Search This Blog

Wednesday 29 March 2023

PENIELEA (3) - 5

  





Simulizi : Peniela (3)

Sehemu Ya Tano (5)



“ Katika maisha yangu sijawahi kukutana na vijana washenzi kama hawa.Bado sielewi mpaka leo hii wamewezaje kufanikiwa kunitia mikononi mwao.Tayari wamekwisha fahamu mambo mengi kuhusu mimi na kila ninachokifanya.Wameipekua kompyuta yangu kila mahala na wamegundua mambo mengi sana.Wamefahamu mambo yangu mengi ninayoyafanya,wamewafahamu washirika wangu wote.Ninaapa sintawasamehe hata kdogo.lazima niwafanyie kitu kibaya sana.Wameuwasha moto wenyewe na hawatauzima tena.Ni nani yuko nyuma yao? Lazima kuna mtu ambaye anawapa nguvu ya kuweza kufanya haya yote.Nina wasi wasi na Deus.Mimi na yeye kwa sasa ni maadui wakubwa na ninahisi yeye ndiye atakayekuwa nyuma ya hawa vijana na anawapa habari zangu kisha wakanivamia na kunishikilia.”akawaza Rose huku uso wake ukiwa umejikunja kwa hasira.Akaitazama mikono yake namna ilivyoumizwa ,akaviangalia vidole vyake vya miguu akakumbuka namna Mathew alivyovikata bila huruma..

“ Yule kijana amenisababishia ulemavu kwa kunikata vidolevyangu viwili.Amenitesa sana na kwa hili ninaapa sintomsamehe.Nitamsaka kila kona ya nchi hadi nihakikishe nimempata naye nimtese kama alivyonitesa mimi.Hataweza kunikimhia nina hakika ndaniyamuda mfupi nitakuwa nimempata.Mtandao wangu ni mkubwa na umesambaa kila kona.Nitampata tu.”akaendelea kuwaza Rose na kuketi kitini kwani alianza kuhisi maumivu mguuni.Akachukua simu yake na kuwapigia tena vijana wake kujua wamefika wapi na wakamuhakikishia kwamba wako karibu sana kufika.

“ Leo ninaiteketeza nyumba hii na watakaporejea watakuta imebaki majivu matupu na kila kitu chao kimeteketea .Lazima niwaonyeshe nguvu zangu.Wao na huyo anayewatuma watanitambua mimi ni nani.Watajuta kwa hiliwalilolianzisha .”akawaza Rose.

Baada ya dakika ishirini jaji Elibariki akaingia ofisini alimokuwa amekaa Rose akiwa ameongozana na vijana sita wakiwa na silaha.Vijana wale walistuka sana kwa haliwaliyomkuta nayo Rose.



“Pole sana madam.Who did this to you? Akauliza kijana mmoja aliyekuwa ameshika bastora na aliyeonekana ni kiongozi wa vijana wale.Rose akamtazama Elibariki kisha akatoa maelekezo kwa wale vijana wake



“Mkamateni huyo jamaa mfungeni,tunaondoka naye.Nimtu muhimu sana kwetu.Mwagieni petrol nyumba nzima na kisha tuichome moto nyumba yote.”akasema Rose na kisha akamuaangalia Anitha aliyekuwa amelala pale chini.

“Mchukueni hata huyu pia.Tunaondoka naye” akasema



“ Rose what is the meaning of this? We had an agreements!!!..jaji Elibariki akashangaa.

Rose akainuka akajitahidi kutembea kwa shida halafu akamnasa kofi.

“ You’ve betrayed your friends do you think I can believe you? Take him away ”Rose akawaamuru vijana wake.jaji Elibariki akafungwa pingu na kuanza kutolewa mle ndani.

“ Rose hivi sivyo tulivyokubaliana” akasema jaji Elibariki kwa nguvu lakini vijana wale wenye miili iliyojengeka wakamchukua kwa nguvu na kumfunga na kamba wakamrushia ndani ya gari.Anitha naye akachukuliwa na kurushwa ndani ya gari pamoja na Elibariki

“ Rose anafanya nini tena? Mbona anafanya kinyume na tulivyokubaliana?.Nimemsaidia kumuokoa lakini amenigeuka.Sikupaswa kabisa kumuamini huyu mwanamke.Maskini nyumba ya Mathew inataka kuteketezwa kwa moto.Sikujua kama huyu mwanamke ni mnyama kiasi hiki.”Mathew akastuliwa mawazoni na mlango uliofunguliwa na Naomi akarushwa ndani.



“ jaji nini kinaendelea? hawa watu ni akina nani? Tumevamiwa? mathew yuko wapi? Akauliza Naomi.

Vijana wawili wakamtegemeza Rose kwani alikuwa akisikia maumivu makali ya miguu kwa sababu ya vidole alivyokatwa na Mathew,wakampeleka katika gari.

Mlango wa nyumba ambayo Mathew huhifadhia magari yake ukavunjwa mle ndani yakakutwa magaloni manne ya mafuta ya akiba wakayachukua na kuyamimina ndani ya nyumba halafu wakapanda katika magari yao .Mmoja wao akawasha kiberiti akakirushia ndani na nyumba ikaanza kuwaka moto kisha wakaondoka.

“This is just the beginning .Wamenichokoza wao wenyewe na sasa ni zamu yangu kuwaonyesha mimi ni nani.Vijana wadogo kama wale hawawezi wakanifanya mimi namna hii.Wamenivamia nyumbani kwangu,wakamuua mpenzi wangu kwa risasi,wakaniteka na kunificha humu katika nyumba yao,wamenitesa mno na katu siwezi kukubali kuteswa na vijana wadogo kama hawa wasiokuwa na adabu hata chembe.Nitawasaka kila mahala na kuhakikisha nimewapata na mimi niwakate vidole vyao kama walivyonikata vyangu.Nitamsaka pia na anayewatumia ili kupambana na mimi ambaye nina hakika lazima atakuwa ni Deus.”akawaza Rosemary Mkozumi



.





*******







“ Peniela!..Peniela !!!..”akaita Mathew lakini Peniela hakuwa na nguvu kabisa.Umati wa watu ulianza kuongezeka katika mtaa ule wakija kushuhudia tukio lile la nyumba ya Peniela kuwaka moto .

Mathew akautazama moto ule mkubwa akavuta pumzi ndefu.

“ Hili si eneo salama tena.Team SC41 wameamua kuichoma nyumba ya Peniela kwa makusudi.They did this to me also and killed my wife.I have to save Peniela”akawaza Mathew na kumuinua Peniela akamuweka begani na kuondoka naye akapita kichochoro kadhaa na kutokea sehemu moja iliyokuwa na nyumba inayoendelea kujengwa akaingia ndani na kumlaza Peniela katika mojawapo ya chumba.Jasho jingi lilikuwa linamtoka akavua shati. Na kuanza kumpepea Peniela

“ Nilifanya vizuri kukataa kukaa pale kwa Peniela kama alivyokuwa ameniomba.Kumbe Team SC41 walikuwa wanamfuatilia kwa karibu sana kutaka kufahamu yuko wapi ,yuko na nani na anafanya nini.Hawa jamaa watamtafuta Peniela kila kona hadi wahakikishe wamempata kwani tayari wamekwisha gundua kwamba amewasaliti.Masikini Peniela jumba lake lote limeteketea kwa moto.Namuonea huruma sana kwa namna anavyoteseka.Ninaapa lazima nihakikishe kwamba ninamlinda kwa kila namna ninavyoweza.”akawaza Mathew na kisha akamuinamia peniea



“ Peniela ! Peniela..”akamtikisa kidogo na Peniela akafumba macho.



“ Ahsante Mungu:”akasema Mathew na kumuegemeza Peniela ukutani..



“ Unajisikiaje Peniela?akauliza Mathew



“ Mwili wote hauna nguvu kabisa.”akajbu Peniela

“Peniela.Jikaze kidogo na tondoke eneo hili.Eneo hili si salama kabisa kwetu kwa sasa”akasema Mathew



“ Mathew wamechoma nyumba yangu.Wameunguza nyumba yangu !! Peniela akaangua kilio

“ Shhh !!Peniela usilie tafadhali.Huu si wakati wa kulia”akasema Mathew



“ Mathew kila kitu changu wamekiteketeza.kwa nini wanifanyie hivi? Nimewafanyia mambo mangapi mazuri hadi wanifanyie hivi? akauliza Peniela huku machozi yakimwagika



“ peniela nadhani sasa umeelewa kwamba Team SC 41 si watu wazuri hata kidogo.Hata uwafanyie nini hawatakuthamini .Tunachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuelekeza nguvu katika kuhakikisha kwamba tunaipata package kutoka kwa Dr Joshua na baada ya hapo tutawageukia Team SC41.Ninakuhakikishia Peniela kwamba nitapambana hadi nihakikishe tumelifyeka kabisa kundi lote la Team Sc41 hapa nchini .Usijali kuhsu vitu vyako vilivyoungua.Utavipata vingine” akasema Mathew.



“ Mathew siwezi kukuficha nimeishiwa nguvu kabisa.Sikuwahi kuhisi kama team Sc41 wanaweza wakafikia hatua ya kunifanyia kitu kama hiki na kusahau mambo yote mazuri niliyowafanyia.Kama wameweza kunichomea nyumba yangu na kila kitu changu basi dakika yote wakinipata wataniua.Nitafanya nini Mathew?akauliza Peniela

“Peniela nitakulinda .Niamini nikwambiavyo kwamba nitakulinda” akasema Mathew



“ Mathew I don’t know if I can do this anymore”akasema Peniela.mathew akamuangalia

“Peniela anahitaji muda wa kutuliza akili yake.Tukio lile la kuishuhudia nyumba yake inateketekea limemuumiza sana” akawaza Mathew halafu akapapasa katika mifuko yake akachukua simu yake akaitazama kama iko salama



“ Thanks God simu yangu iko salama hata baada ya rabsha zile zote”akawaza Mathew na kuzitafuta namba za simu za Anitha akampigia.



“Hallow Mathew .What happened? Akauliza Anitha

“ Anitha tumepatwa na matatizo.Nahitaji msaada.Nataka uchukue gari utufuate sehemu nitakayokuelekeza ili uje utuchukue kwani Peniela hawezi kutembea.” Akasema Mathew lakini hakusikia Anitha akimjibu

“Anitha umenisikia? Akauliza lakini bado kulikuwa kimya na mara simu katika.Akapiga tena lakini simu ya Anitha haikuwa ikipatikana,akapiga namba nyingine za simu zilizomo mle ofisini lakini zote hazikupokelewa.



“ What happened? Kwa nini Anitha hataki kupokea simu? Akajiuliza



“ Nimeanza kuwa na hisia mbaya kwanini Anitha akatike ghafla simuni? Anyway ngoja nitafute msaada sehemu nyingine tena.Nani anayeweza kunisaidia muda huu? Akajiuliza Mathew



“ jason !..japokuwa mara ya mwisho tulikwaruzana lakini nina hakika akisikia kuhusu peniela lazima atakuwa tayari kumsaidia”akawaza Mathew na kuzitafuta namba za simu za Jason akampigia .Simu ikaita mara ya kwanza na kukatika.Ikaita mara ya pili ikapokelewa

“ Hallow Mathew” akasema jason



“ Jason samahani kwa kukupigia usiku huu.Nina shida nahitaji msaada wako.”



“Mathew I cant help you .Mara ya mwisho tulipoachana wakati tukitoka kwa John mwaulaya ulinitamkia maneno mabaya sana ya dharau . Siwezi kukusaidia Mathew hata iweje” akasema Jason

“ Josh its peniela.If you cant help me then help her” akasema Mathew

“ Peniela kafanya nini?



“Amepatwa na tatizo na anahitaji msaada”

Jason alipotajiwa jina la Peniela alishindwa kukataa,Mathew akamuelekeza sehemu ambayo atawakuta .

“ peniela nimempigia simu jason anatufuata .Jikaze tuondoke tuelekee sehemu ambayo tutakutana.” akasema Mathew akamuinua peniela wakatoka nje ya lile jumba.





Moto ule mkubwa uliokuwa unaiteketeza nyumba ya Peniela uliwafanya watu wengi waamke na kutoka katika nyumba zao wakaelekea katika eneo la tukio ili kujaribu kutoa msaada wa uokoaji.Ndani ya kipindi kifupi baada ya kupewa taarifa kikosi cha zimamoto kikawasili wakiwa na gari tatu kubwa zilizojaa maji na kuanza kuuzima ule moto wakisadiana na wananchi.Askari polisi pia walifika mahala pale kwa ajili ya kusaida katika uokoaji na ulinzi wa mali na usalama wa watu.Moto ulikuwa mkubwa sana na moshi mwingi ukaonekana angani.

Wakati jitihada za kuuzima moto ule zikiendelea kati ya kikosi cha zimamoto na wananchi,Mathew na Peniela walikuwa wanajikongoja kuelekea mahala ambako walipanga kukutana na Jason.Peniela hakuwa na nguvu za kutosha kutembea haraka ili kuwahi hivyo kuna nyakati ilimlazimu Mathew kumbeba mgongoni.Walifika katika sehemu ambayo walipanga wakutane na Jason.Ni katika kituo cha basi cha Msagaweni.Mathew akamkalisha Peniela katika kiti cha kupumzikia abiria .

“ Mathew thank you so much.Sintausahau usiku wa leo kwa namna ulivyonisaidia” akasema Peniela kwa sauti dhaifu.Mathew akamtazama na kusema



“ Usijali Peniela.Nilikuahidi kukulinda na nitafanya hivyo siku zote hata kama nitajiweka mimi hatarini ili wewe uwe salama.Tafadhali pumzika wakati tunamsubiri Jaso….”Ghafla akastuliwa na watu watatu waliotokea ghafla wakiwa na mapanga mikononi na kuwaamuru kusalimisha kila walichokuwa nacho.Peniela akatetemeka sana .Ghafla bila kutarajia Mathew akaichomoa bastora yake na kuwalekezea watu wale na kuwataka watimue mbio haraka sana.Kufumba na kufumbua vibaka wale wakatawanyika haraka sana kila mmoja na njia yake.Hawakutarajia kabisa kama Mathew alikuwa na bastora.

“ Mathew,eneo hili si salama hata kidogo .Kama usingekuwa na hiyo silaha vibaka hawa wangetuumza sana.” akasema Peniela kwa uoga..

“ Usiogope Peniela hakuna kibaka anayeweza kutufanya lolote.Nina risasi chache zimebaki katika bastora yangu zinatosha kutulinda” akasema Mathew na kuchukua simu yake akampigia Jason akamfahamisha kwamba tayari wamekwisha wasili katika eneo walilopanga wakutane.Baada ya kuwasiliana na Jason,akampigia tena Anitha lakini bado simu yake haikupatikana na kingine kilichomstua zaid hata zile simu zake nyingine ambazo huzitumia ofisini kwake hazikupatikana tena.



“ Whats going on? Kwa nini simu zote hata zile za ofisini hazipatikani ghafla? Hii haijawahi kutokea hata mara moja.Kuna kitu hakiko sawa hapa “ akawaza Mathew na kuchkua simu akapiga tena lakini hakukuwa na mabadiliko.Simu hazikupatikana.

“ Natakiwa kwenda nyumbani haraka.Something is wrong there” akawaza Mathew halafu akamgeukia Peniela

“ Peniela !!..unajisikiaje?



“ Mathew sina nguvu kabisa.Mwili wote hauna nguvu hata kidogo” akasema Peniela

“ usijali Peniela.Nimeongoea na Jason amesema yuko karibu sana kufika.”

Baada ya kama dakika kumi hivi kwa mbali likaonekana gari linakuja upande ule.Mathew akaweka bastora yake tayari halafu akamuamsha Peniela

“ Peniela kuna gari linakuja upande huu.Inawezekana akawa ni Jason au hata Team Sc41.Inuka tujiweke tayari” akasema Mathew na kumsaidia Peniela kuinuka kisha wakajibanza katika kona ya kituo.Gari lille lilikuwa linakuja kwa mwendo mkali sana na baada ya muda likawasili pale kituoni na kusimama.Mathew bastora ilikuwa mkononi tayari kukabiliana na lolote lile ambalo lingejitokeza lakini kupitia mwangaza wa taa ya gari akamuona Jason akishuka,akashusha pumzi.



“ Peniela Jason amefika” akasema Mathew halafu akajitokeza na kumuita Jason aliyekuwa akiangaza angaza akiwatafuta.Jason akawakimbilia na moja kwa moja akamuinamia Peniela

“ Peniela ! Peniela !..nini kimetokea? Akauliza Jason



“ Jason we need to get out of here fast” akasema Mathew na kusaidiana na Jason kumuinua Peniela hadi ndani ya gari kisha wakaondoka

“ Mathew nini kimetokea? Mbona unavuja damu kiasi hicho? Mmeshambuliwa? Akaulizia Jason kwa wasi wasi baada ya kumuona Mathew namna alivyochafuka damu

“ Jason kuna tukio limetokea usiku huu baya sana.” akasema Mathew na kumsimulia Jason kila kitu kilichotokea usiku ule.Jason akaogopa sana.

“ Mathew mnatakiwa mpelekwe kwanza hospitali mkapate matibabu.Jeraha lako linavuja damu nyingi.Hata Peniela naye anaonekana kuwa katika mshtuko mkubwa sana.Ouh maskini Peniela kwa nini ni yeye kila wakati anakutwa na mambo mabaya? Akasema Jason

“ Hapana Jason nipeleke kwanza nyumbani nikaangalie kama kuna usalama.Nina wasiwasi ana na usalama wa watu niliowaacha kule .” Akasema Mathew



” Sawa Mathew lakini kwa hali hii ulitakiwa kwanza matibabu”

“ Usijali Jason nipeleke kwanza nyumbani.Nina wasi wasi mkubwa kama nyumbani kwangu kuko salama” akasema Mathew akageuka na kumtazama Peniela aliyekuwa amelala katika kiti cha nyuma.

“ Jason samahani sana kwa kilichotokea siku ile.Nilikutamkia maneno ya kuudhi lakini nilifanya vile kwa ajili ya kukulinda wewe mwenyewe kwani nilifahamu ulichokuwa unataka kukifanya ni hatari sana kwa maisha yako.John mwaulaya japkuwa amefariki lakini alikuwa ni mtu hatari sana na mtandao wake pia ni hatari.Umeona kilichomtokea Peniela leo.Amewafanyia Team Sc41mambo mengi lakini hivi sasa wanamsaka kwa udi na uvumba na nyumba yake wameiwasha moto.” Akasema Mathew



“ John mwaulaya amefariki dunia? Akauliza Jason

“ Ndiyo Jason” akajibu Mathew



“ Ouh thank you Lord ! akasema Jason akionekana kufurahia kifo kile cha John lakini Mathew akamgusa na kumfanyia ishara kwamba hatakiwi kufurahia kifo kile cha John mbele ya Peniela.

“Mathew, mimi ndiye ninayepaswa kusema samahani kwa kitendo cha kukukosea heshima kwa maneno niliyoyatamka .Nilikutamkia maneno ambayo sikupaswa kukutamkia mtu kama wewe.Sikujua nini nilikuwa ninakiongea kwani niliongozwa na hisia zangu zaidi kutaka kufanya kitu ambacho sikuwa nakijua undani wake.Samahani sana Mathew naomba tusahau yaliyopita na tushikamane kwa ajili ya Peniela.Kama kuna jambo lolote ambalo unaona ninaweza kusaidia tafadhali usisite kunitaarifu” akasema Jason

“ Ahsante sana Jason.” Akasema Mathew na kuegemea kiti huku akiitumia fulana yake kugandamiza sehemu yenye jeraha kuzuia damu kuendelea kuvuja.

“ Nilichokuwa nataka kukifanya siku ile ni kitu cha kijinga sana.Nashukuru kwa Mathew kunitamkia maneno yale yaliyonifanya nikasirike na nisifanye kile ambacho nilikusudia kukifanya.Nilikuwa najipeleka katika mdomo wa mamba mimi mwenyewe.Hiki kilichomkuta Peniela leo kingeweza hata kunikuta mimi” akawaza Jason.



“ Nadhani ni wakati wa Peniela kuachana na kundi hili analoshirikiana nalo.Si watu wazuri hata kidogo na asipoangalia wanaweza hata kumuua.” Akaendelea kuwaza Jason wakati wakipana kilima na mara walipofika juu ya kilima akastuka baada ya kuuona moto mkubwa ukiwaka kutokea sehemu walikokuwa wanakwenda.

“ Mathew kuna moto mkubwa unawaka maeneo ya kule unakoishi” akasema Jason na kumstua Mathew aliyekuwa amefumba macho akitafakari.



“ ouh my God ! moto ule ni mkubwa sana lazima kuna nyumba nyumba itakuwa inaungua moto” akasema Mathew aliyestuka sana baada ya kuona moto ule



“ Yale ni maeneo ninapoishi kwani ni karibu na ule mnara wa simu.Pale jirani yangu kuna nyumba za wazungu wawili na nyingine za waswahili wenzangu.Ni nyumba ipi itakuwa inawaka moto? Akawaza Mathew



“ Usiku huu tayari nimekwisha ushuhudia moto mkubwa ukiteketeza nyumba ya Peniela na huku tena kuna mto unawaka, tena karibu na eneo ninaloishi.Mbona matukio ya moto yametawala usiku huu? Akajiuliza Mathew

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Bado taswira ya ule ya moto mkubwa ukiiteketeza nyumba na familia yangu inanijia kila usiku na baada ya kuuona moto ule mkubwa ukiiteketeza nyumba ya Peniela ,umekitonesha tena kidonda changu kilichokwisha anza kupona.Ninajiuliza nini lengo la kuichoma nyumba moto nyumba ya Peniela na kumkosesha makazi? Nitawasaka washenzi hawa wote na kuwashikisha adabu.Huu ni unyama uliopitiliza sana .” Akawaza Mathew huku wakikaribia sana maeneo anakoishi.Miale ya magari ya zimamoto ilionekana na ving’ora vya magari ya polisi yakiendelea kuja kwa kasi eneo lile vikasikika.Kadiri walivyozidi kusogea ndivyo moto ulivyoonekana kuwa mkubwa na mara wakakutana na kizuizi cha askari wakasimamishwa.Kulikuwa na magari ya polisi na mengine yameegeshwa pembeni..Askari mmoja mwenye silaha akawafuata na kuwasalimu na kuwaambia

“ Ndugu njia iimefungwa hakuna mtu anayeruhusiwa kupita mtaa huu.Kuna nyumba inaungua na kwa bahati mbaya ndani ya nyumba hiyo inasadikiwa kulikuwa na milipuko kwani baada ya moto kuanza imetokea milipuko mikubwa minne ambayo tunahisi yanaweza kuwa ni mabomu .Hali hiyo imefanya juhudi za kuuzima moto huo kushindikana kwani hatujui kama ndani ya nyumba hiyo kunaweza kuwa na milipuko zaidi ama vipi.Tunachokifanya kwa sasa ni kujitahidi kuzuia moto ule usiweze kusambaa katika nyumba za jirani na kusababisha maafa zaidi ” akasema Yule askari.Kwa mara ya kwanza Mathew alihisi miguu yake inaisha nguvu baada ya kusikia maneno yale ya askari.



“ Afande kuna mtu yeyote ameokolewa kutoka katika nyumba hiyo inayoungua? Akauliza Jason



“ Kwa mujibu wa watu waliowahi kufika eneo la tukio baada ya moto kuanza wanasema kwamba hawakuwahi kuokoa kitu chochote kile na hawajui kama ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na mtu .Eneo hili ni jipya na bado halina wakazi wengi kwa hiyo wengi walistuka kama kuna moto baada ya mlipuko wa kwanza kutokea na wakati huo tayari moto ulikwisha sambaa nyumba nzima kwa hiyo hakuna walichofanikiwa kuokoa zaidi ya kukimbia kujinusuru” akasema Yule askari na kuondoka

“ Mathew kuna nini? Mbona naona magari ya askari polisi na kule kuna moto mkubwa unawak? Akauliza Peniela kwa wasi wasi baada ya kuzinduka toka kwa wasiwasi



“ Peniela huku ni nyumbani kwangu.Kuna nyumba inaungua mta huu ndiyo maana tumezuiliwa hapa.” akasema Mathew huku sauti yake ikionyesha kitetemeshi ,aliogopa sana

“ Jason kwa maelezo ya Yule askari nina wasi wasi sana yawezekana ni nyumba yangu ndiyo inaungua kwa sababu nimehifadhi mabomu matano ya kutupa kwa mkono mle ndani na kuna silaha nyinginezo ambazo zinaweza kusababisha mlipuko” akasema Mathew huku akiufungua mlango na kutaka kushuka.

“ No Mathew usishuke.Umechafuka damu sana na eneo lote limetapakaa askari wanaweza wakataka kufahamu jeraha hili umelipata wapi.Ngona mimi nishuke nikajaribu kufanya uchunguzi nijue ni nyumba ipi inaungua.” Akasema Jason na kushuka



“ Mathew bado jeraha linavuja damu.Tutafanya nini kuzia damu hii isiendelee kutoka? Akauliza Peniela lakini Mathew hakumjibu kitu alikuwa anatetemeka kwa ndani

“ Mungu asaidie nyumba hiyo inayoteketea isiwe ni ya kwangu.” Akawaza.



“ Kama ni ya kwangu sijui nitafanya nini ” akaendelea kuwaza Mathew na kuchukua simu yake akapiga namba za Anitha na zile za nyumbani kwake lakini hakuna simu iliyopatikana akazidi kuogopa

“ Yawezekana Anitha na jaji Elibariki watakuwa wamekimbia na kujificha mahala baada ya moto huo kutokea katika nyumba ya jirani na yawezekana hii ni sababu iliyomfanya Anitha azime kila kitu hata simu zote.Kama ni hivyo watakuwa wapi? Jaji Elibariki anatafutwa na hatakiwi kuonekana hovyo hadharani.Nahisi watakuwa wamejificha mahala Fulani mbali kidogo na hapa ili kuepuka kuonekana.Halafu kule nyumba ya chini alikuwemo Rosemary lakini yeye simuhofii sana kwani hakuna anayeweza kufahamu kama kule chini kuna nyumba .Hata hivyo natakiwa kufahamu mahala walipojificha Anitha ,jaji Elibariki na Naomi na kama wako salama ama vipi” akawaza Mathew huku akiendelea kuangaza angaza kama angeweza kumuona Antha kutoka katika kundi la watu waliokuwepo eneo lile.

Ghafla Jason akarejea mbio na kuingia ndani ya gari akafunga mkanda na kumtaka Mathew naye afunge mkanda kisha akawasha gari.

“ Jason kuna nini ? Mbona umerudi mbio namna hiyo? Akauliza Mathew kwa wasi wasi huku akiufunga mkanda.Jason hakujbu kitu akawasha gari na kugeuza kisha akaondoka kwa kasi

“ Jason kuna nini? Mbona hivyo? Umeona nini kimekustua? Akauliza tena Mathew lakini jason hakujibu kitu akaongeza mwendo.Alionekana kama kuchanganyikiwa hali iliyozidi kumuogopesha Mathew.

“ Jason mbona hutaki kutueleza umeona nini? Tueleze tafadhali nini umeona kilichokustua? Akauliza Mathew

“ Jason kweli unatuogopesha sana.Tueleze ukweli nini umekiona kimekustua hivyo” Peniela naye akasisitiza lakini bado Jason hakuwa tayari kusema chochote bali aliendesha gari kwa mwendo mkali sana

“ Jason !! akaita Mathew kwa ukali lakini bado Jason hakugeuza hata shingo kumtazama bali aliendelea kuwa makini katika usukani.Uso wake ulionekana kuloa jasho .



“ Jason whats wrong with you?? Akauliza Peniela.



“ Something is not right!! Akawaza Mathew

“ Kuna kitu alichoona Jason na ndiyo maana amestuka na hataki kusema chochote.Akili yangu inanituma niamini kwamba yawezekana ni nyumba yangu ndiyo inateketekea na anaogopa kunieleza ukweli.Please help me God isiwe ni nyumba yangu” Akawaza Mathew na kumgeukia Jason



“ Jason stop the car and tell me the truth.!!! Akasema Mathew kwa ukali

“ Mathew not now “ akasema Jason.

“ Jason simamisha gari na utueleze nini umeona kilichokustua .? Naomba hii iwe ni mara ya mwisho sitaki kukuuliza tena.Kama hutasimamisha nitasimamisha mimi mwenyewe,” Akasema Mathew Kwa ukali.

Jason akaogopa namna Mathew alivyobadilika na kusimamisha gari pembeni ya barabara kisha akavuta pumzi ndefu na kusema



“ Mathew ni nyumba yako ndiyo iliyoungua”

“ Ouh My god !!!....

Haya ndiyo maneno aliyoweza kutamka Mathew huku ameiweka mikono yake kichwani.Mstuko alioupata ulikuwa ni mkubwa sana .

“ Mathew !!.mathew !! akaita Peniela lakini Mathew hakuitika.



“ Mathew ! .akaita tena peniela lakini Mathew hakuitika.bado mikono iliendelea kuwa kichwani.



“ Mungu wangu nini kimemtokea Mathew? Hii ndiyo sababu sikutaka kumueleza pale karibu na eneo la tuo kwani niliogopa lazima angepatw ana mstuko mkubwa na lazima angefanya fujo na angekamatwa na askari wale kwani wangetaka kufahamu milipuko ile iliyotokea ndani ya nyumba yake ameitoa wapi.Mambo yangekuwa magumu sana kwa Mathew “ akawaza Jason na kumgeukia Mathew



“ Mathew are you ok? Akauliza Jason lakini Mathew hakujibu kitu.Jason akawasha taa ya ndani ya gari ili kumtazama Mathew .Michirizi ya machozi ikaonekana machoni pake.Ilikuw ani mara ya kwanza kwa Peniela kumshuhudia Mathew akimwaga machozi. Aliogopa sana



“ Nimekutana na mambo mengi ya hatari nikiwa na Team Sc41 lakini sijawahi kukutana na matukio ya hatari yaliyoniogopesha kama ya usiku wa leo.Ni nani ameichoma nyumba ya Mathew? Ni team SC41? Anitha na jaji Elibariki wako wapi? Wameteketea ndani ya nyumba au wamekimbia ? Rosemary mkozumi je yuko wapi? Kwa sababu nakumbuka Mathew alimchukua na kwenda kumuhifadhi mahala pa siri” Akajiuliza Peniela na kuzidi kuogopa naye pia machozi yakaanza kumtoka.

Iliwachukua zaidi ya robo saa wakiwa pale pembeni ya bara bara na Mathew hakuwa ameongea chochote.Bado mikono ilikua kichwani na michirizi ya machozi ilionekana machoni pake.



“ Mathew !!..akaita Jason lakini Mathew hakujibu kitu.Katika kiti cha nyuma Peniela naye akasikika analia.Jason akashindwa afanye nini .

“ Mathew please talk to me” akasema Jason.Bado Mathew aliendelea kuiweka mikono kichwani na machozi kuendelea kumdondoka.

Baada ya dakika ishirini Mathew akatoa mikono kichwani akafuta machozi na kuingiza mkono mfukoni akachukua simu yake akaitazama halafu akatafuta namba Fulani katika simu yake akapiga,akaiweka simu sikioni kisha akafungua mlango wa gari akashuka.Jason akaogopa sana na kutaka kushuka garini lakini Mathew akamfanyia ishara kwamba asishuke garini.Mathew akaenda umbali wa hatua kadhaa ili aweze kuongea na Yule aliyempigia simu bila ya akina Jason kusikia.

“ Jason kwa nini umemuacha Mathew asuke garini? Akauliza Peniela uso wake ukiwa umejaa machozi

“ Kwa sasa amechanganyikiwa na hajui anachokifanya” akasema Peniela

“ Wait Peniela ! akasema Jason huku akimuangalia Mathew kwa makni.Baada ya kama dakika tano hivi Mathew akarejea garini



“ Twende Jamaica night club” akasema Mathew huku akiufunga mkanda .Jason akawasha gari wakaondoka

“ Are you ok Mathew “ akauliza Peniela

“ Yes ! I’m ok” akajibu Mathew

“ He’s not ok.Nmemfahamu Mathew ndani ya kipindi kifupi sana lakini ni mwanaume jasiri mno na asiyeogopa kitu chochote.Kwa mara ya kwanza nimemuona akidondosha machozi hii inaonyesha ni namna gani alivyoumizwa na hiki kilichotokea usiku huu.He’s badly hurt.Ni nani lakini ambaye amefanya jambo hili? Ni Team SC41 au nani? Akajiuliza Peniela



“ Ni vigumu sana kufahamu ni nani aliyefanya kitendo hiki .Nini kitafuata baada ya hapa? Je mipango yetu yote imefikia mwisho wake? Akaendelea kujiuliza Peniela na machozi mengi yakaendelea kumdondoka



“ Tumepambana sana lakini mambo yamekuja kuharibika mwishoni kabisa.Inaniuma sana.Kwa nini iwe hivi? Akashindwa kujizuia na kuanza kulia kwa kwikwi,Mathew akageuza shingo akamtazama na kusema

“ Usilie Peniela.This isn’t over yet” akasema na kisha akafuta machozi.Peniela hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kulia.

Safari iliendelea hadi walipofika Jamaica nigt club.Mathew akamuelekeza Jason sehemu ya kuegesha.Jamaica night club ni mojawapo ya kumbi za burudani inayotoa burudani kwa saa ishirini na nne.Gari zilikuwa zinaingia na kutoka.Walikaa mle garini kwa takribani dakika saba mara ikaja gari moja nyeusi mbele yao na kusimama kisha taa kubwa zikazimwa na kuwashwa haraka haraka mara tatu.Mathew akamgeukia Peniela.

“ Peniela we have to go” akasema na kumshangaza Jason



“ Mathew mnakwenda wapi? Akauliza

“ Jason ahsante sana kwa msaada wako mkubwa.Siwezi kukusahau kwa msaada huu mkubwa ulioutaidia kwa usiku huu wa leo.Muda wowote nikihitaji tena msaada nitakupigia.Tafadhali kuwa muangalifu sana” akasema Mathew na kuufungua mlango wa gari akashuka ,akamfungulia Peniela mlango akashuka ,akamshika mkono akamuongoza hadi katika lile gari lililosimama mbele yao wakaingia na gari likaondoka.Jason akabaki amepigwa na butwaa.



“ wanakwenda wapi? Gari ile iliyokuj akuwachukua ni ya nani? Akajiuliza Jason bila kupata jibu





“ Karibu tena nyumbani madam.” Mmoja wa walinzi wa Rosemary Mkozumi akamwambia Rose huku akimfungulia mlango.Rose akasaidiwa na walinzi wake kushuka ndani ya gari na kuingia sebuleni akakalishwa katika sofa.



“ Ahsanteni sana vijana.Mmefanya kazi nzuri usiku waleo.” Akasema Rose



“ madam kwa niaba ya wenzangu wote ninaomba samahani sana kwa tukio lile lililotokea.Sisi hatukujua kama watu wale walioongozana na Henry ni watu wabaya namna hii.” Akasema Yule mlinzi.



“ Fernando haya mambo si wakati wake sasa,nitakuwa na maongezi na ninyi.Hebu nieleze kuna habari gani hapa nyumbani katika muda wote ambao sikuwepo?



“ Baada ya wewe kuchukuliwa katika lile gari la wagonjwa ,tulipigiwa simu na watu wakatuarifu kwamba kuna mwili wa Henry mle ofisini kwako tuliwasiliana na polisi ambao walifika hapa wakafanya uchunguzi wao wakavunja mlango na kuondoka na mwili wa Henry.Hiyo ndiyo habari kubwa iliyopo.Zaidi ya hiyo hakuna tena habari nyingine yoyote” akasema Fernando.

“ Ok safi sana.Imarisheni ulinzi na kuanzia sasa mtu yeyote asiingie humu ndani bila ruhusa yangu na yeyote atakayeingia humu hata kama ameruhusiwa lazima apekuliwe ili kujua kama hana silaha ya aina yoyote ile.Nitaongea zaidi na ninyi kesho “ akasema Rose



“ lakini madam ni nani aliyefanya ukatili huu ? Huyu aliyefanya hivi anatakiwa asakwe hadi apatikane na afundishwe adabu “Akauliza Fernando.

“ usijali Fernando.Atasakwa na atapatikana tu.kwa sasa wale wote watu tuliowachukua kule wafungieni kila mmoja katika chumba chake.Nitakuwa na maongezi nao nao mmoja mmoja asubuhi.Kwa sasa naombeni mnipeleke chumbani kwangu” akasema Rose na walinzi wake wakambeba hadi chumbani kwake.

“ Ok ahsanteni sana vijana.Naombeni mniache sasa ninahitaji kuwa mwenyewe.”akasema Rose na walinzi wake wakaondoka wakamuacha mwenyewe.Akampigia simu mfanyakazi wake wa ndani akamuomba amtengenezee supu kwani hakuwa ameweka chochote tumboni.Alihisi maumivu makali sana kila sehemu ya mwili wake.Mlango ukagongwa akaingia Dr Imelda daktari binafsi wa Rosemary .



“ madam pole sana kwa mkasa huu.Nani kakufanya hivi? Imelda akashangaa



“ Imelda nashukuru sana umefika kwa wakati.Hali yangu ni kama unavyoniona.Si nzuri hata kidopo”akasema Rose.Dr Imelda akamchunguza Rose majeraha yake halafu akasema

“ Inabidi kabla ya kuanza kutibu nikusafishe kwanza majeraha yote ili tujue ukubwa wake.Can you walk?akauliza Imelda.Rose akasimama na kuuma meno kwa maumivu aliyokuwa akiyasikia.Imelda akamsaidia akamuingiza bafuni na kumuogesha kwani hakuwa akitazamika kwa damu iliyomtapakaa kila mahala.Baada ya kuhakikisha amekuwa safi akamrudisha chumbani na kumlaza kitandani akaanza kumtibu majeraha akianzia na yale makubwa ya miguuni ya kukatwa vidole.

“ Ni katili gani ambaye alifanya hivi madam? Mtu huyu aliyefanya hivi hana roho ya ubinadamu hata chembe. Lengo lake lilikuwa ni kukuua” akasema Dr Imelda wakati akitibu majeraha ya miguuni.

“ Imelda katika hii dunia tunaishi na maadui wengi sana na waliofanya hivi ni watu wenye visasi na mimi na lengo lao ni kuniua.” Akasema Rosemary.



“ Inasikitisha sana kwa ukatili huu kufanyiwa mtu mkubwa kama wewe.Yeyote aliyefanya hivi anatakiwa kuozea gerezani.Alichokufanyia kinatisha sana” akasema Imelda na machozi yakaonekana machoni kwa Rosemary



“ They will all pay..!!..They must pay ! ..akasema Rose.

Dr Imelda akaendelea kumganga Rose majeraha yake na wakati wanaendelea simu ya Rose ikaita matibabu yakasimama kidogo ili aweze kuongea na simu ile kwani alisema ni ya muhimu sana



“ hallow Rose”ikasema sauti ya upande wa pili baada ya Rose kupokea simu



“ Hallow Vincent !!!

“Rose ninataka kuripoti ukosefu wa adabu wanaonifanyia hawa walinzi wako.Dont they know who I am? Akauliza Vincent

“I’m sorry Vincent.Ni mimi ndiye niliyewapa maagizo ya kuhakikisha kwamba kila mtu anayeingia hapa anapekuliwa ili kuhakikisha hana silaha yoyote.I don’t trust anyone right now.Nipe kiongozi wao niongee naye” akasema Rose na baada ya sekunde kadhaa akasikia sauti ya Fernando

“ hallow Madam”

“ Fernando mruhusuni Vincent apite moja kwa moja”akasema Rose na kukata simu na matibabu yakaendelea.

Baada ya dakika kumi mlango ukagongwa Dr Imelda akaenda kuangalia ni nani aliyekuwa anagonga akakutana na Vincent akamueleza aketi sofani katika sebule ya Rose asubiri hadi amalize kazi aliyokuwa anaifanya.

Baada ya saa nzima Dr Imelda akamaliza kumtibu Rose majeraha yake halafu akamchoma sindano na kutoka mle chumbani ili kumpa nafasi Rose ya kuongea na mgeni wake.Vincent akastuka sana baada ya kumuona Rose akiwa na majeraha

“ Ouh my God ! who did this to you Rose? Vincent akashangaa



“ I have so many enemies Vincent” akasema Rose

“ Pole sana Rose.Whoever did this to you,must be pay.Umekwisha mfahamu ni nani aliyefanya unyama huu?akauliza Vincent

“ Tayari nimewajua walionifanya hivi na hata aliyewatuma wanifanyie hivi” akasema Rose.

“ Good.Its pay back time..”akasema Vincent kwa hasira

“ Not so fast Vincent.Wameuwasha moto wenyewe sasa watakosa maji ya kuuzimia.Nitapambana nao taratibu na kuwafyeka mmoja baada ya mwingine. Kwa bahati mbaya waliotumwa wanifanyie hivi hawakutaarifiwa kwamba Rosemary ni nani na sasa watakwenda kunifahamu mimi ni nani.Ninakuhakikishia Vincent yeyote ambaye ana mkono wakekatika jambo hili lazima atalipa.Hakuna atakayesalimika hata kama ni nani.Tuachane na hayo nimekuita hapa kwanza kukujulisha kwamba nimerejea nyumbani ingawa nimechakazwa kila sehemu ya mwili wangu.Nilivamiwa na kutekwa na watu ambao walimuua pia Henry.Watu hao wamenitesa sana kama hivi unavyoona.”

“ Dah ! pole sana Rose.” Akasema Vincent kw masikitiko



“ Ahsante Vicent.” Akasema Rose na kugugumia kwa maumivu kisha akasema



“Jambo la pili ninalotaka ulifahamu wewe kama mshirika wangu ni kwamba kuanzia sasa tuko vitani.Watu hawa walioniteka tayari wanafahamu mambo mengi sana kuhusu mimi na hata wale ambao ninashirikiana nao...”akasema Rosemary na kumfanya Vincent astuke



“ They know ?!! akauliza



“ Ndiyo Vincent.wanafahamu kila kitu kuhusu mimi,wamepekua kompyuta yangu,simu zangu,wamefahamu mambo mengi sana kwa hiyo nimekuita ili kukupa taarifa hizi ili unisaidie kupambana na watu hawa.” akasema Rose.

“ Ni nani hawa watu? Nani kawatuma? Halafu tukio hili lilitokeaje? Akauliza Vincent

“Henry alikuja na watu hao na sifahamu alitoka nao wapi .Kuna kitu nilisahau hivyo nikarejea mara moja ndipo nilipotaarifiwa kwamba Henry amekuja na wageni.Moja kwa moja nikaja mpaka ofisini ili niwafahamu wageni hao ni akina nani na mara tu nilipoingia ofisini Henry akaruka ili anipe taarifa kwamba nisingiie mle ofisini lakini watu wale wakamuwahi na kumpiga risasi akafariki pale pale.Ouh masikini Henry wamemuua mpenzi wangu jamani !!..Rose akasema kwa uchungu mkubwa na kushindwa kuyazuia machozi kumtoka.



“ Pole sana Rose.”akasema Vincent.Rose akafuta machozi na kuendelea.



“ Watu wale sifahamu walitoka wapi na Henry lakini ninachoweza kusema kwamba walimtumia Henry ili kuingia hapa ndani. Ninamfahamu Henry vizuri kwa namna yoyote ili asingeweza kuwaleta hapa kwangu watu ambao anajua ni hatari .Watu wale hadi wakamtumia Henry ni watu ambao tayari wamenifahamu kwa undani na wanajua kila kitu kuhusu mimi na yeye.Wamepekua kila mahala wamechukua kila taarifa waliyokuwa wanaitaka na huko walikonipeleka wamenitesa sana ili niwaeleze baadhi ya mambo “ akasema Rose



“ Dah pole sana Rose.” Akasema Vincent



“ Ahsante sana Vincent.Lakini nimegundua aliyewatuma watu hawa lazima atakuwa ni mmoja wa washindani wangu wa kisiasa na hili ni jaribio lao la kutaka kuizima ndoto yangu ya kugombea urais lakini nakuhakikishia kwamba hawataweza.Nitagombea urais na nitashinda tu”akasema Rose

“ Nakubaliana nawe Rose unapoingia katika siasa na hasa katika jambo kubwa kama kugombea urais lazima utapata maadui wengi na vikwazo vingi.Lakini ni nani basi ambaye unahisi ameianzisha vita hii ? akauliza Vincent



“ Ni Deus “ akasema Rose na kumstua sana Vincent

“ Deus ? akauliza Vinmcnet



“ Ndiyo ni Deus.My x husband”



“ Are you sure Rose? Akauliza Vincent

“ Ndiyo nina hakika kabisa ni yeye.Toka tulipoachana amekuwa ni adui yangu mkubwa na aliposikia kwamba nina nia ya kuwani aurais amekuwa ni mpinzani wangu mkubwa .Nina hakika kabisa kwamba ni yeye ndiye aliyewatuma vijana wale wanifanyie hivi.Lakini ninakuhakikishia Vincent kwamba simuogopi Deus na nitamuonyesha kwamba mimi ni nani.Safari hii ataifahamu nguvu yangu” akasema Rose.Vincent akamtazama Rose na kusema.

“ Rose kuna kitu ninataka kukuuliza.Una hakika gani kwamba ni Dues ndiye aliyewatuma watu hao kwako ?



“ Nina uhakika huo Vincent.Vijana wale walipokuwa wananitesa walitaka kufahamu kuhusu Hasheem Abullah.Ni Deus pekee ambaye anafahamu kuhusu mimi na Hasheem na hii ilikuwa ni sababu kubwa ya mimi na Deus kutengana. Nina hakika aliyewapa taarifa hizo zote ni Deus.Jambo hili ni la ndani sana na wasingeweza kulifahamu kama si kuambiwa na Deus.Kwa hiyo safari hii I swear nitamuonyesha mimi ni nani ” Akasema Rose.

“ Rose kabla hujafanya lolote nataka uwe na uhakika kama ni kweli Deus ndiye aliyekuwa nyuma ya hao watu,kama huna hakika na suala hilo naomba usifanye hilo tafadhali. “ akasema Vincent

“ Vincent nina uhakika mkubwa sana kwamba hakuna mtu mwingine anayeweza kunifanyia hivi zaidi yake.Deus hataki kuniona nyota yangu iking’aa kisiasa na ndiyo maana anafanya kila awezalo kuhakikisha kwamba mambo yangu hayafanikiwi na lengo la kuwatumia vijana wale ni ili kuweza kunivurugia mipango yangu wa kuwania urais kwani anajua kabisa kwamba nina watu wengi wanaoniunga mkono na kwamba lazima nitashinda tu na kuwa rais wa kwanza mwanamke Tanzania.Nimeishi na Deus na ninamfahamu vizuri sana kuliko mtu mwingine yeyote Yule.He’s a monster” Akasema Rose.Vincent akajiweka vizuri na kusema

“ Rose kuna mambo kadhaa ambayo ninataka uyafahamu kabla hujafanya hichounachotaka kukifanya.Kwanza kabisa…” akasema Vincent na simu ya Rose ikaita ikambidi asubiri hadi Rose alipomaliza kuongea akaendelea.



“ Kwanza kabisa ninataka ufahamu for years now I’ve been working with Deus.Mimi nay eye ni washirika wakubwa .”



“ What ?!..Rosemary akashangaa



“ Ina maana kwa muda huu wote umekuwa ukishirikiana na Deus bila ya kunitaarifu? You traitor !!“ akasema Rose kwa ukali

“ Rose tafadhali usihamaki.Nisikilize vizuri.Nimeamua kukueleza jambo hili kwa sababu sitaki ukurupuke katika maamuzi yako na uje kujutia baadae.NInataka kukusaidia kumfahamu muhusika halisi aliyefanya jambo hili.Mimi na Deus tumekuwa marafiki na washirika wakubwa kwa muda mrefu.Tuna kikundi cha watu wachache mabilionea wakubwa ambao tunakifadhili chama anachokiongoza Deus na nyakati ningine tunafanya hata maamuzi makubwa yanayohusu nchi.Hiki ni kikundi cha watu wenye nguvu ya kufanya jambo lolote katika nchi.It’s us who decides who is going to be the next president” akasema Vincent na kumfanya Rose azidi kumtumbulia macho

“ Nimekueleza haya yote ili kukupa picha kwamba katika vikao vyetu vya maamuzi hata siku moja hatujawahi kukuzungumzia wewe na hata siku moja sijawahi kumsikia Deus akikuzugumzia.Katika watu ambao wanazungumzwa kuwa na nguvu kubwa kisiasa na katika uchaguzi ujao wewe haumo hata kati ya tano bora kwa hiyo nina hakika kabisa kwamba Deus siye aliyewatuma hao watu wakufanyie hivyo kwa sababu hana shida na wewe . There is must be someone else behind this and not Deus. We have to find him” akasema Vincent.



“ Vincent umenisikitisha sana.Kumbe siku hizi zote umekuwa ni mtu wangu wa karibu unayeniunga mkono na kunisapoti katika mambo mengi kumbe umekuwa pia na ushirika na Deus? Umenisaliti Vincent na sitaki kabisa kukuona tena hapa kwangu.You traitor !! akasema kwa ukali Rosemary

“ Rosemary Calm down my dear.Nimeamua kukueleza ukweli ili kukusaidia kumtafuta mtu sahihi aliyekufanyia haya na si Deus. Yule ni mtu mkubwa sana na hana mpango wowote na wewe na usijaribu kabisa kucheza naye.Hata sisi pamoja na uwezo wetu mkubwa kifedha lakini tunamuogopa na tunatii kila atakachotuambia.Japokuwa amestaafu lakini bado ni mtu mwenye nguvu sana hapa nchini” Akasema Vincent.Rose alimuangalia Vincent kwa hasira kali

“ Vincent mimi na wewe tulikuwa marafiki wakubwa nilikuamini kwamba ni mtu ambaye ninaweza kukutegemea katika jambo lolote na hata kukupa siri zangu.Na hata usiku huu wewe ndiye uliyekuwa mtu wa kwanza kukupigia simu na kukufahamisha kwamba niko salama lakini sikujua kama una ushirika na Deus ambaye ni adui yangu mkubwa.Kwa kushirikiana na adui yangu ninakuweka nawe vile vile katika kundi la maadui zangu. From now on you are my enemy !!! akasema Rose.Vincent akacheka kidogo



“ Listen to me carefull woman.Dont you ever try to do anything to Deus.Atakumaliza ndani ya sekunde moja kama mbu anavyouliwa kwa kofi moja.Kwa Deus wewe bado ni mtu mdogo sana na anaweza akakufanya chochote muda wowote.There is one more thing I want to tell you.Mtu uliyemtegemea Captain Amos amefariki..!!..Taarifa ile ilimuingia Rosemary Mkozumi moyoni kama vile kitu chenye ncha kali na kwa dakika mbili hakuweza kusema chochote

“Ulimtegemea sana Amos katika mambo mengi lakini hukujua kwamba mtu ambaye ulimuamini kama mshirika wako alikuwa ni moja wa vijana wa Deus.Rose umewekwa kiganjani na Deus na kama angekuwa na shida ya kukudhuru wala asingewatumia hao vijana,angewatumia watu wako waliokuzunguka na wangekumaliza sekunde moja.Endapo utakayothubutu kujaribu kufanya chochote kwa Deus kama unavyofikiria nakuapia atakufinyanga kama udongo so don’t try him” akasema Vincent

“ Vincent please go away !! I’m surrounded by traitors !! Go away !! Akasema Rose huku akibubujikwa na machozi.



“ Rose you called me here because you need my help..Right now I’m the only friend you can count on” akasema Vincent

“ Go away Vincent .I’ll fight this war alone”

“ Rose huwezi kushinda vita hii.Let me help you to find who did this to you” akasema Vincent.Rose akamuangalia kwa jicho la chuki kisha akauliza

“ Who killed Amos and why? Akauliza Rose



“ Siwezi kukutajia ni nani aliyemuua lakini ninaweza kukwambia ni kwa nini aliuawa.Alikuwa tayari kuvujisha siri ambayo hakutakiwa kuitoa” akasema Vincent



“ Ouh Amos nitakulilia kilio gani mimi jamani..!!..akasema Rose huku akimwaga machozi

“ Rose ninadhani sintakuwa na jambo lingile la kuzungumza nawe kwa usiku huu. Endelea kupumzika na tafadhali zingatia hayo niliyokueleza.Dont start war with Deus.Nitakutembelea tena kujua hali yako” akasema Vincent



“ Vincent don’t show your face here again you monster !! akasema Rose kwa ukali .Vincent akaufungua mlango akatoka .



“ Aaaagggghhhh.!!!!! Akalia kwa uchungu Rose na mara Dr Imelda akaingia na kumchoma sindano ya usingizi ili aweze kulala





Anitha alifumbua macho na kujikuta akiwa katika kiza kinene.

“ Where am I? akajiuliza lakini hakupata jibu la mahala alikokuwa.Akajaribu kuinua mkono ili aweze kupapasa akastuka baada ya kugundua kuwa mikono yake imefungwa pingu.

“ Nimefungwa pingu ! ? Niko wapi hapa? Akajiuliza Anitha na kugundua kwamba hata miguu yake pia ilikuwa imefungwa pingu



“ Hapa niko wapi? What happened? Akawaza Anitha na kujaribu kurudisha kumbukumbu nyuma na ndipo alipokumbuka kile kilichokuwa kimetokea



“ Elibariki did this !!.Ni yeye ..ouh my God why him??.. akajiuliza



“ Ninakumbuka alinifuata ofisini akaniomba anitengenezee kahawa nikakataa. Muda huo huo Mathew akanipigia simu nikapokea lakini nilipoanza kuongea naye ghafla nikapigwa na kitu kigumu kichwani nikapoteza fahamu.Lazima ni Elibarki ndiye aliyenipiga na kitu kile nikapoteza fahamu.Dhumuni lake lilikuwa nini ? Kama ni yeye lazima ndiye aliyenileta hapa.Anataka nini toka kwangu? Anitha akaendelea kujiuliza maswali yaliyokosa majibu

“ Mathew hivi sasa atakuwa katika matatizo na anahitaji sana msaada wangu.Naomba Mungu huko aliko awe salama.” Anitha akaanza tena kukumbuka kila kilichotokea usiku ule nyumbani kwa Mathew

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ lazima ni Elibariki aliyenipiga na kitu kile kichwani nikapoteza fahamu. Kwa nini afanye hivi wakati anajua kwamba sisi ndiye wakombozi wake?.Pale nyumbani kwa Mathew ndiyo sehemu pekee ambayo salama kwake.Mwenzetu Noah alipoteza uhai wake wakati akimuokoa Elibariki katika shambulio kwa hiyo sisi ni watu wake wa muhimu sana ,kwa nini basi atufanyie hivi? Kwa nini ametusaliti? Tulimuamini sana Elibariki lakini kumbe katika kipindi hiki chote tulichokaa naye kumbe alikuwa anatuchunguza.Ouh my God sikutegemea kama Elibarikianaweza akatufanyia hivi.Who is he working with? Anyway ngoja nisubiri ili nijue sababu iliyomfanya atugeuke katika dakika hizi za mwishoni.Kinachoniumiza kichwa zaidiamenileta na kunifunga huku katika wakati ambao Mathew anahitaji sana msaada wangu.Nitafanyaje kumsaidia kwani ananitegemea sana katika kuifanikisha mpango mzima wa kuichukua package toka kwa Dr Joshua na tayari tumekwisha fanya kazi kubwa na tulikuwa tunaelekea mwishoni .Ee Mugu nisaidie niweze kutoka humu ndani salama na kumsaidia Mathew.Bila ya mimi kuwepo kila kitu tulichokihangaikia kitakuw akazi bure.” Akawaza Anitha na kuumia sana.



“ Sifahamu dhumuni la kuletwa hapa na sijui nitakaa hapa kwa muda gani .Lazima nitafute akili ya kuweza kunitoa hapa lazima nikaonane na Mathew .Siwezi kukubali kile tulichokipigania Kwa nguvu zote kishindikane wakati tunakaribia sana kufika mwisho.Tusipokuwa makini kirusi kile kitatua mikononi mwa watu wabaya na juhudi zetu zote za kulizima shambulio hili zitakwenda bure.Sitaki kukubali hilo litokee.I cant die in here while Mathew needs me.I must find a way out of here.I better die trying” akawaza Anitha

Katika chumba cha pili jaji Elibariki alikuwa amefungwa pingu kama alivyofungwa Anitha.Kchwa chake kilijaa mawazo



“ Kwa nini Rosemary anifanyie hivi hata baada ya kumsaidia kumuweka huru? Nimewasaliti wenzangu kwa kumsaidia yeye lakini haya ndiyo malipo yake? Nilikosea sana.Ninakijutia kitendo nilichokifanya.Hii ni dhambi kubwa sana ya kuwasaliti wenzangu na hii itanitafuna hadi siku ninaingia kaburini.My plan failed and I don’t know what to do anymore.” Akawaza

“ Ni bora ningeendelea kukaa pale pale kwa Mathew kuliko kufanya usaliti kama huu ambao haujanisaidia lolote na umeniweka pabaya zaidi.Nimeruka jivu nimekanyaga moto.Kinachoniumiza zaidi ni ukatili alioufanya Rose kwa kuichoma moto nyumba ya Mathew.Hii imeniumiza sana na sikutegemea kabisa kama Rose angeweza kufanya jambo kama lile .Sijui Mathew atakuwa katika hali gani akikuta nyumba yake aliyoijenga kwa mamilioni ya fedha imeungua moto na kila klichomo ndani kimegeuka majivu.Sijui sura yangu nitaiweka wapi Mathew akigundua kwamba ni mimi ndiye niliyefanya usaliti huu mkubwa.Naomba hata Rosemary aniue tu ili niepukane na mateso hjaya makubwa ninayoyapata hivi sasa.Sioni tena hata thamani ya kuendelea kuishi.Imefikia hatua sasa ambayo ninatamani kufa kuliko kuendelea kuishi .Akili yangu imechoka na haina tena uwezo wa kupata ufumbuzi wa kudumu wa matatizo yanayonizunguka” akawaza jaji Elibariki na kuanza kuikumbuka historia ya maisha yake.

“ Maisha yangu yalianza kubadilika nilipofunga ndoa na Flaviana.Japokuwa kwa nje tulionekana tunapendana lakini maisha yetuya ndani ni Mungu tu ndiye anayejua namna tulivyokuwa tunaishi.Ghafla Peniela akajitokeza katika picha nikatokea kumpenda hapo ndipo kila kitu kilipokwenda chini.Laiti peniela asingejitokeza katika maisha yangu ningeendelea na maisha yangu ya kukwaruzana na mke wangu Flaviana na wala tusingefika hapa tulipofika sasa hivi.Kwa ajili ya kumpenda Peniela nilitaka kulisafisha jina lake na ndiyo maana nikamuajiri Mathew ili aweze kumsaka muuaji halisi wa Edson lakini badala yake yameibuka mambo mengi makubwa na kunifikisha hapa nilipofika. Nimempoteza mke wangu Flaviana,nimemkosa Peniela,nimewapoteza ma rafiki Mathew na Anithana hili inainuma sana.Mathew ni rafiki yangu mkubwa ambaye aliyatoa maisha yake kunisaidia lakini kwa kutokufikiri kwa umakini nikamsaliti kwa kutegemea kwamba ninatengeneza njia ya kunisaidia kumbe ninabomoa na sasa nimekwama.Now where to run.Ouh my Lord please show me the way..” akaendelea kuwaza Elibariki akiwa amekata tamaa kabisa.

“ Anitha na Naomi nao wamechukuliwa pia .Sikujua kama angemchukua na Anitha .Yule ni msaada mkubwa sana kwa Mathew.Shughuli nyingi za Mathew zinamtegemea sana Anitha .Kwa kutokuwepo anitha kila kitu walichokuwa wanakifanya kitakwama. Huu ni mwisho wa kila kitu ila ninachokiomba Rose asimuue Anitha.Ni bora aniue mimi lakini amuache Anitha.Halafu kuna Yule paka shume Naomi.Yeye ndiye amechangia kwa kiasi kikubwa mimi kupatwa na mawazo haya ya kuwasaliti wenzangu kwa kumuachia Rosemary.Yeye ndiye aliyenishawishi nikafanya naye mapenzi na tukakutwa na akina Mathew na mimi kupata abu kubwa kwa watu ambao wananiheshimu sana.Ni yeye ambaye amesababisha nikamkosa Peniela kwani baada ya kushuhudia kitendo kile hakutaka tena kuendelea na mahusiano na mimi.Nilijaribu sana kumbembeleza lakini alinitolea maneno machafu na sitaki hata kuyakumbuka .” akaendelea kuwaza jaji Elibariki na taratibu macho yakaazna kuwa mazito akalala









******





Kumekucha tena Tanzania .Habari kubwa iliyotawala katika vyombo vyote vya habari asubuhi hii ni matukio makubwa mawili ya nyumba kuteketea kwa moto.Taarifa zilisema kwamba Jeshi la polisi linaendelea kufanya utafitiwa vyanzo vya moto huo navile vile taarifa ziliongeza kwamba mmiliki wa mojawapo ya nyumba iliyongua anatafutwa na jeshi la polisi kwani katika nyumba yake kulitokea milipuko inayosaidikiwa kuwa ni mabomu. Kingine kilichochukua nafasi katika vyombo vya habari hususan magazeti ni kurejeshwa nchini kwa mwili wa Flaviana mtoto wa rais aliyepelekwa nchini afrika ya kusini kwa matibabu baada ya kushambuliwa katikashambulio linalosadikiwa kupangwa na mumewake jaji Elibariki.Taarifa hiyo pia iliambatana napicha kubwa ya jaji Elibariki na ilimuelezea kama mtu anayesakwa kila kona kwa kusababisha kifo kile cha mtoto wa rais.

Saa mbili na nusu za asubuhi Dr Imelda,akaingia chumbani kwa Rosemary akamuamsha.



“ hallow madam unaendelaje?

“ Ninaendelea vizuri ila maumivu bado ni makali sana hasa miguuni Yule kijana alikonikata vidole.Waliniumiza sana wale jamaa.Sijawahi fanyiwa hivi toka nizaliwe.”akasema Rosemary

‘Pole sana madam utapona tu.kwa sasa nitakusafisha majeraha na kisha nitakucho masindano .” akasema Imelda

Baada ya zoezi lile kukamilika Rosemary akaomba kuonana na Fernando mlinzi mkuu wa nyumba yake.



“ Fernando nataka uwaandae wale watu nahitaji kuonana nao mmoja mmoja.Nataka kwanza kuonana na Yule mwanaume halafu Yule mwanamke na kisha kale ka binti”akasema Rose na Fernando akatoka mle chumbani.Baada ya Fernando kutoka akaingia Celine katibu wa Rose.Wakasalimiana na baada ya maongezi machache Rose akasema .

“Celine naomba ufute kabisa ratiba zangu zote kwa muda wa wiki mbili hadi hapo nitakapopona kabisa .” Akasema Rose

“ sawa madam .lakini nimepokea simu kadhaa za watu maarufu wanaotaka kuja kukupa pole.Kuna mawaziri,wafanyabiashara n.k . Sijawapangia chochote kwanza ninasubiri ruhusa toka kwako” akasema Celine



“ Vizuri.Sihitaji kuonana na mtu yeyote Yule siku ya leo.Nitakutaarifu sikuya kuonana nao .Kikubwa ninachokihitaji siku ya leo,andaa ni mkutano na waandishiwa habari.Andaa sehemu ya kukutana nao kule bustanini na nitaonana nao saa nane za mchana wa leo.Hakikisha waandishi toka redio na televisheni zote wanafika na andaa vle vile posho zao ilitaarifa zangu zipewe kipaumbele cha juu .Nina jambo kubwa na la muhimu sana la kuzungumza nao naambalo ninataka litawale katikakila chombo cha habari kwa siku nzima ya leo na kesho.bada ya kulikamilisha hilo,nitakupa tena maelekezo mengine ” akasema Rose



“ Sawa madam,nitalishughulokia suala hilo.Kuna ambo lingine lolote la kufanya madam? Akauliza Celine.

“Kwa sasa ni hilo tu celine.Kama nina jambo lingine ninahitaji nitakujulisha “akasema Rose na Celine akatoka mle chumbani.

“ Hakuna ambaye anaweza akaniambia chochote nikamuelewa kwamba eti Dues hakuhusika katika tukio lile la mimi kutekwa nyara.Najua amekwisha pata taarifa kwamba ninatarajia kuwania urais kwa hiyo jambo hili limemstua sana kwani anafahamu fika nguvu niliyonayo na anafahamu kabisa kwamba nina uhakika mkubwa wa kuweza kushinda uchaguzi.Ameogopa na kusudio la kuwatumia wale vijana ni kuniogopesha ili nisiweze kuendelea na mpango wangu .Alikose a sana kwani badala ya kniporomosha yeye atazidi kunijenga na nitaitumia fursa hii kujijenga kisiasa.”akawaza Rose na kuichukua simu yake iliyokuwa inaita.Akataarifiwa na mlinzi wake kwamba kamandawa polisi wa kanda maalum ya Dare s salaam anahitaji kumuona.Bila kipingamizi akaomba kamanda aruhusiwe kungia ndani



“ Wote hawa niwatu ambao wananipa sapoti kubwa sana.Ameachakazizake zote na amekuja kunitembelea.” akawaza Rose huku akivaa na kujiandaa kuonana na kamanda Yule Ezekiel msonobari

Walitumia zaidi ya dakika thelatjini kwa maongezi na kikubwa kamanda alimuhakikishia Roseary kwamba uchunguzi unaendelea ili kuwabaini wale wote waliofanya kitendo kile kiovu.Kamanda wa polisi alipoondoka Rosemary akamuita Fernando na kumtaka ampeleke akaonane na jaji Elibariki.Fernando akamtegemeza wakatembea taratibu hadi katika chumba alimofungwa jaji Elibariki.

“ Rose is this how you repay me?akauliza jaji Elibariki kwa ukali mara tu Rosemary alipoingia mle ndani



“ jaji ni jadi yetu mnapoonana kwanza mnasalimiana kisha mambo mengine yafuate.Unaedelaje? akasema Rosemary

“ Unategemea niseme ninaendelea vizuri?Kwa nini umenifanyia hivi Rose? Nilijitoa mhanga kukusaidia lakini malipo yake ndiyo haya?.Nashukuru sana Rose.Ninachokuomba ninataka uniue tu ili niepukane na haya mateso niliyonayo.Kill me Rose..Kill me right now !!”akafoka jaji Elibariki

“ jaji usihamaki namna hiyo.Sijakuleta hapa kukuua na kwa nini nifanye hivyo? Siwezi kukuua mtu kama wewe.kwanza ninakushukuru sana kwa kunisadia nikaweza kutoka katikaile jehanamu.Lakini pamoja na msaada mlionisaidia naombanikuweke wazi kwamba sikuamini hata chembe na siwezi kufanya hivyo.Ninazifahamu mbinu zenu zote mnazotumia .Baada ya kuona mmeshndwa kupata kile mlichokuwa mnakihitaji toka kwangu mkapangana wenzako kwamba ujifanye umewasaliti na ili nikuamini na halafu muendelee kunichunguza.Mamboyote haya nimekwisha yapitia kwa hiyo ninayafahamu vizuri sana na hamuwezi kunidanganya kitu.”akasema Rosemary



“ Rose you’re a monster !!..akasemaElibariki

“ Pamoja na maamuzi yale magumu niliyoyafanya bado tu huniamini? Nimewasaliti wenzangu walioniamini sana pamoja na kuivuruga mipango yetu yote bado tu huniamini ? Nifanye nini ili uniamini?

“ Do you think I can easily trust you? No I cant..” akasema Rosemary



“ I betrayed my friends because of you !! !Nifanye nini zaidi ili uniamini? If you don’t tyrust me then kill me..akasemajaji Elibariki.Rosemary akamfanyia ishara Fernando asogee karibu akamnong’oneza kitu kisha Fernando akatoka na baada ya muda akarejea akiwa ameongozana na Anitha.Jaji Elibariki akastuka sana alipogonganisha macho na Anitha



“ Elibariki?!! Rosemary?!! Akasema Anitha kwa mshangao



‘ Jaji uliniambia kwamba una matatizo na unahitaji msaada wangu kwa hiyo ukawasliti wenzako na kuniachia huru ili nikusaidie kutatua matatizo yako lakini bado siamini kama unachoniambia ni kweli.Ili nikuamini kwamba kweli unahitaji msaada wangu ,ninataka umpige risasi huyu mwenzako ambaye ulikuwa unashirikiana naye ,mbele yangu.Ukifanya hivyo utanithibitishia kwamba ni kweli unahitaji msaada wangu na nitakusaidia”akasema Rose kisha akampa ishara fernandoamfungue jai Elibariki.

“ Rosemary ina maana haya yote nliyoyafanya kukuweka huru haujaniamini hadi nimuue mwenzangu? Hapana siwezi kufanya kitu kama hicho”akasema Elibariki



“ Ukikataa utanifanya niamini kwamba unanidanganya na nitakufanyia kitu kibaya sana.Nitakutesa na kukuua taratibu sana”akasema



“ Rose I cant do that”akasema jaji Elibariki



“ Fernando give him the gun !! akasema Rose na fernandoakampatia Rosemary bastora.

“ Shoot her.Prove to me that you are not lying to me .Iwill cont to three..



“ One..! akasema Rose..jaji Elibariki jasho lilikuwa linamtoka .

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Two !..akahesabu tena Rose.Jaji Elibarikihukuakilengwa na machozi akainukana kuchukua ilee bastora akainua mkono na kumuelekezea Anitha



“ Elibariki are you sure you want to kill me? Akauliza anitha

“ I’msorry Anitha !! akajibu Elibariki

“Ok go ahead traitor,shoot me but I’ll haunt you to the grave..!! akasema Anitha huku macho yake yamejaa machozi.



“ I’m sorry Anitha I have to do this”akasema jaji Elibariki na kuilenga bastora ile kichwani kwa Anitha



“ Three !!..

Jaji Elibariki akaizinga bastora ile na ukatokea mlipuko.







“ hahahahaha..!! akacheka Rosemary



“ I’m impressed with you judge ! kidogo sasa nimeanza kukuamini.Hiyo bastora haikuwa na risasi halisi bali ni risasi baridi kwa ajili ya kuogofya.” Akasema Rosemary na kumgeukia Fernando



“ Fernando take thegun” .Uso wa Jaji Elibariki ulikuwa umeloa jasho na midomo ilikuwa inamtetemeka.

“ Fernando take her out of here” akaamuru Rosemary na Anitha akatolewa mle chumbani alikuwa anatetemeka mwli mzima kwa woga.Hakuamini kama bado alikuwa hai.

“ Jaji kitendo ulichotoka kukifanya kimenithibitishia kwamba ni kweli una tatizo na unahitaji sana msaada wangu na ndiyo maana hukusita kuachia risasi ile ambayo kama ingekuwa ni risasi halisi basi mwenzako angekufa.Lakini pamoja na hayo kuna mambo ninataka kufahamu toka kwako.Nataka kufahamu wale wenzako ni nani aliye nyuma yao? Ni nani aliyewatuma kwangu? Akauliza Rosemary

“ No one” akajibu jaji Elibariki

“ Jaji bado hatima yako iko mikononi mwangu.Ni mimi ndiye nitakaye kusaidia na kukutoa katika matatizo yako uliyonayo kwa hiyo ninapokuuliza swali naomba unijibu bila kunificha Ni nani aliyewatuma wale wenzako kwangu? Ni nani aliyewapa taarifa zangu?

“ Nitakueleza ukweli Rose .Hakuna mtu yeyote aliyetutuma kwako lakini ulijitokeza katikati ya uchunguzi aliokuwa anaufanya Mathew na ndipo alipoanza kukufuatilia.”

“ Nilitokea katikati ya uchunguzi? Ni uchunguzi gani huo alikuwa anaufanya ?



“ Mathew alikuwa anachunguza kuhusiana na kifo cha Edson aliyeuawa na kisha Peniela akaangushiwa kesi ile ya mauaji.Mimi ndiye niliyemuachia huru Peniela baada ya kuridhika kwamba hakuwa amefanya mauaji yale ya Edson kama ilivyokuwa imedaiwa.Baada ya hukumu ile kulikuwa na maneno mengi sana yaliyoongelewa kwa hiyo nikataka kukata mzizi wa fitina kwa kumtafuta muuaji halisi wa Edson na ndipo nilipomkodisha Mathew aweze kuifanya hiyo kazi.Katika uchunguzi huo Mathew alibaini kwamba kuna nyaraka za siri ziliibwa ikulu na Edson ndiye aliyeeziiba akishirikiana na Captain Amos.Baada ya kulicghimba kwa undani suala hili akabaini kwamba wewe ndiye uliyekuwa nyuma ya wizi huo na ndiyo maana akaanza kukufuatilia.Hakuna mtu yeyote aliye nyuma yetu.”

“ damn you !!!!. akasema Rose kwa hasira.

“ Mathew anafanya kazi idara gani? Ni polisi?



“ Ni mpelelezi wa kujitegemea. “akajibu Elibariki.Rose akamtazama na kusema

“ Pamoja na maelezo hayo bado ninaamini lazima kuna mtu aliye nyuma yenu.Nieleze ukweli nani amewapa taarifa zangu ? akauliza Rose

“ Hakuna mtu aliyetutuma kwako Rose.kwa nini hutaki kuniamini? Akauliza Elibariki

“ That guy Mathew !alinitesa sana nani wazi kuna kitu alichokuwa anakitaka toka kwangu na ninaamini alikuwa anafuata maelekezo aliyopewa na mtu Fulani.Nataka kumfahamu huyo mtu ni nani? akasema Rose.Elibariki akamtazama kwa hasira na kusema



“ Mimi na Mathew ni marafiki wakubwa na tumekuwa tunasaidiana katika mambo mengi na hata nilipomuomba anisaidie kumtafuta muuaji wa Edson hakusita kukubali.Niko hai leo hii kwa sababu yake.lakini pamoja na hayo yote bado nimekubali kumsaliti kwa kukuachia huru.Unadhani Mathew angethubutu kukuacha huru? Nakuhakikishia ule ndio ungekuwa mwisho wako.Wewe ni mtu hatari sana na asingethubutu kukuachia huru..Wewe na wenzako mnafahadhili makundi ya kigaidi afrika mashariki .Fedha za kufadhili ugaidi zinapitia kwako .Yote haya tayari wanayafahamu unadhani wangekuachia huru? Katu usingeachiwa huru.Lakini pamoja na kufahamu kwamba weweni mtu hatari bado nimeamua kukuachia huru.Nilikua tayari kumuua mshirika wangu Anitha muda mfupi uliopita yote hii ni katika kukufanya uniamini. Unataka nifanye nini kingine ili uniamini? Kama hutaki kunisaidia ninaomba uniue tu.Kill me now.Kill me!! Akasema jaji Elibariki kwa hasira

“ Mathew ni rafiki yako mkubwa na umemsaliti? Unadhani kwa kitendo ulichokifanya akikutana nawe leo hii atakuacha hai?akauliza Rose



“ Sina namna nyingine ya kufanya zaidi ya kutafuta msaada wa kunikamua katika matatizo niliyonayo.Nimechoka kukimbia,nimechoka kujificha.Nataka niwe huru na ndiyo maana nikawasaliti wenzangu ili niweze kupata msaada toka kwako”

“ Ni jambo gani linakufanya ukimbie? Umefanya nini? akauliza Rose

“ Hivi sasa ninasakwa kila kona ya nchi hii kwa kusababisha kifo cha mke wangu Flaviana ambaye ni mtoto wa rais .“



“ You killed her?

“No I didn’t”



“ who killed her then”



“ watu waliotumwa na rais”

“kama wewe hukumshambulia mke wako na kusababisha kifochake kwa nini basi ukimbie?Kwa nini usieleze ukweli?

“ Nimenusurika kuuawa mara moja nikalazimika kuingia mafichoni lakini nikiwa mafichoni nimebambikiwa tena kesi ya kusababisha kifo.Hakuna ninayeweza kumueleza chochote akanielewa..”

“ kwa nini ulitaka kuuawa? Nani anayetaka kukuua? Kwa nini ubambikiwe kesi wakati wewe siye uliyesababisha kifo cha mkeo? Jaji unaonekana unataka kucheza na akili yangu .Mimi si mtu wa kudanganywa hovyo”

“ Wamenibambikia kesi kwa sababu wanataka kuniondoa duniani”

“ Akina nani hao wanaotaka kukuondoa duniani?

“ Rais Dr Joshua na wenzake”

“ kwanini Joshua atake kukumaliza wewe jaji? Umemfanya nini?

“ Kuna jambo nimeligundua ambalo sikupaswa kuligundua”



“ Jambo gani hilo? Akauliza Rose.Jaji Elibariki akabaki kimy



“ You want my help? Tell me everything!!..akasema Rose

“ Niligundua kwamba alimuua mkewe “

“ Dr Flora?!! Aliuawa na Dr Joshua?..Rosemary akashangaa

“ Ndiyo aliuawa na Dr Joshua kwa kumtumia Captain Amos.”

“ Ninawafahamu Dr Joshua na Dr Flora walikuwa wanapendana sana.Hainiingii akilini eti Dr Joshua amuue mke wake !!

“ Flora aligundua jambo kubwa la hatari alilokuwa anataka kulifanya Dr Joshua na ndiyo sababu akauawa.”

“Ni jambo gani hilo?

“ Kuna kirusi hatari kinaitwa Aby ambacho Dr Joshua anataka kukiuza.Nina hakika unalifahamu jambohili kupitia kwa Amos ambaye alikuwa ni mshirika wa karibu wa rais na walikuwa pamoja katika suala hili.Nina hakika hata wewe pia ulikuwa unaifuatilia package yenye kirusi hicho kwani tuliyanasa mawasiliano yako na mtu mmoja anaitwa Samir ,ukimuahidi mtu mmoja aitwaye Samir kwamba muda si mrefu utaupata mzigo kwa kuwa ulikuwa na mawasiliano na mtu wa karibu na rais.”



“ I hate that guy Mathew !!..nitamsaka kila kona mpaka nimpate lakini ninashukuru kwa taarifa uliyonipa kuhusu Dr Joshua kumuua mke wake “ akasema Rosemary

“ Dr Joshua I’ve got you now.Wewe ndiye utakayeikamilisha ndoto yangu .You are going to make me the next president of the united republic of Tanzania.”akawaza Rose na kutabasamu halafu akamgeukia Elibariki

“ I will help you judge!!..http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Thank you Rose.” Akajibu Elibariki

“Unataka nikusaidie nini?



“ Niligundua kwamba Dr Flora aliuawa kwa sumu kwa hiyo nikawa adui mkubwa wa Dr Joshua kwani aliamini kwamba ningeweza kulitumia jambo hilo kumchafua kwa hiyo lengo lake lilikuwa ni kuniua.Kwa bahati mbaya mpango wa mara ya kwanza wa kuniua ulishindikana kwa hiyo toka wakati huo wamekuwa wakinitafuta kwa kila nguvu waliyonayo.Nimejiuliza maswali mengi kwamba nitajificha mpaka lini? Nitaendelea kukimbia hadi lini? Jibu nililolipata ni kwamba vita hii imenishinda.Siwezi kupambana na Dr Joshua kwani yeye ana nguvu kubwa kunishinda mimi.Nimeinua mikono kwa hiyo ninachohitaji ni kujisalimisha kwake ili mambo haya yaweze kuisha.Nisipofanya hivyo maisha yangu yataharibika na nitakosa kila kitu.Siwezi kukubali maisha yangu yaharibike na ndiyo maana niko tayari kufanya jambo lolote lile kwa ajili ya kuyajenga upya tena maisha yangu.Msaada ninaouhitaji toka kwako ni kunikutanisha na Dr Joshua ili niweze kuongea naye” akasema jaji Elibariki.Rose akamtazama kwa makini kisha akauliza

“ Una hakika Dr Joshua atakubali kukusamehe?

“ Nina uhaika huo kwani niko tayari hata kumsaidia katika mpango wake wa kuiuza package ili ufanikwe.Ninaifahamu mipango yote waliyoipanga Mathew na wenzake na kwa sasa baada ya nyumba ya Mathew kuungua moto hakuna tena kitakachoendelea.”

“ Unasema uko tayari kumsaidia Dr Joshua kuuza kirusi Aby? Are you out of your mind? Akauliza Rosemary

“ Kama kwa kufanya hivyo atanisamehe na kuniweka huru basi niko tayari.Rose hii ni fursa kwako na kwangu ambayo tunatakiwa kuitumia.Endapo tutaitumia vizuri fursa hii kila mmoja atafaidika.Rose tunaweza kuwa washirika na tuk……………..”



“ Stop that judge..! akasema Rosmeary mkozumi kwa ukali

“ Usiongelee kabisa suala la mimi na wewe kuwa washirika.Siwezi kamwe kushirikiana na mtu kama wewe ambaye nimekushuhudia ukiwasaliti wenzako.Kwa ajili ya maslahi yako unaweza ukamsaliti mtu yeyote Yule.Wewe si mtu wa kuamini hata kidogo lakini hata hivyo itakusaidia ingawa kwa sharti moja kubwa.”

“ Sharti gani hilo Rose? akauliza Elibariki



“ Promise me that you will help me find Mathew”akasema Rose

Bila kupepesa macho jaji Elibariki akasema

“ I will help you find Mathew.I promise”akasema jaji Elibariki.

“ Thank you.I will help you.Dr Joshua atakapomaliza mazishi ya mwanae nitakukutanisha naye”akasema Rose



“ Naomba unisaidie suala hili kwa haraka zaidi ili niweze kushiriki mazishi ya mke wangu Flaviana” akaomba Elibariki

“ Nitajitahidi kadiri nitakavyoweza “

“Fernando I’m done with Mr Judge,Take me to the next room to see that woman ” akasema Rose na kisha Fernando akamsaidia kuinuka akamshika mkono akamsaidia kutembea wakatoka mle chumbani.





Mlango wa chumba alimofungiwa Anitha ukafunguliwa ,Rosemary Mkozumi akaingia akiwa ameongozana na mlinzi wake Fernando.Anitha alikuwa amekaa kitandani amefungwa pingu mikononi ,alikuwa anatetemeka mwili mzima.Tukio lililotokea chumbani alimowekwa jaji Elbariki muda mfupi uliopita lilimuogopesha mno.Akainua uso na kumtazama Rose,macho yake yalijaa machozi

“ Nilidhani ninyi ni mashujaa na hamuogopi kufa kwa ajili ya kuitetea nchi yenu.!! Sasa mona unalia? akasema Rosemary Mkozumi huku akicheka kwa dharau .Anitha hakuongea kitu akabaki anamtazama kwa jicho la chuki.



“ whats your name ? akauliza Rose.Anitha hakumjibu kitu

“ nakuuliza jina lako nani? Akauliza tena lakini bado Anitha hakujibu kitu

“ Wewe ni bubu hutaki kujibu?.”akasema Rose na Fernando akamsogelea Anitha



“ Umeulizwa jina lako nani? Akasema Fernando kwa ukali

“ Fernando leave her.Atasema tu yeye ni nani hata kama si sasa hivi lakini atasema tu”akasema Rose huku akimtazama anitha kwa hasira



“ Wewe na mwenzako Mathew ndiyo mashujaa wa nchi hii ambao mmekuwa mnawatuatilia watu migongoni mwao kujua wanafanya nini siyo? Hongereni sana vijana wenye uchungu na nchi hii lakini siku zote mashujaa huwa wa kwanza kufa na ndivyo itakavyokutokea kwako kama usiponipatia kile ninachokihitaji”akasema Rose na kuendelea kumtazama Anitha kwa jicho kali

“ Mwenzako Mathew aliingia ndani ya nyumba yangu,akamuua mpenzi wangu na kisha akaniteka na kunipekea nyumbani kwake,akanitesa sana .Ninataka kujua ni nani aliyewatuma kwangu? Nani aliyewapa habari zangu?akauliza Rose.Bado Anitha hakuthubutu kuufungua mdomowake.



“ Wewe ni bubu? Akauliza Rose akionyesha kukerwa na tabia ile ya Anitha kukaa kimya kila alipoulizwa

“ Sikiliza binti,kwa hivi sasa hatima ya maisha yako iko mikononi mwangu na endapo ukinipa ushirikiano ninaoutaka basi ninaweza kukuachia huru lakini ukiendelea na tabia yako ya kiburi ninakuapia kwamba hutaliona tena jua la kesho.Mpaka sasa wewe na mwenzako Mathew ni maadui zangu wakubwa sana na huyu mwenzako nitamsaka kwa udi na uvumba hadi nihakikishe nimemtia mikononi na kumuonyesha mimi ni nani.Nataka liwe fundisho kwenu na kwa wenzenu ili mjue kwamba Tanzania hii ina wenyewe.Kwa taarifa yako ile nyumba yenu mliyokuwa mnaitumia kuwatesea watu nimeiteketeza kwa moto jana usiku.Kila kitucheni hivi sasa ni majivu ”akasema Rosemary na kumstua sana Anitha ambaye aliinuka ghafla na kutaka kumvamia Rose lakini Fernando akawahi kumdaka



“ You devil ! I swear you’ll pay for this Rose..You will pay !! akasema kwa hasira Anitha.



“ Ouh kumbe unaweza kuongea vizuri,basi baadae mchana nitakapomaliza mkutano wangu na waandishi wa habari nitapata nafasi ya kuongea nawe.fernando I need her later in room five” Rosemary akamuelekeza Fernando.



“ Brave woman,me and you we’ll meet later.We’’ hve a nice talk. “ akasema Rose



“ you go to hell !! akasema Anitha kwa ukali.Rose akamsogelea



“ You’ll see how hell looks like,very soon..”akasema Rose.Anitha akamtemea mate usoni na kabla hajakaa sawa Fernando akamnasa kibao kikali kilichompekea chini

“ Thank you brave woman,tutaonana baadae na nitakutemea lita kadhaa za mate “ akasema Rose kisha wakatoka mle ofisini.



“ This woman is brave..haonekani kuogopa hata kidogo.Anaonekana ni mtu mzoefu sana katika shughuli hizi “akasema Rose



“ Ni kweli madam.Anaonekana jasiri sanamlakini akiminywa atasema kila kitu”

“ Ok tutaonana naye baadae.Huyu lazima atuonyeshe mahala alipo mwenzake.Watu hawa ni hatari sana kwetu” akasema Fernando.

Bado Anitha aliendelea kutweta kwa hasira baada ya Rosemary kutoka mle chumbani.Alikuwana hasira kali sana.



“ Ama kweli hawakukosea waliosema ni heri kumfadhili Mbuzi kuliko binadamu.Elibarki anawezaje kweli leo hii kutifanyia sisi namna hii? Tumefanya mambo mengi kwa ajili yake lakini haya ndiyo malipo yake...Mhh !Elibariki !! bado siamini ”akawaza Anitha huku machozi yakimtoka kwa hasira alizokuwa nazo



"Aaaaagghhhh!!!..akapiga ukelele mkubwa.



“ Tulifanya kila tuliloweza kumsaidia na hata Noah akapoteza uhai kwa ajili ya kumuokoa yeye lakini haya yote hayana thamani tena kwake na badala yake amediriki kutusaliti tena kwa mtu ambaye ni hatari sana.Amemuachia huru mtu ambaye anashirikiana na magaidi.Ouh Elibariki kwa nini lakini umefanya hivi?Jitihada zetu zote ni kazi bure.Hatutaweza tena kukipata kirusi kile hatari !! Aaaaghhh !!...akaendelea kulia kwa uchungu.



“ Sipati picha Mathew atakuwa katika hali gani hivi sasa baada ya nyumba yake kuteteketezwa kwa moto.Kama kila kitu kimeungua basi tutakuwa tumerudi nyuma sana na kazi ya kukipata kirusi Aby itakuw angumu sana kwani kila kitu amacho tulikitegemea katika operesheni hii kilikuwamo mle ndani.I must get out of here.I must help Mathew.lakini nitatokajehapa? akajiuliza

Baada ya kutoka chumbani kwa Anitha Rose akaelekea katika chumba alimofungiwa Naomi.Akapata mstuko mkubwa baada ya kugundua msichana aliyefungwa mle ni Naomi.



“ Naomi ?!! akasema kwa mshangao



“ Aunt Rose? Naomi naye akashangaa

“Umejuaje kama niko hapa aunt Rose? Akauliza

Naomi



“ Hapa ni nyumbani kwangu.Ulifikaje kwa Mathew ?Alikuteka nyara? Akauliza Rose



“ Kwa hiyo wewe ndiye uliyetuteka pale kwa Mathew mimi jaji na Aunt Anitha?



“ Naomi nieleze ulifikaje pale kwa Mathew? Alikuteka na kukuchukau kwa nguvu? Akauliza Rose



“ Hapana aunt,Mathew hakuniteka bali ndiye aliyenisaidia kunitoa katika lile jumba baba alimokuwa ananifungia kwa zaidi ya miaka minne na kuniweka huru..”

“Mathew alikusaidia? Rose akashangaa

“ Ndiye aliyenisaidia kutoka ndani ya jumba lile” akasema Naomi bila wasiwasi



“ Naomi hebu nieleze vizuri ilikuajehadi akamuamini Mathew ? Unafahamiana naye? Nieleze vizuri tafadhali”akasema Rose.

Naomi akamsimulia kila kitu kilivyokuwa hadi akafanikiwa kutoka mle ndani na kuishi nyumbani kwa Mathew

“ Naomi ulifanya kosa kubwa sana kumuamini Mathew na utalijutia kosa hili kwa siku zote za maisha yako.Mathew ni mtu mbaya sana na katili na hafai kuaminiwa hata idogo.kwa nini ulifanya vile lakini? Kwa nini ulimuamini? Kwa nini ulikubali akakundanganya kwamba atakupatia maisha mazuri na ukakubali kumuuza baba yako?



“ Aunt wewe mwenyewe unajua maisha yangu yalivyokuwa.Mara kadhaa Ulikuwa unakuja na baba na kunikuta namna nilivyokuwa ninateseka ndani ya lile jumba.Nimekaa kifungoni mle ndani kwa zaidi ya miaka minne na nimechoka .Nahitaji kuwa huru.Nimeteseka vya kutosha .Baba amenitesa mno na siwezi kuvumilia tena”akasema Naomi

“ Naomi unafahamu lakini athari za hiki ulichokifanya?akauliza Rose



“ I dont care aunt.Ninachohitaji ni mimi kuwa huru basi.Nimeteseka vya kutosha na siwezi tena kuendelea kuteseka.Aunt ninaomba uniache huru mimi niende zangu.Sitaki maswali zaidi” akasema Naomi

“ Naomi sikiliza.watu uliowaamini kwamba watakusadia si watu wazuri hata kidogo na hawana lengo wala nia ya kukusaidia,Unafahamu kwamba baba yako ameuawa?

“ Ameuawa? Naomi akashangaa

“Ndiyo kwani Mathew hajakueleza?



“ hapana hajaniambia chochote kuhusiana na baba yangu kuuawa”



“ Hawezi kukueleza kwa sababu ndiye aliyemuua baba yako.Baada ya kupata kile alichokuwa anakihitaji toka kwake alimpiga risasi humu humu ndani mwangu akamuua.Ndiyo maanan nilikuuliza awali kama unafahamu athari za hicho ulichokifanya..Baba yako amefariki dunia na hujui hata kinachoendelea.Masikini Naomi”akasema Rose.Naomi akamtazama Rose halafu akainua mikono na macho juu na kusema

“ Ouh ahsante Mungu.Ahsante kwa kumuondoa huyu mtu huku duniani.Hatimaye shetani karejea kuzimu”akasema Naomi na kumkasirisha sana Rose ambaye alimsogelea na kumnasa kibao kikali



“ Baba yako ameuawa na wewe unafurahia? Wewe ni mtoto wa namna gani? Nina mashaka kama akili yako iko sawasawa” akasema Rosemary kwa hasira



“ Akili yangu haiko sawasawa,kwani aliyeiharibu ni huyo huyo ambaye ambaye wewekwako unamuona ana thamani kubwa kwa sababu alikuwa mshirika wako katika biashara zenu za haramu.Ameniharibu kwa kuniingiza katika matumizi ya unga wa kulevya ,ndoto zangu zote za maisha zimepotea maisha yangu yote hayana muelekeo tena,unadhani nitampenda mtu kama huyo? Ninamsifu Mathew kwa kumuua na kama angechelewa ningemuua hata mimi mwenyewe.Mathew ni shujaa na anastahili pongezi kwa kitu alichokifanya cha kishujaa.Ninamchukia sana baba yangu na ninamuomba huko aliko Mungu amtupe katika moto.”akasema Naomi na kuzidi kumchafua Rose

“ Jaji na Aunt Anitha wako wapi? Jana tulipakiwa katika gari wote.Umewapeleka wapi? ” Akauliza Naomi



“ Naomi umenisikitisha sana .Nilikupenda sana kama binti yangu lakini leo umenisikitisha sana .Sina hakika kama kweli wewe ni mtoto wa Henry.”

“ Aunt Rose wewe na baba hamtofautiani na ndiyo maana mkawa wapenzi.Ninaomba unifungue humu nikamzike huyu anayeitwa baba yangu kisha niendelee na maisha yangu,.nahitaji pia kuonana na mathew nimpongeze kwa kitendo alichokifanya cha kumuua baba yangu."Akasema Naomi.Rose akamtazama kwa hasira halafu akamgeukia Fernando



“ Fernando let’s get out of here.Naomi utaendelea kukaa ndani ya chumba hiki na hutatoka kamwe mpaka hapo akili yako itakapokaa sawa”akasema Rose.Fernando akamfungulia mlango wakatoka mle ndani na kumuacha Naomi akipiga ukele mkubwa akitaka aachiwe huru.

“ dah ! nahisi nimeishiwa nguvu Fernando.Sikutegemea kabisa kama msichana Yule tuliyemchukua kule kwa Mathew ni Naomi. Huyu Mathew ni anapaswa kutafutwa haraka sana kwa kila namna anaonekana ni mtu anayenifahamu vyema.Alifahamu kwamba kuingia hapa nyumbani kwangu kuna ugumu kwa hiyo akaamua kumtumia Henry na ili kumpata henr ilimlazimu kumtumia binti yake Naomi.Dah ! huyu kijana ameniogopesha .”



“ Usijali Madam tutamtafuta huyu Mathew kwa kila namna tutakavyoweza na ninakuhakikishia kwamba tutampata tu.” Akasema Fernando.

Rose akarejea chumbani kwake na kuketi sofani akitafakari.

“ Kwa nini kijana mdogo kama huyu Mathew anataka kuninyima usingizi? Lakini hawezi kushindana na mimi kamwe.Nitamsaka kwa namna yoyote hadi nitampata tu. Nataka kabla ya kuanza kwa harakati zangu za urais niwe nimemtia mikononi huyu kijana na kumnyamazisha kimya kimya.Ni mtu ambaye anafahamu mambo yangu mengi sana na endapo nisipofanya jitihada za kumsaka anaweza akaniharibia kila kitu..lazima ndoto yangu itimie na ili kuitimiza sihitaji vikwazo vyovyote njiani.Nitakiondoa kila kikwazokitakachokuja mbele yangu na kikwazo cha kwanza ni huyu kijana Mathew.Atanitambua mimi ndiye Rosemary Mkozumi.!!akawaza Rosemary na kustuliwa na Celline katibu wake aliyeingia ghafla pale sebuleni.

“ celline siku nyingine ukiingia uwe unabisha hodi ,umenistua sana nilikuwa mbali kimawazo”akasema Rose

“ samahani madam.”akajibu Celline huku akitabasamu

“ madam nimekuja kukutaarifu kwamba lile zoezi limekamilika na mpaka sasa hivi tayari waandishi wa habari wamekwisha anza kuwasili.Kila kitu kitakwenda kama vile ulivyoagiza .Waandishi toka vyombo vyote vikubwa vya habari watakuwepo.kwa hiyo ninaomba sasa uingie ndani na uanze kujiandaa kwa ajili ya kuongea na waandishi wa habari.”akasema Cellne



“ Good Job celline.halafu bado kuna jambo moja ninataka ulifane.Ninataka niwasiliane na Dr Kigomba Yule katibu wa rais.” Akasema Rose

“ Sawa madam ngoja nimtafute simuni halafu nitakupa uongee naye” akasema Celline na kumsaidia Rosemary kunyanyuka akaelekea chumbani kwa ajili ya kujiandaa kuongea na waandishio wa habari



Dege la rais linalotajwa kushika nafasi ya pili kwa ufahari barani afrika lilionekana katika anga ya jiji la Dare s salaam.Ni dege aina ya Boeng 747 inayotumiwa na Dr Joshua rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Mara tu alipoingia madarakani Dr Joshau aliidhininisha kiasi kikubwa cha pesa kwa ajii ya kununua dege hili kubwa la kifahari

Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere ulifurika watu waliokuja kuupokea mwili wa Flaviana mtoto wa rais unaorejeshwa nchini kutokea nchini afrika ya kusini alikopelekwa kwa matibabu .Viongozi mbali mbali wa serikali walikuwepo uwanjani pale kwa ajili ya kuungana na familia ya katika mapokezi ya le ya mwili wa Flaviana.

Taratibu dege lile kubwa la kifahari likaanza kutua kugusa ardhi likienda kwa kasi kubwa na baadae likaanza kureejea taratibu na kusimama.Mlango wa ndege ukafunguliwa na maafisa kadhaa wa usalama pamoja na baadhi ya viongozi wakaingia ndani ya ndege kuonana na rais.Miongoni mwa watu waliongia ndegeni alikuwepo Dr Kigomba katibu wa rais na mshirika wake mkubwa.

“ Pole sana Mr President “ akasema Dr Kigomba mara tu alipoonana na rais



“ Kila kitu kinakwenda vizuri Kigomba? Akauliza Dr Joshua na kisha Kigomba na maafisa wengine wakamuelezea rais namna kila kitu kuhusiana na msiba ule kinavyokwenda na maandalizi yaliyokwisha fanyika.Rais akatoa maelekezo kadhaa na kisha baadhi ya maafisa walioambatana na rais wakaanza kushuka ndegeni na halafu akashuka Anna mtoto pekee wa rais aliyebakia akiwa ameongozana na shangazi yake .Alikuwa amevaa mavazi meusi na macho yake aliyafunika kwa miwani mikubwa ili yasionekane namna yalivyokuwa yamevimba kwa kulia

Baadhi ya ndugu walipomuona Anna wakaangua kilio kikubwa pale uwanjani hali iliyomlazimu Anna naye kujiunga nao kulia .Watu wengi wakiwemo ndugu na marafiki zake walikuja kumpa pole.Baada ya kama dakika kumi hivi Dr Joshua akamaliza kikao kifupi na maafisa wale waliomfata ndegeni , akashuka.Viongozi mbali mbali walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kumpa pole .Dr Joshua akasalimiana nao wote na kisha wakajipanga ili kushuhudia mwili wa Flaviana ukishushwa ndegeni. Taratibu jeneza lenye mwili wa Flaviana likashushwa na kupakiwa katika gari maalum lililoandaliwa kwa ajiliya kuupeleka hospitali .Shughuli uwanjani hapo zikamalizika na Dr Joshua akaingia katika gari lake na kuondoka na msafara wake kuelekea katika makazi yake binafsi ambako ndiko shughuli zote za msiba zingefanyika.Mwili wa Flaviana ukapelekwa kwanza hospitali ambako ungekaa huko wakati taratibu za mazishi zikiendelea.

Katika makazi binafsi ya rais watu walikuwa ni wengi sana.Rais akawasili na kupokewa na vilio vya akina mama ,akasalimiana na watu mbali mbali waliokuja kumpa pole na halafu akaenda kuungana na wazee waliokuwapo pale msibani.Baada ya nusu saa za kukaa na wazee pia kupokea mkono wa pole toka kwa watu mbali mbali, Kareem mmoja wa walinzi ambao Dr Joshua anawaamini sana akamfuata na kumwabia kwamba Dr Kigomba anahitaji kuonana naye katika chumba cha maongezi ya faragha .Dr Joshua akawaomba radhi wale wazee aliokuwa amekaa nao akazunguka mlango wa nyuma na kuingia ndani na moja kwa moja akamfuata Dr Kigomba katika chumba cha maongezi ya faragha.

“ Kigomba mambo yanakwendaje?



“ Dr Joshua samahani kwa kukusumbua lakini imenilazimu kufanya hivyo .Kuna mtu anataka kuongea nawe.Ni mtu muhimu na amesisitiza sana kutaka kuongea nawe sasa hivi.” akasema Dr Kigomba

“ Ninani? Akauliza Dr Joshua

“ Ni Rosemary Mkozumi”



“ Rosemary? Anataka nini ?



“ Atakueleza mwenyewe katika simu lakini kikubwa alichokisema ni kwamba anataka akupe pole kwa matatizo lakini najua lazima kuna suala lingine” akasema Kigomba .Dr Joshua akavuta pumzi ndefu alionekana kushtushwa sana aliposikia Rosemary anataka kuongea naye

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Mbona umestuka sana Dr Joshua? Akauliza Dr Kigomba



“ That woman is a snake.Yeye na mume wake ni nyoka wenye sumu kali sana.Nimeshangaa sana kutaka kuongea nami wakati mimi na yeye hatuna mazoea ya kupigiana simu na kama ulivyosema lazima kuna jambo anataka kuniambia.Vipi kuhusu Peniela uligundua chochote toka kwake kuhusu mahusiano yake na Elibariki? Kuna maendeleo yoyote yamefikiwa kufahamu mahala alikojificha Elibariki?







“ Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za mahala alikojificha Elibariki.Anaonekana amejificha mahala ambako si rahisi kuonekana lakini ninakuhakikishia kwamba lazima atapatikana.Kwa Peniela nilijaribu kumchunguza lakini hakukuwa na dalili zozote kwamba yeye na Elibariki wana mahusiano.Nadhani chanzo cha taarifa hakikuwa na uhakika”

“ Ok good.Hata hivyo lazima tuikamilishe biashara yetu as soon as possible.Kama nilivyokufahamisha awali kwamba Hussein anawasili leo jioni kwa hiyo inabidi ukampokee na kuhakikisha anakuwa salama halafu tujipange ili tuweze kumaliza biashara yetu.Hatutakiwi kuendelea kuchukua tena muda mrefu kwani kadiri tunavyozidi kuchukua muda mrefu ndivyo tunavyozidi kupata athari kwa hiyo suala hili halitakiwi kuchukua zaidi ya siku tatu kuanzia sasa.Nataka baada ya msiba wa Flaviana kumalizika na sisi tuwe tumemaliza biashara yetu .Hakuna tena cha kusubiri kwani jamaa tayari wamekwisha tulipa pesa yote kilichobaki ni kiasi kidogo sana ambacho wanaweza wakakikamilisha muda wowote kwa hiyo anza kufanya maandalizi ya mahala ambako makabidhiano yatafanyika .Iwe ni sehemu tulivu na salama sana.” Akasema Dr Joshua.

“ Sawa Dr Joshua nitashughuilikia kila kitu usijali” akasema Dr Kigomba

“ Tutajadili masuala haya baadae kwa utulivu lakini kwa sasa nataka niongee na huyo Rosemary Mkozumi nisikie anachokitaka” akasema Dr Joshua na Dr Kigomba akachukua simu yake akazitafuta namba Fulani akapiga

“ Hallow Celline ,mheshimiwa rais yuko tayari sasa kuzungumza na madam Rose” akasema Dr Kigomba na kumpatia simu Dr Joshua halafu akatoka nje ya kile chumba kumpa nafasi Dr Joshua

“ Hallow mheshimiwa rais” akasema Rosemary Mkozumi



“ Hallow Rose.Habari za siku nyingi?

“ Habari naweza kusema ni nzuri na si nzuri pia.kwanza pole sana kwa matatizo yaliyokupata wewe na familia yako kwa kumpoteza Flora na mwanao Flaviana” akasema Rose



“ Ahsante sana Rose.Ni mapenzi ya mungu kwa hiyo hatuna budi kukubaliana nayo japo tunaumia.Nimestuka kidogo nilipoambiwa kwamba unahitaji kuzungumza nami” akasema Dr Joshua

“ Ouh Dr Joshua kitu gani kimekustua? Am I an enemy? Akauliza Rose huku akicheka kidogo

“ Hapana si hivyo Rose,unajua mimi na wewe hatuna mazoea ya karibu sana ya kupigiana simu na ndiyo maana nimestuka na kujiuliza maswali mengi kwamba Rose anataka kunieleza jambo gani? akasema Dr Joshua

“ Usiogope Dr Joshua hakuna jambo lolote baya ila ni kweli kama ulivyosema kwamba mimi na wewe hatuna mazoea ya karibu sana ya kupigiana simu lakini from now onwards we’ll be very close friends.” Akasema Rose



“ Nitafurahi sana Rose” akajibu Dr Joshua

“ Dr Joshua samahani sana kwa kukusumbua katika wakati huu wa matatizo lakini dhumuni kuu ni kutaka kuonana nawe.” Akasema Rose



“ Unataka kuonana nami? akauliza Dr Joshua kwa mshangao kidogo

“ Ndiyo ninataka kuonana nawe. Kuna mambo kama mawili matatu hivi ya muhimu sana ambayo nataka kuzungumza nawe ana kwa ana”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Ni mambo gani hayo hatuwezi kuzungumza simuni?

“ Hapana Mr President ni mambo mazito ambayo hayafai kuzungumzwa simuni.Mimi na wewe tunapaswa kuonana na kuongea” akasema Rose

Dr Joshua akafikiri kwa sekunde kadhaa na kusema

“ Ok unataka tuonane lini na wapi?

“ We have to meet today.Tuonane leo hapa hapa nyumbani kwangu mida ya saa tisa kama itawezekana” akasema Rose

“ Saa tisa haitawezekana,nina miadi ya kuonana na mtu muhimu sana mida hiyo na halafu niko hapa msibani wageni wengi wanakuja kunipa pole.Vipi jioni ya leo”



“ Sawa Dr Joshua.Tuonane jioni ya leo ila nakuomba usikose kwani ni mambo ya msingi sana ambayo tunataka kuyajadili na ninakuhakikishia utafurahi mwenyewe” akasema Rose



“ Nitafika Rose bila kukosa” akasema Dr Joshua na kukata simu



“ Huyu Rose anataka kunieleza jambo gani? Nimekwisha sikia taarifa za huyu mama anasemekana ni mtu hatari sana na mwenye mtandao mkubwa.Kuna uwezekano akawa tayari amepata taarifa za kuhusiana na package ? Lazima kuna jambo kwani huyu mama hawezi kutaka kuona na mimi hivi hivi kwa suala ambalo halina maslahi kwake.Anyway nitakwenda kuona anaye nimsikie anataka nini.” Akawaza Dr Joshua .

“ Mchana wa leo ninataka kuona na Peniela.Ninahamu sana ya kuonana na Yule mtoto.Toka aliponipigia simu jana nimekesha ninamuota yeye.Huyu msichana ndiye faraja yangu na wakati huu wa matatizo haya ninamuhitaji sana.Nitampigia simu kumtaarifu kwamba tayari nimekwisha rejea” akawaza Dr Joshua na mlango ukafunguliwa akaingia Dr Kigomba

“ Is everything ok Mr President? Akauliza Dr Kigomb

“ Everything is fine.Rose anasema kuna jambo anataka kuongea na mimi na hajanieleza ni jambo gani.Nitakwenda jioni kuonana naye nyumbani kwake” akasema Dr Joshua

“ Sawa Dr Joshua nimepata taarifa kwamba balozi wa India amekuja.Nadhani uende ukaonane naye” akasema Dr Kigomba na Dr Joshua akatoka kwenda kuonana na balozi wa India.







********





Waandishi wa habari kutoka karibu vyombo vyote vikubwa vya habari waliitika wito na kufika kwa wingi nyumbani kwa Rosemary Mkozumi.Ukaguzi ulikuwa mkali sana kuhakikisha kwamba hakuna kati yao aliyekuwa na silaha ya aina yoyote.Waandishi wote walipokewa na kupelekwa bustanini ambako ndiko Rose angefanya nao mkutano

Saa nane na dakika saba Rose akiwa anasukumwa katika kiti cha magurudumu akajitokeza na kuelekea moja kwa moja katika meza kuu .Celline akawafuata waandishi wale na kuwauliza kama kila kitu kiko tayari na kama wanaweza kuanza.Kila kitu kilikuwa tayari hiyo moja kwa moja mkutano kati ya Rosemary Mkozumi na waandishi wa habari ukaanza



“ Ndugu zangu waandishi wa habari kwanza kabisa ninapenda kuwashukuru sana kwa kuitika wito na kufika kwa wingi japokuwa taarifa zimewafikia kwa kuchelewa sana.Ahsanteni sana kwa kufika kwenu.” Akaanzisha kikao Rose



“ Nimewaiteni hapa kuzungumza nanyi na kupitia ninyi taifa zima la Tanzania liweze kupata habari hii.Nina mambo moja kama si mawili ambayo ninataka kupitia kwenu watanzania waweze kuyafahamu.” Akanyamaza kidogo halafu akasema



“ Jambo la kwanza ambalo ninataka kuwafahamisha watanzania ni kwamba siku ya jana mida ya saa tano asubuhi nilivamiwa hapa nyumbani kwangu na watu wasiojulikana wakamuua mpenzi wangu kwa risasi na mimi wakaniteka.Ninaposema mpenzi wangu najua wengi wenu mtashangaa kwani mnamfahamu Deus Mkozumi kama mume wangu lakini mimi na yeye tulikwisha tengana muda mrefu na kila mmoja kwa sasa yuko huru na maisha yake kwa hiyo mimi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye aliuawa na wavamizi hao.” Akanyamaza kwa sekunde kama tano hivi kisha akaendelea

“ Baada ya kuniteka wavamizi hao walinipeleka mahala nisipokujua wakanifunga na kunitesa sana.Walinitoboa sehemu mbalimbali za mwili wangu kwa kutumia mashine ya kutobolea na kama haitoshi walinikata vidole viwili vya miguu.Walinitesa sana .”

“ Ndugu waandishi wa habari mimi nimekuwa katika siasa kwa muda mrefu na nilimsaidia sana rais mstaafu Deus Mkozumi wakati huo nikiwa mke wake na kama mnavyofahamu kazi ya siasa ina maadui wengi na hasa pale unapokuwa unafanya vizuri .Hata mimi pia kuna watu ambao wananichukia hasa kutokana na kufanikiwa katika shughuli zangu za kisiasa na hasa zile zinazogusa maisha ya watu wa hali ya chini.Nimekuwa mstari wa mbele sana katika kuamsha ari na mwamko wa kisiasa kwa akina mama na vijana hapa nchi.Mimi na taasisi yangu ya mama Rosemary tumekuwa tunazunguka nchi nzima kuhamasisha wanawake na vijana kujiunga katia vikundi na kuwawezesha kiuchumi vile vile tumewahamasisha washiriki atika shughuli za kisiasa na kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali katika chaguzi zijazo.Jambo hili kuna watu ambao halikuwafurahisha na ndiyo maana wakatumia vijana wale waniteke na kunitesa namna hii.Lakini kubwa zaidi nililoligundua ni kwamba watu walionifanyia hivi kuna jambo moja kubwa wanaliogopa.” Akasema Rose na kunyamaza na baada ya muda akaendeleahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“ Ndugu waandishi wa habari na watanzania najua baadhi yenu mmekwisha sikia tetesi tetesi kuhusu mimi kuhusishwa na kuwania urais baada ya muhula wa pili wa Dr Joshua kumalizika lakini sikuwahi kusimama hadharani na kuliongelea jambo hili .Leo kupitia kwenu waandishi wa habari nataka niliongelee suala hili na kuliweka wazi.” Akanyamaza akawatazama waandishi wa habari na kusema



“ Ndugu zangu waandishi wa habari,nimezunguka nchi nzima ,nimezifahamu shida za watanzania ,nimeuona umasikini wa watanzania na nina nia ya dhati ya kuwasaidia watanzania na kuwatatulia shida zao na ndiyo maana kupitia kwenu leo hii ninataka kutangaza rasmi kwamba nitagombea urais katika uchaguzi mkuu ujao.Nitaitisha tena mkutano mwingine mkubwa wa waandishi wa habari na wadau mbali mbali kutangaza vipaumble vyangu na nini nitawafanyia watanzania kama nikipata ridhaa ya kuwaongoza lakini katika mkutano huu wa leo ninataka kutuma ujumbe kwa wale watu wenye nia ya kunikatisha tamaa kwamba hawataweza.Nina dhamira ya dhati ya kuwatumikia watanzania na kwa hiyo juhudi zao hazitafanikiwa.Naomba niwaeleze watanzania kwamba tukio zima la mimi kutekwa nyara na kuteswa limeratibiwa na watu ambao hawataki mimi nigombee urais kwani wanajua wazi kwamba watanzania wananijua na lazima watanichagua .Walinitolea vitisho vingi vya kuniua endapo nitaendele ana harakati zangu za kutaka kuwania urais na mimi kupitia kwenu ninawaambia kwamba sintarudi nyuma nimejitolea kuwatumikia watanzania hata kama ikinibidi kupoteza uhai wangu.Ninaomba watanzania wote bila kujali itikadi zenu mniunge mkono katika dhamira yangu hii kubwa ya kuwatumikia na ninawaahidi kwamba licha ya juhudi nyingi za watu wanaotaka kunirudidisha nyuma sintokata tamaa. Ndugu zangu waandishi wa habari ninawashukuru sana kwa kufika kwenu na watanzania wamesikia kupitia kwenu na kama nilivyowaambia awali kwamba nitakuwa na mkutano nanyi hivi karibuni nitazungumza nanyi mambo mengi ila kwa leo nililokuwa ninataka watanzania walifahamu kupitia kwenu ni hilo.Mtanisamehe kutokana na hali yangu sintahitaji maswali kwa siku ya leo .Nitakapokutana nanyi siku nyingine mtapata nafasi kubwa y a kuuliza maswali “ akasema Rose na kuondoka pale bustanini

“ Mateso waliyonitesa wale washenzi yatanisaidia sana kunijenga kisiasa.Hawakujua kwa kunitesa vile wananitengenezea jina kubwa.Natumai taarifa hii ya leo itaitikisa nchi na hasa kutokana na namna itakavyopewa umuhimu mkubwa na vyombo vyote vya habari.” Akawaza Rosemary wakati anarudishwa ndani.





Taarifa ya Rosemary Mkozumi kutaka kuwania nafasi ya urais ilianza kusambaa kwa kasi ya ajabu mara tu baada ya kumaliza mkutano wake na waandishiwa habari.Ukuaji wa teknolojia ulifanya taarifa ile iwafikie watu wengi ndani ya kipindi kifupi sananakuzua gumzo hasa katika mitandao ya kijamii.Wengi walionekana kumuunga mkono mama huyu hususan vijana ambaoamekuwa akiwawezesha sana kiuchumi.

Rosemary alianza kupokea simu za pongezi kutoka kwa watu mbali mbali wakimpa pole na kumpongeza kwa hatua yake ile ya ujasiri na wakiahidi kumuunga mkono katika mbio zake za kusaka urais.Ilikuwa ni siku njema sana kwa Rose na uso wake haukukaukiwa tabasamu licha ya maumivu ambayo badoaliendelea kuyasikia

Rais mstaafu Deus Mkozumi akiwa amejipumzisha nyumbani kwake alitumiwa video na rafiki yake ya alichokizungumza Rose katika mkutano wakena waandishi wa habarina kumstua sana.

“ Rosemary awe Rais?? Akasema Deus na kucheka kwa dharau kidogo.

“ Hapana haiwezekanai.Hili ni jambo lisilokubalika hata kidogo .Hatuwezi kuichezea nafasi hii nyeti sana kwa kuwaacha watu wachafu kama hawa watie nia ya kutuongoza.Nimeishi na Rose kwa miaka ishirini na nane,ninamfahamu vizuri kuliko mtu yeyote Yule..She’s a devil.Watu wanachanganyikiwa na misaadaya fedha anazowapatia bila hata ya kuhoji anazipata wapi.Ninaapa kamabado niko hai Rose hafanikiwi katika jambo hili” akawaza Deus na kuitazama video ile kwa mara nyingine i.

“ Ni akina nani waliokuwa wamemteka nyara Rosemary? Nakumbuka Peniela aliniambia kwamba anawafahamu watu waliomteka Rose na nikamsihi awaambie watu hao wasithubutu kumuachia Rose kwani ni mtu htari mno ninashangaa amewezaje kuwa huru? Kwa nini wamemuachia? Akajiuliza Deus.

“ nahitaji kuitisha kikao cha dharura haraka sana na timu yangu tulijadili suala hili na tuone namna tunavyoweza kulizuia lisifanyie.Hili si jambo la kufanyia mzaha hata kidogo lazima kwa gharama zozote zile nihakishe lengo la Rosemary halitimii.”akawaza Deus

“ Nimeanza kuwa na hisia kwamba yawezekana Rose akahusika hata katika kifo cha Amos.Nitafanya uchunguzi ili nibaini kama ni kweli alihusika na kama ni yeye ndiye aliyehusika nitamfanyia kitu kibaya sana” akawaza Deus na kuhukua simu akawapigia washirika wake akawataka wakutane kwa dharura jioni ya siku ile kulijadili suala lile la Rose.









*******





Kiza kimeanza kutanda angani .Nyumbani kwa Rosemary Mkozumi ulinzi uliimarishwa kwani rais Dr Joshua alitarajia kwenda kuonana na Rosemary jioni hiyo.

Saa moja na dakika ishirini na mbili Dr Joshua akawasili nyumbani kwa Rose na kupokewa na Rose ambaye alikuwa anatembea kwa kuchechemea wakaelekea bustanini mahala kulikokuwa kumeandaliwa maalum kwa ajili yao



“ Pole sana Rose.nani amekufanya hivi? Akauliza Dr Joshua

“ Ni hadithi ndefu Mr Presdent lakini napenda nichukue nafasi hii nikupe pole sana wewe pia kwa matatizo yaliyokupata”

“ Ahsante sana Rose.Mimi na familia yangu tunapitia kipindi kigumu sana cha majaribu lakini naamini kwa dua zenu tutasimama imara na tutashinda.Habari za siku nyingi Rose? Ni muda mrefu sana hatujaonana na ndiyo maana uliponiambia kwamba unataka kuonana nami nilistuka kidogo.By the way nataka binafsi nikupongeze kwa tamko ulilolitoa leo hii kuhusiana na kusudio lako la kutaka kuwania urais.Hongera sana kwa maamuzi hayo makubwa na ninahisi yawezekana jambo hili likawa miongoni mwa mambo yaliyotukutunanisha jioni hii” akasema Dr Joshua na kumfanya Rose atabasamu



“ Ahsante sana kwa pongezi Dr Joshua ingawa nilitegemea ungewahi kunipigia simu na kunipongeza mara tu baada ya kuzipata taarifa hizo lakini nashukuru hata hivyo kwa kunipa moyo.Suala hili litakuwa ni kama nyongeza tu katika yale masuala makubwa ambayo nimekuitia hapa .Kuna mambo mawli makubwa ninayotaka kuzungumza nawe.” Akasema Rose.Muhudumu wa Rose akafika na chupa ya mvinyo akawamiminia katika glasi



“ Kabla hatujaendelea mbele Rose,vipi maisha yanakwendaje? Akauliza Dr Joshua

“ Maisha yanakwenda vizuri sana .”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Vipi mnawasiliana na Deus?

“ hatuwasiliani kabisa.Mimi na Deus ni kama paka na panya hivi sasa na nina hakika ni yeye ambaye alikuwa nyuma ya vijana wale walionifanya hivi” akasema Rose



“ Are you sure Rose? Akauliza Dr Joshua

“ yes I’m sure.Ni yeye ambaye amekuwa akinipiga vita sana katika mambo yangu.Tulipoachana alitegemea labda ningeadhirika na kumpigia magoti lakini badala yake nimekuwa na mafanikio tofauti na alivyotegemea na ndiyo maana anafanya kila juhudi kutaka kunirudisha nyuma”

“ Deus is a monster.Anatakiwa akamatwe haraka sana na kufikishwa katika vyombo vya dola.kwa nini hukunitaarifu mapema ili tuweze kumchukulia hatua? Mimi sijali kama ni ras mstaafu lakini kama anahusika katika uporaji na utesaji wa watu lazima achukuliwe hatua kali” akasema kwa ukali Dr Joshua

“ Dr Joshua you know how Deus works,right? He’s a very smart person.Kwa sasa sina ushahidi wa moja kwa moja kwa moja wa kuweza kumtia hatiani Deus kwa tukio lile lakini ninakuhakikishia ndani ya siku mbili hizi nitakuwa nimepata ushahidi kamili na wa kutosha kabisa kwamba Deus ndiye aliyewatuma vijana wale waniteke nyara.” Akasema Rose



“ It must be him!!. Akasema Dr Joshua kwa ukali.Rose akamuangalia kisha akachukua glasi ya mvinyo akanywa kidogo na kusema

“ Why do you hate him so much? Akauliza Rose.Dr Joshua akachukua glasi akanywa mvinyo kidogo kisha akasema



“ Nitashindwaje kumchukia kwa mambo kama haya aliyokufanyia? Huu si ubinadamu hata kidogo”akasema Dr Joshua.Rose akaguna kidogo kisha akassema



“ You hate him because of what he did to me of because what he knows about you? Akauliza Rose huku akitabasamu

“ Deus knows me ? akauliza Dr Joshua

“ By the way pole sana kwa kifo cha Amos.” Akasema Rose



“ Ahsante sana.Umejuaje kama Amos amefariki dunia? Akauliza Dr Joshua.Rose akacheka kidogo na kusema



“ Dr Joshua tunaishi katika kijiji na kila kinachofanyika lazima nikijue.Kikubwa zaidi ambacho yawezekana hukuwa unakifahamu ni kwamba Amos alikuwa ni mtu wangu na mimi pia.Alikuwa ni mtu mwenye msaada mkubwa kwangu na alikuwa ananieleza kila kinachofanyika ndani ya ikulu.”

Dr Joshua akastuka akamtazama Rose kwa macho makali

“ Amos alikuwa anaripoti kwako pia? That bastard !! amekueleza mambo gani? akahamaki Dr Joshua

“ Usihamaki Dr Joshua.Amos hakuwa akiripoti kwangu tu vile vile alikuwa ni mtu wa Deus ndani ya ikulu na ndiye aliyekuwa anampatia Deus habari zako zote.”



“ Ouh my Gd !! akashangaa Dr Joshua

“ Ndiyo maana nikawa najiuliza huyu Deus amepataje habari zangu? Kumbe alikuwa anaambiwa na Amos.Dah ! nilikosea sana kumuamini .Kumbe ni yeye ambaye amekuwa ananiuza kwa muda wote huu.Kila kitu tukifanya kilikuwa kinajulikana kabla hata ya utekelezaji wake kumbe chanzo cha yote ni Amos.Tumekumbana na vikwazo lukuki kumbe chanzo ni Amos..Dah nashukuru amekwenda lakini amenistua sana.Kumbe katika hii dunia hupaswi kumuamini mtu yeyote.Nilimuamini sana mke wangu Flora naye akataka kunisaliti na kuvujisha siri nikalazimika kumuondoa.Ni nani basi nitakayemuamini kama watu wangu wa karibu wote wanageuka wasaliti?



“ unawaza nini Dr Joshua? Akauliza Rose na kumstua Dr Joshua toka mawazoni



“ Rose taarifa uliyonipa imenistua sana.Amos ni mmoja wa watu niliowamini kupita kiasi na sikutegemea kabisa kama angeweza kunifanyia kitu cha namna hii.Sikutegemea kabisa mtu kama Amos angeweza kunizunguka na kushirikiana na mtu kama Deus.”akasema Dr Joshua

“ Ulifanya makosa makubwa sana Dr Joshua kumuamini mtu kupita kiasi.Katika siasa hakuna mtu wa kumuamini.Kila aliye mbele yako ni adui yako mtarajiwa kwahiyo hili liwe ni fundisho kwako.Kuanzia leo hii usimuamini mtu yeyote Yule”akasema Rose

“Kinachonichanganya zaidi mambo yangu mengi sana anayafahamu kwa hiyo sijui amemweleza nani kitu gani”akasema Dr Joshua na kunywa mvinyo kidogo



“ he told me everything about your wife.Yeye ndiye aliyemuua Dr Flora kwa kumchoma sindano ya sumu,alinieleza pia kuhusiana na kifo cha Flaviana kilisababishwa na watu uliowatuma wakamuue jaji Elibariki,alinieleza pia kuhusiana na jambo unalotaka kulifanya la kuiuza package yenye kirusi Aby.Kwa ujumla alinieleza mambo mengi.Kila unachokifanya alikuwa ananieleza kwa hiyo ninakufahamu nje ndani” akasema Rosemary.DrJoshua akainama na kushika kichwa kwa mikono yake.

“ Najua umestuka sana Dr Joshua kuona kwamba ninafahamu mambo yako yote unayoyafanya huku ukidhani kwamba watu hatujui kumbe tunajua kila kitu.Lakini usiogope mimi siwezi katu kuufungua mdomo wangu kwa mtu yeyote Yule kwani hata mimi nilikuwa ninamtumia Amos ili niweze kuipata hiyo package.Wote tulikuwa na lengo moja la kujipatia kiasi kikubwa cha pesa kupitia package hiyo lakini kwa sasa baada ya Amos kufariki mimi na wewe tunapaswa kuwa washirika”

“ What !!..Dr Joshua akashangaa



“ Mbona unasangaa Dr Joshua? Sote lengo letu lilikuwa moja tu kupata pesa kwa hiyo ninataka tushirikiane katika suala hili kwani hata mimi nina hitaji pesa.Baada ya mauzo nitahitaji unigawie kiasi fulani cha pesa ili kinisaidie katika kuendesha kampeni yangu ya kuwania urais.” Akasema Rose



“ Hilo haliwezekani Rose.Siwezi kuwa na ushirika na wewe”akasema Dr Joshua

“ Kama haliwezekani then you wont sell the package” akasema Rose huku akitabasamu

“ Now you are threatening me Rose” akasema Dr Joshua

“ This is not a threat Dr Joshua this is a warning.Kama hutataka kushirikiana nami basi hutaweza kuuza huo mzigo.Dr Joshua umezungukwa katika kila kona na kamwe mpango wako huo hautafanikiwa na pindi ukijaribu kutaka kuitoa package ile ikulu ndio utakuwa mwisho wako.You will die in prison.Kuna watu ambao hawalali usiku na mchana wanakuwinda na wanaihitaji hiyo package zaidi ya roho yako.Ninafahamu mipango yao yote ninafahamu kila wanachokipanga na kama ukitaka tushirikiane basi utavuka vikwazo vyote na utafanikiwa lakini endapo utapuuza onyo hili hautasalimika kamwe.” Akasema Rosemary



“ Ouh Rosemary don’t ever try me my former first lady !! akasema Dr Joshua

“ Hilo ni jambo la kwanza Dr Joshua kuna jambo lingine la pili.Nitaendelea kuufumba mdomo wangu kuhusiana na mambo unayoyafanya na hususan kuhusika kwako katika kifo cha mkeo Dr Flora kama ukilikubali na kulitimiza”

“ No body will believe you.Hakuna ushahidi wowote wa kunihusisha na suala hilo”akasema Dr Joshua



“ Usijidanganye dr Joshua.Do you know this guy called Mathew? Huyu ni kijana hatari sana na huyu ameapa hatalala usingizi mpaka ahakikishe amekuangusha.Anafahamu kila kitu kuhusu wewe ana kila ushahidi wa kila unachokifanya.Nakuambia Dr Joshua kijana huyu ni hatari kuzidi hatari yenyewe lakini kama ukinitumia mimi niko tayari kukusaidia kumpata na kama ukimpata huyu then you are a free man..” akasema Rose.Dr Joshua akamtazama na kusema

“ Kitugani hasa unachokitaka toka kwangu Rose?



“ Kuna mambo mawili makubwa nayataka toka kwako.Moja nataka kushirikishwa katika mpango unaoendelea wa uuzwaji wa package yenye kirusi Aby.Nitaka na mimi nipate mgawo wangu sawa kwa sawa.Pili muda wako wa uongozi unaelekea ukingoni .Najua kwa sasa kuna mchakato wa kumpata mrithi wako ndani ya chama ,na mtu kama mimi sina nguvu kubwa ndani ya chama nataka utumie nafasi yako kama rais unipitishe niwe mgombea urais .”

“ What ?!!! akasema Dr Joshua na kusimama

“ Unataka nikufanyie nini? Akauliza kwa ukali

“ You are going to make me the next president of the united republic of Tanzania.”akasema Rose



“ No I cant!! Akasema Dr Joshua huku akigonga meza

“ Yes you can and you are going to do it !!! akasema Rose kw a kujiamini

“ Dr Joshua naomba usihamaki tafadhali.Najua una mipango mingi mizuri ya kuishi maisha mazuri siku za mbele baada ya kustaafu.Mimi ndiye mwenye kuamua hatima ya maisha yako baada ya kustaafu.Ukitaka kuishi maisha mazuri tafadhali kubaliana nami katika yale yote niliyokueleza .Si mambo magumu kwako hata kidogo”

“ You devil !! akasema Dr Joshua kwa ukali



“ I’m not a devil Dr Joshua.I’m your angel.Mimi ndiye msaada mkubwa kwako.I’m going to protect you”

“ Protect me ?



“ yes !! I can protect you.Kukuonyesha kwamba mimi ni msaada mkubwa kwako ninakwenda kukuonyesha kitu ambacho you’ve been dying to see. You will thank me “ akasema Rose na kumchukua Dr Joshua wakaelekea ndani.walipoingia sebuleni Rose akawageukia walinzi wa rais

“ Guys you can wait here.We’ll be fine..”akasema Rose.walinzi wale wakaonyesha kutokukubaliana naye

“ Its ok guys.we’llbe fine”akasema Dr Joshua kisha wakaelekea hadi katika chumba alichofungwa Elibariki.Mlango ukafunguliwa na taa ikawashwa.Dr Joshua akapatw ana mshangao mkubwa baada ya kuonana na jaji Elibariki mtu ambaye amekuwa anamuwinda kwa nguvu kubwa usiku na mchana.





“ Elibariki?!! Dr Joshua akashangaa sana kumkuta Elibariki mle chumbani.Hakuwa ametegemea kabisa kuonana naye ana kwa ana

“ Mr President!! Akasema jaji Elibariki.Hu uso wake ukiwa umejikunja kwa hasira Dr Joshua akamgeukia Rosemary Mkozumi

“ What is the meaning of this Rose? Akauliza kwa ukali

“ Dr JoshuJaji Elibariki ni mtu ambaye ulikuwa unaota kumpata usiku na mchana.Umetumia nguvu kubwa ya vyombo vya dola kumtafuta lakini mpaka sasa hawajafanikiwa kumpata na wasingeweza kumpata kamwe.He wants to talk to you! akasema Rose

“ This man is ..!! akasema kwa ukali Dr Joshua lakini Rose akamzuia



“ Usihamaki Dr Joshua.You have to talk to him.Nakuhakikishia kwamba hutajuta kuzungumza naye” akasema Rose.Uso wa Dr Joshua ulionyesha hasira za wazi

“ hatimaye nimekupata mwanaharamu wewe.Nina hasira nawe sana .Wewe ni chanzo cha matatizo yangu mengi.Ni wewe uliyesababisha hadi mwanangu Flaviana akafariki.Ninakuchukia Elibariki na ninatamani hata nikuvamie na kukuua kwa mikono yangu mwenyewe.” Akawaza Dr Joshua huku akiuma meno kwa hasira halafu akachukua kiti akaketi .

“ Rose sijapendezwa kabisa na hiki ulichokifanya.Huyu mtu ni mhalifu na mida hii anatakiwa awe gerezani.Huyu ni chanzo mwanangu Flaviana kufariki dunia.I hate this man !!.Kwa nini umemuhifadhi hapa kwako?.akasema Dr Joshua kwa hasira

“Dr Joshua kwa nini tusiokoe muda na kuongea mambo ya msingi? Sisi sote hapa tunafahamu kila kinachoendelea na kwamba hayo yote unayoyasema hayana ukweli hata kidogo,Elibarikihahusiki hata kidogo katika kifo cha mkeo wala mwanao.You killed them yourself.” Akasema Rose na Dr Joshua hakujibu kitu akabaki anamtazama kwa hasira

“ Kwa taarifa yako Dr Joshua ni kwamba jaji Elibariki ndiye aliyeniokoa mimi mahala nilikokuwa nimefungwa nikiteswa na aliniokoa kwa dhumuni la kutafuta msaada wangu na msaada aliokuwa anauhitaji ni kuongea nawe.Kuna jambo la muhimu anataka kuzungumza nawe.Tafadhali msikilize” akasema Rose

“ Unataka kunieleza nini? Akauliza Dr Joshua kwa ukali

“ Dr Joshua ahsante kwa nafasi hii na sitaki kuchukua muda wako mwingi nataka nijielekeze moja kwa moja katika kile ambacho kimenifanya nitake kuonana nawe.” Akasema Jaji Elibariki



“ Kwanza ninataka kuchukua nafasi hii kukupa pole kwa msiba wa mwanao na mke wangu Flaviana.Nimeumia sana kwa msiba ule japokuwa ninatuhumiwa kusababisha kifo kile.Mr President sote tunafahamu kwamba sikuhusika kabisa na kilichotokea usiku ule na wala sikuwa nimelipanga shambulio lile na hata siku moja nisingeweza kumdhuru mke wangu na wewe unafahamu kabisa nani waliomuua Flaviana lakini kwa kuwa una hasira mimi ukaamua kuniangushia kesi ile mbaya ya kusababisha mauaji” akasema Elibariki na Dr Joshua akaendelea kumuangalia kwa hasira.Elibariki akaendelea.



“ Yote haya yalianza baada ya kifo cha Dr Flora.Mazingira ya kifo cha Dr Flora yalimfanya Flaviana aingiwe na shaka na hivyo akaniomba nimsaidie kufanya uchunguzi kubaini nini kilichomuua mama yake.Kwa kushirikiana na wenzangu tulifanikiwa kugundua sababu ya kifo cha Dr Flora kwamba aliuawa kwa kuchomwa sindano ya sumu na hapo ndipo nilipoanza kuwindwa.Nilinusurika kuuawa na nikaokolewa na mwanamke mmoja ambaye simfahamu nikaenda kujificha kwa Pen………”



“ Hebu ngoja kwanza Elibariki,Unasema kwamba uliokolewa na mwanamke.Unamfahamu mwanamke aliyekuokoa? Akauliza Dr Joshua

“ Hapana simfahamu .Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuonana naye na sifahamu ni kwanini aliniokoa.”

“ Unaweza ukanielezea muonekano wa mwanamke huyo ? Akauliza Dr Joshua

“ Ni mrefu kidogo,alikuwa na uso mpana na wenye macho madogo.Kingine ninachokikumbuka ambacho kinaweza kunipa urahisi kumtambua hata kama nikikutana naye kesho alikuwa na kovu katika jicho lake la kushoto.Mdom....

“ Wait ….!! Akasema Dr Joshua

“ Mkono wake wa kushoto una kovu la kuungua?



“ Sikuliona kovu hilo lakini alikuwa amevaa glovu mkono mmoja wa kushoto ila shingoni upande wa nyuma alionekana kama vile ana kovu la kuungua “ akasema jaji Elibariki



“ That’s Jesica!!.Ouh my God .I cant believe this.Jessica !!!..akasema kwa mshangao Dr Joshua

“ Unamfahamu? Akauliza Rosemary

“ Ninamfahamu.Anafanya kazi idara ya usalama wa taifa.Aliwahi kuwa mlinzi wangu wakati Fulani nikamuondoa baada ya kutoridhishwa na tabia zake.Ama kweli nimejifunza katika hii dunia usimuamini mtu yeyote Yule.Who sent her to help him??” akasema Dr Joshua.



“ I’ll find her and she will answer to me everything !! akasema Dr Joshua kwa hasira.

“ Endelea na simulizi yako “ Dr Joshua akamwambia Elibariki.

“ Nilipookolewa nilienda kujificha kwa Peniela na baadae nikachukuliwa na Mathew .”

“ Kwa hiyo taarifa za wewe kujificha kwa Peniela zilikuwa za kweli!! Akasema Dr Joshua

“ ni kweli nilijificha kwa Peniela kwa muda halafu nikaenda kujificha kwa Mathew.”



“ Who is Mathew?!!

“ He’s a monster who did this to me !!..akasema Rosemary



“ Mathew ni rafiki yangu ambaye ni mpelelezi wa kujitegemea ambaye ndiye aliyenisaidia katika kufahamu ukweli kuhusiana na kifo cha Dr Flora.Kwa kushirikiana naye tumegundua mambo mengi sana kuhusu wewe na hasa hili kubwa linaloendelea hivi sasa linalohusiana na kirusi Aby.Dr Joshua mambo ya kukuambia ni mengi lakini kwa kuokoa muda ninataka tuongelee mambo yanayotuhusu mimi na wewe.” Akasema jaji Elibariki .Dr Joshua akachomoa kitambaa mfukoni akajifuta jasho.Maneno aliyoambiwa na Elibariki yalimstua sana



“ Mr President ninajua ninatafutwa kila kona kwa agizo lako na endapo nikikamatwa maisha yangu yataharibika kwani nitaozea gerezani.Sitaki hilo linitokee.Nilijifanya jasiri kutaka kushinda nawe lakini hakuna nilichokipata zaidi ya kuwa mkimbizi nikijificha kama Sungura.Nimeinua mikono vita hii imenishinda.Siwezi kupambana nawe mheshmiwa rais kwa hiyo nimekuja kwako kukuomba msamaha sana kwa yale yote niliyokukosea .Nataka unisamehe na unirudishie maisha yangu ya kawaida tena.Nataka unifutie kesi inayonikabili na niendelee na kazi zangu kama kawaida .” akasema jaji Elibariki.Dr Joshua akamtazama akajifuta tena jasho halafu akasema



“ Natamani sana nikuamini tena jaji lakini kwa mambo uliyonifanyia siwezi kukuamini tena.Naomba nikuweke wazi kwamba ninakuchukia sana, sana, tena sana.Wewe ni adui yangu namba moja na lengo langu ni kukukuondoa kabisa katika uso wa hii dunia.Nilikuamini sana Elibariki nikakupa cheo kikubwa cha jaji wa mahakama kuu lakini badala yake ukaanza kunipuuza na hukunisikiliza tena.Sioni namna ya kukuamini tena Elibariki na kwa vile nimekwisha kuona hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kutumia nguvu zangu zote nilizonazo kuhakikisha kwamba unapotea katika uso wa dunia.Ni heri ungebaki katika maficho yako kuliko kujitokeza.Umejileta mwenyewe katika mdomo wa mamba na ninakuhakikishia kwamba huu ndio mwisho wako.!! Akasema Dr Joshua kwa ukali.

“ He can be trusted ! akasema Rose

“ What ? Dr Joshua akashangaa



“ Do you trust this guy? Do you know who he is?akauliza Dr Joshua kwa ukali

“ Yes I do trust him and you have too” akasema Rose.Dr Joshua akamtazama kwa macho makali na kusema

“ Unanishangaza sana Rose.Huyu mtu hafai kabisa kuaminiwa.Amenifanyia mambo mengi sana ambayo siwezi kumsamhehe hata aseme nini !!

“ Dr Joshua naomba unisikilize.Nimekuleta hapa makusudi kabisa ili uweze kuonana na Elibariki mtu ambaye umekuwa ukiota kumpata usiku na mchana.Huyu ndiye aliyekuwa kikwazo kikubwa katika mpango wako wa kuuza kirusi Aby.Unapaswa ufurahi badala ya kukasirika .Kwa sasa huyu ndiye mkombozi wako.Huyu ndiye anayeweza akasababisha ukaimaliza biashara yako kwa amani na salama”



“ Huyu awe mkombozi wangu??? Rose nashindwa kukuelewa kwa nini unamuamini sana huyu mtu.Hafai huyu kuaminiwa hata kidogo.!!!! Akasema kwa ukali Dr Joshua

“ Ninamuamini kwa sababu ndiye aliyeniachia mimi huru kutoka mahala nilikokuwa nimefungwa.Aliwasaliti wenzake na kuniachia huru kwa lengo la kutaka nikukutanishe naye tu.Hata ukimuangalia machoni anamaanisha kile anachokiongea.Amechoka kukimbia kimbia huku na kule kila siku kujificha.He needs his normal life back na mtu pekee ambaye anaweza akalifanya hilo ni wewe. Elibariki alikuwa anashirikiana na watu ambao walikuwa wanakufuatilia usiku na mchana na ambao wana nia ya dhati ya kuhakikisha kwamba mpango wako wa kuiuza package ile haufanikiwi.They are dangerous people and I swear kama ukipuuza basi huu utakuwa ni mwisho wako.Wana kila ushahidi wa kuweza kukutia hatiani.Elibariki anafahamu kila mpango wao namna walivyojipanga kukuangusha na anaweza akawa ni msaada mkubwa sana kwako” akasema Rose.Dr Joshua akamtazama tena kwa makini kisha akasema

“ Ni ya kweli hayo anayosema Rose? Watu hao uliokuwa unashirikiana nao ni akina nani? Wamepanga mipango gani kuhusu mimi? Akauliza Dr Joshua

“ Mr President anachokisema Rosemary ni kitu cha kweli kabisa.Nimeshirikiana na wenzangu ambao lengu letu lilikuwa ni kuhakikisha kwanza mpango wako haufanikiwi na pili ni kuhakikisha kwamba unapatikana ushahidi wa kutosha wa kuweza kukutia hatiani kwa kifo cha mkeo Dr Flora.Nimetafakari sana na nikaona kwamba hata kama tukifanikiwa kuizuia mipango yako na kufanikiwa kukufikisha mbele ya sheria ,hakuna faida yoyote ambayo ninaweza nikaipata kwani mimi bado nina kesi ya kujibu ya kusababisha kifo cha Flaviana.Ni wewe pekee ambaye unaweza ukanirejeshea maisha yangu ya kawaida hivyo nikaona njia pekee ni kuwasaliti wenzangu na kuonana nawe,nikuombe msamaha na tuweze kuyamaliza haya mambo.Dr Joshua tafadhali naomba uniamini kwamba haikuwa kazi rahisi kuwasaliti wenzangu na kumuachia huru Rosemary lakini nimefanya hivyo kwa lengo moja tu la kutaka kuishi maisha yangu ya kawaida” akasema jaji Elibariki



“ Jaji una maneno mazuri ambayo yananifanya nitake kukuamini tena lakini bado hujanishawishi nitawezaje kukuamini mtu ambaye nilikupenda kama mwanangu na nikakuamini lakini ukanigeuka na kunifanyia mambo ya ajabu kama uliyoyafanya? Kama nikikuamini leo hii nitakuwa na uhakika gani kwamba hutakuja kunigeuka tena na kunisaliti? Akauliza Dr Joshua

“ Mr President naomba uniamini.Najua bado haitakuwa rahisi kuniamini moja kwa moja lakini naomba nikuhakikishie kwamba I know things that you want to know so badly .I can tell you all the plans they have on you,nitakusaidia hata kuweza kuwapata hao wenzangu wote lakini nitayafanya hayo tu endapo utakuwa tayari kunisamehe na kunirejeshea uhuru wangu,kunirejeshea maisha yangu ya kawaida,kunirejeshea kazi yangu na kulisafisha jina langu.” Akasema jaji Elibariki.Dr Joshua akamtazama kwa zaidi ya dakika moja halafu akamgeukia Rose na kusema

“ Rose naomba tutoke tuongee nje kidogo”

Dr Joshua na Rose wakatoka nje ya kile chumba



“ Rose unaniweka katika wakati mgumu sana na kunitaka nimuamini huyu jamaa tena.Huyu ni mtu mbaya mno !! akasema Dr Joshua

“ Right now this is the only guy you need to trust with your life” akasema Rose

“ Elibariki anafahamu mambo yako yote na vile vile anifahamu mipango yote waliyoipanga akina Mathew juu yako.Tafadhali usiache kumuamini tena jaji.Hautapoteza kitu kama ukimuamini tena.Utafanikiwa katika malengo yako na wabaya wako wote watashindwa. This is your last call Mr President” akasema Rose..Dr Joshua akainama akafikiri kwa kama dakika mbili hivi halafu akasema



“ Ok nitafuata ushauri wako na nitamrejeshea Elibariki uhuru wake lakini anatakiwa aonyeshe kwanza juhudi za kunishawishi nimuamini kwa kuniwezesha kuikwepa mipango yote iliyopangwa na hao jamaa zake na kuwafutilia mbali na kama nikifanikiwa basi nitamuamini lakini kama ananidanganya I’ll kill him...”

“ That’s good.! Akasema Rose



“ What about me .Bado hujanipa jibu lolote lile kuhusu yale tuliyoongea.Kumbuka Elibariki works under my command !! akasema Rose.

“ Kuhusu suala la kwanza, nitakuweka katika mgawo endapo biashara ikifanikiwa kwenda vizuri.Suala la pili ninaomba niondoke nalo nikalitafakari kwanza na kuona namna ninavyoweza kulifanyia kazi na kisha baada ya msiba wa mwanangu kumalizika mimi na wewe tutakuwa na kikao kulijadili suala hili kwa upana wake lakini nakuhakikishia kamba nitakusaidia kwa sababu hata wewe umenisaidia sana kumpata huyu mtu ambaye vyombo vya dola vimeshindwa” akasema Dr Joshua kisha wakarejea ndani

“ Jaji ,nimeongea na Rose na amenishawishi nikubali kukuamini tena.Nimekubali kulifanya hilo na nitakurejesha uhuru wako.Nitaliondoa agizo la kukusaka,na utaendelea na maisha yako ya kawaida lakini kama tu ukiniwezesha kuwapata hao jamaa zako pamoja na kunieleza mipango yote waliyoipanga juu yangu.Endapo ukishirikiana nami vizuri basi unaweza ukafaidika sana badala ya kutaka mapambano na mtu kama mimi na unaishia kutanga tanga kama ndege.Nakuhakikishia kwamba endapo utanisaidia katika hili basi utafurahi mwenyewe.Utakuwa na maisha mazuri sana na utajilaumu kwa nini hukushirikiana nami toka mapema.Pamoja na hayo nataka nikuonye kwamba tayari unafahamu mambo yangu mengi kwa hiyo ninachokitaka kingine ni kuufunga mdomo wako.Sitaki uropoke chochote kama watu wengine ambao niliwaamini lakini kumbe ni wasaliti wakubwa kama akina Amos.Kitu cha mwisho ninachotaka kuwa muwazi kwako ni kwamba kwa sasa kwa kuwa bado sijarejesha imani kubwa kwako sintakupa nafasi ya kupumua. Nitakufuatilia usiku na mchana na kila mahala uendako utaongozana na mlinzi nitakaye mteua mimi na utachunguzwa katika kila unachokifanya,kila simu unayopiga na kila unayeongea naye.Nikiridhika kwamba unafaa kuaminiwa basi nitakuacha uwe huru kufanya unavyotaka lakini kwa sasa hadi hapo baadae you’ll be under my control!! Akasema Dr Joshua

“ Tumeelewana Elibarki?

“ Ndiyo Mr President,tumeelewana.!! Akasema Elibariki.



“ Mfungueni hizo pingu nitaondoka naye ili akahudhurie msiba wa mke wake” akasema Dr Joshua.Rose akampigia simu Fernando mlinzi wake na kumtaka afike mara moja naye hakupoteza muda akafika akamfungua jaji Elibariki pingu alizokuwa amefungwa

“ Take him somewhere to clean up.Hatakiwi kuonekana kama ametoka kifungoni” akasema Dr Joshua halafu wakatoka mle chumbani wakaongozana hadi sebuleni ambako Dr Joshua akakaribishwa kinywaji wakati akimsubiri jaji Elibariki aweze kuoga na kujiweka safi. Rosemary akamchukua Elibariki hadi katika chumba kilichokuwa cha Henry akamuacha mle ili aweze kuoga .Baada ya kuoga akagongewa mlango na kuletewa suti nzuri ya gharama iliyokuwa ya Henry.Elibariki akavaa na kupendeza kisha akashuka ngazi hadi sebuleni alikokuwako Dr Joshua.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Now you look like a gentleman.” Akasema Dr Joshua

“ Kwa sasa usijibu chochote endapo ukiulizwa mahala ulikokuwa na kuhusiana na shambulio lile ulilonusurika na lile lililosababisha kifo cha mkeo” akasema Dr Joshua kisha akaongozana na jaji Elibariki hadi katika gari wakapanda na kuagana na Rose wakaondoka.

“ Later tonight,me and you we’ll have a long and serious talk” akasema Dr Joshua na jaji Elibariki akatikisa kichwa kukubaliana naye



“ Elibariki anaonekana kufahamu mambo mnegi sana kuhusiana na kila ninachokifanya.Ameamua kurudi mwenyewe na kuomba msamaha .Kama angelifanya hivi mapema wala tusingefika hapa tulipofika.Tungeweza kupiga hatua kubwa sana na wala asinge hitaji tena hata kufanya kazi.Tatizo la hawa vijana wanatafuta ushujaa lakini matokeo yake ndiyo haya amekosa muelekeo na maisha yake yameharbika.Na kama asingestuka mapema na kuja kuniomba msamaha ningemfutilia mbali toka katika uso wa dunia.” Akawaza Dr Joshua



“ Hawa watu anaoshrikiana nao ni akina nani? Wanaonekana ni watu makini sana na wenye ujuzi wa hali ya juu kiasi cha kuweza kufahamu kila ninachokifanya.Watu hawa hawatakiwi kuachwa hai hata kidogo.NI watu ambao natakiwa kuwaondoa haraka sana “ akawaza Dr Joshua





Mining’ono ilianza msibani mara tu baada ya Dr Joshua kurejea akiwa ameongozana na jaji Elibariki mtu ambaye alitajwa kuhusika katika kifo cha Flaviana.

“ Kuonekana kwako hapa kutazua maswali mengi na maneno mengi yatasemwa lakini unatakiwa uwe mvumilivu sana na usionyeshe aina yoyote ya wasi wasi” Dr Joshua akamnong’oneza jaji Elibariki.

Japokuwa ilikuwa ni usiku tayari lakini taarifa za kuonekana kwa jaji Elibariki pale msibani zilisambaa kwa kasi na watu mbali mbali wakaanza kuja kumpa pole na wengi wakitaka kushuhudia kama taarifa zile ni za kweli ama si kweli.

Nusura Dr Kigomba aanguke kwa mstuko pale alipowaona Dr Joshua akiwa ameongozana na mtu aliyemuita kama adui yake mkubwa ambaye ni jaji Elibariki.

“ What the hell is this ?!!! akajiuliza Dr Kigomba kwa mshangao mkubwa .Hakuamini macho yake kama ni kweli Dr Joshua alikuwa amengozana na adui yao mkubwa.



“ Dr Joshua ?!! anadiriki vipi kuongozana na Elibariki mtu ambaye ni hatari sana kwetu? Mtu huyu tayari anafahamu siri ya kilichomuua Dr Flora kwa hiyo ni mtu hatari sana na Dr Joshaua ametumia nguvu kubwa kumtafuta lakini nashangaa leo hii ameongozana naye bila wasiwasi wowote.Whats going on?? Kuna mambo Dr Joshua ananificha hanielezi ukweli? Aliniambia kwamba anakwenda kuonana na Rosemary Mkozumi lakini badala yake anarejea akiwa ameongozana na adui yetu mkubwa jaji Elibariki mbona kama vile kuna kitu kinaendelea hapa nisichokielewa? Akajiuliza Dr Kigomba.



“ Hapana lazima nimuulize Dr Joshua niufahamu ukweli kama kuna jambo linaloendelea na haniweki wazi.Nimeyaweka rehani maisha yangu ili kuhakikisha kwamba mambo yetu yanafanikiwa lakini kwa kitendo hiki cha kuongozana na jaji Elibariki kimenipa mashaka kidogo.I have to know the truth” akawaza Dr Kigomba na kumfuata Dr Joshua akamuomba waongee pembeni kidogo.Dr Joshua akainuka wakasogea pembeni akawaambia walinzi wake wasogee pembeni ili wapate ya kuongea na Kigomba ambaye uso wake ulionyesha ni wazi alikuwa na jambo linalomsumbua



“ Kigomba ninafahamu ulichoniitia.Najua unachotaka kukifahamu.Nitakueleza kila kitu lakini si sasa hivi.”akasema Dr Joshua



“ Dr Joshua mimi na wewe ni watu tunaoaminiana sana na hata siku moja sijawahi kwenda kinyume na maagizo yako na nimekuwa muaminifu sana kwako.Tumetumia nguvu kubwa kumuondoa Elibariki katika ramani lakini ghafla umeonekana ukiwa naye.Kitendo hiki kimezua maswali mengi sana si kwangu tu bali kwa watu wote kwani tayari kila mtu anafahamu kwamba Elibariki ndiye aliyesababisha kifo cha Flaviana.Utatumia sentensi gani kumsafisha Elibariki.Wale wote waliojitokeza hadharani na kutangaza kwamba jaji Elibariki ndiye mtuhumiwa namba moja wa kusababisha kifo cha mkewe wataonekanaje? Huoni kama wataonekana ni waongo na wanaobahatisha kazi zao? Ouh Dr Joshua please explain to me everything,.!! Akasema Dr Kigomba.



“ Dr Kigomba naomba unipe muda nitakueleza kila kitu kuhusiana na jaji Elibariki .Kuna mambo mengi ambayo mimi na wewe tunatakiwa kuyafahamu kuhusiana na jaji Elibariki” akasema Dr Joshua



“ Dr Joshua sikufichi ndugu yangu umeniweka katika wakati mgumu sana wa kuendelea kuifanya kazi hii.Anyway nitasubiri maelezo yako kama ulivyoniahidi.By the way Hussein amekwisha wasili,nimekwenda kumpokea na kumpeleka katika hoteli .Amekuja na msafara wa watu kumi na ulinzi nimeuimarisha sana katika eneo alilofikia ” akasema Dr Kigomba



“ Ahsante sana kwa taarifa hizo Dr Kigomba ila naomba usihofu kitu kuhusu Elibariki.Kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa na zaidi ya yote huyu jama atakuwa ni msaada mkubwa sana kwetu .Believe me” akasema Dr Joshua na kuachana na Kigomba akarejea mahala alikokuwa amekaa jaji Elibariki

“ Najua kutahitajika maelezo ya kutosha kuhusiana na jaji Elibariki lakini hakuna kitakachoharibika.Kila kitu kitakwenda vizuri tu.Potelea mbali watakavyoongea na waongee tu lakini jaji Elibariki ni mtu ambaye ninamuhitaji sana kwa sasa” akawaza Dr Joshua.

Taarifa za kuonekana kwa jaji Elibariki pale msibani zilimfikia pia Anna mtoto wa rais na kumstua sana ,haraka haraka akatoka na kumtafuta Elibariki mahala aliko.Akamkuta amekaa na baba yake akamsalimu kisha akarejea ndani .Hakupata nafasi ya kuongea naye jambo lolote zaidi ya salamu.



“ bado siamini naona ni kama maajabu.Elibariki ametokea msibani?!! Alikuwa amejificha wapi? Kwa nini ameongozana na baba wakati ni yeye ndiye aliyenihakikishia kwamba baba anahusika katika vifo vya mama na Flaviana? Kuna kitu gani hapa kinaendelea? Akajiuliza Anna wakati akirejea ndani.



“ Lazima nipate nafasi ya kumuhoji na kuufahamu ukweli kuhusu yale yote aliyonieleza na kwa nini anashirikiana tena na baba wakati anajua kabisa kwamba ndiye aliyesababisha kifo cha mkewe na mama. “ akawaza







******







Takribani masaa mawili yamekatika sasa Anitha akiwa katika chumba ambacho kimepewa jina la Room 5.Hiki ni chumba ambacho kipo ndani ya jumba la Rosemary Mkozumi ambacho hutumiwa kwa ajili ya kutesea watu. Anitha alikuwa amefungwa miguu na mikono katika kitanda akiwa hoi na hakuwa akitazamika kwa namna alivyochafuka kwa damu.Ndani ya chumba kile alikuwamo Rosemary Mkozumi ,mlinzi wake mkuu Fernando pamoja na mtu mwingine ajulikanaye kwa jina la Gabon.Huyu kazi yake kubwa ni kutesa watu.Ndani ya chumbakile kulikuw ana mitambo mbali mbali maalum kabisa kwa ajili ya kutesea watu.



“ Madam nadhani kwa leo inabidi tuishie hapa kwani tukiendelea zaidi ya hapa anaweza akapoteza masha.Tumuache apumzike na tuendelee tena na zoezi kesho” akasema Gabon .Rosemary Mkozumi akamtazama kwa macho makali na kusema

“ Ni mara ya kwanza leo kukusikia ukimuonea huruma mtu na kupendekeza tusiendelee kumtesa.You’ve let me down Gabon..I’m totally disappointed!! Akasema Rose

“ Madam tumemtesa sana huyu msichana na wewe mwenyewe umeshuhudia .Ninaomba nikiri kwamba katika muda wote wa kuifanya kazi hii hata siku moja sijawahi kumtesa mju jasiri kama huyu.Nimetumia kila aina ya mateso lakini bado hajafungua mdomo wake na kutupatia kile ambacho tunakitaka.Naomba mnisikilize na tumuache kwa leo apumzike hadi kesho.Tukiendelea kulazimisha kumtesa zaidi tunaweza kumuua na kukosa kila kitu”akasema Gabon



“ Gabon hujamminya vya kutosha huyu.Endelea na kazi hadi nitakaposema mwenyewe basi”akasema Rosemary Mkozumi

“ madam nadhani Gabon yuko sahihi.Tumpumzishe huyu msichana hadi kesho.Tunaweza kumpoteza na kukosa kila kitu” akasema Fernando.Rose akamtazama tena Antha halafu akasema

“ ok sawa .Tumpumzishe hadi kesho ila kesho lazima tuhakikishe anafumbua mdomo wake na kutupata kile tunachokitaka” akasema Rosemary Mkozumi na kuinuka akaelekea chumbani kwake.

“ Huyu Mathew na kundi lake wanaonekana ni watu waliokubuhu sana katika hizi kazi.Huyu msichana pamoja na mateso yote lakini bado hajathubutu luufungua mdomowa wake na kutamka hata neno moja.Ujasiri wa namna hii hupatikana kwa wanajeshi ama majasusi pekee. Watu hawa wamekula yamini Ya kutokusema jambo lolote lile na nina hakika hata tukimtesa vipi yuko tayari kufa kuliko kutueleza mahala Mathew aliko.Kama huyu msichana mdogo yuko hivi je huyo Mathew atakuaje? Lakini pamoja na yote lazima nihakikishe kwamba nimemtia mikononi Mathew kwa gharama zozote zile ndani ya kipindi kifupi sana na kama nisipofanya hivyo he will haunt me like a ghost.”akawaza Rose huku akielekea chumbani kwake.

Gabon akisaidiana na Fernando wakamfungua Anitha na kumtoa mle chumbani wakamrejesha katika chumba alichokuwa amefungwa.Hakuwa akitazamika,uso wake wote ulikuwa umetakapaa damu.Hakuwa na hata nguvu za kusimama.Baada ya kumlaza kitandani Gabon na Fernando wakatoka mle chumbani na kukifunga chumba.

“ Fernando simfahamu msichana huyu ni nani na amefanya nini lakini nakuhakikishia kwamba ni mmoja kati ya wanawake majasiri mno.Kwa mateso niliyompa sina hakika kama hata mimi ningeweza kuvumilia ,lazima ningesema tu ninachotakiwa kukisema .Nina hakika hata kama tukiendelea kumtesa tena kesho hatasema chochote.Ana ujasiri wa kipekee sana na yuko radhi kufa kuliko kuonyesha mahala aliko huyo mwenzake.Huyu si mtu wa kawaida lazima atakuwa amepata mafunzo ya hali ya juu sana kuhusiana na kutokutoa siri ..Pamoja na hayo kwa usiku wa leo tunatakiwa tumchome sindano ambayo itampunguzia maumivu na atalala vizuri bila matatizo.madam Rose anatulipa pesa nyingi sana lakini nyakati nyingine lazima tuwe na mioyo ya kibinadamu.Tumsaidie huyu msichana” akasema Gabon .Fernando akafikiri kidogo na kusema



“ lakini endapo Madam akifafahamu kuhusu jambo hili sote tutakuwa matatizoni.”

“ Usjili kuhusu hilo hawezi kujua.Its just you and me” akasema Gabon na kuingia tena chumbani akafungua sanduku lake na kutoa kichupa Fulani cha dawa akamchoma Anitha kisha wakatoka.



“ Nimekuwa mtesaji kwa muda mrefu lakini sijui ni kwa nini kwa huyu dada moyo unaniuma sana kumtesa.Laiti ningekuwa na uwezo wa kumsaidia ili aweze hata kutoroka basi ningefanya hivyo lakini sina uwezo wa kumsaida.”akawaza Gabon wakati akitoka mle chumbani







********





Ni watu wachache walioonekana kuwa macho pale msibani.Wengi tayari walikuwa wamekwisha lala.Wakati wengine wakiwa usingizini ndani ya chumba cha maongezi ya farahgha ndani ya jumba hili ,Dr Joshua na jaji Elibariki walikuwa na maongezi ya muhimu sana.

“ Mr Judge it’s me and you now.We have all the time in the world so tell me everything .”akasema Dr Joshua

“Mr president kwanza kabisa napenda nikushukuru tena kwa kunipa uhuru huu na nimeweza kuhudhuria msiba wa mke wangu kitu ambacho sikuwa natarajia ningekipata.Kama nilivyokueleza awali ni kwamba hii sintofahamu yote ilianza baada ya kesi ya Peniela.Kama utakumbuka mimi ndiye niliyeamua kesi ile na kumuachia huru.Kesi ile ilikuwa na sintofahamu nyingi na baada ya maamuzi yale niliyoyatoa ya kumuachia huru Peniela mambo mengi sana yali zungumzwa na zaidi sana nilipokea lawama nyingi na hata wewe mwenyewe ulinilaumu sana kwa kupuuza kile ulichokuwa umeniamuru kukifanya.Baadaya kesi ile nilijiuliza sana kwa nini nguvu kubwa ilitumika kutaka peniela akutwe na hatia na kufungwa? Nilikosa jibu na nikaamua kuutafuta ukweli ni nani aliyemuua Edson na kumtupia kesi Peniela?.Sikuwa na taaluma ya kufanya uchunguzi hivyo ikanilazimu kumtafuta mtu ambaye ana weza akafanya kazi hii na nikampata Mathew.Mathew aliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi na baadae aliamua kuiacha kazi hiyo baada ya familia yake yote kuteketezwa kwa moto.” Elibariki akanyamaza kidogo kisha akaendelea

“ wakati uchunguzi ukiendelea kuhusiana na nani alimuua Edson,kukatokea kifo cha Dr Flora.Flaviana akaomba nimsaidie kufanya uchunguzi wa kubaini sababu ya kifo chake.Kwa kumtumia Mathew tuliweza kufanikiwa kugundua nini kilimuua Dr Flora na taarifa ile tutakuletea na kwa bahati mbaya ukaikataa na badala yake ukaileta ripoti ile ambayo ulidai ilitoka kwa madaktari wa hospitali kuu ya taifa.Usiku wa siku ile Flaviana akanipigia simu na kuniomba tuonane na akaniomba tuachane na mambo yale ya ripoti zile za uchunguzi kwani hazitatusaidia chochote.Mimi kama jaji na ambaye siku zote ninaitaka haki sikukubaliana naye nikaondoka.Kabla sijaingia katika gari nikapigiwa simu na mwanamke mmoja ambaye simfahamu akaniomba nisiingie katika gari kwani kuna mpango w a kuniua.Nilimpuuza na nikaendelea na safari yangu.Garini nilikuwepo mimi na mwenzangu anaitwa Noah.Baade tulishambuliwa na Noah akapoteza maisha na mimi nikachukuliwa na Yule mwanamke nisiyemjua nikaenda kujificha kwa peniela.Baadae Mathew akaja kunichukua akaenda kunificha kwake” akanyamaza akameza mate na kuendelea

“ Kitendo kile cha mimi kunusurika kuuawa kiliongeza udadisi na kutufanya tutake kuchunguza zaidi na ndipo tukagundua mambo mengine yaliyojificha zaidi.Kwanza tuligundua uwepo wa kikundi kiitwacho Team Sc41.Kikun………….”

“ Wait !! Dr Joshua akamkatisha



“ Umesema Team Sc41? Ni kitu gani hicho? Akauliza

“ Hiki ni kikundi kidogo kinachofanya shughuli zake kwa siri kubwa hapa nchini lengo lao kuu likiwa ni kulinda maslahi ya Marekani hapa nchini.”



“ What ?!! Yaani hapa nchini kuna kitu kama hicho? Kwa nini mimi nisifahamu? Kimeanza lini hicho kikundi?

“ Si rahisi kufahamu kuhusu kikundi hiki kwani ni cha siri sana na kilianza wakati wa awamu ya Deus Mkozumi.Kikundi hiki ni cha watu wachache ambao hujishughulisha na kazi moja tu ya kuhakikisha kwamba maslahi ya Marekani yanalindwa kwa hiyo wamepenyeza mizizi yao katika serikali na wanaweza kupata habari za kila kinachoendelea na hivyo wanaweza kujua kama kuna hatari yoyote katika uwekezaji mkubwa wa Marekani hapa nchini” akasema Elibariki

“ Team Sc41 waliweza kufahamu kuhusiana na biashara uliyokuwa unataka kuifanya ya package yenye kirusi Aby na wana mikakati ya kuipata package hiyo”

“ Hebu subiri kidogo jaji,umesema Team SC41 waligundua kuhusiana na package,nataka kujua waligunduaje wakati suala hili lilikuwa ni siri kubwa na tuliokuwa tunalifahamu ni watu watatu tu,mimi Dr Kigomba na Captain Amos? Hao wenzako uliokuwa unashirikiana nao ,pia ni Team SC41? Akauliza Dr Joshua

“ Watu niliokuwa ninashirikiana nao si washirika wa Team Sc 41 .Kuhusu Team Sc 41 waligunduaje kuhusu mpango wa kuiuza package ile yenye kirusi Aby ni kwamba tayari walikuwa na watu wao waliokuwa wanawatumia kupata habari zote na kila kilichokuwa kinafanyika.”



“ Walikuwa na watu wao?? Akauliza Dr Joshua kwa mshangao



“ Ndiyo.Hukuwa unalifahanmu hili mr President lakini watu waliokuwa wanawatumia ni Captain Amos na Peniela”

“ Peniela !!! Dr Joshua akastuka na Ghafla akasimama akamshika Jaji Elibariki kwa nguvu na kumkaba shingoni







“ Sikiliza jaji,najua wewe na wenzako mmekwisha nichunguza sana na mmefahamu mambo mengi kuhusu mimi kwa hiyo nina hakika tayari umekwisha fahamu Peniela ni nani kwangu so be very carefull when you mention that name in front of me !! asema Dr Joshua halafu akamuachia jaji Elibariki aliyekuwa akikohoa kutokana na kukabwa shingoni .

“ I don’t want the name Peniela to appear in our conversations. Do you understand ? Dr Joshua akamuuliza jaji

“ Mr Preseident ulitaka nikueleze ukwelI na ndicho kitu ninachokifanya hapa.I’m telling you the truth. Ukweli ninaokueleza hapa utakuwa na msaada mkubwa kwako Mr President na ili mambo yako yafanikiwe unatakiwa utulie na unisikilize kila kile nitakachokuambia na ninaomba uniamini hata kama utaumia” akasema jaji Elibariki



“ Vyovyote vile itakavyokuwa lakini nimesema sitaki kusikia jina la Peniela likitajwa humu ndani !! akaendelea kusisitiza Dr Joshua kwa ukali

“ Dr Joshua nimewasaliti wenzangu waliojitolea maisha yao kwa ajiliyangu kwa hiyo sina haja ya kuficha tena jambo lolote lile.Niruhusu nikueleze ukweli wote bila kukuficha hata kitu kimoja” akasema jaji Elibariki.Dr Joshua hakujibu kitu akabaki kimya alionekana kuchanganywa sana na jaji Elibariki kumtaja Peniela



“ Dr Joshua ukimya huo ni ishara kwmba ninaruhusiwa kuendelea .” akasema jaji Elibariki halafu akaendelea.



“ Peniela ni mtu ambaye team Sc41 wanamtumia sana katika mipango yao mingi na walim..”

“ jaji Elibairki tafadhali naomba nisirudie tena kulisema hili,sitaki jina Peniela liingie katika maongezi yetu !! Kwa nini hutaki kunisikia?!! Peniela ni malaika wangu na hawezi katu kunifanyia hayo unayoyasema !! Akasema Dr Joshua kwa ukali

“ What do you want me to say Mr President? You don’t want to know the truth?!! Akauliza jaji Elibariki Dr Joshua hakujbu kitu

“ Kama hutaki kuusikia ukweli ninaokueleza basi hakuna haja ya kuendelea na maongezi haya.Watu ambao hutaki niwaseme ndio hao hao ambao wamekusaliti na kutoa habari zako.Peniela ambaye umekuwa ukimuona kama malika wako hakupendi hata chembe na ndiye anayeongoza mipango yote ya kukuangamiza.Anatumiwa na team SC41 ambao ndio waliompa mafunzo na wakamuunganisha kwako makusudi kabisa wakimtumia captain Amos .Walikuwa na lengo moja tu la kuipata package hiyo.Nakuhakikishia tena Mr President kwamba Peniela ni mwanamke hatari sana ambaye hana mapenzi yoyote kwako bali anayetumiwa ili kukumaliza.Na kama huniamini hili nikwambialo basi usichukue hatua zozopte na baada ya muda utaamini kile nikwambiacho.Peniela amekuwa akiutumia uzuri wake ili kupata taarifa mbali mbali toka kwa watu tofauti tofauti.Unafahamu kwamba mpaka sasa tayari Peniela na Dr Kigomba wana mahusiano ya kimapenzi?

” What ?!! Dr Joshua akastuka sana



“ Lazima ustuke kwa sababu ni kitu ambacho hujakitegemea kabisa lakini huo ndio ukweli.Dr Kigomba na Peniela ni wapenzi.”

“ No I cant believe this !!!..akasema Dr Joshua



“ Ulimpa Dr Kigomba jukumu la kumchunguza Peniela kamaana mahusiano yoyote na mimi si ndiyo?



“ Ndiyo nilimpa kazi hiyo baada ya kupata taarifa kwamba ulikuwa umejificha kwa Peniela “ akasema Dr Joshua



“Basi ulipompa jukumu hilo alijikuta akiingia katika mahusiano na peniela na akasahau hata jukumu ulilomkabidhi.Kukuhakikishia hilo kuna saa ambayo Peniela alimpatia Dr Kigomba ambayo akiivaa humuonyesha kila sehemu alipo kwa hiyo inakuwa rahisi kwao kumfuatilia.Wanamfuatilia Dr Kigomba kwa sababu wanafahamu ndiye unayemtumia sana katika mipango yako mingi na hasa huu wa package.kwa kumtumia Peniela waliweza kuiunganisha simu ya Dr Kigomba katika kompyuta yao kwa hiyo walikuwa na uwezo wa kusikia kila kile ambacho Dr Kigomba alikuwa anakiongea katika simu yake.Kila ambacho ulikuwa unaongea naye katika simu tulikuwa tunakisikia.Tayari wanafahamu kuhusu kila mpango mnaoupanga .Wanafahamu kuhusu ujio wa Hussein ambaye ndiye anayekuja kuichukua package hiyo ,kwa ujumla niseme wanafahamu siri zako nyingi sana na hii yote imewezekana kwa sababu ya Peniela.” akasema jaji Elibairki



“ Ouhmy God !! akasema Dr Joshua na kuinamahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Peniela ..Peniela …!! Akasema kwa uchungu na kusimama kisha kwa hasira akaibinua meza

“ Aaaaghhhh !!! akapiga ukelele mkubwa halafu akakaa chini na kuanza kudondosha machozi

“ Mr President tafadhali naomba unyamaze na tuendelee na maongezi yetu.Wewe ni mtu mkubwa ndiye kiongozi wa nchi hii kwa hiyo hutakiwi kudondosha chozi hata ukiumia vipi. Crying is the sign of defeat and you are the powerful man in this country so don’t let them defeat you.I can help you Mr President” akasema jaji Elibariki na kumshika mkono Dr Joshua akamketisha sofani.

“ Jaji nimeshindwa kuvumilia imenibidi nitoe machozi kutokana na namna nilivyoumizwa na taarifa hizi.Ninampenda Peniela kwa moyo wangu wote na kila ninachokifanya ninakifanya kwa ajili yake.Ouh jamani kwa nini Peniela anifanyie hivi? Nilimpenda Yule msichana na nilikuwa tayari kufanya kila nililoweza ili kumfurahisha lakin kumbe nilikuwa ninamfurahisha nyoka.Nimeumia sana .” akasema Dr Joshua

“ Pole sana dr Johsua .Hivyo ndivyo watu walivyo.Wale unaowapenda na kuwaamini ndio hao hao ambao kesho watakuangamiza.,Unatakiwa uwe makini sana kabla ya kuamini mtu yeyote Yule” akasema jaji Elibariki



“ Ahsante sana jaji kwa kunifumbua macho.Nilikuwa nimepofushwa na Peniela naniliamini yeye ni malaika kumbeni ibilisi aliyekuwa anaitafuta roho yangu.Umeniokoa sana jaji.Sikutegeema kama siku moja ungegeukana kuwa mkombozi wangu.Ninakuahidi nitasakaPeniela kokote aliko na nitampata tu.!!

“Dr Joshua kwanza kabisa kabla ya kuwatafuta Peniela na Mathew kuna mambo ambayo lazima tuyafanye.”



“ Hebu nishauri kijana wangu “ akasema Dr Joshua

“ Kwani peniela umekwisha wasiliana naye toka jana? Akauliza Elibariki.

“ Nilikuwa na miadi ya kuonana naye jana mchana lakini nilimpigia simu na haikuwa ikipatikana.”



“ Basi lengo la kutaka kuonana nawe lilikuwa ni uipata simu yako ili aweze kuzipata namba za simu za Hussein kwani badompaka sasa hawamfahamu na kupitia namba hizo za simu wangeweza kumfahamu kirahisi sana.Lakini endapo akikupigia simu na kutaka muonane usimweleze chochote kuhusu haya niliyokuambia na upange kukutana naye na hiiitakuwa ni njia rahisisana ya kuweza kumkamata kwani mpakassa bado hajafahamu kama niko nawe.Pili n kuhsu Dr Kigomba.Simu yake inatakiwa kuchukuliwa na kuzimwa kabisa na ile saa anayoivaa aliyopewa na peniela inatakiwa kuvuliwa kwani akina Mathew wanamfuatailia na kufahamu kila mahala alipo kwa kutumia vitu hivi viwili. Wanatumia teknolojia ya haliya juu sana na haya yote yanafanyw ana Anitha ambaye ni mshirika wa Mathew.Huyu mwanadada ana utaalamu wa hali ya juu sana wa mamboya elekroniki na ndiye anayebuni programu hizi zote.Kwasasa Anitha anashikiliwa nyumbani kwa Rose na ninakushauri umwambie Rose amchunge sana na asije akamuachia mwanadada huyu kwani ndiye roho ya Mathew.Huyu ndiye anayemuwezesha Mathew kufanya kazi zake kirahisi.Tukimshikilia huyu Mathew atapata wakati mgumu sana wa kutekeleza mipango yake “ akasema Elibariki



“Huyu Mathew anaishi wapi?

“ kwa sasa hana makazi kwa sababu nyumba aliyokuwa anaishi Rosemary aliiteketeza kwa moto na kila kilichokuwamo ndani yake kiliteketea .Kwa hivi sasa sifahamu ni wapi alipo Mathew lakini kwa kumtumia Anitha tunaweza kufahamu yuko wapi.”



“ Elibariki nakushukuru sana kwa kunitoa usingizini.Sikujua kama nina maadui wakubwa namna hii tena walio karibu kabisa na mimi na ambao wangeweza hata kunimaliza sekund e yoyote .Kuanzia sasa wewe ndiye utakayekuwa mshirika wangu mkuu.I’ll give back to you all that I took from you.Nisaidie tuimalize biashara hii na ninakuahidi kwamba uakuwa ni mtu mkubwa sana. kuna jambo ambalo sikuwa nimelifikiria lakini kwa sasa limekuja akilini.I’ll make you the next president of Tanzania”

Jaji Elibariki alibaki mdomo wazi akimkodolea macho Dr Joshua asiamini kile alichoambiwa.



“ Umesema nini mzee? akauliza



“ kwa mambo uliyonifanyia jaji umenifanya nikuthamini ghafla kuliko watu wote kwani bila wewe ningeendelea na mipango yangu yote bila kufahamau chochote na mwisho wangu ungekuwa ni wa aibu kubwa.Ni wewe ambaye nilikuwa nimekuweka katika kundi la adui zangu wakubwa lakini ndiye umekuja na kunifumbua macho.kwa hili ulilolifanya nimesema kwamba nitakufanyia kitu ambacho sikuwa nimekusudia kukifanya.Nitakufanya uwe rais wa jamhuri ya muunganowa Tanzania.” Akasema Dr Joshua.jaji Elibarki machozi ya furaha yakamdondoka.

“ is this true Dr Joshua?

“ Ndiyo Elibarik.Uwezo huo ninao na nitafanya hivyo na hakuna anayeweza kunizuia kufanya hivyo.I’ll make you a very powerfull man in this country na nina hakikani wewe ambaye utaweza kuendelea kuyalinda maslahi yangu.Nilikuwa nafikiria sana ni nani ambaye ninaweza nikampa nchi na akaendelea kuyalinda maslahi yangu lakini nashukuru nimekupata wewe.Nina hakika wewe ni mtu sahihi kabisa na unafaa.”Akasema Dr Joshua.Jaji Elibariki akainuka na kwenda kumpa mkono akamshukuru

“ Dr Joshua sikuwahi kufikiri kuhusu jambo kama hili ! akasema kwa furaha jaji Elbariki

“kwa hiyo kama halikuwa katika ndoto zako anza sasa kuota kwamba umekuwa rais wa Tanzania kwani jambo hili linakwenda kutimia.Nitakuelekeza nini cha kufanya muda utakapofika lakini lazima ukae ukijua kwamba wewe ndiye utakayekuwa rais wa Tanzania baada ya mimi kuondoka madarakani.Lakini pamoja na hayo kuna jambo nataka nikuombe”

“Jambo gani Dr Joshua?

“ Samahani lakini kwa kulisemahilikabla hata hatujamzika Flaviana mkeo lakini ni ukweli ulio wazi kwamba Kwa sasa baada ya Falivana kututoka utabaki mwenyewe na kwa kuwa bado kijana lazima utaoa tena lakini mimi lengo langu kubwa ni kutaka familia yangu iendelee kukaa katika neema ya uongozi kwahiyo basi ninakutaka ujenge mazoea ya karibu na Anna mbaye naye kwa sasa yuko mwenyewe baada ya mpenziwake kufariki.Ninajua umenielewa ninaposema hivyo kwani ninataka utakapokuwa rais yeye awe ni mke wa rais na familia yetu iendelee kutawala.Unalionaje wazo hili? Akauliza Dr Joshua

“ Hilo ni wazo zuri Dr Joshua lakini naomba uniachie kwanza jambo hilo nilitafakari na kulifanyia kazi na nitakupa majibu”akasema Elibarik,.Dr Joshua akafungua mlango na kumuita msaidizi wake akamuomba amuite Dr Kigomba ambaye alifika mara moja .Dr Joshaua akamuangalia kwa macho makali kwa sekunde kadhaa kisha akasema

‘ Kigomba give me your phone” .Huku akishangaa Dr Kigomba akachukua simu yake na kumpatia Dr Joshua.



” Kuanzia sasa hautaitumia simu hii utatafuta simu nyingine.Vua na hiyo saa mkononi”akaamuru Dr Joshua

“ Dr Joshua whats going on? Akauliza Dr Kigomba kwa wasiwasi.

“ Kigomba nadhani umekwisha fahamu nini kinaendelea.Nilikupa kazi ya kumchunguza peniela na badala yake ukaanzisha mahusiano naye.Ulifanya kosa kubwa sana Kigomba”

“ Nani kakueleza habarihizo dr Joshua?

“ Kigomba tayari ninafahamu kila kitu kwa hiyo hakuna haja ya mabishano. Siku zote nimekuwa nkikuonya kuhusiana na udhaifu wako kwa wanawake lakini hukutaka kunisikia.”

“ Dr Joshua sikuelewi una maanisha nini” akasema Dr Kigomba.Dr Joshua akamtazama kwa macho makali na kusema



“ Kigomba unafahamu Peniela ni nani? Unafahamu ni kitu gani alichotufanyia kupitia kwako?

“ hapana Mr President.”akajibu Dr Kigomba



“ Peniela ni nyoka mkubwa na tayari ameunganisha simu yako katika program yao na wanasikia kila kitu unachokiongea kupitia simu yako.Kama hiyo haitoshi alikupa saa hii kama zawadi uivae lakini kwa taarifa yako saa hii imefungwa kifaa maalum ambacho kina uwezo wa kuwaonyesha kila mahala ulipo.Tumshukuru sana Elibariki ambaye ametufumbua macho na kama si yeye tusingeweza kujua chochote kinachoendelea” akasema Dr Joshua.Kigomba alibaki kimya akiwatazama.



“ I’m sorry Mr President,sikuwa ninafahamu lolote kuhusiana na alichokifanya Peniela.” Akasema Dr Kigomba



“ Kigomba mimi na wewe tutakuwa na maongezi yetu baadae lakini kwa sasa naomba nikufahamishe kwamba mipango yetu yote imekwisha gundulika na kama tusipochukua hatua za tahadhari angali bado mapema basi hatutaweza kufanikiwa.Cha kwanza tunachotakiw a kukifanya ni kumuhamisha kwa siri Hussein na ujumbe wake mapema kesho asubuhi na kesho hiyo hiyo jioni kila kitu kikamilike na Hussein aondoke nchini haraka na baada ya hapo tutaendelea na zoezi la kumsaka mtu aitwaye Mathew ambaye huyu ndiye adui yetu mkubwa sana kwa sasa.”akasema Dr Joshua

“Mr President ninaomba niuliz……………”Dr Kigomba akataka kuuliza swali lakini Dr Joshua akamzuia

“ Kigomba hakuna muda wa maswali sasa hivi.Anza sasa hivi kushughulikia hoteli ya kuwahamisha Hussein na ujumbe wake.Tutaongea baada ya mambo yote kukamilika” Akasema Dr Joshua na Dr Kigomba akatoka mle chumbani

Jaji Elibarikina Dr Joshua waliendelea na maongezi na ilipotimu saa tisa za usiku wakaagana.



“ Nenda kalale jaji kesho tuna siku ndefu sana.Kesho tutamzika Flaviana na kisha tutaendelea na mchakato mwingine.Tutaongea zaidi kesho lakini nakushukuru sana jaji.” Akasema Dr Joshua na kumuongoza jaji Elibariki kuelekea katika chumba maalum cha wageni





.MWISHO WA SEASON 3



MATHEW NA PENIELA WAKO WAPI NA WANAFANYA NINI? DR JOSHUA ATAFANIKIWA KATIKA MIPANGO YAKE YA KUKIUZA KIRUSI ABY? MWISHO WA PENIELA SEASON 3 .USIKOSE KUISOMA PENIEAL SEASON 4 HIVI KARIBUNI……….




MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog