Simulizi : Nitakuua Mwenyewe
Sehemu Ya : Pili (2)
Mzee Jonathan alipigwa butwaa.
"Hatuna jeuri ya kufanya chochote lile kundi ni kubwa na hatujui wamejipangaje?"
Masanja aliwasihi wenzake kutofanya chochote.
"Jamani ee hapa ni kuangalia usalama wetu kwanza."
Mzee Jonathan alianza kutimua mbio huku akiwaambia wenzake waokoe roho zao.
"Au tuwashambulie nini kwani huko tuendako hatukujui mwisho wa siku tutakamatwa tu."
Black alitoa wazo baada ya kuona hakuna uwezekano wa kutoka eneo hilo.
Wananchi waliokuwa wamelizunguka gari walisogea ndani ya yale makaburi na wengine kusalia pale kwenye gari hii ni mara baada ya kuona hawatokei washukiwa wao.
" Vijana wangu muwe makini maana hao jamaa hatuwajui vizuri."
Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa kijiji cha Lupa mzee Kaaya na ambaye ndiye baba mzazi wa Robinson aliwasihi vijana wake kuchukua tahadhari.
"Bila shaka mzee usiwe na mashaka." Alijibu kijana mmoja ambaye alikuwa karibu yake.
"Jamani njooni muone viatu vyao vimepita huku." Aliwaita yule kijana ambaye aliwakimbia wakina mzee Jonathan.
Wote walielekea kule kuangalia zile alama za viatu ili kujua zimeelekea wapi na baada ya kuziangalia wakajua hawa watu wako ndani ya makaburi yale au nje kimsitu kinachoelekea mtoni.
" Kwenye gari msiondoke wote wengine wabakie." Mzee Kaaya alitoa tahadhari baada ya kuona wote wanakimbilia kwenye zile alama.
Vijana walisambaa kwenye maeneo yale kuhakikisha wanawatia mikononi wahusika. Makaburi na msitu huo ulivamiwa na kundi hilo ambalo lilikuwa na zaidi ya watu mia moja.
" Wameelekea huku jamani nyayo zao zinaenda huku."
Mmoja aliwaita wenzake baada ya kuziona zikielekea eneo la mto Lupa.
"Jamani hivi tutatoka salama kweli?" Mzee Jonathan alionesha hofu yake baada ya kuona kundi lile likija nyuma yao.
"Tutatoka tu mzee kikubwa uwe na pumzi ya kutosha ya kukimbia." Masanja alimtia moyo mzee Jonathan.
"Inaonekana hawa watu walishajipanga kuwakamata watu wote watakaogusia familia ya mzee Fikirini kutokana na kutambua azma ya yule kijana Surambaya ambaye aliuwawa kwa kuchomwa moto na jeshi la polisi kisha kutoa taarifa zangu kama mtuhumiwa namba moja." Mzee Jonathan aliongea hayo baada ya kukutana na ukinzani ambao hakuutarajia kabisa.
" Mzee huu si muda wa kujilaumu tupambane kuhakikisha tunatoka eneo hili."
"Ni sawa usemayo Masanja lakini huku tuendako unakufahamu?"
"Sikufahamu ndiyo lakini hatuna jinsi kwani gari limetekwa hivyo tutafute njia mbadala kutoka."
Masanja aliendelea kufafanua.
"Oya ee tupiteni njia hii nimeifuatilia mpaka kule mbele inatoka nje."
Black aliingilia maongezi yao.
"Vizuri tuwahini kabla hatujatiwa mikononi jamani na tukitoka salama sitaki tena kuendelea na zoezi hili ni kurudi nyumbani nikajue la kufanya."
"Mzee Jonathan ulianzaje mambo haya ilhali unakiroho cha chipsi yao?"
Masanja alimcheka wakati akimkongoja kwa kumshika mkono.
"Weee usicheze na uhai hujui siku zote huwa tunapanga mipango kwa kuangalia upande mmoja tu bila kujua upande wa pili umejiandaaje."
"Ni kweli kabisa mzee Jonathan."
"Acheni stori nyinyi nitawaacha ohooo."
Black aliwatishia baada ya kuona wenzake mwendo hauridhishi.
"Tunajitahidi sana sema tu basi." Masanja alijitetea.
Baada ya kuona wanazidi kusonga tu mbele bila mafanikio waliamua kugawanyika na wengine kurudi tena mpaka barabarani ambako waliamua kuweka vizuizi uelekeo wa Mbeya na ule wa Tabora kuhakikisha wanawatia nguvuni na
zoezi hilo likikabidhiwa kwa Jilanga ambaye ndiye aliwakimbia na kwamba amewakariri muonekano wao.
***
Wakiwa wamejipumzisha mara mlango ulifunguliwa na kuingizwa chombo ambacho kilikuwa na chakula. Na kisha mlango ulifungwa tena, waliinuka na kukichukua chakula na muda huu hawakuwa na minyororo tena. Ila tu mawazo yalikuwa bado kwa mwenzao Jackline ambaye fahamu zilikuwa hazijamrudia.
"Tuwaite tuwajulishe kuwa mwenzetu hajaamka bado watupe msaada." Jessica alishauri.
"Haiwezekani hiyo Jessica kumbuka wao ndiyo wamesababisha hayo na huyu huyu ndiye aliyewatia huzuni kwa kuwaua wenzao halafu tuwaambie kuwa tunaomba msaada wa tiba si watakwenda kumuulia mbali?" Robinson aliweka upinzani kwenye hilo.
"Ni kweli lakini itakuwa ngumu hapa tukomae nae tu mpaka asubuhi muujiza utakuwa umetokea." Jasmine aliunga mkono.
Hivyo walijongea kwenye chakula, katika kufunua funua vyombo vilivyokuwa vimeletwa pale walikutana na kikaratasi kilichokuwa na maandishi.
"HILO BIRIKA LINA DAWA MNYWESHENI MGONJWA NA NYINGINE MKANDENI MAENEO YENYE VIDONDA."
"Jamani oneni maajabu sijui ni nani aliyefanya haya."
"Tuweni makini isije kuwa ni sumu akanywa ikawa ndiyo kwa heri." Jessica alionesha wasiwasi juu ya dawa hiyo.
"Hapana ngoja tufanye kama ilivyo huoni watu ambavyo walimkubali pale nje hivyo nadhani kuna mtu kaonesha kuguswa na majeraha yake jamani." Robinson alipinga wazo la Jessica.
Jasmine alichukua ile dawa na kuanza kumfanyia tiba Jackline na nyingine wakimnywesha. Na walipo hakikisha kila kitu kiko sawa walichukua mihogo kiasi wakamuwekea pembeni akizinduka ale na mingine walikula wao.
" Jackline akiamka tu tunaanza mchakato wa kupanga namna kutoka humu nimeguswa na moyo wake inatakiwa tuungane naye." Jasmine aliwaambia wenzake juu ya kuguswa kwake na Jackline.
"Hilo neno ndugu zangu na kwanza mpaka hapa naona kuna kila dalili ya kupata msaada." Aliongeza Jessica.
Wakiwa wanaendelea na mazungumzo yao mara walisikia kama ukuta unagongwa hivi.
"Nini hicho?" Jasmine aliuliza.
"Sijui ni nini?" Jessica alijibu.
"Hebu tulieni kwanza." Robinson alinong'ona huku akiinuka na kusogea pale ambapo palikuwa panasikika kugongwa ili kuchungulia ni nini.
Kabla hata hajajua kipi kinaendelea mara aliona kijikaratasi kikipenyezwa kupitia kijitundu kilichotobolewa. Robinson alikivuta na kukifungua.
"MGONJWA AKIPATA NAFUU MSIFANYE CHOCHOTE JIFANYENI WAJINGA ILI MKUU AJIONE MSHINDI AKIONA HIVYO ATAJUA MUMEINGIWA UOGA HIVYO ATAWAPA KAZI ZA NJE KAMA SISI NA HAPO NDIPO TUTAWAUNGA MKONO KWENYE MPANGO WA KUTOKA HUMU KUNA NJIA RAHISI YA KUPITA HATA SISI TUMEUMISS UHURU."
Baada ya kukisoma alimpatia Jasmine ambaye naye alipokisoma alitikisa kichwa kama kukubaliana na kilichoandikwa.
" Kuna sababu hapa Robinson, hebu tufanye kama kimemo kinavyosema then tutajua cha kufanya kwa kushirikiana na huyu mtuma vimemo ambaye hatujamfahamu mpaka sasa."
"Uko sawa kabisa, hebu tutulie ili tuyasome mazingira ambayo yatatuonesha njia ya kutoka au kubaki." Robinson aliunga mkono hoja ya Jasmine.
"Jamani mpaka hapa naiona njia ya kutoka tayari lakini pia msisahau kuwa kuna watu wanakuja nyuma yetu kututafuta."
Jessica aliunga mkono lakini pia aliwakumbusha jambo wenzake.
Nini kitatokea?
USIKOSE KUSOMA SEHEMU INAYOFUATA KUJUA KILICHOENDELEA.
"Jackline na wewe bado tu huamki au tulipewa magumashi na si dawa?"
Robinson aliuliza baada ya kuona Jackline haamki.
"Na nguo zilivyotapakaa matope utafikiri mdoli? Kweli huku ni jehanamu hivi kweli? Lazima tumpe somo mzee Bruno."
Jasmine aliapia wakati akimuangalia alivyolala pale chini na mitope yake.
"Nuru yaja muda ambao giza litakimbia na kulipisha jua huku mwezi ukiwa pembeni umeishiwa nguvu."
Jessica alijipa matumaini kwa msemo wa washairi wa mashariki ya kati.
Wakati bado wakitegemea miujiza ya Mungu kuweza kumzindua Jackline mara alifungua macho na kuwatazama kwa awamu.
" Vipi mpinzani wangu kapotelea wapi? Au anadhani ameshinda la hasha nilikuwa nakusanya nguvu tu, niko tayari sasa."
Maneno ya Jackline yaliwaacha vinywa wazi yaani pamoja na yote yaliyomtokea lakini bado hesabu zake zilikuwa pale pale kushinda mpambano. Na ndiyo maana waswahili hunena kuwa tutaendelea tulipoishia na ndivyo ilivyokuwa kwa Jackline.
" Jipumzishe kwanza love' bado una maumivu."
Robinson alimsihi Jackline.
"Robinson mpenzi wangu nina hasira na wanyama wale au ninyi mmefurahia? Hata tufanye nini wapenzi sisi ni wa kufa tu sasa tunaogopa nini si bora tufe tukijaribu kuliko...."
"Jackline hatujafurahia kwa kilichotokea wala hatujabweteka bado mipango inaendelea na labda nikuhakikishie kuwa hafi mtu kati yetu tutatoka salama kabisa."
Jasmine aliamua kumuondoa wasiwasi Jackline.
"Nawaona si wale ambao tulipambana kwa nguvu zetu zote kule Belem ni kama mmeingiwa hofu hivi hamuoni mwenzenu pamoja na maumivu ya mkono lakini sijakata tamaa napambana.." Alianza kulia kwa kwikwi kitendo kilichowafanya na wenzake kuingiwa na uchungu wa hasira na kuanza kulia. Hakuna aliyemnyamazisha mwenzake si Robinson ambaye ndiye angekuwa kinara kwa wenzake wala Jasmine wala Jessica kila mmoja alikuwa akilia kwa hisia kweli kweli.
"Ila ninaamini bado tuna nafasi ya kutoka humu kwa wakati."
Jackline aliendelea kuwapa moyo wenzake.
"Jackline kwenye hili hatuko peke yetu." Jessica alimwambia Jackline.
"Hatuko peke yetu? Kivipi Jessica."
"Dada hebu mpeni zile jumbe azisome mwenyewe tusije ongeza hata chembe ya neno."
Vile vikaratasi vikaletwa na kumkabidhi avisome vyote kuanzia kile cha dawa mpaka kile cha wao kutofanya kitu chochote, baada ya kuvisoma alishusha pumzi kwa nguvu kama vile alikuwa kabeba zigo kubwa na alikuwa kalitua.
" Mmevipata wapi hivi vikaratasi?"
"Hatuna jibu kwani vilikuja kwa awamu hicho cha maelekezo ya dawa kilikuja pamoja na chakula, we Jessica mletee hiyo mihogo aendelee kuua njaa baada ya kuwashindwa wale washenzi."
Wote waliangua kicheko baada ya Jasmine kukumbushia mtanange uliomfanya Jackline kuzimia.
" Washukuru Mungu walinivizia angekuja mmoja mmoja ndiyo wangenijua mimi ni nani weupe kabisa wale pale walinizidi ndevu tu zilizokosa matunzo, ngoja nishibe kwanza."
"Wewe pata tu, we Robinson si umlishe mgonjwa jamani?"
Jessica alimtania Robinson.
"Kama hanioni vile, hivi ningekufa ingekuwaje Robinson?"
"Ningelia sana na mwisho ningekufa na mimi ili kukufuata huko huko si ninasikia kuna maisha mazuri kuliko huku na ndiyo maana wafao wote hawarudi kutupa taarifa za huko."
"Usituvunje mbavu zetu Robinson, toka lini mtu aliyeoza aishi tena? Usione aibu we sema tu baada ya maziko ungenioa mimi ama?"
Jasmine alitania kidogo.
"Ngumu sana hiyo kutokea eti."
"Natania tu jamani, huko nje pilika zimeanza inawezekana kumepambazuka tayari."
"Hebu Jessica zima hilo litaa linatuletea kiwingu tu."
Jackline aliongea akimalizia kula mihogo.
"We Jackline hapa ndipo kikaratasi cha pili kilipitishwa."
Jessica alimuonesha alipokuwa akizima taa.
"Hivi watakuwa ni wakina nani hao au ni walinzi iweje vikaratasi vipenyezwe wakati huko nje kuna walinzi kila kona na pia angalieni hata chakula kililetwa na mlinzi."
Walitazamana kama kuna picha wanaivuta hivi mara baada ya Jackline kuongea maneno juu ya walinzi.
" Jackline uko sahihi hata mimi naanza kupata shaka juu ya hawa walinzi." Jasmine aliongea kama kuungana na Jackline..
" Kwa hiyo mnataka kusema kuwa hapa kuna kila dalili ya kuchezewa mchezo siyo?"
Robinson aliuliza.
"Roby yote yanawezekana kikubwa ni kuwa makini tu."
Jessica alimjibu.
"Hivi ndani ya hili Jehanamu kuna kuoga kweli maana si kwa uchafu huu utafikiri kinyago cha Kimakonde jamani?"
"Bora umesema mwenyewe yani hapa tulikuwa tukikuangalia ulivyo tunajichekea wenyewe muda mwingine tunalia mpaka basi ila nafikiri kama wanaubinadamu watafanya jambo tu."
Robinson alijibu jibu ambalo mwanzo lilitaka kuharibu hali ya hewa lakini aliiona hiyo akabadilisha gia juu kwa juu.
" Bahati yako Love ningekuchenjia hapa yaani usingeamini hata chembe."
Mara mlango ulifunguliwa na mlinzi mmoja aliingia ndani mle na kuwasabahi. Na kisha kufikisha kilichomleta mle ndani.
"Habari yenu wageni wetu."
"Kikubwa kumekucha ndugu yetu."
Robinson alijibu.
"Ndani ya Ngome ndivyo kulivyo hakuna anayeishi maisha ya raha zaidi ya mkuu mwenyewe tofauti na hapo wote ni tabu tupu."
"Daa itabidi tuzoee tu bwana mkubwa."
Jessica alijibu baada ya kusikia maelezo ya mlinzi.
"Nisipoteze muda nifikishe kilichonileta ndugu zangu."
"Bila shaka afande uwanja ni wako."
Jackline alijibu akiinuka kutoka pale alipokuwa kakaa kitendo ambacho kilimfanya mlinzi ausogelee mlango kwa tahadhari.
"Brother mbona unarudi nyuma natisha eee?"
"Ha-hapana dada kawaida tu."
"Basi ukienda kwa bosi wako mwambie wale wageni wanaomba maji ya kuoga na kama kuna vinguo vya kuvaa ili nguo zetu tufue."
"Mkuu katoka na kaagiza kuwa mnatakiwa kutoka kuna chumba kina nguo maalum mtachagua zinazowatosha ni sare kama muwaonavyo wengine nje na hizo zitafuliwa na watu maalum kwa kazi hiyo."
"Samahani kaka unataka kutuambia kuwa tumeshasajiliwa kuwatumikia?"
Robinson ilibidi aulize baada ya kuchanganywa na maelezo ya mlinzi.
"Hapana brother si hivyo huwa tunafanya hivyo kama njia ya kujilinda na pia ni sheria ya nchi kuwa eneo lolote linalozalisha bidhaa fulani lazima wafanyakazi wake wawe kwenye sare maalum."
"Unaposema kujilinda unamaanisha nini? Samahani kwa maswali mfululizo inawezekana tunakuuliza wewe si mhusika lakini unaweza kutuibia tu."
Jackline alimtupia swali.
Ilikuwa ni asubuhi ya saa kumi na mbili lakini mlinzi alitoa tambala sijui ni maalum kwa kujifutia au ni kinguo kilikatwa tu sehemu fulani na kujifutia jasho ambalo lilianza kuushambulia uso wake.
" Niliposema kujilinda ni kwa upande wenu ninyi kwani mkiwa tofauti na sisi humu itakuwa rahisi kuhisiwa na kudakwa na maadui zenu."
"Aisee kwa hiyo mmeshapewa taarifa kuwa tumefanya nini tulikotoka?"
Jessica alionesha hofu alijua suala lao linajulikana kwa mzee Bruno tu kumbe liko nje tayari.
"Jana baada ya mpambano ule alituita walinzi wote na kutueleza kuwa tusitarajie kupambana na ninyi hata kidogo kwani Ngome ya Santana mmeishinda hivyo kwetu hapa ni ngumu zaidi ya kuwasaidia tu kwa muda wote mtakaokuwa hapa japo shughuli za humu ndani mtazifanya kama kawaida ila tu mtakuwa sehemu maalum ya kulala tofauti na sisi mzee atawakabidhi akirejea."
"Okay tumekupata kidogo afande najua mengi atatueleza mwenyewe mkulu."
Jackline alimkatisha.
"Kingine kasema kama mna simu nipeni nikaziweke sehemu maalum ambayo ni ngumu kwa adui zenu kuzitraki kirahisi."
Hawakuwa na jinsi zaidi ya kutoa simu zao na kumkabidhi kisha walitoka naye nje kwa ajili ya kupewa utaratibu wa mle ndani.
******
sultanuwezo.com
"Chude nipe ripoti fasta."
"Bosi yaani tumezunguka sana lakini hakuna hata dalili ya harufu yao."
"Mko eneo gani?"
"Bado tuko ndani ya mji tunafanya oparesheni kwenye nyumba za kulala wageni pamoja na mahoteli."
"Chude huna akili chizi langu yaani mko ndani mji tena kwenye majumba ya kulala wageni? Ni wajinga kiasi gani mpaka wawepo ndani ya mji kwani wao hawajui kuwa wanatafutwa na jeshi la Ulinzi?"
"Bosi tuliamua kuanzia huku kwanza ili tukitoka nje ya mji tusiwe na mashaka yoyote."
"Okay wewe si ndiyo mwenye zoezi eeh ratiba imekaaje?"
"Baada ya hapa tunaingia kwenye maeneo yote yanayouzunguka mji mfano kwenye mashamba ya maua na maeneo mengine ikiwa ni pamoja na kwenye makazi yasiyo na wakaaji kule kaskazini."
"Vizuri lakini kama ambavyo nilikuambieni nawataka hao kabla hawajatiwa mikononi mwa jeshi."
"Mkuu tuamini majibu utayapata."
Simu ilikatwa na zoezi likaendelea kama lilivyokuwa kabla ya simu ya mkubwa wao Santana.
"Ila boss wetu na yeye anachukulia poa zoezi hili."
Mmoja wa vijana wake aliongea baada ya Santana kukata simu.
"Si unamjua mkuu wako, starehe zake zinatutesa sisi na kipindi kile niliwahi kumshauri juu ya shemeji yetu lakini wee nilikoswa ya kichwa?"
Chude alijazia maneno yale ya mwenzake.
Wakiwa wanaendelea na maongezi yao huku wakiendelea na matembezi mara simu ikaita tena.
" Bosi karudi tena mzee."
"Msikilize anasemaje."
Kisha aliipokea simu ya Santana ili kujua anasemaje.
"Chude hakikisheni washenzi hao wanapatikana iwe wazima au wafu ila ningependa zaidi wafike kwangu wakiwa wazima ili mkono wangu ndiyo uwaondoe duniani."
"Kuna nini bosi?"
"Nilikwenda kuzikagua akaunti zote za Jasmine nimekutana nazo zikiomba msaada tu."
"Kivipi bosi mbona mafumbo?"
"Sijakuta hata senti moja kwenye akaunti zake kazihamisha zoteeee mshenzi yule nitamuuuuaaaa nasema."
Alikata simu na kumuacha mdomo wazi asijue ampigie tena kumuuliza swali au afanyeje.
"Vipi mkuu?"
"Simuelewi bosi anasema eti Shem Jasmine kahamisha fedha zote kwenye akaunti zake zote."
"Sasa ambacho hujaelewa hapo nini brother Chude?"
"Alitakaje sasa Ibrah zile ni akaunti za mke wake alimfungulia yeye mwenyewe sasa alitaka awe anaziangalia tu hata ningekuwa mimi ningefanya hivyo hivyo."
"Mtajuana bwana sisi wengine ni vibendera tu upepo unakoelekea ndiyo huko huko tunakwenda."
Waliendelea kukata mitaa wakiwa na usafiri wao kuelekea nje kidogo ya mji kwa ajili kuendelea kuwatafuta wakina J's na Robinson.
Bruno Gautier kawaza nini kuwaacha huru ndani ya Ngome?
Tukutane katika sehemu inayofuata.
"Na humu ndimo kuna nguo za kubadilisha chagueni saizi zenu kisha hizo mtaingia kwenye kijumba kile pale mtakuta eneo maalum la kufulia fueni zianikeni kisha mengine yafuate." Mlinzi alihitimisha kutoa maelekezo.
"Asante kaka ngoja tufanye yetu."
Jessica alimjibu Mlinzi kisha akawaacha na kuelekea kwenye majukumu mengine.
"Yaani hizi nguo hazina tofauti na za wafungwa." Jackline alizua mjadala.
"Wakati mwingine tunatakiwa kukubali matokeo kikubwa tujifanye wajinga ili tuweze kukutana na aliyeingiza jumbe zile."
Jasmine alimkumbusha wanachotakiwa kukifanya muda huo.
"Sawa jamani nimeelewa na sijalewa vipi Robinson umeipata ya kunifaa?"
"Kitambo sana, jaribu hii naona ni saizi yako kabisa."
Robinson alijibu na kumpatia Jackline sare ambayo ingemkaa vizuri mwilini.
"Shemela tupishe sasa tubadili magwanda yetu kisha na wewe tutakuachia uwanja."
Jessica alimwambia Robinson awapishe wabadili nguo zao.
"Ina maana leo ndiyo mmegundua si wa jinsi yenu ee kule Belem mbona mlizishusha tu bila hofu yoyote?"
"Babu ee kuwa muelewa kidogo basi kule kulikuwa Belem na hapa ni United States of Bruno."
Jasmine alimjibu kwa hasira kidogo kitendo kilichomfanya Robinson kutoka nje bila kutoa mlio wowote.
"Dada na wewe ndo umefanya nini sasa kwa Robinson wa watu?"
"Huku si maskani jamani kila kitu tunakifanya na mkumbuke kuwa kuna vitu ambavyo tukivifanya vinatupa nguvu fulani ya kufanya jambo namaanisha vinatuondoa uoga so kuchukizana ni kawaida sana."
Ilibidi Jackline aingilie kati mgogoro ambao ulianza kumea katikati yao na alipoweka kila kitu sawa alitoka nje na nguo za Robinson ili naye abadilishe.
"Ndiyo nini sasa mbona umejiinamia hapo au vineno kiduchu tu vile vimekukwaza baby?"
"Hapana baby nimejikuta tu picha ya nyumbani inaniijia."
"Picha ya nyumbani?"
"Ndiyo mpenzi."
"Acha mambo yako hayo, unataka kuniambia kuwa hizo picha zimekuja baada ya Jasmine kusema vile au?"
"Usifike huko love, nimejichanganya tu na si vinginevyo."
"Okay sawa ila sijapenda mpenzi, badili nguo zako fasta hapo kwenye kona hiyo."
Robinson alizichukua nguo na kwenda nazo mpaka nyuma ya ile nyumba na kubadilisha na baada ya kumaliza alirejea na kuungana na wakina Jessica pale kwenye kijumba cha kufulia.
" Robinson sikutegemea kama ungekwazika kwa nilichokisema naomba nisamehe bure."
Jasmine alimuomba msamaha.
"Hapana Jasmine sikuchukia bwana."
"Uongo ulichukia unashindwa kuwa muwazi tu Robbie."
Jessica alimtania.
Muda huo waliokuwa wakitaniana zoezi la ufuaji nguo zao liliendelea. Walizifua na kuzianika kwenye vyuma vya mabaki ya magari. Na kisha waliondoka na kuelekea kwenye eneo walilokuwa wamesimama baadhi ya walinzi.
" Hutu tuvijana si twakawaida cheki tulivyojazia hasa kale kadada kalikofanya maafa jana."
Alisikika kijana mmoja alimwambia mwenzake walipokuwa wamekaa wakati huo wakina Jackline walikuwa wanapita hapo.
"Na pia nahisi lile tukio litakuwa limemchanga mzee Bruno mbo..."
Kabla hajamalizia neno lake mara mlio wa gari ulisikika nje ya geti na hapo kila aliyekuwa kakaa akiinuka tayari kwa kupokea oda huku mzee mmoja aliyeonekana kudhoofu kidogo alikimbilia kwenye sehemu iliyokuwa na kengele bila shaka alienda kuigonga. Na Mlinzi wa zamu alifungua geti kuu na gari liliingia ndani likiwa limeongozana na gari jingine aina Tata jeusi. Baada ya kengele watu wote walikuwa kwenye paredi wakisubiri gari lisimame wasogee kushusha magogo na mizigo mingine.
"Habari yenu watu wangu."
"Salama mkuu heshima kwako."
Wote walijibu kwa pamoja ila kwa upande wa akina Jackline kwao ilikuwa tofauti kwani walikuwa wakishangaa kila kitu kilichokuwa kikifanyika muda ule.
"Leo ni siku ya kurudisha faida kwangu kama mjuavyo siku hii huwa ikifika tu baadhi ya wenzenu hupelekwa sehemu nyingine na mimi kuingiza kipato ambacho husaidia kusukuma siku. Hivyo leo nitawaondoa watu wapatao kumi najua hii itawashangaza kwani haijawahi tokea hivyo natoa muda wa dakika kumi tu kwa ajili ya kuagana kwani huwezi jua kama ni wewe utakayechaguliwa. Nimeeleweka?"
"Umeeleweka mkuu."
Wote waliitikia na kuanza kuagana kwa kukumbatiana na kupeana maneno ya kutiana moyo, mara nyingi siku hii huwa ni ya huzuni sana kutokana na ndugu kutengana, marafiki kutengana, wanandoa kutengana na hata wapenzi kutengana hivyo kila mmoja alikuwa akimwaga machozi akijua muda umefika ambao hutokea mara moja kila baada ya miaka mitatu. Hali ilikuwa mbaya sana kwa bibi mmoja ambaye baada ya kutolewa tangazo hilo tu alianguka chini na kuzimia, inasemekana mpaka wakati huo alikuwa amepoteza watoto wake wote ambao idadi yao ni wawili na hivyo kitendo cha kusikia tangazo hilo ni kama alitoneshwa kidonda bado hakijapona vizuri.
"Mbona kama sielewi hivi, anamaanisha nini?"
Jackline alimuuliza mlinzi waliyekuwa naye karibu.
"Dada yangu hii siku mbaya sana kwenye Ngome hii kwani hao watu wanaouzwa hapa inasemekana hupelekwa kwenye migodi mingine iliyosambaa duniani kote na wengine hupelekwa huko Kolumbia na Mexico kwa ajili ya kusafikirisha madawa ya kulevya na hivyo tu wengine hutolewa viungo vyao kama moyo,figo ambavyo inasemekana vina soko sana huko India na ndiyo maana wengi wanalia sana wanajua hawataonana tena na wapendwa wao."
"Mhh kwa hiyo hata sisi tunaweza kuuzwa hapa?"
Robinson aliuliza baada ya kuyasikia maelezo ya mlinzi.
"Hiyo itategemea na mkuu kaamkaje siku hiyo ila kutokana na tukio la jana wewe dada hapo unaweza kuuzwa tu maana huko nyuma imetokea sana kwa wote ambao waliharibu mpango wa mkuu."
"Mungu wangu hivi kwanini hukutupa ishara yoyote mbaya juu ya mtu huyu?"
Jasmine alimlaumu Mungu wake baada ya kusikia hayo.
"Tunafanya.."
Kabla hajamalizia kauli yake Robinson mara mzee Bruno alipaza sauti yake tena.
"Haya leo nakwenda kufanya kitu cha utofauti sana, nikimaanisha kuwa nitakaowauza kwenye mnada huu ni wale wote ambao ni watoto wa kike na bora wa kike tu yaani Warembo na hawa ni wale waliokaa ndani ya Ngome kwa muda usiopungua miaka mitatu, na si vinginevyo nadhani wateja wangu watakuja kuchagua wanaowahitaji wenyewe.
Wateja wangu uwanja ni wenu sasa kuanza kuchagua kikubwa msiende kinyume na makubaliano."
Lakini wakati akiwakaribisha wateja wake kuanza kuchagua Warembo wanaowahitaji macho yake yakagongana na ya Jackline na mara moja akasitisha zoezi kwanza.
"Wageni wangu naomba tusubiri kidogo naona kuna rangi sizioni hapa hivyo naomba askari mmoja aje awapeleke ofisini kwangu wageni wetu ili nijue nini kimetokea hapa."
Wale wageni wakatii amri na kurudi pale juu ni baada ya kushuka kuanza zoezi la kuchagua. Mlinzi mmoja alipanda akawaongoza kuelekea ofisini kwa bosi wao na kisha yeye akavuta hatua kushuka chini moja kwa moja mpaka walipokuwa wamesimama wakina Jasmine.
"Ni nani kawaruhusu ninyi kuja hapa?"
"Walinzi wako ndiyo walioturuhusu."
Alijibu Jasmine.
"Bosi ulipokuwa unaondoka asubuhi uliagiza kuwa tuwatoe kiotani na kisha tuwakabidhi sare na baada ya hapo waungane na wengine mpaka pale utakapokuja na kuwapa utaratibu ni hivyo tu mkuu."
Alijibu mlinzi aliyekuwa karibu yao na ndiye aliyewafungulia.
"Oohh my God nini tena hiki?"
"Bosi au nimekosea?"
"Hapana Mathew si hivyo ila nahisi kuna vitu sikuviweka sawa. Hebu rudini kwenye chumba mlichokuwa haraka msijeharibu soko langu Mbweha ninyi."
Mpaka hapo wakajua kuwa mzee Bruno kavurugwa hii ni kutokana na majibu yake ambayo hawakujua anamaanisha nini lakini ilibidi wao kurudi zao ndani.
****
Walibahatika kutoka ndani ya pori lile na haraka sana walijificha kwenye chaka ambalo lilikuwa karibu na barabara ya Lupa kuelekea Tabora na hapo ilikuwa ni mbele zaidi ya kizuizi cha kwanza ambacho kiliwekwa na wakazi wa Lupa na baada ya muda kidogo lilitokea basi ambalo ilibidi walipige mkono.
"Unahisi litakuwa poa hilo Black?"
"Vyovyote watu wangu mwenzenu nishachoka."
"Kumbukeni huko tunatafutwa hivyo wanaweza kuwa ndani ya basi hili."
Mzee Jonathan aliwasihi wenzake.
"Oyaa vipi mbona mnapiga mkono gari halafu hampandi mnazingua mjue."
Kondakta aliwawashia moto baada ya kuona hawapandi.
"Tunaenda Konda, si unajua lazima tuulizane kuhusu mkwanja? Bila mkwanja tutasafiri bro?"
Masanja alimuuliza Kondakta.
"Hayanihusu hayo kama vipi jikataeni basi."
Kondakta alivurugwa sana na wakina Masanja.
"Jamani ee twenzetu jitu lenyewe hili limevurugwa na safari."
Black aliwaambia wenzake wapande garini.
"Brother tuheshimiane nani kavurugwa, nani kavurugwa? Brother mimi mtu mbaya usiombe kukutana na mimi bora ukutane na manyigu ila siyo mimi nitakugeuza bucha."
Kondakta aliendelea kuwaka mle ndani wakati huo wakina Masanja walikuwa wakitafuta sehemu ya kukaa na gari lilikuwa likishika kasi.
" Kwanza ninyi nimeshawashtukia naombeni nauli zangu maana ukiona kwenye kundi kuna Mfuga minywele halafu hekima sifuri ujue kundi hilo ni la wala mlenda tu."
"Dogo kukaa kwetu kimya siyo kuwa tumekuogopa angalia sana tunabadilisha historia sasa hivi."
Mzee Jonathan ilibidi amtahadharishe Kondakta yule baada ya kuona hana ustaarabu.
"Jamani vipi mbona kelele hazifiki tamati?"
Dereva ilibidi aulize baada ya kuona hakuna dalili ya kukoma kwa fujo zile.
"Muulize Konda wako, kwanza sijui umemtoa wapi mimi nahisi huyu alikuwa muimba taarabu maana si kwa mipasho hii."
Black alifungua kinywa kwa maneno ya shombo.
"Sasa ninyi naona mnataka kunipanda kichwani ngoja nitoe fundisho."
Alisema hayo na kumrukia Black na kumkunja shati.
Ni kama alichokoza nyoka shimoni kwani katika hali isiyo ya kutarajia Kondakta alijikuta uso kwa uso na mdomo wa bastola ya Masanja.
"Brother nini tena hujui bunduki hiyo?"
"Endelea na kelele zako."
"Brother mimi ni mtu wa utani sana na kama huamini waulize abiria watakuambia."
"Sihitaji mashairi yako hapa, ongoza kwa dereva wako haraka kabla sijapasua bichwa lako."
"Hiyo ni rahisi tu kaka twende tu."
Akiwa anageuka kuongoza kwa dereva mara huku nyuma mzee Jonathan na Black walisimama na kutoa silaha zao na kuwataka kutofanya chochote kile.
"Dereva kwa usalama wako na wa abiria wako ukifika pale juu kwenye kilima kile paki gari pembeni sawa."
Mzee Jonathan aliagiza.
"Sawa nimeelewa."
Ndani ya gari utulivu ulikuwa mkubwa huku kila mmoja akisubiri hatma yao baada ya gari kusimama huku dereva akiendelea kupiga gia. Kosa lilifanywa na mzee mmoja ambaye alikaa karibu na dirisha kujaribu kupiga simu akiwa kainama vile vile, Black aliweza kumuona alichokifanya kilikuwa ni kitendo cha kinyama kwani alimfuata na kumuinua kisha akamtaka kwa usalama wake afungue dirisha yeye mwenyewe kisha aruke.
"Nisamehe mwanangu sirudii tena, nakuapia."
"Mzee sirudiagi maneno fanya haraka kabla sijautawanya ubongo wako."
Yule mzee hakuwa na la kufanya zaidi ya kuvuta kioo cha dirisha kisha akajivuta na kujirusha nje ambako huko aliangukia kwenye ukingo wa barabara ambao ulimrudisha na kukutana na tairi za nyuma zilizomsaga na kusikika mlio uliowashtua abiria wenzao.
" Mnashtuka nini endeleeni kucheza na akili zetu kama hamjamfuata mpumbavu mmoja."
Masanja aliwaambia pale walipoonekana kama kushtuka baada ya kusikia mlio ule.
UNAFIKIRI NINI KITAENDELEA?
USIKOSE KATIKA SEHEMU INAYOFUATA KUJUA KAMA MZEE JONATHAN ALISALIMIKA NA PIA WAKINA JACKLINE ILIKUWAJE.
Baada ya umbali kuufikia ule muinuko basi lile lilipaki kwa amri ya Black na liliposimama tu watu wote waliambiwa washuke chini kila mmoja akiwa kaweka mikono kichwani huku wakitakiwa kulala kifudifudi mara baada ya kufika pale chini. Zoezi lilifanyika kama walivyoelekezwa na kisha wakaanza kuwakagua kwa kuwapora kila walichokuwa nacho mifukoni kwa wanaume na kwenye vipochi kwa wanawake na kisha kuvuliwa nguo zote na kubaki kama walivyozaliwa baadaye waliambiwa warudi garini wakiwa uchi na kuamriwa kuwa wanarudi sehemu zako wanakaa na kuingiza vichwa chini viti vya mbele yao. Kitendo hiki kiliwauma sana abiria lakini hawakuwa na la kufanya zaidi ya kutulia kusubiri amri ya watekaji. Walikaa kwa muda garini hakuna amri ambayo ilitolewa na ndipo kiherehere mmoja alipoinua kichwa kuangalia nini kina endelea ndipo alipobaini kuwa hakuna mtu na nguo zao zilikuwa pale pale nje na watekaji hawapo.
"Inukeni wahanga wenzangu jamaa wametokomea kusikojulikana."
Ndipo kila mmoja alipoinuka na kuhakikisha alichoambiwa na walipojiridhisha kuwa ni salama kwa kupitia mlangoni na madirishani kila mmoja alishuka kufuata nguo zake pale chini. Walichambua nguo zao na kuzivaa kisha wakarudi garini ambako lawama zao walianza kuzielekeza kwa kondakta wa basi hilo kuwa bila yeye hayo yote yasingetokea.
Wakati huo huo wakina Masanja na mzee Jonathan walikuwa ndani msitu ule wa Kipembawe wakiwa wamepumzika kwenye pango moja huku Black akiendelea kuhesabu kiasi cha hela walizokomba kwa wasafiri.
"Sasa hizo simu mtazifanyia nini?"
Mzee Jonathan aliuliza baada ya kumuona Masanja naye akihangaika na simu moja aina ya iPhone kuingiza nywila.
"Hizi zitatusaidia kwenye mawasiliano ya kundi letu kwa sasa kila mmoja atamiliki simu ya kijanja si unacheki hizi simu kumi zilivyo?"
Masanja alijibu.
"Acha ujinga dogo kwa kutumia hizo simu tutatiwa mikononi mwa polisi hata kabla ya kufika Itigi."
Black alimtahadharisha Masanja.
"Ni kweli kabisa hapo cha kufanya simu zote zitabaki hapa hapa na sisi kuondoka zetu kitu kitakachotuweka huru."
Mzee Jonathan alitoa wazo lake.
"Lakini mzee hizi simu nilizozishika na za hela kubwa hamuoni tunaacha hela porini?"
"Masanja acha ujinga hizo ni hela? Kama shida yako ni hela si hizo Black anaendelea kuzihesabu?"
Mzee Jonathan alimuwakia Masanja.
"Na ni hela ya kushiba tu mzee."
"Iko ngapi Black?"
"Kama sijakosea nimepata shilingi milioni kumi na saba."
Black alijibu baada ya kumaliza kuhesabu.
"Si umeona sasa milioni kumi na saba hela nyingi sana hiyo na hapo mimi sichukui hata mia mtagawana wenyewe."
"Kwanini mzee?"
Black aliuliza baada ya kusikia mzee Jonathan hatachukua mgao.
"Black mimi ni bilionea hapo hakuna hela ya kuchukua mimi na usifikiri kukaa huku porini nimefilisika ni usalama tu."
"Sawa mzee nimekuelewa."
Waliachana na lile eneo pamoja na zile simu na kuondoka zao kusogea mbele zaidi ya kilometa ishirini ili kuwa mbali na pale walipokuwa kisha mzee Jonathan akampigia simu mke wake.
"Wife tumekwama zoezi huku watu walishajiandaa kukabiliana na yoyote atakayeigusa familia ya mzee Fikirini."
"Mko wapi sasa mume wangu?"
"Tuko ndani ya msitu mmoja hapa hata jina lake silifahamu ila si mbali sana kutoka barabarani."
"Mume wangu ngoja nimtume Rashidi awafuate kabla hamjadakwa na polisi."
"Okay sawa kikubwa mwambie awe hewani muda wote ili kujulishana amefika wapi na sisi tuko wapi na pia mke wangu anza maandalizi nikifika tu hapo tunaondoka kuelekea nchini Uganda kabla ya kupotelea nchini Oman."
"Sawa mume wangu kuweni makini."
Baada ya kukata simu ya mke wake aliona si vibaya amtaarifu na Karatu juu ya kukwama kwao.
"Karatu tumeangukia poa mtu wangu."
Aliongea mzee Jonathan mara baada ya Karatu kupokea simu.
"Sijakuelewa mzee una maanisha nini?"
"Tumekuta wanakijiji wamejipanga si tumetelekeza mpaka gari hivi tuko ndani ya msitu ambao hatuujui lakini ni uelekeo wa kuja Tabora na Singida."
"Kwangu haina tatizo ntajuana wenyewe kama mmekubaliana kurudi mimi nitawabishiaje bwana."
"Ndiyo hivyo na muda huu bila shaka kijana wangu atakuwa njia ni kutufuata japo kwa muda huu inawezekana ikawa kesho."
"Poa mzee ila waambie vijana wangu kesho jioni kuna mchongo unatakiwa kufanyika."
Kisha alikata simu hakutaka kusikia mzee Jonathan anajibu nini na hapo mzee Jonathan aliwajulisha wakina Masanja mkuu wao kasema nini.
****
Baada ya kuhakikisha wakina Jackline wameingia ndani ndipo alipowafuata wateja wake kuja kuendelea na mnada wao.
"Poleni kwa usumbufu uliojitokeza lakini kila kitu kiko sawa tunaweza kuendelea na zoezi letu."
"Bila shaka mzee Bruno sisi tunakusikiliza wewe."
Alijibu mzee mmoja wa makamo.
Walishuka tena mpaka chini lilipo kusanyiko lile la watumwa wale na kuanza kuchagua wanawake wanaowataka.
"Mimi nadhani hawa wawili wananitosha kwani nyumba yangu haina shughuli nyingi sana."
"Mzee Shegah unataka kuniambia unawanunua kwa ajili ya shughuli za nyumbani leo?
Mzee Bruno ilibidi amuulize maana si kawaida yake mzee huyo ambaye ni sapulaya mkubwa wa watumwa kwenye nchi tofauti hasa Mexico na Kolumbia.
" Leo ilikuwa ni kwa ajili ya kijana wangu Maximilian ambaye nategemea ndiye atakayeiendeleza kampuni hivyo lazima ajue soko likoje na ni watu gani wa kufanya nao biashara na mimi ilikuwa ni kumtafutia mama wafanyakazi wa ndani si unajua umri nao unatutupa mkono."
"Ni kweli kabisa na hilo nalo umelifikiria la maana sana hata mimi ningekuwa nayo ningefanya kama wewe sasa si unamfahamu nini kilinitokea kule Vietnam?"
"Nakumbuka vizuri sana mzee mwenzangu lakini unaweza kutafuta familia ya makubaliano ya kuilea ikawa yako kwa kufuata sheria tu zinavyotaka na hapo utaikuta ukiishi maisha mazuri bila stress si kama haya unayoishi."
"Nashukuru kwa ushauri wako mzee Shegah nitautafakari na kuufanyia maamuzi."
"Ni wewe tu."
"Baba kwa leo niliowaona wanafaa ni hawa watano ambao kwa urembo wao tutapiga dollars za kutosha."
"Okay wapigeni cheni kisha waingizeni kwenye gari, mzee Bruno tuelekee ofisini tukamalizane."
"Bila shaka Shegah, haya mliobakia kila mmoja kwenye kazi yake na ninyi mabeba anzeni kushusha magogo kwenye gari."
Wao wakapandisha ofisini ambako walilipana kama ilivyo kawaida yao na kisha waliondoka zao na kumuacha mzee Bruno akihifadhi midollar yake kwenye sefa maalum.
Alipohakikisha kila kitu kiko sawa alishuka moja kwa moja na kuelekea kwenye banda walilokuwa wakina Jasmine.
"Fungua mlango hapa."
Alimtaka Mlinzi aufungue mlango.
Mlango ulifunguliwa na kisha akaingia ndani na kuwakuta wakiwa wamekaa chini wakimuangalia yeye alipokuwa akiwasogelea.
"Siwapendi nyinyi vibwengo hata kidogo na leo mlitaka kutia doa biashara yangu lakini hamjafanikiwa."
"Kosa letu liko wapi mzee kuna kilichofanyika tofauti na maagizo yako?"
Jackline aliuliza.
"Mbabe bado una nguvu eee?"
"Wala mimi sihitaji unachokitaka na ni nani aliyekuambia mimi ni mbabe?"
Jackline naye alimtupia swali.
"Sijafuata maswali humu kilichonileta ni kitu kimoja tu."
"Tunakusikiliza mkuu." Robinson alimjibu kuwa wako tayari kusikiliza.
"Ni hivi kuanzia leo kazi yenu itakuwa ni kule open area' kung'oa mawe kwa ajili ya kokoto mtakuwa huko kwa muda wa wiki moja kisha mtarudi hapa tena."
"Na vipi kuhusu malipo ya kazi hiyo?"
Jessica aliuliza.
"Binti unauliza malipo? Malipo yenu ni kula na kufichiwa siri yenu tu na hakuna zaidi."
"Okay hakuna shida mzee tuko tayari kwa kazi."
Jackline alijibu haraka baada ya kukumbuka kuwa kuna mtu ambaye yupo japo hajioneshi ambaye awali aliwatumia vikaratasi.
"Mtaelekea kwenye banda la chakula baada ya kupata chakula ndipo vijana wangu watawapeleka saiti kuanza kazi rasmi ila tu nawatahadharisha mkileta jeuri tu nawageuza kitoweo."
"Hatuko hivyo mzee wewe tuamini tu."
Robinson alijibu haraka haraka kitendo kilichowafanya wenzake watazamane.
"Okay mfuateni mlinzi huyo mpaka kwenye chakula."
Walitoka na kuelekea kwenye banda la chakula ambako huko walikutana na watu wengine ambao walikuwa wakiendelea kula chakula.
"Chukueni vyombo pale kisha mtakinga chakula pale kwa wapishi."
Waliongoza mpaka pale kwenye vyombo wakachukua na kwenda kukinga chakula kisha wakaongoza kwenye chanja ambalo lilikuwa mfano wa meza na kwenda kukaa kuungana na wenzao waliokuwa pale.
"Mimi ndiye ninayewasiliana nanyi kuweni wapole mpango unaenda vizuri."
Kijana mmoja aliyekuwa karibu na Jackline alimnong'oneza sikioni.
"Mbona sikufahamu?"
"Hakuna jumbe ambazo mlizipata kule ndani?"
"Okay tulipata kumbe ni wewe?"
"Ndiyo mimi."
"OK sawa fanya mambo yako kwa tahadhari kubwa." Jackline alimpa tahadhari kijana huyo.
Lakini wakati wanaongea hayo kuna mtumwa mmoja alikuwa karibu yao alisikia kila kitu na kwenda kumjulisha mlinzi pale nje juu ya kinachopangwa.
"Costantine anaonekana kupanga mpango wa siri na wale wageni."
"Dogo punguza umbeya basi hivi hakuna muda ambao ukawa unawaza kufanya mambo yako badala ya kusambaza ujinga usio na faida."
Mlinzi alinyambua yule aliyepeleka taarifa.
"Ni kweli kabisa afande nimewasikia na inavyoonekana wanataka kutorok..."
Lakini kabla hajamalizia kueleza alikutana na rungu la kichwa na kuanguka chini na kisha mlinzi huyo alipuliza filimbi ambayo hiyo huwa ikisikika kila mmoja hutoka mbio kutoka aliko maana huwa ni kiashiria cha hatari. Hivyo watu karibia wote walitoka kusikiliza kulikoni huku mzee Bruno naye akitoka nje kuangalia kuna hatari gani nje.
"Mnamuona aliye mbele yangu?"
Yule mlinzi aliwauliza waliokusanyika pale.
"Ndiyo tunamuonaaaa." Waliitikia.
"Awadhi kuna nini hapo chini?"
Mzee Bruno aliuliza.
"Mkuu kijana huyu inaonekana kuna mpango alikuwa anataka kuufanya kwani nilimuona akienda huku na kule huku akiwa na hofu na nilipomfuatilia akajaribu kuninyang'anya silaha ndipo nilipomgonga na rungu."
"Haya mbebeni mkamchome moto kwenye tanuru la taka kule chini na wengine kaendeleeni na shughuli zenu."
"Sawa mkuu kama ulivyoagiza."
Wote wakarudi kuendelea na shughuli zao huku tukio lile likiwaacha vinywa wazi wakina Jackline.
"Mnaonekana kushangaa mambo yanayoendelea humu mbona kawaida sana vitu kama hivyo ila huyo aliyeuwawa alitaka kutuchoma ndipo mlinzi akamuwahi."
Yule kijana aliwaeleza wakina Jackline.
"Kutuchoma kivipi tena?".
"Alisikia kila kitu nilichokuwa nawaeleza ndipo alipokimbilia kwa mlinzi kumjulisha..."
Kabla hajamaliza kusimulia tangazo lilipita mle ndani.
"Muda wa chakula umekwisha kila mtu atoke nje kuendelea na shughuli zake kulingana na utaratibu aliopewa na kiongozi."
Hivyo kila mmoja akatoka mle bandani huku Jackline akiwa bado hajapata jibu zuri juu ya alichokisikia kutoka kwa yule kijana.
"Iweje mlinzi apelekewe taarifa zetu lakini amemuua mtoa taarifa kuna nini hapa?"
Ni maswali aliyokuwa akijiuliza kimoyo moyo wakati akitoka mle ndani.
"Tulia hapo weweee unatembeaje hivyo?"
NI NANI HUYO ALIYEMTULIZA JACKLINE?
TUKUTANE KATIKA SEHEMU INAYOFUATA.
Mlinzi wa lango la kuingia kwenye machimbo ya mawe alimfuata kwa nyuma na kumshtua baada ya kugundua kuna kitu anakitafakari Jackline.
"Nimekosa nini tena?"
"Hujakosa kitu ila tu nimeona kama una mashaka fulani hivi na ndiyo maana nikafanya kitu hiki cha kukurudisha kwenye mood yako, sikiliza dada huku ndani hakunaga serikali zaidi ya ile ya mkuu wetu hivyo yanayotokea humu ndani yaache kama yalivyo fanya michakato yako."
Yule mlinzi alijaribu kumshauri baadhi ya vitu vinavyotokea mle ndani avione ni vya kawaida tu.
Jackline alipoona ameachwa na yule mlinzi alitembea haraka na kuwafuata wenzake ambao muda huo walikuwa wakikabidhiwa vitendea kazi kama vile sururu, mtaimbo,nyundo, jembe na spedi.
"Vipi mbona ukataitiwa ghafla na mlinzi?"
Jasmine alimuuliza.
"Mwenzangu yaani acha tu maana naona kama vile niko ndotoni na muda mfupi ujao nitazinduka."
"Alikuwa anakuambia nini kwani?"
"Kaongea vimafumbo fulani hivi ambavyo bado najaribu kuziunganisha hizi doti nione nitapata umbo gani lakini tu ninachokikumbuka kaniambia kuwa yanayotokea humu niachane nayo niangalie mipango yangu."
"Mmhh hapa kuna jambo tunatakiwa kuwa nalo makini na hatutakiwi kujipambanua kwa yeyote tusiyemuamini ndugu yangu."
"Ni kweli kabisa."
Walichukua vifaa vyao na kuelekea ndani ya shimo ambalo lina urefu wa mita mia sita chini kwa chini na kutokea eneo la wazi ambalo limezungushwa ukuta ambao juu yake kuna nyaya za umeme ambazo ni za kusapoti ulinzi huku kila eneo la ukuta kuna kibanda chenye walinzi wa kutosha ambao wanapishana pishana kulinda eneo hilo. Mazingira hayo yaliwashanhaza sana wakina Jackline na kujiuliza maswali yasiyo na majibu, kikubwa walichokuwa wanajiuliza huyu mzee Bruno kwa muonekano wake tu anaweza kumiliki eneo hili ambalo linaonekana limezamisha mamilioni ya dolla? Au kwamba kuna mkwanja aliuotea na kuununua mgodi huu maarufu.
"Jamani mbona tunaendelea kukutana na maajabu ndani ya Ngome hii?"
Jessica aliwauliza wenzake baada ya kuibukia eneo hilo huku huko chini walikopita kuna ulinzi wa kutosha kila baada ya mita kumi kuna kituo kulinda usalama.
"Sisi wenyewe kama wewe tu Jessica kwani ni kama filamu fulani kwani kazee kenyewe hakana muonekano wa kuwa na mabilioni ya dollars' ila mimi nahisi kuna mtu yuko nyuma ya mzee Bruno."
Jackline alieleza kile anachokihisi moyoni mwake.
"Hata mimi jamani nafikiria hivyo hivyo kwanza fikiria mambo yanayofanyika humu ina maana serikali haijui na kama inajua imewahi kuchukua hatua gani dhidi ya mgodi huu."
Robinson na yeye alielezea hisia zake juu ya Ngome hiyo.
Wakiwa bado hawajajua ni wapi pa kuanzia mara alifika mlinzi kiongozi wa machimbo yale ya mawe na kuwataka wamfuate ili akawaoneshe eneo lao ambalo watatakiwa kuanza kufukua mawe na namna ya kuyafukua na kuyatoa kisha kuna mitambo ambayo huyabeba na kuyapakia kwenye viberenge ambavyo huyasafirisha kwenda kwenye mashine za kuyasaga na kutoa kokoto ambazo huwekwa kwenye madaraja mbalimbali kuanzia zile laini za kati na zile kubwa kubwa.
"Nifuateni nikawaoneshe eneo lenu ambalo mtakuwa mnafanyia kazi na eneo la kulala ambapo huku tunatumia Tenti kama zinavyoonekana kule pembezoni."
"Sawa brother, lakini naona hujazungumzia suala la chakula si unajua kazi hii ni ya nguvu inahitaji shibe."
Robinson alimuuliza mlinzi yule.
"Kuhusu chakula wala usijali kaka kuna watu maalum ambao hupita kwenye maeneo yenu ya kazi na kugawa chakula na kwa utaratibu wetu huku ni kwamba chakula hutolewa jioni tu huku asubuhi tunatoa mihogo kama chai."
"Unahisi ni haki namna utaratibu huu ulivyoratibiwa?"
Jasmine aliuliza.
"Dada yangu hata mimi mwenyewe napokea amri kutoka juu."
Walifika na kuoneshwa mlima ambao watatakiwa kuanza kuvunja miamba hiyo na kutoa mawe ya saizi ya kati na kisha aliwapeleka kwenye Tenti ambazo watazitumia kama eneo lao la kulaza mbavu zao.
"Samahani kaka mbona hizi Tenti hazina vya kulalia wala vya kujifunika?"
Jackline aliuliza
"Vya kulalia vitakuja ninyi anzeni kazi ila tu naomba niwajulishe huku ubabe ni nje nje hakuna huruma watu huuwana sana na mkuu huwa hajali zaidi ya kuzitoa maiti na kazi kuelekea, angalieni kule magharibi kuna nini?"
Mlinzi aliona awape pia tahadhari juu ya eneo hilo ambalo inasemekana lina wababe au tuwaite watemi wengi sana.
" Ninaona kuna watu ambao wanaendelea kupiga kazi."
Jasmine alimjibu mlinzi yule.
" Okay sawa, sasa wale ndiyo wale ambao walikushambulia wewe siku ile ya jana na mkuu huwatumia sana inapotokea kuna mtu msumbufu."
"Mbona ulinzi uko vizuri inakuwaje wanafanya ubabe mbele ya walinzi ambao wako kila eneo la machimbo haya?"
Robinson alimchimba swali mlinzi.
"Kaka kama unakumbuka nimesema hawa jamaa ni watemi sana hivyo hupenyeza rupia kwa walinzi na kisha kufanya yao na kwenu nina uhakika na jinsi yenu lazima watawafanyia vurugu tu."
"Kaka tunashukuru kwa kutuweka wazi kwa kila zuri na baya linalofanyika humu ndani tutakuwa makini wala usijali."
Jackline alijibu huku akichukua sururu yake tayari kuelekea muinukoni.
"Haya mimi niwaache muanze kazi."
Mlinzi aliwaaga wakina Jackline na kuondoka zake.
"Jamani ee mmesikia kila kitu hivyo kama sikosei tumeletwa buchani mlinzi kashindwa kutuweka wazi."
Jasmine aliwajulisha wenzake kile alichokihisi.
"Uko sahihi dada mimi mwenyewe nimeona hivyo hivyo kikubwa ni ushirikiano wa dhati."
Jessica aliunga mkono hoja.
"Tuanzeni kazi kikubwa mazingira si mageni kwetu kwa maelezo tuliyopewa."
Robinson aliwaeleza wenzake kuanza kazi.
Na kweli kazi ilianza huku kila mmoja akasimama upande wake na wakati huo hakukuwa na mazungumzo zaidi ya kazi. Kule juu walinzi waliendelea na doria yao huku mmoja wa walinzi ambaye ni kiongozi wa walinzi kule juu alionekana kutoa ishara fulani kwa ile mijitu ya miraba minne huku wakina Jackline wakiwa bize na kuvunja miamba. Kisha ile mijitu ilikusanyika na kuanza kujadili kitu ambacho kilionekana si cha usalama kwa upande wa akina Jackline kwani walionekana mara kwa mara wakionesha upande wa akina Jackline.
"Jamani hii kazi tutaiweza kweli?"
Jessica aliuliza baada ya kuona mikono yake imeanza kuweka damu.
"Dogo unafahamu vizuri katika makuzi yetu hatukuwahi fikiria kutana na mazingira kama haya hivyo kama wasemavyo waswahili 'kuwa uyaone' ulifikiri maghorofa ee? Ni maisha kama hivi."
Jasmine alimjibu mdogo wake.
"Ni sawa dada lakini si kama hivi hii ni too much' we hata saa halijaisha damu mikononi vipi tukimaliza hizo siku?"
Jessica aliendelea kulalamika.
"Nikwambie kitu Jessica?"
"Niambie dada Jackline kamanda wangu wa vita."
"Acha kunipaka mafuta ila tu ninachotaka kukueleza ni kwamba hakuna kazi nyepesi siku ya kwanza lakini kadri siku zitakavyokuwa zinasonga utajikuta umezoea, hebu jiulize mimi hapa hata mwezi haujaisha toka niumie mkono haujapona vizuri na bado nikalianzisha varangati ambalo kama wasingekuwa na jicho la tatu ningewafanya kitu mbaya na mimi huyu huyu leo napiga kazi huku mlimani na ukitaka kujua hali ikoje mdogo wangu tuangalie wote mikono yetu (akimuonesha mikono yake) wote inatoa damu, lakini tunakomaa."
"Dada maneno yako yameniingia hasa nikikumbuka ulivyoumia na vile tulivyotaka kukupoteza machozi yamenitoka tena, naomba nikuahidi kuwa nitakuwa jasiri mara mbili hata ya Robinson."
"Kwa hiyo umeona unitolee mfano wako mimi."
Robinson mzee wa mapaniki alimuuliza Jessica baada ya kuona kaoneshwa mfano yeye.
"Sasa uongo bwana kwenye kundi hili wachovu ni mimi na wewe japo huwa unajikongoja kidogo lakini nataka kuwa zaidi yako."
"Pa pa pa pa....."
Waligeuga kuangalia ni nani aliyekuwa akipiga makofi nyuma yao.
UNAFIKIRI NI NANI HUYO?
JIANDAE KWA SEHEMU YA INAYOFUATA KUJUA KILICHOTOKEA.
"Wao wao naona mnajiingilia tu kwenye miliki za watu bila hodi."
Wakina Jackline walilitazama jitu hilo ambalo sura lake halikuwa geni machoni pao kwani ni siku chache lilikuwa ni miongoni mwa wale waliomzimisha Jackline kwenye uwanja wa mapambano na hapo wakajua kazi imefika kama ambavyo waliambiwa na yule mlinzi aliyewaleta.
"Mbona hatukuelewi una maanisha nini?"
Robinson ilibidi aulize swali ambalo kwa jitu lile liliona swali lile ni kichekesho kwani lilicheka kwa muda kisha likamjibu kwa swali.
"Hujaelewa siyo?"
"Ndiyo na si mimi tu wote hatujaelewa labda utueleweshe vizuri."
"Kifupi eneo lote ni la kwangu mimi haruhusiwi hata panya kufukua shimo sembuse vinyangalika kama ninyi, hivyo itabidi mtafute eneo jingine hapa pisheni kabla sijawafanya kitu mbaya."
"Usitutishe mkubwa hata sisi tunahaki ya kufanya kazi eneo hili ungekuwa ni mmiliki ungekuwa umepauka hivyo kwa jua? Tupishe babuuu wee tufanye yetu siye." Jessica alimshambulia kwa maneno.
"Unasemaje wewe kunguni?"
"Kunguni ni yule aliyeacha kazi aliyopangiwa na kujaribu kuona kama anaweza kupata pa kunyonya damu"
Jessica aliinunua kesi mazima.
"Una maanisha kuwa mimi ndiyo kunguni?"
"Kwani wewe ulimwita nani hilo jina?"
"Wewe hapo."
"Basi na mimi namaanisha wewe ndiyo kunguni una kingine?"
"Kumbe hunijui wewe mtoto?"
"Nani akujue hapa wewe tupishe bwana ndugu zako wenyewe hawakujui sasa sisi tukujue ili iwe nini?"
Robinson alidakia malumbano.
Wakati wao wakiwa kwenye malumbano na jitu hilo Jackline alikuwa pembeni akiendelea kugonga mawe tu na si kwamba hakusikia mkwara uliochimbwa na jitu lile la hasha bali alikuwa na plani yake kichwani ambayo alisubiri muda ufike aifanyie zoezi.
"Halafu natoa agizo la kusitisha kazi hapa naona kingine kinaendelea tu sijui hakijanisikia? Halafu na wewe acha kugusia ndugu zangu." Lilimwambia Robinson likiwa limemshika shingoni.
"Usinitishe kaka kwa kabali laini kama hiyo na pia nakusikitikia sana kwani nahisi wakati unakuja hapa uliwaahidi wenzako kuja kutufanyia timbwili lakini hukuwaambia kuwa haurudi na roho yako kwani mwili utabaki hapa wakati roho yako ikitokomea zake."
Liliposikia maneno ya Robinson yaliyojaa dharau lile jitu lilimuachia na kisha likarusha gumi lake kwa Robinson ambaye aliikwepa na kulifanya jitu kwenda nayo kasi ya gumi lake mpaka chini huko ilitua kwenye jiwe ambalo lilipelekea maumivu makali kwa jitu lile kwani sura yake ndiyo iliongea japo machozi na sauti havikutoa ushirikiano. Aliinuka kwa hasira zote na kumvaa Robinson mzima mzima na kumgonga kichwa kilichopelekea wakina Jasmine kupandwa na hasira baada ya kuona Robinson akitokwa damu puani na mdomoni baada kugongwa kichwa na kusukumiwa kwenye korongo.
"Umevuka mipaka ngoja tukuoneshe kazi."
Jasmine aliongea na kumpiga sururu ya mguu.
"Aggghhhhhhh mguu wangu...."
Jamaa lililalamika kwa maumivu lililoyapata na hapo Robinson aliinuka kutoka alikokuwa na kulisogelea.
"Jasmine naomba uniachie huyu nimuoneshe kuwa na mimi sijavaa suruali kwa bahati mbaya."
Alilifuata na kuligonga jiwe la kichwa lililopelekea paji la uso kutapakaa damu huku lilishindwa hata kuona.
"Nikiinuka nitawafanya kitu mbaya ohhh pona yenu acheni mchezo wenu..."
Kabla hajamaliza kuongea alifuatwa na jiwe jingine kubwa lililomzima kabisa.
"Wanakuja wale kule tufanyaje hapa?"
Robinson aliuliza.
"Tulieni hivyo hivyo ngoja niwaoneshe kitu hapa." Jackline aliwaambia wenzake watulie wakati yeye akiambaa kwenye kilima kile kufuata ule ukuta ambao juu yake kuna wale walinzi ambao muda huo hawakuwa nje walikuwa ndani ya Vibanda ili isionekane kama walikuwepo wakati vurugu zinafanyika. Hivyo Jackline alifika kwenye eneo ambalo lina kingazi akapanda haraka na kufika juu na kisha kujificha sehemu ambayo wakitoka ndani hawawezi kumuona alipo. Huku chini ile mijitu mitatu ilifika na kukitifua pale baada ya kushuhudia mwenzao akiwa marehemu.
Lakini haikuwa nyepesi kwani walikutana na Jasmine aliyewachezesha sindimba la maana. Wakina Robinson na Jessica walicheza na nyundo walizokuwa wakiwagonga nazo kwenye goko zao huku Jasmine akipambana nao na ukumbuke kuwa huyu naye si wa kawaida hata kidogo.
Aliruka na teke moja takatifu lililompata mmoja wao kwenye maeneo yetu nyeti na kulifanya jamaa kulia kama toto na hii ilikuwa masta plani ya Jasmine ambaye alijua kwa mimwili ya hawa watu ni kupiga maeneo nyeti tu.
Walinzi wa upande mwingine waliona chezo lile na kuamua kushuka haraka kuja kutuliza muziki ule huku mwingine akikimbilia kwenye kile kijumba walichokuwa wale walinzi wa karibu ambao ndiyo waliochora mchoro na muda huo walikuwa ndani wakicheza karata. Alifika kwenye kibanda kile lakini kabla hajaufikia mlango alikutana na pigo la shingo lililomtuliza bila kupiga kelele kwani ilikuwa kama kapigwa na shoti ya umeme vile haraka Jackline akamvuta pembeni na kuichukua silaha yake ambayo alitimba nayo mle ndani na kuwachomoa jamaa ambao hawakuwa na hili wala lile kama kuna mtu amewaingilia.
"Umefuata nini humu wewe mwaharamu?"
Jackline ambaye muda huo alikuwa anaonekana macho tu kutokana na kazi ile ya mawe kumchafua vilivyo, hakuwa na muda wa kuwajibu badala yake aliwaweka mtu kati.
"Hivyo hivyo mlivyo mikono juu usiguse chochote jivuteni mbele kwa magoti yenu haraka sina muda wa kusubiri hapa."
Jamaa wakajua wamepatikana hivyo walitii amri na kujongea mpaka nje huku nyuma yao Jackline akiwa kawanyooshea bunduki. Alizibeba na zile bunduki nyingine begani na kuwataka wasonge mbele waongoze njia wanayopitiaga kufika kule chini waliko wakina Jessica. Waliongoza mpaka kule chini ambako wale walinzi wengine na ile mijitu mingine ilidhibitiwa vilivyo na wakina Jasmine na ni baada ya Robinson kuyamwagia mchanga yale majitu huku wale walinzi waliofika pale kichwa kichwa walikutana na mikono na miguu supa ya Jasmine aliyewaonesha kuwa wao ni watu wengine kabisa kwani aliwavizia na kumdaka mmoja na kwa kumtumia huyo aliwataka wale wengine wajisalimishe kabla hajamsambaratisha mwenzao na ikawa hivyo. Na baada ya Jackline kufika waliwaweka mtu kati na kuwataka washike vifaa vya kazi waanze kuvunja miamba, zile silaha za wale wengine walikabidhiwa wakina Jessica na Robinson kwa ajili ya kuwasimamia kisha Jackline na Jasmine waliondoka wakiwa na silaha zao kuwafuata wale walinzi wengine kutoka kwenye vijumba vingine ili kuwateka nao na kuwaleta kazini kisha baadaye kumfuata bosi wao wakiwa kama walinzi wapya.
***
Baada ya mwendo mrefu kijana yule aitwaye Rashid alikuwa ndani ya pori la hifadhi la Rungwa pori ambalo lina usumbufu sana nyakati za masika kwani magari hukwama sana na eneo hili lina umbali wa kilometa zaidi ya kumi hivyo kama gari lako halina uwezo wa kutosha lazima likwame, hivyo baada ya Rashid kufika eneo hili gari lake lilikwama kwa muda wa zaidi ya masaa matano kutoka saa kumi na moja asubuhi mpaka saa nne na hapo ndipo alipopata msaada kutoka kwa wawindaji ambao ilibidi wamsaidie kulisukuma na kulitoa na hapo safari iliendelea, mazingira haya yalimtisha sana kwani njia nzima hakuweza kukutana na watu wengine zaidi ya wale wawindaji. Lakini haikumletea hofu ya kutoendelea na safari alisonga mbele na Cruiser lake lilikubali sheria.
Mara simu yake iliita na kisha aliichukua na kuipokea baada ya kubaini ni bosi wake mke wa mzee Jonathan.
"Ndiyo mama nakusikiliza."
"Vipi mwanangu safari inaendeleaje na umefika wapi muda huu?"
"Kwa muda huu ndiyo napita eneo moja lililosomeka kwenye kibao 'Rungwa Game Reserve' mama."
"Okay sawa mwanangu ngoja nimuulize mzee kuna umbali gani kutoka hapo mpaka walipo wao."
"Sawa mama fanya hivyo kisha utanijulisha lakini pia itakuwa vizuri iwapo utanitumia namba yake na mimi."
"Sawa basi ngoja niwasiliane naye kwanza kisha nitakutumia au yeye mwenyewe atakupigia maana nina uhakika yeye anayo yako."
"Bila shaka mama."
Basi simu ilikatwa na Rashid aliendelea kupiga gia huku ndani ya gari yake kukiwa na burudani murua ikimsindikiza kutoka kwa mwanamuziki mwenye jina kwa sasa ndani ya ardhi ya mjomba Magufuli anayekwenda kwa jina la Cheed kutoka Kings Music iliyo chini ya Mwanamuziki nguli na mwenye jina aitwaye Ali Kiba akiwa kashirikiana na Mwanamuziki mwenzake Marioo kwenye wimbo huu uitwao For you' ni ngoma inayobamba kwa sasa kila kona hivyo kwa Rashid ilikuwa burudani nyuma ya usukani.
Mara simu yake iliita tena na safari hii hakuwa tena bosi wake bali alikuwa ni mume wake mzee Jonathan na ila hakujua kama ni yeye kwani hakuwa na namba yake lakini aliipokea ili kujua mpigaji ni nani.
"Haloo, haooo."
"Naongea na Rashid bila shaka."
"Ndiyo mzee ni mimi."
"Okay unaongea na mzee Jonathan hapa namba yako nilikuwa nayo hivi baada ya mama yako kunipigia na kunijulisha kuwa uko njiani nikaona nikupigie ili unijulishe vizuri ulipo."
"Ndiyo mzee ni kweli nilimjulisha mama niliko, kwa sasa ndiyo nimepita kwenye hili pori la Rungwa."
"Vizuri sana sasa wewe endelea kuja ukifika kuna sehemu inaitwa Kampi Katoto utaulizia Bitimanyanga na hapo utatusubiri kwani sisi tuko ndani ya msitu ulio kijijini hapa."
"Dakika sifuri mzee si unalijua hili ndinga lako linavyoatamia barabara na kumbuka hili ni falme la nyika."
"Najua kijana wangu kikubwa kuwa makini sana."
"Sawa mzee nimekupata."
Simu ilikata na Rashid akazidi kunyonga usukani kuelekea aliko mzee Jonathan ili kuwaokoa baada ya zoezi lao kushindikana la kuisambaratisha familia ya akina Jackline japo hajui kama Jackline yupo matesoni kwa ajili yake yeye.
NINI KITAENDELEA?
"Mzee hii ni sehemu moja inaitwa Kambikatoto kutokana na mtu niliyemuuliza hapa stendi."
Rashid alimwambia mzee Jonathan baada ya kupokea simu yake.
"Okay sasa jitahidi usogee kimji kinachofuata kinaitwa Bitimanyanga hapo ukifika usiondoke paki mpaka tutokee."
Mzee Jonathan alimwelekeza.
"Sawa bosi kumbe ngoja nipoteze dakika chache hapa hapa Kambikatoto nipate chochote kitu."
"Sawa basi tuchukulie na sisi chakula cha kutosha kwani hatuta poteza hata sekunde tukitokeza mjini Bitimanyanga."
"Okay sawa mzee."
Rashid alijibu na kukata simu na kisha aliisogeza gari karibu na mgahawa mmoja uitwao Chekanao na kuzama ndani yake kupata chakula.
"Vipi tutafanikiwa kuibuka salama mzee Jonathan?"
Masanja aliuliza.
"Bila shaka kwani kuna kila dalili za kutoka na ninachoshukuru mpaka sasa gari imeshawasili iko kilometa chache kutoka hapa tulipo." Mzee Jonathan alifafanua.
"Lakini mimi nilikuwa nina wazo jamani." Black aliongea.
"Wazo gani hilo Black?
Mzee Jonathan aliuliza.
" Kwa kuwa hapa tulipo si mbali kutoka hapo mji ulipo kutokana na kusikika kwa kelele za shughuli mbalimbali kama vile magari na makelele mengine inatakiwa tusiende wote ataenda mmoja kwanza kusoma mazingira si unajua tena unaweza shangaa tukawa tumefuatwa mpaka huku."
"Umenena Black hapo itabidi wewe ndiyo utakwenda kucheki ustaarabu kisha utatutonya kwenye simu ili tusogee au tuminye kwanza."
Mzee Jonathan aliunga mkono hoja ya Black.
Waliendelea kujivuta mdogo mdogo kutoka porini na kusogea kijijini. Jua lilikuwa likiwaka kama vile limetumwa kwani ilifikia muda mpaka walivua mashati yao na kubakia na vivesti tu huku Masanja akiwa kavua na buti zake huku akitembea kufuata vivuli vya miti.
"Halafu dogo nakushangaa umevua viatu ikitokea mtanange hapa na wabaya wetu itakuwaje?"
Black alimuuliza Masanja.
"Mbele kwa mbele brother itafahamika tu maana si kwa malengelenge haya labda kwa mchanga huu wa moto yatapona."
"Ongezeni mwendo jamani si mnajua kuwa tunaweza kufia karibu na zizi."
"Kivipi mzee Jonathan?"
Masanja aliuliza.
"Nina maanisha kuwa ng'ombe anapotoka machungoni mara nyingi akikutana na kadhia yoyote hupambana na kwenda kufia karibu na zizi sasa basi isije tokea tukaishia kuliona gari tu likitusubiri huku tukitiwa mikononi mwa wenyewe."
Mzee Jonathan aliwapa tahadhari wenzake.
" Vyovyote vile mzee japo mimi nina amini kuwa tumeshapona na masaa machache yajayo tutakuwa maskani kuungana na familia zetu ambazo mpaka sasa hazijui tunafanya kazi gani ya ziada."
Masanja alijibu muda huo akiwa kakaa chini akivaa viatu.
"Halafu wewe dogo kanisani kwenu si wanakuamini sana?"
Black aliuliza.
"Kaka acha tu, usiongelee hayo kwani ni juzi tu nimekabidhiwa funguo ya chumba cha kuhifadhia vyombo vya muziki kama mtunza stoo."
"Kweli duniani kuna vimbwanga sana na ninachojiuliza itakuwaje siku ambayo Masihi atakuja ghafla na kuwakuta watu wake tuwaaminio kama Wachungaji, Maaskofu, Manabii na Mapadri wakiwa kwenye Vilinge vya Waganga wa kienyeji wakipigwa chale kuhakikisha wanapata waamini wengi na sasa wewe ambaye ni jambazi sugu nchini unapewa cheo kanisani kisa tu misaada ambayo huitoa na huo upole wako, ila siku zaja."
Black alimpa ukweli wake Masanja.
" Black kwenye hilo ikiwa litatokea hata leo basi ni wengi tutaumbuka kwani mimi mwenyewe kanisani kwangu ni miongoni mwa wazee wa kanisa na hata taarifa zangu zilipochapishwa kwenye magazeti sikuamini pale nilipoona waumini wenzangu na viongozi wa kanisa wakichukua jukumu la kunitetea huku wakisema ndivyo ilivyo kwa mtu mwenye mafanikio na hata nilipofikia maamuzi ya kuweka rasta hizi ilibidi niende kanisani kuomba kibali cha safari kuwa nitakuwa nje ya mkoa kwa mwezi mmoja."
Mzee Jonathan alieleza na yeye namna alivyoficha makucha yake kanisani.
" Itakuwaje sasa ikiwa tunarejea bila kufanikisha zoezi lako utawaeleza nini kanisani ukiwa na minywele yako hiyo?"
Aliuliza Masanja.
" Itafahamika kwani mpaka tufike Mwanza na akili mpya nitakuwa nimeipata."
"Bora yangu ambaye nikitimba mjini hata sasa sina shaka na yeyote maana ndivyo nilivyo."
"Acha uongo Black ni nani mitaa ya Makoroboi asiyejua kuwa wewe ni Mshona viatu na muuza maji mashuhuri?"
"Jamani ee bati ndiyo zile pale sasa Black fanya kama tulivyokubaliana."
Mzee Jonathan aliwaelekeza wenzake.
"Sawa mzee."
Black alijibu huku akiikabidhi bastola yake kwa Masanja.
"Nini sasa umechanganyikiwa nini brother mbona unanikabidhi silaha?"
"Inatakiwa niwe mimi kama mimi ili wasinistukie maraia."
"Na mimi naona kweli Black umechanganyikiwa hiyo si ni bastola kwanini usiiweke sehemu yake ndani ya koti au kwenye suruali?"
Mzee Jonathan naye alimshangaa Black.
"Sorry jamani, jua nalo limetuchoma sana utosini."
Alijitetea Black.
"Wahi bwana hatuna muda wa kupoteza hapa."
Mzee Jonathan alimtaka aondoke kuelekea kijijini kusoma mazingira.
Huku yeye akiitafuta namba ya Rashid ili amuulize kama kafika tayari.
"Wapi hapo dogo?"
"Ndiyo naingia hapa stendi ya Bitimanyanga mzee."
"Okay sasa kuna kijana anakuja hapo kavalia jinsi nyeusi na kikoti chake cha jinsi na kiatu cha kaki."
"Sawa mzee nimekupata."
Baada ya simu hiyo alikata na kumpa ishara Black aondoke kwenda.
***
"Mkuu hali ya hewa imechafuka kule machimboni."
Mlinzi mmoja aliyekuwa miongoni mwa walinzi kule mgodini kwenye mawe alikuwa akitoa taarifa kwa mzee Bruno Gautier kwa kile alichokishuhudia kabla ya kutimua mbio ndefu ambazo nusura zimtoboe kisogo kwa buti zake.
" Unasemaje wewe Karumekenge?"
Mzee Bruno alimuuliza.
"Mkuu wale wasichana na bwana wao uliowaleta kule kugonga mawe si watu kawaida hata kidogo yaani hawafai."
Mlinzi aliendelea kumueleza mkuu wake ambaye alikuwa akimshangaa tu.
"Unaongea nini wewe hebu ongea kama mwanaume siyo unabana bana sauti kama mtoto wa kike, kuna nini?"
Mzee Bruno Gautier alimuwakia mlinzi yule ambaye jasho lilikuwa likimtoka utadhani katoka kwenye marathoni zilizokuwa zikifanyika Jangwani.
"Mkuu wale wasichana uliowaleta kule machimboni hawafai hata kidogo waliyofanya kule si ya Ulimwengu huu kwani wamewafyekelea mbali wale mabaunsa wote na mbaya zaidi wameviteka vizimba vyote vya ulinzi baada ya kuwaua wenzangu na wengine wamewapeleka kung'oa mawe na wao wakiwa ndiyo walinzi wao."
Mlinzi aliongea huku akipukuta jasho kwa viganja vya mikono.
" Na kwanini wewe umepona na kuwa hapa?"
" Mimi nilikuwa kujisaidia nilipotoka sikuweza kuwaona wenzangu na wakati nikiwa kwenye harakati za kuwatafuta ndipo niliwaona wale mabaunsa kule chini wakiteswa na wale mabinti wawili wanaofanana kama midoli ya Kichina na huku lile bwana lao likiwamwagia mchanga machoni ili wasione na kisha kuwapiga kirahisi mpaka kuwaua na wakati nikitaka kushuka kuwafuata ndipo nilipomuona yule msichana katili kuliko wote aliyemuua James akiwaongoza wenzangu kuelekea kule maweni, ikabidi nijifiche ili nione atawafanya nini ndipo nilipoona akiwakabidhi vitendea kazi waanze kazi na hapo ndipo nilipoona njia pekee ni kuja kutoa taarifa mkuu."
"Paaaaaaaaaaaa......"
Ilikuwa ni mlio wa risasi ambayo ilifyatuliwa na mzee Bruno na kumtwanga yule mlinzi kwenye paji la uso na kumpeleka chini.
"Shwaini mangamba wewe unaniambia utumbo mimi 'eti nilijificha ili nione' umekuwa mwandishi wa habari wewe na bunduki yako ilikuwa ya kazi gani kwanini usiwatawanye bongo zao?"
Mzee Bruno Gautier kama chizi vile alikuwa akiongea kwa vitendo huku akionyesha ishara ya kushika bunduki na kuzunguka nayo pale aliposema 'kwanini usiwatawanye bongo zao' hakika taarifa hizi hazikuwa nzuri kwake hata kidogo kwani kwa muda ulioishi na kumiliki mgodi ule hakuwahi kukutana na upinzani kama anaokutana nao kutoka kwa hawa viumbe wa ajabu ambao ukiwaona sura na miili yao ilivyo huwezi amini ukiambiwa ndiyo wanaoisumbua akili ya mzee Bruno na Santana.
"Aaaaghhh buuuushiiiiiit, nakuja kuwafyekelea mbali mimi mwenyewe kenge msiokuwa na damu nyinyi."
Aliondoka na kuuacha mwili wa yule mlinzi pale pale chini na kushuka ngazi haraka. Alipofika chini ni kama vile kuna kitu alikikumbuka hivyo aligeuza na kuanza kuzipanda ngazi tena haikuchukua muda hata kabla hajafika mwisho wa ngazi zile alirudi tena mpaka chini na kuanza kutembeatembea kutoka kulia kwenda kushoto mara kushoto kwenda kulia na kama ungekuwa karibu ukimuangalia ungejua labda anahakiki urefu na upana wa shamba lake huku mikono ikiwa nyuma na kichwa chini na kwa mara ya kwanza mzee Bruno alitoa kofia yake mbele ya macho ya wafanyakazi wake na kuanza kuukuna upara wake hapo ni hakika maji yalikuwa yamezidi unga.
"Mkuu nasubiri amri yako."
Mlinzi alimshtua mkuu wake mzee Bruno kutoka kwenye mawazo.
"Tokaaaaa nani kakuita hapa kama una nguvu si uende ukapambane na virusi visivyosikia dawa kule kwenye mawe alaaaaaa."
Mzee Bruno Gautier alitoa sauti kubwa akimfukuza mlinzi wake na kuwafanya wote waliokuwa eneo lile kupatwa na hofu kwani mara nyingi hali kama hii ya kupiga kelele huwa ikimpata tu kitulizo chake huwa ni kutaka aletewe mtumwa mmoja au wawili na kunyongelea mbali au kuwaua kwa kuwafyeka vichwa vyao.
"Jamie kuja hapa haraka."
Alimwita mmoja wa walinzi wake tegemezi.
"Mkuu niko mbele yako tayari kwa kupokea oda yako."
"Kenge wewe unataka oda yangu ipi kama wewe kidume si uende kule mgodini ukaokoe jahazi ambalo limezama."
"Jahazi gani mzee mbona kule mgodini hakuna bahari wala ziwa?"
"Keleleeeee, nitausambaza ubongo wako wewe mtoto wa malayaa ohhhooo nenda kule ofisini katoe mzoga wa ndugu yako na mhakikishe mnauchoma moto sawa?"
"Sawa mkuu."
Mlinzi alijibu na kuondoka eneo lile kuelekea juu kama alivyoelekezwa lakini alipofika kwenye ngazi kama ya tano hivi aligeuka kumuangalia bosi wake ambaye aliendelea kuongea kimya kimya huku vitendo vikitawala zaidi, mlinzi huyu Jamie aliishia kutikisa kichwa tu na kuendelea kuzipanda ngazi.
Alipofika ofisini kwa bosi wake hakuamini macho yake baada ya kumuona rafiki yake akiwa kalalia dimbwi la damu ambayo ilikuwa imeanza kuganda Jamie alilia sana huku akipiga magoti kumkagua vizuri rafiki yake Ogingi ambaye walishibana sana na pia wote wana asili ya Afrika katika nchi ya Kenya.
"Umepatwa na nini rafiki yangu mpaka kuondoka bila kuniaga rafiki yako? Nitamweleza nini mchumba wako pindi atakaponiuliza uliko?"
Aliuliza maswali ambayo hakupata majibu yake na badala yake alitoka ofisini mle na kushuka ngazi haraka silaha ikiwa mkononi na kumfuata mkuu wake huku akitokwa na jasho jingi. Akiwa hatua chache kutoka pale alipo mzee Bruno aliteleza na kuanguka na hapo mzee Bruno aligeuka baada ya kusikia kishindo kile cha kitu kuanguka.
"Unafanya nini hapa wewe? Nimekupa kazi gani?"
"Samahani mkuu nilikuwa namfuata wa kunisaidia."
"Fanya haraka Jamie utamfuata sasa hivi kama unasuasua hapa."
"Samahani mkuu."
Jamie alijibu huku akiinuka kutoka pale chini na baada ya kusimama aligeuka tena kumuangalia mzee Bruno Gautier ambaye muda huu alikuwa akivuta kiko chake na kwa namna ambavyo Jamie alikuwa akimuangalia kwa hasira bila shaka alikuwa akimwambia kimoyomoyo kuwa bahati yako nilidondoka ishukuru ardhi.
NINI KITATOKEA?
TUKUTANE KATIKA SEHEMU INAYOFUATA KUJUA NINI KITATOKEA NDANI YA NGOME YA MZEE BRUNO GAUTIER.
"Ninyi hapo nifuateni haraka."
Jamie aliwataka walinzi wawili aliowakuta nyuma ya jengo la utawala waongozane ofisini kwa mkuu wao kuubeba mwili wa Ogingi.
"Jamie mbona ghafla hivyo tukufuate wapi na kufanya nini?"
Mmoja wa walinzi aliuliza.
"Umeota mapembe siku hizi dogo siyo umesahau tulikokutoa siyo?" Jamie alimuuliza mlinzi huyu.
"Samahani kaka Jamie nilikuwa natania tu twende zetu basi."
"Endelea kuvimbisha kifua wewe si Jemedari mkuu wa Ngome."
"Kaka Jamie na wewe hutaniwi tu mbona yamekwisha kitambo hayo."
"Maamuzi yangu ni haya, wewe baki hapa na maswali yako wewe pale nifuate huku haraka."
"Sawa brother."
Yule mlinzi alimfuata Jamie kule juu mpaka kwenye ofisi ya mkuu wao na kuingia ndani ambako bado mwili wa mwenzao ulikuwa pale pale chini ukisubiri kutolewa na kupelekwa eneo maalum ambalo huichoma kupoteza ushahidi kabisa.
"Jamie hivi tutaendelea kuyafumbia macho matukio haya ya wenzetu kuuawa mpaka lini lakini?"
"Sikiliza dogo sauti zetu hata tuzipaze vipi haziwezi fika popote zaidi ya kuishia kwenye tanuru la moto ambako mwenzetu ndo tunampeleka huko lakini laiti kama tungekuwa na roho za kijasiri kama wale wageni hakika Ngome hii ingekuwa huru na tungepata fidia kwa miaka yote tuliyohudumu humu ndani."
"Ni kweli kabisa kaka lakini bado tuna muda wa kufanya kitu." Mlinzi yule alimwambia Jamie kuwa muda wanao.
"Hebu mshike huko miguuni tufanye kama tulivyoagizwa si unamjua mzee huyu kwa machale?"
"Haya kaka twende zetu mshike vizuri hapo ila kaka fanyia kazi hili tunaweza kufanya jambo."
"Chunga mdomo wako dogo utakuponza shauri yako kumbuka Ogingi tulikuwa naye masaa machache yaliyopita na sasa jina lake limebadilika na zaidi roho yangu inaniuma sana kwani ni juzi tu alinionesha picha ya mpenzi wake ambaye alimuacha nyumbani Kenya akiwa mjamzito kabla hajahadaiwa na maajenti wa mzee Bruno Gautier walioenea bara zima la Afrika wakiwadanganya kuwa huku Brazil kuna fursa nyingi za kazi za migodini na baada ya kufika huku ndoto zetu zote huyeyuka na kufunikwa blanketi zito lenye kiza kinene ambacho hatujui hatma yake ni lini?"
Jamie alionekana kuguswa sana na kifo cha rafiki yake na hivyo kumsihi mlinzi mwenzake kuacha mawazo ya hovyo.
" Mlikuwa bado hamjamtoa tu si ndiyo?"
Mzee Bruno Gautier aliwauliza.
" Ni kweli mzee shida ilikuwa ni namna ya kumbeba ni mzito sana."
Jamie alimjibu.
"Kelele wewe fanyeni haraka kisha mje hapa niwape jukumu jingine sawa?"
"Ndiyo mzee."
Walitoka na kuelekea eneo lililo na tanuru la kuchomea maiti na kisha kumuweka ndani yake wakapanga magogo kisha mafuta ya taa yakafuata na baadaye wakawasha moto ambao ndani ya muda mchache ulimteketeza Ogingi na kuwa majivu na hapo walirudisha taarifa kwa mzee Bruno ambaye mara zote hufurahia matukio hayo ila ilikuwa tofauti kwa tukio hili kwani pamoja na kupokea taarifa hiyo yeye alikuwa mbali kimawazo akivuta zake kiko tu huku mkono mwingine ukigusagusa kifuko cha kuhifadhia bastola.
"Mkuu tunasubiri oda yako."
"Okay hebu ongozaneni na walinzi wengine kumi muelekee kule mgodini mkaniletee wale wageni ambao tuliwapeleka kule kwa mateso."
"Sawa mkuu kama ulivyoagiza."
Waliondoka pale na kuwafuata wenzao na kumuacha mzee Bruno ambaye baada ya maagizo yale alianza kupanda ngazi taratibu kuelekea ofisini kwake kusubiria matokeo ya kile kitakachotokea huko.
"Sijui itakuwaje kwa hawa wakifika huko maana maji yamenifika shingoni daa, Weee naniiii.......! Aisee kumbe tayari wameshakwenda."
Alijishtukia kuwa mawazo yake yalivuka kiwango cha kawaida hadi kufikia kutaka kuwaita watu ambao muda mrefu walishakwenda mgodini.
Alipanda ngazi na kuufungua mlango wa ofisini kwake na kisha aliingia.
Wale walinzi wakiongozwa na Jamie walifika kule mgodini mpaka eneo linalochimbwa mawe na kuanza kulivizia eneo walilokuwepo wakina Jackline kwa tahadhari kubwa.
"Sikilizeni tunakoelekea kuna watu hatari sana na mpaka sasa wameshaua wenzetu kadhaa na wengine wanawashikilia huku huku cha kufanya hapa ni kila mmoja apite njia yake lakini makutano ni pale kwenye zile Tenti ambapo nina uhakika muda huu wa usiku watakuwa pale wakipumzika hivyo tukiwavamia kutoka pande zote itakuwa rahisi kwetu kuwakamata."
Jamie aliwatahadharisha wenzake na kuwapanga pia namna ya kuvamia Tenti za wakina Jackline.
" Tumekusoma kiongozi."
Alijibu mwenzao mmoja wakati wengine wakipotelea kizani.
Kila mmoja akifanya kama walivyokubaliana.
Kwa kuwa eneo lile wao ni wenyeji wakilijua vizuri halikuwasumbua sana kuzifikia zile tenti na kwa ishara ambayo walipanga kuitumia kwa pamoja waliwasili na kuitageti kutoka pande zote.
Baada ya kuhakikisha kuwa wote wako kwenye eneo lengwa Jamie alianza kuisogelea tenti ya kwanza na ili kuwateka waliomo ndani yake na baada ya kuchungulia kupitia kitundu kimoja wapo hakuweza kuona kitu ndani yake zaidi ya vigodoro visivyo na watu juu yake, hali ile ikamrejesha nyuma haraka Jamie kuwafuata wenzake kuwapa taarifa ya alichokiona.
"Kaeni sawa eneo hili si salama kwani ndani ya tenti la kwanza hakuna kitu inawezekana wametushtukia, ngoja niangalie lile la pili kwanza."
"Sawa big fanya yako."
Alirudi tena kwenye tenti la pili na safari hii akienda kwa staili ya kutambaa mpaka lilipo tenti la pili.
Baada ya kulifikia alisimama na kuchungulia kwa staili ile ile lakini bado hali ilikuwa kama ya kwenye tenti la kwanza kwani hakukuwa na mtu yoyote ndani yake na hapo akajua kwa vyovyote vile maadui zao wamewazunguka ikabidi arudi haraka kwa wenzake kuwataka kurudi nyuma haraka kabla hawageuzwa asusa na wakina Jackline. Lakini alishachelewa kwani ile anainuka tu alikutana na ngumi nzito iliyotua vilivyo kwenye shavu la kulia na kumtupa chini alipojaribu kuinuka alipigwa risasi ya mguu na kumfanya Jamie kutoa mlio wenye mchanganyiko wa maumivu makali.
"Usiniue, usiniue tafadhali siyo matakwa yetu ni mkuu wetu mzee Bruno."
Jamie alianza maelezo mwenyewe kabla ya kuulizwa inawezekana kutokana na namna alivyootewa na ile ngumi na kisha risasi akajua ahera inamwita.
"Brother mwili mkubwa namna hiyo kumbe muoga hivyo?"
Robinson alimdhihaki Jamie huku akimkanyaga sehemu ile aliyomtwanga risasi. Na kwa namna ambavyo kimwezi kilikuwa kiking'ara haikuwa tabu kwa mtu kuweza kumuona adui yake.
"Kaka nisamehe kwa kweli sisi si watu wabaya bali ni mzee Bruno ndiye aliyetuagiza kuja kuwakamata."
Aliendelea kujitetea Jamie.
"Anasemaje huyo?"
Jasmine aliuliza.
"Anachochote basi ni stori zile zile za kukikimbia kifo."
Robinson alijibu.
"Sikiliza kaka sisi si watu wabaya kwenu ila mnaweza kutuita Upepo wa Jangwani ambao huwa hauzuiliwi na chochote, na hatuwezi kuwaua ninyi ila tunawaagiza kwa bosi wenu mkamweleze kuwa chimbo limevamiwa na si chimbo tu bali Ngome nzima lakini anaweza fanya jambo ambalo si jingine zaidi ya kumtaka mzee huyo afike kwenye majadiliano."
Jackline alimuagiza Jamie kwa mzee Bruno Gautier.
" Sawa sister nashukuru kwa nafasi nyingine ya uhai wetu nakuhakikishia kulifikisha hili usiku huu huu japo mguu umepata hitilafu."
"Halituhusu fanya kama tulivyokuagiza brother na mkamweleze kuwa kuna kitu anachokitegemea tunakishikilia."
Jasmine aliongeza.
"Sawa dada ngoja tukamwambie."
Baada ya maagizo hayo waliwaachia na wao kurudi kwenye ficho lao ambalo bado halikuweza kufahamika mara moja.
Kwa kukongojana hivyo hivyo waliweza kuwasili ofisini kwa mzee Bruno Gautier na kumgongea mlango. Lakini haukufunguliwa hivyo hali hiyo ikawachanganya kidogo lakini wakaona wajaribu mara kadhaa ndipo mlango ukafunguliwa na mzee Bruno ambaye ilionekana wazi alikuwa kalala kwa namna alivyotoka akipiga miayo mingi.
"Lete taarifa Jamie."
"Mzee hali ni mbaya sana huko kama utuonavyo tulivyochakaa kwa majeraha."
"Keleleeeeeee weweeee unaongea nini majeraha kitu gani mbona hakuna aliyekufa kati yenu?"
"Mkuu wameteka baadhi ya maeneo yako mpaka sasa."
"Unasemaje weweeee?"
Mzee Bruno Gautier alipagawa baada ya kusikia habari za kutekwa kwa maeneo yake.
******
Black alishika njia mpaka ndani ya kijiji cha Bitimanyanga na kuibukia madukani, alipofika alielekea kule ambako aliiona ile Toyota Cruiser imepaki kwa rangi na muundo alijua ndiyo yenyewe. Baada ya kuifikia alijaribu kukigonga kioo cha mbele ili kuona kama kuna mtu ndani yake, lakini kimya kilitawala hivyo ikabidi anyonge kitasa lakini akakutana na lock akachanganyikiwa lakini wakati kijasho cha hofu kikimshika ikajikuta akishikwa bega kwa nyuma.
"Brother vipi kwenye gari langu?"
"Sorry ndugu nimeona imepaki hapa nilijua kuna mtu ndani yake na ndiyo maana nilikuwa nikigonga."
"Ili iweje baada ya hapo?"
"Shida yangu ni lift tu na si kingine ndugu yangu nimetembea kwa umbali mrefu kutoka Isangawana mpaka hapa kwa zaidi ya kilometa thelathini nimechoka hivyo nikaona niombe msaada."
"Isangawana ndiyo wapi na unaelekea wapi?"
"Ni mji ulioko huko nyuma na mimi naelekea Sikonge nilikuwa kwenye matumbaku lakini mambo yamekuwa tofauti na matarajio yangu hivyo nimeona nitoroke tu."
"Ha ha ha ha ha ha ha ha ha, kaka uko vizuri kwenye kutengeneza uongo ee, tuache hayo unamfahamu mzee Jonathan?"
Ilibidi Rashid amuingie kwa kutumia utambulisho wa mtu anayewaongoza wote, na kwa swali lile Black akajua ni mwenyewe ikabidi akubali.
"Namfahamu na ndiye aliyeniagiza kwako."
"Okay okay ngoja nimpigie basi kumjulisha kuwa umefika."
Alitoa simu mfukoni huku akimpa ishara Black ya kuingia ndani ya gari, baada ya kumpata hewani aliongea naye.
"Kijana wako keshafika tayari hivyo ni muda wako kuja tunakusuburi mzee wangu."
"Okay vizuri sana basi tangulieni mbele kidogo mtoke hapo katikati ya mji uelekeo wa Tabora."
"Sawa mzee kama ulivyopendekeza."
Kisha alikata simu na kuingia garini na kumkuta Black akimsubiri.
"Nambie brother habari ya Chunya?"
"Mmhh mimi si mwenyeji wa huku ni mwenyeji wa Mwanza huku tulimsindikiza mzee Jonathan kwenye shughuli zake za uwindaji sema nini tumechoka sana baada ya kupotea porini humo kwa zaidi ya kilometa ishirini."
"Aisee poleni sana."
"Asante sana brother, vipi mbona unaondoa gari kabla mzee hajafika?"
"Usihofu kaka kasema hapa tuondoe gari tukasimamie mbele kidogo."
"Okay sawa."
Wakiwa wanaeleweshana katika hilo mara simu ya mke wa mzee Jonathan iliingia kwenye simu ya Rashid na kisha aliipokea.
"Ndiyo mama nakusikia."
"Vipi umefika?"
"Nimefika ndiyo namsubiri atokee."
"Okay umewasiliana naye lakini kuwa uko hapo?"
"Yaani wakati yeye anakata simu tu na ya kwako inaingia mama."
"Vizuri mwanangu pole kwa usumbufu lakini?"
"Hapana mama kuwa na amani tu."
"Haya mwanangu nikutakieni safari njema muondoke salama na mfike salama pia."
"Asante mama."
Alipofika eneo ambalo barabara ni pana kiasi aliipaki gari pembeni kuwasubiri mzee Jonathan na Masanja. Kisha aliteremka chini kuangalia kama amelipaki sawa sawa na baada ya kujiridhisha alirudi garini na kuchukua moja ya kiboksi cha chakula na kumkabidhi Black huku yeye akishuka na kuelekea madukani kuongeza chakula pamoja na vinywaji.
NINI KITATOKEA?
TUKUTANE KATIKA SEHEMU INAYOFUATA KUJUA KITAKACHOENDELEA.
Rashid aliingia kwenye duka la vinywaji kununua vinywaji kwa ajili ya mzee Jonathan na vijana wake ambapo mara baada ya kumuona Black alibaini kitu kutokana na midomo yake kuonesha kukosa chakula kwa muda fulani maana midomo ilikuwa imemkauka sana hivyo alijiongeza, baada ya kununua alitoka na kuelekea kwenye kibanda cha kuuza vyakula lakini akiwa mdogo mdogo mara aliliona gari la polisi almaarufu kama Tenga likifika stendi na kutia breki zilizosababisha vumbi jingi kutimka kitendo kile kilimshtua sana Rashid lakini kwa kuwa alijiamini kama raia safi asiye na tatizo lolote na mtu yeyote aliendelea na mwendo wake. Lakini ni kama kuna kitu kilimsukuma kuangalia nyuma yake huko aliweza kuwaona askari polisi wakiruka kwenye Tenga hilo na kusambaa eneo lote huku mkuu wa kikosi kile akitoa tangazo kupitia kipaza sauti kilichokuwa kwenye gari.
"Ndugu wana Bitimanyanga nina wataarifu kuwa tuko eneo hili kwenye oparesheni maalum ya kuwasaka wahalifu ambao wako eneo hili, unachoombwa ni kutoa ushirikiano kwa jeshi lako la polisi kwa kutoa taarifa za watu hao ambao picha zao ndiyo zinabandikwa na askari wangu. Sura hizo ukiziona toa taarifa kwetu na kama kuna yeyote aliyewahifadhi kwa kujua au kutokujua ajisalimishe mwenyewe kwetu."
Wakati mkuu wa kikosi huyo akiendelea kutoa tangazo ilibidi Rashid asitishe zoezi lake la kuelekea kwenye banda la vyakula na kuongoza kwenye picha mojawapo iliyokuwa imebandikwa karibu na alipokuwa.
" Hee nini tena? Huyu aliye hapa mbona ni yule brother niliyemuacha kwenye gari? Na hawa wengine ni wakina nani?"
Rashid hakutaka kupoteza muda wake haraka sana aligeuza na kuongoza kwenye gari akamuangalie aliyemuacha ndani ya gari.
"Kijana hapo hapo simama mbona mbio mbio kwenye gari mara baada ya kuliona tangazo lenye picha za wahalifu wetu?"
Sauti hiyo iliyotoka nyuma ya Rashid ilimshtua kwani ilikuwa imeshirikiana na mdomo wa bunduki iliyokuwa tayari kwenye kisogo chake.
"Usijaribu kuvuta hata robo hatua nitausambaza ubongo wako."
Askari huyo aliunganisha maelezo kabla hata ya Rashid kujitetea.
"Afande ngoja tu niwe muwazi kwenye hili."
"Ehee ukweli gani huo? Eleza haraka kabla ubongo wako sijautawanya."
"Mimi nimefika hapa dakika chache kutoka Tabora na...."
"Tabora? Na hapa umefuata nini mbona una hofu?"
"Hofu lazima niwe nayo Afande kwa sababu mimi safari yangu ilikuwa inaishia Kambikatoto kununua asali lakini nikaambiwa huku pia inapatikana ikabidi nije lakini hali ikawa tofauti nikakuta bei iko juu ikabidi niondoke lakini nilipofika pale gari lilipo nikasimamishwa na kijana mmoja ambaye akaniomba lifti na nilipomhoji akasema katokea huko sijui Isangawana kwenye tumbaku na kule alishindwa kuvumilia manyanyaso ya bosi wake hivyo akatoroka na baada ya kufika hapa akawa kachoka sana na ndipo alipoona aombe lift mpaka Sikonge ambako ndiyo kwao basi nikaona nimchukue kama ilivyo kwetu watanzania tumejaaliwa huruma na ndipo nikaona nifuate vocha na hivi vinywaji kisha safari iendelee lakini kilichonishtua mpaka kutembea haraka hivi ni baada ya kumuwahi kwani kwenye ile picha mmoja wao ni yeye hivyo nilikuwa nakimbia kumuwahi."
"Afande Nyigo tufuate haraka.
Simama na wewe hapa kule usiende kwani tayari ni hatari tuachie sisi mchezo huu."
Pale pale Rashid alitoa simu yake mfukoni akaishika kisha akaifungua na kutoa betri kisha laini baada ya hapo aliiweka chini na kuifukia kwa mchanga kwa kutumia raba yake, laini na betri alivirusha pembeni baada ya kuhakikisha hakuna anayemuangalia kisha akasogea pembeni kidogo kutoka pale na hii ilikuwa ni baada ya kubaini kuwa kuna kila dalili ya kutiwa mbaroni kwani alihisi mzee Jonathan hayupo maeneo yale ila tu aliyekuwa garini ni mtu wake na inawezekana ndiye aliyemfuata.
"Kwanini mzee Jonathan na mke wake wanifanyie hivi?"
Rashid alijiuliza swali hilo pasipo kujua miongoni mwa wanaotafutwa na walio kwenye ile picha ni yeye lakini ule muonekano mpya ulimchanganya Rashid.
"We dogo mbona hakuna mtu humu unatuchezea sisi siyo?"
Yule afande alimgeukia Rashid baada ya kukuta gari jeupe halina mtu.
Ilibidi Rashid asogee akajiridhisha mwenyewe kwani ni mtu ambaye alimuacha ndani ya gari wakati akielekea dukani.
"Basi ametoka mbona nilimuacha humu ndani Afande?"
"Kijana usicheze na sisi kumbuka tumechoma mafuta yetu kuwafuata wao?"
Wakati afande huyo akiendelea kumuwakia, Rashid ilibidi ainame chini ya gari na kuchungulia kama anaweza kumuona lakini hakuweza kumuona ila kuna kitu alikiona.
"Afande angalia hapa hii ni alama ya viatu vyake."
Wakati ameshuka alikanyaga pale kwenye mchanga ikabidi yule afande na mwenzake Nyigo kuanza kufuatilia zile kanyagio za Black. Huku nyuma Rashid alibaki ameegemea gari asijue la kufanya.
Lakini akiwa pale kundi la pili la askari lilimpita kuelekea walikoenda wenzao na ndipo Rashid akapata wazo la kutoroka na kuliacha gari kwani alihisi kuwa wakirudi huko walikokwenda wakiwa hawajampata lazima adakwe yeye kwa kulisaidia jeshi la polisi.
Aliacha kila kitu na kuanza kutembea kidogo kidogo kama vile yupo huku anaangalia nyuma na akiwa hatua kadhaa kutoka kwenye gari aliliona pikipiki ikija nyuma yake ambayo aliisimamisha na kuombwa kukimbizwa Rungwa.
"Brother mimi sifiki huko naelekea shambani kupeleka chakula kwa vijana wangu."
"Nikimbize kaka wenzangu wananisubiri wasije niacha huku ni mgeni nitakulipa mara mbili ya nauli ya kawaida ya bodaboda."
"Utaiweza ndugu yangu?"
"Kwani ni shilingi ngapi mpaka nishindwe?"
"Nauli ya kawaida ni shilingi elfu kumi na tano na kwa ulivyosema itakuwa nyekundu tatu."
"Hiyo tu?"
"Ndiyo ni hiyo tu."
"Twende zetu basi ila jitahidi mwendo rafiki yangu."
"Kuhusu mwendo usijali shikilia tu nisijefika peke yangu."
"Poa poa."
Alipanda na pikipiki ilianza kulamba vumbi kwa kasi ya sifa kama alivyoomba Rashid.
********
"Kweli nimepatwa au nimezeeka sana? Yaani vile vitoto vinaniendesha hivi? Lakini nitavifundisha adabu si vinaniona boya fulani hivi ee kwanza havina shukrani hata chembe nimevihifadhi hapa lakini havijaona sijui niwataarifu askari wa jeshi la Ulinzi kutoka kambi ya Milton Camp kwa rafiki yangu Afande Felnando? Lakini hapana mimi mwenyewe nawamudu wale."
Mzee Bruno Gautier alikuwa akiongea peke yake huku akijiuliza na kujijibu mwenyewe ni baada ya kuambiwa anatakiwa kwenda mbele ya wakina Jackline.
" Mkuu fanya maamuzi kabla hawajataifisha mali zako."
Jamie alimkumbusha baada ya kuona anajizungusha tu.
"Jamie usinifanye kichwa cha panzi kumbuka mimi ni kamanda mstaafu wa jeshi la maji hapa Brazil hivyo nina mbinu za kila aina za kumkabili adui natakiwa kupanga ni namna gani niwakabili wale Bweha siendi kichwa kichwa tu kama ninyi."
Alijikanyaga kanyaga pale huku akiwaangalia walinzi wake kwa zamu na mate yakiwa hayamkauki mdomoni, alikichukua kiko chake na kukipeleka mdomoni kisha akawasha na kuanza kuvuta huku walinzi wakiendelea kumshangaa tu kwani si kawaida yake anapoletewa habari mbaya huchukua hatua mara moja, sasa kwanini hili la leo limemchukua muda mrefu kufanya maamuzi?
Na mzee Bruno Gautier ni kama aliyasoma mawazo ya walinzi wake kwani aliwaangalia kisha akawaacha na kupanda zake ngazi kuelekea ofisini kwake na sijui ilikuwa ni kwenda kuchukua nini na alipofika ndani aliufunga mlango na kwenda kujitupa kitini kwake na kutulia huku akikigongagonga kiko chake kwenye meno yake ambayo yalikosa ushirikiano. Lakini ghafla mlango uligongwa na haukugongwa kwa utaratibu aliouzoea kitendo hicho kikamshtua mzee Gautier na kujikuta akianza kujipapasa kuikagua bastola yake kama ipo alipohakikisha kuwa ipo mahali pake alisimama na kukivuta kiti kwa nyuma ili kumpa nafasi ya kuufuata mlango.
"Nani anayegonga mlango bila utaratibu?"
Aliuliza mzee Bruno lakini hakupata jibu lolote kutoka nje hapo akajua si salama akaichomoa bastola yake kisha akausogelea mlango karibu zaidi.
"Nani yuko hapo nje mbona hakuna anayejibu?"
Ajabu badala ya kujibiwa mlango uliendelea kugongwa na safari uligongwa kwa chini hali ambayo iliendelea kumchanganya mzee Bruno Gautier akiwa na bastola yake mkononi.
"Mmhh ni nani huyu anayegonga kwa nguvu kiasi hiki na hataki kujibu? Maana wangekuwa vijana wangu ningeujua ugongaji wao kwa vyovyote vile huyu si miongoni mwao, lakini ngoja kwanza."
Mzee Bruno Gautier alijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu na wakati mwingine alikuwa akijijibu mwenyewe. Lakini mwisho alipata wazo ambalo lingemsaidia.
Aliiendea swichi ya taa na kuizima ili kama likitokea la kutokea aweze kujinusuru na baada ya kuzima alipeleka mkono kwenye kitasa cha mlango akakinyonga kikajibu lakini kwa kasi ya ajabu akaubana tena mlango kwa nguvu na kuulock kisha akauegemea huku akihema kwa nguvu. Aligeuka na kujaribu kuangalia nje kupitia nasi zilizo kwenye mlango kuona kama anaweza kuona chochote lakini hakuona kitu bila shaka nafasi haikuwa rafiki kuweza kuona nje. Aliinuka na kujitengeneza vizuri magwanda yake na kisha akaamua kufungua mlango ili liwalo na liwe tu mlango ulikubali sheria na kufunguka na katika hali ya kujiweka salama alijiviringisha kama gurudumu mpaka upande wa pili wa mlango ule na kusimama bastola mkononi. Lakini katika hali ya kushangaza hakuweza kuona kitu chochote zaidi ya mtu aliyekuwa kalala pembeni kidogo ya mlango, alimsogelea na kumuangalia.
Hakuamini macho yake baada ya kukutana na mlinzi wake ambaye alikuwa kachomwa visu vya maana muda mrefu na kuungana na mauti huku pembeni yake kukiwa na kikaratasi chenye damu damu alikiokota na kukifungua maana kilikuwa kimefinyangwa sana.
"MZEE BRUNO GAUTIER MTU USIYE NA HURUMA NA BINADAMU WENZAKO WATOTO WA WANAWAKE WENZAKE NA MAMA YAKO ALIKUZAA WEWE HESHIMA KWAKO, TUMEAMUA KUJISALIMISHA WENYEWE TUKO HAPA CHINI TUNASUBIRI HUKUMU YAKO."
Hakutaka kusubiri asome mpaka mwisho moja kwa moja akajua ni wakina Jackline tu hivyo haraka sana akazivamia ngazi na kushuka kwa kasi kwenda kukutana nao ili awadhihirishie kuwa yeye si mtu wa kawaida hata kidogo.
Alipofika kule chini hakuweza kuona chochote kama ujumbe ulivyoeleza na hapo ndipo alipopandwa na hasira zaidi na kuanza kuzungukazunguka huku akijipigapiga kichwa chake kwa bastola yake.
"Washenzi sana ninyi si mjitokeze sasa kama miamba ya vita."
Aliongea kwa sauti ambayo bila shaka hakujua kama amepayuka kwa nguvu lakini akiwa anataka kurudi kule juu mara alisikia sauti ya mtu akihema kwa tabu sana ndipo alipogeuka na kuifuata sauti ile.
" Buuuu shiiiiit......! Nitaua mtu mimi haki ya Mungu tena naapa."
Aliongea hayo akienda chini kwa hasira si kwamba alipigwa hapana bali alichokiona ndicho kilimfanya aende chini na kujipigiza kichwa ardhini.
ALIONA NINI MZEE BRUNO GAUTIER?
USIKOSE KUSOMA SEHEMU INAYOFUATA YA HADITHI HII KUPATA MAJIBU.
"Ina maana haya yote yanafanywa na hawa vimburu?"
Mzee Bruno Gautier alijiuliza akiwa bado chini kakaa huku macho yake yakiwa kule kwenye kile anachokishuhudia mbele ya macho yake walinzi karibia wote walikuwa wamepigwa kudu za kutosha nje ya banda ambalo walifungiwa wakina Jackline kwa mara ya pili mara baada ya kutoka kwenye vile vibanda ambavyo walifungwa tofauti tofauti na walinzi hawa walifungwa kila mmoja peke yake na kulazwa eneo moja kama vile wanasubiri hatma yao kutoka kwa Faraoh.
"Jamie nini kimewakuta mbona sielewi elewi jamani?"
Mzee Bruno Gautier alimuuliza Jamie kilichotokea, lakini Jamie hakujibu chochote zaidi ya kumtolea macho tu kitu kilichoendelea kumtisha mzee Bruno.
Alipoona hajibiwi chochote aliamua kufanya maamuzi ambayo alihisi yataleta mafanikio usiku huo hivyo alikiendea king'ora ambacho huwa kikigongwa tu watu wote mle ngomeni hutoka haraka kwani huwa ni kiashiria cha hatari.
Alifika na kupeleka mkono kwenye swichi ya king'ora ili abonyeze lakini katika hali ya kushangaza kabla hajabonyeza alikutana na teke moja matata sana lililompata sehemu nyeti na kwenda kuangukia ukuta wa banda lile lililofungwa king'ora kile huku akipiga ukelele wa maumivu.
"Aaaaghhh pu**u zangu jamani."
"Kelele mzee, hautakiwi kupiga kelele unapokutana na sura hizi sawa?"
"Mmmmmmmmmhhhhh."
Mzee alishindwa kujibu zaidi ya kuguna huku akitikisa kichwa sura akiwa kaikunja kama vile anakamuliwa kijipu uchungu.
"Siyo Mmmmmmmmmhhhhh kwani bubu wewe toa sauti yako ile ya kibabe."
"Nimekukoseeni nini mimi?"
"Unataka kujua?"
"Ndiyo nahitaji kujua."
"Okay vizuri sana sasa nakwenda kubonyeza swichi ya king'ora ili kuwatoa nje watumwa wako uliowafuga humu ndani ili uwaeleze kile ambacho ulilenga kukifanya nilipokukuta."
"Ha... !" Kabla hajamalizia alikatishwa.
"Shiiiiiiiiii funga domo lako mzee utaongea king'ora kikijibu."
Kama vile Jackline alikuwa anatania kumbe alikuwa kadhamiria kweli aliisogelea swichi na kuibonyeza huku nyuma mzee alijipapasa kuangalia kama bastola iko sehemu yake ili amuwahi Jackline kabla hajakipiga king'ora lakini alikuwa kachelewa kwani muda ule kapigwa teke la Ikulu na kuangukia ukutani bastola ilianguka pembeni na kuonwa na Jackline ambaye aliichukua, king'ora kililia kweli na watu waliokuwa ndani ya Ngome ile wake kwa waume na watoto walitoka nje huku kila mmoja akiwa hajui usiku ule kuna kitu gani wanakwenda kuulizwa, waliongoza mpaka eneo la makutano na kusubiri kinachokwenda kutokea muda huo Lakini walishtushwa na tukio ambalo lilitokea muda ule kwani taa zote za ulinzi pamoja na zile za kawaida zilizimwa na kuzua taharuki kutokana na giza ambalo lilitanda mbele ya macho yao. Na baada ya dakika kama nne hivi ziliwaka tena na mbele yao tayari kulikuwa na watu wakiwa wamesimama ambao waliwafahamu vizuri sana.
"Poleni kwa usumbufu ndugu zangu na tunaomba mtusamehe kwa kuwaondoa kwenye malalo yenu lakini tulikuwa hatuna jinsi ilibidi iwe hivi. Mbele yenu kuna sura ambazo si ngeni kwenu hasa huyu mzee Bruno Gautier."
"Ndiyooooo....!"
Waliitikia kwa pamoja na bila shaka tayari walishajiandaa kuzipokea taarifa zile kwani hawakuwa na hofu yoyote ile.
"Kiongozi wenu kuna mambo kadhaa anataka kuongea nanyi msikilizeni tafadhari."
Jackline aliendelea kupaza sauti mbele ya umati ule ambao ulikusanyika.
"Poleni na majukumu watu wangu watiifu kwangu."
Alianza mzee Gautier.
"Asante twashukuru kiongozi."
Walijibu.
"Nimewaiteni usiku huu kutaka kukuelezeni kuwa kuanzia sasa kutakuwa na mabadiliko makubwa ya kiutawala zaidi katika eneo la Ulinzi ambalo siku za hivi karibuni limeonekana kupwaya sana na mfumo wa maisha pia utabadilika kabisa kutoka kwenye mfumo wa kufanya kazi na kutolipwa mpaka kwenye mfumo wa kulipwa kiasi chochote kitu."
"Ubarikiweeeeee milele kiongozi wetuuuuuu....!!!!!"
Walipaza sauti kumshukuru lakini hawakujua kilichokuwa nyuma ya pazia kwani yale yote aliyoyaongea yalikuwa si maamuzi yake mzee Bruno Gautier bali aliamrishwa na Jackline muda ule taa zimezimwa akisogezwa pale mbele bila wao kujua chochote kile ila kuna baadhi yao waliujua mchezo mzima kwani walikuwa wakishirikiana nao katika kutoa taarifa.
Na baada ya shangwe lile kuendelea pale mara taa zilizimwa tena na mzee Bruno aliondoshwa pale na Jackline mpaka ofisini kwake kule juu huku akimuachia maagizo mmoja wa walinzi ambaye tayari alikuwa mshirika wao kitambo kuwasha taa na kuwataka kurudi vyumbani mwao mpaka kesho ambapo watapewa utaratibu.
Taa iliwashwa tena na kila mmoja alishangaa kuona mbele kukiwa tupu hakuna mzee Bruno wala Jackline lakini alifika yule mlinzi na kuwapa maagizo.
"Mnatakiwa kurudi vyumbani kwenu kuendelea kuutafuta usingizi wenu mlioupoteza ghafla mpaka kesho ambapo taratibu nyingine zitafutwa."
Wakatawanyika wote kutoka lile eneo wakiwa na maswali mengi vichwani mwao.
"Mbona kama naota hivi?"
"Kivipi mzee mwenzangu?"
"Mbona kiongozi wetu leo kaongea lugha rafiki sana ambayo sikuwahi itegemea hata siku moja? Na yule binti mbabe mbona alikuwa karibu yake wakati hawapatani?"
"Hayatuhusu hayo sisi tunachotakiwa kuangalia sasa ni maisha yetu mapya tunayokwenda kuyaishi."
"Ni kweli kabisa mzee mwenzangu, sasa nikutakie usiku mwema."
Waliagana na kila mmoja kuingia sehemu yake. Huku nyuma yule mlinzi aliwafuata wale walinzi wenzake wakina Jamie na kuwafungua zile kama walizokuwa wamefungwa na wakina Jackline.
"Sikilizeni jamaa zangu, mnatakiwa kuungana na mimi katika harakati za kuwaunga mkono hawa ndugu zetu kama walivyosema na kwa yeyote atakayekuwa kinyume nao watampoteza."
"Mimi siko tayari kuhatarisha maisha yangu kisa mzee Gautier nitaungana nao kwanza ukizingatia nilishajiwekea kisasi cha siku moja kuja kumuangamiza mzee huyu baada ya kumuua rafiki yangu Ogingi."
Jamie aliongea hayo kwa uchungu mkubwa huku akiwaangalia wenzake ambao nao walisema wanaungana kuupambania Uhuru wao.
" Hayo ndiyo maneno jamaa zangu na muda huu tunaanza ulinzi feki ikiwa ni pamoja na kufuatilia nyendo zote za mzee Bruno Gautier na kuwataarifu wakina Jackline."
"Kazi rahisi sana hiyo kwanza nimeipenda sana ile kombinesheni ya wale madada na yule bro."
Alijibu Jamie na kutoa ya moyoni mwake.
Wakiwa wanapanga yao pale nje kule ndani moto ulikuwa unaendelea kuwaka kati ya mzee Bruno na wakina Jackline.
"Haya mzee tuongee kikubwa sasa kwa sababu tumeagiza jumbe mbalimbali kukutaka uje kule lakini ukatia jeuri na ndiyo maana tuko mbele yako."
Jasmine aliongea kwa mbwembwe akiwa kwenye kiti cha mzee Bruno akizunguka huku na kule kama vile ndiye mmiliki wa kampuni akiwafanyia usaili wafanyakazi wapya.
" Naombeni tuongee mbona haya yanaongeleka kabisa?"
Mzee Bruno Gautier aliongea kwa sauti ya upole.
"Kwa sasa ndiyo yanaongeleka baada ya kukumbana mbavu siyo?"
Jackline alimsogelea mpaka pale alipokuwa kaketi na kumuuliza.
"Mjue pia mimi si mtu mbaya kwenu hata kidogo hayo niliyowafanyia ilikuwa ni katika kutaka kuwajua zaidi kwani nilijua mnanidanganya siku ile na ndiyo maana sijatoa taarifa kokote kule juu ya uwepo wenu hapa kambini."
"Haituhusu hiyo unadhani hata ungetoa taarifa tunaogopa? Haujui kutoa kwako taarifa kutapelekea kupoteza utajiri wako wote na pia kuchukuliwa hatua wewe na jamaa yako Santana au unafikiri hatujui kuwa Santana ana hisa karibia asilimia hamsini na tano na zinazobakia ndiyo zako wewe na mjomba wako aishiye Misri?"
Jackline alimchana ukweli.
" Mmeyajua vipi haya wakati ni mambo ya ndani sana?"
Mzee Bruno Gautier alitokwa na macho baada ya kuambiwa ukweli huu.
" Tumepata wapi taarifa hizi siyo kazi yako ila tu unachotakiwa kujua ni kuwa sisi ni moto wa kuotea mbali kwani ukiotea karibu nini kitatokea?"
" Hapo lazima uungue."
Alijibu mzee Bruno huku akitazama chini.
"Halafu mzee unajiona jeuri sana wewe?"
Robinson aliuliza naye swali.
"Kivipi kijana wangu?"
"Sikiliza mzee Santana unamjua humjui maana uliuliza tu baada ya kuambiwa na kisha ukaishia kuuliza tu swali."
"Ni kweli namfahamu vizuri kama mlivyo sema ni Shareholder mwenzangu ila mimi nina dhamana ya kusimamia mgodi huu kutokana na uzoefu wangu kwenye eneo hili na juzi hapa nilimtaarifu juu ya uwepo wenu na akasema niendelee kuwahadaa ili siku ikifika aje na watu wake kuwakamata na kisha kuwanyofoa viungo vyenu muhimu kama Moyo, Figo, Macho, na Ulimi kisha kuwauwa na kwenda kuviuza vitu hivyo India ambako vina soko sana na ni biashara ambayo tumekuwa tukiifanya kwa kuwafanyia hivyo watumwa wetu wa hapa na wale wanaojipendekeza kwake kupitia Mitandao ya kijamii kama nyinyi... "
" Keleleeeeee..... "
Jackline hakutaka kuendelea kuusikiliza upuuzi ule uliokuwa ukielezwa na mzee Bruno Gautier.
" Sikiliza mzee inatosha sana kwa madhambi yenu mliyofanya kwa damu zisizo na hatia na sasa ni muda wenu kuyalipia haya na mtayalipia vipi itafahamika."
"Wewe ni kama mwanangu najua kwa umri wenu ninyi bado mnayapambania maisha ikiwa na wewe kuzipigania Mali za marehemu baba yako na mama yako hivyo basi mimi niko tayari kutoa msaada kwa kufanikisha kumtia nguvuni mzee huyo aliyedhulumu na pia kuwapa nusu ya utajiri wangu ambao ni mabilioni ya dollar ikiwa tu mtaniacha huru na biashara zangu."
Mzee Bruno Gautier alitoa ahadi hizo mbele ya wakina Robinson. Kitu kilichomfanya Robinson kutoa mimacho kwenye mgao huo ambao alijua umaskini kwa heri lakini akashangazwa na majibu ya wenzake.
" Ndiyo unajidanganya hivyo mzee Bruno Gautier? Hatudanganyiki na vihela sisi ila tu ili uendelee kuishi utapaswa kufanya yale ambayo tutahitaji uyafanye muda huu, sijui uko tayari?"
Jackline alimuuliza.
"Niko tayari hata sasa."
"Lakini watu wangu mnaonaje kama tukijibebea mihela hiyo na kutokomea zetu kwetu?"
Robinson aliwauliza wenzake.
Kitu kilichowafanya wakina Jackline na Jasmine kutazamana kwa sekunde kadhaa kabla ya Jasmine kumjibu.
"Inaonekana una uchu na vihela vya mzee huyu ambaye anachozungumza hakina ukweli ndani yake."
"Hapana Jasmine nilikuwa nauliza tu."
"Dada zangu muwe makini naye huyo tayari kaota pembe zinazoweza kutuchoma."
Jessica aliongezea lake kama tahadhari.
"Kwa hilo Robinson hawezi kufanya namtetea alikuwa akitoa wazo tu jamani tuwaze mbali sana."
Jackline alimtetea mpenzi wake.
"Yameisha hayo tuendelee na mzee Bruno."
Jasmine aliongea akimuangalia mdogo wake kwa jicho la kumtuliza.
KUNA NINI HAPO?
TUKUTANE KATIKA SEHEMU INAYOFUATA.
"Mzee Bruno Gautier ungependa kuendelea kumiliki mgodi wako bila bughudha?"
Jackline alimuuliza.
"Sana tu binti yangu."
"Vizuri sana sasa utatakiwa kufanya mambo yafuatayo muda."
"Mambo gani hayo?"
"Punguza presha mzee, ni hivi ili uwe salama kuna mambo matatu ambayo utayafanya nayo ni kumpigia simu Santana afike hapa kesho jioni, pili ni kuwalipa wafanyakazi wako haki zao ambazo ulizowanyonya na mwisho ni kuhakikisha tunafika Afrika bila tatizo lolote, uko tayari?"
" Ugumu upo ila kwa kuwa napigania mali zangu nitafanya tu nipeni nafasi."
"Haina tatizo muda ndiyo huu mzee." Jasmine aliongeza.
Baada ya hapo walimruhusu mzee Bruno aisogelee simu yake ya mezani na alipobonyeza namba ambazo bila shaka zilikuwa ni za Santana simu ilikuwa kwenye laini.
"Mr Bruno hapa mgodini fanyeni haraka nimevamiwa....."
Kabla hajamaliza kuongea vizuri na simu ile ambayo waliishtukia, Jasmine alimnyang'anya na kuirudisha mahali pake na kumvamia.
"Mzee umefanya?"
"Unafikiri ni rahisi tu kutekeleza matakwa yenu? Bora nife tu."
"Unasemaje?"
Robinson alimuuliza kwa hasira.
"Nimemaliza ninyi subirini matokeo tu."
"Mzee tutakufanyia kitu mbaya umempigia simu nani?"
Jackline alimuuliza.
"Jeshi la Ulinzi."
"Jeshi la Ulinzi?"
Jasmine aliuliza na mara walisikia mlio wa kama ndege hivi na hapo wakajua shughuli imefika hapo hapo Jackline alimvamia mzee Bruno na kumpiga na kitako cha bunduki kichwani kitendo kilichompeleka chini na kukata moto.
"Robinson mbebe huyo tunarudi mgodini mara."
Jackline alitoa maagizo kwa Robinson huku akifungua mlango na kutoka nje kuangalia hiyo ndege inaelekea wapi, alipigwa butwaa baada ya kuona ukimya umetawala kuashiria ilikuwa imetua tayari.
"Hiyo ndege imeelekea wapi?"
Aliwauliza walinzi pale nje.
"Imepita tu hapa lakini ni kama imetua kilometa chache kutoka hapa kwani ilikuwa chini sana."
Alijibu mlinzi mmoja wao na mara ile ndege ilipita tena na safari hii ilikuwa chini zaidi lakini ikielekea juu kitu kilichowaaminisha kuna sehemu ilikuwa imetua.
" Jasmine harakisheni hawako mbali sana. Na ninyi harakisheni hakuna anayetia mguu humu ndani."
Jackline alitoa maagizo na kisha wao kuondoka zao kurudi kule mgodini sehemu wanayoamini ni salama kutokana na muundo wa njia ya kuelekea kule uko vizuri kwani ni moja tu ambayo ni handaki hivyo maadui wakija kule watawadhibiti.
Wakiwa ndiyo wanazama kule chini huku nyuma kikasikika king'ora ikiwa ni ishara ya kuwaamsha watu wote japo tayari ilikuwa ni alfajiri watu walikuwa bado wamejipumzisha vyumbani mwao walitoka kusikiliza kuna nini tena.
"Kila mmoja atafute sehemu salama ajifiche kwa wale wenye nguvu wakae mkao wa mapambano."
Lilikuwa ni tangazo kutoka kwa mmoja wa walinzi ni baada ya watu wote kukusanyika pale. Kila mmoja akafanya kama alivyoagizwa na wale walinzi huku wakina mama wakikimbizana kujificha kwenye baadhi ya mahandaki pamoja na watoto wao.
" Mzee huyu kashaharibu itakuwaje hapa?"
Jackline aliuliza.
"Yani hata sijui itakuwaje lakini kikubwa tubane hapa tunaweza kumtaiti mmoja wao ikawa salama yetu."
Jasmine alijibu.
Lakini haikuchukua muda kule kule mgodini ndiko askari walikoingilia wakilenga kuwashtukiza wavamizi wa mgodi ambao macho na akili zao zingekuwa lango kuu na kuwapa urahisi wa kuwadaka bila shida. Kumbe lile eneo la mgodi lilikuwa na mlango wa siri ambao hawa askari wamekuwa wakiutumia mara kwa mara linapotokea janga lolote mle mgodini na kwa walinzi ambao walikuwa wanajua hilo alikuwa ni James na Ogingi wengine walikuwa hawajui chochote.
"Wametuvamia kwa nyuma fichameni haraka."
Jackline aliwaamuru wenzake.
"Robinson hakikisha unakaa karibu na mzee Bruno ili akishtuka asije asije kimbia."
"Sawa Jackline."
Basi Robinson alimchukua mzee Bruno na kwenda naye kujificha huku Jackline, Jasmine na Jessica wakichukua nafasi zao kuwakabiri wale askari ambao waliongoza kwenye ile njia kuelekea kule juu.
"Hivi hawa waliovamia huu mgodi watakuwa wakina nani?"
Mmoja wa askari alisikika akimuuliza mwenzake walipokuwa wakipita karibu na alipokuwa kajificha Jasmine. Lakini kabla hawajafika hata katikati ya handaki lile ndipo alipotokea Jackline kwa mbele na kupiga risasi moja juu kuwatisha wale askari ambao idadi yao ilikuwa inafikia kama kumi na mbili hivi na walipotaka kurudi nyuma kwanza walishangaa nako kuna watu ambao ni Jasmine na mdogo wake na pale mmoja wao alipojaribu kutaka kuleta upinzani Jackline alimshuti na kumuua kitendo kilichowaogofya wenzao.
"Kwa usalama wenu mikono juu msitingishe hata gwanda."
Jackline aliwaamuru wale askari na hapo Jessica alipita kuchukua silaha zao na kisha kuwaongoza mpaka kwenye jengo kule juu ambako walifungiwa wao siku ya kwanza na kuwafungia humo na kisha kurudi tena kule chini kuangalia kama kuna wengine wamesalia kule nje waliongoza mpaka ile sehemu ambayo walipitia na kukuta kuna mlango wa chuma ambao ukiuangalia kwa haraka unaweza usijue kama ni mlango kwa umetengenezwa kwa mfumo kimfuniko cha shimo la maji machafu na chini yake kuna ngazi zinazokupeleka mpaka nje na hapo wakawa wamebaini njia ya kutoka mle ndani kirahisi zaidi.
"Mambo si haya sasa kumbe njia iko huku? Masaa ya kuishi humu ndani yanahesabika."
Jasmine aliongea baada ya kuchungulia nje kabisa ila kule nje hawakuweza kuona chochote na hapo wakabaini walikuwa ni wale wale waliowatia nguvuni. Na walipohakiki usalama walirudi ndani kwenda kuwahoji mateka wao.
" Robinson mchukue huyo mzee twende naye kule juu."
Jackline aliagiza.
"Lakini mbona hajibu chochote huyu Robinson?"
Jessica aliuliza.
"Hebu ngoja niwaangalie."
Jackline aliongea na kuelekea kule walikokuwa.
Hakuamini macho yake baada ya kukuta eneo tupu halina mtu yoyote na alipojaribu kuangalia eneo la jirani akakuta kuna koti la Mzee Bruno lakini halikuwa na mtu.
"Jackline vipi umewakuta?"
Jasmine aliuliza mara baada ya kumuona Jackline akirejea sura imemshuka.
"Hakuna mtu yeyote Jasmine."
"Watakuwa wamepandisha ofisini kule juu."
Jessica alijibu haraka.
"Sina uhakika hapa napata wasiwasi kidogo kutokana na kauli yake ya muda ule asije akawa kashawishika na dollars za mzee Bruno."
Na hapo haraka sana walipandisha kule juu kwenda kuhakikisha kama wapo au la.
************
"Nikushushie wapi brother?"
Aliuliza dereva bodaboda mara baada ya kuingia stendi ya Rungwa."
"Niache hapa hapa stendi kaka."
Rashid aliomba aachwe stendi.
Alishuka na kumlipa nauli yake dereva bodaboda na kisha kuachana naye na hapo akaingia mpaka kwenye duka la vinywaji.
"Kaka naomba maji ya baridi sana."
"Ya shilingi ngapi?"
"Nipe ya mia tano kaka."
Alipewa maji akayakata fasta na kulitupa kopo pembeni kulipokuwa na kapu la taka kisha akamgeukia muuza duka na kumlipa hela yake.
"Samahani kaka niazime simu yako."
"Lakini haina salio mtu wangu."
"Weka cha shilingi elfu moja."
Alijibu na kuingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi hicho na kumkabidhi muuza duka yule ambaye alianza kuunga kifurushi kwenye simu. Na baada ya kumaliza alimkabidhi Rashid huku akipokea hela yake.
"Mama kimenuka huku."
"Kimenuka nini tena Rashid?"
Mke wa mzee Jonathan aliuliza.
"Kwanini ulinituma kwenye moto?"
"Kwenye moto kivipi mbona sikuelewi?"
"Mzee hakutokea na wala hakuwepo kwani mtu ambaye alisema alikuwa na mzee nikamkuta kwenye bango akitafutwa na hata askari waliponibananisha na kwenda nao kwenye gari hatukumkuta alikuwa ni nani huyo?"
"Kwenye bango? Na hilo bango lilikuwa na picha ngapi mwanangu?"
"Lilikuwa na picha tatu na kwenye hizo niliyemfahamu ni huyu niliyekuwa naye hao wengine sikuwafahamu kwani kuna wengine wana Mirasta yaani tafrani mama."
"Mwenye Mirasta? Naye alikuwa kwenye bango anatafutwa?"
"Mbona unauliza hivyo mama unamfahamu huyo Rasta?"
Alitulia kwa muda mke wa Jonathan akitafakari amjibu nini Rashid lakini mwisho wa siku alimkatalia kuwa hamfahamu.
"Hapana simfahamu hata kidogo kwani kwenye simu hakupatikana?"
"Sikupata muda hata kidogo kwani simu yenyewe nilishaitupa na hii nimeiazima tu hapa dukani na kingine hata gari nimelitelekeza huko huko na kukimbia zangu."
"Rashid weweee yaani gari umeliacha?"
"Ndiyo mama debe naliogopa sana na pia nimegundua ninyi mlinitegeshea bomu hivyo mama naomba niacheni kabisa sitaki mazoea na hilo gari tafuta mtu wa kulifuata na kama mumeo yuko kule mpigie simu alichukue."
Kisha alikata simu akafuta namba na kurudi dukani na kumkabidhi mwenye duka simu yake.
" Kaka nashukuru sana."
"Bila shaka ndugu yangu."
Kisha Rashid aliondoka zake na kukaa sehemu ambayo alijua hawezi kuonekana kirahisi na kusubiri usafiri wa kutoka Singida kuelekea Tabora.
Huko porini nako polisi waliishia patupu kutokana na kumkosa Black na hivyo kurudi haraka mjini pale Bitimanyanga na kama bahati vile mzee Jonathan na Masanja wakiwa hawana A wala B waliibuka na kuongoza kwenye moja ya duka ambako kabla hawajafanya chochote walishtukia wanawekwa chini ya ulinzi.
"Marasta ulijua umefanikiwa kutukimbia siyo?"
"Mbona sielewielewi ndugu zangu kuna nini?"
"Unajifanya kushangaa siyo?"
"Mkuu yule dogo wa ile gari hayupo."
"Atakuwa kaelekea wapi hebu ulizeni au kumuangalia kwenye vibanda humo."
"Sawa mkuu."
Waliondoka na kuanza kumtafuta kwe vibanda kuona kama wanaweza kubahatika kumuona.
NINI KITAENDELEA?
SEHEMU IJAYO INAKUHUSU.
"Mkuu hayupo kote tumezunguka hatujabahatika kumuona na hata baada ya kuuliza wamesema hajaonekana."
"Kitakuwa wapi hiki kitoto, si mbaya nendeni kwenye ile gari hakikisheni inawaka ipelekwe kituoni mhusika atapatikana tu."
"Sawa mkuu."
Aliondoka mpaka kwenye ile Cruiser akafanya mambo milango ikajibu akazama ndani nako akafanya utundu wake na kisha ikawaka akaja nayo mpaka pale ambapo walikuwepo wenzake.
"Kila kitu kiko sawa mkuu."
"Okay subiri kidogo, walete hao mabedui hapa piga pingu safari ianze tuna kilometa nyingi sana kufika Lupa."
"Ndiyo mkuu kama ulivyoagiza."
Alichukua pingu na kuwafunga mzee Jonathan na Masanja ambao mpaka hapo hawakujua nini kimetokea na kilichomshangaza zaidi ni pale alipoliona gari lake jingine likiwa mbele ya macho yake na huku akisikia kuwa mwenye gari katoroka na hapo akaishiwa nguvu na ni kutokana na magari yake mawili kuwa nje ya himaya yake.
"Afande tunaweza kuongea kidogo?"
Mzee Jonathan alimuomba mkuu wa oparesheni waongee kidogo muda ambao alikuwa kapigwa pingu tayari.
"Unataka kuniambia nini wewe?"
"Mimi ni mfanyabiashara maarufu sana hapa nchini ila kuna watu wananichafua na hao ni wale wasiopenda maendeleo yangu."
"Acha kuzunguka nenda kwenye pointi unataka kuniambia nini?"
"Nilikuwa naomba huruma yako afande niko tayari kutoa kiasi chochote kile ilmradi nibaki huru."
"Mnalisikia hili limanywele eti linataka kutoa hongo mbele ya chombo cha dora lina akili timamu kweli hili? Hebu litupeni ndani ya tenga likakutane na vyuma vya kazi kule gerezani Isanga Mbeya."
Zoezi lake mzee Jonathan lilishindikana baada ya mkuu yule kumchomolea nje na kuamuru watupwe ndani karandinga ambalo muda huo lilikuwa kwenye moto kuashiria safari kuanza mara moja kurudi mjini Lupa tayari kwa kufunguliwa mashtaka.
" Mungu wangu yaani naiona jela inaniita hivi hivi sijui kwanini nilikubali kuja huku."
Masanja alikuwa akijiwazia akiwa karibu zaidi na mzee Jonathan ambaye alikuwa akidondosha machozi tu.
"Hivi ni kwanini Black hakututonya wenzake?"
Masanja aliona amuulize mzee Jonathan.
"Hata mimi bado najiuliza swali hilo hilo na kwanini hata yule dogo aliyetufuata naye kaondoka na kuitelekeza gari inavyoonekana lao lilikuwa moja hawa."
Mzee Jonathan alimjibu Masanja kwa kunong'ona ili askari wasijue wanaongea nini.
"Mzee unalionaje hili kuna uwezekano wa kutoka kweli?"
Masanja aliendelea kumswalika mzee mzima.
"Masanja itafahamika tukifika huko."
"Sijui itakuwaje pindi wazazi wangu pamoja na waumini wenzangu watakapopata taarifa kuwa niko ndani kwa tuhuma za ujambazi."
Mzee Jonathan alimtazama Masanja kwa macho ya huruma kisha akatingisha kichwa na kwa namna ambavyo alikuwa akiongea ongea ni dhahiri tangu aanze kazi hii hajawahi kamatwa na ndiyo maana anaumiza kichwa.
" Sikiliza Masanja wako wengi wanaoishi maisha mazuri ambayo kila mmoja anatamani kuyaishi lakini namna siri ya upatikanaji Mali zake ni yeye ajuaye, unaweza kuta kuna wengine ni Wachungaji, watumishi wa Mungu lakini giza linawalinda na sisi ni miongoni mwao ila tu arobaini zetu zimefika, lakini nakuhakikishia kuwa nitatumia akaunti yangu mpaka tutoke."
" Ni ndoto mzee kumbuka tuna kesi mbili za kujibu, moja ni ile ya kuwatoroka wakijiji kule Lupa na ya pili ile ya kuwateka abiria kwenye lile basi ambalo sijui liliendelea na safari au ndiyo lilirudi mpaka Lupa kutoa ripoti ya kutekwa kwao?"
Mzee Jonathan alimgusa kwa mguu kumuashiria anyamaze kwani japo kuwa alikuwa akinong'ona kuna mmoja wa maaskari ni kama alikuwa akiwaangalia sana kama vile alikuwa akifuatilia maongezi yao.
Safari iliendelea na mpaka inafika saa tano usiku walikuwa ndiyo wanaingia kituoni Lupa na kisha walishushwa na kuingizwa moja kwa moja kwenye chumba maalum cha mahojiano ili kama mambo yakienda vizuri kesho yake hatua nyingine zifuatwe.
"Ndiyo kama ulivyosikia, tunawashikilia watuhumiwa wawili wa ujambazi ambao walitelekeza gari baada ya kubaini wameshtukiwa na wanakijiji na inavyoonekana ni wale wale ambao wanaifuatilia familia ya Jackline na pia ndiyo hawa hawa walioliteka basi na kuwapora abiria pesa zao zote pamoja na simu pia ila tu kama bahati kuna abiria mmoja ambaye alibahatika kuwapiga picha wote watatu kabla hajashtukiwa na kisha kuificha simu yake kwenye kiti cha gari."
"Vizuri sana Afande Mkonge sasa wahojini kisha ripoti naihitaji haraka sana."
"Umesomeka mkuu."
Simu ilikatwa na kisha akarudi ndani tayari kwa mahojiano na watuhumiwa ambao tayari walikuwa mbele yake.
"Afande Piliska hebu niletee vitu vyote ambavyo mmewakuta navyo."
"Ndiyo mkuu."
Alichukua vile vitu pamoja karatasi ambayo ilikuwa imeandikwa vitu vyote walivyovikuta kwao. Baada ya kupitia ile karatasi kujua kilichoandikwa macho ya Afande Mkonge yalitua kwenye kitambulisho kimoja ambacho kilikuwa na picha ambayo ni tofauti na mhusika mwenyewe.
"Wewe Afande Piliska mbona sielewi hapa kwenye hiki kitambulisho? Ndivyo ilivyo mkuu."
"Namhitaji huyu Jonathan na bila shaka ndiye yule yule ambaye jalada lake liko mezani kwa mkuu pale Makongolosi."
Afande Piliska alikwenda kumchukua mzee Jonathan na kumleta mbele ya mkuu wake.
"Afande naomba niende chooni mara moja."
Mzee Jonathan alimuomba Afande Piliska.
"Umebanwa baada ya kusikia mkuu anakuhitaji eee?"
"Hapana si hivyo Afande kujisaidia ni haki yangu kumbuka."
"Ni kweli mzee lakini itakuwa baada ya kutoka kwa mkuu."
"Okay ila siyo vizuri hata kidogo nikichafua mazingira huko ndani?"
"Hakuna tatizo kwani wewe utakuwa si wa kwanza kufanya hivyo."
Alimuongoza mpaka kwa mkuu wa kituo kidogo pale Lupa na baada ya kumfikisha alitoka na kurudisha mlango kuwacha huru.
"Haya Marasta naomba kujua uhalisia wako bila kupindisha hata kona moja sawa."
"Sawa Afande, mimi kama kitambulisho kinavyoonekana naitwa Jonathan Ubao ni mfanyabiashara maarufu na kwa sasa niko jijini Mwanza kabla ya hapo nilikuwa Singida."
"Bitimanyanga ulifuata nini? Kwanini uliwakimbia wanakijiji wa Lupa? Vipi kuhusu manywele yako?"
"Afande kama nilivyokuambia hapo awali mimi ni mfanyabiashara hivyo niko huru kuingia sehemu yoyote ambayo nitasikia kuna fursa ya kibiashara na ndiyo maana niliingia Bitimanyanga baada ya kupata taarifa kuwa kuna asali nyingi pamoja na mbao. Na kuhusu kuwakimbia wanakijiji ni kweli niliwakimbia baada ya kuona tumezungukwa wakati sisi tulikuwa tunahitaji kuonana na mzee mmoja aitwaye Fikirini na juu ya nywele zangu si ajabu hata kidogo kwani hakuna sheria inayonikataza kufuga."
"Okay vizuri sana na vipi kuhusu hili gazeti?"
Hapo mzee Jonathan jasho lilimtoka kwani hakutegemea kukutana na gazeti la siku nyingi kidogo ambalo lilikuwa likiwaelezea hasa yeye baada ya kulutwa baadhi ya vitu kwenye mkoba wa jambazi Surambaya ambaye aliuwawa kwa kuchomwa ndani ya msitu ambao alikuwa kajificha. Na hapo mzee Jonathan alijikuta akiishiwa nguvu na macho yakikosa ushirikiano na viungo vingine vya mwili kisha alidondoka na kupoteza fahamu.
"Afande Piliska mwite Afande mwingine mje mumtoe huyu mshenzi humu ofisini nitaendelea naye baada ya kupata fahamu zake kesho."
"Sawa mkuu."
Alimwita Afande mwenzake kisha wakamtoa mzee Jonathan na kumrejesha tena kwenye chumba cha giza lakini hiki kilikuwa ni rafiki kwani kilikuwa na hewa ya kutosha.
sultanuwezo.com:
****
"Mzee Bruno umezinduka tayari?"
"Hapa tuko wapi na wewe ni nani?"
Mzee Bruno aliuliza baada ya kukutana na mazingira tofauti na yale kule Ngomeni kwake.
"Mimi mwenyewe sipafahamu ni wapi ila tu elewa nilikutoa kule ndani kupitia njia ambayo niliwaona wale askari wakipita."
"Kwa hiyo ina maana ile njia ya siri umeibaini?"
"Ndiyo na si mimi tu bali hata wale mabinti niliokuwa nao wameibaini pia na hivi tunaongea wako kututafuta."
"Wewe si ni mmoja wao mbona umeniokoa unanipeleka wapi?"
"Ni jambo moja tu ukilifanikisha tu uko huru mzee wangu na endapo ukienda tofauti tu nakurudisha kule kisha nitawaambia kuwa uliniteka ili unitumie lakini nikafanikiwa kujiokoa."
"Ongea ni kitu gani unakitaka kwangu na kwanini umenifunga mikamba mingi hivi?"
"Kama nilivyokueleza hapo kabla kuwa endapo utafanya kile nikitakacho utakuwa huru lakini kinyume na hapo elewa kifo kitakukabili kwani nitakurudisha kwenye mikono ya mbweha wenye hasira na wewe na hiyo ni baada ya kuwapigia simu wale askari."
"Wale si askari wa jeshi la serikali bali walikuwa ni kikosi maalum kutoka kwa bosi mwenzangu Santana."
"Aaahhh kumbe ndiyo mchezo wako siyo? Na unataka kuniambia kuwa hata Santana atakuwa pale muda huu."
"Hapana yeye yuko nchini Columbia kwenye mishe zake za biashara na huku alituma tu kikosi chake cha kazi na ninajua akirejea ni lazima atakuja tu kujua kinachoendelea."
"Okay sawa hayo hayanihusu kwa sasa ninachokihitaji sasa ni noti tu."
"Kama kiasi gani kijana wangu?"
"Mimi si kijana wako kwanza hilo liweke akilini na pili nahitaji kiasi cha shilingi milioni mia tisa mezani ambazo nikizipata tu naishia zangu Tanzania kuanza maisha mapya ya kitajiri lakini pia ukitaka kufanya kazi na mimi utaongeza kiasi cha shilingi milioni mia nne juu kwani hakuna ambaye ataweza kuwamudu wale mabinti zaidi yangu mimi."
"Hiyo inawezekana kijana ila hebu punguza kidogo hiyo figure' ni kubwa sana."
"Okay unataka nipunguze siyo mzee Bruno?"
"Ni kweli kijana punguza."
"Okay nisubiri hapo hapo."
Robinson alisimama na kuondoka pale na kumuacha mzee Bruno pale alipomfunga na kisha akaanza kukusanya nyasi.
Kule ndani ya Ngome hali ilikuwa ni ya kutisha sana kwani wakina Jessica walipobaini kuwa Robinson haonekani moja wakajua baadhi ya wale askari wamemkamata na kuondoka naye hivyo na wao hasira zote wakazipeleka kwa wale walioamini ni askari.
"Mtatueleza mtu wetu mmempeleka wapi?"
Jackline aliuliza huku akiwa anawararua kwa kipande cha nondo mmoja baada ya mwingine.
"Mtu wenu gani jamani?"
"Unauliza siyo, kwamba hujui lolote?"
"Sister ni kweli kabisa hatujui kitu kama hicho."
"Mtasema tu aliko mwenzetu."
Nondo iliendelea kutembea kwenye kila kiungo cha miili yao. Jasmine hakuna kuwaonea huruma hawa. Lakini wakati kipigo kikiendelea Jasmine alibaini kitu kwa wale askari na ndipo alipomsogelea mmoja wao.
"Nakufahamu vizuri sana nilishawahi kukuona sehemu moja nilipokuwa na Santana unakumbuka?"
"Hapana mimi sikufahamu madam hata kidogo."
"Unasemaje?"
Jasmine aliuliza kwa kutumia mdomo na mkono kwani kibao cha haja kilikuwa kimetua vilivyo shavuni kwa yule askari feki na kujikuta anatema mate yaliyo na rangi nyekundu.
"Narudia tena, nakufahamu vizuri sana Je na wewe unanifahamu?"
"Hapana madam utaniua tu sikufahamu mimi."
"Usipate tabu mdogo wangu nipishe kwanza."
Aliongea Jackline akimtaka Jasmine amuachie kazi hiyo ya kumhoji.
"Naomba ujibu swali uliloulizwa kabla sijaanza kukuhoji mimi."
Jackline alimtisha kijana yule.
"Sifahamu chochote kile."
"Okay inawezekana wewe ulikunywa damu ya kiapo sasa ngoja nikutoe wenge."
Pale pale Jackline alianza kumvua suruali taratibu kitendo kile kiliashiria kitu kibaya kinakwenda kutokea muda si mrefu.
"Vipi niendelee au utaongea?"
"Mtaniua tu lakini sina chochote cha kukuambieni mimi."
"Vizuri inaonekana unajua kucheza na kinywa chako subiri niifanye kazi yangu."
Jackline alimalizia kulishusha suruali ya yule askari feki na kisha alichukua moto na kuanza kuupitisha karibu zaidi na nyeti zake.
"Na hao wengine zoezi kama hili liendelee."
Haraka sana wale walinzi kwa kushirikiana na wakina Jasmine waliwavua nguo na kuanza kupitisha moto kwenye nyeti huku wakizipekecha na kuzichoma choma pini.
"Wacha mimi niongee, aaaaghhh niacheni nitaongea kila kitu."
Mmoja wao uzalendo ulimshinda akajikuta akiropoka huku akijivuta mbele mara nyuma bila shaka ni kutokana na utamu wa muziki walikutana nao.
"Eeehhhh ongea haraka hatuna muda wa kurudia swali ulishalisikia kwa mwenzako."
"Jamani sisi si askari wa Jeshi la Ulinzi la serikali bali ni askari wa jeshi la kujitegemea la mtu binafsi ambaye ni Santana."
"Unasemaje weweee...."
Jessica alijikuta akitokwa na swali lililoenda sambamba na kibao.
"Ni watu wa Santana."
"Shiiiiiiiit......! Ina maana Santana yuko hapa."
Jasmine alijikuta anauliza.
"Hapana hayupo nchini yeye yuko Kolumbia kibiashara ila mara baada ya kupigiwa simu na mzee Bruno naye alitoa maagizo kwetu kuja na ndege haraka."
"Pumb..u sana kwa hiyo ndiyo maana mmemteka mwenzetu na kumpeleka kwa huyo Santana siyo?"
"Hapana madam, sisi hatujafanya hivyo kwani tulikuja kama tulivyo hatukuwa na wengine."
"Vizuri, kwa hiyo ina maana mzee Bruno kamteka?"
"Hata mimi nahisi hivyo hivyo."
"Hebu njooni kwanza."
Jasmine aliwaita wenzake pembeni.
"Jamani ee hapa si shwari la msingi tusubiri mpaka jioni iwapo mzee Bruno hatarejea tunatakiwa kuondoka upesi eneo hili, tutaelekea wapi itafahamika."
"Ni kweli na hawa inakuwaje?"
Jessica aliuliza.
"Hawa tuwaache hapo hapo mpaka hiyo baadaye kisha tutajua kama tuwamalize au la."
"Sawa Sawa."
Jasmine aliunga mkono.
Walirudi na kuwaamuru wale walinzi wao kusitisha zoezi lao na kurudi kwenye maeneo yao ya kazi huku wakiwataka wafanyakazi wengine wote kufanya usafi wa mazingira huku wakishughulikia chakula kazi nyingine ambazo hazijatajwa hapo hazitafanyika kwa siku hiyo.
NINI KITATOKEA?
USIKOSE KUSOMA SEHEMU INAYOFUATA.
Walitulia ofisini kwa mzee Bruno wakiwa wamejiachia wenyewe na kutafakari juu ya yale wanayopitia toka waingie ndani ya nchi hiyo ya Brazil. Upande wa Jackline hata chakula hakikupanda hata robo mawazo yalikuwa kwa Robinson akimuwazia kapatwa na nini kwa namna alivyomfahamu si mtu wa vitamaa iweje apotee.
"Au kile kiwango alichokitaja mzee Bruno kilimtamanisha?"
Aliwaza sana na zaidi aliivuta picha ya nyumbani kwao Lupa na akayaangalia mazingira kuanzia makazi mpaka wenyewe alitikisa tu kichwa kuashilia kuna jibu alilipata ila hakutaka kulikubali.
"Au katekwa?"
Alizidi kuwaza Jackline juu ya Robinson.
"Wewe vipi mbona hauli? Naona muda mrefu tu umeshikilia tu kijiko kulikoni?"
Jasmine alimuuliza baada ya kuona katulia tu akigongagonga kijiko kwenye meno yake.
"Hamna kitu wangu hapa naumiza kichwa namna ya kutoka hapa salama na ukizingatia Santana kashajua kuwa tupo hapa."
Ilibidi adanganye tu kwani kwa vyovyote vile lazima tukio la Robinson litasababisha hata wao kuzua tafrani.
"La msingi hapa ni kuhakikisha tunaondoka leo."
Jasmine alichangia.
"Suala la Robinson linakaaje maana naona mnazungumzia kuondoka hili mmelisahau maana mpaka sasa hatujui alipo."
Jessica aliwauliza dada zake.
"Ila Robinson anatuumiza vichwa atakuwa wapi?"
Jasmine aliishia kuuliza swali badala ya kujibu.
"Yaani hapa akili si yangu mwenzenu nikiyakumbuka maneno ya wazazi wake ambao waliniambia nikawe makini na mtoto wao ambaye hajawahi toka nje ya mji aliozaliwa."
Jackline ilibidi atoe hisia zake.
Waliinuka na kutoka nje ambako wapishi walipowaona pale nje wameegemea nguzo za ofisi ile wao walipandisha na kwenda kutoa vyombo na kufanya usafi.
Mara alitoka yule mfanyakazi na kutoa taarifa fulani kwa Jackline. Na kisha aliongozana naye ndani.
"Mzee nipe ripoti ya huko?"
Ilikuwa ni simu ya mezani ambayo iliita na ndiyo maana mfanyakazi yule alitoka kumuita Jackline.
Simu ikiwa sikioni Jackline hakuongea chochote zaidi ya kumsikiliza tu mpigaji ambaye alikuwa ni Santana aliyekuwa akiuliza kama wamefanikiwa kuwatia mikononi wakina Jackline.
"Mzee mbona kimya haujibu chochote umepatwa na kitu gani ongea basi nijue."
Jackline uzalendo ulimshinda akajikuta akiirudisha simu ile sehemu yake na kutoka zake nje huku akijifuta jasho kwa t-shirt yake.
"Kulikoni huko ndani?"
Jasmine aliuliza baada ya kuona Jackline katoka lakini ni kama ana mawazo sana.
"Hakuna chochote ila tu Santana alipiga nikapokea lakini sikuongea kitu zaidi ya kumsikiliza tu mwenyewe akiuliza kama wamefanikiwa."
"Okay kwa hiyo alijua anaongea na mzee Bruno?"
Jessica aliuliza.
"Ndiyo mawazo yake hayo angejua kilichotokea wala asingeuliza maswali ya kijinga kama hayo. Jamani mimi ngoja nikaoge naona joto limekuwa kali sana.
" Poa poa."
Jasmine alijibu.
Upande wa pili kule porini Robinson alionekana kuendelea kumbananisha mzee Bruno na safari aliamua kumkusanyia nyasi. Alikusanya za kutosha na kurundika kiasi cha kufanya kutoonana.
"Sasa mijani yote hiyo ni ya nini kijana mbona sikuelewi njoo tufanye makubaliano hili suala ni dogo sana."
Mzee Bruno Gautier ilibidi aulize baada ya kuona Robinson yuko bize na mijani haongei na mtu.
"Wewe si mgumu ngoja nikulainishe kidogo mzee."
"Hapana bwana njoo tuyajenge basi."
Robinson kama hakumsikia vile kwani alichukua zile nyasi na kuzisambaza mpaka karibu na pale alipokuwa mzee Bruno. Kisha akaondoka na kumuacha mzee Bruno pale pale alipomfunga. Alitembea kwa muda kisha akafanikiwa kufika sehemu moja ambayo ilikuwa na gogo lililokuwa likiwaka moto na kusogea karibu ambapo alichukua gome na kuzoa mkaa na kuondoka zake na baada ya kufika kule alikokuwa kamuacha mzee Bruno na kuanza kuziwasha zile nyasi. Baada ya kuupuliza ulikubali sheria.
"Kijana naomba uuzime moto niko tayari kutoa kiasi hicho cha fedha."
"Unazingua mzee nataka kukuona ukiwa mkaa mbele ya macho yangu."
"Hapana kijana hujuagi hata utani? Nilikuwa natania bwana zima moto huo au hujui kama unaua huo?"
"Najua na ndiyo maana nimeuwasha."
"Uuzime basi nitaongeza milioni kumi juu ya unayoitaka kwa ajili ya usumbu
fu na itafikia shilingi milioni mia tisa na kumi."
"Nihakikishie mzee hapa hapa kabla ya yote."
"Kwenye mfuko wa koti langu kuna kadi yangu ya benk itoe nikupe maelekezo."
Moto ulikuwa umeshika kasi na sasa ulikuwa umemfikia kabisa mzee Bruno lakini Robinson hakujali hicho aliingiza mkono mfukoni kwa mzee Bruno na kuchukua ile kadi.
"Kijana wangu naungua mzee wako...."
Mzee Bruno Gautier alilalamika mara baada ya moto kumvagaa eneo la kwenye suruali kitendo kilichomfanya Robinson kurukia majani ya mti na kuuzima moto kwa staili ya kumchapa mzee Bruno kwa kichapo kile moto kweli ulizima lakini tayari mzee Bruno alikuwa kachakaa na suruali yake ilikuwa imeungua baadhi ya maeneo na kuonesha ngozi kabisa.
"Kijana unaona sasa nilivyoungua?"
"Nikurudishie moto wako siyo unaweza nionesha ulipoungua kama siyo utani huo, hapo umeguswa tu unalia lia je ungeungua kabisa?"
"Pamoja na hayo lakini nimefungwa kijana wangu."
"Niondolee kelele zako hapa mzee la msingi kwa sasa ni wewe kuongoza mpaka mjini ukatoe kiasi hicho kisha tuachane kimjini mjini."
Aliongea huku akimfungua kamba ambazo alikuwa kamfunga nazo.
"Sawa lakini ilikuwa ni jambo jema nikikuhamishia kwenye akaunti yako kukupa mkononi kiasi kikubwa kama hicho ni hatari sana."
"Toka lini wewe ukawa mshauri wa masuala ya fedha?"
Lakini japo alimtupia swali lile mzee Bruno, kichwani alibakia kuwaza hizo hela itakuwaje hata akaunti hana na akisema akabidhiwe itakuwaje iwapo watagundua amebeba mihela? Hilo lilimuumiza kichwa Robinson akajiona kuwa mjinga aliyekurupuka bila kufikiria. Mwisho alipata wazo jipya ambalo alijua hili lingemlainisha mzee Bruno na kumsogeza karibu kama rafiki yake.
"Mzee hapa nilikuwa naipima imani yako na hivyo nimebaini hizi hela umezikusanya kwa shida sana na kwa muda mrefu huku fungu kubwa likimwendea Santana na mimi kama kijana wa kiafrika niliyepata malezi ya kidini iwapo nitachukua kiasi hiki kikubwa cha fedha tena ambacho umekitoa kwa kinyongo najua sitafanyia chochote hivyo mzee nakupa uhuru wa kunipa kiasi ambacho utaona kinanifaa."
Mzee Bruno hakuamini alichokisikia kutoka kwa Robinson alisimama na kumfuata pale alipokuwa kakaa na kumkumbatia.
" Sasa ndiyo napata jibu ni kwanini uliamua kuniokoa kutoka kwenye mikono ya wale washenzi na hapo ni fika kuwa ulilazimishwa kuungana nao lakini wewe si taipu yao ni mcha Mungu wa kweli."
"Ni kweli mzee mimi niliambiwa tu nimsindikize huku yule msichana anayepiga sana kuwa kuna vitu vyake anafuatilia kwani kule nyumbani ni majirani na baba yake mdogo ambaye kwa sasa ni marehemu nashangaa kufika huku tumekuwa marafiki wa bunduki na damu za watu hapana mzee sijazoea na ndiyo maana nikaamua kuchukua njia yangu ambayo ni salama kwangu na familia yangu nyumbani."
"Sasa hauoni kama itakuwa hatari zaidi iwapo watabaini wewe umewasaliti?"
"Ni kweli mzee lakini najua kwa ujanja wako utafanya kila njia kuniweka salama."
"Okay kuna jambo nitalifanya kwako na juu ya fedha siwezi kukuahidi ni kiasi gani nitakupa ila utakiona tu kwenye akaunti yako."
"Nitashukuru sana mzee."
Robinson aliongea hayo huku akimsogelea mzee Bruno na kumshika mikono kisha wakanyanyuana na kusimama.
Baada ya kukubaliana ni jinsi gani maisha yatakuwa baina yao kwanza waliamua kuondoka eneo na kuelekea mjini ambako huko ndiko kwenye makazi ya mzee Bruno Gautier.
Baada ya kufika barabarani walipanda basi na kuelekea mjini Manaus ambako ndiko kwenye jengo la Mzee Bruno.
"Kijana wangu hapa ndiyo kwangu na utaishi hapa kwa kipindi chote ambacho utakuwa hapa."
"Nashukuru sana mzee kwa huruma yako ambayo leo imenileta hapa na pia naomba nirudie tena kukuomba msamaha kwa yote niliyokufanyia mzee wangu na ninakuahidi kuwa mstari wa mbele kuikomboa Ngome yako."
"Wala usihofu katika hilo Robin mimi nimekusamehe na kikubwa nakuahidi iwapo utafanikisha kuikomboa ngome yangu utafurahi mwenyewe na huko Tanzania nitakusaidia kufungua miradi ambayo itakupa heshima."
"Hata leo niko tayari na kama ambavyo nilikwambia wale kwangu hawana ujanja nitawadaka tu."
"Wala usihofu leo tupumzike kwanza kazi yenyewe ianze kesho na wale walionisaliti pale kambini watajuta kunijua mzee Bruno Gautier."
Walioga wakabadilisha nguo zao ambazo zilikuwa zinanuka moshi na kisha waliingia kwe gari na kuondoka kuingia katikati ya mji.
" Huu mji unaitwaje mzee?"
" Mji huu unaitwa Manaus maarufu kwa uvuvi na biashara nyingine kama ujuavyo mji huu hauko mbali na mto Amazon."
"Okay naona umepangwa vizuri sana mitaa inaonekana siyo kama mji wetu wa Mbeya ambao kuna mitaa ukiingia tu unatokea chooni."
"Aisee huku ni kwa kipekee sana unajua nini Robinson ngoja nikupeleke kwa shemeji yako toto dogo dogo ambayo niliioa baada ya mke wangu mkubwa kufariki alipokuwa akisafirisha madawa ya kulevya ya Santana kuelekea nchini China baada ya pakiti kupasukia tumboni."
"Kwa hiyo na wewe ulimruhusu afanye shughuli hiyo hatari?"
"Hali ngumu ya maisha ilipelekea kuingia kwenye shughuli hiyo na kipindi hicho nilikuwa choka mbaya kwani hata kumi mbovu ilikuwa tatizo kwangu na ndipo siku moja nilikutana na Santana kona moja hivi akanieleza kuwa naonaje nikimtoa mke wangu afanye shughuli hiyo na iwapo akifanikiwa tu maisha yatabadilika nilikubali na hata nilipomshirikisha wife' hakuwa na pingamizi kwani alikuwa amechoka na Maisha ya kutembeza maua mtaani. Lakini Mungu hakupenda iwe hivyo akapoteza maisha."
"Pole sana mzee, kwa hiyo ikaishiaje hiyo?"
"Usiwe na haraka ni stori ndefu ila kwa sasa tumefika kwa mke wangu kipenzi ambaye nilimnunulia hili Kasri kama Kifalme vile."
"Mungu wangu huu ni mjengo wako mzee Bruno?"
"Ukinifurahisha na wewe utamiliki zaidi ya huu mjengo."
"Kweli mzee?"
"Fanya uwadake wale Mambwa jike uone nitakufanyia nini?"
"Kwenye hilo niachie mimi wewe anza kufanya mipango ya nyaraka."
Wakiwa getini kuingia ndani mara simu ya mzee Bruno Gautier iliita akaitoa na kuangalia mpigaji ni nani nafikiri ni mtu ambaye alimtarajia kwani aliipokea kwa tabasamu kubwa.
"Kubwa la maadui niambie sasa."
"Nikuambie nini mzee, naona unajichekesha chekesha tu hapa kama mwanamke hebu nipe ripoti maana napiga simu ya ofisini kwako lakini kimya japo inapokelewa."
"Oohh pole mkuu, kule hali ni mbaya na sijui kinachoendelea kwani mimi mwenyewe kama bahati tu kati yao ndiye aliyeokoa maisha yangu."
"Unasemaje wewe mzee yaani wale mijusi wamekushinda na huyo aliyeokoa maisha yako ni nani?"
"Ni huyu dogo wa kiume anayeitwa Robinson."
"Huyo dogo mzembe mzembe kawezaje kukuokoa wewe haujui inaweza kuwa plani yao hao?"
"Hapana nimeongea naye mengi sana na kaniahidi kuwakamata kwa mikono yake mwenyewe."
"Okay ngoja tuone, lakini kesho mapema nitakuwa hapo kwa lengo moja tu la kwenda kuwashikisha adabu vimburu wale."
"Kwani umerudi safari?"
"Niko ndani ya Belem kitambo toka alfajiri ya jana sema tu niliamua kutuliza akili zangu town kabla ya kuelekea kambini."
Basi simu ilikatwa na kisha mzee Bruno alimgeukia Robinson na kumkaribisha ndani ambako mke wake aliku ameshafika kumlaki na kupokea kibegi kilichokuwa mkononi.
JE, NI KWELI ROBINSON KAUNGANA NA MZEE BRUNO GAUTIER?
TUKUTANE KATIKA SEHEMU INAYOFUATA.
"Hii hapa simu yako Mr Jonathan unaweza kuendelea ila fanya haraka kabla sijabadili maamuzi yangu ambayo hubadilika kama kata upepo pindi upepo unapobadili uelekeo wake."
Afande Mkonge alimkabidhi na kisha alimpiga mkwara.
"Nashukuru Afande nivumilie dakika sifuri tu itakuwa tayari."
Mzee Jonathan alijitetea kisha akabonyeza namba za mhasibu wake na kuiweka simu sikioni.
"Nakusikiliza bosi wangu."
Mhasibu aliitikia.
"Vipi mnaendeleaje hapo?"
"Huku ni kwema tu bosi kazi zinapigwa zaidi tunakuombea umalize ziara yako salama na urudi salama."
"Vizuri sana, sasa naomba ufanye mpango wa kutoa kiasi cha shilingi milioni ishirini na tano na kisha kamkabidhi dada yako pale nyumbani muda huu."
"Sawa bosi nimekuelewa na ninakwenda kufanya kama ulivyoagiza."
Mzee Jonathan alikata simu hiyo na kupiga namba nyingine ambayo ilikuwa ni ya mke wake.
"Mbona mlikuwa hampatikani hewani toka jana? Rashid katelekeza gari porini sijui ni wapi pale kasema?"
Mke wake aliipokea simu kwa maswali mfululizo ambayo mzee Jonathan alijua yatakwenda kutoboa siri zilizofichika hivyo akamkatisha.
"Nitakusimulia mke wangu kila kitu ila kwa sasa kuna fedha italetwa hapo na mhasibu utaipokea na kisha utakwenda Benki kuiingiza kwenye akaunti namba *56*0099 usichelewe mke wangu."
"Kiasi gani hicho?"
"Milioni ishirini na tano."
"Mhh mbona hela zinazidi kuteketea mume wangu au tayari umepata kimada huko umeamua kuwa mfadhili wake?"
"Acha stori hizo mke wangu laiti ungejua sehemu nilipo ungeondoka sasa hivi kumfuata mhasibu na kuacha maswali yasiyo na kichwa wala miguu."
"Si uniambie sasa uko wapi mume wangu nijue?"
"Niko mahabusu hapa Lupa."
Mzee Jonathan alijibu na kukata simu kisha akairudisha kwa Afande Mkonge.
"Inatumwa muda si mrefu Afande nikuachie ulingo mwenyewe."
"Okay sawa lakini mpaka ujumbe wa muamala uingie kwanza maana simu yangu imeunganishwa na mfumo wa kibenki ninyi mahalifu hamuaminiki hata kidogo mnaweza kuzuia juu kwa juu."
"Hapana siwezi fanya hivyo Afande."
"Sasa tunaposubiria muamala utapumzika kwanza wakati mimi nikiendelea na majukumu mengine ya kiofisi."
"Nitakuwa humu humu Afande?"
"Hapana utarudishwa sero namba moja uliyofikia jana na yule mwenzako hii ni sehemu ya mahojiano na kuna wengine wanatakiwa kuingia hapa kwa mahojiano."
"Mmhh, sawa Afande."
Ilibidi agune tu mzee Jonathan baada ya kuambiwa hivyo na muda huo mkuu wa kituo alitoka na kufunga mlango na kumuacha mzee Jonathan kakodoa macho.
"Kamtoe yule mzee mpeleke kwa mwenzake."
"Sawa mkuu."
Afande Piliska aliitikia na kuelekea kwenye chumba cha mahojiano kumtoa mzee Jonathan na kumpeleka kwa Masanja sero namba moja.
"Sasa unaonaje kabla hujanipeleka kwanza ungeenda ukamuulize kama meseji imeingia na umsikilize atasemaje."
"Mzee namtumikia mkuu mmoja tu hapa ambaye neno lake lolote ni amri kwangu hivyo naomba usimame uelekee sero hayo mengine mtajuana naye."
"Binti mimi ni mzee wako lakini?"
"Najua hilo mzee na ndiyo maana maombi yako yalisikilizwa."
"Okay sawa, ila tunaomba msaada wa chakula kama ujuavyo sisi hapa ni wageni."
"Sawa mzee haina tatizo."
Alimuongoza mpaka sero na kumfungia kisha akarudi ofisini kuweka funguo.
"Afande Piliska njoo nikupe mchongo hapa kwanza kabla ya yote."
"Mchongo gani huo bosi?"
"Acha maswali binti utakosa vizuri ooh ooh shauri yako."
"Ndiyo bosi."
"Leo tumepiga bingo ya huyo babu jinga meseji imejibu taslimu shilingi milioni ishirini na tano soma hapa."
Alimkabidhi simu ili asome ile meseji kutoka benki ikionesha muamala uliongia.
"Bosi zote hizi utazifanyia nini?"
"Katika hizo zangu ni shilingi milioni kumi tano tu hizo nyingine kesho nawakabidhi mgawane."
"Bosi hapo tu ndiyo nakukubali kwa hiyo kesho najaa nyekundu nyekundu."
"Ndiyo jibu hilo, utawataarifu wote kuwa kuna mgao huo ila wakikuuliza waambie ni bonasi kutoka mkuu."
"Sawa mkuu."
"Eehh na itakuwaje kwa huyo mwenyewe?"
"Imekula kwake hiyo na hivi tayari nimeshawapigia simu Makongolosi wawafuate jioni ya leo mzigo huu tuuepuke na hii ni rushwa ataidaia wapi binti yangu?"
"Mhhh atasikitika huyo na mimacho yake ile kama namuona atakavyoitoa."
"Achana naye atajua mwenyewe yeye si bingwa wa utapeli?"
Alieleza hayo huku akitoka nje na kumuacha Afande Piliska naye aendelee na majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuwafuatia chakula wakina mzee Jonathan.
"Samahani Afande."
"Mzee Kaaya umekuja?"
"Nimeona nikutembelee maana toka ile jana mlipokuwa mnaenda Bitimanyanga."
"Ni kweli kabisa mzee Kaaya tulikwenda kule tukafanya msako wa kufa mtu, mzee karibu ofisini tunazungumzia hapa kama vile wakimbizi bwana."
Waliongozana mpaka ofisini kwake ambako huko alilenga kumsimulia A to Z ya mwanzo wa safari mpaka kurudi.
"Karibu kiti mzee."
"Asante Afande."
"Eehh ilikuwaje huko?"
"Baada ya kupokea taarifa zile za basi kutekwa na kuporwa vitu mbalimbali ilibidi tuelekee kwanza Isangawana ambapo walitulia kwanza kutokana na dereva kupata mshtuko hivyo akawaomba radhi abiria kuwa badala ya kurudi mpaka hapa akaona asogee mbele kisha watoe taarifa kwetu ndivyo ilivyokuwa na baada ya kufika pale tukapewa mkasa ulivyokuwa na baadaye tukapewa picha za wahusika kwani pamoja na kuwapora simu zao huyu mmoja alibahatika kuwapiga picha na kisha kuificha simu na tulipoziona tuliingia duka moja la kutoa nakala kivuli tukaomba watutolee nakala za zile picha na hapo tukaanzia kuziandika pale kisha Bitimanyanga kama Mungu vile hata saa halikuisha tukambaini kijana mmoja ambaye alikuwa na mashaka nasi na baada ya kumbana alitupeleka kwenye gari akidai kuna mmoja aliye kwenye picha yuko garini lakini cha ajabu hatukumkuta na baada ya kufuatilia nyayo zake ziliendelea porini tukaelekea huko tukamtafuta na kumtafuta lakini wapi ikabidi turudi kumbana huyu kijana aliyekuwa naye, mzee wangu kwani tulimkuta? "
" Hee alielekea wapi?"
" Naelewa basi mzee wangu tulichoambulia ni gari tu ambalo ndiyo hilo hapo nje lakini kama bahati si ndiyo tukawadaka wenzao ambao mmoja wapo ndiye mhusika wetu Mr Jonathan."
"Unataka kuniambia wako hapa tayari?"
"Ndiyo mzee."
"Vizuri sana yaani huwezi amini kama huyu mzee ndiyo chanzo cha vifo vya mzee Fikirini na mke wake na kupelekea mtoto wake kuondoka pamoja na mwanangu kutafuta haki yao."
"Wamenaswa tayari."
"Naweza waona?"
"Nadhani baadaye kwa muda huu wamepewa muda wa kupumzika baada ya kukesha usiku kucha tukiwasulubu."
"Poleni sana."
"Ni majukumu yetu mzee Kaaya."
"Da, Mungu mkubwa sana Afande nikuache nitakuja muda huo ili nikatafute mawasiliano ya Wanangu."
"Sawa sawa mzee."
Waliachana na Afande Mkonge kutoka nje naye kuelekea kule alikokuwa akitaka kwenda.
****
"Twendeni haraka kule mbele ni kama kuna mwanga wa boti vile?"
Jasmine aliwataka wenzake watembee haraka baada ya kuona mwanga kandoni mwa mto moa.
"Ningependa tuikute ambayo iko tayari kuondoka."
Jackline aliwaza hilo kwa sauti.
"Ni kweli kabisa dada Jackline."
Jessica aliunga mkono.
Waliongeza mwendo mpaka kwenye yale maegesho ya boti na kukuta hakuna dalili yoyote ya watu japo boti zilikuwa nyingi.
Waliangaza huku na kule lakini hawakuona mtu yoyote karibu na eneo lile, hali ile iliwapa wasiwasi sana kiasi cha kutojua wafanye nini waite au waondoke? Na anga ndiyo lilikuwa linaonyesha dalili ya kuchafuka kwa wingu la mvua ambayo ingedondoka muda wowote ule.
"Mbona kuna ukimya hivi?"
Jackline aliuliza.
"Hata mwenyewe nashangaa hivyo hivyo au yule dogo katuunguzia ramani?"
Jasmine alionyesha hofu juu ya hali ile.
"Tunatakiwa tuondoke haraka sana eneo hili kabla halijatokea lolote la kutokea."
"Pa pa pa pa pa...." Makofi yalisikika yakipigwa nyuma yao.
"Msijidanganye kuwa mtaondoka hapa mabinti, tunashukuru mmejileta wenyewe."
"Mbona hatukuelewi."
Jackline aliuliza.
"Mtanielewa tu, kifupi mimi ni mfanyabiashara mkubwa kwenye huu ukingo wa mto na biashara yangu hii hulenga wale wote ambao hupotea na kufika huku mtoni mida ya usiku. Huwakamata na kuwatia minyororo na kisha kuwapeleka sokoni wakawatumikie mabwana huko huku sisi tukikunja mihela ya kutosha."
"Tunaomba msaada wako tafadhali."
Jessica aliomba wasaidiwe.
"Msaada? Askari wangu kamata hawa piga kamba tupia kwenye boti kisha tuondoke zetu pambazuko linaanza."
Haraka sana kabla wakina Jackline hawajakaa sawa walijikuta wakikamatwa na kufungwa kamba kisha boti liliwashwa na kuondoka eneo lile.
" Nilifikiria sana masaa machache yaliyopita kuwa tuondoke zetu kwa kukaa eneo hili bila kupata bidhaa hata moja kumbe Mwenyezi Mungu alikuwa anatuletea bidhaa za kutosha."
"Ni kweli kabisa mkuu na kwa namna wanavyoonekana hawa Warembo tutakunja mpunga wa kutosha si unajua vile yule mzee wa Kihispania anavyopenda totoz?"
"Yaa ni kweli kabisa."
Mkuu wao alikubaliana nao.
Wakati wao wakiongea hayo wakina Jackline waliyasikia yote na kubaini kuwa kumbe wanakwenda kuuzwa tena? Waliamua kuanza harakati za kujinasua mikononi mwao hivyo walianza kuzikata zile kamba kwa kila mmoja kumgeukia mwenzake aume kwa meno. Wenyewe walikuwa bize na stori za hapa na pale huku wakinywa mipombe hawakuwa na habari nao hata kidogo sijui kwa sababu waliona ni wasichana tu lakini laiti wangeujua undani wao hata wasingejaribu kukaa nao mbali hata nukta moja.
Kamba zilikatwa na kisha walihesabiana idadi ya kila mmoja anaotakiwa kuwaua kwani idadi yao ilikuwa ni watu wanne tu na nahodha alikuwa wa tano hivyo kilichofanyika ilikuwa ni Jackline kunyata na kuingia kwa nahodha kisha kumteka huku nje wakina Jessica waligawana kila mmoja wawili na halikuwa gumu kwao.
"Wewe kenge ukitingisha kichwa chako nakisambaza, umenisikia?"
Jackline alimvamia nahodha na kumuwekea bastola sikioni.
"Wewe ni nani?"
"Si wakati wake kikubwa ni kufuata maelekezo tu."
"Sawa nimekuelewa dada."
"Ongeza spidi ya boti haraka."
"Huku sisi tumemaliza kazi iliyobaki ni huyo mjusi kutufikisha Rio Branco kabla ya jua kuchomoza."
Jasmine alimwambia Jackline kile ambacho walikuwa wamewafanyia wale watekaji kule nje ya boti.
JE, NINI HATMA YA SAFARI YAO?
TUKUTANE KATIKA SEHEMU INAYOFUATA.
Waliondoka mpaka kwenye helicopter yao kule porini na kujaa ndani ambako walimkuta Robinson akiwa kajikunja kwenye kona akiwa katoa macho baada ya kuwaona Santana na timu yake akajua mwisho wake umefika.
"Niko chini ya miguu yenu naombeni msiniue badala yake nirudisheni nyumbani au nipeni kazi yoyote ya kufanya maana wazazi wangu wananitegemea mimi hawana mtoto mwingine."
Alianza kujitetea Robinson.
"Robinson, Robinson mbona unalialia hivyo kwani ni nani aliyekwambia tuna mpango wa kukuua?"
Santana aliamua kumuweka sawa Robinson.
"Nimeamua kuwa nanyi na si kwingine."
"Hebu mfungueni hizo ringi."
Santana aliamuru.
"Mpatieni chakula huyu najua atakuwa na njaa sana kijana wetu."
Mzee Bruno Gautier aliagiza.
Aliletewa chakula pale ambacho kilikuwa ni mkate wa viazi mbatata ambao aliushambulia pamoja na juisi ya karoti. Na kwa ulaji ule walijua moja kwa moja alikuwa katingwa na njaa.
" Endelea kula tu Robinson chakula bado kipo cha kutosha na ukishiba tuna mvinyo wa kutosha."
Santana aliendelea kumsogeza karibu Robinson aliyeonekana kumuogopa yeye zaidi.
"Asanteni nimetosheka." Alishukuru Robinson.
Baada ya hapo ndipo alipomwita chumba maalum ambacho hicho mara nyingi hukitumia yeye tu Santana ndani ya ndege hiyo. Huku akimuagiza rubani kuzungusha panga za helicopter hiyo kuelekea Belem tayari kuangalia wanamuokoaje mke wa mzee Bruno ndani ya Rio Branco.
"Ni wakati wako sasa kunieleza chochote kinachokuhusu Robinson."
Santana alimueleza Robinson.
"Mkuu mimi kama ninavyojulikana kwa jina la Robinson Kaaya ni mtoto wa pekee kwa wanandoa Mr&Mrs Kaaya. Wazazi wangu ni wakulima wadogo wa zao la tumbaku ambalo mpaka sasa ni kitendawili kutokana na mfumo wake wa uzalishaji nakichukia sana kilimo cha zao hilo la Tumbaku na ndiyo maana nilishawishiwa na Jackline kuja huku kumsaidia mambo yake lakini nilivyotulia nikajikuta natamani kuzifikia ndoto zangu za muda mrefu za kuwa na maisha mazuri na yenye furaha hivyo tu mkuu."
"Vizuri Robinson kumbe wewe ni kijana muelewa sana ee na ndiyo maana nikaona nikuajiri kusimamia kampuni yangu ya usambazaji wa vifaa vya michezo barani Afrika na makao makuu yakiwa hapa hapa Brazil hivyo jukumu lako ni kuhakikisha kuwa unafungua matawi ndani ya nchi za Tanzania, Afrika ya kusini, Misri, Kenya, Rwanda, na Zimbabwe."
"Kweli mkuu?"
"Kama ulivyosikia Robinson ndivyo ilivyo ila tu yote haya yatafanyika mara baada ya kuwatia nguvuni wale Mbwa Koko wasio na makazi na hilo si la leo wala kesho utalifanya kwa wakati wako mwenyewe."
"Niamini mkuu, katika hili wewe mwenyewe utajionea mbona kwangu wale nitawaminya kwa kutumia kwapa langu tu."
Robinson kwa namna ambavyo alitoa majibu ilipelekea Santana kusimama na kumfuata alipokuwa kakaa na kumkumbatia.
"Nimekukubali Robinson kwa namna ambavyo umejieleza nina uhakika tunakwenda kushinda hii vita."
"Kweli mkuu?"
"Niamini Robinson katika hili mimi ni mgumu sana kumuamini mtu lakini kwako naiona imani kubwa sana kikubwa usiniangushe kijana."
"Kijana wangu tumefika tayari maliza haraka mahojiano yako."
Mzee Bruno Gautier alimkumbusha Santana baada ya kuingilia maongezi yao.
"Okay mzee hata hivyo tumekamilisha tayari tunaweza kushuka."
Alijibu Santana.
Wakiwa wanatelemka kutoka kwenye helicopter wakiwa ndani ya kambi ya Santana mzee Bruno Gautier alimuuliza inakuwaje juu ya suala la mke wake.
"Inakuwaje Santana kwenye suala la mke wangu ni masaa takribani mawili sasa na sijui ana hali gani?"
"Mzee punguza wenge yatakwisha tu hayo na muda si mrefu tutamrejesha akiwa salama."
"Tutafanyaje hapo?"
"Si walisema wanamhitaji Robinson?"
"Ndiyo ni moja ya mahitaji yao."
"Kinachotakiwa kufanyika hapo ni wewe mzee Bruno kuwapigia simu na kisha kuwauliza tunakutana nao sehemu gani kwani mtu wao tunaye mikononi mwetu."
"Hiyo itakuwa imekaa vyema Santana hebu ngoja niwapandie huko huko hewani." Aliongea hayo huku akiichukua simu yake mfukoni na akabonyeza namba ya mke wake na kuipiga hapo hapo mbele ya wenzake.
"Haloo halooo halooooo.....!"
Mzee Bruno Gautier aliita baada ya simu kupokelewa na upande wa pili kutoongea chochote.
"Haloo oo mhhh mbona kimya hawaongei chochote hawa?"
Mzee Bruno Gautier alijiuliza swali.
"Vipi mbona unaongea peke yako mzee wangu kuna nini?"
Santana alimuuliza mzee Bruno wakati akiingia ndani mle na kumkuta akiongea peke yake.
"Wanapokea simu lakini hakuna wanachojibu au kuongea chochote."
Mzee Bruno Gautier alieleza.
"Jaribu tena inawezekana mtandao haukuwa vizuri."
Santana alimshauri mzee Bruno.
Kisha alipiga tena namba ya mke wake kwa mara nyingine tena.
"Mume wangu ni-na-ni.... nakufa niokoe kutoka kwa mbweha hawa si watu wazuri hata kidogo na laiti ungejua sehemu niliyofungiwa mume wangu usingekaa hata sekunde sifuri."
"Unasemaje mke wangu? Kwani wamekufungia sehemu gani?"
Mzee Bruno Gautier aliuliza.
"Unataka kujua siyo?"
Huyu mzee mara baada ya kusikia tu swali hilo aliidondosha simu kwa pressure kwani sauti iliyouliza swali lile anaijua vizuri sana.
"Mzee mbona unaangusha simu au ni ya bei dezo?"
Robinson alimuuliza huku akiiokota simu na kumkabidhi mzee Bruno.
"Hapana Robinson imetokea tu."
Aliipokea na kuiweka sikioni kuona kama bado iko hewani au la.
"Halooo...."
Mzee Bruno Gautier aliita.
"Mbona ulikuwa hauongei ni hivi mzee iwapo utachukua muda mrefu bila kumfuata mkeo tutakutumia kichwa cha mkeo kwani hatuna hasara yoyote."
Jackline alimtisha.
"Binti ndiyo tuko kukamilisha mipango ili twende sawa na kwa kuwahakikishia tu hata mwenzenu tunaye hapa."
"Mwenzetu gani mzee?"
"Si ni Robinson?"
"Robinson? Robinson gani huyo?"
Jackline aliuliza.
"Kwani mlikuwa wangapi siku ile tulipokutana kule porini na mpaka kule mgodini kwangu?"
"Hatukumbuki kwani tulikuwa wangapi zaidi ya sisi wenyewe kama tulivyo hapa."
"Sasa mbona mnanichanganya maana hata kwenye vitu mnavyovihitaji ni pamoja na Robinson."
"Mzee masuala ya Robinson hatutaki kuyasikia hata kidogo huyo ni mwenzenu mnafikiri hatujui kilichomfanya akutoroshe?"
"Kitu gani hicho ambacho hata mimi sikijui?"
"Muda ukifika tu utajua mzee Bruno Gautier na huyo msaliti wako."
Jackline alikazia maneno yake.
"Basi ongeeni naye mwenyewe huyu hapa yuko salama kabisa."
Aliongea maneno yale na kumkabidhi simu Robinson alikuwa pembeni yake muda wote akiwasikiliza.
"Haloo ni mimi Robinson niko vizuri kwa sasa na kuhusu kupotea kwangu ile siku nilitekwa na watu wa Santana."
"Huna chochote Robinson wewe ni msaliti na hilo ulilianza toka ile siku ulipokisikia kile kiasi cha fedha cha mzee Bruno."
Kisha alikata simu Jackline na kuwaachia maswali mzee Bruno na Robinson.
****
"Mkuu nakusikia."
Mkuu wa kituo Lupa aliitikia mara baada ya kupokea simu ya bosi wake kutoka Makongolosi.
"Vijana wangu hawajafika bado hapo?"
"Bado mkuu, niliwatafuta muda fulani hivi hawakupatikana ngoja niwapigie tena."
"Fanya hivyo kwani wanatakiwa kurudi hapa hata kama itakuwa ni usiku wa manane maana hapa kuna tukio jingine limetokea Saza Mining' kuna wafanyakazi wamefukiwa na kifusi walipokuwa shimoni huko na hapa hakuna gari jingine la kulitumia."
"Sawa mkuu wakifika tu sitawapa hata sikunde moja ya kukaa hapa."
Akiwa anaongea na mkuu wake wa kazi alisikia gari likipiga breki nje.
"Naona ndiyo wanaingia mkuu."
"Okay niwatakie majukumu mema."
"Sawa mkuu."
Alikata simu na kutoka nje ambako aliwakuta wakiwa tayari kwa kuwabeba wahalifu.
"Vipi mbona mmechelewa sana mpaka mkuu alipata hofu akapiga simu kutaka kujua nini kimewakuta."
"Tulikutana na tatizo kidogo la panja lakini mwisho wa siku tulilikabili na sasa tuko hapa."
"Okay basi subirini kidogo tuwaandae watu wenu maana sisi kazi yetu tushaimaliza Afande George."
"Bila tatizo mkuu."
Afande Mkonge aliingia ofisini kwake na kisha kumtumia ujumbe Afande Piliska.
"Njoo mara moja hapa ofisini kwangu."
Afande Piliska baada ya kuiona ile meseji alitoka na kuelekea kwa mkuu wake kuitikia wito.
"Mambo yameiva tayari utamfuata Afande Miraji aandaye lile faili la hao nyang'ao kisha amkabidhi Afande George pamoja na watuhumiwa."
"Kama ulivyoagiza mkuu."
Afande Piliska aliitikia na kutoka nje kumfuata Afande Miraji kumpa maelekezo ya mkuu.
"Mkuu kasema chukua faili la wale watuhumiwa wa Bitimanyanga na mkabidhi Afande George pamoja nao."
"Okay sawa."
Alitoka Afande Miraji na kufanya kama alivyoelekezwa na Afande Piliska akamkabidhi Afande George faili pamoja na wahusika.
"Mbona siwaelewi jamani? Kila kitu nilishamalizana na mkuu wa kituo juu ya kilichotokea kilichokuwa kikisubiriwa ilikuwa ni tamko kutoka kwake tu."
"Uko sawa kabisa na tamko alilolitoa ni ninyi kuhamishwa Kituo kutoka hapa na kwenda Kituo kikuu cha Makongolosi, umenielewa mzee Rasta?"
Afande Miraji alimkebehi mzee Jonathan kwa muonekano wake wa nywele.
Mzee Jonathan aliishiwa pozi lote na nguvu zilimwisha aligeuka tu nyuma kumtazama Masanja ambaye alikuwa kimya muda wote.
" Mzee Jonathan yako wapi sasa majigambo yako? "
Masanja aliongea hayo kwa sauti ya chini huku akimpita na kuliendea gari lililokuwa likiwasubiri.
"Yakwisha tu haya mimi ndiyo Jonathan Ubao mtu hatari zaidi ndani ya nchi."
Mzee Jonathan aliongea hayo kimoyo moyo huku akimpita Afande Piliska aliyekuwa akiwaangalia kwa jicho la huruma.
NINI KINAKWENDA KUTOKEA?
TUKUTANE KATIKA SEHEMU INAYOFUATA YA HADITHI HII.'
"Mzee Bruno Gautier hebu watafute hao Kenge waambie tuko njiani tunakutana wapi?"
Santana alimuagiza mzee Bruno.
"Sawa kijana wangu ngoja niwaulize mara moja."
Mzee Bruno Gautier alijibu.
"Fanya haraka sana maana siku ya leo nina mzuka hatari."
Mzee Bruno alimpigia simu mke wake kwani mara nyingi ndiyo namba wanayoitumia wakina Jackline pia. Baada ya kuipiga mara kadhaa haikupatikana kitu kilichomchanganya sana mzee Bruno.
"Wasije kuwa wameshamuua mke wangu?"
Mzee Bruno Gautier aliuliza swali huku akipiga piga kichwa kwa simu yake.
"Vipi kwanini unasema hivyo mzee?"
Santana alimuuliza mzee Bruno baada ya kuona hayuko sawa.
"Mhhh hakuna kitu."
Mzee Bruno Gautier hakuwa sawa kabisa.
"Kwanza ngoja, umewapata hewani?"
Santana ilibidi aulize swali la msingi baada ya kuona mzee mzima kama kachanganyikiwa hivi kwa jinsi alivyokuwa akigongagonga bodi ya gari.
"Ndicho kinachonichanganya Santana hapatikani hewani kabisa nimepiga na kupiga lakini hakuna kitu na si kawaida yao au wamemuua mke wangu?"
"Sikiliza mzee usiwe kama boga wewe ni shujaa ninayekuamini kwenye mambo yangu mengi sana sasa nitakushangaa kuchanganyikiwa eti kisa mkeo hapatikani hewani, kwanza nimekwambia wapigie wale wanawake na si mkeo."
"Santana hata wewe hauko sawa hata kidogo nilikwambia wale hawana simu hivyo wanatumia ya mke wangu."
"Ni kweli kabisa simu hawana, sababu ni kwamba simu zetu tuliziacha ndani ya chumba ambacho tulifungiwa mgodini kwako mzee hivyo sina uhakika kama walikumbuka kwenda kuzifukua pale ambapo tulizichimbia."
Robinson alifafanua.
"Si unaona Santana, nilikwambia hawana simu wale."
"Kwani nilikataa juu ya hilo? Mimi nilitaka wapatikane tu haijalishi ni kwa kutumia simu ya nani?"
Santana alipaza sauti ya juu baada ya kuona hawaelewani kila mmoja akiongea lake.
"Okay hebu tuyaache hayo Santana tujadili ni namna gani tunawapata."
Mzee Bruno Gautier ilibidi amrudishe Santana kwenye mstari kwanza ili mambo mengine yaendelee.
"Hebu niitieni rubani wa ndege mara moja." Santana aliagiza.
Baada ya kuja rubani wake alimwambia aikague ndege kama iko vizuri kuna safari wanatakiwa kwenda.
"Kamanda wangu wa anga ifanyie ukaguzi ndege kama iko poa."
"Sawa kiongozi wangu."
Rubani alitoka na kuelekea kwenye egesho la ndege.
Rubani alipotoka tu ofisini kwa Santana, simu yake iliingia ujumbe.
"NAISIKIA HARUFU YA DAMU YAKO SANTANA."
Baada ya kuisoma tu alijikuta jasho likimtoka mfululizo na kama hakuielewa hivi ile meseji akaisoma tena akiamini labda yalikuwa ni mawenge ya macho yake tu lakini alipoirudia kuisoma ilikuwa ni ile ile. Alihisi kichwa kinawaka moto.
" Ni nani aliyetuma ujumbe huu kwa kutumia namba ngeni?"
Aliinuka na kutoka nje ambako wenzake walikuwa wamekaa wakimsubiri yeye waianze safari yao.
"Vipi kijana wangu mbona macho juu kama jogoo anayeangalia muda wa kuwika."
Mzee Bruno Gautier alimuuliza Santana baada ya kumuona kafika pale haongei chochote zaidi kuangalia juu kama vile kulikuwa na kitu kipya angani ambacho hajawahi kiona.
"Nimepokea ujumbe wa kutisha kidogo si sana."
"Ujumbe wa kutisha? Kutoka wapi? Kwa nani?"
Mzee Bruno Gautier aliuliza.
"Sijui uliko toka ila nahisi ni wale wanawake tu kwani namba ya mtumaji haionekani, nimeitafuta na kuitafuta lakini wapi."
"Inasemaje hiyo meseji mkuu?"
Robinson alimuuliza Santana.
"NAISIKIA HARUFU YA DAMU YAKO SANTANA."
Robinson aliusoma ujumbe ule baada ya kupewa simu na Santana.
"Kiongozi si wengine waliotuma huo ujumbe bali ni wakina Jackline tu, eleweni kuwa hawa ndiyo maadui zetu wakubwa kwa sasa na kwa namna nilivyowafahamu hawa wasichana kwa kipindi chote nilichokuwa nao huwa wakisema kitu lazima kiwe hivyo huo ujumbe msiubeze hata kidogo." Robinson aliwatahadharisha wakuu wake wapya.
" Unataka kututisha siyo au ndivyo ulivyoagizwa na hao mapunguani waliopoteza network' za maisha? "
Santana alimgeukia Robinson ambaye alijua anashauri zuri kumbe alikuwa ameharibu.
" Hapana kiongozi nilikuwa najaribu kukuelezeni nilivyowafahamu hawa viumbe na mfanyaje kuwakabili.. "
" Keleleeee.... Unaongea upuuzi gani kama wewe ni muhubiri mzuri si ungekuwa huko kwenye Masinagogi ukihubiri neno la Mungu kwa wanaolihitaji lakini siyo sisi kijana."
"Naombeni msamaha kama nimewakwaza wakubwa zangu."
Robinson alipiga magoti kuomba msamaha baada ya kubaini kuwa amechafua hali ya hewa.
"Santana haina haja ya kuendelea kulumbana hapa zaidi tuangalie mbele tunakutana nao vipi hao viumbe?"
Mzee Bruno Gautier aliingilia kati baada ya kuona Santana hamuelewi Robinson.
"Na wewe mzee elewa kuwa kama mkeo atakufa itakuwa ndiyo mwanzo wetu wa kukuwa kiuchumi hivyo sioni sababu ya kwenda kumkomboa mtu kama yule mzee wangu mbona sisi wengine hatuzungumzii Mahusiano ni wewe tu na huyo kenge wako ana kipi cha kuichanganya akili yako kiasi cha kuacha kufikiria namna ya kuuendeleza mgodi?"
" Hapo umenigusa pengine kijana wangu naona sasa heshima inashuka, mke wangu wa kwanza ulimuua na madawa yako na huyu tena unasema wa nini kwangu kweli Santana? "
Kabla Santana hajajibu chochote kwa mzee Bruno mara alifika rubani kutoa ripoti ya kile ambacho aliagizwa na mkuu wake.
" Mkuu ndege iko tayari kwa safari."
"Okay vizuri kamanda wangu pakia lile boksi la vinywaji na wewe Mtanzania hapo ongozana na rubani kachukue maboksi ya vyakula pakieni haraka tuko nyuma ya wakati."
"Nashukuru mkuu kwa kunisamehe." Robinson alishukuru lakini Santana hakumjibu kitu zaidi ya kuendelea kunywa mvinyo wake na macho yakiwa kwa mzee Bruno ambaye muda huo alikuwa katulia tu akitafakari maneno ya mbia mwenzake ya kumkashifu mke wake Bi Claudia.
" Kila kitu kiko sawa mkuu tunaweza kuondoka sasa." Rubani alitoa taarifa.
"Okay tuondokeni sasa."
Santana aliongea na kuchukua koti lake huku akimuacha mzee Bruno Gautier akiwa bado katulia tu hajafanya maamuzi.
"We mzee hauongozani nasi?"
Santana alimuuliza mzee Bruno baada ya kugeuka na kumuona bado hajainuka zaidi ya kujiinamia tu.
Aliyasikia maneno ya Santana lakini hakujibu chochote zaidi ya kusimama na kuongoza ndege ilikokuwa.
***
Wakina Jackline baada ya kutoka hospitali kumuona mama yake Roberto Stanley ambaye wakina Jackline walimuahidi Roberto kumsaidia. Waliongoza mpaka kwa rafiki yake Jasmine aitwaye Melissa anayefanya kazi kwenye ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Brazil.
"Unajua bado najiuliza sana huku Rio Branco mmefuata nini ninyi Warembo?"
Aliuliza Melissa akiwa nyuma ya usukani akiwapeleka wageni wake kwake maeneo ya North Angle eneo ambalo hukaliwa sana na Waafrika kutokana na hali ya utulivu na hali ya hewa inayofanana na ya Afrika na hata shughuli za kilimo hufanyika kwa wingi eneo hili.
"Unajua nini Melissa? Kwa sasa tumekuwa kama digi digi hatuna makazi maalum hapa Brazil."
"Kivipi Jasmine na vipi kuhusu Santana wako maana nakumbuka kuna siku uliniambia kuna kitu kimetokea unataka kuniomba ushauri."
"Ni kweli kabisa lakini masaa chache nilitiwa pingu na watu wake nikiwa na mdogo wangu Jessica na kisha kushindiliwa madawa ya kulevya lengo likiwa ni kunikomoa kutokana na hatua yangu ya kumsaidia mdogo wangu ambaye alitaka kumtumia kusafirisha madawa yake na bora ingekuwa kwa makubaliano na mhusika lakini yeye alitaka amuue kisha asafirishe kama maiti."
"Mhh makubwa hayo, pole sana Jessica (alimgeukia Jessica) eeh sasa ikawaje mpaka leo mko nje ya mikono michafu ya Santana?"
"Acha tu yaani kama muvi vile walitokea hawa wenzetu nasema wenzetu sababu walikuwa wawili Jackline na mpenzi wake Robinson ambaye ametusaliti na kurudi upande wa pili kisa mkwanja, walituokoa baada ya wao pia kuokoka kutoka kwenye mikono hiyo hiyo ya Santana ambaye aliwaambia waje yeye ana chuo cha mafunzo ya mapigano kumbe tageti yake ilikuwa ni kuwanyofoa viungo vyao na kuvipeleka India lakini kabla hajafanikisha zoezi lake watanzania wenye chale zao wakaiona na kutoroka."
"Poleni sana ndugu zangu, mwenzenu huyu Jasmine nilimkanya sana juu ya Santana lakini masikioni aliweka pamba."
"Ni bora alifanya hivyo kwani angekubali ushauri wako inawezekana mpaka leo angejua wewe ndiye uliyemtenganisha na mpenzi wake."
"Ni kweli Jackline, jamani karibuni hapa ndipo ninapoishi kwa sasa."
"Tunashukuru sana dada Melissa." Aliitikia Jessica ambaye muda wote alikuwa kimya akiwasikiliza tu.
" Dada hivi unamuamini tumemuamini vipi Roberto kumuachia Bi Claudia?"
Jessica aliuliza swali hilo kama vile naye hakuwepo wakati wanamkabidhi.
" Hebu achana na hizo mambo mdogo wangu itajulikana tu baada ya kutoka hapa."
Jasmine alimjibu mdogo wake.
"Hebu mtishe tena Santana bwana ili ajue tuko siliasi."
"Nakujuaga ukisema hivyo tu tayari kichwani una jipya chukua simu hii hapa mfanyia jambo."
"Poa."
Aliipokea simu kutoka kwa Jasmine na kuuandika ujumbe mwingine ambao aliutuma tena kwa Santana nao ulisomeka hivi..
"KESHO ALFAJIRI KWENYE Ufukwe wa PRAIA DO FUTURO ulioko ndani ya mji wa FORTALEZA kuna zawadi yako na ukipuuza tu Utajuta kutufahamu."
Na baada ya kuukamilisha aliwaonesha wenzake ambao waliufurahia kisha alimtumia Santana.
"Nina uhakika baada ya kuusoma ujumbe huo lazima achanganyikiwe na pale atakapojaribu kututafuta hewani hawezi kutupatau."
Jackline alichekelea.
"Sasa lengo lenu ni lipi kwenye mtego wenu huu?"
Melissa aliuliza.
"Kikubwa ni kumfilisi Santana na mshirika wake mzee Bruno Gautier na kisha kumfunza adabu Robinson hata kama itakuwa miaka elfu mia moja wakati huo huo kuhakikisha Mali za marehemu wazazi wangu zinarudi kwangu na wakati huo tutakuwa na mabilioni ya dollars."
Jackline alitoa ufafanuzi zaidi kwa Melissa ambaye aliona kama na anashauku ya kutaka kujua hivi.
" WATU WAKO NINAO NYUMBANI KWANGU "
Melissa alimtumia ujumbe Santana baada ya kuwaacha wenyeji wake sebuleni na yeye kuingia chumbani kwake.
" WAMEFIKAJE KWAKO?"
Santana aliuliza swali.
"WAMEFIKA TU SI UNAJUA MIAKA KADHAA NYUMA NILIKUWA MSIRI MKUBWA WA JASMINE KABLA HAMJAOANA."
"KWELI?"
"NDIYO, MASIKINI JASMINE NA MPAKA LEO ANAAMINI MIMI BADO NAFANYA KAZI UBALOZINI KWETU KUMBE NILIACHA KITAMBO BAADA YA KUUNGANA NA WEWE KWENYE BIASHARA YETU YA VIUNGO VYA BINADAMU."
"ENDELEA KUCHEZA NA AKILI ZAO NA SISI TUTAKUWA HAPO BAADA YA DAKIKA CHACHE KUWAONESHA MIMI NI NANI."
"POA JEMEDARI WANGU."
Alipomaliza kuchati na Santana alirudi pale sebuleni kwa wageni wake waliokuwa wanamsubiria.
"Niwaletee kinywaji gani wageni wangu?"
Aliwauliza huku akiwa na tabasamu pana la ushindi usoni.
UNAFIKIRI NINI KITAENDELEA?
TUKUTANE KATIKA SEHEMU INAYOFUATA.
Baada ya kutaja vinywaji wavihitajivyo Melissa aliiendea friji yake akachukua vinywaji vile na kuwaletea wageni wake kisha akachukua nafasi yake naye akaketi.
"Melissa hivi toka kipindi kile tumeachana ndipo ulipata kazi ubalozini au kabla kuna kona ambayo ulipita kwanza?"
Jasmine alimuuliza Melissa wakiwa wanaendelea kupooza makoo yao.
"Kabla ya Ubalozini nilijiajiri kwanza hapa mjini nikiwa natembeza matunda ya maepo."
"Wee kwa nyodo zako wewe uliwezaje kufanya biashara hiyo ya maepo?"
"Biashara ya maepo kwa hapa bonge la dili kwani huuzwa kwa bei ya juu sana huenda mpaka dola tatu kwa epo moja."
"Lakini nasikia matunda haya yana uhusiano mkubwa sana na madawa ya kulevya sababu kule Afrika ya Kusini matunda hayo yalikuwa yakiuzwa mpaka dola ishirini kwa epo moja na mara baada ya serikali kuyafanyia uchunguzi wakabaini kuwa sura ilikuwa ni epo lakini mfumo wa burudani wa ndani ulikuwa ni madawa ya kulevya ambayo yalipachikwa kitaalam sana na maeneo yalikokuwa yakipelekwa na kuuzwa sana ilikuwa ni kwenye masaluni."
Jackline alichangia hoja hiyo kwa kuelezea namna ambavyo anaijua biashara hiyo.
" Kwa hiyo unataka kusema na mimi nilikuwa nafanya biashara hiyo ya madawa ya kulevya?
Melissa aliuliza kwa kumkazia macho Jackline kama vile aliotea uhalisia wa biashara yake hivyo ilikuwa kama vile kumkata fikra zake.
" Hapana sijamaanisha hivyo nimeelezea tu ninavyoifahamu biashara ya maepo kwa maeneo niliyokuwepo."
"Okay ila kwa upande wangu haikuwa hivyo mpendwa."
"Dada tuwashie muziki tuburudishe ngoma za masikio kwani tuna muda mrefu sana hatujawahi kusikia milio ya muziki zaidi ya milio ya risasi na mabomu."
Jessica aliona dalili hazikuwa nzuri kwa upande wa Jackline na mwenyeji wao Melissa.
"Kweli kabisa mdogo wangu umenena ni muda sana hebu Melissa tufanyie mambo tuzungushe viuno hapa visijekuwa vigumu kama vimeshikwa na kutu bure."
Jasmine aliongea hayo na kuwafanya wote kuachia vicheko huku Melissa akihangaika kutafuta flashi yenye ngoma tofauti tofauti kutoka kila bara.
Katika kuitafuta ndipo akaikuta na kuipachika kwenye Home Theater yake na kama zali vile si ngoma ya kwanza ikawa ni ile ya BEMBELEZA iliyoimbwa na Wanamuziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Quick Rocka akimshirikisha Joh Makini pale sebuleni nani alikaa? Kila mmoja akicheza kwa ustadi wake aliyecheza kwa kuzungusha kiuno haya, aliyecheza kwa kuchezesha tumbo twende kazi ila kituko kilikuwa kwa Melissa aliyecheza kiustadi zaidi kutokana na staili yake ya kuweka mguu wake mmoja juu ya kochi na kuanza kukisasambua kinyonga chake.
"Mmhh mwenzetu umetushinda kwa staili hiyo duu!"
Jackline aliongea baada ya kujikuta akiduwaa kumuangalia tu Melissa. Naye kama vile alifanya makusudi kwani alipoona anatazamwa sana ndipo akaongeza mbwembwe zaidi.
"Bwana eee umeshinda wewe sasa..." Jasmine naye akaona amkatishe kwa kumsukuma.
"Wivu wenu tu hamna lolote kama hamjui hamjui tu ninyi zenu ni silaha tu mambo hizi tuachieni siye."
Melissa akawazodoa na muda huo akaingia chumbani kwake huku akiwaacha wakina Jessica wakijisevia maji ya baridi baada ya kulinunua joto la ghafla.
"NDIYO TUNAINGIA KWAKO HAPO."
Meseji iliingia na ndipo Melissa akaona amtwangie tu Santana.
"Mnaingia na staili gani sasa?"
"Hakuna zaidi ya kuvamia tu na kisha kuwabeba wote kisha tutajua wewe tunakuachaje ."
"Sawa ila changu mapema maneno sitaki. "
"Kitambo sana akaunti yako inapumulia mipira kutokana na kuzidiwa na midola."
"Hayo ndiyo maneno vingine havinihusu ni kazi yenu kucheza na vipanya buku vilivyowashinda midume mizima na kunasa kwenye mtego wangu mdogo tu."
"Haya mama yake andaa mazingira jeshi langu limeshafika nje ya mjengo wako."
"Poa."
Melissa alikata simu na kurejea sebuleni na kuwakuta wenzake wakiwa wameacha kucheza na muda huu walikuwa wanaangalia katuni kupitia kwenye chaneli maarufu ya katuni ya hapo Brazil inayofahamika kama LIVE CARTOON. Aliwaangalia kisha alitikisa kichwa kwani alijua muda wa kunaswa umefika na yeye kuzidi kuchanua kiuchumi.
"Mtanisamehe sana Melissa hana undugu na binadamu mbele ya Mkwanja."
Wakiwa wametekwa na katuni pale sebuleni mara mlango uligongwa, walitazamana na kisha wakahamishia macho kwa mwenyeji wao ambaye alisimama na kwenda kuufungua. Aliusogelea na kuufungua na alipojaribu kuchungulia nje kuona ni nani aliyegonga alikutana na kitako cha bunduki kilichotua kichwani na kumpeleka chini kisha wagongaji wakiingia ndani wakimruka Melissa pale mlangoni.
Wakina Jackline wakiwa bado hawajui kinachoendelea mara waliingia watu watatu wakiwa na mitutu mikononi mwao na usoni wakiwa wamevalia maski.
Jackline akaona njia pekee ya kujinasua ni kuchomoa bastola yake iliyokuwa kiunoni mwake lakini alichelewa kwani walioingia hawakuwa na masihara hata kidogo kwani aliyekuwa katikati yao alifyatua risasi iliyomkosa na kupiga kabati la vyombo. Hapo Jackline akajua akileta za kuleta anakwenda kukutana na pembenne huku tani sita za udongo zikiwa juu yake.
Akalala chini kama wenza huku akiiachia bastola yake.
"Jackline usilete ujuaji kwenye mdomo wa bunduki utakufa mama yangu."
Robinson aliongea hayo huku akivua maski na kuchuchumaa pale alipo Jackline.
"Haaa Robinson ni wewe kweli usiniambie kama umetisaliti wenzako na mimi mpenzi wako?"
Jackline aliongea baada ya kuiona sura ya Robinson ikiwa ndani ya mavazi yale ya rangi ya kijani nyeusi ambayo huvaliwa na watu wa Santana.
"Jackline kwanza naomba unisamehe kwa kukutelekeza kabla ya kufikia lengo lako la kuokoa Mali zenu na pili nikuambie tu mpenzi wangu kuwa chini ya jua hakuna mtu yeyote ambaye ni mjanja mbele hela na ni hela hizo hizo zilikuleta huku Brazil kuzipambania nikaona mwenzangu tayari unazo, Jasmine na mdogo wake wanazo na mimi mtoto wa kapuku nina nini nikaona nifanye maamuzi ya kiume kama haya ikiwa ni kukukamateni na kuwapeleka machinjioni kwa mtu ambaye mmemkimbia weee mwisho wa siku mnarudishwa kwake."
"Keleleeeeee Robinson unaongea nini wewe?"
Jackline aliongea huku kajipindua na kumtandika teke la kisogo Robinson lililompeleka chini na kuachia bunduki ambayo Jackline aliirukia aichukue lakini alichelewa kwani Robinson alifanikiwa kuisukuma kwa teke na kumfikia mmoja wa wale aliokuja nao na wakaichukua. Ndipo Jackline akajipindua na kumvaa Robinson ambaye kwa wepesi wa hali ya juu alimkwepa na kumfanya Jackline atulie kwenye mkono wake ambao aliumia kwenye ajali ya pikipiki na hapo ndipo walimvaa wale wengine na kumpiga cheni. Upande wa Jasmine na Jessica wao ilibidi watulie kwanza kuusoma mchezo unakwendaje lakini wakaona wababe wao walikuwa kamili ikabidi watulie tu. Wote walipigwa cheni za mikono na miguu na hapo ndipo walipofanikiwa kuiona sura ya mtu wa pili kati ya wale walioongozana na Robinson kuwa alikuwa ni mzee Bruno Gautier.
"Jackline mrembo jasiri usiyeogopa kitu chochote kwa hilo nakupongeza sana lakini nikuhakikishie tu safari hii huruki geti aisee."
Mzee Bruno Gautier alipokuwa akiongea hayo mbele ya Jackline alishangaa akitemewa mate usoni na Jackline.
"Asante sana Jackline kwa kitendo hiki na ndiyo maana niliongea mwanzo kuwa wewe si wa kawaida lakini fanya yote unayohisi yatakusaidia kujinasua lakini angalia usije wahi kuzimu kabla ya muda wako.
" Tunawahakikishia kuwa tunakwenda kuibuka tena na kuwasambaratisha kwa mara nyingine tena."
Jessica aliibuka na kuongea maneno ya kujitia moyo.
"Unajidanganya sana Jessica ni muda wenu sasa wa kutangulia kuzimu huku sisi tukibakia kula maisha milele."
"Robinson acha kujidanganya wewe na nikuhakikishie kuwa hata nife leo nitainuka tena na kukuua kwa mkono wangu."
Jackline aliongea huku machozi yakimtoka.
"Shutup your mouth."
Robinson aliongea hayo na kumtandika ngumi ya shavu iliyompeleka chini na kuuangukia mkono ule ule na hapo uzalendo ulimshinda na kujikuta akianza kulia kwa sauti.
"Bibie usiniletee uchuro ndani ya jumba langu lenye bahati ya minoti subiri ukitoka hapa ndani ndiyo uendelee kulia sawa wewe nguchiro? Na wewe mwehu hapo ulijua mimi ni kama wewe eee mwenzako naitwa Melissa Madola upo nyonyoooo." Melissa aliongea mbele ya Jackline na Jasmine kisha aliwapita na kwenda kuongeza sauti ya muziki ambao muda huo ilikuwa ikipigwa ngoma ya BABA LAO ya Diamond Platinum kisha akaanza kucheza na hapo ndipo walipobaini kuwa Melissa ndiye mchawi wao aliyewauza.
"Nipe ripoti mzee Bruno Gautier."
"Kijana wangu tulia basi kila kitu kimekaa sawa chezea Robinson wewe utaugua ugonjwa wa Corona shauri yako."
"Ikoje mzee?"
"Tumewadaka kama nzige wale wadudu wasumbufu kule Kenya pamoja na mbwembwe zao zote lakini walikuwa wakidakwa kiulaini sana na ndivyo tulivyowadaka hawa vibwengo."
"Fanyeni haraka mniletee wakiwa hai ili niwatoe viungo vyao ambavyo kwa utatu wao tunakwenda kuingiza 'a lot of dollars' mzee wangu."
"Tutegemee kijana wangu ila kama utakuwa umekamilisha masuala yako ungana nasi basi kwani hatuwezi kuondoka hapa kabla sijajua mke wangu alipo japo uliniudhi kwa kauli zako juu ya mke wangu."
"Aaah mzee wangu yale yalikuwa ni madawa tu sikuwa mimi muda ule ila yote kwa yote wafanyieni chochote kile but' muwe makini na roho zao tu. Mimi siwezi kuungana nanyi hapo sababu bado namalizia kuingiza pesa kwenye akaunti ya Melissa na pia kwenye akaunti ya bwana mdogo Robinson walau aifurahie kazi mpya siyo kama hao Kenge waliokuwa wakimtumia dere."
"Vizuri kijana wangu basi wewe endelea na yako na sisi na yetu."
"Sawa sawa mzee."
Mzee Bruno Gautier alikata simu na kuwageukia wabaya wake ambao wameichanganya sana akili yake ndani ya muda mfupi kitu ambacho hakuwahi kutana nacho tokea aingie kwenye biashara ya machimbo ya kokoto.
Jackline muda wote alikuwa akimuangalia sana Robinson pamoja na Melissa ambaye bado alikuwa anacheza muziki ikiwa ni furaha baada ya kuingiza mkwanja mrefu ndani ya muda mfupi bila hata kutoa jasho.
Mara simu ya Jackline iliita na kwa kuwa ilikuwa mfukoni hakuweza kuhangaika nayo alitulia tu huku akiwa anaendelea kupiga hesabu zake za kujiokoa.
"Baby hiyo simu si inaita?"
Robinson aliuliza.
"Kwa hiyo kama inaita inakuhusu?"
Jackline alimjibu.
"Nilijua hujaisikia nilikuwa nakujulisha tu."
"Achana na mimi wewe Kinyago cha Kimakonde na tena usinizoee na nikuhakikishie tu kwa namna yoyote ile nikiwa nimekufa au nikiwa hai lazima nitakuua mwenyewe Robinson na lazima utayajutia maamuzi yako na wewe hapo mshenzi wa tabia."
Akimuangalia Melissa.
"Jackline unajua unachekesha sana toka lini maiti isiyo na viungo vyote yaani yenye upungufu wa viungo ikaamka na kuua watu."
Robinson aliongea hao akiwa anauchezea mdomo wa Jessica ambaye muda wote alikuwa katulia tu hasemi chocolate lakini kwa kitendo kile cha kuchezewa na mtu kama Robinson alijikuta akimtwanga Robinson bonge la kichwa kilichomfanya ateme damu za kutosha.
"Paaaaa....."
Ilikuwa ni mlio wa risasi.
NI NANI ALIYEIPIGA HIYO RISASI NA IMEKWENDA KWA NANI?
KAA MGUU SAWA KATIKA SEHEMU INAYOFUATA KUJUA ZAIDI.
"Afande Bupe nawahitaji wale watuhumiwa walioletwa hapa kutoka Lupa."
Mkuu wa kituo aliagiza.
"Kama ulivyoagiza mkuu."
Alijibu Afande Bupe na kisha kutoka ofisini kwa mkuu wake.
Alienda kuwachukua wakina mzee Jonathan na Masanja na kuwaleta mbele ya mkuu wake wa kazi.
"Kaeni bwana msinisimamie kama milingoti hapa."
Mkuu huyu alianza kwa kuwapiga biti walipoingia tu. Na Afande Bupe akafungua mlango ili kutoa nafasi kwa mkuu wake kuweza kuwahoji watuhumiwa hao.
"Unakwenda wapi Afande tulia hapa hapa."
"Sawa mkuu."
Alirudisha mlango na kurudi kuchukua nafasi kando ya watuhumiwa.
"Ehhh naomba kuwafahamu zaidi ya ninavyowafahamu waungwana."
Alianza mkuu wa kituo.
"Sijakuelewa Afande."
Mzee Jonathan alijibu.
"Hujanielewa eee, niambie basi nitumie lugha ipi ambayo utanielewa mzee mwenzangu."
"Hiyo ni juu yako mwenyewe si jukumu langu mimi, watu gani mnakuwa vigeugeu hapa."
Mzee Jonathan aliongea kwa jazba huku kamtolea macho mkuu wa kituo.
"Afande Bupe nitolee huyo kijana kwanza nianze na mzee mwenzangu labda tutaongea lugha moja."
"Sawa mkuu."
Afande Bupe aliondoka na Masanja na kumrudisha sero kisha akarejea tena.
"Sasa nafikiri tutaelewana si ndiyo?"
"Bado sikuelewi Afande."
Alijibu mzee Jonathan.
"Ooohhh kumbe ni mgumu wa kuelewa siyo? Afande mfungue kufuri la uelewa mara."
Afande Bupe hakujibu lolote kwa mkuu wake zaidi ya kumzoa mzee Jonathan na kumsogeza pembeni kidogo ambapo alianza kumtandika viboko na fimbo ilivyokuwa ikitumika ilikuwa kama vile ngozi ya mnyama hivi kwa namna ambavyo ilikuwa ikimzunguka mzee Jonathan maana ilikuwa ikimchapa mgongoni inakwenda mpaka tumboni na kisha Afande huyu mwenye sura ya kazi alikuwa akiivuta na kupelekea makelele.
"Ahhh.. aghhhh inatosha Afande nitaongea kila kitu."
"Ha ha ha kumbe hii ni njia ya kukuelewesha mzee mwenzangu?"
"Afande naomba msaada wako tafadhali."
"Msaada gani huo unaouhitaji kutoka kwangu?"
"Fanya kila unaloweza niondoke hapa maana sijayazoea hata kidogo."
"Okay kwanza niambie haya niliyoyasoma kwenye faili lako ni ya kweli?"
"Inawezekana Afande."
"Kivipi?"
"Sijaona kilichoandikwa hata kimoja Afande sasa nitasemaje ni sawa?"
"Lakini wewe si ndiye uliyetoa maelezo?"
"Ndiyo Afande."
"Basi nataka kujua kutoka kwenye maelezo yako mwenyewe."
"Mimi kwa majina naitwa Jonathan Ubao ni mfanyabiashara nikiwa na biashara nyingi sana nyingine nazimiliki kihalali na nyingine nilifanya dhuluma na hizo ndizo zinanitesa mpaka sasa."
"Ulizidhulumu kutoka kwa nani?"
"Ni stori ndefu Afande lakini kifupi ni kutoka kwa familia ya rafiki yangu mkubwa sana na ambaye aliniinua pale nilipoanguka na hata baada ya kufikwa na umauti wao mzee Fikirini ambaye ni ndugu na hiyo familia alinikabidhi kusimamia Mali za marehemu ambazo ni Hotel Joachim iliyoko Morogoro, kampuni ya utalii iitwayo Joachim Safaris yenye makao yake jijini Arusha pamoja na shamba la mpunga kule Kilombero Morogoro bila kusahau kampuni ya usafirishaji mizigo ya Mzalendo Cargo ya jijini Dar nyingine nyingi."
"Hiyo familia hujaitaja hapo zaidi ya ndugu yake mzee Fikirini."
"Ni ya mzee Joachim Thomas ambaye alifariki pamoja na mke katika ajali ya gari maeneo ya Sekenke Singida na hapo alipona binti yao aitwaye Jackline."
"Okay ndiyo maana unaisaka kwa udi na uvumba ili uiteketeze siyo?"
"Ni kweli kabisa na kwa sasa kazi imebakia ndogo tu kwani mzee Fikirini na mkewe nao nasikia walishalamba lamba mchanga na wanaonisumbua ni Jackline pamoja na watoto wa mzee Fikirini ambao siwafahamu Kiukweli."
"Kwa hiyo pamoja na kukutia mikononi mwetu bado una hesabu za kuwaua?"
"Lazima iwe hivyo nikiwapata Afande kwani iwapo sitafanya hivyo itakuwa shida kwenye maisha yetu hasa huyu Jackline ambaye nimemsomesha mpaka nje ya nchi."
"Hizi picha unazikumbuka mzee Jonathan?"
Baada ya kuziangalia zile picha aliduwaa kidogo na kisha akakubali kuzitambua.
"Nazifahamu vizuri sana huyu ni kichaa wangu Surambaya, huyu mwingine ndiye mzee Fikirini na huyu binti ndiye Jackline anayekisumbua kichwa changu usiku kucha."
"Vizuri sana kwa hiyo unakiri kuwa wewe ndiye kila kitu kwenye matukio haya yote kuanzia ajali ya mzee Joachim mpaka utekaji kwenye lile basi?"
" Ni kweli kabisa Afande ile ajali ya rafiki yangu mzee Joachim m Thomas niliifungia safari mpaka ndani ya kisiwa cha Saa Nane Mwanza kwa mtaalam mmoja ili tu kuwapoteza ambapo niliamini mtoto wao nitamtunza kumbe nilijidanganya bora ningemmaliza tu kumbuka hata huu muonekano nimeutengeneza kwa gharama kubwa ili kujilinda na wabaya wangu lakini nahisi jinamizi la Mzee Joachim linaniandama."
"Aisee basi nikuhakikishie kuwa sisi kama serikali tumeamua kukubadilishia makazi."
"Kivipi Afande?"
*********
Mzee Bruno Gautier baada ya kuona Robinson kapigwa vile na Jessica akaona njia pekee ya kumnusuru kijana wake ni kumtwanga tu risasi ya mguu Jessica.
"Maamaaaaa mguu wanguuuu..........."
Jessica alipiga kelele kiasi cha kuwashtua wenzake ikiwa ni pamoja na Melissa mwenyewe aliyewauza.
"Mzee Bruno Gautier umefanya nini sasa?"
Melissa alimpigia kelele mzee Bruno kwa kitendo kile.
Pamoja na kuwa kwenye cheni waliinuka na kumvaa mzee Bruno na kumzungusha ile cheni na kuanza kumnyonga mzee huyu lakini yule kijana mwingine aliyekuwa na wakina Robinson akaona muziki huo hauwezi na ukizingatia bosi wao anawataka wakiwa hai mabinti hao alichokifanya yeye ni kutoa Kopo fulani mfukoni na akalifungua na kulirusha hewani na kisha kumfuata Robinson kumvutia nje. Mle ndani hali ilibadilika kwani wakina Jackline walijikuta wakiishiwa nguvu na kujikuta wakimuachia mzee Bruno ambaye aliomba msaada kwa wenzake ambapo yule kijana alikuja na kumbeba lakini naye alipofika mlangoni alianguka na kumbwaga mzee Bruno pembeni.
Hali ikawa tete kwani kila aliyekuwa pale alipoteza fahamu, hali ile ilikwenda kwa masaa kadhaa kisha Robinson alikuwa mtu wa kwanza kupata fahamu kutokana na kupigwa na upepo pale nje lakini wengine wote mpaka Melissa naye alikuwa kapoteza fahamu. Aliamua kufanya maamuzi ya haraka ikiwa ni pamoja na kuwatoa nje wote ili wapigwe upepo hasa Melissa, mzee Bruno na yule mwenzao aliyesababisha hilo tukio la watu kupoteza fahamu lakini wengine ambao ni Jackline, Jasmine na Jessica akiwaacha humo humo ndani waendelee kumezwa na ile sumu. Akakaa nje ili akili ikae sawa kwanza wakati akiwasubiri wenzake wapate fahamu.
"Mkuu huyu mtu wako Tom kafanya yake hapa na kusababisha watu kupoteza fahamu."
"Kivipi wewe dogo?"
"Wakati kumetokea vurugu hapa ndani yeye akaona njia pekee ni kupuliza sumu aliyokuwanayo mfukoni."
"Mungu wangu hivi Tom ana akili zote kweli? Ile sumu si ya mchezo hata kidogo sisi huitumia kwenye biashara yetu ya madawa ya kulevya na Mazungu wenzetu na mbaya zaidi ukikosa hewa safi kwa dakika ishirini lazima upoteze maisha kabisa au uzinduke baada ya wiki kadhaa mbele."
"Kwa maelezo yako tu hayo ambao wanaweza kuinuka ndani ya masaa kadhaa yajayo labda mzee Bruno na yeye mwenyewe Tom kama sikosei na Melissa ila hawa wengine sina uhakika kwani mpaka sasa wako ndani ya sebule ambako lile kopo lipo na bado linatoa harufu ile."
"Kazi ishakuwa mbovu hiyo tena, okay hebu tuje na vifaa maalum vya kuvaa ili tuwatoe humo ndani."
"Sawa mkuu nimekupata."
Simu ilikatwa na kisha akarudi mlangoni kuiangalia kama kile kikopo kimeacha kutoa ile hewa ya moshi wenye sumu na baada ya kuangalia hali ilikuwa ni ile ile akarudi alipokuwa kakaa akiendelea kuangalia mdomo wake ambao ulikuwa umechwa sehemu ya chini na mtoto Jessica.
Mara helicopter ilikuwa juu ya anga ikitafuta sehemu nzuri ya kutua na ndipo Robinson alipoinuka na kupunga mkono juu kuwaonesha sehemu walipo na kisha kuongoza upande ambao ulikuwa na uwazi mkubwa na huko akamjulisha Santana kunafaa kwa kutua ndipo ndege ilielekea huko na kutua. Haraka sana hakukua na muda wa kupoteza walianza kuwapakia wakina Tom, mzee Bruno pamoja na Melissa kwenye ndege kisha Wakavalia maski maalum tofauti na zile za nguo ambazo walivaa wakina Robinson wakati wakivamia na kisha wakaingia ndani na kuwabeba wakina Jackline na wenzake wakina Jessica na Jasmine na kuwapakia ndegeni kisha Santana alirudi kwenye ile nyumba akakagua mazingira ya ile nyumba hasa pale sebuleni na kukutana na vilivyokuwa vimeharibiwa na chini kulikuwa na simu moja aliiangalia ile simu ambayo ilikuwa ikifunguliwa na password maalum akaona haina maana akaachana nayo na kisha kutoka na kufunga milango na kuzama kwenye ndege (helicopter) ikaondoka eneo hilo.
"Mnapokuwa kwenye oparesheni kama hizi mnatakiwa kuwa makini hasa kwenye vifaa vyenu msiende kinyume na maelekezo."
"Nimekupata bosi wakati mwingine hilo haliwezi jirudia."
"Na huo mdomo vipi?"
"Ndiyo sababu ya Tom kurusha lile kopo la sumu ni mara baada ya mimi kutaitiwa na huyu Jessica."
"Yaani hawa viumbe huwa hawakati tamaa mapema usije ukashangaa fahamu zikiwarejea tu wanalianzisha."
"Ni kweli kabisa tunatakiwa kuwa nao makini sana."
"Yaani pamoja na kuwa katika hali hiyo watatakiwa kuwa kwenye chumba maalum chini ya ardhi ambako hata Jasmine hajawahi fika na miguu na mikono yao ikiwa kwenye minyororo bab'kubwa na si hiyo."
"Sawa Sawa mkuu."
Baada ya dakika kadhaa hivi helicopter lilikuwa limeinamisha pua likinusa eneo lake la kujidai ndani ya Ngome ya mtu mzima Santana na kisha ilitua.
"Leteni gari ya gari hapa."
Santana aliagiza gari iletwe ili wawachukue wagonjwa na kuwapeleka kwenye vyumba maalum ambako wataanza matibabu.
"Hao kenge wapelekeni kwanza kwenye kile chumba cha barafu kwanza wakaipate freshi wanaweza kuwa wanazuga wamezirai kumbe wanatuchora tu na wakina Bruno kwenye zahanati yetu kwa matibabu."
"Bosi huyu Jessica anajeraha mguuni alilopigwa na mzee Bruno Gautier."
Robinson alimwambia Santana ambaye alionekana kuwa na furaha kidogo baada ya kuwanasa wabaya wake ambao aliamini watainuka ndani ya masaa kadhaa ili zoezi la kuwacharanga lianze mara moja.
" Si muhimu sana achana naye shida yangu si mguu mimi ninahitaji moyo, figo muhimu kwanza vingine ni kwa maelekezo ya mteja kama na Ngozi watahitaji au la."
Basi Robinson aliondoka baada ya kujibiwa vile na Santana akaelekea Kantini sehemu ambayo wafanyakazi wa Santana hupumzika kwa bata lao fulani baada ya kazi hasa ile ambayo huwa matokeo chanya.
JE, NINI KITAENDELEA?
TUKUTANE TENA KATIKA SEHEMU INAYOFUATA YA HADITHI HII.
"Mkuu wakina Tom wamezinduka tayari ila utafikiri akili hazijakaa sawa wanaongeaongea hovyo tu."
Robinson alileta taarifa kwa Santana za kuzinduka kwa mzee Bruno na Tom huku Melissa akiwa bado kazirai.
"Jambo jema hilo Robinson japo furaha yangu itaongezeka baada ya kumuona Jessica, Jasmine na Jackline wakizinduka na mimi kuwaandalia tafrija kubwa kabla ya kukutana na mauti yao ambayo nimepanga kuyatekeleza kwenye kisiwa cha kitalii cha Marajo. Nikiwa kule nitaifanya kazi yangu vizuri sana kulingana na utulivu wa kisiwa hicho."
"Mkuu ni kumuomba Mungu waamke kwanza mengine ndiyo yafuate sababu kupanga mipango ambayo wahusika wenyewe ni nusu wafu ni kazi bure."
Robinson wewe hujui kitu hata kidogo juu ya hii biashara na ukija tambua utakuwa mshirika wangu mkubwa sana kwani nimesikia huko kwenu Tanzania watu wanapenda sana kutoka nje ya nchi."
"Sana tena huamini kuwa mtu akitoka nje ya nchi huyo tayari amepasua kimaisha na hiyo ndiyo ambayo ilinifanya na mimi kutokaa kiboya huku ili hata ninaporudi nyumbani wanione kama bilionea fulani hivi."
"Sikiliza Robinson siyo kama bilionea wewe tayari ni bilionea na si bilionea tu bali ni tirionea mtarajiwa kwani akaunti yako mpaka sasa ina zaidi ya dollar milioni mbili ambazo kwa hela ya kwenu inakwenda zaidi ya shilingi milioni mia nne na ushenzi juu hapo ni mwanzo tu na hata tukiikosa hela ya hawa vimburu wako si mbaya tutakwenda kwenu Tanzania na kuanzisha Kituo cha Sanaa na micheza hapo tutazalisha vipaji vingi sana ambavyo kupitia kampuni yetu tutakuwa tunawatafutia nafasi kwenye platform za kimataifa kama ni wachezaji kwenye vituo vya michezo vya timu kubwa duniani na kwa wale wenye vipaji vingine tunatafanya hivyo hivyo na hii itatufanya sisi kujizolea umaarufu barani Afrika na kwa kupitia humo humo tutakuwa tunawateka mmoja mmoja na kumtoa viungo na kuviuza nchini India na China katika hili tutawatumia wataalamu wetu kwenye masuala ya utekaji hakuna ambaye atatushtukia."
"Mkuu una mipango mingi ila itakuwa nzuri hiyo iwapo hawa viumbe watakufa lakini wakiwa hai kila jambo letu litakuwa likigonga mwamba kutokana na haya wanayokutana nayo yatazalisha visasi."
"Hapo umenena kabla ya yote tutatakiwa kuutengeneza uongo ambao tutauuza Mitandaoni utakaoelezea kijana mmoja kutoka Chunya huko aliyerubuniwa na binti mmoja aitwaye Jackline akijidai ni mpenzi wake na kumshawishi waende Brazil kimasomo kumbe ilikuwa ni janja ya binti huyo kwenda kumuuza kwa mazungu ya unga, lakini kama bahati kijana huyo aitwaye Robinson aliokolewa na kijana wa Kibrazil ambaye ni mvuvi kutoka kwenye mikono ya hao wauza madawa ya kulevya ambao walikuwa wameshamnunua."
"Ni bonge la mkakati huu na kwa Tanzania niwajuavyo pindi wakiusoma na kuuona kwenye television mbalimbali zikirusha hili hakuna ambaye atamuamini Jackline zaidi ya kumfukuza kila huku sisi tukiendelea kuchanua kiuchumi."
"Ndicho ninachokiplani kichwani kwangu kwa baadaye ila kwa kuanzia unatakiwa uingie darasani kuongeza ujuzi zaidi ili tukianza mambo yetu tuyaendeshe kisomi zaidi tofauti na mzee Bruno ambaye kwenye mradi wetu wa kokoto hutumia nguvu zaidi kuuendesha na ndiyo maana hasara hutuandama kila mwaka."
"Tuombe Mungu mkuu kila kitu kitakwenda tu."
"Naombea iwe hivyo na mimi pia."
Santana aliongea kwa kirefu na Robinson juu ya mikakati yake ya baadaye na katika maongezi yao Robinson alikuwa akimuangalia sana usoni kama vile kuna kitu alikuwa anakiangalia lakini wapi ilikuwa ni kumuona vizuri mtu ambaye ni tishio nchini Brazil na nchi jirani lakini kutokana na maongezi yao ndipo Robinson alipobaini kuwa Santana si mtu wa kutisha sana ila tu nguvu ya pesa ndiyo ambayo humpa jeuri kufanya chochote anachojisikia.
Walielekea mpaka zahanati kuwaangalia wakina Melissa, Tom na mzee Bruno ambao walikuwa wamefumbua macho tatizo lilibakia kwenye utimamu wa akili.
"Daktari nipe ripoti yao isemaje?"
Santana alianza baada ya kumkuta Daktari akiendelea kuwafanyia tiba.
"Kwa sasa kama unavyowaona wanaendelea vizuri sana isipokuwa tu tumewadunga sindano za usingizi ili kukamilisha kazi yetu maana walianza vurugu."
"Okay sawa daktari lakini watakuwa sawa baada ya muda gani?"
"Nadhani itakuwa baada ya masaa saba."
"Jitahidi sana mtaalam wangu maana hawa watu nawategemea sana."
"Bosi naomba tuamini katika hili."
"Okay daktari sisi tukuache uendelee na shughuli zako."
"Nashukuru pia bosi wangu."
Santana aliondoka na timu yake mpaka kule chini ambako walikuwa wamewekwa wakina Jackline, Jasmine na Jessica.
Baada ya kuingia Santana alipita kwenye kila kitanda kuwaangalia na alipokifikia kitanda cha Jasmine alitulia kidogo na kuanza kumkagua sijui alikuwa anahakiki kitu gani?
"Mshenzi wewe nilikupenda sana na hakuna kiumbe yeyote mwenye jinsi yako chini jua aliyewahi kuuteka moyo na kuuchezea atakavyo kama wewe Jasmine, kitu kidogo tu kilikufanya unichukie na kuingia kwenye maisha ya mateso kama kama haya lakini nakuapia Jasmine mwisho wako utakuwa mbaya sana na sijui kama unalitambua, kuongea huwezi lakini najua unanisikia vizuri sana na kwa kile mlichowafanyia vijana wangu kwa kuwaua bila huruma hamjui ni kwa namna gani mliugusa moyo wangu mpaka kufikia hatua ya kula kiapo kuwa nitawakamata na kuwaua taratibu ili muweze kuyalipia maumivu yao." Aliondoka na kukisogelea kitanda cha Jackline baada ya kufika alimuangalia sana machoni na mikononi.
" Kwa urembo huu ulionao na mikono laini kama hili uliwashinda vipi maadui zako wewe? Au ni mzimu?
Lakini nikuhakikishie kuwa tamati yako imewadia tayari naomba ujiandae tu kwa hilo."
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment