Search This Blog

Monday 27 March 2023

HEKAHEKA! - 3

  


Simulizi : Hekaheka!

Sehemu Ya Tatu (3)



Yule ofisa wa usalama akaonekana kunipuuza tena badala yake akafungua tena ule mkoba wake mweusi uliokuwa chini ya meza.


Sikuelewa alikuwa akitaka kufanya nini hadi pale alipochukua bahasha moja kubwa ya kaki na kumimina vitu vilivyokuwa ndani ya ile bahasha pale juu meza.


Niliyakaribisha macho yangu kutazama pale mezani na ghafla nikapigwa butwaa huku midomo yangu ikinikauka.


Pale mezani niliziona picha nne kubwa zilizonionesha nikiwa katika maeneo mbalimbali, picha moja ilinionesha nikiwa na watu wawili, mwanamume mmoja mrefu mwenye umbo kakamavu na msichana mrembo aliyefanana sana na Babra.


Tulikuwa tumesimama katika eneo ambalo sikuweza kulifahamu vyema tukionekana kupanga mambo fulani, yule mwanamume sikumfahamu lakini yule msichana niliamini kuwa ndiye Jasmine aliyesemwa na Babra.


Picha mbili zilinionesha nikiwa viwanja viwili tofauti vya ndege katika siku tofauti nikiwa na watu ambao sikuweza kuwafahamu, moja nikiwa uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere na nyingine nikiwa uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro.




Tulikuwa tumesimama katika eneo ambalo sikuweza kulifahamu vyema tukionekana kupanga mambo fulani, yule mwanamume sikumfahamu lakini yule msichana niliamini kuwa ndiye Jasmine aliyesemwa na Babra.


Picha mbili zilinionesha nikiwa viwanja viwili tofauti vya ndege katika siku tofauti nikiwa na watu ambao sikuweza kuwafahamu, moja nikiwa uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere na nyingine nikiwa uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro.


Picha ya mwisho ilinionesha nikitoka kwenye mlango wa ofisi ambao ulikuwa na maandishi ‘Ofisi ya Meneja’ huku nikisindikizwa na mwanamume mmoja mfupi mnene na mweusi, mazingira yalionesha kuwa ilikuwa ni ndani ya benki ambayo sikuifahamu lakini nilihisi huenda ndiyo ilikuwa Benki ya Wananchi.


Nilizitazama kwa makini zile picha nikashangaa sana, zilikuwa ni picha zenye sura yangu kabisa ingawa nilionekana nimenyoa nywele zote na kubaki na kipara na nilikuwa nimefuga ndevu nyingi!


Wazo la haraka likanijia akilini mwangu kuwa zile picha zilikuwa zimetengenezwa kwenye kompyuta kwa kuunganisha sura yangu na kiwiliwili cha mwanamume mwingine aliyekuwa na mwili kama wangu ili kutaka kunimaliza.


Hata hivyo, nililifuta lile wazo kwani nilijiuliza kuwa ikiwa walikuwa wameunganisha sura yangu na kiwiliwili cha mtu mwingine, je, walizipata wapi zile picha zenye sura yangu? Pia ukiziangalia kwa makini zile picha zilionekana kuwa halisi kabisa.


Lakini swali likabaki kuwa, mbona sijawahi kunyoa nywele zote kichwani kwa mtindo ule na wala sijawahi kufuga ndevu nyingi kwa mtindo ule kama ilivyoonekana kwenye zile picha? Kwa kweli nilijikuta nikianza kuchanganyikiwa.


“Mmezipata wapi hizi picha?” nilimuuliza yule ofisa wa usalama kwa mshangao.


“Hizi ni picha zilizopatikana kwenye camera za CCTV zilizowekwa katika maeneo husika isipokuwa hiyo uliyosimama na Jasmine ambayo ilichukuliwa kwa siri kutoka kwenye simu, je, bado unaendelea kusisitiza kwamba tumekufananisha?” alinijibu yule ofisa wa usalama huku akiniangalia kwa tabasamu.


“Huu ni uongo kabisa! Hizo picha siyo zangu, mtakuwa mmezitengeneza kwenye photoshop ili kunipakazia,” nilisema kwa hasira huku nikitaka kusimama pale nilipoketi.


Kabla sijafanikiwa kusimama nikashtukia nikitulizwa kwa kuzabwa kofi la sikioni lililonisababishia maradhi ya ukiziwi kwa dakika kadhaa.


“Tunazo njia nyingi za kukulazimisha uongee ukweli lakini sura yako nzuri inaashiria kuwa u mtu usiyependa matata, hivyo tusingependa kufikia huko endapo utashirikiana nasi,” yule ofisa usalama aliniambia, kisha akaunyanyua juu ule mkoba wake mweusi na kunionesha.


“Bado tuna ushahidi mwingi tu kukuhusu na kuna watu takriban kumi wanaokufahamu ambao wapo tayari kutoa ushahidi dhidi yako, lakini hapa si mahala pake kwa sasa,” alisema na kuirudisha ile bahasha kwenye ule mkoba.


Kisha nikamuona akimwashiria kitu yule ofisa usalama aliyekuja na Babra na mara yule ofisa usalama akaondoka na kutoka nje akiwa ameongozana na Babra.


Wakati Babra na yule ofisa usalama wakitoka mawazo mengi yakaanza kupita kichwani kwangu, nilijiuliza kuwa huenda ni kweli niliitwa Brown Senga na pengine nilikuwa nimekumbwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu maarufu kama ‘amnesia’.


Nikakumbuka kisa cha rafiki yangu Martin (katika mkasa uliopewa jina la Faraja) aliyewahi kupoteza kumbukumbu baada ya ajali, akaishi akiwa mtu mwingine kabisa, akaoa na kufanya kazi za vibarua vya kutwa, huku ndugu na jamaa zake wakiamini kuwa alikuwa amekufa!


Ajali iliyompata Martin ilisababisha ubongo wake kuhama kutoka katika sehemu yake ya kawaida na hivyo kupata tatizo la kupoteza kumbukumbu lililojulikana kama ‘retrograde amnesia’, yaani kutokuwa na uwezo wa kukumbuka taarifa zozote za kabla ya ajali hiyo.


“Okay, bila shaka sasa upo tayari kutueleza bila kuficha, wenzako wako wapi na silaha mlizopora mmezificha wapi?” yule ofisa usalama akaniuliza huku akiwa amenikazia macho.


“Sielewi kwanini mnang’ang’ania kuniuliza swali hilo, si mkawaulize hao watu mnaodai kuwa wana ushahidi dhidi yangu, eh?” nikamuuliza yule ofisa usalama na kabla sijamaliza nikashtukia nikizabwa makofi mawili ya nguvu yaliyonipa kisulisuli.


“Tuambie Brown, washirika wenzako wako wapi na silaha mmezificha wapi?” yule ofisa aliniuliza tena akionekana kuanza kupandwa na hasira.


“Sasa kwanini mnanipiga, kosa langu ni lipi?” nilimuuliza yule ofisa usalama kwa hasira.


“Mimi ningekuwa nafahamu chochote kuhusu hizo silaha mnazozizungumzia ningekwisha waambia mahali zilipo, sina sababu ya kuwasumbua,” nilisema huku nikiwa nimekasirika sana.


“Hivi unafahamu kuwa kushiriki kitendo chochote cha ugaidi na kutaka kuifanya nchi isiwe na amani ni uhaini na malipo yake ni kifo?”


“Nafahamu,” nikajibu kwa kifupi.


“Okay, mmezificha wapi na washirika wenzako ni kina nani?”


Kwa kweli nilijikuta nashindwa kujibu na kubaki nashangaa. Nikiwa bado natafakari neno la kusema mara mlango wa kile chumba cha mahojiano ukafunguliwa, akaingia mwanamke mmoja mrefu mwenye umbo zuri la kimazoezi na haiba ya kuvutia.


Mwanamke yule alionekana mchangamfu sana lakini akiwa makini kuliko hata simba jike, akiwa ameongozana na walinzi wawili.


Alikuwa na ngozi ya rangi ya maji ya kunde mwenye nywele nyeusi ndefu na laini alizokuwa amezifunika kwa kofia nyeusi ya kapelo. Alikuwa na sura ya duara na macho yake yalikuwa makubwa ya kike lakini yaliyokuwa makini zaidi.


Alikuwa amevaa miwani mikubwa ya macho na suruali ya Jamsuit ya rangi ya samawati iliyolionesha vyema umbo lake refu maridadi lenye kiuno chembamba lakini kilichokuwa imara kikiwa kimebeba minofu ya mapaja iliyokaza kutokana na mazoezi. Miguuni alikuwa amevaa buti ngumu za ngozi za rangi nyeusi.


Harufu nzuri ya manukato ghali aliyokuwa amejipulizia mwilini ilitamalaki mle ndani na kuzifanya pua zangu zipate uhai mpya na kunisahaulisha kwa muda masahibu ya kuhojiwa na wale maofisa wa usalama.


Maofisa wote wa usalama mle ndani walipomuona yule mwanamke wakasimama kwa ukakamavu na kwa heshima huku wakionesha utii mkubwa.


Kisha yule mwanamke akageuka kunitazama kwa utulivu kwa kitambo na kuachia tabasamu kabambe kabla hajanisogelea na kusimama jirani na mimi huku akiendelea kunitazama kwa uyakinifu zaidi na kubetua kichwa chake.


Nikamtambua, kwa kuwa nilikuwa nimemuona mara kadhaa kwenye vituo vya runinga vya CNN, Aljazira na BBC, na kusoma habari zake magazetini na kwenye mitandao ya intaneti. Alikuwa ni mwanamke wa kwanza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.


Mwanamke yule aliitwa Pamela au maarufu kama Madame Pamela na alikuwa na umri wa miaka 46. Historia ilionesha kuwa alikuwa amejikita kwenye kazi ya ujasusi kwa takriban miaka 25, hatua hiyo ilikuwa miongoni mwa sifa kubwa zilizomfikisha katika nafasi ile na kuwa mwanamke wa kwanza kuiongoza taasisi hiyo nyeti.


Madame Pamela ambaye alikuwa jasusi mbobezi aliwahi kulihudumia taifa katika masuala mbalimbali aliyopangiwa kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo ya juu na kuthibitishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa na baadaye kula kiapo cha utiifu.


Maelezo zaidi yalieleza kuwa kuthibitishwa kwa Madame Pamela kuwa bosi wa Usalama wa Taifa kulikuja baada ya malalamiko kuwa taasisi hiyo ilianza kupoteza imani na iliaminika kuwa Madame Pamela angeweza kurudisha imani kwa kuwa alikuwa makini na aliyefanya kazi zake kwa weledi mkubwa akiwa ameshiriki kwenye oparesheni nyingi tata.


Madame Pamela alikuwa komandoo, shushushu na jasusi wa kuogopwa aliyekuwa amepata mafunzo ya kijasusi kwa nyakati tofauti katika nchi za Israel, China na Marekani na alisifika kama ‘mwanamke wa chuma’ baada ya kuongoza kwa mafanikio kikosi maalumu cha usalama cha nchi za Afrika Mashariki kilichopewa kazi ya kuwahoji watuhumiwa wa matukio ya ugaidi waliokuwa wamehusishwa na kundi la Al Shabab baada ya matukio ya kigaidi kutawala katika nchi za Afrika Mashariki.




Madame Pamela alikuwa komandoo, shushushu na jasusi wa kuogopwa aliyekuwa amepata mafunzo ya kijasusi kwa nyakati tofauti katika nchi za Israel, China na Marekani na alisifika kama ‘mwanamke wa chuma’ baada ya kuongoza kwa mafanikio kikosi maalumu cha usalama cha nchi za Afrika Mashariki kilichopewa kazi ya kuwahoji watuhumiwa wa matukio ya ugaidi waliokuwa wamehusishwa na kundi la Al Shabab baada ya matukio ya kigaidi kutawala katika nchi za Afrika Mashariki.


Alijiunga na idara ya Usalama wa Taifa akiwa na umri wa miaka 21 tu, ilikuwa ni baada tu ya kuhitimu masomo yake katika Chuo Kikuu cha Kentucky, na amewahi kuwa mkuu wa vitengo mbalimbali vya ujasusi, ikiwamo cha kupambana na ugaidi kilichofanya kazi nzuri sana ili kuhakikisha Tanzania na nchi za Afrika Mashariki zinakuwa salama.


Jina lake kamili aliitwa Pamela Mtokambali akiwa amekulia katika nchi za Tanzania, Uingereza na Canada ambako baba yake, Aleck Mtokambali aliyekwenda kufanya kazi kama balozi akiiwakilisha nchi ya Tanzania katika nchi hizo.


Madame Pamela alianza elimu yake ya msingi nchini Tanzania kisha akaendelea nchini Uingereza na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Kentucky, ambako alihitimu Shahada ya Sanaa katika Sayansi ya Jamii.


Kisha alisoma Shahada ya Umahili katika Mawasiliano, Lugha na Uandishi katika Chuo Kikuu cha Technion – Israel Institute of Technology cha nchini Israel na baadaye akasoma na kuhitimu Shahada ya System Analysis katika chuo hicho hicho.


Tangu alipojiunga na idara ya Usalama wa Taifa akiwa na miaka 21 Pamela ameshiriki operesheni tofauti kama jasusi wa taasisi hiyo katika nchi mbalimbali. Operesheni ya kwanza aliyopangiwa kufanya ilikuwa nchini Sudan katika eneo la Darfur.


Baadaye alishiriki na kusaidia oparesheni za majeshi ya umoja wa nchi za Afrika kukikomboa kisiwa cha Anzuwani kutoka mikononi mwa majeshi ya Muhamad Bakari katika visiwa vya Comoro.


Kisha alishiriki katika oparesheni za kiintelijensia na kijasusi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Cameroon na nchini Lebanon kwenye oparesheni maalumu za kupambana na ugaidi.


Ni huko Lebanon alikofanya oparesheni kabambe ya kupambana na ugaidi iliyofanikiwa sana na kumpa sifa kubwa huku ikikaribia kuyagharimu maisha yake na kumwachia makovu mawili ya risasi yaliyokuwa kwenye paja lake la mguu wa kulia na kovu jingine la kisu lililokuwa kwenye bega lake.


Ilisemekana kuwa kila sehemu aliyopelekwa alifanya kazi kwa umakini mkubwa na kupata mafanikio. Kisha alitajwa kuwa ofisa mtendaji wa kikosi cha kupambana na ugaidi kabla ya kuwa ofisa mtendaji wa idara ya rasilimali watu ndani ya idara ya Usalama wa Taifa.


Pamela Mtokambali aliwahi kuolewa na mwanausalama mwenzake na shushushu aliyebobea, James Gayo ambaye aliwahi kuwa naibu mkurugenzi mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa kabla ya kuteuliwa na Rais kuwa Mbunge na Waziri wa Utawala Bora, na ndoa yao ilidumu kwa miaka tisa tu kisha wakatalikiana.


Ilisemekana kuwa baada ya Madame Pamela kutalikiana na mumewe hakutaka kuolewa tena na walibahatika kuwa na mtoto mmoja wa kike huku ikisemekana kuwa Madame Pamela alikuwa hatumii kabisa mitandao ya kijamii…


‘Hmm… kama baba shushushu aliyebobea na mama naye shushushu aliyebobea sijui mtoto wao atakuaje!’ niliwaza na hapo nikajikuta nikitamani kucheka.


“Mmefanya kazi nzuri sana kumkamata huyu jasusi hatari…” sauti ya Madame Pamela ilinizindua kutoka kwenye lindi la mawazo na hapo nikainua uso wangu kumtazama Madame Pamela kwa makini.


“Kwa taarifa za uhakika, jina lake halisi ni Brown Senga, si Mtanzania kama anavyotaka kuwaaminisha watu ila ni Mnyarwanda wa kabila la Kihutu aliyeingia nchini na wazazi wake akiwa na miaka kumi kipindi kile cha mauaji ya kimbali yaliyoikumba nchi ya Rwanda, na taarifa tulizonazo ni kwamba hajawahi kuukana uraia wa Rwanda ambako ndiko chimbuko la wazazi wake. Alijifunza vizuri Kiswahili na kumalizia elimu yake ya msingi na baadaye akapata elimu ya sekondari hapa Tanzania akitumia jina la Godwin Sengerema. Umri wake ni miaka therathini na mbili…


“Huyu ni jasusi hatari sana, mbobezi wa ujasusi wa kimtandao ambaye amekuwa akikodiwa kupanga matukio ya kigaidi kwenye nchi tofauti za Kiafrika… ndiye aliyeratibu tukio la kigaidi katika mkutano wa Bulawayo nchini Zimbabwe ambao Rais wa Zimbabwe alinusurika kuuawa na guruneti. Tunazo video kutoka uwanja wa michezo wa White City siku ya tukio, na kuna picha zilizopigwa na watu wa usalama siku ile mkutano wa rais wa nchi hiyo uliposhambuliwa na guruneti, baada ya kumshuku kutokana na mazungumzo yake…


“Pia anahusishwa kupanga tukio la mlipuko wa guruneti katika mkutano wa Waziri Mkuu wa Ethiopia kwenye bustani kuu ya Meskel mjini Addis Ababa, ambapo watu 83 walijeruhiwa huku 6 wakiwa katika hali mahututi. Yapo matukio mengine anayohusishwa nayo katika nchi za Rwanda, Burundi, Kenya na mashariki mwa DR Congo,” Madame Pamela alitoa maelezo yaliyonishtua sana.


“Alisoma katika chuo cha Technion – Israel Institute of Technology akitumia jina la Godwin Sengerema na amewahi kuwa Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha TEHAMA, kabla hajaacha kazi na kuamua kwenda nchini Rwanda ambako aliondoka tena kurudi nchini Israel, safari hii akitumia pasipoti ya Rwanda yenye jina la Brown Senga na alijiunga na Chuo kikuu cha Birzeit kusomea uhandisi wa umeme na inasemekana kuwa akiwa nchini Israel alitumia pia mwanya huo kujiunga na programu maalumu ya kijasusi na kupata mafunzo ya kujihami, hasa karate na judo, na kufanikiwa kupata mkanda mweusi, kiwango cha third degree…


“Baadaye akaenda nchini Zambia ambako aliajiriwa kama mkufunzi wa uhandisi umeme katika taasisi ya Electrical Maintenance Lusaka Ltd iliyopo jijini Lusaka, alikofanya kazi kwa miaka miwili tu akaacha na kurudi tena Tanzania akitumia jina la Godwin Sengerema na kuamua kujikita kufanya biashara ya madini.


“Kwa kipindi fulani aliondoka nchini katika mazingira ya kutatanisha akaelekea nchini Rwanda ambako alitumia tena pasipoti ya Rwanda yenye jina la Brown Senga na kwenda nchini Libya, inaaminika kuwa huko alipata mafunzo zaidi ya ujasusi na kuwa 'mhalifu wa daraja la kwanza' na ndipo alipoanza rasmi harakati za ugaidi kwa kukodiwa huku akijificha kwenye kivuli cha mfanyabiashara wa madini kutoka Tanzania…” kufika hapo Madame Pamela akaweka tena kituo kidogo na kuendelea baada ya kukohoa kidogo ili kusafisha koo lake.


“Amekuwa akipanga mambo yake kwa ustadi mkubwa huku akihakikisha washirika wenzake hawajuani na wala hawamjui bosi wa uhalifu na huwa haachi alama, moja ya vitu vinavyomsaidia kufanya matukio ya uhalifu kwa mafanikio bila kuhusishwa wala kuacha alama ni uwezo wake wa kupanga mikakati ya utekelezaji! Ni dhahiri kuwa mafunzo ya kijasusi aliyoyapata yamemsaidia sana kuwa mwanamkakati mzuri wa kiufundi wa matukio!


“Kwanza kabisa Brown huzuru eneo analotaka kufanyia uhalifu kazi ambayo huifanya kwa umakini mno, kisha hutafiti juu ya tukio lenyewe atakavyolitekeleza kwa kusoma mandhari yanayozunguka eneo husika na akishajiridhisha hutafuta washirika anaodhani watamfanyia kazi, huwalenga hasa watu wenye makandokando kwa kuwatishia kutoa siri zao nje endapo hawatampa ushirikiano…


“Kwa mfano, kwenye lile tukio la kigaidi la wizi mkubwa wa pesa katika Benki ya Wananchi alitafiti na kudukua mawasiliano yao ndipo alipojua siku ambazo wanakuwa na kiasi kikubwa cha fedha na kuwatafiti wafanyakazi wa benki husika akizingatia kuhusu zamu zao za kazini, udhaifu wao, vitu wanavyopendelea na haiba zao…


“Alipogundua udhaifu wa meneja wa benki hiyo, Lister Manda kuwa aliwahi kuhusika kwenye mauaji ya watu wenye ualbino, hasa tukio la kumteka na kumuua binti mdogo wa miaka kumi mwenye ualbino kutoka mkoani Geita kisha akachukua viungo vyake na kuvizika katika nyumba yake na eneo hilo kupanda mti wa matunda ili mambo yake yafanikiwe, basi akaamua kumtishia kutoa siri endapo angekataa. Kwa sasa meneja huyo tunamshikilia na tutamfikisha mahakamani…




“Alipogundua udhaifu wa meneja wa benki hiyo, Lister Manda kuwa aliwahi kuhusika kwenye mauaji ya watu wenye ualbino, hasa tukio la kumteka na kumuua binti mdogo wa miaka kumi mwenye ualbino kutoka mkoani Geita kisha akachukua viungo vyake na kuvizika katika nyumba yake na eneo hilo kupanda mti wa matunda ili mambo yake yafanikiwe, basi akaamua kumtishia kutoa siri endapo angekataa. Kwa sasa meneja huyo tunamshikilia na tutamfikisha mahakamani…


“Na ukichunguza vizuri utagundua kuwa matukio mengi ambayo Brown anahusishwa kuyaandaa yametekelezwa jioni ya siku ya Ijumaa ya mwisho wa mwezi na hii ni mbinu inayomsaidia sana na huitumia siku hii kwa sababu za kisaikolojia kwa kuwa jioni ya Ijumaa ya mwisho wa mwezi watu wengi wanakuwa hawako makini kutokana na weekend kuanza, na hata tukio la ugaidi na uporaji wa silaha katika bohari kuu ya silaha kule Kwembe lilifanyika jioni ya Ijumaa ya mwisho wa mwezi,” Madame Pamela alimaliza taarifa yake na kunikazia macho yenye ghadhabu.


Loh… taarifa zile zikasababisha kutokea kitambo kirefu cha ukimya mle ndani ya chumba kile cha mahojiano huku watu wote wakinitazama kwa mashaka utadhani walikuwa wameona kiumbe cha ajabu kutoka sayari nyingine.


Kwa kweli nilishtushwa sana na taarifa zile na kwa kiwango fulani nilijikuta nikianza kukata tamaa ya kuokoka katika mkasa ule. Kwa wasifu ule niliamini kabisa kuwa huyo mtu aliyeitwa Brown Senga alikuwa mtu hatari sana kuliko hata hatari yenyewe. Hata hivyo, sikuacha kujitetea.


“Uongo mkubwa, mimi siyo Brown Senga mnayemzungumzia, nipo tayari kuthibitisha hilo…” nilijaribu kujitetea na kabla sijamaliza kusema ofisa mmoja wa usalama aliyekuwa amesimama karibu yangu akanizaba kibao kikali cha uso na kunisababishia maumivu makali.


“Hujaulizwa, unajibujibu nini!” alisema kwa ukali.


Nilikaa kimya huku nikiugulia maumivu, na muda ule ule nikamshuhudia Madame Pamela akiongea jambo kwa sauti ya chini na yule ofisa mkuu wa usalama aliyekuwa akinihoji, na katika maongezi yao walijitahidi sana kutumia maneno maalumu ya mafumbo ya kiintelijensia ambayo sikuweza kabisa kuelewa yalikuwa yanamaanisha nini.


Baada ya majadiliano mafupi mwishoni nikamsikia Madame Pamela akitamka maneno yaliyoninyong’onyesha zaidi.


“Tunahitaji taarifa zote muhimu kutoka kwa mtu huyu kwa namna yoyote ile. Nimeshawasiliana na Pay Master, ameniambia apelekwe CMI kwa mahojiano maalumu,” alisema Madame Pamela na kuanza kupiga hatua kuondoka huku yule ofisa mkuu wa usalama na wale maofisa usalama wengine wakiinuka.


Muda ule ule wale maofisa wa usalama walionileta mle ndani wakanizingira huku wakinielekezea bastola zao kichwani, kuona hivyo nikafumba macho yangu.


Moyo wangu ukapiga kite huku akili yangu ikisimama na baridi nyepesi ikaanza kusambaa mwilini.


“Mnataka kunifanya nini?” nikawauliza wale maofisa usalama kwa wasiwasi huku nikiitupia jicho saa yangu ya mkononi iliyonitanabaisha kuwa ilikuwa tayari saa tano usiku.


“Unajali nini wewe, tunakupeleka sehemu salama zaidi ambako utaweza kutueleza bila usumbufu kuhusu washirika wenzako na mahali mlikozificha silaha,” alinijibu yule ofisa usalama aliyekuwa ameshika pingu na kusimama mbele yangu huku akiachia tabasamu la kifedhuli usoni mwake.


Nikabaki kimya nikiwatumbulia macho huku jasho jepesi likinitoka sehemu mbalimbali za mwili wangu. Badala ya ubaridi sasa joto la woga wa aina yake likaanza kunitambaa mwilini na mapigo ya moyo wangu yakibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!


Alinifunga zile pingu mikononi kisha nikaongozwa kuelekea nje ya kile chumba nikiwa chini ya ulinzi mkali. Hapo nikajua kuwa safari ya kuelekea kwenye mateso zaidi ilikuwa imeanza na kwa kweli sikuweza kufahamu vizuri ni wapi nilikuwa napelekwa.


Maofisa wawili walibeba mizigo yangu na kutufuata nyuma, hadi tulipotokea kwenye lango moja ambako kulikuwa na eneo tulivu kabisa.


Hapo nje tuliyakuta magari matano maalumu kwa ajili ya misafara ya kusafirisha wahalifu hatari na eneo lote lilikuwa limetanda askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu hatari kama ujasusi, uzandiki, hujuma na ugaidi waliokuwa wamejiweka tayari muda wote kwa ajili ya kuboresha ulinzi.


Wale askari walikuwa wamevaa kofia nyekundu za bereti kichwani, fulana za rangi ya hudhurungi, suruali za kombati na buti ngumu za ngozi miguuni.


Walikuwa vijana warefu na wakakamavu wakiwa imara kabisa. Wote walikuwa wameshika bunduki aina ya Sub Machine Gun mikononi tayari kuzitumia wakati wowote endapo ingetokea rabsha yoyote.


Nilipowatazama usoni sikuona mazingira yoyote ya urafiki katika nyuso zao.


Katikati ya yale magari kulikuwa na gari moja maalumu lenye muundo maalumu wa magari yanayotumiwa kusafirishia watuhumiwa hatari duniani kama wahaini dhidi ya serikali, magaidi hatari au watuhumiwa wa mauaji ya kimbari na wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya waliokamatwa na vyombo vya dola.


Nilifunikwa kichwani na mfuko mweusi ulionifanya nisiweze kuona chochote na kupandishwa sehemu ya kati ya lile gari kwenye chumba kidogo kilichopakana na ukuta wa nyaya ngumu pande zote ili kumtenganisha mtuhumiwa hatari na dereva wa lile gari kwa upande wa mbele na walinzi wa msafara kwa upande wa nyuma.


Muda uleule mlango wa kile chumba cha gari nilichoingizwa ukafungwa kwa nje kisha askari wengine wa kikosi maalumu wakapanda na kukaa kwenye sehemu ya nyuma ya lile gari.


Bila kupoteza muda madereva wakatia moto magari na hapo safari ikaanza. Kwa namna ilivyokuwa nilihisi kuwa msafara wetu wa magari matano uligawanywa kwa magari mawili kutangulia mbele yetu na mawili yalikuwa nyuma yetu.


Safari ya kutoka pale katika eneo la uwanja wa ndege wa Julius Nyerere ikawa imeanza na kwa kweli sikuweza kufahamu vizuri jiografia ya eneo tulilokuwa tukielekea kwa vile usoni nilikuwa nimefunikwa ule mfuko mweusi.


Hata hivyo, hisia zangu zilinitanabaisha kuwa baada ya kutoka pale uwanja wa ndege magari yaliingia katika Barabara ya Nyerere na kukata kona yakiingia upande wa kulia kisha safari ya kuelekea mjini ikashika kasi.


Kwa hisia tu nilibaini kuwa msafara wetu ulitanguliwa na pikipiki maalumu yenye king’ora kwa ajili ya kuyataka magari mengine yaliyokuwa barabarani yakae kando wakati tukipita.


Kwa kweli kwa jinsi msafara ule ulivyokuwa umeshika kasi utadhani aliyekuwa akipita barabarani alikuwa Rais wa nchi nilijikuta nikikata tamaa japo sikuwa na mpango wa kutaka kutoroka.


Wakati tukiendelea na safari nilitamani sana kujua tulikokuwa tukielekea lakini sikuweza. Nilianza kujilaumu sana kwa kutomsikiliza Susan, niliamini kuwa alikuwa na maono aliponitaka niahirishe safari yangu lakini nikakataa.


Nikajikuta nikiilaumu sana siku hiyo ambayo ilikuwa ya hekaheka sana kwangu, maana katika kipindi cha saa kumi na mbili tu tayari nilikuwa nimekwishapata jambajamba mara mbili kwenye viwanja vya ndege viwili tofauti!


Maana kabla ya mkasa huu wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, nilikuwa nimepatwa na mkasa uliofanana na huo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Schiphol jijini Amsterdam, katika siku hiyo hiyo moja ya safari! Kwa kweli siku hiyo ilikuwa ni siku ya hekaheka!




Wakati tukiendelea na safari nilitamani sana kujua tulikokuwa tukielekea lakini sikuweza. Nilianza kujilaumu sana kwa kutomsikiliza Susan, niliamini kuwa alikuwa na maono aliponitaka niahirishe safari yangu lakini nikakataa.


Nikajikuta nikiilaumu sana siku hiyo ambayo ilikuwa ya hekaheka sana kwangu, maana katika kipindi cha saa kumi na mbili tu tayari nilikuwa nimekwishapata jambajamba mara mbili kwenye viwanja vya ndege viwili tofauti!


Maana kabla ya mkasa huu wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, nilikuwa nimepatwa na mkasa uliofanana na huo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Schiphol jijini Amsterdam, katika siku hiyo hiyo moja ya safari! Kwa kweli siku hiyo ilikuwa ni siku ya hekaheka!


Alfajiri ya siku ile nikiwa na Susan na binti yetu, Pamela aliyekuwa na miaka minne, tulitoka nyumbani kwetu Stadsdeel Nieuw-West jijini Amsterdam na kuelekea katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Schiphol.


Tulifika pale uwanja wa ndege asubuhi ya saa kumi na mbili kasoro dakika ishirini, ikiwa ni dakika hamsini kabla ndege niliyotarajia kusafiria nayo haijaruka.


Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Schiphol jijini Amsterdam, ambacho jina lake kamili kwa Kiholanzi kikiitwa Luchthaven Schiphol, kilikuwa kiwanja kikubwa sana cha kisasa kikiwa kati ya viwanja vya ndege vikubwa duniani chenye kupokea abiria zaidi ya milioni 46 kwa mwaka, idadi iliyokifanya kushika nafasi ya tatu barani Ulaya na nafasi ya 12 duniani.


Kiwanja hicho cha ndege kipo kilomita 9 kusini magharibi ya Amsterdam katika manispaa ya Haarlemmermeer kikiwa na kituo (terminal) kikubwa kimoja kilichokuwa kimegawanywa katika vituo vikubwa vitatu vya kuondokea (Departure Halls).


Tulifika pale uwanjani tukaingia moja kwa moja katika eneo la chini la Departure Hall 2 kwenye geti namba E-10 na haraka haraka nilikaanza mchakato wa kukamilisha taratibu zote za uhamiaji pale uwanja wa ndege kabla ya kuondoka.


Niliwaacha Susan na Pamela wakilinda mizigo yangu nikapanga foleni kwenye dirisha la ofisi ya uhamiaji pale uwanjani kisha nikapenyeza vibali vyangu vyote vya kusafiria kwenye dirisha dogo la kioo la chumba kilichomhifadhi msichana mmoja mlimbwende aliyekuwa na sura ya uchangamfu.


Msichana yule ofisa uhamiaji akavipokea vibali vyangu vya kusafiria huku akiliachia tabasamu lake maridhawa na kulifanya lizisumbue fikra zangu.


Japo mchumba wangu Susan alikuwa mrembo kwelikweli lakini nilikuwa mgonjwa kwa walimbwende kama huyu na sikuwa nikiridhika, nilimtamani kila msichana mrembo niliyemuona mbele yangu.


Mambo yote yalikuwa chapuchapu kwani yule ofisa uhamiaji alimaliza haraka kuingiza taarifa zangu kwenye kompyuta yake kisha akagonga mhuri kwenye hati yangu ya kusafiria na hivyo safari yangu kuelekea nchini Tanzania ikawa imeidhinishwa rasmi.


Bila kupoteza muda nikaipokea pasi yangu ya kusafiria na kuitia mfukoni huku tabasamu langu la kichokozi likichomoza na kuzisumbua vibaya hisia za yule ofisa uhamiaji.


Kisha nikanyoosha mkono wangu kumpa, wakati tukipeana mkono wa kuagana na yule ofisa uhamiaji nikapitisha kidole changu cha shahada katikati ya kiganja chake kumtekenya, kitendo kile kikamfanya yule ofisa uhamiaji ashtuke na kuruka huku akiutoa haraka mkono wake kutoka kwenye kiganja changu.


Sikuishia hapo, nikamkonyeza kidogo kumchombeza lakini nikihakikisha Susan haoni kitendo kile. Nikashukuru kuwa Susan alikuwa hajashtukia mchezo ule vinginevyo kwa jinsi nilivyokuwa namfahamu Susan, kwa vyovyote moto ungewaka palepale.


Wakati yule ofisa uhamiaji akiwa bado ana mshangao usoni kwake nikamnong’oneza kuwa siku nikirudi Amsterdam nitamtafuta, kisha nikanza kuzitupa hatua zangu kwa utulivu kuliacha eneo lile.


Yule ofisa wa uhamiaji hakujibu bali alibaki ameduwaa huku macho yake yakinisindikiza nyuma yangu hadi pale nilipopotea mbele ya macho yake.


Kwa kusaidiwa na mchumba wangu Susan tulichukua mizigo yangu na kwenda kupanga foleni kwa ajili ya ukaguzi wa mizigo.


Wakati zamu yangu ikikaribia mara nikahisi mchafuko mbaya wa tumbo huku dalili za kuendesha zikiibuka. Katika hali ile nilijikuta nikihitaji sana kukimbilia maliwatoni hivyo nilikuwa natweta huku jasho likinitoka.


Kutokana na hali ile ya kubabaika, ofisa mmoja wa usalama wa eneo lile aliniona akanishtukia kisha alituchukua kando mimi na Susan kwa ajili ya upekuzi zaidi wa mizigo yetu.


Na baada ya kufanya upekuzi wa mizigo yangu katika kila eneo yule ofisa usalama aliomba usaidizi wa kupata ofisa mwingine ili kufanya upekuzi zaidi.


Wakati tukimsubiri ofisa usalama mwingine afike ndipo nikafanya kosa kubwa kwa kumwambia yule ofisa usalama kuwa nilihitaji sana kwenda maliwato kwa kuwa nilikabiliwa na mchafuko wa tumbo.


Yule ofisa usalama alinitazama kwa makini zaidi kisha akaniuliza ikiwa nilikuwa nimekula au kunywa chochote kibaya usiku wa kuamkia alfajiri ile nami nilimjibu kuwa sikuwa nimekula wala kunywa chochote kibaya.


Aliniuliza tena ikiwa nilimhitaji daktari wa kunichunguza tumbo langu ili kujua kilichokuwa kikinisumbua, nikasema nilikuwa sawa, bali nilichohitaji ilikuwa kwenda maliwatoni tu.


Yule ofisa usalama alinitazama katika mtizamo ambao baadaye niligundua kuwa hatukuwa tumeelewana kuhusu kilichokuwa kikinisumbua. Yule ofisa usalama alisisitiza kuwa mchafuko wa tumbo langu ulisababishwa na kumeza mihadarati niliyokuwa nikijaribu kuisafirisha.


Kwa kuwa hali ya mchafuko wa tumbo ilinifanya kutweta na jasho jingi kunitoka, yule ofisa usalama hakutaka kunipa nafasi ya kutoroka kutoka eneo lile wala kwenda maliwato.


Nilijaribu kumwelewesha lakini hakutaka kunielewa na mara nikawaona maofisa wengine wawili wa usalama wakifika eneo lile wakiwa na mbwa, na wakatuchukua mimi na familia yangu hadi kwenye kibanda maalumu cha walinzi wa uwanja ule na hapo tukasubiri ukaguzi zaidi wa mizigo yetu kwa kutumia mashine maalumu.


Baada ya ukaguzi nikachukuliwa tena hadi kwenye chumba maalumu cha mahojiano, ambako ofisa wa polisi alijaribu kuligusagusa tumbo langu wakati akiniuliza maswali kama nimeshawahi kusumbuliwa na tatizo la aina ile na kama kuna dawa zozote maalumu nilizozoea kutumia nilipotokewa na tatizo kama lile.


Nilimweleza kuwa “bila shaka huwa nakunywa Imodium, lakini sijanywa leo.”


Yule ofisa wa usalama aliniambia kuwa, nilipaswa kuwa na subira wakati tukimsubiri daktari ili anifanye uchunguzi wa tumbo langu.


Nilijaribu kumwelezea kuwa shida yangu haikuwa kumwona daktari bali nilihitaji huduma ya maliwato, lakini haikuwa rahisi kuniruhusu muda ule.


Tulisubiri pale kwa dakika kadhaa, mchumba wangu Susan na mwanetu Pamela walikuwa wanalia kilio cha kwikwi; wale maofisa wa polisi walionekana kucheka kwa dharau na kutusanifu. Hatimaye mtu mmoja alifika ili kunifanyia uchunguzi lakini niligundua kuwa hakuwa daktari bali ni ofisa usalama.


Niliamua kumuuliza yule ofisa usalama kuhusu uwezo wake wa kidaktari lakini niliambiwa kuwa sikuwa na uchaguzi mwingine bali kuwasikiliza. Niliondoka nikiongozana na yule ofisa usalama.


Tulifika kwenye mlango mmoja na kusimama, hapo yule ofisa usalama akanionesha kwa kidole huku akiniambia kuwa niingine maana kile kilikuwa chumba cha maliwato.


“Dah, hatimaye ninapata nafasi ya kujisaidia!” nikawaza kwa furaha.


Nilipoingia ndani ya kile chumba, yule ofisa usalama pia akaingia akinifuata. Nikiwa mle ndani nikagundua kuwa kile chumba kilikuwa ni choo maalumu cha kutolea dawa za kulevya kwa njia ya haja kubwa kama nilichokuja kukikuta katika uwanja wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Nilibaki nimeshangaa nikimtazama yule ofisa usalama lakini yeye aliniambia kuwa alikuwa anataka kushuhudia iwapo nilikuwa nasema ukweli au la! Na aliniambia kuwa iwapo nilitaka kujisaidia mbele yake hakuwa na shida.


Wakati nikitaka kumwomba anipishe kwa muda ili nijisaidie kwa uhuru zaidi nilijikuta nikishindwa kuhimili zaidi mchafuko wa lile tumbo, hivyo sikujali tena kama alikuwa akinishuhudia. Nilishusha haraka suruali yangu, nikaachia mzigo nikimwaga haja kama maji huku nikipiga mabomu ya kutosha.



Na Bishop Hiluka


Nilibaki nimeshangaa nikimtazama yule ofisa usalama lakini yeye aliniambia kuwa alikuwa anataka kushuhudia iwapo nilikuwa nasema ukweli au la! Na aliniambia kuwa iwapo nilitaka kujisaidia mbele yake hakuwa na shida.


Wakati nikitaka kumwomba anipishe kwa muda ili nijisaidie kwa uhuru zaidi nilijikuta nikishindwa kuhimili zaidi mchafuko wa lile tumbo, hivyo sikujali tena kama alikuwa akinishuhudia. Nilishusha haraka suruali yangu, nikaachia mzigo nikimwaga haja kama maji huku nikipiga mabomu ya kutosha.


Wakati nikiendeleaa kushusha mzigo nilianza kujisikia faraja kubwa na muda huo huo nikamtupia jicho yule ofisa usalama huku nikiachia tabasamu la faraja lililokuwa na swali: “vipi bado hujaamini?”


Yule ofisa usalama aliziba pua yake huku akijitahidi kuvumilia kilichokuwa kikiendelea mle maliwatoni. Baada ya takriban dakika moja na ushee, yule ofisa usalama alionekana kuridhika na kutoka huku akiendelea kuziba pua yake na kuniacha naendelea kuachia fataki za kutosha.


Nilimaliza na kujisafisha na niliporudi nilimkuta Susan akimalizia kufungasha vitu vyangu, hata hivyo yeye na mwanetu walikuwa bado wana wasiwasi maana hawakujua maofisa usalama walikuwa wamenipeleka wapi.


Ndege niliyopaswa kuondoka nayo iliondoka na kuniacha japo ilisubiri kwa dakika kadhaa, hivyo ilibidi nilipe tena malipo mengine ya asilimia ishirini ya kiwango halali nilichokuwa nimelipa awali ndipo nikapata nafasi ya kuendelea na safari yangu kuelekea Tanzania.


Sasa huku Tanzania nimekutana tena na hekaheka nyingine iliyofanana na hiyo ya Uholanzi. Lakini hekaheka ya Dar es Salaam ilionekana kuwa kubwa na sikujua ingeisha vipi…


______


“Wewe wacha kulala au unadhani upo gesti? Teremka haraka na usijaribu kufanya ujanja, utajuta!” sauti kali ya ofisa wa usalama aliyekuwa amenishika mkono wangu akinivuta niteremke kutoka katika lile gari ilinishtua na kunikatisha mawazo yangu.


“Nishuke kwani mnanipeleka wapi?” niliuliza huku hofu ikizidi kunizonga.


“Siyo kazi yako kujua unapelekwa wapi,” alijibu kwa ukali huku nikihisi mtu mwingine akiongezeka pale nilipokuwa.


Nilishtukia nikiwa nimedakwa mikono na miguu kisha nikashushwa kwa nguvu kutoka katika lile gari na hapo nikadakwa juu kwa juu ili nisianguke chini huku nikishangazwa na uharaka wa matukio yale.


Kwa uharaka sana na kwa wepesi wa hali ya juu nikashtukia nikibebwa juu juu kama jeneza kisha nikahisi kuwa walionibeba walikuwa wakitembea haraka na kwa hatua za ukakamavu.


Baada ya kitambo fulani cha mwendo wa kijeshi nilihisi walikuwa wanapanda ngazi za jengo na kisha wakaanza kuingia ndani ya jumba kubwa, sikuweza kuielewa vizuri jiografia ya eneo lile kwa sababu nilikuwa bado nimefunikwa kichwa na ule mfuko mweusi.


Kisha walinitupa chini nikaanguka nikifikia kiuno na mgongo, hapo nilihisi maumivu makali sana yakisambaa mwilini. Mikono yenye nguvu ilinishika na kuniinua pale sakafuni nilipokuwa nimeanguka, nikasimama huku nikiugulia kwa maumivu makali.


Niliposimama kwa miguu yangu mwenyewe nikagundua haraka kuwa tulikuwa kwenye jumba kubwa la kale ambalo kwa vyovyote lilikuwa lina ulinzi mkali kila mahali.


Sikujua tulikuwa tumetumia muda gani kutoka uwanja wa ndege hadi kufika katika eneo lile na ni wakati gani tulikuwa pale kabla sijazinduliwa katika lindi la mawazo.


Kisha nilikokotwa kwa nguvu nikiongozwa kuelekea ndani zaidi ya lile jengo, na wakati tukielekea ndani zaidi nilihisi kuwa tulikuwa tunapita katika korido ndefu hadi mbele na hapo nikasikia mlango mkubwa ukifunguliwa kisha tukaingia na kutokea kwenye ukumbi mmoja mkubwa.


Sikuweza kuona tulikuwa wapi hasa na wapi tulikuwa tukielekea, hata hivyo hisia zangu zilinitanabaisha kuwa tulikuwa kwenye ukumbi mkubwa kisha tukashika uelekeo wa upande wa kushoto.


Baada ya kwenda mwendo mfupi tukakata kona na kushika uelekeo wa upande wa kulia kisha kushoto tena na baada ya muda tukaanza kuifuata korido nyingine ndefu. Muda wote huo ukimya ulikuwa umetawala.


Tulikuwa tukikatisha kwenye eneo lililokuwa na mazingira yenye utulivu wa kupita kiasi, wale maofisa usalama waliokuwa wakiniongoza kunipeleka nisikokujua walikuwa kimya kabisa na hapakuwa na maongezi yoyote baina yao.


Baada ya safari ya kitambo fulani tukipita kwenye korido ile ndefu tukaingia upande wa kulia tukikatiza katikati ya ukumbi ambao kwa hisia tu nilijua kuwa ulikuwa mdogo, kisha tukaifuata korido nyingine iliyokuwa ikielekea upande wa kushoto kabla ya kuzikuta ngazi zilizokuwa zikielekea eneo la chini la lile jumba.


Hapo tukaanza kuzishuka zile ngazi na kwa sababu nilikuwa sioni nilijikuta nikikanyaga ngazi vibaya na kuanguka kisha nikaburuzika kwenye zile ngazi hadi katika eneo la chini kabisa huku nikichubuka sehemu mbalimbali za mwili wangu.


Nikiwa hapo sakafuni mikono yenye nguvu ikanishika kwa nguvu na kuniinua na hapo nikagundua kuwa tulikuwa kwenye ukumbi mwingine ambao kwa kutumia mlango wangu wa sita wa fahamu niliweza kuhisi kuwa ulikuwa ukumbi mpana huku eneo lile likitawaliwa na hewa nzito.


Wasiwasi mkubwa ukaniingia, moyo wangu ukaanza kupiga kite kwa nguvu huku mwenendo wa mapigo yake ukianza kwenda katika utaratibu usio wa kawaida, miguu yangu ikaanza kuishiwa nguvu kama iliyoishiwa na damu na hivyo ikikaribia ganzi.


Hapo nikaanza kuhisi kuwa sikuwa sehemu salama bali nililetwa sehemu hatari zaidi isiyokuwa na utu, ambapo ningeweza kufanyiwa unyama wa kutisha na hata kuuawa na huo ndiyo ungekuwa mwisho wangu.


Kwa kweli nikaanza kujuta majuto ya firauni kwa kushindwa kumsikiliza Susan na kuahirisha safari yangu, pengine haya yote yasingenikuta.


Nikiwa bado nimesimama nilishtukia mkono wenye nguvu wa ofisa mmoja wa usalama ukinishika kwa nguvu kama kishada na kuanza kuniburuta huku nikiongozwa kupita katikati ya ule ukumbi.


Ili nisiumie nikajikakamua na kusimama sawasawa kisha nikaanza kupiga hatua nikitembea haraka, tukakatisha katikati ya ule ukumbi mpana na kuifikia korido nyingine iliyokuwa na kona mbili-tatu kwa kuwa tulikuwa tukikata kona kila baada ya hatua kadhaa, mara tupinde kushoto mara kulia.


Kisha tukanyooka mbele zaidi na baada ya kitambo kifupi tukawa tumefika kwenye kona ambayo nilidhani ndiyo ilikuwa kona ya mwisho iliyokuwa upande wetu wa kulia.


Hapo niligundua kuwa kulikuwa na mlango mkubwa madhubuti wa chuma, maana nilimsikia ofisa usalama mmoja akikukuruka kuufungua ule mlango na kisha akauvuta kwa nje. Mlango ukasalimu amri na kufunguka ukituruhusu kuingia ndani.


Niliongozwa kuingia ndani ya kile chumba ambacho sikujua kilikuwa cha ukubwa gani, lakini mazingira yalikuwa ya ukimya mno ulionitisha sana.


Hapo tulisimama kisha ofisa mmoja wa usalama akanifungua ule mfuko mweusi niliokuwa nimefunikwa kichwani. Nikajaribu kuyakodoa macho yangu ili nione kilichokuwemo mle ndani.


Nilijiona nikiwa kwenye chumba kikubwa kilichokuwa chini ya ardhi kikiwa na kuta imara lakini hakina dirisha na kikiwa na kioo kipana ukutani ambacho kilimfanya mtu aliyekuwemo mle ndani asiweze kumuona mtu aliyekuwa nje ya chumba lakini yule mtu wa nje aliweza kumuona vizuri mtu aliyekuwa mle ndani.


Nilipozidi kutupa macho huku na huko nikaweza kuyaona mandhari ya chumba kile kikubwa. Katikati ya chumba kile niliona viti vitatu na meza kubwa ya chuma iliyovitenganisha vile viti katikati, upande mmoja ukiwa na viti viwili na upande mwingine kulikuwa na kiti kimoja cha chuma.


Juu ya meza ile kulikuwa na balbu ya umeme ya mwanga usiokuwa mkali sana kutoka katika dari ya chumba kile ikiwa imening’inizwa kwa waya mwembamba na mrefu kutoka darini.





Nilipozidi kutupa macho huku na huko nikaweza kuyaona mandhari ya chumba kile kikubwa. Katikati ya chumba kile niliona viti vitatu na meza kubwa ya chuma iliyovitenganisha vile viti katikati, upande mmoja ukiwa na viti viwili na upande mwingine kulikuwa na kiti kimoja cha chuma.


Juu ya meza ile kulikuwa na balbu ya umeme ya mwanga usiokuwa mkali sana kutoka katika dari ya chumba kile ikiwa imening’inizwa kwa waya mwembamba na mrefu kutoka darini.


Na kwenye vile viti viwili vilivyokuwa upande mmoja wa ile meza kubwa ya chuma niliweza kuwaona wanaume wawili makamanda shupavu, warefu na wenye miili iliyojengeka imara waliokuwa wameketi wakinitazama kwa makini.


Kwa uelewa wangu kutokana na kupenda kutazama sinema za kijasusi niliweza kubaini kuwa kile kilikuwa chumba maalumu kwa ajili ya kumuhoji mtuhumiwa kwa mdomo bila kumsulubisha. Na hata kama wangetaka kufanya hivyo, basi wangetumia viungo vyao kama ngumi na mateke.


Wale wanaume wawili makamanda shupavu walikuwa wamevaa kombati za rangi ya hudhurungi, kofia nyekundu za bareti vichwani mwao na buti ngumu za ngozi miguuni.


Walikuwa wamekunja mikono ya magwanda yao na kuruhusu misuli yao imara ya mikononi iliyotuna kikamilifu kwa mazoezi ya nguvu yasiyokuwa na kikomo ionekane vyema.


Nilipowatazama kwa makini nikagundua kuwa walikuwa ni makomandoo waliofuzu vizuri katika medani za masuala ya kijeshi, na hata nyuso zao hazikuonesha mazingira yoyote ya urafiki.


Nilipochunguza vizuri nikagundua kuwa nyuma ya wale makamanda wa jeshi kulikuwa na mlango mwingine mkubwa wa chuma uliokuwa umefungwa.


Niliyahamisha macho yangu kutoka kwa wale makamanda na kuyapeleka juu ya ile meza ya chuma, hapo hofu ikaongezeka zaidi na moyo wangu ukashikwa na mfadhaiko huku ukienda mbio na kuunguruma sana kama uliopambana na kazi isiyo ya kiasi chake.


Niliiona nembo kubwa ya CMI – Central Military Intelligence, ambayo ni idara maalumu ya ujasusi ndani ya jeshi. Hapo jasho jembamba likaanza kunitoka huku nikiihisi hatari iliyokuwa mbele yangu, maana hii ilikuwa ni Idara iliyofanya kazi ya kukusanya taarifa hatarishi za kigaidi au za kijasusi dhidi ya nchi.


Sasa sikuwa na shaka yoyote kuwa nilikuwa nimefikishwa kwenye makao makuu ya idara maalumu ya ujasusi ndani ya jeshi ili kuhojiwa! Mara nyingi maeneo kama yale walifikishwa watu walioonekana kuwa hatari zaidi, kama magaidi waliokubuhu au majasusi waliobobea.

ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog