Search This Blog

Monday 27 March 2023

GARI LA KUKODI (2) - 5

  


Simulizi : Gari La Kukodi (2)

Sehemu Ya Tano (5)



“Tom!” Tunu aliita kwa mshangao uliochanganyika na furaha baada ya kumwona akiwa amesimama mbele yake akimtazama kwa tabasamu.


“Tunu!” Tom naye akaita kwa furaha huku akiharakisha kuelekea pale kitandani alipoketi Tunu na kumkumbatia kwa furaha. “Thanks Lord!” Tom alisema kwa sauti ya chini huku akizidi kumkumbatia Tunu.


Walikumbatiana kwa kitambo fulani huku kila mmoja wao akionesha hisia za furaha kwa mwenzake. Tom alipomwachia Tunu na kumtazama usoni alikuwa amelengwa na machozi ya furaha. Tunu alimtazama kwa Tom makini.


“Hivi nimefikaje hapa?” Tunu alimuuliza Tom kwa shauku kubwa ya kutaka kufahamu kile kilichokuwa kimetokea huku wakitazamana kwa furaha.


“Uliokolewa na kina Bob baada ya kutekwa na watu wa Mr. Oduya na kuletwa hapa baada ya Bob kuwasiliana na mimi,” Tom alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


Mara Tunu akakumbuka kuwa kabla hajapoteza fahamu na kulala usingizi mzito akiwa ndani ya ile taxi alikuwa ameliona gari la Bob, aina ya Nissan Patrol.


“Bob yuko wapi?” Tunu aliuliza kwa shauku huku furaha yake ikizidi kuongezeka.


“Ametoka sasa hivi, amempeleka daktari mmoja rafiki yangu aliyekuja kukuhudumia, lakini yule mwenzake yupo sebuleni amepumzika…” Tom alisema huku akimtazama Tunu kwa makini. “Vipi unajisiaje kwa sasa?”


“Nahisi maumivu kwenye mguu wangu wa kulia, kichwa nacho kinauma kidogo na kizunguzungu. Kwani nini kilinitokea?” Tunu alisema huku akifinya macho yake.


“Ulichomwa sindano fulani yenye dawa ya kuupumbaza ubongo wako ili usiweze kuwaletea matata na kama ungeachwa hivyo hivyo bila kupatiwa antidote basi ingekuchukua saa arobaini na nane kuweza kuzinduka na kurudia hali yako ya kawaida,” Tom alisema maneno yaliyomfanya Tunu asisimkwe mwili wake.


“Na begi langu la laptop liko wapi?” Tunu akauliza tena kwa wasiwasi baada ya kutokuliona begi lake la laptop sehemu yoyote mle chumbani.


“Usihofu, lipo mahala salama, begi pamoja na vitu vyako vyote ikiwemo bastola na simu,” Tom alisema huku akimpetipeti Tunu mgongoni katika namna ya kumtoa hofu.


“Basi fanyafanya mpango unitafutie msosi, nina njaa ya kufa,” Tunu aliongea kwa utulivu huku akipiga mwayo hafifu.

“Usijali, tayari chakula kimeshaandaliwa. Kuna mchemsho wa ndizi nyama, mchemsho wa kuku, maziwa fresh na vitafunwa. Chaguo ni lako!” Tom alisema na kumtazama Tunu kwa utulivu huku akitabasamu.


Tunu naye aliachia tabasamu lake jepesi huku akijiinua toka pale kitandani lakini akaketi tena juu ya kitanda baada ya kuhisi kizunguzungu. Akayafumba macho yake huku akivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu.


Tom alimtazama kwa makini, “Pumzika kwanza, Tunu, nitakwenda kukuchukulia chakula na ukila kila kitu kitakuwa sawa,” Tom alisema na kumuaga Tunu kisha akaondoka kuelekea kule jikoni akimwacha pale kitandani.


Mara tu Tom alipoondoka mle chumbani ile hali ya upweke ikamrudia tena Tunu pale kitandani huku akiupisha utulivu kichwani mwake. Alipoitazama saa yake ya mkononi akagundua kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa moja na robo ya asubuhi, hapo fikra zake zikahamia kutafakari juu ya kazi iliyokuwa mbele yake. Alitamani sana aangalie kilichomo kwenye ile memory card kabla ya mambo mengine yote na alikuwa akimuomba Mungu kusiwe na chochote kilichofutwa.





“Basi fanyafanya mpango unitafutie msosi, nina njaa ya kufa,” Tunu aliongea kwa utulivu huku akipiga mwayo hafifu.


“Usijali, tayari chakula kimeshaandaliwa. Kuna mchemsho wa ndizi nyama, mchemsho wa kuku, maziwa fresh na vitafunwa. Chaguo ni lako!” Tom alisema na kumtazama Tunu kwa utulivu huku akitabasamu.


Tunu naye aliachia tabasamu lake jepesi huku akijiinua toka pale kitandani lakini akaketi tena juu ya kitanda baada ya kuhisi kizunguzungu. Akayafumba macho yake huku akivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu.


Tom alimtazama kwa makini, “Pumzika kwanza, Tunu, nitakwenda kukuchukulia chakula na ukila kila kitu kitakuwa sawa,” Tom alisema na kumuaga Tunu kisha akaondoka kuelekea kule jikoni akimwacha pale kitandani.


Mara tu Tom alipoondoka mle chumbani ile hali ya upweke ikamrudia tena Tunu pale kitandani huku akiupisha utulivu kichwani mwake. Alipoitazama saa yake ya mkononi akagundua kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa moja na robo ya asubuhi, hapo fikra zake zikahamia kutafakari juu ya kazi iliyokuwa mbele yake. Alitamani sana aangalie kilichomo kwenye ile memory card kabla ya mambo mengine yote na alikuwa akimuomba Mungu kusiwe na chochote kilichofutwa.


ENDELEA...


Mawazo juu ya ile memory card na kazi kwa ujumla sasa yalichukua nafasi kwenye kichwa cha Tunu hadi pale aliposhtuka baada ya kitasa cha mlango wa kile chumba kuzungushwa taratibu na ule mlango kufunguliwa, kisha ukasukumwa kwa ndani.


Tunu aliyapeleka macho yake kutazama kule mlangoni huku akitabasamu, alimwona Tom akaingia mle ndani huku akiwa ameongozana na Dumba. Tom alikuwa amebeba bakuli kubwa la udongo lenye maakuli na jagi kubwa la maji, na Dumba alikuwa amebeba begi la Tunu lenye laptop na bilauri.


Tunu aliachia tabasamu baada ya kumwona Dumba na kuliona begi lake, akalipokea lile bakuli na kutazama ndani yake, kulikuwa na mchemsho wa ndizi matoke na nyama laini ya ng’ombe. Chakula kile kilikuwa kimepikwa kwa ufundi wa hali ya juu. Tunu hakutaka kujivunga, alianza kukishambilia kile chakula kwa pupa.


Kilikuwa chakula kitamu sana ambacho Tunu hakuweza kukumbuka kuwa mara ya mwisho kula chakula kitamu namna ile ilikuwa linin a wapi. Hakuwa na shaka yoyote kuwa chakula kile hakikuwa kimeandaliwa na Tom, huenda kilinunuliwa katika mojawapo ya migahawa ya kisasa kama Elli’s au Nuru Foods Café.


Hata hivyo, Tunu hakuwa na shida ya kuuliza. Aliendelea kula kwa pupa. Utamu wa kile chakula uliifanya asubuhi ile tulivu mno kuwa ya kupendeza sana kwa Tunu. Alipomaliza kupata kifungua kinywa, alinyanyuka na kuingia bafuni, huko alichukua dakika kadhaa kujimwagia maji na alipotoka humo mwili wake ulikuwa tayari umepata nguvu mpya.


Alijiandaa vizuri na kubadili nguo. Sasa alikuwa katika mwonekano mpya wa gauni lake zuri la kitenge lililoshonwa kwa mtindo wa ‘Ankara midi tube dress’ likiishia juu kidogo ya magoti yake, likaushika vyema mwili wake ulioumbika na kulichora umbo lake maridhawa. Nywele zake fupi na laini alizozitia rangi ya dhahabu alizichana vizuri na miguuni alivaa viatu simpo visivyo na vikanyagio virefu.


Ilipofika saa mbili na robo Tunu alitoka chumbani akiwa amebeba begi la laptop na kuelekea sebuleni. Sebule ilikuwa tulivu mno na kila mtu alikuwa akiwaza lake. Ilikuwa sebule kubwa iliyopo katika mazingira ya upweke kiasi yenye nyumba chache za makazi, eneo la Kinyerezi, watu wanne walikuwa wameketi kwenye sebule kubwa ya kifahari.


Ilikuwa sebule kubwa yenye kila thamani za kisasa yakiwemo makochi ya ngozi ya sofa ya kifahari yaliyopangwa katika mtindo wa kuizunguka na meza nzuri ya kioo yenye umbo la yai ilikuwa katikati, runinga pana kutani na chini yake kulikuwa na meza fupi nyeusi yenye sistimu ya muziki na kisimbuzi chenye chaneli za ndani na za kimataifa. Ilikuwa na madirisha makubwa ya vioo yenye kupitisha hewa safi.


Mbele ya sebule ile kulikuwa na ukumbi wa kulia chakula wenye meza kubwa ya duara iliyozungukwa na viti sita vya sponji. Kwa kweli ilikuwa ni nyumba nzuri ya kupendeza na yenye hadhi ya kukaliwa na kiongozi yeyote wa serikali mwenye cheo cha juu. Hata hivyo, pamoja na ufahari wa nyumba ile lakini ilikuwa haikaliwi na mtu yeyote, Tom alipenda kuifanya makazi yake ya siri kila alipokuwa na kazi za dharura kama ile.


Pale sebuleni Tunu aliwakuta Tom, Bob na Dumba wakiwa wameketi tayari sebuleni wakishushia na mvinyo ghali na mtamu aina ya Madeira wenye kiwango kikubwa cha asilimia 20 cha kilevi. Kulikuwa na bilauri nne, moja ikiwa tupu ikimsubiri Tunu na bilauri nyingine tatu zilikuwa zimejazwa mvinyo. Bob alikuwa ameshika kitabu cha Behind the Presidential Curtain kilichoandikwa na Noble Marara, mpambe wa zamani wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame.


Alikuwa akisoma taratibu aya kwa aya na kifungu kwa kifungu huku akishushia mvinyo aina ya Madeira. Alipomwona Tunu alifunika kile kitabu na kukiweka juu ya meza ndogo ya kioo mbele yake, macho yake yakiwa kwa Tunu.


“Dah! Hakika Mungu kakupendelea, nilidhani unapendeza zaidi ukivaa suruali ya jeans kumbe hata ukiwa katika mwonekano wa vazi la kitenge! Ningekuwa promota wa mitindo ya mavazi ya Kiafrika ningekusajili, sina shaka yoyote wewe ungeweza kuiletea nchi hii ushindi usio na shaka,” Bob alisema kwa mzaha na kuwafanya wote waangue kicheko. Kisha walimkaribisha Tunu mvinyo.


Hakujivunga, alichukua ile chupa kubwa ya mvinyo na kujimiminia kwenye ile bilauri tupu kisha akapiga tarumbeta mafunda kadhaa na kuikita ile bilauri juu ya meza huku akisisimkwa mwili wake. Kisha akaketi kwenye sofa huku mvinyo ule ukionekana kuamsha ari mpya katika mwili wake na kumchangamsha vizuri kiasi cha kupunguza nishai machoni.


* * * * *


Saa mbili na nusu asubuhi ilimkuta Mr. Oduya akiwa bado ameketi kwenye kiti chake, moyo wake ulikuwa bado hauna amani. Hii ilikuwa ni baada ya kuwa na kikao kifupi na washirika wake muhimu sana. Kikao hicho kilifanyika kwenye ofisi yake iliyopo ndani ya jengo lake la ghorofa kumi na mbili lililopo barabara ya Bagamoyo, eneo la Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.


Katika kikao hicho, washirika wake walikuwa wameshtushwa sana kusikia kwamba ni yeye Mr. Oduya aliyekuwa nyuma ya sakata lote la kuvamiwa nyumba ya Sammy na kisha yeye na mkewe kujeruhiwa. Baada ya kuwasihi sana walikubali kumsaidia, japo kwa shingo upande ili kulimaliza tatizo hilo na kuuanza ukurasa mpya.


Sasa Mr. Oduya alikuwa na uhakika wa kumalizana na jambo la kwanza kati ya mawili makubwa yaliyomkabili, sasa alikuwa anawasubiri watu wake maalumu wa kupanga mikakati ili kumalizia jambo la pili. Muda huo alikuwa ametulia mbele ya computer yake, macho yake yalikuwa matulivu yakipitia taarifa muhimu za mpango-kazi zilizokuwa zimetumwa kwake na wahisani walio nje ya nchi.




Akiwa anaendelea kuipitia taarifa ile, akakumbuka jambo muhimu sana na kuinua simu yake ya mezani iliyokuwa kando ya meza yake, kisha akapiga kwa katibu muhtasi wake.


“Mariam, leo nina mambo mengi sana ya kufanya, hivyo sitapenda kusumbuliwa kwa matatizo madogomadogo, sawa?” Mr. Oduya alisema kwa sauti yake nziti ya kimamlaka.


“Sawa, Bosi,” katibu muhtasi wake aliitikia kwa sauti iliyoashiria heshima zote, kisha simu ikakatwa.


Baada ya kukata simu Mr. Oduya alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu kisha akatoa sigara moja toka kwenye paketi na kujiwashia, akaanza kuvuta taratibu huku akiipitia ile taarifa ya mpango-kazi kwa umakini zaidi na kunukuu kwenye kitabu chake kidogo cha kutunza kumbukumbu baadhi ya mambo aliyoyaona ni muhimu zaidi.


Mara simu yake ya mezani ikaanza kuita, Mr. Oduya aliitazama ile simu kwa hasira kwa kitambo fulani na kuamua kuidharau. Ile simu iliendelea kuita na mwito wake ukageuka kero masikioni mwake, aliitazama kwa makini huku akijishauri, mara akashawishika kutaka kuipokea huku akijiuliza, ni nani aliyekuwa akimsumbua kiasi kile!


Alinyoosha mkono wake kuichukua ile simu, hata hivyo, kabla mkono wake haujakigusa kiwambo cha kusikilizia simu ikakatika. Mr. Oduya akaminya midomo yake huku akijiuliza ni nani aliyekuwa akipiga simu, kisha akavuta mkupuo mkubwa wa moshi wa sigara na kuutoa nje kupitia mdomo na tundu za pua huku akiutazama kwa makini.


Akaachana na habari ya simu na kuendelea kupitia ile taarifa kwenye computer huku kitambo kifupi cha ukimya kikipita, mara ile simu ya mezani ikaanza kuita tena. Safari hii hakutaka ile simu iendelee kuita zaidi, hivyo haraka akakinyakuwa kiwambo chake na kukiweka sikioni huku akiipa akili yake utulivu wa hali ya juu. “Hallo!” aliongea kwa sauti tulivu iliyoficha hasira.


“Samahani, Bosi, kuna mgeni anahitaji kukuona...” yule katibu muhtasi wa Mr. Oduya alisema kwa sauti iliyoashiria woga fulani. Mr. Oduya alimkatisha kwa hasira.


“Binti, sikukwambia kuwa sitapenda usumbufu! Sijui umenielewa?” Mr. Oduya aliongea kwa ukali huku akitaka kuikata ile simu.


“Nimekuelewa, Bosi, ila huyu mgeni amesisitiza kuwa lazima akuone sasa hivi kwa hali yoyote,” yule katibu muhtasi aliongea kwa sauti yenye wasiwasi mkubwa.


“Sasa hivi! Amekutajia jina lake?” Mr. Oduya aliuliza huku akihisi donge la hasira likimkaba kooni kutokana na usumbufu ulioanza kujitokeza.


“Anasema yeye ni Inspekta Abel...” sauti ya yule katibu muhtasi ilipenya kwenye ngoma ya sikio la Mr. Oduya na kumfanya ahisi ubaridi mwepesi ukisambaa kwenye mwili wake.


“Nani? Inspekta Abel!” Mr. Oduya alimaka kwa mshtuko kwenye simu kiasi cha kutaka kuipasua ngoma ya sikio la katibu muhtasi wake.


Hakujua kwa nini alishtuka kiasi kile. Mapigo ya moyo wake yalikuwa yakienda mbio isivyo kawaida na jasho jepesi likaanza kumtoka usoni. Hata hivyo, alijikaza na kushusha pumzi za ndani kwa ndani. Hofu ilikuwa imepenya katika moyo wake kiasi cha kumshangaza zaidi ya ilivyomtisha. Alijiuliza, anahofia nini? Kama yule inspekta alifika pale kwa ajili ya suala la Sammy hilo halikumtia hofu. Alijua kuwa hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja ambao ungemuunganisha Mr. Oduya kwenye suala hilo.


Hata hivyo, hofu ilizidi kuutekenya moyo wake! Je, aliogopa nini? Alijiuliza tena. Kuna nini cha kuhofia? Hakupata jibu! Upuuzi ulioje! Akawaza, kwanza Inspekta Abel siyo saizi yake, yeye saizi yake ni kuanzia makamishna wasaidizi wa polisi hadi mkuu wa jeshi la Polisi.


“Sasa, Bosi, nimwambieje?” sauti tulivu ya katibu muhtasi wake ikamzindua Mr. Oduya toka kwenye mawazo yake.


“Okay, mruhusu aingie,” Mr. Oduya alisema na kisha akaiweka ile simu pembeni na kujiegemeza kwenye kiti chake kumsubiri yule mgeni.


Mwanamume mrefu mwenye mwili mpana akiwa ndani ya sare nadhifu za kipolisi zilizokuwa na cheo cha alama mbili za nyota mabegani kwake aliingia, mkononi mwake alikuwa amebeba mkoba mdogo mweusi wa ngozi. Ni Inspekta Abel, aliyekuwa amepewa jukumu la kufanya uchunguzi wa kesi ya shambulio katika nyumba ya Sammy. Inspekta Abel alipoingia alinyoosha mkono wake wa salamu kwa Mr. Oduya na kumsalimia huku akitabasamu.


“Karibu sana, karibu uketi,” Mr. Oduya alisema huku akimwonesha kiti baada ya kusalimiana. Inspekta Abel akaketi.


“Naweza kukusaidia, Inspekta?” Mr. Oduya alimuuliza Inspekta Abel huku akimwangalia kwa makini.


“Naam,” Inspekta Abel aliitikia huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani. Kisha alimweleza Mr. Oduya kuwa alikuwa amefika hapo kwa ajili ya suala la vijana wake waliouawa.


Alimweleza kuwa kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na polisi juu ya vifo vya kutatanisha vya watu watatu akiwemo msichana mmoja, waliouawa kwa kupigwa risasi kwenye nyumba moja huko Karakata, ilibainika kuwa wote walikuwa wafanyakazi katika kampuni zilizokuwa chini ya The Splendid Group, mali ya Mr. Oduya.


Kilichowavutia zaidi polisi ni kwamba mmoja wa watu hao, Dulla Mcomoro, alikuwa amepigwa risasi katika makabiliano na polisi katika uvamizi nyumbani kwa Sammy kule Tabata Chang’ombe na mwili wake kukutwa na wenzake wawili Uledi na Lisa huko Karakata. Kwa hali hiyo, Inspekta Abel aliona kuwa, kulikuwa na haja ya kuonana na Mr. Oduya ili apate kujua tokea kwenye mzizi, juu ya kuhusishwa kwa vijana wake watatu huku akiamini kuwa angekuwa na kitu fulani cha kumweleza.


Mr. Oduya alikubali kuwa wote walikuwa vijana wake na wafanyakazi wake, lakini alipinga kufahamu chochote na kwa namna yoyote ile kama kulikuwa na yeyote kati yao aliyekuwa akijihusisha na uhalifu wa aina yoyote.




“Ofisa, kama umekuja hapa kwa sababu ya hilo basi jua sina chochote cha kukusaidia,” Mr. Oduya alisema huku akimtazama Inspekta Abel kwa makini na kuyatuliza macho yake kwenye uso wake.


“Waweza kuniambia, inakuwaje wafanyakazi watatu wa kampuni zako wakauawa kwa risasi katika usiku mmoja, wawili wakiwa ndani ya nyumba moja, tena nyumba ya mmojawao? Je, walikuwa na ugomvi na mtu yeyote?” Inspekta Abel aliuliza huku akiwa ameyatuliza macho yake usoni kwa Mr. Oduya.


Mr. Oduya alimtazama Inspekta Abel kwa kitambo kidogo kisha akatingisha kichwa chake kulia na kushoto taratibu, “Hayo siwezi kuyafahamu. Walikuwa na maisha yao binafsi nje ya kazi, mimi siwezi kujua, samahani kwa hilo.”


Inspekta Abel aliachia tabasamu kisha akakohoa kidogo kusafisha koo lake kabla hajauliza, “Mr. Oduya, unaweza kuniambia hadi sasa umechukua hatua zipi, hata kuomba uchunguzi baada ya kupokea taarifa za vifo vyao? Kumbuka ndugu wa marehemu wanataka uchunguzi ufanyike...”


“Bwana Inspekta, mimi ni Mwenyekiti Mtendaji wa The Splendid Group, kampuni hii ina kampuni kubwa ishirini chini yake na zote zina wakurugenzi watendaji na mameneja, siyo jukumu langu kuchukua hatua za moja kwa moja kwa wafanyazi kwani sina ‘link’ ya moja kwa moja na wao. Mimi ni mmiliki lakini wao wana viongozi wao,” Mr. Oduya alisema kwa sauti tulivu na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Ni kweli wana viongozi wao ambao ni waajiriwa wako, kwani wewe ndiye mmiliki... kumbuka wana ndugu na wategemezi wao ambao walikuwa wanawategemea!” Inspekta Abel alisema, kisha kukawa na ukimya wa kitambo fulani kabla ya Inspekta Abel kuuvunja ule ukimya, “Na vipi kuhusu tetesi kwamba kampuni yako inawatenga ndugu wa marehemu?”


“Sijapokea malalamiko kama hayo, sijui wewe umeyapata wapi?” Mr. Oduya aliuliza huku akimtazama Inspekta Abel kwa mshangao.


“Wenyewe wanasema kuwa wanatengwa...” Inspekta Abel alisema na kuongeza, “anyway... tuyaache hayo, pia kuna mwanamume mmoja anaitwa Casmir Njoroge ambaye amejeruhiwa kwenye ajali ya taxi iliyogonga nyumba usiku wa kuamkia leo huko Sinza Mori na baadaye kukimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala. Je. Unamfahamu vipi huyu bwana?”


“Hadi sasa sifahamu chochote kuhusu mtu anayeitwa Casmir Njoroge aliyejeruhiwa kwenye ajali ya taxi, labda yeye amekwambia chochote kuhusu mimi?” Mr. Oduya aliuliza kwa sauti tulivu huku akijitahidi kuifanya sauti yake iwe ya kawaida.


“Hapana, kusema ukweli Casmir hakutwambia chochote kuhusu wewe kwani yupo chumba cha wagonjwa mahututi na hawezi kuongea, ila kuna watu wawili wamemtambua kuwa walimwona akifika na kuingia kwenye kichochoro cha nyumba ya Sammy kule Tabata Chang’ombe dakika tano tu kabla hajatoka na bomu kulipuka,” Inspekta Abel alisema huku akiilamba midomo yake.


“Sasa, labda mimi nahusikaje na mtu huyu anayehusishwa na ugaidi?” Mr. Oduya aliuliza kwa sauti iliyoonesha kuwa alikwisha anza kushindwa kuidhibiti hasira yake.


“Katika uchunguzi wetu tumegundua kuwa Casmir Njoroge anatokea nchi jirani ya Kenya na anao uhusiano wa karibu sana na mfanyakazi wako Silas Potela, kwani wote wanatoka Kenya na waliwahi kuhusishwa na vikundi vya uhalifu nchini humo, hasa kikundi cha Mungiki,” Inspekta Abel alisema huku akimtazama Mr. Oduya kwa makini.


“Bado sijaelewa, inspekta, mimi nahusikaje hapo? Silas Potela ni mfanyakazi wangu, historia yake ya yote aliyoyafanya Kenya enzi hizo hayanihusu kwa kuwa hapa kwangu anafanya kazi vizuri na ana tabia njema, pia sina uwezo wa kumzuia mfanyakazi wangu yeyote kuwa na uhusiano na mtu mwingine hata kama mtu huyo ana historia ya uhalifu huko alikotoka. Sidhani kama ni sahihi kunituhumu kwa jambo hili, bwana inspekta!” Mr. Oduya alisema kwa msisitizo huku macho yake yakiwaka kwa hasira.


“Wala hakuna mtu anayekutuhumu, bwana mkubwa... nilidhani ipo haja ya kukuona ili nipate maelezo yako juu ya kuhusishwa kwa vijana wako na matukio ya hivi karibuni ya uhalifu...” Inspekta Abel alisema na kunyamaza kidogo, akameza mate kutowesha koo lake.


“Tumegundua kuwa kwa siku za karibuni yamekuwepo mawasiliano ya simu kati ya Casmir Njoroge na wafanyakazi wako wawili, Silas Potela na dereva wako Madjid Chege, ambaye pia ana asili ya Kenya! Mawasiliano hayo yamemhusisha pia mtu mwingine kutoka Kenya, Robert Kamau, na tunadhani pia yumo humu nchini,” Inspekta Abel aliongeza huku akimtazama Mr. Oduya kwa makini.


“Inspekta, naona sasa unaanza kuvuka mipaka! Nimeshakwambia sihusiki na chochote kuhusu maisha binafsi ya wafanyakazi wangu lakini hutaki kunielewa!” Mr. Oduya alisema kwa kufoka. Kama sauti yake ilivyobadilika, sura yake pia ilikuwa imebadilika.


Kitambo cha sekunde kadhaa za ukimya kilipita, walibaki wakitumbuliana macho kwa namna ya kusomana mawazo yao. Kisha, taratibu tabasamu jipya lilianza kuchanua usoni kwa Mr. Oduya. Halikuwa tabasamu lile ambalo Inspekta Abel alilizoea. Hili lilikuwa tabasamu jembamba, lisilopendeza hata kidogo, tabasamu ambalo lilifuatiwa na swali, “Bado tu unataka maelezo zaidi, bwana inspekta?”


“Vifo vya watu watatu wanaokuhusu vimetokea, mmoja wao ametambuliwa kuhusika na uvamizi kwenye nyumba ya Sammy. Mwingine tena anayehusishwa na watu wako anapata ajali ya kutatanisha, pia amehusishwa kulipua nyumba ya Sammy. Kama unadhani utaweza kuwa na jambo la kuniambia, basi utanitafuta,” Inspekta Abel alisema na kunyanyuka.


Alisimama akamtazama Mr. Oduya kwa kitambo na kuachia tabasamu, “Natumai kupata msaada toka kwako, mzee wangu.” Akasema na kuanza kupiga hatua kuondoka huku akimwacha Mr. Oduya ameketi kimya akimsindikiza kwa macho makali wakati akitoka nje ya ofisi yake.




“Tumegundua kuwa kwa siku za karibuni yamekuwepo mawasiliano ya simu kati ya Casmir Njoroge na wafanyakazi wako wawili, Silas Potela na dereva wako Madjid Chege, ambaye pia ana asili ya Kenya! Mawasiliano hayo yamemhusisha pia mtu mwingine kutoka Kenya, Robert Kamau, na tunadhani pia yumo humu nchini,” Inspekta Abel aliongeza huku akimtazama Mr. Oduya kwa makini.


“Inspekta, naona sasa unaanza kuvuka mipaka! Nimeshakwambia sihusiki na chochote kuhusu maisha binafsi ya wafanyakazi wangu lakini hutaki kunielewa!” Mr. Oduya alisema kwa kufoka. Kama sauti yake ilivyobadilika, sura yake pia ilikuwa imebadilika.


Kitambo cha sekunde kadhaa za ukimya kilipita, walibaki wakitumbuliana macho kwa namna ya kusomana mawazo yao. Kisha, taratibu tabasamu jipya lilianza kuchanua usoni kwa Mr. Oduya. Halikuwa tabasamu lile ambalo Inspekta Abel alilizoea. Hili lilikuwa tabasamu jembamba, lisilopendeza hata kidogo, tabasamu ambalo lilifuatiwa na swali, “Bado tu unataka maelezo zaidi, bwana inspekta?”


“Vifo vya watu watatu wanaokuhusu vimetokea, mmoja wao ametambuliwa kuhusika na uvamizi kwenye nyumba ya Sammy. Mwingine tena anayehusishwa na watu wako anapata ajali ya kutatanisha, pia amehusishwa kulipua nyumba ya Sammy. Kama unadhani utaweza kuwa na jambo la kuniambia, basi utanitafuta,” Inspekta Abel alisema na kunyanyuka.


Alisimama akamtazama Mr. Oduya kwa kitambo na kuachia tabasamu, “Natumai kupata msaada toka kwako, mzee wangu.” Akasema na kuanza kupiga hatua kuondoka huku akimwacha Mr. Oduya ameketi kimya akimsindikiza kwa macho makali wakati akitoka nje ya ofisi yake.


ENDELEA...


Baada ya yule inspekta wa polisi kutoka, Mr. Oduya alijiegemeza kwenye kiti chake na kushusha pumzi ndefu. Sasa aliona kuwa mambo yalianza kwenda mrama na maji kumfika kooni. Vifo vya Dulla, Uledi na Lisa vilianza kumgeuka.


Kama hiyo haitoshi, kushtukiwa kwa Casmir Njoroge na hata Robert Kamau ambaye alikuwa hajatiwa nguvuni kulianza kumweka Mr. Oduya matatani. Sasa akili yake ilianza kufanya kazi mara mbili, aliwaza jinsi ya kujinasua toka kwenye sakata hilo huku akihisi mwili wake ukipata joto zaidi.


Alifikiria kidogo kisha akachukua simu yake ya mkononi na kutafuta namba fulani za mshirika wake muhimu aliyepo ndani ya jeshi la polisi. Alipozipata namba hizo alitaka kupiga simu lakini akashtuka na kuirudisha ile simu, kisha akachukua simu nyingine ambayo hakuwa akiitumia kwa kila mtu, bali kwa watu wachache sana na kwa mawasiliano nyeti kama yale.


Alizinakiri zile namba kisha akapiga na kuiweka sikioni. Simu ikaita mara mbili na kupokelewa. “Hallo, nahitaji sana kukuona, mkuu…” Mr. Oduya aliongea mara ile simu ilipopokelewa.


“Vipi, kuna tatizo lolote?” sauti nzito ilisikika ikiuliza toka upande wa pili wa ile simu.


“Tatizo lipo, ni kuhusu mmoja wa vijana wako, Inspekta Abel… ningeomba tuonane hata sasa hivi kama inawezekana!” Mr. Oduya alisema na kusikiliza kidogo kisha asiongeze kitu, akakata simu na kuinuka lakini kabla hajatoka akakumbuka jambo. Akatafuta namba za Spoiler na kupiga kisha akaiweka ile simu sikioni.


“Silas, ni nini sasa umefanya?” Mr. Oduya alimdaka Spoiler juu kwa juu, aliongea kwa sauti iliyoashiria hasira. Spoiler hakujibu, alibaki kimya.


“Hivi umekuwaje? Mbona umeanza kuwa mzembe kiasi hicho?” Mr. Oduya aliuliza kwa hasira.


“Usijali, mkuu, mambo yatakuwa sawa tu,” Spoiler aliongea kwa wasiwasi.


“Ninahitaji actions na siyo hizo soga zako!” Mr. Oduya alifoka. “Hivi unajua imenigharimu kiasi gani tangu uliposhindwa kutii agizo langu la kuliteketeza lile gari lililonunuliwa na Sammy?”


“Nisamehe, mkuu, naahidi kurekebisha makosa yote na kufuta kabisa ushahidi wote,” Spoiler alisema kwa kujitetea.

“Una uhakika?” Mr. Oduya aliuliza kwa sauti ya kufoka kidogo.


“Ninaamini hilo, mkuu. Kuanzia sasa nalishughulikia kwa umakini zaidi na wala jua halitakuchwa kabla sijafuta ushahidi wote,” Spoiler aliongea kwa msisitizo.


“Omba Mungu mpango huo utimie, vinginevyo hatutaelewana…” Mr. Oduya alisema kwa hasira na kukata simu kisha akaanza kupiga hatua kutoka nje, akaelekea kwenye chumba cha lifti na kushuka hadi chini. Sura yake ilionesha wazi hasira alizokuwa nazo.


Aliposhuka chini ya lile jengo alitembea taratibu huku mawazo yakiwa yamemtawala. Kitendo cha Spoiler kushindwa kizembe kukamilisha misheni aliyotumwa kilimuumiza kichwa, alianza kupoteza imani. Alielekea kwenye gari lake la kifahari aina ya Range Rover Velar la rangi nyeupe, akamkuta dereva wake Chege akimsubiri. Dakika mbili baadaye lile gari lilikuwa linayaacha maegesho yake na kuelekea mjini.


* * * * *


Baada ya kutoka katika jengo la makao makuu ya ofisi za The Splendid Group lililopo barabara ya Bagamoyo, eneo la Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, Inspekta Abel alielekea moja kwa moja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni, ya Mwananyamala.


Ilimchukua takriban dakika arobaini na tano kutoka ofisini kwa Mr. Oduya hadi Hospitali ya Mwananyamala, hali ambayo ilisababishwa na msongamano wa magari na ubovu wa barabara. Aliingia kwenye geti la kuingilia la hospitali hiyo na kwenda hadi katika viunga vya maegesho vya hospitali hiyo, akaliegesha gari lake jirani na gari nyingine aina ya Toyota Alphard jeusi lenye vioo vyenye tinted nyeusi.


Alishuka na kuanza kupiga hatua taratibu kuelekea katika jengo maalumu la wagonjwa mahututi alikolazwa Casmir Njoroge. Nje ya kile chumba maalumu cha wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu alicholazwa Casmir, alimkuta askari wake Koplo Rashid, kijana mwembamba, mrefu, aliyevalia sare rasmi za polisi, akimsubiri.


Wakati Inspekta Abel anapokewa na Koplo Rashid pale nje ya kile chumba alicholazwa Casmir, Spoiler alikuwa analifikia gari lake aina ya Toyota Alphard jeusi na kujipakia kisha akaliondoa taratibu kutoka eneo lile na kutokomea mtaani.


Mara Inspekta Abel akashangaa kumwona muuguzi wa kile chumba alicholazwa Casmir akitoka mle chumbani huku akiwa na uso uliojaa wasiwasi na kukimbilia kwenye ofisi ya daktari wa jengo lile. Kabla hajajua akamwona tena yule muuguzi akiwa ameongozana na daktari wakikimbilia kuelekea kwenye chumba alicholazwa Casmir.


“Nini kimetokea?” Inspekta Abel aliwauliza kwa wasiwasi huku akitaka kuzama ndani lakini lakini akazuiwa kwa kuwa mtu yeyote hakuruhusiwa kuingia humo muda huo. Inspekta Abel alitii na kusubiri pale nje huku akiwa na wasiwasi, alijaribu kuchungulia mle ndani kupitia kioo kidogo cha mlangoni lakini hakuweza kuona kitu


Baada ya dakika zisizopungua tano, yule daktari alitoka nje huku uso wake ukiwa umesawajika na jasho jepesi lilikuwa linamtoka usoni.


“Nini kimetokea, daktari?” Inspekta Abel aliuliza tena kwa wasiwasi. Alikuwa amepigwa na butwaa, mikono yake ilikuwa imeshika kiuno huku akimtazama yule daktari kwa makini. “Ni nini kimetokea?” akauliza tena baada ya kuona hajibiwi.

“Nashangaa, hali ya mgonjwa ilikuwa inaanza kuimarika vizuri na muda mfupi tu uliopita nilimwona, lakini imebadilika ghafla na mapigo ya moyo wake kushuka isivyo kawaida...” yule daktari alisema kwa huzuni na kunyamaza kidogo.




Inspekta Abel alimtazama kwa makini, moyo wake ulipiga kite kwa nguvu, alianza kuomba Mungu ili hali isiendelee kuwa mbaya zaidi, kwani alimhitaji sana Casmir ili kukamilisha kesi yake.


“Kwa hiyo, unataka kuniambia nini, daktari?” Inspekta Abel aliuliza huku akiwa ameyatuliza macho yake kwenye uso wa daktari.


“Tumeshindwa kuyaokoa maisha yake... amefariki dunia,” yule daktari alisema, uso wake ulikuwa umejawa na mashaka na woga.


Ilikuwa ni kama pigo la kisu likipenya mwilini na kuujeruhi moyo wa Inspekta Abel. Katika yote aliyoyatarajia asubuhi hiyo, taarifa ya kifo cha Casmir haikuwamo kabisa akilini mwake. Alimtazama yule daktari kama aliyekuwa anataka ufafanuzi juu ya kifo cha Casmir, akili yake ilikuwa inakataa kabisa kuipokea ile taarifa.


“Ni kweli amekufa, bwana inspekta,” yule daktari alijibu shaka ya Inspekta Abel baada ya kuisoma katika macho yake.

Bila kujua atendalo, Inspekta Abel alijikuta akimkwida yule daktari kwa mikono yake yenye nguvu na kumbana kwa vidole vyake huku akimsogeza karibu yake na kumtazama kwa hasira. “Kwa nini amekufa?” alimuuliza yule daktari akiwa amemkazia macho.


Yule daktari alipigwa na butwaa, alijaribu kujitoa katika mikono yenye nguvu ya Inspekta Abel, hata hivyo ilikuwa ni sawa na kujaribu kujitoa toka katika pingu. Kila alivyojaribu kujitoa ndivyo vidole vya Inspekta Abel vilivyozidi kudidimia katika ngozi yake. Licha ya kuwa alihisi maumivu makali lakini hali ile ilimshangaza zaidi.


“Unaniumiza, Inspekta,” yule daktari alimwambia Inspekta Abel huku akimtazama usoni kwa wasiwasi. Alikuwa amekunja ndita na jasho likimchuruzika usoni.


Ndiyo kwanza Inspekta Abel akashtuka baada ya kugundua kuwa alikuwa amemkwida yule daktari. Alimwachia huku akiomba radhi. “Nisamehe sana daktari, nilichanganyikiwa maana huyu mtu alikuwa muhimu sana kwenye kesi yangu!”


“Najua, lakini ndiyo mapenzi ya Mungu, mimi ni nani hadi nipingane na mapenzi yake?” yule daktari alisema kwa sauti tulivu. Inspekta Abel alibaki kimya akiwa ameduwaa.


* * * * *


Katika viunga vya maegesho ya magari vya klabu ya mabilionea na vigogo wa serikalini ya Paradise Club, Mr. Oduya na kigogo mmoja wa jeshi la polisi walikuwa wameketi kwenye siti ya nyuma ndani ya gari la kifahari aina ya Range Rover Velar la Mr. Oduya. Gari lile lilikuwa linanguruma taratibu na ndani ya lile gari walikuwa wamebakia wao wawili tu.


Yule kigogo wa polisi alikuwa amefika pale Paradise Club akitembea kwa miguu baada ya kumwacha dereva wake katika viunga vya maegesho ya magari vya jengo la mbele la hoteli ya kitalii ya Udzungwa Beach Resort. Hakutaka mtu mwingine ajue kama alikuwa amefika pale kuonana na Mr. Oduya.


Muda huo Mr. Oduya alikuwa ameketi kwa kukunja mguu wake wa kulia na alikuwa akimtazama yule kigogo wa polisi katika namna ya kuhitaji msaada. Uso wake ulionesha kuwa alikuwa ameelemewa na fikra za kukata tamaa.


“Hofu yako ni kwamba, unahisi Inspekta Abel anaweza kuwa amepata ushahidi kamili kukuhusu?” yule kigogo wa polisi alimuuliza Mr. Oduya huku akimtazama kwa makini.


“Sijajua...” Mr. Oduya alisema kwa wasiwasi na kushusha pumzi za ndani kwa ndani. “Ila ni wazi huyu inspekta amekuwa mtu wa kumtazama kwa ukaribu sana, anaweza kuwa hatari zaidi ya yule binti wa usalama wa taifa.”


“Kwa nini unadhani hivyo?” yule kigogo wa polisi aliuliza tena kwa sauti tulivu.


“Kwa sababu yeye ameweza kupiga hatua kwa kuunganisha matukio jambo linaloonesha kuwa amegundua uhusiano uliopo kati yangu na watu waliofanya uhalifu huo. Kitu ambacho bado sina uhakika ni kama ameshagundua uhusiano uliopo kati yangu na wewe,” Mr. Oduya alisema kwa wasiwasi.


Yule kigogo wa polisi alitulia kidogo akitafakari, kisha alikohoa kidogo kusafisha koo lake. “Kwa hiyo, unafikiriaje? Nadhani atakuwa anakushuku tu lakini hana kithibitisho chochote cha kukutia hatiani,” alisema na kuongeza, “Tunachopaswa kufanya ni kuhakikisha hapati anachokitafuta.”


“Hilo ndilo neno! Na ninadhani, kama inawezekana, anyamazishwe mapema! Sijui tutafanyaje?” Mr. Oduya aliuliza huku akimtulizia macho yule kigogo wa polisi.


“Mr. Oduya, you are not serious, brother! Unadhani utaua wangapi?” yule kigogo wa polisi alisema huku akimtazama Mr. Oduya kwa mshangao. Kisha kikaibuka kitambo kifupi cha ukimya, kila mmoja alionekana kufikiria kwa muda na kushusha pumzi.


“Sioni namna nyingine ya kufanya ili kuepuka janga hili, kumbuka kuwa akizidi kuchimba kiundani basi hata wewe huwezi kukwepa kwenye hili, ndiyo maana nadhani kuwa yeyote atakayekaa mbele yetu anapaswa kunyamazishwa haraka!” Mr. Oduya alisema baada ya kitambo kile cha ukimya.


“Hapana, sidhani kama kuua litakuwa jambo jema, kwani hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwako kuliko hata kwangu!” yule kigogo wa polisi alishauri.


“Sasa tutafanyaje wakati naona maji yanaanza kuzidi unga?” Mr. Oduya aliuliza kwa sauti yenye mchanganyiko wa hasira na wasiwasi.


Yule kigogo wa polisi aliwaza kidogo kisha akasema, “Wacha niende, hadi nikifika ofisini kwangu nitakuwa nimeshapata jibu!” yule kigogo wa polisi alisema kisha akaangalia huku na kule ili kuhakikisha hakuna mtu aliyemwona, akashuka haraka toka ndani ya gari la Mr. Oduya na kuondoka.


Muda huohuo simu ya Mr. Oduya ikaanza kuita. Mr. Oduya aliitazama kwa makini na kuliona jina la Spoiler. Akaipokea ile simu mara moja na kuipeleka kwenye sikio lake. ”Niambie!” alisema kwa sauti tulivu huku akiilamba midomo yake iliyoanza kukauka.


“Nimekamilisha kila kitu, mzee. Casmir amekufa,” Spoiler alisema kwenye simu kwa sauti ya ushindi.


“Una uhakika?” Mr. Oduya aliuliza kwa sauti iliyoonesha kutoamini kile alichokuwa akiambiwa.


“Ninao uhakika, mzee... daktari aliyekuwa anamhudumia ndiye ameifanya kazi hiyo kwa umakini na amenihakikishia. Nimetoka kuongea naye sasa hivi kwenye simu, ameniambia kuwa Inspekta Abel amechanganyikiwa kwelikweli baada ya kuambiwa kuhusu kifo cha Casmir!” Spoiler alisema huku akiachia kicheko hafifu.


“Okay, hiyo ni habari nzuri. Sasa nataka na yule binti anayejitia mpelelezi wa kimataifa afuate. Hakikisha unampata kabla jua halijatua,” Mr. Oduya alisema kisha simu ikakatwa.


Endelea kufuatilia simulizi hii ya kusisimua ili kuujua mwisho wake...




“Mr. Oduya, you are not serious, brother! Unadhani utaua wangapi?” yule kigogo wa polisi alisema huku akimtazama Mr. Oduya kwa mshangao. Kisha kikaibuka kitambo kifupi cha ukimya, kila mmoja alionekana kufikiria kwa muda na kushusha pumzi.


“Sioni namna nyingine ya kufanya ili kuepuka janga hili, kumbuka kuwa akizidi kuchimba kiundani basi hata wewe huwezi kukwepa kwenye hili, ndiyo maana nadhani kuwa yeyote atakayekaa mbele yetu anapaswa kunyamazishwa haraka!” Mr. Oduya alisema baada ya kitambo kile cha ukimya.


“Hapana, sidhani kama kuua litakuwa jambo jema, kwani hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwako kuliko hata kwangu!” yule kigogo wa polisi alishauri.


“Sasa tutafanyaje wakati naona maji yanaanza kuzidi unga?” Mr. Oduya aliuliza kwa sauti yenye mchanganyiko wa hasira na wasiwasi.


Yule kigogo wa polisi aliwaza kidogo kisha akasema, “Wacha niende, hadi nikifika ofisini kwangu nitakuwa nimeshapata jibu!” yule kigogo wa polisi alisema kisha akaangalia huku na kule ili kuhakikisha hakuna mtu aliyemwona, akashuka haraka toka ndani ya gari la Mr. Oduya na kuondoka.


Muda huohuo simu ya Mr. Oduya ikaanza kuita. Mr. Oduya aliitazama kwa makini na kuliona jina la Spoiler. Akaipokea ile simu mara moja na kuipeleka kwenye sikio lake. ”Niambie!” alisema kwa sauti tulivu huku akiilamba midomo yake iliyoanza kukauka.


“Nimekamilisha kila kitu, mzee. Casmir amekufa,” Spoiler alisema kwenye simu kwa sauti ya ushindi.


“Una uhakika?” Mr. Oduya aliuliza kwa sauti iliyoonesha kutoamini kile alichokuwa akiambiwa.


“Ninao uhakika, mzee... daktari aliyekuwa anamhudumia ndiye ameifanya kazi hiyo kwa umakini na amenihakikishia. Nimetoka kuongea naye sasa hivi kwenye simu, ameniambia kuwa Inspekta Abel amechanganyikiwa kwelikweli baada ya kuambiwa kuhusu kifo cha Casmir!” Spoiler alisema huku akiachia kicheko hafifu.


ENDELEA...


“Okay, hiyo ni habari nzuri. Sasa nataka na yule binti anayejiita mpelelezi wa kimataifa naye afuate njia hiyo hiyo. Hakikisha anapatikana kabla jua halijatua,” Mr. Oduya alisema kisha simu ikakatwa. Aliwaza kidogo na kutafuta namba ya Robert Kamau kwenye simu yake, alipoipata akapiga simu na kuiweka sikioni. Ile simu ikaita mara tatu na kupokelewa.


“Rob, upo wapi?” Mr. Oduya aliuliza pasipo hata salamu.


“Bado nipo hapa hotelini Udzungwa Beach Resort, nipo na Tom, mkuu,” Job alijibu.


“Naona sasa kazi imekushinda! Umeamua kulala tu, hujui hiyo fedha unayolipwa inatokana na kazi gani?” Mr. Oduya aliuliza kwa hasira na kumfanya Job aduwae kidogo.


“Najua, mkuu,” Robert alijibu kwa sauti tulivu.


“Okay, mwambie Tom ninawahitaji haraka sana hapa Paradise Club, mkifika getini jitambulisheni kuwa ni wageni wa PC.008.19, hakikisheni mnafika hapa ndani ya dakika tano tu, hatuna muda wa kupoteza,” Mr. Oduya aliongea na kukata simu.


* * * * *


Saa tatu asubuhi, kwenye sebule kubwa ya kifahari iliyo katika mazingira ya upweke, eneo la Kinyerezi, sebule yote ilikuwa imetulia sana na wanaume watatu walikuwa wakimwangalia Tunu kwa mshangao mkubwa. Macho yao yalikuwa yametulia yakimtazama usoni. Tunu alikuwa ameketi kwenye sofa akiwa amekunja nne na mikono yake ikiwa imepakata laptop yake.


Japo Tunu alikuwa akiwaangalia kwa tabasamu na mwili wake ukiwa umetulia kwenye sofa, lakini moyo wake ulikuwa unakita kwa nguvu kifuani kwake na akili yake ilikuwa mbali sana. Akili yake ilikuwa nje ya zile kuta nne za ile sebule.


Hali hii ilikuwa imejitokeza baada ya wote kushuhudia mambo ya kutisha kwenye ile memory card baada ya kupachikwa kwenye laptop ya Tunu.


Walikuwa wamesikiliza mazungumzo ya simu kati ya Mr. Oduya na kigogo mmoja wa jeshi la polisi, waliokuwa wanapanga mikakati ya jinsi ya kumteka nyara Jaji Lutego kwa kumtumia mwanadada Lisa, na kisha kutekeleza mauaji yake. Yule kigogo wa polisi alibainisha kuwa alikwishaandaa mipango yote na alikuwa na uhakika Jaji Lutego angenasa kwenye mtego.


“Jesus Christ!” Bob alijikuta akiropoka kwa mshangao mkubwa baada ya kuyasikia yale mazungumzo. “Una hakika kabisa zile sauti ni za Mr. Oduya na Kamishna Omalla, Mkuu wa Kamisheni ya Intelijensia wa Jeshi la Polisi? Siyo kwamba kuna watu wametumia teknolojia wakatengeneza sauti zinazofanana na zao?”


“Hiki si kitu cha kutengeneza, Bob. Hizi ni sauti zao za kweli. Niliyanasa mazungumzo yao mimi mwenyewe kwa kutumia simu yangu,” Tunu alisema huku akiachia tabasamu.


“Dah! Nimeishiwa kabisa nguvu!” Bob alisema huku akipiga mluzi mdogo, mshangao ulikuwa bado haujamtoka usoni.


Baada ya yale mazungumzo ya simu kati ya Mr. Oduya na kigogo wa jeshi la polisi, Tunu aliwawekea video iliyomwonesha Jaji Lutego akipata mateso makali na baadaye kuuawa kinyama. Katika video hiyo, Mr. Oduya alionekana katika picha ndogo akiwasiliana kwa mfumo wa Videotelephony na watu aliowapa kazi ya kuua, waliokuwa katika eneo ambalo halikujulikana.


Mr. Oduya ambaye hakuwa katika eneo la tukio alionekana akitaka kujionea kwa macho yake jinsi jaji huyo alivyokuwa akiteswa kabla ya kifo chake. Alimsomea Jaji Lutego mashtaka yake kama aliyekuwa mahakamani akihukumu kesi, kisha akawaamuru watu wake kummaliza. Dulla na Uledi wakamwelekezea Jaji Lutego bastola zao, wakammiminia risasi nyingi mwilini na walipohakikisha amekufa wakamwekwa kwenye mfuko na kumpakia kwenye buti la gari aina ya Cadillac DeVille lenye muundo wa kizamani. Haikueleweka mwili wake waliupeleka wapi ule.


Video ile iliishia pale Mr. Oduya mwenye furaha alipotamka, “Good bye, my dear judge. This is a die-or-survive world!”


“Na hii video, una uhakika si ya kutengeneza?” Tom aliuliza huku akizidi kushangaa.


“Ndiyo,” Tunu alisema kwa utulivu huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Mimi sina mengi sana ya kutaka kujua isipokuwa hili moja tu... uliwezaje kuyarekodi matukio hayo yote pasipo kushtukiwa?” Tom aliuliza huku akimimina mvinyo aina ya Madeira kwenye bilauri ya Tunu iliyokuwa tupu.


Tunu alimwangalia Tom kwa makini na kuachia tabasamu pana, kisha akawaelezea kisa kizima aliporudi toka Israel na kupata taarifa za mauaji ya rafiki yake Layla, waliyesoma darasa moja katika Shule ya Jangwani, alivyoumia sana kujiingiza kufanya uchunguzi baada ya kuhisi polisi hawakutaka kujishughulisha na kesi hiyo kwa kuwa aliyefanya hivyo alikuwa mtoto wa bilionea.


Alieleza alivyojipenyeza na baadaye kuajiriwa kwenye kampuni ya Mr. Oduya na baadaye kuhamishiwa makao makuu ya kampuni ya The Splendid Group kama mkuu wa kitengo cha ‘tehama’ kutokana na taaluma yake ya Computer System Analysis.


Kwa kutumia laptop yake iliyokuwa na mfumo maalumu wa udukuzi wa taarifa, Tunu aliweza kutengeneza kirusi maalumu aina ya Trojans alichokituma kuiba taarifa za siri za kampuni hiyo baada ya kukituma kwenye kompyuta alizozichagua za kampuni hiyo kikiwa kama keyloggers na RAT (Remote Administration Tools), na aliweza kupata taarifa baada ya mtu kubonyeza kwenye keyboard yake, na bila kujua akawa amekiingiza kwenye mfumo bila kujua na kutuma taarifa zote nyeti kwenye laptop ya Tunu.





Hakuishia hapo, alifanikiwa pia kudukua mawasiliano katika simu ya Mr. Oduya na kuweza kusikiliza maongezi yote kutoka simu zote ambazo Mr. Oduya alikuwa anapiga au kupigiwa. Hapo ndipo alipogundua mambo ya kutisha yaliyokaribia kuyagharimu Maisha yake baada ya kugunduliwa kuwa ni shushushu.


“Hebu subiri kidogo, Tunu... How did you get Oduya’s phone?” Tom aliuliza akiwa katika mshangao mkubwa.


“Kwa mtu mwenye taaluma kama yangu ni rahisi sana, wala sikuhitaji hata kuigusa simu yake bali nilihitaji kujua namba yake tu ya simu, kisha nikamaliza kazi,” Tunu alisema huku akitabasamu.


“Sasa walijuaje kama wewe ni shushushu?” Tom aliuliza tena akiwa bado ana mshangao mkubwa.


“Ex-boyfriend wangu, Nelson Mtokambali ndiye aliyewafanya watambue kuwa mimi ni shushushu baada ya kunikuta ofisini kwa Mr. Oduya. Sikujua kuwa Nelson alikuwa mshirika na mmoja wa watu wa Mr. Oduya. Tena siku aliyonikuta ndiyo siku ile ile niliyofanikiwa kudukua hizi taarifa,” Tunu alieleza.


“Na hiyo memory card ilifikaje kwenye lile gari la kizamani aina ya Cadillac DeVille?” Tom aliuliza tena akionekana kuwa na shauku kubwa.


“Ni hadithi ndefu kidogo, nitaieleza siku nyingine lakini naomba tu ufahamu kwamba, kama nisingeshtuka mapema huenda sasa ningekuwa marehemu, maana Mr. Oduya ni mtu hatari sana tofauti na wengi wanavyomchukulia,” Tunu alisema na kushusha pumzi ndefu, akanyanyua bilauri ya mvinyo na kugida mvinyo wote uliokuwemo ndani ya ile bilauri, kisha akaikita ile bilauri juu ya meza huku akiusikilizia ule mvinyo ulivyokuwa ukisafiri kwenye koo lake na kutua tumboni.


“Hongera, ulifanya jambo zuri na kubwa sana,” Tom alisema huku akivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu.


“This is what I’ve been looking for three years... ni moja ya kazi ambazo zimekuwa ngumu sana kwangu na kukaribia kuyagharimu maisha yangu, lakini siku zote Mungu amekuwa upande wangu,” Tunu alisema kwa furaha.


Mara simu yake ya mkononi ikaanza kuita. Tunu aliitazama ile simu kwa makini na kuliona jina la Victoria, mke wa Elli. Hisia za hofu, kitu ambacho kwa kawaida kilitokea kwa nadra sana katika damu yake, zilianza kumnyemelea. Tunu aliikodolea macho ile simu kana kwamba alikuwa ameona guruneti la kutupa kwa mkono, akili yake taratibu ikaanza kuzama kwenye kuwaza kuwa huenda jambo baya lilikuwa limetokea.


Kilichomtia hofu Tunu ni kwamba hakuwa tayari kupokea taarifa yoyote mbaya kumhusu Sammy wala familia yake. Aliendelea kuitazama ile simu kwa wasiwasi, hata hivyo, hakutaka kuendelea kuiacha ile simu iendelee kuita zaidi kwani ilikuwa mbioni kukatika baada ya kuita kwa muda mrefu. Haraka akaipokea na kukiweka sikioni huku akiipa akili yake utulivu wa hali ya juu.


“Hallo!” Tunu alisema mara tu alipoiweka ile simu sikioni na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Hallow, habari za asubuhi, dada?” Victoria aliongea kwa sauti iliyoonesha kujawa na furaha. Tunu aliihisi ile furaha kwenye sauti ya Victoria upande wa pili wa simu.


Kitendo cha kuisikia sauti adimu ya Victoria ikiwa na furaha kikamfanya Tunu ameze funda kubwa la mate kuutuliza mtima wake huku akianza kuhisi ahueni fulani.


“Nzuri, dada, nipe taarifa za huko,” Tunu aliongea huku ile hofu ikianza kupotea.


“Huku kwema kabisa. Vipi unaendeleaje na mambo yako?”


“Namshukuru Mungu nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa...”


“Okay! Nilitaka kukujulia hali na pia kukujulisha kuhusu maendeleo ya wagonjwa wetu. Nimepigiwa simu asubuhi hii na Elli kuwa Sammy ameweza kuamka ingawa hajaanza kuongea, madaktari wamefanikiwa kuyaokoa maisha yake na sasa hana tena tishio kubwa la kiafya...” Victoria alisema na kumfanya Tunu aruke juu kwa furaha.


“Oh, thanks God!” Tunu alisema kwa sauti yenye kitetemeshi huku machozi ya furaha yakimtoka machoni. Watu wote pale sebuleni walimtazama kwa mshangao uliochanganyikana na shauku ya kutaka kujua kilichomfanya atokwe na machozi. “Thanks God!” alisema tena na kushusha pumzi. Kisha kikatokea kitambo kifupi cha ukimya.


“Vipi kuhusu Joyce?” Tunu aliuliza huku akifuta machozi yaliyokuwa yakimtoka machoni kwake.


“Hali yake imezidi kuimarika, nimepata taarifa kuwa leo madaktari wanamruhusu...” Victoria alisema kwa sauti tulivu lakini yenye furaha.


“Oh, Mungu amsaidie...” Tunu alisema kwa furaha. “Nitapenda kuja kumwona baadaye, nadhani atakuwa hapo kwako?”


“Hapana, atakuwa kwa mama yake, Madame Norah,” Victoria alisema na kumfanya Tunu ashangae kidogo.


“Joyce ni mtoto wa Madame Norah?” Tunu aliuliza ili kupata uhakika, alidhani labda hakuwa amesikia vizuri.


“Ndiyo, ingawa hili tumelijua jana tu na wala Joyce mwenyewe bado hajui kama Madame Norah ndiye mama yake mzazi,” Victoria alisema, maneno yaliyozidi kumshangaza Tunu.


“Kivipi? Mbona sielewi?”


“Ni hadithi ndefu kidogo, ukipata nafasi nitakuelezea...” Victoria alisema na kushusha pumzi.


“Sawa, nitakuja mchana hapo nyumbani tuongee, kwa sasa kuna mambo fulanifulani natakiwa kuyakamilisha,” Tunu alisema kwa furaha kisha wakaagana. Akakata simu.


* * * * *


Gari la Inspekta Abel liliondoka taratibu na kuyaacha maegesho ya magari katika Hospitali ya Mwananyamala. Koplo Rashid ndiye aliyekuwa anaendesha gari na Inspekta Abel alikuwa ameketi kushoto kwake akiwa mtulivu sana. Muda wote akili ya Inspekta Abel ilikuwa kazini ikijaribu kupambanua hili na lile ili kupata jibu endapo kifo cha Casmir kilikuwa kimetokana na hali yake kiafya kudhorota au ulikuwa ni mpango wa mauaji ili asiweze kutoa siri.



Japokuwa katika katika kesi ile Inspekta Abel alikuwa akifanya kazi na Sajenti Mapunda lakini kwenye safari hiyo aliamua kuambatana na Koplo Rashid, ambaye vilevile alikuwa komando wa daraja la pili, kwa kuwa alimwamini zaidi ya askari wengine wa kada yake.


Gari lao lilipotoka kwenye geti la kutokea la hospitali ile ya Mwananyamala Koplo Rashid alikata kona na kuingia upande wa kushoto akiifuata barabara iliyokwenda kuungana na barabara ya Mwinjuma. Walipofika kwenye makutano ya barabara zile wakaingia kushoto wakiifuata barabara ya Mwinjuma iliyokuwa inakwenda Kinondoni. Muda ule wa asubuhi barabara ya Mwinjuma ilikuwa na magari mengi.


Inspekta Abel alikusudia kuelekea katika Hospitali ya Amana ili kuonana na Joyce, katika harakati ya kutaka kupata maelezo zaidi ya kumsaidia katika ile kesi.


Kwa kupitia barabara ile ya Mwinjuma, iliwachukua takriban dakika arobaini na tano, badala ya dakika ishirini, kutoka katika Hospitali ya Mwananyamala hadi kuifikia barabara ya Kawawa, katika eneo la Kinondoni Studio. Hali ile ilikuwa imesababishwa na msongamano wa magari katika barabara ile, hasa daladala.


Taa za kuongea magari barabarani ziliwaruhusu, wakati wakiingia katika barabara ya Kawawa ili kuelekea Ilala, gari kubwa la mizigo aina ya Tata Daewoo likatokea mbele yao kwa mwendo wa kasi na kuwabamiza kwa mbele. Lile gari lilikuwa likitokea katika mtaa wa Togo.


Kitendo kile cha kugongwa kilisababisha sauti ya mshindo mkubwa na moshi mzito ukaanza kufuka toka kwenye boneti la gari lile la polisi ambalo lilikuwa halitamaniki kabisa. Eneo lile likageuka kuwa sehemu ya vurumai na mshikemshike.


Koplo Rashid aliyekuwa kwenye usukani aliumia kichwani na alikuwa anavuja damu katika eneo la kichwa, japo si kwa wingi sana ingawa alikuwa hoi kwa maumivu. Inspekta Abel alikuwa amejeruhiwa zaidi kwa kuwa upande aliokuwa ameketi ndiko ambako lile gari lao lilikuwa limebamizwa zaidi kiasi cha kupinda. Alikuwa amepoteza fahamu na alivuja damu nyingi kichwani na nyingine zilimtoka mdomoni.


Ndani ya lile gari kubwa aina ya Tata Daewoo kulikuwa na mtu mmoja tu aliyekuwa akiliendesha lile gari, alikuwa amevaa kofia pana nyeusi aina ya pama, miwani myeusi mikubwa ya jua iliyoyaficha macho yake na glavu maalumu mikononi mwake. Hakutaka kusimama baada ya kusababisha ajali, aliliendesha gari lake kama aliyepandwa na kichaa na kuvuka barabara ya Kawawa kisha akaingia katika barabara ya Mwinjuma akielekea upande wa Mwananyamala na kuongeza mwendo.


Askari wawili wa usalama barabarani waliokuwepo eneo lile na kuishuhudia ile ajali ya kiutisha waliwasiliana na wenzao waliokuwa katika eneo la Mwananyamala ‘A’ ili wahakikishe yule dereva wa lile gari aina ya Tata Daewoo anatiwa mbaroni. Kisha wao wakatafuta gari nyingine harakaharaka na kuwaingia wale majeruhi ili kuwawahisha hospitali.


Yule dereva wa lile gari kubwa aina ya Tata Daewoo alipofanikiwa kukimbia eneo la tuklio aliendesha kwa mweno wa kasi huku akipishana na magari mengine yaliyokuwa yakitokea eneo la Mwananyamala ‘A’ na alipofika katika eneo la baa ta MK Grand, akakata kona na kuingia kulia akiufuata mtaa wa Kasaba, alikuwa bado katika mwendo wa kasi. Baada ya mwendo wa kama dakika mbili alifika katika baa ya Pachoto, akashuka na kulitelekeza lile gari huku yeye akipotelea uchochoroni, asijulikane alikoelekea.


Dakika iliyofuata pikipiki mbili na gari moja dogo zilifika hapo, askari watatu waliteremka haraka na kulizunguka lile gari lakini dereva alikuwa amekwishatoweka. Walipolikagua vizuri lile hgari wakagundua kuwa nyuma ya lile gari kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa hana fahamu akidhaniwa kuchomwa kiasi kikubwa cha dawa maalumu za kupumbaza akili yake ili asiweze kutambua kitu.


* * * * *


Katika Hospitali ya Amana, Joyce na Bi. Pamela walikuwa wameketi kwa utulivu mkubwa wakimsubiri Madame Norah aliyekuwa amefuata dawa ambazo Joyce alitakiwa kuondoka nazo na kwenda kutumia nyumbani baada ya kuruhusiwa, hii ilikuwa ni baada ya daktari wa zamu kumwandikia Joyce ruhusa ya kwenda kuugulia nyumbani baada ya hali yake kiafya kuimarika.


Hadi muda ule bado Joyce alikuwa ana maswali mengi kichwani kwake ambayo hakuwa ameyapatia majibu. Alikuwa akimwangalia mama yake Bi. Pamela kwa macho yaliyojaribu kuuliza mambo mengi lakini Bi. Pamela alikuwa akiyakwepa macho ya Joyce, kwa kuwa hakuwa tayari kuyajibu maswali yake kwa muda ule. Muda wote alijaribu kumtaka Joyce avute subira na muda si mrefu angefahamu kila kitu, baada ya kufika nyumbani.


Akiwa katika wakati mgumu wa kuendelea kuyakwepa macho ya Joyce mara alimwona Madame Norah akirejea na kuwataka waondoke na kuelekea kule alikokuwa ameegesha gari lake la kifahari aina ya Mercedes Benz E-class limousine jeusi la milango sita.


Walipoingia dereva aliliondoa gari, likatoka kwenye geti la kuingilia la Hospitali ya Amana na kukata kushoto kisha likaifuata barabara iliyokwenda kuungana na barabara ya Uhuru katika eneo la Amana Vijana, kisha dereva akakunja tena kuingia upande wa kushoto akiifuata barabara ya Uhuru. Joyce akashangaa sana maana hakujua walikuwa wanaelekea wapi.


Hata hivyo aliamua kubaki kimya tu akiwatazama Bi. Pamela na Madame Norah kwa kuibia bila kusema lolote. Wote walikuwa kimya kabisa. Lile gari lilipofika eneo la vianda vya wasusi wa Kimasai likaingia kushoto likiufuata mtaa wa Mafao na kuyapita maghorofa ya Ilala kisha likatokea katika barabara ya Kawawa, hapo dereva akaingia upande wa kushoto akiifuata barabara ya Kawawa kama anaelekea Magomeni.


Endelea kuwemo kwenye safari hii ya kusisimua ya ???? ili kuufahamu mwisho wake...




Katika Hospitali ya Amana, Joyce na Bi. Pamela walikuwa wameketi kwa utulivu mkubwa wakimsubiri Madame Norah aliyekuwa amefuata dawa ambazo Joyce alitakiwa kuondoka nazo na kwenda kutumia nyumbani baada ya kuruhusiwa, hii ilikuwa ni baada ya daktari wa zamu kumwandikia Joyce ruhusa ya kwenda kuugulia nyumbani baada ya hali yake kiafya kuimarika.


Hadi muda ule bado Joyce alikuwa ana maswali mengi kichwani kwake ambayo hakuwa ameyapatia majibu. Alikuwa akimwangalia mama yake Bi. Pamela kwa macho yaliyojaribu kuuliza mambo mengi lakini Bi. Pamela alikuwa akiyakwepa macho ya Joyce, kwa kuwa hakuwa tayari kuyajibu maswali yake kwa muda ule. Muda wote alijaribu kumtaka Joyce avute subira na muda si mrefu angefahamu kila kitu, baada ya kufika nyumbani.


Akiwa katika wakati mgumu wa kuendelea kuyakwepa macho ya Joyce mara alimwona Madame Norah akirejea na kuwataka waondoke na kuelekea kule alikokuwa ameegesha gari lake la kifahari aina ya Mercedes Benz E-class limousine jeusi la milango sita.


Walipoingia dereva aliliondoa gari, likatoka kwenye geti la kuingilia la Hospitali ya Amana na kukata kushoto kisha likaifuata barabara iliyokwenda kuungana na barabara ya Uhuru katika eneo la Amana Vijana, kisha dereva akakunja tena kuingia upande wa kushoto akiifuata barabara ya Uhuru. Joyce akashangaa sana maana hakujua walikuwa wanaelekea wapi.


Hata hivyo aliamua kubaki kimya tu akiwatazama Bi. Pamela na Madame Norah kwa kuibia bila kusema lolote. Wote walikuwa kimya kabisa. Lile gari lilipofika eneo la vianda vya wasusi wa Kimasai likaingia kushoto likiufuata mtaa wa Mafao na kuyapita maghorofa ya Ilala kisha likatokea katika barabara ya Kawawa, hapo dereva akaingia upande wa kushoto akiifuata barabara ya Kawawa kama anaelekea Magomeni.


ENDELEA...


Joyce aliendelea kuwa kimya akijaribu kutafakari, muda wote macho yake yalikuwa yakiangalia nje wakati gari waliloabiri likipita katika eneo la Msimbazi Centre, kisha likavuka eneo la Kigogo Sambusa na baadaye Kigogo Mbuyuni, kwenye mzunguko wa barabara za Kawawa na ile ya Kigogo. Kutoka hapo wakaanza kuteremsha katika bonde la Msimbazi na kuibukia Magomeni Mikumi na baadaye waliivuka Barabara ya Morogoro.


Bado Joyce hakujua walikuwa wakielekea wapi, kuanzia hapo alianza kuzama kwenye lindo la mawazo, alijiuliza ni nini kilikuwa kimemtokea Sammy? Kitendo cha kutomwona akimtembelea hospitali kilizidi kumshangaza sana Joyce, alihisi labda Sammy alikuwa bado ana kinyongo kutokana na kile alichokuwa amemweleza, juu ya mwanamuziki Dynamo Plus. Hata hivyo, Joyce aliamini kuwa Sammy hakuwa mtu wa kinyongo bali lilikuwepo jambo ambalo hakuwa akilijua.


Mawazo kibao yaliendelea kupita kichwani kwake kiasi kwamba hakuweza kukumbuka kitu kingine chochote na alipokuja kuzinduka tayari lile gari lilikuwa limesimama mbele ya geti kubwa katika jumba la kifahari la Madame Norah lililopo ufukweni mwa Bahari ya Hindi eneo la Mikocheni.


Joyce aliyatazama vizuri mandhari ya kuvutia ya jumba lile yaliyozungukwa na miti mirefu na mikubwa ya kivuli aina ya ‘Quercus virginiana’ na barabara ya lami yenye usafi wa hali ya juu iliyokuwa ikieleka katika jumba hilo na kupandwa miti ya kivuli iliyovutia na maua aina ya ‘lotus’. Baada ya kuyaona mandhari yale ndipo alipoweza kugundua kuwa alikuwa amepelekwa Mikocheni nyumbani kwa Madame Norah. Joyce akazidi kushangaa.


Joyce hakutaka kuendelea kuumiza kichwa chake kwa maswali yasiyo na majibu, sasa aliazimia kuufahamu ukweli, kwa njia yoyote ile. Aligoma kushuka kwenye gari akitaka aelezwe kwanza ukweli wote kuhusu yote yaliyotokea wakati alipokuwa hana fahamu, na aelezwe Sammy yupo wapi na kwa nini waliamua kumleta pale nyumbani kwa Madame Norah badala ya kumpeleka nyumbani kwake, Tabata Chang’ombe.


Madame Norah na Bi. Pamela waliangaliana katika namna ya kuulizana kama walipaswa kumwambia chochote muda huo, kisha Bi. Pamela akashusha pumzi za ndani huku akionekana kusita sana. Hata hivyo, hawakuwa na namna nyingine ya kumshawishi ili ashuke kwenye gari.


Madame Norah alinyanyua mabega yake juu na kuyashusha huku akiminya midomo yake. Akajaribu kumwomba Joyce aingie kwanza ndani na mambo mengine wangeyazungumza wakiwa ndani lakini Joyce alikataa katakata akitaka aelezwe ukweli wote ndipo aamue kama angeingia ndani au lah.


“Tumeamua kukuleta hapa kwa sababu ndipo nyumbani kwenu, kwa mama yako,” Madame Norah alisema baada ya kufikiria sana. Hakuwa na namna nyingine isipokuwa kumweleza ukweli.


“Nyumbani kwa mama yangu kivipi?” Joyce aliuliza kwa mshangao huku akiwatazama Madame Norah na Bi. Pamela kwa zamu.


“Labda kitu ambacho hujajua ni kwamba Madame Norah ndiye mama’ako mzazi,” Bi. Pamela alisema kwa sauti tulivu.

“Mama’angu mzazi!” Joyce aliuliza kwa mshangao. “Ni mama’angu tangu lini? Mbona sijawahi kuambiwa kuhusu jambo hili! Na vipi kuhusu wewe, mama?”


“Ni hadithi ndefu kidogo, mwanangu. Ila kwa kifupi ni kwamba Madame Norah ndiye mama’ako mzazi. Mimi si mama’ako mzazi ingawa ndiye niliyekulea tangu utoto wako,” alisema Bi. Pamela kwa huzuni.


Joyce alihisi ubaridi mwepesi ukimtambaa mwilini mwake na kuzifanya nywele zake kusisimka. Alitaka kusema neno lakini akasita. Japo hakuweza kuelewa mara moja kama taarifa zile alizozisikia zilikuwa na ukweli wowote au lah, lakini alijikuta akichanganyikiwa zaidi ya kushangaa. Alidhani maelezo yale yangemsaidia kupata majibu sahihi ya maswali yake machache yaliyokuwa yakimsumbua kichwani kwake lakini sasa akajikuta maswali mengi zaidi yakiibuka kichwani kwake.


Aliwaza kuwa huenda ile ilikuwa ndoto tu kama ndoto zingine na mara tu angeamka kutoka usingizini na kukuta kila kitu kikiwa tofauti kabisa. Hata hivyo, hisia zake zilimtanabaisha kuwa ile haikuwa ndoto bali ni kitu halisi kilikuwa kinamtokea. Alitambua kuwa ni kweli alikuwa yupo nyumbani kwa Madame Norah na alipewa taarifa kuwa Madame Norah ndiye mama’ake mzazi! Mama mzazi kivipi? Hilo hakulijua kwani hajawahi kuambiwa. Alijiuliza, ni kwa nini siku zote hizo hakuwahi kuambiwa kuwa Bi. Pamela hakuwa mama’ake mzazi isipokuwa Madame Norah?


Alihisi kutaka kuchanganyikiwa. Hisia za tukio lile zikasababisha koo lake likauke ghafla na milango yake ya fahamu ilikuwa makini zaidi huku akijaribu kuishirikisha akili yake kikamilifu katika kumletea taarifa za kuaminika ili kubaini endapo tukio lile lilikuwa katika mlolongo wa matukio yoyote ya ndotoni au lah!


Baada yah apo hakuweza kukumbuka ni vipi alishuka toka kwenye gari na kuingia ndani, alipokuja kurudiwa na fahamu alijikuta akiwa ameketi juu ya sofa kubwa la kifahari kwenye sebule kubwa ya nyumba ile, huku macho yake yakiwa yamejawa na machozi. Hakuelewa mara moja kuwa machozi yale yalikuwa ya huzuni au ya furaha?


Madame Norah na Bi. Pamela walikuwa wakimtazama kwa makini pasipo kusema neno. Sebule nzima ilikuwa katika hali ya utulivu na ukimya mkubwa. Joyce aliyatupa machjo yake kuangaza pembe zote lakini hakuona dalili za uwepo wa watu wa familia yake, si mwanawe Pendo, Winifrida wala Sammy. Hali ile ikazidi kumtia hofu na kusababisha jasho jepesi lianze kumtoka sehemu mbalimbali za mwili wake huku mapigo ya moyo wake yakibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!


Joyce alimwangalia Madame Norah usoni kwa makini akitaka kuelezwa ukweli, akagundua kuwa kulikuwa na jambo kwenye uso wa Madame Norah, ni kama huzuni fulani japokuwa alijitahidi kulazimisha tabasamu. Hata hivyo, tabasamu lake halikuweza kuiondoa hisia fulani ya majonzi usoni kwake. Madame Norah alikuwa ameketi kimya kabisa huku akionekana kutafuta maneno ya kumwambia Joyce.




“Joyce, najua unayo maswali mengi sana kichwani kwako na hili tulilokwambia limekuzidishia mkanganyiko badala ya kujibu maswali yako. Naomba ufahamu kuwa mimi ndiye mama’ako, nilipata ujauzito wako nikiwa kidato cha nne, nikakatisha masomo na mambo fulani yakatokea, nilipokuzaa nikakuacha na baba’ako Jengo,” Madame Norah alisema kwa sauti ya kutetemeka huku machozi yakianza kumtoka.


“Huwezi kuamini, kwa miaka yote hii nimekuwa nikikutafuta sana, ilifikia kipindi nikaamini kuwa wewe na baba’ako mlikufa kwenye ajali ya moto ulioteketeza nyumba mliyokuwa mkiishi eneo la Ngamiani Tanga. Baada yah apo sikujua ningewapata wapi hadi jana nilipokutana na baba’ako pale hospitali. Nisamehe sana binti’angu, najua sikukutendea haki lakini itoshe tu kusema kuwa najutia sana kitendo changu, kwani tangu wakati huo nimekuwa nikiishi maisha ya huzuni kubwa na majuto mengi ingawa watu wakiniangalia hudhani labda nina furaha...”


Maneno yale yalizidi kumuumiza Joyce, hakujua aseme nini. Hata hivyo, aliendelea kuwa kimya kabisa. Alihisi labda akili yake ilikuwa haifanyi kazi sawasawa. Aliendelea kumtazama Madame Norah kwa makini. Kikatokea tena kitambo kirefu cha ukimya.


Haikuwa rahisi kwa Joyce kuipokea taarifa ile. Ilikuwa ni taarifa ngeni kabisa masikioni mwake na akili yake ilikataa kuikubali. Siku zote alikuwa akimchukulia Madame Norah kama mfano wa mwanamke mwenye mafanikio, akitamani siku moja kufikia japo nusu ya mafanikio yake, hakuwahi kudhani kama angeweza kuwa mama’ake mzazi.


Japo alitaka kuamini lakini akili yake likataa, ila alipowatazama wale wanawake wawili alikiona kitu kwenye macho yao na nyuso zao, kitu kilichomhakikishia kuwa yote aliyoyasikia yakisemwa juu yake yalikuwa kweli kabisa!


Baada ya kitambo kirefu hatimaye Joyce aliwataka wamwache kwanza, kwani alihitaji muda wa kuwa peke yake ili aweze kutafakari kabla hajaamua lipi la kufanya. Hata hivyo, kabla hajajitenga aliomba afahamishwe ni wapi ilipokuwa familia yake. Madame Norah alimtaka kuwa jasiri huku akijitahidi kuifanya sauti yake iwe za kawaida.


Kisha walimweleza Joyce yote kuhusu nyumba yao kushambuliwa na bomu lililotegwa kwenye gari na watu wasiojulikana, wakati huo Sammy na Jengo wakiwa ndani ya nyumba hiyo. Wakamweleza kuhusu majeraha waliyoyapata na Sammy kulazwa Muhimbili, na kwamba hali yake ilikuwa inaendelea vizuri.


* * * * *


Mr. Oduya aliwasili katika jengo la makao makuu ya ofisi za The Splendid Group lililopo barabara ya Bagamoyo, eneo la Kijitonyama. Alikuwa akitokea Paradise Club alikokwenda kuonana wa mshirika wake mkubwa, Kamishna Omalla, Mkuu wa Kamisheni ya Intelijensia wa Jeshi la Polisi.


Kama mtu mkubwa, Mr. Oduya alitumia lifti maalumu ambayo ilimfikisha katika ghorofa ya saba ilikokuwa ofisi yake na kuutumia mlango maalumu ili kuingia ofisini kwake bila kubughudhiwa na mtu mwingine. Alipoingia alijibwaga juu ya kiti chake na kuitazama saa yake ya mkononi, ilionesha kuwa ilishatimia saa nne na nusu asubuhi. Mr. Oduya alishusha pumzi na kupandisha miguu yake juu ya meza na kuinyoosha, akatulia akitafakari.


Japokuwa alipaswa kufurahia kazi nzuri iliyofanywa na Robert Kamau ya kumsababisha ajali ya gari Inspekta Abel, mtu aliyeanza kuwa tishio kwake, huku akihakikishiwa kuwa asingeweza kuamka tena na kama angefanikiwa kuamka basi angekuwa mlemavu maisha yake yote, lakini Mr. Oduya alishangaa kuona kuwa bado hakuwa na furaha wala amani kabisa moyoni.


Alijihisi kama yupo uchi kabisa kwa Tunu na hilo halikuwa na mjadala. Kwanza binti huyo alikuwa amefanikiwa kuepuka mitego yote aliyomtegea kwa miaka mitatu na kusababisha vifo vya watu wake muhimu sana kwenye harakati zake, huku Victor akiwa mahututi akipigania roho yake hospitali, na pili alishagundua mambo yao mengi.


Mr. Oduya alidhani kuwa ili kuwa salama alipaswa kuhakikisha anammaliza Tunu kabla jua halijatua. Hata hivyo jambo la ajabu, hadi wakati huo hakuna yeyote miongoni mwa watu wake aliyejua Tunu alikuwa wapi. watu wote aliowapa jukumu la kumfuatilia Tunu hawakujua alikuwa wapi, tangu alipookolewa na watu wake usiku wa kuamkia siku ile. Alianza kuingiwa na mawazo kuwa huenda alikufa kwenye ile ajali.


Alijikuta akianza kupata furaha moyoni ingawa hakupendaa kuamini, alitoa maagizo kwa watu wake wote kuwa makini sana na kuhakikisha wanafuatilia kila taarifa na maeneo yote waliyodhani huenda Tunu angeweza kuwepo. Maeneo kama Hospitali ya Amana, Muhimbili au katika mgahawa wa kisasa wa Elli’s ambako Tunu aliliacha gari lake.


Muda huo Mr. Oduya alikuwa mchovu aliyechoshwa na fikra nzito. Aliwasha kiyoyozi ndani ya ofisi yake kilichojaribu kuupooza mwili wake. Kisha alianza kumezwa na fikra nzito mpaka pale alipokuja kushtushwa na simu yake ya mkononi iliyoanza kuita kwa fujo. Mr. Oduya aliichukua ile simu na kuitazama kwa makini, akaachia tabasamu baada ya kuliona jina la Kamishna Omalla. Aliipokea ile simu na kuipeleka sikioni.


“Hallo, poti!” Mr. Oduya alisema kwa sauti tulivu huku akibana pumzi zake.


“Ni nini hiki umefanya?” sauti nzito ya Kamishna Omalla ilisikika ikimuuliza Mr. Oduya pasipo kujuliana hali.


“Kwani ulitarajia nini, poti?” Mr. Oduya aliuliza huku akiminya midomo yake kuzuia kicheko kilichotaka kumtoka. “Vipi, amekufa?”


Kamishna Omalla hakujibu mara moja, alibaki kimya kwa kitambo kirefu hadi Mr. Oduya akadhani labda alikuwa amekata simu. Alipotaka kuita akamsikia Kamishna Omalla akikohoa kidogo kusafisha koo lake.


“Oduya, hii tabia ya kutaka kuua watu wote unaodhani ni tishio kwako inabidi uipunguze, imezidi sasa!” Kamishna Omalla alisema kwa sauti ya majonzi. Ilionekana wazi kuwa alikuwa haipendi tabia ile ya mauaji, aliamini kama yangeendelea basi mwisho wake si Mr. Oduya tu ambaye angetiwa hatiani bali hata yeye, endapo angegundulika kuwa ni mshirika wake mkubwa.


“Kamishna, najua huwezi kunielewa,” Mr. Oduya aliongea kwa sauti ya chini, “Ulimwengu huu haupo sawa kama unavyodhani. Muda mwingine yatupasa kufanya hivyo kabla hatujafanyiwa hivyo sisi wenyewe!” Mr. Oduya alisema na kumfanya Kamishna Omalla agune.


“Nakuelewa, lakini nilidhani tulikubaliana nilipokwambia suala hilo nitalishughulikia. Hukupaswa kufanya ulichokifanya,” Kamishna Omalla alisema na kushusha pumzi za ndani kwa ndani. “Hata hivyo, ngoja nione itakavyokuwa.” Kamishna Omalla alisema na kukata simu.


Usichoke kufuatilia simulizi hii ili kuujua mwisho wake...





“Oduya, hii tabia ya kutaka kuua watu wote unaodhani ni tishio kwako inabidi uipunguze, imezidi sasa!” Kamishna Omalla alisema kwa sauti ya majonzi. Ilionekana wazi kuwa alikuwa haipendi tabia ile ya mauaji, aliamini kama yangeendelea basi mwisho wake si Mr. Oduya tu ambaye angetiwa hatiani bali hata yeye, endapo angegundulika kuwa ni mshirika wake mkubwa.


“Kamishna, najua huwezi kunielewa,” Mr. Oduya aliongea kwa sauti ya chini, “Ulimwengu huu haupo sawa kama unavyodhani. Muda mwingine yatupasa kufanya hivyo kabla hatujafanyiwa hivyo sisi wenyewe!” Mr. Oduya alisema na kumfanya Kamishna Omalla agune.


“Nakuelewa, lakini nilidhani tulikubaliana nilipokwambia suala hilo nitalishughulikia. Hukupaswa kufanya ulichokifanya,” Kamishna Omalla alisema na kushusha pumzi za ndani kwa ndani. “Hata hivyo, ngoja nione itakavyokuwa.” Kamishna Omalla alisema na kukata simu.


ENDELEA...


Mr. Oduya aliachia tabasamu pana kwa namna fulani ya kujipongeza kwa kuandaa mkakati mzuri wa kumwondoa yule inspekta wa polisi ‘mwenye kiherehere’ aliyetaka kuwa tishio kwenye harakati na maslahi ya Mr. Oduya. Hata hivyo, hakuona kama tabasamu lilitosha, aliamua kungua kicheko. Kisha aliona kicheko hakitoshi, akainuka na kuliendea jokofu dogo lililokuwa katika pembe moja ya kile chumba kikubwa cha ofisi yake. Alilifungua lile jokofu na kutoa chupa kubwa ya mvinyo ghali kutoka Italia, aina ya Gaja Barbaresco na bilauri moja.


Akaifungua ile chupa na kujimiminia mvinyo wa kutosha kwenye ile bilauri kisha akainyanyua juu na kupiga funda kubwa la mvinyo huku akifumba macho yake na kusisimkwa mwili huku akiusikilizia ule mvinyo ukisafiri toka kwenye koo lake hadi tumboni.


Alikuwa na kila sababu za kusherehekea kwani aliamini kuwa haikupata kutokea kwa mtu yeyote au kwenye mpango wowote aliouandaa ukashindwa kumletea mafanikio. Ni mtu mmoja tu aliyetaka kumharibia rekodi yake, Tunu Michael. Hata hivyo, hakuwa na shaka tena kuwa wakati wowote angepewa taarifa njema kuhusu kifo cha Tunu, taarifa ambazo zingezidisha furaha yake mara dufu. Kwani watu wake walimhakikishia kuwa walikuwa na fununu kuhusu mahali ambapo Tunu angeweza kuwa amejificha na tayari walikwisha anza safari ya kuelekea eneo hilo ili kummaliza. Mr. Oduya alijikumbusha kuwa ili aendelee kufanikiwa katika harakati zake alikuwa na mambo mawili tu: ama kufa akipambana au kushinda vita.


* * * * *


Ni dhahiri kwa yeyote aliyemtazama machoni Naibu Kamishna Mamboleo asingeshindwa kubaini kwamba alikuwa hajapata usingizi wa kutosha kwa siku kadhaa. Mambo mengi yalikuwa yamemkabili kichwani kiasi cha kumpokonya hata hamu ya kula. Angewezaje kupumzika wakati alikuwa hajapata taarifa kamili ambazo zingemsaidia katika kukamilisha faili la upelelezi na kukomesha tishio jipya la uhalifu lililoanza kuibuka jijini Dar es Salaam?


Jioni ya siku iliyotangulia alikuwa ameitwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwenye kikao cha dharura na kutakiwa kutoa maelezo mbele ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Mawaziri wa Mambo ya Ndani na wa Ulinzi na Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.


Ingawa alikuwa na taarifa za awali za upelelezi wa kesi ile zilizoonesha kuwa kwa kiasi fulani mwenendo wa kesi ile, taarifa zile alikuwa ameziwasilisha kishujaa kwenye kile kikao cha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama huku moyo wake ukidunda kwa hofu, alijua kuwa hakuwa tayari kuyajibu maswali yao mengi ili kuwaridhisha. Jasho jembamba lilimtoka baada ya kutupiwa lawama kuwa yeye na vijana wake wote walionekana kutumia mbinu za kizamani katika kukabiliana na wahalifu walioonekana kuwa mbele yao.


Wale wakuu walimtaka Naibu Kamishna Mamboleo awape maelezo ambayo yangewaridhisha iwapo alidhani alikuwa bado anatosha kuendelea kushika nafasi ile ya Ukamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Wale wakuu walimkumbusha kuwa yeye na vijana wake walipaswa kuwa makini muda wote kwani walikuwa wamefundishwa mbinu zote za kuwawezesha kung’amua viashiria vyovyote vya uhalifu kabla havijatokea na kwamba uhai wa jiji zima la Dar es Salaam ulikuwa ukiwategemea wao.


Nusura Naibu Kamishna Mamboleo apate hasira kwa lawama zilizokuwa zikielekezwa kwake ambazo hakuona kama zilimstahili. Ilibaki kidogo tu atangaze kujiuzulu nafasi hiyo, lakini hakuweza kufanya hivyo baada ya kukumbuka kuwa jambo lolote la kihalifu ambalo lingetokea katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ni yeye ndiye aliyestahili kupewa lawama zile, kwani kufanya kazi ni kupata matokeo mazuri ya kazi hiyo na kama hakuna matokeo basi hiyo haiwezi kuitwa kazi.


Naibu Kamishna Mamboleo alikuwa amedhamiria kupata matokeo mazuri ya kazi na kulifunga jalada la kesi ile haraka iwezekanavyo ndani ya wiki ile, lakini muda ule alikuwa amepata taarifa mbaya sana zilizoonesha kumchangaya zaidi. Taarifa kuhusu ajali ya gari na kuumia kwa Inspekta Abel wakati akiwa katika majukumu yake ya upelelezi, na ilionesha wazi kuwa ilikuwa ni ajali ya kupangwa, baada ya kugundulika kuwa gari lililosababisha ajali hiyo aina ya Tata Daewoo lilikuwa limeibiwa mahali na dereva wake kupewa kiwango kikubwa cha dawa za kumpumbaza akili.


Kwa vyovyote mtu au watu waliofanya tukio lile walikuwa watu makini sana katika kazi yao kwa kuwa hawakuwa wameacha alama zozote ambazo zingewawezesha polisi kuwatambua. Tayari mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi yalikuwa yamejaa washukiwa ambao walihojiwa kwa maneno na vitendo. Wale walioonekana kuwa hawana tatizo waliachiwa, walioonekana kutiliwa shaka, japo kidogo, waliandaliwa mashtaka. Hata hivyo, hakuna hata mtu mmoja ambaye alielekea kujua mengi ambayo yangeweza kuwasaidia katika kesi ile.


* * * * *


Saa sita mchana, Tunu na Bob walikuwa peke yao kwenye sebule kubwa ya kifahari iliyo katika mazingira ya upweke, eneo la Kinyerezi. Muda ule Tom na Dumba walikuwa wametoka kwenda mjini, ambako walikusudia kupeleka taarifa za siri kwa Solomon Zirro, Inspekta Jenerali wa Polisi na kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna Mamboleo. Pia walikusudia kufikisha salamu kwa Kamishna Omalla, Mkuu wa Kamisheni ya Intelijensia wa Jeshi la Polisi na kwa Mr. Oduya mwenyewe.




Taarifa na salamu hizo zilikuwa zimebebwa kwenye nakala kadhaa za CD maalumu zilizorudufiwa na kuhifadhi sauti na video kuhusiana na mauaji ya Jaji Mkuu, Sylvester Lutego. Tom na Dumba walipoondoka, Tunu alimtaka Bob ampeleke Kurasini ili akaonane na Victoria. Hivyo aliingia chumbani akajiandaa kwa ajili ya safari ya kuelekea Kurasini.


Baada ya dakika chache Tunu alitoka chumbani akiwa amebadilisha nguo na sasa alikuwa amevaa suruali ya Jamsuit ya rangi ya bluu iliyolionesha vyema umbo lake refu maridadi lenye minofu ya mapaja iliyokaza kutokana na mazoezi ya kila siku. Miguuni alikuwa amevaa viatu vya mchumumio vye visigino virefu vya rangi nyeusi na kujipulizia manukato ghali mwilini yaliyofanya harufu yake itamalaki sebule yote na kuzifanya pua za Bob zipate uhai mpya.


Muda huo huo wakaisikia sauti ya kengele iliyokuwa imewekwa getini ikiita kwa fujo. Tunu na Bob wakatazamana kwa makini katika namna ya kuulizana “huyo atakuwa nani?” huku wakijitahidi kusikiliza kwa makini. Kengele ile iliendelea kuita kwa fujo.


Mlango wa hisia ya sita katika ubongo wa Tunu ulifunguka, ilikuwa ni hisia iliyomfahamisha kuwa yeyote aliyekuwa pale nje anabonyeza ile kengele hakuwa amefika pale kwa jambo la heri. Tunu alikumbuka katika mafunzo ya ushushushu nchini Israel, maendeleo ya hisia ya sita yalikuwa yanapewa uzito mkubwa kwa wanafunzi wa ushushushu, na kadri yalivyosisitizwa ndivyo ambavyo yalimjenga Tunu kutambua umuhimu wa nyenzo hiyo muhimu.


Kwa mara ya kwanza tangu apate sehemu ya maficho katika eneo lile la Kinyerezi alijikuta akigundua kuwa alikuwa amekosea sana kuwadharau watu wa Mr. Oduya kiasi hicho. Mwanzoni aliamini kuwa wasingeweza kugundua uwepo wake katika nyumba ile. Hata hivyo, hakutaka kumfanya mtu yeyote aliyepo nje ya ile nyumba ahisi kuwa alikuwa amegundulika na watu waliokuwemo mle ndani, hivyo akamtumia Bob jicho ambalo lilibeba ujumbe wote, ujumbe ambao masikioni mwa Bob ulijieleza waziwazi “Kazi kwako, mzee!”


Papo hapo Bob akanyanyuka na kutoka nje kisha akaelekea getini huku akiwa makini sana kama mbwa awindaye. Alipolifikia geti akaufungua mlango mdogo uliokuwa pembeni ya lile geti kubwa. Kama walivyotegemea, aliwaona wanaume wawili warefu wenye miili iliyojengeka wakiwa wamesimama nje ya lile geti, wote walikuwa makini sana. Macho yao tu yalitosha kumfahamisha Bob kuwa wale watu walikuwa wazee wa kazi.


“Samahani sana, bro,” mwanamume mmoja alianza kujieleza mbele ya Bob. “Tumelazimika kukusumbua kidogo. Nadhani utatuwia radhi. Mimi ni mwenyekiti wa mtaa huu na huyu ni mjumbe wa eneo hili, nadhani wewe ndiye mwenye nyumba hii?”


Bob aliwatazama kwa makini na kutaka kucheka, lakini hakuweza kufanya hivyo, kwani alishaelewa wale walikuwa kina nani na kwa nini walikuwa pale. Hata hivyo, aliitikia kwa kubetua kichwa chake huku akiendelea kujifanya mjinga aone nini walitaka kufanya. Wakati huo mkono wake wa kulia aliupeleka kiunoni na kuigusa bastola yake, mwili wake ukasisimka.


“Nyumba hii imeonekana kutokaliwa na mtu tangu ikamilike, hivyo tupo katika ziara ya kutembelea wakazi ambao bado ni wageni katika mtaa wetu huu ili kujua mambo mawili matatu ambayo nadhani utatujibu. Uisijali, ni mzunguko wa kawaida tu kwa wakazi wote wageni ili kufahamiana. Samahani kama tutakuwa tumekusumbua kidogo, kwa kawaida hapa mtaani kwetu hatupendi kusumbua wakazi wetu,” yule mwanamume mwingine alidakia.


“Bila samahani, mnakaribishwa sana,” Bob aliitikia, “Karibuni basi ndani,” akasema na kuwapisha ili waingie kisha aliwaongozana kuelekea sebuleni.


“Sijui mwenzetu unaitwa nani?” mwanaume mmoja alimuuliza Bob wakati wakielekea kwenye mlango wa kuingilia ndani.


“Godwin Tyson,” Bob alijibu mara moja pasipo hata kufikiria.


“Wewe ni mwenyeji wa wapi?”


“Hapa hapa Dar es Salaam.”


“Umeoa?”


“Nina mke na mtoto mmoja,” Bob alijibu huku akiufungua mlango na kuwaruhusu waingine ndani.


“Nao wanaishi hapa hapa?”


“Kumbe ulitaka wakaishi wapi?” Bob aliuliza kwa mshangao huku akimtazama yule mwanamume aliyekuwa akimuuliza maswali, kisha akawapisha wale wanaume waingie ndani.


“Sahamani, bwana mkubwa, kama nimekukwaza kwa maswali yangu, nilimaanisha wapo ndani?”


“Wala usijali, ukihitaji kuwaona utawaona tu,” Bob alijibu huku akianza kushindwa kuzizuia hasira zake.


Walipoingia tu sebuleni Bob aliufungua ule mlango wa ufunguo kisha akauchomoa ule ufunguo na kuuweka mfukoni, wale watu wakashtuka na kugeuka haraka kumtazama kwa mshangao, na hapo wakakutana na mtutu ukiwaelekea, lakini ni kama walikuwa wamejiandaa kwa jambo hilo. Walijigawa na kuruka juu huku wakiachia mapigo ya haraka kumwelekea Bob lakini mapigo yao hayakutimiza wajibu wake ingawa walifanikiwa kuidondosha bastola ya Bob iliyokuwa mkononi huku Bob akifanikiwa kuyakwepa mapigo hayo na kujiweka sawa.


Kabla hawajafanya jambo jingine lolote walishtukia wakimwona Tunu akiibuka toka kusikojulikana na kuruka juu huku akijipindua hewani akiwa ametanua miguu yake na kuutanguliza mguu wake wa kushoto usiokuwa na jeraha, ukifuatiwa na mguu wa kulia. Mwanamume mmoja aliyekuwa karibu na Tunu akafanya jitihada za kujikinga na shambulizi hilo huku akiwa tayari amechomoa bastola yake.


Tunu alikiwa bado hewani aliachia pigo moja matata lililomfanya mwanamume yule na kumfanya apepesuke na kugonga kichwa chake kwenye ukuta. Bastola iliyokuwa mkononi mwake ilimtoka na kuanguka kando. Kabla Tunu hajatua sakafuni akampa pigo jingine la judo ambalo lilitua ubavuni mwake na kumlegeza kabisa. Pigo lililofuata lilimlazimisha yule mwanamume kuanguka sakafuni akiwa hana fahamu.


Wakati hayo yakiendelea yule mwanamume wa pili alijikuta akikabiliwa na Bob aliyeachia pigo maridadi lakini yule mwanamume aliliona na kuinua mkono wake juu kulikinga huku mkono wake wa pili ukijiandaa kubonyeza kitufe cha bastola yake. Bob hakuruhusu mkono huo ufanikiwe kuifyatua ile bastola. Aliruka akampiga kichwa kikavu kilichompa kisurisuri na kufanya ateremke sakafuni bila ubishi na kupoteza kabisa fahamu.


Mpambano unazidi kupamba ??????. Je, baada ya kufahamika kwa maficho hayo Tunu na Bob watafanikiwa kutoka salama ndani ya nyumba hiyo? Endelea kusafiri nami katika safari hii ya kusisimua ndani ya ???? hadi mwisho...





Walipoingia tu sebuleni Bob aliufungua ule mlango wa ufunguo kisha akauchomoa ule ufunguo na kuuweka mfukoni, wale watu wakashtuka na kugeuka haraka kumtazama kwa mshangao, na hapo wakakutana na mtutu ukiwaelekea, lakini ni kama walikuwa wamejiandaa kwa jambo hilo. Walijigawa na kuruka juu huku wakiachia mapigo ya haraka kumwelekea Bob lakini mapigo yao hayakutimiza wajibu wake ingawa walifanikiwa kuidondosha bastola ya Bob iliyokuwa mkononi huku Bob akifanikiwa kuyakwepa mapigo hayo na kujiweka sawa.


Kabla hawajafanya jambo jingine lolote walishtukia wakimwona Tunu akiibuka toka kusikojulikana na kuruka juu huku akijipindua hewani akiwa ametanua miguu yake na kuutanguliza mguu wake wa kushoto usiokuwa na jeraha, ukifuatiwa na mguu wa kulia. Mwanamume mmoja aliyekuwa karibu na Tunu akafanya jitihada za kujikinga na shambulizi hilo huku akiwa tayari amechomoa bastola yake.


Tunu alikiwa bado hewani aliachia pigo moja matata lililomfanya mwanamume yule na kumfanya apepesuke na kugonga kichwa chake kwenye ukuta. Bastola iliyokuwa mkononi mwake ilimtoka na kuanguka kando. Kabla Tunu hajatua sakafuni akampa pigo jingine la judo ambalo lilitua ubavuni mwake na kumlegeza kabisa. Pigo lililofuata lilimlazimisha yule mwanamume kuanguka sakafuni akiwa hana fahamu.


Wakati hayo yakiendelea yule mwanamume wa pili alijikuta akikabiliwa na Bob aliyeachia pigo maridadi lakini yule mwanamume aliliona na kuinua mkono wake juu kulikinga huku mkono wake wa pili ukijiandaa kubonyeza kitufe cha bastola yake. Bob hakuruhusu mkono huo ufanikiwe kuifyatua ile bastola. Aliruka akampiga kichwa kikavu kilichompa kisurisuri na kufanya ateremke sakafuni bila ubishi na kupoteza kabisa fahamu.


ENDELEA...


Tunu aliwatazama wale wanaume kwa makini akiwa haamini kabisa kama waliweza kugundua yalipo maficho yake. Moyo wake ulimdunda sana ingawa hakujua au kupata kuhisi hofu katika moyo wake, lakini kitu fulani kilimpanda moyoni na kumtia hasira na kichefuchefu. Mlango wake wa hisia ya sita ulimtanabaisha kuwa wale wanaume hawakuwa peke yao, bali kulikuwa na mtu au watu wengine waliokuwa wameambatana nao na huenda walikuwa sehemu fulani jirani na eneo lile wakijiandaa kuvamia. Sasa Tunu aliamua kupambana na yeyote.


Kwa kusaidiana na Bob, waliwaburuza wale wanaume hadi kwenye chumba kidogo cha maliwato ya jumuia, wakawafungia humo baada ya kuwapekua na kuwakuta wakiwa na chupa ndogo ya dawa ya kusababisha usingizi aina ya Chloroform, bastola mbili, simu na vifaa maalumu vya mawasiliano. Kisha waliwavua nguo wakiwaacha na boksa na kuwafunga pingu miguuni kwa pamoja, mmoja mguu wa kushoto na mwingine mguu wa kulia.


Tunu na Bob walivichukua vile vifaa vya mawasiliano na kuvivaa ili kufuatilia mawasiliano yoyote kati ya wale wanaume na wenzao, hata hivyo walishangaa kuona kuwa tayari mawasiliano yalikuwa yamekatwa. Wakaamua kuviacha vile vifaa na kuweka mtego ili kuwanasa endapo wangejaribu kufuatilia au kuingia mle ndani. Tunu alimtaka Bob atangulie kutoka nje na apande kwenye mti mkubwa uliokuwa sehemu ya mbele ya ile nyumba, ili aweze kumwona kila mtu ambaye angejaribu kuingia mle ndani kupitia mbele. Bob akatoka nje na kukwea mti mmoja kwa tahadhari.


Wakati huo Tunu alikuwa akiandaa mtego kwa yeyote ambaye angefanikiwa kuingia mle ndani, alichukua chupa fulani iliyofanana na chupa ya manukato, akaziba pua na mdomo wake kwa kitambaa maalumu na kuyapulizia yale manukato yote kwa tahadhari kubwa eneo la sebuleni kwenye mlango mkubwa wa kuingilia na jikoni kulikokuwa na mlango mwingine wa kuingilia ndani.


Baada ya muda mfupi eneo lote la jikoni na sebuleni likajaa harufu nzuri ya marashi. Tunu aliporidhika akachukua begi lake lenye vifaa vyake vya kazi na kutoka haraka, aliizunguka ile nyumba, kisha kwa kutumia mbinu yake ya kijasusi aliupanda mti mmoja mkubwa uliokuwa kando ya ukuta uliokuwa ukiizunguka ile nyumba.


Alitafuta sehemu nzuri juu ya tawi moja kubwa la ule mti lililokuwa na majani mengi na kujibanza, ilikuwa ni sehemu ambayo aliweza kumwona kila mtu aliyekaribia au kupita jirani na nyumba ile kwa kupitia eneo la nyuma. Mara simu yake ikaanza kuita kwa kutetema, aliitoa na kuitazama kwa makini huku akikunja sura yake, akaliona jina la Tom na kushusha pumzi huku akiuma midomo yake. Aliipokea ile simu haraka, “Niambie, Tom!” aliongea kwa sauti ndogo yenye tahadhari.


“Vipi kwema huko, mbona kama unaongea kwa tahadhari kubwa sana!” Tom aliuliza kwa wasiwasi baada ya kuhisi kuwa mambo hayakuwa shwari kwa upande wa Tunu.


“Mambo si shwari, watu wa Mr. Oduya wamevamia hapa, hata sijui wamepafahamu vipi...” Tunu alisema kwa sauti ya chini iliyobeba kila aina ya tahadhari.


“What!” Tom aling’aka kwa mshtuko mkubwa. “Lakini wote mko salama?”


“Usijali! Tumewadhibiti kirahisi mno, ila tumeweka mtego kuwanasa wengine watakaokuja,” Tunu alisema na kusita kidogo. “Na wewe nipe ripoti!”


“Huku mambo yamekwenda kama tulivyopanga, tayari ujumbe umeshawafikia IGP Solomon Zirro na Naibu Kamishna Mamboleo, muda wowote kuanzia sasa moto utawaka. Kuhusu Kamishna Omalla na Mr. Oduya ni kama tulivyokubaliana, tusubiri kwanza,” Tom alisema na kumfanya Tunu aachie tabasamu pana la ushindi.


“Okay, tuwasiliane...” Tunu alisema na kukata simu, muda huohuo akawaona wanaume wawili waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki wakipita jirani na ile nyumba, Tunu aliweza kumtambua mtu aliyekuwa akiendesha ile pikipiki licha ya kuwa alikuwa amevaa mavazi yaliyomficha, miwani mikubwa ya jua iliyofunika macho yake na chapeo (helmet) kichwani. Alikuwa Spoiler.


Ile pikipiki ilipita mbele ya ile nyumba pasipo kusimama, hata hivyo wale watu walitupa macho yao kuangalia kwenye ile nyumba katika namna ya kuyachunguza mazingira ya ile nyumba, pikipiki ikaelekea mbele zaidi ikipita kwenye njia nyembamba iliyopita katikati ya vichaka vidogovidogo. Tunu alijua kuwa wale watu walikuwa wakitafuta namna ya kuingia ndani kwa kusoma mazingira. Hakuwa na shaka yoyote kuwa walikwishagundua kuwa wenzao walioingia ndani walikuwa kwenye hatari, huenda ndiyo maana waliamua kuwazima vifaa vya mawasiliano.


“Bob, unanikopi?” Tunu aliwasiliana na Bob ili kumpa taarifa.


“Nakukopi, nadhani na wewe umeona nilichokiona. Ndege wawili wanaruka jirani na kiota, au siyo?” Bob alisema kwa sauti ya chini yenye kila aina ya tahadhari.


“Yap! Basi endelea kufuatilia huko mbele na inabidi tuongeze umakini zaidi,” Tunu alisema huku akitazama upande ilikoishia ile pikipiki, hakusikia tena muungurumo wake.


“Usijali, endapo wakiingia tu kwenye kiota basi watakuwa asusa...”


“Na lazima wawe asusa!” Tunu akadakia kisha akageuza shingo yake kutazama huku na huko kwa makini. “Lazima wanase kwani kila kitu kipo kama tulivyopanga.”


“Basi vema...” Bob alisema na kusita kidogo. “Namwona ndege mmoja akirejea taratibu,” Bob alisema kwa tahadhari.




“Okay! Nakukopi, endelea kufuatilia na ninaomba uzidishe umakini!” Tunu alisema na mara akamwona Spoiler akitembea kwa tahadhari akipita eneo la nyuma ya ile nyumba. Eneo alilopita lilikuwa kama mita ishirini na tano tu kutoka ilipo nyumba ile. Hakuwa na pikipiki, hivyo Tunu aliweza kubaini kuwa waliiacha pikipiki yao sehemu na kuamua kurudi kwa miguu wakiwa wamejigawa, mmoja akielekea upande wa nyuma ya ile nyumba na mwingine upande wa mbele kisha wakakutanie ndani.


Tunu aliweza kugundua kuwa Spoiler alikuwa amevaa kitu fulani sikioni kwake na alikuwa akiwasiliana na mwenzake katika kujuzana kinachoendelea.


Tunu alimtazama Spoiler kwa makini wakati akiisogelea ile nyumba, kisha kwa kutumia mbinu ya hali ya juu ya kikomando, alikwea ukuta na kurukia ndani pasipo kutoa kishindo, kisha alijibanza kwenye banda moja lililojengwa kwa ajili ya kufugia kuku kule nyuma, jirani na ule mti ambao Tunu alijificha. Kabla ya kufanya mjongeo wowote alitulia palepale akayatembeza macho yake kupeleleza mandhari ya ile nyumba, alipogundua kuwa kajificha mahala salama akawasiliana na mwenzake.


Muda mfupi tangu Spoiler awasiliane na mwenzake Tunu alimwona mwanamume mwingine akitumia mbinu ileile ya kikomando kuingia ndani ya uzio wa nyumba bila kishindo kisha akakimbilia kwenye mti mmoja mkubwa wa kivuli na kujificha. Hapo Tunu akagundua kuwa alikuwa anacheza na watu hatari wenye uzoefu mkubwa wa masuala ya kihalifu.


Wale watu waliendelea kujificha kwa muda mrefu huku wakionekana kuyasoma mazingira katika namna ya kujiridhisha na hali ya usalama wa eneo lile. Walistaajabu kuona hali ikiwa shwari kabisa. Hatimaye Spoiler akaondoka pale kwenye banda na kusogea upande wa kulia akiambaa na maua kuizunguka ile nyumba katika namna ya kupata uhakika wa hali ya usalama wa eneo lile, huku akifanya mjongeo makini wa utulivu akitoka eneo moja na kuhamia eneo jingine akiifuata baraza ndogo ya nyuma ya nyumba kwa tahadhari.


Wakati huo yule mwanamume mwingine aliendelea kujibanza palepale akiwa makini zaidi, bastola yake ilikuwa imetulia vyema kwenye kiganja cha mkono wake wa kushoto akiwa tayari kumlinda mwenzake endapo jambo lolote baya lingemtokea.


Kwa tahadhari Spoiler alifika katika baraza ya ile sehemu ya nyuma ya nyumba na kuanza kupanda ngazi chache za varandani kuelekea mlango wa nyuma. Alipoufikia ule mlango wa jikoni alianza kuchunguza, akashika kitasa na kukinyonga lakini mlango haukufunguka, hivyo akatumia pini maalumu kutengulia vitasa cha mlango na kuzama ndani haraka huku akiurudisha mlango. Alikuwa na kila aina ya tahadhari. Kisu mkononi na macho yakiwa yanazunguka huku na kule.


Alisimama pale jikoni na kwa namna ya ajabu akakumbana na harufu nzuri ya marashi. Alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu, lilikuwa kosa kubwa kwani alianza kuhisi akili yake ikiwa nzito na mwili ukimlegea, kabla hajajua afanye nini alidondoka sakafuni na mara usingizi mzito ukameza na kumteka kabisa.


Dakika mbili baadaye yule mwanamume mwingine alionekana akijaribu kuwasiliana na Spoiler bila mafanikio, upesi akafanya namna kuingia ndani lakini kwa tahadhari kubwa, bastola yake iliendelea kutulia vyema kwenye kiganja cha mkono wake wa kushoto akiwa tayari kwa lolote. Aliufungua mlango na kuusukuma huku akiyatupa macho yake kutazama ndani, akamwona Spoiler akiwa sakafuni amemezwa na usingizi mzito.


Yule mwanamume alishtuka sana, akakunja uso wake na macho yake aliyakodoa kwa hofu. Alishafahamu kuwa mambo yalikuwa yameenda kombo. Alitaka kugeuka ili arudi alikotoka lakini alikuwa amechelewa, kwani muda huohuo alihisi ubaridi wa bomba lililomgusa kisogoni. Ulikuwa ni mtutu wa bastola ndogo ya Tunu aina ya Glock 19M.


“Don’t try to do anything stupid, sitasita kukuua. Ingia mwenyewe ndani kimyakimya,” sauti kali ya Tunu ilimwamuru. Yule mwanamume alimfahamu vyema Tunu hivyo aliona hakutakiwa kufanya jambo lolote kwa pupa isipokuwa kutii amri hiyo kisha atafute namna ya kujiokoa. Alipoingia tu ndani ule mlango ukafungwa haraka. Yule mwanamume aliruka juu na kujiviringisha, akatua sakafuni nyuma ya jokofu kubwa huku akigeuka tayari kwa mapambano, bastola yake ikiwa tayari kwa lolote.


Alishangaa kuona akiwa peke yake na muda huohuo mwili wake ukianza kulegea baada ya kuvuta harufu nzuri ya marashi, hakuchukua muda akadondoka sakafuni huku akimezwa na usingizi mzito. Usingizi ambao usingemtoka hadi baada ya saa ishirini na nne.


* * * * *


Naibu Kamishna Mamboleo alikuwa ametulia tuli kwenye kiti chake ndani ya ofisini yake kubwa, alikuwa akiitazama video fupi ya mauaji ya kutisha kwenye runinga maalumu ya ofisini kwake. Alikuwa anaiangalia video ile kwa mara ya tatu kabla hajabaini kuwa haikuwa na kasoro yoyote bali ilikuwa na picha halisi ambazo hazikuchezewa.


Hata sauti alizokuwa amezisikia ndani ya ile CD aliamini kabisa kuwa zilikuwa ni sauti halisi za wahusika, kwani seti ile ya runinga aliyoitumia kuangalia na kusikiliza ilikuwa ni moja ya runinga zenye uwezo mkubwa wa kubaini kama sauti au picha hazikuwa halisi na ziliigizwa kwa kuwa ilikuwa imeunganishwa na mfumo maalumu wa intelijensia ya kidijitali kwa ajili ya kubaini mambo mbalimbali ya uhalifu wa kimtandao.


Naibu Kamishna Mamboleo alishusha pumzi za ndani kwa ndani, alikuwa amechanganyikiwa kwani video ile ilikuwa na sauti na picha zilizowahusisha watu wawili walioheshimika sana nchini: Kamishna Omalla, Mkuu wa Kamisheni ya Intelijensia wa Jeshi la Polisi na Mr. Oduya, bilionea mkubwa Afrika ambaye pia alikuwa akitajwa sana kumrithi Rais Yohana Funguo katika nafasi ya urais wa nchi.


Inaendelea...


NB: Litro ??


(157)


Aliichukua tena barua fupi iliyokuwa imeambatanishwa na ile CD, akaisoma kwa mara ya tatu. Bado ujumbe ulikuwa ni uleule, ujumbe mfupi lakini wenye uzito mkubwa, ikiwa imeandikwa kwa kompyuta:


Naibu Kamishna Mamboleo, pole sana na majukumu, naamini wewe na timu yako bado hamjafanikiwa kuwapata wahalifu japo naamini Inspekta Abel alishaanza kuujua ukweli, ndiyo maana wahalifu hao wakapanga kuyakatisha maisha yake.

Natumaini baada ya kuzisikiliza vyema sauti na kuitazama video hii fupi utabaini ni nani walio nyuma ya sakata la kuvamiwa Sammy na familia yake. Usijiulize video hii inahusianaje na tukio hilo au mimi nimeyabaini vipi haya, unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wahalifu papa wanatiwa mbaroni kisha nitakupa ushahidi mwingine mzito kuhusu mtandao wote wa uhalifu unaowahusisha baadhi ya askari wako wasio waaminifu ingawa wewe unawaamini. Pia usisahau kuwasiliana na IGP Solomon Zirro kwa taarifa zaidi.


Ni mimi raia mzalendo.


Naibu Kamishna Mamboleo alihisi mwili wake ukimtetemeka, akili yake ilijaribu kukataa kabisa kukubaliana na kile alichokuwa amekiona kwenye ile video, alichokuwa amekisikia toka kwenye ile CD na hata ujumbe ule aliousoma, akihisi labda alikuwa ndotoni. Hali ile ikafanya jasho jepesi lianze kumtoka usoni huku mapigo ya moyo wake yakianza kwenda mbio isivyo kawaida.


Alinyanyua simu ya mezani kwake mara mbili akitaka kumpigia simu Inspekta Jenerali wa Polisi, Solomon Zirro, lakini mar azote mbili alionesha kusita sana, hivyo akataka kwanza ajiridhishe kabla hajafanya chochote. Aliinyanyua simu kwa mara ya tatu na kubonyeza namba za katibu muhtasi wake, simu ikaita mara moja na kupokelewa. “Asia, nakuhitaji mara moja ofisini kwangu,” Naibu Kamishna Mamboleo alisema na kuirudisha simu sehemu yake.


Dakika iliyofuata katibu wake, Asia Bilali, mwanamama mwenye umbo kubwa la kuvutia likiwa limesheheni vema na kunesanesa, akiwa amevaa sare maalumu ya kazi aliingia na kusimama kwa ukakamavu mbele yake. Naibu Kamishna Mamboleo alimtazama Asia kwa makini kama aliyekuwa akiyatafuta maneno ya kumweleza. Aliinua ile bahasha iliyokuwa imehifadhi ile CD na kumwonesha Asia. “Ni nani aliyeileta hii bahasha?”


“Ililetwa na mwanamume mmoja anayetoka kampuni ya kusafirisha vifurushi ya Posta...” Asia alijibu huku akimtazama Naibu Kamishna Mamboleo kwa mshangao, kwani alikuwa ameulizwa swali lilelile kwa mara ya tatu tangu alipomkabidhi bosi wake ile bahasha.


Hata hivyo, kilichomshangaza zaidi Asia ni baada ya kumwona Naibu Kamishna Mamboleo akiwa na uso uliosawajika huku jasho jepesi likimtoka usoni.


“Kuna tatizo lolote, afande?” Asia aliuliza huku akiwa ameyatuliza macho yake kwenye uso wa Naibu Kamishna Mamboleo akijaribu kuyasoma mawazo yake.


“Hakuna tatizo. Unaweza kwenda kuendelea na kazi,” Naibu Kamishna Mamboleo alimwambia Asia na kujiegemeza kwenye kiti. Asia alizidi kushangaa, hata hivyo alitoka na kumwacha bosi wake akiwa ametahayari. Mara simu ya meza kwa Naibu Kamishna Mamboleo ikaanza kuita kwa fujo. Naibu Kamishna Mamboleo aliitazama ile simu kwa wasiwasi kisha akanyanyua kiwambo cha simu na kupeleka sikioni.


“Naibu Kamishna Mamboleo, naongea na nani?” Naibu Kamishna Mamboleo alijitambulisha na kumuuliza mpigaji simu.

“IGP Zirro hapa, habari yako, Naibu Kamishna!” sauti kavu ya Solomon Zirro ilipenya kwenye ngoma ya sikio la Naibu Kamishna Mamboleo na kumfanya ahisi mwili wake ukizizima kama aliyepigwa na shoti ya umeme.


“Nzuri, afande!” Naibu Kamishna Mamboleo aliitikia salamu ile kwa sauti iliyotetemeka kidogo.


“Nakuhitaji ofisini kwangu haraka iwezekanavyo,” Solomon Zirro alisema na kukata simu.


Naibu Kamishna Mamboleo hakusubiri. Asubiri nini wakati alikwishajua kuwa hali haikuwa shwari kabisa! Aliinuka na kuchukua ile CD pamoja na barua yake, akatoka nje na kuelekea kwenye gari lake, alijipakia na kumtaka dereva wake ampeleke makao makuu ya polisi. Dereva alilitia gari moto na kufunga safari hiyo ya dharura hadi makao makuu ya polisi.


Naibu Kamishna Mamboleo aliteremka haraka na kuelekea ofisini kwa Solomon Zirro akimwacha dereva wake akitafuta sehemu ya kuliegesha gari lake. Naibu Kamishna Mamboleo alielekezwa kuingia katika chumba maalumu cha faragha. Humo aliwakuta Solomon Zirro na Kamishna Adili Mkwizu, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, wakiwa wameketi wakitafakari.

Naibu Kamishna Mamboleo aliwasalimia kijeshi ingawa moyo wake ulikuwa ukidunda kwa hofu. Aliangalia kiti kilichokuwa tupu, akaketi.


“Umeshakutana na ujumbe huu?” Solomon Zirro alimuuliza Naibu Kamishna Mamboleo mara tu alipoketi huku akimsogezea CD kama ile aliyotoka kuitazama ofisini kwake ikiwa imeambatanishwa na barua fupi kama ile aliyokuwa nayo.


Naibu Kamishna Mamboleo aliitazama na kuitambua mara moja. Hakuwa na haja ya kuvipokea kwani na yeye alikuwa anavyo mkononi, alibetua kichwa chake kukubali huku akimwonesha IGP Solomon Zirro hata yeye alikuwa amepelekewa ofisini kwake.


“Ujumbe umeshanifikia, afande,” Naibu Kamishna Mamboleo alisema na kushusha pumzi ndefu.


“Ulimwona mtu aliyeleta?” IGP Solomon Zirro aliuliza huku akiyatuliza macho yake kwenye uso wa Naibu Kamishna Mamboleo.


“Hapana, alimkabidhi katibu wangu kabla haijanifikia,” Naibu Kamishna Mamboleo alijibu na kumeza mate kutowesha koo lake lililoanza kukauka.


“Unasemaje kuhusu kilichomo ndani yake, kina ukweli wowote?” Solomon Zirro aliuliza tena huku akizidi kumkazia macho Naibu Kamishna Mamboleo.


“Sina shaka kabisa, afande, kuwa niliyoyasikia na kuyashuhudia yote ni halisi kabisa.”


“Hata sisi tumebaini hivyo. Hata hivyo, tunajiuliza, ni nani aliyerekodi matukio haya na kwa nini alikaa nayo siku zote hizo!” Solomon Zirro alisema na kumtupia jicho Kamishna Mkwizu kisha akashusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Ni dhahiri kuwa mtu aliyerekodi matukio haya anayajua mengi kuhusu huu uhalifu unaoendelea sasa na pengine yupo hatua zaidi ya moja mbele ya jeshi la polisi. Kilichotushtua zaidi ni ushiriki wa Kamishna Omalla,” Solomon Zirro alisema na kuongeza. “Sasa nauona ugumu uliokuwa ukiupata katika kuumaliza uhalifu hapa jijini, maana mtu muhimu kama Kamishna Omalla anaposhiriki kwenye mambo haya ni rahisi sana kuingilia na kuvuruga upelelezi!”




“Hata hivyo, kwa sasa naomba mambo haya yabaki kuwa siri kati yetu watatu, ingawa sina uhakika kama hakuna mwingine zaidi yetu anayejua kuhusu jambo hili. Nilichowaitia hapa ni kutaka twende kwa mheshimiwa Rais tukazungumze naye kuhusu jambo hili,” Solomon Zirro alisema kwa msisitizo.


* * * * *


Saa nane na dakika ishirini na tano mchana, Mr. Oduya alikuwa ameketi katika kiti chake kikubwa cha kiofisi, ofisini kwake katika jengo la makao makuu ya ofisi za The Splendid Group, barabara ya Bagamoyo. Alionekana kuwaza mbali sana na muda wote alikuwa akiitupia jicho saa yake ya mkononi.


Moyo wake ulikuwa ukimdunda kwa nguvu, kwa mara ya tatu sasa tangu alipoanza harakati zake wazo la kutaka kutoroka nchi lilizidi kupata nafasi akilini mwake, safari hii alijikuta akiwa katika hali ya wasiwasi na mashaka makubwa. Sasa alipanga kuondoka nchini na kwenda Canada, ambako angekaa huko hadi pale ambapo mambo yangeonesha kutulia.


Moyoni mwake, hofu ilikuwa kubwa ikitishia kuutawala moyo wake na sauti fulani ndani yake ilikuwa ikimweleza kuwa mambo yalikuwa yamekwenda mrama. Kwa mara ya kwanza tangu alipomfahamu Silas Polea, Mr. Oduya alijikuta akianza kumlaumu sana kijana huyo kwa kumwingiza katika matatizo makubwa, ambayo hakujua nini ingekuwa hatima yake. Hii ilitokana na kukaidi agizo lake la kuliteketeza lile gari la kizamani aina ya Cadillac DeVille.


Siku zote Silas alikuwa kijana mtiifu kwake na kila kazi aliyotumwa kuifanya aliifanya kwa uaminifu na umakini mkubwa, isipokuwa hii moja tu. Mr. Oduya hakuwa na shaka naye, hasa kwa kukumbuka mambo mengi aliyowahi kumfanyia. Hata hivyo, hofu kubwa ilishaanza kumshika baada ya kuona kuwa hadi muda ule alikuwa hajapokea taarifa zozote kuhusu Tunu. Si Silas, Robert Kamau wala Job aliyekuwa akipatikana kwenye simu! Ni hayo yaliyomtia mashaka ingawa aliamini kuwa siku ile ingeisha kwa furaha kubwa.


Aliichukua tena simu yake ya mkononi na kupiga namba ya Spoiler, bado sauti ilikuwa ileile kwamba namba hiyo ilikuwa haipatikani. Akashusha pumzi. Kabla hajajua afanye nini, mlango wa ofisi yake uligongwa mara moja na kufunguliwa, katibu muhtasi wake akaingia akiwa ameshika bahasha ya khaki yenye ukubwa wa wastani iliyobandikwa karatasi ndogo yenye maandishi ya Express Mail na ilikuwa na nembo ya Posta, akamkabidhi Mr. Oduya.


Mr. Oduya aliipokea kwa mashaka na kuitazama kwa makini. Hakujua kwa nini alikuwa katika hali ya wasiwasi na mashaka makubwa, labda kwa kuwa hadi muda ule hakuwa amepata taarifa zozote kuhusu watu wake.


“Nani kaileta hii?” Mr. Oduya alimuuliza katibu wake huku akiiangalia ile bahasha kwa makini.


“Imeletwa na kaka mmoja wa Posta.”


“Vyema,” Mr. Oduya alisema na kumruhusu katibu wake aondoke kurudi ofisini kwake, akaanza kuifungua harakaharaka na kutoa nakala moja ya CD iliyoambatanishwa na barua ambayo iliyavuta macho yake kwa hofu kubwa. Mr. Oduya aliyapitisha macho yake harakaharaka kuisoma ile barua. Ilikuwa imeandikwa hivi:


Mr. Oduya, sidhani kama bado una ndoto ya kuendelea na harakati zako chafu zenye kuleta maafa kwa watu wasio na hatia ili kuupata Urais wa nchi hii tukufu. Kama bado una ndoto hiyo nakushauri uachane nayo na ujitokeze kuomba radhi hadharani kisha ujikabidhi mwenyewe polisi kabla ya saa kumi jioni. Usipofanya hivyo hadi muda huo nitakusaidia kufanya hivyo ili kukuonesha kuwa sina mzaha. Si kwamba nakutisha, pengine itapendeza kama utaitazama kwanza video fupi ndani ya CD hiyo niliyokutumia na usikilize sauti zilizomo ili kubaini ni kwa kiasi gani ninaufahamu mtandao wako wote wa uhalifu, orodha yenu, picha zenu, maongezi yenu ya simu na harakati zenu chafu. Usijiulize nimewezaje kupata video hii na sauti zenu, kwani unaelewa fika uwezo wangu katika mambo ya kishushushu.


Tunu Michael.


Mr. Oduya aliirudia kuisoma barua ile mara tatu lakini bado asiyaamini yale aliyokuwa akiyasoma, alidhani labda huo ulikuwa mtego wa Tunu ili kumkamatisha. Hata hivyo, alihisi mwili wake wote ukitetemeka. Bila kusubiri aliichukua ile CD iliyoambatanishwa na ile barua na kuitumbukiza kwenye kompyuta yake.


Aliyoyashuhudia na kuyasikia yaliyafanya mapigo ya moyo wake yaende mbio isivyo kawaida na kijasho chembamba kikaanza kumtoka, hakuwa na uwezo wa kuendelea kukanusha kuwa Tunu aliyafahamu mengi kuhusu harakati zake chafu na asingesita kuchukua hatua kama alivyoahidi kwenye barua yake.


Akiwa bado amechanganyikiwa, moyo wake ukampasuka mara tu simu yake ya mkononi ilipoanza kuita kwa fujo, aliinyanyua na kuitazama kwa makini, ilikuwa namba ya Dk. Masanja. Mr. Oduya aliipokea haraka na kuipeleka sikioni.


“Hallo!” Mr. Oduya aliongea kwa sauti ya kutetemeka mara baada ya kuiweka kwenye sikio lake kiasi kwamba alianza kujishangaa.


“Vipi umesikia?” sauti ya wasiwasi ya Dk. Masanja ilisikika toka upande wa pili wa simu.


“Kusikia nini!” Mr. Oduya aliuliza kwa mshangao.


“Kilichompata rafiki yako, Kamishna Omalla. Amejipiga risasi ya kichwa ofisini kwake muda mfupi uliopita,” Dk. Masanja alisema kwa huzuni.


“What! Ameji...” Mr. Oduya alitaka kusema lakini akahisi maneno yakikwama kooni. Donge lenye mchanganyiko wa hasira na huzuni lilimkaba kooni na kumfanya ahisi koo lake likikauka ghafla huku nywele zikimsimama kichwani kwa hofu. “Hali yake inaendeleaje?” aliuliza huku akihisi moyo wake ukisitisha kazi yake kwa muda.


“Amekufa! Risasi imefumua kabisa kichwa chake...” Dk. Masanja alisema.


Mr. Oduya alihisi kama mwili wake ulikuwa ukicharangwa kwa visu vikali na kubanikwa katika moto mkubwa. Alihisi moto mkali sana ukitambaa kwenye mwili wake na ngozi yake ilikuwa inaungua na kumfanya kuhisi maumivu makali mno. Muda huohuo alihisi hasira kali zikiibuka ndani yake, chumba cha ofisi yake kilionekana kama kilichoshuka nyuzi kumi hivi na kuwa kifupi mno.


Mara simu yake ya mezani ikaanza kuita na kumzindua toka kwenye yale mawazo. Ndipo alipogundua kuwa ile simu ya mkononi ilikuwa bado ipo sikioni ingawa hakuwa akisikia tena kilichoongewa upande wa pili wa simu ile. Hakuweza kukumbuka ilichukua muda gani akiwa ameiweka ile simu sikioni huku mawazo yake yakiwa yamehama toka kwenye maongezi yake na Dk. Masanja hadi muda ule wakati simu ya mezani ilikuwa ikiita.


Hofu ilikuwa imemmeza kabisa, aliitazama ile simu ya mezani kwa wasiwasi huku akianza kuhisi jambo la hatari. Hata hivyo, hakutaka kuendelea kusubiri ile simu iendelee kuita zaidi kwani ilikuwa mbioni kukata baada ya kuita kwa muda mrefu. Hivyo akanyoosha mkono wake kivivuvivu ili kuipokea lakini kabla mkono haujaifikia ile simu ikakatika. Tukio lile likaiongeza hofu yake yake na hivyo akabaki akiikodolea macho ile simu kana kwamba lilikuwa ni bomu la kutegeshwa lililokuwa mbioni kulipuka.


Alianza kujiuliza, mpigaji wa simu ile angekuwa nani na angekuwa na shida gani muda ule, au ni yaleyale ya kupewa taarifa mbaya kuhusu Kamishna Omalla? Wakati akijiuliza mara ile simu ya mezani ikaanza kuita tena. Hakutaka iendelee kuita zaidi hivyo haraka akakinyakuwa kiwambo chake na kukiweka sikioni huku akiipa akili yake utulivu wa hali ya juu.


Mambo bado ni ?????? kwelikweli. Ili kujua mwisho wake, usichoke kufuatilia hadi mwisho...


Mara tu alipoiweka ile simu sikioni sauti ya upande wa pili wa simu ikamtanabaisha kuwa mpigaji simu alikuwa ni katibu muhtasi wake.


“Bosi, kuna vijana wawili hapa wanadai kuwa lazima wakuone, wanasema ni rafiki zako na kwamba utafurahi sana kukutana nao,” katibu wa Mr. Oduya alisema kwenye simu.


“Sikutaka kuonana na mtu kwa sasa, wamekutajia majina yao na wanakotoka?” Mr. Oduya aliuliza kwa shauku.


“Wanasema wanatokea hapahapa Dar es Salaam. Mmoja anaitwa Tunu na mwingine ni Tom...”


“Kina nani!” sauti ya Mr. Oduya ilinguruma kwenye simu, ikapenya hadi kwenye ngoma ya sikio la katibu muhtasi wake na kutishia kuichana. Mr. Oduya aliogopa sana na hakuweza kusikia katibu wake aliongea au kumjibu nini, hakujua afanye nini na wala hakujua kama alikuwa tayari kuonana na vijana hao.


Alibaki ameduwaa asijue kipi cha kumwambia katibu muhtasi wake, mara akashuhudia mlango wa ofisi yake ukifunguliwa, Tunu na Tom wakaingia na kumkuta akiwa bado katika hali ile ya kuduwaa huku kiwambo cha simu kikiwa sikioni.


“Samahani, mzee, kwa kuingia bila ruhusa yako,” Tunu alisema kwa sauti tulivu ya kirafiki, huku akijikaribisha kwenye kiti pasipo kusubiri kukaribishwa. Tom naye akaketi kitini huku akimtazama Mr. Oduya kwa tabasamu.


“Nilipata salamu zako kuwa umekuwa ukinitafuta sana, umetumia rasilimali kubwa kuhakikisha unanipata, hivyo nimeona leo nije mwenyewe ili usipate taabu ya kuendelea kunitafuta. Sijui unasemaje, mzee?” Tunu alisema huku uso wake ukiwa umepambwa na tabasamu bashasha.


Hakuna jibu lililotoka kinywani mwa Mr. Oduya bali aliendelea kuduwaa huku akiwatazama Tunu na Tom kwa mshangao.

“Mr. Oduya, wewe ni mtu mbaya sana usiye na shukrani hata chembe,” Tunu aliendelea kuongea kwa sauti tulivu huku akiyatuliza macho yake kwenye uso wa Mr. Oduya. “Nafasi na heshima uliyo nayo kwenye jamii ya Watanzania ni kubwa sana lakini hujaridhika. Mamilioni ya Watanzania wamekuamini sana kiasi kwa kudhani ungefaa kuwa Rais ajaye lakini kumbe ni mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo! Unadiriki kushiriki katika mipango michafu ili kutimiza lengo lako. Aibu ilioje...”


Mr. Oduya akaonekana kurudiwa na fahamu, aliinuka huku akiwakazia macho Tunu na Tom. Muda wote Tom alikuwa kimya kabisa akimtazama Mr. Oduya kwa makini kama aliyekuwa akiyasoma mawazo yake.


“Get out of my office now!” Mr. Oduya alifoka huku sauti na mwili wake ukitetemeka kwa ghadhabu.


Tunu na Tom waliendelea kuketi kwenye viti vyao wakiwa hawana wasiwasi wowote, walikuwa wakimtazama kwa makini huku nyuso zao zikipambwa na tabasamu.


“Mzee, nilidhani ungefurahi kutuona hapa kwani ulikuwa unatusaka kwa udi na uvumba. Umesababisha vifo vya watu wako na hata rafiki’angu Victor yupo hospitali akipigania uhai wake, yote ni sababu ya kuhakikisha unatupata, sasa...”


“Toka nje! Tokeni kabla sijawafanyia kitu kibaya...” Mr. Oduya limkatisha Tunu huku akifoka kwa ghadhabu. Povu la hasira lilianza kumtoka mdomoni.


“...usijali, nikimaliza kukueleza niliyokusudia tutatoka,” Tunu alisema pasipo kujali vitisho vya Mr. Oduya. “Kumbuka taifa hili siyo kampuni ambayo yeyote anaweza kuimiliki, uliweza kuwanunua watu wengi akiwemo Kamishna Omalla na Victor lakini ukasahau kuwa wapo wenye moyo wa kizalendo kama Faustine Thomas Ndejembi, ambaye wewe unamfahamu kwa jina la Tom...”


“Toka!” Mr. Oduya alifoka huku akivuta mtoto wa meza na kutoa bastola aina ya FNX 45 Tactical. Akaishika vyema mkononi na kuielekeza kwa Tunu na Tom, alikuwa ameghadhabika mno na povu lilizidi kumtoka mdomoni. “Tokeni ofisi kwangu, vinginevyo sitasita kuwaua,” alifoka.


Tunu na Tom waliangaliana, wakaachia tabasamu wakionekana kutokuwa na hofu yoyote. Kitendo kile kikamshangaza sana Mr. Oduya. Kabla hajafanya chochote mlango wa ofisi yake ukapigwa kumbo, Naibu Kamishna Mamboleo na vijana wake sita waliokuwa wamebebelea bunduki na vifua vyao vikiwa vimekingwa na mavazi maalumu yanayozuia risasi wakaingia na kutawanyika ndani ya ile ofisi. Wale askari wote walikuwa na sura ya kazi.


Mr. Oduya akapigwa na butwaa, alimtazama Naibu Kamishna Mamboleo kwa macho yenye mchanganyiko wa aibu na hasira, kisha akayahamisha macho yake kuwataza wale askari kwa zamu kabla hajayarudisha kwa Tunu na Tom, ambao sura zao zilikuwa bado zimepambwa na tabasamu.


“Mr. Oduya, tafadhali weka bastola yako chini na ujisalimishe. Kama ni mipango imeshaharibika. Umemwaga damu zisizo na hatia, umethubutu kununua watu hadi walinzi wa Amani kwa sababu ya kutaka kutimiza mipango yako michafu ili uwe kiongozi wa nchi hii. Jisalimishe ili sheria ichukue mkondo wake,” Naibu Kamishna Mamboleo alimwamuru Mr. Oduya.


Mr. Oduya alimtazama Naibu Kamishna Mamboleo kwa hasira, alionekana kuchanganyikiwa. Aliyasaga meno yake kwa hasira. “Siwezi kukubali kukamatwa na kupelekwa mahakamani, nitaitazama vipi jamii? Nitamtazama vipi Rais?” Mr. Oduya aliwaza na kuielekeza bastola yake kichwani kwake.


Kumbe Tunu na Tom walikuwa wakiyasoma mawazo yake, kwa kasi ya ajabu Tunu alichupa, akaruka juu na kutua mbele ya Mr. Oduya na wakati huohuo Tom aliserereka juu ya meza na kumdaka Mr. Oduya. Tunu aliupiga teke mkono wa Mr. Oduya ulioshika bastola na wakati huohuo ukasikika mlipuko wa bastola.


Naibu Kamishna Mamboleo na vijana wake walipotazama kwa makini wakamwona Mr. Oduya akiwa amedhibitiwa. Tom alikuwa amemkandamiza kwa nguvu huku amembana mikono yake kwa nyuma na Tunu alitoa pingu na kumfunga, kisha wakamwinua na kumkabidhi kwa Naibu Kamishna Mamboleo.


“Kamishna, nasikitika muda hautoshi kuzungumza mengi, kwani kuna mahali tunatakiwa kuwahi,” Tunu alimwambia Naibu Kamishna Mamboleo baada ya kuitazama saa yake ya mkononi.


“Nadhani kesho utapata faili lenye taarifa zote kuhusu mtandao wa uhalifu. Ila huko Kinyerezi kuna nyumba moja ambayo ndani yake tumewafungia wahalifu wanne waliotumwa na huyu mzee kutuua mimi na Tom. Hapo chini kuna wenzetu wawili, Bob na Dumba, watawapeleka kwenye nyumba hiyo,” Tunu alisema huku akimshika mkono Tom tayari kwa kuondoka.


“Pia katika Hospitali ya St. Agatha iliyopo Mikocheni inayomilikiwa ya rafiki wa Mr. Oduya, kuna mtu anaitwa Victor, Ofisa Usalama wa Taifa anayeshughulikia Kanda ya Kinondoni, amelazwa akitibiwa kwa siri baada ya kuvunjwa mbavu alipopambana nami, alitumwa na huyu mzee kuja kuniua,” Tunu alisema huku akipiga hatua kuondoka.


“Kwa nini, vijana?” Naibu Kamishna Mamboleo alifoka. “Kwa nini hamkuyaweka mambo haya wazi mapema hadi damu nyingi imemwagika? Mnajua huyu mtu alikaribia kunifanya nijiuzulu kazi yangu!” Naibu Kamishna Mamboleo alisema kwa huzuni.


“Usijali, Kamishna. Muda ulikuwa haujafika, maana kila kitu kina wakati wake chini ya jua,” Tunu alisema, kisha yeye na Tom wakaanza kupiga hatua kueleka nje ya ile ofisi. Walitoka wakaelekea kilipo chumba cha lifti ambapo Tom alibonyeza kitufe cha kuteremka, milango ikafunguka na kuwaruhusu kuingia ndani. Wakateremka hadi chini na kuelekea kwenye gari lao.


* * * * *


Saa kumi na robo Tunu na Tom walikuwa wanashuka toka kwenye gari lao katika viunga vya maegesho ya magari ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuelekea kwenye jengo la wodi alimokuwa amehamishiwa Sammy katika jengo la Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI). Walitembea wakiwa wameshikana mikono kama wanandoa wapya waliotoka kwenye fungate baada ya ndoa yao.


Wakati wakipita kwenye korido ndefu ya jengo lile la Taasisi ya Tiba ya Mifupa walisikia mazungumzo ya watu waliopishana nao wakizungumza kuhusu kifo cha Kamishna Omalla na kukamatwa kwa bilionea Mr. Oduya. Tunu na Tom wakatazamana wakioneshwa kushangazwa sana jinsi habari zile zilivyoweza kusafiri haraka na kufika katika kila pembe ya jiji la Dar es Salaam.


Hawakupata taabu kuifikia wodi alimolazwa Sammy kwani pale nje walimkuta askari mmoja mwenye silaha aliyekuwa akilinda eneo lile aliyewaelekeza. Askari yule alikuwa amepewa taarifa na Naibu Kamishna Mamboleo kuhusu ujio wao.


Waliingia wodini wakamkuta Sammy akiwa amelala kitandani kwenye foronya laini na mto wa kuegemeza kichwa, alikuwa akiongea na Joyce aliyekuwa pembeni yake ameketi kwenye kiti cha magurudumu. Madame Norah, Bi. Pamela, Rafel Jengo na Elli walikuwa wamesimama kando, wote wakimsikiliza Sammy.


Kwa mwonekano wa haraka Sammy alionekana hakuwa katika hatari kama mwanzo na hata chumba alichohamishiwa hakikuwa na mitambo ya kumsaidia kupumua ingawa alikuwa amewekewa kifaa maalumu cha kuchunguza mwenendo wa mapigo ya moyo wake kwenye vidole vya mkono wa kulia.


Tunu na Tom walipoingia wakawafanya watu wote wageuze shingo zao kutazama kwa makini kule mlangoni. Sammy na Elli waliwatambua mara moja. Sammy hakuamini macho yake. Alimtazama Tunu wakati akipiga hatua zake za madaha kuelekea pale kitandani huku mtikisiko wa umbo lake zuri la kike na matata ukizimeza haraka hisia za Sammy pasipo kujali maumivu ya mwili aliyokuwa nayo muda ule.


“Tunu!” Sammy alijikuta akitamka jina hilo kwa mshangao mkubwa uliochanganyika na furaha huku akitamani kuinuka kutoka pale kitandani ili amkumbatie. Lakini akajionya asifanye hivyo na kumtupia jicho mkewe.


“Sammy!” Tunu naye aliita kwa mshangao huku akiharakisha kwenda pale kitandani, alipofika alinyoosha mkono wake na kumgusa paji lake la uso kwa furaha huku akitokwa machozi ya furaha. Kisha alinyoosha mikono yake juu kumshukuru Mungu. “Vipi unajisikiaje kwa sasa?” Tunu alimuuliza Sammy huku akigeuza shingo yake kuwatazama watu wengine.


“Najisikia nafuu sasa, hasa baada ya kupata taarifa njema kuhusu kukamatwa kwa Mr. Oduya,” Sammy aliongea kwa furaha, kisha kama aliyegutuka akageuza shingo yake kumtazama Joyce. “By the way, huyu ni Joyce mke wangu...” alimtambulisha Joyce kwa Tunu.


Tunu alinyoosha mkono wake kumsalimia Joyce. “Nafurahi kukufahamu, maana juzi asubuhi nilikuja hospitali lakini sikuruhusiwa kukuona. Natumai unaendelea vyema,” alisema huku akiachia tabasamu.


“Naendelea vizuri, namshukuru Mungu kwa kunilinda, maana ni vigumu sana kuamini kuwa hadi sasa nipo hai,” Joyce alisema huku akinyoosha mkono wake kumsalimia Tunu. Waliangaliana kwa muda, kila mmoja alionekana kumhusudu mwenziwe.

Kisha Sammy aliwatambulisha Madame Norah, Bi. Pamela na Rafel Jengo kwa Tunu na Tom kisha akawaeleza kwa kifupi kuhusu Tunu. Wote walibaki mdomo wazi wakimshangaa Tunu, msichana mrembo lakini hatari kuliko hata hatari yenyewe. Ni Elli peke yake ambaye hakushangaa, kwani alimfahamu vyema Tunu.


Kisha kitambo kifupi cha ukimya kikapita mle ndani huku kila mmoja akionekana kuzama kwenye tafakuri juu ya mambo yote yaliyotokea. Simu ya Tunu ikaanza kuita, Tunu aliitazama kwa makini na kuliona jina la Dk. Mgaya Kingoba, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Akamtupia jicho Tom na kuwaomba radhi watu wengine kisha akajitenga nao na kuipokea ile simu.


“Hallo!” Tunu alisema kwa sauti tulivu baada ya kuiweka sikioni.


“Nimepata taarifa zenu, kwanza hongereni sana kwa kazi nzuri,” Dk. Kingoba alisema kwa sauti tulivu.


“Ahsante, mkuu,” Tunu alisema na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


“Katika oparesheni hii ulikuwa nani?”


“Mimi na Faustine Ndejembi, yule wa Ofisi ya Waziri Mkuu. Na watu wengine wawili ambao ni wapelelezi wa kujitegemea.”


“Ndejembi yupo wapi sasa hivi?”


“Ninaye hapa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Vipi mkuu?”


“Rais anahitaji kuonana nanyi leo usiku, hivyo ninaomba mfike ofisini kwangu kabla ya saa kumi na mbili,” Dk. Kingoba alisema na kukata simu.


Tunu alikenua meno kwa furaha na kurudi pale kitandani. “Sahamani, tunawaacha tumeitwa makao makuu haraka,” Tunu alimwambia Sammy kisha akawataka radhi watu wengine. Yeye na Tom wakatoka kuelekea kwenye gari lao wakiwaacha watu wote wakiwasindikiza kwa macho yaliyowahusudu sana.


* * * * *


Tom aliendesha gari lake katika barabara ile ya Umoja wa Mataifa akielekea Makao Makuu ya Idara ya Usalama wa Taifa, eneo la Oysterbay. Macho alikuwa ameyakaza barabarani lakini mawazo yake yalikuwa kwa Tunu, mwanadada jamali na aliyeumbika vyema. Kila nukta iliyopita Tom alijikuta akishindwa kuvumilia. Alihisi pumzi zikimpaa, akajiambia kimoyomoyo kuwa katika maisha yake hakupata kukutana na kiumbe wa shani kama Tunu!


Ingawa aliwahi kuwa na uhusiano na wasichana wengi wasio na idadi, lakini hakuwahi kuhisi hali kama aliyoihisi wakati huo akiwa ameketi pembeni ya mrembo wa shani anayeweza kumsahaulisha yeyote machungu yote ya dunia. Kwa Tom, Tunu alikuwa ua waridi machoni mwake, miski puani mwake na pepo masikioni mwake. Hata hivyo, alihisi donge la wivu likimkaba kooni baada ya kukumbuka kuwa Tunu alikuwa bado anampenda Sammy.


“Inaonesha bado unampenda sana Sammy! Kwa nini usimsahau na kuufungua moyo wako kwa mwanamume mwingine?” Tom alijikuta akimuuliza Tunu.


“Kwa sasa Sammy ninampenda kama rafiki na si kimapenzi, ninaiheshimu ndoa yake,” Tunu alisema na kuachia tabasamu lililoficha uchungu. “Endapo nitampata mwanamume mwenye mapenzi ya kweli na mimi nikampenda basi nitaufungua moyo wangu kwake.”


“I wish I could be that man!” Tom alisema kwa sauti ya chini ambayo iliweza kumfikia Tunu.


“Umesemaje, Tom? Tunu aliuliza huku akimtazama kwa makini.


“Oh! Forget what I said. Kuna nyakati ulimi unatamka jambo bila kuwasiliana kwanza na ubongo,” Tom alisema huku akiachia kicheko hafifu.


“Tafadhali rudia kile ulichokisema, nimesikia ukisema jambo ila sijakupata vyema,” Tunu alisisitiza huku akiyatuliza macho yake kwenye uso wa Tom.


“Nilisema I wish I could be that man!” Tom alisema huku akimtazama Tunu kwa tabasamu.


“Kwa nini utamani, kwani ukitaka iwe hivyo haitakuwa?” Tunu aliuliza huku akiwa bado ameyatuliza macho yake kwa Tom.


“Tunu, wewe ni msichana mrembo uliyejaaliwa sifa zote zimfaazo mke, ni mwanamke wa kipekee kabisa ambaye nimewahi kukutana naye katika maisha yangu. Unastahili kuwa na mume bora. Naamini mwanamume atakayekupata atakuwa na bahati sana. Ninatamani kuwa mwanamume huyo lakini sijui kama ninazo sifa za kuwa na wewe,” Tom alisema kwa huzuni na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.


Kikapita kimya kizito ndani ya lile gari kilichomfanya Tom kushtuka, akageuza shingo yake kumtazama Tunu na kumwona akiwa ameinamisha kichwa chake akionekana kuwa mbali sana kimawazo.


“Tunu... usichukie. Nimeyasema haya kwa sababu sitaki kuendelea kuumia, huu ndiyo ukweli ulio ndani ya moyo wangu… nimenyoosha mikono yangu kuomba zawadi unayodhani itanifaa na sistahili kuona utakachonipa, ni hiari yako kuniwekea mikononi kile unachodhani kinanifaa zaidi hata kama ni kaa la moto...”


“Wala usijali, Tom. Ninaelewa kilichomo moyoni mwako kupitia macho yako. Siwezi kuzuia maana kila kitu hupangwa na Mungu. Ninadiriki kusema kuwa nadhani nimezaliwa kwa ajili yako…” Tunu alisema maneno yaliyoufanya mkondo wa umeme kupitishwa ghafla katika mwili wa Tom. Vita vilikuwa vimekwisha na yeye akiwa kasalimu amri!


“Unasema kweli au unanitania?” Tom aliuliza kwa sauti iliyoonesha wazi kuwa hakuamini alichokisikia. Ni kweli hakutegemea kujibiwa kirahisi namna ile. Aliduwaa kwa muda akiwa hajimudu huku akiajabia sauti iliyovunjika, na macho yaliyolegea. Vyote pamoja vilitoa haiba ya kike ndani mwa Tunu na kumwaia.


“Sina sababu ya kukutania,” Tunu alisema huku akiachia tabasamu pana. Jibu lile likamfanya Tom aachie usukani na kumkumbatia Tunu huku akimporomoshea mabusu, akajisahau kama alikuwa barabarani akiendesha gari. Gari likaanza kupoteza mwelekeo na kuserereka likielekea mtoni kwenye daraja la Selander. Kidogo wapate ajali, kama isingekuwa Tunu kumshtua!


Tom alikanyaga breki, gari likasimama. Kisha wote wawili waliangaliana na kujikuta wakicheka kwa sauti kubwa. Kilikuwa ni kicheko cha furaha isiyopimika!


TAMATI



0 comments:

Post a Comment

Blog