Search This Blog

Thursday 23 March 2023

HUJUMA NZITO - 4

  

Simulizi : Hujuma Nzito

Sehemu Ya : Nne (4)

Kwanza Kachero Manu alivyomuona tu Van-Dubbe taswira yake ikamjia moja kwa moja ndio ile maiti iliyozikwa kule Kijijini Kwembe. Mwili wake Van-Dubbe na mwili wa anayedhaniwa ni marehemu Dr.Chilembwa ulifanana sana.

"Huyu ni Mrakibu wa Polisi Makao Makuu Bwana Samson Komba, namjua fika tumeshakutana nae vikao vingi vya utendaji, kumbe ni mshenzi namna hii ameungana na wahalifu, kuzipiga shoka mali za serikali!" alijikuta Kachero Manu anaropoka kwa kujisahau kuwa pale amejitambulisha ni Mwandishi wa habari wa kujitegemea.

Alikuwa amepigwa na butwaa haamini kama kigogo mzito kama Samson Komba kuja kushiriki kumpoteza kichaa Van-Dubbe. Bahati nzuri, Mr.Bhatti alikuwa ameitwa dukani mara moja na mtumishi wake hivyo hakutilia maanani maneno ya Kachero Manu.

Huyo Mrakibu wa Polisi Bwana Samson Komba ndio kule kwenye genge la "Nyasa Empire Supporters" (NES) ndio akijulikana kama "Chew Master", Afisa Mkuu wa mambo yote ya Ulinzi. Ghafla bin vuu...Mhindi akarejea kwa kasi pale walipokaa Kachero Manu na rafiki yake huku anahema kwa uoga, kama vile amepatwa na kihoro.

"Mtaani kuna vijana fanya fujo navunja maduka naiba bidhaa nataka funge duka haraka sije filisi mtaji wangu, samahani sana" alizungumza huku anatetemeka.

"Bila samahani ahsante sana kwa ushirikiano wako, tunaomba anuani za wale ndugu zake Van-Dubbe kama unazo..!" Alizungumza Kachero Manu huku akiwa na furaha sheshe ya kupata taarifa muhimu alizokuwa anazihitaji sana.

Mr.Bhatti Akaanza kupekua kwa haraka haraka kwenye mafaili yake yaliyohifadhiwa kwenye mtoto wa meza, huku vidole vyake vinamtetemeka kwa hofu ya kukutwa na waandamanaji. Punde tu akakiona anachokisaka, kisha akachomoa kikaratasi fulani akampa Kachero Manu.

Akakipokea kikaratasi hicho na kukipitia kwa haraka haraka kisha akakisunda mfukoni mwake. Wakaelekezwa na Mr.Bhatti watokee mlango wa uwani, tayari duka lilishabugazwa na mtumishi wake kutokana na kuhofia vurugu zilizoanza kushamiri kwa kasi mitaani.

Walipofanikiwa kuwa kwenye eneo salama, wakaamua kugawana majukumu ya kazi kwa mkupuo hakuna tena kupiga ubwete kutokana na muda kwenda sana.
Kachero Manu akabeba jukumu la kufuatilia majibu ya vinasaba (DNA) vya mwili wa Marehemu Dr.Pius Chilembwa kwenye ofisi za "DNA Diagnostics Centre" (DDC), huku Dr.Edson Nkube akienda kufuatilia gari alilopata nalo ajali ya moto Dr. Chilembwa kujua mmiliki wake ni nani.

Walikubaliana kama majibu ya DNA yatakuwa ni tofauti na vipimo vya DNA ya Dr. Chilembwa, itabidi Kachero Manu aelekee kitongoji cha Soweto kwa wazazi wa Van-Dubbe ili awalainishe wakubali kupima kipimo cha DNA.
Kama DNA zao zitaowana na kipimo cha DNA ya sampuli aliyokuja nayo Kachero Manu, basi itathibitika pasina kuacha mashaka kuwa Van-Dubbe ndio maiti iliyozikwa kisanii kama Dr.Chilembwa.

SURA YA TISA

Bwana Molefe Thobakgale anasakwa na Dr.Nkube

Dr.Nkube alikuwa ndio kwanza anaegesha gari yake katika ofisi za kampuni ya kukodisha magari ya "Avis-Car Rental" iliyopo Jijini Johanesburg. Katika video za CCTV walizoziona dukani kwa mhindi, Mr.Bhatti walionekana baadhi ya watu walioambatana na majinuni Van-Dubbe wakiwa wamekodisha gari yenye pleti ya kampuni hiyo.

Lakini kama hiyo haitoshi, Dr.Nkube kwa kutumia watu wake wa intelijinsia waliomo ndani ya jeshi la polisi Jijini Johanesburg wakampatia taarifa nzima ya aina ya gari lililotumiwa na Dr Pius Chilembwa wakati anapata ajali na pleti namba zake.

Kupitia kwenye mtandao wa usajili wa magari nchini Afrika ya Kusini, alitafuta mmiliki wa gari hiyo mpaka akajua kuwa linamilikiwa na kampuni ile ya Avis, tawi la Santon, Jijini Johanesburg. Ndipo kiguu na njia akafanya maamuzi ya kwenda kumfanyia mahojiano mmiliki huyo wa kampuni ya magari ili kuweza kuunganisha nukta ya matukio haya mtawalia.

Aliposhuka tu kwenye gari kitu cha kwanza macho yake yakatua kwenye kidonda chake mkononi, majira yalikuwa yanasoma saa 7:05 adhuhuri, ikiwa ni saa mbili tokea wameachana na sahibu wake wa chanda na pete, Kachero Manu.

Akafanya haraka kupita geti la walinzi ambapo alisainishwa katika kitabu cha wageni. Akaandikisha taarifa za uwongo kuanzia jina lake mpaka namba ya kitambulisho chake. Baada ya kumaliza taratibu hizo za awali hapo getini akaruhusiwa kupita. Kwenye uwanja ule wa wazi wa pale kwenye kampuni kulikuwa na magari zaidi 100 ya kifahari, ya anuwai mbalimbali yakiwa yameegeshwa uwanjani yakisubiria wateja.

Akatembea umbali mfupi kama wa meta 10 akakutana na mlango mkubwa ambapo kulikuwa na mlinzi mwingine ambaye alimkagua tena kwa mara ya pili kuhakikisha haingii na silaha ofisini. Kwa bahati nzuri bastola yake alikuwa ameamua kuiacha kwenye gari lake.

Akaruhusiwa kuingia ndani ya ofisi hiyo ya wakala wa kampuni ya Avis. Baada ya kujieleza nia na madhumuni ya ziara yake kwa Katibu Muhtasi wa ofisi.
Akapewa maelekezo ya kutulia kitini, Mkurugenzi amekwenda kutekeleza ibada ya sala ya adhuhuri. Akitoka kuabudu ana mkutano kwa njia ya mtandao na wadau wake wa kibiashara kisha baada ya hapo ndio atakuwa huru ofisini kwake.




Mkurugenzi wa Ofisi hiyo ya wakala Bwana Jamaly Ashrafy alikuwa ni mtu wa khamsa salati kipindi hakimbanduki msikitini. Swaumu za sunnah za Jumatatu na Alhamisi zilikuwa hazimkosi.

Dr.Nkube aliamua iwe isiwe, iwe mvua iwe jua lazima aonane na Bwana Ashrafy hivyo akakata shauri kumsubiria.

Baada ya kupita kama saa tatu, Bwana Jamaly akawa amesharejea Ofisini kwake. Alikuwa amevalia kanzu nyeupe kama theluji haina hata nukta ya doa la uchafu. Kichwani alikuwa amevalia balaghashia mufti kabisa yenye rangi ya kahawia ya kufumwa kwa mkono.

Miguuni alivalia makubazi ya rangi ya kaki yenye kuachia sehemu kubwa ya miguu yake. Mkononi alikuwa amekamatia tasbihi yake, vidole vyake vina kazi kubwa ya kuchezesha kete za tasbihi katika harakati za kumsabihi Mola wake.

"Karibu kitini Bwana Edson jisikie upo huru, samahani kwa kukuchelewesha, maana nimeambiwa upo muda mrefu sana ila ndio majukumu tena" alifungua maongezi baina yao baada ya kumkaribisha mgeni wake ofisini mwake.

Bwana Jamaly Ashrafy alikuwa na asili ya Tanzania Visiwani, aliyezamia nchini Afrika ya Kusini akiwa ghulamu mdogo tokea alipomaliza kidato cha nne katika sekondari ya Fidel Castro iliyopo kule Zanzibari. Tokea hapo baada ya kula msoto mitaani kwa kujishughulisha na kazi mbalimbali za sulubu, mwishowe ndipo akaibukia kwenye mafanikio kama wakala wa kampuni ya Avis.

Sasa maisha yake yalikuwa pambe sana, alichomoka kwenye kundi la Walalahoi na kuingia kundi la Walalaheri, chambilecho mchumia juani hulia kivulini. Mahojiano ya kirafiki zaidi baina yao yakaanza rasmi baada ya kuwa tayari alishajitambulisha hapo mwanzoni.

Dr.Nkube: "Kama nilivyojitambulisha kwako mwanzoni kuwa natokea chombo cha habari cha "SABC" ujio wangu ni kupeleleza juu ya tukio zima la gari yenu aina ya "Rolls-Royce Phantom" kupata ajali ya moto na kusababisha kifo cha Mkurugenzi wa fedha wa Benki Kuu ya Tanzania Dr.Pius Chilembwa" akaweka kituo kidogo cha maongezi yake, akameza mate kidogo, kisha akaendelea na mazungumzo yake. "Kwanza nikupeni pole kwa hasara mlioipata, lakini ningependa kufahamu Dr.Chilembwa alikodisha mwenyewe gari kwenu au kuna muwakilishi wake alikuja kwenu?"

Bwana Jamaly: "Ahsante sana tumepoa, hakuja mwenyewe, tuliyemkodisha gari ni mwingine kabisa!"

Dr.Nkube: "Unaweza kunipatia jina lake na anuani yake huyo aliyekodisha kwenu? "

Bwana Jamaly: "Hamna shida utapata" alijibu huku ameshika kasa ya kompyuta yake ya mezani anafungua faili lenye kumbukumbu za wanaokodisha magari kwao. Dr.Nkube aligundua kitu toka kwa Bwana Jamaly Ashrafy, viganja vyake vya mikono vilikuwa vinatetema kwa uoga, kuonyesha sio mzoefu wa mahojiano.

Bwana Jamaly: "Huyu hapa aliyekodisha gari yetu..! " alisema huku anamkabidhi Dr Nkube karatasi iliyodurufiwa kwenye printa ndogo ya mule ofisini. Kisha mahojiano yakaendelea kwa muda mrefu, Bwana Jamaly alikuwa anafunguka tu bila mficho.

Dr.Nkube: "OK..Ahsante sana", akaipokea na kuiperuzi kwa umakini mkubwa ile karatasi kisha akaikunja na kuisweka kwenye dayari yake ndogo ya mkononi.

Mahojiano yakaendelea tena kwa muda mchache mpaka yakafika ukingoni.
Alichogundua Dr Nkube kwa haraka haraka ni kuwa Bwana Jamaly Ashrafy alikuwa mweupe kabisa hajui chochote katika njama za washirika wa "Nyasa Empire Supporters" (NES). Kila alichoulizwa kwa anachokijua alikuwa anaropoka tu bila breki wala konakona.

Ila alichokuwa hakijui Dr Nkube ni kuwa Katibu Muhtasi wa Bwana Jamaly alikuwa ni kibaraka wa "Nyasa Empire Supporters" (NES), akilipwa ngwenje za kutosha kila mwezi kwa ajili ya kuchunguza usalama wao dhidi ya vyombo vya dola.

Alipewa vifaa maalumu vya kurekodi kila mahojiano anayoyafanya Bwana Jamaly Ashrafy na watu atakaowahisi kuwa ni wapelelezi, kisha anayatuma kwa njia ya mtandao hayo mahojiano kwa waliomtuma wakayafanyie uchambuzi.

Dr.Nkube wakaagana salama salimini wakiwa wameongea vya kutosha. Akasindikizwa mpaka mlangoni kisha Bwana Jamaly akafunga ofisi yake na kumuacha Dr.Nkube aende zake, kila mmoja akishika hamsini zake.

"Tafadhali naomba kitambulisho chako niweke rekodi za wageni waliokuja kutembelea ofisini, nimesahau pale mwanzoni, samahani sana" alijieleza yule Katibu Muhtasi huku akiwa amesimama kwenye kiti chake na kusogelea dirisha la kioo katika ofisi yake ile iliyozungushiwa vioo tupu tayari kwa kupokea hicho kitambulisho.

"Bila samahani!" alijibu kwa ufupi na kumkabidhi kitambulisho hicho yule dada kwa kutumia mkono wake wa kulia baada ya kukichomoa toka kwenye pochi yake anayoitumia kuhifadhia pesa na vitambulisho mbalimbali. Alipokiskani tu akamrudishia kwa haraka na kuagana naye kwa mara ya pili kwa uso wenye bashasha mpwitompwito.

Katibu Muhtasi yule alikuwa anamuangalia Dr Nkube kwa sura ya kebehi alivyompa tu mgongo, akijua fika hana maisha marefu mbele yake kutoka sasa. Alikuwa hajui kiswahili vizuri ila kitendo cha mazungumzo yao kutaja namba za gari lile alilofia Dr.Pius Chilembwa alihisi moja moja huyu ni mpelelezi katika kesi hiyo. Hivyo alijua taarifa ya uwepo wa huyu mtu ofisini kwao itagombewa kama peremende ikifika kunako wanaomtumia.

Dr.Nkube akatoka nje ya jengo, majira ya magharibi ilishatimu kutokana na nuru ya jua angani kuanza kufifia kutokana na ghurubi ya jua hilo huku kiza taratibu kikianza kulivamia anga katika pande zake zote nne. Akawa anajongea kuelekea mahali alipoegesha gari yake ili apate kuondoka mahali hapo akaendelea na harakati zake nyingine.

Dr.Nkube akaangalia simu yake kama ametumiwa arafa yoyote na muhibu wake Kachero Manu, akakuta hamna ujumbe wowote aliotumiwa wala kupigiwa simu. Akafungua mlango wa gari yake kisha akaingia ndani. Bila kuchelewa akawasha na kutimkia zake mitaani akishika baraste ya kuelekea kitongoji cha "South Western Townships" maarufu kwa jina la ufupisho la Soweto.

Hii sasa ilikuwa ni lala salama kwao hakuna kulala tena kwenye samadari mpaka kieleweke. Wanatwanga kotekote, Kachero Yasmine bado anakaba beki Jijini Dar es Salaam wakati Kachero Manu na sahibu wake Dr.Edson Nkube wanashambulia mahasimu wao wa "Nyasa Empire Supporters" (NES) wakitokea Jijini Johanesburg.

Aliwasili mtaa anaoukusudia majira ya usiku mbichi ukiwa umetimu, kiza kimetanda kimtindo. Mbalamwezi pekee ilikuwa inajitahidi kuangaza lakini ilizidiwa na kiza hicho. Nia na madhumuni ya ujio wake katika kitongoji hicho cha Soweto ilikuwa ni kuja mtaa wa Vilakazi.

Huo ulikuwa moja ya mitaa yenye heshima sana nchini Afrika ya Kusini na duniani kwa ujumla. Umaarufu wake mtaa huu unatokana na kuwa ni mtaa uliotoa washindi wawili wa Tuzo ya Amani ya Nobeli, nao ni Mheshimiwa Nelson Rolihlahla Mandela na Askofu Desmond Tutu.

Pia maeneo jirani na mtaa huo, kipindi cha harakati za ukombozi dhidi ya Makaburu, ghulamu wa miaka 13, Hector Pieterson alipigwa risasi na kufa hapo hapo na askari wa Makaburu na kusababisha machafuko makubwa ya Juni 16, 1976.

Dr.Nkube aliegesha gari yake nje ya Klabu moja maarufu ya starehe. Aliposhuka nje ya gari tu, akachomoa simu yake ya kiganjani toka kwenye mfuko wa suruali yake ya dangirizi iliyombeba vilivyo. Akaanza kumtafuta hewani Kachero Manu, ili afanye nae mawasiliano muhimu ya kikazi. Majibu yaliyokuja upande wa pili ni kuwa simu ya Kachero Manu haipatikani, ajaribu tena baadae.

Kwa bahati mbaya sana bila kukusudia kikaratasi kidogo kilichokuwa kimekunjwa na kuwekwa mfukoni kilikuwa kimemdondoka chini bila kufahamu wakati anatoa simu mfukoni.

Lengo lake la kumpigia simu alikuwa anataka afahamu Kachero Manu yupo maeneo gani hapa Soweto ili kama amemaliza majukumu yake anayatekeleza, waende pamoja anapokusudia kwenda. Akarudisha simu yake mfukoni na kupiga moyo konde kuwa ataenda peke yake kwenye nyumba hiyo anayoikusudia kwenda.




Nikupongeze sana kwa hatua ya upelelezi uliyoifikia mpaka sasa, ulibaki kidogo tu ungegusa kichwa chenyewe. Haya geuka nyuma tukupe zawadi yako ya kazi nzuri ukaisimulie huko jongomeo unakoelekea hivi punde tu" alipewa amri ya kuwapa mgongo akiwa tayari ameshavuliwa viatu, shati lake na sarawili yake amebaki na nguo ya ndani tu. Dr.Nkube hakutaka afe kirahisi kama mgonjwa kiharusi kitandani. Alijipanga lazima apambane nao.


Ghafla bin vuu..Dr.Nkube akasikia sauti ya kulalamika maumivu ya mmoja wa wale maadui. Hakutaka kulaza damu tena, akajirusha pembeni kwa nguvu kuchupia kitanda kama kipa anayechupia mpira kwenye lango lake. Alipotua juu ya godoro kutupa macho na yule adui yake mwingine nae yupo chali chini anagaragara maumivu makali anayoyasikia.


Haraka haraka akaamka pale kitandani na kushuka chini ya kitanda huku akiwa haamini kama kilichotokea ni uhalisia au ni muujiza. Akiwa bado anashangaa mle chumbani hajui ni muujiza gani umetokea akastukia mlango unapigwa teke na Kachero Manu anaingia na mkononi ameshika bastola yake inayofuka moshi yenye kiwambo cha kuzuia sauti.

"Asante Komredi, umeniokoa na kifo chupuchupu" alishukuru Dr.Nkube, huku akishusha pumzi ndefu, wakikumbatiana na Kachero Manu. "Usijali nimelipa kisasi cha wewe ulivyoniokoa kule "New Salama Lodge" kwa kumtuma yule kijana wako" alijibu Kachero Manu huku wote wanaangusha kicheko.


Wakafanya upekuzi wa haraka haraka nyumba nzima, hawakupata chochote kitakachowaisaidia. Kwenye upekuzi wa moja ya ile maiti wakakuta kivuli cha kitambulisho feki cha uanahabari cha Dr.Nkube kile alichompa Katibu Muhtasi wa Bwana Jamaly Ashrafy na kukiskani. Hapo hapo Dr.Nkube akang'amua aliuzwa na yule dada kwa maadui zake.


Ikabidi wote watoke ndani ya nyumba ile haraka haraka kabla hawajafikwa na matatizo toka vyombo vya dola. Wakatembea takribani kama mwendo wa dakika 10 hivi mpaka wakaifikia gari yao. Wakiwa kwenye gari wanarejea ndipo kila mmoja akaanza kumuelezea mwenzake hatua aliyofikia ya kazi tokea walipoachana majira ya dhuha, asubuhi.


Alianza Dr.Nkube kuelezea kuwa hapo Soweto pale alipokuja kuokolewa, alimfuata marehemu Molefe Thobakgale ambaye ndio kutokana na taarifa ya wakala wa Avis, Bwana Jamaly Ashrafy, alikodisha gari lililopata ajali ya moto iliyomuua anayesadikiwa kuwa ni Dr.Pius Chilembwa. Dr.Nkube baada ya kumaliza simulizi yake akashikwa na hamu sasa ya kujua Kachero Manu alinusaje mpaka kujua yeye yupo kwenye hatari ya kupoteza uhai wake.


Kachero Manu Alimhabarisha kuwa walipoachana alifanikiwa kuja Soweto na kumshawishi mama mzazi wa kichaa Van-Dubbe kwenda kupima DNA katika taasisi ya "DNA Diagnostics Centre" (DDC) ambapo majibu watayapata kesho yake. Hivyo akamrudisha nyumbani kwake majira ya jioni kwa kutumia gari la kukodi.


Wakati anataka kuondoka Soweto akaamua arudi mashimashi bila gari kutokana na umati wa washabiki wa mpira waliofurika mitaani. Katika tembea yake ndipo akalikuta gari lao limeegeshwa Klabu. Akadhania labda Dr.Nkube atakuwa Klabu anapata moja moto moja baridi, kumbe Lahasha wa kalla! hakuwepo.
Akashikwa na hofu kidogo na kuanza kulizungukia gari kuangalia usalama wake, ndipo akaokota kikaratasi chini ya ardhi kina anuani ya hapo alipomfumania.

Akaiwasha simu yake aliyokuwa ameizima muda mrefu na kukuta kuna ujumbe wake kuwa mara mbili mtawalia alitafutwa hewani na Dr.Nkube. Akaanza kupigia simu yake kumtafuta bila majibu yoyote, ndipo akaamua kuzitii hisia zake zilizomuelekeza amfuate kwenye nyumba ile ya mshukiwa wake.


Kwa bahati nzuri akamkuta amebananishwa almanusura wainyakue roho ya rafiki yake. "Vipi sasa majibu ya DNA ya mwili unaodhaniwa kuwa ni wa marehemu Dr Pius Chilembwa, majibu yake mbona umeyaficha huyaweki hadharani" Dr Nkube uzalendo ulimshinda aliona rafiki yake anakwepesha kwenye kiini cha upelelezi wao.


"Oooh...Sorry...nilipitiwa habari njema ni kuwa "DNA Disgnostics Centre" (DDC) wamethibitisha pasina kuacha mashaka ya kuwa ile sampuli niliyokuja nayo sio mwili wa Dr Chilembwa" aliongea Kachero Manu huku uso wake umebeba tabasamu kunjufu la ushindi.
"Kwa munasaba huo ninathibitisha pasina kuacha mashaka kuwa Dr.Pius Chilembwa yupo hai, ni jukumu letu sasa kumsaka kwa udi na uvumba popote alipo ajibu kesi yake ya kula njama na kukwapua mabilioni ya pesa za mabenki yaliyokuwa chini yake.

Majibu ya kesho ya DNA toka kwa mama mzazi wa Kichaa Van-Dubbe yatatupa picha halisi ya kuwa kule Tanzania tumezika mwili wa Mwendawazimu Van-Dubbe aliyetekwa na kuuliwa kwa makusudi kwenye ajali ya moto iliyotokea nchini Afrika ya Kusini".


Baada ya kama nusu saa ya msafara wao wakafika nyumbani kwa Dr.Nkube huku wakijipongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya siku ya leo kila mmoja kwa kadri ya uwezo wake. Kachero Manu alipanga kesho kutwa yake arudi nchini Tanzania akamuongezee nguvu Kachero Yasmine kuwatia mbaroni wahusika wote.



"Mtume weeeeeeh.....!! Mtume weeeeeeh..!! Dada unaniua dada nimekoma dadaaaah....Weeh dadaaaah.... Sirudii tenaaaaa...Mama weeeeeh Mama weeeeh...Ooooh Oooh...Nakufaaaaa... Nakufaaaa...!! " yalikuwa ni sehemu tu maneno yaliyoambatana na kilio cha mayowe chenye majonzi na maumivu makali sana yasiyoelezeka.

Alikuwa ni Mohammed Mtoni huyo akipokea mateso ya kuzimu wakati bado yupo hai duniani. Mateso yote hayo muasisi wake ni Kachero Yasmine. Alikuwa amemvua nguo zake, kisha amemtundika kwenye bomba lenye umbo la mstatili kama goli la uwanja wa mpira. Alimfunga kwa kamba kichwa chini miguu juu, huku mikono yote imefungwa pingu, hafurukuti.


Kisha akamchanja na wembe mgongo wake wote, baada ya hapo akampaka pilipili na chumvi. Kisha akaanza kumchapa mgongoni na mkia wa samaki taa, mkia ambao ulikuwa na sifa ya kupasua ngozi vilivyo.


Kachero Yasmine masikioni alikuwa anasikiliza muziki kwa kutumia vifaa maalumu hivyo hakuwa anasikia vilio vya mateso ya "Muddy Comp". Alimpa kila aina ya mateso kwa muda wa saa tatu mfululizo mpaka akawa hatamaniki.

Baada ya hapo akamfungua kamba zote na kumuacha chini anatwetwa kama mbwa koko aliyefukuzwa maili nyingi. "Sasa upo tayari kujibu yale maswali yangu uliyonijibu kifedhuli mwanzoni au nirudie tena dozi?" alikuwa anazungumza Yasmine huku anatabasamu utsema hana mfuko wa uzazi kwa jinsi alivyokosa huruma.

"Dadaa nitasema kila kitu sitaki matatizo mimi tena. Kwanza Shikamoo watu wa usalama popote mlipo..!!" alikuwa ameshachanganyikiwa hataki matatizo tena. Alishajua huyu mwanamke ni hatari sana sura yake na matendo yake ni mbingu na ardhi.

"Eeh...ulikuwa unapewa kazi gani na Nathanieli wa Benki Kuu mpaka unalipwa pesa sufufu namna ile kupitia kwenye kwenye akaunti ya "JUAKALI GENERAL SUPPLIES"?" aliuliza swali la kwanza na Kachero Yasmine huku amejiandaa kumrekodi majibu atakayopewa kwa kutumia simu yake ya mkononi.

"Kazi ilikuwa ni kufoji saini ya Gavana kuidhinisha pesa zinapelekwa nje ya nchi nchini Afrika ya Kusini kupitia nyaraka mbalimbali anazoniletea" alijibu kiufasaha bila kupindisha maneno wala kuleta usani wowote.

"Mlikuwa mnakutania wapi kupeana hizo kazi?" alichomekewa swali la pili. "Alikuwa ananichukua kutoka kijiweni Mkwepu kisha napelekwa kwenye Hoteli za kifahari tofauti tofauti kuifanya hiyo kazi kwa utulivu".

Aliendelea kujieleza huku sasa ameanza kuwa na amani anajua usalama wake umepatikana."Unalo lolote la ziada ungependa serikali yako ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walijue kwenye sakata hili? " aliuliza swali la mwisho kwa siku hiyo Kachero Yasmine.

"Ninalo dadaa ninaloo...kuna mwenzangu mmoja anakaa Sinza sipakumbuki vilivyo aliponitajia, yeye pia anatengeneza ATM-kadi za kuchukulia pesa, sasa kuna siku tulikuwa Hotelini wote, yeye anafyatua ATM kadi mimi nipo kwenye kazi yangu ya saini" aliongea huku analia kwa uchungu akitaka na huyo mwenzake asakwe pia nae apitie suluba kama alizopitia yeye.

"Huyo unayemtaja nafahamu hadithi yake na habari yake usiku huu inaishia usihofu, sasa wewe utapumzishwa jela maalumu kwa ajili ya usalama wako na pia una kesi ya kujibu ya uhujumu uchumi na kula njama za kutaka kuiangusha serikali iliyopo madarakani.

Subiri wenzako mkamilike utaenda kujitetea mbele ya Pilato mimi sina mamlaka ya kukuachia huru au kukutia hatiani" alipomaliza maelezo hayo Kachero Yasmine akaanza kupiga simu kitengo maalumu waje kumchukua Mohammed Mtoni, akaunganishwe na wenzake waliokamatwa asubuhi wale wa "JUAKALI GENERAL SUPPLIES".

"Muddy Comp" alishaanza kuishiwa nguvu alikuwa amelala tu chini, mwili umevimba utasema mwanamasumbi aliyeshindwa kufua dafu ulingoni anasubiri machela tu impeleke hospitalini. Haukupita muda mrefu sana gari maalumu likaja kumbeba ili limkimbize hospitali kisha akipata nafuu akahifadhiwe sehemu salama mpaka kesi yake itakapopelekwa mahakamani.

Kachero Yasmine alipanga alasiri yake aelekee nyumba Namba 29-Sinza-Mori akashughulike na hayawani mwingine, mshirika mkuu wa "Nyasa Empire Supporters" (NES), Bwana Newton Temba.
,
Ilikuwa ni majira ya Alasiri tulivu, adhana ya Allahu-Akbar Allahu-Akbar ikitolewa msikitini, ile inayowataka waislamu swalihina waende kuabudu Mola wao. Kachero Yasmine alasiri hiyo ilimkuta yupo mitaa ya Sinza, saluni ya kike ya kutengeneza nywele. Saluni hiyo ilikuwa katika moja ya jengo refu la roshani moja la kibiashara, lililokatwa fremu nyingi za biashara mbalimbali.

"Hivi kwanini mwenye kiwanja cha mbele yenu asingetafuta mwekezaji amtolee matoleo kama ghorofa hili apige pesa ndefu, hiyo nyumba haivutii kwa kweli" alichokonoa mazungumzo Kachero Yasmine na dada aliyekuwa anamsuka nywele zake. Kama ujuavyo saluni ndio vijiwe vya umbea kwa akina mama. Ukitaka habari motomoto za Mjini nenda kwenye saluni.

Kachero Yasmine alikuwa anaitazama nyumba ambayo anahisi ni namba 29 hapo maeneo ya Sinza Mori. Lakini cha kustaajabisha nyumba hiyo ilikuwa haina kibao chochote ila ya mbele yake ikisoma namba 30 na ya nyuma yake inasoma namba 28, hivyo hiyo kwa vyovyote hisia zilimtuma itakuwa ni namba 29.

Pia nyumba hiyo kimtazamo wa nje haikufanania na hadhi ya huyo mtu anayemtafuta. Mmoja wa watuhumiwa wakuu wa kundi la "Nyasa Empire Supporters" (NES) kama Man-Temba asingeweza kuwa maskani yake ni hapo, ndio maana akaamua aingie hapo saluni huenda akaibuka na umbea wa kuhusu hiyo nyumba.

Mawazoni kabla hajawasili eneo hilo la tukio, alitegemea kuona kumeshushwa mjengo wa adabu, ofisi zenye kupulizwa na viyoyozi na vikorombwezo kedekede vya kustarehesha, tofauti na nyumba mbavu za mbwa aliyoikuta.

"Babu mwenye nyumba anaishi Kibada huko kashaisusa. Madaraka yote kamuachia kichaa mmoja muokota makopo anaitwa Temba na hii ndio mida yake ya kurejea, utamuona hivi punde, anapita kulaanika juani mchana kutwa kuokota makopo" aliongea yule msusi huku akiwa analainisha nywele za Kachero Yasmine kwa mafuta ya nazi na kuanza kupasua njia katikati ya nywele kwa kutumia chanuo la mti wa mpingo.

"Sista Anita usidanganyike mjini shule yule wala sio kichaa ana akili zake timamu wala hazijadaathari, anajifanyisha uzumbwani tu" alidakia mazungumzo mmoja wa wahudumu wa ile saluni ambaye alikuwa anamfumua mteja mwingine rasta. Wajihi wake yule dada ukionyesha kabisa kukerwa na tabia za Man-Temba.

"Kuna siku alikuja dada wa Baba Aika, huyo Mzee Mwakibete wa hilo duka la nguo, alikuja kuosha nywele hapa, kipindi unamuuguza mama yako Muhimbili, mhhh aliongea mambo mengi ya huyu mwehu wetu Temba" akasimamisha mazungumzo wakati anahangaikia kuwasha mashine ya kukaushia nywele aliyoenda kuichomeka ukutani kwenye swichi.

Kachero Yasmine alitulia kimya kama zuzu hata kutikisika hataki, anasikiliza kwa umakini maelezo.
"Basi dada yake mama Aika akasema huyu Temba anamjua fika, kwanza alishtuka kumuona yupo Jijini Dar es Salaam, huko Mbeya wanajua amekufa. Akatusimulia ya kuwa ameshawahi kukamatwa kesi ya wizi wa pesa za kigeni enzi zile iliyovuma sana ya Kasusura.

Alituambia inasemekana huyu ndio alichora ramani yote ya wizi ule uliotikisa nchi ila Mahakama haikumkumkuta na hatia ikamuachia huru. Akazidi kutupasha kuwa utapeli wake alijifunza Naijeria alikokaa miaka mingi sana huko. Mtu mwenyewe huyooo anarudi ha.. ha... ha.. hatari kweli!" wamama wote wa mule saluni wakageuza shingo zao kama feni.

Walikodoka kumuangalia Man-Temba akiwa na mabuti yake ya mvua huku juu amevalia koti la mvua, nywele vuruvuru, amechafuka mavumbi mwili mzima utasema kichaa kwelikweli. Akaanza kuvua shati lake lenye viraka kochokocho na kulitupia pembeni na kukiacha wazi kidari chake kilichojengeka mithili ya mataruma ya reli.

"Ila naweza kuanza kuamini kwa mbali lisemwalo lipo. Anachonishangaza kila siku utamkuta na majarida na magazeti ya lugha ya Kiingereza. Pia kuna siku alikisahau kidaftari chake hapo barazani tukakuta amerekodi bei za manunuzi ya fedha za kigeni kwa kila siku kwenye mabenki mbalimbali, sasa huyo kichaa gani kweli anapenda kujua mambo hayo ya Maafisa..!" Anita alionyesha kukubaliana na dhana ya msaidizi wake kuhusiana na Man-Temba.

Baada ya muda mle saluni, mada ikabadilika sasa zikarudi zile mada zao pendwa za umbea na upashikuna.
Sifa za umbea hakuzipenda, akabaki yupo nao kimwili lakini rohoni anapanga mipango ya mbinu mbalimbali za kumvamia Man-Temba kwenye nyumba yake ya madongo poromoka.

Akili yake ilikuwa haikubali kuwa Babu mmiliki wa nyumba hiyo iliyopo ndani ya kitongoji cha Sinza, Jijini Dar es Salaam akubali tu kiubwete ubwete kichaa akae tu bila malipo yoyote. "Lazima atakuwa analipwa pesa ndefu sana na wahalifu wanaojificha hapo" aliwaza Kachero Yasmine.




Ilipofika majira ya magharibi akiwa tayari kashamaliza kusukwa nywele zake na msusi, akalipia pesa na kuagana nao kwa bashasha. Akarejea kwa miguu hadi kwenye kituo cha mafuta cha Big-Bon alipoomba kuegesha gari yake.


Akalichukua na kuelekea maeneo ya Afrikasana, Hongera Bar kupata nyama choma safi maana tumbo lake lilikuwa linadai haki yake ya kupata maakuli.
Hapo palikuwa ni moja ya maeneo ya kula bata kwa wakazi wengi wa Sinza na vitongoji vya jirani.

Palikuwa usiku huo mbichi pameshaanza kuchangamka kwa wateja kuanza kujazana eneo hilo. Kwa bahati alipoegesha tu gari akaanza kugombaniwa kama mpira wa kona na wahudumu zaidi ya watatu kila mmoja akimtaka ampe huduma kutoka kwenye jiko analolisimamia.

Kachero Yasmine hakuwajali akawa anatabasamu tu huku anatembea kusaka meza huru, kwa bahati akaketi alipopachagua. Mhudumu mmoja wapo akasogelea na kuchukua oda yake aliyoiagiza. Macho yake yalikuwa yanaangalia usalama wa gari yake na alikuwa anashuhudia mubashara magari yanavyotembea kama kinyonga eneo hilo lenye msongamano wa magari hasa kuanzia magharibi na kuendelea.


Ghafla bin vuu wakati analetewa nyama choma yake aliyoiagiza kwa ugali, akamuona hasimu wake Man Temba anakuja kwa kasi anakimbia kuelekea yalipoegeshwa magari. Kisha alipofika kwenye gari la Kachero Yasmine akasimama kidogo na kuanza kulichunguza kwa umakini sana. Akaanza kulizunguka kama askari wa barabarani anavyolikagua gari lenye makosa.


Kachero Yasmine akawa ameganda bado hajaanza kula chakula chake anajishauri kama atoke pale alipo na kumfuata au asubirie aone mwisho wake ni nini haswa. Man Temba Akachomoa kidaftari chake na kuanza kuandika pleti namba za gari kisha alipomaliza akaitia mfukoni na kuelekea moja kwa moja kwa kasi jikoni wanapouza vyakula.


"Dada yangu asikutie presha ni mwehu yule, ndio kawaida kufanya vibweka kila leo!" mhudumu alimtoa hofu Yasmine baada ya kumuona mteja wake aliyemuandalia maakuli amesusa kula kabisa anaangalia gari lake linavyochezewa shere na Man-Temba.

"OK..kama hivyo sawa maana nikijua ni mkora anataka kuchomoa kifaa kwenye gari ila anaigiza uchizi tu..!" alimjibu huku mkono wa kulia wa Yasmine ukianza na Bismillahi kwenye sahani ile ya kuku kwa kunyofoa kipande cha firigisi ya kuku.

"Yule tumemzoea sana hapa, ndio muda wake huu, hapo nae ataagiza kuku wa kienyeji mzima, akitoka hapo ataingia kaunta ya vinywaji atainuka na chupa yake ya Hennessy, huyooo anatimua zake" akazidi kumtoa mashaka Yasmine, mhudumu yule.

"Oooh..Waaooh.. sasa nina amani ya moyo, anapata wapi hizo pesa zote za kunywa pombe ya bei aghali kama Hennessy?" Yasmine akajifanya ni buda akichokoza mjadala ule ili azidi kuvuna taarifa zaidi za hasimu wake Man-Temba.

"Hilo hata sisi linatufikirisha sana, maana hata wale madadapoa wanaojiuza miili yao, huwa siku akiwafuata hapa, wanapigana kumgombania na uchafu wake vilevile alivyo. Wenyewe wanamuita gari la mishahara limekuja wanasema anawalipa vizuri sana kwa huduma wanayotoa kwake.

Changudoa mmoja anasema kuna siku wakati yupo nae mfukoni mwake zilidondoka ATM kadi kama 10 za benki tofauti tofauti. Pia Kuna mteja wetu mmoja ni mfanyakazi wa benki anakuja sana hapa kula, anasema huyu ana rafiki zake wapo nchini Afrika ya Kusini huenda ndio wanaomuwezesha kipesa. Hivyo hapa mjini kila mtu anaishi kwa mtindo wake" akamalizia mazungumzo yule dada huku akiomba udhuru wa kujitoa na maongezi yale akahudumie wateja wengine waliokuwa sasa wameshajazana furifuri kwenye eneo hilo.


Ndani ya robo saa tu kuku mzima wa kienyeji na posheni ya ugali ikawa imeshasambaratisha pale mezani kwa Kachero Yasmine. "Dada yangu hongera sana, Mungu akuzidishie hamu ya kula unajua siku amini kama utamaliza kuku yule" alijisemesha mhudumu yule mbele ya Kachero Yasmine, wakati anaondosha vyombo mezani, akiwa hayaamini macho baada ya kuona sahani imepambwa na mifupa tupu.

"Ha ha ha... Hivyo ulijua utaambulia kitu muwauzie wateja wengine eeh..leo nimekukomesha. Maana sehemu zingine nyie wahudumu Mungu awasamehe tu, maana unaagiza kuku mzima, lakini unaletewa kuku kwenye sahani ana shingo tatu, mpaka unajiuliza huyu jogoo alikuwa na vichwa vitatu nini" alijibu mapigo ya utani ule Kachero Yasmine wote wakajikuta wanakufa kicheko.

"Ni ukweli uyasemayo dada yangu watu hatufanani, wanachofanya ukiagiza kuku mzima kama akikuona umelewa anachomoa shingo anaficha kwenye mfuko wa nguo yake. Akija mteja mwingine anakwapua bawa. Hivyo hivyo wanakwapua mpaka na yeye anakuwa ana kuku mzima yupo mfukoni mwake. Sasa akija mteja wa kuku mzima haendi jikoni tena anauza yule wa vipande vipande alivyokwapua kwa wateja.

Sasa akijichanganya ndio hapo anapokuletea jogoo wa vichwa vitatu ha ha ha ha" alisema huku anapokea pesa yake yenye bahashishi ya huduma nzuri ndani yake kisha Kachero Yasmine akaondoka zake eneo lile na kuelekea maeneo ya "Mlimani City Mall" kutulizana kwanza.


Alitaka afanye uvamizi eneo lile analoishi Man-Temba manane ya usiku. Lakini pia alitaka aombe ofisini kwao atumiwe kwa haraka kesi ya Kasusura ambayo inasemekana Man-Temba ndio alikuwa fundi mkuu wa tukio zima. Alishtushwa sana kuona mtu hatari kama Man Temba yupo uraiani anashiriki kuhujumu uchumi wa nchi kwa mara ya pili mfululizo.

Alipofika "Mlimani City Mall" na kuegesha gari yake hakutoka nje ya gari. Alichofanya ni kuchomeka kifaa aina ya modemu kwenye kompyuta mpakato yake ili kuunganisha mtandao. Alipofanikiwa kupata mtandao haraka haraka akatuma ujumbe ofisini kwao kwa Katibu Muhtasi wao Kokunawa. Kwa bahati nzuri Kokunawa muda huo wa saa 3:15 usiku mbichi alikuwa bado yupo, ofisini hivyo akaahidi kumtumia faili aliloliomba ndani ya nusu saa.

Wakati analisubiria faili hilo litumwe akashuka chini ya gari lake akafungua droo ya upande wa siti ya abiria, akachomoa paketi la sigara. Lilikuwa paketi la sigara aina ya 'Vogue', moja ya sigara ambazo ni gharama ya juu duniani. Kampuni hii ya sigara ilikuwa pia inatengeneza sigara maalumu kwa ajili ya watumiaji wanawake, kama 'Vogue Superslims' na 'Vogue Superslims Menthol'.


Kachero Yasmine alikuwa ni mvutaji wa mara moja moja sana, kwa muda wa miezi mitatu anaweza kuvuta kwa mkupuo sigara hata kumi kutuliza alosto yake. Mara nyingi sana akiwa kichwani kuna jambo linamsumbua na hajaweza kulikamilisha bado ndipo anapopatwa na alosto ya matumizi ya sigara zake pendwa za Vogue.

Akachomoa sigara za kutosha toka kwenye paketi lake, na kurudisha bunda lililobaki kwenye droo, kisha akaibusha moto. Akaanza bandika bandua ya kulichafua anga kwa moshi wa sigara akipingana na mkataba wa Kyoto wa mwaka 1997 unaokataza uchafuzi wa mazingira, huku anazunguka kwenye bustani ya pale "Mlimani City Mall". Tahamaki akajikuta kashateketeza fegi miche kama minane.


Akachomoa peremende kadhaa kutoka kwenye mfuko wa suruali ya dangirizi yake na kuanza kuzimung'unya ili kuupa mdomo wake riha ya kuvutia. Baada ya hapo akarejea kwenye gari na kuwasha tena kompyuta yake kuangalia kwenye barua pepe yake nyaraka aliyoiomba kwa Katibu Muhtasi wao.

Kwa bahati nzuri nyaraka hiyo ilikuwa imeshatumwa punde kama dakika 5 zilizopita. Akalifungua faili hilo na kuanza kulisoma. Ilikuwa ni taarifa ndefu iliyoandaliwa kiustadi mkubwa na mwandishi wao wa habari wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Baada ya kumaliza kusoma ripoti hiyo ndefu isiyochosha kutokana na kuandaliwa kwa ufundi mkubwa, akashusha pumzi ndefu kuonyesha ngoma ni nzito sana. Fikra zake zikawa zinatembea kwenye mafaili mawili aliyoyaona kwa Nathanieli akashindwa kuyafungua.

Faili la kwanza ni MAN-TEMBA FILE?S/N: 532- 'THREE IN ONE-SOWETO-HOUSE NO. 29, SINZA-MORI ?ATM-ISSUES', na faili la pili la 'MAN-TEMBA, FILE S/N: 189- SANDTON CITY CODING SYSTEM'. Akili yake ilikuwa inamtuma ya kuwa lazima akienda pale anapojiegesha Man-Temba atapata majibu yake hayo mafaili yana kitu gani haswa.



Faili la kwanza ni MAN-TEMBA FILE?S/N: 532- 'THREE IN ONE-SOWETO-HOUSE NO. 29, SINZA-MORI ?ATM-ISSUES', na faili la pili la 'MAN-TEMBA, FILE S/N: 189- SANDTON CITY CODING SYSTEM'. Akili yake ilikuwa inamtuma ya kuwa lazima akienda pale anapojiegesha Man-Temba atapata majibu yake hayo mafaili yana kitu gani haswa.

Akazima kompyuta yake na kuirudisha sehemu yake salama anapoihifadhi kwenye gari, kisha akawasha gari lake kuelekea tena Sinza Mori. Alishaghailisha mipango yake. Badala ya kuvamia usiku wa manane, aliamua aende sasa hivi. Aliamua hivyo kwa kigezo cha kuwa Man Temba yupo mitaani, hivyo nyumba ipo huru.

Alipoangalia saa yake ya mkononi wakati anaegesha gari yake mbele ya saluni aliyotoka kusukwa nywele zake, ilikuwa inasoma saa sita usiku kasoro dakika tano na sekunde kadhaa. Maduka yote yaliyopo eneo hilo yalikuwa yamefungwa. Aliposhuka tu akasalimiana kwa bashasha na mlinzi wa eneo lile na kumuachia majukumu ya ulinzi wa gari lake kwa muda.

Mlinzi yule alifurahi mno maana alijua atakapokuja kulichukua gari lake hatomuacha hivi hivi lazima atamtoa kwa chauchau ya kupunguza ukali wa maisha. Kachero Yasmine akavuka barabara na kuzuga kama analipita pagale analoishi Man-Temba halafu ghafla akavamia kuingia ndani huku tayari mkononi amekamata pisto yake pendwa aina ya Glock-G yenye kiwambo cha kuzuia sauti tayari kwa kazi.

Uzuri kulikuwa hamna mlango wa mbele pako wazi tu, pamesitiriwa na pazia kadimu lililojaa mavumbi. Mboni za macho yake zilikaribishwa na giza totoro lisilo na mfano wake.
Akaanza kutembea kwa tahadhari ndani ya nyumba huku miguu yake inakanyaga ardhini kwa unyenyekevu. Miguu hiyo ikamjulisha kuwa sakafu ya nyumba hiyo chini ilikuwa imepondeka pondeka na kutengeneza makorongo, nyufa na mashimo yasiyo rasmi.

Hakutaka kuwasha kurunzi yake akihofia huenda akashtukiwa kama ndani yake kuna mtu. Alikuwa anatembea kwa mwendo wa pole kwa kupapasa kiambaza huku kadri anavyokwenda mbele anasikia sauti za popo kujigonga ukutani na kuanguka chini, wakichagizwa na upepo mwanana unaovuma nje kupitia madirishani.

Akasita kwenda mbele kwa muda baada ya kukumbuka jambo. Alitanabahi kumbe ana kifaa cha kumsaidia kuona gizani halafu anajitaabisha bure. Akachomoa toka kwenye mfuko wa mbele wa dangirizi yake miwani maalumu yenye uwezo wa kumlinda macho yake na kumsaidia kuona kirahisi akiwa gizani. Alipoivaa akatabasamu kwa furaha na kuanza kutembea bila hofu yoyote, kwani alikuwa anaona kila kitu kiufasaha.

Kwa taftishi yake ya haraka haraka aliyoifanya, ilikuwa ni nyumba ndogo ya vyumba vitatu, vyumba viwili vya kwanza vilikuwa vipo wazi huku cha tatu kikiwa kina mlango wa bati chakavu uliofungwa na kufuli linaloning'inia mlangoni.
Hisia zikamtuma achungulie kwenye hivyo vyumba viwili, macho yake yakakaribishwa na mafurushi ya mizigo isiyo na faida yoyote. Akavikacha vyumba hivyo kisha moja kwa moja akaelekea kwenye kile chumba cha tatu chenye kufuli.

Ile kugusa tu kufuli ili afungue kwa funguo zake malaya, wakatokea mapaka wa rangi nyeusi tii kama watatu, macho yao yanang'ara kama taa ya Aladini. Paka hao wakaanza kumfokea kwa makelele kana kwamba wanamtishia Kachero Yasmine asiguse kabisa ule mlango.

Kachero Yasmine akaanza kurudi nyuma nyuma kwa tahadhari kubwa mpaka alipofika ukutani akajiegemeza huku anatwetwa kwa kuogofya viroja vile mbele yake.
Jasho jekejeke likaanza kumtirika mwilini, hakutegemea kukutana na jeshi la Ibilisi usiku ule. Walikuwa sio paka wa kawaida, ukubwa wao ulikuwa unataka kukaribiana na kitoto cha mbuzi.

Halafu ghafla, ukasikika msonyo wa sauti kubwa ya mtu asiyeonekana kisha wale paka watu wakatimua zao kuelekea kusikojulikana. Kachero Yasmine akashusha pumzi ndefu ya ahueni kutokana na vibweka hivyo vya kimazingara vilivyotoweka.

Kwa ujumla alipwaya kama mtu aliyetoka ugonjwani. Alitanabahi kuwa kazi aliyopewa sio rahisi kama kuhesabu moja, mbili, tatu, ni kazi ngumu na ya hatari anaweza kupoteza uhai akiingia kichwa kichwa na kujifanya pofu kama jongoo. Akakumbukia tukio hilo na ugumu walioupata wakati wanamsaka gaidi wa Amboni kijana Maso Maso kutokana na mambo ya mashetani wa mapangoni.
Akiwa anapanga na kupangua kichwani mwake kitu cha kufanya pindi walipotoweka wale paka, ghafla alipoangaza mbele yake akaanza kuona maji kama ya bahari yamefunika eneo lote la upeo wa macho yake.

Kwa ufupi kila chumba kikawa kimetoweka kwenye uoni wake wa macho. Alinyamaza shuuu huku akiwa amejibanza ukutani, amejinyoosha kama maiti anawaza kitu cha kufanya.
Kwa kuwa Kachero Yasmine pia amekomazwa sio mnemba, alishajua hapo hapaingiliki tena, dawa ya moto ni moto. Himahima akageuka na kutoka nduki nje ya ile nyumba haraka sana kuelekea kwenye gari yake. Mbwa wa nyumba za jirani kumuona anatoka na mbio zile wakaanza kubweka wooh wooh...! lakini Yasmine hakujihangaisha nao. Akakimbia mpaka lilipo gari lake.

Akafungua mlango wa gari lake akaingia na kuufunga, huku amefumba macho yake anatweta kwa uoga. "Vipi dada ndio unatimka sio, basi ganji hata ya soda kidogo..!" alizinduliwa Kachero Yasmine na sauti ya yule mlinzi wa nyumba iliyokuwa mkabala na nyumba ya Man Temba akimpiga kirungu cha kuomba pesa.

Bila kumjibu kitu akachomoa noti ya shilingi elfu kumi kutoka kwenye pochi yake na kumpatia huku akipandisha kioo cha gari yake baada ya kumkabidhi pesa hiyo kuonyesha hataki usumbufu. Yule mlinzi aliganda kwa dakika kadhaa akiwa haamini kama amepewa yote hiyo au ameambiwa arudishe chenji.

Alipoona kimya haambiwi kitu chochote, taratibu akaanza kuondoka mlinzi yule akihofia msamaria mwema wake asije kubadilisha mawazo ikala kwake. Kwa mshahara wake wa kilo na nusu anaoupokea kila tarehe 40, na wakati mwingine mpaka tarehe 50, shilingi elfu kumi kwake ilikuwa ni mshahara wake wa siku mbili kamili.

Kachero Yasmine alikuwa bado na fikra pacha, moja inamuambia aondoke ameshachemsha hamuwezi Man Temba ni bahari kuu, yeye kweli ni “Three In One. Kwa maana ya kuwa ni mtabe wa fani ya mawasiliano 'IT', pia yupo vizuri kwenye Juju za Kinaijeria mpaka amemtumia paka watu pia ni mtaalamu wa kupanga matukio ya kiuhalifu wa wizi wa fedha kinyang'anyi na kiteknolojia.

Sifa zote tatu zilijikusanya kwa Man-Temba, jeshi la mtu mmoja. Huku fikra ingine ikimuambia serikali haiamini uchawi hivi akiondoka zake akarudi ofisini ataenda kumueleza nini Bosi wake Mzee Omega Mtanika, ambaye tayari ameshampachika jina la Singeli, mvivu wa kazi.

Ataenda kuelezea simulizi za Ablakadabra kuwa ameona mauzauza nyumbani kwa Man-Temba?. Nani atamuamini na hadithi hiyo ya kufikirika isiyo na kichwa wala miguu. Hivyo huu upelelezi ulikuwa ni muhimu kwake kujijengea heshima hasa ukichukulia anapambana peke yake akiwa nchini bila kubebwa na kivuli cha Kachero Manu.

"Lazima nipambane kwa juhudi na maarifa siwezi kuweka silaha chini, lazima tuwaonyeshe Watanzania kuwa wanawake tukipewa nafasi tunaweza, hatubebwi tu ili mradi kuleta usawa, kama wanavyotushutumu waumini wa mfume dume..!" alijiapiza huku anapiga mikono juu ya usukani wa gari kwa hamasa.

Ghafla bin vuu akatulizana tuli kana kwamba kuna kitu amekikumbuka. Akaunda tabasamu pana la ushindi usoni mwake. Akashuka haraka chini ya gari na kwenda kufungua buti la gari kisha akashusha chini moja ya begi lake la safari. Begi ambalo lilikuwa na nguo na vifaa vya kazi vya akiba, kiasi kwamba akikurupushwa hata usiku wa manane kuhusiana na safari ya pande yoyote ya dunia anasafiri bila tatizo lolote.




Ghafla bin vuu akatulizana tuli kana kwamba kuna kitu amekikumbuka. Akaunda tabasamu pana la ushindi usoni mwake. Akashuka haraka chini ya gari na kwenda kufungua buti la gari kisha akashusha chini moja ya begi lake la safari. Begi ambalo lilikuwa na nguo na vifaa vya kazi vya akiba, kiasi kwamba akikurupushwa hata usiku wa manane kuhusiana na safari ya pande yoyote ya dunia anasafiri bila tatizo lolote.

Alifungua na kuanza kupekenyua ndani ya begi lake. Alikuwa anakitafuta kijitabu chake kidogo alichopewa na marehemu Babu yake mzaa mama siku alipompa taarifa za kuajiriwa kwake kama Afisa Usalama.

"Mjukuu wangu, nakukabidhi kitabu hiki kinaitwa Yasini Mubin ni kidogo lakini penda sana kukisoma kitakupa kinga dhidi ya wabaya wako, hata uchawi na mazingaombwe havitaweza kukudhuru ukikitumia ipasavyo. Mjukuu wangu kazi yako hiyo nzito lazima ujikomaze vilivyo kwa kuwa karibu na Allah Subhanahu Wata'ala" Yasmine alikuwa anayakumbukia maongezi yake na Babu yake siku alipokuwa anamkabidhi kitabu hicho alichokihifadhi ndani ya begi lake.

Bahati nzuri akafanikiwa kukifukunyua kitabu hicho mahali kilipojibanza. Sasa alikuwa tayari ameshakishika mkononi mwake kijitabu hicho, ambacho kimtazamo kilikuwa kimeanza kupoteza nuru kwenye kurasa zake kwa uchakavu wake uliokithiri.

Akafunga begi lake hilo na kulirudisha ndani ya buti na kurudi ndani ya gari yake. Kwa msaada wa mwanga wa ndani ya gari akaanza kuzitafuna nuni na jiimu za kwenye kitabu hicho maktubu kwa lugha ya kiarabu bulbu, kisicho na hata nukta ya kosa la kisarufi.

Ilimchukua kama nusu saa kukimaliza chote. Lakini maajabu kadri alivyokuwa anakisoma kijitabu kile kuna vitu mwilini mwake vilikuwa vinafunguka na mwili wake unaanza kuwa mwepesi na kurudia hali yake ya kawaida na uoga wote umemvuka. Akagundua kumbe alishaanza kufungwa na marogo ya kwenye nyumba ile.

Ghafla mvua nzito ile ya kidindia ikaanza kunyesha kwenye anga ile ya Sinza Mori huku sauti za radi zinalipuka angani mtindo mmoja mithili ya mabomu kwenye uwanja wa vita. Kachero Yasmine hakuwa na muda wa kupoteza ikabidi achomoe koti lake la kujikinga na mvua kutoka siti ya nyuma ya gari na kujivika mwilini. Baada ya hapo akateremka nje ya gari na kuvuka barabara kuelekea kiamboni kwa Man-Temba kwa mara ingine akiwa anatimua mbio.

Safari hii alipoingia tu ndani ya nyumba hiyo akawasha kurunzi yake, akamulika waa nyumba nzima na bastola yake ipo mkononi mwake. Nyumba nzima ilikuwa inavuja utasema imeezekwa na chujio mbovu. Alipoukaribia ule mlango wa bati, ghafla wakajitokeza tena paka wale wale watatu wanaanza kumcheza shere Kachero Yasmine Kama mwanzoni. Safari hii hakutana utani nao tena, akamlenga mmoja wao kwa bastola yake na kumfyatulia risasi moja iliyotua sawia kichwani mwa paka huyo.

Pale pale kiumbe kile kikadondoka chini na kuanza kupwiripwita kwa huruma mpaka kikata roho. Wale paka wengine kuona mwenzao anavuja damu wakatoka nduki huku nyayo zao zinalia pukutu pukutu kutokana na kuzidiwa kwa uzito wa miili yao.

Yasmine alipoumulika kwa kurunzi ule mzoga wa paka akakuta shingoni umefungwa bonge la hirizi nyekundu. Hapo hapo ule mzoga ukaanza kunuka fee fee harufu ya uozo. Hiyo ikazidi kuthibitisha kuwa yule hakuwa paka wa kawaida. Akaachana nao ule mzoga na kuendelea na kilichomleta kwenye nyumba ile.

Akalikorokochoa kufuli lile kwa funguo malaya mpaka likafunguka na kumuwezesha kuingia kwenye chumba kile. Alipokimulika mwangaza vizuri akakuta kuna tandiko moja tu, jembamba mithili ya ulimi wa ng'ombe. Hakukuwa na kitu kingine chochote kile cha thamani, jambo ambalo lilimstaajabisha sana Kachero Yasmine. Tandiko hilo lilikuwa limewekwa juu ya zulia chakavu lililoenea chumba kizima.

Kijasho chembamba cha juu ya pua zake kikaanza kumvuja bila kupenda. Alijiona kama vile Amechezewa kanya boya ya hatari, kuliko mategemeo yake. Fikrani mwake alihisi huenda kitakuwa ni chumba ambacho kimesheheni vifaa vizito vya kazi kama ishara ya meseji alizokuta nyumbani kwa Nathanieli zilivyoashiria.

Akakifanyia speksheni chumba kizima kwa umakini mkubwa, mpaka sehemu za ukutani labda atakuta unafunguka popote, akatoka patupu. Baada ya taftishi ya zaidi ya nusu saa akaamua atimke zake ndani ya chumba kile hamna chochote cha maana anapoteza muda wake tu.

Alipoufikia mlango wa kuingilia anataka sasa ausukumize mlango ule wa bati atoke nje akasita kidogo. Akageuka nyuma na kumulika kurunzi pale kwenye tandiko kwa sekunde kadhaa kama mtu aliyegundua kitu. Akaamua arudi tena mahali ambapo limewekwa godoro. Alipofika akalipiga teke kwa kutumia viatu vyake vya raba vya ngozi, likasogea pembeni lile godoro. Akaanza kumulika kwa umakini mkubwa eneo lote pale sakafuni lililokuwa limezibwa na godoro lile.

Kuna kitu akakigundua katika taftishi yake hiyo. Aliona kuna mkato wa duara juu ya lile zulia katikati ya pale palipozibwa na godoro. Mkato huo ulionekana kuungwa kiustadi mkubwa na sehemu nyingine ya zulia hilo. Akafanya maamuzi ya kuvuta kwa nguvu sehemu hiyo ya zulia kwa bahati ikanyofoka na kuacha eneo wazi la sakafuni lililozibwa na mfuniko wa shaba.

Akajibidiisha kuuvuta huo mfuniko kwa nguvu zake zote, lakini akaukuta umeng'ang'ania ng'ang'anu hauchomoki kirahisi. Akaendelea kujibidiisha mtoto wa kike kwa nguvu zote kuuvuta mfuniko huo bila kukata tamaa mpaka ukakubali kufunguka. Ukalia mlio wa sauti buuuh..! mfuniko ule baada ya kukubali kuachia.

Sasa usoni mwake furaha yake ilikuwa sheshe isiyo na kifani, huku kijasho chembamba cha juhudi kikimtiririka mashavuni mwake. Alipoangalia saa yake ilikuwa inasoma saa nane na robo ya usiku wa manane. Pia huko nje, mvua ilishakata kunyesha kabisa kitambo kirefu.
Alipopiga chabo ndani ya shimo, kulikuwa na kiza totoro kiasi kwamba kurunzi ilikuwa haitoshi mwangaza wake. Akapiga moyo konde na kuanza kuteremka kuelekea chini ya shimo lile huku akiurudishia vizuri mfuniko ule juu, akijipa moyo wa liwalo na liwe. Muda wote alikuwa anawaza huyu mkazi wake hii nyumba, Man-Temba yupo wapi mpaka sasa.

Akaanza kuteremka ngazi moja baada ya ingine kuelekea chini ya shimo. Kadri anavyoshuka chini ndio hali ya hewa inazidi kumchefua chefu chefu, lakini akazidi kupiga moyo konde aendelee na msafara wake bila kusalimu amri.
Alishuka kama mwendo wa dakika 10 hivi ndipo akakiona mbele yake chumba kimoja kizuri ila kidogo sana chenye uwezo wa kuingiza watu wasiozidi watatu tu.

Kwa bahati mlango wake chumba hicho ulikuwa umebugazwa tu. Akausukuma na kuingia ndani mzima mzima. Ndani ya kichumba Kulikuwa na meza ndogo juu yake kuna kompyuta mpakato ndogo na mzinga mkubwa wa konyagi.
Alipomulika zaidi kwenye chumba kile akaona swichi ya umeme na kiyoyozi mle kwenye kijichumba. Akaelekea ukutani na kuwasha batani hizo, kufumba na kufumbua nuru ikaenea chumba kizima na kiyoyozi kikaanza kuleta hewa nzuri ya kuvutia ndani ya chumba kile na kulifukuza kwa kasi joto lililokuwa limeshitadi ndani ya chumba kile.

Akavuta kiti kisha akaketi juu yake na bila kupepesa macho akaanza kuhangaika kuiwasha kompyuta hiyo. Wakati Kompyuta inajiweka sawa kwa ajili ya kuanza kupiga kazi, akavuta droo ndogo ya upande wa kushoto wa meza hiyo, akashtuka kidogo.

Alikutana na lundo la ATM-kadi za benki tofauti tofauti za ndani na nje ya Tanzania na mishumaa isiyopungua mitano. Kadi hizo zilikuwa ni mali za benki mbalimbali za Congo, Gambia, Afrika ya Kusini na nchi nyinginezo. Akakumbuka wameshawahi kupewa mafunzo namna pesa zinavyoibwa kwenye mashine za benki, enzi ATM-Mashine zimeanza kutumika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza.

Aina hii ya kuiba pesa kwa kutumia nta ya mshumaa, hii ni mbinu ya kizamani kidogo lakini bado kwa nchi zinazochechemea kiteknolojia ilikuwa inaweza kufanya kazi kwa asilimia kadhaa. Akaachana na kadi hizo huku akiweka umakini kwenye kompyuta aliyoiwasha punde ili kujitafutia kilichomleta ndani ya chumba hicho cha maajabu..

Kompyuta sasa ikawa imefunguka, akaanza kuyaperuzi mafaili ndani yake kadri atakavyo. Mafaili yote yaliyohifadhiwa ambayo aliyaona yana manufaa kwake alikuwa anayafowadi kwa Kachero Manu kwenye baruapepe yake na kuyahifadhi pia kwenye flashi yake. Alipanga akayasome vizuri nyumbani kwake atakaporejea maana tayari kichwa kilishachoka.

Ghafla wakati anajiandaa kuifunga ile kompyuta ikaja meseji kwenye mesenja yake Man-Temba, anaulizwa swali, "Pesa zinakaribia kusafirishwa wiki ijayo, tunasubiria mtu toka Tanzania atakayesindikiza magari hayo kutoka nchini Afrika ya Kusini kama ulivyoahidi". Ujumbe uliandikwa kuwa umetoka kwa Professor "Potchefstroom". Kachero Yasmine akashtuka na kubaki ameduwaa mdomo wazi kwa sekunde kadhaa kama zuzu hajui atoe jibu gani pale.

"Mbona hutoi jibu haraka, tukichelewa pesa zitagandishwa tushindwe kuzitoa kwa wakati, tekeleza makubaliano yetu kwa kumtuma mtu makini kama ulivyoahidi, hatuna muda wa kupoteza..!" ujumbe mwingine ulitumwa papo kwa papo kwa mtindo wa bandika bandua.

Yasmine akili yake ikachakata mambo kwa haraka sana, ikabidi ajiongeze tu kwa kujibu kwa kubahatisha tu."Sawa ameshafika mtu wetu, mpe mawasiliano namna atakavyokupata.!". Kimya kirefu kikatawala bila majibu yoyote toka upande wa pili mpaka akaanza kuingiwa na wasiwasi Kachero Yasmine kuwa huenda ameshtukiwa kuwa ni mdukuzi.

Mara akaona yule mtu anayejiita Professor Potchefstroom anachapa maneno ya kujibu. Uso wa Yasmine ukarudiwa tena na bashasha mpwitompwito na uchangamfu wake ulioanza kupotea. "OK... atapokewa na Mr. Okworonko, Sandton Gautrain Station kesho saa 6:00 mchana. Akifika ampigie kwa namba +27 83 347 21143. Tusiwasiliane tena kuanzia sasa mpaka siku mzigo wa kwanza unatua Dar es Salaam, Bye..Tchaooo..!!" jamaa akatoka kwenye mtandao.

Kachero Yasmine bila kufanya ajizi akatuma taarifa zote kwenye barua pepe ya Kachero Manu ikiwa na maelezo ya kina ya kumtaka ajifanye yeye ndio wakala aliyetumwa na Man-Temba nchini Afrika ya Kusini kufuatilia fedha. Alipotaka kuifunga kompyuta hiyo hakutaka kuiacha salama. Akairushia moja ya virusi wabaya wanaotafuna mafaili yote yaliyohifadhiwa.

Kirusi hicho kibaya ni Kachero Yasmine pekee ndio angeweza kuyarudisha mafaili hayo pindi akiyahitaji. Baada ya kufanikisha lengo lake hilo akajikuta anaunda tabasamu la ushindi, huku alijiapiza kiwa siku za wanaokula njama za uhaini kukamatwa zinahesabika kwa vidole.

Wakati anajiandaa kuondoka kwenye chumba kile akiwa tayari ameshasimama wima, akahisi kitu kama ubaridi usio wa kawaida juu ya sikio lake la kushoto. Alipogeuka tu akakutana na mdomo wa bastola unamsalimia. "Mrembo karibu kiamboni kwetu, jiskie huru..!" alikaribishwa na sauti nzito, yenye mikwaruzo ya mtu aliyekuwa amejifunika sura yake na kuachia macho yake tu huku akiwa tayari ameitwaa silaha ya Kachero Yasmine iliyokuwa pembeni ya meza yenye kompyuta.

Kachero Yasmine alipigwa na butwaa asijue la kufanya huku akijilaumu kwa uzembe wake wa kupitiliza uliomfanya afumaniwe kiwepesi sana. Nafsini kwake alikubali kabisa kuwa hakuchukua tahadhari ya kutosha. Uso wa Kachero Yasmine ulipigwa na taharuki, fedheha na soni isiyomithilika, akiwa ameishiwa mipango




Wakati anajiandaa kuondoka kwenye chumba kile akiwa tayari ameshasimama wima, akahisi kitu kama ubaridi usio wa kawaida juu ya sikio lake la kushoto. Alipogeuka tu akakutana na mdomo wa bastola unamsalimia. "Mrembo karibu kiamboni kwetu, jiskie huru..!" alikaribishwa na sauti nzito, yenye mikwaruzo ya mtu aliyekuwa amejifunika sura yake na kuachia macho yake tu huku akiwa tayari ameitwaa silaha ya Kachero Yasmine iliyokuwa pembeni ya meza yenye kompyuta.

Kachero Yasmine alipigwa na butwaa asijue la kufanya huku akijilaumu kwa uzembe wake wa kupitiliza uliomfanya afumaniwe kiwepesi sana. Nafsini kwake alikubali kabisa kuwa hakuchukua tahadhari ya kutosha. Uso wa Kachero Yasmine ulipigwa na taharuki, fedheha na soni isiyomithilika, akiwa ameishiwa mipango.

Akili yake ilikuwa inamchombeza "pambana wewe mpaka tone lako la mwisho la damu usikubali kushindwa kibwege" lakini alikuwa anasitasita kuanzisha varangati kwa sababu alikuwa hajui ukubwa wa nguvu za adui yake, kama yupo peke yake au na wenzake.

Akajipa moyo kuwa subira yavuta heri, na daima haraka haraka haina baraka, ngoja aone mwisho wake itakuwaje. Huku akijiapiza kuwa kosa lolote ambalo maadui zake watalifanya dhidi yake atalitumia vizuri ipasavyo kuweza kuwageuzia kibao.

Yule jamaa akaipandisha barakoa yake kichwani kwa juu kidogo na kuachia mdomo wake wazi, kisha akasogeza mdomo wake ampige denda Yasmine. Mdomo ambao meno yote yalikuwa ya njano kutokana na uvivu wa kupiga mswaki, unywaji wa pombe na uvutaji wa bangi na sigara wa kupitiliza huku ukitoa riha mbaya yenye kuchukiza kwenye pua.

Yasmine akili zake zilishafanya kazi yake ipasavyo akaligundua lengo la yule jamaa kuacha mdomo wazi. Akakwepesha mdomo wake usikutane na mdomo wa mjuba yule kwa kukaza misuli ya shingo yake na kufumba mdomo wake.

"Sasa mbona huna ushirikiano Bibie? Ulivyofanya maamuzi ya kuja kwenye gheto la mwanaume wa shoka ulitegemea nini? Pumbavu sana wewe" alizungumza kwa ukali jamaa yule na matusi lukuki huku akimshindilia vibao vya nguvu kwenye uso wa Yasmine. Kisha akapiga mluzi kuelekea juu ya shimo kule juu.

Punde si punde akashuka kijeba cha mtu, mweusi ti ti ti, ana mapengo mdomo mzima amevalia pensi nyeusi ya dangirizi. Chini alikuwa amevaa viatu aina ya buti. Alifika ndani ya kile chumba, wakawa sasa wamembana vilivyo Kachero Yasmine hawezi kabisa kufurukuta wala kujimwayamwaya mbele yao.

Yule kibushuti ukimtazama umbile lake alikuwa anatisha kimuonekano, uso wake wote umepambwa kwa makovu ya suluba mbalimbali alizowahi kukutana nazo kwenye shughuli zake za uhalifu.
Alikuwa akicheka kama analia vile. "Vipi mbona unacheka nae...huyu ni mtu hatari sana, mpaka kafanikiwa kufika hapa ujue amefukunyua mambo yetu mengi sana..!!" aliongea kwa sauti yenye kukwaruza isiyo na chembe ya masikhara yule mtu mfupi.

"Huyu Inabidi tuondoke nae tukambinye taarifa gani alikuwa anazidukua na amezituma wapi. Tatizo Man-Temba amelewa sana, yupo chakari tumsubirie asubuhi atakapokuwa na fahamu ndio ataweza kugundua taarifa gani zimedukuliwa" alijibu yule mjuba aliyejisitiri uso wake.

"Basi kama ni hivyo sasa tukamgeuze kuwa Bibi yetu mpaka asubuhi, hakikisha umebeba kondomu za kutosha maana Binti ni mbichi huyu kabisa chuchu zimemsimama haswa" alichagiza yule kibushuti huku sasa akimkamata kwa nguvu Kachero Yasmine na kuanza kumpapasa kimahaba, akionekana nae pia ni mbovu wa ngono.

Akawa anajaribu kujipapatua bila mafanikio toka mwilini kwa kibushuti yule ambaye alishapandisha ashki ya ngono. Kachero Yasmine hakukubali kirahisi kuliwa denda kibudu bila idhini ya Walii wake na hotuba ya Sheikh, akamng'ata meno shingoni kibushuti yule ambaye alishaanza kulegea kimahaba.

"Aaaaaah...!" Aligugumia kwa maumivu makali wakati Yasmine kanyofoa kipande cha nyama shingoni mwake. Yule kibushuti akajipachua mwenyewe mwilini mwa Kachero Yasmine bila kupenda. Yule mjuba mwingine kuona hivyo akamvaa wanguwangu Yasmine ili amuadabishe.
Kumbe alimuona vizuri anavyokuja, akajipinda kidogo, yule jamaa akapita mzima mzima na kwenda kuiparamia kompyuta pale mezani na kwenda kujigonga ukutani.

Yule kibushuti kumbe alishajipanga zamani, akawahi kudaka kiti cha chuma kilichomo chumbani mule.
Kachero Yasmine alipogeuka, tayari alikuwa ameshachelewa kukipangua kiti hicho kilitua sawia kichwani mwake maeneo ya kichogoni. Hamadi! lilikuwa ni pigo takatifu lililomfanya ahisi kizunguzungu na kuanza kuyumba na kujikuta anaanguka sakafuni kwenye zulia na kupoteza fahamu.

Alisikia kwa mbali sana kauli za wale mahasimu wake wakishauriana watoke nae haraka asije akawafia mle ndani kutokana na upotevu mkubwa wa damu mwilini mwake. Akaanza kuona nyota nyingi usoni mwake. Nyota ambazo wataalamu wa elimu ya anga hawawezi kuzieleza kazi yake. Akajiona anaanza kushuka kwenye shimo lefu lenye kiza kinene lisilo na mwisho, mpaka akapoteza fahamu.

SURA YA KUMI NA MOJA

Professor Potchefstroom..
"Sandton Gautrain Station" ni kituo cha treni cha kisasa kilichopo nchini Afrika ya Kusini, kilichojengwa katika makutano ya barabara za Rivonia na West Streets. Ni kituo kilichojengwa kwa ajili ya kupitisha treni za chini kwa chini zinazoelekea katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa 'OR TAMBO AIRPORT', huku juu yake kukijengwa platifomu mbili za juu, nazo zenye kufanya safari zake sehemu mbalimbali.

Kulikuwa na njia za mabasi ya kisasa yanayowatoa abiria na kuwaleta kituoni hapo, yenye kwenda na kurudi maeneo yasiyo pungua sita. Nazo njia hizo ni,Wendywood (S2), Rivonia (S3), Randburg (S4), Fourways (S5), Rosebank (S6) na Sandton CBD loop (S1). Hicho kituo kilizinduliwa rasmi mwaka 2010 kutokana na umuhimu wa kiuchumi wa eneo hili la Sandton City lililopo ndani ya Jiji la Johanesburg.

Huu Mji mdogo wa Sandton ulikuwa ndio chemchem ya uchumi wa Afrika ya Kusini kwa upande wa biashara. Majengo makubwa ya kibiashara "Malls" yalikuwa yanapatikana ndani ya Mji huo. Kampuni kubwa zote duniani unazozijua wewe zilikuwa na maduka yao ya kuuzia bidhaa halisi ndani ya eneo hilo.

Kuanzia kampuni ya mikoba ya mikononi kama Louis Vuitton, mpaka wauza bidhaa za mapochi, na mikanda, kampuni ya Gucci nao wapo hapo. Bila kusahau kampuni kama za Prada, Patek Phillipe, Dolce & Gabbana hao wote walipiga kambi kwenye eneo hilo dogo lenye ukwasi wa kupindukia.

Kwa ujumla Sandton ni eneo la kifahari sana pale Johanesburg, kuna nyumba za gharama kubwa mno, mahoteli ya kifahari mno, magari ya anasa, yaani kila kitu unachokiona hapo ni cha kifahari. Inasemekana Sandton ndio mtaa wa kitajiri zaidi barani Afrika. Eneo hilo peke yake linakadiriwa kuwa na mabilionea wanane (8), na mamilionea (USD) si chini ya mia moja ishirini na saba (127).

Kiufupi kuishi katika Mji huo inakubidi uwe vizuri zaidi ya sana kiuchumi. Kila mtu unayekutana nae mtaani ana dalili zote za kuwa ni Mlalaheri na sio Mlalahoi, haswa kutokana na gari yake anayoiendesha, nyumba anayoishi, kazi anayofanya na mengineyo.

Kachero Manu kwa upande safari ya kurejea Tanzania ilishakufa tayari kutokana na maelekezo aliyopewa na Kachero Yasmine kuwa aonane na Mr.Okworonko kwa ajili ya kushughulikia pesa zilizotoroshwa Tanzania na kuja kufichwa nchini Afrika ya Kusini namna zitakavyorudishwa kinyemela nchini Tanzania zifanye lengo lililokusudiwa. Alijifanya ndio ametoka Tanzania kuja kwa kazi hiyo aliyoagizwa na Man Temba, kumbe hata kufahamiana hawafahamiani.

Roho yake ilikuwa inamdunda hasa kuogopea kushtukiwa na maadui zake hasa ukichukulia wameanza kuisaka roho yake tokea siku ya kwanza tu anakanyaga nchini Afrika ya Kusini. Alijibadilisha kidogo muonekano wake kwa kunyoa upara na ndevu zake zote, akawa anaonekana ni kijana haswa hasa kutokana na umbo lake la kimazoezi.

Alipowasili tu pale stesheni ya Sandton Gautrain akapiga namba simu aliyopewa na Kachero Yasmine. Bahati nzuri akajibiwa kuwa Mr.Okworonko yupo njiani anakuja. Alipojibiwa hivyo akatafua mgahawa hapo hapo stesheni ili apate kifungua kinywa maana alikurupuka nyumbani bila hata kuuchoma utumbo wake kwa chai.

Ile anamalizia tu staftahi yake akasikia simu yake inaita, bila kufanya ajizi akaipokea. "Hellow....Yap...Al-right..haina noma naja" alijibu Kachero Manu simu ya upande wa pili kisha akakata simu. Alipigwa na bumbuwazi kwa muda akishangazwa na Kiswahili fasaha kinachocharazwa na Mr.Okworonko. Akafanya haraka kwenda kumuwahi kwenye eneo la maegesho ya magari pale stesheni kumlaki.

"Ooh...Nice to meet you, I'm Mr.Okworonko, if you wish call me Mr.OK...that is my nickname, and you?? akatupiwa swali Kachero Manu akiwa ameshapanda kwenye gari, swali ambalo hakujiandaa nalo kulijibu kwa haraka haraka. Hakujipanga kabisa na swali hilo.
"I'm...I'm....call me Ken-D my nickname..!" alipatwa na kigugumizi cha ghafla Kachero Manu. "Ooh..Sorry Be free to speak Swahili najua nyie Wabongo wengi Kiingereza ni tatizo kwenu... teh... teh.. teh..!" alimtoa hofu Kachero Manu, kisha wote kwa pamoja wakaangua kicheko.

Wakaelekea nyumbani kwa Mr.Okworonko.
Kumbe angejua kuwa Kachero Manu, kimombo ndio kimelala kwake utasema kazaliwa nyumbani kwa Malkia wa Uingereza, wakati ni Mmwera tu wa Mahiwa, Lindi. Alipofika nyumbani kwa Mr.Okworonko bila kuchelewa mafunzo yakaanza mara moja, ya namna ya kuendesha mifumo mbalimbali ya utapeli wa kwenye mabenki.



Moja ya lengo la Nyasa Empire Supporters (NES) lilikuwa ni kuweka kituo cha utapeli huo kwa ajili eneo la Afrika Mashariki na Kati. Jukumu la kwanza lilikuwa ni kuhakikisha pesa zilizoibwa na kutoroshwa kwenda kufichwa kwenye Mabenki katika Mji wa Sandton City zinarudi Tanzania kinyemela na kufanya lengo husika lililokusudiwa. Lengo la pesa hizo lilikuwa ni kutumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa kuhakikisha wapiga kura wanahongwa ili wakichague na kukiingiza madarakani kwa kishindo chama cha upinzani cha National Movement Party (NMP) kinachoongozwa na Dr Patrick Ndomba.


Kwa muda wa siku tatu tu Kachero Manu alizoishi katika Mji huo akagundua kitu kimoja, kwamba kuna asilimia kubwa sana ya vijana wadogo kiumri wanaishi hapo Sandton City, na wengi walikuwa ni watu wenye asili ya Afrika Magharibi kuanzia Naijeria, Cameroon na Ghana.
Walikuwa na maisha mazuri mno, wengi wao wakionekana maeneo ya kula bata wakiwa na magari ya thamani sana na kufanya vitu vya anasa. Cha kushangaza hawa vijana hawakuwa na kazi wala biashara yoyote ya maana, hawakuwa na michongo yoyote ya kueleweka hadharani. Lakini waliweza kumudu maisha ya Sandton na anasa za hali ya juu.

Mfano mwenyeji wake Mr.Okworonko alikuwa anamkodishia Kachero Manu kila siku gari la kifahari aina ya 'Rolls-Royce Phantom' kwa gharama ya R4000 kwa ajili ya kumzungusha kwenye mizunguko yake ya mjini kila siku na kumrudisha mahali alipofikia.
Ilipofika siku ya tano, akiwa tayari ameshaanza kuiva na kufundwa mbinu mbalimbali za ukwapuaji wa pesa kwenye Mabenki, siku moja usiku wa majira ya saa 4:00 Kachero Manu akaitwa na Mr.Okworonko sebuleni kwake, wakaketi kwa ajili ya mazungumzo yao ya faraghani yaliyohitaji utulivu mkubwa baina yao.

"Kesho Asubuhi ndio nakupeleka kwa Professor Potchefstroom..!!" alifungua maongezi yake Mr.Okworonko kisha akaweka kituo akawa anajimiminia maji kwenye glasi yake na kuanza kuyagida mfululizo, kisha akaendelea. "Mimi nilichoagizwa nikufundishe nimeshamaliza kazi, Yeye ndio ataenda kukupa mbinu za mwisho namna pesa zitakavyotoka hapa na kurejea kwenu Tanzania.

Onyo ninalokupa ni kuwa Professor Potchefstroom hataki ubabaishaji, usaliti wowote dhidi yake ujue kifo kinakuita. Ana mtandao mpana Afrika nzima mpaka katika bara la Amerika. Una bahati sana kuonana na yeye, mimi nipo hapa nchini Afrika ya Kusini mwaka wa 10 sasa sijabahatika kumuona uso kwa uso zaidi ya kupokea maagizo toka kwa wakubwa zangu waliopo nchini Naijeria ambao nao Bosi wao ni Professor Potchefstroom.

Nikutakie kila la kheri kwenye safari yako ya kurejea nyumbani kwenu Tanzania". Yalikuwa ni mazungumzo mafupi yenye kutoa zaidi maelekezo ya upande mmoja badala kufungua mjadala.
Kachero Manu alikuwa anasikiliza tu kwa umakini mkubwa huku moyoni akifurahia kwenda kukutana na mzizi wa tatizo. Mtu ambaye ndiye aliyehandisi uhaini na ukwapuaji huo mkubwa wa pesa katika mabenki Tanzania, uliotikisa nchi nzima.

Wakatakiana usiku mwema huku kila mmoja akielekea kwenye khurfa yake kulala, tayari kwa Kachero Manu kujiandaa na safari ya kesho yake kuelekea kwa Professor Potchefstroom.


Mama Catherine alikuwa tayari ameshawasili katika viunga vya shule ya sekondari ya wasichana-Kilakala iliyopo takribani kilometa 5 kutoka stendi kuu ya Mabasi ya Msamvu, ndani ya Mji kasoro Bahari, Morogoro.

Ujio wake pale shuleni ulitokana na barua ya wito toka shuleni ukimtaka afike mara moja bila kukosa tarehe 30/07/1970 saa 4:00 asubuhi. Ni barua ambayo ilizua taharuki kubwa katika mioyo ya wazazi wake Catherine Mushi, mwanafunzi wa Kilakala. Kwani binti yao alikuwa hajamaliza hata wiki tatu tokea aripoti shuleni hapo kwa ajili ya kuanza durusu za kidato cha 5.

Catherine alikuwa ni binti yao wa pekee katika ndoa yao ya zaidi ya miaka 20. Alichaguliwa kujiunga na shule ya wasichana Kilakala akitokea sekondari ya Korogwe Girls baada ya kuongoza kitaifa kwa upande wa wasichana katika matokeo ya mtihani wa kidato cha 4 kwa mwaka 1969. Alipata alama 'A' kwenye kila somo alilofanya mtihani wake, likiwemo mpaka somo la ufahamu wa maarifa ya Biblia.
Hivyo mtoto wao huyo wa pekee walimuona kama ni nyota ya baadae kwa Taifa la Tanzania hasa ukichukulia kipaji chake pekee cha kiakili alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu na maadili ya hofu ya Mungu waliyomlea.

Mama Catherine alikuwa amekaa pamoja na wazazi wenzake watatu chini ya turubai maalumu lililowatenganisha wao na watoto wao likiwa nje ya ofisi kuu ya walimu. Ndani ya ofisi hiyo kulikuwa na kikao cha bodi ya shule inarindima huku vigogo wote wa bodi na uongozi wa Mkoa wa Morogoro ukiwa ndani ya kikao hicho. Mabinti hao walikuwa wanaitwa mmoja mmoja ndani ya kikao hicho kuhojiwa.

Wazazi wote walikuwa kama wamechanganyikiwa hawajui maswahibu gani ya kinidhamu yamewakuta watoto wao, hasa baada ya kuona kila binti akitoka kwenye mahojiano hayo anaangusha kilio kama amepewa taarifa za msiba.

Majira ya alasiri wazazi wote wakaitwa ndani ya kikao cha bodi hiyo kupewa nia na madhumuni ya wito wao. Walikabidhiwa rasmi barua za kuwajulisha kuwa watoto wao wamefukuzwa kwa kosa la kinidhamu la kukutwa na mimba.
Katika utaratibu wa kawaida wa shule wa kuwapima wasichana pindi wanaporudi toka likizo, ndio ukawanasa Mabinti hao wanne kuwa na mimba pamoja na Catherine nae akiwemo. Walitulizwa kwa kupewa ushauri nasaha wa kuishi nao kiustaarabu bila kuwanyanyapaa kuogopea wasije Mabinti hao wakachukua maamuzi magumu ya hata kujiua.

Baba Catherine, Meja Mushi alivyopata habari hiyo alicharuka kama mbogo aliyekoswakoswa risasi na jangili. Alitaka hata kumpiga risasi binti yake kwa aibu hiyo aliyoileta kwenye familia. Lakini ndugu, jamaa na marafiki wakafanya kazi kubwa ya kumshusha wahaka wake.
Mama Catherine bado nae akawa haamini anatafakari mwanawe kaipatia wapi mimba hasa ikichukuliwa maadili mufti aliyomkuza nayo bintiye. Jibu la mhusika wa mzigo huo likawa ni gumu kulipata wakabaki na giza zito kwenye mioyo yao.

Siku hazigandi hatimaye muda wa kujifungua ukatimu, akazaliwa mtoto dume. Mjukuu ambaye furaha yake ya kuzaliwa ikawasahaulisha aibu iliyoletwa na Catherine. Mjukuu akaleta neema ya upendo na umoja upya katika familia.
Babu yake akampa jina la 'Asante-Rabbi', akimaanisha Ahsante Mungu kwa zawadi ya mjukuu. Asante-Rabbi huyu Mziwanda wa Catherine ndio huyu Professor Potchefstroom kigogo mzito wa Nyasa Empire Supporters (NES) ya leo inayowatoa jasho na kamasi akina Kachero Manu na Kachero Yasmine na kuutikisa uchumi wa nchi.

Ndio huyo anayeheshimiwa na matapeli wote wa wizi wa mtandao kutoka nchi zote za Afrika Magharibi. Asante-Rabbi huyu alilelewa na kukuzwa kwa upendo na mahaba mazito na familia nzima, walikuwa wanamtunza kama mboni ya jicho. Kwa ujumla alikuwa mtoto wa Bibi na Babu.

Alipofikisha umri wa miaka 7, mwaka 1977 akaandikishwa darasa la kwanza. Kwa jina la Asante-Rabbi Mushi, babu yake hakutaka hata kulisikia jina la baba wa mtoto likitajwa. Alikuwa akitajwa mhusika jina lake anajisikia kichefuchefu.
Mhusika alikuwa ni Shamba-Boi wao aliyekuwa akijulikana kwa jina moja tu la Ngwenyama. Ambaye baada ya kupata penyenye kuwa Catherine kafukuzwa shule kwa sababu ya ujauzito, alilala mitini.

Alishajua ishu ikibumbuluka hawezi kubakia salama. Mchaga Meja Mushi wa jeshi la wananchi JWTZ asingemuacha salama, lazima angempiga risasi au kumtia kilema kwa kumuharibia binti yake.
Asante-Rabbi huko shuleni alipofika umri wa kusoma akageuka moto wa kuotea mbali kwa jinsi kichwa chake kinavyochaji darasani. Mtoto wa nyoka ni nyoka, kama mama yake mzazi Catherine alivyokuwa mtabe wa masomo darasani na yeye alikuwa hivyo hivyo. Matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 1983 ndio yalimtangaza Asante-Rabbi Mushi mbele ya Watanzania wote kwenye redio na magazeti kuwa ni mshindi.

Aliongoza nchi nzima kwa kupata alama ambazo tokea baraza la mitihani ya taifa "NECTA" lianzishwe kulikuwa hamna mwanafunzi aliyewahi kupata alama hizo. Wapo waliomtabiria Asante-Rabbi mazuri, kuwa huenda akaja kuwa mmoja wa Wanasayansi wa kuheshimiwa dunia mfano wa akina Isack Newton, mwanafizikia bobezi.

Akachaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya wavulana, Mzumbe iliyopo Mkoani Morogoro. Shule ambayo ilikuwa ni maalumu kwa watoto wenye vipaji vya kipekee vya kiakili. Huko nako akauendeleza moto wake wa masomo ule ule aliouwasha tokea shule ya msingi.
Tokea kidato cha kwanza mpaka anahitimu kidato cha nne yeye ndio alikuwa kinara kwenye masomo. Maajabu ilikuwa kuna wakati mpaka wanafunzi wa kidato cha tano na sita walikuwa wakikwama kwenye somo la Hesabu na Fizikia, wanamuona Assante-Rabbi anawatatulia.

Ila chambilecho uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti, asiye na hili ana lile. Asante-Rabbi alikuwa mkimya na mpole kupitiliza, jongoo ana nafuu. Alikuwa ni mtu wa kujitenga hapendi kuchanganyika na makundi ya wanafunzi wenzake. Ni mwanafunzi mmoja tu shuleni pale ndio alizoeana nae sana, mpaka watu wakastaajabishwa.

Mwanafunzi huyo akiitwa Newton Temba. Nae alikuwa na silka za kufanana na Asante-Rabbi. Mpaka watu wakawa wanajiuliza hawa hasa wanaunganishwa na kitu gani hasa ukichukulia ya kuwa Asante-Rabbi alimpita madarasa mawili Newton Temba.
Huyu Newton Temba ndio Man-Temba, ambaye ukubwani kwao waliunda tena uwili mtakatifu kati yake na Asante-Rabbi katika mawasiliano ya utapeli wa zile fedha zilizoibwa ndani ya Mabenki matatu makubwa nchini.

Basi pale shuleni wapo waliosema Asante-Rabbi anaringa kutokana na uwezo wa kiakili alio nao ndio maana hataki kabisa kujichanganya na wenzake anawaona vilaza. Wapo waliosema anajidai kwa kuwa anatokea familia ya kigogo wa Jeshi, Meja Mushi hivyo anajiona ni Mlalaheri na wengine wote ni Makapuku Bin Walalahoi.
Ili mradi kila mmoja alizusha lake, lakini hawakujua kitu ambacho kilikuwa kinamtafuna ndani kwa ndani mpaka kumfanya awe mnyonge kupitiliza kiasi hicho.

Kikubwa kilichokuwa kinamkosesha raha ni kitendo cha kutokumfahamu baba yake mzazi. Alishagundua kuwa Mzee Mushi ni Babu yake sasa Baba yake yupo wapi na kwanini hawaishi nae pamoja ndio kitu kilikuwa kinamkosesha sana raha.
Kila alipokuwa anajaribu kumchokonoa Mama yake mada ya kuhusiana na Baba yake mahali alipo, alikuwa anaitolea mbavuni hataki kuijadili hiyo mada. Ndipo ilipokuwa imebaki wiki tatu tu kumaliza mitihani ya kuhitimu elimu ya kidato cha nne, alipoamua kufanya kituko cha mwaka kushinikiza kumjua Baba yake mzazi.

Alitoweka shuleni bila ruhusa na kurejea nyumbani. Babu yake aliwaka akawa mkali kama pilipili mpaka anamtishia kumshushia kipigo kama asiporejea shuleni, lakini wapi hakuweza kufua dafu. Babu, Bibi na Mama yake mzazi walikuwa tumbo joto, wakijua pepo lililomtoa shuleni Catherine na kumkatiza masomo linataka kujirudia upya kwa mjukuu wao Asante-Rabbi, jambo ambalo waliapa kuwa hawatokubali wapo tayari wakeshe kwa maombi, kunuti na funga ili mradi pepo huyo amtoke mjukuu wao.

Licha ya juhudi zote za kumrai kuwa akamalize shule kwanza ndio wajadili jambo hilo kutokana na unyeti wake lakini wapi, walitoka kapa, Asante Rabbi aliwawekea kigingi, jibu lake lilikuwa ni moja tu, tena kwa kimombo "No Father-No School". Ndipo mama mtu akatwishwa mzigo wa kumpasulia ukweli mtoto wake.

Ndio siku miongoni mwa siku, usiku wa manane Catherine aligonga mlango wa ghulamu wake na kumualika kuwa ana mazungumzo ya faragha na yeye.
Wakaketi sebuleni wawili tu wakiwa na lepelepe la usingizi hamna mtu yoyote anayewashuhudia zaidi ya Mungu na Malaika wake. Fikra za Catherine zikarejea nyuma zaidi ya miaka 18 iliyopita akikumbukia hatua mpaka hatua kuanzia jinsi alivyopata mimba ya mziwanda wake Asante-Rabbi mpaka kujifungua kwake. Alikuwa hajasahau kipengere hata kimoja katika matukio hayo.

Alianza kukumbukia peke yake mawazoni mwake kuwa baba yake Asante-Rabbi, Ngwenyama alikuwa ni Shamba-Boi wao wa kazi za nje aliyetokea nchini Malawi kuja kutafuta kazi za nyumbani Jijini Dar es Salaam. Alikuwa ni kijana mtiifu, mwenye kujituma na mchapa kazi, hali iliyomfanya apendwe na kila mwana familia ya Meja Mushi. Kingine cha ziada alikuwa ni umbile lenye mvuto, ukichanganya na kazi zake za shuruba zikamfanya awe na umbo la kuvutia la kiuanamichezo.

Pia alikuwa ni mcheshi sana mwenye kupenda utani na kila mtu katika nyumba ile. Sasa Catherine alipomaliza shule mwaka 1969 akiwa nyumbani anasubiria matokeo ya kidato cha nne, ndipo majaribu ya Ibilisi yalipoanza. Alijikuta ghafla tu anampenda Ngwenyama toka moyoni. Na kwa kuwa alikuwa ni mtoto wa getikali hamna kuzurura ovyo kama mbwa koko wa uswahilini hivyo mwanaume wa maana kwake aliyemzoea machoni mwake ni Ngwenyama.

Kila dalili alizozionyesha kwa Ngwenyama kuonyesha amekufa na kuoza kimapenzi juu yake, hazikufua dafu. Akabakia anateketea moyoni kwa moto mkali wa huba. Mila za Kiafrika zilikuwa haziruhusu msichana kumtakia mvulana kuwa anampenda minghaili wazungu wao kwao ni kitu cha kawaida tu mtu kuelezea hisia zake.

Fursa ya pekee aliyokuwa anaisubiria Catherine ikajitokeza, baba yake Meja Mushi na mkewe walipata safari ya ghafla kuelekea Rombo-Moshi. Kulikuwa na msiba umetokea Kijijini hivyo walipaswa kwenda kuzika. Mzee Mushi akawausia waishi vizuri ndani ya hizo siku tatu, kuanzia Ijumaa mpaka jumatatu watakaporejea safarini.

Sasa nyumba ikabakia watu watatu, dada wa kazi, Catherine na Ngwanyama. Ijumaa ile ikapita salama mpaka Jumamosi. Tatizo lilikuwa kwa Catherine hawezi kumuambia hisia zake asije akaonekana yeye ni ghashi wa mahonyo. Siku ya Jumapili ndipo mpango wa Ibilisi kuwadondoshea Catherine na Ngwanyama katika dhambi ya zinaa ukatimu.

Ilikuwa ni kawaida ya Catherine kila ifikapo siku ya Jumapili kwenda kusali kanisani misa ya kwanza. Hivyo alikuwa anaondoka saa 12:30 shapu kuelekea kanisani, atakaa huko na kurejea nyumbani saa 3 asubuhi. Ratiba ya kazi ya Ngwanyama siku ya Jumapili ilikuwa ni kusafisha madirisha ya nyumba nzima.

Hivyo alipenda kuanza na madirisha ya chumba cha Catherine ili akirudi kanisani awe huru kujimwayamwaya kutumia chumba chake bila usumbufu. Lakini kumbe siku hiyo Catherine alichelewa kuamka hivyo akapanga aingie kanisani misa ya pili.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog