Simulizi : Ukurasa Wa Gaidi
Sehemu Ya : Pili (2)
iliyojengeka katika mwili wake ule.Usoni
alionekana kama mtu aliye na umri wa miaka
mwishoni mwa arobaini au mwanzoni mwa miaka
hamsini.
Mara mtu huyu alipokanyaga ardhi,watu kadhaa
waliokuwepo mahali hapo wakiwa webeba bunduki
zao, walipiga goti moja chini na kukunja mkono wa
kulia mbele huku wakiinamisha ichwa chini usawa
wa mkono uliokunjwa kama ishara ya heshima
kubwa.Kwa kuwaangalia tu, ilionekana huyu
aliyekuwa mbele yao alikuwa mtu mkubwa na
mwenye kuheshimiwa sana na watu hawa.
Bwana yule akawataka watu wale
wasimame,akawakumbatia kila mmoja na
kuwabusu katika paji la uso huku akizungumza nao
kwa lugha ya kiarabu.Wakati huo huo helkopta
nyingine ikawasili eneo hilo.Hii ilikuwa na chapa
ya shirika la utangazaji la CNN. Bwana mkubwa
yule akaongozwa na watu wake hadi katika
helkopta ile na baada ya kupanda ikapaa na
kutokomea kutoka katika eneo hilo. Sekunde
chache baada ya helkopta ile kupaa, ile helkopta
iliyotumika kubeba gari, ililipuka na kuteketea
kabisa.
*********************************************
*****************************************************
"Breaking news".Ndivyo vioo vya luninga
vilivyosomeka siku hiyo.Vituo mbali mbali vya
televisheni vilikatisha matangazo ya kawaida na
kurusha habari hizi mpya zilizokuwa na msisimko
kuliko habari nyingine.Vituo vikubwa vya
televisheni na radio viliripoti moja kwa moja
kutoka eneo la tukio.Makamanda waliohusika
kuongoza msafara ule walihojiwa nao wakatoa
ushirikiano wa kutosha. Vyombo vya habari vya
kimataifa kama BBC,CNN,ALJAZEERA na Sky News
navyo viliripoti kupitia wawakilishi wake.Dunia
nzima ilipata habari hizi za kuogofya moja kwa
moja kwamba yule gaidi aliyeisumbua dunia kwa
uhusika wake katika matukio mbalimbali bwana
'Omar Al-Mahmood' ametoroka tena kutoka katika
ulinzi mkali sana.
Usiku ulipita,siku mpya ikaanza kwa mchaka
mchaka wa hali ya juu.Jua lilichomoza wakati
makachero wa polisi na wanausalama wa vitengo
na idara mbali mbali wakiwa wamemwagwa kila
kona ya nchi. Wanausalama walipewa maagizo ya
kuacha kazi nyingine zote zisizo na uhitaji wa
haraka na kipaumbele chao kiwe ni kesi hii
iliyokuwa mbele yao. Kesi ya kutoroshwa kwa
gaidi aliyesemwa kuwa ni hatari sana zaidi ya
magaidi waliowahi kutokea katika historia ya bara
la Africa.
Baadhi ya wananchi walisikika wakitoa sifa kwa
kituo cha habari cha CNN kwa kuwahi kuelekea
eneo la tukio kabla hata mapambano hayajapoa
vizuri. Watu wengine walienda mbali zaidi kwa
kusema kuwa vyombo vya habari vya Tanzania
vimelala sana.Wapelelezi waliomwagwa kila kona
ya nchi walisikia habari ya helkopta ya shirika la
habari la ' CNN' kuonekana ikielekea eneo la tukio
kabla hata watu hawajajua ni nini kinaendelea.Lak
ini haikuchukua muda kwa wapelelezi kujua kuwa
ilikuwa ni helkopta ya 'CNN feki'. Magazeti nayo
hayakuwa nyuma kiripoti habari hii.
Gazeti la 'MTANZANIA MZAWA' liliandika " Gaidi wa
kimataifa aliyekamatwa na vyombo vya usalama
vya marekani kwa kushirikiana na Tanzania
ametoroshwa kutoka chini ya ulinzi mkali
alipokuwa anasafirishwa mara baada ya kutokea
mapambano makali sana.Gaidi huyo alikamatwa
katika mpaka wa Tunduma mkoani Mbeya wakati
alipokuwa akitaka kutorokea nchini
Zambia.Mapambano haya yalitokea baada ya
msafara huo kuvamiwa na kundi kubwa la watu
wanaodaiwa kuwa ni magaidi kutoka nchini
Somalia. Aidha maswali ambalo watu wengi
wanajiuliza sasa ni kuwa inawezekana vipi kundi
kubwa la magaidi kuvuka mipaka yetu na kuingia
nchini kwetu bila vyombo vya usalama kung'amua?
Na ni vipi watu hawa wavushe silaha nyingi kiasi
kike bila vyombo vya usalama kuona?"
AGOST 7, 1998
Siku hii ni kati ya siku ambazo wanaafrika
mashariki hawataisahau. Ofisi za ubalozi wa
Marekani nchini Tanzania na ubalozi wa Marekani
nchini Kenya zililipuliwa na Magaidi.Wahusika
walikuwa ni magaidi wa kikundi cha Alquaeda.
Moja kati ya watu waliotekeleza kusuka mipango
ya kufanikisha tukio hilo ni Omar Al-Mahmood.
Waweza kujiuliza Omar Al-Mahmood ni nani
kiundani sana? Ni mmoja wa viongozi wa ngazi za
juu wa Al-shabaab.Anasifika sana kwa kuwa na
ushawishi,utashi na kuwa na misimamo mikali
sana. Wakati wa mkakati wa kutekeleza matukio ya
kigaidi katika balozi za marekani nchini Tanzania
na Kenya, kikundi cha alquaeda kilifanya
mazungumzo na kikundi rafiki cha al-
shabaab.Wakati huo kikundi cha Alshabaab
hakikuwa na umaarufu kama ilivyo sasa bali
kilikuw ndiyo kwanza kinachipua bado.Mawasiliano
haya yalikuwa yamefanyika kwa kuwa iliaminika
Somalia iko karibu na Kenya na Tanzania hivyo
wanafahamu vizuri nchi hizi kuliko alquaeda
ambao makao makuu yao yapo Afghanistan. Omar
Al Mahmood alifanikisha tukio hili kwa mipango
yake yenye utashi na utaalamu wa hali ya juu.
Siku hiyo (August 7, 1998) alfajiri,gari lililobeba
milipuko (mabomu) lilionekana nje ya ubalozi wa
Marekani barabara ya Laiboni mahali ambako
ubalozi huu ulikuwepo.Gari hilo lilikuwa likienda
kasi na kutaka kuingia ubalozini moja kwa moja.
Lakini lilizuiliwa na lori la maji lililokuwa
linamilikiwa na ubalozi huo.Baada ya muda kidogo,
gari hili lililipuka kwa kishindo na kujeruhi na kuua
watu kadhaa.
********:*************
C.T.I
Idara ya kupambana na ugaidi Tanzania iliundwa
mwaka 2002. Hii ilikuwa ni miaka minne imepita
tangu lilipotokea shambulio la ugaidi katika ubalozi
wa Marekani nchini.Mara tu baada ya tukio la
ugaidi kutokea, nchi ya Tanzania iliona ni vyema
kuanzishwa kwa idara hii huru. Hili lilishauriwa na
wakuu wa mambo ya usalama kwa kuzingatia
kuwa ,suala la kupambana na ugaida lilikuwa chini
ya idara ya usalama wa taifa (TISS) ambayo ndiyo
idara kubwa ya intelijensia nchini.Kwa kuwa
Tanzania ilikwishaonja joto la ugaidi wakati huo,
ilionekana ni vyema ikianzishwa idara maalum kwa
ajili ya kupambana na ugaidi pekee. Hapo ndipo
idara hii ilianzishwa ikiwa na mamlaka kamili ya
kupambana dhidi ya ugaidi au tishio lolote la
ugaidi kutoka ndani na nje ya nchi.
Idara ya C.T.I(Counter Terrorism Inteligence),il
iundwa na vitengo vikuu vinne. Wapelelezi
walioenda kufanya kazi kwa vitendo uwanja wa
mapambano ( field agent ), wataalamu wa
teknolojia ya kompyuta(information technology/
data analysis), wataalamu wa maabala na kikosi
cha askari maalum wenye weledi wa hali ya juu
kwa mapambano kinachoitwa E.C.S(Elite Combat
Squad).
OFISI ZA C.T.I DODOMA
Mkurugenzi wa idara hii nyeti bwana Eliakim
Makassy alikuwa ana harakati nyingi sana ofisini
mwake.Hii ilitokana na kazi ngumu ambayo ilikuwa
inaikabili idara hii iliyo chini yake.Tangia hapo jana
alipopata taarifa rasmi ya matukio yote
yaliyojitokeza likiwepo la kutoroka kwa gaidi hatari
zaidi Africa kwa kuratibu matukio mbalimbali ya
ugaidi, hakutulia kabisa. Mara ashike karatasi
hili,mara apige simu pale, mara acheze na
kompyuta iliyokuwapo mezani.Yaani ili mradi
alikuwa bize kuliko kawaida.
Kazi kubwa aliyokuwa anaifanya katika kompyuta
iliyokuwa mbele yake, ni kufuatilia kiumakini zaidi
majina mawili.Omar Al-Mahmood na Abdallah
Yusoof.Si kwamba ilikuwa ni mara ya kwanza
kuwafuatilia watu hawa.La hasha.Hata kuanzishwa
kwa idara hii ulitokana na tukio lililomuhusisha
Omar Al Mahmood.Baada ya kuanzishwa kwa idara
hii, kazi yao kubwa ya kwanza ilihusiana na
kukusanya data mbali mbali kumuhusu Omar.Na
hata wakati wakikusanya data mbalimbali
kumuhusu, ndipo jina La abdallah Yusoof
likajitokeza mara kadhaa ndani ya upelelezi
wao.Kujirudia kwa jina La Abdallah Yusoof katika
matukio yaliyofanywa kwa mipango ya Omar Al
Mahmood, kulisababisha waanze kufuatilia haba ri
zinazomuhusu Abdallah Yusoof. Upelelezi huu
ulipofika hatua kadhaa mbele, ulisababisha Yusoof
awekwe katika vipaumbele vyao kati ya watu
wanaotafutwa zaidi.
Eliakim Makassy alikuwa akichambua taarifa
mbalimbali muhimu kutoka katika taarifa nyingi
walizokuwa nazo ndani ya idara.Pengine inaweza
kushangaza.Kwamba mkurugenzi ni mtu mzito
sana.Kwa nini afanye kazi ya kuchambua taarifa
badala ya kumpa kazi hiyo mtaalamu wa
kuchambua data(data analyst)? Makassy alikuwa
mkurugenzi wa tofauti sana. Kwanza alipenda
kujishughulisha kwa kila jambo ambalo lilikuwa
ndani ya uwezo wake. Yaani wakati mwingine
kama mtu angeingia katika ofisi za idara hii,
pengine angeweza kukaa hata masaa mawili bila
kutambua kuwa mkurugenzi wa idara hii ni
nani.Alijichanganya na maajenti wengine na
kufanya nao kazi kila alipopata nafasi. Lakini mbali
na kupenda kujishughulisha tu,Makassy alikuwa ni
mtaalamu wa mambo ya kompyuta.Hivyo wakati
mwingine maajenti wanaohusiana na utaalamu wa
kompyuta wakiwa na majukumu mengi sana
aliwasaidia kazi hii kwa mikono yake.
"Ngrii ngrii". Simu ya mezani iliita.Makassy ni
kama alitegemea simu hii kuita kwa namna ali
yoipokea haraka kabla haijaita mara ya pili.
"Hallow. C.T.I hapa."
"Unahitajika Ikulu haraka kadri inavyowezekana."
Upande wa pili ukaongea
"Sawa . Niko njiani".Alijibu Makassy.Kisha alipanga
makabrasha mawili matatu na kompyuta mpakato
yake katika begi dogo la mkononi kisha
akatokaofisini kwake.Alielekea moja kwa moja
katika kiwanja kidogo kilichokuwa nje ya ofisi za
C.T.I.Hapo alipanda katika helkopta moja iliyokuwa
imepaki hapo, kisha akaipaisha kuelekea Dar es
salaam.
IKULU.Dar es salaam
Baada ya muda,Makassy alitua helkopta yake
sehemu maalum ndani ya viwanja vya ikulu.Mara
baada ya taratibu mbili tatu kukamilika, aliongozwa
na mtu mmoja anayehusika na usalama ikulu hadi
katika ofisi ya Rais George Katumba.Mara
alipoingia katika ofisi hii, alimkuta rais anaongea
katika simu ya mezani.Zaidi ya raisi pia alikuwepo
waziri mkuu wa Tanzania mheshimiwa Abdulahman
Mohamed, pamoja na waziri wa ulinzi
muheshimiwa Michael Josheph Magombe. Rais
akaonesha kwa ishara tu, kumtaka Makassy akae
kwenye moja ya sofa zilizokuwa katika ofisi
hiyo.Mara baada ya kumaliza kuongea na simu,rais
alisabahiana na Makassy kisha akatoka katika kiti
chake cha kiofisi, na kwenda kukaa katika sofa
nyingine iliyokuwa inamtazama kiupande upande
Makassy.
"Ndiyo bwana Makassy, nadhani utakuwa
umekwisha kuhisi jambo tunaloelekea
kuzungumza.Ama niseme nadhani ulikuwa
unasubiri kusikia kutoka kwangu ili uanze mara
moja kufanya jambo hili linaloihusu idara
yako."Alianza kuongea Rais kisha akaendelea"
Sasa ninaweka suala hili mikononi mwako kuanzia
sasa kazi ianze mara moja. Nimeongea na
Marekani ambao ndiyo walikuwa wanaendesha
oparesheni ya kumkamata Omar Al Mahmood
kabla hajakimbia na kukamatwa mpakani akitaka
kwenda Zambia kisha kutoroshwa tena. Wao
wamesema kuwa kwa kuwa haya ni mambo ya
ndani ya Afrika, yanausikiliza umoja wa nchi za
Afrika utakavyoamua. Nimezungumza na umoja wa
Afrika, tumefikia muafaka.Tumepewa miezi mitatu,
kama hakutakuwa hata na mafanikio kidogo, basi
itabidi tuwaachie Marekani wafanye kazi hii. Kwa
hiyo idara yako inatakiwa kuonesha mafanikio juu
ya kazi hii kabla miezi mitatu haijaisha. Serikali
itakuwa bega kwa bega nyuma yako na itakupa
kila msaada utakaohitaji katikakufanikisha
hili.Tambua Afrika yote, na nchi zote zilizo mstari
wa mbele kupambana na ugaidi ziko nyuma
yako."Alimaliza kuongea rais.
"Ahsante sana muheshimiwa kwa kuiamini idara hii
na kuikabidhi kazi kubwa hivi.Naahidi
hatutakuangusha. Ila ninaomba tu vyombo vingine
vyote vya usalama viendelee na majukumu yao ya
kawaida na waachane na kesi hii, hadi pale idara
hii itakapo hitaji msaada wao".Aliongea Makassy.
"Sawa hilo halina shaka".Aliongea rais.
"Sijui kama kuna la nyongeza"Alihoji rais huku
akiwaangalia waziri mkuu na waziri wa ulinzi.
"Nadhani uko sawa kabisa"Aliongea kwa kifupi
waziri mkuu.
"Hata mimi nadhani muheshimiwa umeongea vizuri
sana.Nadhani hii idara inastahili kabisa kufanya
kazi hii kwa kuwa inaongozwa na mtu makini
sana.Nadhani cha msingi tu kuendelea
kushikamana na kuwasiliana kila mahali ambapo
idara hii itafikia. Nadhani tutalifumbua fumbo hili
kwa ustadi wa hali ya juu." Aliongea pia waziri wa
ulinzi.Mmoja wa mawaziri waliosifika sana kwa
kuwa wazalendo.
Baada ya hapo waliongea kuhusu mipango mbali
mbali ambayo Makassy alikwishafikiria kuhusiana
na suala lililokuwa mbele yao.Baada ya hapo
waliagana, Makassy alirudi Dodoma kuanza
kutekeleza kazi ambayo idara ya C.T.I ilipewa.
HISPANIA
Visiwa ya Ibiza
Jua lisilo na miale mikali liliwaka huku upepo
mwanana wa bahari ukivuma taratibu bila
bugdha.Watu wengi walikuwepo katika eneo la
ufukwe wakipunga upepo ,wengine wakiwa na
wenzi wao na wengine na familia zao.Ilikuwa ni
kipindi cha mwisho wa wiki hivyo watu wengi
walifika pale kwa mapumziko ya wikiendi.
Japo wengine walifika kwa mapumzikobya wiki
endi tu, lakini kuna baadhi ya watu walikuwa katika
mapumziko ya likizo ya muda mrefu.Hasa wale
waliokuwa na pesa za kutosha na waliojua
kuzitumbua pesa hizo walikaa mahali hapa
hadibpake limizo zao zilipokwisha. Mmoja wa watu
hawa ni kijana Mmoja wa Kitanzania.Kwa
muonekano wake ,ni mrefu wa wastani mwenye
sura na haiba ya kuvutia, mwenye mwili wa
wastani uliojengeka kimazoezi. Kwa Jina anaitwa
Mick-Reuben Garino.
Wakati huu alikuwa amejilaza katika mchanga
akiwa na mrembo mmoja wa kihispania ambaye
amekuwa akimpa kampani kwa kipindi chote cha
likizo hii.Hadi sasa,Mick alikiwa ni kijana wa umri
wa miaka 28.
Ni mwezi wa pili sasa tangu Mick afike katika
visiwa hivi na amefanya anasa sana tu. Katika
wakati ambao anakuwa nje ya majukumu yake
halisi, Mick alikuwa ni mfanyabiashara wa madini.
Alikuwa na ofisi yake Dar es salaam Tanzania
ambako watu walienda kuuza na wengine walienda
kununua madini na vito aina mbalimbali, biashara
iliyomuingizia pesa nyingi na kumuweka katika
watu waliokuwa na pesa nyingi.
Lakini kitu ambacho wengi hawakukijua,katika
majukumu yake halisi Mick ni ajenti namba moja
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment