Search This Blog

Wednesday 22 March 2023

JINO KWA JINO - 1

  

IMEANDIKWA NA : KAICHI M MUSSA

***********************************************

Simulizi : Jino Kwa Jino

Sehemu Ya : Kwanza (1)



Kwa mara nyingine mtunzi wako wa riwaya za kijasusi nakuletea riwaya ingine ya kuvutia ambayo imechezwa nchi takribani sita. Riwaya ambayo nimeipa jina lililobeba mahudhui ya matukio husika pamoja maneno ya wahusika katika riwaya husika kuwa ni ‘JINO KWA JINO’ na kwa lugha iliyokuja kwa meli za ughaibuni kuja barani Afrika inaitwa “Tooth For Tooth”, kutokana na visasi vya wahusika na kuapia lazima kufanya jambo fulani kama malipizo ya jambo alilofanyiwa yeye au familia yake au rafiki yake.


Riwaya iliyokusanya mikasa mizito na hekaheka za kutisha ambayo kwa asilimia sitini yakitokea nchi za Mexico na Guatemala huku Marekani, Bolivia na Canada zikiingia kwa asilimia zilizobaki. Riwaya ikimrudisha kijana nguli katika michezo ya giza Agent Kai Hamis a.k.a The Sole Cat shushushu na jasusi wa CIA aliye kitengo maalumu cha mashushushu wenye ujuzi wa juu zaidi kitengo kilicho ndani ya shirika hili la kijasusi kiitwacho Special Activities Division (SAD) akihudumu kutokea ofisi ya makamu wa Rais wa Marekani, akiwa na majasusi wengine kadhaa waliojitokeza kwa namna moja ama nyingine kushirikiana naye kwa kazi iliyomkuta kupambana na wahalifu waliokubuhu katika fani ya uhalifu wa ulanguzi wa mihadarati na magenge yao yaliyojikita katika viunga vya maeneo tajwa wakichuma pesa na kujimilikisha utajiri mkubwa kwa njia hii ya kihalifu na inayoacha athari kubwa katika jamii hasa vijana wakiwa waathirika wakubwa.


Baada ya kumaliza operesheni ya mshangao iliyompeleka nchini Malaysia kisha kumpelekea kuingia katika ndoa kwa kumuoa mwanadada wa kiarabu toka Syria aliyekutana naye Malaysia ndoa yao iliyofungiwa jijini Kuala Lumpur. Maharusi hawa waliamua kuelekea fungate katika nchi yake ya kuzaliwa Tanzania walipokula raha kwa siku tisini (miezi mitatu), walirudi Washington DC-Marekani.


Wakiwa na siku tatu toka waingie Washington DC, Agent Kai akipekua pekua akaunti yake ya barua pepe anakutana na barua pepe iliyotumwa kwake wiki mbili zilizopita ya mtu ambaye ni rafiki yake mkubwa sana aliyetoweka miaka mitano iliyopita, jasusi mwenzie aliyepitia naye katika mafunzo mbalimbali katika vituo kadhaa vya mafunzo na kisha rafiki yake huyo kuhamishiwa katika kitengo cha Marekani cha kijasusi cha kupambana na madawa ya kulevya Drug Enforcement Administration (DEA) kutokea kikosi cha makomando cha US Navy Seals sababu ya kupata na tatizo la kukatwa kiganja cha mkono wa kulia.


Hii barua pepe ndiyo aliyoikuta na kuipa umuhimu na uzito mkubwa kuliko barua pepe zote alizozikuta na kuchukua muda wake kuzipitia.


Jasusi huyu wa DEA aliyeandika barua hii pamoja na kuwa ni marafiki waliokuwa kwenye vitengo tofauti vya kijasusi kati ya vitengo vingi vinavyohudumu kiufasaha na maslahi mazito kwa taifa kubwa la Marekani, pia alikuwa ni kama ndugu kwa Agent Kai, ni mwanaume mwenye asili ya kiafrika toka nchi ya Nigeria. Ambaye wazazi wake waliamia Marekani miaka hamsini iliyopita na baada ya miaka kadhaa kwakuwa wote walikuwa ni madaktari bingwa katika hospitali moja iliyopo Oklahoma walichukua uraia wa Marekani na kumleta yeye duniani miaka thelathini na nne iliyopita, hivyo yeye ni Mmarekani wa kuzaliwa tofauti na Agent Kai aliye mmarekani wa kununuliwa kama wanavyonunuliwa wachezaji katika baadhi ya mataifa yaliyokwisha endelea kama Ufaransa na mengineyo na kufanya yatawale soka la dunia.


Barua pepe toka kwa Jasusi wa DEA, Sajenti Johnson Greg Rautolaye ikiwa mwenyewe Agent Kai alipenda kumuita kwa kifupi ‘Jogre’.


Barua pepe ilimshtua kwa kiasi kikubwa kwakuwa:

i)Muandikaji alipotea katika hali ya sintofahamu takribani sasa ni miaka kumi, alipotea akiwa ndiyo kwanza ametoka kumuoa mchumba wake wa toka enzi za balehe yao, aliwapa wakati mgumu sana na sintofahamu kuu kwa wakuu wake wa kazi akiwemo mkurugenzi wa kitengo cha DEA, Licha ya kuwa alipotea na majasusi wawili kwa siku moja wa kitengo cha kijasusi cha Drug Enforcement Administrastion (DEA) Jogre aliwashtua wengi na kuwasikitisha sana kwakuwa alikuwa ametoka fungate ya ndoa yake muda mfupi uliopita pia hakuwa mtu wa kazi za vitendo zaidi kutokana na kutokuwa na mkono mmoja wa kulia uliokatwa kuanzia linapoanzia bega hivyo yeye alikuwa mtu wa mipango zaidi.


ii)Barua pepe iliandikwa kwa kuonyesha muandikaji aliandika akiwa katika wakati mgumu sana, maana maandishi yake ya kimafumbo yaliyofumbwa kwenye mchoro wa kuonyesha kitu kilichoandikwa kimefutwa yalifumbwa haswa na yalikuwa machache sana huku mwisho akiandika ‘Jogre’, kitaalamu sana ambapo kwa mtu wa kawaida hawezi hata kuliona jina hilo ndipo Agent Kai akatambua muandikaji ni nani.


Barua pepe inamuelekeza nini? Agent Kai


Fuatana nami katika safari ndefu ya JINO KWA JINO (Tooth For Tooth) inayopita katika nchi mbalimbali zilizopo Amerika ya kaskazini, karibu utafune na ufyonze asali yenye ladha ya maridhawa ya chakula cha ubongo unaotaka kuburudishwa kwa mambo ya mazuri yenye taharuki,ujasusi wa teknolojia, silaha na mapigo ya kisasa.


KARIBU TUFYONZEA NA KULAMBA ASALI…!


WASHINGTON DC-USA (MAREKANI)

“Ngriiii, ngriiiii, ngriiiii” ulikuwa mlio wa kengele ya getini kuashiria kuna mtu amesimama nje ya geti lililoshikana na ukuta mrefu uliozunguka nyumba namba VB 22214, North Underwood Street, mtaa ulio mita chache na ulipo mtaa 28 Third Street inapopatikana shule maarufu ya upili ya Bishop O’Connell High School katika viunga vya jiji la Washington DC, jiji la shughuli nyingi za kiserikali katika serikali ya Marekani.


Kengele haikuwa imejipiga yenyewe pale getini kusababisha iende kuhanikiza katika vyumba vya nyumba husika hili kuwastua wakazi wa nyumba kuwa kuna mtu anayehitaji kuingia katika nyumba hii, kengele hii ilibonyezwa na kijana shababi aliyekuwa kashuka toka kwenye gari yake aina ya Chevrolet Camaro rangi nyeupe, kichwani akiwa amevaa kofia aina ya kapero ya rangi ya bluu aliyoishusha mpaka ionekane kama inamziba uso kwa juu kuja machoni ikiwa na andishi la herufi moja tu kubwa ya C iliyoandikwa kwa rangi ya njano kisha chini kuna mnyama aina ya paka akifanya mjongeo, fulana ya rangi ya njano isiyo na andishi lolote ndiyo aliyoivaa ikiwa ya kawaida si ya kubana na suruali ya jeans rangi ya bluu ilimfanya aonekane jinsi alivyo mtanashati anayependa umaridadi unaokwenda na wakati wa mavazi.


Alikuwa akitambua anapobonyeza swichi ya kengele basi anatakiwa awe ameelekeza uso wake katika kamera inayochukua matukio ya eneo hili la getini kupeleka ndani, hivyo huku akiachia uso wake kuonekana wenye furaha kwa vizuri aliishika kapero yake kwa kuiinua kwa juu, aliiangalia kamera husika na papo hapo ukatokea mwanga wa kijani, ishara ambayo nayo haikuwa ngeni kwake huyu mbonyeza swichi ya kengele.


Hapo kwa haraka alirudi ndani ya gari yake na alipofunga mlango wa gari tu, geti lililo mbele yake likaanza kufunguka kwa kusogea kutoka kushoto kwenda kulia. Taratibu akaingiza gia isiyofanya gari kutoka spidi akaingiza gari taratibu ndani ya uwa wa eneo hili la nyumba huku nyuma yake geti likijifunga.


Kwa mwendo ule ule wa taratibu akasogea mpaka eneo aliloona ni sahihi yeye kupaki gari lake, akazima gari na kabla hajanyanyua simu yake iliyo kwenye dashboard ya gari, mlango wa mbele wa jumba hili la kisasa ulifunguka na kisha akatoka mwanadada wa kizungu aliyekuwa kavaa suruali taiti nyeusi na kikawoshi cha kimichezo (jezi) ya timu ya basketball ya Milwaukee Bucks, miguuni mwake akivaa ndala za rangi nyeupe, akiwa na uso uliojaa tabasamu pana sana huku akishuka ngazi kwa kasi kuelekea ilipo gari kuonyesha furaha yake kwa mgeni aliyefika.


Mgeni naye uso ukiwa umechanua tabasamu pana akashuka haraka garini kumlaki mwenyeji wake kwa furaha na bashasha tele.


“Hi my love…!” Akasalimu mwenyeji na kuchanua mikono yake kumpokea kwa kumbatio mwanaume aliye mbele.


“Hi my dear… How are you?” Akajibu mgeni kwa lugha wanayoitumia wao wamarekani hawa (ila sisi tutaenda na kiswahili chetu moja kwa moja)


“Niko poa kabisa… Ajabu kubwa sana naona leo…kunitembelea jumapili wee mtu”

“Kwa kweli ni ajabu.. Ukiona hivyo nimekumisi sana, likizo yangu imekuwa ndefu sana mpenzi wangu”

“Aisee! Umekula fungate mpaka na yenyewe nayo imekujibu imetosheka, shavu limetoka kama lote..Waoooh.. hahaha hahaha hahahah, umerudi lini?” Akahoji kwa furaha tele mwanadada mwenyeji.


Mgeni hakujibu zaidi ya kuendelea kutabasamu tu huku anamuangalia mwenyeji juu hadi chini kama anamfanyia usahili wa kumuingiza kwenye mashindano ya urembo.


Walikuwa tayari wanaongozana kuingia ndani ya nyumba wakiwa mbele mwenyeji na nyuma mgeni wake ambaye kama ulivyosoma inasemekana alikuwa fungate ya harusi.


Waliingia ndani ya eneo la ndani la nyumba, mwenyeji akamuomgoza kupandisha ngazi mgeni wake mpaka eneo la juu kidogo wakapita korido iliyonakshiwa uzuri kwa malumalu zenye rangi ya kupendeza wakatokea sebuleni, sebule moja matata sana iliyopambwa kwa fenicha za kuvutia.


“Karibu! Keti sofani bwana harusi… Karibu sana… Kinywaji gani nikuletee?” Mwenyeji akaongea kwa haraka huku akimuonyesha mwenyeji kwa mkono aketi kwenye moja ya sofa kati ya masofa kadhaa ya ngozi na rangi yake ya maziwa yaliyopangwa sebuleni kwake.


“Miezi mitatu imekufanya usahau swahiba yako anatumia kinywaji gani? Hahahah! Acha hizo mwanamke” Akajibu mgeni kisha wote wakafungua kicheko kidogo.


Mwanadada wa kizungu hakuongea tena kitu zaidi ya kuelekea lilipo friji lililo sehemu ya kulia chakula (dinning).


Alirudi na bilauri kubwa lililojaa juisi ya matunda mchanganyiko ikiwa kaikamatia mkono wa kulia na glasi aliyoikamatia mkono wa kushoto.


Vyote hivi akaenda kuvitua juu ya kimeza kidogo cha kioo kilicho pembeni ya sofa alilokaa mgeni wake, akamimina juisi kwenye glasi kisha akainua uso wake ambao muda wote hakuacha kutabasamu na kumfanya kijana aliye mbele yake naye asiache kutabasamu,hii ilionyesha ni jinsi gani watu hawa wamefurahi kuonana.


“Karibu unywe mwenyewe sasa maana umeshakuwa mume wa mtu sasa hivyo siruhusiwi kuvuka mipaka na kukunywesha kama zamani nilivyokuwa nikifanya” Akaongea mwanadada wa kizungu na kicheko kikubwa kikaibuka kwao wote na kugongesha viganja vyao kimchapo kidogo kama wanaepesha mikono yao kumbe wanagonga.


“Hujaacha masikhara yako Lizy?” Akaongea huku ananyanyua glasi yenye juisi kuipeleka mdomoni mgeni.


“Naachaje sasa… au kwakuwa umeniletea mke mwenzangu wa kiarabu?” Aliongea mwanadada wa kizungu ambaye mgeni kashatujuza kwa kumuita jina la Lizy na hii kufanya tujue hapa mwanadada mwenyeji ni Lizy.


Anaitwa Elizabety Robert au kama rafiki zake na hata ndugu zake wengi walipenda kumfupisha kwa kumuita ‘Lizy Rob’ ni mwanadada mwenye umri wa miaka thelathini na tisa, mtaalamu wa kompyuta, msomi wa masters ya teknoliojia ya Tehama katika cyber crime na cyber security.


Ni jasusi wa CIA katika ofisi ya makamu wa Rais, kitengo kinachosimamiwa na katibu wa ofisi ya makamu wa Rais (Chief Of Staff To The Vice President).


Yeye Elizabety Robert akiwa ndiyo mkuu wa kitengo cha Tehama (kompyuta) upande wa ujasusi (intelligence) ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo huko Eisenhower Executive Office Building, Washington DC-Marekani.


“Umeingia lini hapa WDC? Wewe mwanaume mwenye nyayo za paka” Akauliza tena Lizy huku akitupa mwili wake kama anatupa mzigo katika sofa.


“Alhamisi…. Alhamisi ndiyo tumerudi na mke wangu hapa WDC! Maana kesho natakiwa ofisini, likizo yangu ndiyo imeisha hivyo pia niliwakumbuka sana wanangu ambao wao walitangulia kurudi kutoka Afrika sababu ya masomo yao, shule zilipofunguliwa tu”

“Fungate ilikuwa ndefu, mke mwenzangu kaufaidi mwili huo mpaka basi… Na wewe siyo kufaidi utamu wa mtoto wa kiarabu… Lete habari za huko natamani kuzijua angalau kwa kifupi tu”

“Acha zako! Sijaletwa na icho hapa… Nilishakuhadithia siku ile ulivyonipigia simu nikakwambia tupo Serengeti National Park, hakuna kilichoongezeka mwanamke acha umbeya, hahahaha hahahah hahahah!”

“Haya kama hutaki nijue na ulivyokuwa unakunja na kukunjua, ila ujio wako hapa uliokufanya ushindwe kuvumilia kesho tutakapokutana katika mjengo wa Eisenhower lazima utakuwa na jambo.. Niambiee!”

“Ni kweli nina jambo na uzuri wake nikiwa na wewe uwa sikosi ufumbuzi wa jambo hata kama itachukua muda kidogo ila nakushukuru sana uwa unanisaidia kufumbua vile vilivyofungwa ambavyo mimi nashindwa kuvifungua na maana nikaona nisikupigie simu kukujulisha nimerudi WDC ila nilitaka asubuhi hii nifunge safari ya maili nyingi toka kwangu Gillard Street, Northwest hadi huku North Underwood Street ” Akaongea mgeni kisha akainua glasi na kupiga funda moja kubwa la juisi.


“Kai!...Usiniambie shida yako ni kuacha kazi.. Maana fungate uwa na mambo mengi sana.. Mwarabu asije kuwa kashakupangia huko na kukupiga marufuku kuhusu kazi zetu….!”

“Hawezi sababu hakuna anayeweza kunipangia mimi cha kufanya katika vile vitu ambavyo vina husiana na nivipendavyo, naipenda kazi yangu… Niliomba kuachana na kikosi cha US Navy Seals kwakuwa nilichoka kudondosha watu wasio na hatia katika umri mdogo ule niliokuwa nao nikiwa kule ilikuwa inaniuma sana kuua watu ambao sikuwa hata najua idadi yake… Lakini hapa nilipo sasa hata kama nadondosha nakuwa na uhakika wa makosa yao waliyonayo hivyo siwezi kuacha mpaka pale umri wangu utakapoona inatosha mimi kuachana kabisa na mikiki mikiki au nitakapodondoshwa”

“Nakuamini sana Agent Kai… Ni jambo gani unataka tujadili?”

“Wakati niko kwenye likizo ya fungate yangu sikuwai kuifungua kabisa akaunti yangu ya barua pepe lakini jana jumamosi jioni nikiwa nimepumzika niliamua kufungua hili nipitie barua ambazo nitakuwa nimetumiwa na..” Alinyamaza kijana huyu wa kiume ambaye kwa jina sasa tushamtambua ni Agent Kai, Agent Kai Hamis ‘The Sole Cat’ kwa marafiki zake wanavyopenda kumuita kwa a.k.a hiyo inayomfanya na yeye kupenda aitwe kwa utambulisho wa siri ‘TSC’. Alinyamaza hili amimine juisi kutoka kwenye jagi kwenda kwenye glasi.


“Katika barua nyingi nilizotumiwa katika kipindi cha miezi mitatu nilichokuwa sijaacha wazi akaunti yangu ya barua pepe, barua moja iliyoingia tarehe ya wiki tatu iliyopita imetumwa kwa akaunti ambayo siifahamu ya nani? chini ya meseji fupi ile kulikuwa na ufupisho wa jina la siri la rafiki yangu ambaye niliwai kuwa naye katika kikosi cha US Navy Seals…. Nikajaribu utundu wangu kuchunguza ile barua pepe imeandikwa kutokea nchi gani na ni anwani ya nani? Na ndicho kilichonileta hapa unipatie ufumbuzi kwa mautundu yako tujue imetokea wapi na ni kweli ujumbe ule umetoka kwa huyo mtu na moja kwa moja akituma kwangu?” Agent Kai akaanza kueleza ni lipi lililomfikisha asubuhi ya saa tano kwa masaa ya Washington DC katika makazi ya rafiki yake wa kike na mkuu wa kitengo cha Tehama katika ofisi ya Makamu wa Rais.


“Ni nani huyo rafiki yako?” Akauliza Lizy huku akijiweka vizuri sofani aweze kuweka mapokeo mazuri ya atakachoelezewa.


“Mtu huyu aliwai mapema kuondoka katika kikosi chetu US Navy Seals kutokana katika operesheni moja nchini Colombia ambayo mimi sikuhusika alipatwa na tatizo akakatwa mkono wake wa kulia hivyo baada ya matibabu yake haikuwezekana kuendelea kuhudumu kikosi cha US Navy Seals kama ujuavyo kule kulivyo na kashikashi nyingi zisizo na utulivu hasa mazoezi ya kila siku hivyo alivyokaa sawa aliondolewa kikosini na akapelekwa kuwa jasusi wa Drug Enforcement Administrastion (DEA), lakini miaka saba iliyopita mimi nikiwa tayari nimehamia ofisi ya makamu wa Rais kuwa ajenti wa CIA, nilipewa taarifa ametoweka katika mazingira yasiyoeleweka akiwa yeye na maafisa wenzie wa DEA wawili ambao ni Agent Rummenige Brandts na Agent Telizo Munde na kwakuwa inasemekana walipotea huko huko Springfield, Virginia yalipo makao makuu ya DEA moja kwa moja kesi ya kupotea kwao ilishikiliwa na wao wenyewe DEA wakishirikiana na FBI ya Virginia….Maafisa kadhaa waliokabidhiwa kesi hii wakawa wanafuatilia kesi ya kupotea kwao ma-agent hawa wa DEA, hivyo mimi nikawa naulizia ulizia mara kwa mara kujua wanafikia wapi kwakuwa jamaa alikuwa ni rafiki yangu mkubwa tuliyeshibana haswa tukitenganishwa na kila mmoja kuwa mashirika tofauti… Naamini utakuwa ushawai kusikia juu ya mtu huyu anayeitwa Sajenti Johnson Greg Rautolaye, jina la utambulisho wake la siri tukiwa US Navy Seals tulikuwa tukimuita ‘Jogre’…”.Agent Kai akafafanua ni nani anayemuongelea kisha akainua glasi yenye juisi toka kwenye kimeza kilicho pembeni yake moja kwa moja ikatua mdomoni akanywa funda mbili za kufuatana kisha akairudisha mahala pake mezani.


“Si jina geni hilo kwangu sababu lipo katika orodha ya majina ya majasusi wa vitengo mbalimbali vilivyo chini ya NSA ambao wametoweka kiutatanishi na mpaka sasa haijulikani wako wapi na kusambazwa hadi kwetu CIA ila sijawai kumuona hapo kabla mtu huyo… Meseji yake inasemaje? ”

“Meseji imeandikwa kwa mtindo wa fumbo lililo kwenye mchoro uliovurugwa baada ya kuchorwa kana kwamba mchoraji alichora kisha akaona kakosea akaamua kuvuruga vuruga… Si meseji wala mchoro ulio wazi na hii inanifanya kidogo niamini anaweza kuwa yeye ni mafumbo ambayo uwa tulikuwa tunayatumia kikosini US Navy Seals tunapokuwa matatani na mpaka sasa stahili hii bado ipo huko”

“Ok! Shida ipo kwenye nini sasa? Ikiwa ni fumbo ulilofumbua maana nakujua wewe mtambo kwenye kufumbua mafumbo yaliyofichana katika vichaka”

“Fumbo kwangu si gumu kwakuwa linanihusu… shida yangu nataka kujua kile ambacho mtumaji alichoamini mpaka akatuma kwangu barua pepe hii, miaka mitano ni mingi sana kuamini kuwa mtu fulani aliye katika shughuli za kijasusi kuwa bado yupo hai sababu tunakutana na mambo mengi sana ya kuweza kutufupishia maisha yetu… Je barua imeandikwa kutokea nchi gani? Kwanini hakuandika ikaenda kwenye akaunti ya barua pepe ya DIA alipokuwa akifanya kazi? Naamini mengi katika yale ninayoyafikiria lakini pia nina mengi ya kuniwazisha mseto kuwa kuna walakini fulani unaotengeneza mtego maana Agent Kai nina maadui mpaka najiogopa na kutoamini kila ninalolipata likiwa katika taarifa isiyo na uhakika”. Agent Kai akaongea kwa kasi kama ilivyo kawaida yake aongeapo kiingereza kwa lafudhi ya kimtaani kwa wamarekani.


“Ok.. Naanza kukuelewa Kai… Unataka tuchunguze kwa umakini kuhusu mtumaji alituma kutokea wapi? Na akaunti iliyotumika ni ya nani? Je wewe hujachunguza akaunti hiyo ya e-mail ilifunguliwa nchi gani?”

“Hilo nimeweza kutambua inaonekana ilianza kutumika miaka mitatu iliyopita na sehemu yake ya kwanza kutumika kutuma na kupokea barua ni nchini Haiti ila sasa cha ajabu nilivyotaka kupata uhakika nimegundua haipo huko kwa sasa ipo visiwa vya Carribien huko Puerto Rico, shida je Jogre wakati anaitumia hiyo akaunti aliitumia kutokea huko Puerto Rico? Sasa mbona fumbo lake linanibana na kunipeleka mahala pengine ambako alama ya fumbo inaonyesha kijiografia”. Akafafanua tena kwa urefu Agent Kai huku macho yake na macho ya Lizy yakiwa yamegandana bila kupepesa wakiangaliana kwa umakini mkubwa majasusi hawa.


“Fumbo linasemaje? Ebu tuanzie hapo katika hili jambo”. Akauliza Lizy mwanadada makini mwenye ubongo hatari sana katika kujua mambo mengi ya kijiografia na teknolojia, asiyeshindwa katika mambo mengi ya kuweza kujua vilivyo fichwa kitaalamu.


Mwisho wa sehemu ya kwanza (01)


Riwaya yetu ndiyo imeanza safari ndefu katika safari tamu ya kutufurahisha na kutuburudisha kwa mikiki ya kijasusi iliyoambatana na mitwangio ya kisasa pamoja na unyama wa magenge ya walanguzi wa madawa ya kulevya yanayoongozwa na ma cartels (mabosi wakubwa wa mihadarati).


Ni fumbo gani? alilopata Agent Kai katika barua pepe aliyopokea toka kwa mtu aliyetoweka miaka saba iliyopita,rafiki yake kipenzi mtu mwenye asili ya Afrika kama yeye Sajenti Johnson Greg Rautolaye ‘Jogre’.


Je fumbo hili litampelekea Agent Kai kuchukua hatua gani baada ya mwanadada Lizy kwa kushirikiana naye kulifumbua?


Majibu ya yote haya utayapata katika mfululizo unaokujia katika riwaya hii tamu sana.




“Ok.. Nimeanza kukuelewa Kai… Unataka tuchunguze kwa umakini kuhusu mtumaji alituma kutokea wapi? Na akaunti iliyotumika ni ya nani? Je wewe hujachunguza akaunti hiyo ya e-mail ilifunguliwa nchi gani?”

“Hilo nimeweza kutambua inaonekana ilianza kutumika miaka mitatu iliyopita na sehemu yake ya kwanza kutumika kutuma na kupokea barua ni nchini Haiti ila sasa cha ajabu nilivyotaka kupata uhakika nimegundua haipo huko kwa sasa ipo nchini Puerto Rico, shida je Jogre wakati anaitumia hiyo akaunti aliitumia kutokea huko Puerto Rico? Sasa mbona fumbo lake linanibana na kunipeleka mahala pengine ambako alama ya fumbo inaonyesha kijiografia”. Akafafanua tena kwa urefu Agent Kai huku macho yake na macho ya Lizy yakiwa yamegandana bila kupepesa wakiangaliana kwa umakini mkubwa majasusi hawa.


“Fumbo linasemaje? Ebu tuanzie hapo katika hili jambo”. Akauliza Lizy mwanadada makini mwenye ubongo hatari sana katika kujua mambo mengi ya kijiografia na teknolojia, asiyeshindwa katika mambo mengi ya kuweza kujua vilivyo fichwa kitaalamu.


ENDELEA NA DODO…!


WASHNGTON DC-USA (MAREKANI)

“Shika ipad yangu uone mwenyewe halafu jaribu kufumbua wewe kama wewe nione kama kuna utofauti na kile nilichofumbua mimi ni mchoro ulio katika rafu rafu lakini una maana kubwa sana kifundi na ndiyo maana sikuiita barua pepe ya mchoro nimeiita ni barua kamili” Akaongea Agent Kai huku sasa wote wakiwa wamekaa katika sofa moja la kukaa watu wawili na masikhara yao yanayokuwepo mara kwa mara kati yao yakiwekwa kando.


Lizy aliichukua ipad ya Agent Kai na kuangalia barua pepe iliyotumwa na jogre ambao ulikuwa ni mchoro uliochorwa ambao mtu asiyehusika na ujuzi wa vitu kama hivi ukiutizama huwezi kujua kama mtu aliyetuma barua hii alimaanisha nini? Ulikuwa mchoro kama wa ovyo pengine unaweza kusema umechorwa na mtoto anayejifunza kuchora chora vikatuni si vikatuni au uchafu fulani usioeleweka kisha baada ya kuchora akauvuruga vuruga fulani lakini vuruga yenye maana sana kwa mtu kama Agent Kai au Lizy Rob kama anavyoitwa na wenzake katika idara ya shirika la kijasusi la CIA hasa kitengo kilichopo katika ofisi ya makamu wa Rais.


“Hii Kai ni karatasi iliyochorwa kisha ikapigwa picha kwa wizi kama kamera ya simu iliyotumiwa kupiga inavyoonyesha kisha ndiyo ikatumwa kwenye akaunti yako ya e-mail na ni kweli huu ni ufundi wa Navy Seals… Inaonyesha huyu rafiki yako yupo mahali ambapo hata uhuru wa kuchora vizuri mafumbo kama haya haupo, aliipataje simu? Hapa ndipo kwenye njia panda kuu… Duh maskini sijui yuko wapi?” Lizy akaongea huku macho yake kayakazia kwenye ipad.


Wote walikutanisha macho yao kana kwamba kila mmoja anamtathimini mwenzake kwa hisia kali sana kumbe walikuwa wakiunda vitu katika hisia zao kwa kutumia macho yao kwa kila mmoja kuvuta hisia kali za kifundi na si ufundi wa mchezo wa draft au soka ni ufundi wa kazi za michezo ya gizani. Michezo ya kijasusi! iliyokusanya elimu ya jiografia na hesabu kama wewe mvivu kwenye masomo hayo ukiwa ni yungali ni mwanafunzi au ulikuwa mvivu huko kipindi unasomahuwezi kuwa jasusi mwenye kuweza kupitishwa kuwa jasusi katika shirika kubwa la kijasusi la CIA lenye makao yake makuu huko Langley, Virginia, shirika lililo chini ya taasisi kuu ya ujasusi ya National Security Agency (NSA) yenye makao makuu yake huko Fort Meade, Maryland-Marekani.


Hii ndiyo taasisi kuu na namba moja ya usalama nchini Marekani ikiongozwa na mkurugenzi mkuu wa ujasusi Marekani (Director of National Intellgence) ambae vyombo vyote vya usalama vya Marekani vinaripoti na hata kupokea maagizo toka kwao kuanzia Pentagon, CIA, FBI na mengineyo katika wingi wao chini ya slogan (mwito) yao ‘Defending Our Nation. Securing The Future’.


National Security Agency (NSA) wao ndo wanahusika na kulinda taarifa za kiusalama za Marekani pia kulinda mawasiliano ya viongozi wakubwa wa Marekani na kuhakikisha viongozi wake wote wakubwa wanakuwa safe (salama) kwenye mambo yote yanayohusiana na IC&T kumbuka siku hizi ujasusi wa Human Intelligence si chaguo namba moja la taarifa nyingi za usalama kwani kuna sehemu nyingine binadamu hawezi kufika hivyo kunahitajika technology Intelligence, sasa hiyo ndiyo kazi kuu ya NSA katika Marekani.


“Nimekuja kwako najua wewe ndiyo mtu pekee katika Washington hii kama si Marekani yote unayeweza kukusanya nusu ya uliyonayo nikaweka na nusu yangu tukapata nzima itakayoweza kutupa majibu ya fumbo hili na kisha tukafika lilipo jibu la mwisho la kutoa msaada nilioombwa”

“Ni kweli Kai… Kichwa kimoja hakiwezi kufumbua haya… Huyu Jogre ameamini kwa asilimia mia mchoro huu unaoonekana wa kijingaukifika kwako utaupatia jibu, anajua wewe ni genius… Niambie wewe umegundua nini? Hili nami nijipime nimefika ulipofika”

“Umefika wapi Lizy? Usinipime nachoamini, ok! Haina shida ngoja niokoe muda nilichoona mimi katika mchoro huu… Ebu lete laptop yako unayotumia kufanya kazi zako za kazi si zile za kuangalia movie na video..” Agent Kai alitaka kukubali kumuelezea mwanadada Lizy alichogundua kwenye mchoro lakini alisita kidogo akamuomba kwanza asogeze kompyuta mpakato (laptop) ambayo ilikuwa pembeni yao kidogo juu ya meza kubwa iliyo katikati ya sebule.


Lizy alinyoosha mkono tu akainyakua laptop ambayo muda wote alikuwa ameshaiwasha, Agent Kai akaichukua akachomeka waya wa USB kutoka kwenye laptop kwenda ipad yake.


“Nataka nichore mchoro wa ndani ulivyochorwa kabla ya kuvurugwa kama umefutwa, mchoro wa ndani una maana na hata huu mvurugo una maana pia unaokamilisha maana ya mchoro wa ndani.. Kazi zetu hizi muda mwingine zinakufanya uwaze kama unakomolewa vile.. !” Akaongea Agent Kai ingali tayari kashaanza kufungua programu itayompelekea huko kwenye kuchora, huku akiutizama mchoro ambao alishauamisha toka kwenye ipad yake kuja kwenye laptop ya Lizy.


Lizy hakuwa anaongea kitu alikuwa katulia wakati mtaalamu akichora mchoro wa ndani ambao alianza kwa kuchora kitu kama mdomo wa mamba ukiwa na meno yaliyofanya kama yameng’ata kitu lakini kama ujuavyo meno ya mamba uwa hayaumani hivyo alipomaliza hapo akainua macho yake kumtizama Lizy ambaye naye akamtizama kisha akatikisa kichwa kukubali kitu.


Agent Kai akarudisha macho yake kwenye mchoro anaouchora kisha akaendelea kwa juu kuuwekea mfupa unaoonekana kwenye mchoro aliotumiwa unaonekana kama mfupa wa uti wa mgongo wa mamba pia akaishia hapo.


“Sahihi! Ufafanuzi?!!” Akasifu na kuhoji Lizy akitabasamu.


“Mchoro wa ndani uliofichwa huko hivyo bibie… Maana ya mchoro wa mdomo wa mamba na meno yake yasiyoumana lakini yameng’ata kitu ni kuwa Jogre anashikiliwa mahali kwa miaka yote aliyopotea na mchoro wa uti wa mgongo wa mamba wenye mbavu zake kwa uelewa wangu wa haraka usiopotea kwa urahisi hisia zake ni ugumu wa kumfikia na mvurugano ulioongezwa kana kwamba mchoraji alifuta ni kuwa eneo hilo ni eneo lililozungukwa na maji, pengine ni kisiwa au ndani ya maji yenyewe nikimaanisha pengine yupo kwenye nyambizi fulani kati nyambizi nyingi zilizo ndani ya bahari mbalimbali zilizotuzunguka hapa duniani ila kiukweli hisia zangu hazinipeleki huko kwenye nyambizi kuwa ndiko anakoshikiliwa mateka kwa miaka yote hiyo”. Alisimama hapo kimaelezo akiuelezea mchoro aliouchora akiutoa katika mchoro wa katika barua pepe aliyotumiwa.


“Yah! Huko sahihi na pia jina lake akaliweka ndani ya mvurugo wa kana kwamba amefuta picha… Cha kwanza ndugu yangu ningetaka kujua umevutiwa na kutaka kufuatilia hili jambo?”Akaeleza na kuuliza Lizy Rob.


“Aliyenitumia hakunitumia hivi akitaka kunisalimu, ametaka nifanye kitu, ametuma kwangu akaacha kutuma kwa watu wote anaowajua sababu anajua ukaribu wetu ulivyo ni kama ndugu wa damu toka enzi za shule na mafunzo yetu mbalimbali, anajua tulishawai fanya mengi kati yetu huku tukiahidiana mipango mingi ya kuzikabili changamoto mbalimbali katika kazi… Kumbuka mtu huyu kwa sasa ni mlemavu wa mkono mmoja hivyo anajimudu lakini si katika mambo yote ya mapambano na kipindi alichokuwa kakutwa na tatizo husika na kuwa matibabuni nilikuwa naye sambamba nikimsapoti katika hali mpya aliyokuwa nayo mpaka anakwenda DEA akiniacha mimi katika kikosi cha US Navy Seals, bado tuliendelewa kuwasiliana licha kuishi majimbo tofauti na hata mimi kutoka Navy na yeye pia aliniunga mkono na kunishauri mambo kadhaa wa kadha”. Akajibu kirefu Agent Kai.


“Sawa nimekuelewa baba.. Na je huoni ungetoa taarifa ya huu mchoro kwenye uongozi wa ofisi yake DEA wangeweza kuamua kwa uzuri zaidi kuliko sisi hapa kuumiza kichwa kuwa tunafanyaje?”Akaongea Lizy huku akijua anamuuzi Agent Kai hivyo hakumtizama usoni alijifanya yuko bize kuangalia mchoro kwenye laptop.


“Lizy, Lizy. Lizy… Nimekuita mara tatu hili ubongo wako uweze kutambua ni jinsi gani nimekuamini na jinsi gani mtumaji wa mchoro huu aliye matatizoni ameniamini mimi… Kuja kwangu kwako si kama nisingeweza fika kwenye jibu la hashaaah! Nimekuja kwako hili kwa haraka tukajua yale mengine ambayo mimi peke yangu nisingeweza fika kwa haraka.. Ondoa masihara yako na pia sukuma kando upuuzi wa kupuuzia hili nililolileta kwako… Jogre ni binadamu ni mmarekani kama mimi na wewe tulivyo wamarekani hana tofauti na wale wanasayansi nilioenda kuwarudisha kwa familia zao miezi mitatu na nusu iliyopita, Jogre ana mke wake, hakufaidi ndoa yake amekatiliwa sana yeye na hata mkewe….. Mke wake mara ya mwisho mwaka juzi nilisikia ameamua kukata tamaa na kuruhusu kuwa boyfriend, miaka kadhaa nyuma alikuwa anafanya mawasiliano na mimi lakini miaka miwili iliyopita ameacha kufanya mawasilino na mimi, huoni natakiwa kufanya kitu hapo”. Akaongea kwa kasi Agent Kai huku amekunja sura kuonyesha hajaridhika na kile alichoongea Lizy Rob.


“Umekuwa mkali Kai.. Nisamehe sana sikuwa na maana mbaya, basi nafikiri cha kwanza tuchunguze hii simu iliyotumika kukutumia barua pepe yenye mchoro wakati mtumaji anatuma ilikuwa eneo gani?” Akaongea Lizy kuomba msamaha wa masikhara yake ambayo hata naye alijistukia na kuona hapa sasa anatakiwa arudi kwenye mstari maana jamaa aliye pembeni yake ni mtu asiyetabirika sana katika misimamo yake ya anachokitaka hata iwe kwa mfanyakazi mwenzie.


“Yah! Hapa ndipo nilipokwama na ndicho kilichonifanya nikaja kwako ambako nitakula faida mbili tatu katika hili hivyo lolote utakalokuwa unafanya naomba usiache likanipita hili siku nyingine nisikusumbue” Akaunga mkono kile alichoongea mwanadada wa kizungu mwenye nywele za blonde alizoziacha zikimwagika mgongoni kwa urefu wenye kuvutia kuutizama.


Hakuendelea kukaa pale kweny sofa akainuka na kuelekea kwenye meza kubwa iliyo pembeni kabisa ya sebule hii ikiwa na vitabu vitabu kadhaa na mashine moja ya kuchapa, pamoja na kompyuta desktop (ya mezani), pale alichomoa modem akarudi nayo alipo Agent Kai.


Akaichomeka katika moja la tundu la usb la laptop yake, haikuchukua muda akaanza kufanya kazi ambayo Agent Kai alikwama kuifanya akiwa mwenyewe nyumbani kwake, kila hatua aliyokuwa akienda alienda huku aliyeomba asiachwe akihakikisha hamuachi kwa kufanya anachofanya kisha anamuangalia mfuatiliaji.


“Simu iliyotumika kurusha barua pepe hii kwa sasa ipo eneo la mnara ulio mji wa Belmopan, mji mkuu wa nchi ya Belize ni simu aina ya T-Mobile.... Program inasachi barua pepe za wiki tatu nyuma ambapo tutachambua mpaka tuione barua mchoro iliyotumwa kuja kwako ilitumwa muda gani? na eneo gani? …Hivyo kutokana na wingi wa siku kurudi siku tunayoitaka tungetulia kusubiri kwa takribani dakika tano itakuwa tayari” Akafafanua kidogo Lizy kisha akainuka toka walipo na kuelekea tena kwenye meza ambayo kwa haraka kwa mtu yoyote akiitizama atatambua ni meza ambayo mwenyeji huyu mwenye nyumba huitumia kufanya kazi zake mbalimbali anapokuwa hapa sebuleni.


Dakika tano alizosema zilipofika alirudi haraka pale alipo Agent Kai na ni kweli program ilikuwa ishakusanya data za rekodi za barua pepe za mpaka tarehe aliyotega akihitaji iwe mwisho.


“Yes.. Barua yetu inaonekana ipo hapa ila katika simu hii kwa sasa imefutwa na hii inaonyesha mtumajI alipotuma tu alifuta haraka sana… Duh! Miaka mitano yote hakupata nafasi ya kutuma chochote ila siku hii inaonyesha nyota ya jaha ilimuangukia akaokota dodo chini ya mkaratusi… Vizuri sana!, mtumaji alituma akiwa katika mnara ulio nchi ya Guatemala katika milima ya msitu huu kama dira inavyotuonyesha hapa ni milima yaTajumulco ila kando kando ya misitu hii wanalima sana kahawa.... Hii ndiyo maana ya Jogre kukutumia mchoro wa mamba akiwa ameng’ata kitu” Alikuwa akiongea huku amekazia macho kuangalia anachokiona katika screan ya laptop na alipomaliza maongezi yake akainua kichwa macho yake yakagongana nay a Agent Kai ambaye alitikisa kichwa kukubali kitu.


“Vizuri sana Lizy… Jogre yuko amewekwa mateka hapa Tajumulco je amewekwa na serikali ya Guatemala au kuna kikundi kinamshikilia? Maana kama angekuwa anashikiliwa na serikali ya Guatemala tungeweza kujua mapema maana hatuna uhasama wowote na nchi ya Guatemala ingawa nilishawai kusikika kuna magenge mawili ya kimexico yanatumia misitu ya Guatemala kama sehemu za mafunzo ya vijana wanaojiunga na magenge yao..!” Akaongea Agent Kai wakitizamana machoni kwa umakini sana.


“Sijawai kuingia sana kuchunguza juu ya magenge ya mihadarati ya huko Mexico kwakuwa hizo ni kazi mara nyingi wanazisimaia makao makuu Langley na hao DEA.. Hivyo tukitaka habari za magenge hayo itabidi tuombe msaada makao makuu ya CIA au kwakuwa una marafiki zako huko DEA ishu nyepesi kabisa… Sawa tushajua hivi niambie nia yetu sasa nini sasa? Naomba nifafanulie baada ya kujua haya kuna nini kinafuata hili tupange inakuwaje”

“Kwanza tunatakiwa kuijua Guatemala kwa undani na si juujuu kuhusu magenge ya kimexico yanayotumia misitu ya nchi hiyo kisha ndipo tutajua anashikiliwa na kina nani?, hivyo acha mimi nikachunguze mwenyewe sasa kuhusu hii kisha nitakupa jibu inakuwaje au unaonaje?…. Nafikiri kesho tukiwa ofisini tutalijadili hili angalau kidogo ila naomba uingie kazini unisaidie tena kuijua kidogo hii nchi mimi kiukweli sijawai fika Mexico hata Guatemala iwe kutembea tu au kikazi..!”.

“Sawa… Mi nitafanya hivyo.. Pia nitataka nimjue huyu Jogre wako ni mtu wa namna gani ukiacha wewe unavyomjua na kumtambua kama rafiki yako mpendwa… Kuchunguza yote hayo kutatusaidia sisi kuona tunafanyaje kumsaidia”

“Rukhsa kufanya unachotaka na umeweza kuniongoza vizuri katika kuona wapi muhimu kupitia kabla ya yote… Yote kwa yote huyu mtumiaji wa akaunti iliyotumika kunitumia mchoro huu atakuwa wa kwanza kuchunguzwa mawasiliano yake yote na hata kuwa ndiyo msaada wa kujua mengi kuhusu Jogre alipo ila kwa inavyoonekana ukitizama mtiririko wake ni mtu wa kuhama hama na sijui kwanini haipiti siku mbili tatu yeye kutuhama sehemu moja ni nadra sana i truck namba yake katika mfumo wa mawimbi ya sauti hili tuweze kunasa maongezi yake na watu anaoongea nao mara kwa mara.. ”.

“.. Sawa nitaiweka kwenye rada za mifumo yetu, kisha nitakujulisha kila kitu kama nimefanikiwa..Ila wewe ukiamua lako ni king’ang’anizi sana najua wapi tutapoenda na kudondokea kwa hili.. Mwanaume usiyependa kupumzika, safari hii mwarabu atakuonyesha nini maana ya ndoa nakwambia maana si kwa utamu ule hadi mwanamke mwenzie namtamani” Akarudi kwenye masihara yake Lizy Rob kisha wote wakacheka kwa sauti na mara kengele kutoka spika ndogo zilizo juu ya kona moja ya dari gypsum ikahanikiza pale sebuleni walipo na hii ilimaanisha kuna mtu aliye nje huko yupo getini anabonyeza swichi aruhusiwe kuingia.


“Nani huyo?” Akauliza Agent Kai kisha hakusubiri anajibiwa nini akanyanyua glasi na kuitua mdomoni kifuatacho juisi yote iliyo kwenye glasi ikahamishiwa tumboni kwa kasi.


“Mdogo wangu wa kiume amerudi alienda kanisani uwa kila jumapili anaenda kufuata pointi tatu muhimu za kwenda nazo ugenini” Akajibu Lizy Rob alipoangalia screan moja ndogo nchi 14 iliyo pachikwa na kukaa vizuri ukutani.

“Na akiwa hapa uwanja wa nyumbani uwa anapoteza pointi ngapi?” Akahoji Agent Kai uso wake ukiwa umechanua tabasamu pana.

“Hakudhidi wewe pointi unazopoteza uwanja wa nyumbani.. Loooh!!” Akajibu Lizy na wote kucheka kwa nguvu kwa kufurahia matani yao.

“Basi nikuache kifamilia zaidi mi naelekea kwangu kupumzika kisha tutawasiliana jioni tuone wewe umefikia wapi katika upekuzi wako, nami nikifuatilia kwa washikaji zangu walioko DIA kujua nitalipataje faili la kesi ya Jogre kwa waliokuwa wakipeleleza kesi ya kutoweka kwake”


Waliamua kwa pamoja mambo kadhaa wa kadha watani hawa wanaopenda kuitana wapenzi ilihali si wapenzi baada ya makubaliano yao kuhusu mambo hayo waliagana Lizy akamsindikiza hadi nje rafiki yake naye kurudi ndani akiwa kaongozana na mdogo wake wa kike ambaye alikuwa katokea kanisani.


***** ***** *****


MIAKA KUMI ILIYOPITA-MEXICO

Brigedia mfukuzwa wa jeshi la Mexico anayefahamika kwa jina Brigedia Fernandes Carlos Codrado a.k.a Brigedia Feca kama watu wake wa karibu walivyopenda kumuita alikuwa amemaliza kifungo cha miaka saba gerezani, gereza la Acapulco ambalo uwafunga wafungwa wa kijeshi waliofanya makosa wakiwa jeshini, kifungo kilichotokana na kukutwa na hatia akiwa jeshini kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kwa namna ya kificho sana akiwatumia wanajeshi wa vyeo vya chini yake ingawa kati yao walikuwemo wenye vyeo vya kumkaribia ila utii wao kwake ulikuwa mkubwa.


Alikuwa ameunda mtandao ambao ulikuwa umeunganishwa na marafiki zake walio wauzaji wakubwa wa madawa ya kulevya aina zote katika Mexico ambao wao hawakuwa katika genge kubwa linalosifika kwa unyama na ukatili wake genge la Los Zetas, Gulf Cartel au Sinaloa Cartel yeye alijihusisha hasa na wanaounda magenge madogo madogo yanayojihusisha na biashara hii haramu ya ulanguzi wa dawa za kulevya hapa duniani, mara zote alikuwa akichukia sana matendo yanayofanywa na genge la Los Zetas na hata lile la Sinaloa la Joaguin Guzman maarufu kama ‘El Chapo’ bilionea na nguli mkuu wa kimexico katika biashara ya ulanguzi wa mihadarati aliyekuwa akiishi Mexico na Colombia akifanya mengi yale anayojisikia katika pesa akichuana vikali na genge la Los Zetas lenye makao yake makuu Nuevo Laredo ‘lango la Mexico’manispaa iliyopo boda ya Mexico na Marekani jimbo la Tamaulipas.


Brigedia Feca aliingia hatiani pasipo ushahidi uliokamilika ambao ulitokana na watu waliokamatwa na mzigo kusema wao ndiyo wenye mzigo huo na si mtu anayeshutumiwa na kikosi kazi cha kipelelezi cha toka kikosi cha kupambana na mihadarati cha Mexico kiitwacho ‘Drug Trafficking Organization (DTO) kilichofanya upelelezi na kisha kuweka mtego uliowanasa watu wale.


Lakini kwa habari za kwanza za kipelelezi zilizoibua taarifa iliyowafikisha hapo zilikuwa zikitoa taarifa kuwa mtandao huu aliye juu yao ni Brigedia Fernandes Carlos Codrado, hivyo naye akachukuliwa na kisha kufikishwa katika mahakama ya kijeshi ambako hukumu iliposomwa na jaji wa mahakama za kijeshi waliokutwa na mzigo walihukumiwa miaka ishirini kila mmoja na wote kupelekwa kutumikia adhabu zao katika gereza lisilo la kijeshi la Matamoros lililopo manispaa ya Matamoros mji mkuu wa jimbo la Tamaulipas na mtu aliyekuwa ndiyo kinara wao wakiwa wamemsafisha bila kujali wao kuwa wanaingia katika adhabu kali, alihukumiwa miaka saba jela sababu kuna ushahidi ambao wao mahakama ya kijeshi walimuhusisha nao na kumuingiza hatiani na kuamriwa atumukie hukumu yake gereza la kijeshi la Acapulco lililopo jimbo la Guerrero.


Brigedia Fernandes akaingia gerezani na kuanza kuitumikia adhabu yake mpaka akaimaliza ambapo alipotoka jeshi likampa taarifa hawezi tena kulitumikia jeshi hilo aelekee kuanza maisha mapya uraiani.


Kisasi! Mara moja alijiapiza katika maisha yake mapya cha kwanza ni yeye kulipiza alichokiita kisasi kwa wale wote waliosababisha kuingia matatani katika biashara ya haramu aliyokuwa akiifanya, wale wote waliosababisha yeye kukutwa na hatia licha ya wafuasi wake watiifu kumsafisha hakuhusika na mzigo waliokutwa nao.


Kazi ikawa ni kujipanga ni jinsi gani anaweza kuifanya kazi aliyojipa ikiwa hana genge la kumsaidia na je atafanyaje kazi hii nzito?.


Mwisho wa sehemu ya tatu (03)


Agent Kai na bibie mtaalamu wa kompyuta mwenye maujuzi na mautundu yote katika ‘crakers na hackers’ bibie Lizy Robert wameweza kufika kule ambapo waliamini kunaweza kutoa majibu ya nini wafanye? Wapi waanzie na kupeana majukumu madogo ya kuchunguza masuala kadhaa na mwisho Agent Kai akaondoka akiwa na mambo kadhaa katika kichwa chake ambayo alipanga pale pale ataanza kuyafuatilia mara moja katika namna hii na ile.


Pia tumerudi nyuma miaka kumi iliyopita na kuona utokaji jela wa bwana mmoja aliyekuwa Luteni wa jeshi la Mexico ajulikanaye kwa majina ya Brigedia Fernandes Carlos Codrado a.k.a Brigedia Feca, moja kwa moja tukaona kwanini yeye alihukumiwa kwenda jela na kutumikia kifungo cha miaka saba.




Lakini kwa habari za kwanza za kipelelezi zilizoibua taarifa iliyowafikisha hapo zilikuwa zikitoa taarifa kuwa mtandao huu aliye juu yao ni Brigedia Fernandes Carlos Codrado, hivyo naye akachukuliwa na kisha kufikishwa katika mahakama ya kijeshi ambako hukumu iliposomwa na jaji wa mahakama za kijeshi waliokutwa na mzigo walihukumiwa miaka ishirini kila mmoja na wote kupelekwa kutumikia adhabu zao katika gereza lisilo la kijeshi la Matamoros lililopo manispaa ya Matamoros mji mkuu wa jimbo la Tamaulipas na mtu aliyekuwa ndiyo kinara wao wakiwa wamemsafisha bila kujali wao kuwa wanaingia katika adhabu kali, alihukumiwa miaka saba jela sababu kuna ushahidi ambao wao mahakama ya kijeshi walimuhusisha nao na kumuingiza hatiani na kuamriwa atumukie hukumu yake gereza la kijeshi la Acapulco lililopo jimbo la Guerrero.


Brigedia Fernandes akaingia gerezani na kuanza kuitumikia adhabu yake mpaka akaimaliza ambapo alipotoka jeshi likampa taarifa hawezi tena kulitumikia jeshi hilo aelekee kuanza maisha mapya uraiani.


Kisasi! Mara moja alijiapiza katika maisha yake mapya cha kwanza ni yeye kulipiza alichokiita kisasi kwa wale wote waliosababisha kuingia matatani katika biashara ya haramu aliyokuwa akiifanya, wale wote waliosababisha yeye kukutwa na hatia licha ya wafuasi wake watiifu kumsafisha hakuhusika na mzigo waliokutwa nao.


Kazi ikawa ni kujipanga ni jinsi gani anaweza kuifanya kazi aliyojipa ikiwa hana genge la kumsaidia na je atafanyaje kazi hii nzito?.


ENDELEA NA DODO..!


MIAKA KUMI ILIYOPITA, TETAPLAN, GUERRERO-MEXICO

Kila muhusika wa kadhia iliyomkumba ‘Feca’ alijiapiza moyoni mwake lazima alipe, alipe kila baya kwa kiasi anachostahili, jino kwa jino, panga kwa panga, mguu kwa mguu, hakuna jiwe kubaki juu ya jiwe lazima vyote anavishusha chini kuwaenzi wenzake waliopigana kwa kila hali kumuweka kando licha ya mateso makali na vitisho mbalimbali juu ya uhai wao, mwisho wakaenda gereza la watuhumiwa wa unga, Malaya wanaojiuza na wahalifu wengine wakubwa walioshindikana kama magaidi ni gereza linalojulikana kwa mateso makubwa nchini Mexico, gereza la Matamoros huko Tamaulipas kutumikia kifungo kirefu cha miaka ishirini ishirini kwa kila mmoja.


Mawazo yake akiwa ndani ya gari ya abiria itokayo eneo la mji wa Acapulco lilipo gereza la kijeshi yalikuwa ni jinsi gani ataweza kuinuka toka alipoamini ni chini? Wapi anakwenda kufikia ikiwa wakati anaenda kutumikia kifungo chake alikuwa ameiamisha familia yake nchini Marekani jijini Washington DC, mji wa Columbia kwa sababu za kiusalama wa familia yake.


Columbia ni kati ya sehemu ambazo katika nchi ya Marekani yeye ‘Feca’ aliweza itumia faida ya biashara zake za haramu za dawa za kulevya kununua nyumba nzuri akisaidiwa na mmoja wa mshirika wake mmoja wa kimarekani mwenye asili ya nchini kwao Mexico akijulikana kwa jina la Sergio Lopez Valdez katika makaratasi yake ya hati za uhamiaji alizotumia kuingia Marekani huku jina lake la kiasili kabisa alilopewa na wazazi wake nchini Mexico alikuwa akiitwa Puto Sergio Lopez kwa sababu ambazo aliona si sawa yeye kutumia jina la kwanza la Puto kiusalama kwa wanausalama wa Marekani wakati alipokuwa sasa anahitaji kuamia Marekani moja kwa moja Marekani na si alivyokuwa akiingia kiwizi wizi hapo kabla akiishia miji iliyo mipakani katika Mexico na Marekani.


‘Feca’ hakuwa anataka na yeye aende kuishi Marekani kisa ameachishwa jeshi, kisa familia yake haipo Mexico, akili yake ilikuwa ni kisasi tu. Hakuwa ameonewa lakini yeye hakujali hilo katika maisha yake hakuwai kuwa na msemo uliokuwa unasema ‘samehe’,toka yuko gerezani yeye sala zake za kihuni alizokuwa anaomba ilikuwa amalize kifungo chake kisha aingie uraiani kufagia jamaa aliyemdhulumu na visiki vyake au mtu huyo kumrejeshea amana yake yake yote ikiwa na faida maradufu, kisasi kwa aina zote ya vijiti na aina yoyote iliyohusika na kile alichokiita kumfuata fuata na kumkomalia mpaka afungwe.


Lakini wakati akiendelea na safari akapata wazo aelekee Manispaa ya Tetaplan, manispaa iliyopo jimbo hili hili la Guerrero ambako miaka saba iliyopita alimuacha rafiki yake mmoja, akaelekea huko na hakupata tabu kupajua kwa kuwa alikuwa ni mtu anayejulikana na wengi katika mji wa Tetaplan.


“Karibu sana Brigedia, jisikie huko nyumbani kwako… Nimefurahi sana umerudi upya mtaani, Mexico inakusubiri shujaa kama wewe miaka saba uliyopotea umeacha pengo kubwa sana hasa kwa wateja wetu wa jeshini” Alikuwa ni baba mmoja mrefu wa wastani na mwenye mwili usio mnene wala mwembamba, usoni akiwa kachonga ndevu zinazozunguka mdomo wake tunaita stahili ya ‘O’, baba wa kimexico alitoa ukaribisho kwa mgeni wake aliyeingia katika eneo la uwanja wake mkubwa wa kupumzika katika eneo la nyumba yake yenye eneo kubwa za kimraba.


“Asante sana… Nimefurahi sana kurudi mtaani na kukuta ndugu yangu ukiwa unadhidi kustawi kikila kitu, aisee hongera sana Guti” Akaupokea ukaribisho ule Brigedia ‘Feca’ mikono yao ikiwa imeshikana kikakamavu wanaitikisatikisa kwa nguvu kama wanapimana ubavu wa mikono yao.


Eneo walilokuwa lilikuwa ni eneo la katikati katika uwanja mpana uliopandwa nyasi nzuri kama vile ardhi ya hapa imetandikwa kapeti ya nyasi bandia jinsi ilivyokuwa, kulikuwa na maua mazuri ya kunukia yenye rangi mbalimbali, pamoja na miti ya kuvutia ambayo ilikuwa ikileta vivuli vikubwa eneo lote, mikokono iliyopandwa kwa kupangwa vizuri kama ipo kwenye foleni huku mbele hatua kadhaa kulikuwa na bwawa kubwa la kuogelea (swimming pool), kando kando yao walikuwa wanaume kadhaa wa umri ambao haukuwa unakabana kati yao ki rika, walikuwa ni rika tofauti tofauti wakiweka ulinzi kwake yeye Mr. Guti binafsi na eneo hili kwa ujumla.


“Dunia hii kwa sasa viongozi wake wanajifanya kuwa wao hawaihitaji kabisa biashara yetu ya dawa za kulevya lakini papo hapo wanashindwa kujiongeza kuwa hata wao baadhi yao tumewaweka sisi magenge ya dawa za kulevya kutawala nchi zao… Hahahaha hahaha hahah.. Keti kiti mwanajeshi wangu mfalme wangu mtukufu, kiukweli umenifanyia surprise kufika hapa kwangu sikuwa najua kama leo unatoka huko gerezani Acapulco….!” Akaongea Mr. Guti huku akimuelekeza kwa mkono sehemu ambayo swahiba wake ambaye hakuwa ameonana naye kwa miaka takribani saba, akae naye akakaa katika kiti cha kulala cha kistarehe chenye ladha tamu ukikitizama ladha isiyo ya mdomoni.


“Nimerudi, nimetoka kaka yangu, nimerudi tufanye kazi kisasa zaidi… Nina mipango mingi ambayo kama tutaiseti vizuri eneo lote la Amerika litatikisika na kukuna vichwa vyao hakuna cha Los Zetas wala Sinaloa na wengineo wote sisi tutakuwa juu kama utanisikiliza na kuniunga mkono Mr. Guti,wapuuzi wote watalipia upuuzi wao shenzi kabisa itakuwa jino kwa jino kuanzia walionidhulumu hadi mabwana wakubwa wanaotawala mchezo kwa sasa hapa Mexico”. ‘Feca’ akaongea kwa hisia kali zilizojidhihirisha usoni mwake.


“Nakuamini Feca.. Wakuletee kinywaji gani?”

“Wine yoyote iliyo kali sana, nimemisi pombe kali Guti… Gereza la kijeshi unaweza pata karibu vitu vingi vinavyohusu chakula na vinywaji laini lakini pombe kali hawatoi”.

“Hahahah hahahah hahahah! Pole sana.. Walitaka kumgeuza shetani kuwa malaika, hahah hahaha hahahah…!”.Guti akaongea huku akionyesha ishara ya mkono kumuita mlinzi wake mmoja aliyekuwa akiwaangalia, akijua kifuatacho atatakiwa atoe huduma kwa boss na mgeni wake.


Kijana yule alifika pale akapokea maelekezo ya boss wake kinywaji gani amletee mgeni wa boss wake kisha akaondoka kufuata kinywaji.


“Lete habari za mtaani.. Nataka kujua kila kitu kinachohusu mtaani hili nijue naanzia wapi Mr. Guti” Akaongea ‘Feca’ huku wakitazamana na Mr. Guti.


Kijana muhudumu alileta kinywaji alichoamriwa alete na boss wake kwa ajili ya mgeni wa boss wake na mara moja Brigedia Fernandez Carlos Codrado ‘Feca’ akaanza kunywa taratibu kilevi kikali cha kimexico kiitwacho ‘Tequila Tiki Chacha Alc 25%’ na kutokana na kinywaji icho kuwa kikali alikuwa akipiga funda ndogo ndogo huku anakunja sura yake.


“Mmmmh! Mmmh! Hii kitu si mchezo Mr. Guti… Aisee nilimisi sana vyombo hivi ahahahaaa Tequila.. Tunywe huku tunayapanga cha kwanza nataka kujua mtandao wako unafanya kazi vipi? kisha nijue habari za magenge mengine yote yanayoongozwa na Kingpin kama wewe ukiacha haya makubwa ambayo natambua uwezo wao” Akaongea huku akijfaragua faragua kimajivuno kama wababe wengi hasa wanaojihusisha na magenge makubwa ya biashara hizi.

“Biashara hii kwa sasa imekuwa ngumu sana lakini pia naweza kusema ugumu huo umeongeza faida kubwa na faida yake hiyo imeongezeka zaidi kutokana na ongezeko la watumiaji wa madawa haya ya kulevya kama starehe katika nchi za Marekani, Brazil, Australia na mabara ya Ulaya,Asia na hata Afrika... Ugumu wake upo kwenye mapambano dhidi ya vikosi mbalimbali vya kupambana na madawa ya kulevya vinavyoundwa na kuboreshwa kila leo na maserikali yote hapa duniani hasa Marekani” Akaanza kuelezea Mr. Guti kisha akanyamaza kidogo kumtizama Feca.


“Ila pamoja na yote hayo wanashindwa kudhibiti kwenye vyanzo vya mizigo yetu na pia hali imekuwa nzuri upande wetu katika usambazaji wetu katika soko letu kuu huko Marekani na Asia …..”Akaendelea kidogo kisha akasimama sababu mdomo wa Brigedia Feca ulionyesha kutaka kuongea.


“Kwanini huko imekuwa rahisi? Ina maana hakuna hali kama ile niliyoiacha miaka saba iliyopita? Katika nchi hiyo kubwa maana DEA wako vizuri sana”Akauliza Brigedia mfukuzwa jeshini Feca.


“Hali huko kwa sasa ni shwari kwakuwa kuna magenge ya huko yanayofanya vizuri biashara hiyo kwa kutegemea uwepo wetu kuwafikishia mzigo hadi eneo la mpakani kisha wao wakatumia njia za chini kwa chini kuingiza ndani ya Marekani… Hii ndiyo njia ambayo unaona hata nami nina mafanikio kama haya unayoyaona.. Nalipa ushuru vizuri kwa Los Zetas hivyo watu wangu wanapata msaada katika kupitisha mzigo wangu njia za panya ambazo zote huzijuazo kama hulipi ushuru Z basi huwezi pita njia za panya na mzigo bila sapoti yao hasa Marekani”

“Okay!... Oooh.. Los Zetas wanakula faida isiyo yao utafikiri wanagawa mitaji!..Miaka hii nafikiri mbinu zimebadilika zaidi… Ila sijajua kwa hapa mnapata shida gani katika biashara hii? Funguka kila kitu hili nikishapumzika na kutoa uchovu nije nikupe mpango wangu niliokuja nao nikiwa nimeuandaa kwa ufasaha kimkakati muda wote niliokuwa gerezani”

“Hapa serikali kama kawaida tunaweza kuimudu sababu tamaa bado ipo miongoni mwa askari wote na vikosi vinavyoundwa kwa ajili ya kupambana na madawa ya kulevya na hata DTO wenyewe si hatari sana wanachofanya wao ni kuhakikisha amani inakuwepo katika hali ya kuzuia mauaji ya holela kama hujuavyo magenge mengine kuua kwao ni kawaida sana… Bado wanatutegemea sana katika uchumi wa serikali za mitaa hasa katika masuala ya afya… Shida kuu ipo katika kuingiliana kibiashara bila kuachiana mipaka ya kimaeneo ya biashara katika magenge kadhaa wa kadha hasa wale watu wanaopatikana Mexico City, Tabasco, Querretero, Jalisco, Veracruz na hata eneo hili la Guerrero magenge yote ni mwendo wa kuwindana na kuporana mizigo ikiwa mnyonge basi kila siku inakuwa hasara kwako hiki ndicho kitisho kikuu katika biashara hii hapa Mexico” Akaeleza kirefu kidogo kisha akanyanyua paja kubwa la nyama ya kuku akaanza kulila taratibu akiamini maelezo yametosheleza kwa mgeni wake mfungwa aliyemaliza kifungo chake gerezani.


“Gereza la kijeshi nililofungwa ni gereza ambalo kwangu mimi ilikuwa ni ngumu kupokea taarifa kutoka nje ya gereza sababu nilinyimwa uhuru wa hata kuongea na wafungwa wenzangu kitu cha ajabu sana… Kwa miaka mitatu niliyokuwa huko sikuweza ongea na mtu mwingine ambaye si mlinzi wa gereza lile hivyo sikuwa napata au kujua lolote linalohusu nje ya gereza lile la Acapulco, nafikiri walinibana zaidi mimi kwa sababu waliamini kama nitapata fursa chache basi ningeweza endesha walichoamini ni mtandao wangu” Akaeleza Feca kisha akanywa kinywaji chake kwa kubugia funda mbili za dabodabo (kufuatana).


“Nalijua hilo Feca!... Mara mbili nilituma watu wangu waweze kuonana na wewe lakini getini pale pale wanapochukua maelezo ya wageni wanaotembelea wafungwa walizuiliwa kuingia hata ndani tu, ndipo nikapewa taarifa na rafiki yangu mmoja mwanasheria kuwa imetolewa oda toka mamlaka ya juu kuwa wewe hutakiwi kuonana na mtu yoyote mpaka utakapomaliza muda wako”

“Sikupewa mateso mule ndani lakini kuninyima uhuru wa hata kuongea na rafiki zangu au wafungwa wenzangu ni kitu ambacho nilijiahidi kuwa watakilipia wahusika wote waliotoa oda hiyo hadi watekelezaji wa oda hiyo… Nina mipango mingi sana Guti, nachohitaji kwako ni kunipa msaada wa watu wa kufanya kazi ambayo nitataka tuifanye” Akanyamaza hapo akamuangalia usoni Guti na wote wakatizamana na kila mmoja akatikisa kichwa kukubali kitu.


“Endelea nakusikiliza Brigedia….!. Mara zote niliamini ukirudi heshima yangu itaongezeka maradufu na ndicho nachokiona machoni mwako” Guti akaongea macho yao yakiwa angali yanaangaliana kwa umakini mkubwa.


“Kabla halijatokea la kutokea na mimi kukamatwa nilikuwa nimempa Fanuel Miguel Mendoza mzigo mkubwa wenye thamani ambayo naamini mpaka muda huu alifurahi sana mimi kukutwa na hatia kisha kwenda gerezani, nilikuwa nimempa mzigo wa white cocaine ounces 5000 grams lakini wakati kesi yangu inaendelea kusikilizwa katika mahakama ya kijeshi nilimtuma mtu kwake hili anipatie nusu ya pesa ya mzigo niliompa lakini majibu yake aliyoniletea nilijua nishadhulumiwa kwa sababu aliamini siwezi kujinasua katika kesi na akaona kwake ni fursa… Mtu wa kwanza nataka nianze na huyu hili nirudi katika nguvu yangu, nataka maelezo ya kina kuhusu Fanuel!”


“Mmmh! Kwanini hukunipa ujumbe toka kipindi icho kabla hujahukumiwa si ningeshafuatilia na tukajua imekuwaje, Fanuel kwa sasa hapa Mexico ni mmoja wa ma ‘kingpin’ wakubwa hashikiki hata mimi siwezi kukupa tumaini kuwa tunaweza mfuatilia na kupata haki zako kama hujuavyo biashara hizi wewe si mgeni ukishapigwa umepigwa ukidai kama mtu atakuelewa unashukuru na endapo mkashindwa kuelewana mtaanzisha vita kubwa sana au lah usamehe na kuacha mambo yaende kawaida tu”


Brigedia Feca alimtizama Guti jicho kali mpaka anayetizamwa akatupia macho pembeni kwa ukali wa macho ya anayemuangalia.


“Upuuzi huo Guti… Umenisahau? Mimi ni mwanajeshi komando mbobezi mwenye nishani ya juu katika medani za kivita, mimi ni mwalimu wa wanajeshi wengine, huwezi niambia kuwa Fanuel ‘kingpin’ yupo juu kibiashara hii basi nimuache aendelee kutanua kwa mtaji uliotoka katika jasho langu na akili zangu… Anajua mimi nilipataje mtaji wangu? Niambie anapatikana wapi kwa sasa, yupo hapahapa Guerrero au wapi?”


“Yeye kwa sasa ndiye kashika ngome yote ya Tabasco na miji yake yote, yeye ndiye Mfalme wa Tabasco na hata gavana wa jimbo lile anatokana na yeye kumpigania mpaka akashinda uchaguzi kama ujuavyo mwaka huu ndiyo ulikuwa mwaka wa uchaguzi wa majimbo hivyo alitumia fursa ya uwezo alionao kipesa na mengine kumsaidia Gavana Morientes Gao kuchukua ushindi na kwa mantiki hiyo Gao anaongoza Tabasco kwa matakwa na utashi wa Fanuel Mendoza pia ni mwanachama wa Los Zetas, wanampa sapoti kubwa ya kiulinzi katika mambo yake ya kusafirisha mizigo yake inasemekana analipa kwa mwezi pesa nyingi kwao hili asibugudhiwe na magenge mengine licha ya yeye kumiliki genge ambalo mimi silijui jina lake kwakuwa sikuwa namfuatilia kabisa mambo yake zaidi ya kujua juu juu….. Alikimbia hapa Guerrero mwaka ule ule uliofungwa, sikujua kama amehama sababu ya kuhofia kuwa ulimpa mzigo mkubwa… Kwa kweli ounces 5000 ya white cocaine ulimpa mtaji mkubwa sana, mtaji unaompa kichwa mpaka sasa sababu mizigo yote ya kutoka Cali na Peru anapelekewa yeye na genge analolitumikia nalo linapokea mzigo toka huko pia inakosemekana wana mashamba na viwanda vya siri huko.. Nahofia anaweza akataka kukuua akijua umetoka gerezani hata mimi kanisahau kabisa kuwa alikuwa anaonana nami akiwa nawe”


“Hahahah! Hahahah hahahah!... Brigedia Feca nimetoka, Brigedia Feca niko mtaani, sijazeeka bado lazima nifanye kitu na kwakuwa umetahadhalisha basi sina budi kuwa makini… Kwa sasa nitaomba hifadhi hapa kwako kwa huku nikiweka mambo sawa wakati huohuo nifanye mawasiliano na familia yangu huko Coumbia, Washngton DC wahame kwa muda walipo maana nikianza vita yangu wataingia matatizoni nina nyumba Kentucky huko hakuna wa Mexico wengi hivyo wataishi bila kufahamika kirahisi”.


“Ukweli huko hivyo Guti… Utemi wa kukurupuka bila tahadhali kwa sasa hapa Mexico hakuna ilasitaki uwaze kushindwa.. Fanuel ni mtu wa hatari kwa sasa hapa Mexico naye ni mmoja wa watu wanaoogopewa na serikali si wa kumuingilia kizembe lazima utaumia inatakiwa ujipange kweli kweli lazima ukienda na muhemko anaweza akakurudisha ukiwa hujitambui na hujiwezi kabisa… Mimi na kikosi kidogo sana mimi ni muuzaji wa kawaida sana ingawa unaona kama mambo yangu ni safi sana.. Kwa Fanuel hamna kitu kabisa, namiliki watu hawa kwa sababu ya kulinda biashara yangu isiporwe lakini sishiriki michezo kama waliyonayo magenge mengine..”


“Aiseeh! Anaweza kuwa anamiliki jeshi la watu wake wangapi?”

“Ana kikosi kipana ambacho kwangu hiki nilichonacho ni kidogo sana.. Mimi nina walinzi na wasambazaji wa mzigo wangu wachache ambapo pia hao hao ndiyo uwa wananisindikiza ninapoenda chukua mzigo na mzigo wangu wote unatokea Bolivia, sina uwezo wa kuingia njia za watu wanaopokea mizigo yao toka Peru, Colombia na Belize.. Huko ni kwa watu watemi, wababe kama wao kina Fanuel”.


“Shenzi! Fanuel anatambia mzigo wangu, Guti! Pesa anayotumia ni jasho langu na akili yangu”. Akawaka kwa sauti Brigedia Feca mpaka walinzi wa Guti wakaongeza umakini kuangalia pale walipo hawa wanaofanya maongezi, wakihakikisha usalama wa bosi wao Guti.


“Calm down! Feca… Unastua watu kwa kupaniki kwako.. Naona kwanza upumzike hili kesho asubuhi baada ya breakfast tuongee vizuri ukiwa ushapumzisha akili yako… Mambo haya ukiyakurupukia unaweza ukaharibu kila kitu kabisa, mimi kwa kweli mpaka sasa nashukuru sijawai ingia katika vita na wauzaji wenzangu wa uwezo wangu na hata wakubwa zaidi iwe wa hapa Guerrero na hata nje ya hapa, hivyo nakusihi upumzike kwanza kisha kesho tutapata fursa ya kujadili tunafanyaje”


“Ooooopuh! Sawa Guti acha nisubiri asubuhi pengine naweza nikaja na jambo ambalo litaleta wazo zuri zaidi”.


***** ***** *****


Saa mbili na nusu asubuhi ya siku ya pili iliwakutanisha tena kimaongezi Brigedia Fernandes Carlos Codrado ‘Feca’ na Mr.Villa Nandez Guti. Katika chumba cha maongezi cha Mr. Guti katika mjengo wake wa kifahari uliopo eneo la Sierra Madre Del Sul ililopo wilaya ya Petatlan Municipality, moja ya manispaa kati ya manispaa nane zinazounda jimbo la Guerrero.


“Vipi usiku wa kwanza? katika nyumba ambayo huko huru kabisa” Akaanza kwa swali Mr. Guti baba mwenye jumba hili la kifahari na uzuri wake wa kuvutia.


“Nimelala kama mtu aliyeweka mguu sehmu kisha akatoa katika hali ya kukanyaga kupiga hatua.. Sababu nilipojigeuza tu nikiwa macho nilipokuja kustuka jua tayari linapiga usawa wa dirisha wa chumba nilicholala, kumekucha kimatani sana”. Akajibu Brigedia Feca huku akitabasamu.


“Hahahah hahahah hahahah! Lakini ulitumikia kifungo chako ukiwa gereza la kistaarabu… Vipi haukuwa unalala vizuri huko kama ulivyolala hapa?” Akauliza tena Guti.


“Hata kama ningelala kwenye kitanda cha ikulu ya Washngton white house, bila uhuru nisingeweza kulala kwa raha na kufurahi” Akajibu Feca wakagonga mikono yao kuonyesha furaha yao ya maongezi yao yakianza hivyo.


“Umeamua nini? katika yale tuliyoacha jana hili utulie ukiwaza na kupata ufumbuzi” Akabadili gia haraka Mr. Guti kwa kuuliza swali ambalo ndiyo haswa kilichowakutanisha hapa asubuhi.


“Nimeamua kisasi juu ya kisasi” Akaongea kifupi Feca kisha akajiweka vizuri katika sofa alilokaa, mgongo akiwa kauegemeza katika egemeo la sofa la kukaa watu wawili ila yeye alikuwa anajimwaga kwa raha zake peke yake.


“Kwa jinsi nilivyokusiiliza jana nahisi kisasi chako si cha kwenda kwa mtu mmoja tu.. Nyoosha mipango nami nitasimama kama mshauri naweza kutoa mawazo kipi kifanyike na kipi kisifanyike”




“Cha kwanza nataka niwapate watu wangu wote waliofungwa kwa ajili ya kunilinda bila kujali walipoteza nini.. Nawahitaji bila kujali kama ni gharama kiasi gani kuwatoa, ni jukumu langu mimi kulipa fadhila kwao kwa kuwatoa.. Nawaamini sana watu hao sababu kwanza ni wanajeshi wenzangu hivyo ni watu muhimu katika kazi yangu ya kulipa kisasi na kurudisha mali zangu”


“Wamefungwa miaka ishirini kila mmoja, huoni haiwezekani suala hilo?”

“Nia… Nia ndiyo jambo muhimu bila kuwa na woga wowote…. Brigedia wa jeshi mwenye mafunzo ya nguvu hivyo mimi kama mimi sidhani kama nitashindwa kufanya na kutimiza ndoto yangu”


“Mexico ina magereza mengi na kwa mujibu wa idadi ya watu wako waliohukumiwa kipindi icho ni idadi ya watu nane, je unafikiri wanaweza kuwa wote wamefungwa gereza moja?”.


“Hapa ndipo itabidi tuingie kazini tuache kazi tufanye kazi… Piga ua garagaza kati ya nane wale tuwapate angalau watano tu kama wote itashindikana na mpango uanze mara moja hili tusiwe nyuma na wakati ndugu yangu”


“Sawa niko tayari tushirikiane kwanza kuwapata hao watu wako. Naamini bila wao unaamini hauwezi.. Nakusikiliza wewe sasa katika mpango huu, mi nitafuata maelekezo yako na kufanya kile utakachohitaji kimsaada, mi si wale wanaosahau fadhila wewe kwangu una thamani kubwa sana nathamini mchango wako kwangu na laiti ungenipatia mimi hiyo ounces 5,000 ungelikuta jeshi kubwa na faida kubwa hii leo ungekuwa unagawa hisa wewe kama boss”


“Ahsante sana Mr. Guti… Wewe ni jembe kubwa sana nafurahi kwa msaada wako na upendo wako wewe ni kaka yangu sitakuacha kwa vyovyote vile” Akaongea Brigedia Feca kisha wakapeana mikono kwa furaha wakitingishana kwa furaha kama watu wanaopimana ubavu.


“Naomba nitafutie watu wawili watatu unaowajua walio katika mamlaka za magereza hayo yasiyo ya kijeshi”Akaongea tena Brigedia Feca.


“Sawa… Acha nimuite msaidizi wangu yeye ndiyo mara nyingi anashughulika na mambo ya huko magerezani kwa watu wetu wanaokuwa wanashikiliwa na magereza kisha wanakuwa na umuhimu kwetu wa namna moja ama nyingine”


“Vizuri.!”.


ENDELEA NA DODO ASALI..!


MIAKA KUMI ILIYOPITA, GUERRERO-MEXICO

Guti aliinuka sofani alipokaa akamuacha Feca akaelekea kwenye korido ndefu inayokwenda nje ya nyumba, dakika moja mbele akarudi na mwanaume mmoja wa kizungu kama wao walivyo wazungu wa Mexico wenye kufanana kila kitu na wazungu wa kihispaniola, tofauti ya huyu baba wa kizungu na Mr. Guti ni kuwa yeye alikuwa mrefu sana mpaka Brigedia Feca ambaye alikuwa kakaa kwenye sofa ilimbidi kuinua sura yake zaidi hili amtizame usoni mbaba aliyeongozana na Mr. Guti wakifuatana sambamba na hata mavazi yao waliyovaa yalikuwa yamefanana katika mashati yao suruali tu ndiyo walipishana sababu mtu mrefu alivaa suruali ya kitambaa chepesi wakati Guti alivaa jeans nyeusi huku mikono yake ikiwa na michoro ya sura za watoto wake aliyochora kwa mchora tattoo mmoja maarufu huko New York jiji la gharama kubwa kimaisha huko Marekani.


“Brigedia Fernandes kutana na msaidizi wangu anayeratibu mambo yangu yote ya kila siku, anaitwa Ivan Alberto a.k.a ‘alto’… Na Ivan nafikiri unamjua huyu mtu ni nani?” Akatoa utambulisho wa haraka Mr. Guti baada wote kuchukua nafasi za kukaa katika masofa yaliyo pembeni ya sofa alilokaa Brigedia Fernandes.


“Hakuna asiyemjua Brigedia ‘Feca’ hapa Mexico.. Nimefurahi sana kukutana na komando mkubwa sana katika Mexico hii, habari zako hazina kificho… Karibu sana uraiani kaka!” Ivan au pengine unaweza kumuita ‘alto’ kwa kiingereza ‘Tall’ na kwa Kiswahili ‘mrefu’, akasema huku akijitahidi kutaka kutabasamu kitu ambacho ni kigumu sana kwake na si kama anapenda asiwe anatabasamu ni kwamba taya zake zimeshikizwa na waya zilizowekwa kwa ndani katika operesheni iliyotokana na yeye kuumia kwa kuvunjwa taya zake katika pilika pilika zake za kihatarishi, hali hii pia umfanya asipende kuongea mpaka iwe lazima sana na utayari wa kupokea maumivu atakayoyasikia.


Brigedia Fernandes aliligundua hilo kutokana na kumtizama vizuri na kumuona anavyogugumia kulazimisha atabasamu kwa tabu.


“Nawe pia navyokutizama nazisoma alama nyingi kwako kuwa si mtu wa mchezo mchezo, naamini Mr. Guti ana mtu pacha wa mambo yake na ndiyo maana hayumbi anakwenda vizuri katika ushindani wa biashara hii hapa Mexico” Brigedia Fernandes akaongea huku akitabasamu.


“Yah! Ivan ni mtu wa kazi kweli kweli mwenye kujua anafanya nini si mwenyeji wa hapa Guerrero anatokea mji wa Nuevo Laredo lango la Mexico huko Tamaulipas, nilikutana naye Guatemala mji wa Iztapa katika mishe zangu nikaona mtu ndiyo huyu niliyekuwa namuhitaji, mtu mwenye uwezo wa kufanya lolote popote… Muelekeze kila kitu unachotaka mimi sasa ni msikilizaji tu ila yeye mara nyingi anatumia karatasi kuandika maelezo kwa sababu hayuko vizuri kuongea ana matatizo katika taya”. Mr. Guti akaongea kisha akanyanyua mguu wake wa kulia kuupachika juu ya wa kushoto, tunaita kuweka nne sisi waswahili haswa.


“Sawa sawa… ‘Alto’! niko hapa kwa mambo mengi yatakayoleta manufaa kwa pande zote endapo sote tutakuwa makini na kufanya yale ambayo yapo katika mkakati wangu… Kuwa makini unisikilize ‘Alto’ sababu wewe sasa ndiyo utakuwa mhimili wangu na wetu kwa ujumla katika kile ambacho nakifikiria katika kukifanya Mexico, bara lote la Amerika kusini na kaskazini pamoja dunia nzima kutujua sisi ni kina nani? Kama sasa wanavyoijua Los Zetas na hata Sinaloa ya El Chapo.... Ila yote ya hayo kabla sijaenda mbele zaidi tunahitaji nguvu ya kufanya hayo kwa ufasaha huku tukisaidiwa na msaada wa pesa maana hatuwezi kufanya chochote kati ya yale yaliyopo katika mkakati kazi” Alieleza Brigedia Fernandes kisha akapumzika kidogo akaacha kumtizama ‘alto’ akageuza uso kumtizama Mr. Guti alivyokaa mkao wake wa kupiga nne huku akivuta sigara yake aina ya marliboro na sasa akijitwisha na miwani meusi ya kiFBI katika macho yake na si kama anataka madoido fulani, hapana! Mara zote akivuta sigara bwana huyu upenda kuvuta akiwa kavaa miwani kuzuia moshi usimkere machoni mwake (sijui kwa wenzake walio karibu sababu hakuwa anajali hilo).


“Kufungwa kwangu kumefanya watu wengine kuinuka katika biashara hii ya haramu kupitia jasho langu na mtu huyo sasa ana jina kubwa sana katika biashara yetu hapa Mexico hivyo nalitaka jasho langu bila kujali yeye ni nani katika nchi hii, anafanya nini? Na ana nguvu kiasi gani? Nachotaka yeye ni kuwajibika kwa usaliti na dhuluma aliyonifanyia… Ila hakuna nguvu hiyo katika kundi lako lazima tupate nyongeza ya nguvu itakayoweza kutusaidia tukafanikiwa katika mpango nilionao” Akanyamaza tena Feca na safari hii hakuzungusha sura yake zaidi ya kumimina kahawa iliyokuwa kwenye chupa ya chai yenye nakshi nakshi ya dhahabu kwenda kwenye kikombe kizuri cha udongo cheusi kisha akanyanyua kikombe na kupiga funda moja la kahawa kavu na chungu.


“Unanipata Alto? Akampachika swali Ivan ‘alto’ baada ya yeye Feca kushusha kikombe chini kwenye meza ndogo ya kioo yenye maurembo yaliyonakshiwa vizuri madini ya dhahabu kiasi ya kwamba mtu kama mimi nikipewa hii meza na chupa ya chai iliyopo hapa juu ya meza yenye kahawa basi napata kagari kazuri tu cha kuzunguka zunguka mitaani.


“…Nakupata boss!” Akajibu ‘alto’, mwenye sifa ingine ya kulazimishwa na mdomo wake kutopenda kuongea kabisa kama alivyotahadhalisha mapema Mr. Guti kuwa maongezi kwake ni nadra zaidi ni vitendo na maandishi anayoandika kwenye vikaratasi vidogo anavyotembea navyo mfukoni mpaka muda mwingine watu wengine umuhisi ni bubu.


“Cha kwanza nahitaji kuwapata vijana wangu niliokuwa nafanya nao kazi nikiwa jeshini yaani wao wakawa wanasambaza mzigo kwa wanajeshi wateja wetu tuliokuwa nao katika jeshi, wanaume wale walikuwa nane ila hata nikiwapata watano tu itatosha, wale watu ni watu muhimu sana kwangu pia ni waaminifu waliokula yamini juu yangu, hivyo tupo hapa kwa mambo mengi lakini jambo kuu la kwanza ni kupanga misheni itakayofanikisha sisi kuwapata watu ninaosema kwa gharama yoyote ile kisha ndipo tutakuja kwenye operesheni ya pili itakayomuhusu aliyenidhulumu na kuwa sasa anatanua kwa jasho langu ambalo hajui hata nilijikamua vipi jasho hilo” Akaeleza Feca huku mkono wake kulia ukihakisi alilonalo kifuani mwake kwa kuutingisha ukiambatana na ngumi iliyokunjwa barabara.


“Watu hao bwana ‘alto’ ndiyo walionifanya mimi nikuite hapa tuweze kujadili kwa pamoja na kuona tunafanya nini kuweza kuwapata maana kama unavyojua magereza yetu ya Matamoros tukiingia watu wa unga kama sisi mateso yake uwa makali sana na kufanya wengi kupoteza maisha” Akaingilia maongezi Mr. Guti kisha akaendelea kuvuta sigara yake hii ikiwa ya pili sasa.


“Nawaamini vijana wangu, miaka saba ni michache sana kwao haiwezekani wakawa wameshindwa vumilia mateso watakayokuwa wamepewa huko ni wanajeshi wale si raia wa kawaida ni watu wenye mafunzo makali sana si mbugila mbugila na hata kama wangefungwa lile gereza la raia la Acapulco lenye mateso makali zaidi ya la Matamoros pia wangeweza kuvumilia mateso na kusurvive” Brigedia Fernandes akampinga Mr. Guti kwa wazo alilotoa kisha ukimya ukatokea kwa sekunde kadhaa na ‘alto’ akatikisa kichwa na kuonyesha ishara ya mkono kuwa Feca aendelee.


“Cha kwanza katika misheni hii tunatakiwa kuwapata makamishina wa maaskari magereza wenye vyeo angalau watatu au hata wawili wanaweza wakatosha wawe wa makao makuu ya gereza au wenye uwezo wa kutuunganisha na mtu mkubwa aliye makao makuu kama hao ambao wewe au nyinyi hamna mtu wenu katika makao makuu ya jeshi la magereza…. Maafisa hao wa jeshi la magereza wawe wenye kukubali kutusaidia kujua walipo watu wetu na pia kukubali kutusaidia jinsi gani tutaweza kuwapata watu wetu.. Ni hayo alto na sasa ni kazi kwako kuona tunafikaje kwenye mstari ninaoomba uwe wa kwanza kufikiwa na kufanyiwa kazi”Akamalizia hapa Brigedia Fernandes na macho yake makubwa yakazunguka kuwaangalia wanaomsikiliza kwa umakini mkono wake wa kushoto ukichezea ndevu zake zilizotoka kwa urefu kushuka chini kama ndevu za beberu na kukiziba kidevu chake chote, alto alikuwa akitikisa kichwa chake kama mwendo wa kinyonga anayejongea kukatiza bara bara isiyo na magari mengi.


Kukapita ukimya wa dakika mbili kisha Ivan ‘alto’ akatia mkono kwenye mfuko wa suruali akaibuka na peni pamoja na karatasi jeupe dogo tu.


Akaanza kuandika andika kwenye karatasi alipomaliza akaiinua karatasi ile na kumpa mkononi Brigedia Fernandes ‘Feca’.


Kulikuwa na majina katika karatasi ile, majina yapatayo mawili na yakiambatanishwa na vyeo vyao wahusika walioandikwa na hii mara moja ilimfanya Brigedia kutambua majina yale ni watu alioomba watafutwe na kwa vyeo vyao alitambua ni maaskari magereza.


“Itabidi uzoee Brigedia kama nilivyosema awali… Ni kwamba mara nyingi alto hutumia vitendo na maandishi kwenye mawasiliano na akiongea huongea mara chache kutokana ana matatizo katika taya zake aliyoyapata miaka kadhaa iliyopita huko huko kwao Nuevo Laredo.. Ndiyo maana anatembea na peni na karatasi kama hizi, amekuandikia majina hayo sasa ni sisi ndiyo tutakaofanya nao mawasiliano hao aliowaandika kwenye karatasi au tunaweza muachia kazi hii yeye akawatumia wasaidizi wake nako hakutaharibika jambo” Mr. Guti akarudia kufafanua kwanini Ivan hapendi kuongea kama inavyoonekana hapendi.


“Haina shida Guti… Nilivyomuona tu nilijua tatizo nini? Mbona mshono wake huko wazi tu kwa sisi watu wa masuala ya kivita inaonekana kirahisi tu…. Nafikiri hili suala la kufanya mawasiliano na watu hawa tumuachie yeye alto afanye nao mawasiliano kwa nitakachofanya mimi kwa sasa ni kumpa majina ya wafungwa hao na mara moja asubuhi hii hii mawasiliano yaanze maana hatuna cha kusubiri kazi ianze mara moja, ndani ya wiki moja hii ya kwanza tuwe tushawapata watu wetu na kisha tufanye kikao cha pili tukiwa wote na walio gerezani ndipo operesheni yetu itahamia kwenye kusaka nguvu ya kipesa kwa kuchukua mtaji wangu ulio mikononi mwa fedhuli mlima Fanuel Miguel Mendoza ‘kingpin’ anayetanua kwa jasho lisiloliwa na hapo ndipo tutaunda mkakati madhubuti utakaotuwezesha sisi kuwa genge tishio tukikamata maeneo yote yanayoshikwa na watu wanaojifanya majeuri sasa na ndipo dunia itatutambua sisi ni watu wa namna gani” Akaongea kimsisitizo wenye jeuri kubwa Brigedia Fernandes.


“Nimeelewa boss!” Akaongea kifupi Ivan kisha akatoa karatasi ingine toka mfukoni mwake akaandika kwa dakika mbili nzima alipoinua macho yake akamkabidhi karatasi ile Feca naye akaanza kuisoma.


Yalikuwa ni maelekezo apewe siku nzima ya siku hii waliyokuwa wamekutana hapa pia akaelekeza watu hao ambao ni maaskari magereza wenye vyeo kati yao wawili atawaleta pale mjengoni keshokutwa yake na watazungumza nao vizuri tu.


Fernandes ‘Feca’ kwakuwa alishaanza kumuelewa alto naye alitingisha kichwa kumkubalia ombi lake na dole gumba lake likisaidia kusapoti.


***** ***** *****


SIKU MBILI MBELE…!

Ilikuwa ni siku ya jumatano, siku mbili mbele za toka Brigedia Fernandes Carlos Codrado ‘Feca’ atoke katika kutumikia kifungo chake.


Muda wa saa tano na nusu katika eneo lile lile ambalo hajawai kutoka toka arudi mtaani toka huko gerezani, muda huu walikuwa wamefika wageni wawili katika mjengo wa Mr. Guti.


Wakiwa wameletwa na msaidizi wa Guti, Ivan ‘alto’ au kama vile nilivyokwisha elezea ‘olta’ ni kihispania unaweza kumuita kwa kiingereza ‘tall’.


“Karibuni waheshimiwa! Msihofu hao ni walinzi wetu ni wajibu wao kuwakagua hili nasi mabosi zao tukaamini katika usalama wetu” Akaongea akiwa kwa ndani Mr. Guti, kwakuwa naye muda huo ndiyo alikuwa anafika hapa kwake kutokea katika mambo yake mengine ya ulanguzi wa mihadarati alikuwa walinzi wake wa mlango mkubwa wa kuingia ndani ya eneo la uwanja mkubwa ambao wageni wake mara nyingi wakifika uwa wanafikia eneo hili kwa ukaguzi kwanza ndipo waingie ndani.


Ukaguzi ulimalizika na wale wageni wakaingia eneo la ndani kisha kamlango kadogo kalicho pembeni ya geti kubwa la kupita magari, kalifungwa na walinzi wakasogea pembeni kazi yao ikawa imeisha.


Guti akawaongoza wageni wale akiwa sambamba na msaidizi wake Ivan na walinzi wao binafsi wapatao watatu kwa kila mmoja na kwa hapa wakiwa sita na wote wana bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG).


Walitembea wakipita maeneo mazuri yaliyopandwa nyasi bandia zenye kupatiwa huduma haswa inayostahili katika huduma za nyasi, miti mifupi na mirefu ya mikokono inayokwenda juu ikinyooka pamoja na miti yenye kwenda juu na kutawanyika kwa ajili ya vivuli na bustani mpaka karibu na swimming pool (bwawa la kuogelea) hapo walimkuta Brigedia Fernandes ‘Feca’ akiwa ametulia katika moja ya viti vya kulala huku pembeni yake ana mvinyo wa pombe kali aina ya Tequila, hii pombe ilikuwa ishamvutia na mara zote alipenda kupata hii kitu kimiminika toka arudi uraiani kutoka gerezani.


“Karibuni wageni..!” Aliongea haraka baada ya kuwaona kisha akainuka hili apate kupeana nao mikono ya salamu.


“Ahsante sana boss!” Wakajibu kwa pamoja wageni kisha wakasalimiana wote kwa mikono na Mr. Guti akawaonyesha kwa mikono viti mbalimbali vilivyo pale pembeni ya swimming pool wapate kukaa.


Kila mmoja alishika hatamu ya kiti alichoona ni sahihi yeye kukaa wakati Mr. Guti yeye pamoja na Ivan walikaa viti vinavyoangalia upande walipo wageni wao. Wakati huohuo walinzi wakasogea hatua ambazo si rahisi wao kusikia mazungumzo ya mabosi zao waliowaajiri.


Ivan ‘alto’ hakutaka kuchelewa mara moja akatoa karatasi na kumpa Brigedia Fernandes ambaye naye akaikunjua na kuanza kuisoma.


“Wageni msisubiri kuhudumiwa sababu hakuna muhudumu atakayekuja, mbele yenu hivyo vinywaji mnavyoviona vipo kwa ajili yetu kuvishambulia mpaka unapoona umetosheka, karibuni”. Akaongea Mr. Guti huku akiachia tabasamu la ukarimu linaloficha unyama alionao kwa binadamu wenzake kuwaharibu kwa ulevi mbaya wa kutumia madawa ya kulevya.


Wageni wale mmoja akainuka na kuchukua chupa kubwa ya kinywaji cha Martins na glasi mbili akarudi mahali pake kisha akampa glasi mwenzake na wote wakawa wanatabasamu na hili liliwajulisha kina Guti kuwa wageni wao ni watu wanaojuana nyendo zao kwa ufasaha na ndiyo maana wanajuana hadi aina kinywaji wanavyopenda kunywa.


“Wageni huku mkiendelea kunywa naomba nitoe utambulisho maana mimi ndiyo mwenyeji wenu hapa na nyote naamini mnatambua hilo sababu Guti ni jina kubwa hapa Guerrero na miji yake yote” Mr.Guti akaona wakati Brigedia Fernandes anaendelea na usomaji karatasi aliyopewa na alto yeye aendelee na utambulisho kwanza.


“Aliyewaleta hapa alto siwezi sema lolote juu yake, mimi kama nilivyosema naitwa Mr. Guti siwezi jielezea lolote kwenu sababu nyote mwanijua vilivyo na pia tushawai kukutana mara mbili mara tatu kama sikosei… Utambulisho mkubwa kwenu ni kwa mtu aliyeomba nyie mfike hapa ila pia naamini hamtastuka kusikia jina lake sababu naye pia ni jina kubwa sana hapa Mexico… Kutaneni na mheshimiwa wetu mkuu Brigedia Fernandes Carlos Codrado a.k.a Feca na Brigedia Fernandes kutana na wale watu ulioomba wafike hapa kwa ajili ya kazi unayotaka kuwaomba kutusaidia, huyu wa kushoto anaitwa Kamishina Fergata Maxiwell Ginger kutoka makao makuu ya jeshi la Magereza na kulia ni Kamanda Persuan Lureta ni mkuu wa jeshi la magereza ukanda wa jimbo letu la Guerrero” Akatambulisha Mr. Guti, wakati huo huo Brigedia Feca alikuwa amemaliza kusoma karatasi aliyopewa na Ivan ‘alto’.


“Karibuni sana wageni wetu… Kama mlivyoambiwa mimi ndiyo niliyewaita nyinyi hapa kwa kazi ambayo pia nashukuru alto ameshawaeleza kwa mujibu wa hii karatasi kilichoandikwa ni kuwa nyinyi mmekubali kile mlichoambiwa na alto, majina ya watu naowahitaji kujua habari zao ni haya hapa” Akaongea Brigedia Fernandes kisha mwisho akatoa karatasi ambayo ilikuwa katika mfuko wa shati alilovaa akampa Ivan aliye karibu na wageni wao ambaye naye akanyoosha mkono na kukisafirisha kwenye mkono wa aliyetambulishwa kwa jina la Kamishina Fergata Maxiwell Ginger na mara moja akaanza kukisoma kikaratasi kile chenye orodha ya majina ya watu wa kazi anaowaamini sana Brigedia Feca.


Kilipita kimya cha dakika tano Fergata akisoma majina yale na kwa kutumia peni yake akawa anapiga tiki katika karatasi ile taratibu baada ya kuwa katika tafakari kama mwalimu anasahihisha mitihani.


Alipomaliza akampa mwenzake aliyekuja naye Kamanda Persuan Lureta ambaye naye akakipitia taratibu na alipoinua macho yake akamtizama rafiki yake kisha akanyoosha mkono kumrudishia karatasi ile Ivan “alto’.


Ivan kikawa njia moja kwa moja akakipasia kwenye mkono wa Brigedia Feca.


“Hao sita niliowapigia tiki ni kwamba ndiyo ambao najua tunawezaje kuwapata kwakuwa wako sehemu ambayo tunaijua lakini hao wengine wawili mmoja alifariki mwezi mmoja uliopita na huyo Kanali Simon Oli Dogot alipelekwa gereza ambalo wewe ulifungwa humo, gereza la Acapulco na ni kutokana na cheo chake isingewezekana yeye kufungwa gereza za raia wa kawaida… Hivyo umemuacha huko” Akatoa ufafanuzi kamishina Fergata Maxiwell Ginger.


“Duh! Dogot mashine mtu wa hatari sana.. Shenzi! Kumbe walimleta kule Acapulco… Basi Kamishina ninaomba niwapate hao sita na sasa jinsi ya kuwapata mnaweza sema nyie tunafanyaje sasa?” Akaongea na kumalizia kwa swali Brigedia Feca.


Kabla maafisa wa magereza hawajaongea chochote, Ivan akatoa kikaratasi katika mfuko wake kisha akamkabidhi mkononi Feca.




“Karibuni sana wageni wetu… Kama mlivyoambiwa mimi ndiyo niliyewaita nyinyi hapa kwa kazi ambayo pia nashukuru alto ameshawaeleza kwa mujibu wa hii karatasi kilichoandikwa ni kuwa nyinyi mmekubali kile mlichoambiwa na alto, majina ya watu naowahitaji kujua habari zao ni haya hapa” Akaongea Brigedia Fernandez kisha mwisho akatoa karatasi ambayo ilikuwa katika mfuko wa shati alilovaa akampa Ivan aliye karibu na wageni wao ambaye naye akanyoosha mkono na kukisafirisha kwenye mkono wa aliyetambulishwa kwa jina la Kamishina Fergata Maxiwell Ginger na mara moja akaanza kukisoma kikaratasi kile chenye orodha ya majina ya watu wa kazi anaowaamini sana Brigedia Feca.


Kilipita kimya cha dakika tano Fergata akisoma majina yale na kwa kutumia peni yake akawa anapiga tiki katika karatasi ile taratibu baada ya kuwa katika tafakari kama mwalimu anasahihisha mitihani.


Alipomaliza akampa mwenzake aliyekuja naye Kamanda Persuan Lureta ambaye naye akakipitia taratibu na alipoinua macho yake akamtizama rafiki yake kisha akanyoosha mkono kumrudishia karatasi ile Ivan “alto’.


Ivan kikawa njia moja kwa moja akakipasia kwenye mkono wa Brigedia Feca.


“Hao sita niliowapigia tiki ni kwamba ndiyo ambao najua tunawezaje kuwapata kwakuwa wako sehemu ambayo tunaijua lakini hao wengine wawili mmoja alifariki mwezi mmoja uliopita na huyo Kanali Simon Oli Dogot alipelekwa gereza ambalo wewe ulifungwa humo, gereza la Acapulco na ni kutokana na cheo chake isingewezekana yeye kufungwa gereza za raia wa kawaida… Hivyo umemuacha huko” Akatoa ufafanuzi kamishina mdogo Fergata Maxiwell Ginger.


“Duh! Dogot mashine mtu wa hatari sana.. Shenzi! Kumbe walimleta kule Acapulco… Basi Kamishina ninaomba niwapate hao sita na sasa jinsi ya kuwapata mnaweza sema nyie tunafanyaje sasa?” Akaongea na kumalizia kwa swali Brigedia Feca.


Kabla maafisa wa magereza hawajaongea chochote, Ivan akatoa kikaratasi katika mfuko wake kisha akamkabidhi mkononi Feca.


ENDELEA NA DODO ASALI…!


MIAKA KUMI ILIYOPITA, GUERRERO-MEXICO

SIKU MBILI MBELE

Nywele zilimsisimka Brigedia huku akipatwa na hisia kali kutokana na kile kilichoandikwa na huyu msaidizi wa Mr. Guti. Ilibidi Brigedia ainue macho kuyakutanisha na macho ya ‘alto’ ambaye alimtizama tu lakini macho yake yalikuwa yanaonyesha dalili ya kuwa anatabasamu kifuani mwake.


“Aisee alto mpango huu umeupanga saa ngapi? Mbona umenisapraiz sana.. Aisee wewe ni kichwa sana” Brigedia Feca aliongea kisha akashindwa jizuia akampa mkono wa pongezi muandika vikaratasi.


“Safi sana Ivan” Akamwambia.

“Ahsante..!” Ivan akajibu kama ilivyo ada yake kuongea kwa tabu akiwa anaongea haraka kwa kuibia.


“Mr. Guti una kamanda wa hatari sana…. Aisee sahivi ndiyo natambua kwanini umemchagua huyu mtu toka Nuevo Laredo kuwa msaidizi wako na mpangaji wa kila kitu katika genge lako, mtu huyu anastahili mshahara mkubwa sana na usiombe kumpoteza muombee hudumu naye wakati wote mtu huyu asiye na maneno zaidi ya vitendo… Nimeupitisha huu mpango kwa asilimia mia moja” Akaeleza Brigedia Feca na haraka akarudisha macho yake katika karatasi aliyopewa akarudia kuisoma kwa umakini.


“Nilikwambia Brigedia kuhusu alto… Huyu mtu nilivyokutana naye niligundua kipaji kikubwa alichonacho na moja kwa moja nikafanya naye makubaliano nakuja naye hapa Guerrero, anaogopewa, anaongoza na anapanga mipango vizuri kabisa na hakuna ramani aliyochora tukafeli katika game vitendo ni genius” Akatoa sifa zinazostahili kwa msaidizi wake Mr. Guti.


“Hongera sana alto… Jamani nyote naomba mnisikilize kwa makini, huu ni mpango alioupanga kwa umakini kamanda wetu alto…” Akaongea Brigedia Fernandes kisha akasimama na kuwaangalia kila mmoja kwa zamu kati ya wageni wao.


“Cha kwanza mheshimiwa Brigedia tambua watu wako wapo kwenye gereza ambalo mtu yoyote mhalifu ambaye serikali inatambua kiasi cha uhalifu ufungwa huko, gereza la Matamoros katika mji wa Tamaulipas hivyo kuwatoa watu katika gereza hili itahitajika kazi ya ziada na mbinu kubwa ya kusukwa” Akaongea kamishina Fergata Maxiwell Ginger kisha akatulia akimuangalia Brigedia Feca.


“Nilihisi hilo kabla na ninajua yote Kamishina kuwa si kazi rahisi… Ila kwa mpango huu alioundaa alto nafikiri kuna namna pale… Na namna kuu iliyopo ni safari bubu kama mpango ulivyoainishwa” Akaongea Brigedia huku akipitia mistari aliyoona ina maelekezo yaliyo kichwa zaidi.


“Waheshimiwa katika plan hii aliyoiandaa Ivan alto inaonyesha tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja kwa kuucheza mchezo ambao utafanya serikali isijue kama wafungwa wametoroka, wanatakiwa kujua kuwa wamekufa wote”Akaanza Brigedia Fernandes kueleza mpango ulioandikwa katika karatasi moja tu na mutu ya kazi Ivan ‘alto’.


“Kivipi hapo? Sijaelewa itakuwaje?” Akauliza kamishina Fergata ambaye yeye ndiyo alikuwa mwepesi kuuliza maswali na hata kuingiza mawazo yake katika maongezi ya hapa yenye mpango mkakati wenye nia ya kuwatorosha wafungwa anaowahitaji Brigedia Fernandes.


“Yaani kuna njia ya kwanza ambayo mimi upande wangu nimielewa sana na kuipitisha kuwa inaweza ikafaa zaidi ingawa pia nasita kwakuwa itabidi mpango ushirikishe watu wengi na kwa ilivyo mpango wa wengi wasio kambi moja uwa ni mpango hatarishi… Mpango unahitaji watu wetu wasafirishwe kutoka gereza lile kwenda gereza lingine na wakiwa njiani ndiyo tuwatoroshe” Akaeleza tena Brigedia na wakati akieleza ‘alto’ alikuwa akiandika katika karatasi yake na alipoona Brigedia amenyamaza akainua mkono wake akimaanisha wasiendelee kuongea kuna kitu anaandika pengine kufafanua zaidi mpango wake.


“Tusubiri genius alto aandike atakacho, nafikiri kutakuwa na ufafanuzi utakaotusaidia zaidi” Akaongea Mr. Guti kwa mara ya kwanza toka amalize starehe yake ya kuvuta sigara kama tatu mfululizo alizokuwa akizipuliza kwa kasi kana kwamba ni mashindano ya kuvuta sigara.


Alto alimaliza kuandika akampa karatasi Brigedia Feca naye haraka akaanza kupitia kilichoandikwa, dakika tatu zilitosha kusoma kilichoandikwa na kukifikiria katika ubongo wake na akadhidi kumuongezea max za juu huyu mfungwa nyaya kwenye taya zake.


“Safi sana nimelipokea hili alto, ni wazo zuri zaidi… Jamani alto anapendekeza hili tupate urahisi juu ya hili tumshirikishe mtu aliye jeshini, tukimpata mtu huyo mwenye cheo ataomba kwa maafisa wa gereza

la Matamoros kuwa anawahitaji wafungwa wakaendelee na kifungo chao katika magereza ya kijeshi… Hivyo kazi hii itabidi mimi niweke sawa kisha kamishina mkuu wa taifa wa jeshi la Magereza huko makao makuu Mexico City ataingia mtegoni na kusaini na akisha saini wewe Fergata utakuwa unatupa maelekezo yote jinsi itakavyokuwa kwa kutokea huko makao makuu nasi tutajiandaa kuvamia na kuwatorosha watu wetu” Akaongea Brigedia na kuinua macho yake kuwatizama kwa zamu watu waliopo pale.


“Lakini hamuoni itatuwia tabu kumpata huyo mtu wa huko jeshini? kwani atakuwa anajua kuwa mpango ukivuja kazi hana” Akaongea na kuhoji kamanda Persuan Lureta.


“Mexico hii hakuna jambo gumu Kamanda Persuan…. Mimi ni mwanajeshi niliyefukuzwa, mkufunzi wa mafunzo jeshini nina marafiki zangu wengi katika jeshi la Mexico, wengi wao wakiwa ni wanafunzi wangu… Hivyo kesho nitakutana na afisa mmoja atakayefanya kazi ya kimaelekezo vipi naweza fanikisha mpango wa kupata saini ya kuomba uhamisho wa watu wetu kutokea makao makuu ya jeshi ofisi ya sekretarieti ya nidhamu ya jeshini na ndipo mpango utakuwa umetiki kwa wafungwa wa waliokuwa wanajeshi katika gereza la Matamoros huko Tamaulipas kuja gereza la Acapulco, Guerrero” Akaeleza Brigedia Fernandes kwa kujiamini zaidi.


“Ndicho kitu walichokuwa wamesahau maafisa hawa kuwa hapa anayeseti mchongo huu ni Brigedia wa jeshi aliyefukuzwa jeshini na si Brigedia wa mtaani tu” Akaongea Mr. Guti kwa mbembwe nyingi na vitendo maana mikono yote ilikuwa ikimsaidia kusindikiza maneno na kichwa kikifuatisha.


Watu wote walio pale walicheka vicheko vya sauti kidogo ukiacha alto aliyefurahia kifuani mwake bila kuishirikisha sauti katika furaha yake.


“Kwa kweli mimi nilijisahu kidogo si mnajua ni ngumu sana kuingilia mambo ya jeshini huko sisi askari magereza tunadili sana maafisa wa polisi kuliko wanajeshi hivyo nilihisi kutakuwa na zengwe fulani” Akafafanua kamanda Persuan.


“Usijali! Hakuna kufeli naamini tutafanikiwa katika kila tunalopanga” Akasema Brigedia Fernandes ‘Feca’.


“Je? Tukishafanikiwa kuseti mpango kipi kitafanyika maana mlisema mmepanga waonekane wamekufa hili kesi zao zifutwe kimtindo huo” Kamishina akauliza, swali likielekea kwa Brigedia.


“Tutakuwa tumeshaandaa maiti za wanaume wa idadi ya watu wetu, maiti ambazo zitakuwa zimekatwa vichwa, mikono kuanzia kwapani na miguu kuanzia magotini kushuka chini kisha tutazivalisha nguo za wafungwa tutakaokuwa tumewaokoa… Muunda mkakati ameeleza vizuri kuwa kwakuwa tutakuwa tumemuua dereva atayekuwa anaongoza msafara pamoja na askari wengine watakaokuwa na kazi hiyo ya kuwaamisha na kisha kufanya kama nilivyosema, tutaacha karatasi ya onyo kuwa tumelipiza kisasi kwa wanajeshi hawa waliofungwa sababu walikuwa wametudhulumu na hii ndiyo ilikuwa ni nafasi yetu kuwapata na kuwaangamiza” Akajibu Brigedia na wapo walioelewa somo vizuri na wakatikisa vichwa vyao kukubali.


“Maiti hizo mtazipata wapi?” Akauliza kamanda Persuan.


“Kupata maiti rahisi hiyo kazi mtuachie sisi.. Kinachotakiwa kabla ya yote mtu mmoja aende kuwaona wafungwa wetu huko gerezani hili alete jibu la uhakika kwa kuwapiga picha kijanja tukagundua afya za miili yao zilivyo” Akajibu Brigedia kwa umakini.


“Sheria ya magereza yetu hairuhusu kuingia na kamera kuwaona wafungwa na kuwapiga picha”. Kamishina akaeleza alijualo kwa haraka.


“Atakayeenda ataenda na kamera ndogo ya siri, hamjui kama zipo kamera hizo? Au na nyie mlikuwa wafungwa hamjui kuwa kuna kamera hizo za kijasusi kama peni na hata miwani na saa ” Akajibu Brigedia na pia kupachika swali humo humo, huku alto akimtizama kwa umakini akitikisa bichwa lake kukubali maelezo ya Brigedia kuwa yako sahihi na mazuri sana, wengine nao wakakubali.


***** ***** *****


Ilikuwa ni saa saba na dakika arobaini mchana wa siku ya siku ya alhamisi, baada ya lunch time (chakula cha mchana).


Muda huu katika eneo la uwanja wa mashindano ya mchezo wa ng’ombe wakubwa (bulls) wanaotumika katika maonyesho ambayo watu uingia kuangalia binadamu anavyotishana na ng’ombe huku ng’ombe huyo akimshambulia kwa kasi naye kutumia ufundi na maujanja kumuepa, mchezo huu ni mchezo ambao unapendwa sana na wa Mexico wengi sana wake kwa waume mpaka watoto wadogo.


Kiwanja hiki ambacho ni kiwanja kinachomilikiwa na hotel ya nyota tano ya Fiesta Americana Acapulco Villas ni moja ya sehemu maarufu sana ya starehe katika jimbo kubwa la Guerrero, ni sehemu ya aghali sana kimatumizi wanapokutana watu wenye ukwasi wa kutosha kuangalia michezo mbalimbali ukiwemo huu wa ng’ombe (bulls), watu wa matumizi hasa wazungu wa unga (wafanyabiashara wa mihadarati) hapa ni kama kituo kikuu kwa starehe zao za michezo mbalimbali.


Jukwaa la VIP ndipo mahali ambapo Brigedia Fernandes akiwa ameambatanaa na Ivan a.k.a alto walikuwa na kikao cha siri na afisa mmoja wa jeshi la Mexico, mwenye cheo cha Luteni kanali.


Afisa huyu wa kijeshi aitwaye Luteni Kanali Gumendez Cassilato aliomba wakutane eneo hili baada ya Brigedia Fernandes ‘Feca’ kumtafuta usiku wa jana na kumuomba kuwa ana maongezi naye.


Aliona ni vizuri wakakutana eneo hili muda huu kwakuwa kunakuwa hamna watu ukiacha kule kwenye eneo la bar ya hotel na ndani ya hotel yenyewe.


“Kaka! Hujabadilika kabisa licha ya kukaa gerezani miaka saba… Nimefurahi sana kukuona mwalimu wangu”. Akaanza kuongea Luteni Kanali Gume kama wenzake walivyokuwa wanamkatizia kumuita jina lake kwa kifupi Gume.


“Hata wewe hujabadilika kabisa hata hivyo miaka saba haiwezi kumbadili mtu kwa kiasi kikubwa zaidi labda apate tatizo kama ugonjwa na mambo mengine kama hayo yenye uwezo wa kumbadili mtu”


Walikumbatiana kwa furaha kubwa sana huku pembeni yao akiwepo ‘alto’ anawaangalia tu watu wa kazi wa jeshi, mmoja akiwa yupo kazini na mwingine mtimuliwa.


“Nimetoka Ltn.Knl Gume lakini sina kazi tena… Waliotaka nisiwe na kazi wamefanikiwa kwa raha zao” Akaongea Brigedia Feca wakiwa bado wamekumbatiana.


“Lakini hakuna anayeweza kukufanya ukaishi kwa tabu.. Wewe ni mwanaume mwenye nguvu na akili.. Pole sana kamanda wangu na mwalimu wangu, nimeitikia wito sema chochote unachotaka nakusikiliza sababu hatutakiwi kukaa sana hapa kwa usalama wangu na kazi yangu endapo tutakutwa”.


“Sawa kijana wangu sitakuchelewesha… Nina msaada ninaouhitaji kwako” Akaongea Feca na sasa walikuwa wameachiana katika kumbatio lao na kila mmoja kasimama akimtizama mwenzie, walikuwa pembeni ya jukwaa la VIP, kwa chini karibu na geti kuu la kuingilia watu wanaoingia eneo hili jukwaa hili hivyo kulikuwa hakuna viti vya wao kukaa kwa pale walipo.


“Sema mkuu wangu… Niko tayari kukusaidia lolote lile lililo ndani ya uwezo wangu” Luteni Kanali Gumendez akakubali ombi la kumsikiliza anachohitaji.


“Katika makao makuu ya jeshi huko Mexico City kwa sasa nani? anashika kitengo cha nidhamu ya wanajeshi ofisi ya Secretariat Of The Navy”

“Meja Manuel Fuerza Sanz ndiyo anashika kitengo cha nidhamu, bado hajabadilika toka wewe upatwe na matatizo yako, vipi kwani?” Luteni Kanali Gume akajibu na kuhoji.


“Nahitaji msaada wako maana yeye hawezi kunisaidia mimi kama mimi lakini unaweza kunisaidia nikampata mtu aliye katika ofisi ile akafanya jambo la kutusaidia kupata sahihi yake na mhuri wake utakaogongwa juu ya sahihi yake kuhidhinisha jambo fulani” Akaongea Brigedia Fernandes ‘Feca’ kisha akaacha kuongea baada ya kuuona mshtuko katika sura ya Luteni Kanali Gume.


“Ngumu sana hiyo… Ngumu kufanya hivyo Feca, sababu wasaidizi wake walio katika ofisi ile hakuna ninayemjua labda hujaribu njia ingine”

“Njia gani Gume? Nishauri nifanyaje maana bila sahihi yake hakuna tutakachoweza”

“Je haukufikiria hilo wakati unapanga mpango wako? Mwalimu wa wanajeshi katika matumizi ya silaha na mapigano…Unapopanga A lazima uwe umepanga na B hili A ikifeli B ifanye kazi.. Samahani nimekukumbusha maneno uliyokuwa ukiniambia wakati unanipa mafunzo mwalimu wangu… Tuache hayo mwalimu…Niambie jambo gani hilo unalotaka? Unataka kupata haki zako ulivyokuwa kazini?”

“Haki? Haki zangu? Hapana sitaki kufuatilia hizo kwa kwanza sababu bado sijazeeka kama kuzifuatilia nitazifuatilia nikifika miaka sitini na wala pia usifikiri nataka kuomba nirudishwe kazini hapana sitaki kurudi kazini nataka wale vijana waliofungwa kwa sababu yangu katika kesi ile iliyonifanya nami nikafungwa wahamishwe kutoka gereza la Matamoros, Tamaulipas hadi gereza la kijeshi la Acapulco, wale ni wanajeshi hawatakiwi kuendelea kutumikia kifungo chao sawa na raia wengine hasa katika gereza baya na la kutisha lenye ukatili wa kila aina kama gereza la Matamoros,Tamaulipas”Akaeleza Brigedia Fernandes akionyesha sura ya kuwa na uchungu mkubwa sana kwa anachokieleza kuhusu watu wake huko walipofungwa.


“Feca! Watu wako ni wanajeshi kama sisi, jeshini tumefunzwa uvumilivu wa kila hali… Kwangu mimi naona ni sawa tu au labda tungefanya mpango wa kisheria wapunguziwe miaka kama itawezekana”

“Luteni Gume! Sawa inawezekana tukajaribu hilo kwa unavyoona? Mimi sioni kama inawezekana kukata rufaa hiyo na tukafanikiwa, naomba msaada huo na wewe ndiye msaada kwangu sababu wewe ndiyo mtu wangu wa karibu uliye kazini”

“Ebu tufanye ungeenda Mexico City ukaonane na mwanadada aitwaye Koplo Mariana Funtes, huyu dada anashirikiana na magenge ya uhalifu na ni rahisi kumuingia, yupo katika ofisi ya Secretariat Of The Navy na ndiye sekretari wa Meja Manuel Fuerza Sanz na nilivyokwambia sina nimjuaye nilisema vile kwa sababu sikujua unahitaji nini kutoka huko ofisi ya nidhamu ya wanajeshi… Jibu la kazi yako lipo kwa Mariana”

“Namuingiaje wakati hatujuani? Inatakiwa wewe uniunganishe naye na kwakuwa siku zinakimbia sana naomba yafanyike leo leo hayo hili twende na spidi kazi kuwasaidia watu wangu, wamenisadia sana kufanya nisifungwe miaka mingi”

“Nitakuunganisha naye mkuu… Mariana ni swahiba wangu haitakuwa na shida yeye kukusaidia jambo unalotaka tena kwa ufasaha sana maana navyomjua anafanya mengi sana ikiwemo hadi kuuza silaha akifanya hayo kwa kushirikiana na wakuu wengine walioko makao makuu ya jeshi wenye kufanya biashara za kuwauzia silaha magenge ya wauza madawa ya kulevya” Akafafanua Luteni Kanali Gumendez.


“Sawa nitaenda na msaidizi wangu huyu… Nitaondoka hapa Guerrero leo leo, usiku nitataka unikutanishe na Mariana hili kuona anatusaidia vipi?”

“Acha nimpigie usikie navyoongea naye pia nawe utaongea naye hapahapa kumuelekeza kidogo kisha mtapanga muonane wapi huko Mexico City!”


Maongezi yao yaliendelea kidogo kisha Luteni Kanali Gumendez akapiga simu kwa Mariana wakaongea akamuelekeza msaada anaotaka kwake napo pia akampa simu Brigedia Fernandes ambaye naye akajitambulisha wakafikia makubaliano waonane saa ngapi huko Mexico City kilometa 225 tokea Guerrero.


Mwisho wa sehemu ya tano (05)


Bado tupo miaka kumi iliyopita, tukinyumbulika kiufasaha katika fasihi andishi hii yenye ladha tamu toka kwa watu wa kazi.


Tumeona Brigedia Fernandes ‘Feca’ akianza kupiga hatua kuingia ndani ya mpango wake akisaidiwa na mtaalamu mrefu toka jimbo la Nuevo Laredo.


Kikao cha Brigedia Fernandes ‘Feca’ na Luteni Kanali Gumendez Cassilato kilichofanyika uwanja wa mashindano ya ng’ombe wakubwa (bulls) kimefikia kwa maamuzi ya kuwa mwanajeshi aliyeko kazini kumsaidia kwa namna anayoweza yeye mwalimu wake kufanikisha alichoomba wakutane hapa.


Nini kitafuata?




“Feca! Watu wako ni wanajeshi kama sisi, jeshini tumefunzwa uvumilivu wa kila hali… Kwangu mimi naona ni sawa tu au labda tungefanya mpango wa kisheria wapunguziwe miaka kama itawezekana”

“Luteni Gume! Sawa inawezekana tukajaribu hilo kwa unavyoona? Mimi sioni kama inawezekana kukata rufaa hiyo na tukafanikiwa, naomba msaada huo na wewe ndiye msaada kwangu sababu wewe ndiyo mtu wangu wa karibu uliye kazini”

“Ebu tufanye ungeenda Mexico City ukaonane na mwanadada aitwaye Koplo Mariana Funtes, huyu dada anashirikiana na magenge ya uhalifu na ni rahisi kumuingia, yupo katika ofisi ya Secretariat Of The Navy na ndiye sekretari wa Meja Manuel Fuerza Sanz na nilivyokwambia sina nimjuaye nilisema vile kwa sababu sikujua unahitaji nini kutoka huko ofisi ya nidhamu ya wanajeshi… Jibu la kazi yako lipo kwa Mariana”

“Namuingiaje wakati hatujuani? Inatakiwa wewe uniunganishe naye na kwakuwa siku zinakimbia sana naomba yafanyike leo leo hayo hili twende na spidi kazi kuwasaidia watu wangu, wamenisadia sana kufanya nisifungwe miaka mingi”

“Nitakuunganisha naye mkuu… Mariana ni swahiba wangu haitakuwa na shida yeye kukusaidia jambo unalotaka tena kwa ufasaha sana maana navyomjua anafanya mengi sana ikiwemo hadi kuuza silaha akifanya hayo kwa kushirikiana na wakuu wengine walioko makao makuu ya jeshi wenye kufanya biashara za kuwauzia silaha magenge ya wauza madawa ya kulevya” Akafafanua Luteni Kanali Gumendez.


“Sawa nitaenda na msaidizi wangu huyu… Nitaondoka hapa Guerrero leo leo, usiku nitataka unikutanishe na Mariana hili kuona anatusaidia vipi?”

“Acha nimpigie usikie navyoongea naye pia nawe utaongea naye hapahapa kumuelekeza kidogo kisha mtapanga muonane wapi huko Mexico City!”


Maongezi yao yaliendelea kidogo kisha Luteni Kanali Gumendez akapiga simu kwa Mariana wakaongea akamuelekeza msaada anaotaka kwake napo pia akampa simu Brigedia Fernandes ambaye naye akajitambulisha wakafikia makubaliano waonane saa ngapi huko Mexico City kilometa 225 tokea Guerrero.


ENDELEA NA UTAMU..!


MEXICO CITY-MEXICO

Restaurant La Mansion Camino Real, mgahawa uliopo ndani ya hotel maarufu jijini Mexico inayoitwa Hotel Camino Real Aeropuerto Monterrey Fundidora iliyopo mtaa wa Penon de Los Banos, mtaa uliopo karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mexico City, jiji kuu na makao makuu ya nchi ya Mexico.


Mwanadada Mariana Caro Funtes, Koplo wa jeshi la Mexico akihudumu tokea makao makuu ya jeshi alikuwa amekaa katika moja ya kiti kati ya viti vitatu vinavyoizunguka meza moja ya duara iliyopo pembezoni mwa mgahawa huu muda huu wa saa mbili usiku aliokuwa ameekeana ahadi na wageni wake wanaotokea jimbo la Guerrero baada ya kuwa walishamtaarifu wameshatua na ndege iliyowaleta jijini hapa, ndipo akawapa maelekezo wamkute hapa.


Mgahawa ulikuwa umechangamka muda huu kwa watu wa jinsia tofauti wengi wao wakiwa ni wenyeji wa nchi hii walikuwa wamefika kupata maakuli pamoja na vinywaji, vyakula vinavyopatikana hapa vilikuwa ni vyakula vinavyopikwa kwa ustadi na ubora wa hali ya juu toka kwa wapishi walioajriwa hapa wakiwa ni wapishi bora kabisa toka nchi mbalimbali, hivyo kila aina ya chakula kilipatikana hapa ukitaka hata ugali wa kitanzania nao pia ulipatikana endapo tu utatoa oda ya kuutaka basi unapikiwa.


Koplo Mariana aliagiza supu ya kitamaduni inayotengenezwa kwa mchanganyiko wa nyama na ndizi ni supu inayopendwa sana na watu wa Mexico, ikiitwa na wenyeji wa hapa kwa jina la ‘pozole’, akaletewa na kuanza kuipitisha njia zake kwenda kunako tumbo, pembeni akisindikizwa na kinywaji laini cha kimexico kiitwacho Sangria Soft Drinks iliyo katika chupa kubwa inayofana na chupa ya kinywaji cha kilevi cha Grants.


Akiwa katikati ya mlo wake simu yake aina iPhone 5s ilianza kuita akaitazama na kusoma namba na mara moja akamjua mpigaji ni nani? Akatupa macho huku na huko pengine atamuona anayepiga kwake kisha akaipokea.


“Hallow! Mshafika?” Akauliza baada ya kuiweka sikioni.

“Ndiyo…. Huko sehemu gani?” Upande wa mpigaji ukaongea.

“Pembezoni kabisa mwa kona ya mashariki ni karibu na korido inayoelekea kwenye ngazi zinazoelekea yalipo majengo ya hotel”

“Ndiyo tunaingia, nimevaa shati jepesi la rangi ya njano lenye maua maua meusi na ndevu zilizoshuka kidevuni kama beberu na kwakuwa hatufahamiani tunafuata muelekeo uliotuelekeza mwenzangu kavaa suti ya rangi nyeusi na kofia ya pama ni mrefu sana”

“Ha ha ha..... Yes! Nimewaona sogeeni mbele mtaniona niko kwenye meza iliyo na mdada mmoja tu ambaye ni mimi, sogeeni mbele yaaah!” Koplo Mariana aliongea huku mkono mmoja kauinua juu kupunga hili aonekane na ni kweli wageni wake walimuona.


“Waoooh! Mrembo ni wewe?” Akaongea Brigedia Fernandes a.k.a Feca mkono akiwa kaunyoosha hili wakamatane mikono na mwanadada Mariana Funtes.


“Ni mimi Brigedia… Heshima yako mkuu?” Akajibu na kutoa salamu wakiachiana mikono.


Koplo Mariana alitamani kumpigia saluti Brigedia lakini macho ya watu yalimfanya apige kimya asije akazua minong’ono.


“Nashukuru bado ipo na itaendelea kuwepo… Aisee Koplo umependeza sana, mnatunyima nini Mexico City?”

“Hamna kitu zaidi ya kuwanyima ubize na kazi zisizokuwa na mwisho kila siku… Habari za safari yenu huko angani mpaka barabarani mlivyokuwa mnakuja hapa?”

“Nzuri tu… Nafikiri tumefika kwa wakati mrembo”

“Yah! Mmewai tu wala msihofu… Agizeni chakula hili tukianza maongezi yetu tuanze mazima bila usumbufu wowote” Koplo akawaambia na kwakuwa muhudumu alikuwa kashajileta haikuwa tabu wakaagiza kila mmoja chakula anachovutiwa nacho usiku huu, muhudumu akaondoka kufuata alichoagizwa.


“Navyokutizama naona picha yako kuwa nishakuona mara nyingi tu Brigedia ni sahihi?” Akauliza Koplo Mariana huku akitabasamu na kufanya uso wake ung’ae kama ujuavyo wanawake wa kimexico (walatino) wengi wanavutia sana.


“Itakuwa umeziona picha zangu, miaka saba iliyopita nilivuma sana katika media za hapa Mexico ila nashukuru nimetoka hakuna media iliyoandika Brigedia Fernandes kamaliza kifungo chake”


Muhudumu alifika na kapu la chano aliyobebea vyakula alivyoagizwa na akagawa kwa kila mmoja kwa stahili yake.

“Karibuni wateja” Akatoa ukaribisho wa chakula muhudumu na wote waliokuwa pale wakatikisa vichwa vyao kukubali.


“Ni kweli nimekumbuka nilipokuona ni kwenye gazeti na hata ofisini kwetu ila kwakuwa mwaka ule uliokuwa umepatwa na tatizo nilikuwa sipo ofisi niliyopo sikuwa nimefuatilia mambo mengi yanayokuhusu… Okay tuyaache hayo tutajuana zaidi na zaidi mara nyingine tukikutana” Koplo aliongea na kutoa ishara ya mkono maongezi yaliyowaleta pale yaanze mara moja.


“Nimeambatana na msaidizi wangu anaitwa Ivan a.k.a alto yeye si mtu wa maongezi, usishangae kuona kuwa hataongea chochote na kama anataka kuchangia kitu kutumia karatasi kutuandikia… Tumetaka kuja kuonana na wewe moja kwa moja hili tuweze kupanga na kukubaliana mambo kadhaa wa kadha….!”

“Ngoja usiendelee kwanza... Brigedia! Utanisamehe.. Nafikiri uliambiwa taratibu za kuongea nami toka huko Guerrero, niko sahihi au?” Koplo Mariana alimkatizia Brigedia kuongea na kumuuliza swali.


“Ndiyo niliambiwa tuje na mzigo wako kabla ya chochote tukupe” Akajibu Brigedia Fernandes.


“Hamuoni mmevunja makubaliano boss wangu?”

“Kujisahau tu Koplo wangu… Alto toa bahasha ile yenye mzigo umpatie”. Akaongea kujibu Brigedia Feca na kumuomba Ivan ‘alto’ atoe bahasha iliyokuwa kwenye begi jeusi aliokuwa amelibeba toka Guerrero huko mpaka hapa Mexico City katika mgahawa huu.


Ivan ‘alto’ msaidizi wa Mr. Guti ambaye amekuwa kipenzi cha Brigedia Fernandes kutokana na kumkubali jinsi alivyo mwepesi kichwani kuchanganua mambo, alitoa bahasha ndani ya begi la mgongoni, akanyoosha mkono kumkabidhi mwanadada aliyegoma kuendelea na maongezi bila kupewa chochote kitu na hii ni kawaida yake akikutana na watu wenye kujihusisha na mipango ya tofauti na serikali yeye pesa kwanza ndiyo anasikiliza mlichomuitia na pia uamua kama asaidie au asisaidie mnalotaka au unalotaka na hapo uwa kuna dau lingine.


“Dola 2000 hiyo, nadhani imekamilika… Ndizo tulizoambiwa unachukua kabla ya lolote… Utatusamehe kwa kutotanguliza na hii ni kutokana tuna moto sana na jambo husika” Akaongea haraka Brigedia Feca.


“Hapa tunaweza kuendelea, naweza kuwasikiliza ingawa lazima mtambue pesa hii ni ya usumbufu tu wa kunitoa kwangu kunileta hapa kuja kuwasikiliza hivyo natoa angalizo kwamba naweza kukubali jambo husika kutokana na dau nitakalotaka kama mtalikubali na uwa sipunguzi, magenge yote hapa Mexico yanayotaka jambo lao kupitia mimi wanalijua hilo na nyinyi kutoka Guerrero ni watu wa kwanza kuja kuniomba msaada mna haki ya kujua masharti yangu kwanza kabla ya yote”Akafunguka Koplo Mariana huku akihesabu pesa alizopewa zikiwa humo humo ndani ya bahasha yeye akiishika kwa mkono wa kushoto na kulia ukiwa umezama ndani, macho yake kwa kasi yanakata hesabu kupitia vidole vinavyopita kwa kasi kuhesabu dola mia mia.


“Tunaelewa Koplo…. Nafikiri tunaweza anza ombi la hitaji letu kwako?…” Akaongea muongeaji mkuu Feca.


“Nakusikiliza lete mchongo huo… Kuweni na amani kwangu mimi hakuna kinachoharibika niambieni chochote kile kisichohusu mapenzi na mwili wangu” Akajibu Koplo na wote wawili wanaoongea wakatabasamu ukiacha ‘alto’ asiyeweza kutabasamu wala kucheka kama hana bandama kumbe minyaya iliyofungwa kuzuia taya yake isisogee mahala pake ndiyo iliyokuwa ikimfanya hivi.


“Mwili wako hauna mapenzi na watu wengine? Hahah hahahah hahahaha weee kweli mwanajeshi ngangari sana…. Sisi kilichotuleta hapa ni kuwa tuna shida ya wewe utusaidie kwa njia yoyote uiwezayo kikapatikana kibali cha uhamisho wa wafungwa toka gereza la Matamoros, Tamaulipas kwenda gereza la kijeshi la Acapulco ni hilo tu kwa leo” Akaongea Brigedia Fernandes ‘Feca’ macho yake na ya Mariana yakiwa yanaangaliana bila kupepesa ukope.


“Hao wafungwa walikuwa wanajeshi?” Akahoji Mariana.

“Ndiyo… Walifungwa katika kesi ambayo inanihusu mimi pia lakini wao wakapelekwa gereza hilo la mateso kwa ajili ya wauza unga na wahalifu wengine wenye kutishia amani ya nchi, mimi nikaenda Acapulco”

“Wako wangapi?”

“Wakati wanaenda kutumikia kifungo walikuwa nane ila nimepewa taarifa kwa kamishina mmoja wa magereza wamebaki sita, mmoja kapelekwa Acapulco na mwingine alifariki… Hivyo kibali tunachotaka kiwe cha watu sita”

“Mnataka kibali icho kwa lini? Na je kuna mpango gani mwingine nyuma ya pazia wakishahamishwa huko?”

“Watu wale ni watu wangu, nafikiri unajua kesi yetu ilikuwa ikihusu mihadarati… Kuuza unga aina ya cocaine kwa wanajeshi wa jeshi la wananchi wa Mexico, vijana wale licha ya kuwa ni kweli walikuwa wakinitumikia walikataa kuwa na mahusiano nami wakisema biashara ni yao mimi hainihusu na hawajawai kusikia kama nahusika na biashara ya mihadarati ya aina yoyote… Licha ya vitisho vya aina mbalimbali na mateso makali walikataa na kuniweka mbali ila mwendesha mashitaka wa kijeshi akang’ang’ania katika tetesi na upelelezi wa maafisa wa DTO na ndipo nikaingia hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka saba gereza la Acapulco na wale watu wangu jaji wa mahakama ya kijeshi akasema kwakuwa ni viburi bila kujali ni wanajeshi na wana haki ya kufungwa magereza ya kijeshi, wapelekwe gereza la kufunza adabu la Matamoros,Tamaulipas wakatumikie adhabu ya kifungo cha miaka ishirini kila mmoja” Maelezo marefu yalitiririka toka mdomoni mwa Feca kisha akanyamaza kumalizia chakula alichokuwa anakula toka kwenye sahani.


“Okay! Nimekuelewa Brigedia… Shida yenu kuu waondoke kule kwenye gereza la watukutu na wapelekwe gereza la kijeshi… Kazi hii ni ngumu kidogo ila nitaifanya kama pesa nzuri itakuwepo sababu sitaifanya mwenyewe tu, mnataka wahamishwe lini? Au naweza andaa mpango taratibu tu?”


“Sihitaji ipite wiki hii… Naomba iwe haraka, leo alhamisi ikibidi jumanne ijayo wawe wako safarini na jumatano waanze maisha yao ya kifungoni kule Acapulco na tena uandike wasiteswe tena waishi kwa raha kama wafungwa wengine wenye vyeo wanaofungwa Acapulco kama mimi nilivyoishi kana kwamba niko kwangu nkikosa mpenzi tu”


“Nipe wiki moja kufanya hii kazi sababu natakiwa niseti mambo nikiwa mwenyewe kwanza kisha nimuingie mtu nitakayemuona ni sahihi kumshirikisha… Mnaonaje?”


“Sawa… Wiki moja tunaweza subiri ila kibali icho hautatupatia sisi utakituma gereza la Matamoros na wao ndiyo watafanya mpango wa kuwasafirisha kuwapeleka huko”


“Najua hilo Brigedia… Tuje kwenye gharama ya kazi hii…!”


Feca na Ivan ‘alto’ wakaangaliana na kisha kumuangalia bibie huyu ambapo wote wawili walishakuwa wanamjua kuwa mtu wa pesa mbele kama tumbo la mjamzito mwenye mimba kubwa.


“Sema tu gharama yako.. Tuko pamoja” Akatoa mwongozo Feca huku akitabasamu tabasamu lenye siri zilizo ndani ya kifua chake.


“Mtalipia kwa kila kichwa kimoja.. Wako sita, kila mmoja nahitaji dola 2500 hivyo jumla ni dola 15000 na pesa hizo zote mtatoa nusu kabla sijaanza kazi”


Feca na Ivan wakaangaliana kisha Ivan akatoa karatasi na peni kisha kuanza kuandika alichokuwa anajua mwenyewe, wakati Mariana alikuwa akiwatizama tu kichwani mwake mawazo yaakanza kumsonga ‘kwanini mtu huyu haongei kitu?’ .


‘Alto’ alipomaliza kuandika akampa Feca kikaratasi alichokuwa akiandika, haraka Feca akapitia kilichoandikwa.


Dakika moja zilimtosha kusoma akainua macho kumuangalia ‘alto’ na kumuonyesha dole gumba kuhashiria kukubali alichoandika.


“Ndugu yangu anasema uhakika upo? Na si tutangulize tu pesa bila uhakika, ndipo wasiwasi wake ulipo” Akauliza na kufafanua kidogo Feca.


“Gumendez aliwatuma kwangu kwasababu ana uhakika na kazi yangu… Mimi nachojali ni pesa tu na si kingine, nakuhakikishieni hiyo kazi kwangu ni nyepesi sana, nitahidhinisha mwenyewe na hakuna wa kuniuliza mimi mwanamke nina silaha zangu za siri”. Akajibu kwa majigambo Mariana.


“Sawa sisi tutatoa nusu ya pesa, dola 7500 na kisha tutakumalizia nusu yake tukipewa taarifa kibali kishafika gereza la Matamoros…!” Kabla hajaendelea Feca akaona Mariana ana jambo akaacha alitoe jambo lake.


“Angalizo… Watu wenu hawataingizwa kwenye gari litakalotumika kuwasafirisha bila kunimalizia nusu iliyobaki”


“Usiwe na wasi Mariana, tutafanya yote tuliyokubaliana… Hii karatasi ndiyo majina yao watu hao.. Pesa yako nusu tutakupatia asubuhi ya kesho ya saa nne, sema wapi tukuletee mzigo wako”


“Nitakupigia kesho saa mbili asubuhi wapi mniletee mzigo huo… Kisha ya hapo sitapenda kuonana nanyi tena zaidi ya mawasiliano ya simu” Akamaliza yake Mariana kisha akainuka kitini akapeana mikono na wote kati yao akawaaga na kuondoka zake.


“Mwanamke huyu… Duh! Anapenda pesa sana… Kuongea naye tu pesa.. Mexico hii watu wanazijua sana pesa kuliko utu, inatubidi nasi tujifunze kuishi kama wanavyoishi watu wengine” Akaongea Brigedia Fernandes akimwambia jamaa yake Ivan Alberto ‘alto’.


Hawakukaa sana pale kwani waliamua waondoke kutafuta hotel kati ya hotel nyingi zilizopo jiji la Mexico huku pia wakiwa wamekubaliana baada ya kutumiwa pesa walizoomba watumiwe na Mr. Guti hili kumpatia mwanadada huyu machachari mpenda pesa mbele kama kitumbo cha mimba iliyofikisha miezi saba.


Mpango wao wahakikishe hawatatumia tena usafiri wa ndege kurudi Guerrero kwakuwa hawakuwa na haraka hakuna wanachowai tena huko, walipanga watakodi usafiri wa taxi.


Mwisho wa sehemu ya sita (06)


Brigedia Fernandes Carlos Codrado ‘Feca’ na swahiba wake anayemkubali sana Ivan Alberto ‘alto’ walifika jijini Mexico City na kuonana na mwanadada mwanajeshi Koplo Mariana Funtes, sekretari wa mkuu wa kitengo cha nidhamu makao makuu ya jeshi la wananchi la Mexico, sekretariati ya Navy.


Walifanikiwa kuingia naye makubaliano katika kile kilichowafanya wao kutoka Manispaa ya mji wa Tetaplan jimbo la Guerrero mpaka Mexico City, walikubaliana naye watampatia pesa alizohitaji siku ya pili naye kuwaahidi kufanya jambo wanalohitaji katika wakati muafaka na wasiwe na shaka.



“Gumendez aliwatuma kwangu kwasababu ana uhakika na kazi yangu… Mimi nachojali ni pesa tu na si kingine, nakuhakikishieni hiyo kazi kwangu ni nyepesi sana, nitahidhinisha mwenyewe na hakuna wa kuniuliza mimi mwanamke nina silaha zangu za siri”. Akajibu kwa majigambo Mariana.


“Sawa sisi tutatoa nusu ya pesa, dola 7500 na kisha tutakumalizia nusu yake tukipewa taarifa kibali kishafika gereza la Matamoros…!” Kabla hajaendelea Feca akaona Mariana ana jambo akaacha alitoe jambo lake.


“Angalizo… Watu wenu hawataingizwa kwenye gari litakalotumika kuwasafirisha bila kunimalizia nusu iliyobaki”


“Usiwe na wasi Mariana, tutafanya yote tuliyokubaliana… Hii karatasi ndiyo majina yao watu hao.. Pesa yako nusu tutakupatia asubuhi ya kesho ya saa nne, sema wapi tukuletee mzigo wako”


“Nitakupigia kesho saa mbili asubuhi wapi mniletee mzigo huo… Kisha ya hapo sitapenda kuonana nanyi tena zaidi ya mawasiliano ya simu” Akamaliza yake Mariana kisha akainuka kitini akapeana mikono na wote kati yao akawaaga na kuondoka zake.


“Mwanamke huyu… Duh! Anapenda pesa sana… Kuongea naye tu pesa.. Mexico hii watu wanazijua sana pesa kuliko utu, inatubidi nasi tujifunze kuishi kama wanavyoishi watu wengine” Akaongea Brigedia Fernandes akimwambia jamaa yake Ivan Alberto ‘alto’.


Hawakukaa sana pale kwani waliamua waondoke kutafuta hotel kati ya hotel nyingi zilizopo jiji la Mexico huku pia wakiwa wamekubaliana baada ya kutumiwa pesa walizoomba watumiwe na Mr. Guti hili kumpatia mwanadada huyu machachari mpenda pesa mbele kama kitumbo cha mimba iliyofikisha miezi saba.


Mpango wao wahakikishe hawatatumia tena usafiri wa ndege kurudi Guerrero kwakuwa hawakuwa na haraka hakuna wanachowai tena huko, walipanga watakodi usafiri wa taxi.


ENDELEA NA DODO..!


BAADA YA WIKI MOJA MBELE, GUERRERO-MEXICO

“Hallow!” Upande wa pili ulisikika masikioni mwa Mr.Villa Nandez Guti baada ya yeye kupokea simu toka kwa mtu anayemjua kuwa ni Kamishina wa jeshi la Magereza jimbo la Guerrero.


“Halloow! Kamishina Fergata Maxiwell Ginger, habari yako?” Akajibu na kusalimu Mr. Guti.


“Nzuri Mr. Guti… Upo karibu na jamaa yako Feca?”

“Hapana.. Yupo chumbani kwake amejipumzisha… Lete habari?”

“Kibali toka makao makuu ya jeshi la wananchi kimewasili muda si mrefu kikitoa maelekezo juu ya watu mnaowahitaji wahamishwe toka gereza la Matamoros,Tamaulipas kwenda Acapulco, Guerrero mpe taarifa hizo ndugu yako kabla sijatuma ujumbe kwenda Tamaulipas wawaandae hao wafungwa maana Kamishina msaidizi wa taifa ametia saini na kunipa maagizo nitume taarifa kwenda huko..”

“Sawa.. Subiri dakika tano nitakupigia uongee naye”


Simu zikakatwa kwa pande zote mbili, Mr. Guti akamuita mtumishi wake mmoja aende kumuita Brigedia Feca.


Dakika tatu tu Feca alikuwepo pale sebuleni alipo Mr. Guti akipanga mabunda ya noti aliyoletewa na watu wake mbalimbali.


“Kamishina Fergata amepiga simu kueleza mambo yameanza kuiva, kibali mlichompa kazi Koplo Mariana atengeneze kimekamilika na kimeshafika, sasa anahitaji maelezo yako, hivyo mpigie muongee” Akaongea Mr. Guti na papo hapo Feca akakenua meno ya ushindi kufurahia taarifa aliyopewa.


“Kijana! Haraka sana niitie ‘alto’” Akaongea kwa kasi Feca kumuamrisha mmoja wa kijana aliyekuwa amesimama pembeni kabisa ya sebule hii kubwa na kusimama kwake huko ni kuwa tayari kwa huduma yoyote kwa boss yake Mr. Guti.


Wakati kijana akienda, Feca akatumia fursa kupiga simu kwa Kamishina Fergata, kiongozi msaidizi wa jeshi la magereza.


“Hallow!” Upande wa pili ukaongea baada ya kupokea.

“Halloow! Kamishina Fergata… Habari yako?”

“Nzuri tu Brigedia Fernandes.. Vipi hali yako?”

“Niko vizuri, fiti kabisa kama chuma cha reli… Lete habari?”

“Habari ni nzuri upande wetu… Afisa wa jeshi mliyempa kazi amemaliza kazi yake na sasa imebaki kazi ya upande wetu tu, nasubiri maelekezo yako hili nitume ujumbe kwenda gereza la Matamoros huko Tamaulipas wawaandae watu wako kuwasafirisha toka huko hadi Acapulco”

“Kazi nzuri sana amefanya Mariana… Sasa sisi tunachotaka toka kwako ni maelekezo ya aina ya gari itakayotumika kuwasafirisha watu wetu na pia njia ipi itakayotumika hili nasi tujipange kingine nahitaji picha za hao wafungwa wote walivyo sasa kiafya”

“Sawa sawa.. Ila na mimi nahitaji pesa yangu aniletee mtu wenu kabla sijaanza kazi hii mara moja maana hawa watu wenu wakishaingia kwenye mikono yenu sidhani kama itakuwa rahisi tena kuwaona katika namna moja hama nyingine… Pia kosa lolote litakalotokea naomba jina langu lisihusike kwa namna yoyote ile”

“Mr. Guti atamtuma mtu wake aliyeko huko Mexico City kukuletea mzigo wako usiwe na wasi… Hadi jioni mambo yatakuwa poa kabisa, usiku nitakupigia kwa maelekezo zaidi”


Simu zao walizikata zote kwa pamoja, Feca akasogea lilipo sofa na kujipweteka sofani kama mzigo na mara ‘alto’ akatokea pale sebuleni.


Simu ya Feca ikaanza kuita kabla hajakaa vizuri pale sofani na alipoangalia mpigaji ilimbidi atabasamu na kisha akapokea huku tabasamu likiwa bado limeweka makazi usoni mwake.


“Mariana!” Akaongea alipopokea tu.


“Brigedia! Habari yako?”

“Nzuri Koplo… Nimepokea simu ya Kamishina mdogo wa jeshi la Magereza.. Aisee ahsante sana mpendwa… Umecheza kama Chicharito kwa kweli, umetimiza ahadi yako katika wakati uliouahidi”

“Nashukuru sana.. Uwa siharibu ahadi na ukiona nimeharibu ujue kazi hiyo yoyote anaharibu, zile nyaraka Kamishina msaidizi wa jeshi la magereza makao makuu ya jeshi la Magereza asingeweza kuona upungufu wake sababu ni halali na hata sahihi ni halali maana nimemsainisha mtu wakati ambao hata wewe ungesaini, mimi mwanamke na mwanamke ana nguvu kubwa mbele ya mwanaume sema tu wanaake wengine hawatambui nguvu yao… Haya sasa zamu yenu kutimiza ahadi yenu kunimalizia mzigo wangu uliobaki”

“Mr. Guti muda si mrefu atacheza na muamala wa kibenki kuna mtu wake huko Mexico City atakupatia nusu yako… Ahsante sana kwa kazi nzuri na nataka nikwambie ukweli tutazidi kufanya mengi zaidi kati yetu”

“Karibu sana.. Nataka niupate mzigo wangu kabla ya saa kumi na mbili jioni.. Kazi njema” Alipomaliza Hivi Mariana akakata simu.


Fernandes Carlos Codrado ‘Feca’ Brigedia mkufunzi wa kijeshi aliyetimuliwa kazi baada ya kutoka kifungoni alizungusha macho yake kuwatizama watu wawili waliokuwa nao wakimtizama kwa makini sana, akapapasa ndevu zake kwa mbwembwe zenye matumaini kisha tabasamu murua likasindikiza mbwembwe zake.


“Mr. Guti!” Akamuita Mr. Villa Nandez Guti.

“Naam…!”Akajibu kiunyenyekevu zungu la unga (Mr. Guti) hili jambo ambalo hata msaidizi wake Ivan alikuwa kaanza kumshangaa wiki sasa kwanini heshima ya Guti kwa Feca imepitiliza sana siku hadi siku inaongezeka lakini hakuthubutu kuuliza na si kwakuwa kuongea kwake ni shida la hashaa! Ni kwa sababu aliona haimuhusu hili.


“Kama mlivyosikia kazi sasa ndiyo inataka kuanza… Mpango umeenda kama tulivyopanga na ninashukuru Lopez ametuma mzigo wetu katika wakati muafaka, pesa alizotuma zitatusaidia katika operesheni hii…. Mariana anadai dola 7500 na kamishina mdogo anahitaji dola 3500.. Kwa ilivyo Mr. Guti itabidi twende benki ukamuingizie mdogo wako pesa awapatie hawa jamaa hili wafanye mambo ya haraka” Brigedia Feca akatoa muongozo wa haraka kipi kifanyike na kama wameambiana wote wakaangalia saa kama ujuavyo mara nyingi kuangalia saa sawa na kupiga mwayo kunaambukiza labda usiwe umevaa saa ndipo hautaweza kuangalia saa endapo mtu uliye karibu naye ataangalia saa yake.


“Sawa chukua pesa tuondoke kuelekea benki muda unakimbia sana” Mr. Guti akapitisha alichoongea rafiki yake Brigedia Fernandes.


Muda huo ulikuwa saa tisa kasoro robo alasiri, wakiwa na walinzi wao katika msafara wa magari matatu walielekea maeneo ya benki.


***** ***** *****


Saa kumi na mbili jioni katika jumba la Mr. Guti pale pale wanapopenda kupumzika muda wa jioni eneo la swimming pool ndipo palikuwa na kikao cha mpango wa nini kinaenda kufanyika muda watakaotaarifiwa kuwa gari itakayowabeba wafungwa walioombewa kibali cha kuhamishwa kutoka gereza la wafungwa watukutu, gereza la Matamoros lililopo jimbo la Tamaulipas jimbo liliopo pembezoni mwa ghuba ya Mexico, katikati ya majimbo ya Veracruz upande wa kusini mashariki, San Luis Potosi kusini magharibi na Nuevo Leon upande wa magharibi huku kaskazini mwa jimbo hili la Tamaulipas ndipo ilipo boda ya Marekani na Mexico manispaa ya mji wa Nuevo Laredo ambapo ukipitia kutokea eneo kama unahitaji kuingia Marekani basi utaingia jiji la Luredo jimbo la Texas.


Gereza hili la Matamoros ni moja ya gereza kongwe sana katika nchi ya Mexico, likiwa ni moja la gereza ambalo linatumika kufunga wafungwa watukutu haswa, wenye roho kutu zenye ukatili na uvumilivu mkubwa wengi wao wakiwa wauzaji wakubwa na mabosi wa magenge ya mihadarati (Kingpin) ya kila aina kutoka magenge mbalimbali tishio kwa mihadarati nchini Mexico na nchi jirani.


“Picha za watu wetu nimetumiwa kwa whatssap.. Hapa ndipo mahala ambapo mpango wa ‘alto’ ulianzia, itatubidi tupate watu wanaofanana kimwili na watu wetu kabla ya saa tano usiku ya kesho, tunatakiwa twende na wakati kwa spidi inayotakiwa…. Msafara wa watu wetu utaondoka gereza la Matamoros alfajiri ya kesho kwa mujibu wa kamishina mdogo gari watakalotumia ni gari zao za kawaida la kusafirisha wafungwa, kutoka Matamoros, Tamaulipas mpaka Acapulco, Guerrero kwa hesabu zilivyo kama wangetoka bila kukutana na msukosuko ambao sote tunautarajia kwa kawaida ni masaa 17 hadi 20 kwa kutegemea na gari spidi yake…!”Akaanza maongezi Brigedia Fernandes a.k.a Feca kisha akapumzika kuwangalia watu watano waliokuwa wakimsikiliza, akiwemo Mr. Guti, Ivan ‘alto’ na wengine wawili ambao ni makamanda wa ngazi za juu katika genge analolimiliki Mr. Villa Nandez Guti.


“… Mchoro wa Ivan ‘alto’ unaonyesha wataingia eneo la Lazaro Cardenas saa moja asubuhi kama wataondoka saa kumi na moja alfajiri na kwakuwa gari itakuwa inakimbizwa kwa spidi sababu inasafirisha wanaoitwa watu wa hatari basi haitasimama Lazaro Cardenas eneo hili watalipita na moja kwa moja dereva ataenda kusimamisha gari Calle 18 de Marzo ambapo watapata kupumzika kidogo angalau wao askari wasafirishaji na dereva kupata vinywaji kama si chai au kahawa, muda huo kutokana na umbali wa Lazaro Cardenas hadi Calle 18 de Marzo kuwa si umbali mrefu sana na kwa spidi tunayoikadiria basi saa nne ndipo watakuwa hapa… Tukadirie hapa watapumzika nusu saa tu naamini itawatosha ndipo wataondoka..!” Alinyamaza kidogo kugonga eneo lililo kwenye mchoro wa ramani kwa vidole vyake na kupokea kikaratasi kingine toka kwa Ivan ‘alto’ akakisoma kidogo kisha akakiweka kwenye mfuko wa mbele wa shati alilovaa, akamtizama ‘alto’ na kutingisha kichwa kukubali jambo.


Akatupa macho kwenye ramani anayoitumia kutoa maelekezo yake akasoma kidogo kisha akaendelea na maelezo.


“Saa sita kwa kilometa za kutoka Calle 18 de Marzo hadi La Catolica muda huu watakuwa hapa na Tarasco watafika saa nane na robo.. Muda huu wa saa nane na robo sisi huku tutatakiwa tuwe tumeshafika eneo la Segundo Piso del Anillo Periferico, eneo hili watu wetu watafika saa mbili au tatu usiku, hapa ndipo tutafanya yetu katika daraja la kona ya Jalisco kwa kuwa kuna huu muinuko mkubwa wakiupanda tu papo hapo tunawavamia na kufanya yanayostahili, tutaziacha maiti zilizokatwakatwa kubaki viwili wili na pia tutaacha ujumbe tulikuwa tunawataka sana hawa wafungwa kwa ajili ya kisasi na leo tumetimiza kisasi cha wao kumuua boss wetu … Mpango huko hivyo.. Kuna mwenye swali?”


Hakuna aliyeuliza wote walibaki wakiangaliana kwa zamu kisha wakatikisa tu vichwa vyao kukubali mpango ulivyo.


“Naona kila mmoja amekubali mpango ulivyo kilichobaki ni kujua wapi tunaenda kupata maiti za watu sita ambao kila mmoja kati ya watu hawa walio katika picha hizi atatakiwa awe amefanana mwili na mmojawao” Akaendelea Brigedia Fernandes kisha akamkabidhi simu yake Ivan ‘alto’ aangalie picha za wafungwa waliokuwa watu wake wakati wako jeshini.


“Naomba jambo moja boss!... Kazi ya kukata kata miili ya binadamu hao tutakaowapata nitaomba niifanye mimi maana sijaifanya siku nyingi toka niikimbie Los Zetas hivyo nina hamu ya kuchezea damu..!” Mtu mmoja mwenye mwili usio mwembamba wala mnene, mwili wa wastani akiwa kajichora tattoo mwili mzima yaani mpaka uso alikuwa kauchafua aliomba jambo hili la kikatili alifanye yeye hili ajikumbushe aliyokuwa akiyafanya akiwa genge la Los Zetas, genge hatarishi sana lililoanzishwa na wanajeshi walioasi jeshi la wananchi wa Mexico, kijana huyu katili ni Mmexico mwenye asili ya Ujerumani aitwaye Wolfs Klauben Gend a.k.a Hitler.


“Haahaah! Usijali kazi hiyo utaifanya bila shaka muhimu ni kuwapata watu hao kwa wakati… Kumbe ulikuwa Los Zetas? Sikuwa nalijua hili kama kwa Guti kuna vijana walikuwa genge hilo, bora ulivyotoka mapema maana muda si mrefu na wao watapiga magoti kwetu” Akaongea huku watu wote waliokuwa pale wakitabasamu kufurahia ujasisri wa kikatili wa Wolfs Klauben Gend ‘Hitler’.


Ivan alitumia dakika mbili kuangalia picha zile kisha kama kawaida yake akatoa peni na karatasi toka mfuko wa suruali yake aina timberland yenye mifuko mingi kila pande, alitulia dakika tatu akiandika mambo anayojua yeye, alipomaliza akampa kikaratasi Brigedia Fernandes.


“Ivan! Amependekeza jambo ambalo naona linafaa… Anaonelea sisi tungeenda kusubiria mji mdogo wa Segundo mapema kisha baadaye tutasogea daraja la kona ya Jalisco na huko huko tutapata tu watu wa kuwapoteza uhai wao hasa vigenge vidogo vidogo vya wauza unga wa mitaani huko Segundo bwana Ivan anasema vipo vingi na vinawindana sana tu… Pendekezo lingine anasema tutaiteka gari na kwenda nalo kwenye pori la Segundo el collina ambako huko tutafanya yetu na kisha kutelekeza kila kitu na hapo mchezo utakuwa umekwisha na kustukiwa labda wapime DNA… Mr. Guti! Yapi mawazo yako?” Akatoa maelezo Feca kisha akampa nafasi Mr. Guti aongee kama ana jambo.


“Mimi langu ningependa maandalizi yaanze mara moja kwa vijana wote kutaarifiwa kitakachokwenda kufanyika na kisha wote pia wajue kuanzia sasa genge letu linatakiwa kupanuka na kuwa kubwa zaidi kutoka hapa lilipo” Akajibu na kupitiliza na maneno hata ambayo hajaulizwa wala kuombwa azungumzie.


“Waitwe vijana wote ambao nitachagua miongoni mwao wa kwenda nao kwenye operesheni hii ndogo lakini operesheni muhimu kwa mustakabali wa biashara yetu na nguvu zetu…” Akaomba Feca na mara moja Ivan akainuka kuelekea mahali ambapo vijana wao wa kazi za kazi uwa wako tayari kwa lolote muda wowote ukiacha walinzi wao ambao nao muda wote uzunguka zunguka kukagua hali ya usalama wa eneo kana kwamba wao wako kihalali wanalinda nyumba ya mkubwa fulani aliyeko serikalini.


Haikuchukua muda mrefu wakati ukimya ukitamalaki pale sebuleni wakatokea vijana wa kike na wa kiume zaidi ya ishirini pale sebuleni mpaka pakawa kama hapatoshi kwa uwepo licha ya sebule kuwa kubwa sana yenye upana wa kutosha na thamani zake za fenicha za kuvutia.


“Ni muhimu tukaongelea hapa sababu Mr. Guti anatakiwa kuwepo kusikia na kutoa mawazo yake na kidogo hayuko sawa kiafya toka jana mgongo unamuuma… Hivyo nawaomba mwenye kusimama anaweza akasimama tu sina masharti ya kichawi mimi na mwenye kuhitaji kukaa masofa hayo hapo karibuni mkae” Akatoa ukaribisho Brigedia na vijana wale wakagawana masofa kwa kukaa na bahati nzuri wote walitosha hakuna aliyesimama.


“Naamini nyote mko poa, salama wa salimini… Nimewaita hapa kuna jambo muhimu tunatakiwa kuongea kwa pamoja kisha kuna baadhi yetu tutajumuika katika operesheni hiyo kusudiwa..!” Akaendelea Feca kisha akanyamaza kuwaangalia vijana wao kila mmoja kwa zamu kuangalia tention yao machoni mwao.

“Wote naamini mnanijua mimi ni nani kwa majina… Lakini sidhani kama mnajua mimi na kiongozi wenu Mr. Guti tukoje ingawa kwa siku kadhaa za hivi karibuni mnaniona hapa na tunapishana pishana kwa namna moja hama ingine… Mr. Villa Nandez Guti alitakiwa anitambulishe kwenu kama ni nani? Lakini naweza kujitambulisha mimi mwenyewe mimi ni nani katika genge hili kwa sasa, Brigedia mfukuzwa wa jeshi la wananchi la Mexico kwa sasa mimi ndiye mtendaji mkuu wa genge hili na baada ya kazi tutakayokwenda kuifanya tutaongezeka zaidi na ndipo tutakapofanya kikao kingine ambacho mimi binafsi nitaeleza kila kitu kuhusu mfumo mpya nitakaouunda katika genge letu, mfumo utaoleta heshima na manufaa kwetu sote ukizingatiwa na maslahi bora yatakayotokana na mavuno yetu” Akaendelea tena Feca kisha akawatizama tena kwa zamu baadhi ya watu, akanyanyua glasi ya maji ya kunywa akapiga funda kadhaa.


Wafuasi wa Mr. Guti wakawa wanamuangalia kwa umakini huku wengine wananong’onezana kwa chati kwa viganja vyao kuviziba mdomoni, lakini hawakuthubutu kuongea kiuwazi kwa sauti na hii ni kwa sababu boss wao Mr. Guti alikuwepo na alikuwa kimya akisikiliza huku starehe yake ya kuvuta sigara bila kujali uwepo wa watu sehemu ilipo, ilikuwa ikiendelea anakata mti anapanda mti.


“Sipendi uvunjifu wa amani katika sisi wenyewe kwa wenyewe kwa kudhibitiana katika uhuru wa kimaongezi wala uhuru wa kutoongea unachojisikia ila si tunapokuwa kwenye vikao kama hivi vya dharura na hata vya kiratiba kama kikundi na uendeshaji wake unavyotaka, heshima ni kitu cha kuzingatiwa hasa kwa walio juu kimamlaka… Sijawaita leo hapa kuwapa rulling za squad ila ningependa sote tuwe makini na kile ninachoongea tuache minong’ono kama kuna swali unatakiwa kuniuliza mimi pia hata kama ni dukuduku au kutoridhishwa na lolote karibu nyosha kidole uliza, nafahamu sote hapa ni wengi ni watoto mtaani watukutu ila zingatieni haya” Aliishia hapa akamtizama Mr. Guti ambaye yeye alipuliza moshi wa sigara juu kana kwamba anautuma uende kwenye mawingu huku kichwa chake kikitikiswa kwa mbwembwe za kama wale matajiri waliopata utajiri kutoka kwenye urithi wa baba wa kambo.


“Nachoongea kina baraka za kiongozi wenu hivyo msihofu kuwa kuna mapinduzi yamefanyika la hashaah! Guti bado kiongozi ila kuna maboresho na pia mimi pia ni mwanahisa wake ambaye sikuwepo kwa miaka mitatu na sasa nimerudi rasmi ndiyo maana mnaniona mara nyingi nipo na Ivan ‘alto’….Leo usiku tutaondoka hapa Petatlan kuelekea Segundo Piso del Anillo Periferico kwa kazi maalumu hivyo Ivan atachagua watu kumi wa kwenda huko tukiongozana na mimi pamoja naye Ivan mwenyewe, huku wengine mkibaki hapa mkiwa na Mr. Guti kwa wito wa dharura kama itahitajika hivyo… Kama kuna swali naomba liulizwe?” Brigedia Fernandes akaeleza tena kisha akauliza kama kuna mwenye swali.


“Hey! Yaap uliza..!” Feca akamruhusu kijana mmoja ambaye alinyoosha mkono, alikuwa ni kijana aliyejichora mwili mzima kwa tattoo bila kuacha hata usoni mwake kama alivyo ‘Hitler’ wa genge hili dogo Wolfs, weupe wake wa kizungu uliharibiwa kwa michoro meusi iliyojichanganywa na mingine mekundu.


“Tunataka kujua katika mfumo mpya unaosema utaundwa sisi waanzilishi tulioanza kwa pamoja toka Guti akiwa chini tutapangwa vipi na wageni watakaoletwa kama unavyosema?” Akauliza kijana huyu swali ambalo wengine wote kati ya vijana hawa walioitwa hapa sebuleni walitingisha vichwa vyao kuafikiana na swali lililoulizwa na mwenzao.


Mwisho wa sehemu ya saba (07)


Kazi ya kazi za kazi inasogea na kufanya mchezo mtamu ukaribie katika macho yetu utakaojenga utamu wa dodo asali katika ubongo.


Kikao cha kuelekea kufanya ukombozi wa kuwaokoa wafuasi wake kinaendelea katika jumba la Mr. Villa Nandez Guti.



“Nachoongea kina baraka za kiongozi wenu hivyo msihofu kuwa kuna mapinduzi yamefanyika la hashaah! Guti bado kiongozi ila kuna maboresho na pia mimi pia ni mwanahisa wake ambaye sikuwepo kwa miaka mitatu na sasa nimerudi rasmi ndiyo maana mnaniona mara nyingi nipo na Ivan ‘alto’….Leo usiku tutaondoka hapa Petatlan kuelekea Segundo Piso del Anillo Periferico kwa kazi maalumu hivyo Ivan atachagua watu kumi wa kwenda huko tukiongozana na mimi pamoja naye Ivan mwenyewe, huku wengine mkibaki hapa mkiwa na Mr. Guti kwa wito wa dharura kama itahitajika hivyo… Kama kuna swali naomba liulizwe?” Brigedia Fernandes akaeleza tena kisha akauliza kama kuna mwenye swali.


“Hey! Yaap uliza..!” Feca akamruhusu kijana mmoja ambaye alinyoosha mkono, alikuwa ni kijana aliyejichora mwili mzima kwa tattoo bila kuacha hata usoni mwake kama alivyo ‘Hitler’ wa genge hili dogo Wolfs, weupe wake wa kizungu uliharibiwa kwa michoro meusi iliyojichanganywa na mingine mekundu.


“Tunataka kujua katika mfumo mpya unaosema utaundwa sisi waanzilishi tulioanza kwa pamoja toka Guti akiwa chini tutapangwa vipi na wageni watakaoletwa kama unavyosema?” Akauliza kijana huyu swali ambalo wengine wote kati ya vijana hawa walioitwa hapa sebuleni walitingisha vichwa vyao kuafikiana na swali lililoulizwa na mwenzao.


ENDELEA NA DODO…!


BAADA YA WIKI MOJA MBELE, GUERRERO-MEXICO

“Brigedia! Samahani naomba swali hilo nilijibu mimi ingawa hatujaitana hapa kuelezana na mustakabali wa kundi letu… Jamani waasisi wa kundi letu hawawezi kutupwa lazima katika mfumo mpya utakaoundwa kila mmoja kati ya sisi hapa atafaidika katika hali ya ubora wa hali ya juu kinachotakiwa ni kuombeana uzima tu, hivyo wote nawaombeni tufanye kazi hii iliyo mbele yetu na kila atakayepangiwa jukumu aheshimu jukumu alilopewa… Tuna kazi ngumu sana ndani ya mwezi huu na matunda yake yatakuwa makubwa sana kwa wote baada ya operesheni mbili zinazokuja huku operesheni ya kwanza ikiwa ni mzizi wa operesheni kubwa itakayofuata,kama Brigedia alivyosema Ivan atachagua watu kumi wataondoka kwenda kwenye operesheni ndogo tu itakayofanyika kesho huko Segundo, naomba wote mkawe makini kufuata maelekezo ya viongozi wenu wa msafara… Ninawaamini sana vijana wangu wote” Alirukia mkuu wao wa kundi hili na bosi mwenyewe kwa kuwaelekeza kidogo mambo aliyoona anatakiwa aelekeze.


“Sawa bosi..!” Wafuasi wote kwakuwa ni watiifu kwa bosi wao walijibu kwa pamoja na nyuso zao zikakunjua tabasamu.


“Alto! Naomba uchague vijana kumi wa kazi tutakaoenda nao Segundo… Hili baadaye tukae nao tuelekezane nao kuhusu operesheni husika” Brigedia Fernandes akaongea baada ya Guti na wafuasi wake kuwekana sawa.


“Sawa mkuu!” Kwa tabu akaongea sauti iliyosikika kwa mbali Ivan Alto na mara moja akitumia mkono wake na kichwa kusapoti akawa anaita mtu asogee mbele walipo wao.


Dakika zipatazo tano zilitosha kwa Genius ‘alto’ kuchagua watu anaowaamni sana kuwa wana mambo yote anayostahili kuwa nayo mtu wa kazi za kutisha.


MAUAJI YA KUTISHA, VERACRUZ-MEXICO

Kikosi kazi cha wazee wa kazi wenye kujua kazi zao katika sekta ya unyama na ukatili wa kutisha kikiongozwa na katili wa toka enzi alivyokuwa akilitumikia jeshi la wananchi wa Mexico, Brigedia Fernandez Carlos Codrado “Feca’, muda wa saa mbili asubuhi kilikuwa kimeingia katika mji mdogo wa Segundo uliopo jimbo la Veracruz.


“Wakati tuko njiani tunakuja huku nilikuwa nikifanya mawasiliano na jamaa yangu mmoja anayeishi Puebla, amenielekeza kitu ambacho kinachoweza kutusaidia kupata watu tutakaowachinja na kufanya ndiyo maiti za watu ambao ni wenzetu… Hapa Segundo kuna genge la wahuni ambao hatuwezi kusema wanaweza kuwa ni wauzaji wa kimtaa wakubwa wa mihadarati ni wa kawaida tu ila si wa kuwaingia kizembe… Nimepewa mawasiliano ya mtu mmoja ambaye anawajua watu hao nahitaji watu hawa tuende huko tukawafagie wote na tuchukue chochote chenye maana kwetu.. Kambi yao ipo eneo la La Playa, nafikiri hakuna ambaye hajawai isikia mtaa kwa sifa zake…!” Akaeleza Brigedia Fernandes wakiwa wote ndani ya gari moja aina ya Toyota Hiace rangi nyeusi, gari ikiwa imewekwa kwenye maegesho ya magari ya kulipiwa ya katikati ya mji wa Segundo.


“Mkuu! eneo unalolitaja ni eneo la hatari sana katika Vercruz hii una sifa zake hata mapolisi hawakatizi huko ni kama wanajitawala wenyewe, mbinu hiyo huoni itaanzisha vita ndogo hapa Segundo?” Akahoji kijana mmoja mwenye mwili mkubwa wa mazoezi, pia mikono yake yote ikiwa imechafuka michoro, akiwa amevaa shati jeupe pee kote hakuna hata doa, shati la kitambaa chepesi juu ya kawoshi nyeusi inayoonekana vizuri kutokana na shati lake kutofunga vifungo na pensi (kaptura) ya jeans alilolikata magotini lilipokuwa jeans suruali na kutolishona pindo lake.


“Ni kweli mkuu asemavyo Cisco… Mimi nimekulia jimbo la Monterrey lakini katika eneo hili la Veracruz sifa za ‘La Hormiga’ wa La Playa ni sifa sikika sana, kama kuna njia ingine tunaweza itumia ni bora tukaitumia hata tungekuwa tupo makomando tupu ngumu sana kupigana na watu zaidi ya mia tano na zaidi tena wasio na huruma kutokana wamezaliwa eneo hili wakiwa wanaona mauaji kitu cha kawaida..” Akaongea kijana mwingine ambaye muda mwingi wakati wako safarini yeye hearphones zake zilikuwa masikioni akisikiliza nyimbo zinazovuma sana katika Mexico za wanamuziki wanaopendwa sana akiwa amezikusanya za kutosha katika simu yake aina ya LG-Smartphone, lakini hapa alikuwa ameweka heshima kusikiliza maelekezo yaliyoanza punde tu gari lilipopaki mahali hapa. ‘La Hormiga’ kwa kihispaniola lugha inayotumika kwa watu wa Mexico maana yake ni ‘siafu’ kwa kiswahili au kwa kiingereza ni ‘ant’.


“Shida wanaongozana wengi sana kama wafanyavyo vijana wa kihuni wa mitaa ya Rio De Janeiro, kundi moja unaweza kuta lina watu zaidi ya thelathini pia wamekata tamaa kabisa ya maisha wanatumia silaha zote kama visu, mapanga na bunduki za kisasa kabisa” Akaongea dreva aliyewaendesha watu hawa tokea mji mdogo wa Petatlan kuja hapa mji mdogo wa Segundo.


Muda huo wao wakiongea mtu mrefu ‘alto’ alikuwa akiandika anachokijua mwenyewe katika karatasi akiwa amekaa siti ya mbele kabisa alipo dereva.


“Tumekuja huku kufanya kazi… Katika akili ya haraka na akili ya muandaaji wa operesheni hii ameangalia mbali kuwa hatuwezi kuvamia watu wema wa mji huu na kuwafanya tunavyotaka, tunatakiwa tufanye jambo ambalo lina faida mbili kwa wakati mmoja, vijana wa huko mitaa ya Playa sifa yao kuu ni siafu wanaopora mizigo ya watu, wanapora na kuua sana watu wa magenge makubwa ya unga hivyo tunaweza pata faida kama tutaondoa uoga tulionao juu ya sifa zao, tutapata silaha, tutapata mizigo ya maana kwao na pia tutapata maiti tunazozitaka” Akaongea Brigedia Fernandes ‘Feca’ mkuu wa msafara akileta amri ya kiongozi wa kijeshi anayetaka jambo lake litimie.


“Kwanini lazima tutengeneze uadui na siafu? Huoni watatuwinda sana” Akahoji kijana mwingine aliye siti ya nyuma kabisa, ambaye sehemu iliyopita nilimuelezea alijipiga michoro kama ana akili nzuri na kuugeuza mwili wake kuwa ubao wa michoro na maandishi huyu anaitwa Alejandro Lopez a.k.a la culebra, walimuita hivyo wakimaanisha ni nyoka mdogo. Kwa sababu alikuwa anapenda sana kung’ata endapo atazidiwa kwenye mapambano na mwili wake wa kuwa mwembamba jina lilimkaa sana na mwisho naye akalizoea na kupendwa aitwe hivyo.


Tayari mzee wa kuandika ‘alto’ alimaliza kuandika akanyoosha mkono kumpa karatasi kiongozi wao wa hapa Brigedia Fernandes.


Dakika tatu zilifanya ndani ya gari kupitiwe na utulivu wa kutosha ni moshi wa sigara tu uliokuwa ukitoka katika baadhi ya watu wanaume hawa wanaovuta sigara wengi wao wakivuta Marliboro na kutapakaa ndani kuleta kiwingu kwa baadhi ya sehemu kisha ukawa unatoka nje.


Alipomaliza kupitia kilichoandikwa Brigedia akayainua macho yake na kuwatizama baadhi ya watu huku yeye akikaziwa macho na watu wote waliomo ndani ya Toyota hiace van hii hata kama wengine walikuwa wamevaa miwani ya jua rangi nyeusi ila hakuna ambaye alikuwa hamuangalii.


“Mmmh! Mara zote mtu huyu kiongozi wenu amekuwa muongozo mkubwa kwetu anarahisha sana mambo mengi ‘alto’ sasa nakuita ‘alto genius’ kwa ulivyo genius kwa kila jambo unadhidi kunifungua akili pamoja na uzoefu wangu mkubwa lakini wewe ni zaidi ya wote niliyowai kukutana nao… Jamani alto amependekeza tusiunde uhasama na siafu wa mji huu, amependekeza kuwa hapa watu tunaowahitaji tunaweza kuwapata katika danguro moja lililopo mtaa wa Jogos, yeye ameshawai kufika huko anasema kuna wanaume mashoga wengi wanaojiuza katika danguro hili lisilo rasmi ingawa linafahamika na serikali ila serikali haitaki kuhusika nalo kwa mambo yao hivyo ulinzi tu wanajilinda wenyewe kwa wenyewe… Yaani humo mashoga na mabasha kuwaona katika mapenzi ya hadharani ni kawaida kabisa hata ndoa za jinsia moja ufanyiwa sherehe humo kwa mashoga wa Veracruz, Puebla hata kule Guerrero mashoga huja kufungia ndoa zao katika ukumbi huo wa Jogos… Hivyo alto anataka twende mtaa ule karibu na jengo la danguro husika kisha kwa anavyojua yeye anasema uwa haipiti dakika ishirini wanatokea wanaokwenda kuingia ndani na wengine wanatoka, sisi tutakachokuwa tunafanya ni kumkamata kila mmoja anayepita karibu yetu kisha tunamdhibiti ndani ya gari mpaka idadi ya watu sita itakapotosha… Nimemuelewa sana alto katika hili sababu hawana maana watu hawa pia serikali haiwezi kushtuka upotevu wa watu fulani kwa haraka kwakuwa jamii hii ya mashoga ni jamii inayofanya mambo yao kwa siri bila kujulikana idadi kamili kama muonavyo hata kuwafuatilia serikali haifuatilii wanachofanya katika Jogos House’s.. Mnaonaje mpango huu ulioletwa kwetu na alto?” Aliongea kwa urefu Brigedia kisha mwisho alimalizia na swali.


Kama wanashindana vijana waliomo humu walikuwa wakiendelea kupuliza sigara na kuachia mimoshi inatapakaa ndani ya gari, uzuri kati yao hakuna ambaye hakuwa anavuta sigara ila Feca yeye kwa wakati huo hakuwa akivuta yeye na dreva Rude hivyo pona yao ikawa ni kushusha vioo vya siti ya mbele anapokaa dereva kwa pande zote mbili.


“Mimi kwangu naona alto yuko sahihi.. Ni bora tukachukiwa na mashoga kuliko siafu hasa siafu wa Playa, napitisha hoja iliyotolewa kwa mikono miwili” Akaunga mkono dreva.


“Nami pia naunga mkono hoja aliyoandika alto”. Alejandro ‘la culebra’ akaunga mkono.


Wote walipitisha kwenda huko mtaa wa Jogos kwenye danguro maarufu sana katika jimbo la Veracruz, danguro hili likiwa pembeni kabisa ya mji mdogo wa Segundo, danguro hili lilianzishwa miaka mingi nyuma ya miaka kumi lilipotokea tukio la unyama naokwenda kuuelezea mbele.


Mwanzilishi wa danguro, shoga maarufu sana katika kuongoza kampeni ya kutetea mashoga katika Mexico ndiye alianzisha danguro hili kisha alipoolewa na mwanaume mmoja (mweu) wa Mexico City aliyekuwa tajiri sana na mlanguzi wa madawa ya kulevya ikambidi muanzilishi huyu aende kuishi Mexico City kumfuata mume wake katika ndoa yao ya kipuuzi (shubamiit), ndoa isiyo na matunda maana ndoa lazima ilete matunda lakini si ndoa hizi za hawa wanaojiona wako sawa kumbe hawako sawa.


Kuamia kwake huko Mexico City hakukumfanya shoga hili kuu kuliacha jengo lake hivi hivi, bali ndiyo alikarabati vizuri jengo kwa msaada wa mumewe (mende) na kulipa jina danguro hilo kuitwa jogos gay house’s na kuwapa uongozi wa kuliendesha danguro rafiki zake, mashoga wenzake waliopinda kama yeye, laini kama walizaliwa walivyo, hivyo kukawa kuna laana zote toka kwao zikiwashilikisha na wasagaji, kila muda ukifika eneo hili utaona watu hawa wa kusikitisha wakiingia na kutoka kwa wingi tu iwe mchana au usiku, huku ndoa zao zikifungwa na sherehe kufanyika humuhumu.Hakuishiwi sherehe humu ndani.


“Muda huu ni saa sita… Tunaweza kwenda huko?” Akahoji Brigedia, swali ambalo lilitakiwa kujibiwa na mtu yoyote Yule mwenye kujua jibu lake.


“Muda wowote pale kwa nilivyowai kuona kipindi nilichowai kufika pale kupeleka mzigo wa bosi mmoja ambaye naye chakula kama wenzake niliona muda wote kuna pilika pilika za ingia toka kama zote tu.. Hivyo nafikiri twendeni na kwa urahisi zaidi njia inayokwenda huko ipo moja kwakuwa jengo lipo kando kando ya ufukwe wa bahari, hivyo tunaweza tega mahali na tukawanasa kwa mtindo kama unataka kumtumia unamtongoza”. Cisco akaeleza na wote waliomo mule ndani ya gari wakakubali kwa kutingisha vichwa vyao.


“Dereva! Twendeni huko… Gari itatubana sana tukiwapata hao wanaharamu ila tutawaminya humu humu vizuri tu” Akaongea na kutoa hoja aliyojijibu mwenyewe Brigedia Fernandes.


***** ***** *****


Gari ilikwenda na kupaki mahala walipoona ni sawa wao kusubiri kilicho ndani ya makubaliano yao na kweli walifanikiwa kuwapata watu waliokuwa wanawahitaji na wakaondoka nao wakiwa wamewadhibiti kwa stahili ya pumzika bila kupenda maana kila waliyekuwa wakimpata walikuwa wakimnusisha poda yenye sumu isiyo ua inayozimisha kwa usingizi mzito usio na fahamu wala kuhisi chochote.


Waliondoka na watu wale wenye tabia za kishoga bila kushtukiwa na watu wengine wowote iwe wasio na tabia zao na hata wenye tabia kama zao.


“Sasa hapa twendeni tukatafute mahala ambapo tutajituliza zetu hadi muda muafaka utakapofika. Nashukuru katika wote hawa tumefanya machagua mazuri sana maana karibu kila mmoja kuna anayefanana naye kimwili na wafungwa ndugu zetu walio safarini….Wenye kuujua vizuri huu mji waseme chimbo gani lililotulia tunaloweza kwenda tukapata chakula na vinywaji bila kusumbuliwa na chochote kile kama mjuavyo hatutakiwi kujulikana kama sisi ni watu wa aina gani katika Segundo hii” Akaongea Brigedia, wakati huohuo dereva wao alikuwa akipangua gia kurudi katikati ya mji.


“Twendeni Las Lamas Hotel & Club… Huko kuna sehemu nzuri za kupumzika tutaweza kutulia mahala pazuri sana bila kufuatiliwa fuatiliwa sababu hakuna maaskari wanaofika huko kikazi zaidi ya kufuata starehe tu pia kuna mkataba wa amani uliingiwa huko miongoni mwa magenge ya uuzaji mihadarati katika Veracruz” Kijana aliye pembeni ya Brigedia Feca akaongea huku akisinzia sinzia sababu kati ya vijana hawa yeye pekee yake ndiyo alikuwa akitumia unga na bangi wakati wenzake walikuwa ni wavutaji bangi na wanywaji wa mapombe makali, yeye alikuwa pombe si sana kama wenzake ila unga kwake ilikuwa cronic mpaka muda mwingine walikuwa wakienda chukua mzigo onja alikuwa yeye lakini kitu kimoja kikubwa alichonacho yeye mpaka Ivan kumchagua kila mahali anapokwenda kufanya kazi yoyote ni kuwa alikuwa muuaji katili sana na pia mtesaji mwenye kutesa kikatili sana kama alivyo Wolfs ‘Hitler’ ila yeye jina lake Bezela Muricho ‘Animal’.


“Sawa.. Dereva tuelekee aliposema Bezela, njaa inauma nafikiri na wengine nao muda ndiyo huu wa kula” Brigedia Fernandes akakubaliana na alichosema Bezela Muricho ‘Animal’.


Safari ya kuelekea Las Lamas Hotel and Club iliacha watu wote walio ndani ya Toyota Hiace kuwa kimya bila maongezi yoyote, kila mmoja alikuwa akitafakari analolifikiri kichwani mwake na kama kawaida sigara kubwa na ndogo zilikuwa zikichomeka kwa stahili ya bandika bandua.


Dereva alipiga mwendo kwa kasi ya kawaida, dakika ishirini zilitosha kuwafikisha eneo husika ilipo hotel Las Lamas.


“Cisco, Alex, Alejandro na Juan chukueni hii pesa mkalete vinywaji na chakula… Watakaohitaji kwenda ndani ya club kulia hukohuko chakula na kufanya starehe zingine ruhusa kufanya hivyo limradi mkawe makini mambo yasiharibike” Gari ilipopaki kwenye maegesho yaliyo nje ya hotel akaongea Brigedia.


Vijana wote wakiwa na furaha wakashuka kwenye gari wakimuacha mtoa ruhusa mwenyewe na Ivan ‘alto’ tu, Brigedia akitabasamu kwa jinsi walivyoshuka kwa kasi.


“Mmeamua wote kwenda ndani ya club… Vipi hapa kuna totoz za kujiuza?” Akaongea na kuuliza Feca ikiwa vijana washashuka wawili watatu wakibaki kumsikiliza.


“Wa kumwaga yaani kama Segundo yote imehamia hapa.. Watoto wakali kweli kweli pesa yako tu” Akajibu Cisco na wote kwa pamoja wakacheka na kugonga mikono yao kwa furaha.


“Juzi nilitoa ugwadu nilivyokuwa Mexico City.. Huko uvumilivu ulinishinda nikaamua nifanye kweli” Akasema Feca huku sura ya mke wake ikimjia usoni na kutamani angemjulia tu hata hali maana toka atoke gerezani aliongea na familia yake mara moja tu wakati anawapa taarifa waame haraka sana Columbia, Washington.


“Mkuu! Kukaa na ugwadu kwa siku zote hizo wakati huko uraiani si vizuri kabisa” Akaongea tena Cisco.


“Sawa Cisco! Ila kwanza niletee chakula nile nipate nguvu ya kazi, wanawake hata Petatlan wapo wa kumwaga, hii Mexico watoto wa kilatin ni watoto barikiwa sana kwa uzuri nchi yetu ina watoto wazuri sana kwa kweli..”


“Chakula gani utakula?”


“Nimemisi nyama ya nguruwe… kalete kilo mbili tuje tule mpaka itukinai mimi na mwenzangu mpenda mnyama huyo, tuletee na viazi mviringo vya kukaanga sahani mbili, tia pilipili na mboga mboga kwa wingi na vinywaji lete maji ya kunywa tu”

“Ok! Dakika chache nivumilieni nitawaletea msosi…” Kichogo kilishageuzwa wakati akijibu hivi Cisco ‘la culebra’ akatokomea kwenye geti fupi linaloelekeza unakoelekea ni sehemu ya huduma ya maakuli.


Ukiacha Brigedia Fernandes ‘Feca’ na Ivan kubaki kwenye gari wakiwalinda wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ambao waliwateka kwa nia ya kwenda kuwageuza bucha muda utakapofika, kwenye gari hii alibaki na dereva wa safari yao hii toka Petatlan, Guerrero kuja huku Segundo, Veracruz, bwana huyu dereva mwenye sifa zake kwenye kukimbiza gari kuliko madereva wote katika genge analolimiliki Mr. Guti alikuwa akiitwa Maxi Anguelo Rude ‘Bwoy’ kwa genge wakipenda kumuita ‘Rude Bwoy’.


Waliletewa nyama ya nguruwe idadi ya kilo walizotaka na viazi vilivyokatwa katwa kwa mtindo ambao sisi wa tz tunaita ‘chips’ na vinywaji mbalimbali na mara moja upande wao walianza kupiga mambo wakiwa hawana wasiwasi wowote maana mateka wao walikuw na uhakika hawataweza kuamka toka kwenye kuzirai kwao kwa dozi ya madawa waliyowanusisha.


Wakiwa wamepumzika kwa muda mrefu wakibadilishana mawazo na kila mmoja kumjua mwenzie zaidi na zaidi kati yao hasa Ivan ‘alto’ aliyekuwa kama kawaida stori akiwashilikisha wenzake kwa stahili ya kuandika kwa haraka anachotaka kusema kuchangia mada mbalimbali kati ya mada walizokuwa wakibadilishana uzoefu kwa kila mmoja anachojua.


Saa mbili na robo usiku iliingia meseji kwenye simu Brigedia Fernandes cf ikimtaarifu kuwa gari ya wafungwa iliyowabeba watu anaowahitaji ipo kwenye mpaka wa kuingia jimbo la Veracruz.


“Muda wa kazi umefika jamani… Gari iliyobeba watu wetu iko mpakani hivyo Rude ingia ndani waambie jamaa watoke twendeni kazini” Akaongea Feca na dereva akajifuta mikono yake vizuri na kushuka garini kwenda ndani ya club walipo wenzao wakipata starehe mbalimbali na hata wengine walikuwa wameshapata huduma ya ngono inayotolewa na wanawake wanaojihuza katika club hii.


Dakika kumi Rude alirudi nao wote wakaingia ndani ya gari na dereva akawasha gari wakaondoka kwa maelekezo ya Brigedia kuwa waende wakasubiri kwenye barabara ya corner of Jalisco ambapo walipanga kulivamia na kuliteka gari lililowabeba wafungwa wanaohamishwa, ambapo taarifa kamili zilitumwa kwao kuwa haikuwa liko peke yake nyuma yao kulikuwa na gari inayotizama usalama ikiwa na maaskari gereza kama watano.



ILIPOISHIA SEHEMU YA 08…!!

Waliletewa nyama ya nguruwe idadi ya kilo walizotaka na viazi vilivyokatwa katwa kwa mtindo ambao sisi wa tz tunaita ‘chips’ na vinywaji mbalimbali na mara moja upande wao walianza kupiga mambo wakiwa hawana wasiwasi wowote maana mateka wao walikuw na uhakika hawataweza kuamka toka kwenye kuzirai kwao kwa dozi ya madawa waliyowanusisha.


Wakiwa wamepumzika kwa muda mrefu wakibadilishana mawazo na kila mmoja kumjua mwenzie zaidi na zaidi kati yao hasa Ivan ‘alto’ aliyekuwa kama kawaida stori akiwashilikisha wenzake kwa stahili ya kuandika kwa haraka anachotaka kusema kuchangia mada mbalimbali kati ya mada walizokuwa wakibadilishana uzoefu kwa kila mmoja anachojua.


Saa mbili na robo usiku iliingia meseji kwenye simu Brigedia Fernandez ikimtaarifu kuwa gari ya wafungwa iliyowabeba watu anaowahitaji ipo kwenye mpaka wa kuingia jimbo la Veracruz.


“Muda wa kazi umefika jamani… Gari iliyobeba watu wetu iko mpakani hivyo Rude ingia ndani waambie jamaa watoke twendeni kazini” Akaongea Feca na dereva akajifuta mikono yake vizuri na kushuka garini kwenda ndani ya club walipo wenzao wakipata starehe mbalimbali na hata wengine walikuwa wameshapata huduma ya ngono inayotolewa na wanawake wanaojihuza katika club hii.


Dakika kumi Rude alirudi nao wote wakaingia ndani ya gari na dereva akawasha gari wakaondoka kwa maelekezo ya Brigedia kuwa waende wakasubiri kwenye barabara ya corner of Jalisco ambapo walipanga kulivamia na kuliteka gari lililowabeba wafungwa wanaohamishwa, ambapo taarifa kamili zilitumwa kwao kuwa haikuwa liko peke yake nyuma yao kulikuwa na gari inayotizama usalama ikiwa na maaskari gereza kama watano.


ENDELEA NA DODO…!


MAUAJI YA KUTISHA KONA YA JALISCO

Toka walipokuwa hadi huko Corner Of Jalisco kulikuwa na umbali mrefu kidogo hivyo dereva ilibidi aendeshe kwa spidi iliyo kubwa kidogo hili wawai.


Corner Of Jalisco, usiku wa saa tatu uliwakuta kikosi kazi cha vijana wa Mr. Guti wakiongozwa na Brigedia Fernandes Carlos Codrado pamoja naye mzee wa vitendo zaidi Ivan a.k.a alto.


“Nafikiri hatujachelewa Ivan!” Feca akaeleza wakati dereva akitafuta sehemu atakayoweza kupaki gari vizuri zaidi, Ivan akatingisha kichwa stahili ya kukubali asemacho Brigedia.


“Weka gari pembeni ya ukuta wa nyumba ile pale, nafikiri pale pametulia zaidi” Akaelekeza Feca na dereva bila kuchelewa akailekeza gari mahali alipoelekezwa na boss wao kwa hapa.


“Kamishina mdogo amenionya kuwa nisimpigie tena simu kwa usalama wake hivyo nachotaka tuamini tu kuwa tuko sahihi kuwa hapa kwa wakati sahihi… ,Cisco,Alex, Javier na Bezela kasimameni pembeni ya ule mti mkubwa karibu na daraja wakati hapa nitabaki mimi, Maquez, Mikael na Silvestre… Ivan,Wolfs, Alejandro na Klaus chukueni nafasi upande wa pili ule, nyie wa pale mbele nitaomba mkawe makini kuangalia kwa kule bondeni yanapotokea magari kuja huku mtatupa ishara kisha mtajificha kwenye nguzo za daraja wakivuka daraja tu na kuwapita mtaanzisha mashambulizi kulishambulia gari la nyuma lenye maaskari wanaowasindikiza na mkiona wanajibu mashambulizi mtawarushia bomu la kutupwa na mkono.. Nyie kina Ivan mtashambulia matairi ya gari lililowabeba wafungwa kwa upande wenu wakati sisi tutashambulia matairi ya gari kwa upande wetu na mara moja wa kutoka nyuma mtakuja kwa kasi kwenye gari husika na sote tutalizunguka gari lile na kuwaweka chini ya ulinzi na hapo mimi nitavua sox ya usoni wakishaniona tu ndugu zangu naamini watatoa ushirikiano na mchezo wa kufanya tulichopanga utaanzia hapo” Maelezo marefu yakatoka kwa Brigedia Feca na hakuna aliyeremba kila mmoja alichukua zana yake ya kazi za kazi wote wakashuka garini wakimuacha dereva peke yake.


Mateka wao mpaka muda huu walikuwa bado wapo katika hali ya kuzimia nusu kaputi hivyo hawakuogopa kuwaacha wenyewe tu wakiwa na dereva katika gari sababu pia walikuwa wamefunga mikono kwa nyuma kwa kamba za nyaya ngumu za umeme na miguu pia hawakuipa uhuru nayo waliifunga.


Dakika hadi ishirini na tano toka wafike hapa zilipotea walikuwa wakiona magari tofauti tu yakitokea njia inayoingia jimbo la Veracruz mpaka kwa wengine walianza kuhsi pengine wamekosea njia au pengine washapita wanaowatega.


Mshale wa saa kabla haujasogea zaidi kuusogelea muda wa saa nne usiku, kule walipo kina Cisco mmoja wa watu waliokuwa kule aliinua mkono juu kwa kupunga usawa wa saizi ya kichwa chake mara mbili na kusababisha waliokuwa kwa nyuma yao kupata ishara ya kuwa gari kusudiwa limeonekana.


Baada ya ishara ile kikosi kile kilifanya kama maelekezo ya kiongozi wao yalivyoelekeza, wakasogea kwa kasi zilipo nguzo zinazoshika daraja wakajificha kukawa kimya kana kwamba kulikuwa hakuna watu eneo lile.


Gari aina ya Mercedes Benz Sprinte mali ya jeshi la magerezar, rangi nyeusi ilitangulia mbele kuinuka muinuko wa kuingia kwenye daraja la mto Actopan, mto unaokatiza katikati ya jimbo la Veracruz kuja hadi huku pembezoni mwa jiji au waweza kusema mwanzoni mwa jimbo hili kubwa sana lenye mito mingine kadhaa.


Nyuma ya gari hii ya Mercedes Benz Sprinter ambayo kwa huku kwetu unaweza kuifananisha na gari aina ya Noah ila hii kwa kuitizama tu unatambua jinsi gani ilivyo imara zaidi ya Noah za mjapan, mbele ikiwa na kioo ambacho ni proof (kinazuia risasi) na maandishi madogo ya rangi nyeupe ‘Prison’, nyuma yake kulikuwa Land Rover Defender iliyokuwa na maaskari wenye bunduki aina ya riffle gun.


Gari ndiyo ambayo ilikuwa ndiyo kusudio la kikosi kinachoongozwa na Brigedia Fernandes lilimaliza daraja hili lenye urefu wa mita ishirini na tano likaendelea na safari lakini gari iliyobeba maaskari magereza wasindikizaji ilipomaliza daraja tu, kijana mmoja aitwaye Javier mmoja wa vijana kati ya vijana waliojificha pembeni ya nguzo zilizotengenezwa kushikana na mwanzo wa daraja alijitokeza kwa pembeni bila kuogopa magari yaliyokuwa yanakuja nyuma ya magari haya kisha akapiga risasi dirisha la mlango wa upande wa dereva na kwakuwa dereva hakuwa kapandisha kioo risasi toka kwenye bunduki aina ya ‘Agram 2000, Sub Machine Gun’ itengenezwayo nchini Croatia ilikita na kupasua upande wa kulia kichwa cha dreva, ubongo na damu uliruka kwa nguvu toka ndani ya kichwa cha muhusika baada ya risasi ile moja tu kufumua tundu kubwa upande wa kushoto, huku maubongo yaliyojichanganya na damu ya moto kumrukia askari magereza mwingine aliye upande wa pili ambaye alikuwa akivuta sigara ikamtoka mdomoni kwa mshtuko mkubwa.


Gari iliyumbayumba na kujikuta inaelekea kwa bondeni kwa kasi lakini haikufanikiwa kufika katika mstari wa mwisho wa barabara hili itoke nje ya barabara, bomu la kutupwa kwa mkono lilirushwa kifundi na mmoja wa kijana wa Feca aitwaye Juan lilipenya katika dirisha lile lile la dereva na kuzusha taharuki kubwa ndani ya gari kwa maaskari magereza ambao ni kama walikuwa wamepigwa na butwaa kwani hawakuwa wameterajia jambo kama hili walikuwa wakienda wakipiga soga na kupata burudani ya sigara kubwa (bangi) na sigara ya kawaida.


Kabla hawajajua wafanye nini na kwakuwa bomu lilipodondoka lilidondokea kwa chini ya viti na wote waliona na kusikia kitu kimetua lakini kuyumba yumba kwa gari iliyokuwa kwenye kasi kuliweza kuwafanya washindwe tumia akili ya haraka katika kujiokoa kwa namna yoyote ile.


Gari ilipohama kwenye mstari na kutaka kuanza kupinduka ulisikika mlio mkubwa uliombatana na mwangwi mkali wa moto uliolipuka eneo lote la mbele ya kidogo ya daraja la mto Actopan karibu na kona ya Jalisco kuwa kama kumewashwa taa kubwa.


Land Rover Defender ililipuka yote kwa mshindo ule mzito kisha ikaserereka kuelekea bondeni, bonde la mto Actopan.


Mshindo wa mlipuko uliwastua sana wote walio ndani ya gari iliyobeba wafungwa, si askari mmoja aliyekuwa kakaa mbele na dereva wala dereva mwenyewe aliyeacha kushtuka, dereva akapoteza umakini akaanza kuyumba yumba huku wafungwa walio nyuma ya cabin walikuwa wakipiga kelele zisizoeleweka.


Brigedia Fernandes na vijana waliokuwa wamejigawanya pande zote mbele wakati gari inawapita walitokeza na Klaus ambaye yeye na wenzake wengine walikuwa upande wa kulia wa barabara akitumia bunduki inayofanana aina na wenzake wote aina ya ‘Agram 2000, Sub Machine Gun’ alipiga risasi matairi ya gari yote mawili yaliyo upande wake na kabla gari haijalala upande huu wa kushoto matairi yake yalipopigwa risasi ilijikuta ikikaa sawa kwani upande wa kulia tayari Brigedia Fernandes aliyapiga risasi matairi ya upande wake.


Kwa kasi wote waliokuwa nyuma na kufanya shambulizi kwa Land Rover Defender wakiongozwa na kijana jasiri sana mwenye roho ambayo ni roho ambayo kwa kiasi kikubwa ni roho ambazo ni mfanano tu kwa wote kati ya vijana wakiongozwa na mtu katili sana ‘alto’ Ivan mtu mrefu na mwenye silika ya ukimya uliopitiliza umuonapo lakini ni sumu zaidi ya sumu kali za kibaolojia zinazotengenezwa nchi mbalimbali zilizokwisha endelea, vikundi vyote vilivyogawanya kama ni wepesi walikuwa wepesi haswa maana walifika na mara moja gari ile ikazungukwa.


Usoni mwao hakuna aliyekuwa na uso usio na sox, wote walivaa sox nyeusi zilizoacha uwazi machoni na mdomoni.


“Shukeni ndani ya gari..” Brigedia Fernandes ‘Feca’ akatoa amri kwa lugha yao ya Mexico ‘kihispaniola’ kuwapa dereva na askari aliye upande ule na wote wakashuka upesi sana.


“Piga magoti” Akawaamrisha na jamaa bila kupoteza wakati wakaenda chini kwa kasi tena kwa pamoja


“Nyosheni mikono juu hakuna hata kujikuna..!” Akaamrisha tena na kwakuwa wenzake nao wapo waliokuwa wamesimama nao aliwaacha na kwenda mlango wa nyuma walipo wafungwa ambao wao walikuwa wakiangalia mchezo tu huku wakiwa hawaelewi kitu chochote maana hawakuwa wamejulishwa chochote zaidi ya kuona wanaambiwa waingie ndani ya gari hili baada ya kutolewa ndani ya gereza.


Magari yaliyokuwa yakija nyuma yakifuata msafara huu wa magari mawili ya magereza yalisimama kule darajani huku madereva wengine waliokuwa hawajaanza kuingia na magari yao darajani wakirudi nyuma kwa kasi na hata walio mbele mawazo yakawa hivyo hivyo yaani kulikuwa na taharuki kubwa eneo lote.


Brigedia Fernandez hakutaka kuremba alipiga risasi kufuli kubwa lililofungwa kwenye mlango kisha akafungua komeo kwa kasi halafu akafungua milango hii iliyokuwa inafunguka kwa pande mbili kushoto na kulia.


Akatokeza uso wake mbele ya rafiki zake, tabasamu likajikuta linatoka lenyewe katika viunga vya uso wake. Haraka akatoa sox yake usoni kwa kuipandisha kwa juu, wote waliokuwa wakimuangalia tu huku wamepigwa na butwaa kujiuliza nani aliye mbele yao? Anataka nini? Walijikuta wanazifungua nyuso zao ghafla na kumuunga mkono kwa kutabasamu.


“Brigedia… Fecaaa!” Mmoja akajikuta anapayuka kwa nguvu, macho kayatumbua anatamani pengine yatoke katika mipaka yake kuhakiki yanachoona, akajisahau kama kafungwa minyororo miguuni na mikononi akataka kuinuka lakini alishindwa akajikuta anaenda chini na kusababisha asonye na wote kati yao wakacheka kwa sauti kubwa sana.


Brigedia ‘Feca’ akatoa kibunda cha funguo malaya za pingu toka mfuko wa suruali yake ya jeans aliyovaa na kumrushia yule yule aliyesababisha vicheko ndani ya bodi ya gari, jamaa akakidaka kibunda na mara moja akaanza kuzishughulikia pingu na minyororo waliyofungwa.


“Haraka fungueni mshuke nje ya gari mvue nguo hizo.. Kuna kazi ya haraka inatakiwa kufanyika hapa hapa kabla wingu halijaja na kutuletea usiku mwingine tusiouhitaji.. haya haraka Savatel, nimewamisi sana mpaka natamani tungekuwa hapa ndiyo maskani tuanze soga” Akaongea kwa sauti ya kasi sana Brigedia Feca na wakati huo huo Ivan alto alifika pale uso wake ukiwa ndani ya sox, Brigedia alipomuangalia tu naye akavuta sox yake kurudisha izibe uso na hapo Bezela Muricho akasogea ‘Agram 2000 SMG’ ikiwa thabiti mkononi mwake tayari kwa lolote.


“Mshawasogeza wale mashoga?” Akauliza Feca na alto akajibu kwa kukubali kwa kichwa chake.


“Cisco njoo!” Feca akamuita Cisco na mara moja akasogea pale kumsikiliza.

“Mwambie dereva alete gari hapa upesi atuzibe na upande ule wa kule ambako magari yalikuwa yanataka kuingia huku kupitia darajani wasije wakaona tunachofanya kwa mbali huko huko na kuharibu movie yetu na kina Juan waambie wawe makini kulinda upande ule magari yasije mpaka tumalize kazi yetu” Maelekezo toka kwa kamanda mwanajeshi mfukuzwa Brigedia Feca.


Wafungwa dakika mbili ziliwatosha kuondoa minyororo iliyokuwa imefungwa kwa kuzungushwa katika mikono yao na miguu yao kwa pamoja na kwa furaha kubwa kama masokwe makubwa yaliyokuwa yamejificha mvua mapangoni yametoka baada ya mvua kukata.


Gari aliyotaka Feca ifike ilifika na kuziba pale kwa nyuma ya gari ya magereza aina Mercedes Benz Sprinter.


“Vueni nguo hizo za kifungwa haraka sana kisha vaeni hizi” Akaeleza Feca kuwaeleza ndugu zake waliokuwa wakimkosesha usingizi toka yeye amalize kifungo chake.


Jamaa wakafuata maelekezo na kwakuwa ni wanajeshi wakakamavu wenye ujasiri na wepesi wa kimafunzo walifanya mambo yakawa sawa sawia kwa dakika moja tu.


“Morientes.... Tuko barabarani ingieni kwenye gari hii mkiwa mmeinama na mlale chini msikalie siti, hamtakiwi kuonekana kabisa” Feca aliendelea kutoa maelekezo kwa wafungwa rafiki zake.


“Leteni hao mashoga hapa…” Akaamrisha Feca na kwakuwa vijana wote walikuwa wakijua nini kinafuata walishawaleta wanaume wenye tabia za jinsia iliyo tofauti na jinsia yao na kati yao hakuna aliyekuwa ana fahamu mpaka muda huo licha ya kuwa wako hai lakini dawa walizonusishwa hazikuwa saizi yao kabisa, walizirai muda mrefu sana.


Haraka vijana wa kazi walichukua mavazi ya kifungwa waliyokuwa wamevaa wafungwa waliokuwa wamekuja kuwaokoa hapa toka kifungoni.


Wakati hawa wakichukua mavazi yale wengine walikuwa wakiwavua wanaume kama mabinti mavazi waliyoyavaa kisha ya hapo wakawavalisha mavazi ya kifungwa na kuwafunga minyororo pia, wakawapandisha kwenye gari la magereza kwenye bodi walipotoka wafungwa waliokuwa wakisafrishwa.


Wolfs Klauben Gend ‘Hitler’ kijana wa Mexico mwenye asili ya kijerumani muda wote wakati wenzake wakihangaika na yote haya alikuwa akivuta bangi huku mkono wa kushoto akiwa kashika chensoo ya kukatia miti na kuchana chana mbao vipande vipande, walipomaliza kuwaingiza ndani ya gari mashoga wale akatabasamu na kuweka miwani yake ya jua vizuri ambayo licha ya kuwa ni usiku huu yeye aliivaa bila kujali, Bezela naye alisogea akiwa na bunduki yake haraka akaiweka mgongoni kwakuwa ilikuwa na kamba yake ya kuining’iniza.


Wolfs Akatupa kipisi cha bangi pembeni kikiwa bado kinawaka akatoa gloves kubwa kama wanazovaa wasafisha vyoo vya public (jumuiya) sehemu wanazojali afya za wananchi wao.


Haraka wanaume hawa wenye mioyo ya kipekee wakaingia ndani ya bodi ambapo wafungwa wanaosafirishwa kupelekwa iwe mahakamani au kwingine kokote ukaa na hapa sasa wakiwa wamewaweka wasiokuwa wafungwa, watu waliowateka barabara ya kuelekea club ya mashoga ya Jogos gay’s.


Bezela akiwa mwenye kukenua meno kwa furaha akakamata kichwa cha aliye mbele yake akiwa kafumba macho hajitambui kutokana na kuwa kazirai, Wolfs akamchinja shingo kwa kutumia chensoo bila huruma kama anakata mti kumbe anamchinja binadamu mwenzake, damu zilikuwa zinaruka kama mpira wa maji uliopasuka ghafla na kuacha tundu na maji kutapakaa ovyo lakini hapa si maji ni damu nzito iliyo ya moto haswa.Sekunde ishirini kichwa kiliachana na shingo akawa kakikamatia mkono wa kushoto akakirusha nje ya bodi ambapo wenzake wawili waliokuwa nyuma yake mmoja akakipokea kama anapokea mpira wa soka.


Wolfs katili hakuzubaa kwa kasi akaamia mikono akaiondoa kwa kuikata kwapani na kuacha kiumbe huyu kuwa kama kawoshi (singilendi), hakusubiri kasi akaondoa miguu akikata kuanzia gotini (ukatili mkubwa) na vyote akawapa wanaomuangalia kazi anayofanya ambapo na wao waliweka katika mfuko mkubwa wa nailoni viungo na kichwa.


Zoezi gumu la kikatili liliendelea kwa dakika nane kwa Wolfs kufanya ukatili mkubwa wa kutisha kwa kuwakatakata kwa stahili inayofanana viumbe waliowateka na wote wakawa viwili wili tu, wote waliaga dunia wakiwa wamezimia na wote waliuliwa kwa mauaji yanayotisha sana tena na mtu mmoja Wolfs akisaidiwa na mshikaji miili inapokatwa Bezela Muricho ambaye kwa kweli kama ungemuona ungehisi labda alitumbukia ndani ya pipa la damu, alitapakaa damu nguo na mwili wote kwa ujumla.


Akashuka garini akiwa na chensoo yake mkononi, harufu kali ya damu iliyochanganyika na harufu kali ya vinyesi vya binadamu ilitapakaa pale na mita kadhaa toka pale, wachinjwaji ilionyesha dhahiri shahiri wote wakati wakichinjwa haja kubwa ziliwatoka huku mchinjaji hakuwa anajali lolote lile.


“Nashauri hii gari ya magereza tuichome moto ikiwa na hizi maiti tulizozicharanga sababu miili yao asilimia nyingi sana haifanani na miili ya ndugu zetu”. Katili Wolfs akaongea na papo hapo akaanza kutoa magloves mikononi mwake nayo yakatupiwa ndani ya mfuko uliobeba vichwa na viungo vingine vya binadamu wenzao.


“Sawa wazo zuri.. Tupige bomu maana ving’ora vya magari ya polisi vinazidi kusogea kwa kasi” Akajibu Feca na tayari kijana mwingine chakaramu haswa Cisco alishakuwa na bomu la kutupwa na mkononi mwake kana kwamba mpango wa bomu alikuwa amekubaliana na Wolfs.


Kwa mbali kulikuwa kukisikika milio ya ving’ora vya magari ya polisi, hivyo waliokuwa wakiangalia Wolfs na Bezela wakifanya ukatili wake na Wolfs na Bezela wenyewe bila kujali chochote wana madamu yamewatapakaa walijirusha ndani ya gari na kukaa kwa chini na dereva hakusubiri amri toka kiongozi wao Brigedia aliondoa gari kwa kasi, walipozunguka gari ya magereza iliyobeba wafungwa ndugu zao Cisco akatupia bomu la mkono kwenye mdomo wa tanki la mafuta na mlipuko ulifuata bila kukopesha na kukajibu kile kilichotakiwa kutokea gari kushika moto, wao wakitimua vumbi la lami na kwakuwa mbele mita kadhaa kulikuwa na magari ya watu waliokuwa wamesimama wanashindwa wafanye nini kutokana na kuwa hawakuwa wanaweza kupindua magari yao walipo na kwakuwa hawakuwa karibu sana na eneo la tukio walibaki tu.


Alejandro alitoa kichwa uso wake ukiwa umefunikwa na sox akawa anapiga risasi juu magari yasogezwe na mara moja kukazuka kizaazaa chenye taharuki kubwa sana eneo lote magari yakipiga honi na miseleleko kadhaa ya matairi hili kupisha.


Brigedia na kikosi wakawa nyuma wameacha hali isiyoelezeka watu walitokea eneo lile kwa wingi na kufanya misongamano ya magari iwe kama ndiyo mji mkuu wa Mexico linapotokea tatizo la ajali au milio ya risasi kama iliyotokea hapa na kisha waliofanya tukio kukimbia.


Dereva Rude Bwoy, mzungu mwenye kufuga nywele stahili ya rasta, nywele zake za rangi ya blonde zilizosukwa vizuri zilimfanya kuvutia sana hasa kwa mabinti, alikimbiza gari ile hadi pwani ya beach ya Playa Villa Rica ambako wote walishuka kisha gari waliyokuwa wakiitumia wakaipiga moto ikiwa pembezoni kabisa mwa bahari.


Mwisho wa sehemu ya tisa (09)


Hali bado ipo katika maandalizi kwa upande wa Brigedia Feca, maandalizi ya kutaka magenge ya Mexico yanamsujudia yeye na genge ataloliunda, maandalizi ya kufanya awe na heshima heshimika na tukuka kwa atakavyo.


Watu wake aliokuwa akiwataka sana aliokuwa nao jeshini jeshi la wananchi wa Mexico kambi ya Chiapas, furaha yake haikujificha mbele yao na hata mbele ya waliomsaidia kuwapata rafiki zake waliomtetea kwa hali na mali asifungwe lakini mambo hayakuwa vile tarajiwa na bahati mbaya akaenda jela kama walivyoenda watu wake.


Ukatili mkubwa wa kinyama ndani ya Veracruz karibu na mji mdogo wa Segundo kwenye daraja la mto Actopan kwenye kona ifahamiakayo kama kona ya Jalisco.





Kwa mbali kulikuwa kukisikika milio ya ving’ora vya magari ya polisi, hivyo waliokuwa wakiangalia Wolfs na Bezela wakifanya ukatili wake na Wolfs na Bezela wenyewe bila kujali chochote wana madamu yamewatapakaa walijirusha ndani ya gari na kukaa kwa chini na dereva hakusubiri amri toka kiongozi wao Brigedia aliondoa gari kwa kasi, walipozunguka gari ya magereza iliyobeba wafungwa ndugu zao Cisco akatupia bomu la mkono kwenye mdomo wa tanki la mafuta na mlipuko ulifuata bila kukopesha na kukajibu kile kilichotakiwa kutokea gari kushika moto, wao wakitimua vumbi la lami na kwakuwa mbele mita kadhaa kulikuwa na magari ya watu waliokuwa wamesimama wanashindwa wafanye nini kutokana na kuwa hawakuwa wanaweza kupindua magari yao walipo na kwakuwa hawakuwa karibu sana na eneo la tukio walibaki tu.


Alejandro alitoa kichwa uso wake ukiwa umefunikwa na sox akawa anapiga risasi juu magari yasogezwe na mara moja kukazuka kizaazaa chenye taharuki kubwa sana eneo lote magari yakipiga honi na miseleleko kadhaa ya matairi hili kupisha.


Brigedia na kikosi wakawa nyuma wameacha hali isiyoelezeka watu walitokea eneo lile kwa wingi na kufanya misongamano ya magari iwe kama ndiyo mji mkuu wa Mexico linapotokea tatizo la ajali au milio ya risasi kama iliyotokea hapa na kisha waliofanya tukio kukimbia.


Dereva Rude Bwoy, mzungu mwenye kufuga nywele stahili ya rasta, nywele zake za rangi ya blonde zilizosukwa vizuri zilimfanya kuvutia sana hasa kwa mabinti, alikimbiza gari ile hadi pwani ya beach ya Playa Villa Rica ambako wote walishuka kisha gari waliyokuwa wakiitumia wakaipiga moto ikiwa pembezoni kabisa mwa bahari.


ENDELEA NA DODO….!



VERACRUZ MPAKA GUERRERO-MEXICO

“Mr. Guti ndiyo amenielekeza kwa meseji kuwa tulichome hili gari moto kisha twende kwenye maegesho ya beach kuna watu wake wanatusubiri hivyo msiwe na wasi maana naona mmeshangaa sana nilivyosema tunaiunguza hii Town Hiace… Haya twendeni tuondokeni haraka hapa tayari ishakuwa imekolea tena muda wowote italia mzinga”. Haraka akaongea Feca na mara moja na watu wake wote wakaanza kumfuata kwa nyuma kwa kasi kama yeye atembeavyo kasi.


Msafara wao huu sasa ulikuwa na watu kumi na nane, kumi na mbili waliotokea Petatlan, Guerrero na sita wafungwa waliotolewa ufungwani kwa raha zao.


Hatua hazikuwa nyingi sana toka walipokuwa wanaanza maeneo ya majengo kutokea yanapoanza maji ya bahari, hatua zao zilisita kidogo kwa baadhi ya watu kwakuwa mlio wa kishindo kikubwa cha mlipuko wa gari ulisikika, gari iliyowaleta toka Petatlan ililipuka na kupoteza muonekano wake wote.


Wazee wa kazi za kazi wakiongozwa na Brigedia Feca walifika kwenye maegesho na muda huu wa usiku kulikuwa hamna watu waliokuwepo muda huu wakizagaa hapa maegeshoni, watu walikuwa wakionekana kwenye eneo la mgahawa ingawa siyo kwa wingi pia.


Kutokea kwao tu, kulisababisha milango miwili ya magari mawili aina ya Ford Ranger Wildtrack zinazofanana rangi kufunguka na kisha kila mlango mmoja alitoka kijana mmoja.


“Karibuni Brigedia Fernandes 'Feca'..!” Akakaribisha mmoja aliyeshuka gari ya upande wa kulia.

“Ahsante sana… La Bruto kama sikosei?” Akajibu salamu na kuuliza swali na papo hapo aliupokea mkono wa salamu.


“Yah! Ni mimi hujakosea, naitwa Serim La bruto… Ni meneja wa kampuni ya uuzaji wa magari ya La Bruto Car Sales iliyoko hapa , Mr. Guti alinipigia simu muda wa saa kumi na mbili jioni kuwa anahitaji kununua magari manne kwa mpigo aina hii ya Ford Ranger Wildtrack na nyie ndiyo mtakuja kuchukua hapa Playa Villa Rica” Akaeleza kwa sauti ya utaratibu kabisa ikiwa ni tofauti kidogo wanavyoongea wamexico wengine wa maeneo mengine.


“Nashukuru kukufahamu.. Kwahiyo ni mali zetu? Vijana wachukue nafasi ndani ya gari” Akauliza Feca kupata uhakika zaidi.


“Ni mali zenu… Nimeshamalizana kila kitu kipesa na Mr. Guti, alimtuma mtu wake anayeishi hapa Veracruz hivyo ruhusa wenyewe kuyafanya mnachotaka ni mali za boss wenu hizi” Akajibu Serim La Bruto pia akamkabidhi bahasha Feca.


“Hizi ni nyaraka za gari… Mnaweza kuendelea na mambo yenu” Akaeleza tena Serim.

“Ahsante sana…!” Akapokea bahasha na kumalizia kwa maneno haya, waliagana jamaa (Serim) akiwa na madereva wake wawili wakasogea hatua kadhaa wakaingia kwenye dude kali na la aina ya Maserati juu likiwa halijafunikwa, dreva aliyekuwa akiwangoja akaliondoa kwa mbwembwe sana.


“Tuko kumi na nane, hizi gari ziko nne hivyo aina budi tujibane bane hili tuondoke hapa Veracruz” Feca akawaeleza wenzake na zoezi la kuingia ndani ya magari likaanza na wote wakaenea kwa kubanana haswa.


PETATLAN, GUERRERO-MEXICO

Ilikuwa ni furaha kubwa sana katika jumba la kifahari la Mr. Guti lililopo eneo la Sierra Madre Del Sul,Petatlan Manispaa pembezoni mwa bahari ya Pacific, jimbo la Guerrero.


Koplo Maxiwell Zuantejo, Koplo Lavatel Santos, Sajenti Lara Moentes, Stafu Sajenti Morientes Gudrado, Aristos Mosquera na Mireles Gonzalez, hawa wawili wa mwisho hawakuwa na vyeo walipokuwa huko jeshini kabla hawajakutwa na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya, pamoja na kuwauzia wanajeshi wenzao madawa hayo yaliyopigwa marufuku kutumika.


Watu hawa sita ndiyo waliokuwa wasaidizi wakuu wa Brigedia Fernandes katika shughuli ya kuhakikisha biashara ya madawa ya kulevya inafanyika kwa ufasaha katika viunga vya kambi mbalimbali za jeshi la wananchi la Mexico kwa wapenzi na waathirika wa kilevi icho chenye ubaya wa kutisha katika mwili wa binadamu.


Muda wa saa kumi jioni ya siku ya pili toka usiku uliopita baada ya Brigedia na kikosi chake cha vijana wa kazi wa Mr. Guti kufanikisha zoezi la kuwatorosha wanajeshi hawa waliokuwa kifungoni, kulikuwa na tafrija fupi iliyoandaliwa na Brigedia Fernandes a.k.a ‘Feca’ akisaidiwa na mwenye nyumba hii Mr. Villa Nandez Guti.


“Mpango wetu umefanikiwa ghiliba kwa asilimia mia…! Hahhahah hahahahah hahahaha… Eee eeeeh ee shiiih raha sana… Media zote zimenukuu zile karatasi tulizozitupa tupa eneo lote lile wakati tunaondoka….Zimechukuliwa karatasi zile kuwa vile tulivyotaka, huu ni ushindi kwetu na pia ni dalili nzuri kuwa tunakwenda kufanikiwa kila jambo katika mipango yetu…!” Brigedia Feca aliongea huku lafudhi yake ikitoka kufuatana na pombe alizoanza kunywa toka asubuhi hivyo ilitoka kipombe pombe ingawa kiukweli yeye si mtu kulewa ovyo ovyo hata anywe vipi.


“Mimi ni gwiji… Na.. Sasa wasubiri mziki huu uliotoka jela kuipindua Mexico na bara zima la Amerika kusini na kaskazini kichwa chini miguu juu… Naapa kwa jina la mzazi wa Fernandes Corlos Codrado, Brigedia kigogo, Brigedia mwamba kazi imeanza simba mtawala karudi mtaani na kapewa uhuru wa kuwatumikia wahuni kwa ufasa..ha..!” Akajigamba tena Brigedia Fernandes huku akijipiga piga kifuani kwa kiganja chake, akiwa kazungukwa na wanawake mabinti watano wadogo wadogo kabisa wenye umri unaoshabahiana kwa kiasi sawa karibu wote, miaka ishirini na moja mpaka ishirini na mbili.


“Bosi wa nyika… Brigedia fundi na gwiji ambaye serikali hii itajutia kukupoteza… Hongera kaka kwa utu wako, nakuahidi kukutumikia mpaka tone langu la mwisho la pumzi yangu” Huyu alisogeza mdomo wake sikio la kulia la Brigedia Feca akawa anamnong’oneza huku anayumba yumba kwa kuzidiwa na pombe, wakashikana mikono kisha wote wakajitupa sofani.


“Naomba tusinywe tena jamani..!” Mr. Villa Nandez Guti akapaza sauti baada ya kuangalia hali iliyopo pale na kuona hakutaweza kuwa na lolote lingine.


“Kwanini boss?.. Tuna furaha heti…!” Akasema Koplo mfukuzwa na mfungwa mtoroshwa Maxiwell Zuantejo ambaye yeye alikuwa katika sofa moja na Mr. Guti, kwenye paja lake la kulia akiwa kampakata binti mrembo wa kimexico, sigara aina ya marliboro ikipulizwa na kimiminika cha pombe kali kikimburudisha kwa fujo.


“Tuna kikao leo usiku na sherehe hii ilikuwa ya chakula tu lakini tumevuka mipaka na kunywa sana, sasa tutafanya kweli kikao hiyo jioni” Akaeleza Guti kwa sauti aliyohakikisha haimfikii Koplo Maxiwell peke yake bali inafika hadi sofa za jirani hapa walipo pembezoni mwa ufukwe wa bahari ulio nyuma ya jumba hili la kifahari.


Mr. Guti ambaye siku hii hakuwa anakunywa sana kutokana na kuwa alikuwa akiumwa hivyo hajisikii vizuri kunywa pombe kali kama ilivyo kawaida yake, pia alikuwa ana hamu ya kujua kitu gani rafiki yake na swahiba yake mkubwa Brigedia Fernandes anataka kuzungumza kama alivyokubaliana naye asubuhi kuwa kabla ya yote atataka wao kama wao wakae kikao kitachokuwa ndiyo muhtasari wa maongezi yao na wafuasi wao wa chini yao, alikuwa akijua Brigedia Fernandes ana mipango mingi ambayo itawafanya wapae toka mahala walipo lakini alikuwa na wasiwasi mwingi sana nini kitajiri baadaye katika maisha yake na genge litakalokuwa na watu watakaongezwa na Brigedia.


Alikuwa akijua kuna faida na hasara ya kufanya ushirika na Feca lakini hakuwa tena na ubavu wa kudhibiti hili tena, hakuwa na uwezo wa kuinua mdomo kusema ‘Fernandes' sitaki muunganiko wowote kati yetu, chukua watu wako kaanzeni maisha yenu wenyewe, niachie watu wangu ulionikuta nao’, kiburi hiki hakuwa nacho licha ya kuwa alikuwa akijiamini kutokana na roho za kazi za kazi za vijana wake ambao yeye akisema fanya hivi walikuwa hawarudi nyuma wanafanya kweli bila kujali huyo mtu ni nani? Anakumbuka mke wake kipenzi alijifanya kutaka kumuharibia mambo yake na alipowapa amri vijana wake wamchinje na kumtumbukiza kwenye pipa lililojaa kimiminika cha tindikali. Dakika kumi tu aliporudi eneo la tukio alikuta mkewe si mtu tena bali kageuka rojorojo iliyojichanganya na maji yale ya tindikali.


Kujiamini kwa Brigedia Fernandes ‘Feca’ hakukuwepo alikuwa akimjua a to z mwanajeshi huyu, pia alikuwa anatambua bila mtu huyu yeye asingekuwa hapo alipo, mtaji wa biashara hii ya haramu ilitokana na mzigo mdogo aliopewa na Feca kama malipo ya kumsaidia kupeleka mzigo kilo kadhaa Texas, Marekani.


Anakumbuka enzi hizo alikuwa pusha mdogo tu akitumwa tumwa na matajiri mbalimbali wa unga kusafirisha vimizigo vidogo lakini hakuna aliyewai kumlipa kiasi kikubwa kama alichompa mwanajeshi huyu na hapo ndipo yeye akatoka, naye akawa ana mzigo wake ingawa si mkubwa na upinzani mkubwa aliupata kwa watu wa kazi walio na uwezo, akakwepa vikwazo vingi sana na kila alipoteleza basi Feca alimuinua kwa kumpa sapoti kidogo lakini sapoti iliyomfanya aendelee na mambo yake na hivi alisaidiwa mara zaidi ya tatu.


Hivyo kwa haya yote hakuwa na uthubutu wa kumkwepa Feca na hata kipindi hiki Feca alichotoka gerezani yeye kama yeye Mr. Guti alimsaidia mambo ya kama kikosi hiki chake katika kuwapata rafiki zake na pia siku za kwanza alimsaidia kipesa katika matumizi na mambo mengine yaliyohusu pesa na kisha Feca alirejesha pesa alizoomba na kuzidisha baada ya kutumiwa na marafiki zake wa Brazil na Argentina.


“Kaka! Naomba usiendelee kunywa acha tuwaache vijana waendelee, kumbuka baadaye tuna mazungumzo sasa ukiwa umelewa sana tutashindwa kuongea..!” Mr. Guti akaongea sikioni mwa Brigedia Feca huku kamuinamia kwakuwa yeye alikuwa kasimama na Feca kaka kwenye sofa kati ya masofa mengi ya ngozi waliyokuwa yameletwa na wafanyakazi maalumu waliopamba eneo hili kwa ajili ya tafrija fupi hii.


“Sijalewa Guti, niko sawa kabisa… Mimi uwa silewi kabisa uwa nachangamka tu hivyo usiwe na wasiwasi kabisa” Akajibu Brigedia Fernandes na kisha akainuka kumuonyesha Mr. Guti yupo ngangari kivipi.


“Unaona.. Umeona! Niko sawa si unaniona.. twende kule kwenye maegesho ya boti yako hili tuongee kabisa mambo yawe vipi maana kesho nataka tufanye operesheni ya yule mpuuzi wa Tabasco, nahitaji kurudisha heshima na mali zangu kwa kuwapata hawa tuliowapata Mr. Guti nakuapia Villahermosa na Tabasco kwa ujumla tutaitia mikononi mwetu kwa nusu saa tu hata kama Fanuel Miguel Mendoza anamiliki jeshi la watu mia moja..… Kwa kikosi chetu na vijana wako tutawafagia kwa mshangao wa hali ya juu na tutarudi na kila kitu hapa” Akaongea Brigedia Feca wakiwa wameshikana mikono wanaume hawa wote wakiwa wamevaa pensi ya vitambaa vya hariri na shati pia kama kitambaa icho cha mapensi waliyovaa, ikiwa wametofautisha rangi mwingine full yake ina rangi ya bluu na mwingine njano na wote hawakuwa wamefunga vifungo vya shati na kichwani Mr. Guti alivaa kofia aina ya pama wakati Brigedia hakuwa na kofia na wote kila mmoja alikuwa kavaa miwani ya jua rangi nyeusi.


Walijisogeza hadi eneo ambalo kuna boti ya Mr. Guti inaelea elea baharini na kamba zake za kuzuia isiondoke ikiwa imefungwa kwenye nguzo, wakakanyaga ngazi za kidaraja kinachopeleka kwenye boti na moja kwa moja wakapitiliza hadi ilipo boti yenyewe wakakaa kwa mbele ya boti.


“Hapa tunaweza ongea kwa uzuri Mr. guti… Kwanza hongera kwa boti nzuri kama hii” Walipofika tu na kuweka vitako vyao mahali pa kukaa akaongea Feca akimpiga piga begani rafiki yake.


“Kawaida Feca.. Ningependa tutulie hapa katika kuelekezana zaidi jinsi gani tutafanya kazi tukiwa pamoja kwa maslahi yetu sote, maana siku ulipofika hatukuongea kuhusu hili tulizama katika kuona jinsi gani unawapata watu wako unaowaamini katika kazi.. Watu wako wamepatikana lakini sasa nini kinafuata baada ya kuwa pamoja sasa… nafahamu kinachofuata ni operesheni Fanuel Mendoza ila je tukishafanikisha operesheni hiyo nini kinafuata? Maana mimi tayari nilikuwa na genge dogo naloliongoza kwa ulinzi wangu tu binafsi na wewe hawa tuliowapata jana ni genge dogo unaloliongoza ambalo linakutii na kukuheshimu kama mimi watu wangu wanavyoniheshimu na kunitii… Hivyo hapa kuna makundi mawili tayari na maslahi yako vipi? Nafahamu kundi langu watataka kujua ingawa leo umewalipa kiasi cha pesa ambacho wote wamefurahi sana” Mr. Guti alitoa maelezo marefu kidogo huku wakiwa wanatizamana kila mmoja kakaa upande wake wakiangaliana kwa umakini.


“Nalijua hilo Mr. Guti, natambua kuna changamoto fulani… Lakini nataka nikwambie kitu kimoja una kiongozi wa kundi lako aliye bora sana ni mtu mzuri kupitiliza katika kazi na hata pasipo na kazi, mtulivu na muaminifu na mtiifu kwako.. Ivan nimetokea kumkubali sana na kwa jinsi ilivyo katika genge lako hakuna ambaye havutiwi na uwepo wangu… Naomba nikuweke wazi Mr. Guti kuwa hakuna kitakachoharibika hasa tutakapokuwa tumemaliza operesheni ya Tabasco… Nitakuja na maelezo mazuri sana ambayo kila mmoja aliye shirika nasi atakubaliana na hili, nakuambia itasababisha tuwe tuna nguvu Amerika nzima kama si duniani miongoni mwa magenge ya uuzaji wa mihadarati.


“Kwahiyo jinsi gani itakuwa ni mpaka pale tutakapokuwa tumerudi kutoka kwenye operesheni Fanuel Mendoza? Na je unasemaje kuhusu genge la Los Zetas?” Akahoji Mr. Guti.


“Ndiyo… Kuwa na subira na acha leo vijana waburudike kwa manyama nyama, mapombe na mikasi ya kiutu uzima ila kwa kuanzia nataka tukimaliza operesheni marejesho tutaunda mfumo mpya wa kundi letu tukiwa unit hivyo vumilia kwanza Mr. Guti na hata wapuuzi wa Los Zetas wasikubabaishe nawajua viongozi wao wote katika uwezo wao wa kijeshi hivyo hawawezi kututisha mimi na kina Koplo Maxiwell Zuantejo” Feca akamalizia kwa hivyo kisha wakendelea na maongezi mengine huku wanakunywa pombe, sigara nazo kwa stahili ya panda mti kata mti.


***** ***** *****


VILLAHERMOSA, TABASCO-MEXICO

Tabasco ni moja kati ya majimbo 31 yanayounda nchi ya Mexico likiwa upande wa kusini mwa nchi, mji mkuu wa jimbo hili na makao makuu ya jimbo ni mji wa Villahermosa. Jimbo likiwa limepakana na jimbo la Veracruz, Campeche na nchi ya Guatemala hivyo jimbo hili ni jimbo lililo mpakani kati ya mpaka wa Mexico na Guatemala.


Mtaa wa Avenida Pasco Usumancita kiwanja namba 526 kilichojengwa amursement park kwa kuielezea kasri kubwa la kifahari lililozungukawa na eneo kubwa sana lililokusanya bwawa la samaki wa maji baridi aina mbalimbali la kutengenezwa lenye upana wa mita za mraba 255 na urefu mita za mraba 305, miti mizuri ya matunda mbalimbali pamoja miti ya mikokoni iko kama minazi lakini yenyewe ikinyooka ikiwa kama mapambo kwa jinsi inavyopangwa mstari pia kulikuwa na maua mbalimbali ya kunukia ya kuvutia sana yalipandwa kuzungukwa eneo hili la bwawa,wanyama kama swala na pundamilia pia walikuwepo kupendezesha eneo hili, ndege wakubwa kwa wadogo wanaoruka na kutambea kama tausi nao waliranda randa eneo la hifadhi hii ndogo unaweza kuita kitalu ndani ya eneo la mtu binafsi.


Huku eneo la nyumba yenyewe iliyo na jumba tunaloweza sema ni kasri nyuma lilikuwa na mabwawa ya kuogelea (swimming pool). Uwa mkubwa uliojaa magari ya kifahari toka kila kampuni ya magari ya kifahari unayoijua wewe yalikuwepo hapa yakiwa katika rangi tofauti tofauti huku ya rangi ya nyeusi yalitawala zaidi, uwa huu ulikuwa mbele ya kasri hili jeupe lenye kung’aa.


Kasri la ghorofa (losheni) tano la rangi nyeupe kuanzia juu mpaka chini ukiacha bati juu lenye rangi la kijani lilifanya eneo hili lote la Avenida Pasco Usumancita watu wakipita karibu na jumba kusifia ujenzi uliofanywa na wajenzi wa kasri hili na hata wengine kati ya hao wakifika eneo hili huko kwa nje kuona tu uzuri wake sababu ilikuwa si ruhusa mtu asiyejulikana na wenye kasri hili kusogea karibu na hata uzio mkubwa wa senyenge ilindwayo kwa umeme na makamera iliyozunguka eneo lote ambalo unaweza kujenga viwanja nane vya mpira wa miguu na bado zikabaki mita kama hamsini hivi.


Kasri hili kwa wenyeji wa mitaa iliyopo kando kando ya manispaa ya Villahermosa na hata wenyewe wakazi wa kasri hili walikuwa wakipaita ‘Miguel Palace’ kwa kuwa mwenye jumba hili ni mfanyabiashara mwenye jina kubwa sana na ushawishi wa kutosha katika Tabasco yote, Mr. Fanuel Miguel Mendoza.


Alikuwa ni mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya ‘Miguel La Plancha Compania Limitado’ kwa kiingereza unaweza kuita ‘Miguel Iron Co. Ltd’, kampuni inayomiliki viwanda vya kuyeyusha na kuunda vyuma vilivyopo katika majimbo matatu makubwa ya Mexico, jimbo la Tabasco ambalo ndipo anapoishi yeye mwenyewe manispaa ya Villahermosa, jimbo la Jalisco na jimbo la Guanajuto. Viwanda alivyofungua miaka miwili tu iliyopita tena kwa mara moja kwa pamoja na kuanza kazi ya uzalishaji kwa mara moja pia, wakikamata soko kwa makampuni makubwa ya ujenzi.


Fanuel Miguel Mendoza hakuwa mwanasiasa lakini kwa jinsi alivyokuwa mtu wa kupenda sana kutoa misaada kwa wananchi hasa manispaa yake anayoishi Villahermosa ambapo alijenga hospital kubwa yenye kutoa huduma kwa wagonjwa wa kila aina kwakuwa aliweka madaktari wenye uwezo mkubwa akiwalipa vizuri, umaarufu wa hospitali yake ulikuwa mkubwa ukivutia hadi watu wa kutoka manispaa zingine zinazounda jimbo la Tabasco. Hii ilimaanisha laiti angetaka kugombea chochote katika jimbo hili angepata iwe useneta wa manispaa au hata ugavana wa jimbo.


Huyu mtu mwenye kujipenda sana kimavazi katika mwili huku akipenda sana kufanya mazoezi ya kukimbia kila asubuhi ya kila siku akizunguka katika eneo lake analoishi, alikuwa na mwili wa minyama ya kitipwa tipwa pamoja na kujitahidi kwake kufanya mazoezi bado vyakula anavyopenda kula kwa wingi vilimfanya aendelee kuwa tipwatpwa, urefu wa wastani na sura ya kawaida kama wanaume wengi wa Mexico huku akipenda kuvaa hereni kubwa za kuning’inia akibadili badili aina za madini kila siku kulingana na nguo alizovaa, mabangili ya madini mikononi, saa ya gharama na macheni pia ya madini ya gharama kama tanzanite, dhahabu na silva. Huyu ndiye mtu ambaye Brigedia Fernandes alimuulizia kwa rafiki yake Mr. Guti na kupewa jibu yupo Tabasco akiwa ni ‘Kingpin’ taita mkubwa sana wa biashara ya ulanguzi wa mihadarati.


Kampuni ya ‘Miguel La Plancha Compania Limitado’ ilikuwa ni kampuni ya siri ya utakatishaji wa fedha kwa bwana mkubwa huyu, alianzisha viwanda anavyovimiliki na hospital yake pia kwa ajili ya pesa nyingi sana anazoingiza katika biashara haramu ya madawa ya kulevya alikuwa akiingiza mzunguko wake katika biashara halali zinazofahamika kwa serikali na hapa ndipo lilipotimia neno la utakatishaji wa pesa.


Mwisho wa sehemu ya kumi (10)


Sherehe inaendelea Tetaplan, Guerrero.

Sherehe ya ushindi wa kuwakomboa toka kwenye gereza la Matamoros kwa njia ya kuwalaghai wakuu wa magereza kwa karatasi nyaraka zilizofanyiwa utundu na bibie mrembo mwanajeshi wa jeshi la wananchi wa Mexico, sekretari wa ofisi ya kiongozi wa nidhamu jeshini Koplo Mariana Funtes.


‘Kingpin’ aliyeibuka na kupata jina miaka minne hadi mitano iliyopita akiushika ukanda wa jimbo la Tabasco, Mr. Fanuel Miguel Mendoza naye anaibuka na kutokea kwenye riwaya yetu.


Nini kitafuata?



Fanuel Miguel Mendoza hakuwa mwanasiasa lakini kwa jinsi alivyokuwa mtu wa kupenda sana kutoa misaada kwa wananchi hasa manispaa yake anayoishi Villahermosa ambapo alijenga hospital kubwa yenye kutoa huduma kwa wagonjwa wa kila aina kwakuwa aliweka madaktari wenye uwezo mkubwa akiwalipa vizuri, umaarufu wa hospitali yake ulikuwa mkubwa ukivutia hadi watu wa kutoka manispaa zingine zinazounda jimbo la Tabasco. Hii ilimaanisha laiti angetaka kugombea chochote katika jimbo hili angepata iwe useneta wa manispaa au hata ugavana wa jimbo.


Huyu mtu mwenye kujipenda sana kimavazi katika mwili huku akipenda sana kufanya mazoezi ya kukimbia kila asubuhi ya kila siku akizunguka katika eneo lake analoishi, alikuwa na mwili wa minyama ya kitipwa tipwa pamoja na kujitahidi kwake kufanya mazoezi bado vyakula anavyopenda kula kwa wingi vilimfanya aendelee kuwa tipwatpwa, urefu wa wastani na sura ya kawaida kama wanaume wengi wa Mexico huku akipenda kuvaa hereni kubwa za kuning’inia akibadili badili aina za madini kila siku kulingana na nguo alizovaa, mabangili ya madini mikononi, saa ya gharama na macheni pia ya madini ya gharama kama tanzanite, dhahabu na silva. Huyu ndiye mtu ambaye Brigedia Fernandes alimuulizia kwa rafiki Mr. Guti na kupewa jibu yupo Tabasco akiwa ni ‘Kingpin’ taita mkubwa sana wa biashara ya ulanguzi wa mihadarati.


Kampuni ya ‘Miguel La Plancha Compania Limitado’ ilikuwa ni kampuni ya siri ya utakatishaji wa fedha kwa bwana mkubwa huyu, alianzisha viwanda anavyovimiliki na hospital yake pia kwa ajili ya pesa nyingi sana anazoingiza katika biashara haramu ya madawa ya kulevya alikuwa akiingiza mzunguko wake katika biashara halali zinazofahamika kwa serikali na hapa ndipo lilipotimia neno la utakatishaji wa pesa.


ENDELEA NA UTAMU…!


VILLAHERMOSA, TABASCO-MEXICO

“Bosi tumefuatilia vizuri habari zilizotokea jana huko Veracruz kona ya Jalisco ni kweli kama taarifa zinavyosema wafungwa waliokuwa wanajeshi waliohukumiwa kufungwa katika gereza la Matamoros manispaa ya Tamaulipas na kisha kutaka kutakiwa kuhamishwa kwenda gereza la kijeshi la Acapulco wameuliwa kwa kukatwa katwa na kisha gari yote ya magereza iliyokuwa ikiwasafirisha imelipuliwa kwa bomu la kutupwa la mkono” Alikuwa ni mwanamke mrembo mwenye sura ya kuvutia, mrefu, mwenye nywele nyingi nyeusi ndefu zilizojimwaga kichwani mpaka mgongoni, alikuwa amefika ofisi ya nyumbani ya mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya ‘Miguel La Plancha Co. Ltd’ na kuingia tu akatoa maelezo haya.


“Nimeshafahamishwa kwa uzuri juu ya jambo hilo pale tu nilipowapa taarifa mfuatilie kwa undani kama ni kweli kuhusu habari iliyotokea, nikapokea simu kutoka kwa mkuu wa polisi akanieleza kila kitu… Ila sikuwa ninajua kumbe yule niliyekuwa nimekwambia tunatakiwa tumdhibiti kwa kumsafirisha usingizi wa milele akiwa huko huko gerezani, amemaliza kifungo chake na yuko mtaani sasa sijui kwanini ilitokea watu wake walitakiwa kuamishwa ghafla gereza wakati yeye ndiyo amemaliza kifungo chake… Hili ndiyo la sisi kujiluliza kwa mapana na marefu! Maria” Akaeleza Mr. Fanuel Miguel Mendoza.


“Habari ni mkanganyiko sana maana si La Hormiga wanaotawala Veracruz si Los Zetas wala Sinaloa waliotangaza wao wenyewe kuhusika na mauaji yale ya kutisha pengine wanaogopa au wana kingine au ni genge lingine lililofanya vile na kwa ujumbe ulioachwa ni Z peke yao wanakuwa tabia ya kuacha karatasi za onyo au kujieleza kwanini wamefanya hivyo..! Najaribu kuunganisha na icho unachosema juu ya mtu tuliyetakiwa kumfyeka akiwa gerezani nasi kuzubaa…Bosi huoni ni hatari kwa hatua mbaya ya uzubaifu tuliyotumia kipindi chote wakati yupo gerezani? Huoni nafasi yetu kubwa ilikuwa kipindi icho akiwa kule?” Akahoji Maria huku uso wake na macho ukimkazia bosi wake katika hali ya wasiwasi na mambo yanayotokea yakiwa yamejifunga funga.


“Miaka naona kama imekimbia isivyo kawaida hata na mimi nimeshtushwa sana na taarifa za kuwa amemaliza kifungo chake cha miaka saba na pia jeshi limemfukuza kazi… Brigedia Fernandez ni mtu wa hatari kuliko kawaida yenye kawaida ni hatari kuliko mtu wa aina yoyote katika Mexico hii ukiacha El Chapo wa Sinaloa Cartel, Luteni Salinas muanzilishi wa Los Zetas na hata waajiri wao Gulf Cartel kimtizamo wangu hakuna anyefika kwa mtu huyu Brigedia Fernandes kwa uhatari wake..! ” Akaongea Mr. Fanuel, mgongo wake akiuegemeza kwenye mtoto wa kiti cha kistarehe kinachonesanesa na kumfanya anesenese taratibu kwa raha zake.


“Uliwai niambia hilo bosi lakini kipindi cha mwaka juzi ndiyo ulikuwa ukimuongelea kila mara lakini cha ajabu hapa kati mwaka jana hata mwaka huu sikuwai kukusikia ukimuongelea kabisa nikajua labda hakuna tena habari za kutisha juu yake… Mmh! Kwa ilivyo itatubidi tuzidishe umakini juu yake au tumtafute kwa haraka tumzime pumzi au pia tunaweza kumtafuta ukafanya maelewano ukamlipa pesa zake na faida juu… Unaonaje? Bosi!”.


“Ounces Grams 5000… Ounces Grams 5000 za cocaine nyeupe, miaka saba na nusu iliyopita ndiyo alinipatia unafikiri atasema nimlipe MX Peso ngapi? Siko tayari sababu namjua atataka kulipa na nilivyoukataa ujumbe wake kipindi kile alipotaka nimpatie nusu ya pesa ya mzigo wa ounces gram 5000.. Hapa haraka sana nataka uimarishe ulinzi wa hapa nyumbani kwangu na ma godown yangu yote ya mzigo… Pia tuma watu wawili wa intelejensia wakachunguze yuko wapi ingawa nahisi anaweza kuwa kwa sasa kaenda kwa familia yake Columbia, Washngton DC, hivyo nitatuma taarifa kwa Washingiton Boy’s watupie macho yao kwa jicho la tatu ilipo familia yake wakimuona endapo watamuona wanitaarifu haraka” Akaeleza Mr. Fanuel kisha akatoa sigara toka kwenye dash ya kuhifadhia sigara iliyopo pembeni ya meza ya ofisi yake hii ya nyumbani, maana alikuwa na ofisi hii pia ana ofisi inayofahamika na serikali iliyopo katikati ya mji huu wa manispaa ya Villahermosa.


Alipoweka sigara yake mdomoni tu huyu mwanadada aitwaye kwa ushapu mkubwa akatoa kiberiti cha gesi toka mfuko wa suruali ya jeans aliyovaa akakiwasha na kumsogezea kwenye kichwa cha sigara, bosi akasogeza mdomo wenye sigara mbele, sigara ikawashwa. Sigara aina ya Fortuna kutoka kiwanda cha sigara cha Altadis.


“Sawa..Basi acha niende kwa Ximo kiongozi wa ulinzi hapa kasri tukapange juu ya ulinzi kwanza kisha nitakujulisha juu ya nani na nani watafanya kazi ya kuchunguza juu ya mtu huyu alipotoka jela alielekea wapi? Pia nitamuagiza na kiongozi mkuu wa ulinzi Mauro ajehapa kwako na kule ofisini afike kupanga safu kali ya ulinzi wako binafsi na familia yako ya watu wa kuaminika na wenye utiifu wa hali ya juu... Wee endelea na mambo mengine bosi usiwe na wasiwasi maana naona umepooza sana.. Kiongozi wako niko makini mimi na ninaowaongoza mara moja tutampata huyu mtu kabla ya yote hawezi shindana nasi”. Bibie Maria Rodgruez ‘Baby Beauty’ kama wamuitavyo wa karibu yake katika kuficha jina lake la ukweli. Wakimaanisha kuwa mzuri kama unavyoweza kumuona ikiwa utabahatika kumuona lakini wao walikuwa wakimaanisha kinyume kabisa katika usiri mkubwa sababu mwanadada huyu mpaka kuteuliwa na Mr. Fanuel kuwa kiongozi mkuu wa kikosi chake cha kazi za mihadarati katika nchi babu kubwa kwa biashara hii ikiwa yenye upinzani na ushindani mkubwa ilikuwa si mchezo.


Mwanadada huyu si wa mchezo mchezo hasa katika mapigano ya ana kwa ana na hata kutumia silaha, hapo kabla alikuwa ni mfanyakazi wa idara ya ujasusi ya Mexico (MIA) Mexico Intelligence Agency. Alifukuzwa baada ya kukutwa na kosa kumjeruhi aliyekuwa kiongozi wa idara hii wakiwa katika mapambano na moja kati ya genge kati ya magenge yaliyo mengi katika nchi ya Mexico vinavyojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.


Maria Rodgruez alionekana akili zake haziko sawa ndipo akaachishwa kazi na hasira zake ndipo akajiunga na mambo ya biashara za madawa ya kulevya mpaka alipokutana na Mr. Fanuel Miguel Mendoza aliyemchukua kwenye kikundi chake cha siri ingawa wakubwa wengi wa serikalini walikuwa wakijua juu ya kikundi hiki na hata vikundi vingine vingi tu vilivyo Mexico.


***** ***** *****


MEXICO CITY-MEXICO

Abraham Gonzalez 49 Juara Street, mtaa iliyopo ofisi ya waziri wa mambo ya ndani wa nchini Mexico katika jiji kuu na makao makuu ya serikali ya Mexico, Mexico City.


Asubuhi ya saa nne na robo mkuu wa wizara hii ya mambo ya ndani, waziri wa mambo ya ndani ya nchi alikuwa ametoa maagizo ya kuitishwa kwa kikao na wakuu wa usalama wa nchi katika sekta mbalmbali za ulinzi zinazohudumu kwa kupokea maagizo chini ya wizara yake.


Alikuwepo katibu wa wizara hii aliyekuwa akiitwa Mr. Saul Nuahin, mkuu wa jeshi la polisi wa nchi aliyekuwa akiitwa Inspekta Jeneral Ernesto Manuel Calderon, aliyekuwa mkuu wa idara ya usalama wa taifa Meja Fransisco Calisto Mugiera na aliyekuwa mkuu wa jeshi la magereza Kamishina Nieto Luna Spreto.


Kikao hiki kilichoitwa kwa dharura kwakuwa hakikuwa kwenye ratiba zao hawa wakuu wote ila kwa hali ya mauaji ya kutisha iliyotokea jimbo la Veracruz karibu na mji mdogo wa manispaa ya Jalisco ni jambo ambalo liliwastua wao kama wana usalama wa wakuu katika nchi.


Mauaji katika nchi ya Mexico katika kila kona yanayohusisha magenge ya wauzaji wa madawa ya kulevya na biashara zingine za haramu yalikuwa si mambo mageni miongoni mwa masikio ya watu wengi walioko Mexico na hata majirani zao lakini mauaji yaliyofanywa siku mbili zilizopita yalikuwa ni mauaji ambayo vyombo vyote vya habari vya Mexico viliyapa jina kuwa ‘mauaji ya kutisha’.


Vichwa, mikono na miguu kukatwa na miili kuachwa kiwiliwili tu yalikuwa ni mauaji mapya kwao, mauaji ya kimateso kwa marehemu husika waliofanyiwa ukatili ule. Hali ya kuogofya ilitamalaki miongoni mwa wananchi wa maeneo mbalimbali mpaka wao wana usalama.


Waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa Castillo Zuguzaleta alipokea simu kadhaa kutoka kwa mabosi wa juu yake, mkuu wa nchi Rais wa wa mexico, makamu wa Rais na hata waziri mkuu wakitaka kujua kama mauaji yale yanamaanisha nini? Kuna ujumbe gani umetaka kufikishwa kwa waliofanya mauaji yale kwenda serikalini? Hivyo kwa kuanzia aliwaita hawa walio chini yake kufanya nao mazungumzo ya kina.


“Nieto! naomba utuelezee ilikuwaje? Kwakuwa wewe jambo hili limetokea katika jeshi lako la Magereza” Viongozi waliokuwa wote wako katika mavazi aina ya suti, ambapo wawili walivaa rangi nyeusi inayofanana na mmoja haikuwa suti ya rangi nyeusi ilikuwa rangi ya kijivu na wengine wawili mmoja alikuwa kavaa suti ya rangi ya kijani, rangi inayopendwa sana na watu wa jamii hii ya Mexico na mwingine alivaa suti ya rangi nyeupe kabisa. Kifupi wote walipendeza ndani ya mavazi haya ya suti ingawa kuna mwanadada mmoja mwanamitindo aliwai kuniambia mimi mwandishi na mtunzi wa riwaya hii kuwa ‘vazi la suti halimchukui mtu, awe mwembamba awe mnene wote wakivaa vazi hili watapendeza tu na kuheshimika pia’. Waziri wa mambo ya ndani aliomba mkuu wa jeshi la magereza Kamishina Nieto aelezee anachojua juu ya wafungwa ambao wao na kila mtu aliye kando ya mpango anajua kuwa wameuawa vifo vya kikatili na kutisha sana.


“Mkuu hata mimi sikuwa najua lolote juu ya jambo la uhamisho wa ghafla wa wafungwa wale, nafikiri jambo hili ameshiriki zaidi kamishina msaidizi wa jeshi naloliongoza Mr. Geraldo Muriel… Ila sikuja nae hapa kikaoni sababu yupo Veracruz kufuatilia jambo hili” Akaeleza mkuu wa jeshi la magereza Kamishina Nieto Luna Spreto.


“Simu zipo! Mkuu ningeshauri hili kikao hiki kilete majibu utakayoweza kumfahamisha Mheshimiwa Rais, ningeomba Mr. Geraldo apigiwe simu tumfanyie mahojiano akiwa huko huko Veracruz” Mkuu wa jeshi la polisi wa nchi Inspekta Jeneral Ernesto Manuel Calderon hakusubiri waziri ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hiki apanue kinywa chake kuongea jambo lingine, akatoa wazo lake.


“Naunga mkono ombi la Ernesto… Waziri mpigie simu kamishina msaidizi wa jeshi la Magereza aweze kutuambia ilikuwaje? Kwakuwa mahakama ilitoa hukumu yake kwa kile ilichokuwa inaona ni sahihi kwa wafungwa wale kutumikia vifungo vyao wakiwa gereza la adabu la Matamoros, Tamaulipas” Mkuu wa idara ya usalama wa taifa Kamishina Meja Fransisco Mugiera akaunga mkono wazo la Inspekta Jenerali.


“Sawa kama muonavyo… Naomba namba yake za simu ya mkononi” Mwenyekiti wa kikao waziri wa mambo ya ndani akakubaliana na wanavyotaka waliotoa pendekezo kamaishina msaidizi wa jeshi la Magereza kuwa apigiwe simu na ahojiwe na kamati kuu hii ya ulinzi ya taifa.


Mkuu wa magereza Kamishina Nieto mara moja alitoa simu yake ya mkononi aina ya Samsung Galaxy S8 kisha akatafuta namba ya msaidizi wake na alipoipata hakumpa waziri bali akapiga yeye mwenyewe kwa kutumia simu yake.


Simu haikuita kwa miito zaidi ya mitatu ikapokelewa na anayepigiwa.


“Hallooo!” Sauti ya Mr.Geraldo ikasikika punde tu alipopokea.


“Mr. Geraldo, niko kwenye kikao na Waziri pamoja na maafisa wengine wa polisi na usalama… Naomba uongee na Waziri ana mambo anataka kujua kutoka kwako mambo ambayo mimi nilisema tutayaongea vizuri ukirudi Mexico City..!” Akaongea Kamishina Nieto.


“Okay! Haina shida niko hotelini nilikuwa naangalia angalia picha za CCTV zilizochukuliwa karibu na daraja” Akaeleza Kamishina msaidizi wa jeshi la magereza Mr. Geraldo na mara moja simu ikatoka kiganjani mwa Kamishina Nieto kwenda kwa Waziri wa Mambo ya ndani.


“Halloo Mr. Geraldo! Habari za Veracruz?” Akaongea Waziri wa mambo ya ndani alipoipokea tu simu na kuiweka mezani ikiwa imewekwa kwenye loud speaker.


“Nzuri mheshimiwa! Habari za Mexico City na nyie?”

“Huku tunashukuru Mungu mambo yanaendelea vizuri ni majukumu ya kazi tu ndiyo yanayotutinga na kutufanya tuwe busy kama hivitulivyo sasa… Naomba nisikuchelweshe Mr. Geraldo na majukumu yako ya kikazi huko, nilikuwa nahitaji kujua ilikuwaje wafungwa waliohukumiwa na mahakma kutumikia kifungo chao katika gereza la Matamoros, Tamaulipas kuhamishwa ghafla kwenda gereza la kijeshi la Acapulco.. Tunataka kuanzia kwa yule aliyetia sahihi ya kuridhia kuhamishwa kwao ambaye ni wewe” Maelezo yenye maswali ndani yake yalitolewa na mheshimiwa waziri.


“Makaratasi nyaraka ya kuhitaji sahihi zangu niliyakuta mezani mwa ofisi yangu, makaratasi ya nyaraka yaliletwa na sekretari wangu wa ofisi Mrs. Magdalena Cralla Heus… Nilipomuuliza nyaraka zile zimeletwa na nani akasema zimeletwa na mjumbe kutoka makao makuu ya jeshi kuwa wanawahitaji wafungwa wao wakaendelee na kifungo katika gereza lao la Acapulco…” Akajibu Mr. Geraldo.


“Hizo nyaraka toka makao makuu ya jeshi zilikuwa zina saini ya nani? Maana kwa nijuavyo wao waliridhia hukumu ya mahakama kuwa wafungwa wao kwakuwa walihusika na ufanyaji biashara haramu ya marijuana ni bora wakapelekwa gereza la watu hatari zaidi la Matamoros huko Tamaulipas na kama hujuavyo katiba yetu inazuia mhimili mmoja kuingilia juu ya maamuzi yaliyokwisha kuchukuliwa na mhimili mwingine hasa huu wa mahakama unaosimamia sheria za nchi yetu” Akahoji na kutoa maelezo kidogo Waziri.


“Saini niliyoiona kwenye nyaraka na mhuri vilinishawishi mimi kufanya vile bila kutaka uhakika zaidi.. iliuwa ni saini ya Meja Sanz Manuel Fuerza mkuu wa kitengo cha nidhamu jeshini Secretariat Of The Navy makao makuu”

“Nyaraka uliyosaini iko wapi kwa sasa?” Akauliza mheshimiwa Waziri.

“Kopi nilibaki nayo ipo katika meza yangu sababu ni juzi tu hivyo sidhani kama itakuwa imeondolewa mezani mwangu na kopi ingine nilimkabidhi aliyesimamia suala hili Kamishina mdogo Maxiwell Fergata… Na hata kama itakuwa imeondolewa itakuwa imehifadhiwa mahala salama.. ufuo ilienda gereza la Tamaulipas” (Ufuo ni Kiswahili cha neno original). Akafafanua zaidi Kamishina msaidizi Muriel Geraldo.

“Tutaihitaji hiyo kopi iliyo kwako na ufuo wake huko Tamaulipas”

“Haina shida mheshimiwa Waziri.. Nafikiri mngetuma ujumbe ofisini kwangu mi nitampigia sekretari wangu ataitoa tu”

“Sawa! Mr. Geraldo nafikiri wewe huko ungerudi tu huku Mexico City kwa uchunguzi zaidi ambao sote tutatakiwa kuufanya maana kiukweli suala hili lina ukakasi mwingi wenye giza jingi pia ndani yake.. Mauaji yaliyofanyika yanatutisha tunataka kujua ukweli kama ni nani ameshiriki kucheza upuuzi huu unaofanywa mara nyingi na magenge haya ambayo mheshimiwa Rais wakati anaomba kura aliahidi kuzuia mauaji ya holela na kujitahidi kwa hali na mali kuyafuta magenge ya uhalifu na mihadarati..”. Akaeleza mheshimiwa Waziri kisha hakusubiri jibu toka kwa Mr. Geraldo, akakata simu na kushusha pumzi nzito macho akiyazungusha kwa kila mmoja aliye katika mzunguko wa kuizunguka meza iliyozungukwa na viti walivyokalia.


“Majibu ya Kamishina msaidizi wa jeshi la magereza ni majibu mepesi lakini yenye uzito ukiyasikiliza kwani kwa vyovyote lazima hata mimi ningefanya alichotaka Meja Sanz… Cha kufanya cha kwanza kabla ya yotetungepata nyaraka husika alizosaini Mr. Geraldo ziwe kama ushahidi dhidi ya Meja Sanz, kisha mpira huu tumtupie waziri wa ulinzi aongee na watu wake huko jeshi la wananchi kuleta majibu imekuwaje mi sitaki kuhisiana vibaya kama mjuavyo hali ya sasa kila aliye serikalini katika nafasi ya juu ana wasiwasi na mwenzie aliye katika nafasi nyingine kuwa anahusika na magenge haya ya mihadarati na uhalifu… hali ni mbaya sana Mexico nzima” Akaongea Waziri na kisha ya hapo akafunga kikao kwa kuahidiana wakutane kesho wakiwa na nyaraka husika kisha yeye aende kwenye ofisi ya waziri wa ulinzi.


Mwisho wa sehemu ya kumi na moja (11)

Kichwa moto kwa tajiri na mlanguzi wa mihadarati Mr. Fanuel Miguel Mendoza.


Serikali nayo chini ya Rais wa nchi wamestuka kwa hali iliyotokea ikiwa mwaka tu toka serikali mpya iingie madarakani.


Nini kitafuata?



mezani mwangu na kopi ingine nilimkabidhi aliyesimamia suala hili Kamishina mdogo Maxiwell Fergata… Na hata kama itakuwa imeondolewa itakuwa imehifadhiwa mahala salama.. ufuo ilienda gereza la Tamaulipas” (Ufuo ni Kiswahili cha neno original). Akafafanua zaidi Kamishina msaidizi Muriel Geraldo.

“Tutaihitaji hiyo kopi iliyo kwako na ufuo wake huko Tamaulipas”

“Haina shida mheshimiwa Waziri.. Nafikiri mngetuma ujumbe ofisini kwangu mi nitampigia sekretari wangu ataitoa tu”

“Sawa! Mr. Geraldo nafikiri wewe huko ungerudi tu huku Mexico City kwa uchunguzi zaidi ambao sote tutatakiwa kuufanya maana kiukweli suala hili lina ukakasi mwingi wenye giza jingi pia ndani yake.. Mauaji yaliyofanyika yanatutisha tunataka kujua ukweli kama ni nani ameshiriki kucheza upuuzi huu unaofanywa mara nyingi na magenge haya ambayo mheshimiwa Rais wakati anaomba kura aliahidi kuzuia mauaji ya holela na kujitahidi kwa hali na mali kuyafuta magenge ya uhalifu na mihadarati..”. Akaeleza mheshimiwa Waziri kisha hakusubiri jibu toka kwa Mr. Geraldo, akakata simu na kushusha pumzi nzito macho akiyazungusha kwa kila mmoja aliye katika mzunguko wa kuizunguka meza iliyozungukwa na viti walivyokalia.


“Majibu ya Kamishina msaidizi wa jeshi la magereza ni majibu mepesi lakini yenye uzito ukiyasikiliza kwani kwa vyovyote lazima hata mimi ningefanya alichotaka Meja Sanz… Cha kufanya cha kwanza kabla ya yotetungepata nyaraka husika alizosaini Mr. Geraldo ziwe kama ushahidi dhidi ya Meja Sanz, kisha mpira huu tumtupie waziri wa ulinzi aongee na watu wake huko jeshi la wananchi kuleta majibu imekuwaje mi sitaki kuhisiana vibaya kama mjuavyo hali ya sasa kila aliye serikalini katika nafasi ya juu ana wasiwasi na mwenzie aliye katika nafasi nyingine kuwa anahusika na magenge haya ya mihadarati na uhalifu… hali ni mbaya sana Mexico nzima” Akaongea Waziri na kisha ya hapo akafunga kikao kwa kuahidiana wakutane kesho wakiwa na nyaraka husika kisha yeye aende kwenye ofisi ya waziri wa ulinzi.


ENDELEA NA MAMBO


PETATLAN, GUERRERO-MEXICO

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog