Search This Blog

Wednesday 29 March 2023

PENIELEA (4) - 2

  


Simulizi : Peniela (4)

Sehemu Ya Pili (2)









“ Nimestushwa sana baada ya kumuona baba akiwa na Elibariki.How it happened? Akajiuliza Anna ambaye alikosa kabisa usingizi.

“ Kwa mujibu wa maelezo aliyonipa Elibariki nikiwa afrika ya kusini alisema kwamba baba ndiye mhusika mkuu wa vifo vya mama na dada .Alinieleza kwamba hata yeye kutaka kuuawa ulikuwa ni mpango wa baba na ndiyo maana akaenda mafichoni.Kitendo cha kuibuka tena na kuonekana akiwa na baba kimenishangaza sana.Nini kinaendelea hapa? Lazima nifahamu kinachoendelea kati yao kwa sababu hainiingiii kabisa akilini kuwaona wawili hawa wakiwa wanaongozana pamoja .Tayari Elibariki anatafutwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mke wake iweje basi mtuhumiwa wa mauaji aonekane ameongozana na rais? Anna akazidi kuumiza kichwa kwa mawazo.





********



Hali ilikuwa ya ukimya mkubwa katika jumba la John Mwaulaya.Kila aliyekuwamo ndani ya jumba hili alionekana kuwa katika tafakari .Kilichotokea usiku ule kiliwastua wote.Kwa takribani masaa mawili sasa wageni waliotoka Marekani walikuwa wamejifungia katika mojawapo cha chumba wakijadiliana.Mlango wa chumba walimokuwamo ukafunguliwa na Nickson Strawberry akawataka watu wote wakusanyike sebuleni

“ Ndugu zangu poleni sana kwa mkasa mzito uliotokea .Usiku wa leo tumewapoteza wenzetu wanne katika shambulio na wengine wawili hali zao ni mbaya sana.Hatukutegemea jambo kama hili kutokea lakini limetokea. “ akanyamaza kidogo kisha akaendelea



“ Siku ya leo imekuwa ni ya majanga makubwa kwa Team SC41 kwani tumempoteza pia mtu muhimu sana katika kundi letu ,John Mwaulaya.Huyu ni mtu aliyeanzisha Team SC41 hapa Tanzania .Ni mtu anayeifahamu Team Sc41 kwa undani sana.John Mwaulaya amefariki katika wakati ambao mchango wake ulikuwa unahitajika sana ili kufanikisha operesheni 26B. Ili operesheni hii muhimu ifanikiwe kuna watu wawili ambao tuliwategemea sana na kuwaweka m stari wa mbele,Captain Amos na Peniela.Kwa bahati mbaya kwetu,Captain Amos hatumjui na kati yetu hakuna aliyewahi kumuona.Ni John Mwaulaya pekee aliyemuingiza Team SC41 na alikuwa anaripoti kwake kwa hiyo sisi itakuwa vigumu sana kumpata.Mtu pekee ambaye tumebaki tunamtegemea ni Peniela.Katika hali isiyo ya kawaida Peniela naye alianza kuonyesha ushirikiano mdogo kwetu na baada yua kifo cha John Mwaulaya alitoweka ikatulazimu kuanza kumfuatilia.Tulikuwa tunamtafuta kwa mambo mawili makubwa.Kwanza atupe muelekeo wa operesheni 26B kwa sababu yeye ndiye tuliyemtanguliza mbele .Pili ni kuhusiana na mazishi ya John Mwaulaya.Katika wosia wake John Mwaulaya ameandika kwamba baada ya kifo chake mali zake zote atakabidhiwa Peniela.Hii inatufanya tuamini kwamba Peniela alikuwa ni mtu muhimu sana kwa John kwa hiyo yeye ndiye atakayekuwa na sauti kubwa kuhusiana na namna ya kumzika John Mwaulaya.Baadae usiku kamera za siri zilizofungwa nyumbani kwake zikamnasa akiingia nyumbani kwake akiwa ameongozana na mwanaume mmoja.Haraka haraka tuliwatuma vijana wetu kumfuatilia.” Akanyamaza kidogo na kuendelea



“ Peniela na jamaa aliyeongozana naye hawakukaa sana mle ndani ,wakatoka na kuondoka ,vijana wetu wakawafuatilia ili kufahamu wanakwenda wapi.Kwa mujibu wa vijana wetu ilionekana Peniela na huyo mtu aliyekuwa naye,waling’amua kwamba wanafuatiliwa kwa hiyo wakajihami na ndiyo m aana kulitokea upinzani mkubwa na tukawapoteza wenzetu wanne.Hatukufanikiwa kumpata Peniela kwani alifanikiwa kutoroka na huyo mwenzake.Mwanaume ambaye alikuwa ameongozana na Peniela ametambuliwa na Dr Martin kwamba aliwahi kufika hapa nyumbani kwa John akiwa ameongozana na mwenzake na akamtolea John vitisho vya kumuua.Mtu huyu anaonekana kufahamiana na Peniela na jina lake anaitwa Mathew.Peniela na Mathew wanaonekana ni washirika na na kuna siri wanayo kwa hiyo ili kuipata package tunayoitafuta toka kwa Dr Joshua lazima tumpate Peniela kwa namna yoyote ile kwani ndiye kiungo pekee kati yetu na rais.Bila yeye hakuna kinachoweza kufanikiwa.Kwa sasa Peniela yuko katika mstuko baada ya makazi yake kuchomwa moto na tumefanya hivi ili kumfanya Peniela akose makazi na arejee kwetu.Kwa sasa kumpata Peniela ni kipaumbele cha juu kuliko vyote lazima tufanye kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha tunampata kabla ya kesho mchana.Bila ya yeye juhudi zetu zote tulizozifanya kwa miaka kadhaa ili kuipata package hiyo zitakuwa ni bure.Hatuwezi kukubali hilo litokee kwa hiyo basi tutumie kila aina ya uwezo tulionao kuhakikisha Peniela anapatikana.” Akasema Nickson



“ Josh kesho asubuhi utashughulikia mazishi ya watu hawa tuliowapoteza.Kumbuka ni mazishi ya kimya kimya na asifahamu mtu yeyote.Vile vile kwa sasa wewe ndiye utakayekaimu uongozi wa Team SC41 kwa hapa Tanzania kwa hiyo waongoze wenzako kuhakikisha Peniela anapatikana.Sisi tunakwenda kuwataarifu ofisi kuu Marekani kilichotokea” akasema Nickson halafu akaongozana na wale wenzake wakaondoka kuelekea ofisi kuu ya Team SC41.

“ Siamini kama nimepewa uongozi wa Team SC41 Tanzani.Hili ni jukumu zito na na nimepewa kama mtego.Nahisi hawa jamaa wanahisi kitu Fulani kuhusu mimi na Peniela.Mimi ndiye niliyempigia simu kumfahamisha kwamba anafuatiliwa .Nashukuru niliwahi kumpa taarifa ile ambayo naamini imemsaidia sana kwani bila hivyo wale jamaa wangemkamata.Where is she now? Imeniuma sana kusikia eti nyumbayake wameichoma moto.Huu ni unyama mkubwa sana.Mtu kama Peniela hakupaswa kabisa kufanyiwa ukatili kama huu hasa kwa mambo makubwa ambayo ameyafanya katika Team SC41.Watu hawa ni wanyama na hawafai kabisa.Nadhani mwisho wa Team SC41 umewadia.Wamekose a sana kunipa uongozi .Nitamtafuta Peniela na kwa kushirikiana naye we’re going to take down team SC41 “ akawaza Josh na kuelekea chumbani kwa John Mwaulaya.







******





Gari walilopanda Mathew na Peniela lilitawaliwa na ukimya mkubwa.Dereva aliyekuwa anaendesha gari lile alionekana kutohitaji maongezi ya aina yoyote

“ Mathew who is this guy? Where are wre going? “ akauliza Peniela kwa kunong’ona



“ Vuta subira Peniela utafahamu kila kitu.Usiwe na wasi wasi ,we’re going somewhere safe” akasema Mathew.Peniela akamtazama kwa sekunde kadhaa na kusema

“ Thank you Mathew for everything.Thank you for saving my life”

Mathew hakujibu kitu akatabasamu halafu akalitazama jeraha lake lililokuwa linavuja damu

“ Damu hii inayomwagika haiwezi kupotea bure.Lazima ilipwe” akawaza halafu akakiegemeza kichwa katika kiti na kuzama katika tafakari nzito

“ Nini kimesababisha nyumba yangu kuungua moto? Ni team SC41 ndio waliofanya unyama huu.Nalazimika kuamini hivyo kwa sababu hata nyumba ya Peniela imechomwa moto pia na matukio haya yote yametokea kwa wakati mmoja.Team SC41 wanamtafuta Peniela wa gharama zozote zile kwani ndiye tegemeo lao kubwa katika kukipata kirusi Aby.Bila yeye hawataweza kufanikisha lolote.Nina hakika walimfuatilia Peniela na kugundua kwamba alikuwa nyumbani kwake na ndiyo maana wakaamua kufanya vile walivyofanya.Kwa mara ya pili tena team SC 41 wanateketeza makazi yangu kwa moto.Mara ya kwanza alikuwa ni John mwaulaya aliyeteketeza nyumba yangu kwa moto na familia yangu yote ikateketea.Safari hii wameiteketeza tena na …” picha ya Anitha ikamjia na kumfanya aume meno kwa uchungu

“ Oh my God !! Anitha ..!!. She was in there with Elibariki,Naomi and Rosemary Mkozumi.Are they all dead? Jamani Anitha n itamlilia kilio gani mimi? Amekuwa ni mtu wangu na mshirika wangu wa karibu mno.Ufanikishaji wa k azi zangu nyingi kwa kiasi kikubwa unamtegemea yeye.Anitha ni mwanamke jasiri asiyeogopa kitu.Kuna nyakati tumekumbana na hatari kubwa lakini bado alisimama bila woga na tukashinda.Sijawahi na sintakutana na mwanamke kama Anitha.Sitaki kabisa kuamini eti Anitha amekufa.I know her she knows how to fight.Nafsi yangu inakataa kabisa kukubali kwamba Anitha aliteketea ndani ya ule moto” akawaza Mathew



“ Lakini kama hakuteketea ndani ya ule moto yuko wapi ? Jaji Elibariki,Naomi na Rosemary Mkozumi wako wapi? Nao pia watakuwa wameteketea ? Rosemary Mkozumi ni mwanamke hatari kwa nchi yetu ambaye anashirikiana na mtandao wa kigaidi na kwa kupitia kwake tungeweza kufahamu mambo mengi na mipango yote ambayo imepangwa kutekelezwa na magaidi katika ukanda huu wa afrika mashariki.Kumpoteza Rose kutarudisha nyuma juhudi zote za kupambana n a ugaidi.Ngoja kwanza nitulize akili yangu na kutakapopambazuka tayari nitakuwa nimepata akili n ifanye nini lakini kwa yeyote aliyefanya unyama huu wa kunichomea nyumba kwa lengo la kuharibu mipango yangu amekosea sana na ameuwasha moto ambao hataweza kuuzima.Safari hii watauona upande wangu wa pili ulivyo” akawaza Mathew huku akiuma meno kwa hasira ,akageuka na kumtazama Peniela.



“ Namuonea huruma sana Peniela.Inaonekana katika maisha yake hajawahi kukutana na mikasa ya namna hii.Sura yake inaonyesha wazi amekata tamaa kabisa.Kilichotokea usiku huu kimemuogopesha mno.Hata hivyo nitamlinda .Sintaruhusu hatari yoyote imkaribie.Kwa maneno yake mwenyewe kabla hajakata roho ,John Mwaulaya alinisisitiza kwamba nimlinde Peniela kwa namna yoyote ile hata kama ni kwa kuyaweka maisha yangu hatarini.Thats what I’m going to do.Nitamlinda Peniela zaidi ya mboni yangu ya jicho” akawaza Mathew



“ Whats going to happen from tomorrow is a victory or death.Chochote kinaweza kutokea lakini nitapambana kuhakikisha Peniela anakuwa salama na mipango yetu yote inakwenda kama tulivyoipanga” akawaza Mathew akajaribu kuinua mkono akahisi maumivu makali



“ Nahtaj kulitibu jeraha hili haraka.” Akawaza Mathew na taratibu mwendo wa gari ukapungua,walikuwa wamelikaribia geti kubwa jeusi.Yule dereva akatoa kifaa kidogo akakielekezea katika geti na kubonyeza kidude Fulani chekundu na geti likaanza kufunguka wakaingia ndani.Lilikuwa ni jumba zuri la ghorofa moja llilozungukwa na taa nyingi ,mbele ya jumba lile kuliegeshwa gari tatu .dereva akawageukia akina Mathew



“ Safari yenu bado inaendelea.Mtaingia katika gari lingine na mtapelekwa mahala mnakotakiwa kwenda.Ila nawatahadharisha .There is only one rule you’ll have to obey.Follow instructions and don’t ask question.Tumeelewana?

Mathew na Peniela wakatazamana na kujibu kwa pamoja

“ Tumeelewana”



“ Good.Now follow me” akasema Yule dereva na kushuka garini akina Mathew nao wakashuka wakamfuata,akawaelekeza waingie katika mojawapo ya magari yaliyokuwa yameegeshwa nje ya jumba lile halafu yeye akaingia ndani.



“ Mathew who are these people? Do you real know them? Akauliza Peniela kwa wasi wasi

“ Relax Penny.We’re going to be fine” akajibu Mathew kwa ufupi.

“ Mathew mienendo ya hawa jamaa inanipa shaka sana na ndiyo maana nahitaji kufahamu kama tuko salama ama vipi.Kilichotutokea usiku wa leo kimenipa fundisho la kuwa na mipaka katika kumuanini mtu.Kwa hiyo Mathew naomba unieleze ukweli unawafahamu hawa watu?

Kabla Mathew hajajibu kitu ,mlango wa kuingilia ndani ya ile nyumba ukafunguliwa akatoka jamaa mmoja aliyevalia fulana nyeupe na kofia nyeupe pia akaingia garini

“ Hi “ akawasalimu akina Mathew bila hata ya kuwatazama usoni halafu akawasha gari.Hakupita katika geti lile waliloingilia badala yake akazunguka nyuma ya nyumba kulikokuwa na geti lingine wakaondoka

“ Watu hawa ni akina nani? Mathew amewafahamuje? Huku tunakoenda wanatupeleka wapi? Akajiuliza Peniela



“ Napatwa na wasi wasi sana hasa nikikumbuka kilichotokea usiku wa leo.Team SC41 wamenifanyia kitendo cha kinyama sana.Kila kitu changu wamekiteketeza na kuniacha kama nilivyo.Nyaraka zangu ,kumbu kumbu zangu zote za muhimu zimeteketea.Huu ni ukatili usiovumilika.Nimefanya mambo mengi na mengine ya hatari kubwa kwa ajili ya team SC41 lakini haya ndiyo malipo yake? Kwa namna yoyote ile lazima nihakikishe ninaimaliza Team Sc41.Hata hivyo namshukuru sana Josh kwani bila yeye kunistua kuwa ninafuatiliwa na team SC41 sijui n ini kingetokea.Baada ya kunikosa sasa ni zamu yao.Moto huu lazima uwageukie wao” Akawaza Peniela huku safari ikiendelea.

“ Nyumba yangu naamini imechomwa moto na Team Sc41 lakini nani kaichoma moto nyumba ya Mathew na kwa nini ? Je ni team SC41? Kama ni wao walifahamu vipi niko pale? Kwa upande Fulani nalazimika kuamini watakuwa ni wao kwani tukio la kuchomwa moto nyumba yangu na ile ya Mathew vimetokea kwa wakati m moja.Nahisi aliyechoma nyumba zetu tayari alikuwa anafahamu mipango yetu na alifahamu kuwa mimi na Mathew tuna mashirikiano na ndiyo maana akaamua kuchoma nyumba zetu ili kuvuruga mipango yetu yote.Halafu bado sijapata jibu,Anitha,jaji Elibariki,na Yule kahaba Naomi wamesalimika katika moto ule? Au nao wameteketea?Haitaniuma kabisa kama jaji Elibariki na Naomi watakuwa wameteketea kwa moto kwani wanastahili ila nitaumia sana kama Anitha atakuwa amefariki.Anitha hastahili kufa kifo kigumu kama cha moto..Nitashirikiana na Mathew kuhakikisha wale wote waliofanya kitendo hiki wanalipa uovu wao” akawaza Peniela na kugeuka akamtazama Mathew.



“ Sijawahi kukutana na mtu jasiri kama huyu katika maisha yangu lakini pamoja na ujasiri wake kwa mara ya kwanza nimeshuhudia akimwaga chozi.Kitendo alichofanyiwa cha kuchomewa nyumba yake kimemuumiza mno.Anatakiwa kupata faraja ili apunguze hasira na machungu aliyonayo.Kwa kuwa niko k aribu naye nitajitahidi kwa kila niwezavyo kuhakikisha kuwa anapata faraja.He needs someone by his side.Vile vile ninapaswa kumshukuru sana kwani bila ya yeye leo nisingeweza kuwaponyoka team SC41.He’s my hero and this is the man I deserve to be in love with.Ni mwanaume wa kipekee kabisa ambaye yuko tayari kuhatarisha maisha yake kwa ajili yaw engine.After everything is over I hope me and him we’re going to be together for good.Japokuwa tuko katika matatizo lakini lazima nikiri kwamba najihisi kuanza kumpenda Mathew.Sielewi kama h isia hizi ni za kweli kwa sababu hisia zangu zimekuwa zikibadilika mara kwa mara mare leo kwa huyu,kesho kwa huyu lakini naamini safari hii hisia zangu ni za kweli.Imekuwa ni kawaida yangu kila nimuonapo mwanaume mzuri akanivutia basi hutokea kumpenda .Siwezi kuendelea na maisha ya namna hii..Natakiwa kubadilika.Mabadiliko yataanzia kwa Mathew.Hisia kwamba ninampenda zinazidi kukita mizizi yake ndani ya moyo wangu japokuwa sifahamu kama na yeye anahisi chochote juu yangu.” Peniela akamtazama tena Mathew aliyeonekana kuzama katika mawazo mazito



“ Kuna jambo bado linanipa mawazo mengi.Mathew na John Mwaulaya waliongea nini pale hospitali? Kwa nini John hakutaka nisikie mazungumzo yao? Kuna kitu gani hakutaka nikifahamu? Kwa nini M athew amekuwa mgumu sana kunieleza kile alichoelezwa na John ? Hapa lazima kuna jambo kubwa ambalo John alimweleza Mathew kwani nakumbuka baada tu ya kumaliza maongezi yao kulikuwa na mabadiliko katika sura ya Mathew.Kwa mujibu wa maelezo aliyowahi kutupa Mathew ni kwamba Team Sc41 wakiongozwa na John mwaulaya waliiteketeza nyumba yake ka moto miaka kadhaa iliyopita a katika tukio hilo familia yote ya Mathew pia iliteketea kwa moto.Tukio hili lilimfanya Mathew na John Mwaulaya wawe maadui wakubwa na siku zote Mathe alikuwa anatafuta nafasi ya kulipiza kisasi.Kinachonishangaza na kunipa udadisi ni kwamba baada ya mazungumzo yao Mathew hakuonyesha tena ile hasira yake kubwa kwa John Mwaualaya.Kitu gani basi John alimweleza Mathew kiasi cha kumfanya asiwe tena na hasira juu yake?Haiwezekani watu waliokuwa maadui wakubwa waongee na kupeana mikono baada ya kumaliza maongezi yao bila ya kuwa na jambo muhimu lililomaliza tofauti zao.Kuna kitu hapa ambacho nakikosa na ambach o lazima nikifahamu” akawaza Penila

Gari lilivuka daraja la Nyerere na kuelekea the Blue city au jiji la bluu.Huu ni mji mpya kabisa wa kimataifa ulioko Kigamboni.Waliwasili katika jengo moja kubwa llilozungushiwa uzio na dereva akapunguza mwendo wa gari akawasha taa ya kushoto kuashiria kwamba alikuwa anaingia katika jengo lile.Juu ya geti kulibandikwa kibao kikubwa kilichosomeka Calvary Ministry.

“Church?!!!..Peniela akashangaa





“ Tumekuja kufuata nini hapa kanisani? Akajiuliza Peniela wakati gari likivuka geti la kanisa na kufuata bara bara iliyoelekea kushoto iliyoelekea katika jumba moja kubwa la ghorofa lililokuwa mita kadhaa toka katika kanisa lile kubwa.Kwa upande wa kaskazini mwa kanisa kama mita mia tano hivi kulionekana majengo sita makubwa ya ghorofa .

“ Sijawahi fika mahali hapa.Tumefuata nini? Tumemfuata nani? Maswali yangu hayataweza kupata majibu kwani Yule jamaa kule tulikotoka alitupa sharti la kutouliza chochote. Ninachopaswa kufanya ni kunyamaza na kusubiri kujua kinachoendelea” Akawaza Peniela

Nje ya jengo lile walilokweda kulikuwa na magari mawili, dereva akaegesha karibu kabisa na zile gari mbili halafu akawageukia akina Mathew

“ We’re here.You can get out now.” Akasema huku akiufungua mlango akashuka.Mathew na Peniela nao wakashuka wakaongozana na Yule dereva hadi katika mlango mkubwa wa kuingilia ndani.Yule jamaa akatoa kadi na kuipitisha katika sehemu maalum ya kupitishia kadi na mlango ukafunguka wakaingia ndani,akawaongoza katika lifti wakapanda hadi ghorofa ya nne.Mara tu milango ya lifti iilipofunguka wakajikuta wakitazamana na watu wawili waliovalia suti nyeusi.Yule kijana akaongea nao kwa kama dakika mbili pembeni halafu mmoja wao akawafanyia ishara akina Mathew wawafuate.Namna mambo yalivyokuwa yanakwenda yalizidi kumpa maswali mengi Peniela lakini alipata nguvu kila alipomtazama Mathew na kumuoana akiwa hana hata chembe ya wasi wasi.

Walipelekwa katika sebule kubwa lililosheheni samani za kupendeza .Baada ya dakika nne wakatokea wanawake wawili waliovalia mavazi ya wauguzi na kuwataka akina Mathew waongozane nao.Kila maelekezo yalipotolewa Peniela alimtazama kwanza Mathew kabla ya kufanya chochote.Bila wasi wasi Mathew akainuka na kuanza kuwafuata wale akina dada Peniela naye akafuata nyuma yake huku wale jamaa wawili wenye suti nyeusi wakiwa nyuma yao.Walipanda ghorofa ya tano wakaingia katika chumba kimoja chenye vifaa kama hospitali.Mmoja wa wale wauguzi akamtaka Peniela amfuate katika chumba kingine.Peniela akasita na kumtazama Mathew



“ It’s ok Penny.Go…” akasema Mathew na Peniela akaongozana na yule muuguzi hadi katika chumba kingine ambacho nacho kilikuwa na vifaa kama vile vilivyokuwa katika chumba kile alikomuacha Mathew.Yule muuguzi akamtaka avue nguo zote na aingie katika bafu akaoga na kisha akamuelekeza apande katika kitanda na kumtaka asubiri hapo.

“ Hapa ni wapi? Watu hawa ni akina nani? Mbona mambo yao wanayafanya kimya kila bila ya maelezo yoyote?Mbona Mathew anaonekana kuwaamini sana amewafahamuje watu hawa? Anyway ngoja niendelee kuvumilia nione kitakachotokea”

Peniela akaondolewa mawazoni baada ya mlango kufunguliwa na mtu mmoja aliyevalia koti la kidaktari akaingia

“ Hallow naitwa Dr Lucious Wade.Nataka nikufanyie uchunguzi wa mwili wako ili nijue kama kuna tatizo lolote umelipata.Naomba uendelee kulala hapo hapo kitandani” akasema Dr Lucious aliyeongea kiingereza chenye lafudhi ya Marekani .Alikaa katika kiti na kutazama mambo kadhaa katika kompyuta yake halafu akabonyeza vitufe kadhaa na mtambo Fulani uliokuwa juu ukashuka taratibu na kumfunika Peniela



“ Oh my God ! haya ni mambo gani sasa? Akawaza peniela akwa amefunikwa na mtambo ule.Baada ya dakika tano mtambo ukapanda juu.Dr Lucious akaendelea kucheza na kompyuta yake halafu akainuka na kumfuata Peniela

“ Uchunguzi unaonyesha hauna tatizo lolote kwa ndani wala nje.Uko salama “ akasema na kumtaka Peniela ainuke pale kitandani



“ Ninyi ni akina nani? Peniela akashindwa kuvumilia akajikuta akiuliza swali.Dr Lucious akamtazama kwa sekunde kadhaa na kusema

“ Mlipokuwa mnaletwa huku hamkupewa masharti yoyote?

“ Tulipewa sharti la kutouliza chochote”

“ Vizuri.Zingatia sharti hilo” akasema Dr Lucious na kutoka..Dakika mbili baadae akaingia tena Yule muuguzi akamtaka Peniela amfuate wakaelekea sebuleni.Baada ya muda mfupi Mathew naye akaingia pale sebuleni .Tayari alikwishatibiwa jeraha lake.Wakiwa bado sebuleni wakaletewa chakula chepesi wakala kimya kimya huku wakisimamiwa na wale jamaa wawili wenye suti nyeusi na walipomaliza kula wakaombwa wapumzike na wasubiri maelekezo mengine.Zilipita dakika kama kumi hivi akaingia sebuleni mwanamke mmoja mrembo akawasalimu akina Mathew halafu akawaelekeza kwamba kesho ndipo watakapopata nafasi ya kuonana na askofu.



“ Ninyi ni wapenzi? Akauliza yule mwanamke na kabla Mathew hajajibu Peniela akajibu

“ Ndiyo sisi ni wapenzi”

“ Vizuri.Nilifikiria kuwatenganisha lakini kwa kuwa ninyi ni wapenzi itawalazimu mlale katika chumba kimoja.Twendeni nikawaonyeshe mahala pa kulala” akasema na kuinuka ,akina Mathew nao wakamfuata.Aliwapeleka katika chumba kikubwa na kizuri.



“ Hiki ndicho chumba mtakacholala.Endapo mtahitaji chochote mtabonyeza kitufe kile cha rangi ya kijani na endapo kuna tatizo lolote na mnahitaji msaada basi mtabonyeza kitufe chekundu.Msihofu hapa mko sehemu salama kuna ulinzi wa kutosha “ akasema Yule mama na kutoka akawaacha akina Mathew peke yao.Peniela hakutaka kupoteza wakati akamvaa Mathew kwa swali

“ Mathew tell me,whats going on? Who are these people?

Mathew akageuza shingo akamtazama na kusema

“ Usihofu Peniela we’re safe here.Go to sleep and wait for tomorrow.It’s going t be a very long day.Go to sleep” akasema Mathew .Peniela hakuwa na la kusema .

“ Sawa Mathew tulale tujiandae na siku ya kesho”

“ Lala Peniela mimi sintalala,nitakesha macho nataka nihakikishe usalama wako.” Akasema Mathew na kwenda kuketi katika sofa lililokuwamo mle chumbani.







******





Kwa zaidi ya saa moja Dr Joshua alikuwa anaongea na mkuu wa polisi kanda ya Dar es salaam simuni.Kikubwa walichokiongea ni namna ya kulimaliza suala la jaji Elibariki ambaye tayari anatuhumiwa kwa kosa la kusababisha kifo cha Flaviana.Ulikuwa ni mjadala mrefu lakini mwishowe wakaelewana na kamanda wa poliisi dar es salaam akakubali ombi la Dr Joshua la kumsafisha jaji Elibariki dhidi ya tuhuma zote zilizokuwa zinamkabili .



“ Uuupppphhh !!!...Dr Joshua akasha pumzi baada ya kumaliza kuongea na kamanda wa polisi kanda ya Dar es salaam

“ Haikuwa rahisi kumshawishi kamanda amsafishe jaji Elibariki.kweli ni kazi ngumu kwa sababu tayari umma wote wa Tanzania unafahamu kuwa yeye ndiye aliyesababisha kifo cha Flaviana.Inahitaji kazi ya ziada kumsafisha tena mbele ya umma kwamba hakutenda kosa lile alilokuwa anashukiwa kulifanya.Hata hivyo nashukuru amekubali na ataifanya hiyo kazi” akawaza Dr Joshua akachukua kitambaa na kujifuta jasho

“ I have many things to solve tonight.Next is Kigomba” akainuka na kufungua mlango akamtuma mlinzi wake akamuite Dr Kigomba.Haikuchukua muda Dr Kigomba akawasili na Dr Joshua akamfanyia ishara aketi



“ Kigomba tuna mambo mengi ya kuzungumza mimi na wewe lakini muda umekwenda sana kwa hiyo tutazungumza kwa kirefu baada ya kumaliza shughuli za msiba hapo kesho” akaanzisha mazungumzo Dr Joshua.Dr Kigoma hakujibu kitu akatikisa kichwa na kumpa nafasi Dr Joshua ya kuendelea

“ kwa usiku wa leo kuna mambo mawili au matatu ambayo nitakufahamisha .Jambo la kwanza ni kuhusu biashara yetu na Hussein.Kutokana na hali halisi ilivyo hivi sasa nimeamua kusimamisha kwanza kila kitu hadi hapo baadae hali itakapotulia.”

Kauli ile ikamstua Dr Kigomba na mshangao haukujificha katika uso wake.

“ Mr President how???...Why ??!! we’re so close to finish everything…” akasema Dr Kigomba

“ Kigomba you don’t know whats going on right now na ndiyo maana umestuka na unashangaa.Nimefanya maamuzi haya kwa faida yetu sisi .Endapo tutaendelea na mipango yetu tutakuwa tunajiweka katika matatizo makubwa”

“ Mr President can you explain to me why you are doing this? We’ve sacrificed a lot for this.Maisha ya watu yamepotea ,iweje kila kitu kivurugike katika usiku mmoja?

“ Dr Kigomba mpango wetu umevuja.Tayari kuna watu wanaofahamu kila tunachokfanya na kila hatua tunayoichukua.Wapo watu ambao hawalali wanakesha wanapanga mipango ya kuipata package hiyo” akasema Dr Joshua

“ Who are they? Do you know them? Akuliza Dr Kigomba.Dr Joshua akamtazama na kusema

“ Do you trust me Kigomba? Akauliza Dr Joshua na kusimama



“ I do trust you me President and you know that..”|



“ Good..Naomba basi uniamini ninapokwambia kwamba tuko katika hatari na tutaendelea kujiweka katika hatari kubwa endapo tutaendelea na mipango yetu.”

Dr Kgomba akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Dr Joshua kama hutanieleza ni akina nani hao wanaohatarisha mipango yetu na kukushawishi uahirishe kila kitu ,sintakubaliana nawe hata kidogo.Mimi ni mshirika wako katika suala hili na nina haki ya kufahamu kila kinachoendelea katika mpango wetu.Tayari Hussein amekwisha lipa fedha zote na tayari amekwisha wasili ili kuchukua mzigo wake unadhani nini kitatokea iwapo utaahirisha kumpatia mzigo wake? Akauliza Dr Kigomba na kutazamana na Dr Joshua



“ What’s happening Dr Joshua? What’s going on? Tell me the truth and I’ll understand you.Kuna mambo yametokea ghafla ambayo nashindwa kuyaelewa na kubwa ni suala la kuibuka kwa jaji Elibariki mtu ambaye sote tunamfahamu kwamba ndiye kikwazo namba moja kwetu na tayari tumetumia nguvu kubwa kumsaka ikiwamo hata kulitumia jeshi la polisi.Nchi nzima wanafahamu kwamba Elibariki anasakwa kwa tuhuma za kusababisha mauaji lakini ghafla anaibuka na unaonekana ukiwa umeongozana naye na baada ya yeye kutokea tu ndipo kila kitu kimevurugika.Why Mr president..why???....” akauliza Dr Kigomba.Dr Joshua akaonekana kukerwa na maneno yale ya Dr Kigomba.Akavuta pumzi ndefu n a kusema

“ Jaji Elibariki ameibuka toka huko alikokuwa na kuja kunifumbua macho kuhusiana na kinachoendelea.Nilikupa jukumu la kumchunguza Peniela na kumfahamu kwa undani badala yake ukasahau jukumu lako na kuanzisha mahusiano naye.You did a very stupid thing Dr Kigomba !!!!..

Dr Kigomba akahamaki kwa kauli ile ya Dr Joshua



“ Dr Joshua don’t insult me because of that prostitute.Mwanamke Yule ni kahaba na hakatai mwanaume yeyote mwenye pesa.Ni yeye ndiye aliyenitaka na mimi sikufanya ajizi nika…….” Dr Joshua hakutaka kumuacha Dr Kigomba amalize kile alichotaka kukisema ghafla akamrukia na kumkaba koo.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Iwe ni mara ya kwanza na ya mwisho kumsema vibaya Peniela mbele yangu.You don’t know anything about her.Ukithubutu siku nyingine kumtukana au kumdharau Peniela I swear I’ll forget that we’re friends and I will destroy you!!! Do you understand me Kigomba? Akauliza Dr Joshua kwa ukali

“ Yes I understand” akajibu Dr Kigomba

“ Good.” Akasema Dr Joshua na kumuachia Kigomba



“ Sasa nisikilize vizuri,kuanzia sasa mipango yetu yote naisitisha hadi hapo nitakapotoa maelekezo mengine kwa hiyo naomba siku nyingine usijaribu kubishana na mimi pale ninapokuwa nimetoa maamuzi yangu.Kwa sasa nenda kapumzike kesho tuna siku ndefu.Nitaongea nawe zaidi baada ya msiba kumalizika” akasema Dr Joshua.

“ Sawa Dr Joshua”

“ It’s Mr President don’t forget that..!!! akasema Dr Joshua

“ Sawa Mr President ila kabla sijaondoka nahitaji kufahamu jambo moja.Kama kila kitu kimesimama tunafanyaje basi kuhusu zile fedha ambazo tayari tumelipwa? Ni wazi fedha zile haziwezi kurudi kwa hiyo nahitaji nipatiwe mgao wangu kabisa ili hata kama baadae biashara ikiendelea iwe ni kumkabidhi tu Hussein mzigo wake.”

Dr Joshua akamtazama Dr Kigomba kwa hasira na kusema

“ Masuala ya fedha ile nitaamua hapo baadae ndiyo maana nikakwambia kwamba tutaongea zaidi hapo baadae tutakapokuwa tumepata muda mzuri lakini kwa sasa kila kitu nimekiweka pembeni ili tuone upepo unavyokwenda.Nenda kapumzike Kigomba tayari ni usiku mwingi” akasema Dr Joshua.



“ Ok Mheshimiwa rais tutaonana kesho. “ Akasema Dr Kigomba na kuondoka



“ Kisiki kingine hiki nimeking’oa.Kwa sasa baada ya kumuweka pembeni Kigomba,mambo yangu yakwenda vizuri bila wasi wasi na pesa yote itakuwa yangu peke yangu.Kesho nitazihamisha zile fedha zote kutoka katika ile akaunti zilimowekwa na kuziweka katika akaunti nyingine .Sitaki kugawana na mtu yeyote Yule.Ili kujihakikishia kwamba pesa yote inakuwa yangu kuna watu wawili au watatu ambao lazima niwafumbe midomo haraka sana .Kwanza ni Rosemary Mkozumi pamoja na mumewe Deus Mkozumi.Hawa ni watu hatari sana kwangu.Hawa wote wanafahamu kuhusu jambo hili na Deus aliwahi hata kunipigia simu na kunitolea vitisho.Niliwahi kuwa na mpango wa kumuua lakini yalitokea mambo mengi kwa haraka na kunisahaulisha lakini safari hii lazima nimuondoe.Dr KIgomba yeye japokuwa bado ni mshirika wangu wa karibu sana na bado sijamuingiza katika orodha ya watu wanaotakiwa kukatwa ndimi zao lakini naye nadhani anastahili kabisa kuondolewa kwani anayafahamu mambo yangu mengi na anaweza kuwa mtu hatari sana kwangu.” Dr Joshua akaondoka pale sebuleni akaelekea chumbani kwake kujipumzisha







******





Baada ya kuondoka katika makazi ya Dr Joshua ,Dr Kigomba alihisi kuchanganyikiwa .Mambo mengi yalizunguka ndani ya kichwa chake lakini kubwa ni lile la Dr Joshua kusimamisha mipango yao yote ya kuiuza package yenye kirusi Aby kwa Hussein.

“ Lazima kuna jambo linaloendelea hapa.Haiwezekani Dr Joshua aahirishe kila kitu katika hatua hizi za mwishoni .Kuna mchezo unataka kuchezeka hapa.Hata mimi ni mwerevu na tayari nimeng’amua kinachoendelea .Ni wazi Dr Joshua anataka aniondoe kimya kimya katika mpango wetu na pesa yote abaki nayo yeye mwenyewe.Kwa hilo amekosea sana” akawaza Dr Kigomba halafu akachukua simu yake na kumpigia Jacob Kateka mkuu wa idara ya usalama wa taifa.

“ Hallow Kigomba? Akasema Jacob



“ Halow Jacob,samahani sana ndugu yangu kwa kukuamsha najua umepumzika mida hii”

“ Usijali Kigomba.Niambie kulikoni usiku huu?

“ Jacob nahitaji kukuona usiku huu”

“ Usiku huu” akauliza Jacob kwa mshangao kidogo

“ Ndiyo Jacob.Kuna suala la dharura nataka tulijadili.Ni muhimu sana tafadhali “

Jacob akafikiri kwa muda halafu akauliza

“ Kwani wewe uko wapi mida hii Kigomba na unataka tuonane wapi?

“ Usisumbuke tafadhali ninakuja nyumbani kwako sasa hivi”

“ Sawa Kigomba utanikuta hapa ninakusubiri.” Akasema Jacob.Dr Kigomba akamuelekeza dereva wake sehemu anakotaka kwenda.

Barabara nyingi hazikuwa na magari usiku huu hivyo haikumchukua muda mrefu Dr Kigomba kuwasili nyumbani kwa Jacob Kateka.Walinzi tayari walikuwa na taarifa zake hivyo mara tu alipofika geti likafunguliwa akaingia ndani.Jacob akamlaki Dr Kigomba akamkaribisha sebuleni

“ Karibu sana Dr Kigomba” akaanzisha mazungumzo Jacob

“ Ahsante Jacob.Samahani sana kwa kukusumbua usiku huu mkubwa.”

“ Bila samahani Kigomba.” Akajibu Jacob

Dr Kigomba akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Jacob nimekuja kwako usiku huu kuna jambo nataka nikueleze na nitaomba nitakachokueleza kibaki kati yangu na wewe.”

“ Usihofu Kigomba ,chochote tutakachokiongea hakitatoka nje ya kuta hizi.”



“ Good.” Akasema Dr Kigomba halafu zikapita sekunde kadhaa akasema

“ Dr Joshua amekupigia simu usiku huu?

“ Hapana sijapokea simu yoyote toka kwa mheshimiwa rais usiku wa leo.’



“ Vipi kuhusu Abel Mkokasule amekupigia simu usiku huu? Hajakutaarifu chochote?

“ Abel Mkokasule?!!..Jacob akashangaa

“Ndiyo.Hajakueleza chochote?

“ Hapana .Sijawasiliana kabisa na Abel siku nzima ya jana.Kwani kuna nini Kigomba?

“ Usiku huu Abel ameitwa ikulu na rais walikuwa na kikao cha siri “ akasema na kunyamaza



“ Abel anaongoza kitengo ambacho kiko chini ya ofisi ya rais na anaripoti moja kwa moja kwa rais.Kwa hiyo si ajabu kukutana usiku huu” akasema Jacob

“ Nalifahamu hilo lakini kikao cha leo hakikuwa kwa ajili ya mambo ya kawaida ya kikazi.Kuna jambo Dr Joshua alimuitia Abel.”



“ Ni jambo gani hilo? Unalifahamu?



“ Ndiyo ninalifahamu.Kuna biashara mimi na Dr Joshua tulikuwa tunaifanya.Kuna kitu tulikuwa tunataka kukiuza.Ni Package ambayo imehifadhiwa ikulu”

“ Hebu subiri kidogo Dr Kigomba.Unasema kuna package ambayo mnataka kuiuza? Kuna nini ndani ya package hiyo ? akauliza Jaco

“ Hata mimi sifahamu kuna nini ndani ya hiyo package ,anayefahamu ni Dr Joshua pekee lakini ninachofahamu mimi ni kwamba kilichomo ndani ya hiyo inayoitwa package kuna kitu cha thamani kubwa sana kwani fedha ambazo tulitegemea kupata kwa mauzo ya hiyo package ni nyingi mno.Its billions of money.Hapa siongelei bilioni mbili, tatu ,kumi au ishirini ni mamia ya mabilioni.” Akasema Dr Kigomba na kumfanya Jacob astuke



“ Dah ! basi kuna kitu cha thamani kubwa sana ndani ya hiyo package.” Akasema Jacob



“ ndiyo hivyo Jacob.Kuna kitu cha thamani kubwa mno.Mimi na Dr Joshua tumeshughulikia mchakato wa kuiuza package hiyo toka mwanzo na hadi kufikia hatua ya kukabidhiwa pesa na hatua iliyokuwa imebaki ni kumkabidhi mnunuzi aitwaye Hussein mzigo wake kwani tayari amekuja nchini kwa ajili ya kuuchukua lakini ghafla yakatokea mabadiliko usiku huu.Dr Joshua anadai kwamba kuna mambo yametokea na anasitisha biashara yetu.Nimemtaka anieleze ni mambo gani hayo yaliyotokea lakini hakuwa tayari kunieleza.Ninachofahamu mimi hakuna jambo lolote katika biashara yetu ile lililotokea bali ni njia ya Dr Joshua kuniondoa katika mpango halafu pesa zote abaki nazo yeye mwenyewe.” Akanyamaza wakatazamana kwa sekunde kadhaa

“ Kigomba kwa nini umeamua kunieleza mambo haya yote? Akauliza Jacob

“ Kwa sababu nataka tuungane na tufanye kitu kuhusiana na jambo hili” akasema Dr Kigomba bila kupepesa macho.

“ Unataka tuungane na tufanye kitu.” Akasema Jacob na kufkiri kidogo halafu akauliza

“What do you want me to do?



“ Nataka tutafute namna ya kuipata package hiyo na kuiuza “



“ Unataka tufanye nini?? Akauliza Jacob kwa mshangao

“ Nataka tuchukue biashara ile sisi wawili.Jacob nakuhakikishia package hiyo ina thamani kubwa.Ni fedha ambayo watakula hadi watoto wa vitukuu wetu.”



“ Kigomba bado umeniacha njia panda kwa maneno hayo uliyoniambia .Naomba unifafanulie kwa kina ili nielewe nini hasa unachokihitaji” akasema Jacob.Dr Kigomba akamueleza Jacob kwa kirefu kila kitu kiivyo

“ Kwa hiyo Jacob nahitaji kufahamu jambo moja tu kutoka kwako,kama umekubali tufanye jambo hili lenye manufaa makubwa kwetu na kwa vizazi vyetu.”

Jacob akafikiri kidogo na kusema



“ Kidogo nimeanza kukuelewa Kigomba lakini bado sijafahamu uhusika wangu ndani ya mpango huo endapo nitaamua kuubali.”

“ Usiogope kuhusu hilo.Ninachohitaji kukifahamu kwanza ni iwapo umekubali kujiunga nami katika mpango huu”

“ Kigomba ninakuamini na ninaamini kitu ulichonieleza ni cha kweli.Kama isingekuwa kweli usingenifuata usiku huu.I need money and we all need money na kwa kiwango hicho ulichonitajia ni wazi hakuna anayeweza kukataa labda awe malaika,kwa hiyo nimekubali kujiunga nawe na kikubwa kinachonifanya nikubali bila kusita ni kwa sababu ninamchukia sana Dr Joshua.Kitu kikubwa ninachokitaka ni sisi kukaa na kupanga mikakati namna ya kufanya kuipata hiyo package”

“ Nafurahi sana kusikia hivyo Jacob.Kwa kuwa hivi sasa muda umekwenda sana ,nitaonana nawe kesho ili tuongee zaidi na nikupe maelezo ya kina kuhusu mpango huu na kwa pamoja tuone nini cha kufanya.Narudia tena kukuhakikishia Jacob kwamba endapo mpango huu utafanikiwa basi tutaingia katika orodha ya mabilionea kwa hiyo nakuomba usije ukabadili mawazo” akasema Dr Kigomba

“ Only a fool can do that.Nakuhakikishia Kigomba siwezi kubadili mawazo.Nimekuwa mtiifu katika kazi yangu lakini hakuna chochote cha maana nilichokipata zaidi ya kujenga maadui wengi.Nadhani ni wakati wangu na mimi kufanya mambo ambayo wengine wanafanya yaani kujitengenezea maisha mazuri baada ya kustaafu” akasema Jacob



“ Ahsante Jacob kwa kuwa na muono huo.Muda wa uzalendo umepita na sasa ni wakati wa kujijengea maisha mazuri baada ya kustaafu.Tutaongea vizuri zaidi na kwa kirefu kesho.” Akasema Dr Kigomba na kisha wakaagana na Dr Kigomba akaondoka kuelekea nyumbani kwake



“ Kama ulifikiri una akili sana,ulikuwa unajidanganya Dr Joshua .Sasa nitakuonyesha kwamba kuna watu wana akili zaidi yako” akawaza Dr Kigomba wakati akielekea nyumbani kwake kupumzika.





Kumekucha Tanzania .Taarifa ,kubwa iliyoliamsha taifa asubuhi hii ni tukio la polisi kupambana na majambazi wenye silaha katika msitu wa Makenge na kufanikiwa kuwaua majambazi wanne.Kwa mujibu wa kamanda wa polisi kanda ya Dare s salaam aliyehojiwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya tukio lile kutokea ni kwamba walipokea taarifa kuhusu kuwapo kwa kambi ya majambazi katika msitu wa Makenge kutoka kwa jaji Eibariki.



Kamanda Yule aliendelea kusema kwamba jaji huyo wa mahakama kuu ambayealikuwa anatuhumiwa kwa mauaji ya mke wake ambaye ni mtoto wa rais,alikuwa ametekwa na watu hao siku kadhaa zilizopita na alipelekwa katika msitu wa Makenge ambako alifichwa katika pango



“ Akiwa mafichoni“ akaendelea mkuu wa polisi kanda ya Dare s salaam

“ Watu wale walimtaka jaji Elibariki ampigie simu mke wake na kumtaka afike mahala walikopanga.Lengo lao lilikuwa ni kumteka Flaviana mtoto wa rais na kudai kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa rais ili wamuachie.



Jaji Elibariki alifanya kama alivyoelekezwa na Flaviana alipofika sehemu walikopanga wakutane majambazi wale walijitokeza na kutaka kumteka lakini kwa bahati nzuri alikuwa ameongozana na walinzi na hapo ndipo walipoanza kushambuliana na katika tukio hilo Flaviana alijeruhiwa kwa risasi akafariki akiwa katika matibabu nchini Afrika ya kusini.



Jaji Elibariki ,alifanikiwa kutoroka toka mafichoni alikokuwa anashikiliwa na majambazi hayo na kunipigia simu akanifahamisha kila kitu na kutuelekeza mahala wanakojificha majambazio hao .Usiku wa kuamkia leo polisi walivamia maficho ya majambazi hayo na pakatokea majibizano ya risasi kwa zaidi ya nusu saa lakini polisi walifanikiwa kuwadhibiti .



Majambazi wanne waliuawa na wawili walifanikiwa kutoroka.Katika eneo walilotumia majambazi hayo kama maficho yao kulikutwa na silaha mbili aina ya smg , na risasi mia moja na kumi.Kwa sasa jeshi la polisi linaendelea na msako mkali kuwatafuta majambazi waliotoroka pamoja na mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Mathew ambaye inasemekana ndiye anayeshirikiana na majambazi hayo na kuwasaidia katika kufanikisha mipango yao ya kihalifu”



Hii ilikuwa ni taarifa fupi iliyotolewa na kamanda wa polisi kanda ya Dar es salaam kwa baadhi ya waandishi wa habari,muda mfupi baada ya kutokea kwa tukio lile la majambazi na polisi kushambuliana kwa risasi katika msitu wa Makenge tukio lililotokea mida ya saa kumi na moja za alfajiri.



Dr Joshua ambaye kwa kawaida huwa hakosi kutazama taarifa ya habari .Aliitazama taarifa hii iliyopewa umuhimu mkubwa akatabasamu



“ he did it…!! Akasema kwa furaha



“ hawa ndio watu ninaopenda kufanya nao kazi.Ukimpa maelekezo yanafanyika kama unavyotaka.Nimeongea naye jana usiku na usiku huo huo akatafuta namna ya kulimaliza suala ambalo lilikuwa linanila sana akili yangu.I’m very Impressed .



Kabla ya uongozi wangu kumalizika lazima na huyu kamanda wa kanda ya Dare s salaam nimuache katika nafasi nzuri.” Akawaza Dr Joshua na kuchukua simu akazitafuta namba za kamanda wa polisi kanda ya Dar es salaam akampigia

“ hallow mzee.” Akasema Kamanda wa polisi baada ya kupokea simu



“ Habari yako Kamanda”



“ Habari nzuri sana mzee.Samahani nimechelewa kukupigia simu kukutaarifu kuhusiana na kukamilika kwa ile kazi uliyonipa”



“ Usijali kuhusu hilo kamanda,nimeona katika taarifa ya habari muda mfupi uliopita.Thank you so much”



“ Mzee,jana baada ya kumaliza kuzungumza nawe ,nilianza kuchekecha akili namna ya kufanya nikakumbuka niliwahi kupewa taarifa za kuwapo kwa majambazi wanaotumia msitu wa Makenge kama maficho yao .Taarifa hii haikuwa imefanyiwa kazi bado kwa hiyo nilikuwa nayo mimi pekee hivyo niliwaandaa vijana na kuwapa maelekezo na mimi mwenyewe nikaongozana nao hadi katika msitu wa Makenge na kweli tulifanikiwa kuwakuta majambazi hao tukawavamia na kushambuliana nao tukawaua wanne, wawili wakatoroka.



Hiyo ilikuwa ni njia nyepesi niliyoweza kuifanya ya kumsafisha tena Elibariki na kumuondoa katika zile tuhuma zilizokuwa zinamkabili.Kwa sasa mpira umerushwa kwa huyu Mathew na Elibariki amesafishika na hahusiki tena katika tuko lolote.



Nitaonana naye na kumpa maelekezo ya namna ya kuzungumza na waandishi wa habari ambao watapenda kumuhoji au mtu yeyote atakayemuuliza kuhusuana na tukio hili lakini hadi hapo nitakapokuwa nimeongea naye naomba asihojiwe na mtu yeyote Yule au chombo chochote cha habari”



“ Kamanda nimefurahi sana kwa namna ulivyo mbunifu.Sitaki nikuahidi chochote kwa sasa ila naomba unisubiri kwa kama wiki mbili hivi na utaona nitakachokufanyia.Watu watiifu kama ninyi mnastahili pongezi ya kiwango cha juu mo” akasema Dr Joshua



“ Nashukuru sana mheshimiwa rais” akasema Kamanda wa polisi

“ Hata mimi nashukuru sana na kwa kuwa hivi sasa bado nimebanwa na mambo mengi nitakuita hivi karibuni ili tujadili kuhusiana na huyu Mathew.”



“ Hakuna shaka mzee.Muda wowote ukinihitaji utanipa taarifa”



“ Ahsante kamanda .Nakukumbusha vile vile kuwa leo ni siku ya mazishi ya mwanangu na kutakuwepo na wageni mbali mbali marafiki zangu wa kutoka nje ya nchi kwa hiyo naomba suala la ulinzi lipewe kipaumbele kikubwa.”



“ Tayari nimekwisha toa maelekezo ya kuwepo kwa ulinzi wa kutosha eneo hilo kwa hiyo usihofu mheshimiwa “ akasema kamanda wa polis Dar es salaam wakaagana Dr Joshua akakata simu.



“ Lazima nimfanyie mambo makubwa huyu kamanda kwa namna alivyonisaidia katika suala hili.Kitakachofuata baada ya Elibariki kusafishika ni kuanza kumuandaa kwa ajili ya kushika madaraka makubwa.Najua kuna taratibu zake kwa mtu kama Elibariki ambaye ni jaji wa mahakama kuu kuingia katika mambo ya siasa lakini hilo si tatizo litakalonisumbua.



Elibariki kwa sasa tayari jina lake linafahamika,kwanza kama mhalifu na sasa anajulikana kama shujaa.Nitawaita wanamtandao wangu ili kwa pamoja tuanze kulijadili suala hili la kumuandaa Elibariki kwa nafasi ya urais” akawaza Dr Joshua.



“ Ngoja kwanza niachane na mambo haya ya jaji Elibariki,leo ni siku ndefu na ngumu.Ninamzika mwanangu Flaviana” akanyamaza na kuinamana na kuzama katika mawazo



“ Sikutegemea kama suala hili lingenifikisha hapa.Sikujua kama jambo hili lingewapoteza mke na wanangu.Hakuna wa kumlaumu kwa haya yote yaliyotokea,kwani ilikuwa ni lazima yatokee.Ninachopaswa kukifanya kwa sasa ni kuhakikisha lengo langu halikwami na ninafanikiwa kulimaliza suala la package .



Siko tayari kuyakosa mabilioni yale ya fedha ambayo tayari yametua mikononi mwangu.” Akawaza Dr Joshua halafu akaanza kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo.Wakati akijiandaa mara mlango ukagongwa,akatoka na kukutana na mwanae Anna

“ Anna,how are you my princess??



“ I’m fine dady” akajibu Anna na kuingia akateti sofani



“ Nashukuru umekuja Anna kwani nilikuwa natazamia kukuita asubuhi hii ili tuongee kuhusiana na siku ya leo” akasema Dr Joshua halafu akanyamaza kidogo akamtazama Anna aliyekuwa amesawajika sana na kuendelea



“ Leo ni siku nyingine ngumu kwetu kama familia.Tunakwenda kumpumzisha dada yako Flaviana.Its hard but we have to be strong.Anna nakuomba sana uwe jasiri siku ya leo”



“ I’m trying dady.Najaribu sana kuwa jasiri lakini najikuta nashindwa .Why this is happening to us? Why always us” Anna akasema huku akilia



“ Usilie Anna.Kila jambo hutokea kwa sababu maalum na kifo ni mapenzi ya Mungu.Hatuwezi kujua Mungu ana makusudi gani kutuchukulia wapendwa wetu wawili ndani ya kipindi kifupi.Hata kabla ya arobaini ya mama yako haijawadia,ametutoka tena dada yako.



Japo ni mapenzi ya Mungu na yeye ndiye mwenye kutoa na kutwaa lakini inauma sana” akasema Dr Joshua na kuinama akionyesha majonzi makubwa.Sekunde kadhaa za ukimya zikapita Anna akainua kichwa na kusema

“ Who will be next??.

Swali lile likamstua Dr Joshua

“ Umesemaje Anna?



“ Nimeuliza nani atafuata kati yetu? Alianza mama ,akafuata Flaviana na sasa tumebaki wawili mimi na wewe kwa hiyo nani atakayefuata? Akauliza Anna.Dr Joshua akamtazama mwanae kwa sekunde kadhaa akashidwa ampe jibu gani

“ kwa nini umeuliza hivyo Anna?



“ kwa sababu naona kama kuna kitu kinaiandama familia yetu na ndiyo maana najiuliza hivyo”

Ukimya ukatanda mle ndani.Baada ya muda Anna akasema

“ Anyway dady forget what I said. Mambo haya yaliyotokea yamenichanganya mno akili yangu.Kitu kikubwa kilichonileta hapa kwako asubuhi hii ni kutaka kufahamu kuhusu jaji Elibariki.Nimemuona uko naye jana usiku.What is he doing here? Kwa nini hakamatwi? Akauliza Anna



“ Mimi ndiye ninayepaswa kulaumiwa kwa kutokukufahamisha mapema kuhusu jaji Elibariki.There is an explanation” akasema Dr Joshua

“ Explanation? What explanation dady?? He killed my sister so what can you explain to me? Akauliza Anna

“ Calm down Anna.Umetazama taarifa ya habari leo asubuhi?

“ Hapana sijaitazama.Kuna nini ?



“ Basi kama ungekuwa umetazama tayari ungekuwa na jibu Elibariki siye aliyemuua Flaviana”



“ What ???!! Anna akashangaa

“ Ndiyo Anna,Elibariki siye aliyemuua Flaviana”



“ Dady I don’t understand what you are talking about. Jeshi la polisi walilithibitisha hilo na wakaanzisha msako wa kumsaka Elibariki ,nini kimetokea ?



“ Ukweli umebainika kwamba Elibariki alitekwa na watu wasiojulikana na kwenda kufichwa katika msitu wa Makenge.Lengo kuu la watu hao ni kujipatia fedha na ndiyo maana wakamtumia ili awasiliane na Flaviana wakapanga wakutane sehemu ambako wale majambazi walikuwa wamejipanga ili wamteke Flaviana.



Kwa bahati nzuri kulikuwa na walinzi wa siri ambao walikuwa wanamlinda Flaviana ambao walipambana vilivyo na majambazi hao na katika mapambano hayo Flaviana akajeruhiwa kwa risasi.Jana Elibariki alifanikiwa kuwaponyoka majambazi wale na kukimbia na mtu wakwanza kumpigia simu baada ya kutoroka alikuwa ni mimi.



Alinieleza kila kitu na mahala alipo nikampiga simu kamanda wa polisi kanda ya Dare s salaam nikamtaarifu kuhusu suala hili na usiku wa kuamkia leo polisi walivamia maficho ya majambazi hao na kufanikiwa kuwaua watatu na wawili wakakimbia.



Kwa sasa jeshi la plisi linawasaka majambazi yaliyokimbia pamoja na mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Mathew ambaye ndiye mfadhili wao.Kwa maana hiyo basi jaji Elibariki hahusiki kabisa na kifo cha dada yako.” Akasema Dr Joshua wakabaki wanatamana.Anna akataka kusema kitu lakini mlango ukafunguliwa akaingia mlinzi wa rais



“ Mzee kuna mgeni wako amefika anakusubiri pindi ukimaliza maongezi”

“ Ni nani? Akauliza Dr Joshua

“ Abel mkokasule”

Dr Joshua hakutaka kupoteza muda akamtaka Anna aende akajiandae ili yeye apate muda wa kuongea na mgeni wake .Anna akatoka japo kwa shingo upande.



“ hallow Abel,karibu sana “ akasema Dr Joshua

“ Ahsante sana mzee.Samahani kwa kukuvamia asubuhi asubuhi namna hii.

“ Bila samahani Abel.I hope you have something for me this morning”

“ Ndiyo mzee” akajibu Abel



“ Tell me good news Abel..” akasema Dr Joshua huku akitabasamu

“ Tulipoachana jana usiku niliwapanga vijana wangu na tukaanza kazi mara moja.Kama ulivyoelekeza ,usiku huo huo tulianza kumfuatilia Dr Kigomba.Alipotoka hapa kwako,aliekea moja kwa moja kwa mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa Jacob kateka” akasema Abel.

“ Alikwenda kuonana na Jacob Kateka?..Dr Joshua akashangaa



“ Ndiyo mzee”



“ Alikwenda kumueleza kitu gani? Mlifanikiwa kunasa maongezi yao?

“ Hapana mzee hatukufaikiwa kunasa maongezi yao”

Taarifa ile ikaonekana kumchanganya kidogo Dr Joshua



“ Kama baada ya kutoka hapa alikwenda kuonana na Jacob basi lazima kuna jambo alikwenda kumueleza.Waliongea mambo gani? Naanza kuhisi lazima Kigomba atakuwa amemueleza Jacob kuhusiana na mpango wetu.Kigomba anaanza kudhihirisha ni kwa namna gani alivyo hatari kwangu.



Anafahamu mambo yangu mengi na anafahamu mipango yangu yote na ninahisi atakuwa na mipango ya siri ya kunivurugia mipango yangu.Natakiwa kufahamu kitu ambacho wawili hawa wanakipanga na kikubwa zaidi natakiwa kumshughulikia Kigomba haraka iwezekanavyo .



Endapo nitamuacha huyu jamaa basi lazima kuna jambo anapanga kulifanya.Na kama amemweleza Jacob basi lazima wawili hawa watakuwa wameungana na kupanga njama za kunihujumu.I’m going to deal with them “



“ Mr President..!!” Abel Mkosasule akamstua Dr Joshua toka mawazoni



“ Oh Samahani Abel kuna jambo nilikuwa nawaza.Ahsante sana kwa taarifa hii.Endeleeni kumfuatilia Kigomba kila aendako na kila anachokifanya kisha unipe taarifa.Nataka kufahamu watu anaokutana nao na kama ikiwezekana nataka kujua hadi kile wanachokiongea.



Kitu kingine ambacho kinaweza kuwasaidieni kumpata vizuri Kigomba ni kwamba ni mdhaifu mno kwa wanawake.Utumieni udhaifu huo kufanikisha kazi yenu” akasema Dr Joshua



“ Ahsante sana mzee kwa wazo hilo.Tutaendelea kumfuatilia Kigomba na nitakupa taarifa kamili jioni ya leo.Tukiachana na suala la Kigomba kuna kazi ulinipatia ya kumpata Jessica na kumpeleka Dark house.Napenda kukutaarifu pia kuwa alfajiri ya leo tumefanikiwa kumpata na tayari amepelekwa dark house tunasubiri maelekezo yako”

Dr Joshua akaachia tabasamu kubwa na kusema



“ Good Job Abel.Najuta kwa nini nisingekutumia wewe toka awali,ninsingefika hapa nilipofika”



“ Unasemaje mzee? Akauliza Abel



“ Oh sorry,forget what I said.Kazi nzuri sana umeifanya Abel .Endelea kumuweka Jessica Dark house hadi hapo nitakapokupa maelekezo mengine.Jioni ya leo nataka tuonane kuna kazi ambayo nataka uifanye.



Nilikudokeza kwamba kuna mtu yuko sehemu Fulani anashikiliwa kwa hiyo nataka mtu huyo akachukuliwe toka mahala hapo naye pia apelekwe dark house.Ni kazi ya hatari kidogo kutokana na mahala aliko huyo mtu kuwa ni sehemu yenye ulinzi mkali kwa hiyo waweke tayari vijana wako” akasema Dr Joshua

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Usijali Dr Joshua.Vijana wako tayari kwa kazi muda wowote”

“ Ahsante sana Abel kwa taarifa nzuri.Nenda kaendelee na kazi na tutaonana hapa jioni ya leo.Nitakufahamisha muda nitakaokuwa na nafasi” akasema Dr Joshua na kuagana na Abel akaondoka



“ Dr Kigomba alikwenda kufanya nini nyumbani kwa Jacob usiku ule mwingi? Kuna kitu gani kinaendelea kati yao? Naanza kuhisi Kigomba kuna jambo analipanga na Jacob na lazima jambo lenyewe litakuwa ni kuhusiana na ile package.



Ngoja kwanza nimalize shughuli za msiba wa mwanangu halafu nitaamua niwafanye nini lakini wakae wanajua kwamba kama wana mipango yoyote mibaya juu yangu wanajisumbua bure kwani hawatafanikiwa .Kushindana nami ni sawa na kushindana na moto wa nyika..



Mimi ndiye raia namba moja hapa nchini na kila kitu kipo ch…..” Mlio wa simu ukamstua Dr Joshua akaichukua na kutazama mpigaji.Alizifahamu namba zile ni namba za zamani za Dr Kigomba



“ Hallow Kigomba” akasema Dr Joshua

“ Mr President habari za asubuhi ?

“ Habari nzuri Kigomba.Kuhusu ile simu yako nataka kuikabidhi kwa vijana wetu wa usalama waifanyie uchunguzi na kubaini kama kweli imeunganishwa halafu utarejeshewa.Habari za toka jana?



“ Habari nzuri mheshimiwa rais.Nitashukuru sana mzee kama nitarejeshewa simu yangu kwani watu wengi wanaifahamu ile namba wananitafuta na kunikosa” akasema Dr Kigomba na kunyamaza kidogo halafu akasema



“ Dr Joshua kuna jambo limenistua na ndiyo maana nimekupigia simu.Nimekuja katika hii hoteli ambako Hussein na ujumbe wake walifikia kwa lengo la kutaka kuhakikisha wako salama lakini kitu cha kushangaza Hussein na ujumbe wake wamehamishwa alfajiri ya leo.Unafahamu chochote kuhusu jambo hili? Akauliza Dr Kigomba



“ Ndiyo ninafahamu Kigomba na mimi ndiye niliyetoa maelekezo hayo”

Kupitia spika za simu Dr Kigomba akasikika akishusha pumzi.

“ Kigomba kuna tatizo lolote kwani? Akauliza Dr Joshua

“ Hakuna tatizo Dr Joshua kama wamehamishwa kwa amri yako.Naweza ukaniambia wamehamishiwa wapi?



“ No I cant tell you now.” Akasema Dr Joshua na kuzidi kumkasirisha Dr Kigomba

“ Dr Joshua whats going on? Kwa nini unanificha na hutaki kunieleza kitu gani kinachoendelea ? Don’t you trust me?

“ Kigomba nimekwisha kueleza kwamba subiri kwanza tuyamalize masuala ya msiba halafu tutakaa na nitakueleza kila kitu kinachoendelea.Do you understand me Kigomba? Akauliza Dr Joshua.

“ Yes I do” akajibu Dr Kigomba

`

“ Good.Now come over here.I’m waiting for you.Shughuli zinatakiwa kuanza mapema” akasema Dr Joshua na kukata simu

“ Damn ! you Joshua.Unajifanya wewe una akili sana basi nitakuonyesha namna ulivyo mjinga!!.akawaza Dr Kigomba akiwa garini akielekea kwa Dr Joshua .Akachukua simu na kumpigia Jacob Kateka.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog