Search This Blog

Monday 27 March 2023

KIZUNGUMKUTI ! - 5

  


Simulizi : Kizungumkuti !

Sehemu Ya Tano (5)



Ndani ya dakika mbili Jonas alikuwa amefika katika ofisi ya bosi wake Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kuitika ule wito. Alikuwa kijana mrefu wa wastani na hakuwa na umri wa zaidi ya miaka thelathini.


Alikuwa amevaa shati jeupe la mikono mirefu na juu yake alivaa koti jeusi lililokuwa na mistari myeupe, na saa ya mkononi. Chini alivaa suruali ya kadeti ya rangi ya kaki na buti ngumu za ngozi miguuni.


Yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano alimweleza yule kijana kilichowaleta pale wale maofisa wa polisi na kumpa zile namba nne ambazo ASP Komba na Sajenti Mapambano walikuwa wamezitilia shaka kutoka katika simu ya Yusuf.


“Jonas, tafadhali fuatilia hizi namba kwenye kompyuta na utupatie taarifa zote muhimu za wateja wenye kumiliki namba hizi, ikiwemo majina yao, namba za vitambulisho vyao walivyotumia kusajili, locations zao, na namba zote ambazo zimekuwa zikiwasiliana na namba hizi kwa tarehe husika na saa… sijui itakuchukua muda gani kuifanya kazi hii, maana taarifa hii inatakiwa haraka sana,” yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano alimwambia Jonas huku akimkazia macho.


Jonas aliipokea ile karatasi yenye zile namba akaziangalia zile namba kwa kitambo nkifupi huku akifikiria kidogo, “Wala haitachukua muda, boss. Yote hayo yamo kwenye Kompyuta.”


“Kama nusu saa?” yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano aliuliza kwa shauku.


“Haifiki, ni kama dakika kumi hadi kumi na tano tu zinanitosha kuimaliza kazi.”


“Ooh, basi itakuwa vyema!” yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano alisema huku akitabasamu.


Jonas aliwatupia jicho ASP Komba na Sajenti Mapambano haraka haraka na kuachia tabasamu kisha alitoka haraka huku macho ya wale maofisa wa polisi yakimfuata hadi alipotoka kabisa na kuufunga mlango wa ile ofisi.


“Huyu kijana ndiye tegemeo letu hapa ofisini kwa sasa, kwa kweli anastahili makubwa zaidi… hamtaamini jinsi atakavyoifanya kazi hii kwa uharaka sana na kuleta majibu chanya,” yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano aliwaambia wale maofisa wa polisi baada ya Jonas kuondoka.


“Anaonekana tu kwa jinsi anavyojiamini,” ASP Komba alisema akionekana kuafiki.


“Je, mnadhani hii inaweza kuwa njia sahihi ya kuwakamata hao wezi? Na kama hawakutumia mawasiliano ya simu…” yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano alimuuliza ASP Komba huku akimkazia macho lakini ASP Komba alimkatisha kabla hata hajamaliza kuongea.


“Kwetu, hilo si suala la kudhani, tumekwisha fanya kazi nyingi na ngumu za uhalifu hatari zaidi wa mtandaoni na kufanikiwa. Vyovyote iwavyo lazima tuwatie mbaroni tu,” ASP Komba alisema katika namna ya kujigamba huku akimtupia jicho Jacob.


Kisha yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano aliamua kubadilisha maongezi, na baada ya takriban dakika kumi na tano Jonas alirejea ofisini kwa Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano akiwa ameshika karatasi kadhaa zilizokuwa zimechapwa kwa maandishi ya kompyuta zikiwa na taarifa zote muhimu zilizohitajika.


Alipoingia alizikkabidhi karatasi zile kwa Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Yule Mkurugenzi alizipokea zile karatasi na kuanza kuzipitia papo hapo huku uso wake ukichanua kwa tabasamu dogo la kuridhika na alichokiona. Kisha alimkabishi ASP Komba.


“Naona kijana amefanya kazi nzuri sana, kila ulichohitaji kuhusu hizo namba kimo humo, hebu zipitie kwanza hapa hapa ujiridhishe kabla hujaondoka ili uone kama bado kuna chochote ungependa kutafutiwa.”


ASP Komba na Sajenti Mapambano walizipitia zile karatasi haraka haraka kwa kupokezana kisha ASP Komba alisimama kutoka kwenye kiti alichoketi na kumpa mkono yule Mkurugenzi kumshukuru huku akionesha furaha yake.


“Naona mtaalamu kafanya kazi kubwa na nzuri sana, tunashukuru kwa kweli,” ASP Komba alisema kwa furaha huku akimpa mkono kwa pongezi Jonas.


“Hata hivyo, kuna namba moja kati ya hizo imenisumbua kidogo, ilikuwa imewekewa mfumo maalumu wa kiulinzi,” Jonas alimwambia ASP Komba huku akimtazama kwa makini.


“Una maana gani unaposema mfumo maalumu wa kiulinzi?” ASP Komba alimwuliza Jonas huku akimtulizia macho yake.


“Inaonekana wazi mtumiaji wa namba hiyo ni mtaalamu aliyebobea sana kwenye masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano na ana ufahamu mkubwa sana wa masuala ya kompyuta, aliiwekea namba yake programu maalumu ambayo inamuwezesha mtumiaji wa namba hiyo kutojulikana mahali alipo na ameweza hata kuzuia mawasiliano yake yasiingiliwe na watu wengine, na pia aliifanya namba hiyo kutumika katika simu yake tu.”


“Duh, natumai umefanikiwa kuiondoa hiyo programu ya kiulinzi, siyo?” ASP alimuuliza Jonas kwa shauku huku akimtulizia macho kwa makini.


“Ndiyo, nimeweza kuiondoa programu hiyo japo imenipa shida kidogo, sasa mtaweza kuona jinsi anavyoweza kuwasiliana na watu wengine ingawa mahali alipo wakati anawasiliana na watu bado inaweza kuwa shida,” Jonas alisema huku akishusha pumzi ndefu.


“Hata hivyo, umetusaidia sana… enhe, ni namba ipi kati ya hizi?” ASP Komba alimuuliza Jonas kwa shauku huku akimsogezea zile karatasi.


“Ni hii hapa!” Jonas alisema huku akimwonesha ASP Komba ile namba baada ya kuzitazama zile namba kwa makini.



“Ndiyo, nimeweza kuiondoa programu hiyo japo imenipa shida kidogo, sasa mtaweza kuona jinsi anavyoweza kuwasiliana na watu wengine ingawa mahali alipo wakati anawasiliana na watu bado inaweza kuwa shida,” Jonas alisema huku akishusha pumzi ndefu.


“Hata hivyo, umetusaidia sana… enhe, ni namba ipi kati ya hizi?” ASP Komba alimuuliza Jonas kwa shauku huku akimsogezea zile karatasi.


“Ni hii hapa!” Jonas alisema huku akimwonesha ASP Komba ile namba baada ya kuzitazama zile namba kwa makini.


Endelea...


ASP Komba alibetua kichwa chake huku akiiwekea alama ile namba, “Asante sana, na hii ndiyo namba tutakayoanza nayo katika uchunguzi wetu tukifika tu ofisini,” alisema huku akimtupia jicho Sajenti Mapambano.


“Kazi ya kwanza ambayo tutaweza kuifanya ni kuichunguza kwa umakini zaidi hii namba ya simu yenye programu maalumu ya mfumo wa kiulinzi ili tufahamu Yusuf alikuwa akiwasiliana na nani kwa siri. Nina hakika lazima kuna sababu iliyomfanya mtumiaji wa namba hii kuamua kuificha namba yake hii isionekane na mtu yeyote,” ASP Komba alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Ninatumaini kila kitu kipo sawa, kama kutakuwa na chochote sitasita kuja tena hapa kutaka msaada, tafadhali msinichoke tu,” ASP Komba alimwambia Jacob huku akitabasamu, kisha akampa mkono Jacob.


“Ndugu yangu, tusameheane kwa yote, nadhani umeyaona mazingira ya kazi zetu jinsi yalivyo magumu,” ASP Komba alisema huku akimpa mkono.


“Usijali,” Jacob alisema kwa kifupi huku akiuma mdomo wake wa chini na kushusha pumzi.


Wakaagana kisha ASP Komba na Sajenti Mapambano wakatoka nje ya ile ofisi. Walitembea kwa utulivu huku mawazo mengi yakipita kichwani kwa ASP Komba na walipozifikia zile ngazi wakaanza kuzishuka taratibu na baada ya muda mfupi hatimaye wakawa wamefika eneo la chini la lile jengo na hatimaye wakatokea eneo la Mapokezi. ASP akaona ni vyema wapiti kwanza pale Mapokezi ili kwenda kuaga


“Vipi mmefanikiwa?” yule mhudumu wa Mapokezi alimwuliza ASP Komba huku akitabasamu mara baada ya kuwaona.


“Sana! Wala hatuna cha kulalamikia,” ASP Komba alisema kwa utani huku akiachia tabasamu.


“Haya, karibuni tena,” yule mhudumu alisema huku akiangua kicheko hafifu.


“Nitarudi mara tu nikimaliza kazi hii, lakini safari hii sitakwenda tena ghorofa ya pili bali nitaishia hapa hapa Mapokezi,” ASP Komba alisema kwa utani na wote watatu wakacheka.


* * * * *


“Everything is in position now,” ASP Komba alimwambia Sajenti Mapambano huku akiziangalia taarifa nyeti kwenye kompyuta maalumu ya ofisi iliyokuwa mbele yao ikiwa imeunganishwa na mfumo maalumu wa kiintelijensia uliowawezesha kupata taarifa mbalimbali za kiintelijensia kwa ajili ya kubaini mambo mbalimbali ya uhalifu wa kimtandao.


ASP Komba na Sajenti Mapambano walikuwa wameketi ndani ya chumba cha ofisi ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu katika jengo la Kituo Kikuu cha polisi Dar es Salaam, maarufu kama Central Police.


Chumba cha ofisi ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu kilikuwa kikubwa kilichokuwa upande wa kushoto kabisa mara baada ya kumaliza kupanda ngazi za kuingia katika ghorofa ya tatu kwenye korido pana, kilikuwa hatua chache baada ya kuzipita ofisi za Idara ya Intelijensia ya Jinai na ile ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali.


Kilikuwa chumba kipana na sakafu ya ofisi ile ilifunikwa kwa zulia maridadi jekundu huku katikati ya lile zulia likiwa na nembo kubwa ya Jeshi la Polisi la Tanzania. Chumba kile kilikuwa na meza ndefu ya mikutano iliyozungukwa na viti kumi na mbilii. Viti vitano upande wa kushoto, viti vingine vitano upande wa kulia, kiti kimoja mwanzoni mwa ile meza na kiti kimoja kilikuwa mwisho wa meza.


Upande wa kushoto wa chumba kile kulikuwa na picha kubwa tatu, ya kwanza ilikuwa ni ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, picha ya pili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na picha ya tatu ilikuwa ya Inspekta Jenerali wa Polisi, sote zikiwa zimewekwa kwenye fremu maalumu za vioo na kutundikwa ukutani.


Mbele ya kile chumba ukutani kulikuwa na ramani mbili kubwa. Ramani moja ya nchi ya Tanzania na ramani ya pili ya Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Upande wa kulia kulikuwa na rafu kubwa ya mbao iliyosanifiwa kwa ustadi wa hali ya juu. Ndani ya rafu ile kulipangwa vitabu na majarida mbalimbali.


Kulikuwa na meza kubwa mbili za ofisini zenye majalada mengi juu yake. Bendera ndogo nne zilionekana juu ya zile meza, mbili zikiwa bendera za Taifa na nyingine mbili zilikuwa bendera za Jeshi la Polisi. Vitabu kadhaa vya Katiba ya Tanzania, kidau cha wino, mhuri na kichupa kidogo chenye wino mweupe wa kufutia maandishi.


Nyuma ya meza zile kulikuwa na viti vikubwa vya ofisini vyenye foronya laini na kwenye kiti kimojawapo nyuma ya meza moja yenye kompyuta aina ya IMac alikuwa ameketi ASP Komba na Sajenti mapambano alikuwa amesimama kando yake wakifuatilia taarifa kwenye ile kompyuta.


Pembeni ya ile meza ya ofisini chini yake kulikuwa na mashine ndogo ya kidijitali ya kurudufu, mashine maalumu ya kuchapa barua na nyraka za kiofisi, mashine ya picha na mashine moja ya nukushi.


Upande wa kulia wa ile meza aliyokuwa ameketi ASP Komba kulikuwa na kabati kubwa nadhifu la chuma lenye droo sita. Pia ukutani kulitundikwa saa kubwa ya mshale na pembeni ya saa ile kulikuwa kalenda moja kubwa. Na kando yake kwenye ukuta juu ya rafu kubwa kulikuwa na runinga bapa iliyounganishwa na chaneli tofauti za kimataifa iliyokuwa imetundikwa ukutani.


Kulikuwa na seti moja ya makochi mazuri ya ngozi laini ya sofa yaliyoizunguka meza ya kioo yenye umbo duara na chini ya meza ile kulikuwa na magazeti na majarida kadhaa tofauti na kando ya makochi yale kulikuwa na rafu kubwa ya vitabu na majalada yaliyopangwa kwa ustadi wa hali ya juu. Kulikuwa na kiyoyozi kikubwa mle ndani kilichokuwa kikisambaza hewa safi.


Ki ujumla ofisi ile ilikuwa ya kistaarabu sana yenye samani za kisasa na iliyopangiliwa vizuri na muonekano wake uliendana kabisa na ule kipelelezi wa makosa ya jinai.


ASP Komba alikuwa katika uso wa kusawajika kidogo huku akiwa ameegemea kiti chake. Alikuwa kimya kabisa akiziangalia zile taarifa kwa makini walizokuwa wamepewa kule kwenye ofisi za kampuni kubwa ya simu na kujaribu kulinganisha na taarifa walizokuwa wakizipitia kwenye ile kompyuta. Sajenti Mapambano alisimama akipitia taarifa zile kwa utulivu.


Sajenti Mapambano alibofya kitufe fulani kwenye ile kompyuta na kuanza kupandisha maandishi akitafuta taarifa fulani kisha akaingiza taarifa za namba waliyokuwa wakiichunguza, akaipachika katika kifaa fulani kidogo mithili ya mkebe na kuanza kuibonyeza ile kompyuta. Mara akaguna


“This is very strange! Inawezekanaje hii namba yenye mfumo wa ulinzi ikawa imetumika kuwasiliana na watu wawili pekee yake!” Sajenti Mapambano alisema kwa mshangao huku akikodolea macho kwenye ile kompyuta.


ASP Komba alimtazama kwa makini kisha akaziangalia zile taarifa na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku naye akionesha kushangaa.




Sajenti Mapambano alibofya kitufe fulani kwenye ile kompyuta na kuanza kupandisha maandishi akitafuta taarifa fulani kisha akaingiza taarifa za namba waliyokuwa wakiichunguza, akaipachika katika kifaa fulani kidogo mithili ya mkebe na kuanza kuibonyeza ile kompyuta. Mara akaguna


“This is very strange! Inawezekanaje hii namba yenye mfumo wa ulinzi ikawa imetumika kuwasiliana na watu wawili pekee yake!” Sajenti Mapambano alisema kwa mshangao huku akikodolea macho kwenye ile kompyuta.


ASP Komba alimtazama kwa makini kisha akaziangalia zile taarifa na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku naye akionesha kushangaa.


Endelea...


“Ni kweli, imewasiliana na watu wawili tu! Kwa mujibu wa taarifa za kampuni ya simu namba hizo ni za Yusuf na nyingine ni ya mtu anayeitwa Joram Mbezi. Inaonesha huyu mwenye namba hii na hawa watu wamekuwa wakiwasiliana zaidi katika wiki hizi mbili za mwisho kabla ya kutokea kwa wizi wa mabilioni pale benki,” ASP Komba alisema huku akizikodolea macho zile namba.


“Na kwa mujibu wa taarifa kutoka kampuni ya simu namba hii inamilikiwa na mtu anayeitwa Belinda Jackson,” Sajenti Mapambano alisema huku akizitazama zile karatasi walizozitoa kampuni ya simu, kisha akabonyeza kifute fulani kwenye ile kompyuta na baada ya dakika kama tatu hivi akasimama na kuvuta pumzi ndefu.


“Inabidi kupata taarifa za hawa watu wawili, Belinda Jackson na Joram Mbezi ili tuwajue ni kina nani hasa kabla hatujawaunganisha kwenye hili tukio la wizi, nadhani tunaweza kufuatilia taarifa zao kwenye mtandao wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Nida, na ule wa kiintelijensia wa Jeshi la Polisi,” ASP Komba alisema huku akiminya midomo yake.


Sajenti Mapambano alibofya kwenye ile kompyuta na kuingia kwenye mtandao maalumu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ambao ulikuwa umeunganishwa na ile kompyuta ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu.


Baada ya kuperuzi kwa dakika kadhaa na kupata taarifa kamili za Joram Mbezi, Sajenti Mapambano aliingia kwenye mtandao mwingine wa kiintelijensia na kutafuta taarifa zaidi za Joram Mbezi ili kuona kama amewahi kuhusishwa na matukio yoyote ya uhalifu, mara akaonekana kushtuka kidogo.


Alisimama akafikicha macho yake na kuzitazama tena zile taarifa akiwa haamini macho yake.


“Joram Mbezi, mfanyabiashara wa kuuza madini ya rubi, tanzanite na mengineyo, anaishi eneo la Sinza jijini Dar es Salaam na ana umri wa miaka takriban hamsini. Historia yake imekuwa yenye utata kidogo kwa kuwa amewahi kuhusishwa mara kadhaa na matukio ya uhalifu katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania…” Sajenti Mapambano alisema huku akisoma zile taarifa kutoka katika ile kompyuta ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu.


“Ila huyu Belinda Jackson inaonekana habari zake zinakanganya sana inawezekana ni mtu hatari mno kuliko tunavyoweza kudhani kwani taarifa zinadai kuwa alikuwa daktari bingwa wa afya ya akili katika Hospitali ya Milembe mkoani Dodoma na alifariki miaka mitatu iliyopita. Inashangaza kuona kuwa hii namba yake imesajiliwa miezi mitatu tu iliyopita na imetumika zaidi wiki mbili za mwisho kabla ya tukio la wizi pale benki…” Sajenti Mapambano alisema huku akimtazama ASP Komba. Wakatazamana kwa kitambo kifupi, kila mmoja akijaribu kutafakari kwa kina.


“Kwa hiyo maana yake ni kwamba marehemu Belinda aliisajili hii namba wakati tayari akiwa marehemu kwa takriban miaka mitatu!” ASP Komba aliuliza kwa mshangao huku akihisi uwepo wa kitu kisichokuwa cha kawaida kwenye ile namba.


“Hapa ndipo penye utata wenyewe, nadhani kuna namna hapa, ndiyo maana hii namba ikawekewa mfumo wa siri wa kiulinzi ili mtu huyu asiweze kufuatiliwa katika mawasiliano yake na hawa watu wawili, Yusuf Akida na Joram Mbezi. Inawezekana kabisa kwa kumbana Yusuf tutaweza kumtambua huyu mtu anayejiita Belinda, na huenda akawa na laini nyingine za siri ambazo huzitumia kuwasiliana na watu wengine zaidi,” Sajenti Mapambano alisema na kuanza kutafuta taarifa zaidi.


ASP Komba alichoka kabisa, aliamua kusimama na kuelekea kwenye dirisha, kwa dakika kadhaa alitulia pale dirishani huku akitazama nje kupitia ukuta msafi wa kioo cha lile dirisha, aliyatazama magari mbalimbali yaliyokuwa yakipita barabarani huku akionekana kuyachunguza kwa utulivu, mikono yake alikuwa ameiegemeza pale dirishani.


Kisha macho yake yakahamia kutazama pale chini ya lile jengo kulipokuwa na magari machache yaliyoegeshwa katika sehemu ya maegesho ya magari ya lile jengo. Na hapo akaliona gari aina ya Toyota Lexus RX la rangi nyeusi likiegeshwa sehemu ile. Lile gari ASP Komba alilitambua mara moja kuwa lilikuwa gari la Jacob.


* * * * *


Ilikuwa saa kumi na mbili na nusu wakati Jacky alipokuwa akiingia katika sebule kubwa yenye masofa mazuri nyumbani kwa Jacob.


“It’s a nice place, I really liked your home,” (Ni sehemu nzuri, nimepapenda sana nyumbani kwako) Jacky alimwambia Jacob wakati akiingia katika sebule ile kubwa huku akiitazama kwa makini. Sakafuni kulikuwa na zulia zuri la rangi nyekundu huku katikati ya sebule ile kukiwa na meza fupi ya kioo yenye umbo la yai.


Upande wa kushoto wa ile sebule kwenye kona kulikuwa na runinga pana iliyofungwa ukutani huku chini yake kukiwa na meza fupi nyeusi yenye sistimu ya muziki, deki ya Dvd, kingamuzi cha DStv na vinyago vya Kimakonde vilivyokuwa vimepangwa kwa ustadi wa hali ya juu.


Upande wa kulia wa ile sebule kwenye kona nyingine kulikuwa na meza fupi ya mapambo. Kutoka pale alipokuwa amesimama Jacky upande wa kulia kulikuwa na mlango mkubwa wa sebule ile katikati ya madirisha mapana ya vioo yaliyofunikwa kwa mapazia marefu. Ulikuwa ni mlango wa kuelekea kwenye vyumba vya kulala vya ile nyumba.


Nyumba ya Jacob ilikuwa nzuri na kubwa ya kisasa iliyozungukwa na miti mizuri ya vivuli na sehemu za wazi zenye bustani nzuri ya maua na nyasi za kijani kibichi zilizokatiwa vizuri.


Nyumba ile ilikuwa na ukuta mfupi kuizunguka wenye nakshi za hapa na pale kiasi cha kumruhusu mtembea kwa miguu kuweza kuona mle ndani kwa shida kidogo. Mbele ya ile nyumba kulikuwa na geti kubwa jeusi na kando ya lile geti kulikuwa na kitufe cha kengele.


Ilikuwa ni nyumba kubwa ya kisasa ya ghorofa moja iliyokuwa na madirisha makubwa ya kisasa ya vioo na baraza kubwa mbele yake.


Nje ya nyumba ile upande wa kulia kulikuwa na banda la wazi la kuegeshea magari na alipochunguza akaona kuwa kulikuwa na magari awili ya kifahari aina ya Mercedes Benz E-class limousine jeusi lenye milango sita na gari aina ya Toyota Lexus RX la rangi nyeusi.


Sehemu nyingine ya mandhari ya nyumba ile ilizungukwa na miti mirefu na mikubwa ya kivuli, hata hivyo matawi makubwa ya miti ile yalikuwa yametengeneza vichaka vilivyosababisha kiza fulani.


Sehemu ya mbele ya ile nyumba ilikuwa imezungukwa na bustani nzuri ya maua ya kupendeza yaliyotoa harufu nzuri na katikati ya bustani ile kulitengenezwa njia nzuri ya kutembea kwa miguu kwa vitofali vidogo vilivyokuwa vinavutia.


“Sijui unatumia kinywaji gani?” Jacob alimwuliza Jacky huku akimtazama kwa makini.


“Mvinyo mwepesi tafadhali,” Jacky alisema, na hapo Jacob akainuka na kuelekea kwenye jokofu kubwa la vinywaji.na kurudi na chupa ya mvinyo, akamimina katika bilauri mbili, moja akampatia Jacky na nyingine akabaki nayo mwenyewe, kisha waligongesha zile bilauri kutakiana afya njema huku Jacob akiachia tabasamu pana.




“Sijui unatumia kinywaji gani?” Jacob alimwuliza Jacky huku akimtazama kwa makini.


“Mvinyo mwepesi tafadhali,” Jacky alisema, na hapo Jacob akainuka na kuelekea kwenye jokofu kubwa la vinywaji.na kurudi na chupa ya mvinyo, akamimina katika bilauri mbili, moja akampatia Jacky na nyingine akabaki nayo mwenyewe, kisha waligongesha zile bilauri kutakiana afya njema huku Jacob akiachia tabasamu pana.


Endelea...


Alikunywa kidogo na kuiweka bilauri yake juu ya meza huku akimtazama Jacky katika namna ya kuuajabia uzuri wake. Jacky alikuwa amevaa gauni jepesi jeusi la kata mikono lililokuwa limelichora vyema umbo lake na kuishia juu ya magoti yake na hivyo kuifichua hazina nzuri ya miguu yake. Miguuni alikuwa amevaa viatu vyekundu vyenye visigino virefu.


Kope zake zilikuwa zimekolea wanja mwembamba mfano wa mwezi mwandamo na kuyafanya macho yake makubwa, meupe na legevu yaifanye akili ya Jacob isikinai kumtazama muda wote. Kila wakati tabasamu lake lilizisogeza kingo pana za mdomo wake wa juu na wa chini na hivyo kufanya meno yake meupe yaliyopangika vizuri kuonekana bila kificho.


Alikuwa amevaa hereni nzuri za madini ya tanzanite kwenye masikio yake huku mkufu mwembamba wa dhahabu safi ukiizunguka vyema shingo yake nyembamba na kisha kidani chake kupotelea katikati ya matiti yake.


“When you called me you really confused me a lot, and so far I don’t know what’s exactly the problem can be that makes you want to see me so quickly!” (Uliponipigia simu kwa kweli ulinichanganya sana, na hadi sasa sijajua una tatizo gani kiasi cha kutaka kuniona haraka kiasi hiki!) Jacob alisema huku akipiga funda jingine la mvinyo na kuketi karibu ya Jacky huku akimtazama kwa makini.


“First I must thank you for giving me such great honor to welcome me to your home. A great person like you to invite someone like me is not a small thing,” (Kwanza nakushukuru sana kwa kunipa heshima kubwa kama hii kunikaribisha nyumbani kwako. Mtu mkubwa kama wewe kukubali kunikaribisha mtu kama mimi si jambo dogo) Jacky alisema kwa mzaha huku akilazimisha tabasamu.


“Stop flattering me, here is your home and you don't need to ask to come here, you’re welcome anytime, by the way, I’d not want to miss an angel like you. You don’t know the joy I had after receiving your phone call. After many years of escaping me today I am lucky to be with you, just the two of us, alone, my heart is full of joy,” (Acha kunizingua, hapa ni nyumbani kwako na huna haja ya kuomba kuja, muda wowote unakaribishwa, hata hivyo, nisingeweza kukosa kuonana na malaika kama wewe. Huwezi kujua furaha niliyokuwa nayo baada ya kupokea simu yako. Baada ya miaka mingi ya kunikimbia hatimaye leo hii nimepata bahati ya kuwa na wewe, tukiwa wiwili tu, faragha, moyo wangu umejaa furaha sana) Jacob alisema huku akiupitisha mkono wake mmoja nyuma ya Jacky na kuanza kumpapasa nyama za mgongo.


Jacky alijitahidi kutabasamu lakini uso wake haukuonesha furaha na wala haukuwa na tashwishwi yoyote, alionesha kuwa alikuwa jambo zito lililokuwa likimtatiza sana moyoni, alikuwa na huzuni moyoni iliyojionesha wazi wazi kwenye macho yake ingawa alijitahidi sana kuificha hali ile lakini hakufanikiwa.


Jacob alimtazama Jacky kwa makini na kuhisi uwepo wa jambo lisilo la kawaida, moyo wake ukaingiwa na ganzi huku akijaribu kujiuliza nini kilichokuwa kikimtatiza Jacky?


Jacob alijikuta akiiona siku ile kama siku iliyokuwa imebeba matukio mabaya yenye kumuumiza roho yake, kwanza rafiki yake Yusuf alikuwa mahabusu baada ya kuhusishwa na tukio la wizi wa mabilioni, alikwenda kituo cha polisi mara mbili, mara ya pli akiwa ameongozana na mke wa Yusuf, Mama Jasmine kujaribu kumshawishi ASP Komba ili waweze kumwekea dhamana Yusuf.


Ushawishi wake uligonga mwamba mara mbili, hasa kwa kuwa ilionekana dhamana ile ingeweza kusababisha mchakato wa upelelezi wa kesi ile uwe mgumu zaidi. ASP Komba alimweleza Jacob kuwa kulikuwa na watu wawili wahusika katika wizi ule wa mabilioni, Joram Mbezi na Belinda Jackson waliopaswa kupatikana kwanza…


Jacob aliyakumbuka yote, na sasa alikuwa sebuleni na Jacky, alijikuta akimtazama Jacky machoni kwa udadisi zaidi na kumsogeza zaidi karibu yake huku akimkumbatia, “Ni nani aliyekuudhi mpenzi wangu?” Jacob alimuuliza Jacky, hata hivyo Jacky hakujibu badala yake alikilaza kichwa chake kwenye kifua cha Jacob.


“Niambie mpenzi wangu, nani aliyekuudhi nimshughulikie, you know I don't want to see you so sad!” (…unajua sipendi kukuona ukiwa una huzuni kiasi hiki!) Jacob alisema na kumfanya Jacky ainue uso wake kumtazama Jacob usoni huku macho yake yakionesha kuzingirwa na malenge lenge ya machozi.


“Hakuna aliyeniudhi, mpenzi,” Jacky alisema kwa sauti laini ya chini lakini iliyokuwa imebeba uchungu mwingi.


“Now what makes you so sad?” (Sasa nini kinachokufanya kuhuzunika kiasi hiki?) Jacob aliuliza kwa udadisi.


“It’s you,” (Ni wewe) Jacky alijibu na kumshtua sana Jacob, kitendo kilichomfanya Jacob akamkazie macho kumtazama kama ambaye hakuwa amemsikia vizuri.


“Mimi!” Jacob aliuliza kwa mshangao.


“Ndiyo, ni wewe,” Jacky alisisitiza huku akiendelea kumtazama Jacob kwa huzuni.


“What have I done to you, my love?” (Kwani nimekufanya nini, mpenzi?) Jacob alimuuliza Jacky huku akimtazama kwa makini.


Jacky alivuta pumzi ndefu kisha akazishusha taratibu na kuminya midomo yake huku akimtulizia macho, “To be honest, I began to forget you, but now you’ve come back into my life and hurt the sore that started to heal,” (Kusema ukweli, nilianza kukusahau, lakini sasa umerudi katika maisha yangu na kutonesha kidonda kilichoanza kupona) Jacky alisema huku akijiegemeza kifuani kwa Jacob.


“I’m so sorry for what happened, but the truth is that I still love you very much, I couldn’t stop myself from following you,” (Nasikitika samahani kwa kilichotokea, lakini ukweli ni kwamba bado nakupenda sana, sikuweza kujizuia kukufuatilia) Jacob alimwambia Jacky huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


Jacky alimtazama Jacob machoni na kutabasamu, “How many of you live here?” (Hivi humu ndani mnaishi wangapi?)


“For now I’m all alone… but I live with my two siblings, a young sister Daisy and a young brother Goodluck, they’ve gone for a short vacation in Songea…” (Kwa sasa niko peke yangu… ila naishi na ndugu zangu wawili, wa kike Daisy Haule na wa kiume Goodluck Haule, ambao wapo Songea kwa likizo fupi…) Jacob alisema huku akimtazama Jacky na kutabasamu.


“What is it?” (Kwani vipi?) kisha Jacob akamuuliza Jacky kwa shauku.


“I’m just curious, you live alone in a big building like this! No wife, no servant to serve you?” (Najiuliza tu, unaishi peke yako kwenye jumba kubwa kama hili! Huna mke, huna hata mtumishi wa kukusaidia kazi?)



“What is it?” (Kwani vipi?) kisha Jacob akamuuliza Jacky kwa shauku.


“I’m just curious, you live alone in a big building like this! No wife, no servant to serve you?” (Najiuliza tu, unaishi peke yako kwenye jumba kubwa kama hili! Huna mke, huna hata mtumishi wa kukusaidia kazi?)


Endelea...


“I told you I've never get married since you ran away from me… but I have a maid who leaves after she has finished her chores.” (Nilikuambia sijawahi kuoa tangu uliponikimbia… lakini nina mfanyakazi ambaye huondoka mara tu akishamaliza kazi zake).


“Ooh!”


“I don't like a crowd of servants, because I’m not the king…” (Sipendi kundi kubwa la wafanyakazi wa kunihudumia, kwa sababu mimi siyo mfalme…) Jacob alisema na kuongeza, “By the way, you called me, right? What were you saying?” (Hata hivyo, ulinipigia, au siyo? Ulikuwa unasemaje?)


“I have nothing, I just wanted to be with you,” (Sina, nilitaka tu kuwa na wewe) Jacky alisema huku akiangalia chini kuyakwepa macho ya Jacob. Jacob alimtazama kwa makini na kutingisha kichwa chake.


“Come on, darling… just tell me! I know you have something to tell me, I promise you, from now on I’m going to protect you. I’m going to make you the happiest woman on earth. Nobody will never hurt you,” (Niambie mpenzi… niambie! Najua una jambo la kuniambia, nakuahidi, kuanzia sasa nitakulinda. Nitahakikisha unakuwa mwanamke mwenye furaha kuliko wote duniani. Hakuna atakayeweza kukuumiza) Jacob alisema huku akimtazama Jacky kwa uadisi.


“I just wanted to see you… I wanted to spend this moment with you, now I feel like I’m in heaven,” (Nilitaka kukuona… nilitaka kuwa na wewe muda huu, sasa najihisi kama nipo mbinguni) Jacky alimwambia Jacob huku akiachia tabasamu pana na kuongeza, “…though I’m married and I’ve tried very hard to get rid of you but I have failed…” (…ingawa nimeolewa na nimejitahidi sana kukutoa moyoni mwangu lakini nimeshindwa…)


“I'm glad to hear it, but when I lost you I lost something worth more than the wealth I have, I didn't see how I would live without joy or peace in my heart,” (Nina furaha kusikia hivyo, lakini nilipokupoteza nilipoteza kitu cha thamani kuliko hata utajiri nilio nao, sikuona nitaishi vipi bila furaha wala amani moyoni mwangu,” Jacob alisema kwa hisia huku akimtazama Jacky.


“Jacob, you never lost me. I was there and I’ll always be there by your side. But there is one important thing I want to tell you…” (Jacob, hujawahi kunipoteza. Nilikuwepo na siku zote nitakuwa na furaha nikiwa na wewe. Lakini kuna kitu cha muhimu nataka kukueleza…) Jacky alisema na kuonekana kusita.


“What is that?”(Kitu gani?) Jacob alimuuliza Jacky baada ya kumuona akisita huku akimtazama kwa makini.


Jacky akamshika Jacob mikono huku akimtazama usoni, “I love you so much. I love you from my heart. The love I have for you cannot be expressed. What I feel for you is more than love. The love I have for you cannot be expressed. I think to run away from my marriage so that I can open a new page of life with you…” (Nakupenda sana. Nakupenda toka ndani ya moyo wangu. Upendo nilio nao kwako siwezi kuueleza. Ninavyojihisi juu yako ni zaidi ya pendo… Ninafikiria kutaka kuikimbia ndoa ndoa yangu ili nifungue ukurasa mpya wa maisha pamoja nawe…)


“Darling, you don’t have an idea how many days and night I’ve been waiting to hear those words you’ve just said to me. I believe our encounter was not unfortunate, God had His purposes even though on the one hand today has been my sad day…” (Mpenzi, hujui ni kwa muda gani nimekuwa nimekuwa nikisubiri kusikia maneno hayo uliyoniambia. Naamini kukutana kwetu haikuwa bahati mbaya, Mungu alikuwa na makusudi yake japokuwa kwa upande mmoja siku ya leo imekuwa ya huzuni kwangu…)


“I wanted to ask you, how it went to the police station?” (Nilitaka kukuuliza, ilikuwaje kule kituo cha polisi ulikokwenda?) Jacky alimuuliza Jacob kwa sauti tulivu kisha akamvuta na kumbusu huku akimpapasa sehemu mbali mbali za mwili wake.


“The police have refused to give him bail for fear that the investigation can be destroyed…” (Polisi wamekataa kumpa dhamana kwa kuhofia kuvurugwa kwa upelelezi…) Jacob alisema kwa huzuni.


“So, what have they found so far? You told me they came to your office to monitor the phone numbers that were communicating with your friend Yusuf,” (Kwa hiyo, wamegundua nini hadi sasa? Uliniambia walikuja ofisini kwenu kufuatilia namba za simu zilizokuwa zinawasiliana na huyo rafiki yako anayeitwa Yusuf) Jacky aliuliza kwa shauku.


“They have already found about a man named Joram Mbezi, and they are still struggling to find someone who calls herself Belinda Jackson…” (Tayari wamegundua kuhusu mtu mmoja anayeitwa Joram Mbezi, na bado wanahangaika kumtafuta mtu mwingine anayejiita Belinda Jackson…) Jacob alisema na kumfanya Jacky ashtuke.


“So they have already catched up Joram?” (Kwa hiyo tayari wameshamkata huyo Joram?) Jacky aliuliza huku akionesha kushtuka sana, alimkazia macho Jacob.


“Not yet, tomorrow they’ll start chasing him… but what has that to do with us?” (Bado, kesho wataanza kumfuatilia… lakini haya yanahusianaje na sisi?)


“It's just humanity… just to care for one another joy and sorrow.” (Ni ubinadamu tu… ni kujaribu kujali furaha na huzuni za watu wengine).


“Good. Now let’s leave this and focus our own issues. Let’s enjoy life my angel,” (Vizuri. Sasa tuachane na hayo na tuangalie masuala yanayotuhusu. Tufurahie maisha malaika wangu) Jacob alisema kisha akamvuta Jacky na kumbusu, akaanza kumpapasa sehemu mbalimbali za mwili wake.


Jacky alijilegeza, akamkumbatia Jacob na kuanza kumchezea maeneo nyeti ambayo ghafla yalifura kwa hasira kali, “I know you have been waiting for this for so long, this’s what you want Jacob…” (Najua umekuwa unasubiri kitu hiki kwa muda mrefu, hiki ndicho unachokitaka Jacob) Jacky alimwambia Jacob na kumporomoshea mabusu mfululizo yaliyomchanganya zaidi.


“Jacky, in my life I’ve met many women but none of them are like you, I love you very much Jacky,” (Jacky, katika maisha yangu nimekutana na wanawake wengi lakini hakuna kati yao aliye kama wewe, nakupenda sana Jacky) Jacob alisema na kumkumbatia Jacky kwa nguvu.


Jacky aliachia tabasamu kisha akalipandisha juu gauni lake na hapo nguo yake ya ndani ikaonekena, taratibu akaanza kuishusha ile nguo na kuiweka pembeni huku akimtazama Jacob kwa namna iliyozidi kumchanganya mno.





“Jacky, in my life I’ve met many women but none of them are like you, I love you very much Jacky,” (Jacky, katika maisha yangu nimekutana na wanawake wengi lakini hakuna kati yao aliye kama wewe, nakupenda sana Jacky) Jacob alisema na kumkumbatia Jacky kwa nguvu.


Jacky aliachia tabasamu kisha akalipandisha juu gauni lake na hapo nguo yake ya ndani ikaonekena, taratibu akaanza kuishusha ile nguo na kuiweka pembeni huku akimtazama Jacob kwa namna iliyozidi kumchanganya mno.


Endelea...


Muda huo huo Jacky alimsogelea Jacob akaanza kuufungua mkanda wa suruali yake na mara suruali hiyo ikaanguka chini huku Jacob akibakiwa na boksa tu. Kisha aliivuta taratibu ile boksa ya Jacob, akaishusha hadi magotini na kuupeleka mkono wake ikulu. Jacob alianza kuhema ovyo utadhani bata, hakujiweza tena.


Jacky alimtazama Jacob kwa makini kisha akamsukuma, Jacob alianguka sakafuni kwenye zulia laini. Kabla hajajua afanye nini, Jacky alikuja juu yake na kumkalia, na muda mfupi uliofuata walikuwa pale sebuleni juu ya zulia, Jacob chini na Jacky juu huku Jacob akiishuhudia mijongeo ya Jacky ya taratibu alipokuwa akipanda juu na kushuka chini…


* * * * *


Saa tatu usiku wa siku ile iliwakuta Kabwe na Liston wakiwa katika ukumbi wa chini wa baa ya Masai Club iliyokuwa katika Barabara ya Mwinjuma, Kinondoni mkabala na benki ya ACB jijini Dar es Salaam.


Masai Club ilikuwa ni klabu ya usiku ya kisasa kabisa yenye kila kionjo cha burudani cha daraja la kimataifa ikiwa na kumbi tatu za baa, ukumbi mmoja ulikuwa katika eneo la chini na kumbi mbili zilikuwa ndani ya klabu.


Kulikuwa na ukumbi kwa ajili ya kujipatia vyakula vya kimataifa wenye meza ndefu za kisasa zilizozungukwa na viti vizuri vya sofa vyenye foronya laini pamoja na ukumbi mwingine mkubwa wenye jukwaa zuri lililokuwa linatazamana na viti vingi vya kisasa kwa ajili ya kufanyia shughuli za muziki na mikutano mbalimbali.


Kila ukumbi ulikuwa umejitenga na hivyo kutengeneza mgawanyo mzuri wa starehe tofauti zenye utulivu zilizoweza kufanyika kwa wakati mmoja.


Kabwe na Liston walikuwa katika ukumbi wa chini wa baa uliokuwa mkubwa na wenye uwezo wa kumeza watu wengi bila bugudha yoyote huku ukiwa na meza nyingi ndogo fupi na pana zilizozungukwa na viti vya mbao na vya plastiki.


Pia kulikuwa na meza nyingi za mchezo wa Pool table na kulikuwa na taa nzuri zenye mwanga hafifu zilikuwa zikiangaza mle ndani.


Kabwe na Liston walikuwa wameketi kwenye stuli ndefu katika kaunta ya ile baa, Kabwe alikuwa kaegemea kaunta na mbele yake kulikuwa na chupa kubwa ya pombe kali aina ya Grant’s Blended Scotch Whisky na bilauri.


Liston alikuwa akiongea na msichana mmoja mfanyakazi wa pale baa, aliyekuwa ameketi upande wa pili wa ile kaunta.


Kwenye ukumbi ule kulikuwa na wateja wengi waliokuwa wameketi kwa utulivu huku wakijipatia vinywaji na vyakula na wengine wakiendelea na maongezi yao.


Mzee mmoja alikuwa ameketi kwenye meza ya pembeni kabisa na msichana mzuri ambaye kimuonekana angeweza hata kuwa mjukuu wake na pengine ilikuwa hivyo, na walikuwa wakinywa soda.


Hapa na pale kulikuwa wasichana warembo kama machangudoa, waliokuwa wanazunguka zunguka wakiwa wamevaa nguo zilizokuwa zinaonesha sehemu kubwa ya miili yao na kuwavutia mno wanaume.


Kutokana na pilika pilika zao wakijipitisha huku na kule walionekana bila shaka yoyote kuwa walikuwa wakingoja kuopolewa.


Kulikuwa na wahudumu wa kike warembo waliokuwa wakihudumia wateja waliokuwa mle ndani ya ukumbi. Muziki laini ulikuwa ukisikika taratibu mle ndani ya ukumbi na hivyo kuzikonga vizuri nyoyo za watu waliokuwa ndani ya ule ukumbi.


Runinga pana zilizokuwa zimetundikwa ukutani mle ukumbini zilikuwa zimejikita katika kurusha burudani mbalimbali.


Kabwe na Liston walikuwa wameanza kulewa na muda ule Kabwe alikuwa akipiga kelele zilizokuwa zikiwakera wateja wengine ndani ya ule ukumbi wa baa. Wateja waliokuwemo ndani ya ule ukumbi walikuwa wakimtazama Kabwe kwa mshangao.


Kabwe aliinuka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia akiwa ameshika ile chupa kubwa ya pombe kali na kuimimina yote chini huku akipiga kelele na kuyumba.


“Hii ni trela tu, picha kamili keshokutwa! Hakyamungu keshokutwa hakai mtu hapa… mi naapa! Nitakunywa na nitatembea uchi ukumbi mzima. Mademu wakinimaindi poa tu au vipi kichaa wangu?” Kabwe alipiga kelele na kuwafanya watu wote wageuke kumtazama kwa mshangao.


Muda ule Liston alikuwa analazimisha kumshika matiti dada mmoja asiyemjua, aliyepita karibu yake. Yule dada alikuwa amevaa t-shirt laini ya rangi nyeupe, sketi fupi ya rangi ya pinki, viatu virefu vya rangi ya pinki vyenye visigino virefu na wigi lenye nywele ndefu aligeuka kumtazama Liston kwa hasira na kusonya.


Kuona vile Liston alimvuta yule dada kwa nguvu na kumkumbatia kwa kuzungusha mikono yake kwenye kiuno cha yule dada. Yule dada alimsukuma Liston kwa nguvu, akamtazama kwa dharau kuanzia juu hadi chini, kisha akabinua midomo yake kwa dharau na kusonya.


“Wewe kaka vipi! Unadhani kila mwanamke anayeingia hapa ni malaya? Mimi siko hapa kujiuza,” yule dada alisema kwa hasira huku akimkazia macho Liston.


“I don’t care who you are! Kama siyo malaya unatafuta nini hapa? Si ungekaa na mumeo nyumbani!” Liston alisema kwa sauti ya kilevi huku akiyumba.


“Wewe ni nani hadi unipangie maisha?” yule dada alisema kwa hasira na kusonya huku akibinua midomo yake kwa dharau.


“Mijanaume mingine sijui vipi, sijaja kwako kuomba msaada, kwa kipi kwanza ulichokuwa nacho!” alisema na kuanza kupiga hatua kuondoka.


“I don’t give a shit!” Liston alisema huku akimdaka mkono yule dada na kuung’ang’ania huku akimvutia kwake huku akimfinyia macho yake kilevi.


“We mwanamke, unadhani mimi bwege kama hao mabwana zako, eh? Mimi nina hela ya kuulisha ukoo wenu wote kwa mwaka mzima,” Liston alisema huku akitema mate ya ulevi.


Yule dada aliutoa mkono wake kwa nguvu kutoka kwenye mkono wa Liston na kumchapa kibao cha uso huku akionekana kupandwa na hasira. Kisha aliondoka haraka kutoka eneo lile na kukimbilia nje ya ukumbi. Liston alijipangusa uso wake huku akisonya kwa hasira, kisha aligeuka kumtazama Kabwe.


“Eti yule malaya ananiletea pozi! Sasa keshokutwa ndiyo atanitambua mimi ni nani labda nisimuone, nitafanya mambo juu ya kaunta…” Liston alisema.


“Umeona eh! Yule bwana si katuahidi kutukatia hamsini zetu! Keshokutwa ndo watajua sisi ni nani, watu tumefanya kweli bladikenge, keshokutwa ndo keshokutwa, hapakaliki hapa,” Kabwe alipaza sauti yake na kurusha mkono wake hewani kitendo kilichomfanya kumpiga mwanamume mmoja aliyekuwa akipita karibu yake.


Wakati yule mwanamume akitaka kuzozana na kabwe mara yule dada aliyemkimbia Liston akarudi mle ndani ya ule ukumbi akiwa ameongozana na Meneja wa ile klabu na kuonekana akinyoosha kidole chake kuelekeza walipokuwa Kabwe na Liston.




“Eti yule malaya ananiletea pozi! Sasa keshokutwa ndiyo atanitambua mimi ni nani labda nisimuone, nitafanya mambo juu ya kaunta…” Liston alisema.


“Umeona eh! Yule bwana si katuahidi kutukatia hamsini zetu! Keshokutwa ndo watajua sisi ni nani, watu tumefanya kweli bladikenge, keshokutwa ndo keshokutwa, hapakaliki hapa,” Kabwe alipaza sauti yake na kurusha mkono wake hewani kitendo kilichomfanya kumpiga mwanamume mmoja aliyekuwa akipita karibu yake.


Wakati yule mwanamume akitaka kuzozana na kabwe mara yule dada aliyemkimbia Liston akarudi mle ndani ya ule ukumbi akiwa ameongozana na Meneja wa ile klabu na kuonekana akinyoosha kidole chake kuelekeza walipokuwa Kabwe na Liston.


Endelea...


Yule Meneja alikuwa mwanaume mfupi mwenye sura ya umbo duara, miwani iliyokuwa imetuama kwenye macho yake makubwa, pua ya kibantu na mdomo wenye kingo pana uliokuwa umezungukwa na ndevu zilizokuwa zimenyolewa vizuri mtindo wa “O”. Alikuwa na kitambi cha ukwasi huku akiwa amevaa suti ya rangi nyeusi, shati la rangi ya kijivu na tai nyekundu shingoni.


Aliwafuata Kabwe na Liston na kuongea nao kwa kitambo kifupi akiwasihi kunywa pombe kistaarabu na kutowabughudhi wateja wengine au kama hawawezi basi waondoke. Kabwe na Liston hawakufurahishwa kupangiwa jinsi ya kutumia fedha zao, walionekana kuchukia sana na kuondoka kwa hasira, lakini waliahidi kurudi tena siku nyingine.


* * * * *


Saa tatu kasoro robo usiku Jacky alikuwa amesimama sebuleni katika nyumba ya Jacob akiwa tayari amekwisha vaa nguo zake akitaka kuondoka. Hiyo ilikuwa ni baada shughuli pevu ya raundi mbili mfululizo kutoka kwa Jacob iliyomuacha hoi.


“You are so wonderful Jacky. I swear in heaven and earth, I'll never find a woman who knows how to make love like you. You are so amazing,” (Wewe ni ajabu sana Jacky. Naapa kwa mbingu na ardhi, sitakuja kumpata mwanamke anayeyajua mapenzi kama wewe. Unashangaza sana) Jacob alimwambia Jacky baada ya mzunguko wa kwanza kumalizika.


“Where are you going, come here, darling,” (Unaenda wapi, njoo hapa, mpenzi) Jacob alimwambia Jacky baada ya kumuona akijiinua kutoka pale sakafuni.


“I need to call my husband first, I don't want to make him worried,” (Nahitaji kumpigia simu mume wangu kwanza, sitaki kumfanya apate wasiwasi) Jacky alimwambia Jacob huku akichukua simu yake na kuelekea bafuni.


Alijifungia mle bafuni na kumpigia simu Carlos, akamweleza yote aliyoyasikia kutoka kwa Jacob kuhusu Kisu. Alimtaka Carlos afanye kila awezavyo kuwasiliana na Kisu na kumgawo wake ili atoroke nchi kabla polisi hawajamfikia, na alipomaliza kuongea na Carlos alirejea pale sebuleni na kumkuta Jacob akimsubiri kwa hamu.


“Hmm! It was not unfortunate, I wanted this to happen. Although I don't like but I needed to do this for a special reason. It has also helped me discover what was hidden inside me, obviously I do love Jacob. I deeply love him and for that I can't argue with my soul…” (Hmm! Haikuwa ni bahati mbaya, nilihitaji kitu kama hiki. Japo sipendi lakini nilihitaji kufanya hivi kwa sababu maalumu. Pia imenisaidia kugundua kilichokuwa kimejificha ndani mwangu, ni wazi bado nampenda Jacob. Nampenda sana na kwa hilo siwezi kubishana na nafsi yangu…) Jacky aliwaza wakati akimfuata Jacob aliyekuwa bado kajilaza pale sakafuni.


Jacob hakusema chochote alimvuta Jacky huku akimtazama kwa macho ya uchu kama fisi aliyeona mfupa na kumkumbatia kwa nguvu huku akimporomoshea mabusu mazito mazito. Jacky alijikuta hajiwezi tena na alihitaji huduma kwa mara nyingine tena.


Jacky alikifahamu alichokihitaji Jacob, hakumkawiza akaanza manjonjo yake na kumpatia huduma, wakaingia katika mzunguko wa pili huku ile sebule ikijazwa na vilio vya mahaba toka kwa Jacky kuashiria raha aliyokuwa akiipata. Walichezeshana gwaride la uhakika na hadi wanamaliza mzunguko wa pili wote walikuwa hoi bin taaban.


“Jacky, you are still hot, my love,” (Jacky, hakika bado unadai mno, mpenzi wangu) Jacob alimwambia Jacky huku akitweta baada ya kumaliza ule mzunguko wa pili. Jacob alikuwa amejilaza chali pale sakafuni juu ya zulia nene la manyoya akitiririkwa na jasho jingi. Shughuli aliyoifanya haikuwa ndogo. Jacob alishusha pumzi na kujiinua kutoka pale katika zulia alikokuwa amelala, akajimiminia mvinyo katika bilauri yake na kunywa huku akitweta.


Jacky alichukua nguo zake na kukimbilia bafuni na baada ya muda mfupi alitoka akiwa tayari amekwisha vaa nguo zake zote na kuchukua mkoba wake.


“I thought today you would spend the night with me, darling?” (Nilidhani leo ungekesha nami, mpenzi?) Jacob alimuuliza Jacky huku akimtazama kwa makini na kumfanya Jacky anyanyue mkono wake na kuitazama tena saa yake ya mkononi.


“It’s quarters to nine, my love, I don't want to upset my husband, see you tomorrow,” (Ni saa tatu kasoro robo, mpenzi, sitaki kumuudhi mume wangu, tutaonana kesho) Jacky aliongea kwa sauti hafifu ya kirafiki na hapo akamuona Jacob akimtazama kwa macho yaliyokuwa yamejaa wivu.


“But I thought…” (Lakini nilidhani…) Jacob alisema lakini Jacky akamkatiza.


“Another day, darling, please…” (Siku nyingine, mpenzi, tafadhali) Jacky alisema huku akirembua macho yake kisha akaanza kuondoka.


“Jacky…”


“Abee”


“I love you so much until I feel confused,” (Nakupenda sana hadi najihisi kuchanganyikiwa) Jacob alisema huku akijiinua pale sakafuni.


“Me too,” (Mimi pia) Jacky alisema huku akimtazama Jacob kwa makini.


“Please don't let me down, my love, see you tomorrow,” (Tafadhali usiniangushe, mpenzi wangu, kesho tuonane).


“Until death separates us,” (Hadi kifo kitakapotutenganisha) Jacky aliongea kwa utulivu huku akiruhusu tabasamu lake kuchanua usoni, kisha alimsogelea Jacob na kumbusu mdomoni.


Taratibu akageuka na kuanza kuondoka akimwacha Jacob anamsindikiza kwa macho huku akiutazama mtikisiko maridhawa wa umbo lake zuri. Jacob alibaki akimkodolea macho jacky huku akihisi nafsi yake ilikuwa imepata utajiri mkubwa wa furaha isiyoelezeka.


Jacky alitoka ndani ya lile jumba la Jacob na kuingia ndani ya gari lake aina ya kisha aliliondoa gari lake aina ya Range Rover Sport L494 la rangi nyeupe taratibu.


Muda ule ile hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam ilikuwa imepoa zaidi, manyunyu hafifu ya mvua yalikuwa yakianguka kutoka angani kulikotanda wingu la mvua kiasi cha kuweza kuizuia nyota. Muda wote alikuwa akiwaza namna ya kujikwamua na lile balaa kutokana na kushiriki katika wizi wa mabilioni pale Benki ya Biashara.


Wakati akiendesha gari macho yake yalikuwa makini kutazama kila mahali katika namna ya kuchunguza kuwa hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa akimfuatilia nyendo zake.





Jacky alitoka ndani ya lile jumba la Jacob na kuingia ndani ya gari lake aina ya kisha aliliondoa gari lake aina ya Range Rover Sport L494 la rangi nyeupe taratibu.


Muda ule ile hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam ilikuwa imepoa zaidi, manyunyu hafifu ya mvua yalikuwa yakianguka kutoka angani kulikotanda wingu la mvua kiasi cha kuweza kuizuia nyota. Muda wote alikuwa akiwaza namna ya kujikwamua na lile balaa kutokana na kushiriki katika wizi wa mabilioni pale Benki ya Biashara.


Wakati akiendesha gari macho yake yalikuwa makini kutazama kila mahali katika namna ya kuchunguza kuwa hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa akimfuatilia nyendo zake.


Endelea...


Alipofika nyumbani kwake ilikuwa tayari imekwisha timia saa nne za usiku lakini hakumkuta Carlos, hata alipompigia simu ilikuwa inaita tu pasipo kupokelewa.


* * * * *


Saa tatu usiku kwenye chumba cha ofisi ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu katika jengo la kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam, ukimya ulikuwa umetawala.


ASP Komba alikuwa ameketi nyuma ya ile meza ndefu mwisho wa kile chumba upande wa kushoto akiwa katika uso wa kusawajika huku akiwa ameegemea kiti chake.


Mche wa sigara ulikuwa ukiteketea taratibu kwenye pembe ya mdomo wake na macho yake yalikuwa yakitazama picha kadhaa za mnato zilizochukuliwa wakati gari aina ya Ford Transit lililokuwa na nembo ya NeoVision Security lilikiungua nmoto a kubaki chuma chakavu.


Kwenye kiti kingine kilichokuwa jirani na kile cha ASP Komba alikuwa ameketi kachero wa polisi, Sajenti Mapambano, ambaye alikuwa kimya akizitazama zile picha za gari na kisha akasoma nyaraka fulani za taarifa kutoka Idara ya Intelijensia ya Jinai.


ASP Komba na Sajenti Mapambano walizipitia kwa makini zile taarifa kutoka katika ofisi ya Idara ya Intelijensia ya Jinai ambazo zilikuwa zimebeba taarifa nyingi na nyeti kumhusu Joram Mbezi.


Hii ilikuwa ni baada ya kuzipitia kwa makini picha za video zilizonaswa na kamera za ulinzi za ile benki maarufu kama CCTV zikionesha tukio lote la wizi pale katika Benki ya Biashara tawi la barabara ya Lumumba Mnazi Mmoja.


Kabla hajaziangalia zile picha za CCTV ASP Komba aliamini kuwa kiongozi wa wizi ule alikuwa mzungu kama ilivyosemwa na watu lakini zile picha ya video kutoka katika kamera za ulinzi zilimuonesha kwa uwazi kabisa kuwa mtu waliyedhani ni mzungu alikuwa Joram Mbezi, ambaye yeye ASP Komba alimfahamu fika.


Alimfahamu kwa kuwa mara mbili alishamwekwa ndani lakini akalazimika kumwachia kwa sababu ya kukosekana ushahidi wa kutosha kumfungulia kesi.


ASP Komba alichukua tena remote ya runinga na kucheza tena ile picha ya video iliyonaswa na kamera za ulinzi huku akiliangalia lile tukio la wizi wa benki kwa mara ya kumi na mbili. Alikiangalia kwa umakini zaidi kile kipande cha picha ya CCTV kilichokuwa kikimuonesha Joram Mbezi akitangulia kuingia na kutembea kwa madaha huku akifuatwa na wanaume wengine wawili.


Kisha akakirudia na kile kipande ambacho kilimuonesha wakati anatoka huku mmoja wao akiburuza begi la magurudumu hadi pale walipoingia kwenye gari aina ya Ford Transit lililokuwa na nembo ya NeoVision Security.


Sasa ASP Komba aliafikiana kabisa na maelezo yaliyokuwa yametolewa awali na mfanyakazi wa Benki ya Biashara aliyeshuhudia lile tukio, Elibariki, aliyeonesha wasiwasi wake kuhusu mzungu aliyeingia benki kuiba kuwa hakuwa mzungu ila alikuwa mweupe kama mzungu na alivaa nywele bandia kuwahadaa watu wadhani alikuwa mzungu.


Ile picha ya video iliyonaswa na kamera za ulinzi ilimuonesha Joram Mbezi akiwa na nywele ndefu zilizolalia mgongoni na alikuwa amevaa miwani mikubwa myeusi ili kuficha utambulisho wake lakini hiyo haikumzuia ASP Komba kumtambua katika picha ile.


ASP Komba aliisimamisha tena ile picha ya video na kuirudisha nyuma kisha alizitazama zile sura nyingine kwa umakini ili kujiridhisha. Hata hivyo, bado hakuweza mara moja kuwatambua wale wengine, alidhani kuwa ingemchukua muda kuweza kuwatambua endapo angeituliza akili yake, hivyo aliigandisha ile picha ya CCTV na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Ukimtazama haraka haraka huwezi kabisa kudhania kama huyu mtu ni Joram Mbezi…” ASP Komba alisema kwa sauti yenye utulivu huku akiendelea kuiangalia ile picha, kisha alishusha pumzi ndefu huku akiminya midomo yake na kumtupia jicho Sajenti Mapambano. “Labda nikuulize, ni lini, mara ya mwisho ulikutana na huyu mtu?”


“"Kama wiki tatu hivi zilizopita... nakumbuka ilikuwa Jumamosi pale Masai Club,” Sajenti Mapambano alisema baada ya kutafakari kwa sekunde chache.


“Ilikuwa kama saa ngapi hivi?" ASP Komba alimuuliza Sajenti Mapambano huku akimtulizia macho.


"Ilikuwa saa tano na nusu za usiku, siku hiyo tulikwenda kwa ajili ya kuwakamata madada poa na makaka poa. Tukamkuta yuko na yule mwanamke wake Doris. Sisi tukafanya kazi yetu na kuondoka.”


“Yeye mkamwacha?”


“Tungemfanya nini, afande, wakati alikwenda pale kutumia kama watu wengine?” Sajenti Mapambano alimuuliza ASP Komba huku akimkazia macho.


“Mngewakamata wote, yeye na bibi yake, mkawaweka ndani!” ASP Komba alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Japokuwa ana historia ya uhalifu lakini ni mjanja sana, nakumbuka mara mbili ulishamwekwa ndani, ukamtoa kwa sababu ya kukosekana ushahidi wa kutosha kumfungulia kesi,” Sajenti Mapambano alimwambia ASP Komba.


“Sasa naanza kupata wasiwasi, inawezekana kabisa Doris ndiye Belinda Jackson tunayemtafuta,” ASP Komba alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Inawezekana akawa ni Doris, lakini kinachonichanganya, Doris aliwezaje kuwasiliana kwa siri na Joram wakati watu wote wanajua kuwa ni mzazi mwenziye na wana watoto wawili? Kama waliwahi kuishi pamoja na kupata watoto wawili ni wazi hawakuwa na wasiwasi wa kuficha mawasiliano yao, nadhani hapa kuna jambo ambalo hatulifahamu lililomfanya mtu anayejiita Belinda Jackson kuficha utambulisho wake ili mtu mwingine asifahamu!” Sajenti Mapambano alisema huku akimtazama ASP Komba kwa makini.


“Yeah, you’re right… nadhani kwa leo inatosha. Leo imekuwa ni siku ndefu sana kwetu. Tukapumzike na kesho asubuhi tuanze kazi rasmi tukianzia Sinza nyumbani kwa Joram,” ASP Komba alimwambia Sajenti Mapambano na kugeuza uso wake, akaitazama tena ile picha ya video iliyogandishwa kwenye runinga na kushusha pumzi. Safari hii uso wake ulijenga matuta ya hasira.


“This time you are no longer smart, Joram, I must put you in prison,” (Safari hii huna tena ujanja, Joram, lazima nikutie mbaroni) ASP Komba alisema kwa sauti tulivu lakini iliyobeba hasira.


* * * * *


Asubuhi ya saa moja na dakika ishirini na tano katika barabara ya Igesa eneo la Sinza Makaburini Carlos alikuwa amesimama karibu na baa ya Mwika. Alifika katika eneo lile muda mrefu, takriban dakika ishirini na ushee zilizokuwa zimetangulia akasimama kando ya makaburi akiangalia kila kilichokuwa kinaendelea katika nyumba moja jirani na yale makaburi.


Tangu alipopigiwa simu na Jacky siku iliyokuwa imetangulia na kuelezwa kuhusu maofisa wa polisi kumtilia shaka Kisu kuwa alikuwa mmoja wa walioshiriki katika ule wizi wa mabilioni pale Benki ya Biashara, Carlos hakuweza kulala.


Usiku ule ule alianza harakati za kumtafuta Kisu na bahati mbaya simu yake ilikuwa haipatikani. Alikwenda katika viwanja alivyodhani angeweza kumuona Kisu lakini hakuwepo, hatimaye aliamua kwenda nyumbani kwa Doris, mwanamke aliyewahi kuishi na Kisu na walikuwa na watoto wawili. Hata hivyo Doris alimwambia Carlos kuwa hakuwa ameonana na Kisu kwa takriban wiki tatu, tangu walipoachana Masai Club Kinondoni baada ya kutofautiana.





Tangu alipopigiwa simu na Jacky siku iliyokuwa imetangulia na kuelezwa kuhusu maofisa wa polisi kumtilia shaka Kisu kuwa alikuwa mmoja wa walioshiriki katika ule wizi wa mabilioni pale Benki ya Biashara, Carlos hakuweza kulala.


Usiku ule ule alianza harakati za kumtafuta Kisu na bahati mbaya simu yake ilikuwa haipatikani. Alikwenda katika viwanja alivyodhani angeweza kumuona Kisu lakini hakuwepo, hatimaye aliamua kwenda nyumbani kwa Doris, mwanamke aliyewahi kuishi na Kisu na walikuwa na watoto wawili. Hata hivyo Doris alimwambia Carlos kuwa hakuwa ameonana na Kisu kwa takriban wiki tatu, tangu walipoachana Masai Club Kinondoni baada ya kutofautiana.


Endelea...


Carlo alikuwa amerudi nyumbani kwake saa saba usiku akiwa amechoka sana na kumkuta Jacky akiwa amelala kwenye sofa kubwa pale pale sebuleni baada ya kumsubiri kwa kitambo kirefu. Hata hivyo, baada ya kurudi Carlos hakuweza kupata usingizi, usiku wote alikuwa akipanga hili na lile na alfajiri ya siku iliyofuata aliondoka nyumbani ili kwenda kumtafuta Kisu.


Alichukua gari lake aina ya Toyota Landcruiser GX V8 na kuingia barabarani ili kuelekea Sinza Makaburini, alipokuwa akipita jirani na meza moja ya magazeti alimuona yule muuzaji akiwa anapanga magazeti kwenye meza.


Carlos alivutiwa na kichwa kimoja cha gazeti pale macho yake yalipoangukia kwenye maneno makubwa yaliyokuwa yamekolezwa wino mweusi yakiwa na kichwa cha habari: ‘Mfanyakazi benki akamatwa akihusishwa na wizi wa mabilioni, wenzake wasakwa’. Moyo wa Carlos ulipiga mshindo, hata hivyo hakuwa na muda wa kupoteza.


Akaamua kuendelea na safari yake na wakati akiingia katika barabara iliyokuwa inatoka Kinyerezi alimuona mwanamume mmoja, mtu mzima aliyekuwa anapita akiwa na baiskeli iliyobeba madafu akielekea Kariakoo.


Mara Carlos akapata wazo na kumsimamisha yule mtu, alimuuliza bei ya yale madafu na baada ya kuelezwa alimtaka yule mtu amuuzie madafu yote pamoja na ile baiskeli lakini yule mtu alionesha kusita. Lakini alipooneshwa kitita cha fedha shilingi milioni moja alikubali mara moja na kumwachia yale madafu pamoja na baiskeli yake.


Carlos aliipakia ile baiskeli na madafu yake kwenye gari lake kisha alirudi nyumbani kwake na kuvaa kanzu juu ya nguo zake, kichwani akavaa baragashia na miguuni alivaa makubazi, na baada ya hapo safari ya kuelekea Sinza ikaanza.


Jacky alimtazama Carlos kwa wasiwasi, alipotaka kujua alikuwa anaelekea wapi na mavazi yale Carlos alimtaka asubiri angerudi kumpa taarifa na kumtaka asiondoke nyumbani hadi atakapokuwa amerudi.


Carlos alipofika eneo la Sinza Palestina ilikuwa tayari saa moja ya asubuhi, watu walikuwa katika pilika pilika za hapa na pale kuelekea kwenye shughuli zao, Carlos akaamua kuliegesha gari lake jirani na Hospitali ya Sinza Palestina, kisha akaishusha ile baiskeli ya madafu na kuanza kuendesha taratibu.


Kwa yeyote ambaye angemuona Carlos asingeshindwa kumtofautisha na wauzaji wengine wa madafu. Aliendesha hadi alipofika Sinza makaburini na kuiegesha baiskeli yake eneo lile akijifanya kuuza madafu huku macho yake yakiwa makini kufuatilia nyendo zote zilizokuwa zikiendelea eneo lile.


Mara akamuona Kisu akifika kwenye ile nyumba ambayo Carlos alikuwa akiichunguza muda wote na kuegesha pikipiki yake pale nje, kisha aliharakisha kuingia ndani ya ile nyumba akionekana mwenye wasiwasi mkubwa.


Carlos alitaka kumfuata lakini akasita baada ya kuwaona wavulana wawili wa umri wa miaka kumi na kumi na mbili wakisogelea pale kwenye baiskeli yake na kusimamia kando yake huku wakimtazama kwa makini.


“Madafu shilingi ngapi?” mtoto mmoja alimuuliza Carlos huku akimtazama kwa makini.


Carlos alimtazama yule mtoto, akachukua madafu mawili na kuwapa kila mmoja na dafu lake. “Haya, ondokeni!”


Wale watoto waliyapokea yale madafu kwa furaha lakini hawakuondoka. Walibaki wamesimama wakimkodolea macho kwa mshangao, huku wakiwa wameshikilia yake madafu.


Carlos aliwatazama na kutaka kuwafukuza lakini akasita na kuyaondosha macho yake kutoka kwa wale watoto, akayaelekeza kule kwenye ile nyumba. Muda huo Kisu alikuwa anatoka ndani akiwa amebeba begi dogo la mgongoni na kuanza kupiga hatua zake kuifuata piki piki yake.


Muda ule ule Carlos alitoa bastola yake iliyokuwa na kiwambo cha kuzuia sauti, akamlenga Kisu na kuachia risasi iliyompata Kisu katikati ya paji la uso wake, ikamrusha na kumtupa hatua tatu nyuma yake. Watu wachache waliokuwepo eneo lile karibu na Kisu wakataharuki na kumtazama kwa mshangao wakiwa hawajui alipatwa na nini!


Carlos akateleza taratibu akiiacha ile baiskeli na madafu yake katika eneo lile! Aliingia kichochoroni karibu na duka la mavazi la Kitaani Classic na kutoka mtaa wa Social kisha akazidi kusonga mbele kwa mwendo wa haraka, alipita kwenye kichochoro kimoja kilichokuwa na lundo la takataka, Carlos akaivua ile kanzu na kuitupa pale.


Alipoibuka katika mtaa wa Gandabahari alikuwa tayari amebadilika na kuingia kichochoro kingine kilichokwenda kumfikisha mtaa wa Mjiasali, kisha akaufuata mtaa wa Ramala uliomfikisha nyuma ya majengo ya hospitali ya Sinza Palestina. Wakati akifika alipokuwa ameegesha gari lake aliliona gari moja aina ya Nissan Patrol la rangi nyeusi lililokuwa na maandishi ya POLISI ubavuni likipita pale kwa mwendo wa kasi likielekea Sinza Makaburini.


Carlos aliachia tabasamu huku akiingia ndani ya gari lake na kuliondoa kwa kasi na kuyafanya magurudumu yachimbe ardhi wakati akiliingiza lile gari barabara ya Shekilango.


Alielekea upande ule ule lilikoelekea lile gari la polisi na kulivuka eneo la Sinza Makaburini, alitupa macho yake kutazama upande ule wa kushoto na kuwaona watu wengi wakiwa wamekusanyika eneo lile huku maofisa wa polisi, ASP Komba na Sajenti Mapambano wakionekana kuwahoji baadhi ya watu walioshuhudia tukio lile.


Carlos alishusha pumzi na kuongeza mwendo akilipita eneo la makaburi, akavuka eneo la Sinza Kwa Remi hadi alipofika eneo la Sinza Mori akakunja kuingia kushoto akiifuata barabara ya Mori hadi alipokwenda kutokea katika barabara ya Sam Nujoma jirani na Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, maarufu Kanisa la Kakobe.


Hapo akakunja na kuingia kushoto akiifuata ile barabara ya Sam Nujoma kuelekea eneo la Ubungo.


______


Hazikupita hata saa tatu baada ya tukio la mauaji pale Sinza Makaburi, mwili wa Kisu ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti maarufu kama mochuari katika hospitali ya Sinza Palestina, habari zilizagaa karibu kila mahali jijini kupitia mtandao wa WhatsApp.


Waandishi kadhaa wa habari walikuwa wamefika na kusimama nje ya jengo la Kituo Kikuu cha Polisi wakitaka maelezo ya tukio zima, na nani anayeshukiwa. Waliambiwa kuwa suala lile lilikuwa likishughulikiwa na ASP Komba, ambaye hata hivyo, kutokana na kuchanganyikiwa hakupenda kuongea hata na mmoja wao.


ASP Komba alijilaumu sana kwa kushindwa kumpata Joram Mbezi akiwa hai kwani aliamini kuwa Joram ndiye alikuwa kiungo kikubwa kati ya mtu aliyejiita Belinda Jackson na Yusuf na sasa kazi ilianza kuwa ngumu pasipo Joram.


Alikuwa amebakiwa na kazi moja tu, kumbana Yusuf ili amweleze uhusiano wake na wale watu wawili, Joram Mbezi ambaye sasa alikuwa marehemu na Belinda Jackson, ambaye hawakuwa na taarifa zake hadi muda huo. Alipaswa kupata majibu ya uchunguzi wake haraka iwezekanavyo.




ASP Komba alijilaumu sana kwa kushindwa kumpata Joram Mbezi akiwa hai kwani aliamini kuwa Joram ndiye alikuwa kiungo kikubwa kati ya mtu aliyejiita Belinda Jackson na Yusuf na sasa kazi ilianza kuwa ngumu pasipo Joram.


Alikuwa amebakiwa na kazi moja tu, kumbana Yusuf ili amweleze uhusiano wake na wale watu wawili, Joram Mbezi ambaye sasa alikuwa marehemu na Belinda Jackson, ambaye hawakuwa na taarifa zake hadi muda huo. Alipaswa kupata majibu ya uchunguzi wake haraka iwezekanavyo.


Endelea...


ASP Komba alionekana kuchoka sana asubuhi ile alikumbuka kuwa baada ya kurudi tu ofisini mkuu wake wa kazi, Kamanda wa Polisi wa kanda maalumu alimuuliza, “Unadhani kuna haja ya kukuongezea mtu mwingine katika kazi hii?”


“Hapana, afande! Naamini sisi wawili tunatosha. Nikihitaji msaada, nitakujulisha,” ASP Komba alijibu.


Picha ya maiti ya Joram Mbezi iliyokuwa imefumuliwa kichwani iliendelea kumjia ASP Komba akilini mwake, baada ya uchunguzi wa mwili wa Joram Mbezi waliwahoji takriban watu watano, wakiwamo wale watoto wawili waliopewa madafu katika eneo la tukio.


Watu hao watano, watatu wakiwa watu wazima ambao kati yao mmoja alikuwa mwanamume na wawili wanawake, walichukuliwa hadi kituo cha polisi na kuhojiwa na ASP Komba, wote walieleza kuwa walimwona muuza madafu kwa mbali na wala hawakumtilia maanani, hivyo wasingeweza kumtambua endapo wangemuona tena.


Ila wale watoto waliopewa madafu walikiri kumwona kwa ukaribu yule muuza madafu akitumia bastola. Walieleza kuwa waliitambua bastola kwa kuwa waliwahi kuona zikitumika kwenye sinema walizoziangalia kwenye mabanda ya video.


Baada ya mahojiano, wale watu wazima watatu, isipokuwa wale watoto, waliachiwa. ASP Komba na Sajenti Mapambano wakabaki peke yao na wale watoto.


ASP Komba aliwatazama kwa macho ya upole wale watoto. Aliamini kuwa ilikuwa ni mara yao ya kwanza kushuhudia mauaji na kufikishwa kituo cha polisi kutoa maelezo. ASP Komba alikumbuka kuwa pamoja na mambo mengi aliyowauliza wale watoto lakini alitaka kujua kama wangeweza kumtambua yule mtu aliyewapa madafu endapo wangemuona kwenye picha.


“Mkimwona tena yule baba aliyekupeni madafu mtaweza kumtambua?” ASP Komba aliwauliza wale watoto.


“Sura yake?” aliuliza mtoto mmoja aliyeonekana mjanja zaidi.


”Ndiyo, sura yake”


“Naweza,” yule mtoto alijibu pasipo hata kufikiria mara mbili.


“Hata ukimuona kwenye picha?” ASP Komba alimuuliza kwa upole huku akimkazia macho.


“Ntamjua.”


ASP Komba aliinuka akafungua kabati moja la chuma lililokuwa ukutani na kuvuta droo iliyokuwa ndani yake upande wa kulia, akatoa faili lililokuwa na picha kadhaa za wahalifu, akawawekea mbele wale watoto.


“Angalieni vizuri kama picha ya huyo mtu imo humo. Msifanye haraka,” ASP Komba aliwaeleza kwa sauti ya upole.


Pamoja na kuchukua muda mrefu kufunua na kuziangalia zile picha kwa utulivu mkubwa, wakipitia kila moja kwa msaada lakini hawakuweza kumuona mtu waliyekuwa wakimtafuta. Jambo lile likazidi kumuumiza ASP Komba.


* * * * *


“I killed Kisu, he had to die…” (Nimemuua Kisu, alipaswa kufa…) maneno ya Carlos ambayo bado yaliendelea kupita kichwani mwa Jacky na kumsumbua. Baada ya kuambiwa maneno yale Jacky hakusema lolote, alijiondosha pole pole pale alipokuwa amesimama akaketi juu ya sofa.


Uso wake ulionesha mchanganyiko wa huzuni na hasira. Alimtazama Carlos huku akipumua kwa nguvu. Carlos alimtazama Jacky kwa mshangao, akapitisha ulimi wake chini ya midomo yake. Hakuweza kuelewa mara moja ni kipi kilichomkera Jacky.


Carlos alimsogelea Jacky, akaketi karibu yake huku akimtulizia macho yake usoni akimtazama kwa makini.


“Why you look so serious?” (Vipi, mbona unaonekana hivyo?) Carlos alimuuliza Jacky huku akiendelea kumkazia macho.


Jacky alimtazama Carlos, akashusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani, “There was no reason to kill Kisu,” (Hapakuwa na sababu ya kumuua Kisu) alisema, uso wake akiwa kaukunja, kisha akaongeza, “We agreed to bring him here, give him his share and then let him leave the country,” (Tulikubaliana kuwa umlete hapa, umkatie chake kisha atoroke nchi).


Carlos alitazama kando akaonekana akiwaza kwa kitambo kifupi kisha akayarudisha macho kwa Jacky, “So, is this what makes you so distressed?” (Kwa hiyo, ndicho kinachokukera sana?)


“Kwani wewe hakikukeri?” Jacky alimuuliza huku aakimtulizia macho.


“Kinikere kwa vipi? Carlos aliongea kwa sauti iliyoanza kuonesha dalili za hasira. “Si alikuwa akisakwa na polisi kwa udi na uvumba, na ilibaki kidogo tu wangemtia mbaroni, sasa weweulitakaje?”


Jacky alibaki kimya akimtazama Carlos kwa makini, kisha alitazama kando, akashusha pumzi za ndani kwa ndani.


“I don't understand, what are you trying to tell me, Jacky?” (Sijaelewa, unajaribu kuniambia nini, Jacky?) Carlos alimuuliza Jacky huku akimkazia macho yaliyokuwa yanawaka kwa hasira.


“Listen, Carlos. We have everything that man has to have that can buy anything, I didn't see a reason to start killing people who helped us!” (Sikiliza, Carlos. Tuna kila kitu ambacho binadamu anatakiwa kuna nacho ambacho kinaweza kununua chochote, sikuona sababu ya kuanza kufanya mauaji kwa watu waliotusaidia!) Jacky alisema huku akiminya midomo yake.


Carlos aliachia tabasamu la mbali, akatingisha kichwa taratibu, “Jacky,” alisema kwa sauti ya upole. “Hivi tangu lini mwenzangu umeanza kuwa mlokole?”


“Nani mlokole?” Jacky alimuuliza Carlos huku akitoa macho. “Yaani mimi niwe mlokole, are you kidding?”


“Kama si mlokole basi ni nini hiki unachomaanisha?” Carlos alisema huku akimkazia macho Jacky.


”Basi tuyaache hayo, tayari yameshatokea na hakuna namna ya kumrudishia Kisu uhai wake,” Jacky alisema huku akiinuka pale kwenye sofa. Akaingia jikoni. Carlos alimsindikiza kwa macho kisha akainuka na kutoka nje.


Baada ya kuandaa kifungua kinywa, Jacky alitoka na kuelekea sebuleni, hakumkuta Carlos, akaanza kuita akidhani labda Carlos alikuwa chumbani, kimya. Akaamua kuchukua simu yake na kumpigia simu lakini simu ilikuwa inaongea na simu nyingine na baada ya muda alipokea ujumbe mfupi, “Nimetoka kidogo, nitarudi baada ya nusu saa…”


Saa tano asubuhi Jacky alikuwa amejipumzisha kwenye kochi kubwa la sofa pale sebuleni, hadi muda huo Carlos hakuwepo nyumbani. Jacky hakuwa na furaha kabisa kama alivyozoea siku zote, alijikuta akiwa na mawazo mengi yaliyokuwa yakizunguka kichwani kwake kiasi cha kutaka kumtia wendawazimu.


Jacky alikwisha anza kuchoshwa aina ile ya maisha waliyokuwa wakiyaishi yeye na mumewe Carlos, alijiona ni mtu mwenye hatia kuishi maisha kama yale, ya kuuza utu wake na hata kuhatarisha maisha kwa sababu ya kutaka kuendelea kupata mabilioni ya fedha.


Alianza kujishangaa, kwa nini aendelee kuishi maisha ya uhalifu wakati tayari walikuwa na fedha nyingi za kutosha kufanya chochote na hata kuishi nchi yoyote!


Nyumba waliyokuwa wakiishi lilikuwa kasri lililokuwa na thamani kubwa ya zaidi ya mabilioni ya fedha na walikuwa na nyumba nyingine tatu jijini Dar es Salaam, zenye thamani ya mabilioni ya fedha na miradi kadhaa iliyokuwa ikiwaingizia fedha nyingi, japo hazikufikia mabilioni. Pia walikuwa na magari kadhaa ya kifahari.


Kila alipofikiria mambo aliyokwisha yafanya na wanaume kadhaa kwa maelekezo ya mume wake Carlos, alianza kuona kinyaa na kujiona mjinga kukubali kutumika kama chambo cha kuingiza mabilioni ya fedha. Alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akihisi thamani ya utu wake ilikwisha toweka siku nyingi na sasa alikuwa akiishi maisha ya majonzi!




Nyumba waliyokuwa wakiishi lilikuwa kasri lililokuwa na thamani kubwa ya zaidi ya mabilioni ya fedha na walikuwa na nyumba nyingine tatu jijini Dar es Salaam, zenye thamani ya mabilioni ya fedha na miradi kadhaa iliyokuwa ikiwaingizia fedha nyingi, japo hazikufikia mabilioni. Pia walikuwa na magari kadhaa ya kifahari.


Kila alipofikiria mambo aliyokwisha yafanya na wanaume kadhaa kwa maelekezo ya mume wake Carlos, alianza kuona kinyaa na kujiona mjinga kukubali kutumika kama chambo cha kuingiza mabilioni ya fedha. Alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akihisi thamani ya utu wake ilikwisha toweka siku nyingi na sasa alikuwa akiishi maisha ya majonzi!


Endelea...


Muda ule Jacky alikata shauri kuwa tukio lile la wizi wa fedha katika Benki ya Biashara tawi la barabara ya Lumumba pale Mnazi Mmoja lingekuwa la mwisho, kwani hakutaka kuendelea na maisha kama yale, potelea mbali, kama Carlos angechukia, yeye alikuwa tayari kwa lolote.


Alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani na kujiegemeza kwenye sofa huku akifumba macho yake.


Hadi muda ule hakuwa ametia chochote tumboni japo alipika na wala hakuwa akihisi njaa, aliamua kuliendea jokofu na kujimiminia juisi ya passion ya boksi iliyokuwa ndani ya lile jokofu, kisha alirejea pale kwenye sofa na kuanza kunywa taratibu huku akiendelea kuwaza hili na lile.


Kando ya lile kochi kulikuwa na meza ndogo na juu ya ile meza kulikuwa na magazeti kadhaa ya siku ile yaliyokuwa yamepitishwa pale na kijana mmoja muuza magazeti ambaye walikuwa wamempa kazi ya kuwapitishia magazeti kila siku asubuhi. Lakini cha ajabu, Jacky aliyapokea na kuyabwaga pale juu ya meza na hakuwa amesoma gazeti lolote hadi muda ule.


Jacky aliyatazama kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani, kisha alijinyanyua na kuchukua gazeti moja akaanza kulipekua akitafuta ukurasa wa mwendelezo wa riwaya moja aliyoipenda sana ya “Hadi Lini!” iliyoandikwa na mtunzi mahili nchini, ambayo ilikuwa ikiendelea kwenye gazeti lile.


Hata hivyo, alisoma paragrafu mbili tu za mwanzo na kulitupa gazeti lile kando akiwa hajisikii kufanya chochote. Muda ule ule alisikia muungurumo wa gari la Carlos wakati lilipokuwa likiingia kwenye uzio wa ile nyumba, kisha mlango mkubwa wa sebuleni ulifunguliwa na Carlos aliingia ndani akionekana mwenye wasiwasi mwingi.


Carlos alisimama akamtazama Jacky kwa kitambo kirefu bila kusema neno kisha kama aliyegutuka alimtupia Jacky gazeti moja alilokuwa amelishika mkononi.


Jacky alimtazama Carlos kwa mshangao na kulitupia jicho lile gazeti lililokuwa limeangukia kwenye mapaja yake, na hapo akapigwa butwaa akiwa haamini macho yake.


Moyo wake ulipiga mshindo pale macho yake yalipoangukia kwenye maneno makubwa yaliyokuwa yamekolezwa wino mweusi yakiwa na kichwa cha habari: ‘Mfanyakazi benki akamatwa akihusishwa na wizi wa mabilioni, wenzake wasakwa’.


Jacky aliinua uso wake kumtazama Carlos kwa wasiwasi, na wakati huo huo Carlos alikuwa akimtazama Jacky kwa makini, wakatazamana kwa kitambo kisha Carlos akatingisha kichwa chake kwa huzuni.


Kwa haraka Jacky aliyarudisha macho yake kwenye lile gazeti na kupitisha macho yake kwenye maandishi ya habari iliyoandikwa chini ya kichwa hicho cha habari, akayatuliza na kuona kuwa jina la Yusuf halikuwa limetajwa kabisa, japo benki aliyofanyia kazi ilitajwa.


Habari ile ilieleza kuwa mfanyakazi mmoja (jina lake kapuni) alikuwa anashikiliwa na polisi kwa kujihusisha na wizi wa mabilioni ya fedha akiwa mfanyakazi wa benki, na kwamba alishirikiana na watu wengine watatu (majina yamehifadhiwa) ambao walikuwa wanatafutwa.


Habari ile iliendelea kueleza kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu alikuwa anawaomba raia wema washirikiane na jeshi la polisi katika kuwafichua wote watakaowatilia shaka.


Jacky aliinua uso wake na kumtazama Carlos, alilifunga lile gazeti na kuketi huku akiendelea kumtazama Carlos, lakini alishangaa kwa kutoiona ile habari mwanzo pale alipokuwa akilipitia lile gazeti lililokuwa na hadithi ya Hadi Lini! ambalo alilitupia pale mezani.


“Kukamatwa kwa Yusuf inaweza isiwe kitu kinachoninyima raha, kwa kuwa hana information nyingi za kuwaeleza polisi… hata kama watambana sana bado hana ufahamu mzuri kuhusu wewe, ila kinachoninyima raha ni kama watambana aeleze wapi mlikutana na wao kufuatilia katika hoteli mlizokutana ili kutafuta picha za video za CCTV…” hatimaye Carlos alisema kwa huzuni akivunja ukimya.


“Ndiyo hapo sasa! Kwa upumbavu wake anaweza kuropoka kila kitu akidhani kuwa anawapunguzia kazi ya upelelezi ili wamsamehe,” Jacky alijibu huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


Carlos alimtazama Jacky kwa makini na kubetua kichwa chake kukubaliana naye, kisha kilipita kitambo kirefu cha ukimya kila mmoja akionekana kuzama kwenye mawazo.


Carlos alijiinamia akawaza kidogo, kisha akashusha pumzi. Alipoinua macho kumtazama Jacky, akasema, “Now what do you think?” (Sasa una mawazo gani?)


“Let us leave the city first, if possible we can leave the country and stay there for several months.” (Tuondoke mjini kwanza, ikiwezekana tuhame nchi tukakae huko kwa miezi kadhaa tukisikilizia).


“Where do we go?” (Tuelekee wapi?)


“I don't know ... anywhere, we just have to leave. We have enough resources to take us anywhere,” (Sijui… popote pale, mradi tuondoke tu. Tuna mali nyingi za kutosha kutupeleka popote) Jacky alisema huku akishusha pumzi.


“Is it really that you’ve reached that decision, Jacky?” (Ni kweli umefikia uamuzi huo, Jacky?)


“Unauonaje, wa kipumbuvu, ee?”


“Sijasema hivyo!”


“Kumbe?”


“Nataka nithibitishe tu kwamba kweli tunataka kuikimbia nchi!”


“Carlos, if you would like to stay here, I do not force you to leave,” (Carlos, kama unapenda kuendelea kuishi hapa, sikulazimishi uondoke) Jacky alisema huku sauti yake ikianza kuwa na mikwaruzo ya hasira. “Continue to live here, look for another woman, do…” (Endelea kuishi hapa, tafuta mwanamke mwingine, fanya…)


“Jacky!” Carlos alimkatiza.


“What?” (Nini?) Jacky aliuliza huku akimtolea Carlos macho.


“Mbona unataka kuvuka mpaka?” Carlos alisema huku akimkazia macho Jacky.


Wakabaki kimya wakitumbuliana macho. Na wakiwa katika ukimya ule mara Carlos akaonekana kugutuka akionekana kupata wazo na kumkazia macho Jacky.


“Oh my God, Jasmine!” Jacob alisema huku midomo yake ikitetemeka kama aliyekuwa amemuona malaika mtoa roho akimjia mbele yake. Jacky alimtazama Carlos kwa mshangao.


Carlos alianza kuranda randa pale sebuleni akiwa ameinamisha kichwa chake chini akitafakari kwa kina. Jacky aliendelea kumtumbulia macho Carlos kwa mshangao bila kusema neno.


“I've got an idea,” (Nimepata wazo) Carlos alisema huku akiketi taratibu kwenye sofa. Jacky aliendelea kumtazama kwa makini bila kusema neno lolote.


“We need to find a quick way to silence Kabwe and Liston before things get worse, and then I’ll find out how to deal with Yusuf in jail,” (Itabidi tutafute njia ya haraka ya kuwanyamazisha Kabwe na Liston kwanza kabla mambo hayajaharibika, halafu nitatafuta namna ya kudili na Yusuf kule kule mahabusu) Carlos alisema huku akiachia tabasamu.


Jacky alishtuka sana na kumkazia macho Carlos kwa hofu kana kwamba alikuwa akitazama kitu cha ajabu sana chenye kutisha.


“What do you mean to silence them, Carlos?” (Unamaanisha nini kuwanyamazisha, Carlos?) Jacky aliuliza huku akionekana kuanza kuchanganyikiwa.


“To kill them, like Kisu,” (Wauawe, kama Kisu) Carlos alisistiza huku akiendelea kutabasamu.


“Aah, sasa unataka kutafuta matatizo mengine. Haya bado hayajaisha unataka kuzua mambo mapya!” alisema Jacky kwa huzuni.


Kila kitu sasa kimegeuka kuwa KIZUNGUMKUTI, hata mimi sijui nini kitatokea, tuzidi kufuatilia stori hii ya kusisimua kujionea jinsi hiki



“We need to find a quick way to silence Kabwe and Liston before things get worse, and then I’ll find out how to deal with Yusuf in jail,” (Itabidi tutafute njia ya haraka ya kuwanyamazisha Kabwe na Liston kwanza kabla mambo hayajaharibika, halafu nitatafuta namna ya kudili na Yusuf kule kule mahabusu) Carlos alisema huku akiachia tabasamu.


Jacky alishtuka sana na kumkazia macho Carlos kwa hofu kana kwamba alikuwa akitazama kitu cha ajabu sana chenye kutisha.


“What do you mean to silence them, Carlos?” (Unamaanisha nini kuwanyamazisha, Carlos?) Jacky aliuliza huku akionekana kuanza kuchanganyikiwa.


“To kill them, like Kisu,” (Wauawe, kama Kisu) Carlos alisistiza huku akiendelea kutabasamu.


“Aah, sasa unataka kutafuta matatizo mengine. Haya bado hayajaisha unataka kuzua mambo mapya!” alisema Jacky kwa huzuni.


Endelea...


“Bila hivyo hatutakuwa salama kabisa, kwanza siamini kabisa kama tangu jana Kabwe na Liston hawajazua balaa lolote huko waliko… I don't believe at all!” Carlos alisema huku akishusha pumzi.


Jacky alimtazama kwa makini na kutaka kusema neno lakini akasita na kushusha pumzi za ndani kwa ndani kisha akabaki akimtazama Carlos kwa wasiwasi. Alimtazama kwa kitambo kisha akaamua kuvunja ukimya, “And what about Jasmine?” (Na vipi kuhusu Jasmine?) Jacky aliuliza huku akiwa bado amemtulizia Carlos macho.


“I want to follow her right now and bring her here, we’ll give her the money belongs to her and ask her to leave the city completely,” (Nataka kumfuata sasa hivi nimlete hapa, tutamkatia anachostahili na kumtaka aondoke kabisa hapa mjini) Carlos alisema na kuinuka kisha akaanza kupiga hatua kutoka, mara akakumbuka jambo na kugeuka kumtazama Jacky.


“By the way, be careful when you want to get out of here, because I feel like there are people going to be tracking our movements,” (Hata hivyo, kuwa mwangalifu unapotaka kutoka humu ndani, maana nahisi kama kuna watu watakuwa wanafuatilia nyendo zetu) Carlos alimwambia Jacky kisha akatoka kabla Jacky hajasema neno lolote.


Carlos aliingia kwenye gari lake aina ya BMW X6 xDrive 50i la rangi ya samawati kisha akabofya remote kufungua lile geti kubwa na kuliondoa gari lake kwa mwendo wa kasi, alichukua uelekeo wa barabara iliyokuwa ikielekea Kinyerezi akiwa hataki kuelekea moja kwa moja Vingunguti ili kuwapoteza watu aliodhani wangeweza kuwa wakifuatilia nyendo zake.


Aliyachunguza magari yaliyokuwa yakija nyuma yake, na kuona magari mawili miongoni mwa magari yaliyokuwa nyuma yake ambayo aliyaanza kutilia shaka.


Magari yale, moja lilikuwa ni gari aina ya Landcruiser Hardtop la rangi nyeusi na jingine lilikuwa ni gari aina ya Land Rover 110 jeupe, na yote mawili yalikuwa yakielekea upande ule ule aliokuwa akienda. Katika muda ule barabara ile haikuwa na msongamano mkubwa wa magari, hivyo mwendo wake ulikuwa wa kuridhisha.


Alipoitupia macho saa yake ya mkononi ilimuonesha kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa sita mchana na wakati huo jua lilikuwa limeanza kushamiri huku hali ya hewa ikiwa ya joto kama ilivyokuwa kawaida katika jiji la Dar es Salaam.


Carlos alianza kuteremsha mteremko mkali na baada ya kulivuka gereza la Segerea alikwenda mwendo wa kasi zaidi na mbele kidogo alifika eneo la Mbuyuni Njiapanda.


Hapo aliamua kuiacha ile barabara iliyokuwa ikielekea Kinyerezi na kukata kuelekea upande wa kushoto akiifuata barabara ya Mbuyuni.


Ilikuwa ni barabara ya kawaida yenye kiasi kidogo cha magari na iliyokuwa ikikatisha katikati ya makazi ya watu. Carlos aliendelea mbele na safari yake huku akifanya tathmini nzuri ya barabara ile iliyoonekana kuwa na watu wachache waliokuwa wanatembea kwa miguu.


Baada ya mwendo mfupi wa safari yake akayaona yale magari Landcruiser Hardtop jeusi na Land Rover 110 jeupe yakiwa nyuma yake, moyo wake ukapiga kite na kumfanya aongeze mwendo ili kuhakikisha kama yale gari yalikuwa yakimfuata.


Wakati akiendelea na safari yake na akiwa hajui afanye nini mara mbele kidogo upande wake wa kushoto akaiona gereji ya Wantong, hivyo ili kuhakikisha kama ni kweli alikuwa anafuatwa aliamua kuchepukia upande ule wa kushoto na kuliingiza gari lake kwenye eneo lile la gereji.


Lile gari jeusi Landcruiser Hardtop lilipunguza mwendo na kuonekana kama vile dereva alikuwa anajishauri kama asimame au lah, lakini akaonekana kuendelea na safari huku lile gari jingine Land Rover 110 jeupe likipitiliza bila kusimama.


Carlos aliyasindikiza kwa macho yale magari huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani na kujipa matumaini kuwa alikuwa salama. Alisubiri kwa dakika tano kisha akaliondoa gari lake kuendelea na safari yake akiifuata ile barabara.


Alipokwenda mbele zaidi alikipita kituo cha mafuta cha Meru kilichokuwa upande wake wa kushoto na mbele kidogo kulikuwa na kituo kingine cha mafuta cha Anna ATN kilichokuwa upande wa kulia kwenye kona ya ile barabara huku kushoto kwake kukiwa na MTN Bakery.


Carlos alishtuka sana alipoliona lile gari Landcruiser Hardtop jeusi likiwa limeegeshwa kando ya barabara jirani na Anna ATN Petroleum huku dereva wake akionekana kufungua boneti la gari.


Carlos aliongeza mwendo huku akilitupia jicho lile gari, na baada ya mwendo mfupi mara akamuona yule dereva akifunga haraka boneti na kuingia kwenye gari kisha gari likaingia barabara na kumfuata nyuma.


Hata hivyo, tukio lile bado lisingekuwa kigezo cha kumridhisha Carlos kuwa sasa alikuwa amefungiwa tera, hata hivyo kwa namna nyingine ile ilikuwa ni ishara mojawapo ya kumtahadharisha kuwa alipaswa kuwa makini na nyendo zake.


Hakujua lile gari jingine Land Rover 110 jeupe lilikuwa wapi muda ule, hivyo mara hii alijikuta akilitazama lile gari Landcruiser Hardtop jeusi kwa utulivu wa hali ya juu katika namna ya kutafuta hakika kama alikuwa akifuatwa au lah!


Aliongeza mwendo na kuivuka baa ya Darajani White kisha alilivuka daraja katika Mto Msimbazi, na kuzivuka baa nyingine za Ndindindii, Elegant Lodge na baadaye Kilimani Bar huku akifikira kama aingie kwenye mojawapo ya zile baa kujifanya kuwa safari yake ilikuwa inaishia pale.


Lakini akaamua kuendelea mbele na baada ya mwendo mfupi wa safari yake akakifikia Kituo cha Decent na kuiacha barabara ile kisha akachepuka na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara finyu ya vumbi iliyokuwa ikielekea Da Prince Lodge.


Aliongeza mwendo na wakati akiifikia Da Prince Lodge, aliliona lile gari jeusi Landcruiser Hardtop nalo likichepuka na kuingia kwenye ile barabara finyu ya vumbi na kufuata uelekeo wa Da Prince Lodge likiwa katika mwendo wa taratibu.


Kitendo kile kikamfanya Carlos ashtuke kidogo baada ya kuridhishwa vizuri na tathmini za hisia zake. Sasa aling’amua kuwa lile gari Landcruiser Hardtop jeusi nyuma yake lilikuwa kazini kumfuata kama alivyokuwa amehisi pale awali.


Hivyo, aliamua kuongeza mwendo bila kujali makorongo katika barabara ile finyu ya vumbi huku kijasho chepesi kikianza kumtoka usoni. Moyo wake nao ulikuwa umeanza kupoteza utulivu, hata hivyo kwa kila hali alijitahidi kupambana kikamilifu na hali ile.


Akili yake ikiwa mbioni kupoteza utulivu sasa alikuwa makini sana kulichunguza lile gari kupitia vile vioo vya ubavuni. Hatimaye akafika mwisho wa ule mtaa na kuchepuka akiingia upande wa kushoto.


Kisha aliongeza mwendo katika barabara ile, hata hivyo hadi alipokuwa mbioni kufikia mwisho wa barabara ile lile gari halikuwa limejitokeza. Carlos hakutaka kuamini kuwa lilikuwa linaishia katika mtaa ule, aliongeza mwendo na kuchepuka tena akiingia upande wa kushoto akiifuata barabara nyingine pana kidogo ya vumbi iliyokuwa inakwenda sambamba na reli ya kati.




Akili yake ikiwa mbioni kupoteza utulivu sasa alikuwa makini sana kulichunguza lile gari kupitia vile vioo vya ubavuni. Hatimaye akafika mwisho wa ule mtaa na kuchepuka akiingia upande wa kushoto.


Kisha aliongeza mwendo katika barabara ile, hata hivyo hadi alipokuwa mbioni kufikia mwisho wa barabara ile lile gari halikuwa limejitokeza. Carlos hakutaka kuamini kuwa lilikuwa linaishia katika mtaa ule, aliongeza mwendo na kuchepuka tena akiingia upande wa kushoto akiifuata barabara nyingine pana kidogo ya vumbi iliyokuwa inakwenda sambamba na reli ya kati.


Endelea...


Ilikuwa barabara iliyokuwa ikikatisha kwenye makazi ya watu upande mmoja na upande wa pili kulikuwa na reli, na hakukuwa na msongamano mkubwa wa magari katika barabara ile.


Hivyo mwendo wake ulikuwa wa kasi zaidi akiwa hataki mtu au watu waliokuwa ndani ya lile gari jeusi Landcruiser Hardtop, ambalo aliamini lilikuwa linamfuatilia ingawa hadi pale lilikuwa halijajitokeza nyuma yake, wafahamu alipokuwa akielekea.


Alihakikisha analipoteza lile gari kabla hawajajitokeza katika barabara ile, hivyo alipofika katika makutano ya barabara ile na barabara ya lami iliyokuwa ikitokea Segerea alivuka na kukunja akiingia upande wa kushoto kuifuata barabara ndogo ya vumbi iliyokuwa inaelekea Kituo cha Polisi cha Stakishari kabla lile gari Landcruiser Hardtop halijatokea katika ile barabara.


Carlos alikwenda mwendo mfupi na kuiacha barabara iliyokuwa inaelekea Kituo cha Polisi cha Stakishari, akachepuka na kuingia katika uchochoro wa barabara finyu zaidi iliyokuwa ikiyazunguka maghala ya Ushirika ambayo kwa wakati huo yalikuwa yakitumiwa kama nyumba ya ibada.


Alisimamisha gari lake kwenye uchochoro ule jirani na yale maghala ya ushirika na kuchungulia nyuma yake akilichunguza kila gari lililopita kwenye ile barabara ya lami iliyotoka Segerea. Baada ya kukaa hapo kwa takriban dakika kumi, mara akaliona lile gari Landcruiser Hardtop jeusi kwa mbali likipita katika ile barabara ya lami iliyokuwa ikitoka Segerea kuelekea eneo la Njia Panda ya Segerea katika Barabara ya Nyerere.


Carlos alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kusubiri pale kwa dakika zingine kumi kisha aligeuza gari lake na kurudi hadi kwenye ile barabara ya vumbi iliyokuwa ikienda sambamba na reli ya kati. Alipofika pale alichukua uelekeo wa upande wa kushoto akiifuata ile barabara ya vumbi ambayo haikuwa na magari mengi, hivyo kumfanya kuongeza mwendo wake.


Alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi katika barabara ile iliyokuwa ikikatisha kwenye makazi ya watu bila kujali kwamba maeneo yale ya uswahilini yalikuwa na watu wengi.


Mara kadhaa alikosakosa kuwagonga watembea kwa miguu na hata waendesha bodaboda aliopishana nao katika barabara ile iliyokuwa ikielekea eneo la Vingunguti.


Baada ya mwendo wa dakika kumi alivuka katika eneo la Chuo cha Ufundi Stadi, VETA, kisha akaanza kuzivuka shule za msingi na sekondari za Ilala na Majani ya Chai.


Wakati akivuka eneo la shule kijana mmoja alikuwa anavuka barabara bila kuwa makini, Carlos aliliyumbisha gari lake huku na huko ili kumkwepa yule kijana lakini hakuweza, hivyo alimgonga na kumrusha kando ya ile barabara.


Carlos alisonya kwa hasira na kukanyaga pedeli ya mafuta, gari likafanya magurudumu yake kuchimba ardhi na kuongeza kasi licha ya baadhi ya watu waliokuwa jirani na eneo lile kumpigia kelele kumtaka asimame.


Aliendelea na safari yake huku akijitahidi kuwakwepa watu waliokuwa katika pilika pilika hadi alipofika kwenye kiwanda cha mabomba cha Pipes Industries.


Hapo alikunja na kuingia upande wa kushoto akiifuata barabara finyu ya vumbi ambayo hata hivyo haikwenda mbali, akachepuka akishika uelekeo wa upande wa kulia akiifuata barabara nyembamba ya lami iliyokuwa ikipita katikati ya makazi ya watu upande mmoja na viwanda upande mwingine.


Akiwa bado katika mwendo wa kasi alilivuka eneo lile la viwanda na hatimaye aliingia katika eneo la Vingunguti Sahara, hapo alipunguza mwendo kutokana na magari kadhaa yaliyokuwa yakipita eneo lile, kisha aliiona nyumba ya Jasmine mbele yake na kufunga breki akiliegesha gari lake umbali wa mita kama therathini hivi kutoka ilipokuwa ile nyumba ya Jasmine.


Aliangaza macho yake huku na kule kwa makini akiangalia kama angeweza kumuona Jasmine lakini hakumuona popote, kwa takriban dakika mbili hivi aliendelea kuangalia huku na kule bila kumuona, akapata wazo la kumpigia simu lakini wakati akitoa simu yake ili kumpigia mara akamuona Jasmine akitokea nyumba moja iliyokuwa upande wa pili wa ile barabara na kuvuka kuelekea nyumbani kwake akiwa ameshika gazeti mkononi.


Carlos alipiga honi huku akimtazama Jasmine kwa umakini. Jasmine alishtuka na kugeuza shingo yake kutazama upande ule ilikotokea ile sauti ya honi na kuliona gari la Carlos. Carlos alitoa mkono wake na kumpungia Jasmine akimwashiria amfuate kwenye gari.


Jasmine alimfuata Carlos pale kwenye gari na alipofika alimsalimia kwa heshima zote, japo alionekana kuwa na uso uliosawajika.


“Tena ilikuwa nije nyumbani kwako leo jioni,” Jasmine alimwambia Carlos baada ya kumsalimia huku akimtazama kwa umakini usoni.


“Nimekufuata, ingia ndani ya gari tuongee,” Carlos alimwambia Jasmine huku akilitupia jicho lile gazeti lililokuwa mkononi kwa Jasmine.


Jasmine hakusita, alifungua mlango wa mbele wa lile gari upande wa kushoto wa dereva na kuingia bila huku akiendelea kumtazama Carlos kwa umakini.


“Vipi, umesoma magazeti ya leo?” Carlos alimuuliza Jasmine huku akimkazia macho mara baada ya kuingia ndani ya lile gari na kuketi.


“Gazeti mojawapo ni hili hapa nimelitoa kwa shoga yangu,” Jasmine alisema huku akimwonesha Carlos lile gazeti.


“Umeshaongea na watu?” Carlos alimuuliza huku akiwa amemtulizia macho.


“Watu gani?” Jasmine aliuliza kwa mshangao huku akimkazia macho Carlos.


“Sijui, labda shoga zako ama…”


“Hmm… kwa mambo kama haya nitaongea nao nini?” Jasmine aliuliza kwa mashaka huku akishusha pumzi.


“Nilitaka tu kujua kama kuna yeyote umeongeaa naye… vipi ulishafika kazini siku mbili hizi?”


“Akah, si nilikwambia siendi tena kazini, naogopa sana…” Jasmine alisema huku akibetua mabega yake juu kukataa.


“Okay, sasa sikiliza, mambo yamekwisha haribika, hivyo nimekufuata twende nyumbani nikakupe pesa zako uondoke kabisa hapa mjini, au unasemaje?” Carlos alimwambia Jasmine huku akimkazia macho.


“Nitashukuru sana maana naogopa wasije wakanifuata hapa nyumbani,” Jasmine alisema huku wasiwasi ukizidi kujionesha usoni kwake.


Carlos aliingiza gia ili kuondoka lakini wakati Carlos akitaka kuliondoa gari lake mara akaliona gari moja aina ya Range Rover SV Autobiography LWB la rangi nyeusi lililokuwa na vioo vyeusi visivyoonesha watu waliomo ndani likifika katika eneo lile na kuegeshwa mbele kabisa ya nyumba ya Jasmine.


Carlos alilitazama lile gari kwa umakini mkubwa huku akionekana kulitilia shaka, hakuta kuondoka, hivyo alisubiri kidogo kuona ni watu gani waliokuwemo ndani ya lile gari na walikuwa wanatafuta nini pale.


“Twende basi,” Jasmine alimwambia Carlos baada ya kumuona akiwa amezubaa akilitazama lile gari.


“Ngoja kwanza, unaliona lile pale gari, nina shaka watakuwa ni askari,” Carlos alisema huku akimwonesha Jasmine kwa kidole lilipokuwa limesimama lile gari aina ya Range Rover SV Autobiography LWB jeusi.


Jasmine aligeuza shingo yake na kuliona lile gari na hapo hapo moyo wake ukapiga mshindo kwa mshtuko mkubwa, alilitambua lile gari na kumaka kwa mshangao.


“Ha! Ni gari la bosi Nassos!” Jasmine alisema kwa mshtuko mkubwa.





“Ngoja kwanza, unaliona lile pale gari, nina shaka watakuwa ni askari,” Carlos alisema huku akimwonesha Jasmine kwa kidole lilipokuwa limesimama lile gari aina ya Range Rover SV Autobiography LWB jeusi.


Jasmine aligeuza shingo yake na kuliona lile gari na hapo hapo moyo wake ukapiga mshindo kwa mshtuko mkubwa, alilitambua lile gari na kumaka kwa mshangao.


“Ha! Ni gari la bosi Nassos!” Jasmine alisema kwa mshtuko mkubwa.


Endelea...


“Unamaanisha ni gari la bosi wako, wa kampuni ya The Jacarandah…” Carlos alitaka kumuliza Jasmine lakini alijikuta akikatisha swali lake baada ya kuwaona watu wanne wakishuka kutoka ndani ya lile gari.


Wa kwanza kushuka alikuwa mwanadada mweupe mfupi aliyeitwa Zena Chande na kufuatwa nyuma na mwanamumke wa Kigiriki, Nassos.


“Huyo msichana ni rafiki yangu anaitwa Zena, na yule mzungu ndiye bosi wangu…” Jasmine alimwambia Carlos huku akiwaangalia Zena na Nassos kwa umakini.


Wakati wakiendelea kuwaangalia wale watu mara wakawaona maofisa wa polisi, ASP Komba na Sajenti Mapambano nao wakishuka kutoka ndani ya lile gari na kujiunga na kina Nassos na Zena. Carlos aliwatazama kwa umakini ASP Komba na Sajenti Mapambano na kuwatambua. Akahisi moyo wake ukibadili mapigo na kuanza kwenda kasi isivyo kawaida.


Wakati huo huo wakamuona Zena akimfuata mwanamke mmoja aliyekuwa amesimama nje ya ile nyumba ya Jasmine na kuonekana akimuuliza jambo. Yule mwanamke alimwonesha Zena kwa kidole lilipokuwa limeegeshwa lile gari la Carlos. Na hapo Nassos, ASP Komba na Sajenti Mapambano wakageuka kulitazama lile gari la Carlos.


Carlos alishtuka sana, akakanyaga pedeli ya mafuta na hapo magurudumu ya gari yakachimba lami huku lile gari likiondoka kwa kasi ya ajabu, muda ule ule kijana mmoja alikuwa akikatisha barabara hivyo lile gari likakosa kumgonga.


Muda ule ule ASP Komba akawaamuru watu wote waingie haraka ndani ya gari walilokuja nalo, wote wakaingia na dereva akaliondoa lile gari kwa mwendo wa kasi kulifukuza lile gari la Carlos ambalo muda ule lilikuwa limekwisha waacha mbali.


Kwa kuwa barabara ile ilikuwa finyu na ilikuwa ikipita katikati ya makazi ya watu katika eneo la Uswahilini la Vingunguti lililokuwa na msongamano mkubwa wa watu, hali ile ilimfanya Carlos asiweze kwenda kwa kasi aliyoitaka.


Hata hivyo, alifanikiwa kufikia katika makutano ya barabara ile na barabara zingine za kuelekea machinjio ya Vingunguti na ile ya kuelekea Buguruni kwa Mnyamani. Carlos alikunja kona na kuingia kushoto kwake akiifuata ile barabara iliyokuwa ikielekea machinjio ya Vingunguti.


Kwa mbali akaliona lile gari aina ya Range Rover SV Autobiography LWB jeusi likizidi kumsogelea likiwa katika mwendo wa kasi, huku taa za mbele za lile gari zikiwa zimewashwa kuashiria hali ya hatari. Carlos alijitahidi kuwakwepa watembea kwa miguu na pikipiki zilizokuwa zikija katika uelekeo wake.


Lile gari aina ya Range Rover SV Autobiography LWB jeusi nalo lilipoyafikia makutano ya barabara zile likakunja na kuingia kushoto likiifuata barabara ile iliyoelekea kwenye machinjio ya ng’ombe ya Vingunguti, na hivyo kuyafanya yale magari kuanza kufukuzana.


Purukshani za yale magari mawili zilisababisha mtafaruku mkubwa katika barabara ile huku watembea kwa miguu na watu waliokuwa wakifanya biashara pembezoni mwa ile barabara wakikimbilia mbali kabisa kukwepa kugongwa na yale magari.


Baada ya kuyapita machinjio ya ng’ombe ya Vingunguti, gari la Carlos lilianza kushusha mteremko mkali katika bonde la Mto Msimbazi na lilipokuwa likikaribia kwenye daraja la Mto Msimbazi lililounganisha Vingunguti na Tabata kuna lori moja lililokuwa limebeba mchanga lilionekana kukatisha kwa mbele, hivyo kumfanya Carlos aliyekuwa katika mwendo wa kasi ajitahidi kufunga breki huku akiliyumbisha gari lake kujaribu kulikwepa lile lori.


Kutokana na mwendo wake kuwa wa kasi mno alishindwa kuhimili na hivyo gari lake liliyumba na kuserereka huku magurudumu yakilalamika kwenye ile barabara ya lami, likaacha barabara na kupinduka likitumbukia kwenye daraja la Mto Msimbazi. Sauti ya mshindo mkubwa sana ilisikika na mara vumbi kubwa likatimka katika eneo lile likifuatiwa na yowe kubwa la hofu.


Lile gari aina ya Range Rover SV Autobiography LWB jeusi walilokuwa wamepanda ASP Komba na wenzake liliserereka huku dereva akijitahidi kuepusha ajali na kusababisha magurudumu yake yalalamike kwenye ile barabara ya lami, likayumba na kufunga breki za ghafla huku likiingia kwenye kibanda kidogo kisichokuwa na mtu kilichokuwa kando ya ile barabara jirani kabisa na lile daraja.


ASP Komba na Sajenti Mapambano walishuka haraka kutoka ndani ya lile gari, wakasimama wakiangalia kule ambako gari la Carlos lilikuwa limeangukia huku wakiwa hawaamini macho yao. Muda ule ule watu walianza kusogea na kukusanyika katika eneo lile.


* * * * *


Siku ile ilionekana kuwa ndefu sana kwa Jacky kuliko kawaida, hadi muda ule alikuwa bado ameketi peke yake pale sebuleni akijihisi upweke mkubwa, alipoitupia jicho saa yake ya mkononi alishangaa sana kuona kuwa ilikuwa imeshatimia saa saba na ushee!


Hakujua kwa nini siku ile hakuwa na furaha kabisa na alishangaa kuona kuwa tangu asubuhi alipokuwa ameamka hakuwa akihisi njaa ingawa hakutia chochote tumboni zaidi ya ile bilauri moja ya juisi ya passion ya boksi. Kwa miaka miwili na ushee aliyoishi na Carlos hapakuwa na hata siku moja aliyowahi kuwa katika wakati mgumu kama siku ile.


Alijikuta akitafakari jinsi alivyokutana na Carlos kwa mara ya kwanza kule jijini Arusha, walivyoanza uhusiano hadi walipofunga ndoa. Siku zote tangu walipooana aliishi kwa furaha na kujikuta akimsahau kabisa Jacob, mwanamume aliyewahi kumpenda sana kuliko chochote.


Kitu ambacho hakukijua ni kuwa hakuwaza kama ingetokea siku ambayo angekuja kuwa na wakati mgumu kama siku ile. Alipigiwa simu mara kadhaa na Jacob lakini hakuweza kuzipokea simu zake, na hata alipopigiwa na kuona namba ngeni bado hakupokea simu.


Akiwa bado anatafakari mara alisikia sauti ya kengele ya getini ikiita kuashiria kuwa kulikuwa na mtu nje ya uzio wa ile nyumba, moyo wake ukapasuka pah! Jasho jepesi likaanza kumtoka mwilini na hakujua kwa nini alishtuka kiasi kile, alianza kuhisi ubaridi mwepesi wa woga ukimtambaa mwilini huku mapigo ya moyo wake yakabadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!


Aliinuka huku mwili wake ukitetemeka na kuchungulia nje kupitia ukuta msafi wa kioo cha dirisha lakini hakuweza kumuona mtu yeyote. Ile kengele ikaendelea kuita tena na tena, Jacky aliamua kutoka na kwenda moja kwa moja hadi kwenye lile geti, kisha akachungulia nje.


Aliwaona wanaume wawili wakiwa wamesimama pale kwenye geti huku wakiendelea kubonyeza kile kitufe cha kengele kwa fujo, Jacky alipowatazama kwa makini akapatwa na mshangao uliochanganyika na wasiwasi baada ya kuwatambua Kabwe na Liston wakiwa wamesimama nje ya ile nyumba.


“Karibuni,” Jacky alisema baada ya kuwafungulia lile geti na na kusimama kando huku akiwatazama kwa umakini, hata hivyo, uso wake ulishindwa kuficha mshangao aliokuwa nao wakati akiwakaribisha ndani. Kabwe alimtazama kwa makini na kuachia tabasamu huku akiingia ndani na kufuatwa nyuma na Liston.


“Vipi hapa?” Kabwe alimuuliza Jacky huku akimkazia macho mara baada ya kuketi kwenye sofa pale sebuleni.



“Karibuni,” Jacky alisema baada ya kuwafungulia lile geti na na kusimama kando huku akiwatazama kwa umakini, hata hivyo, uso wake ulishindwa kuficha mshangao aliokuwa nao wakati akiwakaribisha ndani. Kabwe alimtazama kwa makini na kuachia tabasamu huku akiingia ndani na kufuatwa nyuma na Liston.


“Vipi hapa?” Kabwe alimuuliza Jacky huku akimkazia macho mara baada ya kuketi kwenye sofa pale sebuleni.


Endelea...


“Ah, ndo’ kama mlivyosikia!” Jacky aliongea kwa sauti ya unyonge huku akiwa amesimama akiwatazama wote wawili kwa makini.


“Kusikia nini, mbona sikuelewi, shem?” Kabwe alimuuliza Jacky huku akimkazia macho kwa mshangao.


“Kwani hamsomi magazeti, jamani au hamperuzi hata mitandao kujua yanayoendelea duniani?” Jacky aliwauliza huku akiwatazama kwa mshangao.


“Tunasoma lakini habari za magazetini hazituhusu…” Kabwe alijibu huku akionekana kupuuza kile alichokuwa akiambiwa na Jacky. Jacky alitaka kusema neno lakini Kabwe alimkatisha kwa ishara.


“Sikiliza shem, watu wa magazeti wanafanya biashara yao, watu wa mitandao wanaingiza fedha zao na sisi tunayafanya ya kwetu. Ndiyo nchi ya viwanda inavyokwenda, kila mtu na mambo yake, au siyo?” Kabwe alisema huku akicheua, na muda huo huo ile sebule ikaenea harufu ya pombe.


“Lakini habari zilizotoka leo kwenye magazeti zinatuhusu, ni kwamba mambo yetu ndiyo yamekwama…” Jacky alisema kwa huzuni na kukatishwa na sauti ya Liston aliyepiga ngumi juu ya meza huku akifoka.


“Haiwezekani! Kwani ile fedha mmeirudisha benki?” Liston alimuuliza Jacky huku macho yake yakiwaka kwa ghadhabu.


“Fedha yote ipo!” Jacky alisema huku akimtazama Liston kwa wasiwasi.


“Sasa kilichokwama ni nini? Unajua shem, usituchanganye hapa… kwanza niambie ukweli, ni kweli Kisu ameuawa maana tumesikia habari juu juu?” Kabwe alidakia huku akimkazia macho Jacky kisha akaendelea bila hata kusubiri jibu lake, “Mmemuua Kisu na sisi hatujui hatma yetu ni ipi! Naomba usituchanganye kabisa…” Kabwe alifoka.


Jacky alimtazama Kabwe kwa makini huku akijaribu kutafakari namna ya kukabiliana na hasira za wale wanaume endapo wangeamua kuanzisha vurugu.


“Kwanza mzee yuko wapi? Tunataka kuongea naye kama wanaume,” kabwe alimuuliza Jacky huku aakimkazia macho.


“Katoka kidogo lakini atarudi muda wowote kuanzia sasa.”


“Kama kakuachia mzigo wetu, tupe tusepe ili kila mtu afe na chake, maana sasa naona mnaanza uswahili,” Kabwe alimwambia Jacky huku akionekana kuanza kupandwa na jazba.


“Hajaniachia mzigo wowote wa kuwapeni leo, ninachojua kesho ndiyo mnatakiwa mje kuchukua mzigo wenu… labda nimpigie simu kumjulisha kuwa mmekuja leo,” Jacky alisema huku akiichukua simu yake iliyokuwa juu ya meza, kisha alibofya namba ya Carlos, akapiga na kusikiliza. Simu ya Carlos ilikuwa haipatikani!


Jacky alishtuka sana na kuitazama ile simu kwa mshangao kisha alipiga tena lakini bado simu ya Carlos ilikuwa haipatikani! Akashusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiwatazama Kabwe na Liston katika hali ya kukata tamaa. “Simu yake haipatikani,” Jacky alisema kwa wasiwasi.


“Naona sasa mnatuchanganya, Kisu ameshakufa na sijui kama mlishamkatia chake, na sisi mnaanza kutuletea ngonjera… sikiliza tunachotaka ni hela yetu ama sivyo nyumba hii itawaka moto,” Kabwe alisema kwa ghadhabu.


“Msiwe hivyo jamani, hebu jaribuni kuwa na subira kama ni hela yenu ipo…” Jacky alisema kwa sauti laini huku akiachia tabasamu na kulegeza macho yake akijaribu kuwalainisha.


“Bwana ee, usitulegeze macho yako hapa ukadhani utamrusha mtu roho. Harushwi mtu roho hata kwa nini! Tunachotaka ni mzigo wetu tu, au kama vipi tutalianzisha!” Kabwe alifoka kwa sauti kubwa huku akiinuka kutoka kwenye lile sofa alilokuwa amekalia.


Jacky alimtazama Kabwe kwa makini huku akijiandaa kwa lolote endapo wangetaka kuleta vurugu kisha akayahamishia macho yake kwa Liston ambaye muda wote alikuwa ametulia kwenye kochi akimtazama huku macho yake yakiwaka kwa ghadhabu.


“Basi naomba mvute subira tu jamani, hakawii kurudi,” Jacky alisihi huku akiupima upepo.


Liston na Kabwe wakaangaliana. “Unasemaje kamanda wangu, tumsubiri au tukautwike halafu tuwajie jioni?” Kabwe alimuuliza Liston.


“Jioni ya saa ngapi? Wanaweza kutukimbia hawa,” Liston aliuliza huku naye akiinuka kutoka kwenye sofa.


“Tuwazukie mapema tu…”


“Poa, twen’zetu!” Liston alisema na hapo hapo wakaondoka wakimwacha Jacky amepigwa butwaa.


* * * * *


Saa tisa alasiri, gari lenye maandishi ya POLISI ubavuni aina ya Nissan Patrol la rangi nyeusi liliingia kwenye lango kuu la kuingilia katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala ya Amana, katika eneo la Amana Ilala jijini Dar es Salaam.


Walinzi wa hospitali ile ya Amana waliokuwa nadhifu kwa sare zao za ulinzi walimwelekeza Sajenti Mapambano aliyekuwa akiendesha lile gari sehemu maalumu ya kuliegesha gari lake katika maegesho maalumu ya magari.


Baada ya lile gari kuegeshwa katika eneo lile la maegesho ya magari, ASP Komba, ambaye muda ule alikuwa amevalia sare rasmi za polisi na cheo chake cha nyota tatu kikionekana vyema kwenye mabega yake, alishuka kutoka katika lile gari.


Sajenti Mapambano naye aliteremka na hapo wakaanza kupiga hatua kikakamavu wakielekea kwenye jengo la ofisi za madaktari wa hospitali ile. Walifika na kusimama mbele ya mlango mmoja na hapo ASP Komba akagonga mlango ule mara moja kisha akakishika kitasa, akakinyonga na kuusukuma mlango.


Mlango ulisalimu amri na kumruhusu ASP Komba kuingia ndani ya ile ofisi, Dk Fadhili Masha ambaye alikuwa ameinamisha uso wake akisoma taarifa fulani za mgonjwa kwenye faili alilokuwa amelishika mkononi aliinua uso wake na macho yake yakakutana na yale ya ASP Komba, akaachia tabasamu huku akiinuka kuwalaki ASP Komba na Sajenti Mapambano.


Dk Masha alikuwa mwanamume mrefu mnene na alikuwa mweupe kama chotara, akiwa na umri wa miaka takriban hamsini alionekana mwenye nguvu na misuli imara ya mikononi iliyotuna kikamilifu. Alikuwa na upara mpana uliokuwa unawaka na uso wake ulikuwa mpana huku miwani yake mikubwa ikiwa imeyahifadhi macho yake makubwa.


Alikuwa amevaa suruali ya bluu yenye mistari myeupe, shati la rangi ya samawati lililokuwa na mistari ya bluu ya pundamilia na juu ya lile shati alivaa koti refu jeupe la kidaktari na kuning’iniza shingoni kwake kifaa cha kupimia mapigo ya moyo ambacho kitaalamu kiliitwa stethoscope. Miguuni yule daktari alikuwa amevaa viatu vizuri vyeusi vya ngozi.


“Naona mmeniwahi, sasa hivi nilikuwa namalizia kuisoma hii taarifa kisha niondoke!” Dk Masha alisema baada ya kuwakaribisha wale maofisa wa polisi.


“Majukumu yametubana, dokta… vipi habari za muda?” ASP Komba alisema huku akinyoosha mkono wake kumsalimia Dk Masha.


“Nzuri tu, karibuni,” Dk Masha aliitikia huku akimpa ASP Komba mkono, kisha akamsalimia Sajenti Mapambano na wote wakaketi kwenye viti. Walipoketi tu Dk Masha alivuta droo ndogo ya meza yake na kutoa humo kitabu kidogo cha kumbukumbu.


“Kitu pekee nilichokipata kutoka kwenye mfuko wa suruali ya marehemu ni hiki kitabu chake cha kumbukumbu,” Dk Masha alisema huku akinyoosha mkono wake kumpa ASP Komba kile kitabu.


ASP Komba alikipokea kile kitabu cha kumbukumbu, maarufu kama Diary na kukigeuza geuza huku akikiangalia kwa umakini. Kilikuwa kitabu kidogo cha rangi ya bluu.


“Pia kuna karatasi zingine mbili tatu, labda zitaweza kuwasaidia,” Dk Masha alisema tena huku akichukua zile karatasi na kunyoosha mkono wake kumpa ASP Komba.




“Nzuri tu, karibuni,” Dk Masha aliitikia huku akimpa ASP Komba mkono, kisha akamsalimia Sajenti Mapambano na wote wakaketi kwenye viti. Walipoketi tu Dk Masha alivuta droo ndogo ya meza yake na kutoa humo kitabu kidogo cha kumbukumbu.


“Kitu pekee nilichokipata kutoka kwenye mfuko wa suruali ya marehemu ni hiki kitabu chake cha kumbukumbu,” Dk Masha alisema huku akinyoosha mkono wake kumpa ASP Komba kile kitabu.


ASP Komba alikipokea kile kitabu cha kumbukumbu, maarufu kama Diary na kukigeuza geuza huku akikiangalia kwa umakini. Kilikuwa kitabu kidogo cha rangi ya bluu.


“Pia kuna karatasi zingine mbili tatu, labda zitaweza kuwasaidia,” Dk Masha alisema tena huku akichukua zile karatasi na kunyoosha mkono wake kumpa ASP Komba.


Endelea...


ASP Komba alizipokea zile karatasi na kuzitupia jicho mara moja kisha akayarudisha macho yake kwenye kile kitabu cha kumbukumbu. Akakifungua na macho yake yakatua kwenye ukurasa wa kwanza tu ambapo alikutana na jina la mmiliki wa kile kitabu, “Carlos Mwamba” likiambatana na taarifa zingine binafsi ikiwemo mawasiliano yake.

ASP Komba akaonesha kushtuka kidogo kwa kuwa alimfahamu vyema Carlos Mwamba, ni wiki chache tu zilizokuwa zimepita walikutana wakaongea na Carlos Mwamba alimuahidi kuwa alitaka kulisaidia Jeshi la Polisi kiasi cha shilingi milioni 100 katika operesheni zake mbalimbali.

ASP Komba alishusha pumzi kisha akaanza kuangalia kurasa mbili tatu na hapo macho yake yakatua kwenye karatasi mbili zilizokuwa zimepachikwa kwenye ukurasa mmoja wa kile kitabu cha kumbukumbu.

ASP Komba alizitoa zile karatasi na kuzitazama kwa umakini, karatasi moja ilikuwa ni nakala kivuli (photocopy) ya hundi ya The Jacarandah Group iliyokuwa na saini na karatasi nyingine ilikuwa imeandikwa namba kadhaa za simu.

ASP Komba alizitazama zile namba kwa umakini mkubwa na kugundua kuwa namba mbili kati ya zile zilikuwa ni namba alizokuwa ameziona kwenye simu ya Yusuf, moja ikiwa ni namba ya Joram Mbezi, ambayo pale ilipewa jina la Kisu na namba ya Belinda Jackson, ambayo pale ilipewa jina la beloved coordinator.

Pia katika orodha ile kulikuwa na namba aliyoifahamu kuwa ni ya Yusuf na namba nyingine mbili ambazo hakuweza kuzifahamu. ASP Komba alijikuta akiachia tabasamu pana ambalo baadaye lilitengeneza kicheko hafifu na hivyo kuwafanya Dk Masha na Sajenti Mapambano wapate shauku ya kutaka kujua kilichokuwa kimeandikwa kwenye zile karatasi.

“Vipi, afande, kuna lolote umegundua?” Dk Masha alimuuliza ASP Komba kwa shauku huku akijitahidi kurefusha shingo yake ili ajionee kilichokuwemo kwenye zile karatasi.

“Huwezi kuamini, umenisaidia sana, dokta… nilikuwa nina hamu kubwa sana ya kukutana na huyu mtu,” ASP Komba alisema huku akiendelea kutabasamu.

“Nani, huyu marehemu?” Dk Masha alimuuliza ASP Komba kwa mshangao.

“Naam! Lakini tayari kajihukumu mwenyewe…” ASP Komba alisema na kusita kidogo, kisha kama aliyegutuka akauliza, “Na hali ya yule binti aliyekuwa na marehemu ikoje?”

“Yule binti kama atavuka kesho jioni basi ataweza kuongea,” Dk Masha alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

ASP Komba aliinuka kutoka kwenye kiti chake huku akiendelea kutabasamu kisha akampa ishara fulani Sajenti Mapambano ambaye pia aliinuka, wakamuaga Dk Masha.

“Nakushukuru sana, dokta, huwezi kujua ni kwa kiasi gani umeifanya kazi yangu kuwa rahisi mno, nitakutembelea kesho au keshokutwa kutegemea na hali ya yule binti itakavyokuwa, maana nina hamu kubwa ya kutaka kuongea naye.”

“Karibuni sana,” Dk Masha alijibu huku akiinuka kutoka kwenye kiti chake na kuwasindikiza ASP Komba na Sajenti Mapambano. Wakatoka nje na kuelekea walikokuwa wameegesha gari lao.

Waliingia kwenye gari lao na dereva akaliondoa, waliamua kurudi ofisini. Walipofika ofisini ASP Komba aliketi kwenye kiti chake, akaanza kupitia maandishi yaliyokuwa yameandikwa kwenye kile kitabu cha kumbukumbu cha Carlos Mwamba, ukurasa mmoja baada ya mwingine.

Kuna wakati alijikuta akisisimkwa mwili wake kutokana na kusoma mipango ya hatari iliyokuwa imeandikwa kwenye kile kitabu cha kumbukumbu ikionesha tarehe ya kutekeleza mipango ile na aina ya watu ambao wangetumika kufanikisha mipango ile.

ASP Komba hakuamini kabisa kile alichokuwa akikisoma kwenye kile kitabu cha kumbukumbu cha Carlos Mwamba, mtu aliyekuwa rafiki yake, yeye na mkewe Jackline Mgaya Mwamba. Siku zote ASP Komba aliamini kuwa Carlos ni mfanyabiashara mwenye mafanikio na raia mwema aliyependa kusaidia wengine kwa hali na mali, kumbe ni mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo!

Hadi wakati ule ASP Komba alikuwa bado akikkikodolea macho kile kitabu cha kumbukumbu akiwa haamini kama ni kweli Carlos Mwamba alikuwa nyuma ya uhalifu ule, akaamua kuingiza jina la Carlos Mwamba kwenye ile kompyuta maalumu ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu iliyokuwa pale ofisini ili kutafuta taarifa zake.

Alipoingiza tu lile jina zilikuja taarifa nyingi zilizoonesha kuwa Carlos Mwamba alikuwa mfanyabiashara wa madini mwenye mafanikio makubwa akimiliki kampuni mbili, Mwamba Mines iliyojihusisha na biashara ya madini na Jaco Investment (ikiwa ni kifupi cha Jackline na Carlos) iliyokuwa ikihusika na ujenzi wa majumba (estates), na hakuwa na rekodi yoyote ya uhalifu.

Taarifa zile zilibainisha kuwa jina lake kamili aliitwa Carlos Michael Mwamba, mzaliwa wa jijni Mwanza, umri wake ulikuwa miaka arobaini na mbili, alikuwa na mke Jackline Mgaya Mwamba na aliwahi kupata mafunzo na kuhitimu Shahada ya Kwanza ya System Analysis and Design katika Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza na baadaye alifanya mafunzo ya shahada ya uzamili katika masuala ya takwimu (Statistics) huku huko Oxford nchini Uingereza…

ASP Komba alishusha pumzi ndefu huku akimtazama msaidizi wake, Sajenti Mapambano, kisha akakohoa kidogo kusafisha koo lake huku akizitazama kwa makini picha kadhaa za Carlos zilizokuwa zimeambatana na taarifa ile.

“Niseme wazi, taarifa hizi zimenishtua sana, sikutegemea kama Carlos Mwamba anaweza kuwa ndiye Master Planner aliye nyuma ya uhalifu huu!” ASP Komba alisema huku akishusha pumzi.

Kisha alitoa paketi ya sigara na kuiweka kwenye pembe ya mdomo wake na kuchukua kiberiti kutoka mfukoni, akawasha ile sigara kwenye pembe ya mdomo wake na kusimama, akaelekea dirishani.

Alisimama pale dirishani na kutazama nje kupitia ukuta msafi wa kioo cha dirisha akiyatazama mandhari ya jiji la Dar es Salaam yaliyokuwa yakipendeza katika muda ule wa alasiri. Hata hivyo, hakuwa na tashwishwi yoyote katika sura yake.

Alivuta sigara yake kwa utulivu huku akiutoa moshi mwingi na kuutazama kwa makini kisha akapiga mkupuo mwingine mkubwa wa moshi na alipoitoa sigara mdomoni akapuliza moshi wake pembeni huku akiutazama kabla ya macho yake kuweka kituo kwenye magari machache yaliyokuwa yameegeshwa katika sehemu maalumu ya kuegesha magari yaliyokuwa na kesi au matatizo katika lile jengo la polisi.

Alilitazama gari la Carlos Mwamba aina ya BMW X6 xDrive 50i la rangi ya samawati lililokuwa limeharibika vibaya baada ya kupata ajali kule kwenye daraja la Mto Msimbazi katika eneo la Vingunguti.

Wakati akiwa bado amesimama pale dirishani akitazama chini mara mlango wa kile chumba ukagongwa na kufunguliwa, ASP Komba na Sajenti Mapambano wakageuza shingo zao kutazama kule mlangoni na kumuona askari mmoja aliyekuwa na cheo cha Koplo akiingia na kutembea kwa ukakamavu hadi pale dirishani kisha akasimama karibu na ASP Komba na kupiga saluti ya ukakamavu.

“Afande, kuna mtu mmoja amepiga simu akijitambulisha kama raia mwema anayeishi Tabata Segerea, amesema kuwa amesikia mzozo mkali kwenye nyumba ya jirani yake anayeitwa Carlos Mwamba kuhusiana na mgao wa fedha,” yule askari mwenye cheo cha Koplo alisema.

Maneno yale yakawafanya ASP Komba na Sajenti Mapambano waangaliane kwa makini. Kikatokea kitambo kifupi cha ukimya, kisha ASP Komba akashusha pumzi za ndani kwa ndani.





“Afande, kuna mtu mmoja amepiga simu akijitambulisha kama raia mwema anayeishi Tabata Segerea, amesema kuwa amesikia mzozo mkali kwenye nyumba ya jirani yake anayeitwa Carlos Mwamba kuhusiana na mgao wa fedha,” yule askari mwenye cheo cha Koplo alisema.

Maneno yale yakawafanya ASP Komba na Sajenti Mapambano waangaliane kwa makini. Kikatokea kitambo kifupi cha ukimya, kisha ASP Komba akashusha pumzi za ndani kwa ndani.


Endelea...


“Mzozo huo umetokea lini na saa gani?” ASP Komba alimuuliza yule askari mwenye cheo cha Koplo.

“Leo kama dakika therathini au therathini na tano hivi zilizopita zimesikika sauti za vitisho kutoka kwa vijana fulani wawili wakimweleza mke wa Carlos Mwamba kuwa wanataka fedha yao vinginevyo nyumba itawaka moto, pia wamesikika wakilaumu kuhusu kifo cha mwenzao anayeitwa Kisu…” yule askari mwenye cheo cha Koplo alisema huku akimkazia macho ASP Komba.

“Huyo jirani amepata kuwaona hao vijana?”

“Ndiyo, afande! Anasema ni vijana wawili ambao kimuonekano wanaonekana kabisa kuwa ni wahuni, na jinsi alivyowaelezea ninadhani wanashabihiana sana na wale walioonekana kwenye tukio la wiza pale benki kama ambavyo picha za video za CCTV zimewaonesha…” yule askari mwenye cheo cha Koplo alisema na kuongeza, “Amesema wale vijana wametoka lakini wameahidi kurudi tena jioni…”

ASP Komba alishusha pumzi ndefu na kuweka sigara yake mdomoni, alivuta akipiga mkupuo mkubwa wa moshi kisha aliutoa ule moshi huku akiutazama kwa umakini, alionekana kuzama katika lindi la mawazo.

“Kwa hali hiyo, kuna uwezekano mkubwa kwamba fedha iliyoibwa pale Benki ya Biashara ipo ndani ya nyumba ya Carlos,” ASP Komba alisema huku akiendelea kuutazama moshi aliokuwa akiutoa mdomoni, kisha aligeuza shingo yake kumtazama yule askari mwenye cheo cha Koplo na kuachia tabasamu.

“Koplo!” ASP Komba alimwita yule askari mwenye cheo cha Koplo.

“Ndiyo, afande!” yule askari mwenye cheo cha Koplo aliitikia kwa ukakamavu.

“Kawaite kachero Haji na Seba wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu, kisha na wewe uje ili muwe watatu, nataka kuanzia sasa muanze kufuatilia kwa siri nyendo zote zinazoendelea kwenye hiyo nyumba, na mhakikishe hakuna mzigo wowote unaotoka katika nyumba hiyo, sawa?” ASP Komba alimpa amri yule askari mwenye cheo cha Koplo.

“Sawa, afande!” yule askari mwenye cheo cha Koplo alijibu kwa ukakamavu.

“Okay, unaweza kwenda,” ASP Komba alisema na hapo hapo yule askari mwenye cheo cha Koplo alipiga saluti ya ukakamavu kisha akaondoka haraka kwa ukakamavu.

“Sasa, tunahitaji tena kumhoji Yusuf,” ASP Komba alimweleza Sajenti Mapambano.

* * * * *

Jacky aliitazama saa yake ya mkononi kwa mara ya mia moja. Alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani na kutingisha kichwa chake kwa huzuni huku akisonya. Alishangaa sana kwa kuwa hadi muda ule wa saa kumi jioni Carlos alikuwa hajarudi na wala simu yake ilikuwa haipatikani.

Alitamani sana atoke nje akamtafute lakini aliogopa, hasa alipokumbuka kauli ya Carlos alipomuonya kuwa makini. Akaanza kuhisi kuwa huenda labda Carlos alikuwa amekamatwa na polisi. Hata hivyo, wazo la kukamatwa kwa Carlos likamfanya aogope sana, akawaza kutoroka lakini akajikuta akijiuliza angekimbilia wapi!

Alijiuliza, akimbilie kwa wazazi wake waliokuwa wakiishi jijini Tanga ambako Jacky alifanikiwa kuwajengea nyumba kubwa ya kisasa na kwa kumtumia Carlos, walikuwa na maisha mazuri wakimiliki kiwanda cha kusindika majani ya chai mkoani Tanga na miradi mingine kadhaa!

Hata hivyo, aliona isingekuwa busara kukimbilia Tanga kwa wazazi wake, hakutaka kuwaingiza kwenye matatizo, hivyo akajiuliza, akimbilie kwa jijini Mwanza, ambako pia yeye na mumewe Carlos walikuwa wamejenga nyumba kubwa ya kisasa iliyowagharimu mabilioni ya fedha? Ni huko huko jijini Mwanza ambako pia dada wa Carlos na wifi yake, Anita Mwamba alikuwa akiishi.

Au achukue fedha zote walizoiba katika Benki ya Biashara kisha akimbilie nje ya nchi akaanze maisha mapya?

Mawazo hayo na mengine mengi yalipita kichwani kwa Jacky kisha akayapuuza, alijipa moyo kuwa Carlos hakuwa mtu wa kukamatwa kirahisi namna ile, kwani alikuwa na mtandao mkubwa wa marafiki wakiwemo viongozi wakubwa serikalini na baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa polisi. Hivyo isingewezekana kukamatwa kwa muda ule.

Swali likabaki, Carlos alikuwa wapi muda wote ule na kwa nini simu yake ilikuwa haipatikani? Simanzi ilimjaa Jacky moyoni mwake, hata hivyo alipiga moyo konde na kuamua kusubiri majaliwa ya Mungu.

Muda wote aliokuwa akiwaza hili na lile simu zilikuwa zinapigwa kwa fujo, alipozitazama namba zilizokuwa zikimpigia aliweza kuona namba ya Jacob, baadhi ya namba za rafiki zake na namba zingine ambazo hakuzifahamu kabisa.

Na wakati mwingine uliingia ujumbe mfupi wa maandishi lakini vyote hivyo Jacky alivipuuza, hakutaka hata kusoma ujumbe uliokuwa ukiingia kwenye simu yake. Ilifikia wakati ile simu iligeuka kuwa kero kubwa kwake na hata kuna wakati alitamani kuizima.

Kwa kweli siku ile ilionekana kuwa ndefu sana kwa Jacky. Ile simu haikuacha kuita, ikafika wakati sasa Jacky aliichukua ile simu kwa kusudi moja tu, la kuizima kabisa, kwani alishachoshwa na zile simu zilizokuwa zikipigwa mfululizo.

Lakini alipoichukua na kuiangalia vizuri namba iliyokuwa inaita akakutana na jina la mama yake mzazi. Jacky akashtuka kidogo, ingawa hakujua kwa nini alishtuka kuona mama yake akimpigia simu. Jacky aliikodolea macho ile simu wakati ikiita hadi ikakatika pasipo kupokea.

Akiwa bado anatafakari akijiuliza mama yake alitaka kumwambia kitu gani, mara ile simu ikaanza kuita tena, Jacky alijishauri kama aipokee au aachane nayo lakini kuna sauti ndani yake ikawa inamsisitiza kuipokea ile simu, hivyo alishusha pumzi na kuipokea kisha akaiweka sikioni.

“Hello, mama, shikamoo!” alisema kwa sauti tulivu ya chini iliyokuwa na kitetemeshi.

“Marhaba, mwanangu, pole sana kwa msiba, mwanangu! Tupo pamoja nawe…” sauti ya majonzi ya mama yake ilisikika kutokea upande wa pili wa simu na kumfanya Jacky apate mshtuko mkubwa.

“Msiba wa nani, mama?” Jacky aliuliza huku akiitazama ile simu kwa makini, na hapo hapo akaanza kuhisi kizunguzungu.

“msiba wa nani! Kwani aliyekufa siyo mumeo?” sauti ya majonzi ya mama yake ilisikika tena ikiuliza kwa mshangao na kumfanya Jacky ahisi kama ile nyumba yake ilikuwa ikizunguka kama tufe kubwa lililokuwa likining’inia angani. Kwa sekunde chache Jacky alibaki kimya akiwa ameganda kama sanamu.

Jasho lilianza kumtoka, alijiona kama aliyekuwa amepigwa na shoti mbaya ya umeme huku akiuhisi mwili wake wote ukiwa mzito sana kama uliogeuka kuwa kipande cha chuma na moyo wake ukisahau mapigo yake kwa sekunde kadhaa.

Aliitazama ile nyumba yake na kujiona kama aliyekuwa yumo ndani ya pango kubwa lililotisha sana. Hakuwahi kuwaza hata siku moja kwamba nyumba yake aliyoipenda ingeweza kuwa kitu cha kutisha kiasi kile na hata kufikia hatua ya kumfanya kupagawa na kuogopa mno. Ilikuwa ni siku ambayo hangeweza kuisahau kabisa katika maisha yake!

Kwanza alidhani kuwa labda alikuwa kwenye usingizi wa mang’amung’amu kwa sababu tangu alipoamka asubuhi alikuwa na mawazo mengi yaliyokuwa yanapita kichwani kwake kiasi cha kumchosha, na kwamba yote aliyokuwa ameambiwa na mama yake kwenye simu yalikuwa ni mambo yaliyotendeka wakati akiwa yupo ndotoni.



Kwanza alidhani kuwa labda alikuwa kwenye usingizi wa mang’amung’amu kwa sababu tangu alipoamka asubuhi alikuwa na mawazo mengi yaliyokuwa yanapita kichwani kwake kiasi cha kumchosha, na kwamba yote aliyokuwa ameambiwa na mama yake kwenye simu yalikuwa ni mambo yaliyotendeka wakati akiwa yupo ndotoni.

Endelea...

Hali ile ikasababisha jasho jingi lizidi kumtoka sehemu mbalimbali za mwili wake, huku akihisi joto fulani ambalo alishindwa kulitafsiri likimtambaa mwilini mwake na mapigo ya moyo wake yakibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!

Wakati akiwa katika hali ile mara hisia zake zikamtanabaisha kuwa ile haikuwa ndoto bali kilikuwa kitu halisi kilichokuwa kimetokea na muda huo mama yake alikuwa akimfikishia taarifa zile. Hisia za kifo cha mumewe Carlos zikasababisha koo lake likauke ghafla huku nywele zake zikimsimama kichwani kwa hofu.

Hata hivyo, mara hii milango yake ya fahamu ilikuwa makini zaidi huku akijaribu kuishirikisha akili yake kikamilifu katika kumletea taarifa za kuaminika ili kujaribu kubaini endapo tukio lile lilikuwa katika mlolongo wa yale matukio ya ndotoni au la!...

“Jackline!” sauti ya upole ya mama yake ikamzindua Jacky kutoka kwenye yale mawazo. Jacky alishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Mama, kwani wewe taarifa hizi umezipata wapi?” Jacky alimuuliza mama yake huku akiwa bado haamini kile alichokisikia kwenye simu.

“Mbona zimesambaa kila mahali kwenye mitandao ya kijamii! Kuna mfanyakazi mmoja wa baba yako kule kiwandani ndiye aliyeanza kutupa habari hizi kuwa Carlos Mwamba amekufa kwenye ajali ya gari eneo la Vingunguti, sijui alikuwa anawakimbia polisi… tena wameweka hadi picha ya gari lake likionekana jinsi lilivyoharibika… Inamaana wewe hufahamu kama mumewo amekufa?” sauti ya mama yake ilisema maneno yale yaliyomfanya Jacky azidi kuchanganyikiwa.

Jacky aliuma midomo yake, akataka kuongea neno lakini akashindwa, kwani aligundua kuwa sauti yake ilikuwa haitoki, hivyo akaamua kukata simu.

Alipokata tu, mara simu ikaanza kuita tena, alipoitazama akaiona namba ya wifi yake Anita Mwamba. Jacky hakujiuliza tena, alibonyeza kitufe cha kupokelea na kuiweka ile simu sikioni, mara akasikia sauti ya Anita aliyekuwa akilia kwa uchungu mkubwa huku akiongea maneno ambayo Jacky hakuweza kuyasikia vizuri. Hakuona sababu ya kuendelea kuisikiliza ile simu, akaikata na kuitupia kando.

Hadi hapo hakuweza kuamini kama kweli Carlos alikuwa amekufa kwenye ajali, akafumba macho na kujiegemeza kwenye sofa huku akihema kwa nguvu, kisha kama mtu aliyekumbuka kitu, akaichukua ile simu na kuwasha data, na haikuchukua muda akaona ujumbe wa kifo cha Carlos Mwamba uliokuwa ukisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya WhatsApp na Instagram ukiambatana na picha ya gari aina ya BMW X6 xDrive 50i la rangi ya samawati lililokuwa limepondeka vibaya.

‘Mfanyabiashara maarufu wa madini ambaye pia anamiliki biashara kadhaa jijini Dar es Salaam amepata ajali eneo la Vingunguti wakati akiwakimbia askari, ajali hiyo imetokea mchana wa saa sita baada ya gari lake kupinduka na kutumbukia katika daraja la Mto Msimbazi, eneo la Vingunguti jijini Dar es salaam… pia ndani ya lile gari kulikuwa na binti mmoja ambaye bado haijulikani kama naye alikufa au alinusurika…’

Jacky alishtushwa sana na taarifa ile, alijikuta akisimama wima, mikono yake ikiwa kichwani huku akili yake ikikataa kabisa kukubali kile alichokuwa akikisoma. Ilikuwa ni habari mbaya sana aliyowahi kuisikia maishani kwake. Jacky aliendelea kusimama wima huku akiikodolea macho ile simu yake akiwa bado haamini, mawazo mengi yalizidi kupita kichwani mwake hukusu hatma yake.

Simu ziliendelea kupigwa, Jacky hakutaka kupokea simu yoyote, aliitupia kando ile simu huku ile picha ya gari BMW X6 xDrive 50i la rangi ya samawati lililokuwa limebondeka vibaya baada ya kupata ajali ikikataa kufutika akilini kwake.

Alianza kuhisi kuchanganyikiwa, sebule yote ilienea hali ya hewa ya joto kali sana ambalo lilianza kutambaa mwilini na kumfanya atamani kuvua nguo zake ili abaki mtupu. Kisha kama mtu aliyezinduka kutoka usingizini, akaanza kulia kwa uchungu mkubwa.

* * * * *

Saa kumi kasoro dakika tano jioni, kwenye chumba maalumu cha mahojiano cha Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam, Yusuf alikuwa ameketi kwenye kiti mbele ya meza ndefu yenye umbo mstatili. Alikuwa mnyonge sana huku akimtumbulia macho Ibrahim Komba kwa wasiwasi.

“Hii inaweza kuwa mara ya mwisho kukuita hapa na kukuhoji kuhusiana na wizi uliotokea pale Benki ya Biashara, kuwa makini sana katika majibu yako, umenielewa?” ASP Komba alisema huku akimkazia macho Yusuf.

“Nimekuelewa,” Yusuf alisema kwa unyonge huku akiwa bado anamtumbulia macho ASP Komba.

“Je, unamfahamu mwanamke mmoja anayeitwa Belinda?” ASP Komba alimhoji Yusuf huku akiwa amemkazia macho.

Yusuf alisita kidogo na kuangalia chini kwa kitambo, alishusha pumzi za ndani kwa ndani kisha akainua uso wake, “Belinda! Wa wapi?” aliuliza huku akionesha kushangaa kidogo.

“Belinda Jackson,” ASP Komba alimjibu Yusuf huku akiendelea kumkazia macho.

Yusuf akainamisha tena kichwa chake chini huku akishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani, “Simkumbuki mtu mwenye jina hilo,” hatimaye alijibu huku akiangalia kando kuyakwepa macho makali ya ASP Komba.

“Ni kweli humkumbuki Belinda Jackson?” ASP Komba aliuliza tena huku akiendelea kumkazia macho Yusuf. Yusuf alitingisha kichwa chake kukataa. ASP Komba alimwangalia kwa makini kwa kitambo kifupi na kuachia tabasamu pana.

“Nilikwambia uwe makini sana katika majibu yako, ukasema umeelewa,” ASP Komba alisema huku akiendelea kutabasamu, lakini tabasamu lake lilikuwa limeficha ghadhabu aliyokuwa nayo.

“Ndiyo nimekuelewa sana, afande. Huyo Belinda Jackson simkumbuki kweli,” Yusuf alijaribu kujitetea.

“Unasema uongo, nimelikuta jina lake na namba yake ndani ya simu yako. Unaweza kuniambia vimefikaje?” ASP Komba alimuuliza kwa sauti tulivu huku akimtulizia macho usoni bila kupepesa.

Yusuf alishtuka, jasho jepesi lilianza kumtoka sehemu mbalimbali za mwili wake huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio isivyo kawaida. ASP Komba alizidi kumkazia macho.

“Nijibu, vimefikaje?” ASP Komba aliuliza kwa ukali.

“Alinipa mwenyewe,” Yusuf alisema kwa unyonge huku akiangalia chini.

“Alikupa lini?”

“Muda mrefu.”

“Muda mrefu… lini?”

“Kama wiki mbili hivi zilizopita.”

“Wiki mbili zilizopita, eh?”

“Ndiyo afande.”

“Mlikutana wapi?”

Yusuf alitaka kusema neno lakini akasita, na hapo machozi yakaanza kumlenga lenga machoni. Kikapita kitambo kifupi cha ukimya huku Yusuf akifuta machozi, “Tuli… tulikutana hotelini,” hatimaye alisema huku akifuta machozi.

“Mlikutana katika hoteli gani?” ASP Komba alizidi kumsaili Yusuf.

“Kwanza tulikutana Southern Sun na baadaye tukakutana Amariah Hotel,” Yusuf alijibu kwa unyonge.

ASP Komba alivuta droo ndogo na kutoa picha kadhaa za Carlos na Jacky alizokuwa amezipakua kutoka kwenye mtandao, kisha akachukua picha ya Jacky na kumuonesha Yusuf, “Belinda Jackson ndiyo huyu, siyo?”

Yusuf aliitazama ile picha ya Jacky kwa kitambo kirefu pasipo kusema neno lolote huku midomo yake ikimtetemeka kwa hofu. Machozi yalizidi kumlenga lenga machoni.

“Nijibu, huyu ndiye Belinda Jackson, siyo?”

“Ndiyo, afande,” Yusuf alijibu kwa unyonge.




Yusuf alitaka kusema neno lakini akasita, na hapo machozi yakaanza kumlenga lenga machoni. Kikapita kitambo kifupi cha ukimya huku Yusuf akifuta machozi, “Tuli… tulikutana hotelini,” hatimaye alisema huku akifuta machozi.

“Mlikutana katika hoteli gani?” ASP Komba alizidi kumsaili Yusuf.

“Kwanza tulikutana Southern Sun na baadaye tukakutana Amariah Hotel,” Yusuf alijibu kwa unyonge.

ASP Komba alivuta droo ndogo na kutoa picha kadhaa za Carlos na Jacky alizokuwa amezipakua kutoka kwenye mtandao, kisha akachukua picha ya Jacky na kumuonesha Yusuf, “Belinda Jackson ndiyo huyu, siyo?”

Yusuf aliitazama ile picha ya Jacky kwa kitambo kirefu pasipo kusema neno lolote huku midomo yake ikimtetemeka kwa hofu. Machozi yalizidi kumlenga lenga machoni.

“Nijibu, huyu ndiye Belinda Jackson, siyo?”

“Ndiyo, afande,” Yusuf alijibu kwa unyonge.


Endelea...


“Kwa hiyo, ni rafiki yako, siyo?” ASP Komba alizidi kumbana Yusuf huku akizidi kumkazia macho. Yusuf alisita tena, akamwangalia ASP Komba kwa wasiwasi.

“Siyo sana, afande,” Yusuf alisema kwa sauti ya unyonge.

“Si sana, eh? Ulijua kama alikuwa amekuongopea jina na wala haitwi Belinda Jackson?”

Yusuf akaonekana kushtuka sana na kumtazama ASP Komba kwa mshangao. Hata hivyo, hakujibu bali alibaki kimya mdomo ukiwa wazi kwa mshangao.

“Je, ulijua kama ana mume?” ASP Komba alimuuliza tena huku akimkazia macho.

“Sikupata kumuona!”

“Jibu swali langu, sijakuuliza kama ulipata kumuona… Ulijua kama ana mume?”

“Aliniambia kuwa hajaolewa,” Yusuf alisema huku akitaka kulia.

“Alikwambia hajaolewa… na ukamuamini na kufanya naye urafiki?” ASP Komba aliuliza huku akitingisha kichwa chake kwa huzuni.

“Siyo sana, afande. Si nimekuambia?” Yusuf alisema huku akifuta machozi.

ASP Komba alimtazama Yusuf kwa umakini kwa kitambo kirefu, kisha akatingisha kichwa chake na kuvuta jalada la kesi lililokuwa mbele yake. Alilifungua lile jalada na kutoa nakala kivuli ya hundi ya benki ya kampuni ya The Jacarandah Group iliyokuwa na saini, akaiwekea mbele ya Yusuf.

“Hii ulimpa nani? Carlos Mwamba au Jackline Mgaya ambaye wewe unamfahamu kwa jina la Belinda Jackson?” ASP Komba alimuuliza Yusuf huku akiisogeza ile nakala kivuli ya hundi karibu zaidi ya Yusuf.

Yusuf alinywea sana mara alipoiona ile nakala kivuli ya hundi ya benki ya kampuni ya The Jacarandah Group iliyokuwa na saini, alianza kutetemeka, machozi yakaanza kumwagika machoni utadhani milizamu iliyopasuka. ASP Komba aliendelea kumkazia macho pasipo kupepesa.

“Ulimpa nani, mbona hujibu?” ASP Komba alimuuliza kwa ukali.

“Lakini, afande…” Yusuf alitaka kujitetea lakini ASP Komba alimkatisha kwa sauti ya ukali.

“Hutaki kujibu, eh?”

“Nilimpa Belinda,” Yusuf alisema huku akifuta machozi. ASP Komba alibetua kichwa chake huku akiachia tabasamu, lakini akiwa bado amemkazia macho Yusuf bila kupepesa.

“Je, unamjua Jasmine Kombo?” ASP Komba alimtupia Yusuf swali jingine. Yusuf alimtazama ASP Komba kwa unyonge na kufuta machozi yaliyoendelea kumtoka kwa fujo na kutitirika mashavuni.

“Kwa kweli huyo simjui kabisa!” Yusuf alisema kwa huzuni huku akiinamisha kichwa chake chini kwa majonzi.

“Hukupata hata kumsikia?”

“Hata mara moja.”

ASP Komba aliichukua ile nakala kivuli ya hundi na kuirudisha kwenye lile faili, kisha alipaza sauti yake kumwita Sajenti Mapambano, na mara aliingia Sajenti Mapambano na kusimama mbele yake kwa ukakamavu.

“Mrudishe huyu rumande,” ASP Komba alimwambia Sajenti Mapambano huku akiinuka na akusimama dirishani.

Sajenti Mapambano alimchukua Yusuf na kutoka naye nje ya kile chumba cha mahojiano. ASP Komba alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuingiza mkono wake kwenye mfuko wa gwanda lake na kutoa pakiti ya sigara kisha akatoa sigara moja na kuibana kwenye pembe ya mdomo wake, akaiwasha na kuanza kuvuta taratibu huku akitafakari kuhusu kazi iliyokuwa mbele yake.

* * * * *

Saa kumi na mbili jioni katika eneo la Tabata Segerea katika mtaa wa majumba ya kifahari ya watu wenye ukwasi mkubwa, vilio na nyimbo mbalimbali za maombolezo vilikuwa vikisikika kutoka ndani ya nyumba kubwa ya kifahari ya Jacky na Carlos.

Muda ule taarifa za msiba mzito wa Carlos zilikuwa zimeenea kila mahali na watu wengi waliomfahamu na hata wale waliokuwa wakimsikia tu walifika pale kuomboleza kifo kile cha ajali.

Ndani ya lile jumba la kifahari Jacky alikuwa analia kwa uchungu mkubwa kilio cha kwikwi akiwa pale sebuleni huku akiwa amezungukwa na waombolezaji kadhaa wanawake, wengi wakiwa rafiki na jamaa zake wa karibu.

Pamoja na maombolezo hayo bado hakukuwa na taarifa rasmi zilizokuwa zimetolewa kuhusiana na nini sababu ya ajali iliyosababisha kifo cha Carlos. Salamu za rambirambi zilikuwa zikimiminika kutoka kila pembe ya nchi, watu mbalimbali waliomfahamu au kufanya biashara na Carlos walikuwa wakimpa pole Jacky kwa kufiwa na mumewe Carlos.

Na kwa watu waliokuwa wamefika pale kwenye msiba kila mmoja alijaribu kuuliza hili na lile ili kupata uhakika kama kweli ajali iliyosababisha kifo cha Carlos ilitokana na kuwakimbia polisi, kama ilivyokuwa imeelezwa kwenye taarifa zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao.

Makachero wa polisi, Haji Adam, Sebastian Masesa na Koplo Victor Shirima, waliokuwa wamevaa mavazi ya kiraia walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa katika eneo lile wakiomboleza msiba ule mzito uliogusa nyoyo za watu wengi. Hata hivyo, wao hawakuwepo pale kama waombolezaji bali walikuwepo pale kwa kazi maalumu waliyokuwa wamepewa na ASP Komba.

Kila aliyekuwepo katika eneo lile la msiba kama hakuwa katika sura ya huzuni basi alikuwa kazungukwa na maswali mengi yasiyo na majibu. Eneo la nje katika barabara ya mtaa ule kulikuwa na magari kadhaa ya kila aina ya ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa wamefika kuomboleza msiba ule na kumpa pole Jacky kwa kifo cha mumewe Carlos Mwamba.

Ki ukweli kifo cha Carlos kilikuwa pigo kubwa kwa vijana wa eneo lile na kileta simanzi nzito, ulikuwa ni msiba wa mtu mashuhuri sana katika eneo lile ambaye alikuwa akisaidia watu na alijitoa kwa hali na mali, na kila mtu aliyefika pale kwenye msiba alionesha kuguswa kwa namna moja au nyingine kwa jinsi Carlos alivyokuwa akijitoa kusaidia watu, alikuwa mcheshi aliyeopenda kucheka na kila mtu na mkarimu ambaye mfano wake ulikuwa haujapata kuonekana katika eneo lile.

“Ama kweli wema hawadumu!” kijana mmoja aliyekuwa ameketi nje ya fensi ya ile nyumba yenye msiba, chini ya mti mkubwa wa kivuli akiwa na vijana wenzake alisikika akisema kwa kauli ya kukata tamaa huku akivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu.

* * * * *

Saa moja na nusu ya asubuhi ilimkuta ASP Komba akiwa bado ameketi kwenye kiti chake ofisini mwake akiyapitia baadhi ya makaratasi aliyokuwa akiyafanyia kazi, kuhusiana na upelelezi wa wizi wa mabilioni ya fedha katika Benki ya Biashara tawi la barabara ya Lumumba, jijini Dar es Salaam. Alikuwa ameketi pale tangu saa kumi na mbili na nusu akijaribu kuhakikisha anakamilisha kazi ile haraka. Muda ule alikuwa amevaa nguo za kiraia.

Simu yake ya mkononi iliyokuwa mbele yake juu ya meza iliaza kuita kwa fujo, ASP Komba akaitupia jicho mara moja tu na kuiona namba ngeni, akaipuuza. Alikuwa ametingwa na kazi ngumu mbele yake na kitendo cha kupokea simu kingemchelewesha kwani alitaka akamilishe ile kazi haraka iwezekanavyo ili kesi ipelekwe mahakamani.




Simu yake ya mkononi iliyokuwa mbele yake juu ya meza iliaza kuita kwa fujo, ASP Komba akaitupia jicho mara moja tu na kuiona namba ngeni, akaipuuza. Alikuwa ametingwa na kazi ngumu mbele yake na kitendo cha kupokea simu kingemchelewesha kwani alitaka akamilishe ile kazi haraka iwezekanavyo ili kesi ipelekwe mahakamani.


Endelea...


Ile simu iliendelea kuita hadi ikakatika, kisha ikaanza kuita tena kwa muda mrefu na kumfanya ASP Komba ayaondoshe macho yake kutoka kwenye yale makaratasi, akainyakua ile simu kwa hasira.

“ASP Komba… nani mwenzangu?” ASP Komba huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Dk Masha hapa. Habari za saa hizi, afande,” sauti ya Dk Masha ilisikika wazi ikiongea kutoka upande wa pili wa ile simu.

“Ooh, dokta! Habari ni nzuri tu, za huko?”

“Nzuri kabisa. Mbona simu imeita weeee…”

“Ah, nilidhani napigiwa simu na jamaa fulani hivi wanataka mchango wa harusi. Enhe mnaendeleaje huko?” ASP Komba alisema huku uso wake ukichanua tabasamu.

“Tunaendelea vyema.”

“Vipi hali ya yule binti?”

“Hali yake inazidi kuimarika. Enhe jana ilikuwaje ndugu yangu?” Dk Masha alimuuliza ASP Komba.

“Vipi?”

“Nimekutafuta sana kwenye simu yako ya mkononi sikukupata.”

“Ni kweli, niliizima kabisa simu kukwepa kero.”

“Kero ipi tena?”

“Nilikuwa napigiwa simu nyingi kuulizwa maswali ambayo sikuwa na majibu yake, na mengine yalionesha kuingilia utaratibu wangu wa kazi.”

“Basi nilitaka kukutaarifu kuwa yule binti kwa sasa yuko fit, ukipata nafasi mchana baada ya madaktari kupita round unaweza kuja kuongea naye,” Dk Masha alisema na kumfanya ASP Komba aachie tabasamu.

“Okay, ninashukuru kwa taarifa, dokta.” ASP Komba alisema na kushusha pumzi. Simu ikakatwa.

ASP Komba aliinuka kutoka pale kwenye kiti chake, akaingiza mkono wake kwenye mfuko wa suruali yake na kutoa pakiti ya sigara kisha akatoa sigara moja na kuibana kwenye pembe ya mdomo wake, akaiwasha na kuanza kuvuta taratibu huku akitafakari.

Baada ya kitambo kirefu aliamua kutoka ndani ya ile ofisi yake kisha akashuka ngazi na kuelekea kule chini, kwenye mahabusu, akamkuta Yusuf akiwa amekaa akiwa amejikunyata kwa huzuni jirani na uzio wa nondo. ASP Komba alimtazama Yusuf, akatingisha kichwa polepole.

“Afande, vipi sasa kuhusu dhamana yangu?” Yusuf alimuuliza ASP Komba mara baada ya kumuona.

“Nani aliyekuambia unaweza kuwekewa dhamana? Unashirikiana na majambazi waliokubuhu, halafu upewe dhamana?”

Yusuf alibaki kimya akiwa anamtumbulia macho ASP Komba, uso wake ulisawajika na alionesha kupoteza kabisa matumaini ya kutoka. ASP Komba alitoka na kumwita Koplo Victor, “Twende zetu hoteli ya Southern Sun na baadaye Amariah,” alimwambia. Wakatoka nje ya lile jengo la kituo kikuu cha polisi na kuliende gari lao.

Muda ule ule Mama Jasmine akiwa ameambatana na mwanamke mmoja mtu mzima walifika na kuingia ndani ya lile jengo, walifika pale kaunta ya polisi na kusimama huku wakimwangalia ofisa mmoja wa polisi mwenye cheo cha sajenti. Mama Jasmine alikuwa amekuja na chai.

“Wewe ndiye uliyetakiwa kumletea chai huyu… Yusuf?” yule ofisa wa polisi mwenye cheo cha sajenti aliyekuwa pale kaunta alimuuliza Mama Jasmine baada ya kujitambulisha.

“Ndiyo.”

“Ni ndugu yako?”

“Mume wangu.”

“Fungua hiyo chai, mimina kidogo unywe!”

Mama jasmine alifanya kama alivyoambiwa na yule ofisa wa polisi mwenye cheo cha sajenti, akaonja na kitafunwa alichokuwa ameleta na baada ya yule askari kuridhika akamfuata Yusuf na kumpa ile chai.

* * * * *

Saa sita za mchana, katika wodi moja ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Amana, Jasmine alikuwa amejilaza kitandani kwenye foronya laini na mto wa kuegemeza kichwa. Alikuwa na majeraha kwenye kichwa chake na kwenye mkono wake wa kushoto.

Muda ule Jasmine alikuwa anaongea na jamaa zake wawili waliokuwa wamefika pale hospitalini kumletea chakula na kumjulia hali. Dk Masha aliingia akiwa ameongozana na ASP Komba, ambaye hakuwa amevaa mavazi rasmi ya kazi, wakatembea taratibu hadi kwenye kitanda alichokuwa amelazwa Jasmine.

“Vipi, unajisikiaje sasa?” Dk Masha alimuuliza Jasmine huku akiachia tabasamu pana usoni kwake.

“Kidogo afadhali, ila kichwa ndiyo bado kinaniuma,” Jasmine alimwambia Dk Masha huku akipeleka mkono wake kichwani.

“Usijali… utapata nafuu na kupona kabisa,” Dk Masha alimwambia Jasmine huku akigeuza shingo yake kumtazama ASP Komba. Wakatazama kwa kitambo fulani huku Dk Masha akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Sasa Jasmine, nimekuja na mgeni ambaye atajitambulisha, anahitaji kupata maelezo fulani kutoka kwako,” Dk Masha alisema kwa sauti tulivu huku akiachia tabasamu.

Jasmine alishtuka sana na kumtumbulia macho ASP Komba kwa wasiwasi. Alimtazama kama aliyekuwa akimfananisha, “Kwema lakini?” Jasmine aliuliza huku akizidi kumkazia macho ASP Komba.

“Usihofu, hapa uko kwenye mikono salama kabisa, binti,” Dk Masha alimwambia Jasmine huku akigeuza shingo yake kumtazama tena ASP Komba.

“Okay! I wish you a good success, let me go back to the office,” (Nakutakia mafanikio mema, ngoja mimi nirudi ofisini) Dk Masha alimwambia ASP Komba na kuondoka bila kusubiri jibu lake huku akimwacha ASP Komba akiwa amesimama akimtazama Jasmine kwa makini. Jasmine na rafiki zake waliendelea kumtazama ASP Komba kwa wasiwasi.

“Unajisikiaje sasa, Jasmine?” ASP Komba alimuuliza Jasmine huku akiwatupia macho wale jamaa zake.

“Sijambo kiasi, nashukuru Mungu kwa kuwa bado naongea.”

“Pole sana!”

“Asante, lakini mimi sikufahamu, sijui mwenzangu nani?” Jasmine alimuuliza ASP Komba huku akitabasamu.

“Naitwa Ibrahim Komba, mimi ni ofisa wa polisi na ninatokeaa kituo kikuu cha polisi,” ASP Komba alimwambia Jasmine huku akiachia tabasamu pana usoni kwake.

Jasmine alibadilika ghafla na kunywea, uso wake ulisawajika na muda ule ule aliwatazama wale jamaa zake na kushusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani. “Sawa… karibu,” aliitikia kwa unyonge.

“Asante sana… nadhani ndugu zako wangetupisha kidogo, nahitaji kuongea na wewe,” ASP Komba alimwambia Jasmine kwa sauti tulivu ya chini.

Jasmine alisita kidogo na kuwatupia jicho wale jamaa zake, kisha alimtazama ASP Komba na kukunja sura yake. “Kuongea na mimi kuhusu nini?” alimuuliza ASP Komba huku akimkazia macho.

“Mambo mawili matatu. Wala usiwe na wasiwasi, binti.”

“Mungu wangu! Mambo gani tena jamani?” Jasmine alilalama huku akiwatupia jicho wale jamaa zake.

ASP Komba aliwageukia wale jamaa wa Jasmine na kuongea kwa sauti tulivu ya kirafiki, “Samahani, naomba mtupe nafasi kidogo, nahitaji kuongea na ndugu yenu.”

Wale wanawake waliinuka kwa unyonge bila kuhoji chochote na kutoka nje huku wakimtazama Jasmine kwa wasiwasi. ASP Komba alimkazia macho Jasmine akimtazama kwa umakini.

“Jasmine, wewe ni mfanyakazi wa The Jacarandah Group, ile kampuni iliyoibiwa mabilioni ya fedha hivi karibuni, sawa?” ASP Komba alimuuliza Jasmine huku akiendelea kumkazia macho pasipo kupepesa.

“Sawa,” Jasmine alijibu bila kusita.

“Lini uliacha kwenda kazini?” ASP Komba aliuliza huku akiketi kando ya kitanda.

“Mi sijaacha kwenda kazini, nani kakwambia kuwa mimi siendi kazini?” Jasmine alisema huku akikunja sura yake.




“Jasmine, wewe ni mfanyakazi wa The Jacarandah Group, ile kampuni iliyoibiwa mabilioni ya fedha hivi karibuni, sawa?” ASP Komba alimuuliza Jasmine huku akiendelea kumkazia macho pasipo kupepesa.

“Sawa,” Jasmine alijibu bila kusita.

“Lini uliacha kwenda kazini?” ASP Komba aliuliza huku akiketi kando ya kitanda.

“Mi sijaacha kwenda kazini, nani kakwambia kuwa mimi siendi kazini?” Jasmine alisema huku akikunja sura yake.


Endelea...


“Sijaambiwa na mtu yeyote,” ASP Komba alijibu huku akiachia tabasamu.

“Kumbe umejuaje?”

“Jasmine, najua ni vigumu sana, lakini ningependa ujibu maswali yangu bila kuhoji chochote. Tumeelewana?” ASP Komba alisema kwa sauti tulivu.

“Yaani miye ninyamaze tu?” Jasmine alisema na kugeuka pembeni huku akiwa amenuna.

“Hujanielewa, sijasema wewe unyamaze tu. Nasema jibu maswali yangu bila kunihoji chochote, tumeelewana?”

“Haya,” Jasmine alijibu huku akiwa bado kaangalia pembeni.

“Tunaanza mwanzo, tangu lini hujaenda kazini?”

“Nimeshakujibu, sijaacha kwenda kazini.”

“Hata siku moja?”

“Ndiyo, hata siku moja.”

“Unaweza kukumbuka ni lini fedha za kampuni yenu ziliibwa benki?”

“Hata sikumbuki, kwani wakati wizi huo unatokea mimi nilikuwa nyumbani naumwa,” Jasmine alisema huku akimtupia jicho kali ASP Komba.

“Ulikuwa ukiumwa nini?”

“Malaria.”

“Umeugua siku ngapi?”

“Siku tatu.”

“Ulitoa taarifa kwa mwajiri wako?”

“Sikuweza, nilizidiwa sana.”

“Kwa nini usimtume mtu akatoe taarifa, au hata kupiga simu?”

“Nimtume nani, kila mtu ana shughuli zake,” Jasmine alisema huku akinyanyua juu mabega yake juu.

“Na hawa ndugu zako niliowakuta hapa?” ASP Komba alimuuliza huku akimkazia macho.

“Wale siyo ndugu zangu, ni majirani tu.”

“Na kwa nini usipige simu, kwani huna simu?” ASP Komba alizidi kumuuliza Jasmine huku akiwa amemkazia macho bila kupepesa.

“Simu yangu imeharibika, ndiyo nilikuwa natarajia kununua simu nyingine hivi karibuni nikipata mshahara,” Jasmine alijaribu kujitetea.

“Ulimfahamu vipi marehemu Carlos Mwamba?” ASP Komba alimuuliza swali ambalo lilionekana kumshtua kidogo Jasmine.

“Alikuwa rafiki wa marehemu baba yangu, kwani amekufa?” Jasmine alijibu na kuuliza swali hapo hapo huku akiinamisha uso wake na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Ndiyo amekufa. Kwa maana hiyo, alikuwa rafiki wa baba yako ndiyo maana akaamua kukutumia kufanikisha wizi wa hundi kutoka ofisini kwenu, Uongo?” ASP Komba alisema huku akiwa amekunja sura yake akimkazia macho Jasmine.

Jasmine alishtuka sana, moyo wake ukashikwa na mfadhaiko huku ukianza kwenda mbio isivyo kawaida. Kwa sekunde chache aliyasahau maumivu yake na jasho jepesi likaanza kumtoka sehemu mbalimbali za mwili wake, akamtazama ASP Komba huku akitetemeka kwa mbali.

“Hebu nieleze ukweli, Jasmine, na ole wako ukijaribu kuficha… ujue Carlos Mwamba hayupo lakini wewe upo… hivyo kukana ni kujichongea,” ASP Komba alisema na kunyamaza kidogo huku akizidi kumtazama Jasmine kwa makini.

“Ni wewe uliyempa ile hundi Carlos Mwamba?” ASP Komba alimuuliza Jasmine kwa sauti tulivu. Jasmine alionekana kunywea sana, alimtazama ASP Komba kwa chuki pasipo kujibu lile swali.

“Jibu swali langu, Jasmine,” ASP Komba aliuliza huku akizidi kumkazia macho.

“Ndiyo,” Jasmine alijibu kwa sauti ya unyonge huku akitazama kando.

“Uliipata vipi?”

“Kitabu cha hundi huwa kipo mezani kwa bosi, na mimi huwa naingia ofisini kwake kila siku,” Jasmine alisema huku machozi yakimlenga lenga machoni.

“Carlos Mwamba alikuahidi kukupa kiasi gani cha fedha akifanikiwa?”

“Shilingi milioni mia moja.”

“Ooh… kwa hiyo wewe sasa hivi ni milionea, siyo? Nadhani tayari amekwisha kupa!”

“Bado, ndiyo alikuwa amenifuata ili akanipe, bahati mbaya tena ikatokea ajali,” Jasmine alisema kwa huzuni huku akifuta machozi yaliyoanza kumtoka.

ASP Komba alimtazama Jasmine kwa kitambo kirefu, huruma ikaanza kumwingia lakini hakutaka kuiruhusu iingilie majukumu yake ya kazi, hivyo alitingisha kichwa chake taratibu huku akimtazama Jasmine kwa makini.

Mara simu yake ikaanza kuita, ASP Komba aliitazama ile simu kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani, kisha akamtaka radhi Jasmine na kutoka nje haraka.

ASP Komba alifika nje ya lile jengo la wodi ya wanawake akamkuta Sajenti Mapambano akiwa amesimama na muuguzi mmoja wakiongea. Wakazungumza mawili matatu kwa kitambo kifupi, kisha ASP Komba akaelekea ofisini kwa Dk Masha kumuaga akiahidi kurudi baadaye.

Alipotoka wakaongozana hadi kwenye gari lao aina ya Nissan Patrol la rangi nyeusi lililokuwa na maandishi ya POLISI ubavuni, wakaingia ndani ya lile gari na kuondoka haraka.

* * * * *

Jua la saa saba mchana lilishaanza kuchukua nafasi yake juu ya anga, hali ambayo waswahili waliita jua la utosi, na hivyo kuifanya hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam kuwa ya joto sana. Katika barabara ya Mandela kulionekana foleni ya magari, na miongoni mwa magari yale lilionekana gari polisi aina ya Nissan Patrol la rangi nyeusi lililokuwa na maandishi ya POLISI ubavuni liikuwa katika mwendo wa kasi.

Ndani ya gari lile kulikuwa na watu watatu, dereva wa gari lile, Koplo Victor Shirima, ASP Komba aliyekuwa ameketi kwenye siti ya mbele kushoto kwa dereva na Sajenti Mapambano aliyeketi siti ya nyuma.

Sajenti Mapambano alikuwa akimweleza ASP Komba kuhusiana na taarifa mpya za kipelelezi alizozipata kutoka nyumbani kwa marehemu Carlos Mwamba.

Gari lile la polisi lilipofika katika eneo la taa za barabarani za kuongozea magari katika eneo la Tabata liliiacha ile barabara ya Mandela na kukunja kushoto likiingia katika barabara iliyokuwa ikielekea Tabata.

Kuanzia pale maongezi ndani ya lile gari yalikatika ghafla na kila mmoja alikuwa kimya akitafakari kuhusu kazi ile iliyokuwa mbele yao.

ASP Komba aliangaza macho yake kuangalia nje akiyatazama magari mbalimbali waliyopishana nayo katika mitaa ile ya Tabata huku kichwani akiwaza kuhusu hatma ya mshikemshike wa kila siku wa kukimbizana na wahalifu. Alishangaa kwa nini watu hawakutaka kuacha uhalifu na kusihi maisha mema ya kumcha Mungu, huku akijiuliza hali kama ile itaisha lini!

Alijikuta akizikumbuka ndoto zake za ujanani alipokuwa akiota kuja kuwa na mafanikio makubwa kwa kucheza soka, kwani alipokuwa shuleni alikuwa mcheza soka mahili sana na alisifiwa na kila mtu, na wakati mwingine alikuwa na ndoto ya kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa nchini.

Hata siku moja hakuwahi kuota kuja kuwa ofisa wa polisi, na ilitokea tu siku moja pale alipokuwa katika kumalizia masomo yake pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alijikuta akishawishiwa na hatimaye kuvutiwa kuchukua fomu akiomba kujiunga na Jeshi la Polisi.

ASP Komba alizidi kuwaza hili na lile na mara akajikuta akikumbuka siku zake za mwanzo kabisa baada ya kufuzu mafunzo yake ya upolisi katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi (MPA).

Alikumbuka baada ya kumaliza mafunzo ya uaskari kituo chake cha kwanza cha kazi kilikuwa mkoani Mwanza na baada ya kuripoti pale Mwanza, haikupita hata miezi sita kukatokea mapambano makali sana kati ya polisi na majambazi sugu waliokuwa wamejificha katika mapango ya milima ya Utemini, yaliyochukua zaidi ya saa 12.

Wakati ule hayo yakitokea ASP Komba alikuwa bado hajapewa cheo chochote, na baada ya mapambano yale polisi walishinda na majambazi wale wakakutwa na silaha nzito za kivita walizokuwa wamezificha mapangoni.



Alikumbuka baada ya kumaliza mafunzo ya uaskari kituo chake cha kwanza cha kazi kilikuwa mkoani Mwanza na baada ya kuripoti pale Mwanza, haikupita hata miezi sita kukatokea mapambano makali sana kati ya polisi na majambazi sugu waliokuwa wamejificha katika mapango ya milima ya Utemini, yaliyochukua zaidi ya saa 12.

Wakati ule hayo yakitokea ASP Komba alikuwa bado hajapewa cheo chochote, na baada ya mapambano yale polisi walishinda na majambazi wale wakakutwa na silaha nzito za kivita walizokuwa wamezificha mapangoni.


Endelea...


Pia ASP Komba aliyakumbuka makovu mawili ya risasi yaliyokuwa kwenye paja lake la mguu wa kulia na kovu jingine la kisu lililokuwa kwenye bega lake ambayo alikuwa ameyapata kwenye harakati mbalimbali za kupambana na uhalifu mkubwa. Alijikuta akimeza funda kubwa la mate kuzitowesha kumbukumbu zile mbaya.

Mawazo yake yaliporudi tena mle ndani ya gari alishtuka kuona kuwa tayari walikuwa wamefika eneo walilokuwa wakienda, kwani walikuwa wakipita katika barabara tulivu ya mtaa wenye majumba ya kifahari yaliyozungukwa na miti mirefu ya kivuli na kuta zenye usalama wa uhakika.

Hawakuchukua muda wakawa wamefika katika nyumba ya kifahari aliyokuwa akiishi Carlos Mwamba na mkewe Jackline Mgaya. ASP Komba na Sajenti Mapambano walishuhudia magari mengi ya kifahari na mengine ya kawaida yaliyokuwa yameegeshwa kwenye barabara yote ya mtaa ule.

Pia kulikuwa na watu wengi waliofika pale kuomboleza msiba na kumpa pole Jacky kwa kifo cha mumewe Carlos waliokuwa wameketi kwa utulivu kwenye maturubai maalumu yaliyokuwa yamefungwa kwenye eneo kubwa la wazi mbele ya ile nyumba.

Muda ule sauti ya nyimbo za maombolezo kutoka kwenye spika kubwa zilizokuwa zimesambazwa katika eneo lote ziliendelea kusikika katika eneo lile, nje na ndani ya nyumba ile, huku watu wakizidi kufika pale kuomboleza msiba ule mkubwa wa mtu mashuhuri.

Koplo Victor alipunguza mwendo wa gari huku akiyatembeza macho yake huku na kule akitafuta sehemu nzuri ya kuegesha gari lao na baada ya muda mfupi hatimaye akawa amepata sehemu nzuri na kuliegesha lile gari.

ASP Komba na Sajenti Mapambano waliteremka kutoka kwenye lile gari na kuanza kutembea taratibu wakirudi nyuma kuifuata ile nyumba, kisha wakaanza kukatiza wakipenya penya katikati ya watu waliokuwa wamejaa eneo lile ili kuingia ndani ya ile nyumba. Baadhi ya waombolezaji waliokuwepo eneo lile waliwatazama kwa wasiwasi huku wakiwapisha.

Walifanikiwa kupenya na kulifikia geti kubwa jeusi, kisha wakaingia ndani ya uzio wa lile jumba la kifahari na baadaye wakafanikiwa kuingia sebuleni na kukaribishwa. Walikwenda moja kwa moja hadi alipokuwa ameketi Jacky akiwa analia taratibu kilio cha kwikwi pale sebuleni huku akifarijiwa na ndugu, jamaa na rafiki zake.

Pale sebuleni pia walikuwepo ndugu wengine kama wifi zake, shemeji zake, wakwe zake na wazazi wake ambao wote kwa pamoja waliendelea kuomboleza msiba ule wa mpendwa wao.

Jacky aliinua uso wake na kuwaona wale maofisa wa polisi, akashtuka sana na kupunguza kulia. Aliwatazama kwa umakini na kufuta machozi yake huku akijitahidi kutengeneza sura ya kirafiki. ASP Komba na Sajenti Mapambano walimsogelea huku wakionesha huzuni yao.

“Pole sana kwa msiba,” ASP Komba alimwambia Jacky kwa sauti tulivu ya chini huku akichuchumaa na kumpa mkono.

“Asante, kazi ya Mungu,” Jacky alijitahidi kujibu huku akionesha unyonge na kujiweka vizuri pale sakafuni alipokuwa ameketi huku akimpisha ASP Komba apate nafasi ya kuketi. Sajenti Mapambano naye alimsalimia na kuketi kando.

Wale watu wengine waliokuwa wakiomboleza na wengine waliokuwa wakimfariji Jacky waliwatazama ASP Komba na Sajenti Mapambano kwa umakini huku wakiwa na maswali kibao kichwani. ASP Komba alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiwatazama wale kina mama waombolezaji.

“Jacky, kwanza nichukue nafasi hii kukupa pole sana… mimi naitwa Ibrahim Komba na mwenzangu hapa ni Venance Mapambano, nadhani sisi siyo wageni kwako kwani tumeshawahi kukutana mara kadhaa…” ASP Komba alijitambulisha kwa Jacky kwa sauti tulivu ya chini.

Jacky alibetua kichwa chake kukubali huku akishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani, “Nawafahamu vizuri sana, wala hamna haja ya kujitambulisha kwanu” alisema huku akiinamisha sura yake kutazama chini.

“Okay, basi tuna sababu muhimu sana ya kuja hapa kuongea na wewe. Tunajua uko kwenye msiba mkubwa sana kwa kuondokewa na mume wako mpenzi, lakini tutahitaji nafasi kidogo ili kukuuliza maswali mawili matatu kama hutojali,” ASP Komba alimwambia Jacky kwa sauti tulivu ya chini.

Jacky aliwatupia jicho ndugu na jamaa zake kwa wasiwasi waliofika kwenye msiba kumfariji kisha akamtazama ASP Komba akionekana kusita kidogo, kisha alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiminya midomo yake.

“Usijali, tunaweza kwenda kuongea chemba kidogo ili tusiingilie shughuli za watu wengine,” ASP Komba alimweleza Jacky huku akiinuka. Jacky aliweatupia tena jicho wale ndugu na jamaa zake kisha akainuka na kuwaongoza ASP Komba na sajenti Mapambano hadi eneo moja chini ya mti wa kivuli lililoonekana tulivu kwenye ile fensi ya nyumba.

Eneo lile kulikuwa na vijana wameketi wakibishana kuhusiana na nani mkali kati ya Messi na Cristiano Ronaldo. Jacky aliwaomba wale vijana wapishe kidogo kwani alihitaji kuongea na wale maofisa wa polisi. Wale vijana waliinuka na kuondoka eneo lile mmoja mmoja huku wakiwaacha wale maofisa wa polisi na Jacky wakiwasindika kwa macho.

“Karibuni, sijui mnasemaje maana sijajua sababu ya ujio wenu,” Jacky alimwambia ASP Komba mara baada ya kuachwa peke yao huku akijiweka sawa kwenye kiti chake.

“Ni kuhusu wizi wa bilioni moja na milioni mia tatu zilizoibiwa katika Benki ya Biashara juzi, sisi polisi tunaamini kuwa wewe na mumeo mmehusika,” ASP Komba alimwambia Jacky kwa sauti tulivu huku akimkazia macho.

“Mimi na mume wangu!” Jacky aliuliza akijifaanya kushangaa sana.

“Ndiyo, wewe na mumeo Carlos Mwamba. Nadhani unamfahamu Yusuf Akida, yule mfanyakazi wa benki iliyoibiwa pesa!” ASP Komba alimuuliza Jacky huku akiendelea kumkazia macho.

Jacky alimwangalia ASP Komba kwa kitambo kifupi akionekana kufikiria kidogo. “Nimepata kumuona mara kadhaa pale pale benki, mimi ni mteja wao.”

“Je, una uhusiano naye?”

“Sina uhusiano naye wowote!”

“Unajua unachokisema?”

“Nakijua sana,” Jacky alisema huku akimtazama ASP Komba kwa jicho la chuki.

“Aliipataje namba yako ya simu?” ASP Komba aliuliza akiwa amemkazia macho Jacky bila kuyapepesa.

“Nina uhakika kuwa hana namba yangu ya simu.”

“Si hii namba uliyosajili kama Jackline Mgaya, bali namba yako kama Belinda Jackson, iliyowekwa mfumo maalumu wa ulinzi…” ASP Komba aliendelea kumuuliza huku akimkazia macho.

“Sina namba yoyote iliyowekwa mfumo wa ulinzi na wala simfahamu huyo mtu mnayemwita Belinda Jackson.”



“Aliipataje namba yako ya simu?” ASP Komba aliuliza akiwa amemkazia macho Jacky bila kuyapepesa.

“Nina uhakika kuwa hana namba yangu ya simu.”

“Si hii namba uliyosajili kama Jackline Mgaya, bali namba yako kama Belinda Jackson, iliyowekwa mfumo maalumu wa ulinzi…” ASP Komba aliendelea kumuuliza huku akimkazia macho.

“Sina namba yoyote iliyowekwa mfumo wa ulinzi na wala simfahamu huyo mtu mnayemwita Belinda Jackson.”


Endelea...


“Mbona tunafahamu kuwa hilo ni jina ambalo Yusuf alikuwa akikuita, je alilipata wapi?”

“Sijui, mi sijamwambia aniite hivyo.”

“Kama hukumwambia yeye alilijuaje?”

“N’tajuaje, labda kamuulize mwenyewe,” Jacky alijibu kijeuri huku akigeuza shingo yake kuangalia kando, alikunja sura yake kwa hasira.

“Nimeshamuuliza, kasema wewe ulijitambulisha kwake kwa jina hilo na ulimpa ile namba ili muwasiliane. Na kanieleza mengi, mengine ambayo sidhani hata kama marehemu mumeo aliyafahamu,” ASP Komba alimwambia Jacky huku akimtazama kwa tabasamu.

“Sasa hayo yana uhusiano gani na haya?” Jacky alimuuliza ASP Komba huku akitazama pembeni kuyakwepa macho yake.

“Yana uhusiano wa karibu sana, kama ulivyo wewe na Yusuf Akida,” ASP Komba alisema na kutoa kitabu kidogo cha kumbukumbu za kila siku cha Carlos Mwamba.

“Unakikumbuka hiki kitabu?” ASP Komba alimuuliza Jacky huku kamkazia macho. Jacky alikiangalia kile kitabu cha kumbukumbu mara moja tu na kuonekana kunywea. Alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akitazama kando, alihisi kijasho chembamba kikianza kumtoka mwilini.

“Ndiyo, cha marehemu mume wangu,” Jacky alisema kwa unyonge.

ASP Komba alikifungua kile kitabu na kuitoa ile nakala kivuli ya hundi ya The Jacarandah Group iliyokuwa na saini, akamuonesha Jacky huku akiendelea kumkazia macho. “Yusuf alimpa nani hii nakala, wewe au marehemu Carlos Mwamba?”

Jacky aliitazama ile nakala kivuli ya hundi ya The Jacarandah Group iliyokuwa na saini na kuinamisha uso wake chini.

“Nataka kujua, Yusuf alimpa nani hii nakala ya hundi?” ASP Komba alimuuliza tena Jacky, safari hii kwa ukali kidogo. Jacky alinyanyua uso wake uliosheheni maumivu na kumtazama ASP Komba kwa huzuni, michirizi ya machozi ilikuwa inaonekana kwenye mashavu yake.

“Jamani, bora mniuwe tu nikapumzike kama mume wangu. Shida yote ya nini?” Jacky alilalama huku akifuta machozi. ASP Komba aliendelea kumkazia macho bila kupepesa.

“Alimpa nani? Naomba ujibu swali langu,” ASP Komba aliuliza kwa ukali huku akisisitiza.

“Alimpa mume wangu,” Jacky alijibu kwa unyonge.

“Mbona yeye anadai alikupa wewe?”

“Alimpa mume wangu, kwa nini niongope?”

“Okay, na hawa wahuni wawili wanaokuja kuja hapa nyumbani kwako kudai mgao wao wa fedha ni kina nani?” ASP Komba alimuuliza Jacky huku akimtupia jicho Sajenti Mapambano.

“Carlos ndiye aliyekuwa akijuana nao.”

“Wewe huwajui?”

“Siwajui.”

ASP Komba alimtazama Jacky kwa umakini kwa kitambo kirefu na kutingisha kichwa chake. “Huwajui, eh? Okay, fedha mlizoiba kule Benki ya Biashara mmezificha wapi?”

Jacky alibaki kimya akiwatumbulia macho wale maofisa wa polisi. Mara akawaona Kabwe na Liston wakaingia kwenye ule uzio wa ile nyumba huku wakiangaza macho yao kutazama huku na kule huku wakitembea kwa ubabe wakionekana kuwa na hasira.

Walitaka kuingia lakini wakasita baada ya kumuona Jacky akiwa ameketi na wanaume wawili chini ya kivuli cha mti, wakamfuata. Walifika pale na kuketi bila hata kukaribishwa huku wakiwakazia macho ASP Komba na Sajenti Mapambano.

“Habari zenu wakubwa?” Kabwe aliwasalimia ASP Komba na Sajenti Mapambano huku akiwatazama kwa dharau.

“Nzuri, za kwenu?” Jacky peke yake aliitikia ile salamu. ASP Komba na Sajenti Mapambano walibaki kimya huku wakiwatazama kwa umakini.

“Poa. Poleni kwa msiba,” Kabwe alijibu na kugeuka kumtazama ASP Komba, “Habari yako braza?” alimsalimia huku akimkazia macho.

“Nzuri!” ASP Komba alijibu kwa sauti tulivu huku akimtazama Kabwe kwa umakini zaidi. Kisha kikazuka kimya cha kitambo fulani huku wakiangaliana kwa makini. Kisha Liston na Kabwe wakaangaliana na Kabwe alionekana kumkonyeza Liston.

“Jamani, sisi tuna mazungumzo na huyu bibie hapa, tunaomba mtupishe kidogo, au kama vipi twende naye pembeni tukatete kidogo,” Kabwe aliwaambia ASP Komba na Sajenti Mapambano huku akiuma mdomo wake wa chini.

“Zungumzeni tu hapa hapa hamna taabu, au vipi mwenzangu?” ASP Komba aliwaambia huku akigeuka kumtazama Sajenti Mapambano na kuachia tabasamu la kifedhuli.

“Sawa kabisa, wazungumze tu, hata sijui wasiwasi wao ni nini?” Sajenti Mapambano alionekana kuafiki huku akiwaangalia Kabwe na Liston kwa umakini zaidi.

“Aa, noma hiyo washkaji. Haya ni mambo yetu na bibie nyinyi yanawahusu nini? Kama mmekuja kwenye msiba basi fateni ya msiba haya mengine hayawahusu, sawa?” Kabwe alisema kwa sauti ya kibabe huku akiwatazama ASP Komba na Sajenti Mapambano kwa umakini, tayari alikuwa ameanza kupandwa na hasira zisizoelezeka.

“Kama mambo yenu ni ya siri, basi kasubirini kwanza kule ili sisi tumalize maongezi yetu. Lakini hapa hatoki mtu. Mnalazimisha nini wakati watu wengine wamekaa huko pembeni, au mnadhani wao hawataki kuongea na bibie,” ASP Komba alisema huku taratibu akizilamba kingo za mdomo wake kwa ulimi.

Liston alionekana kupandwa zaidi na hasira, alimtazama ASP Komba kwa hasira huku akionekana kutaka kuanzisha matata muda wowote. Kabwe alishtukia na kumtuliza.

“Achana nao mafala hawa…” Kabwe alimwambia Liston huku akionekana kuwapuuza ASP Komba na Sajenti Mapambano, kisha akaongeza. “Oya shem, fanya mambo tuondoke isiwe taabu hapa.”

“Ndiyo ishakuwa taabu. Hawa mnaowaona hapa ni maofisa wa polisi kutoka kituo kikuu cha polisi,” Jacky alimwambia Kabwe kwa sauti tulivu.

Liston na Kabwe walitazamana kisha wakawatupia macho ASP Komba na Sajenti Mapambano huku wakiwatazama kwa makini na hatimaye wakamgeukia tena Jacky.

“Hebu acha kutuwekea mkwara wa kitoto, unataka kutuchezea picha sisi. Hadhulumiwi mtu hapa,” Kabwe alisema huku akimnyooshea kidole Jacky kwa hasira.

“Wala hakuna anayetaka kuwachezea picha, mnataka au hamtaki lakini huo ndiyo ukweli wenyewe…” Jacky alimwambia Kabwe huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

Muda ule ule kabwe aliinuka ghafla kwa pasipo kutegemea alichomoa bastola yake iliyokuwa imehifadhiwa kiunoni. Aliikamata vyema ile bastola na kuielekezea kwenye kichwa cha Jacky huku akionekana kugadhabika sana. Muda ule midomo yake ilikuwa ikimtetemeka kwa hasira.


Mambo yamezidi kupamba moto, kila mahali ni kizungumkuti tu, na sasa ASP Komba na Sajenti Mapambano wameingia katika anga za Kabwe na Liston, ambao wanahisi kutaka kudhulumiwa. Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia stori hii ya kusisimua.



Liston na Kabwe walitazamana kisha wakawatupia macho ASP Komba na Sajenti Mapambano huku wakiwatazama kwa makini na hatimaye wakamgeukia tena Jacky.


“Hebu acha kutuwekea mkwara wa kitoto, unataka kutuchezea picha sisi. Hadhulumiwi mtu hapa,” Kabwe alisema huku akimnyooshea kidole Jacky kwa hasira.


“Wala hakuna anayetaka kuwachezea picha, mnataka au hamtaki lakini huo ndiyo ukweli wenyewe…” Jacky alimwambia Kabwe huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


Muda ule ule kabwe aliinuka ghafla kwa pasipo kutegemea alichomoa bastola yake iliyokuwa imehifadhiwa kiunoni. Aliikamata vyema ile bastola na kuielekezea kwenye kichwa cha Jacky huku akionekana kugadhabika sana. Muda ule midomo yake ilikuwa ikimtetemeka kwa hasira.


Endelea...


ASP Komba alikwisha ihisi hatari ambayo ingeweza kutokea mbele ya macho yao muda wowote, hivyo aliwahi kuinuka na kuruka juu akajibetua kwa sarakasi ya samasoti na kumchapa Kabwe pigo moja takatifu la flying kick lililomtia udhaifu mkubwa kifuani na kichwani kwake.


Pigo lile lilimfanya Kabwe arudi kinyumenyume na kupepesuka ovyo huku akipiga mayowe ya hofu. ile bastola ikamtoka na kuanguka kando. ASP Komba hakutaka kumkawiza, kwa haraka aliruka tena hewani na kumchapa pigo lingine la teke la kijapani ambalo lilikata mzizi wa fitina, kwani Kabwe aliangukia juu ya kiti kikubwa ambacho kilivunjika vipande viwili.


Kuona vile Liston alitaharuki na kunyanyuka haraka huku akiitoa bastola yake tayari kwa mapambano kisha aliielekeza kwa ASP Komba. Kwa haraka sana Sajenti Mapambano alikusanya nguvu za kutosha kisha kufumba na kufumbua aliruka juu na kutua karibu na Liston, akajibetua na kuuzungusha chini mguu wake wa kulia akimchota mtama maridadi wenye ufundi wa hali ya juu.


Liston alishikwa na taharuki ya aina yake wakati alipokuwa akirushwa hewani na alipotua chini akajikuta tayari ameenea vizuri kwenye kabari matata ya Sajenti Mapambano iliyomnyima nafasi ya kuhema vizuri, huku macho yake yakiwa yamemtoka pima kama mjusi aliyebanwa na mlango.


Tukio lile lilikuwa limesababisha hata ile bastola yake mkononi imponyoke na kuangukia mguuni kwa Sajenti Mapambano. Mahesabu ya Sajenti Mapambano yalikuwa yameenda vizuri kwani kwa haraka aliinama na kuiokota ile bastola huku Liston akiendelea kufurukuta bila ya mafanikio.


Wakati Liston akiwa kadhibitiwa vyema na Sajenti Mapambano, Kabwe alijaribu kuinuka huku akigugumia kwa maumivu makali na kujiweka sawa kumkabili ASP Komba, kisha akaanza kumfuata kwa hasira kama Mbogo aliyejeruhiwa.


ASP Komba alikusanya nguvu za kutosha kisha alimtandika kichwa cha nguvu na kuupasua vibaya mwamba wa pua yake. Kabwe alipiga yowe kali la maumivu huku akiyumba, na hapo ASP Komba akamtupia pigo jingine kali la kareti shingoni lililomfanya apepesuke na kurushwa juu, akapiga yowe kali la maumivu wakati alipojipigiza kichwa chake kwenye ukuta wa ile fensi ya nyumba kisha akaanguka chini na kutulia kimya.


Shingo yake ilikuwa imevunjika na damu ilikuwa inamtoka puani, mdomoni na masikioni. Jacky aliziba macho yake huku akitoa ukelele hafifu wa hofu. Watu waliokuwa wamekuja pale msibani walianza kukaa mbali na eneo lile na wengine kupanda juu ya ukuta wa fensi huku wakichungulia kile kilichokuwa kikiendelea pale nyumbani kwa Jacky wakati ASP Komba na Sajenti Mapambano wakiwadhibiti wale wahuni.


Mara eneo lote likageuka kuwa kisiwa chenye ukimya wa kutisha, hakuna cha nyimbo za maombolezo wala vilio, watu wote walikuwa kimya kabisa. Liston alikubali yaishe na hivyo kusalimu amri mbele ya wale maofisa wa polisi wenye mafunzo maalumu katika sanaa ya mapigano. Wakamfunga pingu mikononi na kumtuliza pale chini, kisha ASP Komba aliwaita makachero Haji Adam na Sebastian Masesa waliokuwa sehemu ya wale waombolezaji.


Kisha akatoa simu yake akawapigia kituoni akiwafahamisha kilichotokea pale nyumbani kwa Jacky na kuwaomba walete haraka gari la kubebea maiti. Muda ule ule wale makachero makachero Haji Adam na Sebastian Masesa walimnyanyua Liston wakamkokota msobe msobe hadi kwenye gari la polisi na kuondoka naye.


ASP Komba aliutazama kwa makini mwili wa Kabwe uliokuwa umelala pale chini ukiwa hauna uhai na kuminya midomo yake, kisha akampa maelekezo Koplo Victor ya kubaki hapo hadi gari la kubebea maiti litakapofika na kuuchukua ule mwili.


ASP Komba akamtazama Jacky kwa makini na kushika vyema bastola yake, akamuelekezea kichwani.


“Haya sasa nieleze, ziko wapi?” ASP Komba alisema kwa sauti iliyokuwa imebeba hasira.

“Nini, afande?” Jacky alimuuliza ASP Komba huku akionekana kugwaya sana.


“Fedha, mmezificha wapi?” ASP Komba alimuuliza Jacky huku sura yake ikiwa mbali kabisa na mzaha, safari hii sura yake haikuonesha aina yoyote ya utani wala kubembelezana.


“Zipo kwenye kabati maalumu ndani ya chumba maalumu cha ofisi ya siri.” Jacky alisema na kuwafanya ASP Komba na Sajenti Mapambano watazamane.


“Tupeleke haraka kwenye hicho chumba cha ofisi ya siri,” ASP Komba alimuamuru Jacky.

Bila ubishi wowote, Jacky akaanza kupiga hatua taratibu kuelekea ndani ya lile jumba huku akifuatwa na wale maofisa wa polisi, wakaivuka ile sebule kubwa ya lile jumba iliyokuwa imejaa waombolezaji ambao waliwatazama kwa wasiwasi wale maofisa wa polisi ambao muda wote walikuwa wamemuelekezea Jacky bastola kichwa wakati wakipita, wakaelekea katika chumba cha chakula.


Kule kwenye chumba cha chakula wakavuka na kuelekea jikoni ambako waliukuta mlango mwingine ulioonekana kama mmoja wa milango ya makabati ya ukutani ambao juu yake kulikuwa na taa ndogo nyekundu na pembeni yake kulikuwa na kisanduku kilichokuwa na namba.


Walipoufikia ule mlango Jacky aligeuza shingo yake kuwatazama ASP Komba na Sajenti Mapambano na kuiona ile mitutu ikiwa bado imemuelekea kichwani, akashusha pumzi na kubonyeza namba nne za siri kwenye kile kisanduku kilichokuwa pembeni ya mlango kisha akaweka dole gumba la mkono wake wa kulia katika sehemu maalumu iliyokuwa ikiwaka taa ya kijani.


“Thank you, Jackline Mgaya, you’re welcome…” sauti maalumu kwenye spika ndogo pembeni ya mlango ikasikika ikimkaribisha Jacky huku ikiambatana na maandishi “Welcome Jackline Mgaya” na mara mlango ule ukafunguka.


ASP Komba na Sajenti Mapambano wakatazamana na kutweta, kisha wakaingia ndani ya kile chumba wakimfuata Jacky huku wakiendelea kumuelekezea bastola zao kichwani, wakiwa tayari kwa lolote. Na hapo walijikuta wakiwa ndani ya ofisi ya siri iliyoonekana kama ofisi ya kawaida tu yenye samani chache za kiofisi ikiwa na kiyoyozi aina ya Singsung kilichokuwa kikisambaza hewa safi.


Ofisi ile ilikuwa na zulia zuri la rangi nyekundu sakafuni, meza kubwa ya kiofisi ambayo juu yake kulikuwa na kompyuta mbili, IMac Retina 5K ya inchi 27 na PC aina ya Acer i5 yenye kioo cha flat.


Kwenye kona moja ya ile ofisi kulikuwa na mashine iliyokuwa ukutani mfano wa zile mashine za kutolea fedha (ATM), lakini hii ilikuwa ikisoma alama za vidole.


Jacky alishusha pumzi huku akionekana kujishauri, kisha akaingiza tena namba nne za siri na kuweka kiganja cha mkono wake wa kulia mahala palipochorwa alama ya vidole na baada ya sekunde kumi ile mashine ikasoma na kuwaka taa ya kijani huku maandishi yakitokea kwenye kioo, “Thank you, Jackline Mgaya, Now the door will open in a few seconds”.


Ndani ya sekunde tano mlango fulani uliokuwa unafanana na ule ukuta ukaanza kusogea ukifunguka taratibu, na hapo wakaliona kabati la ukutani likijitokeza, na begi kubwa la magurudumu lililoonekana kwenye kamera za usalama za benki likaonekana likiwa limehifahiwa kwenye shelfu za lile kabati la ukutani.


Bila wasiwasi wowote, Jacky akalivuta lile begi na kubonyeza namba fulani zilizokuwa juu ya lile begi, likafunguka. Mabunda ya fedha ya noti nyekundu nyekundu yaliyopangwa vizuri yakaonekana ndani ya lile begi kubwa. ASP Komba na Sajenti Mapambano wakapigwa butwaa.


Ghafla Jacky akafanya jambo ambalo hakuna yeyote aliyekuwa amelitarajia, aliruka hewani kutoka pale alipokuwa amesimama na kutua nje ya kile chumba na kubonyeza namba fulani kwenye kile kisanduku kilichokuwa na namba kando ya ule mlango wa ofisi. ASP Komba alishtuka na kuruka juu kumfuata Jacky, bastola ikiwa mkononi, lakini alikuwa amechelewa! Mlango ukajifunga.


Kwa sekunde kadhaa ASP Komba na Sajenti Mapambano wakachanganyikiwa wasijue wafanye nini, fahamu zilipokuja kuwarudia, ASP Komba alishusha pumzi ndefu kana kwamba alikuwa ametoka kwenye mbio ndefu za marathoni.




Ghafla Jacky akafanya jambo ambalo hakuna yeyote aliyekuwa amelitarajia, aliruka hewani kutoka pale alipokuwa amesimama na kutua nje ya kile chumba na kubonyeza namba fulani kwenye kile kisanduku kilichokuwa na namba kando ya ule mlango wa ofisi. ASP Komba alishtuka na kuruka juu kumfuata Jacky, bastola ikiwa mkononi, lakini alikuwa amechelewa! Mlango ukajifunga.


Kwa sekunde kadhaa ASP Komba na Sajenti Mapambano wakachanganyikiwa wasijue wafanye nini, fahamu zilipokuja kuwarudia, ASP Komba alishusha pumzi ndefu kana kwamba alikuwa ametoka kwenye mbio ndefu za marathoni.


Endelea...


“What are we going to do?” (Tutafanyaje) Sajenti Mapambano aliuliza kwa wasiwasi.


“The bastard has escaped. We must do something to get out of here,” (Mwanaharamu katoroka. Lazima tufanye kitu tutoke humu) ASP Komba alisema huku akijaribu kuufungua ule mlango uliokuwa umejifunga bila mafanikio.


“Inaonekana chumba hiki kina mambo makubwa tusiyoyafahamu. Tunachotakiwa ni kutafuta namna ya kujiokoa kutoka humu ndani haraka kabla hayajatukuta makubwa,” ASP Komba alimwambia Sajenti Mapambano huku akionesha kukata tamaa.


Kisha kama mtu aliyekumbuka jambo alichukua simu yake kisha akapiga simu ofisini kwake akiwafahamisha kilichotokea na kuwaomba waongeze nguvu na wamlete mtaalamu wa Tehama.


* * * * *


Saa kumi na mbili jioni, ndani ya ofisi za Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu, kwenye jengo la kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam, ASP Komba alikuwa ameketi kwenye kiti chake cha kuzunguka.


Mkononi alikuwa ameshika faili kubwa ambalo alikuwa akilipitia na kuhakiki zile taarifa. Mara mlango wa ile ofisi ukagongwa mara moja na kufunguliwa, kisha Nassos Chatzopoulos, mkurugenzi mkuu wa The Jacarandah Group akaingia na kutembea taratibu huku akionekana mnyonge sana.


ASP Komba alimtazama Nassos Chatzopoulos na kuachia tabasamu huku akimuelekeza kiti. Nassos aliketi kwenye kile kiti huku akimtazama ASP Komba kwa umakini.


“I’m sorry to bother you, Mr Nassos, but I’ve called you to give you a final report of our case on the part of the investigation,” (Samahani nimekusumbua, bwana Nassos, lakini nimekuita ili nikupe taarifa ya mwisho ya kesi yetu kwa upande wa upelelezi) ASP Komba alimweleza Nassos huku akiendelea kutabasamu.


“Okay, officer, but I'm desperate to get back my money, however, I don't know where you've got?” (Sawa, afande, lakini mimi nimeshakata tamaa kabisa ya kuzipata fedha zangu, hata hivyo, sijui mmefikia wapi?) Nassos Chatzopoulos alisema na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


“All your money was found…” (Fedha zako zote zimepatikana…)


“Impossible, all!” (Haiwezekani, zo-te!) Nassos aliuliza huku akinyanyuka kutoka kwenye kile kiti kwa mshtuko mkubwa, alimkodolea macho ASP Komba kwa mshangao akiwa haamini kile alichokisikia.


“All and have been stored within the central police cabinet of the stolen money. You’ll be given once the case has ended,” (Zote na zimehifadhiwa ndani ya kabati kuu la polisi la fedha zilizoibiwa. Utakabidhiwa mara tu kesi itakapomalizika) ASP Komba alisema huku akishusha pumzi.


“When?” (Lini?) Nassos aliuliza kwa shauku kubwa.


“It won't take long. The defendants will be brought to court tomorrow morning, and we’ll make sure the case goes quickly because all the evidences are there,” (Haitachukua muda. Washtakiwa watakafikishwa mahakamani kesho asubuhi, na sisi tutahakikisha kesi inakwenda haraka maana vielelezo vyote vipo) ASP Komba alimwambia Nassos huku akilifunga lile faili na kuliweka kwenye droo ndogo ya meza yake.


“How many defendants are there?” (Kwani washtakiwa wenyewe ni wangapi?) Nassos alimuuliza ASP Komba kwa shauku huku sura yake ikianza kuonesha nuru.


“They were three defendants but now they are only two. Yusuf Akida, the employee of the Commercial Bank and the notorious criminal called Liston George. The first defendant, a woman who was the key arranger of all strategies, called Jackline Mgaya has managed to escape,” (Walikuwa watatu lakini kwa sasa wapo wawili tu. Yusuf Akida, yule mfanyakazi wa Benki ya Biashara na mhuni maarufu anaitwa Liston George. Mshtakiwa wa kwanza mwanamke aliyekuwa mratibu mkuu wa mipango yote, anayeitwa Jackline Mgaya amefanikiwa kutoroka) ASP Komba alisema na kumfanya Nassos kushangaa kidogo.


“I heard even my attendant, Jasmine Kombo is involved in theft! Will she not be brought to court?” (Si nilisikia hata yule mhudumu wangu, Jasmine Kombo kuwa amehusika kwenye wizi! Kwani yeye hatafikishwa mahakamani?) Nassos aliuliza kwa mshangao.


“She’d have been brought if she were present,” (Kama angekuwepo angefikishwa) ASP Komba alisema huku akizilamba kingo za midomo yake kwa ulimi.


“If she were present! What do you mean, officer, I’ve heard she’s admitted in hospital?” (Kama angekuwepo! Unamaanisha nini, afande, si nimesikia amelazwa hospitali?) Nassos aliuliza huku akizidi kushangaa. ASP Komba alivuta pumzi ndefu kisha akazishusha taratibu.


“She has also escaped this midday after the interrogation,” (Pia katoroka leo mchana baada ya mimi kutoka kumhoji) ASP Komba alisema, Nassos akaguna. Wakatazamana kwa kitambo kifupi na kuangua kicheko.


Kicheko chao kilikatizwa na simu ya ASP Komba iliyoanza kuita, ASP Komba alitaka kuipuuza ile simu lakini alipoitazama kwa makini akashtuka sana baada ya kugundua kuwa ilikuwa inatoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Evance Hiza. Akaipokea haraka na kuiweka sikioni.

“Hello!” ASP Komba alisema kwa unyenyekevu.


“Habari yako, ASP?” sauti nzito ya IGP Hiza ikasikika kutoka upande wa pili wa ile simu.


“Nzuri, afande!” ASP Komba alijibu kwa sauti ya ukakamavu.


“Umefikia wapi huko?” IGP Hiza aliuliza kwa shauku.


“Tumekamilisha kazi, afande,” ASP Komba alijibu kwa ukakamavu.


“Unasema…?”


“Nasema tumekamilisha ile kazi, afande.”


“Mmefanikiwa kuzipata fedha zote zilizoibwa?”


“Ndiyo, afande, fedha zote zipo salama na zimehifadhiwa ndani ya kabati kuu la polisi la fedha zilizoibiwa,” ASP Komba alisema huku akimtupia jicho Nassos.


“Vipi watu walioshiriki katika wizi wa mabilioni pale benki, mmefanikiwa kuwakamata?”


“Ndiyo, afande, tunao watuhumiwa wawili na mmoja ametoroka… wengine watatu wamekufa katika operesheni,” ASP Komba alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


IGP Hiza alinyamaza kwa sekunde kadhaa, kisha akaibuka, “Mbali na wewe, ni nani mwingine alikuwa mstari wa mbele katika kuongoza upelelezi huo?”


“Msaidizi wangu, Sajenti Mapambano.”


“Yupo ofisini sasa hivi?”


“Hapana, nimempa mapumziko ya siku mbili, ataingia kazini keshokutwa asubuhi. Vipi afande?” ASP Komba aliuliza huku akionekana kupata shaka kidogo.


“Wanasema mcheza kwao hutunzwa. Kuna nafasi zimetoka za askari kwenda masomoni Toronto, Canada mwezi ujao, nataka nimpe nafasi hiyo Sajenti Mapambano akaongeze ujuzi…” IGP Hiza alisema na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Na wewe jina lako tayari lipo mezani kwa Rais, utakuwa mmoja wa maofisa wa polisi watakaopewa kamisheni na Rais wa Tanzania kuwa Makamishna wasaidizi wa Polisi, kwa hiyo utapanda nafasi mbili zaidi kutoka Mrakibu Msaidizi wa Polisi hadi Kamishna Msaidizi wa Polisi. Na ukishapewa kamisheni tu nakuhamishia Arusha kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa,” IGP Hiza alisema na kumfanya ASP Komba akenue meno yake kwa furaha.


“Ninashukuru sana, afande, ninashukuru sana…” ASP Komba alisema kwa nyenyekevu. IGP Hiza akakata simu.



MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog