Search This Blog

Wednesday 22 March 2023

MSHANGAO - 4

Simulizi : Mshangao 

Sehemu Ya : Nne (4)

Kifupi Mr. Michael Joram alikuwa ni shushushu wa kijerumani nchini Marekani na hata alipotoka na kuletwa nchini Malaysia kufanya kazi za kidiplomasia kazi yake iliendelea kwa usiri mkubwa tena bila kugundulikana na watu wa usalama wa Marekani. Hakuna alichojali zaidi ya maslahi yake na kuamini nchi anayoifanyia kazi si nchi yake.

Hakuwa anajua juu ya kina nani waliowateka wanasayansi wa Marekani alitumia kila jitihada hili angalau ajue ni nani aliyefanya jambo lile lakini hakufanikiwa ingawa aliamini ipo siku atajua ni nani aliyefanya vile. Bwana Logan Puteri alifanya jambo hili katika usiri mkubwa bila kushirikisha watu walio nje ya watu wake na wengi wanaomjua hawakuwa wakijua kama yeye kama anamiliki kikosi kinachofanya mambo ya tofauti na ndiyo maana bwana Logan alikuwa na kile kikundi alichokuwa anajifanya kama anakifadhili kinachohusiana na mambo ya boxing na mambo mengine ya kimichezo, kikundi cha SDB.

Huyu Michael alikuwa anajua machafu kidogo aliyonayo Logan Puteri na ujanja wake wakupiga pesa haramu na kuzitakatisha lakini hakuwai kujua kama ana kikosi kipana cha kazi, hivyo mambo mengine aliyokuwa akishirikishwa naye alikuwa akishiriki bila kujua anashirikishwa kwa mpango gani unaoendelea alichojalia yeye ni akaunti yake kuingizwa pesa alizoomba ziingizwe naye akatoa msaada alioombwa. Aligusiwa kilichohitajiwa na bwana Logan nay eye akafanya uchunguzi wake mdogo na kupata baadhi ya majibu kutokana na kuaminiwa kwake na watu wawili walio juu yake pale ubalozini, balozi mwenyewe na mkuu wa kitengo chake.

Dakika ishirini mbele toka waongee kwa simu bawana Logan Puteri na bwana Michael Joram Schweinsteiger gari ya kifahari aina ya Chevrolet rangi nyekundu ilikuwa imeelekezwa kwenye geti la jumba la kifahari eneo Batu Caves barabara ya Jalan Kepong akisubiri geti lifunguliwe baada ya maelekezo aliyopewa na mwenye akifika tu yeye atamuona katika CCTV Monitoring room na kumfungulia geti.

Kweli dakika moja tu mbele aliona geti lenye vitairi likisogea kutoka kulia kuelekea kushoto naye akalipitisha Chevrolet lake kisha akaenda kulipaki pembeni ya mahali alipoona gari aina ya Hammer rangi ya kijivu imepaki ni gari ambayo alikuwa akiijua vilivyo ni ya rafiki yake kipenzi aliyemuita hapa.

“Karibu Mr. Michael… Karibu sana nyumbani kwangu kwingine na ujisikie huko nyumbani kwa Zahra Logan ulipozoea mara nyingi kufika”. Akatoa ukaribisho Bwana Logan akiwa katoka ndani na Michael akashuka wakapeana kumbatio la salamu marafiki hawa waliofahamiana miaka takribani nane sasa.

“Ahsante Mr. Logan Puteri…. Eeeeh! Hongera sana maana umenunua jumba zuri na kubwa… Anaishi nani hapa?”. Akajibu Mr. Michael huku wakiachiana kwenye hugh (kumbatio).

“Hii nyumba nimenunua kuna jambo nataka nimuombe Zahra baada ya kumaliza mambo fulani yanayonikabili sasa na kama atanikubalia basi jumba hili litapata mkaaji… nimenunua majumba mawili makali kama hili Mr. Michael na yote haya Zahra hajui, hiyo ingine ipo Kota Damansamara”.

“Pesa imekuzidi Logan unafanya yale unayojisikia kwa raha zako… Nafikiri utakalomuomba mkeo ni kuongeza mke wa pili, dini yenu inaruhusu naamimi Zahra muelewa atakuruhusu tu”.

Tayari walikuwa wakiongozana kuelekea Mr. Logan alipotaka ndiyo wakaongelee kwenye viti vilivyokuwa kwenye bustani iliyo mbele ya bwawa la kuogelea (swimming poo).

“Nina binti mmoja chotara wa kihindi na kizungu namuelewa kweli kweli nimefikiria ni bora nikamuoa kabisa maana damu changa na vijana wenzie navyomfanya wa akiba wanamsumbua sana nami sitaki vurugu na vijana wa kisasa, nimeona ni bora nikamuoa na ndiyo uwa nakuja naye hapa kupumzika weekend moja moja pale ninapoweza kumzuga Zahra kuwa nimesafiri, kifupi hii nyumba na ile ingine ni kama nimenunua kwa ajili yake binti huyo aliyeiteka akili yangu… Nataka jumba lile kota damansamara niwahonge wazazi wake hili wasilete ubishi wa umri wakati wa kumposa binti yao”

“Wewe bwana saivi huko juu sana, biashara zako zishakuingizia faida sana acha ule matunda ya uvumilivu wako… Nasubiri mualiko wa harusi tu tuje tufurahi lakini uwe makini wakati wakumeleza mu Iran wako Zahra”.

Walikuwa washafika kwenye viti maalumu vinavyokuwa mara nyingi vinatumika kwa watu wanaojua starehe zao na kuwa pembeni ya mabwawa ya kuogelea na hata beach, kila mmoja akakaa sehemu yake wakitenganishwa na meza nzuri ya kioo rangi nyeusi na nyeupe iliyokuwa ina vinywaji vya gharama chupa za aina tofauti tofauti kama mizinga mitano hivi.

“Karibu vinywaji nimeandaa aina zote za mivinyo unayoipenda hili ufurahi maongezi Mr. Michael”.

“Leo nataka niamie kwako mnywaji wa luc belaire, nasikia hiyo chupa ya dhahabu ina ladha tamu sana”.

“Yah! Ni kweli luc belaire gold iko vizuri sana… Achana na ma Whisky yako makali sana”. Maongezi yao yalikuwa yamezungukwa na furaha sana isiyoisha vicheko na kugongesha viganja vyao, vinywaji vikamiminwa kwenye glasi zao.

“Mmmh! Lete habari Mr. Michael, vipi kuhusu nilivyokuomba unisaidie?”. Akaanzisha maongezi ya kuhusu kikao chao hiki Mr. Logan akiwa na shauku ya kujua juu ya aliyoomba asaidiwe.

“Nimelifanyia kazi uliloniomba… Unajua mara zote mimi kama msaidizi wa mwanadiplomasia wetu uwa nashirikishwa kila kitu juu ya yanayoendelea hapa Malaysia na hata yanayokuja kutoka nchini kwetu Marekani, mimi ndiyo mtu mzoefu mwenye kujua kila kitu kinachohusu ubalozi wetu hapa Malaysia… Lakini Mr. Logan sikuwa najua lolote kuhusu mtu uliyeniagiza kukupa taarifa zake na si kama simjui namjua sana Agent Kai hasa kwa sifa zake za kikazi toka kipindi yupo US Navy Seals na mpaka awe CIA… Leo nataka nikupe siri rafiki yangu kuwa mimi ni nani haswa licha ya unijuavyo kama afisa msaidizi wa mwanadiplomasia”. Akatoa maelezo marefu kidogo Mr. Michael kisha akanywa funda kadhaa za kinywaji na kuendela baada ya kutizamana usoni na bwana Logan.

“Ila kabla sijakwambia chochote bwana Logan ningependa kujua juu ya upande wako wewe kwanini unataka kujua habari za huyu mtu na uwepo wake hapa Malaysia na kwanini? anakunyima raha kama ulivyoniambia asubuhi, kuna jambo gani lililo nyuma yake mpaka uwe na wasiwasi na jasusi wa CIA?”.

Kijasho chembamba kilianza kumtoka Mr. Logan Puteri, hakutegemea kukutana na maswali kama aliyoulizwa kutoka kwa rafiki yake Mr. Michael, alijiuliza anawezaje kuongea kitu kinachogusa masuala ya wamarekani kwa mwanadiplomasia wa taifa hilo? Je anaweza akamuamini? Je ataharibu kila kitu? Alijifanya amenogewa na kunywa kwa kupiga funda kadhaa wa kadhaa kupisha akili yake anayoiamini sana kwenye maamuzi ya jambo lolote, mwisho akaamua jambo ambalo aliamini ndiyo msaada kwake.

“Mr. Michael tumekuwa marafiki kwa kikpindi kirefu nafikiri toka tujuane kwa mara ya kwanza ni takribani miaka nane na miezi kadhaa sasa…. Ndani ya miaka hiyo umeweza kujua baadhi ya mambo yangu na mengi uliyoyajua yapo uliyonisapoti punde tu nilipoomba sapoti yako…. Nina jambo ambalo upande mwingine naona kama linaweza niletea matatizo makubwa sana lakini kwakuwa mimi ni mwanaume nimeamua kupambana nalo kiume”. Akasema na kukata tena kinywaji kulipa burudani koo lake.

“Wewe Mr. Michael kama ulivyowai niambia siku moja utaifa wako wa asili unakufanya muda mwingine ufanye kazi huku ukiwa na uchungu kwanini usingekuwa unawafanyia kazi Wajerumani iliko asili ya wazee wako, hivyo nina imani kuu leo hatuwezi vunja urafiki wetu kwa yale utakayoyasikia sababu ya kuwa kinagusa maslahi ya nchi yako…. Tumesaidiana mengi sana Mr. Michael na imani yangu huwezi nitupa kwenye hili na haliwezi kuwa lina hasara yoyote kwako”. Akaendelea na kupumzika kusubiri labda anayeongea naye ana jambo la kutia hapo lakini akaonyeshwa kwa ishara aendelee.

“Nakumbuka kuna siku uliniuliza juu ya wanasayansi wa Marekani waliopotea hapa KL, kuwanaweza kuwa na fununu nani amehusika na upoteaji wake kutokana na mimi kuwa ni miongoni mwa watu unaojua nafahamiana na watu wengi hapa KL”. Hapa alisimama kuongea pale alipoona macho ya kijani ya mzungu wa kijerumani yamemuangalia yakiwa na shauku wa kujua nini kinafuata toka mdomoni mwake.

“Yah! Nakumbuka nilikuuliza na nakumbuka jibu ulilonipa kuwa hujui chochote na utajaribu kufuatilia kwa watu wengine unaowajua wanaweza kuwa wamehusika na jambo hili na mpaka leo hatujawai kuongelea hilo suala hadi sasa unavyonikumbusha”.

“Ningependa nijue utajisikiaje? nikikwambia najua muhusika wa tendo lile”.

“Logan… Logan unanijaribu au? Unaniulizaje swali kama hili? Unafikiri naweza kujisikiaje zaidi ya kufurahi… Maana ni jambo la kheri kujua hivyo sababu sifa zitakuja kwangu na hata kwako toka kwa wamarekani na pia nataka nikupe siri kuna donge nono litalipwa kwa hata tetesi tu zitakazo saidia kuonekana kwao”. AKajibu Mr. Michael na kumfanya Mr. Logan kuanza kuogopa kumwambia.

“Michael rafiki yangu donge nono hilo ni shilingi ngapi na limetangazwa lini?”.

“Sisi watu wa ubalozini tulitangaziwa dau… Dau lenyewe ni pesa ambazo unaweza nunua hayo ma hammer yako unayoyapenda kama manne hivi na kama Chevrolet hizi za kisasa kama yangu unapata tatu na chenchi inabaki”. Michael akajibu huku akiamini anachoongea yeye kina ushawishi kwa Mr. Logan.

Mwisho wa sehemu ya ishirini na mbili (22)

Kama kawaida mwisho wa sehemu inayopita uwa mwanzo wa sehemu inayoanza, naomba nisikuchoshe na maneno ya ufafanuzi wa sehemu iliyopita, twen’zetu mbele.

ENDELEA NA UTAMU!

HATUA MOJA MBELE II

“Mr. Michael, Mr. Michael tuliza akili na unisikilize kwa umakini…. Ooooopuh! Mpaka nahema.. Maana dau ulilonitajia ni dogo kwangu… Sikiliza rafiki yangu mi naomba uwe upande wangu katika suala hili”.

“Mr. Logan sikuelewi kabisa.. Ebu funguka kuwa muwazi kwangu kwa sababu mpaka saivi sielewi ni kitu gani kinachokuumiza na kukupa mawazo mpaka umeamua kuniomba kufuatilia habari za Agent Kai na hata sielewi kwanini wewe umejua juu ya Agent Kai kuwa hapa Malaysia wakati mimi mtu wa ubalozini sikujua kuhusu hilo mpaka uliponiambia… Unajua rafiki yangu unanipa ukakasi na kunifanya nifikirie mbali bila sababu”.

Kikapita kimya wakiendelea kunywa vinywaji vyao.

“Muda unakwenda Logan”.

“Michael wale watu mi ndiyo muhusika wa suala lile”. Aliongea Mr. Logan Puteri na kumfanya Mr. Michael kupaliwa na kinywaji chake, akakohoa kwa sekunde thelathini.

“Umesema?”. Akauliza kwa sauti ya kustukiza huku macho kayatoa pima.

“Mimi ndiyo muhusika wa mpango wote na watu wote wale ninao mimi…. Mr. Michael sijakurupuka kukuamini nimeamua kukuamini sababu naamini wewe ndiyo msaada kwangu lasivyo naingia matatizoni… Mr. Michael safu yangu ya uongozi wa kampuni yangu ya Logan Group of Business ni watu wa kazi, nimeajiri watu waliokuwa wanajeshi, majasusi na hata magaidi… Hivyo namiliki timu ya watu wa kazi wakiwa kwenye kivuli cha kuwa wafanyakazi wangu… Hakuna aliye nje ya kampuni yetu ambaye anajua hili kwa nguvu zake mwenyewe bila mimi mwenyewe kumwambia”.

Alisimama kuongea Mr. Logan baada ya kuona jamaa anamuangalia macho ya kijani kama paka yaking’aa kwa kutokuamini aambiwayo.

“Mr. Logan unajiamini nini kufanya jambo kubwa kama hili? Na kwanini unawashikilia watu wale wasio na hatia?”. Akampachika swali huku akitizama huku na huko katika maeneo yanayozunguka jumba lile wasiwasi ukimtanda moyoni isije kuwa naye anaingizwa kwenye matatizo ya kutekwa.

“Michael! Nilifanya baada ya kushawishiwa na pesa… Pesa ndiyo inanifanya mpaka leo niwashikilie watu wale, nachoomba kwako ukubali tuwe jambo moja katika hili sababu hakuna madhara kwako zaidi ya faida”.

“Faida gani Mr. Logan? Unajua umenipa mshangao mkubwa sana katika hili, sikujua kama unaniitia jambo kubwa kama hili”.

“Nakuandikia cheki sasa hivi hapa ya dola laki moja na ishu ikitiki nakuingizia dola laki moja ingine”.

Ilibidi Mr. Michael atoe miwani yake toka machoni akajifuta kwa kitambaa machoni kisha akajifuta uso mzima jasho lililokuwa linachukua hatamu.

“Wewe watu wale wa nini? Unataka kutengeneza silaha za kibaiolojia au nini hasa ulichonacho kwa ajili ya watu wale?”.

“Wale watu kuna tajiri anawahitaji lakini hakuishia hapo anamtaka na Agent Kai akiwa na watu hao na yeye ndiye anagharamia huu mchongo wote na ndiye aliyenishawishi mimi kufanya hivi”.

“Logan ujue mimi siamini unachoniambia, hao maprofesa wako wapi? Na wapo na familia zao vilevile au?”.

“Siwezi kukwambia wako wapi rafiki yangu… Nakuamini lakini si kwa kufikia hadi kukwambia walipo”.

“Lakini unao wewe bwana Logan… Unajua Mr. Logan mimi na wewe ni marafiki wakubwa sana ila hukunishirikisha kuanzia kwanza kuhusu jambo hili… Je wale wapelelezi wetu wawili wa kiume na yule wa kike wote hao kikundi chako kikiongozwa na wewe mnahusika pia?”.

“Michael maswali yako yananiogopesha ni kama unanifanya nianze kujutia maamuzi ya kutaka kuomba msaada wako… Tafadhali usinifanye nijutie kujuana na wewe na usinilazimishe nikavunja ukaribu tulionao”. Mr. Logan alianza kupatwa na wasi wasi na msimamo wa kiuongo aliokuwa akiuonyesha Mr. Michael huku dau na kutokuwa na upendo wa kweli dhidi ya taifa lake la Marekani kulishamshawishi atoe huo msaada.

“Kwanza mi nataka nijue tajiri gani anawahaitaji hao watu na kwanini anawahitaji? Na unaona kama mimi mjinga navyokuuliza haya maswali… Ukweli maswali haya ni muhimu mimi kukuuliza hili ubongo wangu upokee unachokihitaji wewe sababu licha ya kuwa mimi asili yangu si Marekani lakini kumbuka wamarekani wengi sisi ni wahamiaji tu hivyo mimi ni mmarekani na sifa kuu ya mmarekani ni uzalendo kwa nchi yetu, nitakuwa tayari kushawishika baada ya wewe kunifungua akili yangu nikapata kuyajua mengi nisiyoyajua… Dola laki mbili ni pesa ndefu lakini je? naingiza hasara gani kwa taifa langu, ndicho hasa kilichopo… Wewe umeamua kunishirikisha kwakuwa unaniamini unaonaje ukiniamini kwa yote na kunijibu yale nayoyaona ni sahihi mimi kuyajua Mr. Logan”.

“Michael! Ulianza vizuri sana wakati tunakaa hapa.. Ulitaka kujua kitu gani kinanisumbua rafiki yako ndipo unisaidie na msaada wenyewe naotaka kwako ni kutupa maelezo wapi kafikia, wapi yupo katika muda huo ambao wewe utakuwa umemuona… Kwa sababu naamini mtu kama yule lazima afike ubalozini kwenu au nyinyi maafisa wa ngazi za juu ubalozini lazima mjue amelala wapi kwakuwa anawaamini wenyeji wake”.

Dakika mbili zilipita kila mmoja akitafakari lake huku wakiyaburudisha makoo yao kwa luc belaire. Kimya kilichofanya Mr. Logan kuwasha sigara anayovuta mara kwa mara aina ya Dunhill akapiga mikupuo mitatu baada ya kutoa moshi tu, Mr. Michael akachomoa na yeye pakti yake toka kwenye mfuko wa shati alilovaa na kuibuka na sigara yake anayopenda kuvuta aina ya Pall Mall akaiwasha wakaanza kuvuta wakitafakari maongezi yao ambayo hayakuwa yamefikia muafaka.

“Logan………….. Nafikiri siwezi kukuangusha rafiki yangu… Niko tayari kukusaidia… Leo huyu nilijaribu kufuatilia habari zake kwa kweli habari zake ziko kisiri sana lazima uwe makini na lazima akuogopeshe huyu mtu anapochunguza jambo uwa kama ana kismati kwakuwa mambo kwake uwa si magumu sana maana ni kama yanakuwa yanamfuata yeye, katika masiha yangu sijawai kuonana naye hivi kwa hivi bali nishawai kumuona Washington akiwa ana pewa tuzo ya heshima baada ya kumaliza kazi ambayo Raisi wa wakati huo alifurahi sana hivyo namjua vizuri kwa sura…. Pale ubalozini kuna mwanamke kamuweka alimleta jana usiku, naomba nipe muda kesho asubuhi nikifika kazini nianze kufuatilia yule mwanamke ni nani na kwanini kataka apewe hifadhi pale na kisura ni mtu wa hapahapa Malaysia si mmarekani”. Kama vile sigara ilimbadili mawazo bwana Michael aliamua kukubali kuwa atamsaidia bwana Logan akakubali kuwa msaliti wa wenzake kwa maslahi yake.

“ Ahsante Michael kwa kukubali kunisaidia, unajua jamaa ananitisha haonekani kwenye rada zetu ila tunapata taarifa ya matukio tu, huwezi kuamini mtu mmoja huyo mpaka sasa ameua watu saba waliokuwa chini ya malipo yangu… Huyo mwanamke aliyeletwa ubalozini kwenu ni mwanamke wa aliyekuwa mtu wangu wa kazi, amemuokoa wakati alipovamia jengo letu la Broga hill 1st Hiltop… Tulipitisha mwanamke huyo auwawe kwakuwa tunahisi ana siri anazozijua juu yetu”.

“Hii kazi atakuwa amepewa moja kwa moja Balozi bila ushirikiano hata wa kiongozi wangu wa kitengo cha kidiplomasia Mr. Abraham… Sababu nilimuingia Abraham kijanja leo akanijibu majibu yaliyoonyesha hajui lolote juu ya Kai”.

“Kazi ipo Michael… Naomba unisaidie nilichoomba mambo mengine niachie mimi… Muda umeenda sana naona meseji za Zahra zimeanza kuingia kwenye simu, acha nikusainie hundi ya pesa niliyokuahidi wewe kesho asubuhi ukiingia ofisini jaribu kuangalia inakuwaje pia mfuatilie mwanamke niliyekwambia anatakiwa kuuwawa kisha unijulishe kama anaweza kuingia mtu wangu mmoja akammaliza humohumo ubalozini”.

“Mmmh! Hilo gumu sana Logan… Ubalozi wa marekani unalindwa vizuri sana pengine akubali mtu wa mulemule ndani kummaliza hasa wapishi lakini kuingia mtu kutoka nje sahau hilo acha tuangalie njia zingine na ninaamini kesho asubuhi nikiingia tu nitayapata mengi kwa kutumia cheo change na kuaminiwa wangu”.

“Nitashukuru sana Mr. Michael naomba usivunje uaminifu wangu kwako”.

Mr. Logan alisaini hundi akijaza dola laki moja na kumkabidhi Mr. Michael kisha ya hapo wakaagana.

** ** ***

“Sura hii unaonekana kama wengi wa wenyeji wa watu wa hapa Malaysia ile ya Ramji ilikuwa na uarabu mwingi ndani yake, hahahahahah hahahahah! Kazi yenu kiboko uwa mnaandaa kabisa na hivi vitu…. Nitakuita jina gani kwa sura hii?”. Alikuwa akiongea Shufania Mahamud wakiwa kwenye gari na Agent Kai aliyekuwa akimalizia kuvaa sura ya bandia itakayomuonyesha muonekano wa tofauti na ule wake wa asili na hata aliokuwa akiutumia hapo awali muonekano uliomtambulisha kama Faheem Ramji.

“Lakini si nimependeza? Vipi rangi yangu na rangi ya hii ya sura vinaendana?”. Hakujibu swali aliloulizwa bali naye alimtandika maswali mawili.

“Hata hujapendeza… Anayependeza machoni mwangu ni Kai Hamis wengine wote hawapendezi machoni mwangu…. Rangi! Rangi tofauti ipo kwa mbali lakini mpaka mtu achunguze, watu wenye rangi ya chocolate kama yako hapa Malaysia ni wengi tu, hivyo hilo usitie shaka… Natamani niipe jina hii sura”. Walitizamana sana kwa sekunde mbili kisha Agent Kai akamkonyeza Shufania wakajikuta wanacheka kwa sauti.

“Jina tayari lipo.. Ila si mbaya ukitoa lako ingawa halitatumika ila unaweza bahatisha ukakuta umelenga maana na wewe si jasusi hivyo vingi unaweza kuwa unavihisi halafu vinakuja kwenye usahihi”. Kicheko cha furaha kati yao kiliendelea wakifurahi kwa vitendo zaidi.

“Akhuuu! Mi si mtabiri kama lipo liseme lianze kutumika”.

“Akhuu ndiyo nini? Kiarabu icho au?... Okay! Fungua zipu ya chini hapo kwenye begi utakutana na bahasha kubwa ya plastiki itoe”. Kai akamuelekeza Shufania cha kufanya na binti akanyanyua begi ambalo mara zote na kila mahali Agent Kai uwa nalo kisha akaliweka kwenye mapaja yake halafu akafungua zipu na kuitoa bahasha aliyoelekezwa akainua macho kumtizama Agent Kai.

“Fungua ndani kuna vitambulisho toa cha rangi ya bluu chenye bendera ya Malaysia, kisha soma ndani kimeandikwa jina gani na kina picha yenye sura gani?”. Akaongea Kai huku anatabasamu.

“Eeeh! Ulishaandaa hadi kitambulisho?... kina picha yenye sura hii uliyovaa… Aiseee sikuwezi Kai… Wewe hivi ulipiga muda gani picha hii na ukatengeneza kitambulisho kabisa?”.

“Hahahahahah! Hahahahah hahahahaah! Fundi… Fundi hatari, fundi wa hatari ndiye aliyeandaa hivi vitu baada ya kuwa kayasoma mazingira ya hapa akaamua kucheza sehemu yake kwa mtindo huu, hata mimi sikujua kama ataniandalia vitu hivi katika kiwango kikubwa kama hiki sababu mara nyingi vitu hivi uwa jasusi mwenye kiwango cha juu kama mimi ujiandalia mwenyewe lakini baada ya kusoma mazingira…. Hivi vitambulisho vyenye hati ya uraia mi nisingevijua viko vipi? Vina alama gani? Hadi sura hizi alizozitengeneza ni yeye ni Balozi wetu hapa Malaysia anaitwa Kapteni Jones Lebrons”.

“Kweli fundi.. Jina la kwenye kitambulisho Abdul Raheem Yussuf, fundi wa lifti cheni za maghorofa, mkazi wa jimbo la Pokok Sena mkoa wa Kedah”. Alikuwa akisoma huku anacheka kwa furaha.

“Kuanzia sasa nikiwa kwenye sura hii naitwa Abdul Raheem Yussuf, niite Abdul tukiwa pembeni au katikati ya watu”.

“Sawa jasusi wa CIA, Jasusi wa kimataifa mume wa fulani.. Hahahah! Sitaki umbeya”.

“Mmmh! Sawa jasusi la kike Shufania bint Mahamud mke wa fulani mtarajiwa”.

“Hahaha! Acha kucheka, sikia… Umenikumbusha… Tukiwa kwenye watu wasiojulikana nitakuwa nakuita …. Mume wangu Abdul”.

“Hahaha! Nami naitikia naaam mke wangu”.

Waliangua kicheko kikubwa sana na kugongesha viganja vyao vikalia pwaah!

Muda huo saa moja kasoro dakika chache sana magharibi ikiondoka kwa kasi kukimbilia insha walikuwa wako ndani ya gari aina ya Range Rover waliloenda kulichukua kwenye maegesho ya magari ya jengo la River Bank mtaa wa James Mosque, wakaondoka nalo hadi hapa walipo sasa mitaa wanayoishi wahindi kwa wingi sana katika jiji la Kuala Lumpur, wakapaki gari karibu na hekalu wanaloabudu wahindi wanaomuabudu wanayemuita mtakatifu Shiva eneo la Batu Caves, mtaa huu ulikuwa umetulia kabisa tofauti na mitaa mingine iliyo karibu na katikati ya jiji hili kulikuwa hakuna pilika pilika za watu kwa wingi zaidi ya wale wanaoenda kwenye jengo la hekalu la Shiva.

“Ratiba yetu Mrs. Abdul inaonyesha unatakiwa kumpigia simu shosti wako Sheila umuulize juu ya yale tuliyopanga utamuuliza”. Akakumbusha Agent Kai

“Nilizima simu Mr. Abdul kwa maelekezo yako… Vipi niiwashe au kuna namna kwanza?”.

“Iwashe tu halafu ukimaliza kuongea utaizima tunaondoka hapa Shiva Temple… Kama kuna wanaofuatilia simu yako watakuja huku tukiwa tushaondoka”. Akajibu mtaalamu.

Shufania akaitoa simu yake aina Samsung GalaxyNote8 baada ya kutoa akaiwasha baada ya dakika mbili ikawa tayari ishakaa sawa, akatafuta namba za rafiki yake Sheila na kuziendea hewani. Baada ya kuita miito mitatu tu ikapokelewa na upande wa pili.

“Niambie shost?”. Sauti ya upande wa pili ikaongea ikionyesha dhahiri ina shauku.

“Shosti niko poa, vipi hali yako wewe?”.

“Mi niko poa! hofu yangu kwenu tu, vipi baba anaendeleaje?”.

“Mwenzangu eeeh! baba sijui hali yake toka nikuage asubuhi nikikwambia napokwenda mpaka saivi mwenzio sijafika nyumbani siku imekuwa ndefu sana kwangu”.

“Eeeeh! Shufania unaniambia kweli au unanitania?”.

“Ndiyo! Sheila niko na Ramsey mpaka sasa”.

“Shosti ndiyo kusema umenogewa kwa mmarekani mweusi mpaka saivi?... Shufania kwa hiyo ina maana hujui kama baba yako amelazwa?”.

“Eeeeh! Baba amelazwa?”. Akaongea kwa sauti kubwa mpaka Agent Kai akainua uso kumuangalia maana muda wote huo alikuwa na jambo anafuatilia kwenye simu yake.

“Ndiyooo Shufania, baba yako amelazwa alipelekwa hospitali na mama yako muda wa saa kumi na moja jioni… Na walikupigia simu kukupa taarifa wakakukosa hewani ikabidi mama anipigie mimi kunipa taarifa, mi kwakuwa uliniaga unakwenda wapi nikawaambia nitakufuatilia ulipokwenda na kukupa taarifa”.

“Mamaa yangu! Nilizima kweli na kulikuwa kuna sababu mimi kufanya hivo Sheila sikufanya makusudi, ipo siku utajua sababu shosti wangu.. Mungu wangu msaidie baba yangu… Nilimuacha anakohoa sana asubuhi sikujua kama itafikia kulazwa ingawa nilimshauri aende hospitali kama anavyoenda kila mara anaposhikwa na kifua chake hiki”.

“Habari ndiyo iko hivyo shosti, usiniambie ulizima simu hili mmmm na mmmh! Katika mtoko wako wa kwanza naye, najua shosti ulisema haki hiyo ni ya mumeo atakayekuoa… Tuyaache hayo sababu ni yako binafsi na una uhuru na chochote ulichonacho… Nilitamani niende hospitali kumpa kampani mama lakini na mimi mtoto wangu anaumwa na niko peke yangu, baba yake ameenda kikazi Sarawak”.

“Usijali rafiki yangu mpenzi… Ahsante kwa taarifa yako”.

“Ahsante na wewe pia, tafadhali kuwa makini shosti wangu wazazi wanakutegemea sana kama unavyojua wadogo zako wao wako chuo muda wote, hivyo wewe ndiyo kila kitu… Tuombe Mungu awe amesharudi katika hali yake ya kawaida baada ya huduma za kidaktari”.

“Inshaallah! Tunamuombea iwe hivyo… Atakuwa ameenda hospitali ya rafiki yake dokta Qassim?”.

“Ndiyo! Mama ameniambia jina hilohilo la Dokta Qassim hospital ya Gleneagles Hospital wodi ile ile anayowekwa mara zote anapolazwa kwa ugonjwa wake huo wa kifua”.

“Basi nitaenda mara tu nimalizapo kuongea na wewe… Nina shida shosti inayohitaji msaada wako na ndicho hasa kilichonifanya niwashe simu muda huu kukupigia na kukutana na taarifa hii ambayo kama ningeendelea kutoipata ingeleta picha tofauti kwa wazazi wangu”.

“Niambie tu mdogo wangu, kama unataka niwe msimamizi wa harusi niko tayari huna haja ya kuniambia shosti”.

“Mmmh! Bado sijafika huko shosti ikifikia utajua tu… Ningependa kujua kama kuna mtu aliyekuuliza chochote kuhusu mimi na Ramsey?”.

“Yupo… Yupo ni yule mzee Abubakar Morsi aliniuliza juu ya duka la baba yako la kuuza kanzu liko wapi?”.

Kwakuwa Shufania alikuwa kachomeka earphones masikioni na alipofikia kumuuliza swali hili shosti wake aliona ni wakati wa kuwa ana share na Agent Kai hili naye asikie akampa earphone ya upande wa kushoto naye akaipokea na kuchomeka kwenye tundu la sikio lake.

“Eeeh!”. Kabla hajaendelea kuongea Agent Kai akamuonyesha ishara azibe maiki ya kuongelea na Shufania haraka akaziba.

“Huyo mzee Abubakari anajua kama baba yako ana duka la kuuza kanzu?”. Agent Kai akamuuliza kwa kasi.

“Mi sijui sababu sijawai kumwambia pengine kaambiwa na mtu mwingine”.

“Kumbe wapo wanaojua?”.

“Wapo baadhi ya watu wanaojua kati ya wafanyakazi wenzangu”.

Kai akamuonyesha ishara ya dole kuwa aendelee kuongea na upande wa pili.

Mwisho wa sehemu ya ishirini na tatu (23)

Kuungua kwa mpini si mwisho wa kulima,

ENDELEA NA UTAMU..!

“Shosti!” Akaita baada ya upande wa pili kuita mara kama tatu na ulipoona kimya nao ukanyamaza.

“Shosti nipo, mbona ulikuwa huongei?”.

“Network nafikiri maana nami nilikuwa sikusikii… Nilitaka nijue mzee Abubakari kwani anajua kama mimi baba yangu ana duka la kuuza kanzu?”.

“Mimi sijui ila sikuona haja ya kumuuliza lolote zaidi ya kumuelekeza lilipo maana si mteja bwana”.

“Sawa sawa! Vipi yule Mzee Rafael aliyetukuta tunaongea akatuambia kuwa kuna mgeni wa Ramsey anataka kujua kama yupo. Alikuuliza chochote kingine?”.

“Hapana hakunifuata tena ila nilimuona ana pilika nyingi sana leo tena za ndani ya hotel kitu ambacho si kawaida yake maana mara nyingi uwa anaishia huko zilipo kazi zake… Nafikiri ana wageni wake ambao ni rafiki zake waliopanga hotel hii leo sasa alikuwa anawaonyesha ukarimu wake”.

“Hivi ushawai kusikia anaishi wapi yule mzee maana kuna jambo amenichanganya sana natamani kujua zaidi toka kwake”.

“Shosti toka lini na wewe? Achana naye asikuumize kichwa mzee kama yule… Sidhani kama ana lolote lingine”.

“Sheila ujue mzee yule hajawai kuongea na wewe wala na mimi huoni kuna kitu hapo?... Okay! Sikiliza naomba msaada wako kama nilivyotangulia kukwambia awali na ukanijibu nikwambie tu na hilo ndiyo hasa nalohitaji kwako”.

“Sawa mdogo wangu siwezi kugoma chochote kwako ingawa sikufikiria kama lina umuhimu sana kwako… Yule mzee mimi sijui anapoishi ila kuna mtu ambaye ndiyo rafiki yake mkubwa ni huyu huyu mzee Abubakari Morsi mfanya usafi wa jikoni kwetu”.

“Ooooh! Good huyo huyo atatusaidia na mimi nishawai kuwaona wakiondoka wote tukiwa kwenye treni ya mwendo kasi… Namba yake naamini unayo maana alikuwa anakusumbua sana kizee kile kilikuwa kinakutaka kipindi kile”.

“Nakutumia muda si mrefu mpaka niiangalie kwa kupekua simuni”.

“Haya naisubiri unitumie… Na acha niwai hospitali kumuona baba”.

“Haya shosti… Wai ukamuone baba na umtoe wasi wasi mama, mpe hi shemeji yangu mtarajiwa”.

“ Haya ahsante dada kwa yote”.

Waliagana na kukata simu, hali ilibadilika usoni mwa Shufania alipooza ghafla baada ya maongezi yale habari za kusikitisha juu ya kulazwa kwa baba yake zilimuuma sana.

“Pole sana mpendwa… Anasumbuliwa hasa na nini? Baba”.

“Baba ana matatizo ya kifua mpaka anatoa damu akianza kukohoa, tatizo lilimuanza wakati tunakimbia vita Syria. Tulikimbia kwa chombo cha jahazi bahari ya pacific tukiwa watu wengi tuliokaa kwa kubanana, sasa wakati tupo katika safari chombo kilikuwa kinasukwa sukwa kwa mawimbi makubwa hali ikawa ya kutisha sana na bahati mbaya ilimkumba baba baada ya jahazi kupigwa na wimbi kubwa zaidi watu tuliokuwemo tukiwa tumeshikana kwa mikono katika miili yetu wanawake wengi tukiwekwa katikati hatukupatwa na tatizo kubwa zaidi ya wote kupiga mayowe ya uoga lakini muda kidogo makelele ya walio pembeni yakazidi zaidi sababu baba na wanaume wengine wanne walitupwa baharini… Bahati nzuri kwetu miongoni mwa wanaume tuliokuwa tukikimbia nao vita katika jahazi lile walikuwemo wanaojua kuogelea hivyo walipiga mbizi kuwaokoa watu wale wanne… Lakini hiyo ikawa ndiyo tatizo kuu la baba maana katika maji mengi aliyokunjwa ipo aleji fulani iliyo mdhuru, amekuwa katika hali hii ya kurudiwa na kifua kama hiki kilichomtokea leo, akicharukwa inakuwa kama hivyo, hata kazi yake ya udaktari bingwa wa magonjwa ya macho aliifanya katika hospitali hiyo hiyo aliyolazwa lakini ilibidi wamuachishe kutokana na kuwa katika hali isiyotabirika”.

“Poleni sana na pole yake… Twende tuwai ukamuone, pia nafikiri mama atakuwa yupo huko huko hospital tunatakiwa kumuwai hili asirudi nyumbani kwa usalama wetu na wasiwasi na urafiki wa Mzee Rafael na Mzee Abubakar Morsi pamoja na uulizaji wao wa duka la kuuzia kanzu kwa baba yako”.

“Ni kweli inaweza kuwa na uhusiano kama usemavyo, nimeanza kuwa na wasiwasi sana na maisha ya familia yetu Kai”.

“Usiwe na wasiwasi mrembo wangu, anapokuwepo Agent Kai ujuwe hakuharibiki kitu kabisa upande aliopo uwa salama… Shufania ningependa unijue zaidi mimi ni nani lakini si kirahisi sana … Nitafanya yote kwa haraka kuwaweka wazazi wako nje ya tukio lolote baya na hata wewe pia”.

Akasema Agent Kai huku anarudisha gari nyuma toka pale walipokuwa wamepaki kwa ajili ya kuondoka.

** ** ***

Saa tatu kamili usiku ndani ya nyumba iliyo kama ghala tu kwa muonekano wa haraka ambayo wenyewe walikuwa wakiita nyumba ya nyoka kwa matumizi yasiyofahamika, sababu ilikuwa ni nyumba ya siri ambayo ndani yake yalikuwa yakifanyika mambo yasiyo mazuri lakini yalikuwa hayajulikani kwa serikali ilikuwa ni nyumba iliyojulikana mmiliki wake kuwa ni mmalaysia mwenye asili ya India anayefanya kazi kampuni ya Logan Group Of Business ajulikanaye kwa jina la jina la Ghulam Qaresh.

Ilikuwa ni nyumba ghala ambayo serikali ilikuwa ikijua Bwana Ghulam Qaresh ameipangisha kampuni anayofanya kazi kuhifadhi baadhi ya mali zao ambazo zilimaliza matumizi lakini hazina pa kwenda yaani kama magari mabovu na vifaa vyake, mashine za kwenye vituo za mashine (Petrol station) ambazo wamefungua na kuweka mpya na mambo mengine mengi tu.

Lakini kazi ingine ya nyumba hii ilikuwa ni kuleta watesi wao wanaowasumbua katika kazi zao zisizojulikana kwenye macho ya watu wengine na hata wanasayansi walipotekwa wakiwa na familia zao mahala pa kwanza waliletwa hapa wakafichwa mpaka walipoondolewa kupelekwa huko walipo sasa, wapelelezi wa kiume wawili waliotekwa mwanzo na hata wa kike detective Marie hapa ndipo baada ya kuanzia kule Nadia Golf kwa vijana waliokuwa wakiunda kikundi cha SDB kwakuwa ndiyo waliwatia mitegoni kituo cha pili kilikuwa hapa kabla hawajapelekwa huko walipo pamoja na wanasayansi walio na familia zao.

Nyumba hii ipo eneo linalofahamika kama Kepong Metropolitan Park ambalo ni eneo lililo pembezoni mwa ufukwe wa ziwa linalojulikana kama Metropolitan Lake nje kidogo ya jiji la Kuala Lumpur, hili nalo serikali Malaysia imelitenga eneo hili ukubwa wa hekta 95 kama hifadhi ukiiacha hifadhi ndipo yapo makazi ya watu na ndipo ilipo nyumba hii eneo la kijani kibichi kuanzaia misitu hadi nyasi zilizo pembeni mwa barabara.

Usiku huu ulikuwa usiku wenye nusu presha nusu amani kwa bwana Logan, aliamua kuja kukutana na watu wake katika nyumba hii ya nyoka kutoa aliyonayo na pia na yeye kusikiliza wenzake wana jambo gani, eneo hili la Kepong Metropolitan lilikuwa ni eneo lenye upepo unaojikusanya na ubaridi lakini kwake bwana Logan bado alikuwa hajisikii amani na alikuwa akijua anapokuwa anajisikia hivi basi kwake uwa ni tatizo licha ya muda wa saa moja kuwa alifanya kikao na bwana Michael Joram na kupewa matumaini fulani lakini hakuwa na amani na hakuwa anajua kwanini anakuwa hana amani licha ya kujiamini kote alikokuwa nao miaka yote na kutokuwai kufeli kwa mpango wake wowote katika kipindi chote.

Mambo yaliyotokea siku mbili tu yalimshusha amani aliyokuwa nayo, moyo wake ulikuwa ukidunda mdundo wa tofauti kila alipopekua simu yake na kukutana na picha ya Agent Kai na muda mwingine alikuwa akiiangalia picha hiyo na kujikuta anasonya mwenyewe na akijiambia sifa zote anazoambiwa na marafiki zake toka sehemu mbalimbali anazowaamini ni kama wanamdanganya.

Muda mfupi toka aingie kwenye nyumba alikuwa kamaliza sigara tatu kwa kuvuta ikikaribia kuisha anaitupa alifanya hivi hili ajiweke katika hali ya kawaida huku akisubiri idadi ya aliowaambia wafike hapo mara moja itimie.

Kwenye veranda hakuwa peke yake alikuwa na baadhi ya watu wake waliowai kufika na hata wengine walikuwa wakifika kwa muda ambao unafuatana na mara wakaenea idadi aliyohitaji iwepo.

“Tumebakiza masaa kama ishirini na sita kati ya masaa ambayo nimepewa mimi niwe najibu kwa watu walionipa dili la kazi hii iliyo mikononi mwetu ni masaa machache sana kwetu, yamekuwa machache kutokana na ugumu wa jambo ambalo limepewa umuhimu na watu walioshika biashara hii”. Akasema Mr. Logan kisha akawaangalia kwa zamu watu waliokaa kwenye veranda hii yenye masofa ya rangi nyeusi lakini ikiwa ni veranda isiyo na mbwembwe za maurembo mengi mengi zaidi ya masofa yaliyopangwa pembeni yakirandana sambamba na ukuta ulioizunguka hii veranda.

Ilikuwa toka kikundi hiki kisicho rasmi kiundwe walikutana eneo hili wakiwa wote kama mara mbili tu na hii ndiyo ilikuwa mara ya tatu, mara zote walikutana wakiwa wachache tu. Ilikuwa si kawaida kwa Mr. Logan Puteri kuwaita wote kwa mara moja huku nyumba ya nyoka, mara zote alipenda kuwaita kwenye mahotel, night club au zilipo nyumba zake zisizo nyumbani kwa mke wake Zahra.

“Jioni hii nimetumiwa e-mail toka Secret police officer wa Korea Kaskazini anasema hawatatuma ndege kisiwani Borneo bila sisi kuwahakikishia kuwa mikononi mwetu tuna Agent Kai”. Akaendelea kuongea Mr. Logan na kufanya wote walioko pale kuinua vichwa vyao kumuangalia kiongozi wao.

“Msistuke sana, siamini kama masaa ishirini na sita yatapita bila kumpata mtu huyu ikiwa mimi Logan Puteri nimeamua kutumia akili yangu hadi ya akiba kumtia nguvuni mtu huyu mtu mweusi anayependa kuua watu wetu kwa kuvizia… Lakini lingine ambalo mimi linanipa imani kwa nguvu zote ni kuwa muda mfupi wakati niko njiani nakuja huku rafiki yangu mmoja wa Iran anayefanya kazi shirika la kijasusi la Iran alinipigia simu na kuniambia maongezi yake na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo yanaendelea vizuri asubuhi ya kesho kunaweza kuwa na badiliko moja sababu wao wanamtaka profesa mmoja na familia yake ila fungu lao si kubwa sana kama fungu la Pyongyang, hivyo pale Putatan tuna uhakika jumapili kichwa cha profesa moja kinaweza kutuingizia dola milioni 100 tofauti ya dola milioni 50 ambazo kichwa kimoja serikali ya N.K wako tayari kutoa dau la dola milioni 150… Ni pesa nyingi sana inayoweza kutusababishia tukaacha hii kazi nakuendelea na biashara zetu kitajiri zaidi maana tutakuwa mabilionea kwa pesa ya Malaysia Ringiit… Tunaweza tukafanya biashara hiyo na Iran huku tukisubiri biashara na Korea Kaskazini bila kujali mtu mmoja atakuwa kapungua katika idadi yao na hata pesa waliyotanguliza kama posho kwetu hili iturahisishie kufanya kazi hii.. Nafikiri kuwaambia kuwa alijaribu kutoroka walinzi wakamshuti risasi na kwakuwa ilimpata sehemu mbaya akafa”. Aliongea Mr. Logan Puteri kisha akawasha sigara na kuvuta mikupuo mizito kama mitano kisha akatoa moshi kwa madaha akiupuliza kuelekea juu.

“Kichwa kinaniuma sana juu ya huyu mtu kidudu mtu ngozi nyeusi, amekuja hapa KL na kaharibu mipango mizima ilivyokuwa inakwenda… Laiti asingekuwa amefika hapa au hata kama amefika na ningekuwa sijamtaarifu LI-Nam Jo wa Special Secret Police tusingesumbuka naye zaidi ya kumkwepa tu… Ukitaka kuona hapa lazima vichwa vituume dau waliloweka na wao wenyewe kuna habari walijaribu majaribio sita ya kumtia mikononi mwao wakashindwa, hili ni jaribio la saba kwao na wamesema hawawezi kupata nafasi ya wazi kama hii… Angalia dau la profesa mmoja wameniambia ni dola milioni 150 na dau la Agent Kai ni dola milioni 200 na tizama waliposikia tu juu ya uwepo wake tu walinipa posho pale pale hili zisaidie juu ya hili”. Alinyamaza kidogo hapa baada ya Mr. Nawaz Patrash kuonyesha ana swali la kuuliza.

“Sema Nawaz”. Akamruhusu.

“Ni kweli kuna kitu kikubwa sana kwa huyu mtu na ninaamini tusipokuwa na umoja hatutafika popote… Mimi leo nilikuwa nawasiliana na mtu ambaye najuana naye yupo humo humo Special Secret Police ya Korea Kaskazini ameniambia jamaa huyu alimuu kiongozi mkuu wa kikosi chao miaka mitatu iliyopita nchini Syria na kuna watu wao wanne wenye uwezo wa hali ya juu sana leo usiku wanaingia hapa Kuala Lumpur kuhakikisha wanampata wao wenyewe, nafikiri hili Mr. Logan hulijui lakini habari iko hivyo”. Akafikisha alilonalo Mr. Nawaz Patrash.

“Eeeeh! Kweli mi sijui hilo… Itabidi nimuulize Li-Nam Jo, kwanini wananificha?...” Akanyamaza tena baada ya Ghulam Qaresh naye kuhitaji kuongea.

“Mmmmh! Ghulam sema!”. Akamruhusu.

“Logan… Dola milioni 200 ni nyingi sana na kama ulivyosema awali inaweza kutufanya wote hapa tukawa na kipato ambacho mtu akiamua kufanya biashara ni mtaji tosha icho atakacho gawiwa… Lakini kama N.K wameona watume mtu hapo hamuoni kuna walakini? Hamuoni wanatuingilia kazi waliotupa?”. Akaongea Mr. Ghulam.

“Ghulam! Maswali yako ni mazuri sana itabidi tuyapatie majibu hapahapa au kabla ya asubuhi… Ila naamini wao hawatamfikia kirahisi sababu sisi ndiyo tushaweka mipango sawa.. Ebu Nawaz tueleze wote hapa mipango ilivyoenda ingawa haina mafanikio mpaka sasa’. Akasema Mr. Logan kisha akamgeukia Mr. Nawaz na kumpa nafasi aeleze mbele ya kabineti yote pale.

“Kila tulichopanga na kutaka kiwe kama njia ya kutusaidia tunampata Agent Kai kilikwenda kama tulivyopanga, tatizo kama ulivyonena hakuna lililofaulu kwa upande wetu imekuwa hasara kwa kuwa tumepoteza rasilimali watu wawili na gari moja, jamaa ametutangulia hatua mbili mbele kwa kweli ni mtu wa hatari ambaye sijawai kukutana naye lakini hisia zinaniambia hivyo… Kosa kubwa ambalo tumefanya au niseme mimi muongoza mpango nimefeli nilipowaambia Meloo na Daus wamfuatilie yule binti ambaye mahitajio yetu atusaidie kutufikisha kwa mlengwa wetu, walipomuona yupo na mwanaume hatukumtilia maanani kuwa anaweza kuwa ndiyo Agent Kai ila baada ya tukio ndiyo nilikumbuka kuchukua kompyuta na kulinganisha picha za mlengwa wetu na zile za kama mwarabu au mhindi katika upana wa mwili na urefu nikapata jibu tumedanganywa ni kweli ni Agent Kai, nilistuka tukiwa tushachelewa alishatuacha kwenye mataa kwa uzembe mkubwa sana… Naomba niwaahidi wote hapa nikiwa kama muongoza mpango huu ulioshikilia uti wa mgongo wa pesa tunazotamani ziingie kwenye akaunti zetu, sitafanya uzembe tena wa kitoto kama niliofanya leo kana kwamba mimi ni mgeni wa mchezo huu”. Nawaz akajieleza kwa wenzake na boss wao.

“Makosa yapo katika michuano kama hii… Mpaka saivi naamini huyu mtu licha ya kuwa yupo hatua moja mbele lakini hana analolijua juu ya watu wao waliopo Putatan… Ima tupigane tuwawai majasusi wa Korea Kaskazini watakaoingia usiku huu wa leo.. Wanatakiwa wao watupe pesa sisi sababu kama wameanza hivi ujue kuna wasiwasi tunaweza tukagongana nao sehemu tukajikuta tunapambana nao bila sababu na kusababisha taharuki kwa serikali hizi mbili ambazo tayari zina uhasama kutokana na mauaji ya juzijuzi ya kaka yake na Raisi wa Korea Kaskazini aliyeuliwa kwa sumu poda ya kibaiolojia pale airport na mwanamke wa Indonesia anayejulikana kama Siti Asiyah, bado Korea Kaskazini wanasema hawahusiki ingawa sumu ile inatoka nchini kwao na hata dola elfu tisini aliyoahidiwa kulipwa Siti Asiyah inasemekana imeingizwa kwenye akaunti ya ndugu yake huko Indonesia ikitokea Korea Kaskazini… Angalia serikali ya hapa imewatimua wahamiaji zaidi ya 500 toka Korea Kaskazini waliokuwa wakiishi kisiwa cha Borneo, kwa kisingizio wanaishi bila kibali… Ukweli uhusiano baina ya ncho hizi umedorora sana, Hofu inatakiwa iwepo”. Akaongea kirefu Mr. Logan kisha akajifuta jasho kwa kitambaa cha jasho alichotoa mfukoni mwake kisha akasogea kwenye meza yenye vinywaji akanywa funda nne za kinywaji chake Luc Belaire ambacho uwa hakosi chupa kadhaa kwenye gari kila anapokwenda uenda nazo kama vile anakitangaza kibiashara kinywaji hiki.

“Ebu tusawafikirie sana… Tuangalie mpango ulivyo sasa… Endapo mambo yataenda kama tunavyotaraji ndege hazitatua tena nchini Laos kama nilivyowai kuwaambia baadhi ya wenzangu hapa, ndege itatua kisiwa cha Borneo mkoa wa Sarawak, divisheni ya Bintulu district. Kama mjuavyo kisiwa kile kimegawanywa pande tatu nchi ya Brunei, Indonesia na Malaysia. Hivyo kwa maelekezo niliyopewa leo kule Bintulu kuna kijiji kinaitwa Jepak kwenye mpaka wa hifadhi ya Tanjung Batu Beach ambapo kama una darubini unaweza kupavuta Indonesia eneo la Kalimantan na ukaliona vizuri kabisa. Ndege ndogo za watalii mara moja moja utua kijijini hapo, inasemwa mara moja moja sababu mara nyingi ndege uenda kutua kusini magharibi mwa kisiwa sehemu ijulikanayo kama Miri ambako mbuga za Similaju Park na Tumbina Park zimepakana ambako kuna maporomoko ya maji yanayowavutia watalii kwenda kule kwa wingi.. Utulivu na kutotumika mara kawa mara ndiyo imekuwa ni uzuri sisi kupeleka mali zetu kijijini Jepak na kuwakabidhi wahusika nasi tukaingiza pesa tunayoitarajia.. Tayari kibali cha ndege cha kutua kwenye uwanja ule kinatengenezwa kuwa kuna watalii wamekodi ndege hiyo moja kwa moja kuwachukua pale”. Maelezo marefu ya Mr. Logan yalitiririka kwa urefu kisha akalowanisha koo lake kwa kupiga funda kadhaa za kinywaji.

“Usiku huu wataondoka hapa Kuala Lumpur, Mr. Hassan Saddiq na Mr. Zhing Lae kuelekea walipo mateka wetu Putatan, Sabah State… Nawatanguliza sababu kazi ya kutengeneza sura za bandia tutakazowavalisha mateka wetu wakati tunawasafirisha imekamilika kwa asilimia themanini… Mimi nitaelekea Putatan bila kujali lolote ifikapo kesho saa moja jioni, nafanya hivyo hili kwenda kuandaa wale watu waondoke pale kwenda Putatan siku ya jumapili…. Usiku wa kesho mpaka siku ya jumapili kutakuwa hamna kulala kutokana na pilika pilika za kuhakikisha yote yanatimia, nimeshaandaa minibus aina ya Coaster baada ya kufanikisha kukubaliana na rafiki yangu aitwaye Razdal anayeishi Putatan, huyu anamiliki kampuni ya kusafirisha watalii iitwayo Razdal Car Tours hivyo atatukodishia Coaster yake itakayotutoa kutoka Putatan hadi Sarawak ambapo napo kuna boti zake hivyo pale tutachukua boti hadi kisiwa cha Borneo huko ndipo kazi hii naamini tutaenda ifanikisha”. Aliongea mpango kazi Mr. Logan Puteri huku kakunja ngumi ya mkono wa kulia anaipiga piga kwenye kiganja chake cha mkono wa kushoto.

“Mpango huko vizuri ila bado unahitaji utekelezaji unaotutegemea sisi wote hapa, nia yetu thabiti inahitajika katika kazi hii, hatuwezi shindwa kitu ambacho tulishakianza ni biashara ambayo tayari ipo mikononi mwetu itakuwa ni ujinga sana tukishindwa itimiza sababu ya Agent Kai… Kuna timu ulaya hazijawai kumuuza mchezaji wao nyota yoyote kwa timu zingine kwa pesa ambazo sisi tutaingiza kwa kumuuza profesa mmoja akiwa na familia yake. Pesa ambazo klabu tajiri au zenye wawekazaji wenye nazo zinatoa kununua wachezaji nyota watano mpaka sita, sisi tunatakiwa tuzipate kwa mtu mmoja akiwa na familia yake, pia tuanatakiwa kuzipata pesa nyingi zaidi kwa kuwafikishia mtu mmoja tu… Hapa jamani tupigane tutimize lengo tusilete masikhara kama pesa ndiyo hii jamani”. Aliongea Mr. Ghulam maneno ya kuwahamasisha wenzake.

“Naamini wote tuliomo humu ni waelewa na tunajua kila kitu tunachotakiwa kufanya… Mmemsikia Mr. Ghulam alichoeleza na mimi pia nimemuelewa anachosema… Kuna lingine hapa kati kwa mtu mwingine tulisikie kabisa”. Akakazia Mr. Logan na kisha kutoa fursa kama kuna lingine.

“Tumsikilize Damia maana kuna jambo nilimtuma afuatilie… Damia uwanja ni wako”. Akasema Mr. Nawaz Patrash.

“Nilienda mtaa wa Pudu ulionielekeza kuwa kuna duka la kuuza kanzu na mabaibui la baba yake na yule binti aitwaye Shufania.. Nililipata duka lakini lilikuwa limefungwa na kwa habari nilizozipata toka kwa wauza duka wa majirani wameniambia duka lile leo halikufunguliwa na hakuna anayejua sababu, ikabidi niulize anaishi wapi wakanielekeza mtaa wa Block D, Jalan Putra Perdana nyumba namba 234 nako nilipoenda sikuwakuta na mtaa ule wanaishi watu wa jamii mchanganyiko hivyo sikupata ushirikiano wa kutosha.. Kuna kijana anaishi nyumba inayopakana na ile ameniahidi atanitumia namba zake kutokana na kuwa ana mdogo wake wa kike anasoma chuo kimoja na wadogo zake Shufania ambao kwa taarifa zilizopo ni mapacha wote wa kike na wanasoma chuo cha kiislamu cha International Islamic Unniversity Of Malaysia… Mpaka sasa bado sijapata simu kutoka kwa huyo kijana, nilimuachia namba yangu ya simu hili akiipata tu anitumie, nafikiri bado hajaipata sababu ina mlolongo kidogo, hivyo ndiyo kitu nachosubiri icho kwa upande wangu. Ingawa naamini namba ile tunaweza ipata kazini kwake Shufania, Alamanda Hotel”. Alieleza Damia a.k.a Language girl mwanadada ambaye hakuwa akijua kama hakuna mtu ambaye Agent Kai anamtamani kama yeye wakutane tu.

“Umefanya kazi nzuri Damia lakini namba ya binti huyo tayari ninayo niliipata mida ya saa kumi na moja na nusu lakini niliijaribu kwa simu ya vibandani haikuita inaonyesha amefunga simu…. Na niseme tu hili sisi wote tuelewe tunayumuwinda huku naye akituwinda ni fundi pengine kama sisi au katuzidi hivyo binti huyu lazima atakuwa kashaamua kumuwekea kava kumlinda… Nitakupa namba hii Damia”. Akasema Mr. Ghulam Qaresh.

“Basi nafikiri tukaendelee na msako wetu… Wale mliochukua chumba Alamanda muende kulala huko na wengine msicheze mbali na kule pengine muwindwa anaweza akafika huko… Nachopenda kusisitiza hakuna kulala mpaka tujue mbichi na mbivu… Bado nitapiga simu kwa mawakala wetu wa hotel kadhaa wa kadhaa kujua kama kuna sehemu kaonekana huyu mtu, club zote na sehemu zote za starehe mzunguke wale mtakaokuwa mpo kwenye doria”. Akasema Mr. Logan.

“Sawa boss…. Nafikiri muda huu tuutumie kwa mimi, Language girl na Uugun twende Block D kuvizia kama watakuwa wamerudi wazazi wa Shufania, tutakaa huko mpaka usiku mnene tukitazamia.. Naomba wengine mtakaokuwa around mtupe taarifa lolote litakalokuwa limetokea… Mr. Saddiq na Mr. Zhing Lae nawatakia safari njema ya Putatan usiku huu”

Kikao kilipitisha maamuzi hayo, wakiwa wenye kujiamini sana kuwa wanakwenda kwenye mafanikio, kikao kikaahirishwa wote wakaondoka wakiwaacha walinzi wanaokuwa wapo kila siku kulinda jengo hili.

Mwisho wa sehemu ya ishirini na nne (24)

Picha imeanza kuonekana taratibu ikipanda kuelekea kwenye kutimia ule unaoitwa MSHANGAO…!

Agent Kai hatua moja mbele kama wapinzani wake walivyo na wasiwasi kuhusu hilo.

Tumejionea Mr. Logan Puteri uoga ukizidi kutamalaki mpaka kuamua kuchukua maamuzi ya kuomba msaada kutoka kwa mwanadiplomasia msaidizi wa ubalozi wa marekani mwenye tama ya pesa amsaidie katika kujua nyendo za Agent Kai.

Tumesikia majasusi wanne wa kutoka shirika la kijasusi la Korea Kaskazini ikisemekana nao wanakuja Kuala Lumpur kwa ajili ya kazi moja tu ya kumtia nguvuni Agent Kai aende akajibu anayotakiwa kujibu nchini mwao.

Je kipi kitatokea katika mipango yote iliyopangwa?

25

Saa tatu na dakika moja ilimkuta Agent Kai akipaki gari katika maegesho ya magari ya Hospitali ya binafsi iitwayo Gleneagleas Hospital of Kuala Lumpur (GKL) iliyopo mtaa mtaa wa Kampung Berembang, eneo la Jalan Ampang, Persekutuan District.

“Twende wote ukamuone na kumjua baba na pia ukamjue na mama yetu”. Akatoa pendekezo Shufania baada ya Agent Kai kuzima injini ya gari na kisha macho yao kugongana.

“Una uhakika ni sawa mimi kufanya hivyo?”.

“Ni sawa Kai… Mimi kwangu hakuna shida na nitafurahi ikiwa hivyo”.

“Hapana si kwa muda huu… Nina uhakika wote hao nitawaona hata masaa ishirini na nne hayatafika kwa sababu tayari wameingia kwenye mpango wangu. Nenda tu mimi nitakusubiri hapahapa ndani ya gari ila hakikisha unarudi na mama”.

“Au unahisi wale watu watakuwa wamejua kama baba yangu amelazwa?.. Okay! Haina shida, ndiyo vizuri nikamueleze mama sababu ga….!”. Aliishia hapo akakatiza alichokuwa anataka kumalizia, dhahiri alionyesha kustuka, macho yakawa yanafuatilia jambo nje ya gari kupitia kioo cha mlango wa siti aliyokaa sababu hawakuwa wameshuka kutoka garini.

“Vipi Shufania? Umeona nini tena nishirikishe basi?”. Agent akamuuliza baada ya kufuatilia macho yake yanapoangalia na kutokuona kwake yeye ni kipi binti anakiangalia kwa kustuka vile.

“Mama… Nimemuona mama, yaaah! Ni yeye …. Ngoja nimuwai anatoka kupitia geti la wanaotoka kuelekea kituo cha mwendokasi”. Akajibu Shufania bila kusubiri Kai ataongea nini tayari akawa ashafungua mlango wa Range Rover Sport na hata mlango hakuurudisha akatoka mbio za kike mikono yote miwili akiwa kakamata baibui lake lisiburuzike chini wakati anakimbia pia iwe rahisi kwake kupiga hatua za kukimbia, ni baibui alilovaa jioni baada ya kulinunua jioni hiyo hiyo akiwa na Agent Kai na kubadili nguo zile alizokuwa kavaa asubuhi ya siku hii inayoelekea kuisha.

“Mam! Mam!.... Mam! Mama Ilham”. Akapaza sauti Shufania kumuita mama yake aliyekuwa naangalia magari yanavyopita hili yakisimama tu avuke kwenda upande wa pili kilipo kituo cha treni za mwendokasi zinazopiga tripu jijini Kuala Lumpur.

Mama Shufania au kama wenyewe wana familia yake wanavyomuita mama Ilham akageuza shingo kuona ni nani anamuita.

Naam! Macho yake yalikutana na macho anayoyatambua, macho yanayofanana na macho yake kwa kila kitu utafikiri aliyatoa kopi, macho ya binti yake kipenzi Shufania.

Haraka akageuka mwili mzima na kumlaki mwanae ambaye bado alikuwa kwenye mbio akapunguza spidi kisha kusimama pindi tu alipoingia ndani ya kumbatio (wakakumbatiana).

“Asallaam aleykuum”. Akatoa salamu Shufania.

“Aleykuum salaam… Vipi hali mwanangu?”.

“Nzuri mama…. Poleni sana mama, pole kwa kushughulika peke yako na mgonjwa… Naomba nisamehe mama kwa kuchelewa kuja kumuona mama”. Akaongea Shufania baada ya kuachiana toka kwenye kumbatio wakabaki wameshikana mikono yao yote miwili kwa kila mmoja.

“Ulikuwa wapi mwanangu? Mbona si kawaida yako kukaa bila kupiga simu muda wa jioni na hasa pale unapoona utachelewa kurudi nyumbani”.

“Mama ni stori ndefu kidogo… Vipi baba anaendeleaje?”.

“Anaendelea vizuri ameacha kutapika damu na hakohoi mfululizo kama tulivyokuwa tumekuja toka nyumbani, ilikuwa bahati kwetu tulifika wakati dokta wake Zakaria Tareek bado hajatoka kamsaidia sana kwa huduma nzuri na dawa”. Akajibu mama Ilham.

“Naweza kwenda kumuona?”.

“Unaweza lakini hautaweza kuongea naye, sababu nilipomaliza kumlisha tu akaniomba alale tukaomba dua akalala na dokta alisema akilala tu tumuache maana kama alivyokwambia mwenyewe asubuhi wakati unamuaga unaenda kazini kuwa hakulala usiku… Haihitajiki tumsumbue tena, nashauri tudamke asubuhi kuja kumuona wote”.

“Uliwataarifu kina Ilham?”. Huku macho yanayoonekana peke yake katika uso wote maana alivaa nikabu (ninja) yalikuwa yakiangalia kitu pembeni.

“Baba yako alikataa nisiwaambie lolote kwa sababu ambayo hata wewe unawajua ndugu zako tabia yao ya kutaharuki wasikiapo baba yenu au mimi mama yenu nimelazwa kiasi wanaondoka chuo bila hata ku… kua..gaa”. Alibabaika mwishoni wakati anajibu sababu aliona Shufania anaangalia nini. Agent Kai alikuwa kasimama hatua tano toka walipo akiwa kazibwa na kivuli cha kuti la mnazi ulio kando ya njia na angalia yake kwao haikumficha mama Ilham kuwa anawaangalia wao.

Wote wakawa wanawaangaliana hivyo ikabidi Agent Kai asogee karibu hili atoe salamu.

“Assalaam aleykuum mama!”.

“Aleykuum salaam”. Akajibu mama akishindwa kuongeza neno lingine sababu alikuwa akijua kuongea kiarabu tu.

Agent Kai muda mwingine uwa kama anaingia kwenye ubongo wa mtu na kumuelewa anawaza nini? Hivyo haraka akajiongeza.

“Poleni na matatizo ya kuumwa kwa baba”. Akaongea kwa kiarabu na hapo akaliona tabasamu limechanua toka kwenye uso wa mama na uso wa Shufania pia uliofichwa ndani ya nikabu ukatabasamu.

“Tushapoa baba yangu… “. Akajibu mama Ilham huku anamtizama usoni akitafuta picha wapi ashawai kumuona mtu huyu.

“Anaendeleaje saivi ulivyomuacha?”.

“Anaendelea vizuri kabisa… Nimemuacha amelala na imekuwa vizuri sana maana hakulala usiku wa jana kwa kukohoa mpaka mchana wa leo akaanza kukohoa damu ndipo nikamleta hospitali”.

“Tatizo inaelekea ni kubwa… Lakini kwa Mungu hakuna jambo kubwa inshaallah atarudi katika hali yake ya kawaida na kufanya kazi zake”. Agent Kai aliongea taratibu akiweka heshima kubwa kwa mama aliye mbele yake huku akitoa tumaini la kiimani.

“Amen! Inshaallah itakuwa hivyo mwanangu”. Akajibu mama Ilham kisha akageuka kumuangalia Shufania aliye pembeni yake upande wa kushoto, na bila shaka macho yake yakaonyesha anataka kujua jambo toka kwa mwanae lakini mdomo ukigoma kuuliza. Sura yake ilihitaji jibu toka mdomoni mwa mwanae na kwakuwa binti anamjua vizuri mama yake akampa tabasamu.

“Mama huyu ni rafiki yangu… kwa sasa sina mengi ya kukwambia ingawa najua haujawai kuniona nikiongozana na mwanaume na hilo ndiyo kitu kinachokuchangaya ila naomba uwe na amani utamjua vizuri tu”. Akaongea Shufania.

“Haya sawa mwanangu… twendeni tuondoke basi”. Ikabidi mama amkubalie mwanae ingawa kwa shingo upande maana hakutajiwa hata jina.

“Agent! Chukua gari utatukuta kule kwenye kivuko cha kuingia stendi ya treni tunakusubiri”.

Akasema Shufania kwa kiingereza kumwambia Agent Kai, ambaye naye hakusubiri neno lingine akachanganya miguu kuelekea kwenye maegesho ya gari walipoacha gari lao.

“Hayupo sasa, nafikiri unaweza kuniaambia… Ni nani yule kijana? Mwanangu… Wenyeji wa hapa wengi ninaokutana nao mimi hawawezi kuongea kiarabu fasaha kama anavyoongea yule kijana”. Akauliza na kutia maneno mengine baada baada ya kuona Kai kashatokomea machoni mwao.

“Mama! Yule kijana si mwenyeji wa nchi hii… Nafikiri ungevuta subira kidogo tu mwenyewe atajitambulisha ni nani? Twende tumuwai kule chini, acha haraka zako shosti”. Shufania akasema na kuanza hatua za haraka kuondoka, mama ikabidi aunge tela.

Walipokanyaga tu mistari ya pundamilia iliyochorwa barabarani kama ishara ya watu kuvuka kwa usalama kuelekea upande wa stesheni ya treni ya mwendokasi inayofanya kazi ya usafiri wa ndani ya jiji la Kuala Lumpur, Range Rover Sport ikasimama hatua chache toka walipo.

“Twende Mam!” Akasema Shufania huku kamshika mkono mama kumuongoza, akafungua mlango wa nyuma ya siti ya dereva kisha akampa ishara mama yake aingie kwenye gari na mama akapanda ndani ya gari na mlango ukafungwa. Kisha haraka akazunguka upande wa pili na kuingia siti ya mbele.

Kai akatia gia na kukanyaga mafuta gari ikaondoka.

“Umeshamwambia mama tunaenda wapi?”. Kai akamuuliza Shufania baada ya kuona wanaukaribia mzunguko wa magari wa Ampang-Kuala Lumpur Elevated Highway.

“Hatukuongea tunaenda wapi… Au uliniambia wapi tunapoenda? Pengine nimesahau… Niambie nimwambie tunaenda wapi?”.

“Twendeni mahali ambapo tutakula na kuongea kwa amani, huku ninawasiliana na balozi nyumba niliyoomba aandae iko wapi”. Akajibu Kai huku akitabasamu.

“Twende mgahawa wa Botanical Garden wana mgahawa unaotoa huduma siku hizi hadi usiku na watu hawajai kutokana na bei”. Akaongea Shufania.

“Hapa naelekea barabara ipi?”. Akamuuliza.

“Fuata hiyo Jalan Tun Razak Road”.

“Okay! Nishaujua huo mgahawa ulio kwenye hiyo garden… Perdana Botanical Garden niliuona kwenye ramani ya jiji, karibu na jumba la makumbusho la taifa”.

“Huko sahihi… Ni eneo la Tugu Negara unapita hiyo Jalan Tun Razak kisha tunaingia Jalan Damansara tunaliona jengo la makumbusho ya taifa lakini hatulifikii tunaingia kushoto ndipo tunaiona garden ya Perdana Botanical Garden…. Haya sasa hapo kwakuwa nimemuelekeza jasusi genius sina lingine la kuelekeza tena”.

“Hahahahah ahahahah! Tugu Negara, Alamanda putrajaya ni eneo zuri sana ningekuwa naweza ningenunua moja ya jengo nikafungua biashara fulani ambayo inalipa… Haya ndiyo umwambie mama tunaenda wapi”.

“Okay”. Maongezi yao ya kutumia lugha ya kiingereza yakasimama hapo, Shufania akageuka mwili kiupande hili aweze kumwambia mama yake walichokuwa wakijadili.

“Mama tunaenda kula kwenye mgahawa mmoja ulio Alamanda Putrajaya, sababu tuna maongezi muhimu tunatakiwa kufanya baina yako na yetu”. Akamwambia.

“Sawa tu, ilimradi tusichelewe sana huko kwa kukaa muda mrefu”. Mama akakubali.

Walifika Perdana Botanical Garden na moja kwa moja wakaingia ndani ya maegesho ya magari na baada ya kupata sehemu aliyoona Agent Kai dereva wa gari hii ni poa akasimamisha gari na kisha wote wakashuka toka ndani ya gari.

Walitafuta sehemu nzuri ambayo ilikuwa karibu jiko la mgahawa wakapata viti na muhudumu akaja kuwasikiliza mahitaji yao wote kila mmoja akaagiza chakula alichotamani kula kwa usiku huo pamoja na kinywaji alichohitaji kunywa.

Vyakula na vinywaji vikaletwa wakanaishwa mikono na wote wakaanza kula huku kukiwa na ukimya na mara moja moja ikisikika midomo yao ikitoa milio ya kutafuna.

“Mama samahani…. Najua siku zote toka wanao sisi tukiwa watoto mpaka sasa watoto wako wote tumekuwa wakubwa ulituzuia wakati wa kula kuongea, lakini natanguliza samahani na kukuomba tuongee hili tuongee muda, naomba ruhusa yako mama yangu”. Shufania akavunja ukimya oliokuwa umetawala kwao.

“Hakuna shida, mimi mwenyewe nilitamani tuongee sababu ya muda… Natoa ruhusa wanangu tuonge, muda mwingine inatubidi tuziache mila zetu za kawaida na kufuata zisizokuwa mila zetu kama hizi za kuongea wakati wa kula kwa sababu ya dharura”. Mama akakubali ombi la mwanae.

“Ahsante sana mama kwa ruhusa yako, Shufania usiogope nitambulishe kwa mama bila kumuweka gizani kuhusu mimi”. Akasema Agent Kai akiomba atambulishwe yeye kama Agent Kai Hamis.

“Samahanini kwanza wanangu… Kabla Shufania hajaniambia chochote naomba niweke sawa lile nalofikiri mimi hili msivuke mipaka… Mimi namjua mwangu Shufania kwa kila hali, najua nini anakwenda kuniambia. Sitaki mnione mimi mama mpenda kuingilia uhuru wa watoto, naweza kutambulishwa kwenu lakino sina mamlaka ya kuidhinisha uhusiano wenu. Yupo baba Shufania mzee Mahamud yeye ndiye aliyepewa mamlaka na Mungu kuwaunganisha ninyi kwa utaratibu maalumu wa kindoa. Nitawasikiliza tu lakini tafadhali Mungu muweza wa yote akawe kati yenu na mkamuogope kwa kufanya yale anayoyapenda na kuyaacha yale yamchukizao”. Mama akiwa hajui kipi kilichowafanya waje kwenye mgahawa huu usiku huu kupata chakula cha pamoja, alisema anachohisi ambacho si sahihi sababu haikuwa wakati wake na haikuwa mawazoni kwa vijana wale.

Shufania akamuangalia Kai na macho yao yalipogongana akamkonyeza wkatabasamu mama akishuhudia, aibu ikahushusha uso wa mrembo wa Shufania chini.

“Mama huko sahihi kwa hayo uyasemayo lakini umewai sana, ni kweli sisi tunafikiri kufika huko ulipofikia lakini tumemtanguliza Mungu mbele sote sisi ni waislamu tunafuata sheria za dini yetu. Mpango wetu ni mzuri na ikifika muda muafaka utaujua sababu ni mpango ambao kwa kila mzazi yeyote atapenda kuusikia…. Lakini kwa sasa kuna kazi imeingilia kiasi imesababisha mimi leo kutowai kufika hospitali isivyo kawaida kama mlivyonizoea uwa nakuwa sambamba na nyie mara zote baba au wewe mama mnapopata tatizo.. hii ilitokana na simu yangu kufungwa ikiwa sababu ni hilo jambo”. Alitoa maelezo Shufania kisha akanywa juisi yake iliyo kwenye glass na kujiweka vizuri kwenye kiti akawaangalia wote alionao pale kwa zamu wakimsikiliza kisha akaendelea.

“Mama ushawai sikia habari ambayo ilivuma sana masikioni mwa watu wiki tatu zilizopita ikishika vichwa vya mbele vya magazeti hapa Malaysia na kutawala mijadala kwenye mitandao ya kijamii, habari ya kupotea kwa kutekwa wanasayansi wa Marekani maprofesa wataalamu wa silaha za kinyuklia pamoja na kibaiolojia… Nasema umesikia sababu baba alikuwa akipenda sana kuliongelea jambo hili tulipokuwa tunaangalia taarifa mbalimbali za habari katika vituo mbalimbali vya televisheni… Kupotea kwao kwa wanasayansi wale ni jambo la hatari sana kiufundi kwa serikali ya Marekan pia hata kwa ndugu na jamaa hivyo hawajakaa kimya kufuatilia jambo hili hivyo walituma wapelelezi wawili ambao hao wanaohusika na utekaji huu waliwateka hao wapelelezi akaja mwingine naye akamuwai ndipo amekuja huyu unayemuona hapa mbele yetu na alipo hapo kiuhalisia hayupo hivyo kama unavyomuona… Ameamua kuwa mkweli kwetu sababu ametuamini wote… Unaweza ukajiuliza kwanini amesogea karibu yangu wakati yeye ni jasusi ni kwamba alifikia hotelini pale napofanya kazi na katika kuwa namuhudumia aliniomba anitume sehemu ndipo likawa kosa kwake au kwetu yeye kunituma”. Hapa alisimama tena akanywa tena juisi kisha akaendelea.

“Kwanini mimi na wewe mama tupo hapa?.. Jibu usilishangae mama ni la kweli na wala lisikustue ingawa najua lazima utastuka, mimi mwanao hao waliofanya matukio hayo ya kuteka wanasayansi hadi wapelelezi wananitaka kwa wanachoamini mimi nipo karibu na huyu mtu hivyo wakinipata mimi watampata huyu kaka… Kwanini wao hawampati huyu mtu? Mtu huyu ni kama nilivyokueleza ni jasusi na si jasusi wa kikawaida ana mbinu nyingi za kufanya kuwakwepa huku anawafuatilia na ndiyo maana nimekwambia hapo nilipoanza kuwa hayupo kiuhalisia na alivyo yaani amevaa sura ya bandia na huwezi kuiona sura yake halisi kwa yeye kuitoa sura hiyo aliyoivaa hapa tulipo ila utamuona alivyo hata kesho tutakapokuwa sehemu sahihi… Mimi nimegeuka ngazi kwa hao watu wanaomtaka huyu kijana kwa wao kumuua au kufanya lingine wanaloona kwao liko sahihi… Anaitwa Kai Hamis Mkarambati ni jasusi wa wa shirika la kijasusi la CIA la Marekani, anaishi Washington DC, Marekani”.

“Nimekuelewa mwanangu… Lakini wewe umejuaje kama unatafutwa na hao watu hili uwe ngazi yao kuwasaidia wampate mtu huyu?”.

“Asubuhi walikuja watu wasioeleweka kuniuliza maswali niliyoyashuku si maswali ya kawaida baadaye nikapata wazo nimpigie Kai wakati huo nikimjua kwa jina aliloandika pale hotelini jina la Ramsey Bronze, nilipomueleza tu nikagundua ameshangaa na akaniomba tusiendelee kuongea kwenye simu nitafute muda huko ndiyo tutaongea vizuri.. Nikataka nisubiri hadi jioni lakini moyo wangu ukakataa kumtafuta muda huo nikamuomba tukutane kwa ajili ya lunch, wakati naenda kukutana naye sikuwa najua kuna watu wananifuatilia lakini yeye nilipofika tu aligundua maana mwenye fani yake mara nyingi uwa hakosei hivyo tukatumia mbinu tukawatoroka, icho ndicho kilichonihakikishia kuwa mimi nasakwa, natafutwa, nahitajiwa”.

“Mama! Samahani kwa kuingilia maongezi yenu, baada ya kujua jina langu ningependa ufahamu mimi ni mzoefu wa kazi nayofanya. Najua hila zote za magaidi, majasusi wenzangu na wahalifu wa kimataifa waliobobea kwenye michezo kama hii, najua saivi wanachowaza ingawa sijajua wako wapi watu wetu wanaowashikilia lakini napenda kuahidi hawana muda mrefu watagundua kwanini maji hayapandi mlima na mlima wanaotaka kuupnda haupandiki… Nachoomba kwenu wakubwa wangu mnisaidie msirudi mtaa wenu yaani msirudi nyumbani kama inavyotakiwa mpaka kazi hii iliyonileta hapa nitakapoimaliza… Tuombe Mungu iishe salama na kwa wakati ulio sahihi, naamini siku tatu au nne tokea siku hii ya leo kazi itakuwa imekwisha na kuwapa mshangao. Nyumba yenu si salama kwenu”. Akaingilia maongezi ghafla Agent Kai.

“Sasa tutaenda wapi mwanangu?” Mama Ilham akauliza huku akiweka aibu au tuseme heshima fulani ya kidini kwa kuyakazia macho ya Kai macho yake.

“Swala mtaenda wapi? Hilo mniachie mimi… Sababu lipo ndani ya uwezo wangu licha ya kuwa mimi ni mgeni hapa Malaysia lakini wenyeji wangu wapo kwa ajili ya misaada kama hii”.

“Je? Hao watu hawawezi kufuatilia na kujua mume wangu yupo hospitali? Maana ninaanza kuhofia kila kitu”.

“Wanaweza au wasiweze, kinachotakiwa sisi tuombe wasifike huko kabla hatujachukua tahadhari”.

“Kwa ilivyo.. Ule mtaa wetu watu hatushirikiani sana kwa mambo mengi tunapeana salamu tu halafu kila mtu anaendelea na hamsini zake…. Icho kitu kinanipa imani kuwa hawawezi pata habari juu ya baba kuwa amelazwa”. Akaingilia Shufania kuwatoa wasiwasi wanaomsikiliza.

“Sawa wanangu nimekubaliana na hilo ilimradi mimi, wanangu na mume wangu wawe salama”.

“Ahsante mama kwa kukubali maombi yetu kwa ujumla … Acha tuokoe muda hii ni saa nne na robo usiku , naombeni niongee kwa simu kidogo hili niweke mambo sawa”. Akasema Agent Kai kisha akainuka kitini na kutembea hatua kama kumi toka walipo.

Mwisho wa sehemu ya ishirini na tano (25)

Sehemu hii tumeshuhudia Agent Kai na Shufania binti Mahamud wakiwa katika maongezi marefu na mama mzazi wa Shufania (Mama Iham).

Uzuri mama aliweza kuelewa na kukubaliana na matakwa ya Agent Kai yeye na familia yake kupelekwa mahala salama.

Tusipoteze wakati, twende sehemu inayofuata kujua mengi zaidi.. Karibu tena!

ILIPOISHIA….!

“Umefanya kazi nzuri Damia lakini namba ya binti huyo tayari ninayo niliipata mida ya saa kumi na moja na nusu lakini niliijaribu kwa simu ya vibandani haikuita inaonyesha amefunga simu…. Na niseme tu hili sisi wote tuelewe tunayumuwinda huku naye akituwinda ni fundi pengine kama sisi au katuzidi hivyo binti huyu lazima atakuwa kashaamua kumuwekea kava kumlinda… Nitakupa namba hii Damia”. Akasema Mr. Ghulam Qaresh.

“Basi nafikiri tukaendelee na msako wetu… Wale mliochukua chumba Alamanda muende kulala huko na wengine msicheze mbali na kule pengine muwindwa anaweza akafika huko… Nachopenda kusisitiza hakuna kulala mpaka tujue mbichi na mbivu… Bado nitapiga simu kwa mawakala wetu wa hotel kadhaa wa kadhaa kujua kama kuna sehemu kaonekana huyu mtu, club zote na sehemu zote za starehe mzunguke wale mtakaokuwa mpo kwenye doria”. Akasema Mr. Logan.

“Sawa boss…. Nafikiri muda huu tuutumie kwa mimi, Language girl na Uugun twende Block D kuvizia kama watakuwa wamerudi wazazi wa Shufania, tutakaa huko mpaka usiku mnene tukitazamia.. Naomba wengine mtakaokuwa around mtupe taarifa lolote litakalokuwa limetokea… Mr. Saddiq na Mr. Zhing Lae nawatakia safari njema ya Putatan usiku huu”

Kikao kilipitisha maamuzi hayo, wakiwa wenye kujiamini sana kuwa wanakwenda kwenye mafanikio, kikao kikaahirishwa wote wakaondoka wakiwaacha walinzi wanaokuwa wapo kila siku kulinda jengo hili.

ENDELEA NA UTAMU…!

HATUA MOJA MBELE VI

ENDELEA NA DODO..!

HATUA MOJA MBELE VII

“US First!”.

“US First! Habari yako mzee?”.

“Safi mwanangu, lete habari?”. Akasema balozi.

“Ahsante kwa gari.. Napenda kujua juu ya lile suala nililokuachia ufuatilie vipi maendeleo? Maana tulipanga tuonane usiku huu lakini mpaka sasa bado naweka sawa jambo fulani”.

“Mambo mawili ndiyo uliniachia kufuatilia, moja nimefuatilia kwa kiasi nilichoweza lakini ni vizuri tuonane hata kama ikiwa ni saa nane usiku kama hautajali… Na kuhusu nyumba nishalishughulikia suala hilo, nyumba ipo tayari nimeandaa walinzi wanne ambao ni kati ya walinzi kumi na sita tulionao pale ubalozini, nafikiri hao watu wanaweza wakajihudumia wenyewe masuala ya kupika na vitu vingine kama hivyo, hivyo ulinzi tu utawatosha”.

“Good! Nafikiri ulinzi utawatosha hakuna shida… Vipi huyo mgeni niliyekuletea naweza naye mkanikabidhi leo? Yaani usiku huu huu hili akaungane na wengine katika nyumba hiyo”.

“Mimi nipo nyumbani unamtaka mtu huyo aletwe na mtu mwingine au ni vipi? Maana wewe ndiyo unajua kipi kinaendelea”.

“Hilo huko sahihi kapteni, bado sijajua waliopo hapo ubalozini yupi ni yupi na yupi ni yupi ila wewe ni mtaalamu unaweza ukajua yupi aliye msafi zaidi ingawa kazi sana kujua msaliti kiwepesi… Naomba mtu aliye safi amlete mahali ambapo mimi nitakuwa na hawa nilionao na huyo mtu ndiyo atampeleka mama wa rafiki yangu na huyo mgeni kwenye nyumba niliyoomba”.

“Kwa sasa mpo wapi?”.

“Perdana Botanical Garden mtaa wa Alamanda Putrajaya”.

“Ok! Hiyo nyumba ipo nje ya jiji eneo la Istana Negara, Jalan Istana nyuma ya Royal Klang Club pembezoni tu mwa Klang River ni nyumba ambayo naijua mimi na katibu wetu Mrs. Rose Thompson yaani hata viongozi wetu wa kidiplomasia Mr. Abraham na msaidizi wake Michael hawaijui hiyo nyumba sababu tulipewa sisi kama sisi na ambaye wao hawakuwa wanamjua tukaona itakuwa vizuri kama ikiwa nyumba yetu ya siri kama litatokea tatizo na haikuwa shida sababu hatukuinunua hivyo hatukuogopa tuhuma za ufisadi iwapo itagundulika na mtu ambaye atawapeleka anaitwa Clark, nyumba ilikuwa hii anakaa kijana wa Mrs. Rose Thompson hivyo nimekubaliana na Rose kuhusu kijana huyo kuwa atarudi nyumbani kwake kwa muda … Kwa hapo mlipo naomba msogee hadi jalan jalil perkasa 1 kuna kanisa kuu la Calvary Convention Center mtamkuta kijana na mgeni wetu wanawasubiri hapo, huyo kijana ninayemuagiza yupo smart kabisa usimuhofie kabisa ndiye ninayemtumia katika mambo mengi ya siri yanayonihusu ”

“Ahsante sana Kapteni, nimefurahi sana kufanya kazi na wewe hapa KL… Naamini hii kazi tunakwenda kuimaliza”.

“Nipo kwa ajili yako kijana wangu… Lakini kuna jambo lingine unatakiwa kulifanyia kazi halafu muda tutakaonana nitakueleza kuhusu lile lingine… Jambo lenyewe ni chief executive amenitumia ujumbe muda wa saa moja kuwa uhakikishe unampigia simu au mnawasiliana kivingine vyovyote ni muhimu sana”.

“Ahsante sana kwa mara ingine tena!! Nitamcheki nikishawakabidhi watu hawa kwa Clark”.

“Fanya hivyo! Ameniambia leo umenyamaza kutwa yote bila taarifa yoyote mpaka ana wasiwasi na kama ujuavyo operesheni ipo chini ya makamu wa rais hivyo wanataka kujua kila linaloendelea kama linaenda sahihi”.

“Lakini niliamini wewe utampa taarifa zile ninazokupa mkuu… Basi usijali nitafanya hivyo”.

“Maliza hayo kwanza… Nafikiri tuonane asubuhi kule kwenye nyumba watakayokwenda watu wako”.

“Sawa tutaonana huko Istana Negara… Kama kuna chochote kitatokea kinachohitaji msaada wako kwa haraka nitakucheki kwenye simu, kuna harufu naisikia usiku huu utakuwa usiku mrefu”.

“Nipo kwa ajili yako nicheki muda wowote”.

Waliagana na simu ikakatwa.

“Mama samahani kwa kukuchelewesha kwenda kupumzika, siku yako imekuwa ndefu sana bila sababu, tunaweza kuondoka sasa… Tushapata nyumba nzuri mtakayoitumia kwa kipindi na hata mkitaka make milele ni rukhsa”. Akaongea Agent Kai bila hata kukaa kitini, muhudumu alipowaona wapo mkao ule wenye nia ya kuondoka alisogea haraka na akachukua haki yake ya malipo.

Mama Ilham na mwanae Shufania wakainuka vitini kisha wakaunga tela kumfuata Kai kwa nyuma aliyekuwa katangulia kutoka.

Mwendo hadi kwenye maegesho ya Perdana Botanical Garden, wote wakazama ndani ya gari ikaondoshwa na dereva Agent Kai bila kulemba.

Wakiwa washaiacha barabara ya Jalan Tun Razak moja ya barabara yenye urefu mkubwa sana katika barabara za jiji la Kuala Lumpur ikiziunganisha barabara nyingi tu za jiji hili, wakaingia barabara ya Tuanku Abdul Rahman, simu ya Shufania iliita na safari hii aliisikia vizuri sababu ilikuwa ipo mkononi mwake.

Alipoangalia jina la mpigaji ilisoma ni Safia ambaye ni mdogo wake kati ya wadogo zake wawili walio mapacha aliopishana nao miaka minne. Familia yao yam zee Mahamud aliyekuwa daktari nchini Syria, walizaliwa watoto watano, wakitangulia kaka zake Shufania waliozaliwa mapacha wakifungua uzazi wa wanandoa hawa Kulwa akiitwa Hemed Mahamud na Doto akiitwa Himid Mahamud, kisha baada ya miaka mitatu akazaliwa Shufania yeye akiwa peke yake baada ya hapo miaka minne mbele ndipo walipozaliwa mapacha wengine wa kike Kulwa akiitwa Safia Mahamud na Doto wake akiitwa Ilham Mahamud. Baada ya vita kulipuka nchini Syria ikiwa pia katika nchi nyingi za kiarabu ilitokea hali hii ya vita za wenyewe kwa wenyewe, watoto wa kiume wa Dokta Mahamud walikuwa ni waajiriwa katika kikosi cha usalama wa taifa na vita ile iliwakuta sehemu mbaya na wakauwawa na watu wa dola ya kiislamu. Hivyo baada ya kufariki kwa kaka zao hawa likafa jina la mama Himid na likaja jina la mama Ilham. Dokta Mahamud alichanganyikiwa sana kufa kwa watoto wake baada ya miezi kadhaa vita ilichanganya sana ndipo wakatafuta mbinu ya kutoroka nchi hii.

Na kwa sasa Ilham na Safia wanasoma chuo cha Kiislamu cha International Islamic University of Malaysia wakiwa mwaka wa kwanza.

“Assalaam Aleykuum”. Upande uliopiga simu ulitoa salamu papo hapo baada ya kugundua simu imepokelewa.

“Aleykuum salaam … Vipi hali mdogo wangu?”.

“Safi tu dada za huko?”.

“Huku safi tu, vipi wewe na yako mnaendeleaje?”.

“Tunaendelea vizuri dada… Vipi wazazi wanaendeleaje?”.

“Wako poa”. Shufania hakutaka kuwajulisha ndugu zake kuhusu baba yao kulazwa.

“Nilipiga simu ya baba sikuipata hewani na hata ya mama nayo kadhalika haipatikani, nikapatwa na wasiwasi maana si kawaida yao.. Na hata Ilham alipiga hadi yako muda fulani mchana pia hakukupata”.

“Utakuwa ni mtandao tu, sababu hata mimi niliwatafuta wazazi mchana lakini sikuwapata na wao pia walinitafuta ikawa hivyo hivyo… Hapa KL leo mtandao haukuwa vizuri mpaka saivi usiku ndiyo umerudi katika hali yake, mnamaliza lini michezo yenu huko Sarawak?”.

“Jumapili tunamaliza na jumatatu tunarudi KL… Dada! Muda si mrefu yaani kama dakika kumi zilizopita kuna rafiki yangu mmoja tunasoma naye chuo lakini yeye si mwanamichezo aliniomba namba zako za simu kwa shida kuwa ana kaka yake kamaliza mafunzo ya hotel management anataka umsaidie kupata kazi, nimemwambia mpaka nikuombe mwenyewe ruhusa ndipo nimpe”.

“Mmmh! Sasa mbona mimi sijawai kumsaidia mtu mambo kama hayo na si utaratibu wa wetu huo… Okay mpe nitaongea naye kumsaidia afanye nini”.

Waliishia hapo wakatakiana kila la kheri na kisha wakaagana na tayari walikuwa washafika Jalil Perkasa Street , taratibu Agent Kai akawa anaendesha gari kuelekea maegesho ya magari ya kanisa kuu la Calvary Convention Center.

Wakati anasogea taratibu gari aina ya Toyota Hilux rangi nyeupe ilipiga honi kwa kurudia mara mbili huku taa zikiwashwa kiishara na hapo Agent Kai akajua wanaitwa wao akasimamisha gari kisha akashusha kioo baada ya kumuona dereva wa ile gari akishuka, alikuwa ni kijana wa kizungu na dhahri hakujificha machoni mwa Agent Kai kumtambua ndiyo mlengwa waliyemfuata hili wakutane hapa.

“Naitwa Clark!”. Akaongea baada ya kufika kwenye dirisha la upande wa dereva akimwambia Kai.

“Hi!”. Agent Kai akamsalimu salamu ya kimarekani ikiwa ndiyo mbinu yake ya kwanza kujua anayeongea naye ni wa kwao au vipi.

“Hi..”.

“Clark wa Mrs. Rose Thompson?”.

“Hujakosea ni mimi… Nimeagizwa kuna watu nakuja kuwachukua hapa toka kwako kuwapeleka Jalan Negara, Klang River na pia kuna dada nimekuja naye”.

“Yah! Nimefurahi kukujua… Huyo mwanamke nitamuona baadaye, naomba uwapeleke yeye na mama mmoja nipo naye humu. Tafadhali uwawaishe wakapumzike, mimi kuna sehemu naenda… Unaishi wapi wewe hapa KL?”.

“Naishi Villa Mont Kiara”.

“Mpigie simu Mrs. Kuwa leo hautarudi, naamini hautakuwa umekosea kikazi… Sababu nahitaji ulale huko Jalan Negara nikiwa nakuja nitakupigia unielekeze”.

“Niko peke yangu kwa sasa, mke wangu ameenda Marekani kujifungua. Hivyo haina shida boss nitakusubiri huko”.

Kai akachukua namba za simu za Clark na kuzisevu kwenye simu yake wakati wote huo yeye hakuwa ameshuka toka ndani ya gari.

“Mama utaondoka na huyu kijana kwenda huko nilipokwambia kabla ndipo patakuwa makazi yenu kwa muda… Shufania nitakuja naye mimi sababu kuna mawasiliano nataka anisaidie”.

“Sawa mwanangu ila naomba msichelewe huko muendako”. Mama akakubali, Shufania akashuka toka ndani ya gari kisha akazunguka upande wa pili akamfungulia mama yake mlango wa gari na kumuongoza mama yake hadi ilipopaki gari ya aina Toyota Hilux aliyokuja nayo Clark akiwa na dada aliyekuwa kahifadhiwa ubalozini mwao.

Clark hakupoteza muda akaondoka akiwaacha Agent Kai na Shufania wakiwa bado wamepaki pale pale.

“Vipi umechoka sana?”. Akaongea Agent Kai baada ya kumtizama machoni Shufania ambaye alikuwa kaondoa nikabu (ninja) uso unaonekana vizuri, naye akamjibu kwa tabasamu kisha kutikisa kichwa bado hajachoka.

“Vipi umepokea meseji tuliyokuwa tukiisubiri?”.

“Ndiyo nimeiona wakati unaongea na Clark”.

Alikuwa ni Sheila ametuma namba ya mzee Abubakari Morsi.

“Vizuri hapa tuna laini moja ya adui yetu aliyetangulia mchana, kiuharaka sidhani kama yeye huyo mzee Abubakari atakuwa anaijua namba hii… Naiweka kwenye kifaa maalumu kisha naichomeka kwenye kompyuta tutampigia utaongea naye ukijifanya wewe ni Sheila ila kabla ya yote mpigie Sheila mpe taarifa utakachofanya”.

Shufania hakusubiri zaidi sababu taratibu naye alishaanza kuwa kama jasusi kwa kukaa kwa muda mfupi karibu na ua waridi. Akapiga namba za Sheila.

“Shosti!”. Akaongea baada ya kupokelewa.

“Shosti hujalala! Vipi huko hospitali?”. Akajibu na kuuliza Sheila.

“Hospitali safi kabisa namshukuru Mungu, baba anaendelea vizuri … Ahsante kwa namba uliyonitumia”. Akajibu Shufania na kuongezea.

“Haya ahsante na wewe kwa kwenda hospitali na kunipigia kunijulisha kuwa mzee anaendela vizuri… Vipi ulimpigia mzee Morsi?”.

“Hapana sijampigia bado lakini ndiyo nataka nimpigie kwa namba ingine… Ila naomba uzime simu yako kwa muda kidogo sababu nikimpigia nitajifanya ni wewe umempigia kwa namba ingine”.

“Halafu utamueleza nini?”.

“Nitamwambia uliongea na mimi unaomba kujua naishi mtaa upi na nyumba namba ngapi kisha kitakachofuata kesho nitamfuata mimi mwenyewe… Naomba Sheila unisaidie juu ya hili na usimwambie mtu kama umenipa namba ya huyu mzee”.

“Hivi kuna nini shosti unachonificha?... Tafadhali Shufania niambie mimi dada yako kuna tatizo gani maana sikuelewi elewi toka uwe karibu na Ramsey Bronze tena mmejuana hata siku tatu bado”.

“Usihofu shosti.. Mambo mazuri hayahitaji haraka… Fanya hivyo nilivyokuomba kwanza”.

“Sawa nazima sasa hivi kwakuwa nalala na nishaongea na Sabry”.

“Okay! Usiku mwema nitakupigia asubuhi tuonane wapi maana wote kesho ijumaa tupo mapumziko”.

Simu zikakatwa Shufania akamgeukia Agent Kai aliyekuwa akiunganisha kifaa chake kilicho na ukubwa kama modem hili waongee kwa namba waliyotumiwa.

“Nisomee namba hiyo”. Akamuomba Shufania amsomee namba.

Shufania akasoma namba Agent Kai akaandika kwenye kompyuta yake mpakato (laptop) kisha akapiga ikaanza kuita.

“Inaita… Iga sauti ya Sheila, jitambulishe kisha elekea kwenye moja kwa moja anaishi wapi”.

Alipomaliza kumuelekeza tu simu ikapokelea na upande wa pili.

“Halloo!”.

“Halloo! Asallaam Aleykuum!”.

“Aleykuuma sallam! Nani mwenzangu usiku huu?”.

“Sheila Isaiyah wa Alamanda hotel!”.

“Oooh! Ni wewe, namba ngeni hii, umebadili au ndiyo unazo nyingi?”.

“Hamna mzee Morsi, hii namba ya mdogo wangu… Samahani kwa kukupigia usiku”.

“Bila samahani… Niambie Sheila?”.

“Samahani tena, hivi mzee Rafael anaishi wapi?”.

“Mzee Rafael wa nini usiku wote huu?”.

“Simuhitaji usiku huu ila ninahitaji kujua anakaa wapi maana aliniambia ana ndugu yake anataka tumtafutie nafasi kule jikoni”.

“Kwa hiyo hapo ni namba au anakaa wapi?”.

“Anakaa wapi moja au hata namba mbili ila vizuri ukanielekeza anakaa wapi sababu kesho mi nipo mapumziko nitaenda kukubaliana naye vitu”.

“Ok! Umesema hii ni namba ya mdogo wako, wewe simu yako iko wapi?”.

“Mzee Morsi mbona maswali mengi sana… kama hutaki kunielekeza anakaa wapi nikate simu na iwe mara ya mwisho kuwasiliana mimi na wewe na hata paled kazini kuniongelesha”.

“Hahahah hahahah! Usifike huko… Dunia imebadilika sana Sheila hasa hapa Kuala Lumpur, hivyo tunatakiwa kuwa makini hasa kwa nyinyi wanawake watu wanawatumia sana…. Sawa nitakuelekeza ila usije ukasema kama mimi ndiyo nimekuelekeza huko, anaishi Block B Jalan Aman Putra nyumba namba 304 BJAP/Selangor”. Mzee Morsi akafunguka baada ya Shufania kumpa tishio dogo la kutotaka kuongea naye, mzee huyu toka mara ya kwanza anaingia kufanya kazi Alamanda Hotel pamoja na uzee wake wa miaka inayokaribia hamsini na tano alionyesha kuvutiwa sana na Sheila, hivyo akaamua kufunguka na mara kwa mara kumsumbua Sheila akimuhitaji kimapenzi bila mafanikio ingawa binti alikuwa akimridhisha kwa kupenda kuongea naye na hata kumuonyesha kana kwamba anaelekea kumkubali.

“Ahsante sana mpendwa, naomba nikuache upumzike tutawasiliana kesho”. Shufania alikyekuwa kajifanya Sheila akaongea.

“Haya Sheila nikutakie usiku mwema ila usirudie kupiga usiku utanisababishia matatizo kwa mke mkubwa”.

“Hahahahah hahahahah! Na yuko wapi?”.

“Amelala! Leo amechoka sana mjukuu anamsumbua anaumwa sana hivyo akimbembeleza mpaka alale ndipo naye alale…. Haya tusije tukamstua akacharuka… Usiku mwema”.

Shufania hakujibu maana Agent Kai alikata simu huku kabinya midomo yake hili asiongee kitu maana alitamani aongee kitu.

Mwisho wa sehemu ya ishirini na sita (26)

Nisifafanue lolote sababu naamini msomaji unafuatilia kwa umakini mkasa huu! Kama ni ufafanuzi utakuja katika sehemu ziingine ambazo itakuwa hakuna budi kufafanua kidogo.

Endelea kuwa nami mtunzi na mwandishi wako.

ILIPOISHIA….!

“Sheila Isaiyah wa Alamanda hotel!”.

“Oooh! Ni wewe, namba ngeni hii, umebadili au ndiyo unazo nyingi?”.

“Hamna mzee Morsi, hii namba ya mdogo wangu… Samahani kwa kukupigia usiku”.

“Bila samahani… Niambie Sheila?”.

“Samahani tena, hivi mzee Rafael anaishi wapi?”.

“Mzee Rafael wa nini usiku wote huu?”.

“Simuhitaji usiku huu ila ninahitaji kujua anakaa wapi maana aliniambia ana ndugu yake anataka tumtafutie nafasi kule jikoni”.

“Kwa hiyo hapo ni namba au anakaa wapi?”.

“Anakaa wapi moja au hata namba mbili ila vizuri ukanielekeza anakaa wapi sababu kesho mi nipo mapumziko nitaenda kukubaliana naye vitu”.

“Ok! Umesema hii ni namba ya mdogo wako, wewe simu yako iko wapi?”.

“Mzee Morsi mbona maswali mengi sana… kama hutaki kunielekeza anakaa wapi nikate simu na iwe mara ya mwisho kuwasiliana mimi na wewe na hata paled kazini kuniongelesha”.

“Hahahah hahahah! Usifike huko… Dunia imebadilika sana Sheila hasa hapa Kuala Lumpur, hivyo tunatakiwa kuwa makini hasa kwa nyinyi wanawake watu wanawatumia sana…. Sawa nitakuelekeza ila usije ukasema kama mimi ndiyo nimekuelekeza huko, anaishi Block B Jalan Aman Putra nyumba namba 304 BJAP/Selangor”. Mzee Morsi akafunguka baada ya Shufania kumpa tishio dogo la kutotaka kuongea naye, mzee huyu toka mara ya kwanza anaingia kufanya kazi Alamanda Hotel pamoja na uzee wake wa miaka inayokaribia hamsini na tano alionyesha kuvutiwa sana na Sheila, hivyo akaamua kufunguka na mara kwa mara kumsumbua Sheila akimuhitaji kimapenzi bila mafanikio ingawa binti alikuwa akimridhisha kwa kupenda kuongea naye na hata kumuonyesha kana kwamba anaelekea kumkubali.

“Ahsante sana mpendwa, naomba nikuache upumzike tutawasiliana kesho”. Shufania alikyekuwa kajifanya Sheila akaongea.

“Haya Sheila nikutakie usiku mwema ila usirudie kupiga usiku utanisababishia matatizo kwa mke mkubwa”.

“Hahahahah hahahahah! Na yuko wapi?”.

“Amelala! Leo amechoka sana mjukuu anamsumbua anaumwa sana hivyo akimbembeleza mpaka alale ndipo naye alale…. Haya tusije tukamstua akacharuka… Usiku mwema”.

Shufania hakujibu maana Agent Kai alikata simu huku kabinya midomo yake hili asiongee kitu maana alitamani aongee kitu.

ENDELEA NA UTAMU..!

HATUA MOJA MBELE VIII

“Shenzy! Kumbe lina mke zee zima linatamani wanae”. Akaongea Agent Kai.

“Una wivu hadi na Sheila… Hahahahah hahahah, nipe ratiba haraka hili tukalale”. Akasema Shufania huku akitabasamu tabasamu tamu la kumchanganya kidume aliye pembeni yake.

‘Mmmh! Mtoto huyu kwa huu uzuri atanifanya niwe na haraka kupiga hii kazi iishe hili nimalizane na yeye pia’ Akawaza Kai.

“ Kazi yako kwa usiku huu imeisha, nikupeleke Klang River, Jalan Negara”. Akaongea Agent Kai huku anawasha gari.

“Ukishanipeleka wewe unatoka?”.

“Ndiyo! Siwezi kulala mpaka nimuone mzee Rafael anielekeze vizuri alikuwa anali dalalia shamba lipi kununua mbolea yetu”.

“Eeeh! Mnauza mbolea?”. Akauliza Shufania huku akijizuia kucheka kwa kuukinga mdomo.

“Mi uwa natumia neno la mbolea lakini hatuuzi mbolea Mrs.Abdul”.

“Naomba huko kote twende wote halafu ndiyo turudi wote Klang River…”.

“Utamtia mama wasiwasi halafu huwezi juwa nitamalizana nao saa ngapi wateja wa mbolea nataka wakiamka wakute kuna jipya lililofanywa na Agent Kai… Tafadhali naomba nikupeleke ukapumzike umenisaidia mengi leo bila wewe mwenyewe kujua kama umenisaidia mengi”.

“Basi sawa nipeleke ila sijaridhika kwa kweli”.

“Ahsante kwa kukubali ushauri wangu… Nielekeze japo kwa ufupi huyo mzee Rafael yukoje?”

“Oooh! Ni mrefu wa urefu wa kama wako hamjapishana kwenye urefu ni mmalaysia asiye na weupe mkali kama wengine anafuga ndevu nyingi lakini si ndefu ingawa zimefanya mzunguko mashavuni hadi kidevuni”.

“Inatosha nishachora picha yake alivyo.. Anaongea lugha gani?”.

“Kigezo cha kwanza cha kupata kazi katika hotel yetu ni mtu kujua lugha za kigeni angalau kiingereza, mi uwa naongea naye kwa kiingereza”.

“Okay! Nimekuelewa… Twen’zetu”

***** ***** *****

Ilikuwa ni saa sita na robo fundi ‘the sole cat’ Agent Kai, Sajenti wa zamani wa kikosi bora cha makomamndo kinachofahamika kama US Navy Seals alikuwa akipanda ngazi kama vile ni mwenyeji wa ghorofa lililo na urefu wa flour (losheni) tano. Ghorofa hili lililojengwa sambamba na maghorofa mengine yanayofanana (flat) kama kumi yakipangwa kwa mpangilio wa kufuata barabara ya mtaa inavyokwenda,yalikuwa maghorofa makubwa yenye changanyikeni kweli kweli maana mpaka muda huo ulioenda sana kikawaida kwa muda wa watu kupumzika bado alikuwa akipishana na watu waliokuwa wakishuka na wengine wakienda juu na hakuna aliyemjali.

Agent Kai alikwenda juu huku akisoma kibao kinachoonyesha flour aliyopo inaanza na nyumba namba ngapi hakutaka kuuliza kati ya wale anaopishana nao sababu hakihofia lugha gongana.

Flour ya nne aliiona namba aliyokuwa akihitaji korido hii ilikuwa kimya huku baadhi flat zikiwa zikiwa milangoni wameweka taa na zingine hawajaweka alihesabu namba mpaka akaifikia namba Flat 304 BJAP.

Akatoa miwani yake mfukoni kisha akavaa akasogea kwa mwendo ambao hata laiti ambapo angetokea mtu asingemuona kama yupo kwenye mnyapio akinyapia jambo. Alipofika usawa wa dirisha ambalo alishajua toka anapanda toka chini huko flour ya kwanza kuwa limeunganisha kwa kuanza dinner (sehemu ya kulia) halafu mbele sehemu ya kupumzikia, hivyo alijibanza na kuchungulia kwa chati macho yaliyo ndani ya miwani ya kazi yaliona pote sehemu hii hakuna mtu hii.

Kwa haraka ilimjuza wenyewe washalala, akapita hapa mpaka mlangoni kwa haraka akaminya kitasa na kusukuma mlango akakutana na kigingi akaacha na kusogea mbele ambapo pana dirisha dogo lililo juu kiasi ya kwamba kwa Agent Kai akinyoosha mikono kwenda usawa wa juu analifikia linapoanzia. Hapo aliganda sekunde thelathini akisikilizia utulivu uliopo maeneo yale kisha akanyoosha mkono wake na kukamata nyavu iliyotengenezwa kwa juu dirishani ikizuia mbu kwa nguvu akaivuta ikajiachia na kutoa mlio hafifu akauweka chini usawa wa ukuta.

Hapo akatulia tena sekunde chache kisha akajifyatua kuruka juu hadi usawa wa dirisha dogo mikono yake ilikamata kama paka ama kweli ‘the sole cat’ nalo pia hakuwa amekurupuka alishapima toka flat za chini na kuona kwake anaweza kupenya, hivyo kama mwendo wa nyoka anayekimbia moto kwenye kichaka chake alipenya na akajikuta ametokea chooni tena bila kishindo cha kumstua mtu aliyesinzia. Sekunde ishirini zilimtosha kuupima utulivu uliopo akasogea mlangoni alipotaka kugusa kitasa tu akasikia miguu upande wa pili wa mlango ikisogea na mara ikasikika komeo ikifunguliwa ‘Alhamdullilah kumbe kulifungwa na komeo kwa nje’ akajinong’oneza huku akipiga hatua mpja ndefu kuwai nyuma ya mlango. Alishukuru sababu komeo ilikuwa kizuizi kwake na ingembidi atumie nguvu kufuungua na ingewastua wenyeji.

Mtu aliyeingia alikuwa na binti mwenye umri wa haraka kwa kukadiria alikuwa na miaka kama kumi na sita kusogea kumi na saba, nane. Macho ya binti yaligongana na sura iliyovaa miwani akastuka kiasi kikubwa sana akataka kupiga kelele na ilikuwa Agent Kai amezubaa asijue amfanye nini binti yule aliyevaa nguo nyeupe ya kulalia.

Lakini hakuwa na jinsi alimvaa mwilini kisha akamkamata usoni mkono wa kulia ukamziba mdomo kwa nguvu, binti kwakuwa alibanwa kwa nguvu huku akiwa kabanwa ukutani hakuweza kukuruka sana maana alishikwa na mtu anayejua kumshika mtu na akatulia. Akili ikafanya kazi haraka kichwani kwa mtaalamu haraka akampiga judo hafifu ya kimshipa kinachounganisha shingo na sikio binti akapoteza fahamu.

Bila kupoteza taratibu akambeba begani hakutaka kumuacha chooni binti wa watu akatokea naye kwenye veranda hapo akamlaza chini na bahati nzuri wakati anamlaza akaona kuna chumba mlango umeachwa wazi akasogea kwenda kuchungulia na mara moja akatambua ndiyo chumba alichotoka yule binti na alikuwa peke yake, hivyo KaI akarudi alipomlaza akamnyanyua pale na kumpeleka chumbani kwake akamlaza vizuri kitandani.

“Samahani binti niko kazini, pole sana kwa kukulaza hapa ukiwa hujajisaidia haja yako”. Akaongea kwa sauti ya chini huku anatoka mule chumbani.

Akaelekea upande wa kulia na mlango uliofuata akaminya kitasa ukakubali akachungulia ndani kwenye kiuwazi kidogo hapo akakutana na watu walio katika umri wa miaka ambayo kwa haraka akajua mwanaume aliyopo pale ndiyo mlengwa wake na tayari walikuwa katika lepe la usingizi maana walilala kila mmoja upande wake feni ikiwapepea.

Agent Kai akaingia taratibu na kunyata kusogea hadi kitandani macho yakaiona picha ambayo alishaichora kwenye ubongo wake wa ubunifu wa kazi, sura yam zee Rafael ikiwa ndani ya usingizi alikuwa akiiangalia. Kama kawaida yake akiwa maeneo haya akili yake uwa ishapanga anafanya nini bila kusubiri akamgonga kingumi konzi hafifu ya shingo mama aliyelala upande wa juu akiwa amevaa gauni la kulalia na papo hapo akazirai.

Akatoa bastola yake na kumtingisha kwa nguvu mzee Rafael ambapo alistuka na kutumbua macho baada ya kukutana na mdomo wa bastola. Akababaika na kuongea lugha ambayo Agent Kai akajua hiki ni ki melay bahasa.

“Asallaam aleykuum!”. Kai akamsalimu huku akimfanyia ishara kwa mdomo wa bastola kuwa ainuke kitandani.

“Aley.. Aleykuuum Sallaam”. Macho hayakuwa yakitulia aliangalia kila upande wa kila chumba kana kwamba yeye ni mgeni wakati yeye ndiyo mwenyeji, alikuwa akijiuliza anaota au ni kweli anaangalia mdomo wa bastola na anaangaliwa kwa macho makali ya mtu asiyemjua akiwa kapandisha miwani yake kwa kuiweka kwenye paji la uso.

“Usitetemeke mzee… Najua unajiuliza mambo mengi kichwani mwako usiumize kichwa kujiuliza hayo unayojiuliza sababu yapo nje ya uwezo wako”. Kai akamuongelesha kwa kiingereza.

“Wewe ni .. wewe ni nani?”. Akaweza kuuliza naye akitumia kiingereza kibovu.

“Haina haja ya kunijua… Ila nina angalizo dogo kwako… Mimi si mtu wa kipoa poa kama utaenda tofauti na yale ninayoyataka kujua kutoka kwako”.

“Samahani, samahani kijana wangu, umemfanyaje mke wangu?”.

“Nimekupa ruhusa muda gani wa kuniuliza?.... Nimekupa angalizo kuwa wewe ni wa kujibu niyatakayo tena kwa ukweli ukiweka uongo kando nikigundua umenidanganya tu nitafanya jambo ambalo litakufanya ujutie kufika hadi umri huo ukiwa hai, mke wako msubiri akiamka utamuuliza imekuwaje upande wake”.

“Sawa, sawa ila kijana haufanyi vizuri kwa unachofanya”.

“Ongoza sebuleni tukaongee huko ninayotaka”. Akampa ishara atangulie kutoka chumbani, walikwenda mpaka sebuleni huku bwana Rafael akitamani kujua binti yake naye yuko kwenye hali gani.

“Mr. Rafael hakuna chochote kinachoweza kutokea kukupa msaada maana naona unahangaika kuangalia kila sehemu kana kwamba unamuangalia mtu… Siingiagi kwenye nyumba ya mtu nikiwa sijahakikisha usalama wangu hivyo achana na hayo unayoyafikiria.. Tafadhali kaa sofani tuongee kirafiki”.

“Kirafiki! Kivipi?” mbona umeshika bastola mkononi?”.

“Ndiyo kirafiki mkuu lakini siamini utulivu wako ndiyo maana nimeshika bastola na si kwamba nakuogopa mzee wangu naogopa kelele zako hivyo bastola itazuia kelele yako yoyote ile… Nataka tuongee kirafiki na kwa utulivu”.

“Kitu gani unataka tuongee? Na umeingilia wapi? Mbona mlango umefungwa, wewe ni mtu kweli?”.

“Shit! Ujue unanipotezea muda… Tafadhali keti lasivyo nitakulazimisha kuketi bwana mkubwa”. Hapo Mr. Rafael alikaa sofani na bado alikuwa aamini anachoona kashikwa na mshangao kweli kweli.

“Mr. Rafael, meneja wa mazingira ya nje hotel Alamanda… Leo ulikuwa na pilika pilika nyingi sana unaweza kunifafanulia pilika pilika zote zile ulikuwa unatumiwa na nani?”.

“Sijakuelewa kijana kwanini unaniuliza hivyo?”.

“Hivi mzee una miaka mingapi?... Kwanini huelewi? Au unafikiri nimekuja kucheza hapa… Nakuonya mara ya mwisho hii bastola nimeifunga kiwambo cha kuzuia sauti muda si mrefu nitakugeuza jina, sitaki nisikie swali lolote toka kwako mpaka nitakapokuruhusu kuniuliza… Haya haraka sana nijibu nilichokuuliza na usidanganye sababu najua vingi ila nahitaji uhakika tu toka kwako”.

“Samahani sitarudia tena kijana wangu… Ni kweli kazini kulikuwa na pilika pilika nyingi ila samahani ungenifafanulia ni pilika pilika zipi ulizomaanisha”.

“Unaleta ujanja wa kizamani na sitaki nikuumize… Pilika pilika nazotaka kujua ni juu ya mpangaji wa hotel ile mgeni toka Marekani anaitwa Ramsey Bronze”.

“Haaaah! Mi nilitumwa tu sina makosa”.

“Alikutuma nani? Naomba unieleze vizuri mpaka huyo aliyekutuma umuelezee vizuri bila kukosea lasivyo nautawanya ubongo wako sekunde tu”.

“Naomba usinifanyie hivyo nitakueleza…Boss mmoja ambaye kiukweli mimi uwa simjui jina na sijawai kuonana naye zaidi ya kumsikia sauti yake kwenye simu anaponipigia tu”.

“Ulijuana naye vipi bila kuwai kuonana naye? Namaanisha namba zenu za simu pia mlibadilishana vipi? Kama kuna mtu wa kati aliyesababisha kubadilishana kwenu namba zenu za simu huyo ndiyo muhimu kwangu nitafurahi kama nitamjua na nitaachana na wewe sasa hivi hapa uendelee kulala kwa raha zako”.

“Alianza kunipigia simu yeye wiki kama mbili tu zilizopita, alipata namba yangu kutoka kwa kijana wangu mmoja anaitwa Othman Awadh”.

“Hukumuuliza Othman kwanini boss anataka namba yako?”.

“Nilimuuliza hivyo wakati ananiomba kuna mtu anaomba namba je atoe nami nikamuuliza mtu gani huyo akaniambia ni boss wake na yeye na ni mwanamke, nilisita kumruhusu kwakuwa ni mwanamke lakini akanisihi sana nikubali tena akaniahidi kunipa pesa ndipo nikakubali kama ujuavyo kijana wangu shida zetu cha ajabu baada ya kumpa namba siku ya kwanza akanipigia mwanamke kama alivyosema Othman baada ya kujitambulisha yeye nani akaniomba niongee na boss wake ndipo nikaongea na huyo mwanaume”.

“Huyo mwanaume alikwambia nini?”.

“Aliniambia kuna kazi anataka kunipa na atanilipa mara mbili ya mshahara wangu ninaolipwa Alamanda”.

“Kazi gani hiyo?”.

“Ya kufuatilia kila mgeni anayefika kupanga hotel pale kazini akiwa anatokea Marekani.. Sikuona haja ya kukataa suala dogo kama hilo kufuatilia tu na nikawa nafanya hivyo lakini siku zote zile za mwanzo hakukutokea mgeni toka Marekani kuja kupanga Alamanda”.

“Unawajua uliokuwa ukipanga nao mipango leo?”.

“Mimi sikuwa nikipanga mipango bali wao ndiyo walikuwa wakipanga mipango mimi nikiwasaidia kwa nilivyoweza tu”.

“Suala unawajua ni kina nani hao?”.

“Ni hao watu wa huyo anayejiita boss mkubwa”.

“Huwajui majina yao na je walifikaje pale Alamanda bila mawasiliano na wewe?”

Mwisho wa sehemu ya ishirini na saba (27)

Kazi imeanza kukolea kwenye reli yake!

Agent Kai akipanga mipango yake na huku ikionekana ikienda vile anavyotaka..!

Akifanikiwa kuwakwepa adui zake mpaka siku inaisha wasijue wapi alipo.

Tumeona Agent Kai akisogea hatua ingine kwa kukaribia kujua kidogo walio kwenye mpango..!

Je Othman ni nani?

Na ni mwanamke gani aliyetajwa na Othman kuwa ndiyo boss aliyetaka namba ya Mr. Rafael?

Je Agent Kai atapata muda wa kupumzika siku hii iliyokwisha ama toka alhamisi kwenda ijumaa?

Majibu ya yote haya yapo katika sehemu inayokuja na zinazokuja mbele…!

“Hukumuuliza Othman kwanini boss anataka namba yako?”.

“Nilimuuliza hivyo wakati ananiomba kuna mtu anaomba namba je atoe nami nikamuuliza mtu gani huyo akaniambia ni boss wake na yeye na ni mwanamke, nilisita kumruhusu kwakuwa ni mwanamke lakini akanisihi sana nikubali tena akaniahidi kunipa pesa ndipo nikakubali kama ujuavyo kijana wangu shida zetu cha ajabu baada ya kumpa namba siku ya kwanza akanipigia mwanamke kama alivyosema Othman baada ya kujitambulisha yeye nani akaniomba niongee na boss wake ndipo nikaongea na huyo mwanaume”.

“Huyo mwanaume alikwambia nini?”.

“Aliniambia kuna kazi anataka kunipa na atanilipa mara mbili ya mshahara wangu ninaolipwa Alamanda”.

“Kazi gani hiyo?”.

“Ya kufuatilia kila mgeni anayefika kupanga hotel pale kazini akiwa anatokea Marekani.. Sikuona haja ya kukataa suala dogo kama hilo kufuatilia tu na nikawa nafanya hivyo lakini siku zote zile za mwanzo hakukutokea mgeni toka Marekani kuja kupanga Alamanda”.

“Unawajua uliokuwa ukipanga nao mipango leo?”.

“Mimi sikuwa nikipanga mipango bali wao ndiyo walikuwa wakipanga mipango mimi nikiwasaidia kwa nilivyoweza tu”.

“Suala unawajua ni kina nani hao?”.

“Ni hao watu wa huyo anayejiita boss mkubwa”.

“Huwajui majina yao na je walifikaje pale Alamanda bila mawasiliano na wewe?”

ENDELEA NA MBUTE

WASIWASI NA MASHAKA I

“Alinipigia simu nayemuita boss akiniomba nichunguze katika majina ya wageni waliorodheshwa mapokezi kama wageni katika hotel nayofanya kazi, akitaka jina la mtu anayejiita Ramsey Bronze, ndipo nilipoanza kushughulika kuhusu jina hilo nikienda mapokezi na nikatumia uzoefu wa kujulikana pale hotelini niliweza kupata daftari la orodha nikaliona jina hilo nikamjibu lipo”.

“Endelea ikawaje? Nimekuja hapa kuhakikisha tu sababu ninajua kila hatua ulizoshirikiana na watu hao wakiongozwa na boss unayesema hujawai kumuona”.

“Akanitumia picha ya huyo mtu hili nihakikishe kama ni sahihi lakini mimi huyo mtu pia sijawai kumuona nikamjibu kama nitamuona nitamjulisha lakini akaniomba nikutane na watu wake aliowatuma na hao watu waliniita Madam Stang’s Food Restaurant eneo la china town, huko ndipo nilipokutana nao”.

“Hao uliokutana nao hawana majina?”.

“Hakuna ninayemjua jina kati yao na sikuona umuhimu wa kuuliza jina la hata mmoja wao ingawa wao wananijua mimi”.

“Ajabu sana … Mr. Rafael Khamdushin wewe unawafanyia kazi watu na unapokea malipo kwao bila kuwajua kina nani? Okay si tatizo sana, naomba uainishe mipango yote uliofanya au uliyowasaidia kufanya hao watu wasiojulikana na kumbuka mengi ninayajua ukinidanganya nafyatua bastola kutawanya ubongo wako”.

“Waliomba niwasaidie kupanga vyumba vilivyo karibu na Ramsey Bronze, kimoja walipata kilichopakana naye na kingine kipo kwa nyuma kama vyumba vinne kupita ilipo ilipo lifti… Kingine waliomba niwasaidie kuwakutanisha na mtunza kumbukumbu cctv control room nikawakutanisha na wakafanikiwa kununua video zilizorekodiwa kuanzia siku aliyoingia Ramsey, kingine nimewasaidia gari lao wanalohifadhi vifaa vyao kupaki kwenye maegesho yanayotumiwa na watu maalumu tu wa hoteli… Ni hayo tu niliyosaidia kijana wangu”.

“Gari yao ni aina gani?”.

“Toyota Hiace rangi nyeupe”.

“Nataka kujua anapoishi Othman, anaishi wapi?”.

“Othman najua eneo analoishi ila sijawai kufika kwake hivyo sijui anakaa nyumba namba ngapi najua mtaa tu… Anaishi Taman Desa Street”.

“Anajishughulisha na kazi gani katika kumuingizia kipato”.

“Hana kazi maalumu zaidi ya kuwa matajiri wengi wa hapa Kuala Lumpur ni marafiki zake wanamtumia katika kuwapata mabinti wazuri na kazi zingine za udalali wa magari mazuri ambayo kama tajiri akilichoka anataka kuuza akimpa yeye haraka analiuza na watu wengine wanasema anajihusisha na wizi wa magari… Ni kijana anayejipenda sana na ana marafiki wengi sana wa kike hasa wanaojiuza kimataifa na kwa matajiri”.

“Naomba namba yake”.

“Simu yangu ipo chumbani tumeiacha kule”.

“Twende ukachukue unipe namba nikuache upumzike”.

Walienda chumbani Mzee wa watu akiwa chini ya uangalizi makini akachukua simu aliyokuwa kaichomeka kwenye chaji baada ya kutoa lock kama zilivyo smartphone nyingi akapekua namba na kutaka kuisoma.

“Nionyeshe hiyo namba usinisomee”. Akampa angalizo mzee akampa simu Agent Kai huku ikiwa kafungua sehemu za majina.

“Ipi namba ya unayemuita boss?”

“Kuna namba nimeisevu kwa jina la Unknown 1”.

“Okay nimeiona… Ya aliyekuita Madam Stang’s Food, umesevu vipi?”.

“Unknown 2!”.

“Ya Othman?”

“Nimeandika Born Shine sababu ya anajipenda sana”.

“Ahsante naona umesevu majina katika lugha ninayoielewa maana nilianza kuhofu inaweza kuwa ki-melayu bahasa… Utanisamehe mzee hii simu nina kazi nayo hivyo naichukua na kuondoka nayo… Naitwa Abdul natokea Pokok Sena, naomba twende ukanifungulie niondoke zangu sababu siwezi kutokea nilipoingilia….. Mke wako na binti anayelala chumba cha kwanza wamezimia na muda si mrefu watazinduka usifosi kuwazindua utawaumiza na kunipa ubaya uwaache watazinduka wenyewe kila mmoja kwa muda wake… Angalizo! Tafadhali kuanzia kesho nisikuone na wale watu usiowajua majina lakini wanakutumikisha, Ramsey atakuwa na watu wengine kukuchunguza kama umekiuka masharti haya ninayokupa kila hatua utakayopiga tutakuwa tunaifuatilia kama leo tulivyofanya… Mzee umri ulionao hutakiwi kuwa na tamaa ya pesa hadi watu wabaya wanakutumia kuwaumiza watu wasio na hatia kwa faida yao… Haya ongoza twende ukanifungulie mlango”.Akatoa maelezo marefu Agent Kai huku akiwa kamkazia macho Mzee wa watu ambaye mpaka sasa hakuwa anajua huyu mtu ameingiaje mule ndani.

Waliongozana hadi sebuleni mzee Rafael akafungua mlango na kumpisha Agent Kai aondoke.

“Usiku mwema mzee wangu… Nisamehe kwa kuleta ugeni ambao kwako wa ajabu sana lakini kazi ndiyo iliyonileta kwako usiku huu kama usiowajua majina walivyokuja kwako kutaka uwasaidie kuhusu kijana anayeitwa Ramsey Bronze.. Mi si jini wala mchawi mimi ni mtu kama wewe na kukikucha tu utajua niliingiaje humu”.

Akaongea Agent kisha akatimka kwa hatua za mwendokasi akimuacha mzee Rafael Khamdushin kaganda mlangoni kumshangaa akijipa maswali lukuki yasiyo na majibu kamili.

Alikwenda mpaka alipopaki gari lake kwenye Bar moja ndogo ambayo mpaka muda huo ilikuwa haijafungwa baadhi ya wakazi wa maghorofa ya mtaa huu walikuwa wakikata maji.

Alipoingia na kuketi kwenye kiti cha dereva akaangalia simu yake iliyomjuza ni saa saba na dakika tano usiku, alifikiri kama dakika tatu kipi afanye kisha akanyanyua simu yake toka kwenye dashboard.

Akaishika huku anafikiri halafu akaona hakifai anachofikiri akairudisha simu kwenye dashboard kisha akawasha gari na kuitoa pale kwenye maegesho ya bar ile iliyo ndogo kama glocery.

Mwendo wa kasi alikwenda hadi mtaa wa Taman Desa, mtaa anaoishi kijana aliyetajiwa jina anaitwa Othman, alisogea kuingia mtaa unapoelekea ambao nao ulikuwa ni miongoni mwa kama mitaa mingi iliyopo Kuala Lumpur iliyotengenezwa kisasa na kwa mpangilio ikiwa na mataa ya barabarani pamoja na lami.

Alitafuta sehemu ambayo nyumba yake ilikuwa ina wigo wa michongoma pamoja na miti akapaki gari kisha akatoa laptop yake toka kwenye begi akaiwasha na kuchomeka kifaa ambacho ukitumia katika mambo mengi anayotaka kuyafanya kama kumsaidia katika mawasiliano mbalimbali.

“Halloo!”.Upande wa pili uliongea baada ya Agent Kai kupiga namba hiyo.

“Halloo! Kapteni samahani kwa kukusumbua usiku mwingine tena… Kama nilivyokwambia mwanzo tulivyoongea kuwa nauona usiku wa leo kuwa utakuwa mrefu kwangu, niko na haraka sana sababu kuna kitu kingine nje ya kazi nataka kukimaliza”. Akaongea Agent Kai.

“Ni sawa mwanangu… Ila tafadhali uwe makini usifanye pupa sana kumaliza kilichopo unaweza ingia kwenye tatizo na kushindwa kuimaliza kazi”.

“Niko makini Kapteni… Kingine ambacho sikujua mara ya kwanza na sasa nimekijua na nina uhakika kipo sahihi watu wanaohusika na huu mchezo ni wahalifu wa kawaida ambao wanapewa msaada na kikundi au serikali fulani yenye nia ovu juu ya Marekani”.

“Ok! Naamini katika kila hatua yako… Ila nahisi hujaongea na chifu, kwanini unafanya hivyo… Na hata e-mail hujafungua”.

“Ni kweli sijafungua e-mail yangu na sijampigia ni kwa sababu sijafika hatua nayoona ni sahihi mi kuongea naye kwa leo”

“Yeye ndiyo ana jambo muhimu la kukwambia… Kanitumia e-mail anasisitiza hivyo nikampa hii namba yako unayotumia hapa.. Nafikiri atakupigia muda si mrefu… Tuache hayo, lete habari”.

“Niko mtaa wa Taman Desa kuna dalali wa wateja wa mbolea namuhitaji ila sijui anaishi nyumba gani? Anaitwa Othman naomba unisaidie kumtoa huko alipo aje nilipo lakini naomba upige kwenye namba ya kifaa changu ulichonipa kisha nitaunganisha kwenye hiyo namba nataka wasijue namba yako na hata huko wapi wakati umepiga”.

“Haahaahaah! Jasusi huna haja ya kunielekeza mengi tupo kwenye mchezo mmoja hata kama nimestaafu nitajie hiyo namba ya kifaa chako nipige maana nimeisahau na sina hapa… Lakini nielekeze naongea nini? na huyo Othman”.

“Haya mkuu! Naona tunazeeka mpaka kifaa kilichokuwa chako unasahau namba yake… Okay! Namba ni 124569-5678. Utamwambia jina lolote unaloona ni la wenyeji wa hapa kisha utamuomba muonane nje ya nyumbani kwake usiku huu unataka kununua gari kwa bei mtakayokubaliana ikiwa utaimudu, akisema yupo nyumbani mwambie akuelekeze nyumba uende kisha mimi nitaenda kumchukua”.

“Sawa napiga sasa hivi wewe unganisha tu”.

Dakika mbili kompyuta ilionyesha namba za Kapteni Jones Lobrens ikiita papo hapo Agent Kai akaiunganisha na namba ya Othman aliyoisoma toka kwenye simu ya Mr. Rafael. Ikasachi kidogo na kuanza kuita na pia ilionyesha alama ya kuwa simu inayopigiwa ipo mita chache toka kifaa hiki kilipo.

“Halloow!”. Sauti ya upande wa ile namba iliyopigiwa ikasikika kwa Agent Kai kutokea kwenye spika za laptop na kwa Balozi Kapteni Jones huko alipo kwenye simu.

“Halloow! Asallaam Aleykuum!”. Akaongea Kapteni akitoa salamu.

“Aleykuum sallaam, nani mwenzangu?”. Akaongea Othman.

“Naitwa Jayl Wang… Naongea na Othman?”.

“Huko sahihi ni mimi, mbona umenipigia usiku huu na tena kwa namba nisiyojua ya nchi gani”.

“Hii namba ni ya hapahapa Malaysia iangalie vizuri tu utaijua”.

“Wewe Jayl Wang wa wapi?”.

“Natokea Padang Pesar, nina gari nahitaji mteja usiku huuhuu nilikuwa club kuna kijana nilimuuliza kama anamfahamu dalali mzuri wa magari nataka kuuza gari yangu niliyokuja nayo toka Padang Pesar, akanitajia jina lako kisha akanipa hii namba yako ya simu”.

“Okay! Ni sawa… Hiyo gari aina gani na ina muda gani toka itumike?”.

“Range Rover Sport ina miezi kama sita tu sema nina matatizo nimemleta mama yangu kupata matibabu hapa KL, sasa gharama zimekuwa kubwa sana hivyo nikaona cha kwanza cha kufanya nikuuza kitu changu kilicho na thamani hili niyaokoe maisha ya mama”.

“Rangi gani? Na unayo kadi yake?”.

“Nina kila kitu chake ni rangi nyeusi”.

“Huko wapi saivi?”.

“Niko Bangsar Baru karibu na mzunguko wa Jalan Telawi natokea Bangsar and Mid Valley Nightlife nilipokuwa nimekuja kupoteza mawazo kwa kunywa mbili tatu… Wewe huko wapi?”.

“Ndiyo nimefika kwangu nami nilikuwa Fuze Club hata kuoga sijaoga bado”.

“Aisee niko na shida ndugu yangu, tafadhali naomba nielekeze kwako nije niache gari na uione kadi yake unisaidie hata pesa kidogo niweze kumsaidia mama yangu kisha siku nyingine yoyote utanimalizia iliyobaki nakupa kadi ya gari tunakuwa tumemalizana”.

“Sawa inawezekana kufanya hivyo, njoo niione hiyo gari… Kama ipo kwenye hali hiyo unayoisema siku mbili tu tutamalizana”.

“Nitashukuru sana kwa msaada wako, gari ipo vizuri sana utaiona tu”.

“Okay! mimi naishi Taman Desa street nyumba namba TD 367 KL ukifika mtaa huu ndiyo nyumba pekee yenye bati lenye rangi ya kijani kwa usiku huu unaweza usilione kwa urahisi lakini nina alama ingine ipo kwenye kimlima hivi na ina geti jeusi lenye taa za rangi ya bluu nyeupe pande zote mbili za geti”.

“Sawa tusicheleweshane kimaongezi nakuja na hivi hakuna foleni ya magari usiku huu nitegemee baada ya dakika chache nafika siunajua Range Rover Sport inavyotimua kishada”.

“Okay! Ukifika utapiga honi nitatoka nje”.

Kapteni akamuaga na kukata simu.

Agent Kai hakutaka kupiga tena kwa balozi Kapteni Jones kama msaada alishaupata na maongezi aliyasikia yote. Alichofanya alitoa kifaa alichokichomeka na kuizima laptop yake.

Akatoa gari pale alipopaki kwa mwendo wa taratibu na kuelekea unapoendelea ule mtaa alikwenda hadi kona na kweli akakiona kimlima kidogo alichosikia Othman akielekeza na akaiona nyumba husika akapitiliza hadi mwisho wa mtaa ambapo akapaki gari tena hili kuvuta muda kidogo.

Dakika ishirini za kufanya subira zilitimia akiwa amefungua e-mail yake na kuangalia ni meseji ipi aliyoambiwa na balozi kuwa katumiwa na kiongozi wake wa kazi. Meseji ilikuwa ikimsisitiza wawasiliane kabla hakujakucha. Akaamua atampigia akishatoka kuongea na Othman ambaye aliamua atamchukua na kuondoka naye.

Aliondoa gari pale na kwa mwendo wa kuonekana kama toka alipotoka alikuwa akikimbiza alikwenda na kufunga breki kali hatua chache ya geti mpaka matairi yakalalamika gari ilipotulia akapiga honi na haikuchukua muda wa dakika zaidi ya mbili geti likafunguliwa akatoka kijana wa kiarabu aliyevaa jezi kawoshi ya timu ya mpira wa kikapu ya Marekani iitwayo Warriors na pensi (kaptura) aina ya timberland, kifuani alining’iniza cheni tatu kubwa kubwa zenye kumeremeta madini kama wapendavyo kuvaa wanamuziki mbalimbali wa Marekani.

“Karibu Mr. Jayl”. Akaongea baada ya kufika usawa wa dirisha la gari huku akitabasamu.

“Ahsante sana Othman, vipi hali?”.

“Safi sana… Hujapotea na umefika haraka sana… Hii kitu nimeikubali, hii tunafanya biashara haraka sana kesho tu”.

“Range Rover Sport si mchezo ndugu yangu, dude kama linapaa yaani shaaa kwenye lami au hata barabara za vumbi mwendo tu unakimbia hakuna wasiwasi wowote… Nimewai kufika ndugu nafikiri vizuri ukaingia ndani ya gari tuongee”.

“Huingii ndani hata? Au ndiyo unataka ukimbilie hospitali?”.

“Usiku huu kaka… Nitaingia siku nyingine acha tuongee niende zangu’.

Othman akakubali akaingia kwenye gari ambapo alipokaa kwenye siti Agent Kai akamuangalia vizuri kwa kuiibia.

“Othman! Samahani sana kwa kukusumbua usiku huu mi siuzi gari nimekuja kwako nina shida ambayo inahitaji msaada wako”.

“Unamaanisha nini Jayl?”.

“Utajua ninachomaanisha muda si mrefu, sitaki nitumie nguvu ila nataka kukwambia jambo moja sihitaji kutumia nguvu yoyote kwako nachoomba uwe mtiifu hili twende sawa bila kutishana tishana chochote”.

“Wewe mbona unanichanganya sana… Mi pia ni muhuni kama wewe hili jiji lote wananijua mimi nani, ulitakiwa uniambie kwenye simu shida yako hili nione kama naweza kukusaidia.. Halafu nani aliyekupa namba yangu? Sina muda wa kukusaidia chochote”. Akajibu huku mkono wake ukiminya kitasa cha ndani cha mlango wa gari na alipousukuma uligoma hii ikimaanisha umelock, alistuka akageuka upande wa Agent Kai kwa hasira akiwa kakunja uso mpaka macho yamejifinya lakini alichokiona moyo wake ulipiga mkambi puuuh, mdomo wa bastola aina ya Glock 42.

“Sitaki usumbufu wowote na kwakuwa umesema wewe ni muhuni basi sina budi kukuchukua kihuni… Tunaondoka wote sababu muda umeenda sana naomba utulie tuli kama unanyolewa lasivyo sitasita kukunyofoa roho kwa risasi”.

“Bro! unajua sikuelewi kabisa… Wewe ni polisi?”.

“Siruhusu kuulizwa chochote na wewe mpaka niamue mimi mwenyewe, upo chini yangu Othman na usijaribu ujanja wowote…. Funga mdomo wako”. Akaongea Agent Kai kisha akawasha gari na kuligeuza kasi matairi yakilalamika kwa fujo akabinya breki lilipokaa sawa na kuliondoa kwa kasi mtaa ukiwa umetulia kabisa.

Mwisho wa sehemu ya ishirini na nane (28)

Usiku umekuwa mrefu sana kwa ‘The Sole Cat” katika sehemu ya ishirini na nane.

Mbio za marathoni kuwasogelea maadui waliosababisha yeye awe hapo Malaysia awe katika jiji la Kuala Lumpur muda na nyakati hizi.

Tuendelee kufuatilia nini kitatokea katika sehemu inayofuata na zitakazofuata, tafadhali nipe muda wako hili uone nini nilichonacho katika hazina ya kichwa changu.

Mwisho wa sehemu moja uwa ndiyo mwanzo wa sehemu ingine ya Riwaya hii tamu yenye mtiririko mzuri ambao ukiwa msomaji utaona huko sahihi lakini kama huvutiwi na riwaya za kijasusi zilizo ndefu utaona haifai.

“Utajua ninachomaanisha muda si mrefu, sitaki nitumie nguvu ila nataka kukwambia jambo moja sihitaji kutumia nguvu yoyote kwako nachoomba uwe mtiifu hili twende sawa bila kutishana tishana chochote”.

“Wewe mbona unanichanganya sana… Mi pia ni muhuni kama wewe hili jiji lote wananijua mimi nani, ulitakiwa uniambie kwenye simu shida yako hili nione kama naweza kukusaidia.. Halafu nani aliyekupa namba yangu? Sina muda wa kukusaidia chochote”. Akajibu huku mkono wake ukiminya kitasa cha ndani cha mlango wa gari na alipousukuma uligoma hii ikimaanisha umelock, alistuka akageuka upande wa Agent Kai kwa hasira akiwa kakunja uso mpaka macho yamejifinya lakini alichokiona moyo wake ulipiga mkambi puuuh, mdomo wa bastola aina ya Glock 42.

“Sitaki usumbufu wowote na kwakuwa umesema wewe ni muhuni basi sina budi kukuchukua kihuni… Tunaondoka wote sababu muda umeenda sana naomba utulie tuli kama unanyolewa lasivyo sitasita kukunyofoa roho kwa risasi”.

“Bro! unajua sikuelewi kabisa… Wewe ni polisi?”.

“Siruhusu kuulizwa chochote na wewe mpaka niamue mimi mwenyewe, upo chini yangu Othman na usijaribu ujanja wowote…. Funga mdomo wako”. Akaongea Agent Kai kisha akawasha gari na kuligeuza kasi matairi yakilalamika kwa fujo akabinya breki lilipokaa sawa na kuliondoa kwa kasi mtaa ukiwa umetulia kabisa.

ENDELEA…!

WASIWASI NA MASHAKA II

“Clark! Habari za muda mfupi uliopita?”. Akaongea kwa simu huku bastola akiwa kaiacha kwenye dashboard macho yakiwa makini na vyote anavyovifanya kuhakikisha hakuna ujanja wowote unaofanywa na Othman pia alikuwa kashamjua hana uzoefu na mchezo anaoucheza bila kujua.

“Safi brother! Vipi huko salama?”. Upande wa pili ukajibu.

“Huku safi nakuja Klang River niko na dalali mmoja wa mbolea naomba nikukute nje sababu sitaki tuwastue waliokwisha lala?”. Akaongea kwa haraka.

“Sawa brother utanikuta tu bado sijalala”.

“Sawa! Sawa! Nikukute nje”. Alikatizia kuongea kwa haraka akakata simu baada ya kumuona Othman akijisogeza karibu yake.

“Kwanini unasogea kwangu? Na wewe washakufunza ujinga?”. Akamuuliza huku akikata kota kutoka barabara waliyokuwa kuelekea inayoelekea Klang Rver. Haraka Othman akasota huku anatetemeka kurudi kwenye siti yake, alikuwa akijaribu kufanya kitu huku tayari moyo wake na ujasiri wake wa kikawaida ukiwa haupo kabisa.

Dakika ishirini na tano mbele wakawa wamefika Klang River na Agent Kai akapunguza mwendo wa gari akaifuata njia inayoingia eneo la nyumba ambayo ipo kwa ndani ikiwa imezungukwa na miti mingi ya kupandwa na ikiwa imepangwa kwa ustadi wa hali ya juu, moja kwa moja akaenda palipoonyesha ndiyo parking ya magari ya nyumba ile. Nje aliwaona watu watatu wawili wakiwa wameshika bunduki na mmoja ni Clark na wote wakaja maegeshoni.

“Sema mkuu?”. Akaongea Clark huku anasogea taratibu, Agent Kai akashuka toka garini huku Othman naye akishuka toka kwenye gari.

“Safi Clark! Vipi hapa?”.

“Hapa safi tu, wageni wameshalala mi nilikuwa nacheki tv kukusubiri ufike”.

“Nimechoka nahitaji kupumzika… Kuna vyumba vingapi ambavyo havina watu?”.

“Ni kimoja tu ndiyo kimebaki, sababu mama na binti yake wamelala chumba kimoja, wakati yule niliyetoka naye ubalozini amealala chumba cha peke yake, kingine nipo mimi na kingine ndicho kipo free hakina mtu”.

“Basi mimi nitalala na huyu mgeni kwenye icho chumba”. Akasema Kai huku akilock milango ya gari akawasalimia tena walinzi ambao alishasalimiana nao mara ya kwanza alivyomleta Shufania.

“Sikuwa nimeona kule kuna nyumba ndogo ya nini ile?”. Akamuuliza Clark huku kasimama kwakuwa walikuwa wameongozana kuelekea ndani.

“Ni nyumba ambayo walinzi wanapumzika na kuhifadhi vitu vyao”.

Hapo Agent Kai akawageukia walinzi na kuwaita kwa mkono.

“Naomba wote mkalale sababu bado hapa kwa leo ni mahali salama kabisa”. Akawaambia walinzi wale wa kizungu kama alivyo Clark.

“Othman wewe utalala na mimi chumba kimoja, relax sababu hakuna baya litakalokukuta shida ulinitishia ndiyo maana huko hapa laa sasa hivi ungekuwa kwako unatafuta usingizi”. Akamwambia Othman baada ya kuingia sebuleni ambaye bado mpaka muda huo hakujua kwanini amechukuliwa toka kwake.

“Clark.. Usiku mwema”. Akaagana na Clark baada ya kuwa kashaonyeshwa chumba anachotakiwa kwenda kulala.

“Nawe pia boss!”. Akajibu Clark na kuongoza kuingia chumba anacholala.

Agent Kai akamuongoza Othman kuelekea chumba ambacho naye atalala wakaingia ndani ambako kulikuwa na kitanda kimoja, sofa la kukaa watu wawili moja na lingine la kukaa mtu mmoja, kabati dogo la nguo pia kulikuwa na meza.

“Naweza kukuacha nikakuamini na ukatulia kirafiki?”. Akamuuliza wakati anaweka begi lake na briefcase juu ya kabati ambavyo uwa havikosi kwenye gari.

“Naweza nikatulia brother… Shida mpaka sasa sijajua kwanini umenitoa nyumbani kwangu? Nimekukosea nini? Na nyinyi ni kina nani? Maana nimeona wenzako wote ni wazungu na wewe ni Mmmalaysia kama sikosei”.

“Unataka kujua sisi ni kina nani?... Keti kwenye sofa nikwambie sisi ni kina nani na kwanini huko hapa”. Akamjibu kisha akamuelekeza akae. Othman akakaa kwenye sofa la kukaa mtu mmoja.

Agent Kai akatumia fursa kuivua sura ya bandia aliyovaa mbele ya Othman na kumfanya Othman ashikwe na mshangao anachokiona.

“Mbona umestuka? Hii sura ushawai kuiona mahali?”.

“Nimestuka sababu kumbe umevaa sura ya bandia kaka.. Dah! Sijui kwanini umenifuata mimi? Ukiwa hivyo…. Lakini nahofia maisha yangu nahisi yapo hatarini sana kwako”.

“Maisha yako yatakuwa hayapo hatarini kwako kama utafuata niyatakayo… Naitwa Agent Kai kutoka shirika la kimataifa la kijasusi la kimarekani linaloitwa CIA… Kuhusu wale wengine nafikiri sasa ushawajua ni kina nani, nimekufuata wewe sababu unayajua robo ya yale ambayo tunayahitaji”.

“Kaka mi sijui chochote… Mi sijihusishi na ubaya wowote zaidi ya mambo ya magari pia sina lingine nilijualo kaka”.

“Othman mi nakujua na mpaka makao makuu ya CIA yanakufahamu wewe ni nani hivyo kuwa makini ninapokuuliza kitu na kunijibu tena haraka maana uongo wowote ni uongo ambao mimi nitaujua haraka sana sababu kazi ninayofanya inafungamana na uongo kwa asilimia sabini”.

“Kwani kaka unataka nini nikusaidie labda naweza kukusaidia maana najua mengi hapa Kuala Lumpur, nipo tayari kushirikiana na wewe kila kona utakayotaka nikupeleke ilimradi mimimsinitese wala kuniumiza kwa namna yoyote ile”. Alidhidi kuwa mpole Othman na hata machozi yalishaanza kumtoka alikuwa akijua na hata kuona kwenye baadhi ya movie ambazo wamarekani wameekti ikiwa wametoa visa na mikasa toka CIA, alijua watu hawa wanatesa sana watakapo majibu naye hakuna anachokipenda kama kubaki akiwa katika sura yake inayowapendeza mabinti. Agent Kai aliligundua hilo la uoga wa kweli aliokuwa nao Othman hivyo akaamini iwapo huyu atakuwa anajua mengi leo atayapata kirahisi.

“Sawa sitaruhusu kibaya chochote kitokee kwako kama utanifurahisha na kunijibu kwa ufasaha niyatakayo… Pia hautarudi kwako mpaka mimi nitakapokuruhusu urudi kwako… Kukikucha nitakufanyia mpango ukaenda kukaa sehemu nzuri na salama zaidi ya hapa”.

“Ahsante kaka! Niambie tu nikusaidie nini?”.

“Okay! Cha kwanza napenda kujua unamfahamu bwana mmoja anaitwa Rafael Khamdushini wa Alamanda hotel?”. Kazi ikaanza akambambika swali ambalo lilimfanya Othman kustuka dhahiri kisha akapoteza kiaina usoni kitu ambacho mtaalamu alishakipata.

“Vipi hujalisikia swali nilirudie?”. Akamuuliza tena baada ya kumuona anafikiria.

“hapana nimelisikia… Najaribu kuvuta kumbukumbu kaka”.

“Sawa nijibu”.

“Namfahamu, namfahamu bwana Rafael Khamdushini”. Akajibu huku akijiuliza huyo Rafael kafanyaje tena?.

“Umeshawai kulisikia jina la Ramsey Bronze mahali popote pale?”.

“Hapana sijawai kulisikia hilo jina kaka”.

“Umeshawai kulisikia jina langu nililokutajia?”.

“Lipi hilo? Kaka, maana ulivyonitajia nilikuwa so confused”.

“Agent Kai?”.

“Mmmh! Hapana mi kiukweli sijawai lisikia hilo jina zaidi ya unavyonitajia hapa”.

“Wiki mbili zilizopita ulimuanganisha bwana Rafael Khamdushin na dada mmoja hivi hili wawe wanawasiliana, je unaweza kunitajia jina la huyo dada ni nani?”.

Hapo Othman alistuka dhahiri mpaka akajistukia kuwa amefanya kosa, Agent Kai akamtikisia kichwa aongee.

“Dada mmoja rafiki yangu wa siku nyingi aliniomba nimsaidie kumuanganishia kwa kila mtu mmoja nayemjua katika hotel zote za nyota tano za chini yake na hata ndogo ndogo za mitaani… Nilikubali kumfanyia hiyo kwakuwa ni rafiki pia alinilipa pesa nzuri ambayo sikutegemea ikiwemo kunijazia mafuta gari yangu kwa siku tatu niliyofanya kazi hiyo… Sijui yeye kwanini alitaka nimuunganishe hivyo”.

“Nimekuelewa… Anaitwa nani? Na kwanini alikupa kazi hiyo wewe na si kuifanya yeye mwenyewe?’.

“Jina lake analopenda kuitwa na watu wengi ambao mimi nawajua anapenda kuitwa Language girl kwa kifupi LG na alinipa kazi kwakuwa anajua nina marafiki wengi katika mahotel ya hapa KL”.

LG kifupi cha jina a.k.a la Language girl liligonga kichwani kwa Kai na mara moja akakumbuka kuliona jina hilo katika kurasa ya majina ya simu ya marehemu aliyewasababishia ajali yeye na mwenzie.

“Wengi wanamjua kwa jina hilo na yeye anapenda kuitwa hivyo, wewe unamjua kwa jina gani ambalo ni jina lake halisi?”.

“Mi sina jina lingine ninalolijua zaidi ya uwa ananitania mi namuita Sweet naye ananiita Honey”.

“Una mahusiano naye ya kimapenzi?”.

“Hapana sina mahusiano naye ya kimapenzi zaidi ya utani na mara nyingi akitaka kwenda club ananitafuta mimi twende wote”.

“Ana shughulika na nini?”.

“Kwa kweli sijui ila ana pesa sana na kwakuwa ni mwanamke na ni mzuri sijawai kuwaza kumuuliza zaidi ya kuitikia wito anaponiita”.

“Yukoje kiumbo na sura?”.

“Mrefu, ana umbo namba nane, sura yake ndefu macho yake makubwa kiasi na ana midomo mipana pia akicheka ana mwanya mwembamba kiasi”. Maelekezo yalipoisha tu toka mdomoni mwa Othman, umbo la LG likamjia machoni Agent Kai.

“Anapenda kuvaa nguo za aina gani?”.

“Suruali za aina ya jeans rangi tofauti akibadili kila siku na blauzi zenye mikono mirefu, kichwani uwa anavaa hijabu ambayo mara nyingi rangi yake urandana na rangi ya viatu si blauzi”.

Kengele ikagonga kichwani mwa Kai, picha ya mdada aliyeenda kumpokea Airport akijifanya ndiyo Detective Marie ikajaa taswira yote huku akifuta sura na kuipachika sura aliyoambiwa papo hapo akaivalisha kilemba cha hijabu.

“Anaishi wapi?”.

“Siku ambazo alikuwa ananichukua hadi kwake au hata siku nyingine kunikaribisha alikuwa akiishi Pangsapuri Cempaka mtaa wa Merdeka Villa barabara ya Jalan Merdeka, alipanga nyumba nzima huko lakini kuna siku za hivi karibuni aliniambia amehamia kwenye nyumba yake aliyonunua mtaa wa Taman Bukit Kalil barabara ya Jalan Bayan, eneo la Melaka”.

“Ni mtu muhimu sana ninayemuhitaji”.

“Kwani kaka amefanyaje? LG”.

“Anahusika na kundi la utekaji nyara wa wanasayansi toka nchi nayotoka ya Marekani… Sina tatizo lolote na wewe Othman na ninaomba unisamehe kwa haya yote yanayokufika sasa, naomba unisaidie kumpata huyu mwanamke”.

“Sasa kaka ulivyonichukua ulinichukua nikiwa bila simu yangu na hiyo ndiyo ina namba ya watu wote wanaonizunguka ikiwemo ya LG”.

“Sawa imeshatokea hivyo, nafikiri asubuhi twende wote kwako halafu utampigia kwa simu yako… Basi kwa leo tuishie hapa naona sasa una amani na uko upande wa kutotaka kufanya jambo lisilofaa”.

“Nashukuru kaka … Sikujua kama LG si mtu mzuri na wala sijawai kufikiri kama wanasayansi waliopotea hapa KL kwa kutekwa inawezekana mimi nipo karibu na ninatoa msaada kwa namna moja ama nyingine”.

“Si rahisi kujua unaposhirikishwa katika mambo kama haya bila kuambiwa… Sikia Othman mi nakuacha kwenye chumba hiki ulale mwenyewe tu mi naenda kulala sebuleni sababu kuna mambo natakiwa kuyamaliza usiku huuhuu… Nachoomba kwako usijaribu chochote kingine zaidi ya kwenda bafuni kuoga au chooni kufanya jambo lolote huko, vyumba vya kulala vya nyumba hii vina huduma zote zinazohitajika kwa binadamu”.

“Kaka mimi purukushani sijawai kuziweza pamoja na uhuni wote nilionao kaka mimi ni mtu muoga sana hasa kwa watu wa usalama nawaogopa sana… Usihofu kabisa katika yote yale na wala usiwaze”.

“Okay! Pumzika sasa, tutaonana asubuhi… Angalizo ni kuwa nakufungia kwa nje hautaweza kutoka nje ya chumba mpaka nitakapokuja kukufuata utoke muda nitakaoamka”.

Akasema Agent Kai na kuchukua vyote vinavyomuhusu ikiwemo shuka ambalo alilipata humohumo chumbani.

Agent Kai alitoka kwenye kile chumba na kuelekea sebuleni ambapo alipofika na kuweka vitu vyake mezani katika mpangilio anaotaka, alichukua simu yake akapiga namba za mkuu wake wa kazi Chief Executive of the vice president.

“Halloo! Kijana wa mie”. Mpokeaji wa upande wa pili aliongea baada ya kupokea simu.

“Niambie kitu, mzee wa mie”. Akajibu Agent Kai.

“US First!”.

“Siku zote ni namba moja”.

“Vipi treni linaenda?”

“Yaap! Ndiyo limetoka stesheni mzee wangu hivyo bado halijakolea mwendo”.

“Hahahah hahahahah! Lisije kuwa la enzi ya mkoloni wakati sisi tunataka litembee kasi”.

“Si kwa mwanao,au unajisahaulisha? Mzee wee jumapili nipigie kabla ya saa sita za Malaysia niulize limefika kituo cha mwisho au halijafika”.

“Nikikusahau nitakuwa nipo kaburini, naujua udereva wako ulivyo… Sasa mwanangu kuna duru ya kiintelejensia kanipenyezea rafiki yako ambaye alikutafuta kwakuja hapa ofisini, huyu rafiki yako anaitwa Kristian Lee”. Akanyamaza kidogo na papo Agent Kai akamrushia swali.

“Yupo Marekani? Kristian”.

“Yah! Yupo hapa… Lakini ameacha kazi shirika la ujasusi la Russia FSB toka mwaka juzi kwa jinsi alivyonieleza kwa sasa anafanya kazi zake binafsi”.

“Eeeeh! Hizi kazi bwana inafika kipindi unaona bora ufanye mambo mengine kazi sana kuchunguza vitu vilivyojificha huku vikilindwa na kikundi, serikali au hata mtu mmoja akijitahidi kujilinda tena kwa gharama yoyote… Turudi kwenye duru husika niambie inasemaje? Maana mimi kusema ukweli simuamini jasusi wowote kuacha mimi mwenyewe, sisi tabia zetu hazitabiriki zinajificha ndani ya mioyo yetu hasa tunaotoka nchi kama yetu ya Marekani na wanaotoka nchi zingine kama Russia na zingine ambazo wewe jasusi mstaafu unazijua”.

“Ni kweli hata mimi nilishangaa kwanini anakuulizia na kusema ana jambo muhimu sana anataka kukupa taarifa ambayo ni muhimu sana… Tulimchukua tukampeleka kwenye ofisi yetu ya kiintelejensia na tukamuhoji mimi na mkuu wa CIA, anasema mlisoma wote shule ya msingi china kisha wewe ukamuacha ukachukuliwa Marekani na yeye akachukuliwa na wa Russia lakni mkakutana tena katika mafunzo ya kininja. Achana na hayo, tuliamua kumbana ni kitu gani kilichomfanya kukutafuta akatuambia kuna rafiki yake mmoja ambaye ni mchina anafanya kazi shirika la kijasusi la China la Ministry of State Security (MSS), huyu mchina inasemekana naye ulikuwa naye shule moja ya Acrobatic’s hivyo anakujua kwa sifa zako ulizowapa shule ile kipindi icho… Kristian amepewa taarifa ambayo ipo ndani ya MSS kwa sasa kuwa kuwa majasusi wanne wa Korea Kaskazini usiku wa leo wanaingia huko Malaysia kwa kazi ya kuzuia jitihada zako pia wamepewa oda ya kuhakikisha wanaondoka na wewe kwenda Korea Kaskazini wana kisasi na wewe”.

“Mpya hii mzee wangu… Lakini nishazoea kusakwa na hao watu wa mashirika mengine na wengi wana kisasi na mimi kwa niliyoyafanya kwa nchi zao… Mmefuatilia vizuri habari hii?”.

“Nilimpa kazi mkuu wa CIA amefuatilia jambo hili kitaalamu na amenipa jibu ni kweli inaonyesha shirika la ndege la Malaysia Airways kuna wakorea kaskazini wanne wamesafiri usiku huu wakipitia Airport ya China ambayo kwa sasa ndiyo kiwanja cha ndege wanachotumia wakorea kaskazini.. Amepata picha za wawili kwakuwa ni majasusi wakubwa kabisa katika Korea Kaskazini, mambo mengi makubwa ya nchi hiyo katika ujasusi kimataifa wamefanya hao na nafikiri utakuwa unawajua tu ukiona picha zao utaligundua hilo”.

“Ni kweli majasusi wengi wa nchi hiyo nawajua maana tulivyoingia kisiri miaka mitano iliyopita katika operesheni ya kuwaokoa military agency nikiwa na Scott tulikutana nao… Mnitumie picha zao”.

“Sawa nitakutumia muda si mrefu… Mkuu wa CIA amenishauri tukuongezee mtu haraka iwezekanavyo apitie Indonesia, vipi kuhusu hilo?”.

“Nitachagua mimi kama nitahitaji mtu, hahahahh hahahah naona mmeingia uoga sababu ya wakorea kaskazini hahahah hahah msipaniki wazee kazi wanayo hawataweza kiwepesi.. Nafikiri giza litakalofuata nitakuja najibu, ahsante kwa taarifa mlizonipa”.

“Ok! Nikutakie usiku mwema mwanangu na kazi njema kukikucha, kumbuka Marekani na umuhimu wake kwanza kabla ya yote”.

“Usijali… US First!”

ENDELEA NA MOTO..!

WASIWASI NA MASHAKA III

Mtu aliyepita sebuleni alisababisha Agent Kai kustuka usingizini na kufungua macho kisha kukutana na mwangaza wa asubuhi, hapo akajizoa zoa kujiinua kisha akakalia matako huku akifikicha macho yake ambayo bado yalikuwa yana usingizi wa kutosha lakini kwakuwa pale sebuleni na kuendelea kulala aliona si vizuri. Alipopindua macho kuangalia ni nani aliyekatiza macho yakagongana na macho ya Clark.

“Za asubuhi? Kaka”. Clark akamsalimu.

“Safi! Vipi wewe? Clark”. Akamjibu.

“Niko poa kaka, namshukuru Mungu… Nataka nielekee kazini ubalozini”.

“Ooooh! Basi sawa… Vipi wageni wetu wameamka? Maana wana ratiba ya kwenda hospital tuna mgonjwa huko”.

“Ndiyo nimetoka kuongea na dada sasa hivi alinigongea mlango kunipa taarifa hiyo… Mlinzi mmoja atawapeleka kwa gari yao, nishampigia simu kumpa taarifa anatakiwa awapeleke hospitali wageni”.

“Saa hivi ni saa kumi na mbili na dakika kumi, acha niwapeleke mimi mwenyewe ila yule ambaye ulitoka naye kule ubalozini naomba umpe maelekezo ya sehemu ya kupikia aandae chai wakirudi wenzake wanywe pia muelekeze na kuhusu chakula cha mchana na hata usiku, kifupi yeye leo ndiyo awa mkuu..!”.

Agent Kai alirudi kwenye chumba alichomfungia Othman na kufungua mlango akaingia na kumkuta Othman bado kalala, hakutaka kumuamsha alichofanya akaufunga mlango kwa funguo kwa ndani kisha akaelekea maliwatoni kushughulika na shughuli zote zinazohusu haja zote za chooni na usafi wa mwili akifanya vyote katika uspidi. Alipotoka ndipo akamkuta Othman kafumbua macho yupo kitandani lakini bado kajifunika shuka mwilini”

“Za asubuhi? kaka”.

“ Safi Othman, za kwako?”.

“Safi kaka… kumekucha!”.

“Yah! Kumekucha… Uwa unakunywa chai au kahawa? Au hutumii chochote kati ya hivyo?”.

“Kahawa natumia lakini kama ipo supu itapendeza zaidi”.

“Ok! Naenda hospitali… Nikiwa narudi nitakuchukulia supu, endelea kupumzika tu nitarudi baada masaa mawili au matatu hivi”.

Akatoka n akumuacha Othman akiendelea huku akimfungia kwa funguo kwa nje.

Moja kwa moja akaelekea chumba alichoonyeshwa na Clark kuwa ndiyo chumba walicho Shufania na mama yake akagonga kistaarabu na unyenyekevu.

“Nakuja kufungua”. Sauti tamu aipendayo akitamani aisikie muda wote ikasikika kwa ndani.

“Asallaam aleykuum!”. Akamsalimu Shufania baada ya mlango kufunguliwa tu na wote kutanguliza tabasamu pana wakifurahi kuonana tena Agent Kai akiwa katika sura yake halisi.

“Aleykuum salaam warahmatullah wataallah wabarakatuh! Za asubuhi?”.

“Safi sana.. Huko poa?”.

“Niko poa kabisa… Ulirudi saa ngapi?”.

“Saa tisa na nusu… Vipi mama amaeamkaje?”.

“Mmmh! Ndivyo ilivyo hivyo unachelewa kulala namna hiyo?... Mama yuko poa ameshajiandaa tulikuwa tunasubiri aje dereva tuondoke”.

“Haya dereva nimekuja twendeni”.

“Unatupeleka wewe? Hupumziki?”

“Nitapumzika nikimaliza hii kazi iliyonileta Malaysia.. Mstue mama twende”.

Baada ya dakika hamsini walikuwa wamefika hosptali ya Gleneagles (GKL), Agent Kai akaenda kupaki kwenye maegesho na kuzima injini.

“Nawasubiri hapa mama… Hakikisheni mnamuuliza dokta kama inawezekana tukarudi na mzee”. Akawaomba wafanye kuomba mzee Mahamud wakaondoka naye.

“Sawa mwanangu.. Naamini atakuwa yuko poa na tutaruhusiwa kwenda naye”.

“Shufania utanijuza juu ya gharama au mambo mengine humo ndani”.

“Sawa sawa… Hatutakaa sana hili tusikucheleweshe kupumzika na kufuatilia mambo yako”.

Mama Ilham na mwanae Shufania wakashuka kwenye gari na moja kwa moja wakelekea eneo la ndani la hospitali wakimuacha Agent Kai akibaki kwenye Range Rover Sport.

***** ***** *****

Saa kumi na mbili kamili alarm aliyotegesha kwenye saa ndogo inayokuwa siku zote kwenye kimeza kidogo kilicho pembeni ya kitanda chake cha kifahari ilimstua usingizini Mr. Logan Puteri na haraka akanyosha mkono kwenye kimeza icho icho kunyanyua simu yake ya mkononi aina Iphone X rangi nyeupe akatizama zinapoingia notification akakutana na meseji zilizoonyesha zimeingia, haraka akatoa lock huku akimtizama mke wake upande wa pili wa kitanda ambaye alikuwa bado yupo ndani ya usingizi mzito.

Mzee baba master plan akafungua meseji moja moja kusoma. ‘Ina maana hakuna jipya? Ina maana adui yetu usiku wa leo hajafanya jambo baya kwetu.. lakini kwanini hakuna habari yake yoyote?’ Aliwaza Logan kisha akajiinua kitandani na kujinyosha nyosha viungo vyake.

Akamuangalia tena mke wake akamsogelea na kumbusu kwenye paji la uso kuonyesha upendo wake kisha akatoka mule chumbani moja kwa moja akaelekea kilipo chumba chake cha mazozezi (gym).

“Halloow! Hassan”.Akaongea baada ya kupiga namba za simu za Hassan Saddiq kiongozi wake wa mambo ya kitaalamu zaidi.

“Halloow! MP”. Upande wa pili ukajibu.

“Vipi hali?”.

“Ndiyo tumeingia Sarawak muda huu”.

“Basi utanijulisha kinachoendelea… Nampigia Khalid muda si mrefu hili awaandae watu wetu kabisa”.

“Sawa mkuu fanya hivyo, ingawa niliongea naye muda si mrefu sababu alinipigia kuniulizia tuko wapi”.

“Huku bwana mpaka sasa hivi naamka hakuna mpya kuhusu mteja wa hapa, nafikiri hata yeye toka afanye alichofanya mchana atakuwa hajafanya lingine lililokuwa baya upande wetu”.

“Mmmh! Usipende kujiaminisha hivyo MP, mi mwenyewe hapa tuko na Takasho lakini kila mara tunaangalia usalama wetu nyuma isije kuwa kuna mtu anatufuata, ujue sijawai kukaa kimya toka afike KL mtu huyo.. Uchunguzi niliofanya jamaa si wa kitoto, nitakutumia faili nililotumiwa na rafiki yangu wa MOSAD, Palestina. Faili lake linatisha kaka, mambo aliyoyafanya US Navy Seals kwa kweli si mtu poa kabisa Korea Kaskazini wana haki ya kutaka tuwatafunie wao wameze tu sababu duru inasema si vikundi tu vya kigaidi na kihalifu kama Mafia na mengineyo yanayomuhofia huyu mtu bali hata mashirika ya kijasusi ya nchi zenye uadui na Marekani yanamuhofia sana na wanatamani leo kesho wampate”

“Siyo kama najiaminisha, nina vyanzo vingi vya habari lakini hakuna habari iliyopo inayogusa maslahi yetu zaidi ya ile habari ya mchana ya ajali Bambino Village…. Basi acha niwacheki na wengine nijue ratiba inasemaje, nikutakie safari njema”.

“Sawa mkuu”.

Simu zikakatwa hapo Mr. Logan akatafuta namba ingine na kupiga.

“Mkuu!”. Upande wa pili ukaongea haraka baada ya kupokea.

“Yaap! Niambie?”.

“Hakuna jipya kaka… Haijulikani amelala wapi, mfano mimi nimekuwa macho muda mrefu kuangalia kamera tulizotega Alamanda hotel lakini hakuna kitu kabisa yaani ni kama amerudisha chumba vile”.

“Kwani walivyopekua kwenye chumba kulikuwa hamna vitu vyake?”.

“Hamna vitu vyake… Hakuacha begi la nguo wala kingine chochote”.

“Isije kuwa ameshastuliwa na wale ambao mliwahoji na kuwaomba baadhi ya msaada?”.

“Inawezekana … Okay! Ngoja nimpigie Nawaz nijue ilikuwaje walivyokwenda walikosema wataenda kwa binti aliyekuwa anafanya kazi hapo hotelini, nafikiri tukutaneni jumba la nyoka saa tano sababu mchana nitaelekea Sarawak… Asubuhi hii nitaenda ofisini mpaka saa nne nitatoka”.

“Sawa sawa mkuu… Mi nitatoka hapa hotelini muda si mrefu nami nakuja ofisini kusaini nitawaacha wengine waendelee na uangalizi kuona kama anaweza akajisahaulisha na kutokea”.

“Sawa… Baadaye!”.

Simu ya Mr. Logan ikaendelea kutumika akapiga namba ingine ya Nawaz Patrash.

“Nilitaka nipige kwako sasa hivi hapa umeniwai umepiga”. Upande wa pili ukaongea.

“Kawaida… Lete habari za huko zinaendaje?”. Akaongea kwa kasi Mr. Logan.

“Aisee! Inaonyesha jamaa katuwai yupo makini na kazi kwa kweli acha tumsifie”.

“Eeeeh! Kwanini?”.

“Tulikaa nje ya nyumba ya wazazi wa binti muhudumu wa Alamanda na wazazi wake mpaka saa nane usiku tukachoka tukaamua kuondoka mimi na LG, muda huu tumerudi tena mtaa huu tumepewa taarifa na majirani kuwa hawapo hawakurudi jana na wanahisi kuwa yule mzee wa familia hii alipelekwa hospitali na atakuwa amelazwa maana aliondoka kwa taxi muda walioondoka kitu ambacho uwa kinatokea endapo mmoja kati ya watu wa familia hii anaumwa, mara nyingine wao uwa wanatumia usafiri wa jumuiya kama treni na mabasi ya mwendokasi tu pale watokapo au warudipo toka kwenye shughuli zao”.

“Hapo kama usemavyo… Mteja katuwai karibu kila kona kafika yeye, hatujui tu ametufikia kwa kiasi gani na kutufikia huko kumesababisha amejua ni na nini kuhusu watu pesa…. Basi nafikiri tusubiri habari toka kwa Michael akifika kazini atatufanyia uchunguzi utakaoweza kutusaidia juu ya hili la mtejapesa… Saa hivi nataka nijiandae nielekee ofisini kuna viraka naenda kuvikazia kisha naomba tufanye kikao saa tano jumba la nyoka nitakuwa nina mpango mpya baada ya kuongea na Michael”

“Sawa.. Tunaona sisi tuondoke hapa hili nami nifike ofisini kuna faili natakiwa kuwasainia pale, nampeleka Damia kwake akapumzike saa tano tutaonana wote huko jumba la nyoka”.

Simu zikashuka chini kisha Mr. Logan akakata na kutoa pumzi nzito kama mara mbili akaviangalia vyombo vya gym akitamani kupiga kiakili lakini hamu ya kimwili haikuwepo kabisa.

Mwisho wa sehemu ya thelathini (30)

Tumeona mipango inavyozidi kuwekwa sawa kwa pande zote mbili zinazowindana, huku kama ni mpira basi asilimia za kumiliki mpira zikionekana bado zinampendelea Agent Kai.

Taarifa zinasema majasusi wa kikorea kaskazini wameamua na wao watumie fursa ya Agent Kai kuwepo Malaysia kikazi na wao kuja kumtia katika himaya wakiwa hawaamini utendaji kazi wa Mr. Logan na watu wake.

Je? Mipango ipi kati ya mipango inayozidi kupangwa na pande zote mbili itatimia

Je? Majasusi wa Korea Kaskazini watafanikiwa kutimiza kilichowaleta Malaysia

Majibu ya yote haya yanapatikana katika sehemu zinazofuata za MSHANGAO…

WASIWASI NA MASHAKA IV

“Habari yako Othman?”. Agent Kai aliongea baada ya kufungua mlango wa chumba alichomuacha Othman alale mwenyewe tu huku yeye akienda kulala sebuleni, alimkuta Othman ilihali ameamka anaangalia luninga iliyomo kwenye chumba kile.

“Safi tu kaka, vipi hali yako?”.

“Safi! Ndiyo tumerudi toka hospitali… Sasa hivi ni saa mbili na nusu, nafikiri ni muda mzuri wa kwenda kwako kwa ajili ya wewe kutumia simu yako kama tulivyokubaliana usiku uliopita”.

“Sawa kaka… Naomba tukishamaliza lako uniache huru, nakuhakikishia sitamwambia yeyote juu ya ujio wako kwangu”.

“Yah! Ni kweli sitakuwa na sababu ya kuendelea kukushikilia lakini nina kosa la kiufundi nimefanya ambalo litanifanya nisikuamini kama utakuwa kimya kama unavyoniahidi”.

“Lipi kaka?... Kaka nina masuala ya kibiashara nilikuwa nayafuatilia yatasimama nisipokuwa huru, please nisaidie”.

“Othman! Nimekuja na wewe huku bila kukuzuia kuona unaelekea wapi, niliamini unaweza kunisumbua sana kwenye mahojiano, niliamini nitatumia nguvu kukuhoji na kupata niyatakayo hivyo hautarudi kwako lakini umekuwa mtiifu kwangu na kunipa ushirikiano tena bila hata kujaribu ujanja janja wowote… nafikiri nikuache huru lakini kwa masharti ambayo nitakupa”.

“Sawa kaka nipe masharti hayo”. Akajibu kwa haraka Othman huku akijiweka vizuri kitini kusikia masharti atakayopewa. Agent Kai alimtizama kwa makini kana kwamba anaingia kwenye ubongo wake kufikiri anachowaza.

“Nataka nikuamini, ukishanikutanisha na LG.. Sitataka ukutane na mwingine yeyote awaye ambaye anahusiana na unaowajua wako karibu na Sweet LG, lolote litakaloonekana katika macho yangu au akili yangu limesogea eneo hili na kuhatarisha maisha ya watu waliopo hapa utahusika moja kwa moja ndugu Othman na mara moja utawajibika tena kwa kifo si mateso, mkono wangu ni mrefu uliojaa ufundi na mafundi, nakuonya kuhusu hili na niko serious unatakiwa uendelee na mambo yako kama kawaida tu sababu nikimpata LG sitamuachia tena na hivyo hautakuwa matatizoni”.

“Nakuahidi hilo kaka.. Hujanifanya lolote baya umenitendea wema sana tofauti na mtu mwingine mwenye uwezo kama wako angetaka kunidhuru kwa jinsi nilivyokuwa nakujibu”.

“Usihofu kuhusu usalama wako, huko salama kwa asilimia mia moja unachotakiwa na kujiweka kando kabisa na masuala haya uache sisi tuucheze huu mchezo”.

“Nitashukuru sana kaka kubaki na uhuru wangu, nitakaa mbali kabisa na LG na ninashukuru siwajui wenzake wengine”.

“Okay! Jihudumie supu nimekuletea na vitafunwa aina ya chapati.. Mi ninafanya maongezi na wengine waliopo hapa nijue wanaendeleaje na kuwapa ratiba yangu itakavyokwenda”. Akaongea Agent Kai kasha akamuacha Othman anajiandalia supu aliyoletewa.

Kama kawaida alimfungia kwa nje na kwenda hadi sebuleni alipokuwa amewaacha Shufania, mama yake mama Ilham na baba Ilham, mzee dokta Mahamud ambaye Shufania na mama yake walifanikiwa kumuombea atoke hospitali na kumuelekeza kuhusu mambo yanayoendelea na juu ya usalama wao na wakafanikiwa kumshawishi kuja naye huku kutokana mzee mwenyewe kuwa anajua mambo kama hayo haraka akaelewa.

“Dokta umejitahidi kula kama nilivyosema?”. Akamuongelesha kwa lugha yao wanayopenda kuitumia familia hii ya kisyria, lugha ya kiarabu.

“Nimekula mwanangu.. Supu imeisha na hata mikate nimekula ya kutosha tu, ahsante sana mwanangu”.

“Heti mama! Amekula kweli?”. Akamuuliza mama Ilham aliyekuwa kakaa pembeni ya mume wake sofa moja.

“Kwa kweli amejitahidi sana.. Tunatakiwa kumshukuru kwa kweli, ahsante sana”. Akajibu mama Shufania huku akikwepesha macho yake kuangaliana na Agent Kai.

“Sawa! Ahsanteni na nyie kwa ushirikiano wenu… Shufania yupo chumbani?”. Akawauliza.

“Hapana yupo jikoni anaosha vyombo tulivyotumia”. Akajibu mama Ilham.

“Nataka nitoke, acha nimuone kwanza yeye”. Akasema Agent Kai na kuondoka pale sebuleni kuelekea alipoambiwa yupo Shufania.

Alinyata taratibu kama anamyatia adui sababu binti mzuri wa kiarabu alikuwa kampa mgongo anaosha vyombo hana habari. Alipomfikia hatua mbili tu toka aliposimama alipuliza upepo toka mdomoni kuelekea shingoni kwa binti huyu na kusababisha binti ageuke upesi huku dhahiri mshtuko ukiwa usoni mwake lakini kwa alichokutana nacho machoni kilimfanya atabasamu na kutamani hata angekumbatiwa na amuonaye na hata Agent Kai alitamani kufanya hivyo lakini alizijua tamaduni za kiislamu hazikutaka hivyo kama hawajaoana. Naye alijibu tabasamu lile pana.

“Natoka Shufania, naingia kazini mapema leo… Wateja wa mbolea wananihitaji asubuhi hii”. Akaongea na kusababisha cheko kubwa kulipuka baina yao mpaka Kai akavunja taratibu mpaka iliyopo kati yao akamziba mdomo kwa kiganja chake na papo hapo wakakumbatiana.

“Wazazi watasikia macheko yetu si adabu Shufania… Hahahahah! Samahani nimekukumbatia”. Akaongea Kai na kumtoa mikononi mwake Shufania.

“Bila samahani Kai…. Upande wangu natambua tumekosea lakini ni bahati mbaya na hapo siku zijazo Mungu atatufanyia wepesi itakuwa halali”.

“Napenda nikwambie kitu muhimu sana”. Akasema Agent Kai huku kakutanisha viganja vya mikono yake (kunyenyekea).

“Niambie Kai”. Shufania akatoa ruhusa huku leo akimudu kuvumilia kuyaangalia macho ya Agent Kai ambaye kumkazia mtu macho kwake uwa ni kawaida sana.

“Sitaacha busara zako na hekima zako zikae nje ya nyumba yangu, nahitaji uwepo wako pembeni yangu, nahitaji uwepo wako kwenye malezi ya wanangu.. Nakupenda sana, nakuhitaji”. Akasema huku ikiwa ahadi iliyotoka ndani ya moyo wake.

Machozi yalianza kuporomoka toka machoni mwa Shufania, viganja vyake akavifumbata kifuani mwake, uso wake ulidhihiri furaha kubwa sana alitamani aruke kumkumbatia kijana aliyesimama mbele yake.

“Furaha niliyonayo imeambatana na machozi ya furaha, natamani furaha hii ningewashirikisha ndugu zangu wote wakajua nimeletewa mwanaume wa moyo wangu, kijana mwenye asili ya kiafrika, shujaa wa Marekani… Nakupenda pia, nakuhitaji pia Kai Hamis”.

“Unanipa sababu ya kufanya kazi hii kwa ufanisi na spidi hili lengo letu ambalo limeingia katika ratiba… Wewe ni wangu wa maisha nakuahidi kufunga ndoa na wewe haraka”.

Hapa wote hawakuvumilia kwani Shufania alijisogeza alipo Kai naye akampokea kwa kumuweka kifuani mwake wakakumbatiana. Kumbatio la dakika tatu lilipita huku wakitamani wasiachiane.

“Acha nikafanye kile nilichokuja kukwambia hapa… Nimefurahi sana leo”.

“Mimi pia nimefurahi sana… Wazazi waliniuliza kuhusu uhusiano wetu nikwakwepa kujibu, nenda salama huko uendako naomba ukawe makini sana mtarajiwa wangu nakutegemea, natamani niwaone watoto wako baadaye ukirudi unionyeshe hata picha zao nianze kuwajua”. Akaongea Shufania huku anapapasa mgongo wa Agent Kai.

***** ***** *****

Saa mbili kasoro dakika tano Mr. Michael alikuwa akisimamisha gari yake katika parking ya magari ya ubalozi wa marekani wanapopaki wao maofisa wa ubalozi na wafanyakazi wengine wa ubalozini. Alishuka kwenye gari na mara akakumbuka jambo aliloahidiana na Mr, Logan Puteri. Papo hapo akaahirisha kuelekea ofisini kwake akanyoosha kuelekea ofisi ya afisa wa ulinzi wa ubalozi.

Kwakuwa walikuwa ni marafiki waliozoeana sana hakuona haja hata ya kugonga mlango ambao ulikuwa ni mlango wa kioo na mtu aliyekuwa akimfuata alimuona yupo kwenye meza ya ofisi akisoma baadhi ya mafaili yaliyopo mezani kwake. Mr. Michael alisukuma mlango na kuingia na kupokelewa na tabasamu lililochanua toka usoni mwa mwenye ofisi hii.

“Karibu Mr. Michael…. Hahahah! Leo umekurupushwa na nini huko? mpaka umeniamkia mimi ofisini kwangu”. Akaongea mwanaume huyu wa kizungu katika lugha yao ya kiingereza.

“Ahsante sana Mr. Cowel… Nimekuota usiku unaondoka na maji katika mto mkubwa sana wenye mamba na mamba hao wakakugeuza msosi mbele ya macho yangu na mtu mwingine ambaye sikumtambua”. Kilifumuka kicheko kikubwa na viganja vya mikono vikalipuka mlio wa kugongana pwaah!

.

“Walikuachaje wewe hao mamba? Fuckin! Walikutafuna wewe tu hao sema unanizuga mimi wamenila mimi”.

“Wewe ni mnyama na wamekutafuna wewe sababu wewe ni mnyama”.

“Mmmh! Hizo ndoto zitupe kule.. Monster!... Niambie cha kweli kilichokuleta hapa, maana wewe huwezi kuja ofisi hii bila kuwa na sababu maalumu”. Akasema Mr. Cowel.

“Ni kweli mkuu wa kazi nina shida kwako..!”.

“Shida hiyo ya asubuhi asubuhi inamalizwa na mimi? Na si wakuu zako?”.

“Acha udunguaji … Tushakuwa watu wazima sisi, ingekuwa inamalizwa na balozi au hao wengine ungeniona hapa kufuata nini?”

Wakagonga mikono yao kuonyesha furaha yao katika maongezi yao ya utangulizi.

“Lete mpya kaka!”. Mr. Cowell akaongea baada ya Mr. Michael kuvuta kiti na kukaa.

“Ndugu yangu na jambo nataka tulijadili kidogo… Ni jambo linalohusu mambo yanayoendelea hapa ubalozini”.

“Mmmh! Mr. Michael jambo gani hilo? ambalo mimi kama mkuu wa kitengo cha ulinzi silijui”.

“Hivi una lolote unalojua juu ya ugeni wowote uliopo hapa KL ukiwa umekuja katika kuchunguza juu ya wale wanasayansi wetu pamoja na wapelelezi wetu waliotekwa na kikundi au watu wasiojulikana?”.

“Najua kuhusu hilo kaka, kwani wewe hujui?”.

“Sijui kwa sababu sikushirikishwa kwa mara ya kwanza hapa ubalozini linafanyika jambo bila mimi ninayeijua Kuala Lumpur kwa miaka zaidi ya nane sasa”.

“Mimi mwenyewe sikulijua hilo mpaka mtu huyo alipokuwa ameomba kwa balozi amlete mwanamke mmoja kwa ajili ya hifadhi na sikumuona sababu alimleta usiku mnene ambao kama ujuavyo siwezi kuwepo muda mpaka kwasababu maalumu, nilipokuja asubuhi nikapewa taarifa na vijana waliokuwa zamu usiku kuwa tuna mgeni mwanamke aliyeletwa kuhifadhiwa kwa ajili ya usalama wake, nikamuuliza ameletwa na nani ndiyo nikaambiwa ni mtu huyo mgeni unayesema”.

“Bado stori yako haijakaa sawa, nielekeze vizuri Mr. Cowell… Ni nani huyo mtu?”. Akauliza Mr. Michael huku akijifanya hajui ni nani huyo mtu wanayemuongelea kuwa ni mgeni.

“Balozi mwenyewe aliniita kuniambia juu ya mtu huyo jana asubuhi, akaniambia walifanya siri juu ya ujio kutokana na ombi la makamu wa Raisi wetu… Na hii ilitokana na kutokuwa na uaminifu toka wapotee wapelelezi watatu wa kabla yake, ni mtu ambaye hata wewe utakuwa unamjua kutokana na umaarufu wa kisifa aliokuwa nao toka akiwa US Navy Seals ni Sajenti Agent Kai Hamis”.

“Kazi kweli kweli hii Mr. Cowell, inaonekana hadi mimi siaminiki sasa… Okay! Unasema hujawai kuonana naye hii inamaanisha anafanya kazi kwa muongozo wa Kapteni peke yake?”. Sura ya Mr. Michael ilionyesha kuwa na hisia fulani ya kutopendezewa kabisa na hali ya yeye kutoaminiwa tena.

“Ndiyo anafanya kazi kwa muongozo wa balozi Kapteni Jones”.

“Sawa haina shida ni jambo jema waliloamua… Vipi mwanamke aliyemleta yupo hapa?”.

“Nilivyofika leo asubuhi taarifa ya kwanza kukabidhiwa ni ya kuondolewa huyo mwnamke hapa ubalozini na inasemekana ni kwa amri ya Agent Kai… Vipi Michael kuna tatizo katika jambo hili? Maana naona uso wako unadhihirisha machoni mwangu kuwa hujaridhika na yanayotokea haya ya kisiri siri wakati sote tupo hapa Malaysia kama timu”.

“Shauri lao… Mimi Agent Kai ni mtu ninayejuana naye lakini sina urafiki naye wa kivile zaidi ya salamu pale ninapokutana naye, wangefanya iwe wazi kwa sisi watu wa juu tungeweza msaidia zaidi katika safari zake za kupita huku na huko… Sawa acha wafanye wanavyojisikia nawaombea mafanikio katika kazi hii sababu wakishinda wao tumeshinda Marekani”.

“Kwa kweli Michael… Mi wakiniomba msaada wa vijana wangu nitawapa tu haina wasiwasi juu ya hilo”.

“Poa! Cowell, acha na mimi nikale viporo vyangu vya kazi ofisini kwangu, saa sita nina kikao na waziri wa mambo ya ndani wa hapa kisha saa tisa nina kikao kingine na waziri wa mambo ya kigeni hivyo nina siku ndefu kidogo”.

Aliaga Mr. Michael na kutoka ofisini kwa mkuu wa kitengo cha ulinzi wa pale ubalozini Mr. Cowell.

***** ***** *****

Saa tatu na dakika tatu iliwakuta Agent Kai na Othman wakiwa sebuleni kwa Mr. Othman kijana barobaro wa kimalaysia ambaye usiku uliopita Agent Kai alimchukua kwa nguvu na kuelekea naye Istana Negara, Klang River.

“Unaishi na nani hapa?”. Agent Kai akamuuliza Othman, sasa walikuwa ni kama marafiki na ilikuwa ni kama bahati kwa Agent Kai huyu kijana barobaro kuvutiwa na anachofanya na kujiona kuwa na rafiki mtu wa Marekani na ni mtu wa CIA kwake ni bahati sana, alikuwa na hamu ya siku moja kutembelea Marekani lakni alikosa rafiki wa kumfanyia mialiko hivyo aliona fursa imejisogeza aliona ni wakati wake wa kuitumia kwa kumsaidia kila atakachohitaji Kai na yeye baadaye kuja kuomba ombi hili.

“Ninaishi mwenyewe, niliwai kuishi na ndugu zangu katika wakati tofauti tofauti lakini mama yangu alipostaafu akahama hapa Kuala Lumpur na kwenda kwenye asili yetu alipotokea yeye na baba huko Kedah aliondoka na wadogo zangu mpaka ambao walikuwa wanakaa hapa”.

“Umejitahidi sana una nyumba nzuri sana kwa kijana kama wewe kumiliki nyumba jiji kama hili la Kuala Lumpur si mchezo”.

“Kwa kweli kaka nilipigana sana ingawa marehemu ndiyo alinunua mjengo uliokuwa chakavu na kutuachia na mimi nikamuomba mama nivunje nijenge hivi unavyoiona kwakuwa mama hakuwa mkazi wa hapa alikubali…. Marekani unakaa jimbo gani?”.

“Nipo Washngton DC… Ulisemaulivyopiga simu ya LG hakuwa anapokea?”. Agent Kai alibadili maongezi baada ya kutizama saa ya ukutani iliyo katika sebule hii ya Othman iliyopambwa kisasa.

“Acha nijaribu tena… Bado asubuhi hii pengine bado kalala”. Akajibu Othman.

Akanyanyua simu yake iliyokuwa juu ya meza kubwa ya duara ya vioo na kisha akabonyeza namba ya simu ya Language girl ambapo sisi tunamjua kama Damia. Simu ikaanza kuita upande wa pili miito mitano bahati ikapokelewa.

“Hi!”. Sauti ya kike ikatamalaki kwenye masikio yao wote wawili Agent Kai aliyekuwa kakaa kwenye sofa kubwa la ngozi ya rangi nyeupe lililo upande wa pili wa meza na mpiga simu mwenyewe na hii ilitokana simu anayotumia ukiweka sauti mpaka mwisho inasikika vizuri kwa mtu aliye karibu.

“Hi!”. Akajibu Othman lakini hakufanikiwa kuongeza neno kwani muongeaji wa upande wa pili aliingiza maneno.

“Niambie mtu wangu una nini mpaka unanisumbua unanikatishia usingizi wangu?”. Kwa anavyolaza kiingereza chake haraka Agent Kai mwenye utaalamu wa kunasa sauti kwenye halmashauri ya kichwa chake aliigundua hii ndiyo ile sauti ya mtekaji wake hata kama inasikika kutoka simuni lakini haikuwa na kificho chake aliinakshi vilevile ilivyo.

“Una raha kweli mwanamke sukari mpaka sasa unajipindua pindua kitandani kwa raha zote”.

“Sasa nina shida gani, kama pesa najua kuzitafuta kushinda hata baadhi ya wanaume… Nilikumisi sana mchizi wangu sema nimebanwa sana mtu wangu wa nguvu wiki hii imekuwa ina mishemishe nyingi mpaka nachelewa kulala, weekend nitakutafuta tukale raha kiwanja”.

“Nakuaminia my sweet… Sasa sweet naomba kuonana na wewe asubuhi hii nina shida kubwa sana”.

“Ya kipesa au ya nini?”.

“Ni shida ya kifursa kuna fursa naitaka lakini inahitaji ushauri wa mtu kama wako”.

“Mmmh! Wee dalali una fursa gani tena?”.

“Usiwe na haraka … Fursa hii haihitaji kuongelewa kwenye simu lakini pia ina changamoto ya muda wenye haraka sana”.

“Nina ratiba ngumu sana Honey O, wewe ndiye umeniamsha na wewe ndiye utanifanya niende maliwatoni kujiswafi… Nataka nikupe siri moja Honey! Usiku uliopita ulikuwa mrefu sana lakini si kama vile unavyoweza kuhisi labda nilikuwa kwenye starehe, kuna dili la pesa litakalofanya tutanue jijini kwa raha zaidi. Hiyo fursa nahisi imenusa pesa nitakazoingiza… Fanya hivi Othman, saa tano nina kikao na watu wangu wa mipango ila wakati ninaoenda huko kikaoni kama kweli fursa ina umuhimu wa kupita mikononi mwangu tuonane Taman Bukit Kalil, barabara ya Jalan Bayan huko Melaka”.

“Sawa sawa Sweet! Nimefurahi sana kunikubalia sasa ni kama naiona fursa machoni mwangu ikifanikiwa na hata supu yangu niliyotaka nisiinywe kwa kuchanganyikiwa nitainywa sasa, hii inaitwa pesa haijawai kushindwa”. Furaha ya bandia iliundwa kwa Othman, kijana ambaye alikuwa ni mjanja sana na anayejua kutumia fursa za kupata pesa, mapenzi na starehe zingine anazozipenda.

“Ila uwe unanitafutaga na siku ambazo hauna fursa, wewe ni mwanaume wa ajabu sana hujawai nitaka kimapenzi mpaka mimi nishikwe hamu ya kufanya hivyo na wewe… Kunywa supu yako haraka tukutane pale paki gari yako kwenye duka la mavazi ya Gucci&Cabbana tutaongea palepale… Sitashuka kwenye gari wewe ndiyo utakuja kuongea ndani ya gari yangu”.

“Okay! Baby byee!”.

Waliagana na Othman akakata simu na wakaangaliana na Agent Kai.

Mwisho wa sehemu ya thelathini na moja (31)

Tumeshuhudia Agent Kai akimtumia Othman kupiga hatua kuwasogelea maadui zake ama wateja wake wa mbolea.

Ushirikiano mzuri uliotoka kwa Othman umemfanya asisumbuliwe na Agent Kai kiasi cha kuufanya moyo wa kazi wa mtaalamu Kai ukifurahia kurahisishiwa ayatakayo.

Tumeshuhudia msaliti Mr. Michael anafika asubuhi kazini na moja kwa moja kwenda ofisini kwa kiongozi wa kitengo cha ulinzi Mr. Cowell huko anakutana na habari ambayo alikuwa akiitarajia na kuijua lakini anakutana na mshangao kwanini mwanamke aliyeletwa kuhifadhiwa ubalozini ameondoshwa na hapo ndipo anapokumbuka kuwa Agent Kai sifa yake kuu ni kuhisi hatari inayokuja baada ya muda fulani mbele.

Nini kitafuatia?

Mara zote nakwambia songa nami mbele upate utamu..!

Ilipoishia sehemu ya thelathini na moja…..!

“Nakuaminia my sweet… Sasa sweet naomba kuonana na wewe asubuhi hii nina shida kubwa sana”.

“Ya kipesa au ya nini?”.

“Ni shida ya kifursa kuna fursa naitaka lakini inahitaji ushauri wa mtu kama wako”.

“Mmmh! Wee dalali una fursa gani tena?”.

“Usiwe na haraka … Fursa hii haihitaji kuongelewa kwenye simu lakini pia ina changamoto ya muda wenye haraka sana”.

“Nina ratiba ngumu sana Honey O, wewe ndiye umeniamsha na wewe ndiye utanifanya niende maliwatoni kujiswafi… Nataka nikupe siri moja Honey! Usiku uliopita ulikuwa mrefu sana lakini si kama vile unavyoweza kuhisi labda nilikuwa kwenye starehe, kuna dili la pesa litakalofanya tutanue jijini kwa raha zaidi. Hiyo fursa nahisi imenusa pesa nitakazoingiza… Fanya hivi Othman, saa tano nina kikao na watu wangu wa mipango ila wakati ninaoenda huko kikaoni kama kweli fursa ina umuhimu wa kupita mikononi mwangu tuonane Taman Bukit Kalil, barabara ya Jalan Bayan huko Melaka”.

“Sawa sawa Sweet! Nimefurahi sana kunikubalia sasa ni kama naiona fursa machoni mwangu ikifanikiwa na hata supu yangu niliyotaka nisiinywe kwa kuchanganyikiwa nitainywa sasa, hii inaitwa pesa haijawai kushindwa”. Furaha ya bandia iliundwa kwa Othman, kijana ambaye alikuwa ni mjanja sana na anayejua kutumia fursa za kupata pesa, mapenzi na starehe zingine anazozipenda.

“Ila uwe unanitafutaga na siku ambazo hauna fursa, wewe ni mwanaume wa ajabu sana hujawai nitaka kimapenzi mpaka mimi nishikwe hamu ya kufanya hivyo na wewe… Kunywa supu yako haraka tukutane pale paki gari yako kwenye duka la mavazi ya Gucci&Cabbana tutaongea palepale… Sitashuka kwenye gari wewe ndiyo utakuja kuongea ndani ya gari yangu”.

“Okay! Baby byee!”.

Waliagana na Othman akakata simu na wakaangaliana na Agent Kai.

ENDELEA NA UTAMU WA DODO..!

WASIWASI NA MASHAKA V

“Natumaini umesikia maongezi yetu kaka?”. Akaongea Othman huku akiizungusha zungusha simu yake mkononi.

“Vizuri kabisa nimesikia… Nafikiri tungeanza safari ya kwenda huko muda huu maana ni mbali kutokea hapa au naongopa?”.

“Hapana hauongopi ni kweli ni mbali”.

“Sasa nataka nisikuunguze kwa vyovyote vile, nataka uonekane msafi kwake kwa kila aina… Tutaondoka hapa wewe ukiwa kwenye gari yako na mimi kwenye gari yangu, tukifika huko mlipokubaliana utaonana naye kama alivyotaka lakini kwakuwa nipo ndani ya sura hii ya bandia hataweza kunijua hivyo wakati mkiendelea na maongezi mi nitakuja na kumteka nikikuacha wewe na hapo utaendelea na mambo yako kazi yako itakuwa imeisha lakini hatutaacha kuwasiliana na kumbuka kutakuwa kuna watu wanaopishana zamu kukufuatilia kila unachofanya kuhakikisha hukutani na watu ambao tunahisi wako pamoja na LG… Na si kama sikuamini ni kazi yangu inasema hivyo kwa usalama wangu kwa ujumla”.

“Kaka amini nikuambiayo… Mimi niko upande wako kwa kila sapoti utakayohitaji”.

“Vizuri, lakini hukuniambia kama una uhusiano wa kimapenzi na LG… Na katika maongezi yenu nimesikia kumbe uwa anakutamani kimapenzi na mnafanya mapenzi”.

“Huko sahihi kaka, naomba unisamehe kaka… LG amenizidi umri na hilo analijua hata yeye kuwa nipo kwake kumlizisha tu pale anapojisikia hamu ya mapenzi hivyo hata nikimuona na mwanaume sijiumizi kichwa pia hata yeye akiniona na mwanamke uwa haniulizi sana na haimuumizi pia, naomba usijali kabisa kuwa nitakaa upande wake sababu ya mapenzi. Yupo nimpendaye kwa dhati”.

“Sawa! Tutaenda pamoja na ipo siku utafurahi kwa ushirikiano unaoutoa kwangu”.

***** ***** *****

Kama walivyokubaliana wakati wanatoka mtaa wa Taman Desa, Agent Kai aliacha barobaro Othman apaki gari yake duka kubwa la mavazi ya Gucci wakati yeye akipaki jengo la tatu kabla hujafika duka la Gucci.

Dakika kumi na moja mbele kwa mwendo wataratibu iliingia kwenye maegesho yale gari aina ya Verosa rangi ya silva yenye vioo vya tinted, taratibu ikaenda ikapaki upande wa kulia aliopaki gari yake Othman haina ya Honda Civic new model rangi ya bluu nyeupe. Gari ya Verosa ilipopaki tu, mlango wa gari ya Othman ukafunguka na akashuka kisha akafungua mlango wa Verosa na kuzama garini.

Agent Kai alisubiri dakika tatu kisha akatoa bastola yake aina ya Glock 42 akatizama magazine katika kipakio cha bullets (risasi) alipoona iko sawa akaibusu na kushuka kwenye gari yake Range Rover Sport, hakutaka kuchelewa sababu alihisi kumuacha Othman aongee kwa muda mrefu na LG atasababisha mambo kwenda tofauti, moyo wake ulitokea kuukubali uwezo binafsi wa ujanja aliokuwa nao LG.

Hivyo kwa mwendo wa haraka kama anawai kitu alijiunga katika misafara ya watu wanaokwenda wakipishana eneo hili la wapita kwa miguu linaloelekea kwenye maegesho ya duka la mavazi la Gucci.

Macho yaliyo ndani ya miwani aliyovaa yalikuwa yakizunguka huku na huko kutizama usalama wa eneo hili hatua zikisogea kwa kasi ileile kuelekea upande wa dirisha la dereva ambao ndiyo upande aliokaa LG tunayemtambua kama Damia The Language Girl.

Paaah waaaahaa! Ulisikika mlio mdogo wa uvunjikaji wa kioo cha gari, lilikuwa ni tendo la kasi lililotumiwa kwa nguvu kwa kiwiko (kipepsi) cha mkono wa kushoto wa Agent Kai, kiwiko kilikitwa kwa nguvu kwenye kioo cha dirisha cha upande aliokaa LG kilivunjika na kumwagika huku baadhi ya vipande vikimrukia usoni LG ambaye pamoja na ujasiri wake alionao mstuko uliojidhihiri usoni mwake uliokuwa ni mstuko wa kiwango cha zege la ikulu ya mjerumani.

Haraka bastola ilikuwa imewekwa usawa wa pua yake tundu likiwa limekandamizwa barabara kwenye pua na kuifanya ijiminye na kumpa ukakasi wa maumivu fulani ya karaha.

“Tulia hivyo hivyo la sivyo natawanya muonekano wote wa hii pua nzuri ukafa kifo cha kuondoka duniani maiti yako ikiwa haina pua… Na wewe barobaro kama kweli unampenda mpenzi wako nitapenda kukuona ukiwa kwenye utulivu huohuo kiasi ya kwamba ujanja wako wowote utagharimu uhai wa utamu wako wa kuta zenye pembe nne”. Haraka aliongea Agent Kai huku akijitahidi bastola yake isionekane kwa wapiti njia na uzuri kila mtu alikuwa bize na mambo yake.

“Samahani kaka yangu unataka nini kwetu? tukupe utuachie uhai wetu”. Akaongea Othman huku akijifanya anatetemeka kwa kuogopa anachokiona kiasi ya kwamba moyo wa Kai uliachia tabasamu.

“Ndiyo.. Ndiyo kaka…. Sema tu unataka nini? Hata kama hii gari chu chu chukua tu… Tunachoomba utuachie tu”. Akaunga mkono LG huku akitetemeka baada ya bumbuwazi la mshangao kuisha, hakutegemea kabisa kukumbwa na kitu kama kile.

“Weka mikono juu!”. Agent Kai akamuhamulisha LG, na wakati anaangalia afanye nini Othman aliinua mikono yake juu akijifanya naye kama kaambiwa hivyo LG akafuatia kuinua mikono juu akipita kichwa.

“Wewe mwanaume… Sikia sihitaji chochote toka kwenu zaidi ya huyu mwanamke wako, wewe baki humo humo kwenye gari… Wewe shuka kwenye gari taratibu ukiwa na pochi yako tunaondoka wote”.

“Kaka nimekukosea nini? mpaka unaniteka, naona uniue tu mi siwezi kwenda popote nimuache mpenzi wangu”. LG akauliza huku akijaribu kuangalia huku na huko kama ataweza pata msaada hata wa mapolisi maana haraka alishamjua anayetaka kumchukua ni Agent Kai.

“Sikia mwanamke… Uliingia kwenye michezo hii kwa tamaa ya pesa lakini imani yako ilikwambia hakuna siku utakutana na mkono usiokunjuka, tafadhali usije ukanikera na kwangu uwa hakuna maswali.. Upesi nyanyua pochi yako ushuke ndani ya gari tuondoke”. Agent Kai akaongea huku anarudi nyuma bastola ikiwa bado iko sambamba na uso wa LG.

“Othman utatoa taarifa polisi uwaambie nimetekwa”. LG akaongea huku anashuka toka ndani ya gari baada ya kuona mwanaume hana masikhara na anachokiongea.

“Mumeo jina lake Othman?.... Okay Othman utatoa taarifa kama anavyokwambia mkeo, waambie katekwa na paka wa gizani asiye na masikhara”. Kauli hii iliyotoka mdomoni mwa Agent Kai laiti kama Language girl angegeuza sura kumtizama Othman angemfumania akitabasamu.

“Shusha mikono yako geuka kulia na uongoze kwenda mbele na usije ukahisi nitaogopa watu wanaopita hapa kukufanya uwe marehemu endapo tu utafanya janjajanja yoyote, usigeuke nyuma tafadhali uende mpaka nitakapokuambia panatosha utasimama papo hapo”.

LG aliongoza mbele akiwa ndani ya mavazi yake anayoyapenda suruali ya jeans ya rangi nyeusi na shati la jeans pia likiwa juu ya kifulana cheupe ilihali chini akiwa na viatu vya kutumbukiza rangi nyeupe, nywele zake ndefu aliziacha zikimwagika pande zote kujia mgongoni hakika alipendeza na hata sura yake ilikuwa ya kuvutia pia.

Kuambiwa asigeuke nyuma kulimfanya Agent Kai amfuate kwa nyuma hatua tatu huku mkono wa kulia akijifanya anajikuna mgongoni kumbe anaigusa gusa bastola yake aliyoirudisha nyuma ya kiuno ikifunikwa na fulana aina ya lacrose aliyoivaa na laiti ungekuwa nawe ni miongoni mwa wapita njia wa mtaa huu wa kibiashara usingehisi kama dada wa mbele yuko chini ya uangalizi wenye mwelekeo wa kuwa mateka.

“Simama hapo pembeni ya mlango wa gari hiyo nyeusi Range Rover Sport”. Akaongea Agent Kai na LG akasimama na ikiwa yupo mlango wa nyuma wa kiti cha dereva. Kai akasogea hadi pale kisha akafungua mlango wakaangaliana usoni na mwanamke yule akamkonyeza na kumtingishia kichwa aingie ndani ya gari.

Ile anageuza shingo hili ainue mguu apande garini alistuka akigongwa karete ya shingo iliyopigwa kasi na kifundi kiasi ya kwamba giza lilimtanda machoni akataka kudaka mlango akashindwa Kai akamdaka na kumsukumia ndani ya gari kisha naye akazama haraka na kuufunga mlango.

Lilikuwa tendo la haraka sana kiasi ya kwamba pamoja na watu kuwa wanapita hakuna aliyeona kiutimilifu tukio lile ingawa wapo walistuka fulani kuwa kuna kitu kimetokea lakini kitu gani hakuna aliyekuwa na uhakika.

Agent Kai mtaalamu alitoa kamba kwenye begi lake na kumfunga LG miguuni na mikononi kisha akamziba mdomo na plasta, alipoona kamili alivyotaka akashuka kwenye gari akafunga mlango na kuingia upande wa siti yake ya dereva akawasha gari na kuondoka eneo lile.

“US First!”. Upande wa pili uliongea haraka baada ya kupokea simu ni Kapteni Jones Lebrons alikuwa kapigiwa na Agent Kai.

“US First! Za asubuhi Kapteni?”.

“Nzuri tu, za kwako?”.

“Bado Mungu yuko upande wetu mapambano yanaendelea, hapa nina mtu muhimu nimetoka kumteka katikati ya jiji.. Mwanzo nilipanga niende naye kule Istana Negara lakini wageni wetu sihitaji wasikie au waone chochote kinachohusiana na kazi hususani baba na mama wa Shufania”.

“Oooh! Kwa hiyo huna pa kwenda kufanya kazi yako kwa uzuri?”.

“Ndiyo mzee… Na si kama hatatoka mikononi mwetu tena sababu ni yule aliyekuja nipokea Airport akijifanya Detective Marie”.

“Sawa sawa… Huyo ni muhimu sana katika mfereji wetu wa kuelekea lilipo bwawa… Sasa hapa tuna mtihani kidogo wa nyumba nafikiri ungeenda naye nje ya jiji ndiyo ingekuwa vizuri zaidi”.

“Una nyumba huko nje ya jiji?”.

“Sina nyumba ila kuna Mmarekani anayemiliki kampuni inayojihusisha na kilimo cha korosho na uuzaji wake ana mashamba nchini Vietnam lakni soko lake lipo hapa Kuala Lumpur… Naweza kumuomba nyumba yake kati ya nyumba zake zilizopo hapa jijini sababu zipo tatu zilizo nje ya wilaya hii ya Persekutuan”.

“Sawa sawa mkuu kama inawezekana fanya hivyo”.

“Cha kufanya kwa sasa endesha gari kuelekea wilaya ya Kuala Langat wakati ukiwa unaelekea njiani nitakupa mrejesho nyumba ipi katoa na ramani nitakutumia ya kufika huko”.

Agent Kai alipunguza mwendo wa gari akatoa simu yake na kufungua upande wa ramani hili ajue afuate barabara ipi kuelekea Kuala Langat, dakika chache tu kwa kufuata google map ya jiji alipata jibu aelekee wapi.

Kabla hajafika Klang River Banting Bridge simu yake iliita na alipoiangalia alikuwa ni Balozi Kapteni Jones.

“Kapteni”. Akaongea baada ya kusugua pa kupokelea.

“Ukivuka daraja la Klang River Banting Bridge kuna mji mdogo unaitwa Bazar Banting hapo utakwenda na barabara mpaka kwenye kituo cha wauza samaki maarufu kama bazar fish sales ukifika hapo unaingia kushoto ukiiacha barabara inayoelekea Uptown Banting kuna mtaa ambao ukifika tu utaujua ni wenyewe sababu umetulia sana kuliko mitaa yote ya mwanzo mwanzo mwa mji huo mdogo…Nyumba zimepangika vizuri tu kwa maelekezo ya mwenye nyumba ni nyumba ya tano upande wa kulia kwa unavyoingia mtaa huo kwa njia hiyo niliyokuelekeza nyumba imezungushwa ukuta mrefu kikawaida tu ikiwa juu kuna nyaya senyenge za security electricity pia ina geti pana la rangi ya bluu, utakuta mlinzi mmoja ambaye mara zote uwa ndiyo anailinda nyumba hiyo”. Maelezo marefu yaliyosikilizwa kwa umakini na Agent Kai yalitoka upande wa Balozi.

“Uwa anaitumia yeye mwenyewe huyo bosi au uwa inatumika kama nini?”.

“Kwa majibu wake anasema nyumba hiyo kwa nyuma kuna magodown uwa anahifadhi korosho lakini msimu huu hakuweza kuyatumia magodown yale kwakuwa alipata mengine karibu na Airport hivyo nyumba ipo free tu ikiwa inalindwa kwa zamu na walinzi”.

“Sawa Kapteni! Ombi langu nahihitaji hii nyumba isiwe na mlinzi tena… Mwambie awape amri walinzi wake wakishanikabidhi funguo wasirudi tena patanifaa kwa kuhifadhi watu kama hawa”.

“Umeingia kwenye mawazo ya Mr. Edwin naye alipendekeza hili uwe huru kwa kazi zako na kwakuwa yeye yupo Vietnam mlinzi aondoke”.

“Fanya mawasiliano naye itakuwa vizuri ikiwa hivyo”.

Simu ikakatwa na akatia gia gari ikaongezeka mwendo .

Alijitahidi kufuata maelekezo aliyoelekezwa na kwakuwa alikuwa makini na ubongo ulio mwepesi katika kunasa mambo aliupata mtaa aliolekezwa na wakati anahesabu nyumba kama maelekezo yanavyoelekeza, simu yake iliita akatizama kioo na kuona ni balozi tena.

“Kapteni!”. Akaongea baada ya kupokea.

“Kila kitu kimeenda sawa, utajitambulisha kwa jina la Moses Mcnitosh kwa mlinzi atakukabidhi funguo zote za nyumba hiyo”.

“Kazi nzuri Kapteni… Acha niingie kazini sasa… Chifu niliongea naye na amenipa habari alizotaka kunipa, naamini leo nitakuwa na hekaheka nzito sana”.

“Nakuamini kijana wangu”.

“Okay! Nyumba nimeiona… US First!”.

“US First!”

Agent Kai akakata simu na kuisogeza gari karibu na geti la nyumba aliyoelekezwa kisha akafunga breki na papo hapo mtu akachungulia kupitia uwazi ulio na pembe nne kwa kutokea ndani ya geti la uwa wa nyumba kisha akapotea halafu ukafuatia mchakato wa kuonyesha geti linatolewa makomeo hili lifunguliwe.

Mwanaume wa makamo ya umri unaoendea uzee alisukuma geti na kuruhusu Agent Kai apitishe Range Rover Sport na mtaalamu akaliongoza gari kuingia kwenye uwa mpana ulio kama uwanja wa basketball kiukubwa, akasimama katikati ya uwa ule.

“Karibu mkuu jisikie huko nyumbani”. Mwanaume yule akaongea baada ya Agent Kai kushuka toka kwenye gari.

“Ahsante sana mzee wangu.. Habari za hapa?”. Agent akampa salamu huku anampa mkono kwa salamu.

“Nzuri boss! Nimepewa taarifa zako toka kwa boss Edwin kuwa Mr. Moses Mcnitosh utakuwa kwenye nyumba hii mpaka utakapoondoka Malaysia kurudi Marekani”.

“Huko sahihi mzee!”.

“Mimi uwa naingia kulinda hapa mchana na ifikapo saa moja usiku uwa anakuja mwenzangu lakini kwa mujibu wa boss Edwin amenipa taarifa sote tupumzike utakuwepo wewe hapa… Huko nyuma ya hii nyumba kuna magodown mawili ya kuhifadhia korosho na eneo la hapa ni kubwa sana na uzuri kote kumezungushwa ukuta”. Alitoa maelezo marefu mlinzi na kisha akamkabidhi funguo Agent Kai.

“Ahsante kwa maelekezo yako mkuu… Nakutakia mapumziko mema”. Akasema Agent Kai kisha akatoa wallet toka mfuko wake wa nyuma wa suruali aliyovaa akachomoa noti za kimalaysia ‘malaysia ringiit’ MR zipatazo tatu na kumpatia mlinzi yule.

“Ahsante, ahsante sana boss… Ukae salama”.

Maongezi yao yalishia hapo mlinzi akaondoka na kumuacha Kai peke yake ambapo sasa akaanza kuichunguza nyumba ile kwa nje akiwa kasimama ilikuwa nyumba kubwa nzuri na ya kisasa, alisogea akafungua mlango wa mbele ulio pembeni na mbao katikati kioo kigumu chenye tinted nyeusi akaingia na kutokea kwenye korido iliyomtembeza mpaka kwenye sebule kubwa iliyowekwa vitu vya kisasa. Aliachana na pale sebuleni akapanda ngazi iliyoonyesha inampeleka vilipo vyumba vingine na mambo mengine huko akakuta vyumba vya kulala vine vikiwa katika mtindo wa self container akachagua chumba cha mwisho kabisa kuwa ndicho chumba atakachomleta LG kwa ajili ya mahojiano hivyo alitoa godoro kitandani na kuliweka sakafuni kisha akafungua kitanda ambacho kilikuwa cha chuma cha futi tano kwa sita akakibeba na kutoka nacho moja kwa moja akakipeleka alipoona ni stoo.

Akashuka chini na moja kwa moja akatoka nje alipoacha gari akafungua upande siti iliyo upande wa nyuma akamkuta LG amezinduka ikionyesha alikuwa akijitahidi kufungua kamba alizofungwa.

“Ooooh! Ooooh! Waoooh madam umepatwa na fahamu.. Vizuri sana”. Akamwambia huku anatabasamu, uso wa Damia ukiwa kwenye hasira kali iliyochanganyika na uoga ulisinyaa ghafla baada ya mlango tu ulipofunguliwa.

“Wewe ni nani? Na kwanini umeniteka?”. Akauliza kwa sauti ya ukali akijifanya hajui aliyemteka ni nani.

“Pumbavu zako Malaya wa bei rahisi , leo ndiyo utajua ubaya wa kufanya ubaya na sitaki kelele zako kabla sijakuruhusu kuongea akamwambia kisha akamkata kamba alizomfunga mguuni kutumia kisu huku Agent Kai umakini ukiwa mkali isije ikatokea janja yoyote pale kwakuwa mara nyingi hata yeye hutumia fursa kama hiyo kujikwamua matatizoni.

“Haya shuka chini malkia wa lugha hili ukanijue huko ndani kuwa mimi ni nani?”. Akampa amri huku bastola iliyo kwenye mkono wake wa kushoto, mkono wa dhahabu tundu lake likiwa limemuelekea.

LG akamtizama machoni lakini kwa jicho alilokutana nalo ubongo wake wa hisia ukamwambia aliye mbele yake ni fundi na kwa utaalamu alionao alihisi sura hii ni ya bandia na moja kwa moja akili ikamtuma atakuwa ni Agent Kai ingawa alijiambia kama ni kweli kaisha na anajutia kutekwa kibwege, alijiuliza mengi sana kuhusu Othman kama ataweza kutoa taarifa polisi hili aliyemteka atafutwe, muda mwingine akahisi pengine Othman amemuuza kwa mtekaji wake maana alichokuwa anaongea naye pindi walipoingia kwenye gari ilikuwa amenza na mambo ya kukumbukana na mapenzi zaidi kabla hajamwambia alichomuitia wanavamiwa na yeye anatekwa Othman anaachwa, lakini napo alipingana na hilo akasimama kwenye mtekaji wake kuwa alimfuatilia toka anatoka nyumbani kwake.

Mwisho wa sehemu ya thelathini na mbili (32)

Tumeshuhudia Agent Kai akimtumia Othman kupiga hatua kuwasogelea maadui zake ama wateja wake wa mbolea.

Ushirikiano mzuri uliotoka kwa Othman umemfanya asisumbuliwe na Agent Kai kiasi cha kuufanya moyo wa kazi wa mtaalamu Kai ukifurahia kurahisishiwa ayatakayo.

Tumeshuhudia msaliti Mr. Michael anafika asubuhi kazini na moja kwa moja kwenda ofisini kwa kiongozi wa kitengo cha ulinzi Mr. Cowell huko anakutana na habari ambayo alikuwa akiitarajia na kuijua lakini anakutana na mshangao kwanini mwanamke aliyeletwa kuhifadhiwa ubalozini ameondoshwa na hapo ndipo anapokumbuka kuwa Agent Kai sifa yake kuu ni kuhisi hatari inayokuja baada ya muda Fulani mbele.

Nini kitaendelea katika sehemu inayofuata?

Endelea kufuatilia mkasa huu mtamu wa kijasusi na kipelelezi unaoendeshwa na mtu wa mipango, mtu wa mikakati.

ILIPOISHIA….!

Akashuka chini na moja kwa moja akatoka nje alipoacha gari akafungua upande siti iliyo upande wa nyuma akamkuta LG amezinduka ikionyesha alikuwa akijitahidi kufungua kamba alizofungwa.

“Ooooh! Ooooh! Waoooh madam umepatwa na fahamu.. Vizuri sana”. Akamwambia huku anatabasamu, uso wa Damia ukiwa kwenye hasira kali iliyochanganyika na uoga ulisinyaa ghafla baada ya mlango tu ulipofunguliwa.

“Wewe ni nani? Na kwanini umeniteka?”. Akauliza kwa sauti ya ukali.

“Pumbavu zako, leo ndiyo utajua ubaya wa kufanya ubaya na sitaki kelele zako kabla sijakuruhusu kuongea akamwambia kisha akamkta kamba alizomfunga mguuni kutumia kisu huku Agent Kai umakini ukiwa mkali isije ikatokea janja yoyote pale kwakuwa mara nyingi hata yeye hutumia fursa kama hiyo kujikwamua matatizoni.

“Haya shuka chini malkia wa lugha hili ukanijue huko ndani kuwa mimi ni nani?”. Akampa amri huku bastola iliyo kwenye mkono wake wa kushoto, mkono wa dhahabu tundu lake likiwa limemuelekea. LG akamtizama machoni lakini kwa jicho alilokutana nalo ubongo wake wa hisia ukamwambia aliye mbele yake ni fundi na kwa utaalamu alionao alihisi sura hii ni ya bandia na moja kwa moja akili ikamtuma atakuwa ni Agent Kai ingawa alijiambia kama ni kweli kaisha na anajutia kutekwa kibwege, alijiuliza mengi sana kuhusu Othman kama ataweza kutoa taarifa polisi hili aliyemteka atafutwe, muda mwingine akahisi pengine Othman amemuuza kwa mtekaji wake maana alichokuwa anaongea naye pindi walipoingia kwenye gari ilikuwa amenza na mambo ya kukumbukana na mapenzi zaidi kabla hajamwambia alichomuitia wanavamiwa na yeye anatekwa Othman anaachwa, lakini napo alipingana na hilo akasimama kwenye mtekaji wake kuwa alimfuatilia toka anatoka nyumbani kwake.

ENDELEA NA MAPIGO..!

WASIWASI NA MASHAKA VI

Macho yake yakichunguza eneo lote la nyumba ile anayoongozwa afuate mlango wake waingie LG mikono yake ikiwa imefungwa thabiti kwa waya umeme wa ndani wa rangi nyekundu, alisogea huku akitamani utokee muujiza wowote anasuke katika anachohisi jambo baya kwake, binti yake mdogo wa umri wa miaka mitano naye alikuwa akisumbua ubongo wake katika mawazo yake.

Safari iliitimishwa katika chumba alichochagua Agent Kai ndiyo kitakuwa chumba chake cha mahojiano kati yake na mwanamke huyu.

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog