Simulizi : Mshangao
Sehemu Ya : Pili (2)
“Yupo na muda si mrefu ndiyo amerudi maana alitoka”
“Naweza kuongea naye au utaongea naye?”.
“Ndiyo! Itabidi uongee naye wewe si mimi… Lete simu nikubonyezee namba za ofisini kwake uongee naye” Akasema Shufania huku akinyoosha mkono kuomba asogezewe simu ya pale sebuleni, Kai akampa sababu ilikuwa pembeni ya sofa alilokaa ikiwa juu ya meza ndogo ya kioo.
“Tayari inaita… Shika! … Shika ongea naye uwa hachelewi kupokea”. Baada ya kubonyeza namba anazozijua na simu upande wa pili kuita Shufania alimpa chombo cha kuongelea (risiva) Kai.
“Halloow! Akasema ilipofika sikioni tu.
“Hallow! Habari yako ndugu mteja wetu?”.
“Nzuri boss….. Samahani sana bwana mkubwa, ninahitaji huduma nje ya hotel hii lakini ifanywe na mmoja wa wafanyakazi wako na nitalipia huduma hiyo kwako moja kwa moja kwa kiasi utakachoona ni sahihi mimi mteja wako kukitoa….”. Akaanza Kai kuongea huku akiwa makini kusubiri majibu toka upande wa pili.
“Kuna mtu uliyemchagua tayari?”. Meneja akauliza.
“Ndiyo kuna binti nimemchagua sababu ya uaminifu wangu kwake ninaoamini ni mikono salama kwake”
“Sawa kama utalipa hapa kwangu moja kwa moja hili iwe kinga kwake kama mkurugenzi atatokea ghafla”
“Usiwe na wasi mkuu, nitalipa pesa utakayoona ni sahihi mi kulipa kama nilivyokwisha tangulia kusema”
“Okay! Amekwambia jina huyo binti?”
“Yes! Anaitwa Shufania na ninamuagiza kwenye maduka ya simu na nguo”
“Okay! Ruksa unaweza muagiza tu… Utalipa dola hamsini na naomba utampa yeye aipitishe hapa ofisini kwangu kwanza ndiyo aende huko”
“Shukrani… Atapitisha bila wasi”
Simu ikakatwa, Kai akatabasamu na Shufania akafuatia na kuachia tabasamu mujarabu.
Nguo ya juu aliyovaa Kai muda huo ilikuwa ni shati haina ya jeans aliyochukua katika chumba cha marehemu Jeong Low, mbaya wake aliyempiga na kitako bunduki na yeye alipopata nafasi ya kumkuta anga zake kajilalia akiwa na mpenziwe alimjibu kwa kumtoa uhai wake kama kisasi tena kwa kumchinja akiwa usingizini kama tulivyosoma sehemu ya pili, shati hili lilikuwa lina kiharufu fulani cha jasho kilichokuwa kikimkera na kumkosesha amani ingawa aliikuta kabatini kwa kiongozi yule wa SDB tena ikiwa safi maana ilionyesha imepigwa pasi vizuri tu, hiki kiharufu kama ulikuwa si mtu wa kusikia harufu ya vitu vizuri usingeweza kuisikia maana ilikuwa kwa mbali sana.
“Twende zetu unipeleke nikatoe pesa”. Akasema Kai kisha akainuka toka sofani, alijikuta hatua zake zikienda kasi ambayo hakupanga hadi pembeni kidogo ya sofa alilokaa Shufania ambaye naye alipigwa na butwaa na kujikuta akinyosha mkono wake kuupokea mkono wa Kai uliokuwa umenyooshwa kwake kwa nia ya kumuinua kwa kumvuta, nukta kudunda tu walijikuta wamekutanisha viganja vyao na wote ikatokea misisimko fulani haswa kwa Shufania na kijikuta anamuangalia Kai usoni na mate kujipitisha kooni bila taarifa maalumu toka kwake.
Kai akamuinua kwa kumvutia karibu yake kisha akamuachia mkono haraka wakatoka ndani ya sebule ile mlango ukafungwa kwa kadi maalumu ya vitasa vya hoteli hii ambavyo ufungwa na kufunguliwa kwa kadi inayosoguliwa kwenye kauwazi kembamba kalipo katika eneo lililo na kiminyio cha kitasa.
Wakiwa wameongozana huku Shufania aibu ikiwa imempungua na moyo wake kuuhisi amani kubwa kuwa karibu ya Kai, walienda hadi kwenye lifti wakaingia ikawafikisha hadi mapokezi wakatoka hadi kwenye korido zinazoelekea upande wenye jengo la Square B ambapo pana vyumba vidogo vilivyoongozana kwa ajili ya huduma ya ATM, akatoa kiasi cha pesa alichoona sawa kwa matumizi ya wakati huo na kumkabidhi Shufania hili aelekee kumtafutia mahitaji yake aliyomuelekeza. Yeye akarudi juu kilipo chumba chake.
Alipofika chumbani kwake akachukua saa yake maalumu ambayo alifanikiwa kuipata kwa marehemu Jeong Low baada ya Damia kuiona kama ya kawaida hivyo hakuichukua ikawa imepona na kuikuta kwa adui yake.
Aliseti sehemu ambayo uitumia kama simu na kupiga namba ambazo ni kati ya namba tatu tu za simu zilizo ndani ya saa ile.
“Agent Kai” Upande wa pili uliongea kwa lugha yao waitumiayo kama kawaida yao lugha ya kiingereza.
“Habari za Marekani chifu?” Akaongea Kai, alimpgia kiongozi wake wa kikazi katika ofisi ya makamu wa Rais anayeongoza kitengo cha ujasusi kilicho chini ya ofisi wa makamu wa Rais kilicho na wafanyakazi watatu tu, yeye mwenyewe Chief of Staff to the Vice Pressdent of America, secretary na Agent Kai lakini bosi mkuu akiwa ni makamu wa Raisi.
“Huku tuko salama na muda si mrefu nimetoka kuongea na balozi wetu wa huko KL, anasema hamjawasiliana toka ufike… Nini tatizo mwanangu?” Akaongea na kuuliza papo hapo chifu.
“Nimepoteza simu mkuu… Nilipokewa na maadui baada ya Detective Marie, walifanikiwa kunighilibu kwa kuniletea Detective Marie fake nilichelewa kumstukia mpaka akanichukua na kunipeleka mpaka kwenye gari lao”
“Eeeeh! Usiniambie Detective Marie naye ameingia kwenye mkumbo wa kupotea.. niambie?” Chifu alijkuta akipayuka kwa pupa huku kijasho chemba kikimtoka makwapani mwake.
“Kama wameweza kutengeneza sura ya bandia ya Detective Marie tena ndani ya siku mbili tu toka aingie Kuala Lumpur unafikiri kuna nini hapo?”.
“Shiiit… Son of bitch! Hao ni wahuni gani wanafanya mambo haya?”.Niambie kwa kifupi ilikuwaje baada ya kupokewa na hao maadui?”
“Wateja zetu walimtanguliza huyo Detective fake akaja kunipokea airport… Ujanja nilionao ulifeli kutokana na maisha yangu yote sijawai kuonana na detective Marie hivyo siljui umbo lake halisi zaidi ya zile picha ulizonipa hivyo alinifuata na akanipata tena alikuwa akiongea kama wanavyoongea wadada wengi wa nchini kwetu aliweza kulanda sauti kwa ustadi mkubwa mpaka sikuweza mstukia, kama ujuavyo sisi cha kwanza uwajua maadui zetu kwa sauti zao hasa wakiwa si wamarekani… Ila wakati tunaelekea katikati ya jiji nikashangaa tunaenda safari ndefu maana katika maelezo niliyojiandikia kwenye sehemu ya siri iliyo ndani ya simu yangu niliandika maelezo mafupi juu ya jiji la KL katika maelezo yale niliweka nyota kwenye umbali wa kutoka maeneo ya baadhi ya maeneo muhimu ya jiji hili kwa ukitokea Airport ambapo ndiyo kitovu changu cha kazi katika kila nchi nayoenda kufanya kazi… Alinitembeza masaa mawili kasoro mpaka ikabidi nimuulize wapi amepanga kunipeleka ukizingatia nilikuwa na uchovu wa safari ndefu toka huko Washington DC hadi KL, majibu yalikuwa ya kujigonga na pia alikuwa akiniangalia uangaliaji usio na shaka ana kitu hivyo macho yangu nikayapa kazi yamchunguze kwa chati hapo ndipo nikaiona ngoz iiliyoshindwa kwenda vyema katika jicho lake nikahakiki tena na tena uhakiki ukapita ngozi ya juu ilikuwa plastiki sura ya mfano wa sura ya detective Marie. Nikajipitishia maamuzi nitulie nisimuonyeshe dalili zozote kuwa nimemstukia pia dalili za kazi zilinifika lakini nazo nikazisihi niwe na subira hili nione napelekwa wapi halafu hukohuko ndiyo nitajua nafanyaje”. Alitoa maelezo marefu Agent Kai lakini alisima chifu alipokoa kwa kutoa ishara asiendelee na yeye ana jambo anataka kuongea.
“Usipende kujiamini hivyo Agent… Ulitakiwa kumdhibiti mapema na pengine angerahisisha kazi zaidi upande wetu, anyway endelea na maelezo hili nije nimueleze makamu wa Raisi maana aliniuliza juu yako”.
“Nilipoacha na iwe nilivyowaza alinipeleka hadi eneo la Nadau golf ambako ndiyo wana jengo lao la ghorofa huko tuliposhuka kwenye maegesho alinijibu majibu mengine yasiyoridhisha nikapanga tukishuka tu nimuweke chini ya ulinzi wangu lakini haikuwa hivyo niliposhuka garini nilivamiwa na wanaume sita mmoja akanipiga na kitako cha bunduki fupi kichogoni nikazirai… Nilipokuja kuzinduka nilijkuta niko katika chumba kidogo kama chumba cha choo au stoo, nashukuru hakukuwa na mlinzi waliyeniwekea na kama ujuavyo kutoniweka chini ya uangalizi ni moja ya makosa makubwa ya kazi ambayo watu huyajutia kipindi wakiyafanya kwangu, walikuwa wamenifunga kamba lakini za katani ambapo kuzifungua kwangu uwaga si shida, bahati ingine hawakuwa wamenivua raba zangu hivyo niliweza kujiondoa ndani ya chumba kile kisha nikafanikiwa kulipa kisasi kwa watu wawili niliwapa wanachostahili kwa kosa la kuniteka bila kupumzika na roho yao mbaya lakini nikiwa katika harakati za kuwapunguza na kumpata yule dada aliyeongoza utekaji walinistukia ikabidi nitumie mbinu ya ziada kuwatoroka” Maelezo yalifika alipoona yanatosha akasima kisha wote kama wameambiana wakavuta pumzi kubwa kwa pamoja kana kwmaba wameambiana.
“Pole sana Agent… Ila pole yangu inatembea na hongera kwa kufanikiwa kujitoa mikononi mwao, kwa haraka naamini hao waliofanya tukio lako ndiyo wanaohusika na matukio ya kuteka watu wetu au kuwadhuru watu wetu”.
“Yah! Nachelea kusema inawezekana kabisa … Sababu moja inayowaingiza katika tuhuma ni uwezo wa kutengeneza sura bandia ya detective Marie na kwa utaalamu wangu wa haraka katika watu wale sidhani kama kuna walakini kuhusu wao kuhusika moja kwa moja na kupotea kwa maprofesa na watu wetu wengine wa FBI NA CIA, naamini ndugu zetu wa kijasusi waliingia kwenye mtego kama wangu… Pia kuna connection ipo huko Marekani na watu hawa…”
“Mmmh! Inaweza ikawa kuna connection kweli?”
“Yah! Chifu umefanya kazi hizi huko nyuma, wewe si mwanafunzi wa ujasusi unajua mengi lakini usitake niamini huwezi kuhisi kuwa kuna connection huko nchini kwetu… Watu hawa wanajuaje juu ya mambo ya Kai anafika muda fulani Airport?... Ukijiuliza hili tu moja kwa moja unapata jibu kuna mtu au watu wanawapenyezea taarifa…. Kazi nimeishika na nashukuru nimepata pa kuanzia tutayajua yote tena kwa haraka sana” Akasema Kai kwa hisia kali huku akijiweka vizuri kitandani alipolalia mgongo macho yake yakiangalia dirishani na kwenda mbali ya eneo lile nje ya hotel sababu dirisha lilikuwa wazi aliondoa mapazia kwa kuyasukuma upande kwa pande zote na lilikuwa dirisha kubwa la futi sita, macho yalikuwa yakiona mandhari ya majengo ya karibu na hotel hii.
“Nakuamini sana… Sasa unataka nikuongezee mtu toka Langley? Au inakuwaje?
“Hilo nitakujibu keshokutwa, nipeni siku ya kesho nicheki upepo unakwendaje… Muda si mrefu nitapata simu na laptop, uzuri wa hapa kuna huduma ya WI-FI nikishapata tu naomba Betty anitumie code secret ya simu yangu ya niliyoipoteza pamoja code secret ya laptop yangu… Kingine nitumie humu namba za balozi pia hakikisha tukimaliza kuongea naye tu umpe taarifa hii niliyokupa pia aandae vitu nilivyoomba aniandalie ifikapo usiku nivipate” Akatoa maelekezo komandoo Agent Kai Hamis Mkarambati mwenye a.k.a kibao toka mashirika ya kijasusi mbalimbali wanaojua juu yake kuwa yeye ni nani katika medani za kijasusi ikiwa mashirika mengine yashawai kupambana naye kiasi cha kumfanya yeye ni adui yao kwa alichowafanyia ilimradi kiwe na maslahi kwa nchi anayoitumikia.
“Okay! Yote nitayatimiza katika muda unaostahili… Nikutakie umakini katika kazi… Mara zote kumbuka kuwa sisi kama serikali ya United States of America tunakutegemea na familia za walioingia matatani huko Kuala Lumpur wanalia na wewe ndiye mfuta machozi wao, pia tunaongozwa na slogan ya US First!”.
“Yes! US First! Akasema na kukata simu iliyo ndani ya saa yake ya mkononi.
***** ***** *****
Saa kumi na moja na dakika na tano jioni ya siku ya jumatano gari mbili zilizoongozana zilipaki kwenye maegesho ya YOUTH MUSCLE’S & BOXING TRAINING mtaa wa Nadau Golf, gari zote mbili zilikuwa ni za aina moja ya Hammer moja nyeusi ingine ya rangi ya nyeupe zote zikiwa zinapendeza sana uziangaliapo.
Gari ya rangi nyeusi ambayo ndiyo ilikuwa gari ya nyuma kati ya gari zile kwenye siti ya mbele mlango wa abiria alishuka mtu mmoja mwanaume mwenye miraba minne kisha akaenda mfungulia mlango aliye siti ya nyuma ya hammer ile nyeusi, kabla aliyefunguliwa mlango hajashuka kwenye gari ya mbele wakashuka wanaume watatu kutokea milango ya siti waliyokuwa wamekaa kisha baada ya wao kushuka wakashuka wengine tena wawili toka kwenye hammer nyeupe ambayo ni kama ilikuwa inaongoza msafara ule uliokuwa na magari mawili tu tena yaliyofanana aina na kupishana rangi tu, kwenye magari walimuacha dereva pekee aliyekuwa akiwaendesha.
Ndipo mtu aliyefunguliwa mlango akashuka toka kwenye gari na papo hapo alimfungulia mlango akampisha na kukaa nyuma yake kisha wale watatu walioshuka mara ya wakawazunguka wote wakiwaweka katikati wawili walioshuka baada ya wao kushuka na mmoja huyu ambaye alivaa suti nyeusi na miwani meusi akionekana ni baba wa makamo mtu mzima lakini mwenye kamnuko kapesa, kundi lile lilikuwa na watu wawili waliovaa suti zilizofanana rangi na mmoja akiwa kavaa suti ya kijivu na wengine walivaa jeans tu na fulana nyeusi na ndiyo waliwazunguka watu hawa kama wakiwalinda.
Kwa mwendo wa haraka kama watu wanaowai kitu wakikataa kupoteza muda wakasogea kwenye korido waliyotembea nayo ikawafikisha kwenye ngazi zinazopanda ngazi kuelekea juu ya jengo hili ambalo asubuhi Agent Kai alifanya yake na kuwatoroka waliomteka.
Mwisho wa sehemu ya saba (07)
Alamanda Hotel imewakutanisha Agent Kai na binti mrembo wa kiarabu aitwaye Shufania Mahamud, binti anayefanya kazi katika hotel ya kimataifa yenye hadhi ya nyota tano.
Nini kitakwenda kutokea baina yao?
Mara hii tena napenda nikuombe msomaji wangu kuwa ‘subira ndiyo jambo la kheri’
Twende nami katika sehemu inayofuata.
Kwa mwendo wa haraka kama watu wanaowai kitu wakikataa kupoteza muda wakasogea kwenye korido waliyotembea nayo ikawafikisha kwenye ngazi zinazopanda ngazi kuelekea juu ya jengo hili ambalo asubuhi Agent Kai alifanya yake na kuwatoroka waliomteka.
ENDELEA NA UTAMU…!
Walipanda ngazi katika kasi ileile mpaka floor ya tatu bila ya wao kugonga hodi kutaka wafunguliwe na mwenyeji aliye ndani kuna mtu alikuwa ndani alifungua mlango.
“Karibuni… Karibu boss Mr Logan” Akatoa ukaribisho aliyefungua mlango huku akiwapisha wapiti kwa kujibana sambamba na mlango pembeni.Hakuna aliyejibu kati ya wote wale zaidi ya kila mmoja kumuangalia kila anapopita kuingia ndani na moja kwa moja wakaenda sebuleni ambako kulikuwa na watu waliokuwa wanausubiri huu ujio.
Wageni hawa walikuwa ni Mr Logan Puter tajiri bilionea mjanja mjanja mwenye kufanya shughuli za nusu halali na nusu zisizo halali katika utafutaji aliingia katika nchi yake hii masaa mawili yaliyopita akitokea nchini Korea Kaskazini alipokwenda baada ya kupewa mualiko na shirika la kijasusi la nchi nchi hiyo na idara ya usalama wa taifa wa nchi hiyo na kuchukua baadhi ya mikakati itakayomsaidia yeye na watu wake kufanikisha mchongo wa kuwasafirisha raia wa Marekani waliokuwa wanawashikilia baada ya kuwateka.
Huko Korea Kaskazini aliongozana na walinzi wake watano pamoja na watu wake wa kazi wawili ambao ni Mr Nawz Patrash na Mr Ghulam Qaresh na ndiyo aliofika nao hapa makao makuu ya ‘SDB’ sehemu inayosifika Kuala Lumpur kwa vijana wengi kufanya mazoezi ya gym na boxing sababu ya walimu wazuri jamaa wa ‘SDB’.
Waliwakuta wanaume waliopo pale wakiwa na mwanadada mmoja wote wakiwa katika sura za huzuni sana hasa Mr Malaysia bwana Jeong Low ambaye bado alikuwa na machungu makubwa sana kuuliwa kwa mdogo wake aitwaye Jack Low kwa kuvunjwa shingo kwa karate aliyopigwa na Agent Kai, muda wote alikuwa ahamini kama mdogo wake amefariki walikuwa wakipendana sana katika maisha yao hawakauwai kuachana katika safari zao za kimatembezi iwe nchini majimbo mbalimbali ya Malaysia au nje ya nchi ya Malaysia, katika kazi zake za kutunisha misuli bwana Jeong alimfanya mdogo wake Jack kuwa ndiyo meneja wake aliyeingia mikataba mbalimbali na makampuni yaliyomuhitaji kaka yake, ilikuwa ni haki yake kuumia kuhusu kifo cha mdogo na kiukweli alikuwa amempania sana Agent Kai akiweka ahadi lazima amuue katika kumuenzi mdogo wake.
Mr Logan alipoingia pale sebuleni moja kwa moja alikwenda na kukaa kwenye sofa alilokaa Jeong kisha akavua miwani yake na kumshika bega sekunde kadhaa halafu akampigapiga kwa kiganja pale pale begani.
“Pole sana Jeong..!”. Akasema kwa utulivu Mr Logan kitu ambacho toka Jeong amjue hakuwai kumuona au kumsikia akiongea kwa sauti ya unyenyekevu kama aliyoongea muda huo ilionyesha naye aliguswa na huzuni aliyoiona mule ndani sababu toka vikundi vyao wavianzishe hawakuwai kumpoteza mtu iwe kwa ugonjwa au kuuliwa, hivyo vifo viwili vya watu wao vilikuwa pigo kwao kutokana na kutozoea hali hiyo wakati wao walikuwa washatoa roho za watu wengi tu hasa huyu Jeong alikuwa na mudder case zisizojulikana serikalini kuwa zimefanywa na yeye zenye idadi ya watu wapatao kumi na zaidi.
“Asante sana mkuu… Imeniuma sana kwa mdogo wangu na hata rafiki na kiongozi wetu Nabeel, amegusa sehemu zisizogusika kwa kweli… Sijui nitamfanyaje nikimkamata, msiniambie na yeye mnamtaka akiwa mzima kama ulivyotoa oda kwa Damia…. Nakuheshimu Mr Logan… Tafadhali mniachie huyu mtu na mimi nimfanye kama alivyomfanya mdogo wangu” Akasema kwa uchungu huku machozi yakiporomoka mashavuni mpaka Mr Logan akatoa kitambaa jasho mfukoni mwake na kumpa hili ajifute machozi.
“Mimi pia upewa oda na wateja wangu si kama napenda kuwashikilia watu hawa na kuwalisha chakula changu pamoja na kuwanywesha maji yangu…. Yule mtu wa jana ni mtu anayetakiwa na SPNK wakiongozwa na serikali yao, sasa kazi inakuwa si rahisi lakini ni faida kati yetu sote” Logan akamjibu kwa kumnong’oneza sikioni kwa sababu anazozijua yeye.
“Hili nimuache hai yule mtu nitaomba nimtese vya kutosha, pia utahitajika unilipe pesa zitakazofuta hasira nilizonazo … Boya kama yule anataka nishindwe kujieleza kwa wazazi wangu wapi alipo Jack, amesababisha mpaka saivi nisijue natoaje taarifa juu ya kifo chake.
“Usijali Jeong nitaruhusu ufanye utakavyo ila usimuue nitakupatia pesa ya kutosha… Kuhusu kuwaambia wazazi wako juu ya kifo cha nduguyo naomba usiogope uende ukawaambie, nitamwambia daktari wetu kupitia clinic yake aandike alikunywa dawa nyingi za kuongeza nguvu mpaka akafa tutafanya hivyo sababu yeye hakufa kwa kuchinjwa kama nilivyopewa maelezo toka kwa Damia itakuwa ni sahihi, sisi tukitoka tu hapa utaenda kwa wazazi wako kuwapa taarifa juu ya hili, shughuli zote za msiba nitazigharamia kwa kukupa pesa ya shughuli nzima… Kuhusu Nabeel kwa stahili ya kifo alichouliwa endapo tutawapa taarifa ndugu zake tutakutwa na kesi ya kujibu serikalini, uzuri yeye anatokea jimbo la Padang Besar hapa KL hana ndugu hivyo naomba yeye mtaenda kumzika kule shamba letu la siri za maiti… Natambua inauma sana yeye kuzikwa kule kusikokuwa na heshima tunakowazika watu ambao tunawaua katika harakati zetu, inauma sababu atazikwa bila heshima tena usiku ila mtamuaga hapa hapa… Nawaombeni muongeze umakini sana sababu adui tunayepambana naye ni mtu wa hatari sana ten asana natambua anaweza kurudi hapa muda wowote imarisheni ulinzi na msilale au kukaa kizembe” Akatoa maelezo marefu kwa watu wote walioko pale sebuleni, wote walikuwa kimya wakimsikiliza kwa makini.
“Fanyeni siri kuhusu mauaji yaliyotokea humu ndani sitaki vyombo vya usalama vya nchi vikaanza kutushuku kwa namna moja hama nyingine… Damia tutaondoka wote hapa sababu nina maongezi marefu sana na wewe maana wewe ndiye uliongea naye kwa muda mrefu mtu yule”. Akaongea tena kisha akainuka sofani na akamnyanyua kwa mkono Jeong wakaanza safari ya kutoka pale sebuleni akiwa sambamba naye, hakuna aliyeshangaa sababu ilikuwa ni kawaida kwake anapomaliza maelezo kutokutoa ishara au neno la kuwa kamaliza alikuwa akimaliza anainuka na kuondoka hivyo wote walimzoea sana.
Aliokuja nao na wao waliinuka na kuanza kuchapa mwendo na walinzi wakijitahidi kuweka ulinzi wao uliozoeleka kwa kasi kama wanavyojipanga mara zote.
Msafara wake na Jeong ulienda hadi yalipo magari waliyokuja nayo akamvuta pembeni kidogo na kuanza kumnong’oneza sikioni.
“Sikia ‘SDB’ sasa ipo chini yako… Kuna kazi kubwa inakuja mbele yetu, kesho mkimaliza shughuli za mazishi nitakuita kwenye kikao ambacho hukuwai hudhuria kabla alikuwa akihudhuria Nabeel mara moja moja nilipomuita. Unakwenda kujua mambo mengi yanayonihusu mimi na wenzangu wa karibu naomba uwe msiri katika utakayoyasikia kwenye vikao vyetu vya siri. .. Kingine sikumuona yule mwanamke aliyelala na Nabeel mliyesema yeye alizimia, yuko wapi?”.
“Tumemuweka chumba cha huduma bado hajisikii vizuri”
“Sikia yule mwanamke nataka awemo katika msafara mtakapokwenda kumzika bwana yake mkifika huko mumuue huko huko na kumzika sababu hafai tena kuishi kwa usalama wenu na hatuwezi juwa aliambiwa mangapi na Nabeel, sitapenda mkosee kitu katika maelekezo niliyotoa… Asubuhi utakuja ofisini kwangu kufuata pesa”. Akasema tena hili likiwa na msisitizo zaidi.
***** ***** *****
MTAFUTANO PANDE MBILI
Saa moja kamili juu ya alama jua likiwa linaishia kuashiria siku inaenda kuisha kwa saa za Asia mashariki ilimkuta Agent Kai akiwa bado yupo ndani ya chumba namba 105, Square A, Alamanda Hotel. Ikiwa ameshafanya kazi nyingi katika kompyuta mpya aliyoletewa ikiwa ni miongoni mwa vitu ambavyo alimuagiza muhudumu Shufania binti Mahamud muhudumu wa hotel upande wa vyumba vya Square A, aliweza kuingiza code secret za simu yake iliyochukuliwa pia aliweza kuingiza namba ambazo ikiwa kompyuta itawashwa tu basi hii kompyuta yake itamjulisha imewashwa muda gani na eneo gani iliwashwa kama nilivyokwisha sema awali kompyuta yake ambayo wao upewa na kampuni ya Apple ilikuwa ni kompyuta yenye mfumo maalumu uliotengenezwa kwa ajili yao majasusi CIA, ikiwa uambatanishwa na simu yenye teknolojia ya hali ya juu kama tulivyoona saa yake, vyote hivi vilikuwa ni vitendea kazi vya ukweli vyenye teknolojia iliyo ya hali ya juu.
Baada ya kumaliza kazi ile alielekea bafuni kujimwagia maji na mambo mengine kufika huko akaanza kufikiria miaka ya nyuma wakati yupo mdogo nchini Tanzania mkoa wa Morogoro akiwa anasoma shule ya msingi Bungo ilikuwa historia tamu sana na ndefu.
> {Kila mtoto uwa na kipaji chake iwe kwa kumuona mtu anafanya hivi au vile basi naye upenda kufanya anachofanya huyo mtu. Kai alikuwa akipenda michezo miwili katika makuzi yake akiwa na umri wa miaka mitano alipenda kucheza mchezo wa mpira wa miguu wa makaratasi (chandimu) kama ilivyokuwa watoto wengi wa umri wake aliokuwa anasoma nao chekechea na hata watoto wengine wa mitaa yao, licha ya mpira wa chandimu aliokuwa akiutandaza na watoto wenzake pia alikuwa akipenda mchezo wa kuruka sarakasi tena kwa stahili ya juu sana kila siku akianza kwa kwenda yalipokuwa yanamwagwa mapumba.
Taratibu mchezo mmoja kati ya hiyo ulianza kuingia katika damu kati ya michezo miwili hiyo (soka na sarakasi) mpaka alipofika kuanzishwa darasa la kwanza akiwa na miaka sita baada ya kuonyesha maendeleo makubwa kwenye masomo yake ya chekechea. Alikutana na watoto watatu waliokuwa wanapenda mchezo wa sarakasi kama yeye kila walipokuwa mapumziko shuleni walishindana sarakasi za aina mbali mbali,
Kai alipoona muda mwingine kuna mmoja kati ya wale watoto watatu anawashinda akaamua kitu sababu katika umri wake wa utotoni mpaka saivi yupo mkubwa hakuna kitu anakichukia kama kushindwa jambo na hii imekuwa ikimsaidia sana. Aliamua kuwa lazima amshinde yule mtoto mwenzake kwa stahili mpya za sarakasi.
Eneo alilokuwa akiishi kuna mtaa alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa akifunza watoto sarakasi kisha anazunguka nao siku za weekend (mwisho wa wiki) mtaani akilipisha watu kiasi fulani cha pesa kwa kuchangisha mpaka kilipofika kiasi cha kuridhisha kwa wale wanaovutiwa na mambo ya kuona show za sarakasi, hivyo Kai alikwenda mtaa ule akawa anawaangalia wanapofanya mazoezi baada ya kumuomba mwalimu wao ruhusa aweze kuwa anawaangalia.
Aliweza kwenda mara kwa mara kila alipotoka shuleni mwisho yule mwalimu akampa nafasi naye ajiunge nao baada ya kupata habari kwa mtoto mwingine kuwa Kai akiwa shuleni anaruka sarakasi.
Nafasi ile adimu alikuwa akiiota kila siku alionyesha juhudi kubwa kwa kufuata maelekezo ya mwalimu wake ambaye aliwaongezea na silaha kwa kuwafundisha mchezo wa karate sababu alikuwa na mkanda mweusi katika Shotokan na mweusi katika Taekwondo.
Miezi miwili tu jina la Kai mtoto likaanza kupaa miongoni mwa watoto, vijana mpaka watu wazima, alikuwa ni mwepesi ajabu katika kushika mafunzo ni kipaji halisi kweli kweli kilijionyesha na kujiibua machoni mwa watu.
Bidii yake na kutokutaka kushindwa katika kila jambo lenye ushindani lilimfanya kila alichofanya kama ushindani kukifanya vizuri na kuongoza, mtihani wa kumaliza mwaka wa darasa la kwanza aliwaburuza kwa mbali wanafunzi wenzake akishika namba moja kwa maksi za juu kabisa.
Likizo ya kufunga muhula ule wa kumaliza mwaka akaenda bwagamoyo kwa dada yake huko napo hakuacha kipaji chake kisubiri tu alianza yeye mwenyewe kupita mtaani akiwa na ringi maalumu alilokuwa akilitumia kuonyesha show ya sarakasi akawa anakusanya pesa mpaka watu wa viunga vya bwagamoyo mjini mitaa ya Magomeni, majengo na mitaa mingine ya katikati katikati jina lake likawa midomoni kwa watoto, vijana na baadhi ya watu wazima.
Wakati akiendelea na pilika pilika zake pale kwa dada yake alipofikia walifika wachina watatu kumtembelea shemeji yake aliyemuoa dada yake.
Mume wa dada yake alikuwa anapiga muziki wa utamaduni akimiliki bendi ya muziki huo wa kiasilia wa kigogo iliyokuwa maarufu miaka hiyo kutokana na kazi iliyokuwa ikifanywa na shemeji yake huo ile bendi mpaka sasa bado ipo ingawa si kwa kasi ile iliyokuwa nayo miaka hiyo Chibite Band ilikuwa Chibite kweli, wale wachina walifika pale kujifunza mambo mbalimbali ya kuhusu mziki huo kama kupiga marimba, filimbi, nyanga na hata mazumari pamoja na kuimba baadhi ya nyimbo zilizokuwa maarufu katika bendi hiyo ambayo ilikuwa kwenda Ulaya, Asia na Amerika kitu cha kawaida sana.
Wachina siku ya kwanza tu walipomuona Kai maeneo ya sokoni karibu na uhindini kakusanya watu anaonyesha show walivutiwa na kusogea na wao kushangaa anayoyafanya Kai wakiwa hawajui kama wanapokwenda kufanyaga mazoezi asubuhi na jioni ndipo alipofikia Kai au ndipo anapokaa Kai.
Ilipofika jioni wakiwa na mwenyeji wao katika mazoezi ya kawaida ya muziki wa asili walimuona mtoto waliyemuona mitaa ya uhindini akiwaonyesha show watu na kufanya mkusanyiko usio na kibali mkusanyiko usio rasmi, alikuwa ni Kai. Wakamuuliza mwenyeji wao ambaye ni shemeji yake na Kai kuhusu mtoto huyo. Akawajibu ni mtoto wa mjomba na mke wake. Pale pale wakiwa na mwenyeji waliweza kuongea kwa lugha yao ya kichina wakimzungumzia Kai kuwa anaweza akawafaa katika mambo yao fulani fulani wanayowajua wao.
Ikabidi shemeji wa Kai awaache wazungumze yeye aliwaaga anaingia ndani kuna kitu anafuata. Wale wachina wote watatu wakapitisha uamuzi kuwa mtoto Kai anafaa katika mpango wao, wakaamia kwenye mjadala watampataje hapo mmoja akatoa wazo watumie pesa kidogo kumshawishi shemeji wa Kai awasaidie kutoka kwa mzazi wa Kai hili wamchukue waende naye China.
Wachina awa walikuwa na rafiki yao ana kikundi cha watoto huko kwao China akiwafunza michezo mbalimbali ya kimapigano huku akiwasomesha katika shule mbalimbali za pale China, alikuwa na faida anayopata kwa kuwauza katika vikundi mbalimbali vya kijasusi na hata vya kimafia baada ya kuona wameiva, alikuwa na kibali kabisa cha kuwa na watoto wao alichokuwa akikilipia katika serikali ya China hivyo Haikuwa tabu kwake kutafuta watoto wenye vipaji.
Hivyo wale wachina kumuona mtoto kama Kai waliona kama bahati maana walikuwa na uhakika wakimpeleka na kumuonyesha ndugu yao walikuwa na malipo mazuri. Maongezi yao yalifikia maamuzi wamuingie shemeji na kumpa taarifa ya nia yao. Shemeji aliporudi alikuta ni kama vile ni mtu anayesubiriwa kwa hamu.
Wachina wakaona hakuna kuremba dhahabu lazima iandaliwe miundo mbinu ya kuchimbwa.
“Bwana mkubwa samahani sana…” Mmoja akaanzisha maongezi baada wa waliyekuwa wakimsubiri kukaa kwenye kiti alichokiacha wakati anaingia ndani.
“Vipi kuna tatizo gani? Mbona umeanza kwa samahani mkuu!”. Alishikwa na mshangao sababu si kawaida kwa wale wageni wake kuongea neno samahani katika maongezi.
“Hakuna shida kabisa, kuna kitu kimetuvutia sana tukaona tukushirikishe sababu kipo chini yako, kipo juu ya uwezo wako” Akajibu yule yule huku akiwaangalia wenzake kwa zamu kisha akamuangalia Mr Chibi.
“Mko huru kusema chochote mkitakacho katika nyumba hii, jisikieni mko China… Karibuni” Akawapa ruhusa waseme wanachohitaji wasiwe na wasi wasi kabisa.
“Tumetanguliza samahani sababu unaweza ukashangaa icho ambacho tutakachokwambia … Hapa kuna mtoto tumemuona anaingia kwenye nyumba yako na kutoka kama mara mbili mara tatu hivi hatujui kama ni mtoto anayehusika na nyumba hii maana hapa watoto wengi sana na wewe hauna utaratibu wa kututambulisha kwa watoto” Aliongea kirefu kidogo na akanyamaza baada ya kumuona mzee Chibi akipepesa macho kama anayetafuta huyo mtoto kati ya watoto wanaocheza cheza hapo.
“Endelea Mr Cheong nakusikiliza”.
“Hapa mkuu kuna kipaji cha hatari sana tumekiona” Alisema akasimama na kunywa maji kisha akaendelea kuongea, wengine nao wakaiga kunywa maji.
“Tumemuona mtoto mitaa ya uhindini ameweka mkusanyiko wanamuangalia halafu kuna mtoto mwingine ambaye pia hapa tumemuona naye anakusanya pesa, yeye alikuwa akiruka sarakasi na kutumia baiskeli yenye tairi moja kwa ufasaha kabisa”
“Eeeeh!.... Ooooh, kumbe mnamsema shemeji yangu…. Yule leo amevaa fulana ya jezi ya njano?” Akamkatizia kwa kumuuliza.
“Yah! Ni huyo huyo….. Hivi ni mtoto wako?”
“Hapana si mtoto wangu, ndiyo maana nikasema shemeji yangu… shemeji yangu ina maanisha ni mdogo wake na mke wangu, kati ya wake zangu wanne nilionao, mke wangu mdogo kabisa ndiyo dada yake na huyo mtoto mnayesema”.
“Okay! Mzazi wake yuko wapi?”
“Amekuja likizo ana siku tatu tu toka amefika ila ni mtoto mchangamfu sana na mwenye akili nyingi sana kifupi ni miongoni mwa watoto genius…. Yupo vizuri sana darasani na kwenye huo mchezo mliouona anaucheza ni mchezo anaoupenda sana”
“Umesema ana akili sana ya darasani, yupo darasa la ngapi?”
“Ndiyo ana akili sana toka chekechea yeye anaongoza tu, yupo darasa la kwanza, bado mdogo sana ila anayoyafanya ni tofauti na umri wake… Ana miaka sita sasa na yupo darasa la kwanza, ingekuwa nchi zenu mtoto huyu angepelekwa shule maalumu”
“Ni kweli kwa nchi zetu zilizoendelea mtoto kama huyu mwenye kipaji na akili za ajabu angesomeshwa na serikali mzazi wake asingetoa pesa na angeandaliwa kwa kazi maalumu”. Mjadala uliendelea ukiwa baina ya shemeji wa Kai na Mchina ambaye yeye alikuwa akiongea kiingereza kwa ufasaha zaidi kuliko wenzake.
“Wazazi wengine wana bahati sana…. Eeeeh niambieni mna mawazo gani juu yake? Maana kwa maelezo yenu mlivyoanza mliniambia mmeona kipaji cha hatari”.
“Sisi tumemuona kwa anayoyafanya kwa vitendo… Sasa ulipotuambia ana akili za kipekee darasani, huyu mtoto ni hazina, huyu mtoto ana kipaji kisichoelezeka. Hatakiwi kuendelea kuwa hapa Tanzania mtoto kama huyu anatakiwa kusoma nchi yenye kujua vipaji vya watoto na mahitaji yao katika kuviendeleza, nchi yenu atapotea huyu” Akaendelea kusema mchina yule huku wenzake ambao walikuwa wakijua kiingereza kwa kwa kiasi kidogo walitikisa vichwa kuonyesha wapo pamoja.
“Angekuwa ni mtoto wangu mara moja ningetoa go ahead mkiondoka muondoke naye” Akasema Mr Chibi kisha akachukua chupa ya maji akanywa funda kubwa la maji na kuishusha chini.
“Tutakulipa pesa kadhaa tutakazokubaliana ilimradi utusaidie kwenda kumshawishi baba yake atupe huyu mtoto”. Akasema mchina yule baada ya kumuona mtu wanayeongea naye anaonyesha kusitasita.
“Kwani nyinyi mkishampata mtampeleka wapi?” Akauliza
“Sisi hatutaki kukuficha bwana Chibi, mtoto huyu atatupa faida kubwa sana kati yetu sisi sote wakati mzazi wake atafaidika na mtoto kama kila mzazi anavyofaidika na mtoto wake kwa kula matunda ya kumlea vizuri…. Hivyo usiwe na wasiwasi kabisa”
“Hujanifafanulia… Fafanua vizuri hili nitakapoinuka hapa kwenda kuongea na dada yake nijue naanzia wapi, maana ndiyo mtu wake hapa bwagamoyo kamfuata yeye licha ya kuwa wote wapo kwangu”.
“Chibi …. Kule China kuna vituo vya kulea watoto wenye vipaji mbalimbali, kaka yangu mimi ana kituo chake kinacholea huku kikiwapa watoto msaada wa kuwasomesha shule mbalimbali za watoto kulingana na mtoto alivyo na kipaji, wapo watoto wanaoruka sarakasi, wenye akili zilizopindukia, wacheza boxing, wacheza karate na hata wacheza mpira wa basketball na football… Sasa huyu mtoto wenu ana vipaji vingi kwa kumuangalia tu, hivyo huyu tukifika na kumkabidhi baada ya kumpa sifa zake huyo kaka yetu miezi mitatu atajua anamfaa kwenye nini ingawa sisi tushamjua kwamba mtoto ni genius kwenye masomo na kwenye michezo ni mwanasarakasi na mengine hatujayajua lakini kifupi ana mengi”
“Ok! Nimeelewa, akishamaliza miezi mitatu anakuwa mtu wake kwa kuingia mkataba naye au ni vipi?”
“Akishampima kwa vipimo vyake vya mazoezi atakayompa atajua anamuweka wapi lakini masomo ya kawaida yataenda sambamba na shule atakayompeleka… Miezi mitatu ya uangalizi uwa haiendi bure uwa anatoa malipo ya gharama za nauli tulizofanya kwa mtoto mwenyewe, sisi na atakayeongozana naye sababu mtoto uwa hachukuliwi bila mwakilishi kwenda nchi ya mbali na nchi yake”
“Sawa nakubali kuingia kwenye dili hilo… Nipeni dakika kadhaa za kuongea na dada yake” Aliwaomba wampe muda kidogo akaongee na dada binamu na Kai.
Mwisho wa sehemu ya nane (08)
Nafahamu msomaji wangu umeingia sehemu ambayo unaweza usipende kwa stori ambayo naielelezea juu ya star wetu wa riwaya hii ya Mshangao.
Ila hii ndiyo riwaya yangu ya kwanza kumleta nyota huyu, hivyo nimeona kifupi nimuelezee kidogo wasifu wake na hata kwanini anaitumikia Marekani na si Tanzania ilipo asili yake na wazazi wake.
Utanisamehe kidogo ila naomba nikuambie ni muhimu sana kupitia na kuisoma historia ya nyota huyu hili kujua unamsoma mtu wa aina gani katika vitendo na hata kihisia.
“Sisi hatutaki kukuficha bwana Chibi, mtoto huyu atatupa faida kubwa sana kati yetu sisi sote wakati mzazi wake atafaidika na mtoto kama kila mzazi anavyofaidika na mtoto wake kwa kula matunda ya kumlea vizuri…. Hivyo usiwe na wasiwasi kabisa”
“Hujanifafanulia… Fafanua vizuri hili nitakapoinuka hapa kwenda kuongea na dada yake nijue naanzia wapi, maana ndiyo mtu wake hapa bwagamoyo kamfuata yeye licha ya kuwa wote wapo kwangu”.
“Chibi …. Kule China kuna vituo vya kulea watoto wenye vipaji mbalimbali, kaka yangu mimi ana kituo chake kinacholea huku kikiwapa watoto msaada wa kuwasomesha shule mbalimbali za watoto kulingana na mtoto alivyo na kipaji, wapo watoto wanaoruka sarakasi, wenye akili zilizopindukia, wacheza boxing, wacheza karate na hata wacheza mpira wa basketball na football… Sasa huyu mtoto wenu ana vipaji vingi kwa kumuangalia tu, hivyo huyu tukifika na kumkabidhi baada ya kumpa sifa zake huyo kaka yetu miezi mitatu atajua anamfaa kwenye nini ingawa sisi tushamjua kwamba mtoto ni genius kwenye masomo na kwenye michezo ni mwanasarakasi na mengine hatujayajua lakini kifupi ana mengi”
“Ok! Nimeelewa, akishamaliza miezi mitatu anakuwa mtu wake kwa kuingia mkataba naye au ni vipi?”
“Akishampima kwa vipimo vyake vya mazoezi atakayompa atajua anamuweka wapi lakini masomo ya kawaida yataenda sambamba na shule atakayompeleka… Miezi mitatu ya uangalizi uwa haiendi bure uwa anatoa malipo ya gharama za nauli tulizofanya kwa mtoto mwenyewe, sisi na atakayeongozana naye sababu mtoto uwa hachukuliwi bila mwakilishi kwenda nchi ya mbali na nchi yake”
“Sawa nakubali kuingia kwenye dili hilo… Nipeni dakika kadhaa za kuongea na dada yake” Aliwaomba wampe muda kidogo akaongee na dada binamu na Kai.
ENDELEA NA STORY…!
MTAFUTANO PANDE MBILI II
Baada ya dakika kama arobaini alirudi na jibu kuwa dada kakubali kuwasaidia wafunge safari hadi Morogoro kwenda kuwaona wazazi wa Kai kwa ajili ya kumuomba mtoto wao. Siku ya pili mtoto Kai, wachina watatu, dada yake binamu na shemeji wakitumia gari binafsi la Bwana Chibi walielekea mkoa wa Morogoro, wilaya ya Morogoro mjini.
Huko napo hawakupata pingamizi kwa wazazi wa Kai sababu walikuwa wakijua nini maana ya elimu na nini maana ya elimu bora inayoambatana na mafunzo bora, baada ya wiki tatu ikiwa wamekamilisha taratibu zote mtoto Kai akiwa na baba yake mzazi wakiongozwa na wachina watatu waliofika kwa shemeji yake Kai kwa nia ya kujifunza kupiga vyombo vya muziki wa asili waliondoka Tanzania kuelekea China katika jiji la Beijing.
>>Mr. Chang Jie Lou ndiye aliyekuwa mchina mjasiriamali aliyekuwa akituma skauti wake kila pembe ya dunia katika nchi mbalimbali kutafuta watoto wenye vipaji mbalimbali kisha ana watatafutia shule na kuwalea kwa upendo mkubwa sana akiwapa mahitaji yote ya kuhakikisha hawaharibikiwi katika vipaji walivyonavyo pamoja na masomo yao.
Kai alifikishwa kwa mtu huyu na alipomuona kwa utaalamu wa saikolojia kwa watoto aligundua mtoto aliye mbele yake ni mtoto mwenye kipaji, wachina wenzake walikaa naye pembeni wakamueleza jinsi walivyogundua kipaji cha mtoto yule na wepesi wake katika masomo, baada ya maelezo marefu walirudi walipowaacha Kai na baba yake kisha mazungumzo ya itakuwaje mtoto atakapokuwa pale China.
Baada ya makubaliano maalumu kati ya Mr. Chang Jie Lou na Mr. Hamisi Mussa baba yake na Kai ilipitishwa maamuzi Mr. Hamisi Mussa atatumiwa tiketi ya kurudi tena China baada ya miezi mitatu ikiwa kusaini mkataba maalumu baina yake yeye mzazi na Mr. Chang Jie ambaye atakuwa kama mlezi wa mtoto Kai.
Alilipwa pesa kidogo mbele ya wanasheria ambao si mkataba wenye kumfunga kuwa kamuuza mtoto ilikuwa kama bakshishi tu ya dola kadhaa, baada ya wiki moja Mr. Hamisi akiwa katembezwea tembezwa sehemu mbalimbali za jiji la Beijing alirudi Tanzania na kufikisha yote yaliyojiri kwa mama mzazi wa Kai ambaye muda wote alikuwa na wasiwasi juu ya mwanae pengine ndiyo kaenda kuuzwa huko China.
Mtoto Kai alipelekwa shule ya kujifunza lugha ya kichina na kiingereza kwa pamoja ikiwa ni tofauti na watu wengine wanaoingia kusoma China au kufanya kazi nchini China, ilikuwa wanajifunza kusoma na kuandika lugha ya kichina peke yake miezi mitatu.
Lakini bwana Chang aligundua mtoto aliyeletewa anaweza kujifunza mambo mengi kwa wakati mmoja na akaelewa haraka na kwa ufasaha. Haikuwa tofauti na alivyowaza Kai hakumuangusha hakumuacha hapoteze muda na pesa zake bure, miezi miwili tu ya kwanza alijua lugha zote mbili kwa wakati mmoja akawa akiongea kichina na kukiandika pia hata kiingereza alikiweka kichwani haraka akawa akimudu kukisoma, kukiandika pamoja na kukiongea kwa ufasaha, mwezi mmoja uliobakia mwalimu wake wa kichina alimkazia katika kuongea kichina kwa kuvuta lafudhi na kuulanda ulimi vile wanavyovuta na kulanda wao wachina.
>>Yalipopita mambo ya lugha, Mr. Chang alifanya mawasiliano na wachina wake waliofanya mpango wa mtoto Kai kuamia China kupata China kupata elimu na mafunzo mengine yanayohusu kipaji chake. Wale wachina ya kupewa taarifa kuwa kuna mafanikio makubwa yamefikiwa kwa Kai wakafurahi sana, Mr. Chang akionyeshwa kufurahishwa zaidi aliwapa motisha ya zawadi iliyo nje ya makubaliano ya pesa fulani kila mmoja.
Furaha yake ilienda mbele kwa kuamua kutuma tiketi mbili za ndege kwa mzazi wa Kai Mr. Hamisi hili aongozane na mama Kai hadi China kwenda kusaini mkataba maalumu kuhusu mtoto wao.
Wazazi wa Kai walifika jijini Beijing China na wakapewa habari nzuri kuhusu mtoto wao kuwa ameonyesha jinsi gani yeye ni mtoto mwenye vipaji vingi. Mkataba uliingiwa kuwa Mr. Chang Jie Lou
atamsomesha Kai elimu ya kawaida kwa wanadamu mpaka chuo kikuu, atampeleka shule za mafunzo ya Acrobatics mpaka atakapomaliza mafunzo yote pia atamtafutia ajira. Wazazi wa Kai walikubaliana na mkataba huo sababu haukuwa unawafunga pia ulikuwa msaada mkubwa kwao wao na mtoto wao kwa ujumla.
Walilipwa pesa nzuri wao na hata wale wachina watatu nao walichukua pesa nzuri. Wazazi wa Kai walikaa nchini China miezi miwili wakiwa na mtoto wao wakiishi katika hoteli nzuri kwa kugharamiwa na Mr. Chang Jie Lou.
Walipoondoka waliacha Kai akiwa kaandikishwa shule ya kawaida ya kimataifa iitwayo Yew Chung International School of Beijing (YCIS Beijing) na pia shule ya mafunzo ya mchezo wake iitwayo Beijing Acrobatics School, akiingia shule ya masomo ya kawaida asubuhi ya saa mbili mpaka saa tisa mchana kisha akirudi shule anapumzika mpaka saa kumi na mbili jioni anaingia shule yake ya Acrobatics (sarakasi) ambapo huko alikuwa mafunzoni kuanzia muda huo hadi saa tatu usiku.
Bidii ilikuwa kubwa sana kwa mtoto Kai katika mambo yote hayo kwa pamoja kwa muda wa miezi sita tu alimaliza mafunzo yote yanayohusu acrobatics za aina mbalimbali akionyesha wepesi wa hali ya juu sana mpaka yalipofika mashindano ya michezo mbalimbali inayohusu shule za sarakasi zilizopo jiji la Beijing, alichaguliwa katika timu ya shule iliyowakilisha shule yao ya ambapo alifunika kwenye mashindano na kuacha jina kubwa sana miongoni mwa wanafunzi wa shule za jijini Beijing.
Baada ya kurudi toka mashindanoni na medali kadhaa za sarakasi za aina mbalimbali, mlezi wake alifurahi sana na kuona kweli kapata mtu ingawa katika watoto zaidi ya ishirini aliokuwa akiwamiliki kama anavyomiliki Kai wote walikuwa ni watoto wenye vipaji ila Kai alikuwa kivutio kikubwa kwake. Mitihani ya mwisho ya darasa lake la kwanza katika shule yake ya Primary aliweza kukaa juu ya wanafunzi wengine wapatao mia na tano akishika namba moja kwa maksi za juu sana.
Walimu wakamuita mlezi wake Mr Chang Jie na kumuomba aingie katika uangalizi maalumu kwa wao walimu mwaka wa pili kama ataendelea na nidhamu aliyoionyesha na bidii yake basi watamvusha darasa.
Na kweli mwaka uliofuata aliendeleza spidi yake ile ile ikabidi arushwe darasa, kwenye acrobatics napo aliongezewa mafunzo ya Acrobatics and Circus skills, aerial, equlibirium, contortion, tumbling and juggling.
Msimu uliofuata wa kumaliza mwaka waliingia katika mashindano ya shule zilizo jiji la Beijing ambako mwaka huo watu wengi toka mataifa mbalimbali walifika kushuhudia mashindano yale, mtoto Kai alitisha mbaya katika mashindano yale. Walikuwepo watu wawili toka Marekani walionyeshwa kuvutiwa mno na mtoto Kai wakaondoka na jina lake wakiahidi kurudi tena kumchunguza. Shule zilipofungwa Mr. Chang Jie Lou alimsafirisha yeye mwenyewe kilikizo kwenda naye Tanzania ambako walikaa wiki tatu wakienda sehemu mbalimbali za kitalii ambazo napo waliongozana na wazazi wa Kai kwa gharama za Mr Chang Jie Lou.
Likizo ilipoisha walirudi Beijing, China kama kawaida kuendelea na masomo pamoja na mafunzo, walimu wake wa mafunzo walimuongezea mafunzo mapigano ya Karate, Wushu, Kung Fu na Judo. Bado aliendelea kufanya vizuri, ilipofika mashuindano ya mashule safari hii aliongezewa katika fani ya mapigano (Martial arts) ambapo alivunja rekodi mwenyewe aliyejiwekea mwaka uliopita kwa kubeba medali katika acrobatics kwa ujumla, Kung fu na judo.
Wale wamarekani walioahidi watarudi kumuona tena safari hii waliona itakuwa si busara kwao kukaa kimya wakauliza kwa walimu wake wa mafunzo juu ya habari ya kijana huyu pekee katika asili ya Afrika huko walielekezwa kwa mlezi wake Mr. Chang wakaenda kumjua Mr Chang na akawapa taarifa za mtoto Kai, ambaye alikuwa amebadilika mwili kutokana na mazoezi anayoyafanya ukimuona unakuwa huamini kama ana miaka tisa kwa wakati huo.
Baada ya maongezi Mr Chang kwakuwa ilikuwa ndiyo biashara yake kuuza watoto kwa vikundi mbalimbali vya kiserikali mpaka vya kihalifu wa kimataifa alifurahi sana kuona dhahabu yake ishaanza kuonekana kwa watu wanaojua kama yeye umuhimu wa kuendeleza vipaji vya watoto.
Wakamuahidi watakuwa wanarudi kila mwezi wa kumi na mbili kuona anaendeleaje kingine walistaajabu baada ya kupata taarifa darasani napo yupo sawa sawa. Habari zikafika katika kitengo maalumu cha serikali ya Marekani juu ya mtoto huyo, wakatumwa watu kuanza kumfuatilia ikiwezekana watumie hila yoyote kumpata Kai, mwisho wa mwaka mwalimu mkuu wa shule alimuita tena mlezi Mr Chang kumpa taarifa wanataka Kai afanye mtihani wa darasa la nne na wanafunzi wa darasa hilo alipokubali mtoto Kai akafanya mtihani napo akaonyesha kipaji chake masomo ya sayansi na hesabu aliyatendea haki na kwa ujumla akawa wa pili akifungana maksi na watoto wawili waliokuwa wao la nne.
Shule zikafungwa zilipofunguliwa aliingia la tano, ndipo akawa akipata wageni mara kwa mara wakifika shule yake ya mafunzo na mara nyingine ya masomo ya kawaida, wengi wao walikuwa waandishi wa habari kwa utambulisho wao wakifika mapokezi na wengine walikuwa watu wa mashirika ya kijasusi na hata ya magenge ya kihalifu ya nchi mbalimbali.
Mr Chang alijitahidi kumlinda kwa kumpatia ulinzi kila aendapo shule na anaporudi na pia anapotaka kufanya matembezi yake mbalimbali. Mtoto Kai alikuwa kivutio na kwakuwa katika watoto aliokuwa nao Mr Chang kulikuwa na watoto kumi wanaruka sarakasi kama arukavyo Kai aliona ni bora akaunda kikundi kitakachokuwa kinatoa burudani kama vikundi vingine vingi vilivyokuwa ndani ya China aliona ni wakati wake kuwatumia watoto wale kupata pesa.
Kikundi kilisajiliwa na kwa muda mfupi kilipata umaarufu sababu Kai alikuwa mburudishaji mkubwa mwenye uwezo mkubwa sana wa kuruka juu sana na kuunganisha kwa haraka na kwa wingi sarakasi za aina mbalimbali, kikundi kilikuwa kinmapatikana kila jumapili katika kumbi mbalimbali kikitoa burudani kwa kukodishwa.
Serikali ya China ilimfuata Mr Chang nakumuomba wafanye mpango mapema mtoto yule apewe uraia wa China hili waje kumtumia katika michezo ya Olimpiki na kumuingiza katika mipango yao mbalimbali ya kinchi wakiona anafaa wapi maana mpaka wakati huo kwa utaalamu wao na maendeleo yake ya darasani walihisi anaweza kufiti kwenye mambo ya sayansi au kwenye mambo ya kijeshi au kwenye mambo ya kijasusi. Mr Chang aliwaambia yupo tayari kumkabidhi awe chini ya uangalizi wa serikali.
Lakini wakati wao wakiwaza hivyo serikali ya Israel ilizipata habari zake, serikali ya Uingereza nayo ilizipata habari za mtoto mwenye kipaji na kwakuwa walionyesha nia ya kumtaka habari zile zikavuja na kufika kwa Marekani ambao kwao ni kawaida sana kutafuta watoto wa sampuli hii, hivyo wao walikuwa na uzoefu uliowasaidia kuwa na mbinu nyingi za kuwapata watoto kama hao waligundua kumuacha mikononi mwa Wachina ni kuwapa faida wachina.
Kipindi wanawaza hivyo ulikuwa ni mwaka wa mwisho wa kimasomo wa Kai akiwa namaliza darasa la sita ambalo ni darasa la mwisho kwa shule za msingi za China alikuwa bado mdogo ana miaka kumi na moja kutokana na kurushwa darasa kutoka la tatu alilotakiwa kuingia akitokea darasa la pili hadi darasa la tano baada ya kupewa mtihani wa darasa la nne kuufanya.
Watu wawili mmoja mwanamama na mwingine mwanaume toka kitengo maalumu cha kutafuta vipaji vya watoto kutoka Marekani walifika Tanzania mkoani Morogoro na kufika moja kwa moja kazini kwa mzazi wa kiume wa Kai. Baada ya kujitambulisha wapi wanatokea wakaomba nafasi ya kimaongezi jioni ya siku hiyo baada ya muda wa kazi.
Jioni hiyo kweli walikutana na Mr Hamisi Mussa aliyewakaribisha nyumbani kwake, baada ya kueleza nia yao ni nini kwa kweli yalikuwa mazito sana kutokana na bwana Hamisi kutokubaliana nao akimuogopa Mr Chang kutokana toka mwaka uliopita baada ya Mr Chang kuunda kile kikundi cha watoto na kukipa jina Chang Acrobatics Children Talents ‘CACT’ kila mwezi alikuwa akimtumia bwana Hamisi dola elfu moja mia tano kiasi kikubwa sana cha pesa katika miaka ile ya mwishoni mwa miaka ya tisini kila alipozibadili kwa ela ya kitanzania, alizigawa kwa mama mzazi na Kai na wote wakawa wanafanyia mambo ya maana kama kumalizia nyumba zao na hata kupata gari ndani ya mwaka mmoja tu. Wale watu wote wakiwa ni wazungu ilibidi waage kuwa watarudi siku yapili ambayo ni jumamosi kwa maongezi zaidi, iliwabidi wafanye hivyo hili wakaombe ushauri toka kwa mkuu wao wa kazi.
Siku ya pili walifika mapema kwenye kikao chao ambacho pia aliongezeka mama mzazi wa Kai akiwa na kaka yake ambaye kwa Kai anamuita mjomba. Pia alikuwepo kaka binamu wa Kai, wale wazungu cha kwanza tu waliuliza kitu gani kama familia kinapata kupitia mtoto wao, bwana Hamisi alieleza jinsi gani anavyoona ugumu wa jambo hili, ndipo mzungu mwanaume aliyekuwa amejitambulisha anaitwa Joseph Mackson akasema walichoshauriwa na mkuu wao wa kazi, ambaye naye alipewa ushauri na watu kutoka wizara inayomiliki kitengo chao ikiwa wao walishapewa taarifa za kiuchunguzi toka kwa shirika la kipelelezi la FBI na shirika la kijasusi la CIA kuwa wakimtaka mtoto yule wakamshirikisha Mr Chang wanampata mtoto yule sababu kazi yake ni kulea kusomesha watoto na kisha kuwauza katika nchi mbalimbali na hata vikundi mbalimbali.
Basi walishauriana kwa pamoja yafanyike mawasiliano haraka ikiwezekana Mr Chang aombwe afike Tanzania. Taarifa ingine ambayo iliwastua wazazi wa Kai ni kusikia kuwa Mr Chang uwa anawauza watoto wafikapo miaka ya kumaliza masomo na mafunzo yao.
Walikutwa na hofu ya ghafla mpaka waliitana kifamilia na kujadili kidogo baada ya kikao kile kilirudi na jibu la kutaka kujua na wale wazungu wanamtaka Kai kwa dhumuni gani haswa baada ya kumaliza masomo yake. Ikabidi Mr. Mackson aelekeze vizuri nia yao kuwa ni nia ya serikali nzima ya Marekani kipindi icho ikiongozwa na Rais Bill Clinton na hata wakifanikiwa kumpata mtoto Kai basi wataongozana na wazazi wote wawili mpaka Marekani na kisha moja kwa moja hadi kwa waziri anayehusika na masuala hayo na kisha hadi kwa Raisi wa nchi.
Mr Hamisi alichukua jukumu la kupiga simu kwenda nchini China kwa Mr Chang Jie Lou na kumuomba afanye anavyoweza afike nchini Tanzania, Mr Chang alihoji mbona ghafla sana ikabidi atumie mbinu ya uongo kidogo kuwa kuna tatizo kidogo la kifamilia linalomuhusu Kai lakini kama akifika yeye Mr Chang ndiyo itakuwa vizuri zaidi.
Mr Chang akakubali kufika lakini baada ya siku tatu hili afanikishe kufika na Kai aliyekuwa ana jambo anamalizia katika mafunzo yake. Ikabidi Mr Hamisi aombe kupigiwa baadaye kwanza aongee na ndugu wengine wa familia juu ya ombi lake kuwa waje Tanzania baada ya siku tatu. Baada ya kukata simu alishauriana kwanza na wageni wao kisha akapiga tena China na kumpa jibu amekubali waje baada ya siku tatu. Mr Mackson na mwanamama aliyekuwa akiitwa Lilian Traizer waliona siku tatu si nyingi wakapanga hotel wakisubiri mtoto Kai na Mr Chang wafike.
>>Baada ya siku tatu Mr Chang na mtoto Kai walifika na kupokelewa kwa furaha sana mpaka Mr Chang akashangaa kutokukuta tatizo kama alivyokuwa ametaraji hata kujiandaa kisaikolojia, kisha baada ya masaa mawili watu wa kwa ajili ya kikao walifika Mr Mackson na bibie Lilian Traizer.
Baada ya salamu na utambulisho maalumu kikao kilianza ambapo kwa bwana Chang ilikuwa si tatizo kwake lakini hofu yake ilikwenda kwa serikali ya nchi yake, dau lililowekwa mezani lilimfanya akubali kwa urahisi lakini je atawajibu nini watu wa serikali ya nchi yake aliyowaahidi kuwa atawakabidhi mtoto Kai pindi atakapomaliza sekondari kwa alivyoamini yeye atakuwa kashamtumia sana Kai katika kuingiza pesa za matamasha na hata medali alizokuwa akizipa shule zake zote mbili moja ya mafunzo ya Acrobatics na ile ya msingi amabapo sasa alikuwa akienda sekondari, shule zile zilikuwa zikimlipa pesa yeye kila Kai alipokuwa akizipa ushindi katika mashindano.
Mr Mackson alipoona kuna ugumu katika maongezi yao ukijengwa na woga wa Mr Chang kwa serikali ya China akaona aombe udhuru kidogo hivyo haraka aliomba ruhusa aongee na wakuu zake nao kwa haraka walimuomba bora aongeze dau mara tatu ya alilowaahidi Mr Chang na familia ya Kai pamoja na wale wachina watatu wa mara ya kwanza waliofika bwagamoyo na kugundua kipaji cha mtoto Kai, dau la mara ya pili lilimfanya Mr Chang kukubali kumuachia Kai katika himaya yake. Mikataba ikasainiwa siku ya pili yake na hapo ikawa mwanzo mwa mtoto Kai mwaka mpya kusherehekea akiwa na wazazi nchini Marekani katika jiji la New York.
>>Mpaka wazazi wa Kai wanaondoka wakiwa wameshajihakikishia mtoto wao atakuwa katika mikono iliyo salama ya serikali ya Marekani ilikuwa wamekaa Marekani kwa miezi miwili. Mtoto Kai alikabidhiwa kuishi kwa kiongozi msaidizi wa shirika la kijasusi la Marekani la CIA ‘Deputy Director’. Ilikuwa hivyo bado ya wao serikali ya Marekani kuamini mtoto mwenye vipaji vingi kama Kai alikuwa na akili za kipelelezi na hata kimapigano hivyo ujasusi ndiyo fani halisi aliyozaliwa nayo.
Ingawa yeye mwenyewe Kai alipoulizwa anatamani kuwa nani atakapokuwa mkubwa aliwajibu anataka kuwa ‘ninja komando’, watu wa mambo ya kijasusi wa Marekani waliona ni mtazamo mzuri na kwa mtu mwenye akili kama zake na uelewa wa haraka chochote anachokitamani kwake akipewa muongozo tu basi ataweza kukifanya kwa ufasaha tu.
Lakini wakaona wakimpeleka jeshini moja kwa moja kwa umri wake haitawezekana mpaka afike umri wa miaka kumi nane. Rais wa Marekani wa wakati huo Mr. Bill Clinton akashauri apelekwe shule za kijasusi ajengwe katika ujasusi na atakapofika umri wa miaka kumi na nane apelekwe kujiunga na jeshi la marekani US Army na huko moja kwa moja apelekwe kwenye mafunzo ya ukomando na mafunzo ya uninja atapewa huko huko ingawa yeye alishaanza mafunzo ya uninja akiwa China.
Baada ya kukabidhiwa kumlea mtoto yule kutokana na yeye familia yake ilikuwa haijafanikiwa kuwa na mtoto Deputy Director aliahidi kumlea Kai kama ni mtoto wake ingawa gharama za kusoma hazikuwa juu yake na wala gharama za maradhi, chakula na hata mavazi lakini yeye alitaka kuonyesha ni jinsi gani amekosa baraka za kuwa na mtoto yeye na mke wake lakini si kutokuwa mlezi bora si kutokuwa mfano wa bora.
Hata wazazi wa Kai mwezi mmoja wa mwisho kati ya miezi miwili waliyokuwa kama wamepewa ofa ya kukaa Marekani waliumalizia kwa huyu kiongozi msaidizi wa CIA. Shule zilipofunguliwa Kai alipelekwa shule inayomilikiwa na shirika la kijasusi la CIA ikiwa inawaandaa watoto wenye vipaji kama Kai walioonyesha ishara ya wao kuwa wanafaa kuwa majasusi baada ya uchunguzi maalumu inayojulikana kwa jina la Sherman Kent School For Intelligence Analysis iliyopo Williamsburg, Virginia.
Ni shule iliyokuwa ikifundisha masomo ya kijasusi na masomo ya kawaida ya sekondari pia wakipata mafunzo ya vitendo. Kai aliendelea kuonyesha yeye ni kipaji halisi aliweza kuwashinda wenzake kila wanapofanya mitihani akishika namba moja katika masomo yote iwe ya sayansi au arts mpaka walimu wakawa hawajui wamuweke wapi kama inavyotakiwa katika shule zote ndipo alipofiika mwaka wa pili akachagua mwenyewe kuwa atasoma masomo ya sayansi baada ya kupewa ushauri na mzazi wake wa kiume.
Miaka minne ikapita akifaulu kwa grade ya kwanza katika masomo ya sayansi yote unayoyajua wewe yakisindikizwa na hesabu ambalo nalo alipata A na kipindi icho chote kila likizo ya mwezi wa sita alikuwa akipelekwa chuo cha mafunzo ya uninja kilichopo Sloatsburg, New York ambako ulikuwa akikaa kambini mwezi mzima mpaka shule zinapofunguliwa anaondoka kurudi shuleni ambako napo walikuwa wakiishi kambini huko huko.
Baada ya kufaulu hapo alirudi likizo Tanzania akakaa mwezi mmoja aliporudi Marekani kuendelea na masomo moja kwa moja akapelekwa chuo cha CIA University (CIAU) kilichopo Chantilly, Virginia. Ambako alifunganisha masomo mbalimbali, alipomaliza ndipo akapelekwa chuo cha US Navy Seals Training BASE, Coronado, California kambi iliyo mpakani mwa jimbo la California na San Diego.
Huko alipotea miaka mitatu bila kuonekana Tanzania wala uraiani pale New York alipokuwa akilelewa kwenye familia ya Deputy Director wa CIA.
Alipokuja kurudi alikuwa komando rasmi tena aliyefudhu kwa maksi za juu kuliko wanafunzi wenzake kumi alioingia nao kwa wakati mmoja. Kwa uwezo aliounyesha kiongozi wa US Navy Seals aliiomba serikali ya Marekani atumikie kwanza kikosi chao sababu mwaka huo alipomaliza kulikuwa na vita ya ghuba ya uajemi ya pili iliyokuja kumuondoa Saddam Hussein, hivyo Kai akawa komandoo mdogo kabisa aliyeingia katika vita hiyo akiwa na kundi la US Navy Seals.
Na hii ndiyo ilikuwa ndiyo historia ya Agent Kai na sababu iliyomfanya kujikuta anaitumikia Marekani baada ya nchi ya Tanzania<<.
Mwisho wa sehemu ya tisa (09)
Sehemu iliyopokea historia ya nyota wa Mshangao kutoka sehemu ya nane ambako nilitanguliza ombi la kuomba subira yako msomaji kumjua nyota huyu.
Naam tushajua mengi juu ya Agent Kai tokea akiwa mdogo nchini Tanzania na ilikuwaje akaangukia mikononi mwa taifa la Marekani, akifanya kazi kwa maslahi mapana ya taifa hili kubwa lililokusanya watu asili mbalimbali toka nchi mbalimbali wengine wakiwa wanunuliwa kama Agent Kai.
Nisikuchoshe, pata break kisha uendelee na sehemu ya kumi (10)
TUKUTANE SEHEMU YA KUMI (10)
Miaka minne ikapita akifaulu kwa grade ya kwanza katika masomo ya sayansi yote unayoyajua wewe yakisindikizwa na hesabu ambalo nalo alipata A na kipindi icho chote kila likizo ya mwezi wa sita alikuwa akipelekwa chuo cha mafunzo ya uninja kilichopo Sloatsburg, New York ambako ulikuwa akikaa kambini mwezi mzima mpaka shule zinapofunguliwa anaondoka kurudi shuleni ambako napo walikuwa wakiishi kambini huko huko.
Baada ya kufaulu hapo alirudi likizo Tanzania akakaa mwezi mmoja aliporudi Marekani kuendelea na masomo moja kwa moja akapelekwa chuo cha CIA University (CIAU) kilichopo Chantilly, Virginia. Ambako alifunganisha masomo mbalimbali, alipomaliza ndipo akapelekwa chuo cha US Navy Seals Training BASE, Coronado, California kambi iliyo mpakani mwa jimbo la California na San Diego.
Huko alipotea miaka mitatu bila kuonekana Tanzania wala uraiani pale New York alipokuwa akilelewa kwenye familia ya Deputy Director wa CIA.
Alipokuja kurudi alikuwa komando rasmi tena aliyefudhu kwa maksi za juu kuliko wanafunzi wenzake kumi alioingia nao kwa wakati mmoja. Kwa uwezo aliounyesha kiongozi wa US Navy Seals aliiomba serikali ya Marekani atumikie kwanza kikosi chao sababu mwaka huo alipomaliza kulikuwa na vita ya ghuba ya uajemi ya pili iliyokuja kumuondoa Saddam Hussein, hivyo Kai akawa komandoo mdogo kabisa aliyeingia katika vita hiyo akiwa na kundi la US Navy Seals.
Na hii ndiyo ilikuwa ndiyo historia ya Agent Kai na sababu iliyomfanya kujikuta anaitumikia Marekani baada ya nchi ya Tanzania<<
ENDELEA NA DODO..!
MTAFUTANO PANDE MBILI III
.
“Ramsey Bronze hapa!” Aliongea Kai baada ya kupiga namba za simu alizopewa upya na kiongozi wa operesheni zote zinazofanyika kupitia ofisi ya makamu wa Raisi (Chief Of Staff to the Vice Pressdent of America) na kuzihifadhi sehemu ya kuhifadhia namba za simu kwenye simu yake mpya aliyoletewa na binti muhudumu wa hotel Shufania baada ya kumtuma akamnunulie, alimletea simu aina ya Samsung Galaxy Note 8, namba alizopiga zilikuwa za balozi wa Marekani nchini Malaysia.
“Nilikuwa na wasiwasi sana juu yako mwanangu, nimefurahi sana kusikia sauti yako”
“Usiwe na wasiwasi baba yangu naamini unanijua mwanao nilivyo mtambo… Tusiongee sana kwenye simu naomba tuonane, saa hivi ni saa moja na dakika thelathini na tatu. Nielekeze wapi nije”.
“Kwani huko wapi saa hivi?” Akauliza balozi.
“Nipo Alamanda Hotel, unaonaje ukija kwenye moja ya migahawa iliyo karibu na huku?” Akamjibu na kumpachika swali.
“Oooh, ushapanga wapi tuonane?”
“Sijapanga mkuu…. Nimekuuliza, nimehisi pengine unaweza kuwa unaujua mgahawa ulio mzuri ulio maeneo haya ya karibu na Alamanda Hotel”.
“Okay! Muda huu niko kwenye gari naelekea ikulu ya kiongozi wa nchi hii, Waziri mkuu. Saa mbili kamili tuna kikao baina yake, mabalozi wa nchi za umoja wa ulaya pamoja nami”.
“Ikulu ya waziri mkuu iko wapi?”.
“Ipo eneo la Putrajaya”
“Basi nitasogea karibu na eneo hilo nafikiri sitakosa mgahawa mzuri tutakaoweza kuongea, ukishamaliza kikao utanitumia meseji halafu mimi nitakuelekeza nipo mgahawa gani”.
“Eeeh! Ipo migahawa mingi mizuri tu eneo la Putrajaya, ukifika utanielekeza tu nami nikimaliza kikao tu nitakucheki, ila jitahidi kuwai kutoka huko kutokana kuna umbali kutoka Sepang hadi Putrajaya”.
“Ahsante sana kwa maelekezo… Ila naomba utume mtu aniletee gari na kibali ulichoniandalia cha kuendesha gari nchi hii… Pamoja na mzigo nafikiri mlishaongea juu ya huo mzigo wewe na Chifu hivyo naamini Meja unafahamu ni mzigo gani na umeshauandaa kutokana wewe si mgeni wa michezo hii”.
“Nikikata simu tu kwako napiga kwa mesenja wangu anakuletea, niliandaa mwenyewe toka juzi baada ya kupewa maelekezo na Chifu, uzuri wake vingine vilikuwa vipo tayari siku zote vikihitaji watumiaji tu kama wewe tu…. Mzigo huko kamili una kila kitu muhimu”.
“Nakuamini Meja… Nakutakia kikao chema uendako”.
“Nashukuru kijana wangu mtambo wa sheria genius… Naomba usubiri papo hapo hotelini, mtu nitakayemtuma kuleta gari ataleta gari aina ya Nissan Frontier rangi nyeusi ataiacha kwa mlinzi wa magari wa hapo Alamanda Hotel, ukitoka utajitambulisha kwa jina hilo hilo la Ramsey Bronze”.
“Huko vizuri Meja… Nafurahi sana kufanya kazi tena na wewe baada ya miaka mingi, pamoja na umri wako kusogea hujasahau kazi”.
“Siwezi sahau sheria za kazi na usalama wake… Bye! … US First!”.
“US First”
Simu zikakatwa pande zote mbili.
Baada ya dakika arobaini toka atoke kuongea na balozi wa Marekani nchini Malaysia Kai akiwa tayari kashapigilia mavazi aliyoletewa na binti Shufania kwa maelekezo aliyompa alipomtuma, alitizama saa ilikuwa ilikuwa saa mbili na dakika ishirini na nane usiku, alitoka kwenye chumba alichokuwa kapanga (appartiment) na kufunga mlango kwa kutumia kadi, moja kwa moja akaenda kwenye lifti ya hoteli hili imteremshe hadi chini yalipo mapokezi na mgahawa wa hoteli.
Akiwa kwenye lifti ikiwa imeanza kushuka ndipo alipomkumbuka binti Shufania kwani alishuka naye kwenye lifti mchana wakati wanaongozana kwenda ATM kutoa pesa, uzuri wake ulimbabaisha sana Kai na ubongo wake kuwa unatamani afanye kitu.
Agent Kai katika umri alionao wa miaka thelathini na tatu aliwai kuoa miaka saba iliyopita mwanamke kimarekani mzungu wakaachana miaka mitatu tu ya ndoa yao, kutokana mwanadada huyo wa kizungu alikuwa havutiwi na kazi anazofanya Kai sababu alimuoa kipindi yeye Kai akiwa ni komandoo wa jeshi la Marekani kitengo cha makomandoo spesho (US Navy Seals) akatumia uwezo wake wa kuwa ndani ya penzi zito na ndoa tamu yao kumshawishi Komandoo Kai aachane na kazi afanye mambo mengine.
Kai aliporudi toka kwenye janga la milima ya tolabora nchini Afghanistan mwanamke yule alipigana kweli kweli mpaka Kai akakubali kuandika barua kwa mkuu wa majeshi akimuomba ajiondoe katika kikosi cha US Navy Seals lakini serikali ya Marekani kwa kujua umuhimu wa Kai na gharama walizotumia kumnunua na kumsomesha walijitahidi kumshawishi na hata kumkumbusha wapi wamemtoa mwisho wakaona atafutiwe sehemu muhimu ambayo itamfanya aendelee kuitumikia Marekani katika mambo yale yale waliyomsomesha ingawa yeye alipenda arudi chuo kuchukua degree ya udaktari, ndipo akaombwa arudishwe kule alikopita wakati anafika Marekani alisoma shule na vyuo vya CIA lakini napo hili wampunguzie kashikashi atafutiwe sehemu atakayokuwa hafanyi shughuli za mara kwa mara.
Ikatokea nafasi ya uwakala wa CIA katika ofisi ya makamu wa Raisi nafasi ikamuangukia. Mke akafurahi kuwa kashinda lakini miezi sita tu Agent Kai akajigundua hatakiwi kukaa ofisini tu akaomba awe anapewa kazi zitakazomfanya alipe kwa kuutumikia mshahara wake, hapo zikaanza kuja kazi alizozifanya katika ustadi wa hali ya juu na kujikuta anapanda chati ya juu miongoni mwa majasusi wa CIA na hata wapelelezi wa mashirika mengine.
Kazi nyingi zilizoshindikana alizifanya yeye na kuleta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali na hata kuharibu vikundi mbalimbali vya kihalifu vya kimataifa hadi kuwakamata au kuwaangamiza kabisa watu aliotakiwa kuwafanyia hivyo.
Hapo mke akaona hakuna alichokwepa hawezi kuendelea kuishi mwanaume aliyezoe kufukuzana iwe kwa miguu, pikipiki, magari na wahalifu kukwepa mishale, risasi, ngumi na kujibu mapigo kwa stahili iliyotumika yeye kushambuliwa akajaribu kama utani kuomba taraka na Kai naye kwakuwa alikuwa amemchoka kutokana alikuwa mwanamke wa kununa nuna mara nyingi na anachokitaka ilikuwa lazima kitimie alikubali akamuandikia taraka.
Mwanadada alilia sana kwa kusema alikuwa anatania lakini Kai hakurudi nyuma hakuchana taraka zikaanza hatua za kupeana baada ya mwezi taraka ikakamilika wakagawana mali na habari kati yake na yule mwanamke zikaishia hapo, ndoa yao ilileta mtoto mmoja wa kikechotara (shombeshombe baby), pia ana mtoto mwingine wa kiume alizaa na mwanamke ambaye hakufunga naye ndoa walikuwa ni marafiki wapenzi ambao ulikuwa upendo wa dhati sababu walikaribia kuvishana pete za uchumba alikuwa ni chotara kihispania na kiafrika.
Hawakufanikiwa kutimiza nia yao ya kuvishana hata pete za uchumba kwani mwanadada yule alikufa mwaka jana kwa kuuliwa na magaidi huko Pakistani alikuwa kazini sababu naye alikuwa ni jasusi wa shirika la kijasusi la CIA kama alivyo Kai, lakini yeye alikuwa ofisi ya Washington DC, alimletea Kai mtoto wa kiume akiwa na mwaka mmoja na sasa huyo mtoto ana miaka miwili wakati dada yake ana miaka mitano.
Watoto hao wote anaishi nao kwake wakiangaliwa kwa ukaribu na dada yake mkubwa wa kwanza katika kuzaliwa kwao ambaye anaishi naye Marekani akiwa na mume wake na familia yake ambaye Kai amemfungulia biashara ya duka kubwa la kuuza fenicha, pia wapo wasaidizi wa kazi wawili mmoja wa kiume ambaye ni kama dereva wa familia, pia yupo mdada mwingine ambaye anahusika na mambo ya mapishi na mambo ya mapishi na wote aliwatoa Tanzania. Watoto wake wote wanasoma shule na wa kiume amerithi utundu uleule aliokuwa nao baba yake wakati mdogo.
Baada ya kutoka kwenye lifti moja kwa moja alitoka kwenye eneo la mapokezi ambako kando yake kuna mgahawa mkubwa wa hotel, yeye akaelekea nje kuliko na bustani za hotel na kutafuta sehemu iliyo karibu na geti la kuingia kwenye maegesho ya hoteli hili iwe rahisi kuliona gari atakaloletewa likiingia. Alipopata kiti ambacho chenyewe na meza yake hakukuwa na mtu yeyote akakivuta na kukaa. Haikuchukua muda muhudumu wa kiume alifika pale akiwa na daftari mkononi.
“Habari yako kaka?”. Akasalimiwa na muhudumu yule.
“Safi sana!... Naomba niletee juice ya embe”. Akamjibu salamu na kumuomba.
Muhudumu akaondoka, Kai akatumia fursa kuitoa simu yake toka mfukoni kisha akatoa lock na kuitafuta namba ya Shufania alizopeana naye mchana wakati alipomuomba binti yule amfundishe kuingiza salio anaponunua vocha za simu kwa mtandao wa kampuni ile ambayo laini hii iliyo kwenye simu hii ni ya kampuni ya Malaysia, alitabasamu wakati anaiangalia ile namba kisha akaibonyeza na mara moja ikaanza kuita.
“Hallow”. Akaongea baada ya kusikia ikipokelewa upande wa pili.
“Hallow!.... Asallaam aleykuum!”. Sauti tamu ya upande wa pili ikasikika ikijibu na kutoa salamu.
“Aleikum sallam! Habari yako Shufania?”.
“Nzuri tu… Hofu kwako Ramsey, upo poa?”.
“Nashukuru Mungu niko poa kabisa, wala usiwe na hofu… Huko wapi muda huu?”
“Nipo nyumbani Ramsey, sina pakwenda mimi kila ikifika usiku kama huu napatikana nyumbani tu… Saivi naandaa chakula baada ya kupika… leo zamu yangu kupika, napikia familia”.
“Safi sana… Natamani nionje mapishi yako… Nafikiri ni matamu sana”.
“Karibu nyumbani uyaonje, kwetu si mbali na hapo Alamanda Hoteli… Utayaonja mapishi yangu pia utafurahi kuwajua wazazi wangu na wao watafurahi kukujua mtu mcheshi na mzuri kama wewe”
“Mmmh… Haaah! Naogopa wazazi wako”.
“Kwanini unawaogopa wazazi wangu?.... Wazazi wetu sisi si simba wala mbwa mwitu, kwetu hatufukuzi wageni”.
“Mmmh! Yah kweli hayo? Nisije nikaja nikaanzisha kesi zingine… Mara umemtoa wapi huyu mtu mweusi” Kai akaongea na kuunganisha na kicheko kidogo.
“Kweli Ramsey…. Yaani kwetu hatubagui rangi, dini wala imani yoyote ya mtu, kila mtu anaruhusiwa kufika kwetu, usije ukaogopa kabisa kufika kwetu”.
“Basi nitapanga siku kabla sijarudi kwetu nije kuwaona wazazi wako”
“Kweli?”. Akauliza Shufania akiwa ahamini alichosema Kai kama kitakuja kutokea.
“Ninapoahidi kitu kwa watu wa ukweli wasio fake basi uwa naahidi ahadi ya ukweli”.
“Ikiwa ni kweli nitafurahi sana… Kuna kitu natamani kukuuliza lakini naogopa kukuuliza muda huu kwenye sababu nilipanga nitakuuliza kesho… Hivyo nitakuuliza kesho tukikutana”.
“Tafadhali niulize leo Shufania… uwa sipendagi kulaza jambo linalowezekana leo… Mama yangu alinifunza neon moja ambalo uwa nalithamini sana kuwa linalowezekana leo lisingoje kesho”
“Alikufunza mama neno zuri lakini sidhani kama katika mafunzo yake alisahau kukufunza kuwa subira yavuta kheri na akasahu kukwambia kama haraka haraka haina baraka”. Akajibu Shufania na kusababisha wote wacheke kiasi ambacho kicheko kile kilimsababisha Shufania aangaliwe na binti wa kazi anayemsaidia mama yake kazi za nyumbani kwao hasa za jikoni na usafi usafi wa nyumba ambaye muda huo wote walikuwa jikoni wanaisubiri mboga iive vizuri.
“Hahahahah…. Nachokumbuka aliniongezea na ngoja ngoja inaumiza matumbo… ila kwakuwa umedhamiria na iwe hivyo unavyotaka nitakusubiri hadi kesho ila sitakukumbusha”.
“Mambo mazuri hayahitaji haraka Ramsey… Ujue unanifanya niongee huku muda wote nimetabasamu… wewe mwanaume huishiwi maneno umenifanya nami kwa siku moja tu niwe na maneno kama wewe, utanifanya nisilale usiku wa leo kama ulivyonifanya nifanye kazi mchana wa leo huku nikiwaza ucheshi wako”.
“Hahahah.. Ha ha hah!Basi nikuache uendelee kuwaandalia wazazi chakula, kesho tutaonana”. Ilibidi amkatizie baada ya kuiona gari aliyoahidiwa ikiingia kwenye maegesho.
“Haya usiku mwema, lala salama na urelax kesho utajua nachotaka kukuuliza”
“Nawe pia ulale salama, wasalimie ndugu zako”. Akaongea Kai huku macho yake yakiwa kule maegesho ambapo dereva wa kizungu alishuka toka ndani ya gari ile na kuanza maongezi na mlinzi wa pale maegeshoni.
“Haya asante… Kuwa makini na watu wa jiji hili, natamani kesho iruke nionane na wewe tena”
“Usijali! Inshaallah tutaonana”. Akasema tena Shufania huku moyoni mwake akihisi kuna kitu fulani kimeongezeka toka amuone Kai. Shufania Mahamud Binti mhamiaji toka Syria alikuwa akiishi na wazazi wake eneo linaloitwa Pasar Seni Street, toka waamie katika jiji la Kuala Lumpur baada ya kuingia Malaysia wakitokea Syria mzazi wao Dokta Mahamud Zubeir alifanikiwa kupata nyumba hii ya kupanga iliyo mtaa huu wa Pasar Seni, walipanga nyumba nzima katika msururu wa nyumba hizi zilizo kwa stahili ya kota. Walikuwa wakiishi yeye Shufania, baba yao na mama yao na wadogo zake mapacha wa kike ambao wako chuo.
Familia yao ilikuwa imepungua maana walizaliwa watoto watano yaani yeye Shufania akiwa katanguliwa na kaka zake wawili na kisha hao wadogo zake mapacha. Kaka zake wawili wa kwanza wote wameshatangulia mbele za haki sababu waliuwawa wakati wanajaribu kutoroka nchini Syria katika mji wa Damascus baada tu ya vita kati ya serikali na kundi la kigaidi la Islamic State, wao walikuwa ni wafanyakazi katika ikulu ya Rais wa nchi yao mmoja akiwa fundi wa kompyuta na mwingine na mwingine mmoja wa walinzi wa karibu wa watoto wa Rais.
Kai alimalizia juisi ya embe aliyoletewa na muhudumu kwa haraka kisha akalipa na kuinuka moja kwa moja akaelekea yalipo maegesho.
“Habari yako kaka?”. Akamsalimu mlinzi wa pale maegeshoni aliyemuona akiongea na yule mtu aliyeleta gari baada ya kumfikia.
“Nzuri tu, za kwako?”. Mlinzi akajibu salamu na kuuliza yake.
“Alhamdulillah, niko sawa… Gari yangu ni hii, nilimuachia rafiki yangu akaifanyie service. Pia nikamuachia maagizo akuachie funguo atakapoileta”. Akamueleza huku anainyoshea kidole gari iliyoletwa muda si mrefu huku yeye akishuhudia toka alipokuwa amekaa.
“Unaitwa nani?”
“Naitwa Ramsey Bronze”.
“Ndiyo bwana mkubwa… Funguo hii hapa”. Mara alipojibiwa jina alikenua meno yake kuonyesha ameridhishwa na jibu kisha akainua funguo aliyoiweka juu ya stuli na kumpa Kai.
Kai akaipokea kisha akazama mfukoni na kutoka na noti moja ya dola mia akamnyoshea mkono wa kulia na kumpa huku naye akitabasamu kama anavyotabasamu mlinzi yule.
“ Kamata asante yangu ndugu yangu hii”
“Alhamdulillah… Ubarikiwe sana ndugu yangu wewe na kizazi chako…. Aisee kaka nakuona kama malaika uliyetumwa kunisaidia..! Jamaa alifurahi sana maana aliipokea ile pesa huku akiinamisha kichwa chini ishara ya kushukuru.
“Asante kwa kushukuru, Mungu atazidi kukubariki na wewe pia… Mi ni mpangaji wenu kwenye hii hotel, hivyo tutazidi kuonana mara kwa mara na hata nitakapohitaji msaada wako sitasita kukuomba unisaidie nawe pia usiogope kuniambia chochote utakachohisi ninaweza kukusaidia” Kai akasema huku akipeana naye mkono. Ilivyo Kai anapokuwa yupo sehemu za ugenini kikazi basi hujaribu kujenga ukaribu na watu wale walioingia kwake kinamna moja hama ingine. Akaagana naye na kuingia ndani ya gari akiwa na begi lake lililokuwa na laptop yake na vitu vingine muhimu zikiwemo na nguo zake mbili tatu, pia hii ni kawaida yake anapokuwa sehemu kikazi uwa haachi begi lake lenye vitu kama hivi maana yeye uwa hana makazi maalumu. Alitulia ndani ya gari akichunguza vitu alivyoomba awekewe akakuta kila kitu kipo, akawasha gari na kulitoa pale maegeshoni na kuondoka.
Mwisho wa sehemu ya kumi (10)
Hrakati ndiyo zinaanza kukokwa kwa kutumia kipepeo, msosi unaotakiwa kuliwa ndiyo ushaanza kuandaliwa na kuanza kukokwa kwa moto ni dalili za tumbo kupata linachostahili kwa chanzo hiki.
Mtaalamu wetu taratibu muda huu wa usiku akienda kuonana na Balozi wa nchi yao katika nchi ya Malaysia.
Nisimalize kwa kufafanua zaidi yale ambayo utaenda yasoma sehemu inayofuata…
TUKUTANE SEHEMU YA KUMI NA MOJA (11)
“Habari yako kaka?”. Akamsalimu mlinzi wa pale maegeshoni aliyemuona akiongea na yule mtu aliyeleta gari baada ya kumfikia.
“Nzuri tu, za kwako?”. Mlinzi akajibu salamu na kuuliza yake.
“Alhamdulillah, niko sawa… Gari yangu ni hii, nilimuachia rafiki yangu akaifanyie service. Pia nikamuachia maagizo akuachie funguo atakapoileta”. Akamueleza huku anainyoshea kidole gari iliyoletwa muda si mrefu huku yeye akishuhudia toka alipokuwa amekaa.
“Unaitwa nani?”
“Naitwa Ramsey Bronze”.
“Ndiyo bwana mkubwa… Funguo hii hapa”. Mara alipojibiwa jina alikenua meno yake kuonyesha ameridhishwa na jibu kisha akainua funguo aliyoiweka juu ya stuli na kumpa Kai.
Kai akaipokea kisha akazama mfukoni na kutoka na noti moja ya dola mia akamnyoshea mkono wa kulia na kumpa huku naye akitabasamu kama anavyotabasamu mlinzi yule.
“ Kamata asante yangu ndugu yangu hii”
“Alhamdulillah… Ubarikiwe sana ndugu yangu wewe na kizazi chako…. Aisee kaka nakuona kama malaika uliyetumwa kunisaidia..! Jamaa alifurahi sana maana aliipokea ile pesa huku akiinamisha kichwa chini ishara ya kushukuru.
“Asante kwa kushukuru, Mungu atazidi kukubariki na wewe pia… Mi ni mpangaji wenu kwenye hii hotel, hivyo tutazidi kuonana mara kwa mara na hata nitakapohitaji msaada wako sitasita kukuomba unisaidie nawe pia usiogope kuniambia chochote utakachohisi ninaweza kukusaidia” Kai akasema huku akipeana naye mkono. Ilivyo Kai anapokuwa yupo sehemu za ugenini kikazi basi hujaribu kujenga ukaribu na watu wale walioingia kwake kinamna moja hama ingine. Akaagana naye na kuingia ndani ya gari akiwa na begi lake lililokuwa na laptop yake na vitu vingine muhimu zikiwemo na nguo zake mbili tatu, pia hii ni kawaida yake anapokuwa sehemu kikazi uwa haachi begi lake lenye vitu kama hivi maana yeye uwa hana makazi maalumu. Alitulia ndani ya gari akichunguza vitu alivyoomba awekewe akakuta kila kitu kipo, akawasha gari na kulitoa pale maegeshoni na kuondoka.
ENDELEA...!!
MTAFUTANO PANDE MBILI IV
Saa nne na dakika tano usiku mgahawa unaoitwa Leboh Ampang Food & Drinks Restaurant ulionekana kuchangamka sana, maana jiji la Kuala Lumpur mida kama hii ndiyo uchangamka sana. Watu wanaoingia na kukaa kupata huduma na wanaoondoka baada ya kupata huduma idadi ilikuwa kama ni sawa.
Hali ile ilitosha kumtambulisha Kai huduma ya sehemu hii ilikuwa ni huduma bora.
Baada ya kutumia dakika mbili kuzunguka taratibu ndani ya mgahawa akitafuta sehemu ambayo atakaa akiwa yeye mwenyewe hili iwe rahisi atakavyofika Kapteni na wakafanya maongezi yao katika hali ya usalama zaidi.
Karibu na kona iliyo mwisho wa mgahawa ambako ni mbali na eneo la jiko (kitchen)aliikuta meza ikiwa imezungukwa na viti vitatu lakini kiti kimoja ndicho alikuwa kakaa mwanadada wa asili iliyoonyesha kama si mkorea basi ni mchina akila nyama iliyokuwa iko ndani ya sahani huku akisindikiza kwa kunywa kimiminika kilichojionyesha ni juisi.
Ilikuwa ni meza pekee iliyo na mtu aliyekaa peke yake hivyo Kai hakuona kama kuna jinsi ya kupata sehemu ingine zaidi ya kwenda kwenye meza ile na kumuomba mwanadada yule wakae wote pale akiamini muda mpaka atakaofika Kapteni pale basi huyu mwanadada atakuwa kamaliza nyama zile zisizoeleweka anazokula.
Kai alisogea pale akasimama kwa usoni mwa dada yule na kumfanya ainue uso wake kuangalia nani amesimama mbele yake, Agent Kai alifanya hivi sababu alikuwa anajua tabia za wachina na hata wakorea hivyo kwa kutumia ishara ndipo uwatambua, walipotizamana akainamisha kichwa chini kumsalimu kwa vitendo alivyojibiwa moja kwa moja akajua yule ni mchina hivyo akatabasamu na kumsalimu kwa kichina maana kichina kwa Kai sawa sawa na mimi mtoto wa uswahilini na Kiswahili.
“Habari yako?”
“Nzuri, za kwako?” Mwanadada akajibu huku akionyesha uchangamfu kama ilivyo kwa wachina wengi kuwa ni wachangamfu sana.
“Nzuri tu... Naweza kukaa hapa?”
“Haina shida, keti,keti na karibu sana tule”
Agent Kai akavuta kiti na kukaa upande wa ubavu wa aliokaa mwanadada yule wa kichina na baada ya kukaa ndipo akamuona yuko na simu mkono wa kushoto akichati huku wa kulia anakula na kwa ujuzi wa Kai na umri wake aliokaa China kipindi cha miaka kadhaa aligundua mwanadada yule anakula nyama ya nyoka, akatabasamu na kumfanya dada naye atabasamu na kumkonyeza.
“Mgeni Malaysia au?”. Akauliza dada na papo hapo muhudumu akawa kafika kumsikiliza Kai.
“Yah! Natokea Tanzania, Afrika”. Akamjibu huku akitabasamu.
“Naomba niletee supu ya ng’ombe, chapati tatu na maziwa safi yasiyo ya moto wala baridi”. Papo hapo Kai akaagiza kwa muhudumu kisha akamgeukia mchina mwanadada na wote wakatabasamu.
Kisha mchina akasema kwa kiingereza cha kama wachina wengine wanapoongea kiingereza.
“Kumbe unaongea kiingereza na kichina ulijifunzia wapi?”.
“Watanzania tunaongea kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha tu ingawa kuna wengine hawajui kiingereza… Kichina nimejifunzia china maana shule ya msingi nilisoma china baba yangu alikuwa anafanya kazi ubalozi wa Tanzania nchini china”
“Oooh! Kumbe ni ndugu yangu,ndiyo maana unaongea vizuri sana kichina watanzania ni ndugu zetu sote sisi ni wajamaa”
Alipojibu vile tu simu ya Kai ikaita na alipocheki jina lililotokea kwenye kioo moja kwa moja akamjua akapokea kwa bila kusubiri iendelee kuita zaidi lakini alimuomba samahani yule dada kwa ishara.
“Kapteni”. Akasema baada ya kupokea.
“Mwanangu, huko wapi?”.
“Leboh Ampang Food, lakini kuna watu utafikiri mji wote umeamia hapa… Nipo kwenye meza iliyo kwenye kona ya upande wa kushoto unapoingia ni mwisho kabisa”. Akajibu na kutoa maelekezo.
“Ok! Mi ndiyo natoka hapa kikao kilikuwa kirefu sana, nipe dakika kumi au kumi na tano maana si mbali na hapa na barabara ya kuja huko kutokea huku uwa haina foleni hasa muda wa huu wa usiku”
Alipomaliza tu kuongea Kai akakata simu.
“Kuna mgeni anakuja?”. Mchina akamuuliza.
“Si mgeni ni mwenyeji wangu”. Akamjibu na tayari muhudumu alikuwa kaleta alivyoagiza Agent Kai.
Waliendelea na maongezi ya kawaida katika kutaka kufahamiana zaidi na baada ya dakika kumi hivi mchina akamaliza nyama na kiminika chake akamuaga Kai na kuondoka.
Ni mzee wa makamo, umri wa miaka 62 lakini bado anaonekana ni mtu anayehitajika katika shughuli za nchi bado hajachoka.
Alikuwa ni mwanajeshi mstaafu wa jeshi la majini la Marekani (US Marine) aliyestaafu akiwa na cheo chake cha uKapteni, alikuwa na sifa kede kede zilizovuma na zinazovuma mpaka sasa akiwa anafahamika kwa jina la Kapteni Jones Lebrons.
Usiku huu alivalia kama wazee wengi wa nchi hii ya Malaysia wanavyopenda kuvaa hasa nyakati kama hizi za usiku. Kichwani alikuwa bagharashia, koti jeusi la suti ya mikono mirefu akiwa kalivaa juu ya kanzu ndefu iliyopita hadi ugoko wake chini kanzu ya rangi ya bluu na miguuni akivaa sandlozi nzuri inayovutia kuitazama kwa kweli mzee huyu wa kizungu mwenye umbo la kawaida na urefu unaorandana na wa Kai.
Kuonana na Kai kulimfanya alipuke kwa furaha akamsogelea kwa kasi kisha wote wakarukiana na kupeana hugh (kumbatio la salamu)matabasamu tele yenye kusindikizwa na vicheko vya chini kuzuia kicheko kikali kitakachowashangaza walio meza za jirani, hii ikiwa inadhihirisha ni jinsi gani wamefurahi kuonana.
“Miaka mingi sana Kapteni” Baada ya kupeana hugh Kai akasema huku wakigawana upande kuizunguka meza iliyo kati na wakaketi vitini.
“Hubadiliki kijana wangu, bado huko vile vile toka tulivyoonana miaka kumi iliyopita nikaja nikasikia umetoka US Navy Seals huko CIA… Yote ni kazi, ningesikitika kama ungeenda kuwa daktari au mwanasheria au ungejiunga kwenye siasa”. Akasema Kapteni Jones huku akikaa vizuri kitini.
“Mmmh! Kwa kweli hata wewe hujabadilika… Nilikuwa sijui huko wapi mpaka juzi nilipoambiwa natakiwa kuja huku kwa kazi maalumu ndiyo kuambiwa balozi wetu huku ni wewe Kapteni Jones Lebrons… Bado huko fiti sijaijua miaka yako lakini umebadilika kidogo sana toka mara ya mwisho nikuone tukiwa wote kwenye operesheni ya kuiokoa nyambizi yenu iliyotekwa kwenye bahari ya Medditerranian ikitoea Israel…. Nakumbuka baada ya kuiokoa na walioiteka kukimbia tuliongozana makomaando wanne ukiwemo wewe hadi nchini Ukraine tukawafagia watekaji wote… Operesheni ile ilikuwa tamu sana sitaisahau daima sababu iliniweka karibu na mama mtoto wangu wa kwanza mpaka nikamuoa”. Akaonyesha kukumbuka Kai na wote wakagongesha viganja vyao vikatoa mlio ‘pwaaah’
“Wee ni mtu wa hatari sana mwanangu…. Nilipendekeza uletwe huku siku ya kwanza baada ya kupotea kwa wanasayansi na dalili kuonyesha hawatapatikana kiwepesi wala kimazungumzo lakini CIA wakanijibu wewe ni mtu wa operesheni zilizoshindikana, ilinivunja moyo sana maana siku zote nilitamani kukuona tena mara zote toka tuimalize ile operesheni Ukraine nimekuwa nikiyakumbuka matukio mengi uliyokuwa ukiyafanya sisi tukidhani unaingia kwenye hatari lakini ukawa unajiondoa hatarini kwa stahili kama vile star wa Hollywood anatengeneza filamu ya action. Nakumbuka vile ulivyokuwa komando mwenye umri mdogo kuliko makomando wote wa US Navy Seals na ukawa unafanya na kuelekeza kwetu mambo ambayo yalikuwa muongozo ni kipaji kikubwa sana ulikuwa unatuonyesha ulikuwa gumzo kubwa kwetu”. Akakumbusha Kapteni Jones Lebrons.
“Hahahah! Tuliwakomesha na wakawa mfano kwa wengine… Maana lile lilikuwa fagio la chuma, tuliwafagia wote tena kwa siku mbili tu walikwisha kikosi chote… Saivi sidhani kama unaweza tena kashikashi kama zile… Nakumbuka ulinifunza mambo mengi sana kutokana na uzoefu wako kwenye maji makubwa ya bahari kubwa kama ya Mediterranian”
“Bado namudu mwanangu na hii kazi nitakusaidia bega kwa bega nitakuwa na sura ya bandia”
“Mmmh! Baba hapana… Wewe ni ndiyo kiongozi wa wamarekani waliopo hapa Malaysia… Nitajibu nini white house wakigundua uzembe wangu ndiyo umesababisha kukuingiza matatizoni…. Pia mzee kuna umenishangaza sikuoni ukiwa na walinzi. Unataka kuniambia huko ikulu ulienda bila walinzi?”.
“Nilienda nao kikaoni ila na hata hapa nimekuja nao wapo huko nje wananisubiri niliwaambia kuna mtu na mazungumzo naye lakini sitaki wawepo wakatii amri, sitaki wakujue mapema kuwa upo hapa wewe ni mtu maarufu kwa watu wa Marekani wanakujua kwa zile medali za ushindi ulizokuwa ukipewa ikulu kipindi kile komando wa US Navy Seals”.
“Ina maana uwaamini?”.
“Nawaamini sana lakini katika ofisi yangu ujio wako tunaujua watu tusiozidi watatu na ndiyo maana nilimwambia Chifu ni vizuri ukifika usifike ubalozini. Kuwapoteza detective Hansen Morris na Agent Caesar North kumenichanganya sana walikuwa watu muhimu lakini nikaja nikagundua kujakuja kwao pale ubalozini kulisababisha kwa namna moja hama ingine kujulikana haraka kwa adui zetu… Sasa angalia na taarifa niliyopewa mchana kuwa tumempoteza na Detective Marie na hata wewe umenusurika kwenye mdomo wa mamba, hizi ni habari mbaya sana inabidi tusimuamini mtu katika operesheni hii”
“Sikuchukia mi kuingia mikononi mwa adui mapema na ninashukuru sana niliwatoroka kabla sijafanywa chochote chenye madhara ingawa muda mwingine nafikiria pengine ningevuta subira nione inakuwaje mbele ingawa pia ni kamari kufanya hivyo ingawa pia ni mbinu ambayo uwa tunaitumia ikiwa tumejua udhaifu wa adui kwenye ulinzi pamoja na uzoefu wao wa kazi hizi”.
“Kwa upoteaji wa ndugu zako si nzuri hiyo mbinu ni vizuri ulivyojinasua kabla hata hayajakufika mengine”
“Hahahah! Kazi nitaanzia pale pale waliponianzishia… Moyo wangu huko baridi naamini hii kazi naenda kuwapa mshangao mwingine kati ya mishangao mingi niliyowai kuifanya… leo ni jumatano hadi jumapili wanasayansi na mateka wote wanaoshikiliwa watakuwa wanarudi Marekani”. Akasema Kai kama ilivyo ada yake kujiamini kupitiliza kuwa hashindwi kitu.
Maongezi yao yalikuwa yakiendelea huku wakinywa vinywaji vyao ambapo Kapteni yeye alikuwa akinywa soda haina sprite na Kai alikuwa akimalizia maziwa aliyoagiza kila anapopumzika kuongea kwa kumsikiliza Kapteni basi alikuwa akinywa kwa kadiri inavyoruhusu.
“Napenda sana unavyojiamini… Wewe ni mwamba ulioshondikana … Umechunguza begi nililotuma?” Akauliza Kapteni huku akitizama saa yake ya mkononi ambapo ilimuonyesha ilishatimu saa sita na dakika mbili usiku ikiwa siku ya alhamisi ndiyo imeanza.
“Nimechunguza… Asante sababu haujaacha kitu kila kitu kipo sawa… umecheza sana kuniwekea sura za bandia haina tatu na zote kila moja umeandaa hadi kitambulisho chake… Nimecheka mwenyewe nilipoiona sura ya bandia ya kichina maana wachina wenye mwili kama wangu adimu kabisa” Akasema na kumalizia kwa wote kucheka kwa nguvu kisha wakagonga mikono kwa furaha.
“Anza kwa kuzivaa zingine na ukihitaji nyingine nitakupa tu”
“Usiku huu nitarudi kule kwa wateja wetu nilipotoroka nataka niende kikazi zaidi ingawa najua leo watakuwa wamejiandaa kwa nilichochowafanyia jana mshangao wa mwaka…. Kesho usiku nitaomba tukutane tena sehemu ambayo tutaongea tena kama hivi na nitakuwa na lolote la kukwambia”
Maongezi yao muhimu yaliishia hapo wakaagana na Kapteni akaanza kuondoka kisha Kai akafuata.
Mwisho wa sehemu ya (11)….!
Tumeona katika sehemu hii jinsi MTAFUTANO ulivyoanza kwa Kai kukutana na balozi Marekani nchini Malaysia ambapo walielekezana mambo yanayohusu kazi na kukumbushana mambo mengi waliyowai kuyafanya kwa pamoja wakati Agent Kai akiwa hajawa Agent Kai aikwa ni komando wa US Navy Seals!
Nini kitafuata katika sehemu ya kumi na mbili ambako kazi ya MTAFUTANO inaendelea rasmi
Tuendelee kufuatilia kisa hiki cha nguvu chenye mikasa ya kimapigano ya kisasa toka kwa mtaalamu wetu komandoo Agent Kai Hamisi Mkarambati.
Maongezi yao yalikuwa yakiendelea huku wakinywa vinywaji vyao ambapo Kapteni yeye alikuwa akinywa soda haina sprite na Kai alikuwa akimalizia maziwa aliyoagiza kila anapopumzika kuongea kwa kumsikiliza Kapteni basi alikuwa akinywa kwa kadiri inavyoruhusu.
“Napenda sana unavyojiamini… Wewe ni mwamba ulioshondikana … Umechunguza begi nililotuma?” Akauliza Kapteni huku akitizama saa yake ya mkononi ambapo ilimuonyesha ilishatimu saa sita na dakika mbili usiku ikiwa siku ya alhamisi ndiyo imeanza.
“Nimechunguza… Asante sababu haujaacha kitu kila kitu kipo sawa… umecheza sana kuniwekea sura za bandia haina tatu na zote kila moja umeandaa hadi kitambulisho chake… Nimescheka mwenyewe nilipoiona sura ya bandia ya kichina maana wachina wenye mwili kama wangu adimu kabisa” Akasema na kumalizia kwa wote kucheka kwa nguvu kisha wakagonga mikono kwa furaha.
“Anza kwa kuzivaa zingine na ukihitaji nyingine nitakupa tu”
“Usiku huu nitarudi kule kwa wateja wetu nilipotoroka nataka niende kikazi zaidi ingawa najua leo watakuwa wamejiandaa kwa nilichochowafanyia jana mshangao wa mwaka…. Kesho usiku nitaomba tukutane tena sehemu ambayo tutaongea tena kama hivi na nitakuwa na lolote la kukwambia”
Maongezi yao muhimu yaliishia hapo wakaagana na Kapteni akaanza kuondoka kisha Kai akafuata.
ENDELEA NA UHONDO!
MTAFUTANO PANDE MBILI V
Saa sita na robo usiku juu ya alama ilimkuta fundi mtaalamu komandoo Agent Kai akiwa ndani ya gari Nissan Frontier aliyopewa na balozi Kapteni Jones Lebrons mwendo wa taratibu kama vile anahesabu nyumba za mtaa anaopita.
Ungekuwa umekutana naye muda huo usingeweza kumjua kama ni yeye alikuwa amejibadili muonekano kwa kuvaa sura ya bandia akionekana kama miongoni mwa wanaume wengi wa mji huu, nywele za kimalaysia na sura ya kimalaysia ni macho tu ndiyo ungeweza kuyatambua ni macho ya Agent Kai tena mpaka uwe unamjua haswa kama mama yake mzazi.
Alisogea mpaka kwenye kijumba kidogo chenye dirisha mbele kilichoonyesha ni kijumba cha mlinzi kilicho kama kastoo kadogo, eneo hili lenye mita nyingi za mraba ambao kwa kukadiria inaweza kuwa inafikia mita mia nane ulikuwa ni uwanja wa gofu wa Nadau na kile kijumba ndiyo kilikuwa cha mlinzi anayeulinda huu uwanja wakati wa usiku.
Agent Kai alipiga honi mara tatu hili kumstua mlinzi maana alikuwa kalala huku dirisha likiwa wazi tu kwa maana alikuwa limejengewa wavu, nondo au kitu kingine chochote sababu kulikuwa hakuna haja ya kujengewa hivyo hakuna kilichokuwa kinalindwa hapa zaidi ya mtu au watu walikuwa hawaruhusiwi kupita na ndiyo maana uwanja ulizungushiwa senyenge kote kwa kuuzunguka, pia palikuwa na jengo lingine ambalo lilikuwa limefungwa na hii ilimaanisha pale ni mahala pa kubadilishia nguo kwa wachezaji wa gofu na hata kuhifadhia vifaa vyao (dressing room).
Honi ile ilimstua mlinzi na akajitokeza kwa kuuinua uso wake mkononi akiwa na gobore (bunduki inayotengenezwa kikawaida sana) alipoiona gari imeelekezewa kwenye kijumba chake alijiinua.
“Samahani mkuu kwa kukusumbua… Unaweza kuzungumza kiingereza?” Kai akamuuliza kwa kiingereza akiwa kazima injini ya gari.
“Kwanini? Kwani wewe si mwenyeji wa hapa Malaysia?”. Akujibu swali bali aliuliza tena kwa kiingereza fasaha tu mpaka Kai akajilaumu kwanini alimuuliza swali baada ya kuanza tu kuongea naye (sura aliyoivaa ilimbadili sana) ila kwake uwa hakuna linaloshindika anapolikabili hivyo alitabasamu (genius ni genius tu)
“Ni jana tu ndiyo nimerudi nchi hii ya wazazi wangu, miaka yote toka nazaliwa mpaka nasoma hadi sasa nafanya kazi nilikuta tunaishi Uingereza, hivyo wazazi wangu hawakunifundisha kibahasa”. Haraka aliunda uongo unaoweza kukaa kwenye ubongo wa mtu mwingine yeyote.
“Nazungumza… Ongea shida yako mkuu!” Akajibu mlinzi yule huku akionyesha hajafurahi kumuona Kai eneo lile, ikabidi Agent Kai ashuke toka ndani ya gari na kumfuata wakawa wametenganishwa na dirisha mlinzi ndani na Kai nje.
“Samahani kwa kukusumbua na kukukatizia usingizi wako, pole sana na ninaomba usijali sababu nitailipia hii karaha, ila nina jambo ambalo bila msaada wako sitaweza kulijua jambo hilo”. Akaongea Kai huku akimchunguza mlinzi yule atakachomueleza kama itawezekana kumsikiliza.
“Jambo gani hilo?”
Agent Kai alimsaili sekunde tano kisha akaingiza mkono mfukoni katika mfuko wa kanzu fupi aliyovaa na kuibuka na wallet yake kisha akaifungua huku akiionyesha kwa ndani ilivyokuwa imenona kama kunguni wa bwenini aliyenenepa kwa kunyonya damu za wanafunzi wasiojali usafi wa kuoga na kufua mashuka yao mara kwa mara, akamnyoshea mkono na kumpa huku anatabasamu.
“Najua usingizi ni mali sana hivyo hii ni samahani yangu kwa usumbufu”.
“Asante sana ….. asante sana mkuu, Mungu akubariki… Ruhusa , uwanja ni wako sema tu nikusaidie nini?”. Alipokea pesa mlinzi kisha meno yalichanua baada ya kinywa kupanuka kama kiboko aliyeibuka majini na kuona adui, pesa fimbo hakuna kilicho kigumu mbele ya pesa hapa chini ya jua.
“Wewe ni mwenyeji mtaa huu?”. Kai akarudi kazini.
“Kwa kweli mi uwa nakuja tu nakaa kota damansamara ila si kama naweza shindwa kukusaidia juu ya habari za mtaa huu.. Sema tu shida yako?”. Akajibu mlinzi huku akiliegemeza gobore lake ukutani na papo hapo akahamia kuhifadhi ela alizopewa kwenye mfuko wa koti kubwa alilovaa.
“Kabla sijaja huku nilipewa maelekezo na mama yangu kuwa kuna mtu alimuachia biashara zake azisimamie, huyo mtu ni mdogo wake na mama yangu lakini ni ndugu yake binamu ni mtoto wa shangazi yake na mama…!”. Alianza Kai kupanga uongo kama vile ameuandika sehemu akimuangalia kwa makini mlinzi ambaye naye alikuwa makini kumsikiliza.
“Biashara mama aliyomuachia huyo ndugu yake ilikuwa ni siri baina yao haikuwa inajulikana na baba, hivyo miaka yote zaidi ya thelathini ambayo baba na mama wameamia uingereza na kuanza shughuli zao za kujiingizia kipato kwa baba kuajiriwa kwenye duka la kuuza spea za boti la rafiki yake na mama kuwa mama wa nyumbani, baba hakuwai kumpa mama ruhusa ya kurudi nchi hii… Nilipotaka kujua kuhusu huku nilikuwa nikikaa na mama ndiyo ananihadithia kila kitu kuhusu hii nchi ya asili kwetu… Mwaka huu nikaona nitembelee nchi hii, ndipo mama akanielekeza kwa baadhi ya ndugu zangu anaowakumbuka na katika maelekezo yake huyo ndugu yake wa kiume aliyemuachia biashara yake aisimamie aliniambia amemuacha mtaa huu na walikuwa na nyumba yao na ilikuwa nyumba ya kawaida kabisa kwa maelekezo lakini nimepita saivi nyumba ile iliyo kwenye maelekezo yake nimeona imekuwa ni ya ghorofa na imewekwa bango la matangazo kuwa ni sehemu ya mazoezi ya viungo”. Alitoa maelezo marefu Kai na kukatizia kidogo hili ampe nafasi anayemsikiliza naye kusema chochote baada ya kumuangalia na kugundua ana shauku ya kusema kitu.
“Una uhakika ni mtaa huu?”. Akauliza mlinzi.
“Sijakosea naamini hivyo…!”
“Nyumba unayosema kuna bango kuwa ni sehemu ya kufanya mazoezi ya viungo ni kule mbele au?” Akauliza mlinzi huku akionyesha upande wa kidole cha shahada cha mkono kulia inapoelekea barabara lilipo jengo la ghorofa ambalo Agent Kai alipotekwa aliletwa.
“Ndiyo limeandikwa YOUTH MUSCLE’S & BOXING TRAINING”. Akamjibu.
“Anaitwa nani mjomba wako?”.
“Medel… Medel James!”. Akajibu jina la kubuni papo hapo.
“Kwa miaka thelathini ni miaka mingi sana inavyoelekea mjomba wako aliuza nyumba kwa mtu mwingine naye ndiye akaivunja na kujenga nyumba ya ghorofa, sababu nipo nafanya ulinzi katika uwanja huu wa golf mwaka wa nane na toka niwe nafika huku nyumba ile machoni mwangu ni ya ghorofa vile vile na iliuzwa kwa wamiliki wa sasa ambao wameifanya kuwa vile ulivyoiona”.
“Okay! Unaweza kumkumbuka aliyeiuza nyumba ile kwa jina? hili anielekeze kwa dalali aliyefanya mpango wa nyumba kuuzwa sababu naamini dalali atakuwa anajua anwani ya mjomba wangu na nikaweza kumpata”.
“Namkumbuka anaitwa madam Groly na dalali aliyedalalia nyumba kuuzwa ni kampuni ya udalali ya Cook”
Wakati mlinzi anajibu swali aliloulizwa kwa namna hiyo kule mbele ambako kuna jengo wanalolijadili Kai na mlinzi ulitokea mwanga wa gari na ukiwa unakujia huku walipo wao, hapo Kai akaongeza umakini kuangalia itakuwa gari gani, ilikuja kwa mwendo wa kasi ya kawaida ya mtu anayewai kitu lakini si ya anayekimbizwa au kukimbiza kitu, ilipokaribia ndipo Kai akaona kwa nyuma pia kuna gari inaifuata ile gari ni kama wanaongozana sababu walikuwa wako kwenye spidi inayolandana.
“Hiyo gari ya nyuma unayoiona ni gari ambayo hutumiwa mara nyingi na vijana wanaofundisha mafunzo katika ile gym unayosema ipo kwenye ghorofa lililokuwa nyumba aliyeachwa mjomba wako”. Akasema mlinzi huku akiiangalia gari aina ya Noah nyeusi na kustua mawazo ya Kai ilikuwa ni Noah ile ile aliyoiona jana usiku ikishuka aliokuwa anawavizia usiku huu. Gari ya mbele ilikuwa ni aina ya Nadia.
“Katika gari hii ya mwisho uliyonionyesha nimeiona sura ya anayeendesha inafanana na sura ya mjomba, anaweza kuwa ni mwanae wamefanana… Ngoja nijaribu kuwafuatilia pengine nitawaona …. Asante sana kwa maelekezo yako na muda wako”. Akaongea kwa haraka Kai (akidanganya) bila kupoteza wakati akatoka kwa hatua za nusu mkimbiaji hadi hatua chache alipopaki gari akaingia na kuiwasha ikaitikia akatia gia na kuiondoa kwa mwendo kasi kinyumenyume na ilipokaa sawa kiuelekeo anapotaka kwenda akasimama na kubadili gia isongeshe kwa kasi akaanza kufukuza zilipoelekea zile gari, kulikuwa hamna magari barabarani lakini zile gari aliziona kwa mbali taa zake za nyuma hivyo alikanyga mafuta zisije zikampotea zitakapobadili bara bara na kuingia barabara ingine sababu huu mtaa wa Nadau golf ground club ulikuwa na barabara inayochepuka si barabara kuu.
Kwa kasi ile alifanikiwa kuwakuta akiwa nyuma yao mita thelethini wakiwa katika bara bara ya mwendo kasi ya Jalan Ampang Road hii bara bara kwa muda wa mchana uwa ni barabara yenye magari mengi, pikipiki na hata baiskeli lakini vyote hivyo uwa vinapita katika njia zilizopangiwa, Kai alichukua miwani yake ya kijasusi ambayo ni mikongoni mwa vifaa kazi alivyovikuta kwenye briefcase alilopewa na Kapteni Jones likiambatana na begi.
Alibonyeza kitufe kilicho pembeni kulia ya miwani aliyovaa akaivuta gari anayoifukuza kwa ukaribu zaidi na kuona vichwa vya watu kama vinne hii ni kutokana ile gari ilikuwa na vioo vya tinted na kwa umbali waliokuwa miwani ile haikuwa na uwezo wa kuingia ndani kabisa, alirudisha macho nje akaisoma namba ya gari na papo hapo akaziingiza kwenye simu yake na kuzisevu.
Msafara ulikuwa una gari moja tu ndiyo lililowaachanisha lakini uzuri barabara hii ilikuwa ni ya mwendo kasi hivyo kwa kasi ile ingekuwa si rahisi walio ndani ya Noah kuona kama wanafuatwa na Agent Kai, msafara ulipofika kituo cha traffic jam cha Jalan Ampang Road MRR2 gari iliyowaachanisha ikaingia barabara ya kuelekea Pahang north lakini wale wa kwenye Noah wakapandisha inayoelekea Kampung Ampang Campuran na kwa uzuri likatokea gari kubwa tu aina ya lori likaingia kule hapo Kai akapunguza mwendo na kulionyesha taa za ishara lipite lilipompita akawa analifuata nyuma na hii ilikuwa bara bara ambayo unaweza kwenda mwendo wa kawaida au wa kasi unayotaka wewe kwa kuchagua upande tu, msafara ulitembea kasi ileile hadi state road ukaingia Hulu Langat District na bado bahati ililala kwa Agent Kai kwani lori nalo liliingia inapoelekea Noah.
Walikwenda mwendo dakika ishirini na tano kwakuwa kulikuwa hamna magari barabara hii mwendo ulikuwa wa kasi sana mpaka Kai akawa anahofia lori linaweza sababisha akawapoteza watu wake lakini walipokipita chuo cha The Unniversity of Nottingham (Malaysia Camp) lori lilipunguza mwendo na kuonyesha ishara linaingia kulia hivyo kwa tahadhari ya kupoteza wateja wake akalipita katika kasi ileile dakika nne mbele jamaa wakaanza kupunguza mwendo ikiwa wanakaribia Broga Hill 1st Hilltop ikiwa imepunguza mwendo kabisa ikachepuka kuingia njia iliyokuwa ina barabara ndogo ya kupishana gari moja tu.
Hapo Kai akaona akiingia naye mtaa ule atakuwa panya kwenye ujasusi alipitiliza lakini naye akiwa kapunguza mwendo akawaona wakiwa wamesimama gari ikiwa imeonyesha ishara inataka kuingia kulia lakini imesimama ile ni ishara ya kuwa kuna kizuizi, hapo Agent Kai kwa uzoefu na mahesabu yaliyolala kichwani alipima umbali kwa macho tu kisha akaenda kidogo na kusimamisha gari kabisa akatizama saa yake ya mkononi ilimuonyesha ni saa nane kasoro dakika tatu hii ilimdhihirishia wametembea umbali mrefu toka walipotoka wilaya ya Persekutuan hadi wilaya ya Hulu Langat, zote hizi ni wilaya zinazounda jiji la Kuala Lumpur lakini Hulu Langat ni wilaya iliyo pembeni ya jiji.
Kwa haraka alipisha dakika moja kisha akapindua gari na kwenda bila kusita akiingia ule mtaa na hapo akaziona tu mwanga wa taa wa gari ukipotea kuingia sehemu na alipofika eneo lile akakuta geti likiwa linafungwa kwa kuvutwa kulia kwenda kushoto yeye macho yake yakiwa ndani ya miwani kwa kasi yalifanya usaili wa kutosheleza huku akiendesha gari kwa mwendo wa taratibu kabisa.
Aliendesha gari hadi juu kabisa ya mtaa ule ambapo alikuta nyumba iliyozungushiwa wigo na miti mikubwa mikubwa ikiwa imeizunguka nyumba ile iliyojengwa kwa ndani hapo Kai aliitizama nyumba ile kwa umakini sana na kuona ipo tulivu na wenyeji wake wanaonyesha wamelala na hakuna ulinzi wowote, hapo hakujiuliza aliichepua gari pembeni na kuichomeka katikati ya miti mikubwa miwili kisha akazima injini ya gari na uzuri ni kuwa Nissan Frontier ilikuwa haina kelele yoyote iliyo kubwa itembeapo hivyo aliamini hapo hajastua yeyote kati ya watu walio mtaa hususani wa nyumba hii iliyozungushiwa wigo aina ya mchongoma.
Akatoa bastola moja toka kwenye begi aina ya SCCY CPX-1 yenye uwezo wa kuingia magazini inayobeba risasi kumi lakini ikiwa na uwezo wa kuruka umbali wa mita thelathini alipo adui, kisha akatoa na ingine aina ya Berreta Nano zao la Italia yenye uwezo wa kubeba risasi sita kwenye magazine yake ila kwenye mruko inaruka umbali wa mita ishirini zote akazifunga vichuma vinavyofahamika kama viwambo vya kuzuia sauti akaziweka kwenye mifuko ya kanzu fupi aliyovaa (kanzu fupi yaani inakuwa kama shati haifiki chini inaishia katikati ya mapaja kwenda magotini) ila ina mikono mirefu kama kanzu nyingi zilivyo.
Alipomaliza kuhifadhi bastola zake akatoa gloves maalumu za kupandia ukuta kama aliouona unazunguka nyumba ile waliyoingia watu ambao aliuona ni mrefu sana kiasi ya kwamba ingempa tabu kupanda kwa kutegemea miti iliyo pembeni yake, gloves zinazojulikana kwa majasusi kwa jina la Magnetic Fingertrip Gloves nazo akazitia mfuko wa nyuma wa suruali aina ya kitambaa kama cha kanzu aliyovaa.
Hivyo vitu aliamini ni tosha kwake, akazungusha macho yake huku na huko kisha akaiweka miwani yake vizuri machoni taratibu akashuka toka ndani ya gari na kuipiga lock milango ya gari akapiga hatua mbili tatu kisha macho yakazunguka huku na huko kucheki usalama wake halafu akaanza kutembea akijiamini kama mpita njia yeyote mwenye kujiamini atembeapo ikiwa yeye ni mtu salama tu.
Alikwenda kwa mwendo uleule akijitahidi kujificha kwenye vivuli vya miti sababu mzoefu kama yeye uwa anajua jinsi ya kutembea sehemu kama hizi bila kuleta hali ya kutiliwa shaka hasa kwa mbwa ambao uwa hawakosekani maeneo kama haya katika nchi nyingi alizowai tembea kikazi au kistarehe.
Mlima wa bahati ulilala kwake mpaka anakaribia eneo la nyumba husika hakukutana na chochote, miwani yake kama nilivyokwisha tangulia sema awali ilikuwa ni miwani yenye uwezo wa tofauti na miwani ya kawaida ilikuwa ikiweza kuona mbali.
Macho huku na huko kila anavyosogea alipoona amefika unapoanza tu ukuta alipotea kwa kasi kama siyo yeye akazama eneo lenye giza lenye miti miti inayoambatana na ule ukuta macho tena yalizunguka haraka akaona ni salama hivyo alitoa gloves toka mfuko wa nyuma wa suruali kisha akazivaa katika kasi ileile na zilipokaa tu aliruka mruko ambao laiti ungekuwa upo karibu na umemuona mzee wa kazi huyu ungestaajabu mwili ule kuwa mwepesi katika kiasi kile , mruko ule ulimfikisha kwenye tawi la mti lilio juu futi kumi na mbili toka usawa wa ardhi napo alipofika hakuganda hata sekunde mbili yaani alikamata tu akaachia na kuruka hadi juu ya ukuta ambapo palikuwa na waya zimezungushwa kwa stahili ambayo yeye alishajua ni waya zenye shoti ya umeme unapozikamata bila gloves kama alizovaa yeye unarushwa na ikiwa una maji mwilini unanasa na kufa papo hapo.
Kai alizikamata nyaya zile kisha akajivuta na kuchuchumaa juu ya ukuta aliweza kuuona upande wote wa jengo lile na hakukuwa na mtu ila mbwa wawili walionekana na walihisi kitu kutokana walivyofika karibu na eneo alipo kwa chini ya ukuta huku wakionekna dhahiri kuna jambo wamelihisi ni la tofauti wanavuta harufu kwa pua zao kuziinua juu na masikio yamesimama.
Nyumba yenyewe iliyozungukwa na ukuta huu ilimchangaya Kai na akastaajabu sana ilikuwa nyumba ndogo ya kawaida isiyo ya kisasa tena ipo katikati ikiwa imepigwa rangi nyeupe juu na nyeusi chini, kichwani alikuwa amejenga imani ndani uwa huu wa ukuta atakuta kasri la maana kwani ukuta ulio na urefu kama huu na ukizungushiwa nyaya kwa kuu zikiwa na umeme mara nyingi uzunguka majumba makubwa ya kifahari (kasri), miti na bustani mbali mbali za maua ndiyo zilitawala eneo kubwa na ukuta ukionekana umezunguka mita nyingi kulizunguka eneo hili ambalo kama mmiliki au wamiliki wangetaka wangejenga nyumba kubwa tatu.
Agent Kai hakufikiri alichokuwa akifikiri baada ya kustaajabu na alichojiaminisha wakati anaona geti linafungwa pindi tu aliokuwa akiwafuata alipoona wameingia humu na mfungua geti kufunga, akatoa bastola haina ya SCCY CPX-1 kisha haraka akalichunguza tena eneo lile kwa macho kwa sekunde kumi na ushei hivi aliporudisha macho kwa mbwa wale ambao walikazana kutafuta walichohisi huku kila mmoja dhahiri akionyesha muda wowote uvumilivu utamshinda na kubweka, kitu ambacho Kai alikigundua alipowatizama tu papo hapo hakutaka hali itokee akafyatua risasi zinazofuatana zikiwalenga kichwani kila mmoja akadondoka chali ikiwa ni mmoja tu aliyetoa sauti ndogo sana.
Agent Kai kilichofuata hakuona sababu ya kuendelea kuganda juu pale akajifyatua na alipotua akatulia ncha za mbele za raba alizovaa (hii ni stahili nyepesi sana kwa maninja) alipotua tu moja kwa moja akajirusha na mikono yake yote miwili ikitangulia kwenda chini mgongo ukafuata akajiviringisha kama tairi mbingiriko wa kasi raundi tano ukamfikisha usawa wa ukuta wa nyumba ndogo aliyokuwa akiitizama wakati yupo juu ya ukuta.
Mwendo wa mnyato akasogea hadi kwenye dirisha lililopo upande ule wa nyuma akakuta dirisha ni la kioo lakini kwa kulitizama tu hakuona namna kama anaweza kulifungua kwa muda ambao utakuwa rafiki kwake na pia lisilete kelele kwa walio katika nyumba hii ambayo ilikuwa na eneo za mita za mraba thelethini kwa upande huu alipo Kai wakati ukuta unaozunguka nyumba ukizunguka kwa ukubwa wa mita za mraba themanini, kiwanja kikubwa sana kati ya viwanja vikubwa vinavyopimwa eneo hili la Broga 1st hilltop.
Safari ya Kai ilimpeleka hadi kwenye kona ya nyumba ambapo wakati anasogea alishaanza kusikia watu wakiongea kwa mbali akisimama kama mti akiwa kanyooka kabisa sambamba na upande wa kona aliyopo aliweza kuchungulia anaposikia watu wakiongea, ndipo alipoona toka pale alipo kuelekea kule walipo waongeaji kuna swimming pool toka mita chache aliposimama hii limtambulisha Kai nyumba hii zamani ilikuwa ni ya kisasa lakini ni ya miaka mingi na wanaoimiliki hawakutaka kuifanyia mabadiliko licha ya eneo kuruhusu.
Mwisho wa sehemu ya kumi na mbili (12)
Patamu hapa lakini kurasa zimegoma kunipa ruhusa ya kuendelea kuchapa..!
Agent Kai ndani ya minyapio aliyojikuta inampeleka mpaka eneo la Broga First Hilltop, adui zake bila kujua nyuma yao kuna mkia wa hatari kama mkia wa taya unawafuatilia.
Nini kinaenda kuwakuta watu hawa ambao bado hawajanusa harufu ya hatari iliyo mbele yao?
Twende nami katika sehemu inayofuata sehemu ya kumi na tatu (13) huko kuna mengi ya kuyajua katika riwaya yetu hii ndefu na tamu yenye mapigo matamu na ya kisasa.
Agent Kai hakufikiri alichokuwa akifikiri baada ya kustaajabu na alichojiaminisha wakati anaona geti linafungwa pindi tu aliokuwa akiwafuata alipoona wameingia humu na mfungua geti kufunga, akatoa bastola haina ya SCCY CPX-1 kisha haraka akalichunguza tena eneo lile kwa macho kwa sekunde kumi na ushei hivi aliporudisha macho kwa mbwa wale ambao walikazana kutafuta walichohisi huku kila mmoja dhahiri akionyesha muda wowote uvumilivu utamshinda na kubweka, kitu ambacho Kai alikigundua alipowatizama tu papo hapo hakutaka hali itokee akafyatua risasi zinazofuatana zikiwalenga kichwani kila mmoja akadondoka chali ikiwa ni mmoja tu aliyetoa sauti ndogo sana.
Agent Kai kilichofuata hakuona sababu ya kuendelea kuganda juu pale akajifyatua na alipotua akatulia ncha za mbele za raba alizovaa (hii ni stahili nyepesi sana kwa maninja) alipotua tu moja kwa moja akajirusha na mikono yake yote miwili ikitangulia kwenda chini mgongo ukafuata akajiviringisha kama tairi mbingiriko wa kasi raundi tano ukamfikisha usawa wa ukuta wa nyumba ndogo aliyokuwa akiitizama wakati yupo juu ya ukuta.
Mwendo wa mnyato akasogea hadi kwenye dirisha lililopo upande ule wa nyuma akakuta dirisha ni la kioo lakini kwa kulitizama tu hakuona namna kama anaweza kulifungua kwa muda ambao utakuwa rafiki kwake na pia lisilete kelele kwa walio katika nyumba hii ambayo ilikuwa na eneo za mita za mraba thelethini kwa upande huu alipo Kai wakati ukuta unaozunguka nyumba ukizunguka kwa ukubwa wa mita za mraba themanini, kiwanja kikubwa sana kati ya viwanja vikubwa vinavyopimwa eneo hili la Broga 1st hilltop.
Safari ya Kai ilimpeleka hadi kwenye kona ya nyumba ambapo wakati anasogea alishaanza kusikia watu wakiongea kwa mbali akisimama kama mti akiwa kanyooka kabisa sambamba na upande wa kona aliyopo aliweza kuchungulia anaposikia watu wakiongea, ndipo alipoona toka pale alipo kuelekea kule walipo waongeaji kuna swimming pool toka mita chache aliposimama hii limtambulisha Kai nyumba hii zamani ilikuwa ni ya kisasa lakini ni ya miaka mingi na wanaoimiliki hawakutaka kuifanyia mabadiliko licha ya eneo kuruhusu.
ENDELEA NA DODO..!
MTAFUTANO PANDE MBILI VI
Bwawa la kuogelea lililo hatua chache toka kona aliyosimama Kai lilikuwa na ukubwa wa kutosha kuogelea kistarehe na hadi mtu kuridhika ikiwa ni mpenzi wa kuogelea, baada ya kupita bwawa lile ndipo walipokuwa watu wale wakionekana na kitu wamezunguka kitu huku wanelekezana walikuwa takribani watu watano, wanaume wanne na mwanamke mmoja ambaye yeye alikaa kwenye gogo kubwa la mti lililokuwa pembeni ya mchanga ulioonekana kama umechimbwa akiwa na majonzi dhahiri usoni mwake licha ya kuwa alijifunga nguo stahili ya Panjabi ya kihindi.
Kai akabonyeza kitufe kilicho upande wa kulia wa miwani aliyovaa na kuwavuta karibu akianza na yule mwanamke alipomtizama mara moja akamkumbuka ni yule aliyempiga pigo la ngumi nyepesi lililomfanya azirai baada ya kumchinja bwana wake alipowakuta katika chumba kile, kitu walichokizunguka hakuweza kukiona ni kitu gani hivyo shauku ilimkumba asogee mbele kwenda karibu na eneo lile hili aone wamezunguka kitu gani na kwanini kuna kifusi kikubwa pembeni alipokaa yule mwanamke juu ya gogo la mti huku machozi yakiwa hayaishi kutiririka machoni mwake na kuporomokea mashavuni kama maji ya mvua yatiririkayo juu ya bati.
Alitokeza toka kwenye ile kona kisha akainama kama ana rukuu bastola zake zote mbili zilikuwa mkononi akaanza kwa kwenda sambamba na miti na maua makubwa yaliyo pembeni ya swimming pool kwa hatua ndefu lakini zisizotoa ukelele wowote ‘The Sole Cat’ alisogea bila kustukiwa hadi kwenye mti ulio mita tano tu toka walipo watu wale na hapo miwani aliyovaa ambayo uonyesha kwenye giza kwa mwanga wa rangi ya kijani aliweza kuwaona wote kwa uzuri.
Alikuwepo mtu mfupi mwenye nywele nyingi kichwani ambazo anaziacha zikimwagika pande zote kisha nyuma anazifunga kama mchicha (Mabrouk) usiku uliopita alikuwemo katika kikosi kilichomteka Agent Kai na kisha kushuhudia akiwafanyia kitu roho inachukia kukiona mubashara lakini kwenye movie utafurahia kukiona.
Pia alikuwepo Awan Razal a.k.a Fighter pia alikuwepo Krish ambaye alijeruhiwa bega lake kwa risasi katika usiku uliopita wakati Agent Kai akijitetea kwa kujibu shambulizi.
Walikuwa wanashusha maiti kwenye shimo wakiwa wameifunga kwenye sanda, ilikuwa ni maiti ya Nabeel ambapo ni agizo la boss wao Mr. Logan kuwa azikwe na wao tu bila kuwafahamisha ndugu zake, Nabeel alikuwa ndiyo kiongozi wa Six Dangerous Boys (SDB) kabla hajakutwa na mauti kwa kuchinjwa na Agent Kai na mpenzi wake kupigwa pigo jepesi lakini yule mwingine anayefahamika kwa jina la Jack ndugu yake na Jeong ambaye yeye Jack alivunjwa shingo na kufa yeye alizikwa jioni ya siku hiyo kwa heshima zote alizopewa na awa rafiki zake pia kaka yake Jeong na ndugu zake wote wakiwemo wazazi wake ambao pia ni wazazi wa Jeong ambaye sasa amepewa cheo cha kuongoza SDB Na boss wao Mr. Logan Puter.
Yeye Jeong hakuwepo hapa, mtu mwingine aliyekuwepo pale alikuwa ni mtu anayeiangalia hii nyumba na ndiye aliyewafungulia geti na kisha kulifunga huyu mtu yeye analipwa vizuri na Mr. Logan Puter kwa ajili ya kuilinda hii nyumba na vitu vinavyoletwa hapa na hata kushiriki zinapoletwa maiti ambazo mara nyingi watu wanahofia kwa siri kwenye mikono yake Logan au ya watu wake basi huletwa kuchomwa moto katika nyumba hii na ndiyo kisa cha nyumba kutojengwa toka alivyoinunua kwa mkorea aliyekuwa anarudi kwao korea kingine aliongeza kwa kupanda miti mingi na bustani mbalimbali zilizokuwa zikihudumiwa vyema na huyu anayeishi hapa, leo maiti hii ya Nabeel.
Ilikuwa lazima waizike kistaarabu sababu alikuwa ni muislamu pia si adui yao hivyo kuichoma maiti moto ilikuwa si heshima kwake marehemu Nabeel na hata kwao wao ingawa watu wengine wowote ambao walipewa amri ya kuleta maiti zao huku bila kujali dini gani alichomwa moto na majivu kuchimbiwa shimo kuzikwa.
Wakati akiendelea kuwaangalia huku akipanga awafanyaje mmoja wa vijana wale ambaye yeye hakuwa anamjua ni nani simu yake iliita kwa sauti ambayo hata yeye Agent Kai aliisikia vizuri tu alikuwa ni Awan Razal, alipoipokea haraka na akaanza kuongea akajibu salamu kwa lugha ya kiarabu na hata maongezi akayafanya kwa kiarabu, Kai alifurahi kusikia anaongea kiarabu ingawa ilibidi azidi kujibanza kwenye mti aliojificha nyuma yake maana jamaa aligeukia upande alipo na giza alikuwepo eneo lile sababu walikuwa na taa ya betri inayowasaidia katika shughuli yao.
“Ndiyo tumeanza shughuli….!”. Akaongea
Kikapita kimya akimsikiliza wa upande wa pili.
“Bado… Usiwe na wasiwasi, najua …. Nasema hivyo sababu nina uhakika”.
Akanyamaza na kupisha jamaa anayeongea naye aongee.
“Ni mkristo na ni wa hapahapa Malaysia hivyo ni ngumu sana kujua kiarabu…. Uhakika nilionao ndiyo maana sijasogea hata mbali na tulipo sababu kati yetu sisi SDB na muangalizi wa nyumba ya hapa ndiyo tunajua kiarabu lakini si yeye sababu hata Nabeel alikuwa akitaka kumteta kwetu alikuwa akitumia kiarabu”. Akajibu Awan huku akisogea tena hatua tatu mbele kuukaribia mti aliopo Kai kwa ukaribu kabisa na kumfanya Kai aiinue bastola yake iliyo mkono wake wa kushoto iwe tayari.
Kimya kikakatiza tena kama sekunde arobaini hivi.
“Sawa sawa boss… Jeong alituelekeza kufanya hivyo lakini tulitaka ashuhudie tunavyomzika kwanza mume wake maana toka mchana tulimdhibiti hakuwa na uhuru kabisa kitu ambacho si kawaida, uwa anatupikia na kufanya usafi katika nyumba ile lakini leo tulimuomba apumzike kabisa na tulishamfahamisha kwanini tunamzika Nabeel katika hali ya uficho na akatuelewa… Ila kwakuwa umetaka nimuue sasa hivi ukishakata simu tu basi usihofu baada ya dakika tano unazosema utapiga tena itakuwa tushatimiza matakwa yako boss!”. Akaongea na kugeuka kuwatizama wenzake ambao nao walikuwa wakimtizama kasoro yule mwanamke tu hakuwa akiangalia alipo Awan, yeye alikuwa kainamisha kichwa chini na mara kwa mara alikuwa akijifuta machoni kwa ushungi alioshika mkononi.
Aliposhusha simu chini ilimaanisha kwa Kai amemaliza maongezi ambayo genius komandoo Agent Kai aliyaelewa hasa mwishoni haraka akili yake ilimpa jibu yule mwanamke aliye pale yupo hatarini kufa dakika chache zijazo papo hapo akatamani kuyaokoa maisha yake sababu aliamini mwanamke yule hana makosa kabisa na jana usiku yeye alimuacha sababu aliamini hastahili adhabu ya kifo hivyo alimfanya azimie kwa kuwa hakuwa salama kwake kumuacha hai, ‘nimeelewa na ninahitajika niyaokoe maisha ya huyu mwanamke kwa mara ingine anahitaji huruma yangu’.Aliwaza Kai kisha akarudisha mwili wake alipokuwa kabla hajarudi nyuma jamaa aliyeongea na simu alivyosogea.
“Logan anataka tumalize kazi haraka bila kuchelewa”. Akaongea Awan kwa kiarabu tena na hapo tena Kai akajua kumbe awa jamaa wanapotaka kumficha maongezi wanaoongea huyu dada basi huongea kiarabu.
“Tumesikia ulivyokuwa ukimjibu… Haina haja ya maongezi mengi sisi sote watatu tuliokuja na shemeji huku hatuna ubaya na shemeji lakini amri ndiyo ishatoka… Tufanyaje hapo?”Akasema mtu mfupi (Mabrouk)
“Mi naona si lazima kuitekeleza kila amri ya kishenzi toka kwa Logan”. Akaongea Krish huku akimtizama mwanamke alipojiinamia akilia huku kakaa juu ya gogo hana hili wala lile anajionea kawaida na ukiunganisha majonzi ya kuona mume wake aliyefunga naye ndoa miezi miwili tu iliyopita leo tena usiku ulioenda amekuja kushuhudia akizikwa tena bila heshima ya kuagwa na watu wengi kama vile mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa ebola au kipindupindu, kiarabu hajui atafanyaje sasa.
“Sawa siyo kila amri ya kutekelezwa lakini mmeshafikilia maana zote mbili na kuziweka katika mzani ipi yenye uzito?”. Mabrouk mtu mfupi akasema na kuwatizama wenzake kwa zamu.
“Ni kweli kama asemavyo Mabrouk…. Huyu hajawai kuwakosea kama msemavyo lakini hana siri nyingi zinazowahusu na zinazotuhusu, hamuoni maana ya boss ilivyo nzuri?”. Kwa mara ya kwanza akachangia wazo anayeiangalia hii nyumba kama kuilinda ingawa naye ni mfuasi wa Logan kwenye kazi zake. Kai yeye alikuwa makini kusikiliza kila neno wanaloongea watu wale akiwa kafichwa na upana wa mti na vivuli vyake vilivyochanganyika na giza iliyokosa mbalamwezi sababu ya mawingu juu ya dalili za kutaka kunyesha kwa mvua.
“Ndiyo watoe vitambaa vyao machoni … Kama boss tunayemuona si boss ingawa anatulipa ameliona la kuhusu kumuua huyu mwanamke na auliwe tu lasivyo tujipe kazi ya kumlinda muda wote… Nani mwenye uwezo huo kati yetu?”. Mabrouk akasema na kisha kutema mate pembeni.
“Na nani asiye na huruma juu yake ampige risasi au amchome kisu au amuue vyovyote anavyoona kwake rahisi?”. Awan akaongea huku akionyesha mikono kama yeye hayumo kwenye dhahama hiyo.
“Mimi nitafanya hiyo kazi, sababu nyinyi mnamuona kama dada yenu kwakuwa mliishi naye huko lakini mimi nitamtwanga risasi bila kuuliza”. Mwenyeji akajipa dhamana ya kumuua yule mwanamke.
“Sawa… Lakini yeye tutaichoma moto maiti yake kisha wewe mwenyewe Samilang utayazika majivu yake kama ilivyo ada. Sasa kazi ni kwako”. Awan akasema huku akimkazia macho mwenyeji wao ambaye naye tayari bastola ilikuwa mkononi mwake akaanza kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti.
Wakati huo huo Agent Kai alipiga hesabu za haraka kati ya wote wale yupi amuache asimuue wakati huo hili afanye naye mahojiano akishawafagia wenzake na papo hapo akapata jibu.
Yule mwenyeji alipoinua mkono wake wa kulia kuelekeza tundu la bastola kichwani kwa mwanadada kwa minajili amuue kwa kumtwanga risasi ya kichwa sababu mwanadada bado alikuwa kainamisha kichwa chini habari, Agent Kai alijitokeza kwa kasi bastola mbili mkononi akawai kufyatua risasi moja ikatua kisogoni kwa aliyejitolea kumuua mwanadada ubongo ulifumuka damu zikaruka na kuwastua watu wote ambao macho yao yalikuwa kumuangalia anavyokwenda kuu kumbe anauwawa yeye.
Mshangao mkubwa ukawakumba ni mmoja tu aliyefanikiwa kugeuka upande alipo Kai kwani wawili nao risasi moja moja kwa mmoja ya vichwa vyao iliwarusha wakajikuta miili yao inaparamiana mmoja aliyegeuka risasi moja ilitua kwenye moyo na kuuchana moyo wote na wote kwa pamoja walikata roho, aliyebaki mzima kati ya wanaume wale alikuwa ni Krish mtu aliyejeruhiwa kwa risasi ya bega usiku uliopita alitaka kukimbia kisha akageuka upande alipo Kai na kwa uwoga akapiga magoti na mikono akanyoosha juu katika hali ya kutii sheria bila kushurutishwa mwili wake ulikuwa ukitetemeka sana na wala hakuweza kuongea chochote kile, wakati mwanadada na yeye baada ya kurukiwa na madamu yaliyochanganyika na ubongo ikiwemo mtu mfupi kumuangukia juu baada ya kurushwa kwa mpigo wa risasi iliyomfumua kisogoni, naye dada yule alishindwa kunyanyua mdomo haraka akakimbilia pale alipopiga magoti Krish naye akapiga magoti na kumkumbatia kwa nyuma.
“Mbona unatetemeka sana?”. Agent Kai akamuuliza Krish kwa lugha ya kiarabu huku anawasogela kwa ukaribu mikono yote ikiwa na bastola na kawaelekezea.
“Huwezi kujibu?”. Akamuuliza tena baada ya kuona anaangaliwa tu usoni.
“Unataka nikuwaishe kama wenzako?, usijifanye hujui lugha nayoongea… Unajua kwanini nimekuchagua wewe ubaki hai mpaka saivi?.... Unafikiri ziliisha risasi?” Alidhidi kumuuliza maswali yanayofuatana na kudhidi kumuweka katika hali ya uwoga mtu yule ambaye kuuwawa kwa wenzake kulimfanya achanganyikiwe sana na kutoamini kabisa kwamba aliokuwa akiongea nao na kupanga nao mipango dakika tano zilizopita wanavujwa damu kwenye matundu yaliyosababishwa na kupigwa kwao risasi na israel malaika mwenye sifa tuliyofundishwa na manabii na hata vitabu kuandika kuwa ni kutoa roho alashafanya kazi wamelala chini hawawezi kufanya lolote.
“Wewe…. Wewe ni …ni …ni nani?” Akajibu kwa lugha kiarabu tena akibabaika kuongea.
“Haikusaidii kitu kunijua mimi ni nani… na upo chini yangu saivi hivyo hutakiwi kuniuliza lolote kama mimi mwenyewe sijataka kuulizwa…. Nina mengi nahitaji kuyajua kutoka kwako na ukinijibu na nikaridhishwa na majibu nitakuacha huru”. Akamwambia.
“Sina mengi niyajuayo naomba usiniue ni bora ukanipeleka polisi”. Akaongea Krish akiwa yuko vilevile kapiga magoti mikono yote miwili ipo juu utafikiri aliambiwa apige magoti.
“Hauna kosa la kukupeleka polisi… Nijibu tu hata kidogo ulichonacho”
“Cha kwanza ningependa ujue ndani ya nyumba kuna watu wan…….!”. Aliishia hapo kwani maneno hayo ya uongo wake aliona kama yamefanikiwa baada ya Agent Kai kugeuza kichwa upande ilipo nyumba, Krish aliinuka pale alipo kwa kasi kisha akatupa teke kwa nguvu kuelekea kwenye mikono ya Kai iliyoshika bastola lakini bahati haikuwa kwake, teke lile lilipiga hewa jamaa akayumba sababu alikuwa kalirusha kwa nguvu zake zote hadi za ziada.
Agent Kai akamchota mtama mguu uliobaki alipodondoka ilikuwa hatua mbili toka alipo Agent Kai alimuongezea teke kisu (dochi) la mbavu akitumia mguu wa kulia mwili wa Krish ulirudi nyuma kwa pigo lile kwa kuburuzika na mbavu moja ya upande wa kushoto ikatoa mlio wa kama ubao uliovunjwa aliousikia mpigwaji tu, hapo uso ulikunjwa mikono ikaamia kujishika mbavuni huku kajikunja kama anasikia baridi, Agent Kai akasogea na kutaka kutandika teke lingine.
“Basi, basi…. Basi ni… ni…. Hahahaha umeniumiza mbavu zaaa nguuu…Naomba…… ni….samehe sitaleta tena ujanja….. mwingine”. Jamaa pigo la teke la mbavu lililomfanya ahisi kama anataka kukata fahamu kutokana na nyota nyota alizokuwa akiziona zilimfanya akubali kushindwa na kujutia jaribio lake la kutaka kujiokoa yalikuwa maumivu ambayo hakuwai kuyasikia hapo kabla licha ya kuwa alikuwa mfanya mazoezi mzuri na mpiganaji aliyewai kupigana mara nyingi na kupigwa maeneo kadha wa kadha lakini teke alilopigwa leo lilipigwa kifundi na mpigaji alijua wapi anapiga wakati anapiga.
“Mzembe sana wewe… Kwani ulifikiri ujanja wako sikuujua? Unafikiri mimi sawa na wengine uliowai kukutana nao na ukawadanganya?.. Mimi ni mtu mwingine tena nisiye na masikhara hata kidogo niwapo kazini…. Sasa naomba ujisachi mwilini mwako na utoe kila ulichonacho bila kuacha kitu na ufanye kwa haraka sina muda wa kuremba hapa”. Akasema Agent Kai huku akirudisha bastola moja mfukoni, Krish huku akitetemeka mwili na maumivu ya mbavu yake iliyoumizwa ilimchanganya sana, alianza kutoa vitu alivyonavyo mfukoni akatoa bastola moja, kisu kidogo cha mkunjo na funguo moja pamoja na wallet.
“Nina hivi tu mkuu…. Tafadhali naomba.. naomba nisa…nisai…nisaidie mbavu yangu imevunjika inaniuma sana”. Akasema alipoona amemaliza kutoa alivyoombwa kisha akavirusha pembeni hatua kama tano na alipo, wakati huohuo dada aliyekuwa amekuja nao hakuwa anaongea chochote akili yake ilikuwa kama haipo vile akiona vyote kama ni ndoto fulani mpaka akawa anafikicha macho yake.
“Huyu mwanamke anajua lugha gani ukiacha anayoongea”. Kai akamuuliza tena Krish ambaye aliamua kukaa kwa kuweka matako yake ardhini mikono yote miwili akiifumbata mbavuni.
“Uki… ukiacha…. kibahasa anajua… anajua… kidogo kiingereza tu”. Akajibu kwa tabu.
“Vipi hali yako?”. Agent Kai akamsalimu kwa kiingereza yule mwanamke aliyekuwa amepiga magoti bila kuambiwa apige magoti.
“Nzuri, nzuri kaka yangu”. Akajibu kwa haraka huku anahema muhemo wa kiuwoga.
“Ulijua wamekuja huku na wewe kufanyaje?”. Akamuuliza tena.
“Tulileta maiti ya mume wangu kuja kuizika, aliuliwa jana na mtu ambaye walimteka…. Mume wangu alichinjwa”. Akajibu na machozi yakaanza kumtoka machoni kiasi ya kwamba Agent Kai akamuonea huruma sana.
“Ulijua mume wako anafanya kazi gani kabla hajauliwa na huyo mtu?”
“Mume wangu alikuwa mwalimu wa michezo ya kimapigano na mtunisha misuli ndivyo nilivyojua”. Akajibu mwanadada mkono wake wa kulia akijfuta machozi na kuvuta makamasi juu puani kwake.
“Unaitwa nani?”. Agent Kai akamuuliza tena.
“Saky… Saky Mofsi!”.
“Saky hujui lugha ya kiarabu… Si ndiyo?”.
“Ndiyo najua kibahasa lugha yetu na kiingereza kidogo nacho nilijifunzia Hong Kong nilienda kufanya kazi za ndani huko”.
“Basi ndiyo maana awa jamaa walikuwa wanatumia kiarabu kuongea hili usisikie wanaongea nini”
“Ndiyo lugha yao kuu waongeapo kukiwa na watu wengine mi siielewi na nilikuwa nikitaka kuongea nao au wao wakitaka kuongea na mimi walitumia kibahasa”.
“Saky… Pole sana kwa kuifiwa na mume wako, uwa tunasema kazi ya Mungu haina makosa na mumeo hakuwa anapata pesa za kukutunzia wewe kupitia kazi ulizozijua, mumeo alikuwa na kazi ambayo imempelekea yeye kuuwawa kati hali aliyouwawa nayo kama awa wengine uliowaona nawaua leo… Mimi nipo kazini nipo katika kusaidia watu wema dhidi ya makundi mabaya kama haya alilokuwa marehemu mumeo… Huyu unayemuona anaugulia mbavu umeona vitu alivyotoa mfukoni?” Akaongea Kai huku akiwatizama kwa zamu Krish na Saky.
“Nimeona kaka yangu”.
“Kwanini anamiliki bastola?”
“Mara nyingi nilikuwa naziona kwao na hata kwa mume wangu… Nafahamu hawakuwa watu wazuri.. Hilo kaka yangu mimi silipingi… Naomba unisamehe kwa kunikuta hapa mimi niliongozana nao kuja kumzika mume wangu… Sijawai hata siku moja kufika kwenye nyumba hii… Wewe ni askari kaka yangu?”. Akaongea kama kawaida yake uongeaji wa maneno kwa haraka na kumuuliza Kai.
“Utanijua tu lakini si kwa haraka hivyo, kifupi mimi siyo askari… Jamaa hawa walikuleta huku hili wakuue kwa amri ya boss wao”.
“Eeeeh! Sikujua hilo… Kwa kweli sijui kama waliagizwa hivyo… Asante kwa kuniokoa kaka”.
“Inuka nenda kakae pale… Ngoja nimalizane na huyu jamaa”. Akamwambia na Saky akaamka kwenda alipoelekezwa akakae.
“Ndiyo ndugu yangu… Mwarabu mwenzangu naomba inua uso wako tuongee”. Akabadili lugha toka kiingereza kuja kiarabu.
“Pole sana na maumivu uliyonayo lakini ndiyo haki yako uliyoihitaji… Nataka kujua boss wenu nani?... Nakutahadharisha unapojibu swali nalokuuliza unijibu kwa umakini na uhakika… sina maskhara kabisa katika kazi… Nitakuua kwa kipigo kikali nitakachokupa nikiona unakwenda tofauti na ninavyotaka”. Akamwambia baada ya Krish kuinua uso kumtizama.
“Usiniangalie tu … Unanichelewesha, huu ni usiku mzito nahitaji kupumzika… Naomba nijibu”. Akamuongelesha kwa sauti ya ukali na kumfanya jamaa kutishika.
“Boss wetu simjui sababu mimi sikuwa mtu mkubwa katika kundi letu… Tuliyekuja kumzika ndiye alikuwa kiongozi wetu”. Akajibu na Kai alipomtizama vizuri akauona ukweli kwenye macho yake.
“Anaitwa nani jina lake?”.
“Hapo naomba … nisamehe …. Sababu simjui kama nilivyosema uliponiuliza ni nani nikakujibu kuwa simjui boss wetu ni nani ni hivyo tu simjui na nilimaanisha sina nilijualo kuhusu yeye”
“Nilikuonya mapema kuwa mimi uwa sidanganywi… Naona unajifanya chizi, nijibu swali langu kama ninavyotaka”.
“Ukweli ni huo”. Akajibu kifupi huku maumivu yakimfanya muda wote kukunja uso wake.
“Bwana Logan ni nani?”. Akamsindika swali la ghafla huku akimnyoshea tundu la bastola, Krish akastuka kusikia jina hilo kutamkwa mdomoni mwa Kai.
“Mbona umestuka na unaninyamazia… Ujue unanichelewesha… Nijibu Logan ni nani? Na ninakuonya risasi moja ikitoka hapa kama unavyoijua itazima kila kitu maishani mwako”.Akamuonya baada ya kumuona ananyamaza tu akiwa kakunja uso licha ya dalili kuonekana amestuka.
“Unamjua, unamjua Logan?”
“Hivi wewe ni chizi au unajifanyisha? Unawezaje kuniuliza swali wakati nilikwambia utaniuliza swali endapo nitahitaji kuulizwa… Sasa utanijibu kilazima”. Akamfokea na kumsogelea mpaka alipo kisha akainua mguu hili amkite kwenye mikono yake iliyojishika mbavuni.
“Nitasema mkuu, nitasema.. Tafadhali usinipige tena” Akapaza sauti.
“Haya haraka sana sema Logan ni nani?”
“Logan ni boss wetu lakini sisi hakuwai kutufanya tukamjua zaidi ya kuwa ni mfanyabiashara maarufu hapa Malaysia”.
“Kwanini jana mlimteka yule kijana mwenye asili ya afrika kwa kumtumia dada aliyejifanya anamjua kwa kuvaa sura ya bandia? Na yule dada ni nani?”
“Tulipewa taarifa na bwana Logan kupitia yule dada unayetaka kumjua ni nani kuwa kuna mtu anaitwa jina Agent Kai anakuja toka Marekani tunatakiwa kumpokea na kisha kumzuia mpaka yeye boss atakaporudi toka Korea alipokwenda”. Kitisho kilimfanya Krish aanze kufunguka ukweli.
Mwisho wa sehemu ya kumi na tatu (13)
‘The Sole Cat’ kazini no doubt, kazi inafanyika, minyapio ilifika hapa katika nyumba iliyozungushiwa ukuta mrefu sana kwenda juu lakini baada ya kufanikiwa kupanda juu ya ukuta huu kutumia uzoefu wa kazi, kama fundi nguo anapokata kata kitambaa mpaka mteja kuhisi anaharibiwa nguo zake kumbe ndiyo kazi yenyewe. Ndicho mtaalamu wetu alivyoweza kukwea ukuta kwa msaada fulani fulani na kukutana nyumba iliyomshangaza kwa ilivyo.
Fyeka fyeka bila huruma iliwakuta Six Dangerous Boys waliobakia na kujikuta rasmi kikundi kikifutwa duniani na mtu ambaye walimuanza wenyewe kwa sababu zilizo kuwa zipo katika wajibu wao.
Nini kinafuata katika sehemu inayofuata, vuta muda itakujia hapa hapa ulipokutana nayo mwanzo..!
“Boss wetu simjui sababu mimi sikuwa mtu mkubwa katika kundi letu… Tuliyekuja kumzika ndiye alikuwa kiongozi wetu”. Akajibu na Kai alipomtizama vizuri akauona ukweli kwenye macho yake.
“Anaitwa nani jina lake?”.
“Hapo naomba … nisamehe …. Sababu simjui kama nilivyosema uliponiuliza ni nani nikakujibu kuwa simjui boss wetu ni nani ni hivyo tu simjui na nilimaanisha sina nilijualo kuhusu yeye”
“Nilikuonya mapema kuwa mimi uwa sidanganywi… Naona unajifanya chizi, nijibu swali langu kama ninavyotaka”.
“Ukweli ni huo”. Akajibu kifupi huku maumivu yakimfanya muda wote kukunja uso wake.
“Bwana Logan ni nani?”. Akamsindika swali la ghafla huku akimnyoshea tundu la bastola, Krish akastuka kusikia jina hilo kutamkwa mdomoni mwa Kai.
“Mbona umestuka na unaninyamazia… Ujue unanichelewesha… Nijibu Logan ni nani? Na ninakuonya risasi moja ikitoka hapa kama unavyoijua itazima kila kitu maishani mwako”.Akamuonya baada ya kumuona ananyamaza tu akiwa kakunja uso licha ya dalili kuonekana amestuka.
“Unamjua, unamjua Logan?”
“Hivi wewe ni chizi au unajifanyisha? Unawezaje kuniuliza swali wakati nilikwambia utaniuliza swali endapo nitahitaji kuulizwa… Sasa utanijibu kilazima”. Akamfokea na kumsogelea mpaka alipo kisha akainua mguu hili amkite kwenye mikono yake iliyojishika mbavuni.
“Nitasema mkuu, nitasema.. Tafadhali usinipige tena” Akapaza sauti.
“Haya haraka sana sema Logan ni nani?”
“Logan ni boss wetu lakini sisi hakuwai kutufanya tukamjua zaidi ya kuwa ni mfanyabiashara maarufu hapa Malaysia”.
“Kwanini jana mlimteka yule kijana mwenye asili ya afrika kwa kumtumia dada aliyejifanya anamjua kwa kuvaa sura ya bandia? Na yule dada ni nani?”
“Tulipewa taarifa na bwana Logan kupitia yule dada unayetaka kumjua ni nani kuwa kuna mtu anaitwa jina Agent Kai anakuja toka Marekani tunatakiwa kumpokea na kisha kumzuia mpaka yeye boss atakaporudi toka Korea alipokwenda”. Kitisho kilimfanya Krish aanze kufunguka ukweli.
ENDELEA NA UHONDO…!
MTAFUTANO PANDE MBILI VII
“Yule dada anaitwa nani?”.
“Anaitwa Damia … Ndiyo mtu anayetuletea habari za boss anachokitaka”.
“Anaitwa Damia tu hana jina la baba?”.
“Damia Abdulrahman…!”.
“Anaishi wapi hapa Kuala Lumpur?”.
“Sijawai kumuuliza wapi anaishi na wala kufuatilia kuhusu hilo”.
“Unajua nini kuhusu wanasayansi wawili waliotekwa wakiwa na familia zao mwezi uliopita?”.
“Hilo analijua Damia, ukimpata yeye analo jibu la kukupa”. Akajibu na Kai akatizama saa aliyovaa iliyomuonyesha ni saa tisa kasoro dakika mbili tu usiku wa manane. ‘Nahitaji kupumzika’ Akawaza na papo hapo akapiga mwayo wa usingizi.
“Sawa nitamtafuta Damia Abdulrahman… Ila hapa nitaondoka na huyu dada, wewe sina mpango na wewe lakini sikuamini na ninaposema sikuamini kwakuwa umejiingiza katika michezo hii naamini utakuwa unajua kwanini nasema hivyo… Ningependa kukuacha huru je nakuachaje huru halafu ukanisababishia matatizo”. Akasema kwa urefu Agent Kai na kumfanya Krish kutoa macho kutoamini anachokisikia akatamani asogee kwenye miguu ya Kai kumshika kama watu wengi wan chi wanavyofanya wanapoomba msamaha lakini Agent Kai hakusubiri aishike miguu alifumba macho na kumkita kwa nguvu nyuma ya shingo kwakuwa alikuwa kainama kwenye miguu ya Kai, Krish mkito ule ulimfanya aage duniani papo hapo sababu alivunjwa maungio ya uti wa mgongo na shingo aliishia kutoa yowe hafifu.
“Saky tunatakiwa tuondoke hapa lakini kabla hatujaondoka natakiwa kuingia kwenye hii nyumba ndogo nichunguze kuna nini…. Je naweza kukuamini?”. Alibadili lugha kurudi kwenye kiingereza katika kuongea akimuongelesha Saky ambaye bado alikuwa akitetemeka.
“Niamini kaka yangu… Mi siwezi kufanya chochote sina lolote nijualo”.
“Kanisubiri pale… Mi naingia ndani..!”. Akasema Kai na kwa mwendo wa haraka alikwenda ulipo mlango wa kuingilia nyumba ile na uzuri aliukuta umeegeshwa tu akausukuma na kuzama ndani ambapo macho yalikutana na sebule ndogo iliyokuwa na masofa matatu na meza moja katikati iliyotengenezwa kwa miti ya mitete na kamba kushoto kulikuwa na dinning na upande wa kulia palikuwa na kompyuta ya desktop.
Kai akafuata kwenye mlango mwingine ulioonekana upande uleule wa kulia alipoufikia nao ulikuwa wazi akaingia na kukuta vitu ambavyo yeye hakuwa anavihitaji akapekua pekua kwa haraka haraka sehemu alizoona anahitajika kuziangalia napo hakuona linaloweza kumsaidia kwa chochote kile hakuendelea kupoteza muda alioona anaupoteza.
Wakati anatoka aliuona mtungi wa gesi mkubwa chini ya meza na kwa juu akaliona jiko la gesi lenye sehemu tatu za kupikia. Agent Kai akatabasamu na kusogea pale ambapo hakusubiri haraka akaliwasha sehemu zote tatu kisha akavuta pazia ililo dirishani akakata kipande kidogo na kukiweka katika hali ya mkusanyiko kisha akakiweka katikati kati ya sehemu zile tatu za jiko akachukua kamba moja akaifunga na pazia lenye pande tatu ambalo alilisambaza mpaka kwenye sofa kisha ya hapo akayapanga masofa yagusane na kutoka mule, dakika tatu mbele sebule hii itawaka moto mkubwa kisha nyumba yote itakuwa marehemu kama wakazi wake walivyo marehemu sasa’ Akawaza.
“Twende zetu…. Kuna dakika chache sana hapa patakuwa panawaka moto”. Agent Kai akamwambia huku analisukuma geti kuendea upande wa kulia kulifungua.
Wakatoka nje Kai akalirudisha tena geti, akamkamata mkono Saky akamuongoza kuelekea alipoliacha gari lake. Hatua za nusu wanakimbia zilimfanya Saky ahisi kama ni adhabu fulani.
“Pole binti naona umeumia nilivyokukimbiza lakini ni hali ya kawaida hii”. Akasema Agent Kai huku kwa kichwa akimuonyesha ishara azunguke upande wa pili wa gari kuingia maana walishalifikia.
“Ahsante kaka yangu, najua”. Akajibu Saky huku akielekea upande wa pili wa gari.
Agent Kai akawasha gari na kutia gia kuirudisha nyuma akapindua na kuiweka sawa akatia gia na kuiondoa kasi akirudi njia ya kuingilia mtaa ule ambayo waliingilia wakati wanaipita nyumba ile akatupia macho na kwa kweli juu kulianza kuonyesha moshi.
“Tayari kushalipa… Watu kama hawa ndugu zako hawatakiwi kubakiza kitu”. Akasema Agent Kai wakati anakata kona kuingia barabara ya lami kutoka vumbi ya mtaa wanaoondoka sasa.
“Nahitaji kukutafutia sehemu utakayo kaa kwa muda wa siku mbili tatu pengine mpaka wiki moja, sehemu utakayokuwa salama kutoka kwa watu wengine kati ya watu hawa ambao washakufa…. Hawa watu wanaonekana wana kundi kubwa lililo juu yao”. Akasema tena Agent Kai.
“Nitashukuru sana… lakini sijajua kwanini walitaka kuniua wakati mume wangu ameuliwa jana na mtu mwingine asiyehusiana na wao… Na samahani kaka naweza kujua ulifikaje pale na ulijuaje kama walitaka kuniua? Na wewe ni nani?”. Akaongea na kuuliza papo hapo Saky.
“Nilifika pale kwa kuongozana nao kutoka kule nadau, nilisikia pale pale wakipewa maagizo na bosi wao kuwa wakuue… Walifanikiwa kukuongelea kwa sababu hujui kiarabu… Kuhusu mimi ni nani tafadhali usiwe na haraka utanijua tu mi ni nani siku itakayoruhusu kujua hivyo”.
Baada ya ukimya wa dakika tano Agent Kai kwenye usukani wa Nissan Frontier akipangua gia, alitoa simu yake na kubonyeza namba za Balozi Kapteni Jones Lebrons. Simu iliita mara ya kwanza ikakata akarudia tena ikaita ikakata, Kai hakukata tamaa alijua ni usiku mnene watu wapo kitandani na usingizi kwa muda huo uwa unakolea haswa, akabonyeza tena hapo iliita kidogo tu ikapokelewa.
“Halloow!”. Upande wa pili sauti ya mtu aliyeamshwa toka usingizini ikasikika.
“Kapteni…. Pole na kukustua usingizini usiku mnene huu mzee wangu”.
“Haina haja ya pole mwanangu… Tuko kazini muda wote hata iwe tuko kitandani tunaumwa tunakuwa tupo kazini.. Lete habari mwanangu”.
“Mpaka sasa sijafanikiwa kulala hata kusinzia chembe kidogo… Nilikwenda kuzengea kule nilipokwambia nitakwenda kwa wateja wetu wa mbolea za korosho. Walipotoka nikawafuata ndiyo wakanileta hadi huku Hulu Langat District walileta kumzika yule mteja aliyepanda ngazi ya kuzimu jana, waliongozana na mwanamke mmoja kumbe naye waliamliwa kumuua uzuri nikawawi kabla hawajamuua ndiyo niko naye hapa narudi naye katikati ya jiji”.
“Ooooh! Safi sana, mafanikio yakoje?”.
“Asilimia tisini yapo sababu nimejua vingi tulivyokuwa hatuvijui kabla, kesho tukikutana tutaongea na kuelekezana vizuri… Nimepiga kwako usiku huu nina ombi ambalo linahitaji msaada wako… Huyu mwanamke naomba akakae pale ubalozini mpaka pale nitakaposema aondoke kwenda kuendelea na mambo yake, asisumbuliwe kwa lolote lile na sitahitaji mtu yeyote kuhojiana naye lolote kuwa yeye ni nani katoka wapi na nini na nini, sitataka hilo litokee kama kuongea nitaongea naye mimi tu”.
“Sawa napiga simu ubalozini wee mpitishe pale na watampokea getini”
“Nashukuru sana… Pumzika Kapteni, tutaonana baadaye”.
“Ahsante sana mwanangu… USA First!”.
“USA First!”.
Simu zilikatwa kwa pande zote mbili.
***** ***** *****
Mwanadada Damia a.k.a Language girl akiwa na Jeong a.k.a Mr Malaysia ndiyo waliokuwa wa kwanza kumpita Agent Kai wakiwa kwenye gari aina ya Nadia pale Agent Kai alipokuwa anaongea na mlinzi wa uwanja wa golf wa Nadau.
Wao walikwenda wakiongozana na wenzao waliokuwa kwenye gari ya nyuma aina ya Noah iliyowapakiza kina Awan wakiwa na shemeji yao Saky na walipofika muunganiko wa fly over (barabara ya juu chini) waliwaacha kina Awan wakiendelea na Jalan Tun Razak Road wao wakaingia Jalan Alor Road kisha wakaenda nayo hadi mtaa Berrangan city centre kisha Damia akaiongoza gari hadi Changkat Bukit Bintang Nightlife hii ni club maarufu sana katika jiji la Kuala Lumpur ikiwa eneo hili la katikati ya jiji hili likijulikana kama eneo la Bukit Bintang. Wakaingia kwenye maegesho ya club hii na kupaki gari.
“Mara nyingi uwa tunakutana na boss kwenye hii club, boss wetu ni mbinafsi sana hapendi sisi tupajue kwake wala kujulikana kama anapenda kukutana na sisi na ndiyo maana akija maeneo kama haya uwa anavaa sura ya bandia”. Akaongea Damia baada ya kuzima injini ya gari.
“Mmmh! Hamuoni anatugeuza wajinga kwake?”. Akauliza Jeong ambaye yeye ni mmoja wa watu wenye misimamo sana anapoona kitu hakiendi sawa uwa hafichi anaongea papo hapo kwa muhusika.
“Kivipi Jeong?”. Akamuuliza huku anamuangalia usoni.
“Kwanini na sisi asitutafutie sura za bandia tukawa tunazivaa na tukabaki wasafi kwenye macho ya watu kama yeye anavyopenda kubaki msafi? Ushawai jiuliza juu ya hilo? Au nyinyi hamjui kama tunafanya makosa katika hizi kazi tunazofanya?”. Akauliza Jeong huku anajifungua mkanda wa siti alichokalia.
“Jeong hujazuiliwa kuvaa sura ya bandia kama yeye anavyofanya lakini wewe huna unachokihitaji katika vile anavyovihitaji yeye… Mfano mdogo ni kwamba yeye ni mfanyabiashara na uwa anatoa misaada mingi sana kwa jamii, kama ulivyosikia hivi karibuni anataka kuinunua timu ya mpira wa miguu ya Johor Darul Takzim na pia anataka kugombea ubunge ifikapo mwakani”
“Basi tuyaache hayo… Ila tuwe makini na sisi pia watu, imeniuma sana kifo cha mdogo wangu”. Akaongea Jeong na kushuka toka ndani ya gari ikabidi Damia naye ashuke huku akijilazimisha
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment