Search This Blog

Wednesday, 22 March 2023

JINO KWA JINO (2) - 2

   

Simulizi : Jino Kwa Jino (2)

Sehemu Ya : Pili (2)


   “Sisi sote tuko vizuri kiongozi… Tunamshukuru Mungu kwa kweli” Austin akajibu kwa niaba ya mwenzake vijana hawa walio kama ndugu wanaofanya kazi kwa mazoea kwa ukaribu sana.

   “Vizuri na karibu sana msisite kuongea chochote kama mnaona si sawa au kinawakwamisha katika lolote lile sisi sote hapa ni ndugu moja tunaofanya kazi kwa ushirikiano tusiokubali kuona mwenzetu hata mmoja anapatwa na tatizo lolote lile… Na nyie warembo wetu jamani mmeamkaje?” Aliongea tena Kai na kumalizi kwa swali lililoenda kwa madada waliopo hapa ambao muda si mrefu wote walikuwa jikoni kuandaa hii ‘breakfast’ na sasa wote wako hapa sebuleni.

   “Mimi leo niko sawa sana na nina amani sana” Akajibu Angelica Linares mwanadada  mwenye tunu ya urembo akiwa nimrembo haswa kwa kweli yaani sifa zake nashindwa zielezea kwa urahisi ila msomaji juwa tu mwanadada huyu wa kilatini anastahili tuzo ya urembo.

   “Najua kwanini una amani hivyo… Nitakwambia tukiwa wawili tu” Akaongea na kuunganisha cheko dogo Agent Kai, wengine nao wakamjibu juu ya wajionavyo kuanzia Special Agent Rebecca hadi mwanadada aliyebanjuka amri ya sita na Miller nesi Avon ambaye naye kiukweli si haba naye alibeba nini maana ya warembo wa kilatini ingawa si kwa kiwango cha Ange.

Stori hapa zilipigwa vya kutosha kisha Agent Kai ‘TSC’ aliwaomba udhuru wa kazi wakamuacha Miller na wanawake wawili ambao ni Avon na Ange wakiendela na soga jumlisha matani mbalimbali na wanawake hawa wacheshi sana, ucheshi uliotokana na kuzoea kwao uwepo wao hapa.

Chumba cha mahojiano chenye meza moja kubwa iliyotengenezwa kwa bati juu na miguu ya nondo waliletwa wakiwa wamefungwa vitambaa usoni Mwanamke ambaye ndiye haswa anayetafutwa na ‘The Sole Cat’ ila hamjui kwa sura pia aliletwa mmoja watu muhimu sana katika usalama wa taifa la Guatemala katika mambo ya ujasusi akiwa muajiriwa wa ‘Guatemala Intelligence And Security’ bwana huyu anaitwa Mr. Eddie Mauro miongoni mwa watu walionusurika kwa mabomu ya kudondoshwa na wanajeshi wa jeshi la Marekani wakiwa katika operesheni ndogo ya kuwaokoa raia wenzao wa Marekani na wanausalama wenzao.

Watu hawa mwanamke na mwanaume walikalishwa kwenye viti vya chuma mikono yao iliyo na pingu ikafungwa katika moja ya nondo za juu ya meza ambazo ni maalumu kufunga watu hivyo.

  “Watoe vitambaa usoni tuoanane vizuri..!” Akaongea Kai kumwambia Austin aliye karibu na watu hawa naye bila kusita akatekeleza kwa kuwavuta kwa juu vitambaa vyeusi kila mmoja ikiwa toka wanaletwa ndani ya nyumba hii wakiwa hata njiani vitambaa hivi havikutoka usoni mwao wakiwa walifungwa punde tu gari ilipoondoshwa eneo walilotekewa huko ‘Las Anonas’.

Mwanga mkali wa taa ulikuwa ukiwamulika na kuwafanya wafinye macho yao kwa nguvu kisha wakawa wanafungua kidogo kidogo hili wazoee mwanga waliokuwa wameukosa kwa masaa mengi.

   “Karibuni waungwana katika jengo la burudani itakayoendeshwa na ma mc pamoja na ma dj sisi… Kwa majina mimi naitwa Agent Kai Hamis ni mwanajeshi niliyebadilishwa kazi na kupelekwa shirika la kijasusi la Marekani CIA kitengo maalumu cha Special Activities Division, niliacha jeshi nikiwa na cheo cha Sajenti miaka nane iliyopita hivyo msihofu sana mko mikono salama kabisa sisi si majambazi ni wanausalama tu… Mwenzangu aliye kulia kwangu anaitwa Special Agent Fransis Simone Silla huyu ni mwanausalama toka Drug Enforcement Administration, kushoto kwangu ni Special Agent Miss Rebecca Smith na hao walio pembeni zenu wa  kushoto ni Austin Contreras na wa kulia ni Jairo Jimenez Lezcano, sote tupo hapa kwa ajili ya kusikia tunayotaka kusikia toka kwenu… Hapa pana masharti yaliyo salama kama mtataka kuwa salama na yaliyo na shari kutegemea na uhitaji wenu wa shari hiyo.. Kwa kuanzia mimi nimejitambulisha kwa majina na pia kuwatambulisha wenzangu kwa majina pia, ningependa kujua majina yenu tafadhali?” Aliongea kwa kirefu Agent Kai huku simu yake ikifanya kazi ya kuwapiga picha si kwa kuficha alikuwa akiwapiga tu kila anapohitaji kufanya hivyo.

Watu hawa waliangaliana kisha walirudisha vichwa vyao wakiwa wamenyamaza kana kwamba wao ni viziwi hakuna walichosikia au ni mabubu hawawezi jibu lolote.

   “Dada unaitwa nani?” Akauliza Agent Kai tena akimuuliza mwanadada Mariana wakiwa wanaangaliana, hakuinua mdomo kujibu swali alimtizama Agent Kai kwa jicho la ukali na hasira kisha akaama akiwaangalia mmoja mmoja watu waliosimama mbele yake upande wa pili wa meza inayowatenganisha.

   “Austin! Lete ndoo ya maji kisha fungua kwenye bomba ijaze maji nafikiri njaa zinawauma wanataka tuongee huku wanakunywa chai..!” Akaelekeza ‘TSC’.

Austin alifanya alivyoelekezwa ndani ya chumba hiki hiki kuna mabomba ya maji mawili, maji yanayotoka yakiwa ya moto na bomba lingine linatoa maji ya baridi kama barafu ambayo yanatengenezwa kwenye kimtambo maalumu kilichofungwa upande wa pili wa chumba, ndoo ya maji ya baridi ilisogezwa karibu na walipo ‘mabubu wa bandia’.

   “Nauliza mara ya mwisho waungwana.. Nachukia sana kumtesa mtu sababu mimi mwenyewe ninapotekwa na adui zangu uwa mwepesi kuongea hili nisiteswe sababu naupenda mwili wangu sipendi mateso anikute bila msingi wowote… Dada tunaomba kufahamu majina yako kamili unayotumia” ‘TSC’ Kazini uso taratibu ulianza kujenga matuta ikimaanisha maamuzi yanaweza kushika hatamu yake.

Kama kawaida mateka walinyamaza, Rebecca alizunguka kusogea upande ule walipo kisha akamsogelea mwanadada akimtizama kwa hasira.

   “Kwanini unataka kutuchelewesha mwanamke mwenzangu… Hauna jina? Wewe ni bubu?” Aliongea Rebecca akiwa kakikamata na kukibetua kidevu kwa nguvu cha Mariana ambaye ni mwanamke wa shoka kweli kweli mwenye mafunzo ya kijeshi tena asiyependa kushikwa kwa nguvu mwili hivyo alivyoshikwa ilimfanya aheme kwa nguvu kwa hasira akitamani ainue kichwa chake kwa nguvu ampige kichwa Rebecca.

   “Usinishike hivyoo..!” Kwa mara ya kwanza alijikuta akipayuka kwa nguvu bila kupenda hasira tu ndizo zilimfanya akiuke alichokiahidi wakati akiletwa kwenye chumba hiki.

   “Unataka ushikwe vipi?” Rebecca naye jeuri sana alizidisha kumkandamiza akimvuta juu kisha anamrudisha nyuma kwa nguvu akamsukuma kwa kumpigiza kwenye kingo ya kiti kisha akamuachia akachota maji kwa jagi toka kwenye ndoo akammwagia kichwani mwanadada huyu aliyehisi kama kachomwa msumari utosini sababu hakujua kama maji haya baridi hivi, moyo wake ulianza kwenda mbio.

Rebecca akapiga hatua kama anaelekea upande wa pili akimuacha kwenye dimbwi zito la hasira mwanamke mwenzie tena akiwa kazidiwa miaka mingi na mwanamama huyu lakini hatua zile hazikwenda sana aligeuka kwa kasi ya umeme akafyatua kibao kikali na kizito kikitua kwenye shavu la bibie Mariana ambae kilimfanya atake dondoka kitini alijikuta akichia yowe dogo ununda mbele ya kibao kilichostukizwa haukuwepo.

   “Nitakuongeza kibao kingine kama utaendelea kuwa kiburi..!” Akamuonya akimnyoshea kidole cha shahada, sura ya Mariana upande wa shavu la kushoto uliwiva kwa wekundu wa kizungu kwa mlatini huyu.

   “Chai umeonja kidogo.. Tayari Lizy amenitumia meseji anaitwa nani huyu mwanamke..” Aliongea Agent Kai kwa ujumbe ulioenda kwa Mariana na mwingine ulioenda kwa washirika wenzake walio timu moja kikazi na macho yake yakiendelea kusoma meseji zinazoingia kwenye whatssap yake zikitoka kwa Liz Rob.

   “Unaitwa Mariana Caro Funtes uliyeacha kazi katika jeshi la wananchi la Mexico baada ya kufanya hujuma za kughushi nyaraka za kuonyesha watu fulani waliofungwa kwa kosa la kukutwa na hatia ya kujihusisha kwao na uuzwaji wa madawa ya kulevya ndani ya kambi za jeshi, ulighushi sahihi na kuiba muhuri  wa kiongozi wa nidhamu jeshi uliogongwa kwenye haraka za kuwaamisha toka magereza ya wafungwa wote ukisema wafungwa wanaenda kufungwa magereza ya kijeshi baada ya kughushi kwako kufanikiwa ghiriba watu wale walikutwa wamekufa kwa kukatwa katwa kikatili kama wanyama katika sehemu inayoitwa kona ya Jalisco huko Mexico.. Uchunguzi ulipoanza ndipo wewe ulipotoweka ikisemekana umejiunga na moja ya magenge ya wauzaji wa madawa ya kulevya.. Namba yako ya simu imesajiliwa kwa jina la Valentina Aurelio Moschi hili ni jina lako la bandia unalolitumia katika passport yako unayosafiria sehemu mbalimbali kuficha jina lako la ukweli kwa serikali ya Mexico inayokusaka.. Una lipi la kuongea mwanamke?” Aliongea kirefu akimalizia kwa kumbandika swali Mariana ikiwa hajshangazwa sana kwa anachokisikia toka kwa Agent Kai sababu kupigwa picha tu alikuwa anajua kitakachofuata ni nini?.

Mwisho wa sehemu ya themanini na mbili (82)

Mariana ndani ya chumba cha maswali na majibu, chumba ambacho popote pale kinapokuwepo kisha anakuwa yumo Rebecca Smith basi chumba icho uwa ni hatari.

Sina mengi ya kufafanua, twen’zetu epsd inayofuata!





Rebecca akapiga hatua kama anaelekea upande wa pili akimuacha kwenye dimbwi zito la hasira mwanamke mwenzie tena akiwa kazidiwa miaka mingi na mwanamama huyu lakini hatua zile hazikwenda sana aligeuka kwa kasi ya umeme akafyatua kibao kikali na kizito kikitua kwenye shavu la bibie Mariana ambae kilimfanya atake dondoka kitini alijikuta akichia yowe dogo ununda mbele ya kibao kilichostukizwa haukuwepo.

   “Nitakuongeza kibao kingine kama utaendelea kuwa kiburi..!” Akamuonya akimnyoshea kidole cha shahada, sura ya Mariana upande wa shavu la kushoto uliwiva kwa wekundu wa kizungu kwa mlatini huyu.

   “Chai umeonja kidogo.. Tayari Lizy amenitumia meseji anaitwa nani huyu mwanamke..” Aliongea Agent Kai kwa ujumbe ulioenda kwa Mariana na mwingine ulioenda kwa washirika wenzake walio timu moja kikazi na macho yake yakiendelea kusoma meseji zinazoingia kwenye whatssap yake zikitoka kwa Liz Rob.

   “Unaitwa Mariana Caro Funtes uliyeacha kazi katika jeshi la wananchi la Mexico baada ya kufanya hujuma za kughushi nyaraka za kuonyesha watu fulani waliofungwa kwa kosa la kukutwa na hatia ya kujihusisha kwao na uuzwaji wa madawa ya kulevya ndani ya kambi za jeshi, ulighushi sahihi na kuiba muhuri  wa kiongozi wa nidhamu jeshi uliogongwa kwenye haraka za kuwaamisha toka magereza ya wafungwa wote ukisema wafungwa wanaenda kufungwa magereza ya kijeshi baada ya kughushi kwako kufanikiwa ghiriba watu wale walikutwa wamekufa kwa kukatwa katwa kikatili kama wanyama katika sehemu inayoitwa kona ya Jalisco huko Mexico.. Uchunguzi ulipoanza ndipo wewe ulipotoweka ikisemekana umejiunga na moja ya magenge ya wauzaji wa madawa ya kulevya.. Namba yako ya simu imesajiliwa kwa jina la Valentina Aurelio Moschi hili ni jina lako la bandia unalolitumia katika passport yako unayosafiria sehemu mbalimbali kuficha jina lako la ukweli kwa serikali ya Mexico inayokusaka.. Una lipi la kuongea mwanamke?” Aliongea kirefu akimalizia kwa kumbandika swali Mariana ikiwa hajshangazwa sana kwa anachokisikia toka kwa Agent Kai sababu kupigwa picha tu alikuwa anajua kitakachofuata ni nini?.

ENDELEA NA NONDO..!!

PANDE MBILI ZA SHILINGI IV

CHIMALTENANGO, GUATEMALA CITY-GUATEMALA

Mariana alimuangalia ‘TSC’ kana kwamba anamfanyia usahili ampitishe kwenye uhusiano wa kimapenzi baada ya kulishwa swaga (kutongozwa) za maana.

   “Kunyamaza kwako Madam uliyesajili laini yako ya simu kupitia mamlaka ya simu ya Guatemala mtandao wa T-mobile kwa jina la uongo la Valentina Aurelio Moschi, hivyo unaponyamaza unanifanya nijijibu mwenyewe kila kitu kiko kama ninavyokudonyolea moja moja juu yako Koplo Mariana Caro Funtes” Agent Kai akaongea tena mikono na mwili wake kwa ujumla ukifuata kiishara mbalimbali wakati anaongea.

   “Pengine boss tunaongea kwa lugha ambazo hawa watu hawazielewi” S.S Rebecca Smith akaongea kisha akafungua mkoba wa ngozi ulio juu ya meza alipomaliza kuufungua akamwaga vitu vilivyomo juu ya meza, kiukweli Mariana na Eddie Mauro walikuwa wanakera kwa jinsi walivyokuwa wanasikiliza tu lakini hakuna anayeinua papi (lips) za mdomo wake kuongea chochote ni macho yao tu ndiyo yalikuwa yakitizama huku na huko kana kwamba hawahusiki na yanayozungumzwa au ni mabubu.

   “Pengine.. Endeleeni na kazi ya kupanua midomo yao mi acha niwe shahidi tu kwa sasa.. Msiowaonee huruma sababu wasifu wa mwanamke huyu nilivyousoma ni kweli anastahili kuwa mbishi.. Hivyo ubishi una dawa moja tu ambayo ni ubishi pia” Akaongea ‘TSC’ kisha akasogea pembeni kuliko na kiti akavuta na kukaa simu yake ikiamia mkononi kutoka mfukoni.

   “Madam kama tulivyokusikia unaitwa mara kadhaa katika mawasiliano yako ya simu tuliyokuwa tunayadukua na kukusikiliza ukipanga mipango kadhaa wa kadha kuhujumu usalama kwa kulinda maslahi ya genge lako la ‘THE RED JAGUAR’, leo hii kiukweli mi  nimefurahi sana kuona mtu aliyetutoa Marekani kuja hapa Guatemala tumekutana naye na ni mwanajeshi hivyo ana ujasisri wa kijeshi akiwa na jina la bandia ambalo ni jina la kwanza sisi kulijua kwakuwa ulisajilia laini yako ya simu jina la Valentina lakini kwa mujibu wa boss wangu hapa wewe jina lako kamili ni Koplo Mariana umeacha jeshi ukiwa na cheo kikubwa tu hongera na pongezi nyingi kwako mwanamke mwenzangu” S.S Rebecca akaongea huku anaandaa bomba la sindano ya kudungia wanyama kama ng’ombe nakadhalika kama hao, alipomaliza alivaa gloves kama wanazovaa madaktari na manesi mahospitalini wanapokuwa wanatoa huduma zao kwa wagonjwa.

   “Austin.. Naomba mkamate kichwa mwanaume mwenzao nianze na yeye kuwajulisha kuwa hapa sisi hatuko kutangaza injili ya bwana Yesu Kristo..!” Aliongea kisha akasogea alipo Eddie Mauro ambaye tayai uoga fulani ulianza kupanda moyoni mwake na ule ujasiri wa bandia uliotokana na jeuri kuwa hapa hakuna kuongea kitu ilianza kuyeyuka kama kipande cha mfupa kilichotupwa kwenye pipa la asidi.

Rebecca uwa hanaga huruma awapo mahala kama hapa alisogea na bomba la sindano kubwa ya kudungia wanyama akalenga jicho la kushoto la Eddie ambaye akawa analazimisha kuusogeza uso wake pembeni kwa nguvu asichomwe na sindano lile lakini mikono yote miwili ya Austin ilikamata kichwa kwa nguvu na ncha ya sindano iliposogea ‘zero distance’akashindwa vumilia Eddie akafumba macho sindano ikaanza kuzamishwa kwenye ngozi ya kopi ya jicho.

   “Khaaaaah!....Usinitoboeeee… Mimi sijui loloteeee! Mnanionea bure…!” Yowe kubwa lililoambatana na kuomba asitobolewe lilitoka kwa Eddie lakini tayari kope ya jicho ilikuwa inavuja damu maana Rebecrca aliingiza ncha mpaka ilipo mboni ya jicho akasimama hapo kwa kelele zile akaitoa sindano.

   “Unaonewa bure… Hujui kitu? Unaitwa nani?” Maswali ya kuongozana yalitoka mdomoni mwa mwanadada mwenye sura na shepu ya kuvutia (English figure) Special Agent Rebecca Smith akitumia kilatini lugha mwenyeji kwa mateka wao.

Baada ya kujibu maswali na kwakuwa aliyemkamata kichwa chake alikuwa amemuachia aligeuka kumuangalia Madam Mariana kama anavyomjua yeye kwa majina yake wakaangaliana yeye akiwa na sura iliyotepeta na kujaa ishara kuwa tisho alilopewa linamfanya sekunde ama dakika zijazo mdomo wake unafunguka kusema lakini sura ya Mariana ilikuwa sura chachu iliyokunjwa na kuupoteza ukike wake ikawa sura kopi ya baba yake mpaka ikamfanya kwa haraka mwanaume waliyetizamana kuhofu akaurudisha uso wake kawaida kisha akainua macho kumtizama Rebecca aliye hatua moja tu mbele yake akihitaji jibu kama si majibu ya yale aliyouliza.

   “Umelisahau jina lako?” Aliuliza tena Rebecca kisha akakita kwa sindano juu ya jicho akiigonga kingo ya fuvu inayoshika jicho, damu ziliruka jamaa naye alirudisha kichwa chake kwa nguvu nyuma mpaka akajigonga kwenye mgongo wa kiti alichofungwa akifuatiwa na yowe dogo la mshtuko.

   “Naitwa Joao… Joao Gonclales..!” Akajibu jina la uongo ambalo ni zoeleka kwake pale anapokuwa matatani au anapohitajika kusema jina la uongo popote pale alipo jina hili uja haraka kwenye mdomo wake na kujitambulisha hivi.

   “Austin.. Unamjua huyu mtu?” Agent Kai akaingilia kwa kuuliza swali lililoenda moja kwa moja kwa Austin mesenja wa Kamanda Muniain huku yeye akiwa pale pale alipokaa anachati na kuperuzi mitandaoni.

   “Ndio nishawai onana naye mara mbili mara tatu sehemu mbalimbali bila yeye kujua na wala kufahamu kama nami nimo katika masuala ya usalama wa taifa wa nchi ..!” Akajibu Austin na kufanya bwana mkubwa Eddie Mauro kugeuza shingo amuone vizuri Austin wakatizamana vizuri kwakuwa wote walipigana macho hili waonane vizuri, kengele ya mlipuko wa moyo kuruhusu damu ipite kwa pupa kwenye mishipa inayoshiriki na nyama kuunda moyo maana Eddie alikumbuka kitu kichwani mwake kuwa aliwai muona mtu huyu maeneo ya ikulu ya Rais.

   “Bwana mkubwa nafikiri tushaonana kama sikosei ilikuwia ugumu kujua kama nami nimo kwenye mfumo wa kiintelejensia kwakuwa sisi ni miongoni wa watu wachache wa siri kubwa tunaofahamika kwa siri na watu wachache walio kwenye mfumo… Naitwa Austin Manuel Contreras kama mkuu pale alivyonitambulisha na wewe kama sikosei ni Eddie Mauro ni assistant plan wa GIS makao makuu.. Hukupaswa kuwa muongo kwa kufuata jeuri ya mwanamke huyu hii itakugharimu sababu inaweza kukufanya upoteze maisha na si kama ambavyo hata nasi tunajua kuwa uhai wako ungeachwa tu tena bila hata kuumizwa ukikabidhiwa kwa watu wa mamlaka ya juu..!” Aliongea kirefu kidogo na kwa mbwembwe Austin wakiwa wanaangaliana na mtu aliyeonyesha sasa amechoka na kukata tamaa huku akijutia mengi katika yaliyopita.

Kunyamaza kwa Austin na aibu iliyotamaladi usoni mwa Eddie ilifuatiwa na kitu kama mzuka au tuseme stukizo jicho la Eddie la kulia ambalo alikuwa limejeruhiwa mwanzo wakati S.S Rebecca anagonga kingo ya fuvu inayozunguka jicho la kushoto la Eddie na kufanya damu kuwa inatoka kama mpira bomba uliotoboka na kuleta mvujo wa maji basi hili jicho lililkuwa likivuja lakini hili sasa alikuguswa lilikuwa la upande wa kulia sasa tena katikati ya mboni ya jicho sindano la kudunga wanyama tena si wanyama hawa wafugwao ni wanyama wa porini, ilikita na kuzama mpaka mwisho wa jicho kwa ndani na kulifanya lipoteze uhai wake giza likatanda upande mmoja.

   “Haaaayaaaah! Umeuaaa jich…ooo laanguuu!” Hii ilikuwa kelele iliyopazwa yaani kama laiti kungekuwa na dirisha kubwa katika chumba hiki kelele zingeenda mbali lakini kulikuwa na kadirisha kadogo sana kakiwa juu kabisa kakuleta hewa walau kidogo ya oxygen.

   “Mshenzi weeeh… Si nilishaonya kuwa hapa hakuna muinjilisti wala mhadhiri wa mihadhara ya kiislamu pokea adhabu ya kwanza ya upofu wa jicho moja kama mshahara wa kujibu uongo.. Nikiuliza tena ukajibu upumbavu uutakao naondoa lililobaki usione milele kisha nitawaomba wenzangu uachwe uende mtaani ukiwa ulivyo ukikumbuka huna macho utakuwa unajutia usaliti wako kwa wananchi na wakuu waliokuamini na kukupa wadhifa muhimu..!” Aliongea kwa ukali Rebecca kifua kikipandisha na kushuka kwa jazba aliyonayo.

   “Mr. Eddie una mke na watoto?” Akauliza swali lililowashangaza hata wasikilizaji wengine wakiongozwa na Agent Kai maana waliona kama halihusiani kwa hapa, wote wakamtizama Rebecca baada ya kumtizama muulizwa maswali.

   “Ndi.. Ndi..yo-oo..! naombeni .. naombeni..msaada kunifunga.. majeraha nitasema ukweli wa niyajuayo msiendelee kunipa adhabu jamani..!” Akajibu na papo hapo Rebecca alichukua kichupa chenye dawa ya maji ya kuzuia damu isitoke sehemu mtu anapokuwa amepatwa majeraha, alifungua akaweka kwenye pamba akambandika jicho la kushoto kwa juu ambako alikuwa kamshambulia mwanzo kisha jicho lililopasuka alichukua pamba akafuta maji ya jicho yaliyojichanganya na damu nzito inayomtoka akaitupa pamba kisha akakata pamba ingine kubwa zaidi akaziba pale na kugandamizia na plasta Mr. Eddie akabadilika sasa akawa Mr. Kijicho malipo ya ukaidi na kujifanya bingwa.

   “Wee mwanamke mwenzangu nitarudi kwako muda si mrefu hili nikujuze kama wewe unajifanya chizi mpya mimi chizi wa zamani nishapinda kitambo ila ukiniona smart kwakuwa najielewa kwa mbali.. Kulinga kutakuisha maana ulipo hakuna wa kukuokoa zaidi yako… Kwako Mr. Eddie! Anaitwa nani huyu mwanamke jeuri?” Chumba hiki cha mahojiano na mateso alikuwa akitamba mwanadada Rebecca mwenye sifa zake upande wa kuhoji hana masikhara.

  “Jina lake si alishalitaja boss pale..!” Akajibu kwa sauti ya ‘tafadhali nionee huruma’.

   “Ukiacha mheshimiwa Ceni ni nani kiongozi wa serikali unayemjua yumo katika mtandao wake?” Akauliza muuliza maswali Rebecca.

  “Katika safu ya mawaziri au viongozi wapi uliomaanisha?

  “Safu ya mawaziri, wabunge na hata maafisa wakubwa wanaoshika nyadhifa muhimu serikalini tunahitaji kuwajua hili tujue operesheni ya wanausalama wema kwa nchi hii wanaelekea wapi kuondoa virusi vyote vilivyowekwa na genge la TRJ hapa GTL.. Eleza!”

   “Mimi nawaju wachache hasa wale niliokuwa nawaongoza mimi nitaomba peni niwape orodha na kuhusu TRJ kwa upande wangu nilikuwa sihusiki nao sana zaidi ya kukutana nao katika operesheni za kimsaada tu ambao wao wanatutumia sisi zaidi kwa faida ya boss wetu mheshimiwa Ceni… Hivyo nashauri mpate majibu mazuri toka kwa muhusika hapa” Aliongea hivi Eddie kisha akaelekeza kwa kuyumbisha uso wake kidogo upande alipo Mariana.

  “..Rebecca subiri!... Mfungue vifungo vya shati vya kifuani huyo mwanamke… Liz amenitumia habari hapa kuhusu THE RED JAGUAR maana aliwasiliana na maafisa wa Drug Trafficking Organization kupata maelezo juu yao na majibu ameniandikia kwa kirefu..!” Agent Kai aliomba asiendelee kuhoji afanye hivi kwanza.

Rebecca alimtizama kidogo boss wake kama anavyomuita kisha akapiga hatua mbili alipo Mariana na Jairo aliye nyuma ya madam Mariana alisogea kuongeza msaada akamkamata mabega, shati likafunguliwa vifungo mpaka usawa wa tumbo kisha mfunguaji akasimama hapo kusubiri maelekezo.

  “Mtoe sidiria haina haja ya heshima hapa!” Akaongea tena kuelekeza ‘TSC’.

S.S Rebecca akafanya bila kusita maziwa yaliyolala kistaarabu ya mwanamama madam Mariana yakawa wazi macho ya kila anayemtizama akaona tattoo za kinachoonekana ni majina na maandishi mengine ya kilatino lakini kwenye titi la kushoto kwa pembeni sehemu za chini kulikuwa na mchoro wa mjusi kafiri ameng’ata kifurushi, Agent Kai alitoka kwa haraka toka eneo alilokuwa amekaa kwenye kiti akapiga hatua za haraka mpaka pale kisha akamuelekeza kitu kwa kichwa Jairo na jamaa akamuelewa akauvuta mkono wa kushoto wa Madam Mariana kwa nyuma licha ya kuwa ulikuwa umefungwa pingu kwa chuma iliyo juu ya meza.

Agent Kai alitulia akiungalia mchoro ule wa tattoo kwa umakini kisha akitumia simu yake akapiga picha kama tatu za kufuatana, mchoro huu uliweza kumrudisha nyuma siku kadhaa zilizopita wakati alipokutana na barua pepe toka kwa ‘Jogre’ iliyotumwa kupitia akaunti ya barua pepe ya mwanamke huyu, ‘TSC’ akatabasamu.

Mchoro hapa aliuona vizuri mubashara, mchoro wa tattoo ya mjusi kafiri na si mamba kama alivyoweza kuuona ule mchoro ulio kwenye barua pepe, huyu ni mjusi kafiri ameng’ata kifurushi na kwa maelezo ya afisa wa ‘Drug Trafficking Organization’ (DTO) shirika la kupambana na madawa ya kulevya huko Mexico ni kuwa alama hii ndiyo alama ya utambulisho na kujuana wafuasi wa genge la ulanguzi wa mihadarati la ‘THE RED JAGUAR’ wake kwa waume huku maafisa wa juu wakiekewa nyota mbili na wale wa juu zaidi nyota tatu na boss mwenyewe wanasema ana nyota tano.

   “Mariana Caro Funtes! Koplo wa zamani wa jeshi la Mexico… Una nyota tatu ndani ya genge la TRJ na wewe ni mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu kabisa ndani ya GTL… Naomba utupe ushirikiano hili tukuache huru uendelee na mambo yako kwakuwa kwa uzoefu nilionao nimegundua wewe ni mpiga dili tu uliostukiwa dili lako hivyo haraka ukakimbilia kwenye genge hili usiingie matatani kutoka ndani ya jeshi la wananchi wa Mexico na ndiyo maana ukaletwa huku hili kuwakwepa maafisa wa serikali waliokuwa wakikuhitaji miaka nane iliyopita na mpaka leo hawajui kama wewe huko wapi? Wewe ndie unayeongoza genge lenu hapa Guatemala tunaweza kuambiwa nawe mwenyewe kuwa pale Tajumulco kuna nini haswa ukiacha shamba la kahawa la Mr. Alexis?” Aliongea kirefu kidogo ‘TSC’ kisha akaweka tako lake moja upande juu ya meza hii ndefu kwenda juu mpaka usawa wa viuno vya watu hawa karibu wote.

   “Sioni hilo la kuachwa huru kwenye macho yenu” Akaongea kwa mara ya kwanza Mariana uso wake akiwa kauinamisha chini kana kwamba anaangalia ubora wa simenti uliojengewa sakafu ya chumba hiki.

   “Unataka uachwe huru kivipi?” Akahoji Agent Kai huku akiwa anatuma picha alizompiga Mariana kwa ‘Liz Rob’.

   “Ni kweli naweza saliti wenzangu na kuongea mengi kwenu lakini sina hakika nay ale mnayoweza kuniahidi kuwa nitaachwa huru kama mlivyosema” Akajibu macho yakiendelea kuangalia sakafu.

   “Bila kashikashi zile za kuhusika na kughushi nyaraka za kuwaamisha jela wafungwa wa kijeshi mpaka leo ungendelea kuwa sekretari wa ofisi ya mkuu wa nidhamu jeshi la wananchi la Mexico kama wenyewe mnavyoiita ofisi hiyo kuwa ni ofisi ya ‘secretariaty of Navy’ iliyopo makao makuu ya jeshi huko Mexico City boss wenu akiwa Meja Manuel Sanz.. .. Uliingia kwa Brigedia mfukuzwa jeshini bwana Fernandes Carlos Codrado hili akupe hifadhi na kukuficha akakuleta huku GTL kuongoza genge lake upande wa huku… Hivyo basi ukinifungukia ukweli na bet kukuacha huru uende mbali nje ya ukanda wa mabara ya Amerika kuendelea na maisha yako” Kete ya Agent Kai hili wapate habari nyingi wanazohitaji kuhusu genge la ‘TRJ’ hapa Guatemala ilikuwa ni kumuahidi hiki alichoahidi ingawa mara nyingi Agent Ka ufanya makosa kama haya kwa waalifu kuwaahidi kitu hili na yeye afaidike kujua anayohitaji.

Ahadi hii ilifanya bibie Mariana kufunguka kila kitu kuhusu genge la hatari la ‘THE RED JAGUAR’ chui hawa wa kiamerika na maelekezo jinsi gani wao kina Agent Kai wanaweza fanikisha litokomeza upande huu wa Guatemala.

‘TSC’ naye alimueleza kwanini walifika hapo ikiwa ni barua pepe yake yeye Mariana na ilipofika kumuonyesha picha ya Johnson Greg Rautollaye, mwanamam huyu alistuka sana na kusema mara nyingi akiwa katika kambi yao ya Tajumulco basi alikuwa anaomba aletewe mtu huyu kisha analala naye akifanya naye mapenzi anampenda sana na alipanga siku moja amtoroshe waanze naye maisha ya kuishi kama wapenzi walio huru, ilimshangaza ujanja uliotumiwa na ‘Jogre’ kuwasiliana na Agent Kai kupitia simu yake akaunti yake ya barua pepe.

Mwisho wa sehemu ya themanini na tatu (83)

‘Timu Kai’ imepiga hatua na kupata faida kubwa sana juu ya siri za genge la ‘TRJ’

Mwanadada Mariana amelegea na kubwabwaja karibu yote kwa ahadi ya kuachiwa huru.

Je ni kweli Agent Kai atatimiza ahadi yake?

Nini kitafuata baada ya kusikia juu ya Tajumulco Mountain na kusikia juu ya jasusi anayeshikiliwa mateka kwa miaka zaidi ya saba?

Tusogee mbele kwa mengi zaidi!




   “Bila kashikashi zile za kuhusika na kughushi nyaraka za kuwaamisha jela wafungwa wa kijeshi mpaka leo ungendelea kuwa sekretari wa ofisi ya mkuu wa nidhamu jeshi la wananchi la Mexico kama wenyewe mnavyoiita ofisi hiyo kuwa ni ofisi ya ‘secretariaty of Navy’ iliyopo makao makuu ya jeshi huko Mexico City boss wenu akiwa Meja Manuel Sanz.. .. Uliingia kwa Brigedia mfukuzwa jeshini bwana Fernandes Carlos Codrado hili akupe hifadhi na kukuficha akakuleta huku GTL kuongoza genge lake upande wa huku… Hivyo basi ukinifungukia ukweli na bet kukuacha huru uende mbali nje ya ukanda wa mabara ya Amerika kuendelea na maisha yako” Kete ya Agent Kai hili wapate habari nyingi wanazohitaji kuhusu genge la ‘TRJ’ hapa Guatemala ilikuwa ni kumuahidi hiki alichoahidi ingawa mara nyingi Agent Ka ufanya makosa kama haya kwa waalifu kuwaahidi kitu hili na yeye afaidike kujua anayohitaji.

Ahadi hii ilifanya bibie Mariana kufunguka kila kitu kuhusu genge la hatari la ‘THE RED JAGUAR’ chui hawa wa kiamerika na maelekezo jinsi gani wao kina Agent Kai wanaweza fanikisha litokomeza upande huu wa Guatemala.

‘TSC’ naye alimueleza kwanini walifika hapo ikiwa ni barua pepe yake yeye Mariana na ilipofika kumuonyesha picha ya Johnson Greg Rautollaye, mwanamam huyu alistuka sana na kusema mara nyingi akiwa katika kambi yao ya Tajumulco basi alikuwa anaomba aletewe mtu huyu kisha analala naye akifanya naye mapenzi anampenda sana na alipanga siku moja amtoroshe waanze naye maisha ya kuishi kama wapenzi walio huru, ilimshangaza ujanja uliotumiwa na ‘Jogre’ kuwasiliana na Agent Kai kupitia simu yake akaunti yake ya barua pepe.

ENDELEA NA NONDO..!!

PANDE MBILI ZA SHILINGI V

PETATLAN, GUERRERO-MEXICO

Ukumbi wa mikutano ulio juu kabisa katika kasri la ‘Secreto Potential La Feca Palacio’ kasri la kifahari na lenye mvuto kuliko majumba makubwa yote yaliyo katika mji mdogo wa manispaa ya Petatlan jimbo la Guerrero nchini Mexico, asubuhi hii ya siku ya jumapili ulikuwa umekaliwa na watu wapatao kumi walikuwa wamekaa kwenye viti vya plastiki rangi nyekundu ambavyo miguu ya viti hivi ilikuwa ya chuma kilichonakshiwa na kuwa kama alluminium kwa rangi yake, viti vinavyotengenezwa na moja ya kiwanda kati ya viwanda viwili vya mheshimiwa mwenye kasri hili ‘Kingpin’ Feca ambaye licha ya kujulikana kwake kuwa ni mmoja wa walanguzi wakubwa wa dawa za kulevya lakini kumiliki viwanda vyake ilimfanya kuonekana kama hajihusishi na biashara ya haramu ukweli uliofichwa kwenye nguo ya kaniki nyeusi.

Mijadala mbali mbali ilikuwa ikipigwa hapa katika eneo la mikutano ilikuwa si ya mpangilio nakuwa kama soga miongoni mwao sababu wapo waliokuwa wakiongea kutokana na ukaribu wa viti vyao huku pia wapo waliokuwa wakisikiliza huku na huko na kuishia kutabasamu au kutikisa vichwa vyao tu hawa ni kama Mr. Alexis Carlos Codrado na mheshimiwa waziri Ceni wao walikuwa kimya wakiguswa na maongezi wanainua vichwa kwa kila mmoja na wakati kufurahi au kutingisha vichwa vyao lakini kuchati kwa simu zao ilikuwa kila wakati jibu meseji soma meseji iwe kawaida au mitandaoni hasa whatssap.

Dakika tano za soga na stori mbalimbali za kuhusu genge lao na hata watu inaosemekana wanaongoza upambanaji juu yao huko Guatemala, zilipita ilipofika dakika ya sita alitokea ‘Kingpin Feca’ katika moja ya mlango unaomleta mtu hapa kutokea kwa ndani soga zikakata kila mmoja akanyamaza.

   “Tiiii Araaa Jeeiiii!!” Akatoa salamu ya genge lao huku anavuta kiti kukaa kiti kilicho mbele na kikiwa kimegeukia upande walipo hawa ndugu zake nao wakiwa kwenye viti vilivyogeuziwa upande wa mbele.

   “Tiiii Emmm Jiiiii!!!!” Wote wakatoa sauti ilitokusanya maneno haya kujibu salamu ya genge wakiwa wamesimama kwa pamoja.

   “Ahsanteni! Mwaweza kukaa tu..!” Akawashukuru na kuwaomba waketi vitini kama ilivyokuwa kabla hajaingia hapa.

   “Awali ya yote naomba niwashukuru kwa uwepo wenu hapa kwa ajili ya mjadala wa kuhusu mustakabali wa biashara yetu unaoonekana unaenda ndivyo sivyo juu ya usalama wake kimsingi.. Naomba sote tunyamaze kwa dakika moja kuweza kuwakumbuka na kuwarehemu ndugu zetu wengi waliopoteza maisha jana kwa kiasi ambacho ni rekodi toka tuasisi genge letu, genge tishio ukanda wote huu..!” Akaongea tena Feca kisha akaianamisha kichwa chake chini na wote walio hapa wkafana kama yeye kuinamisha vichwa vyao chini kuweza kunyamaza kimya wakiomb a dua zao za kimoyo moyo au kifuani fuani waweza sema pia na ndivyo ilivyo.

Dakika moja ya ukimya ilipita Feca akapiga viganja vyake kuonyesha sasa tayari wainue vichwa vyao.

   “Sote twaweza  sema tujipe pole kwa kilichotokea jana na pia tunaweza sema kilichotokea wiki hii inayoisha siku ya leo jumapili… Ni kuwa tulifuga kidonda na sasa limegeuka na kuwa donda.. Athari za dharau zimetugharimu na sasa tunahofu kubwa na mashaka tele juu ya tusichokijua kuhusu maisha yetu binafsi  na biashara yetu iliyo kichwa cha biashara zingine” Alianza kuongea kile kilichopo kwa wakati huu ambao kila mmoja alikuwa na hofu kweli kama asemavyo ‘Kingpin Feca’.

   “Taarifa za awali ambazo hazina uhakika sababu tunakosa habari iliyokamilika kutokana na mtu ambaye ni tegemeo kwetu naye tunaye hapa kutokana na hali ya hatari iliyo katika nchi ya GTL kwa sasa… Hatuna hakika juu ya Mariana kama naye katika mabomu yale ya kivita yaliyoshushwa bila huruma na kikosi cha kijeshi cha Marekani kama kanusurika ama vipi na kama kanusurika yuko wapi? Ingawa uhakika ni kuwa kama amenusurika kama tunavyohisi basi atakuwa anashikiliwa mateka na watu hawa wa Marekani ambao hata sijui tumewakosea nini kwa kipindi hiki ambacho tumekuwa tukifanya mambo yetu bila kuwadhuru watu wao wa DEA na wana usalama wao wengine wa mipakani tukijitahidi kuwaepa kwa kuwahonga baadhi yao hili tu mambo yetu yaende bila kuacha makovu ya kuumizana” Aliendelea kuongea Feca kisha akasimama toka kitini alipokaa akiwa na Ipad mkononi akaiwasha akawatizama watu wake uso wake ukiwa hauna ile hali ambayo uwa anayo mara nyingi hali ya ujivuni.

   “Kikosi cha awali ambacho Mariana alikiongoza kikiwa na watu wa GIS walio katika malipo na maelekezo ya mheshimiwa Ceni kilikuwa ni kikosi cha watu kumi wa GIS wakiwa katika gari zao mbili za kazi zinazofahamika kwa serikali yao na sisi TRJ pale Las Anonas tulikuwa na gari mbili pia zikiwa na watu kumi pia kila gari watu watano wakiwemo Molina Gudrado huyu ‘mwamba wa La Playa’, Stafu Sajenti Morientes Gudrado ambao kwa jinsi ambavyo anasema mheshimiwa kwa taarifa alizopewa na afisa wa polisi ni kuwa hakuna maiti ya Stafu Sajenti Morientes Gudrado na hata Molina waliyoikuta na hakuna maiti ya Mariana katika miongoni mwa maiti zilizokutwa pale katika vifusi vya juu juu ambazo nyingi zimeharibika kwa kiasi kikubwa kiasi ambacho huwezi kumgundua mtu kwa urahisi pengine waangalie vizuri wanaweza wakawaona hao watu wetu muhimu ambapo pia alikuwemo Eddie Mauro huyu ni assistant plan wa GIS naye tunasubiri ripoti ya pili itasemaje juu ya vifusi vinavyofukuliwa eneo la tukio lakini kwa taarifa za Petr Batromelo mkuu wetu wa kitengo cha silaha Tajumulco Camp anasema kwa hesabu za haraka ambazo bado anahitaji kuzifanyia uhakiki zaidi ni kuwa wale kumi kwanza waliongozana na Mariana na baadaye ikapigwa simu kuomba vikosi zaidi toka kwa Mariana kumpigia muongoza vikosi vyetu, waliondoka watu kama mia moja katika msafara wa gari kumi na nne aina ya Toyota Van Hiace  kama mjuavyo kwa sasa pale Tajumulco tuliacha watu wengi wa kiwanda cha siri wasio na uzoefu wa kazi za kazi wao wakiwa kwa ajili ya kutufanyia kazi za uzalishaji tu hivyo kwa hesabu hizo pale Las Anonas tumeondokewa na idadi kubwa ya watu wetu na mbaya zaidi jeshi la GTL toka usiku uliopita wamesambaa mipakani wakitumia anga na ardhi kudhibiti watu wanaotaka kutoka kwa njia zisizo halali na pia wanaotaka kuingia bila uhalali hivyo amri niliyoitoa awali kuwa vikosi vilivyo katika majimbo yote viende kulinda Tajumulco Camp nimeisitisha kwanza mpaka hali itakapotulia kwa sasa hali inaweza kugeuka na kuwa si hali kama itakuwa ndugu zetu wanashikiliwa mateka wanaweza shindwa vumilia mateso au kupewa ahadi inaoweza wafanya wakatoa siri pale Tajumulco Camp lilipo shamba la mdogo wangu Alexis kama inavojulikana kuna siri kubwa ikiwemo kiwanda na maghala ya kuhifadhi malighafi za mihadarati na mihadarati iliyo tayari shehena kwa shehena, pale Tajumulco kuna watu ninawaoamini sana lakini kwa mambo haya ya kushambuliwa na vikosi vya kijeshi wakitumia ndege na helkopta mambo yanaweza kuharibika zaidi kule ndipo ulipo mtaji wetu” Maelezo marefu yaliendelea kutoka kwa ‘Kingpin’ alipumzika akanyanyua chupa ya kinywaji mzinga wa ‘Zacapa Centenario’ moja ya pombe kali ambazo wanakunywa watu walio na uzoefu sana na pombe katika maisha yao maana ni pombe kali haswa ambayo unywapo hii unatakiwa uwe umeshiba haswa.

   “Tuko hapa kuona tunachukua tahadhari yetu binafsi na pia kuona tunajibu vipi mapigo yaani si kusubiri tunapigwa tu kama ng’ombe anayesubiri fimbo ya mfugaji imchape, uzuri hali ya hapa Mexico kwetu ni shwari mambo yamekuwa mabaya GTL tu lakini hatuwezi sema tuko salama hadi huku lolote linaweza pinduka kama ilivyo shilingi kuwa na pande mbili.. Niko kusikia mnafikiri tufanye nini kudhibiti hazina yetu na usalama wetu!” Alitoa fursa ya kuwasikiliza watu wake ambapo pia hapa leo alikuwepo master plan aliye smart kuliko watu wote wa genge la TRJ wenyewe wakimuita ‘alto genius’ tena akiwa amefanyiwa operesheni ya kurekebishwa taya yake.

   “Ningeomba niwe wa kwanza kuchangia niliyonayo pamoja na kuleta ombi la hitaji langu kwenu kwa sababu hali iliyotokea Guatemala kwa kiasi kikubwa ninastahili lawama kwakuwa mimi ndiyo nilikuwa kivuli chako mheshimiwa Brigedia Feca ingawa nilivyofika uliniomba nisijali kwa yote yaliyotokea sababu ukisema kuwa sote tuna wajibu na sote tuna wajibika kwa yote… Awali ingine naomba radhi kwa wana TRJ wote kwa ujumla kwa kutokuwa makini licha ya fursa zote nilizokuwa nazo nikikamata vyombo vya usalama vya kidola, waheshimiwa mnisamehe sana na pia nataka mjue kuwa mimi ni mjanja tu wa mambo ya kwenye makaratasi tu lakini si mjanja sana katika sekta za kazi kama hizi kivitendo” Alianza kuongea mheshimiwa waziri wa usalama wa nchi ya Guatemala ambaye mpaka wakati wapo hapa habari za kufutwa kwake kazi zilikuwa bado hazijatangazwa hadharani wanancrhi wakapata kujua, alisimama kuwaangalia watu wanaomsikiliza akiwa ameweka ombi la kusamehewa kwakuwa nafsi yake ilikuwa ikimsuta kuwa amewaangusha sana wenzake pamoja na yeye mwenyewe kwa ujumla.

   “Nafurahi wote mmeniruhusu niendelee na ninachohitaji kusema mbele yenu.. Nianze na kwanini niko hapa nanyi muda huu? Wakati si kawaida yangu kufika hapa HQ na kuhudhuia kikao kama hiki ingawa pia si mara ya kwanza kama wengine wanavyoweza kudhania juu ya ujaji wangu hapa, nimekuwa nikifika hapa na kufanya vikao vya watu wawili au watatu ikiwa pamoja na boss Feca kisha haraka napnda chombo kurudi GTL… Niko hapa kwa ajili ya habari za haraka nilizopenyezewa juu ya kilichomo kwenye flash tuliyokuwa tukihitaji sana kujua ina jambo gani mule lililoandaliwa na mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa marehemu Jota Mariapan ni kwamba ni ushahidi wa mimi kuhusika moja kwa moja na ushawishi mkubwa wa vyombo vya kiusalama kufanya mambo yaliyo kinyume na majukumu yao, mheshimiwa Rais aliwaandaa vijana wakuja kunichukua ifikapo alfajiri lakini bahati nzuri kwangu katika vijana wale kulikuwa na mmoja ambaye ni kati ya wawili anaowaamini sana ni mtu niliyempachika bila mheshimiwa Rais kujua, vijana hawa wawili waaminiwa sana walitaarifiwa kuwa kukikucha tu asubuhi niwekwe chini ya ulinzi kisha nipelekwe kwenye kambi ya jeshi makao makuu.. Kijana akanitaarifu ndipo nikaomba msaada wa Feca anitumie helkopta haraka sana na hii ndiyo sababu niko nanyi hapa.. Kuhusu hali ilivyo sasa nchini kwetu kwa kweli hali ni mbaya sana tumepoteza uwezo wetu kwa muda mfupi sana bila kutegemea ni ghafla sana, wamarekani wameleta kikosi cha kijeshi kikiongozwa na watu wao wa kiintelejensia toka DEA na CIA wakipewa sapoti na Rais wetu akimtumia ndugu yake binamu Kamanda Muniain mkurugenzi wa OCLA kanda ya Guatemala kama mnavyomjua amekuwa mwiba mkali kwa miaka mingi huyu Muniain lakini tumekuwa tukihofia kumfanya jambo baya kwa hofu ya kuwachokoza OCLA na pia kumchokoza kaka yake… Mara zote uwa tunasema mbaya kumfuga nyoka aliyekwisha onyesha si nyoka wa kuhitaji kufugwa ni nyoka wa hatari kama nyoka swila.. Kaman..!” Aliongea kwa kirefu Mheshimiwa Ceni lakini kuna swali lilitaka kuulizwa hivyo akasimama kusikiliza swali linalotaka kuulizwa na mmoja ya wasikilizaji.

   “Mheshimiwa Ceni… Ni kweli wewe ndiye mtu pekee tuliyekuwa tukikutegemea katika kujua serikali yenu inapanga nini kama tulivyowaweka watu wengine katika nafasi za ukaribu na serikali za nchi mbalimbali za ukanda huu ni kwa sababu ya wao kuwa masikio na macho yetu ndani ya serikali na kushiriki moja kwa moja kutulinda kwa hali na mali… Swali langu ambalo ninahitaji jibu lake ni swali linaloniumiza sana kichwa toka niko kwenye matibabu nikiwa nasikia mambo mengi ya kuchanganya toka GTL, imekuwaje mpaka ubalozi wa Marekani unaingiza kikosi cha kijeshi bila wewe kama waziri wa usalama kujua nia na madhumuni yake?” Swali liliulizwa na makamu wa Rais wa genge la ‘TRJ’ Mr. Guti Villa Nandez.

   “Mimi kwenye masuala ya kijeshi sihusiki sana kwakuwa katiba imeniwekewa mipaka makubaliano yoyote baina ya serikali yetu na jeshi la nchi nyingine uwa yanasimamiwa na wizara husika, wizara ya ulinzi… Hivyo basi nililetewa taarifa tu ya kimaandishi kuwa ubalozi wa Marekani umewaombea eneo la kutia nanga manowari ya kijeshi ya jeshi la wananachi la Marekani ‘US Army’ nilipouliza dhumuni nikaambiwa ni makubaliano baina ya jeshi letu na wao kutoa mafunzo kwa wanajeshi wetu wa jeshi la wanamaji pia kuilinda pwani na ghuba zetu kutokana na maharamia wa baharini… Tokai we hivi ni miezi nane sasa na ndipo walipokuja hawa majasusi wanaongozwa na Agent Kai wa CIA” Akajibu kiufafanuzi kidogo kisha kukawa na swali lingine.

   “…Mmh!.. Je ulishirikishwa kwa namna yoyote juu ya uingiaji wao? Na je unajua idadi ya kikosi anachoongoza huyo Agent Kai?” Swali lilitoka tena kwa Mr. Guti.

   “.. Sikushirikishwa na ilinistaajabisha kidogo sababu hata hao OCLA wanaripoti kwa GIS ikiwa wana jambo linalohitaji kuvuka mipaka ya nchi, nilipomuuliza mkuugenzi wangu wa GIS akasema ishu ya hao watu inaonekana hata yeye alifichwa wanafanya kazi za kiuchunguzi bila kibali kutoka kwao hivyo anamtafuta mtu anayeonekana nao akifanya nao kazi bega kwa bega ambaye ni Muniain sasa… Walipowasiliana akanipa jibu kibali cha watu hao kufanya kazi kimetoka ikulu moja kwa moja kwa mheshimiwa Rais na katibu wake mkuu hapa moja kwa moja nikapata jibu Muniain ametumia undugu wake na Rais kuingiza watu wa kutuangamiza kwa kushirikiana kikosi kinachotoa mafunzo kwa wanajeshi wetu” Akajibu Ceni kisha akajimiminia kinywaji katika glasi hili apate kulowanisha koo lake.

   “Huu ni mpango ulioandaliwa na Kamanda Muniain kwa pamoja na marehemu Jota Mariapan wakitumia ukaribu wao na mheshimiwa Rais akawapa Baraka zote wakaomba msaada Marekani bila kukushirikisha wewe na hapa ndipo palipo na ukakasi sababu na wewe ni mmoja wa watu waliokuwa na ukaribu mkubwa na Rais, je ulistukiwa kuwa si muaminifu ndiyo maana wakakutenga licha ya usiri mkubwa uliokuwa ukiufanya” Feca akaongea akiwa amesimama mwisho kabisa wa ukumbi huu ambao huko baraza ya juu kabisa katika kasri hili linalong’aa sana kwa rangi nyeupe iliyopigwa kuta zote toka flour (losheni) ya chini mpaka ya juu.

  “Au katika watu ambao unawaamini kuwa ni wa siri katika mipango yetu aliweza kutoa siri kuwa wewe hutakiwi kushirikishwa kwa lolote… Nilivyokuwa naondoka kwenda Canada kwa matibabu yangu nakumbuka nilikutumia onyo kwa meseji kuwa uwe mwangalifu na wigo mpana wa watu wapya unaowaongeza katika mfumo wa ulinzi wako na wetu, hao ndiyo wameweza kuharibu amini usiamini mheshimiwa” Ivan Alberto ‘alto genius’ akaongea kuongezea alipoishia Feca kumwambia mheshimiwa Ceni.

  “Kuna ukweli kati ya mengi muyasemayo… Bado niko nafanya mawasiliano nao wale walio waaminifu kujua kunaendeleaje huko nyumbani, nafahamu kuna kikao kwenye ukumbi wa ikulu ifikapo saa tano asubuhi hii na ajenda ya kikao ni kufutwa kwangu kazi na kuwa natafutwa na serikali kwa kesi mbalimbali nikihusishwa moja kwa moja.. Nyepesi nyepesi zinasema watatangaza kutaifishwa na mali zangu zote” Mheshimiwa Ceni akajibu hoja zilizotolewa.

  “Kuna namna ya kuzuia hayo?” Akahoji Sergio Lopez Puto huyu ni mwana genge wa ‘TRJ’ anayetokea Marekani nilishamuelezea mwanzo mwanzo wakati ambao Feca ametoka gerezani kutumikia kifungo chake, alifika hapa makao makuu ya genge lao baada ya kuombwa na kiongozi wao Rais wa genge Feca ahudhurie kikao hiki kitakachoamua mustakabali wa genge.

  “Usiku huu nilikuwa naongea na mwanasheria wangu kuona tunafanyaje kuzuia kutaifishwa tu bila sheria kupitiwa kuona inakuwaje hivyo anasubiri hotuba ya Rais itakaosomwa juu yangu na maamuzi yake kisha ya hapo atanicheki tutapanga cha kufanya” Akajibu mheshimiwa Ceni na kusubiri swali lingine.

  “Wakati wa uchaguzi uliopita katika kampeni unakumbuka tulichangia kiasi gani kwa mheshimiwa Rais? Kupitia kwako akiamini umetoa mwenyewe tu” Akauliza ‘Alto Genius’.

  “Ni pesa nyingi na nilimwambia si mkopo nimetoa kama msaada wangu tu kwake, kunani hapo?” Akajibu na kuhoji Ceni.

  “Nataka utumie kete ya kumpatia msaada uliompatia kuzuia asitaifishe mali zako.. Kumbuka unamiliki mtandao wa simu ambao kwa sasa pale GTL ni maarufu sana ukiwa na wateja wengi nyumbani hadi nchi za jirani, angalia una vituo vya mafuta na kampuni kubwa ya gesi kuliko kampuni yoyote, kufilisiwa kwako kutakufanya ufe maskini” Akafafanua Ivan ‘Alto Genius’.

  “…Oooh! Lakini.. Lakini kuna ugumu fulani yeye sasa ni Rais ana dola mkononi mwake analindwa na katiba ya nchi… Unashauri nipite njia gani?” Akakubali lakini akataka afafanuliwe anaweza fanyaje kwa wazo mbadala.

  “Usiogope utaondoka hapa Petatlan kwenda Mexico City kisha utampigia kumwambia utautangazia uuma kuwa ulimuomba pesa anazosema za haramu kiasi kikubwa kutumia kwenye kampeni zake na kwa pamoja mlishirikiana kusambaza pesa na zawadi nyingine kwa wananchi kinyume cha sheria mpaka akashinda urais” Akafafanua ‘Alto Genius’ na watu wote walio pale wakaunga mkono ikawa kama soga kila mmoja akiongea lake na mwisho ikapita njia hii kuzuia mali za Ceni kutaifishwa na serikali na cha msingi waliona kwanza wasikilize kitakachoongelewa na Rais katika mkutano wake na waandishi wa habari ndipo waanze kuchukua maamuzi kamili kwa kuanzia hapo katika hotuba yake.

Mwisho wa sehemu ya themanini na nne (84)

Kamati kuu ya genge la ‘TRJ’ imekutana makao makuu ya genge lao katika kasri la boss wao huko manispaa ya mji wa Petatlan jimbo la Guerrero nchini Mexico.

Tuweke kando maneno twen’zetu tumalizie malizie epsd hizi za mwisho mwisho katika jino kwa jino.




  “Usiku huu nilikuwa naongea na mwanasheria wangu kuona tunafanyaje kuzuia kutaifishwa tu bila sheria kupitiwa kuona inakuwaje hivyo anasubiri hotuba ya Rais itakaosomwa juu yangu na maamuzi yake kisha ya hapo atanicheki tutapanga cha kufanya” Akajibu mheshimiwa Ceni na kusubiri swali lingine.

  “Wakati wa uchaguzi uliopita katika kampeni unakumbuka tulichangia kiasi gani kwa mheshimiwa Rais? Kupitia kwako akiamini umetoa mwenyewe tu” Akauliza ‘Alto Genius’.

  “Ni pesa nyingi na nilimwambia si mkopo nimetoa kama msaada wangu tu kwake, kunani hapo?” Akajibu na kuhoji Ceni.

  “Nataka utumie kete ya kumpatia msaada uliompatia kuzuia asitaifishe mali zako.. Kumbuka unamiliki mtandao wa simu ambao kwa sasa pale GTL ni maarufu sana ukiwa na wateja wengi nyumbani hadi nchi za jirani, angalia una vituo vya mafuta na kampuni kubwa ya gesi kuliko kampuni yoyote, kufilisiwa kwako kutakufanya ufe maskini” Akafafanua Ivan ‘Alto Genius’.

  “…Oooh! Lakini.. Lakini kuna ugumu fulani yeye sasa ni Rais ana dola mkononi mwake analindwa na katiba ya nchi… Unashauri nipite njia gani?” Akakubali lakini akataka afafanuliwe anaweza fanyaje kwa wazo mbadala.

  “Usiogope utaondoka hapa Petatlan kwenda Mexico City kisha utampigia kumwambia utautangazia uuma kuwa ulimuomba pesa anazosema za haramu kiasi kikubwa kutumia kwenye kampeni zake na kwa pamoja mlishirikiana kusambaza pesa na zawadi nyingine kwa wananchi kinyume cha sheria mpaka akashinda urais” Akafafanua ‘Alto Genius’ na watu wote walio pale wakaunga mkono ikawa kama soga kila mmoja akiongea lake na mwisho ikapita njia hii kuzuia mali za Ceni kutaifishwa na serikali na cha msingi waliona kwanza wasikilize kitakachoongelewa na Rais katika mkutano wake na waandishi wa habari ndipo waanze kuchukua maamuzi kamili kwa kuanzia hapo katika hotuba yake.

ENDELEA NA NONDO….!!

BUTWAA I

SAN MARCOS-GUATEMALA

   “Hakuna mtu hapa, tumesachi nyumba yote bila bila..!” Upande wa pili wa simu uliongea baada ya Agent Kai kupokea simu yake ya mkononi akiwa kakaa siti ya upande wa pili wa dreva wakiwa wanaelekea kupaki gari kwenye maegesho ya mgahawa unaoitwa Restaurant Hana, mgahawa unaotoa huduma zake kwa vyakula aina mbalimbali toka mataifa mbalimbali ulioko eneo la Panajachel a.k.a Pana mji mdogo katika mkoa wa San Marcos.

  “Basi haina shida.. Mje huku Panajachel kuendelea na ratiba iliyo mbele yetu kama tulivyopanga..” Akajibu Agent Kai ‘The Sole Cat’ na simu ikakatwa na wa upande wa pili aliyepiga.

  “Ni Silla ananipa taarifa kuwa hawajakuta mtu kwenye makazi tuliyoelekezwa na Ange kuwa ni nyumba aliyonunuliwa na Alexis hapa San Marcos na uwa bwana wake anafikia anapokuwa hapa San Marcos kwa shughuli zake kama boss wa ‘Alexis Farm’s and Industrie’s’… Naamini huko Tajumulco usiku wa leo tutakuta mengi sana..” Akaongea Agent Kai akiwa anawatizama wenzake alio nao ndani ya gari kwa zamu.

  “Mungu awe nasi” Aliongea Kamanda Muniain ambaye naye alijumuika na vijana hawa kwa ajili ya kuwa msaada kwa lolote ambalo linaweza kuwa tofauti kwao.

   “Mheshimiwa Rais ametuamini sana na ametupatia baraka zake zote katika jambo tunaloenda kulifanya..” Akaongea tena ‘TSC’  na papo hapo Special Agent Rebecca akafunga breki na kupaki mahala alipoona ni sahihi kupaki gari yao haina ya Toyota Hiace Van.

  “Hotuba yake mbele ya waandishi wa habari asubuhi ya leo imefungua njia ya Guatemala mpya bila madawa ya kulevya, Guatemala mpya kwa usalama wa wananchi wake..” Kamanda Muniain akaongea akiwa kainamisha kichgwa chake chini akifikiri kwa kina yaliotokea katika nchi yake siku tatu mpaka nne zilizopita matukio kadhaa yakipita kichwani mwake kisha akatabasamu kwa furaha akiamini kuna mafanikio kamili yanakuja kwao kama kikosi na kwao kama nchi ya Guatemala.

  “Mimi nimefurahi alipovunja baraza lote la mawaziri na kuahidi kuunda baraza jipya la mawaziri baada ya mwezi mmoja.. Hii itampa nafasi ya kusubiri na kuona virusi vyote vinaondolewa” Rebecca akaongea na wengine wakakubali kwa kutingisha vichwa vyao.

  “Inahitajika umakini sana katika hali kama hii maana wale tuliokwisha wabaini wengi ni wa kutoka wizara ya usalama, hatujui cheni kama iliishia huko tu… Je hawakuweka mtandao wao hadi wizara zingine? Mwezi mmoja utatosha kujua yote haya cha muhimu ni usiku wa leo kuona tunaenda kufanyaje pale Tajumulco juu ya wenzetu tunaoamini wako pale wanashikiliwa mateka” Agent Kai akaongea huku anasoma meseji anazotumiwa na swahiba wake ‘Liz Rob’ meseji za maelekezo mbalimbali kwa njia ya whatssap.

Walishuka wote kwa pamoja wakiwa takribani watu wanne hapa huku huko Main Street ilipo nyumba ya Angelica Linares walienda Special Agent Silla akiwaongoza Austin na Jairo kwa dhumuni walilokubalina kuwa pengine inaweza kuwa Alexis amejihifadhi huko kuukimbia mkono wao na wa serikali, ingawa ni kweli wakati anaondoka Guatemala City alikimbilia hapa lakini walimchelewa muda huu upo kwa kaka yake huko Petatlan, Guerrero nchini Mexico.

  “Tukakae viti vya kule pembezoni mwa ziwa, tukapate hewa mwanana ya ziwa Atitlan.. Hapa nilifika miaka minne iliyopita mahala pazuri sana..!” Kamanda Muniain akaelekeza mahala ambapo wakakae kusubiri muda muafaka wa kuelekea Tajumulco Mountain huko karibu na mpakani mwa nchi ya Guatemala na Mexico.

Wakuu hawa wa kazi za kazi waliendelea kuwa hapa mpaka Silla na wenzake alioenda nao huko Main Street walipofika kujumuika nao, saa tano usiku baridi ikiwa imekolea sana eneo hili kwa kila mmoja wao licha ya mavazi waliyovaa kuwa ni kwa ajili ya kudhibiti baridi kama hii lakini nyuso zao zilionyesha wamechoka kuwepo hapa.

  “Baridi hapa limekuwa si rafiki tena hata tukisema tusogee kule juu yalipo majiko ndiyo patatufanya tulemae zaidi… Ni wakati wa kuelekea Tajumulco bila kujali si muda tuliosema ni mzuri kuelekea huko kutokana na kiulinzi watu wanakuwa wamechoka kuanzia saa nane usiku.. Nafikiri tuanze safari!” Akaongea ‘TSC’ akimalizia kahawa kwenye kikombe chake sababu yeye kwakuwa si mnywaji pombe aina yoyote ile mara nyingi anapokuwa sehemu kama hizi basi uagiza kahawa kama njia ya kuzuia usingizi na baridi.

  “Muda mzuri sababu kuna umbali kidogo kutoka hapa Panajacheli hadi Tajumulco.. Tutaenda taratibu tu na kufika kama saa saba hivi” Kamanda Muniain akafafanua kisha wote wakainuka toka vitini mwao.

  *****  *****  *****

BUTWAA II

TAJUMULCO, SAN MARCOS-GUATEMALA

Kwa njia waliyoijia Agent Kai na timu yake anayoiongoza wakiwa na gari lao rangi nyeusi maalumu kwa kubeba watu zaidi ya nane aina ya Toyota Hiace Van, njia iliwafikisha hadi mahala ambapo ni uwanja wa mpira wa shule ya msingi inayotumiwa na wakazi wa eneo la kijiji kilicho karibu kabisa na mwanzoni mwanzoni mwa milima ya Tajumulco, milima inayochukua eneo kubwa sana kwenda eneo la mpakani mwa nchi hii ya Guatemala na Mexico.

Eneo la kijiji hiki ni eneo lililojengwa nyumba za kufanana (kota) kabla ya hata shamba la kahawa lililo eneo hili kando ya milima lililokuwa la serikali halijachukuliwa na mwekezaji Alexis Carlos Codrado, walifika gari ikiendeshwa na Austin Manuel Contreras mzungu huyu mwenye za blonde, mwembamba na mrefu alisimamisha gari karibu na goli la upande wa kusini mwa uwanja wa mpira ambako kulikuwa na miti mikubwa iliyofanya eneo hili kuwa na giza zito sana la kuweza kukupa tabu ukiwa kwa hapa kumuona hata aliye jirani yako labda awepo kwa upande wa uwanjani kule ambako kuna angalau kidogo katika uzito wa giza.

  “Hizi nyumba za hapa ni kota za wafanyakazi wa shamba la Alexis Farm’s na mbele ya uwanja ni shule ya msingi ambayo inatumiwa na watoto wa wafanyakazi wa shamba na pia watu wa vijiji vya jirani na hapa Tajumulco, upande wa pili ukishazunguka eneo la hii la shule kuna nyumba za walimu ukipita eneo hilo unaikuta bara bara kisha ya hapo ndipo linaanza shamba la Alexis Farm’s likiwa limezungushiwa senyenge kwa upande wote wa barabara… Maelekezo haya alinipa Norman kwakuwa aliwai kufika kuchunguza eneo hili” Gari ikiwa imetulia tuli na watu wote waliomo kuanza kushugulisha macho yao kwa kutizama huku na huko, Kamanda Muniain alivunja ukimya uliotaka kuteka hatamu ndani ya gari.

  “Sisi tulivyokuja huku hatukuingilia eneo hili tulizungukia upande wa chini mbali na hapa kuna mto mkubwa sana tukaishia pale kwa kushindwa kwenda upande wa pili, ulinzi wa upande ule tuliuona ni mkali sana, tuliishia upande ule wa mtoni tukatumia darubini kuona tuliyoyaona..!” Investigator Miller akaongea.

   “Yaaah! Walinzi ni wengi hata Norman kilichomshinda kuingia ndani ya hata eneo la shamba ni icho icho kitu ambacho ni cha kushtua kidogo sababu hapa GTL kuna mashamba mengi tu ya wawekezaji mbalimbali lakini si mashamba yanayolindwa kwa kiasi kikubwa kama shamba hili” Akaunga mkono Kamanda Muniain.

  “Leo tuko na nguvu kazi, tuko na silaha na tayari tushawaandaa watu wa jeshi wa katibu na hata mheshimiwa Rais anajua muda huu wa usiku tuko hapa Tajumulco.. Tutaelekea huko kwa tahadhari tukiwa kwa miguu gari tutaiacha hapa hapa ikiwa inaangaliwa na mzee wetu, tukifika huko  tutajua tunajigawa vipi” Agent Kai akawatia nguvu ya imani ya kazi wenzake kisha wote wakaanza kuchukua kile walichokiandaa kwa ajili ya kazi za kazi zikiwa ni zana za kazi za kisasa.

Safari yao ilifuata maelekezo ya Kamanda Muniain ambaye aliomba awasindikze halafu ndiyo arudi kuwasubiri kama alivyopanga kiongozi wa timu ‘TSC’.

Walipofika eneo la barabara iliyokuwa si pana sana na ya vumbi waliiona senyenge iliyosemwa hapa wakasimama wakijiweka sawa na miti mbalimbali iliyo kando ya barabara.

   “Hapa ndipo mwisho wa mpaka wa nyumba za walimu kuanzia upande wa pili ukivuka barabara kuna bonde mtaingia hapo mkiibuka kuna kimlima kama mnavyokiona juu yake ndipo ilipoanza kusukwa senyenge inayozunguka eneo lote la shamba ikisambaa kwa urefu wa heka zaidi ya thelathini kama unafuata barabara hii inakwenda mpaka lilipo geti la kuingilia ndani ya eneo la shamba… Huko aliposema Silla kuwa walikwenda wakakuta mto upande ule haujaweka uzio wowote wakiutegemea tu mto kama kinga ya kuzuia watu kupita kufika eneo lao ni eneo la misitu minene yenye wanyama na majoka hivyo si salama kupita huko na kidogo ilinishangaza kwa ndugu zetu kupita huko na kurudi salama bila kuzuliwa hata na nyoka wa kawaida wenye sumu kali” Yalikuwa ni maelezo ya Kamanda Muniain akiyatoa huku kina Agent Kai wanamsikiliza kila mmoja akiwa makini sana kutizama huku na huko.

  “Haina shaka mzee.. Sisi tutalazimisha kupitia hapa ulipotuelekeza kuwa kuna bonde… Wewe nenda katusubiri kwenye gari na muda wote uwe makini kusikiliza kwenye mtambo wetu yanayoendelea.. Sisi wengine naomba kila mmoja wetu aweke sawa saa simu na vifaa vyetu vya Earphone Bluetooth kwa ajli ya SCNG” Agent Kai aliona ni vizuri mzee wao Kamanda Muniain arudi walipoacha gari ambako kuna kamtambo kidogo kinachowaunganisha kimawasiliano kupitia mtandao wao mdogo wa ‘SCNG’ (Small Call Network Group) kisha ya hapo waliagana na mzee wao akiwapa mkono wa kheri walivuka kwenda upande wa pili kila mmoja akiwa na begi mgongoni mwake wakiwa wameinama kama mwendo wa masokwe, kikosi chwa watu sita kilikuwa kimeongozana kila mmoja akiwa katika mavazi meusi kuanzia suruali zao walizovaa mpaka makoti yaliyo juu ya fulana maalumu zilizo kama vizibao hizi zikiwa hazipenyi risasi (bulletproof) na miwani maalumu ya kijasusi ya kuonea gizani katika macho yao iliwafanya wawe kamili na wenye kujiamini vya kutosha.

Ni kweli waliposhuka kwenye bonde walikiona kilima kama kichuguu kukiwa na nyasi haina ya magugu zilizoshuka mpaka bondeni na eneo lote pamoja na mawe mawe makubwa ya wastani na madogo, wakakwea kilima kwa stahili ya kutambaa ndipo wakauona uzio wa senyenge ambayo kwa ilivyo na uzoefu wao walitambua ni senyenge inayotumia umeme kwa shoti kuzuia mtu kuigusa kwa muda huu wa usiku maana kwa juu kabisa zilisambaa nyaya maalumu kwa kazi hii.

Macho ya kila mmoja yakisaidiwa na miwani waliyoivaa waliweza kuona wakishavuka kwa ndani basi watakutana na miche ya mikahawa katika eneo ambalo kiutaalamu ni mahala inapozalishwa miche ya miti ya kahawa kwa uwingi ikiwa imetambaa eneo kubwa la heka moja  au na zaidi, macho yasiyo na pazia yaliama na kusogea mbele zaidi ndipo haswa palianza kutimiliza nia ya shamba kuwa ni shamba la kahawa.

   “Haina haja ya kugawana na kujitawanya… Tutapita kuingia ndani ya eneo la shamba tukiwa pamoja, endeleeni kuwa kama tulivyo hapa hapa mi naenda kukata senyenge eneo la kupita” Baada ya kuacha macho yao tu yazunguke huku na huko kuangalia mazingira yalivyo walipo na maeneo mengine wakitumia wasaa wa dakika kumi na mbili kapteni wa kikosi akaongea huku begi lake likiwa mbele ya kichwa chake akiwa amelala chini, akafungua zipu na kutoa gloves kisha akafunga zipu na kurudisha begi mgongoni akazitwaa gloves kuzivaa viganjani mwake.

Mtambao kama nyoka mkubwa ulianza kwa kasi kukwea kilima safari iliyomfikisha kwenye senyenge  akatulia akiacha kazi ya macho kufanya usahili ishike hatamu kwa takribani dakika moja, alipoona hali haina kokoro akaleta tena begi mbele yake toka mgongoni akafungua zipu na kutoa mkasi mkubwa kidogo wenye makali ya kukata nyaya haraka akakata kwa mtindo wa kipenyo cha duara chenye uwezo wa kumfanya apite bila bugudha wala zuio la senyenge ya umeme.

Aliporidhika akageuza shingo kule alipotoka na kuwaonesha ishara iliyoeleweka kwa wote, mkasi ukarudishwa kwenye begi likafungwa bila kuremba akatanguliza kichwa chake kupenya akihakikisha nyaya hata moja aliyoiacha kwa bahati mbaya kumgusa.

Miguu ilipomaliza kupita tu kwenye tundu akaona mwanga wa tochi unaokwenda mbele kisha unarudi nyuma unajia upande huu na kwa mbali kimluzi kikihanikiza, mluzi ulikuwa wa stahili fulani hivi na kila mwanga wa tochi ulivyokuwa unazidi kusogea na ndipo usikikaji mzuri wa mluzi katika masikio ya ‘TSC’ uliongezeka.

  “Msianze safari ya kupanda kilima sababu kuna mteja anajia upande nilipo nafikiri ni mlinzi wa doria” Akaongea ‘TSC’kwa sauti ya chini kabisa mkono wenye saa ulikuwa sawa na mdomo wake, taarifa iliwafikia wote wana .

Mtambao ulianza tena ikiwa dakika hii Agent Kai ‘TSC’ akitambaa kwa spidi kubwa bila kuacha athari, breki ya kwanza ilikuwa ni kumfanya asimame wima kwa mnyooko wa kama mwamba wa goli sambamba na mti ambao kwa giza lililopo hapa ilikuwa ngumu yeye kuujua na kuweza kunijuza niandikaye (lol).

Kwa chati alitokeza kichwa apate kuweza kuchungulia kule kuliko na mwanga wa tochi unaokuja taratibu ikiwa ishara ya kuwa mtu anayekuja anatembea taratibu sana na anapotokea kuna njia nyembamba kama ujuavyo mashamba yanavyokuwa na vinjia kama hivi, kwa ukaribu na alipo ‘TSC’ akisaidiwa na miwani aliyovaa yenye uwezo mzuri wa kuona vizuri gizani na hata kwa umbali fulani usiowezekana kuonekana na macho ya kawaida aliweza kumuona mwanaume anayekuja akiwa kavaa mavazi ya kama askari au mwanajeshi kwa kuzuia baridi aliweka koti zito mwilini, mkono wake wa kulia alikuwa kashika bunduki aina ya ‘shot-gun’ akiishika katikati kana kwamba kashika mua mfupi, uso wake ukionekana kidogo sana kwakuwa alivaa kofia inayomziba kuanzia masikio, eneo lote la paji la uso akiacha machoni mpaka kidevuni ambako kofia la nguo nzito ya sufi ilikamatia.

‘TSC’ aliacha asogee sogee huku akihakikisha hakuna mwingine ajaye nyuma yake alipokaribia mti aliojificha kwa tahadhali kubwa Agent Kai akazunguka mti hili wapishane lakini alipoona ashapita hatua mbili aliruka hatua moja tu kwa nyuma  yake na kumstua kwa kiasi kikubwa mwanaume huyu akageuka kwa kasi iliyotarajiwa na fundi muwindaji ambaye alishamuandalia shambulizi.

Mwisho wa sehemu ya themanini na tano (85)

Kazi imeanza ndani ya ngome ya kambi ya Tajumulco, kambi yenye usiri mzito na matumizi yake, ikifahamika kama ni eneo la shamba la mwekezaji Alexis Carlos Codrado.

Nini kitatokea hapa Tajumulco?

Kwa majibu mazuri ya kuvutia na kutia taharuki twen’zetu sehemu inayofuata.




Miguu ilipomaliza kupita tu kwenye tundu akaona mwanga wa tochi unaokwenda mbele kisha unarudi nyuma unajia upande huu na kwa mbali kimluzi kikihanikiza, mluzi ulikuwa wa stahili fulani hivi na kila mwanga wa tochi ulivyokuwa unazidi kusogea na ndipo usikikaji mzuri wa mluzi katika masikio ya ‘TSC’ uliongezeka.

  “Msianze safari ya kupanda kilima sababu kuna mteja anajia upande nilipo nafikiri ni mlinzi wa doria” Akaongea ‘TSC’kwa sauti ya chini kabisa mkono wenye saa ulikuwa sawa na mdomo wake, taarifa iliwafikia wote wana .

Mtambao ulianza tena ikiwa dakika hii Agent Kai ‘TSC’ akitambaa kwa spidi kubwa bila kuacha athari, breki ya kwanza ilikuwa ni kumfanya asimame wima kwa mnyooko wa kama mwamba wa goli sambamba na mti ambao kwa giza lililopo hapa ilikuwa ngumu yeye kuujua na kuweza kunijuza niandikaye (lol).

Kwa chati alitokeza kichwa apate kuweza kuchungulia kule kuliko na mwanga wa tochi unaokuja taratibu ikiwa ishara ya kuwa mtu anayekuja anatembea taratibu sana na anapotokea kuna njia nyembamba kama ujuavyo mashamba yanavyokuwa na vinjia kama hivi, kwa ukaribu na alipo ‘TSC’ akisaidiwa na miwani aliyovaa yenye uwezo mzuri wa kuona vizuri gizani na hata kwa umbali fulani usiowezekana kuonekana na macho ya kawaida aliweza kumuona mwanaume anayekuja akiwa kavaa mavazi ya kama askari au mwanajeshi kwa kuzuia baridi aliweka koti zito mwilini, mkono wake wa kulia alikuwa kashika bunduki aina ya ‘shot-gun’ akiishika katikati kana kwamba kashika mua mfupi, uso wake ukionekana kidogo sana kwakuwa alivaa kofia inayomziba kuanzia masikio, eneo lote la paji la uso akiacha machoni mpaka kidevuni ambako kofia la nguo nzito ya sufi ilikamatia.

‘TSC’ aliacha asogee sogee huku akihakikisha hakuna mwingine ajaye nyuma yake alipokaribia mti aliojificha kwa tahadhali kubwa Agent Kai akazunguka mti hili wapishane lakini alipoona ashapita hatua mbili aliruka hatua moja tu kwa nyuma  yake na kumstua kwa kiasi kikubwa mwanaume huyu akageuka kwa kasi iliyotarajiwa na fundi muwindaji ambaye alishamuandalia shambulizi.

ENDELEA NA NA MAPIGO…!

BUTWAA II

SAN MARCOS-GUATEMALA

Mwanaume huyu ambaye tayari ilishajidhihiri ni mlinzi aliyekuwa akifanya doria kucheki usalama wa eneo la mipaka ya shamba kama walivyotahadharishwa mapema asubuhi ya siku iliyopita kuwa wawe makini sana alitoka mahala alipolala na wenzake kuzunguka kupita kwa pembeni kuangalia hali ilivyo kwa tahadhali tu usiku huu wa saa nane na robo baridi ikiwa imekolea kiasi ya kwamba mikono kwa mtu ambaye anakuwa hajavaa gloves anaweza hisi damu haitembei imeganda.

Mstuko wake wa kutoamini kuwa kumbe alikuwa anaviziwa ulimfanya azubae na ashindwe kuepa teke kisu alilopigwa kwa nguvu sehemu za katikati ya suruali, Agent Kai akiwa kavaa viatu aina ya ‘timberland’ au wahuni wanapenda kuita ‘buyu’ aliachia teke kali sehemu za siri (unapopatikana ukoo) za mtu huyu kiasi ya kwamba alizipasua kende (pumbu) zote mbili zilizo ndani ya suruali ya kitambaa kama cha kijeshi kama nilivyoeleza kuwa mavazi ya mwanaume huyu yalifanana na mavazi ya kijeshi.

Maumivu makali yalimfanya mshambuliwa atake kupiga kuinua mdomo wake hili apige kelele lakini haikuwa ndani ya uwezo wake konde zito la mkono wa kushoto wa Agent Kai ‘mkono wa dhahabu’, mkono uliojaliwa nguvu na shabaha, lilitua katika mdomo wake na kumng’oa meno yote ya sebuleni ya chini na juu akaenda chini akiwa tayari fahamu zake za uzima zimemtoka hilo alikujulikana kwa ‘TSC’ alikwenda naye sambamba kwa kasi ile ile alipoona ametua akitulia mgongo guu la kushoto likikunjwa kwa stahili ya ‘nje’ (outer) lilikita eneo la shingo ya mtu na kumvunja shingo uhai wa mtu huyu aliyekuwa akivuta pumzi sekunde mbili tu zilizopita ulipitiwa kwa kasi na yule anayesemekana ni malaika mtoa roho kwa jina lake sifika kuwa ni ‘Israel’.

  “Njooni.. Israel kashafanya yake!” Akaongea ‘TSC’ akiwa kausogeza mkono wake wa kulia wenye saa karibu na mdomo aweze kusikika vizuri akiwaambia wana timu wenzake wanaosubiri kwa upande wa pili juu ya kilima kati ya safu mbalimbali ya milima iliyopo eneo hili lote kwa ujumla.

Sekunde hamsini zijazo wote waliokuwa chini wakitanguliwa na Special Agent Rebecca walifika na kumkuta Agent Kai akiuburuza mwili wa marehemu kuusogeza kichakani.

  “Alipotokea jamaa kwa umbali wa mita hamsini kama sikosei kuna jengo dogo nimeona paa kwa juu.. Upande ule mtaelekea wawili kuchunguza kwenye jengo kuna nini? Ingawa hisia zinaniambia ni jengo la walinzi wa eneo hili.. Silla na Austin muelekee mkikutacho mtatupa taarifa… Miller na Jairo muelekee alipokuwa akielekea marehemu, mimi na Rebecca tunaingia katikati ya shamba hatuna hakika wapi yalipo majengo lakini hatuwezi choka shambani tushafika acha tuvune kinachotustahili.. Nawatakia kazi njema, umakini ndio nguzo yetu na kanuni yetu kuu wai kumuona adui kabla hajakuona” Agent Kai ‘The Sole Cat’ aliongea kimaelekezo akiwa anaangaliana na watu wake wa timu, mdomo wake ukitoa mvuke mzito wa unaonekana vizuri machoni mwa wanaomsikiliza hii ilitokana na baridi kali lililopo.

Kila mmoja alimgeukia mwenzie wakawa wanagonganisha mikono yao ikiwa imekunjwa ngumi zilizo ndani ya gloves mapaka wote wakamaliza kupeana hamasa kila aliyepangwa kuondoka na mwenzie wakaondoka kuelekea walikopangiwa na nahodha wao kukiwa hakuna aliyetoa neno lolote.

Wakiwa wameongozana sambamba na bastola mkononi huku bunduki zao kila mmoja na aina anayovutiwa nayo Special Agent Silla kijana wa kizungu mwenye umri unaokimbilia miaka thelathini na tano pamoja kijana wa ki Guatemala Austin Manuel Contreras wakiwa kwenye tahadhari ya hali ya juu walifika kwenye kijumba kilichojengwa juu ya muinuko mita chache kwa mbele toka inapoanza mikahawa na nyuma yakekukiwa na miti mingi ya matunda kama machungwa, machenza na hata mipapai kisha ya hapo kwa nyuma kuna senyenge inayozunguka eneo lote.

  “Zunguka kwa nyuma mi naenda mbele kabisa kutizama kwa mlangoni kama kuna uwezekano nikaingia ndani” Akanong’ona S.S Silla karibu na sikio la Austin.

  “Sawa..!” Akajibu Austin ikiwa pia kwa kunong’ona ambaye uoga kwake ulikuwepo ila hakutaka kuuonyesha kabisa ikiwa kwa ukweli hajawai nyatia kwa namna kama hii hapo awali katika kazi yake yeye na hata Jairo wao kazi zao ilikuwa ni kumchunguza mtu kwa usiri baada ya kupewa maelekezo na boss wao Kamanda Muniain, lakini si Agent Kai wala wengineo kati ya majasusi toka Marekani waliokuwa wakijua hili wao walijua watu hawa wanaweza kazi ya kufanya chochote kile kinachohitajika kama ilivyo kwa Norman wakati si kweli vijana hawa hawajawai hata kuua mtu katika maisha yao licha ya mafunzo waliyonayo yanayoruhusu wao kufanya hivyo kibinadamu na kikazi inapohitajika ingawa ni kosa na dhambi kubwa kwa muumba wetu.

Austin akinyata kwa hatua ndefu ndefu alisogea akirandana na ukuta mpaka kwenye pekee la nyuma la jengo hili dogo, lilikuwa ni dirisha la kioo cha kusukumwa kilichofungwa katika fremu za alluminium lakini kwa muda huu wa usiku wenye baridi kali la mpaka mtu kujihisi anaweza ganda endapo atakuwa hajavaa nguo maalumu kwa ajili ya kuzuia baridi dirisha lilikuwa si tu limefungwa bali kulikuwa na pazia zito kwa ndani lililozuia kijana huyu Austin ashindwe kuona ndani akabaki ameganda pale pale asijue ana jambo gani analoweza kufanya ukizingatiwa si mzoefu wa michezo hii ya giza.

Special Agent Silla alikwenda akiwa katika tahadhari inayohitajika akapanda juu ya kibaraza akasogea hadi mlangoni ulikuwa ni mlango wa mbao kukiwa na kitasa akaminya kitasa kisha akausukuma mlango akitumia upande wa juu wa bega lake hapo mlango ukagoma kusukumika, ulikuwa umefungwa.

Alitamani azunguke zaidi kuelekea nyuma kama angekuwa peke yake aliyesogea hapa kwenye kijumba hiki lakini hakuwa peke yake huko kwa nyuma alikuwa ameelekezana na mwenzake Austin azunguke huko kuangalia na hata ikiwezekana apite kuingia ndani kupitia huko kama kanuni ya mgawanyo wa kazi hizi za giza a.k.a kazi za kazi, hivyo basi alijisachi kwenye mfuko mmojawa wapo kati ya mifuko mingi ilio katika suruali ya ‘timberland’ aliyovaa moja ya suruali zinazopendwa sana na watu wanaofanya shughuli za kijasusi wanaoenda sehemu za mapambano ikiwa wao hawawezi kuvaa suruali za kijeshi zinazoweza kumfanya mtu mwingine hata wa kawaida kuhisi jambo juu ya vazi hilo licha ya kuwa nchi nyingi za nje ya Afrika ni ruhusa kuvaa mavazi kama haya tena bila wasiwasi lakini usithubutu kuvaa katika baadhi ya nchi za kiafrika.

Sachi yake katika mfuko ule ilimfanya atoke na burungutu la funguo za kijasusi maalumu maarufu kama ‘funguo malaya’ (Master Key) kwa ajili ya kufungua vitasa mbalimbali, akazungusha shingo yake kutizama huku na huko macho yake yakisaidiwa na miwani aliyovaa kisha akarudisha kwenye kilicho mbele yake akainamisha uso wake kusoma aina ya kitasa alipoweza kuona ni kitasa gani? Toka kampuni gani, akarudisha macho yake mkononi mwake alikoshika burungutu la funguo ambapo kidogo tu macho yake yakaiona funguo inayoweza kazi ya kukifungua kitasa kile.

Akaichomeka na kuzungusha mara moja tu ikakubali ikitoa mlio ambao masikio yake yalisikia uzuri mlio ule hivyo akatulia kwanza kupisha umakini zaidi, sekunde ishirini na tano zilimtosha kuwa hasikii kitu kingine zaidi ya vimilio vya wadudu wa porini wanaomudu kucheza cheza kama si kutafuta riziki kwenye giza na baridi kama hili la usiku huu ndani ya eneo la milima ya Tajumulco.

Mkono wake wa kushoto uliminya kitasa taratibu huku bega la upande wa juu likiusukuma mlango kwa tahadhari ya kiwango cha juu, mkono wake wa kulia ukiwa umekamata bastola iliyoinuka na kuwa saizi ya kifua chake tayari kwa matumizi endapo atatokea kiumbe mwenye madhara, mwanga hafifu wa taa ulijitokea katika uwazi wa mlango wakati anausukuma, macho yake ukumbi uliosogea kutoka pale mlangoni mpaka mwisho wake ambako kuna ukuta na dirisha lenye pazia iliyoziba pale dirishani kiasi ya kuwa Silla hakuweza liona dirisha husika zaidi ya pazia tu, haukuwa ukumbi mkubwa ulikuwa ukumbi wa mita kumi na mbili kimakadirio aliyoweza kuyakadiria mvamizi huyu na pia kulikuwa hamna chochote ukumbini hapa zaidi ya kuta huku na huku (kushoto na kulia).

S.S Silla akausukuma mlango ukasogea nusu kisha akapita na kuingia ndani akivuka kizingiti kisha akaubugadha (kuurudisha) mlango akiusukuma kwa mgongo taratibu kuhakikisha hautoi mlio wa juu wa ‘kwiiiiii iiii’ kwakuwa ulikuwa ni kawaida kutoa mlio huo kutokana bawaba zake zilikuwa kavu sana hili Silla alilijua wakati anausukuma punde tu alipoufungua, macho ya jasusi huyu wa DEA yaliweza kuona upande wa kushoto mlango wa kwanza katika safu iliyofuatiwa na mlango mwingine baada yamita kadhaa na upande wa kulia wa ukuta nao ulikuwa na milango miwili kama iliyo kushoto.

Sekunde ishirini za utulivu na kufikiri zilimalizika kwa kupiga hatua ya kwanza kusonga mbele, alipotupa ya pili mtu anayekohoa alisikika akikohoa kutokea chumba cha kwanza akikohoa mara mbili zinazofuatana, hii ikamjuza jasusi kuwa chumba cha kwanza upande wa kulia kwake kuna mtu mwenye ugonjwa kifua hivyo anatakiwa kwanza adili naye lakini akili mwake akapata wazo lingine hili likija baada ya kuwa ametizama saa yake ya mkononi iliyomjuza kuwa ni dakika kumi na tano sasa toka waachane na kina Agent Kai.

Akaandika meseji kwenda kwa Agent Kai akimuomba afanye kitu fulani kisha akasubiri jibu ambalo halikuchelewa alijibiwa vile anavyohitaji yeye kuwa afanye tu.

Begi lake la mgongoni liliamia mbele haraka akililieta kwa kasi kwa mkono wake kulia kisha ya hapo akafungua zipu na kutoa mabomu madogo ukubwa wa kama chaji za ‘laptop’ ni madogo lakini yana uwezo mkubwa wa kulipua nyumba kubwa tu kama yatategwa mahala pazuri, kidume cha kizungu kikanasisha ukutani kwa juu kidogo ya mlango wa chumba cha kwanza upande wa kulia kisha akanyata kusonga mbele mpaka mwisho kabisa wa korido kuliko na chumba cha pili na cha mwisho nako akanasisha bomu juu ya ukuta, bomu ya kufyatuka kwa rimoti, alipohakikisha kila kitu kiko sawa hakusubiri zaidi akanyata kutoka nje akiufunga mlango kwa ufunguo kama alivyoukuta.

  “Austin! Austin.. Huko wapi?” Akaongea mkono wake wenye saa ukiwa umesogea karibu na mdomo.

 “Niko huku kuna mlinzi nilikuwa namvizia nimeshamminya.. Wewe huko wapi?” Akajibu na kuuliza ikiwa amedanganya si kweli kuwa alikuwa amekutana na mlinzi wa kumvizia huko nyuma lakini Silla alimuamini tu.

  “Njoo mbele ya nyumba.. Tutapita kwa mtindo wa yai” Akamalizia kwa kuelekeza Special Agent Silla.

Austin akaja alikoitwa akiwa na hofu anayojitahidi kuificha isionekane kwa Silla wakati akimsogelea ‘team mate’ (timu moja) wake katika mgawanyo wa majukumu yao.

   “Ni kweli hiki kimjengo ni kimjengo cha walinzi kupumzika, sasa sielewi kama ni walinzi wote wa eneo hili ama ni vipi.. Nimeingia ndani kuna vyumba vine na wote waliomo wamelala kama ujuavyo saa nane inayokaribia saa tisa hii kikawaida binadamu muda kama huu usingizi totoro hata wachawi ufanya kazi zao mida kama hii na sisi majasusi tulio wabobezi mida hii ndiyo mida yetu, nimetegesha mabomu mawili ndani ya kufyatua kwa rimoti… Vipi na wewe huko ulipotoka?” Alitoa maelezo Silla baada ya Austin kumfikia.

  “Kama nilivyokueleza nilimkuta mlinzi mmoja anavuta bangi huko, naona aliona kuvutia ndani itawakera wenzake ndiyo maana akawa anavutia huko nyuma nashukuru nimemdhibiti na kumficha vichakani, tunaendelea mbele?” Akajibu na kuuliza.

  “Ndiyo ila ngoja tuwaulize na wenzetu kina Miller wanakopita kukoje?” Akajibu na kuelekeza nini anataka kufanya kwenye simu saa yake, alikuwa akitafuta ‘code number’ anazotumia Miller katika mfumo wao mdogo wa mawasiliano katika timu yao.

   “… Halloo Miller!” Akauliza baada ya upande wa pili kuruhusu waongee.

   “Naam… Nilipo hali ni shwari kuna kimjengo kama tulichokiona huko mkajongea kutizama ndani kuna nini? Nafikiri mambo yameenda sawia?”

   “Naam! Yameenda sawia kabisa nilikuta wote wamelala hivyo nimetega mabomu mawili na kwa sasa tunaelekea kunakoonekana taa za mjengo mwingine.. Vipi na wewe salama?”

   “Ni kama tumeelekezana sisi tumedhibiti walinzi wawili tuliwakuta wanavuta sigaa huku wanaota moto karibu na jengo dogo linalofanana na hilo la huko, pia nasi tumetega mabomu kama matatu hivi hatukuingia ndani baada ya kuwamaliza walinzi tuliowaona hatukuona haja ya kuingia ndani na kwa sasa tuko karibu na geti kuna kibanda kidogo cha walinzi wa getini pia kuna mnara wa watch tower kwenye kona ya barabara kote kuko kimya yaonyesha hakuna aliye macho hivyo tunataka kutumia fursa hii kutega mabomu getini, kibanda cha walinzi na kwenye miguu ya watch tower”

   “Kazi nzuri sana… Ndani ya lisaa limoja mbele patakuwa na patashika eneo lote moto kuwaka kama jehanamu ndogo, niwatakie kazi njema sisi pia tukilifikia lile jengo ni mwendo wa kupachika milipuko tu..!”

  “Kazi njema na nyinyi pia” Walimalizia kihivi maafisa wa DEA hawa walio wabobezi wakubwa licha ya umri kutofika miaka arobaini lakini kiukweli ofisi ya DEA inajivunia sana watu hawa wa kazi.

Jengo linalofuata Special Agent Silla na mshirika wake anayemuongoza walifika na kulizunguka kiukaguzi wa nje bila kuingia ndani walichungulia madirishani lilikuwa ni jengo lenye kuhifadhi zana za kilimo ikiwa kama stoo ya kuhifadhi vitendea kazi hivi kwa ajili ya wafanyakazi wanalo lihudumia shamba hili la mikahawa.

Kama ilivyo katika maelekezo yao bila kujali kama na wao wanaweza ingia matatizoni walipachika mabomu katika kuta zake kisha yakawa unganishi na rimoti katika mfumo mmoja na yale ya jengo walilolala walinzi, walipomaliza wakasonga mbele kwa matumaini na bashaha tele katika baridi kali linalomwaga mambo yake kana kwamba limeambiwa kesho ni kiama chake alitakuwepo tena duniani.

Ujumbe ukatumwa kwa nahodha wa timu kuwa upande huu majengo yanayopatikana huku tayai yamepachikwa mabomu na wao wanasonga mbele kutafuta kama kuna kingine cha kutega milipuko hii isiyo na huruma pale inapokushambulia ukiwa umeingia kwenye anga zake barabara.

Upande wao Investigator miller na kijana wa kiguatemala Jairo wa OCLA walifanikisha adhima yao ya kutega milipuko katika sehemu walizokubaliana kuwa watatega milipuko baada ya kuwavizia mbwa watano waliolala karibu na kibanda cha mlinzi kulikokuwa kumewashwa moto kupunguza makali ya baridi, raha ya moto ni utamu uliowafanya kusahau majukumu yao walichapwa risasi wote watano hakuna aliyeweza kuinua hata pua yake kunusa harufu ya damu ya mwenzake umauti wenye roho ya kikatili ulichukua chake, cctv kamera za hapa ziliweza kuchukua matukio ya wageni hawa vizuri tu lakini waliokuwa katika kazi ya kufuatilia matukio ya cctv kamera muda huu walikuwa ndani ya blanketi nzito wana koroma bila kujali kama wanaokuwa zamu katika chumba hiki hawaruhusiwi kulala wala kusinzia ndiyo maana wana shift (mabadilishano ya kazi).

Baada ya kazi ya kuwaua mbwa kupata mafanikio ilifika zamu ya walinzi na wao wakaogelea katika bwawa la mauti kwa mikito ya visu vyenye ncha kali ambao na wao mpaka wanaingiliwa katika banda na kina Miller joto joto la moto wa kuni uliogeuka kuwa mkaa waliouwasha liliwafanya kujisahau kama wajibu wao ni kulinda getini na maeneo ya jirani na getini hakuna mtu kuingia, walikuwa watatu walikufa usingizini wakiwa wamejifunika gubigubi.

Mwisho wa sehemu ya themanini na sita (86)

Timu ya kazi iko ‘site’ ni mwendo wa kutega milipuko ya mabomu katika sehemu muhimu za kiulinzi wa pembeni.

Tusile muda zaidi twende kazi katika sehemu zinazofuata tumalize malize dodo asali na nondo za mapigo 




Kama ilivyo katika maelekezo yao bila kujali kama na wao wanaweza ingia matatizoni walipachika mabomu katika kuta zake kisha yakawa unganishi na rimoti katika mfumo mmoja na yale ya jengo walilolala walinzi, walipomaliza wakasonga mbele kwa matumaini na bashaha tele katika baridi kali linalomwaga mambo yake kana kwamba limeambiwa kesho ni kiama chake alitakuwepo tena duniani.

Ujumbe ukatumwa kwa nahodha wa timu kuwa upande huu majengo yanayopatikana huku tayai yamepachikwa mabomu na wao wanasonga mbele kutafuta kama kuna kingine cha kutega milipuko hii isiyo na huruma pale inapokushambulia ukiwa umeingia kwenye anga zake barabara.

Upande wao Investigator miller na kijana wa kiguatemala Jairo wa OCLA walifanikisha adhima yao ya kutega milipuko katika sehemu walizokubaliana kuwa watatega milipuko baada ya kuwavizia mbwa watano waliolala karibu na kibanda cha mlinzi kulikokuwa kumewashwa moto kupunguza makali ya baridi, raha ya moto ni utamu uliowafanya kusahau majukumu yao walichapwa risasi wote watano hakuna aliyeweza kuinua hata pua yake kunusa harufu ya damu ya mwenzake umauti wenye roho ya kikatili ulichukua chake, cctv kamera za hapa ziliweza kuchukua matukio ya wageni hawa vizuri tu lakini waliokuwa katika kazi ya kufuatilia matukio ya cctv kamera muda huu walikuwa ndani ya blanketi nzito wana koroma bila kujali kama wanaokuwa zamu katika chumba hiki hawaruhusiwi kulala wala kusinzia ndiyo maana wana shift (mabadilishano ya kazi).

Baada ya kazi ya kuwaua mbwa kupata mafanikio ilifika zamu ya walinzi na wao wakaogelea katika bwawa la mauti kwa mikito ya visu vyenye ncha kali ambao na wao mpaka wanaingiliwa katika banda na kina Miller joto joto la moto wa kuni uliogeuka kuwa mkaa waliouwasha liliwafanya kujisahau kama wajibu wao ni kulinda getini na maeneo ya jirani na getini hakuna mtu kuingia, walikuwa watatu walikufa usingizini wakiwa wamejifunika gubigubi.

ENDELEA NA NA MAPIGO…!

BUTWAA III

SAN MARCOS-GUATEMALA

Agent Kai na Special Agent Rebecca walipita wakifuatisha njia ndogo nyembamba zinazoonekana ndiyo njia ambazo zinatumiwa na watu wanaopitaga maeneo haya ya shamba, walitembea eneo la urefu wa heka mbili ndipo kwa mbali mbele kabisa ya shamba kupita mikahawa mingi ndipo taa za majengo zilianza kuonekana.

   “Tumeanza kuziona taa za majengo nayohisi ndiyo majengo ya ofisi… Kama nilivyoelekeza kwa meseji tanueni mpaka kando kando kabisa ya shamba kisha mtapita kufuata urefu wa umbo la yai naamini mtaanza kuziona taa za majengo kama haya tunayoyaona sisi kama bado hamjayaona.. Kazi njema” Maelekezo ya kazi yalitoka kwa Agent Kai akiwaelekeza Silla na Austin pamoja na Miller aliyeongozana na Jairo ambao hajaongozana nao yeye ‘TSC’.

Ukubwa wa shamba kwa upande huu kwenda kwenye majengo ulikuwa ni mkubwa wa heka tano eneo hili likiwa na mikahawa ya kutosha kwa kweli shamba lilikuwa kubwa na lenye zao hili la kahawa lenye afya kama zote vile hii ilidhihirisha huduma ilikuwa makini sana kwa wahudumu wa shamba hili na hata boss wao alionyesha kujali haswa shamba lake.

ikiwa wamebaki mita zipatazo kama themanini kukaribia unapoonekana mjengo wa kwanza huku pia kukiwa na majengo mengine kadhaa kwa nyuma na hata kando yake Special Agent Rebecca aliyekuwa anatangulia mbele zaidi kuliko Agent Kai aliyekuwa naye anakwenda kwa mwendo fanana na mshirika wake lakini hakuwa anaacha kutizama kila pahali kila hatua wanayosogea mbele, alisimama na kuinama chini kwa haraka kuwa sawa na mmoja wa mmea wa zao la kahawa kisha taratibu akajisogeza pembeni hili aweze kujificha zaidi na ishara ya mkono wake wa kushoto iliwekwa kumtambulisha aliye nyuma yake kuwa kuna jambo, Agent Kai naye hakuzubaa aliruka akiwa kainama mpaka mahala alipoona ni sahihi kufanya kama aliye mbele yake alivyofanya.

  “Kuna kamera za cctv kuanzia kwenye nguzo ile inayoonekana pale yalipo maua… Pia kuna mbwa wengi wamekaa mbele kidogo ya nguzo zilizojipanga ambazo nafikiri uwa zinawekwa bendera kunapopambazuka kwa sauti ndogo inayokaribia kunong’ona aliongea Rebecca kumwambia Agent Kai aliyekuwa anainua shingo yake hili kichwa kinachomiliki eneo la macho yake aweze kuona mwenyewe.

   “Swadakta! Nimeona kazi ipo.. Wapo wengi kweli na si wapo eneo lile tu inaonekana wako eneo lote la mbele ya yale majengo na kulala kwao pale si kama wamelala wapo wengine wako macho kabisa ila wamekaa tu kujikunyata baridi hili ambalo si saizi yao..!” Agent Kai akasema kwa kunong’ona kisha akajiinua kidogo toka alivyo amepiga goti moja chini akavuka kwenda upande alipo Rebecca.

  “Mariana Caro Funtes anasema nyuma ya majengo haya ya mbele kuna kiwanda kidogo cha kuchakata kahawa kisha ukisogea kusini ya kiwanda kuna maghala ya kuhifadhi kahawa iliyotoka kuvunwa na ndipo ndani yake kuna mfuniko wa kuelekea kwenye handaki lenye kuleta maana ya Tajumulco Camp” Rebecca akaongea wakiwa wamesogeleana na boss wake sambamba kabisa.

  “Nimeanza kuamini kila kitu alichotuambia ila hakusema kama kuna mi mbwa mingi namna hii” Akaongea Kai akiendelea kuinua shingo yake juu juu aweze kuona kwingine na kwingine.

  “Lakini alitahadharisha kuwa kuna ulinzi ulio makini sana ambao kama unataka kuja kuvamia hapa unatakiwa uombe bahati ilale sana kwako ndiyo utafanikiwa kufika kwenye ghala lenye mfuniko wa handaki.. Tuwape taarifa kina Silla na pia tujue mpaka sasa wamekutana na nini na wao” S.S Rebecca akaongea kisha wakatizamana na boss wake wote wakatabasamu hii ilizoeleka sana kwao wanapokuwa sehemu yenye changamoto kupeana morali wanapotizama kwa kutabasamu.

   “Sawa! Ila nafikiri tuachane na njia hii tuingie kwenye vitalu tutatakiwa tutambae..!” ‘TSC’ akaongea na kumgonga kwa kiganja mgongoni swahiba wake, wakatizamana tena wakiwa bado wanatabasamu.

  “Pamoja sana boss.. Twende tu!”

  “Ndiyo ndiyo.. Silla na mwenzake na Miller na mwenzake kama wana mkwamo watatujulisha kilicho mbele yetu ni kuyafikia majengo kutega milipuko na kuingia kwenye ghala tuliloelekezwa huko chini ndiyo kila kitu katika shamba hili la kahawa” Akaongea tena ‘TSC’ sasa akiwa anajilaza chini ardhini kifudi fudi.

Safari ya kutambaa kwa tumbo ikaongozwa na mwenyewe Agent Kai akifuatiwa kwa pembeni yake na S.S Rebecca, ilikuwa wanakwenda mbele lakini wanatanua zaidi mpaka walipokaribia eneo lenye maua yaliyopandwa vizuri kwa mpangilio maalumu yakiwa yamejengewa eneo la kuishia kwake kisha mbele yake kuna barabara iliyotiwa lami inayotenganisha upande huu wa shamba na upande wa majengo, eneo lilikuwa linavutia sana kukiwa na mwanga mkali wa mataa makubwa yaliyo kwenye majengo na manguzo ya barabarani unaofanya kuwe kweupe kama mchana hadi eneo walilo ‘TSC’ na mshirika wake wakiwa wamelala chini hatua chache kutoka mwisho wa shamba kwenda yalipoanza maua.

  “Nilisema hawa mbwa wapo mpaka huku na tayari kama wanahisi kuna kitu kigeni..!” Aliongea Agent Kai wakiwa wamelala chini ardhini kwa pamoja wakitegemea vivuli vya miti ya mikahawa ya mwanzo kuendea barabarani.

  “Ndiyo! upepo ukipuliza kuelekea upande ule wale wa upande ule wanainua vichwa vyao kumaanisha wanaijiwa na harufu ya tofauti ila kuna mkanganyiko na haya maua na hili kudhibiti hili nina wazo boss” Special Agent Rebecca aliongea akimtizama Agent Kai aliyeweka umakini kumsikiliza ikiwa hamuangalii anazungusha akili nini kifanyike hapa.

  “Sema tu! Naamini litatusaidia”

  “Kushoto kwako kuna mti wa mpira tuutumie kuzipaka nguo zetu kuweka harufu tofauti kwa mbwa hawa wakishaacha kusikia harufu hii inayowachanganya wataendelea kuupiga usingizi sisi tutafanya yetu bila kuwagusa kwakuwa hatutaweza fanya lolote kwa uwingi wao… Yaani wajinga wanafuga mbwa wengi kama wanafuga mbuzi..!” Aliongea Rebecca kisha hakungoja tamko la kuungwa mkono toka mdomoni mwa Agent Kai ajiviringisha akamruka kwa kasi akipita juu ya mgongo mpaka kwenye mti aliosema na tayari mkononi alikuwa na kisu akaanza kukata magamba ya mti utomvu ukaanza kumwagika kwa kasi hapo naye akaanza kuukinga kiganjani kisha anampaka boss wake.

Kazi iliwalia dakika tano nzima hapa mpaka walipokuwa wananukia kiutomvu wa mpira na ni kweli mbwa wale waliokuwa wakiinua pua zao kuweza kupata harufu vizuri wakarrudisha vichwa vyao kuvilaza kwenye sakafu.

  “Aisee! Weee mwanamke ni genius.. Sijui hata ulijifunza wapi njia hii?” Tabasamu zito toka usoni mwa Kai lilifanya wote watabasamu na kukumbatiana wakiwa wamelala ardhini vile vile bila kujali hawako sehemu salama.

  “Boss! Umejisahau kuwa kuna cctv kamera pia..!”Akanong’ona Rebecca sikioni kwa boss wake na habari hii ya tahadhari ilikuwa muhimu lakini kunong’onezwa na kuwa amemisi mambo Fulani ilimfanya mwanaume huyu kusisimkwa lakini heshima yake kwa mwanamke huyu ilikuwa ya kiwango kikubwa sana akapuuzia tamanio lake la kupata hata ‘deep kiss’.

Meseji iliingia kwenye simu saa yake wakaachiana kisha akaifungua meseji kuisoma ilikuwa ni ujumbe toka kwa Silla akielekeza kuwa na wao sasa wameanza kuyaona majengo baada ya safari ya dakika kadhaa wakitembea kwa kujificha ficha ikiwemo na kutega milipuko sehemu mbalimbali, Agent Kai akatumia fursa hio kumuelekeza hali ilivyo na wapi wao wamekwama na ni hatua gani inafuata, hakuishia hapo alimtafuta na Miller kwa meseji akamjuslisha kile alichomjulisha Silla na pia Mller alimjulisha na wao wako wapi sasa wanavyochati na kuwa wametega milipuko sehemu zote muhimu za ulinzi wa pembeni ikiwemo getini wako wapi na pia akashauri kule Silla alikotega milipuko alipue nay eye atalipua walikotega hili kuifanya kambi iwe na taharuki ndipo wanaweza kufanikiwa kufika kwenye ghala. Agent Kai alikubali wakaamua iwe vita sasa kila mmoja ashike bunduki ajiweke tayari kwa mashambulizi.

   “Jamaa zetu wameshafanya kazi nzuri sana washatega milipuko sehemu za majengo ya pembeni ikiwemo na getini wametega milipuko…Tumekubaliana miili iwe tayari kwa mapambano toa mabomu ya mkononi ikishatokea milipuko kule sisi huku tutasubiri kuona wanakotokea watu wanaoilinda hii kambi wakitokea tutaanza na mabomu ya kutupa tutatupa kwa mbwa hadi kwa watu wowote wale kisha ya hapo ni risasi tu kwa kwenda mbele” Akanong’ona ‘TSC’ macho yakizunguka haraka huku na huko kama anajisaidia haja kubwa porini anaogopa kufumwa.

Mara mpango uliitika milio miwili ya milipuko ya kufuatana ikiachiana sekunde tatu tu ilisikika ukifuatiwa na mwanga mkubwa wa moto kutokea kule yalikotegwa mabomu ya kulipuka kwa rimoti za kilipuzi na Silla sekunde kumi na tano mbele upande wa kule walikotega Miller na Jairo nako kulijibu ikiwa ni milipuko mizito na ya kufuatana ikifuatishwa na milio ya vitu vilivyo sambaratishwa ikwemo kelele za mbwa na watu walioathirika na milipuko lakini uhai wao ulikuwa bado unapigana kugoma kutoka miilini mwao.

  “Tayari kumeitika!” S.S Rebecca akaongea na kisha akafuatisha kitendo kilichofanywa na Kai aliyejiinua na kuchuchumaa, mbele yao mbwa wote waliokuwa wanajikunyata baridi waliinuka na mara jengo la mbele kikaanza kusikika king’ora cha taarifa za hatari kikilia mfululizo mlio wa ‘tiiiii tiiiii tiiiiii’ bila kuacha sekunde thelathini mbele vikasikika vishindo vya watu wanaokimbia kutokea pembezoni mwa jengo ambalo Agent Kai na Rebecca wanaliangalia kwa mbele likiwa ni jengo la ghorofa mbili juu kabisa kukiwa na maandishi makubwa ‘ALEXIS COFFEES FARM’S & INDUSTRY’.

Mbwa walikuwa wanakimbia kimbia tu kwa kupishana hawana muongozo maalumu kuwa waende wapi, ikasikika milio ya magari inatokea kule kule ambako vilisikika vishindo vya watu pia wakiongea kwa bila mpangilio ikawa makelele sasa huku milango ya magari inafunguliwa kwa fujo kisha inafungwa kwa kubamizwa halafu gari la kwanza likatokeza kutokea upande ambao sasa majasusi hawa walikuwa makini kuangalia kuona nini kitatokea.

Gari ilipotokea wakaishuhudia ikiwa ni aina ya Jeep iliyo wazi juu na watu ikafuata ingine kama hii iliyotangulia nayo ikiwa na watu ndani nyuso zao zikiwa na taharuki kubwa sana kwa kila mmoja wao na kuonyesha walikurupuka toka usingizini wengi wao walikuwa hawajavaa viatu walikuwa pekupeku.

  “Shambuliaaa..!” Akaongea kwa kunong’ona Agent Kai akimnong’oneza Rebecca kisha wote kila wakarusha bomu la kutupwa na mkono maarufu kwa jina la uswahilini ‘kiazi’, wakigawana kwa kila mmoja gari yake, mlipuko mwingine mzito ukasikika wa magari yakiambatana na makelele ya watu waliokuwa juu ya gari hizi na tena yakirushwa juu na kufanya wapandaji na dreva wao na wao kurushwa huku wengine wakiwa wamekatwa shingo, viwili mpaka wanatua hakuna aliyekuwa hai zilitapakaa maiti chini za watu kama kumi na sita na maiti zingine za mbwa waliokuwa wakijifanya na wao wanataka kuongozana na magari haya iliposikika milio ya milipuko.

  “Rusha tena kwa mbwa kisha tukimbie kutoka hapa tulipo wewe utaendea kushoto kwako mimi kulia” Akaelekeza ‘TSC’ kisha wakaangaliana wakatoa kilimi cha bomu kila mmoja akiwa kalishika na kilimi wakitoa kwa kuking’ata kwa meno kisha wakarusha mabomu kuelekea walipo mbwa ambao walikuwa wako kwenye taharuki wanabweka wakiwa hawajui wanambwekea nani?

Wako waliojeruhiwa na kuwafanya kuwa wapole ghafla hawabweki wananung’unia maumivu chini na wapo waliokufa papo hapo na wengine wakifa kwa kupishana muda kutokana na muathiriko wa bomu za kurushwa.

Kama ‘movie fulani vile’ majasusi wa CIA hawa wanaopendana sana katika safari za kazi waliruka juu toka vichakani kulipo na mikahawa wakiyaruka maua wakatua chini kwa mgongo kifundi zaidi mafundi hawa kwenye barabara ya lami waliyokuwa wakiiona tokea vichakani na wote kubingirika kama tairi la gari linapotembea kwenda mbele, kichwa kikitua unafuata mgongo nao unazunguka kufuatisha uti wa mgongo yanakuja makalio nayo yanapita kasi inatua miguu (sinema tamu) ilitia raha kushuhudia majasusi hawa tena wakienda kasi kila mmoja na upande wake walipokuja kusimama napo walisimama kana kwamba wanatumia ubongo mmoja, kuna baadhi ya mbwa waliopona katika mashambulizi ya mabomu pamoja na ukali wao wa kimafunzo macho yenye kuona ‘black n white’  kushuhudia viumbe vinabingirika kwa kasi kama tairi ilikuwa ni miujiza kwao walikimbia mbio mikia wakiwa wameifyata kuokoa maisha yao hakuna kubweka ni visauti vya kutaka huruma ndivyo vilivyosikika miongoni mwao wakielekea kwa kasi kusikojulikana.

‘TSC’ aliposimama tu akakutanisha macho ya ana kwa ana mita kama kumi tu toka alipo na watu wa kazi wenye bunduki mikononi mwao wakiwa na wao wanakimbia kuja kona washuhudie kunani? Kusimama kwa ‘TSC’ kwa ghafla toka katika hali ya kuwa anavingirika kama tairi na ghafla kuwa mrefu iliwafanya wapigwe na butwaa.

Bunduki iliyoko mikononi mwake tayai ilikuwa ishasetiwa kwa matumiz akakoki kisha akamwaga risasi kama njugu kuwaelekea wale watu walio katika hali ya kutoka usingizini kama nilivyoeleza wengi hata viatu hawakuvaa, ‘TSC’ alidondosha chini mmoja mmoja kwa wingi wao huku akikimbia upande kuelekea kwenye ukuta wa jengo lingine hili ajizibe maana walikuwa wemgi pale licha ya kudondosha wengi sasa nay eye alianza kushambuliwa ikawa shukrani kwa bulletproof alilovaa ndani na jamaa kutolenga kichwa chake, risasi tano zilitua mwilini mwake mbili kifuani eneo ambalo kama ingepenya basi moyo wake ungeharibiwa vibaya na tatu zikipiga eneo la tumboni wakati anakimbia kiupande upande huku anashambulia.

Special Agent Rebecca kuona majibizano ya risasi yameshika kasi alikwenda hadi kwenye kona ya ukuta akachungulia eneo zinapotoka risasi anazoshambuliwa ‘TSC’ , ndipo macho yake yakashuhudia miili kadhaa ikiwa imelala katika madimbwi ya damu zinazozidi kutoka katika miili hiyo hiyo na kufanya harufu ya damu za binadamu imfikie hadi alipo kama ujuavyo watu hawa wamezoea kusikia harufu za damu mara kwa mara.

Akiwa pale kwa uzuri kabisa aliwaona watu wengine wake kwa waume wengi wao wakiwa ni wenye tattoo hadi usoni mwao ingawa kwa baridi hili la usiku wote walivaa masweta na majaketi mazito, wakiwa wanatoka na ngao zinazotumiwa mara nyingi na mapolisi wanaotuliza ghasia na pia kuzuia waandamanaji wanaondamana kupinga au kutaka kitu flani, akili zao wote zilikuwa kule alipokimbilia Agent Kai, walikuwa wanatoka wanapiga goti moja chini lingine linakunjwa tu ngao zikiwekwa mbele yao huku wawili wa mbele zaidi kati yao walishika silaha aina ya ‘Rocket-Propelled Grenade’ (RPG), kuona silaha hizi za kilipuzi kulimstua Rebecca haraka alitoa bomu moja la kurushwa toka kwenye mfuko wa kati wa suruali aliyovaa akang’ata kipini akakivuta kisha akatokeza mwili wake kwa kasi toka alipojificha akalirusha kwa nguvu kuelekea kule akilenga safu ya mbele ya watu walio na ‘RPG’.

Mwisho wa sehemu ya themanini na saba (87)

Mashambulizi ya kushtukiza toka kwa timu inayoongozwa na Agent Kai iliwachanganya sana wafuasi wa genge la ‘THE RED JAGUAR’ waliokuwa wamelala wakiamini hakuna baya linaloweza kuwakuta muda wa saa nane kwenda tisa usiku kutokana na hali hewa nzito yenye ubaridi mkali sana eneo la Tajumulco licha ya maboss zao kuwasisitiza kuwa dalili za kambi yao kuvamiwa ni kubwa sana, kukiwa ni msimu wa baridi katika nchi nzima ya Guatemala na nchi zingine za jirani zenye sifa ya hali hii ya hewa si rahisi kwa mtu au watu kuvumilia kuwa nje eneo kama hili na sasa ndiyo wamevamiwa na haina budi kupambana au kujisalimisha kwa wavamizi wao.

Dozi zinaendelea kumwagwa kwa vijana hawa walio na butwaa!

nini kitafuata sehemu ijayo?




‘TSC’ aliposimama tu akakutanisha macho ya ana kwa ana mita kama kumi tu toka alipo na watu wa kazi wenye bunduki mikononi mwao wakiwa na wao wanakimbia kuja kona washuhudie kunani? Kusimama kwa ‘TSC’ kwa ghafla toka katika hali ya kuwa anavingirika kama tairi na ghafla kuwa mrefu iliwafanya wapigwe na butwaa.

Bunduki iliyoko mikononi mwake tayai ilikuwa ishasetiwa kwa matumiz akakoki kisha akamwaga risasi kama njugu kuwaelekea wale watu walio katika hali ya kutoka usingizini kama nilivyoeleza wengi hata viatu hawakuvaa, ‘TSC’ alidondosha chini mmoja mmoja kwa wingi wao huku akikimbia upande kuelekea kwenye ukuta wa jengo lingine hili ajizibe maana walikuwa wemgi pale licha ya kudondosha wengi sasa nay eye alianza kushambuliwa ikawa shukrani kwa bulletproof alilovaa ndani na jamaa kutolenga kichwa chake, risasi tano zilitua mwilini mwake mbili kifuani eneo ambalo kama ingepenya basi moyo wake ungeharibiwa vibaya na tatu zikipiga eneo la tumboni wakati anakimbia kiupande upande huku anashambulia.

Special Agent Rebecca kuona majibizano ya risasi yameshika kasi alikwenda hadi kwenye kona ya ukuta akachungulia eneo zinapotoka risasi anazoshambuliwa ‘TSC’ , ndipo macho yake yakashuhudia miili kadhaa ikiwa imelala katika madimbwi ya damu zinazozidi kutoka katika miili hiyo hiyo na kufanya harufu ya damu za binadamu imfikie hadi alipo kama ujuavyo watu hawa wamezoea kusikia harufu za damu mara kwa mara.

Akiwa pale kwa uzuri kabisa aliwaona watu wengine wake kwa waume wengi wao wakiwa ni wenye tattoo hadi usoni mwao ingawa kwa baridi hili la usiku wote walivaa masweta na majaketi mazito, wakiwa wanatoka na ngao zinazotumiwa mara nyingi na mapolisi wanaotuliza ghasia na pia kuzuia waandamanaji wanaondamana kupinga au kutaka kitu flani, akili zao wote zilikuwa kule alipokimbilia Agent Kai, walikuwa wanatoka wanapiga goti moja chini lingine linakunjwa tu ngao zikiwekwa mbele yao huku wawili wa mbele zaidi kati yao walishika silaha aina ya ‘Rocket-Propelled Grenade’ (RPG), kuona silaha hizi za kilipuzi kulimstua Rebecca haraka alitoa bomu moja la kurushwa toka kwenye mfuko wa kati wa suruali aliyovaa akang’ata kipini akakivuta kisha akatokeza mwili wake kwa kasi toka alipojificha akalirusha kwa nguvu kuelekea kule akilenga safu ya mbele ya watu walio na ‘RPG’.

ENDELEA NA MAPIGO..!!

BUTWAA IV

SAN MARCOS-GUATEMALA

Bomu halikuacha salama safu yote ya mbele iliteketea kwa bomu moja tu ukizingatia walikuwa wameshika vitu vinavyolipuka, mbele tu kulikuwa na watu wapatao sita wakiwa wanapiga hesabu ya kushambulia alipo Kai, waliobaki waliokuwa safu ya mwisho walikimbilia ndani kwa kasi kunakoonekana ni ghala la kuhifadhi kama si mazao au kingine chochote ka jinsi kulivyojengwa.

Kai alipokuwa alikuwa akimuona Rebecca vizuri na pia Rebecca alikuwa akimuona wakapeana alama ya dole gumba kuonyesha kazi nzuri imefanyika, upande wa barabara inayojia huku alionekana Miller akija kwa kujificha katika nguzo za majengo yanayoonekana ni ofisi na alikuwa amemuona S.S Rebecca ikabidi apige mluzi unaofahamika kwao wote hili asishambuliwe akiwa hajui Agent Kai alishamuona na akamuonyesha ishara Reb ecca aangalie nyuma kuna mtu na kwakuwa ulipigwa mluzi anaouelewa aligeuka bila wasiwasi akitambua anayekuja ni ndugu yake akakutana na uso wa Miller nyuma yake akiwepo mshirika wake Jairo.

   “..Mko wapi Silla?” Akauliza Agent Kai akiwa amesogeza mkono wake wenye simu saa karibu na mdomo wake hili aweze kuongea bia tatizo ikiwa ameruhusu kuongea.

  “Tunatokea kwenye kona ya kujia barabarani tumeona mlipuko wa bomu kutokea kwa mbele ya ghala.. Na nyie mko wapi?”

  “Kwenye majengo ya mbele ya ghala mnalosema mmeona mlipuko kuna wateja wetu kwa ndani ya ghala hivyo nyie zungukeni kwa nyuma ya hili jengo kuona kama mnaweza kuingiaje ndani wakati sisi tunajaribu kulazimisha kwa mbele..!!”

  “Sawa tunafanya hivyo ila huyu niliyenaye na wasiwasi si mzoefu au ana uoga flani hivyo kama Miller anaweza kuja nikaenda naye ni vizuri kama mko naye hapo muombeni hivyo nyinyi mtakuwa na hawa wawili”

   “Sawa nafanya hivyo..!”

Vitufe vya kukata vikabonyezwa kwa pande zote kwa kutumia ishara tu bila kuongea kitu kwa mdomo Agent Kai alielekeza kitu kwa kina Rebecca na wote wakaelewana na kukubaliana.

Fundi ‘TSC’ akatoa bomu la kutupa (kiazi) toka kwenye moja ya mifuko yake ya katikati katika suruali yake, akaonyesha ishara ingine kwa kina Miller ambayo nayo ilieleweka hapo mtaalamu akatoa ‘lock’ ya bomu kisha akalirusha kwa nguvu kuelekea kwenye lango kuu la ghala lilipofika na kulipuka likiwa limekwaa kisiki kwakuwa lango lilikuwa limefungwa kwa ndani na ni lango la bati ngumu na chuma hivyo hakukuwa na athari zaidi ya mlio wa kustua wakati mlipuko unatoka kwa mbio za kasi Miller alikatiza kutoka upande walipo na Rebecca kwenda alipo Agent Kai na kufanikiwa kufika salama bila shambulizi lolote toka kule kwenye ghala ikawa mbinu aliyopanga ‘TSC’ imefanikiwa, wakati Miller akifanya hivyo kwa mbio zake na Rebecca alimshika mkono Jairo wakatokea toka walipojificha kwa kasi wao hawakwenda mbele bali walifuata ukuta unavyokwenda mbio zilizowafikisha karibu na lango la ghala wakajiweka pembeni  wakiinama karibu na lango kuu kukiwa moshi na moto wa bomu lililotupwa vinamalizika malizika kitu hiki hata Agent Kai hakuwa amemuelekeza ila moyoni alifurahi kujiongeza kwa mwanadada huyu akausifu moyo wake wa imani kubwa aliyonayo kwa binti huyu wa kizungu.

   “Nimehitaji u..!” Alitaka kuongea Agent Kai lakini aliishia hapo nyuma yao walisikia mluzi wao wa kupeana ishara ukitokea kwa nyuma yao, wakageuka na kukutana na Silla akiwa katika umakini wa hali ya juu pembeni yake akiwepo mtu ambaye alishautambua udhaifu wake kwa muda mfupi waliokuwa pamoja.

  “Hafadhali tumekutana.. Ghala tuliloelekezwa ndimo kuna mdomo wa kuingia ilipo maana ya kambi ya Tajumulco na genge lao ‘TRJ’ Ndimo kwa sasa watu wote waliobaki kwenye kambi hii wamo humo wanajua wanachofanya wanalinda mahala ambapo wanajua tukiingia tumeingia kwenye moyo hivyo nilitoa wazo Silla na Austin wapite kuzunguka hili jengo hili wakatokee nyuma  ya ghala kuona kama inawezekana kuna njia tunaweza pita kuingia ndani wakati mimi na Rebecca tukiangalia namna tunaweza ingia kupitia mbele kwa kulazimisha kwa mashambulizi” Akaongea Agent Kai.

  “Naona Rebecca kashamuongoza Jairo… Dada yuko vizuri sana!”Miller akaongea na wote wakatabasamu huku wakichungulia kule walipo S.S Rebecca na Jairo.

   “Muda unakimbia… Austin utakuwa hapa ukiangalia usalama wetu kwa kutokea huku nje.. Silla mtu wako huo elekeeni huko mara moja” Macho yake na akili yake yakiwa kule lilipo lango kuu alielekeza huku hawaangalii wahusika lakini kabla hajafanya lililo mawazoni mwake alijikuta akipigwa kikumbo tokea mgongoni.

  “Araaa Piii Jiiii!” Aliyempiga kikumbo kwa nyuma alipaza sauti huku akiutwisha mwili wake nguvu kubwa aweze kumdondosha ‘TSC’ chini na ni kweli sentimeta chache sana kutokea vilipo vichwa vyao bomu la kutoka kwenye silaha ya kulipuka ituapo mahala husika aina ya ‘Rocket-Propelled Grenade’ (RPG) lilipita likitoa mlio wake wa kutisha kwa wale watu wa kazi za kazi na wazee wa vita wanaujua ikikukosa inavyolia kwa hasira kama kimluzi flani kisha mruko wake wa hasira na kasi ukaenda kukita ukuta wa upande wa pili, hapa wote walikwenda chini ikiwa Silla ndiye aliemvamia ‘TSC’ na kwa upande wa Miller na Austin wote walikuwa wa kwanza kuliona linavyokuja na wote walijitupa chini kwa pembeni macho yakiwa makini kuangalia lilipotokea.

  “Haraka kila mmoja akae mahala penye kizuizi, washambulizi wamezima taa kutokea mahala walipo katika jengo linaloonekana linajengwa..” Akaongea Miller huku tayari anatambaa kwa kasi kama mjusi kwenda mahala ambapo pana ukuta kingo wa baraza, ‘TSC’ na Silla nao walitambaa kwa stahili ile ile kufuata kona ya ukuta na ile wanamalizia miguu tu ‘RPG’ lilitua tena mahala walipokuwa kwasasa ikiwa mlengaji alilituma litue walipokuwa.

‘TSC’ alijigeuza haraka binadamu huyu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri kiwango ambacho kinabebana na ‘IQ capacity’ kubwa aliyobarikiwa na mola wetu alipolalia mgongo tu bunduki iliinuka akafyatua risasi kwenye taa kubwa iliyo kwenye nguzo ndefu za chuma zilizo karibu yao pembezoni mwa barabara, hakuishia hapo akaachia zingine kuvunja balbu ndefu mbili zilizoundwa kuacha hatua tano kwa tano zilizo juu kabisa ya ukuta waliojiweka kama kinga, giza likaweka kivuli chake mahala walipo ingawa alikuwa giza la kuwafanya wasionekane lakini ilikuwa ni hafadhali kwao kuliko mwanga uliokuwa ukiwaanika kwa kiasi kikubwa.

Kulikuwa na mawasiliano baina ya ‘TRJ’ walioko kwenye ghala kusudiwa na kina Agent Kai kuwa wanatakiwa waingie humo kutokana na maelekezo waliyopewa na Madam Mariana, walioko ghalani walikuwa wakiwasiliana na kikosi cha ulinzi kilichokuwa hakikuonekana na timu ya kina ‘TSC’ hawa ni walinzi waliokuwa wanalinda upande wa nyuma kabisa wa shamba kunakopita mto na walikuwa na silaha nzito kama hizi ‘RPG’ na nyinginezo hivyo wakipokea mawasiliano walifika na kuingia kwenye jengo ambalo lilikuwa bado katika ujenzi wake wakawaona Kai na wenzake wakipanga mikakati ndipo mara moja wakaanza kurusha makombora madogo yanayopachikwa kwenye silaha hii aina ya ‘RPG’.

Waliweza kupeana mawasiliano kuwa mashambulizi yamewatawanya wavamizi hivyo walio ghalani wanaweza fungua lango kuu la kuingilia hili kushambulia lakini wasishambulie mpaka kombora lingine lirushwe ndipo na wao watoke kasi wakiwa na silaha hii waliyoona kwao ni muhimu zaidi kutumika  kwa sasa kuzuia watu hawa kuweza kugundua siri iliyofichwa miaka takribani mitano katika eneo la chini ya ardhi ya Tajumulco.

Agent Kai akiwa makini mwili ukiwa umelazwa ardhini kwenye vitofali vilivyopangwa kiustadi juu ya ardhi na kulifanya eneo lote kuwa hivi watu wapitapo wanapita kwa raha zao pasipo kukanyaga vumbi wala tope kama ni wakati wa mvua, alijivuta mpaka kwenye kona ya ukuta akautokeza mdomo wa mtutu na kisha kichwa akiangalia kule zinakotokea ‘RPG’, si yeye tu na Silla alifanya kama yeye.

  “Rebecca! Tulinde na hao wa ndani sisi tunaangalia wanaotushambulia tunaweza wadhibiti vipi!” Akaongea Agent Kai kupitia ‘SCNG’.

Ile anarudisha mkono wake kwenye kifyatulio ‘RPG’ lingine lilitua pembeni yao likitawanyika ardhini mpaka cheche zingine zikiwafikia pamoja na vumbi la vitofali vilivyoshindwa himili vishindo na kuvunjika kwa juu hali ya vumbi ikiwa bado alisikika mtu akilalamika maumivu.

  “Bega langu.. Wakuu bega limejeruhiwa” Aliongea kwa sauti ndogo asisikike mbali lakini akiamini wote walio karibu wamesikia, alikuwa ni Austin pale alipojificha kipande kimoja cha makali ya ‘RPG’ yalimfika na kumuumiza bega hapo Miller akamvuta kwa kasi kuja alipo yeye hili awezekumsaidia jeraha lake.

Lango kuu la ghala ulipotua mshindo wa ‘RPG’ tu ulifunguliwa kwa kasi na kisha watu wawili wakatokeza wakitokea kwa ndani wakiwa na nia moja tu kushambulia kule walipo ‘TSC’ na Silla wakiwa wamelala kichalichali lakini wanaonekana walipo na watu hawa, watu hawa hawakuwa wanajua kuwa pembeni tu ya lango kuu kuna watu wawili, mwanamke wa hatari Special Agent Rebecca Smith na kijana wa ‘OCLA’ Jairo.

Bila kuangali pembeni kushoto na kulia watu hawa moja kwa moja kwa kasi ile ile waliyotoka nayo ndani walipiga kila mmoja goti la miguu yao ya kushoto huku mguu wa kulia ukiwa umekunjwa tu  silaha zao za ‘RPG’ kwenye kipando cha bega mikono ikatoa sapoti wakaseti kuvuta silaha lakini hakuna aliyeweza ruhusu silaha kufyatuka kwani bastola aina ya ‘Automatic Colt 45’ ilitema risasi nne za kufuatana mpigaji akiamisha kutoka kushoto kwenda kulia na kuwadondosha wazungu hawa wote wa kiume miili ikilaliana bila ukelele wala kikili kakara maubongo yalifumuliwa kutokea visogoni mwao kwenda kwenye paji zao za uso wakifa vifo vya kufanana haswa, Rebecca Smith akawa ameongeza idadi ya watu anaowakatizia hamu ya kuendelea kuvuta pumzi ya bure ya duniani.

Walio ndani waliona wenzao wakidondoka baada ya kupigwa risasi na mtu ambaye wao hawakumuona lakini sasa walijua kuwa kuna mtu kama si watu pembeni ya lango kuu nje ya ghala walilopo.

Mwanadada Rebecca alisogea karibu kabisa na lango likiwa halijafungwa lakini hakuwa mzembe kuweza kutoa hata kipande cha ncha ya pua yake kuchungulia alisimama tu mgongo wake akiwa kaugemeza ukutani hapo akaweza kusikia waliopo kwa ndani wakiongea kwa kupishana pishana bila mpangilio kana kwamba wako kwenye ukumbi wa disko na disko limekolea na watu wanahitaji kucheza na hata stori kupigwa.

Walio ndani ya jengo linalojengwa kwa urushaji wao wa ‘RPG’ waliamini mashambulizi yamezaa matunda, mtu mmoja akatoka akiwa na bunduki yake kaikamatia uzuri akiwa katika tahadhari akashuka toka barazani kwa kasi na kwakuwa kulikuwa na giza jepesi aliamini anaonekana kwa tabu alikwenda akiwa ameinama mpaka palipo na matofali ya ujenzi mbele ya jengo akajiweka hapo yakawa yamemziba kwa mbele kutokea walipo ‘TSC’ na wenzake na wote walimuona ila kana kwamba waliambiana walimuacha tu waone anafanyaje au wamepangaje, wangeweza kumdungua vizuri tu.

Dakika moja ilipita akatoka mwingine akipita kwa kasi ile ile aliyopita aliyotangulia safari yake naye ikaishia kwenye matofali, kukawa kimya tena ikapita dakika moja ingine toka aliyetoka toka ndani ya boma atoke, akatoka mwingine naye akipitia mule mule walipopita wenzake, alipofika matofalini tu mlio wa ‘RPG’ ilioachiwa ulisikika kutokea ndani ya boma (Jengo lisiloisha) ukilengwa kutua kulekule eneo lengwa walipo Agent Kai na wenzake lilikwenda na kupiga ukutani likitibua vumbi lakini halikuacha madhara katika miili ya walengwa kwakuwa walikuwa wamejibanza kwenye kingo ambazo labda lingepigwa bomu la kufumua ardhi ndiyo wangeweza kuzulika hata Austin alizulika katika shambulizi la ‘RPG’ lililopita kwa sababu hakuwa amejiweka mahala palipo na kingo ya kuta nzito kama walipo sasa wakijikinga na ngazi za baraza hivyo masalia ya vyuma toka kwenye mruko wa bomu hizi za ‘RPG’ yalikuwa yakikumbana na kigingi.

Mlipuko ulipotua na kuwafanya kina ‘TSC’ kujivuta zaidi wasizulike ilikuwa ni mbinu ya kivita tu kwani jamaa walio kwenye matofali, walitokea kwa mbele bunduki zao zikiwa tayari kuua yoyote atakayetokeza pua katika macho yao, hawakuwa wanajua kama hawapambani na wanafunzi wa kijeshi wanapambana na watu wenye uzoefu na kujua kila aina ya mbinu za kivita eneo la mapambano, vumbi  lililotibuliwa na ‘RPG’ likiwa halijatulia ‘TSC’ aliona kwa kutokea chini alipojilaza watu wakija kwa kunyata kuja eneo lao kwa hatua ndefu wakiwa wameinama.

Mdomo wa mtutu wa bunduki aina ya M240 Machine Gun bunduki ya kivita ya kimarekani  uliinuka kwa chati kisha mkono wa kushoto ukasogeza vidole vyake kwenye ‘trigger’ (kifyatulio), wa mbele akiwa anakaribia eneo ambalo endapo angefika tu basi angemuona Austin,r isasi moja tu iliyotua katikati ya eneo la chini ya pua na juu ya mdomo ilimpaisha huku damu nazo zikiruka kufuatana na mwili unavyoruka wenzake waliokuwa nyuma wakimfuata waliinama chini mwili wa mwenzao ukakatiza juu ya migongo yao kwa kasi na kisha kujibwaga chini, jamaa walipojiinua tu nao walishambuliwa kwa risasi za aina ile ile iliyotumika kuondoa uhai wa mwenzao hapa wakishambuliwa na Miller pamoja na Silla kana kwamba wameambiana bunduki zilitema risasi kama sindano ya cherehani inatoboa nguo ndipo na wale jamaa wawili walivyotobolewa tobolewa kabla hawajasalimu amri ikiwa wamekata mauno ya kutosha Israel akachukua stahiki yake.

Miili ilipojibwaga tu kando ya matofali, Investigator Miller alichomoa ‘lock’ ya bomu la kurushwa kwa mkono kisha kwa nguvu akalirusha kwenye boma linalojengwa walipo adui zao likitua langoni na kulipuka, papo hapo Miller akainuka akakamata mkono wenye bega lililo salama la Austin akainuka naye sambamba kisha kwa mwendo wa nusu mbio nusu tembea wakiwa wameinama kwa mbele walielekea kwenye kona ya ukuta walipo Agent Kai na Silla, safari ya kuzunguka nyuma ya ghala ikawa imefia hapa walipokaribia kona wakajitupa chini na wote kuanza kutambaa wakapotea sasa wale waliobaki bomani hawakuwa wanawaona tena.

  “Kazi nzuri! Austin pole sana..!” Akaongea Agent Kai baada ya macho yake kushuhudia jeraha lililopo begani mwa Austin.

  “Ahsante sana… Ajali kazini kaka!” Akajibu Austin hapo akiwa anafungwa kwa kitambaa eneo aliloumia na Investigator Miller.

Mwisho wa sehemu ya themanini na nane (88)

Wenye mamlaka wa kuilinda kambi ya Tajumulco wako matatani, wanajaribu kuzuia uvamizi wakati wavamizi wakiwa na kiapo lazima kabla hakujakucha wawe wamejua mbivu na mbichi zilizopo hapa ndani ya eneo la shamba lililopo ndani ya milima ya Tajumulco.

Nini kitafuatia katika mapambano ya kuonyeshana maujuzi baina ya ‘timu Kai’ na walinzi wa ‘TRJ’ ndani ya Tajumulco?

Jipe nafasi ya kusogea mbele, sogea sogea kumalizia riwaya yetu katika epsd chache zilizobaki baada ya kupita katika epsd nyingi zilizopita.




Mdomo wa mtutu wa bunduki aina ya M240 Machine Gun bunduki ya kivita ya kimarekani uliinuka kwa chati kisha mkono wa kushoto ukasogeza vidole vyake kwenye ‘trigger’ (kifyatulio), wa mbele akiwa anakaribia eneo ambalo endapo angefika tu basi angemuona Austin,r isasi moja tu iliyotua katikati ya eneo la chini ya pua na juu ya mdomo ilimpaisha huku damu nazo zikiruka kufuatana na mwili unavyoruka wenzake waliokuwa nyuma wakimfuata waliinama chini mwili wa mwenzao ukakatiza juu ya migongo yao kwa kasi na kisha kujibwaga chini, jamaa walipojiinua tu nao walishambuliwa kwa risasi za aina ile ile iliyotumika kuondoa uhai wa mwenzao hapa wakishambuliwa na Miller pamoja na Silla kana kwamba wameambiana bunduki zilitema risasi kama sindano ya cherehani inatoboa nguo ndipo na wale jamaa wawili walivyotobolewa tobolewa kabla hawajasalimu amri ikiwa wamekata mauno ya kutosha Israel akachukua stahiki yake.


Miili ilipojibwaga tu kando ya matofali, Investigator Miller alichomoa ‘lock’ ya bomu la kurushwa kwa mkono kisha kwa nguvu akalirusha kwenye boma linalojengwa walipo adui zao likitua langoni na kulipuka, papo hapo Miller akainuka akakamata mkono wenye bega lililo salama la Austin akainuka naye sambamba kisha kwa mwendo wa nusu mbio nusu tembea wakiwa wameinama kwa mbele walielekea kwenye kona ya ukuta walipo Agent Kai na Silla, safari ya kuzunguka nyuma ya ghala ikawa imefia hapa walipokaribia kona wakajitupa chini na wote kuanza kutambaa wakapotea sasa wale waliobaki bomani hawakuwa wanawaona tena.


“Kazi nzuri! Austin pole sana..!” Akaongea Agent Kai baada ya macho yake kushuhudia jeraha lililopo begani mwa Austin.


“Ahsante sana… Ajali kazini kaka!” Akajibu Austin hapo akiwa anafungwa kwa kitambaa eneo aliloumia na Investigator Miller.


ENDELEA NA PIGO NONDO..!!!


BUTWAA V

SAN MARCOS-GUATEMALA

Jibu la Austin lilikuwa la kishujaa mpaka wanaume wenzake walio pembeni ambao muda si mrefu kulikuwa na taarifa kuwa ana uoga ikiwa ni taarifa toka kwa Silla kuwa anahitaji nguvu mpya toka kwa Miller na huyu aelekee kwa ‘TSC’ na alishapangiwa kazi ya kulinda kwa nje ya ghala na eneo lote la mbele ya majengo yaliyo mbele ya majengo yote ya eneo la maofisi ya shamba hili kubwa la mwekezaji Alexis.


“Safi sana! Kazi hizi zina mengi na kiukweli tunajivunia kuwa na kila mmoja hapa” Akaongea Agent Kai kisha akasogea kwenye kona ya chini kabisa yenye kiambaza cha baraza aweze kuona kule walipo washambulizi wao ambako kulikuwa kimya kabisa kana kwamba hamna mtu.


“Tuachane na wale au mnaonaje?” Akatoa wazo pia akahoji kama inawezekana kwa wenzake.


“Hapa nje wabaki watu wawili.. Majeruhi wetu nafikiri anaweza kubaki hapa kama ulivyokwisha mpanga hapo mwanzo awe na Jairo ndani twendeni sisi sote tukiwa na Super Girl!” Wazo la Silla likawa hivi huku yeye umakini wa macho yake ukiwa kule kwenye lango kuu la ghala ambalo iwe kumekucha, giza linaendelea kuna watu wenye silaha nzito au kuna kitu gani cha kuzuia majasusi hawa hawawezi kuondoka bila kuingia ndani.


“Austin! Utakuwa na Jairo hapa kuhakikisha walio ndani ya boma lile hawatoki kuja kuongeza nguvu katika hili ghala, naamini hakuna njia ingine ya kuingia katika ghala hili zaidi hili lango tunaloliona mbele yetu… Psiiiii psiiiiii!!” Aliongea Agent Kai kisha akaunganisha na mluzi uliosapotiwa na mkono wake aliokuwa akiupunga walipo Special Agent Rebecca na Jairo ambao walikuwa bizi kuona wanaingiaje ndani ya ghala, wote waligeuka kule uliposikika mluzi wakakutana na mkono unaopunga kisha mkono ule ule ukaendelea kutoa maelekezo ya vitendo, wakaelewa na papo hapo Jairo akaanza kupiga hatua ndefu ndefu za kinyumenyume mdomo wa mtutu wa bunduki iliyo mikononi mwake ikiwa imeelekezwa kule lilipo ghala hili kama kutatokea shambulizi lolote au kufunguliwa lango kuu aweze kushambulia.


Alifika walipo Agent Kai na wengineo wakiwa wamelaza miili yao ardhini naye akajilaza kichalichali kama aliowakuta akijiweka ubavu kwa ubavu na Agent Kai wakasogeleana hili apewe maelekezo.


“Ndani ya ghala lililo mbele yetu ndiyo mahala ambapo tunatakiwa kuingia kukamilisha kilichotuleta hapa lakini uliona RPG zikidondoshwa eneo hili kutushambulia. Tunashukuru hakuna madhara makubwa kwetu licha ya washambulizi kujitahidi kwa kila hali kushambulia wakiamini washatuangamiza wakatoka watatu kuja kuhakiki kama wamefanikiwa wakaangamia wao hivyo imekuwa onyo hakuna anayetokea kutoka huko mafichoni kuja tena kufanya uhakiki kwa chai ya kuondoa baridi iliyowapata wenzao na hata kushambulia kwa RPG wameamua kusitisha kwakuwa washaona kuwa walikuwa wakitwanga maji kwenye kinu… Katika mashambulizi yao walimjeruhi ndugu yetu Austin kidogo kwenye bega na tayari tumempatia huduma ya kwanza damu haitoki tena kwenye bega husika.. Muda unaenda kwa kasi na kwa ilivyo walio ndani ya ghala wanajua kama wavamizi tuliofika hapa tayari tunajua mahala tunapotaka kwenda na umuhimu wake hivyo nguvu kubwa kwao kwa sasa ni kutuzuia sisi kuingia ndani kwa stahili yoyote kama nasi tulivyo tayari kwa stahili yoyote ile kuingia ndani hivyo kwa tulipofikia kunahitaji kujitoa na uzoefu mkubwa sana tumeshauliana nyinyi wawili mbaki hapa mkiakikisha hakuna mbuzi yoyote inayotoka kwenye boma kuja huku kuongeza nguvu yaani mkiona mtu ni risasi tu kuelekea kwake hii itawafanya wakose mbinu ya haraka kuja kuongeza nguvu pia kutupa taarifa kama kuna watu wanaoongezeka kwa namna yoyote ile… Hatujui njia wanayoingilia kwenye boma lakini tunaijua njia ya kuja hapa hili kuelekea kwenye ghala hivyo mtadhibiti hilo, nafikiri tumeelewana wote kwa ujumla!” Aliongea kirefu Agent Kai muda wote kichwa chake hakikuwa kimetulia kinahama huku na huko pale pale chini walipolaza miili yao.


“Mi binafsi nimeelewa na naamini tayari ndugu yangu Austin anaelewa hilo!” Akajibu Jairo kisha akageuza shingo yake kumuangalia Austin wote wakatikisa vichwa vyao kukubali majukumu wanayopewa.


“Vizuri! Acha sisi tukaone kama yaliyomo yamo..!” Alimalizia Agent Kai kisha wote wakapeana mikono ya kuhamasishana kikazi kwa stahili ya kugonga ‘tano’.


“Acha moto uwake.. Muda wa kazi za kazi sasa!” Silla akaongea kauli ambayo upenda kuongea anapokuwa eneo kama hili ni kauli ambayo ndugu yake Miller ameizoea sana hivyo waliangalina na kutabasamu wakainuka kwa pamoja kama ambavyo nahodha wao ‘TSC’ alivyokuwa ashainuka na anamuelekeza jambo kwa ishara Rebecca.


Kwa hatua za kunyata lakini si hatua fupi wala za kutembea ni nusu mbio nusu kutembea kwa hatua ndefu wanaume hawa walikimbia hadi usawa wa ukuta wa mbele wa ghala, wakigawana kila mmoja na mtu anayemuelewa zaidi kikazi na hata maisha ya kawaida, Kai akivuka upande ule alipo Rebecca na Silla na Miller wakienda kwa pamoja upande wa kulia wa lango kuu waliloliacha katikati.


Agent Kai hakuremba alipofika tu hata kumuangalia Rebecca kama ilivyotakiwa waangaliane kwanza ndiyo yaendelee mengine hakumuangalia alijiweka sawa na ukuta kisha akaamisha begi lake toka mgongoni kuja mbele akiwa ameiweka bunduki pembeni yake akiigemeza ukutani, mule kwenye begi akatoa baruti kati ya baruti moja mbili alizozichukua wakati anaondoka ‘sign street’ manispaa ya Chimaltenango jijini Guatemala kuja huku mkoa wa San Marcos, hizi ni baruti maalumu za kulipua miamba na vitu vingine vizito.


Akalisogelea lango geti akiwa anajisogeza mgongo wake ukiegemezwa ukutani, alipolifikia alichunguza kisha akapata jibu akapachika baruti kwenye kingo ya chini kwakuwa lilikuwa ni lango geti la kupanda juu si kufungukia upande wala kusogea upande mmoja kutoka mwingine hivyo jibu lilikuwa chini kuna ‘lock’ zake, uzi wa baruti alirudi nao nyuma wakati anarudi nyuma aliweza kuangalia juu kabisa kabisa lilipo paa bati la ghala hapo akaiona kamera ya ‘cctv camera’ ikiwa imewekwa kwa ndani kidogo na inachukua video zake kuja eneo lote la hapa lango kuu.


“Ina maana hukuiona ile kamera juu?” Akamuuliza Rebecca wakaangaliana kisha macho yao yaliyo ndani ya miwani yaliinuka kwa pamoja kuelekea ilipo kamera, hapo Rebecca akashangaa kwakuwa hakuwa na wazo hilo kabla akarudisha macho kumtizama akakuta naye anamuangalia na papo hapo Kai akatabasamu kumtoa wasiwasi licha ya kuwa alichukia kwa uzembe wa mtu huyu anayemuamini sana kuwa kama makosa ufanya kwakuwa bado anajifunza kisha akashusha ‘sox’ aliyovaa kichwani imzibe usoni.


“Basi bibie.. Usijali..!” Akasema ‘TSC’ kisha akachukua bunduki yake toka alipoiegemeza ukutani ilipotulia mkononi akakoki akaiinua kwa kasi kulenga kamera ya cctv ilipo ilikuwa ni ndogo sana na mpaka uione ilikuwa uwe na macho yanayopekua sana, mlio wa risasi ulisikika kisha ukimya ukafuata pale nje kikamera kilisambaratishwa chote huko waliokuwa wakiangalia kila linalofanyika hapa walikutana na wanachostahili kwa muda huu wanaume hawa wa kazi waliopo hapa kisha akakaza mikanda ya begi hili lisimsumbue tena litulie mahala pake huko mgongoni mwanaume kazini rasmi.


“Bila kamera ile hii baruti ingeondoka na watu kadhaa walio kwa ndani.. Rudini nyuma kabla hatujalipua kila mmoja aandae bomu la kurushwa na mkono pakivunjika tutakuja kasi bila kujitokeza tutatupia kwa chati ndani iwe karibu na hata wengine kwa mbali kuelekea ndani halafu mimi nitajitosa kujitupa ndani! Mungu siku zote usimama ilipo haki tunamuomba alizie kila tarajio letu, kila tutakapokanyaga baraka zake zianze kukanyaga, atutangulie kwa kila jambo..Inshaallah!” Alielekeza akaunganisha na dua lake la jumla analopenda kulitanguliza kimoyo moyo (kifuani) akiwa mahala peke yake na kwa sauti akiwa na wenzake na kisha akawasha uzi wa baruti kwa kutumia kiberiti cha gesi, moto wa uzi ulio ‘doto’kwa kasi ukawaka na kuanza safari yake kufuata ‘kulwa’ wake alipo.


Mshindo mkuu ulisikika ukilifumua ‘lango geti’ kwenye ‘lock’ zake za chini kama bingwa alivyoamini kuwa itatokea hivyo kwa uzoefu wake, mlio wa mshindo wa mlipuko ulipopoa tu wazee hawa wa kazi kama wanatumia mashine ‘mota’ zenye kasi walifika na kutupia mabomu ya kurushwa kwa mkono kuelekea ndani ikatokea milipuko mingine na ikunganika na baadhi ya vilio vya watu.


‘The Sole Cat’ hakuhofu tena tundu za pua zake zilikuwa zinasikia harufu ya damu ya binadamu na akishasikia hivi akili yake uwa inahitaji kufanya kile inachojituma tu na ilishokwisha panga tu katika kujitetea na kuangamiza adui tu, aliruka mtupu-mtupu mtu huu mwenye mwili ambao ukimuona huwezi amini kama ana wepesi huu lakini ndiyo hivyo ndiyo kipaji chake mwaya hata mimi namuonea wivu kwakuwa natamani mengi anayoyafanya nami ningeweza kuyaweza ila wapi (Lol), alipotua kwa miguu tu akaunganisha kwa kujifyatua tena kwa sasa ikiwa kwa mbele napo alipotua akajidindosha chini kwa kasi macho yake yakaona kiumbe kingine kikija kwa kasi kwa stahili ya kujiviringisha kwa mbele kama tairi alikuwa ni Special Agent Rebecca hakutaka kumuacha mshirika wake aende ndani mwenyewe tu.


Taa za ndani ya eneo la ghala ilikuwa imezimwa lakini wakati wanahama kutoka eneo la wazi kwenda kwenye mabelo yaliyopangwa ‘stake’ taa ziliwaka na zilikuwa taa katika eneo lote la dari tena mataa makubwa yenye mwanga mkubwa lakini watu hawa wajanja walishafika pembeni kila mmoja akasogea eneo ambalo atakuwa anazibwa, akili za bwana mkubwa Kai zilifanya kazi hakuutaka ule mwanga kama kanuni ya kazi zao anayoitilia mkazo kanuni ya kuucheza mchezo wa ‘roho’ kukiwa na giza aliinua bunduki yake akaapasu mbili zilizo juu yake kisha kwa kasi akahama upande kukwepa vyupa vunjika vya balbu zile na mara ukasikika mlio mwingine wa risasi alikuwa ni Rebecca akivunja zilizo juu yake.


Walionekana walipo na adui ambao wao hawakuwa wanajua haswa wako eneo gani kati ya eneo kubwa la ghala hili refu na pana ukubwa ambao ni mita mia mbili urefu na upana mita mia moja na kote kumepangwa ‘stake’ za mabelo ya viroba vyeupe inayoonekana ni kahawa kwa ndani sababu ingine ilikuwa imemwagika chini kutokana na mabomu yaliyotupwa awali na timu ya Kai.


Ulisikika mlio usiojificha mlio wa silaha pendwa na watu hawa wa ‘TRJ’ silaha ya ‘RPG’, mlio uliowafanya Agent Kai na Rebecca kujibwaga chini na kujisogeza kwa kasi zilipo vitako vya chuma vilivyotengenezwa pembe nne kisha vikapangwa hivi viroba vya kahawa iliyokwisha sindikwa, ‘RPG’ ilitawanya eneo lote la juu la ile ‘stake’ na kahawa kuwamwagia majususi hawa ambao nao walitoa mabomu ya kurushwa kwa mkono wakarusha kwa mbele kwa pamoja huko lilwalo na liwe, mlipuko ukatokea ukifuatana.


“Ingieni jamani tusije tukajichanganya ni bora tuwe pamoja.. Tukirusha mabomu mengine tu muingie” Aliongea Agent Kai akiwa ameruhusu ‘SCGN’ Hili awaelekeza Silla na Miller ambao waliganda kwa nje wakiwa na sintofahamu.


“Vipi katika angalia yako hujaona cctv?” Akauliza Kai akimuuliza Rebecca ambaye alimuangalia wakaangaliana akatikisa kichwa kuwa hajaona.


“Twende tuzunguke tuelekee kwenye kona mwisho upande huu” Akaongea tena Kai kisha wakaondoka walipo wakiwa wanainama kuakikisha miili yao haionekani.


Mwendo ule ule wa kunyata uliwafikisha kwenye kona ambako kulikuwa na ‘stake’ ya mwisho hapo walikwea na kupanda juu kwa pamoja huku kulikuwa na balbu ambayo hawakuivunja na waliona hawawezi kuivunja watawafahamisha adui zao walipo ikizingatiwa wao hawakuwa wanajua rasmi wapi wapo hao adui zao.


Kitaa cha kijani kiliwaka kwenye saa yake ‘TSC’ ikamjulisha kuwa kuna mtu anampigia anahitaji kuongea naye wakiwa wamejilaza juu ya ‘stake’ ya viroba vya kahawa, akabonyeza kitufe kuruhusu.


“Tuko tayari!” Alikuwa ni Miller akitoa taarifa kuwa yeye na Silla wako tayari.

“…Subirini kidogo hatujajua kama hawa jamaa wamejificha kwa wapi? Hatuwezi rusha kila bomu la bure tu tunataka liondoke na mtu, tunataka nasi tucheze kipanya kama wao wanavyocheza kipanya..” Akanong’ona Kai sauti ambayo mtu aliye hatua tano asingeweza kusikia.

“Msichelewe… Maana tuliona kama vipi turudie mbinu kama ile mliyotumia!”

“Mkisikia mlipuko wa chochote kile iwe bomu au risasi muingie kwa kukimbilia zilipo ‘stake’!”

Alimalizia Agent Kai kisha akarudisha mkono wake ukamate vizuri bunduki aliyoshika, wakaangaliana na mshirika wake kisha yeye akaanza kutambalia tumbo kuhama ‘stake’ hii kwenda ingine ambazo zilikuwa zimepangwa kwa kubanana zikiacha njia katikati za kupita wahusika wanaotoa huduma katika ghala au hata watu wa kukagua.


Wakiwa wamesogea ‘stake’ ya tatu kule kule juu mita zipatazo sitini za upeo wa macho yao yanayosaidiwa na miwani ya kijasusi waliweza kuona miili ya watu inayojongea kwa taratibu kama wafanyavyo wao lakini wao walikuwa wakielekea kule mwanzo walipokuwa wao wakarushiwa ‘RPG’, taa zilikuwa zimezimwa katika eneo wanalopita watu hawa hawakuwa wanafikiri kama wanaopambana ni ‘full’ maujanja na ni wazoefu, ingia yao tu ilitakiwa iwe funzo kwao lakini wao hisia zilikuwa hisia bishani pale walipokuwa wakipeana mawazo na kujadiliana kila mmoja aliweka wazo pengine ‘RPG’ zao zilikuwa zimemaliza kazi, adui zao wamekufa au kujeruhiwa ile ya kutojiweza kabisa hivyo wazo la haraka lilikuwa kutumia njia ya panya ya juu ya ‘stake’ kwenda kuona wako sahihi na kile ambacho kila mmoja anaamini akiwemo kiongozi wao ambaye usiku huu wa uvamizi wa ‘timu Kai’ alikuwa yupo kati ya wale watu wa juu ndani ya ‘TRJ’ mtu mzito Koplo wa zamani wa jeshi la Mexico Mr. Maxiwell Zuantejo ambaye alishatoa taarifa kuwa wamevamiwa na wamarekani tokea tu kina Kai wako nje walionekana kwenye kamera za cctv na yeye na wasaidizi wake waliwaona.


“Mbuzi zinasota kuelekea kule tulipokuwa.. Kwa tulivyolaza miili juu ya stake hatuwezi rusha bomu kufika kule pengine nasi tungekuwa na RPG kama wao” Akaongea kwa kunong’ona S.S Rebecca bila kumuangalia anayemwambia.


“Tusogee stake tatu toka hii ila itatubidi turuke safu hii mpaka ile.. Utulivu ni kitu muhimu sana tuzingatie hili”Kai naye akaleta wazo lake ambalo halikuwa na mjadala lilipita bila kupingwa.


Walifanya ilivyotakiwa wakisogea kutoka ‘stake’ kwa ‘stake’ za belo za viroba vya kahawa ikawa si tatu kama walivyokubaliana mwanzo walijikuta kila wanavyokwenda na kuona hakuna dalili ya kustukiwa nao wanaongeza ingine mpaka ikawa zimebaki mita thelathini tu kwa kipimo cha macho yao wote wawili.


“Inatosha hapa.. Utanilinda mimi nawasogelea kwa kasi kisha nitarusha mabomu nikikaribia palipo na uwezo wa kufanya hivyo.. Moja, mbili, tatu!” Aliongea Kai akielekeza kisha akahesabu mpaka tatu akainuka nusu kimo chake akiwa kainama bila kujali kama anaweza onekana akiwa kaiweka bunduki yake mgongoni ikining’inia usawa na bega lake.


Hatua tano tu za mbio zake ziliweza shtua baadhi ya wale walio katika msafara ulio kama siafu hapo ilikuwa wamestukizwa kwa kiasi kikubwa kila mmoja ambaye walikuwa wanatumia mwendo wa kutambaa wakiwa wamelala juu ‘stake’ kifudifudi alitumbua asijue kama anayekuja akiwa kainama ni ndugu yao ama vipi kwakuwa usiku huu wao kwa ujumla hawakuwa katika jezi maalumu wengi waliamshwa usingizini na kukurupuka tu.


Mwisho wa sehemu themanini na tisa (89)


Kazi inaendelea!


‘The Sole Cat’ kama mzimu machoni mwa wana ‘TRJ’ waliokuwa nao juu ya stake za viroba vilivyojazwa kahawa kama ilivyo yeye lakini upande anaotokea uliwachanganya jamaa wakabaki wameduwaa sababu alifika eneo lao la giza waliloweka mpaka wa kuzima taa kuwa wao watakuwa wa kwanza kuwaona maadui zao waliowavamia lakini wao wasiwe wanaonekana.


Nini kitatokea hapa?




“Mbuzi zinasota kuelekea kule tulipokuwa.. Kwa tulivyolaza miili juu ya stake hatuwezi rusha bomu kufika kule pengine nasi tungekuwa na RPG kama wao” Akaongea kwa kunong’ona S.S Rebecca bila kumuangalia anayemwambia.


“Tusogee stake tatu toka hii ila itatubidi turuke safu hii mpaka ile.. Utulivu ni kitu muhimu sana tuzingatie hili”Kai naye akaleta wazo lake ambalo halikuwa na mjadala lilipita bila kupingwa.


Walifanya ilivyotakiwa wakisogea kutoka ‘stake’ kwa ‘stake’ za belo za viroba vya kahawa ikawa si tatu kama walivyokubaliana mwanzo walijikuta kila wanavyokwenda na kuona hakuna dalili ya kustukiwa nao wanaongeza ingine mpaka ikawa zimebaki mita thelathini tu kwa kipimo cha macho yao wote wawili.


“Inatosha hapa.. Utanilinda mimi nawasogelea kwa kasi kisha nitarusha mabomu nikikaribia palipo na uwezo wa kufanya hivyo.. Moja, mbili, tatu!” Aliongea Kai akielekeza kisha akahesabu mpaka tatu akainuka nusu kimo chake akiwa kainama bila kujali kama anaweza onekana akiwa kaiweka bunduki yake mgongoni ikining’inia usawa na bega lake.


Hatua tano tu za mbio zake ziliweza shtua baadhi ya wale walio katika msafara ulio kama siafu hapo ilikuwa wamestukizwa kwa kiasi kikubwa kila mmoja ambaye walikuwa wanatumia mwendo wa kutambaa wakiwa wamelala juu ‘stake’ kifudifudi alitumbua asijue kama anayekuja akiwa kainama ni ndugu yao ama vipi kwakuwa usiku huu wao kwa ujumla hawakuwa katika jezi maalumu wengi waliamshwa usingizini na kukurupuka tu.


ENDELEA NA MAPIGO..!!


BUTWAA VI

SAN MARCOS-GUATEMALA

Udhaifu wao wa kustuka na kuchelewa kuchukua maamuzi licha ya wingi wa o wa watu zaidi ya kumi na mbili ulimpa nafasi Agent Kai kutoa ‘lock’ ya mabomu ya kurusha mawili walipokuwa wanajipindua na hata wengine kusimama hili waweze kutumia bunduki zao mabomu mawili ya kufuatana yalitua katikati yao ukijumlisha na giza pamoja na ujuzi wao wa kutambua mabomu ya kurushwa yanapotua hatua gani stahiki kwa muhanga wa kushambuliwa anatakiwa aitumie kwa kasi, mabomu yalilipuka na kuwasambaratisha walipiga makelele ya kulia maumivu ya kifo kilichowapitia kiukatili wa kuchanwa chanwa miili yao wakisambaratika na michaniko ya viroba vya kahawa, vipande vya viungo na damu zinazotoka katika viungo hivyo ndiyo kitu pekee alichokuwa anakiona ‘TSC’ kwa sasa, akageuka kumuangalia Special Agent Rebecca ambaye alikuwa anatambaa kama kenge kuelekea boss wake na mshirika wake.


Special Agent Silla na mshirika wake wa karibu na swahiba wake milio ya mabomu ya kufuatana ikirandana na vilio vya watu wazima wanaotokwa roho wakilalamika kwa lugha yao ya kilatin iliwafanya wadunde na kuingia ndani ya eneo la ndani la ghala kutokea nje wakipita kwenye lango kuu ambalo walikuwa wakiogopa kupita bila tahadhari, walielekea upande ambao walielekezwa waelekee katika safu ya ‘stake’ za viroba vya kahawa upande wa kulia uingiapo ndani ya ghala ukiacha na upande wa kushoto walio Kai na Rebecca sasa.


“Mmeingia?” Akauliza Agent Kai huku kwa sasa wakiwa wanashuka toka juu ya ‘stake’ kubadili stahili ya mahala walipo wakipita pembeni kidogo ya ‘stake’ zilizoharibika na bomu muda si mrefu zikiwa zinafuka moshi unaotaka kubadilika kuwa moto lakini damu za marehemu walioondoka duniani kilazima muda mfupi uliopita ambayo kiuhalisia ni kimiminika ilikuwa ikizuia kutokea kwa moto.


“Ndiyo! Tumeelekea safu ya kulia” Akajibu Miller kwa niaba ya mwenzake.


“Sawa.. Kuweni makini kwa pamoja tutafute mdomo ulipo”

“Sawa.. Kazi njema..!”Akamalizia Miller kisha wakaminya vitufe vya kukata, ‘TSC’ hakushusha mkono akabonyeza ‘code’ ingine.


“Halloo! Austin” Akaita baada ya aliyempigia kupokea.

“Naam kaka!”

“Kuhali gani?”

“Bado na wao wana mashaka hakuna anayethubutu kutokeza wala kurusha RPG zao kama ilivyokuwa”

“Vizuri! Sisi bado tunatafuta mdomo.. Msifanye chochote cha kuhatarisha maisha yenu zaidi ya ulinzi madhubuti. Poleni na baridi kali la nje!”

“Ahsante.. Na msihofu juu yetu”

“Haya.. Kazi njema!”

“Nanyi pia!!”

Walimalizia hivyo hapa vitufe vikaminywa kwa pande zote, Agent Kai akamgeukia Rebecca ambaye hakuwa tena karibu alikuwa amesogea mbele hatua sita anachungulia huku na huko kama paka shume anayetaka kuzama kwenye banda la kuku akapige vitu vitamu, ‘TSC’ akapiga hatua mnyato hadi alipo akamgusa bega wakageukiana.


“Ni vizuri sasa tukagawana nafasi za kuendea..!” Rebecca akatoa wazo wakiwa wanafichwa na kivuli cha safu za ‘stake’ zilizo maeneo walipo.


“Ndiyo! Elekea kushoto mi naingilia hapa kati.. Muda unakimbia sana inakaribia alfajiri.. Tunatakiwa tuuone mdomo wa kutupeleka mahala husika haraka iwezekanavyo” Wazo la Rebecca likaungwa mkono wakapeana ‘tano’ ya kuhamasishana wakimalizi na kumbatio (hugh).


Walivyoachiana hakuna aliyemuangalia tena mwenzie waliondoka kila mmoja akishika njia yake katika hali ya umakini na tahadhali ya hali ya juu maana hatua zilikanyagwa kana kwamba nyayo za miguu zina misumari zinapita juu ya ngoma zilizowambwa ngozi nzuri ya ngamia.


Koplo Maxiwell Zuantejo ‘The Big Man’ kama wengi walivyopenda kumuita watu wengine walio ndani ya ‘THE RED JAGUAR’, muda huu wakati kina Kai wanawinda kujua mdomo walioambiwa unapatikana katika ghala hili, mdomo huo ukiuona na ukaingia ndiyo utakuwa umeingia kwenye maana ya neno linalofahamika ‘Tajumulco Camp’, mwanaume huu pandikizi la mtu wa miraba minne alikuwa katika chumba cha mawasiliano akiwasiliana na wakuu wa ‘TRJ’ waliopo Mexico ikiwemo ‘Kingpin’ wa genge hili lenye sifa zake miongoni mwa magenge ya mihadarati yaliyopo ndani eneo la mabara yote ya Amerika kuanzia Kusini, kaskazini na kati.


“Tumieni kila aina ya njia kuzuia hao ngedere kuingia ndani ya ngome yetu.. Helkopta imeondoka hapa ikiwa na watu watano wa kazi ambao naamini watazuia upumbavu wao wa kuamini kuwa wanaweza kutuingilia na kutufanya vile wanavyojisikia hao wajinga” Koplo mfukuzwa wa jeshi la Mexico Maxiwell Zuantejo alipopokea simu tu alikutana na maneno haya toka kwa mmiliki wa simu iliyotumika kupiga kwenye simu yake na pia ni boss wake aliyemuajiri Brigedia mfukuzwa wa jeshi la Mexico Fernandes Carlos Codrado, ikiwa yeye na viongozi wengine wa juu wako makao makuu wakiwa wameamshana punde tu walipopokea taarifa ya kuwa ngome yao kuu katika uhifadhi wa biashara yao kuu ya ulanguzi wa mihadarati imevamiwa.


“Juu niliacha vijana arobaini kuhakikisha hawafiki kwenye lango letu la kuja huku chini.. Kosa lililopo eneo la juu la hapa alikuwa limefungwa cctv kamera za kutosha hivyo tunaona sehemu muhimu tu kama tulivyoweza kuwaona wakiwa kwenye lango kuu kule nje mpaka walipostuka wanaonekana wakaharibu kamera ya pale.. Nimetega mtego endapo watafanikiwa kumaliza vijana wetu kisha kuuona mdomo wa kuja huku chini na pia kuiona kamera wakaiharibu hawataweza kupita salama na kukwepa mitego yetu” Zuantejo akajieleza kwa boss.


“Wako wangapi kwa ulivyoona?”

“Watano au sita kwa jinsi kamera za kwanza zilivyowachukua wanaonekana hivyo”

“Mimi umenitumia video inayowahusu zikiwa zinajirudia rudia aina ya mavazi… Kiongozi wao ni adui yetu namba moja hata kama mtaweza zuia wasiingie na wakakimbia sitamuacha salama kabisa yeye na familia yake watalipia huu upuuzi wa kuingilia maisha ya watu”

“Nimesikia mlipuko wa mabomu.. Mungu wangu isiwe tu vijana wanazidi kupungua.. Naomba nikuache nitakucheki kitaarifa muda si mrefu acha niwasiliane na walio juu kwanza” Zuantejo akaomba kwa boss wake.


“Sawa.. ‘Alto Genius’ na wenzake wanakuja huko.. Msihofu kila kitu kitakuwa salama..Nakuamini sana Koplo!” Akamalizia na hawakufanikiwa kuagana simu ikakatwa.


Maxiwell akasogea haraka zilipo skrini (screan) za cctv kamera zote zinazozunguka eneo lote la majengo mbalimbali yaliyopo ndani ya eneo la kambi ya Tajumulco.


“Aisee hawa guard three wazembe sana.. Jamaa kawalipua na mabomu kizembe.. Toka nje ya chumba wape tahadhari guard two kuwa wawe makini na walipue yoyote atakayeonekana kuusogelea mdomo wa Tajumulco Camp!” Akaongea Maxiwell baada ya kurudisha nyuma na kuweza kuona tukio la Agent Kai kuwalipua kwa mabomu watu waliokuwa wakitambaa juu ‘stake’.


Mtu aliyepewa maelekezo alitoka katika chumba kile kwa kasi akiwa full na silaha zake tayari kwa lolote, akimuacha Maxiwell Zuantejo na wenzake wengine wanaohusika na chumba hiki cha mawasiliano.


Agent Kai njia aliyoifuata ilikuwa ni njia ya katikati ya safu ya ‘stake’ na ‘stake’ lakini alikwenda huku masikio yake akihakikisha yanasikia hata unyayo huo umekanyagwa na mtu anayefanana na jina lake la utani kutokea kwa juu ya ‘stake’.


Mita karibu hamsini hakukutana na kiumbe chochote zaidi ya kelele za wadudu mbalimbali wanaopenda kuishi katika sehemu kama hizi kama panya nakadhalika, alipokaribia kona akasikia mlio wa bunduki kisha ya hapo yakaanza majibishano ya risasi ikiwa ni bunduki tu zinazosikika kwa kukadiria na alipo ilikuwa ni karibu sana na kwa jinsi alivyoelekezana na Rebecca wake ilimjuza akilini majibizano yanatokea alipoelekea.


Haraka akapanda juu ya ‘stake’ mojawapo mpaka juu hapo akaweza kuona kule inapoonekana ndipo kuna majibishano ya risasi baina ya upande unaopiga kwa wingi zaidi tena kwa mpangilio wa kiasi kidogo na upande unaopiga risasi kama kwa kuvizia lakini kwa hesabu zenye umakini sana na ni mpigo mmoja au miwili ya kufuatana kisha ukimya upande huo unatamaladi kidogo halafu mambo yanaendelea.


Juu ya ‘stake’ mwamba ulitambalia tumbo mikono ikiwa imara na madhubuti haswa kukamatia bunduki iliyokwisha ruhusu risasi kukaa kwenye chemba yake iruke kwenda kupeleka madhara kwa adui, mtambao uliendea akahama ‘stake’ hii na kwenda ingine na hapo pande zote zilikoma kushambuliana ikawa ni harufu ya baruti tu za kutokea kwenye bunduki husika ndizo zilizokuwa zimetanda eneo hili na kuweza kusikika uzuri kwenye tundu mbili za pua za Agent Kai zilizo ndani ya ‘mask’ aliyovaa usoni mwake.


Harufu ilimfika kwa ukaribu sana mijongeo yake ikasita kutokana na ukaribu huo, kichwa akikutulia sehemu moja hata sekunde mbili tu kama kenge katoka kichakani mwake, kushoto, kulia kwake, mbele yake na hata nyuma yake umakini wa kiwango kikuu akiwa katika hali hiyo akaona kivuli kinajongea toka pande moja za safu za ‘stake’, kiumbe chenye kivuli wakilisha kilionekana kinanyata hatua za moja kisha anaganda anapeleka ya pili nyayo ikitua anaganda tena kisha ya hapo akatokea dhahiri shahiri machoni mwa ‘TSC’ hapo akamuangalia vizuri kwa kutokea juu alipo wakati anaendelea kumfanyia usahili kikatokea kivuli kingine kikpiga hatua zile zile kama ilivyokuwa kwa huyu wa kwanza, vikaongezeka kuwa viwili kisha kwa pamoja wakatokea wanaume wengine wawili wakimfuata kwa nyuma yule aliyetangulia lakini wa mbele hakupiga hatua zaidi alionekana akipaa kurudi nyuma huku katikati ya paji lake la uso kukipasuka kufuatana na mruko wa kulazimishwa huku mlio mmoja wa bunduki ukitokea kutoka kwenye ‘stake’ aliyo ‘TSC’ hatua chache tu, wale wa nyuma walistuka na wote bunduki zao zikatema miale ya moto iliyolandana na milio ya risasi ya kufuatana kuelekea huko walipoamini aliyempiga risasi alye mbele yao ameweka kambi.


‘TSC’ alijiinua na kupiga goti moja katika kiroba cha kahawa huku lingine likiwa limekunjwa bunduki akaielekeza kwa watu wale kisha akaruhusu kutema risasi tano za kufuatana mfululizo watu wale wote walidondoka bunduki zao zikitupwa toka mikononi mwao mrusho wa miili yao ukiifanya miili yao kujipiga katika bomba za ‘stake’ na viroba vya kahawa kisha kutupwa chini matundu ya risasi zilizopenya kwenye miili yao zikiacha athari kubwa ya kurusha damu zao kama mabomba ya maji yaliyopasuka, Israel alishafanya kilichofanya yeye kuitwa ‘Israel’.


“Boss! Nimehama upande… Nashukuru kwa msaada wako!” Aliongea Rebecca ambaye alipomshambulia mtu wa mbele alihama upande kwa kuzunguka safu ya pili kwa kasi na wepesi wa hali ya juu, aliongea kwa kutumia mfumo wao wa simu saa na ‘bluetooth earphones’ (SCNG).


“Nilijua tu ni wewe dear! Niko juu ya viroba wee endelea kuwa chini.. Usha..!” Kabla hajaendelea kuongea kasauti ka ‘RPG’ kakasikika kakija kwa kasi kwenye masikio yake haraka mwamba ukakamatia vizuri bunduki kisha akabingirika kwa kasi kuhama kule juu kisha alipofika kingoni akajifyatua na papo hapo kama kwamba nyota ya jaha ililala kichwani mwake mlipuko mzito ulitua mahala alipokuwa hata stamina aliyokuwa nayo ilikata alivamiwa kwa mgongoni na kiroba kisha akajikuta anatupwa kuhama toka alipo kwenda kujipiga katika moja ya nguzo bomba pana inayokwenda juu kabisa kushika bati za godown (ghala) hili, bunduki ilimtoka mkononi akabwaga mwili chini akitulia mgongo akajipindua na kisha kutambaa kwa mikono na miguu iliyokunjwa bila kujali maumivu ya shambulizi hili la silaha ya ‘RPG’, haraka akaokota bunduki akaacha kutambaa na kuwa ameinama tu akiweka hatua za haraka kuondoka eneo alipo, kitaa cha kijani kikawaka kwenye saa hapo akatambua anapigiwa.


Hakutaka kuongea akiwa pale alikuwa akitimua nusu mbio kama paka jinsi kishindo kilivyokuwa hakuna kwa mwanaume huyu, hatua zilimfikisha kwenye uchochoro ambao hakuuingia kwa kukurupuka bali alisimama akachuchumaa chini kabisa, mkono wake mmoja ukaiweka miwani vizuri kwa hapa kulikuwa na giza la wastani kichwa akakipeleka eneo la chini kabisa akachungulia unapoelekea uchochoro hapo hakuganda zaidi kwakuwa kulikuwa na watu wawili wanakuja kwa huku alipo tena wakiwa wananyata wa mbele akiwa ameshika bunduki mdomo umeelekea mbele na wa pili akiwa amebeba begi ambalo kwa haraka isingekuwa rahisi kwa ‘TSC’ au mwingineyo yoyote kujua kuna nini?.


‘TSC’ alihesabu kwa kifuani mwake mpaka tatu kisha kwa kasi akaulaza mwili wake chini na kisha kugala gala akitokeza kwenye upenyo mlango wa uchochoro husika bunduki ikiwa imekamatwa vizuri licha ya kuwa ana galagala mkono wa kushoto ulioweka kidole chake cha shahada katika ‘trigger’ (kifyatulio) ulipapasa kidude hiki kidogo lakini kikiguswa na kuvutwa na mtu kama yeye uwa ni nadra icho kilichosukumwa (risasi) kutofanya kile alichokusudia, watu hawa wote wawili hakuna aliyeweza fanya lolote zaidi ya wa nyuma kupaishwa kumvamia wa nyuma kisha wote kudondoka chini wakiwa wanagaligali mauti roho zao zikipambania kubaki kwenye miili ilihali mnyofoa roho kashazikamata kiganjani mwake (hakuna ujanja wala hongo).


Alikuwa ameshajua mahala ambapo panakuwa pamesikika mlio wa silaha yoyote basi wenyeji wa godown hili uwa wanakuja kujibu mashambulizi alichofanya hakuuingia ule uchochoro akapiga hatua kuvuka toka safu hii hadi ya pili ambapo akiwa anajongea kwa kasi macho huku na kule walikutana na S.S Rebecca wakijuana haraka wajihi wao wa mavazi waliyovaa, wakasogeleana na kugonga ‘tano’ kana kwamba ‘masela’ flani wamekutana katika anga zao.


“Wajinga hawa wanatumia sana RPG.. Natamani nipige simu kwa Norman atuulizie kwa Mariana lango la siri tunaweza kulionaje kwa kweli maana ni kama hawaishi na hatuoni mahala tunapohitaji kufika palipotuleta hapa Tajumulco” Akaongea Special Agent Rebecca ikiwa wamesogezeana vichwa vyao kwa ukaribu mkubwa hata pumzi zao zilikuwa zikisikizana kwa ukaribu mkubwa.


“Silla na Miller wako kimya.. Ngoja tuongee nao… Nilinde wakati naongea nao tuweze kupeana maelekezo kidogo” Kai naye akaongea kisha akachuchumaa chini na Rebecca akabaki kasimama mgongo wake akiwa kauegemeza kwenye moja ya kiroba cha kahawa vilivyopangwa kwa kubebana katika stake yake zilizo katika safu ya msururu mmoja.


“Mko wapi? Mko kimya hatusikii hata mlio wa bastola. Vipi?” Akauliza Agent Kai baada ya simu ya mfumo wao wa mawasiliano ilipopokelewa na upande wa pili.


“Tuko karibu na lango ambalo nafikiri ndiyo unapopita unaelekea huko kwenye ‘flour’ ya chini tunakohitaji kwenda.. Sisi hatujastukiwa kabisa kama tumefika hapa ni mita chache tu na pia wao wanachojua na kuzuia ni nyie kusogea huku tunawasikia wakipokea maelekezo walinzi walio hapa na idadi yao kwa haraka tu huwezi kuhesabu maana wengine wamejificha hawaonekani kwa dhahiri” Akajibu kwa sauti ambayo msikilizaji utambua ananong’ona kwa sababu hayuko mahala salama.


Mwisho wa sehemu ya tisini (90)


Mapambano bado yanaendelea!


Agent Kai ‘TSC’ na mshirika wake wa karibu Special Agent Rebecca Smith wameendelea kusonga mbele wakikutana na vikwazo vya juu toka kwa wapinzani zao ambao walilishwa yamini kuhakikisha hakuna mtu anasogea na hata kuliona lango au waweza ita mdomo wa kuingilia mahala palipo na siri nzito katika genge la ‘TRJ’.


Je muziki utachezekaje?






Alikuwa ameshajua mahala ambapo panakuwa pamesikika mlio wa silaha yoyote basi wenyeji wa godown hili uwa wanakuja kujibu mashambulizi alichofanya hakuuingia ule uchochoro akapiga hatua kuvuka toka safu hii hadi ya pili ambapo akiwa anajongea kwa kasi macho huku na kule walikutana na S.S Rebecca wakijuana haraka wajihi wao wa mavazi waliyovaa, wakasogeleana na kugonga ‘tano’ kana kwamba ‘masela’ flani wamekutana katika anga zao.


“Wajinga hawa wanatumia sana RPG.. Natamani nipige simu kwa Norman atuulizie kwa Mariana lango la siri tunaweza kulionaje kwa kweli maana ni kama hawaishi na hatuoni mahala tunapohitaji kufika palipotuleta hapa Tajumulco” Akaongea Special Agent Rebecca ikiwa wamesogezeana vichwa vyao kwa ukaribu mkubwa hata pumzi zao zilikuwa zikisikizana kwa ukaribu mkubwa.


“Silla na Miller wako kimya.. Ngoja tuongee nao… Nilinde wakati naongea nao tuweze kupeana maelekezo kidogo” Kai naye akaongea kisha akachuchumaa chini na Rebecca akabaki kasimama mgongo wake akiwa kauegemeza kwenye moja ya kiroba cha kahawa vilivyopangwa kwa kubebana katika stake yake zilizo katika safu ya msururu mmoja.


“Mko wapi? Mko kimya hatusikii hata mlio wa bastola. Vipi?” Akauliza Agent Kai baada ya simu ya mfumo wao wa mawasiliano ilipopokelewa na upande wa pili.


“Tuko karibu na lango ambalo nafikiri ndiyo unapopita unaelekea huko kwenye ‘flour’ ya chini tunakohitaji kwenda.. Sisi hatujastukiwa kabisa kama tumefika hapa ni mita chache tu na pia wao wanachojua na kuzuia ni nyie kusogea huku tunawasikia wakipokea maelekezo walinzi walio hapa na idadi yao kwa haraka tu huwezi kuhesabu maana wengine wamejificha hawaonekani kwa dhahiri” Akajibu kwa sauti ambayo msikilizaji utambua ananong’ona kwa sababu hayuko mahala salama.


ENDELEA NA PIGO ZA NONDO..!!


BUTWAA VII

SAN MARCOS-GUATEMALA

“…Hafadhali kwa hilo… Mmeweza kupiga hatua ambayo tulikuwa tunahisi ni changamoto kubwa kwetu, je hapo mlipo mnaweza kulifikia lango ikiwa ni hatua ngapi kwa kukadiria?” Akapongeza na kuhoji Agent Kai.


“Ni kama hatua ishirini tu ila walinzi wapo kwa kuanzia hatua kama kumi na moja kama si kumi na mbili toka tulipo”

“Mlijua wanalinda lango kwa kushuhudia likifungwa na kufunguliwa na watu kuingia na kutoka humo au liko wazi tu?”

“Kuna mtu alitoka humo… Linazibwa na moja ya safu za stake mbili zilizopangwa viroba vilivyo tupu kukiwa na meza kama tano kwa pembeni zikiwa na makopo ya rangi pamoja na mabrashi ya kuchorea juu hii ikimaanisha ni sehemu au kitengo cha waandishi na wachoraji wa viroba hivi ambavyo baadaye wanapaki kahawa iliyokwisha sagwa humo kama uonavyo stake zingine zikiwa na viroba vilivyokwisha wekwa kahawa..!”

“Mabomu ya kurushwa upande wenu hatujaona au kusikia kabisa mkitumia.. Hapo ndipo pakutumia hatuwezi kuendelea kuchelewa zaidi hapa..Tutaanza sisi kuwafanya wawaze huku tulipo ndipo nanyi mtafanya kuwastukiza kutokea mlipo”

“Ni kweli hatujatumia.. Mimi nilibeba matano sijatumia hata moja mpaka sasa na hata Silla ni hivyo hivyo pia, anzisheni tu nasi tutafanya kinachotakiwa kisha tutasogea ulipo mlango”

“Kazi njema!!”

“Nanyi pia!”

Walimaliza na kutakiana heri katika kinachofuata.


Dakika tatu mbele baada ya mawasiliano baina ya ‘TSC’ na Silla, kile kilichopangwa ndicho kilichotokea, milio ya bunduki mbili zikishambulia kutokea kwenye moja ya kona ya safu za ‘stake’ ilisikika ikimwaga njugu (risasi) na hata kuwadondosha baadhi ya walinzi waliokuwa wanazunguka kana kwamba hakuna hatari karibu na eneo ambalo walipewa maelekezo kuwa wahakikishe adui zao waliowavamia hapa katika kambi yao kutosogelea sehemu muhimu zaidi.


Pilika pilika za kujibu mashambulizi na hata kuchukua nafasi zilizo salama zilianza na kulifanya eneo lile liwe na vurumai na kelele zilizochanganya bila mpangilio watu na vitu, watu ikiwa ni baadhi maumivu zingine za mtu mwingine akimpa taarifa mwenzake wapi ashike nafasi au yupi apewe msaada maana risasi za kutoka kwa washambuliaji Agent Kai na mshirika wake Rebecca Smith hazikuwa zinachagua wa kumtwanga pale tu walipoinua bomba (bunduki) zao kuelekeza eneo walilopo walinzi wale.


Waliosalimika kutokana na mashambulizi yale ya kushtukiza walishika nafasi za kujiweka kando ya ‘stake’ zilizo pembeni ambazo zilikuwa na viroba, maiti kadhaa zikiachwa chini huku baadhi ya majeruhi nao wakisaidiana kujiweka mahala salama na yanapotokea mashambulizi wakiwa hawajui kwa nyuma yao wanaviziwa na watu wengine wawili, mashambulizi waliyoshambuliwa ni gelesha tu ingawa wenzao waliokuwa na bahati mbaya ya mti wa mkenge kutoota matunda wala mizizi yake na majani kutokuwa dawa (uliza waganga wote ila usiulize wachawi maana hawaeleweki), hawa walikatiziwa uhai wao na wengine kuachwa na maumivu makali ya majeraha ya risasi zilizowachana sehemu ambazo salama kiuhai lakini pia inaweza kuwa kwa muda tu huo uhai kama ujuavyo majeraha ya risasi utegemeana na sehemu mtu aliyopigwa na haina ya upotezaji wake wa damu mwilini.


‘TSC’ na Rebecca waliacha kushambulia wakarudisha miili yao kwa chini maana walipo mbele yao walipanga viroba vyenye kahawa, wakatizamana kisha wakakonyezana kwa kuinua vichwa vyao ishara ya mkonyezo inayokuwa ndani ya uso ilifichwa na sox walizovaa usoni, ishara hiyo iliwafanya kuondoka kwa kujiviringisha kwa pamoja kama tairi gari lililo mwendoni, maadui wakawaona kama vivuli vya paka vinapita kutoka pale kuelekea zilipo safu za ‘stake’, adui wawili kwa kasi wakashambulia risasi lakini kasi yao ya ufyatuaji risasi kwa iamrisha ‘trigger’ (kifyatulio) kwa vidole vyao haikuendana na kasi ya wahamaji wale waliokuwa sambamba wakienda kama sinema vile kwa wanaoshuhudia, walikoswakoswa wakafanikisha lengo lao.


Milipuko ya mabomu ya kutupwa ilianza kusikika ikipishana ‘booooom!, boooooom!, boooom!, booooom! Milio minne ikimaanisha viazi (mabomu) vinne vimetupwa eneo lile na kusababisha maafa kwa kiumbe kilicho pale, tena wakiwa wameshambuliwa kwa uwazi kabisa kutokea kwa nyuma na washambulizi waliowaweka kwenye ‘target’ kali kabisa hakuna aliyesalimika, maiti zilitapakaa, damu zilimwagika na vipande vya viungo vya viungo vya binadamu navyo havikukosekana kama ujuavyo mabomu yanapopata kile kinachotakiwa kupatikana na mtu aliyedhamiria kazi yake ifanyike.


Ukimya wa dakika tano ukashika hatamu hata wale waliokuwa wakilia maumivu kwa chini chini kuwa wamejeruhiwa kwa risasi na kina ‘TSC’ walipiga kimya, kimya cha kulazimishwa, kimya cha kurudisha haki ya roho zao mahala panapostahili kuwepo kwa milele si hapa duniani tupitapo, Rebecca akachungulia eneo lile, macho yakapokelewa na hali ambayo kama mwanamke mwingine pengine angetapika au kupiga kelele za uoga lakini kwake haikuwa hivyo ndiyo kwanza akageuka alipo Agent Kai kisha akamuonyesha alama ya dole gumba kuwa mambo safi.


“Sidhani kama kuna aliyebakia eneo lile”Akaongea S.S Rebecca wakitizamana na mshirika wake na boss wake kisha akatizama saa yake.


“Saa kumi na robo… Silla na Miller mnanisikia?” Akaongea Rebecca baada ya kutizama saa kisha akiuinua mkono ule wenye saa kuusogeza karibu na eneo la mdomo wake hili aweze kuongea na walio upande wa pili wakiwa wametengenishwa na safu moja iliyopangwa ‘stake’.


“Nakusikia Rebecca.. Hapa hatujaacha aliye mzima.. Sijui sehemu zingine huko..!” Akajibu Miller.


“Vizuri! Tumeona kazi nzuri mmefanya.. Sidhani kama kuna wengine nafikiri tuangalie jinsi tutakavyo weza kuingia mahala tunapohitaji kufika…!” Akaongea tena Rebecca kisha akatokeza toka walipo yeye na Kai ambaye naye alimfuata nyuma, kichwa kikizunguka huku na huko kunyata kwa kila hatua hakukuachwa kana kwamba wanaiogopa ardhi iliyosakafiwa pengine itatoboka kwa aina ya viatu walivyovaa.


Walipotokeza wote kwa ujumla wakawaona S.S Silla na Investigator Miller lakini na wao hawakuwa wamesimama tu nao walikuwa wanatembea tembea wakikagua kila maiti inayoonekana haina majeraha ya kuharibika miili pengine wataweza kuta mmoja mzima.


Rebecca aliyekuwa kamtangulia ‘TSC’ mbele alipokuwa anaruka kiroba aliona mwili wa mtu ukijivuta akaacha kupiga hatua na kusababisha hata Kai kusimama hatua mbili tu nyuma yake, hapo akakaza macho kuangalia kulikoni ndipo akashuhudia kiwili wili kilichokatwa eneo lote la kuanzia katikati ya mapaja kuja miguuni hivyo hana miguu yote miwili, alikuwa akimwaga damu kwa wingi na kufanya eneo lote analopita kwa nyuma yake kuwa na dimbwi la damu lakini hakuwa anapiga makelele ya maumivu alikuwa akijiburuza kuingia mahali ambapo aliamini anaweza kujificha asionekane.


Rebecca akamsogelea na kisha akamkanyaga matakoni kwa buti alizovaa akimkandamiza kwa nguvu kumfanya ashindwe kujongea mbele, majeruhi huyu nguvu za mguu unaokanamiza eneo la tako lake moja ulimfanya kuacha kujongea akatoa ukulele wa maumivu akitamani ajigeuze aweze kuuona uso wa aliyeamini ni mtu katili anayemuongezea maumivu zaidi.


“…Aaaaa..Aaaaah…Shiiiiih! nakufaaa.. Ni..Ni.. Nisaidieni jamani.. Nimeumia, nimeumia saaana..!” Akaongea kwa kilatini mtu yule mwili wake akitamani kuugeuza lakini hakuwa anaweza kujigeuza kama matamanio yake yalivyokuwa yanahitaji kufanya kwa hakika, Rebecca akaligundua hilo akatoa mguu kijamaa kwa kutumia mikono yake akajipindua uso wake ukiwa umejaa machozi wote, maumivu makali yaliakisi katika kila kilichopo usoni mwake kwa jinsi alivyoukunja uso wake kijana huu wa kizungu mwenye tattoo mbalimbali hadi usoni mwake.


“Ndiyoo! Umeumia sana… Pole sana.. Lakini wenzako karibu wote wamekufa… Ni mabomu ya kurushwa yamefanya hivi baada ya kurushwa na binadamu kama wewe.. Ni kweli unahitaji msaada wetu lakini nasi kabla hatujasema tunakusaidia vipi tunapenda nawe upate ujasiri wa kutusaidia kwa namna moja tu” S.S Rebecca akaongea kisha akatoa miwani aliyovaa machoni mwake halafu akapandisha juu sox ya kininja aliyovaa usoni aweze kuonana vizuri na anayeongea naye aliye ndani ya maumivu ambayo hakuwai kuota kabla kuwa ipo siku atasikia maumivu makali kama haya tena usiku mzito wenye baridi kali sana.


“Nisa..nisa..nisaidie da….da.. Nakufaaaa, nakufaaa, nakufaaa mi.. miye..nisaidie..!” Akaongea tena majeruhi huyu baada ya kuuona uzuri uso wa Rebecca, eneo hili lilikuwa na mwanga hafifu wa taa zinazotokea juu ukutani ambazo zilisalimika katika hali ya ajabu maana Kai na mshirika wake walikuwa wakishambulia huku wanazipiga risasi na taa kila wanapopata nafasi.


“..Huko tayari tukusaidie?” Agent Kai akamuuliza naye akiwa kapandisha sox aliyovaa juu ya kichwa na miwani yake kaishikilia mkononi.


“Ndi..Ndiyoooo..Macho yangu..Macho yangu… Nisai die eni..damu.. Nao nao nao na gi za” Kwa tabu akaongea, hapo haraka Rebecca akamuinamia akaikamata suruali ya mtu yule akaikaza kwa juu eneo zilipoishia zana zake za kazi ya kuongeza ukoo na starehe tamu isiyoisha utamu kwa watu wazima wenye afya zao, alimkaza bila kujali kijamaa kilivyokuwa kinalia na kukaza meno kwa maumivu makali ambayo sina uwezo wa kuyasimulia hapa.


“Msaada wetu wa kwanza ni huu.. Umenielewa? Ila upo wa pili wa kukukimbiza hospitali angalau uendelee kuishi hata kama hautakuwa na uwezo wa kutembea mwenyewe bila sapoti kama zamani… Lakini msaada wa pili unahitaji utayari wako wa msaada wako kwetu.. Jitahidi utuambie jinsi ya kuingia chini huko ilipo maana ya Tajumulco Camp?” Rebecca akaongea mdomo akiuweka karibu ya sikio la majeruhi.


“Nisaidieni kwa nza.. Ma..Ma cho haya hayana ngu u uvuu.. Nime ishiwa daa..!” Alishindwa kuendelea mdomo wake ulianza kuwa mzito, pilika pilika zake za awali kutumia mikono yake kuvuta mwili wake kwa nguvu toka mahala alipoona si salama akikutwa zilisababisha apungukiwe kwa haraka damu kuliko ambavyo kama angeamua kujituliza na kusubiri matokeo ya kijacho.


“Sema upesi.. Nakupa dawa ya kutuliza maumivu.. Tunafunguaje lango la kwenda chini?” Agent Kai naye alipiga magoti kisha kumuinamia mtu yule, magoti yakiwekwa kwenye sakafu iliyokuwa na dimbwi la damu pamoja na harufu kali ya damu, vinyesi vya binadamu na mautumbo yaliyotapakaa karibu kila baada ya hatua kadhaa eneo lote walilopo.


“Kwa…Kwa.. ka ka ka di” Alijitahidi kufungua mdomo lakini papi (lips) za mdomo wake hazikuweza kuongea zaidi, giza liliteka nuru ya macho yake fahamu zikamtoka, hapo Kai na Rebecca walisimama nakuona mbele yao wapo wenzao (Silla na Miller) wakiwaangalia na kulinda usalama pia.


“Kwisha habari yake.. Hawezi kupona.. Amesema kadi.. Je tunaipataje kadi?” ‘TSC’ akaongea na kuhoji swali ambalo hata yeye muulizaji aliamini wenzake wote hakuna atakayejibu.


“Twendeni mlipoona wakifungua kuingia na kutoka..!” Special Agent Rebecca akaongea kisha wote wakatizamana kwa zamu kifuatacho wakaanza kuongozana kuelekea ilipo ‘Stake’ ambayo ilikuwa imesambaratishwa kwa bomu na sasa iko fremu tupu ya chuma, maviroba yanawaka moto ambao ukiutizama unagundua muda si mrefu eneo hili lote litakuwa eneo lililotapakaa moto utakaounguza kuanzia kila kilichopo kisha eneo lote la jengo kama si majengo yote kama usipozimwa kwa haraka.


“Natamani tungekuja na mwanamke yule kiongozi Madam Mariana” Miller akaongea akiwa amesogea mahala ambapo ni ukutani kuna kisehemu ambacho kadi iliyosemwa na marehemu aliyeondoka muda si mrefu.


“Amepoteza fahamu akiwa hajakamilisha maelekezo yake kwa ufasaha.. Kadi.. Kadi.. Je kadi hiyo inashikwa na nani?” S.S Rebecca akaongea na kisha kumtizama Agent Kai ambaye alikuwa ndani ya tafakuri nzito akifikiri wanapitaje na hapa.


“Swali kuu lililo kichwani mwangu kwa sasa, je tukishafungua huko ndani kuna watu wa kiasi gani? Wamejiandaaje? Watatupokeaje?” Agent Kai akaongea na kisha kuuliza tena maswali ambayo uwa haana majibu kwa kweli mara nyingi uwa ni maswali ambayo yeye ujiuliza mwenyewe anapokuwa mahala kama hapa.


“Kazi kweli kweli… Jamaa walio ndani watakuwa wamejipanga haswa.. Tujaribu njia ya kulipua kwa bomu eneo la kumulika kadi kisha ya hapo tutajua tunafanyaje” Waza la Silla likasikika akasubiri kama litapita.


Ulipita ukimya wa sekunde kadhaa kisha fundi Agent Kai akasogea kilipo kifaa kinachopokea kadi maalumu ya kumulika kisha ndiyo kiruhusu lango kufunguka, alipokifikia akakitizama kwa muda wa dakika moja kisha akainua kitako cha bunduki akakita kwa nguvu, mkebe wa juu ukaachia na kudondoka kukaonekana ndani yake huku vicheche kadhaa vikitokea, hapo akaacha sekunde chache kutulie kwakuwa mikononi alikuwa amevaa gloves hakusita wala kujiuliza mara mbili akazikamata nyaya zinazosababisha mawasiliano ya hapa nazo zilibaki vidoleni akiwa kazishika macho akifanya usahili kwa umakini mkubwa sana komando huyu mwenye kichwa chenye ufukunyuku uliobobea kama si utundu usio na hasara toka utotoni mwake.


Nyaya aliweza kuzisoma kwa umakini zikimrudisha miaka kadhaa nyuma wakati wa mafunzo ya vitendo ya kufungua milango kama hii, alitulia akiweka sawa kumbukumbu zake kisha akaanza kuzivuta zitoke kwa juu kidogo, akatoa kisu toka mfukoni mwake.


Shughuli ya kielekroniki ikaanza akizifumua nyaya zile kisha akaziunganisha kivingine ajuavyo yeye tofauti na ilivyokuwa mpaka ilipofika mahala alipopataka, yaani laiti kungekuwa hakuna baridi kali kama lililopo eneo hili la safu ya milima ya Tajumulco na eneo la nchi nzima ya Guatemala kwa ujumla msimu huu basi kijasho kingemtiririka vya kutosha na kumlowanisha mwili mzima.


Nyaya ziliwekwa katika mfumo mpya lakini mfumo ambao ungeleta jambo ambalo yeye au wao wanauhitaji kwa wakati huu, alipomaliza akatoa kifaa kwenye moja ya mifuko ya pembeni ya begi lake mgongoni, kifaa kilicho kama pima simu kwa wale mafundi wa simu za mkononi ambacho utumika kupima uzima wa simu pale fundi simu anapopelekewa simu ya kutengeneza inapoharibika na wateja zake.


Kifaa kile kiliweza kumtambulisha nyaya zile zipi akizigusanisha kwa kuambatana na kifaa basi ataweza kuamrisha jambo, akaunganisha kisha akabonyeza vitufe kadhaa mara ukuta ukaanza kujiachia kwa kupanda juu eneo la upana mkubwa wa kuweza kupita gari kubwa kama basi tena zikipishana, haraka kwa kuendana na kasi ya ufungukaji Special Agent Rebecca na Silla wakakimbilia wakawe pembezoni mwa ukuta huku Agent Kai na Investigator Miller wakibaki kwa upande huu ilipo swichi waliyoifanyia mambo ya kiintelejensia lango kufunguka.


Mwisho wa sehemu ya tisini na moja (91)


Maisha ya majasusi hawa yatakuwaje baada ya kufanikiwa kukisambaratisha kikosi kilichokuwa kikilinda eneo la ndani ya godown (ghala) la uhifadhi wa kahawa?


Je nini kitatokea ndani ya eneo paniwa na timu inayoongozwa na Agent Kai?

Kuna mafanikio gani na kitu gani kitakutwa huko na hata kutokea?


Majibu ya maswali yote haya yatakuja katika sehemu inayokuja na zinazokuja katika hatua za mwisho mwisho za jino kwa jino.





ILIPOISHIA SEHEMU YA 91…!!

Ulipita ukimya wa sekunde kadhaa kisha fundi Agent Kai akasogea kilipo kifaa kinachopokea kadi maalumu ya kumulika kisha ndiyo kiruhusu lango kufunguka, alipokifikia akakitizama kwa muda wa dakika moja kisha akainua kitako cha bunduki akakita kwa nguvu, mkebe wa juu ukaachia na kudondoka kukaonekana ndani yake huku vicheche kadhaa vikitokea, hapo akaacha sekunde chache kutulie kwakuwa mikononi alikuwa amevaa gloves hakusita wala kujiuliza mara mbili akazikamata nyaya zinazosababisha mawasiliano ya hapa nazo zilibaki vidoleni akiwa kazishika macho akifanya usahili kwa umakini mkubwa sana komando huyu mwenye kichwa chenye ufukunyuku uliobobea kama si utundu usio na hasara toka utotoni mwake.


Nyaya aliweza kuzisoma kwa umakini zikimrudisha miaka kadhaa nyuma wakati wa mafunzo ya vitendo ya kufungua milango kama hii, alitulia akiweka sawa kumbukumbu zake kisha akaanza kuzivuta zitoke kwa juu kidogo, akatoa kisu toka mfukoni mwake.


Shughuli ya kielekroniki ikaanza akizifumua nyaya zile kisha akaziunganisha kivingine ajuavyo yeye tofauti na ilivyokuwa mpaka ilipofika mahala alipopataka, yaani laiti kungekuwa hakuna baridi kali kama lililopo eneo hili la safu ya milima ya Tajumulco na eneo la nchi nzima ya Guatemala kwa ujumla msimu huu basi kijasho kingemtiririka vya kutosha na kumlowanisha mwili mzima.


Nyaya ziliwekwa katika mfumo mpya lakini mfumo ambao ungeleta jambo ambalo yeye au wao wanauhitaji kwa wakati huu, alipomaliza akatoa kifaa kwenye moja ya mifuko ya pembeni ya begi lake mgongoni, kifaa kilicho kama pima simu kwa wale mafundi wa simu za mkononi ambacho utumika kupima uzima wa simu pale fundi simu anapopelekewa simu ya kutengeneza inapoharibika na wateja zake.


Kifaa kile kiliweza kumtambulisha nyaya zile zipi akizigusanisha kwa kuambatana na kifaa basi ataweza kuamrisha jambo, akaunganisha kisha akabonyeza vitufe kadhaa mara ukuta ukaanza kujiachia kwa kupanda juu eneo la upana mkubwa wa kuweza kupita gari kubwa kama basi tena zikipishana, haraka kwa kuendana na kasi ya ufungukaji Special Agent Rebecca na Silla wakakimbilia wakawe pembezoni mwa ukuta huku Agent Kai na Investigator Miller wakibaki kwa upande huu ilipo swichi waliyoifanyia mambo ya kiintelejensia lango kufunguka.


ENDELEA NA MAPIGO YA NONDO…!!


BUTWAA VIII

SAN MARCOS-GUATEMALA

Uwazi ulikuwa kwa kila macho ya mmoja wao, kila mmoja aliweza kuona kwa macho yake korido fupi yenye urefu wa hatua tano kuingia ndani kisha mwisho wake ni ukutani hii ikiwa kwa mbele yao kwa uwezo wa macho yao.


Agent Kai aliwatizama kwa zamu wenzake kisha akautokeza mwili kutoka kwenye kona aweze kuvusha kichwa kupita kiambaza ambako sasa aliweza kuona korido ikiendelea kiupande hapo akashawishika kutaka kuchungulia korido inaendeleaje lakini mwili wake ulipingana na anachokiwaza kimipango hapo akatoa begi lake toka mgongoni kwa mara nyingine tena.


Ndani ya begi akatoa kifaa kidogo kilicho na darubini ya kuchukua ama kuangalia matukio ya moja kwa moja akakifanyisha kiweze kufanya kazi yake kwa kukiwasha kisha akakitokeza kwa chati kiweze kuchukua ama kudukua taarifa za moja kwa moja (live) upande wa pili yeye akiwa anaangalia kutokea pale pale kwenye chati ya kona aliyosimama pembezoni mwa lango kuu ama mdomo kama walivyokuwa wakiuita kuwa ni mdomo wa Tajumulco Camp.


Upande ule hakuweza kuona kiumbe chochote ila kulikuwa na mwanga mkali wa balbu na korido inayoendelea mbele kidogo kisha kuna uwazi unaotumbukia chini mbele ukuta hapo kiujuziwa majengo aliweza tambua kuna ngazi zinazoshuka chini, aliendelea kuchunguza kila anachokiona kwa umakini mkubwa sana mpaka akaweza kugundua jambo katika balbu ile iliyo upande ule inayoleta mwanga wake mpaka eneo hili kuwa si balbu tu pia ilikuwa ni cctv-balbu inayochukua matukio eneo hili lote mtu au chochote kikitokea basi balbu hii yenye kamera ya cctv ilikuwa ikichukua na kupeleka taarifa kwa wafuatiliaji iwe imeunganishwa na skrini au hata simu kulingana na aliyefunga alivyotaka.


‘TSC’ akarudisha kifaa kile kwenye begi lake wenzake wote walikuwa wakimuangalia tu pia wakiangalia kwa umakini na sehemu zingine iwe nyuma yao au mbele wakiwa na silaha zao kwa umakini wanasubiri maelekezo toka kwa mtu waliyekuwa wakimuamini kuwa ndiyo nahodha wao wakifuata na kutii kila elekezo lake kama inavyokuwa jeshini kwa kamanda mkuu anavyoongoza kikosi uwa inatakiwa kwa wengine kumtii na kufuata maelekezo yake bila kujali umri au hata akili za ziada shida ni yeye kuaminiwa tu kuongoza kikosi husika na cheo alichonacho ndiyo awa kwa Agent Kai walikuwa hivi na pia walipenda sana kufuata maelekezo yake kwakuwa walikuwa wanamuamini na kuamini kila alisemalo kuwa lina mantiki na uzoefu pia.


Bunduki ilikamatiwa vizuri mikononi mwake kisha akaonyesha ishara iliyoeleweka kwa wote kuwa ana jambo anataka kufanya wenzake wakaielewa ishara ile wakajibu kwa pamoja alama ya dole kuwa ruksa yeye kufanya kile anachokusudia, Kai alitokeza nusu mwili mdomo wa mtutu wa bunduki ukitangulia mbele ukiwa umeinuka sawia tayari kufanya jambo ambalo alikuwa amelikusudia paaap shabaha kali kutokeza tu mtutu wa bunduki ulitema cheche ukiachia risasi moja tu kana kwamba alikuwa ameilenga taa kwa kuiangalia dakika moja, taa ilivunjika giza likashika hatamu kisha jamaa kwa kasi ile ile akarudisha mwili alikotoka kusikilizia kifuatacho kama ni habari mpasuko (breaking news) ama habari kamili.


Hapo wakaangaliana na wenzake kisha akawaonyesha ishara kuwa watulie kwanza wasikurupke kusonga mbele kwakuwa tayari katika kichwa chake aliamini utulivu uliopo hapa una jambo na jambo hilo ni jambo madhubuti litakaloweza kuwaathiri wasipokuwa katika hali ya kuchukua tahadhali yenye umakini ndani yake, lakini jambo moja muhimu kwa mafundi wakutanapo uwa hakiharibiki kitu hasa mafundi wanaosapotiwa na sayansi ya teknolojia ya hali ya juu iliyopo katika vyombo vya kiusalama na kijasusi vya nchi kubwa iliyopiga hatua kubwa katika mambo ya kiitelejensia kama Marekani, begi lililetwa mbele kisha fundi ama binadamu mwenye nyayo zisizotoa sauti hawapo sehemu za mapambano alitoa ipad ndogo toka kwenye begi lake dogo lakini uwa na vifaa mpaka waweza kujiuliza bwana mkubwa huyu ruka ruka zake na mibingiriko yake inayoambatana na mibingirisho uwa havunji vifaa hivi? Jibu ni kuwa vifaa hivi vimetengenezwa katika hali ya kuwa na ugumu mkubwa sana wa kuzuia kuharibika kwa wepesi kwa sababu watengenezaji hawakukurupuka walitengeneza kwa ombi maalumu toka taasisi kuu ya kijasusi ya Marekani kwa ajili ya watu wake kama hawa kina Agent Kai.


Ipad ilitangulia kutoka begini ikifuatiwa na ki drone kidogo hiki ni kifaa maalumu kwa kuchukua picha na matukio mengine kama ni video na mengineyo kama haya kikiongozwa kuruka kama helkopta maana uwa na upanga juu unaokiwezesha kuruka na si lazima kikafanye kazi ya kupiga picha ama kuchukua video uwa kinafanya na kazi zingine kulingana na mtumiaji ametaka kifanye kazi gani kwa wakati huo hata wizi wa kuiba kitu kitakachoweza kubebeka kwa uzito unaofanana nao uwa inawezekana, hapa tutaona ‘TSC’ alitaka kufanya nini?.


Aliwasha kifaa hiki ‘dronne’ kisha akaunganisha haraka na ‘Ipad’ kimfumo kisha akakiiweka chini ‘dronne’ ikiwa tayari panga zake zinazunguka yeye akatumia ‘Ipad’ kuanza kuongoza kufanya kile anachohitaji ikiwa anaona kinavyopaa katika moja ya sehemu kipande cha juu cha ‘ipad’ na kipande cha chini anaona kinavyochukua kila kitu inachokipita kwa mtindo wa video, kiliruka mpaka eneo linakoanzia ngazi akapeleka kikaleta kuanzia ngazi ya kwanza ya juu kushuka chini mtaalamu akawa anafuatilia lakini hakuwa anafuatilia mwenyewe tu aliye pembeni yake Investigator Miller naye alikuwa akifuatilia, ngazi zilikuwa zikishuka kwenda chini kwa kirefu tu mpaka karibu na mwisho kulionekana mwanga wa taa na aina ya mwanga wake ilikuwa kama balbu iliyovunjwa hapa mwanzo muda si mrefui hivyo balbu hizi zilikuwa ni balbu zinazofanana ‘cctv-balbu’ hapo ‘dronne’ ilichezeshwa chezeshwa kutafuta kuna nini kinachoweza kuwa kikwazo kwa wao kusogea ‘TSC’ akiogopa kusogea unakotokea mwanga kwakuwa tayari kulikuwa na dalili kuwa kuna watu.


Kwa kasi akakiongoza kurudi kilipotoka kifaa hiki ‘dronne’ aliporudisha kwenye begi vyote hivi akamtizama Miller kisha wakatabasamu.


“Ukimya unatisha sana.. Ila hatujaja kuogopa vitisho twendeni… Tutangulia mimi na Miller kwakuwa ndiyo tumeshatangulia kuona njia ilivyo ingawa nahisi kuna hatari sana tuendako hivyo tahadhari itatakiwa kuwa mara kumi ya ilivyokuwa mwanzo wa ndugu” Akaongea Agent Kai kwa sauti ambayo wote waliopo hapa waliisikia vizuri na kuelewa lakini endapo ungekuwa upo hatua saba nyuma sidhani kama ungemsikia au kama ungesikia sidhani kama ungeelewa kwa maana kama ujuavyo wa Marekani kiingereza chao na kasi yao katika uongeaji ni shida.


Bunduki aina ya M240 Machine Gun ilikamatiwa barabara mdomo wake unaotoa chuma kidogo ambacho kikiruhusiwa kutoka uwa kinatoka kwa kasi na kwenda umbali ulioagizwa kutokana na aina ya kitu kilicholengwa kilivyo na umbali wake iwe karibu zaidi na hata umbali wa hatua kadhaa huku kwa watu ambao kama Agent Kai ikiwa washaonja ladha ya chuma (risasi) inaporindima na kupenya katika nyama ya mwili, ladha ya ubaridi wenye maumivu makali sana hasa inapopenya katika mfupa iwe kuuvunja (kuupasua) ama kingine chochote kinachofanana na icho na hata kuugusa tu mfupa kama si kupenya na kuweka makazi humo, hatua za kunyata ilikuwa ni jadi kwa ‘TSC’ katika maisha yake ya kikazi na pia kikawaida kwake kutembea ananyata ni mazoea kabisa yanayokuwa yanawashangaza wengi ikiwemo watu wa familia yake pamoja nao rafiki zake, ajabu lililoweza kumstaajabisha mwanadada kijacho wetu Shufania Mahamud a.k.a Mrs Kai, kisha akalizoea ajabu hilo akiona ni kawaida sasa akiamini naye anatakiwa kuiga utulivu huo wa kutembea akiiheshimu ardhi anayoikanyaga.


Hakutembea ilihali akinyata akiwa katikati ya korido toka upande na upande bali alitembea mwili wake upande wa bega la kushoto ukiwa unasugua ukuta huku kulia kwake kwenye ukuta mwingine unaounda hii korido akiwemo Investigator Miller naye akijitahidi kunyata kimafunzo kama anavyonyata ndugu yake kikazi na nahodha wao Agent Kai wakiwa sambamba kihatua ikiinuka ya mguu wa kulia ya huyu basi na upande wa mwingine naye aliinua hatua ya mguu ule ule kusonga mbele silaha mbele tayari kwa matumizi.


Walisogea hadi zinapoanza ngazi zinazoshuka huku walipo wakiwa kwa juu hivyo wakitakiwa kuteremka chini kuzifuata zinavyoelekea, wakatizamana kwa macho yao yaliyo ndani ya miwani iliyoundwa kwa teknolojia ya hali ya juu waliyovaa ikiwasapoti kwa hali ya juu, kuangaliana kwao huku nyuso zao zikiwa zimefunikwa kwa mask haikuwazuia kufanya mawasiliano kwa ishara kuwa yeye Agent Kai atashuka mwenyewe hadi mwisho wa ngazi na Miller abaki pale juu akisubiri kwanza.


“Bismillah!!” Akasema kwa sauti ya kifuani aliyoisikia yeye mwenyewe akimaanisha anamtanguliza mola mbele kisha taratibu kama anaziogopa ngazi akaweka mguu wa kwanza wa kulia ukasimama kwa sekunde mbili kisha akaiunua ukasonga ngazi inayofuata kushuka ukanyanyuka wa kushoto, mtembeo mnyato ulikuwa ukienda ‘step by step’(hatua kwa hatua) anashuka macho mbele kwenye kona inayoonekana lakini kwa upeo hana analoweza tambua wapi inaelekea.


Alipokuwa akikaribia ngazi za mwisho kengele ya tahadhari ikagonga kichwani mwake kwa ishara zilizojenga mazoea ndani ya mwili wake pale anapoiendea hatari zaidi awapo mahala pa hatari, misuli iliyojengeka kwenye tumbo lake (six packs) kutokana na mazoezi makali ya tumbo anayoyafanya ilianza kukaza na kumletea hali zoea kwake kuwa kifuatacho kitakuwa si habari ‘mpasuko’ bali ni habari kamili, harufu ya damu ilifuatia ikirindima ndani ya tundu za pua zake ingawa hakukuwa na umwagaji damu kwa wakati huo eneo hili la ngazi, hali hii ni kama hali barikiwa aliyonayo binadamu huyu mwenye maajabu yake.


Mwili na akili vilishirikiana kupeana muongozo way eye Agent Kai kutosogea zaidi ya pale ikiwa zimebaki ngazi tatu tu kufika mwisho wa ngazi, alizidi kujiegemeza katika ukuta kana kwamba anausukuma kwa mgongo, kichwa alikigeuza juu alikotokea macho yake yaliyo ndani ya miwani yakawaona wenzake wawili sasa aliyekuwa kaongozana naye kama utaratibu mpango wao ulivyokuwa ukisema Investigator Miller aliyeshuka kidogo ngazi tatu kwa nyuma yake akiwa kaongezeka Special Agent Rebecca.


Aliporudisha kichwa anapohitaji kujongea ndipo kile alichokuwa akikifikiri kilisikika kwa mbali katika masikio yake, kengele iliyokuwa ikigonga kuwa aongeze umakini iliweza kutimiza dhamira yake, aliweza kusikia mlio wa kitu anachokijua ni mlango ukifunguliwa au kufungwa katika hali ambayo mfunguaji au mfungaji alikuwa akitaka asisikike kama anafungua au anafunga mlango hii iliweza kumjuza ‘TSC’ kuwa kikorido hiki cha mwisho baada ya ngazi zilizomleta hadi hapa kuna kona inayoelekea ulipo mlango ambao hakuwa anaujua yeye kama yeye kuwa unaelekea wapi?.


Jasusi mbobezi aliyebobea kwenye fani hii ya giza aligeuka tena kwa mara ingine juu walipo wenzake kisha akaonyesha ishara iliyoeleweka kwa wenzake lakini aliporudisha kichwa hili afanye kile alichowaelekeza kitu kama kopo la bati kilitupwa kwenye korido hii ndogo na kilipojipiga tu kwenye ukuta kikafunuka mfuniko wake, hatari! Macho yalimtoka Agent Kai akili ikfanya kazi kwa kasi kubwa sana akaruka hatua moja kilipo kikopo kile kikionyesha ishara ya kuanza kutoa moshi wake kusudiwa na aliyekirusha kwenye kibaraza cha korido ya mwisho wa ngazi, kidume alipokifikia akatupa macho kwa kasi kule kilipotokea hapo alishuhudia mlango wa vioo mkubwa usionyesha upande wa pili ukimalizikia kufungwa na mtu aliyerusha kikopo hiki, Agent Kai akainama na kukiokota kikiwa kimeanza kutoa moshi wake ilikuwa inahitajika spidi kubwa kudhibiti hili kopo na kwakuwa mikononi mwake alikuwa kavaa gloves cha kwanza akaziba kwa nguvu moshi usitoke kwa kutumia kiganja cha mkono wake wa kulia huku wa kushoto ukiwa umelikamata kopo kwa spidi akiwa kalishika akakimbia kupanda ngazi juu walipo kina Miller ambao na wao walikuwa washaelewa nini anachofanya mwenzao licha ya kuwa hakuwa ameongea chochote zaidi ya vitendo tu.


Alikuwa kopo ambalo yeye Agent Kai au wenzake wote kwa ujumla ambao wasingeweza kujua ni kopo la nini na madhara gani yatatokea likiachwa bila kushughulikiwa kama alivyoamua kulishughulikia mzee wa kazi, mbio zile zilikwenda akiwapita wenzake akatokea korido ya juu huko akamkuta Special Agent Silla ambaye alistuka sana na kutaka naye akimbie lakini kusimama kwa Rebecca tena akimpisha Kai kulifanya asimame macho yakielekezwa mikononi mwa Agent Kai.


“Nifuate Silla…Sumu ya ngozi.. Wajinga wana silaha hadi za sumu kama hizi..” Agent Kai hakumpita hivi hivi Silla akampa taarifa ikiwa pia amemuomba amfuate.


Walitoka wakiwa katika hali ya mbio vilevile mpaka kwenye lango mdomo walilopita, breki ya kwanza ikawa kwenye moja ya stake ya viroba vya kahawa.


“Inua viroba viwili vya juu..” Kai akamuomba na Silla akafanya vile vile akiinua viroba viwili kisha ya hapo ‘TSC’ akaingiza kopo lile katikati akatoa kiganja kilichokuwa kinazuia moshi usiendelee kutoka, viroba vikaachiwa na kufunika kopo lile kwa ndani.


“Sumu itasambaa na kuweza kudhuru sisi ama watu wengine… Maana hii ni hewa ya moshi sumu kapteni..” Alikuwa swali lakini kwa alivyoongea yoyote angeweza tambua ni kama swali linalohitaji majibu kwakuwa liliulizwa kitaalamu pia.


“Kuzuia hili tulipue au kuwasha moto eneo hili lote moshi wa viroba, kahawa na mambo mengine yatajichanganya pamoja na kupunguza nguvu yake”. Agent Kai akaongea akiwa anazungusha macho yake kuangalia kila eneo upande na upande kuona anachosema kama kitakuwa nma faida isiyo na madhara kwao.


“Lakini ni hatari upande wetu kwakuwa hatuwezi umeme unaweza kuleta madhara ya kufika kwa kiasi gani toka eneo hili hadi ndani tunakofikiri ndiyo kutakuwa salama kwetu” Silla akakubali wazo lakini akaweka wazo lililofika kichwani mwake ikiwa naye anakagua mazingira kama anavyofanya ‘TSC’.


“Nafikiri tutatambua huko huko ndani… sisi ni wanajeshi, majasusi wabobezi hatuwezi shindwa pata sehemu ambayo tutajiweka kiusalama hivyo tufanye lililo mbele yetu bila kujali hasara ya wapinzani wetu ambayo hasara yao ni faida kwetu” Akajibu Agent Kai kisha ya hapo akatoa kiberiti cha gesi katika moja ya mfuko kati ya mifuko mingi iliyo katika suruali aliyovaa.


Dakika tatu mbele moto ulikuwa umeanza kuwaka eneo hili, wawashaji wakikimbilia ndani walikotoka ambapo sasa mstari wa mbele kabisa eneo alilokuwa yupo Agent Kai kabla hajaokota kopo la moshi wa sumu sasa alikuwa kasimama Investigator Miller kuja kwa juu yupo Rebecca, ‘TSC’ alimpita Rebecca akateremka hadi chini kabisa sasa akienda kwa upande wa kushoto hili kulia aendelee kuwa Miller.


“Tumewasha eneo la juu moto tukijumlisha na ule moto wa mabomu ya kurushwa hivyo huko juu ndani ya godown muda wowote kutakuwa na mwanga mkali kama mchana wa jua kali kwa mwanga wa moto… Ima tufanye kazi iliyotuleta” Akaongea kwa kasi Agent Kai, wakaangaliana na Miller sababu iliyowafanya waangaliane ilikuwa ni kusikika mlango uliofungwa ukifunguliwa kwa funguo kwa hali inayoonyesha mfunguaji amechukua tahadhali ya hali ya juu asiweze kusikika sema tu tundu la funguo lilikuwa ni tundu kavu lililojaa unafiki wa kutovumilia utaratibu na ukimya.


Haraka Agent Kai aliruka kwa spidi kubwa hatua moja ndefu kana kwamba anaruka mfereji wenye upana wa mita kadhaa hali iliyoweza mshangaza hata Miller tena bila kishindo wakati nyayo zake za miguu yake yote miwili inatua haikutoa kishindo chochote maana alinata vizuri pembeni ya mlango unaofunguliwa akageuka kasi kumuangalia Miller kisha akamuonyesha ishara arudi kwenye kona kujificha amuache yeye peke yake pale.


Mwisho wa sehemu ya tisini na mbili (92)


Mambo ni moto! Agent Kai na wenzake wakiwa wanatafuta mbinu ya kuingia mahala ambapo hakuna hata siku moja tokea ngome yaTajumulco Camp inajengwa aliwai kuingia mtu asiyehusika.


Je kutatokea nini kwa majasusi hawa na watu walio ndani ya ngome husika?


Tusogee mbele kujua mengi zaidi.



“Lakini ni hatari upande wetu kwakuwa hatuwezi umeme unaweza kuleta madhara ya kufika kwa kiasi gani toka eneo hili hadi ndani tunakofikiri ndiyo kutakuwa salama kwetu” Silla akakubali wazo lakini akaweka wazo lililofika kichwani mwake ikiwa naye anakagua mazingira kama anavyofanya ‘TSC’.


“Nafikiri tutatambua huko huko ndani… sisi ni wanajeshi, majasusi wabobezi hatuwezi shindwa pata sehemu ambayo tutajiweka kiusalama hivyo tufanye lililo mbele yetu bila kujali hasara ya wapinzani wetu ambayo hasara yao ni faida kwetu” Akajibu Agent Kai kisha ya hapo akatoa kiberiti cha gesi katika moja ya mfuko kati ya mifuko mingi iliyo katika suruali aliyovaa.


Dakika tatu mbele moto ulikuwa umeanza kuwaka eneo hili, wawashaji wakikimbilia ndani walikotoka ambapo sasa mstari wa mbele kabisa eneo alilokuwa yupo Agent Kai kabla hajaokota kopo la moshi wa sumu sasa alikuwa kasimama Investigator Miller kuja kwa juu yupo Rebecca, ‘TSC’ alimpita Rebecca akateremka hadi chini kabisa sasa akienda kwa upande wa kushoto hili kulia aendelee kuwa Miller.


“Tumewasha eneo la juu moto tukijumlisha na ule moto wa mabomu ya kurushwa hivyo huko juu ndani ya godown muda wowote kutakuwa na mwanga mkali kama mchana wa jua kali kwa mwanga wa moto… Ima tufanye kazi iliyotuleta” Akaongea kwa kasi Agent Kai, wakaangaliana na Miller sababu iliyowafanya waangaliane ilikuwa ni kusikika mlango uliofungwa ukifunguliwa kwa funguo kwa hali inayoonyesha mfunguaji amechukua tahadhali ya hali ya juu asiweze kusikika sema tu tundu la funguo lilikuwa ni tundu kavu lililojaa unafiki wa kutovumilia utaratibu na ukimya.


Haraka Agent Kai aliruka kwa spidi kubwa hatua moja ndefu kana kwamba anaruka mfereji wenye upana wa mita kadhaa hali iliyoweza mshangaza hata Miller tena bila kishindo wakati nyayo zake za miguu yake yote miwili inatua haikutoa kishindo chochote maana alinata vizuri pembeni ya mlango unaofunguliwa akageuka kasi kumuangalia Miller kisha akamuonyesha ishara arudi kwenye kona kujificha amuache yeye peke yake pale.


ENDELEA NA MAPIGO..!!


BUTWAA IX

SAN MARCOS-GUATEMALA

Mlango ulifunguliwa kwa chati na tahadhali ya hali ya juu ukiachwa uwazi mdogo sana wa mtu kuchungulia na ndipo mdomo wa mtutu wa bunduki ukaanza kutoka ukishuhudiwa na Agent Kai aliye pembeni upande wa kulia wa mlango aliacha kuona mtu huyo aliyetanguliza mtutu wa bunduki aendelee kutokeza kichwa kwakuwa michezo hii yeye si migeni nayo.


Ilipoanza kutokea mikono iliyokamata bunduki, mikono iliyovaa gloves na jaketi rangi nyesusi alilolikunjia kwenye viwiko, kikafuatia kichwa komwe likitangulia hapo Agent Kai hakusubiri pua ndefu ya kizungu iliyokuwa ikianza kutokea isogee zaidi hili macho yaweze kuona anapotaka kuona mtu yule kwa kutumia mguu wa kushoto alikita kwa nguvu mikono akilazimisha katika mkito huo mtu huyo avutwe kuifuata bunduki yake iliyokamatwa na mikono na kama alivyohitaji mwili ulivutwa na nguvu ya mkito wa mguu wa fundi mapigo, akatokeza mabega yote akifuatiwa na mwili uliojipigiza mlangoni na kuufanya mlango ufunguke ukimuumiza maeneo ya mkono wa kulia kwa kumuacha na michubuko kati ya kiwiko na kiganja.


Njemba ilistuka kwa shambulizi la kustukiza kujikuta anavutwa kwa nguvu kwenda nje alijitahidi kujizuia lakini teke mkito alikupigwa na mtu ambaye hajui pigo analotoa lina maana gani ni pigo tu ilimradi limepigwa ilikuwa kama mchezaji mzuri wa soka kama Messi anapokuwa anapiga chenga karibu na goli uwa tayari kashajua nini kitafuata na kikizuiliwa atafanya nini na kikitimia atafanya nini, shingo ya adui ilianikwa ikitokeza kwa kasi papo hapo ‘TSC’ akitumia kitako cha bunduki aliikita shingo ya mtu Yule eneo la pembeni ya shingo lakini karibu kabisa na koromeo, pumzi zikaziba ukiunganisha na mshtuko aliokuwa nao uhai wake ulikuwa unacheza kwenye uzi mwembamba alitoa mguno tu na kudondoka kifudi fudi miguu yake sehemu ya kisigino ikizuia mlango kufunga ukabaki wazi nusu.


Risasi za kufuatana zilichapwa kutokea kwa ndani tena milio ya bunduki zinazotumika kupiga risasi zilikuwa kwa wingi bila mpangilio wakipiga kulenga eneo la wazi la mlango na nyingine zikipiga mlango huu wa vioo na fremu ya alluminium na kuvunja vunja muonekano wake, kama paka aliyejikunyata mvua Agent Kai akiwa ameng’ata meno kwa nguvu kutokana na kelele za milio ya bunduki zinazorusha risasi, alijisimamisha kwenye kona ya pembeni ya mlango kana kwamba mlingoti wa goli (nguzo chuma) akiwa sambamba na kaupana kadogo cha ukuta kanachoshika mlango.


Milio ilikata kwa pamoja kana kwamba wapigaji wameambiana waache kushambulia, kule kwenye kona ya kujia huku mlangoni zinapoishia ngazi zinazojia huku mlangoni sasa kulikuwa na majasusi wote watatu wa kimarekani, Miller akachungulia kuona ndugu yao Agent Kai ana hali gani ingawa hakuwa na wasiwasi juu ya uzima wake pamoja na milio ya risasi zilizokuwa zikipigwa kama mvua inanyesha, alimuona ndugu yao akiwa kasimama kwenye kiukuta kile akiwa kanyooka kimya kabisa hata kutingishika hatingishiki mkononi akiwa na silaha yake tayari kwa matumizi lakini macho ya Ivestigator Miller yalishuhudia mwili ukiwa umelala chini mbele yake pale chini kukiwa na bunduki aina ya Norinko QBZ-97 ikionekana muda kabla hajadondoshwa chini kilazima alikuwa ameikamata bunduki na aliyefanya kazi hii lazima ni kapteni wao ‘TSC’.


Kwa ndani ya mlango ulikochakazwa kutokea pale alipo Miller anapochungulia akiwa kainama chini kabisa aliweza kuona kukiwa giza lakini si giza totoro la kufanya mtu asiweze kuona kulivyo hasa kwa yeye na hata wenzake wote wanaotumia miwani ya kazi za kazi hivyo eneo likiwa kama kaunta ya hoteli jinsi kulivyo.


Agent Kai pale alipo aliweza kumuona Miller akiwa katokeza kichwa chake kwa chati kutokea kwenye kona ya ukuta kwa chini kabisa kama paka anayechungulia, wakaangaliana akamuonyesha ishara kuwa wazungumze kwa ishara hivyo atokeze mikono lakini kabla hajaendelea Miller akamuonyesha ishara kuwa kwa ndani hakuko sawa wapo waviziaji walio tayari kudungua chochote kutokea hukohuko.


‘TSC’ akamuelewa hivyo akamwambia atulie afanye jambo akitanguliwa na kutizama saa yake iliyomfahamisha ni saa kumi na dakika tano usiku, alileta begi lake mbele haraka akalifungua na kutizama ndani kuona kipi anaweza akakichukua kikaleta tofauti na kuwasaidia wao wote kwa ujumla kufanya humu hakuona kinachoweza endana na mtizamo wake wa haraka, hapo akalifunga na kulirudisha mgongoni, akajisachi mifuko ya pembeni eneo la chini ya magoti katika suruali ya kazi aliyoivaa hapo akatabasamu tabasamu kavu alikutana na kitu ambacho kifikra aliamini kitasaidia na kuleta mabadiliko yatakayowafanya waendelee mbele, alikuta kiazi (kibomu) cha kurushwa kikiwa kimoja kati ya viazi kadhaa alivyobeba wakati anakuja huku Tajumulco, San Marcos.


Utulivu mkubwa ulikuwa ukiendelea kana kwamba maeneo haya hayana watu wenye nia mbili za tofauti na hata huko juu ya eneo hili lilipo godown la kahawa na viroba kuna moto unawake.


Pin inayozuia bomu la kurushwa kulipuka ilitolewa kwa kuvutwa kwa meno likiwa mkononi mwa Agent Kai kisha ya hapo akamuonyesha ishara kadhaa za maelekezo Miller tokea kule alipo ambapo pamoja na kuwa alikuwa amejificha kwa kujilaza chini ya sakafu kichwa kikichungulia kwa kutokezwa eneo la paji la uso, miwani aliyovaa ilimsaidia kumvuta ndugu yake na kufanya naye mawasiliano kwakuwa wote walikuwa wakionana kwa ukaribu kwa kusaidiwa nah ii miwani.


Maelekezo ya ishara kwa haraka yalipokamilika ‘TSC’ alivuta hatua ya kujisogeza kutoka alipo mpaka kingo ya mlango kisha akakirusha kiazi kwa ndani akirusha tu bila kuangalia kama kuna watu au mtu au kitu gani alichotaka kitue ndani tu na kuleta anachotaka.


Mlipuko wa bomu lile la kurushwa ulisikika ukiacha tafrani nguo kuchanika kwa watu walio ndani eneo la karibu, mlipuko ulipokuwa umeanikiza mlio wake tayari Investigator Miller alikuwa ameinuka toka alipojilaza akifuata maelekezo ya kiishara aliyopewa, alikuwa akikimbia kuelekea kwa mlangoni vumbi la bomu la kutupwa na miale yake ya moto ilipotuama tu yeye akaongeza bomu jingine la kurushwa kuelekea ndani tena na kwakuwa yeye alikuwa akiona wapi analirusha lilitua kwenye kioo cha kilicho katika dirisha ambalo ni kama kaunta zinazokuwa katika mahotel ambapo uwa na uwazi flani ambao utegemea na watu wa eneo hilo au tuseme wenyeji wa mjengo husika wanataka uwe wa kiasi gani, basi yeye Miller kurusha kwake akishabaha bomu analolirusha likaingie ndani ya kichumba husika sababu hisia zake zilimtuma kuna watu mule na ndiyo kikwazo chao kikubwa cha kwanza.


Kelele za watu wanaolilia uhai wao zilisikika kutokea ndani ya chumba kile tofauti na bomu alilorusha Agent Kai ambalo hakuna kelele ya watu iliyosikika ikililia kama lilivyo bomu hili alilorusha Miller akiwa katika mbio kana kwamba anarusha kizibo cha soda kwenda mbele, Mbio za Miller hazikukwama popote alipitiliza akiuruka mwili uliotolewa roho na Agent Kai muda mfupi uliopita akaingia ndani akijitupa chini kana kwamba anapiga mbizi ndani ya maji akaserereka chini akitumia tumbo mpaka kwenye ukuta wa kaunta aliokuwa anauona kwa mbali dakika kadhaa zilizopita hapo akajiviringisha na kuchuchumaa tuli muhemo wa kasi akijitahidi kuudhibiti aweze kuhema kawaida.


Hali ya watu waliokuwa wamepatwa na bomu la kurushwa ikiwa wamezubaa baada ya bomu la kwanza lililotupwa na Agent Kai kuwafanya wainame katika chumba cha mapokezi na ukaguzi kilichopo hapa ambapo kimtizamo nilishapaelezea kuwa pako kama kaunta nyingi za hoteli zinavyokuwa na hata kaunta za mabenki ambapo uwa panatolewa huduma za kuweka na hata kutoa pesa, bomu lililorushwa na kuwazamia ndani kabisa ya eneo lao kutahamaki wakashindwa kujitetea liliondoa uhai wa watu saba papo hapo huku wengine watano wakiachwa na hali mbaya isiyo na ahueni kwao muda wowote wakielekea kukata uzi, kelele zao za kuwa wako katika maumivu makali yanayohitaji msaada ilifanya Miller ainue mwili wake kusimama kutoka kwenye mchuchumio kwa chati akawachungulia kupitia eneo wazi ambalo muda wa dakika mbili tu zilizopita kulikuwa na vioo madirisha yote na sasa vimevunjika.


Aliweza kuwaona wakiangaika ndani ya chumba kilichojaa damu na uvunjikaji wa vitu kwa kazi ya bomu alilolirusha, hapo alijitokeza vizuri akainua bunduki na kuwamiminia risasi za mfululizo akipiga kila mmoja moja moja kisha anarudia tena moja moja mpaka zilipofika idadi ya risasi nne kwa kila mmoja wote wakanyauka tuli miili ikivuja damu huku mtoa roho akiwa kashachukua stahiki yake.


Milio ya risasi mfululizo toka kwenye bunduki ya Miller ilimfanya Agent Kai achungulie kuona ni shughuli kweli ya Miller au kuna mtu anayefanya kazi hiyo, alipoona ni ndugu yake Miller alichuchumaa chini kisha akaingia mahala husika akipita juu ya mwili uliolala pale mlangoni kuchuchumaa hakukumzuia kuingia kwa kasi ya kuruka kichura chura mpaka usawa aliosimama Miller hapo naye akasimama.


“… Dah! Safari imekuwa ndefu sana..!” Akaongea Agent Kai huku macho yakikagua eneo la ndani ya kaunta iliyogeuka kuwa dimbwi la damu na miili iliyoumizwa vibaya sana hii ikiwa ni kazi ya bomu la kurushwa alilorusha Investigator Miller.


“.. Wamejenga kwa mtindo huu hili kuhakikisha usalama wao wa kufanya mambo yao.. Hatua za kupita hizi zote zinadhihirisha umakini wao katika michezo hii” Akajibu hoja Miller kisha akasogea kwenye kona kuchungulia mbele kuona wataelekea wapi kama watasongesha.


“..Mbele kuna mlango mwingine.. Hapa ni mahala ambapo uwa anayefika anachukuliwa maelezo kama ni mgeni na kama si mgeni basi kuna saini yake uhitajika.. Tuna kazi nzito kila hatua ina mtihani mzito sana” Akaongea Miller macho yake yakizidi kufanya upembuzi yakinifu.


Agent Kai hakutia neon tena bali alikamata kwa viganja vyake eneo la dirisha akajivuta kwa nguvu na kasi akatua ndani ya chumba chenye maiti, akili yake sasa alihihitaji ifanye kazi za ziada, muda unaokwenda kasi kuufanya usiku kuisha kuelekea alfajiri ulikuwa unamchanganya kila anapotizama saa yake ya mkononi.


Alisogea hadi mahala ambapo alikuwa ameona kitu ambacho ndicho kilichomvutia kudunda humu ndani ya chumba, ilikuwa kadi ambayo aliamini ndiyo itakayowawezesha wao kufungua mlango unaofuata.


“Naamini hii ni funguo ya mlango..!” Akaongea huku anaipangusa damu kwa kipande cha karatasi alichokikata toka katika kitabu kilichoandikwa mambo kadha wa kadhaa.


“Silla mje haraka tupange tunasogeaje mbele… Kuko shwari hivyo njooni tu” Miller akaongea kupitia simu saa yake.


Dakika moja tu tayari Special Agent Rebecca na Special Agent Silla wakawa wamefika pale kaunta, Kai aliamua kuzima taa ya pale kwakuwa aliiona swichi yake katika kichumba cha kaunta, giza likashika hatamu.


“..Vipi moto huko juu?” Akauliza Agent Kai, swali lililokuwa linahitaji jibu toka kwa wenzao waliofika toka huko juu.


“Kwa hali ya baridi ukiwa huko huko juu unaweza pata hamu ya kukaa papo hapo hili joto la moto liendelee kukupa burudani… Umesambaa sana umeshika kasi inayostahili..!” Akajibu S.S Rebecca.


“Sa..!” Hakuendelea na alichohitaji kusema ulisikika mlio mkubwa wa kitu ambacho kimelipuka kama bomu basi ni bomu lenye uzito wa hali ya juu maana hata wao pale walipo kulitetema kama tetemeko dogo la ardhi lisilo na madhara ndiyo haswa kilichotokea, umeme ulikatika giza likashika hatamu ghafla.


“Yah! Kile tulichohitaji kimetimia.. Umeme umekatika..!” Akaongea Agent Kai akiachana na kile alichotakiwa kusema mwanzo akakikatizia.


“Huo mlipuko nafikiri ni mlipuko wa tanki la mafuta tuliloliona karibu na viroba visivyo na kitu..!!” Miller akaongea na wenzake wakakubali kichwa.


“Kadi haina kazi.. “Kai akaongea na kuiweka mfukoni kadi kwa mwendo wa kawaida akaenda hadi pale ulipo mlango unaotumia elektroniki, nyuma yake wenzake wote walimfuata kama mkia mpka pale.


“Tukipita hapa ndiyo tutakuwa tumeingia ndani ya tumbo la The Red Jaguar..” Akaongea tena Kai bila kuwatizama wenzake.


“Ndiyo ndiyo! Hakuna njia ingine ya kuingia ni njia ambayo kama ni mtego unaweza kutufanya sote tuingie mtegoni..!” Silla akaongea naye akijipa fursa ya kukichunguza kitasa ikiwa ‘TSC’ amesogea pembeni.


Macho ya Special Agent Rebecca yaliyo ndani ya miwani yalivutiwa na kitu, alikuwa ameona jambo ambalo akili yake ilimtuma asogee kwenda kuona kama anachokiwaza kinaweza kuleta jibu ambalo wote hapa walikuwa wakitamani.


Upande wa kulia kwao kwa juu kulikuwa na wavu uliotengenezwa kufunika katika bomba la umbo la mstatili, alipolifikia kwa urefu wake asingeweza kulifikia bali alibaki akilichunguza kutokea pale chini yake aliposimama ndipo wenzake wote wakavutiwa na wao walipoona mwenzao anashangaa jambo gani.


Wote wakajikusanya pale na kila mmoja alivutiwa bila kuongea jambo lolote wakatizamana na kugonganisha viganja vyao vikiwa ndani ya gloves walizovaa.


Dakika haikufika tayari walikuwa na jibu la kufanya, Miller aliweka ngazi mgongo wake na Silla akapanda kwenda juu alipofika akachungulia na kuona ni bomba la kupitisha hewa kutokea ndani kuja hapa likiwa na upana na urefu wa kupitisha mtu mmoja atakayepita kwa kulala akitambaa katika miongoni mwao wote hakuna ambaye asingeweza kupita hapa, Miller akatabasamu kisha akawaonyeshea alama ya dole wenzake kuwa sasa kuna jibu la kuleta matumaini.


Alichukua dakika moja nzima akichunguza jinsi gani anaweza akautoa ule wavu mgumu wenye unene wa kiasi cha ukubwa wa peni ya speedo.


Wakati akiendelea kufikiria alistuka akiguswa guswa mgongoni mwake na kitu alipogeuka kuangalia ni kitu gani? Akakutana na kifaa kilichoshikwa mkononi na Agent Kai na kwakuwa yeye pia si mgeni wa kifaa icho alikipokea haraka kilikuwa na ukubwa wa chupa ya soda ndogo haina ya mwala kwa wale wanaojua soda aina ya mwala ikoje ni rahisi kwao kung’amua sasa naongelea kifaa chenye ukubwa wa namna gani?.


Kifaa hiki kinafanya kazi kama jeki pia kinafanya kazi ya kuvuta msumari kama umepigiliwa sehemu, Silla hakuwa mgeni na kifaa hiki mara moja akaanza kazi iliyodumu dakika nne na nusu tu wavu ukatoka akautupa chini kisha akakamata kingo zake akajivuta na kuzama ndani yake akitanguliza kichwa ambako mtu akishatangulia hivi uwa hana uwezo wa kupinduka akiwa anapita eneo la bomba la hewa kama hili ambalo si njia maalumu kwa viumbe hai.


Mwisho wa sehemu ya tisini na tatu (93)


Shughuli bado ni pevu kweli kweli ndani ya Tajumulco Camp, majasusi wanaumiza vichwa vyao wanaingiaje ndani ya tumbo la ‘TRJ’.


Tuweke maneno mengi pembeni tukiwaachia wazaramo!




Wote wakajikusanya pale na kila mmoja alivutiwa bila kuongea jambo lolote wakatizamana na kugonganisha viganja vyao vikiwa ndani ya gloves walizovaa.


Dakika haikufika tayari walikuwa na jibu la kufanya, Miller aliweka ngazi mgongo wake na Silla akapanda kwenda juu alipofika akachungulia na kuona ni bomba la kupitisha hewa kutokea ndani kuja hapa likiwa na upana na urefu wa kupitisha mtu mmoja atakayepita kwa kulala akitambaa katika miongoni mwao wote hakuna ambaye asingeweza kupita hapa, Miller akatabasamu kisha akawaonyeshea alama ya dole wenzake kuwa sasa kuna jibu la kuleta matumaini.


Alichukua dakika moja nzima akichunguza jinsi gani anaweza akautoa ule wavu mgumu wenye unene wa kiasi cha ukubwa wa peni ya speedo.


Wakati akiendelea kufikiria alistuka akiguswa guswa mgongoni mwake na kitu alipogeuka kuangalia ni kitu gani? Akakutana na kifaa kilichoshikwa mkononi na Agent Kai na kwakuwa yeye pia si mgeni wa kifaa icho alikipokea haraka kilikuwa na ukubwa wa chupa ya soda ndogo haina ya mwala kwa wale wanaojua soda aina ya mwala ikoje ni rahisi kwao kung’amua sasa naongelea kifaa chenye ukubwa wa namna gani?.


Kifaa hiki kinafanya kazi kama jeki pia kinafanya kazi ya kuvuta msumari kama umepigiliwa sehemu, Silla hakuwa mgeni na kifaa hiki mara moja akaanza kazi iliyodumu dakika nne na nusu tu wavu ukatoka akautupa chini kisha akakamata kingo zake akajivuta na kuzama ndani yake akitanguliza kichwa ambako mtu akishatangulia hivi uwa hana uwezo wa kupinduka akiwa anapita eneo la bomba la hewa kama hili ambalo si njia maalumu kwa viumbe hai.


ENDELEA NA MAPIGO NONDO..!!


BUTWAA X

SAN MARCOS-GUATEMALA

“Lete habari Maxi?”

“Hali bado tete mkuu.. Naomba kuongezewa nguvu haraka sana ya mashambulizi ya anga, sisi tujitahidi kuzuia wasiingie ndani ya eneo muhimu waishie huko huko..”

“Helkopta imeruka nusu saa sasa.. Hali ikoje kwa sasa?”

“Hali tete.. Umetokea mlipuko mkubwa sana ambao umesababisha umeme kukatika eneo lote na kama ujuavyo jenereta tunalolitegemea liko juu huko hivyo kwa sasa tunatumia tochi kuonana”

“Watakuwa wameuzima kama si kulipua miundo mbinu hao si hitilafu za shoti ya umeme.. Basi jitahidini kama ulivyosema kuwazuia wasiingie eneo la ndani ninaamini hawawezi kupita kufika huko mkiwa makini”

“.. Tunahisi wamefika korido ya ukaguzi, pale chumba cha ukaguzi niliwaweka watu wazoefu wa kazi na ujuzi wa hali ya juu waliahidi kuzuia chochote kile kupita pale”

“Unasema unahisi! Kwani hakuna cctv kamera kufuatilia kila kinachofanywa na hao wavamizi kama ilivyokuwa mwanzo?”

“Zote zimezimika hakuna inayoonyesha chochote.. Tena baadhi zilizima kabla ya hata umeme kuzimika hivyo hakuna chochote mimi nimetoka chumba cha mawasiliano na skrini za cctv niko hapa walipo watu wote tukisubiri taarifa toka walio chumba cha ukaguzi wakidhibiti wasifanikiwe kuingia”

“Dah! Jamaa wanafanya mambo kifundi sana.. Ila msihofu hapo labda waombe msaada wa jeshi lao la Marekani ndiyo wataharibu plan yetu… Helkopta iliyowabeba kina Ivan itafika muda si mrefu.. Kuweni makini pia jiandae kufanya nao mawasiliano mlipo na adui walipo hili wawashambulie”

“Sawa mkuu!”

Simu ilikatwa na upande ambao ndiyo ulikuwa umepiga simu hii, alikuwa ni Brigedia Fernandes Carlos Codrado ‘Feca’ akiwa amempigia Koplo mfukuzwa wa jeshi la wananchi wa Mexico, Maxiwell Zuantejo kiongozi mwandamizi wa genge la ‘TRJ’ wakipeana maelekezo juu ya hali inayoendelea ndani ya eneo lao muhimu sana kwa mustakabali wa genge lao, eneo la Tajumulco Mountain Camp.


Hakuna aliyekuwa ametulia kati ya watu zaidi ya mia na ishirini ambao usiku huu walikuwa katika eneo muhimu la ‘TRJ’, sabini wakifanya kazi ya kiwanda cha siri kinachohusika na kubadilisha mimea ya madawa ya kulevya kuwa unga wake kwa matumizi ya watu wabishi wasiojali afya zao, pia watu wengine hamsini usiku huu walikuwa hapa kwa ajili ya ulinzi wa eneo hili la ndani kama wenyewe wanavyoliita ni eneo muhimu au ‘moyo wa TRJ’.


Kila mmoja kwa wakati huu wapo waliokuwa wakitumia bangi kuvuta hili kuwaongezea mizuka ikiwa wengi wao wameamshwa toka usingizini hivyo vinywaji vikali vilihusika mchanganyiko na bangi, silaha zao za bunduki ambazo ni kama zoeleka zaidi kwakuwa ni aina ambayo kila mmoja alikuwa anaitumia, Norinko QBZ-97 hii ni silaha aina ya bunduki rahisi zaidi kupatikana kwa magenge ya wahalifu itokayo nchini china kama ujuavyo soko la China katika kila aina ya bidhaa limekuwa soko linalojali maslahi zaidi ya kukua kwao kiuchumi hivyo kuwa na masharti nafuu zaidi kupata kila unalolihitaji ilimradi pesa yako iwe ile muafaka kwao kifaida.


Eneo lote hili lilikuwa likinuka harufu ya bangi, pia walikuwepo wale wanaotumia madawa ya kulevya ya unga kama cocaine, heroine na methamphesine katika kujiweka sawa na kupokea chochote kitakachotokea katika hali ya utayari iwe kufa au kupona ni mzuka tu uliohusika hapa ikiambatana na kuhamasishana kuwa hakuna mpuuzi yoyote kuingia eneo la mstari wa ‘moyo wa TRJ’ , walikuwa wakisubiri kuona kiumbe gani kitajitokeza kupitia lango kuu la kuingia eneo walilopo kwa hamu wakiwa wamefurahi pia kuruhusiwa kuua chochote kitakachojitokeza licha ya kuwa wapo waliokuwa na wasiwasi juu ya mustakabali wa maisha hasa ambao kazi yao ndani ya mjengo huu wa chini uwa kwenye kiwanda cha usindikaji wa madawa ya kulevya baada ya kushuhudia kupitia skrini kubwa zilizokuwa zikipokea matukio kupitia cctv kamera, muziki wa Agent Kai na wenzake uliweza kuwajuza kuwa waliowavamia siyo ‘vinzila’ (wapuuzi) wa kuwapuuza ni makomandoo wenye sifa zao.


Koplo Maxiwell Zuantejo naye kwa wakati huu alikuwa macho yake kayaelekeza lango kuu, akiwa na siri ya kuwa mawasiliano baina yake na watu walio chumba cha walinzi wa ukaguzi yalikuwa sasa hapokelewi simu zake na karibia watu wote hii ikimaanisha kuna jambo si zuri linaendelea lakini hii ilibaki kwake tu hakutaka mwingine ajue.


***** ***** *****


Special Agent Silla aliongoza msafara akiwa mbele wote wakitambaa vichwa vyao vikiwa vimetangulia mbele, hakuna aliyebaki kule kwenye chumba cha ukaguzi , mtu wa mwihso akiwa ni Agent Kai yeye akiwa ametanguliza miguu kwenda mbele na kichwa kikiwa kinaangalia kule wanakotoka kuhakikisha usalama wao hivyo alikuwa akienda kinyumenyume macho yake yakiwa makini kuangalia wanapotoka.


Bomba hili lililo katika muundo wa boksi (pembe nne) ambalo kimsingi kulikuwa na nyaya zilizopita zinazotumika kwenye mfumo wa intaneti na hata zinazounganisha kamera mbalimbali za cctv kamera kutokea juu huko na sehmu mbalimbali za jingo hili kwenda kwenye chumba kikuu cha mawasiliano, lilikuwa na vumbi jingi sana kiasi ya kwamba kila wanavyokwenda hasa aliye mbele alikuwa akikomba vumbi la kutosha kana kwamba nguo alizovaa zinapangusa vumbi lile ambalo lilikuwa jepesi linapokuja humu lakini linapotua katika kuta bomba linajenga makazi mpaka kutengeneza kitu kama poda laini sana, yote hii ilikuwa ni kutowai kufanyiwa usafi kwa kipindi kirefu hata mtu kuchungulia tu mpaka imekuwa njia ya panya wakubwa.


Waliweza kutambaa kwa urefu wa mita mia na hamsini mpaka walianza kuchoka na iliwashangaza sana kuwa pengine bomba linaweza kuwa linawatoa nje kabisa ya eneo wanalolitaka wao kutokea kama ‘plan’ yao ilivyotaka, muongoza msafara alifika mahali akakutana na mwisho wa bomba kukiwa kuna wavu mkubwa unaofanana kila kitu na ule wa kule alioweza kuuondoa kisha wakaingia humu ndani ya bomba, hapa alijisogeza zaidi kisha akachungulia katika matundu aweze kuona wapi watatokea endapo watautoa wavu husika.


Macho yake yalikutana na kichumba kidogo lakini kina maboksi ya plastiki mbalimbali yaliyofungwa katika kuta za chumba kwa idadi kadhaa pande zote ya kichumba kulikuwa hamna dalili kuwa uwa kunakuwa na mtu anayekaa kwa muda mrefu katika kichumba hiki zaidi ya kuwa na dalili kuwa kama kuja kwa mtu hapa basi uwa anafika mara moja moja, kulikuwa na giza zito sana lakini kama ujuavyo miwani wanayoivaa watu hawa majasusi wabobezi, miwani ya kazi za kazi iliweza kumfanya usahili wake wa macho ufanyike vizuri sawa sawia.


Alijipinda kidogo hili aweze kuweza kuiona sura ya mtu anayemfuata kwa nyuma yake ambaye ni Inv. Miller na kwa tabu wakaweza kuangaliana macho kwa macho kisha akamuonyesha ishara asogee mbele alipo bila kujali udogo wa eneo Miller akasogea wakiminyana mpaka usawa wa kichwa cha mwenzake.


“Mwisho wa safari ndefu ya bomba hili la nyaya kama uonavyo mbele yako” Akaongea S.S Silla wakiwa wote wanachungulia ndani ya kachumba kadogo.


“Acha nishuke kwenda kufanya uchunguzi kisha nitakujulisha nini ni nini!!” Miller hakugeuza sura kumtizama mwenzake kama na mwenzake naye alivyofanya wote walikuwa bize kuangalia kila mahala ndani ya kachumba kale, aliomba ruhusa ashuke yeye kwanza.


Walishirikiana kufungua pini za misumari zilizoshika wavu mgumu mpaka ukaachia wakaukamata kwa pamoja usidondoke chini na kuwaletea mambo mbovu mbovu, Miller akapenya akiupitisha mwili wake juu ya mwili wa mwenzake akitanguliza miguu akajiachia na kutua ndani ya chumba ambapo Silla akanyoosha mkono uliokamata wavu kumpa mshirika mwenza naye akaupokea na kuuweka juu ya moja boksi moja ambalo ndani yake hakuna aliyekuwa akijua kuna nini?.


Macho ya Inv. Miller yalizunguka haraka haraka kutizama kila pembe ya kachumba haka kadogo ambacho muda huo mfupi aliweza kutambua ni chumba kidogo chenye mitambo midogo inayopeleka mawasiliano sehemu mbalimbali za majengo ya hapa kambi ya Tajumulco, wakati huo wote juu yake Silla alikuwa kalalia tumbo kichalichali anamtizama ndugu yake.


Dakika mbili nzima zilipita Miller akipekua pekua kwa baadhi ya vitu akitumia sekunde chache kukipitia kila kimoja kisha ya hapo akamuangalia Silla akatingisha kichwa kumaanisha jambo ambapo Silla akamuelewa naye akajivuta na kuhuruhusu mwili wake kutua ndani ya kachumba sasa wakawa wawili huku juu kwenye bomba akasogea S.S Rebecca aliyekuwa nyuma muda wote akipumua kwa tabu na kumfanya akereke na hali ya pale ndani ya bomba akitamani kushirikishwa kuona nini kinaendelea mbele walipo Miller na Silla.


Inv. Miller alisogea kwenye kidirisha kinacholeta hewa mule ndani akachungulia na kukutana na chumba chenye skrini mbalimbali pande mbili za ukuta kati ya pande nne zinazounda chumba, kulikuwa na viti kadhaa vya plastiki vya kisasa pamoja na meza ya mbao ya umbo la mstatili ikiwa na mafaili kadhaa pamoja na kompyuta mpakato kama tatu zikiwa zote zimezimwa kama vilivyo vitu vingine ambavyo vilikuwa navyo zoimezimwa ama kuzimika pengine kwake Miller aliamini umeme ndiyo umesababisha chumba hiki muhimu kwa sasa kuwa na ukimya huu mzito.


Silla naye hakutaka kuwa nyuma kama mkia wa fisi alijisogeza pale kwenye kidirisha naye aweze kushuhudia kile anachokishuhudia ndugu yake katika kazi.


“Chumba cha skrini za cctv kamera na mambo mengine ya kiteknolojia… Ni chumba muhimu sana, hili jingo la chini limejengwa jingo kubwa sana kwa jinsi tulivyopita tumepita urefu wa mita zaidi ya mia moja hii ndiyo inanidhihirishia kuwa TRJ watu wanaojua wanafanya nini katika kazi yao..” Akaongea Miller kumwambia mwenzake.


“Naam.. Naenda ndani wewe utanilinda kutokea kwa hapa dirishani kwa chochote kile kitakachokuwa cha tofauti” Silla akaeleza kisha hakusubiri jibu lolote toka kwa Miller akasogea ulipo mlango unaoleta mtu au watu ndani yah aka kachumba kadogo.


S.S Rebecca alishuhudia yote hayo na alipoona Silla anasogea ulipo mlango, akajivuta na kujirushia ndani alifanya hivi hili Agent Kai asogeaa naye apate kuona kinachoendelea si kusubiri tu ndani ya bomba lenye hewa mbaya ya harufu ya mavi ya panya na mchanganyiko wa vumbi, ni kama fursa ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na mzee wa fursa kuondoka kwa Rebecca kulimfanya ajipindue kama joka lililo mawindoni miguu iliyokuwa mbele kurudishwa nyuma kisha kichwa kuja mbele halafu kwa kasi akajiburuta mpaka ukingoni macho yake majanja yaliyojaa umbeya mwingi wa kiuchunguzi kuweza kushuhudia nini kiko mbele na kinafanyiwa kazi gani eneo hilo.


Silla alishika kitasa akakinyonga kikawaida tu bila kuchukua tahadhali ya kuhakikisha kuwa hakitoi mlio wowote akausukuma mlango bila hiyana ukasukumika, chumba hiki kidogo hakikuwa kinafungwa kwa funguo zaidi ya mlango wake kurudishwa tu, jasusi wa kizungu Special Agent Silla akaingia ndani ya chumba husika huku kwa nyuma yake akifuatiwa na Rebecca aliyeona hakuna haja ya kusubiri subiri.


Kupotea kutoka katika kichumba hiki kulimfanya ‘TSC’ kujiachia naye kutoka juu mpaka ndani ya kichumba sasa wote wakawa wametoka kwenye bomba, wote walikuwa kama wametoka kuchimba madini ni vumbi nguo zote hakuna kulikokuwa salama katika athiriko hili la mavumbi kati yao na hata hakuna aliyethubutu kujikung’uta angalau kulipunguza vumbi.


Miller aliangaliana na Kai kisha akamuonyesha ishara naye aondoke pale kwenda walikoelekea kina Silla.


Chumba cha mawasiliano cha eneo muhimu na moyo wa ‘THE RED JAGUAR’, eneo ambalo kiukweli hakuna mtu baki na asiye na cheo kikubwa ndani ya genge hili ambaye alikuwa amewai kuingia humu, muda huu majasusi wa Marekani walikuwa wamo humu wakipekua na kufungua kila droo na kila kasiki ambayo waliikuta humo ndani, wakisoma kila nyaraka waliyokutana nayo kwa haraka na kila iliyoonekana muhimu basi kuna begi moja ambalo ni begi la mwanadada S.S Rebecca iliwekwa humo, mwisho walichukua ipad tatu walizozikuta mezani na laptop mbili nazo zikiwa kwenye mbili tofauti tofauti ikionyesha zimezimwa muda si mrefu kwa watumiaji wa vitu hivi utambua hili, hizi walizipakia katika begi moja ambalo walilikuta humu ofisi hii ya mawasiliano.


“Tunatoka katika chumba hiki… Hii mizigo tutaificha mahali humu humu ila tusije kusahau hivi ni vithibitisho muhimu sana katika kesi na operesheni hii..!” Agent Kai akaongea akiwa kasogea katika mlango unaotumika kuingia na kutoka katika chumba hiki.


Rebecca aliangalia wapi anaweza kuweka mizigo yao iliyosemwa na Agent Kai kuwa ni vidhibiti muhimu, alipoangalia njia iliyowaleta haraka alisogea pale akiwa na mabegi mawili akayapandisha juu na kuyasukumia kwa ndani kisha akarudisha wavu kama ulivyokuwa kabla hawajaung’oa hili kupita kuingia humu ndani.


“Safi! Hapo kwa haraka mtu asiye sisi kujua umeweka kitu atachelewa sana..!” Miller akaunga mkono uhifadhi wa vidhibiti mahala alipoweka Rebecca.


“Tutatangulia kutoka mimi na Silla humu ndani… Dakika mbili mbele mtafuata nyinyi” Akaelekeza Agent Kai akiwatizama kwa zamu wenzake kisha ya hapo akaiweka bunduki yake vizuri mkono wake wa kushoto, mkono wa kulia ukaminya kitasa taratibu akauvuta mlango ukagoma kuvutika ikimaanisha umefungwa kwa nje ya chumba, akainama kukisoma kitasa ni uzao wa wapi? Alipopata jibu mkono wa kulia ukazama kwenye mfuko wa mbele kulia wa suruali aliyovaa ambao kuna funguo rundo katika fungu moja akalitwaa na kulikamatia mkononi, bunduki akaiegemeza ukutani pembeni ya mlango.


Hakupata tabu kuipata ‘master key’ (funguo Malaya) ya kufungua aina ya kitasa kilicho mbele yake, haraka akaipachika tunduni ikazungushwa kifundi mizungusho kadhaa mlango ukatii amri ukafunguka hapo akautoa akakamatia fungu lote likarudi mfukoni ( kawaida kwa majasusi hawa waendapo kazini makorokoro ya kazi uwa kibao katika mifuko yao ndiyo maana uwa wanapenda kuvaa suruali aina za timberland zenye mifuko mingi hili kuweza kubeba kila aina ya vifaa vya kazi).


Mlango ukavutwa taratibu ikihakikishwa hautoi ukelele utakaoweza kumfanya aliye karibu na mlango kwa nje astuke kwa kuusikia tu labda kwa kuuona ukifunguka, kiuwazi kidogo cha kuweza kuona angalau kidogo kifuatacho mbele kiliweza kumuwezesha Agent Kai kuona eneo la korido iliyonakshiwa kama chumba hiki kilivyonakshiwa kwa malumalu (tiles) sakafuni mpaka kuta zake na kufanya kung’ae licha ya hali ya ugiza iliyokuwepo kumbuka yeye ana miwani ya kazi za kazi machoni mwake hivyo aliweza kuona hali ya unadhifu wa mahala hapa, akauvuta zaidi kidogo kumuwezesha kutoa kichwa chake hapa akaiona korido ndefu inayoendelea mbele na hakukuwa na kiumbe chochote hapo akatokeza kabisa ikiwa kashaiinua bunduki alipoiweka ila aliitupia upande wa nyuma wa bega, mkono wake wa kushoto akakamatia bastola yake aipendayo ‘Glock-7 Pistol’ ikiwa kaifunga kiwambo cha kuzuia sauti (sailensa).


Akatokeza hatua mbili mbele kutoka mlangoni akiwa mgongo kauegemeza ukutani macho mbele, nyuma yake akafuata Silla kama ratiba yao ilivyoelekeza.


Mwisho wa sehemu ya tisini na nne (94)


Mziki mzito wenye ‘sound’ zenye ujazo wa kutosha unaenda kufunguliwa muda mfupi ujao, mziki ambao unatusogeza sehemu ambayo hatma ya Tajumulco Camp itaweza kujulikana kama itaanguka au kina Agent Kai na wamarekani wenzake ndiyo watakaoanguka na maisha yao kuishia katika jingo hili la hatari sana katika ukanda wa Amerika kusini na kaskazini kuliko majengo ya magenge yote yanayojihusisha na ulanguzi wa madawa ya kulevya.


Nini kitafuata?




“Tutatangulia kutoka mimi na Silla humu ndani… Dakika mbili mbele mtafuata nyinyi” Akaelekeza Agent Kai akiwatizama kwa zamu wenzake kisha ya hapo akaiweka bunduki yake vizuri mkono wake wa kushoto, mkono wa kulia ukaminya kitasa taratibu akauvuta mlango ukagoma kuvutika ikimaanisha umefungwa kwa nje ya chumba, akainama kukisoma kitasa ni uzao wa wapi? Alipopata jibu mkono wa kulia ukazama kwenye mfuko wa mbele kulia wa suruali aliyovaa ambao kuna funguo rundo katika fungu moja akalitwaa na kulikamatia mkononi, bunduki akaiegemeza ukutani pembeni ya mlango.


Hakupata tabu kuipata ‘master key’ (funguo Malaya) ya kufungua aina ya kitasa kilicho mbele yake, haraka akaipachika tunduni ikazungushwa kifundi mizungusho kadhaa mlango ukatii amri ukafunguka hapo akautoa akakamatia fungu lote likarudi mfukoni ( kawaida kwa majasusi hawa waendapo kazini makorokoro ya kazi uwa kibao katika mifuko yao ndiyo maana uwa wanapenda kuvaa suruali aina za timberland zenye mifuko mingi hili kuweza kubeba kila aina ya vifaa vya kazi).


Mlango ukavutwa taratibu ikihakikishwa hautoi ukelele utakaoweza kumfanya aliye karibu na mlango kwa nje astuke kwa kuusikia tu labda kwa kuuona ukifunguka, kiuwazi kidogo cha kuweza kuona angalau kidogo kifuatacho mbele kiliweza kumuwezesha Agent Kai kuona eneo la korido iliyonakshiwa kama chumba hiki kilivyonakshiwa kwa malumalu (tiles) sakafuni mpaka kuta zake na kufanya kung’ae licha ya hali ya ugiza iliyokuwepo kumbuka yeye ana miwani ya kazi za kazi machoni mwake hivyo aliweza kuona hali ya unadhifu wa mahala hapa, akauvuta zaidi kidogo kumuwezesha kutoa kichwa chake hapa akaiona korido ndefu inayoendelea mbele na hakukuwa na kiumbe chochote hapo akatokeza kabisa ikiwa kashaiinua bunduki alipoiweka ila aliitupia upande wa nyuma wa bega, mkono wake wa kushoto akakamatia bastola yake aipendayo ‘Glock-7 Pistol’ ikiwa kaifunga kiwambo cha kuzuia sauti (sailensa).


Akatokeza hatua mbili mbele kutoka mlangoni akiwa mgongo kauegemeza ukutani macho mbele, nyuma yake akafuata Silla kama ratiba yao ilivyoelekeza.


ENDELEA NA MAPIGO NONDO…!!


BUTWAA XI

SAN MARCOS-GUATEMALA

Ukumbi huu uliokuwa na milango ya zinazoonekana ni ofisi zilizopangana kulikuwa na giza lisilo na kero kwao wote haukuwa na kikwazo kwao cha kiulinzi kwa hali iliwajuza wajuzi hawa mambo kuwa wahusika wa ofisi hizi usiku uwa hawapatikani katika ofisi kwa jinsi kulivyokuwa kimya, TSC alitembea akiwa katangulia mbele nyuma yake akifuatwa na Special Agent Silla mpaka kwenye mlango wa vioo ulioweza kuwaonyesha eneo uwazi mkubwa upande wa pili kama ukumbi mkubwa wa mikutano au michezo kama si show za miziki.


Akiwa bado anachungulia upande huo wa pili pembeni yake akiwa Silla naye anachungulia waliweza kuona kwa mbali gizani watu wawili wanatokea upande mmoja kwenda upande mwingine wakiwa wanakimbia kimbia kama ya mwendokasi hivyo kuepusha wasionekane kila mmoja akajiweka kando ya lango hili la vioo, walipoona wamepita tayari ndipo Agent Kai akavuta mlango ule ulioandikwa kwa huku walipo wao maneno mawili la kwanza la kilatin ‘JALA’ kisha mstari wa kugawa kati mwisho likaandikwa neno la kiingereza ‘PULL’ kwa Kiswahili chetu ikimaanishwa ‘VUTA’ neno hili la Kiswahili alikuwepo hapo msomaji wangu ila nimeeleza maana ya maneno ingawa naamini hili la pili si geni kwako.


Alitangulia kutoka akiwa amechuchumaa kana kwamba yupo kwenye choo cha kulenga (choo cha shimo) anashusha mambo kupunguza taka ngumu tumboni maisha yaendelee mbele kama ilivyo ada ya viumbe hai wote duniani, Silla naye alifuata kisha akachuchumaa kama alivyofanya ndugu yake kwa kasi kwa pamoja wakaruka hatua zinazofanana na kichura chura kuelekea usawa mmoja wenye masofa ya ngozi ya kisasa yaliyopangwa eneo hili lenye uwazi mpana mbele yakiwa pembeni ya kuta itokayo kule wanakotoka wao.


Macho yao kwa mbele ndipo waliona watu wengi wake kwa waume wakiwa wamewapa mgongo wakiwa na silaha aina ya bunduki karibu kila mmoja pia walikuwa na silaha zingine za ziada kama silaha pendwa na watu wa hapa aina ‘RPG’ hata walioshika bunduki na mapanga hata visu walikuwepo pia, mavazi yao ya makoti meusi marefu kwa kila mmoja yaliwafanya wawe wamependeza na giza lililokuwepo likiwafanya kuonekana kama vivuli.


Umakini ulihitajika hapa kuliko sehemu yoyote ile toka walivyoingia katika kambi hii hawakuwa wameona uwingi huu wa watu, kilichosaidia kwao ni kuwa hakuna aliyekuwa akiwaza kuwa tayari wamezungukwa kwa nyuma na adui zao ambao wao wanaimarisha ulinzi wasipite kuingia ndani kupitia mlangoni bila kukumbuka kama kuna njia za panya zinazoweza kugeuzwa kuwa za binadamu na wataalamu kama hawa ambao uwa hawachoki kutafuta chochote cha kufanya kutimiza hitaji lao.


Mawasiliano ya Kai na Rebecca yalifanyika na kuwafanya wenzao hao kujiunga kwakuja na wao pale yalipo masofa bila kuleta haina yoyote ya mshtuko toka kwa adui zao ambao hamu yao kuu ni kuona pua ya adui zao zikifungua mlango na hata kuufunga waliufunga kiwepesi tu ikiwa ni mtego kwakina Agent Kai na wenzake.


“Wameelekeza nguvu kwenye lango la kuingilia humu.. Aiseeh hawa TRJ hatari hili jengo la chini ya ardhi ni kubwa sana ni kama wamejenga juu ya ardhi tu ingekuwa umeme haujakatika tungeona mengi zaidi” Aliongea Miller baada ya kufika tu walipo Silla na Kai.


“Upande wa juu kulia kwetu kuna mahala ambapo natamani tungepata nafasi ya kuchunguza zaidi kuna nini nahisi kuna kitu cha ziada upande ule unaonekana una madohani makubwa ya kutolea moshi” Agent Kai akaongea kwa sauti ya chini kama iliyotumika na Miller kuongea wakati anafika walipo wenzake.


“Mnafikiri tunaweza tukawaacha tu hawa watu waendelee kuzubaa sisi tukaenda chunguza kile kilichotufanya tuje humu?”Swali likaulizwa na Special Agent Rebecca akiwa kainama chini kuchungulia mita hamsini kutoka walipo ambapo ndipo vikosi vilivyojikusanya kulinda lango vilipo kuanzia pale kwenda mbele na hata kutawanyika huku na kule.


“Inawezekana tukafanya hivyo.. Wazo zuri sana umelitoa Miss.. Kai unaonaje hilo?” Inv. Miller akaongea akiwa ameunga mkono wazo lililotolewa na Rebecca akataka kujua na nahodha wao anafikiria nini?.


“Sawa tufanye hi…!”Hakufanikiwa kumalizia alichotaka wote walishtushwa na mlio mkubwa wa mlipuko kutokea kwa nje ya huku walipo, taharuki kubwa ikawa kwa watu wanaowatizama huku na wao pia wakiangaliana.


“Mzinga mkubwa huo.. Kazi ya moto tuliouwasha inaendelea kuleta athari tuliyoitarajia..!” S.S Silla akaongea akitabasamu wakagonga tano na S.S Rebecca kushirikishana furaha zilizopo mioyoni mwao.


“Wanahangaika na hawana wazo lolote juu ya huku tulipo kama kunaweza kuwa tayari kushaingiliwa na wamarekani.. Nafikiri tutumie fursa kuondoka kuelekea upande ule ambao kwa hakika naamini kuna mengi ya siri yanayohusu hii kambi ya siri” Agent Kai aliongea akiwatizama wenzake kisha akaanza kuondoka akiwa kainama usawa wa kimo cha mbuzi beberu kubwa la mfugaji mzuri si mfugaji mbabaishaji.


Nyuma yake alifuata Rebecca huku Miller na Silla wakilinda usalama wa wenzao maana walikuwa wanapita gizani lakini eneo la wazi kiasi ya kwamba kati ya watu wale walio katika mita hamsini tu kutoka eneo hili walilo wao wangeweza kuangalia wangeweza kuwaona, safari ikiwa wameinama silaha zao haina ya bastola zilikuwa mikononi bunduki zikiwa zimepachikwa mgongoni kwa kamba zake iliwapeleka zaidi ya mita sitini ndipo wakafika mahala ambapo kulikuwa na nguzo kubwa za zege ambazo zimekwenda mpaka juu zikiwa ni nguzo za katikati zinazoleta uwiano wa nguvu za eneo hili la chini na la juu hapo waliegemea nguzo hii yenye pembe nne kwa migongo yao, macho wakiwa wameyaelekeza kule walipo wenzao na walipo adui zao.


“Mnaweza kuja sasa.. Tunalinda..”Akaongea Agent Kai akitumia ‘SCNG’ mfumo wao wa mawasiliano unaotumia saa na kifaa kidogo cha kupachikwa kwenye tundu la sikio ‘bluetooth earphones’.


“Sisi tutapita tukifuata ukuta hatutapita kwenye uwazi kama mlivyofanya nyinyi sababu tayari jamaa mara kwa mara wanaangalia na nyuma yao.


“Sawa!” Akakubali Kai na kushusha mkono wake aliokuwa kausogeza karibu na mdomo.


Haikuwa na haja tena Agent Kai na mshirika wake Rebecca kuangalia tena kule walipo adui na Miller bali waliangalia eneo ambalo walikuwa wakitamani kwenda, wakazunguka nguzo na hapo ndipo wakaona vigari vidogo vitatu vya kunyanyua mizigo ‘folko lift’ mara nyingi uwa vinatumika viwandani au katika mabandari, wakanyata mpaka vilipo wakapita kila mmoja na upande wake kwa pembeni kisha wakakutana mbele yake kukiwa na ukimya wa kuvutia watu kama wao wenye kupenda masikio yao yawe yanasikia kila kinachofanya mlio wa aina yoyote.


Hatua kumi mbele wakaona jengo kubwa lililo katika aina ya ‘godown’ (ghala) mbele yake kukiwa na lango kubwa juu likiwa na bango dogo lililoandikwa kwa maandishi yaliyokuwa hayaonekani vizuri ikionyesha yameandikwa bila mpangilio wenye umakini kwa aliyekuwa anaandika.


Wote wawili wakasogea hadi lilipo lango lakini kabla hawajaamua wafanye lipi S.S Silla na mshirika wake wa karibu Inv. Miller wakafika, hawakuongeleshana neno lolote.


Agent Kai akasukuma lango lile kubwa la mbao hakukuwa na utata halikuwa limefungwa kwa ndani na hata kwa nje, kiuwazi kidogo kilimtosha kuchungulia ndani macho yake yakaona kitu ambacho kilimjuza ni mtambo akasogeza zaidi kisha akapitisha kichwa chake kuhakiki akionacho hapo akaona aingie kabisa akaingia ndani akasimama kwa ndani moyo wake ukiwa umebadili mapigo kabisa unadunda isivyo kawaida yake.


Akawaonyesha ishara ndugu zake waingie nao wakaingia na wote wakastaajabu walichokuwa wanakiona katika macho yao.


“Hii mitambo ya kiwanda..”Akaongea Rebecca macho yakiwa kayatumbua ndani ya miwani aliyovaa.


“…Ndiyo na haijawekwa tu kama kuhifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya kile kiwanda tulichokiona nje hiki ni kiwanda kingine.. Swali la kujiuliza kwanini kimewekwa huku chini kisiwe juu?” Akaongea Agent Kai kisha akamalizia kwa swali ambalo hata asingekuwa na wenzake angejiuliza hivyo.


“Ni kiwanda cha siri… Hii ni mitambo ya kusaga mihadarati.. Aiseeeh!” Special Agent Silla akaongea kisha akaanza kuzunguka kwenye mtambo wa mashine wa kwanza ambao ulikuwa mbele yao, walizunguka eneo lote wakikagua kwa joto lililokuwepo iliweza kuwajuza mitambo hii ilikuwa ikifanya kazi usiku huu kabla umeme haujakatika.


“Walikuwa wakifanya kazi usiku huu… Hatari sana ndiyo maana hili genge linapalinda eneo hili kwa nguvu kubwa sana kumbe kuna siri kubwa hivi” Inv. Miller akaongea akiwa anaendelea kupiga picha kwa kamera yake ndogo ya kidigital, wengine walikuwa noa wanapiga picha kila wanachokiona kwa kutumia simu zao.


Walipomaliza eneo ilipo mitambo ya kiwanda kidogo kilichochukua eneo la ukubwa wa mita za mraba sitini (eneo kama la nusu ya uwanja na ziada ya mita zake kumi), mbele kulikuwa na tambala kubwa jeupe likiwa limetenganishwa eneo hili na upande huo ambao wao walikuwa hawaoni kilichopo upande wa pili.


Silla na Miller wakaongoza kuingia huko wakifunua tambala kila mmoja alipoingia alistuka na kuguna kwa mshangao mkubwa sana.


“Shehena ya unga uliokwisha tengenezwa.. Huu unga ina maana uwa wanaingiza sokoni?” Silla akauliza ikiwa anatambu ni ngumu kupata jibu la uhakika wa moja kwa moja.


Kai na Rebecca nao wakaingia na wao walipigwa na bumbuwazi kutoamini wanachokiona mbele yao ni viroba vyeupe ambavyo kwa mimi kama ningekuwa sijui lolote kuhusu viroba hivi basi ningejua ni viroba vya unga wa ngano vilivyopangwa katika ‘stake’ vikiwa toka chini mpaka juu.


Kila kiroba kilipata shambulizi la kutobolewa tobolewa kwa kisu na kufanya view vinamwaga unga taratibu kitu ambacho mtu kama Feca angeona wanafanya hivi angelia kwa sauti au kimya kimya machozi ndiyo yakimuonyesha analilia anachokiona kwa uchungu mkubwa.


“Tunawasha moto tena na huku… Tayari ni alfajiri muda wa dakika kumi na tano mbele kutakuwa kunaanza kukuchwa, usiku ushaisha huu..!” Agent Kai akaongea akiwa anarudisha simu yake mfukoni anayoitumia pia kama kamera ya kupiga picha na kuchukua video ya kumbukumbu kama hizi ikiwa ni ushahidi.


“Wazo zuri tuwashe moto tutoke kuanza mapambano ya ana kwa ana… Ingekuwa hatujamaliza milipuko ya kutegwa tungetegesha na kulipua tukiwa kwa nje” Silla akakubaliana na wazo la kuchoma moto mitambo na kila kitu kilichopo ndani ya jengo hili la kiwanda cha siri.


Kwa pamoja lilipita wazo la kuchoma moto wakashusha tambara kubwa chini kisha wakakusanya na matambara mengine yaliyofungwa katika mabomba yanayoshusha unga uliokwisha sagwa vizuri, wakayasambaza huku na huko kisha kiki moja tu ya kiberiti cha gesi ulifanya moto uanze kushika kasi ikifuata matambara! Moto ukawaka katika matambara ukifuata vilipo viroba katika ‘stake’ zao.


Moto ukiwa unakolea kwa kasi majasusi hawa wa kimarekani wakatoka nje wakiwa katika tahadhali ya hali ya juu, wote mbio zao zikawapeleka zilipo ‘folko lift’ bastola zao zilirudi kwenye hifadhi zake (mahala salama) bunduki zikahamia mikononi mwao.


“Upande ule wa chini nahisi kuna jambo lingine.. Mnakumbuka yule mwanamke alisema humu kuna gereza la siri ambalo alikuwa akimchukua Agent Jogre kwenda kufanya naye mapenzi, tuelekee huko haraka kabla moto haujaweza kuwafanya watu wale kuanza kuelekeza macho yao huku” Agent Kai akakumbusha kilichowafanya kuja katika nchi ya Guatemala na hata kuja katika kambi hii.


Walizunguka wakitembea sambamba na ukuta mpaka kona ya mwisho wakalizunguka jengo upande wake wa pili ndipo mita ishirini mbele wakaona kama bwawa kubwa la kujengwa si la asili. Katika ubongo wa Agent Kai akaanza kuhisi jambo.


Wakasogea wote wakiwa katika tahadhali na umakini mpaka yanapoanza maji kabla hawajakaribia kingo za kuta zilizojengwa kuzuia maji yale kupanda juu kuyafanya yawe kwa bondeni waliona mamba wakisogea ndani ya maji kwa kwenda huku na huko, bwawa kwa hapa karibu lilionyesha jinsi lilivyo pana likizunguka eneo za mita za mraba mia moja na zaidi kisha katikati kuna mjengo mkubwa kidogo uliojengwa ukiwa umezungukwa na bwawa hili kwa kila upande.


“Mnakumbuka mchoro wa Agent Jogre?” Akauliza Agent Kai akiwa hawatizami wenzake anaangalia ndani ya maji kutokea kwa mahali ambapo wote walikuwa wamelala chini.


“Ndiyo… Gereza alilomo ni jengo tunaloliona.. Hivi ni kweli watu wote wamekimbilia kule? Nafikiri tusiamini sana” Akajibu kwa niaba Inv. Miller akaweka swali ambalo pia akalijibu yeye mwenyewe.


“Moto ukijitokeza nje ya jengo la kiwanda chao tu hali ya taharuki italipukwa ndipo tutakapojua mbivu na mbichi… Kuna namna ya kwenda kule kwenye jengo la gereza ambayo kati yetu kaiona?” Akaeleza na kuhoji Agent Kai.


“Sioni boti wala daraja na maji haya mamba wanaonekana muda wote wana hamu ya kula nyama za watu, majamaa yanaonekana yamezoesha chakula cha miili ya binadamu hawa mamba” Akaongea S.S Silla.


Moto ulishika kasi ukiunguza kuanzia mitambo ya mashine pamoja malighafi unga mpaka unga wenyewe ukashindwa kuvumilia ukaanza kutoka nje na kujidhihirisha hapo Koplo Maxiwell Zuantejo na wafuasi wake walistuka na kuanza kutokea lililo tabiriwa na wazee wa mipango.


Mwisho wa sehemu ya tisini na tano (95)


Sehemu ya tisini na sita ni sehemu ambayo si ya kuikosa kwa jinsi hata mimi ninayehadithiwa stori hii kutoka katika mamlaka za ubongo wenye akili za ziada natamani kusoma ilikuwaje?



Wakasogea wote wakiwa katika tahadhali na umakini mpaka yanapoanza maji kabla hawajakaribia kingo za kuta zilizojengwa kuzuia maji yale kupanda juu kuyafanya yawe kwa bondeni waliona mamba wakisogea ndani ya maji kwa kwenda huku na huko, bwawa kwa hapa karibu lilionyesha jinsi lilivyo pana likizunguka eneo za mita za mraba mia moja na zaidi kisha katikati kuna mjengo mkubwa kidogo uliojengwa ukiwa umezungukwa na bwawa hili kwa kila upande.


“Mnakumbuka mchoro wa Agent Jogre?” Akauliza Agent Kai akiwa hawatizami wenzake anaangalia ndani ya maji kutokea kwa mahali ambapo wote walikuwa wamelala chini.


“Ndiyo… Gereza alilomo ni jengo tunaloliona.. Hivi ni kweli watu wote wamekimbilia kule? Nafikiri tusiamini sana” Akajibu kwa niaba Inv. Miller akaweka swali ambalo pia akalijibu yeye mwenyewe.


“Moto ukijitokeza nje ya jengo la kiwanda chao tu hali ya taharuki italipukwa ndipo tutakapojua mbivu na mbichi… Kuna namna ya kwenda kule kwenye jengo la gereza ambayo kati yetu kaiona?” Akaeleza na kuhoji Agent Kai.


“Sioni boti wala daraja na maji haya mamba wanaonekana muda wote wana hamu ya kula nyama za watu, majamaa yanaonekana yamezoesha chakula cha miili ya binadamu hawa mamba” Akaongea S.A Silla.


Moto ulishika kasi ukiunguza kuanzia mitambo ya mashine pamoja malighafi unga mpaka unga wenyewe ukashindwa kuvumilia ukaanza kutoka nje na kujidhihirisha hapo Koplo Maxiwell Zuantejo na wafuasi wake walistuka na kuanza kutokea lililo tabiriwa na wazee wa mipango.


ENDELEA NA MAPIGO..!!


BUTWAA XII


SAN MARCOS-GUATEMALA


“…Chucho! Kuna hali ya ujoto fulani unaosababisha baridi kushuka kila dakika inayosogea mbele.. Ni kwangu tu ama na nyie?” Swali hili liliulizwa na kiongozi mkuu katika usiku unaoendea kuisha na kuianza siku mpya rasmi kwakuwa tayari ilishakuwa ni alfajiri, Koplo Maxiwell Zuantejo aligundua kuna mabadiliko ya hali hewa ghafla kitu ambacho si cha kawaida katika eneo lao kambi ya Tajumulco iliyopo eneo hili la safu za milima ya Tajumulco.


“Ni kweli kuna hali unayoisema mkuu… Nuno unaonaje upande wako?” Aliyetajwa kwa jina la Chucho alijibu swali aliloulizwa kisha naye akataka uhakika toka kwa mtu mwingine aliye pembeni yake anayeitwa Nuno.


“Mi nasikia harufu ya kitu kinachoungua.. Na hata fukuto mlisemalo nalisikia pia” Nuno akaongea kisha akanyamaza kuwaangalia baadhi ya watu ambao nao wengi wao na wao waligeuka kuwaangalia wao waliokuwa kwenye kona moja ya ukuta mbele yao kukiwa na meza kubwa ya umbo la mstatili.


“Hali imebadilika kwa mbali kuna fukuto kidogo na sijui kwanini? Kifupi nahisi linatokea kwa juu” Akajibu mtu mwingine kutokea kwa walio karibu na lango wanalosubiri muda wote kitokee chochote mara akageuka kwa kasi baada ya watu kadhaa kuwaona wakiwa wamegeuka nyuma yao ikiwa mmoja aliongea jambo ambalo Maxiwell na wenzake walio karibu walistuka.


Moto uliokuwa umewashwa katika eneo la kiwanda ulikubali makali yake ikiwa kwa muda mfupi ambao harufu ya kitu kinachoungua kusikika, macho ya kila mmoja yalielekea kwenye majengo ya kiwanda chao cha siri.


“…Shiiit! Moto …Moto.. Moto! Kiwandani ..”Mmoja wao alikuwa mahala ambapo aliweza kuona upande ule kwa uzuri ndiyo alipaza sauti hiyo kubwa sana iliyopeleka mawimbi yake uliojibiwa kwa mwangwi hadi walipo Agent Kai na wenzake kando kando ya bwawa.


“Wengine endeleeni kuwa makini na mlango mkuu.. “ Maxiwell Zuantejo alipaza sauti kuwaelekeza jambo walio chini yake uso akiwa kaukunja pamoja na mwili mkubwa wa mazoezi alipita juu ya meza kwa wepesi kwa mtindo wa kujibiringisha mpaka upande wa pili kisha watu wengi wakaungana naye kukimbilia zilizpo ‘folko lift’ ambazo zilikuwa zimepokea moto utokao kiwandani kwa kasi huku moto mziti ukiendelea kushika kasi kutokea kwa ndani.


“Shenzi kabisa.. Nitaeleza nini kwa Feca?” Zuantejo alijikuta akiongea huku hajatulia anaruka ruka kama punda aliyejeruhiwa kwa mng’ato wa meno na chui kisha akaachwa kidogo.


“Maji.. Sogezeni gari za zima moto haraka.. Candrea na Nicholaus fanyeni haraka kwenda gereji ya magari ya zima moto huu moto utatukausha humu ndani” Bado Zuantejo aliendelea kutoa maelekezo huku moshi mzito unaotokea ndani na vilipo vi ‘folko lift’ ukianza kutapakaa kwa kasi kubwa kwakuwa vilivyowashwa vingi ni vitu vya kulipuka na kushika moto kwa urahisi.


Candrea na Nicholaus walizunguka wakiwa katika mbio kuelekea nyuma ya jengo linalowaka moto, ndani humu hakuna ambaye alikuwa hana hofu hata kina Agent Kai nao walikuwa na hofu ingawa wao si hofu kubwa sana lakini walikuwa nayo, waliwaona watu wawili wanakuja wakikimbia wakifuata barabara inavyoelekea.


Bastola ya Agent Kai aina ya Glock-7 Pistols iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti (sailensa) iliinuka kima cha juu kidogo ya paji la uso wake mkono wake wa kushoto akiwa kalala chini kabisa akawalenga na kuachia risasi moja moja za kila kichwa cha mmoja wa watu ambao kwakuwa walikuwa katika mbio walijikuta wakidondoka chini vichwa vyao vikipasuka kila mmoja akitupwa upande wake.


“Kazi imeanza.. Sijui walikuwa wanakimbilia wapi?.. Muhimu sasa ni kuingia ndani ya jela, asilimia mia Agent Jogre yumo humo” Akaongea Agent Kai.


“Hatujui jinsi ya kwenda huko.. Hatuwezi juwa bila kumpata muhusika mmoja..!” S.A Silla akaongea naye akiwa kaulaza mwili wake kama ilivyo kwa wengine wote.


“Tutafute namna ni viz..!” Alikuwa ni Rebecca anataka kueleza kitu lakini kwa ghafla walistushwa na kishindo kikubwa cha mlio ulioleta mtikisiko ndani ya eneo hili na hata eneo la jirani, mlio ulikuwa umetokea kwenye lango la kuingilia kiwandani, mshindo mzito uliolivunja hadi lango likarushwa huko kwa mbele.


Lango kuchomoka kwa kasi toka kwenye kizingiti chake liliwafanya walio mbele yake kuruka kwa pembeni likitua kwa kuwakosa kosa, mayowe yakasikika hali ya taharuki inayoambatana na makelele yasiyo na mpangilio yakaanza, moto ulikuwa mkali haswa.


“Toa taarifa kwa Feca.. Na watu waliosemwa watafika kwa helkopta wamekwama wapi?” Alielekeza kitu Chucho kisha akauliza swali likielekea kwa Zuantejo.


“Meseji ya mwisho kutoka kwao ilifika muda mfupi uliopita kuwa helkopta imepoteza mawasiliano nao.. Na hawajui ni kitu gani kimewakuta” Akajibu swali aliloulizwa Koplo Zuantejo huku wote wanarudi kinyume nyume maana moto ulikuwa ukizidi kukamata kila kilicho karibu na kiwanda chao cha siri.


“Kiongozi nashauri umtaarifu Feca juu ya huu moto..!” Nuno akashauri wakati huo huo kuna kijana mmoja alifika akiwa katika mwendo wa mbio akiomba kupishwa na wenzake walio nyuma ya Zuantejo.


“…Vipi?” Macho yalivyomtoka kijana yule wakati anaangaliana na Zuantejo ilimstua sana mkuu wake ikabidi amuulize kabla hata hajamfikia karibu.


“Moto haupo kiwandani tu.. Upo hadi nje ya hapa huko juu.. Na ndiyo maana kuna joto tunalolisikia juu yetu kuna moto unaowaka ukiteketeza kiasi kikubwa..!” Akaongea kasi kijana macho hayakuacha kutumbuka kama anataka kuyatoa nje ya fremu yake inayoshika na kuhifadhi macho.


“Umejuaje?” Akauliza Zuantejo kwakuwa hakuna aliyefungua lango kuu ikiwa ni kudhibiti maadui zao wasiingie.


“Kumekucha mkuu.. Tayari wanaotakiwa waingie zamu asubuhi hii katika kiwanda cha kahawa na hata wanaohudumia shamba la kahawa wameamka na ndiyo wamestushwa na moshi mzito juu ya paa zetu, walio wa kwanza kwanza kuona wakawaamsha wenzao.. Spreto ni mshikaji wangu akanipigia kunitaarifu.. Wanasema hata viongozi wa kijiji nao wameshafika” Akaeleza kijana yule.


“Kama ni kweli hakuna haja ya kusubiri humu ndani tu, tutokeni kwenda kupambana ana kwa ana na adui zetu… Sisi tuko wengi na tuna mafunzo kama wao pia” Nuno akaingilia kati mazungumzo kwa kuleta wazo lake.


“… Sawa anavyosema Nuno… Mkuu tufanye hivyo, fungueni lango kisha tuone moto wa huko juu kama umesogea hadi chumba cha maulizo mapokezi!” Chucho akaongea naye, hapa moto ulikuwa haujaweza kukamata dari kwakuwa dari kama hujuvyo eneo la chini ya ardhi linapojengwa uwa na zege juu.


“Adui zetu watakuwa wameshaondoka eneo hili kama wameweza kuona watu kutoka kijijini wameshafika hawataweza kuendelea kuwepo mpaka sasa hivi maana na wao wanaogopa kitakachowakuta wakifosi kuingia bila umakini wowote” Nuno akaongea tena akimuangalia mkuu wake wa kazi ambaye shingo yake ilikuwa ikikishurutisha kichwa chake kuangalia huku na huko na giza sasa alikuwepo kama lile lililokuwa mwanzoni walau dakika ishirini zilizopita, aliitizama simu yake ya mkononi kisha akasogea kando kidogo akikiacha kikundi kilichomzunguka.


Alipiga namba za boss wao, boss wa The Red Jaguar ‘Kingpin’ Fernandes Carlos Codrado, simu ikaanza kuita kwa haraka ikapokelewa.


“Zuantejo!” Sauti aina ya kukaripia au kama ya mtu aliye kasirika sana ilisikika ikilipuka sikioni mwa Zuantejo toka katika spika za simu.


“Hali si shwari kaka… Tajumulco imezungukwa na moto kuanzia juu na hata humu ndani umeibuka moto ndani ya kiwanda na ghala kuu la mali yetu na sijui umewakaje”


“Shenzi!!!” Ilisikika sauti hii tu kisha simu ikakatika mpaka Zuantejo akaileta mbele kutoka sikioni afanye uhakiki kwa kukiangalia kioo kuona imekuwaje.


Koplo wa jeshi la wananchi wa Mexico miaka ya nyuma alirudisha simu mfuko wa mbele wa suruali akasogea walipo wenzake.


“…Mbona Candrea na Nicholaus hawaleti gari za zima moto.. Nuno waangalie nini tatizo” Zuantejo akaongea tena na kisha akatoa kitambaa cha jasho (leso) akajifuta jasho lililokuwa linatoka kichwani na usoni mwake.


Nuno alitoka mbio akipita pembeni pembeni asigusane na ukuta wa kiwanda ambao kwa ndani kulikuwa kunawaka moto, mbio zake kama kafunga mota zilimfikisha hadi eneo ambalo upande wa pili kuna bwawa linalozunguka jengo ambalo Agent Kai na wenzake wanaamini ndiyo gereza ambalo barua pepe iliyo katika fumbo la mchoro aliyotumiwa ‘TSC’ ilikuwa ikielekeza hapa.


Gereji yenye magari yenye zima moto ilikuwa inaonekana kwake ikiwa kama mita kumi tu ndiyo afikie lakini ilimstaajabisha kuwa lango la mbele lililo kama geti la kupanda juu halikuwa limefunguliwa hivyo anaowafuata watakuwa hawajalifungua, swali kuu kwake ‘wako wapi?’, taratibu akaanza punguza mwendo mara akahisi anaguswa na kitu chenye ubaridi katika shingo yake alipotaka kugeuka akasikia mlio wa bunduki inayokokiwa magazine tayari kwa matumizi.


“Tulia vivyo hivyo, usigeuke wala usisogee!” Sauti nzito yenye kitisho ndani yake iliunguruma, alikuwa ni Agent Kai kazini.


“Nani wewe… Umetokea wapi?” Maswali mawili ya kufutana yalitoka mdomoni mwa Nuno akitamani ageuze shingo kumuangalia aliye nyuma yake akiwa kamuwekea mdomo wa mtutu wa bunduki katika shingo yake.


“Mtu kama wewe.. Sikia hatuna muda wa kupoteza.. Tunataka kujua juu ya jengo lililo ndani ya bwa hili lenye mamba ni jengo la nini?” Akauliza Agent Kai na papo hapo S.A Rebecca akajitokeza mbele ya Nuno akitokea pembeni kidogo alipokuwa kajibanza.


“Nyie kina nani? Mmefikaje hapa?” Hakujibu swali bali aliuliza tena kitu ambacho kilimkera Agent Kai akamtia ‘mbata’ (kibao cha chini ya kichogo na juu ya shingo kwa nyuma) kilikuwa kizito mpaka Nuno akasogea mbele bila kupenda ambako napo Special Agent Rebecca akamuongeza kibao kingine kikali cha uso kiganja kikitua katikati ya macho yote mawili.


“Pata chai kwanza, kumekucha!” Akaongea Rebecca akitabasamu.


“Haya jibu haraka sana… Ukileta kujua jua tena kutuzungusha kama unamzungusha mtoto wako kwenye bembea nakutoa roho uwafuate wenzako ambao tushawarushia kwenye bwawa washazikwa kwenye matumbo ya mamba” Onyo kali likafuata baada ya chai ya vibao vya moto.


“Jengo lile?” Akauliza akibabaika kugeuka kwa uoga kule lilipo bwawa.


“Ndiyo.. Ongea haraka lasivyo naenda kukurushiwa kwenye bwawa ufe kifo cha kuliwa na mamba kaburi lako liwe ndani ya matumbo yao..” Agent Kai akaongea kisha akamkamata ukosi wa jaketi alilovaa akaanza kumvutia kama wanaenda kwenye bwawa la mamba kumbe geresha.


“Basi! Basi! Nitasema mkuu..” Akajibu kijana huyu wa kizungu ambaye kwa jinsi alivyo ilikuwa tosha kusema ni mmexico aliyekuja hapa GTL kwa kazi tu na hata lafudhi yake haikufanana na lafudhi za watu hapa, alijifuta mdomo kwa kiganja chake kisha akamtizama Rebecca umbali uliopo baina yao kana kwamba anataka kufanya kitu lakini nafsi yake ikamuonya bunduki iliyoelekezwa kwake ilimnyima fursa hiyo.


“Tajumulco Prison… Hapa ndipo uwa tunawafunga bila hukumu watu kadhaa wanaoenda kinyume na utaratibu wetu ikiwemo wale wanaoingilia mipango yetu kama maafisa wa DTO, OCLA, DEA na wengineo wengi kutoka nchi mbalimbali ambazo TRJ zina maslahi nazo katika biashara zetu” Akaeleza Nuno akili yake ikiwa ishaona watu hawa mwanamke na mwanume hawana masikhara anaweza kugeuzwa hasusa ya mamba kweli kama ataleta umaandazi.


“Tumeona kote kumezungukwa na maji ya bwawa kama inavyoonekana mnaenda vipi pale?” Akauliza tena Agent Kai.


“Umeme hamna haiwezekani kutumia njia ambayo uwa tunaitumia mara zote” Akajibu kwa haraka kwa kilatino chake cha kimexico.


“Kivipi?” Akahoji Rebecca, wakati huo S.A Silla na Inv. Miller walikuwa makini kuangalia kwenye njia inayoji upande huu kutokea mbele ya kiwanda cha siri.


“Pale katika sanduku lililo kama sanduku za mtaani za barua ndani ya box ukishalifungua kuna swichi iko moja tu hiyo ukibonyeza kuna daraja utokeza kwenye ngazi zile hapo uwa linaenda mpaka kwenye baraza ndipo unafika kama unataka kufika Tajumulco Prison na ndiyo maana nimesema lenyewe linatumia umeme kufanya kazi hiyo na ukiwa haupo umeme basi uwa kuna jenereta kubwa linaloleta umeme eneo lote juu na chini” Akajibu jibu ambalo majasusi hawa wa kimarekani wakaangaliana usoni jinsi kazi ilivyo ngumu huku kukiwa kunazidi kupambazuka.


“Walinzi wanaolinda gereza hili wapo ndani ya gereza au?” Akauliza tena Rebecca.


“Hapana! mamba wa bwawa na milango isiyofunguliwa na mtu aliye ndani ndiyo walinzi wa gereza hili” Akajibu Nuno.


“Hapa ndiyo nimezidi kufunguliwa ubongo wangu juu ya mchoro alionitumia Jogre.. Aisee tunafanyaje? Hata sijui sasa nimechoka mwili mpaka akili” Akaongea Agent Kai kitu ambacho ni aghalabu kwake kuongea katika maisha yake uongea mara chache maneo haya.


Mwisho wa sehemu ya tisini na sita (96)


Agent Kai amekiri kuwa kuna ugumu wa wao kufanya jambo juu ya kulifikia gereza linaloitwa ‘Tajumulco Prison’, gereza linalohifadhi wafungwa ambao hawajahukumiwa na mahakama na hata makosa yao si makosa ya kuwatia hatiani kutoka kwa jamii ni kosa la tu kuonekana ni mtu wa hatari katika maslahi ya genge la ‘THE RED JAGUAR’.


Majasusi hawa watafanyaje?


Je nini watafanya na kitu muhimu kwao ni kitu kilichowafanya wafike hapa Guatemala ni kumpata Agent Jogre wa DEA?.


Kwa uhondo kamili wenye ujazo wa nondo za mapigo ya kisasa ni kusogea episode inayofuata..




“Tajumulco Prison… Hapa ndipo uwa tunawafunga bila hukumu watu kadhaa wanaoenda kinyume na utaratibu wetu ikiwemo wale wanaoingilia mipango yetu kama maafisa wa DTO, OCLA, DEA na wengineo wengi kutoka nchi mbalimbali ambazo TRJ zina maslahi nazo katika biashara zetu” Akaeleza Nuno akili yake ikiwa ishaona watu hawa mwanamke na mwanume hawana masikhara anaweza kugeuzwa hasusa ya mamba kweli kama ataleta umaandazi.


“Tumeona kote kumezungukwa na maji ya bwawa kama inavyoonekana mnaenda vipi pale?” Akauliza tena Agent Kai.


“Umeme hamna haiwezekani kutumia njia ambayo uwa tunaitumia mara zote” Akajibu kwa haraka kwa kilatino chake cha kimexico.


“Kivipi?” Akahoji Rebecca, wakati huo S.A Silla na Inv. Miller walikuwa makini kuangalia kwenye njia inayoji upande huu kutokea mbele ya kiwanda cha siri.


“Pale katika sanduku lililo kama sanduku za mtaani za barua ndani ya box ukishalifungua kuna swichi iko moja tu hiyo ukibonyeza kuna daraja utokeza kwenye ngazi zile hapo uwa linaenda mpaka kwenye baraza ndipo unafika kama unataka kufika Tajumulco Prison na ndiyo maana nimesema lenyewe linatumia umeme kufanya kazi hiyo na ukiwa haupo umeme basi uwa kuna jenereta kubwa linaloleta umeme eneo lote juu na chini” Akajibu jibu ambalo majasusi hawa wa kimarekani wakaangaliana usoni jinsi kazi ilivyo ngumu huku kukiwa kunazidi kupambazuka.


“Walinzi wanaolinda gereza hili wapo ndani ya gereza au?” Akauliza tena Rebecca.


“Hapana! mamba wa bwawa na milango isiyofunguliwa na mtu aliye ndani ndiyo walinzi wa gereza hili” Akajibu Nuno.


“Hapa ndiyo nimezidi kufunguliwa ubongo wangu juu ya mchoro alionitumia Jogre.. Aisee tunafanyaje? Hata sijui sasa nimechoka mwili mpaka akili” Akaongea Agent Kai kitu ambacho ni aghalabu kwake kuongea katika maisha yake uongea mara chache maneo haya.




ENDELEA NA MAPIGO NONDO..!!



BUTWAA XIII

SAN MARCOS-GUATEMALA

“Kwa mara ya kwanza ni leo kukusikia umechoka boss wangu..!!” S.A Rebecca akaongea akimtizama machoni Agent Kai.


“Kwani wewe hujachoka Rebecca?” Akahoji swali ‘TSC’ naye macho yake yakiwa yametuhama kwa Rebecca huku kamuwekea mtutu wa bunduki mateka wao wa muda mfupi ambaye walikuwa wamemkalisha chini kwa kumlazimisha.


“Mmmh! Sijakuelewa kuchoka kivipi? Naona swali lako lina kamtego ndani yake”

“Unaogopa kujibu? Unakwepa swali langu?”

“Ndiyo nalikwepa swali hilo sababu wewe ni boss wangu nitakavyojibu jibu ambalo lipo nafsini mwangu linaweza kuwa si jibu la mfanyakazi kumjibu boss wake” Akajibu akitabasamu Rebecca kisha akazungusha macho yake kuangalia alipo S.A Silla akamuona haraka akazungusha kwa Inv. Miller akamuona yuko makini kuangalia kona ambayo mtu akiwa anakuja huku walipo basi utokea.


“… Kumbe uwa unaniogopa kwa sababu ni boss.. Hahahah hah.. Mi pia binadamu si malaika hivyo nachoka… Hatujalala usiku wote tumetoboa tukiwinda na kutumia akili nyingi sana katika kila jambo hii ni moja ya ngome ngumu sana kuwai kukutana nayo toka nibadili kutoka jeshi kuja kwenye kazi hii.. Kichwa kimekuwa kizito kwa sababu ya usingizi ambao kibinadamu hatuukwepi ni ngumu kutoboa kirahisi rahisi bila kujihisi ninavyohisi..!”


“Ni kweli boss! Khaah! Ni kweli kabisa maana mimi nishawai lala nikiwa kwenye mafunzo tena silaha na milipuko ikipasua kwa sauti kuu” Akaongea Rebecca akitabasamu kana kwamba hawapo eneo ambalo maamuzi yanatakiwa kufanyika kwa haraka sana na hii ilikuwa ni moja ya njia ya kawaida kwao katika kujiweka au kujirudisha katika hali ya kufumbua vitendawili vilivyo ndani ya mafumbo kikazi.


“Umeona.. Nami ni kama wewe ila mimi nilishapitiwa na usingizi eneo la mabomu mazito mazito yakirindima katika moja ya vita niliyoshiriki na si vita moja tu… Sishangai sana watu pia uwa wanalala viwandani mitambo ikiwa imechachamaa kufanya kazi.. Vipi ushafikiria tunafanyaje na bwawa hili?” Aliongea kirefu tena na ghafla kubadili maongezi kwa kumpachika swali Rebecca.


“…Hah..Mmmh mmh! Bado sijafikiria bado niko njia panda ingawa nafikiria tena kwa hesabu kali mbali mbali lakini kila nikiangalia hali ilivyo sioni njia boss!”


“Kijana maisha yako mikononi mwetu.. Tunaweza ingia mktaba ambao una maslahi kwako na kwetu.. Kama utaweza kufanya vile ambavyo sisi tunatamani tutakuacha huru hatutakudhuru kwa namna yoyote ile, upo tayari kwa hilo?” Maongezi yalibadilika toka kwa Rebecca kuja kwa Nuno mateka wao wa muda mfupi, kichwa chake kilikuwa kimeinuliwa hili uso wake uweze kumuangalia Agent Kai aliyesimama mbele yake sasa yeye mateka akiwa chini kakalishwa na hata mask aliyovaa usoni Kai aliirudisha juu waweze kuangaliana ana kwa ana.


“Kivipi boss?.. Mbona nimeshajibu kila mlilotaka kujua kutoka kwangu baada ya kuniambia nisipojibu nitakuwa kifungua kinywa cha mamba asubuhi hii” Akajibu Nuno huku moyoni mwake akitamani wenzake watokee huku nyuma ya jengo la kiwanda cha siri linalowaka moto kwa ndani unaoleta joto hadi wao walipo kwakuwa ukuta unaozunguka jengo la kiwanda ulikuwa ukuta wa bati nzito yenye unene fulani zao la moja ya viwanda vya chuma vya ‘Kingpin’ Feca, kitu ambacho hakuwa anajua Nuno ni kuwa ‘TSC’ na Rebecca hawakuwa peke yao kama anavyodhania yeye kwakuwa hakuwa amewaona Silla na Miller wanaowalinda watu hawa wanaotaka kujua habari za gereza la siri la Tajumulco Prison.


“Kitu pekee kilichotuleta humu ndani ni hili gereza… Sisi ni majasusi wa moja ya mashirika ya kijasusi ya Marekani kati ya mashirika kadhaa ya kijasusi.. Kuna wafungwa ambao ni majasusi wenzetu wa moja ya shirika kijasusi la Marekani wanashikiliwa humo, upelelezi wetu umetufikisha hapa hivyo hatuna chochote tutakachokuwa tumefanya bila kuingia ndani ya gereza hili” Agent Kai akaeleza tena kumueleza Nuno.


“Nyinyi ndiyo tuliokuwa tunawazuia msiingie kupitia lango kuu?” Akauliza Nuno swali ambalo kwa Kai na hata Rebecca ilikuwa ni karaha lakini hawakuwa na njia zaidi ya kuweka subira wapate lolote la kuwasaidia.


“Ndiyo… Na tafadhali usituulize zaidi lingine sababu muda si rafiki ila kama utatujibu vizuri kile tunachotaka nakiri kwako nikiweka kiapo kuwa utakwenda kujua mengi juu yetu.. Naomba kujua zaidi juu ya njia ya ziada kuingia ndani ya gereza hili na kuweza kuangalia hao tunaosema ndugu zetu”

“Lakini uvamizi wenu kaka umeharibu miundo mbinu ya umeme hivyo kiukweli kuna ugumu mkubwa” Nuno alikuwa anawazubaisha akiamini kuzidi kwake kuchelewa kutasababisha Koplo Zuantejo kutuma watu zaidi kuja kuangalia kulikoni na yeye arudi toka aagizwe kuzunguka huku gereji ya gari za zimamoto kuja kuwaangalia wenzao wawili waliogizwa na kuchukua muda mrefu kutorudi.


“Hatukuwa tunajua hili hatukuwa na mchoro wa kutuonyesha mengi ya humu, aliyesababisha tuje hapa ambaye ni mwenyeji wa hapa alitupa maelekezo yasiyotosheleza sababu alitaka tushindwe katika jaribio hili.. Na kiukweli naamini wewe unajua njia ya ziada ya kuweza kwenda kule sababu si rahisi muweke njia ya kuhusu umeme wakati umeme si kitu kilichoumbwa moja kwa moja na Mungu, umeme ni kazi ya binadamu na kazi ya binadamu uwa haikosi mahala pa kukwama siku zote maishani mwake… Naomba tuambie njia ingine ni ipi haraka?”


Wakati wanaendelea kumbana aweze kueleza njia ingine watu watano walitokea toka kona ya mbele wakiwa wanakuja kwa tahadhari kana kwamba wameshahisi tatizo, pia moto ulikuwa umechanganya mpaka sasa ndani kukawa na kelele za watu zinazoleta fujo wakielekezana mengi ya kufanya kana kwamba wanabishana kumbe ni maelekezo wafanye nini ikiwa wamegundua na hata njia ya kwenda nje imeshika moto hali ni tete kwao hofu kwao ikiwa si adui zao tu hofu ikiwa ni kufa au kuzuliwa na moto unaowaka kwa hasira ukiteketeza kila unachokumbana nacho kwa hasira kali kama uujuavyo moto unapokosa kudhibitiwa na mwendo wa kulipuka tu vya kulipuka kila unapofikia na kuleta taharuki masikioni kwa kila mtu aliyemo humu ‘flour’ ya chini.


Silla na Miller waliwaona watu wale wakija kwa mwendo wao wa kunyata bunduki zao zikiwa zimetangulia mbele, wote Silla na mwenzie kama wameambiana waliangalia viwambo walivyofunga mbele ya mdomo wa bunduki zao vinavyozuia mlio wa bunduki kuwa wa kuogofya masikioni mwa watu (sailensa), S.A Silla alivusha macho yake kumwangalia Miller kisha akayarudisha kwa watu wale akiwa kwenye nguzo inayomfanya aonekane kama kivuli kama mtu atasogea umbali mdogo na alipo.


Wawili walio mbele walijikuta wakirushwa kurudi nyuma kwa shambulizi la ghafla toka kwenye bunduki ya Silla likiwa shambuliz la ghafla bila hata Miller kuhisi itaweza kuwa mapema hivyo lakini naye hakuzubaa aliwaondoa wawili wa nyuma na Silla akammalizia mmoja wote wakadondoka chini wakiwa wameshabadili majina yao ya kwanza yaliyokuwa ndiyo yanaanza yakisogea mbele baada ya hilo lililoongezeka la marehemu au hayati.


Silla akatokeza alipokuwa amejificha kisha akaruhusu mawasiliano ya ‘SCNG’ kufanya kazi akabonyeza kitufe iite kwa wenzake alipoona imepokelewa akasogeza mkono wake karibu na mdomo bunduki akiwa kaikamatia mkono wake wa kulia ambao hakuwa amevaa saa.


“Mnanipata wote? Tutasogeza mamba sehemu hii juu kwa kila maiti kuitupa ndani ya bwawa navyojua mimi mamba wote wa sehemu zingine watakimbilia huku kisha tutajaribu tutakachoweza” Akaongea Silla bila kusubiri jibu akawa kashaifikia ile miili iliyojibwaga chini damu zikiwa zinaendelea kutoka kwenye miili ile na kuleta harufu kali ya damu mbichi ya binadamu.


Miller alielewa naye akatoka alipojificha akasogea ilipo miili wakaanza kuiburuza kwa kasi mpaka ilipo kingo ya ukuta iliyojengwa kwa chini ndipo kuna bwawa hapo wakaisukuma miili ndani ya maji wakafanya hivyo wakirudia na iliyobaki, mamba kama walivyofikiri walisogea kwa kasi laiti kusingekuwa na kelele za watu wanaoongea bila mpangilio katika kuangalia uwezekano wa kuzuia moto matukio haya yangeweza kusikika kwa uzuri na watu walio mbele ya jengo la kiwanda.


Kwakina Agent Kai mahojiano yalikuwa yakiendelea na hili kumuogopesha zaidi waliweza kumsimamisha kisha akaonyeshwa kula walipo kina Silla wakiitupia miili kwenye maji ndipo kijana Nuno akatambua kumbe kuna watu wengine zaidi.


“Muda si mrefu na wewe utaongezeka katika kuwa kifungua kinywa cha mamba mnaowafuga kwa ajili ya kuwala maadui wenu wa genge la TRJ.. Ipi njia ingine tutakayoweza kuitumia? Na kuhakikishia ukitujibu vizuri hautakuwemo kati ya watu ambao tutawahesabia ni adui zetu wanaostahili kukutwa na jambo baya… Maana muda si mrefu jeshi la Marekani lenye wanajeshi makomandoo zaidi ya mia moja wanafika hapa hivyo salama yako ni kujisalimisha kwetu kwakuwa mkweli tu” Rebecca aliongea akiwa kamshika kidevu kijana yule kama anamminya kumalazimisha kumbe anamlazimisha aangalie walipo kina Silla wakifanya kazi ya kusogeza maiti za watu kwenye makaburi ya matumbo ya mamba.


“Ipo njia lakini si salama sana.. Ukizunguka kwa nyuma kuna boti ambayo haitumiki mara kwa mara kwakuwa ilishawai kupinduliwa na mamba na kuua wenzatu wanne” Akajibu Nuno.


“Siku hiyo mamba walikuwa na njaa kali leo tayari washakula asubuhi asubuhi chakula kitamu.. Twende ongoza huko” Agent Kai akaongea akiwa anamuinua Nuno.


“Silla na Miller akikisheni hasogei mtu kuvuka mstari mliojichorea pia huduma kwa mamba iwe endelevu tunataka mamba wote waamie mbele…!” Agent Kai ‘TSC’ akaongea tena safari hii akitumia kifaa cha mfumo wao wa mawasiliano (SCNG) hili aweze kuwafikishia ujumbe wenzao.


waliongozana kuzunguka kando kando ya bwawa mpaka wakawa wanaliona gereza kwa upande si kwa mbele tena huku kule walikotoka karibu na ‘yard’ ya magari ya zimamoto wakiwa hawapaoni pia.


“Hii hapa!” Akaonyesha Nuno boti iliyofungwa kamba yake katika moja ya nguzo zilizo juu kukiwa na ngazi inayoteremka kwenda chini lilipo bwawa lakini kabla hazijaanza ngazi kule kule chini kulikuwa na geti lililosukwa kwa nondo hii likiwa ni kwa ajili ya kuzuia mamba kupanda ngazi kuja juu.


“Ahsante .. Kuna njia moja ya kukulinda kwa sasa nayo ni hii..” Aliongea Agent Kai akitanguliza shukrani kisha kama bondia mwenye kasi ulingoni ngumi yake ya mkono wa kushoto ilitua pembeni ya shingo ya Nuno kwenye vimishipa ambavyo watu wenye mafunzo kama yeye Agent Kai uwa anapomshambulia mtu uwa kashajua nini anafanya na wapi anapalenga hata iwe gizani kama hapa miwani yake ilimsaidia kuona shingo vizuri, alimdaka mwili hili asiporomekee kwenye bwawa na kusababisha mamba wengine kufanya ziara za upande huu haraka akamlaza chini.


“Twen’zetu!” Akaongea ‘TSC’ wakitizamana na mshirika wake, wakaruka kizuizi na kukanyaga ngazi zilizowateremsha kwa pamoja mpaka kwenye geti lililosukwa kwa nondo wakaruka na kihs akwa kasi ya pamoja wakarukia ndani ya boti ikiwa wameshafungua kamba inayozuia isiondoke eneo hili wakati haitumiki.


Kwakuwa hawakuwa na funguo Agent Kai alitumia ujuzi wake wa kuwasha injini kama hizi za vitu vya moto kwa kufumua nyaya zilizo eneo la funguo kisha akaziunganisha anavyojua yeye boti ikawaka akaiondoa akiendesha yeye mwenyewe huku Rebecca akiwa analinda usalama wao bunduki mkononi macho yakitupwa huku na huko.


Mita arobaini za kutoka ukingoni mwa bwawa kuja katikati ndipo jengo la gereza la kificho lilikuwepo walifika katika kibaraza wakashuka na kuifunga boti kwenye nguzo za kibaraza wakawa wanauangalia ukuta mrefu unaokadiria futi kumi kwenda juu uliozunguka jengo lililo ndani, ukuta ambao juu yake kulikuwa na nyaya ambazo ukizitizama ukiwa mzoefu utaweza tambua ni nyaya zilizounganishwa na umeme kuzuia mtu kuuparamia ukuta iwe kwa ndani au kwa nje.


“…. Tutapanda ukuta bila kujali nyaya unazoziona kwa sababu umeme hamna hivyo hakuna madhara yoyote” Akaongea Agent Kai huku macho yake yakiwa yanaangalia juu kabisa ya ukuta zinapooneskana nyaya zimesukwa sukwa.


“Sawa boss.. Nikiuangalia ukuta huu unanikumbusha Putatan, Sabah huko Malaysia kulikuwa na mvua kubwa inanyesha tukiwa tunaangalia juu tunawezaje kukwea kwenda juu… Hahaha hahaha hatari sana.. Niambie tunakweaje na leo hapa?” Akaongea Rebecca ana kuuliza.


“Gloves zangu zenye sumaku ya ukuta ninazo.. Ila wewe nahisi huonagi umuhimu wa kuwa nazo.. Hahaha hahahah…”

“Kwahiyo mimi mbuzi nisiyejifunza? Mimi siyo binadamu?” Akaeleza Rebecca akiwa anatabasamu mikono yake ikiwa kaitumbukiza kwenye begi anatafuta cha kutafutwa.


“Ooooh! Kumbe umekumbuka kubeba safari hii… Safi sana miss wangu!”


Dakika moja mbele walikuwa wote wako juu wamezikamata nyaya ambazo kikawaida uwa na umeme lakini kwa hapa muda huu hazikuwa na umeme na hata zingekuwa na umeme mbele ya gloves walizovaa ilikuwa ngumu wao kudhulika.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog