Search This Blog

Wednesday, 29 March 2023

PENIELEA (3) - 1





 IMEANDIKWA NA : PATRICK CK




*********************************************************************************



Simulizi : Peniela (3)

Sehemu Ya Kwanza (1)



PENIELA SEASON 3



EPISODE 1







ILIPOISHIA SEASON 2





“ John this is the last chance ..are you Peniela’s father? Akauliza Mathew kwa ukali.John akajibu kwa kumfanyia ishara kwamba haelewi chochote.Mathew akakasirika na kuchomoa bastora yake.Peniela akaogopa sana

“ Mathew what are yo doing? Akauliza lakini Mathew hakumjali

“ Mathew unataka kufanya nini? Akauliza Peniela kwa wasi wasi



“ I’ll count to three and if you cant answer me I’m going to kill you John ! akasema kwa ukali Mathew



“ Mathew No ! Don’t do that !! akasema Peniela huku akilia

“ Jason hold her” Mathew akamuamuru Jason amshike Peniela ili asimsogelee.

“ Three…..!!!akaanza kuhesabu Mathew huku amemuelekezea John bastora



“ Two ….!!!!



“ Mathew noo!!!!..dont do that !!..akapiga kelele peniela.

“ On………..” Kabla Mathew hajamaliza kutamka John Mwaulaya akasema

“ Ok ok..I’ll tell you..put your gun down” akasema John mwaulaya aliyekuwa akitetemeka



“ ok tell her the truth! akasema kwa ukali Mathew huku akimtazma John kwa macho ya hasira

John akamfanyia ishara peniela asogee karibu na kuanza kumsimulia kilichotokea kuhusiana na wazazi wake.Alisimulia mkasa mzima uliotokea na kupelekea kuwaua wazazi wote wa peniela.Peniela alibubujkwa na machozi mengi.John akamgeukia Mathew



“ Hiyo ndiyo historia ya Peniela.Nilishindwa kabisa namna ya kumueleza nikiogopa kumuumiza na ndiyo maana nilitaka afahamu kuhusu yeye baada ya mimi kufariki dunia.Nilijua lazima atanichukia sana akifahamu kwamba mimi ndiye niliyewaua wazazi wake.Nilimuwekea kila kitu kuhusiana na historia yake katika makasha matatu ikiwamo na picha za wazazi wake.” Akasema John.Peniela alimuangalia kwa hasira huu machozi yakimtoka.



“Leo nilikuja kwa ajili ya Peniela.Safari ijayo nitakuja rasmi kwa ajili yangu.Jiandae “ akasema Mathew na kutoka Peniela akamfuata

“ Mathew thank you so much.Umenisaidia nimefahamu jambo kubwa sana.Sikuwa nikifahamu chochote kuhusiana na wazazi wangu.John amenificha siri hii kwa miaka mingi.I hate that bastard so much.”akasema Peniela

“ Elibariki aliniomba nikusaidie kuufahamu ukweli kuhusiana na asili yako na ninashukuru ukweli umedhihiri.Naomba ukweli huu usivuruge mipango yetu.”

“hakuna kitakachovurugika Mathew.I’m a very strong woman.Kila kitu kitakwenda kama tulivyokipanga.hata hivyo nina swali nataka kukuuliza.”



“ Uliza Peniela”



“ Ulipomuelekezea John bastora na kuanza kuhesabu,ulidhamiria kumpiga risasi kama asingesema chochote ?

Mathew akatabamu kidogo na kusema



“ No ! I just wanted him to talk”

“ ahsante Mathew.Ahsante sana.Tutaonana jioni .Mwambie Elibariki nashukuru sana kwa kunijali.Bila yeye kuwa na mawazo haya nisingeufahamu ukweli kuhusu wazazi wangu“ akasema peniela na kurejea tena ndani akakuta hali ya John mwaulaya imebadilika ghafla.Ikawalazimu wawaite haraka wale madaktari wawili waliokuja toka marekani kwa lengo la kuja kuangalia afya yake.







ENDELEA SEASON 3

EPISODE 1 ……………………..





Saa saba na dakika ishirini za mchana,gari zipatazo saba ziliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Anna mtoto wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akashuka toka mojawapo ya magari yale na kuongozana na maafisa wa usalama pamoja na ndugu wengine alioambatana nao hadi katika sehemu ya kupumzikia.Katika siku hii ya leo binti huyu mrembo aliyafunika macho yake yaliyokuwa mekundu kwa miwani myeusi . Ni wazi ilionyesha alikuwa Amelia sana.

Dakika kumi baadae kikasikika king’ora cha gari la wagonjwa likiwasili pale uwanjani.Gari hili lilimbeba Flaviana akitokea katika hospitali kuu ya taifa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda afrika ya kusini kwa matibabu zaidi.Bila kupoteza muda madaktari na wauguzi wakasaidiana kumshusha Flaviana toka ndani ya gari lile la wagonjwa akiwa bado hana fahamu na kuingizwa moja kwa moja katika ndege iliyokwisha andaliwa maalum kwa ajili ya kumsafirisha kuelekea afrika ya kusini.Taratibu zilipokamilika Anna akaagana na ndugu zake na watu wengine alioambatana nao na kuanza kupiga hatua kuelekea ndegeni.Kabla hajakanyaga ngazi za ndege ,mmoja wa walinzi akamkimbilia na kumpa simu



“ Mzee anataka kuongea nawe” akasema Yule mlinzi.Anna akachukua simu na kuiweka sikioni.

“ Hallow dady “ akasema Anna.Dr Joshua akasikika simuni akivuta pumzi ndefu kisha akasema

“ Hallow Anna.Tayari kila kitu kimekamilika?

“ Ndiyo baba.Kila kitu kimekamilika na kwa sasa tunaingia ndegeni tayari kwa safari”

“ Sawa Anna.Ningependa sana kuongozana nanyi kuelekea huko afrika ya kusini lakini kikao kile cha wakuu wa nchi za afrika ya mashariki ni cha muhimu sana kuna mambo ya msingi sana ambayo yananilazimu niwepo .Hata hivyo jioni baada ya kumaliza kikao nitakuja kuungana nanyi huko afrika ya kusini” akasema Dr Joshua

“ Usijali baba ninaelewa majukumu uliyonayo .Tuzidi kumuombea Flaviana aweze kupona” akasema Anna.

“ Ni kweli Anna inatubidi tusimame pamoja kama familia na nina hakika Mungu atamponya Flaviana.Mungu awatangulie katika safari yenu na mfike salama” akasema Dr Joshua na kuagana na Anna kisha akakata simu. Anna akarejesha simu kwa Yule afisa wa usalama akapanda ndegeni na mlango ukafungwa.Haikuchukua muda mrefu ndege ikapaa na kuelekea afrika ya kusini.Michirizi ya machozi ikaonekana machoni kwa Anna.

“ Ee Mungu msaidie dada yangu Flaviana aweze kupona.Bado ninamuhitaji sana katika maisha yangu.” Anna akaomba kimya kimya huku akijifuta machozi.Shangazi yake aliyekuwa pembeni yake akamuonea huruma sana na kumshika bega



“ Anna usilie,utazidi kuumiza kichwa.Flaviana atapona tu” shangazi yake akamfariji



“ Shangazi ninaumia sana kwa mambo yanayotokea katika familia yetu.Kwanza alifariki mama,Elibariki mume wa Flaviana akanusurika katika shambulio na hata muda haujapita Flaviana naye anapatwa na janga hili kwa kweli mambo yanayoumiza sana.Mambo mazito yametokea katika kipindi kifupi sana” akasema Anna.Shangazi yake akamtazama akamuonea huruma sana na kusema



“ Anna unatakiwa uwe jasiri sana kwani kwa sasa sote tunapita katika kipindi kigumu sana.Ni wakati wa kumuomba Mungu awape nguvu ya kuhimili misuko suko hii mizito.Nina hakika kabisa vyombo vya usalama viko macho na vitamsaka na kuhakikisha vinampata huyu aliyemfanyia Flaviana ukatili huu mkubwa.Sikuwahi kufikiria hata siku moja kama jaji Elibariki angeweza kufanya jambo kama hili la kikatili kwa mke wake wa ndoa.Sijui ni shetani gani aliyemuingia na kumshawishi akafanya ukatili huu mkubwa uliopitiliza.Ninakuhakikishia Anna kwamba hataweza kujificha kamwe na na atapatikana tu ili aweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria” akasema shangazi yake anna

“ Kwa kweli inashangaza sana kwa kitendo alichokifanya Elibariki.Ni wazi alikuwa na lengo la kuua kabisa” akasema Anna halafu ghafla akakumbuka kitu

“ Kuna kitu bado kinanipa mashaka sana kuhusiana na tukio hili la kushambuliwa Flaviana.Katika taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi inasema kwamba Elibariki alipanga shambulio lile kutokana na wivu wa mapenzi akitaka kulipiza kisasi kwa Flaviana baada ya kugundua kwamba Flaviana alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine nje ya ndoa.Ninapata mashaka kidogo kukubaliana na kauli hii kwa sababu ninamfahamu vyema Flaviana hakuwa na tabia hii na hata siku moja hakuwahi kunieleza kama ana mahusiano ya siri nje ya ndoa yake.Ninafahamu ndoa yao ilitawaliwa na migogoro mingi lakini hata siku moja Flaviana hakuwani kunieleza chochote kuhusiana na kuwa na mpenzi nje ya ndoa na wala kuwa na hisia za kuwa na mahusiano mbadala.Kama ingekuwa ni kweli tayari angekwisha nieleza kwani mimi ndiye niliyekuwa msiri wake mkubwa na hata siku moja hajawahi kunificha jambo lolote hata liwe kubwa kiasi gani.Hii inanipa ugumu sana kukubaliana na kauli hii eti ya kwamba shambulio lile lilikuwa ni kwa ajili ya kulipiza kisasi.Kingine kinachonipa mashaka nisikubaliane moja kwa moja na kauli hii ya jeshi la polisi ni utayari wa Elibariki kutenda jambo kama hili la kutaka kumtoa uhai mke wake.Mimi na Elibariki hatukuwa katika maelewano mazuri kwa muda mrefu na baada ya kufanya maamuzi ya kesi ile iliyomkabili Peniela tulizidi kuwa maadui zaidi lakini pamoja na yote yaliyotokea kati yetu ninamfahamu vizuri Elibariki hana roho mbaya kiasi hicho hadi kufikia hatua ya kutaka kuua.Ni mmoja kati ya wanaume wavumilivu sana .Ninamfahamu dada yangu ni mkorofi na ana matatizo yake lakini Elibariki amevumilia mambo mengi sana toka kwa Flaviana kwa sababu alimpenda sana.Nakumbuka wakati wa msiba wa mama ni Elibariki aliyehatarisha uhai wake kwa kufanya uchunguzi kuhusiana na kile kilichomuua mama na alifanya hivi kwa ombi la Flaviana.Amenusurika katika shambulio ambalo polisi wanadai kwamba lilifanywa na mtu ambaye anasadikiwa kuwa katika mahusiano na Flaviana kwa lengo la kutaka kumuua Elibariki na baada ya hapo Elibariki akapotelea mafichoni.Akiwa huko aliwasiliana na Flaviana usiku ule na kumtaka afanye juu chini ili aipate taarifa ile ya madaktari bingwa waliofanya uchunguzi kuhusiana na kilichosababisha kifo cha mama.Kuhusiana na taarifa ile ninapata shaka kidogo namna baba alivyoweza kumpatia taarifa ile kwa haraka na wepesi wakati hapo kabla hakuwa tayari kabisa taarifa ile iguswe na mtu mwingine yeyote zaidi yake.Kuna picha ambayo nimeanza kuipata hapa nikiunganisha matukio haya yote nikianzia na kifo cha mama na hadi shambulio la Flaviana.” Akawaza Anna

“ Ukiunganisha mtiririko wa matukio utagundua kwamba kuna jambo linaloendelea.Kwa picha ninayoipata nashawishika kuamini kwamba si Elibariki aliyefanya kitendo kile cha kumshambulia Flaviana.Alichokuwa akihitaji Elibariki usiku ule ni taarifa ile ya madaktari na hakuwa na lengo la kumdhuru Flaviana.Kama si yeye aliyefanya shambulio lile nani basi alitaka kumuua Flaviana na kwa nini? Akajiuliza Anna

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Kuna kitu nimekumbuka.Siku ile usiku Flaviana alikuja chumbani kwangu na kutumia simu yangu kuwasiliana na Elibariki.Bado zile namba alizotumia zipo katika simu yangu.Nadhani ni yeye ndiye ana majibu yote ya kilichotokea usiku ule.Kwa kuwa nimeondoka na simu yangu nikifika afrika ya kusini nitafanya mawasiliano na Elibariki kwa kutumia namba ile ya simu .Ni yeye pekee kwa sasa ambaye anaufahamu ukweli wa kilichotokea usiku ule” Anna alizama katika mawazo mengi sana.

“ Nakumbuka usiku ule tulijadiliana na Flaviana kuhusiana na mambo yanayotokea ndani ya familia yetu tukianzia na kifo cha mama.Tuligundua kwamba baba hakuonyesha kabisa kuweka uzito katika kufuatilia chanzo cha kifo cha mama Tabia aliyoionyesha baba toka wakati wa msiba wa mama inatia shaka sana.Nilimsikia kwa masikio yangu Dr Kigomba akitoa amri ya kuwakamata madaktari waliokuwa wakitaka kufanya uchunguzi wa kilichomuua mama lakini baba alidiriki kusimama na kumtetea Dr Kigomba kwa nguvu zote.Hata mimi ninaanza kupata picha Fulani ambayo si nzuri kuhusiana na baba na matukio yaliyotokea.Kuna ulazima wa kulifanyia uchunguzi jambo hili na kwa hili Elibariki anaweza kuwa na msaada mkubwa sana kwangu” akaendelea kuwaza Anna halafu akajiegemeza kitini na kijiusingizi kikampitia







********



Madaktari wawili waliongozana na Nickson Strawberry kutoka Marekani walirejea haraka sana nyumbani kwa John Mwaulaya baada ya kutaarifiwa kwamba hali ya John Mwaulaya ilibadilika ghafla.Wote walishangaza sana na mabadiliko yale ya ghafla ya hali ya John.Si muda mrefu sana walipoongea naye na alionekana kutokuwa katika hali mbaya sana kama aliyokuwa nayo sasa.Bila kupoteza wakati wakatoa mashine zao na kuwaomba Peniela na John watoke mle chumbani isipokuwa Martin ambaye ana taaluma ya udaktari na ambaye amekuwa akimuhudumia John kwa muda mrefu.



“ I’m so scared Josh.I don’t know if he’s going to make it…” akasema Peniela kwa wasi wasi mkubwa wakiwa nje ya mlango wa chumba cha John Mwaulaya .John akamtazama na kumshika bega

“ Usiogope Peniela.John atapona.He’s a strong man and he’s going to survive” Josh akampa Peniela maneno ya faraja.Peniela akafuta machozi na kusema

“ Pamoja na mambo mengi mabaya aliyoyafanya John Mwaulaya kwangu na kwa wengine lakini yeye ni sababu ya mimi kuwepo hapa nilipo.Alipewa amri aniue lakini hakufanya hivyo na badala yake aliniacha hai na akahakikisha ninalelewa vyema.Japokuwa nimeishi bila ya wazazi wangu lakini nimeishi maisha mazuri na kupatiwa kila kitu na hii yote ni kwa sababu ya John .Ingawa ni mtu mwenye roho ngumu na ya kikatili lakini ana sehemu ndogo ya huruma na upendo ndani ya moyo wake na ndiyo maana hakudiriki kuniua.Nikipima kati ya mazuri na mabaya aliyonifanyia ninakuta mazuri ni mengi kuliko mabaya kwa hiyo nina deni kwake” akasema Peniela

“ Uko sahihi Penny.John ni mtu katili lakini ana huruma sana.Yeye ndiye aliyeniokota toka katika maisha yangu mabaya niliyokuwa nayo na akanifikisha hapa.Nimekuwa mlinzi wake kwa muda mrefu na nimejifunza mambo mengi toka kwake .John ameniamini sana kuliko mtu mwingine yeyote na kwa mambo mengi aliyonifanyia hata mimi ninadiriki kukiri kwamba nina deni kuwa kwake” akasema Josh



“ Mungu amsaidie John apone” akasema Peniela akiwa ameifumbata mikono kifuani.Josh akakaa kimya halafu akasema



“ Peniela do you trust these guys? Are they real doctors?



“ Kwa nini unauliza hivyo Josh ? akauliza Peniela



“ Nina mashaka kidogo na hawa watu wanaotoka Marekani wakidai kutaka kumtibu John.Awali John hakuonyesha kukubaliana nao na ndiyo maana alinituma nimuue Dr Burke.Aliniambia kwamba Dr Burke hakuwa na lengo la kuja kumtibu bali kumuua” akasema Josh na Peniela akamtazama Josh kwa wasi wasi na kuuliza



“ John alikueleza ni kwa nini Dr Burke alitaka kumuua? Kwa nini Team Sc41 wanataka kumuua?

“ Peniela mimi nimekuwa mtu wa karibu na John Mwaulaya kwa muda mrefu lakini nakuhakikishia John ni mtu msiri sana.Maisha yake yamezungukwa na siri nyingi kwa hiyo sifahamu mpaka leo sababu ya Dr Burke kutaka kuja kumuua” akasema Josh.Peniela akainama kidogo akafikiri na kusema

“ Josh hisia zako zinaweza kuwa za kweli.Hatupaswi kuwaamini hawa watu hata kidogo.Nina hakika lazima ipo sababu iliyopelekea Dr Burke kutaka kumuua John.Nilikwisha wasiliana na daktari mmoja ambaye ni rafiki yake mkubwa na John na anajiandaa kuja kumfanyia John upasuaji.Maandalizi yamekwisha kamilika na wanaosubiriwa ni madaktari hao tu wafike na kuifanya operesheni hiyo.Kinachonishangaza ni kwamba nimewaeleza akina Edwin kuhusiana na suala hili na wamelipinga vikali.Hawataki kabisa mtu yeyote ambaye hawamjui ashughulike na ugonjwa wa John.Wanadai kwamba hakuna haja ya kuwaleta madaktari kwa kuwa wao wanatosha na wamekuja kwa ajili ya kazi hii moja ya kumtibu John,hata hivyo sina kabisa imani na watu hawa na ndiyo maana nimefikiria ku…..” Peniela akataka kusema kitu lakini akastuka

“ Ouh my gosh ! nimejisahau na kutaka kutamka mpango wangu wa kuimaliza team SC41 mbele ya josh.Huu ni mpango wa siri ambao hatakiwi kuufahamu mtu mwingine yeyote toka ndani ya team sc41” akawaza Peniela

“ Umesema unafikiria kufanya nini Peniela? Akauliza Josh



“ Nafikiria namna ya kumsaidia John.We cant just sit here and give these guys chance to kill him.We have to get in there and see what they are doing” akasema Peniela huku akianza kupiga hatua kuuelekea mlango wa chumba cha John lakini Josh akawahi kumshika mkono.



“ Hapana Peniela hatuwezi kuingia humo ndani kwa sasa.Tuwaache kwanza wafanye kazi zao ila tusiache kuwafuatilia kwa karibu kuona kama kweli wana lengo la dhati la kumtibu John” akasema Josh

“ Ndani ya chumba cha John Mwaulaya madaktari wale wawili toka marekani wakisaidiana na Dr Martini ambaye amekuwa akimuuguza John mwaulaya kwa muda mrefu waliendelea na jitihada za kuhakikisha hali ya John inarejea kuwa ya kawaida.Wakati kazi hiyo ikiendelea mmoja wa madaktari wale ambaye alikuwa karibu sana na Martini akamuuliza

“ Dr Martin hebu nieleze nini hasa kilichotokea na kusababisha hali ya John kubadilika ghafla na kuwa mbaya kiasi hiki? Kuna dawa yoyote au sindano uliyomchoma iliyopelekea hali yake kubadilika ? akauliza Dr Edwin Hurdosn.Swali lile likambabaisha kidogo Martin kulijibu.



“ Martin nini kilitokea na kusababisha hali ya John iwe hivi? Akauliza tena Dr Edwin

“ Hakuna dawa niliyompa ambayo imebadilisha hali yake kuwa hivi.Dawa alizotumia ni zile ambazo amekuwa akizitumia kila siku .Hali yake ilibadilika ghafla tu” akasema Martin



“ Martin tumekuja sisi toka Marekani kwa ajili ya kazi moja tu ya kushughulikia ugonjwa wa John na kulifahamu tatizo lake.Hili si suala dogo kama unavyofikiria kwani John ni mtu mwenye nafasi ya juu sana ndani ya Team Sc 41 kwa hiyo ugonjwa wake unapewa uzito mkubwa.Mimi na mwenzangu ni mabingwa katika mishipa ya fahamu na tuna hakika tutaokoa maisha ya John lakini tunahitaji sana taarifa kamili za kuhusiana na ugonjwa wake.Najua tutayaongea hayo baadae kidogo lakini kwa sasa tunatakiwa kufanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kurejesha hali yake iwe kawaida ndipo tuanze kuchukua vipimo na kugundua tatizo lake kwa maana hiyo tunahitaji kufahamu ukweli kama kuna dawa yoyote ulimpa au kuna sindano ulimchoma kabla ya kuendelea na matibabu mengine”

Martin akabaki kimya akitafakari



“ Martin !!!!..Edwin akamstua



“ Toka asubuhi hali ya John ilikuwa nzuri na alitumia dawa zile zile ambazo amekuwa akizitumia siku zote .Kilichotokea ni kwamba baada ya nyie kuondoka kuna watu Fulani waliingia ghafla kuja kuonana na John” akasema Martin

“ Watu ?!!..Andrew akashangaa

“ Watu gani hao? Walifuata nini? Akauliza

“ Watu hao mimi siwafahamu ila wanafahamiana na Peniela”

“ Hauwafahamu? Hujawahi kuwaona watu hao hapo kabla? Unakumbuka waliongea nini na John? Dr Edwin akauliza maswali mfululizo.Wakati huo mwenzake aitwaye Alexander Piscat aliyekuwa akishughulika kuweka sawa baadhi ya mashine alikwisha maliza kuunganisha mashine ile na kuwasogelea akina Edwin.

“ Edwin kila kitu tayari sasa tunaweza kuendelea na kazi yetu” akasema Dr Alex

“ Kabla hatujaendelea ,nilitaka kufahamu kilichotokea na kusababisha hali ya John kubadilika ghafla.Kuna jambo Martin amenieleza limenistua kidogo.Anasema kuna watu walifika nyumbani kwa John ambao hawafahamu na hajawahi kuwaona pale na walizungumza na John na baada ya hapo ndipo hali yake ilipobadilika ghafla” akasema Dr Edwin



“ Martin ni akina nani hao waliokuja nyumbani kwa John? Akauliza Dr Alex



“ Siwafahamu watu hao ni mara yangu ya kwanza kuwaona lakini wanafahamiana na Peniela” akasema Dr Martin halafu akasita kidogo na kuendelea

“ Martin tafadhali naomba utueleze kila kilichotokea.Watu hao walihitaji nini na waliongea kitu gani na John? Akasema Alex



“ Nilikuwa humu chumbani nikiwa na Peniela na mara mlango ukafunguliwa akaingia Josh akiwa ameongozana na watu wawili ambao siwajui ila Peniela alionekana kuwafahamu watu hao kwani aliwaita hata kwa majina yao Mathew na Josh.Kwa jinsi nilivyoona watu wale walikuwa wakifahamiana na John kwa sababu baada tu ya kuwaona John alistuka sana.Yule jamaa aitwaye Mathew alimtazama John kwa ukali na ninakumbuka maneno Fulani aliyasema.Alisema kwamba japokuwa ni miaka mingi imepita lakini ana uhakika John atakuwa akimkumbuka vyema.Aliendelea kusema kwamba kwa siku ya leo hakuja kwa ajili yake bali kwa ajili ya Peniela.”

“ alikuja kwa ajili ya Peniela? Dr Alex akauliza



“ Ndiyo .Alitaka John aeleze ukweli kuhusiana na historia ya Peniela.Alimtaka John aeleze wazi wazi mahala waliko wazazi wa Peniela.”

“ John alijibu nini? Akauliza Edwin

“ John alikataa kutofahamu chochote kuhusiana na walipo wazazi wa Peniela ndipo Mathew alipochomoa bastora na kumlenga John.Alitishia kumpiga risasi na akaanza kuhesabu .Kabla hajafika tatu John akakubali kueleza ukweli.Alieleza kila kitu kuhusiana na wazazi wa Peniela kwamba ni yeye aliyewaua kisha akamchukua Peniela na kumlea”

Dr Edwin na Alex wakabaki wanatazamana



“ Siku zote huwa ninamuita John ni shetani mweusi.Ni mtu wa kuogopwa sana” akasema Edwin kwa sauti ndogo



“ Nini kilifuata baada ya hapo ? Dr Alex akauliza



“ Baada ya John kueleza ukweli kuhusiana na Peniela ,Mathew akamwambia John kwamba anaondoka lakini atarejea tena mara ya pili na atakaporejea itakuwa ni maalum kwa ajili yake.John alionekana wazi kuogopa sana na mara tu Mathew na Jason walipoondoka ndipo hali yake ilipobadilika” akasema Martin na kuwaacha Alex na Edwin wakitazamana



“ Huyu Mathew ni nani? .Anaonekana kumfahamu sana John na kwa hiyo kuna uwezekano atakuwa akifahamu kuhusiana na Team Sc41.Huyu anaweza akawa ni mtu hatari sana kwetu” akasema Edwin



“ Ahsante Dr Martin kwa maelezo hayo.Tutayafanyia kazi lakini kwa sasa tunatakiwa kuyaokoa kwanza maisha ya John.Tutaongea mambo mengine baadae” akasema Alex na kumshika mkono Edwin akamvuta kuelekea katika kitanda cha John Mwaulaya wakaendelea na zoezi la kujaribu kurejesha mapigo ya moyo ya John katika hali ya kawaida







***********





“ Mathew kwa kweli sikutegemea kabisa kusikia yale niliyoyasikia toka kwa John kuhusu Peniela.Huu ni ukatili mkubwa sana amemfanyia .Ninaapa lazima nimsaidie Peniela kwa kila namna niwezavyo ili aweze kuipata haki yake.John Mwaulaya ni mtu katili sana na ambaye hastahili kabisa kuwa huru katika jamii iliyostaarabika.Ninaapa nitapambana hadi nihakikishe haki imetendeka na John amefikishwa mbele ya sheria. Bado sijasahau namna walivyoniteka na kunifanyia ukatili mkubwa ndani ya jumba lile. Maskini Peniela ameteseka sana.Nitapambana kwa ajili ya kumsaidia kuipata haki yake !! akasema Jason kwa masikitiko makubwa wakiwa garini baada ya kutoka nyumbani kwa John Mwaulaya.

“ Hakuna haja ya kufanya hivyo !!!..akasema Mathew

“ What ?!!...Jason akashangaa

“ John mwaulaya amewaua wazazi wa Peniela kwa mkono wake .Unajua ni maumivu kiasi gani aliyo nayo sasa Peniela baada ya kuufahamu ukweli kuhusiana na wazazi wake? Japokuwa hataki kuonyesha lakini ni wazi ameumia.Kama mimi imeniuma hivi vipi kuhusu muhusika mwenyewe? John is a monster na anatakiwa akafie gerezani.Nakuhakikishia Mathew siwezi kukaa kimya katika jambo hili,lazima nihakikishe John anatupwa gerezani kwa kitendo hiki alichokifanya.Sintojali ugonjwa wake ninachojali mimi ni haki itendeke.Hakuna anayeweza kunizuia katika hili.I swear no bo body is going to stop me on this” akasema Jason.



“ Achana kabisa na suala hili Jason.Hutakiwi kufanya chochote kuhusiana na suala hili” akasema Mathew kwa sauti ya juu kidogo.Jason akamtazama Mathew kwa macho makali na kusema

“ Are you out of your mind Mathew? Are you real want to let this go ? No ! Peniela is my friend,I love her and her pain is my pain as well so I swear I wont let this go.I must do something !!.Mimi ni mwanasheria na siku zote lengo langu ni kuhakikisha kwamba haki inapatikana .I must fight for her “ akasema Jason

“ No Jason !!.You cant do anything..” akasema Mathew kwa ukali

“ You cant do anything about this.You cant take down team Sc41.You cant fight John.He’s on bed right now but he’s still a very dangerous man and above all you don’t know anything about him.If you love Peniela and you want to help her,stay out of this !!!!... akasema Mathew .Jason akamtazama kwa hasira kisha akasema

“ Mathew mimi na Elibariki ndio tuliokupa kazi hii kwa hiyo kama sisi ndio tunaokulipa huwezi ukatupangia nini cha kufanya.Kuniambia kwamba siwezi kufanya lolote kuhusiana na suala hili ni sawa na kuniambia I’m not a real man.Hufahamu chochote bado kuhusiana na mimi na nini ninaweza nikafanya.Hufahamu chochote kuhusu mimi na Peniela na nimefanya mambo mangapi hadi sasa Peniela yuko huru.Kwa maana hiyo nina..!!..” Kabla hajamaliza alichotaka kukisema Mathew akamkatisha

“ Stop it Jason !! akasema Mathew kwa ukali



“ Naomba nikuweke wazi kwamba ni kweli mlinikabidhi kazi hii lakini nilikubali kuifanya kwa sababu ya ukaribu wangu na Elibariki na wala sikuwa nikikufahamu wewe.Japokuwa ilikuwa ni kazi yenu lakini kwa sasa hii ni kazi yangu na ninaifanya kwa namna ninavyotaka mimi kwa hiyo naomba ukae pembeni na uniache niifanye kazi yangu na usijihusishe na suala lolote linalohusiana na Peniela.Huna sababu yoyote ya kuhatarisha maisha yako kwa sababu ya Peniela.She loves Elibariki and no matter what you try to do, she’ll never change her mind and love you.Kwa hiyo Jason usitake kujiumiza bure kwa jambo hili.This is my job,this is my mission let me finish it !!..” akasema Mathew.Jason akamuangalia usoni kwa hasira na kusema

“ Stop the car !!!..akasema Jason kwa ukali



“ Unataka kushuka? Akauliza Mathew



“ Mathew simamisha gari nishuke !!!..akasema Jason .Mathew hakujibu kitu akaendesha gari hadi katika kituo cha daladala kilichokuwa karibu akasimamisha gari na Jason akashuka kwa hasira na kuubamiza mlango na kutamka neno ambalo Mathew hakulisikia vizuri.Mathew hakumjali akaingiza gari barabarani na kuendelea na safari yake



“ stupid !!..akasema Mathew



“ Katika maisha yangu yote ndani ya kazi hii nimekutana na watu wengi makatili lakini si kama John Mwaulaya.Mtu huyu aliiteketeza familia yangu bila huruma na ametoa roho za watu wengi.Hata hivyo siku zake zinahesabika .Nitarudi tena kwake kwa mara nyingine na hii itakuwa ni zamu yangu.Picha za moto ule mkubwa ulioiteketeza familia yangu bado haijafutika kichwani kwangu.Nitamuua John taratibu sana na kwa mateso makali ” akawaza Mathew huku akiuma meno kwa hasira





Hatimaye baada ya jitihada kubwa Dr Edwin na Dr Alex wakisaidiana na Dr Martini walifanikiwa kuirejesha hali ya John Mwaulaya katika hali yake ya kawaida.Mapigo ya moyo yalirejea katika hali ya kawaida japokuwa bado John bado hakuwa na fahamu.

“ Ouh ahsante Mungu ! akasema Dr Edwin baada ya mashine inayoonyesha mwenendo wa mapigo ya moyo kuanza kuonyesha kwamba sasa yalianza kwenda kawaida.Kwa takribani dakika mbili wote walibaki kimya wakimtazama John.Dr alex akamuita Edwin pembeni wakaongea kwa zaidi ya dakika kumi huku wakielekezana jambo fulani halafu wakamfuata Martin

“ Martin tunahitaji kuonana na Peniela” akasema Dr Alex.Martin akatoka na baada ya dakika tatu akarejea akiwa ameongozana na Peniela na Josh



“ Dr Alex vipi hali ya John? Akauliza Peniela kwa wasi wasi.Dr Alex akamshika mkono na kumketisha sofani



“ Peniela hali ya John mwaulaya siwezi kusema ni nzuri kwa sasa japokuwa mapigo ya moyo yamerejea katika hali yake ya kawaida.Inaonekana alipatwa na mstuko mkubwa na ndiyo maana hali yake ilibadilika ghafla.Tumejitahidi kwa kila tulivyoweza na tumefanikiwa kuyarejesha mapigo ya moyo katika hali yake ya kawaida.Pamoja na hayo ninaomba niwe muwazi kwako kwamba tatizo la John linaonekana ni kubwa tofauti na tulivyokuwa tunafikiria.” Akasema Dr Alex na kuzidi kumuogopesha peniela

“ Dr Alex mmegundua nini kinamsumbua John? Akauliza Peniela

“ Ni mapema sana kutamka chochote kwa sasa hadi hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika.Kwa sasa kuna kitu tunahitaji “



“ Kitu gani Alex? Sema chochote “



“ Kutokana na hali ya John ilivyo kwa sasa anatakiwa afanyiwe uchunguzi mkubwa sana katika mfumo wake wote wa fahamu.Kwa vifaa tulivyo navyo hapa zoezi hilo haliwezi kufanikiwa kwa hiyo tunahitaji kupata hospitali yenye vifaa ambavyo tunaweza tukafanya uchunguzi wa kina na kubaini kile kinachomsumbua John hospitali yenye usalama mkubwa kwani matibabu ya John yanatakiwa yawe ni siri kubwa” akasema Dr Alex



“ Hospitali itapatikana bila wasi wasi .Naomba dakika mbili nifanye mawasiliano ” akasema Peniela na kutoka mle chumbani akachukua simu yake na kumpigia daktari mkuu wa hospitali ile kubwa yenye aliyosaidiwa na Dr Joshua na kumtaarifu kwamba angempeleka John muda si mrefu kutokana na hali yake kuzidi kuwa mbaya.Baada ya kuwasiliana akarejea tena chumbani

“ Gari la wagonjwa litafika hapa muda si mrefu kwa hiyo tuanze kumuandaa mgonjwa.Tunampeleka katika hospitali kubwa ambayo huwatibu viongozi wakuu wa serikali na hata rais mwenyewe hutibiwa hapo.Kuna vifaa vyote mnavyovihitaji na hata usalama wake ni mkubwa sana” akasema Peniela



“ Josh gari la wagonjwa litafika hapa muda si mrefu nenda kawasubiri nje uwapokee.Dr Alex,Edwin na Martini tuanze kumuandaa mgonjwa” akaamuru Peniela

Gari la wagonjwa lilifika kwa haraka na John Mwaulaya akachukuliwa na kuwahishwa hospitali.Ndani ya gari hilo walipanda Dr Alex ,Dr Edwin na Martin.Peniela na Josh wao walifuata nyuma kwa gari la Peniela.Mara tu alipofikishwa hospitali John akapokelewa na bila kupoteza muda madaktari wa hospitali ile wakisaidiana na akina Dr Edwin wakaanza taratibu za kumfanyia uchunguzi wa kina .Madaktari katika hospitali ile walijitahidi kwa kila wawezavyo kutoa huduma za kiwango cha juu kwa John wakijua ni ndugu wa rais.

Kwa kuwa hakufahamu uchunguzi ule ungechukua muda gani , Peniela akaamua aondoke akaendelee na majukumu mengine kwani alikuwa na miadi na Anitha .Walipanga waonane ili aweze kumkabidhi vifaa maalum ambavyo vitawasaidia katika kumfuatilia Dr Kigomba.



“ Josh utaendelea kukaa hapa na kufuatilia kila kinachoendelea.mimi ninatoka kidogo nina miadi ya muhimu na mtu.Utanifahamisha kila kinachoendelea hapa” akasema Peniela na kuondoka zake







********



Mathew aliwasili nyumbani kwake akashuka garini na kumkuta jaji Elibariki peke yake sebuleni wakasalimiana



“ Anitha yuko wapi? Akauliza Mathew



“ Aliondoka hapa muda si mrefu na kusema kwamba anakwenda kuonana na Peniela kwa ajili ya kumpatia vifaa vile vya kusaidia kumfuatilia Dr Kigomba.”



“ Ok good.Kuna habari yoyote mpya? Akauliza Mathew



“ Hakuna habari yoyote mpya Mathew.Mimi niko humu ndani na sijui ni kitu gani kinachoendelea huko nje kwa hiyo nategemea sana kupata habari na taarifa toka kwako.Kwema huko utokako? Akauliza jaji Elibariki.Mathew akachukua glasi ya maji akanywa halafu akaketi sofani akavuta pumzi ndefu na kusema



“ Ulikuwa sahihi jaji Elibariki,kuna mambo mengi ambayo Peniela hakuwa akiyafahamu kuhusiana na wazazi wake.John lied to her.Lakini nashukuru leo tumeufahamu ukweli wote.Peniela amefahamu kila kitu kuhusiana na historia ya maisha yake na kuhusu wazazi wake.” Akasema Mathew na kumsimulia jaji Elibariki kila kitu kilichotokea.Hii ilikuwa ni habari iliyomstua sana jaji Elibariki

“ Masikini Peniela.Sipati picha maumivu aliyonayo sasa baada ya kuufahamu ukweli kuhusiana na wazazi wake.Hata mimi nimeumizwa sana na jambo hili. Peniela needs someone to comfort her right now.Huyu John mwaulaya ni shetani mkubwa.Amemuumiza sana mwanamke ninayempenda kwa moyo wangu wote.Hana hata chembe ya ubinadamu huyu mtu na laiti kama ningekuwa karibu yake ningeweza kumfanya jambo lolote baya” akasema jaji Elibariki kwa hasira

“ Ni kweli inauma sana jaji Elibariki.John Mwaulaya ni mtu katili na ameumiza watu wengi sana .Picha ya moto ule mkubwa ukiiteketeza nyumba yangu ambayo ndani yake ilikuwamo familia yangu bado haijafutika kichwani kwangu” akasema Mathew halafu akainuka na kwenda ukutani kulikokuwa na picha kubwa iliyowaonyesha watu wawili mwanamke na mwanaume wakiwa katika tabasamu kubwa.Picha hii ikamkumbusha mbali sana Mathew ,hizi zilikuwa ni siku za furaha alipokuwa na mke wake aliyempenda sana



“ Get ready John.Your days are numbered.Kipimo kile kile ulichokitumia kuiteketeza familia yangu ndicho hicho nitakachokitumia kuhakikisha kwamba unakufa kwa mateso makali sana” akasema Mathew kwa sauti ndogo

“ Kwa hiyo nini kinaendelea hivi sasa Mathew? Huyu John tunamfanya nini? akauliza jaji Elibariki



“ Just relax judge.I’ll handle this ,don’t worry” akajibu Mathew halafu akaelekea katika ofisi yake

“ Sasa ni wakati wa kuufahamu ukweli wa kile kilichomo katika zile nyaraka zilizopoteza uhai wa Edson na wenzake nyaraka ambazo zina thamani ya mabilioni ya fedha.” Akawaza Mathew huku akiiwasha kompyuta yake na kuitafuta barua pepe kutoka kwa Yash.Barua pepe hiyo iliandikwa hivi





“ Mathew,nimechelewa kidogo kurudisha majibu ya kile ulichoniomba nikusaidie kukifanyia uchunguzi.Hii ni kutokana na jambo lenyewe kuwa kubwa tofauti na nilivyokuwa nikilifikiria.Ilinilazimu kuwashirikisha jopo la mabingwa wa sayansi ili kwa pamoja waweze kutambua kilichoandikwa katika zile karatasi.Baada ya uchunguzi wa kina imebainika kwamba kilichoandikwa katika karatasi zile ni kanuni ya kutengeneza kirusi hatari sana ambacho kinaweza kufanya maangamizi makubwa endapo kitatumika kama silaha.Hiki kitu kimetustua sana sote.Wamenihoji sana wakitaka kujua mahala nilikozipata karatasi zile hatari na ni mwanasayansi gani aliyeandika kanuni zile lakini sikuwaeleza chochote kwa kuhofia kuingilia uchunguzi wako lakini Mathew ukae ukijua kwamba yeyote uliyemkuta na karatasi hizi ni mtu hatari sana na lengo lake si zuri hata kidogo.Yeyote uliyemkuta na karatasi hizi anatakiwa ashikiliwe kwa nguvu zote ili aweze kutoa maelezo ya kina kuhusiana na karatasi zile.Nimekuwekea pia viambatanisho kadhaa ili uweze kupata picha halisi ya nini kinaweza kutokea endapo kirusi hicho kikiweza kutengenezwa kwa kutumia kanuni hizo.Mathew jambo hili ni hatari sana kwa usalama wa nchi yako na dunia kwa ujumla kwani sifahamu mtu aliyekuwa na karatasi hizi alikuwa na malengo gani ila ninachokuomba jitahidi kufanya kila kinachowezekana kuzuia kirusi hiki kisitengezwe na kama tayari kimetengenezwa fanya kila uwezavyo kuhakikisha kwamba kinapatikana mahala kilipo kabla ya kuleta maangamizi makubwa.Binafsi niko tayari kukupa msaada wa namna yoyote ile utakaouhitaji muda wowote .Najua kwa sasa uko katika uchunguzi wako na mimi sihitaji kuingilia jambo unalolichunguza ila narudia tena kukuomba kwamba jambo hili ni hatari kwa nchi yako na dunia kwa ujumla kwa hiyo jitahidi kwa kila utakavyoweza kuhakikisha kwamba wale wote wenye lengo ovu hawafanikiwi lengo lao.Ninategemea kupewa tena taarifa nyingine kutoka kwa wanasayansi ambao bado wanaendelea kufanyia uchunguzi kanuni zile kwa kina zaidi na mara tu nikiipokea taarifa hiyo nitakutaarifu mara moja.”





Hivyo ndivyo ilivyosomeka barua pepe ile kutoka kwa Yash kijana anayefanya kazi katika shirika la kijasusi la Israel Mossad .Mathew akairudia tena kwa mara ya pili kuisoma barua pepe ile pamoja na viambatanisho vyake vyote kwa lengo la kuwa na uelewa mpana sana kuhusiana na kile alichokisema Yash .Alipomaliza kusoma akavua shati na kubakiwa na fulana ya ndani,alihisi joto kali



“ Anything wrong Mathew?

Sauti ya jaji Elibariki ikamstua Mathew.Kwa muda wa dakika kadhaa Elibariki alikuwa amesimama mlangoni akimtazama Mathew bila ya yeye kuwa na habari.



“ Ouh ! Elibariki.Karibu” akasema Mathew



“ Nimesimama mlangoni kwa dakika zaidi ya kumi .Akili yako yote umeihamisha katika hicho unachokisoma katika kompyuta yako. Is Eeverything ok Mathew? Akauliza jaji Elibariki.Mathew akamfanyia ishara avute kiti aketi,akamtazama kwa sekunde kadhaa na kusema

“ Eli,kila uchao jambo hili linazidi kuwa kubwa na kuchukua sura mpya.” Akasema Mathew

“ Kazi ya kwanza uliyoniomba nikufanyie ilikuwa ni kuchunguza kuhusiana na kifo cha Edson .Tumekwisha fahamu ni kwa nini Edson aliuawa lakini yameibuka mambo mengine makubwa.Katika uchunguzi huo tumefanikiwa kugundua mambo kadhaa makubwa kiasi cha kutulazimu tuendelee kuyachimba hadi mzizi wake.Tumefanikiwa kuzipata karatasi ambazo zilisababisha kifo cha Edson na wenzake na kama utakumbuka karatasi zile ziliandikwa lugha ya kisayansi kiasi kwamba sote tulishindwa kuelewa nini kilichokuwa kimeandikwa.Ilinilazimu kuomba msaada toka kwa washirika wangu .Ninaye rafiki yangu mmoja anaitwa Yash yeye anafanya kazi katika shirika la ujasusi la Isrel Mossad na ni mtaalamu sana wa masuala ya silaha za kibaolojia.Pamoja na utaalamu wake katika sayansi lakini alishindwa kutambua kilichoandikwa ikamlazimu kuwashirikisha wanasayansi wakubwa.Kwa kushirikiana na jopo la wanasayansi wakubwa wamezifanyia utafiti karatasi zile na kugundua kilichoandikwa na leo hii Yash amenitumia majibu ndiyo maana nilikuwa nimeelekeza akili yangu yote huko nikiisoma taarifa yake.” Akasema Mathewhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Wow ! That’s good news.Amegundua nini? Akauliza jaji Elibariki.Mathew akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Katika uchunguzi wao wamegundua kwamba kilichoandikwa katika karatasi zile ni kanuni za kutengeneza kirusi hatari ambacho kinaweza kusababisha maangamizi makubwa endapo kitatumika kama silaha iwapo kitatua katika mikono isiyo salama.Kwa mujibu wa Yash,kirusi hicho ni hatari mno iwapo tayari kimetengenezwa au kikitengenezwa.” Akasema Mathew

“ Ouh Mungu wangu !!!...” jaji Elibariki akastuka sana.Kikapita kimya kifupi .



“ Kwa taarifa hii ya Yash,tayari tumeanza kupata picha ni kwanini karatasi hizi zilitaka kuuzwa kwa thamani kubwa sana.Kumbuka mtu ambaye anatajwa kutaka kununua karatasi hizi alitaka kuzinunua kwa mabilioni ya fedha.Ilitia shaka kidogo kwa mtu kutaka kununua karatasi kwa fedha nyingi kiasi kile kumbe alifahamu kilichoandikwa katika karatasi hizo.” Akasema Mathew



“ mambo yanazidi kuwa makubwa.Sikutegemea kabisa kama suala hili lingekuwa kubwa kiasi hiki.Ni nani aliyetaka kununua karatasi hizo kwa fedha nyingi kiasi hicho na alitaka kuzipeleka wapi? Do you know him? Akauliza jaji Elibariki



“ Tayari tunamfahamu mtu aliyetaka kuzinunua karatasi hizo.Anaita Habib Soud ni tajiri toka nchini Saudi Arabia.Bado hatujui ni kwa nini alizihitaji karatasi zile na kwa sasa inabidi tumfanyie uchunguzi mkubwa sana huyu mtu ili tufahamu nini hasa lilikuwa lengo lake la kutaka karatasi zile .Yawezekana akawa na mafungamano na makundi ya kigaidi na yawezekana akawa alihitaji karatasi zile kwa ajili ya kutengeneza kirusi ambacho wangekitumia katika mashambulio ya kigaidi.Tutafahamu haya yote baada ya kufanya uchunguzi wa kina.Pamoja na hayo bado kuna maswali ya kujiuliza mfano Ni nani aliyeandika kanuni zile? Ni wazi hazikujiandika zenyewe lazima kuna mtu ambaye aliziandika,kama ni hivyo ni nani basi aliyeandika? Tutanatakiwa tulitafutie majibu swali hili.Pili karatasi zile zilifikaje katika ikulu yetu na kuhifadhiwa pale? Tatu ,kama nyaraka zile zilihifadhiwa ikulu basi ni lazima kuna mtu au watu waliokuwa wakifahamu mahala zilipo na katika hao wachache lazima kuna mmoja wao aliyevujisha siri na kupelekea kuibiwa. Kwa unyeti wake karatasi hizi lazima zilikuwa zikihifadhiwa sehemu ya siri sana ambako si rahisi kwa mtu kama Edson kufahamu kwa hiyo ninapata picha kwamba Edson lazima alielekezwa mahala zilipo na akaziiba.Kama ni hivyo mtu huyo ni nani? Tunatakiwa kumfahamu pia.Kingine kikubwa ambacho tunatakiwa tukifahamu ni je kirusi hicho tayari kimekwisha tengenezwa au bado? Kama tayari kimekwisha tengenezwa kiko wapi? Kama bado lazima tufute kabisa mipango yote ya kukitengeneza kwa kuwatia nguvuni wale wote wanaohusika katika suala hili.Lazima tulichimbe jambo hili hadi mzizi wake na hakuna hata mmoja ambaye anahusika na suala hilo atabaki salama.” Akasema Mathew



“ Mathew nimekosa neno la kusema lakini ni wazi nimestushwa mno na taarifa hii” akasema jaji Elibariki



“ Hii ni taarifa ambayo hata mimi imenistua mno .Wakati ninaisoma taarifa hii mwili ulikuwa unanitetemeka.Sikuamini kama jambo hili linaweza kuwa kubwa kiasi hiki.Hapa nilipo ninahis joto kali sana na ndiyo maana unaniona nimevua hadi shati.Si kwamba nimeogopa ila nimestuka tu kwani ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kupatikana hapa nchini kwetu.Pamoja na ukubwa wa jambo lenyewe lakini lazima tutalichimba hadi mzizi wake na kuhakikisha tunazizuia njama zote ovu .Tutafahamu karatasi hizi zimetoka wapi, nani kaandika na zilifikaje ikulu na nini lilikuwa lengo la Yule aliyetaka kuzinunua.” Akasema Mathew halafu akasita kidogo na kusema



“ Kuna wazo limenijia.Suala hili haliwezi kuwa na mahusiano na lile suala tunaloendelea kulichunguza kuhusiana na package ambayo Dr Joshua anataka kuiuza? Mpaka sasa hakuna yeyote ambaye anafahamu chochote kuhusiana na kilichomo ndani ya package hiyo .Dr Joshua yuko tayari kufanya chochote kile kuhakikisha kwamba mpango wake unafanikiwa na hii inaonyesha uthamani mkubwa wa package hiyo. Lakini hata hivyo ni mapema sana kusema chochote.Kila kitu kitajulikana baada ya uchunguzi.” Akasema Mathew na kuinama chini akafikiri kwa sekunde kadhaa halafu akasema



“ Katika nyakati hizi ninamkumbuka sana Noah.Alikuwa ni mtu mwenye msaada mkubwa sana kwangu na katika wakati huu angenisaidia sana.” Akasema Mathew

“ Mathew tafadhali usinikumbushe kuhusu Noah.Picha ya usiku ule bado haijafutika haijafutika kichwani kwangu.Kama si yeye tayari ningekwisha kuwa marehemu sasa lakini Noah aliyatoa maisha yake kwa ajili yangu.Nina deni kubwa sana kwake na namna pekee ya kuweza kulipa deni hilo ni kuwapata wale wote waliosababisha kifo chake.I don’t know how I’m going to do this but I promise you we’re in this together.” Akasema jaji Elibariki kwa hisia kali sana.

“ Samahani Elibariki kwa kukukumbusha kuhusu Noah.He was a good guy.Binafsi nimefanya naye kazi kwa muda mrefu and that’s why it’ll take a long time to forget him. Hata hivyo hakijaharibika kitu na tutaifanya kazi hii mpaka mwisho.Niko mimi ,Anitha pamoja na wewe.Tunaweza kuifanya kazi hii.Anitha ni mtu ambaye atatusaidia sana katika suala hili.Ni mtaalamu mkubwa sana wa teknolojia na ni mwepesi sana katika kufikiri na kuchambua mambo.Binafsi ninapokuwa naye katika kazi Fulani basi huwa sifikirii kushindwa hata kidogo katika jambo lolote na hata katika hili nina hakika tutafanikiwa tu” akasema Mathew halafu akachukua simu na kumpigia Anitha



“ Hallow Mathew ,uko wapi? Akauliza Anitha baada ya kupokea simu

“ Tayari nimerejea nyumbani.Wewe uko wapi? Akauliza Mathew



“ Niko njiani ninarejea nyumbani.Nimetoka kuonana na Peniela na tayari nimemkabidhi vile vifaa na jioni ya leo atakapokutana na Dr Kigomba tutaanza kupata kila taarifa toka kwa Dr Kigomba.” Akasema Anitha



“ Good job Anitha.Ninakusubiri hapa nyumbani.Kuna suala zito linalotukabili”



“ Kuna jambo jipya ? akauliza Anitha kwa wasi wasi kidogo

“ Si jipya sana lakini ni mwendelezo wa kile ambacho tumekuwa tunaendelea nacho” akasema Mathew

“ Sawa Mathew .Niko njiani ninakuja sasa hivi” akajibu Anitha na kukata simu







Baada ya kuachana na Anitha ,Peniela hakutaka tena kwenda sehemu yoyote ile zaidi ya nyumbani kwake.Alihisi kichwa chake kizito sana hivyo alihitaji mapumziko.Mambo mengi yalikuwa yametokea ndani ya muda mfupi.

Alifika nyumbani kwake na moja kwa moja akaelekea chumbani ,akajitupa kitandani.Kichwa kilijaa mawazo mengi sana.Picha ya kile kilichotokea chumbani kwa John bado iliendelea kuzunguka kichwani kwake na kumjaza mawazo .Sauti ya John Mwaulaya akitamka namna alivyowatoa uhai wazazi wake bado iliendelea kupenya na kusikika masikioni mwake.Machozi yakamtoka



“ Nilijitahidi nisiseme chochote kwa wakati ule kwani sikutaka watu wagundue kwamba nimeumizwa na taarifa ile lakini ukweli katika maisha yangu sijawahi kuumizwa kama nilivyoumizwa leo na taarifa ile kuhusiana na wazazi wangu.John ni binadamu mwenye roho ya kishetani kabisa.Hana hata chembe ya utu ndani yake.He killed my parents !!..Sikupata hata nafasi ya kuonja upendo wa mama yangu kipenzi.!!..akawaza Peniela na kuangua kilio .Aliumizwa mno kwa kuufahamu ukweli kuhusiana na wazazi wake.

“ Kwa mujibu wa maelezo ya John ,baba yangu alikuwa ni mtu mwenye wadhifa mkubwa serikalini na kutokana na nafasi yake kubwa aliyokuwa nayo hakutaka kuwa na kashfa yoyote ya kumpa mimba mama yangu ambaye alidhamiria kwenda kumshtaki mahakamani kwa kitendo cha kumtelekeza yeye na mtoto yaani mimi.Kwa kuogopa kashfa hiyo ,baba akaamuru John akamuue mama pamoja na mimi.The first monster was my own father.He ordered me killed.Hakuwa na huruma hata kidogo na damu yake kupotea.Natamani niione sura ya binadamu huyu ambaye hakuwa na hata chembe ya huruma kwa mtoto wake mwenyewe ambaye yeye kwake wadhifa ni muhimu zaidi kuliko hata damu yake.” Akawaza Peniela na kuendelea kulia kwa uchungu mkubwa.



“ Kwa maelekezo ya baba,John alimuua mama yangu lakini kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yake,John akaingiwa na moyo wa huruma na akaenda kinyume na amri aliyopewa akaamua kuniacha hai,akanichukua na kunihudumia akahakikisha ninapata huduma zote na ninaishi maisha mazuri.Kwa hili ninamshukuru sana kwani bila yeye nisingeweza kufika umri huu. Kwa upande Fulani sipaswi kumchukia au kumlaumu sana John kwani alikuwa anatekeleza amri aliyopewa na baba yangu.Mtu pekee ambaye ninapaswa kumchukia hapa ni baba.How could he be so cruel?? Akajiuliza Peniela na kuendelea kulia .Alihisi mwili wote kumuisha nguvu.



“ Tayari nimekwisha fahamu historia yangu na nimelia vya kutosha.Nimemwaga machozi mengi kumlilia mama yangu ambaye aliuawa kwa sababu yangu.Aliuawa akiwa katika harakati za kunitetea mimi.Ninachotakiwa kukifanya kwa sasa baada ya kuufahamu ukweli ni kumfahamu vyema mama yangu.Kuifahamu familia yake,kuwafahamu ndugu zake na kujua kama alikuwa na mtoto au watoto wengine.Pamoja na unyama na ukatili wake lakini nitahitaji pia kumfahamu baba yangu pia ili nijue alikuwa ni mtu wa namna gani,vile vile nifahamu kama nina ndugu zangu wengine.” Akawaza Peniela na kuchukua kitambaa akajifuta machozi

“Siku ile nilipoonana na John kwa mara ya kwanza alinikabidhi kasha na akaniambai kwamba kama akifariki nihakikishe ninayakamilisha makasha matatu na baada ya kukamilika yote ndipo nitakapoweza kufahamu mimi ni nani.Ninahisi historia yangu yote iko ndani ya makasha hayo.Inavyoelekea katika makasha hayo kuna mambo makubwa na ya msingi sana.Nitahakikisha ninayapata yote.” Peniela akastuliwa toka mawazoni na mlio wa simu .Ilikuwa ni simu ile ambayo huitumia kuwasiliana na Dr Joshua.Akainuka na kwenda kuichukua akabonyeza kitufe cha kupokelea.



“ Hallow” akasema Peniela.Zikapita sekunde kadhaa bila kujibiwa,Peniela akapatwa na wasi wasi



“ Hallow Dr Joshua” akasema tena .Safari hii akasikia mtu akivuta pumzi ndefu na kusema

“ Hallow Peniela ,unaendeleaje malaika wangu? Sauti ile ya Dr Joshua ikamshangaza kidogo Peniela kwani haikuwa ile ambayo amezoea kuisikia.

“ Dr Joshua are you ok? Akauliza Peniela



“ I’m ok Peniela.Hofu yangu ni kwako tu.You sound so strange today na ndiyo maana ulipopokea simu nilisita kidogo kuongea.Have you been crying? Akauliza Dr Josha



“ No Dr Joshua.Nimerudi sasa hivi nyumbani and I’m very tired.Vipi maendeleo ya Flaviana?



“ Pole sana kwa uchovu lakini sauti yako inaonyesha wazi kwamba ulikuwa unalia.Any way kuhusu Flaviana tayari amesafirishwa leo kwenda afrika ya kusini kwa matibabu zaidi na kwa taarifa nilizozipata muda si mrefu tayari wamefika salama na tayari ameanza kushughulikiwa japo bado hali yake si nzuri.Tuzidi kumuombea” akasema Dr Joshua

“ Pole sana Dr Joshua.Tuzidi kumuombea na Mungu atamponya.By the way aren’t you suppose to be there with your family right now? Akauliza Peniela

“ Ni kweli Peniela,natakiwa nikaungane na familia yangu sasa hivi lakini kilichonifanya nisiambatane nao ni kikao kikubwa cha wakuu wa nchi za afrika mashariki. Lakini usiku wa leo nitaondoka kwenda kuungana na familia yangu afrika ya kusini.Natamani sana kama ningeonana nawe kabla sijaondoka.Hiki ni kipindi kigumu sana kwangu and I think I need some comfort and the only person who can comfort me is you Peniela.” Akasema dr Joshua

“ Dr Joshua pole sana .Nafahamu ni wakati gani ulio nao sasa hivi lakini nasikitika kwamba sintaweza kuonana nawe kwa leo kabla hujaondoka.Nitaonana nawe utakaporejea toka afrika ya kusini ila naomba ufahamu kwamba niko pamoja nawe katika kipndi hiki kigunmu sana kwa familia yako” akasema Peniela

“ Sawa nimekuelewa Peniela.Nitaonana nawe baada ya kurejea .Tuzidi kumuombea Flaviana ili Mungu amjaklia nafuu ya haraka.Kabla hatujaagana una tatizo lolote? Kama kuna chochote kinachokusumbua na kukuumiza kichwa tafadhali naomba usisite kunieleza.” Akasema Dr Joshua

“ Ahsante sana kwa kunijali Dr Joshua ila kwa sasa sina tatizo lolote isipokuwa ni Yule mjomba wangu niliyekueleza hali yake imezidi kuwa mbaya na tayari nimempeleka katika ile hospitali na wamekwisha anza kumshughulikia”

“ Pole sana Peniela.Pole sana malaika wangu.Ulipaswa kunitaarifu mapema walau na mimi nifike nimjulie hali. “Akasema Dr Joshua

“ Usijali Dr Joshua,huna haja ya kupoteza muda wako kwa kwenda hospitali.Una mambo mengi yanayokukabili kama mkuu wa nchi .Msaada mkubwa ulionipatia wa hospitali unatosha sana.”

“ Ouh Peniela my queen usiseme hivyo.Kukusaidia wewe ni jukumu langu.Thamani yangu kwako hailinganishwi na chochote kile kwa hiyo ninajiona ni mwenye bahati sana kuwa ni sehemu ya msaada kwako.Hata hivyo nitawasiliana na daktari mkuu wa hospitali ile ili walipe uzito unaostahili suala la ugonjwa wa mjomba wako” akasema Dr Joshua

“ Nashukuru sana kwa kunijali Dr Joshua.Nakutakia safari njema na tafadhali unijulishe maendeleo ya Flaviana mara utakapowasili afrika ya kusini.”

“ Nitakutaarifu Flaviana .Ubaki salama na ninaomba nikukumbushe kwamba ninakupenda kuliko kitu chochote” akasema Dr Joshua na kumalizia kwa busu kisha akakata simu.Peniela akaitupa simu kitandani



‘ Hili zee halina akili nzuri hata kidogo.Laiti lingenifahamu mimi ni nani lisingethubutu kuniita mimi malaika wake.Siku inakuja na atanitambua mimi ni nani” akawaza Peniela halafu akainuka na kuelekea bafuni.

“ Imekuwa ni siku mbaya na ngumu sana kwangu.Hata hivyo namshukuru sana Mathew kwa kunisaidia kuufahamu ukweli.Bila yeye katu nisingefahamu chochote kuhusiana na wazazi twangu.Natamani hali ya John ingekuwa nzuri ili anieleze kwa kina kuhusiana na wazazi wangu.Kuna mambo mengi ambayo nahitaji kuyafahamu kutoka kwake namuomba Mungu asimchukue mapema kwani yawezekana kuna mambo mengine mengi nisiyoyafahamu kuhusu mimi” akawaza Peniela na picha ya John ikamjia

“ Pamoja na yote aliyonifanyia lakini najikuta bado nikimuonea huruma sana Yule mzee.Nadhani ni kwa sababu ya wema wake mkubwa kwangu.Toka nikiwa mdogo alihakikisha ninapata matunzo na malezi mazuri .Hakuna kitu ambacho nimewahi kupungukiwa.Ni kwa sababu yake nimesoma vizuri,nimeishi maisha mazuri.Kuwa na hasira naye kwa sasa haitanisaidia chochote.John ni mtu ambaye nimekuwa nikitamani sana kumuona toka nikiwa mdogo lakini nimepata bahati ya kukutana naye katika kipindi kama hiki akiwa mgonjwa na hajiwezi,anahitaji msaada wangu.Anyway ngoja niyaweke pembeni mambo ya John na nielekeze akili yangu katika suala kubwa lililoko mbele yangu.Jioni ya leo nina miadi na Dr Kigomba.Huyu ni mtu muhimu sana ambaye atatusaidia katika kufanikisha operesheni yetu .Ninashukuru kwa sababu tayari naye amekwisha nasa katika himaya yangu na kwa sasa nina uhakika mkubwa kwamba operesheni yetu itakwenda vizuri.Nataka tulimalize suala hili na niachane kabisa na aina hii ya maisha .Nimekuwa nikitumika kwa muda mrefu na Team SC41 kama chombo chao cha kuwatafutia taarifa na katika hilo mwili wangu umekuwa ni kama bidhaa kwa kutumiwa na wanaume ili nipate taarifa muhimu.Sitaki kuendelea na aina hii ya maisha na kitu pekee kitakachonifanya nisiendelee kuishi maisha ya namna hii ni kujiondoa kutoka team Sc41 na kuimaliza kabisa.Najua ni kazi ngumu lakini lazima nipambane hadi nihakikishe nimefanikiwa kuimaliza team Sc41.” Akawaza Peniela halafu akatoka bafuni na kupanda kitandani kujipumzisha kabla ya kuonana na Dr Kigomba jioni ya siku hiyo





********



Bado zoezi la uchunguzi wa ugonjwa unaomsumbua John Mwaulaya liliendelea.Dr Edwin na Dr Alex waliendesha uchunguzi ule wakishirikiana na madaktari bingwa wengine watatu toka katika ile hospitali.Josh na Dr Martin Desmond walikaa katika sehemu ya kupumzikia wakisubiri kupewa taarifa ya matokeo ya uchunguzi pindi utakapokamilika.

Wakiendelea na maongezi ya kawaida,mara akatokea Dr Edwin na kumuita Josh wakaenda kusimama mahala kusikokuwa na watu

“ Dr Edwin nini kinaendelea? Uchunguzi umekamilika? Akauliza Josh kwa wasi wasi.

“ Josh ni mapema mno kusema chochote kwa sasa kwani uchunguzi bado haujakamilika.Tutakapokuwa tayari tutakutaarifuni.Kwa sasa nimekuita kwa jambo moja la muhimu” akasema Edwin na kunyamaza ,akatazama huku na huko na kuhakikisha hakuna anayesikia kile wanachokiongea kisha akasema

“ Hali ya John Mwaulaya ilibadilika ghafla baada ya sisi kuondoka pale nyumbani kwake na kwa mujibu wa Martin ni kwamba kuna watu wawili walifika chumbani kwa John na kuanza kumuhoji na kumsababishia mstuko mkubwa.Je ni kweli? Akauliza Dr Edwin.Josh akainama

“ Niambie ukweli Josh kwani tayari tunafahamu kila kitu.Nataka tu unithibitishie kwamba suala hili ni la kweli.” Akasema Dr Edwin



“ Ni kweli.Kuna watu wawili walikuja kuonana naye baada ya nyie kuondoka na hapo ndipo hali ya John ilipobadilika” akajibu Josh



“ Vizuri .Unawafahamu watu hao ni akina nani? Nimeambiwa wewe ndiye uliyekuwa mlinzi wa John kwa kipindi kirefu je uliwahi kuwaona watu hawa nyumbani kwa john hata mara moja? Ni watu ambao wamekuwa wakishirikiana na John? Akauliza Dr Edwin



“ Watu wale siwafahamu vizuri ila ninamfahamu mmoja wao anaitwa Jason.Huyu niliwahi kupewa maelekezo na John ya kumfanyia mahojiano ili kufahamu mambo kadhaa kutoka kwake .Huyu mwingine aitwaye Mathew leo ndiyo nimemuona lakini wote hawa ni marafiki wa Peniela.Nadhani endapo utamuuliza Peniela anaweza akakueleza vizuri zaidi kuhusiana na huyu Mathew”

“ Ahsante Josh.Ila kwa mujibu wa Martin ni kwamba huyu Mathew aliahidi kurejea tena kwa John.Inaonekana yeye na John ni watu wanaofahamiana na nina wasi wasi lazima kuna jambo ambalo sisi hatulifahamu kuhusiana na John na Mathew.Nina wasi wasi kwamba kama mtu huyu anamfahamu sana John basi anaweza akawa anaifahamu team Sc41.Nina hitaji kumfahamu mtu huyu.Pale nyumbani kwa John kuna kamera za ulinzi naomba unipatie picha zote zilizopigwa na kamera wakati wale jamaa wakiingia.Nahitaji sana kumfahamu huyu Mathew” akasema Dr Edwin



“ Usijali Dr Edwin.Ninakwenda kushughulikia suala hilo” akajibu Josh



“ Nashukuru sana Josh” akajibu Dr Edwin na kurejea ndani.







********







Anitha alirejea nyumbani na kusalimiana na jaji Elibariki aliyekuwa amekaa sebuleni akitazama filamu.Anitha alionekana kuchoka sana.

“ Pole sana Anitha.Unaonekana umechoka sana leo” akasema jaji Elibariki

“ Ni kweli ninahisi uchovu mwingi.Nahisi nahitaji mapumziko.Mathew yuko wapi?

“ Mathew naye amejipumzisha chumbani kwake.Vipi huko utokako mambo yanakwendaje?

“ Mambo yote yamekwenda vizuri kama tulivyopanga na tayari nimempatia Peniela vile vifaa kwa hiyo tutaanza kupokea taarifa jioni ya leo pindi atakapoonana na Dr KIgomba.Kila kit………” Anitha akakatisha maongezi baada ya kusikia sauti ya Mathew



“ Hallow Anitha” akasema Mathew aliyetoka chumbani kwake alikokuwa amejipumzisha

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Ouh Mathew .Jaji kaniambia ulikuwa umejipumsisha”



“ Ndiyo .Nilikuwa nimejipumzisha kidogo.Kichwa changu kilikuwa kizito sana.Vipi huko utokako kila kitu kimekwenda vizuri?



“ Huko kila kitu kimekwenda vizuri.Tayari nimempatia Peniela vile vifaa na jioni ya leo tutaanza kupokea taarifa toka kwa Dr Kigomba.Vipi huko ulikokwenda ulifanikiwa? Uliniogopesha kidogo uliposema kuna jambo zito” akasema Anitha

“ Nilikokwenda kuna mafanikio.Elibariki alikuwa sahihi kuhusiana na asili ya Peniela.Tumefahamu kila kitu kuhusiana na Peniela.” Akasema Mathew kisha akamsimulia Anitha kila kitu kilichotokea na alichokigundua

“ Ouh Mungu wangu.Nimestushwa sana na taarifa hiyo.Huyu John mwaulaya ni shetani kabisa.Nimesikia taarifa zake za kikatili lakini sikuwahi kuhisi kama anaweza akawa mkatili kiasi hiki.Lakini mbona nilipoonana na Peniela hakuonyesha dalili zozote za kama kuna jambo zito lilimtokea.Alikuwa katika hali ya kawaida kabisa” akasema Anitha



“ Peniela is a strong woman.Hata kama kuna jambo linamsumbua huwa si rahisi kuonyesha kwa nje but I know she’s deeply hurt” akasema jaji Elibariki



“ Namuonea huruma sana Peniela” akasema Anitha

“ Anyway tuachane na masuala hayo ya peniela,kwa sasa kuna suala lingine kubwa limejitokeza.Yash amerejesha majibu ya zile karatasi “



“ Real ?!!...Amegundua nini? Akauliza Anitha

“ Anitha its something very serious” akasema Mathew na kuwafanyia ishara Elibariki na Anitha wamfuate ofisini.

“ Yash kwa kushirikiana na jopo la wanasayansi wamegundua kwamba kilichoandikwa katika karatasi zile ni kanuni za kutengeneza kirusi ambacho kinatajwa kuwa hatari sana na ambacho kinaweza kutumika kufanya maangamizi makubwa .” Akasema Mathew

“ Ouh my God !..Anitha akastuka sana.

Mathew akaendelea kumueleza kwa undani kuhusiana na kile alichokiandika Yash.

“ Sasa picha imeanza kuja” akasema Anitha baada ya Mathew kumaliza kumpa maelezo

“ Ni kweli ,lakini kuna maswali ambayo lazima tujiulize na tuyatafutie majibu.Kwanza tunatakiwa kumfahamu aliyeandika kanuni zile ni nani? Yuko wapi ? Karatasi zile zimefikaje katika ikulu yetu? Kitu kingine ambacho tunatakiwa tukitafutie majibu ni kwamba kama karatasi zile zilikuwa ikulu basi kutokana na unyeti wake ni lazima zilikuwa zimehifadhiwa mahala pa siri kubwa na ambapo si rahisi kwa mtu kama Edson kuweza kuzifikia na kuziiba.Edson alikuwa ni mfanyakazi wa kawaida katika idara ya habari ikulu na asingeweza kabisa kujua mahala nyaraka nyeti kama hizi zilikohifadhiwa kwa hiyo basi nashawishika kuamini kwamba lazima kuna watu au mtu ambaye alifanikisha kwa Edson kuweza kuzipata kirahisi.Nahisi Edson alitumiwa tu ili kuweza kuzipata kirahisi nyaraka zile.Na kama hisia zangu ni kweli basi lazima mtu huyo ndiye atakayekuwa kinara wa mpango huu wote.Kingine kikubwa ambacho tunatakiwa tukifahamu ni kama kirusi hicho kimekwisha tengenezwa ama bado na kama tayari kiko wapi? Kama bado hakijatengenezwa ni kufuta kabisa mpango wowote wa kukitengeneza kwa kuhakikisha tunalichimba jambo hili hadi mzizi wake na kuwapata wahusika.Guys we’re going into something very dangerous so we need to get prepared for this.This is a victory or death.Siwaogopeshi lakini hiyo ndiyo hali halisi na ninapenda niwe muwazi kwenu.” Akasema Mathew

“ Binafsi hufurahi sana ninapofanya kazi pamoja nawe Mathew.Una akili kubwa ya kuchambua mambo.Ni kweli tunalazimika kutafuta majibu ya maswali hayo uliyoyaorodhesha.Katika jambo ulilolisema mwishoni kuhusiana na mtu ambaye anaweza akawa nyuma ya mpango huu nakubaliana nawe kabisa.Si rahisi kwa akina Edson peke yao kulifanikisha jambo kubwa kama hili.Kufanikiwa kuiba nyaraka ikulu si jambo dogo lazima ni mpango mkubwa uliobuniwa na watu makini na ambao walifahamu mahala nyaraka hizo zilipo.”akasema Anitha



“ We need to find out who is behind this.Tukimpata huyo anaweza akatusaidia sana katika kupata majibu ya baadhi ya maswali yetu” akasema Mathew

“ Jamani kwa mtazamo wangu mimi nadhani mtu ambaye yuko nyuma ya jambo hili lazima atakuwa ndani ya ikulu.Si rahisi kwa mtu wa nje akafahamu kuhusu uwepo wa karatasi muhimu kama hizi na mahala ziliko.Nina wasi wasi sana na Dr Joshua mwenyewe au wasaidizi wake.” Akasema jaji Elibariki



“ Hapana .Sina hakika kama Dr Joshua anaweza akahusika katika jambo hili.Yule ni mtu mkubwa na hawezi kufanya jambo kubwa na la hatari na watu wadogo kama akina Edson.Nina wasi wasi na wasaidizi wake.Lakini tusiseme chochote kwa sasa hadi hapo tutakapofanya uchunguzi wa kina wa jambo hili.Nadhani sehemu nzuri ya kuanzia uchunguzi wetu ni kwa wale wazee wawili waliokuwa katika mtandao mmoja na Edson.Mzee Kitwana na mzee Matiku” Akasema Mathew



“ Lakini Mathew wazee hawa,Kitwana na Matiku wamekwisha fariki kitambo,unadhani tutafanikiwa kupata taarifa zozote za kuweza kutusaidia kupata ufumbuzi wa jambo hili kutoka kwao? Wazo langu mimi ni kwamba ,kwa kuwa tayari tunamfahamu mtu ambaye alikuwa akihitaji kuzinunua karatasi hizo ni kwa nini basi tusimfanyie uchunguzi yeye na kufahamu kwanza alikuwa akiwasiliana na akina nani hapa nchini na pia tunaweza kujua alikuwa na lengo gani na zile karatasi? Akasema Anitha



“ Anitha wazo lako ni zuri sana na hapo kabla nilijadiliana na Elibariki kuhusiana na kumfanyia uchunguzi wa kina huyu mtu anayetajwa kuzitaka karatasi hizo.Tutalifanya hilo lakini kabla ya kulifanya hilo nadhani ingekuwa vizuri kama tungewafanyia uchunguzi hawa wazee wawili tukizipitia taarifa zao za mawasiliano ya mwisho ili tuweze kuwafahamu watu ambao walikuwa wakiwasiliana nao mara kwa mara na katika hao tunaweza tukampata kinara wao.Katika hili Eva atatusaidia sana.Kama nilivyowahi kuwaambia kwamba Eva anafanya kazi katika idara ya usalama wa taifa kwa hiyo ana taarifa nyingi sana na katika hili hatashindwa kutusaidia.” Akasema Mathew



“ Are you sure she will help us? Nakumbuka mara ya mwisho alipoondoka hapa alikuwa na hasira mno na baada ya Yule msichana Sabina kufariki sina hakika kama bado atakuwa tayari kutusaidia” akasema Anitha

“ Believe me Anitha,she will help us” akasema Mathew



“ Nitakwenda kuonana naye sasa hivi.Wewe utabaki hapa ukisubiri taarifa toka kwa Peniela.Sintakawia sana.Endapo kuna jambo lolote kubwa litajitokeza utanitaarifu” akasema Mathew na kuingia chumbani kwake akajiandaa na kuondoka kuelekea kwa Eva.





Tayari kiza kimekwisha anza kutanda angani wakati Mathew alipowasili katika baa inayomilikiwa na mwanadada Eva.Alishuka garini na kuingia ndani ya baa hii maarufu sana mahala ambako vigogo wengi wa serikali na matajiri hupendelea kwenda kupumzika na kupata vinywaji.Wakati akielekea katika ofisi ya Eva iliyoko juu kabisa mwa baa hii maarufu ,mara akamuona Eva akiwa amekaa katika meza moja na baadhi ya wazee Fulani walioonekana kuwa na nyadhifa kubwa kubwa.



“ Kama kawaida yake huwa haachi kukaa na vigogo na wengi huvutiwa na uzuri na uchangamfu wake.Hii ni njia inayomsaidia sana Eva kuweza kupata kila aina ya taarifa anayoitaka” akawaza Mathew halafu akaelekea kaunta akaagiza kinywaji halafu akamuita muhudumu mmoja wa kiume aliyekuwa amevalia nadhifu ,suti nyeusi na tai nyekundu akamuelekeza aende akamuite Eva na baada ya dakika mbili Eva akatokea.Akastuka sana alipokutanisha macho na Mathew aliyekuwa akitabasamu kwa m bali.Eva akageuka na kuanza kupiga hatua akiondoka , Mathew akamfuata

“ Samahani Eva kwa kukuvamia mida hii.I need to talk to you” akasema Mathew .Eva akamtazama kwa hasira halafu akageuka na kutembea kwa kasi kuelekea ofisini kwake .Mathew akamfuata .Walipoingia katika ofisi ya Eva ,akamtazama Mathew kwa macho makali na kusema



“ Sikutegemea kabisa kama unaweza ukaleta sura yako hapa.Mathew you are a monster” akasema Eva kwa ukali

“ Calm down Eva..!!” akasema Mathew na kuzidi kumpandisha Eva hasira



“ Calm down? Do you think its easy? No ! Mathew I wont calm down.What you did to that girl is unforgivable.You killed her.You are a monster” akasema Eva huku midomo yake ikimtetemeka kwa hasira

“ Eva please listen to me.!!” Akasema Mathew kwa sauti ya upole

“ No Mathew.I don’t want to hear anything from you.Please get out of my office now !!..akasema Eva kwa ukali

“ Eva please..I need your help” akasema Mathew

“ I’m not going to help you ever again.You are a monster” akasema Eva.

“ Stop calling me a monster.!! Akasema Mathew kwa ukali kidogo



“ Iwe mwanzo na mwisho kunilaumu kwa kifo cha msichana Yule.Sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya vile nilivyofanya .Eva wewe unafahamu namna kazi zetu zilivyo.Kuna nyakati tunalazimika kufanya maamuzi magumu sana ili kupata kitu muhimu tunachokitafuta.Kwa hiyo tusiendelee kulaumiana kwa kilichotokea.Sabina alikuwa na taarifa muhimu sana ambazo ilikuwa lazima tuzipate na kwa taarifa zile tulizozipata toka kwake tumeokoa maisha ya mamilioni ya watu waliokuwa hatarini.Kwa hiyo Eva nakuomba sana usahau yale yote yaliyopita na unisaidie.Nahitaji sana msaada wako.Siku zote umekuwa ni kimbilio langu kila pale ninapokuwa na tatizo.Please Eva..” akaomba Mathew.Eva akamtazama Mathew kwa macho yake makali halafu akakaa mezani na kushusha pumzi

“ What do you need? Akauliza Eva.Mathew akavuta kiti akaketi na kumweleza kitu anachohitaji Eva amsaidie.Eva akainama akafikiri na kusema



“ Ok nitakusaidia japokuwa uliniumiza sana kwa kitendo ulichomfanyia Sabina”



“ Ahsante sana Eva” akasema Mathew halafu ukimya mfupi ukatanda



“ Nina mahusiano ya karibu na wakuu wa polisi kwa hiyo haitakuwa kazi ngumu kupata taarifa hizo unazozitaka.Mpaka kesho asubuhi nina uhakika nitakuwa nimepata kitu na nitakufahamisha” akasema Eva.

“ Eva nakushukuru sana sana kwa kukubali kunisaidia.This is very important to me” akasema Mathew na kumfanya Eva atabasamu

“ Mathew sijui unatumia dawa gani kwa sababu dakika kumi zilizopita ulikuwa ni mtu ambaye ninakuchukua kuliko wote lakini baada ya kukupa nafasi nimejikuta nikisahau yote yaliyotokea na nimekubali tena kukusaidia.Anyway tusahau yaliyopita na tuangalie yajayo.By the way unaendeleaje na chunguzi zako? Akauliza Eva.

“Eva nakushukuru sana kwa kusahau yaliyotokea na kukubali kunisaidia tena.Kuhusu chunguzi zangu zinaendelea vizuri” akasema Mathew.Eva akamtazama kidogo halafu akasema



“ Mathew unachunguza jambo gani? Can you tell me? Akauliza Eva

“ Ni mapema sana kukueleza chochote kwa sasa lakini its something very important and dangerous” akasema Mathew.Wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha Mathew akasema

“ Eva naona nisiendelee kuchukua muda wako mwingi nitawasiliana nawe kesho asubuhi ili kupata taarifa za kile ambacho utakuwa umekipata”



“ Ok Mathew nitajitahidi” akasema Eva.Mathew akaufungua mlango na kutoka akamuacha Eva bado amekaa juu ya meza akitafakari.











******





Anitha akiwa ofisini nyumbani kwa Mathew akiendelea na kazi zake,mara simu iliyokuwa mezani ikaita akaipokea



“ Hallow !..akasema Anitha



“ Hallow habari yako” ikajibu sauti ya mwanadada upande wa pili

“ Habari yangu nzuri.Naongea na nani? Akauliza Anitha



“ Naitwa Anna mtoto wa rais wa Tanzania ,napiga simu kutokea afrika ya kusini”



“ Ouh Anna.Nafurahi kukufahamu.Nikusaidie nini?

“ Nahitaji kuongea na jaji Elibariki.Aliwahi kuwasiliana na dada yangu Flaviana ambaye ni mke wake kupitia namba hii na ndiyo maana nimepiga ili niongee naye.Kama yuko karibu tafadhali naomba unipe niongee naye.It’s very important” akasema Anna



“ Ok Anna,naomba usubiri kidogo.” Akasema Anitha na kutoka mle ofisini akaelekea sebuleni alikokuwako jaji Elibariki

“ Jaji Elibariki samahani kwa kukusumbua kuna dada mmoja amepiga simu akitokea afrika ya kusini anaitwa Anna amejitambulisha kama mtoto wa rais”

Jaji Elibariki akastuka sana baada ya kusikia taarifa ile

“ Anna !!. amepataje namba za Mathew? Amejuaje kama niko hapa?



“ Relax jaji .Kumbuka ulitumia simu ile kumpigia mkeo Flaviana” akasema Anitha

“ Sawa nimekumbuka.Anasemaje Anna? Anataka nini?



“ Hajanieleza anataka nini ila bado yuko kwenye laini ya simu anakusubiri.Go talk to her” akasema Anitha.Jaji Elibariki akainuka na kwa kasi akaelekea katika ofisi ya Mathew akachukua simu



“ Hallow Anna“ akasema

“ Hallow Elibariki” akasema Anna.Jaji Elibariki akashusha pumzi na kusema

“ Anna how are you?



“ I’m ok Eli.How are you?

“ I’m fine too” akajibu Elibariki halafu kikapita kimya kifupi

“ uhhm Elibariki nafahamu utakuwa umestuka sana kwa mimi kukupigia simu mida hii hasa kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri baina yetu kwa kipindi kirefu...” akasema Anna .

“ Ni kweli Anna nimestuka kidogo kwani ni kitu ambacho sikuwahi kukitegemea.Ok !Tusahau yaliyopita.Niambie hali ya Flaviana anaendeleaje?



“ To be honest She’s not good.Tumemuhamishia huku afrika ya kusini kwa matibabu zaidi lakini bado hali yake si nzuri.Madaktari wanajitahidi kila wawezavyo kuhakikisha anakuwa salama.We need to pray for her” akasema Anna.Zikapita sekunde kadhaa za ukimya



“ Dah ! masikini Flaviana” akasema jaji Elibariki kwa sauti ndogo na kukawa kimya tena.Baada ya sekunde kadhaa za ukimya Elibariki akasema

“ Anna nakushukuru sana kwa kunipa taarifa za maendeleo ya Flaviana .Kwa hivi sasa mimi niko mafichoni na sielewi chochote kinachoendelea huko nje kwani siwezi kutoka ninasakwa kila kona.” akasema jaji Elibariki



“ Elibariki ninalifahamu hilo na ndiyo maana nimekupigia ili kukupa taarifa za mkeo.Pamoja na hayo kuna jambo ambalo nataka tuongee.Ni kuhusiana na kilichotokea usiku ule ulipokwenda kuonana na Flaviana .Kuna mambo ambayo nataka kuyafahamu kutokak wako.What real happened that night? Who shot Flaviana? Nimejiuliza maswali mengi sana kuhusiana na suala hili na kile kinachosemwa lakini inaniwia ugumu kukubaliana na kile ambacho kinasemwa na upande mmoja na nikaona ni bora endapo nitasikia na kwako ili niweze kuufahamu ukweli halisi.Elibariki siku si nyingi nimempoteza mama yangu katika mazingira ya kutatanisha.Nimebakiwa na dada yangu ambaye nampenda sana lakini kwa sasa naye anapigania maisha yake.Please Elibariki tell me the truth what real happened that night? Akasema Anna.Jaji Elibariki akavuta pumzi ndefu kisha akasema

“ Do you believe on what they say? Do you believe I shot my wife?

Anna akavuta pumzi ndefu ndefu na kusema

“ Nafahamu wewe na Flaviana ndoa yenu ilitawaliwa na migogoro mingi na ya mara kwa mara isiyokwisha lakini pamoja na hayo ,toka ndani kabisa ya moyo wangu ninaamini kwamba wewe si muuaji na hukufanya kitendo kile.lakini ni nani basi aliyefanya kitendo kile cha kikatili?”



“ Ahsante sana Anna kwa kulitambua hilo.Ahsante kwa kutoamini kile kinachosemwa juu yangu.Nitakueleza ukweli” akasema Elibariki na kukaa kimya kidogo halafu akasema

“ Anna kuna jambo zito linaloendelea hivi sasa na ili uweze kupata picha halisi nitaanzia alipofariki Dr Flora” akasema Elibariki



“ Mazingira ya kifo cha Dr Flora yalimpa shaka sana Flaviana na hasa baada ya kutolewa amri ya kutoufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora ili kubaini sababu ya kifo chake.Flaviana alikuwa mtu wa kwanza kutilia shaka jambo lile na kwa hiyo akaniita na kuniomba nimsaidie kufanya uchunguzi wa siri kubaini ukweli wa kilichosababisha kifo cha Dr Flora.Kwa mapenzi makubwa niliyonayo kwa mke wangu nilikubali kufanya kazi ile ya hatari kubwa.Ninafahamiana na watu wengi kwa hiyo walinisaidia na tukafanikiwa kuufahamu ukweli.Anna I swear in heaven and earth taarifa ile niliyoileta ilikuwa ya kweli kabisa na uchunguzi ulifanywa na madaktari bingwa wawili.Katika harakati za kuutafuta ukweli tulimpoteza daktari mkuu wa hospitali ile ya jeshi.Anna ninakueleza haya yote ili uweze kupata picha halisi ya nini kilitokea na kinaendelea.” Jaji Elibariki akanyamaza kidogo na kumeza mate kisha akaendelea

“ Anna nafahamu bado itakuwa vigumu sana kwako kuamini lakini ukweli ni kwamba Dr Flora aliuawa ,tena na watu toka ndani ya ikulu.Amri ya kutoufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora ilitolewa na Dr Kigomba ambaye ni mtu wa karibu sana na rais. Hebu jiulize kulikuwa na sababu gani ya kutoufanyia uchunguzi mwili wa mke wa rais ili kujiridhisha na kilichosababisha kifo chake? Halafu jiulize tena Dr Kigomba ambaye ni katibu wa rais alipata wapi nguvu ya kuweza kuzuia madaktari wasiufanyie uchunguzi mwili wa Dr Flora? Kwa picha ya haraka haraka unaweza kuona kwamba kuna jambo lililokuwa linafichwa.Kitu cha kushangaza zaidi ni kwamba Dr Joshua aliitupilia mbali taarifa yangu ile ya uchunguzi na kuiita ni ya kihuni na badala yake ikatolewa taarifa nyingine ikidaiwa ni ya uchunguzi uliofanywa na madaktari bingwa na mkaaminishwa kwamba ndiyo matokeo ya kweli ya uchunguzi wa kile kilichomuua Dr Flora.Kama unakumbuka baada ya kikao kile nilikasirika na kuondoka zangu.Baadae Flaviana akanipigia simu na kuniomba nirejee pale nyumbani kuna jambo anataka tuongee.Nilirejea nyumbani kuonana naye na suala alilotaka kunieleza ni kuachana na masuala yale ya kuhusu ripoti ya kifo cha Dr Flora.Alitambua kwamba nilikuwa nimekasirishwa sana na kitendo cha baba yake kuidharau taarifa yangu na kuiita ya kihuni.Alinitaka niachane na mambo hayo na maisha yaendelee kwani Dr Flora amekwisha fariki na hatarejea tena.Mimi kama jaji na ambaye siku zote kazi yangu ni kuhakikisha haki inatendeka sikukubaliana naye na hivyo tukashindwa kuelewana nikaondoka zangu.Nikiwa barabarani usiku ule baada ya kuachana na Flaviana ndipo likatokea shambulio lile ambao nilinusurika kwa namna ya ajabu kabisa” akasema jaji Elibariki akanyamaza kidogo halafu akaendelea.

“ Nikiwa mafichoni kwa kuogopa kuuawa niliwasiliana na Flaviana na kumjulisha kwamba niko salama na vile vile nilimuomba afanye kila awezalo ili aipate ripoti ile ya madaktari na aniletee.Nilimuelekeza sehemu ya kukutana na mara tu alipofika likatokea shambulio la kustukiza ambalo lilifanywa na watu ambao siwafahamu na Flaviana akajeruhiwa .Inaonekana kuna watu waliokuwa wakimfuatilia nyuma na walifahamu kabisa kwamba anakuja kuonana nami.Mlengwa katika shambulio lile nilikuwa mimi na si Flaviana ila alijeruhiwa wakati wa jitihada za kumkinga asishambuliwe .Pamoja na Flaviana kujeruhiwa lakini nilifanikiwa kuipata taarifa ya uchunguzi aliyokuwa ananiletea.Baada ya kuifanyia kazi tumegundua kwamba taarifa ile haikuwa ya kweli.Madkatari bingwa walioorodheshwa katika ripoti ile kwamba ndio walioufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora hawapo katika orodha ya madaktari bingwa kutoka hospitali kuu ya taifa na hata katika orodha ya madaktari wa hapa nchini.Kwa maana hiyo taarifa ile ambayo Dr Joshua aliwaaminisha kwamba ndiyo sahihi haikuwa ya kweli hata kidogo.Hapo unapata tena picha nyingine kwamba bado nguvu kubwa inaendelea kutumika kuhakikisha kwamba chanzo cha kifo cha Dr Flora hakijulikani.Ukweli halisi ni kwamba Dr Flora aliuawa kama nilivyowaeleza.Kwa sasa mimi na watu wangu tunaendelea kuchunguza nini sababu ya kifo chake kwa hiyo Anna huo ndio ukweli wote wa nini kilitokea. I didn’t shoot my wife” akasema jaji Elibariki.Ukimya ukatanda.Kila mmoja akasikika akivuta pumzi ndefu .Baada ya sekunde kadhaa Anna akasema



“ Elibariki nashukuru sana kwa maelezo yako and I believe you.Ahsante sana kwa kunithibitishia kwamba hisia zangu zilikuwa sahihi.Kifo cha mama hata mimi kilinipa mashaka sana namna kilivyotokea.Pole sana kwa masahibu yote yaliyokukuta.Nina hakika waliomuua mama ndio hao wanaokuwinda wakuue kwa sababu tayari unaufahamu ukweli.I wish tungekuamini toka mwanzo……” akasema anna na kudondosha machozi



“ Anna najua unaumia sana lakini huu si wakati wa kuendelea kudondosha machozi.Huu ni wakati wa kusimama imara na kupambana na wale wote walioamua Dr Flora na kumjeruhi Flaviana dada yako.Bado hatujachelewa bado nafasi tunayo.” Akasema Elibariki na kukawa kimya tena.Baada ya sekunde kadhaa Anna akasema

“ Elibariki I want to ask you one thing and please be honest with me.Tell me the truth even if its going to hurt me badly” akasema Anna



“ What do you want to know Anna?

“ Baba yangu anahusika katika jambo hili? Tafadhali niambie ukweli Elibariki”

Jaji Elibariki akabaki kimya kwa muda akitafakari

“ Elibariki are you there?



“ I’m here Anna” akajibu

“ Anna kwa kuwa umeomba nikueleze ukweli hata kama utakuumiza basi nitakueleza.Katika uchunguzi tulioufanya tumegundua kwamba baba yako anafahamu kinachoendelea kwani amekuwa sehemu ya kuhakikisha kwamba ukweli haujulikani.Ninasema bila kuogopa kwamba baba yako kuna kitu anakifahamu kuhusiana na kifo cha Dr Flora ingawa bado hatuna ushahidi wa moja kwa moja wa kumuhusisha na jambo hili lakini nakuhakikishia kwamba tutaupata” akasema Elibariki

Huku akisikika kulia kwa kwikwi Anna akasema



“ Ahsante sana Elibariki kwa kunieleza ukweli.Kwa asilimia kubwa nakubaliana na hicho ulichokisema.Hata mimi na Flaviana tumewahi kujiuliza sana kuhusu hilo na kwa sasa nimefahamu ukweli.Elibariki naomba kama kuna chochote ambacho ninaweza kukifanya ili kufanikisha kupatikana kwa ushahidi wa kumuhusisha baba na jambo hili usisite kuniambia.Niko tayari kutoa kila aina ya ushirikiano katika jambo hili”.akasema Anna

“ Anna hili si jambo rahisi hata kidogo.Ni jambo zito na la hatari.Naomba nikuweke wazi huyu ni mkuu wa nchi na kuupata ushahidi wa kuweza kumtia hatiani si kitu rahisi kukifanya.Zaidi ya yote huyu ni baba yako mzazi kwa hiyo ukiingia katika jambo hili kwanza wewe mwenyewe utajiweka katika hatari kubwa na pili damu ni nzito kuliko maji.Utaumia sana pale utakapoona baba yako mzazi akipandishwa mahakamani lakini kama umeamua kwa moyo mmoja kuitafuta haki basi ninashukuru sana.Nakuhakikishia mimi na wenzangu tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba tunapata kila aina ya ushahidi.Kuna mambo mengine mengi ambayo ningeweza kukueleza lakini sintoweza kukueleza simuni.Kama ikitokea bahati nikaonana nawe nitakueleza mambo mengi” akasema jaji Elibariki



“ Elibariki hakuna anayeweza kujua namna nilivyoumizwa kwa kifo cha mama.Pili kila ninapomuona Flaviana akipigania uhai wake ninapatwa na hasira sana na niko tayari kwa lolote lile katika kuhakikisha kwamba yeyote aliyehusika katika kusababisha kifo cha mama au katika kumshambulia dada yangu Flaviana anakamatwa.Hata kama ni baba yangu kama anahusika , niko tayari kushirikiana nanyi kuhakikisha anakamatwa na kufikishwa mbele ya haki.Kwa hili sintakuwa na huruma hata kidogo” akasema Anna



“ Ahsante sana Anna.Ahsante sana kwa kunielewa na ahsante kwa kuniahidi ushirikiano mkubwa.Naomba nikukumbushe kwamba haya ni mapambano na tunaopambana nao ni watu wenye uwezo na nguvu kwa hiyo naomba asifahamu mtu yeyote Yule kama mimi na wewe tuna mawasiliano.Kuwasiliana nami kwa sasa ni jambo la hatari kubwa kwako.Kingine ninachokiomba naomba uwe ukinipa taarifa za maendeleo ya Flaviana kwa kutumia namba hii ya simu uliyotumia leo.Nakukumbuisha tena uwe makini sana unapowasiliana name,asifahamu mtu mwingine yeyote na hata siku moja usije ukatumia simu yako ya mkononi kwani nina wasi wasi simu zenu zitakuwa zinafuatiliwa ”



“ Usijali Eli.Kuanzia sasa nitakuwa makini sana na nitachukua tahadhari kubwa kwa kila nitakachokifanya” akasema Anna halafu akasita kidogo na kusema



“ Elibariki I’m sorry for everything I did or say to you in the past.I’m real very sorry.Eli I have to go now naona kuna muuguzi ananiita.Nitakutafuta tena kesho” akasema Anna na kukata simu





Ni mlio wa simu uliomstua Peniela toka usingizini.Alikuwa amelala muda mrefu toka aliporejea kutoka hospitali.Kwa uchovu akajiinua pale kitandani akanyoosha mkono na kuchukua simu.Josh ndiye aliyekuwa akipiga

“ Hallow Josh habari ya huko? Akauliza Peniela



“ Hallow Peniela.Sauti yako inaonyesha ulikuwa umelala.Samahani sana kwa kukusumbua”



“ Bila samahani Josh.Nini kinaendelea hapo? Kuna taarifa zozote madaktari wametoa?

“ Hapana Peniela.Mpaka muda huu hawajasema chochote lakini kuna jambo nataka kukwambia”

“ Jambo gani Josh? Akauliza Peniela.



“Martin amewaeleza wale madaktari kilichotokea na kusababisha hali ya John kubadilika” akasema Josh

“ He told them?

“ Yes he did.Dr Edwin alinifuata na kunieleza kila kitu na kwa sasa wanahitaji kumfahamu Mathew ni nani na ana historia gani na John Mwaulaya.Ameagiza nimpelekee picha za kutoka katika kamera ili aweze kumuona Mathew.Nimeona nisifanye hivyo bila ya kukutaarifu kwanza wewe” akasema Josh

“ You did great Josh.Ninashukuru kwamba hukufanya hivyo alivyotaka Edwin and please don’t do it” akasema Peniela



“ Peniela who is this guy Mathew? Akauliza Josh



“ Josh you don’t need to know him for now.Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba Dr Edwin hazipati hizo picha.Nenda nyumbani sasa hivi na ufute kumbukumbu zote.Hatakiwi kabisa kumfahamu Mathew.Umenielewa Josh?

“ Nimekuelewa Peniela.Ninakwenda kufanya hivyo sasa hivi” akajibu Josh na kukata simu

Peniela aliendelea kukaa kitandani akiwa na mawazo mengi

“ Watu wale hawatakiwi kabisa kumfahamu Mathew kwani wakimjua kiundani inaweza kuwa mbaya kwa usalama wake na hivyo kupelekea hata mipango yetu isiende vizuri.I wont let that happen.Nimedhamiria kuifuta team SC41 na lazima nifanye hivyo” akawaza Peniela

“ Ouh ! Kumbe leo nina miadi na Dr Kigomba.Ngoja nijiandae kwani mida tuliyokubaliana inakaribia”

Peniela akainuka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kukutana na Dr Kigomba jioni hiyo

Hadi inagonga saa mbili kamili za usiku ,tayari Peniela alikwishamaliza maandalizi tayari kwa kukutana na Dr Kigomba



“ Now I’m ready.Ngoja nimsubiri huyu kibwengo ambaye naye kama walivyo wengine amechanganyikiwa na mimi” akawaza Peniela akiwa ameketi sofani.Usiku huu alikuwa amevaa gauni refu jeupe lenye kuonyesha dhahiri kila kitu cha ndani

“ kwa nini Dr Edwin anataka kumfahamu Mathew? Kuna kitu gani amekihis…” Peniela akastuliwa mawazoni na mlio wa kengele ya getini iliyoashiria kuna mtu

“ Nadhani atakuwa ni Dr Kigomba kwani sina miadi na mtu mwingine jioni hii” akawaza Peniela na kuinuka akatoka akaelekea getini akalifungua na kukutana na Dr Kigomba,Peniela akamfuata akamkumbatia na kumwagia mabusu mfululizo



“ Nilikuwa na wasi wasi sana pengine huwezi kuja akasema Peniela akiwa amemshika mkono Dr Kigomba akimuongoza kuingia ndani

“ Siwezi kusahau miadi hii ya muhimu.Hata kama baba yangu angefariki leo hii nisingeshindwa kuja kwako.” Akasema Dr Kigomba huku akimtazama Peniela kwa makini

“ What ! Mbona unanitazama namna hiyo? Akauliza Peniela

“ Peniela you are beautiful.Uzuri wako sijui niufananishe na nini.Ninapokuona ninakuona ni kama malaika uliyeshushwa toka juu.You are amazing.Ninakosa neno zuri la kukusifia Peniela” akasema Dr Kigomba na kumfanyia Peniela atoe tabasamu zito akamkumbatia Dr Kigomba na kumpiga mabusu mfululizo.

Dr Kigomba akashindwa kuvumilia na akajikuta maeneo yake nyeti yakichachamaa.Peniela alifanya makusudi kuupeleka mkono wake maeneo nyeti ya Dr Kigomba.Hakutaka kupoteza muda akaendelea kuyachezea na kumfanya Dr Kigomba azidi kuchanganyikiwa zaidi.Peniela akazidisha manjonjo na Dr Kigomba akashindwa kuhimili manjonjo ya Peniela wakajikuta wakijitupa katika zuria na kuanza mambo.Peniela akampeleka Dr Kigomba barabara na kumfanya aweweseke na kuongea maneno kama chizi



“ Leo utaongea mambo yote paka mkubwa we ! akawaza Peniela huku akiendelea kumpagawisha Dr Kigomba

Dakika kumi na tano za mzunguko mmoja zilimfanya Dr Kigomba abaki hoi akihema mfululizo huku jashio jingi likimtirirka



“ Peniela umeichanganya akili yangu mno.Sijawahi kuchanganywa na mwanamke kiasi hiki.Peniel……” akasema Dr igomba huku akihema kwa nguvu.Peniela akamzuia asiendelee kuongea kwa kumuwekea kidole mdomoni



“ Shhhh..!!!

“ Don’t say anything yet.I still have so much suprises for you tonight.Huu ulikuwa ni utangulizi tu” akasema Peniela akamshika mkono Dr Kigomba wakaelekea katika bafu la chumbani kwake na kuingia katika jaccuzi wakaanza kuoga huku wakipata na mvinyo.Baada ya muda Peniela akasema

“ I need some ice” akasema na kumuomba Dr Kigomba amsubiri kwa muda wakati akienda kuchukua vipande vya barafu.Alipotoka bafuni akachukua simu yake na kwa haraka akaelekea sebuleni ambako Dr Kigomba alivua nguo zake na kwa haraka akapekua katika koti la Dr Kigomba na kuipata simu yake.Haraka haraka bila ya kupoteza muda akampigia simu Anitha.Baada ya sekunde kadhaa Anitha akaipokea

“ Hallow Peniela” akasema Anitha baada ya kuipokea simu

“ Anitha tayari ninayo simu ya Dr Kigomba.Tell me what to do? Akasema Peniela

“ Ok Good.Utafuata maelekezo nitakayokupa.Tafadhali jaribu kwenda kwa haraka na kwa umakini mkubwa “ akasema Anitha.

Anitha akaanza kumpa maelekezo ya namna ya kufanya na baada ya kama dakika tatu tayari kila kitu kikakamilika



“ Sasa kila kitu tayari.Good job Peniela.Sasa rudisha kila kitu namna kilivyokuwa ili asiweze kustuka.Kwa sasa tayari tunaweza kuona kila atakachokifanya katika simu yake.Jitahidi pia umvishe na ile saa ili tumalize kila kitu” akasema Anitha



“ Sawa Anitha .Ngoja niwahi ili asije akastuka” akasema Peniela na kukata simu akaelekea jikoni akachukua vipande vya barafu na kurejea tena chumbani

“ Sorry I’m late Dr Kigomba” akasema Peniela na kuingia tena katika jaccuzi

“ welcome back my angel” akasema Dr Kigomba.Peniela akanywa funda moja la mvinyo



“ Peniela wewe ni kiumbe wa kipekee kabisa kuwahi kukutana naye.Toka nilipokutana nawe haujapita hata sekunde moja ambayo sijakuwaza.Ndani ya kipindi kifupi tu umeniingia katika kila mshipa wa mwili wangu.Peniela sijui umeniwekea nini kiasi cha kunichanganya namna hii.I want to be with you forever.I want to……”

Dr Kigomba akaongea maneno mfululizo.Peniela akamkatisha

“ Dr Kigomba bado tuna muda mwingi tutaongea mambo hayo yote lakini kwa usiku wa leo kuna jambo moja tu ambalo tunatakiwa kulifanya” akasema Peniela na kumsogelea Dr Kigomba akaanza kumchezea nyeti zake ambazo zilifura kwa hasira.Peniela hakutaka kupoteza muda akaanzisha tena mtanange mwingine humo humo ndani ya maji

Mambo ambayo Peniela alimfanyia Dr Kigomba yalimpagawisha mno.Alibaki akiweweseka na kuongea maneno yasiyoeleweka.Baada ya kumaliza mzunguko wa pili walitoka ndani ya maji na kukaa kitandani Peniela akaenda jikoni na kuleta nyama za huku na kuweka mezani wakaendelea kula huku wakinywa mvinyo.Chumba kilitawaliwa na vicheko na maongezi ya kimahaba.Mara Dr Kigomba akastuka na kusema



“ Peniela nimesahau simu yangu sebuleni .Naomba nikaichukue kwani nahisi nitakuwa nimetafutwa sana mpaka sasa” akasema Dr Kigomba

“ Relax Kigomba.Ngoja nikakuchukulie” akasema Peniela akatoka hadi sebuleni na kuzichukua nguo za Dr Kigomba na moja kwa moja Dr Kigomba akachukua simu yake .Peniela kiroho kikamdunda baada ya kuona sura ya Dr Kigomba imebadilika ghafla na kukunja ndita



“ Ouh My God ! Amegundua kama simu yake imechezewa? Akajiuliza Peniela

“ Dr Kigomba mbona umestuka ghafla? Is everything ok? Akaulizia Peniela



“ I missed an important call from Mr President.Naomba dakika mbili ni jaribu kumpigia” akasema Dr Kigomba huku akijifunga taulo na kutoka mle chumbani akaelekea sebuleni huku simu yake ikiwa sikioni akimpigia rais.

Wakati Dr Kigomba akimpigia Dr Joshua simu ,nyumbani kwa Mathew kompyuta ya Anitha ilionyesha ishara kwamba Dr Kigomba alikuwa akipiga simu.Tayari simu ya Dr Kigoba ilikwisha unganishwa katika kompyuta ya Anitha kwa hiyo kila kitu atakachokifanya katika simu yake kilionekana katika kompyuta ya Anitha .Haraka haraka akawaita Mathew na jaji Elibariki ambao walifika haraka sana ili kusikia simu nje ya kwanza kupigwa na Dr Kigomba toka walipoiunganisha simu yake.Simu iliita kwa mara ya kwanza bila kupokelewa,akapiga tena safari hii ikapokelewa.

“ Hallow Dr Kigomba” akasema Dr Joshua

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Halow Mr President .Samahani nilikuwa mbali na simu mbali pale uliponipigia”

“ Dr Kigomba hutakiwi kuacha simu.Wewe ni mtu muhimu sana unatakiwa muda wote uwe na simu.hata kama unakwenda chooni hakikisha unakwenda na simu yako.” Akasema Dr Joshua kwa sauti iliyoonyesha amri Fulani ndani yake

“ Sawa nimekuelewa mzee.” Akajibu Dr Kigomba

“ Bye the way nilikupigia kukutaarifu kwamba muda si mrefu nitaondoka kuelekea afrika ya kusini kufuatilia hali ya Flaviana.Nisipoenda familia yangu haitanielewa kabisa.Hata hivyo sintokaa sana.Kesho jioni nitarejea.Nitakaporejea sitaki kuendelea kupoteza muda nataka tumalize muda nataka tumalize biashara yetu haraka iwezekanavyo kwani tayari kumeanza kujitokeza vizingiti vingi.Kila uchao mambo mapya yamekuwa yakiibuka.Tayari tumekwisha kuwa na maadui yupo huyu Deus Mkozumi na yupo huyu shetani Elibariki.Mzee Deus yeye anafahamu kila kitu kuhusiana na kinachoendelea kwani aliambiwa na Flora na amewahi kunitolea vitisho kwamba nisiendelee na biashara hii.Tayari nimekwisha anza mpango wa kumshughulikia huyu mzee .Nategemea nitakaporejea toka afrika ya kusini nitahakikisha mzee huyu anashughulikiwa ipasavyo na kufumbwa kabisa mdomo wake.Huyu ana sumu kali sana.Kwa upande wako endelea kushughulika na suala la Elibariki.Kama taarifa zile za kwamba Elibariki alikuwa amejificha nyumbani kwa Peniela ni za kweli basi itakuwa rahisi sana kwetu kuweza kumpata kwa hiyo endelea kumchunguza Peniela.Jambo la mwisho nimeongea na Omar amedai kwamba kila kitu kipo tayari na kuanzia kesho wataanza kuingiza fedha katika akaunti.Baada ya zoezi hilo kukamilika tutawapatia mzigo wao .Kigomba gari ziko tayari zinanisubiri kunipeleka uwanja wa ndege tutaongea zaidi nikifika afrika ya kusini “



“ Sawa mheshmiwa rais .Nitayafanyia kazi hayo yote uliyoniagiza.Nakutakia safari njema” akasema Dr Kigomba na kukata simu



“ Dah sasa mambo yameiva.Tayari nimeanza kusikia harufu ya mabilioni ya fedha.Si muda mrefu sana toka sasa nitakuwa bilionea na sintaishi tena katika nchi hii .Nitakwenda kuishi mbali kabisa na hapa nikitumia mabilioni yangu” akawaza Dr Kigomba huku akitabasamu ,mara akakumbuka kitu

“ Peniela anaweza kweli kuwa na mahusiano na jaji Elibariki? Hapana .Taarifa hizo hazikuwa za kweli.Sijaona dalili zozote za kuonyesha Peniela ana mahusiano na jaji Elibariki.Lakini hata kama ningegundua ana mahusiano na Elibariki katu nisingemweleza chochote Dr Joshua .Penzi la kigoli huyu limenikolea na kuniingiza katika kila mshipa wa mwili wangu.Sielewi binti huyu anatumia uchawi au nini hadi akanichanganya kiasi hiki” akawaza Dr Kigomba na kurejea chumbani kwa Peniela

“ Sorry I’m late my queen.Nilikuwa na maongezi kidogo na mheshimiwa rais.Unajua mimi ni mtu wa karibu sana na mheshimiwa rais kwa hiyo kuna maagizo alikuwa ananipa.Usiku huu anaondoka kueleka afrika ya kusini ambako mwanae Flaviana amepelekwa kwa matibabu zaidi” akasema Dr Kigomba

“ Nilisikia kuhusu shambulio alilofanyiwa binti yake vipi anaendeleaje? Akauliza Peniela kana kwamba hafahamu chochote kilichotokea kuhusiana na Flaviana

“ Hali yake bado si nzuri hata kidogo na ndiyo maana akamuhamishia afrika ya kusini kwa matibabu zaidi”

“ Lakini ni nani aliyefanya kitendo hicho cha kikatili? Tayari amekwisha kamatwa? Akauliza Peniela



“ Taarifa za awali zinaonyesha aliyefanya kitendo hicho ni mume wake,jaji Elibariki ambaye ni jaji wa mahakama kuu”



“ Jaji Elibariki?Peniela akashangaa



“ Ndiyo.Do you know him? Akauliza Dr Kigomba

“ Ndiyo namfahamu .Ni jaji ambaye alisikiliza kesi yangu na akanitolea hukumu.NImestuka kwa sababu kwa kumtazama ni mtu mpole sana na huwezi kudhani kwamba anaweza akafanya jambo kama hilo”



“ Peniela dunia ya sasa imebadilika sana.Binadamu wa sasa ni wazuri usoni lakini moyoni ni wakatili kuzidi wanyama pori.Ni vigumu sana kuamini kama Elibariki alidhamiria kumuua mke wake wa ndoa.Kwa hivi sasa anasakwa kila mahali na atapatikana tu muda si mrefu.Anyway tuachane na hayo tusije tukauharibu usiku wetu bure.” Akasema Dr Kigomba na kumsogelea Peniela akambusu



“ I love you Peniela and tonight I have a surprise for you” akasema Dr Kigomba

“ Wow ! I like suprises.I have a surprise for you too.Kwa hiyo nani aanze ? akauliza Peniela huku akitabasamu

“ Ladies first” akasema Dr Kigomba

Peniela akaenda katika kabati lake kubwa la nguo akalifungua na kuta kiboksi kidogo kilichofungwa uzuri na kimetiwa nakshi za kupendeza.Akampatia Dr Kigomba



“ Open it ! akasema Peniela.Taratibu Dr Kigomba akaanza kukifungua kile kibokisi huku akitabasamu na ndani ya kiboksi kile akakutana na kiboksi kingine kidogo.Akakishika na kumtazama Peniela

“ Open it ! akasema Peniela.Dr Kigomba akakifungua na kupatwa na mshangao kwa alichokikuta ndani

“ wow ! akasema Dr Kigomba na kuitoa saa nzuri sana ya dhahabu akaishika mkononi ,akamtazama halafu akamkumbatia Peniela kwa nguvu

“ thank you Peniela.Thank you so much” akasema Dr Kigomba.Peniela akaichukua ile saa ,akaishika mkononi

“ Dr Kigomba from now on you’ll wear this watch.Kila utakapoitazama saa hii itakukumbusha kuhusu mimi.Sitaki unisahau hata sekunde moja.” Akasema Peniela huku akimvalisha Dr Kigomba ile saa mkononi halafu akabonyeza kidude kimoja wapo kati ya vitatu vilivyokuwapo



“ Clock starts now “ akasema Peniela .Dr kigomba ambaye alionekana kuchanganyikiwa kwa penzi alilopewa na Peniela akambusu mfululizo

“ Peniela saa hii uliyonipa hautabanduka mkononi.Nitaivaa kila siku na kila nitakapoivaa itanikumbusha sura ya malaika mwenye uzuri wa kipekee.Ahsante sana Peniela.Ninakupenda sana”

“ nafurahi kusikia hivyo Dr Kigomba.Sasa ni zamu yako.Suprise me” akasema Peniela

Dr Kigomba akamshika mkono na kumtazama usoni kwa makini halafu akasema



“ Kipindi cha pili cha uongozi wa Dr Joshua kinaelekea ukingoni na kwa mujibu wa katiba hatagombea tena .Wengi wa tuliohudumu katika kipindi chake hatutarejea tena katika ulingo wa siasa na mimi nikiwa mmoja wao.Ninataka nipumzike siasa na niishi maisha ya kawaida.Nimepanga baada ya kumaliza utumishi wangu nitaondoka hapa nchini na kwenda kuishi nje ya nchi.Nina nyumba uingereza,Norway,Canada,Marekani n.k.Ninakupa ofa ya kuchagua nchi yoyote ile ambayo ungependa kwenda kuishi na mimi nitakununulia jumba kubwa la kifahari na utaishi kama malkia” akasema Dr Kigomba

“ Wow ! Do you mean it Kigomba? Akauliza Peniela akijifanya kushangaa

“I mean it Peniela.Nakuhakikishia nchi yoyote ile unayotaka kuishi na mimi nitakununulia jumba kubwa la kifahari na nitaishi nawe.”



“ I’m hapy to hear that.What about your family?



“ Foregt about my family.Fo you I can forget everything”



“ Ouh Dr Kigomba unanisisimua sana.This is real a big surprise for me.Before I say anything about this can you give me sometime to think about it?

“ You have all the time in the world Peniela.Think about it” akasema Dr Kigomba

“ Thank you so much Dr Kigomba.I love you” akasema Peniela na kuanza kumporomoshea mabusu mfululizo na mara ikulu kukachachamaa,taratibu Peniela akalivuta taulo alilokuwa amejifunga Dr Kigomba halafu akaupeleka mdomo wake kunako ikulu na kuanza majonjo tena.Dr Kigomba alijikuta akitoa miguno na kuongea maneno yasiyoeleweka



“ Leo nimekupata kenge we.Muda si mrefu utanifahamu mimi ni nani” akawaza Peniela huku akiendelea kumpagawisha Dr Kigomba





KIla kitu walichokiongea Dr Kigomba na Dr Joshua kilisikika wazi wazi kupitia kompyuta ya Anitha iliyokuwa tayari imeunganishwa na simu ya Dr Kigomba

“ That’s why I call you a devil Anitha.Kitu ulichokifanya ni cha kipekee kabisa.Ahsante sana Anitha ,bila ya wewe haya yote yasingewezekana.” Akasema Mathew kwa furaha baada ya Dr Kigomba na Dr Joshua kumaliza maongezi na kukata simu.Jaji Elibariki naye alishindwa kujizuia akajikuta akimkumbatia Anitha



“ Hongera sana Anitha.Kitu ulichokifanya kimenishangaza .Teknolojia imekua sana siku hizi.Nilikuwa ninasikia kuhusiana na teknolojia kama hii lakini leo hii nimeshuhudia kwa macho yangu.Hongera sana” akasema

“ Ahsanteni sana ila sifa za pekee anastahili Peniela kwani bila ya yeye hakuna ambacho kingefanikiwa.Yeye ndiye aliyefanya haya yote yakawezekana .Haikuwa kazi rahisi hata kidogo kuipata simu ya Dr Kigomba na kuingiza program hii.Kuanzia sasa chochote kile ambacho atakifanya Dr Kigomba kupitia simu yake lazima tutakiona kwani program hii inaweza kurekodi kila kinachofanyika katika simu ile.Akipiga simu au kupigiwa tutasikia maongezi yote na hata kama tutakuwa mbali maongezi hayo yatarekodiwa na ukija unasikia kila kitu.Programu hii ni mpya sana na kwa mara ya kwanza imefanyiwa majaribio na shirika la ujasusi la marekani C.I.A na imeonyesha mafanikio makubwa na wameweza kuwakamata watu kadhaa waliokuwa wakishukiwa kuhusika na ugaidi.” Akasema Anitha

Wakati Anitha akiendelea kuwaelewesha akina Mathew namna mfumo ule unavyofanya kazi mara kiboksi kikatokea katika kompyuta chenye maandishi kadhaa na Anitha akatabasamu



“ Tayari Peniela amekwisha iwasha ile saa na kuanzia sasa tutafahamu kila mahala atakakokuwapo Dr Kigomba endapo atakuwa ameivaa ile saa. “ akasema Anitha na kuendelea kuwalekeza akina Mathew



“ Sasa tumewapata.Kupitia mfumo huu tutapata kila tunachokihitaji.Dr Joshua na genge lake wanaelekea mwisho wao.” Akasema Mathew



“ Katika maongezi yao,Dr Joshua anaonekana wazi hakutaka kwenda afrika ya kusini lakini anakwenda kwa ajili tu ya kuonekana na kuiridhisha familia yake.Fisadi Yule hajali mtu yeyote Yule hata wanae.Kwake yeye cha muhimu ni pesa tu.” Akasema jaji Elibariki kwa hasira

“ Pole sana jaji,najua umeumia kwa kilichompata mkeo .Tunachoweza kukifanya kwa sasa ni kumuombea Mungu amjalie nafuu ya haraka” akasema Mathew

“ Thanx” akajibu jaji Elibariki



“ Ukifuatilia maongezi ya Dr Joshua na Kigomba kuna watu wawili ambao wametajwa kama watu hatari katika kufanikisha mpango wao.Amekutaja wewe jaji pamoja na mzee Deus mkozumi.Nadhani nyote mnamfahamu huyu mzee ni rais mstaafu na ndiye aliyemuachia kiti Dr Joshua.Mpaka aingie katika orodha ya watu wanoonekana hatari kwa Dr Joshua kuufanikisha mpango wake lazima atakuwa akifahamu kuhusu anachotaka kukifanya Dr Joshua na ndiyo maana kama ukifuatilia vizuri maneno ya Dr Joshua anasema kwamba Deus aliwahi kumpigia simu na kumpa vitisho ili aachane na hicho anachotaka kukifanya .Dr Joshau anadai kwamba tayari amekwisha andaa mpango wa kumshughulikia Deus na mpango huo anategemea ukamilike mara tu atakaporejea kutoka afrika ya kusini.” Akasema Mathew na kunyamaza kidogo kisha akaendelea.



“ Kwa sasa tayari tuna mtu ambaye anaweza akatutegulia kitendawili hiki kuhusiana na hicho kitu anachotaka kukiuza Dr Joshua na washirika wake.Deus Mkozumi anaonekana kufahamu mambo mengi sana kuhusiana na jambo hili na kwa sasa ndiye hasa mtu ambaye tunamuhitaji.Swali ni je tutampata vipi? Akauliza Anitha.

“ Anitha uko sahihi kabisa.Deus Mkozumi ndiye mtu tunayemuhitaji sana kwa sasa lakini kumpata ndiyo suala gumu.Huyu ni rais mstaafu na kumfikia si jambo rahisi.Kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza akaifanya kazi hii ya kutukutanisha na Deus.Huyu ni Peniela” akasema Mathew



“ Peniela again?! Akastuka jaji Elibariki



“ Ndiyo jaji.Deus ni mtu muhimu sana kwetu na ili mpango huu ufanikiwe hatuna budi kumpata na tutafanikiwa kumpata kama tutamtumia Peniela.” Akasema Mathew



“ Hapana Mathew.Tutafute njia nyingine lakini si kwa kumtumia tena Peniela.Kwa nini kila mara tunamuweka katika hatari? Hamuoni hatari aliyonayo sasa? Imetosha jamani.Tutafute namna nyingine ya kumpata Deus bila ya kumtumia Peniela” akasema jaji Elibariki

“ Elibariki naomba unielewe tafadhali.Deus ni mtu muhimu sana katika suala hili na ni Peniela pekee anayeweza akatufikisha kwa Deus.Unajua kwa nini Team SC41 wanamtumia katika shughuli kama hizi? Its because she’s is trained for this.She’s good at this.” akasema Mathew .Jaji Elibariki akafikiri kidogo na kusema

“ Ok ! Let us use her”

“ Thank you Eli.Kwa hiyo itabidi tuongee naye kuhusu jambo hili kesho kwa sababu kwa usiku huu yuko na Dr Kigomba na hatuwezi kumkatisha kwani hata Kigomba naye ni mtu muhimu sana kwetu.Siku ya kesho tunatarajia pia kupata taarifa toka kwa Eva kuhusiana na uchunguzi niliomuomba anisaidie kuufanya kuhusu watu waliokuwa wakiwasiliana na wale wazee wawili washirika wa Edson.Lengo ni kutaka kumfahamu mtu ambaye yuko nyuma ya mpango huu wa kuziiba karatasi zile toka ikulu.Tunahitaji sana kumfahamu mtu huyo ni nani .Kwa sasa tupumzikeni ila tujiandae kwa siku ya kesho ambayo itakuwa ni siku ndefu sana.Mambo mengi yatafanyika siku ya kesho.Anitha usisahau kuendelea kumfuatilia Kigomba na kama kuna chochote utakachokipata kinachohitaji kufanyiwa kazi haraka utaniamsha mara moja” akasema Mathew na kila mmoja akaelekea chumbani kwake kupumzika







*******



Saa kubwa ya ukutani ilionyesha ni saa sita na dakika nane za usiku.Peniela alikuwa amekilaza kichwa chake kifuani kwa Dr KIgomba ambaye alikuwa amepitiwa na usingizi mzito.Alikuwa amechoka mno kutokana na mchaka mchaka aliokimbizwa na Peniela

“ Natumai ile progaramu ya Anitha ilifanya kazi.Naomba Mungu atusaidie ili mipango yetu yote iweze kwenda kama tulivyopanga il tuweze kuisambaratisha team SC41 pamoja na kuipata hiyo package.Ndiyo maana sikutaka Josh awaonyeshe wale akina Edwin picha za Mathew kwani nina hakika lengo lao ni kutaka kumfuatilia Mathew na kumfahamu ni nani na jambo hilo linaweza likarudisha nyuma sana mpango huu wa kuimaliza team SC41.Katika jambo hili Mathew ni tegemeo langu kubwa kwa hiyo nitahakikisha ninamlinda dhidi ya hatari zote za tea……” Peniela akastuliwa toka mawazoni na mlio wa simu.Akanyosha mkono akaichukua,mpigaji alikuwa ni Josh



“ Josh anataka nini usiku hu? Akauliza Peniela na kubonyeza kitufe cha kupokelea simu

“ Hallow Josh !

“Peniela,samahani kwa kukusumbua mida hii ,niko hapa hospitali” akasema Josh



“ Nini kinaendelea hapo hospitali Josh? Madaktari wamemaliza uchunguzi wao? Wametoa ripoti gani? akauliza Peniela

“ Tayari wamemaliza uchunguzi wao na wanahitaji kukuona sasa hivi”

“ Hawajakueleza chochote?



“ Hapana hawajanieleza chochote zaidi ya kuniambia kwamba wanahitaji kukuona haraka hapa hospitali.Inavyoonekana kuna jambo la haraka sana wanataka kukueleza” akasema Josh



“ Sawa Josh ninakuja .” akajibu Peniela na kukata simu



“ Ouh Mungu wangu,nini kimetokea? Is john Ok? Is he still alive? Yawezekana amekwisha fariki ila wanaogopa kuniambia.Ngoja niwahi nikajue kinachoendelea” akawaza Peniela na kumuamsha Dr Kigomba aliyekuwa amelala fofofo

“ Dr Kigomba samahani sana nimepata dharura.Nimepigiwa simu sasa hivi natakiwa hospitali.Mjomba wangu amelazwa hospitali na hali yake si nzuri.I need to go there now” akasema Peniela



“ What? .Dr Kigomba akashangaa



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog