Search This Blog

Wednesday, 29 March 2023

PENIELEA (4) - 4

   


Simulizi : Peniela (4)

Sehemu Ya Nne (4)

Edmund akatikisa kichwa kukubaliana naye.

“ Kama ni hivyo basi John Mwaulaya pamoja na mabaya yake mengi aliyoyafanya akiwa na Team SC41 anastahili pongezi na heshima ya kipekee kwani bila ya yeye maelfu na maelfu ya waafrika wangeteketea .Hata hivyo kuna maswali ambayo nahitaji kupata majibu yake,ilikuaje kirusi hiki kikahifadhiwa ikulu Dar es salaam” akauliza Mathew

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Jambo hili lina maelezo marefu na hata mimi kuna vitu ambavyo sivifahamu .Haya niliyowaelezeni ni mambo aliyonieleza John Mwaulaya mwenyewe.Aliniambia kwamba baada ya kufanikiwa kukipata kirusi Aby pamoja na Chang Ling,John alihitaji kukiweka kirusi hicho sehemu salama kwani ni hatari mno kwa dunia hivya akalaziika kumueleza ukweli rais wa wakati huo Leonard Aduma ambaye walikuwa na mahusiano ya kirafiki.Wakati wa uongozi wake Leonard ndiye aliyetoa ruhusa kwa Team SC41 kufanya shughuli zake kwa siri nchini Tanzania baada ya kupatiwa utajiri mkubwa wa mabilioni ya dola.Rais Leonard au Leo kama alivyokuwa amezoeleka kuitwa alikubaliana na ushauri wa John na kirusi aby kikahifadhiwa ikulu katika sehemu salama na kila rais aliyefuata baada ya Leonard alikabidhiwa kirusi hicho akitakiwa akilinde kwa kila namna atakavyoweza.” Edmund akanyamaza kwa sekunde kadhaa akwatazama akina Mathew waliokuwa wakimsikiliza kwa makini akaendelea

“ Wakati wa safari hiyo ya kuja kufanya majaribio ya kirusi Aby,Chang ling alikuwa na kifaa kidogo cha kielektroniki ndani ya mkono wake wa kushoto ambacho kiliwawezesha majasusi wa Korea kaskazini kumfuatilia kwa kutumia satelaiti na kwa njia hiyo waliweza kufahamu kila mahali alipo.Lengo la kumuwekea kifaa hiki ni hofu ya kumpoteza Chang ling kwani sehemu aliyokuwa anakwenda kufanya jaribio la kukiachia kirusi hicho ni mbali huko jangwani.Hata baada ya ndege aliyopanda Chang ling kutangazwa kupotea kifaa hicho kidogo katika mkono wa Chang kiliendelea kuonyesha muelekeo wake na baadae kilizimikia Dar es salaam Tanzania.Hii ni sababu Chin Sun alitumwa nchini Tanzania kwa kazi moja tu ya kutafuta alipo Chang Ling ambaye wanaamini bado yuko hai.Hata mimi ninaamini hivyo lakini hii imebaki ni siri kubwa ya John Mwaulaya.Yeye ndiye anayejua mahala aliko Chang Ling” akasema Edmund na baada ya sekunde kadhaa akaendelea

“ Baada ya kufanikisha kukitwaa kirusi Aby na kumdhibii Chang Ling,Bill Madsan na John mwaulaya waliingia katika mtafaruku mkubwa.Bill hakupendezwa na kitendo alichokifanya John mwaulaya cha kukiweka kirusi kile Ikulu kwani mipango yake ilikuwa ni kukitumia kutengeneza fedha nyingi.Wiki mbili baadae Bill aliokotwa akiwa amekufa .Mambo hayakuishia hapo,miezi mitatu baada ya kumaliza kipindi chake cha uongozi,Leonard Aduma alifariki katika ajali ya helkopta alipokwenda kutalii katika mbuga za wanyama akiwa na familia yake.Hapa mtaona kwamba wale wote waliofahamu kuhusiana na kirusi kile walipoteza maisha yao kwa hiyo ni John pekee aliyebaki na siri kubwa ya kuhusiana na kirusi hicho.Alifanya hivi kwa makusudi ili kuzuia kirusi hiki hatari kisiweze kutoka kikulu na kutua katika mikono ya watu wenye kuweza kukitumia kusababisha maangamizi makubwa duniani.” Akanyamaza tena akamtazama Peniela kwa muda halafu akasema



“ Alipoanza kusumbuliwa na ugonjwa wake ,John mwaulaya aliniita na siku hiyo nilikuwa na maongezi naye marefu na kuna jambo alinieleza”



“ John alinieleza kwamba kwa ugonwa huu unaomsumbua hana uhakika kama atapona kwa sababu hawezi kutibiwa katika hospitali kubwa nje ya nchi.Hakunieleza sababu na hata nilipotaka kufahamu kwanini Team SC41 wasishughulikie matibabu yake hakutaka kabisa tuongelee suala hilo.John alinieleza kila kitu kuhusu Peniela .Ni historia ya kuhuzunisha sana na kwa mara ya kwanza toka nimfahamu John Mwaulaya nilimshuhudia akitoa machozi.Aliumia sana kwa maisha anayoishi Peniela na alijutia kitendo hake cha kumuingiza Peniela Team Sc41” akanyamaza kdogo halafu akaendelea

“ John alinieleza azma yake ya kutaka kuyabadili maisha ya Peniela ikiwa ni kumtoa kabisa katika Team SC41 lakini aliingiwa na hofu kuwa jambo hilo linaweza lisifanikiwe kwa muda anaoutaka kutokana na afya yake kuzidi kuzorota.Aliniomba endapo ikitokea akafariki kabla lengo lake halijatimia basi nichukue jukumu la kumsaidia Peniela.Baada ya wiki moja akaniita tena na kunipa ufunguo.Akaniambia kwamba niutunze ufunguo ule na atakapokuwa amefariki Peniela atakuja kwangu na nimpatie ufunguo huo.Ufunguo huo nimeuhifadhi katika sehemu yangu ya siri ambayo ninaitumia kuhifadhi vitu vyangu vya siri .Tukitoka hapa tutaelekea huko na nitawakabidhi funguo hiyo.” Akasema Edmund .Ukimya wa sekunde kadhaa ukapita halafu Peniela akauliza



“ alikueleza ufunguo huo ni wa nini?



“ Hapana hakunieleza ila alisema kwamba nitakapokupa ufunguo huo tayari atakuwa amekupa maelekezo .Je kuna maelekezo yoyote John amekupa?

Peniela akavuta kumbu kumbu na kusema



“ Ndiyo..Mara ya kwanza kuonana naye alinipa kasha moja la chuma na akaniambia kwamba kasha hilo lina kila kitu kuhusu mimi na kwamba nilihifadhi sehemu salama na kwamba nisilifungue hadi hapo atakaponielekeza yeye mwenyewe au ikitokea akafariki dunia.Aliniambia kwamba kasha hilo peke yake bado halijakamilika bali lina sehemu nyingine tatu ili liwe kamili.Alinieleza kwamba nionane na mchungaji Edmund Dawson ambaye ni wewe na ndiye utakayenielekeza yalipo makasha hayo mawili yaliyobakia” akasema Peniela.Mathew akainama na kutikisa kichwa kwa masikitiko



“ Mbona unasiktika Mathew? Akauliza Edmund.



“ Nasikitika kwa sababu nyumba ya Peniela imeteketezwa kwa moto jana usiku na watu ambao tuna imani ni Team SC41 na kwa hiyo kila kitu kimepotea.Nina hakika kabisa funguo hiyo ambayo John alikupa ni kwa ajili ya kufungulia kasha hilo alilompa Peniela.Ndani ya kasha hilo nina hakika kabisa John Mwaulaya aliweka mambo muhimu mno yanayomuhusu Peniela na ndiyo maana akachukua tahadhari kubwa na hakutaka mtu mwingine afanikiwe kujua kilichomo ndani ya kasha hilo zaidi ya Peniela pekee.Peniela kwa nini hukunitaarifu mapema kuhusu suala hili? Tungetafuta sehemu salama na kulihifadhi kasha hilo” akasema Mathew kwa masikitiko.

“ Relax Mathew.John aliisisitiza mno kuhusu kulitunza kasha lile na nilifahamu umuhimu wake kwa hiyo sikuliweka nyumbani kwangu kwani hapakuwa sehemu salama.Nililihifadhi sehemu ambayo nina uhakika ni salama.”



“ Good .Umelihifadhi wapi hilo kasha? Akauliza Mathew

“ Dr Joshua alinipa nyumba ya kuishi kwa dhumuni la kurahisisha makutano yetu mimi na yeye.Ni sehemu salama sana na huko ndiko nilikolihifadhi hilo kasha”

“ Kuna ulinzi katika jumba hilo?

“ Hakuna ulinzi mkubwa zaidi ya walinzi wawili mchana na wawili usiku kwani jumba hilo halikaliwi na mtu kwasasa zaidi yangu.”

“ Good.Tutafanya mchakato wa kwenda kulichukua hilo kasha ili tujue ndani yake kuna nini” akasema Mathew



“ Vipi kuhusu hilo kasha la tatu liko wapi? Tutalipataje? Mathew akamuuliza Edmund.

“ Sifahamu ni wapi tutalipata hilo kasha la tatu kwa sababu John hakuwahi kunieleza kuhusu jambo hilo zaidi ya funguo hiyo aiyonipatia.Kitu kikubwa ambacho ninashauri nguvu kubwa ielekezwe ni katika kulipata hilo kasha alilompa Peniela na nina hakika ndani ya hilo kasha kutakuwa na maelekezo fulani ya namna ya kulipata kasha la tatu.” Akasema Edmund



“ Chin sun amegundua lolote hadi hivi sasa kuhusu Chang ling au kirusi aby? Akauliza Mathew



“ Mpaka sasa Chin sun hajafanikiwa kugundua lolote kuhusu Chang ling wala kirusi Aby na hana taarifa zozote kama kirusi Aby kinahifadhiwa ikulu.”



“Good.Tunashukuru sana Edmund kwa maelezo yako ambayo yametupa mwanga mkubwa kuhusiana na John na ninathubuu kusema kwamba kwa mara ya kwanza leo nimemfahamu John Mwaulaya ni nani.Alikuwa n mtu mwenye sura mbili.Sura ya kwanza malaika na sura ya pili shetani.Tuachane na hayo na tuangalie mambo mengine yaliyoko mbele yetu” akasema Mathew na baada ya sekunde kadhaa akaendelea



“Mimi na Peniela tutaendelea na opereheni yetu ya kuhakikisha tunakipata kirusi Aby na kuepusha maangamizi makubwa yanayopangwa kufanywa kwa kutumia kirusi hicho.Nakuhakikishia kwa gharama zozote lazima kirushi hicho tukipate.Baada ya kukipata tutaanza operesheni mpya ya kumtafuta Chang ling na kama tukifanikiwa kumpata basi tutaweza kufahamu nini kilitokea katika ndege iliyopotea.Kuna mambo mengi bado tunahitaji kuyapatia majibu.Wewe utaendelea na operesheni yako ya kumchunguza Chin sun na tutakuwa tunawasilana kwa siri bila ya mkeo kufahamu.Endapo kuna taarifa zozote ambazo zitakuwa na msaada kwetu basi utatutaarifu mara moja kwa njia ya siri tutakayokuwa tunaitumia kuwasiliana” akasema Mathew



“ Nimekuelewa Mathew.Tutawasiliana kwa siri sana ili Chin sun asiweze kugundua lolote.Niambieni ni vitu gani hasa mnavihitaji ili muendelee na operesheni yenu?

“ kwanza tunahitaji sehemu salama ya kuishi kwa sababu hatuna makazi.Nyumba zetu zote mbili ziliteketezwa na moto jana usiku.Tunahitaji makazi salama yatakayotuwezeha kuendesha operesheni yetu kwa uhuru.Baada ya makazi tunahitaji pia fedha za kutumia.Operesheni hii inahitaji fedha kwa hiyo tutahitaji kiasi kikubwa cha kutosha cha fedha .Tunahitaji vile vile usafiri.Gari mbili zinahitajika.Kuna nyakati tutalazimika kwenda sehemu tofauti toauti mimi na Peniela kwa hiyo kila mmoja atalazimika kwenda na gari lake.Tunahitaji vile vile vifaa vya mawasiliano kama simu na vingine vya kutuwezesha kuwasiliana na mwisho kabisa tunahitaji silaha kwani watu tunaokabiliaa nao tayari wamejihami kwa silaha.Hii ni kama vita bila silaha hatuwezi kushinda.” Akasema Mathew.Edmund akatafakari kwa sekund ekadhaa na kusema



“ John mwaulaya aliniamini sana na kuniomba nimsaidie Peniela kwa hiyo nitahakikisha kila kitu mnachohitaji mnakipata.Kwa upande wa makazi,ipo nyumba nzuri ambayo naamini itawafaa sana.Kuna rafiki yangu mmoja alirejea Marekani hivi karibuni baada ya kuishi hapa nchini kwa zaidi ya miaka kumi na alikuwa na jumba kubwa aliloniachia niliuze kwani alikosa mnunuzi wa haraka kutokana na bei yake kuwa kubwa.Mtaishi hapo hadi hapo operesheni itakapokamiika.Kuhusu magari nayo pia yapo.Mtatumia magari ya huo rafiki yangu ambaye aliacha magari manne.Vifaa vya mawasliano navyo mtapata.Fedha pia mtapata za kutosha.Silaha pia mtapata .”

“ Tunashukuru sana Edmund kwa msaada huu mkubwa.Nina hakika kila mpango wetu tunakwenda kufanikiwa.”



Baada ya maongezi yale hakukuwa tena na muda wa kupoteza wakarejea katika makazi ya Edmund ambaye alichukua funguo za gari na hakutaka kuongozana na dereva au mlinzi yeyote akapanda katika gari na akina Mathew wakaondoka.

“ This is going to be the last chapter .Ama zao ama zangu.” akawaza Mathew wakati wakitoka katika makazi ya askofu Edmund Dawson





Ni saa tano na dakika kumi na saba za asubuhi,Rosemary Mkozumi akiwa chumbani kwake amekaa mbele ya meza kubwa iliyojaa vipodozi vya kila aina akiwa na mtu wake maalum wa urembo.Baada ya kumaliza kurembwa akatabasamu kwa namna alivyopendeza halafu huku akijitegemeza kwa fimbo akasimama.



“ Siwezi kukosa fursa hii muhimu ya kuhudhuria mazishi ya Flaviana.Pale ni sehemu nzuri kwa kuanzia harakati zangu za kuwania uteuzi wa kuwa mgombea urais.Tayari nchi nzima wanafahamu kilichonitokea na ninatakiwa kuwaonyesha kwamba niko imara .Pamoja na misuko suko yote iliyonipata lakini bado ninaweza kufanya mambo yangu kama kawaida .Rais anatakiwa kuwa jasiri na asiyetetereka na mimi nitalidhihirisha hilo pale nitakapoonekana katika msiba wa Faviana.Karibu viongozi wote wa serikali watakuwepo pale.Watu wengine wakubwa na muhimu watakuweo pia.Natakiwa kuanza kutengeneza timu itakayoniwezesha nikafanikiwa kupata uteuzi” akawaza Rosemary Mkozumi na kutembea hatua kadhaa



“ Bado nahisi maumivu makali mguuni.I curse you Mathew.Nitakusaka kokote uliko na nitahakikisha nimekupata na usiombe nikakupata ,nitakutesa zaidi ya ulivyonitesa” akawaza Rosemary na kuuma meno kwa hasira akampigia Fernando mmoja wa walinzi wake ambaye humtumia kwa kutesa,akamtaka aonane naye mara moja.Hazikupita dakika tatu Fernando akafika



“ Fernando ninatoka kidogo ninakwenda kuhudhuria mazishi ya mtoto wa rais.Ninachotaka muandae Yule msichana ili nitakaporejea zoezi lianze upya na leo l azima aongee.I don’t care what will happen but today she must talk.Do you understand me Fernando?? Akauliza Rose kwa sauti kali.Fernando hakujibu kitu akabaki anamtazama.

“ Fernando do you understand me? Akauliza tena Rose

“ Yes madam I do” akajibu Fernando

“ Good.Leo nakupa nafasi ya mwisho na endapo Yule msichana atashindwa kuongea basi utakuwa umeshidwa kazi na nitatafuta mtu mwingine wa kunifanyia kazi yagu ninavyotaka kwa hiyo jitahidi ufanye kila linalowezekana ili msichana Yule aweze kufungua mdomo na aseme ninachokitaka toka kwake.” Akasema Rosemary Mkozumi huku akimtazama Fernando kwa macho makali.Wakatazamana kwa sekunde kadhaa halafu Fernando akatoka.Rosemary Mkozumi akawaita walinzi wake wawili akaambatana nao hadi katika gari lake na kuondoka kuelekea katika shughuli ya mazishi ya Flaviana.

Baada ya Rosemary Mkozumi kuondoka,Fernando akaelekea katika c humba alimo Anitha ,aliyekuwa amelala kitandani hajiwezi.Mikono na miguu yake vilifungwa kwa pingu.Uso wake ulikuwa umetapakaa damu

“ Msichana jasiri mno huyu.Yaani pamoja na mateso yale yote hajathubutu kabisa kufungua mdomo wake .Ni nani huyu mwanamke? Akajiuliza Fernando huku akimsogelea Anitha akamshika shingoni akatazama kwa makini akamuonea huruma

“ Nimemtesa mno na bado Madam Rose anataka niendelee kumtesa tena baadae.She’s so weak na endapo nitaendelea kumtesa zaidi kuna uwezekano akapoteza maisha.” Akawaza Fernando akiwa amesimama akimtazama Anitha

“ Madam Rose ni mwanamke katili mno.Nimefanya kazi zake nyingi chafu lakini kwa mara ya kwanza ninasikia uchungu kwa namna alivyonilazimisha nimtese mwanamke huyu .Mateso haya anastahili mtu katili na si huyu dada.Laiti ningekuwa na uwezo wa kumsaidia lakini namuogopa Madam ni mtu katili na ana mtandao mrefu.Nikifanya lolote linalokwenda kinyume na matakwa yake lazima atanisaka na kuniua.NIfanye nini basi kumsaidia huyu mwanamke? Akawaza Fernando.

“ Ninachotakiwa kufanya kwanza ni kumfahamu vizuri mwanamke huyu ni nani.Pengine naweza kufanikiwa kumshawishi akaniambia kile ambacho ameshibndwa kumueleza Rose.Si kila wakati njia ya mateso huwa inafanikiwa.” Akawaza Fernando akafungua sanduku jeusi lenye vifaa vya kutesea akavuta dawa Fulani katika bomba la sindano na kumchoma Anitha.Baada ya dakika tatu Anitha akafumbua macho na kuinua kichwa.Akakutanisha macho na Fernando akamkumbuka kwamba ndiye mtesaji akaingiwa na woga akayakumbuka mateso aliyoteswa asubuhi.Fernando akamsogelea.

“ Usihofu mrembo.Siko hapa kwa ajili ya kukutesa.Tafadhali ondoa hofu.”

“ Kama bosi wako kakutuma uje unitese tena mwambie kwamba niko tayari kufa lakini si kumueleza hicho anachokitaka.She wont get anything from me” akasema Anitha kwa sauti dhaifu

“ Sikiliza mrembo,Rosemary hayupo na hapa niko peke yangu.Amenipa maagizo ya kukutesa hadi nihakikishe unamwambia kile anachokitaka.Lakini sitaki kufanya hivyo anavyotaka madam.Nataka kwanza nikufahamu wewe ni nani?

Anitha akamtazama Fernando kwa macho makali ya dharau halafu akauliza



“ Unataka kufahamu mimi ni nani?

“ Ndiyo nahitaji kukufahamu lakini utanieleza ” akasema Fernando na kutoka mle chumbani na baada ya dakika kadhaa akarejea akiwa na bakuli lililojaa supu ya kuku akamywesha Anitha na kuhakikisha ameimaliza yote halafu akasema

“ sasa tunaweza kuongea”

Anitha akamtazama na kusema



“ kwa nini unataka kunifahamu? Hata kama ukinifahamu nitakusaidia nini?

“ nataka nikufahamu kwa sababu naweza kuwa na msaada mkubwa kwako.Please time to tell me who are you?

Anitha akamtazama kwa sekunde kadhaa na kuuliza

“ How much she’s paying you?



“ What ?? Fernando akauliza .



“ Nimekuuliza bosi wako anakulipa kiasi gani cha fedha kwa kazi hii ya kunitesa?



“ Usitake kufahamu chochote kuhusu mimi.Nijibu nilichokuuliza”



“ Your name is Fernando ,right? Akauliza Anitha

“ Ndiyo naitwa Fernando.Wewe unaitwa nani?



“ Fernando ,Rosemary Mkozumi anakulipa shilingi ngapi kwa kazi hii ya utesaji?



“ Please young lady ,you don’t need to know anything about me”

“ You are doing this for money ,right? If so this is your chance to make much money than she’s paying you” akasema Anitha



“ Unamaanisha nini ? akauliza Fernando

“ Namaanisha kwamba nataka nikusaidie Fernando.Nataka kuyabadili masha yako.Kazi hii ya utesaji utaifanya hadi lini? Rosemary Mkozumi anakutumia kwa manufaa yake mwenyewe na wewe hufaidiki na chochote naamini hata ujira anaokulipa katu haukutoshi.Nikikutazama naona sura ya kijana mwenye kiu ya mafanikio,kijana mtafutaji lakini swali umeridhka na kazi hii ya kumtumikia Rose? Hutaki kuwa na maisha yako mazuri na ambayo hakuna mtu atakayekupa amri nini ufanye? Fernando wewe ni kijana mwenye nguvu na unaweza ukafanya kazi zako binafsi na si kuajiriwa na mtu tena kwa kazi kama hii ya kutesa watu. Una muda mchache wa kufanya maamuzi ya nini unahitaji katika maisha yako ya usoni..Kama uko tayari naweza kukusaidia” akasema Anitha.Fernando akabaki kimya.maneno yale aliyoyasema Anitha yalionekana kumuingia

“ Kunisaidia ? Kivipi? Akauliza Fernando

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ I’m rich.Very rich.I have lots of money.Ninaweza kukupa kiasi kikubwa cha fedha ili uanze maisha yako bila ya kumtegemea Rosemary Mkozumi” akasema Anitha na kumfanya Fernando acheke

“ Unanifurahisha sana .Huna hela ya kunipa mimi”



“ Nimekwambia mimi ni tajiri.Unahitaji kiasi gani? Ten million? Twenty? Sema kiasi unachokihitaji na ninaweza kukuhamishia sasa hivi katika akaunti yako ya benki.” Akasema Anitha kwa kujiamini.Tayari alikwisha msoma Fernando na kugundua alikuwa na tamaa ya fedha



“ Huyu mwanamke yawezekaa akawa ananiambia jambo la kweli.Ni kweli nimechoshwa na maisha haya ya kutumikishwa na Madam Rose.Mpaka lini maisha haya? Lini na mimi nitakuwa na maisha yangu mazuri na kujitawala mwenyewe? Huyu mwanamke yuko sahihi kabisa kwa analolisema lakini je ni kweli ana pesa za kunipa? Akawaza Fernando

“ Fernando muda unakwenda ,tafadhali fanya maamuzi ni kiasi gani unahitaji? Akauliza Peniela

“ Fifty Million ” akatamka Fernando.

“ Nitakuongeza million kumi na zitakuwa million sitini.I can send that money right now to your account but I need something in retun.”



“ What do you need?

“ Mpaka hapa nadhani tayari unafahamu kile ninachokihitaji .I want you to let me go..Once I transfer that money to your account you’ll let me go.Do we have a deal?

Fernando hakujibu kitu akabaki anamtazama Anitha



“ Do we have a deal fernando? Akauliza tena Anitha



“ Jambo unalolitaka ni gumu sana na haliwezekani.Rose ana mtandao mkubwa na endapo nitakuachia huru utakuwa ndio mwisho wangu kufanya kazi kwa madam Rose na kwa kuwa ana mtandao mkubwa atanisaka na akinipata adhabu yake ni moja tu,kifo.Kwa hiyo siwezi kufanya hivyo unavyotaka” akasema Fernando.Anitha akamtazama na kusema

“ Seventy Million..!!

“ I cant!! Akajibu Fernando.

“ Millioni themanini .!!

Fernando akamtazama Anitha kwa macho ya tamaa ya fedha na kuuliza

“ Are you sure ?



“ Yes I’m sure.Ukikubali nakutumia kiasi hicho sasa hivi katika akaunti yako.” Akasema Anitha.fernando akafikiri kidogo na kusema

“ Ok lets do it !!

“ Good.Nitahitaji kompyuta iliyounganishwa na intaneti sasa hivi” akasema Anitha.Fernado akatoka mle chumbani kwa kasi kufuata kompyuta yake

“ Potelea mbali,liwalo na liwe tu ,siwezi kuiacha pesa hii yote ambayo hata kama nikifanya kazi kwa Rosemary hadi nizeeke sintaweza kuipata.Nitaendelea kumfanyia Rose kazi zake chafu hadi lini?Siwezi kuiachia fursa hii iliyojitokeza.Ni wakati wa mimi kuanza kuyapanga maisha yangu.” Akawaza Fernando wakati akifungua mlango wa gari lake na kutoa mkoba mkoba wenye kompyuta mpakato akarejea chumbani aliko Anitha akaiweka kompyuta mezani



“ Good.sasa naomba unifunge ili niweze kukuhamishia fedha katika akaunt yako.” Akasema Anitha,fernando akasita



“ Usiogope Fernando.Usiponifungua unategemea nitakuthamishiaje fedha?

Fernando akawaza kidogo halafu akatoa bastora yake akamuelekezea Anitha



“ If you try anything Stupid I’m going to kill you.” Akasema na kumsogelea akamfungua mkono mmoja halafu akampa ufunguo ili aweze kujifungua mkono uliobaki.Anitha akainuka na kukaa akafumba macho kwa maumivu makali ya mwili aliyoyasikia,akajikaza na kuchukua kompyuta ile akaanza kucheza nayo.Fernando hakufahamu kitu alichokuwa anakifanya Anitha katika kompyuta ile .Alikuwa amesimama karibu na mlango akimuelekezea Anitha bastora



“ Huyu mjinga amekutana na mchawi wa kompyuta .Kosa hili alilolifanya atalijutia katika maisha yake yote.” Akawaza Anitha huku akiendelea kubofya haraka haraka kisha akamtaka Fernando amtajie namba za akaunti yake ya benki ambako anataka fedha itumwe.Fernando akachomoa pochi akatoa kadi yake ya benki na kumsomea Anitha namba,hakumtaka ainuke mahala alipokuwa amekaa.Anitha akamtaka vile vile ampe na namba zake za simu na bila kusita Fernando akamtajia namba zake.Anitha akaendelea kubofya ile kompyuta na baada ya dakika kama nne hivi ujumbe ukaingia katika simu ya Fernando,Anitha akamtaka ausome.

“ Nimetaarifiwa kwamba kiasi cha shiilingi milioni themanini kimetumwa katika akaunti yangu ya benki.”



“ Good.Nataka tukitoka hapa tuongozane wote hadi benki ukahakiki kama ni kweli fedha hizi zimetumwa halafu baada ya hapo utanipeleka nyumbani kwani siwezi kutembea mjini nikiwa katika hali hii.” Akasema Anitha

“ Millioni themanini dah !! hata kama ningefanya kazi kwa Madam Rose kwa miaka hamsini katu nisingeweza kupata kiasi hiki cha pesa.sasa maisha yangu yanakwenda kubadilika.mwanamke huyu anaonekana kweli ni tajiri sana kama anavyodai mwenywe.Anafanya biashara gani? Ngoja nimsaidie na hii ni kwaheri kwa madam Rose.Hataniona tena katika maisha yake.” Akawaza Fernando.

“ Fernando !! akaita Anitha

“ Nimemaliza kwa upande wangu,sasa ni zamu yako.Take me out f here” akasema Anitha.

“ sasa ni hivi’ akasema Fernando

“ Eneo lote la kuzunguka nyumba ya hii kuna ulinzi mkali .Nitakufunga pingu halafu utajilegeza kabisa ili uonekane una hali mbaya sana na mimi nitasema kwama hali yako imebadilika wakati ninakutesa kwa hiyo ninakukimbiza kwa daktari “ akasema Fernando na kumtaka Peniela ajifunge pingu.Alipohakikisha amejifunga pingu akamsogelea na kumfunga vizuri



“ Time to go” akasema Fernando halafu akamuinua Anitha na kumuweka begani akatoka mle chumbani.Kama alivyoelekezwa na Fernando Anitha alikuwa amejilegeza mno na kama ungemuona ungedhani labda tayari amepoteza uhai.Katika lango mkubwa wa kuingilia sebuleni,walinzi wawili walimuona fernado akitoka akiwa amembeba Anitha haraka haraka wakaenda kumsaidia.



“ Nini kimetokea? Akauliza moja wao

“ Huyu mwanamke amekuwa mgumu sana kufumbua mdomo.Madam aliniachia maagizo niendelee kumtesa lakini wakati naendelea na kazi hali yake imebadilika na nina wasi wasi asije akapoteza maisha kabla madam hajapata kile anachokihitaji toka kwake hivyo nataka kumkimbiza kwa daktari Feruzi haraka .” akasema Fernando huku akimlaza Anitha katika kiti cha nyuma na kwa kasi akaondoa gari .Hakuna yeyote aliyemtilia shaka kwani ni moja wa watu wanaoaminiwa mno na Rosemary Mkozumi

“ Nikupeleke wapi? Akauliza Fernando baada ya kuyaacha makazi ya Rosemay Mkozumi.



“ Una hakika hakuna anayetufuatilia?

“ hakuna .Unataka nikupeleke wapi? Akauliza Fernando

“ Ahsante sana Fernando kwa msaada huu.Kabla ya kwenda sehemu yoyote ile nataka kwanza nipate sehemu ambayo nitaoga na kujiweka vizuri kabla ya kuonekana na mtu yeyote.Tupite kwanza pale malaika tower nataka ukaninunulie mavazi .Nikishajiweka vizuri nitakueleza mahala ninakotaka unipeleke.” Akasema Anitha.Fernando akamfungua pingu na kumtaka ahamie kiti cha mbele

Walikwenda hadi Malaika tower ,jengo refu lenye maduka mengi ya nguo na urembo.Anitha akamuelekeza Fernando aina ya nguo anazozihitaji Fernando akatoka garini na kuingia ndani ya jengo lile kwa dhumuni la kumnunulia Anitha mavazi.Aliondoka na funguo za gari.Anitha akahamia katika kiti cha dereva na kwa kutumia chuma alichokipata mle garini akaipiga sehemu ya kuchomekea funguo ikapasuka akazivuta nyaya akazichuna na kuziunganisha zikatoa cheche na gari ikawaka ,akageuza na kuondoka.

Fernando alifanya manunuzi ya nguo na baadhi ya vitu ambavyo Anitha alivihitaji.Kisha maliza manunuzi akatoka na kuelekea eneo la megesho alikoegesha gari .Aliangaza huku na huko lakini gari lake hakuliona,akahisi kuanza kuchanganyikiwa.Akautupa mfuko aliokuwa ameushika na kuanza kukimbia kulizunguka jengo lile akilitafuta gari lake lakini hakulipata.Alihisi miguu yake inaisha nguvu akakaa katika maua. Aliwaza akatoe taarifa polisi juu ya upotevu ule wa gari lakini akaogopa,mara akapata wazo kwamba aende benki akahakiki kama ile fedha aliyotumiwa na Anitha imefika kweli kwani tayari alikwisha anza kuwa na wasi wasi.Alikodisha teksi iliyompeleka moja kwa moja hadi benki akaomba atazamiwe katika akaunti yake kama kuna fedha imeingia.Taarifa aliyopewa ilitaka kumpasua moyo.Hakukuwa na fedha yoyote iliyotuwa katika akaunti yake.Fernando alipingana na watu wale wa benki na kuwaeleza kwamba ametumiwa pesa kiasi cha shilingi milioni themanini.Aliwatajia jina la benki iliyomtumia fedha ile na wafanyakazi wa benki walifanya uchunguzi na baada ya nusu saa wakaja na jibu ambalo Fernando hakuwa amelitarajia.Hakukuwapo kokote duniani benki yenye jina lile .Hii ilikuwa ni njia mpya ya utapeli wa hali ya juu mno .Fernando aliishiwa nguvu akaanguka





“ Ahsante Mungu nimetoka salama katika mikono ya Yule mama mwenye roho ya kikatIli zaidi ya shetani.Endapo nisingefanikiwa kutoroka leo lazima angeniua.” Akawaza Anitha na kuuma meno kwa maumivu makali aliyoyahisi.



“ Bado nahisi maumivu makali ya mwili kutokana na mateso makali niliyoteswa.Ile sindano aliyonichoma Fernando ndiyo bado inanipa nguvu za kuweza hata kuendesha gari.Rosemary Mkozumi ni mtu katili sana .Inaonekana ni kawaida yake kuwatesa watu na ndiyo maana akajenga hadi chumba maalum kwa ajili ya kutesea watu.Mwanamke Yule ni hatari na hapaswi kabisa kuachwa huru.Ni hatari hata kwa taifa.Naapa sintafumba macho hadi nihakikishe Rosemary mkozumi amepatikana.Pamoja naye kuna huyu mwingine ambaye naye lazima apatikane kwa gharama zozote,jaji Elibariki.Tulimuamini mno na kuyaweka maisha yetu rehani kwa ajili yake lakini kumbe hakuwa mwenzetu.Tulikuwa tunakaa na nyoka ambaye ametugeuka na kutuuma wenyewe tuliomfuga.Ni vigumu sana kuamini lakini huo ndio ukweli jaji Elibariki ndiye aliyetusaliti na anashirikiana na Rosemary Mkozumi mtu ambaye anashirikiana na magaidi.!!Haikuwa kazi nyepesi kumkamata Rose lakini Elibariki amesahau hayo na akachagua kushirikiana naye.Sina hakika kama Mathew anafahamu kuwa ni Elibariki ambaye amesababisha haya yote yakatokea.Nina hakika bado hajafahamu kwa kuwa wakati matukio haya yote yanatokea yeye na Peniela hawakuwepo pale nyumbani.” Anitha akatolewa mawazoni na mlio wa simu.Simu ya Fernando ilikuwa inaita,akatabasamu.

“ Kumbe Yule mjinga alisahau simu garini.Mungu bado yuko upande wangu na sasa amenipa njia nyepesi ya kuwasiliana na Mathew.Ninakumbuka namba ya simu ya Mathew ambayo ilikuwa anaitumia usiku ule allipoondoka na Peniela”

Anitha akapunguza mwendo wa gari na kuegesha pembeni akaichukua ile simu na kuziandika namba za Mathew akapiga lakini simu ya Mathew haikuwa ikipatikana.Akapiga tena lakini jibu likawa lile lile,simu ya Mathew haikuwa ikipatikana.



“ Ni nadra sana kumpiga simu Mathew na kumkosa.Something is not right …nakumbuka usiku ule alinipigia simu kuna kitu alitaka kunieleza lakini Elibariki aliwahi kunipiga na kitu kichwani nikapoteza fahamu .Ngoja nielekee moja kwa moja nyumbani kwake yawezekana nikamkuta kule na yeye anaweza kuwa katika harakati za kunitafuta” akawaza Anitha na kuendelea na safari

Hakukuwa na msongamano mkubwa wa magari hivyo haikumchukua muda mrefu Anitha kuwasili katika mtaa ilipo nyumba ya Mathew lakini alikutana na mstuko mkubwa ambao hakuwahi kuupata katika maisha yake.Kulikuwa na uzio wa polisi na hakuruhusiwa mtu yeyote Yule kuingia mahala pale palipowekwa uzio.Ukuta imara uliokuwa umelizunguka jumba la Mathew ulikuwa umeanguka na ni sehemu ndogo tu iliyobaki imesimama.Jumba la kifahari lililozoeleka kuonekana hapa halikuwepo tena bali kuta zilizotapakaa moshi,majivu na masalia ya baadhi ya vifaa vilivyoungua moto.Anitha aliomba kitu alichokiona kiwe ni ndoto na si kweli lakini kadiri sekunde zilivyosonga akajikuta akiamini ile haikuwa ni ndoto bali ni kitu cha kweli kimetokea.Jumba la Mathew lilikuwa limeteketea kwa moto na hakukuwa na ktu hata kimoja kiichosalimika.Alihisi kuanza kuishiwa nguvu akaamua kuondoka eneo lile ili asije hisiwa kuwa ana mahusiano na Mathew.

“ kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nahisi akili yangu imefika mwisho wake wa kufikiri” akawaza Anitha baada ya kuondoka maeneo yale ya ilipokuwa nyumba ya Mathew



“ I real don’t know what to do.” Akaendelea kuwaza .

“ Mathew na peniela wako wapi? Are they still alive? nani kaichoma moto nyumba ya Mathew na kwa nini? akajiuliza maswali mengi bila majibu

“ Mathew cant be dead.He must be safe somewhere and I must find him.I must find him..!! akawaza

Aliendesha gari taratibu na kwa tahadhari kubwa hadi alipofika ufukweni mwa bahari.Alimshukuru Mungu kwa kumuwezesha kufika salama pale ufukweni kwani kichwa chake kilijaa mawazo mengi sana.Akainamia usukani huku akihisi nguvu kuanza kumuishia.Ghafla akakumbuka kitu Fulani haraka haraka akainua kichwa na kuchukua kompyuta ya Fernando Iliyokuwa mle garini

“ Nimekumbuka njia rahisi ya kumpata Mathew.Mimi na yeye tuliwahi kuwa na pete Fulani za kuvaa vidoleni lakini hizi hazikuwa pete za kawaida za urembo.Hizi zilikuwa ni vifaa maalum kwa ajili ya kufahamu mahala mwenzako alipo endapo itatokea hatari.Kuna programu maalum ya kuitafuta pete hiyo kwa kutumia satellite ambayo hutafuta mawimbi yanayotoka katika hiyo pete na moja kwa moja itakuonyesha mahala mwenzako alipo.Pete yangu mimi nilikwisha ipoteza muda mrefu lakini Mathew ya kwake bado anayo na hajaitoa bado kidoleni.Kwa vile kompyuta ya Fernando imeunganishwa na mtandao wa intaneti .” Anitha alihisi kupata nguvu ya ghafla akaanza kubonyeza kompyuta ile haraka haraka.Ilimchukua zaidi ya nusu saa mara akatoa ukulele wa furaha baada ya kukipata alichokuwa anakitafuta.Katika kompyuta kulionekana ramani ya jiji la Dare s salaam na sehemu Fulani ndani ya jiji hili kuliwa na mduara mwekundu akashusha pumzi.

“ Oh Thank you Lord.Nimempata Mathew.” Akasema na kuanza kulitafuta eneo lile lenye mduara mwekundu ni eneo gani akagundua kwamba ni Kigamboni karibu na bahari ya hindi.Hakutaka kupoteza muda akawasha gari na kuondoka kuifuata ramani ile



“ Ee Mungu nisaidie nimpate Mathew akiwa mzima” akaomba Anitha akiendelea na safari yake ya kuelekea Kigamboni mahala kulikoonyesha ndiko Mathew alikokuwa.Wakati anakaribia daraja la Nyerere akastuka baada ya kuona mduara ule mwekundu ukihama toka sehemu ulipokuwa.

“ He’s moving ” akasema na kusimamisha gari ili aweze kufuatilia ni wapi mduara ule ulielekea.

“ Inaonekana kama vile Mathew yuko garini kutokana na kasi hii ya mduara unavyokwenda.” Akawaza Anitha na kuanza kubonyeza tena kompyuta lakini intaneti ilikuwa inamsumbua sana



“ Please Lord help me find Mathew.Naona huu mtandao unataka kuniletea shida kwa wakati huu ambao tayari nimempata Mathew” akawaza na kuendelea kufuatilia muelekeo wa Mathew





*******







Toka ilipotimu saa mbili za asubuhi watu walianza kuwasili katika makazi binafsi ya rais uliko msiba wa Flaviana.Hadi ilipotimu saa tano za asubuhi tayari viongozi wengi wa chama na serikali walikwisha wasili.Hakukuwa na nafasi tena kwa watu kukaa kutokana na eneo lote kujaa watu.Nafasi chache zilikuwepo upande wa viongozi.Dr Joshua tayari alikwisha wasili na kilichokuwa kinasubiriwa ni mwili wa marehemu kuwasili kutoka hospitali ili shughuli zianze.

Hali ilikuwa ni ya simanzi kubwa .Kila aliyekuweo eneo hili alionekana kuwa na sura ya huzuni .Kwaya maalum ilikuwa inaimba nyimbo za maombolezo kuwafariji waombolezaji wakati wakiusubri mwili uwasili toka hospitali ulikoenda kuchukuliwa.

Dr Joshua akiwa amekaa katika hema la viongozi huku pembeni yake akiwepo rafiki yake mkubwa Dr Benedict Kinyanjui rais wa Kenya ,alifika mlinzi wake na kumpata kijikaratasi kidogo



“ Mzee huu ujumbe umetoka kwa Dr Kigomba” akasema Yule mlinzi na Dr Joshua akaikunjua karatasi ile akasoma kilichoandikwa .





“ Kuna mgeni anaitwa Donald mcNeel ametumwa na serikali ya Marekani ,kuna mambo muhimu anataka kuzungumza nawe leo baada ya shughuli za mazishi kumalizika”





Dr Joshua akarudia tena kuusoma ujumbe ule halafu akachukua kalamu na kuandika chini ya ujumbe ule na kumpa mlinzi aupeleke kwa Kigomba



“ Nitaonana naye leo saa mbili usiku katika nyumba yangu ya mapumziko kule ufukweni.Anza kufanya maandalizi” hivi ndivyo alivyojibu Dr Joshua



“ Huyu Donald mcNeel ni nani? Ametumwa nini kwangu? Nitafahamu nitakapoonana naye jioni ya leo .Baada ya kuonana naye nitakuwa na maongezi na Abel Mkokasule na baadae usiku huo huo natakiwa kwenda Dark house kwenda kuonana na Jessica nifahamu watu ambao anashirikiana nao.Nataka Abel amuhoji ili nifahamu ni nani aliyemtuma akamuokoe jaji Elibariki? Sitaki kuamini eti alifanya vile bila ya kutumwa au kushirikiana na mtu yeyote.Lazima kuna mtu au kikundi cha watu kiko nyuma yake.Nahisi kuna watu wengi tu wanaonisaliti ambao sijawafahamu bado.Katika usiku wa leo pia nataka vijana wa Abel wavamie nyumbani kwa Rosemary Mkozumi na wamchukue Yule msichana ambaye Rose anamshikilia ambaye ana taarifa za mahali alipo huyu mtu anaitwa Mathew.Huyu Mathew ni mtu ambaye natakiwa kutumia uwezo wangu wote hadi nihakikishe ninampat…” Ghafla Dr Joshua akastuliwa toka mawazoni baada ya Rosemary Mkozumi kuwasili pale msibani.Alikuwa anatembea taratibu huku ameambatana na walinzi wake watatu pamoja na msaidizi mmoja .Watu wote walielekeza macho yao kwake na wengine wakimuonea huruma kwa namna alivyokuwa anatembea kwani alionekana kuwa katika maumivu.Muongozaji shughuli akawatangazia wambolezaji kwamba tayari mwili wa marehemu umewasili na muda wowote utaingizwa pale uwanjani ili shughuli ianze.

“ Huyu shetani amekuja!! Akawaza Dr Joshua akikasirishwa na kitendo cha Rosemary Mkozumi kuwasili palemsibani

“ Najua kilichomleta hapa msibani.Kwanza anatafuta ukaribu na mimi vile vile anatafuta huruma ya watu.Huyu mwanamke hatari sana kwangu.Tayari anafahamu mambo yangu na anaonekana atakuwa kikwazo kikubwa katika kutekeleza mipango yangu.Japokuwa kwa kupitia kwake nimeweza kuwatambua wasaliti wangu lakini hata yeye mwenyewe bado ni hatari kwani mambo anayoyataka nimfanyie kama malipo ya kunisaidia kuwabaini wabaya wangu katu siwezi kuyatekeleza.Anataka nimgawie sehemu ya fedha zitakazopatikana kwa kuuza package.Hilo halitawezekana katu.Pesa ile sintogawana na mtu yeyote Yule.Vile vile anataka nimsaidie ili aweze kuteuliwa na chama chetu kuwa mgombea urais .Hilo katu haliwezekani .Mtu pekee ambaye ninamuandaa ili chama kimpitishe ni jaji Elibariki na hakuna mwingine.Kwa mantiki hiyo basi Rosemary Mkozumi ni jipu linalotakiwa kutumbuliwa haraka sana.Lazima nimuondoe haraka” akawaza Dr Joshua huku akiendelea kumtazama Rosemary Mkozumi kwa macho makali







******http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





Askofu Edmund Dawson aliondoka na akina Mathew bila ya kuongozana na mlinzi yeyote hadi katika nyumba Fulani ndogo lakini nzuri iliyokuwa na walinzi wawili .Ilikuwa ni nyumba nzuri iliyojengwa kwa ustadi mkubwa .Edmund akafungua mlango na kuwakaribisha ndani akina Mathew.Ilikuwa ni sebule ndogo lakini nzuri.

“ Karibuni sana Mathew na Peniela.Najua mtakuwa mnajiuliza kwa nini nimewaleta hapa.Hii ni nyumba yangu ya siri na ndiyo ninayotumia kama ofisi yangu ya siri.Chin sun hafahamu chochote kuhusu nyumba hii.Kila kitu changu cha siri kiko humu.Hata ninyi pia mnaweza kutumia ofisi hii pale mtakapohitaji.Humu kuna kila kifaa ambacho mnaweza mkakihitaji.” Akasema Edmund na kuwaacha Mathew na Peniela pale sebuleni akaelekea chumbani.Baada ya dakika kumi akarejea akiwa ma sanduku akaliweka mezani.

“ Nimewawekea kila kitu mnachokihitaji nani ya sanduku hili.Kuna silaha ndogo ndogo na vifaa vingine ambavyo naamini vitawasaidia .Hiki kisanduku kidogo ni mtambo wa mawasiliano ambao nadhani Mathew unaufahamu vyema namna ya kuutumia.Nimewapeni simu sita na kila moja ina namba mbili tofauti.Kwa ujumla karibu kila mlichokitaka kiko ndani ya sanduku hili” Akasema Edmund.Mathew akavikagua vitu vile halafu akalifunga sanduku



“ Ahsante sana Edmund kwa msaada huu mkubwa.Vifaa hivi ulivyotupa vitatusaidia sana katika kukamilisha operesheni yetu na kuhakikisha kwamba kile tulichokianza tunakimaliza na kirusi Aby kinapatikana na kuwekwa katika sehemu salama.Vifaa hivi vichache ulivyotupa vinakwenda kuiokoa Tanzania .Mwisho wa Dr Joshua na genge lake umekaribia” akasema Mathew

“ Mathew mimi na ninyi, sote tuko kitu kimoja kwa hiyo muda wowote mtakapohitaji msaada au kitu chochote kile mtawasiliana nami na nitahakikisha mnakipata.Kwa sasa tuondokeni nikawaonyeshe makazi yenu ili kazi ianze bila kuchelewa.” Akasema Edmund kisha wakangia garini wakaondoka

“ Naamini huko waliko hivi sasa Dr Joshua na wenzake wanasherehekea ushindi wakiamini kwamba wametumaliza nguvu kwa kitendo chao cha kuiteketeza nyumba yangu.They are totally wrong.Safari hii watanifahamu mimi ni nani.Jumba langu la thamani kubwa wameliteketeza ,watu wangu wa muhimu Anitha,jaji Elibariki mpaka sasa sifahamu mahala waliko” akawaza Mathew wakiwa garini wakielekea katika nyumba ambayo wataitumia kama makazi yao ya muda



Hatimaye wakawasili katika nyumba moja iliyozungushiwa ukuta wa rangi nyeupe.Edmund akatumia kifaa cha kufungulia geti kwa mbali na kulifungua geti wakaingia ndani

“ Mathew na Peniela haya ndiyo makazi yenu mapya ya muda.” Edmund akawaambia akina Mathew baada ya kushuka garini

“ Ni nyumba nzuri na usalama wake ni mkubwa sana.Mkiwa hapa mtaweza kufanya shughuli zenu zote kwa uhuru na mimi nitakuwa karibu nanyi kuhakisha kila kitu kinakwenda vizuri na operesheni yenu inafanikiwa.” Akasema Edmund na kuwatembeza katika sehemu zote za nyumba ile nzuri

“ Mtahitaji mtumishi wa kuwasaidia kazi za ndani? Akauliza Edmund wakiwa sebuleni baada ya kumaliza kuizunguka nyumba ile.

“ Hapana Edmund sisi wenyewe tunaweza kufanya kila kitu hatuhitaji mtumishi,isitoshe makazi haya ni kwa muda tu” akajibu Mathew



“ Sawa Mathew mimi na ninyi hatutakuwa tukionana mara kwa mara kwa sababu sitaki Chin sun ajue kuna kitu kinaendelea kati yetu.Bado sijakamilisha uchunguzi wangu kwa hiyo sitaki kuharibu mambo ila nitakuwa ninawasiliana nanyi mara kwa mara karibu kila siku kufahamu maendeleo yenu na kuwapeni msaada pale unapohitajika.Endapo kuna chochote nitakipata toka kwa Chinsun kuhusiana na Chang ling nitawataarifu mara moja” akasema Edmund



“ Edmund ahsante sana kwa msaada huu mkubwa uliotusaidia.Wewe endelea na kazi yako ya kumchunguza mkeo na endapo utapata lolote lile ambalo unaona linaweza kuwa na msaada kwetu usisite kutueleza tutalifanyia kazi.Tutawasiliana nawe mara kwa mara kukujulisha maendeleo yetu na kila pale tutakapokwama na kuhitaji msaada wako hatutasita kukutaarifu” akasema Mathew

Waliagana na Edmund ambaye alitakiwa kuongoza ibada jioni hiyo katika kanisa lake akaondoka

“ Mkono wa Mungu bado uko juu yetu na anatuelekeza njia ya kupita.Jana tumepoteza kila tulichokuwa nacho lakini leo kwa namna ya ajabu kabisa tuna kila kitu tunachokihitaji kwa ajili ya kuendeleza mapambanao yetu.” Akasema Mathew baada ya Edmund kuondoka.Peniela akainuka na kwenda kukaa karibuni na Mathew akamtazama machoni kwa sekunde kadhaa na kusema

“ Mathew”

“ Unasemaje Peniela?

“ Nina mengi ya kusema lakini kabla sijasema chochote kuna ktu naomba nikuulize na tafadhali namba unipe jibu la kweli”



“ Uliza Peniela” akasema Mathew



“ Do you trust me?

Mathew akamtazama na kusema

“ Yes I do”

“ How much do you trust me?



“ With my life”



“ Are you sure?

“ Yes I’m sure”



“ If you do trust me that much why you hide things and you don’t tell me the truth? Why you didn’t tell me about Edmund? Kwa nini hutaki kunieleza ni kitu gani mliongea na John Mwaulaya kule hospitali? Akauliza Peniela



“ Peniela ni kweli kuna mambo mengi ya msingi John alinieleza lakini huu si wakati wake kuyaongelea kwani bado tuna kazi kubwa iliyoko mbele yetu.Nitakueleza kila kitu hapo baadae lakini kwa sasa akili zetu naomba tuzielekeze kwanza katika mambo makubwa yanayotukabiili.Kwanza kulipata kasha ambalo John alikupa ili tujue ndani yake kuna nini ,pili tunatakiwa kuendelea na operesheni yetu ya kukinusuru kirusi Aby.Watu tunaopambana nao wana mbinu za kila aina katika kuhakikisha suala lao lifanikiwa na kwa muda huu mchache tuliopoteza toka jana usiku tayari watakuwa wamebuni mikakati mingine mikubwa ya kufanikisha lengo lao.Hatupaswi nasi kupoteza hata dakika moja .Wenzetu hatujui mahala waliko lakini hatupaswi kurudi nyuma wala kukata tamaa.Machungu na maumivu yetu ya kuwapoteza wenzetu tuyaelekeze katika kazi inayotukabili.Nakuahidi Peniela mara tu baada ya kumaliza sakata hili nitakueleza kila kitu nilichoongea na John Mwaulaya kwa hiyo basi naomba kwa sasa tupange namna ya ….” Mathew akanyamaza baada ya kengele ya getini kulia.Wakatazamana

“ Ngoja nikatazame katika ile luninga iliyounganishwa na kamera nani aliyeko getini kwa sababu hatutegemei mgeni yeyote na sina hakika kama atakuwa ni Edmund.” Akasema Mathew na kuelekea katika chumba kidogo kilichokuwa na mitambo yote ya usalama.Nyumba hii ilikuwa na kamera nne za ulinzi ambazo zote ziliunganishwa katika luninga moja kubwa .Mathew akaingia katika chumba kile na moja kwa moja akaelekeza macho katika kamera ya getini.Kulikuwa na mtu amesimama alikuwa ni mwanamke.Mathew akaivuta sura ya mwanake Yule ili afahamu ni nani.Ghafla akapatwa na mstuko mkubwa.Alichokiona kilimstua mno

“ Oh my God this is a miracle !!!!...Anitha !! akasema Mathew kwa mshangao



“ Is that real her?? Akajiuliza huku akimtazama tena kwa makini



“ Its her.Ni Anitha…She’s not dead.Amejuaje kama tuko hapa? Akajiuliza Mathew halafu akatoka mbio na kumfuata Peniela .

Kama ilivyomtokea Mathew ,ndivyo ilivyomtokea pia Peniela ,alistuka sana .Hakuamini alichokiona



“ Oh my Gosh ! This is a miracle..She’s alive !! akasema Peniela kwa furaha huku akiruka ruka.

“ What are you waiting Mathew? Go get her in” akasema Peniela.

“ Lazima tuchukue tahadhari .Yawezekana akawa anatumiwa na watu .We must be very carefull” akasema Mathew halafu akachukua bastora na kuelekea getini.Taratibu akafungua mlango mdogo wa geti na kuruka nje kama kima huku akielekeza bastora pande zote kujihami endapo kuna adui



“ Don’t shoot ! Its me Anitha” akasema Anitha



“ Anitha !! akasema Mathew baada ya kuhakikisha Anitha alikuwa peke yake



“ Mahew !! akasema Anitha wakakumbatiana kwa furaha.





“ Oh my angel you are back!! You are alive !! akasema Mathew.Anitha alikuwa anatokwa na machozi mengi ,alionekana mchovu na alikuwa na michubuko mingi iliyosababishwa na mateso aliyoyapata nyumbani kwa Rosemary Mkozumi.



“ What happened to you Anitha? Akauliza Mathew akimtazama Anitha .

“ Mathew fungua kwanza geti tuingie ndani tutaongea vizuri,” akasema Anitha na kwa haraka Mathew akafungua geti Anitha akaingiza gari ndani .Tayari Peniela alikwisha toka ndani na mara tu Anitha aliposhuka garini akamkumbatia kwa furaha kubwa huku wote wawili wakitokwa na machozi



Anitha akakaribishwa ndani na kabla ya yote Peniela akampeleka bafuni ambako alioga ,akasafishwa majeraha yoye aliyoyapata halafu akampeleka katika chumba apumzike.Mathew akaja na kisanduku kidogo cha dawa ambacho ni miongoni mwa vitu walivyopewa na askofu Edmund.Akakifungua na kuanza kumganga Anitha majeraha yake yote.Kisha mtibu majeraha yake akamchoma sindano huku Peniela akishangaa

“ Sikujua kama una taaluma ya mambo haya ya tiba” akasema .Mathew akatabasamu kidogo na kusema

“ Katika hizi kazi zetu lazima ufahamu mambo mengi na suala la tiba ni moja ya mambo ambayo lazima kuyafahamu.Kwa sasa tumuache Anitha apumzike twende jikoni tukaangalie kitu cha kumuandalia,she looks so weak.Huko alikokuwa sina hakika kama amekula hata chakula” akasema Mathew

“ No Mathew,we have to talk now.Mimi nimewapata ninyi sina wasi wasi tena.Nimepata nguvu kubwa” Akasema Antha



“ Anitha pumzika tutaongea baadae”

“ Hapana Mathew hatuwezi kusubiri.Something big is going on.I have to tell you whats going on”

Mathew na Peniela wakatazamana



“ Whats going on Anitha? What real happened? Where were you? Umefahamuje kama tuko hapa? Akauliza Mathew.Anitha akainuka na kuketi ,akafumba macho kidogo kwa maumivu makali akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Ni hadithi ya kusikitisha sana na kila kitu kilianzia usiku ule wewe na Peniela mlipoondoka kwenda nyumbani kwa Peniela.Nilikuwa peke yangu ofisini na mara akaja jaji Elibariki tukaongea kidogo akasema kwamba anakwenda kuniandalia kahawa,na muda huo huo ukanipigia simu na nilipopokea tu nikapigwa na kitu kizito nikapoteza fahamu” akanyamaza kidogo na kuendelea

“ Nilipozinduka nikajikuta katika chumba chenye giza na baadae nikafahamu kwamba pale ni nyumbani kwa Rosemary Mkozumi”

“ Rosemary Mkozumi??? Is she alive?akauliza Mathew kwa mshangao



“ Yes she’s alive.Rosemary alikuja katika chumba nilichokuwa nimefungwa akanitaka nimueleze mahala ulipo kama ninataka nibaki hai.Sikuwa tayari kufanya alivyotaka .Alimtuma mmoja wa walinzi wake akamlete mtu Fulani na sikuamini macho yangu nilipomuona mtu aliyeletwa ni jaji Elibariki”

“ Elibariki ??? !!..Mathew na Peniela wote wakauliza kwa mshangao mkubwa

“ Hata mimi nilishangaa sana kumuona Elibariki akishirikiana na Rosemary Mkozumi .Inaonekana walikuwa na makubaliano Fulani kwani Rose alimwambia Elibariki endapo anataka amuamini basi adhihirishe hilo kwa kunipiga risasi ,akapewa bastora akanilenga kichwani akaizinga lakini kumbe bastora ile haikuwa na risasi.Endapo bastora ile ingekuwa na risasi Elibariki alikuwa tayari kuniua. ” akasema Anitha kwa uchungu huku machozi yakimtoka.Peniela ambaye naye machozi yalikuwa yanamtoka akamsogelea Anitha akamfuta machozi .

“ This is unbelievable ..Elibariki ??? Akasema Mathew .Anitha akaendelea

“ Elibariki alitusaliti na akaamua kushirikiana na Rosemary mkozumi” akasema Anitha



“ Baada ya hapo nikaingizwa katika chumba cha mateso”

“ Ndani ya jumba la Rose kuna chumba cha kutesea watu?

“ Ndiyo Mathew.That house is like hell .Kuna chumba cha mateso ambacho kina kila kifaa cha kutesea.Vile vile kuna mtu maalum ambaye kazi yake ni kutesa watu anaitwa Fernando.Walinitesa mno wakitaka niwaonyeshe mahala ulipo lakini sikuthubutu kufungua mdomo wangu.” Akasema Anitha akanyamaza kidogo kisha akaendelea

“ Leo asubuhi niliingizwa tena katika chumba cha kutesea ,wakanitesa mno hadi nikalazimika kujifanya nimepoteza fahamu lakini bado Rosemary Mkozumi hakuridhika akamwambia Fernando aendelee kunitesa hadi nitakaposema Mathew yuko wapi.Baadae Fernando alinifuata akanieleza kwamba alitaka kunifahamu mimi ni nani.Alionekana kunionea huruma .Nilipomtazama niligundua ni mtu mwepesi kushawishika.Nilitumia mbinu ya kumshawishi kwa fedha na akakubali .Nilimwambia atafute kompyuta iliyounganishwa na intanet akaniletea na nikaitumia teknolojia ya benki bandia kumuhamishia fedha katika akaunti na akaamini baada ya kupokea ujumbe uliomtaarifu kwamba kiasi cha fedha kimetumwa katika akaunti yake.Fernando aliridhika akanitorosha .Baada ya kutoka katika makazi ya Rose nilimulekeza tuelekee katika duka la mavazi akanichagulie mavazi .Wakati akiwa dukani nikatokomea na gari lake” akasema Anitha



“ Dah ! pole sana Anitha” akasema Mathew



“ Ahsante Mathew” akajibu Anitha.Ukimya mfupi ukapita halafu akaendelea.

“ Nilikwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwako na kukutana na kitu cha kusikitisha .Hakukuwa na nyumba tena bali majivu.Nyumba ilikuwa imeteketea .Nimewakuta polisi wakifanya uchunguzi wao.Nilichanganyikiwa nikashindwa nifanye nini nikaondoka.Baadae nikapata wazo nikazikumbuka zile pete tulizowahi kuwa nazo.Mimi yangu ilipotea lakini wewe bado unayo

" Mathew akastuka na kutazama vidoleni.Ni kweli katika mkono wake wa kulia alikuwa na pete kubwa ya dhahabu .Anitha akatabasamu



“ Kwa kutumia kompyuta ya Fernando iliyokuwamo mle garini nilianza kuitafuta pete hiyo kwa kutumia satellite na nikafanikiwa kuipata.Kwanza niliiona maeneo ya Kigamboni na baadae ikaondoka nikaendelea kuifuatilia hadi ikafika hapa.Teknolojia imefanikisha tumeweza kuonana tena japo haikuwa rahisi kutokana na intaneti kuwa na kasi ndogo mno”



“ Pole sana Anitha” akasema Peniela

“ Ahsante Penny.Hiyo ndiyo hali halisi ilivyokuwa.Hayo ndiyo mambo yaliyonikuta.Mtu ambaye tulimuamini na kuyaweka rehani maisha yetu kwa ajili yake ametugeuka na kutusaliti.” akasema Anitha.

Mathew alihisi mwili unamtetemeka kwa hasira alizokuwa nazo.Hakuweza kuongea chochote akabaki amejiinamia akiwaza



“ Mathew say something” akasema Peniela



“ I don’t know what to say.Hizi ni taarifa mbaya mno ambazo sikuwa nimetegemea kuzisikia.Sikutegemea kabisa mtu kama Elibariki angeweza kutufanyia sisi kitu kama hiki.Nilimuamini kupita kiasi na ndiyo maana nimestuka sana kusikia kitu alichokifanya.” Akasema Mathew na kuzama katika mawazo mengi

“ Kwa nini jaji Elibariki afanye jambo kama hili? Ni yeye aliyetuomba tufanye kazi yake ya kumtafuta muuaji wa Edson kwa nini basi abadilike na kutufanyia hivi? Nakosa majibu ya maswali haya kwani Elibariki anafahamu ni kitu gani kinachoendelea na kitu gani tunachokipigania,kibaya zaidi amediriki kumuachia huru na kushirikiana na Rosemary Mkozumi ambaye anafahamu wazi kuwa anashirikiana na magaidi.Kwa nini Elibariki????? Akajiuliza Mathew huu mwili ukizidi kuchemka kwa hasira.



“ Kwa upande wenu nini kilitokea? Imekuwaje hadi mkafika hapa? Hii nyumba ya nani? Akauliza Anitha



“ Usiku ule” akasema Mathew

“ Tulikwenda kwa Peniela ambako aliwasiliana na Dr Joshua kisha tukaanza safari ya kurudi .Sikutaka Peniela abaki peke yake pale nyumbani kwake nikamtaka turudi wote nyumbani kwangu,Tukiwa njiani ukatutaarfu kwamba kuna simu ya Peniela .Aliyempigia simu ni kijana mmoja anaitwa Josh ambaye alikuwa mlinzi wa John Mwaulaya.Josh alimtahadharisha Peniela kwamba kuna watu wa Team SC41 wametuwa kumfuatilia kwa hiyo achukue tahadhari.Ni kweli tuligundua kwamba kuna watu walikuwa wanatufuatilia na hapo ndipo mapambano makali yakatokea.Tulipambana sana tukafanikiwa kuwaponyoka wale jamaa waliokuwa wamejiandaa kwa lengo la kumpata Peniela.Nahisi tayari walikuwa na wasi wasi na nyendo zake na ndiyo maana walianza kumfuatilia. Nilikuwa nimejeruhiwa kwa risasi hivyo tukataka kurejea nyumbani kwa Peniela nikatibu jeraha lililokuwa linatoa damu nyingi lakini tulipofika tukakuta moto mkubwa unaiteketeza nyumba ya Peniela .Mpaka sasa hautujui nani alifanya kitendo kile lakini tunahisi lazima watakuwa ni team SC41.Ilitulazimu kuomba msaada toka kwa Jason tukaelekea hadi nyumbani kwangu ambako nako tulikuta tukio kama tulilolikuta kwa Peniela.Nyumba yangu ilikuwa inateketea kwa moto.Hatukuwa na namna nyingine ya kufanya ikanilazimu kumtafuta askofu Edmund Dawson” akanyamaza kidogo halafu akaendeleahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Kabla ya kifo chake ,John Mwaulaya alizungumza nami.Nyote mnafahamu kwamba mimi na John Mwaulaya ni maadui wakubwa kutokana na kitukibaya alichonifanyia na nilikubali kwenda kuonana naye kwa sababu ya Peniela.Katika muda mfupi tulioongea alinileza mambo kadhaa mazito ambayo nitawaeleza hapo mbeleni lakini kubwa zaidi alinitaka kwa gharama zozote zile nimlinde Peniela na nihakikshe namfikisha kwa askofu Edmund Dawson.Alinipa namba za siri za kuwasiliana na Edmund na alinitaka niwasiliane naye mara tu nitakapokamilisha zoezi la kukipata kirusi Aby.Alinisisitiza kwamba kwa gharama yoyote ile lazima nihakikishe ninakipata kirusi Aby.Alinionya nisikubali katu kirusi kile kiingie mikononi mwa team Team SC41 au kwa watu ambao wanataka kukinunua toka kwa Dr Joshua kwani litakuwa ni angamizo la dunia.Niliamua kuwasiliana na Edmund mapema kabla hata ya kulikamilisha zoezi lile la kukipata kirusi Aby kwa sababu hatukuwa na namna nyingine ya kufanya na tulihitaji msaada .Edmund Dawson anafanya kazi na shirika la ujasusi la Marekani C.I.A na yuko hapa nchini kwa kazi maalum ya kumchunguza Chin sun ambaye ni mke wake. Edmund na John Mwaulaya walikuwa ni marafki wakubwa na wa siri,na ndiye aliyetusaidia kila tulichokihitaji pamoja na nyumba .Kwa ufupi hicho ndicho kilichotokea kwa upande wetu .Namshukuru sana Mungu ametukutanisha tena Anitha.Nilichanganyikiwa na sikujua ningekuliliaje endapo ungekuwa mepoteza maisha.Ouh Anitha give a big hug !! ” akasema Mathew na kukumbatiana na Anitha kwa furaha,Peniela naye akaungana nao wakakumbatiana wote .



“ Kwa hiyo kitu gani kinachoendelea hivi sasa ? akauliza Anitha.

“ Bado kazi yetu ya msingi ni kuhakikisha tunakipata kirusi Aby.Kwa vyovyote itakavyokuwa ni lazima tuhakikishe tumekipata kirusi hicho.John Mwaulaya alinisisitiza mno jambo hili.Viongozi wakuu wa Team SC41 wanataka kukipata kirusi hicho kwa ajili ya kukiachia hapa Tanzania.”



“ Tanzania ?? akasema Peniela kwa mshangao



“ Ndiyo wanataka kukitumia nchini Tanzania”



Peniela na Anitha wakatazamana.Taarifa zile ziliwastua sana,Mathew akaendelea



“ Wakati wakifanya utafiti wa mafuta na gesi katika kina kirefu cha bahari,watafiti wa kampuni ya mafuta na gesi ya Solenergy ya Marekani waligundua uwepo wa madini aina ya Gramonite ambayo ni madini yenye thamani kubwa kuliko madini mengine yote tunayoyafahamu .Baada ya ugunduzi huo kampuni hiyo haikutaka kutoa taarifa za uwepo wa madini hayo kwa serikali ya Tanzania na mpaka leo hii serikali ya Tanzania haifahamu chochote kuhusu uwepo wa madini hayo ya thamani kubwa chini ya bahari.Taarifa hizi ziliwasilishwa kwa siri kwa serikali ya Marekani nao wakaanza mikakati itakayowawezesha kuyapata madini hayo.Njia pekee na rahisi ambayo wangeweza kuitumia na ambayo imefanikiwa sehemu nyingi afrika ni kwa kuanzisha migogoro ya ndani ya nchi.Walianza kuwatumia wanasiasa ili wapandikize chuki miongoni kwa watanzania na kuchochea machafuko lakini njia hiyo ilishindwa japokuwa nchi ilitikisika.Walijaribu kutumia njia ya kupandikiza chuki za dini lakini pia njia hii haikufanikiwa na ndipo walipoikabidhi kazi hiyo kwa team SC41 ili waweze kukipata kirusi hicho na kukisambaza kwa lengo la kusababisha maangamizi makubwa.Wakati nchi ikiwa katika taharuki wao watakuja kama wafadhili na wakati huo huo kuchimba na kuondoka na kiasi kikubwa kama si chote cha madini.Huu ni mpango wa siri kubwa sana na John mwaulaya ni miongoni mwa watu wachache sana waliobahatika kuufahamu na ndiyo maana akanisisitiza kwamba tuhakikshe Team SC41 hawakipati kirusi hicho.Endapo tutashindwa na team Sc41 wakafanikiwa kukipata nchi yetu itashuhudia maangamizi makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa.Kila nyumba itakuwa na msiba na hakutakuwa na wa kumzika mwenzake.Maelfu kwa maelfu ya watu watateketea ndani ya muda mfupi kwa hiyo ndugu zangu tuna jukumu zito la kuhakikisha tunakipata kirusi hicho kwa gharama zozote zile.Tunatakiwa kuja na mikakati mizito ya namna ya kukipata kirusi hicho kabla Dr Joshua hajakikabidhi kwa Hussen ambaye ndiye mnunuzi na tayari amekwisha fika kwa ajili ya kukichukua “ Mathew akawatazama wanawake wale wawili ambao nyuso zao zilionyesha woga mkubwa.

“ Mara ya mwisho” akaendelea Mathew

“ Taarifa iliyokuwa mezani kwetu ni kwamba siku ya leo yatafanyika makabidhiano ya kirusi Aby na Dr Kigomba ndiye anayetakiwa kumkabidhi Hussein kirusi hicho kwa hiyo basi mtu pekee ambaye anaweza akatukuongoza katika kukipata kirusi hicho ni Dr Kigomba.Kama mtakumbuka tayari simu yake ilikuwa imeunganishwa katika mifumo yetu na vile vile tulimpa saa ambayo nayo iliunganishwa na mifumo yetu na tulikuwa na uwezo wa kufuatilia na kujua kila mahala aliko lakini kwa kuwa kila kitu kiliteketea Anitha una jukumu la kurudisha tena mifumo yote iliyopotea na tuanze tena kumfuatilia Kigomba.Hilo linawezekana? ” Akauliza Mathew

“ Ndiyo inawezekana Mathew lakini tunahitaji kupata kompyuta mpya yenye uwezo mkubwa na kasi.Kompyuta hii ya Fernando haitaweza kumudu program zile kwani uwezo wake ni mdogo.”

“ Ok hilo halina shaka.Tutapata kompyuta hiyo.Itatulazimu kwenda katika maduka yanayouza kompyuta pamoja na kufanya manunuzi ya vitu vingine ambavyo tutavihitaji humu ndani.Mimi na Peniela tutakwenda na wewe Anitha utabaki hapa unapumzika.Usihofu hapa ni sehemu salama”

“ Mathew are you sure you are going to be safe out there? Akauliza Anitha kwa wasi wasi

“ Usihofu Anitha,I’ll be fine” akasema Mathew



Anitha akampa orodha ya vitu ambavyo anavihitaji halafu Mathew na Peniela wakaingia katika mojawapo ya magari yaliyokuwapo hapo wakaondoka kuelekea madukani kufanya manunuzi

“ Bado naona ni kama muujiza kuonana tena na Anitha.Sikutegemea kabisa” akasema Mathew wakiwa garini.



“ Hata mimi sikutegemea kabisa.Nilijua lazima wote waliteketea kwa moto.Lakini kuna mtu mmoja ambaye Anitha hajatueleza yuko wapi ? Naomi.Naye alikuwemo mle ndani usiku ule.Where is she?

“ Nina hakika lazima Rosemary alimchukua.Simuhofii Naomi bali jaji Elibariki.Yule alikuwa nasi toka awali na anafahamu kila tulichokipanga.Kama ameamua kutusaliti na kumfungua Rosemary Mkozumi basi hatasita kuanika mipango yetu yote .Kitu ambacho nashindwa kupata jibu lake ni kitu gani kimembadilisha Elibariki ghafla namna hii na kumshawishi afanye hivi alivyofanya? Kwa nini atufanyie hivi wakati huu ambao tumekaribia kabisa kufanikisha operesheni yetu? Kuna jambo gani baya tumemkosea akaamua kututenda hivi? Where is he now? Akasema Mathew

“ Kweli nimeamini kikulacho ki nguoni mwako.Angetufanyia hivi mtu mwingine ningeweza kumsamehe lakini Elibarki !!! I’ll never forgive him.Tulimchukulia ni mwenzetu kumbe ni chui katika kundi la kondoo.Noah rafiki yangu alipoteza maisha wakati akimuokoa asiuawe lakini yote haya ameyasahau.” akasema Mathew kwa hasira



“ Kokote aliko lazima nihakikishe ninamsaka na kumpata.hata kama si leo wala kesho lakini nitamsaka hadi siku ninaondoka katika dunia hii.Kwa sasa amekuwa ni adui yangu mkubwa .Usalti alioufanya ni mkubwa mno na hauvumiliki hata kidogo. Ameifanya kazi yetu kuwa ngumu zaidi.Kutokana na jambo aliolifanya jaji elibariki hatuwezi tena kuendelea na mipango yetu ya awali kwani hatujui lengo la kutufanyia hivi ni nini:” akasema Mathew



“ Unashauri tufanye nini Mathew? Akauliza Peniela aliyekuwa katika usukani.Mathew akainama akazama mawazoni.

“ Unawaza nini Mathew? Akauliza Peniela .Bado Mathew aliendelea kuinama na hakujibu chochote.Safari ikaendelea kimya kimya.Kichwa cha Mathew kilijaa mawazo mengi



“ Lazima anafikiria kitu kikubwa sana.Ngoja nimuache aendelee kuumiza kichwa ili kufikiri kitu tutakachokifanya kwani sisi sote tunamtazama yeye” akawaza peniela





“Kwa heri mwanangu.Hukustahili kufa kifo hiki na wala hayakuwa mategemeo yangu kukupoteza.Najua mimi ndiyo sababu ya kifo chako so forgive me my daughter.I’ll akways miss you” Dr Joshua aliyatamka maneno haya kimya kimya wakati akiuaga mwili wa mwanae Flaviana.Aliumia mno kumuona mwanae aliyempenda sana akiwa ndani ya jeneza kana kwamba amelala usingizi.Baada ya Dr Joshua akafuata mume wa marehemu ambaye ni jaji Elibariki halafu Anna mdogo wake Flaviana.Baada ya familia kumaliza wakafuata ndugu wengine halafu vongozi wa kitaifa na mwisho ikawa zamu ya waombolezaji wengine.Wakati zoezi la kutoa heshima za mwisho likiendelea Dr Kigomba alikuwa katika heka heka nyingi.Hakutulia sehemu moja.Alijitenga mbali kidogo sehemu kusiko na watu akanogea na simu kwa muda mrefu na baada ya kumaliza kuongea na simu ile alionekana kutokuwa katika hali ya kawaida.Haraka haraka akaelekea katika gari lake na kumtaka dereva wake ampe funguo akaondoka peke yake.Baada ya kuyaacha makazi ya Dr Joshua akasimamisha gari pembeni na kuvuta pumzi ndefu



“ Damn you Joshua.Naapa nitakuonyesha kwamba kuna watu wana akili zaidi yako.!! Akawaza Dr Kigomba akiwa amefura kwa hasira.Akachukua simu na kumpigia Jacob Kateka mkuu wa idara ya usalama wa taifa



“ Hallow Kigomba.Kuna habari gani? akauliza Joseph



“ Joseph that man is a devil!!

“ Amefanya nini tena? Akauliza Jacob



“ Nimetoka kuzungumza na ile benki ambako fedha za mauzo ya kirusi Aby ziliwekwa na nimeambiwa kwamba tayari zimeondolewa na kuwekwa katika akaunti mpya ambayo hawako tayari kuniambia ni ya nani.Nimechanganyikiwa Joseph kwani mpaka hapa tayari Dr Joshua amenizidi ujanja” akasema

“ So what are we going to do Kigomba? Kama fedha hazipo tena ,ina maanisha kwamba hakuna sababu ya sisi kuendelea na mipango yetu kwani dhumuni kuu lilikuwa ni kuzipata fedha hizo”



“ Usiogope Joseph.Bado tutaendelea na mipango yetu.Tunachotakiwa kukifanya ni kuipata hiyo package na ili tuipate lazima tumfuatilie Abel Mkokasule ambaye ndiye anayefanya kazi ni rais kwa sasa na nina hakika atamtumia yeye kuipeleka hiyo package kwa Hussein ” akasema Kigomba na ukimya mfupo ukapita

“ Joseph are you there? Akauliza Dr Kigomba

“ Yes Kigomba.Where are you now?

“ Kwa sasa nimetoka msibani kuna kazi nimepewa na Dr Joshua ninakwenda kuitekeleza.Nitaonana nawe leo saa mbili usiku ili tuongee zaidi” akasema Dr Kigomba na kukata simu



“ Dah ! huu ndio ule wakati ambao rafiki yako mkubwa hugeuka adui mkubwa.Dr Joshua tayari ametengeneza uadui mkubwa kati yetu.Naapa nitamuonyesha mimi ni nani.Hatafanikiwa kamwe katika mipango yake” akawaza Dr Kigomba akawasha gari na kuondoka







*******





Mathew na Peniela walifanikiwa kurejea salama katika makazi yao mapya wakitokea madukani kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali walivyovihitaji.Katika nyumba ile kulikuwa na chumba cha maktaba ambacho walikiteua kuwa kama ofisi yao .Pamoja na maumivu aliyokuwa nayo Anitha ,aliungana na wenzake katika kuandaa ofisi .Bila kupoteza muda akaanza kuandaa kompyuta ambayo Mathew na Peniela waliinunua ,ilikuwa ni kompyuta nzuri ambayo Anitha aliihitaji.Baada ya kuhakikisha kila kitu kiko sawa akaanza kazi.Mathew na Peniela wakabaki kimya wakimtazama Anitha aliyekuwa anacheza na kompyuta .Baada ya dakika kumi akatabasamu na kusema

“ Nimefanikiwa kuirejesha ile program yetu lakini simu ya Dr Kigomba inaonekana imezimwa na hakuna simu yoyote iliyoingia au kutoka toka jana saa saba za usiku” akasema Anitha



“ This is weird .Kigomba ni mtu wa karibu mno na rais na si rahisi kuizima simu yake kwani ndiyo anayoitumia kwa mawasiliano ya kikazi..Something is not right” akasema Peniela



“ It is simple.Tayari wanafahamu mipango yetu yote.Elibariki !! ..oh my gosh !! akasema Mathew kwa hasira

“ Are you sure it’s him? Anatafutwa na jeshi la polisi kwa kusababisa kifo anawezaje kushirikiana tena na akina Kigomba watu ambao wanamtafuta usiku na mchana? Akasema Anitha



“ Tayari nimepata picha kamili kwa nini Elibariki aliamua kutufanyia vile alivyofanya.He wanted back his normal life and the only way to get back his freedom is to face his enemies na njia pekee ambayo ingemuwezesha kupokelewa na maadui zake na kukubaliwa ni kwa kuwaeleza ukweli wa kila kitu tunachokipanga dhidi yao. Na ndiyo maana wameweza kugundua kuhusu simu ya Dr Kigomba kuunganishwa na mfumo wetu unaotuwezesha kusikia maongezi yake yote “ akasema Mathew.Anitha na Peniela wakatazamana.




ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog