Search This Blog

Wednesday 22 March 2023

JINO KWA JINO - 3

   

Simulizi : Jino Kwa Jino

Sehemu Ya : Tatu (3)



Mtu mmoja aliyekaa pembeni ya dreva katika gari la mbele alikuwa ameshika darubini akiwa makini kuangalia kule eneo la uwanja ambako watu walikuwa furahani wakicheza na hata wengine kuangalia michezo inavyoendelea.


Wakati wao walio kwenye magari wakiwa bize kuangalia matukio yote ya upande husika hasa wakiwalenga vijana waliofika na mipira mingi lakini wakatoa miwili na kuanza kucheza tena wao wakiwa si watu wa maeneo yale na pia si wanafunzi wa shule hii wala zilizo jirani yake, mchezo ukiwa umekolea ilitokea gari aina ya Nissan Land Cruiser ya rangi ya kijani nyeupe si kijani iliyokolea na waliposogea hadi kwenye eneo la uwanja wanapocheza wale vijana wasio wanamichezo kutokana tu na walivyovaa ilijuza hivyo, alishuka kijana mmoja wa kizungu mwenye nywele za blonde na alishuka na akiwa mfuko wa mipira unaofanana na ule ambao wale wa kwanza kufika pale walikuwa wameuweka kwa pembeni, akaenda na kuingia kwenye gati la kuingilia uwanja wa shule.


Yule kijana alikwenda kana kwamba hana lolote alilonalo fikrani mfuko alioubeba ukiwa mgongoni huku mkono wa kulia ukiwa umeushika kwa kutokea bega lake la kulia, alipiga hatua kisha akaubwaga ule mfuko wa mipira sambamba na ule mwingine halafu bila kuchelewa akainama na kunyanyua ule mwingine mchezo wa nukta kumeta tena bila kuwasalimu wale wengine ambao hawakuwa wanamuangalia licha ya kuwa alisogea karibu yao kabisa.


Kijana yule wa kizungu aliyevaa jeans ya rangi nyeusi na fulana iliyokatwa mikono kukiwa na kofia linaloning’inia nyuma rangi ya kijivu nyeupe, machoni alikuwa na miwani ya rangi nyeusi alisogea akiwapita wale wafanya mazoezi wasio wafanya mazoezi (wanazuga tu) kisha gari aliyokuja nayo ikaja karibu yake akafungua mlango na kuingia ndani ya gari ikaondoka mwendo wa taratibu kama ule waliokuja nao.


“Boss! Wamarekani uliosema walipora mzigo wa Angela pamoja na pesa hapa Nuevo Laredo tumewanasa kwenye rada… Wamefika kama ulivyosema juzi kuwa watafika hapa na gari ile ile mliyotupa taarifa ndiyo uwa wanatumia..” Ilikuwa ni simu iliyopigwa na mtumia darubini akiwa pembeni ya dreva ya gari la mbele kati ya magari mawili yaliyopaki mita sabini toka eneo la uwanja wa shule ya upili.


“Nissan Land Cruiser ya rangi ya kijani nyeupe si kijani iliyokolea namba NLK-67-200?..!” Akauliza aliyetamkwa kuwa ni boss.

“Ndiyo mkuu…!”

“Akikisheni hawawapotei pia… Na ni kama vile vile intelejensia yetu ilivyotujuza?”

“Ndiyo mkuu.. Alishuka kijana mmoja ambaye kimaelekezo tu nilivyomuona nikajua ni yeye katika wale wahusika, alikuwa na mipira ya soka akaibadilisha na mipira iliyowekwa pembeni ikiwa ndani ya mfuko wa kambakamba uliofanana na wake”

“Sawa… Chukueni na mzigo ulio kwenye mabadilishano pia nawataka wamarekani hao maana hao ndiyo walipora mzigo wetu kwa Sylivia, wamevuka mipaka kwa sasa sifa zao sifika katika eneo la Nuevo Laredo kana kwamba hawaijui TRJ tuna mwaka sasa hata Los Zetas hawaangilii mambo yetu toka tusaini mkataba wa Puebla”

“Sawa boss!”

Simu ikakatwa jamaa akamuangalia dreva wote wakatabasamu akabonyeza namba za simu nyingine na mara ikaita muito mmoja tu ikapokelewa.


“Chasco sogeeni uwanjani chukueni mipira toka kwa wale wapuuzi na wakileta ubishi msiogope wingi wa watu chalaza risasi… Sisi tunaifuata gari ya wamarekani..!” Akaongea baada ya upande wa pili kupokea na hakusubiri jibu akakata simu huku tayari dreva wake akisha fuata barabara inayochepuka toka mtaa huu wa Durango Madero kuelekea mtaa wa pili wa Ejido Avenue Street..


Kwa mwendo mdogo waliokuwa wakiendesha waliokuwa ndani ya gari ya Nissan Land Cruise namba NLK-67-200, hawa walio ndani ya Nissan Dualis 2006 waliwaona punde tu walipofika kwenye makutano ya barabara ya Pasco Colon Road na Ejido Highway wakazunguka makutano haya na mara wakaiona gari waliyokuwa wakiifukuzia kutokea mtaa wa Durango Madero.


“Itabidi twende nao hadi eneo ambalo wanakwenda au inakuwaje?” Akauliza dreva wa gari akimuuliza kiongozi wao kwa hapa ambaye pia alikuwa akipeleka na kupokea taarifa kwa mkuu wao, mkuu wa kikosi cha Red Jaguar kanda ya mpakani Nuevo Laredo, jimbo La Tamaulipas lililopo mpaka wa Mexico na Marekani ikiwa upande wa Marekani kuna jimbo la Texas.


Ukanda huu wa jimbo hili ulikuwa unaongozwa na Sajenti Lara Moentes akisaidiwa na mtu katili mmexico mwenye asili ya ujerumani Wolfs Klauben Gend a.k.a Animal pamoja naye Cisco Murlindo a.k.a ‘tocon’ kihispaniola hiki wakimaanisha ‘kisiki’ kwa Kiswahili chetu, hawa ndiyo walikuwa viongozi wa ‘The Red Jaguar’ katika eneo hili la mpakani wakilinda maslahi ya genge lao hasa inapofanyika biashara ya kuvusha mizigo yao kwenda nchi ya Marekani.


Mwisho wa sehemu ya ishirini na nne (24)


Genge lisilojulikana la wazungu toka Marekani lilifanya jambo ambalo ‘The Red Jaguar’ (The Monster).


Kundi gani hili ambalo lilikamata sharubu za genge lililobadili siasa ya mihadarati katika eneo la Mexico?


Tusichoshane twende sehemu inayofuata kujua zaidi.




“Chasco sogeeni uwanjani chukueni mipira toka kwa wale wapuuzi na wakileta ubishi msiogope wingi wa watu chalaza risasi… Sisi tunaifuata gari ya wamarekani..!” Akaongea baada ya upande wa pili kupokea na hakusubiri jibu akakata simu huku tayari dreva wake akisha fuata barabara inayochepuka toka mtaa huu wa Durango Madero kuelekea mtaa wa pili wa Ejido Avenue Street..


Kwa mwendo mdogo waliokuwa wakiendesha waliokuwa ndani ya gari ya Nissan Land Cruiser namba NLK-67-200, hawa walio ndani ya Nissan Dualis 2006 waliwaona punde tu walipofika kwenye makutano ya barabara ya Pasco Colon Road na Ejido Highway wakazunguka makutano haya na mara wakaiona gari waliyokuwa wakiifukuzia kutokea mtaa wa Durango Madero.


“Itabidi twende nao hadi eneo ambalo wanakwenda au inakuwaje?” Akauliza dreva wa gari akimuuliza kiongozi wao kwa hapa ambaye pia alikuwa akipeleka na kupokea taarifa kwa mkuu wao, mkuu wa kikosi cha Red Jaguar kanda ya mpakani Nuevo Laredo, jimbo La Tamaulipas lililopo mpaka wa Mexico na Marekani ikiwa upande wa Marekani kuna jimbo la Texas.


Ukanda huu wa jimbo hili ulikuwa unaongozwa na Sajenti Lara Moentes akisaidiwa na mtu katili mmexico mwenye asili ya ujerumani Wolfs Klauben Gend a.k.a Animal pamoja naye Cisco Murlindo a.k.a ‘tocon’ kihispaniola hiki wakimaanisha ‘kisiki’ kwa Kiswahili chetu, hawa ndiyo walikuwa viongozi wa ‘The Red Jaguar’ katika eneo hili la mpakani wakilinda maslahi ya genge lao hasa inapofanyika biashara ya kuvusha mizigo yao kwenda nchi ya Marekani.


ENDELEA NA MOTO…!


MAPAMBANO NUEVO LAREDO-MEXICO

“Hakuna hatutaenda nao mbali kama wanakwenda mbali… Itatubidi tuwafuate kisiri siri kisha tujionyeshe kuwa tunawafukuza endapo watapita barabara isiyo na magari mengi kama hii hili washikwe na mshtuko kuwa wanafuatiliwa kwa haraka watajua sisi ni kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya hapo itakuwa kazi rahisi kwetu kutokana na uzoefu wetu wa kona zote za barabara za mji huu hata vichochoro vyake” Akajibu muongoza shughuli hii.


Upande wa uwanja wa michezo wa American School Academy, vijana waliokuwa wakijifanya wamekuja pale uwanjani kwa ajili ya mazoezi licha ya kuwa walivaa mavazi yasiyotumika michezoni hasa huu waliokuwa wakiucheza wao(soka) kama suruali zao karibu wote zilikuwa za jeans na huku juu wakivaa fulana za aina mbalimbali na rangi tofauti tofauti kwa kila mmoja na kama tulivyokwisha juwa hapo juu ni kuwa hawa walikuwa ni watu wa kazi wa genge la ‘MPD’ lililo chini ya Mr. Fanuel Miguel Mendoza mfanyabiashara tajiri na mlanguzi wa mihadarati wa Villahermosa, Tabasco.


Gari aina ya Toyota Hiace Van rangi nyeusi waliyofika nayo hapa uwanjani hapo awali kisha kuwashusha na baada ya kuwashusha wakiwa na mipira yao, gari ile iliondoka sasa ilirudi kwa mwendo wa taratibu na ililpopaki tu milango ikafunguliwa vijana walipoona gari imepaki kwa barabarani wakaacha kucheza pasi walizokuwa wakipasiana wakarudisha mipira miwili waliyokuwa wakiichezea katika mfuko mkubwa wa kambakamba ulio maalumu kwa kubebea mipira iwe ya soka ama mingineyo, mipira ile ikaungana na mipira iliyokuwemo mule ila hii ikiwa imeletwa na walio katika gari aina ya Nissan Land Cruiser ambao kwa sasa tumewajua kuwa ni wamarekani kutokana na maelekezo ya kiongozi aliyekuwa akielekezana kwa njia ya simu na muongoza msafara wa ‘The Red Jaguar’.


Walipokuwa tayari wakacheki huku na huko kila mmoja kwa wakati wake kisha kwa mwendo wa taratibu kana kwamba hawana haraka wakaisogelea gari kisha wakaingia dreva akatia gia ikaondoka kwa kufuata barabara inapoelekea na ndipo hata gari ya Nissan Land Cruiser ya rangi ya kijani nyeupe si kijani iliyokolea namba NLK-67-200 ya wamarekani ilielekea.


Gari la pili la genge la Red Jaguar aina ya Nissan Prado nalo lilichomoka toka mahali lilipopaki na dreva akaliamuru liunge kwa kasi kuelekea inapoelekea inapoelekea Toyota Hiace Van ambayo yenyewe haikuelekezwa upande walipoelekea wazungu wa kimarekani iliyoelekea mbele hii ilifuata upande huu walipokuwa hawa ‘Red Jaguar’ ikiwapita hawa waliobakia na gari wakisubiri kuwafuatilia hawa.


Toyota Hiace Van ilikwenda kwa mwendo taratibu kama iliyoondokea eneo walilotoka lakini walipokaribia mzunguko wa Paseo Colon Road na Avenida Reforma Highway gari ikazunguka mzunguko na kufuata Avenida Reforma Highway ikiachana na ile ya Paseo Colon Road iliyokuwa ikiendelea mbele na ilipo kaa sawa dreva wake aliongeza mwendo kwa ghafla kisha ikapita majengo ya ofisi za Posta ya Nuevo Laredo ikiwa katika mwendo ule ule wa kasi ikakimbia mpaka barabara kuu ielekeayo boda ya Mexico na Marekani barabara ya Avenida Luis Donaldo Colosio ila kabla hawajaingia taa zinazoongoza magari ziliwasimamisha hivyo dreva akasimanisha gari kwenye foleni.Highway.


Chasco na wenzake walihisi pengine wamestukiwa kuwa wameunga mkia kuifukuza gari hii na maongezi yao yalikuwa hivi.

“Wameongeza mwendo… Hii inamaanisha wametustukia tunawafuata….”Akaongea Chasco kisha naye akaongeza spidi ya gari anayoendesha Nissan Prado.


“Wameuona mkia… Tuchukue tahadhari maana hatujui kama walikuwa peke yao pale..” akaongea aliye siti ya nyuma ya siti ya dreva.


Dreva Chasco aliingia mzungukoni wakauzunguka kama wanaowafuata walivyofanya kisha naye akaachana na barabara ya Colon Paseo akafuata Avenida Reforma Highway barabara iliyo na njia mbili kulia na kushoto ila ni pana sana hivyo inatoa nafasi kwa muendeshaji kucheza barabarani atakavyo licha ya kuwa kuna magari mengi, naye hakuwa na budi zaidi ya kufunga breki kusimama sababu ya foleni kutoruhusu gari zitokazo barabara watokayo kuingia barabara kuu iendayo Mexico boda ambayo na yenyewe ni yenye njia mbili pana sana kama barabara wanayotaka kuhama.


Taa ziliruhusu magari yanayoingia barabara kuu iendayo mpakani kuingia ndipo magari yaendayo njia hii yakafumuka kasi kama ilivyo ada kila mmoja anayeendesha vyombo hivi akijitahidi kutosumbua aliye mbele yake na hata aliye nyuma yake, magari na hata pikipiki zilikuwemo zikipita kwenye njia yake kutokana na michoro inavyoonyesha.


“Hawa jamaa vipi? Hawa ni watu wa MPD ya Mr. Fanuel.. Wanaenda boda ya kuingilia Marekani ina maana wanapeleka pesa walizopewa huko?” Akauliza Chasco, kuwauliza wenzake watano alio nao kwenye gari moja huku yeye akiwaendesha kwa kasi kuwai aingie kwenye barabara ya mwendo kasi.


“Mpigie Castillo mpe hii taarifa maana sielewi tunawapataje hawa watu wanoelekea barabara hili lenye ulinzi wa serikali zote mbili zinazomiliki huu mpaka..” Akaongea aliye mbele katika siti sambamba na dereva.


“Chukua simu yangu piga… Pattern yake ni kama pattern yako niliwai kuona ukitoa yako kwenye simu yako..!” Chasco akamjibu kwa maelekezo huku yeye akikanyaga mafuta gari iongezeke spidi zaidi, jamaa akachukua simu.


“Castillo mko wapi?” Akaongea aliyeelekezwa na Chasco apige simu ya Castillo.

“Mtaa wa Boy’s town… Nyinyi mko wapi?”

“ Bara bara ya Avenida Luis Donaldo Colosio… Jamaa wanaonekana wamejua tunawafuatilia hivyo wameamua waelekee lango la Mexico”

“Sidhani kama watakwenda hadi kwenye lango… Nafikiri hao watakunja barabara mojawapo kati ya nyingi zinazochepuka”

“Kwahiyo tuendelee na kuwafuat…”

“Tiiiiiiiiihhh!!!!” Ulisikika mlio mzito wa kitu kama bomu kubwa, gari waliyomo Chasco na Wwenzake ilipaishwa juu huku ikiwa imelipuka na hivyo moto tu uliokuwa ukionekana machoni mwa watu wengine wengi wakiwa ndani ya magari yaliyo karibu, taharuki kubwa ilitokea kwakuwa kelele za lami ya barabara inayosuguliwa na matairi ya gari yanayofungishwa breki kilazima na madreva wayaendeshayo kwa kuogopa tukio lililoikumba gari wanayoiona, taharuki kubwa kwa kila aliye karibu na eneo hili.


Nissan Prado ilitua ikiwa chakari tena iligeuzwa juu chini na moto ukiendelea kuteketeza na kuharibu kila kilicho ndani na nje, hakuna kiumbe aliyebaki hai (pigo kwa The Red Jaguar), hakuna aliyekuwa anajua kwa haraka vile jambo gani limetokea hapa Avenida Luis Donaldo Colosio Highway, barabara ya kimataifa inayotoka ndani ya Mexico mpaka boda ya kuingia ndani ya Marekani.


Tayari Chasco na wenzake wote watano walichakazwa na silaha aina ya Rocket-Propelled Grenade-7 (RPG-7) iliyotumwa toka kwenye jengo la ghorofa nne lililo pembeni mita mia moja hamsini, silaha hii ya kivita yenye uwezo wa kushambulia kiufasaha kwa kutokea mita mia mbili ililengwa kwenye gari ya akina Chasco na kuwaletea maafa ya umauti kuanzia wao na kila kitu kilichokuwa chao, gari hii mfu sasa iliburuzika ikiwa juu chini mpaka pembeni ya kingo kuu za barabara hii kubwa na pana hapo ikatulia huku ikiendeelea kuwaka moto bila mtu yoyote kuthubutu kusogelea kutokana na sintofahamu kuu iliyotawala na hofu kutoka kwa kila aliye jirani na eneo la tukio.


Ni hivi! Wakati vijana wa Mendoza Potentia Distributio (MPD) wanaondoka eneo la uwanja wa kwenye jengo moja lililo karibu na shule kulikuwa na vijana wawili kila mmoja akiwa na pikipiki aina ya Baja 1000 Race ambazo ni maalumu kwa mashindano, walikuwa wakijifanya wanatengeneza moja ya pikipiki ya mmoja kati yao muda wote wakati huo huo wakifuatilia nyendo kila wanachohisi hakiko sawa, walikuwa wataalamu katika kazi hii ya kufuatilia.


Gari ya kwanza iliyofika pale uwanjani na mtu wao mmoja kushuka na mipira ikiwa katika mfuko uliofanana na waliofika kabla kisha akabadilisha kijanja kwa kuchukua usio wake na kuuacha ulio wake aliporudi kwenye gari na dreva kuondoa gari, wao wa kwenye pikipiki waliendelea na uongo wao kuwa wanatengeneza pikipiki na kweli subira yao iliwapa jibu wakaiona gari aina ya Nissan Dualis 2006 ikipita na kiukweli walikuwa wakiijua hii gari uwa inatumiwa na watu wa genge gani, wakaacha iendelee kuwafuata iendelee kuweka mkia wake kwa wanaowafuata.


Msafara wa pili wa wacheza mpira wa uongo ulipoondoka tu kwa gari yao ya Toyota Hiace Van dakika moja ilipoipita gari aina ya Nissan Prado iliyoachwa wakati Nissan Dualis inaondoka iligeuzwa kisha kuunga mkia, hapo jamaa hawa walio kwenye ufundi uongo wakawa washaunganisha majibu yale waliyokuwa wanayahitaji wakakubaliana wagawane mmoja aende kwa walioenda magharibi na mwingine aende kwa walioenda mashariki.


Aliyeelekea barabara ya Avenida Reforma Highway inayoenda mpaka barabara ielekeayo aliwakuta wakiwa wamesimama wanyatiwaji na wanyatia kwenye mataa yaongozayo barabara yaliyo kwenye makutano ya barabara hii ya Avenida Reforma na Avenida Luis Donaldo Colosio, hivyo yeye alisogea akipita magari yaliyojipanga akasogea mpaka mstari wa mwisho wa mchoro wa barabarani ambako mbele palikuwa na magari yaliyo katika zamu yakitoka kulia kuelekea kushoto, taa ziliporuhusu tu magari ya upande yaanze kuingia bara bara kuu ielekeayo mpakani yeye alikuwa wa kwanza kuingia akiwa kwenye spidi kubwa.


Papo hapo akafanya mawasiliano na wanyatiwa kuwa wapite upande wa pembeni kabisa ambao magari yanayopita huku uwa hayaendi kwa spidi kubwa kwakuwa uwa yanaingia kwenye barabara mchepuko zinazoingia na kutoka katika barabara hii kuelekea sehemu nyingine huku yale ya kati uwa yanaenda kasi.


Piki piki Baja 1000 Race ilikimbizwa mpaka msafara wa maduka makubwa ya kimataifa ya Supermanzana 39 yaliyo jipanga pembezoni mwa barabara hii kubwa ndipo dreva wa pikipiki hii akaingia na moja kwa moja akaelekea lilipo ghorofa linalotumika kama makazi ya kupangisha wageni wanaofika hapa Nuevo Laredo hasa watokao Marekani, muhuni huyu akapaki pikipiki na kwakuwa kulikuwa hakuna watu waliokuwa wakifuatilia ya mwingine alikwenda mbio mbio hadi kwenye chumba ambacho wao wamefikia akachukua RPG-7, akapanda juu ya roof ndipo akafanya shambulizi la silaha hii ya kivita aina ya Rocket-Propelled Grenade-7.


***** ***** *****


Kishindo kilisikika na simu ikakatika ghafla, alishtuka akaitoa simu yake toka sikioni. Macho alivyoyatoa yalifanya wenzie wote kumtizama nao katika hali kama ile aliyoonyesha yeye aliyekuwa akiongea na simu.


“Vipi Castillo?!!!!” Maswali toka kwa watu watatu walioinua vinywa vyao kwa pamoja wakatamka maneno haya sambamba kama wanaimba kiitikio cha nyimbo waipendayo kwa sauti.


“Aiseeh! Nimesikia mlio mkubwa ‘Tiiiiiiihhh’ kisha simu ikakatika ghafla wakati sijamalizana na Chasco kimaongezi…”Akajibu Castillo huku anawaangalia wenzake kwa shahuku kubwa.


“Piga tena simu haraka… Shiit! Nini tena?!!...” Akaongea Zamorano a.k.a Zamo mmoja wa vijana waliotokea genge la vijana wa mtaani la ‘La hormiga’ lililopo Veracruz mitaa ya La Playa.


Castillo akainua simu yake tena na kupiga tena namba zilizompigia muda wa dakika moja tu iliyopita, simu iliganda sikioni dakika moja ikisachi mwisho akajibiwa na huduma kwa wateja mtandao wanaotumia watu wengi wa Mexico mtandao wa T-Mobile kuwa namba anazopiga hazipatikani ajaribu tena baadaye.


“Namba hazipatikani… Shenzi ina maana gari yao imepata ajali au ni nini?” Akauliza Castillo swali kama lile ambalo watu wawili wako ndani ya ngome ya magereza halafu mmoja anamuuliza mwenzie huo mlio wa gari linalopita huko nje wa gari gani? Maana ni swali gumu kujibika kirahisi.


“Unasema umesikia mshindo mkubwa? Ebu ngoja mimi nimpigie Andreas tutapata jibu ni n..” Kabla hajamaliza kuongea walijikuta wakipaa juu na kisha wote kujikuta wanaona giza machoni mwao.


Ni Rocket-Propelled Grenade-7 tena! Gari hii ilirushwa juu ikiwa tayari imesambaratishwa na hakuna kilichokuwa salama kati ya vilivyokuwa ndani ya gari hadi nje ya gari ikiwa juu hadi inatua chini ikiwaka moto. RPG-7 ilifanya kazi ambayo wao walikuwa wakitafuta jibu nini kimewakuta wenzao huko walipo,wakiwa wamepaki mahali ambapo kwao waliona ni salama wakiwa wametega kama walivyoamini wenyewe kuwa wametega (uzembe).


Kumbe wao wakiwa wanatega na wao walikuwa wametegwa tena mtego uliokuwa umeandaliwa vizuri na hawa jamaa ambao kwao kwa sasa wanawaona ni maadui zao wakuu, wakiwa hawawajui vizuri zaidi ya kusema ni wamarekani.


Pigo kwa ‘The Red Jaguar’ ndani ya ngome ambayo inaitwa ngome ya pande mbili hasimu ambazo ziliamua kuingia mkataba wa kuondoa uhasama kati yao kila genge lifanye kazi zake bila kuingilia kazi za mwingine.


“Bon!..” Akiwa kapiga simu alianza kuongea hivyo baada ya upande wa pili kupokea.

“Ray usiniambie bado hujawafagia..” Akajibu wa upande wa pili.

“Toka lini nimewai kukosea…. Mtego umeenda kama tulivyotarajia… Washenzi hawa mpaka waione Nuevo Laredo chungu, mpaka waamishie nguvu yao yote hapa sisi.. Mavics na wenzake wakaingie kilaini kambini mwao tuchukue watu wetu kilaini … Mbwa wa haramu hawa..” Akajibu Bon akijiweka kola yake vizuri mahala alipo, mtaa huu alipo kwa sasa uligeuka mtaa wa watu kujaa kulizunguka gari linalowaka moto huku kila aliye ndani ya gari akionekana amechakaa.


“Mimi pia tayari… Washaenda kuzimu… Waelekeze hao kina Fraizer tukutane maskani kwa kikao cha haraka jinsi gani tunajiaandaa kwa majibu toka kwa wajinga hawa..”Akaongea aliyeitwa Bon na mwenzie ambaye tushamtambua kuwa ni Ray.

“Sawa! Ndiyo nachukua pikipiki hapa.. Wao wapo kwenye maegesho ya mini super market.. Tulipowaelekeza watapaki wakati tunaunda mchongo kama kawaida… Dah! Plan ilikuwa fantastic hii wamenasa kilaini sana..”

“Haraka Guadalupe Street.. Msichelewe..!” Akaongea tena Bon na wote wakakata simu zao.



***** ***** *****


TEN SPECIAL ASSASSIN’S (WAUAJI KUMI MAALUMU)

Kundi la vijana mchanganyiko kumi, kukiwa na wanaume sita na wanawake nne. Vijana hawa wauaji wa kukodishwa wakiwa wanapatikana viunga vya jiji la Denver, mji mkuu na mkubwa wa jimbo la kujitawala la Colorado, moja ya majimbo yaliyoungana kuunda muunganiko wa nchi kubwa ya Marekani.


Kundi lililoanzishwa miaka kumi iliyopita na vijana wa mji huu wa Denver waliokuwa wametoka shiriki vita ya pili ya Iraki na Marekani iliyokuwa na mshirika mwenza Uingereza vilivyoanza kurindima kati ya mwezi wa machi na aprili mwaka 2003 taratibu kisha kushika kasi mpaka pale washrika wenza walipoona wametimiza mengi kati ya waliyoyapanga kwa taifa hili la mafuta lililokuwa lipo chini ya kiongozi wao Rais Saddam Hussein.


Wakiwa katika kikosi cha wadunguaji waliopitia mafunzo yao kwa pamoja katika kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Fort Benning kilichopo Columbia, Georgia na baada tu yao tu wakaangukia mwaka ambao Marekani ilikuwa imeanza fukuto la mgogoro uliokuja kuzua vita ya ghuba uajemi awamu ya pili, hawakuwa na njia ya kukwepa maana na sit u kwenda kuonekana makwao kusalimia na kupeleka taarifa wamemaliza mafunzo salama wao walipandishwa ndege kwenda kwenye manowari za kivita zilizopiga kambi karibu na ghuba ya uajemi.


Vita ilivyochanganya vijana hawa walipiga kazi kama timu kwa ufasaha na kama ujuavyo siri kuu ya jeshi ukiwa kikosi cha udunguaji wewe mwanajeshi mdunguaji kuna asilimia nyingi sana kwenda na kurudi vitani sababu wadunguaji wengi wanasogea eneo la vita huku wakiwa sehemu zile za kujificha kwa ajili ya kulinda wenzao wanaokwenda mstari wa mbele, kazi yao maalumu si kuwalinda tu wenzao kwa kutokea mbali wakitumia viona mbali (darubini) pia kuwapa taarifa ya waendapo kuna nini na nini.


Timu hii yote katika awamu ya kwanza ya watu waliorudi Marekani kutoka vitani wakiwa wamekamilisha kwa asilimia za kutosha kazi waliyoiendea na wao walirudishwa ikiwa ni ombi maalumu la wazazi na walezi wao kutaka kuwaona watoto wao maana Iraki tu walihudumu huko kwa miaka mitatu.


Vijana kwa yale waliyoyaona huko Iraki walikubaliana lazima kwa mbinu zote waache jeshi, wawe raia wa kawaida na katika hili walifanikiwa kwa visingizio mbalimbali kuhusu mifumo mbalimbali ya kibinadamu wakisema kwa kila mmoja amepatwa na kasoro fulani katika mfumo wake fulani na anahisi hawezi kuendelea na jeshi.


Baada ya kuacha jeshi waliangaika na mambo mengine kila mmoja akifanya lake hadi pale siku moja mwenzao mmoja alipowashauri waunde kundi la kukodishwa, kundi litakalofanya kazi za kukodishwa katika mambo ya kisasi, mauaji hata kuteka kwa ofa maalumu ya pesa kutoka kwa watu binafsi na hata serikali mbalimbali hapa duniani ambazo nazo pia uamua kumuondoa fulani bila kuonekana wao wameshiriki basi kundi hili la siri lilifanya kazi hiyo likiwa limejipa jina la ‘Ten Special Assassin’s’ wakimaanisha kuwa wao ni ‘wauaji kumi maalumu’.


Kwa muda mfupi walipata sifa zilizotapakaa ndani ya Marekani hasa kwa matajiri waliokuwa wakihitaji kufanyiwa kazi baada ya kuona maslahi yao yameingiliwa na mtu, watu au kikundi fulani, sifa zao zilizagaa na kutapakaa mwsiho zikavuka mipaka na kupata nafasi ya kufanya kazi na serikali kadhaa za ulaya na hata bara la Asia, wakikodiwa kufanya mengi ya siri na kisha kujiondokea wakiwa wameacha sintofahamu kwa watu wasiohusika.


Mwisho wa sehemu ya ishirini na tano (25)


‘The Red Jaguar’ (The Monster) ndani ya Nuevo Laredo jiji lililopo jimbo la Tamaulipas hali ilikuwa ya sintofahamu baada ya siku kadhaa mabinti watano warembo wanaosifika katika genge hili kwa kazi ya kupitisha mizigo ya mihadarati waliporwa mizigo yao na watu waliosemekana wametokea Marekani, hivyo haraka kiongozi wa ‘TRJ’ alitoa amri wasakwe waliohusika na uporaji huo bila kujua ni kina nani waliwapora wanawake wale.


Tukaona ufuatiliaji na umakini ukianza katika kuwafuatilia watu wale na kupelekea silaha aina ya ‘RPG’ kutumika kuwaondoa duniani watu wa ‘TRJ’.


Je ni kina nani waliofanya matukio haya mawili makubwa wakitumia usafiri wa tukiwa tumesoma majina yao kuwa mmoja anaitwa Bon na mwingine Ray.


‘Ten Special Assassin’s’ nao wameingia na tumeisoma historia yao.

Je ni nani hawa mpaka wasogee katika kurasa zetu?


Majibu ya yote haya yanapatikana sehemu zinazokuja.



Timu hii yote katika awamu ya kwanza ya watu waliorudi Marekani kutoka vitani wakiwa wamekamilisha kwa asilimia za kutosha kazi waliyoiendea na wao walirudishwa ikiwa ni ombi maalumu la wazazi na walezi wao kutaka kuwaona watoto wao maana Iraki tu walihudumu huko kwa miaka mitatu.


Vijana kwa yale waliyoyaona huko Iraki walikubaliana lazima kwa mbinu zote waache jeshi, wawe raia wa kawaida na katika hili walifanikiwa kwa visingizio mbalimbali kuhusu mifumo mbalimbali ya kibinadamu wakisema kwa kila mmoja amepatwa na kasoro fulani katika mfumo wake fulani na anahisi hawezi kuendelea na jeshi.


Baada ya kuacha jeshi waliangaika na mambo mengine kila mmoja akifanya lake hadi pale siku moja mwenzao mmoja alipowashauri waunde kundi la kukodishwa, kundi litakalofanya kazi za kukodishwa katika mambo ya kisasi, mauaji hata kuteka kwa ofa maalumu ya pesa kutoka kwa watu binafsi na hata serikali mbalimbali hapa duniani ambazo nazo pia uamua kumuondoa fulani bila kuonekana wao wameshiriki basi kundi hili la siri lilifanya kazi hiyo likiwa limejipa jina la ‘Ten Special Assassin’s’ wakimaanisha kuwa wao ni ‘wauaji kumi maalumu’.


Kwa muda mfupi walipata sifa zilizotapakaa ndani ya Marekani hasa kwa matajiri waliokuwa wakihitaji kufanyiwa kazi baada ya kuona maslahi yao yameingiliwa na mtu, watu au kikundi fulani, sifa zao zilizagaa na kutapakaa mwsiho zikavuka mipaka na kupata nafasi ya kufanya kazi na serikali kadhaa za ulaya na hata bara la Asia, wakikodiwa kufanya mengi ya siri na kisha kujiondokea wakiwa wameacha sintofahamu kwa watu wasiohusika.


ENDELEA KUFYONZA UTAMU!


TEN SPECIAL ASSASSIN’S (TSA) (WAUAJI KUMI MAALUMU)

Mr. Marcus Daniel Tier mmarekani mwenye asili ya Afrika ni ‘Kingpin’ wa genge la siri la ‘IF U WANT’ lililo na maskani yake katika jiji la Carson City, jiji lililo katika jimbo linalojitawala la Nevada huku jiji kuu na jiji kubwa zaidi la jimbo ambalo ni miongoni mwa majimbo muunganiko yanayounda nchi kubwa ya Marekani ni jiji maarufu lenye sifa zake jiji la Las Vegas, jiji la mastaa kibao wanaoishi Marekani.


Genge la ‘IF U WANT’ ni genge linalojihusisha na ulanguzi wa mihadarati aina zote katika maeneo yote ya jimbo hili la Nevada huku likihusika sana na jamii ya watu weusi katika mfumo wake wa kibiashara zao za haramu.


Miezi miwili kabla, vijana kumi wa genge hili walienda mpaka wa Marekani na Mexico eneo la mto Colorado, mto uliopo katika bonde kubwa la Grand Canyon ni mto ulio Marekani na Mexico. Ukianzia katika nchi ya Mexico katika chanzo cha ziwa La Poudre Pass Lake, ziwa lililopo nchini Mexico na kisha kumalizia katika ghuba ya Calfornia.


Wahuni hawa wa ‘IF U WANT’ walifika hapa kwa kazi maalumu ya kupokea mzigo wa dawa za kulevya aina ya ‘white cocaine’ toka kwa genge la ‘Los Zetas’ lakini wakati wakiwa katika makabidhiano ndiyo kilikuwa kipindi ambacho vita kati ya magenge yaliyokuwa hasimiana katika hali ya juu sana kwa genge kuona lenyewe ndiyo linastahili kufanya biashara za ulanguzi katika maeneo ya mipaka yote ya Marekani na Mexico.


Wazee wa kazi wa ‘RTJ’ walivamia na zikamwaga njugu (risasi) za kumwaga, dakika kumi mbele si watu kumi na tano wa Los Zetas wala watu kumi wa ‘IF U WANT’ waliokuwa hai kila mmoja alilishwa risasi za mwili za kutosha na wote wakaaga dunia.


‘TRJ’ wakachukua pesa zilizokuwa zimeletwa na niggas kutoka Marekani na pia wakachukua mzigo wa white cocaine ounces gram 1500 kipimo kikubwa sana ambacho walitia hasara kubwa sana upande wa makundi haya makubwa moja toka nje ya Mexico na lingine lile walilo na uhasama.


Los Zetas walipoulizwa na Mr. Markus wakatoa taarifa waliofanya uhuni ule ni watu wa ‘TRJ’ ndipo Mr. Markus hasira zake akatuma watu wake ishirini kuingia Mexico kwa dhumuni kuu kusudiwa ni kuhakikisha wanamuua kiongozi wa genge la ‘TRJ’ lakini vijana ishirini wale wakiwa ndiyo kwanza wameingia tu katika mji walioambiwa ndiyo haswa bwana mkubwa Brigedia Feca uwa anapatikana wakashtukiwa wakiwa kwenye kikao cha kujipanga wanafanya nini katika kazi iliyowapeleka jimbo la Guerrero katika moja ya nyumba waliyopanga kwa muda mfupi.


‘TRJ’ wakiwa na kikosi kilichoongozwa na Koplo Savatel Santos waliwavamia na kuwapiga kwa mashambulizi ya mabomu ya kivita wakiisambaratisha nyumba yote.


Hapo taarifa zikamfikia mkubwa wa ‘IF U WANT’ Mr. Markus ambaye haraka akaamua kubadili gia kwa kuwa genge lake lilikuwa likijulikana ni la watu wa jamii ya watu weusi, akaonelea atafute kikundi cha kukodi cha wazungu tupu ndipo akili yake ikaangukia kwa ‘Ten Special Assassin’s’.


Ambao wao baada ya kupewa kazi maalumu ya kumuua Brigedia Feca waliona kwanza watume wasichana wao wawili kati ya wasichana wanne walio katika kundi lao wakiongozana na mwanaume mmoja aitwaye Taylor Brovas, mdunguaji wa zamani wa jeshi la Marekani aliyehudumu katika jeshi la Marekani kwa kiwango sawa na wadunguaji wenzake waliounda genge la ‘Ten Special Assassin’s’ (TSA) akiongozana na wanawake walio ndani ya kundi hili ambao nao walikuwa nao bega kwa bega toka wakiwa jeshini mpaka wakati huu.


Jamaa hawa nao pamoja na ujanja wote na ujuzi wote walio nao huku pia wakiwa na sifa lukuki nao waliingia katika mikono ya ‘TRJ’ na kusababisha Los Zetas kuingiwa na uwoga mkubwa waliposikia taarifa toka Guerrero kuwa watu waliokodishwa na ‘IF U WANT’ kwenda Guerrero kuhakikisha wanamdungua Brigedia Feca wamekamatwa.


‘IF U WANT’ wakapewa taarifa na Los Zetas kuwa mabinti wawili na mwanaume mmoja wametiwa mikononi na ‘TRJ’, taarifa ile ikatumwa kwa kiongozi wa ‘Ten Special Assassin’s ambao wao tayari walikuwa na taarifa kutokana na wale wanawake wawili na yule mwanaume kila mmoja alikuwa na chip maalumu iliyowekwa katika kila tako la kila mmoja wao, micro-chip ambazo zilitengenezwa kwa plastiki na hivyo mashine za kusachi zinazo sensor kupitia jamii ya sindano na chuma ilikuwa inazunguka na kukuta kavu mwili hauna micro-chip.


Hivyo ilifika wakati wao wakiwa wanajiandaa kwenda kikazi katika nchi ya Mexico huku huko Mexico kukiwa na kikao kilichosimamiwa na watu maarufu walio ndani ya serikaliambao wana maslahi na magenge haya na hata wasio ndani ya serikali lakini nao pia wana maslahi na magenge yanayojihusisha na mihadarati hasa yanaoongozwa na mabosi wakubwa kikao kilicholeta muafaka wa mkataba wa amani baina ya Los Zetas na ‘The Red Jaguar’.


Mkakati wa kwanza wa kundi la ‘Ten Special Assassin’s’ (TSA) ulikuwa kuwaokoa kwanza ndugu zao ambao mitambo yao ilionyesha wapo eneo la milima ya Tajumulco, mkoa wsa San Marcos nchi ya Guatemala, safari yao ikawapeleka hadi maeneo hayo na ndipo wakakutana na ngome kubwa ambayo hawakuitaraji, ngome ya genge la ‘TRJ’.


Kwa kweli ‘Ten Special Assassin’s (TSA) wakaogopa wakarudi Marekani kisha kiongozi wao akaenda kwa Mr. Markus na kumuomba awape muda wajipange na waone ni vipi wataifanya kazi husika na pia wakisema kuwaacha ‘TRJ’ wajisahau itawafanya wakasahau kama kuna jino waliling’oa kipindi fulani na wao wanatakiwa kurudisha jino hilo kwa stahili ya ‘Jino kwa Jino’.


Ilipopisha mwaka mmoja na miezi miwili wakiwa wamesajili watu wengine watatu walioacha jeshi kama wao na kufanya idadi yao kuwa ya watu kumi kama ilivyokuwa mwaka mmoja na miezi mitatu iliyopita walirudi ndani ya Mexico na ndipo wameianza kazi rasmi ya kulipiza kisasi na hata kuwaokoa ndugu zao, wao ndiyo walipora mzigo toka kwa wanawake wa genge la ‘TRJ’ huku wakiwaacha huru wanawake wale waondoke zao kwa dhumuni wakatoe taarifa kuwa wamevamiwa na kuporwa.


Na kweli ujumbe wao ulifika na mara moja kiongozi wa ‘TRJ’ kanda ya mpaka wa Mexico na Marekani alistuka lakini hili asionekane mzembe kwa Feca na viongozi wenzake wengine akaamua kuwa atalishughulikia suala hili yeye mwenyewe na ndipo wakaanza msako wakiwa wamekariri namba za gari walizopewa taarifa na wanawake wao kuwa waliowapora walikuwa wakitumia gari hiyo.


Mtego! Mtego waliotegwa uliwanasa uliwapelekea kupoteza watu kazi kumi na gari mbili wanazotumia katika misheni zao.


‘Ten Special Assassin’s (TSA) ndani ya kazi, wapo Mexico kufanya kitu ambacho walikipa subira ya mwaka mmoja na miezi mitatu wakiwaacha ‘TRJ’ wasahau kama waliwai kufanya jambo ambalo watalijutia ama vipi? Walijisahau kama katika magereza yao wanawashikilia na kuwatesa raia wa Marekani wanaounda kikosi kazi cha ‘TSA’.


***** ***** *****


SOLEDAD DE MACIEL, PETATLAN-GUERRERO

Moto wa maneno ulikuwa ukifoka toka kwenye kinywa cha Brigedia wa zamani wa jeshi la Mexico, Brigedia Fernandez Carlos Codrado ‘Feca’, matusi yote ya kimexico yalikuwa yakimtoka bila kuacha lolote bila kujali anaowatukana kama wapo hapa alipo au hawapo.


Kona zote za ambazo zipo kwenye ukumbi waliokuwa wameitisha kikao zilikuwa zikifikiwa na yeye tu, alijawa na gadhabu iliyojidhihiri dhahiri shairi machoni kwa kila mmoja aliyeko pale, alifoka alinyamaza akitingisha kichwa kwa masikitiko akisikitikia yale yaliyotokea ambayo yaliwafanya kwa sasa wawe hapa kwenye kasri ambalo kwao wao wanaoruhusiwa kufika hapa walikuwa wakiliita ‘Secreto Potentio La Feca Palacio’.


“Kazi hii inawasumbulia wapi Morientes? Nimechoka kufoka… Mnafikiri nikiendelea kufoka huku nyinyi nyote mkikaa kimya kuna faida?” Aliwaswalika swali huku macho yake mekundu ya kung’aa yakiwa ndani ya gadhabu yakiwaangalia kana kwamba anawatisha wamuogope, kumbe ni hasira tu alizonazo bwana mkubwa na bado hakuna aliyejibu wote walibaki wamekaa tu kwenye viti vyao na hata Mr. Guti hakuweza sema chochote katika wakati huu alibaki akiwaangalia tu watu wengine walio katika bodi kuu.


“Nataka maelezo ya kina iweje tunapoteza nguvu kazi na mali zetu kwa urahisi kwa watu ambao kwetu sisi tunaweza cheza nao kirahisi sababu wameingia nchini mwetu... Sajenti Lara! Tafadhali lete habari.. Tupo hapa kujadili tunachoweza kufanya kudhibiti kupoteza watu wetu na mali zetu..!” Akaongea tena Brigedia Feca kisha akapiga hatua kilipo kiti chake akakaa huku anajifuta jasho kwa kitambaa cha jasho (leso).


“Angel akiongoza kikosi cha ‘dominae duo’ waliporwa mzigo wa white cocaine eneo ambalo ni karibu kabisa na Bridge Convent Street kona ya kwanza tu pale walikuta gari aina ya Nissan Land Cruiser ya rangi ya kijani nyeupe imepaki na hapo ndipo wao wakati wanawapita wakiwa kwenye gari yao walijikuta wanashambuliwa kwa risasi katika matairi ya gari yao hivyo gari yao ikaserereka kwenda kando ya barabara na kabla hawajajihami akatokea mtu mbele yao akiwa na silaha aina ya RPG kisha akawaamrisha washuke wote ndani ya gari la sivyo anawalipua kwa RPG… Ikabidi Angel na wenzake washuke, muda huo ulikuwa saa tano usiku nilikuwa nimewaagiza waelekee hapo kuna matajiri wawili wa kiarabu toka Canada walifika kwa ajili ya biashara.” Akajibu Sajenti wa zamani wa jeshi la Mexico.


“Mnawaamini hao matajiri toka Canada?” Akauliza Mr. Guti baada ya muda wote kuwa kimya akisikiliza bosi mwandamizi akiongea.


“…Mara mbili tunafanya nao biashara .. Na kama hujuavyo hili jambo ni mara ya kwanza linatokea toka tuingie mkataba wa amani na ‘Z’… Na ndiyo maana sikuomba msaada huku makao makuu nilitaka nidhibiti hali ile sisi kama sisi wa ukanda wa mpakani..!” Akajibu Lara.


“Mna uhakika watu hao wanatokea Marekani?” Akauliza Brigedia Feca.


“Si hakika sana lakini kwa maelekezo ya Angel Ortiz ni hivyo sababu walisikia lugha yao na lafudhi yao ni watu watokao Marekani..!”

“Mh! Kwa ilivyo basi wanaweza wakaijua ngome yetu ndogo iliyoko pale Nuevo Laredo na wakatutia hasara… Sasa naomba nitoe maelekezo ambayo yafanyiwe kazi mara moja..” Akaongea Feca kisha akaachia mate yalowanishe koo lake halafu akaendelea.

“Koplo Maxiwell Zuantejo na S.S Morientes Gudrado muelekee huko Nuevo Laredo leo leo usiku huu huu bila kuchelewa ukafanyike msako mkali wa kundi hili na kama mtafanikiwa kuwakamata itakuwa bora zaidi hili tujue adui yetu ni wao wenyewe au kuna mtu amewatuma kufanya wanachofanya kana kwamba hawaijui ‘TRJ’… Mtaongozana na vikosi na vikosi vyenu mnavyotembea navyo… Nachotaka baada ya siku mbili au tatu nisikie mmemaliza kazi hii..” Yalikuwa na maelekezo toka kwa bwana mkubwa ‘Kingpin’ wa genge la ‘TRJ’ ambayo uwa yakitoka hakuna mjadala zaidi.


“Mr. Guti naomba usiondoke, kuna jambo naomba tuongee kidogo sisi wawili tu..” Akaomba Feca akimuomba kiongozi mwenzake katika ngazi ya juu katika genge hili, mtu wa pili katika hisa za genge.


Waliinuka pale kisha wakapanda ngazi zilizowapeleka kwenye baraza ya juu ya kasri hili wakiwaacha walinzi wao chini kule kwenye ukumbi wa mikutano.


“Ndiyo Brigedia.. Lete habari!” Akaanzisha Mr. Guti baada ya kuweka viwiko kwenye kuta kingo ya baraza.


“Unaonaje juu ya hili mzee mwenzangu?” Akaanza kwa swali Feca.

“Lipi mkuu?”

“Mchezo unaotokea huko Nuevo Laredo.. Huhisi ni mchezo wa ndugu zetu tunazungukana hili kupata zaidi?”

“Kivipi? Mi sifikirii hili Feca… Nafikiri kuna ukweli katika maelezo yao, tunaweza nasi tukaweka wapelelezi wetu wa siri wakapeleleza haya nyuma ya pazia..”

“Shetani wa mawazo mabaya naomba apite mbali, nimetoka mbali sana na Lara.. Mara ya kwanza wakati wanafika hapa na kuomba kikao na bodi kuu yote nilishangaa sana lakini nilipokuwa nakupigia simu wewe kuomba mfike hapa simu yangu nyingine nayotumia kuongea na maafisa wa DTO walio huko Nuevo Laredo iliita ndipo nikakata yako upesi na kupokea.. Nikapewa taarifa ya mauaji yaliyotokea huko hivyo nikawa nishajua Lara amekuja na nini” Akatoa maelezo Feca.


“Hivi unawakumbuka wale wamarekani wawili wa kike na mmoja wa kiume tuliowaweka hadi leo tunawashikilia huko Tajumulco?” Akauliza Guti huku wakikaziana macho mabosi hawa.


“Ndiyo nawakumbuka… Kule sasa kwa maelezo ya Savatel kuna wafungwa toka Marekani saba na wengine kama ishirini… Vipi? Unahisi kuna kitu na yanayotokea?”

“Nahisi hilo maana ni mwaka na aa sasa toka tuwaweke kule na mpaka leo hawajasema kama walitumwa na nani kukufuatilia wewe na hata genge zima..!”

“Wale watakuwa majasusi wa DEA… Ila hawa wazungu wanaosemekana wameanza uchokozi huko Nuevo Laredo nafikiri ni kati ya yale magenge kama lile genge la ‘IF U WANT’ lililotaka kujitutumua kupambana nasi na tukazima chokochoko zao’

“Mi naomba umwambie Savatel akafanye nao mahojiano watu wale kule Tajumulco kuna jambo nahisi wanaficha wale ingawa wao wanasema walitaka kupata fedha kwetu”

“Sawa sawa ila pia nahitaji nimtaarifu Koplo Mariana Caro Funtes naye awepo kwenye kuwahoji wale wanawake kwakuwa ndiyo watu pekee ambao naamini tukiwaahidi jambo zuri kwao watakubali kusema ukweli wao kwa ujumla wamechoka kuwa jehanamu ile..!”

“Sawa.. Tufanye hivyo… Bado kunafuka moshi, moto bado haujaanza kuwaka na lazima tuzime kila kitu kikiwa katika moshi kabla haujawa moto, adui zetu wanatutia hasara na bado wanaona hawaridhiki hiki kitakuwa ni kisasi tu ndugu yangu…!”

“Ni haya tu mkuu nilitaka nisikie kwa wewe binafsi unahisi nini katika mambo haya kama hujuavyo katika biashara yetu ya ulanguzi wa mihadarati hali ilivyo watu wana tamaa sana na wengi hawaridhiki na kitu unachompa anaweza taka apate zaidi na zaidi..”

“Sawa Feca… Acha niwai kwangu..!”

“Sawa! Usiku huu kuwa makini na RPG.. Haha hah.. Maana wananitisha sana hao wahuni waoga wanaotumia RPG..!”


Mr. Guti alishtuka sana kusikia neno RPG toka kwa Feca, akamtizama kwa haraka kisha akatizama eneo la nje analoliona kutokea pale baraza ya juu walipo.


“Basi nitalala hapa hapa na watu wangu… Uzuri mke sina nina kimada hana sauti kwangu… Umeniambia jambo la maana, wajinga sana wanaua kwa kuvizia kama watu wanaojifunza kuua..”

“Ni vizuri ukalala hapa… Asubuhi utaondoka kutokea hapa” Feca aliridhia ombi lake lilillokubaliwa na rafiki yake.


Waliomba waletewe vinywaji na nyama toka kwa wahudumu wa kasri vyote vikaletwa haraka na wao wakaanza kushambulia taratibu huku wakiongea mipango yao mbalimbali.


Mwisho wa sehemu ya ishirini na sita (26)


Mwaka mmoja na miezi mitatu ya uvumilivu wa kisasi cha jino kwa jino imewafanya kikundi chenye kikosi hatari cha ‘TEN SPECIAL ASSASSIN’S (TSA) kurudi Mexico kwa ajili ya kuwaokoa watu wao toka mikononi mwa ‘The Red Jaguar’ (TRJ) ‘The Monster’.


Je watafanikiwa kuwaokoa wenzao na je ilikuwaje Jasusi wa DEA, Sajenti Johnson Greg Rautolaye ‘Jogre’ kuingia katika mikono ya watu wanaomshikilia?


Kaa nami weka uvumilivu na umakini jibu linakaribia.




“Ndiyo nawakumbuka… Kule sasa kwa maelezo ya Savatel kuna wafungwa toka Marekani saba na wengine kama ishirini… Vipi? Unahisi kuna kitu na yanayotokea?”

“Nahisi hilo maana ni mwaka na aa sasa toka tuwaweke kule na mpaka leo hawajasema kama walitumwa na nani kukufuatilia wewe na hata genge zima..!”

“Wale watakuwa majasusi wa DEA… Ila hawa wazungu wanaosemekana wameanza uchokozi huko Nuevo Laredo nafikiri ni kati ya yale magenge kama lile genge la ‘IF U WANT’ lililotaka kujitutumua kupambana nasi na tukazima chokochoko zao’

“Mi naomba umwambie Savatel akafanye nao mahojiano watu wale kule Tajumulco kuna jambo nahisi wanaficha wale ingawa wao wanasema walitaka kupata fedha kwetu”

“Sawa sawa ila pia nahitaji nimtaarifu Koplo Mariana Funtes naye awepo kwenye kuwahoji wale wanawake kwakuwa ndiyo watu pekee ambao naamini tukiwaahidi jambo zuri kwao watakubali kusema ukweli wao kwa ujumla wamechoka kuwa jehanamu ile..!”

“Sawa.. Tufanye hivyo… Bado kunafuka moshi, moto bado haujaanza kuwaka na lazima tuzime kila kitu kikiwa katika moshi kabla haujawa moto, adui zetu wanatutia hasara na bado wanaona hawaridhiki hiki kitakuwa ni kisasi tu ndugu yangu…!”

“Ni haya tu mkuu nilitaka nisikie kwa wewe binafsi unahisi nini katika mambo haya kama hujuavyo katika biashara yetu ya ulanguzi wa mihadarati hali ilivyo watu wana tamaa sana na wengi hawaridhiki na kitu unachompa anaweza taka apate zaidi na zaidi..”

“Sawa Feca… Acha niwai kwangu..!”

“Sawa! Usiku huu kuwa makini na RPG.. Haha hah.. Maana wananitisha sana hao wahuni waoga wanaotumia RPG..!”


Mr. Guti alishtuka sana kusikia neno RPG toka kwa Feca, akamtizama kwa haraka kisha akatizama eneo la nje analoliona kutokea pale baraza ya juu walipo.


“Basi nitalala hapa hapa na watu wangu… Uzuri mke sina nina kimada hana sauti kwangu… Umeniambia jambo la maana, wajinga sana wanaua kwa kuvizia kama watu wanaojifunza kuua..”

“Ni vizuri ukalala hapa… Asubuhi utaondoka kutokea hapa” Feca aliridhia ombi lake lilillokubaliwa na rafiki yake.


Waliomba waletewe vinywaji na nyama toka kwa wahudumu wa kasri vyote vikaletwa haraka na wao wakaanza kushambulia taratibu huku wakiongea mipango yao mbalimbali.


ENDELEA NAYO…!!!


GUADALUPE STREET, NUEVO LAREDO

Sebule moja yenye futi kumi kwa futi kumi na mbili ilikuwa imewakaliza katika zulia lililotandikwa chini wanaume wanne na wanawake wawili, nyumba hii iliyopo mtaa huu wenye jina la Guadalupe. Wanaume hawa wa kizungu toka nchi ya Marekani ndiyo wanaounda kundi ‘Ten Special Assassin’s’.


Nyumba hii walikuwa wamekodisha nyumba yote wakikaa wao peke yao kwa kuwa ni moja ya nyumba zilizopo mtaa huu wa Guadalupe ambazo zinapangishwa kwa mtu anayehitaji kupanga anapanga, aina tatizo analipia tu kwa wahusika wenye nyumba hizi zilizojipanga mtaa huu zikiwa katika muundo wa apartment.


“Mambo yameenda vile tulivyotaka… Taharuki imekuwa kubwa sana, wakati nakuja huku nimetumiwa meseji na Carlos Morza wa Los Zetas kuwa kapigiwa simu na ndugu yake aliyeko ‘TRJ’ kuwa viongozi wao wakuu katika bodi yao wametoka kufanya kikao juu ya hali iliyowakumba… Sasa ndiyo watajua kwamba jino kwa jino inauma sana” Alianza kuongea mwanaume wa kizungu aliyeenda juu na mwili wake mkavu lakini misuli inayoonekana katika mikono na sehemu zingine ukiwa mtu wa kazi lazima utambue unayemuona mbele yako hata kwa kumuibia kwa chati ni mtu wa kazi haswa, nywele zake za rangi ya blonde zilizofungwa nyuma kama fungu la mchicha na ndevu chache zilizosambaa kuanzia mashavuni kama uchafu wa sumaku hazikumfanya awe karaha bali zilimfanya apendeze vizuri tu.


Anaitwa Boniface W Montreal wenyewe walipenda kumkatizia wakimuita ‘Bon’ ndiye mpanga mipango mkuu wa kundi hili la ‘Ten Special Assassin’s’ (Wauaji kumi maalumu) wakiwa na imani kuwa wao ni watu maalumu walioletwa duniani kwa kazi maalumu ya kuua na si ingine.


“Lazima wachanganyikiwe kunguni hawa… Heti wanajiita wanyama.. Na sijui kwanini tumechukua muda mrefu kufika hapa kuwaokoa watu wetu mi sifikirii kwa ujuzi wetu ilifaa kusubiri mpaka heti wasahau kama walitufanyia ubaya” Akaongea mwingine ambaye yeye hakuwa na nywele za blonde ingawa naye pia ni mwanaume wa kizungu, nawaita wanaume sababu wao washaondoka kwenye ujana, huyu anaitwa Rayson Blair pia kundini na hata rafiki zake wengine umuita ‘Ray’.


“Subira ni jambo la heri, sote hapa sisi ni wanajeshi na jeshini tulifunzwa uvumilivu tunapokuwa kazini na hili tulilofanya ni moja ya uvumilivu… Kuna njia nyingine ambayo nimeipokea kama ushauri toka kwa Carlos Morza, anasema tunaweza tumia mbinu ya kuwateka watu wawili au watatu walio karibu na Brigedia Feca kisha tukamuomba mabadilishano na watu wetu anaowashikilia… Nimeona nililete kwenu kama inawezekana tukabadili gia angani!” Bon akatumia busara aliyonayo kuomba Ray apunguze munkari maana siku zote yeye alikuwa akitaka wafike hapa Mexico kutafuta wenzao wanashikiliwa wapi ukizingatia mmoja kati ya wanaoshikiliwa mateka ni mpenzi wake ila mara zote alizotaka hata aje mwenyewe peke yake Mexico, wenzake walimsihi awe na subira na mpenzi atampata tu, pia Bon alifikisha ombi baada ya kupokea wazo toka kwa mtu anayemtaja kuwa anaitwa Carlos Morza wa genge la ‘Los Zetas’.


“Wazo zuri sana… Muhimu kwetu ni wa kuwapata watu wetu, sababu kwa kweli hata sidhani kama walitarajia sisi tutakaa kimya kwa muda wote huu na kwa mawazo ya kijeshi waliyonayo wao hawako katika kile ambacho sisi tulipanga kwa sababu si kawaida yetu toka tuanzishe kundi letu kuwa tufanye subira tena subira iliyo ndefu kama subira hii ya kina Rosa kushikiliwa mateka na sisi tukakubaliana tuvute subira na ukweli mara zote mimi nilikuwa nawaambia tuna lawama kubwa sana toka kwa hawa wenzetu… Mawazo waliyonayo ni kuwa tulijaribu kuwaokoa na sote tumekutwa na umauti hivyo wamekata tamaa kabisa!” Ray akaongea tena katika hali ya kila mmoja kuchangia anachoona ni sahihi kwa wakati huu.


“Sote sisi ni mashujaa na wenzetu nao ni mashujaa, natambua Ray ndugu yangu huba ulilonalo ndiyo lilikusukuma kulazimisha tuchukue maamuzi ya haraka lakini kama utakumbuka miezi mitano iliyopita majasusi wawili wa DEA walikutwa na jambo ambalo hata serikali yetu ilipigwa butwaa tena ndani ya mpaka wetu na ikisemekana ni watu wa Brigedia Feca… DEA haina watu walio ovyo watu walio DEA niwa tu makini sana lakini ‘TRJ’ inawatetemesha sana na kwa habari za chinichini watu wa DEA wameliweka genge la ‘TRJ’ katika magenge ya hatari zaidi ulimwenguni na huku Feca akiweka katika watu wanaosakwa haswa kwa ajili ya mambo mengi aliyowafanyia DEA na hata DTO ya hapa Maexico.. Je Ray hatukwenda wote hadi Tajumulco?” Akaeleza kirefu Bon na kumalizia kwa swali alilomuuliza Ray.


“Tulikwenda sote… Ni uwingi wa walinzi wa pale ndiyo ulitufanya tugeuze kurudi Colorado tukasema tukajipange na ikiwezekana turudi na silaha za kivita maana wenzetu ni kama jeshi dogo..!” Akajibu Ray huku akijiweka vizuri kwenye sofa la mtu mmoja alilokaa.


“Tulirudi tukavumilia mwaka mmoja tukiwa tumewaongeza wenzetu wengine walioamua kuacha jeshi, tunashukuru wako vizuri na mambo yanaenda vizuri na tumekuja huku tukiwa na mbinu ya kuanzisha uchokozi utakaowafanya wasijue lengo lipo wapi, tulitaka kuwe na mvutano kwanza tuwashambulie watu wao wanaowatumia kwenye biashara, tulitaka tupige maslahi yao yaliyoko mijini hili wao waelekeze nguvu zao hapa… Hakuna asiyejua juu ya huu mpango na tayari tumeanza kuufanyia kazi ingawa naamini pia tutakuwa tumemuingiza matatizoni Fanuel na MPD yake, watataka wajue sisi ni kina nani kutoka kwao MPD.. Ningependa sote pamoja tuamue jambno ambalo litarahisisha kumaliza kazi hii ambayo kiukweli naomba niwambieni kila tutakavyokuwa tunachlewe kuitimiza ndivyo ugumu na kuharibika kwa kazi kutakavyo ongezeka kwetu na kupelekea hatari tusiyoitarajia kama mjuavyo kufanya kazi kama hii katika nchi ya Mexico ni hatari sana hata kama sisi ni watu wa hatari tuliozoea hatari zozote..” Maelezo marefu ya Bon yaliishia hapa hili aweze kuwapa nafasi na wenzake waongee kwakuwa ni kawaida yao kuheshimu na kusikiliza wazo la kila mtu.


“… Mmmh!... Upande wangu mimi ningependa tulifanyie kazi wazo la kuteka watu wa karibu wa Feca ingawa kumpata yeye mwenyewe kungeleta tija zaidi lakini pia kuwapata watu wake pia ni vizuri zaidi..” Mwanadada ambaye laiti ungekuwa umebahatisha kukutana naye siku angalau moja tu basi ungeweza kudhania pengine ni mwanaume kwa jinsi alivyo, alikuwa na vigimbi vya mkono na mwili uliojaza kama wacheza mieleka wa kike na hata sura yake ilikuwa sura iliyokwenda sana kwenye sura za wanaume wa shoka na hii yote kutokana na mazoezi magumu anayoyafanya bila kujali jinsia yake wala kuharibu muonekano wake wa kike, anaitwa Suzane Michael a.k.a Suzy M.


“Safi… Vipi Jean! Wewe unapendekezaje?.. Ungependa tuendelee na wazo la mbinu yetu ya kwanza au twende kwenye wazo geni toka kwa mtu asiye kati yetu?” Akauliza Bon akimuuliza mwanaume mwingine aliye katika kundi hili ambaye kwa hapa alikuwa amekaa sofa lililo karibu na sofa alilokaa Bon.


“Wazo la pili lina rahisisha zaidi… Hii mbinu inasemekana ndiyo mbinu aliyoitumia Feca kupata mali zake kwa kingpin wa MPD, hivyo itakuwa ni jino kwa jino, alichofanya ndicho anachofanyiwa hivyo wazo langu kama vipi tuijue familia yake ilipo kisha haraka tufanye utaratibu unaofanana na utaratibu aliotumia yeye..” Akajibu Jean Claude Xavo mwenye sifa zinazofanana na wenzake maana walichofanya na kupitia wote walio katika kundi hili ni aina moja ya mapito kotekote.


“Tulikuja na wazo la kisasi zaidi na hata kuhitaji kufanya kama onyo fulani kwa ‘TRJ’ lakini sasa tumeona jinsi ilivyo kuna ugumu fulani kufanya kazi kama zetu hapa Mexico sababu adui zetu hawana alama ya nje wana alama ya ndani na tunataka tuwapige na kuwaangamiza pale wanapojitokeza kwenye mitego yetu kama tulivyofanya leo lakini magenge ya mihadarati hapa Mexico ni mengi na ubaya wajihi wa watu wanaowafanyia kazi cartels wa hapa wanafanana katika kujichora chora na hata katika hali za kujiweka mionekano yao..!” Mwanadada Suzane Michael akatoa maelezo.


“Ni kweli usemavyo Suzy.. Sisi tuko tofauti na vikundi vingine vya mauaji, sisi tuna mipaka na uhadilifu wetu tuliojiwekea, hatuwezi kuua watu wasiohusika na genge la TRJ… Tunatakiwa tumwage damu husika.. Na sasa naomba niseme sote kwa pamoja ni busara tu tukubalianae kupokea mawazo toka kwa mtu mwingine asiye ndani ya kundi letu na kwa nijuavyo hii itakuwa ni mara ya kwanza kubadili maamuzi tukiwa ndani ya misheni na pia tukipokea wazo la mtu aliye nje ya kundi..!” Bon akaongea kisha akainuka toka kwenye sofa aliloketi akasogea lilipo friji akafungua mlango wa friji kisha akaibuka na whysk ya baridi aina ya Martins akagonga tarumbeta pale pale bila kusogea tena tarumbeta la kuganda kimiminika kikizama kinywani kwa mwendo mrefu kidogo.


“Basi nafikiri… Nguvu zetu ambazo tunatakiwa tuzifanye sasa ni upelelezi na upelelezi huo naomba ufanywe na Suzy akishirikiana Jean, tena mkitoka kwa miguu na kama utahitajika usafiri mtatumia usafiri wa jumuiya kwenda mnapohitaji kwenda popote pale huku mkitupa maelekezo wapi mlipo na inakuwaje kwa kila baada ya nusu saa… Upelelezi mtakaoenda kuufanya ni kwanza ni kujua kama Feca ana familia na iko wapi familia yake na kama mtashindwa kujua pia ni kujua nani tukimchukua kama si kina tukiwachukua na kuwaweka sehemu yeye Feca atashtuka na kutupa tunachotaka kwa mabadilishano… Sisi wengine naomba kila mmoja awe na subira pia tutawaataarifu wenzetu walio San Marcos watulie kabisa kwenye hotel waliyofikia tena wakae tu kama watalii, tuache Suzy na Jean wafanye kazi hii maalumu!” Bon akatoa maelezo ya mwisho, maelezo ya kufunga kikao.


***** ***** *****


BAADA YA SIKU MBILI MBELE, PUEBLA-PUEBLA

“Suzy…!”Alikuwa Bon amepokea simu aliyopigiwa akiwa katulia katika alichokiweka katika uwa wa nyumba waliyopanga, simu toka kwa Suzy M.

“Napiga simu toka mji wa Puebla, upelelezi umetufikisha huku… Bwana mkubwa Brigredia Feca, familia yake ameificha huku na kwa taarifa za chini chini tulizozipata jana alikuja kuitembelea familia yake..” Akaanza kutoa taarifa hiyo baada ya kuanza mazungumzo yao ikiwa hata salamu hakuitoa kwa kiongozi wao huyu.


“Aiseeeh! Mna uhakika na icho mnachosema?” Akahoji Bon.

“Kabisa yaani mtu aliyetuambia tuje huku Puebla kuna jambo ambalo linaweza kutusaidia shida yetu ni jasusi wa Drug Trafficking Organization kwa kweli kwanza tulitaka kujua kuna nini huku Puebla akatujibu kuna kitu ambacho tukifika Puebla tumuone dada mmoja aitwaye Linares ambaye ni mmoja wa wasichana makahaba wanaojiuza katika mji huu wa Puebla ndipo mi na mwenzangu tukaja, tulivyofika tukamtafuta na kumuona dada tuliyeelekezwa ndiyo tukastaajabu kusikia yeye ni mtoto wa mama ambaye ni muhudumu wa ndani wa mke wa Feca… Hapa tulipo tupo mtaa ulio karibu na nyumba ya ghorofa yenye flour (losheni) mbili, nyumba ya bwana mkubwa Feca anayoificha familia yake iwe salama wakati yeye familia za wenzake anazisumbua…” Akatoa maelezo Suzy M.


“Safi sana…. Mmepata malekezo yote au kuna kikwazo chochote cha kuwazuia kufanya yenu?”

“Kikwazo hakipo kikubwa sisi wawili tu tunaweza fanya jambo hapa na likakamilika vizuri tu kwa mujibu wa maelezo ya huyu muuza papuchi”

“Basi msikawie fanyeni la kufanya kisha mtatujulisha inakuwaje na sisi tunajiandaa kuja huko Puebla, msibakishe kitu zoeni wote walio ndani ya nyumba hiyo chochote kile cha tofauti mtatujuza haraka… Msifanye kosa na pia mwambie Jean kama hamna uhakika wa kazi kwenda vizuri kwa uchache wenu mtusubiri tufike…. Na hakika hapa Nuevo Laredo hatutarudi tena..!”

“Sawa kiongozi.. Tutawajulisha kama tutaona kuna mkwamo wowote wakati tutakapoisogelea nyumba husika ila kwa maelekezo ya muuza papuchi hakuna ulinzi wa kutufanya wanajeshi kama sisi tushindwe kuingia, jamaa ameweka ulinzi wa kawaida hili isionekane kama nyumba hii wanakaa wa familia ya juu sana au hatarishi mpaka iwe na ulinzi kama analindwa Gavana wa jimbo ama Rais wa nchi… Na habari ingine bwana mkubwa akifika huku uwa anakuja akiwa na walinzi wawili tu tena akiwa kavaa sura ya bandia na gari aina moja tu anayokuja nayo hapa na yote ni katika kuwaziba macho wasigundue juu ya familia yake..”

“…Mshenzi mjanja sana… Ila safari hii kazi anayo, basi nawatakia kazi njema nasi tunaomba tuwe na safari njema wakati tukija huko..”

“Amini… Amini..!!”


Pande zote zikakata simu ikiwa washamaliza na kuelewana kila linalohitajika kwenda kwenye mstari.


“Wakuu kumekucha… Safari ya Puebla… Kusanyeni kila kitu chetu tunaelekea huko, waamsheni walio lala haraka tunaanza safari usiku huu huu, maana msako wa kutusaka hapa Nuevo umeshika kasi sana..” Akaongea Bon kuwaambia wenzake wawili aliokuwa amepumzika nao kwenye uwa wa nyumba waliyopanga toka wanafika hapa Nueva Laredo.


“Inatakiwa tusiongozane kama kumbikumbi au msafara wa siafu.. Sababu wengine itabidi waondoke na pikipiki na wengine kwa gari na si gari ile ambayo adui wetu tumepata taarifa wanapita kuuliza imeonekena eneo gani kwa wananchi wa hapa Nuevo..” Akaongea Ray akiwa kainuka toka kitini macho yake akiwa akayaelekeza kwenye pikipiki iliyo pembeni kidogo ya uwa karibu na kona ya ukuta unaozunguka eneo la nyumba hii.


“Wazo zuri.. Nafikiri itakuwa vizuri tumpigie simu Maria kumuomba msaada..!”


***** ***** *****


FAMILIA YA FECA MATATANI, PUEBLA-PUEBLA

Tayari alikuwa na maelekezo ya jinsi hali ilivyo anapovizia kuingia, mwanadada Suzy M akiwa kavaa raba nyepesi aina ya sneakers rangi nyeusi, zilimfanya awe katika mnyato unaorandana na karatasi iliyotupwa chini, jeans rangi nyeusi na fulana rangi ya bluu iliyokolea vilimfanya aonekane kama kivuli kama si kutoonekana kabisa machoni kwa watu walio umbali wa mita hamsini na hii ilitokana na giza lililokuwa totoro nyuma ya nyumba anayoinyatia aweze kuingia ndani.


Bastola yake ya aina aipendayo ikipewa jina la DB380 Firearms (Diamondback 380 Firearms) na watengenezaji wake kampuni ya Firearms ya Marekani akiikamata kwa mikono yote miwili, macho yakizunguka kwa kasi lakini iliyo na umakini yakisindikizwa na shingo aliyokuwa akiizungusha huku na huko, mjongeo ulimfikisha mahala ambapo ilimbidi asimame na kujiegemeza kwenye mti wa mchikichi kati ya miti ya michikichi mingi iliyopandwa hapa eneo la nyuma la ukuta uliozunguka nyumba ni eneo lililokuwa lina mwanga mkubwa wa taa uliolifanya eneo hili kuwa na nuru na hivyo kwa mwanadada huyu ilibidi lazima atulie kuchunguza zaidi ni vipi naweza kuendelea mbele kusogea mbele hadi ulipo ukuta wenyewe unaozunguka nyumba ya ghorofa.


Dakika mbili kama si kukaribia tatu kabisa alibaki pale akichunguza kila anachokiona kina utofauti mpaka macho yake yalipoweza kuiona kamera ya cctv ikiwa eneo la juu kabisa ya nyumba hii ya flour (losheni) mbili mita moja tu kuanza mbao zinazoshika bati la nyumba ambalo ni giza ila kwakuwa kamera ni ya rangi ya silva ilionyesha mng’ao wake.


“Jean!, Jean!...” Akaita akiwa kausogeza mkono wake wa kushoto wenye saa karibu na papi (lips) za mdomo wake na mara sikio la kulia kwake ambalo alikuwa kaweka kifaa kidogo cha Bluetooth wireless kinachoendana na saa simu aliyovaa kulitoa kimkoromo kidogo kisha ikasikika sauti.


“Nakupata Suzy… Vipi ushafanikiwa kuiona kamera tuliyoelekezwa?” Akahoji Jean.

“Nimeiona… Vipi na wewe upande wako?”

“Yaah! Safi, nami pia nimeiona na tayari nimeishughulikia kwa kuigeuza uelekeo hivyo niko juu ukutani naangalia ndani ya eneo uwa wa nyumba..”

“Safi sana… Sasa itakubidi ukaigeuze na hii inayochukua eneo hili nilipo lenye mwanga mkali hli nami niingie kupitia ukutani”

“Nipe dakika tano… Tulia papo hapo..!”

“Sawa…!”


Maongezi yao yaliishia hapo kila akashusha mkono wake kawaida hili kazi iendelee, Jean alitambaa juu ya ukuta kama nyoka akielekea upande wa pili na uzuri ukuta ulikuwa mrefu lakini hauna chupa wala nyaya za umeme kama ma ukuta mengi yanayozunguka watu wanaojilinda vizuri zaidi wasiweze kuvamiwa katika majumba yao.


Safari ya kutambaa akiwa katika tahadhari ya hali ya juu asije kuonekana kwa walinzi walio mbele kwenye kibanda cha walinzi kilichojengwa pembezoni mwa geti karibu na bustani nzuri iliyo mbele ya nyumba, bustani yenye maua mazuri, nyasi zilizokatwa vizuri na bembea za watoto aina tofauti tofauti, kifupi lilikuwa ni eneo la watoto kufanya michezo yao.


Alikwenda mpaka karibu kabisa na ilipo kamera ya cctv na kwakuwa ilipo kwenye paa la nyumba na alipo yeye alikuwa kwa upande haikumuwia tabu kunyosha mkono na kuigeuzia upande mwingine kisha akaangalia upande wa nje akiwa kalala palepale juu ya ukuta, akaona kivuli cha mtu anayenyata kikifanya mjongeo kuelekea eneo la chini ya ukuta ambao yeye kajilaza kwa juu.


Jean akatabasamu, alikuwa ni Suzy M, alishuhudia jinsi mtu wa kazi mwenzie anavyotambaa kama nyoka juu kabisa ya ukuta mpaka ilipo cctv kamera na kisha akaigeuza kamera ile hivyo yeye Suzy akaona ni muda wake wa kusogea.


Jean akamtizama kwa kutokea juu alipo kisha wakaelekezana kitu ambacho kwa ishara walizopeana walielewana wanahitaji nini? Aliye juu akatoa kamba ndefu na ngumu ya katani toka kwenye begi dogo alilovaa mgongoni.


Akainyoosha vizuri kisha akaitupia chini ikitokea juu alipo kwenda kwa Suzy M, ambaye naye aliidaka wakaivuta kila mmoja akiivutia kwa upande wake kuhakikisha ubora wake kisha Jean akajigeuza miguu toka pale alipo ikanasa kwenye moja ya nguzo zilizo usawa na nyumba upande huu wa nyumba ya jengo hili la ghorofa, miguu ilipachikwa mahala ikishikana kama kabala kuzunguka bomba.


Alipoona amekaa vizuri akamtolea ishara Suzy aanze kupanda kutumia kamba na hapo Suzy hakuremba, miguu yake yote miwili akaikandamiza ukutani kisha akaanza kupanda kwenda juu akikamata kamba kwa mono wa kulia anaachia anakamata kushoto anaachia na miguu ikifanya kama hivyo ikihama hatua kwa hatua ukutani, akawa anapanda juu akitumia kasi kidogo kuupanda ukuta huu mpaka juu alipofika akapewa mkono na Jean kisha akavutiwa juu ya ukuta, sasa wakawa wote wako juu.


Mwisho wa sehemu ya ishirini na saba (27)


Ten Special Assassin’s gia imebadilishwa hewani kwa mara ya kwanza katika historia ya kikundi chenye watu wachache lakini uwezo walionao ni wa juu sana. Wakifuata maelekezo ya mtu asiyehusika na kundi lao ikiwa wao walishapanga plan yao tena ikiwa ina plan B ikiwa watafeli paln A, lakini plan A iliyoanza kutumika iliachwa na B haikufuatwa kabisa.


Plan ya Carlos Morza imeshika njia na ndiyo inayofuatwa sasa!


Jean Claude Xavo na Suzy M! Wapo katika inayosemekana ni nyumba wanayoishi familia ya bwana mkubwa Fernandes Carlos Codrado.


Nini kitajili katika sehemu zinazofuata?



Jean akatabasamu, alikuwa ni Suzy M, alishuhudia jinsi mtu wa kazi mwenzie anavyotambaa kama nyoka juu kabisa ya ukuta mpaka ilipo cctv kamera na kisha akaigeuza kamera ile hivyo yeye Suzy akaona ni muda wake wa kusogea.


Jean akamtizama kwa kutokea juu alipo kisha wakaelekezana kitu ambacho kwa ishara walizopeana walielewana wanahitaji nini? Aliye juu akatoa kamba ndefu na ngumu ya katani toka kwenye begi dogo alilovaa mgongoni.


Akainyoosha vizuri kisha akaitupia chini ikitokea juu alipo kwenda kwa Suzy M, ambaye naye aliidaka wakaivuta kila mmoja akiivutia kwa upande wake kuhakikisha ubora wake kisha Jean akajigeuza miguu toka pale alipo ikanasa kwenye moja ya nguzo zilizo usawa na nyumba upande huu wa nyumba ya jengo hili la ghorofa, miguu ilipachikwa mahala ikishikana kama kabala kuzunguka bomba.


Alipoona amekaa vizuri akamtolea ishara Suzy aanze kupanda kutumia kamba na hapo Suzy hakuremba, miguu yake yote miwili akaikandamiza ukutani kisha akaanza kupanda kwenda juu akikamata kamba kwa mono wa kulia anaachia anakamata kushoto anaachia na miguu ikifanya kama hivyo ikihama hatua kwa hatua ukutani, akawa anapanda juu akitumia kasi kidogo kuupanda ukuta huu mpaka juu alipofika akapewa mkono na Jean kisha akavutiwa juu ya ukuta, sasa wakawa wote wako juu.


ENDELEA NA MUENDELEZO…!


FAMILIA YA FECA MATATANI, PUEBLA-PUEBLA

Kamba ilivutwa toka chini kuja juu ukutani kisha ikachukuliwa na kurudishwa kwenye begi la Jean Xavo ilipotoka.


“Tutaingia bila wa kuwastua walinzi walio mbele, au unaonaje?” Akauliza Jean baada ya wao wote kwa pamoja kuganda wakilalia tumbo juu ya ukuta kwa dakika moja na sekunde kadhaa.


“Kuna ubaya wa kutokuwashughulikia maana tutahitaji kuondoka… Nafikiri mmoja wetu ashuke chini akawafagie kimya kimya huku mmoja wetu akiingia ndani ya nyumba akipitia hapa kwenye hii baraza..!” Akajibu kimaelezo elekezi Suzy M.

“Sawa! Mimi naona nishuke chini niende kuwafagia hao walinzi na kuangalia kama kuna kikwazo kingine chochote nitakishughulikia inavyo stahili, wewe endelea na safari ya ndani… Fuata maelekezo ya dada yule maana hata kama tulikuwa hatumuamini sana kwa maelekezo yake mpaka sasa hajatupoteza kila kitu kipo ndani ya maelekezo yake..” Jean akatoa pendekezo na kisha akajiinua toka alivyolala akakalia matako pale pale juu alipokuwa, Suzy M akaiga naye akajizungusha na kukalia matako.


Wakaangaliana kisha wakasogezeana midomo yao papi kwa papi (lipa) zikagusana kisha ndimi zao zikatoka wakamatana vichwa wakivutiana kila mmoja kwa mwenzake wakaanza kulana mate huku papi zikisindikiza kwa raha, ni wapenzi hawa na ndiyo maana Bon aliwapanga eneo la upelelezi huu wao wenyewe.


Waliachiana kisha mwanaume akamgonga gonga mabegani mpenzi wake kisha wote wakatabasamu, nukta kumeta Jean akarukia bomba ndefu isiyo pana sana inayotoka chini mpaka karibu na usawa wa baraza ya juu ya flour ya mwisho ya ghorofa hili, alipoipata akaikumbatia kwa miguu na mikono akiikaba kama kabali ya vyote hivyo na kutereza ikimpeleka chini kwa kasi.


Suzy M alimtizama mpenzi wake akatabasamu kwa jinsi alivyomuonyesha mautundu yake na yeye akajibu kwa kuhama toka ukutani mpaka kwenye kingo ya baraza iliyo nyuma ya mjengo akakamata kingo kwa mikono kisha akajivuta kwa kasi ndani ya baraza akiwa amechukua tahadhari kuzuia aina yoyote ya sauti yoyote kutokana na aliyoyafanya.


Jean Claude Xavo! Alivuta kumbukumbu zake vizuri akayaleta maelekezo ya mwanadada aliyekuwa anawaelekeza jinsi nyumba hii ilivyo kwa ndani ya uwa mpaka ndani ya nyumba yenyewe, mwanadada aliyelamba fungu zuri kwa hadhi aliyonayo ya saizi ya kati tena akiutumia mwili wake kupata ridhiki kukutana kwake na Suzy M akiwa na Jean Xavo kwake ilikuwa sawa na nyota ya jaha kumdondokea.


Ramani yote ilikuwa kama anaiona machoni mwake, alinyata akifuata maelekezo mpaka alipotokeza kwenye kona ya jengo la ghorofa kisha akatuliza mwendo wake alipoiona bustani ya michezo ya watoto akakaa sambamba na kona ya ukuta akijitahidi kunyooka kabisa hili asitokeze hata kipande cha nguo lakini sura ilisogea kuruhusu macho yapepese huku na huko kuangalia kulikoni.


Dakika moja ya kufanya usahili wa eneo hili la mbele ya nyumba liliyarusha macho yake ng’ambo ya bustani na kwenda kuyatuhama katika kibanda chumba kilichojengwa vizuri na kupakwa rangi inayofanana na rangi ya jengo la ghorofa, rangi ya khaki inayong’aa inayofanya ukiangalia kwa haraka ujue ni rangi ya njano.


Haraka akiinama akatimua mbio mnyato akilipita eneo la bustani kwa kuruka baadhi ya bembea mzani za watoto, safari iliyompeleka mpaka kwenye ukuta wa jengo na hapa sasa akasikia sauti ya watu wanaofanya jambo! Jean akatabasamu kwani zilikuwa ni sauti alizozijua fika za watu waliokolea katika kufanya mapenzi moja ikibembeleza kusuguliwa vizuri hii ilikuwa sauti nyororo ya kike na ingine ikiwa ile ambayo madume mengine yanapokaribia kileleni na wao uwa yanahanikiza sauti hii ya kuunguruma kuwa anakuja, anakuja!.


Haraka kwa uelewa wa Jean alitambua chumba hiki cha walinzi kina watu wawili tu, sababu haiwezekani kuwe na watu zaidi ya wawili halafu wengine washuhudie wenzao wakipeana starehe, alichungulia lilipo geti mara moja tu kisha akatoka mzima toka kwenye kona mpaka karibu na dirisha hapo akatulia tena na sasa kelele za wanaopeana burudani ziliongezeka masikioni mwake mpaka nay eye akaanza kushikwa na hisia kwa jinsi sauti iliyokuwa ya kike ilivyokuwa ikirembwa kupitia puani hili dume lizizidishe spidi.


Jean Claude Xavo mwanajeshi mdunguaji wa jeshi la Marekani aliyeomba kuacha kazi kwa hiyari kwa kisingizio cha uongo alisogeza kichwa chake kwenye dirisha ambalo alikuwa na chochote, lilikuwa wazi halina pazia wala nondo wala wavu. Laahaulaaah! Moyo wake ulipiga mshindo mkubwa akahisi kama unataka kutoka kwenye mashiko yake, macho hayakuamini yalichokishuhudia.


Ni wanaume kwa wanaume (laanakum), mwanaume alikuwa kakunjwa kwenye stuli ndefu miguu kaichanua na kuikamata ikawa sawa na mabega yake, vitako vyake kamuachia jamaa anamsukuma bila woga kabisa, wazungu hawa wakosa haya walikolea kwenye starehe yao, aliyelazwa kwenye stuli ndefu ndiye aliyekuwa akitoa sauti ya kike ikitokea puani mwake na dume jinga lisilojitambua limekuja duniani kufanya nini? Jasho inamminika kushamiri tobo la mwenzie.


Jean! Kikawaida anachukia sana vitendo licha ya kukulia katika nchi ambayo ushoga na usagaji ni kawaida kwake haikuwa hivyo, alisisimkwa mwili akajikuta anachomoa kisu kikubwa toka katika ala yake iliyo sambamba na mkanda wa kiunoni, dume mende lilikuwa limempa mgongo hivyo yeye bila hata tahadhari ya kuwahofia kuwastua aliruka kupitia mruko wa mvumo wa radi na kutua kwa kishindo nyuma ya jamaa ambaye utamu wake wa kishenzi wenye laana ulikuwa uko kwenye bomba la chini huku tundu la naniii yake likiwa limejitanua kurusha vitu kwenye tobo la mwenzie ambalo halistahili kwa vyovyote vile.


Bisu kubwa toka kwenye mkono mkakamavu lilitua inapoanzia gololi ya kwanza inayoanza katika kukamilisha uti wa mgongo kwa kila binadamu. Bisu lilizama haswa hakupata fursa ya kuendelea kuunguruma kama simba dume kama ilivyokuwa kabla hajashtuliwa na mshindo wa mtu aliyetua nyuma yake kisha yeye kunyamaza ghafla.


Aliishia kutumbua macho, damu zikiruka kumrukia Jean Xavo kwakuwa alichomoa bisu kwa nguvu kubwa, mende akamuangukia mwendawazimu mwenzake kifuani, hapo hasira za Jean bado zilikuwa zimekaa kilele cha juu kabisa alimsogeza kwa nguvu dume marehemu bila kujali madamu yanayoruka kama mpira wa bomba uliopasuka, kidume jike kilichokuwa kinasuguliwa shimo lake la taka ngumu kilitaka kuendelea kupiga kelele kikiwa akiamini kinachoshuhudia.


Jean Claude Xavo! Alimtishia anamkita kwa kisu tumboni kikaruka na kujipigiza ukutani kwa nguvu ya mruko wa uwoga, hasira zilidhidi kwa Jean akamsogelea kasi na kumshindilia bisu la moyo, bisu lililoanza kupenya juu ya kiganja kwakuwa shoga huyu alikinga kifuani kwa viganja vyake vya mikono yake yote miwili ikiwa kavifunika baada ya kuona shambulizi linavyokuja, shubamiit! Bisu lilipenya likitatua kiganja likapenya kifuani na kwenda kuukata moyo katikati, kishenzi hiki nacho hakikuomba maji kilimfuata mshenzi mwenzie jehanamu wakiwa na janaba lenye najsi mbaya kabisa.


“Mbwa wa haramu nyieee, tangulieni kuzimu mimi nitakuja kwa makosa mengine si makosa kama yenu.wanaume hamna aibu kabisa...!”Jean alifoka kwa sauti kubwa tu bila kuogopa kama kuna mtu au watu wanasikia akapiga hatua zilipo nguo za wajahili hawa waliokuwa tayari marehemu akiwonyesha kuwa ana kinyaa hata kuzishika nguo akanyanyua shati la moja na kuanza kujifuta damu zilizomrukia karibu kuanzia uso wote mpaka kifuani.


Upande wa Suzy M alipotua tu baraza iliyo juu flour (losheni) ya pili katika jengo hili lenye flour mbili alipiga hatua moja ndefu iliyomsogeza kwenye dirisha kubwa lililo hapa hapa kwenye hii baraza likiwa limezingwa kwa kioo kilichozungukwa pande zote nne kwa aluminium, dirisha ambalo kwa ndani kulikuwa na pazia kubwa iliyoziba kote huku taa ya mwanga mkali ikiwaka ila mwanga huu haukumfanya Suzy M kuona chochote kilichomo ndani kwa uzito wa pazia iliyowekwa dirishani.


Kushoto kwa dirisha kulikuwa kuna mlango unaotumika kwa mtu mwenye mahitaji ya kuja kukaa baraza hii iliyo nyuma ya jengo na pia ikiweza kumfanya atakayekuja hapa kuona mandhari nzuri iliyopo nyuma ya ukuta uzungukao jengo hili.


Suzy M aliusogelea mlango na cha kwanza kilicho cha kawaida kwa wanajeshi wengi mafundi wabobezi waliopita mafunzoni vizuri kama yeye ni kuchungulia kwenye tundu la funguo, hivyo aliinama lilipo tundu la funguo kitasani akabinya jicho la kushoto huku akiacha la kulia ndiyo lichungulie akakutana na funguo ikiwa imeachwa kwenye tundu la kitasa, bila kuendelea kuchelea kufikiria alitoa kitambaa chake cha jasho (leso) akakikunjua toka kilivyokunjwa mkunjuo mmoja tu kisha akapiga magoti chini akautizama uwazi wa mlango ulio chini kabisa na hapo ukamfanya atabasamu, tabasamu la ushindi.


Kitambaa kilipenyezwa vizuri kwa chini kikiwekwa kwa usawa wa kitasa kilipo kwa mahesabau sahihi na ya upesi, akasimama na mkono wake wa kushoto ukazama tena katika mfuko wa suruali aliyovaa hapo akaibuka na peni ya kubonyeza na hapa hakuibonyeza bali alitoa kizibo cha peni akaifungua ndani kwa kuachanisha ilivyo ikajigawanya kisha akatoa kibomba chembamba cha ndani kinachohifadhi wino wa peni.


Kibomba kikatumbukizwa kwenye tundu la funguo na hapo kililazwa lazwa na kuzungushwa zungushwa kama anachokonoa chokonoa na mara ikawa vile alivyotaka funguo ikajitema toka ndani ya tundu lake na moja kwa moja ikadondokea juu ya leso tena bila kutoa mlio wake wa kawaida pale inapokuwa imedondoka toka juu mpaka chini kwenye simenti au tiles (malumalu) ukiacha kwenye udongo wa kawaida ardhini ambako ni nadra kuisikia funguo ikitoa mlio na mara nyingi watu upoteza funguo zao zinapodondokea kwenye udongo labda ziwe fungu basi zitagongana na kumjulisha mdondoshaji.


Kitambaa (leso) ikavutwa nje ikaja ikiwa na funguo hapo bibie Suzy M hakuzubaa akaizamisha kwenye tundu akazungusha mara moja tu kwa utaratibu kitasa kikajibu kiko tayari kuruhusu mtu kuingia ndani endapo aanyonga kitasa na kuusukuma mlango na ndicho Suzy alichofanya akazama ndani na mara moja kujikuta yuko sehemu ambayo bila shaka hata kama yeye ni mgeni eneo hili aliweza kutambua ni stoo ya kuhifadhia vyakula ghafi na vifaa vya upishi, macho yake yalizunguka kote kisha akitumia matako yake akausukuma mlango urudi mahala pake nao ukatii amri ulivyopelekwa na bibie akausindika kabisa.


Safari ikamtoa pale mpaka kwenye mlango mwingine ambao haukuwa umefungwa ulikuwa umewekwa nusu wazi, akapita pale na kujikuta sasa jikoni kwenyewe nako hakutaka kupoteza muda akakumbuka jinsi Linares alivyokuwa akiwaelekeza akatikisa kichwa kukubaliana naye kuwa aliweza kujua mengi ya humu kwa kuwa mama yake ni mpishi wa boss wa nyumba hii maana kila maelekezo yalikuwa sahihi sana hakuna walipoelekezwa tofauti kama tulivyoona upande wa Jean Xavo na sasa yeye Suzy M.


Alipapita pale eneo la jikoni pua zake zikinasa harufu nzuri ya vyakula vilivyopikwa siku hii ya leo ambayo muda mfupi ujao inaenda kuisha na hatimaye kuianza siku mpya.


Alipotokeza akajikuta anapokelewa na eneo la kulia chakula (dinning room) ambapo macho yalizunguka kote mkononi akiwa imara kaikamatia ‘DB380’ yake akavuta kumbukumbu maelekezo ya kahaba Linares binti wa mama mpishi wa mwenye nyumba hii.


Aliweza kutambua vyumba vya kulala vyote vilivyo flour hii ya pili na ya mwisho kwenye mjengo huu kwa kutumia maelezo hivyo alichofanya alitoa tena kifaa kilicho kama maski ya kukinga pua na mdomo zinazovaliwa sana viwandani na kwa wafagizi wa mabarabarani wenye kujaliwa na mabosi zao kwa afya zao, hiki kilikuwa tofauti kidogo na maski nazosema kwakuwa yenyewe ilikuwa kubwa ya kuziba pua, mdomo na hata nailoni ngumu inayokwenda kwenye ugumu wa vioo vya miwani mara nyingi kifaa hiki uvaliwa maalumu kwa ajili ya kujikinga na silaha za kikemikali kinaitwa kwa kimombo ‘face mask protection’ haraka akajivalisha usoni na kwenda hadi kwenye korido iendayo chumba kikuu (chumba cha mama mwenye nyumba).


Alipofika hakuremba aliinama na kupuliza hewa iliyomo kwenye kichupa kilicho kama vichupa vya pafyumu kwa kurudia mibonyezo mitatu tu kisha akapiga hatua kama kumi zikamfikisha katika mlango wa chumba kingine napo akainama na kupuliza hewa ile ikipitia chini ya mlango kwenda ndani kama haitoshi akasoge mlango mwingine napo akafanya kama alivyofanya vyumba vilivyopita akarudi katikati ya korido akiwa karudisha chupa mfukoni.


Alisubiri dakika tano kisha akaenda mlango wa chumba kikuu akaminya kitasa ukajiachia bila hiyana hakuwa tena anahofia kitu akaingia ndani na moja kwa moja macho akayatupa kitandani, kitanda ambacho ni cha duara kipana klichonakshiwa dhahabu na hapo kiukweli kitanda tu kiliweza kumjulisha aliyelala pale ni mtu tajiri si ‘oyee hayee’, hata kama Feca aliificha familia yake na kuifanya kwa nje ionekane familia ya kawaida lakini kwenye mambo kama haya ya ndani hakuweza kuficha uwezo alionao, kitanda hiki ni kitanda ambacho naye ulala tena mara nyingi akiwa na huyu mke wake mpendwa, chumba nacho kilishindwa ficha ukwasi alionao mwenye kulala chumba hiki thamani haikuficha kile kilicho ndani yake.


Tayari sumu ya hewa iliyopulizwa humu ndani inayosababisha mtu kupoteza fahamu dakika moja tu toka hewa hii iingiapo ndani ya pua hama mdomo wa aliyepuliziwa akiwa hajajikinga kwa kifaa kama hiki alichojikinga nacho Suzy M. Hewa iliweza kumuondoa katika kujielewa kikawaida hata kama yuko usingizini na sasa mwanamama huyu mrembo wa kimexico aliyeishi miaka saba katika jimbo la Columbia,WDC angeweza kufanywa chochote na asijue mpaka pale atakapopewa huduma ya kumrudishia fahamu baada ya masaa mawili (hatari sana).


“JX! JX… JX!..” Akaita kifupi cha jina la Jean hii ndiyo ‘secret name’ wakiwa eneo la kazi za kazi aliita akiwa kainua mkono wake hadi katika eneo ambalo kwa sasa kulikuwa na kava iliyotokeza kwa mbele katika maski aliyovaa lakini sauti ilikuwa inatoka ila katika muungurumo wa tofauti na sauti halisi.


“Nakupata nakupata SM.. Nakupata SM… Lete habari?.!” Akajibu Jean.

“Mafanikio huku tayari… Vipi huko?”

“Huku napo nishafagia uchafu, sikupata tabu sababu niliwakuta majahili wakifanya ufirauni hivyo sikupata upinzani kabisa..” Akajibu na mara akahisi kitu upande wa pili wa anayengea naye.

“Vipi SM.. kunani tena?” Akahoji kwa kupayuka.

“Signal… Signal… Chumba kina signal inabidi tuondoke haraka hapa… Njoo juu haraka tuwatoe hawa watu kabla hawajafika wahusika wa signal hii..” Akajibu Suzy M kwa sauti ya haraka sana kisha akasogea kitandani alipo mwanamama.


Ni hivi kitanda alicholala huyu mwanamke mwenye chumba hiki mke wa Brigedia Fernandes Carlos Codrado kilikuwa kimetegeshwa ‘signal’ (ishara) endapo mtu asiyehusika na familia hii akisimama kando yake kwa dakika moja tu basi kinapeleka taarifa ya mfumo data kwenye saa ya mkononi anayovaa Feca na kisha yeye kutambua ni hatari ipo kwenye chumba chake na mke wake katika hii nyumba yake ya siri ambayo inajulikana kwa watu alionao katika genge lake bodi ya juu tu ambao hawazidi sita huku akiwa kawalisha kiapo cha kutomwambia mtu yoyote kuwa familia yake iko hapa eneo la Heroica Puebla De Zaragoza, eneo maarufu sana kwa watu wenye kutaka kumiliki maeneo ya viwanja vikubwa ambavyo wataweka mahitaji mengi mazuri mazuri katika majumba ya matajiri wenye pesa zao.


Suzy M aliweza kuigundua ‘signal’ kwakuwa naye saa yake aliyovaa ilikuwa ni saa inayompa ishara kuwa kuna kitu cha tofauti eneo la karibu na alipo, kama kuna bomu la kutegwa au vifaa vya kisasa kama hivi basi saa hii aliyoivaa iliweza kumjuza katika ishara tofauti kutokana na kile kilichofichama (hatari).


Hakujali ishara ya taa nyekundu iliyokuwa ikiendelea kumweka kila baada ya sekunde mbili na kuzima kila baada ya sekende mbili katika kioo cha saa bila kutoa mlio wowote wakati kukiwa na bomu saa hii utoa mlio mdogo sana ambao yeye usikia katika kifaa cha mawasiliano alichovaa masikioni na pia uenda mpaka kwa ambaye ameunganika naye katika mfumo wa ‘small group call network’ na ndiyo maana Jean naye saa yake ilimjuza kuna jambo kwa aliyeunganika naye kimawasiliano, Suzy alimnyanyua mwanamama huyu licha ya kuwa yeye na huyu mama uzito wao ni tofauti akajitwisha begani kwa kumlaza kiuno kikiwa begani mwili wa juu nyuma yake yeye Suzy na miguu mbele.


Akaanza kupiga hatua za kutoka kwa ugumu maana uzito ulikuwa si mchezo mama alishiba sana (mwili mkubwa), ikawa bahati alipotokeza tu akakuta Jean Claude Xavo amesimama mlango wa kujia kutokea nje kwenye korido hii ya vyumba vya familia akiwa kajiziba pua kwa kitambaa cha jasho (leso) hivyo Suzy akamtoa begani kiumbe mzito na kumlaza chini karibu na Jean na saa zao ziliacha ku sencor ile hali na hii kila mmoja alitambua chumba kile alichotoka Suzy M kwa huyu mama mwenye mjengo ndipo kulikuwa na ‘signal network’, wakaonyeshana alama ya dole gumba kuwa ‘safi’ kisha yeye Suzy akaenda kuingia chumba cha pili kupuliza hewa yenye madhara.


Mwisho wa sehemu ya ishirini na nane (28)


Suzy M na mpenzi wake ambaye pia ni mshirika wake kikazi ndiyo wamevamia mjengo wa ghorofa mbili ambao kwa mujibu wa maelekezo toka kwenye duru wanazoziamini ni kuwa mwanamama anayeishi hapa ni mke wa Fernandes Carlos Codrado ‘Feca’


‘Ten Special Assassin’ (TSA) nao wako mbioni kuikimbia Nuevo Laredo baada ya muongozo wa maelekezo toka kwa wataalamu wao wa kiintelejensia.


Je nini kitatokea katika muendelezo?



Suzy M aliweza kuigundua ‘signal’ kwakuwa naye saa yake aliyovaa ilikuwa ni saa inayompa ishara kuwa kuna kitu cha tofauti eneo la karibu na alipo, kama kuna bomu la kutegwa au vifaa vya kisasa kama hivi basi saa hii aliyoivaa iliweza kumjuza katika ishara tofauti kutokana na kile kilichofichama (hatari).


Hakujali ishara ya taa nyekundu iliyokuwa ikiendelea kumweka kila baada ya sekunde mbili na kuzima kila baada ya sekende mbili katika kioo cha saa bila kutoa mlio wowote wakati kukiwa na bomu saa hii utoa mlio mdogo sana ambao yeye usikia katika kifaa cha mawasiliano alichovaa masikioni na pia uenda mpaka kwa ambaye ameunganika naye katika mfumo wa ‘small group call network’ na ndiyo maana Jean naye saa yake ilimjuza kuna jambo kwa aliyeunganika naye kimawasiliano, Suzy alimnyanyua mwanamama huyu licha ya kuwa yeye na huyu mama uzito wao ni tofauti akajitwisha begani kwa kumlaza kiuno kikiwa begani mwili wa juu nyuma yake yeye Suzy na miguu mbele.


Akaanza kupiga hatua za kutoka kwa ugumu maana uzito ulikuwa si mchezo mama alishiba sana (mwili mkubwa), ikawa bahati alipotokeza tu akakuta Jean Claude Xavo amesimama mlango wa kujia kutokea nje kwenye korido hii ya vyumba vya familia akiwa kajiziba pua kwa kitambaa cha jasho (leso) hivyo Suzy akamtoa begani kiumbe mzito na kumlaza chini karibu na Jean na saa zao ziliacha ku sencor ile hali na hii kila mmoja alitambua chumba kile alichotoka Suzy M kwa huyu mama mwenye mjengo ndipo kulikuwa na ‘signal network’, wakaonyeshana alama ya dole gumba kuwa ‘safi’ kisha yeye Suzy akaenda kuingia chumba cha pili kupuliza hewa yenye madhara.


ENDELEA NA MUENDELEZO….!


FAMILIA YA FECA MATATANI, PUEBLA-PUEBLA

Akafungua mlango na kuzama ndani napo alipoingia alikutana na kitanda ambacho stahili yake kilifanana na kitanda kilichopo chumba kikuu lakini hiki kilikuwa si kitanda kikubwa sana kama kile na alipoanza kusogea saa yake ikapokea ishara kama ile na hapo Suzy akatabasamu na kufuatia na kutikisa kichwa chake maana alitambua ni vitanda ndivyo vimewekwa ‘signal’, kitanda hiki walilala watoto wawili wa kike wenye umri unaofuatana ukiwaangalia kwa kukadiri mmoja kwa umbo lake na walivyo walatino wa Mexico ungeweza kumkadiria umri wake miaka kumi na moja na huku mwingine miaka yake tisa ama nane.


Aliwainua watoto wote wawili akawaweka begani na kisha kutoka nao mpaka kwenye korido ya kuelekea sebuleni ukitokea kwenye vyumba hivi vya kulala, huko alimkuta mpenziwe na mshirika wake wa karibu wa kazi hayupo na mwili uliozirai wa mama mwenye nyumba haupo yeye akajua nini maana ya hali ile akawaacha chini watoto wadogo wale wa kike, mbio akaingia kwenye chumba cha mwisho akafungua mlango na huko akakuta kitanda kinachofanana na vitanda vya vyumba alivyokwisha ingia na kuchukua watu waliowazima kwa spray yenye inayofanya watu kupoteza fahamu.


Chumba hiki alimkuta kijana wa kiume amelala akiwa hajajifunika shuka, hapa aligundua kuko tofauti na vyumba vingine ambavyo vitanda alipovisogelea tu ‘signal’ ilisoma kwenye simu yake hapa hakukuwa na ‘signal’ (ishara) kama zile, Suzy alisogea kitandani akamzungusha shuka mwilini licha ya mwili wake kuwa amejaa jaa haikuwa kazi ngumu alimnyanyua akampachika begani na kutoka naye koridoni na ndipo akakutana na Jean ndiyo anaingia kutokea nje.


“Nimechagua gari aina ya Range Rover Vogue ndiyo tutaondoka nayo…. “ Akaongea Jean na kisha kutega bega lake akimaanisha Suzy amuwekee begani mwili uliozirai alioubeba.


“… Funguo ya gari umeipata?” Akahoji Suzy M huku akimuweka vizuri kijana aliyemtoa kwenye chumba chake.


“Ndiyoo ..! zingine kama unavyoziona pale kwenye meza yenye kompyuta ya mezani…!”

“Wanajifanya maskini kwa nje… Shenzi magari ya kifahari…”

“Twende tuondoke hapa si eneo rafiki… Nafikiri familia yote imeenea..!”


Walitoka katika hali ya kukimbia huku Jean akiwa na mtu kambeba begani anamuongoza mpenziwe na mshirika wake wa kazi mwanadada wa kizungu Suzy M.


Hawakujighulisha na kurudisha milango ya jengo hili wao waliwaweka mateka wao katika siti za nyuma kisha Jean akafungua geti wakati Suzy akikaa kwenye usukani wa gari hii, jamaa yake aliporudi tu gari liliondolewa kwa kasi kwenda nje ya geti.


Kabla hawajafika mita thelathini gari nyingine ilitokea mbele waendako ikija upande wao wanapotoka kwa mwendo ambao lazima ukiiangalia ukiwa mtu wa michezo hii ya sanaa ya giza utagundua kuna kitu.


“Shenzi..! Signal imeharibu Jean, hao wanaotokea juu tuendako watakuwa wanawai kutudhibiti baada ya signal kuwajulisha kuna sintofahamu hapa..!”

“Geuza gari haraka wako mbali.. Tushukuru tumewai kuwaona toka kwa mbali…”

“Sawaaa…!” Akakubali Suzy kisha gari ikiwa vile vile kwenye kasi alikamata breki ya nyuma ghafla kisha akazungusha usukani gari ikageuka watokako akatia gia na kutimua vumbi la kokoto ndogo ndogo zilizomwagwa kwenye barabara hii.


“Safi… Hatuwezi pambana nao wako wengi… Ongeza mwendo baby..!”


Gari iliyokuwa inakuja mtaa huu na wao kuiona kwa mbali kwakuwa mtaa ulikuwa na barabara ndefu iliyonyooka ikianzia juu mlimani huku kwa huku ilipo jengo wanalotoka wao kulikuwa bondeni, ilikuwa aina ya Nissan Patrol ST-L-Wagon huku kwa Mexico wao uziita Nissan Armarda mfululizo wa gari za kijapan zenye four wheel driver ikiwa na watu waliobanana ndani ya gari wote wanaume wapatao nane.


Walio ndani ya gari walishuhudia gari ikija kasi wanapotokea wao na kisha wakaiona ikifungishwa breki na dreva wake na papo hapo ikapinduliwa ilipotokea, hapo kwa haraka wote walijua ni gari ambayo itakuwa imetoka katika nyumba ya mke wa bosi wao.


Jamaa anayeendesha hakusubiri maelekezo aliongeza mwendo zaidi na kuanza kuifukuza gari ile aina ya Range Rover Vogue.


“Mko wapi Bon?!” Akauliza Jean simu yake ya mkononi ikiwa sambamba na sikio la kulia, kichwa akikilaza kidogo kushoto hili aweze kuiona side mirror vizuri gari inayowafuata kama inaonekana kwa umbali wao kuwa salama kwa mashambulizi yoyote.


“Tunakaribia kufika Puebla ila nafikiri walioondoka na mapikipiki watakuwa ndani ya Puebla muda huu.. Vipi mmefanikiwa?”

“Tumefanikiwa kuipata familia yote kama maelekezo tuliyopewa kuwa wako idadi fulani… Tuko ndani ya gari aina ya Range Rover Vogue tuliichukua uwani kwa wenyeji wetu hili tuwabebee, lakini bahati mbaya ni kuwa tunafukuzwa na watu walio ndani ya gari aina ya Nissan Patrol ST-L-Wagon, tunaomba uwasiliane na waliokwisha fika hapa watupe msaada maana wanaonekana wako wengi ndani ya gari na hatuwezi juwa pengine wanafanya mawasiliano na wengine watutande..” Akaongea Jean gari likiwa linaruka ruka kutokana na barabara waliyoifuata ilikuwa barabara yenye matuta tuta ila dreva bibie Suzy M hakujali hilo


“Mnajua mnaelekea barabara gani au mitaa gani hiyo?” Akauliza Bon.

“Ngoja nimuulize Suzy maana mimi siijui mitaa hii… Suzy eneo gani hili?” Aliongea na watu wawili kwa mara moja akiomba kwa Bon na pia akiuliza kwa Suzy.


“Tuko eneo la Paradise Town… Mtaa huu kama sikosei unaitwa mtaa wa La Puebla.. Mwambie muda si mrefu tunatokea 24 Placita Road hivyo wafanye hima kuja barabara ya Placita kutukava..!” Akajibu Suzy akiwa kasogezewa simu karibu na mdomo wake na yeye akaongea kwa haraka lakini kimpangilio unaoeleweka.


“Umemsikia?”Akahoji akiwa kairudisha simu kwenye sikio lake Jean.

“Ndiyo nimemsikia… Ingieni 24 Placita Road… Ray na wenzake watafika muda si mrefu kuwapa msaada..” Bon akatoa maelekezo kisha simu zikakatwa kwa pande zote mbili.


Suzy alimuangalia kwa kumuibia Jean kisha akarudisha macho yake mbele wakati yeye Jean alikuwa yuko makini kuangalia side-mirror kama wanaowafukuza wanawakaribia.


“Ni kama wanatukaribia Suzy… Aisee maliza zote hizo unaogopa kufa kwa ajali au unaogopa misheni kufeli?” Akahoji kwa sauti yenye msisitizo Jean.

“Natakiwa niingie 24 Placita Road hivyo nataka jamaa wapotee maboya nawafanya waone wanatukaribia kisha nitafanya jambo ambalo watashangaa sana.. Usijifanye hunijui Jean!” Akajibu kwa maelezo marefu Suzy M na kutabasamu.


Gari hakuiongeza mwendo akawa anawasogeza adui kwa kila mita kati ya mita nyingi walizokuwa wamewaacha na kwakuwa barabara hii yenye mchanga wa kichanga changa alikuwa yeye Suzy akiujua fika alikadiria mita alizokuwa akizijua kuwa ndiyo wataikaribia kona ya kuingia 24 Placita barabara ambayo ni ya lami na kubwa kutokea eneo hili.


Aliongeza mwendo spidi zaidi ya ile aliyokuwa akikimbia mwanzo kabla hajawa anaipunguza kijanja, dude ni kama lilitaka kupaa na kama alivyotaraji akitizama kioo cha ndani cha dreva aliweza kuwaona jamaa nao wakiongeza spidi zaidi ya ile na hapa ndipo alipopataka yey Suzy M kwani kwa ghafla alifunga breki kali ya ghafla kisha akaulazimisha usukani kukunja kuielekeza gari kona ya kuingilia bara bara kuu ya 24 Placita lilitibuka vumbi kubwa sana mtaa wa La Puebla na gari lilipokaa sawa akaachia breki na kuruhusu mafuta gari ikapaa tena spidi ile ile, hatari! Lakini salama.


Wakimbiza liliwakuta la kuwakuta kwani dreva licha ya kuwa alikuwa mjuzi wa kukimbiza gari bila uoga kona ya ghafla ilimshinda alipitiliza akakamata akaanza kupangua gia hili akamate breki walijikuta wameeenda mita mia na zaidi kutoka kona ya kuingia 24 Placita.


“Nilikwambia niache nifanye yangu… Shenzi kabisa tumeshawaacha mpaka warudi barabara hii watakuta harufu ya kashata za matairi ya gari yetu! Mimi ndiyo Suzy M sikwenda jeshini kutembea” Akajigamba Suzy na wote wakacheka kwa sauti.


Kweli jamaa walioamriwa na boss wao Feca wawai kuja nyumbani kwake kuna uvamizi wadhibiti hali inayokwenda kutokea na wao walipokuwa wanakuja mtaa wa La Puebla walikuja wakiwa wamechelewa kwani tayari wavamizi ambao ni Suzy M na Jean walikuwa wamemaliza kufanya walichofuata nyumbani kwa mke wa Feca, mpaka wanarudi kwenye kona wao wenyewe walishajua wameachwa wakaingia barabara ya 24 Placita kiushahidi hata kasi dreva hakuwa na hamu nayo tena.


“Jean… Hamajapata msaada?.!”

“Hapana… Ulisema kina Ray watatupa msaada tutakapofika barabara ya 24 Placita, tumeshawakwepa adui zetu.. Wape maelekezo mengine na pia nasi nafikiri ni vizuri tukaondoka kabisa jimbo hili la Puebla na hawa mateka..”

“Safi sana.. Sisi ndiyo tunaingia Puebla.. Mko wapi muda huu?”

“Ndiyo tunapita kituo cha zima moto tunaelekea barabara inayoenda La Puebla Park..!”

“Nimeshapata wazo sisi hatutaingia mjini tena tunafuata barabara kuu ya kwenda jimbo la Hidalgo kwakuwa wewe na Jean si wageni sana Mexico najua mnajua njia za mkato kuja barabara kuu ya kuja Hidalgo State, hivyo fanyeni hivyo”

“Sawa usihofu… Mtatusubiri wapi?”

“Kwakuwa kati yetu sisi mkiacha nyie huko hatuijui sana miji ya majimbo ya Mexico itabidi kuzuia kupotezana na muda ambao tutafika naomba tukutane Pachuca De Soto mji mkuu wa jimbo la Hidalgo na iwe eneo la Pachuca Monument Clock kuna mgahawa nauona kwenye ramani yangu hapa upo pembezoni mwa eneo la mnara huu wa saa..”

“Sawa tunabadili njia na kuhusu watu wetu msiwe na wasi hawatazinduka mpaka tuwasaidie kuzinduka..”


***** ***** *****


PACHUCA DE SOTO, HIDALGO-MEXICO

Pachuca De Soto Manispaa ni mji mkuu wa jimbo la Hidalgo moja ya majimbo yanayounda nchi ya Mexico, manispaa hii iliyopo kusini-kati mwa jimbo hili, jimbo maarufu kwa uchimbwaji wa madini na ni kituo kikuu cha uuzwaji wa madini katika nchi hii ya Mexico.


Clock Monument ya Pachuca ni alama ya mji wa manispaa ya Pachuca ni mnara uliojengwa kwa pande nne katika mtindo ambao wenyewe wenyeji wa hapa wanauita ‘Neo Classic’, ukijengwa kwa mawe yaliyonakshiwa rangi nyeupe ‘cantera’, ukiwa na urefu wa mita 40 kwenda juu, katikati kuna nyuso nne za kuchongwa za sura za wanawake wenyeji wakiziita ‘marble’ na Carrara zikiwa zinaashiria uchumi, mageuzi, uhuru na katiba.


Muda wa saa tisa na nusu usiku kwa saa za Mexico msafara wa mwisho uliokuwa ukisubiriwa kuwasili katika mgahawa wa Cornshmen ulioko mkabala mwa ofisi ya kampuni kubwa na kongwe ya uchimbaji wa madini katika nchi ya Mexico iitwayo ‘BIG BEN’ ambayo majengo ya ofisi yamepakana ubavu na mnara wa Clock Monument, Suzy M na Jean wakiwa na mateka wasiojitambua ndiyo walikuwa wakiingiza gari ndani ya eneo la maegesho ya mgahawa kisha wote wakashuka ndani ya gari waliloliiba nyumbani kwa mke wa Feca, gari aina ya Range Rover Vogue.


“Idadi imetimia… Gari mliyokuja nayo inaweza kuwa dira ya kutukamatisha kwa adui hivyo inatakiwa tuondoke mara moja hapa na kwa haraka tumefikia maamuzi na wenzangu hapa kabla hamjafika kuwa twendeni nao hawa watu nchini mwetu kisha huko ndipo tutafanya makubaliano na Feca… Hivyo tunataka na nyie mawazo yenu kabla hatujaondoka” Akaongea Bon huku akiwatizama wenzake ambao nao wote kama ilivyo yeye usiku huu walikuwa wamekaa kwenye viti vya mgahawa huu unaofanya shughuli zake masaa ishirini na nne licha ya kuwa ni hatari kiusalama kwa kampuni kubwa ya madini kama ‘BIG BEN’. Kilichoangaliwa ni usalama uliokuwa haukosekani eneo hili la kitalii.


“Tunaweza kuondoka kama mtakavyo ila mara moja tunatakiwa tukalitekeleze gari hili eneo la nje kimuelekeo na eneo hili, hili kuwapoteza maboya watu wa Feca maana kama mjuavyo kukikucha kitakachokuwa kinafuatiliwa ni gari aina ya Range Rover Vogue kujua wapi wameelekea familia ya Feca…!” Akajibu Jean kisha akaangalia saa na kuwaambukiza wengine nao kuangalia saa zao hakuna ambaye hakuangalia saa.


“Nafikiri tunaweza kwenda nalo tukitoka hapa mpaka mitaa miwili mitatu kisha tukaliacha na kwakuwa huu ni usiku hatutapata tabu tunaweza liingiza hata kwenye uwa wa nyuma ya mtu mmojawapo wa hapa Pachuca na gari hii ikakutwa kwake na msala utamuangukia yeye…” Suzy M akatoa hoja yake haraka bila kufikiri akiwatizama wenzake alio nao karibu katika maongezi haya.


“Tuanondokea njia gani? Maana kiukweli kama mjuavyo si rahisi sana kuondoka na familia hii ya mtu mwenye genge kubwa sana ndani ya Mexico hivyo tahadhari itahitajika na si masikhara…” Akaongea Rayson kisha akaendelea kuvuta sigara yake pafu kadhaa na kuutoa moshi kwa madaha akiuelekeza hewani.


“Tunachotakiwa ni kubadili vyombo vyetu vya usafiri haraka.. Kisha mengine tutapambana nayo huko mbele kwa kadiri tutakavyokuwa tunakutana nayo..” Bon akatoa lake na uwa akitoa lake kwa heshima aliyonayo kwa wenzake basi ufuatia vitendo tu.


“Nafikiri tukipitia baharini kutapunguza maswali ya wanausalama na kwakuwa sisi ni wamarekani tukiipata boti ya uvuvi itakuwa vizuri zaidi.” Akashusha maoni yake mtu ambaye katika kundi hili yeye ndiyo alikuwa mrefu zaidi ya wengine wote anaitwa Fred Blank (FB).


“Hata mimi nilivyokuwa nikiitizama ramani na kutoka hapa mpaka Marekani kwa usafiri wa barabara tungepata tabu sana, hivyo naunga mkono hoja ya kutumia bahari kuondoka hapa Mexico… Twendeni huko huko nafikiri tukifika tutapata chombo cha kukodisha..” Akaunga mkono Ray na wote katika maongezi haya alikubali.


Walikubaliana na kisha wote kwa pamoja wakitumia maelekezo ya ramani ya mji wa Pachuca inayoelekeza mitaa, barabara na maofisi muhimu ya huduma mbalimbali waliondoka ikiwa imetimia saa kumi kasoro za usiku safari iliyowapeleka hadi eneo ilipo Autolavado Daytona Beach ambako kuna ofisi ya kampuni ya uvuvi ya Baroque Fish Sales and Boat Sailling inayohusika na uvuaji wa samaki na ukodishwaji wa boti kubwa na nzuri kwa ajili ya utalii na jata usafiri.


Hapa walifanikiwa kukodi boti ambayo walikubaliana kiasiambacho kitawafikisha hadi Marekani eneo la pwani ya Cincinnati jimbo la Ohio, kampuni hii kwakuwa iliahidiwa pato kubwa zaidi kwa wamarekani hawa kukodi boti yao haikuwa tabu kukubali licha ya kuona kwa macho yao mama wa makamo na watoto wake wakiingizwa wakiwa wamebebwa wao hawakuwa na la kuhoji (pesa iliongea).


Mwisho wa sehemu ya ishirini na tisa (29)


Mambo yamedhidi kuwa bam bam, hali ni tete kambi ya boss na kingpin Feca wa TRJ.


Familia yake ambayo mara zote alijitahidi kuificha isijulikane kama ameirudisha Mexico sasa iko mikononi mwa watu wa kazi wa ‘Ten Special Assassin’s’ (TSA)


Nini kitatokea sehemu inayofauata tukimalizia malizia mambo yaliyotokea miaka kadhaa yaliyopita?


Subira yako na uvumilivu wako pamoja na muda wako ndiyo vitakufanya wewe msomaji wangu kujua mengi zaidi.



“Nafikiri tukipitia baharini kutapunguza maswali ya wanausalama na kwakuwa sisi ni wamarekani tukiipata boti ya uvuvi itakuwa vizuri zaidi.” Akashusha maoni yake mtu ambaye katika kundi hili yeye ndiyo alikuwa mrefu zaidi ya wengine wote anaitwa Fred Blank (FB).


“Hata mimi nilivyokuwa nikiitizama ramani na kutoka hapa mpaka Marekani kwa usafiri wa barabara tungepata tabu sana, hivyo naunga mkono hoja ya kutumia bahari kuondoka hapa Mexico… Twendeni huko huko nafikiri tukifika tutapata chombo cha kukodisha..” Akaunga mkono Ray na wote katika maongezi haya alikubali.


Walikubaliana na kisha wote kwa pamoja wakitumia maelekezo ya ramani ya mji wa Pachuca inayoelekeza mitaa, barabara na maofisi muhimu ya huduma mbalimbali waliondoka ikiwa imetimia saa kumi kasoro za usiku safari iliyowapeleka hadi eneo ilipo Autolavado Daytona Beach ambako kuna ofisi ya kampuni ya uvuvi ya Baroque Fish Sales and Boat Sailling inayohusika na uvuaji wa samaki na ukodishwaji wa boti kubwa na nzuri kwa ajili ya utalii na jata usafiri.


Hapa walifanikiwa kukodi boti ambayo walikubaliana kiasiambacho kitawafikisha hadi Marekani eneo la pwani ya Cincinnati jimbo la Ohio, kampuni hii kwakuwa iliahidiwa pato kubwa zaidi kwa wamarekani hawa kukodi boti yao haikuwa tabu kukubali licha ya kuona kwa macho yao mama wa makamo na watoto wake wakiingizwa wakiwa wamebebwa wao hawakuwa na la kuhoji (pesa iliongea).


ENDELEA NA DODO ASALI!


CINCINNATI, OHIO-MAREKANI

‘TSA’ kama kifupi cha jina lao la ‘The Special Assassin’s’ walifanikiwa kuondoka ndani ya Mexico bila kikwazo wakitumia passport zao za nchi kubwa ya Marekani zinazowaruhusu kupita katika boda za nchi nyingi katika ukanda huu wa Amerika na hata nchi nyinginezo hapa duniani bila maswali mengi ya kukera tofauti na watu wa mataifa mengine hivyo ilikuwa si rahisi kwao kupata vikwazo kuondoka jimbo la Hidalgo jiji la Pachuca De Soto, waliingia katika jiji la Cincinnati moja ya miji mikubwa inayounda jimbo kubwa la kujitawala la Ohio lililopo kaskazini mashariki ya Marekani likiwa limepakana na majimbo ya Pennisylvania, Michigan, Indiana, Kentucky na West Virginia huku upande wa kaskazini ikiwa ni mpaka wa kimataifa ng’ambo yake likiwa jimbo la Ontario, Canada.


Saa tano ya asubuhi ya siku ya ijumaa mwaka 2001 tarehe 04 mwezi wa 10 siku ya ijumaa, mwezi mmoja na siku kadhaa tokea kwa shambulio la kigaidi la septemba 11 nchini Marekani mashambulizi yaliyolengwa na magaidi wakitumia ndege za abiria katika makao makuu ya jeshi Pentagon, ikulu ya Marekani na kituo kikuu cha biashara ‘World Trade Center’ (WTO) mwaka huohuo wa 2011 wakati ‘TSA’ walipokuwa wamepata nyumba ya kukodi toka katika kikundi kinachohusika na mambo ya uuzwaji wa silaha na biashara zingine zisizo na halali katika jiji la Cincinnati, kikundi hiki kwakuwa kilikuwa ni kikundi mtambuka kwa baadhi ya watu walio katika ‘TSA’ hivyo ilikuwa rahisi kwao wao walipoingia tu ndani ya jiji hili wakawatafuta kwa simu na moja kwa moja wakaingia makubaliano ya kuomba hifadhi katika moja ya nyumba kati ya nyumba tatu wanazozimiliki watu hawa.


Nyumba ilikuwa eneo la nyuma ya hotel maarufu ya Radisson Hotel Cincinnati River iliyopo hatua chache toka uwanja wa mpira wa Paul Brown Stadium mtaa wa 10 Blocks ndipo walipowekwa hifadhi mke wa Feca na watoto wake, jamaa waliamua kuwahifadhi chumba kimoja na ndipo wakawazindua toka katika hali ya kupoteza fahamu na kuwapa taarifa kwanini wanawashikilia na wasiwe na wasi ikiwa mkuu wa familia yao atatekeleza wanachohitaji basi kwao hakutakuwa na pingamizi la kuendelea kuwashikilia.


‘TSA’ wote walishughulika na kuiweka miili yao katika hali ya usafi kisha Bon, Jean, Suzy na Ray wakatoka eneo lile la 10 Blocks wakaelekea eneo la Fountain Square Carew Tower mnara uliopo karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa mji huu wa Cincinnati kwa ajili ya kikao chao cha kupanga wanafanyaje katika kuamua juu ya familia ya Feca.


Kikao kikifanyika katika mgahawa wa hotel ya Best Western Plus Riverfast Restaurant, mgahawa wenye hadhi zake ukiwa unapendwa sana na wakazi wa mji huu wa Cincinnati jimbo la Ohio lenye miji mikubwa na yenye hadhi kubwa sana ukiwemo mji mkuu na makao makuu ya jimbo Columbus.


“Nimepata taarifa ya hali ya taharuki ilivyo sasa huko Mexico… Aisee kumbe Feca anaipenda sana familia yake na huu ni ushindi mkubwa sana mpaka natamani tungemlipa Morza kiasi kikubwa cha pesa kwa wazo lake alilotupa la kuiteka familia hii ya Feca na pia kuwa kwake na uhakika iko wapi..” Alianza mazungumzo Bon baada ya kila mmoja kuwa kashahudumiwa kinywaji alichohitaji kunywa.


“Ni pigo kubwa sana kwake na kwa habari zaidi nilizopewa na watu Los Zetas ni kuwa bwege yule kaelekeza shutuma kwa Fanuel Miguel Mendoza kuwa anahusika na utekwaji wa familia yake..!” Akaongea Ray huku kila mmoja akiwa na furaha kubwa sana, furaha ya kujiona wao ndiyo washindi kabla hata hawajafanyia kazi kile ambacho kilichowafanya waiteke familia ya bwana mkubwa huyu.


“Mh! Ila kwa Fanuel ishakuwa tatizo kwake… Itaamka vita kati yao na mchezo huu tuliwashiriisha katika plan ya kwanza hii ya pili ambayo tulipewa na Morza wao hawaijui kabisa ukiacha sisi wenyewe ni Morza na yule binti Malaya pekee ndiyo wanajua kuwa familia ya Feca tunayo sisi TSA lakini nao watakuwa hawajui kama tumevuka nao boda na kuja nao mbali huku Cincinnati..!” Ray akaongea na kugonga viganja vyao na Jean aliyeketi kiti cha pembeni ya kiti alichokaa yeye.


“Mpaka sasa ushindi tayari upo mikononi mwetu kwa jinsi hali ya taharuki ilivyo Mexico sasa… Mara zote imekuwa ni siri kwa Kingpin wa genge lolote kuvuja habari zake za kutekwa kwa familia yake lakini kwa Feca imekuwa ni tofauti kabisa... Amekuwa akiifanya familia iishi kifichoni lakini kutekwa kwao imekuwa si siri hii inadhihirisha yeye muhusika alivyoshikwa na taharuki kubwa…!” Akaongea Suzy M, kila mmoja aliyekuwa akiongea hapa licha ya kuwa walikuwa wanapata vinywaji hakuna ambaye hakuwa akitabsamu muda wote.


“Sasa nina imani tunakwenda wapata ndugu zetu… Nimemmisi sana mpenzi wangu… Na sijui nitamwambiaje kwa kuacha awe mikononi mwa wajinga wale kwa muda mrefu… Leteni mpango ulivyo naona kuchelewa tu” Akaongea Rayson.


“Mpango wa kwanza nataka mpuuzi huyu na genge lake wasijue kama tuko hapa Cincinnati na ndiyo maana yule nahodha wa boti tuliyokodi kutuleta hapa nilimdanganya sisi ni maafisa wa DEA, nilifanya vile makusudi hili kama ikigundulika kama yeye ndiye alituvusha huku lazima watataka kumuhoji na yeye atasema DEA ndiyo wameiteka familia ya Feca” Alianza kuweka mipango mezani Bon akanyamaza kuweka koo sawa kwa juisi aliyopiga funda mbili kisha akaendelea.

“Sasa katika mpango wetu wa kwanza nataka mchana wa leo watu wanne tuondoke hapa Cincinnati kwenda Springfield, Virginia yalipo makao makuu ya CIA na DEA, tukifika huko ndipo tutapiga simu kwa FECA tukimpa taarifa majasusi wa kikosi cha kupambana na mihadarati DEA tunaishikilia familia yake na hatuna shida naye yeye kama yeye, shida yetu sisi ni kufanya mabadilishano kati ya familia na watu watatu wanaowashikilia tukisema watu wale ni maafisa wa DEA!” Akaanza kuanika mipango Mr. mipango Bon na kiongozi mwanadamizi wa kundi hili la ‘The Special Assassin’s’.


Kila mmoja alinyanyu glasi kana kwamba wameambiana na wote wakanywa vinywaji kati ya vinywaji vilivyo katika glasi zao ingawa mmoja alikuwa akipiga tarumbeta hivyo yeye mdomo wa chupa ya pombe kali ulikuwa kwenye mdomo wake akipata burudani.


“Mpango mzuri… Nia sisi ni kuwapata watu wetu na kama kuna kisasi tutakipanga baadaye maana TSA mara zote hatutaki kukiri kushindwa katika kisasi…!” Akaongea Jean na wote watatu waliokuwa wanamsikiliza wakatikisa vichwa vyao kukubali.


“Springfield tutaenda mimi mwenyewe, Rayson, Mark Becks na Linda Walk… Hapa Cincinnati ambako kwa misheni hii tutapafanya kitovu chetu mtabaki nyie mliofanya kazi kubwa ya kuwapata mateka wetu Jean na Suzy na wale walioenda Guatemala nimeshawataarifu waje hapa wakiwa na ndugu zetu wengineambao sijawataja hapa ni haya kwa sasa” Bon alifafanua tena na sasa kila mmoja alikuwa katika sura makinika akisikiliza kwa umakini.


“Tumekuja kufanya mazungumzo yetu huku makusudi kwakuwa nilikuwa nishapanga itakuwaje bila kuwaambia ndugu zangu hivyo nisubirini hapa mimi naenda kukata tiketi za ndege itakayoondoka masaa muda ujao kuelekea Springfield” Akamalizia hivyo Bon na kisha kuinuka kitini kuelekea aliposema ni eneo la uwanja wa ndege ambapo si mbali na eneo hili la la Fountain Square Carew Tower.


***** ***** *****


SPRINGFIELD TOWN, VIRGINIA-MAREKANI

Mji mdogo kunakopatikana makao makuu ya shirika kuu la kijasusi la kupambana na mihadarati Marekani wakiwa wao ndiyo wanamiliki kikosi kikuu cha kuzuia na kupambana na mihadarati aina yote wakifahamika kwa jina la ‘Drug Enforcement Administration’ (DEA).


The Special Assassin’s kikundi kiboko kwa shughuli za mauaji chenye maskani yake viunga vya jimbo la Colorado muda wa saa kumi na mbili jioni siku ya ijumaa kama walivyopanga katika kikao chao kilichofanyika katika eneo la Fountain Square Carew Tower mgahawa maarufu katika eneo hili lililo karibu na uwanja wa ndege uitwao Best Western Plus Riverfast Restaurant, kikao kilichopokea maamuzi toka kwa kiongozi wao mwandamizi Bon kuwa waje mji wa Springfield kupoteza malengo kwa bwana Feca watakapompigia simu.


Wakiwa eneo la bustani ya Lake Accotink Park katika moja ya mabenchi marefu yaliyotengenezwa kando ya ziwa Accotink eneo zuri hili la wanajamii wa Springfield maeneo ya jirani na hata wageni kuja kufurahia mandhari nzuri ya eneo hili linalovutia.


Kwenye pochi la mwanadada Linda Walk kulikuwa na kifuko kidogo cha nailoni kama vifuko vile ambavyo mara nyingi wanapaki dawa kama vile panadol na nyinginezo, lakini yeye Linda mmoja ya wadada wapya wawili waliongizwa katika kundi la ‘TSA’ kifuko hiki kilikuwa kina laini za simu kadhaa na simu moja ndogo aina ya LG.


Alitoa moja ya laini kati ya laini zile ambazo zimo mule hii ikiwa laini ya kampuni ya mtandao wa simu wa T-Mobile moja ya mtandao mkubwa kati ya makampuni mawili makubwa ya mtandao iliyopo Marekani mpaka nchi kadhaa za jirani ya Marekani zikitumika huko nako, laini aliyoitoa na kuipachika kwenye simu ile ya LG iliyokuwa nayo imo katika kifuko kidogo alichokitoa kwenye pochi lake, wenzake aliokuwa nao eneo lile walikuwa wakimtizama huku pia wakizungusha macho yao huku na huko.


Laini ilipoweza kutulia katika simu na mnara wa T-Mobile kukaa sawa akawaangalia wanaume wale kwa zamu hakuna aliyeongea kitu basi yeye akamkabidhi mkononi bwana mipango Bon akaipokea


Bon alichukua simu yake toka kwenye mfuko wa suruali na kusoma namba alizonazo kwenye ‘phone book’ yake kisha akaamishia kwenye simu aliyopewa na Linda Walk na moja kwa moja kuruhusu kupiga kwenda alipotaka ikasachi kidogo na kuanza kuita upande huo.


“Halloow!’ Upande wa pili ukatoa sauti baada ya kupokea tu, ilikuwa sauti nzito ya kiume.

“…Mmm mmh…Habari yako Brigedia Feca..!!”

“Salama tu… Nani mwenzangu?”

“Unaongea na Agent wa DEA… Napiga simu kutoka Springfield, Virginia Marekani…!”

“Sawa mheshimiwa … Agent wa DEA hauna jina?”

“Kumbe kuna ulazima ukanijua jina… Sikuwa naona kama kuna umuhimu wa kujua jina langu kuliko kujua kwanini nimekupigia simu Brigedia, sawa inaweza kuwa sina budi ukanijua hilo jina kama unaona kwako ni muhimu naitwa Frank Brown… Agent Frank unaweza kuniita hivyo tu haina shida..”

“Hapo sawa mheshimiwa… Ilikuwa lazima nijue naongea na nani maana wewe tayari unajua unaongea na Brigedia Feca, sawa naweza juwa kwanini umenipigia simu?”

“Kwenye kambi yako ya Tajumulco Campamento iliyopo milima ya Tajumulco nchini Guatemala unawashikilia maafisa watatu wa DEA mpaka sasa ni mwaka mmoja na miezi mitatu na mpaka leo tukiangalia rada zetu zilizounganishwa nao watu hao bado wako pale… Tungeweza kufika pale tukiwa na jeshi letu ambalo unatambua kama jeshi letu likishikilia operesheni ndogo kama ya genge lako la mihadarati ni nusu saa tu tunakuwa tushaimaliza kambi yako yote bila kujali chochote ila tumeona tutumie njia nyingine ambayo hata na wewe unatambua njia kama hii ni njia rahisi na nyepesi kwa watu wengine kupata haki zao… Upo bwana mkubwa?” Aliongea kwa kirefu kidogo Bon kisha akampachika swali mpigiwa simu.


“Nakusikiliza Agent Frank… Naomba uende kwenye mzizi wa maana ya simu hii uliyopiga maana nina mambo mengi sana yananiumiza kichwa muda huu”

“Mara zote Feca uwa haujali uzuri sisi tayari tunajua majivuno yako ya pesa zako za haramu unazoingiza… Sikia sikupiga kukupa mwaliko wa sherehe aina yoyote, najua unatafuta mke na watoto wako na unajua waliochukua familia yako mahasimu wako wa kibiashara lakini ukweli kazi kama ile haiwezi kufanywa na hivyo vigenge vyenu hata mmiliki watu wengi wa mji mzima… Mke na wanao tunao DEA na tunakupa siku moja uweze kuwaachia watu wetu kwa mabadilishano nah ii familia yako lasivyo nasi tutawashikilia kama mnavyowashikilia watu wetu”

“Eeeh! Kumbe nyie ndiyo mnawashikilia wanangu na mke wangu… Watu wenu walio Tajumulco kina nani kwa majina?”

“Wadada wawili na mwanaume mmoja… Nafikiri nilivyosema hivi umeshawajua bwana mkubwa..”

“Watu wote wanaoshikiliwa Tajumulco hakuna aliyewai kutuambia yeye afisa wa DEA hivyo mimi siwajui wao wala majina yao ila naweza kumuuliza mkuu wa kambi yangu ya huko Koplo Mariana… Au mnaweza kunitajia majina ya watu hao, kingine naomba msiwadhuru watoto wangu na mke wangu nitafanya mnachotaka mara moja..”

“Sawa mkuu! Mwaka mmoja mliowashikilia watu wetu inatosha na ndiyo maana tukatumia njia hii… Mwambie mtu wako Mariana kuwa watu hao ni Rosa Hellen Marsh, Alicia Glover na mwanaume anaitwa Allen Pearce tunawataka watu hao haraka iwezekanavyo na kwakuwa mmewatesa basi mtalipia kwa gharama ya pesa kiasi ambacho tutawatajia baada ya kupata mrejesho toka kwenu mabadilishano hayo yanafanyikaje?”

“Najua hilo mkuu… Nachotaka familia yangu iwe salama name sitataka kuona mmewatesa watoto wangu na hata mke wangu, mnisamehe kwa kuwashikilia watu wenu kwa muda mrefu”

“Wee andaa pesa yetu na watu wetu tunataka kiasi cha dola elfu kumi inatosha kwa wote watatu na najua ni kiasi kidogo sana kwako kwa kosa ulilofanya kuwashikilia wamarekani nje ya sheria”

“Lakini mambo haya yapo Bon.. Namba mnayopatikana ni hii?”

“Ndiyo namba ni hii muda wote piga utanipata mimi ama patna wangu naofanya nao hii kazi”

Bon hakuona tena kuna haja ya kuendelea kuongea naye akakata simu tabasamu likiwa usoni mwake.


“Siku zote ‘Kingpin’ dawa yao kuwachukulia familia zao tu.. Tulikuwa tunajizungusha kutaka kuanzisha nao vita wajinga hawa kumbe akili inatosha kuwafanya wakafanya kila kitu ambacho tunaamua sisi… Tumeshika tako lake hawezi ruka tena amekubali kufanya tunavyotaka, kumbe kambi yake ya Tajumulco inaongozwa na Koplo Mariana, jamaa anayeitwa Ivan alto na Sajenti Lara yule aliyefungwa miongoni mwa wafungwa waliofungwa naye kwa tuhuma za madawa ya kulevya ndani ya kambi za jeshi la Mexico” Akatoa maelezo kwa wenzake kisha wakainuka toka pale kwenye benchi na kuanza safari kutembea pembezoni mwa ziwa huku wakiongea mpango endelevu.


“Tunataka ionekane misheni ya DEA hivyo nafikiri tungepata sura za bandia za maafisa wa DEA angalau watano wakati tutakapoenda mahala tutakapoelekeza mabadilishano yatafanyika hapo, mnaonaje hili?” Akapendekeza wazo mwanadada Linda Walk.


“Wazo zuri lakini tutahitajika tupate mtaalamu wa kutengeneza hizo sura hapa Springfield tena afanye kwa haraka”Boniface W Montreal ‘Bon’ akaongea na hapa kila mmoja alikuwa akichanganua jambo hili katika mamlaka ya ubongo wake kwa umakini na mantiki kubwa.


“Bon jambo hili muhimu sana mi nawajua wafanya kazi hizo katika jimbo hili kwakuwa nimezaliwa na kukulia jimbo hili kama mjuavyo, yupo mtaalamu mmoja aliacha jeshi kama sisi ila yeye alikuwa daktari wa jeshi na sasa amejiajiri kwa kazi za plastic surgery, amefungua clinic yake inayoitwa Saga Clinic huyu jamaa anaitwa Dokta Straiford Saga anapatikana Annandale District” Akaongea Mark Becks.


Walikubaliana kuwa waondoke hapa Springfield kuelekea wilaya ya Annandale anapopatikana Dokta Straiford Saga na clinic yake ya Saga Clinic kwa kazi ya kutengenezewa sura za bandia za maafisa wa DEA watakao wachagua wao wenyewe.


Mwisho wa sehemu ya thelathini (30)


Mambo ni bam bam utafikiri TSA wamechanganya damu ya ushindi bam bam wenye mashamu mashamu maana mpango wao ulienda watakavyo, wakiwa wamewamisi sana rafiki zao na ndugu zao sasa kuna kila dalili wanakwenda kuwapata.


Je hakuna aliyeumizwa au kujeruhiwa ndani ya mwaka mzima licha ya mateso makali waliyokuwa wakipewa ndani ya Tajumulco toka kwa vijana wa TRJ.


Yote haya tutayajua katika sehemu inayofuata




“Siku zote ‘Kingpin’ dawa yao kuwachukulia familia zao tu.. Tulikuwa tunajizungusha kutaka kuanzisha nao vita wajinga hawa kumbe akili inatosha kuwafanya wakafanya kila kitu ambacho tunaamua sisi… Tumeshika tako lake hawezi ruka tena amekubali kufanya tunavyotaka, kumbe kambi yake ya Tajumulco inaongozwa na Koplo Savatel yule aliyefungwa miongoni mwa wafungwa waliofungwa naye kwa tuhuma za madawa ya kulevya ndani ya kambi za jeshi la Mexico” Akatoa maelezo kwa wenzake kisha wakainuka toka pale kwenye benchi na kuanza safari kutembea pembezoni mwa ziwa huku wakiongea mpango endelevu.


“Tunataka ionekane misheni ya DEA hivyo nafikiri tungepata sura za bandia za maafisa wa DEA angalau watano wakati tutakapoenda mahala tutakapoelekeza mabadilishano yatafanyika hapo, mnaonaje hili?” Akapendekeza wazo mwanadada Linda Walk.


“Wazo zuri lakini tutahitajika tupate mtaalamu wa kutengeneza hizo sura hapa Springfield tena afanye kwa haraka”Boniface W Montreal ‘Bon’ akaongea na hapa kila mmoja alikuwa akichanganua jambo hili katika mamlaka ya ubongo wake kwa umakini na mantiki kubwa.


“Bon jambo hili muhimu sana mi nawajua wafanya kazi hizo katika jimbo hili kwakuwa nimezaliwa na kukulia jimbo hili kama mjuavyo, yupo mtaalamu mmoja aliacha jeshi kama sisi ila yeye alikuwa daktari wa jeshi na sasa amejiajiri kwa kazi za plastic surgery, amefungua clinic yake inayoitwa Saga Clinic huyu jamaa anaitwa Dokta Straiford Saga anapatikana Annandale District” Akaongea Mark Becks.


Walikubaliana kuwa waondoke hapa Springfield kuelekea wilaya ya Annandale anapopatikana Dokta Straiford Saga na clinic yake ya Saga Clinic kwa kazi ya kutengenezewa sura za bandia za maafisa wa DEA watakao wachagua wao wenyewe.


ENDELEA NA DODO ASALI..!


SPRINGFIELD TOWN, VIRGINIA-MAREKANI

Mipango ilikwenda kama vile walivyotaraji, Clinic ya Saga iliwapa huduma ya haraka zaidi kama wao walivyohitaji wakifanikiwa kutengeneza sura za bandia za kufanana majasusi wa shirika la kupambana na mihadarati, huduma ambayo ilifanyiwa kazi kwa masaa thelathini na sita na baada ya kukabidhiwa walirudi hotel waliyofikia katika mji wa Springfield.


Chumba namba 20 katika hotel ya Comfort Inn mtaa wa 6560 Loisdale mtaa wenye hotel kama tatu za nyota tano hapa Springfield ndipo kulikuwa na kikao kidogo cha watu wanne wa ‘TSA’ waliofika katika mji huu kwa kazi ya kumghilibu bosi wa genge la mihadarati la ‘TRJ’ kuwa wao ni majasusi wa Drug Enforcement Administration ‘DEA’.


“Kazi leo ni kumpigia Feca kama tulivyomuahidi jana kuwa tutampigia leo simu kwa ajili ya kumuelekeza aje wapi kuifuata familia yake akiwa na watu wetu” Akaanza Boniface W Montreal akiwa kasimama karibu na dirisha baada ya wao wote kutizama kazi nzuri iliyofanywa na watu wanaopatikana Saga Clinic, Clinic inayojihusha kutengeneza sura za bandia, kurekebisha sura kama mtu atahitaji kufanya hivyo na hata akitaka operesheni ya kujibadili sura basi hawa watu ufanya operesheni hizi.


“Bon! Habari zilizopo ni kwamba hatuwezi kumuita Feca akaingia Marekani kumbe ni miongoni mwa windo hatarishi ambalo DEA na CIA wanaliwinda kwa udi na uvumba wakimuwinda kimya kimya ndani ya Mexico na hata hapa Marekani wanawatafuta sana watu walio kwenye mtandao wao, hivyo angalizo letu tutakapoongea naye tusimpe sharti la yeye mwenyewe kufika eneo tutakalomwambia ndiyo tutafanya mabadilishano..!” Haraka akaongea Mark Becks kitu ambacho alikuwa sahihi kabisa.


Wote walikubaliana naye na wakapitisha maamuzi kuwa watamuomba familia yake atume watu wake wakaichukulie Canada ila kwa makabidhiano ya nipe nikupe zikitumika simu.


“Natoka na Linda hili tukampigie simu Feca tukiwa nje ya hapa maana anahaha sana kujua ukweli akitumia watu mbalimbali alio na ushirikiano nao, pia nitawapa taarifa kina Jean waanze safari na mateka wetu kuelekea Ontario tutawaachia huko familia ya Feca…” Akaongea Bon kisha akamuangalia Rayson aliyeonyesha na jambo.


“Canada itabidi twende na sisi pia Bon… Hatuwezi juwa itakuwaje huko wakienda kina Jean peke yao sisi tukibaki hapa tukifanya mawasiliano na Feca iala hapa anaweza akabaki mtu mmoja kati yetu halafu yeye ndiyo atakuwa anafanya mawasiliano na Feca kisha anafanya na sisi mpaka makabidhishiano yatakapokuwa tayari hapo atakayebaki ataua mawasiliano yote kwa kuivunja simu na laini pia..” Alishusha mpango Rayson, kundi hili karibu kila mtu alikuwa ni mtu makini sana kwa kila jambo na wenye vichwa vyepesi vya kung’amua tatizo na kuweka sawa mara moja.


“Huko sahihi… Hapa atabaki Mark Becks.. Sisi sote tutaenda Canada jimbo la Ontario tutaondoka hapa kwa ndege leo jioni wakati kina Jean wanatakiwa waondoke kwa magari mawili toka huko Cincinnati muda mfupi ujao… Tutakutana huko wote kwa pamoja na kwa sababu hii naomba kwa sasa tusimtaarifu chochote Feca na anajua tumemwambia asithubutu kupiga simu bila sisi kumpigia kwanza” Akaweka sawa mambo Bon.


“Halloo!”

“Bon!”

“Sikia Jean… Naomba muwapige sindano za usingizi hao watu kisha mara moja mtumie gari zetu ambazo zimeletwa leo kutoka Colorado, muondoke kuelekea jimbo la Ontario Canada na taka boda mkapite usiku mkubwa hili muweze kupita nao bila bughudha watu hao mnaweza sema wamepumzika usingizi hivyo au mwaweza tumia njia zingine mtakazoona kwenu ni sahihi”

“Sawa sawa.. Na sasa hivi hapa tumemaliza kuzicheki gari hizi hivyo tunaondoka mara moja hapa”

“Vizuri… Tutapanga mkishafika wapi tukutane”

Alikuwa ni Bon akiongea na kiongozi mwenzake mwandamizi wa kundi Bwana Jean, ratiba zingine walizikatizia na kuendelea na ratiba hii iliyopangwa muda huu.


***** ***** *****


MABADILISHANO MATEKA, ONTARIO-CANADA

Jimbo la Ontario nchini Canada, jimbo wa upande wa ghuba inayoitwa Hudson ni jimbo la pili kwa ukubwa likiwa nyuma ya jimbo la Quebec. Mji mkuu wa jimbo hili ni Toronto ambao pia ni mji mkuu na makao makuu ya shughuli za kiserikali ya Canada.


Keele street! Mtaa unaounganishwa na barabara za kukutana za north-south road eneo la Vaughan pembezoni mwa shule ya Howlett Academy Private kulikuwa na nyumba za makazi ya watu za ghorofa zilizojipanga mstari na kulifanya eneo hili kuwa eneo linalopendeza kama maeneo mengi yaliyo ndani ya jiji la Toronto, jiji zuri kubwa lenye kupendeza.


Ghorofa la pili katika mpango upande wa kushoto wa shule kulikuwa na mpangaji kijana wa kimarekani lakini akiwa ameweka shughuli zake katika jiji hili, akiwa ni wale vijana ambao licha ya umri kusogea ndoa kwake haikuwa na umuhimu aliendelea na tabia zake za kubadili wanawake kuwatumia kisha kuwatema kila siku.


Kijana huyu ndugu yake na bwana mipango Boniface W Montreal kiongozi mwandamizi wa kundi la ‘TSA’ alipewa taarifa na ndugu yake Bon kuwa kuna ugeni unafika katika jiji hili na ombi ni kuwa wanaomba awapokee wageni hao na kuwapa hifadhi ya muda kwa shughuli ya muda mfupi itakayofanywa nao.


Alex W Montreal mara zote upendo kwa ndugu yake wa damu kaka yake toka nitoke ulisabababisha mara zote kumuweka kipaumbele ndugu yake na mara moja akakubali kuwapokea watu aliolekezwa na kuwafikishia kwenye apartment ya flour nzima aliyopanga kwenye ghorofa hizi za shirika la nyumba la kiserikali ya jimbo la Ontario.


Haikuishia hapo ilipofika saa kumi jioni ndipo Bon na wenzake wawili waliokuwa jimbo la Virginia mji wa Springfield waliwasili eneo la Vaughan na kufanya kikosi kazi chote cha TSA kinachoriki operesheni ‘Bring back’ kutimia.


Ilipotimia saa kumi na moja na nusu Bon akachukua simu wanayotumia kuwasiliana na Brigedia Feca na kumpigia


“Halloo Feca!”

“Halloo mkuu habari yako?” Brigedia Feca aliongea baada ya kupokea simu ikishangaza jinsi shetani Feca aliyegeuka malaika kwa muda huu tena bila kutarajia aliongea sauti ya kinyonge sana kujibu.


“Tunapenda kukutaarifu familia yako tumeileta Canada kwenye moja ya ofisi ndogo za siri za CIA hivyo una masaa kumi na mbili ya wewe kuhakikisha Rosa Hellen M arsh, Alicia Glover na Allen Pearce wakiletwa hapa Toronto kwa mabadilishano na familia yako…. Tumekuja Canada kwa sababu operesheni ya kuwapata hao ndugu zetu inaendeshwa na sisi wafanyakazi wenyewe bila viongozi wetu wa juu kuhusika hivyo tumeona endapo tungebaki Marekani basi ingekuwia vigumu kumaliza suala hili bila viongozi wa DEA kujua.


“Nilikuwa nawatafuta toka asubuhi… Kuna taarifa za kuokotwa maiti ya mwanamke mwenye asili ya Mexico huko Marekani nimepatwa na wasiwasi sana”

“Kwahiyo DEA tunaweza kufanya uhuni kuua mtu asiye na kosa?”

“Naipenda sana familia yangu ndiyo maana nimekuwa nikitumia njia nyingi kuweka salama… Niambie muda gani mtakuwa tayari kwa mabadilishano? Watu wenu ninao hapa nyumbani kwangu nitatumia helkopta yangu kuwaleta Canada tena haraka sana bila kuchelewa muda mtakaokuwa mpo tayari”

“Saa tatu usiku Markham Town eneo la Richmond Hill pembezoni ya mto Rouge mwisho wa East Beaver Creek Road kuna bonde kubwa likifuata maporomoko ya maji yanayodondoka si lazima ufike mwenyewe kwakuwa serikali ya Canada nayo inakusaka kama serikali ya Marekani inavyokusaka… Sisi hatuna shida na wewe ila tunaamini huwezi ku risk ukaja wewe mwenyewe” Akaongea Bon akaacha kuendelea kuongea hili asikie upande wa Feca kuna lipi.


“Sawa nitatuma vijana wangu watatu tu hili mjihakikishie sihitaji mapambano nanyi.. Watatumia helkopta ambayo itakuwa na jumla ya watu sita yaani watu wenu na wao watatu, wakiwa na mzigo wenu wa dola elfu kumi mlizotaka..”

“Vizuri sana Feca na ahsante sana kwa ushirikiano wako.. Nitakupigia saa mbili na nusu kuuliza kama helkopta ishaondoka hapo kwako!”

“Ahsante nawe pia… Naamini huu ndiyo mwanzo wa kujuana kati yetu naamini bila kujali tofauti zetu kati ya sisi cartel wa mihadarati na nyie DEA ila sidhani kama tunaweza tusifanye mambo mazuri kwa faida ya maisha yetu… Shukrani kwenu kwa uamuzi wa busara mliotumia kuwapata watu wenu..”

“Shukrani hizo tutapeana baada sisi kuwapata watu wetu na wewe kuipata familia yako tuna masaa mengi kati yetu kufika muda tuliopanga hivyo tusiusemee muda acha muda uongee… Kwaheri Brigedia Feca!”


Bon alikata simu na kuwageukia wenzake waliokuwa wakifuatilia maongezi yale kwakuwa kila mmoja aliunganishwa kwa njia ya Bluetooth earpnones ndogo walizozipachika kwenye masikio yao.


“Nadhani nyote mmesikia mipango ilivyokwenda sawa kwa maneno tukisubiri vitendo ambavyo vitaamua operesheni yetu imeenda sawa kwa namna gani” Akaongea Bon.


“Ni kweli nikusubiri vitendo tu, uzuri pia tushafanya opesheni moja kule Richmond Hill hivyo kila mmoja kati yetu ukiacha kina Linda tunalijua eneo lile” Akaongea Suzy M akiwa kaka sofa moja na mpenzi wake Jean.


“Hakiharibiki kitu ikifika saa mbili usiku tutachukua watu wetu kwenda nao, kuna bar ipo Yonge Street pale wengine mtaweka kambi kama mmefuata burudani zenu za vinywaji wakati huohuo mimi na kina Linda tutaenda kukagua eneo kila kona” Rayson akaongea kila mmoja akakubali.


Waliendelea kupanga kila walichoona kinastahili kupangwa kwa ajili ya usalama wa operesheni yao ya kubadilishana mateka mpaka saa moja na nusu wakajianda na wote bila kubaki mtu wakaondoka kwa magari kuelekea Markham Town inakopatikana milima ya Richmond, milima iliyo na chanzo cha mto Rouge wenye kuanzia hapo na kuingiza maji yake ziwa Ontario.


***** ***** *****


RICHMOND HILL, MARKHAM, ONTARIO-CANADA

Linda Walk, Jean, Rayson na Mark Becks walikuwa kila mmoja kajificha katika kichaka vilivyo sehemu mbali katika eneo Richmond Hill karibu na mapromoko ya maji ya mto Rouge akiwa na bunduki aina ya Alejandro Sniper Rifle bunduki maalumu kwa wadunguaji wanaopenda kutumia bunduki nyepesi zisizo na uzito pia ambazo akitaka kuifunga na kuifungua aina mambo mengi ya kumfanya apoteze muda mrefu ni bunduki toka kiwanda cha silaha cha Union De Industrias Militares cha nchini Cuba kilicho chini ya serikali ya nchi hiyo.


Karibu na maporomoko ya Richmond Hill Falls ya mto Rouge kulikuwa na mti mkubwa ambao hata watalii wengi wajao eneo hili ufika hapa kama eneo zuri la kuyaona maporomoko kwa uzuri wakichukua na picha za kumbukumbu, kwa muda huu kulikuwa na watu saba.


Kwa mara ya kwanza mke wa Feca aitwaye Millian Zabarelo na watoto wake watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume ambaye yeye umri wake alikuwa mkubwa zaidi wa wadogo zake wa kike, wote leo ndiyo ilikuwa ni kama wameiona dunia upya walitolewa vitambaa vyesusi machoni mwao ikiwa toka waingie mikononi mwa watu hawa wa ‘TSA’ hawakuwai kuondolewa vitambaa hivi mara walipopata fahamu walijikuta wako hivi na hata chakula walikula wakiwa wamefunguliwa mikono kwa sharti la kutogusa kitambaa kilicho machoni.


Mbele yao walisimama wanaume ambao wao kwa haraka waliwaona wa kizungu wawili na mmoja mwenye asili ya watu weusi ila huyu pekee yake alikuwa kava kofia aina ya kapero akiigandamiza sana kichwani kufanya asionekane vizuri usoni na wote walipiga miwani ya kijasusi wakiwa wamevaa sutiza rangi nyeusi wakiwa na vitambulisho vinavyoning’inia kwa kamba zilizo shingoni mwao, vitambulisho vikiwatambulisha wao ni maafisa wa shirika la kupambana na madawa ya kulevya la Marekani ‘Drug Enforcement Administration’ (DEA) huku sura zao zikiwa si sura halisi kwa watu wenye kuwajua, sura hizi zilikuwa sura bandia, sura zifananazo na maafisa wa DEA waliowachagua wao na kisha kutengeneza hadi vitambulisho vyenye picha za kufanana na sura walizovaa na hata majina.


Kwa haraka mwanamama Millian alisoma majina yaonekanayo kwenye vitambulisho vya watu vikiwatambulisha majina na vyeo vyao, mwanamama akakalili majina yale kwa ufasaha zaidi kwa minajili yake yeye aliyoona ni sahihi yeye kufanya vile.


Kati ya wanaume hawa waliovaa sura bandia hakuna aliyetoa sauti kuwaongelesha yeye Bi. Millian Zabarelo na watoto wake zaidi ya kuwaonyesha kwa ishara kila kitu na wao wakitii kufuata maana hata eneo walipo hakuna aliyekuwa analijua eneo hilo walipo na wanaume hawa walio kimya wakiwatizama kwa umakini mkubwa kama wanawalinda magaidi au wahalifu wenye ngazi ya juu kabisa.


Saa tatu na dakika tatu kwa mbali walio eneo hili walianza kusikia muungurumo wa helkopta inayokuja eneo hili kwa mbali na mara wakaiona ikitokea kwa mbali ulipoishia upeo wa macho yao kuona kwa juu ya milima na misitu hii ya Richmond.


Helkopta ilisogea ilipofika kwa juu ya walipo wakaiona ikizunguka kutafuta muelekeo wa kutua dakika mbili mbele ilipata muelekeo ikatua mita hamsini toka eneo lile walipo watu waliowaona toka wao wakiwa juu wakifuata maelekezo ya bosi wao ambaye naye alikuwa anapata maelekezo toka kwa mtu aliyekuwa na simu ambayo mara nyingi alikuwa akiitumia Bon ambaye alikuwa hapa kwa ajili ya makabidhiano.


Bon na wenzake wote walioko eneo hili la Richmond Hill walikuwa wakisikia mawasiliano yanayofanyika kati ya Daniel Dawson ‘Double D’ aliyeko chumba namba 20 katika hotel ya Comfort Inn mtaa wa 6560 Loisdale akiongea kwa niaba ya ‘THE SPECIAL ASSASSIN’S’ (TSA) na Brigedia Feca aliyeko kwenye kasri lake liitwalo ‘Secreto Potentio La Feca Palacio’ lililoko eneo la Soledad De Maciel nje kidogo ya manispaa ya Petatlan jimbo la Guerrero nchini Mexico.


Helikopta ilipotua hakuna aliyeshuka kwanza utulivu wa eneo hili ulivurugwa na upanga uliokuwa ukiendelea kuzunguka kumalizia malizia mizunguko yake.


Dakika tatu mbele maelekezo yalipita kwenye mawasiliano ambayo kwanza yalifanyika makubaliano baina ya Double D na Feca ambayo Bon na ‘TSA’ wengine waliyasikia ndipo mlango wa helkopta ukafunguka akashuka mtu mmoja na kupunga mkono juu halafu akatoka kabisa karibu na mlango mkono wake mmoja ukizuia kofia ya pama aliyovaa kuzuia upepo wa upanga wa helkopta usiidondoshe.


Bon akamuinua kwa mkono mwanamama Millian toka mahala alipokalia jiwe na kisha akasogea mbele hatua tano wakiwa wameongozana akiwa kamtanguliza mbele kisha naye akatoa ishara ambayo aliyeshuka kwenye helkopta akaielewa akageuza shingo mlango wa helkopta, papo hapo akashuka mwanamke wa kizungu aliyevaa suruali ya jeans ambayo licha ya kigiza giza eneo ilionekana ilivyochakaa, juu alikuwa na kikoti cha jeans nacho kikiwa kimechakaa sana, mwanadada huyu wa kizungu akasogezwa mbele.


“Sniper one..!” Akapaza sauti Bon aliye ndani ya sura ya bandia.

“Baghdad, Irak kwa mara moja..!” Akajibu mwanadada aliyeshushwa kwenye helkopta tena bila kufikiri lakini sauti iliyoonyesha kabisa hakuwa sawa kiafya maana ilkikwaruza licha ya kujitahidi kuipaza tena akiwa na furaha isiyoamini alichosikia.


“Huyo sawa bwana mkubwa! Muachieni aje mwenyewe wapishane na mtu wenu..!” Akaongea kwa sauti Bon kumwambia yule aliyeshuka.


“Haya mama nenda kwa mtu wenu… Mumeo ametuma watu wakufuate kuwarudisha Mexico… Nafikiri hujaumizwa sana na tukio hili kwakuwa unafahamu shughuli za mumeo na kama uonavyo hapa ni mtu kwa mtu jino kwa jino..!” Bon akamwambia mwanamama mke wa Feca ambapo mwanamama huyu alikuwa akiwaangalia wanae na kufanya awe anasita sita kuondoka kuelekea ilipo helkopta.


“Wanangu nao vipi? Nawaacha?” Akahoji Bi. Millian macho yake yakisoma kitambulisho alichovaa shingoni na kuning’inia mpaka kifuani Bon ambaye wala hakujali akamtizama tu.


“Siwezi kuwaacha wanangu… Nafikiri haya si maagizo ya Fernandez mume wangu!” Akaongea tena Bi. Millian.


“Mama nenda.. Wanao wanakuja nao kwenye helkopta ila mpaka wewe ufike kwanza tafadhali acha jeuri tumalize mambo haya kabla wenye mamlaka na nchi hii hawajafika hapa..!”


“Madam njoo tu… Kuna utaratibu wa haraka tunatakiwa tuumalize haraka sana hapa kisha tuondoke kuelekea Mexico!” Akaongea kwa sauti huku akisogea mbele mwanaume aliyeshuka kwenye helkopta huku mwanamke ambaye naye alishuka kwenye helkopta alishakuwa anakaribia walipo kina Bon, Bi. Millian kuona vile naye akaanza kupiga hatua wakapishana.


Bon na mwanadada wakakumbatiana na kupeana mabusu ya kila mmoja akimbusu mwenzie kwenye mashavu wakaachiana kisha mwanadada akahama na kwenda kumkumbatia Mclean Welch mmoja wa wanaume waandamizi wa ‘TSA’ walibusiana pia wakaachiana na mwanadada kumalizia kwa kukumbatiana na Fred Blank (FB) huyu si mwandamizi ni mgeni kwenye waliongezwa kuziba mapengo ya hawa waliowafuata hapa ambao walikuwa mikononi mwa genge la ‘TRJ’.


Mwanamama Miliian alipoingia tu kwenye helkopta, Bon akawanyanyua watoto wawili wadogo kisha akaonyesha ishara kama ya mwanzo hapo bwana mkubwa anayeongoza wenzake akageuka mlangoni na papo hapo akashuka mwanadada mwingine naye akiwa kavaa suruali ya jeans ila huyu ni jeans nyeusi na fulana tu aina ya lacrosse ya mistari ya kama pundamilia.


Hapa kulikuwa hakuna kusimama simama wala nini mpishano ukafanyika haraka na furaha upande wa kina Bon ikaongezeka licha ya sura za bandia walizovaa ndugu zao hawa waliweza kuwatambua wenzao waliokuja kumalizia mpango wa mabadilishano, waliwajua kwa kutumia maneno ya mafumbo.


Mabadilishano yalikamilika na kila kundi likaondoka na watu wake ikiwa pamoja na kina Bon kukabidhiwa bahasha yenye pesa dola elfu kumi taslimu.


Mwisho wa sehemu ya thelathini na moja (31)


Hatimaye ‘TSA’ wamewakomboa watu wao watatu waliokuwa wakishikiliwa kwa mwaka mmoja na nusu na kundi la ‘TRJ’.


Nini kilifuata baada ya makabidhiano haya?


ILIPOISHIA SEHEMU YA 31…!!

“Siwezi kuwaacha wanangu… Nafikiri haya si maagizo ya Fernandez mume wangu!” Akaongea tena Bi. Millian.


“Mama nenda.. Wanao wanakuja nao kwenye helkopta ila mpaka wewe ufike kwanza tafadhali acha jeuri tumalize mambo haya kabla wenye mamlaka na nchi hii hawajafika hapa..!”


“Madam njoo tu… Kuna utaratibu wa haraka tunatakiwa tuumalize haraka sana hapa kisha tuondoke kuelekea Mexico!” Akaongea kwa sauti huku akisogea mbele mwanaume aliyeshuka kwenye helkopta huku mwanamke ambaye naye alishuka kwenye helkopta alishakuwa anakaribia walipo kina Bon, Bi. Millian kuona vile naye akaanza kupiga hatua wakapishana.


Bon na mwanadada wakakumbatiana na kupeana mabusu ya kila mmoja akimbusu mwenzie kwenye mashavu wakaachiana kisha mwanadada akahama na kwenda kumkumbatia Mclean Welch mmoja wa wanaume waandamizi wa ‘TSA’ walibusiana pia wakaachiana na mwanadada kumalizia kwa kukumbatiana na Fred Blank (FB) huyu si mwandamizi ni mgeni kwenye waliongezwa kuziba mapengo ya hawa waliowafuata hapa ambao walikuwa mikononi mwa genge la ‘TRJ’.


Mwanamama Miliian alipoingia tu kwenye helkopta, Bon akawanyanyua watoto wawili wadogo kisha akaonyesha ishara kama ya mwanzo hapo bwana mkubwa anayeongoza wenzake akageuka mlangoni na papo hapo akashuka mwanadada mwingine naye akiwa kavaa suruali ya jeans ila huyu ni jeans nyeusi na fulana tu aina ya lacrosse ya mistari ya kama pundamilia.


Hapa kulikuwa hakuna kusimama simama wala nini mpishano ukafanyika haraka na furaha upande wa kina Bon ikaongezeka licha ya sura za bandia walizovaa ndugu zao hawa waliweza kuwatambua wenzao waliokuja kumalizia mpango wa mabadilishano, waliwajua kwa kutumia maneno ya mafumbo.


Mabadilishano yalikamilika na kila kundi likaondoka na watu wake ikiwa pamoja na kina Bon kukabidhiwa bahasha yenye pesa dola elfu kumi taslimu.


ENDELEA NA DODO ASALI…!


PETATLAN, GUERRERO-MEXICO

Soledad De Maciel eneo lilipo kasri la kifahari la ‘Secreto Potentio La Feca Palacio’ (nguvu ya siri kasri la Feca) katika viunga vya manispaa ya Petatlan jimbo la Guerrero, katika chumba cha kulala (apartment) cha mheshimiwa Brigedia Fernandes Carlos Codrado ‘Feca’ kwa mara ya kwanza mke wake wa halali alikuwa amekaa kitandani akimuangalia mumewe aliyemgeuzia mgongo hatua chache mbele akiwa ametoka kuoga anavaa pajama lake la kulalia usiku huu wa saa saba na dakika kumi muda wa arobaini toka mkewe na watoto wake kuwasili katika kasri hili wakiletwa kwa helkopta moja kwa moja wakitokea milima ya Richimond karibu na chanzo cha mto Rouge kitongoji cha Markham jimbo la Ontario nchini Canada.


“Nimeumia sana kwa tukio hili… Uliniahidi miaka iliyopita kuwa hata kama unafanya biashara hii ya haramu haitatokea hata siku moja mimi na watoto wetu kuguswa kwa namna yoyote ile, tumeishi tofauti kama si mke na mume kwa miaka mingi kwa sababu ya biashara zako za mihadarati… Naomba kujua baada ya hili unahisi kuna nini tena litakalotutokea familia hii?” Mazungumzo yalianzishwa na mwanamama Millian baada ya kumgundua mumewe ni kama anamkwepa hataki wazungumzie suhala hili kwa kujifanya anaendelea kujipa huduma pembeni ya kioo cha ‘dressing table’.


“Kunyamaza kwako si dawa wa hili jambo… Nina haki ya kuishi kwa amani bila kusumbuliwa vivyo hivyo watoto hawahitaji kuishi kana kwamba tuliwazaa kwa bahati mbaya bila makubaliano yetu sisi wawili licha ya kuwa pia tulikuwa tukistarehe kwa raha zetu, naomba unielekeze vizuri nini kilichotokea mpaka sisi tujikute mahala tusipopajua tukiwa tumefungwa midomo kwa vitambaa tusiweze kuongea na hata macho yetu yakiwa yamenyimwa uhuru wa kujua kama sasa ni usiku au mchana mpaka pale walipotuletea chakula kwa ajili ya kutulazimisha kula ndipo walitufungua mikono na kututoa vitambaa vyeusi machoni tukalazimishwa kula vyakula ambavyo waliamua wao sisi tule tena wakiwa wametusimamia watu wawili waliofunika kwa mask nyuso zao.. Ukweli hakuna kitu ambacho kitatufanya tulale Fernandes zaidi ya ukweli wote.. Niambie kila kitu?” Akaendelea kuongea Bi. Millian akainuka na kukaa kitako juu ya kitanda.


Feca akageuka na kumtizama mkewe uso wake licha ya kuwa ulikuwa na hasira sana lakini alijitahidi kwa mbinu zote kuuweka kawaida na kuwa mpole mbele ya mkewe, akapiga hatua kusogea kitandani bwana mkubwa huyu ambaye alivyo si kama ma ‘kingpin’ wengine wanaongoza magenge ya cartels.


“Kwanza napenda nikuombe msamaha mke wangu kwa mara ya kwanza kuivunja ahadi niliyokuahidi juu ya usalama wako na familia yangu kwa ujumla, napenda niahidi tena siku ya leo tarehe 07 mwezi wa kumi usiku wa siku ya jumapili kuingia jumatatu ambayo kitarehe tushaianza jumatatu mi mi Brigedia Fernandes Carlos Codrado nitahakikisha ninailinda familia kuliko navyojilinda mwenyewe, sikuwa najua kama mlipewa manyanyaso yoyote jamaa waliniahidi hawatawadhuru wala kuwapa kashikashi zitakazowavuruga kisaikolojia kwa namna yoyote ile” Akiwa kamsogelea mkewe kwa ukaribu kabisa ingawa yeye alikaa kwenye kona ya kitanda wakati mkewe akiwa katikati ya kitanda kakaa kitako magoti akiyakunja na kuyafanya yasogee karibu na kidevu chake.


“Waongo wale… Waongo kabisa wametufanyia mambo ambayo si ya uungwana ikiwa mmoja akinidhalilisha kwa kuniingilia Fernandes bila ridhaa yangu nikiwa nimefungwa mdomo nisipige kelele na mikono yangu akiifunga kwa nyuma.. Ha hah ahaha haha eeeh shit..!” Alishindwa kuendelea akaanza kulia mwanamama Millian, moyo wa Feca ulibadili mapigo ukadunda kwa tofauti na udundavyo kikawaida, alistuka sana kusikia mkewe alibakwa.


“Shenziiii… Fuckin, fuckin… Wanaharamu kabisa wanakubaka wakati walisema hawajawagusa kabisa.. Aisee hili jambo siwezi kuliacha likapita, ametumia condom?” Akapayuka kwa nguvu akiwa kapaniki kupitiliza Brigedia Feca.


“… Ame.. ametu..mia nashukuru hilo mume wangu.. Alivizia wenzake hawapo kwakuwa walikuwa wakiwekeana zamu kutulinda alitumia fursa hiyo juzi jumamosi usiku akanibaka wanangu hata kama walikuwa wamefungwa kamba na kuzibwa macho walisikia purukushani za mimi mama yao kudhalilishwa… Nimeumia Ferna, nimeumia sana Ferna.. Najiona msaliti wa kulazimishwa mume wangu” Alidanganya kwenye kutumia condom sababu jamaa alimbaka kavukavu na hata manii zenye uzito wa kutosha alimmwagia ndani ya kitumbutua bila kujali chochote iwe magonjwa au kumpa mimba ila hapa aliona amdanganye mume wake maana alihofu anaweza kujijengea tatizo hadi yeye, tatizo la kutengwa.


“Watu wale watanifanya leo nisilale… Siwezi vumilia mke wangu kipenzi ubakwe kizembe namna hii bila na wao kulipia walichofanya nasema kila afisa wa DEA atalipa kosa la mwenzake bila kujali amehusika au hakuhusika jino kwa jino”

“Nimeshika majina yao na vyeo vyao hawa wa mwisho waliotufungua macho wakati tupo kule helkopta yako ilipotufuata nina hasira nao naomba usiwaache hata kama utafuata sharti langu la kuacha hii kazi ya kuuza mihadarati tukazama zaidi kwenye biashara zitakazotupa heshima yetu na kutufanya tuishi kwa amani”

“Sema sema niambie majina yao haraka…!”Akaongea Feca huku akiinuka kisha akapiga hatua tatu mpaka kwenye dressing table ambako akachukua peni.


“Aliyekuwa akifanya maongezi na mtu wako wakati wa mabadilishano anaitwa Agent Telizo Munde, mwingine anaitwa Agent Rummenige Brandts na wa mwisho ambaye ndiye nahisi alinibaka kutokana na umbo lake nilivyoliona linaendana na mbakaji aliyenibaka hata kama sikuwa namuona kitambulisho chake kimeandikwa Agent Johnson Greg Rautolaye huyu ni mtu mweusi tofauti na wengine wazungu..” Akaeleza majina ya watu waliokuwa wakiwashikilia yakiwa ni majina ya bandia ya maafisa wa DEA lakini si wenyewe na hapa ndipo mtoa wazo watumie majina na sura bandia alicheza ghiliba ya nguvu ikaenda kufanikiwa kwa kiasi walichohitaji kina Bon, Brigedia akiwa kakunja uso pua imepanda juu kama inataka iyapite macho yalipo aliyaandika majina yale kwenye kitabu chake kidogo ‘note book’.


“Watu weusi ndiyo maana nawachukia sana shenzi zao wnapenda sana kubaka… Nitamtafuta mbwa huyu nakwambia nakupa wiki tu atakuwa kaingia katika mikono ya TRJ… Nasema wamechokoza nyuki wasiopigika risasi… Shenzi nawalipa hadi pesa ya msamaha kumbe wana mbwa wao mweusi mmoja anakubaka mke wangu mpendwa, sikubali kama mbwai na iwe mbwai tu…” Alifoka Feca kisha akainuka kitandani akasimama akitikisa kichwa meno kayang’ata kwa hasira.


“Sikia mke wangu mpenda.. Kukikucha tu nitamuita daktari wangu daktari bingwa akuchunguze wewe na watoto afya zenu, mbwa wa DEA wamenitibua sana na wasiwasi pia na watoto afya zao zinaweza kuwa siyo sawa na pia watakuwa wameathirika kisaikolojia watoto wangu..”

“Sawa mume wangu… Itakuwa vizuri sana rudi kitandani tulale usiku umeenda sana… Kukikucha tu panga mambo sawa yule mbakaji nataka ateswe na awekwe gereza la kudumu mpaka afie gerezani huko huko chini ya mateso makali sana maana kutushikilia siku mbili yeye na wenzake ni kosa la kulipia miaka ishirini ya mateso tutamuua akiwa mzee kaisha kabisa” Akaongea Mrs Fernandes au waweza muita Madam Millian.


“Sitalala mpaka majina haya matatu ya hawa washenzi yaingie mikononi mwa TRJ wa Mexico… Watasema kikosi chote kilichokuja kufanya utekaji wenu..”


Walimalizia maongezi kidogo kisha wakalala ikiwa imefika saa nane na nusu usiku wa manane kwa saa za Mexico hususani jimbo la Guerrero.


***** ***** *****


Jumatatu saa mbili asubuhi kwa saa za Mexico zilimkuta kiongozi mkuu wa ‘TRJ’ brigedia Feca akiwa katika ofisi yake kuu iliyopo ndani ya kasri lake, aliwai kufika lakini hakuwa amefanya jambo lolote kiutendaji zaidi ya kuwapigia simu watu walio kwenye bodi yake ya uongozi ambao kwa siku hiyo walikuwa wako jimbo kuu kiutawala wa genge la ‘TRJ’ kuwa anawahitaji wafike mara moja kwenye ofisi yake kuu.


Kwa kuvuta muda hili anaowahitaji wawe wamefika alichukua magazeti ya siku hii akawa anayapitia habari zilizoripotiwa na waandishi wa magazeti hasa zile zilizopewa kipaumbele na wahariri wa magazeti.


Saa mbili na dakika thelethini na tano wale aliowahitaji walifika mule ofisini wakiwa wameongozana wote kwa pamoja kana kwamba walilala sehemu moja.


Alifika Koplo Savatel Santos, Mr. Villa Nandez Guti na Aristos Mosquera, walikuwa wamekubaliana wakutane getini hata kwa kusubiriana kisha ndipo waingie ndani kumsikiliza Feca kiongozi wao mkuu, ambaye siku mbili tatu hakuwa vizuri kisaikolojia akishughulikia suala la kushikiliwa mateka na watu waliosema wao ni majasusi wa ‘DEA’.


Awa wote watatu walishirikiana kumsaidia katika jambo hili kimawazo mpaka walipoona mwenyewe kaamua kufuata matakwa ya watekaji wa familia yake wakamuacha atembee mwenyewe kwenye njia alioona ni sahihi kupita, shukrani boss akafanikiwa kuipata familia yake usiku uliopita.


“Karibuni sana jamani… Na poleni kwa kazi nzito mnazofanya kuhakikisha gurudumu la TRJ haliyumbi hata kidogo licha ya vikwazo vingi” Alianza kuongea mwenyeji, mwenye ofisi yake, ofisi kuu ya boss mkuu wa TRJ. Wageni waliitikia kiheshima inayomstahili kiongozi wao.


“Kwa niaba ya wenzangu wote napenda kushukuru kwa kufanikisha kuirudisha familia yake mikononi mwako, pia tuwashukuru watekaji hawakuwadhuru shemeji na watoto wetu kama walivyoahidi” Akaongea Koplo Savatel kauri ilipomalizika wote wakauona uso wa Feca ukijenga twasira ambayo uwa wakiiona utambua hayuko sawa.


“Vipi Brigedia! Kuna tatizo?” Akauliza Aristois Mosquera.

“Ndiyo kuna tatizo, watu wa DEA wamefanya uhuni ambao si vizuri kusema ila kwakuwa nyie ni watu wangu wa karibu sina budi kusema….. Aibu lakini nitawaambia, mmoja wa watu wao amembaka mke wangu inasemekana ni mtu mweusi kati ya watu waliokuwa wakiishikilia familia yangu, najua amefanya hivyo kwakuwa kiukweli hata watu hao tuliokuwa tunawashikilia naamini lazima watakuwa wamebakwa na watu wetu wanaowalinda hivyo ni kisasi kimelipwa ni jino kwa jino lakini jino kwa jino si kwa mke wangu, mke wangu hahusiki na mambo yangu, kuiteka familia yangu tu ni kosa kubwa sana wamefanya” Akaongea Feca kisha akakatizia kuwaangalia wanaomsikiliza huku wakimuangalia kwa umakini mkubwa.


“Aisee pole sana Brigedia… Kumbe wamefanya kisasi cha kishenzi kwa washenzi mpaka leo najiuliza walijuaje kama watu wao tunawashikilia maana mwaka mmoja mkiwa mmepoteza mtu wenu sidhani kama mnaweza juwa walipo kirahisi, sitaki kuwaza kwenye genge letu kuna vijana wameanza kuuza siri zetu kwa maadui zetu” Alikuwa Aristos tena akiongea kwa kutanguliza pole yake kwa boss wao.


“Pole sana ndugu yangu… Shemeji hajadhurika?” Akahoji Koplo Savatel.

“Daktari ndiyo amefika asubuhi hii kumcheki kitaalamu kama kuna gonjwa lolote kampa, kama mjuavyo watu weusi malaya sana si wanaume wala wanawake hawajatulia hawa watu… Tuacheni habari za shemeji yenu, ahsanteni sana… Nimewaita hapa kutaka mara moja tuwatafute ambao nimepata majina yao kuwa wao ndiyo waliongoza operesheni yao ya kuwarudisha watu wao, natambua tuna wasaliti genge kubwa kama letu haliwezi kukosa wasaliti kila siku tunazidisha umakini kudhibiti watu kama hao, tuachane nao tujikite kwenye operesheni ya siri ya kuwapata hawa watu”Brigedia Feca akaweka hadharani alichowaitia.


“Majina umeyapataje Brigedia? Maana nakumbuka walikataa kukutajia majina yao ulituambia hivyo” Akaongea Mr. Villa Nandez Guti kiongozi mkuu msaidizi wa genge ambaye hali yake kiafya bado haikuwa sawa mgongo wake ulikuwa wakamsumbua mara kwa mara hivyo mara mbili kwa mwezi uwa anakwenda clinic kwa dokta mtaalamu wa magonjwa ya mgongo nchini Canada.


“Walijisahau wakavaa vitambulisho vyao wakati wa mabadilishano huko kwenye milima ya Richimond, mke wangu alisoma jina la kila mmoja wao na akayashika kichwani… Aliyekuwa akiongoza operesheni ile kwa upeo wa mke wangu Millian anaitwa Agent Rummenige Brandts na kama mjuavyo awa DEA kuna maajenti wa siri kwa ajili ya ushushushu na ukachero pia wapo maajenti wa operesheni maalumu hivyo kikosi hiki ni kikosi cha operesheni maalumu, aliyembaka mke wangu inasemekana ni mtu mweusi licha ya kuwa hakumuona na alifanya kwa siri wenzake wasijue lakini watu weusi tabia zao hazitabiriki aliwavizia wenzake akafanya ubakaji hatuna hakika sana ila mke wangu anasema kati ya wale waliopeleka pale Rogue Richmond Falls alikuwepo mtu mweusi mmoja mbaye kitambulisho chake kinasomeka jina la Agent Johnson Greg Rautollaye hivyo mtu huyu ni muhimu sana kwa kisasi changu pia alikuwepo Agent Telizo Munde huyu alivyo kiasili ni mjapan nafahamu historia yake ingawa mke wangu kasema naye ni mzungu… Nawataka watu hawa wote watatu ingawa nilitaka kundi lote kama mke wangu alivyonieleza walikuwepo na wanawake, nataka wawe wamewaokoa wenzao lakini wawe wamepishana nao kisha ndiyo watajua kama Brigedia Feca na TRJ hatutaniwi, TRJ ni genge la watu waliokamilika si genge la mashoga” Akaongea kirefu Feca akiwa kauegemeza mgongo wake kitini mkononi anachezea simu yake.


“Operesheni hii si ni utekaji tu?” Akauliza Koplo Savatel.

“Ndiyo!” Akajibu kifupi Feca na kuendelea kutulia kitini akiwatizama wenzake.

“Operesheni ya utekaji ndani ya Marekani, aisee itabidi tuchague watu walio na uzoefu mkubwa katika masuala ya utekaji na kiufundi itabidi wakawatekee majumbani mwao… Hivyo itabidi wakafanye kazi ya upelelezi Springfield, Virginia kujua makazi ya watu hawa kisha ndipo tuwateke na pia zitayarishwe njia sahihi za kupita na watu hawa” Maelekezo toka kwa Koplo Savatel Luca Santos yakanyooshwa.

“Kikosi cha wapelelezi makini wawili napendekeza kama kawaida aende Nasco Dos Santos mwingine mtachagua nyie” Mr. Guti akampendekeza mtu wake anayemuamini katika kazi za kiintelejensia.


“Koplo Marianna Caro Funtes hajatoka Guatemala muda mrefu toka tumuweke kule kiusalama na serikali yetu inayomuwinda, ataongozana na Nasco pia kikosi cha watu sita kitaenda kabisa huko Springfield kikosi icho kitaongozwa na Koplo Maxiwell Zuantejo,Mireles Gonzales, Rude Bwoy watu watatu watakutana na watu wetu watatu walio Nevada, nitawapigia simu kuwaelekeza operesheni hii natakaje na ifanyike kwa haraka ya namna gani, nawaamini sana Juan na wenzake” Aliendeleza maelekezo Feca.


Kisha wakakubaliana na mambo mengine ya msingi ambayo waliona yakifanyika yataweza kuwafanya operesheni kisasi inakwenda watakavyo kisha kila mmoja akaondoka mahala pale wakikubaliana kuwapa taarifa waliowachagua kwa ajili ya kwenda ndani ya Marekani jimbo la Virginia mji wa Springfield yalipo makao makuu ya shirika la kupambana na madawa ya kulevya la Marekani ‘Drug Enforcement Administration’ (DEA).


Kila mmoja aliona ni sahihi asemavyo Feca kila kitu hasa operesheni moja kwa moja ikielekezwa mji wa Springfield kwa sababu majasusi wa shirika la upambanaji wa madawa ya kulevya karibu wote habari zao ukizihitaji basi utazipata miongoni mwa mwenzao aliye ndani ya shirika hili na wengi wanapatikana hapa hivyo majina waliyonayo yalilengwa yatapatikana habari kamili hapa na hata makazi yao yatajulikana hapa.


Mwisho wa sehemu ya thelathini na mbili (32)


JINO KWA JINO linadhidi kushika hatamu tayari TSA wamefanya ukombozi wa watu lakini wakifanikisha kufanya ghiliba ambayo imesababisha kitu ambacho aliye plan mchezo alijua wakishafanya hivi basi kitaamka kitu ambacho kitasababisha genge la TRJ kujizidishia uadui mkubwa na shirika la kupambana na madawa la Marekani ‘Drug Enforcement Administration’ (DEA).


Hisia mpango kwao TSA ni kama umefanikiwa pakubwa ghiliba imewanasa Feca na watu wake tayari wanatuma watu waende mji wa Springfield jimbo la Virginia kwa ajili ya kufanya malipizi ya utekaji kisha nao wafanye walichokiita JINO KWA JINO.


Nini kitatokea mbele?




“Operesheni hii si ni utekaji tu?” Akauliza Koplo Savatel.

“Ndiyo!” Akajibu kifupi Feca na kuendelea kutulia kitini akiwatizama wenzake.

“Operesheni ya utekaji ndani ya Marekani, aisee itabidi tuchague watu walio na uzoefu mkubwa katika masuala ya utekaji na kiufundi itabidi wakawatekee majumbani mwao… Hivyo itabidi wakafanye kazi ya upelelezi Springfield, Virginia kujua makazi ya watu hawa kisha ndipo tuwateke na pia zitayarishwe njia sahihi za kupita na watu hawa” Maelekezo toka kwa Koplo Savatel Luca Santos yakanyooshwa.

“Kikosi cha wapelelezi makini wawili napendekeza kama kawaida aende Nasco Dos Santos mwingine mtachagua nyie” Mr. Guti akampendekeza mtu wake anayemuamini katika kazi za kiintelejensia.


“Koplo Marianna Funtes hajatoka Guatemala muda mrefu toka tumuweke kule kiusalama na serikali yetu inayomuwinda, ataongozana na Nasco pia kikosi cha watu sita kitaenda kabisa huko Springfield kikosi icho kitaongozwa na Koplo Maxiwell Zuantejo,Mireles Gonzales, Rude Bwoy watu watatu watakutana na watu wetu watatu walio Nevada, nitawapigia simu kuwaelekeza operesheni hii natakaje na ifanyike kwa haraka ya namna gani, nawaamini sana Juan na wenzake” Aliendeleza maelekezo Feca.


Kisha wakakubaliana na mambo mengine ya msingi ambayo waliona yakifanyika yataweza kuwafanya operesheni kisasi inakwenda watakavyo kisha kila mmoja akaondoka mahala pale wakikubaliana kuwapa taarifa waliowachagua kwa ajili ya kwenda ndani ya Marekani jimbo la Virginia mji wa Springfield yalipo makao makuu ya shirika la kupambana na madawa ya kulevya la Marekani ‘Drug Enforcement Administration’ (DEA).


Kila mmoja aliona ni sahihi asemavyo Feca kila kitu hasa operesheni moja kwa moja ikielekezwa mji wa Springfield kwa sababu majasusi wa shirika la upambanaji wa madawa ya kulevya karibu wote habari zao ukizihitaji basi utazipata miongoni mwa mwenzao aliye ndani ya shirika hili na wengi wanapatikana hapa hivyo majina waliyonayo yalilengwa yatapatikana habari kamili hapa na hata makazi yao yatajulikana hapa.


ENDELEA NA DODO ASALI..!


SPRINGFIELD, VIRGINIA-MAREKANI

Best Western Hotel chumba namba 15 hotel ya nyota mbili iliyopo Commerce Street mji wa Springfield jimbo la Virginia nchini Marekani, ndani ya chumba hiki chenye sebule moja kwa ajili ya wageni mpangaji wa chumba na chumba chenyewe cha kulala mpangaji huyo.


Kwenye chumba hiki kulikuwa na watu mchanganyiko wake kwa waume wakiwa wameitana kujadili jambo lililowafanya wao kuwa ndani ya jimbo la Virginia wao kuwa ndani ya mji mzuri wa Springfield, wote wa waliopo hapa walikuwa katika mpango nia wa mheshimiwa wao kiongozi wa genge la ‘THE RED JAGUAR’ (TRJ).


“… Naamini wote tuliotakiwa kuwepo hapa kwa ajili ya mpango mkakati tumefika hivyo hakuna cha kupoteza, Nasco tungeoomba utueleze ulipofikia maana wewe upo hapa Springfield toka siku tatu zilizopita na leo ijumaa ni siku tano toka tukabidhiwe hii misheni..!” Alikuwa ni Koplo Savatel Dos Santos kiongozi wa misheni hii waliyoipa jina ‘misheni heshima’ (respect mission).


“Siku tatu nimefanikisha kwa asilimia mia moja kile ambacho mimi kama mpelelezi nilitakiwa kukamilisha…. Nimeweza kujua makazi ya wasakwa wetu wote na pia nimeweza kujua hadi mienendo yao na kiukweli wanaonekana ni wahusika wakuu wa operesheni iliyofanyika wiki moja tu iliyopita kwa sababu ni watu wanaoandamana sana hasa wakati wanapokuwa wametoka kwa shughuli zao za kiofisi ila mmoja ambaye picha yake niliyotumiwa kwenye mtandao wa whatssap ikiwa na alama kichwani imenishangaza ni kuwa mlemavu wa mkono na haonekani kama ni mtu wa kazi za vitendo” Akaeleza Nasco Dos Santos alichoweza kukipata katika uchunguzi wake toka aingie Springfield akitokea Guerrero, Mexico.


“Kazi nzuri sana umefanya Nasco.. Kazi itaanzia kwa kufuata maelekezo yako hivyo eleza yote unayoona sawa nasi tutafanya vile maelekezo yalivyo” Savatel akaeleza.


“… Kwa ilivyo kuna namna mbili… Moja kwa uchunguzi niliofanya jamaa wale wawili uingia kazini kwa muda ambao wanahitajika kufika kazini na mkuu wao wa kazi ambaye sikufanikiwa kumjua moja kwa moja ni nani? Maana laiti ningemjua pengine tungeweza mjua aliyepanga operesheni ya kuwaokoa wenzao waliokuwa mikononi mwetu ila sasa mmoja kati yao ndiyo huyu mwenye mkono ambao ni wa bandia yule ufika kazini asubuhi ya saa mbili na kutoka muda wa kazi unapoisha huyu ni Agent lakini ni afisa kati ya maafisa wengi wenye vitengo mbalimbali ndani ya DEA huyu ndiye yule mweusi kati ya watatu tuliopewa kazi ya kuhakikisha tunawatia kwenye mikono yetu haraka iwezekanavyo jina lake Agent Johnson Greg Rautollaye anaishi Chelsea Square Apartments barabara ya Blacklick Road hapa Springfield nimemuunganisha yeye ingawa si mtu wa kujichanganya sana na hawa wengine lakini kila jioni uwa wanakutana watu hawa watatu na kwenda katika bar mojawapo kati ya bar zilizopo ndani ya mji huu wakienda huko kupata vinywaji na kubadilishana mawazo hivyo mnaweza ama nitumie neno tunaweza wavamia huko na kuwachukua wakiwa pamoja… Uchunguzi wangu unasema pia inawezekana kila mmoja akafuatwa nyumbani kwake usiku na kuchukuliwa kama kifaranga anavyochukuliwa na mwewe na hii ndiyo njia ya pili ambayo humo humo pia tunaweza tukaunda mtego maana marafiki wana uwezo wa kuwa wanashirikiana kwa mengi hivyo inawezekana tukamtumia mmoja kuwaita wenzie kitu ambacho si salama sana kwetu kwakuwa hawa ni majasusi na majasusi wa Marekani wa mashirika haya kama DEA uwa si majasusi wa kuchezelewa chezelewa wanafanya mambo kwa uhakika na umakini sana… Ni haya ambayo ninaweza kuwakilisha kwenu kama kuna swali nakaribisha swali!” Alitoa maelezo marefu Nasco Dos Santos.


“Umesema umeweza kujua makazi yao watu hawa lakini hukueleza makazi ya wengine tumeweza juwa juu ya Agent Johnson tu. Je awa wengine?” Aliuliza Savatel huku wengine wote wakiwa kimya kusikiliza kwa umakini.


“Agent Rummenige na Agent Telizo Munde wote wanaishi eneo moja linaloitwa Sullivan Place mtaa wa Vincent Gate Alexandria nyumba zao zimeachana nyumba tatu yaani inaanza ya Agent Munde kisha baada ya nyumba tatu muongozano inakuja ya Agent Rummenige… !” Akajibu Nasco.


“Umesema uwa haieleweki bar gani maalumu watakayoelekea kwa kila siku lakini ni kawaida yao kwenda bar, je ushawafuatilia nyendo zao na kugundua jinsi usalama wao unavyokuwa? Maana majasusi wanajilinda vizuri kila dakika bila kufanya kosa litakalosababisha wao kuingia hatiani kwakuwa wanajijua wana maadui wengi wanaowawinda” Savatel aliendelea kuhoji na kufanya kikao kiwe kama cha wazungumzaji wawili huku wengine wakiwa wasikilizaji tu.


“Jana nilifanya hivyo kama ilivyokuwa juzi pia nilifanikiwa kufanya hivyo katika mionekano tofauti ambayo isingewezekana kustukiwa… Juzi walienda bar ya Shooters Sports Bar, bar maarufu sana hapa Springfield kuna mchanganyiko wa starehe zinazopatikana bar inapatikana eneo la Spring Garden Dr na jana walienda bar ya Crossroads Bar & Grill Restaurant Reviews hii nayo inafanana na ya juzi kwa uchangamfu iko 8100 Loisdale Road na kote huko hawakujumuika na familia zao ingawa aliyenipa msaada wa habari anasema wikiendi uwa wanatoka na familia zao kwenda sehemu zenye utulivu hasa beach” Nasco akatiririka.


“Je wanatumika kwenye ulevi kwa kiasi gani?” Akauliza Savatel na mara zote wakati Nasco anatoa maelezo yeye alikuwa akiandika kwenye kitabu kidogo (note book) baadhi ya pointi alizoona ni muhimu zaidi.


“Unamaanisha wanakunywa vipi?... Ni kwamba wanachangamka tu hawalewi kama walevi wengine ingawa chupa za pombe wanazokunywa ni pombe kali na wanagonga glasi nyingi lakini inavyoonyesha pombe katika vichwa ni starehe ya kuwafanya wachangamke huku wakibadilishana mawazo na si kwenda kulewa”

“Unafikiri tunaweza wavamia wakiwa wanatoka kwenye starehe? Je wanaongozana katika usafiri mmoja wote watatu au wawili au mmoja mmoja?”

“Hawaongozani kila mmoja anatumia gari yake ingawa pia uwa wanatumia pikipiki hasa wanaotokea Sullivan Place, nafikiri yule mtu mweusi hatumii pikipiki kwa sababu ya mkono wake wa kulia kuwa ni mkono wa bandia wenyewe umekatwa… Ningependa nitoe pendekezo langu la njia ambayo ningeoneelea itakuwa sahihi zaidi ni njia ya kuwateka pamoja wakiwa wanatoka kwenye satrehe zao maana mara zote mbili nimeona wakitoka na kuagiana kwenye maegesho ya magari ya bar husika hivyo hapo ndiyo wa kuwafika na kuwachukua kwa pamoja..!” Alijibu na kutoa pendekezo Nasco kisha akainua kikombe kidogo cha kunywea kahawa akanyanyua na birika mkono wa kushoto kisha akamimina kahawa kwenye kikombe na kujiunga na baadhi yaw engine waliokuwa wakisikiliza mahojiano na maelezo huku wakinywa kahawa ingawa wapo waliokuwa wakinywa pombe kali za mizinga mbalimbali toka makampuni mengi makubwa ya vinywaji pombe yaliyopo Marekani.


“Sawa sawa hilo halina kasoro naomba wengine wote tukubaliane nalo na kila mmoja atambue hapa hatupo Mexico hapa tupo Marekani na tunachezea sharubu pana za vyombo bora vya usalama hivyo umakini unatakiwa uwe mkubwa sana, kesho kazi itafanyika… Ningependa kujua jambo moja la mwisho, je kesho jumamosi tunaweza fanikisha mpango?” Akafafanua kidogo kwa wenzake wote kwa ujumla kisha akarejesha swali jipya kwa Nasco.


“Kama nilivyoeleza awali siku kama ya kesho DEA uwa wana siku fupi kazini kwa mujibu wa mpatia habari wangu Agent Johnson ufika kazini asubuhi na ifikapo saa sita ofisi zote uwa zinafungwa na ndipo baadaye familia zao ukutana kwa chakula cha mchana kwa pamoja katika nyumba ya mmoja wao wana ratiba kabisa baada ya chakula icho jioni wote uenda sehemu ambayo si mtambuka kwa wengine ukiacha wao ambao wana ratiba juu ya yote kati yao hiko hivyo!” Akajibu kiufafanuzi Nasco, jamaa alikuwa ameweza kuzikusanya habari chache kuhusu watu wanaotaka kuwateka wakifikiri ndiyo walihusika na misheni ya kuiteka familia ya Brigedia Feca kumbe changa la macho waliofanya kazi ile ni kundi la ‘THE SPECIAL ASSASSIN’S’ (TSA), kazi ambayo iliwahusu kwakuwa waliokuwa wakishikiliwa mateka na ‘THE RED JAGUAR’ (TRJ) walikuwa ni watu wao.


“Iko vizuri sana… Sasa bwana Nasco kazi yako imemalizika nusu na robo lakini bado hujamaliza robo yako ambayo itakuwa ni kuhakikisha tunafikia hatua tunayoitaka kikamilifu bila kosa, utaendelea kushirikiana na Mariana Caro Funtes katika kuwinda wanakwenda wapi na familia zao? Ingawa kiusalama hatutaweza kuwateka na familia zao kwakuwa kuondoka na watu wengi hapa Springfield ni shughuli kubwa sana na ya hatari sana” Alieleza mkakati mfupi ujao ambao utawapelekea kwenye mpango madhubuti kukamilisha kilichowatoa Guerrero mpaka hapa Springfield.


Waliendelea na mazungumzo ya wote kwa ujumla jinsi gani itakavyokuwa hatua kwa hatua baada ya hili kwenda lile wakafika hadi jinsi watakavyoweza kuondoka na maafisa wa DEA ndani ya Marekani jimbo la Virginia jimbo bora sana kwa usalama kwakuwa ndipo yalipo mashirika makubwa ya usalama wa nchi hii kubwa.


***** ***** *****


DEA WADUWAZWA, SPRINGFIELD, VIRGINIA-MAREKANI

Ilikuwa zamu ya familia ya Agent Johnson Greg Rautollaye afisa wa shirika la upambanaji wa madawa ya kulevya Marekani ‘Drug Enforcement Administration’ (DEA), familia yenye watu wawili mume na mke ikiwa hata mama mwenye nyumba bado hajaanza dalili za kuwa ana kiumbe kigeni ndani ya mwili wake tena mke akikataa kuwa na msaidizi wa kazi zake za nyumbani pia ikiwa ni tofauti na baadhi ya familia nyingi ambazo wao uwa na wanyama wale wafugwao majumbani kama paka au mbwa lakini Bwana na Bi. Raotollaye hawakuwa na wanyama hawa. Familia ambayo ni miezi miwili tu toka wafike kanisani mbele ya madhabahu ya mchungaji wa kanisa la First Baptist Church Of Springfield lililopo Gary Street.


Jumamosi ya wiki hii iliwakuta familia marafiki wakiwa na ratiba ambayo iliwaleta katika mtaa wa Chelsea Street Apartments barabara ya Backlick Road kwa ajili ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na wanandoa mpya hawa mke akiitwa Anita (Mrs. Anita Johnson) na mume akiitwa Mr. Johnson Greg Rautollaye au kwa cheo cha kijeshi kwakuwa alikuwa amepita jeshini aliachia jeshi akiwa na cheo cha Sajenti Johnson Greg Rautollaye huku katika shirika la upambanaji wa madawa ya kulevya akiitwa Agent Jahnson Greg Rautollaye kijana wa kimarekani mwenye asili ya Nigeria akimuoa mke mwenye asili ya Liberia wote hawa ni wamarekani weusi.


Ni kawaida ya familia tatu ambazo wanaume wote wanafanya kazi ya ujasusi shirika la kupambana na madawa ya kulevya la Marekani kuwa na utaratibu wa kuwafanya wawe karibu kiushirikiano ulio kama undugu tena wakiunganisha mpaka kwa wake zao, hivyo inapofika jumamosi basi familia zote ukusanyika katika nyumba ya mmoja wao wakiwa na watoto wao kama familia husika imejaliwa kuwa na watoto wao na hata wasaidizi wa kazi za nyumbani nao hujumuika pamoja nao katika mlo wa mchana na kisha baadaye yake ya jioni wanakwenda kwa pamoja sehemu za michezo au zinginezo kati ya wao wanazoona kwa pamoja wakiwa na familia zao kutafaa zaidi kuwapa furaha ya pamoja.


Nasco Dos Santos! Kachero na mnyakuzi fundi wa kudukua habari za wengine kwa kutumia upeo wake wa kipaji cha asili alichonacho katika kushawishi mtu au watu kujua habari za watu wengine anaowahitaji, alifika mapema mtaa wa iliyopo makao makuu ya DEA akiwa katika muonekano tofauti na alivyowai kufika nyakati za siku mbili zilizopita, alijihifadhi mbali na pale akihofia kamera za CCTV zilizo nyingi katika mtaa huu lakini kuwa kwake mbali hakukuweza kumzuia kuona kule kwakuwa alikuwa akitumia kiona mbali kilichochanganywa na miwani aliyovaa ambayo laiti angeweza kuonakana uzuri kwa kamera zilizopo mtaa ule zikiwa zimeunganishwa moja kwa moja na mitambo iliyopo katika moja ya chumba chenye huduma za kupokea taarifa za moja kwa moja za CCTV kamera ndani ya jengo la DEA, basi angeweza kufuatiliwa kwa umakini sababu hakuna teknolojia inayoweza kukatiza katika kamera za maofisi ya kiusalama ya Marekani ikafanikiwa kupita bila kujulikana nao.


Agent Johnson Rautollaye alimaliza shughuli zake zinazomfanya kufika kwa ratiba yake ya kila siku ndani ya ofisi za DEA kisha akatoka na kuchukua gari yake aina ya Audi A6 2010 rangi nyeusi na baada ya kuondoka maegeshoni aliingia barabara kuu akiwa kwenye mwendo wa wastani muda ukiwa ni saa tano na dakika kumi asubuhi na mara moja Nasco akaunga mkia akiwa kachukua tahadhari ya usalama wake.


Mkia ulimfuata bila mfuatiliwa kustuka mpaka anafika Backlick Road kilometa nyingi tu toka makao makuu ya DEA, jasusi wa DEA hakuwai kuhisi kama kuna siku atakuwa anafuatiliwa hakuwai kufikiri kama yaweza kutokea watu wenye shida naye, akiamini kuweko kwenye ofisi za DEA makao makuu akifanya kazi za ofisi tu akalewa na kuamini yuko salama salimini.


Akafika maeneo yake ya kujidai mtaani kwake mtaa wa Chelsea Square Apartments ambapo aliwakuta shemeji zake wote wawili wake wa rafiki zake washafika wakiwa na watoto zao kwakuwa familia hizi nyingine kwenye ndoa zilikuwa na miaka kadhaa na tayari zilileta kile wengi wanachotaraji pale wanapooana mke na mume, yaani kuwa na watoto.


Rafiki zake ambao ni Agent Rummenige Brandts na Agent Telizo Munde hawakuwepo na mara moja yeye Agent Johnson akapewa taarifa wako kwenye moja ya sehemu maarufu inayoitwa Springfield Hard Times Café & Cue ambapo watu wanaopenda kuangalia michezo kupitia televisheni ufika hapa kwa wingi kuangalia mechi za michezo mbalimbali kama soka, NFL, rugby na basketball. Kuna screan kubwa za flat zilizofungwa kila kuta za bar hii hivyo kumfanya mtu achague anakaa wapi kwa mchezo anaouhitaji iwe kwa muda na masaa yoyote kwa saa za hapa bila kujali huko unakochezwa ni saa ngapi ukifika hapa utaona mechi unayohiitaji mubashara.


Agent Johnson hakuwa na jinsi akawaaga mke na shemeji zake akaekea huko na alipofika ndipo akagundua muda huo kuna mechi kali ya watani wa jadi wa ligi ya Uingereza maarufu kwa jina la EPL, wakimenyana ni Liverpool na Manchester United na ndicho kilichowafanya rafiki zake wasikae nyumbani kumsubiri atoke kazini wakaamua waje hapa bar muda wa saa sita na nusu mchana kwa saa za jimbo la Virginia.


Swahiba zake walifurahi sana kumuona mwenzao kafika wakajumuika kwa pamoja yeye Agent Johnson Rautollaye akiwa shabiki wa Manchester United na swahiba zake wote wawili wawili ni shabiki wa Liverpool, mechi ikiwa inaendelea kipindi cha kwanza.


Walikaa pale mpaka mechi ilipoisha timu zikitoka sare pacha ya kutokufungana ikiwa Manchester United wakionyesha kandanda dhaifu sana la kujilinda chini ya mkufunzi wao mwenye hulka ya kucheza soka la kujihami David Moyes, walitia aibu kwa kukaa nyuma stahili ya kupaki basi (lol) inasikitisha sana lakini kwa sasa Moyes wakaja mameneja wengine kama Louis Van Gaal naye akaondoka baada ya kutoleta faraja akaja ambaye watu walidhania itakuwa Man Utd yenye matumaini lakini naye alirudi kwa Moyes kwa soka bovu la kujihami licha ya msimu wa kwanza kuipatia Man Utd vikombe viwili cha Europa na Carling Cup naye alikuja kutimuliwa kwa aibu na sasa amefika kocha anayeitwa wa muda mfupi timu inacheza kwa falsafa tunayoijua mashabiki kindakindaki wa timu yetu hii ikileta faraja na hamasa kwa mashabiki hata kuangalia mechi na inapoelekea kocha huyu wa ‘Care taker’ anaweza kuwa kocha wa mkataba mrefu kwa stahili yake maarufu tunayopenda kuiita ‘Oleball’.


Hawakuwa wanajua kama wanawindwa walitoka kwa furaha kubwa marafiki hawa kila mmoja akifurahia na kumtania mwenzie hasa Telizo na Rummenige wakimzonga sana Johnson kwa soka la mkufunzi wao man utd, soka bovu la kujihami.


Simu zao kila mara zilikuwa zikiita ikiwa ni namba za wake zao kuwa wanawasubiri wafanye hima kurudi nyumbani kwa Mr. Rautollaye kwa ajili ya chakula cha pamoja cha mchana.


Ikabidi kila mmoja aelekee ilipo gari yake katika maegesho kwa ajili ya kuondoka pale Springfield Hard Times.


Agent Telizo Munde aliingia kwenye gari yake ya kifahari aina ya Mitsubishi Outlander Sport, motokaa toka japan hii na alipokaa tu kwenye siti nyuma ya kiti cha dereva alichokaa aliibuka mtu kwa kasi mikononi akiwa kavaa gloves akamkamata kichwa kwa nguvu huku akimziba kwa kitambaa cheupe kilichokuwa na poda ambayo kwakuwa Agent Telizo alikuwa kwenye mshtuko aliweza vuta hewa ya poda ile kwa nguvu na mara moja mwili wake ulikosa nguvu macho yakakosa nuru, koo likakauka akapoteza fahamu.


Hapo mtu mmoja alirukia upande wa mbele wa siti akitokea siti za nyuma za abiria za gari hii na akamsogeza Telizo upande wa siti ya abiria kisha akamfunga mkanda wa usalama wa kiti kile kisha akamuongezea kofia aliyovaa yeye kumfunika kichwani ionekane mtu aliyelala baada ya uchovu fulani.


Kama ilivyokuwa kwa Agent Telizo Munde ndivyo vivyo hivyo ilivyokuwa kwa Agent Rummenige Brandts jasusi huyu wa DEA kijana wa kimarekani mwenye asili ya ujerumani gari yake naye haikuwa mbali na ilipoegeshwa gari ya Telizo yeye aliingia kwenye gari yake aina ya Audi A6 2010 aliyonunua siku moja na gari ya Agent Johnson zikiwa zimefanana aina ila rangi tofauti yeye yak wake ikiwa ya bluu mng’ao.


Wakati anajifunga mkanda wa siti yake ya dreva alihisi kitu katika kichwa chake haraka akaachia kujifunga mkanda wa siti akainua macho kuangalia kwenye kioo cha ndani ya gari kilicho juu ndipo akaona kitu lakini kabla hajafanya chochote akaguswa na tundu la baridi la bastola aina ya Automatic Colt 45 Ikabidi awe mpole naye akazibwa pua kwa kitambaa yakamtokea kama yale yaliyomtokea Agent Telizo Munde, fahamu zilihama toka kwenye dunia yake ya kawaida, akazimia.


Yakafanyika kama yale yaliyokwisha fanyika kwa wa mwanzo akahamishwa siti ila yeye akiwekwa siti ya nyuma huko.


Agent Johnson Greg Rautollaye hakuweza kukwepa mtego uliowanasa wenzake akiwa anakwenda mkononi wake wa kushoto akiwa na simu yake anaandika hili kujibu meseji kwa mke wake aliingia kwenye gari na alipofunga mlango wa gari na kuitupia simu yake kwenye dashboard tu alijikuta anabanwa shingo kwa nguvu na mtu mmoja tokea nyuma ya gari na kisha akazibwa pua na mdomo kwa mara moja kwa kitambaa cheupe naye hakuchukua raundi mara moja akaingia dunia ya kipekee, dunia ya giza totoro.


Watekaji walifanya kazi waliyohisi hapo kabla kuwa ingeweza kufanyika jioni ya siku hiyo lakini chini ya maelekezo ya Nasco kazi lifanyika muda wa saa nane na dakika kumi na saba mchana wa siku ya jumamosi katika maegesho ya Springfield Hard Times Café & Cue.


Mwisho wa sehemu ya thelathini na tatu (33)


Safari yetu ndefu ya kujua sababu kuu ya Agent Johnson Greg Rautollaye kushikiliwa mateka hapa ndipo ilifika mwisho wake.


THE RED JAGUAR chini ya ‘Kingpin drug dealer’ Brigedia Feca ndiyo wanamshikilia Agent Johnson Greg Rautollaye ambaye sehemu ya kwanza ya riwaya yetu tuliona Agent Kai akiwa anapekuwa barua pepe zake zilizotumwa katika anwani yake ya barua pepe alikutana na barua mchoro toka kwenye anwani ya mtu asiye mjua lakini muandikaji akiwa ‘Jogre’ kama anavyoitwa kwa sectret name.


Tunarudi kwenye muendelezo wa riwaya tukiachana na miaka iliyopita, karibu kwa uhondo zaidi wa dodo asali, karibu Agent Kai na wenzako wengine uendelee kwa uhondo kamili ulio ndani ya wakati kamili tuliopo.



ILIPOISHIA SEHEMU YA 33…!!

Kama ilivyokuwa kwa Agent Telizo Munde ndivyo vivyo hivyo ilivyokuwa kwa Agent Rummenige Brandts jasusi huyu wa DEA kijana wa kimarekani mwenye asili ya ujerumani gari yake naye haikuwa mbali na ilipoegeshwa gari ya Telizo yeye aliingia kwenye gari yake aina ya Audi A6 2010 aliyonunua siku moja na gari ya Agent Johnson zikiwa zimefanana aina ila rangi tofauti yeye yak wake ikiwa ya bluu mng’ao.


Wakati anajifunga mkanda wa siti yake ya dreva alihisi kitu katika kichwa chake haraka akaachia kujifunga mkanda wa siti akainua macho kuangalia kwenye kioo cha ndani ya gari kilicho juu ndipo akaona kitu lakini kabla hajafanya chochote akaguswa na tundu la baridi la bastola aina ya Automatic Colt 45 Ikabidi awe mpole naye akazibwa pua kwa kitambaa yakamtokea kama yale yaliyomtokea Agent Telizo Munde, fahamu zilihama toka kwenye dunia yake ya kawaida, akazimia.


Yakafanyika kama yale yaliyokwisha fanyika kwa wa mwanzo akahamishwa siti ila yeye akiwekwa siti ya nyuma huko.


Agent Johnson Greg Rautollaye hakuweza kukwepa mtego uliowanasa wenzake akiwa anakwenda mkononi wake wa kushoto akiwa na simu yake anaandika hili kujibu meseji kwa mke wake aliingia kwenye gari na alipofunga mlango wa gari na kuitupia simu yake kwenye dashboard tu alijikuta anabanwa shingo kwa nguvu na mtu mmoja tokea nyuma ya gari na kisha akazibwa pua na mdomo kwa mara moja kwa kitambaa cheupe naye hakuchukua raundi mara moja akaingia dunia ya kipekee, dunia ya giza totoro.


Watekaji walifanya kazi waliyohisi hapo kabla kuwa ingeweza kufanyika jioni ya siku hiyo lakini chini ya maelekezo ya Nasco kazi lifanyika muda wa saa nane na dakika kumi na saba mchana wa siku ya jumamosi katika maegesho ya Springfield Hard Times Café & Cue.


ENDELEA NA DODO ASALI…!


JUMATATU

EISENHOWER,WASHINGTON DC-MAREKANI

Eisenhower Executive Office Building, ofisi ya makamu wa Rais wa Marekani ni miongoni kati ya ofisi nyingi kubwa za kiserikali zinazopatikana katika jengo hili lililo eneo la West Wing, ikiwa yenyewe ndiyo ofisi maarufu zaidi, katika ofisi ya sekretari wa katibu wa ofisi ya makamu wa Rais asubuhi ya siku ya jumatatu aliingia kijana mmarekani mwenye asili ya Afrika na mara moja uso wake ukakunjua tabasamu pana.


“Mwanamke umewai ofisini au umelala hapa hapa?” Akauliza kijana huyu aliye ndani ya vazi aina ya suti rangi ya kijivu na tai ndefu rangi ya bluu aliyoivaa sambamba na shati jeupe, huku kitambulisho cha kazi kikining’inia usawa wa tumbo kamba zake zikiwa zimeenda na kuzunguka shingo.


“Likizo imekwisha bwana harusi kumbe ndiyo maana usiku niliota nakula ugali nilipostuka niko usingizini nikawaza huu ugali wapi ambapo uwa nakula, ndipo mara moja nikapata jibu uwa nakula nyumba ya mtu mtundu toka Afrika.. Hahahah hahahah lini tena umeingia WDC?” Akauliza dada wa kizungumrembo mwenye nywele ndefu nyeusi zilizomwagika pande zote za kichwa zikisogea mpaka katikati ya mgongo ambaye akiwa kavaa suti ya kike rangi inayofanana na rangi ya suti aliyovaa mgeni aliyeingia ofisini hapa na kwa mahali alipokaa ukipaona tu hautakosa jibu la haraka kuwa huyu ndiyo mwenye chumba cha ofisi hii.


“Ulikula ugali wa majini ya Washington.. Hahaha hahaa hahahaa unakubali kula ugali wa ajabu… Nimerudi alhamisi toka Afrika” Akajibu kijana huyu kisha akakaa tako moja la upande wa kulia juu ya meza na kufanya mguu wake wa kulia uwe umening’inia na wa kushoto ukiwa umekanyaga sakafu, mwili wake akaugeuza kuangalia alipo mwanamke anayeongea naye ambaye yeye alikuwa amesimama upande wa pili wa meza kilipo kiti chake akiendelea na kazi aliyokutwa akiifanya ya kupanga mafaili kadhaa vizuri.


“Khaaah! Majini ya kutoka Tanzania au Syria kwakina wifi, huku WDC hatuna mijini yenu ya sehemu hizo… Mambo vipi?”

“Wifi yako Syria hakuna majini na pia mbona yeye mwarabu wa Malaysia… Majini hayana mahali yapo mpaka nyumba za ibada yatakosa kuwepo nyumbani kwako, kitandani kwako unapolala… Mambo safi kabisa hofu kwenu tu niliwamisi sana”

“Hahaha!Kumisi, kumisi ofisi.. Khaah! Ndiyo maana umeingia kwa kuwai kazini si kawaida hii mpaka kuwe na ishu inayohusu wewe ndiyo uwa unawai, vipi baba?”

“Kwani vipi? Siruhusiwi kuwai ofisini, ebu achana na habari zingine maana wewe nakujua ukianza stori tutachanika hapa, habari za hapa? Habari za masiku tele?”

“Habari nzuri tu kazi ngumu sana kila siku inadhidi kuwa bora ya jana”

“Hellen anasema kazi imekuwa ngumu… Mmmh! Uzoefu wote na kukaa katika ofisi yenye kila kitu chenye kuleta urahisi kazini unasema kazi ngumu… Pole sana! Nimerudi kazini likizo yangu mliyopanga iishe ijumaa iliyopita ndiyo imeisha”

“Kwahiyo mimi sipati ugumu wa kazi kwakuwa mimi mzoefu hivyo siruhusiwi kulalamika kazi ngumu… Sawa bwana mkubwa, kaka mkuu…. Karibu kazini na pia hongera yangu ya moja kwa moja kwako bwana harusi na pia bibi harusi, natumaini mmemaliza salama fungate yenu na pia imani yangu mambo ya fungate yamelipa tutarajie damu ya kiafrika na kiarabu kutuletea motto mzuri miezi kadhaa ijayo..!”

“Kwa niaba ya mwenzangu ahsante sana na..!” Hakuweza kuendelea mlango wa kuingia ofisi hii ulifunguka na akaingia mwanadada mwingine wa kizungu akiwa katika mavazi aina ya suti ya kike lakini ikifanana na ambazo hawa waliokuwa wakiongea wamevaa na hii mara moja lilinifahamisha mimi mwandishi na mtunzi wa riwaya hii kuwa wafanyakazi wa ofisi hii siku hii ya jumatatu walitakiwa kuvaa suti za rangi hii.


“Agent Kai! Umelala Eisenhower?” Mwanadada aliyeingia akaongea punde tu alipotokeza uso wake kuingia ndani ya ofisi hii.


“Mnaona ajabu mimi kuwai au mnapenda kuuona uso wangu katika siku yangu ya kwanza kurudi hapa kikazi?” Akajibu aliyeitwa Agent Kai na mwanadada aliyeingia.


“Yaah! Watu mpaka walikuwa wanakuota mchana mchana.. aha haha hahaha… Karibu sana, karibu tena Eisenhower”. Akaongea mwanadada huyu aliyeingia mwenye nywele za blonde.


“Nimewai sababu natakiwa niongee kidogo na chifu kisha nije ofisini kwako tuongee ile ishu yetu halafu nitaenda ofisi ya makamu wa Rais nikamsalimu nikimaliza hayo yote ndipo nitaenda wasalimia walioko ofisini kwangu…!” Akaongea kwa haraka Agent Kai kisha akasimama toka pale alipo wakapeana mikono na yule aliyeingia.


“Natumaini kila kitu kimeenda sawa?” Akamuuliza huku bado wamekamatana mikono.

“Yaah! Kwa kweli kila kitu kimeenda nilivyohitaji na hata wewe ulivyohitaji, nimejua mengi zaidi”

“Ahsante Lizy… Wewe mtu hujawai niangusha.. Sawa acha nikawaone wengine katika ofisi zingine hili na wao nipate kuwasalimu na kuwajulia hali nikisubiri katibu awasili”. Akaongea Agent Kai akimtaja mwanadada aliyeingia kwa jina la Lizy na hii kuleta taswira kwetu mwanadada aliyefika hapa ni Elizabeth Robert au kwa kifupi kama tulivyoweza kumsoma katika mwanzoni alikuwa akikatiziwa kwa kuitwa ‘Lizy Roby’.


Agent Kai hakukaa kwa dakika nyingi zilizofuata pale ofisini kwa sekretari wa ofisi ya katibu mkuu wa ofisi ya makamu wa Rais ambaye alikuwa akifahamika kama chief executive of the vice president, aliondoka kwenda kwenye maofisi mengine ambako katika jengo hili kubwa na bora sana zilikuwa zikipatikana ofisi kubwa serikalini kama tatu hivi ukiacha ofisi kuu husika katika jengo hili ofisi ya makamu wa Rais.


Saa mbili na robo ilimkuta Agent Kai akiwa anagonga mlango wa ofisi ya katibu mkuu wa makamu wa Rais ambaye kimsingi ndiyo boss wake yeye katika ofisi hii ya makamu wa Rais, kuna wanausalama wengi wanaohusika na ulinzi wa makamu wa Rais na wasaidizi wake na hata yeye katibu mkuu, walikuwepo wanajeshi wa jeshi la Marekani wakihusika na ulinzi wa jengo husika na pia walikuwepo wanausalama wengi wa mashirika ya kijasusi ambao wanahusika na usalama viongozi wakubwa wa Marekani wakiongozwa na taasisi kuu inayoratibu mambo yote ya kijasusi katika nchi ya Marekani ‘National Security Agency’ (NSA) na hata shirika la kijasusi la‘Central Intelligence Agency’ (CIA) walikuwepo wakifanya ulinzi makini kwa viongozi wao mbalimbali.


Aliruhusiwa kupita naye bila hiyana akaingia ndani na mara uso wake ulipoonekana kwa mwanaume wa kizungu mwenye nywele zilizokuwa zina weusi baadhi ya sehemu na sehemu zingine zikiwa na weupe (mnvi).


“Karibu!!” Akakaribisha baada ya nyuso zao zikiwa ndani ya tabasamu murua na bashasha tele wanaume wa rika tofauti.


“Ahsante nimekaribia mheshimiwa! Habari za hapa kwa ujumla?” Akajibu ukaribisho aliopewa mkono wa kulia ukiwa umesogea mbele kuelekea ulipo mkono wa katibu wa ofisi ya makamu wa Rais, kwa kasi kama wanawaiana walikamatana viganja vyao na kwakuwa mara zote wakionana uwa na furaha tele mikono yao ilitikisana kama wanapimana ubavu.


“Habari za hapa nzuri kwa ujumla mambo yanaenda vizuri tu hakuna tatizo kiofisi ingawa ki nchi mambo ni mengi sana muda mdogo” Akajibu huku wakiwa wameshikana na wote wamesimama.


“Safi sana chifu, nimefurahi kukuona na nimefurahi kurudi tena kazini katika ujenzi wa taifa…!”

“Mimi pia nimefurahi sana kijana wangu umerudi salama salimini. Nafurahi umejilinda vizuri na maadui zako na wa taifa kwa ujumla… Habari za kifamilia nazo vipi?”

“Familia! Nashukuru Mungu wote wako salama si wa hapa Marekani na hata wale waliopo Tanzania kote Mungu anatulinda na kutupigania kwa namna ya kipekee kwa kweli anastahili shukrani zilizo kuu na wewe vipi mambo yako ya kifamilia wadogo zangu na mama yangu?”.

“Wako sawa pia… Tunashukuru hakuna tatizo na hata hapa Makamu wa Rais na wengineo katika kazi za hapa wako safi sana hakuna tatizo na ni jana usiku Makamu wa Rais alikuulizia wakati nilipokuwa nimemtembelea nyumbani kwake nikamjibu duru zinasema umerudi Marekani toka alhamisi na huko salama salimini”

“Sawa sawa chifu, nafahamu asubuhi unakuwa na mambo mengi ya kuyapitia hasa jumatatu kama ya leo zinahitajika sahini nyingi sana zinazokuhusu katika kupitisha na kuidhinisha mambo mbalimbali ya ujenzi wa taifa, hivyo naomba nikuache nielekee ofisni kwangu kuna mambo ambayo nahitaji kuyapitia na kama kuna lolote litaibuka linalohitaji muongozo wako haraka nitafika kukuona”

“Ni sawa mwanangu kama kawaida kwa taifa letu kubwa licha ya teknolojia ya hali ya juu tuliyonayo katika sekta mbalimbali bado mambo ni mengi sana na muda hautoshi… Baraka tele zikushukie katika siku yako ya kwanza kazini.. Ratiba yangu nitatoka kwenda kwenye kikao na makamu wa Rais kisha nitarudi hapa kuendelea na kupitia nyaraka mbalimbali za kazi”

“Kazi njema chifu!”

“Nawe pia kazi njema kijana wangu… USA kwanza!”

“USA kwanza!”


Agent Kai alitoka katika ofisi ya katibu wa ofisi ya makamu wa Rais na moja kwa moja akaingia kwenye lifti iliyompeleka hadi kwenye flour (losheni) ilipo ofisi kuu ya kitengo cha Tehama upande wa ujasusi ofisi ya makamu wa Rais, lift ikamfikisha akashuka na kuingia korido pana ambayo ilimpeleka mlango wa mkuu wa kitengo hiki akagonga hodi kwa kubonyeza kitufe chenye kazi hiyo.


Mlango ukajifungua kuashiria kashaonekana na walioko ndani ya ofisi hivyo wakamruhusu kiteknolojia kwa kuamrisha mlango huu wa vioo kufunguka naye Agent Kai akapita na kutokea kwenye ofisi pana sana yenye watu wengi wake kwa waume wengi wakiwa ni vijana walio katika mavazi yanayofanana na kila mmoja alikuwa bize akishughulika na kompyuta zao zilizo katika meza zao zilizojipanga pahala mbalimbali, wapo walioinua macho kumtizama na wengine waliendelea kuwa makini na wanachokifanya katika shughuli husika.


Kuna walio msalimia kwa kupunga mkono maana wengi wao walikuwa wakimjua yeye ni nani naye aliwajibu kama inavyotakiwa huku tabasamu likiwa limeweka makazi kwenye viunga vya uso wake mujarabu.


Kwakuwa alikuwa akijua wapi anatakiwa aelekee alipita kando kando ya meza za hapa akasonga mpaka alipoifikia korido ambayo alipokun ja hili asongeshe nayo akakutana na mlango wa kioo lakini unaomuonyesha vizuri aliyeko ndani akiwa katulia bize kwenye meza ya kiofisi akitumia kompyuta yake katika kumsaidia yale anayoyafanya katika wakati huu.


Agent Kai hakugonga hodi hapa bali aliusukuma mlango na kuingia ndani na ndipo mwenye ofisi akainua uso wake kumuangalia ambao haukuweza kuvumilia ukafungua tabasamu murua kufurahia ujio wa Kai pale ofisini kwake.


“Karibu sana mwanaume wangu wa zamani uliyeninyima fursa ya mimi kuwa nawe ndani ya ndoa nikiufurahia ushababi wako, roho mbaya tu!” Akaongea kwa matani mwenye ofisi na wote wakaangua kicheko wakisaidiza mikono yao kuziba midomo hili sauti isiende mbali.


“Mara ngapi nilisema nataka kukuoa ukakataa, ukasema unataka mimi nibadili dini niwe mkristo ndipo nitaweza kukuoa, basi mi nikaona hauko siriasi na uhusiano wetu… Akatokea aliyeona umuhimu wangu kanipa moyo wake nimempa wangu acha tufurahie raha ya ujana wangu wa mwisho mwisho…!” Akajibu Agent Kai wakacheka tena vicheko vilivyogongana tena na wakagonga viganja vyao ‘pwaaah’ vikishinikiza kwa vitendo na papo hapo mgeni akavuta kiti cha mgeni kilichopo ndani ya ofisi ile na akakaa.


“Na kweli ujana wa mwisho mwisho… Ndoa ya ngapi hii?”

“Acha upuuzi, ndoa ya ngapi wee ya nini?”

“Basi mwanaume wewe sikuwezi kwa ubishi wako wa kuuliza swali kwenye swali yote hayo unajiona kama unawahoji washindani wako katika duru za kazi zako”

“Ndiyo unatakiwa uachane na stori zisizo na msingi maana jana nilimaliza kila kitu nilivyokuja kwako… Lete habari, umesema umejua mengi nataka kujua upande wako umejua mengi yapi?” Akaongea Agent Kai akimalizia kwa kuhoji swali.


Hapa alikuwa amekuja ofisi ya Tehama upande wa ujasusi katika ofisi ya makamu wa Rais ambao wako chini ya katibu wa makamu wa Rais, mwanadada Elizabeth Robert ndiyo alikuwa akiongoza kitengo hiki katika masuala yote makuu akiwaunganisha na walioko makao makuu ya CIA yaliyoko mji wa Langley huko jimbo la Virginia.


“Nilivyopata nafasi jioni ya jana niliweza kuanza uchunguzi na kuifuatilia namba kwa umakini ikiwemo na kui trak katika mawasiliano yake hasa mawimbi ya sauti ikanisumbua sana lakini baadaye kidogo niliweza kuchunguza kwa umakini meseji za e-mail alizokuwa anatuma na kutumiwa kwakuwa kabla hujaondoka uliona mwenyewe nilivyofanikiwa kudukua namba za siri za e-mail yake, nilicheza sana nikaona kuna ugumu katika kuiona wapi hasa tunaweza kuiweka kwenye rada zetu kimsaada zaidi, nikaweza fanikiwa hilo baada ya kuomba msaada kwa mtu aliye idara ya usalama wa taifa ya Mexico ‘MIA’ Ni rafiki yangu hivyo nilimcheki kwa simu nikamuelekeza namba nayotaka taarifa zake akaifutilia kwenye mtandao husika wa simu huko waliweza muibia namba ya simu inatumika katika simu ya aina gani akanitumia nilipoipata nikawacheki kampuni waliotengeneza ile simu ndipo nikaweza iweka katika mfumo wangu shika ipad uione jinsi nilivyo i track na kuingilia maongezi yake toka jana usiku akipiga na kupigiwa maongezi yana jirekodi nayakuta ni mwanamke… Leo asubuhi mpaka sasa hajapigiwa simu wala kupiga ingawa usiku aliongea sana kwa simu na watu tofauti tofauti zaidi ya wanne jina alilosajilia laini ya simu anaitwa Valentina Moschi, nikapekua kumtafuta ni nani hasa na kukutana na majibu yasiyo na majibu kamili katika mahitaji yetu” Alitoa maelezo marefu mwanadada Lizy Roby huku wakitazamana bila kupepesa macho na rafiki yake, swahiba yake na ndugu yake wa kazi za kazi ambaye wakiwa kazini uwa wanatulia wakifanya mambo licha ya mautani kwao uwa ni kawaida sana.


“Umefanya kazi nzuri sana Lizy, ulipofikia ni parefu sana ingawa naamini kwa ulivyo una mahala umefika zaidi, endelea nijue wapi umefika” Akatoa pongezi Agent Kai kisha akajiweka vizuri kitini.


“Laini kama tulivyoona awali kuwa imesajiliwa nchini Guatemala lakini jina lililotumika kusajili laini haliko katika rekodi za watu wa eneo husika ndicho kinachonichanganya ndugu yako mpenzi wangu.. Kwakuwa ilikuwa ni usiku sana wakati namaliza kufuatilia hili nikaishia katika kutafuta jina hili la nani haswa? Na kwanini halipo katika orodha ya wakazi wa Guatemala? Na pia walisajili vipi jina tu hakuna picha ya msajiliwa laini si kawaida hii!”


Mwisho wa sehemu ya thelathini na nne (34)


Kazi imerudi Marekani!

Kazi imerudi ndani ya Marekani na kumleta tena jasusi wa CIA kutoka kitengo cha siri cha ndani ya idara ya shirika hili la kijasusi, kitengo kifahamikacho kwa jina la Special Activities Division (SAD).


Mipango bado inaendelea ya kuichunguza barua pepe iliyotumwa kwenye sanduku la barua pepe la Agent Kai.


Lizy Roby mkuu wa kitengo cha Tehama ndani ya ofisi ya katibu mkuu wa makamu wa Rais upande wa ujasusi anaendelea kufafanua kile alichoweza kuking’amua yeye kama yeye akikifikisha mazima kwa Agent Kai.


Nini kitafuata?



Hapa alikuwa amekuja ofisi ya Tehama upande wa ujasusi katika ofisi ya makamu wa Rais ambao wako chini ya katibu wa makamu wa Rais, mwanadada Elizabeth Robert ndiyo alikuwa akiongoza kitengo hiki katika masuala yote makuu akiwaunganisha na walioko makao makuu ya CIA yaliyoko mji wa Langley huko jimbo la Virginia.


“Nilivyopata nafasi jioni ya jana niliweza kuanza uchunguzi na kuifuatilia namba kwa umakini ikiwemo na kui trak katika mawasiliano yake hasa mawimbi ya sauti ikanisumbua sana lakini baadaye kidogo niliweza kuchunguza kwa umakini meseji za e-mail alizokuwa anatuma na kutumiwa kwakuwa kabla hujaondoka uliona mwenyewe nilivyofanikiwa kudukua namba za siri za e-mail yake, nilicheza sana nikaona kuna ugumu katika kuiona wapi hasa tunaweza kuiweka kwenye rada zetu kimsaada zaidi, nikaweza fanikiwa hilo baada ya kuomba msaada kwa mtu aliye idara ya usalama wa taifa ya Mexico ‘MIA’ Ni rafiki yangu hivyo nilimcheki kwa simu nikamuelekeza namba nayotaka taarifa zake akaifutilia kwenye mtandao husika wa simu huko waliweza muibia namba ya simu inatumika katika simu ya aina gani akanitumia nilipoipata nikawacheki kampuni waliotengeneza ile simu ndipo nikaweza iweka katika mfumo wangu shika ipad uione jinsi nilivyo i track na kuingilia maongezi yake toka jana usiku akipiga na kupigiwa maongezi yana jirekodi nayakuta ni mwanamke… Leo asubuhi mpaka sasa hajapigiwa simu wala kupiga ingawa usiku aliongea sana kwa simu na watu tofauti tofauti zaidi ya wanne jina alilosajilia laini ya simu anaitwa Valentina Aurelia Moschi, nikapekua kumtafuta ni nani hasa na kukutana na majibu yasiyo na majibu kamili katika mahitaji yetu” Alitoa maelezo marefu mwanadada Lizy Roby huku wakitazamana bila kupepesa macho na rafiki yake, swahiba yake na ndugu yake wa kazi za kazi ambaye wakiwa kazini uwa wanatulia wakifanya mambo licha ya mautani kwao uwa ni kawaida sana.


“Umefanya kazi nzuri sana Lizy, ulipofikia ni parefu sana ingawa naamini kwa ulivyo una mahala umefika zaidi, endelea nijue wapi umefika” Akatoa pongezi Agent Kai kisha akajiweka vizuri kitini.


“Laini kama tulivyoona awali kuwa imesajiliwa nchini Guatemala lakini jina lililotumika kusajili laini haliko katika rekodi za watu wa eneo husika ndicho kinachonichanganya ndugu yako mpenzi wangu.. Kwakuwa ilikuwa ni usiku sana wakati namaliza kufuatilia hili nikaishia katika kutafuta jina hili la nani haswa? Na kwanini halipo katika orodha ya wakazi wa Guatemala? Na pia walisajili vipi jina tu hakuna picha ya msajiliwa laini si kawaida hii!”


ENDELEA NA DODO ASALI..!


JUMATATU

EISENHOWER, WASHINGTON DC-MAREKANI

“Okay! Nimeelewa ugumu upo kwa kuipata picha ya mwanadada huyo na laiti tungeipata nafikiri ingeturahisishia kuona uhusika wake ndani ya uso wake maana tungeweza search kwenye google mfanano wa picha kama mara nyingi tunavyoweza kufanikisha katika hili… Ila kingine nafikiri tracking ya mawimbi ya simu zake na hao anaoongea nao inaweza kutufanikishia kumpata yeye au mwingine mwenye kutuwezesha kumpata yeye” Akaongea Agent Kai na kisha kuwasha ipad yake ambayo toka anaingia ndani ya ofisi hizi ilikuwa ndani ya begi dogo la kushikwa mkononi ambalo uweka vitu mbalimbali vya msaada wa kazi zake ndogondogo.


“Huko sahihi kabisa… Kingine nashauri tusimpigie kabisa simu sababu akizima hii simu hatutaweza kabisa kufanikisha lolote lile katika kumsaidia Jogre… Hivyo tutumie maongezi ya simu aliyoyafanya ambayo nimeyanasa usiku naamini mtu mwenye mishe za kiuhalifu katika simu nne au tano alizopigiwa haiwezekani kusiwe na simu ambayo itatupa majibu husika kati ya ambayo yanaweza kuwa mwanga kwetu” Akaongea Lizy Roby huku akiendelea kuunganisha nyaya mbalimbali toka kwenye laptop yake kuja kwenye ipad ambayo ilikuwa imeungwa kufuatilia mawasiliano ya simu ya msajiliwa wa laini iliyotumika kutuma barua pepe kwa akaunti ya barua pepe ya Agent Kai.


“Lizy ndiyo maana uwa sijutii kukufahamu… Najua wapi umekwama, najua uwezo wako kwenye lugha ya kilatin ambayo huyo mwanadada anatumia, fungua hizo audio tuzisikilize kwa pamoja”


Lizy Roby alifungua audio za maongezi ya simu alizokuwa amepigiwa mwanadada ambaye walivyofuatilia laini yake katika mamlaka za mawasiliano za Guatemala ilikoonekana ndipo laini ilisajiliwa ilikutwa imesajiliwa kwa jina la Valentina Aurelia Moschi.


Audio zile zilisikilizwa vizuri tena kwa kurudia rudia hili kila mmoja aelewe vizuri wakienda kwenye ufafanuzi wafafanue kwa pamoja vizuri na kwakuwa Agent Kai yeye ndiyo alikuwa akijua zaidi kilatini kuliko Lizy Roby aliweza kumfafanulia kila jambo kwa usahihi na katika maongezi ya simu zile waliweza kung’amua simu mbili ambazo ziliweza kuwajuza mengi katika harufu ya uhalifu wa mwanadada anayewasumbua kutaka kumjua zaidi.


“Namba za laini ya simu iliyopigwa na mwanaume wa kwanza kabisa na mazungumzo yao nahisi huyu mwanamke yupo katika shughuli au malipo ya magenge anayoyafanyia kazi, maana mpigaji wa simu ameeleza kuwa kuna mtu anatakiwa amfuatilie na ahakikishe amapotezi hata mara moja katika kila nyendo anazofanya na mtu huyo jina lake limetajwa moja kuwa anaitwa Mr. Valdez, hii ni simu muhimu sana kwa kweli hivyo ni kuifuatilia hii namba zaidi tumjue ni nani? Kazi ni kwako sasa Lizy Roby..!”

“Sawa acha nifanye udukuzi kidogo katika kampuni ya simu iliyosajiliwa hii namba, nipe dakika kadhaa kidogo” Lizy aliomba aifanyie kazi namba waliyoamua itakuwa ya kwanza wao kuichunguza.


Zilifika dakika zipatazo kumi na tano ndipo Lizy Roby alipoweza kufanikiwa kuingia katika orodha ya majina waliosajiliwa kampuni ya simu iliyosajili namba ambayo ilitumika kupiga kwa mwanadada ambaye kwao alijulikana kuwa jina lake ni Valentina Aurelia Moschi.


Namba ile iliingizwa katika mfumo na kuanza kusachi hili kuleta mfanano na ndipo ilipokubali na kuonyesha mmiliki wa namba ile anaitwa Sergio Jesus na hata picha yake ilikuja alikuwa ni mwanaume mwenye sura ambayo ukiiona kwa ghafala unaweza kustuka sana maana ungeweza kusema pengine umekutana na mchezaji wa timu ya mpira wa miguu inayopatikana viunga vya Cataluhna, jiji la Barcelona nchini uhispania, walifanana haswa haswa na mshambuliaji machachari mchana nyavu mashuhuri Luis Suarez kila kitu ama kweli duniani wawili wawili, hadi meno ya juu kwenda offside basi huyu mtu aitwaye Sergio Jesus alikuwa kama ameamisha mdomo wa Suarez kuuleta kwake.


“Copy picha haraka haraka itumbukize kwenye mitandao ya kijamii tuone kama yaliyomo yamo… Ila kwa kweli leo nimeamini msemo wa duniani wawili, hii sura ni Luis Suarez kabisa… Dah!”

“Luis Suarez ndiyo nani?”

“Mmmh! Nilijua naongea na mjua soka kama mimi”

“Luis Suarez ni mcheza soka?”

“Ndiyo! Mchezaji wa timu moja kubwa huko ulaya inaitwa Barcelona… Sasa jamaa picha yake imepeleka kila kitu katika sura pengine ni plastic surgery maana si kwa mfananano huu” Akafafanua Agent Kai huku akiitizama vizuri picha ambayo kwa sasa alikuwa kashaiamishia kwenye ipad yake.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog