Search This Blog

Thursday 23 March 2023

ZAWADI TOKA IKULU - 4

 

Simulizi : Zawadi Toka Ikulu

Sehemu Ya : Nne (4)

“vipi Jesca mbona usumbufu rafiki yangu?”


“Usinichukie Jamie najua umeumia sana juu ya tarifa nilizokupa, najua umechukia kuliko kawaida kumbuka haya yote sikuyapanga mimi ni tofauti zetu na kukosekana kwa mawasiliano na ushahidi wa kutosha ndo kilichotufikisha yatokee haya”


“najua Jesca lakini ukashindwa kweli kunisubiri japo dakika moja tu…. Yani moja tu mpenzi yangu” niliongea kwa kwikwi huku machozi yakinitoka.


“Nikweli inauma na naweza kusema nibora kungekuwa na mawasiliano lakini ujinga wangu wakutokukusikiliza ona sasa naumia mwenzio nitaiweka wapi mimi sura yangu, nitamueleza nini mimi baba yangu mpaka akanielewa, huu ni mtihani na najuta kukutenda mpenzi wangu.”


“No!... usiseme hivyo Jesca wangu hakuna aliyejua nini kinaendelea katika maisha yetu.”


“nikweli Jamie mimi ndo chanzo ningekusikiliza haya yote yasingetokea ona sasa nilijifanya mwenye hasira na leo ona ninakupoteza mpenzi wangu inaniuma sana mme wangu niliyekutarajia, leo sina haki yakukupata tena?”


“Nakuomba mpenzi wangu, nakuomba tafadhali haya yamesha pita tafadhari acha kulia, acha kulaumu Mungu atakusaidia hata huyo uliyempata atakuwa mme mwema kwako, naamini mnapendana na Mungu atawasimamia” najua nilikuwa ninaumia kuliko kawaida ila sikuwa na budi kumpa moyo.


Mazungumzo yetu yalitawaliwa na vilio hayakuwa mazuri, ila uchungu kwa kila mmoja wetu, Jesca ilimuuma sana kunipoteza na hata mimi iliniuma sana kumpoteza. Kulingana na vilio kutawala mazungumzo yetu hayakudumu ,yalishindikana na vilio vikashika nafasi. Hakuna aliyekumbuka kuzima simu iliendelea kuwa hewani, huku tukiendelea kulia kwa uchungu hakuna aliefurahishwa na kilichokuwa kikiendelea kati yetu. Naamini kila mtu alitamani penzi letu lirejee lakini haikuwa kazi rahisi.


Nilimuomba Jesca avunje uhusiano, alikataa na akautaja ugumu wa kuvunja uhusiano huo na nilimuelewa maana kulikuwa na ugumu na ulikuwa ni ugumu kweli. Jesca aliniambia ameingia kwenye mahusiano na mtoto wa kiongozi wa zamani wa nchi hii ambaye amewahi kuitumikia kama waziri mkuu miaka ya zamani na sasa ni bilionea Kenedy Gao mtoto wake ajulikanaye kwa jina la Pius Von Gao ndiye hasa alitaka kumuoa Jesca.


Von Gao alipomuona alimtuma baba yake nyumbani kwao Jesca kulingana na ukaribu uliokuwepo kati yake na baba yake Jesca ilikuwa rahisi sana kushawishika na kujikuta akiingia kwenye mahusiano. Kulingana na kuwa yuko single kwa kipindi hicho hakuona sababu ya kumuangusha baba yake alikubali. Ukaribu wa familia zao ndiyo uliolirahisisha swala hili na pia Jesca alikuwa akitafuta furaha na aliamini huenda Von Gao anaweza kutoa furaha kubwa kwa Jesca.


Mazungumzo yaliyofanyika kutoka pande zote mbili yalifikia mwisho na makualiano ya mahali yalifikiwa. Jesca alitolewa mahali kimyakimya. Nihadithi aliyonisimulia na iliniumiza mno, aliendelea kusema kuwa “Von Gao ni mtu ambaye haishi hapa nchini na siwezi kusema kuwa namfahamu kiundani zaidi ya kumjua juu juu tu.


Niliamua kuolewa tu kwasababu nilijua umeniumiza na niliamini sina mpenzi kwa wakati huu. Jamie umerejea na wewe ndiye mtu pekee katika maisha yangu niliekuchagua na kukulidhia bila shuruti uwe mpenzi wangu naamini Mungu alikuwa na maksudi nasisi lakini huenda nimeharibu, na ninaamini nimevuruga.


Natamani kuurudisha moyo wangu lakini kunakitanzi kimening’inizwa mbele yangu. Nitamueleza nini baba yangu na nitaipokeaje hali hii, mbaya zaidi nilikubali kwa hiali yangu sasa itakuwaje na nitawashawishi vipi wazazi wangu kuliahilisha zoezi hili.


Naamini siyo kitu kidogo hili ni tatizo kubwa na utatuzi wake unahitaji busara wala siyo nguvu. Niliamini ukitumia nguvu unaweza kuharibu kila kitu.” Nikweli alikuwa na kitanzi shingoni familia ya Rais ni familia mashuhuri mno, kuvunja uchumba ambao tayari wazazi wameshiriki kwa asilimia miamoja na mhusika alikubali itakuwa ni skendo kubwa kuwahi kutokea. Kwa unyonge niliamini hapa sina changu na nilikuwa mpole na kukubaliana na maelezo.


Ilikuwa ni siku ya Jumamosi nilifika ofisini kwangu majira ya saa mbili asubuhi mitaa ya Karuta Katikati ya jiji la Mwanza hapa ndipo yalikuwa makao makuu ya Himaya ChapaKazi niliegesha gari langu na nilipo ingia ndani mapokezi nilimkuta msichana mrembo kajiinamia nilimsogerea maana alikuwa peke yake.


Nilimgusa alipoinua uso alikuwa ni Jesca Manguli kwanza nilishituka maana ni kitu amabacho sikukitarajia kabisa. Nilimwinua na kumkumbatia kwa nguvu alikuwa akilia na nilipomkumbatia alilia kwa nguvu kiasi kwamba wafanyakazi wangu baadhi walitoka ofisini wakitaka kujua nini kinaendelea.


Kwa kifupi sikuona kama ni hali nzuri kuwepo pale nilijikaza nikamshika mkono, Jesca nikamuingiza kwenye gari sikutaka mazungumzo naye niliwasha gari na safari ilielekea nyumbani kwangu Isamilo ambako nimehamia hivi karibuni baada ya kununua nyumba karibu na kituo cha utafiti wa magonjwa ya mifugo na binadamu. Nilimkaribisha ndani ya jengo langu la kifahali nilililinunua toka kwa mmiliki wake wa awali shirika la Care international na ilikuwa ni nyumba ya mkurugenzi wa shirika hili nchini Tanzania ambaye alihamisha makazi yake hapa jijini.


Nilimkaribisha nyumabani kwangu baada ya kufika, alikuwa akishangaa na sikujua kama anashangaa uzuri wa nyumba au ubaya wa nyumba maana Ikulu ni pazuri kuliko kwangu sasa alikuwa akishangaa nini. Naamini nilijitahidi kwa kiwango changu lakini sikuweza kuufikia uwezo na uzuri wa jengo la Ikulu. Tulipita mpaka ndani na tulipofika sebuleni tulikumbatiana na kubusu, nilikuwa nimemkubuka kwelikweli na naamini hata yeye kanikumbuka.


Hakukuwa na mazungumzo kwani Jesca aliniomba nifunge mlango na kwenda kujipumzisha chumbani kwani alikuwa kachoka sana. Nilifanya hivyo nilifunga milango na kumpeleka chumbani. Baada ya kufika chumbani alinirukia na kuanza kupata denda kilichofuata baada ya hapo ni mabusu na hatimayae nguo zilitupwa pembeni na mahaba mazito yalifuata asubuhi ile.


Ilikuwa yapata saa saba mchana nilikuwa jikoni nikiandaa chakula na nilipokamilisha nilienda chumbani kwangu nikamkuta Jesca kajilaza na usingizi ulikuwa umemkamata vilivyo.


Sura nzuri, uso wa upole wenye ngozi laini na macho yaliyokuwa yamepambwa vyema kwa nyusi na kope zenye mvuto ulimfanya Jesca azidi kuonekana mrembo na kunivutia kila wakati. Kulingana na umhimu wake sikuona haja yakumwamsha Jesca. Niliandaa chakula hukohuko chumbani na siku hiyo nilimwandalia chakula kizuri na niliamini atakipenda.


Baada ya kukamilisha kuandaa nilimwamsha na kumuomba akaoge, alionekana kuchoka sana hivyo nilimpa msaada mpaka bafuni alipofika nilimsaidia kufungua taulo na kumuweka kwenye thinki la kuogea. Nilifungua maji na nikaanza kumwosha naweza kusema Jesca alikuwa na furaha muda wote baada ya kumaliza kuoga, nilimpeleka kwenye kioo cha kujilemba alijiremba kadri alivyoweza na alipokamilisha nilimkaribisha mezani kwa chakula.


Nilikua nimeandaa chakula kuku aliyekaangwa vizuri na ndizi wakuchoma, kachumbari na matunda yakutosha, pembeni kulikuwa na chupa ya mvinyo. Tulikula kwa furaha na jesca akakifurahia chakula alichokula mpaka kusaza.


“kwanza kwako pazuri nimepapenda ni pazuri mno, hebu niambie umepanga au nyumba yako?”


“ni nyumba yangu nimeinunua hivi karibuni”


“wow! Umejuaje kama ninahamu na kuku leo, nahii kachumbari harufu yake tu inanitia wazimu”


“haha nimeamua leo nikupikie mwenyewe”


“usiniambie unamaanisha umepika wewe?”


“ndiyo nimekupikia wewe ule chakula kitaamu mpenzi wangu”


“No “J” usiniambie wewe ndiye umepika hiki chakula…. Si kwa utamu huu utakuwa umenunua hotelini”


“nimepika na kama huamini usiku pia nakupikia”


Wote tualiangua kicheko, pamoja na kwamba nilikuwa nimepika mimi chakula kilikuwa kitamu mno kilivutia na kila mmoja wetu alikipenda. Na baada ya kila mmoja kushiba Jesca alichukua vyombo na kwenda kuosha. Nilimzuia lakini alilazimisha nilimuacha akaosha vyombo na kufanya usafi ndani.


Mnamo saa tisa alasiri nilipigiwa simu nilihitajika ofisini, sikuwa na budi kumuacha mgeni wangu nilimuaga akaniruhusu nikaondoka kwenda kushughulikia maswala ya kazi. Nikiwa njiani nilianza kuwaza mengi sana juu ya maisha yangu na ujio wa Jesca nyumbani kwangu.


Nilifika nikakamilisha shughuli iliyonipeleka na kugeuza nyumbani, nilipita supermarket ya Uturn kuchukua baadhi ya bidhaa na nilipokamilisha nilishika barabara ya kuelekea nyumbani. Ndani kwangu kuligeuka na kuwa pazuri ghafla ndani ya muda mfupi, mpangilio ni mzuri na muonekano wa makochi ulikuwa mzuri zaidi.


Nilipokelewa vizuri sana nyumbani kwangu Jesca Manguli alipendeza sana tu kuwa mama mwenye nyumba katika himaya yangu lakini Jesca ni mke wa mtu mtarajiwa. Nilipokuwa nikifika hapo roho iliniuma marambili.


Usiku wa siku hiyo Jesca alidai anahamu na samaki wakuchoma niliamua kumpeleka Tai five hotel maeneo ya kirumba, ambako tulipata samaki wa kuchoma wa kila aina na waliochomwa kwa mitindo tofauti. Mlo wa usiku tuliukamilishia huko huku tukisindikizwa na mziki mtamu na mwanana.


Majira ya saa mbili tulikuwa nyumbani kwangu sebuleni tumejipumzisha na sasa huu ulikuwa ni muda mwafaka wa kuzungumza.


“Jesca unadhani tufanyeje juu ya haya maisha, maana hatujaongea nimekupokea tu na sijajua unataka kunieleza nini”


“nikweli Jamie nimeamua kuja ili tuzungumze, sikotayari kuolewa na Von Gao wakati ninakuona kipenzi changu, lakini kwa hili najua wazazi wangu hawatanielewa”


“unadhani huu ni uamzi sahihi kama unajua wazi kuwa wazazi hawatakuelewa?”


“sijui itakuwaje lakini sikotayari kukupoteza Jamie, nimetoka nyumbani leo saa kumi na mbili asubuhi nimedanganya nakwenda Geita kwenye kikao nitakuwepo hapa kwako kwa siku tatu. Jamie nakupenda na ninakuheshimu mpenzi wangu tusahau yaliyopita hebu tuanze moja mpenzi wangu kipenzi na tufikirie namna bora ya kulirejesha penzi letu”.


“Jesca tafadhali usinitafutie matatizo unanijua sina mbele wala nyuma ndo napigana kujikomboa kimaisha sasa ukitumia force utaniumiza mpenzi wangu.”


“Sijaja kukuumiza nimekuja kukupa neema nilikukumbuka acha tufurahi pamoja”. Nyumba yenye furaha, tabasamu na upendo wa dhati naweza kusema ndiyo nyumba bora kuliko muonekano wa majengo samani na mvuto wa nakshi. Nyumba yangu sasa ilikuwa na upendo wa dhati na furaha kutoka mioyoni mwetu.


Maisha ya furaha na chungu ndani yake yalikuwa yakinisakama, nilifurahi kuwa na Jesca nyumbani kwangu ila nilikuwa sina furaha nilipowaza juu ya maisha yangu. Nampenda Jesca ila sina furaha na maisha tuliyoishi, nilijiuliza tutaendelea kuishi hivi mpaka lini. Hitaji langu ni kumwoa Jesca na siyo kupunguza tamaa za mwiili.


Nilimpenda sana ila roho yangu ilikuwa inaniuma sana, katika maisha yangu sikutegemea hata sikumoja kuwa nitakuja kuishi kwa maumivu. Kila nilipomuangalia Jesca roho ilizidi kuniuma.


Usiku wa siku hiyo kulikuwa na mazungumzo mazito yaliyoanza na utani na hatimaye yalizalisha utata na baadae kuleta mgogoro uliokuwa hivi ambao pia uliumiza moyo wangu.


“Jamie staolewa na Von Gao, nikama natania lakini ninaamini wewe pekee ndiye furaha yangu nitafanya kila niwezalo kuhakikisha hii ndoa haifungwi”


“utafanya nini mpaka kumshawishi baba kukubaliana na ombi lako, ambapo walikuuluiza toka nawali ukawakubalia kuwa utaolewa?”


“ni rahisi mno nilikuja huku kukamilisha hilo, nilikuja kwako kuhakikisha kama bado unanihitaji na niamehakikisha bado unanipenda na unanihitaji niwe wako, yaliyobaki yaache kwangu nitamaliza”


“hapana Jesca mimi ni mdogo sana kiuwezo, kiumri na hata nguvu, siwezi kupambana na mzazi wako na hata siwezi kupambana na mkwewe mtarajiwa mzee Gao,hawa watu wana pesa, wana nguvu, wana ushawishi wakufanya lolote katika taifa hili na kufanya chochote kwangu”


“ni kweli lakini kumbuka mapenzi hayalazimishwi, mimi nakuhitaji wewe na naamini utanioa kabla Von Gao hajanioa”


“unamanisha nini kusema hivyo Jesca?”


“ndani ya miezi michache utaelewa ninachokizungumza”


“Niambie unamanisha nini ili nikae nikijua, Jesca kesho ukiondoka nyumbani kwangu tafadhari usirudi, nakuomba usirudi ninaona nia yako juu yangu siyo nzuri na mimi siko tayari kupapana na serikali, siko tayari kupambana na mzee Manguli, baba yako ni rais wa nchi hii, kutaka kupambana naye uwezo huo sina tafadhari ya thamini maisha yangu”


“kwahiyo hutaki tena nikanyage nyumbani kwako?”


“Hicho ndicho ninachokimaanisha Jesca nakupenda ila kwa hatua iliyopo bora iwe hivyo”


“sawa kumbuka nakupenda ndiyomaana niko hapa kwako leo, usingeniona nahangaika kwa ajili yako, lakini kumbe thamani yangu hujaiona?”


“staki matatizo nakwambia Jesca, hujui tu yaliyonikuta mwanzo leo tena nirudi huko? Hapana!”


“Naondoka na ukae ukijua nakupenda sana, staolewa mpaka utakapo nihitaji sawa Jamie, endelea kunichukia ukinihitaji utakuja, hutaki kuniona kwako, umesema ninaondoka sasa hivi na stalala hapa wala Mwanza nitalala nyumbani Dar Es Salaam. Ndege zipo nitakodi usiku huu baki salama mpenzi wangu”


Jesca ni kama alikuwa anatania, alinyanyuka na kuondoka, sikuwa na lakufanya aliondoka akiwa amechukia usiku ule bila kujali chochote, sikuwa na lakufanya aliondoka na alikuwa kakasirika................


Kuna mapito mengi katika dunia hii na mmoja ya watu wanao kabiliana nayo ni mimi Jamie Justine. Kuishi kwingi kuona mengi na ili uishi vyema kutana na watu. Nilikuwa nimeingia kwenye matatizo makubwa, kwani uhusiano wangu na Jesca ulikuwa ukizidi kuharibika kila kukicha na kuukamilisha usemi wangu wa kila siku kuwa kamwe stokaa niwe na furaha ya mapenzi na nikapata furaha maishani mwangu.


Jesca Manguli aliondoka nyumbani kwangu usiku na mpaka sasa hapatikani, najaribu kumtafuta kifupi hakupatikana. Huwa hakuna njia mbadala ya kumpata Jesca asipopatikana kwenye simu basi usitegemee kumpata kwa njia nyingine na hufanya hivi kwa sababu za kiusalama.


Niliamua kulidhika na kuendelea na maisha yangu. Jamie, nilijua katika maisha yangu hakuna muujiza utatokea juu ya kumuoa Jesca mwana wa rais maana tayari alikuwa amechumbiwa na Von Gao mtoto wa waziri mkuu wa zamani na bilionea mkubwa ndani ya taifa hili na mbaya zaidi taratibu za harusi yao zilikuwa zikiendelea kimyakimya.


*********************


Jesca hakuwa na furaha nyumbani kwao huko Ikulu, alionekana akiwa amejilaza na maskitiko kila kukicha hakuwa tayari kulikosa penzi langu kwa sababu ya mkataba wa mahali ambao familia yake iliingi na familia ya Mzee Gao. Asubuhi mchana na jioni kilikuwa ni kilio majonzi na hakuwa na amani muda wote tangu ametoka kwangu.


Katika imani yake daima aliamini ipo siku dunia itamuelewa na kukielewa anachokifanya. Mapenzi yalimutia wazimu na kumfanya achanganyikiwe na hata kujiona hana haki katika jamii hii ya kitanzania. Kulingana na hali ya binti yake kuwa ya ukiwa mama mzazi wa Jesca ambaye ni mke wa rais Manguli aliamua kuliingilia kati swala hilo baada ya kupokea malalamiko ya mgomo wa chakula kwa siku ya pili mfululizo kutoka kwa wafanyakazi. Mama aliamua kwenda mwenyewe chumbani kwa mwanae.


“mwanangu umeamkaje?”


“siko vizuri mama nayachukia haya maisha, kwanini iwe kwangu tu, kwanini mimi?”


“unamaanisha nini binti yangu?”


“wewe ni mama yangu sina haja yakukuficha ni mapenzi… kuna mtu ninampenda toka zamani nampenda ila anaitesa nafsi yangu”


“una maanisha Von Gao ameanza usumbufu kabla hata hamjafunga ndoa?”


“hapana mama yangu Von Gao hanisumbui ila pia hajali, ni mtu ambaye hajali kuhusu mapenzi, zipite sikumbili na hata wiki bila hata kukujulia hali kwake ni kawaida mfano sasa hivi ana siku tano hajapiga simu wala kutuma ujumbe wa maandishi”


“kwahiyo hilo tu ndo linalokutesa?”


“hapana mama ni Jamie… ni mwanamume pekee niliemjua na kujikuta nikimpenda kwa hiali yangu, Jamie ni chaguo langu ananipenda ila pia ninampenda sijui itakuwaje?”


“Unamaanisha nini unaposema Jamie? mwanangu inamaana unamwanaume mwingine unayempenda zaidi ya Gao? Huoni huo ni ukahaba? Hiyo tabia ya kuchanganya mabwana imeanza lini ndani ya nyumba hii, na itakuwaje iwapo baba yako atajua?”




“mama Nampenda Jamie nampenda saana na niko tayari kwa lolote lile ili tu niwe na furaha maishani, kuhusu baba sijui nitamueleza nini… Mungu wangu!”


“Jesca inamaana ulimkubalia Gao kuleta posa ilihali unamwanamume mwingine uliye na mipango naye?”


“kuna watu mama, watu wabaya walitugombanisha nikamchukia na kumuacha lakini baadae nimegundua nilimkosea na tayari nimemruhusu Gao kutoa posa”


Hakuwa na sababu ya kumficha mama yake ilimbidi amueleze kila kilichotokea kati yangu mimi na yeye tangu tumekutana siku ya kwanza mpaka leo.


Mama ilimsikitisha lakini aliahidi kuwa upande wa binti yake kwani alivutiwa na maelezo aliyopewa kuhusiana na mimi. Jesca alinipamba sana kwa mama yake juu ya kujali, kumheshimu na hata kumtunza kitu ambacho Gao hakuwa anafanya.


Tabia za Jesca zilianza kubadilika taratibu, hakuwa na mapenzi ya wazi tena kwa Gao alianza kutomjali hata akija pale nyumbani, hakupenda kuongozana naye hata kumsindikiza tu na mama alikuwa mstari wa mbele kuliunga mkono swala hilo.


Mzee Manguli na mzee Gao wao walikuwa bize kuandaa shughuli ya ndoa ya watoto wao na walitamani ndoa iwe ya kifahari na ikibidi ivunje rekodi ya kuwa ndoa nzuri na ghali zaidi kuwahi kutokea Afrika.


Kwa upande wao hawakujua kuwa mahusiano ya watoto wao yalikuwa yakidolola kila kukicha maana imefikia mahala Jesca hapokei kabisa simu za Von Gao ambaye pia alikuwa akimpigiaakijisikia. Siri ya mawasiliano ilibaki kuwa ya wapenzi wenyewe na mama Jesca pekee ndiye aliijua lakini kwa upande wa Mzee Manguli na rafiki ya Gao hali ilikuwa shwali na waliamini kila kitu kinaenda poa.


Upendo hukutana na changamoto nyingi Jesca Manguli alikuwa hajalidhia kuolewa na Von Gao na maisha yake sasa yalikuwa yakisua sua hakujua nani atakuwa mtetezi wake maana alikubali kwa hiali yake kuolewa na Von Gao, sasa itakuwaje abatilishe tena na kukataa kuolewa na Gao. Kwa kifupi ilikuwa ni hesabu isiyoingia akilini mbaya zaidi ilikuwa ni ndoa ya familia mashuhuli zote mbili.


Familia ya waziri mkuu wa zamani Mzee Gao na rais wa sasa Mzee Joseph Manguli. Jesca aliwaza kila kukicha atawezaje kuukwepa huu mtego wa uchumba, atawezaje kulivunja kufuli la mahusiano alilojifunga na funguo zake kuzipoteza. Mara kwa mara alijuta na kulia lakini haukuwa msaada kwake, maana isingekuwa kazi rahisi kumshawishi Mzee Manguli ili aipokee aibu ya mwaka tena aibu ya karne kutoka kwa rafiki yake kipenzi iwapo atakubali kubatilisha posa ya vijana wao. Siri kuitunza ni mtihani lakini raha ya maisha ni kukipata ukipendacho, furaha ya maisha ya Jesca ni kuwa na Jamie na sasa inamlazimu kuingia kwenye mahusiano ambayo hakuyatarajia hali hii ilimuuma sana.


Von Gao sasa alianza kushitushwa na tabia za Jesca kwani zilizidi kumkera kila kukicha, simu hapokei na hata akifunga safari kwenda kumuona bado hakuwa tayari kuonana naye. Von Gao alikuwa akijiuliza kuna nani nyuma yake alianza kuhisi kuna mtu anaingilia penzi lake.


Kulingana na kwamba awamu hii alikuwa na muda mwingi wa kuwepo Tanzania. Aliamua kufanya utafiti ili kujua nini kinamsibu mpenzi wake na pia alitaka kujua kama kuna mtu anaingilia penzi lake na aliapa kumshikisha adabu mara tu atakapomgundua. Gao akiwa mwenye hasira kila wakati alikuwa akisonya ndani ya gari lake wakati akiondoka baada ya Jesca kugoma hata kumsindikiza.


********************************************


Maisha huwa hayanyooki siku zote nilikuwa na furaha ya pesa, furaha ya maisha mazuri kila nilichokitaka nilikipata kwa wakati lakini sikuwa na furaha ya mapenzi. Kila nilipoyawaza mapenzi nilimuwaza Jesca Manguli mtoto wa rais niliyempenda kwa dhati.


Ni mwanamke niliyempenda kwa dhati ni chaguo langu la pekee mwanamke niliyemweka moyoni ni Jesca pekee. Kuna wakati nilikosa raha na kushindwa kufanya kazi kabisa nilikuwa nikimwaza mwanamke kipenzi na furaha yangu Jesca akinililia kila mara na kujitoa kwa ajili yangu niliumia sana na sasa nilikuwa nalihitaji penzi lake la dhati, lakini nilichelewa maana siwezi kumpata na sina mawasiliano naye hali hii ilizidi kuniumiza na kunitesa kimawazo.


Natoka ofsini jioni ya siku hiyo nikiwa nimechoka nikiwa kwenye foleni ya mataa makutano ya barabara ya Nyerere na barabara ya Uturn kuna mtu aliita nilipogeuka alikuwa ni Dominic. Kwanza nilishangaa imekuwaje leo huyu mtu kunikumbuka, niliendesha gari baada ya taa kuruhusu nilivuka na kwenda kuegesha gari langu karibu na ofisi za barmedas nilimsubiri alikuwa akija haraka.


“Jamie habari kaka”


“poa inakuwaje Domi ?”


mimi niko poa ila mambo siyo mazuri”


“siyo mazuri kivipi tena?”


“nishafukuzwa kazi ndugu yangu, sina kazi hapa mjini mwenzio unavyoniona hivi nimeuza kila kitu na sina hata pakuishi Maria kanisitiri kwake naye maneno tu hayaishi. Aliletwa boss mpya anaroho mbaya kama nini usiombe ukutane naye”


“sababu ya kukufukuza ni nini?”


“Fitina kaka, watu wana roho mbaya asikwambie mtu”


“kauli ile ilinifanya nitabasamu, kumbe wafitini nao hufitinishwa?”


“Na hapa nina madeni kaka, nilijisahau mpaka nafukuzwa kazi sikuwa nimeweka akiba hata kidogo, najuta sana kaka starehe hizi zimeniponza hapa unaponiona na sina begi wala nguo yaani natembea na kila kitu.”


“kwahiyo ulikuwa unasemaje?”


“kazi ….. natafuta kazi ndugu yako, fanya mpango najua tulikwazana sana ila wanaume husameheana fanya mpango nipate kazi kaka nadhalilika mwenzio”


Niliyatafakali sana maneno ya Dominic, alikuwa anatia huruma sana kulingana na hali aliyokuwa nayo, niliyakumbuka mambo mengi aliyonifanyia lakini kama binadamu nilimuonea huruma nikajikuta nikimuahidi kazi nilimwambia aje ofisini kwangu mtaa wa Karuta kesho asubuhi.


Kama mwanaume sikuyajali yaliyotokea kati yetu na niliendelea na majukumu yangu kama mkurugenzi mtendaji wa Himaya Chapakazi. Nilimpokea kesho yake Dominic alipangiwa kazi na alianza kazi kama kibarua, niliona anafanya vizuri baadae alipandishwa cheo na Hatimaye nilimuajiri kama Afisa masoko katika Kampuni yangu. Dominic namjua, madhaifu yake pia ninayajua, niliamua kumdhibiti aachane na pombe na sitarehe na alinielewa akawa ni mtu mwema.


Kulingana na utendaji wake mzuri tulikuwa tukishauliana maswala mengi na yalileta manufaa tulipoyaweka kiutekelezaji na kiutendaji. Dominic alikuwa mtu wa kwanza kunishauri tufungue matawi ya viwanda katika nchi za Burundi na Congo DRC, tulifanya hivyo na kampuni ilizidi kukua kila kukicha tena kwa mafanikio kwani matawi haya yalikuwa yakiingiza kipato kikubwa. Dominic chini ya utawala wangu hakuwahi kukosea kunishauri na kama tulitofautiana basi ni makosa ya kibinadamu na huyu ndiye Domi niliyemjua toka awali.


Kulingana na mahusiano yetu kuwa makubwa alinishauri kuuza hisa za kampuni yangu ili kufungua milango ya uwekezaji mkubwa zaidi na kutoa fursa kwa wananchi wengine kumiliki sehemu ya mapato ya kampuni yetu nilifanya hivyo na tukapanua soko kubwa zaidi.


Manufaa ya uwepo wa Domi ndani ya kampuni yangu yalikuwa yakionekana kila kukicha, na sasa ninamuona kama rafiki wa kweli na aliyejifunza kutokana na anguko alilolipitia. Naufurahia uwepo wake na sasa niliamua kumweka karibu zaidi nilimpandisha cheo na kuwa makamu wa mkurugezi alikuwa ni msaidizi wangu na nilikuwa namlipa mshahara mnono na alifanya kazi kwa bidii na kunifanya nifurahie kila wakati. Nilikuwa nikipambana kila kukicha ili maisha yangu na yawafanyakazi wangu yawe bora maana niliamini juu ya maisha bora na maisha bora yangejengwa na unufaikaji bora wa kipato cha shughuli tulizozifanya. Sasa Himaya chapa kazi ilikuwa bora zaidi na ilizidi kuiteka Afrika hasa Afrika mashariki na kati kupitia mavazi yake yaliyobuniwa kwa ubunifu mzuri.


**********************


Mahusiano ya Von Gao na Jesca yalizidisha dosari na sasa inafikia sehemu Jesca anaishi kwa kuigiza. Mzee Manguli akiwa karibu wanakuwa kama wapenzi wanaopendana kwelikweli lakini wakiwa wao pekee yao walikuwa ni maadui wakubwa. Ni siku moja walikuwa wakizozana sebuleni Von Gao akilalamikia tabia za Jesca za kutokupokea simu na kutokumjali mpenzi wake, pia Von Gao alilalamikia kupungua kwa mapenzi na kumjali na sikuhii ndipo Jesca alipomtamkia Von Gao kuwa hamtaki. Gao alipouliza sababu aliambiwa na Jesca kuwa “mpenzi wangu amerudi na nilimpenda kwa dhati tuache tutaoana” kauli hii si tu kumshitua Von Gao bali ilimkera kuliko kawaida.


Hasira zilijidhihilisha wazi na Jesca hakuzijali maana alijua hawezi kufanya lolote. Na kweli asingethubutu kuchukua hatua ya ainayoyote alijikuta akinywea na kuanzisha mjadala.


“haya huyo unaemwita mpenzi wako anaitwa nani?” Von Gao alihoji.


“Ni Jamie Justine mkazi wa Mwanza huyu ndiye mtu ninayempenda sana na samahani kwa kutokukueleza ukweli mapema”


“Wow! Lakini siyo jina geni, kwani anajishughulisha na nini?”


“ni mfanya biashara”


“C.E.O wa Himaya ChapaKazi” Von Gao alidakia wakati Jesca akimhadithia.


“Ndiyo na naamini hata Mungu ananiona mapenzi yangu ya kweli yako kwa huyu kijana, najua ninaweza kukukwaza ila hakuna aliyekamilika katika dunia hii hivyo nisamehe” Jesca aliongea huku akitokwa machozi.


“hicho kikampuni ndicho kinakuzuzua au umaarufu ndiyo unakusumbua?” Von Gao alikejeli.


Mzee Manguli anaingia na kusalimiana na Von Gao walianza kupiga soga na Rais Manguli alikuwa akisisitiza juu ya mipango anayoendelea nayo juu ya harusi yao amabayo ingefanyika mwaka utakaofuata kwa mujibu wa ratiba waliyokubaliana. Maongezi haya hayakumfurahisha hata kidogo Jesca, ingawa alishiriki kwa shingo upande na alichangia aliposhirikishwa lakini alikuwa akifanya hivyo kuuficha ukweli, baba yake asijue kama kuna mgogoro mkubwa ingawa hatua hiyo ilikuwa ikileta mkanganyiko kwa Von Gao.


Mchezo aliokuwa anaucheza Jesca ulimkera sana Von Gao na sasa alikuwa na taarifa sahihi juu ya uwepo wa mtu aliyependwa zaidi yake. Kulingana na uwepo wa Mzee Manguli pale sebuleni kunatoa nafasi ya Jesca kumsindikiza Von Gao kitu ambacho hakikutokea kwa muda mrefu. Jesca anafanya hivi ili baba yake asijue kama kuna mgogoro.


Walitoka ndani huku wakijaribu kuyapangua baadhi ya majengo ya Ikulu kabla hawajaifikia barabara ya kulifuata geti la kutokea walikuwa wakizozana.


“Jesca kwanini unanifanyia hivi mpenzi wangu, kwanini?” Von Gao alikuwa akibwata


“unapaswa kukubaliana na maamzi yangu, nilikubali kuolewa na wewe baada ya kuwa kwenye sintofahamu mimi na mpenzi wangu, kwa sasa nitakuwa siitendei haki nafsi yangu, simtendei haki mpenzi wangu na hata jamii yangu kuona ninamuumiza tena mtu niliyemuumiza mwanzo aliponikabidhi penzi lake na moyo wake naamini ilitokea kwa bahati mbaya niache nimuoneshe na aamini kuwa ilitokea kwa bahati mbaya nampenda sana Jamie staki kujua anahali gani na anasifa zipi”


“Jesca kumbuka familia yangu haitakubali kuaibika kwa ajili yako fikiri kuhusu hilo pia kabla hujafanya maamzi, familia yangu inakila sifa yawewe kuishi na jamii ikakuheshimu kutokana na wewe kuolewa katika familia tajiri na mashuhuli ndani ya taifa letu, nakupenda na stokubali kuona nakupoteza kizembe, wewe ni wangu na kama ulikubali kuposwa nami na familia zetu zikaridhia basi amini haitatokea siku ukaniacha.”


“mapenzi hayalazimishwi na kaa ukijua hayatalazimishwa ndugu yangu, najua unatoka familia mashuhuli, inapesa, inajina lakini furaha yangu itakamilika iwapo nitafunga ndoa yangu na Jamie mtu ninaye mpenda kutoka moyoni kuhusu utajiri, jina sijui sifa…. hayo ni matokeo tu kila mtu anaweza kuyapata kuolewa na huyu kijana hilo ndilo hitaji namba moja la moyo wangu.”


“Itakuwaje baba yako akigundua, huoni kama hatakuelewa?”


“Stasubiri agundue kabla sijamjuza?”


Yalikuwa ni mazunguzo yaliyojaa hasira na chuki ndani yake kila mtu alikuwa amejaa sumu akijaribu kuutetea upande wake. Mazungumzo haya yalimchanganya Von Gao kulingana na hali ilivyokuwa ikiendelea aliona anamkosa mke aliyemtarajia na dalili hizi zilijidhihirisha kutokana na misimamo ya Jesca.


Baada ya kukatisha mazungumzo yao na kutawanyika kila mmoja akiwa na hasira Von Gao anaona njia pekee ya kutatua hili tatizo ni Kuja Jijini Mwanza anakuja kumtafuta Jamie Justine.


Van Gao hakulala nyumbani siku hiyo kulingana na hasira aliyokuwa nayo aliamua kupanda ndege majira hayo ya jioni na aliingia jijini Mwanza majira ya saa mbili usiku. Hakupata taabu kuipata sehemu ya kufikia kwani aliamua kufikia Mwanza hoteli kwani alikuwa anapapenda na pia kulikuwa na wahudumu na wafanya kazi aliofahamiana nao na kuzoeana nao toka kitambo. Mtoto wa mfanyabiashara mashuhuli mzee Gao ni kijana Von Gao amekuja kufatilia matatizo yanayomkabili yeye na mpenzi wake Jesca Manguli.


Alikuwa na hasira na Jamie akiamini kuwa Jamie ndiye chanzo cha mgogoro wa penzi lake, Jamie ndiye anaemfanya mtoto wa Rais kutokuwa karibu na Von Gao na mgogoro huu sasa unachukua sura mpya baada ya Von Gao kunifungia safari kuja Mwanza. Gao alikuwa anahasira na kiburi aliamini kuwa familia yake kuwa tajiri na kuwa na jina kubwa ndiyo kumaliza kila kitu katika ulimwengu huu. Kama alivyozoezwa na wazazi wake kila alichokitaka alikipata kwa wakati na aliamini kuwa hawezi kukosa kitu chochote katika hii dunia atakachokihitaji na aliamini hawezi kulikosa penzi la mtoto wa rais kwa sababu ya Kabwela mmoja anaejifanya ana mapenzi ya kweli.


Asubuhi nilikuja ofsini mapema niliwahi sana maana siku hiyo nilikuwa na kazi nyingi zakufanya, nilipita huku nikiwasalimia wafanyakazi wenzangu mpaka ofsini kwangu. Bila kuchelewa nilianza kukagua barua pepe zilizotumwa usiku wa siku hiyo nilianza kupitia taarifa mbali mbali za mahitaji, mapendekezo na mahitaji ya huduma. Mlango uligongwa na msaidizi wangu niilimruhusu kwa sauti.


“ingia” aliingia


“kuna mgeni anakuhitaji boss”


“oooh anaitwa nani?”


“sikumbuki vizuri ila nikama kasema anaitwa Gao” jibu hili lilinishitua kidogo jina hili ni maarufu sana kila mtu aliijua familia hii ya matajiri wa kutupwa nchini kwetu anafuata nini kwangu.


“ okey mwambie aingie” Gao aliruhusiwa”


Alipita na kuingia mpaka ofisini kwangu alifika nikamkaribisha akaketi kwa dharau lakini hali hiyo sikuijali sana maana watu wa familia za kitajiri na maarufu wanakasumba zao.


“naitwa Jamie Justine ni mkurugenzi mtendaji wa Himaya Chapakazi” nilijitambulisha huku nikimpa mkono lakini hakuupokea


“naitwa Pius Von Gao ni mtoto wa mwisho wa Waziri Mkuu wa zamani, tajiri na mtu mshuhuli hapa nchini”.


“nikusaidie nini Mr. Gao?”


“chakunisaidia huna ila nimeamua mimi kukusaidia wewe maana huna pesa yakunisaidia wala kunipa, huna lolote lakunisaidia we masikini mkubwa chakufanya, achana na Jesca Manguli.” Kauli ile ilinifurahisha kidogo.


“Jesca Manguli …. Kitambo sana bro siko naye na kama kakwambia niko naye alikuwa akiichezea akili yako”


“ninauwezo wakufanya lolote acha kujitia kiburi, naweza kukufilisi nikitaka ndani ya siku moja hautakuwa na hata senti yakununua kiberiti masikini wewe, unajiita unapesa? pesa gani hii haijai hata kwenye kikombe cha kahawa?, naweza kukuua nikitaka muda wowote ule pia naweza kukupoteza uraiani muda wowote nitakaotaka, nina pesa, ninanguvu na naweza kufanya nitakacho katika taifa hili.


"Lakini haya yote sitaki yatokee hebu achana na Jesca Manguli yule binti ni mke wangu mtarajiwa. Acha kujitia unamapenzi yakweli, acha kujitia wewe ndo kidume unayejua kuwapagawisha wapenzi wa wenzio. Kama huujui uchungu wa mke basi endelea nitakufanya uujue mapema tu na kama hautanisikia ninachokueleza hapa basi jiandae kukisikia ukiwa kwenye jeneza au kaburini.”


Alimaliza huku akifungua mlango na kuondoka zake, nilishusha pumzi na kutafakari kwa muda maana ni maneno makali yaliyosemwa mbele yangu. Staki kujua Jesca amemjibu nini huko alikotoka maana habari za Jesca nilisha malizana nazo na kuanza maisha yangu binafsi, sasa inakuwaje Jesca anasababisha nafungiwa safari ya vitisho. Staki mapenzi na sihitaji mpenzi hii ndiyo imekuwa kauli mbiu yangu lakini yanaibuka mapya tena kila kukicha.


Unaweza ukatoka nyumbani umepania kufanya jambo Fulani lakini mwingiliano wa matatizo na changamoto ukakuharibia kila kitu, naweza kusema hali yangu haikuwa sawa tena na niliona nikiendelea na kazi huenda nikaharibu. Niliingia ofisini kwa Dominic nikasingizia naumwa ili asijue nini kinaendelea, nilimwachia maagizo na mimi nikaondoka eneo lile. Baada ya kufika nyumbani kwangu, hali haikuwa nzuri nilikuwa nikivitafakari vitisho vya Von Gao kiuhalisia sikuwa tayari kujikuta naangamia kwa kosa ambalo sijashiriki.


Maranyingi watoto wa viongozi huamua mambo yao watakavyo maana huamini wameushika mkono wa dora na hakuna mtu wakuwaingilia katika maamuzi. Ninajua Von Gao anauwezo wa kufanya lolote alitakalo kwangu kwani pamoja na baba yake kumaliza muda wake kwenye uongozi, bado ana ushawishi wa kiutawala na bado familia yake inaushawishi mkubwa katika serikali na jamii kwa ujumla kutokana na umaarufu wa baba yao.


Lakini nguvu kubwa ya pesa wanauwezo wa kunizamisha muda wowote na hata kuniangamiza wakitaka. Picha iliniijia akilini nilihisi huenda nikauwawa kimyakimya na wazazi wangu wasijue wapi nimetupwa au kuzikwa.


Nilijaribu kuitafuta namba ya Jesca lakini haikupatikana, hii nayo inakuwa ni miongoni mwa siku mbaya kuwahi kunitokea hapa duniani. Siku nzima sina furaha wala chochote nilikuwa nikihangaika kutafuta ufumbuzi wa swala hili lakini kila kukicha lilichukua sura mpya.


Nilianza kujuta na majuto yangu yalikuwa juu ya kumjua Jesca kwanini nilimjua na kwanini ananifanyia hivi ilifika wakati nilitamani hata penzi la Maria maana Jesca nanipeleka kubaya. Nilijilaumu mno mpenzi wangu alikuwa akizidi kuichanganya nafsi yangu, siioni faraja ya kuachana na Jesca maana sasa si mapenzi tena maana yamefikia mahala vimegeuka vitisho na chuki. Natishwa na kuonywa kama mhalifu lakini sikuwa na mapenzi yoyote na Jesca maana kwangu mimi naamini tulishaachana na sikutegemea kama ipo siku atarudi ingawa roho ilikuwa ikiniuma kila kukicha kwa kumpoteza. Mawazo yasiyo na ufumbuzi huzalisha ugonjwa wa kichwa, uoga na kukosa amani, kichwa kinauma sana nilikunywa dawa za maumivu lakini hazikunisaidia kabisa maana niliona maumivu ndo kwanza yanazidi nikaamua kulala.


Dominic nilikuwa nimemuachia ofisi kwa siku mbili sasa, Maria ana kuja pale ofsini na kuanza kujahadiliana mambo yao ya umbea jasiri haachi asili na mimi sikuwa na hili wala lile kwa kile kilichokuwa kikiendelea ofisini kwangu.


“mmnh! Domi huyu chizi aliipata wapi hii hela yote yakujenga hiki kiwanda?”


“Du! Mimi mwenyewe nilikuwa sijui lakini aliniambia ni nyumba ya baba yake iliuzwa na hivyo baba yake akampa mtaji, ila jamaa ana akili sana aliutumia vizuri mtaji na hapa ameajiri watu wengi na nawalipa vizuri kiukweli Jamie anajituma”


“anajituma wapi zisinge kuwa juhudi zako wewe Domi angekuwa hapa? hebu acha kumpa kichwa wewe ndiye unampa dira huyo mjinga angetoa wapi hii akili bila juhudi zako? Wewe hujiulizi kwanini kakuweka hapa?”


“nikweli lakini hata mimi nanilipa vizuri pamoja na kujituma kwangu”


“anakulipa shilingi ngapi kwani?”


“ni zaidi ya kule pa mwanzo ninakula kama milioni saba kwa mwezi na marupurupu kibao”


“sasa milioni saba ndo unalingia na kumsifia kumbe na wewe hamnazo eeh!? Huoni kama anakupunja wewe si ni kaimu mkurugenzi unafanya kazi ngumu na unapitia mangapi?”


“ndiyo unachosema ni kweli”


“najua unauwezo wa kufanya chochote hasa Jamie asipokuwepo hapa ofisini wewe ndiye mwenye maamzi ya mwisho sasa endelea kulala wakati mali umekabidhiwa za bure kabisa, nitakushangaa kufa masikini na ufunguo wa sefu unao wewe. Ningekuwa mimi mbona kitambo ningekuwa nimesha hamisha changu na ikibidi nilishatimukia nchi za mbali”


“duh! Hilo nalo neno!”


*****************************


Jesca alikuwa akisumbuliwa na mawazo, Jamie Justine ni jina pekee lilliloutawala moyo wake wala alikuwa hahangaiki kuhusu Von Gao. Naweza kusema alidhamilia kuolewa na mimi maana msimamo wake ulikuwa ukijidhihilisha mbele ya mama yake mzazi na kila kukicha alitamani baba yake ajue kuhusu maamzi haya ya kubadilisha msimamo wake pamoja na kuwa familia yake ilikuwa imekwisha kupokea fedha na mali za thamani kubwa kutoka familia ya kitajiri ya Mzee Gao.


Mama Jesca hakuchoka kumtia moyo mwanae na aliamini atasimama mpaka mwisho kuhakikisha mwanaye anayashinda majaribu. Mama Jesca alitamani kumweleza mmewe juu ya hili lakini matokeo yake alijua huenda yakawa siyo mazuri maana alimjua vyema mume wake maana huwa na maamzi magumu na wakati mwingine yanaweza kuleta madhara makubwa. Tahadhari na kuihakikishia familia ya rais usalama, mama Jesca alijifanya halijui kabisa jambo hili nikama ndo kwanza analisikia kwa mara ya kwanza alikuwa akimwambia mwanawe kuwa, Jesca anaweza kwenda kumueleza baba yake ukweli lakini ahakikishe mama hahusishwi na lolote juu ya kilichokuwa kinaendelea.


Jesca anajaribu kutafakari ataanzaje kumueleza baba yake juu ya uamzi wake mpya uliofuta k wa zamani. Wakati huo Von gao anaamini kabisa kwa matusi na vitisho alivyonipa aliamini wazi kuwa penzi lake litakuwa limeimarika. Tangu arudi kutoka Mwanza ni siku ya tatu anaamua kwenda Ikulu kumuona mpenzi wake na kujua maendeleo ya Jesca lakini, lengo kuu halikuwa kumuona Jesca bali kujua kama kuna mabadiliko ya aina yoyote kwa mpenzi wake maana aliamini kunifokea huenda kungebadili mtanzamo wa Jesca. Alifika na kupokelewa vizuri na wafanya kazi na aliomba kuonana na Jesca lakini haikuwezekana Jesca aliendelea kuwa na msimamo wake hakumhitaji tena Von Gao mtu aliyekuwa akilazimisha mapenzi kwa nguvu na sasa penzi lake alilielekeza kwangu ingawa hakukuwa na mawasiliano yoyote kati yetu. Von Gao alijawa na hasira maana aliamini tunawasiliana mimi na Jesca na baada ya Jesca kuendelea kumkazia sasa anagundua kuwa bado ninamtia kiburi, alijua kuwa sijakielewa alichoniambia na hapo ndipo hasira zilimpanda mithili ya mbogo aliyekoswa risasi.


Alikuwa sebuleni akijitathimini jinsi anavyodhalilika ukweni na hapo ndipo anagundua yeye hana thamani kwa Jesca kwa sababu yangu. “inawezekanaje Jesca anidhalilishe mimi tena hapa kwao mbele ya wafanyakazi wao namwita anakataa kuja sababu ya huyo masikini wake?” alijisemea. Von Gao alikuwa kaketi pale sebuleni kama mjinga peke yake alikuwa akijaribu kutafakari ni aibu gani hii inayompata kwa sababu ya Jamie. Alitafakari sana kama unavyojua watu wanaopenda kujikweza maranyingi huwa hawawezi kuhimili fedheha. Alinyanyuka na kuondoka zake, huku akizungumza peke yake nadhani hata yeye ukimuuliza alizungumza nini asingekujibu.


Alifika nyumbani na kutafakari kwa kina juu ya hatima ya maisha yake na sasa anaamua kufanya maamzi magumu ambayo hakutarajia kuyafanya, lakini kulingana na hali aliyokumbana nayo Von Gao anajikuta akichukua simu na kumtafuta mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Evarist Kimbo.


Kimbo ni mtu hatari sana naweza kumuita hivyo ana umri wa makamo ni kama umri wa miaka 38, kazi zake huwa hazieleweki kwani amewahi kuitumikia serikali na huenda bado anaitumikia maana haeleweki anafanya nini huyu mtu. Inasemekana ni mtu hatari sana hasa akitumwa kukufatilia maranyingi Kimbo ni mtu wa mwisho kwa watu walioshindikana kufatiliwa, ukimwona Kimbo anakufatilia jua wewe ni mtu sugu na hatari.


Na kama huna sifa hizo na Kimbo katumwa kwako basi Maisha yako yako hatarini. Kimbo amekuwa akiagizwa na serikali pamoja na viongozi mashuhuri katika kutekeleza shughuli zao hasa za kumpoteza mtu anayewasumbua. Katika historia inasemekana amepoteza watu wengi muno mashuhuli na watu wakawaida, ukikutana na Kimbo ukapona basi sali sana maana Mungu bado anakupenda. Von Gao kitu alichokuwa akihitaji kukizungumza na Kimbo hakikutakiwa kuzungumzwa kwenye simu hivyo alimuomba wakutane sehemu na Kimbo alikubaliana na wito huo Huku Von Gao akikata simu na kushusha pumzi kwa hasira.

Mzee Manguli alikuwa keketi sebleni baada ya kutoka safari katika mkoa wa jilani alikokwenda kutekeleza majukumu yake yakiserikali. Mzee Manguli alimpenda sana binti yake na sasa alikuwa hajaonana naye siku nzima. Alimuagiza mfanyakazi wake mmoja amuite Jesca maana alitaka kuonana naye.

“oooh binti yangu naona unazidi kupendeza mama”

“ahsante baba shikamoo”

“marihabaaa, mimi sijambo ni majukumu tu maana hapa tunasiku kama mbili hatujaonana mwanangu”

“nikweli baba pole nimekuona ukihutubia kwenye Runinga mkoa wa jilani na hujaniaga leo asubuhui baba yangu”

“nikweli ni safari ya dharula mwanangu ila shukuru nimerejea salama baba yako”

“haha mungu azidi kukujalia uzima baba”

“vipi mama Von Gaooo hajambo?”

“enh!... eeh ndiyo ha haajambo tu”

“sawa tulikuwa na maongezi na baba yake Von Gao juu ya ndoa yenu nahisi itafanyika January au February mwakani, kusema ukweli anajitolea sana huyu mzee na naamini atakuwa mkwe mzuri kwako”

“oooh! Ni vizuri”

“hahahaaa lakini mbona kama hauna furaha mama?”

“Nikweli dady kuna kitu hakiko sawa” wakati Jesca akitaka kuzungumza mama naye alikuwa anakuja pale subuleni.

“shida gani mama niambie wewe ni binti yangu pekee, na mimi ni baba yako kipenzi nitafanya lolote katika ulimwengu huu ili kuhakikisha una amani mwanangu”

“Mapenzi baba … mapenzi ya kweli baba yangu natamani niwe na furaha na niwe na amani moyoni mwangu”

“ na ndiyo maana ukamchagua kijana mtanashati, mtiifu, mfanyabiashara, musomi, anatoka familia mashuhuli na anayekupenda kwa dhati”

“nikweli lakini ninampenzi wangu sorry kwa kutokuwa mkweli, mnapaswa kuniamini kwa hili nilikuwa na mpenzi tulichonganishwa na watu nikamuacha kwa hasra but ananipenda sana baba yangu, najua nilimkosea na kwa hasra hiyohiyo nilijikuta nikikubali kuolewa na Von Gao kabla sijaujua ukweli na baada ya kuujua ukweli mimi nilijuta sana na sasa siko tayari kuolewa na Von Gao baba mnaspaswa kuliheshimu hili na muyaheshimu maamzi yangu pia.”

“ mbona unataka kutuchanganya humu ndani? Huyo kijana yuko wapi na anaitwa nani?”

“ Yuko Mwanza na anaitwa Jamae Justine.”

“usiniambie ni huyu mmiliki wa kampuni tuliyoenda wote kuizindua miezi kadhaa iliyopita?”

“Ndiyo baba ni yeye”

“inamaana kuongozana na wewe tu siku hiyo tayari umepata na mchumba? Hebu tumia akili basi usiwe mjinga”

“tunafahamiana siku nyingi saana na kama unakumbuka miaka miwili nyuma nilikuwa nasafiri saana kwenda mwanza wakati huo mahusiano yetu yakiwa yamepamba moto lakini tulifalakanishwa na watu wenye hira”

“Jesca maji umeyavulia nguo kwa hiali hakuna namna ya kuyakwepa, nazungumza kama mzazi nilikuuliza marambili ukakubali kuolewa na Von Gao, tukakupa muda bado ulileta jibu la ndiyo. Nilipokea mahali kwa hiali yako, watu wakaalikwa viongozi wakubwa wa ndani na nje ya nchi, siko tayari kuibeba aibu hii begani kwangu. Ninakuomba kwa usalama wako tu mama na ninaongea kama mzazi, rafiki yako kipenzi na pia naongea kama rais wako wa nchi hii kuwa utake utaolewa usitake utaolewa I’m done”

Mzee alinyanyuka na kwenda zake.


Ukimya ulitawala pale sebuleni na hakukuwa na mazungumzo tena Jesca alikuwa akitizamana na mama yake wasijue cha kuzungumza mzee Manguli amesha wavuruga kwa maamzi yake magumu ndani ya himaya yake. Hali ya ukimya ilitawala ikiwa imeambatana na uoga na kukosa amani.

“Hatuna Jeuri tena mwanangu unapaswa kukubaliana na maamzi ya baba yako hakuna njia nyingine”

“Siwezi mama, siwezi kuisariti nafsi yangu maana baba ananionea siko tayari kuolewa na Von Gao.”

“ni sawa lakini kumbuka ulisha mthibitishia kuwa unampenda na familia zikajiridhisha sasa kugeuka kwako kutaleta mtafaruku na kuichanganya jamii”

“najua lakini mimi ndiye niliamua na wakati mwingine maamzi hubadilika, nia yangu si kuolewa familia ya kifahali na kujulikana kila kona, natamani kuolewa na mtu atakaenipenda na kuniheshimu kama mke wake, na siyo kuwa na mtu anaetaka kukuoa ili aoneshe ufahari kwa jamii na kujigamba mbele za watu kuwa yeye ni kidume anaweza kumuoa mke yeyote amtakaye.”

Familia ya Manguli ilikuwa imeingia kwenye mgogoro mkubwa habari kubwa alikuwa ni Jamae Justine kuyavuruga mahusiano ya binti yao.




Mama anaonekana kuwa upande wa binti yake lakini anajua msimamo wa mume wake na maamzi magumu ya mumewe pale anapokosewa ingawa hayuko tayari kumuona binti yake akikosa furaha kutokana na mapenzi ya dhati aliyokuwanayo kwa mpenzi wake wa siku zote mimi Jamae.


Mama alimuonya binti yake akimwambia awe makini na maamzi yake yasije yakaleta athari ndani ya familia ya rais na kulea mtafaruku. Naweza kusema maneno yote aliyoambiwa na kuonywa kamwe hayakubadilisha azma ya binti yao kuolewa na mimi, bado alibaki na ndoto yakweli moyoni mwake kuhakikisha siku moja anafunga ndoa na mimi.


Jesca hakuwa na furaha tena alikuwa akilia kila wakati akijaribu kumbembeleza mama yake aweze kumshawishi Mzee Manguli kukubaliana na binti yake kubadilisha mawazo na kumruhusu kuvunja uchumba uliokuwa ukiendelea. Mama aliumia sana lakini alimjua vizuri mmewe najua asingeweza mfuata kwenda kumshawishi mumewe juu ya hilo aliamini huenda angehatarisha mahusiano yake ndani ya familia hiyo.


Mzee Manguli ni mtu makini sana na kawaida yake huwa hayumbishwi akiweka msimamo wake huwa hauyumbi. Mama aliamua kuwa mpole na kutii kila alichokuwa akiambiwa na mumewe. Lakini Jesca hakuchoka kumshawishi mama yake ili aweze kumpatia msaada ingawa alijua ni ngumu ila aliamini mama anaushawishi mkubwa kwa baba huenda baba akamuelewa.


Pamaoja na juhudi zote za mama kuongea na kumshauri mzee Manguli lakini vikwazo havikuisha mzee Manguli hakuwa tayari kudhalilika, hakuwa tayari kukwazana na rafiki yake Mzee Gao, hakuwa tayari kuiona heshima yake ikishushwa na mwanawe wa kumzaa, hayuko tayari kuona wanasiasa wakitumia madhaifu ya familia yake kumzungumzia na kumkejeli, Manguli hakuwa tayari kabisa kushushwa hadhi yake kwa sababu ya mahusiano ya binti yake.


Von Gao anamtuma baba yake kwenda kwa mzee Manguli kulizungumza swala la uchumba wake, wazee hawa wanakutana na kuzungumza. Makubaliano yao yalijikita katika kukwepa aibu huenda waliyatathimini mapenzi ya watoto wao lakini walijua watakaporuhusu tu kufanya ambavyo Jesca anvyotaka aibu ingekuwa yao na ingewatafuna mpaka kufa.


"Bw. Gao tusilichukulie hili swala kiurahisi, kumbuka tunagusa familia ya rais, tunaizungumzia familia ya ikulu nadhani hii inaigusa serikali moja kwa moja hivyo tunapaswa kuwa makini."


"Nikweli unachokizungumza Mh. rais nadhani tunapaswa kuwa na msimamo juu ya maamzi yetu, watoto tumewazaa wenyewe harafu watushinde kweli"


"Mzee Gao kuna kijana anayevuruga mahusiano ya hawa watoto nadhani anapaswa kupokea onyo la mapema zaidi".


Mazungumzo yaliendelea kati ya raisi Manguli na rafikia yake wa karibu mzee Gao na muafaka ukafikiwa kuwa ndoa ya Jesca na Von Gao ni lazima ifungwe.


***************************


Ni Evarist Kimbo ndani ya jijini la Mwanza mimi sikujua na nilikuwa nikiendelea na shughuli zangu, naamini alikuwa kapewa ramani yakunipata kiurahisi hivyo hakufanya kosa kulingana na maelekezo aliyoyapata. Ni majira ya saa nane mchana narudi kutoka kula chakula cha mchana nakuta taarifa ofisini kwangu kuwa kulikuwa na mtu amekuja kunitafuta na ameahidi kurudi tena. Nilitaka kupata taarifa zaidi lakini ilikuwa ngumu maana msaidizi wangu aliniambia hata yeye hamfahamu mtu huyo.


Nikama dakika tano baada ya kuketi kwenye kiti mlango ulifunguliwa na liliingia jibaba refu pande la mtu jeusi tii. Ni jamaa wa makamu na alikuwa kavaa suti nyeusi na shati jeupe lakini kapanda hewani sekunde huku kifua kikionekana kimejazia vilivyo na usoni katinga miwani mieusi.


“Habari za saahizi?” alinisalimia.


“Salama kaka karibu sana”


“Okey wewe ndiye Jamae si ndiyo?”


“Yes ndo mimi”


“Sawa, unaweza kunyanyuka taratibu maana ninakuhitaji sasa hivi”


“Wewe ni nani na kwanini unihitaji bila kuwa na taarifa?”


“Naitwa Mr. Kimbo nimekuja kukuchukua kuna mashitaka unapaswa kuyajibu”


"Mashitaka gani?"


"Hupaswi kujua"


"Ni haki yangu kujua kabla sijanyanyuka hapa nilipo"


Niliona anafungua koti lake sehemu ya kiunoni alinionesha bastora nilikuwa mpole maana ni kitu ambacho sikukitarajia alininyanyua juu taratibu, niliomba kuaga lakini hakuniruhusu. Basi nilichukuliwa kwa siri hakuna mtu aliyejua pale ofisini kama nimetekwa alinipandishwa kwenye gari na nikajikuta nafunikwa uso kwa mfuko mweusi na sikujua kilichoendelea.


Nilizinduka nikiwa ndani ya jengo kubwa lililochoka ilionesha ni jengo la muda murefu sana kutokana na muonekano wake wa kuzeeka. Ndani ya jengo hilo nilifanikiwa kuangaza huku na kule sikuona chochote lilikuwa wazi kuanzia chini mpaka juu ya paa, zaidi niliinua macho yangu kulikuwa na meza moja iliyokuwa na vitu vyenye ncha kali kama vile, visu vya aina tofauti toafauti kama vile sindano, shoka , mkuki, mkasi, visu na hata upinde na mishale.


Kulingana na hali niliyokuwa nayo naweza kusema nilikuwa tayari nimekata tamaa maana sikujua kosa langu lakini sehemu niliyokuwepo haikuwa salama. Mikononi nilifungwa mnyororo mkubwa ambao haikuwa rahisi kuukata au kuufungua mnyororo ule uliunganishwa na kiti cha chuma nilichokuwa nimeketishwa. Sikuijua azma ya Kimbo kuniweka pale nilikuwa nikiwaza sana juu ya maisha yangu na nilijuta kwanini nimekubali kirahisi kuchukuliwa kazini kwangu nilishakata tamaa.


Nikiwa kwenye dimbwi la mawazo, nilishuhudia mlango ukifunguliwa kwa ghadhabu niliinua macho alikuwa ni Kimbo alifika karibu yangu alinitungua ngumi ya kushitukiza, ilikuwa ni ngumi ya shavu aisee iliniuma balaa. Kulingana na baridi lile la asubuhi asikwambie mtu ile ngumi iliniuma balaa. Kimbo alivuta kiti na kunisogelea huku akiwa na kisu cha bapa kisu hiki sikijui jina lake ila huwa nakiona maranyingi kikitumiwa na wauza nyama kwenye maduka ya nyama alikiangalia bila kusema lolote kisha akatikisa kichwa.


"Unaweza kuniambia kwanini uko hapa?"


Hapana sijui bro, sijamdhulumu mtu, sijamuibia mtu najitahidi kuwa mwema kila kukicha sidhani kama kuna kosa nimekukosea bro."


"Unamjua Von Gao?"


"Ndiyo ninamjua"


"Basi kaniagiza hutakiwi kuwepo duniani kuanzia muda huu"


Maelezo ya kimbo yalikuwa magumu mno kuyasikiliza licha ya kuyaamini lakini yaliuchoma moyo wangu na kunifanya niishishiwe nguvu. Kimbo alikuwa akipekua siraha kwenye chombo kimoja cha shaba ambacho kilikushanya mikasi, visu sindano na hatimaye alikipata alichokuwa akikitafuta a kusimama mbele yangu. alikuwa kashika kisu na kilionekana kuwa kikali mno na sasa dakika zangu zilikuwa zinahesabika tu.


"kimbo maisha yangu yamekuwa hatarini tangu niingie kwenye mahusiano na Jesca sishangai haya yanayonipata leo kwasababu hata wewe unatekeleza ulichoagizwa tu ila hujui ndani yake kuna nini"


"Von Gao anataka kumuoa Jesca nimejitahidi kumueleza ukweli Jesca ili aachane na mimi na aimarishe mapenzi yake na Von Gao lakini imeshindikana kila siku ni vibweka tu Jesca na mimi tulishaachana kitambo , lakini mgogoro wangu na Gao unaeletwa na imani yake ya kuamini kuwa Jesca bado niko naye kwenye mahusiano." Kimbo wakati namueleza haya alikuwa kimya kwa muda kisha akauliza.


"ulimfahamu Von hapo kabla?"


"hapana "


Kimbo aliniangalia sana baada ya kunijibu, kisha alinishushia kipigo cha mbwa mwizi, naweza kusema ni kipigo changu cha kwanza kuwahi kutokea maishani mwangu. Pamoja na kuanguka na kiti pale chini bado aliendelea kushusha kipigo pale chini mithili ya mtu aliyepagawa.


Chakushangaza kipindi akinipiga Kimbo alikuwa akilia kwa hasira na baadhi ya maneno alikuwa akiyaongea niliyasikia alidai ameua watu wengi sana bila hatia. Hayuko tayari kuua tena kwasababu ya pesa. "siko tayari kuua tena maishani mwangu nilishatubu dhambi zangu ninaamini ulikuwa ni mtu wa mwisho kukuua ila Mungu bado anakupenda stakuua Jamae. Kimbo alionekana kukosa nguvu alianza kujivuta na kwenda kuegemea kwenye kona ya nyumba huku akilia kwa uchungu.


********************


Siku ya tano sijaonekana ofisini ilikuwa ni nafasi pekee kwa Dominic maana hakujua nilipo na aliponitafuta hakufanikiwa kunipata. Aliamua kukomba pesa nyingi kwenye kampuni yangu na kuzihamishia kwenye akaunti yake kisha alichoma ofisi computer zote ziliteketea na kuuharibu mfumo mzima wa tarifa katika kampuni yangu. Habari hii ilienea kwa kasi Afrika nzima na kumshitua kila mtu na hapo ndipo taarifa za kupotea kwangu zilipovuma kama upepo kwenye vyombo vya habari. Jesca anakutana na habari za kupotea kwangu alishituka kidogo alianza kufuatilia. Jesca alijua moja kwa moja kupotea kwangu lazima kunamhusisha Von Gao na alijua moja kwa moja Von atakuwa pia kahusika na kuchomwa kwa ofisi zangu za makao makuu.


Jesca alinyanyua simu kwa Von Gao na kumwambia anamhitaji nyumbani kwao mara moja na hapo ndipo Gao alijipa moyo kuwa huenda alikuwa akiitiwa suruhu ya mapenzi kati yake na Jesca.


"nimekuita hapa kwa lengo moja tu, umechoma ofisi za Jamae ninajua kwa asilimia tisini umehusika ili kumfirisi, pili Jamae anakaribia wiki sasa hajaonekana inasemekana umemteka, ninakuongezea wiki nyingine awe ameonekana tofauti na hapo tutapimana nguvu ni nani kashika dora kati ya baba yako au baba yangu na tatu sahau kuhusu ndoa na unaweza kuaondoka kuanzia sasa"


yalikuwa ni maongezi ya kibabe yaliyomchanganya Von Gao alishangazwa na kuhusishwa na taarifa za kuchomwa kwa makao makuu ya Himaya chapakazi lakini kuhusu kutekwa kwa Jamae alihusika kwa asilimia miamoja na ni yeye pekee aliyekuwa akijua Jamae alipo. kila kukicha ni picha za Jamae Justine kwenye magazeti, mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari. walitamani nionekane lakini haikuwezekana kwani nilipokuwa nimefichwa hata mimi mwenyewe sikupajua.


Kipigo naweza kusema kiliendelea kuwa haki yangu chakula na maji nilipewa kwa kiasi kidogo sana lakini namshukuru Mungu niliendelea kupumua ingawa kipigo ilikuwa ni dozi kwangu na wakati mwingine ni zaidi ya dozi. Mwili wangu ulikuwa ukiniuma mno mara kwa mara. Nilikuwa nikisikia mara kwa mara Kimbo akiwasiliana na Von Gao Kimbo alikuwa akiamlishwa aniue na Von Gao lakini alikuwa akikataa katakata kwani hakuwa tayari kufanya hivyo alikuwa akijibu kwa msimamo. " Gao siwezi kumuuwa huyu kijana maana hajakukosea na nasema mbele yake hata yeye atakuwa shahidi, najua hujui alipo nakamwe hautajua na ukijua utakuwa umekufa wewe badala yake naapa kwa jina la baba Gao malizia pesa zangu za nyuma la sivyo nitaanza kushughulika na familia yenu mwambie na baba yako kabla sijakanyaga Dar akaunti yangu iwe imenona madeni yote yalipwe mimi siyo mbwa wenu wakunitumia mtakavyo". kulikuwa na malumbano kila kukicha kati aya Von Gao na Kimbo lakini kila wakilumbana balaa hunipata mimi hasira zote za kimbo huishia kwangu kwa kichapo kikali.


Wazazi wa pande mbili wanakutana na walihitaji kufikia makubaliano ya mwisho juu ya maamzi yao kuhusu ndoa ya Jesca na Von walikuwa wakizungumza na katikati ya mazungumzo Jesca aliibuka na kuropoka kwa sauti mbele ya baba yake.


siwezi kuolewa na jambazi, siwezi kuolewa na mharifu, siwezi olewa na gaidi. Baba mwambie mwanao amuachie huru mtoto wa watu aliyemteka huko Mwanza, pili mwambie juhudi anazofanya kuteketeza mali za Jamae ni laana tosha katika maisha yake. Kumbukeni hata mkalale kwa papa mkiniombea katu siwezi kubadili mawazo yangu nikaolewa na huyo masikini wa akili."


"kaa kimya we mwendawazi, ninaongea kama baba yako na kama hapa ni kwako basi endelea kuropoka ila kama ni kwangu funga hilo tungi lako."


Mzee Manguli alikasilishwa sana na kitendo cha binti yake kuja kufoka mbele za wakwe zake na alionekana kukosa nidhamu na mbaya zaidi alionekana kuropoka maneno yaliyokera na kumkwaza kila mtu aliyekuwa eneo hilo. Si kitu kizuri kimtazamo lakini maneno yake yalikuwa na maana kubwa sana kuyatafakari lakini kulingana na ufinyu wa fikra na kutaka kulinda masilahi yao binafsi Mzee Manguli anatumia sheria binafsi ili kulinda masilahi yake.


Mazungumzo yaliendelea baada ya Jesca kuondolewa eneohilo na maamzi yalipitishwa ndoa yao ingefungwa mwezi utakaofuata ili kuepusha aibu ambayo ilikuwa mbele yao. Jesca Manguli hakulijua hili na hakujua kikao hicho kilifikia maamzi gani yeye aliendelea kuwa na mawazo mazito amabayo kamwe hayakukatika na yaliendelea kuutesa moyo wake kila kukicha maana alitamani kuolewa na mtu aliyempenda.


Von Gao alifikishiwa taarifa na mzazi wake na alianza kujiandaa kufunga ndoa na Jesca mwanzoni mwa mwezi utakao fuata na hali ya shamra shamra ilianza kushika kasi na taarifa zilianza kutapakaa kila mahali huku familia zote mbili zikiunda kamati za maandalizi ya hiyo harusi ya kifahali amabayo hata eneo itakapofanyika bado lilibaki kuwa kitendawili na hata bi harusi mtarajiwa hakuhusishwa.


Jesca anashitushwa na maandalizi ya kila aina yaliyokuwa yakiendelea nyumbani kwao ilimbidi kumuuliza mama yake na mama alimficha hakutaka kumwambia ukweli kulingana na kiapo alichokuwa amekiapa kutoka kwa mumewe, basi mandalizi yalizidi kushika kasi na tarehe zilikaribia Jesca hakujua nini kiliendelea ndani ya familia yao.

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog