Search This Blog

Wednesday, 22 March 2023

JINO KWA JINO - 4

   

Simulizi : Jino Kwa Jino

Sehemu Ya : Nne (4)


“Mwarabu wako anajua habari za soka?” Lizy akaendelea kuhoji huku akiendelea na kazi ya kuseti seti mambo picha iweze kuleta mambo wanayoyahitaji.


“Nishamuambukiza ingawa si mgonjwa kama mimi… Hahaha hahaha hahahaha… Hata ingekuwa wewe ungelala nami nyumba moja mwezi ungekutwa na ugonjwa penda soka hata kama si kwa kiasi changu lakini kingetosha kujua mawili matatu kama si matano sita” Akajibu Agent Kai na wote wakacheka kwa chini chini huku wakiangaliana, mwanadada akiwa ndani ya miwani ya kumsaidia kuona vizuri ikiwa na uwezo wa kupunguza na mwanga wa vioo vya kompyuta na luninga anavyocheza navyomuda wote akiwepo hapa ofisini.


“Picha haiwezi kuwa iko sawa ni kweli haijaweza kuleta jibu sahihi sababu zote hizi ni za Luis Suarez… Mshenzi sana huyu mtu na fundi pia ameweza kufanya fitina nzito” Kazi ilimalizika kwenye ‘google searching pictures’.


“Aiseeh! Kazi hii ina kaugumu kidogo… Sura hii ni plastic surgery, Lizy tubadili gia tudili na muhusika mwenyewe hata kama hatujui anahusika na nini? Naamini muda si mrefu tutajua anashughulika na nini? Kama ni mlanguzi wa mihadarati au anajihusisha na makundi ya kigaidi au vingine vyovyote vinavyohusiana na uhalifu tutajua leoleo…. Simu zake alipigiwa akiwa wapi?”

“Zote alipigiwa akiwa Iztapa, Guatemala ila hii simu tuliyoifuatilia ilimpigia kutokea mji wa Tetaplan jimbo la Guerrero nchini Mexico”


“Sprint wanasajili vipi namba kwenye mtandao wao bila uhakiki wa picha? Kuna kamchezo kwa watu wa Sprint waliopo Mexico na nchi zingine watu wahalifu wanasajili laini zao za simu huko kwakuwa mara nyingi ninapokuwa nachunguza laini za simu ambazo ziko mtandao wa Sprint ambazo zinakuwa na majina yenye walakini basi uwa zimesajiliwa Mexico au Guatemala nilikuwa sijatilia maanani lakini sasa sina budi kuingia kwa umakini kuangalia hili suala”

“Ni kweli kuna malalamiko hayo mengi… Kifupi Mexico takataka nyingi za kimawasiliano ambazo zinakuwa na ugumu kwetu uwa zinafanyika huko sijui kwanini mamalaka ya mawasiliano ya huko hawako makini, mambo haya tulikuwa tumezoa kupata nayo tabu kutokea nchi za afrika lakini kwa sasa na wao wamebadilika…. Sasa tunafanyaje?”

“Nataka nionane na huyu mwanamke ndani ya siku mbili zijazo”

“Mmmh! Unaenda alipo au kivipi?”

“Ndiyo kazi inaanza Lizy… Natakiwa kujua Jogre yuko wapi na huyu mwanamke ndiyo njia yetu ya kujua tunampataje Jogre..!”

“Kazi ya nje ya kazi za ofisi, pia mpaka sasa hatujui kwenye meza yake mkuu kuna kazi gani inayotakiwa kufanywa na wewe?”

“Kama kungekuwa na kazi basi angenigusia nilivyokuwa ofisini kwake na hii kazi naamini inaweza kuwa ya muda mfupi sababu cheni yake nahisi ni fupi tu, nikimpata huyo dada tu nitakuwa nimefika alipo Jogre”

“Jogre nimesoma wasifu wake naamini hata kama hana mkono mmoja kwa wasifu wake sidhani kama angekuwa sehemu nyepesi nyepesi kama unavyosema basi angeshindwa kujiondoa mikononi mwao.. Kazi unayotaka kuifanya Kai ni ngumu sana na usijiamini hivyo, fikiria hilo ndugu yangu”

“Sijalala vizuri usiku sababu ya jambo hili hivyo siwezi achia bila kujali lolote baya naamini nina uwezo wa kujilinda na kuleta ushindi upande wangu usiwe na wasi Lizy, acha tufanye kazi ya kumrudisha rafiki yetu na ndugu yetu”

“Sawa… Nipe mchakato utakavyokuwa maana mimi nitakusaidia kwenye masuala ya teknolojia ya kumfikia muhusika wetu lakini huko kwingine upo wewe”

“Safi kwa kukubali… Hili suala tunapeleka ombi wote kwa chifu hivyo inuka unisindikize..!”

“Sawa! Kuna kazi namalizia kuifunga haraka tunaenda nisubiri dakika nne au tano”


Dakika kumi mbele ziliwakuta katika ofisi ya katibu wa makamu wa Rais wa nchi ya Marekani na kama bahati kwao walimkuta bado hajaenda kwenye kikao ambacho muda ujao wa kama masaa mawili mbele kilitakiwa kufanyika ndani ya ukumbi wa ofisi ya makamu wa Rais.


“Mmeongozana kuna jambo nafikiri!” Chief executive of the vice president (katibu wa ofisi ya makamu wa Rais) akawahoji baada ya kuwakaribisha na wao kuvuta viti vinavyowahusu kuketi.


“Ndiyo mkuu tuna jambo ambalo tunatakiwa kuliwakilisha kwako na kisha likafanyiwa kazi kama utakubaliana nalo” Akajibu Agent Kai.


“Vizuri sana niko tayari kuwasikiliza… Vipi kwanza ofisini kwako vijana wako watatu hujawaona ndiyo umekuja kuuliza walipo?” Waliruhusiwa kuongea walilonalo lakini pia alimuuliza swali Agent Kai.


“Natambua watakuwa kwenye majukumu ya kiofisi hivyo niliwaulizia kwa wenzao niliowakuta wakanielekeza kazi ambayo wameenda kufanya na watu wa makao makuu huko Romania, nawaombea dua njema wafanye kazi kwa mafanikio na warudi salama!” Akajibu Kai.


“Amini! Amini… Leteni habari” Akaongea Chifu kama wenyewe walio ofisi hii walivyopenda kumuita.


Agent Kai akiwa muongeaji mkuu alieleza yote yalivyo kuhusu barua pepe iliyotumwa kwenye akaunti yake, ilivymshangaza kwa jinsi mtumaji alivyoonekana alitumia ufundi mkubwa wa kuficha pia kutoweka kwake kwa muda mrefu wa miaka zaidi ya saba, alieleza uamuzi wake wa kuomba msaada wa Elizabeth Robert (Lizy Roby) ambapo alimuelezea mahala alipofikia naye chifu alimsikiliza msemaji mkuu kwa umakini.


“Nimeelewa na pia nimeguswa sana na jambo hili kiukweli… Kama mjuavyo mimi uwa sijui habari nyingi kuhusu watu wasiohusika na ofisi ya makamu wa Rais ingawa nina uzoefu mkubwa wa mambo haya ya kijasusi, je huoni ni sahihi kuwapa taarifa DEA?” Akaanza kwa maelezo mafupi na kuhoji Chifu baada ya muda wote kuwa msikilizaji tu ya kile alichojua ni ombi la Agent Kai kuifanya kazi yeye kama yeye.


“Tunaweza kuwataarifu ila naomba nisinyimwe fursa ya mimi mwenyewe kuifanya kazi hii ya kuhakikisha Jogre anarudi Marekani toka popote anaposhikiliwa mateka”.Akajibu Agent Kai akiangaliana kwa umakini na boss wake.


“Kumbuka pia nikimtaarifu tu mkurugenzi wa DEA jambo la kwanza ataomba wao wakabidhiwe kazi kwakuwa kama ulivyokwisha eleza mwanzo kuwa DEA walikuwa wakifuatilia hii kesi ya kupotea kwa watu wao watatu bila miili yao kuonekana kama wamekufa na hivyo wakawa wanatilia shaka kuwa watu wao wako mateka mahala fulani na hatuwezi kukwepa kuwataarifu kama sheria zetu za shughuli za kijasusi zinavyotutaka pale tunapotaka kuingilia kuchunguza jambo ambalo tayari lilikuwa chini ya uchunguzi wa shirika lingine la usalama” Akafafanua chifu anachoona ni sahihi.


“Huko sahihi katibu… Agent Kai amechukulia hili katika uzito kwakuwa barua pepe imetumwa kwake moja kwa moja na mtumaji si kama haijui anwani ya barua ya pepe ya DEA la hashaah! Anajua lakini ametuma kwa mtu ambaye anaamini akiupata ujumbe hawezi kaa kimya, lazima atachukua hatua sahihi na yeye kwa imani yake ataondoka toka mahala alipo na kurudishiwa uhuru wake” Kwa mara Lizy Roby akaongea akileta hoja yake ikienda moja kwa moja kwa katibu.


“Sawa Lizy! Naelewa hilo lakini kazi zetu zina mipaka… Napenda nyote mjue kazi hii ambayo Kai anaomba aifanye ni kazi ambayo hatujui ugumu wake kuna kudhulika au hata kupotea kwa mtu kiuhai, je mmeshafikiria hilo?... Ninaposema sioni sababu ya sisi ofisi ya makamu wa Rais kulichukua hili moja kwa moja uwa na maana ya dharura kama hizo na si kama waliotekwa na kupotea siwajali au hawana maana kwa wamarekani la hashaah! Wote wana maana ila ni kesi iliyokuwa tayari mikononi mwa wahusika wa watu hao na pia kumbukeni ofisi yetu uwa inafanya kazi kwa ombi maalumu au kwa dharura na wote nyinyi mnajua hilo si wageni wa sheria zetu… Ningependa kwanza tuwataarifu DEA kisha tuone kama inawezekana wao kukubali kutupa kazi hii kama dharura na si kwakuwa wameshindwa kazi kama ambavyo mkurugenzi wa taasisi kuu ya ujasusi ‘NSA’ anavyoweza kulipokea katika meza baada ya taarifa kufikishwa kwao” Ufafanuzi wa kisheria za kazi ulidhidi kufafanuliwa na katibu mwenye kitengo chake.


“Ni kweli Chifu unachozungumza nimeona hilo liko sahihi zaidi maana mara ya kwanza niliamini kwakuwa tu niko CIA basi naweza kufanya lolote lenye kuhusu ujasusi kwa manufaa ya nchi yangu hasa pia kwakuwa niko Special Activities Division”

“Kuwa ‘SAD’ si tatizo, sheria zetu zote zinapata maelekezo toka ‘NSA’ na ninaamini unazijua ila ni morali uliyonayo juu ya kumsaidia rafiki yako ndiyo icho kinachokufanya mpaka uone hakuna mipaka kuliko na mipaka… Basi ebu mnipe masaa kama matano hivi niwasiliane na mkurugenzi wa ‘DEA’ huko Springfield nitajitahidi kufanya kile ambacho kitasababisha wao kutupa kazi hii sisi kwa dharura”

“Nakuamini Chifu… Mi nachokuahidi kazi itafanyika haraka na sifa zitaongezeka zaidi kwa ofisi hii”


Walikubaliana kama ilivyo kuwa Chifu afanye mawasiliano na mkurugenzi wa shirika la kupambana na madawa ya kulevya la Marekani ‘Drug Enforcement Administration’ (DEA) kisha kama kuna jambo ambalo litaweza kuwa lina ruhusa ya Agent Kai kuifanya kazi ya kumtafuta rafiki yake basi ataruhusiwa kufanya kazi hiyo.


Mwisho wa sehemu ya thelathini na tano (35)


Bado Agent Kai yuko katika kuhangaikia kibali cha kufanya kazi ya kumtafuta rafiki yake Agent Johnson Greg Raotullaye ‘Jogre’.


Nini kitafuata?

Maneno mengi tupa kule twende sehemu inayofuata.



“Sawa Lizy! Naelewa hilo lakini kazi zetu zina mipaka… Napenda nyote mjue kazi hii ambayo Kai anaomba aifanye ni kazi ambayo hatujui ugumu wake kuna kudhulika au hata kupotea kwa mtu kiuhai, je mmeshafikiria hilo?... Ninaposema sioni sababu ya sisi ofisi ya makamu wa Rais kulichukua hili moja kwa moja uwa na maana ya dharura kama hizo na si kama waliotekwa na kupotea siwajali au hawana maana kwa wamarekani la hashaah! Wote wana maana ila ni kesi iliyokuwa tayari mikononi mwa wahusika wa watu hao na pia kumbukeni ofisi yetu uwa inafanya kazi kwa ombi maalumu au kwa dharura na wote nyinyi mnajua hilo si wageni wa sheria zetu… Ningependa kwanza tuwataarifu DEA kisha tuone kama inawezekana wao kukubali kutupa kazi hii kama dharura na si kwakuwa wameshindwa kazi kama ambavyo mkurugenzi wa taasisi kuu ya ujasusi ‘NSA’ anavyoweza kulipokea katika meza baada ya taarifa kufikishwa kwao” Ufafanuzi wa kisheria za kazi ulidhidi kufafanuliwa na katibu mwenye kitengo chake.


“Ni kweli Chifu unachozungumza nimeona hilo liko sahihi zaidi maana mara ya kwanza niliamini kwakuwa tu niko CIA basi naweza kufanya lolote lenye kuhusu ujasusi kwa manufaa ya nchi yangu hasa pia kwakuwa niko Special Activities Division”

“Kuwa ‘SAD’ si tatizo, sheria zetu zote zinapata maelekezo toka ‘NSA’ na ninaamini unazijua ila ni morali uliyonayo juu ya kumsaidia rafiki yako ndiyo icho kinachokufanya mpaka uone hakuna mipaka kuliko na mipaka… Basi ebu mnipe masaa kama matano hivi niwasiliane na mkurugenzi wa ‘DEA’ huko Springfield nitajitahidi kufanya kile ambacho kitasababisha wao kutupa kazi hii sisi kwa dharura”

“Nakuamini Chifu… Mi nachokuahidi kazi itafanyika haraka na sifa zitaongezeka zaidi kwa ofisi hii”


Walikubaliana kama ilivyo kuwa Chifu afanye mawasiliano na mkurugenzi wa shirika la kupambana na madawa ya kulevya la Marekani ‘Drug Enforcement Administration’ (DEA) kisha kama kuna jambo ambalo litaweza kuwa lina ruhusa ya Agent Kai kuifanya kazi ya kumtafuta rafiki yake basi ataruhusiwa kufanya kazi hiyo.


ENDELEA NA DODO ASALI..!!


JUMATATU

EISENHOWER, WASHINGTON DC-MAREKANI

Mawasiliano kati ya katibu wa ofisi ya makamu wa Rais (Chief executive of the vice President) na mkurugenzi wa shirika la kupambana na madawa ya kulevya ‘Drug Enforcement Administration’ (DEA) yalifanyika kwa haraka sana kitu ambacho katibu aliona kuna umuhimu mkubwa ya kuliangalia hili suala kwa umakini baada ya Lizy na Agent Kai kutoka ndani ya ofisi yakehaikuchukua dakika kumi katika tafakari yake ya yale yaliyoletwa kwake na vijana wake, aliona kuna umuhimu wa kufanyika kama walivyoona vijana hawa na pia kuvalia njuga kuwa wanataka lifanyiwe kazi hata kama liko katika mipaka mingine lakini bado ofisi ambayo yupo yeye ipo juu ya yote hayo na inaweza kuomba kufanyiwa kazi jambo kama serikali kuu.


Aliweza kumpata kwenye simu mkurugenzi wa shirika la DEA na habari ile kwake ilikuwa na ugeni masikioni mwake lakini si ngeni katika kuisoma katika mafaili ya waliokuwa wafanyakazi wa DEA nakupotea katika mazingira yenye kutatanisha, hii ilitokana na kuwa mkurugenzi huyu alikuwa ni mkurugenzi mpya akiwa na miaka miwili tu toka Rais mpya wa Marekani mpya aliyeingia madarakani akipokea kiti cha ikulu kutoka kwa aliyekuwa chama cha Democratic ambaye alikuwa ni Rais wa kwanza mwenye asili ya kutoka Afrika (mweusi), Rais mpya alipoingia mkurugenzi wa DEA aliyemkuta alikuwa anatakiwa kustaafu kutokana na umri wake kufikia hivyo mzee baba akateua mtu mwingine.


Wakati Agent Telizo Munde, Agent Rummenige Brandts na mtuma barua pepe Agent Johnson Greg Raotullaye walipokuwa wanapotea kipindi alikuwa mkurugenzi mwingine kama ilivyo shirika la ujasusi la CIA miaka miwili iliyopita walikuwa wamebadilishiwa mkurugenzi na Rais mpya aliyeko madarakani tokea chama cha Republican na hata taasisi kuu inayoongoza mashirika haya ya kijasusi ‘National Security Agency’ (NSA) pia mkurugenzi alikuwa mpya.


Ilikuwa habari nzuri ambayo kuisikia tu alihisi kuna fanikio linakuja, habari iliyopelekwa kwa katibu wa makamu wa Rais na mtu ambaye yeye mkurugenzi wa DEA alikuwa akizijua habari zake nyingi na hata pia kuvutiwa na ufanisi wake kazini kiasi cha kumtamani angekuwa yuko DEA ambako kwa Marekani katika mashirika ya ujasusi ukiacha CIA nao walikuwa kazi nyingi sana zisizo wa pumzisha kwakuwa biashara ya ulanguzi wa madawa ya kulevya ilikuwa na mipambano isiyoisha hasa majimbo yaliyo mipakani.


Mkurugenzi alikubali kazi ya kuchunguza nyuma ya pazia kukoje kufanywe na Agent Kai lakini wawepo watu wawili wa DEA wa kumsaidia sababu watu waliotekwa ni majasusi waajiriwa wa DEA na kwa ilivyo watu hawa watakuwa wanashikiriwa na moja ya kundi ya ulanguzi wa madawa wa kulevya, aliamini haiwezekani magaidi waamue kuteka jasusi au askari wa DEA sababu kimantiki haileti maana ingawa pia inawezekana.


Katibu (chifu) hakuwa na pingamizi juu ya hilo sababu Marekani kiusalama kila mmoja ni mlinzi wa usalama wa mwingine kama ilivyo nchi zingine zote ‘mtu kuwa mlinzi wa mtu’, alipokea hilo akatoa ruhusa mkurugenzi aandae watu wake anaojua ni safi katika kazi za kazi tena wenye uwezo na akili ya kazi ikiwemo kuzingatia uzoefu wa kazi za kishushushu na ukachero na hata katika mapambano ya aina zote silaha na ana kwa ana.


Wakakubaliana waliyoyaona ni sahihi katika kila jambo na katibu akichukua jukumu la kumtaarifu mkurugenzi wa shirika la kijasusi la CIA kuhusu kuwa kuna kazi ambayo iliitwa ya ‘dharura’ kwa pande zote, makubaliano ya mwisho yalikuwa kesho yake ambayo ni siku ya jumanne ifikapo saa nne asubuhi mkurugenzi aende nao Eisenhower vijana ambao watakabidhiwa kushirikiana kazi na Agent Kai bila kujali kazi ni ndogo, fupi ama kubwa, ndefu.


Saa tano katibu alienda kwenye kikao ambacho kiliitishwa na makamu wa Rais kikiwa pia kimehudhuriwa na Agent Kai na pia Elizabeth Robert naye alihudhuria, baada ya kikao kumalizika na makamu wa Rais kuongea mambo kadhaa na baadhi ya watuwaliohudhuria kikao pia alipata fursa wa kuzungumza na Agent Kai binafsi kuhusu ndoa yake na safari yake Afrika katika fungate huku akimpa na salamu za pongezi za Rais kuhusu kazi aliyoifanya Malaysia kwakuwa kipindi chote icho hakuwa amepata wasaa wa kukutana na Rais wa nchi.


Baada ya hapo katibu naye aliweza kuongea naye makamu wa Rais juu ya habari alizohadithiwa na Agent Kai juu ya mpango kazi ulio katika ombi, Makamu wa Rais alifurahi sana moyo wa upendo na kujitolea wa Agent Kai katika mambo yanayowahusu wa marekani wenzake na moja kwa moja akaruhusu kazi iende kufanyika kwa Baraka zake kwakuwa kulikuwa hakuna kazi ingine ambayo ingetakiwa kufanywa na Agent Kai kwa wakati huu aliomaliza likizo yake ya fungate.


Yakafanyika maongezi ya kushirikishwa wote kwa pamoja, wakapanga mambo kadhaa wa kadha na kupitishwa kimaamuzi na baraka zake makamu wa Rais kila mmoja akaondoka ndani ya ukumbi wa mikutano wakiwa na ridhiko ya kila hitaji lililohitajika.


Waliondoka pale kwa pamoja na Chifu lakini baada kutoka kwenye lift ya kuendelea flour zilipo ofisi za makamu wa Rais, Agent Kai na Lizy Roby wao hawakurudi flour (losheni) zilipo ofisi zao na katibu wa makamu wa Rais, wao walielekea kwenye mgahawa wa chakula cha mchana kwa ajili ya wao kupata mlo wa mchana kwakuwa muda wa chakula ulikuwa umetimia.


***** ***** *****


JUMANNE

EISENHOWER, WASHINGTON DC-MAREKANI

Ndani ya ukumbi mdogo wa mikutano ya kikazi uliopo ndani ya flour (losheni) ya katibu wa makamu wa Rais, kulikuwa na kikao kidogo cha utambulisho na kuelekezana kilichohudhuriwa na Katibu mwenyewe wa Makamu wa Rais, mkurugenzi wa shirika la kupambana na madawa ya kulevya ‘Drug Enforcement Administration’ (DEA) aliyeongozana na vijana wawili mmoja akiwa na asili ya Afrika na mwingine ni mzungu, wakifunga safari iliyowaleta hapa Washington DC toka Springfield, Virginia kwa kutumia helkopta.


Kwa pamoja nao alikuwepo Elizabeth Robert (Lizy Rob) mkuu wa kitengo cha Tehama katika ofisi ya katibu wa makamu wa Rais yeye Lizy akihusika na upande wa intelejensia, alikuwepo Agent Kai ambaye naye alikuwa kaongozana na mwanadada wa kizungu aitwaye Rebecca Smit, mwanadada ambaye ni jasusi wa CIA aliyehamishiwa kutoka Malaysia alikokuwa kapangiwa kazi kwa miaka zaidi ya sita mpaka Agent Kai alipofanya naye kazi miezi kama sita iliyopita kisha kuvutiwa na ufanyaji wake wa kazi akapendekeza aletwe ofisi ya makamu wa Rais awe naye karibu kikazi chini ya boss wao Chief Executive Of The Vice-President.


Mwenyekiti wa kikao hiki alikuwa katibu wa makamu wa Rais mwenyewe na kifupi aliwaalika wote hawa yeye mwenyewe.


“Awali ya yote napenda nitoe shukrani zangu za dhati kwa mkurugenzi wa DEA kwa kufanya uchaguzi wa watu wake haraka sana kwa pamoja na nilipofika asubuhi hii nilikuta tayari katika email ya ofisi nina mafaili ya wasifu ya watu hawa uliongozana nao, nimefurahi ni watu wenye sifa lukuki katika medani ya kazi za giza, naamini kuwa nao kwa pamoja na jasusi wa ofisi hii Agent Kai watafanya kazi ikawe nyepesi na laini zaidi, ahsanteni sana sana wote kwa ujumla…! Baada ya shukrani naomba mimi kama mwenyekiti wa kikao nifanye utambulisho wa wote tuliopo hapa ambao ni wenyeji wa ofisi hii… Sina sababu ya kujisemea mimi ni nani sababu naamini hakuna aliye serikalini hasa katika mambo ya usalama ambaye hamjui katibu wa makamu wa Rais hapa Marekani…”. Alinyamaza hapa na kuwatizama kwa zamu watu wote walio mbele yake na pambeni pia.


“Aliye kushoto kwangu ni Special Agent Rebecca Smith ni Ajenti wa CIA katika ofisi yangu ni chaguo letu bora kabisa katika medani ya kazi za giza, kwa waliowai kufanya naye kazi wanajua uwezo wake, aliye pembeni yangu kulia nafikiri nyote mnamjua yeye ni nani? Huyu ndiye Agent Kai kama labda hamumjui” Akaendelea kutambulisha “Na wa mwisho wetu hapa ni mwanadada mtaalamu wa kompyuta katika ofisi yangu upande wa intelejensia anaitwa Elizabeth Robert… Upande huo nafikiri ni uwanja wako mkurugenzi kuwatambulisha huku ikiwa haina haja wa wewe kujitambulisha kwakuwa sote tunakujua toka huko ‘NSA’ makao makuu mpaka sasa huko ‘DEA’”.


“Ahsante sana Chifu… Kwa kweli ni heshima kubwa sote kuwepo tukiwa na nia moja ya kusaidia wenzetu ambao hawajabarikiwa kupata fursa hadhimu kama tuliyopata ya kuwaakilisha katika ulinzi na usalama wa taifa letu kubwa…. Aliye upande wa kulia kwangu anaitwa ni Investigator Joseph January Miller na aliye kushoto kwangu ni Special Agent Fransis Simone Silla wote hawa ni watu ambao DEA wameifanyia mambo mengi ya kufurahisha katika operesheni zetu mbalimbali” Akatoa utambulisho wa vijana wake wa kazi aliofika nao pale kwa madhumuni ya kuwakabidhi kwa Agent Kai kumsaidia katika operesheni ndogo ya dharura ambayo iliibuliwa ghafla kwao.


“Nimefurahi sana kuwajua vijana wenzangu tulionao katika mchezo mmoja, naamini wote watakuwa wananijua kwa namna mbalimbali juu ya machache na mengi niliyoyafanya katika kazi zetu za giza… Naamini watakuwa washagusiwa kidogo kipi ambacho tunatakiwa kukifanyia kazi, niko sahihi mkurugenzi?” Akaongea Agent Kai akimalizia kwa swali na papo hapo akiwa kaiunuka toka kwenye kiti alichokaa kwa zoezi la kurudia mara ya pili kupeana mikono na majasusi wa DEA waliotambulishwa na boss wao.


“Nimefanya hilo ila kwa maelezo zaidi utalifanya wewe kiongozi wa misheni hii ya kuwarudisha ndugu zetu tuliowapotea miaka mingi sasa… Na uzuri ni kuwa mmoja niliyekuja naye hapa alishiriki katika majaribio kadhaa ya kuchimbua na kutafuta ukweli juu ya upoteaji wa wenzao miaka miwili ya kwanza kabla ya kukata tamaa kuliacha fahili…!” Akajibu Mkurugenzi huku akiwaangalia vijana wake tabasamu likiwa limeundwausoni mwao kati yao wote.


“Safi sana! Naamini pia mmekumbuka kubeba na fahili husika la kesi hii mpaka pale mlipofikia katika uchunguzi pia naamini fahili halikufungwa kwa sababu kazi haikufikia mwisho” Ilikuwa ni Agent Kai na mkurugenzi wa DEA katika maongezi ya jumla ambayo muulizaji alikuwa akitaka kujua mambo kadhaa.


“Ndiyo fahili zote tatu za wahusika tumekuja nazo, pia nilivyoingia mimi ofisini sikukuta mafahili haya yakiwa wazi hii inamaanisha uchunguzi juu yao mkurugenzi niliyemrithi aliufunga lakini sheria zinaturuhusu kufungua tena na kesi ya uchunguzi kuendelea sababu jamaa zetu hazikupatikana taarifa kuwa wao ni marehemu wameuwawa… Naamini kwa utaalamu wako tunaenda kuwaona ndugu zetu… Silla na mwenzake wako tayari kufuata maelekezo yako kwa sasa wewe ndiyo boss wao na kioo chao ingawa wote kwa pamoja mkasaidiane hii kazi” Mkurugenzi aliendelea kufafanua katika jibu ya kila swali analoulizwa.


“Basi wakuu naomba muache mikononi mwetu hii kazi baraka zenuzinahitajika katika jambo hili na kifupi niseme nawashukuru sana watu wa DEA, kuanzia mkurugenzi mpaka wafanyakazi wote kwa ujumla… Nina maswali mengi sana ya kuuliza kwa dhumuni la mimi na washirika wangu Rebecca na Lizy tutataka kujua hivyo ni vizuri tukaondoka hapa tukaenda Planning Room kupanga tunaanzia wapi?” Akaongea Agent Kai huku kama kawaida yake akisugua viganja vyake taratibu.


“Sawa tu! Tutahusika kama itahitajika uhusika wetu… Mnaweza ongozana kwenda kujipanga wenyewe kazi inafanywaje sisi bado tunataka wasaa wa kubadilishana mawazo kidogo” Kwa niaba ya Mkurugenzi akaongea Chifu.


Vijana wote wakainuka baada ya kuona Agent Kai amesimama kwa ajili ya kuondoka kwenda kunakoitwa ‘Planning Room’.


Waliwaacha wakuu wao wa kazi kisha kwa pamoja wakaongozana hadi ofisi ambazo Agent Kai na majasusi wengine walio Special Agent wa CIA ni ofisi zao kiongozi wa kitengo hiki cha ujasusi kilicho chini ya Katibu wa makamu wa Rais ni Mr. Kai Hamis Mkarambati.


Chumba ambacho ni kikubwa katika mapana na marefu yake ambacho kilikuwa na viti kadhaa na meza zake katika kila kiti na mbele kukiwa na skrini kubwa pande zote ambazo zimeunganishwa na kompyuta kadhaa zilizo meza kuu ambayo ina viti viwili tu viliwekwa vikiangalia mbele baada ya kuwa zimeigeukia meza, pia kulikuwa na ubao wa plastiki wa rangi nyeupe.


Agent Kai na Lizy Roby walikaa kwenye meza kuu huku viti vingine vitatu vilivyo kwa nyuma hatua kama tano hivi walikaa Special Agent Rebecca Smith huyu mwanadada anayependwa kikazi na Kai mwenyewe, Special Agent Fransis Simone Silla na Investigator Joseph January Miller.


“Jamani karibuni maabara yetu ambayo utuletea majibu na pia utuunganisha kwa pamoja kwa kutokea hapa tunapokuwa na kazi iwe nje ya Marekani au hapa Marekani… Hapa tutaweza kufahamiana vizuri katika maongezi yetu ni ruhusa kuuliza swali lolote ambalo linahusu kazi yetu… Kwa kuanza ningepanda kwanza mtupatie mafahili tuweze kuyapitia tuone wenzetu walioshika uchunguzi huu walikwama wapi?” Kila mmoja alipoweza kukaa tu katika kiti chake Agent Kai akatoa ukaribisho wa chumba hiki na papo hapo akaomba mjadala wa kazi ukaanza kwa wao kupatiwa mafahili ya kesi iliyochunguzwa kwa miaka mitatu iliyopita mfululizo bila kuleta jibu halisi la kutosheleza.


Dakika thelathini na tano ziliweza kuwafanya Lizy Roby, Special Agent Rebecca Smith na Agent Kai kuwa wakimya kabisa wakisoma kwa umakini mstari kwa mstari, nukta kwa nukta na kurasa chache zilizo katika kila fahili huku mmoja akimaliza hili basi alimpa mwingine ikawa mwendo wa kusoma na kubadilishana mafahili kati yao huku wageni wao na washirika wao wapya toka DEA wakiwatizama kwa umakini huku na wao wakijiweka katika utulivu kwa kupitia pitia baadhi ya vitabu ambavyo wamevikuta katika mojawapo ya meza iliyopo katika chumba hiki, vikiwa na vitabu vya habari mbalimbali za shirika la kijasusi la Marekani ‘CIA’.


“Nani alikuwepo wakati ule inafuatiliwa upoteaji wa hawa ndugu zetu?” Agent Kai akawauliza swali wageni wao na washirika wao wapya sasa.


Mwisho wa sehemu ya thelathini na sita (36)


Agent Kai amefanikiwa kuweka ushawishi kwa boss wake na kiongozi wake wa kikazi ambaye ni katibu mkuu wa katika ofisi ya makamu wa Rais wa Marekani.


Ushawishi ulioweza kumfanya akubaliwe kuchunguza juu ya upoteaji wa maafisa usalama wa shirika la kupambana na madawa ya kulevya Marekani ‘Drug Enforcement Administration’ akipewa na sharti la kuwashirikisha watu wa DEA pia.


Nini kitafuatia? katika hatua zetu zijazo za ukwaju wetu.


Fuatana nami sehemu zijazo kwa kuanza na sehemu ijayo kwanza.




ILIPOISHIA SEHEMU YA 36…!!

Chumba ambacho ni kikubwa katika mapana na marefu yake ambacho kilikuwa na viti kadhaa na meza zake katika kila kiti na mbele kukiwa na skrini kubwa pande zote ambazo zimeunganishwa na kompyuta kadhaa zilizo meza kuu ambayo ina viti viwili tu viliwekwa vikiangalia mbele baada ya kuwa zimeigeukia meza, pia kulikuwa na ubao wa plastiki wa rangi nyeupe.


Agent Kai na Lizy Roby walikaa kwenye meza kuu huku viti vingine vitatu vilivyo kwa nyuma hatua kama tano hivi walikaa Special Agent Rebecca Smith huyu mwanadada anayependwa kikazi na Kai mwenyewe, Special Agent Fransis Simone Silla na Investigator Joseph January Miller.


“Jamani karibuni maabara yetu ambayo utuletea majibu na pia utuunganisha kwa pamoja kwa kutokea hapa tunapokuwa na kazi iwe nje ya Marekani au hapa Marekani… Hapa tutaweza kufahamiana vizuri katika maongezi yetu ni ruhusa kuuliza swali lolote ambalo linahusu kazi yetu… Kwa kuanza ningepanda kwanza mtupatie mafahili tuweze kuyapitia tuone wenzetu walioshika uchunguzi huu walikwama wapi?” Kila mmoja alipoweza kukaa tu katika kiti chake Agent Kai akatoa ukaribisho wa chumba hiki na papo hapo akaomba mjadala wa kazi ukaanza kwa wao kupatiwa mafahili ya kesi iliyochunguzwa kwa miaka mitatu iliyopita mfululizo bila kuleta jibu halisi la kutosheleza.


Dakika thelathini na tano ziliweza kuwafanya Lizy Roby, Special Agent Rebecca Smith na Agent Kai kuwa wakimya kabisa wakisoma kwa umakini mstari kwa mstari, nukta kwa nukta na kurasa chache zilizo katika kila fahili huku mmoja akimaliza hili basi alimpa mwingine ikawa mwendo wa kusoma na kubadilishana mafahili kati yao huku wageni wao na washirika wao wapya toka DEA wakiwatizama kwa umakini huku na wao wakijiweka katika utulivu kwa kupitia pitia baadhi ya vitabu ambavyo wamevikuta katika mojawapo ya meza iliyopo katika chumba hiki, vikiwa na vitabu vya habari mbalimbali za shirika la kijasusi la Marekani ‘CIA’.


“Nani alikuwepo wakati ule inafuatiliwa upoteaji wa hawa ndugu zetu?” Agent Kai akawauliza swali wageni wao na washirika wao wapya sasa.


ENDELEA NA DODO ASALI


JUMANNE

EISENHOWER, WASHINGTON DC-MAREKANI

“Mimi ndiyo nilikuwepo kipindi na nilishiriki mwanzo mwisho katika timu iliyoundwa kuchunguza utowekaji wa wenzetu” Alijibu Special Agent Fransis Simone Silla ambaye ni mzungu huku mwezie Investigator Joseph January Miller alikuwa ni mmarekani mweusi ambaye asili yake ya wazazi wake wa pande wa mbili ilikuwa si ya kueleweka kama wamarekani wengi weusi ambao uwa hawajui hasa wao asili yao ni nchi gani katika bara wanaloamini ndiyo bara lao la asili Afrika.


“Ripoti za mafahili yote zinaonyesha hamkutoka nje ya Marekani kuchunguza, je mliamini watekwaji hawakutekwa na watu wa kutoka nje ya Marekani?” Akauliza Agent Kai, watu wengine waliopo hapa walikuwa kimya kabisa kusikiliza maswali na majibu.


“Mara moja tulipopata taarifa toka kwa mmoja wa mke wa watekwaji tulikimbilia inaposemekana walikuwepo kwa mara ya mwisho kama maelezo yanavyoeleza katika fahili zote na kisha tukaomba cctv kamera za pale ambazo cd zake zimeambatanishwa katika kila fahili tunaweza angalia na nyie pamoja mkajionea hapo ndipo hasa tulivyoweza kuhisi watekaji wanaweza kuwa wa hapa hapa Marekani miongoni mwa magenge ya mihadarati ambayo mara nyingi ndiyo tunayopambana nayo” Akajibu Special Agent Fransis Simone Silla.


“Tutaangalia video hizo za cctv kamera.. Barua pepe inaonyesha ilitumwa kwangu na simu iliyotumika kutuma inaonekana kimnara kuwa wakati inatumiwa kutuma mtumiaji wa simu alikuwa eneo la milima ya Tajumulco, mkoa wa San Marcos nchini Guatemala hivyo kama mlikuwa sahihi sijui ila mlikuwa mkicheza mahala ambapo si sahihi Agent…. Si laumu kuhusu hilo maana kulikuwa hakuna kiashiria kingine kama watekwaji kuwa wameondolewa nje ya mipaka ya Marekani kwa namna yoyote labda kama ingetokea ishara kama hii iliyonifikia mimi kupitia barua pepe” Akaendelea Agent Kai na akapisha kusikia Silla anasemaje.


“Ni kweli tulipambana sana na magenge ya hapa na kama watu wale waliondolewa hapa Marekani basi waliondolewa bila kushirikishwa kwa genge lolote la mihadarati yaliyokuwepo kipindi icho hapa Marekani na hata yaliyopo sasa ambayo si kama yale ya kipindi kile sababu mengi yao tumeyamaliza nguvu kwa kiasi kikubwa” Akafafanua Silla.


“Ni jambo la kujivunia sana… DEA mmefanya kazi kubwa katika upambanaji na mambo haya ya kishenzi kwa kikubwa sana, mnastahili tuzo ya ushindi… Sisi katika hatua ya kwanza ambayo tumeona inafaa kuiendea ni kupita katika njia ya kufuatilia mawasiliano ya mwanamke anayejiita Valentina Aurelia Moschi sababu ya kudili na huyu mwanadada namba yake ndiyo inayotumia anwani ya barua pepe ya Valentina1899@gmail.com mpaka sasa ila mpaka sasa tunavyoongea hapa hatujamsikia akipigiwa simu yake wala kupiga ila ipo hewani hivyo tunasubiri kwa hamu afanye mawasiliano ya aina yoyote ile ambayo tunaweza kumjua yeye ni nani na anahusika na nini? Kupitia mawasiliano atakayoyafanya mu..!” Hakuweza kuendelea kwani Investigator Joseph January Miller alinyosha kidole kuomba ruhusa ya kuuliza swali.


“Hatuwezi kumfuata alipo?” Akauliza.

“Tunaweza mfuata ila shida nilitaka nione kama movement zake hawezi kurudi Tajumulco kwa maana mpaka sasa ninavyozungumza hapa ameshazunguka nchi tatu kwa siku ambazo zimetuchanganya sana kwa biashara gani au kazi gani anayofanya mpaka asiwe mtu wa kutulia sehemu moja ila mpango uliopo ni kumfanya yeye kuwa njia yetu kuu” Akajibu kiufafanuzi.


“Hatuwezi subiri mkuu… Fursa yetu ni kumpata yeye” Akaingizia Special Agent Rebecca Smith mwanadada msaidizi wa Agent Kai.


“Ndiyo hatuwezi kusubiri Rebecca ila hawa wenzetu wanahitaji maelekezo yetu na pia tukawasikiliza mawazo yao… Naamni mawazo yao yana umuhimu sana kwetu na pia ilikuwa ni kuweza kujua kwa kifupi kesi hii iliishia wapi, nafikiri umenielewa?.... ebu naomba tuangalie cd ambayo zimeambatanishwa na mafahili haya pengine zinaweza kuwa msaada kwetu” Agent Kai alikubaliana na Rebecca kisha akaomba waangalie cd zilizorekodiwa toka katika cctv kamera zilizochukuliwa miaka saba iliyopita eneo la nje la maegesho ya magari ya Springfield Hard Times Café & Cue.


Lizy Roby alichukua cd zile kisha akaweka katika mlango wa cd ya laptop yake ya kazi ambayo mara zote uwa katika chumba hiki lakini mtu ambaye uwa anaitumia mara nyingi ni yeye.


Kila mmoja hata wale waliokuwa wamekuja na cd hii waliweza kuona kila jambo lililofanyika kipindi cha miaka saba iliyopita katika maegesho ya magari ya Springfield Hard Times & Café, video ilionyeha vizuri tukio la kila gari kati ya magari yote matatu ya waliotekwa. Ilionekana kila gari wakisogea wanaume wawili kisha wakijifanya hawana wasiwasi wowote ule wakaingia ndani ya magari husika na kutulia mpaka muda ambao mpira uliokuwa unafuatiliwa na wapenzi wa soka katika ukumbi unaoonyesha mpira wa aina mbalimbali ulipoisha na watekwaji nao walienda kwa kila mmoja kuingia katika gari lake kile kilichoendelea ndani ya gari hakikuonekana lakini magari yakaondoka kwa kuongozana kuondoka eneo la maegesho ndipo video ile ikaishia pale.


“Kuna haja ya kuirudia?” Akauliza Lizy akimuangalia kila mmoja kisha macho yake yakasimama kumtizama Agent Kai.


“Rudisha kwa wale wa kwanza kuingia katika gari ya kwanza… Tuanze hapo!” Akaelekeza Agent Kai baada anaangaliwa na kila mtu.


Lizy akafuata maelekezo akafanya alivyotakiwa alipofika mahala husika akagandisha akiwa amezigandisha wote wawili wakionekana vizuri katika skrini kubwa iliyo ukutani.


Hapa kwa upande wa Lizy kwa uzoefu wake hakuitaji maelekezo toka kwa Agent Kai au kwa mtu mwingine yoyote, alikuza muonekano na kusogeza sura za wahusika mbele zaidi na papo hapo akaweza kuzibadili na kuziweka katika picha mnato, kisha akaziweka katika mfumo wa kusachi image katika mitandao kazi ambayo ilizunguka (loading) kwa muda wa dakika tano picha moja sura moja ikaleta jibu, mmoja wa wahusika wa picha ile aliweza kukutwa kimfanano na picha ya profile ya akaunti ya imo free video and chat, macho ya watu wote yakawa makini kufuatilia mtaalamu Liozy anachofanya ambapo dakika mbili aliweza kuifungua akaunti husika na kuweza kuikuta ilitumika miaka kumi na moja iliyopita kutoka siku hii waliyopo katika chumba hili na kutokea hapo katika kipindi icho ilionekana mtumiaji aliacha kasumba ya kutumia mtandao wa imo kwa mara kwa mara kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe lakini uzuri hakuweza kufuta matukio kadhaa ya chat zake na marafiki zake.


“Anaitwa Maquez Molito… Ameandika anaishi wapi hapo katika wasifu wake maana nahisi kama hakuweka hilo?” Akahoji Agent Kai na papo hapo Lizy akafungua mahala pa wasifu na ikaonekana akiwa ameweka anatokea jimbo la Veracruz, Mexico.


Agent Kai akaandika katika kitabu chake cha note book baadhi ya maelezo akiyatoa katika chating zake jamaa yule ikiwa anatumi lugha ya kihispaniola (kilatin)


“Kiongozi hamkufika kuchunguza picha hizi?” Lizy Roby akamuuliza Special Agent Fransis Simone Silla.


“Tulichunguza lakini nafikiri teknolojia yetu kwa miaka ile kulikuwa na ukakasi katika intelejensia ya kimtandao katika vifaa vyetu ndiyo maana pamoja na kusachi hatukufika imo” Akajibu.


“Sawa sawa Silla… Ilivyo Lizy! Imo kwa miaka kadhaa huko nyuma walikuwa wanalinda haki ya mmiliki wa akaunti mpaka pale zilipowekwa sheria ya kuruhusu kuchunguza habari za watu wote wanaotumia mitandao kwa majasusi wa CIA na mashirika mengine ya kupambana na ugaidi kama CTU nakadhalika..” Akafafanua Agent Kai.


“Hizi picha zingine zote zimegoma kuleta majibu hii inamaanisha watu hawa hawapo katika mitandao ya kigaidi na wala si watu wakufahamika sana katika magenge ya madawa ya kulevya yaliyoko ukanda wetu wa bara la Amerika na hata kwingineko ila kila mmoja atatakiwa kuwa na picha hizi katika hifadhi yake maana tunakwenda watafuta hawa watu huku mlengwa wetu mkuu akiwa mwanadada anayejiita Valentina Aurelia Moschi” Akaeleza Lizy Roby.


“Jogre na wenzake wote ni maafisa wa DEA… Naamini watu hawa waliuofanya utekaji huu ni walanguzi wa madawa ya kulevya na pengine walifanya hivyo kwa nia ya kisasi au kwa jambo lingine wanalolijua wao…. Katika maelezo yalioandikwa humu kuna mahala panaelezwa wakati wa utafutaji wenu mlikwenda mpaka Nevada kupambana na kikundi mlichohisi kinahusika na utekaji ule kikundi kilichokuwa kikiongozwa na mwanamke aitwaye Camilla Boxer lakini mligundua mmekosea wao si watekaji ingawa walikuwa wakijihusisha na biashara ya ulanguzi wa madawa ya kulevya, kikundi kile mlikisambaratisha na asilimia hamsini kati yao wako gerezani baada ya kukutwa na hatia na mahakama ya kesi zao za mihadarati,.. Nilichogundua mimi watekaji walipowateka watu wetu walikimbia nao nje ya Marekani siku ile ile au siku mbili za mbele yake hizi sura zinafanana na watu mliowavamia ukizitizama wao na ukitizama picha za watu wa kikundi hiki lakini kuna jambo moja ambalo limejificha na linahitaji uzoefu wa hali ya juu… Naomba Lizy utoe hapo ulipogandisha na upeleke video mbele mpaka kwa walioingia katika gari ya mwisho ambayo kimaelezo inaonyesha ni gari aliyokuwa akiitumia Mr. Jogre” Agent Kai akaongea na mara moja Lizy akafanya alichoelekezwa.


“Niigandishe video au niache inatembea?” Lizy akamuuliza.


“Itembeze taratibu kabisa kisha kuza eneo la usoni… Hao walipokuwa wakifika kwenye gari kabla hawajagusa vitasa vya mlango waliongea nataka kuona papi zao zikicheza kwahiyo unatakiwa ucheze na eneo hilo tu” Akafafanua Agent Kai huku mwanadada akifanya atakavyo mtaalamu.


“Vuta eneo la mdomo la huyo wa kushoto kuna kitu alianza kuongea yeye…!” Akaelekeza tena huku akisogeza kichwa mbele zaidi hili aweze kuona kwenye skrini vizuri zaidi.


“Yah!... Nimepata jibu na ni hakika… Jamaa midomo imecheza lips kutamka matamshi yaliyo katika kilatino si kiingereza lugha inayotumika na wamarekani wote, hawa ni wageni 100%, hivyo tunatakiwa tujue sote hapa safari ya kazi yetu iko nje ya Marekani kwa vigezo vya barua ilipotoka, picha imo akaunti ikiwa inaelekeza mwenye profile picha ni mtu aliyejitanabaisha ni mtu wa Veracruz, Mexico… “ Akafafanua Agent Kai na kila mmoja aliyepo pale akatikisa kichwa kukubali maelezo yake.


“Mi napendekeza kazi ingeanza mara moja kwa watu wawili kati yetu waelekee kumtafuta mwanadada huyu huku wengine wawili waelekee kuchunguza huko kwenye milima ya Tajumulco, San Marcos kuona dalili za mfanano wa mchoro uliotumiwa maana katika maelekezo ya kuhusu mchoro uliotumiwa kuna maelekezo ambayo umeyafafanua kuwa unahisi yupo mahala ambapo pamezungukwa na maji ila haijulikani kama ni maji ya bwawa, bahari, ziwa au mto? Ni hayo mkuu”. Akatoa maelezo yake kwa mara ya kwanza Investigator James Miller.


“Sahihi tunaweza anza hivyo hili tupate majibu yote mawili yanayotusumbua, tunaweza kufuata chanzo na pia tunaweza fuata maelekezo ya muandikaji wa barua pepe… Nafikiri Rebecca Smith na mimi tungeelekea kumtafuta mwanadada Valentina wakati huo huo na nyinyi wawili kwakuwa mmezoeana kikazi mngeenda kufanya upelelezi Guatemala mji wa San Marcos na hapa kituo kikuu tutabaki na muongozaji wetu wa kila kitu Lizy…!”Akakubaliana Agent Kai na kuongezea aonavyo ni vizuri ikawa hivyo.


“Hatuna pingamizi tunafuata maelekezo yako tu.. Nadhani I vizuri sisi tukaanza safari leo kwakuwa tunajua tunaenda mji gani kufanya upelelezi wetu wakati nyinyi mnatakiwa kumfuatilia mtu ambaye ni kama mtu hewa mnaweza panga kufuata baada ya yeye kuonyesha ishara yuko wapi kwa wakati huo” Akaongea Special Agent Silla.


“Sawa! Lizy atashughulikia juu ya usafiri wenu sababu nafikiri itapendeza mkianzia safari ya kutoka hapa mpaka Canada kwa basi au treni kisha mkiwa Canada mtaondoka kwa usafiri mtakaoona kwenu ni sahihi kuondoka nao na kuingia nchini Guatemala na muda wote tutakuwa sote tunawasiliana na hasa muongozaji wetu. Atawawekea maelezo ya kwanza ya kuweza kuwasaidia mtakapofika San Marcos ingawa nami nitakuwa nawasiliana nanyi kila hatua..” Akafafanua mambo mengi zaidi Agent Kai.


Walielekezana na mabo mengine kadhaa wa kadha ambayo waliona ni muhimu kwa kazi yao kisha ya hapo Lizy akashughulikia juu ya kusafiri kwa treni ya mwendokasi toka Washington DC mpaka Toronto, Canada pia aliwapatia na kiasi cha pesa kitakachoweza kuwasaidia katika gharama mbalimbali za matumizi mbalimbali.


Kikao hiki cha kupanga na kuweka sawa yote katika hatua ya kwanza kiliisha ikiwa ni mchana na wote wakafuata hatua zingine ikiwa Agent Kai, Lizy Roby na Special Agent Rebecca wao waliondoka kwa pamoja kwenda zilipo ofisi zao za kawaida ambako walipanga wakutane asubuhi huku wakivizia endapo mwanadada anayejiita Valentina kama atafanya mawasiliano waweze kum track yuko wapi? Maana mpaka muda huu alikuwa kimya simu yake ikiwa haijatumika kupiga, kupigiwa, kutuma meseji wala kutumiwa.


Mwisho wa sehemu ya thelethini na saba (37)


Kumekucha ndani ya jino kwa jino!

Hatua ya kwanza ya mguu imeinuka kwa Special Agent Fransis Simone Silla na Investigator James Miller majasusi wa DEA wakipangiwa na Agent Kai waelekee nchini Guatemala kwa ajili ya upelelezi wa eneo ambalo ndipo barua pepe iliyotumwa kwenye akaunti ya barua pepe ya Agent Kai inaonyesha mtumaji akituma kutokea eneo hilo.


Pili Agent Kai na mtu wake anayemkubali sana katika kazi za kazi za giza mwanadada Rebecca Smith wakiwa wanasubiri simu ya mwanadada Valentina ipige au ipigiwe na hapo upande wao wajue wanaanzia katika misheni hii.


Kuungua kwa mwiko siyo mwisho wa kusonga ugali!




“Sawa! Lizy atashughulikia juu ya usafiri wenu sababu nafikiri itapendeza mkianzia safari ya kutoka hapa mpaka Canada kwa basi au treni kisha mkiwa Canada mtaondoka kwa usafiri mtakaoona kwenu ni sahihi kuondoka nao na kuingia nchini Guatemala na muda wote tutakuwa sote tunawasiliana na hasa muongozaji wetu. Atawawekea maelezo ya kwanza ya kuweza kuwasaidia mtakapofika San Marcos ingawa nami nitakuwa nawasiliana nanyi kila hatua..” Akafafanua mambo mengi zaidi Agent Kai.


Walielekezana na mabo mengine kadhaa wa kadha ambayo waliona ni muhimu kwa kazi yao kisha ya hapo Lizy akashughulikia juu ya kusafiri kwa treni ya mwendokasi toka Washington DC mpaka Toronto, Canada pia aliwapatia na kiasi cha pesa kitakachoweza kuwasaidia katika gharama mbalimbali za matumizi mbalimbali.


Kikao hiki cha kupanga na kuweka sawa yote katika hatua ya kwanza kiliisha ikiwa ni mchana na wote wakafuata hatua zingine ikiwa Agent Kai, Lizy Roby na Special Agent Rebecca wao waliondoka kwa pamoja kwenda zilipo ofisi zao za kawaida ambako walipanga wakutane asubuhi huku wakivizia endapo mwanadada anayejiita Valentina kama atafanya mawasiliano waweze kum track yuko wapi? Maana mpaka muda huu alikuwa kimya simu yake ikiwa haijatumika kupiga, kupigiwa, kutuma meseji wala kutumiwa.


ENDELEA NA DODO ASALI!!


JUMANNE USIKU

GILLARD STREET, NORTHWEST, WASHINGTON DC-MAREKANI

Ndani ya chumba cha kulala katika moja ya nyumba iliyo katika mtaa wa Gillard uliopo kaskazini magharibi mwa jiji la Washington DC, kitanda kilikuwa tayari kupokea wanaokilalia kitanda hiki wakiwa mke na mume wa halali si wa kuibana ibana, ndoa yenye miezi mitatu na nusu, ndoa mpya mpya hata wenye ndoa wenye ndoa wakiwa wamezoeana kwa asilimia zisizofika mia, bado maswali hasa kwa mke kumuuliza mume mambo mengi kila apatapo nafasi basi uuliza maswali ya kutaka kumjua mume zaidi na hofu ya kuogopa kumkera itakapotokea akafanya jambo la tofauti.


Bwana Kai Hamis na mkewe Shufania Mahamud ndiyo wanandoa wenyewe, ndoa ambayo katika miezi mitatu ya fungate iliongeza furaha kwa wanandoa hawa baada ya mke kunasa ujauzito ambao una kwa sasa una mwezi mmoja na nusu, bwana Kai alishafanya yake wakiwa kwenye fungate yao huko Tanzania barani Afrika na kufanya mtoto wa kike binti mrembo haswa wa kiarabu muda mwingi kupenda awe karibu na mumewe, adeke, abembelezwe katika mengi kazi ambayo Agent Kai aliiweza haswa licha ya kuwa mimba hii haikuwa ya mtoto wake wa kwanza ila alitambua jinsi binti kama huyu mgeni wa mambo ya ujauzito, ujauzito wa mtoto wake wa kwanza, ujauzito wake wa kwanza anahitaji mume makini na mwema kama yeye. Unaweza kujiuliza mimba ya kwanza, yeye Agent Kai anajuaje? Ni kwamba binti wa kiarabu hakuwa muongo kwa mtaalamu wetu, jamaa alikuta kitu ndani ya box, box lililozungushiwa nailoni jipya lililofungwa vizuri kwa gundi, mume akatoa nailoni, akamuingiza binti kutoka kwenye binti kigori mpaka kuwa mwanamke mkubwa.


Dume komando mwenye mafunzo ya hali ya juu furaha yake ilikuwa kubwa sana, hakuwai kumtoa binti uwanawali wake, hakuwai kupata zawadi hii katika maisha yake yote, alipendwa na wanawake wengi, anapendwa na wanawake wasio na idadi kila siku wanajitokeza iwe kwa bahati mbaya (ghafla) au kwa kuonekana mahala fulani na kisha kuwekewa mitego ya muda mrefu, aliuahidi upendo wake kutoka ndani ya hisia zake kuwa iwe mvua, iwe jua, kimbunga, mabalaa yote yeye Agent Kai Hamis jasusi wa CIA kitengo cha SAD hatakuja kumuacha binti huyu, atampenda zaidi na zaidi mpaka pale Mungu anayemuamini kuwa ni Mungu mmoja muumba mbingu na ardhi na kila kilicho kinachoonekana na kisichoonekana atakaposema Kai rudi upumzike, rudi sasa ukamilishe ubinadamu maana kabla hujaumbika ni msemo lakini ni msemo unaokamilisha utu wa binadamu wote pamoja na viumbe vingine.


Asante Mungu aliyetuumba wanadamu, hii ni kweli tupu mwanamke ni nadra sana akikutana na mwanaume kwa mara ya kwanza kumpenda kwa asilimia hata ishirini inaweza ikawa ila ni asilimia kumi au na zaidi kidogo, lakini mwanamke huyo huyo upendo wake uanza kupanda kwenda kila anapodhidi kumuona mwanaume aliyevutiwa naye kwa asilimia zisizodhidi kumi na tano, Shufania bint Mahamud naye ndivyo ilivyokuwa kwa Agent Kai alivutiwa naye lakini hakuamini nzima nzima kuwa huyu ndiye mume wake, lakini kuongea naye mara kwa mara taratibu akajikuta hisia zinakimbia kwenda juu na kama hujuavyo hii ni fact (kweli ya juu) mwanamke akishapenda huwezi tena kumfuta kwenye upendo huo, mahala alipo Shufania ni hatari natamani nimvushe asilimia za kawaida amefika kilele cha upendo binti, anaona penzi analopewa ni tamu mpaka anaona wivu hata kwa wale wanwake waliokuwa na uhusiano na Kai na kisha kuzaa nae (hatari sana).


“Siku yangu leo ilikuwa ndefu sana… Jana uliwai kurudi ila leo umechelewa mume wangu, kwema huko kazini?” Akauliza mke kwa sauti isiyokinaiwa kwenye masikio ya Agent Kai, binti huyu ambaye tunatakiwa tumpe kombe la dunia ya wepesi katika kujifunza kuongea Kiswahili kwa bidii na sasa alikuwa akiongea mumewe kwa Kiswahili kwa kiasi cha kuridhisha.


“Kwema tu mke wangu… Nafurahi sana kwa kutoniuliza swali hili wakati tupo na watoto kule sebuleni, nakupenda sana mke wangu una busara na unaijua ndoa inahitaji nini… Leo kazi zilidhidi mama kijacho si unajua ni siku ya pili ya mimi kurudi hivyo kazi mezani kwangu zinazotakiwa kufanyiwa ufumbuzi ziko nyingi sana mpaka hatari, naomba uvumilie hali hii wala usikereke kwa hili kama nilivyokwambia tulivyokuwa Tanzania kuhusu kazi yangu inahitaji mwanamke muelewa asiye na machozi ya karibu, sababu machozi ya mke yana madhara kwa mume” Akajibu swali aliloulizwa huku wakiwa wamekumbatiana wanaangaliana uso kwa uso, mke akiwa kauinua uso wake hili waweze kutazamana vizuri kwakuwa hawakuwa sawa katika kimo cha urefu licha ya kuwa hakuwa mfupi ila kwa dume hili ilikuwa bure urefu wake.


“Nakumbuka mume wangu maneno yako.. Kiukweli licha ya kuelewa yote yale uliyoniambia bado nilikuwa nikitamani siku zisimame usirudi kama usirudi kazini maana kwa muda mfupi umenionyesha dunia ni nini? Sizuii usifanye kazi kwakuwa nilikubaliana na wewe wakati unaniambia jinsi vile unavyoipenda kazi yako, tuko pamoja mume wangu namuomba Mungu tudhidi kuwa pamoja maradufu daima na milele..” Akaongea Shufania huku papi za mdomo wake zikitafuta papi za mdomo wa mumewe na hapo wakaamia dunia ya raha ya kidogo wakibadilishana ladha za mate yaliyo kwenye vivywa vyao huku ulimi na papi (lips) zikisindikiza kwa raha zote kwa wapendano hawa, zoezi lililochukua dakika tatu mpaka hisia zao zilipotaka kuwapeleka sayari ingine wakaachiana kwa busu zito toka pande zote mbili likigongana kwa sauti kali.


“Bado hatujamaliza mke wangu… Nina jambo nataka ulijue kabla hatujaamia kwenye jambo linguine lolote” Akaongea Agent Kai wakiwa mikono yao wote imekamata mashavu ya mwingine huku na huku (zero distance) pumzi zao kila mmoja akiisikia ya mwingine kwa ukaribu.


“Niambie mume wangu kipenzi..!” Kwa sauti ya chini kana kwamba anaogopa isisikike kwa mwingine akaongea Shufania.


“Kesho katibu wa ofisi ya makamu wa Rais ambaye ndiyo kiongozi wangu wa kikazi anasafiri kwenda Mexico… Mexico si nchi nzuri kiusalama kwa upande wa viongozi wetu wakuu wa taifa letu hivyo msafara wa mtu mkubwa kama yeye unakuwa msafara wenye mahitaji mengi ya kiulinzi na usalama… Hivyo naomba nikupe taarifa fupi kuwa na mimi nitakuwa miongoni wa watu usalama watakaongozana na Chifu kuelekea Mexico… Na…!” Hakuweza malizia kutaka kuongea alichotaka kuongea kwani bibie alijitoa toka kwenye kumbatio na kurudi hatua mbili nyuma.


“Eeeeh! Siku mbili tu umerudi kazini tayari unaanza safari? Kweli mume wangu?!” Akauliza kwa sauti ya kawaida ila yenye msisitizo bibie huyu na mwili wake ulianza kubadilika toka rangi ya kawaida aliyonayo na kuanza kuwa mwekundu fulani (mshtuko mdogo).


“Mke wangu! Nilishakwambia lakini kuhusu safari za mara kwa mara nikiwa kama mkuu wa usalama wa makamu wa Rais na katibu wake katika ofisi yao upande wa kiintelejensia… Naomba usistuke hivyo mke wangu kumbuka umebeba nini? Na kumbuka kile tulichoongelea, usiwe kama mama aliyongea mengi wakati anatusomea risala yake, siku zote mama hapendi kumuona mwanae akifanya kazi zinazohusiana na usalama wa viongozi waliopewa dhamana ya nchi hasa nchi kubwa kama hii… Safari fupi ya siku chache unapatwa na wasiwasi, je ningesema naenda kwenye shughuli za kutafuta jambo fulani ingekuwaje?” Aliongea kirefu kidogo Agent Kai kisha akamalizia kwa swali kwa mke wake mikono yake ikisogeza viganja vyake kushika viganja laini vya mikono vya mke wake.


“Sogea karibu mke wangu mpenzi… Tafadhali rudi kwenye kumbatio langu mke wangu nahitaji joto lako tamu na pumzi yako nzuri isogee karibu iweze kunipa burudani kwenye ngoma za masikio yangu…” Akabembeleza kidume cha mbegu papo hapo mke akajivuta kurudi katikati ya mikono ya mumewe na mara miili yao ikagusana wakakumbatina , mwanamke akamkamata kwa nguvu mume.


“Nakupenda mume wangu… Nahisi vibaya kufikiria kesho sitakuwa nawe ndani ya nyumba hii, sitalala na wewe ndani ya chumba hiki na bado unasema unaenda huko kwa siku chache hii inamaanisha unaenda zaidi ya siku tatu na zaidi ya hapo pengine.. Huoni nitadhulumika mume wangu?”

“Unadhulumikaje mke wangu?... Ziara ya chifu inaweza chukua siku zaidi ya tatu ndiyo lakini mke wangu tutakuwa tunawasiliana mara kwa mara hili usiwe mpweke na hapa kuna wifi yako, wapo watoto wako na pamoja na ugeni wako wameanza kukuzoea kwa furaha kubwa”.

“Unaona rahisi Kai… Unaona rahisi mimi kukaa mwenyewe tu siku zaidi ya tatu na pengine zaidi, halafu unasahau kuwa uliniambia wewe unahusika na safari za Makamu wa Rais tu, vipi leo unaniambia na katibu wa makamu wa Rais?”

“Katibu wa makamu wa Rais ndiye boss wangu mimi kwa pale nafanya kazi kwa maelekezo yake na ruhusa zake ingawa nimeajiriwa na CIA kitengo cha SAD… Ziara ya kwenda Mexico ilibidi aende makamu wa Rais lakini makamu wa Rais ana majukumu mengine pahala pengine hivyo ikabidi aagize katibu wake aelekee huko”.

“Sawa mume wangu.. Lakini yeye katibu anaenda huko na anahitaji usimamie usalama wake, je wewe usalama wako unasimamiwa na nani?”

“Mimi mwenyewe najisimamia kama hapa navyojisimamia mimi mwenyewe na nyie wote familia yangu”

“Makamu wa Rais anaenda mahala pengine. Si ndiyo?”

“Yupo hapa hapa Marekani kuna vikao anavisimamia huko Pentagon, Virginia hivyo asingeweza kujigawa huko na huko”

“Yeye hakuhitaji wewe huko Pentagon mpaka uambatane na katibu wake huko Mexico?”

“Mimi nimerudi likizo jana tu na usalama na ulinzi wa makamu wa Rais au hata Rais mwenyewe wa nchi uwa unaandaliwa na timu yake kwa siku kadhaa nyuma na hata miezi kadhaa nyuma kama anatoka nje ya nchi hii hivyo sikuwemo katika maandalizi ya yeye kwenda Pentagon” Kwa mara ya kwanza katika ndoa yao ilimbidi Agent Kai aongee uongo mtupu kwa mkewe hili amlainishe katika safari anayotakiwa kuifanya, safari ambayo mpaka muda huo alikuwa hajui itampeleka wapi lilipo windo lao.


“Sikuwezi unajua kupanga maneno katika kujitetea kwako… Lakini waambie wakuu wako kuwa umetoka kuoa ndoa yako haina hata miezi sita na tayari mke wako ana ujauzito wako hivyo wasijaribu kutuweka mbalimbali na wala kukuingiza hatarini katika kazi zako, waambie waweke utu mbele wakuache ufanye kazi za ofisini tu kwakuwa Marekani ina sifa kuu ya kuwa na watu wengi wenye kufanana na wewe katika ufanisi wa ufanyaji wa kazi zenu” Akaongea Shufania kisha akajitoa toka kwenye kumbatio akageuka na kuelekea kilipo kitanda chao cha kulala toka walipokuwa wamesimama.


“Sawa nitafikisha ujumbe wako… Nina furaha kuu kupata mke mzuri sana anayenijali na kunipenda kwa dhati ya moyo wake” Akaongea Agent Kai naye akiwa anafuata kwa nyuma kama dume la samba linapomfuata jike lake baada ya kutoka kula nyama ya mnyama wanayependa ladha yake.


***** ***** *****


JUMATANO ASUBUHI

EISENHOWER, WASHINGITON DC-MAREKANI

“Mtu wetu amewasiliana kama mara tatu hivi usiku uliopita..” Ilikuwa simu aliyopigiwa Agent kai na Lizy Roby akiwa ndani ya gari yake anaendesha kuelekea zilipo ofisi zao ofisi ya makamu wa Rais eneo la Eisenhower kutokea nyumbani kwake mtaa wa Gillard Street.


“Ushafika ofisini?” Akamuuliza kana kwamba hajasikia alichoambiwa.


“Niko ndani ya lift napanda kuelekea na kwakuwa niko peke yangu nikachukua fursa hii kukupigia… Wewe huko wapi?”

“Niko barabarani naendesha, nafika hapo muda si mrefu… Naomba nimkute na Rebecca ofisini kwako, nasikia harufu ya safari asubuhi hii”

“Sawa dear!”


Simu ilikatwa na wa upande wa aliyempigia, yeye akairudisha kwenye dashboard ya gari kisha akaongeza mwendo wa gari yake aina ya Mitsubishi Outlander Sport rangi ya silva aliyokuwa ametoka nayo asubuhi ya siku ya leo kati ya gari kadhaa za kisasa zilizo katika yard yake ya magari nyumbani kwake.


Dakika kumi na mbili alikuwa akiingiza gari kwenye maegesho ya magari ya wafanyakazi wanaofanya kazi katika ofisi ya makamu wa Rais, alitafuta sehemu aliyoweza kuipaki gari yake ikiwa ni sehemu ambayo mara nyingi yeye upenda kupaki gari yake anapofika hapa.


Haraka kana kwamba amefika amechelewa alifanya mambo haraka kuchukua vitu alivyohitaji kuvichukua ndani ya gari kisha akatoka na kuelekea kwenye lifti iliyompeleka mpaka ofisi ya Lizy Roby.


“Imekuwa vizuri na Rebecca umefika kwa wakati maana leo naiona safari yetu machoni mwangu sasa sijui na wewe macho yanaona kama mimi!” Akaongea Agent Kai punde tu alipoingia kwenye ofisi ya Lizy na kukuta yupo Lizy mwenyewe na pia yupo S.A Rebecca Smith (S.A ni kifupi cha Special Agent).


“Nilipokuwa napaki gari yangu maegeshoni nikapigiwa simu na dada Lizy umetaka unikute hapa hivyo hima nikaja hapa kwa haraka boss!... Kuhusu safari na kusikiliza wewe bado nina mengi ya kujifunza toka kwako boss wangu hivyo macho yangu yanaona kama yako ” Akajibu S.A Rebecca akitabasamu.


“Safi sana… Habari zenu wote kwa ujumla?” Akaongea na kuuliza Agent Kai naye akiwa kachanua tabasamu usoni mwake.


“Habari zetu kama utuonavyo tuko poa salama wasalimini mimi na mdogo wangu tumejaa kama pishi ya maharage sokoni, karibu uketi tuanze kazi!” Akajibu kwa niaba Lizy Roby kisha akamkaribisha aketi.


“Kuna taarifa yoyote toka kwa ndugu zetu Guatemala?” Akauliza Agent Kai akiwa anajiweka vizuri katika kiti alichokaa ambacho kiko sambamba na kiti alichokaa Rebecca lakini wote wanamuangalia Lizy ambaye walikuwa wametenganishwa naye upande na meza kubwa ya umbo mstatili iliyoko katikati yao.


“Walinitumia ujumbe wa sauti kuwa wamefika salama jimbo la San Marcos ilikuwa ni usiku wa saa saba na wakasema asubuhi hii wanaanza kazi iliyowapeleka huko” Akajibu Lizy.


“Vizuri! Nitaongea nao baadaye… Lete habari kamili sasa!”


“Mwanadada aliongea kwa simu tatu, mbili akiwa amepigiwa na moja alipiga yeye mwenyewe… Simu ya kwanza upande wangu nimefeli kidogo maana aliongea lugha nisiyoitambua si kilatin wala kiingereza, nafikiri itakuwa vizuri ukisikiliza rekodi unaweza juwa waliongea nini maana waliongea dakika zipatazo kama ishirini na tano” Akajibu kwa maelezo marefu Lizy kisha akaruhusu audio aliyoirekodi ikiwa kwenye ipad isikike.


Wote waliweza kusikiliza vizuri kukiwa na utulivu mkubwa kati yao majibishano katika lugha iliyo ngeni kwa Lizy na hata Rebecca, audio ilipomalizika wanawake hawa wakamuangalia usoni kaka yao Agent Kai.


“Kireno hiki… Na ni muhimu sana hayo, naomba nirushie kwenye ipad yangu…. Mwanamke alipigiwa na mtu akiwa anapiga simu kutokea nchini Brazil na alikuwa akimuomba amfanyie mpango wa kupata ounces 500 za unga aina ya methamphetamines kutoka kwa mabosi zake maana yeye huyo mtu ametofautiana na hao mabosi hivyo anaomba msaada kwake na imesikika akimtaja kwa jina la kwa ufupi kuwa CPL nafikiri alimaanisha Koplo hii inamaanisha mwanamke tunayemfuatilia atakuwa ni afisa wa jeshi au aliwai kuwa afisa wa jeshi” Akafafanua Agent Kai macho yakihama toka kwa huyu kwenda kwa huyu kwa zamu zamu.


“Jina la mwanaume aliyepiga hukulisikia? Maana wakati mwanamke mpigiwa anacheka cheka alitaja jina” Akahoji Rebecca.


“Alitaja jina la mahali ambapo yupo huyo mwanaume ndiyo maana nikasema yupo Brazil…!”Akafafanua Agent Kai, mikono ikicheza na ipad yake kupokea audio alizokuwa anatumiwa na Lizy.


Walisikiliza audio nyingine mbili ikasogea ingine ambayo ni ya mwisho mwanadada akiwa kaongea kwa kilatini akiwa kapiga yeye, waliisikiliza ingawa ilikuwa imeongelewa kimafumbo haikupatikana tabu kwao, hii ilikuwa mwanadada amewasiliana na mtu ambaye jana aliongea naye na alimpa maelezo kuwa kuna mtu anahitaji kufuatiliwa.


Mwisho wa sehemu ya thelathini na nane (38)

Tayari S.A Fransis Simone Silla na Agent na Investigator Joseph January Miller kwa taarifa walizotuma wapo nchini Guatemala jimbo la San Marcos.


Huku ndani ya Washingiton DC! Agent Kai na majasusi wenzake wa kike wakiwa katika kikao ambacho walikuwa wanaamini kikao kitawapelekea katika safarfi ya huko alipo mwanamke windo lao.


Nini kitafuta?



ILIPOISHIA SEHEMU YA 38…!!

Wote waliweza kusikiliza vizuri kukiwa na utulivu mkubwa kati yao majibishano katika lugha iliyo ngeni kwa Lizy na hata Rebecca, audio ilipomalizika wanawake hawa wakamuangalia usoni kaka yao Agent Kai.


“Kireno hiki… Na ni muhimu sana hayo, naomba nirushie kwenye ipad yangu…. Mwanamke alipigiwa na mtu akiwa anapiga simu kutokea nchini Brazil na alikuwa akimuomba amfanyie mpango wa kupata ounces 500 za unga aina ya methamphetamines kutoka kwa mabosi zake maana yeye huyo mtu ametofautiana na hao mabosi hivyo anaomba msaada kwake na imesikika akimtaja kwa jina la kwa ufupi kuwa CPL nafikiri alimaanisha Koplo hii inamaanisha mwanamke tunayemfuatilia atakuwa ni afisa wa jeshi au aliwai kuwa afisa wa jeshi” Akafafanua Agent Kai macho yakihama toka kwa huyu kwenda kwa huyu kwa zamu zamu.


“Jina la mwanaume aliyepiga hukulisikia? Maana wakati mwanamke mpigiwa anacheka cheka alitaja jina” Akahoji Rebecca.


“Alitaja jina la mahali ambapo yupo huyo mwanaume ndiyo maana nikasema yupo Brazil…!”Akafafanua Agent Kai, mikono ikicheza na ipad yake kupokea audio alizokuwa anatumiwa na Lizy.


Walisikiliza audio nyingine mbili ikasogea ingine ambayo ni ya mwisho mwanadada akiwa kaongea kwa kilatini akiwa kapiga yeye, waliisikiliza ingawa ilikuwa imeongelewa kimafumbo haikupatikana tabu kwao, hii ilikuwa mwanadada amewasiliana na mtu ambaye jana aliongea naye na alimpa maelezo kuwa kuna mtu anahitaji kufuatiliwa.


ENDELEA NA DODO ASALI..!


JUMATANO

EISENHOWER, WASHINGTON-MAREKANI

“Afisa wa shirika la upambanaji wa mihadarati la ukanda wa Latin Amerika ‘Organized Crime in Latin America’ kwa kifupi ‘OCLA’ ofisi ya Guatemala City anasakwa na mtu anayempa maelekezo huyu mwanamke, inaelekea afisa huyo ameingilia mambo yao, hii inanisukuma kufikiri watu hawa wanajihusisha na madawa ya kulevya moja kwa moja” Akaongea Agent Kai baada ya kuwa wametulia wanazitathimini audio walizozisikiliza wote kwa pamoja watatu.


“Boss! Huko sahihi kabisa na afisa mwenyewe ametajwa cheo na jina moja kama sikosei ingawa siko vizuri sana katika lugha ya kilatin” Akaongea S.A Rebecca katika hali ya kuhitaji ufafanuzi toka kwa wenzake anaowaamini wamemzidi uwezo katika uelewa wa lugha ya kilatini.


“Ndiyo ametajwa jina moja anaitwa Norman na hapo unaposema ni cheo ni kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya nchini Guatemala ambacho wao ukiita Organized Crime in Latin America ‘OCLA’ hivyo wamemuita OCLA Norman ni mtu ambaye wanayeonekana wanamtafuta siku nyingi lakini hawafanikiwi kumpata na ndiyo mtu anayeharibu mambo yao mengi” Akafafanua Agent Kai.


“Inaelekea huyu Norman ndiyo Kai wao.. Hahaha hahahah!” Lizy akawachekesha na wote wakacheka kwa alichoongea.


“Acha masikhara yako… Weee kila muda ni muda wa kunitania… Ila Norman kwa jinsi maongezi yalivyoongelewa anaonekana mtu wa kazi, huyu mwanamke ni nani haswa? Simu yake jana usiku ilikuwa inatumika tokea Guatemala wakati juzi tu alikuwa Mexico, hivi kwanini anahama sana? Kwanini hatulii nchi moja? Kwanini anapotea muda mrefu kutoongea kwa simu yake? Ni maswali magumu sana sababu pia wakati ilivyokuwa jumapili wakati tunaanza ifuatilia hii namba na akaunti yake ya barua pepe ilionekana yuko Brazil sasa huyu si mtu itabidi tumpe jina la siri tumuite Vasco girl kwa udhururaji wake.. Hatari!!” Akaongea Agent Kai akikuna kidevu chake stahili ya mpapaso wa mbwembwe ambacho uachia ndevu fupi fupi zilizochongwa kistaarabu.


“Muongozo wako ni muhimu sana lakini ni kama tunakwama katika teknolojia na hapa uhakika uliopo na taratibu zilivyokaa mtu huyu uwa anaacha masaa mengi sana kuongea katika muda wetu ambao sisi tunakuwa tunahitaji kumpata hewani yeye anakuwa hayupo hivyo kuna ugumu fulani…” Akaongea S.A Rebecca akimtizama anayemuita boss wake Agent Kai.


“Norman!” Akaongea hivyo tu Agent Kai kisha akainuka na kusogea ilipo meza yenye vikombe vidogo vya udongo na chupa moja ya chai ambayo kikawaida uwa na kahawa kutokana na hali ya hewa ya baridi iliyopo ndani ya jiji la Washington.


“Norman ndiyo mtu wa kuweza kutufikisha alipo huyu mwanamke” Akaongea tena kiufafanuzi mdogo Agent Kai kisha akawaangalia wanawake ambao na wao walikuwa wakimtizama kwa umakini.


“Anaishi kwa kujificha kwa mujibu wa mpigaji wa simu na majibu ya mwanamke tunayemuhitaji, tutampataje?” Akauliza Lizy Roby.


“Wao wanasema anajificha sisi tunajipa imani hajifichi na tunaweza kumpata sababu mtu huyu ni muajiriwa wa shirika la kupambana na madawa la Guatemala hivyo tunaweza pata habari zake kirahisi sisi si hao wanaotaka kumdhuru!” Akajibu swali aliloulizwa.


“Kweli wewe bichwa… Hivi ulizaliwa usiku au mchana?” Akaongea Lizy Roby akimalizia kwa swali la kizushi na kusababisha wanawake wawili hawa kuachia kicheko kidogo kilichorandana na viganja vyao vya mkono wa kulia kuzuia midomo yao kicheko kisipae zaidi kikakera.


“Tuwasiliane na kina Silla kujua kwanza wao wamefikia wapi? Kisha kama tutaweza tutawaomba waondoke huko walipo na kwakuwa wao ni maafisa wa DEA waende ofisi kuu ya OCLA huko Guatemala City… Fanya mawasiliano Lizy!” Akatoa maelekezo kaka mkuu.


Lizy alitafuta namba za Investigator Joseph January Miller kwa kutumia Ipad yake na mara moja simu ya upande wa pili ikaanza kuita miito mitatu tu ikapokewa.


“Halloo!” Akaongea mpigiwaji sauti iliyosikika kutokea kwenye Ipad kwa wote waliopo pale.

“Habari za asubuhi Miller?” Akaongea Lizy macho yakiwa yamekazia kioo cha Ipad iliyo kwenye kiganja chake cha mkono wa kulia.

“Nzuri tu Lizy… Habari za huko na nyie?”

“Huku nzuri tu ila pia si nzuri sababu Agent Kai na S.A Rebecca wamesimama mpaka muda huu bila kwenda sawa na ratiba kama ilivyohitaji, nyie mmefikia wapi mpaka sasa hivi?”

“Tuliingia usiku mzito hapa San Marcos hivyo tuliona tupumzike kwanza kisha asubuhi hii ndiyo tujue tunaanzia wapi baada ya upelelezi wetu juu ya eneo la milima ya Tajumulco ila kwa ilivyo usiku ndiyo tutafunga safari ya kulichunguza eneo hilo”

“Eneo la milima ya Tajumulco ni eneo lililozungukwa na mashamba ya kahawa pamoja na makazi ya wakulima wa kahawa huku pia eneo la mwanzo mwanzo kuna kiwanda cha kahawa pia nyepesi nyepesi zisizo na uhakika mimea ya cocaine inapandwa kwa siri katikati ya mashamba ya mikahawa, ni vizuri mkienda usiku kama mnavyosema kwa nyepesi za kuwa pia kunakuwa na ufanyikaji wa kilimo cha mazao ya madawa ya kulevya hivyo hisia zetu patakuwa si mahala salama” Akaongea kwa urefu Lizy akielekeza vile ambavyo anavijua juu ya eneo la jimbo la San Marcos na eneo lake la milima ya Tajumulco.


“Ahsante kwa kutufunulia njia ya huelewa wa eneo husika hii itasababisha tusiwe na maswali mengi kwa wenyeji wa eneo hili, vipi nyie mlipokwama ni wapi?”

“Ongea na Agent Kai!” Akaomba Lizy kisha akaisogeza Ipad toka mkononi mwake mpaka mkononi mwa Agent Kai.


“Habari yako Mr. Miller?” Agent Kai akaanza hivyo.

“Nzuri ‘TSC’! nafikiri umesikia niliyomwambia Lizy?”

“Nimesikia… Lakini kuna jambo moja ninaomba mlifanyie kazi leo hii kabla hamjaenda huko mlipokuwa mnaelekezana na Lizy… Kuna mtu mmoja anaitwa Norman ni afisa upelelezi wa shirika la kupambana na madawa katika jumuia ya ushirikiano wa mataifa ya Latin Amerika, huyo mtu ni muhimu sana sisi kumpata katika operesheni yetu” Akaongea Agent Kai kisha akanyamaza kumeza mate.


“Tunampataje? Na Guatemala City mpaka hapa San Marcos ni masaa matano na nusu kwa usafiri wa jumuiya wa mabasi ya abiria, je tutaweza kwenda na kurudi?”

“Upelelezi wetu kwa sasa utaanzia kwa Norman…Huyu mtu kwa sasa anaweza kuwa ndiyo mwanzo wa mwanzo zote tunazotakiwa kuanza nazo kwenda katika majibu ya yote yanayotuwazisha sasa mpaka tunashindwa amua moja la kufaa!”

“Tukifika hapo unaposema tutampata yeye moja kwa moja au inakuwaje?”

“Kwa sasa inasemekana anaishi kwa kujificha ficha sababu anasakwa sana na watu ambao sisi tumeyanasa mazungumzo yao mara zaidi ya mbili, ofisi inaitwa Organized Crime in Latin America ‘OCLA’ mkifika Guatemala City mtaitafuta hiyo ofisi kisha muombe kuonana na mkurugenzi wa OCLA mkifanikiwa kuonana naye mtamwambia nyinyi kina nani kisha mtamuomba aongee nami kwa simu ndipo nitamuelekeza shida yetu..!”

“Sawa sawa mkuu… Basi acha tukatize kila kitu tujiandae kwenda uwanja wa ndege kuona kama tutapata ndege ya kwenda huko jijini”

“Sawa nawatakiwa kazi njema na Mungu awatangulie kwa kila hatua akiweka ulinzi wake kwenu” Akamalizia Agent Kai na kukata simu.


***** ***** *****


JUMATANO ALASIRI

GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Colonia El Panorama mtaa uliopo barabara ya Ciudad Vieja makao makuu ya vyombo kadhaa vya usalama nchini Guatemala ikiwemo makao makuu ya polisi likiwa ndiyo jengo kubwa zaidi pia ndipo linapopatikana jengo la Organized Crime In Latin America ‘OCLA’ shirika linalohusika na upambanaji wa madawa ya kulevya ukanda wote wa Latin Amerika.


Saa tisa na dakika kumi na tatu alasiri Investigator Joseph January Miller akiwa sambamba na mshirika wake mkuu Special Agent Fransis Simone Silla walikuwa wapo kwenye benchi moja kati ya mabenchi kama matatu ya wageni wanaotaka kuingia ndani kuonana na mkurugenzi wa shirika hili la ‘OCLA’ yakiwa yameekwa katika korido inayoelekea lango kuu la kuelekea ofisi ya muhusika wanayehitaji kuonana naye.


Dakika kumi mbele alitokea mwanaume mmoja aliyevaa sare ya kujulikana ni ya askari wa ulinzi wa pale ambayo pia ndiyo ya askari wa jeshi la polisi la Guatemala na mara alipowaangalia kwa zamu watu kama watano walioko pale kwenye benchi wakiwa wamekaa mbali mbali nafikiri kutokana na ukaribu wao au kufahamiana kwao.


Mtu yule akanyoosha mkono wake kiishara kuelekea walipo S.A Silla na Investigator Miller ishara iliyowainua kwenye benchi kwa pamoja kana kwamba wamekalia kiungo kimoja, haraka wakapiga hatua kumsogelea tena wote wakiangalia saa katika macho yao yaliyo ndani ya miwani meusi inayoonekana kama ni miwani ya jua kumbe ni miwani ya kazi mbalimbali ikiwemo hivyo pia kuzuia ukali wa jua machoni ila elewa hivyo si miwani ya kawaida ndugu msomaji ni miwani ya kazi za kazi za watu wa kazi wanaojua kazi hasa hizi kazi za giza.


“Nifuateni” Akawaongelesha kwa kiingereza fasaha lakini chenye ukakasi katika lafudhi ambayo wao kina Silla wameizoea huko kwao Marekani.


Lango lilifunguliwa na wao wakapita na kujikuta wapo kwenye korido ndefu iliyonyooka mpaka mwisho ukionekana, eneo safi kabisa lililonakshiwa vizuri kwa sakafu ya malumalu (tiles), kwa kasi waliongozana mpaka karibu na kona wakakuta kuna mlango wa vioo ambapo waliposimama tu mlango ule ukajifungua wakajikuta wameingia sehemu ya ofisi ambayo kuitizama tu unapata jibu hapa ni sehemu ya kazi za kisekretari kutokana na makabati yaliyopangwa vizuri yakiwa na mafahili katika shelfu zake na mbele akiwemo mwanadada wa kizungu mwenye nywele nyeusi akionekana ni kati ya wa Guatemala wengi walio na asili ya kihispaniola akiwa katika meza yenye kompyuta moja aina ya desktop, mashine ya kuchapa na mashine ya photocopy.


Alipowaona aliacha kazi aliyokuwa akiifanya katika kompyuta yake na akaganda kuwatizama kidogo kisha akaachia tabasamu pana la kupendeza meno yake meupe ya kung’aa yakaufanya uso wake mzuri kumfanya apendeze machoni kwa wanaume hawa wageni na nafikiri na hata jamaa aliyewafuata kina Silla kule chumba cha kusubiri uso huu na tabasamu haliwezi kuwa linamuacha salama kila anapoliona nap engine lina muathiri kisaikolojia maana mtoto wa kilatino mashaallah sura alipewa ni miuongoni mwa wasichana warembo sana wa kilatino.


“Karibuni!” Akawakaribisha kwa kiingereza safi kabisa tabasamu lake bado likiwa limeweka makazi ya uenyeji katika viunga vya uso wake murua.


“Ahsante sana! Habari yako?” Wakajibu kwa pamoja wamarekani hawa kana kwamba wanatumia koo moja kuunda maneno na kisha kuyatoa mdomoni kwa haraka na mpangilio sawa.


“Waooh! Nimefurahi sana mmejibu vizuri kwa pamoja… Mimi niko vizuri sana na ombi lenu limekubaliwa kwa haraka na mkuu wetu hivyo nisiwacheleweshe mpite ofisini kwake maana muda wa kazi unakaribia kuisha hapa ofisini… Mkitoka nafikiri tutaongea zaidi maana napenda sana ucheshi wa waamerika pia kupendana kwao bila kujali rangi zenu” Akaongea bibie yule maneno mengi na hii kwa wote kina Silla waliweza tambua hali ya binti yule ya ucheshi wake kwa watu hivyo nao walitabasamu tu.


Mvaa sare za uaskari akaongoza tena hatua chache ulipo mlango pembeni kabisa ya ofisi hii na hapo akanyonga kitasa na kuwafungulia mlango kisha akausogeza akiwapisha wapite na wao bila hiyana wakapita ndani wakajikuta wameingia ofisi yenye meza moja kubwa ya mstatili nyuma ya meza akiwa mwanaume wa makamo mnene mwenye upara unaong’aa kichwani akiwa kavaa miwani ya macho yenye lenzi kubwa kwa maana ya kioo kuwa kipana, alikuwa ameulaza mgongo wake kwenye kiti na kumfanya aonekane kama amekalia kiuno katika kiti cheusi cha kunesa nesa.


“Amerikani! Karibuni wa Marekani… Karibuni sana na nimefurahi leo kutembelewa na nyie hapa ofisni kwangu na natumaini ujio wenu ni ujio mzuri na salama kwetu na kwenu” Akaongea kwa kiingereza baba huyu ambaye umri wake ukimuangalia kama ni mtu wa kukadiria umri vizuri utamuweka katika umri wa watu wanaokaribia kustaafu kazi kisheria.


“Ahsante sana mheshimiwa… Tumefurahi sana kutupa kipaumbele sisi kwanza kuonana na wewe baada ya mapokezi huko chini kutuuliza maswali kadhaa na kujieleza ukweli wetu na nia yetu ya kuonana na wewe.. Usihofu kuhusu usalama ni kwema kabisa pande zote ingawa kwa kazi zetu si rahisi kukubali muda wote kama tupo salama” Akaeleza S.A Silla.


“Ketini tuongee wanausalama wenzangu, jisikieni mko katika ofisini zenu za DEA huko Springfield, Virginia Marekani na ninaamini hakuna haja ya vinywaji vingine zaidi ya maji tu yaliyopo hapa ofisni na mnaweza jichukulia tu hapo kwenye meza kama kuna uhitaji huo karibuni” Akaongea tena mkurugenzi.


“Upande wangu haina haja sijui kwa mwenzangu hapa?” Akajibu S.A Silla kisha akamuangalia Investigator Miller ambaye yeye akatabasamu kisha akatikisa kichwa kukataa.


“Guatemala kipindi hiki kuna kaubaridi ingawa si kama ile ya huko mlipotoka nafikiri ndiyo maana mmeona maji ya kunywa si kitu ila kuna kipindi kila mgeni nayempata hapa kutokea Marekani nikimkaribisha maji tu ufurahi sana na kupokea…. Karibuni sana naitwa Kamanda Muniain Salivita Muniero mkuu wa shirika la upambanaji wa madawa ya kulevya ukanda wa Latin Amerika” Akaongea kirefu kidogo katika yale matamanio yake ya kuona wageni wake hawa wanapata angalau maji ya kunywa licha kukataa kwao kisha akajitambulisha.


“Usijali kuhusu maji mheshimiwa hali ya hewa si ya kukausha makoo pia njiani wakati tunakuja hapa tulipata maji mpaka getini mwa jengo hili… Naitwa Special Agent Fransis Simone Silla” Akajitambulisha S.A Silla.


“Na mimi naitwa Investigator Joseph January Miller, sote sisi tunatokea Drug Enforcement Administration makao makuu… Tumefika hapa kwa maelekezo ya Afisa wa CIA aitwaye Agent Kai baada ya sote kuwa tuko katika operesheni moja tunayoshirikiana” Akaongea Investigator Miller kisha akanyamaza alipoingiza mkono wake mfuko wa suruali yake na kutoa kitambulisho chake cha kazi akamuonyesha mkurugenzi jambo ambalo liliigwa na S.A Silla kumuonyesha pia kitambulisho mwenyeji wao.


“Ahsanteni sana.. Tunafanya kazi na DEA kwa ushirikiano mkubwa sana hasa mipakani ila kwa mujibu wenu mmepewa maagizo ya mtu anayeitwa Agent Kai afisa wa CIA, sijamjua huyo ni nani haswa? Tafadhalini naombeni maelezo anataka nini kwangu afisa?” Akaongea na kuuliza Kamanda Muniain.


Mwisho wa sehemu ya thelathini na tisa (39)


Ujanja na uzoefu wa kazi wa Agent Kai bado haujaweza kumfanya afanikiwe kupata mwelekeo maalumu wa wapi anaweza kumpata mwanamke anayejiita Valentina.


Katika kuendelea kuipanga mipango sawa akabadili mbinu ambayo alikwisha ipanga na washirika alioletewa kutoka DEA akaamua kuifuata njia ambayo hisia zake zilimuonyesha itakuwa sahihi zaidi wakiifuata kuliko kufuata zile za kwanza walizopanga kwa pamoja, akamuomba Lizy apige simu kwa kina S.A Silla na Investigator Miller kisha akawaomba waende ofisi za shirika la upambanaji wa madawa kulevya ukanda wa Latini Amerika.


Special Agent Silla na Investigator Miller wapo ofisi ya mkurugenzi wa ‘OCLA’ nini kitafuata?”


Majibu ya yote yapo sehemu inayokuja na zitakazokuja.




“Ketini tuongee wanausalama wenzangu, jisikieni mko katika ofisini zenu za DEA huko Springfield, Virginia Marekani na ninaamini hakuna haja ya vinywaji vingine zaidi ya maji tu yaliyopo hapa ofisni na mnaweza jichukulia tu hapo kwenye meza kama kuna uhitaji huo karibuni” Akaongea tena mkurugenzi.


“Upande wangu haina haja sijui kwa mwenzangu hapa?” Akajibu S.A Silla kisha akamuangalia Investigator Miller ambaye yeye akatabasamu kisha akatikisa kichwa kukataa.


“Guatemala kipindi hiki kuna kaubaridi ingawa si kama ile ya huko mlipotoka nafikiri ndiyo maana mmeona maji ya kunywa si kitu ila kuna kipindi kila mgeni nayempata hapa kutokea Marekani nikimkaribisha maji tu ufurahi sana na kupokea…. Karibuni sana naitwa Kamanda Muniain Salivita Muniero mkuu wa shirika la upambanaji wa madawa ya kulevya ukanda wa Latin Amerika” Akaongea kirefu kidogo katika yale matamanio yake ya kuona wageni wake hawa wanapata angalau maji ya kunywa licha kukataa kwao kisha akajitambulisha.


“Usijali kuhusu maji mheshimiwa hali ya hewa si ya kukausha makoo pia njiani wakati tunakuja hapa tulipata maji mpaka getini mwa jengo hili… Naitwa Special Agent Fransis Simone Silla” Akajitambulisha S.A Silla.


“Na mimi naitwa Investigator Joseph January Miller, sote sisi tunatokea Drug Enforcement Administration makao makuu… Tumefika hapa kwa maelekezo ya Afisa wa CIA aitwaye Agent Kai baada ya sote kuwa tuko katika operesheni moja tunayoshirikiana” Akaongea Investigator Miller kisha akanyamaza alipoingiza mkono wake mfuko wa suruali yake na kutoa kitambulisho chake cha kazi akamuonyesha mkurugenzi jambo ambalo liliigwa na S.A Silla kumuonyesha pia kitambulisho mwenyeji wao.


“Ahsanteni sana.. Tunafanya kazi na DEA kwa ushirikiano mkubwa sana hasa mipakani ila kwa mujibu wenu mmepewa maagizo ya mtu anayeitwa Agent Kai afisa wa CIA, sijamjua huyo ni nani haswa? Tafadhalini naombeni maelezo anataka nini kwangu afisa?” Akaongea na kuuliza Kamanda Muniain.


ENDELEA NA DODO ASALI!


JUMATANO ALASIRI

GUATEMALA CITY, GUATEMALA

“Agent Kai Hamis ni jasusi wa CIA aliye katika ofisi ya makamu wa Rais… Mara nyingi majasusi wa DEA uwa tunafanya kazi na majasusi toka CIA kwenye operesheni za nje ya nchi na pia utokea uwa tunafanya kazi za mashirikiano na mashirika ya kupambana na mihadarati yaliyopo nje ya Marekani hasa DTO ya Mexico ila sina hakika kama watu wa DEA hawajawai fanya operesheni iliyohusiana na nyie OCLA nafikiri kama si kwa namna inayoweza kuwa ya hata ya kuomba msaada basi ni kwa operesheni ni kutokuwa na rekodi kwa upande wangu..!” Alinyamaza kuendelea kuongea S.A Silla kwani Kamanda Muniain alipanua kinywa kuonyesha ana jambo.


“Tushafanya operesheni kadhaa mpakani kwa ushirikiano naamini kutokuwa kwenu katika kikosi cha maafisa wa mipakani inasababisha msiwe na rekodi kamili juu ya hili..! Endelea nataka kumjua haswa Agent Kai na anasemaje? Ndiyo mkuu wenu?” Akafafanua kamanda kisha akauliza maswali mawili kwa mpigo.


“Si bosi wetu! Yeye hayupo DEA ila CIA hawana mipaka katika shughuli za kuipigania Marekani katika maslahi yake… Katika nchi yenu kuna watu wetu wanashikiliwa mateka n…!” Hakuweza endelea akakatiziwa kwa swali.


“Watu hao ni wanausalama wa Marekani?” Akauliza.

“Ndiyo mkurugenzi ila hawashikiliwi na vyombo vya usalama vya Guatemala bali wanashikiliwa na kikundi ambacho sisi hatukijui ni kikundi gani?” Akajibu S.A Silla.

“Miongoni mwao yumo Agent Kai? Mmmh!”

“Hapana.. Watu waliotekwa wametekwa miaka saba iliyopita lakini miongoni mwao hayupo Agent Kai wa CIA lakini yeye ndiye aliyelifufua jalada la kesi ya kuwatafuta hawa ndugu zetu waliopotea katika mazingira ya kutatanisha na ndiye aliyetuagiza tufike hapa kuonana na wewe baada ya yeye kupata barua pepe katika akaunti yake ya mmoja ya watu waliopotea miaka saba iliyopita” Akajibu kirefu S.A Silla.


“Mlisema operesheni hii imewaleta sehemu moja nyie na CIA, yeye Agent Kai amefika hapa Guatemala na je kwangu mnataka msaada wa aina gani? Kibali cha kazi yenu au ni nini?”

“Ndiyo operesheni yetu imetuweka pamoja kikazi na wenzetu wa CIA walio makao ofisi ya makamu wa Rais Eisenhower, Washingiton DC na mkuu wa shughuli hii ni Agent Kai na ndiyo maana tunafuata maelekezo yake akiwa bado yupo Marekani na elekeza yake ya kwanza ilitutaka tufike hapa kuonana nawe kisha tukuombe uongee naye kwa simu ana jambo la kuongea na wewe” Akaongea Investigator Miller ambaye muda mwingi alikuwa msikilizaji lakini sasa aliona ni wakati wa kupokea kijiti cha maswali na majibu kutoka kwa ndugu yake.


“Sasa naanza kuelewa ugeni wenu unamaanisha nini kufika hapa ofisini kwangu… Sawa pigeni simu nimsikie anasemaje kama ni jambo lililo kwenye uwezo wa ofisi yangu basi nitasaidia mara moja bila kusita” Akatoa ruhusa kifanyike kilichokusudiwa na kilicho kikuu kilichowaleta watu hawa katika ofisi hii.


Investigator Miller akatoa simu yake toka mfukoni na kupiga namba anazotumia ofisini Lizy Roby na kwakuwa walikuwa washatoa taarifa kuwa wameingia ofisi hizi tayari wakae tayari kwa lolote hivyo hawakuwa na hofu muda huu wa mchana lazima Agent Kai atakuwa pembeni ya Lizy Roby.


Simu ilisachi kidogo kisha ikakamata mawasiliano na upande wa pili ikaanza kuita na miito mitatu tu ilitosha upande wa pili kupokea.


“Silla!” Upande wa pili sauti ya Lizy ya kike ikasikika.

“Naam… Tuko na mkurugenzi wa OCLA hapa… Agent Kai aongee naye!”

“Oooh! Vizuri sana… Huyu hapa” Akajibu Lizy na mara ukasikika mlio wa kiti kinachosogezwa pembeni ukimya wa sekunde mbili ukavuta hewani.


“Halloo Investigator Silla… Agent Kai hapa!” Ikavuma sauti ya kiume iliyosikika vizuri kwa wote kwakuwa simu ya Silla ilikuwa imewekwa loud speaker hili wote wasikie.

“Naam mkuu… Ongea na mkurugenzi tayari tumemuelewesha kidogo juu ya ujio wetu hapa GTL” Akaongea Investigator Silla kisha akanyoosha simu kuelekea kwenye kiganja cha mkono wa kulia wa kamanda Muniain ikiwa tayari ameondoa loud spaker.


“Habari yako Agent Kai?” Akaongea Kamanda baada ya kuiweka sikioni simu.

“Nzuri kabisa mkurugenzi.. Habari za GTL?”

“Hapa nzuri tunamshukuru Mungu kwa hili.. Vipi za Washington DC?”

“Huku pia kuko shwari kabisa, poleni na changamoto iliyopo ukanda wenu juu ya magenge ya mihadarati”

“Aisee! Changamoto hii imekuwa kubwa sana inatishia sana kwa ukweli hasa wenzetu wa Mexico wanakoshindwa kudhibiti hali ya magenge ya huko mpaka yanasogeza huduma yao ya uhalifu katika nchi zetu”

“Lakini na nyie mnaruhusu kilimo cha madawa haya kiurahisi mnashindwa kudhibiti na madawa hayo kwa kilimo chake ambapo ni doto kulwa na magenge ya mihadarati, mkurugenzi sitaki nitupe lawama kwako kwakuwa najua kudhibiti magenge hayo ni kazi nzito sana ambayo inaishinda hadi nchi yenye nguvu kubwa sana katika usalama kama yetu na bado watu wanafanya biashara, watu wanaathirika na maunga hayo kila siku idadi ya waathirika wanaotakiwa kwenda sober kliniki ya kutumia madawa inaongezeka mapak mtu unajiuliza tunafeli wapi?… Hatari sana!”

“Hilo liko wazi… Kukata matawi haitoshi ikiwa tunashindwa kata mizizi hizi biashara kwa ukanda wetu zinafanywa na watu ambao ukiambiwa nyadhifa zao katika serikali na hata heshima kwenye jamii unaweza kushangaa kabisa na ndiyo wanaotupa ugumu wana pesa nyingi sana ambazo zinaharibu mifumo yetu ya usalama kabisa, mexico magenge yanafanya mambo ambayo unaweza ukastaajabu kabisa ndugu yangu”

“Inauma sana na ni rahisi kupambana na magaidi kuliko kupambana na magenge haya ya mihadarati, natamani kumaliza mizizi yao kuokoa jamii yetu lakini nikitizama cheni na mtiririko naogopa kujiumiza mwenyewe hata kama najiamini kujiamini kwangu hakuwezi kushindana na woga napoangalia giza lenyewe lilivyo zito… Mkurugenzi tuna mengi sana ya kuongea mimi na wewe na kubadilishana mawazo lakini muda si rafiki licha ya mengi hayo ambayo yanaweza kufunua mengi yaliyo chini, nitaomba namba yako siku nyingine kati ya siku hizi tutaongea vizuri na pengine hata kuonana kabisa… Na jambo ambalo limenisukuma mimi kuwaagiza ndugu zangu hao kufika hapo ofisini kwako… Katika ofisi yako kuna mtu anaitwa Norman nina shida naye!” Akajieleza na kuweka maneno ya mtego kwa mkurugenzi (ufundi).


“Norman… Norman Cabrera! Una shida naye kafanyaje kijana wangu? Anatafutwa sana huyu kijana” Mkurugenzi Kamanda Muniain alijiingiza mtegoni hakuwa anajua kama Agent Kai hamjui Norman hajui kama anaitwa Norman Cabrera zaidi ya kujua kuwa kuna mwanausalama wa Guatemala ambaye anapambana katika kudhibiti biashara haramu ya ulanguzi wa madawa ya kulevya akiwa anahudumu katika OCLA akiwa anatafutwa auwawe au apatikane katika hali yoyote ile hivyo alichofanya ni kuongea akijiaminisha kuwa anatambua anachotaka kwa kamanda hali ambayo ilimsaidia kwa kupewa jibu la urefu wa jina lote la kwanza na la pili.


“Ndiyo ni Norman Cabrera… Yuko hatarini anasakwa sana na watu ambao mpaka sasa najua wako wawili na nina namba zao za simu watu hao mmoja akiwa ni mwanamke na mwingine ni mwanaume na ndiyo huyu anayetoa amri Norman Cabrera auwawe haraka sana kwa manufaa ya biashara zao kwakuwa kijana wako ndiyo kikwazo kwa biashara zao hapo Guatemala” Akafafanua Agent Kai.


“Natambua kijana huyu yuko hatarini lakini sikuwa najua na nyinyi mnafuatilia jambo hili mpaka mpatwe na msukumo uliowasukuma kutaka kujua zaidi… Nahitaji kujua unamuhitaji katika hali ya kumsaidia kumkinga na watu hao au unatakaje? Mkuu”

“Naamini washirika wenzangu hapo wamekwambia nia ya dhumuni lililowaleta hapo GTL… Hivyo katika kuunganisha mambo kijasusi tumeona kuna muingiliano ambao unaweza kutusogeza katika dot kadhaa kufika mahala tunapopataka na dot ya kwanza ni kuonana na Norman na kama tutakubaliana kuna mambo ambayo yanayoweza kutusaidia pande zote mbili zikanufaika”

“Oooh! Taratibu naanza kuelewa mkuu… Norman mnahisi anaweza kuwa anawajua wanaomsaka kumdhuru na hao wanaotaka kumdhuru ndiyo na nyie ni lengo lenu?”

“Ndiyo mheshimiwa! Watu hao ndiyo tunahisi wanaweza kuwa wanashikilia mateka ndugu zetu wamarekani katika sehemu ya siri huko GTL sababu tuna ushahidi wa kimawasiliano kutoka kwa mwanamke ambaye mara nyingi anakuwa hapo Guatemala ingawa si mtu wa kukaa hata siku mbili sehemu moja katika nchi zinazozunguka eneo hilo la Latin Amerika… Hivyo mheshimiwa tunaomba utusaidie kwa hali na mali sisi kuonana na kijana wako na ikibidi utuombee atupe ushirikiano wa kikazi nasi tutampa ushirikiano katika mengi anayoyahitaji ambayo kimantiki ndiyo hitaji la ofisi yako hapo”

“Sawa sawa Agent! Nitafanya hivyo lakini kuna mambo siwezi kuongea kwenye simu nafikiri ni vizuri kama nitaongea na vijana wako… Nataka nikwambie ukweli hali katika nchi hii si nzuri sana katika mapambano dhidi ya mihadarati kila sehemu si salama kabisa hakuna kuaminiana kabisa hivyo ilitufanya mimi na Norman tufanye jambo ambalo tunalijua watu watatu tu, yaani yeye, mimi na mkuu wa polisi na ndiyo linalofanya mpaka sasa Norman kuwa salama na kufanya kazi kwa siri hivyo kiusalama ningependa tusiongelee kwenye simu ingawa naamini hizi simu zenu ni salama hakuna uchakachuzi wowote lakini simu nayotumia mimi pia si salama sana… Nimekuelewa na nakuahidi niko tayari kutoa ushirikiano katika shughuli yenu” Akaeleza kamanda Muniain kwa kirefu.


“Sawa nimekuelewa na ninashukuru kwa kukubali kutupa ushirikiano acha mimi na mwenzangu tufanye mpango wa usafiri tuje Guatemala hili kuongeza nguvu ya misheni hii kwa wenzetu pamoja na nyinyi” Akamalizia Agent Kai na kukata simu upande wake.


“Ahsanteni sana! Nimeongea na Agent Kai na nimeweza tambua mengi kati ya mahitaji yenu” Akasema Kamanda Muniain huku akirudisha simu mkononi mwa Investigator Miller.


“Sisi pia tumefurahi kwa wewe kumuelewa kiongozi wetu wa misheni hii na nafikiri kwa ushirikiano wenu mtakaotupa tutaweza fanikisha kwa urahisi yale tunayotamani kufanikisha katika misheni” Akaongea S.A Silla kisha wakaangaliana na Miller kwa chati.


“Muda wa kufunga ofisi upande wangu ndiyo umefika… Leo nilipanga kuonana na Norman saa moja usiku hivyo kwakuwa hali ya hapa si nzuri sana kwa vikao vya mtu kama mimi na watu wengine nafuatiliwa sana na watu wenye maslahi na mihadarati ambao wako kila mahala kila sekta muhimu unayoijua wewe imechafuka na wote maisha yao yanaona uwepo wangu ni kikwazo kikubwa… Nitawapigia simu kuwataarifu wapi tutakutana hili niwakutanishe naye”


“Sawa sawa mkuu tutasubiri muda huo ila sidhani kama muda huo Agent Kai atakuwa kashafika hapa GTL kwa ilivyo muda huu mlioongea na muda watakaoweza kupata usafiri” Akaongea S.A Silla.


“Msiwe na wasi juu ya hilo muda wowote ambao atafika akitaka kuonana nami tutapanga wapi tuonane na kuonana kwetu naomba niwaambie ukweli itakuwa vizuri ikiwa ni usiku tu sababu hata Norman uwa naonana usiku tu na uwa ni mahala pa siri sana hivyo nanyi itakuwa hivyo na muda tutakaokutana nitawaeleza sababu ya kufanya hivyo ila kifupi elewa tu hali si shwari kwa sisi tulio na kazi kama katika ofisi hii yaani hata walinzi wangu siwaamini” Akaeleza tena Kamanda Muniain.


Waliendelea kuelekezana mambo kadhaa wa kadha kisha wageni wa ofisi hii waliagana na mwenyeji wao kwa ahadi watakutana muda wa saa moja atawajulisha kuwa waonane wapi katika hali ya usalama zaidi.


Investigator Miller na S.A Silla walitoka nje ya ofisi wakaagana na walinzi na kwakuwa hawakuwa na usafiri wa binafsi waliofika nao hapa iliwalazimu kutembea kwa miguu wakiwa katika mavazi yao ya kufanana suti rangi nyeusi wakifunga na tai pia zinazofanana, walivaa hivi kwakuwa walikuwa na hofu wakati wanakuja ofisi za OCLA pengine watapata vikwazo kuonana na mkurugenzi wao kwa stahili ambayo walipenda wao wavae hivyo kiafisa zaidi kuwakilisha uafisa wao ndiyo waliona ni sahihi zaidi.


Ilikuwa ni jioni barabara zote kuanzia za katikati zinazopitisha vyombo vya usafiri kama magari na pikipiki kulikuwa na uwingi wa kutosha katika barabara hii ya Ciudad Vieja itokayo mtaa wa Colonia El Panorama, pembeni mwa barabara ambapo ni njia za wapita kwa miguu ambako Investigator Miller na mshirika wake walikuwa wakiongozana kwa wakitembea kawaida huku wanaongea mambo ya kawaida tu napo kulikuwa hakunaunapoweza hata kutema mate kutokana na uwingi wa watu wanaopita kwa miguu wake kwa waume wanakwenda huko na huku mipishano tu.


“Nahisi kuna watu wanatufuatilia Silla… Wako wawili nyuma yetu niliwaona nje kwenye maegesho ya magari ya upande wa pili wa ofisi za OCLA lakini toka tuondoke kule barabara hata kama ya kunyooka nikigeuka kwa wizi nikiwa najifanya naangalia sehemu mbalimbali nawaona wanavyojitahidi kuonekana kama wako na mambo yao tu” Akaongea kwa sauti ya chini Invetsigator Miller huku wakiendelea kutembea kwa mwendo ule ule waliokuwa nao.


“Nilijua nimehisi mimi tu kumbe na wewe umewaona… Hahahahaha shiit! Alivyosema Kamanda Muniain ni sahihi… Nimewaona mmoja kavaa suti ya rangi ya kijivu na mwingine kavaa suti ya rangi nyeusi ila wana tattoo zinazoharibu muonekano wao wa kuigiza ustaarabu” Akajibu S.A Silla kwa stahili ambayo ni kama ile aliyoambiwa yeye sauti ya chini lakini inayosikika vizuri kati yao tena hakuna aliyegeuka nyuma kati yao.


“Tunafanyaje?” Akahoji Miller.

“Tunaingia kazini moja kwa moja hakuna kuremba tuko GTL kwa kazi na hii ni kazi imejileta kaka tuwatege na mpango unaanza tunaingia sehemu ya vinywaji tutakayoiona mbele yetu” Akaelekeza Investigator Miller.


Walitembea mita kadhaa walipokuwa wanakaribia mzunguko wa unaogawanya barabara hii na barabara ingine ambayo kwao hawakuweza kujua ni barabara yenye jina gani? Waliiona bar iliyochangamka sana kutokana na uwingi wa watu mbele kabisa ya eneo la kuingilia kukiwa na bango kubwa la kuifahamisha bar ile ikiwa inaitwa ‘La Casa De Cervants Beer and Restaurant’, kweli hawakuremba waliingia ndani ya eneo la Bar kisha wakatafuta mahala ambapo waliona wakikaa wataona kila anayeingia na kutoka hapa Bar.


Wakati wakiweka viti kabla hata hawajakaa watu waliokuwa wana wasiwasi juu yao waliingia nao na walipoingia walijifanya wanaangali huko na huko kana kwamba ni watu wanaomtafuta mtu wanayemjua au watu wanaowajua na hata walipowaona kina Silla walijifanya bado wanatafuta tafuta kisha wakaenda kwenye meza ambayo haikuwa na watu lakini ipo karibu na lango kuu la kutokea hapa, hapo walivuta viti wakakaa.


Hapo upande wa Investigator Miller na S.A Silla walikuwa wameshahakikisha ni kweli wasi wasi wao ulikuwa sahihi ni kweli wao wanafuatiliwa na watu hawa wasiowajua wao ni kina nani katika Guatemala City hii.



Timu yote ambayo mara kwanza walijipangia kuwa ingejigawanya pande mbili kwa wawili kuelekea Guatemala na wawili kuelekea Mexico imekuwa ni tofauti tayari Agent Kai na S.A Rebecca wanatafuta usafiri utakaowafikisha Guatemala.


S.A Silla na Investigator Miller wakiwa na wao wamemaliza mazungumzo na Kamanda Muniain mkurugenzi wa shirika la kupambana na madawa ya kulevya ukanda wa Latin Amerika wakiwa wanatoka wanastuka kuwa wanafuatiliwa.


Je wanafuatiliwa na kina nani? Na kwanini wanawafuatilia wamejua jambo gani? Na wamejuaje?


Jibu la haya yote nafikiri ni subira yako na kuhama kurasa hii kwenda kurasa inayofuata na zitakazofuata kwa majibu ya mengi ambayo utapenda kuyajua katika mwendo wa JINO KWA JINO.




   “Nilijua nimehisi mimi tu kumbe na wewe umewaona… Hahahahaha shiit! Alivyosema Kamanda Muniain ni sahihi… Nimewaona mmoja kavaa suti ya rangi ya kijivu na mwingine kavaa suti ya rangi nyeusi ila wana tattoo zinazoharibu muonekano wao wa kuigiza ustaarabu” Akajibu S.A Silla kwa stahili ambayo ni kama ile aliyoambiwa yeye sauti ya chini lakini inayosikika vizuri kati yao tena hakuna aliyegeuka nyuma kati yao.

   “Tunafanyaje?” Akahoji Miller.

   “Tunaingia kazini moja kwa moja hakuna kuremba tuko GTL kwa kazi na hii ni kazi imejileta kaka tuwatege na mpango unaanza tunaingia sehemu ya vinywaji tutakayoiona mbele yetu” Akaelekeza Investigator Miller.

Walitembea mita kadhaa walipokuwa wanakaribia mzunguko wa unaogawanya barabara hii na barabara ingine ambayo kwao hawakuweza kujua ni barabara yenye jina gani? Waliiona bar iliyochangamka sana kutokana na uwingi wa watu mbele kabisa ya eneo la kuingilia kukiwa na bango kubwa la kuifahamisha bar ile ikiwa inaitwa ‘La Casa De Cervants Beer and Restaurant’, kweli hawakuremba waliingia ndani ya eneo la Bar kisha wakatafuta mahala ambapo waliona wakikaa wataona kila anayeingia na kutoka hapa Bar.

Wakati wakiweka viti kabla hata hawajakaa watu waliokuwa wana wasiwasi juu yao waliingia nao na walipoingia walijifanya wanaangali huko na huko kana kwamba ni watu wanaomtafuta mtu wanayemjua au watu wanaowajua na hata walipowaona kina Silla walijifanya bado wanatafuta tafuta kisha wakaenda kwenye meza ambayo haikuwa na watu lakini ipo karibu na lango kuu la kutokea hapa, hapo walivuta viti wakakaa.

Hapo upande wa Investigator Miller na S.A Silla walikuwa wameshahakikisha ni kweli wasi wasi wao ulikuwa sahihi ni kweli wao wanafuatiliwa na watu hawa wasiowajua wao ni kina nani katika Guatemala City hii.

ENDELEA NA DODO ASALI!

JUMATANO JIONI

GUATEMALA CITY-GUATEMALA

   “Hapa sasa ndugu yangu kama ulivyojionea mbuzi zenye mkia zinatusotea.. Tutazionyesha Amerikani si watu wa kusotewa kibwege bwege na mbuzi zisizoota hata ndefu za kijasusi zinafuata kama nzi anavyofuata kidonda kilichokosa uangalizi” Vinywaji vilipoachwa mezani tu na muhudumu S.A Silla alianzisha mazungumzo baada ya kupiga funda kadhaa za utangulizi za bia.

   “Dakika kumi mbele mi nitaenda chooni wewe utakaa kuangalia watafanyaje? Kwa ninavyoamini kama kweli ni mafundi hawatainuka kuja kunifuata iwe wote au mmoja lakini mbinu hiyo itaendelea baada ya dakika chache nawe utaomba kwenda chooni wakati ukiwa huko mi nitatoka nje nikijifanya naongea kwa simu, wewe ukitoka utalipia vinywaji nakuja nje wakati huohuo nitachukua taxi.. Wewe ukitoka utaondoka na kuchukua taxi pia hapo lazima wao watataka kukufuata wewe maana tutakuwa tumewachanganya sana… Vipi hii?” Akaeleza Investigator Miller mpango alioona huko sahihi.

   “Mpango huko sahihi lakini hauoni kuwachanganya kwetu tunaweza kuwapoteza?” S.A Silla akauliza.

   “Lakini unaona walivyo na shida na sisi na hatujui kwanini wanatufuata ila ni kawaida kwetu majasusi kufuatiliwa hivyo ni juu yetu kuwaweka na wao mawindoni na kujilinda pia… Nataka kusikia tunafanyaje katika lililo muhimu kwetu kwa muda huu”

   “Tuwateke!”

   “Kivipi? tutafanikisha..!”

   “Tukimaliza hivi vinywaji tutatoka nje kwa pamoja na wakitufuata papo hapo tunawageuka maana tutasimama tuone watatupita ama vipi?”

   “Sawa tufanye utakavyo ..!” Akakubali Ivestigator Miller ambaye kiumri amepitwa miaka kama minne na Special Agent Silla ambaye ni mzungu na Miller ni mwenye asili ya Afrika (mweusi).

Kwakuwa ilikuwa ni jioni na walitaka kufanya jambo mbele yao walijikuta wakinywa na kuagiza kuongezewa kwa mizunguko ipatayo mitano mbele kwa maana kila mmoja alikunywa bia aina ya Brahiva Extra bia ya chupa inayotengenezwa na kiwanda kinachoitwa Ambev Centro America Brewery kilichopo eneo la Teculutan ndani ya jiji la Guatemala City, wao walitaka kunywa bia hii hili kutoonyesha ugeni wao maana wamarekani wengi uwa wanapenda kunywa vinywaji vya kutoka nchini mwao ila kwa wao majasusi walikuwa na funzo juu ya hili mara zote wakitoka nje ya nchi kikazi basi ujifanya wanaenda na mazingira.

Walipoona giza giza la saa moja linakaribia walimuita muhudumu na kulipia vinywaji kwa idadi waliyokunywa kwa pesa ambazo walibadili kiasi kidogo cha pesa walizokuwa nazo kutoka dola hadi quetzal Guatemala  pesa za nchi hii toka wako uwanja wa ndege wa kimataifa wa La Aurora International Airport uliopo kusini mwa jiji la Guatemala.

Majasusi wa DEA waliinuka kwa pamoja wakionyesha furaha kubwa sana na wote wakijifanya wamelewa sana mpaka wanasaidiana kuinuka kwa kuvutana mikono na kufanya baadhi ya watu kuwaangalia maana kucheka cheka na kuyumba yumba kuliteka macho ya watu wengine.

Walitoka wakijifanya wanajizuia kuonekana wamelewa lakini kwa mtazamaji anayewatizama ataamini hawa vyombo kichwani vimekolea lakini wanajitahidi kuzuia hali itakayowastaajabisha watu wengine.

Hatua kwa hatua mikono yao mifukoni yumba yumba ya kujifanyisha na wakinakshinakshi na sauti za kilevi walitoka mpaka nje, wakanyoosha kufuata barabara ya wapita kwa miguu kigiza giza kikiwa kinafukuza mwanga wa jua kwa kasi na kuleta mwanga fulani mwekundu.

Walevi wa maigizo walinyoosha kisha walipofika zilipo alama za pundamilia wakasimama usawa wa kuonyesha wanahitaji kuvuka kwenda upande wa pili, hii ikiwa ni geresha maana hapa lazima waangalie usalama wao kama kawaida ya watumia barabara hasa wa miguu pale wanapotaka kuvuka usimama kando ya barabara na kutupa macho huku na huko wakianza kulia kisha kushoto.

Waliweza kutupa macho kulia kisha kushoto na ile ya kwanza ya kulia walifanikiwa kuona mikia miwili bado inajifanya ina mambo yao lakini si mambo yao ni mambo ya kuwafuatilia watu kwa agizo maalumu walilopewa.

S.A Silla na Inv. Miller waliruhusiwa na mataa ya barabarani kuwa wapiti kwa miguu sasa wanaruhusiwa kuvuka barabara kuko salama salamini magari yamesimama kuwapisha wao.

Mikia bila aibu wala kuonyesha uwezo wao thabiti katika ufuatiliaji wa watu waliokubuhu kama kina Silla, wao nao waliwai kwa mwendo wa kukazana nusu mbio nusu kutembea kawaida.

Bara bara hii ni barabara yenye njia mbili hivyo walipomaliza njia ya kwanza  ikawabidi wasimame kwa kuwa ile inayofuata yenyewe mataa yalikuwa hayasimamisha magari yanakwenda kwa ile ile, walikuwa watu wengi waliosimama, mikia haikuwa na budi na yenyewe ikafika pale na kwa aibu fulani wakajitenga hatua cheche toka walipo Silla na Miller.

Dakika mbili mbele magari yalisimama kwa amri ya mataa yanayoongoza utaratibu barabarani huku yale ya upande wa nyuma yao yakiwa yameruhusiwa, Silla na Miller wakavuka kwa kasi hadi upende wa pili ambao maduka karibu yote ya eneo hili yalikuwa yamefungwa.

Mikia nao kama kawaida wakavuka na sasa mmoja wao alikuwa akiongea kwa simu na macho yake yote mawili yakiwa yanafanya janja janja kuangalia mawindo yao yasiwapotee na huku akiongea kwa simu.

Uwingi wa watu muda wa magharibi uliwafanya wajichanganye sababu macho yao hayakuwa tena yanaona mawindo yao.

Taharuki! Kubwa ilionekana kati yao wakaanza kuangalia huku na huko bila kufanikiwa kudanganya tena maana sasa ilikuwa dhahiri si kificho kuwa wamepagawa kwa kuwapoteza watu walioambiwa na boss wao kuwa ni watu muhimu sana wasiwapoteze hata chembe ya mchanga, wakaangaliana kisha wakaanza kukimbia mwendo nusu tembea nusu kimbia (kukazana). 

Walipofika karibu na maegesho ya taxi wakapunguza mwendo maana hapa palikuwa na watu lakini si wengi kama walipokuwa wanatoka.

Hamadi! Laaulah wa lakwatah! Wakiwa wanakanyaga sakafu iliyopangwa vitofali vidogo vidogo vinavyozunguka eneo la madereva wa taxi na taxi zao nyuma yao ilisikika sauti katika lugha ya kilatin.

   “Simameni vivyo hivyo mlivyo! Na mnyooshe mikono juu!” Sauti nzito ya kiume iliyo na ugeni kwenye masikio ya mikia hawa  ilisikika, jamaa walistuka sana maana sauti kimakadirio ilikuwa ikitokea kwa nyuma yao hatua tatu au nne toka walipo wao, wote wakageuza shingo zao kuona nani anaongea.

Macho yakawatoka wote kwa pamoja walikutana na mkono mmoja wa kulia wa mzungu ukiwa kiganjani umekamatia bastola kwa chati huku aliye pembeni akiiziba bastola isionekane kwa wapita njia wengine na hata madreva.

Sura hazikuwa na utani hazikuwa na masikhara hata kidogo, sura ziliongea kile kilicho ndani ya mioyo yao, wanaume walikuwa wameweka sura katika hali ambayo mtu yoyote aliye katika michezo ya giza michezo katili ya kupoteza roho ya mtu mwingine kana kwamba umemkanyaga sisimizi hili kulinda maslahi ya nchi yako maslahi ya roho yako na hata mwili wako usikutwe na dhahama ya kuharibu kiungo chako.

   “Mko chini ya ulinzi wetu kuanzia dakika hii na hamuhitajiwi kufanya ujanja wowote kwa kudhani pengine mimi niliyewaelekezea tundu la bastola huku vidole vyangu vikiwa kwenye kifyatulio nitaogopa kuruhusu kilimi kishushe risasi kwa ajili ya matumizi yake… Miller usinizibe watu wasiione hii bastola tayari jiji hili watu washazoea mambo haya, kodisha taxi tuondoke nao” Akaongea S.A Silla na papo hapo Miller hakuzubaa kama alivyoelekezwa akasogea katika taxi ambayo kulikuwa na dreva ndani yake akisoma gazeti kana kwamba haihitaji wateja muda huo wa masaa ya jioni ya magharibi.

Inv. Miller akagonga kioo cha upande ule ule aliokaa msoma gazeti na kumfanya ainue shingo yake haraka sana kana kwamba hakutegemea kama kuna mtu atafanya kilichofanywa bila kujiuliza mara mbili akashusha kioo haraka akitabasamu na kuruhusu uso wake uliozungukwa na masharafa yasiyochanwa hivyo yalikuwa vululu vululu na kumfanya uso wake kuonekana kisiwa kilichozungukwa na maji.

   “Habari yako?” Investigator Miller akawai kumsalimia kwa lugha ya kiingereza hili asije akaongeleshwa kwa lugha zoeleka katika Guatemala kugha ya kilatin.

   “Yeeeh… Safi kabisa!” Akajibu kwa kubabaika sababu hakuwa vizuri kwenye kuongea lugha aliyosalimiwa nayo.

   “Sogeza  gari pale walipo watu watatu na usihoji sana juu ya wale walionyanyua mikono juu, wee jail pesa yako” Akaongea Miller na tayari alishazunguka upande wa pili akawa ameshafungua mlango na kuzama ndani ya gari husika.

Dreva wasiwasi ulimkumba lakini hali ya kuona walionyosha mikono juu huku mtu mwingine amewaonyoshea bastola ilimfanya awe katika hali hii pia alimuhofu huyu mtu aliyezunguka kwa kasi kubwa upande wa pili, aliwasha gari na akaelekeza kasi alipoambiwa.

   “Geukeni nyuma haraka!” Akaamrisha S.A Silla na jamaa wakazunguka kama walivyoelekezwa hapo Silla na Miller aliye ndani ya gari waliongea kwa ishara hali iliyofanya Miller atoe bastola yake toka mahala salama anapohifadhi bastola yake na haraka akafyatua kilimi kuruhusu risasi ikae mkao wa kula ikiwa kawelekezea mateka wao waliokuwa wamepewa amri wageukie ilipo gari lakini hawakuwa wamepewa amri ya kunyanyua miguu yao ifanye mjongeo wowote.

S.A Silla alichukua fursa hii kurudisha bastola yake aina ya 357 MAGNUM toleo la Derringer iliyo nyepesi kushikika kiganjani hata kwa mkono mmoja lakini ni bastola inayoruhusu mtumiaji kuitumia kushambulia kwa haraka sana, akasogea walipo mateka wao mikono ikakusanywa akazungusha pingu ya plastiki pingu za kijasusi hizi zikakamata mkono wa kushoto wa jamaa aliye upande wa kulia na mkono wa kulia kwa aliye upande wa kushoto kisha akawasukuma wasogee mbele kidogo akawasachi kwa stahili ya kuwapapasa sehemu zenye mifuko na wote aliwakuta na bastola katika vifuko maalumu vya kuhifadhi bastola ambavyo vilikuwa vimezibwa na makoti yao ya suti walizovaa, Silla akazitwaa zote halafu akawagusa wote kwa pamoja kwa bastola zao ambazo sasa zilikuwa mikononi mwake.

   “Ingieni ndani ya gari upesi kama mmekurupushwa na bomu lililorushwa kuwalipua..!” Akanong’ona karibu ya masikio yao wote wawili na jamaa hawakuwa na hiyana wakasogea kwenye gari taxi huku mlango ukiwa ushafunguliwa na Investigator Miller.

Mateka wakaingia ndani ya gari wakiwa wamejibana sambamba kutokana na pingu plastiki waliyofungwa ikiwa imewabana haswa mikononi.

   “Nje ya mji wa Antigua peleka huko gari kwa kasi ya kawaida ila tuwai kufika huko… “ Dereva akaelekezwa na Special Agent Silla  na akafuata maelekezo kwa kutia gia akazunguka kutoka pale maegeshoni ikiwa watu wachache sana walioona tukio lile na wasiwasi kwao kuwa mkubwa sana pengine hadi dreva mwenzao yupo matatani lakini wengi wao kati ya walioona tukio waliamini polisi wa usalama haswa wa madawa ya kulevya watakuwa wamewakamata wahalifu wa mambo hayo lakini rafiki yao na dreva mwenzao walishindwa kuelewa kwanini kaingia katika tukio waliloliona.

Dreva alikamata barabara ya Chimaltenango Road  ambayo walikwenda nayo mpaka kwenye makutano ya barabara ya Jocotenango Road ambapo walikwenda hadi mji wa Antigua ambako huku walipita barabara hii hii ya Jocotenango iliyokuwa ikipita kando kando ya bahari ya Pacific eneo la mahotel makubwa ya kitalii kama hotel 4A Calle Poniente 9 Antigua na mengineyo ambayo ufanya eneo hili liwe tulivu na la kupendeza sana, walipokuwa wanatoka eneo hili tu Silla akaona mahala hapa patafaa kuachana na dreva huyu wa taxi na taxi yake.

   “Punguza mwendo kisha simama chini ya mti mkubwa pale kwenye muinuko” Akaelekeza Silla huku akiruhusu sekunde chache kutizama nje kisha macho yake kwa kasi yakarudi kuendelea umakini wa kuwalinda mateka wao alionao siti za nyuma.

Dreva alisimamisha gari alipoelekezwa Investigator akampatia pesa walizokubaliana ndiyo zinatosha kutoka Ciudad Vieja mtaa wa Colonia El Panorama mpaka hapa waliposimama karibu na eneo maarufu la Carratera San Felipe a Jocotenango.

Mateka waliamrishwa washuke toka garini na kisha dreva wa Taxi akaruhusiwa aondoke eneo lile kurudi walipotoka.

   “Tuna maongezi na nyie maongezi ambayo kama tutaweza fika pale ambapo sisi mabosi zenu tumeridhika tutawaachia bila kadhia yoyote ile…” Akaongea Silla huku wote wakisogea pembeni kabisa ya barabara kulipita gari kubwa la mizigo lililokuwa likiwapita.

   “Twendeni tukaongelee kwa chini pwani naamini patatufaa kuongea na wenzetu hawa… Mikia si mizuri mmejikuta matatani sababu ya kujifanya nyie manyani wenye mikia” Akaongea Investigator Miller na mara moja hakuna aliyeongeza neon linguine wakaanza kuelekea kwa bondeni wakikatiza barabara hii kubwa mpaka upande wa pili walipoifika barabara ya vumbi la  michanga meupe ya baharini.

Mateka wao walikuwa wapole sana wakiwa hawaonyeshi ubishi wowote ule mpaka wenyewe watekaji kila mmoja bila hata kuongea kumwambia mwenzake anachofikiri ila mawazo ndiyo yaligongana.

Walifika kando ya bahari (pwani) ya Jocotenango Beach iliyopo mji mdogo wa Antigua kati ya miji kadhaa inayounda jiji la Guatemala makao makuu na jiji kuu la biashara nchini Guatemala.

   “Hapa patatufaa bila ya shaka kuongea vizuri na rafiki zetu waliojitoa ufahamu na kuwa mikia.. Rafiki zangu ningeomba wote mngekaa tu chini hapo kwenye mchanga mzuri mweupe usio na siri hata gizani” Akaongea Silla na jamaa wakatii sheria bila shuruti wakatupa matako yao mchangani huku yakisikika mawimbi yanayosukwa sukwa kutoka eneo lake kuja nchi kavu, eneo likiwa kimya kabisa ni mataa tu ya mahotel kadhaa yaliyopo eneo hili ndiyo yaliyokuwa yanatamba kwa uwazi kwa kutokea kwenye majengo mbali mbali ya hotel za kitalii ziliyoko kwenye fukwe hizi.

Mwisho wa sehemu ya arobaini na moja (41)

Wanaume wasiojulikana wakiwa wanawafuatilia kwa stahili waliyoamini hawajastukiwa wanaingia matatani kwa kutekwa kirahisi sana na majasusi wa DEA ndani ya viunga vya Guatemala City.

Wanaume ni kina nani?

Tusipoteze muda wa kuchoshana kwa mengi tusogee sehemu ya arobaini na mbili kwa mengi zaidi.




Dreva alisimamisha gari alipoelekezwa Investigator akampatia pesa walizokubaliana ndiyo zinatosha kutoka Ciudad Vieja mtaa wa Colonia El Panorama mpaka hapa waliposimama karibu na eneo maarufu la Carratera San Felipe a Jocotenango.

Mateka waliamrishwa washuke toka garini na kisha dreva wa Taxi akaruhusiwa aondoke eneo lile kurudi walipotoka.

   “Tuna maongezi na nyie maongezi ambayo kama tutaweza fika pale ambapo sisi mabosi zenu tumeridhika tutawaachia bila kadhia yoyote ile…” Akaongea Silla huku wote wakisogea pembeni kabisa ya barabara kulipita gari kubwa la mizigo lililokuwa likiwapita.

   “Twendeni tukaongelee kwa chini pwani naamini patatufaa kuongea na wenzetu hawa… Mikia si mizuri mmejikuta matatani sababu ya kujifanya nyie manyani wenye mikia” Akaongea Investigator Miller na mara moja hakuna aliyeongeza neon linguine wakaanza kuelekea kwa bondeni wakikatiza barabara hii kubwa mpaka upande wa pili walipoifika barabara ya vumbi la  michanga meupe ya baharini.

Mateka wao walikuwa wapole sana wakiwa hawaonyeshi ubishi wowote ule mpaka wenyewe watekaji kila mmoja bila hata kuongea kumwambia mwenzake anachofikiri ila mawazo ndiyo yaligongana.

Walifika kando ya bahari (pwani) ya Jocotenango Beach iliyopo mji mdogo wa Antigua kati ya miji kadhaa inayounda jiji la Guatemala makao makuu na jiji kuu la biashara nchini Guatemala.

   “Hapa patatufaa bila ya shaka kuongea vizuri na rafiki zetu waliojitoa ufahamu na kuwa mikia.. Rafiki zangu ningeomba wote mngekaa tu chini hapo kwenye mchanga mzuri mweupe usio na siri hata gizani” Akaongea Silla na jamaa wakatii sheria bila shuruti wakatupa matako yao mchangani huku yakisikika mawimbi yanayosukwa sukwa kutoka eneo lake kuja nchi kavu, eneo likiwa kimya kabisa ni mataa tu ya mahotel kadhaa yaliyopo eneo hili ndiyo yaliyokuwa yanatamba kwa uwazi kwa kutokea kwenye majengo mbali mbali ya hotel za kitalii ziliyoko kwenye fukwe hizi.

ENDELEA NA DODO LENYE LADHA YA ASALI!

JUMATANO JIONI

GUATEMALA CITY-GUATEMALA

  “Nyinyi ni akina nani? Na kwanini mnatufuatilia?” Akaanza kuhoji Investigator Miller akiwa kasimama kwa mbele ya mateka wao huku pembeni akiwa kasimama Special Agent Silla akitizama huku na huko kucheki usalama wao kwa ujumla na papo hapo akifuatilia kwa umakini kinachoendelea.

  “Mmekosea sisi hatuwafuatilii kwa ubaya.. Kama ingekuwa kwa ubaya msingeona tukiwafuata kama mbuzi anayefuata majani yasiyo na uwezo wa kukimbia” Akajibu aliyevaa suti ya kijivu akiwa anajitahidi kujiweka sawa maumivu ya mkono aliofungwa sambamba na mwenzake yasiwe makali.

   “Siyo kwa ubaya kwani mna undugu na nani kati yetu?” Akauliza Inv. Miller baada ya kutizamana na Silla.

   “Ni agizo toka mamlaka ya juu ya OCLA kuwa tuwafuatilie kila kona mtakayopita hili tujue ukweli wenu juu ya kumuona mtu muhimu Norman… Ni kawaida ya ofisi yetu kumuwekea ulinzi maalumu mtu mnayetaka kuonana naye na udanganyifu ni mwingi sana” Akajibu tena yule mtu macho yake yakiwa yako makini kabisa kuangaliana na Inv. Miller.

Silla na Miller wakaangaliana tena kwa sekunde tano na macho yao yakaongea kitu walichoelewana.

   “Kamanda Muniain… Kamanda Muniain Salivita Muniero ni boss wenu? Nyinyi ni majasusi wa OCLA?” Akauliza maswali mawili ya kufuatana Investigator Miller.

  “Ndiyo wakuu… Sisi tulielekezwa tu na mkuu tuwafuate kila mahala ila msijue kama tunawafuatilia ni kawaida kila anayekuja katika ofisi zetu hata kama watampa boss wetu ushahidi mkubwa namna gani juu yao ni sheria yetu kumjua zaidi kwa usalama wetu maana magenge mengitunayopambana nayo yana mbinu nyingina mengi yanatoka nje ya nchi yetu” Akaeleza tena ambaye yeye ni kama alijitolea kujibu kila kitu wanachoulizwa kwa pamoja.

   “Tulikubaliana na Kamanda Muniain kuwa tutaonana naye mahala atakapo tuelekeza tuelekee kuonana naye muda wa saa mbili usiku na saa mbili ndiyo inakaribia… Tutataka kujiridhisha kwa muyasemayo hili tuwaache, thibitisheni na katika hili hatuna maelekezo mtathibitisha vipi sababu majasusi wote wanajua jinsi ya kuthibitisha juu ya hili”

   “Tunafahamu tuna namna nyingi za kuthibitisha, tuna vitambulisho vyetu na pia mnaweza mpigia kwa simu zetu mkuu wetu kumuuliza juu yetu..!”

   “Naomba vitambulisho vyenu… Na..!” Hakumaliza kuongea alichotaka kuongea alijikuta anageuka upande wa S.A Silla maana simu ya Silla ilikuwa ikiita tokea kwenye mifuko ya suruali ya suti yake nyeusi aliyovaa.

Special Agent Silla akaitoa simu yake aina ya HTC Smartphone mfukoni ikiwa bado inaita akasoma jina kwenye kioo kisha bila kuinua uso wake akaruhusu kupokea.

   “Kamanda Muniain! Habari za muda huu?” Alivyopokea tu akaongea kwa lugha ya kuelewana na huyo mpigaji simu.

   “Nzuri kabisa… Habari za ugeni wenu hapa GTL?” Akahoji wa upande wa pili wa mpigaji wa simu Kamanda Muniain baada ya kujibu salamu aliyopewa.

   “Nzuri pia mpaka sasa tuko kamili mkuu.. Niambie mkuu?”

   “Safi… Na mpaka sasa navyoongea nanyi nimepokea taarifa toka kwa ndugu yenu wamepanda ndege saa kumi na moja kuja GTL akiwa na mwenzake… na pia muda si mrefu nitaonana na Norman maana ndiyo nimefika mahala ambapo ni kati ya sehemu uwa tunakutana…. Niachieni nifanye maongezi naye kisha nitawajulisha wapi mtakuja tuonane kwa maongezi ya wote kwa ujumla..!”

   “Sawa mkuu haina shida upande wetu tunakusikiliza wewe na kufuata muongozo wako tu… Ila kuna tatizo jingine hapa kidogo”

   “Lipi tena hilo?”

   “Kuna watu wanasema uliwapa taarifa watufuatilie nyendo zetu… Ni sahihi?”

   “Mko nao hapo mlipo au ni vipi?”

   “Tupo nao hapa ufukweni mwa bahari eneo ambalo dreva wa taxi aliyetuleta huku alituambia kunaitwa Jocotenango Beach..”

   “Majina yao tafadhali… Au hamjawauliza hivyo?”

   “Nina vitambulisho vyao mkononi hapa…. Mmoja anaitwa Austin Manuel Contreras na mwingine ni Jairo Jimenez Lezcano..”Akajibu huku akisoma majina katika vitambulisho ambavyo Investigator Miller alivipokea toka kwa mateka wao.

   “Ndiyo ni vijana wa OCLA hao ni maalumu kwa ulinzi wa nje wa ofisi yetu… Ni wazembe sana hao imekuwaje mpaka wako chini ya ulinzi wenu?

   “Si wazembe walikuwa wanawafuatilia watu ambao ni kazi yao kuwafuatilia watu wengine… Samahani kwa yote na uzuri hatujawadhuru na hata wao hawajatudhuru pia… Nafikiri sasa tutakuwa nao au kama wakitaka kuachana nasi wakaendelea na mambo yao ni sawa tu” 

   “Samahani niwaombe mimi… Ila eleweni tu ni kwa ajili ya usalama wetu na wala si kosa upande wetu sababu tunachofanya ni kuhakikisha hatutakiwi kutumika vibaya kwa adui zetu wanaotuwinda kila kona”

   “Bila samahani na uhakiki katika kujihakikishia usalama ni jambo la heri sana… Basi tukuache Kamanda hasa na sisi tuombane msamaha hapa kwa yote”

   “Sawa sawa… Nitakupigia baada ya maongezi yetu na Norman maana ndiyo anaingia hapa mahala husika”

Maongezi yao yaliishia hapo upande wa S.A Silla akakata simu na macho yake yakaangaliana na ya ndugu yake katika kazi Investigator Miller.

  *****  *****  *****

JUMATANO USIKU

GUATEMALA CITY-GUATEMALA

   “Tayari taxi tuliyopanda dreva wake ametufikisha eneo la Carratera San Felipe! Tupo karibu na geti kuu la kuingia hotel ya Casa Madelaine” Aliongea kwa simu yake ya mkononi Investigator Joseph January Miller akiwa kakaa kwenye siti ya upande wa kushoto wa dreva wa taxi ambaye yeye alikuwa kwenye siti yake ya dreva upande wa kulia akiendesha kwa maelekezo ya waliomkodisha kuja eneo hili la Carratera San Felipe, eneo lenye hotel kadhaa zenye hadhi ya nyota tano, tatu mpaka mbili.

   “Endeleeni kunyosha kisha mtaiacha bara bara ya Jocotenango na kuingia kushoto hapo mtamwambia dreva akuacheni papo hapo, mkihakikisha ameondoka mtafuata moja kwa moja uelekeo wa barabara unavyoenda mpaka mtaona bango la Filadelifia Coffee Resort & Tours mtafuata mshale unavyoelekeza na kuuona huu mgahawa sisi tupo mgahawa wa juu tutawaona mkitokea sababu eneo lote la chini linamulikwa kwa mwanga mkali wa taa mbalimbali..!” Akajibu aliyekuwa akiongea naye kwa njia ya simu.

Simu ikakatwa dreva akaelekezwa vile ambavyo Investigator Miller alikuwa ameelekezwa kwa njia ya simu na mtu aliyempigia.

Gari aina ya Toyota Cresta Super Lucent ambayo ni taxi ilifunga breki kwenye kona mchepuo ya barabara ya kuu ya Jocotenango ikiiacha na kufuata barabara inayoingia hii barabara waliyojia wao kina Inv. Miller, dreva akalipwa kilichomstahili kwa umbali wa walikotoka hadi hapa kisha wote wawili wakodishaji wakashuka kukiwa ni eneo lenye mwanga hafifu kutokana na kuwa ni usiku pia kuna miti miti mingi iliyopandwa kandokando mwa barabara hivyo taa zilizopo kwenye nyumba za makazi ya watu zilizopo kando kando mwa barabara ya mtaa zilishindwa nguvu ya matawi ya miti na kufanya sehemu zingine kufikiwa na mwanga wa taa kidogo kisha vivuli vya matawi.

Dreva wa taxi alipindua gari na kurejea alipotoka ambako ndipo kilipo kituo chake cha kupaki taxi yake kama ilivyo ada ya kazi hii ya udreva wa taxi lazima muendeshaji awe na kituo maalumu kwa kazi hii.

Wakiongozana kwa pamoja mapacha wa kazi hawa mmoja mzungu na mwingine mweusi wa maji ya kunde (chocolate) walikwenda wakifuata barabara hii ya mtaa lakini yenye ubora wa kiwango cha lami na si lami mchuzi juu kama lami za nchi zingine za kiafrika hasa za mitaani kama huu mtaa, walikwenda karibu na kona inayoingia barabara ingine inayojia huu mtaa wakaliona bango lililoandikwa Filadelifia Coffee Resort & Tour’s.

   “Bango ndiyo hili… Tufuate mshale unapoelekeza” Akaongea Inv. Miller akiangaliana na S.A Silla ambaye hakujibu kitu zaidi ya kuangalia saa yake ya mkononi akasoma muda na kusababisha ambukizo kwa mwenzake kwani naye aliinua mkono wake akatizama saa yake aina ya Rolex zisizo za kawaida saa za kazi za kazi yenye mambo kadhaa ya kusaidia katika ukachero na ushushushu (ujasusi).

Hatua chache mbele walipanda muin uko mkubwa wa barabara walipoumaliza tu wakauona mgahawa walioambiwa hapo wakaongeza umakini kama ilivyo ada ya majasusi walio makini wanapoitwa au kama ni mmoja peke yake anapoitwa mahali na kulifikia eneo husika basi huongeza umakini mkubwa sana katika ulinzi wake binafsi kiakili na kimwili.

Macho ya Investigator Miller yaliinuliwa kuangalia eneo la juu la mgahawa ambako kulikuwa na watu wachache wakipata vinywaji na chakula na mara akainuka mtu mmoja kule kule juu akapunga mkono kisha akavua kofia lake aina ya pama uso wake ukaonekana dhahiri na ndipo Silla na Miller wakatambua wenyeji wao washawaona, Miller akapunga mkono kwa stahili ya zima kaa moja la moto kwa maji.

Wakafuata ngazi wakakanyaga mmoja akitangulia mbele zikawafikisha hadi juu ambapo wakasogea hadi kwenye meza yenye wanaume wawili, waliovaa mavazi yanayotaka kufanana, kitambaa cha shati wote rangi ya nyeusi na suruali zao za kitambaa cha rangi nyeupe na kufanya kama sare, mmoja akiwa ni mtu wa makamo ambaye ndiyo huyu aliyepunga mkono kutoa ishara kwa kina Miller na upande wa pili alikuwa ni kijana wa kumkadiria umri wake anacheza kwenye miaka thelathini kwenda thelathini na moja hivi.

Kijana huyu yeye alivaa kapero ya rangi nyeusi yenye maandishi meupe yaliyolala yakiwa yameandikwa ‘Arrow’ (Mshale) pia kijana huyu alikuwa ni chotara wa kilatini na kiafrika hivyo alionekana kupendeza sana usiku huu jinsi alivyo maridadi.

   “Karibuni wageni..!” Akatoa ukaribisho ambaye ndiye haswa alikuwa akiwajua hawa wageni ni akina nani?

   “Tumeshakaribia mheshimiwa… Habari za kututangulia? kufika hapa kwenye mgahawa mzuri sana” Akajibu na kuuliza S.A Silla kwa niaba ya mwenzake Miller.

  “Viti kwa ajili yenu, karibuni mketi!!” Akawakaribisha mkono wake ukionyesha kwa vitendo wakae kwenye viti vilivyokuwa viwili upande wa pili.

Investigator Miller na Special Agent Silla wakaweka viti vizuri kwa ajili ya wao kukaa kisha wakaweka kitako macho yao yakiwa makini kuangalia huku na huko, shingo zao zikiwasaidia.

  “Norman kijana wangu kutana na Special Agent Fransis Simone Silla na Investigator Joseph January Miller wote wanatokea shirika la Marekani la upambanaji wa madawa ya kulevya ‘DEA’ makao makuu Springfield, Virginia” Akaongea kwa lugha ya kilatini Kamanda Muniain Salivita Muniero huku akimuangalia kijana aliyevaa jeans, fulana ya mikono mirefu yenye kofia lake nyuma kwa shingoni na pia akiwa na kofia aina ya mzula kichwani mkononi mwake alikuwa kashika miwani ya kioo cha rangi nyeusi.

   “Maafisa wa DEA! Huyu ndiye Norman Cabrera ni kachero wa OCLA muaminifu na mwenye kufanya kazi kwa weledi mkubwa sana kiasi ya kwamba ndiyo tegemeo langu kuu hivyo kutaneni na kijana bora na namba moja katika shirika la kupambana na madawa ya kulevya ukanda wa Latin Amerika” Kamanda Muniain akiwa na uso wenye bashasha tele alimtambulisha kijana aliyekutwa naye pale katika meza waliyoizunguka na mara alipomaliza kuongea kijana yule alivua kofia yake ya mzula toka kichwani mwake na kufanya aonekane vizuri usoni kisha akanyoosha mkono wake kusalimiana na maafisa wa ujasusi aliotambulishwa wanatoka DEA.

   “Nimefurahi sana kukutana nanyi maafisa wa DEA toka Marekani… Karibuni sana GTL na mjisikie mko nyumbani na mimi ndiye Norman mliyeambiwa munitafute kwa misaada mingi zaidi ya kikazi…” Akaongea kijana yule tena kwa kiingereza fasaha, uso wake ukiwa umeruhusu kuchanua tabasamu pana, sauti yake ikiwa sauti nzito sana kuliko kati yao wote, sauti ya kiume haswa maana besi lilivuma haswa toka kinywani mwake.

   “Tumefurahi kukutana na detective matata sana na sote kwa pamoja tunaamini tumepata mtu sahihi kwa wakati sahihi” Akaongea Investigator Miller huku akitikisa mkono wa Norman kana kwamba wanapimishana ubavu na ukakamavu wa miili yao.

   “Nilipata taarifa muda wa saa kumi na mbili kwamba nahitajiwa na maafisa wa usalama toka Marekani na mara moja nikataka kuwafahamu kwa undani kwa njia zangu haswa kupitia majina yenu hivyo niliomba msaada kwa watu ninao wajua huko DEA na uzuri wakanihakikishia ni kweli majina yenu ni miongoni mwa maafisa bora na wa juu sana katika Drug Enforcement Administration na pia nikatafuta maafisa wa CIA kutaka kujua juu ya mliyesema ndiye haswa aliyewaagiza mfike OCLA kunitafuta! Agent Kai kwake iliniwia vigumu kupata maelezo ya kuridhisha maana inaonekana rafiki zangu wa CIA walitaka kwanza kujiridhisha kwanini namuulizia lakini mwisho wa siku nilitumiwa uhakika kuwa ni afisa wa CIA lakini hairuhusiwi kujua zaidi ya hilo nikaona nisiendelee sana na lolote zaidi ya kujitokeza toka mafichoni kuja kuwasikiliza mnanihitaji kwa lipi haswa?” Akaeleza kirefu Detective Norman Cabrera kijana wa ki Guatemala mwenye weupe wa kizungu ambao haujakolea kiasi ya kuwa anaonekana ana rangi ya chocolate.

Mwisho wa sehemu ya arobaini na mbili (42)

Majasusi wa DEA wamefanikiwa kukutanishwa na mtu ambaye Agent Kai kutokea ndani ya chumba maalumu kilichopo ndani ya jengo la makamu wa Rais wa Marekani, alifikiri kwa haraka na kuona hili kufika wanapotaka kufika lazima wapiti kwa mtu anayesakwa na yule ambaye akaunti yake ya barua pepe ilitumika kutuma barua pepe kwenye akaunti yake.

Kamanda Muniain anakubali kuwakutanisha na pia kuwaunganisha kiushirikiano kati ya wana usalama wa Marekani na kijana wake Detective Norman Cabrera.

Nini kitafuta?





   “Maafisa wa DEA! Huyu ndiye Norman Cabrera ni kachero wa OCLA muaminifu na mwenye kufanya kazi kwa weledi mkubwa sana kiasi ya kwamba ndiyo tegemeo langu kuu hivyo kutaneni na kijana bora na namba moja katika shirika la kupambana na madawa ya kulevya ukanda wa Latin Amerika” Kamanda Muniain akiwa na uso wenye bashasha tele alimtambulisha kijana aliyekutwa naye pale katika meza waliyoizunguka na mara alipomaliza kuongea kijana yule alivua kofia yake ya mzula toka kichwani mwake na kufanya aonekane vizuri usoni kisha akanyoosha mkono wake kusalimiana na maafisa wa ujasusi aliotambulishwa wanatoka DEA.

   “Nimefurahi sana kukutana nanyi maafisa wa DEA toka Marekani… Karibuni sana GTL na mjisikie mko nyumbani na mimi ndiye Norman mliyeambiwa munitafute kwa misaada mingi zaidi ya kikazi…” Akaongea kijana yule tena kwa kiingereza fasaha, uso wake ukiwa umeruhusu kuchanua tabasamu pana, sauti yake ikiwa sauti nzito sana kuliko kati yao wote, sauti ya kiume haswa maana besi lilivuma haswa toka kinywani mwake.

   “Tumefurahi kukutana na detective matata sana na sote kwa pamoja tunaamini tumepata mtu sahihi kwa wakati sahihi” Akaongea Investigator Miller huku akitikisa mkono wa Norman kana kwamba wanapimishana ubavu na ukakamavu wa miili yao.

   “Nilipata taarifa muda wa saa kumi na mbili kwamba nahitajiwa na maafisa wa usalama toka Marekani na mara moja nikataka kuwafahamu kwa undani kwa njia zangu haswa kupitia majina yenu hivyo niliomba msaada kwa watu ninao wajua huko DEA na uzuri wakanihakikishia ni kweli majina yenu ni miongoni mwa maafisa bora na wa juu sana katika Drug Enforcement Administration na pia nikatafuta maafisa wa CIA kutaka kujua juu ya mliyesema ndiye haswa aliyewaagiza mfike OCLA kunitafuta! Agent Kai kwake iliniwia vigumu kupata maelezo ya kuridhisha maana inaonekana rafiki zangu wa CIA walitaka kwanza kujiridhisha kwanini namuulizia lakini mwisho wa siku nilitumiwa uhakika kuwa ni afisa wa CIA lakini hairuhusiwi kujua zaidi ya hilo nikaona nisiendelee sana na lolote zaidi ya kujitokeza toka mafichoni kuja kuwasikiliza mnanihitaji kwa lipi haswa?” Akaeleza kirefu Detective Norman Cabrera kijana wa ki Guatemala mwenye weupe wa kizungu ambao haujakolea kiasi ya kuwa anaonekana ana rangi ya chocolate.

ENDELEA NA UTAMU WA DODO ASALI!

JUMATANO USIKU

GUATEMALA CITY-GUATEMALA

   “Jambo la heri kutaka kuujua ukweli kwa watu ambao huwafahamu undani wao kama sisi…” Akaongea akitabasamu S.A Silla baada ya Detective Norman kumaliza mpangilio wake wa maneno.

   “Dunia ya kijasusi imejaa majasusi ambao wengi wako kwa maslahi yao binafsi na si nchi wanayoitumikia hivyo unapokuwa unatakiwa na watu walio katika mchezo mmoja kutoka nchi ingine ama shirika linguine kama si kitengo kingine lazima ujiridhishe ukweli ulivyo lasivyo unaingia matatani na mara zote uwa nasema ndivyo majasusi wanavyotakiwa kuwa…!” Akaongea Kamanda Muniain na kusababisha wote waliopo pale kufurahia kwa kicheko cha sauti isiyoenda mbali zaidi ya pale waliopo.

  “Ni vizuri na mko sahihi… Sababu maafisa wa DEA wapo wanaotembea na kufanya wakiwa na kofia za utambulisho pia tupo ambao tunafanya kazi ndani ya kivuli tukiaminishwa na vitambuliusho vyetu kama ilivyo kwa baadhi ya maafisa wengine wa polisi tunaowaita askari kanzu na maafisa wengi wa CIA wanavyofanya kazi kama secret agency… “ Akafafanua S.A Silla baada ya kicheko kukata upande wake.

   “Safi sana nafikiri ni muda wetu wa kuweza kuongea juu ya kazi yetu iliyopo maana mimi binafsi ningependa kujua kwanini majasusi wa Marekani wamehitaji kukutana nami  haswa maana sikuweza kufafanuliwa lile lililowafanya mnitafute kwakuja hapa GTL na kusema mnahitaji kuonana na Norman!” Akaongea Norman Cabrera na kurudisha umakini kati yao.

   “Ndiyo ndiyo… Nimetimiza wajibu wangu kama bosi wa Norman kwa kuwakutanisha na sasa mnaweza kuongea naye nini haswa lililowafanya muwe na hitaji la kukutana naye na huku mimi nikiwa msikilizaji tu” Kamanda Muniain akaweka msisitizo wake akijiweka vizuri kitini macho yake yakibwenza bwenza na hili liliwafanya hata hawa wageni kujua ni kawaida iliyopo katika kope za macho ya mkurugenzi huyu wa OCLA.

  “Ahsanteni sana kwa heshima ya pamoja mliotupa.. Cha muhimu ambacho sisi tunachoweza kukisema kwa muda huu ni kuomba ruhusa yako Norman kuwemo katika misheni yetu ambayo kimsingi imetutoa Marekani mpaka tukiwa na muunganiko wa majasusi wa DEA ambao ni mimi na mwenzangu hapa tukishirikiana na majasusi wawili wa CIA ambao wao ndiyo walioibua suala hili”Akaanza kuongea Investigator Miller kisha akapumzika kwa kunywa bia aipendayo ambayo hapa katika mgahawa huu ulio kando ya mji wa Antigua ulioko Guatemala City aliweza kuzipata bia azitakazo zitokazo huko kwao Marekani, kisha akaendelea.

  “Mratibu wa misheni hii iliyotuleta hapa na kiongozi wetu kwa ujumla ni Agent Kai, muda wa dakika ishirini zilizopita alitutumia meseji kwa njia ya whatssap kuwa wanakaribia kutua uwanja wa ndege wa La Aurora International Airport hivyo kwakuwa amesema yeye akifika hakuna kupumzika nafikiri tumpe nafasi kuu ya yeye kuja kueleza kwa ufasaha kusudio la kutukutanisha sisi na nyie… Kwa muda wote huu uliopita toka anatutaarifu naamini hakutakuwa na ucheleweshaji wowote wa muda kati yetu… Tuvute subira sababu subira mara zote ndiyo jambo muhimu na la kheri katika shughuli zetu za kijasusi”

   “Ila ni muhimu tukakugusia jambo lenyewe sababu umesema mkuu wako hajakugusia la zaidi ya kukwambia sisi majasusi wa kimarekani tunahitaji kuonana na wewe… Ni hivi! Miaka saba iliyopita maafisa watatu wa Drug Enforcement Administration walipotea katika mazingira yaliyothibitishwa wametekwa nyara na watu wasiojulikana eneo maarufu kwa watu kuangalia mubashara michezo mbalimbali kupitia televisheni huku wakipata vinywaji katika mji wa Springfield, Virginia eneo hilo linaitwa Springfield Hard Times Café & Cue walitekewa kwenye maegesho tena kila mmoja akiwa ndani ya gari yake kwakuwa wote walifika pale wakiwa kwenye magari yao kuangalia mechi ya watani wa jadi Liverpool na Manchester United za Uingereza katika ligi yao maarufu kama English Premier League ‘EPL’… Baada ya kutekwa watu wale na sisi watu wa DEA kupata taarifa haraka sana tulifika eneo la utekaji sababu mimi mwenyewe nilikuwepo kipindi icho na kuchaguliwa na mkuu wangu wa kazi kuongozana na wenzangu wengine saba, tulifika pale na kuanza uchunguzi wa tukio lilivyokuwa tuligundua baadhi ya vitu kwa msaada wa CCTV Camera lakini tulikuja kukwama kwa kushindwa kuwajua wahusika haswa ni hakina nani wa tukio…!” Aliamua kuweka ufafanuzi Special Agent Silla kwa kuanza na maelezo marefu kidogo kisha akanyamaza kwa kunywa funda kadhaa za bia anayokunywa ambayo ilikuwa kwenye glasi kisha akajilamba papi (lips) za mdomo wake akawaangalia waliokuwa wakimtizama kwa umakini akajikohoza kidogo na kuendelea.

   “Tuliweza kuunganisha matukio kadhaa ya kimapambano na vikundi kadhaa wa kadha vya uuzaji na usambazaji wa madawa ya kulevya vilivyopo Marekani na tukafika kupambana navyo tukiongeza nguvu na silaha nzito hili kuwatisha waweze kuwaachia maafisa wenzetu wa kijasusi lakini tuliishia kusambaratisha vikundi hivyo bila kufanikiwa kuwapata ndugu zetu mpaka pale tulipoamua kuanza upelelezi wa chini chini bila kutumia nguvu zaidi lakini napo ilikatika miaka miwili bila kusikia tetesi zozote juu ya ndugu zetu hao ambao ni Agent Johnson Greg Rautollaye, Agent Telizo Munde na wa mwisho ni Agent Rummenige Brandts.. Tukaona pengine tunaweza kuwa tunatafuta watu ambao walishauliwa na kuzikwa hivyo mkuu wetu wa wakati ule akafunga mafahili… Lakini jumanne ya wiki hii baada ya miaka saba jambo hili liliibuka tena ila safari hii likitokea CIA branch ya ofisi ya makamu wa Rais chini ya mtendaji mkuu wa ofisi ile ndipo mahala hapa palipoweza kutuleta kwa pamoja sisi DEA na CIA maana Agent Kai akiwa katika likizo yake ya fungate aliamua kutotumia akaunti yake ya kimtandao ya barua pepe kwa sababu zake binafsi lakini ilipoisha likizo na kurudi Marekani toka Afrika aliamua kuzipitia sasa barua alizotumiwa ndipo akakutana na barua pepe ya mtu ambaye alitumia akaunti ya mtu mwingine kufikisha ujumbe kwa njia ya mchoro mafumbo kwenye akaunti ya Agent Kai… Ujumbe ule ulio katika mfumo wa fumbo la kuchorwa uliweza kumfanya Agent Kai kugundua mtumaji wa ujumbe ule ni Agent Johnson Greg Rautollaye tena akituma kutokea mnara ambao ulisomeka huko mkoa wa San Marcos eneo la milima ya Tajumulco baada ya yeye kugundua hivyo akapeleka taarifa kwa mkuu wake wa kazi, ndipo mkuu wake wa kazi akasema hawezi kumruhusu kufanya uchunguzi na hata kujaribu kufanya anachohitaji bila kuishirikisha DEA..!” Alinyamaza S.A Silla baada ya simu ya Investigator Miller kuanza kuita akaiinua huku akiwaangalia kwa zamu alionao wamezunguka meza ya vinywaji kwenye viti walivyokaa.

  “…. Ni Agent Kai… Nafikiri ameshaingia mtaani sasa..!”Akaongea Investigator Miller baada ya kuona macho ya kila mmoja yanamuangalia kwa umakini na hakusubiri mwingine yoyote apanue papi zake za mdomo kuongea chochote yeye Silla akasugua kioo cha simu yake ya smartphone kupokea.

   “Naam mtaalamu…!” Akaongea na kusikiliza upande wa pili.

   “Niko San Miguel Duenas Road! Dreva wa taxi niliyokodi amenijuza hivyo na nikajiridhisha yuko sahihi, mko wapi? hili anisogeze karibu”

   “Ongea na Kamanda Muniain hili akupe maelekezo yeye mwenyeji maana ni rahisi zaidi…” Akajibu Investigator Miller kisha kwakuwa Agent Kai aliyekuwa kapiga simu alinyamaza moja kwa moja akajua ombi limepita hivyo akaitoa simu sikioni mwake na kuikabidhi mkononi mwa Kamanda Muniain.

   “Halloo mtaalamu… Muniain hapa..!”

   “Ni furaha kubwa kuongea nawe tena muda huu… Habari za wakati huu mkuu?”

   “Nzuri kijana wangu… Pole na safari ya mawinguni..”

   “Ahsante sana… Nafikiri tutaongea zaidi nikifika hapo.. Naomba dira mkuu..!”

   “Mwambie dreva akulete barabara kuu ya Jocotenango kisha aje akuache eneo la Carratera San Felipe hapo ukishashuka utanipigia nikupe maelekezo ya mwisho… Uliniambia mko wawili na mwanadada ambaye ni msaidizi wako, sasa unasema ukifika unamaanishaje?”

   “Namaanisha niko mwenyewe ninayekuja huko kwa mazungumzo na usihofu juu ya mshirika wangu sababu mimi kuwepo hapo inatosha kumuwakilisha yeye…”

   “Sawa sawa.. Mwambie dreva akimbie maana pana ka umbali huku Jocotenango na hapo mlipo..!”

Simu ilikatwa bila kurudishwa mikononi mwa mwenye simu yake Inv. M iller.

..”Wakati tukimsubiri bwana Kai.. Nafikiri tungeendelea na utangulizi kama ulivyokuwa ukieleza mwanzo Special Agent Silla kabla simu ya Investigator Miller haijapigwa na kutukatizia maelezo mazuri sana..!” Norman Cabrera akaomba Silla aendelee na maelezo yake ya kiufafanuzi aliyokuwa akiyatoa mwanzo.

  “…. Ndiyo ndiyo! Tuliishia pale mtendaji mkuu wa ofisi ya makamu wa Rais wa nchi ambaye mtendaji huyu kimsingi ndiyo mkuu wa kazi wa Agent Kai na maafisa wengine wa usalama wote wanaohudumu kazi katika ofisi ile iwe wa FBI au wa CIA ambao wote wana majukumu yao ya tofauti lakini wote wakiwa katika kuhakikisha Marekani yetu na hata dunia kwa ujumla inakuwa salama kuishi wanadamu na mali zao bila bugudha ya wasiopenda amani na wahalifu wa aina zote… Mtendaji mkuu aliona haiwezekani kwa Agent Kai na wenzake waliopeleka ombi la kuufanya huu uchunguzi wao wenyewe bila kuishirikisha DEA ambayo tayari ilishaanza jambo hilo kabla ya fahili kufungwa baada ya kuona kuna mengine  mengi ya kufanya, lilipoletwa suhala hili kwetu mkurugenzi wetu akaomba nasi tushiriki ndipo tukachaguliwa mimi na Investigator Miller kushirikiana na wao walioomba kuifanya kazi hii ya kutafuta wapi walipo mashushushu wenzetu” Akaeleza kirefu kidogo S.A Silla akapumzika kupisha kama kuna swali.

   “Mimi Norman niliingiaje katika misheni yenu ikiwa hata hamkuwa mmeinua mguu wenu kuja GTL?” Akahoji Detective Norman.

Lakini kabla halijajibiwa swali lake yeye Norman aliona gari mbili zilizoongozana zikipita barabarani yaani nje ya geti kuu la kuingilia kwenye eneo la ndani la mgahawa huu hivyo aliinua mkono wake kidogo kiishara kama si salama na wote wakanyamaza kana kwamba hakuna chochote kinachoendelea maana waliganda vile vile walivyo.

  “Gari mbili aina ya Land Rover Discover 3 zenye mkonga mfupi wa mawasiliano mbele ya gari ambazo hutumiwa na watu wa TRJ… Naomba tuongeze umakini na yoyote aliyepo hapa maana ukiona hivyo tu ujue wanakwenda kufanya jambo sehemu au wanatuzunguka sisi kwa ajili ya lolote lisilo zuri kwetu” Aliongea kwa maneno ya haraka Norman Cabrera huku akizungusha macho kwa watu waliokaa kwenye meza kadhaa zilizopo pale kaunta ya juu ya mgahawa huu.

   “Hapa kuna mtu mmoja yupo meza ya mwisho upande wa kulia yuko peke yake sikumuona wakati akiingia hapa, huyu mtu anaonekana ndiyo katuchoresha… Sasa hapa na hakika walengwa ni sisi… Mkuu tunatakiwa kuondoka haraka kabla hawajavamia TRJ hapa!” Akaongea tena kwa kasi ile ile akitumia lugha ya kilatin ambayo wote waliopo hapa walikuwa wakiijua vizuri katika kuisikia na hata kuongea maana wao kina Norman ndiyo lugha ya taifa lao la Guatemala na upande wa maafisa wa DEA kujifunza lugha ni wajibu wa kila shushushu anapoingia kuanza kazi baada ya mafunzo maana wanaopambana nao kwa asilimia tisini wanatoka inapotumika lugha hiyo ukiacha magenge ya wamarekani ambao ndiyo kiingereza lugha kuu.

  “Huyu kijana ameingia dakika ishirini zilizopita kabla hata simu iliyopigwa na Bwana Kai… Nilimuona na nilimshuku kitu kwakuwa alituangalia kifundi kwa macho ya kazi kisha akaenda kukaa meza ambayo aliweza kutuona vizuri.. “ Akasema Kamanda Muniain huku akimimina kinywaji chake toka kwenye chupa kuja kwenye glasi katika hali ya kuendelea kufanya waonekane bado wako katika mazungumzo ya kawaida tu hawajui chochote na uzuri wanayemuongelea alikuwa mbali hatua zaidi ya thelathini toka meza hii ilipo na hata eneo la chini kwa mbele ya mgahawa hakuwa analiona hivyo hakuziona gari ambazo zilikuwa zinaongelewa na Norman kuwa zimekatiza kwa barabarani.

   “Tuondokeni hapa haraka wakuu…” Akaongea S.A Silla na akainuka kitini kisha akaanza kupiga hatua kwenda kaunta ya juu ambayo ilikuwa ipo karibu na meza aliyo kijana mzungumziwa.

Akauliza gharama za vinywaji kwa kutumia lugha husika ya wa Guatemala tena akiongea kwa sauti hili mtu yule asikie naye aone ishara ambazo alizihitaji toka kwa mtu yule na kweli jamaa hakuweza kukwepa mtego alijifanya anajiweka vizuri huku akikunja shati la mikono mirefu aliyovaa halafu akatega sikio uzuri jambo ambalo kwa Silla lilikuwa la kitoto papo hapo akatoa wallet yake mfukoni na kulipa gharama za vinywaji vyote vilivyopelekwa meza katika meza yake huku jicho lake la kijasusi likiusoma mchezo kwa jamaa akamuona alivyokuwa akiandika meseji kwa haraka sana kupitia simu yake aina LG Smartphone hapo kwa Special Agent Silla ikawa kapata uhakika.

Akatizama walipo wenzakelugha ya ishara za vidole ikafanya kazi kisha akatizama kwa wizi umbali wa kiti alichokaa mtu yule na yeye hatua zilikidhi mahitaji yake papo hapo aligeuka kwa kasi bila kujali watu wachache waliopo pale katika kaunta ya juu, mguu wake wa kulia uliinuka na kumkita kwa nguvu kijana yule katika bega la kushoto na kumfanya arushwe na kiti chake mzima mzima kwenda chini kisha akaburuzika na kiti kile cha plastiki mpaka karibu na kingo ikiwa chupu chupu atoke kutoka juu ya kaunta hii ya juu kwenda chini kabisa huko, manusura yake ilikuwa Silla aliyefanya shambulizi la kumkita alidaka mguu wa kushoto wa mtu yule na kiti ndicho kilichopenya katika uwazi na kikaenda chenyewe chini kikifuatiwa na simu iliyokuwa mkononi mwa kijana yule mshambuliwa.

Hapo S.A Silla kama mbogo mjeruhiwa alimkamata vile vile mguu na kumzungusha kwa nguvu naye akijizungusha kana kwamba wale warusha matufe katika mashindano ya Olimpiki na mengineyo kama ya umoja wa madola mizunguko ya kasi miwili ilifanya baadhi ya viti na meza zilizokuwa karibu kuangushwa na kichwa cha kijana kilichokuwa mhanga wa shambulizi, halafu bila huruma alimuachia mguu na kumfanya afyatuke huku akipiga mayowe mpaka karibu na katikati ya eneo hili akiangusha tena meza ya plastiki aliyoipitia kati ya meza na viti vya plastiki vilivyopangwa hapa.

Kijana kizunguzungu kilichojichanganya na nyota nyota giza na mwanga vilimfanya ajishike machoni damu zikimtoka sehemu mbalimbali za mwili wake na mara aliinuliwa juu na Investigator Miller akiwa kazungukwa na wote waliofika pale, watu wengine walikuwa wanashangaa tu hawaelewi nini kinatokea hapa sehemu maarufu sana kwa watalii kupata huduma za kitalii na hata huduma ambazo zinapatikana katika nchi watokazo kama vyakula,chai, kahawa, juisi na pombe kali.

   “Twendeni tutatumia mlango wa wahudumu kuondoka hapa… !” Akasema Detective Norman na mara ikasikika kelele.

   “Lala chini risasi..!!” Akapaza sauti kwa kiingereza S.A Silla ambaye yeye hakuwa amesogea kwa wakati alipomrusha kijana aliyekuwa akimuadhibu bila huruma.

Wote wakajitupa chini wakimlazimisha na kijana muadhibiwa ainame kwa nguvu chini na risasi zisizo na idadi zikapita na kwenda kuvunja taa kadhaa za ukutani na kufanya eneo la karibu na kaunta kuwa na giza hafifu.

   “Twendeni!” Akaongea tena Silla huku akiwa tayari kashafika akitambaa katika mlango unaotumiwa na wahudumu kuja eneo la kaunta ya juu la mgahawa na bar hii.

Wenzake akiwemo Kamanda Muniain walifuata kwa kasi ile ile wakitambalia matumbo kama nyoka wasije wakaonekana kwa wanaowashambulia kutokea mbele ya mgahawa kwa chini.

Mwisho wa sehemu ya arobaini na tatu (43)

Mapambano ndani ya mgahawa na bar ya Filadelifia Coffee Resort, Restaurant &Tours yameibuka ghafla bila kutarajiwa na walioitana hapa kwa ajili ya kikao cha kutambulishana.

Agent Kai akiwa hajafika eneo hili wenzake wanavamiwa na watu wa genge la TRJ walio nchini Guatemala baada ya mtu aliyekuwa akifuatilia nyendo za mmoja wao kati ya Kamanda Muniain au Detective Norman.

Je nini tukitarajie katika sehemu inayofuata?

Vuta subira sogea sehemu inayofuata kwa usomaji wa dodo lenye ladha ya asali…!



Akatizama walipo wenzakelugha ya ishara za vidole ikafanya kazi kisha akatizama kwa wizi umbali wa kiti alichokaa mtu yule na yeye hatua zilikidhi mahitaji yake papo hapo aligeuka kwa kasi bila kujali watu wachache waliopo pale katika kaunta ya juu, mguu wake wa kulia uliinuka na kumkita kwa nguvu kijana yule katika bega la kushoto na kumfanya arushwe na kiti chake mzima mzima kwenda chini kisha akaburuzika na kiti kile cha plastiki mpaka karibu na kingo ikiwa chupu chupu atoke kutoka juu ya kaunta hii ya juu kwenda chini kabisa huko, manusura yake ilikuwa Silla aliyefanya shambulizi la kumkita alidaka mguu wa kushoto wa mtu yule na kiti ndicho kilichopenya katika uwazi na kikaenda chenyewe chini kikifuatiwa na simu iliyokuwa mkononi mwa kijana yule mshambuliwa.

Hapo S.A Silla kama mbogo mjeruhiwa alimkamata vile vile mguu na kumzungusha kwa nguvu naye akijizungusha kana kwamba wale warusha matufe katika mashindano ya Olimpiki na mengineyo kama ya umoja wa madola mizunguko ya kasi miwili ilifanya baadhi ya viti na meza zilizokuwa karibu kuangushwa na kichwa cha kijana kilichokuwa mhanga wa shambulizi, halafu bila huruma alimuachia mguu na kumfanya afyatuke huku akipiga mayowe mpaka karibu na katikati ya eneo hili akiangusha tena meza ya plastiki aliyoipitia kati ya meza na viti vya plastiki vilivyopangwa hapa.

Kijana kizunguzungu kilichojichanganya na nyota nyota giza na mwanga vilimfanya ajishike machoni damu zikimtoka sehemu mbalimbali za mwili wake na mara aliinuliwa juu na Investigator Miller akiwa kazungukwa na wote waliofika pale, watu wengine walikuwa wanashangaa tu hawaelewi nini kinatokea hapa sehemu maarufu sana kwa watalii kupata huduma za kitalii na hata huduma ambazo zinapatikana katika nchi watokazo kama vyakula,chai, kahawa, juisi na pombe kali.

   “Twendeni tutatumia mlango wa wahudumu kuondoka hapa… !” Akasema Detective Norman na mara ikasikika kelele.

   “Lala chini risasi..!!” Akapaza sauti kwa kiingereza S.A Silla ambaye yeye hakuwa amesogea kwa wakati alipomrusha kijana aliyekuwa akimuadhibu bila huruma.

Wote wakajitupa chini wakimlazimisha na kijana muadhibiwa ainame kwa nguvu chini na risasi zisizo na idadi zikapita na kwenda kuvunja taa kadhaa za ukutani na kufanya eneo la karibu na kaunta kuwa na giza hafifu.

   “Twendeni!” Akaongea tena Silla huku akiwa tayari kashafika akitambaa katika mlango unaotumiwa na wahudumu kuja eneo la kaunta ya juu la mgahawa na bar hii.

Wenzake akiwemo Kamanda Muniain walifuata kwa kasi ile ile wakitambalia matumbo kama nyoka wasije wakaonekana kwa wanaowashambulia kutokea mbele ya mgahawa kwa chini.

ENDELEA NA DODO ASALI!

JUMATANO USIKU

GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Hali ya taharuki iliikumba eneo lote la mgahawa huu maana milio ya risasi haikuwa milio ya bastola ndogo, zilikuwa ni bunduki kubwa za kivita aina ya Norinko QBZ-97 ambazo ndizo silaha aina ya bunduki zinazotumiwa na magenge mengi ya kihalifu toka ukanda wa Amerika Kusini, Kati na Kaskazini sababu ya wepesi wa upatikanaji wake kutoka China zinakotengenezwa.

Ngazi zilizowateremsha Silla na wenzake wakiwa wanamburuta na kijana aliyekula mkong’oto wa kijeshi toka kwa Silla, ziliwafikisha kwenye korido ya flour ya chini ambako kulikuwa na milango miwili ya alluminium na vioo katikati, mmoja ukiwa mbele ambako ndiyo mwisho wa korido huu ulionyesha kwa nje kwa uzuri tu na mwingine ukiwa katikati huu haukuwa ukionyesha kilichomo ndani.

Hapa wote wakainuka kila mmoja akiwa na bastola mkononi mwake na haraka wa mbele ambaye ni S.A Silla alisogea hadi kwenye pembe ya mlango unaoonyesha mandhari ya nje akachungulia apate kuona kwa uzuri kama wanaweza wakatoka bila mushkeri yoyote.

Kulikuwa na mwanga wa taa zikimulika eneo lile la nje kwa uzuri tu ambako kwa haraka aliona watu wakikimbia katika hali ya kuokoa maisha yao na wengi wakitokea upande wa kushoto kuelekea kulia ambapo kwa uzoefu wake ilimjengea picha kipi kitakachojiri, akageuka kuwatizama wenzake ambao wote walikuwa wakimuangalia na hata mahututi wao alikuwa akimtizama damu zikimchuruzika sehemu mbalimbali.

Aliporudisha macho kutizama tena kwa nje na huku mkono wake wa kushoto ambao haukuwa umeshika bastola ukiminya kitasa papo hapo taa zote za eneo hili zilizimika ikimaanisha umeme umekatwa eneo lote la mgahawa.

Hapo S.A Silla hakusubiri alifungua mlango na kuusukuma upande akatoa miwani ya kazi toka mfuko wa shati lililo ndani ya koti la suti aliyovaa akaivaa na kuiruhusu iweze kumsaidia kupambana na giza kwa kubonyeza batani iliyopo pembeni ya kioo cha miwani, kisha akatokeza uso wake na mara watu waliokuwa wakikimbia wakamalizika wakawa hawapiti hapo ikambidi kuongeza umakini na kupata jibu wamechelewa kujiunga nao (kazi ipo).

Macho yakiwa ndani ya miwani yalizunguka kote hakuona dalili kama kuna dalili la mtu kuwa karibu. Kimya kabisa! Ukimya ulioweza kumtisha jasusi fundi kama yeye mwenye uzoefu wa mapambano na magenge mbalimbali ya mihadarati.

Toka mlangoni aliposimama akiwa sambamba na ukuta unaoshika fremu ya mlango kwenda hatua mbili mbele kulikuwa na pipa refu kwenda juu la plastiki ambalo ni maalumu kwa kutupia uchafu mdogo mdogo (dustbin), Silla akili ikafanya kazi inayostahili akanyoosha mkono na kulivuta pipa kwake, alifanikiwa kwakuwa alikuwa na uchafu mzito zaidi ya makaratasi kidogo ya watu waliolia vyakula na tishu kadhaa za kujifutia mikono na midomo kwa walaji.

Alipoweza liweka karibu zaidi akakamata mshikio wake na kujitoa mzima akiliweka kinga kule upande wa kushoto walipokuwa wanatokea wakimbiaji waliokuwa wakijiokoa toka hatarini kwa kuelekea kulia pipa la dustbin likimziba maana aliinama nakuwa saizi sawa na urefu wa pipa, hakuacha miguu yake ionekane na upande wa pili alirudi hadi kwenye kona ya ukuta bila kutokea shambulizi lolote hali ambayo ilimfanya asiamini na huko anapotaka kutokea kwakuwa aliamini atashambuliwa kutokea upande wa alipoweka kinga ya pipa.

Hivyo Silla alisimama kutembea hapo kwenye kona bila kuruhusu mwili wake kutokea upande wa pili hapo akageuza shingo na kuchungulia ndipo vumbi la ukuta wa kona ile liliruka kwa kasi, shambulizi! Risasi za kuongozana zikitokea upande wa pili zilivunja kona ya ukuta saizi ya uso wake na mlio mkubwa wa risasi ulisikika na kumfanya naye kuogopeshwa sana haraka akarudi pale pale na mara ikaisikika milio mingine ya risasi ambayo ilikuwa ikitokea mahali ambapo ndipo hasa alijua ndipo shambulizi litatokea lakini hakuwa ameshambuliwa na milio mitatu tu kufuatana ndiyo iliyosikika, Silla akachungulia aone wapi kuliko shambuliwa macho yake yakielekezwa mlangoni yakakutana na michirizi ya damu.

Haraka S.A Silla akatoa simu yake na kupiga namba za Investigator Miller na ikapokelewa kwa haraka sana.

   “Vipi hapo?” Akaongea kwa pupa Silla huku shingo yake ikizunguka huku na huko asije akashambuliwa au kuingizwa ndani ya mtego wa kuwa mateka.

   “Norman kashambuliwa kwa risasi imempata kwenye mkono alipokuwa anataka kutokeza mlangoni punde aliposikia milio ya risasi akataka aone nini kinaendelea upande wako…” Akajibu kwa haraka Investigator Miller.

   “Aiseeh! Hii nchi sijui vipi yaani milio ya risasi inasikika polisi hawafiki… Kazi sana… Tumezungukwa kote Miller na hapa nilipo kama mtu atatokea kwa upande wa juu ya ukuta nitashambuliwa kwa urahisi nakuomba nilinde sababu siwezi kwenda mbele wala kurudi nilipotoka hivyo wewe kwa kutokea hapo mlangoni angalia pande zote za ukuta unazoziona” Akaongea tena kwa spidi kama hujuavyo wamarekani wanapoamua kuongea haraka kiingereza chao ni kama mtu ana rap.

   “Nimemtaarifu kwa meseji Agent Kai nimempa hali halisi amenijibu ndiyo ameshushwa 

Carratera San Felipe na amesikia milio ya bunduki anakuja kamili kuona anatusaidiaje na sasa atakuwa kashafika eneo hili”

   “Safi sana.. Ila awe makini sana..!” Akaongea na kisha akakata simu na kuirudisha mfuko wa mbele wa suruali yake ya suti aliyovaa, umakini ukiwa A na bastola yake mkononi.

Agent Kai baada ya kushushwa tu kwenye taxi ambayo ilimleta eneo hili la Carratera San Felipe masikio yake yalisikia milio ya bunduki zikifyatua risasi ambao aliweza kujua ni bunduki lakini ikawa ngumu kujua aina yake.

Harufu ya damu ilimjia katika pua yake na mwili wake ukasisimka, ishara ya hatari ikagonga katika kichwa chake na si kama amechanja dawa katika mwili wake kama msomaji unavyoweza kuhisi la hashaa! Ndivyo alivyo anaposogea eneo ambalo aliko salama hali hizi umtokea na utegemea na aina ya hatari hiyo ila hii ya kusikia harufu ya damu uanza popote pale ingawa ipo ishara ingine ambayo yeye hujua ni michale pale inapomtokea hii ni tumbo kumbana katika six packs zake.

Alimuacha dreva aondoke ambaye baada ya abiria wake kumlipa tu hakutaka kusubiri aliondosha gari kasi akiungana na magari mengine yanayotokea upande huu ambayo yalikuwa yakiondoka kwa spidi kukimbia hatari pia wapo waliokuwa wakikimbia kwa miguu.

Agent Kai ‘The Sole Cat’ (TSC) akiwa kavaa kapero kichwani ya rangi nyeusi ikiwa na picha ya paka anatembea, suruali ya jeans ya rangi ya bluu na juu akiwa kavaa sweta la rangi nyekundu likiwa na kofia ya nyuma na kamba zake endapo angehitaji kulibana shingoni kwa uzuri angeweza, aliweka begi dogo alilobeba mgongoni vizuri akilipachika katika mabega yote kwa nyuma kisha akamsimamisha kijana ambaye alikuwa akikimbia kutokea kule iliposikika milio ya risasi lakini cha jabu hajaacha chupa ya bia alikuwa kaishika mkononi anakimbia kwa kasi ya kawaida si kasi ya kishada ama kimbunga (lol).

  “Najua una haraka lakini pia nami na haraka kuwai kutoa msaada mnapotoka kuna mke wangu huko nahitajika nimsaidie..” Akaongea kwa haraka Agent Kai tena bila kusita akitumia kilatin moja kwa moja.

   “Nenda uwai kaka… Acha mi nijiokoe bado napenda kuishi huko ni hatari sana ila kwakuwa ni mkeo huo ni upendo wako na huwezi ruhusu upendo kutoweka kabla ya wakati… TRJ wamevamia huko wanasema kuna watu wanawataka wawe wamekufa au hai” Akaeleza kijana yule huku mguu mmoja akiwa kauweka tayari kwa kuendelea kukimbia lakini wema wake ulikuwa tayari kumsikiliza Kai.

   “Nilitamani kujua TRJ ni nini? Lakini nitajua siku nyingine kwanza uhai wa mke ni muhimu… Nataka uniambie hao watu wanaodhibiti eneo wako wapi na wapi? kama uliwaona!”

   “Wamezunguka eneo lote lakini watu wanaowahitaji inaonekana wanawajua iwe kwa sura au mavazi na wamewadhibiti kwenye kona moja maana niliwasikia wakiwasiliana wenyewe kwa wenyewe kuwa wamewadhibiti wote mahala ambapo hakuna wa kutoka..!”

   “Huku njiani mpaka unafika kwenye geti hawapo?”

   “Kuna wawili wapo kwa kule mbele kwakuwa ndiyo niliyochepukia hao wako kwenye gari zao nafikiri wao ni madreva hivyo nashauri kama unaenda upite hapa kwenye uchochoro lakini pia naamini mkeo atakuwa ameshatoka mule kwakuwa hakuna mwanamke anayezuiliwa kutoka”

   “Mke wangu muhudumu wa katika mgahawa huu sidhani kama ashatoka, acha niende! Ahsante na ufike salama kwako” Agent Kai akamalizia hivyo akampiga kishikaji begani kama kumshuru zaidi.

Alitizama huku na huko kisha akaangalia uchochoro alioelekezwa anaweza kupita akili ikamuelekeza afuate hapo akapiga hatua na kuingia ndani ule uchochoro ukiwa una umezungukwa na miti mirefu huku na huku pamoja wigo haina za michongoma, alipita kwa mwendo wa kawaida lakini umakini ukiwa A, uchochoro ulimpeleka hadi mwisho wake akajikuta amefika mahala ambapo kuna ukuta mrefu unaozunguka eneo ambalo kwa ndani kulikuwa na jengo la ghorofa ambazo kwa kutizama tu akatambua kwa mbele kumejengwa kwa sanaa ya mbao na miti hapo Agent Kai akajua ni mgahawa wa chakula au bar akatizama vizuri pande zote na jibu likaja mahala husika ndiyo hapa na ametokea kwa ubavuni.

Akainama na kusogea pembeni ya mti alioamini anaweza kuona zaidi kwa mbele papo hapo akatoa begi lake mgongoni na kulileta mbele kisha akafungua zipu ya eneo dogo la nyuma ya begi hapo akatoa miwani ya kazi za kazi ikaamishiwa machoni ikinasa vizuri kabisa kisha aka swichi batani ndogo ambayo si rahisi kuiona na kujua kama ni batani ya kufanya mengi katika miwani hii ya kijasusi na hata jeshi la Marekani kwa makomando wa vitengo mbalimbali utumia miwani hii ikiwa na teknolojia ya hali ya juu sana.

Akavuta zipu kubwa ambako huko kuna mambo kadhaa ambayo ukilifungua begi hili dogo kwa haraka huwezi kuona maana utaanza kukutana na vitu vya kawaida kama Ipad, Laptop na chaji zake kisha chaji ya simu, lakini kwake mwenye begi hili alipofungua hapo aliinua laptop akavuta zipu ingine kwa ndani yake akakutana na bastola yake kipenzi aina ya Glock 17 iliyo na urefu wa milimita 9 ambayo ni moja ya bastola bora sana kwa wazee wa kazi za kazi za gizani (majasusi) ni nyepesi na yenye kasi sana katika matumizi yake katika hali yoyote ile.

Akaifunga kiwambo cha kuzuia sauti kisha akarudisha begi lake mgongoni akiwa kalifunga vizuri likatulia, mtaalamu akaanza zile hatua zake zilizomfanya aitwe ‘nyayo za paka’ kwa sababu ya uwezo wa kunyata kama hajaikanyaga ardhi kama ilivyo kwa paka anavyotembea kama hajataka umsikie huwezi kumsikia kwa urahisi utaona kama upepo kapita.

Akiwa kainama akitembea sambamba na vivuli vya miti aliweza kuona mbele kabisa lilipo lango la kuingilia kuna wanaume watatu waliovaa suruali za jeans za kufanana aina mpaka rangi nyeusi kama jeans aliyovaa yeye kampuni ya Levi’s juu wakiwa wamevaa majaketi meusi na vichwani wote wakiwa wamefunga vilemba ambavyo licha ya giza Agent Kai akisaidiwa na miwani aliyovaa aliweza kuona rangi ya vile vilemba kuwa rangi nyekundu, mikononi mwao wote walikuwa wamekamatia bunduki ambayo mtaalamu alipotizama kwa mbali kule kule akagundua ni bunduki zao la uchina aina Norinko QBZ-97.

‘The Sole Cat’ alipiga hatua ndefu toka pale chini ya kivuli akirukia ulipo ukuta kisha akajinyoosha kusimama nao sambamba, alisimama vile sekunde tatu kisha akachungulia kule langoni ambapo sasa aliweza hata kuwasikia wakiongea, mmoja wao aliyejiweka pembeni kidogo alikuwa akiongea kwa simu akitumia lugha yao walatin hawa na mtaalamu ‘TSC’ aliweza kusikia akatega sikio lipokee zaidi kile kinachoongeleka na muongeaji yule licha ya kuwa yeye atoweza sikia upande wa anayeongea naye.

  “Wanasema hawawezi kuwashambulia tu sababu kama mjuavyo na wao ni watu wa kazi kama sisi hivyo haiwezekani unavyotaka bosi..!” Akaongea mtu yule bunduki yake akiwa kaiachia kwa kwapani.

Kikapita kimya akisikiliza mtu yule huku shingo yake ikipeleka kichwa chake huku na huko kama kenge kaibuka toka kichakani akihofia uzima wake eneo alipo.

   “Mkuu wa polisi kama amesema hivyo haina shida itatubidi tusubiri dakika tano kama hamna lolote itabidi tuondoke… Ingekuwa Norman si muhimu sana kwetu tungelipua pote hapa wafie humo humo ndani maana wao kina Gudrado wanataka Muniain auwawe kwa tetesi tulizozipata ameomba msaada DEA kuangamiza mipango yetu ya hapa GTL na hawa wamarekani aliwaita hapa kwa kikao lakini wewe unasema Norman muhimu ana flashdisk muhimu sana tuangamize wengine yeye abaki haiwezekani kwa hilo mkuu sababu wako bega kwa bega humo ndani..!” Akaongea tena akiwa hajui kuna mtu hatua tano toka aliposimama anamsikiliza tena anapata madini muhimu ambayo uwa asahau akishasikia.

Kimya cha sekunde arobaini kikapita eneo lote likiwa kimya kabisa kana kwamba hakuna watu maana kila aliyesimama alisimama eneo lake bila kupiga hatua ni macho tu yaliyokuwa yakisaidizana na shingo zao kupeleka vichwa vyao huku na huko bunduki zikiwa midomo yake imetangulia mbele tayari kumwaga damu na kutoa roho ya mtu kama si kuutia majeraha mwili husika.

  “Sawa sawa… Basi ngoja tujifanye tumeondoka kama muda wa askari kuja umefika.. Mwambie inspekta dakika nane mpaka kumi zinatosha aruhusu askari kuja sisi tutakuwa tayari tumeondoka..” Akaongea mtu yule baada ya maelezo marefu toka upande anaopokea maelekezo kisha akaonekana anaondoa simu yake toka masikioni kwa kushusha mkono wake chini halafu akaonekana akiiweka mfukoni akageuka walipo wenzake ambao mmoja alikuwa kasimama upande wa pili wa geti na mwingine kasimama upande ambao ni karibu na alipo mwenzake na pia ni hatua chache na kona ya mwisho alikojificha ‘TSC’ mwindaji huyu wa hatari.

Mwisho wa sehemu ya arobaini ya nne (44)

Hatari! Moto… Kwenye kona ya mwisho kulia mwa mgahawa wa Filadelifia Coffee Resort Restaurant Bar & Tours, alikuwa amejificha mtu wa hatari akitafuta anachokitafuta kwa hisia kali ikiwa tayari kashasikia taarifa toka ndani ya viunga vya mwili wake na akili zake, taarifa ya kusikia harufu ya damu ambayo ni taarifa ya kuwa kwa mara ingine anaingia katika umwagaji wa damu.

Nini kitatokea? kwa hawa watu waliozunguluka jengo la mgahawa huu wa kitalii eneo hili la pembeni ya mji wa Antigua jijini Guatemala.

Majibu naamini yanakuja na mengi yanayokuja katika sehemu zinazofuata.





  “Wanasema hawawezi kuwashambulia tu sababu kama mjuavyo na wao ni watu wa kazi kama sisi hivyo haiwezekani unavyotaka bosi..!” Akaongea mtu yule bunduki yake akiwa kaiachia kwa kwapani.

Kikapita kimya akisikiliza mtu yule huku shingo yake ikipeleka kichwa chake huku na huko kama kenge kaibuka toka kichakani akihofia uzima wake eneo alipo.

   “Mkuu wa polisi kama amesema hivyo haina shida itatubidi tusubiri dakika tano kama hamna lolote itabidi tuondoke… Ingekuwa Norman si muhimu sana kwetu tungelipua pote hapa wafie humo humo ndani maana wao kina Gudrado wanataka Muniain auwawe kwa tetesi tulizozipata ameomba msaada DEA kuangamiza mipango yetu ya hapa GTL na hawa wamarekani aliwaita hapa kwa kikao lakini wewe unasema Norman muhimu ana flashdisk muhimu sana tuangamize wengine yeye abaki haiwezekani kwa hilo mkuu sababu wako bega kwa bega humo ndani..!” Akaongea tena akiwa hajui kuna mtu hatua tano toka aliposimama anamsikiliza tena anapata madini muhimu ambayo uwa asahau akishasikia.

Kimya cha sekunde arobaini kikapita eneo lote likiwa kimya kabisa kana kwamba hakuna watu maana kila aliyesimama alisimama eneo lake bila kupiga hatua ni macho tu yaliyokuwa yakisaidizana na shingo zao kupeleka vichwa vyao huku na huko bunduki zikiwa midomo yake imetangulia mbele tayari kumwaga damu na kutoa roho ya mtu kama si kuutia majeraha mwili husika.

  “Sawa sawa… Basi ngoja tujifanye tumeondoka kama muda wa askari kuja umefika.. Mwambie inspekta dakika nane mpaka kumi zinatosha aruhusu askari kuja sisi tutakuwa tayari tumeondoka..” Akaongea mtu yule baada ya maelezo marefu toka upande anaopokea maelekezo kisha akaonekana anaondoa simu yake toka masikioni kwa kushusha mkono wake chini halafu akaonekana akiiweka mfukoni akageuka walipo wenzake ambao mmoja alikuwa kasimama upande wa pili wa geti na mwingine kasimama upande ambao ni karibu na alipo mwenzake na pia ni hatua chache na kona ya mwisho alikojificha ‘TSC’ mwindaji huyu wa hatari.

ENDELEA NA DODO ASALI

JUMATANO USIKU

GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Licha ya kibaridi ambalo kwa sweta alilovaa ilikuwa haliwezi kufunika usoni mwake lakini cha ajabu kijasho chembamba, kijasho kilichotoka eneo la paji la uso kilikuwa kinateremka kuja puani. Akatumia kiganja cha mkono wa kulia kufuta jasho lile kwakuwa kwa mahala alipo hakuweza ingiza mkono wake mifuko ya nyuma ya jeans aliyovaa hili atoe kitambaa cha jasho, hapa akili yake ilikuwa ni kutoa roho tu, roho za watu watatu anaowaona kutokea kwenye kona aliyojificha tena wakiwa na umakini wa kuangalia ndani ya geti la kuingia mgahawani.

Unaweza ukasema ni hisia ndizo zilizokuwa zinafanya kazi hapa maana Agent Kai ‘TSC’ macho yake yaliyo ndani ya miwani na hata shingo yake iliyosindikiza kichwa chake kuchungulia alishupaza kuwaangalia kwa umakini bila kuacha watu wale lakini mkono wake wa kushoto mkono wa dhahabu uliojaliwa shabaha na nguvu uliitokeza bastola aliyoikamatia na kumlenga mtu wa kwanza aliyetoka kuongea simu ingawa alikuwa akimtamani ampate mzima, haikuwa hivyo hisia ndizo zilizokuwa zikifanya kazi na kuipeleka akili yake inayosimamia vitendo vya mwili kushindwa kusimamia anachowaza wake alijikuta akifyatua risasi moja kuelekea kichwani kwa mtu yule, risasi iliyoenda kupenya barabara juu ya sikio la mtu yule na kumrusha hadi nyuma ya mwenzake aliye karibu naye ambaye alistuka na kujikuta anageuka nyuma kwa kasi lakini naye alijikuta anapachikwa ndonya ya kama watu wa jamii ya kabila la wagogo waliokuwa wanaendeleza mila ya kujiweka alama katikati ya paji la uso. Njemba hii yenyewe ilichimbwa ndonya ya kutoboa si ile ya kuunguzwa na moto ya juu juu, ndonya yake ilimtoboa na kumtawanya ubongo mpaka kichogoni kukafumuka naye akajikuta anaukwaa mwili unaurusha miguu kuachia roho yake.

Njemba iliyobaki ilihamaki kuona wenzake wakidondoka bila kujua kwanini wanadondoka kwa ghafla ile lakini kabla hajachukua maamuzi yoyote risasi ilitua katika jicho lake kwakuwa alitaka kujitupa chini kukwepa kama ni shambulizi, upande wa ‘TSC’ akili yake ilifikiri anaweza kuwa kakwepa akaongeza risasi ingine iliyokwenda sambamba na utosi wa mtu yule akiwa anadondoka hapo roho ilitoka bila mwili ule kufika vizuri chini maana kichwa kilipasuka kwa risasi zile mbili toka ndani ya Glock-7 Pistol ambayo tulishasoma kuwa aliifunga kibomba kidogo kitaalamu kikiitwa ‘kiwambo cha kuzuia sauti ya bastola inapotumika (sailensa).

Mahala kama hapa kwa ‘TSC’ ni uwa mahala kazi za kazi hakuna kuzubaa alizungusha shingo yake na huko macho yakaona hali ilivyo ni shwari kwake haraka alitoka mahala alipo akatembea hatua za haraka lakini bado usingeweza kusikia kukanyaga kwake hii inaleta maana kuu ya code name yake ‘The Sole Cat’.

Alifika eneo la geti harufu ya damu ilikolea katika pua zake zikiwa ni harufu za damu za marehemu waliolala kwa kulaliana kama magunia ya vitunguu yaliyorundikwa bila mpangilio, marehemu aliowatoa roho kwa kuwashambulia vichwani kwa risasi sehemu ambayo ukiona mtu kashambuliwa na risasi halafu kapona ujue risasi ile imemchuna haijampata barabara, akawatizama katika hali ya uhakiki kama kweli Israel mtoa roho kafanya kazi yake akahakiki kazi ya mkono wake haikuwa na makosa.

Akalitizama geti na kulikuta limefunguliwa nusu na robo yaani kuna upande limetoka kushoto kuja kulia likipita nusu na kusogea karibu na robo ya upande wa kushoto na hapo kwa uzoefu wake akatambua kwanini yule mtu wa mwisho aliyemuua kwanini alikuwa amejisogeza pembeni kabisa ya nguzo iliyoshika papi za geti za chuma.

‘TSC’ akachungulia kwa kutokeza kichwa fremu ya miwani ikatangulia kwenye uwazi ulioachwa kwa geti kwa uelekeo aliokuwa hakuona kiumbe akavusha macho kwa kuangaza zaidi mpaka kwenda juu ya flour ya pili ambako kuna kaunta ya pili ambayo kama angekuja kabla ya tukio na kuwawai kina S.A Silla angewakuta wako kaunta ile ya juu wakipata vinywaji na maongezi, kote kulikuwa giza na hakukuwa kunaonekana kiumbe kinachojongea ikabidi ausogeze uso na kuchungulia pande ambazo hakuwa anaziona huko ndipo alifanikiwa kuona watu wawili karibu na kona ya ukuta wakiwa wamevaa kama aliowatoa roho dakika chache zilizopita wakiwa wamelala usingizi wa milele nyuma tu aliposimama akichungulia ndani.

Miwani iliweza kumsaidia kuona upande mwingine karibu na miti ya mikokono iliyopandwa kwa mstari kupendezesha upande ule sambamba na bustani za maua, chini kukiwa na nyasi nzuri zilizokatwa chini chini kabisa eneo likionekana la kupendeza haswa, hapo aliweza kuona watu watatu wakiwa kwenye mavazi ya suruali ya jeans na jaketi nyeusi kama wale wengine hii ilimjuza Agent Kai kuwa hizi ni sare za wavamizi hawa.

Watu hawa wa upande huu walikuwa wamejificha kila mmoja katika mkokono wake huku wako makini kuangalia eneo ambalo yeye ‘TSC’ hakuwa analiona sababu ni upande mwingine wa ubavuni mwa mgahawa huu, lakini kujificha kwao kwa kule wanakokuvizia jambo ilikuwa wamejificha lakini si wamejificha kwa alipo fundi mwindaji mwenye uwezo mkubwa wa kunyata maana alikuwa anawaona vizuri toka alipo

‘TSC’ akarudisha kichwa alipotoka kisha akanyanyua moja ya bunduki ya marehemu iliyokuwa imelala kwa mgongoni wa maiti, akaifuta damu kwa kuigandamiza kwenye suruali jeans ya yuleyule maiti aliyempiga risasi mbili ikiwemo ya utosini ikafutika vizuri ikiwa tofauti na ilivyokuwa, akaitizama magazine kisha akatikisa kifyatulio  (trigger) kucheki hali yake ikiwa hajaikoki.

Bastola yake ikarudi anapopaita mahala salama nyuma ya kiuno, bunduki aina ya Norinko QBZ-97 ikawa kaikamatia mikono miwili kamba ya kuishikiza ikikaa bega la kulia, hizi bunduki wengi uziweka kwa mkono wa kulia mbele ambao ukamata kifyatulio huku wa kushoto ukiweka sapoti kwenye kitako lakini kwa ‘TSC’ kwake ni tofauti yeye mkono wa kushoto ndiyo utumia kukamata kifyatulio (trigger) na mkono wa kulia uweka sapoti kwenye kitako hapo kwake ndiyo burudani anaweza kuondosha idadi kubwa ya watu akikamata mashine kubwa kama hii Norinko QBZ-97 zao la mchina.

Akasogea kwenye uwazi wa geti kisha akatizama saa yake ya mkononi ambayo ni saa ya kazi kama ilivyo kawaida yake vingi anavyovaa uwa ni kifaa cha kazi za kazi au silaha ikiwa kwa mtu asiyeelewa hawezi juwa kama ni vitu msaada kwake zaidi ya kazi yake anayoijua ilimuonyesha ni saa tatu na dakika tano, ‘TSC’ alisimama sawa sawa na eneo la uwazi wa geti ambapo kama mtu angetokea kwa upande wa kaunta ya juu ya mgahawa angeweza kumuona dhahiri shahiri.

Alianza kuhesabu kwa sauti ya kifuani ‘moja, mbili, tatu’ alipomaliza ‘tatu’ tu alijirusha kwa ndani akijiviringisha kwa kasi kama gurudumu mwendo wa mizunguko mitatu kisha kwa kasi ile ile akafunga breki akaweka goti moja chini katika ardhi iliyosakafiwa vipande vya matofali mchanga na udongo usionekane ndani ya uwa huu wa mbele ya mgahawa.

Norinko QBZ-97 ikatema mlio wake wa kutisha risasi akizivurumisha kwenda upande wa jamaa wawili aliowaona wakilinda upande wa kona ya ukuta, kama kawaida alilenga vichwa jamaa wakirushwa na kujipigiza ukutani na damu zikiweka alama na michirizi ya miruko yake katika ukuta miili iliyokuwa ya binadamu wazima ilidondoka chini kila moja mahala pake ikiwa tayari mtoa roho anatoa roho kikatili maana ni miguu yao tu iliyokuwa ikionekana kuruka ruka kwa mbali kama mgonjwa wa kifafa aliyekumbwa na kifafa chake.

Haraka kama kafunga mota katika mwili wake alijiviringisha tena kwa kasi kana kwamba hana begi mgongoni wala hajakamata bunduki iliyo na magazine iliyoshiba, mviringiko ule ulimpeleka hadi karibu na mahala alipoona hapo ni sahihi kisha akacheza tena kifyatulio cha bunduki akipiga mashambulizi ya risasi za kufuatana kuelekea kule walipo waviziaji wakiwa wao wanaona wamejificha na kuvizia kwenye mlango asitoke mtu.

Milio ya risasi ilisikika ikifuatana na mwanga ukitoka katika mdomo wa bunduki watu watatu waliondoka kwa risasi zile ila mmoja aliwai kuzunguka upande wa pili wa mkokono akiwa amekoswa koswa na risasi za kustukizwa za ‘TSC’.

Kuzunguka kwake kwa haraka kulimfanya asahau kuwa kwanini alijificha mahala alipokuwa kajificha kwani alijianika kwa mtu ambaye wao walikuwa wakimdhibiti asitoke nyuma ya pipa la plastiki, akasahu kama mtu yule alikuwa akisubiri kwa hamu ujio wa kiuokozi toka kwa ‘The Sole Cat’.

Ni kama nyota ya jaha kwake milio ya risasi ilimjuza S.A Silla kuwa kumekucha akili yake yatakiwa kufanya kazi sasa asiogope uoga atupe kule mkombozi kafika na ndiye anayeliza milio ya bunduki.

Jamaa kwa uoga akafyatua risasi ovyo kuelekea hisia zake zilipomtuma ndipo alipo anayewashambulia ikiwa kwa upande wa getini lakini ghafla giza lilitanda machoni mwake akajikuta anarushwa bila kupenda toka ulipo mkokono, risasi ya shingo toka kwenye bastola ya Special Agent Silla ilimkata pumzi akajikuta anakwenda chini akajaribu kuinuka kwa kuinua magoti ayasimamie bunduki yake ikiwa imetoka mikononi na mikono yake yote miwili imekamata ilipozama risasi.

‘TSC’ macho yake yakiwa ndani ya miwani alimuona kwa uzuri jamaa anavyotapatapa kujaribu kuokoa roho yake pale kwenye nyasi, aliiweka vizuri bunduki kisha akamwaga njugu (risasi) kuelekea pale kilipo kiumbe cha mwenye mamlaka yake kwa binadamu, risasi zilimfanya azime ghafla ukawa mwisho wake.

Kabla hajakaa uzuri vikasikika vishindo vya watu wanaokimbia kutokea upande wa kulia wa eneo la jengo la mgahawa, hapo ‘TSC’ hakuhitaji kujiuliza mara mbili anatakiwa kufanya nini? Mzoefu kama yeye aliyepitia kwenye vita na mapambano mbalimbali toka US Navy Seals uwa hakosei sana katika eneo la mapambano aliruka hatua mbili ndefu hatua zisizotoa mlio hadi usawa wa ukuta wa kaunta ya chini ya mgahawa kisha akasimama dede sambamba na dirisha macho yaliyo ndani ya miwani yakiangalia kule aliposikia vishindo vya mbio na kweli sekunde tatu tu mbele walitokea wanaume wawili na walioonekana ni wanawake wawili, mavazi waliyoyavaa yalimjulisha Agent Kai watu hawa ni wale wale.

Walitokea wakiwa katika mbio ni kama wamechanganyikiwa maana walipotokea na kuona miili ya wenzao na madamu katika ukuta walisimama wote kisha wakarudi nyuma kama wanataka kurudi walipotokea halafu wa mbele akasita tena wakarudi kwa pamoja tena upande wa ukuta uliokuwa hatua chache wa mbele akaruka kwenye mti ulio kama mti wa maua maana ulikuwa si mkubwa na una maua ya rangi nyekundu na kijani.

Akaanza kwenda juu wenzake nao wakafanya kama yeye hapo masikio ya kila aliyepo eneo hili la mgahawa vikasikika ving’ora vya magari ya polisi.

‘TSC’ akaona hakuna namna ngoja awapopoe toka juu ya mti huu usio na nguvu lakini umeelekeza matawi yake juu ya ukuta ulizozunguka mgahawa.

Alijitoa usawa na ukuta akakamata bunduki vizuri kisha kilichotokea hapo ni harufu kali ya damu mbichi maana ni kama alikuwa anamwaga maji katika mti ule kumbe anapiga risasi, Norinko QBZ-97 ni bunduki ya hatari sana sekunde chache wake kwa waume wale walikuwa chini ya mti wapo waliofika chini wakiwa tayari maiti na wapo wawili waliofika wakitapatapa kubishana na Israel malaika mtoa roho asitoe kwa nguvu roho zao kwa maumivu makali, sekunde kumi mbele hakuna aliyekuwa mzima.

Taa za magari ya polisi zenye mchanganyiko wa rangi ya bluu na nyekundu zilionakana zikihanikiza kwa barabarani huku ving’ora vikiacha kuhanikiza kwa sauti yake kali hii ilimaanisha maaskari polisi walifika pale lakini hakuna aliyethubutu kusogeza gari karibu.

   “Jeshi la polisi liko nje ya mgahawa huu wa Filadelifia Coffee… Wote mlio ndani ya eneo hili mnaamrishwa kutii sheria kwa kujisalimisha wenyewe mkiwa bila silaha kwa maana mikono yenu ikiwa juu..” Sauti ya lugha ya kilatini itokayo ndani ya spika za matangazo ilisikika eneo lote ikitoa amri.

‘TSC’ hakujali akaweka bunduki vizuri na kusogea kwenye kona upande wa kushoto ya jengo la mgahawa akachungulia ndipo akaiona sura ya S.A Silla akinyata kuja mbele.

   “TSC! Hapa…!” Akaongea kwa sauti aliyohakikisha inamfikia Special Agent Silla.

   “S.A Silla..!” Akajibu Silla na papo hapo Agent Kai akajitokeza kabla hajasogea zaidi wakutane kwa mlangoni akatokea Investigator Miller akitabasamu kwa furaha, nyuma yake wakaongozana wanaume wawili ambao kimtazamo kwa upande wa Agent Kai hakuwa anawajua kwa sura lakini kifikra zake akatambua hawa ni Kamanda Muniain na aliyefuatana naye akiwa kafunga mkono kwa kitambaa kinachoonekana ni leso ni Norman, alikuwa amejeruhiwa na hili kuzuia damu kutoka zaidi alifunga hivi.

  “Vipi ulipotokea kuko safi?” Akauliza ‘TSC’ macho yakizunguka huku na huko kama kibaka aliyeingia sebuleni kwa watu usiku wa manane.

   “Kama kwako safi basi huku naamini kuko safi maana baada ya milio ya risasi zitokazo kwenye bunduki waliokuwa wananizuia walishauriana nikiwasikia kuwa wakimbie haraka maana polisi wanakuja..” Akajibu S.A Silla.

   “Poleni sana na matatizo..” Akawaambia wote kwa ujumla kisha akamkumbatia Silla kumbatio la furaha ya kukutana, akaachana naye akaamia kwa Inv. Miller napo walipoachana akaamia kwa Norman kisha akamalizia kwa Kamanda Muniain.

   “Kamanda Muniain hapa…!” Walipoachiana kamanda Muniain akaongea kumwambia akijitambulisha huku kashikana mikono na ‘TSC’.

   “Ahsante sana Kamanda Muniain…. Agent Kai Hamisi kutoka CIA… Nimefurahi kukutana nawe mzee wangu” Akajibu Agent Kai akiutingisha mkono alioshikana nao Kamanda Muniain.

   “Mi nimefurahi pia… Pia ahsante kwa kutuokoa maana Investigator Miller alisema ukifika hakuna cha kutuzuia kubaki humu ndani wala kudhulika… Nimeamini alichosema…!” Akaongea tena Muniain kisha akageuka upande wa Detective Norman Cabrera.

    “Detective Norman Cabrera… Na Norman mwanangu huyu ndiye aliyesababisha muda huu tuwepo hapa na kufika tu kakutana na changamoto ambazo tunapambana nazo… Ndiye Agent Kai kama alivyojitambulisha yeye mwenyewe..”

   “Nimefurahi sana kukutana nawe kaka… Aisee sifa zako zimetamalaki mpaka zinashangaza maana ni nyingi sana kaka… Karibu GTL” Norman akaongea na mara tangazo la mkuu wa msafara wa maaskari polisi waliofika kwa nje ya mgahawa huko likasikika tena.

   “Twendeni tuondokeni hapa.,.. Tutaongelea sehemu ingine lakini sitapenda hao maaskari kutuona sisi yaani mimi na wenzangu wawili” Akaongea Agent Kai akielekeza jambo baada ya sauti kumaliza kutoa kinachoitwa amri kwa kutokea huko ikipaa kuja kwa ndani kwakuwa inatoka mdomoni mwa muongeaji kuja kwa spika.

   “Sawa… Mimi na Norman tutatoka kuongea nao… Nyinyi bakini kidogo hapa ndani kisha tutawafuata..” Akaelekeza Kamanda Muniain macho yake yakiangalia maiti zilizolala ilipo miti ya mikokono.

Mwisho wa sehemu ya arobaini na tano (45)

Mzee wa kazi za kazi, kazi za giza kama ambavyo majasusi wengi upenda kuita kazi zao kuwa ni kazi za kazi au kazi za giza alifanya linalostahili kufanywa na mtu wa hadhi yake, komandoo mzoefu mwenye ujuzi wa mapigano ya ana kwa ana na kutumia silaha.

Akiwa ndiyo anaingia Guatemala City mji wa Antigua, mji mmojawapo katika ya miji inayounda jiji la Guatemala makao makuu ya serikali ya nchi ya Guatemala, Agent Kai anakaribishwa na mkono wa kutoa roho anafanikiwa kujiongezea idadi ya watu aliowaua kwa mikono yake kwa sababu ya kazi yake.

Mambo mazuri ndiyo yameanza ndani ya Guatemala!

Kwa mengi zaidi!




   “Poleni sana na matatizo..” Akawaambia wote kwa ujumla kisha akamkumbatia Silla kumbatio la furaha ya kukutana, akaachana naye akaamia kwa Inv. Miller napo walipoachana akaamia kwa Norman kisha akamalizia kwa Kamanda Muniain.

   “Kamanda Muniain hapa…!” Walipoachiana kamanda Muniain akaongea kumwambia akijitambulisha huku kashikana mikono na ‘TSC’.

   “Ahsante sana Kamanda Muniain…. Agent Kai Hamisi kutoka CIA… Nimefurahi kukutana nawe mzee wangu” Akajibu Agent Kai akiutingisha mkono alioshikana nao Kamanda Muniain.

   “Mi nimefurahi pia… Pia ahsante kwa kutuokoa maana Investigator Miller alisema ukifika hakuna cha kutuzuia kubaki humu ndani wala kudhulika… Nimeamini alichosema…!” Akaongea tena Muniain kisha akageuka upande wa Detective Norman Cabrera.

    “Detective Norman Cabrera… Na Norman mwanangu huyu ndiye aliyesababisha muda huu tuwepo hapa na kufika tu kakutana na changamoto ambazo tunapambana nazo… Ndiye Agent Kai kama alivyojitambulisha yeye mwenyewe..”

   “Nimefurahi sana kukutana nawe kaka… Aisee sifa zako zimetamalaki mpaka zinashangaza maana ni nyingi sana kaka… Karibu GTL” Norman akaongea na mara tangazo la mkuu wa msafara wa maaskari polisi waliofika kwa nje ya mgahawa huko likasikika tena.

   “Twendeni tuondokeni hapa.,.. Tutaongelea sehemu ingine lakini sitapenda hao maaskari kutuona sisi yaani mimi na wenzangu wawili” Akaongea Agent Kai akielekeza jambo baada ya sauti kumaliza kutoa kinachoitwa amri kwa kutokea huko ikipaa kuja kwa ndani kwakuwa inatoka mdomoni mwa muongeaji kuja kwa spika.

   “Sawa… Mimi na Norman tutatoka kuongea nao… Nyinyi bakini kidogo hapa ndani kisha tutawafuata..” Akaelekeza Kamanda Muniain macho yake yakiangalia maiti zilizolala ilipo miti ya mikokono.

ENDELEA NA DODO ASALI!!

ALHAMISI ASUBUHI

PETATLAN, GUERRERO-MEXICO

Soledad De Maciel eneo linapopatikana kasri la ‘Secreto Potentia La Feca Palacio’ (Nguvu ya siri kasri la Feca) ni miaka ilipita likiwa ni kasri la starehe kwa wafuasi wa ‘THE RED JAGUAR’ kwakuwa palikuwa ni mahali pa sherehe zao walizokuwa wakizifanya kwa mualiko wa bosi wao mkuu ‘Kingpin’ Fernandes Carlos Codrado ‘Feca’ mmiliki wa kasri hili linaloitwa ni kasri lenye nguvu ya siri ambayo ni wao ndiyo wenye kujua ni siri gani iliyopo hapa ambayo nilidokeza mwanzoni wakati nalielezea hili kasri lililopo manispaa ya Petatlan jimbo la Guerrero nchini Mexico.

Asubuhi ya siku ya alhamisi saa tatu katika chumba cha mikutano kilichopo katika flour ya chini ambako ndiko ofisi ya mipango yote ya bwana mkubwa Kingpin Feca upanga akiwa na wataalamu wake wa kumsaidia mipango yake ya kibiashara ziwe haramu au zile za kutakatisha pesa zake anazozipata kwa njia haramu ya ulanguzi wa madawa ya kulevya, kikao cha dharura kiliitishwa hapa baada ya habari isiyo nzuri kwao toka mahala ambapo kwao ‘TRJ’ ni ndiyo moyo wa biashara yao ya mihadarati ni mahali ambapo uzalishaji na uhifadhi wa mizigo ufanyika hapo ikisemekana wanakula na watu wa serikali hili kurahisisha mambo yao hivyo ni kama walikuwa hawaingiliwi wakiachwa kufanya yao bila kikwazo na hata kupewa ulinzi wa siri na baadhi ya watu walio serikalini kana kwamba hawafanyi mambo yanayopingwa na jumuiya zote serikali za kidunia.

   “Nimewaita hapa asubuhi hii ni kwa sababu ya matukio yaliyotokea jana huko Antigua Guatemala.. Nimeshtushwa sana na tukio la watu wetu kumi na tatu kuuwawa kiwepesi bila ya wao kufanikisha kumuondoa hata mtu mmoja kati ya watu ambao kwa maelezo ya Marianna waliwafuata katika mgahawa ule kwa ajili ya kumtia mikono Detective Norman Cabrera… Maelezo yanasema Norman toka apewe flashdisk iliyoandaliwa na mkurugenzi wa taasisi ya kupambana na rushwa wa nchini Guatemala mwezi mmoja uliopita amekuwa mtu wa kujificha sana mpaka ikabidi Mariana amuue mkurugenzi yule kwa usaliti aliofanya maana na yeye ni mmoja wa watu walio katika malipo yetu nchini Guatemala… Kabla hajauliwa alijitetea flashdisk aliiandaa ikiwa haihusiani na mtandao wetu wa wanaotusaidia katika biashara yetu nchini mwao kama mlivyosikia kipindi kile lakini bado haijulikani katika flash ile kuna nini zaidi? …. Marianna aliona hakuna haja ya kuendelea kuamini anayosema mkurugenzi ndipo akamuua ila bado tunaitaka flashdisk ile sababu kama itakuwa imewekwa mambo ambayo tunayahisi yamo… Kazi itakuwa ngumu na imenistua kwa kweli sababu siamini katika OCLA kuwa wanaweza kufanya mauaji haya bila msaada toka kwa watu ambao hawajui cheni yetu iliyopita ndani ya OCLA na serikali zote zinazounda ushirika wa OCLA na pia DTO ya hapa Mexico!”Alianza kuongea hivi kirefu ‘Kingpin Feca’ baada ya idadi ya aliowahitaji kufika asubuhi kwa maongezi na kisha maelekezo kuenea ikapita salamu yao ya genge lao la ‘TRJ’kisha maongezi yakaanza kama hivi yakianzishwa na boss mwenyewe, alipumzika kupitisha mate kooni akawaangalia kwa zamu walikokuwa mbele yake kisha akaendelea.

   “Mtu wetu anayeitwa Gaudiano Soria ambaye kwa maelezo ya Mariana aliyonipatia ni kijana anayemudu kumfuatilia mtu kwa ufundi mkubwa ni moja ya vijana ambao hawakutokea la hormiga, huyu aliletwa na Koplo Savatel toka jeshi la Cuba ni jasusi wa kijeshi… Yeye alipewa kazi ya kumfuatilia Kamanda Muniain wiki sasa hili kama atakutana na Norman popote pale amjulishe haraka sana Marianna… Ndani ya wiki hii katika mara zote alizokuwa akimfuatilia kifundi akikwepa hadi watu wanaomlinda kwa siri Kamanda, aliweza kugundua uwa anakutana na watu mbalimbali baada ya muda wa kazi ila si wa aina moja wanabadilika badilika jinsia, umri na hata maeneo anayokutana nao lakini siku ya jana akiwa kamfuatilia hadi mgahawa lilipotokea tukio la mauaji aliweza kumuona kijana aliyekutana naye kuwa ni Norman akiwa kajificha sura kwa kuvaa kofia aina ya kapero iliyokandamizwa sana kuficha sura… Ndipo Gaudiano akatuma meseji kwa Mariana kumjulisha… Na Mariana akatuma vijana kumi na tano kwenda huko kwa ajili ya kuwatia nguvuni wote Norman na boss wake na bahati mbaya yakatokea ya kutokea ikiwa kwa mara ya mwisho Mariana aliwasiliana na Maquez Molito kiongozi aliyeongoza msafara wa kwenda huko akaambiwa jinsi ya ugumu wa kazi ulivyo na kwakuwa kazi uwa tunafanya kwa mawasiliano na polisi wafanye kuchelewa kufika muda wa kufika polisi ulitimia ikabidi Marianna awaambie watoke pale wakatege njiani na kwa mujibu wa Maquez hawakuwepo Norman na Kamanda Muniain peke yao, walikuwepo na wanaume wengine wawili wakati wanawavamia mmoja mzungu na mwingine mwenye asili ya Afrika…!” Maelezo marefu yalitoka kinywani kwa boss Feca kisha akanyamaza na kunyanyua chupa ya kahawa akamimina kwenye kikombe kidogo cha kunywea kahawa yote akaibugia mdomoni akishusha kikombe kikiwa cheupe.

   “Nimewaita hapa tuliangalie hili suhala kwa umakini na mapana kisha nitoe amri nini kifanyike huko Guatemala sababu kama mjuavyo moyo wetu upo kule, tumeweza kuwadhibiti kwa asilimia sitini maafisa wa serikali na vingozi wao wakuu wa kiserikali… Guatemala imetufanya tutanue biashara yetu bila nongwa kabisa, imefanya tujenge kiwanda cha siri katika Tajumulco tukisaga mihadarati kwa amani na kutufanya kuwa genge lenye pesa ambazo zinaweza simamia bajeti ya miaka minne ya nchi kama hii ya Mexico… Watu wachache wasio upande wetu huko Guatemala miongoni mwao ni Rais wa nchi lakini naye tumemzungushia watu wanaotusikiliza na kutuacha tufanye tunalojisikia kwa hili lazima tujivunie na tulinde maslahi yetu… Tumejaribu njia kadhaa kumuondoa Muniain sababu ya ubishi wake wa kukataa kutusikiliza lakini Waziri wa Usalama amekuwa akimlinda kwa kusema tukimuua itamuuma Rais wa nchi sababu ni ndugu yakehivyo anaweza omba msaada nje wa upelelezi juu ya kifo chake na hivyo kuwakaribisha watu kama wamarekani na vyombo vyao bora vya kiuchunguzi na hili linaweza kuwaharibia wao… Nahitaji maoni yenu ndugu zangu na kisha ya hapo nitaomba miongoni mwenu watatu au hata wanne mtaelekea  huko Guatemala” Alingea tena Feca na kusimama hapo akitaraji sasa kuwasikiliza waliokuwa wakimsikiliza.

   “Cha kwanza upande wangu ningeomba tujue ni kina nani waliokuwa na kina Kamanda Muniain maana kwa maelezo niliyoyasikia hapa si watu wanaojulikana kwa jasusi wetu aliyekuwa akifuatilia nyendo za Kamanda… Aliye pembeni ya boss Feca aliongea huyu alikuwa ni Koplo Maxiwell Zuantejo.

   “Mimi upande wangu katika maelezo haya niliyoyasikia toka kwako mkuu ni watu kumi na tano waliagizwa kwenda pale mgahawani na waliouliwa ni kumi na tatu. Je wawili walirudi kambini? Na vipi kuhusu aliyekuwa anamfuatilia Kamanda Muniain muda wote mpaka kufika mgahawani?” Huyu aliyehoji alikuwa ni Aristos Mosquera mmoja wa makamanda wa juu wa genge la ‘TRJ’.

   “Wawili walirudi… Hawa ni madreva sababu kama mjuavyo tunafanya kazi kama timu hivyo wao walibaki kwenye magari kama kawaida ila sasa nilipohoji juu ya mcuba nilijibiwa hajulikani alipo” Akajibu Feca akijifikicha macho kwa vidole vyote vya mikono yake yote miwili.

   “Inatubidi tupate taarifa kamili kutoka kwa maafisa wa polisi ambao ni waaminifu kwetu… Ushauri wangu wa kwanza ningependa iwe hivyo maana kama mcuba atakuwa ametekwa na watu hao polisi watatujuza na kama yuko mikononi mwa polisi pia watatujuza ndipo tutajua tunafanyaje kuliko tukawa tunajadili juu ya watu waliokufa wakati yupo ambaye anaweza akawa msaada kwetu na hata pia msaada kwa adui zetu kujua mambo ambayo pengine anayajua..!”Aristos Mosquera akafafanua kwanini ametaka kujua juu ya mcuba.

   “Sikufikiria hilo… Nilihisi pengine atakuwa amerudi kwa Mariana… Na sijui kwanini Mariana hajaniambia juu ya hili, ngoja nimpigie sote tujue kabla hamjaondoka..!!” Akaongea Feca kisha akainua simu yake iliyokuwa mezani ambayo alikuwa kaweka vitanga vyake vya mikono kuiegemeza pale anapoiunamisha mwili wake kwa mbele akiacha mgongo wa kiti cha kistarehe alichokaa.

Alipopiga tu akaipata laini hewani na simu ikaanza kuita upande aliopiga miito kama mimtano ikapokelewa.

   “Halloo..!”Akaongea baada tu ya upande wa Marianna kupokea simu.

   “Mkuu nakusikia..!”

   “Nataka kujua juu ya kijana aliyekuwa anamfuatilia Kamanda Muniain… Maana nakumbuka wakati unanijuza hukuniambia lolote juu yake kama alirudi kwako au yuko wapi?”

   “Nilighafirika sana muda ule! Nisamehe boss! wakati nimekupigia kukupa taarifa pia sikuwa na habari za uhakika juu yake ni Gadiano Soria …!”

   “Je muda huu unazo habari zake za uhakika?”

   “Ndiyo mkuu! Yupo mikononi mwa Norman na watu wake… Inatia hasira sana..”

   “Lazima itie hasira kwakuwa ni uzembe mmefanya wewe na kina alto, haiwezekani operesheni ya kuipata flashdisk ambayo tunahisi ina mambo yatakayoharibu mipango yetu hapo GTL mnaichukulia kiwepesi sana… Hamjapanga safu vizuri ni hatari sana… Sasa naongeza nguvu ya watu wa huku watakuja huko baadhi, nitampigia alto huko alipo Canada kumueleza na yeye masikitiko yangu na wenzangu wote wa huku makao makuu..”

   “Sawa mkuu! Nakubaliana na wewe ni uzembe mkubwa lakini lazima huelewe Norman ametuzidi ujanja kwenye hili suala yuko mbele zaidi yetu katika kujificha na mambo mengine lakini si moja kwa moja, mkono wetu ni mkubwa sana hawezi kwenda mbali zaidi..!”

   “Haya nigusie mmejipanga vipi?”

   “Tumejipanga kwanza kufuatilia nyendo za Muniain siku ya leo kama kawaida ikibidi hata kuiteka familia yake hili aweze kutusaidia maana kikawaida amekuwa kiburi hadi kwa mawaziri ambao tumewaomba mara kadhaa kutusaidia juu yake”

   “Masaa mawili yajayo watakuja huko Aristos Mosquera, mtu mzito Koplo Maxiwell Zuantejo na Molina Qadrado kuongeza nguvu katika operesheni hii… Nahitaji siku ya kesho jioni Norman na flashdisk au flashdisk peke bila Norman” Akamalizia Brigedia wa zamani Fernandes Carlos Codrado na kukata simu.

   “Kama mlivyosikia kijana wa kicuba hajauwawa… Ni kosa kubwa la kiufundi kuacha mtu ambaye alikuwa anatumika katika masuala yetu ya kijasusi kutekwa na watu wa OCLA ambao hawako upande wetu wanapigana kuangamiza biashara zetu” Akaongea baada ya kuisogeza simu mahala alipoiweka mwanzo.

   “Nafikiri mkuu tusipoteze muda… Acha sisi tukaungane na kina Marianna huko GTL, tukafukue kote kuhakikisha tunampata huyo Norman na Flashdisk au Flashdisk yenyewe..” Koplo Maxiwell Zuantejo akaongea baada ya kutizama saa punde mkuu wake aliponyamaza.

   “Sawa haina shida.. Haina maana kuendelea na mipango huku wakati wako watu huko na ni wazoefu kama sisi huku ni uzembe na dharau tu ndizo zilizowaharibia… Mtu mmoja anatusumbua kwa muda mrefu toka apewe hiyo flashdisk ni miezi miwili inakaribia”.

Walimaliza kikao chao cha dharura kilichoitishwa na boss wao mkuu ‘THE RED JAGUAR’ (TRJ) katika kasri lake la ‘Secreto Potentia La Feca Palacio’ (Nguvu ya siri kasri la Feca).

   *****  *****  *****

ALHAMISI ASUBUHI

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Simu ya kiganjani aina ya iPhone8 kutoka kampuni ya Apple iliyokuwa ikiita ikiwa pembeni ya mto uliolaliwa na Agent Kai katika chumba namba thelathini na mbili flour (losheni) ya nne katika hotel ya nyota tatu inayoitwa El Convento Boutique Hotel iliyopo mtaa wa 5A Avenida karibu na kota za serikali zilizopo eneo Sacatepequez Department, mtaa huu ukiwa kwa juu ya muinuko na mitaa ya kota ikiwa kwa chini hivyo ukiwa upo kwenye hotel hii unayaona maeneo ya kota kwa chini tena mandhari yake ikiwa ya kuvutia sana (kijani kibichi cha miti na misitu ya kimjini mjini).

Haraka Agent Kai ‘The Sole Cat’ alifumbua macho kwakuwa wakati inaanza kuita tayari akili yake ilishakuwa imehama toka kwenye dimbwi la usingizi kuja katika uhai uliokamilika kama hujuavyo usingizi ni nusu ya kifo, shida iliyokuwepo alikuwa bado anautaka utamu wa kuwa katika usingizi hivyo macho yake alikuwa kayafunga na kalala kifudifudi akiwa kajifunika shuka gubigubi mpaka kichwani kama pipi iliyo ndani ya ganda lake ikiwa ni katika kujizuia na hali hewa ya ubaridi.

   “Lizy..” Akaita baada ya kupokea akiwa kaiweka simu sikio analopenda kusikilizia simu sikio la kushoto kwake.

   “Ulikuwa bado umelala? Pole sana”

   “Ahsante sana… Jana nilikuwa na maongezi na wenzangu marefu sana halafu pia tulikuwa na mteja wa mbolea mbishi sana alikataa kununua mbolea yetu licha ya yeye mwenyewe kuja dukani kwetu… Leo nimepanga atanunua mbolea iwe isiwe lasivyo arudishe namba”Akajibu Agent Kai kisha akataka kujua ni saa ngapi mpaka anashutumiwa kalala sana, akageuza shingo hadi pembeni ya kitanda upande aliolaza kichwa kulikuwa na kameza kadogo kalichobebana na dressing table juu yake kulikuwa na saa ndogo ya mezani akasoma saa na kugundua ni kweli amelala sana maana ilikuwa imetimia saa tatu kasoro dakika tano tu asubuhi hii.

   “Pole sana ndugu yangu… Nimeongea na RS dakika kumi zilizopita anasema mliachana kwa kushuka kila mmoja kivyake baada ya kutoka ndani ya ndege na hamkuonana tena”

   “Ndiyo… Kwa usalama wa mizigo yetu ya mbolea tuliona tufanye hivyo”

   “Kwahiyo unaposema ulikuwa na maongezi..yeye hakuwepo?”

   “Nilitaka apumzike kwanza na usijali juu ya hilo sababu nitamjulisha kila kitu mimi mwenyewe… Lete habari za huko?”

   “Habari nzuri… Simu ya mteja mkuu imetumika zaidi ya mara tatu toka jana saa nne mpaka leo asubuhi ya muda si mrefu uliopita nakutumia maongezi kwenye whatssap yako utasikiliza kisha tutajadili kama utahitaji tujadili pamoja nami au kama kuna lingine la zaidi utanijuza nijue..”

   “Sawa tuma… Nikitoka kuoga nitazipitia kabla sijaanza ratiba ya leo”

   “Imeripotiwa mauaji huko GTL, vipi hapo?”

   “kumi na tatu… Makali ya paka yalipita.. Mteja wa mbolea mbishi zao moja”

   “Nilihisi… Sawa nikutakie asubuhi njema, usiache kumpigia mwarabu kumjulia hali kitumbo”

   “Leo uende mtembelea ukae kae kidogo… Kisha utapumzika kesho na kwenda keshokutwa kumuona tena wifi yako na wanangu”

   “Sawa  nitaenda kumtembelea mke mwenzangu, nitafanya kama utakavyo”

   “Wasalimie sana..!”

Waliagana na simu ikakatwa hapo sasa Agent Kai ‘TSC’ akasukuma shuka pembeni na kuinuka kukalia matako akiwa na bukta ya kulalia akatafuta namba ya mke wake na kupiga simu.

   “Mbona usiku hukunipigia? Sijalala vyema mume wangu sababu ya hili” Simu ilipopokelewa tu sauti nyororo inayoongea kwa Kiswahili cha kulazimisha ilisikika, sauti ya mke wa mtaalamu ‘TSC’ mwanadada wa kisyiria Shufania ambaye mara zote akiongea na watoto wa mumewe anapenda kuwaongelesha kwa Kiswahili hili aweze kujifunza zaidi ingawa katika watoto hawa na wao si wazaliwa wa lugha hii kwa mama zao hivyo walikuwa wakiongea sababu baba yao alipenda kuwaongelesha zaidi kwa Kiswahili hili na wao wajue kwa asili ya baba yao nako kuna lugha na ni lugha kubwa na nzuri.

   “Ndiyo salamu hiyo mke wangu?” Akahoji Agent Kai bila kutaka kujibu alichoulizwa na mama kijacho.

   “…Nisamehe mume wangu… Asallaam aleykuum”

   “Waleykuum Sallam! Hayo ndiyo mambo na ndiyo sheria, shurti tusalimiane kwanza hata kama kuna lawama gunia zimekaa kooni wahisi kukereketa zisubirishe kwanza zije baada ya salamu mke wangu kipenzi mwenye ladha ya utamu wa adimu… Vipi hali yako? mama kijacho wangu!!”

   “Tayari naliona jumba liko ndani ya maji kupumua kwa tabu bila uwepo wako laazizi wangu..!”

   “Kazi mke wangu.. Si kama napenda kuwa mbali nawe… Kwa mapenzi yako na uzuri wako wa shani uliotukuka hakuna mwanaume wa kuthubutu wala kudiriki kuacha penzi lako limpite walau kwa siku moja, mtoto wa kiarabu mwenye utamu wa dhabibu mbivu asali nivumilie kama mimi navyojikaza na kuvumilia kisa kazi na si kingine… Amini nakaukiwa na koo na kutamani maji kila nikiivuta sura yako kwenye mboni za macho yangu”

   “Unarudi lini mume wangu kipenzi?”

   “Jana tu nimeondoka… Ukweli sijajua narudi lini ila haifiki wiki nitakuwa nimerudi “

   “Sawa mume wangu… Watoto wameenda shule wote nimepooza nyumbani hapa kuliko kawaida”

   “Kawaida hiyo… Mpigie simu mama Kai hili muongee kuondoa hali ya upweke… Mimi nitakupigia tena usiku acha kwa sasa nifuate ratiba inavyosema. ..Jioni atakuja wifi yako Lizy kukuona, nimemuomba awe anakuja mara kwa mara kukuona wakati wote ambao nitakuwa sipo huko”

   “Sawa mume wangu..,\. Inshaallah! Mungu akutangulie na kukupa ulinzi wake huko ulipo… Muda wote muweke Mungu mbele kisha mengine baadaye, usisahau kila unapotaka kutoka kusoma dua niliyokufundisha”

   “Ahsante sana kwa kunikumbusha, ahsante sana kwa dua zako na swala nyingi juu yangu.. Hakika umeniwekea ulinzi kwa upendo wako… Mkae salama na hakikisha walinzi wote wanafika kwa wakati na wanaofika kushika zamu nao wanafika kwa wakati hilo alisimamie sana wifi yako Ashura..”Alimalizia Agent Kai kisha kila mmoja akamwaga busu zito la baraka kwa ampendaye simu zikakatwa.

Mwisho wa sehemu ya arobaini na sita (46)

Brigedia wa zamani astushwa na habari ya kuwa ‘TRJ’ imepoteza watu wake kumi na tatu, watu waliokula mafunzo ya aina zote kwa ufasaha katika kambi ya siri ya Tajumulco mountain.

Haraka mkuu akaitisha kikao ambacho kilifika muafaka watoke wa tatu kwenda kuongeza nguvu katika kikosi kinachomtafuta Detective Norman ambaye inasemekana alipewa flashdisk yenye siri na mkurugenzi wa kupambana na mihadarati.

Flashdisk ina nini?

Kwa majibu yasiyo na shaka wala kuyumba endelea kufuatilia riwaya hii kali na tamu kama dodo asali.



   “…Nisamehe mume wangu… Asallaam aleykuum”

   “Waleykuum Sallam! Hayo ndiyo mambo na ndiyo sheria, shurti tusalimiane kwanza hata kama kuna lawama gunia zimekaa kooni wahisi kukereketa zisubirishe kwanza zije baada ya salamu mke wangu kipenzi mwenye ladha ya utamu wa adimu… Vipi hali yako? mama kijacho wangu!!”

   “Tayari naliona jumba liko ndani ya maji kupumua kwa tabu bila uwepo wako laazizi wangu..!”

   “Kazi mke wangu.. Si kama napenda kuwa mbali nawe… Kwa mapenzi yako na uzuri wako wa shani uliotukuka hakuna mwanaume wa kuthubutu wala kudiriki kuacha penzi lako limpite walau kwa siku moja, mtoto wa kiarabu mwenye utamu wa dhabibu mbivu asali nivumilie kama mimi navyojikaza na kuvumilia kisa kazi na si kingine… Amini nakaukiwa na koo na kutamani maji kila nikiivuta sura yako kwenye mboni za macho yangu”

   “Unarudi lini mume wangu kipenzi?”

   “Jana tu nimeondoka… Ukweli sijajua narudi lini ila haifiki wiki nitakuwa nimerudi “

   “Sawa mume wangu… Watoto wameenda shule wote nimepooza nyumbani hapa kuliko kawaida”

   “Kawaida hiyo… Mpigie simu mama Kai hili muongee kuondoa hali ya upweke… Mimi nitakupigia tena usiku acha kwa sasa nifuate ratiba inavyosema. ..Jioni atakuja wifi yako Lizy kukuona, nimemuomba awe anakuja mara kwa mara kukuona wakati wote ambao nitakuwa sipo huko”

   “Sawa mume wangu... Inshaallah! Mungu akutangulie na kukupa ulinzi wake huko ulipo… Muda wote muweke Mungu mbele kisha mengine baadaye, usisahau kila unapotaka kutoka kusoma dua niliyokufundisha”

   “Ahsante sana kwa kunikumbusha, ahsante sana kwa dua zako na swala nyingi juu yangu.. Hakika umeniwekea ulinzi kwa upendo wako… Mkae salama na hakikisha walinzi wote wanafika kwa wakati na wanaofika kushika zamu nao wanafika kwa wakati hilo alisimamie sana wifi yako Ashura..”Alimalizia Agent Kai kisha kila mmoja akamwaga busu zito la baraka kwa ampendaye simu zikakatwa.

ENDELEA NA DODO ASALI..!

ALHAMISI, ASUBUHI

ANTIGUA, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Nusu saa mbele yaani ikiwa imetimia saa nne kasoro dakika kumi ‘TSC’ alitoka bafuni sasa akawa anavaa mavazi aliyochagua kuvaa siku hii ya alhamisi, siku ya kwanza inayomkuta kuanzia asubuhi akiwa ndani ya Guatemala City jiji la kibiashara, jiji kuu na makao makuu ya shughuli za kiserikali za nchi ya Guatemala.

Dakika kumi zilimtosha kujiweka katika hali ya utanashati kwa mavazi ya kisasa aliyovaa siku hii ya leo ambayo ratiba yake aliyonayo mbele yake ilimfanya achague mavazi ambayo yatamuweka katika hali ya wepesi wa mwili wake akivaa suruali ya jeans ya rangi nyeusi iliyoiva haswa jeans ya kisasa toka kampuni ya kutengeneza mavazi anayoipenda kuvaa kampuni ya Levi’s, jeans isiyo na mbwembwe nyingi kama ma jeans mengine wanayovaa vijana wengine yaani anaenda dukani kununua lakini tayari inakuwa imechanwa chanwa (ukisasa huo), ukisasa ambao ‘TSC’ mara zote akiwa kama kiongozi wa familia asingeweza kuvaa hata mara moja, juu ya kiwili wili chake alitinga fulana nzito (sweta) la rangi ya bluu iliyoiva kabisa tena ikiwa na mikono mirefu hivyo yeye alifanya kuivuta kwa juu mpaka viwikoni na chini kabisa akivaa raba nyeusi yenye chata ya NIKE.

Kwa kweli kijana huyu mwanaume wa shoka alipendeza kwa jinsi alivyovaa ikiwa ni mavazi machache aliyobeba toka kwenye chumba cha nyumbani kwake anachotumia yeye na mkewe kuhifadhi nguo zao kikiwa na makabati, mashine ya kufulia pamoja na meza ya kupiga pasi nguo, chumba kilicho ndani ya chumba cha kulala.

Hakuona haja ya kujitizama kwenye kioo sababu mara zote alikuwa ni mtu wa kujiamini yeye akivaa basi kwa wengine wanaomuangalia uwa kapendeza tu na hana shida ya kumpendezesha mtu maana ilivyo kila anachovaa uwa ni kwa ajili ya kujisitiri mwili na hata haina ya shughuli iliyo mbele yake.

Alipoona yuko sawa alitizama saa ikiwa tayari sasa imegota saa nne na dakika tano alinyanyua simu na kupiga namba alizotaka kupiga kwa wakati huo, simu ikaita na kupokelewa kwa haraka sana.

   “Boss!” Upande wa pili sauti ya kike nyororo ikavumisha toka kwenye spika za sauti za simu kuja kwenye ngoma ya sikio la kushoto la Agent Kai.

   “Pole na uchovu, pole na kukususa..”

   “Nimeshangaa hata kunijulisha umefikia hotel gani usiku kama tulivyokubaliana, wapi! Mwenzangu ukachuna, mpaka nikatamani kukiuka makubaliano nisikutafute mpaka unitafute”

   “Hahaha hahahah! Nilitaka upumzike maana huku usiku kuna baridi kuliko WDC… Hata hivyo naamini haukuchukia na ukaweka uvumilivu wako”

   “Sikuchukia nilijua hamna tatizo ila wakati wa usiku nikiwa naangalia tv nikashangaa mauaji ya watu eneo linaloitwa Carratera San Felipe karibu na barabara waliyosema kuwa inaitwa Jocotenango… Watu kumi na tatu wameuliwa na watu wasiojulikana, asubuhi hii nikawai magazeti nikafanikiwa kupata moja linalochapwa kwa kiingereza lililoandika habari za mauaji hayo… Muuaji au hao wauaji ni hatari sana kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mji wa Antigua… Umesikia na wewe juu ya hilo?” Aliuliza mwanadada alikuwa ni Special Agent Rebecca Smith msaidizi wa Agent Kai.

   “Ndiyo nimesikia… Mtungi wa maji hautakiwi kupasuka…” Akajibu kwa mafumbo Agent Kai na mara moja S.A Rebecca alimuelewa kuwa hawatakiwi kuliongelea kwa zaidi hili jambo kwenye simu kwa maana ya kuwa jana usiku wakati wakifanya maongezi na kina Detective Norman, Kamanda Muniain na majsusi wenza wao toka DEA walitahadharishwa wote kwa pamoja kuwa mawasiliano ya simu katika Guatemala hayako salama sana yanadukuliwa sana na watu wabaya wanaojihusisha na biashara ya ulanguzi wa madawa ya kulevya hivyo wajitahidi kuonana ana kwa ana kwa maongezi ya siri na si simu kuongelea mambo ya mipango yoyote ile inayohusiana na upambanaji, hivyo mtungi hautakiwi kupasuka wakimaanisha ukipasuka utavujisha maji na maji yenyewe ni siri itakayosikilizwa na wengine bila wao kuwajua.

  “Asante sana… Tunaonana wapi boss?”

  “Muda huu ni saa nne inakaribia na robo… Mimi sijapata kifungua kinywa mpaka sasa hivyo kwa ninavyoitazama ramani ya mji wa Antigua naona kuna mgahawa unaitwa Posada La Merced Antigua tukutane hapo tupate wote kifungua kinywa… Dakika ishirini za mimi kutoka nilipo nafikiri zitanitosha ila wewe pia ukitizama ramani yako hapo ulipo niambie dakika ngapi kwa taxi zinakuonyesha utakuwa umefika?”

   “Haha! Kwangu mimi sipandi taxi… Dakika kumi kwa miguu hazifiki nipo karibu na Posada La Merced Antigua… Wee anza kusogea ukikaribia nami nitaanza safari…”

   “Salama iko salama pale inapokuwa salama, fanya salama” Akaongea tena Agent Kai ikiwa kwa mafumbo tena.

   “Usijali salama itakuwa salama namba moja salama” Akajibu akiwa kaelewa naye akajibu inavyotakiwa hii wakiwa wamemaanisha kiusalama yeye Rebecca aanze kufika kwanza mahala hapo kulinda usalama wao maana toka waambiwe huduma ya simu si salama hawakuwa na amani kabisa kuongea kwa kujiachia na kupanga mipango katika simu bila wasi.

‘TSC’ alikata simu na kisha akachukua katika vitu alivyoona vinafaa kutoka navyo kwa muda huo, ikiwemo bastola yake ndogo, akavaa miwani yake ambayo ukiitizama unaweza kuona ya kukinga jua tu alipomaliza akatoka akiwa amehakikisha pia chumba kakiacha katika hali ya kimitego endapo atatokea mtu ataingia yeye akiwa hayupo basi taarifa zitamfikia kupitia simu na saa yake ya mkononi aliyovaa.

   *****  *****  *****

SAA SITA MCHANA

TAJUMULCO CAMP, SAN MARCOS-GUATEMALA

Helkopta aina ya Robinson R-22 mali ya Brigedia mfukuzwa wa jeshi la wananchi la Mexico Fernandes Carlos Codrado ‘Feca’ ilitua kwenye uwanja mdogo wa kutua ndege ndogo na helkopta aina yoyote, uwanja uliopo eneo la shamba kubwa la mwekezaji mkubwa wa kilimo cha kahawa kutoka Mexico aliyeamua kuwekeza katika katika kilimo cha kahawa eneo kubwa la kando kando ya milima ya Tajumulco jimbo la San Marcos nchini Guatemala.

Abiria waliofika na helkopta wakitokea Mexico walishuka baada ya rubani wa helkopta kushuka yeye kwanza kisha kuwafungulia mlango wa upande wa kulia.

  “Karibuni! Karibuni sana Camp Tajumulco.. Poleni na safari makamanda” Akaongea mmoja ya watu muhimu waliofika kuwapokea wageni hawa ingawa si wageni sana katika kambi hii ya siri ambayo watu wengi wa wanausalama wa serikali walikuwa wakijua juu ya siri ya shamba hili ambalo lilikuwa likimilikiwa na mwekezaji wa kimexico aitwaye Alexis Carlos Codrado huyu ni mdogo wake na Feca tajiri wa kimexico ambaye ndiye haswa mmiliki wa ukweli kabisa wa eneo hili hivyo Alexis yeye alikuwa ni kivuli.

  “Ahsante sana Mariana… Habari za hapa?” Akaongea Koplo Maxiwell Zuantejo kwa niaba ya wenzake ambao kila mmoja alikuwa akiangalia huku na huko pembeni pembeni ya uwanja huu ambako kote kulikuwa na walinzi walioshika silaha wakiwa katika sare maalumu za kiulinzi wakizunguka kulinda eneo hili.

Wageni waliongozwa na wenyeji wao waliokuwa kama watano hawa wakiwa hawana silaha za kuonekana hadharani ila hakuna ambaye alikuwa hana silaha kama bastola na kisu katika hifadhi ya mavazi waliyovaa pia hawa hawakuwa na sare kama wanaonekana pembeni wakiwa wanazunguka huku ni mmoja sana ambaye unaweza kumuona havuti sigara na pia wengi wao muda huu walikuwa wamevaa miwani ya jua, kwa kweli eneo hili tu la uwanjani lilikuwa linalindwa hivi huko kwingine kama ndiyo wafika hapa kwa mara ya kwanza ni mpaka uende kujionea mwenyewe.

   “Mtahitaji kupumzika au tunaweza kuongea kabisa na kupanga kila kitu?” Akauliza mwanaume ambaye kwa hapa Tajumulco Camp alikuwa anahusika na ulinzi mkuu wa ghala la kuhifadhia silaha za genge lao la ‘THE RED JAGUAR’ akifahamika kwa majina ya utani ya ‘The Gun Control’ code name ‘TGC’ kwa watu wake wa katika ‘TRJ’ iwe masalanga wasio na vyeo au walio na vyeo kotekote umuita hivyo lakini yeye jina lake ni Petr Batrolomelo miaka miwili iliyopita alikuwa ni mkufunzi wa mafunzo ya silaha katika chuo cha mafunzo ya upolisi nchini Mexico.

   “Kazi iliyotuleta hapa GTL inaweza kuwa ngumu kama tutataka na pia inaweza kuwa nyepesi kama tutataka iwe hivyo, hivyo sidhani kama tunahitaji kupumzika moja kwa moja twendeni kwenye kikao mapumziko yetu yatakuja tukiwa humo humo kazini au tukiwa tayari tushapanga majukumu yetu” Akajibu wazo lililotolewa la wao kupumzika kwa namna hiyo Koplo Zuantejo.

  “Sawa.. Twendeni juu kuna eneo zuri la kuongea… Vipi watahitajika na watu wa zaidi yetu?” Akaelekeza na kuhoji Petr ‘TGC’.

   “Hilo anatakiwa kiongozi wenu Mariana ajibu yeye… Tulivyokuwa Guerrero tulijua yale tuliyoambiwa ni yeye ndiye kiongozi wa misheni hii ndogo na yupo hapa” Akajibu Koplo Zuantejo huku akimuangalia usoni bibie Mariana Caro Funtes ambaye ni Koplo aliyekimbia jeshi huko Mexico miaka saba iliyopita kama tulivyomuona mwanzoni alikuwa ni sekretari wa Kiongozi wa nidhamu jeshini Meja Sanz.

   “Haina haja masalanga wote uwa tunawaambia tu ikiwa tayari tushapanga sisi wenyewe tulio ngazi ya juu yao na hili TGC Petr unalijua fika…. Wageni hawa wote ni TRJ hivyo wanajua kila kitu twendeni juu kwa ajili ya kuelekezana kila kitu hakuna haja ya kusimama hapa koridoni..!!” Akaongea Mariana na kisha kuanza kuelekea juu kwa kupandisha ngazi.

Walifika ambako uwa vikao vinafanyiwa juu ya flour ya ghorofa dogo ambalo watu wa kawaida wanapofika hapa kwa ajili ya kutembelea shamba hili kubwa la kahawa ufikishiwa kwa chini huko ambako kuna maofisi ya uongo lakini unaofanana ukweli.

Kila mmoja alichukua kiti kati ya viti vya plastiki vilivyopangwa kwa kupachikana mpaka vikafanya kama ngazi kwenda juu, kila aliyechukua alifuta vumbi na kukiweka alipoona sahihi kukaa ila akihakikisha anajenga duara la kufanya waangaliane.

   “Ruhusa sasa kuanza kuongea lile ambalo limesababisha bwana mkubwa wetu Feca kutuagiza nasi tufike hapa GTL.. Mariana karibu utueleze kwa kifupi..!” Koplo Maxiwell Zuantejo akaongea, toka watu watatu hawa waliofika hapa Tajumulco Camp kwa helkopta yeye Maxiwell mwanaume wa shoka mwenye mwili mkubwa aliyekwenda juu na kujaa mwili wa mazoezi kama wacheza mieleka wale ambao hawajaa jaa kihasara kwa miili ya ovyo ovyo, hapa mazoezi yalikubali na si mtu wa kuacha siku mbili zimpite bila kuingia gym na kukamua haswa ni mkufunzi wa kijeshi aliyetoroshwa gerezani akiwa anatumikia kifungo cha miaka ishirini mwanzoni 

  “Naamini hapa sote twajua historia ya TRJ hapa GTL..” Alianza hivyo Mariana kisha akawaangalia kwa zamu wanaume wanaomuangalia kwa umakini akaendelea baada ya kuridhika na umakini wao.

   “… Tumekuwa tukitegemea usalama wetu kwa biashara yetu kwa kuungwa mkono na wakubwa kadhaa muhimu walio katika sekta muhimu katika serikali hii, wamekuwa wakitulinda kwa hali na mali kiasi ya kwamba hakuna kikao kinachofanyika serikalini ambacho sisi hatufahamishwi ni kikao cha aina gani na kwanini kimekaliwa hadi vingine ambavyo hatuna haja ya kujua mimi kama kiongozi msaidizi wa TRJ hapa GTL nimekuwa nikifahamishwa… Wiki mbili zilizopita kiongozi wetu wa hapa katika TRJ Ivan alto alienda Canada kutibiwa mdomo wake kwakuwa umekuwa ukimsumbua sana kwa miezi ya hivi karibuni, madaraka yote nikaachiwa mimi hivyo nimekuwa si mtu wa kupumzika sehemu moja maana masuala mengi nafanya mwenyewe lakini siku ya jana ilinikuta nikiwa hapa San Marcos ndipo yakatokea yaliyotokea kama mlivyoyasikia na si kama ni uzembe wa vijana wetu ni kuzidiwa ujuzi na waliowakuta na pia kujibweteka kwetu sote kwa ujumla tukiamini tunaweza fanya lolote popote katika wakati wowote na tukafanikisha…!” Alianza hivyo Mariana kisha akaacha koo lipitishe mate na hata mdomo wake nao kujipatia pumziko.

   “Pole yake Ivan Alto… Amekuwa mhimili wetu mkuu hapa katika kambi yetu… Siwezi laumu moja kwa moja ila ni kweli kama usemavyo kazi zako zimekuwa nyingi na hujaletewa mtu mwenye kariba ya uwezo wa Alto hili ni kosa letu makao makuu tumekuwa tukipambana na namna gani masoko yawe tukiamini huku hakuhitaji nguvu ya ziada kwakuwa serikali ya huku iko viganjani mwetu lakini tunakosea Tajumulco Camp ndiyo moyo wa TRJ wakati kichwa tukiamini kipo Mexico lakini mimi naweza kusema kichwa na moyo viko hapa na umakini unatakiwa kutiliwa mkazo hapa zaidi” Maxiwell akaunguruma akisaidiwa na mikono yake kwa jinsi alivyokuwa akitumia vitendo katika ongea yake.

  “Ni kweli! Lakini naamini kuja kwenu kuniongezea nguvu kutasababisha kazi kuisha kwa haraka… Kazi kuu ambayo inatuumiza kichwa ni kuwa tulikuwa na mtu ambaye yumo kwenye malipo yetu yeye alikuwa askari polisi kamanda wa mji wa Antigua, huyu mtu baadaye Rais wa nchi alimteua kuwa mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na Rushwa kwa yeye Rais alivyoaminishwa na vyanzo vyake kuwa bwana mkubwa yule ni mtu anayechukia sana rushwa… Miezi mitano mbele baada ya kuteuliwa tuliona kama anatukwepa sana pale tunapohitaji atusaidie katika mambo kadhaa ambayo tunaona kuna miingiliano fulani ambayo inaweza kuyumbisha kazi zetu za hapa Tajumulco, mara akaanza kukamata watu ambao tuliokuwa tunawatumia yaani wapo katika malipo yetu akiwatega kwa mitego mbalimbali ya kukutwa wanachukua rushwa hii ilitustua sana ikabidi tumtumie ujumbe wa kumuonya asiendelee kufanya hivyo alitumiwa ujumbe na mheshimiwa waziri lakini mwenzetu hakutujibu ndipo tukapata taarifa kwamba ana orodha ya watu ambao anaamini akisha watia nguvuni katika mitego yake atavunja nguvu zetu na kisha hata wale wanaotulinda kwa Rais wa nchi itawashinda kutulinda na tutaangamizwa kwa njia ambazo ni kuomba msaada wa OCLA pamoja na vyombo vingine vya kupambana na mihadarati vya nchi za nje ya GTL kama Marekani na hata Mexico yetu kama mjuavyo mpaka sasa kwa miaka yote tumekuwa salama zaidi hapa GTL kuliko sehemu ingine sababu ya mwenzetu waziri wa mambo ya ndani hata kama hatushambuliwi na sehemu zingine lakini kuwa na kiwanda hapa Tajumulco magenge mengi inawauma sana!” Akaeleza tena kwa kirefu Mariana lakini kulikuwa na mtu anataka kutia neno.

   “Flashdisk tunayoitafuta ambayo inasemekana mheshimiwa Rafael alipewa siri na mmoja wa walinzi wa mkurugenzi wa taasisi ya kupambana na rushwa kuwa bwana huyu alimpa Detective Norman wa OCLA kabla haujawasili kwenye makazi yake, mnahisi ina siri gani kubwa?” Aliuliza Aristos Mosquera mmoja wa watu watatu walioongozana na Koplo Maxiwell Zuantejo kuja Guatemala kwa kazi maalumu.

   “Taarifa inasema Norman na boss wake walikua na mpango wa siri ambao sisi hatuujui hivyo waliomba msaada kwa mkurugenzi wa taasisi ya kupambana na rushwa ndipo akawaambia atawaandalia flashdisk kisha atawatumia na kabla sisi hatujafika kumuhoji ni jambo gani wanataka kina Norman tulipishana na Norman bila kumuona akiwa kashatoka kupewa flashdisk na tulipomlazimisha mkurugenzi aseme flasdisk ina siri gani aligoma katukatu kusema chochote ndipo nikaona anatusumbua nikampiga risasi kumuua kisha tukaondoka tulienda na vijana wangu watano..!” Akafafanua Mariana kisha akawatizama kwa zamu wanaume wanaotizama kwa makini kana kwamba wana mtamani kimapenzi kumbe wako na makini na anayoyazungumza.

   “Kwanini mnashindwa mpaka leo kumpata Norman?” Akauliza tena Aristos.

   “Nyendo zake upande wa wataalamu wetu tuliowaweka jijini Guatemala zimekuwa ngumu kung’amua hasa anapatikanaje! Sababu kiukweli kijana huyu amekuwa hajawai kuwa na familia na hata makazi yake maalumu si ya kueleweka, tunazo picha zake aina zote kuanzia video hadi picha mgando lakini kumuona ndani ya nchi hii imekuwa mtihani sana na hatuelewi kwanini anatuzidi akili wakati yupo hapa hapa GTL pia kumbukeni sisi tuna mtu mkubwa zaidi katika serikali hii upande wa usalama naye ana wasiwasi mkubwa juu ya flashdisk lakini bado kuna ugumu mkubwa unaotuzidishia mashaka kwetu”

Akajibu Mariana na kuwafanya wanaomsikiliza wamkazie macho yenye maswali mengi sana yeye akatabasamu maana alielewa kwanini wanamtaza vile.

Mwisho wa sehemu ya arobaini na saba (47)

Agent Kai ‘TSC’ anafanya mawasiliano kadhaa baada ya kuamka yanayomsogeza katika kazi za kazi na kuamua sasa wakutane na msaidizi wake na swahiba wake Special Agent Rebecca Smith.

Kikao nchini Mexico jimbo la Guerrero katika manispaa ya Tetaplan, eneo la Soledad De Maciel linapopatikana kasri la ‘Secreto Potentia La Feca Palacio’ (Nguvu ya siri kasri la Feca), kikao kinazaa kikao kingine kilichokwenda kufanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano ulioko katika jengo la maofisi ya shamba kubwa la kahawa.

Nini kitafuata? Vuta hatua mbele msomaji kwa ajili ya mengi mazuri..



   “Flashdisk tunayoitafuta ambayo inasemekana mlipewa siri na mmoja wa walinzi wa mkurugenzi wa taasisi ya kupambana na rushwa kuwa bwana huyu alimpa Detective Norman wa OCLA, mnahisi ina siri gani kubwa?” Aliuliza Aristos Mosquera mmoja wa watu watatu walioongozana na Koplo Maxiwell Zuantejo kuja Guatemala kwa kazi maalumu.

   “Taarifa inasema Norman na boss wake walikua na mpango wa siri ambao sisi hatuujui hivyo waliomba msaada kwa mkurugenzi wa taasisi ya kupambana na rushwa ndipo akawaambia atawaandalia flashdisk kisha atawatumia na kabla sisi hatujafika kumuhoji ni jambo gani wanataka kina Norman tulipishana na Norman bila kumuona akiwa kashatoka kupewa flashdisk na tulipomlazimisha mkurugenzi aseme flasdisk ina siri gani aligoma katukatu kusema chochote ndipo nikaona anatusumbua nikampiga risasi kumuua kisha tukaondoka tulienda na vijana wangu watano..!” Akafafanua Mariana kisha akawatizama kwa zamu wanaume wanaotizama kwa makini kana kwamba wana mtamani kimapenzi kumbe wako na makini na anayoyazungumza.

   “Kwanini mnashindwa mpaka leo kumpata Norman?” Akauliza tena Aristos.

   “Nyendo zake upande wa wataalamu wetu tuliowaweka jijini Guatemala zimekuwa ngumu kung’amua hasa anapatikanaje! Sababu kiukweli kijana huyu amekuwa hajawai kuwa na familia na hata makazi yake maalumu si ya kueleweka, tunazo picha zake aina zote kuanzia video hadi picha mgando lakini kumuona ndani ya nchi hii imekuwa mtihani sana na hatuelewi kwanini anatuzidi akili wakati yupo hapa hapa GTL”

Akajibu Mariana na kuwafanya wanaomsikiliza wamkazie macho yenye maswali mengi sana yeye akatabasamu maana alielewa kwanini wanamtaza vile.

ENDELEA NA DODO ASALI..!!

SAA TANO, MCHANA

TAJUMULCO CAMP, SAN MARCOS-GUATEMALA

   “Tumefika kumaliza hili tatizo.. Nafikiri uwepo wetu haujawai kuharibu operesheni yoyote toka kuunda kwa TRJ… Hivyo uondoe tena unyonge wa kusema anajificha na haieleweki wapi anaishi ilimradi yeye ni mtu wa GTL hatuwezi shindwa mpata, hatuwezi mruhusu kidudu mtu mmoja au wawili waharibu mfumo tulioufuma kwa pesa na jasho letu lililojichanganya na damu” Akaongea Zuantejo kisha akatoa miwani yake ya rangi nyeusi yenye kioo kipana na sasa macho yake makubwa na mekundu yakaonekana kwa kila mmoja ingawa wengi walishawai muona hivi alivyo walikuwepo ambao hawakuwai kumuona hivi.

   “Kwani mkuu wa hapa Guatemala wa OCLA ni kitu gani kinachozuia asishikiliwe akalishwa adabu itakayomfanya atusogezee huyo mpuuzi wake?”Akauliza Aristos Mosquera.

   “Katika kikao hiki anakosekana mtu muhimu mheshimiwa waziri wa usalama kutokana na itifaki za kisiri katika uwepo wake katika genge letu lakini yeye ndiyo mwenye jibu kamili juu ya sisi kumuangalia tu Kamanda Muniain muda wote huu.!”Akajibu Mariana Caro Funtes.

   “Uwoga mwingi umetawala katika hili na ndicho kitu ambacho kina tuzuru kwa hali kubwa sana katika nchi hii ambayo kwetu ni muhimu sana katika mizizi yetu..!” Aristos Mosquera akaongea tena uso akiwa kaukunja mzungu huyu mwenye kufuga midevu mingi kama waarabu wenye itikadi kali za kiimani.

   “Inawezekana kufanya hivyo lakini katika watu ambao hatujawatia mikononi mwetu na anatafuta kila njia kujua mengi yanayohusu mihadarati katika nchi hii ni huyu Rais wa sasa wa Guatemala…. Toka ameingia Amejitahidi kutekeleza baadhi ya mambo aliyoahidi wakati anaomba kura za wananchi wake katika ahadi zake aliahidi atapambana na rushwa pamoja na mihadarati kwa nguvu zote… Hivi alivyoviahidi ni vitu ambavyo kiukweli ni vitu kera sana kwa wananchi wa GTL hasa kwa watu wazima na vijana wengine ambao hawafungamani na mambo hayo… Hivyo cha kwanza alipoingia aliweka watu ambao aliamini kwa asilimia mia moja kuwa hawawezi shindwa tekeleza ahadi yake kwa wananchi na wakamuangusha, Kamanda Muniain ni mtoto wa mjomba wake hivyo ni binamu hawa akamuweka OCLA kwakuwa licha ya kuwa iko katika nchi zinazoshirikiana katika mambo ya ulinzi wa nchi za latin America lakini mkurugenzi wake katika nchi husika uchaguliwa na Rais husika wa nchi… Na ndipo katika taasisi ya kupambana na rushwa akamuweka rafiki yake mkubwa ambaye alishirikiana naye katika kampeni za uchaguzi bega kwa bega.. Ila tunakoendea tutachukua maamuzi yetu sisi wenyewe bila kumshirikisha mheshimiwa waziri Ceni ambaye lolote lililopo hapa GTL tuliambiwa na Feca  tutalifanya kwa maelekezo ya huyu tu lakini anaharibu sasa tena bila kujijua anaharibu hadi kwake si genge peke yake” Akajibu kirefu Mariana akitizamana na Aristos bila kupepesa muda wote.

   “Hiyo ndiyo inayozuia nyinyi kudhibiti hatari inayotukaribia? Kumbukeni sisi TRJ hatuwezi shindwa kuondoa uhai wa Rais wa nchi kama hii endapo kutakuwa na hatari ya kuharibika mambo yetu… Hilo linawezekana kwa huyo, iweje tushindwe kwa mtu anayeonekana kutaka kutuingilia tena akiwa yeye tu na watu wachache?” Aristos akaongea na kuuliza maswali mawili kwa Mariana tena.

   “Hatujawai fikiria kufikia huko kwenye kutaka kuua nembo ya nchi… Rais wa nchi ni nembo kuu ya taifa ni taasisi kubwa namba moja katika nchi yoyote lakini pia kama inaonekana ni muhimu sisi kumtia kiganjani Kamanda Muniain hilo si tatizo kwangu lakini mimi siko peke yangu katika maamuzi hapo GTL nilikuwa na kiongozi wangu na yeye katika vipaumbele vya kujilinda alivyoviweka aliweka na hilo la kutomgusa Kamanda Muniain akisisitiza kama tunahitaji kuendelea kuishi kwa maelekezo ya waziri Ceni na yeye Ceni anasema tukitaka tuishi kwa starehe ndani ya GTL basi ni kutogusa watu wa familia ya Rais wa nchi hii maana anatutafuta kwa udi na uvumba na hataki kujenga ukaribu na watu wetu walio na ushawishi katika serikali yake” Akajibu Mariana.

  “Je mnafikiri hajui juu ya uwepo wa TRJ katika Guatemala?” Akahoji tena Aristos.

   “Watu wetu ambao wapo karibu naye wanasema anajua hata kabla hajawa Rais wa nchi hii ila tunaweza kusema ni nafuu kwetu anachojua ni genge hatari la Mexico lenye tawi lake katika nchi yake likifanya njia ya kupitisha mihadarati kutoka nchi sifika kwa kilimo na uzalishaji wa mihadarati hivyo hajui kama tuna mitambo ya kiwanda cha kusaga mihadarati ndani ya nchi yake.. Mara nyingi anawekeza nguvu katika kuzuia njia za usafirishaji lakini kuwepo kwa Ceni kunafanya mambo yawe laini… Pia Rais wa hapa anamuamini sana Alexis amekuwa mtu anayemsikiliza sana kwa sababu ya kiwanda kikubwa alichofungua hapa San Marcos cha usindikaji kahawa pamoja na hili shamba hapa ambalo miezi minne iliyopita Rais na waziri wake wa kilimo na viwanda walitembelea hapa wakaongea na watu wetu tuliowafanya wajifanye wao ndiyo wanaotusaidia katika kilimo cha kahawa na mwenyeji wao pia Mr. Alexis akaongea nao na hata kuwatembeza sehemu ambazo si rahisi mtu kuelewa kama kuna jambo la kujificha” Akajibu kirefu tena Mariana ambaye maswali yalianza kumkera lakini hakuwa na njia zaidi ya kujibu kila analoulizwa tena akitakiwa kujibu kiufafanuzi zaidi.

  “Mimi upande wangu nimeelewa shida ilipo ni Mheshimiwa Ceni kumfuga nyoka na natoa angalizo kazi hii inaweza kuwa ngumu endapo hatutamtumia Kamanda Muniain Salivita Muniero… Kwanini? Kwasababu yeye ndiye mtu ambaye kwa pamoja na mtu wake waliamua kuomba msaada kwa mkurugenzi wa taasisi ya kupambana na rushwa akawaahidi kuwapatia msaada kwa njia ya flashdisk ambayo hamjui ina nini? Ajabu ni kuwa pamoja na yeye Ceni Kujua hatari kubwa kuhusu hilo ameshindwa kuwa makini na kuchukua hatua stahiki ni hatari kwa mustakabali wetu ndani ya GTL, hivyo pendekezo langu tutengeneze Plan A ambayo iwe na plan B bila kumshirikisha moja kwa moja mheshimiwa Ceni… Plan A ni sisi wenyewe tukishirikiana na vijana wetu tutamtafuta Norman na tukiona leo imepita ikiwa bila bila kesho tutamtumia Muniain kumpata huyo mtu ambaye kwa habari nilizopata ameshaua watu kumi na sita wa TRJ! So sad, hapo kabla akiwaua watatu na jana kumi na tatu… Hii haingii akilini mtu mmoja kufanya uthubutu mkubwa kama huo” Kwa mara ya kwanza bingwa wa kuvuta sigara kwa stahili ya panda mti fyeka mti aitwaye Molina Qadrado ambaye muda wote toka wameingia Guatemala alikuwa mtu kimya akivuta sigara zake na kusikiliza wenzake wanavyoongea sasa aliongea.

   “Kwa mauaji ya jana sidhani kama ni Norman peke yake amefanya mauaji yale… Moja kwa moja kwa uzoefu wangu namuingiza kwenye mauaji haya Kamanda Muniain na watu aliokuwa nao, watu aliokuwa nao tunatakiwa kuwajumuisha wote kwa ujumla ndiyo wamefanya mauaji wakiwa wamewazidi ujanja watu niliowaagiza pale Filadelifia..!” Akajibu hoja kwa yeye aliyewaagiza watu wake kufanya kazi mgahawa wa Filadelifia, bibie Mariana.

   “Kumbe hawakuwa wenyewe tu, hapo sawa… Kumbe kuna kikosi kilicho tayari kwa mapambano juu yetu TRJ halafu nyinyi mnasubiri kuchukua hatua stahiki, mnasubiri mpaka wafike hapa kambini watuvuruge… Aisee mnafikiri watakuja wanne au watano wakiwa washafanya uchunguzi wao na uhakika juu ya tunalolificha hapa, msijidanganye jamani jamaa watakuja na jeshi hapa na mara moja tutashindwa kuhimili sababu kama mjuavyo TRJ tuko wengi lakini tumegawana majukumu kambi yetu sasa haiwezi kuhimili uvamizi wa jeshi dogo tu hata kama jeshi la wananchi la GTL… Haraka tunatakiwa tuchukue tahadhari tuzuie maji kabla ya hayajavunja kingo” Aristos Mosquera mtu anayependa sana umakini katika kazi kiasi ya kwamba amekuwa mtu wa kuaminiwa sana na Fernandes (Feca) mwenyewe.

   “Mariana! Mara moja naomba tupange safu iliyo na vijana walio na uzoefu na umakini katika uchunguzi wenye urafiki na watu walio katika OCLA nataka waende kufanya uchunguzi ni kina nani waliokuwa na kina Norman jana usiku pia uwapatie pesa ya kuwasaidia katika kazi kama kilainishi kwa watu walio OCLA… Huu si wakati wa kusubiri kuzima moto wakati ukiwa ushakolea ni wakati wa kuzima fukuto la moshi tu lililoanza hivyo si wakati wa kutoa malipo yaliyokwisha pangwa ni wakati wa bonasi” Amri elekezi ikatoka kwa kiongozi wa operesheni hii Koplo Maxiwell Zuantejo waliyoiita operesheni ndogo tu.

Amri hii ndiyo ilikuwa hitimisho la wao kuongea katika ukumbi wa juu wa mikutano wa kampuni inayomiliki shamba la kahawa lililoko hapa pembezoni mwa mlima Tajumulco.

Mariana akatumia simu yake kuwaita vijana ishirini anaoamini wanao watu ambao wako katika Organized Crime Latin America (OCLA) pia wako vizuri katika masuala ya kiuchunguzi, akawapa maelekezo akisaidiana na wakuu wengine waliofika Camp Tajumulco kisha vijana wale wakaondoka baada ya masaa mawili kuelekea Guatemala City kutokea San Marcos.

  *****  *****  *****

SAA TANO, ALHAMISI

GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Mtaa wa 4 A Calle Poniente 49 uliopo mjini Antigua ndipo ulipo mgahawa wa hotel ya Posada La Merced Antigua, Special Agent Rebecca Smith alikuwa mtu wa kwanza kufika akiwa amefika kwa miguu tu kutokea hotel aliyopanga toka usiku wa saa moja baada ya kuingia jijini Guatemala kwa ndege ambayo walikuwa wote yeye na Agent Kai ikiwatoa Washington DC kuja Guatemala.

Kiusalama wao waliamua kuwa wakiwa ndani ya ndege hadi watakapofika Guatemala wasiwe watu kama wanaojuana kabisa na watawasiliana asubuhi ikiwa kila mmoja amechukua hotel atakayopendezewa.

S.A Rebecca alitafuta mahala ambapo akikaa atamuona kila anayeingia katika mgahawa mzuri na wa kisasa katika miongoni ya migahawa mizuri inayopatikana katika jiji la Guatemala hususani mji huu wa manispaa ya Antigua alipata mahala ambapo angeweza kupata hitaji lake akaomba kwa muhudumu wa kiume aliyefika kumuhudumia aweze kumsaidia meza ile iwe na viti viwili tu sababu kuna mtu yeye anamsubiri kisha ya hapo akaagiza supu ya kuku na juisi ya embe, akasubiri kuletewa akipitia magazeti ya kiingereza yalioandikwa mambo mbalimbali yanayochapwa na vyombo vya habari vya Guatemala.

Dakika tano mbele akiwa anaendelea kupata supu ya kuku huku juisi ikimsubiri na akiwa makini kuangalia mlango mkuu wa kuingilia pale eneo la mgahawa alistuka akishikwa bega kwa pembeni na siyo siri alistuka haswa mpaka alitaka kuruka toka kitini lakini akaishia kukiburuza kiti kikisogea sambamba na mwili wake, akageuza shingo kwa kasi macho yake yakagongana na sura ya Agent Kai ikitabasamu.

   “Bosii!! Umepitia wapi?” Akajikuta anahoji bila kufikiri huku akitoa pumzi kwa nguvu Rebecca.

   “Khaaah! Unauliza paka kapitaje kwenye njia nyingi zilizopo hapa… Unakosea ni kama huzijui tabia za paka vile” Akajibu Agent Kai ‘TSC’ huku akivuta kiti alichoachiwa akae kikiwa kinaangalia upande wa pili wa meza alikokaa Rebecca Smith.

  “Ni uchawi wa Tanzania mnatumia paka katika uchawi au ni nini?” Akahoji akitabasamu Rebecca.

  “Uchawi? Uchawi sihujui mimi… Wewe unaamini uchawi?”

   “Sijauthibitisha ila nausikia hasa kwa watu wa huko unakotoka Afrika leo nina fursa ya kusikia mengi tena juu ya yale unayoyajua hasa kuhusiana na Afrika na uchawi”

   “Umechemka sababu sijui mengi ingawa wapo wale wasiojua kuhusu imani yangu ya kidini uwa wanaamini mimi mchawi heti kwa sababu ya kukubali jina la nyayo za paka na kulifanya kama nembo yangu ya siri”

   “Ni kweli wengi wanasema hivyo utashangaa hata wale ambao ni wakubwa wenye vyeo katika CIA na hata FBI uwa wanasema Agent Kai ni mchawi kutoka Afrika mwenye kuisaidia Marekani kupitia uchawi wake… Nishawai kuta mjadala huo Langley makao makuu ya CIA kwa mabinti kama watano walikuwa wanakuongelea kipindi umeenda kuoa Malaysia, waliponiona kuna wawili nilisoma nao na wanajua kama ulinitoa Malaysia kuja ofisi ya makamu wa Rais wakaniomba ufafanuzi kwa niyajuayo juu yako na hasa imani ya chata ya paka na code name yako”

   “Hahahaha hahahahaha… Ukawaambia ndiyo jamaa mchawi anamiliki jini la paka… Hahahaha hahahaha…!!” Akaongea Agent Kai akiwa kaunga na kicheko cha furaha ya stori zao na mara muhudumu yule aliyemuhudumia  S.A Rebecca alifika na kuagizwa supu ya samaki iliyochanganywa na njegere za kuchemshwa pamoja na chapati na juisi ya matunda ya mchanganyiko ikaagizwa ije kusindikiza.

  “Achana na mambo ya wachawi hayo… Kuna audio nimetumiwa tunatakiwa kuzisikiliza kwa pamoja maana kwa zilivyo sisitizwa ni muhimu naamini hizi audio zitatufanya kupata mwangaza wa kazi iliyotuleta hapa” Akaongea TSC akiomba mada ya paka na uchawi iachwe waongee kuhusu kazi kwanza.

  “Tunaweza kusikiliza hapa bila shida au?”

  “Haina shida weka Bluetooth earphone nami naweka tutasikiliza kutokea katika ipad yangu kwakuwa wakati nakuja nikiwa kwenye taxi nilizitupia toka kwenye simu yangu”

   “Basi maliza kula supu yako kwanza tukianza juisi tutaanza huku tunasikiliza audio…!”

   “Mjanja kakutana na mjanja… Hakuna ujanja utakaofanikiwa hapa leo”Akaongea TSC akiunganisha na cheko dogo macho yake yakiwa yameinamia bakuli kubwa la supu.

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog