Search This Blog

Wednesday, 29 March 2023

PENIELEA (3) - 2

 





Simulizi : Peniela (3)

Sehemu Ya Pili (2)





“ Mbona hukuniambia kama una mgonjwa hospitali Peniela?

“ Sikuwa na wasi wasi kuhusiana na hali yake kwani tayari alikuwa katika uangalizi mkubwa wa madaktari lakini inaonekana hali yake imebadilika na ndiyo maana ninahitajika nifike mara moja”

“ I’m going with you” akasema Dr Kigomba”



“ Hapana Dr Kigomba.Endelea kupumzika nitarejea muda si mrefu.Samahani sana kwa suala hili kuingilia usiku wetu huu mzuri”



“ Usijali kuhusu hilo Peniela.Una hakika kwamba utaweza kuendesha gari mwenywe hadi hospitali?



“ Ndiyo Dr Kigomba nitaweza.Wewe endelea kupumzika,nitakufahamisha kama kuna tatizo lolote.Nyumba hii ni salama na hakuna tatizo lolote kwa hiyo kuwa na amani ” akasema Peniela

“ Peniela nilikuja hapa kwa ajili yako tu kwa hiyo kwa vile imetokea dharura hii basi na mimi ngoja niende zangu nyumbani kwani siwezi kukaa hapa ndani peke yangu.Ninaomba unijulishe hali ya mgonjwa inavyoendelea pindi ukifika hospitali na kama kuna lolote ninaloweza kulifanya kusaidia tafadhai usisite kunitaarifu.Kingine lifanyie kazi lile suala nililokwambia jana usiku ” akasema Dr Kigomba huku akivaa nguo

Dr Kigmba ndiye aliyekuwa wa kwanza kuondoka zake na dakika tano baadae Peniela akafunga nyumba yake na kuondoka kuelekea hospitali

“ Kwa hali ya John ilivyokuwa nina wasi wasi sana kama atakuwa mzima.Yawezekana amekwisha fariki .Nasikitika sana kwa kukutana na John katika siku za mwisho za uhai wake.Hata hivyo ninawashukuru Mathew na Elibariki kwa kunisaidia nikaufahamu ukweli kuhusu masha yangu toka katika kinywa cha John mwenyewe.” Akawaza Peniela akiwa njiani kuelekea hospitali

Hakukuwa na magari mengi usiku huu kwa hiyo alikuwa anakwenda kwa mwendo mkali sana.

Aliwasili hospitali na mtu wa kwanza kuonana naye alikuwa ni Josh

“ Tell me Josh ,what happened? Is he ok? Akauliza

“ Peniela sifahamu chochote kinachoendelea hapa ,madaktari wametoka katika chumba na kuagiza uitwe haraka.Wako katika ofisi ya daktari mkuu wanakusubiri” akasema Josh



“ Ok Josh.Ngoja kwanza nikaonanane nao .Ulikwenda kuifanya ile kazi niliyokuagiza?



“ Ndiyo Peniela nimekwisha ifanya”

“ Good” akasema Peniela na kutembea kwa kasi kuelekea katika ofisi ya daktari mkuu.Ndani ya chumba kile kulikuwa na madaktari watano

“ Karibu sana Peniela.” akasema Daktari mkuu

“ Ahsante sana.Poleni na kazi”



“ Ahsante sana” wakajibu kwa pamoja .Peniela akavuta kiti akaketi .

“ Nimestushwa sana na mwito wenu wa dharura.Is everything ok? Akauliza Peniela kwa wasi wasi

“ Samahani sana Peniela kwa kukupa mstuko kwa kukutaka ufike hapa haraka.Tumekuita kwa dharura usiku huu ili kukueleza kile kinachoendelea na matokeo ya uchunguzi ambao tumekuwa tukiufanya toka jana jioni. Tumefanya uchunguzi wa kina kwa mgonjwa wako .Imetuchukua muda mrefu kwa sababu tulitaka tulichimbe tatizo lake kwa undani kabisa.Katika uchuguzi wetu tumegundua kwamba ndugu yako anasumbuliwa na tatizo kubwa.Anasumbuliwa na kansa ya ubongo”



“ Ouh my God !!..akasema Peniela kwa mtuko na kuweka mikono kichwani.Daktari akaendelea

“ Hali ya John si nzuri na sisi kama madaktari bingwa tunaomba tuwe wazi kwako kwamba kwa hali ya ugonjwa wake ilipofika hatuna namna yoyote tunayoweza kufanya ili kumsaidia John.Tiba pekee ambayo ingeweza kufanyika na kumsaidia John ni upasuaji lakini mpaka kwa hatua hii tumekwisha chelewa sana.Kwa ufupi ni kwamba hakuna namna tunayoweza kumsaidia John katika kuutibu ugonjwa wake na kwa hali yake ilivyo hatakuwa na muda mrefu sana wa kuishi.”

Kauli ile ikamstua mno Peniela.Alibaki kimya kwa kama dakika mbili hivi halafu akauliza



“ John amebakiwa na muda gani?

“ Ni vigumu kusema ni lini kifo chake kitatokea lakini kuanzia sasa lazima kujiandaa kwa sababu muda wowote lolote linaweza kutokea”

“ I’m so sorry Peniela.Najua unaumia sana lakini huo ndio ukweli na hakuna lugha nyingine ya kuweza kulieleza jambo hili.Hiki ni kipindi kigumu sana kwako na kwa familaia yako lakini ninakuomba uwe jasiri.Sisi hapa hospitali tutaendelea kumpatia huduma zote hadi hapo Mungu atakapomuita” akasema Daktari.Peniela akatazama chini kwa sekunde kadhaa halafu akasema



“ Daktari kwanza kabisa ninawapeni pole sana kwa kazi kubwa na ngumu mliyoifanya.Ninawashukuru vile vile kwa kuwa wakweli.Si jambo rahisi kumweleza mtu kwamba mgonjwa wake atafariki muda si mrefu.Pamoja na hayo naomba nirudie kuwauliza tena kwa mara ya pili.Ni kweli mna hakika hakuna namna yoyote ya kuweza kumtibu John?

“ Peniela sisi sote utuonao humu ni madaktari bingwa na kama kungekuwa na namna yoyote ya kuweza kumtibu ndugu yako tusingekueleza hayo tuliyokueleza.Ni kweli hakuna namna tunayoweza kufanya kumsaidia John akapona.” Akasema Daktari mkuu Peniela akainama chini



“ Peniela kuna suala lingine” akasema daktari mkuu.Peniela akainua kichwa.

“ John is awake na he wants to see you” akasema daktari na uso wa Peniela ukajikuta ukitengeneza tabasamu



“ Thank you Lord ! akasema na kufuta machozi akainuka na kuongozana na madaktari hadi katika chumba alimolazwa .Ni kweli John alikuwa ameamka na alikuwa amelala kitandani huku kitanda chake kikiwa kimezungukwa na mitambo mingi.Peniela machozi yakamtoka

“ Stop crying my queen” akasema John kwa sauti dhaifu sana.Peniela akamsogelea pale kitandani.Madaktari wakatazamana kisha wote wakatoka na kuwaacha Peniela na John pekee mle chumbani

“Stop crying Peniela.” Akasema John.Peniela akafuta machozi na kumshika mkono

“ The’ve told you already? Akauliza John

“ Tell me what?

“ Penny suala hili si la kuficha tena na ninatumai kwamba kabla ya kuja hapa tayari wamekwisha kueleza kila kitu kuhusu mimi”



“ Ndiyo wamenieleza kila kitu” akajibu Peniela huku akiendelea kudondosha machozi

“ Usilie Peniela ,huo ndio ukweli halisi.I don’t have much time to live.I’m going to die very soon” akasema John

“ Please john don’t give up.There is must be a way out”

“ Peniela lazima sote tukubaliane na ukweli kwamba hakuna namna nyingine ya kufanya ili niweze kupona.Madaktari wamekwisha thibitisha hilo kwa hiyo hakuna haja ya kuwa na matumaini yasiyokuwepo.Mimi nimelikubali hilo na ninaomba hata wewe ulikubali hilo.Ninashukuru sana kwa jitihada zako za kuhakikisha kwamba ninapona.Pamoja na hayo kuna mambo ambayo nataka kukwambia “ akanyamaza kwa sekunde kadhaa halafu akaendelea



“ kwanza kabisa nakuomba samahani sana kwa mambo yote niliyokufanyia wewe binafsi.Sioni neno zuri ambalo ninaweza kulitumia kukuomba msamaha.Nilitoa uhai wa wazazi wako na kusababisha ukakua bila ya wazazi.Hili ni jambo ambalo linaniumiza mno.Pili nilikuingiza katika team Sc41 na kuyabadili kabisa maisha yako.Peniela nash……” John akashindwa kuendelea kuongea kwani alionekana kuanza kupumua kwa shida

“ John stop.Usiseme chochote tena” akasema Peniela



“ No Peniela.Kuna mambo ambayo lazima niyaweke sawa kabla ya pumzi zangu kukatika.Nahitaji kumuona Yule kijana aliyekuja jana pale nyumbani kwangu na kunitaka nikueleze historia yako”

“ Mathew?!!! Peniela akashangaa

“ Exactly !!..Mathew.I need to see him now.Find him” akasema John

“ John!..” Peniela akataka kusema kitu lakini John akamzuia

“ Please Peniela take the phone and call him now.Tell him to come immediately.” Akasema John

Peniela hakutaka kubishana na John akatoka nje ya chumba na kuchukua simu akampigia Mathew

Si kawaida ya Mahew kulala fofofo na ndiyo maana simu yake ilipoita akaamka mara moja na kukuta ni Peniela ndiye anayepiga.Akastuka kidogo kwani hakutegemea kabisa kama angeweza kumpigia simu usiku ule.Bila kupoteza muda akaipokea

“ Hallow Peniela” akasema Mathew



“ Mathew samahani sana kwa kukusumbua mida hii.”



“ Bla samahani Peniela.Is everything ok? Are you ok? Akauliza

“ I’m ok Mathew na wala usiwe na hofu kuhusu mimi.Jambo lililonifanya nikupigie simu usiku huu ni kwamba jana ulipoondoka nyumbani kwa John mwaulaya hali yake ilibadilika sana na ikatulazimu kumkimbiza hospitali.Baada ya uchunguzi imegundulika kwamba John ana saratani ya ubongo na kwa mujibu wa madaktari hawezi kupona.Hapa ninapoongea niko hospitali .Mathew the man is dying.Kuna mambo ambayo anataka kunieleza lakini kutokana na hali yake inamuwia ugumu lakini kuna jambo ameliomba na kulisisitiza sana.He wants to see you “

Mathew akastuka

“ Unasema ?!!...

“ Najua umestuka Mathew na hata mimi nilistuka hivyo hivyo aliponieleza lakini amesisitiza kwamba anahitaji kukuona haraka usiku huu.Inaonekana kuna kitu cha muhimu sana anataka kukueleza.Naomba uje hapa hospitali Mathew” akasema Peniela .Mathew akafikri kidogo na kusema

“ Ok Peniela ninakuja sasa hivi”

Bila kupoteza muda akamuamsha Anitha na kumfahamisha kwamba anatoka kwenda hospitali







Peniela alipomaliza kuwasiliana na Mathew akarejea chumbani kwa John

“ Thank you Peniela.Come sit here” akasema John.Peniela akaenda kuketi katika kitanda .John akamtazama kwa sekunde kadhaa kisha akasema



“ Peniela kuna mambo mengi ambayo ningependa nikueleze ila kutokana na hali yangu ilivyo kuna mambo machache ambayo nitakueleza ” akanyamaza na baada ya muda akaendelea



“ Ninatamani kama ningekuwa na muda mrefu wa kuishi ili niweze kuyabadili maisha yako ambayo kwa kiasi kikuwa nimechangia mimi kuyaharibu kwa kukuingiza katika team SC41.Ninalitambua kosa langu na nina nia ya dhati ya kuyabadili maisha yako na kuyafanya bora zaidi .Kuna mambo mawili au matatu ambayo nataka uyafanye” akanyamza na baada ya muda akaendelea



“ Kitu cha kwanza kukifanya nitakapokuwa nimekufa ni kufuata maelekezo niliyokupa kuhusu kuhakikisha umeyapata yale makasha matatu.Wafuate watu niliokuelekeza na utayaunganisha makasha yote.Yakikamilika yote utafahamu mambo mengi hususan jistoria yako japokuwa tayari umeifahamu lakini bado unatakiwa kuifahau kiundani zaidi.” John akanyamaza na kufumba macho kana kwamba kuna kitu anakikumbuka halafu akafumbua macho na kusema



“ Kitu cha pili ninachotaka ukifanye ni kujitahidi kwa kila uwezavyo kuikamilisha operesheni ile inayoendelea na hakikisha kwa kila namna ile package inapatikana na ukishaipata hakikisha haitui katika mikono ya mtu yeyote Yule zaidi yako”



“ Hata team SC41? Akauliza Peniela



“ Especially team SC41” akajibu John

“ Kwani package hiyo ina kitu gani ndani yake John? Akauliza Peniela



“ Siwezi kukwambia kwa sasa lakini ina umuhimu mkubwa sana.Ukiipata keep it somewhere safe ambako haitaweza kufikiwa na mtu yeyote zaidi yako”

Kabla John hajaendelea ,simu ya Peniela ikaita alikuwa ni Mathew

“ Halow Mathew”



“ Peniela ninakaribia kufika hapo hospitali.Uko sehemu gani kwa sababu hospitali hiyo ina majengo mengi”

“ Mathew utanikuta getini ninakusubiri”akasema Peniela na kutoka mle chumbani kwenda kumsubiri Mathew.





********



Mathew aliwasili hospitali na kumkuta Peniela getini akimsubiri

“ Samahani sana Mathew kwa kukusumbua usiku huu” akasema Peniela



“ Bila samahani Peniela.John anaendeleaje?

“ Bado hali yake si nzuri japokuwa anaweza kuongea .Bado anasisitiza kutaka kukuona”



“ This is weird Peniela.Mimi na John Mwaulaya ni maadui wakubwa na yeye analifaamu hilo.Kitu gani basi anachotaka kunieleza? Akauliza Mathew



“ Sifahamu chochote Mathew.Nadhani tusiendelee kupoteza muda twende ukaonane naye kwani kadiri dakika zinavyokwenda ndivyo anavyozidi kudhoofika.Lakini kabla hatujakwenda huko kunajambo ninataka nikuweke wazi.Usijitambulishe kwa mtu yeyote Yule.Kuna madaktari wawili wa team Sc41 wako hapa na wanahitaji kukufahamu.Nimemwelekeza Josh akafute picha zako zote katika kamera za kule nyumbani kwa John.Watu hawa ni wabaya na wanaweza wakavuruga mipango yetu yote” akasema Penielahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Ahsante sana Peniela kwa kunitahadharisha mapema.Wamenifahamuje?

“ Walimuhoji Martn Yule daktari ambaye amekuwa akimuuguza John kwa muda mrefu na kutaka kufahamu sababu ya hali ya John kubadilika ghafla naye akawaambia ukweli kwamba hali yake ilibadilika kutokana na vitisho ulivyompa na ndiyo maana wakataka wakufahamu wewe ni nani kwani wana wasi wasi kwamba unaweza ukafahamu mambo mengi kuhusiana na Team SC41 kitu ambacho hawakitaki”



“ Sawa Peniela.Twende tukamuone John” akasema Mathew na Peniela akamuongoza hadi chumbani kwa John.Mara tu Mathew alipomuona John,picha ya moto mkubwa ukiiteketeza nyumba yake pamoja na familia yake ikamjia kichwani



“ I hope when you die you’ll go straight to hell you devil.” Akawaza Mathew huku akimtazama John kwa macho makali



“ John,mtu uliyekuwa unamuhitaji huyu hapa amefika” akasema Peniela.Mathew na John wakatazamana kwa sekunde kadhaa



“ Ahsante sana Mathew kwa kuja” akasema John

“ What do you want from me? Akauliza Mathew kwa sauti ya ukali.John akamtazama Peniela na kusema

“ Peniela naomba utupishe nina maongezi muhimu sana na Mathew”

Peniela akaonyesha wasi wasi Fulani na hasa baada ya kuona namna Mathew alivyokuwa amebadilika

“ Its ok Peniela.Give us a room” akasema Mathew na Peniela akatoka japo kwa shingo upande.Alitamani sana kusikia kile ambacho John na Mathew wanakiongea

“ What is he doing in there? Akauliza Josh kwa wasi wasi huku akimtazama Mathew kupitia kioo kidogo kilichokuwa mlangoni

“ Relax Josh.John mwenyewe ndiye aliyetaka kuonana naye” akasema Peniela

“ What ?! John ametaka kuonana na Mathew? Josh akashangaa



“ Ndiyo” akajibu Peniela



“ Kwa nini?

“ hata mimi sifahamu “ akajibu Peniela

“ Bado sijamsahau Yule jamaa namna alivyoingia chumbani kwa John na bila kujali hali yake ya afya akamfanyia vitisho na kupelekea hali ya John kubadilika.Sina amani kabisa nikimuona Mathew karibu na John” akasema Josh

Kupitia kioo kilichokuwa katika mlango Mathew na John mwaulaya walionekana kuongea kwa kuelewana kana kwamba ni watu wanaofahamiana sana.

“ Kwa nini John ametaka kuonana na Mathew? Kwa mujibu wa Mathew ni kwamba John akishirikiana na team SC41 waliiteketeza familia yake.Mathew bado ana hasira kubwa na John na inanishangaza sana kwa John kutaka kuonana na adui yake” akawaza Peniela halafu akageuka na kuungana na Josh kuwaangalia Mathew na John mwaulaya wakiongea

“ What are they talking about? Akajiuliza Peniela



“ Natamani nifahamu wanachokiongea.Natamani pia nipate walau dakika chache za kuongea na John mwaulaya ili anipe ufafanuzi kuhusiana na wazazi wangu.Walizikwa wapi na vile vile nataka kufahamu kama anawafahamu ndugu zangu .Kitu kingine ambacho ninataka kukifahamu ni kuhusu John mwenyewe.Katokea wapi.Familia yake iko wapi.Ndugu zake wako wapi? Nahitaji kuyafahamu haya kwa sababu John hana maisha marefu na kila mtu ananiangalia mimi wakijua ndiye ninayefahamu kila kitu kuhusu John Mwaulaya.” Akawaza Peniela

Maongezi kati ya John Mwaulaya na Mathew yalichukua zaidi ya dakika hamsini.Hakuna aliyesikia walichokiongea.Walionekana kuongea kwa kuelewana sana na kuna nyakati Mathew alionekana kuandika mambo Fulani aliyoelekezwa na John katika kijitabu kidogo

Baadae Mathew akaonekana akimshika mkono John Mwaulaya wakaagana kisha akatoka mle chumbani na kuwakuta Peniela na Josh mlangoni



“ Thank you Peniela.I have to go now” akasema Mathew na Peniela akamsindikiza

“ John anasemaje? Alikuitia nini? Akauliza Peniela



“ Nothing important.It was just a normal talk” akajibu Mathew



“ Normal talk? Peniela akashangaa



“ Ndiyo Peniela.It was just a normal talk.John alitaka tumalize tofauti zetu mimi na yeye.Thats all” akasema Mathew Peniela akasimama na kumtazama Mathew



“ Mathew hainingii akilini hata kidogo eti John akuite na atake kumaliza tofauti zenu.Alisema nikuite kwa sababu kuna jambo ambalo hakutoka mimi nilijue.Mathew me and you we’re team now so in order to win this war we have to trust each other.I told you everything I know and you must do the same.Tell me the truth” akasema Peniela .Mathew akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema

“ Ni kweli kuna mambo amenieleza ambayo hakutaka kumweleza mtu mwingine yeyote .Ni mambo mazito ambayo sintaweza kukwambia kwa sasa hadi hapo tutakapokuwa tmeipata package toka kwa Dr Joshua na kundi lake.Kwa hiyo kwa sasa inabidi tuelekeze nguvu zetu nyingi katika kuhakikisha kwamba package hiyo inapatikana.” Akasema Mathew na kumshika mkono Peniela

“ Peniela the man is dying so if there is anything that you want to know from him,this is the time” akasema Mathew

“ Ni kweli Mathew,kuna mambo mengi ambayo nahitaji kuyafahamu toka kwa John lakini kila nikimuona katika hali ile ninashindwa kumuuliza chochote najikuta nikilia.Japokuwa kuna mambo mengi ambayo amenifanyia lakini kwa hali aliyonayo sasa namuonea huruma sana” akasema Peniela



“ John hana maisha marefu.Go get what you want from him.Nitakupigia simu asubuhi “ akasema Mathew na kuingia katika gari lake akaondoka.Baada ya Mathew kuondoka,Peniela akarejea chumba cha John



“ Peniela come close “ akasema John

“ Peniela kuna mambo kadhaa ambayo nataka nikueleze lakini kubwa ni kwamba baada ya mimi kufariki Mathew ndiye atakayebaki ngao yako.Nimempa maelekezo yote na amenihakikishia kwamba atafanya yale yote niliyomuelekeza”



“ John umeongea nini na Mathew? What did you tell him? Akauliza Peniela



“ Kuna mambo ambayo nimemweleza aliyotakiwa kuyafahamu yeye pekee.Kitu kingine ni kwamba mwanzo nilikueleza kuhusu kwamba ukifanikiwa kuipata ile package uiweke mahala ambako hakuna anayeweza kuifikia lakini kwa sasa ninakuomba ukifanikiwa kuipata salama mkabidhi Mathew.Nimekwisha mpa maelekezo yote. Yeye ndiye atakaye kusaidia hata kukutoa ndani ya Team Sc41.” akasema John Mwaulaya.Peniela alisikia uchungu mwingi na kujikuta akitoa machozi

“ John you’ve been like my father so it hurt me a lot that I cant do anything to save you”

“Peniela ahsante sana kwa maneno yako mazito.Ninakupenda sana Peniela na siku zote nimekupenda kama mwananngu.Naamini toka ndani kabisa mwa moyo wako utanisamehe kwa yale yote mabaya niliyokufanya .” akasema John

“ John pamoja na yote uliyonitendea ambayo unayaita mabaya nakuhakikishia kwamba toka ndani ya moyo wangu nimekusamehe.Umenifanyia mambo mengi mazuri na siwezi kuusahau wema wako kwangu.Toka nikiwa mdogo ulihakikisha ninaishi maisha mazuri na ninapata kila ninachokihitaji..Ahsante sana John” akasema Peniela.Kikapita kimya kidogo Peniela akauliza



“ John where is your family?

John akamtazama Peniela kwa makini na kusema

“ Hakuna anayefahamu historia yangu wala aliyewahi kuniuliza chochote kuhusu historia yangu.Wewe umekuwa ni kwanza kutaka kunifahamu na kwa kuwa ninakupenda nitakeuelza ukweli kuhusu mimi.” John akanyamza halafu akaendelea.

“ I don’t have a family.I grew up without a family.Siwafahamu wazazi wangu wala ndugu zangu.Nmelelewa katika kituo cha watoto wa mitaani.Nikiwa na umri wa miaka kumi na moja niliondoka katika nyumba ya malezi na kujiunga na kundi la watoto wa mitaani na huko ndiko nilikoanza kujifunza mambo mengi mabaya.Siku moja tukiwa bondeni tukicheza kamari ghafla akatokea mzee mmoja tuliyemfahamu kama mzee Mgomba.Huyu alikuwa ni mwanajeshi na tulimuogopa sana.Wote tukatimua mbio lakini akatusihi tusikimbie kwani hakuwa na tatizo lolote na sisi.Wenzangu wote walitokomea bondeni isipokuwa mimi.Mzee Mgomba akanipa kazi ya kumtafuta mbwa wake aliyepotea.Aliahidi kunilipa fedha nyingi endapo ningefanikiwa kumpata mbwa wake.Sikuwa muoga nikamtafuta Yule mbwa na baada ya siku mbili nikafankiwa kumpata,alikuwa ameibiwa.Mzee Mgomba alifurahi sana na akanipatia shilingi laki mbili.Pamoja na fedha alizonipa lakini aliniuliza mahala nikaoishi nikamueleza historia yangu akasikitika sana akaomba nikubali kubadilika ili anisaidie.Alinipatia kazi ya kuhudumia mbwa wake wawili .Niliifanya kazi hiyo kwa ustadi mkubwa na kumfurahisha sana na akamua kunipeleka shule moja nzuri ya gharama ambako nilianza kusoma.Mzee Yule alinipenda kama mwanae” John akanyamaza kidogo ,akaendelea



“ Nilisoma kwa bidii sana na nikawa mmoja wa wanafunzi hodari kila mwaka.Nilifaulu na kuendelea na elimu ya sekondari .kidato cha nne nikafaulu pia nikaendelea na kidato cha tano na sita.Baada ya hapo nikajiunga na jeshi la wananchi na baadae nikachaguliwa kuingia katika mafunzo ya urubani wa ndege za vita.Nilipelekwa nchini Marekani kwa mafunzo zaidi na hapo ndipo nilipojiunga na Team SC41” akasema John na kuvuta pumzi ndefu kwa taabu



“ John basi imetosha.Usiongee tena” akasema Peniela

“ Peniela acha niongee.Historia yangu ni ndefu lakini mbaya sana.Imejaa mambo machafu na jambo pekee ambalo kwangu mimi ninaliona ni zuri ni kitendo cha kukataa kukutoa uhai kama nilivyoelekezwa na baba yako.Nadhani ni hicho pekee kizuri nilichokifanya katika maisha yangu lakini historia yangu imejaa uchafu wa kila namna na haifai hata kuisikiliza.Nimetoa roho za watu wengi na kwa sasa ninasikia watu niliowaua wakinililia.” Akasema John na kumshika Peniela mkono



“ Peniela wewe ndiye ndugu yangu pekee ninayekufahamu kwa sasa na hata kama nikifa ni wewe ndiye mwenye uamuzi na kila kitu kuhusiana na mazishi yangu.Narudia tena kukukumbusha kwamba baada ya mimi kufariki hakikisha unafuata maelekezo yote niliyokupa” akasema John.Peniela hakusema kitu akabaki anamtazama John kwa huzuni kubwa.Baada ya muda John akasema

“ Ninasikia sauti za watu niliowakatikli maisha yao wananililia na kuniuliza kwa nini niliwakatili haki yao ya kuishi? Katika dakika zangu za mwisho ninadiriki kusema kwamba ninahitaji msamaha wa Mungu.Japokuwa sijawahi kujiunga na dini yoyote ile lakini naamini kwamba kuna Mungu na anaweza akanisamehe.Peniela naomba unitafutie padre nahitaji kutubu makosa yangu na kumuomba Mungu msamaha.I can feel death and I can feel the fire.I can feel hell.I don’t want to go to hell.Please Peniela go now! Akasisitiza John na hali yake ikaanza kubadilika.Peniela akatoka na kwenda kuwaita madaktari ambao walifika haraka

“ Josh natakiwa kumtafuta Padre.John anahitaji padre na sijui nitampataje kwa sababu toka nilipoondoka nyumbani kwa bi Bernadetha sijwahi kushiriki ibada yoyote ile.” Akasema Peniela



“ Tutafanya nini sasa Peniela? Akauliza Josh

“ Kuna kitu nimekumbuka.Twende tukamuone mtu Fulani yeye ndiye aayeweza kutusaidia katika hili” akasema Peniela na bila kumuaga mtu yeyote wakaingia garini na kuondoka

“ John amekiona kifo chake na ndiyo maana anataka kutubu dhambi zake .Do you think God will forgive him? Akauliza Peniela

“ I don’t know Peniela” akajibu Josh.Safari ikaendelea hadi walipofika nje ya nyumba Fulani iliyokuwa na geti kubwa na walinzi wawili



“ Hapa ni wapi? akauliza Josh huku akiufungua mlango na kutaka kushuka

“ Usishuke Josh.Kuna walinzi wakali sana hapa na unaweza ukajeruhiwa” akasema Peniela na kuchukua simu akazitafuta namba Fulani akapiga.Simu ikaita bila kupokelewa,akapiga tena ikaita bila kupokelewa

“ C’mon mom pick up the phone” akasema na kupiga kwa mara ya tatu.



“ Hallow Peniela! Ikasema sauti ya upande wa pili baada ya kupokea simu.Peniela akaitambua sauti ile akatabasamu

“ mama Bernadetha shikamoo”



“ marahaba Peniela,Habari za siku nyingi? Unaendeleaje wewe mtoto? Kulikoni usiku huu? Akauliza bi Bernadetha



“ Mama nina tatizo na niko hapa nje kwako”



“ Uko hapo nje?



“ Ndiyo mama nahitaji sana msaada wako.”



“ Ok nakuja” akajibu bi Bernadetha



“ Hapa ndipo nilipolelewa “ Penielea akamwambia Josh na mara geti likafunguliwa akatokea bi Bernadetha akiwa ameongozana na walinzi wawili.Peniela akashuka garini na kwenda kukumbatiana naye halafu wakaelekea ndani.

“ Habari za siku nyingi Peniela? Pole sana kwa matatizo .Kwa nini umepata matatizo bila ya kunitaarifu” akauliza bi Bernadetha



“ Mama utanisamehe sana .Nitakuja siku nyingine na nitakueleza kila kitu lakini kwa sasa kuna jambo moja kubwa lililonileta” akasema Peniela na kumsimuliza Bernadetha kila kitu kuhusiana na John Mwaulaya.

“ Kwa hiyo mama nimekuja kuomba msaada wako.Nafahamu wewe uko karibu sana na hawa viongozi wa dini na unaweza knisaidia kumpata mmoja” akasema Peniela

Kwa msaada wa bi Bernadetha walifanikiwa kumpata padre ambaye waliongozana naye hadi hospitali.Baada ya kuwasili hospitali watu wote wakatolewa mle ndani ya chumba cha John akabaki yeye na Padre tu.

Padre alitumia zaidi ya dakika hamsini ndani ya chumba cha John.Walionekana kuongea na baadae akamuombea na kumpaka mafuta usoni baadae Padre akatoka.

“ Ndugu zangu kama nyote mnavyofahamu kwamba kutokana na ugonjwa wake ndugu yetu hatakuwa na maisha marefu sana kwa hiyo basi nimempatia huduma ya mwisho kabla ya mwenyezi Mungu kumuita.John Mwaulaya amekubali kwa hiari yake kubatizwa na amekuwa mpya tena . John ametubu dhambi zake zote na kwa mamlaka niliyopewa na kanisa nimemuondolea dhabi zake. Amepokea komunyo takatifu na Yesu yuko ndani yake.Kwa sasa hata kama akiitwa na Mungu dakika yoyote tuna hakika atakuwa sehemu salama.Kitu cha msingi ni kuzidi kumuombea ili hata atakapoondoka katika maisha haya aweze kupokelewa Mbinguni” akasema Padre na kuwabariki wote kisha Peniela akamrudisha nyumbani kwake.



Mlio wa simu ulimstua Mathew toka usingizini .Haraka haraka akaichukua simu yake na kutazama mpigaji.Alikuwa ni Eva



“ Hallow Eva? Akasema Mathew

“ Mathew habari za asubuhi? Bado umelala?

“ Ahsante sana kwa kuniamsha Eva.Nilikuwa katika usingizi mzito sana.Kuna habari gani? Akauliza Mathew

“ Mathew nimekupigia kukupa taarifa kuhusiana na ile kazi uliyoniomba nikufanyie.Kuna kitu cha ajabu ambacho kimetokea na kunishangaza sana.Hakuna taarifa zinazoonyesha mawasiliano ya simu ya wale wazee kwa muda wa miezi sita ya mwisho kabla hawajauawa.Taarifa hizo zimefutwa kabisa katika kumbu kumbu kwa hiyo ni vigumu kufahamu walikuwa wakiwasiliana na akina nani kabla hawajafariki.Hii imenishangaza sana Mathew.” Akasema Eva.Mathew akakaa kimya kidogo na kusema

“ Thank you Eva.

“Kuna chochote kingine nikusaidie? Akauliza Eva

“ No thank you Eva.Nikihitaji msaada tena nitakujulisha.Ila nashukuru sana kwa msaada huu mkubwa” akasema Mathew na kukata simu.

“ Kwa miezi sita hakuna taarifa za mawasiliano ya simu za wazee wale.Ni wazi taarifa hizi zimeondolewa makusudi kabisa na lengo hapa ni kumficha Yule mtu ambaye alikuwa nyuma yao.Watu hawa wako makini sana kwani walifahamu fika uchunguzi ungefanyika na yangefuatiliwa mawasiliano kati ya wazee wale na mtu huyo angefahamika na ndiyo maana wakawahi kufuta kabisa kumbu kumbu zote za mawasiliano .Lakini hata hivyo kuna njia nyingine ya kuweza kumfahamu mtu huyo ni nani.Ngoja turudi sasa katika lile wazo la Anitha la kumchunguza Habib ambaye anatajwa kutaka kununua karatasi zile.Nina hakika kupitia yeye basi tunaweza kugundua jambo Fulani.Nina rafiki yangu katika shirika la ujasusi la C.I.A yeye anaweza akanisaidia sana katika jambo hili kwani C.I.A wamejipenyeza karibu kila kona ya dunia na ni rahisi sana kumfuatilia mtu yeyote Yule” akawaza Mathew na kutoka mle chumbani.Tayari Anitha alikwisha amka kitambo na alikuwa jikoni akiandaa mlo wa asubuhi.Mida hiyo ilipata saa moja na dakika kumi na saba za asubuhi

“ Hallow Anitha” akasema Mathew huku akifungua kabati na kutoa chupa ya mvinyo akamimina kidogo katika glasi akagugumia yote.Anitha akamtazama na kusema

“ Is something bothering you? I know you.Ukinywa mvinyo kama hivyo lazima kuna jambo linalokusumbua.” Akasema Anitha

“ nataka kuchangamsha mwili tu ,naona umechoka sana” akajibu Mathew.Anitha akaacha shughuli aliyokuwa akiifanya akamtazama Mathew na kusema

“ Ulionana na John jana? Anaendeleaje? Alikuitia jambo gani? .

Mathew akaongeza tena mvinyo katika glasi akanywa na kusema

“ Nothing important.Hali yake si nzuri na kwa mujibu wa uchunguzi wa madaktari john anasumbuliwa na saratani ya ubongo kwa hiyo hakuna tegemeo la kupona.Aliniita na kuniomba msamaha kwa kitendo kile cha kuiteketeza familia yangu vile vile akanitaka nimlinde Peniela na kuhakikisha anakuwa salama siku zote.Thats all” akasema Mathew na kunywa funda lingine la mvinyo.

“ Anything from Kigomba? Akauliza Mathew



“ hakukuwa na simu ya maana aliyopiga tena zaidi ya kuwapigia simu waanwake wawili na akamuahidi mmoja wao kwamba anakwenda kulala kwake.Vile vile alimpiga simu mke wake na kumweleza kwamba hataweza kurejea nyumbani usiku ule kutokana na kuwa na kikao kizito.Kigomba anaonekana ni mpenda wanawake sana.”akasema Anitha



“ Usimweleze jaji Elibariki chochote kuhusiana na simu hizo za Kigomba alizowapigia wanawake wengine,si unajua anavyompenda peniela.By the way Eva amenipigia simu muda si mrefu na amenipa taarifa kuhusiana na kazi ile niliyomuomba anisaidie kuifanya.Hakuna kumbu kumbu zozote za mawasiliano za wazee wale kwa miezi sita kabla ya kufariki kwao.Zimefutwa kwa makusudi kabisa kwa ajili ya kumficha huyo ambaye walikuwa wakiwasiliana naye.Kwa sababu hiyo basi tunarejea katika lile wazo lako la kumchunguza Habib ambaye anatajwa kutaka kuzinunua karatasi zile.”akasema Mathew



“ Nina rafiki yangu mmoja anafanya kazi katika idara ya ujasusi ya marekani C.I.A.Nina hakika anaweza akatusaidia katika suala hili.” Akasema Mathew halafu akaongozana na Anitha hadi ofisini na kumpigia simu huyo rafiki yake afanyaye kazi katika shirika la ujasusi la marekani.Baada ya sekunde kadhaa mwanadada mmoja akaonekana katika luninga kubwa iliyokuwa ukutani.

“ hallow Mathew” akasema mwanadada Yule mwenye asili ya afrika



“ hallow Kerry.habari za siku ?

“ habari nzuri sana .habari za Tanzania?

“ Tanzania kwema.Samahani kwa kukusumbua Kerry,ninashida naomba unisaidie”

“ Bila samahani Mathew.Nikusaide nini?



“ Kuna mtu mmoja ambaye ninahitaji unisaie kumchunguza.Anaitwa Habib soud ni raia wa Saudi Arabia.Ninataka kufahamu kama ana mawasiliano na mtu yeyote kutoka Tanzania.Kuna jambo ninalichunguza na yeye amejitokeza katika picha .Najua ni kinyume na taratibu zenu za kazi lakini naomba unisaidie Kerry,Ni muhimu sana kwangu” akasema Mathew..Kerry akaonekana kufikiri kidogo kisha akasemahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ sawa Mathew nitakusaidia.Nisubiri dakika mbili.”akasema Kerry na kukata simu

“ Unapofanya kazi kama hizi kuna ulazima wa kuwa na marafiki wengi toka katika mashirika mbali mbali ya kijasusi na kipelelezi duniani ili unapohitaji taarifa Fulani basi inakuwa rahisi sana kuipata.Mimi nina marafiki karibu katika mashirika mengi makubwa ya ujasusi duniani.C.I.A,KGB,MOSSAD,MSS la china,BND ujerumani,MOIS Iran,na mengine mengi” Akasema Mathew na mara Kerry akarejea hewani

“ Mathew huyu Habib Soud ni mtu ambaye amekuwa katika orodha ya watu wanaochunguzwa na C.I.A kwa kufadhili vikundi vya kigaidi.Habib ana utajiri mkubwa sana na inasemakana anautumia utajiri huo katika kufadhili ugaidi.Baba yake alikuwa ni mfadhili wa siri wa Alqaeda na aliuawa na vikosi vya Marekani .” akasema Kerry na kusogeza tena taarifa nyingine katika tablet yake.



“ C.I.A tumekuwa tukimfuatilia pia mawasiliano yake .kwa upande wa Tanzania taarifa zinaonyesha kwamba amekuwa na mawasiliano ya mara na mtu mmoja anaitwa Rosemary Mkozumi.Huyu aliwahi kuwa mke wa rais wa Tanzania na ana taasisi yake inayojishughulisha na miradi mbalimbali ya kuwawezesha akina mama kiuchumi .Kupitia taasisi hii amekuwa akipata wadhili toka sehemu mbali mbali duniani na mmojawapo wa wafadhili wa taasisi hii ni Habib.Amekuwa akitoa pesa nyingi kama misaada kwa taasisi hii kwa dhumuni la kuwawezesha wanawake kiuchumi.Habib anafanya hivi ili kuificha ile dhana kwamba anafadhili makundi ya kigaidi.Mathew hizo ndizo taarifa ninazoweza kukupa kwa sasa kuhusiana na habib.Sisi bado tunaendelea kumchunguza na kama kuna lolote ambalo unaona linaweza likatusaidia katika kupata ushahidi wa kutosha kuhusu Habib kujihusisha na makundi ya ugaidi basi naomba unitaarifu mara moja na endapo utahitaji tena msaada wowote mimi niko tayari kukusaidia muda wowote.” Akasema Kerry



“ Kerry nakushukuru sana kwa msaada wako huo mkubwa.Endapo nitapata jambo lolote la kumuhusu Habib katika uchunguzi wangu nitakutaarifu mara moja” akasema mathew na kuagana na Kerry akata simu.Muda huo huo jaji Elibariki akaingia mle ofisini



“ Kuna taarifa yoyote mpya imepatikana? Akauliza jaji Elbarki

“ Ndiyo jaji.Kuna taarifa tumezipata .Kwanza ni kutoka kwa Eva.hakuweza kupata taarifa zozote za mawasiliano za mzee Mustapha na Ktwana.Inaoenaka zimefutwa kabisa kwa makusudi.Tumewasiliana na trafikiyangu mmoja aanayefanya kazi katika shirika la ujasusi la marekani na ametutaarifu kwamba mtu ambaye alitajwa kutaka kuzinunua karatasi zile zilizoibwa ikulu Habib soud amekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Rosemary Mkozumi mke wa rais mstaafu Deus Mkozumi.Amekwenda mbali zaidi na kusema kwamba Habib amekuwa akiifadhili taasisi inayoongozwa na bi Rosemary kwa kuimwagia mabilioni ya fedha .” Mathew akanyamaza kidogo kisha akaendelea

“ Jana tumemsikia Dr Joshua akimtaja adui yake namba moja katika mpango wa kuiuza package ni Deus mkozumi.Leo tena tunasikia kwamba mke wa Deus mkozumi anapokea mamilioni ya fedha toka kwa mtu anayedaiwa kuufadhili ugaidi.Hapa kuna picha inajengeka.Ninapata picha kwamba package hiyo anayotaka kuiuza Dr Joshua ilikuwepo hata wakati wa uongozi wa Deus na anaifahamu fika na ndiyo maana amekuwa kinyume na mpango wa Dr Joshua wa kutaka kuiuza.Pili nina hakika kabisa kwamba hata hizo karatasi zilizoibwa zilikuwepo ikulu wakati wa uongozi wa Deus na nina hakika kabisa kwamba Rosemary kwa kuwa naye alikuwepo ikulu wakati huo alifahamu uwepo wa karatasi hizo.Ninaweza kutamka bila wasi wasi kwamba Rosemary ndiye aliyekuwa nyuma ya mpango wa kuziuza karatasi zile.Kumbu kumbu za mawasiliano za mzee Kitwana na mzee Mustapha zimefutwa kwa sababu ya kumficha ili asijulikane kama alikuwa akiwasiliana nao.” Akasema Mathew akawaangalia akina Anitha na kusema

“ kama Habib anashukiwa kuufadhili ugaidi basi ni wazi alihitaji sana karatasi zile ili kuweza kuzitumia kanuni zilizomo ndani yake katika kutengeneza kirusi hicho hatari ili kitumike katika mashambulio ya kigaidi.Hii ni sababu pekee ambayo ilimfanya Habib kutaka kuzinunua karatasi zile kwa mabilioni ya fedha.Mnaona namna picha inavyojengeka? Akauliza Mathew



“ Nakubaliana nawe kabisa Mathew.Maelezo uliyoyatoa yanatoa taswira ya wazi ya namna Rosemary Mkozumi alivyohusika katika uibwaji wa karatasi zile ikulu.Kwa mantiki hiyo basi Rosemary naye atakuwa ni mtu wa muhimu sana kwetu .Kuna mambo mengi ambayo tutahitaji kuyafahamu kutoka kwake.” Akasema Anitha



“ Jamani kuna jambo na mimi naomba niliseme.” Akasema jaji Elibariki

“ Ninamfahamu huyu Rosemary Mkozumi .Alikuwa ni mke wa rais mstaafu Deus Mkozumi lakini baada ya Deus kumaliza awamu yake ya pili ya uongozi walitengana.Hakuna sababu iliyowekwa wazi kuhusiana na kutengena kwao.Rosemary anamiliki jumba kubwa la kifahari ufukweni mwa bahari na vile vile anamiliki pia biashara nyingine nyingi kubwa kubwa.Ni mwanamke tajiri na mpaka sasa haijawekwa wazi utajiri wake ameupataje.Ninaweza kukubaliana na maneno ya mathew kwamba Rosemary aliingiwa na tamaa ya pesa na akaamua kusuka mpango wa kuziuza karatasi zile. Edson alitumiwa tu katika kuziiba lakini maelekezo yote yalitoka kwa Rosemary.” Akasema jaji Elibariki na mara ikasikika kengele ya getini.

“ Ngoja nikaangalie nani anagonga” akasema Mathew na kutoka



“ Is Mathew ok? Akauliza jaji Elibariki baada ya Mathew kutoka.Aligundua kwamba Mathew hakuwa sawa.

“ There is must be something bothering him.Jana usiku alipigiwa simu na peniela kwamba john Mwaulaya anamuhitaji.Aliondoka na kwenda hospitali kuonana na John.Nimemuuliza ni kitu gani John alichomuitia lakini bado hajanipa jibu la kweli.Amekuwa akificha ficha.Ninamfahamu Mathew ,kuna jambo aliambiwa na John” Akasema Anitha



“ Umesema alikwenda kuonana na John mwaulaya? Jaji Elibariki akashangaa

“ ndiyo alikwenda kuonana naye jana usiku na….” kabla Anitha hajaendelea akaingia Mathew akiwa ameongozana na peniela.Jaji Elibariki na peniela walipoonana wakajikuta wakikumbatiana kwa nguvu na kupeana mabusu



“ Are you ok my love?akauliza jaji Elibariki



“ I’m ok Elibariki.What about you,are you ok?



“ I’m ok peniela” akasema jaji Elibariki .Anitha na Mathew wakatazamana wakatabasamu



“ karibu sana peniela” akasema Mathew

“ Ahsante sana Mathew.mambo yanakwendaje hapa?

“ mambo yanakwenda vizuri .Anaendeleaje John? Akauliza Mathew

“ Bado hali yake si nzuri.Jana ulipoondoka hali ilizidi kuwa mbaya akaomba tumtafutie padre.Tulifanikiwa kumpata Padre kwa usiku ule na akampatia huduma ya kiroho kumuandaa kwa lolote linaloweza kutokea.Nimeondoka kule saa kumi na moja alfajiri bado hali yake haikuwa nzuri.Nimewapigia tena simu madaktari kabla sijaja huku na wakaniambia kwamba kwa sasa hali yake imezidi kuwa mbaya .Anything can happen at anytime.” Akasema peniela na chumba kikawa kimya.Mathew akauvunja ukimya



“ Tuko pamoja Peniela katika wakati huu mgumu” jaji Elibariki na Anitha wakamuhakikishia peniela kwamba wako pamoja naye pia



“ Ahsanteni sana kwa ushirikiano wenu.Nimepita hapa ili kufahamu ni kitu gani kinachoendelea kwani toka jana hatukuwasiliana.Vipi ule mpango wetu ulifanikiwa? Akauliza Peniela



“ Ulifanya kazi kubwa sana jana na kila kitu kimeenda vizuri kama tulivyopanga Tayari tunaweza kufuatilia kila kinachofanyika katika simu ya Dr Kigomba.Mfano jana tumeweza kusikia maongezi yote aliyoongea na Dr Joshua akiwa afrika ya kusini.Vile vile tunaweza kufahamu kila mahala aliko Dr Kigomba endapo atakuwa ameivaa ile saa” akasema Anitha na kumuelekeza Peniela namna program ile inavyofanya kazi.Akayafungua maongezi ya simu kati ya Dr Kigomba na Dr Joshua na wote kwa pamoja wakayasikia.

“kumbe Yule mzee ni mtu katili sana.Amekwenda afrika ya kusni shingo upande.Kwake yeye fedha ni muhimu sana kuliko uhai wa binadamu tena mtoto wake mwenyewe” akasema peniela kwa hasira



“ kwa mujibu wa maongezi yao inaonekana wanajiandaa kuifanya biashara hii haraka iwezekanavyo.Alimuachia Dr Kigomba jukumu la kuhakiki kama fedha tayari imekwisha ingia katika akaunti zao za siri nje ya nchi na mara tu wakihakikisha kwamba fedha yote imelipwa basi wataikabidhi hiyo package.Mtu wa muhimu na wa kuchunga sana hapa ni Dr Kigomba kwani ndiye atakayefanya makabidhiano kwa niaba ya Dr Joshua Kwa vile tayari tuna uwezo wa kumfuatilia Dr Kigomba .Peniela unatakiwa ukae karibu sana na Dr Kigomba.Ongeza ukaribu pia na Kaptain Amos ambaye mko naye team SC41 na yuko timu moja na akina Kigomba .Katika team SC41 mmejipanga vipi katika kuichukua hiyo Package? Akauliza Mathew

“ Jana walikuja watu watano kutoka makao makuu ya team SC41 Marekani na dhumuni lao kubwa ni kuja kusimamia suala hilo la uchukuaji wa hiyo Package na kuondoka nayo.Leo kutakuwa na kikao cha watu wote wa team SC41 kwa ajili ya kuweka mikakati ya mwisho kuhusiana na package hiyo.Team SC41 wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanaipata package hiyo na katika operesheni hiyo wanatutegemea sana sisi wawili mimi na captain Amos.

"

“ Mpaka sasa hivi hujafanikiwa kufahamu kilichomo ndani ya hiyo Package? Akauliza Anitha



“ Hapana bado.Mpaka sasa hakuna ajuaye ndani ya hipo package kuna nini.Nmejaribu kuwadadisi wale jamaa waliotoka Marekani lakini hawako tayari kuweka wazi.”

“ Ok vizuri.Basi utaendelea kutufahamisha mipango yote ya team SC41 kuhusiana na package hiyo Kitu cha muhimu sana kuzingatia jihadhari wasije wakagundua kwamba unashirikiana nasi” akasema Mathew

“ Ninalifahamu hilo na niko makini sana katika kuhakikisha kwamba hawagundui lolote.Hata nijapo huku huwa ninatumia mbinu za hali ya juu sana. Ili nisiweze ku…..” Peniela akastushwa na mlio wa simu yake.Akaitazama ikiita akaogopa kuipokea.



“Mbona hupokei simu? Akauliza Mathew

‘ Its Josh.Yuko kule hospitali” akasema Peniela kwa wasi wasi

“ Pokea ufahamu anataka kukwambia nini.Yawezekana ana jambo la muhmu sana la kukwambia”akasema jaji Elibariki .Peniela akabonyeza kitufe cha kupokelea na kuweka simu sikioni



“ hallow Josh ” akasema.Zikapita sekunde kadhaa bila ya Josh kuongea kitu

“ Josh are you there? Akauliza peniela

“ Peniela where are you? Akauliza Josh

“ Josh kuna nini?

“ Naomba uje mara moja hapa hospitali” akasema Josh na kukata simu.Peniela akapatwa na wasiwasi mwingi



“ Is everything ok peniela? Akauliza Mathew

“ Josh ananitaka nifike haraka hospitali .Sijui kuna nini.I’m so scared.”akasema Mathew



“ Usiogope peniela .Yawezekana kuna jambo la msingi analokuitia..I’ll take you there.” Akasema Mathew



“ No thank Mathew I can manage” akasema peniela



“ Peniela uko katika mstuko na ni hatari sana kuendesha gari ukiwa katika hali hiyo.Naomba usiweke ubishi katika hilo.Nitakupeleka hospitali.Anitha endelea kumfuatilia Dr Kigomba na kama kuna jambo lolote la dharura utanitaarifu mara moja” akasema Mathew na kuingia chumbani kwake akavaa kisha akaongozana na Peniela akamuendesha kuelekea hospitali.

“ Anitha ninakubaliana nawe kwamba mathew leo hayuko sawa sawa.Kuna jambo linalomsumbua kichwa chake.” Akasema jaji Elibariki.



“ Ninavyofahamu mimi,Mathew na John Mwaulaya ni maadui wakubwa.Ni John mwaulaya aliyeiteketeza familia ya Mathew.Siku zote Mathew alikuwa akitafuta nafasi ya kulipiza kisasi kwa John Mwaulaya na ndiyo maana aliponiambia kwamba John amemuita hospitali nilistuka sana .Lakini tumuache kwanza atulie na atatueleza “akasema Anitha

Mathew na Peniela wakawasili hospitali.Safari yao haikuwa na maongezi mengi kwani Peniela alionekana kuzama katika mawazo na Mathew hakutaka kumsumbua



“ Mathew ahsante sana .Ulikuwa sahihi.Nisingeweza kuendesha gari kwa hali hii.Miguu inanitetemeka ” akasema Peniela huku akifungau mlango na kushuka wakaelekea katika jengo alikolazwa john.Mtu wa kwanza kuonana naye alikuwa ni Josh.Macho yake yalionekana kuwa mekundu .Peniela akazidi kujawa na wasi wasi.Josh alipomuona akamfuata na kumkumbatia



“ Peniela I’m sorry.He’s gone.John is gone”akasema Josh.Peniela akaishiwa nguvu na kuzirai.Haraka haraka akachukuliwa na kupelekwa kupatiwa huduma ya kwanza .Wakati Peniela akiendelea kupatiwa huduma ya kwanza simu ya Mathew ikaita.Alikuwa ni Anitha



“ hallow anitha.Nilikuwa katika harakati za kukupigia simu kukufahamisha mambo ya huku .Kuna habari gani hapo? Akaulzia Mathew

“ Dr Joshua amempigia simu Dr Kigomba muda si mrefu.Flaviana is gone.She’s dead.” Akasema peniela .Ilimchukua Mathew zaidi ya dakika moja kutamka lolote



“ How’s Elibariki?

“ ameishiwa nguvu.Nimempeleka chumbani kupumzika.”akasema Anitha



“ Ok Endelea kumpa uangalizi wa karbu sana.Huku nako mambo si mazuri.John is gone too” akasema Mathew







Kimya kikatawala halafu Mathew akasema

“ Anitha ,Jaji Elibariki na Penile ni watu wa muhimu sana .Kutokana na matatizo yaliyowakuta kwa pamoja kwa wote kuondokewa na watu wao wa muhimu inaweza kuwachukua muda ili waje kukaa sawa tena.Kutokana na suala zito linalotukabili hatuna huo muda wa kusubiri.Tunawategemea sana wao na hasa peniela kwa hiyo pamoja na uchungu walio nao lazima kila kitu kiende kama kilivyopangwa.Kwa maana hiyo jitahidi kwa kadiri uwezavyo kumtuliza jaji Elibariki ili aweze kurejea katika mstari na mimi hapa ninajitahidi nionane na peniela pindi akizinduka na niweze kumuweka sawa arejee katika mstari ili kifo cha John mwaulaya kisiathiri mipango yetu” akasema Mathew

“ Sawa nimekuelewa Mathew,lakini kwa namna Elibariki alivyostuka sina hakika kama anaweza akareja katika mstari hivi karibuni.Hata hvyo nitajitahidi kumuweka sawa.”

Wakati Mathew akionge ana Peniela ghafla kukatokea jambo Fulani lililomstua kidogo Mathew

“ Anitha nitakupigia simu baadae kidogo..” akasema Mathew na kukata simu.Macho aliyaelekeza katika kundi la watu zaidi ya kumi waliowasili pale hospitali.



“ Team SC41” akaongea mwenyewe kwa sauti ndogo.

“ Tayari wamekwisha pata taarifa za kufariki kwa kiongozi wao.hapa sintoweza tena kuipata nafasi ya kuongea na Peniela.” Akawaza Mathew na kumuona Josh amesimama mlangoni akamuita kwa ishara.

“ hallow Mathew” akasema Josh

“ Nikumbushe jna lako” Akauliza Mathew



“ naitwa josh”

“ Ok Josh.Ninahitaji sana kuongea na Peniela kuna jambo la muhimu nataka kumwambia lakini kutokana na mkanganyiko uliopo sintoweza kuonana naye kwa sasa .Ninakuachia maagizo pindi akizinduka mwambie kabla ya kufanya jambo lolote awasiliane kwanza na mimi” akasema Mathew



“ Sawa Mathew nitamweleza” akasema Josh na Mathew akaondoka zake.Gari alilolitumia kuja hospitali lilikuwa la peniela kwa hiyo ikamlazimu kuchukua taksi kurejea nyumbani.Wakati akielekea katika kituo cha taksi akachukua simu na kumpigia Eva

“ hallow Mathew” akasema Eva



“ Eva Uko wapi mida hii?



“ Kwa sasa ninajianda kutoka nyumbani kuelekea mizungukoni.Unahitaji kuniona?



“ Ndiyo Eva,.Nina shida nahitaji kukuona kama hutajali”

“ sawa Mathew.basi nenda kanisubiri pale ofisini kwangu,nakuja tuonane hapo.” Akasema Eva.mathew akakodisha taksi iliyompeleka hadi katika baa ya Eva ambako aliagiza supu ya kuku na kuanza kunywa akimsubiri Eva

“ Ninashindwa kupata jibu kwa nini mtu kama Rosemary Mkozumi ajihusishe katika jambo la hatari kama lile la kumuuzia nyaraka nyeti mtu ambaye ana mafungamano na vikundi vya ugaidi.? Je haelewi kilichomo ndani ya karatasi zile au ni tamaa tu ya fedha? Nitakula naye sahani moja lazima nihakikishe nimemtia mikononi na kuufahamu ukweli na atanieleza ukweli kwa nini anataka kufanya jambo la hatari kama lile.Ninaanza kupatwa na hisia kwamba yawezekana hata huyu mama naye akawa na mafungamano na vikundi vya ugaidi.Nitahakikisha nimeuchimba mtandao wake wote na hakuna atakayesalimika” akawaza Mathew na mara mawazo yake yakakatishwa baada ya kuliona gari la Eva

Eva mwandada mwenye nywele ndefu nyeusi zenye kung’aa akashuka toka ndani ya gari lake na kuanza kutembea kwa mwendo wake wa madaha kuelekea ofisini kwake.Mathew akainuka na kumfuata



“ karibu sana Mathew” Eva akamkaribisha Mathew ofisini kwake



“ Ahsante sana Eva”

“ sikuwa na ratiba ya kuja hapa asubuhi hii lakini imenilazimu kuja kwa ajili yako.Una tatizo gani Mathew?

“ Eva ahsante sana kwa kuahirisha shughuli zako na kuja kunisikia shida yangu.Nimekuja kuomba msaada wako tena.Kuna mtu ninahitaji kumpata ili nimuhoji anaitwa Rosemary Mkozumi”

Eva akastuka na kumtazama kwa sekunde kadhaa akasema



“ Rosemary mkozumi? Akauliza Eva kwa mshangao kidogo



“ Ndiyo”akajibu Mathw .Eva akashusha pumzi

“ Amefanya nini Rosemary?



“ Amejitokeza katikati ya jambo ninalolichunguza kwa hiyo basi ninahitaji kumfanyia uchunguzi naye pia.Kuna mambo ninayohuitaji kuyafahamukutoka kwake na kubwa ni kwamba ninataka kupata kumbu kumbu za mawasiliano kati yake na mtu mmoja raia wa Saudi Arabia anaitwa Habib soud”

Eva akamtazama Mathew kwa sekunde kadhaa na kusema



“ Mathew you are playing with fire my friend.Kwa sisi tunaomfahamu Rosemary Mkozumi tunaelewa kwamba huyu ni mwanamke hatari sana.Huyu aliwahi kuwa make wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania .Huyu ni mwanamke mwenye sura mbili.Katika jamii anafahamika sana kama mtetezi hodari wa haki za wanawake na amekwisha pewa tuzo nyingi kutokana na kuwa na mchango mkubwa katika kuchochea maendeleo ya wanawake nchini.Hii ni taswira nzuri sana aliyojijengea katika jamii.Upande wa pili wa Rosemary ambao wengi hawaufahamu ,ni mwanamke katili na hatari.Ana mtandao wake mkuwa wa watu hatari ambao wako tayari kufanya jambo lolote lile la hatari muda wowote.kwa sasa ninasikia tetesi kwamba ana mpango wa kutaka kugombea urais baada ya Dr Joshua kumaliza muda wake na kutokana na mtandao mkubwa alio nao kuna uhakika mkubwa akaweza kushinda uchaguzi.” Eva akanyamaza na kuendelea

“ Rosemary anatajwa kuwa na utajiri mkubwa sana na anatajwa kama mmoja wa watu matajiri wakubwa sana hapa nchini.Ninamfahamu vizuri mama huyu na ndiyo maana uliponiambia kwamba unataka kumchunguza nilistuka sana.She’s powerfull and very dangerous woman na kama unataka kumchunguza basi inakubidi ujiandae sana kwa lolote”akasema Eva

“ Eva ahsante sana kwa kunitahadharisha mapema kuhusiana na Rosemary na hata hivyo nilikwisha jiandaa toka awali kukabiliana naye kwa hiyo usihofu”akasema Mathew.Eva akabaki anamtazama bila kusema chochote



“ Eva are you going to help me or not?akauliza Mathew



“ Mathew sina sababu ya kukataa kukusaidia lakini ninajaribu kutafakari ombi lako ninashindwa kupata jawabu nitawezaje kufanya kazi hiyo.Rosemay kama nilivyosema ni mtu mwenye mtandao mkuwa na hata ndani ya idara ya usalama wa taifa ana watu wake wanaomsaidia katika mambo yake na ndiyo maana huwa ni vigumu sana kumchunguza huyu mama.” Akasema Eva



“ Ok sawa nimekuelewa Eva.basi nitakuomba kitu kimoja.Nisaidie niweze kuingia ndani ya nyumba yake ili nikafanye uchunguzi mimi mwenyewe.Kazi yako ni kunifanyia uchunguzi ni namna gani nitakavyoweza kuingia ndani ya nyumba ya Rosemary.” Akasema Mathew.Eva bado aliendelea kumtazama Mathew kwa makini



“Are you sure you want to do this Mathew” akauliza Eva



“ Eva katika dunia hii ninayemuogopa ni Mungu peke yake .Please find out how I will get in there “akasema Mathew

“ok Mathew nitajitahidi”akasema Eva



“ Ahsante sana Eva,nakutegemea sana” akasema Mathew na kuagana na Eva akaondoka







********



Baada ya kuondoka ofisini kwa Eva,Mathew akarejea nyumbani kwake



“ Elibariki yuko wapi? Akamuuliza Anitha



“ Yuko chumbani .” akajibu Anitha.Moja kwa moja Mathew akaelekea chumbani kwa jaji Elibariki akagoga mlango na sauti ya Elibariki toka ndani ikamruhusu aingie ndani.Jaji Elibariki alikuwa amekaa kitandani ,alionekana kuzama katika mawazo mengi sana.

“ Pole sana Elibariki.Jambo hili ni zito na limetustua sote”akasema Mathew



“ Ahsante sana Mathew” akajibu jaji Elibariki na kukaa kimya kidogo halafu akasema

" Mimi na Flaviana ndoa yetu ilikuwa na misuko suko mingi sana na kuna nyakati niliamini kwamba hakuwa mwanamke ambaye Mungi alonipangia niwe naye.Nilivumilia misukosuko yote kwa sababu nilikuwa nampenda sana.Nimeumizwa sana na kifo chake.Mathew siwezi kuongea sana lakini ninataka nikuombe jambo moja kwamba fanya kila uwezavyo na uhakikishe kwamba yeyote aliyehusika katika tukio hili anapatikana na analipa uovu wake.Can you promise me that? Akauliza jaji Elibariki

“ yes Elibariki.I promise you .Yeyote ambaye ana mkono wake katika kusababsha kifo cha Flaviana hatasalimika.Nitafanya kazi usiku na mchana na nitahakikisha wote wanatiwa nguvuni na kukutana na mkono wa sheria.kazi hii si rahisi na ninahitaji sana msaada wa watu wanaonizunguka.Anitha,wewe na Peniela ndiyo watu wangu wa karibu .Sote tumeumizwa sana na tukio hili lakini pamoja na uchungu wote tulio nao we have to focus what is ahead us.Mbele yetu kuna suala kubwa na zito.Tunatakiwa tuipate package muhimu sana na vile vile kuwatafuta na kuwapata wote waliosababisha kifo cha Flaviana ,kwa hiyo basi nitakuomba usimame imara na tupambane sote kwa pamoja” akasema Mathew



“ Mathew I’m deeply hurt .Siwezi kuelezea ni kwa kiasi gani nimeumizwa na jambo hili.Kibaya zaidi nikwamba siwezi hata kwenda kumuaga mke wangu katika safari yake ya mwisho.Siwezi kuhudhuria mazishi yake.Hii inaniumiza sana Mathew.Ninachoomba mniache kwa kwanza hadi hapo akili yangu itakapotulia lakini kwa sasa siwezi kufanya jambo lolote” akasema jaji Elibariki



“ Elibariki I know you are deeply hurt so do we all.Flaviana is gone and we need to pay back what they did to her.The only way to pay back is to stand up and fight.kwa hatua inayofuata sote lazima tuingie katika mapambano.So I need you to stop everything and get ready to fight” akasema Mathew na kumpiga piga jaji Elibariki mgongoni halafu akatoka na kuelekea ofisini ambako alimkuta Anitha



“Anitha naomba nisikie maongezi ya Dr Joshua na Kigomba aliyomtaarifu kuhusu kifo cha Flaviana”akasema Mathew.Anitha akafungua faili anakohifadhi maongezi yote ya Dr Kigomba yakaanza kusikikika

“ hallow Mr President” Ikaanza kusikika sauti ya Dr Kigomba

“ hallow Kigomba ,habari za huko?



“ habari za huku nzuri .Vipi huko,Flaviana anaendeleaje ?“ akauliza Dr Kigomba halafu kukawa kimya na baada ya muda ikasikika sauti ya Dr Joshua

“They tried all they could but they didn’t succeed .She passed away few minutes ago.”akasema Dr Joshua kwa masikitiko halafu kukawa na ukimya

“I’m so sorry Mr President for your loss” akasema Dr Kigomba halafu kukawa kimya tena.

“ Niliwasiliana na Hussein jana usiku na akaniambia kwamba tayari fedha imekwisha ingia yote katika akaunti.Ulifanya uhakiki? Akauliza Dr Joshua



“ Ndiyo Mr President.Nimewasiliana na benki leo asubuhi na wamenitumia barua pepe na kunihakikishia kwamba pesa yote imeingia .Katika akaunti ya kwanza kuna shilingi Trilioni tatu na bilioni mia nne na akaunti ya pili ina shilingi trilioni mbili na bilioni mia saba.Katika kiasi tulichokuwa tumekubaliana tayari wamekilipa chote kwa hiyo kilichobaki ni sisi kuwakabidhi mzigo wao”



“ sawa Kigomba.Nitawasiliana na hussen li tupange namna ya kuwakabidhi mzigo wao.Nimechoshwa na mambo yanayoendelea kutokea kila uchao.Biashara hii tayari imeingia mkosi .Mpaka sasa nimepoteza mke na mtoto ndani ya kipindi kifupi na wote wamepotea ili biashara hii iweze kufanikiwa.Imetosha sasa .Nataka tulimalize suala hili ili maisha yakaendelee.Vipi kuhusu jaji Elibariki kuna taarifa zozote kuhusiana na mahala alipo? Kuna chochote ulikigundua kwa Peniela? Akauliza Dr Joshua



“ Mpaka sasa bado sijafanikiwa kupata taarifa zozote za mahala aliko jaji Elibariki au hata kitu cha kuweza kumuunganisha na Peniela.Ninahisi chanzo kilichotokea taarifa kwamba jaji Elibariki amejificha kwa Peniela hakikuwa chanzo cha uhakika.” akajibu Dr Kigomba

“ Dr Kigomba.Tutaongea zaidi nitakaporejea kwani tunatarajia jioni ya leo kuwasili na mwili wa marehemu.Hatuna sababu ya kuendelea kukaa huku .Kwa hiyo anza kuandaa shughuli za msiba” akasema DrJoshua.

“ sawa mheshimiwa raisi ninaanza sasa hivi kushughulikia suala hilo.Kwa mara nyingine tena napenda kuchukua nafasi hii kukupa pole sana wewe na familia yako kwa msiba huu mkubwa”



“ Ahsante sana ninashukuru.Nitawasiliana nawe tena baadae kidogo kukupa taarifa zaidi.” Akasema Dr Joshua na kukata simu



“ Huyu mzee ana roho ya kishetani kabisa.Hana uchungu wowote na kifo cha mwanae anachowaza yeye ni pesa tu” akasema Anitha

“ Kamwe hatakuweza kufanikiwa katika mipango yake.kwa mujibu wa maelekezo aliyompa Dr kigomba inaonekana wanakaribia kufika mwisho wa biashara yao kwani tayari fedha zimekwisha ingizwa katika akaunti zao za siri walizozifungua nje ya nchi.Ni fedha nyingi sana ambazo wamelipwa.Ninajiuliza ni kitu gani hiki ambacho kinaweza kugharimu fedha nyingi kiasi hiki? Halafu katika maongezi yao kuna mtu ametajwa kwa jina moja tu la Hussein.Inaonekana huyu ndiye mnunuzi mkuu wa Package hiyo.Tungeweza kumfahamu huyo mtu ni nani ingeweza kuturahisishia kujua kile kilichomo ndani ya hiyo Package” akasema mathew



“ Sehemu pekee ya kuweza kumfahamu huyu Hussein ni nani ni kwa kuipata simu ya Dr Joshua na anayeweza kuifanya kazi hiyo ni Peniela pekee” akasema Mathew



“ Kwa tukio hili lililompata unadhani anaweza kuifanya kazi hii kwa ufanisi? Ulifanikiwa kuzungumza naye? Akauliza Anitha



“ Sikufanikiwa kuongea naye kama nilivyotaka kwani watu wa team SC41 waliwasil ghafla .hata hivyo nitajitahidi nionane naye ili nimpe hali halisi .Ninam……………….” Mathew akanyamaza baada ya simu yake kuita.Mpigaji alikuwa ni Eva



“ Hallow Eva” akasema Mathew

“ Mathew unaweza kuja hapa ofisini kwangu mara moja? Kuna jambo nataka tujadili kuhusiana na lile suala uliloniomba nikusadie” akasema Eva

“ Tayari kuna jambo umelipata?

“ Ndiyo Mathew.Tukutane ofisini kwangu” akasema Eva na kukata simu



“ Nilipotoka hospitali niilikwenda kuonana na Eva na nikamuomba anisaidie kutafuta namna ya kuweza kuingia ndani ya nyumba ya Rosemary Mkozumi .Mama huyu lazima tumfanyie uchunguzi tubaini kama ni kweli yeye ndiye kinara wa kutaka kuuza karatasi zile kwa mtu anayesaidikiwa kufadhili ugaidi.Nilipata pia maelezo mengine toka kwa Eva kwamba mama huyu ni hatari sana na ana mtandao mkubwa wa watu hatari unaojishughulisha na mambo mengi maovu.Tunaposhughulikia suala hili ni lazima tuuchimbe kwa undani mtandao huu hadi mzizi wake na wote wanaohusika tuwatie nguvuni.” Akasema Mathew

“ Nina hakika kwa simu hii ya Eva kuna jambo la msingi sana ambalo ameligundua.Ngoja nikaonane naye.Wewe endelea kumfuatilia Dr Kigomba na kama kuna jambo lolote la dharura utanitaarifu mara moja” akasema Mathew na kuondoka kuelekea kwa Eva



“ Wakati Elibariki akinikabidhi kazi hii sikutegemea kama ingeweza kuwa kubwa kiasi hiki.Kila uchao linaibuka jambo jipya na kulifanya suala hili kuzidi kuwa kubwa .Tayari maisha ya watu kadhaa yamekwisha potea kwa sababu ya suala hili na maisha ya mamilioni wengine yapo hatarini endapo kirusi kile kitatua katika mikono isiyo salama.” Akawaza Mathew wakati akielekea ofisini kwa Eva

“ Sikutegemea kama siku moja mimi na John Mwaulaya tunaweza kuongea kama marafiki kutokana na kitendo alichonifanyia.Nilikuwa na hasira kali juu yake na kwa miaka mingi nilikuwa ninaisubiri siku ya kulipiza kisasi lakini imekuwa tofauti na nilivyotegemea.Nimefanikiwa kuonana tena na John na katika dakika zangu za mwisho nimejikuta nikishindwa kutekeleza mpango wangu wa kulipiza kisasi.Hali yake nilivyoiona jana ilikuwa mbaya na mimi mwenyewe nikamuonea huruma .Alikiri kosa lake na nikakubali kumsamehe.John alinieleza mambo makubwa na mazito sana na ninapaswa kumshukuru sana kwa kunichagua mimi niyafahamu mambo yale.Amekufa na siri nyingi kubwa kubwa na laiti kama ningepata muda wa kutosha wa kuongea naye angeweza kunieleza mambo mengi makubwa zaidi lakini ninashukuru hata kwa hili alilonieleza.Kitu kingine kizuri ni kwamba katika dakika za mwisho za uhai wake alipata huduma ya kiroho na kama maandiko yanavyosema hata kama tukiwa na dhambi nyingi kiasi gani tukifanya toba ya dhati Mungu hutuondolea dhambi zote na kutufanya wapya tena.Mungu amrehemu na ampe pumziko la milele” akawaza Mathew wakati akikaribia sana kufika katika baa ya Eva





Mathew aliwasili katika baa ya Eva.Watu hawakuwa wengi sana.Wengi wa waliokuwepo hapa mida hii walikuwa wakipata supu,kwani sifa nyingine ya baa hii ni kuwa na supu nzuri .Mathew aksshuka garini na moja kwa moja akelekea katika ofisi ya Eva,akagonga mlango , Eva akamruhusu aingie.

“ Hallow Eva” akasema Mathew



“ Karibu sana Mathew.” Akasema Eva

“ Ahsante Eva..Niambie kuna kitu chochote ulichokipata? akauliza Mathew huku akivuta kiti na kuketi.Eva akasubiri hadi Mathew alipoketi na kutulia kisha akasema

“ Ulipoondoka niliacha shughuli zote na kulishughulikia lile suala uliloniomba.Kuna jambo nimeligunuda ambalo linaweza kuwezesha kupata nafasi ya kuingia ndani ya nyumba ya Rosemary na ukafanya uchunguzi wako.” Akasema Eva

“ Ahsante sana Eva.Umegundua nini? akaulzia Mathew kwa shauku ya kutaka kulifahamu jambo hilo.

“ Baada ya kuachana na Mzee Deus Mkozumi,Rosemary aliingia katika mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa aliyewahi kuwa waziri wa kilimo katika serikali ya Deus Mkozumi anaitwa Henry Alois Chibuma.” Akanyamaza kidogo kisha akaendelea

“ Henry Chibuma ni mmoja kati ya waliokuwa mawaziri vijana sana katika serikali iliyopita na anasemekana kuwa na utrajiri mkubwa.Katika uchunguzi wangu nimegundua kwamba mke wa ndoa wa henry alikwisha farikiki dunia na ana mtoto wake mmoja tu aitwaye Naomi.Huyu ni muathirika wa dawa za kulevya na kwa sasa anafungiwa ndani ya jumba kubwa lenye ulinzi mkali ili asiweze kutoka wala kuonekana.Taarifa zinasema kwamba Henry ndiye chanzo cha mwanae kuathirika na dawa hizo kwani yeye pia alikuwa ni muingizaji na mtumiaji mkubwa wa dawa hizo .Nina hakika tukimpata Naomi tukaongea naye tunaweza kufahamu mambo mengi sana na hii inaweza ikawa ni njia rahisi ya kumpata Henry atakayetupeleka kwa Rosemary..” Akasema Eva.

“ Unasema waziri Henry naye ni muingizaji na mtumiaji wa dawa za kulevya? Akauliza Mathew

“ Ni kweli Mathew.Henry ni muingizaji mkubwa sana wa dawa za kulevya hapa nchini lakini nakuwa vigumu kumtia nguvuni kutokana na mtandao walio nao.Ndiyo maana nilikutahadharisha toka awali kwamba watu hawa ni hatari sana.Hata wakati akiwa wazidi alikuwa akijihusisha na biashara hii” akasema Eva

“ Huyu Naomi umeweza kuipata historia yake japo kwa ufupi? Akauliza Mathew

“ Ndiyo nilifanikwa kupata historia yake.Ni binti wa miaka kumi na tisa sasa na inasemekana alishindwa kuendelea na masomo kutokana na kuathirika na dawa hizo.Pili rafiki yake wa kiume alipigwa risasi na watu wasiojulikana.Inaaminika aliuawa kwa amri ya Henry. Naomi anaishi maisha ya upweke mkubwa ndaniya jumba hilo alimofungiwa.Nina hakika tukienda kuonana naye atatusikia na atakubali kushirikiana nasi.Nimefanikiwa kupata hadi jina la Daktari anayemtibu anaitwa Dr Marina.Huyu ni daktari toka hospitali kuu ya taifa kitengo cha kuwahudumia waathirika wa dawa za kulevya. ” Akasema Eva.Mathew kama kawaida yake hutumia muda kidogo kutafakari kila jambo kabla ya kufanya maamuzi akainama akatafakari na kusema

“ Sawa Eva twende tukaonane na Naomi.Lakini kabla ya kwenda huko lazima tuhakikishe tumejiandaa vya kutosha kwani kama ulivyosema kuna ulinzi katika jumba hilo.Nina hakika hatutaruhusiwa kuonana na Naomi kwa hiyo tunaweza kulazimika kutumia nguvu.” Akasema Mathew.Naomi akainuka akafungua kasiki lake lililoko ukutani ambalo huhifadhia silaha kwa matumizi ya dharura akamuita Mathew aangalie silaha ambazo zingeweza kuwasaidia.Mathew akachagua silaha na vifaa ambavyo vingeweza kuwasadia halafu bila kupoteza muda wakaingia katika gari la Mathew na safari ya kuelekea kwa Naomi ikaanza.

“ Nadhani sasa umeanza kupata picha ya watu wanaomzunguka Rosemary ni watu wa namna gani.Mtandao wao ni mkubwa na hatari.Henry anajihusisha na biashara nyingi haramu ikiwemo uingizaji wa dawa za kulevya lakini kumtia hatiani inakuwa ni mtihani mgumu kwa sababu wamezishika karibu sekta zote muhimu.Wana watu wao ndani ya jeshi la polisi,hata ndani ya usalama wa taifa kuna watu wao kwa hiyo ni rahisi sana kwao kujua chochote kinachoendelea dhidi yao na wakajihami.Ndiyo maana nilikutahadharisha toka mapema kwamba unatakiwa uwe makini sana unapomfuatilia Rose .” akasema Eva



“ Nimeamni maneno yako Eva,lakini dhumuni kuu la kazi yetu ni kushughulika na watu kama hawa. Hatupaswi kuwaogopa hata kidogo.Lazima tuhakikishe watu kama hawa ambao wanakwenda kinyume na taratibu na sheria za nchi wanafikishwa katika vyombo husika.Endapo tukiogopa kupambana nao siku moja nchi hii itashindwa kukalika kwani itakuwa ikiongozwa na genge la wahuni na wahalifu.Wewe mwenyewe uliniambia kwamba Rosemary anafikiria kuwania urais.Kwa nguvu ya pesa,ushawishi na mtandao mkubwa alio nao akipata nafasi hiyo ya kugombea anaweza akawa rais,sasa hebu pata picha mtu kama Rosemary akiwa rais wa nchi hii nini kitatokea? Hatupaswi hata kidogo kuacha jambo kama hilo likatokea.Lazima tupambane naye kwa kila nguvu na uwezo tulio nao.Binafsi nina roho ngumu kama jiwe na huwa siogopi kitu chochote zaidi ya Mungu pekee” akasema Mathew.Eva akatabasamu na baada ya muda akasema

“ Mathew naomba nikuulize kitu na tafadhali naomba unijibu”



“ Uliza va usijali”

“ Ni jambo gani ambalo unalichunguza?



“ Eva , mimi na wewe tumekuwa karibu kwa muda mrefu sana na kila pale ninapokuwa na tatizo nimekuwa nikikukimbilia wewe kwa msaada.Natamani sana nikueleze nini ninachokichunguza lakini ninaomba unipe muda kidogo ili niliweke vizuri suala hili na kisha nitakueleza kila kitu.” Akasema Mathew



“ Don’t you trust me? Akauliza Eva

“ I do trust you with my life Eva” akasema



“ No you don’t.Kama unegkuwa unaniamini usingesita kunieleza kile unachokichunguza.Mathew ninaweza kuwa na msaada mkubwa sana kwako tofauti na unavyodhani.Au unahisi kwamba ukinieleza jambo hilo ninaweza kuvujisha siri na kuharibu uchunguzi wako? Akauliza Eva

“ Si hivyo Eva.Ninakuamini sana na ndiyo maana nimekwambia kwamba nipe muda kidogo na nitakueleza kila kitu .Naomba ufahamu vile vile kwamba bado ninahitaji sana msaada wako.” Akasema Mathew aliyekuwa makini katika usukani

“ Sawa Mathew..” akajibu Eva kwa shingo upande na safari ikaendelea kimya kimya.Baada ya muda Eva akauliza



“ That woman,Anitha is she your girlfried? Akauliza Eva na kumfanya Mathew atabasamu

“ Kwa nini umeuliza ?

“ Nimehisi tu kwamba anaweza akawa ni mchumba wako kwa namna mnavyopendana.” Akasema Eva na Mathew akatoa kicheko

“ Anitha si mpenzi wangu na wala hatuna mahusiano yoyote mengine zaidi ya kazi.Unaponiona mimi na Anitha tuko mahala basi ujue ni kazi tu inafanyika na hakuna lingine.Mimi ni kazi tu mambo hayo ya mapenzi nilikwisha achana nayo muda mrefu.Toka familia yangu ilipoteketea sitaki tena kuijingiza katika mahusiano mengine.” Akasema Mathew

“ Mathew ni miaka sasa imepita toka litokee tukio lile.Usiendelee kujitesa tafadhali.You have to move on.Au bado una mpango wa kulipa kisasi kwa waliofanya kitendo kile? Do you know them? Akauliza Eva.Mathew akanyamaza kidogo kisha akajibu

“ Ni kweli ni miaka mingi imepita sasa lakini bado picha za tukio lile zinanijia akilini kila siku na ninaona ni kama tukio lile limetokea jana.Nimejitahidi sana kulisahau tukio lile lakini nimeshindwa.Bado linanitesa na nitateseka hadi siku ninaingia kaburini.Kuhusu kulipiza kisasi ni kweli nilikuwa na mpango huo lakini kwa sasa nimeachana nao.Sintolipiza kisasi kwani aliyefanya kitendo kile tayari amekwisha fariki dunia na ni Mungu pekee atakayemuhukumu” akasema Mathew

“ Kwa hiyo ulimfahamu? Ni nani huyo shetani? Akauliza Eva



“ It doesn’t matter for now.Eva kama hutajali naomba tusiendelee kuliongelea suala hilo”



“ Sawa Mathew na samahani kwa kukukumbusha mbali lakini kuhusu kuingia katika mahusiano mengine hili sintaacha kukukumbusha kwani umri unakwenda sana.Promise me you’ll think about that” akasema Eva.Mathew akatabasamu na kusema



“ Ok Eva.I’ll think about it” akajibu Mathew na safari ikaendelea.

Waliwasili katika mtaa lilipo jumba analoishi Naomi.Ni jumba kubwa lililozungushiwa ukuta mkubwa wa rangi nyeupe.Haikuwa rahisi kwa mtu aliyeko nje kuona chochote kilichomo ndani ya jumba lile kutokana na ukuta ule mkubwa.Kilichoonekana ukiwa nje ni bati zuri la rangi ya bluu.

“ Ni hapa” akasema Eva.Mathew akalitazama jumba lile na kupunguza mwendo wa gari na kusimama katika geti.Wakashuka na kubonyeza kengele na mlango mdogo wa geti ukafunguliwa na mtu mmoja aliyevaa mavazi meusi aliyeonekana kushangazwa sana na ujio wa akina Mathew

“ Habari zenu? Akawasalimu



“ Nzuri.Habari za hapa? Wakajibu Mathew na Eva kwa pamoja

“ Niwasaidie nini ? Akauliza Yule jamaa.

“ Sisi ni wanasihi tumetoka katika hospitali ya taifa kitengo cha kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya.Tumetumwa hapa na Dr Marina kwa ajili ya kumfabnyia unasihi Naomi.” Akasema Mathew.Yule jamaa akastuka kidogo

“ Ninamfahamu Dr Naomi lakini mbona hakunitaarifu kama kuna watu watakuja hapa leo?Isitoshe huwa anakuja mwenyewe iweje leo atume watu wengine?



“ Una namba zake za simu? Akauliza Mathew



“ Ndiyo ninazo.” Akajibu Yule jamaa

“ mpigie na atakupa maelekezo.” Akasema Mathew na yule jamaa akaingiza mkono mfukoni akatoa simu na kuanza kuzitafuta namba za Dr Marina.Wakati ameiinamia simu yake Mathew akamfanyia ishara Eva na kwa kasi ya umeme Eva akampiga Yule jamaa pigo moja la haraka na kumpeleka chini.Mathew akamuwahi pale chini na kumkaba kabala hadi akapoteza fahamu.Eva akachungulia ndani na hakuona mtu mwingine yeyote.

“ Its clear.No body is here! Akasema Eva kisha Mathew akamvuta Yule jamaa na kumuigiza ndani akamficha katika maua.Akaichukua simu ya yule jamaa kisha wakaelekea katika mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni.Wakagonga lakini hakuna mtu aliyejibu.Wakagonga tena na safari hii mlango ukafunguliwa na msichana mmoja aliyeonekana kama ni mfanyakazi za ndani.Alistuka sana alipowaona akina Mathew akawasalimu kwa uoga.

“ Naomi yuko wapi? Akauliza Mathew

“ Yuko chumbani kwake” akajibu Yule msichana

“ Tupeleke haraka chumbani kwake.” Akasema Mathew kwa ukali na yule msichana akawaongoza hadi katika mlango wa chumba cha Naomi

“ Chumba cha Naomi ni hiki hapa.” Akasema Yule msichana na mara sauti ikasikika toka ndani

“ Chiku unaongea na nani huko ?

Yule msichana akawafanyia akina Mathew ishara kwamba sauti ile ni ya Naomi.

“ Naomi kuna wageni wamekuja kukutembelea.” Akasema Chiku

“ Waambie waondoke.Sihitaji kuonana na mtu yeyote Yule.Nani kawaruhusu waingie humu? Akauliza Naomi kwa ukali toka ndani.Eva akamnong’oneza jambo Chiku akasema

“ Naomi ni watu toka hospitali wanataka kukuona”

“ Nimekwambia waambie waondoke zao.Leo si siku ya tiba” akasema Naomi



“ Eva she’s not going to open” akasema Mathew na kuupiga teke mlango ukafunguka wakaingia ndani.Naomi alistushwa sana na kitendo kile akapiga ukulele mkubwa.Mathew akamfuata na kumtuliza

“ Naomi naomba tafadhali usipige kelele.Hatuko hapa kwa ajili ya kukudhuru.Tuko hapa kwa ajili ya kukusaidia” akasema Mathew.Naomi akawatazama Mathew na Eva halafu akauliza



“ Kwani ninyi ni akina nani?

Mathew akamgeukia Eva aliyekuwa amemshikilia Chiku Yule mtumishi wa ndani



“ Mfungie bafuni huyo” akasema Mathew na Eva akamchukua Chiku akaenda kumfungia katika bafu la Naomi,akamsachi na kuhakikisha hana simu wala kifaa chochote cha mawasiliano .

“ Naomi naomba usituogope tafadhali.Sisi si wanasihi kama tulivyojitambulisha.Sisi ni maafisa toka idara ya usalama wa taifa.Ninaitwa Mathew na Yule dada anaitwa Eva.Tumekuja hapa kuzungumza nawe mambo kadhaa lakini dhumuni kubwa likiwa ni kukusaidia” akasema Mathew



“ Nitaaminije kama unasema kweli? Ninyi si watu wa mtandao wa baba?

“ Hapana sisi si watu wa mtandao baba yako.Tuamini Naomi tuko hapa kwa lengo la kukusaidia.Lakini tutakusaidia endapo na wewe utakuwa tayari kutusadia.” Akasema Mathew

“ Mnataka kunisaidia kivipi? Akauliza Naomi



“ Tunataka kukutoa katika maisha haya unayoishi sasa na kukusadia kuanza maisha mapya na uweze kutimiza ndoto zako za maisha.Naomi tunafahamu kila kitu kuhusu historia yako .Ulikuwa ni msichana mwenye akili sana darasani na ulikuwa na malengo mengi ya maisha yako kwa siku za usoni lakini malengo na ndoto zote za maisha yako zilikatishwa baada ya kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.Tunafahamu ni baba yako ndiye aliyesababisha haya yote yatokee.Tunafahamu anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya . Tunafahamu amekufungia humu ndani na hataki utoke kabisa nje ili watu wafahamu hali yako.Unaishi maisha ya upweke mkubwa humu ndani.Naomi tunataka kukusaidia ili uweze kuachana na maisha haya upate tiba upone na uendelee kutimiza ndoto zako.” Akasema Mathew.Naomi akashindwa kujizuia akaanza kulia.Eva akamfuata akakaa pembeni yake na kumbembeleza.



“ Nyamaza kuliza Naomi.Historia yako inaumiza sana .Tutakusaidia Naomi ..Naomba usiendelee kulia ili tuongee kwani muda wetu ni mfupi sana hapa kwako.” Akasema Eva.Naomi akafuta machozi na kusema



“ Nawaona ninyi ni kama malaika mliokuja kunikomboa.Kwa miaka minne sasa nimekuwa nikiishi kama mfungwa ndani ya jumba hili.Sina hamu tena ya kuendelea kuishi kwani siioni tena thamani yangu.Hakuna mtu anayenipenda tena wala kunijali.Yote hii imesababishwa na mimi kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.” Akasema Naomi huku akiendelea kububujikwa na machozi

“ Ilikuaje ukajiingiza katika matumizi ya dawa hizi za kulevya? Akauliza Mathew.Naomi akamtazama na kusema

“ Ni frank.Huyu ndiye aliyenishawishi mimi kujiingiza katika dawa za kulevya.”

“ Frank ni nani?

“ Alikuwa boyfriend wangu,kwa sasa amekwisha fariki alipigwa risasi.”

“ Pole sana” akasema Eva

“ Haikuwa dhamira ya Frank mimi kujiingiza katika maisha haya ya dawa za kulevya kwani alikuwa ananipenda sana lakini huu ulikuwa ni mpango wa baba niwe hivi.”

“ Mpango wa baba yako? Kivipi? Akauliza Mathew

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Baba alimtumia Frank aniingize katika matumizi ya dawa za kulevya.Niligundua kwamba baba alikuwa anamtumia Franki katika biashara ile kwa hiyo akamtumia yeye kunishawishi niingie katika matumizi hayo ya dawa za kulevya.”

“ Naomi tunafahamu kwamba baba yako anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya na ni mtumiaji pia lakini hatuelewi ni kwa nini akuingize na wewe katika matumizi haya ya dawa za kulevya wakati anazifahamu athari zake? Akauliza Mathew



“ Ni kwa sababu ninafahamu mambo yake mengi.Ninazifahamu siri zake nyingi.Baba alihusika katika kifo cha mama na nilipoligundua niliumia sana na nilimuweka wazi kwamba lazima nihakikishe ninamfikisha katika vyombo vya sheria.Hapo ndipo ugomvi kati yangu na baba ulipoanza na ndipo alipomtumia Frank kuningiza katka dawa za kulevya ili nichanganyikiwe akili yangu nisiweze kufanya kile nilichokusudia kukifanya.Baada ya kuona nimeathirika vibaya Frank aliumia sana na alikuwa tayari kwenda kutoa siri hii ndipo alipouawa kwa risasi na watu wa baba.Nilichukuliwa na kufungiwa humu ndani na katika miaka yote hii minne sijawahi kutoka kwenda nje ya nyumba hii.Nikitoka humu chumbani ninakaa hapo bustanini na si nje ya hapo. Baba amenitafutia daktari wa kunitibu na ameweka hadi walinzi na hakuna yeyote anayeruhusiwa kuingia ndani humu zaidi ya daktari wangu tu.Ninaishi maisha magumu sana na ndiyo maana ninawaona ninyi ni kama malaika mliokuja kunikomboa kama kweli lengo lenu ni hilo” akasema Naomi



“ Naomi sisi tutakusaidia kwa kila namna tuwezavyo ili uweze kurejea katika maisha yako ya kawaida.”

“ Tafadhali naombeni msiniache humu ndani.Mkiondoka ondokeni na mimi” akasema Naomi

“ usijali Naomi tutaondoka nawe.Lakini kabla ya yote kuna jambo ambalo tunahitaji sana msaada wako.” Akasema Mathdew

“Tunafahamu baba yako anajihusisha na mambo mengi ya haramu ikiwemo na biashara hii ya dawa za kulevya.Tumekuwa tukimfuatilia kwa muda na tumegundua kwamba anao mtandao mkubwa wa watu wanaojishughulisha na mambo mengi ya hatari. Kwa sasa baba yako na mtandao wake wanajihusisha na jambo moja kubwa na la hatari lenye kuhatarisha uhai wa mamilioni ya watu duniani.Tunatafuta namna ya kuweza kumzuia yeye na mtandao wake wasiweze kutekeleza mpango wao huo lakini njia pekee ya kufanya hivyo ni kwa kupitia kwako.” Akasema Mathew

“ NInamfahamu baba yangu .Ana roho ya kishetani.Ni mkatili kupindukia.Yeye ndiye aliyenifanya mimi kuishi maisha ya namna hii.Simpendi na ninatamani kama siku moja ningekuwa na uwezo ningemuua.”akasema kwa uchungu Naomi huku akilia



“ Basi usilie Naomi .Hili tutalimaliza.Tunachokuomba ni ushirikiano wako.Baba yako kwa sasa yuko katika mahusiano ya kimapenzi na mke wa rais mstaafu.nadhani unalifahamu hilo”

“ Ndiyo ninalifahamu hilo na kuna nyakati huwa wanakuja wote kunitazama” akajibu Naomi



“ Basi Yule mama ndiye kiongozi wa mtandao alimo baba yako.Mambo mengi anayoyafanya baba yako yanaratibiwa na Yule mama kwa hiyo tunataka kuingia ndani ya jumba la Yule mama na kufanya uchunguzi lakni mtu pekee anayeweza kutuingiza humo ni baba yako kwa hiyo tunaomba utusaidie tuweze kumpata baba yako”

“ Mnataka niwasaidiaje? Akauliza Naomi



“ Tunataka uwasiliane naye na kumtaka afike hapa nyumbani haraka sana kwamba una tatizo na akisha fika sisi tutamtia mikononi mwetu na atatupeleka katika jumba hilo la Rosemary kufanya uchunguzi wetu.Wewe tutakuchukua na kukupeleka sehemu salama,tutakutafutia tiba na tutakupatia ulinzi na tutakusaidia kwa kila namna tuwezavyo kuhakikisha kwamba unakuwa na maisha mazuri na ya uhuru” akasema Mathew



“ Kwa kweli natamani sana baba yangu akamatwe na afungwe gerezani maisha au ikiwezekana anyongwe kabisa lakini ninashindwa namna ya kuwasaidia.Kwanza mimi na baba yangu hatuna mahusiano mazuri na siwezi kuwasiliana naye kwa sababu sina mawasiliano yoyote humu ndani.Sina simu wala kitu chochote cha kuniwezesha kuwasiliana na watu huko nje.” Akasema Naomi.Mathew akatoa simu ya Yule mlinzi aliyepoteza fahamu



“ Simu hii ya mlinzi wa getini.Wasiliana na baba yako.Tafuta namna ya kumfanya aweze kufika hapa mara moja” akasema Mathew na Naomi akaishika ile simu huku mikono ikimtetemeka akazitafuta namba za baba yake na kupiga





Mathew akamuelekeza abonyeze kitufe kitakachowafanya wote wasikie kile watakachokiogea.Simu ikaita bila kupokelewa ikakatika.Akapiga tena na safari hii ikapokelewa



“ Hallo Francis”ikasema sauti ya upande wa pili



“ Hallow dady ni mimi Naomi” akasema Naomi na kumstua kidogo Henry



“ Naomi kwa nini umechukua simu ya Francis wakati nilikwisha kukanya kutumia simu? Akauliza Henry



“ Dady nimelazimika kumuomba mara moja simu yake niwasiliane nawe.”

“ Ok siku nyingine usirudie tena kuchukua simu ya Francis.Muda wowote kama una tatizo mwambie Francis na yeye ndiye atakayenitafuta .Haya niambie una tatizo gani?

“ dady nina tatzo kubwa nahitaji kukuona mara moja”

“ Una tatizo gani Naomi?

“ Dady siwezi kukueleza katika simu.Naomba uje mara moja “

“ Naomi kwa sasa siwezi kufika nina kazi ya muhimu sana.Nitafika baadae baada ya kumaliza kazi hiyo.kamakuna tatizo kubwa mweleze Francis tafadhali”

“ No Dady ! tafadhali achana na kila ulichonacho na uje mara moja.Siwezi kumweleza Francis matatizo yangu ya ndani .He’s not my father”

“ Naomi kama huwezi kumweleza Francis nieleze basi katika simu nijue una tatizo gani?

“ Dady sijawahi hata siku moja kukuomba ukatishe kazi zako uje unitazame.Leo nina tatizo kubwa na ninaomba uje unisikilze.Just this once can you be a father to me and listen to what I want? .Hakuna mwingine ninayeweza kumweleza tatizo langu zaidi yako” akasema Naomi.Kukawa kimya kidogo halafu Henry akasema



“ Sawa ninakuja sasa hivi.Naomba niongee na Francis” akasema Henry.

“ Francis !!.Francis !!!......Francis…!!!!!!!.akaita Naomi kwa nguvu



“ Dady inaonekana Francis ametoka nje nadhani ameenda kutafuta sigara.Nitamwambia akupigie simu akirejea.”



“ Sawa Naomi.Ninakuja sasa hivi” akasema Henry na kukata simu

“ Good.Umefanya vizuri sana Naomi. Ahsante sana kwa msaada wako huu mkubwa.Endapo jambo hili litafanikiwa basi utakuwa umechangia kuokoa maisha ya watu wengi.” Akasema Mathew



“ Nimefanya mlivyotaka nifanye ni zamu yenu sasa kutimiza kile mlichoniahidi.To get me out of here” akasema Naomi

“ Usihofu Naomi.Utapata kila ulichoahidiwa.Tutakutoa hapa na kukupeleka sehemu salama ambako utaishi na tutakusaidia kutimiza malengo yako” akasema Mathew

“ Wakati tukimsubiri baba yako afike,naomba utueleze kama kuna vitu vingine anavyofanya baba yako ambavyo unaona ni vyema tukavifahamu “ akasema Mathew.naomi akainamana kufuta machozi kisha akasema



“ I hate my father.Ni kwa sababu yake maisha yangu leo hii yameharibika na kufika hapa.I hate him so much.Baba yangu anajihusisha na mambo mengi sana haramu lakini leo hii nitakueleza kuhusu jambo moja.Baba na watu wake wana kiwanda cha kutengeneza pesa bandia.Chini ya jumba lake analoishi kuna kiwanda cha kutengeneza fedha bandia.Niliwahi kunyata siku moja na kuingia ndani yua kiwanda hicho wakati baba hayupo na nilifanikiwa kuchukua video ya kiwanda hicho ambayo ninayo na kuna sehemu nimeificha .Sikujua kama ndani ya kiwanda hicho kuna kamera zilizokuwa zinanichukua picha .Hili ni mojawapo ya mambo yaliyomfanya baba aamue kunifanya hivi.Kuna kitu niliwahi kumuomba na akanikatalia nikamtishia kuvujisha siri zake kwaniushahdi ninao kwamba ana kiwanda cha kutengeneza noti bandia akaogopa sana na kwa kuogopa kwamba siku moja ninaweza kuweka siri zake hadharani akaona njia pekee ya kunizuia nisiweze kufanya hivyo ni kuniharibu kwa dawaza kulevya.” akasema Naomi huku akilia kwa uchungu.Aliwaeleza akina Mathew mambo mengi anayoyafahamu kuhusiana na baba yake.Baada ya kuridhika na maelezo yale ya Naomi,Mathew akamchukua Eva pamoja na Yule msichana wa kazi wakaelekea getini kumsubiri Henry.



“ Ama kweli dunia hii inawatu makatili kupindukia.Yaani unadiriki kumfanya vile mtoto wako wa kumzaa mwenyewe ! akasema Eva kwa uchungu

“ Toobad.But Naomi will be fine.Ametupa msaada mkubwa sana na nitahakikisha anapona na kurejea katika hali yake ya kawaida.” Akasema Mathew

Baada ya dakika ishirini za kusubiri mara ikasikika honi nje ya geti.Mathew akamuelekeza Yule msichana wa kazi achungulie kama ni henryndiye aliyekuwa anapiga honi ile.Msichana yule akachungulia na kuwataarifu kwamba ni Henry.Wakajiweka tayari na kumwambia alifungue geti.Taratibu msichana Yule akalifungua geti na Henry akaingiza gari ndani.Alistushwa kidogonakufunguliwa geti na msichanawa kazi badala ya mlinzi.Akafungua mlango na kushuka akitaka kujua aliko Francis lakini ghafla akajikuta akitazamana na watu wawli waliomuelekezea bastora.Akastuka sana kwani hakuwa amelitegemea tukio kama lile.Haraka haraka Mathew akamuamuru ashuke garini na bila ubishi Henry akashuka garini .Mathew akamuongoza kuelekea ndani.

“ Who are you guys? Mnataka nini kwangu? Nani kawatuma kwangu? Akauliza henry huku akiwa ameinua mikono akielekea ndani.Waliingia sebuleni na Mathew akamuamuru aketi sofani.



“ kwa nini mnanifanyia hivi? Ninyi ni akina nani? Nani kawatuma mnifanyie hivi? Hamuogopi kwa hili mnalolifanya? Anawalipa shilingi ngapialiyewatuma?Akauliza Henry.



“ Shut up !! akafoka Mathew na kumuamuru Eva akamchukue Naomi chumbani kwake.Baada ya dakika mbili Naomi akafika pale sebuleni.henry akashangaa sana akabaki mdomo wazi

“ I cant believe thisNaomi !!!...kumbe ni wewe uliyekubali kunisaliti mwanangu? Wamekulipa shilingi ngapi hawa na ukakubali kumsaliti baba yako mzazi? Jambo gani nimekukosea mwanangu kiasi cha kunisaliti namna hii? Akauliza Henry



“ Huyu ni mwanao? Akauliza Mathew



“ Ndiyo ni mwanangu” akajibu Henry

“ kwa nini umesababisha akawa hivi?

“ Amewaeleza kwamba mimi ni sababu ya yeye kuwa hivi? Si mimi niliyemfaya akawa hivi.Yeye mwenyewe alijiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya na ndiyo maana akafikia hali hii.Mimi sihusiki na hali hii kwa namna yoyote.Nimejitahidi kumlea kwa kadiri nilivyoweza lakini bado hakuridhika na akajiingiza katika starehe nadawa za kulevya” akasema Henry

“ Liar !!!..akapaaza sauti Naomi huku akilia

“ Henry hatuna muda mrefu wa kuongea nawe hapa.Tayari tunafahamu mambo yako mengi unayoyafanya ya haramu.Tunafahamu kuhusu biashara yako ya dawa za kulevya.Tunafahamu kuhusu kiwanda chako cha kutengeneza noti bandia chiniya nyumba yako.Tunafahamu kila kitu unachokifanya na ushahidi tunao wa kuweza kukutia hatiani wewe na mtandao wako wote.” Akasema Mathew na kumfanya Henry atetemeke.Mathew akaendelea

“ Henry tunafahamu mambo yako mengi sana na endapo utafikishwa mbele ya sheria huwezi kukwepa kifungo cha maisha gerezani kwa mambo unayoyafanya.Hata hivyo kwa sasa tunayaweka yote pembeni kwanza.Kuna jambo tunalitaka toka kwako na endapo utatupatia tunachohitaji basi tutakuacha uendelee na shughuli zako ila Naomi tutamchukua na kumpeleka katika tiba and She’ll never talk about anything she knows about you”akasema Mathew



“ Who are you guys? Ni jambo gani mnalitaka toka kwangu? Akauliza henry

“ Huna haja ya kutufahamu sisi ni akina nani lakini sisi ni watu wabaya sana na una bahat mbaya ukutana na sisi.We can destroy you in a second” akasema Mathew

“Nielezeni mnataka nini toka kwangu? Akauliza Henry .Mathew akamsogelea karibu na kumuwekea bastora kifuani



“ Tunafahamu kwa sasa una mahusiano ya kimapenzi na Rosemary Mkozumi.Ninataka uniingize ndani ya jumba la Rosemary Mkozumi kwani wewe pale ni kama kwako .Unaweza ukaingia na kutoka muda wowote unaotaka..” Akasema Mathew na kumstua sana Henry

“ What ?!!Unataka kuingia kwa Rosemary? Unataka kwenda kufanya nini?



“ Henry shida yetu si wewe ,shida yetu ni Rosemary.Kuna jambo ninalotaka kulichunguza katik a mawasiliano ya Rosemary ndiyo maana nikakwambia kwamba ukinisaidia kulifanikisha hilo sintakuwa na shida na wewe .”akasema mathew

“ Hapana sintaweza kufanya hivyo mnavyotaka nifanye.Hamumfahamu vizuri Rosemary ninyi.Nawaonya msithubutu kucheza na Yule mama.”akasema Henry

“ Henry utanipeleka ndani ya jumba hilo na utafanya kila nitakachokuamuru umesikia? Usipofanya hivyo ndani ya dakika chache zijazo wewe na mtandao wako wote akiwemo na mpenzi wako Rosemary mtajikuta katika nondo za gereza..Unataka tulifanye hilo? Do you want to go down? Unataka nchi yote ifahamu mambo mnayoyafanya wewe na mtandao wako?akasemamathew.Heny akaonekana kuingiwa na woga

“ Jamani naomba basi muweke silaha zenu chini ili tuongee kama watu wazima na tuelewane.Ninakubali mnafahamu mambo yangu mengi na mmekuja kwangu mkiwa na shida yenu ambayo ili ifanikiwe inanihitaji sana mimi.Ni kweli sitaki mambo yangu yajulikane kwani heshima yangu niliyoijenga ndani ya nchi hii itashuka sana na hii ni mbaya sana kwangu kisiasa.Niko tayari kuwasaidia kile mnchokitaka lakini kwa sharti kwamba binti yangu asiondolewe humu ndani ya hii nyumba kwani akitoka humu ataendelea na tabia yake ya kutumia dawa za kulevya.Huyu ni binti yangu wa pekee na sina tena mtoto mwingine na ndiyo maana ninafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba anakuwa salama na haijihusishi tena na dawa za kulevya.Ili niwasaidie ninaomba mnihakkishie hilo kwanza’ akasema Henry



“ Henry suala hilo halitawezekana kwani kwa miaka minne sasa umemfungia Naomi ndani ya jumbahili na kwa sasa anahitaji kuwa huru.Sisi tutamchukua na kumpeleka katika sehemu atakakopatiwa matibabu na usiwe na wasiwasi hatasema chochote kuhusu wewe na wala hataendelea tena kutumia dawa za kulevya.Naomba uniamini katika hilo’ akasema Mathew.Henry akafikiri kidogo kisha akasema



“Ni kitu gani unachotaka kwenda kukichunguza kwa Rosemary?



“ Nataka kuchunguza mawasiliano yake ya ndani na nje ya nchi” akasema Mathew

“ Nyumba ya Rosemary ina mfumo wa kisasa sana wa ulinzi na kuna baadhi ya vitu vyake kama vile komyuta zake au sehemu anakohifadhi nyaraka zake muhimu vikiwashwa basi taarifa inatumwa moja kwa moja katika simu yake ya mkononi.Kwa hiyo ni vigumu sana kuweza kuwasha kitu chochote cha Rosemary kilichomo katika ofisi yake.”akasema Henry

“ Henry will you take me there or not?akauliza Mathew.Henry akakaa kimya kidogo na kusema



“ sawa nitakupeleka huko lakini tafadhali tukubaliane kwanza kuhusu binti yangu.Haendi kokote”



“ Naomi is in safe hands.Usiogope.She’ll be fine” akasema Mathew



“ Dady fanya kama ulivyoombwa kufanya na ushofukuhusu mimi.I’m free now”akasema Naomi.Henry akamtazama kwa jicho kali

“ Henry muda unakwenda sana.Tuondoke sasa”akasema Mathew.Henry akainuka pale katika sofa

“ Eva mchukue Naomi kamuhifadhi kwa muda ofisini kwako hadi zoezi hili likamilike kisha tutamchukua na kumpeleka sehemu salama.Mimi nitaongozana na Henry kwenda nyumbani kwa Rose.”akasema Mathew



“ Are you sure yo want to go teher alone Mathew? Akauliza Eva

“ yes Eva..” Akasema Mathew na kisha akamgeukia Naomi

“ Naomi utachukua mizigo yako na utaongozana na Eva atakupeleka sehemu salama” akasema Mathew kisha akaongozana na henry wakatoka hadi katika gari la henry .Bado bastora ya Mathew ilikuwa mkononi.Henry akageuza gari wakaondoka pale nyumbani.Mathew akachukua simu na kumpigia Anitha



“ hallow Mathew”akasema Anitha baada ya kupokea simu

“ Anitha kuna habari zozote mpya ?

“ Hapana mpaka sasa hakuna habari mpya ,Dr Kigomba alikuwa anapiga sehemu mbalimbali kufanya maandalizi ya msiba wa Flaviana”

“ Ok good.Niko njiani hivi sasa ninaelekea kwa Rosemary Mkozumi.Inasemekana nyumbani kwa Rose kuna mfumo wa kisasa wa ulinzi na kwa hiyo si rahisi kuingia katika kompyuta ya Rose .Nadhani ingekuwa vizuri sana kama ningeongozana nawe ili uweze kunisaisia katika kazi hi.Ukiwa karibu tunaweza kufanya kazi kwa haraka zaidi.Tafadhali chukua vifaa unavyoona vinaweza kutusaidia na uchukue gari.Utatukuta tunakusubiri pale picha ya samaki ili tuongozane ” akasema Mathew



“ sawa Mathew.Nisubirihapo picha ya samaki ninakuja si muda mrefu.” Akasema Anitha

“ Who are you guys? Mnatafuta kitu gani kwa Rose? Akauliza Henry

“shut up !!akasema Mathew na mara simu ya Henry ikaita.

“ Nipe hiyo simu”akasema Mathew

“ Mmeniweka chIni ya ulInzi na mnanilazimisha nifanye kile mnachokitaka,lakini bado mnanizuia hadi kutumia simu yangu? Akafoka Henry

“ Nimesema nipe smu yako”akasema Mathew na Henry akaogopa kwa namna Mathew alivyokuwa anamaungalia akampatia simu yake ,akaizima nakutoa kabisa betri



“ Twende hadi picha ya samaki kuna mtu tukamsubiri pale.” Akaamuru Mathew

Walifika eneo la picha ya samaki wakaegesha gari wakimsubiri Anitha.Ilimchukua anitha zaidi ya dakika thelathini kuwasili eneo lile.Haraka haraka akiwa na begi lake lenye vifaa muhimu vinavyoweza kuwasaidia akashuka katika piki piki aliyokodi na kuingia katika gari walimokuwamo akina Mathew na safari ikaendelea.

Waliwaisli katika jumba la Rosemary Mkozumi lililojengwa ufukweni mwa bahari .Toka kwa mbali uzuri wa jumba hili ulionekana,barabara iliyoeleka katika jumba hili ilipandwa maua na miti mizuri ya kuvutia sana.Kulikuwa na ukimya mkubwa eneo hili

Wakafika katika geti kubwa jeusi Henry akasimamisha gari.Getni pale walionekana walinzi wanne na wawili kati yao walikuwa na silaha.Walivaa sare za kampuni binafsi ya ulinzi.Mmoja wa walinzi wale akalisogelea gari,Henry akashusha kioo cha gari wakasalimiana halafu geti likafunguliwa na henry akapita.Hawaku muuliza maswali yoyote kwa kuwa walimfahamu.Baada ya kulivuka geti la kwanza wakakuta tena geti la pili,wakafunguliwa wakpita na mwisho wakalifikia geti la tatu nalo wakafunguliwa wakapita bila kuhojiwa.

“ Mhh kwa ulinzi ulioko hapa sina hakika kama ingekuwa rahisi kuingia.Huyu mama amejimarisha sana katika ulinzi.”akawaza Mathew

Kisha livuka geti la tatu lililokuwa na walinzi wawili,wakaanza kulitazama jumba kubwa la ghorofa nne.Lilikuwa ni jumba la kifahari mno.Henry akaegesha gari wakashuka na kuingia ndani.Aliwakaribisha ndani huku akitabsamu ili watumishi wasiweze kugundua chochote kilichokuwa kinaendelea.

Moja kwa moja henry akawapeleka Mathew na Anitha katika ofisi ya Rosemary.Juu ya mlango wa ofisi ile kulikuwa na taa nyekundu ikiwaka napembeni ya mlango ule kulikuwa na kijisanduku chenye namba.Henry ajkabonyeza namna kadhaa halafu akawekamkonokatika sehemu fulaniiliyowaka taa ya kijani na baada ya sekunde kadhaa yakatokea maandishi

“ Welcome Henry” na mlango akafunguka..

“ Hii ndiyo ofisi ya Rosemary lakinihata mimi huitumia pia.Kompyuta yake ile pale,na lile pale ni kabati ambalo huhifadhi nyaraka zake nyeti.Ili kufungua vitu vyake unahitaji namba za siri ambazo hata mimi sina.Ni yeye pekee anayezifahamu” akasema Henry.

Anitha akafungua begi lake akatoa vifaa Fulani akaviweka mezani akaiwasha kompyuta yake ndogo ,halafu akachukua kifaa kingine kidogo akakichomeka nyuma ya kompyuta ya Rose.Akakaa katika komyuta yake na kuanza kubonyeza bonyeza kompyuta yake kwa takribani dakika saba hivi huku Mathew na Henry wakimshangaa wasielwe alichokuwa anakifanya.Akainuka tena na kwenda kuiwasha kompyuta ya Rosemary na kisha akarejea tena katika kompyuta yake. Akaanza kubonyeza tena na baadaya dakika tano akasema



“ Done,we’re in…”

Henry akabaki anashangaa



“ Thank you anitha.You are always the best” akasema Mathew

“ Progarmu hii niliyoiweka inatengua mfumo huu wa usalama aliouweka Rose kwa muda wa dakika thelathini kwa hiyo tufanye haraka kutafuta kile tunachokitaka” akasema Anitha na kumuelekeza Anitha aanze kupekua katika mawasiliano ya barua pepe kama anaweza akapata mawasiliano kati ya Rose na Habib

Anitha akaanza kupekua mawasiliano ya Rose na watu kadhaa lakini ghafla akasimama


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog