Simulizi : Zawadi Toka Ikulu
Sehemu Ya : Tatu (3)
Nikiwa pale chini polisi walifika kwani walikuwa wamesha pigiwa simu nilikabidhiwa kwa polisi na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Mwanza niliwekwa mahabusu.
Mazingira ya chumba cha mahabusu yalitia kinyaa, yalikuwa machafu yasiyo na mvuto kamwe sikupenda kuyaangalia. Ukigeuka huku ndoo ya kinyesi hapa chini mkojo, watu wamekojoa hovyohovyo. Harufu ya mle ndani haikuwa rafiki kwa afya ya binadamu, hapafai hata kupakanyaga lakini ningefanya nini mimi ambaye tayari niko matatizoni.
Nilikuwa mle ndani kimwili ila mawazo yangu sasa yalikuwa yakimuwaza rafiki yangu Domi, niliwaza juu ya afya yake maana nilijua huenda akapoteza maisha na hii ingekuwa mbaya zaidi kwangu sit u kufungwa lakini hata mahusiano mabaya na familia.
Niliyawaza maisha ya mle ndani na nikayatafakari maisha ya jera iwapo ikitokea bahati mbaya akafa, nilitikisa kichwa huku nikijiuliza kama mahabusu kupo hivi itakuwaje huko gerezani?. Nilitikisa kichwa na kumuomba Mungu aepushe lisitokee la kutokea maana nilikuwa katika hali tete ya sintofahamu iliyoniweka njia panda.
Kwa hali niliyokuwa nayo nilijaribu kumfikiria mpenzi wangu iwapo atazipata hizi taarifa itakuwaje, wakati wote huu nilikuwa nikitiririkwa machozi maana nilijuta kwa kile nilichokifanya.
Baada ya mchanganyiko wa moshi wa sigara za vijana niliokuwa nao ndani, harufu ya viroba ukichanganya na harufu ya mikojo na kinyesi, ilikuwa bangi tosha ya kuivuruga akili yangu na kunijengea ujasiri hakuna mtu aliyethubutu kunisogelea. Huku nikiwa na tahadhali ya simulizi za jera maana nilikwisha zisikia toka kitambo kuwa ukilemaa kuna ndoa hiyo nilichuykua tahadhari yakutosha.
Usiku wa siku hiyo nilikuwa nimejikunyata kwenye kona kama kifaranga yatima mwenye ugonjwa wa kideli, nikiwaza na kuwazua, mbu nao walinishughulikia ipasavyo na walifurahia uwepo wangu. Maana koti, shati langu, mkanda, viatu na suluali niliviacha mapokezi na hapo nilikuwa nimebaki na sing’iendi na kikabutula cha ndani.
Nikiwa nimejikunyata mpweke huku nikilisikilizia baridi kali lililotoka ziwa vikitoria na kupenya vyema kwenye nondo za madirisha ya chumba cha mahabusu na kuifanya sakafu na kuta kuongeza baridi.
Radi ngurumo na mvua kali ya upepo iliyonyesha usiku huo, ilizidi kuubadilisha ule usiku na kuufanya kuzidi kuwa moja ya siku mbaya kuwahi kutokea maishani mwangu, kwani upepo ulikuwa ukipuliza na maji yalipenya kwenye madirisha ambayo hayakuwa na viooo na kuingia mpaka ndani ambapo yalituosha na kutuacha tumelowa huku tukitetemeka.
Asubuhi kulikucha nikiwa nimelowa, maji yakiwa yamejitenga mle ndani tukawa tunayakanyaga, ni mchanganyiko wa mkojo na kinyesi wenzangu niliona wakikanyaga bila kujali kwa upande wangu sikulidhishwa na hali hiyo nilibaki nimejikunyata kwenye kisehemu kikavu ambacho hakikufikiwa na maji.
Kwa kweli mahabusu hapafai na kamwe hapata kuja kufaa milele. Siku ya kwanza ilipita hakuna aliyekuja kuniona, mtu wangu wa karibu ni Domi ambaye sikuwa najua kama yuko hai ama kuna lolote lililotokea. Upande wazazi wangu bila shaka walikuwa hawajapewa taarifa au walizipata kwa kuchelewa kwasababu hakuja kuniona.
Jesca niliamini hajui chochote kilichoendelea maana simu yangu ilikuwa haipatikani nimeiacha mapokezi kabla sijawekwa ndani. Siku hii ya leo ilikuwa ni siku ya matarajio makubwa kwangu maana niliamini watu wengi watakuja kuniona.
.
Majira ya saa mbili asubuhi alikuwa ni baba yangu, mzee Justine Mathias akiongozana na mama yangu kipenzi Bi Helen Moga. Nilifurahi kuwaona wazazi wangu baada ya kuitwa kuja kuwaona ndugu zangu, pamoja na kwamba nilikuwa kwenye matatizo makubwa lakini faraja yao ilihitajika na uwepo wao ilikuwa ni fahari kubwa kwangu.
Mama yangu alikuwa akilia sana lakini niliuona uwepo wake kama faraja kwangu. Ninawapenda sana wazazi wangu maana wao walikuwa ni faraja kubwa maishani mwangu, naweza kusema ni faraja pekee katika maisha yangu maana hakuna mwingine aliyeweza kuitunza thamani yangu kama walivyofanya wao kila siku.
Baada ya mama kunisalimia na sasa alikuja baba tukasalimiana na kuongea mengi. Kubwa alinilaumu kwanini nimechukua hatua ya kumuadhibu Domi ambaye ni rafiki yangu kipenzi. Alisema “unajijua ulivyo mwanangu kipenzi, hupaswi kupigana kwanini unajitafutia matatizo mwanangu? Harafu mbaya zaidi uliyepigana naye hana mafunzo uliyonayo wewe. Ulimwengu unamaudhi nalijua hilo ila kuzaliwa kwako mwanaume ni somo tosha la wewe kupambana na hayo matatizo, si kwakupigana bali kuyakabili kwa busara.” Baba alinilaumu saana kwa kile kilichotokea na akaniambia anajaribu kuhangaikia dhamana.
********************************************************
Baada ya kuitafuta simu yangu kwa muda mrefu bila mafanikio Jesca hakuwa na amani alijaribu kwenda kazini kwangu jioni ile lakini hakufanikiwa kumkuta mtu yeyote zaidi ya gari langu lililokuwa limeegeshwa pale nje na bahati mbaya zaidi hakuwa anapajua kwangu alirudi nyumbani akiwa kanyong’onyea. Naweza kusema hakulala usiku kucha maana hakujua nini kimenipata, Jesca alikuwa akilia usiku kucha huku akizidi kuitafuta simu yangu bila mafanikio.
Siku iliyofuata, majira ya saa 12 asubuhi alikuwa tayari amefika ofisini kwetu aliketi nje akinisubiri aliamini lazima nitakuja, lakini mpaka inafika saa tatu asubuhi hakukuwa na matumaini ya kuonekana. Aliamua kuingia ndani kuulizia lakini kwa bahati mbaya alikutana na Esta ambaye ni rafiki wa Maria wakati huo Maria alikuwa jilani akisikiliza nini kinaendelea.
Jesca alimuuliza Esta ili ajue nilipo na nikwanini sipatikani kabla hajajibu aliguswa begani na Maria huku akidakia kabla Esta hajajibu “jamani yuko kwake na mke wake asubuhi asubuhi kuulizia waume za watu hamuoni hata aibu?” ni kauli tata ambayo ilimuvuruga Jesca. “unamaanisha Jamie ameoa?” Jesca aliuliza kwa hofu na sauti ya chini zaidi. “Shosti unaishi dunia hii? Na wewe ni nani mpaka ikuume ndoa ya watu isiyokuhusu, mpaka ukailalie mlango wazi?.” Maria aliendelea kukoleza na maneno ya kuuchoma moyo wa Jesca
Sasa Jesca hakuwa anaelewa nini kinaendelea maana aliona kama dunia imemuangukia, wakati kichwa chake kikijaribu kuchambua zipi chuya upi ni mchele Esta aliongeza “bibie kama ulidanywa ukadanganyika basi yule ni mume wa mtu, anafamilia yake ya mke na watoto wawili tena ndoa changa kabisa. Kwa msaada tunaomba tu umuache kabla hatujayafikisha huko kwa mkewe, mke mwenyewe mkurya yule anapiga kwa mapanga ila kama hujipendi endelea kushindania usichokiweza utaharibu reception bure” Esta akamaliza kupigilia msumali wa mwisho.
Jesca machozi yalianza kumtoka kwa uchungu huku akijuta kunijua, hakukuwa na ukweli wowote kwa yote yalyosemwa lakini ndo hivyo amejikuta akikutana na watu wasio sahihi kwake na ndiyo maana wakaamua kuniharibia. Jesca aliingia ndani ya gari na kurudi zake Kapri-point maana alikuwa ameesha kasirika mno.
Hakuwa anahitaji hata kuniona maana alichokisikia alikiamini na tayari alijenga taswira kuwa nilikuwa namdanganya na kumpotezea muda wake bure. Aliwaza mengi saana na kujaribu kuhusianisha na matukio yaliyopita alizidi kuchoka, alimkumbuka vyema Maria kuwa ni mmoja wa wafanyakazi wenzangu ambaye yuko bega kwa bega na Domi.
Jesca alijiuliza maswali mengi hawa watu nimewakosea nini mpaka wakae wananisingizia kila kitu? Aliona huenda yapo ya kweli yanayosemwa hivyo hakutaka kukiumiza kichwa chake. Mengi walikuwa wakiyasema na kuyaonyesha lakini nilijitetea kwa kusema hawa si watu wazuri kwangu hivyo alipaswa kuwaepuka. Lakini siku hiyo alionekana kuwaamini zaidi nadhani ni sababu ya uwepo wa Esta rafiki yake maria ambaye Jesca hakumjua hapo kabla. Imani yake ilisimama upande wao na kujikuta akilibwaga penzi langu kwa uchungu.
Baada ya kuingia ndani alianza kuvuruga vitu kama vile, nguo, makabati aliyabamiza chini huku akilia kwa uchungu. Ni mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwangu alihisi kama ameyatoa sadaka, aliniona kama sikustahili kupewa penzi hilo kwasababu mimi ni laghai, mwizi na tapeli wa mapenzi alilia sana. “Jamae hujui tu ni nini nilikuwa nakiwaza juu yako, huwezi jua niliiweka akili yangu kiasi gani kwako, huwezi jua nilikupenda kiasi gani iwapo haukuwa tayari kuutambua uhalisia wa mapenzi yangu” kilio cha kwikwi kilichukua nafasi.
Kisha akaendelea “Umeesha nivuruga, kwa usaliti huu sizani kama nitakusamehe namaanisha haitajirudia tena, mimi na Jamie ndo basi tena baki na huyo mkewako” alikuwa aikiongea peke yake chumbani huku akilia bila kujua kuwa amechezewa akili na hawa vikalagosi.
Ilikuwa ni siku ya majonzi kwa Jesca, ukweli alikuwa kaumia sana, alilia sana lakini kilio hakikusaidia kuuridhisha moyo wake, bila shaka aliamini amenipoteza mtu mhimu sana katika maisha yake, aliamini amenioteza mtu pekee katika maisha yake na aliamini kutokuwa na Jamie ni sawa na kutoitimiza ndoto yake.
Furaha ilipotea siku nzima, Jesca alishinda kama mgonjwa, hali chakula, hanywi maji wala chochote na zaidi alikuwa akilia tu, hii ni sababu ya mapenzi ya dhati aliyokuwa kayawekeza kwangu.
Nikweli nilimpenda sana Jesca nilimthamini na kumheshimu sana kama mke pekee wa ndoto zangu. Mawazo juu ya mapenzi mazito ndani ya penzi letu changa ambayo hatujapata hata bahati ya kuyarudia yalikuwa yamekitawala kichwa chake na kukiadhibu kwa mawazo.
Jesca hakuwa anaaamini kama kweli ndo tunaachana, kama kweli ndo nimemsaliti lakini hakukuwa na budi maana hadithi aliyopewa aliamini kabisa na akaona suruhu ni kuniacha hakukuwa na namna nyingine alikwisha fikia muafaka.
Macho yalikuwa yamemvimba kama kaumwa nyuki. Alikuwa akiitafuta walau hiyo sauti yakulia lakini ilimkauka kau kutokana na kulia kwa muda murefu na kubaki akikoroma kama jenereta lililoishiwa oili.
Nywele kichwani zilimvurugika kama kichaa aliyetoroka Milembe na uzuri wake ulikuwa umefifia kutokana na majonzi aliyokuwa nayo. Usiku kucha analia na anakesha kwa siku ya pili mfululizo. Alikuwa akijilaumu huku akibamiza kichwa kwenye ukutani “hivi kwanini? Ni kwanini nilikubali kumvulia nguo huyu mwanaume? Kwanini nilikuwa mwepesi kiasi hiki na leo amenitenda hivi aaah! jamani mungu huyu kwanini hutuoneshi mapema kuhusu ukweli… sasa naanza kuamini huyu huenda anaazima mpaka mavazi ili avutie wanawake. Huenda kilichosemwa nikweli nakiamini huwezi ukazima simu siku mbili, Jamie nikweli anamke huu ni ushahidi tosha” Jesca sasa alikuwa kayaamini maneno ya Esta na rafiki yake Maria kwa asilimia miamoja.
***
Baba alifanikiwa kuniwekea dhamana na sasa nilikuwa huru kwa masharti, huku nikiacha hati yangu yakusafiria na pia kulihitajika wadhamini kadhaa ambao walijitokeza kunidhamini hilo halikuniumiza kichwa maana lilikuwa ni juku la baba , nilimuachia yeye na kilichoniuma ni kumpata Jesca niliwaza ninampata wapi.
Nilikuwa huru ingawa masharti yalikuwa mengi. Baada ya kupewa vitu vyangu kitu cha kwanza nilichokiwaza ilikuwa ni kumpata Jesca nilipowasha simu nilikuta sms nyingi zikinilaumu kwanini sipokei simu. Masikini hakujua yaliyonisibu kwa wakati huo nilijaribu kumpigia simu iliita lakini haikupokelewa. Nilipiga tena ikaita na baadae kukatwa na mwisho simu ilizimwa kabisa. Nilijaribu sana kupiga lakini hakukuwa na majibu, nilianza kupata mashaka ikanilazimu niende mpaka ofisini nilifika na kuchukua gari yangu nikaelekea Kapri-point.
Nilipofika nilikuta utaratibu ni uleule, sikuwa naruhusiwa kuingia na hata kulisogelea geti. Nilijua nimemkwaza mpenzi wangu lakini hakukuwa na namna maana sikuruhusiwa hata kulisogelea geti, maana lilikuwa limefungwa na mashart yake nayajua huwezi kulisogelea zaidi utakuwa unayasaka mauti kwa udi na uvumba.
Nilipopiga simu ilikuwa haipokelewi na hakukuwa na njia nyingine yakumpata zaidi ya hiyo. Pamoja na kufika pale nje lakini lile geti nililiona ni hatari sana kwangu kulingana na mfumo uliowekwa kiulinzi nilijua nikikiuka masharti huenda lolote linaweza kutokea. Iliniuma sana kuona Jesca alikuwa hapokei simu yangu na nilijua lazima kunakitu ambacho hakiko sawa lakini nampataje iwapo mule ndani siruhusiwi kuingia. Niliamua kuondoka na kurudi nyumbani, maisha hayakuwa mazuri kwangu maana naona dunia imenielemea.
Baada ya muda mfupi nilikuwa nimepata taarifa kuwa Domi yuko nyumbani karudi toka hospitali, nilipita nyumbani kwake kumjulia hali, nilimkuta uso umemuumka kama andazi za sabasaba nilimsalimia, huku nikiwa na furaha moyoni maana ile sura ilinichekesha kidogo. Midomo ulikuwa umeshonwa kama nyuzi tatu hivi na kuonekana kama kiroba cha korosho.
Alijibu salamu yangu kwa nidhamu bilashaka alikuwa ameshika adabu na alionekana hana tatizo na mimi. Sikuona haja ya kumwomba msamaha maana lilikuwa ni jukumu lake na kama nilivyo tarajia hakukawia kuanguka miguuni mwangu alinitaka radhi, sikuwa na kinyongo tuliyamaliza kama wanaume ila kidogo adabu niliiona imerejea kwa kasi.
Mchana ule niliutumia nyumbani kwangu nikijaribu kumtafuta Jesca lakini kwa bahati mbaya hakupatikana kabisa. Sikujua nilichomkosea Jesca, nilijiuliza ni nini kimesababisha asipokee simu yangu maana sikuwa najua kinachoendelea kati yetu sikujua kama kunamtu analiharibu penzi letu.
Nikweli Jesca Jones Manguli hakuwa ananihitaji tena sikulijua hilo nilizidi kujitumainisha kuwa labda kabanana au kapoteza simu ingawa hofu ndiyo ilitawala zaidi.
Siku iliyofuata nilienda kumsubili Jesca pale Ikulu na niliapa statoka bila kumuona. Nilifika nikakaa nje tangu asubuhi mpaka jioni na ilipofika majira ya saa kumi na moja jioni geti lilifunguliwa. Ziliongozana gari mbili zikitokea ndani moja ilinipita pale nikiwa nimesimama na gari ya pili ilikuwa imembeba Jesca alikuwa kashusha vioo akiwa kiti cha nyuma lakini baada ya kuniona alipandisha kioo na gari iliondoka bila hata kusimama.
Nilijua huenda hajaniona nilijaribu kumuita bila mafanikio, haraka haraka niliingia ndani ya gari yangu ili kuifatilia ile gari lakini haikuchukua hata kilometa moja zile gari zilisimama na walinzi wake walishuka na kutoka na siraha nzito.
Walikuja kunionya kuwa sikupaswa kuongozana na hizo gari kwa karibu zaidi maana nahatarisha usalama wa kiongozi wao, hivyo nilipaswa kuwa umbali wa mita mianne ilinibidi kupaki mpaka angalau wafikie umbali huo na mwisho waliniacha sikujua walikoelekea.
Uwezekano wa kumpata Jesca haukuwepo tena maana pamoja na juhudi zote za kumtafuta bado ziligonga mwamba. Maisha yangu sasa hayakuwa na furaha tena, mpenzi wangu alikuwa amenikimbia, hakuwa ananihitaji tena. Nilijitahidi sana kumsaka Jesca bila mafanikio, nilizunguka sana katika jiji hili bila mafanikio ukweli Jesca aliupasua moyo wangu. Kwa kipindi hiki sikuwa na rafiki tena Dominic pamoja na kuniomba msamaha tukasameheana lakini ilikuwa ni vigumu mno kuurudisha urafiki wetu kutokana na mapito. Naweza kusema hatukuwa marafiki tena na kama tulikuwa marafiki basi ni urafiki wakuogopana yaani urafiki wa tahadhali.
Baada ya kufungiwa kwenda kazini kwa muda wa mwezi mmoja leo tunaruhusiwa, kufika kazini baada ya kuitumikia adhabu hiyo ambayo pia naweza kusema haikuwa adhabu kamili maana tulipisha uchunguzi wa tukio lililotokea baina yetu yaani mimi kupigana na Dominic.
Niliingia kazini mapema siku hiyo na ilipofika saa mbili na nusu tulikuwa ndani ya chumba na kamati ya maadili swala letu likijadiliwa. Naweza kusema nilikuwa tumbo Joto maana nilijua huenda hawa wazee wakaenda mbali kimaamzi kutokana na kosa nililolifanya. Ukweli uko wazi Dominic alinichokoza lakini kosa langu nilimpiga, masharti ya mkataba hayaniruhusu kupigana wala kumvunjia heshima mtu haijalishi ni mafanyajkazi mwenzako, mteja na hata mtu yeyote ndani ya ofisi maana ile ni ofisi ya umma na mimi tayari nimeesha pigana.
Nilikuwa nimeketi pembeni na mkono wangu wa kushoto alikuwepo Dominic akiwa ameketi, Sikuwa na hofu maana nilijua kitakacho tokea kwasababu Dominic alinichokoza. Basi tulipewa nafasi ya kujieleza Dominic alianza alieleza kwa kusema uongo.
Ni uongo uliopikwa na ukapikika haswaa kwa maelezo yake alieleza kuwa nilimpania siku nyingi kuwa nitampiga na nilikuwa nikimwambia kila mara kuwa nitampiga na hatimaye nilimpiga. Pia alisema nimekuwa na dharau hata kwa wafanyakazi wenzangu nawatolea lugha za matusi amekuwa akinionya yeye kama bosi wangu lakini sikumuelewa alisema kuwa nawadhalilisha sana wafanyakazi wenzangu hasa wanawake na akaeleza mashahidi wa hilo ni Maria na Esta “sikuwa nimekosana na Jamie, sikuwahi mkosea hata siku moja bali anatabia ya ubabe maana anacheza ku-nfu msimuone hivi ni mtu hatari, sikujua kumbe anamkanda mweusi wa mafunzo hatari ya ngumi, kunawakati huwa anaamua tu kuwa mbabe kwa watu, na siyo mimi tu hata mtaani huwa naamua sana kesi zake.” Dominic aliieleza ile kamati ya maadili, maneno yake yaliniuma na kunifanya nijae sumu moyoni mwangu nilikasilishwa sana na uongo aliokuwa akizidi kunitungia.
Nikapewa nafasi ya kusikilizwa nilijaribu kuieleza ile kamati ya maadili kilichotokea ingawa nilificha juu ya mahusiano yangu na Jesca kuwa chanzo cha mgogoro huo. Niliieleza sababu za mimi kupigana na Dominiki ni dharau za kunidhalilisha mara kwa mara. Wale wazee walinisikiliza kwa makini, waliniuliza maswali mengi niliyajibu kadri nilivyoweza ingawa kuna mengine yalikuwa magunu lakini nilipambana nayo hivyohivyo kuyajibu baada ya kulidhika niliruhusiwa nikarudi kukaa.
Nikiwa nimeketi aliitwa shahidi namba moja, alikuja Magreth kulingana na uhusiano wake na Maria nilijua huu utakuwa ni mlolongo wa uongo uliosukwa ukasukika, alifika akajieleza aliulizwa maswali akayajibu bila wasiwasi. Maelezo ya Magreth yalishabihiana sana na Dominic kiuhalisia yalinikandamiza na kwa ushahidi wake ilishawishi kwa kiasi kikubwa mimi kuonekana nina makosa.
Kesi ilikuwa imenigeukia na sikuwa na namna ila kukubali. Shahidi namba mbili aliitwa na kwa kuwa, ng’ombe wa masikini hazai, sura iliyokuja ni nafuu na ile ya mwanzo alikuwa ni Esta huyu ndiye hafai kabisa maana nimuongo kapitiliza, maana hata ndani ya mwaka mmoja unaweza kukuta kakualika birthday mara tatu sasa utajaza mwenyewe alizaliwa marangapi kwa mwaka. Lakini mbali na umbeya na uchonganishi ni maarufu kwa kupika majungu na kuchonganisha pale ofisini.
Aliposimamishwa pale mbele hakuwaangusha wenzake, alipita walimopita na kuupamba ule uongo na hatimaye kukaribiana na ukweli kabisa, huwezi amini alikuwa akiongea kwa uchungu mpaka wale wazee wanafuta machozi maana maneno yaliwagusa. “wazee wangu huyu Jamie siyo mtu mzuri, muoneni tu hivyo amekuwa akitumia ubabe wake hata kututaka kimapenzi kwa lazima wafanyakazi wenziye na ukimkataa yatakupata mazito huwa tunaogopa hata kusema maana huwa anatutishia tukisema tu atatufanya kitu kibaya” moja ya kauli iliyonivunja nguvu na kujikuta natokwa machozi sikutamani kuendelea kukaa nikanyanyuka niondoke.
Mzee yusuph Gabi alinirudisha kwa heshima yake nilirudi na kuketi sikujua kama kuna shahidi namba tatu na sasa aliitwa. Mbele yangu alikuwa kasimama Maria Kimaro, alisimama na kuanza kuieleza ile kamati jinsi nilivyokuwa nikimnyanyasa kwa kumtaka kimapenzi kwa lazima, alisema pamoja na kunikubali, nimekuwa nikimpelekesha kwa ubabe kitu ambacho kinamfanya asiishi kwa amani. “Jamie ni mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo anamatendo mabaya huyu kijana wazee wangu Eheee! Naamini matendo yake hata shetani angeyaogopa, nawaeleza ukweli, staki kuwadanganya.,huyu mtu hafai.” Maria alikuwa akiieleza ile kamati. Maelezo hayakuishia hapo yakaendelea “Jamae alinitaka kimapenzi kwa lazima na alisema nisipo mkubali atanifukuzisha kazi, nisiwadanganye alinitishia mpaka ikafika wakati sikuwa na jinsi nilimkubalia na anachonitenda ni zaidi ya unyama siwezi kusema mbele zenu huyu hapo akatae kama mimi si mpenzi wake” Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Bi Sada mmoja wa wanakamati aliniita wakati Maria akiendelea kusimulia
“Jamie”
“Naam mama” niliitika
“anayoyasema huyu binti niyakweli? Na vipi huhusu wale waliopita?. Hivi ulivyo nadhifu wewe niwakufanya huu uchafu kweli?”
“hapana mama najua huujui ukweli ndiyo maana unakiamini wanachokisema”
“Jamie huwezi kusingiziwa na watu wanne wote, kwani umewahi kuwa kwenye mahusiano na Maria?” Yule mama alihoji tena.
“ndiyo tumewahi ila si kwa hicho anachokieleza yeye”
“kelele wewe! Sasa naanza kupata picha Jamie hutufai na hufai katika jamii nadhani hata kesi yako iliyoko polisi sasa naahidi kuipa ushirikiano wa karibu ili haki itendeke. Kwa maelezo haya wewe siyo binadamu nibora ukafie jera” Yule mama alihitimisha kikao huku wenzake wakimuunga mkono.
Nilipita mapokezi nikapitia barua yangu ya kuachishwa kazi rasmi nikiwa mnyonge nisiye na mbele wala nyuma, nilikuwa na utitiri wa mawazo kichwani mwangu. Nilipofika nje niliikuta kamati ya wanafiki wakifurahia na kupongezana.
Nilipita wakaangua kicheko kwa dharau sikuwajali nikaelekea nilikopaki gari yangu nilisikia sauti za kejeli “ngoja tumuone mkwe wa rais sasa kama ataendelea kuvaa suti mpya” aliropoka Esta wakati huo Maria akidaki “mbona mpaka hicho kigari kitauzwa mwaka huu” hayakuwa maneno mazuri ilinilazimu nigeuke kwasababu wameesha mwaga mboga mimi niliwaza kumwaga ugali maana dawa yao naijua ni kichapo tu.
Nilipiga hatua mbili nikielekea walipo, lakini kabla sijawafikia nafsi ilikataa nikaamua kuendelea na safari zangu. Ugomvi niliuona hautasaidia kuyapunguza machungu niliyonayo. Wala hautatatua matatizo niliyojisababishia, niliamua kuondoka kimya kimya.
Dominic amesababisha sasa sina kazi na sina uelekeo, familia yangu inanitegemea baba umri umeenda mama naye malazi ya kisukari yanamsumbua anahitaji matibabu ya mara kwa mara. Maisha yangu yamevurugika sidhani kama nitapata kazi ya haraka tena maana dalili za kukwama naziona kabisa, niliona ndoto zangu zinaanguka.
Hapo ndipo nilipouona umhimu wa msemo wa kiswahi usemao kuwa “umhimu wa kupata kazi hauta ujua ukiwa na kazi, ila kosa kazi uone ilivyo kazi kuisaka kazi ili upate kazi maana kusaka kazi nayo ni kazi inahitaji kozi”.
Niliwasha gari huku nikijipa matumaini kuwa mimi ni mtoto wa kiume nitafanikiwa, nilijikaza kiume hakuna aliyejua kuwa nimeumia kutokana na kuikosa kazi yangu niliyoisotea na kuipenda mno kabla.
Nilipofika nyumbani kwangu sasa uchungu ndiyo ukanirejea nililia asikwambie mtu, nilikumbuka mengi sana mojawapo ni hili, nilivyotoka chuoni na kusota mtaani kwa miaka miwili nikitafuta kazi na leo nimefukuzwa kazi kizembe kwasababu ya mihemko ya kijinga nilijiona nilifanya kosa la kitoto ambalo nitaonekana mpumbavu milele na hata akihadithiwa mtoto kosa hili ataniona mjinga.
Hasira zangu nilizielekeza kwa Dominic na sasa nilikuwa namchukia kuliko kawaida. Nilitafakari mengi nikiwaza na kuwazua sikuwa na lakufanya maana maisha yangu sasa yalikuwa yameharibika.
Nilikuwa nikiitafakari kesi iliyokuwa mbele yangu niligundua maisha yangu yanaeleka kubaya. Nilijua Dominic hawezi akatoa msamaha wa aina yoyote kwenye kesi yangu na nilijua ataongeza ushawishi kwa hao mashahidi wake na timu nzima ya uongozi wa juu wa kampuni ili nionekane nina makosa. Niliamini nikileta mzaha nitafungwa au kupewa adhabu nyingine kali zaidi.
Maisha yaliniendea kombo maana sikuwa na akiba yakutosha benki, mbaya zaidi nilikuwa na deni kubwa la kama Milioni themanini na tano niliyokopa ili kununua gari langu. Niligundua nikifanya mzaha watanifirisi na kujikuta ninahali mbaya zaidi, wasiwasi wangu ilikuwa ni kuuzwa kwa nyumba yangu. Nyumba ya ndoto zangu niliyoijenga na kuikamilisha kwa jasho na damu.
Kwa kujihami niliamua kuiuza ile gari yangu mpya nilitafuta fedha ya haraka ili nilipe lile deni kwa haraka zaidi na bahati mbaya hali za watu kiuchumi hazikuwa vizuri na ukilinganisha na kuuzia shida niliambulia fedha kidogo sana tofauti na gharama halisi ya gari. Baada ya ilinibidi niuze na gari yangu ya pili ili kukidhi mahitaji, namshukuru Mungu nilikuwa salama baada ya kulipa hilo deni lote na kubaki na nyumba yangu ambayo ndiyo niliipigania kila siku maana nimepata taabu sana kuipata.
Niliamini hata nikilala njaa katu sitakuja kuiuza nyumba yangu nitaendelea kujikaza huenda ipo siku nitajikomboa ila nikiwa nyumbani kwangu. Ni nyumba ya kisasa kabisa niliyoijenga kwa thamani ya milioni mia mbili za kitanzania nimetumia kila senti yangu kuhakikisha naishi kwenye nyumba ya kifahali niliyoitaka na Mungu kaniwezesha kulikamilisha hilo. Mbaya zaidi ndoto zangu za mafanikio zinarudishwa nyuma kila nikipiga hatua moja kunamjinga ananivuta nyuma hatua kumi na sasa nilibaki sina hata baiskeli lakini jina la ababa mwenye nyumba halikufutika.
Nilikuwa nahangaika huku na kule kutafuta kazi lakini kila nilipokaribia kupata kazi viliibuka vikwazo na visingizio, nilijaribu kuomba kazi kwenye kampuni pacha za simu za mkononi nilifanya mpaka usahili na nilifauru lakini nilipopangiwa kazi siku nakwenda kulipoti kazini niliambiwa maamzi yamebatirishwa, nilijaribu kuwasiliana na uongozi hawakuwa na jibu la kuniridhisha kwanini wamebatirisha, niliumia lakini nikaona siyo kesi huenda haikuwa ridhiki.
Nilijaribu kampuni nyingine nikapata niliitwa kwenye usahili lakini siku naenda kufanya usahili sikuruhusiwa hata kuingia kwenye chumba cha usahili, niliondolewa kwenye usahili bila huruma tena kwa ulinzi mkali. Sikulijua kosa langu ila ninachokikumbuka nilifukuzwa tena na walinzi watatu. Nilijaribu kuitafuta sababu kwanini nafukuzwa hivi? Sikuipata.
Sasa nilijua Mungu ameamua kuniadhibu hali iliyonifanya nizikumbuke pesa nilizozitumia kutanua na marafiki, kununua vitu vya thamani na nilizozipoteza kumtunza Maria jike lisilo na shukrani. Nilitamani zirudi huenda zingeokoa maisha yangu lakini haikuwezekana.
Sasa nilikuwa nimebisha hodi karibu kila ofisi niliyoijua nikiomba kazi bila mafanikio. Jamie nilikuwa nimepoteza uelekeo, nilianza kuiona dunia imenigeukia. Matumaini ya kuipata kazi mpya yalikwama siyo Mwanza pekee bali hata mikoa ya jirani na sasa matumaini ya kuikomboa familia yangu yalizidi kufifia kila siku.
Naweza kuiita miezi mitatu ya mateso tangu nimeachishwa kazi maana familia yangu haikuwa inajua chochote juu ya mimi kuachishwa kazi. Sikuwa napenda kukutana na mama yangu maana nilijua ataniuliza maswali mengi ambayo sikuwa na majibu yake.
Ndani kwangu ilifikia wakati nakosa hata mia ya chakula, lakini nilijikaza kuvumilia, nilijitahidi kuificha aibu niliyokuwa nayo huku nikiamini mwanaume huwa hashindwi daima. Mara nyingi nilikuwa nikipishana na Dominic akizidi kutanua na timu yake mpya ya wanafiki ni yeye Esta Maria na Magreth.
Wenzangu walizidi kuishi maisha ya kifahari maana walilipwa mishahara minono na marupurupu mengi ambayo mimi sasa sina nimeesha fukuzwa kazi.
Kazi ilizidi kuwa kitendawili kigumu kukitegua katika maisha yangu. Jamie nilikuwa nikibadirika kila kukicha na maisha yangu kuzidi kuwa magumu. Kesi yangu nayo ilikuwa inapigwa tarehe kila kukicha ili kupisha uchunguzi, mwenendo wake ulikuwa unanipa mashaka maana niliziona kila dalili za mimi kukutwa na hatia.
Mwanasheria wangu Steven Bwire alikuwa akijitahidi kupambana nayo lakini alikuwa akizidiwa na utawala wa rushwa uliokuwa ukitoka upande wa mshitaki.
Hata hivyo ni uvumilivu tu ndiyo ulikuwa ukitumika, huenda engekuwa ameesha achana nayo, maana maamzi yaliyokuwa yakitolewa na mahakimu yalimkatisha tamaa sana mwanasheria wangu, kwani yalijaa upendeleo na ukandamizaji wa wazi wazi kila siku.
Jumatatu hii naamka na matumaini mapya baada ya kuitwa kwenye usaili wa kampuni ya usafirishaji wa vifurushi na mizigo ya kimataifa DHL, nilikuwa nimevaa suti yangu safi na tai nilipokelewa vizuri nikafanya usahili niliamini nilifanya vizuri nikaacha mawasiliano na kuondoka.
Nilitoka nikiamini nimefanya vizuri tena vizuri sana, ila ilishakuwa ni tabia kwangu kufanya usahili vizuri na kusubiri na mwisho huwa naambulia patupu. Jioni ya jumatatu hiyo nilipokea simu ikinipongeza kuchaguliwa kuwa mmoja wa watu waliopita katika usahili huo.
Nilitakiwa kuripoti kazini siku iliyofuata nilimshukuru Mungu, nilijiandaa vizuri nikiamini mambo sasa yameenda vizuri. Kesho yake nilijitahidi kufika kazini mapema nikakaa nje kumsubiri boss afike ili nipangiwe majukumu. Lakini nikiwa nimeketi pale nje nikisubiri niruhusiwe kuingia, nilishituka kumuona Dominic akitoka mle ndani kwa boss asubuhi asubuhi niliinama akapita ili asinione. Uwepo wa Dominic eneo hilo asubuhi hiyo ulinifanya niwe na maswali mengi niliojipa muda huo na kukosa majibu ya maswali hayo.
Niliitwa ofisini kwa bosi na nilikutana na maelezo ya kubatirishwa kwa barua yangu ya wito wa kazi na aliniomba samahani kwa usumbufu, akidai kuwa wamekaa chini kwa muda na wamependekeza kubatirisha uamzi wa kuniita kazini kwani niliitwa kimakosa.
Hasira ilinipanda na nikajua aliyefanya haya ni Dominic na sasa nilikuwa nimeesha mjua mwanga wa maisha yangu, mchawi mkubwa asiye na huruma. Wakati akieleza hayo Yule boss nilikuwa nikimkata jicho ambalo liliashiria shali ila alikuwa mgumu kujiongeza. Wakati akinieleza huo upuuzi nilijikaza nisiharibu utaratibu pale ofisini lakini roho kama ilikuwa ikinisuta hivi siku hizi sina uvumilivu tena. Basi niliyasikiliza maelezo yake yakipuuzi na mwisho nilimkubalia nikaamua kuondoka lakini baada ya hatua kadhaa uzalendo ulinishinda nikaamua kurudi. Nilifika nikamkwida kwa mkono wa kushoto shati lake jeupe na tai yake shingoni vyote nilivikusanya pamoja na kuanza kumhoji huku mkono wangu wa kulia ukima umemuelekezea kalamu shingoni niliyoikamata kwa ustadi.
“unaweza kuniambia Dominic aliijia nini hapa leo asubuhi? Na usiposema unaniona hii kalamu itazama shingoni sasa hivi” niliamua kupata taarifa kwa nguvu sasa maana majadiliano hayakuwa na nafasi tena.
“Dominic simujui kaka” alijibu kwa uoga.
“narudia tena na naapa starudia kukuuliza mara ya pili Dominic alifuata nini hapa ofisini?”Nilikibamiza kichwa chake juu ya meza ni kahoji tena mara hii kalamu iliielekeza jichoni.
“Alikuja kutuzuia tusikuajili, alipiga simu jana usiku na akaahidi kuja leo, kiukweli hataki kuona ukiajiliwa, amesema amezuia kazi nyingi ulizozipata na anaapa hauto ajiriwa labda awe kaburini” alijieleza huku akitetemeka.
“Alizipata wapi hizi habari za mimi kuomba kazi hapa?” nilihoji.
“sijui kaka, sijui mimi utaniua bure tu kaka mkubwa sijui chochote kabisa” alikuwa akitetemeka kama kawekewa mashine yakusaga tumboni.
“kakupa nini mpaka unikatae au kakueleza nini zaidi….” Alikaa kimya
“baba unanijua huwa sirudii maswali kama unautaka upofu endelea kukaa kimya” nilimkumbusha wajibu wake kwa vitisho.
“Kanipa milioni tano hizi hapa kwenye bahasha, na kasema nikimsaliti kaahidi atanifanya kitu kibaya kaka tafadhali sikudhamiria” alijieleza kwa hofu.
Nilizichukua zile pesa nikamuachia na kisha kumuacha akijaribu kujirekebisha kikoti na shati lake nililokuwa nimevifinyanga mithili ya unga wa kukandia tambi na kuwa na mwonekano kama shati lililotafunwa ndama na kutemwa.
Safari hii ilielekea jengo la NSSF niliwapita wafanyakazi wote wakinishangaa mpaka ofisini kwa Dominic niliingia na kufunga mlango alijaribu kuinuka kwa hofu lakini tayari nilikuwa ndani. Nilifika nikaiweka ile bahasha mezani. Domi alijua nimekuja kwa shari muda wote tangu nimeingia alikuwa kanyoosha nikono na kutandaza mikono ishara ya kuzuia shari. Najua alijilaumu kwanini walinzi hawajanizunia maana sura niliyoingia nayo mle ndani ilikuwa ni sura ya kazi.
“Nataka kuujua ukweli nini kinachezwa katikati ya maisha yangu?” Domi alikaa kimya na akabaki kama mjingamjinga tu.
“unapesa sana sikuhizi si ndiyo rafiki yangu?” nilimuongoezea swali
“ulidhani unaweza sasa kupambana na mimi kwa nguvu ya milioni tato na hizo ulizotoa huko kwingine sijui zinakaribia milioni ishirini mwenyewe ukajiona kidume balaa.” Alikuwa yuko kimya lakini wakati namhoji alifanya kosa la kuachia kiganja cha mkono wa kushoto nilikidaka kidole cha kati nikakikunja alilia kama beberu.
“waweza nieleza kwanini unayafatilia maisha yangu? Kwanini umedhamiria kuniharibia maisha yangu?” Domi alikuwa kimya na alikuwa akitokwa machozi na kulia kwa uchungu.
“umekuwa rafiki yangu kwa muda mrefu, unanijua vizuri nikifikia hatua ya kuzungumza kitu kinachonikera ujue nimekeleka vya kutosha na hili kamwe stalifumbia macho, leo nataka kujua kwanini unanifanyia hivi?” Domi alisema ni hasira tu ndizo zimepeleka kunifanyia hivyo. Nilimuuliza nimemuudhi nini hakujibu alibaki kimya.
Niliendelea kukikunja kile kidole bila kujali maumivu aliyokuwa akiyapata Domi alilia kwa uchungu sana mpaka kuna wakati huruma ilinirudia lakini niliona ukimchekea nyani shambani jiandae kuvuna mabua. Domi ni miongoni mwa watu hatari katika maisha yangu ambao nimewafuga kwa muda mrefu ananijua vizuri pengine kuliko mtu yeyote niliyewahi kuishi naye hii hali ndiyo inayomfanya kuwa mtu hatari zaidi kwangu kuliko chochote na yeyote, maana kuwa na adui anayekujua inahitaji moyo sana tofauti na hapo unaweza kujikuta ukiumia kila kukicha.Mlango uligongwa bila shaka watakuwa ni walinzi nilimzuia asifungue na nilimuonya asithubutu kunijaribu juu ya hilo.
“Nikiuliza nilichokukosea huenda usinijibu ngoja nikubadilishie swali, ni nini unachokitaka kwangu ni nikupe ulidhike na uachane na mimi?” Nilihoji kwa mara nyingine.
“hapana Jamie ni matatizo tu rafiki yangu kiukweli mimi nilitaka kukusaidia ili uachane na kile kibinti kilikuwa kinataka kukuibia lakini hukunisikia, na sasa unaiona ulivyo firisika, rafiki yangu wewe niwakukosa hata baisikeli leo?… Aaah Jamie unapotea rudi turudishe urafiki wetu tusichukiane ndugu yangu mimi nakupenda sana na staki upotee ndiyo maana nakuhitaji na nauhitaji mchango wako na nakuapia ungenisikiliza mimi leo usingekuwa hapo ulipo” nilikuwa nikimsikiliza kwa makini na nikagundua anatafuta namna ya kunipoza.
“wewe ulikuwa unamjua Jesca vizuri kuliko mimi?” nilihoji swali la miujiza.
“ndiyo nakajua kale nikakahaba tu tunakutana nako kila sehemu za kujiuza mara makoroboi usiku, villa park, mala vitunguu , mwanza hotel na sehemu kibao. Yule mwanamke ni kahaba asipokuua kwa maradhi basi jiandae kuendelea kufirisika.” Maelezo yake yalinikera na kujikuta namsukumia konde lililotua vyema kifuani alibinuka mpaka chini na kiti chake cha kuzunguka.
Nilichukua mtungi wa gesi uliokuwa pembeni, niliufungua gesi ikaanza kutoka harufu yake ilikuwa kali ila niliipunguza kwa kuziba na kitambaa puani, mkononi nilikuwa na kiberiti cha gesi pia tayari kwa kulipua. Kiukweli nilikuwa nimeesha kata tamaa na maisha na sasa nilikuwa tayari hata kufa. Nilimwambia naitaka sababu halisi ya wewe kuniletea marumbano na mwisho kuleta mgogoro usioisha kati yetu. Nakupa dakika moja nikikiwasha hiki kiberiti hakuna atakaye baki kati yetu. Si wewe, si mimi na ikiwezekana hili jengo zima kama hazitachukuliwa hatua za haraka litateketea pia.
Niliongea hayo huku nikilia, niliamini kile kiberiti kikiwaka tu basi hakuna mtu ambaye angebaki hai kati yetu. Niliweka dole gumba kwa juu sehemu ya kuwashia, alidhani natania nilibonyeza mara ya kwanza baada ya dakika moja kuisha, zikatoka cheche na hakikushika moto vizuri, Dominic hakuamini alijikuta akipiga kelele.
“Inatooosha Jamie acha niseme… ninasema please … ninasema kaka…..” alijitetea huku akilia kwa uchungu, nilimsikiliza.
“Ukweli ni wivu juu ya Jesca nilimpenda toka siku uliyonionesha tu kule Nyakato, ni msichana mzuri ambae hata mimi nilivutiwa naye sana tu, kiukweli nilikuwa nikiona wivu wa nyinyi kuwa pamoja wakati moyo wangu unaumia kwa mapenzi ya dhati. Jamie nimekuwa nikishindwa kujizuia nampenda sana Jesca, na ndiyo maana kila kukicha huwa nazua visa ili umuache niliahidi kutumia hata pesa zangu zote ili nihakikishe hamuoani na Jesca” sasa nilianza kuupata ukweli.
“Bado sijakuelewa ujue, hebu niweke wazi maana naona unazunguka tu hebu toa yote ya moyoni unayoyajua. Maana hapa nilipo ninaroho ngumu zaidi ya msumali siogopi kifo na ukileta utani tutakufa wote hapa. Wakati nikisema hayo wote tulikuwa tukipiga chafya kwa harufu kali ya gesi.
“Jamie hakuna asiyependa kuwa mkwe wa rais na hakuna asiyependa maisha mazuri mimi binafsi natamani saana kuitwa mkwe wa rais kwani haya .Maisha bwana hubadirika tu niliamini siwezi kuyaona maisha yako yakibadirika na kunizunguka mara miamoja huku nikibaki katika maisha haya yakijinga tuliyo yaanza wote, na hapo ndipo niliamua kuungana na Maria ili tuhakikishe haufanikiwi kumuoa mtoto wa rais. Jamie siyo kama hatujui kuwa Jesca ni mtoto wa rais tunajua sana mimi na timu nzima ya akina Maria, tunajua vizuri tu na hayo maneno ya kejeli huwa tunafanya tu ila ukweli uko wazi. Wewe hujui Jesca aliko ila mimi na Maria tunajua na huwezi amini hata kutokukutafuta kumesababishwa na sisi. Maria alimwambia una mke na siku umelala lumande, ulitumika huo mwanya wa simu yako kutokupatikana kumjaza sumu maria kuwa umezima simu sababu uko na mkeo. Jesca alikasirika akaondoka na sasa hayupo Mwanza yuko Kwao Dar Es Salaam na mbaya zaidi Maria bado anawasiliana naye na anazidi kukuharibia.” Kwa maelezo hayo nilijikuta nahisi njaa na kuishiwa nguvu.
Ghafla ilisikika sauti ya king’ora cha jengo watu wote tulitoka nje hii ni baada ya harufu ya gesi kutapakaa walihofia mlipuko huenda ukatokea ndani ya lile jingo, hivyo watu wote waliombwa kuwa nje ya jengo na watu wa zima moto walikuwa pale muda mfupi tu kwa tahadhari. Nilitoka haraka nikaondoka eneo lile kabla Domi hajazungumza chochote kwa watu wengine maana nilijua akitibua kilichotokea ndani huenda mambo yakaniendea vibaya. Baada ya kuondoka eneo lilie nilifika nyumbani kwangu na kazi yangu ya kwanza ilikuwa ni kuyapata mawasiliano ya Jesca na niliambiwa aliye na mawasiliano alikuwa Maria.
Nilijaribu kumpigia simu hakuwa anapokea, nilimtumia sms “Baby nimepata kazi mpya na ina mshahara mnono nitalipwa dolla za kimarekani 3000/= kwa mwezi ni pesa nyingi na bado wameniahidi gharama za usafiri na malazi ni kazi nzuri kwakweli, mshahara tu ni zaidi ya milioni sita huwezi amini. Sasa nina zawadi nzuri kwaajiri yako mpenzi maana wewe ni mtu mhimu mno katika maisha yangu nimeligundua hilo baada ya kuachana” babu yangu aliwahi niambia dawa ya mbwa mkali rusha mifupa yakukaangwa lazima awe rafiki alijibu ule ujumbe haraka maana kaisha ona pesa akajua mapenzi yamerejea na atakuja kupiga pesa. Walipigiana simu na kujazana ujinga na sifa za kijinga na wambea wenzake huko wakati huo mimi nilimuandalia viboko kama viwili hivi chumbani kwangu ni mwendo wa kunyoosha tabia tu.
Jioni ya siku hiyo bila kuchelewa alikuwa ameegesha kitoyota saloon chake pale nje ya nyumba yangu. Nilimpokea kwa mapenzi kama mpenzi nikamkaribisha mpaka chumbani. Kwa kuwa hakujua kilichomleta alifika na kujitupa kitandani. Na hapohapo nikambadirikia
“Maria hapa nataka kitu kimoja tu kukijua katika maisha yangu,unawasiliana nini na Jesca, ulimueleza nini na yuko wapi kwa sasa?”
“hahaaa we bwege kweli ndo ulichoniitia kuja kuniuliza habari za huyo kahaba wako?” alikurupuka na maneno yake yasiyo na staha.
“kahaba? Nilihoji kupata uhakika
ndiyo kahaba, kwani ulikuwa hujui au ndo kujitia uchizi husikii na huelewi?” aliendelea kunijibu kwa kejeli. Nilichukua kiboko nilichokiandaa maana wanawake hawachapwi makofi wasije kupata sababu au kisingizio uso ukiwaumka. Nilichalaza bakora kwelikweli mpaka alishika andabu yake
“haya Jamie nasema ukweli …. Nilimwambia una mke na watoto wawili na tulisha mjaza maneno hakupendi tena na tunawasiliana naye kila mara yuko Dar- huwa anatupigia simu mara kwa mara kiukweli sisi ndiyo tuliwatenganisha mimi nilitaka uendelee kuwa na mimi au wote tukose” alieleza huku akilia kwa uchungu
“Namba yake iko wapi?” nilihoji wakati huo staki hata senti yautani kiboko kikiwa juu tayari kwa kushuka alipochelewa tu kujibu kikashuka tena na kutua vyema mgongoni
“aaaah Mungu wangu Jamie utaniua, mimi mtoto wa watu, nipe mkoba wangu kuna kadi ya mawasiliano alinipa, chukua baba na hela zimo chukuaa” kiboko kilikuwa kinanipa matokeo mazuri maana kila nilichokihitaji kilipatikana kwa wakati, nilikagua kwenye mkoba kweli nikaikuta kadi ya mawasiliano. Na mwisho nilitoa amri.
“kuanzia leo staki kukuona nyumbani kwangu sawa” nilimuonya juu ya kukanyaga nyumabani kwangu.
“sawa Jamie nakuelewa baba yangu” alijibu huku akilia na kuniangalia kwa huruma
“Kamwe naapa stakanyaga hapa na nikikuona nitakimbia” aliongeza na vionjo vya maneno ambavyo hajaulizwa
“haya nyanyuka na upoteee maramoja” alikurupuka kama mwizi na kutoka nduki.
Kadi niliyopewa ilikuwa na namba tatu za simu nilijaribu namba yakwanza haikupatikana, nikajaribu namba ya pili haikupatikana pia. Nilijaribu namba ya tatu ilikuwa bize sana kila nilipojaribu kupiga ilikuwa inatumika. Niliendelea kuvumilia huku nikiijaribu mara kwa mara lakini sikuona matunda mapya na baadae nilipiga ikawa haipatikani pia. Nilikaa na masikitiko yangu moyoni na nilijuta kwanini nimmemuachia Maria akaondoka kabla sijapata uhakika kama kweli zinapatikana sikujua huenda Maria kanidanganya na bahati mbaya nimemuacha kaondoka sijui itakuwaje maana namba nilizopewa hazifanyi kazi zingine hazipatikani na zinazopatikana hazipokelewi. Baada ya muda niliamua kujaribu tena ile namba ya kwanza iliita kwa muda mfupi na ikapokelewa ilikuwa ni sauti ya Jesca.
Niliachia kicheko cha mana nilimshukuru aliye juu na kisha kuendelea kuisikiliza ile simu iliyokuwa ikiendelea kuwa hewani.
“Mambo Jesca” nilimsalimia
“safi nani mwenzangu” aliuliza kwa hofu.
“Oooh jamani hata namba yangu umefuta?” nilimtupia lawama kwa kutonikumbuka
“Pole nimebadilisha simu jamani nimepoteza karibu namba zote, nikumbushe basi we ni nani?” alijiteteta na kuhoji akitaka kujua.
“staki kuamini kama hata sauti huikumbuki?” niliendelea kumchokoza.
“nikweli siikumbuki maana hata hii simu yangu haina usikivu mwanana” naye akazidi kujitete kwa kutia uongo.
“Naitwa Jamie Justine” Niliamua kujitambulisha. Kitendo cha kulitaja jina langu tu Jesca alikata simu na ikawa haiapatikani tena, nilijaribu kila nilivyoweza lakini haikupatikana …Jesca alizima simu na ilionesha hakunihitaji tena.
Nilitumia kila mbinu niliyoijua ili nihakikishe mawasiliano yanarejea kati yangu na mpenzi wangu lakini haikuwezekana. Na nilichokigundua ilikuwa wazi kuwa maneno aliyojazwa na aliyokuwa akiendelea kujazwa yalimtia uchungu na hakuwa tena na imani na mimi.
Hakuna kitu kinaumiza kama mtu kukutengenezea chuki kwa watu mnaopendana au kufahamiana, mnagombanishwa bila wewe kujua, waswahili husema “ishi na mchawi kuliko muongo.” Nilikuwa nauona ukweli juu ya kilichotabiliwa na wahenga wa Kiswahili. Nilijiuliza maswali mengi saana moja Jesca atanielewa tena na kuniamini kama zamani, iwapo nitapata nafasi ya kukutana naye?, swali la pili lilikuwa gumu hata kulitafakari, nitampata wapi Jesca?. Ni swali lililokuwa likikiumiza sana kichwa changu kutokana na kwamba Jesca hapatikani kiurahisi na ratiba zake hazijulikani mpaka uwe na miadi naye nyumbani kwao hapaingiliki kirahisi. Sikuwa na namna sasa nilianza kutafakari namna ya kumpata Jesca mrembo aliyeteka akili yangu na kunifanya niyathamini mapenzi na kuyaheshimu.
Leo hanitaki tena sababu ya watu wachache walioamua kutugombanisha iliniuma sana na kunifanya nikose amani. Ninampenda sana Jesca na ninaamini ananipenda pia, lakini ni changamoto za maisha tu ndiyo zinazotutofautisha mimi nayeye. Nilikuwa mwingi wa mawazo usiku ule na kusababisha nikose usingizi usiku kucha. Nilikuwa nikizunguka mara niende sebuleni mara nirudi chumbani mara nizunguke huku na kule na nisijue nilikuwa natafuta nini usiku ule.
Nilijitahidi sana kuusahaulisha moyo wangu lakini ilikuwa ngumu hasa kumbukumbu ilipokuwa ikinirudia juu ya penzi letu tamu lililoshamili kwa muda mfupi na kuyeyuka kati yangu na Jesca kipenzi changu, malikia wangu. Usiku ule niliwaza mengi jinsi nilivyohangaika kulifukuzia penzi letu toka siku ya kwanza mpaka siku tuliyojipumzisha katika kitanda kimoja mimi na Jesca wangu lakini iliniuma zaidi tulivyokuja kutenganishwa kiulaini na watu wasio na mapenzi mema. Niliwaza na kuwazua na kila kukicha iliniuma sana na tena sana tu, sikuamini kama mapenzi yetu ndo yanayeyuka hivi na kubaki patupu. Mara kwa mara nilikipapasa kifua changu nikilikumbuka joto safi la mpenzi wangu Jesca nilijisemea kwa uchungu Jesca inamaana stakuoni tena katika maisjha yangu? Lilikuwa ni swali gumu mno kwangu lakini hakukuwa na jinsi, huo ndiyo ulikuwa uhalisia. Baada ya kulitazama saana paa hatimaye nilipitiwa usingizi japo ilikuwa kwa taabu sana.
Asubuhi hii niliamkia nyumbani kwa mama yangu kipenzi nilienda kumsabahi, nilifika nikapokelewa vizuri sana. Baada ya kupata kifungua kimywa niliamua kuwaweka chini wazazi wangu na kuwaeleza mkasa mzima juu ya matatizo yanayonikabri. Mama hakuamini kuwa nilisha fukuzwa kazi na sasa inakaribia miezi minne na sina gari hata moja, magari yote nilishauza.
Wazazi wangu walikosa nguvu na kushindwa kabisa kunielewa hasa mama. Nilijitahidi kuwaelewesha kwa upole na hatimaye walinisikiliza na kuniamini. Baba alisikitishwa sana na hadithi yangu na Dominic, urafiki wetu ulipoishia najua ilikuwa ngumu sana kuamini kwamba Dominic amekuwa chanzo cha kuharibu maisha yangu, amekuwa mzalisha chuki asiye na mfano. Dominic kwa sasa anapambana na mimi nisipate kazi na hata kutumia pesa zake kuhakikisha anayavuruga maisha yangu.
Mama aliumizwa sana na matukio yaliyozidi kuni sakama kila siku, alihoji juu ya kesi yangu nilimjibu bado inaendelea na matukio mapya yanazidi kunisakama. Wazazi wangu wananipenda kuliko kawaida maana mimi ndiye mboni yao, ni mtoto pekee katika familia yao, hivyo daima walipambana kuhakikisha ninaishi maisha bora na kunisaidia ili niweze kupambana na changamoto zote zilizonikabili kwa wakati huo. Baada ya kueleza matatizo yote na sasa nilimgeukia mama nikamuaga ili nikaendelee na shughuli zingine. Baba alikumbuka kitu akamunong’oneza mama na baada ya kukubaliana, baba alinyanyuka na aliporejea alikuwa na funguo za gari mkononi.
Jamie huwezi kuishi bila gari mwanangu kuna hii Prado hatuitumii sana hapa nyumbani na kutokana na matumizi makubwa ya mafuta basi ichukue itakuwa ina kusaidia saidia mizunguko ya hapa na pale”. Nilipokea funguo nikawashukuru wazazi wangu niliondoka lakini nilipofika nje baba aliniita nikageuka.
“Jamie unapaswa kusahau kuhusu ajira” kauri ile ilinishitua kidogo, wakati huo baba alikuwa akinisogerea karibu zaidi wakati akinieleza hayo.
“Nenda benki nimekuwekea kiasi cha kutosha kuanzisha biashara yako nimetumia akaunti yako ya DTB najua ulisha isusa na ndiyo maana hata taarifa huna. Ni wakati wa kuanzisha biashara yako binafsi sasa” maelezo ya baba yalizidi kunichanganya. Ninavyoijua familia yangu haina kiasi cha kutosha kunifanya mpaka nimiliki biashara yangu.
“baba…. pesa umetoa wapi? Au ndo umejikamua ka pensheni kote lakini naamini hakata nitosha kabisa kufikia malengo yangu. Nilijibu Ninaifahamu vizuri familia yangu, ninakujua wewe huna fedha baba na hiyo pesa ya biashara inatoka wapi?” nilimhoji kwa hofu sana maana nilijua kipato na hali ya familia yangu niliyozaliwa.
“nimeiuza ile nyumba yangu ya Masaki, nimelipwa kiasi kikubwa sana cha pesa na ndicho kilichonishawishi kuiuza, ni pesa nyingi mno niliahidiwa milioni miatisa na hamsini” baada ya kauli hiyo nilibaki nimeduwaa.
“siri hii sikumshirikisha mtu maana wewe usingekubali na mama yako asingekubali, niliamua kufanya peke yangu nimeesha uza tayari na pesa ziko benki, nilikuwekea milioni miatano ila naona kuna umhimu wa kukuongeza na kiasi kidogo nimerjenga nyumba huko mtaa wa Mwananchi twende nikupeleke zilizobaki zitatumika tukizihitaji zitakuwepo benki.” Baba alinishangaza kwa kila alichokizungumza
“baba inawezekanaje uiuze ile nyumba tena bila kutujulisha kama familia?” Baba alikuwa katukosea saana kama familia.
“kuna sababu nyingi tu, kwanza ilikuwa imechoka sikuwa na fedha za kuikarabati kuwavutia wateja wapya watakao tulipa vizuri wakipanga, pili wapangaji walikuwa wananisumbua nikaona ni bora kuiuza, tatu ile ni mali yako nadhani imeuzwa muda mwafaka hauna kazi na sasa inaweza kukusaidia kujitegemea,nne na mwisho imesaidia kurudisha hadhi ya maisha yetu. Majibu ya baba yalinifurahisha tulikumbatiana na nikampongeza.
Niliingia kwenye gari nikiwa na furaha sana lakini baba aliniomba kushuka nayeye alikaa kwenye usukani huku akinionyesha kwa ishara nizunguke mlango wa upande wa pili. Nilifanya hivyo ndani ya gari na mzee Justine, kutoka Igoma kwa watu wazito mpaka maeneo ya mwananchi alifunga breki kwenye nyumba mpya ambayo ujenzi ulikuwa unaendelea katika hatua za mwisho.
“nilinunua kiwanja hiki milioni hamsini ujenzi unakadiliwa kuchukua milioni kama mia themanini ikikamilika mpaka vitu vya ndani tuanweza kufika miambili, haya yatakuwa makazi yangu mapya mwanangu, mara tu itakapokamilika.
“very nice daddy nimependa … binafsi sina chakukwambia zaidi ya kukusifu baba yangu, wewe ni zaidi ya mzazi unayejali familia yako nakupenda sana baba, daima utakuwa mwongozo katika maisha yangu… I love you so much daddy”
“your welcome son ….. huu ni wajibu wangu ninafanya ninachopaswa kufanya kama mzazi, nilikupeleka chuo na nikakuhimiza ukasome uchumi na sasa nataka ulichokisoma kioneshe impact katika maisha yako, achana na habari za kuwatumikia mabwana na kuwatajirisha watu waliojaa kejeli na dharau… think about your future.” Baba alimaliza huku akinibusu kwenye paji la uso.
Tuliingia ndani mwa ile nyumba, sikutarajia maana nilikuta matengenezo mazuri ya hali ya juu ni nyumba ya kisasa, mafundi walikuwa wakimalizia kuweka vifaa kama vile bomba, taa, masinki na kumalizia kupaka rangi kwenye kuta za nje, nilitokwa na machozi, maana kila siku nilikuwa nikiwaza kuwajengea wazazi wangu nyumba nzuri yakisasa lakini leo baba amenitoa kimasomaso.
Tulizunguka huku na kule huku tukipiga soga ,baba alinielekeza “hii ni sehemu yangu yakusomea vitabu na magazeti stahitaji bughuza, pale juu mama yako na natarajia kumfungulia ka ofisi kake na shughuli zake za ubunifu nadhani atakuza soko lake”. Nilikuwa nikimsikiliza baba kwa upole maana alikuwa kanishangaza kwa hicho alichonifanyia.
Tulirudi baada ya shughuli ya kuiona na kuikagua ile nyumba kuisha na baada ya kufika Nyakato National, baba aliomba ashuke nisihangaike kumpeleka nyumbani. Basi alipanda daladala na mimi nikaelekea nyumbani kwangu Busweru.
Nikiwa kwenye gari nilikuwa nasikiliza radio na kwa bahati nzuri ulipigwa wimbo unaitwa Nipeni dili wa Albert Magwea, ni moja ya wimbo ninaoupenda sana lakini sikuhiyo kuna maneno ndani ya wimbo huo yalinigusa sana, maneno hayo katika wimbo huo ni… “kulala masikini na kuamka tajiri” ulinihusu na sasa nilikuwa nimelala masikini na kuamka tajiri, ama kweli niliamini Mungu hamtupi mja wake.
Nilifika nikapaki gari yangu nilingia ndani nilirukaruka kwa furaha huku nikimshukuru Mungu kwa mapenzi yake. Siku ilienda vyema saana naweza kusema nilikuwa na furaha niliyoikosa kwa siku nyingi sana. Jioni hiyo nilitinga suti yangu ya kijivu nikaamua leo acha nikatulize mawazo.
Nilikuwa na gari yangu niliyopewa na baba si unajua tena wazee wanavyojua kutunza magari?, ilikuwa inaonekana mpya lakini ni ya kitambo saana. Niliiegesha nje ya ufukwe wa Jembe ni Jembe nilipo geuka kulia nilimuona Dominic na timu yake wamesimama......
Niliitumia hiyo siku kuiliwaza nafisi yangu, nilihakikisha nakipumzisha kichwa changu kutokana na matukio yaliyonizonga hapo mwanzo tukianza na mapenzi yangu kuvurugwa, kufukuzwa kazi na sasa natamani kurudi katika maisha halisi yatakayonipa furaha.
Nilikuwa nimejiachia kwenye kiti cha kulala huku nikiwa na chupa kubwa ya mnvinyo ni Dodoma wine niliamua kuvienzi vya nyumbani siku hiyo. Nilikuwa natiririsha kooni huku nikisogeza muda. Wakati huo mawazo yangu sikuyaruhusu tena kuwaza shida ila furaha tu na shukrani zangu nilizielekeza kwa baba yangu kipenzi maana nilimuona kama mkombozi.
Niligeuka upande wa pili nilimkuta Maria na Dominic siku hiyo walikuwa wameongozana na Magreth Esta hawakuwa naye bilashaka walikuwa wakila bata kama walivyozoea. Tulikuwa tukingaliana kwa wizi wizi na nilikuwa sina wasiwasi kabisa, maana najua uwepo wangu tu hapo ufukweni ilikuwa ni gumzo kwao najua hawakupiga stori zingine bila shaka Jamie ndiye alikuwa mada kuu yakuzungumziwa siku hiyo.
Baaada ya kuhakikisha chupa yangu ya wine imekatika na sasa niliamua kuondoka. Nilipita jirani na walipokaa nilitoka mpaka nje nikachukua gari langu na kuondoka. Mapumziko yangu yaliendelea pale KingDom hotel mtaa wa Ghana nilijipumzisha hapo kwa siku tano mfululizo na sasa akili yangu niliiona imekaa sawa. Siku ya sita niliondoka pale majira ya saa nne asubuhi nilienda mpaka nyumbani kwangu amabako nilianza kutafakari ni biashara gani itanifaa.
Niliwaza biashara nyingi sana zitakazonifaa kwa mtaji huo, niliorodhesha biasha kama ishirini, zakuanzisha mwenyewe na zakuwa mshirika baada ya hapo nilianza kuchambua kila moja na changamoto zake na faida, vikwazo na upungufu.
Niliifanya kazi hii kwa siku tano na hatimaye nilikuja na biashara moja ambayo niliamini lazima itanitajirisha haraka. Na baada ya kuibuni nilianza kuifatiria kwa karibu ili kuijua zaidi na hata kutafuta uzoefu. Wakati nafanya haya nilikuwa nayawaza mafanikio kwa karibu na niliamini hii ni njia pekee ya kunitoa. Naamini biashara hii hakuna aliyedhani ni mhimu na najua kila mtu aliipuuza. Nilitafuta kampuni ya kiitaliano inayotengeza mavazi ya kike na tukaingia makubaliano ya kunitengenezea nguo za ndani za kike zenye kiwango cha hali ya juu, tulifikia makubaliano nilisajiri kampuni yangu ya Himaya ChapaKazi na baadae kuanzisha matawi mbalimbali katika sehemu tofauti tofauti. Na kazi ikaanza mara moja nilianza kuingiza nchini aina mbalimbali za nguo za ndani kama vile Chupi, blezia, magauni ya kulalia, na nguo zingine za ndani za aina tofauti tofauti.
Himaya chapa kazi ndo lilikuwa jina la kampuni yangu na ilizalisha bidhaa za African Angel, asikwambie mtu ndani ya miezi mitatu nililiteka soko la afrika mashariki kwani bidhaa bora na sasa zilikuwa hazitoshi, nilijitahidi sana kuagiza kila niwezavyo bidhaa hazikutosha, kwa hali hiyo bidhaa zangu zilikuwa zikijipandisha bei zenyewe sokoni na sasa nilikuwa natengeneza faida kubwa kuliko nilivyotarajia. Nilikuwa na mawakala wengi mno kila kona ya nchi na kila mtu alianza kushitushwa na jinsi bidhaa hizi zilivyoshika kasi.
Himaya sasa ilikuwa ni bland kubwa mno na sasa nilianza mpango wa kujenga kiwanda hapa nchini niliruhusiwa kukopa benki kiasi kikubwa sana cha pesa na nikajenga kiwanda kikubwa nachakisasa. Himaya Chapa Kazi ilikamilika nikiwa namiliki hisa zote kwa asilimia miamoja, nikaleta watalamu na wabunifu kutoka ng’ambo, bidhaa zangu ziliendelea kuwa bora kwani nilianza kuingia kwenye ushindani wa kimataifa nikiwa na mwaka mmoja tu katika soko.
Jamie Justine ni majina amabyo hayakufahamika matajiri wengi walikuwa wakimtafuta huyu mtu ni nani, lakini hawakubahatika kumpata, ndani ya muda mfupi sana nilikuwa na mafanikio makubwa. Nilijidharau sana kwanini nilipenda kuajiriwa wakati kujiajiri kuna mafanikio makubwa hivi. Mafanikio yangu yalikuwa makubwa mno katika maisha yangu, nilikuwa mtu tofauti ndani ya muda mfupi sana. Sasa jina la Himaya ChapaKazi lilikuwa kubwa mno likiwakilishwa na bland mama ya Himaya ChapaKazi Industries Group.
Kila kukicha nilikuja na bidhaa mpya ambayo pia haikukosea kuingia sokoni niliteka soko la mavazi Afrika Mashariki ndani ya mwaka mmoja na nusu, Afrika Mashariki ukikutana na watu watano watatu lazima watakuwa wamevaa mavazi kutoka Himaya ChapaKazi.
Nilikuwa bize sana na shughuli za kila siku na ikafikia wakati nilimsahau Jesca sikutaka tena kuhangaisha kichwa changu juu yake. Mwaka wa pili ulikuwa na mafanikio zaidi na nilifanya upanuzi mkubwa wa kiwanda changu ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali. Wafanyakazi walinishauri wakati tukitafakari nani awe mgeni rasmi katika uzinduzi wa kiwanda chetu awamu ya pili. Kuna mmoja alisema mkuu wa mkoa, mwingine alipendekeza waziri mkuu au waziri wa viwanda.
Kunammoja alisema basi tumualike Mh. Rais maana HimayaChapaKazi imekuwa ni moja ya kampuni mama katika taifa hili ni kampuni inayokua kwa kasi kuliko kawaida. Tulikubaliana na barua ikatumwa Ikulu, na kwa bahati nzuri ilikubaliwa. Maandalizi yalifanyika yakumpokea Mheshimiwa Rais tulijiandaa, hatimaye siku ilifika. Ilikuwa ni saa nne asubuhi watu wakiwa wamejaa kuliko kawaida. Jamie lilikuwa ni jina jipya midomoni mwa watu ila Himaya Chapakazi ilitambulika mpaka kwa watoto. Watu walikuwa wakifika eneo la kiwanda changu walishangaa waliulizana ni nani mwenye kiwanda hiki.
Kila mtu alijibu alivyojua, mara wa China, mwingine wa Canada, mara wa Marekani. Nilikuwa kimya nikiwasikiliza ulipofika muda nilimpokea Mh. Rais na timu yake ya viongozi mbalimbali, lakini hii ni mara nyingine nashikana mkono na Jesca akiwa kaongozana na baba yake Mzee manguli…………
Haikuwa rahisi kutazamana usoni tulijikaza kwa aibu, kiukweli Jesca alipendeza na alivutia mno alipendeza kwa mavazi yake ya kitenge na kiatu chake cheusi, shingoni alivaa mkufu wa shanga uliorembwa vyema. Uso wake ulitakata mithili ya malaika aliyetoroka peponi, nawezakusema hakuna mfano wa mwanamke mzuri katika dunia hii kama Jesca Manguli alivutia sana.
Lakini ilikuwa ngumu mno kwani Jesca hakutaka kabisa kuinua uso wake kuniangalia kutokana na nilivyomkazia macho maana nilimkumbuka sana, Jesca Manguli alikuwa ameinama muda wote sikujua kama ni aibu au hasira huenda hakutegemea kukutana na mimi leo, na ndiyo maana kaishiwa raha. Jesca alikuwa ameongozana na baba yake kwenye uzinduzi wa HimayaChapaKazi nilijitahidi saana kushughulika na swala la kumkaribisha mgeni wangu mheshimiwa rais kuliko chochote maana mimi ndiye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo.
Mheshimiwa Rais alifika nikamkaribisha akapita na kuketi lakini alikuwa na mashaka alikaa pamoja na timu yake nzima aliangaza huku na kule sikujua alimtafuta nani. Najua hakuna aliyejua kuwa naweza kuwa mkurugenzi mtendaji wa Himaya Chapakazi, kwanza kimuonekano nilikuwa mwembamba sana, pili kiumri nilikuwa mdogo sana umri wangu nilikuwa na umri wa miaka ishirini na sita tu lakini mwili ulinibeba zaidi nilionekana mdogo zaidi kwa kuniangalia. Huenda hali hii ndiyo ilimtia hofu Rais kuona kijana mdogo ndiye akimkaribisha.
Baada ya kuwakaribisha wageni ilikuwa ni zamu ya Mkurugenzi mtendaji kuzungumza, watu walikuwa na kiu kubwa si yakumsikia mkurugenzi wa Himaya ChapaKazi bali kumjua ni nani. Baada ya kukaribishwa nilisimama, Mheshimiwa Rais aliniangalia na kutikisa kichwa sikujua kwanini. Nilipiga hatua mpaka mbele umma wote ulinishangilia kwa makofi, nilifika nikawasalimia na nikatoa shukrani zangu na kuutambua uwepo wa viongozi wote huku nikihitimisha na Mheshimiwa Rais.
Nilitoa hotuba nzuri kwa kujiamini na nilikuwa nimejipanga. Jamie Justine kuanzia siku hiyo nilitambulika kilakona, naweza kusema ni busara zangu na uwezo wangu mkubwa wakujituma na kuhakikisha sishindwi na jambo lolote katika ulimwengu huu. Kila nilichokizungumza nilikisema kwa ustadi mkubwa na nilijitahidi kuchagua maneno ambayo hayatasababisha mikwaruzano ya hapa na pale aidha na viongozi au jamii na hata wafanyakazi wenzangu.
Nilianza kuzungumza na kutoa hotuba yangu kama ifuatavyo:-
“Mh Rais HimayaChapakazi ni Kampuni mama ya uzalishaji wa mavazi nchini mwetu ni kampuni niliyoibuni mimi, na mpaka sasa inajiendesha kwa kiwango kikubwa, ndani ya miaka miwili nimetengeneza ajira kwa maelfu ya Watanzania maana ninaamini kuwa Tanzania itajengwa na Watanzania, hivyo niwajibu wangu na wetu vijana wa kitanzania kuijenga Tanzania” nilisita kidogo kisha nikaendelea………
“Kuna watu hawaamini kuwa mimi na umri wangu huu ndiye mmiliki haswaa wa himaya Chapakazi, napenda kuwahakikishia kuwa Mkurugenzi mtendaji wa Himaya ChapaKazi ni Jamie Justine ni huyu aliyesimama mbele yenu, ni huyu anaezungumza mbele yenu. Hana ndevu, mnvi, kipara wala kitambi kama walivyo wakurugenzi wengine tuliozoea kuwaona ingawa sitavikataa hapo baadae vikinivamia” kauli ya mwisho iliwafanya wote waangue kicheko. Niliendelea na hotuba yangu iliyovutia kuisikiliza kwani kila mtu alinisikiliza kwa makini na nilishangiliwa kwa kila nilichokizungumza maana vyote vilikuwa vya msingi na mhimu katika maisha ya kila siku na ujenzi wa taifa letu.
Baada ya hotuba yangu ndefu kama mmiliki wa Himaya nilikuwa nimeeleza mafanikio ya Kampuni iliyofanya vema pia katika kulipa kodi ya uzalishaji, sikuishia hapo tu bali nileleza pia changamoto zote zinazotukabili na matatizo mbalimbali huku nikikisukuma kilio hicho kwa Rais kuomba utatuzi. Rais alisimama baada ya ukaribisho uliozingatia itifaki, alizungumza mengi sana.
Mheshimiwa Rais alisema maneno haya na kuongeza
“Kwa mara yakwanza katika utawala wangu nimeshangazwa na uwezo wa kijana huyu mdogo Jamie Justine, unajua haka kakijana kamenipokea nikawa nashangaa,haka katoto mbona kana kihelehele?, maana tumezoea tuki arikwa huwa tunapokelewa na wazee au watu wa makamo. Leo imekuwa ni safari ya ajabu kwangu maana ni muujiza kuja kufungua kampuni kubwa kama hii na nikakuta mmiliki wake na ndiye mwanzilishi akiwa na umri mdogo kuliko matarajio yangu. Mwanzo sikujua,.. nimekuja kujua Mc alipomtaja mkurugenzi ndipo kakaamka haka kajamaa, Hongera sana mwanangu vijana igeni mfano wa huyu mwenzenu hapa”
Jamie nimekuwa nikihimiza viwanda, vijana wajishughulishe na leo umenitoa kimasomaso stakuacha hivi hivi wewe ni mwanangu, sasa orodhesha matatizo yote uliyonayo ndani ya kampuni hii yaliyondani ya uwezo wangu nitayakamilisha mapema iwezekanavyo”. Rais alieleza mengi huku akinichagua kuwa mfano wa kuigwa ndani ya Taifa hili, Mh. Rais alikamilisha uzinduzi na kuendelea na safari zake na nilipata muda tena wa kuagana na Jesca awamu hii alikuja na kunikumbatia aliniachia namba za simu kisha akaondoka.
Jamie Justine na Himaya ChapaKazi ni majina yaliyolitesa taifa. Jioni ya siku hiyo radio, television na mitandao ya kijamii ilikesha na jina moja tu Jamie Justine. Kesho yake magazeti yote yalinifahamu na jina langu likawa ni moja ya sentensi mhimu nayalazima kutajwa na kila chombo cha habari si cha lugha ya Kiswahili wala lugha za kigeni. Magazeti muhimu kama Tanzania Gwiji liliandika “Jamie Justine mjasiliamali mdogo zaidi anaisumbua Tanzania”. Habari weekend likaandika “Jamie amfurahisha Manguli” na gazeti la Habari za Asubuhi nalo likaandika “Hatimaye mmiliki wa Himaya Chapakazi ajulikana nalo Gazeti la Hapa Kwetu lilisomeka kwenye ukurasa wa mbele limeandikwa “Rais Afurahishwa na Ndoto za Tajiri Kijana aliyedhani ni Mtoto au Mc”. Kila gazeti liliandika walichokijua ili tu kuwafurahisha wasomaji wao. Jamie Justine lilikuwa ni jina maarufu sana ndani ya muda mfupi.
Kilichofuata ni kuhudhuria inter- view katika radio na television mbalimbali nilikuwa nikihama vituo vya radio, magazeti, television na mwisho wa siku jina langu lilizidi kupaa na nikazidi kuwa mtu mashuhuli zaidi. Habari ziliwafikia ndugu zangu Dominic na Maria hawakuamini maana walianza kunisoma kwenye magazeti na mbaya zaidi hawakuwa na chakufanya maana nikombali na uwepo wao, lakini sina ushirikiano nao tena.
Iliwauma sana kuona na kujua kuwa nimefanikiwa kuliko wao.Mwanzo waliijua Himaya ChapaKazi lakini hawakumjua mmiliki na leo mmiliki nimejitokeza ni mimi Jamie Justine. Maisha akipanga Mungu binadamu hawezi kupangua, na sasa safari yangu ya maisha ilizidi kuwa nzuri na tamu kuliko kawaida, nilikuwa naingiza kiasi kikubwa mno cha pesa.
Huwezi amini kwa wakati huu baada ya uzinduzi wa pili kuanza kazi, Himaya ilikuwa na uwezo wakuniingizia pesa nyingi kwa wakati mfupi kutokana na uzalishaji kuwa mkubwa. Na sasa pesa kwangu tena halikuwa tatizo ila tatizo ni penzi la Jesca.
Leo nimepata muda wa kutosha nikiwa nimepumzika nyakati za jioni, niliamua kumpigia Jesca, namba aliyoniachia Jesca ilipatikana baada ya kujaribu kuipiga na akapokea bila wasiwasi, kwanza nilisita maana sikuamini kama ni yeye lakini bila wasi wasi alianza kunisalimia.
“habari?”
“aaaah! Poa Jesca vipi?”
“aaah! Kumbe ni wewe Jamie?”
“yes ni mimi Jesca wangu”
“Mkeo hajambo?”
“hapana sijaoa Jesca nani alikwambia nina mke?”
“ulidhani sitajua?, wasamalia wema waliniambia una mke na watoto wawili, ila ahsante kwa uongo”
“hapana walikudanganya sina mke Jesca wangu”
“acha kunifanya mtoto mdogo Jamie au ndo umempiga chini baada ya kufanikiwa kimaisha, tafadhari usifanye hivyo bwana”
“hapana ukweli ni kwamba sina mke na sina mtoto, nilikwambia toka mwanzo wewe ndiye chaguo langu na wewe ndiye furaha yangu”
“Utahangaika tu ndugu yangu kuendelea kunidanganya bora uwe mkweli na muwazi, jifunze kuwa mkweli kwani uongo utakugharimu siku moja”
Basi mjadala wetu niliona hautakamilika ilinibidi nimhadithie mkasa wote ilivyokuwa mpaka kupelekwa lumande na nikalala huko.
Nilimwambia ndiyo maana nikawa sipatikani, na wabaya wetu waliutumia mwanya huo kukushawishi uamini kuwa niko kwa mke wangu, ndo maana nimezima simu, baba yangu ni shahidi kaja kunitoa ndani na wadhamini watatu baada ya kumtwanga yule mbeya ya kiume, nilimueleza hayo yote ili ajue kilichotokea.
Hao watu waliokueleza haya huwezi amini wamenifanyia fitina mpaka nikafukuzwa kazi, niliuza mali zangu zote na kubaki mikono mitupu. Mpaka leo sitaisahau gari yangu niliyoipenda zaidi Rav4 niliiuza kwa hasara na chanzo ni hao wajinga.
Walihakikisha natengana na wewe walipofanikiwa waligeukia maisha yangu na wakahakikisha wanaya vuruga. Huwezi amini waliniharibia kila kazi niliyopata tena kwa kuhonga nilifukuzwa kila nilipoajiriwa. Pamoja na juhudi zote za kukupata nilizofanya kugonga mwamba lakini nilipowabana walinipa namba zako cha ajabu nilipokupigia nikueleze ukweli ukakata simu na ukazima simu hukutaka kunisikiliza hatakidogo.
Jesca alisikitishwa sana na maelezo niliyompa, na hakuamini nilichomueleza alibaki kinywa wazi huku akisikitika sana.
“Jamie unachokisema ni kweli?”
“hakika ninachokueleza ni kweli”
“na imekuwaje ukawa mkurugenzi wa Himaya ChapaKazi aliyokuja kuizindua baba yangu?”
“baada ya kupoteza uelekeo na maisha kuniendea kombo baba yangu aliamua kuuza nyumba yake iliyokuwa Masaki jijina Dar Es Salaam. Baba alinikabidhi pesa nyingi nikaanzisha biashara na nilijitahidi kuwa makini maana sikuwa na kimbilio jingine, nilitumia maarifa na weledi mkubwa huku nikiruhusu ushirikiano na makampuni makubwa. Nilifanya hivyo kwa muda wa mwaka mmoja ilikwenda vizuri nilishawishika kukopa benki kiasi kikubwa tu cha pesa na nikafanikiwa kupanua wigo zaidi wa uzalishaji ndani ya Kampuni yangu na leo unaniona hapa nilipo ni Jamie Justine wa Himaya ChapaKazi”
“unamaanisha Himaya ChapaKazi ni yako huja ajiriwa?”
“bila shaka mimi ndiye mwanzilishi na ninamiliki hisa alisilimia miamoja”
“kwa hiyo wale watu walinidanganya…. Ooooh! my God!..... kumbe ni waongo eeh?”
“Jesca, Maria unamjua alitufuata mpaka kule Victoria Hotel akiwa na Dominic siku ile akatuharibia maongezi na ukanionya juu yake, sasa ilikuwaje ukamuamini kiulaini kiasi kile?”
“Jamie mapenzi… mapenzi ndugu yangu …. Mapenzi yanauma na uongo huwa haufai katika mapenzi. Katika maisha yangu naogopa sana kuumizwa nilifanya hivyo ili nisiumie kumbe ndo nilikuwa nakuumiza masikini wa Mungu … I m sorry sikujua, mpenzi wangu… sikujua baby nisamehe sweet haert”
“usijali nilisamehe maana nilijua mapema kuwa hukujua na ndiyo maana sikuumiza kichwa juu ya hili.”
Siku hii ilikuwa ya furaha sana kwangu nilifurahi sana kuzungumza tena na Jesca na kilichonifurahisha zaidi nikumueleza ukweli sasa roho yangu ni nyeupe, sina tatizo tena maana ameujua ukweli.
Basi tuliendelea kupiga stori huku tukikumbushana hili na lile lakini hatukuusahau usiku tuliolala pamoja pale Ikulu ndogo tulikumbushana mengi tukataniana huku tukifurahi pamoja. Naweza kusema ulikuwa ni usiku mwanana kuwahi kutokea katika maisha yetu si yeye tu bali hata mimi Jamie. Mazungumzo yetu yalivutia sana na ilionyesha kila mtu alikuwa kammisi mwenzake tulisimuliana hadithi tukacheka na kukumbushana mengi.
Katika mazungumzo yetu kulikuwa na furaha isiyo ya kawaida Jamie Justine nilifurahi sana kumrejesha Jesca Jones Manguli mikononi mwangu.
“Jesca sasa staki kukuchelewesha mambo jiandae anytime nitaleta posa na kama itapokelewa na kukubaliwa ni mwaka huu ujiandae kuolewa, nitakuoa mwaka huuhuu staki kupoteza hata dakika maana waswahili husema chelewachelewa utakuta mwana si wako”
“No.. nooo! please no usiseme hivyo Jamie!”
“kwanini?”
“Jamie nisamehe, ni miaka miwili imepita, na mengi yamepita katikati yetu, kulingana na swala lenyewe lilivyokuwa nilikuwa na hasira na ikafika wakati nilijilazimisha niusahau uwepo wako na sasa bila kutarajia niko kwenye mahusiano na mtu mwingine na mbaya zaidi jamaa kaishatoa mpaka mahali.
“What?”……..
“najua inauma lakini pole sana, sina budi kukueleza ukweli.. .
Nilikata simu na kubaki mdomo wazi, kiukweli haikuniingia akilini, “hivi kweli Jesca kachumbiwa?” nilijikuta nikicheka si kwakufurahi bali ni maumivu makali yaliyo umiza nafsi yangu. Haikuwa rahisi kuyaamini yaliyokuwa yakizungumzwa na Jesca lakini amini usiamini Jesca hakuwa wangu tena.
.
Nilitafakari sana juu ya maisha yangu, inawezekanaje kila ninapokaribia kuipata furaha matatizo huibuka tena na kunikatisha tamaa. Inamaanisha katika maisha yangu haitatokea siku nikawa na furaha hasa katika mapenzi. Nimetafuta pesa kwa nguvu zote na bado najaribu kuitafuta kwa hali na mali lakini bado furaha kwangu limebaki kuwa neno la kichina lililoandikwa kwa lugha ya kichina kwa upeo wangu stokaa nilisome katu.
Sikutaka kuyasikia maneno yaliyosemwa na Jesca yaliniumiza mno, nadhani kwa mara ya kwanza katika mapenzi nakutana na jeraha kubwa lenye maumivu makali moyoni mwangu.
Naweza kusema sikuhii ilikuwa ni moja ya siku zilizoharibu furaha yangu na kuyaona maisha niliyonayo na pesa nilizonazo si lolote na si chochote. Sikuwa na amini kuwa ipo siku nitaikosa furaha kwa kulikosa penzi la Jesca kipenzi changu, lakiniu leo imetimia. Nilijiona sina mbele wala nyuma, kushoto wala kulia. Hakuna maumivu mabaya kama kumpoteza unayempenda tena kizembe, naweza kusema nimempoteza kizembe sana mpenzi wangu.
Wakati kichwa kiuma kwa mawazo simu iliita na nilipoitazama alikuwa inaonesha jina la Jesca Manguli, sikuipokea maana moyo wangu ulikuwa unaniuma mno kumpoteza mpenzi wangu niliyempenda kwa dhati. Simu ilizidi kunisumbua na sikutaka kabisa kuipokea maana moyo wangu umeesha umia na sikutaka kuumiza tena. Kulingana na hali niliyokuwa nilijikuta nikiiogopa kabisa simu yangu. Simu iliyokuwa ikiita muda wote na sikutegemea kuipokea lakini kulinganza na usumbufu na kutokuchoka kwa mpigaji nilijikuta nikiipokea.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment