IMEANDIKWA NA : EMMANUEL VENANCE
***********************************************
Simulizi : Zawadi Toka Ikulu (2)
Sehemu Ya : Kwanza (1)
Baada yakufunga safari kutoka Mbezi beach nilikokuwanaishi na familia yangu niliamua kwenda kumtembelea rafiki yangu Goodluck Bembe rafiki yangu kipenzi sana, aliyehamia hivi karibuni maeneo ya Kibaha Maili moja sikuwahi kufika na pia sina mawasiliano yake ila kwa alivyo nielekeza naamini ninakumbukumbu yakutosha hivyo siwezi kupotea.
Ni majira ya jioni yapata saa kumi na moja nilikuwa tayari niko eneo la maili moja wilayani Kibaha, nageuka kushoto kwangu ninauona ubao mweupe ulioandikwa kwa mandishi ya buluu na mekundu kwakukolezwa yalisomeka hivi “Mkunguni High School” bila shaka ilikuwa ni shule ya Sekondari ya binafsi iliyokuwa mashughuli sana wilayani Kibaha na Dar es salaam kwa ujumla na alama hii ni moja ya alama nilizoelekezwa na mwenyeji wangu naamini nilikuwa karibu sana kumfukia alipo.
Kushoto kwangu kulikuwa na jumba moja la kifahari ambalo hakika sina mfano wake, ni jumba lililomvutia kila mpita njia, halikuwa jumba tu bali waweza kuliita hekalu kulingana na ukubwa wake lakini pia uzuri wa muonekano wake. Hakuna mpita njia ambaye aliizuia shingo yake na kuyanyima uhondo macho yake wakuliangalia jumba hili la kifahari lililokuwa sehemu hiyo. Kuitizama tu ile nyumba ilikuwa ni ufahari, niufahari pia kwenda kuwaeleza ndugu jamaa na marafiki kuwa kuna nyumba nzuri na yakifahari katika eneo Fulani ambayo niyakwanza kukutana nayo katika taifa hili masikini. “Dar wanajenga ila kibaha aaah! wanajenga zaidi.” Nilijisemea kimoyo moyo.
Ilinilazimu kuegesha gari maana sasa sikuwa na namna, hakuna mpita njia aliye nishangaa maana ilikuwa ni jadi kwa eneo hili kukuta watu wamefurika wakiliangalia jengo hili lisilo na gorofa hata moja ila ni kivutio kikubwa kwa wapiti njia. Katika akili yangu nilijuaa wazi jengo lile ilikuwa ni hoteli wala sikuwa na shaka nikamuuliza jamaa mmoja wa makamo mpita njia mwenzangu.
“samahani kaka hii hoteli inaitwaje kaka?”
“hoteli?.. hoteli ipi unayohoji?
“si hii kaka?... “
“Au unamaanisha hii nyumba?”
“ndiyo…. Hii nyumba”
“nyumba ya mtu hiyo kaka, siyo hoteli ni nyumba yakuishi kaka”
“una maanisha kuna mtu anaishi kwenye hili jumba lakifahari?”
“bila shaka hujakosea. Watu wanapesa zao bwana”
“humu wanaishi watu?”
“kaka eeh! Unataka waishi punda siyo?, umeuliza MASWALI nimejibu sasa maswali mia nane yanini…..” Bila shaka maswali yangu yalikuwa yememkera jamaa alikuwa ameesha kasirika …. yule! alitokomea huku akinung’unika na maneno sikuyasikia.
Ukuta ulionakishiwa na rangi pamoja na maumbo ya kufinyanga yenye michoro ya wanyama mbalimbali mashughuli duniani, unakwenda kukutana na geti la rangi ya dhahabu lililokuwa na mvuto usioelezeka, ni geti lakuvutia ambalo kwa kuliangalia tu halikuwa geti lakawaida kuwahi kuliona katika taifa hili, mimi nimtembezi ila hili geti hapana sina chakusema maana lilikuwa nijipya katika upeo wa macho yangu na kumbukumbu zangu zilinielez wazi ndo kwanza nakutana nalo.
Bustani nzuri iliyotiririka maji kama chemichemi ya asili iliyojengwa kwa majabali ilionekana kupitia sehemu,mbalimbali za uwazi pembezoni mwa ukuta ule wa lile jengo huku sehemu hizo zikizibwa na nondo ngumu ila ziliruhusu kuona. Kibwawa kikubwa kilicho nakishiwa kwa vigae na marumaru pembezoni kiliifanya hiyo sehemu kuvutia zaidi. Mita kama hamsini toka bwawa lilipo ilionekana nyumba ya kifahali iliyojengwa mjengo wakimagharibi, iliezekwa kwa vigae vya kijani kwa mitindo yakuvutia, madirisha yake ya vioo yalionekana mwanana huku mbele ikipambwa na bustani nzuri ya majani ya ukoka yaliyohifadhiwa vizuri ili kuongeza mvuto.
Muonekano ule ulinifanya nisogee nikitamani kujua zaidi niliposogea nililiona eneo kubwa la wazi lililozungushiwa ukuta kushoto mwa lile bwawa niliona kuna sehemu iliyojengwa kiasili namaanisha iliezekwa kwa majani lakini ilipambwa na kuvutia na kulipangwa vinywaji vya kila aina. Nje kulipaki magari ya bei ghali kama vile Mercedes Benz, Hummer, Jeep nakadharika, hali iliyozidi kunikata nguvu. Macho yangu sasa yalitamani kushuhudia zaidi maana nilivutiwa zaidi nahii nyumba lakini pindi nageuza jicho mkono wakulia nilikutana na mashine zitumikazo kwenye sheli zamafuta zilikuwa na nembo ya kampumi kubwa ya mafuta hapa nchini GBP.
Hamaki iliongezeka na nikataka kuupata ukweli wakati nazidi kuzungusha macho nilikutana na mandishi yaliyokuwa yameandikwa kwa rangi nyeupe “Barclays Bank ATM 24hours” yakiwa na maana ya mashine yakutolea fedha ya benki ya Barclays inafanya kazi masaa 24.”bila shaka mwenye hii nyumba siyo mtanzania ….. siyo mtanzania!” Nilijisemea huku nikishusha pumzi ndefu. Hakuna mtanzania mwenye fedha kiasi hiki, toka nizaliwe sijawahi kuona mtanzania wa dizaini hii, fedha mpaka zakuweka sheli nyumbani kwake hapana hii ni zaidi ya kukufuru, lakini vipi kuhusu ATM mashine… hili sidhani hata sheria za nchi kama zinakubali.
Sasa nilishapoteza uelekeo kwanza sikumbuki nilifuata nini huko maili moja, nilikuwa nanung’unika mwenyewe huku nikitembea kurudi lilipo gari langu. Nilifungua mlango na kuubamiza kwa hasira niliiwasha kwa hasira na kuondoka zangu. Yanini kuwa na mali kiasi hiki huku watu wanakufa njaa, yanini kumiliki fedha mpaka zikakufanya mwendawazimu?, yanini! Manung’uniko haya hayakuishia moyoni tu bali yalijidhilisha wazi usoni kwangu, sikupendezwa na hali hii iliniumiza na iliendelea kunitesa ndani ya moyo wangu.
Sijui ni wivu, chuki au maumivu tu sikukubaliana kabisa na utaratibu alioutumia yule sijui bwana/bibi katika uwekezaji wa pesa yake. “hata kama unafedha kiasi gani huwezi… huwezi kuustajabisha ulimwengu kwakujifanya wewe ndiye fahari waajabu katika huu ulimwengu. Sidhani kama hata tajiri namba moja wadunia amewahi kuwaza kufanya ujinga kama huu.
Nilipokelewa na mke wangu kipenzi baada ya kufika nyumbani akiwa mwenye furaha nilijitahidi kuificha hudhuni niliyokuwa nayo maana haikumhusu, ingawa nilijua roho inaniuma balaa sikujua kwanini niliumia vile yule jamaa kuwa na nyumba nzuri, sikuiona sababu lakini niliumia sana, pamoja na kujaribu kuikwepa hali ile lakini sikufanikiwa. Jesca mke wangu kipenzi alinikaribisha ndani nikaketi na pembeni kulikuwa na kitanda kidogo kilichokuwa kimembeba mwanangu kipenzi Eric Jamae akiwa na miezi miwili tu tangu amezaliwa nilikisogelea na kumkuta akichezesha mikono nilimbusu na kumpapasa kisha nikaingia zangu bafuni kulipunguza joto na kujaribu kukituliza kichwa kilichokuwa na lundo la mawazo kwa maji ya baribi.
Baada ya kupata maji nilibadili nguo na kumfuata Jesca alikuwa jikoni akihangaika kuandaa chakula, nilifika na kuanza kumtania kidogo tulicheka nilijaribu kumsaidia lakini hakukubali alikataa kabisa akaniomba nikapumzike. Mke wangu hakupenda kuniona namsaidia kazi za jikoni ingawa mimi nilipenda sana kufanya hivyo. Haijalishi alitoka familia gani ila Jesca alipenda kuishi katika uhalisia aliamini jiko ni mahali pa mwanamke.
Na alipokuwa jikoni aliamini yuko sehemu sahihi. Niliondoka zangu na kwenda kujipumzisha sebuleni. Niliketi Tv ilikuwa ikiendelea na vipindi vyake ambavyo havikunivutia lakini sikuhangaika hata kubadili stationi maana nilijua nitapoteza muda wangu bure. Picha iliyokuwa ukutani ni picha ya Jamae Justine na Jesca Manguli vijana waliopitia mikikimiki mingi mpaka kuya vaa mavazi waliyokuwa nayo hapo pichani. Ni picha ya ndoa kati yangu na Jesca ndoa iliyopitia vikwazo vingi lakini ilifungwa.
********
Kimbo alibaki akikilinda chumba chetu nilikuwa niko ndani na mpenzi wangu ambaye ameuvuruga uchumba wake na Von Gao na kulilejesha penzi letu lililokuwa limeyumba. Baada ya aibu iliyomtokea Von Gao na baba yake Mzee Gao. Wageni walisambaa kwani hakukuwa na harusi tena, kila mtu aliongea akijuacho, mwenye kunung’unika alinung’unika, mwenye kutukana alitukana, kila mtu aliongea alichokiona kinafaa, hasa waliotoka upande wa mzee Gao waliishutumu familia ya Rais kwa kuivunja ndoa tarajiwa ya kijana wao makusudi ingawa dua lao halikuwa si chochote wala lolote kwetu.
Tulijipumzisha tukipewa huduma zote na niliamini kwa pigo hilo mzee Manguli nitakuwa nimemuweza. Ni saa saba za usiku tukiwa tumejipumzisha mlango uligongwa nilijua ni Kimbo aliye Gonga nilikwenda kufungua na nilipofungua nilimkuta Kimbo akigugumia kwa maumivu ameanguka chini. Nilikamatwa na kufunikwa nguo usoni nilishushwa ngazi mpaka chini kisha nilipandishwa kwenye gari nilipelekwa sehemu nisiko kujua. Ni mwendo wa saa nzima na ulikuwa ni mwendo wakasi kuliko kawaida.
Hatimaye nilishushwa na kuketishwa kwenye gogo la mti. Lilikuwa ni giza totoro, sikujua lilikuwa ni eneo gani na walionichukua ni kina nani? Akilini mwangu nilijua huu utakuwa ni mwendelezo wa matukio niliyokuwa nikikutana nayo na hali hii ilidhihilisha wazi kuwa Mzee Manguli bado hani hitaji ndani ya familia yake.
Ni ujinga, maana kila nikiyawaza maisha yangu ninaviona vikwazo vikizaliwa vipya kila kukicha. Tangu nimemjua Jesca naweza kusema nimekutana na kila aina ya siraha ingawa nyingio hazijanidhuru ila nimetishiwa karibu kila aina ya siraha tukiachana na mabomu, makombora na vifaru. Si visu pekee, wala bastora pekee, nimekutana na AKA47, SMG, mapanga, jambia na kila takataka pia niekutana na kila aina ya mateso.
Lilikuwa ni eneo la wazi ambalo nilishushwa, hakuna mtu aliyenisemesha bali walikuwa wakipokea simu mara kwa mara huku wakinizunguka na siraha zao nzito ambazo baadhi ndo ilikuwa mara yangu yakwanza kuziona. Usiku ulikatika kukapambazuka nikiwa nimeketishwa kwenye pande la gogo na sasa nilikuwa ninasali sara zangu za mwisho maana niliamini vita yangu na uwezo wangu wakupambana sasa ulifika kikomo. Nilikuwa na sura ngeni zimenizunguka, hazikuonesha hata tone la huruma. Watu walionizunguka wao kwa wao hawasemeshani itakuwaje kwangu kabwela? Ni swali lakujiuliza lakini halikuwa na maana hata kidogo.
*****
Tangu nimeondolewa nyumbani vurugu ziliibuka ni kati ya Jesca na baba yake Jesca alikuwa akimtahadhalisha mzee Manguli kuhusiana na vita yake na mimi. Ilikuwa yapata saa nane na nusu usiku Jesca aliamua kwenda chumbani kwa baba yake usiku huo kwenda kuitafuta suruhu maana alijua hakuna mtu mwingine aliyehusika na kupotea kwangu na pia kuumizwa vibaya kwa Kimbo bali mzee Manguli na mara tu mlango ulipofunguliwa walianza kurushiana maneno.
“ baba hii vita hauta iweza iache tu kama ilivyo”
“vita gani?”
“na sema hauta iweza maana najua hauta iweza, hii vita ni nyingine kabisa”
“Jesca siwezi kupambana na mwanangu hata siku moja, nimeweza kuendesha nchi naamini familia haitanishinda, wewe ni mwanangu wala sitapigana vita na wewe najua utashindwa mwenyewe wala sitapambana”
“nakupa huu usiku mzima na ikifika kesho asubuhi Jamae awe hapa namaanisha siyo kuwa huru bali kuwa hapa nyumbani.
“sijawahi kuendeshwa na mtoto”
“kipindi hiki utaendeshwa…. Na usipo angalia utaendeshwa kwelikweli”
“unasemaje wewe mwendawazimu?”
“nimesema usipotenda haki utaendeshwa…. Nibora ukaendeshwa na mwanao wakumzaa kuliko kuendeshwa na mafisadi, wauza madawa na wapenda sifa, kujigamba na kupenda kutukuzwa.” Kimya kilitawala bila shaka Mzee Manguli alikuwa akitafakali namna yakufanya.
“Baba najua kila kitu kuhusu hili, usitake tufike mbali… staolewa na Gao aibu muliitaka wenyewe na mmeipata kama mlivyoitaka. Niliwaonya mapema sana juu ya hili lakini hamkutaka kunisikiliza. Baba kama familia ya Gao unaipenda sana … tenasana hebu olewa wewe.” Jesca alimaliza na kuondoka huku akimuacha mzee Manguli akifula kwa hasira.
“mpumbavu huyu… ni ujinga! ….. hahaaaa dah! Mimi niolewe na Von siyo? Hapa sasa mama umetosha kunidharau kama tumefikia hatua mpaka yakuozeshana, baba yako unamuozesha… tena si baba tu rais wanchi hii unamuozesha kwa kidumee aaaah! Jesca mwanangu hii dharau ni too much.”
“lakini unapaswa kutafakari kwanini mmefika huku?” mama Jesca alidakia.
“kutafakari …. Kwa kauli hii hapana…. Acha nimuoneshe kuwa mimi ni baba, maana sasa amevuka mipaka…. Acha nimshikishe adabu Jamae ndiye anampa kiburi nadhani hatutakuwa naye ndani ya dakika kadhaa”
“tafadhari baba Jesca kwa hilo nakuomba usijaribu kumkosea Mungu wako kumuua kijana wa watu hana hatia … amekukosea nini mpaka ufanye uamzi huo? No sikubaliani na uamzi huo na nitaupinga mpaka kifo.
Jesca alikuwa ndani ya chumba chake akitiririkwa machozi, hudhuni imekitawala nafsi yake anajaribu kutafuta ufumbuzi wa kunipata lakini haikuwezekana. Kimbo alikuwa kwenye chumba cha watu mahututi kalazwa akikoroma kuipigania nafsi yake haijulikani alipuliziziwa sumu gani kipindi wanakuja kuniteka lakini alikuwa yuko chumba mahututi cha dharula hapo ikulu madakitari wakijaribu kunusuru maisha yake.
******
Nilikuwa nimepokea kichapo cha mbwa mwizi huku kisu kikali kikiwa kimemea kwenye upaja wangu wa mguu wa kulia, nimechapika vilivyo kumbukumbu yangu kidogo iliyokuwa imebaki niliitumia kumkumbuka Mungu wangu, na hatimaye kichwa changu kilianza kuipoteza kumbukumbu na uono wa macho yangu ulianza kufifia. Mauti yalikuwa yameninyemelea.
Ni kipigo cha kitako cha bunduki nilichoanza nacho, nilikutana na sumbwi la mkono wa kushoto kutoka kwa mmoja wa wale watekaji, kabla ya mmoja kunishindilia nisu cha pili kwenye paja lilelile la mguu wa kulia, nilianguka na kupiga magoti lakini maumivu na bwawa la damu lilitapakaa, kwa uono hafifu namtizama jamaaa akijiandaa kuigawanya shingo yangu kwa upanga ilikuwa ni kutenganishwa kichwa na kiwiliwili ndicho kilichokuwa kimebaki. Hawakuwa wanatania maana mmoja wao alisikika akiesema tumeambiwa huyu jamaa hatakiwi kuwa duniani ndani ya dakika tano zijazo na ameagiza twende na kichwa chake. Hayo ndiyo yalikuwa ni maneno ya mwisho kuyasikia hapa duniani siku hiyo.
Nausikia muungurumo kwa mbali pia inanichukua muda kujua nini kunaemdelea masikioni mwangu ni maumivu makali ya kichwa, huu ni muungurumo wa feni au panga boi kama waitavyo waswahili najaribu kuyafungua macho lakini haikuwezekana, najitahidi kuutikisa mkono wangu ulionekana kuwa mzito kutikisika, vidole vyangu sikuweza hata kuvichezesha.
Maumivu yalikuwa makali tena makali mno, kichwa kiliuma isivyo kawaida, muungurumo wa feni pia ulionekana kuwa kero kwangu masikioni mwangu. Taratibu nilijitahidi nikafumbua macho, nilifanikiwa kwa uono hafifu niligundua kuwa niko kwenye chumba cheupe sikumbuki nini kilitokea ili juu yangu niliona mlingoti ulioning’iniza chupa mbili ya moja ya damu na moja ya maji huku mirija ikielekea moja kwa moja kwe mikono yangu. Hii ilikuwa ni ishara kuwa nilikuwa Hospitali.
Shingo yangu ilikuwa haiwezi hata kugeuka, pia sikuweza hata kujitikisa kila sehemu nilihisi maumivu makali. Hatimaye uono wangu ulianza kurejea katika hali ya kawaida, lakini maumivu yakikuwa makali mno. Niliwaona watu wawili wamelala kushoto kwangu kila mtu alionekana kuwa mahututi zaidi. Hii ilidhidi kudhihilisha kuwa nilikuwa hospitali na nikawaida ya hospitali mgonjwa unaweza kujiona unaumwa kumbe kuna wanao umwa zaidi yako.
Baada ya kuzinduka nikama nusu saa hivi dakitari alikuja kuniona alinisalimia nilikuwa naweza kumuona na kumsikia kwa taabu sana lakini sikuwa na uwezo wa kuongea, kwani ulimi na taya zangu zilikuwa zimekakamaa na nilikuwa nahisi maumivu yasiyo ya kawaida. Daktari alinitizama na alifungua mboni zangu kwa kuzipenya na vidole vyake huku akimlika kwa kitochi chake alisikika akisema “angalau damu imerejea kiasi, unabahati sana kwa upungufu ule wa damu nibahati sana mtu kupona” aliongea akionesha masikitiko makubwa.
Aliandika alichokijua yeye kwenye kijitabu chake, wakati huo wauguzi wakihangaika kunibadilisha nguo kwani nilikuwa nimeesha chafua bila kujua maana hali yangu ilikuwa tete kuliko kawaida na haijulikani nimekuwa hapo tangu lini maana hali yangu ilitishia amani.
Ilikuwa ni siku ya tatu tangu nimerejewa na fahamu, najaribu kujigeuza sasa angalau hali yangu ilianza kutia matumaini, nilikuwa nasikia vizuri kuliko awali na sasa niliweza kuongea japokuwa ilikuwa nikwa taabu sana. Kwa wakati huo wote sikumbuki nini kilinitokea, ila ninachokijua nilikuwa hospitali na sikumbuki ilikuwa ni hospitali gani.
Niliendelea kupata matibabu kila kukicha naleo nilipata bahati ya kumuangalia vizuri mgonjwa aliyekuwa karibu yangu. Nina gundua ni Evaristi Kimbo ndiye mgonjwa aliyekuwa kalazwa karibu yangu na hali yake ilionekena kuwa mbaya zaidi. Nilishituka kidogo na nikataka kujua kilicho msibu nilijibiwa na dakitari “ kazi yangu hapa nikutibu wagonjwa sitakiwi kujua kimetokea nini juu yao, mgonjwa akiletwa nitaangalia kama kunauwezekano atatibiwa kama hakuna nitatoa rufaa apelekwe kwingine” maelezo yake yalinishitua kidogo niliuliza tena swali la kizushi “kwani huyu unamjua?... anaumwa nini na aliletwa lini hapa? “ kaka uliyoyakuta hapa yaache hapa kama ulivyo yakuta” lilikuwa ni jibu la mkato kutoka kwa daktari. Ikanibidi kuuliza tena kwa mshangao “kwani hii ni hospitali gani?” ………………. “hupaswi kujua unachotakiwa kujua hapa ni juu ya afya yako tu na si kitu kingine sawa kaka… na sitarajii maswali mengine zaidi sawa” jibu hili lilitolewa jamaa akionekana kuwa kauzu zaidi, nadhani mazungumzo yalifungwa kwa mtindo huo.
Wiki mbili baadae mwili wangu sasa ulikuwa na nguvu tena nguvu haswaa nilikuwa nimeanza mazoezi huku nikizidi kuponyesha majeraha yangu ya paja ambayo yalichukua muda sana kupona, nilikuwa nachechemea kila kukicha na niliamini nitapona na kurejea katika hali yangu ya kila siku. Kumbukumbu za matukio yote yaliyonikuta zilikuwa zikirejea taratibu maana nakumbuka vizuri sana nilivyotekwa na kuteswa usiku wa manane kipigo juu ya kipigo na hatimaye sijui nini kiliendelea nikajikuta hospitalini hapa.
Kulikuwa na maswali mengi najiuliza, ule upanga uliokuwa shingoni kwangu mara ya mwisho kabla sijapoteza kumbukumbu ulininusuru vipi? Mpaka nisiuawe, lakini kulikuwa na swali gumu kulitafakari ambalo mara kwa mara huliwaza nimemkosea nini mimi mzee Manguli mpaka anisurubishe kiasihiki? Maana kila kukicha na adhabu mpya.
Kulingana na mapito ninayopitia nilihisi ninawaza ujinga nakweli huenda ulikuwa ni ujinga maana matokeo ya hiki ninachokiwaza ni kifo.
Ulinzi ulikuwa ukiimalishwa pale hospitali kila kukicha, ni hospitali ya kifahari inakila kitu ndani nazungumzia, sehemu yakupumzika, kuangalia Tv, magazeti ya kila aina utayapata, vinywaji baridi kama juisi, soda, chai na kahawa havilipiwi ni haki ya kila mgonjwa kupewa, chakula kilikuwa kizuri kila mgonjwa alihudumiwa alivyojisikia. Ni hospitali ndogo iliyojazia vifaa vya kisasa na wataalamu waliobobea. Wagonjwa hatufiki watano ila ulinzi uliopo ni zaidi ya askari ishilini swali hawa askari walikuwa wanalinda nini? baada ya kutafakali sana nilijua hiyo siyo hosipitali bali ni sehemu hatari tuliyohifadhiwa.
***************
Nyumbani kwa mzee Manguli tangu nitoweke hapakaliki, vita kati ya baba na binti yake baada ya kujibizana kwa maneno makali, vitisho na kutishiana ubabe. Sasa Jesca hakuiona haja yakuendelea kuishi tena akiwa ndani ya chumba chake aliamini ni heli kuiaga dunia kuliko kuishi na mzazi asiye jali hisia zake.
Mzazi asiye na huruma kwa bintiye ni mzazi wa ajabu kuwahi kutokea katika huu ulimwengu. Alilifungua kabati na kuichukua bastora yake ambayo hutumika kujilinda kama tahadhali mbali na ulinzi alionao. Aliikagua na kugundua magazine ilikuwa ina lisasi nne aliiweka sawa huku akilia kwa uchungu alikuwa kadhamilia kupoteza maisha alikoki mara ya kwanza na kabla hajailekeza kichwani alikosea na kujikuta akifyatua risasi kwa bahati mbaya, kukasikika kishindo kikubwa kilicho washitua walinzi wake walivunja mlango na kuingia kwa kasi ya ajabu huku baba na mama wakichuana kwa mbio kwenda kuyaokoa maisha ya binti yao. Lakini walikuwa wameesha chelewa tayari walinzi walifika ndani kwa tahadhali kubwa huku wasiamini walichokikuta.
Mzee Manguli aliingia huku akijaribu kumsihi binti yake asifanye alicho dhamilia kufanya, tahadhali ilikuwa kubwa kwani kilichokuwa kikiendelea lilikuwa ni swala nyeti na hatari sana ndani ya familia ya rais. Jesca ameweka bastora kwenye kichwa chake lakini baba na mama yake wanaonekana kumsihi asijiue. Mama alikuwa akilia kwa uchungu akimuomba binti yake aachane na maamzi hayo kwani si yeye, atakuwa ni shetani yuko kati yake hivyo asiruhusu kamwe shetani akaiteka akili ya binti yake. Ilikuwa ni vita kali ambayo hakuna aliye thubutu kumsogelea maana tayari salamu ya mlio wa risasi wameesha isikia kwa kawaida akili ya Jesca haikuwa sawa iwapo kungetokea kosa lolote basi alikuwa tayari kughalimu maisha yake au ya yeyote ambaye angemsogelea.
Pamoja na juhudi zote za kumuomba ashushe siraha kugonga mwamba, vilio vilitawala mule ndani kila mtu alijitahidi kumsihi binti huyu asijiue. Ni mmoja wa walinzi mashuhuli na anaye aminika alijulikana kama Cloud Kwambe maarufu kama “Robo” wakati rais na mkewe wakimsihi binti yao asifanye maamzi yakujidhuru Robo pamoja na timu nzima ya ulinzi walikua wakiandaa mtego wakumuokoa Jesca kabla hajajiua Robo alikuwa akisogea taratibu ili amdake na kumnyang’anya siraha lakini kabla hajakamilisha zoezi hilo alilopanga kulifanya alijikuta akishitukiwa na kushushwa risasi ya mguu. Bila shaka zilikuwa ni salamu mbaya sana kwa watu wote waliokuwa eneo hilo. Rais alikuwa chini hajui aliangushwa vipi na walinzi wake huku wakiwa wamelala juu yake mama pia vivyo hivyo na Robo alikuwa akilia kwa uchungu mguu wake ulikuwa umepigwa risasi.
Iliwachukua dakika tano kunyanyuka walipokuwa, na timu ya ulinzi na siraha nzito sasa ilikizunguka chumba kile madirishani na mlangoni kulijaa siraha nzito zikimlenga Jesca lakini Jesca alijua hakua na wakuthubutu kumgusa maana mambo ya familia hayaingiliwi na walinzi. Rais alikuwa akitetemeka kwa uoga, mkewe pia vivyo hivyo vilio vya hofu vilitawala. Hali ilikuwa mbaya zaidi, ilikuwa ngumu na hatari kufyatua risasi kwa walinzi maana aliyefanya hivyo ni binti wa rais nani achukue hetua juu yake bila kupokea amri akuna mtu ange thubutu. Baada ya kuhakikisha kuna usalama walinyanyuka na kutaka kumtoa raisi mule ndani Jesca alikataa.
“Hapana! mnampeleka wapi huyo mzee? namuhitaji hapa, nasema muleteni hapa!” kauli ile ilizidi kuwachanganya walinzi.
“hapana sheria hazituruhusu na kumbuka huyu ni baba yako Jesca you can’t do that.” Ali lalama huku akichombeza na kiingereza.
“nasema hivi mleteni huyo mzee hapa au tunabishana?” maelezo ya awamu hii yalionekana kuwa Jesca yuko serious zaidi.
“Jesca mwanangu unanini leo enh? … unataka kufanya nini mwanangu?” mama alihoji.
“sifanyi kitu mama nataka nimuoneshe huyu mzee kuwa kunawatu wanaumia zaidi kutokana na upuuzi anaoufanya nadhani asipojifunza leo hatojifunza tena maishani”
“what….?”
“umenisikia vizuri sana sina haja yakurudia … ninaomba mnikabidhi huyo rais wenu tafadhali, nyie si waajiliwa hapa au mmekuwa mabisi kama mimi?, rais ni cheo tu hata mimi nikitaka kesho nitakuwa rais hii ni vita ya familia haiwahusu namuomba baba yangu hapa mwachieni”
“hapana Jesca mwanangu nisamehe mama … jamani msimuruhusu akanichukua ataniua… mnamuona alivyo msimuruhusu jamani na…. nani …. Walinzi msimuruhusu jamani … enh …. Aah… bwanaaa! Nakufa najionaa ”
“nina kuomba njoo hapa! .. baba ulitangaza vita nimeamua kupigana vita … haya nakuomba njooo hapa!”
“au unataka nipige hatua nikufuate?”
“aaah! Mama kwanini tufike huko?... yaishe mwanangu nimesha kubali yameisha.”
“Nije siyo?”
“Hapana nakuja… jamani niachieni niende ataniua huyu hataniii ila naomba msiondoke mkatuacha wawili ataniua huyu shetani” walinzi hawakuwa na namna iliwabidi kumkabidhi mzee Manguli kwa binti yake maana mgogoro wa kifamilia hauwahusu, Jesca anampokea baba yake huku mzee akilia kwa uchungu maana alijua wazi binti yake hatomuacha salama.
*** Je ni nini kitaendelea……
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment