Simulizi : Zawadi Toka Ikulu (2)
Sehemu Ya : Nne (4)
********
Von kijana aliyekulia kwenye familia ya kitawala naweza kusema anajua kila kitu kuhusu utawala, amezaliwa na kulelewa mazingira ya kiutawala huku akiandaliwa kuwa mtawala. Wazo alilopewa na rafiki yake Domi linakuwa ni wazo jipya kuwahi kulisikia katika mapito yake anajua vizuri mapito na nyendo za wazazi wake katika utawala.
Nikweli ameshuhudia baba yake akiingia mikataba bubu na kuiuza serikali na rasilimali zake kwa mashirika na makampuni mbali mbali ya kigeni. Ameshutumiwa maranyingi kipindi baba yake akiwa waziri na hata kipindi alipokuwa waziri mkuu. Ameshuhudia baba yake akitumia mamlaka aliyonayo kujifaidisha kupitia miradi mbalimbali ya serikali si hayo tu kaka zake wako serikalini mmoja ni waziri na mwingine ni mkurugezi wa shirika moja la mfuko wa jamii.
Lakini pamoja na mapito haya yote baba yake hana historia yakuumiliki utajiri mkubwa kama aliotajiwa na Domi kuwa wanaweza kuumiliki tena kwa njia rahisi tu ni kufanya mabadilishano ya familia ya Jamae na Fedha hizo ambazo waliamini baba mkwe wa Jamae angezitoa bila wasiwasi.
Ilikuwa ni idea kubwa mno na nadhani ilikuwa ni biashara kubwa na nzito kuwahi kufanyika duniani kupitia ugaidi, ni biashara ambayo Von aliiona inaweza kumfaya akawatajiri mkubwa ndani ya dakika moja mara tu muamara utakapokamilika Von akiwa na chupa lake kubwa la mvinyo aghali mvinyo aupendao kila anapoketi ni JackDaniels alikuwa akitumbukiza mapande ya barafu huku akimimina kidogokidogo kwenye glass yake na kuimimina kooni huku kaikunja sura utafikiri anakunywa kaa la moto.
Mawazo ya kitajiri kama kijana aliyetabiri matokeo ya mpira na akiangalia matarajio ya pesa atakayoshinda ni milioni hamsini wakati yeye kaweka shilingi miatano kama mtaji, vijana hupanga bajeti mpaka yakununua nyumba na gari ilihali hata mechi alizotabiri hazijaanza kuchezwa.
Gao hakuwa mbali na ujinga huo, hapo anawaza kwenda kuishi marekani na akifika huko atatafuta nyumba ya kifahari ya kama bilioni miamoja za kitanzania ili aishi kifalme, gari ya kifahari na kuwekeza kwenye makampuni makubwa ya mafuta barani afrika hasa nchi za kiarabu na Naijeria.Biashara walio iwaza waliiona nyepesi na hawakuwa na presha kabisa maana waliamini mzee Manguli atakuwa tayari kutoa fedha hizo bila hata kuhoji ,ni ndoto za kijuha kwa mtu mwenye akili timamu lakini ilikuwa ni rahisi sana kwa vijana hawa kujiaminisha kuwa inawezekana.
********
Pasipo kumshirikisha mtu yeyeote sasa wanaanza maandalizi, timu iliyoandaliwa na Dominic kwaajili ya udhibiti wa mawasiliano ilikuwa imeweka kambi jiji Mwanza pembezoni kidogo mwa mji eneo la Nyamhongoro ambako kulikuwa na jumba moja la kifahari linalomilikiwa na Dominic. Walifunga mitambo yao ya kidigitali.
Ni vijana wawili wenye asili ya Asia ambao walitoka korea ya Kaskazini, wanaungana na kijana mmoja kutoka Islaeli na kulikuwa na msichana mmoja wa kirusi na timu inakamilika kwa kuwa na watu watatu hawa ni wadukuzi wakimataifa ambao hulipwa pesa nyingi kwa kucheza dili hatari kama hizi wanazokwenda kucheza muda huu “international hackers”.
Domi alikuwa pembeni akiangalia mitambo ikifungwa na ilikamiliaka baada ya siku mbili vijana walionekana kuchapa kazi kadri wawezavyo na hatimaye walikamilisha kazi yao ya kufunga mitambo na waliijaribu na kuhakikisha ilikuwa sawa.
Safari ya kujaribu mitambo inaanzia kwenye kampuni za simu vijana wanatumia dakika moja tu wanafanikiwa kuingia na kudukua nyaraka vile watakavyo. Pili wanahamia wizara ya ulinzi napo wanafanikiwa kudukua nyaraka bila kizuizi na tatu wanamthibitishia Dominic kuwa inawezekana kudukua popote kwani wanaingia mpaka mamlaka ya kudhibiti mawasiliano nchini hii ndio mamlaka inayohusika na ulinzi wa kimtandao nchini lakini vijana hawa wanatumia sekunde chache tu kuudhofisha mfumo wa ulinzi na kiusalama wa shirika hilo wananingia na kuvuruga nyaraka na kusimamisha huduma kwa muda. Hii ni kama salamu lakini ilikuwa ni salamu mbaya mno kwa taifa.
Siku iliyofuata kulikuwa na taarifa mbaya mno kwa taifa taarifa za udukuzi wa nyaraka za siri za serikali, magazeti, mitandao, redio na televisheni vililipoti. Na hii ikawa ni furaha kubwa na yenye mafanikio makubwa kati ya Dominic na Von Gao.
“ kaka nilikwambia vijana wangu ni hatari sasa unakubalina na mimi kuwa hata asipotulipa pesa yetu tunauwezo wakuingia benki kuu na kuchota nyaraka au kitita tutakacho?”
“Nimeiona kazi yako kaka sasa maisha yakifalme yamewadia wewe ni rafiki wakweli uliyechelewa kuja maishani mwangu”
“usijari kaka waache wajisahau kwanza baada ya hapo tunakuja na kubwa kuliko zote”
Wote walicheka kwa dharau huku wakijipongeza kwa madaha.
Ni udukuzi wa kihistoria kwa televisheni ya taifa wakati wakirusha matangazo ya moja kwa moja ya taarifa ya habari kulitokea matatizo ya kiufundi kidogo kisha zilingia picha ambazo hawakuzitarajia na hawakujua nani kaziingiza kwenye mitambo yao yakurushia matangazo. Ni picha za video zilizomuonesha Jamae Justine na familia yake namaanisha mkewe Jesca pamoja na mtoto wao Eric wakiwa wamefungwa kwenye jumba bovu mithili ya banda la mbwa huku Jamae akionekana kuwa katika hali mbaya zaidi kiafya kutokana na kipigo kilichoonekana dhahiri kupitia makovu na uvimbe usoni kwake pia shati lilitapakaa damu iliyogandiana. Mkewe naye akikuwa katika hali mbaya huku akimnyonyesha mwanaye kipenzi mwenye umri wa miezi minne ndani ya mahabusu hiyo iliyotumiwa na watekaji.
Vijana waliofunga nyuso zao huku wakiwa na siraha mikononi wanaonekana kwenye Television ya Taifa wakati huo wa taarifa ya habari ya saa mbili usiku wakiwa wamesimama na kuiweka kati familia hii huku wakiwa na siraha nzito. Juhudi za mafundi mitambo kuiondoa video ile ziligonga mwamba kwani pamoja na juhudi zote na ujuzi wao bado walishindwa kufanikisha kwani iliingizwa kwa mfumo usiojulikana. Sauti ilisikika kutoka kwa kiongozi wao sauti hiyo ambayo iliwekewa mawimbi ili kuupoteza uhalisia ilisikika ikisema.
“ndugu wananchi tunapenda kumjulisha rais wenu kuwa tunamshikilia binti yake Jesca pamoja na mumewe na kijukuu chake kwa takribani wiki mbili sasa. Tumeamua kutoa taarifa hii ili ajue walipo maana nasikia wanakamata watu ovyo, kama mnavyoona ndugu wanachi familia iko salama kabisa. Ombi letu ni kwamba hatutahitaji mahojiano na mtu juu ya hili ngoja tuliweke wazi tu familia hii itaendelea kuwa salama na hata kuachiwa huru ikiwa salama iwapo mam bo mawili yatatekelezwa ndani ya siku mbili zijazo. Swala la kwanza ni ndugu rais kutulipa fedha taslimu shilingi trioni nane ndani ya siku mbili zijazo, msiniulize zitatoka wapi ngoja tumuachie yeye mwenyewe maana hili nilakwake na linamhusu vyema. Swala la pili kama atashindwa kulitimiza swala la kwanza ndugu rais atalazimika kuachia madaraka ndani ya siku moja ijayo na sisi wenyewe tutamtangaza mrithi wake hapahapa. Kumbuka tunayoyasema yanamaana kubwa sana hivyo naomba mfikishie ndugu rais maana wao huwa wako bizebize tu, hivyo mwambieni asipuuze na akijaribu kufanya udanganyifu wowote ajue atayagharimu maisha ya familia ya binti yake kipenzi Jesca Manguli.”
Tarifa ile ilitoweka kwenye runinga na kuacha tafakuri kuu kila mtu akijaribu kutafakari ni namna gani waweze kuafanya ili kuepukana na adha hiyo. Mtangazaji wa televisheni ya taifa aliekuwa akisoma tarifa siku hiyo Geturude Nkoni aliomba radhi watazamaji kwa kaarifa ya kidukuzi iliyoingia kimakosa wakati wa kurusha matangazo ya taarifa ya habari mara baada ya matangazo kurejea katika hali yake. Lakini pamoja na kuomba radhi haikuwa na maana kwa watazamaji wa tarifa hiyo ambao walikuwa wameupata ujumbe halisi kuhusiana na familia ya binti wa mh. Rais kuendelea kuwa mateka wa kikundi cha magaidi wasiojulikana.
Kwenye mitandao ya kijamii vilianza kutendea vipande vya video vya magaidi ambao ni wadukuzi na wahusika wa utekaji wa familia ya Jesca Manguli pamoja na familia yake. Hiyo haikuwa habari tena ila mjadala uliegemea upande wa pili ambapo amri yakulipa shilingi trioni 8 huu ulikuwa ni mjadala wakukata na shoka huko mitandaoni majukwaa ya kijamii kama “Sema usikike”, “Longa nasi”, “Tuambie” na mengine mengi sasa yalipata mada za kujadili kwa siku hiyo. Naweza kusema hakuna mzalendo aliyelala siku hiyo kwani kila mtu aliguswa na tatizo hilo kwa namna yake na hasa chama cha mlengo wa kushoto kilichokuwa kikipingana na uongozi wa bwana Manguli sasa walilishupalia vilivyo swala hilo.
Viongozi mbalimbali waliungana na familia ya rais kukilaani kitendo kile cha magaidi kuwateka nyara familia nzima na hasa mtoto wa miezi minne Eric Justine. Watu wa haki za binadamu hawakuacha kulisemea walipaza sauti lakini wapo walioligeuza tukio hilo kuwa mtaji wakisiasa, waliwapongeza magaidi na kuhimiza raii ajihudhuru ili kunusuru maisha ya familia ya binti yake kipenzi. Mitandao ya kijamii ilijaa jumbe mbalimbali zanazohusishwa na tukio hilo hasa mtandao wa watu mashughuli wa twitter dunia nzima wanasiasa waliandika. Mabarozi wa mataifa mbalimbali na marais pia waliungana kumtia nguvu rais na familia yake ili wavuke salama katika kashikashi hizo walizokuwa wakikumbana nazo kila mtu aliandika ujumbe wa kulaani kitendo hicho na pia kuitia nguvu familia ya kiongozi huyo mashughuli kwa lugha yake na kuonesha mshikamano uliobora zaidi.
Kila gazeti limebeba kichwa cha habari nzito iliyolitikisa taifa, ni kutekwa kwa familia ya binti wa rais habari zimetapakaa kila kona ya dunia, mitandao ya kijamii, redio na televisheni zote zilizungumza lugha moja. Naweza kusema lilikuwa ni tukio la kwanza kwa nchi hii maarufu kwa kuwa na amani duniani kote lakini leo kwa mara yakwanza taifa linakutana na kitendo cha aibu na kustajabisha huku raia wake wakilia na kujuta kwanini imekuwa hivi kwa kiongozi wao mpendwa waliye muamini sasa taifa linachukua sura mpya na kuwa kambi ya mateka.
Majira ya saa nne asubuhi waziri wa ulinzi alikuwa katikati ya waandishi wa habari na kila mwandishi alisubiri kwa hamu kujua ni nini kinaendelea ndani ya familia ya rais na bila kuchelewa alianza kuzungumza na wandishi
“ndugu wandishi wa habari nimewaiteni hapa kwa jambo moja tu, nalo ni kutaka kuwajuza ni nini kinachoendelea kuhusiana na tukio lililotokea wiki mbili zilizopita ni tukio la kutekwa kwa familia ya kiongozi wa taifa hili namaanisha Mh. Rais” pamoja na utekaji huo wakati tukifanya juhudi na maarifa kuweza kuokoa familia hii ya binti wa rais, jana tukio hili lilikuja na sura mpya, sura ya kustajabisha na kuhudhunisha zaidi. Magaidi waliojitambulisha kuwa ndio wahusika wa utekaji huo walidukua kipindi cha taarifa ya habari ya televisheni ya taifa na wakafanikiwa kurusha taarifa yao waliyoikusudia na ikafanikiwa kwa asilimia miamoja kutokana na tekenolojia yao kuwa kubwa mamlaka ya mawasiliano ilishindwa kulidhibiti hilo. Tukumbuke matukio ya udukuzi yametuandama kwa wiki mbili sasa na naona yanazidi kushika kasi ni wadukuzi wale wale ambao katika maandishi yao husomeka kwa lugha kikorea, hivyo hatuna shaka ndio waliodukua kwenye mamlaka ya mawasiliano, na sina shaka pia kusema ni walewale waliodukua tarifa kutoka kwenye wizara yangu na sasa wamehamia kwenye vyombo vya habari.
Ni habari ya kuhuzunisha kwani wamempa rais wetu mpendwa siku moja yakujihudhuru na kama hiyo siku ikipita basi ajiandae kuwalipa fedha taslimu shilingi trioni nane. Ni pesa nyingi sana nadhani hizi ni pesa za kwanza kuwahi kuombwa na magaidi tangu nizaliwe na kuiona dunia si hapa tu bali ni duniani kote” alisema waziri huyu aliyekuwa amevalia mavazi ya kijeshi, alitoa miwani yake na kufuta macho yake kisha akaendelea tena.
“hatuwezi kuwapata tukiwapigia simu maana hatuna mawasiliano nao wanatumia code hizi ni lugha za kompyuta ila wanaweza kutupiga na tukazungumza kwani wanatumia namba za siri katika kuwasiliana, tumefanya juhudi zote ili angalau kupata uelekeo walipo lakini kwa kutumia udukuzi wameeshaharibu mfumo wetu wote wa mawasiliano unaoendeshwa na mamlaka ya mawasiliano nchini. Labda niwaombe ladhi wanachi kwa yaliyotokea na pia nihimize kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu, Jesca na familia yake watarejea wakiwa salama salmini na ninaamini sisi ni chombo cha ulinzi na usalama hivyo niwahakikishie hii ni oparesheni na ni hatari sana kwa taifa ila ninaamini tutaikamilisha salama” alimaliza kuzungumza, wakati waandishi wakijiandaa na maswali waziri alikuwa amekwisha nyanyuka na kuelekea kwenye gari lake na msafara wake ukatoweka eneo husika. Masaa yalizidi kuyoyoma ndani ya chumba cha habari ni kijana Young Yi kutoka korea ya kasikazini akishirikiana na jopo lake waliendeleza udukuzi huku wakichukua nyaraka za taarifa mbali mbali za siri ndani ya serikali ya rais Manguli ili ziwasaidie wao na jopo lao katika kukamilisha dhamira yao.
Muda unazidi kuyoyoma nyumbani kwa rais Ikulu shughuli zilikuwa zimesimama ilikuwa ikitafutwa njia ya amani kulimaliza tatizo hili lakini ilishindikana kwani magaidi hawakuwa tayari kukaa meza moja na serikali, kila walipojaribu kuingia katika mazungumzo upande wa magaidi walikatisha mazungumzo kwa madai walihitaji fedha hizo na si vinginevyo. Mzee Manguli na mkewe walikuwa wameketi sebuleni kila mmoja alikuwa akiwaza alichokijua yeye juu na hatima ya maisha ya binti yao. Vituo vikubwa vya televisheni vya kimataifa vinalivalia njuga swala hili na sasa kilikuwa ni kituo cha habari cha Aljazera, BBC, ABC, CNN, VOA na vingine kedekede vituo hivi vilirusha matangazo yake kwa lugha ya kiingereza vilikuwa vimelivalia njuaga swala la kupotea kwa mwana wa rais na familia yake. Na kuifanya kuwa habari iliyoshika namba moja kwa kufatiliwa duniani kote.
Ilipotimu saa saba mchana nchi ilikubwa na mshituko tena mara hii vyombo vyote vya habari vilizungumza lugha moja na kipindi kikawa kimoja. Ni tarifa ya magaidi ilivuja vipindi vyote na kurusha kipindi chao ni mfumo ule ule uliotumika jana usiku kwenye tarifa ya habari televisheni ya taifa lakini leo unatumika kwenye televisheni zote na redio zote nchini wamefanikiwa kuingia na kuvunja vipindi vyote wakarusha kipindi chao. Ni jambo la hatari ambalo hakuna aliyelitarajia na linaweza kuwa ni jambo lakwanza kuwahi kutokea duniani. Marahii tarifa hii ilijikita zaidi katika kukumbusha ukamilishwaji wa maombi yao hawakuacha kukumbusha ndugu rais ikifika saambili usiku ni lazima Rais ajihudhuru la sivyo atapaswa kulipa fedha walizoomba ili kuokoa maisha ya wapendwa wake.
Ikulu haikuwa sehemu salama kabisa kwa bwana Manguli kuishi maana hali ilibadilika kila mara na hasa ilipofika saa moja na nusu usiku, jopo la washauri walikuwa wamejazana ndani ya ukumbi mdogo wa mikutano pale ikulu, wandishi wa habari za ikulu ndio walioruhusiwa tu kuingia katika mkutano huo pasipo mwandishi mwingine wa chombo cha nje. Ulipaswa kufanyika mkutano wa dharura kwa dakika chache zilizosalia ili kuamua nini hatima ya rais Manguli ndani ya Ikulu. Majaji wastafu, viongozi wa dini, mawaziri akiwemo waziri mkuu wa zamani Mzee Gao, marais wastaafu na watu wengine mashuhuri walihudhuria.
Kilichojadiliwa kilikuwa ni siri lakini hatima ya kikao hicho ilikuwa ni kuamua rais atabaki madarakani au la!, na kama atabaki madarakani wafanyaje juu ya kuwalipa hawa magaidi? Waliokuwa wakidai pesa nyingi mno. Ndani kulikuwa kwa moto mwanzo kuna walioongea kwa jaziba lakini mwisho wa siku busara ilitawala zaidi kuliko nguvu katika mazungumzo yao maana walizungumzia roho za watu namaanisha ni maisha ya raia wa taifa hili Jesca na mumewe pamoja na mtoto wao bado wanayo nafasi yakuishi katika taifa lao na waliotakiwa kuliamua hili ni hao wazee waliokaa kwa muda mfupi. Lakini kwa upande mwingine walizungumzia fedha za wananchi namaanisha trioni nane za walipakodi wakipewa hao magaidi haitakuwa busara. Nini kifanyike mimi na wewe hatujui lakini ikifika saa mbili kamili inabidi wawe na jibu kamili litakalookoa pande zote mbili, waokoe maisha ya raia hawa na pia waokoe fedha za walipa kodi. Muda uliongojewa kwa hamu na sasa uliwadia ni saambili kamili usiku rais alikuwa mbele ya vyombo ya habari akilihutubia taifa.
“Ndugu wananchi nimeamua kuchukua maamzi magumu kwa mstakabari wa taifa letu”
Je, ni maamzi gani atakayoyachukua mzee huyu tukutane toleo lijalo.
Hotuba iliendelea “nimeamua kuzungumza nanyi ndugu zangu wananchi wa taifa hili kutokana na kimya kirefu tangu tumeandamwa na matatizo haya kama taifa. Ni Matatizo yanayolikumba taifa na pia kuihusisha familia yangu… kila mtu ameona na mmesikia kinachoendelea kwenye familia ya binti yangu Jesca ni wazi kabisa kuwa watu hawa wamejipanga vyema kuja kupambana na wanahakikisha wanashinda. Si kitu kidogo walichokifanya hivyo ni watu makini na wanaijua vizuri familia yangu naamini hawajakurupuka.
Naomba nitoe rai mapema kuwa sitajihudhuru… ninarudia tena stajihudhuru kama wanavyotaka ila niwaombe tu wakubali kukaa kwenye meza ya mazungumzo hakuna kitakachoshindikana. Hawa watekaji ni raia wetu na hata kama wanashirikiana na watu wa mataifa mengine ila bado ninaamini msingi mkubwa upo hapa nchini ninasema hivi kwasababu hata anayesema kuwa ndiye kiongozi mkuu wa kundi hili anazungumza lugha yetu ya taifa kwa ufasaha hivyo hakuna shaka kuwa ni vijana wetu tuliowalea na kama si wazawa wa taifa hili lakini ninaamini ni watu tuliowalea kwa muda mrefu.” Raisi alizungumza mengi na akaweka msisitizo kuwa kamwe hatojihudhuru.
Hotuba ya rais iliacha maswali mengi mtaani kwani kila mtu alitarajia rais angejihudhuru ili kuinusuru familia ya binti yake na pia kuzinusuru pesa za walipa kodi zilizoombwa na magaidi lakini imekuwa kinyume chake, kitendo cha yeye kugoma kujihudhuru inamaanisha magaidi watalipwa shilingi trioni 8. Haikuwekwa wazi ila kiuharisia itakuwa hivyo. Hakuna namna maana tayari maamzi ya kwanza yameesha chukuliwa na uliobaki ni uamzi wa pili na wamwisho kulingana na taratibu zilizowekwa na hawa magaidi.
Manguli amebaki na aina mbili za maamzi, maamzi ya kwanza ni kulipa fedha aliyoombwa au kufikia makubaliano na magaidi, jambo la pili ni kuiacha familia ya binti yake iteketee kwa manufaa ya taifa zima. Jambo ambalo si rahisi kwa baba kumuacha mwanae afe kizembe ilhali uwezo wakumuokoa upo hiki kingetazamwa kama ni moja ya kitendo cha kinyama kuwahi kutokea duniani.
Tamaa ya pesa ilikuwa ikiwawaka vijana hawa Dominic na Von Gao kila mmoja alijua tayari ameeshaweka shilingi trioni nne mfukoni mwake ni dili la watu wawili wanaousaka u bilionea kwa nguvu na wanaelekea kufanikiwa. Asilimia tisini za kuzipata fedha hizo imekamilika inaashiria kunauwezekano mkubwa mno kwani rais hajajihudhuru na huo ndioulikuwa mtego wa mwisho kwake, kitendo cha rais kubakia madarakani hii ni ishara ya wazi kuwa atailipa hiyo fedha waliyoiomba. Shangwe lililindima mara baada ya rais kusema hatajihudhuru chupa za mvingo zilizunguka meza huku wakigonga glasi kwa furaha. Ni Dominic na Von Gao walikuwa wakichekelea na kupongezana kwa furaha.
“Tumemshika pabaya huyu mzee, hawezi kufurukuta, ni lazima asalimu amri Domi unamawazo makubwa sana rafiki yangu kwanini tulichelewa kufahamiana?”
“Nikweli tumefanikiwa maana hofu yangu angekubali kujihudhuru sijui nani angechukua hayo madaraka”
“hakuna hofu juu ya hilo mbona ni dakika tu tungemtangaza mzee Gao akachukua mamlaka”
“Ha! Mzee Gao? Kwani anakijua kila kinachoendelea huku?”
“hapana ninaamini hakuna asiyependa jina zuri, kuwa rais si kitu cha kitoto naamini huyu mzee wala asingehoji kwanini awe rais”
“Hakika na hapo tungekomba kila kilicho chetu na kutokomea”
“Aah! Wapi, mzee ameeshachukua nchi tutokomee twende wapi? Hapo ni wazi kuwa tungejichukulia madaraka makubwa tu… ungesikia Von ni waziri wa fedha na Domi kawa waziri mkuu na tukabaki tunakula maisha tu nchi yetu tayari tutoke tumuachie nani? Na ili iweje? Ila anabahati yake huyu mwanaharamu angelogwa akajihudhuru saa hivi ningekuwa nishatia maguu Ikulu kumuapisha mshua usiku huu huu na kesho tungetangaza baraza la mawaziri” wote waliangua kicheko na kupongezana kwa kugonganisha viganja vya mikono.
*********************
Ni muda mfupi umepita Kimbo ameesha wasili nchini akitokea Marekani, kimbo hajui ataanzia wapi kwani kunakiashiria cha uzembe katika kuyaokoa maisha ya rafiki yake Jamae Justine na bosi wake aliyemuajili kwenye makampuni ya Himaya ChapaKazi. Ishara ya uzembe imeonekana toka awali na kusipochukuliwa hatua madhubuti bilashaka maisha ya familia ya Jamae yanaweza kupotea. Kimbo ameamua kurejea nchini kwa kazi moja tu nayo ni kuhakikisha usalama wa Jamae Justine.
Anachukua taxi kutoka uwanja wa ndege kuelekea Mbezi beach haijulikani anakwenda kwa nani maeneo hayo. Ukiuangalia uso wa Kimbo ulikuwa kwenye hali isiyo ya kawaida kulingana na matukio yanayozidi kuoneshwa na vituo vya televisheni aliona kama ni udhalilishaji kwa bosi wake na rafiki yake kipenzi ambaye sasa kageuzwa mbuzi wa kafara yeye na familia yake. Jamae amegeuzwa thamani na atumiwe katika mabadilishano kati ya serikali na magaidi na dunia inaangalia, serikali iko kimya na inashangilia. Ni kitendo cha kinyama kisicho na uungwana Kimbo analivalia njuaga swala hili na kuhakikisha linaisha na anamrudisha Jamae na familia yake wakiwa salama.
Kwa haraka haraka safari hii ya Mbezi ilimhusu mzee Gao, Kimbo aliamini wazi kuwa hakuna magaidi wanaohusika na swala hili la utekeji isipokuwa familia ya mzee Gao. Tax ilimshusha karibu na geti moja Jeusi alilisogelea huku akigeuka nyuma, kulia na kushoto. Alihakikisha yule dereva tax amesha ondoka na hakuna mtu aliyemuona alichomoa bastora yake na kuiweka sawa kisha anasogea na kubonyeza kengele ya getini mlinzi alichungulia na kuhoji.
“Wewe ni nani?”
“ naitwa Alfred Mwaka”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment