IMEANDIKWA NA : PATRICK CK
*********************************************************************************
Simulizi : Peniela (4)
Sehemu Ya Kwanza (1)
ILIPOISHIA SEASON 3
“ Elibariki nakushukuru sana kwa kunitoa usingizini.Sikujua kama nina maadui wakubwa namna hii tena walio karibu kabisa na mimi na ambao wangeweza hata kunimaliza sekund e yoyote .Kuanzia sasa wewe ndiye utakayekuwa mshirika wangu mkuu.I’ll give back to you all that I took from you.Nisaidie tuimalize biashara hii na ninakuahidi kwamba uakuwa ni mtu mkubwa sana. kuna jambo ambalo sikuwa nimelifikiria lakini kwa sasa limekuja akilini.I’ll make you the next president of Tanzania”
Jaji Elibariki alibaki mdomo wazi akimkodolea macho Dr Joshua asiamini kile alichoambiwa.
“ Umesema nini mzee? akauliza
“ kwa mambo uliyonifanyia jaji umenifanya nikuthamini ghafla kuliko watu wote kwani bila wewe ningeendelea na mipango yangu yote bila kufahamau chochote na mwisho wangu ungekuwa ni wa aibu kubwa.Ni wewe ambaye nilikuwa nimekuweka katika kundi la adui zangu wakubwa lakini ndiye umekuja na kunifumbua macho.kwa hili ulilolifanya nimesema kwamba nitakufanyia kitu ambacho sikuwa nimekusudia kukifanya.Nitakufanya uwe rais wa jamhuri ya muunganowa Tanzania.” Akasema Dr Joshua.jaji Elibarki machozi ya furaha yakamdondoka.
“ is this true Dr Joshua?
“ Ndiyo Elibarik.Uwezo huo ninao na nitafanya hivyo na hakuna anayeweza kunizuia kufanya hivyo.I’ll make you a very powerfull man in this country na nina hakikani wewe ambaye utaweza kuendelea kuyalinda maslahi yangu.Nilikuwa nafikiria sana ni nani ambaye ninaweza nikampa nchi na akaendelea kuyalinda maslahi yangu lakini nashukuru nimekupata wewe.Nina hakika wewe ni mtu sahihi kabisa na unafaa.”Akasema Dr Joshua.Jaji Elibariki akainuka na kwenda kumpa mkono akamshukuru
“ Dr Joshua sikuwahi kufikiri kuhusu jambo kama hili ! akasema kwa furaha jaji Elbariki
“kwa hiyo kama halikuwa katika ndoto zako anza sasa kuota kwamba umekuwa rais wa Tanzania kwani jambo hili linakwenda kutimia.Nitakuelekeza nini cha kufanya muda utakapofika lakini lazima ukae ukijua kwamba wewe ndiye utakayekuwa rais wa Tanzania baada ya mimi kuondoka madarakani.Lakini pamoja na hayo kuna jambo nataka nikuombe”
“Jambo gani Dr Joshua?
“ Samahani lakini kwa kulisema hili kabla hata hatujamzika Flaviana mkeo lakini ni ukweli ulio wazi kwamba Kwa sasa baada ya Falivana kututoka utabaki mwenyewe na kwa kuwa bado kijana lazima utaoa tena lakini mimi lengo langu kubwa ni kutaka familia yangu iendelee kukaa katika neema ya uongozi kwahiyo basi ninakutaka ujenge mazoea ya karibu na Anna mbaye naye kwa sasa yuko mwenyewe baada ya mpenziwake kufariki.Ninajua umenielewa ninaposema hivyo kwani ninataka utakapokuwa rais yeye awe ni mke wa rais na familia yetu iendelee kutawala.Unalionaje wazo hili? Akauliza Dr Joshua
“ Hilo ni wazo zuri Dr Joshua lakini naomba uniachie kwanza jambo hilo nilitafakari na kulifanyia kazi na nitakupa majibu”akasema Elibarik,.Dr Joshua akafungua mlango na kumuita msaidizi wake akamuomba amuite Dr Kigomba ambaye alifika mara moja .Dr Joshaua akamuangalia kwa macho makali kwa sekunde kadhaa kisha akasema
‘ Kigomba give me your phone” .Huku akishangaa Dr Kigomba akachukua simu yake na kumpatia Dr Joshua.
” Kuanzia sasa hautaitumia simu hii utatafuta simu nyingine.Vua na hiyo saa mkononi”akaamuru Dr Joshua
“ Dr Joshua whats going on? Akauliza Dr Kigomba kwa wasiwasi.
“ Kigomba nadhani umekwisha fahamu nini kinaendelea.Nilikupa kazi ya kumchunguza peniela na badala yake ukaanzisha mahusiano naye.Ulifanya kosa kubwa sana Kigomba”
“ Nani kakueleza habarihizo dr Joshua?
“ Kigomba tayari ninafahamu kila kitu kwa hiyo hakuna haja ya mabishano. Siku zote nimekuwa nkikuonya kuhusiana na udhaifu wako kwa wanawake lakini hukutaka kunisikia.”
“ Dr Joshua sikuelewi una maanisha nini” akasema Dr Kigomba.Dr Joshua akamtazama kwa macho makali na kusema
“ Kigomba unafahamu Peniela ni nani? Unafahamu ni kitu gani alichotufanyia kupitia kwako?
“ hapana Mr President.”akajibu Dr Kigomba
“ Peniela ni nyoka mkubwa na tayari ameunganisha simu yako katika program yao na wanasikia kila kitu unachokiongea kupitia simu yako.Kama hiyo haitoshi alikupa saa hii kama zawadi uivae lakini kwa taarifa yako saa hii imefungwa kifaa maalum ambacho kina uwezo wa kuwaonyesha kila mahala ulipo.Tumshukuru sana Elibariki ambaye ametufumbua macho na kama si yeye tusingeweza kujua chochote kinachoendelea” akasema Dr Joshua.Kigomba alibaki kimya akiwatazama.
“ I’m sorry Mr President,sikuwa ninafahamu lolote kuhusiana na alichokifanya Peniela.” Akasema Dr Kigomba
“ Kigomba mimi na wewe tutakuwa na maongezi yetu baadae lakini kwa sasa naomba nikufahamishe kwamba mipango yetu yote imekwisha gundulika na kama tusipochukua hatua za tahadhari angali bado mapema basi hatutaweza kufanikiwa.Cha kwanza tunachotakiw a kukifanya ni kumuhamisha kwa siri Hussein na ujumbe wake mapema kesho asubuhi na kesho hiyo hiyo jioni kila kitu kikamilike na Hussein aondoke nchini haraka na baada ya hapo tutaendelea na zoezi la kumsaka mtu aitwaye Mathew ambaye huyu ndiye adui yetu mkubwa sana kwa sasa.”akasema Dr Joshua
“Mr President ninaomba niuliz……………”Dr Kigomba akataka kuuliza swali lakini Dr Joshua akamzuia
“ Kigomba hakuna muda wa maswali sasa hivi.Anza sasa hivi kushughulikia hoteli ya kuwahamisha Hussein na ujumbe wake.Tutaongea baada ya mambo yote kukamilika” Akasema Dr Joshua na Dr Kigomba akatoka mle chumbanihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jaji Elibarikina Dr Joshua waliendelea na maongezi na ilipotimu saa tisa za usiku wakaagana.
“ Nenda kalale jaji kesho tuna siku ndefu sana.Kesho tutamzika Flaviana na kisha tutaendelea na mchakato mwingine.Tutaongea zaidi kesho lakini nakushukuru sana jaji.” Akasema Dr Joshua na kumuongoza jaji Elibariki kuelekea katika chumba maalum cha wageni
ENDELEA SEASON 4
Dr Joshua akarejea sebuleni kwake na kuketi sofani akavuta pumzi ndefu halafu akavua koti na kulegeza tai .Alihisi joto .Mambo aliyoelezwa na jaji Elibariki yalimchanganya mno.
“ I’m confused .Totaly confused !!!.... akawaza na kuinuka akaenda katika kabati kulimokuwa na chupa kadhaa za pombe kali akachukua moja akamimina katika glasi akagugumia yote na kukunja sura kutokana na ukali wa pombe ile,halafu akaenda moja kwa moja chumbani kwake ,akavua tai na kuitupa kitandani akasimama kwa sekunde kadhaa akionekana kujawa na mawazo mengi mara ghafla akaibinua m eza kwa hasira na kumwaga kila kilichokiwa juu yake
“ Aaaagghhhh…!!!!” akapiga ukulele kwa hasira huku akihema mfululizo,na uso wake ukiwa umeloa jasho.Mara mlango wake ukagongwa kwa nguvu akainuka na kwenda kuufungua akakutana na sura zenye wasi wasi za walinzi wake.
“ Is everything ok Mr President?..akauliza mmoja wao.
“ I’m fine guys..I’m ok dont worry” akajibu Dr Joshua
“ Are you sure Mr President?
“ Vijana nimewaambia I’m ok..Nimekunywa kidogo pombe kali ili kuondoa mawazo ya kifo cha mwanangu mpendwa .Msijali vijana wangu I’m fine ,so if you’ll excuse me I n eed to be alone” akasema Dr Joshua na kuufunga mlango wake akaketi sofani na kuinamisha kichwa akaweka mikono kichwani
“ Mambo aliyonieleza jaji Elibariki ni mazito na magumu kuyaamini lakini kwa namna alivyonieleza nalazimika niamini ila nimestushwa mno kusikia eti Peniela ametumwa kwangu na kikundi kiitwacho Team SC41 kwa lengo la kunichunguza na kuhakikisha wanakipata kirusi Aby” akawaza na kuivuta akilini sura ya Peniela
“ Hivi kweli Peniela anaweza akanifanyia hivi alivyosema Elibariki ? Sura yake ya kimalaika iliyojaa mahaba haionyeshi kabisa kama ni msichana anayeweza kufanya hayo aliyoyasema Elibariki.Peniela ni mwananmke nnayempenda mno ,tayari ameniin gia katika kila mshipa wa mwili wangu na ndiyo maana inaniwia ugumu sana kuamini maneno aliyoyasema Elibariki juu yake.” Kichwa cha Dr Joshua kikaendelea kuuma kwa mawazo mengi .Akayakumbuka maneno fulani aliyoambiwa na jaji Elibariki
“ Peniela ambaye umekuwa ukimuona kama malaika wako hakupendi hata chembe na ndiye anayeongoza mipango yote ya kukuangamiza.Anatumiwa na Team Sc41 ambao nio waliompa mafunzo na wakamuunganisha kwako makusudi kabisa wakimtumia Captain Amos.Walikuwa na lengo moja tu la kukipata kirusi Aby.Nakuhakikishia tena mheshimiwa rais kwamba Peniela ni mwanamke hatari sana ambaye hana mapenzi yoyote kwako bali anatumiwa kukumaliza.Kama huamini hiki ninachokwambia usichukue hatua zozote na utaona kitakachotokea.Peniela ni nyoka mwenye sumu kali ,anautumia uzuri wake ili kupata kile ambacho yeye na team yake wanakitaka kwa manufaa yao.Amekuwa akiwalaghai kimapenzi watu mbali mbali na mmoja wao ni katibu wako Dr Kigomba”
Dr Joshua akahisi kama vile kichwa kinapigwa na kitu kizito alipoyakumbuka maneno haya ya jaji Elibariki
“ Natamani nisimuamini Elibariki lakini kwa mambo aliyonieleza yananilazimisha nimuamini.Kwanza ni kweli nilimpata Peniela kwa kumpitia Captain Amos.Hakuna aliyekuwa analifahamu hili zaidi yangu na Amos.Kwa Elibariki kulifahamu hili ananilazimisha niamini kuwa kile anachokisema kinaweza kuwa kweli.Kitu kingine ni kuhusu Peniela na Kigomba kuwa katika mahusiano.Sikuwa nikilifahamu hili lakini Elibariki amenifumbua macho na hata Kigomba ameshindwa kukataa mbele yangu kwamba ana mahusiano na Peniela.Kitendo cha kufuatilia mawasiliano ya Kigomba na kujua nyendo zake zote kinanifanya niamini yale aliyonieleza Elibariki yanaweza kuwa kweli.Ni wazi Peniela anahusika katika jambo hili na kama alivyosema Elibariki ni kwamba Peniela anatumia uzuri wake kufanikisha mambo yake.Oh !! Peniela ..Peniela !! Why she did this to me?!! Alinipofusha kwa penzi lake zito nikajiona nimepata malaika kumbe niko na shetani mtoa roho.I’m so stupid to trust her that much.Kwa nini sikuwa mwangalifu na kuligundua hili toka mapema?..Dr Joshua akauma meno kwa hasira
“ Sijui nitampa nini jaji Elibariki kwa jambo hili kubwa alilonifanyia la kuwasaliti wenzake na kuja kunipa siri hizi ambazo zimenitoa katika usingizi mzito ulionifanya nisijtambue kwa kufunikwa na blanketi la penzi la Peniela.Kumbe nilikuwa najikaanga mwenyewe na mafuta yangu bila kujua.Hayakuwa maamuzi mepesi kuwasaliti wenzake na kuja kwangu na kwa hili I must reward him na zawadi kubwa kuliko zote ambayo naweza kumpatia ni kumfanya awe rais ajaye wa Tanzania.” Akasimama na kuzunguka zunguka mle chumbani
“ Yes ! I will make him a president of Tanzania.Uwezo huo ninao na Elibariki anafaa kabisa.Anaweza akakalia kiti vizuri na zaidi ya yote atakuwa anafuata yale yote nitakayokuwa namuelekeza.Hata kama kuna mambo mengi mabaya nimeyafanya wakati wa uongozi wangu akija mtu kama Elibariki atayafukia yote na nitaendelea kukaa kwa amani na salama nikitumia utajiri wangu.” Akaendelea kuwaza Dr Joshua halafu akamkumbuka Peniela
“ Oh Peniela sijui nikufanye nini pindi nikikuweka mikononi mwangu lakini pamoja na yote uliyonifanyia bado taswira yako imekitawala kichwa changu.Ninahisi yawezekana akawa anatumia uchawi kwani sijawahi kuchanganyikiwa kwa mwanaume yeyote kama alivyonichanganya Peniela namna hii.Ninamuwaza kila dakika japokuwa bado ninahasira naye..” akawaza Dr Joshua na kuanza kukumbuka namna alivyokutana na Peniela
2012 JOHANNESBURG – AFRIKA YA KUSINI
Mkutano mkubwa wa siku sita wa kujadili athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa nchi masikini duniani ulikuwa unafanyika katika jiji la Johannesburg Afrika ya kusini.Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo uliongozwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Joshua ambaye alitarajiwa kutoa hotuba katika mkutano huo.
Akiwa jijini Johannesburg Dr Joshua alifikia katika hoteli ya kifahari ijulikanayo k ama four season hotel
Kazi ya kwanza aliyoifanya Dr Joshua akwa jijini Johannesburg ni kukutana na jumuia ya watanzania waishio nchini Afrika ya kusini Katika mkutano na wanajumuiya hao Dr Joshua aliwaasa wakumbuke kuwekeza nyumbani na vile vile kuzingatia sheria za nchi wanakoishi.Kwa upande wao watanzania waishio afrika ya kusini walimueleza rais changamoto wanazokutana nazo nchini afrika ya kusini ambazo rais aliwaahidi kuzifikisha sehemu husika ili zipatiwe majibu.Baada ya mkutano kumalizika Dr Joshua akaondoka akarejea hotelini alikofikia.
Tayari ilikwisha timu saa kumi na moja jioni.
Akiwa chumbani kwake amejipumzisha,Captain Amos daktari wa familia ya rais akaingia
“ Hallow Mr President” Amos akamsabahi Rais
“ Hallow Amos” akasema Dr Joshua .Captain Amos akaiendea chupa ya mvinyo mezani na kumimina katika glasi mbili akampatia moja Dr Joshua
“ Maneno uliyoyaongea katika kikao chako na wanajumuiya ya watanzania waishio afrika ya kusini yamewagusa sana na kwa namna walivyoguswa nina imani yale yote uliyowaeleza watayafanyia kazi.” Akasema Captain Amos
“ Niliona niwakumbushe umuhimu wa kuwekeza nyumbani na kuijenga nchi yao .Wengi wao wakiwa huku nje ya nchi husahau kabisa kwao.Tuachane na hayo, mambo yanakwendaje? Have you found me something? I’m getting bored in here”
“ Tena ni hilo lililonileta kwako mheshimiwa” akasema Amos na kumfanya Dr Joshua atabasamu
“ Tell me the good news Amos” akasema Dr Joshua
“ Good news is that I’ve found you something very special.Utakubaliana nami utakapomuona” akasema Amos
“ Nakuamini Amos.Ukimsifia mwanamke namna hiyo basi ni kifaa hasa.Tell me who is she?
Captain Amos akanywa funda moja la mvinyo na kusema
“ Her name is Peniela.Ni mtanzania ambaye amekuja Afrika ya kusini kibiashara .Anamiliki maduka makubwa mawili ya nguo na urembo.Nakuhakikishia Mr President she’s an angel.Hadhi yake ni ya juu mno .Naamini hata wewe ukimtia machoni utakubaliana nami”
“ Unafahamiana naye? Unamuamini? Unajua sitaki mtu ambaye anaweza kuwa kidomo domo .Si unajua hawa wanawake ikitokea akatembea na rais basi huanzisha matangazo ili ajulikane kila mtaa kuwa anatoka na rais wa nchi”
“ Usihofu kabisa kuhusu hilo mzee.Peniela ni mwanamke ninayefahamiana naye na niamuamini sana.Hana mambo kama hayo ya ajabu ajabu.”
“ Good to hear that then.Nashukuru kwa kunipa uhakika huo.Nakuamini sana Captan na ndiyo maana sijawahi kukuacha katika safari zangu zote za nje ya nchi”
“ Hata mimi nashukuru sana mzee kwa kuniamini na ninatumai sijawahi kukuangusha hata mara moja katika kila kazi unayonipa”
“ Ni kweli Amos hujawahi kuniangusha .Katika safari zote tunazosafiri nje ya nchi umekuwa unaniletea wanawake wazuri wenye hadhi yangu.Nipatapo safari kama hizi za nje ya nchi huwa ni fursa yangu na mimi kujivinjari na watoto wazuri.Kama ujuavyo mama yenu ni mgonjwa sana siku hizi halafu mahaba yamepungua kutokana na umri kwa hiyo ninapokuwa huku nje ninapata nafasi nzuri ya kujivinjari na damu changa.Nashukuru unalifahamu hitaji langu na kila mara umekuwa unaniletea aina ya wanawake ninaowataka” akasema Dr Joshua na Amos akatabasamu
“ Saa tatu za usiku baada ya chakula nitakuwa na maongezi na balozi wetu hapa afika ya kusni kwa hiyo nitamuhitaji Peniela kuanzia saa sita za usiku.Atakapowasili mkabidhi kwa Kareem na yeye atajua namna ya kumleta kwangu” akasema Dr Joshua halafu wakaendelea na maongezi mengne na baada ya muda Amos akaondoka na kumuacha Dr Joshua peke yake.
“ Peniela ..” akasema kwa sauti ndogo huku akitabasamu
“ Jina hili linafanya nijenge taswira ya mwanamke mwenye uzuri zaidi ya tausi.Amos amemsifia sana na kwa sifa zote zile nina hakika uzuri wake utakuwa zaidi ya Cleopatra Yule aliyewahi kuwa mtawala wa Misri ambaye vitabu vinatueleza kwamba alikuwa na uzuri usioelezeka.Halafu kuna kitu nimekuwa nakifikiria kwa muda mrefu.Kadiri siku zinavyozidi kusonga ndivyo mapenzi na mke wangu Flora yanazidi kupungua.Flora hana tena ule mvuto wake wa asili na kutokana na maradh ya moyo yanayomsumbua hana tena ule uwezo wa uweza kuniridhisha kitandani.Japokuwa umri wangu umekwenda lakini bado damu inanichemka na ninao uwezo mkubwa kitandani .Kama ni hivyo basi kwa nini nisitafute mwanamke mzuri mwenye hadhi ambaye atakuwa wangu moja kwa moja? Mwanamke huyo nitakuwa naonana naye kwa siri kila pale ninapokuwa na hamu ya kufanya mapenzi,mwanamke ambaye ataniliwaza na kuniondolea mawazo.Hili niI wazo la msingi na ninatakiwa kulipa uzito wa kipekee.Ngoja nimuone huyo Peniela ni mwanamnke wa aina gani na kama anaweza akanifaa kuwa naye katika mahusiano ya siri.Kama atafanikiwa kuniridhisha na kama ni mwanamke mwenye staha na si wale wanaitwa micharuko basi nitamfanya awe mpenzi wangu wa kudumu.Nitamfanyia mambo makubwa na kufanya aishi maisha ya kifahari “ akawaza Dr Joshua huku akiendelea kupata mvinyo taratibu
SAA SITA USIKU FOUR SEASON HOTEL
Saa sita na dakika saba za usiku gari moja lenye rangi nyeusi likainga katika hoteli ya four seasons .Toka ndani ya gari hilo akashuka daktari wa rais Captain Amos akiwa ameongozana na mwanamke mmoja mwenye uzuri wa kipekee.Alikuwa mwembamba ,mrefu wastani aliyevaa suti nzuri nyeusi iliyomkaa vyema.Moja kwa moja wakaelekea katika chumba cha rais ambako Captain Amos akakamkabidhi Yule mwanamke kwa Kareem mmoja wa walinzi wa rais.
“ Karibu sana Peniela” akasema Kareem baada ya kutambulishwa.Captain Amos akaondoka na Kareem akamuomba Peniela amfuate.Ulinzi ulikuwa mkali na kila aliyepita eneo lile alipokuwa rais alilazimika kusachiwa kwanza lakini Peniela alipita bila wasi wasi kwa kuwa alikuwa ameongozana na mlinzi wa rais Kareem.Katika mlango wa kuingilia chumba cha rais kulikuwa na walinzi ,Kareem akawapa ishara Fulani nao wakaitika kwa ishara halafu akaufunga mlango na kuingia sebuleni.
Dr Joshua alikuwa peke yake mle sebuleni akitazama Luninga,huku pembeni yake kukiwa na chupa ya mvinyo.Akageuza shingo kutazama mtu aliyeingia mle sebuleni .Kwa sekunde kadhaa akabaki ameduwaa akitazama mlangoni ambako alikuwa amesimama mlinzi wake kareem akiwa na Peniela
“ Oh my Gosh !!!..what a beautifull angel..” akanong’ona Dr Joshua huku akimkazia macho peniela.Alistushwa mno na uzuri wake.
“ Amos wa right.Peniela ana uzuri wa kipekee mno.Katika wanawake wote ambao amekuwa ananiletea kila tuwapo nje ya nchi hajawahi kuniletea mwanamke mzuri kama huyu.This is exactly the the type of woman I want.” Akaendelea kuwaza Dr Joshua huku akimkazia macho Peniela
“ Samahani mzee kwa usumbufu,nimekuletea mgeni.Anaitwa Peniela” akasema Kareem halafu akamgeukia Peniela
“ Peniela huyu ni Dr Joshua ,rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Baada ya utambulisho ule Peniela akatembea kwa mwendo wake wa maringo na kumfuata Dr Joshua akamsalimu kwa adabu.
“ Hallo Mr President” akasema huku akitabasamu
“ Hallo Peniela.Karibu sana.Nimefurahi kukuona”
“ Hata mimi nimefurahi kukuona mheshimiwa rais” akasema Peniela ,halafu Dr Joshua akamgeukia Kareem
“ Kareem ahsante kwa kumfikisha mgeni wangu” akasema na Kareem akaondoka zake.Dr Joshua akaenda katika meza iliyosheheni vinywaji mbali mbali
“ Peniela unatumia kinywaji gani? Akauliza .Peniela akatabasamu na kusema
“ anything that you can choose for me” Sauti laini ya Peniela ikazidi kumpagawisha Dr Joshua.Akachukua chupa ya mvinyo na kumimina katika glasi mbili akampatia moja Peniela
“ Karibu sana peniela.Ninafuraha kubwa mno kuwa nawe kwa usiku huu.Amos alinieleza sifa nyingi juu yako na baada ya kukuona ninakubaliana naye”
“ Amos alikueleza nini kuhusu mimi? Akauliza Peniela
“ Kikubwa alichonieleza ni juu ya uzuri wako.Alinieleza kwamba peniela ni mzuri hata Yule Cleopatra wa Misri hafikii uzuri wako.Baada ya kukuona nakubaliana na kauli yake.You are an angel Peniela” akasema Dr Joshua na kumfanya Peniela atoe kicheko kidogo halafu akasema
“ Thank you”
Dr Joshua akanywa mvinyo funda moja halafu akasema
“ Pamoja na yote aliyonieleza Amos lakini nahitaji kukufahamu zaidi Peniela”
“ Unahitaji kufahamu kitu gani kuhusu mimi Mr President?
“ Just call me Dr Joshua .I need to know everything about you.Your life,relation ship,everything”
“ Why do you wat to know me Mr Presi…..Oh Sorry Dr Joshua? Amos told me its just a one night stand but now it looks like an interrogation” akasema Peniela.Dr Joshua akatabasamu na kusema
“ Usinielewe vibaya Peniela.Ni sawa alivyokueleza Amos ninahitaji mwanamke mrembo kwa usiku wa leo na katika siku hizi chache nitakazokuwa hapa afrika ya kusini kwa mkutano lakini hata hivyo si vibaya kufahamiana zaidi.”
Peniela akanywa funda dogo la mvinyo na kuuliza
“ Don’t you tust Amos?
“ I do trust Amos with my life lakini ukweli ni kwamba nina sababu zangu bnafsi za kutaka kukufahamu kiundani”
“ Can you tell me what are the reasons?
“ The only reason is that I want you to be my woman”
“ Your woman??!” akauliza Peniela
“ Yes my woman” akajibu Dr Joshua
“ Dr Joshua you have a wife so why do you need me to be your woman?
“ Mke wangu ni mgonwa siku hizi na hawezi kunihudumia .Nahitaji huduma za kimwili na kama mke wangu hana uwezo wa kunihudumia basi nalazimika kuzitafuta huduma hizo sehemu nyingine na ndiyo maana nahitaji mwanamke mzuri mwenye hadhi ya kutembea na rais.Peniela nataka uwe mwanamke huyo.Nitakupa kila kitu unachokihitaji katika maisha yako.I’ll make you the most beautifull woman in the world.I’ll give you all luxuries..” akasema Dr Joshua na kunyamaza baada ya Peniela kuangua kicheko.
“ Peniela I’m serious about this.Its not a joke.” Akasema Dr Joshua
“ I know Dr Joshua but if you need love and comfort from me I’m ready to give you but not in exchange for money or anything.Nina kila kitu ninachokihitaji katika maisha yangu labda nilichokuwa nimekikosa ni kutembea na rais wa nchi” akasema Peniela na wote wakaangua kicheko.Dr Joshua akamtazama Peniela kwa sekunde kadhaa na kusema
“ So what do you say Peniela?
“ Say what? Akauliza Peniela
“ Kuwa mpenzi wangu”
“ Naomba unipe muda wa kulifikiri jambo hili Dr Joshua.Unajua kuwa na mahusiano na rais si jambo jepesi kwa hiyo nahitaji kufikiria kwanza kabla sijasema lolote”
“ Are you scared to be in relation with me? Akauliza Dr Joshua na kumfanya Peniela aangue kicheko.
“ Ofcourse I’m scared.You are the most powerfull man in the country so I must be scared.”akasema Peniela.Waliendelea na maongezi mengine na mwishowe wakajikuta kitandani
Dr Joshua akafumba macho baada ya kumbu kumbu ile kumjia kichwani.
“ For the first time in my life I enjoyed sex with her.Sikuwahi kuyafurahia mapenzi hadi nilipo kutana na Peniela.Usiku ule nilipokutana na Peniela ulikuwa ni usiku wangu wa kwanza kuyafurahia mapenzi na Peniela ndiye mwanamke pekee ambaye nakiri kwamba amefanikiwa kunipa penzi lile la kiwango cha juu mno.Ni mwanamke pekee aliyefanikiwa kunichanganya na kuniteka akili.” Akaendelea kuwaza Dr Joshua.
“ Kwa penzi ambalo Peniela amekuwa akinipa sikukumbuka tena kumchunguza na kumfahamu kiundani.Sikujua kumbe nilikuwa najipeleka mwenyewe katika mdomo wa mamba.Maelezo ya Elibariki yananifanya nikubaliane naye kwamba Peniela alipandikizwa kwangu kwa lengo maalum.Damn you Amos !!..Una bahati umekufa ama sivyo ningekuua kifo kibaya sana kwa usaliti ulioufanya.Ninachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuvuruga mipango yote niliyokuwa nimeipanga na kuipanga upya.This time I’ll be more carefull na nitashirkiana na watu ambao ninawaamini.Mtu pekee ambaye ninaweza nikamuamini kwa sasa ni jaji Elibariki.Nitashirikiana na huyu.Dr Kigomba is a traitor and weak siwezi tena kufanya naye kazi.Siwezi kumuamini tena mtu kama Yule wala kushirikiana naye katika jambo lolote .Nitaikamilisha mipango yangu kimya kimya na baadae baada ya kuhakikisha nimemkabidhi Hussein mzigo wake nitalazimika kumuondoa kabisa Kigomba ili kufagia kabisa nyayo zote zisibaki nyuma.Nilimuamini sana Kigomba lakini ameniudhi mno kwa kitendo chake cha kutembea na mwanamke wangu ninayempenda kuliko wote.Tamaa zake zimenilazimisha nimuweke katika kundi la maadui zangu.” Dr Joshua akaendelea kuwaza.
“ Sasa nimeanza kupata picha kwamba Peniela alipoanzisha siri na Yule kijana Edson hakuwa anampenda bali alichokuwa anakitafuta ni zile nyaraka za siri alizoziiba Edson toka katika maktaba yangu ya siri.Inaonekana hao team Sc41 ni mtandao mpana na ni watu wanaofahamu mambo mengi.Kuna haja ya kuchimba kiundani mtandao huu na kuufutilia mbali hapa nchini kwetu.Ninaapa nitahakikisha lazima ninaufuta mtandao huo wa team sc41 katika nchi yangu.” Akawaza Dr Joshua halafu akachukua simu yake akazitafuta namba za mkuu wa kitengo cha siri cha usalama wa nchi kilichomo ndani ya idara ya usalama wa taifa aitwaye Abel Mkokasule.
“ Hallo mheshimiwa rais” akasema Abel
“ Mr Abel,habari za usiku huu?
“ Habari nzuri mzee” akasema Abel
“ Abel nahitaji kukuona usiku huu hapa katika makazi yangu binafsi uliko msiba wa mwanangu Flaviana”
“ Sawa mheshimiwa rais nitafika hapo muda si mrefu” akasema Abel na Dr Joshua akakata simu
“ Pamoja na ugumu wote uliopo wa kuikamilisha biashara ya ile package lakini katu siwezi kukata tamaa na kuishia kati kati.Endapo nitashindwa kumpatia Hussein package ile nitalazimika kurejesha fedha zote alizotoa , jambo ambalo siko tayari kulifanya.Nitapambana hadi nihakikishe ninamkabidhi Hussein mzigo wake.Ili mpango huu ufanikiwe ninahitaji sana watu nitakao waamini na mmoja wao ni huyu Abel.Ni kijana mtiifu sana kwangu na hajawahi kuniangusha katika kila kazi niliyowahi kumpatia.Nitamuondoa Kigomba na nafasi yake ataichukua Abel” Akawaza Dr Joshua
*******
Uso wa Dr Kigomba ulibadilika mara tu alipotoka kuonana na rais Dr Joshua.Alikuwa amejawa na hasira ,akatafuta sehemu akakaa.Kichwa kilijaa mawazo mengi mno
“ Bado siamini kilichotokea.Jaji Elibariki ni mtu hatari na ni kikwazo kikubwa mno kwetu na tayari anazifahamu siri zetu nyingi na kikubwa anachokifahamu ni kuhusiana na kifo cha Dr Flora.Tumetumia gharama kubwa kumsaka kila kona hata tukadiriki kutumia vyombo vya dola na kwa sababu yake uhai wa watu umepotea akiwemo Flaviana.Dr Joshua anayafahamu haya yote lakini nashangaa sana kwa kuonekana ameongozana naye usiku huu, kama vile hakuna chochote kilichotokea.Whats going on here?? Akajiuliza Dr Kigomba
“ Lazima kuna kitu kinaendelea hapa si bure.Hainiingii akilini mtu ambaye Dr Joshua alikuwa halali akiwaza namnaya kumpata leo wanashikana mikono na kucheka pamoja kama watu marafiki.Halafu ninachojiuliza Elibarki alikuwa amejificha wapi? Amefahamuje kwamba nimefanya mapenzi na Peniela? Amefahamuje kama Peniela amenipa zawadi ya saa? I’m confused” Dr Kigomba ni kweli alionekana kuchanganyikiwa.Akainuka alipokuwa amekaa na kuanza kuzunguka zunguka
“ Elibariki amemueleza dr Joshua kuwa eti Peniela ameiunganisha simu yangu na mfumo wao unaowawezesha kufuatilia kila ninachokiongea katika simu yangu.Sijui taarifa hizi Elibariki amezitoa wapi kwa sababu ninavyokumbuka mimi Peniela hajawahi kugusa simu yangu.Huu ni uongo mkubwa ambao ameutunga Elibariki kwa sababu anazojua yeye mwenyewe.Kama zawadi ya saa ni kweli Peniela alinipa lakini hajawahi kugusa simu yangu hata mara moja.Kingine kinachonishangaza na kunifanya nijiulize maswali ,huyu jaji Elibariki amefahamuje mambo haya yote? Au yawezekena ni kweli wakawa na mahusiano na ndiyo maana Dr Joshua akanituma niende kumchunguza Peniela kama ana mahusiano na jaji Elibariki? Inawezekana kabisa kwamba jaji Elibariki na Peniela wana mahusiano na ndiyo maana amefahamu mambo yote ya kuhusu mimi na Peniela .Ninachopaswa kukifanya kwa sasa ni kufahamu mambo yote ambayo jaji Elibariki amemwambia Dr Joshua.Lazima kuna mambo mengi atakuwa amemw……” Dr Kigomba akastuka kidogo baada ya kumuona mtu mmoja mwenye mwili uliojengeka vyema akishuka ndani ya gari
“ Abel Mkokasule !!!..What is he doing here at this time? Akajiuliza
Mmoja wa walinzi wa rais akampokea Abel na kuongozana naye kuelekea ndani.
“ What’s going on here? Mimi si mtoto mdogo wa kushindwa kutambua kwamba kuna jambo linaloendelea hapa.Lazima kuna kitu kati ya Dr Joshua,jaji Elibariki na Abel Mkokasule.I need to find out” akawaza Dr Kigomba na kupiga hatua za haraka akaingia ndani lakini alipokaribia tu sebule ya Dr Joshua akazuiwa na walinzi .
“ Samahani mzee huruhusiwi kuingia humo sebuleni.Rais ana maongezi muhimu na mgeni wake.” Akasema mmoja wa walinzi
“ Mimi ni katibu wa rais na ninaruhusiwa kuingia sehemu yoyote aliko rais.Nina jambo la muhimu ninalotaka kuzungumza na rais sasa hivi”
“ Mzee itakulazimu usubiri hadi hapo rais atakapomaliza maongezi ndipo uonane naye” akasema mlinzi wa rais na kuzidi kumpandisha hasira Dr Kigomba
“ Nyie vijana hamnijui mimi ni nani? Don’t you all know me ? Samweli ,Victor nini nyote hamnifahamu mimi ni nani? Akasema Kigomba huku akiwataja kwa majina wale walinzi
“ We know who you are Sir,but that’s the order from president himself.” Akasema mmoja wa walinzi .Jibu lile likazidi kumnyong’onyeza Dr Kigomba akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Ok nitaonana naye baadae” akasema na kuondoka kwa hasira
“ Mr President “ akasema Abel Mkokasule baada ya kuingia sebuleni kwa rais.
“ Mr Abel.Karibu sana.Ninashukuru umefika kwa wakati” akasema Dr Joshua wakapeana mikono na kuendelea na maongezi
“ Samahani sana Abel kwa kukuita muda kama huu ambao ni wa mpumziko.” Akasema Dr Joshua huku akimiminia Abel mvinyo katika glasi
“ Don’t worry Mr President .Muda wowote mimi niko kazini” akasema Abel halafu kila mmoja akanywa funda moja la mvinyo.
“ Mr President naomba nichukue nafasi hii kukupa pole sana kwa msiba mkubwa wa mwanao.Nakuahidi ushirikiano wangu mkubwa katika kuhakikisha wale wote waliosababisha kifo cha mwanao wanapatikana na kufikishwa katika mkono wa sheria” akasema Abel
“ Nashukuru sana Abel .Muda wowote nitakapohitaji msaada wako sintasita kukutaka unisaidie” akasema Dr Joshua.Akanyamaza na kunywa mvinyo kidogo halafu akaendelea
“ Abel nimekuita usiku huu nina kazi yangu ambayo nahitaji ifanywe na mtu makini ninayemuamini na wewe ndiye pekee ninayekuamini kuifanya kazi hiyo kwani umekwisha nifanyia kazi nyingi na hujawahi hata mara moja kuharibu kazi yangu yoyote” akasema
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Ahsante sana kwa kuniamini mheshimiwa rais.Nakuahidi kuifanya kazi hiyo kwa uamini na weledi mkubwa” akasema Abel
“ Nina kazi mbili ama tatu ambazo nataka uzifanye.Kwanza nina mgeni wangu binafsi anaitwa Hussein Abdullah Hussein ambaye amefikia 790 hotel.Ameongozana na watu kama kumi hivi .Nataka kesho asubuhi na mapema ,Hussein na watu alioongozana nao wahamishwe hoteli na kupelekwa Rainbow hotel.Kazi ya pili nataka umsake Jessica Alfredo Yule anayefanya kazi katika idara ya usalama wa Taifa.Nadhani unamfahamu .Ukimpata mpeleke Dark house na umuhifadhi kule hadi nitakapokupa maelekezo mengine. Kuna vitu ninavihitaji toka kwake.Jambo la tatu nataka ufuatilie nyendo za Dr Kigomba.Nataka kufahamu anakutana na nani ,sehemu zote anazotembelea,nataka kufahamu kila anachokifanya.Ripoti hii naihitaji kila baada ya masaa matatu.Mambo hayo matatu yanahitaji utekelezaji wa haraka .Lakini lipo jambo la nne ambalo nataka unisaidie pia.Kuna msichana mmoja yuko mahala ameshikiliwa na ana taarifa za muhimu sana.Nataka naye umchukue na umuhifadhi dark house ili nizipate hizo taarifa alizonazo.Lakini hili litasubiri kidogo hadi nitakufahamisha litakapokuwa tayari.Nadhani umenielewa Abel”
“ Nimekuelewa mzee na ninakuahidi kwamba kazi hizo zote zitafanyika kwa ufanisi mkubwa na kwa kuzingatia muda”
“ Good.Naomba vile vile nikukumbushe kwamba usiri na umakini mkubwa vinatakiwa sana katika kufanikisha kazi hizi “ akasema Dr Joshua
“ Usihofu mzee.Hayo yote yatazingatiwa .” akasema Abel halafu wakaendelea na maongezi mengine na baadae wakaagana Abel akaondoka.
“ Namuamini sana Abel Mkokasule hajawahi kuniangusha.Endapo atanifanyia vizuri kazi hizi nilizompa kabla sijamaliza uongozi wangu lazima nihakikishe nimemuweka sehemu nzuri ikiwa ni shukrani yangu kwake kwa kazi nzuri “ akawaza Dr Joshua na kunywa funda kubwa la mvinyo
“ Baada ya kumalizana na Abel natakiwa pia kuongea na mkuu wa polisi ili kulimaliza suala la Elibariki kwani tayari vyombo vya dola vilikuwa vikimsaka akihusishwa na kifo cha Flaviana.Hakuna namna nyingine ninayoweza kumtumia Elibariki bila ya kumsafisha kwanza kutokana na tuhuma zilizokuwa zinamkabili za kusababisha kifo cha Flaviana.Lazima niyalambe matapishi yangu kwani nisipofanya hivyo kutatokea sintofahamu kubwa kuhusu suala hili la jaji Elibariki kuwa huru wakati vyombo vya dola vimekwisha tangaza kumtafuta kwa tuhuma za mauaji.Ni wakati kama huu ambao ninal;azimika kutumia nguvu na madaraka yangu kama rais wa nchi” akainuka na kwenda kuegemea meza
“ Kuna suala lingine pia. Rosemary Mkozumi alimtaja mtu mmoja anaitwa Mathew kwamba ndiye aliyemteka na kwamba ndiye anayeongoza harakati zote za kuhakikisha mipango yangu yote inakwama.Kwa mujibu wa jaji Elibariki huyu Mathew ni rafki yake na anafanya kazi za upelelezi wa kujitegemea na tayari anafahamu mambo yangu mengi .Kila kitu ninachokifanya huyu jamaa anakifahamu na ana mikakati mizito ya kuhakikisha hakuna mpango wangu hata mmoja unafanikiwa.Huyu pia ni mtu hatari sana kwangu na lazima nimtafute kwa nguvu zangu zote hadi apatikane.Nikimpata huyu nitakuwa nimempata pia Peniela kwani kwa maelezo ya jaji Elibariki wawili hawa wameungana a wanafanya kazi zao pamoja ili kuhakikisha mambo yangu hayafanikiwi na wanaipata package kabla sijamkabidhi Hussein.” Akawaza Dr Joshua na mara sura yake ikabadilika
“ Kila nikimtamka au kumuwaza Peniela mwili wote unanisisimka.Sifahamu ni hasira au nini kinanitokea nilitamkapo jina hili .Mpaka hapa nakiri kwamba Yule msichana ameniteka akili yangu kabisa.Tayari ameniingia katika kila mshipa wa mwili wangu na ndiyo maana mpaka sasa ninashindwa kupata jibu nimfanye kitu gani kwa jambo alilonifanyia.Natamani nimpatie adhabu kali mno lakini bado kuna sauti ndani yangu inaniambia Peniela hawezi kunifanyia mambo hayo aliyonieleza Elibariki.Yawezekana ni kutokana na mapenzi mazito niliyonayo kwa mwanamke huyu ndiyo maana moyo wangu unakuwa mzito kupata ni adhabu gani nimpatie. Peniela amekosea sana kwa mambo anayonifanyia kwani hiki ninachokifanya ni kwa ajili yetu mimi nay eye ili tuwe na maisha mazuri pindi nitakapomaliza kipindi changu cha uongozi.Nilimpa chaguo achague nchi yoyote duniani anayotaka kwenda kuishi na ningemnunulia nyumba ili aishi maisha a kifahari kama malkia ,sijui ni shetani gani amemuingia Peniela na kumfanyanya akatae maisha haya mazuri ambayo wanawake wengi wanayaota usiku na mchana.Why Peniela?? Akajiuliza Dr Joshua akainama akatafakari.
“Ninadhani inawezekana kabisa Peniela anafanya mambo haya si kwa kupenda bali kwa shinikizo.Kuna nguvu kubwa iliyo nyuma yake inayomwelekeza na kumsukuma nini cha kufanya.Ni Team SC41.Namfahamu Peniela ananipenda na yeye kama yeye hawezi katu kunifanyia mambo kama haya.Anafahamu fika kwamba ninampenda na nina nia nzuri kwake ” akakuna kichwa na kuzama tena mawazoni
“ Kwa mujibu wa jaji Elibariki ni kwamba Team Sc41 ni kikundi cha siri kinachofanya kazi zake kwa siri hapa nchini na katika nchi nyingine afrika na kazi yao kubwa ni kulinda maslahi ya Marekani.Kwa nini Deus Mkozumi wakati ananikabidhi ofisi hakunieleza chochote kuhusu jambo hili ? Nani kiongozi wa kikundi hiki hapa Tanzania? Je ni kweli kwamba kazi yao ni kulinda maslahi ya Marekani hapa nchini au wanafanya shughuli nyingine za ujasusi ?Hili jambo limenistua mno kwani inaonekana hawa team SC41 tayari wamekita mizizi yao hadi ndani kabisa ya serikali na ndiyo maana wana uwezo wa kufahamu kila kinachoendelea ndani ya serikali.Kama wameweza kuniingia hata mimi kwa kuwatumia watu wa karibu na ninaowaamini ,hawawezi kushindwa kwa viongozi wengine.Hii ni hatari mno kwa usalama wa nchi yetu.Katika hili ,serikali ya Marekani inatakiwa kutoa ufafanuzi wa kina ni kwa nini wanaruhusu kikundi hiki kifanye kazi kwa siri ndani ya nchi yetu? Halafu kingine kinachonishangaza kwanini hadi leo hii bado vyombo vyetu vya usalama havijaweza kugundua uwepo wa kikundi hiki hapa nchini? Akawaza Dr Joshua na kukunja sura kwa hasira
“ Lazima nikifutilie mbali kikundi hiki na potelea mbali kama nitaanzisha mgogoro na serikali ya marekani .Lazima Team SC41 waondolewe hapa nchini na kuhakikisha jambo kama hili halijirudii tena hapa nchini kwa siku zijazo.Ni kweli Marekani wamefanya uwekezaji mkubwa sana katika sekta ya mafuta na gesi hapa nchini lakini hiki si kigezo cha wao kufanya kila wanachokitaka hapa nchini.Hii ni nchi huru na ina sheria zake.Kitendo cha kuruhusu kikundi cha siri kuingia nchini na kufanya shughuli zake kwa siri ni kitendo cha uchokozi mkubwa.Hawakuwa na haja ya kufanya hivyo wakati tayari tumewahakikishia maslahi yao yatalindwa .Suala hili lazima lifikishwe katika vyombo vya usalama wa nchi lakini kabla ya kufanya hivyo lazima niongee kwanza na rais wa Marekani nimuulize kama analifahamu jambo hili na kwa nini hajanieleza.Hili si suala dogo na linaweza kuweka doa katika mahusiano mazuri tuliyonayo baina ya nchi zetu.Kesho mara tu baada ya mazishi nitaongea na rais wa Marekani kuhusu suala hili.Sikutegemea kabisa kama jambo hili lingefika hapa lilipofika na kuibua mambo haya mazito”
Kichwa cha Dr Joshua kikaendelea kuzunguka kwa mawazo mengi
“ Kama Team Sc41 tayari wanafahamu kuhusu mipango yangu ya kukiuza kirusi Aby basi ni wazi hata serikali ya Marekani watakuwa wanalifahamu jambo hili na wamekaa kimya wakitegemea kwamba wana kikundi chao hapa nchini wanachokitumia kukitafuta kirusi hicho.Je tayari wanafahamu kuwa ninataka kumuuzia Hussein ? Hapo awali niliwahi kufanya utafiti mdogo kuhusiana na Hussein nikagundua kwamba ni mtu ambaye anatajwa kuhusiana na mitandao ya kigaidi na ninajua lengo la kukitaka kirusi Aby kwa gharama zozote lazima wanataka kukitumia katika mambo ya kigaidi.Ninachojiuliza itakuaje iwapo wanataka kukitumia kirusi hicho kuishambulia Marekani? Itakuaje iwapo uchunguzi utafanyika na nikabainika kwamba ni mimi ndiye niliyemuuzia Hussein kirusi hicho? I’m confused” akaendelea kuwaza huku akinywa funda kadhaa za mvinyo
“ Pamoja na hatari iliyopo siwezi kuyaacha mabilioni haya mengi ambayo tayari nimekwisha yapokea.Potelea mbali kama Hussein na wenzake wanataka kukitumia kwa shughuli za kigaidi ama la mimi ninachohitaji ni pesa tu.Nimeitumia nchi hii kwa miaka kumi sasa na siwezi kustaafu nikiwa masikini.Nataka niwe na maisha mazuri baada ya kumaliza uongozi wangu.Zaidi ya yote hakuna mwenye ushahidi au atakayekuwa na ushahidi kuwa kirusi Aby kimetoka Tanzania.Nitaendelea na mipango yangu kama nilivyoipanga and nobody can stop me.Muda umekwenda sana ngoja nizungumze na kamanda wa polisi kuhusiana na suala la kumsafisha jaji Elibariki.
Ni tayari usiku wa manane na karibu watu wote waliokuwepo katika makazi ya binafsi ya rais Dr Joshua ulipo msiba wa mwanae Flaviana ,walikuwa wamelala lakini kwa jaji Elibariki hali ilikuwa tofauti.Macho yake yalikuwa makavu na hakuhisi hata tone la usingizi.Kichwa chake kilikuwa kizito kwa mawazo mengi aliyokuwa nayo.
“ I don’t know if I’m doing the right thing” akawaza akiwa ameinama na mikono ikiwa kichwani.
“ Sikuwahi kufikiria hata mara moja kama siku moja nitajiunga na kikundi hiki cha mashetani wa nchi.Mtandao wa Dr Joshau naweza kuuita ni wa mashetani kwa namna wanavyofanya mambo yao ya kifedhuli bila kuwa na hata chembe ya huruma.Wanatoa roho za watu bila hata huruma yoyote.Wamelewa madaraka na wanafanya chochote wakitakacho katika nchi hii.Wapo wazalendo wachache ambao wameyatoa maish a yao sadaka kwa kupambana na mtandao huu na miongoni mwao ni Mathew na Anitha lakini badala ya kuwaunga mkono nimechagua kuwasaliti .Si kuwasaliti pekee bali nimezirudisha nyuma juhudi zao zote za kujaribu kulifutilia mbali kundi hili la mafisadi wanaoitafuna nchi bila huruma wakiongozwa na rais Dr Joshua.Mipango yao yote nimeiweka wazi kwa Dr Joshua na kwa sababu hiyo hawana tena namna nyingine ya kutimiza malengo yao na Dr Joshua lazia atafanikisha mpango wake wa kukiuza kirusi Aby.” Akawaza na kujipiga kichwani kwa hasira
“ Shetani gani amenipitia na kunishawishi kufanya hivi nilivyofanya? Akazidi kuumia kwa mawazo kila alipokumbuka kile alichokifanya.
“ Lakini sipaswi kujilaumu sana kwa nilichokifanya kwani sikuwa na namna nyingine ya kufanya .Tayari maji yalikwisha nifika shingoni na sikuwa na uwezo tena wa kupambana na Dr Joshua.Nilishika makali wakati yeye ana mpini kwa hiyo kwa namna yoyote ile lazima angenikata tu.Nilikuwa nataka kushindana na mtu mwenye nguvu kuliko wote hapa nchini.Vyombo vyote vya dola viko chini yake kwa hiyo nisingeweza kujificha kwa muda mrefu lazima ningepatikana tu.Nilikuwa najitengenezea mwenyewe njia ya kujipoteza katika ramani ya dunia kwa hiyo nilichokifanya kwa upande mmoja si sahihi lakini kwa upande wa pili ni sahihi.Hata vitani mwanajeshi anayeshindwa hujisalimisha .Vita nilivianzisha mimi mwenyewe kwa shauku yangu ya kutaka kufahamu mambo yasiyonihusu na sikujua kama vita hii ingenifiisha hapa.Nimepoteza mke wangu Flaviana na mimi mwenyewe nilikuwa katika hatari ya kupotea.Nilihitaji maisha yangu tena.Nilihitaji kuwa huru na ili hilo lifanikiwe njia pekee ilikuwa ni kunyanyua mikono na kujisalimisha.Najua Mathew na wenzake wataumizwa sana na jambo hili lakini sina namna nyingine ya kufanya ,tayari limekwisha tokea na kwa hilo lazima wakubaliane nalo.Hapo mwanzo hata shetani aliwahi kuwa malaika na akaasi kwa hiyo uasi sikuuanza mimi.I hope they’ll understand japokuwa sijui mwisho wake utakuaje kwani sina hakika kama Mathew ataliacha jambo hili lipite hivi hivi.Lazima atataka kulipiza kisasi .Namfahamu Mathew ni mtu mzuri sana lakini ukimkorofisha ni mbaya kuliko shetani.He will haunt me till the day he die.Kwa ajili ya usalama wangu nitamwomba Dr Joshua anipatie ulinzi wa kutosha Anyway nisipoteze muda kuwawaza akina Mathew kwani nguvu ya kuwadhibiti ninayo na isitoshe baadae mwaka huu nitakuwa rais wa Tanzania .Dr Joshua amenihakikishia hilo na uwezo huo anao kwa hiyo ninachopaswa kukiwaza sasa ni namna gani nitatokea mbele ya umma wa watanzania n a kujisafisha kwani hapa nilipo nina tuhuma za kusababisha kifo..Nitatakiwa kueleza nilinusurika vipi katika shambulio ,baada ya hapo nilikwenda wapi ,natakiwa vile vile kukanusha tuhuma za kuhusishwa na kifo cha Flaviana.lakini haya yote yanatajkiwa kufanywa na Dr Joshua kwani uwezo huo anao.Mtu pekee ambaye nitapata wakati mgumu kwake ni Anna.Nilimuhakikishia kwamba baba yake anahusika na vifo vya mama na dada yake .Nilimueleza vile vile kwamba hata mimi kunusurika kuuawa ulikuwa ni mpango wa Dr Joshua na washirika wake baada ya kugundua sababu ya kifo cha Dr Flora.Lakini ghafla ananiona nikiwa nimeongozana na baba yake mtu ambaye anataka kuniua.Ni wazi hapa kunahitajika maelezo ya kutosha sana kumfanya aniamini.Halafu Dr Joshua kuna kitu alinigusia.Alisema kwamba kwa kuwa anataka kunipigania ili niwe rais basi nianzishe mahusiano na Anna ili nitakapokuwa rais basi Anna awe katika nafasi ya uongozi.Sina hakika kama hilo litawezekana kwani mimi na Anna hatujawahi kuwa katika mahusiano mazuri kwa muda mrefu na tumeanza kuzungumza vizuri hivi majuzi .Baada ya tukio la kushambuliwa kwa Flaviana Mwanamke pekee ambaye moyo wangu uliridhia kuwa naye ni Peniela .Yule ana kila kitu ninachokihitaji kwa mwanamke lakini kwa bahati mbaya sintaweza kumpata tena.Anyway ngoja niachane na mawazo haya ili kichwa changu kipumzike .Kesho itakuwa ni siku yangu ndefu sana” akawaza jaji Elibariki na kujilaza kitandani
******
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment