IMEANDIKWA NA : PATRICK CK
*********************************************************************************
Simulizi : Peniela (5)
Sehemu Ya Kwanza (1)
“ Dr Joshua is here? Akamuuliza Yule
mlinzi
“ Yes he’s here and I’m going to ask him if
he knows you.Kama umedanganya utakuwa
umejiweka katika matatizo makubwa sana kwa
kuhatarisha usalama wa rais.” Akasema Yule jamaa na kumkabidhi Peniela kwa mlinzi
mwanamama ili amkague na alipohakikisha hana
silaha yoyote akaelekea ndani
“ Stay Calm Peniela.Usionyeshe woga wa
aina yoyote” Mathew akamwambia peniela kupitia
kifaa cha mawasiliano Peniela alichokivaa sikioni.
ENDELEA SEASON 5
“ Dr Joshua “ akasema Donald baada ya
chumba kutawaliwa na ukimya
“ Baada ya kukueleza suala la pili lililonileta
hapa, sasa turejee katika suala la kwanza.”
Akasema Donald
“ Sawa endelea” akasema Dr Joshua
“ Awali nilikueleza kwamba tayari
tumekwisha fanya mipango yote ya kumuua
Andrew Rodney na Deus Mkozumi na kazi hiyo
itafanywa na Alqaeda na litaonekana ni shambulio
la kigaidi.Serikali ya Tanzania wala Marekani hazitahusishwa kabisa na tukio hilo badala yake
nchi zote zitaulaani kwa nguvu mtandao wa
Alqaeda kwa kitendo hicho.” Donald akanyamaza
kidogo halafu akaendelea
“ Ili kuutekekeleza mpango huo,Alqaeda
wametoa masharti mawili.Sharti la kwanza
tumuachie huru mmoja wa watu wao muhimu
ambaye tunamshikilia katika mojaya magereza
yetu.Hilo tayari tumelikubali na tutamuachia huru
kiongozi wao.Sharti la pili kuna kiongozi wao
muhimu sana anashikiliwa nchini Saudi Arabia
ambaye wanataka aachiwe.Serikali ya Saudi
Arabia haiku tayari kumuachia kiongozi huyo kwa
hiyo Alqaeda wanataka kuilazimisha serikali ya
Saudi Arabia kumuachia kiongozi wao na hilo
wataklifanya kutokea hapa nchini Tanzania”
“ Tanzania tena??!!...Dr Joshua akauliza
“ Ndiyo .Wanataka jambo hilo lifanyikie
hapa Tanzania” akasema Donald na kukawa
kimya.Mara mlango ukagongwa Dr Joshua
akaenda kuufungua.Alikuwa ni mmoja wa walinzi
wake Unasemaje Peter?
“ Mzee kuna kitu kimetokea hapa nyumbani
sasa hivi”
“ Kitu gani? akauliza Dr Joshua kwa wasi
wasi
“ Kuna mwanamke mmoja amefika hapa
anasema anaitwa Peniela na anadai kwamba
anaishi hapa na anakufahamu na wewe ndiye
uliyemruhusu aishi hapa”
Mwili wa Dr Joshua ukastuka kama vile
umepitiwa na chaji za umeme
“ Peniela ???..where is she? Akauliza
“ Yuko nje tunamshikilia”
“ Muachieni haraka aingie ndani ila mpitishe
kwa mlango wa nyuma aende moja kwa moja
chumbani kwake na asiruhusiwe kutoka hadi
nitakapomaliza maongezi na mgeni
wangu”akaamuru Dr Joshua
“ sawa mzee” akajibu Peter na kuanza
kuondoka Dr Joshua akamuita
“ Peter sitaki jambo hili alifahamu mtu
mwingine zaidi ya ninyi mlioko hapa.Kuhusu wale polisi pale getini tafuta namna yoyote ya
kuwadanganya .Tell them she’s my relative or
anything.”
“ Sawa mzee nitafanya hivyo” akajibu Peter
kwa adabu
“ Another thing,umewasiliana na Kareem?
Akauliza Dr Joshua
“ Ndiyo mzee nimewasiliana naye
ameniambia kwamba yuko maeneo ya kule
msibani”
“ Ok Good” akasema Dr Joshua na Peter
akaondoka
“ Peniela !!!.Finaly I’ve got her...” akawaza
Dr Joshua huku akihisi mwili unamtetemeka kwa
ndani kiasi cha kumshangaza hata yeye
mwenyewe ...
“ Sijui kwa nini kila ninapolisikia jina
Peniela,mwili wote hunitetemeka.Ngoja kwanza
nimalize maongezi na Donald halafu nitakwenda
kuonana naye nifahamu kitu gani kilichomleta
hapa.Nashukuru amejileta mwenyewe ,nilikuwa
naumiza kichwa ningempata wapi.Nilikwisha sahau kabisa kama nilimkabidhi nyumba hii aishi.”
Akawaza Dr Joshua aliyekuwa amesimama karibu
na mlango mara akastuliwa na Donald
“ Dr Joshua kuna tatizo lolote limetokea?
Mbona umebadilika ghafla?
“ Oh hapana Donald…Tuendelee na
maongezi yetu.Tuliishia wapi?
“ Nilikueleza kwamba Alqaeda wana
kiongozi wao anayeshikiliwa nchini Saudi Arabia
na wanataka kuishinikiza serikali ya Saudi Arabia
imuachie huru na jambo hilo litafanyika kutokea
hapa Tanzania” akasema Donald
“ Naomba unifafanulie vizuri
Donald.Wanataka kufanya nini kuishinikiza serikali
ya Saudi Arabia imuachie kiongzo wao? Akauliza
Dr Joshua ambaye macho yake yalionyesha wazi
alikuw ana wasi wasi mwingi
“ Binti mfalme wa Saudi Arabia aitwaye
Salhat Abdullah atatembelea Tanzania kwa
mwaliko wa rafiki yake ambaye ni Dr Lucia
Mkozumi .Salhat na Dr Lucia wanafanya kazi
pamoja katika shirika la fedha la umoja wa mataifa kwa hiyo ni marafiki wakubwa.Binti mfalme huyo
ambaye anapendwa mno na baba yake
atakapofika hapa Tanzania atatekwa nyara na
atatumika katika kuishinikiza serikali ya Saudi
Arabia imuache kiongozi wa Alqaeda ili Salhat
aachiwe huru.Kwa jinsi Salhat anavyopendwa na
baba yake lazima atakubaliana na matakwa ya
Alqaeda tu.”akasema Donald
“ Wanataka kumteka mtoto wa mfalme?
Hebu nifafanulie Donald watafanyaje hilo? Mbona
mambo mengi yanataka kutokea hapa nchini
ndani ya kipindi kifupi?
“ Mpango mzima uko hivi.Lucy ambaye
ndiye aliyemualika salhat kuja hapa nchini
ataongozana naye hadi katika jengo la biashar ala
Dar city shopping mall kwa lengo la kufanya
manunuzi ya vitu mbali mbali kwa ajili ya kupeleka
zawadi katika vituo vya watoto wanaoishi na virusi
vya ukimwi kwani Salhat anayo taasisi yake
inayojishughulisha na kuwahudumia watoto wa
aina hiyo .Katika msafara huo Dr Lucia anapaswa
kuhakikisha kuwa baba yake Deus Mkozumi anaambatana nao .Wakati manunuzi yakiendelea
Lucia atampeleka Salhat katika duka moja
linalouza vinyago..Atakapofika huko Alqaeda
watalivamia jengo hilo na kuwachukua mateka Dr
Lucia na Salhat na hapo ndipo Deus Mkozumi
atakapouawa”
Dr Joshua akatoa kitambaa na kujifuta
jasho lililoanza kumtoka usoni.Alihisi joto kutokana
na mambo mazito aliyoelezwa na Donald
“ Nini kitafuata baada ya hapo? Akauliza Dr
Joshua kwa wasi wasi
“ Dr Lucia Mkozumi ataachiwa huru,Salhat
ataendelea kushikiliwa na magaidi na ili aachiwe
huru watashinikiza kuachiwa huru kwa kiongozi
wao kwanza” akasema Donald
“ Itakuaje endapo madai yao
yasipotimizwa? Akauliza Dr Joshua
“ Ikitokea kwamba madai yao yasipotimizwa
wataondoka na Salhat na itakulazimu kuwasaidia
kuondoka hapa nchini lakini kwa utafiti uliofanyika
tunaamini lazima madai yao yatatekelezwa kwani
mfalme anampenda mno mtoto wake.Kiongozi wao atakapoachiwa huru watamuachia Salhat na
watapotea zao”
Dr Joshua akafikiri kidogo halafu akasema
“ Nina wasiw asi katika shambulio hilo
litakalofanyika Dar city shopping mall,watu wasio
na hatia watapoteza maisha yao.”
“ Ni kweli hilo unalolisema Dr Joshua na
haliwezi kuepukika.Lazima watu wapoteze
maisha .Nadhani unafahamu namna
mashambulizi ya kigaidi yanavyokuwa,lazima
idadi kadhaa ya watu wapoteze maisha”
“ Naogopa sana Donald kusema chochote
kwa sasa hasa nikivuta picha ya watu wasio na
hatia wakiwa wamelala chini hawana
uhai...Inaniogiopesha sana.Damu ya watu hao
wasio na hatia itatuandama sisi tuliosaidia
kufanikisha shambulio hilo.” Akasema Dr Joshua
“ Usiogope Dr Joshua.Kazi ya urais ni
ngumu na kuna nyakati unatakiwa kufanya
maamuzi magumu sana kwa maslahi mapana ya
nchi.Wakifa watu kumi au ishirini si kitu kwani
kuna mamilioni ya watu waishio vijijni watakwenda kunufaika na huduma za maji,afya,elimu,kilimo
n.k.Kwa hiyo usiogope Dr Joshua kufanya
maamuzi kwani maamuzi utakayoyafanya leo
yanaakisi maendeleo makubwa kwa Tanzania
kwa miaka mingi ijayo.Nakuhakikishia Dr Joshua
baada ya miaka kumi Tanzania hii uionayo sasa
haitakuwa kama unavyoiona leo.Itakuwa na
mabadiliko makubwa mno lakini haya yote
yanategemea maamuzi utakayoyafanya kuhusu
suala hili” akasema Donald.Dr Joshua
akainamisha kichwa akiwaza na baada ya muda
akasema
“ Dr Lucia Mkozumi anafahamu kuhusiana
na baba yake kutakiwa kuuawa ?
“ Anafahamu kila kitu na ameshiriki katika
kuandaa mpango huo.Dr Lucia mkozumi
hafahamiki kabisa hapa nchini na tukio hili
litachangia sana katika kumtangaza.Dunia yote
watamfahamu yeye ni nani ndani ya kipindi kifupi
sana na atakapotangaza kuwania urais wa
Tanzania haitakuwa kazi ngumu kumnadi.Dr
Joshua kila jambo lina sadaka yake na Dr Lucia Mkozumi yuko tayari kwa lolote ili aweze kuupata
urais wa Tanzania” akasema Donald..Dr Joshua
akakosa neno la kusema
“ Dah ! huyu Lucia lazima atakuwa ni
mwanamke mwenye roho ngumu sana.Kama
kweli amekubali baba yake auawe na magaidi
basi ni mwanamke anayefaa kabisa kuwa rais
kwani urais unahitaji mtu mwenye kuweza
klufanya maamuzi magumu kama aliyofanya Dr
Lucia.She’s a monster just like me.Lakini hata
hivyo siwezi kuukataa mpango huu kwani
umekuja kwa wakati muafaka kabisa.Kwa muda
mrefu nimekuwa nkitafuta namna ya kumuondoa
Deus Mkozumi kwani amekuwa akiingilia sana
mambo yangu na sasa nafasi hiyo imejitokeza na
siwezi kuiacha.Nitaitumia fursa hiyo kumuondoa si
Deus Mkozumi peke bali na mke wake Rosemary
Mkozumi.I hate that woman so much.Najua
atakuwa ni kikwazo kikubwa kwangu kufanikisha
mambo yangu .Lazima nimuondoe haraka sana
Yule mwanamke ili mpango huu usiingiliwe na
kikwazo chochote” “ Dr Joshua !!” akaita Donald na kumstua
Dr Joshua toka mawazoni
“ Donald mambo uliyonieleza ni makubwa
na mazito sana lakini ninaiona faida kubwa mbele
yake.Japokuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa
kasi kubwa lakini idadi kubwa ya raia wake bado
masikini na kwa ahadi hizi ambazo serikali ya
Marekani imeziahidi ninayaona mabadiliko
makubwa kwa Tanzania.Kwa upande wangu mimi
sina tatizo katika hili ilimradi tu ahadi zote
zuilizoahidiwa zitekelezwe.Najua baada ya
matukio hayo kutokea mtikisiko kidogo wa
uchumi lakini nina imani ndaniya kipindi kifupi hali
tarejea kuwa ya kawaida.” Akasema Dr Joshua
.Donald kwa furaha aliyoipata akainuka na kumpa
mkono Dr Joshua
“ Hongera sana Dr Joshua.Wewe ndiye rais
unayeona mbali.Una mtazamo mpana sana kwa
nchi yako.Ninakuhakikishia kuwa maamuzi yako
ya leo yatakuwa na faida kubwa sana kwa nchi
yako siku za usoni.Nakuhakikishia wananchi wa
Tanzania watakukumbuka daima kwa kuwaachia rais kama Dr Lucia ambaye wakati wa uongozi
wake serikali ya Marekani itamwaga misaada
mingi sana kwa serikali yake itakayowanufaisha
mamilioni ya watanzania.Nataka nikuondoe wasi
wasi pia kwamba mambo yote yatakayotokea si
Tanzania wala Marekani watakaolaumiwa bali ni
mtandao wa Alqaeda.Wakati dunia ikiwalaani
magaidi ,mamilioni ya watanzania watakuwa
wanapata huduma za maji safi ya
kunywa,huduma bora za afya,elimu nishati ajira
pamoja na mambo mengine mengi toka kwa
serikali ya Marekani.Kwa kauli yako hiyo
mheshimiwa rais unaniruhusu niwataarifu
wakubwa zangu kwamba umekubali ili tuweze
kuendelea na hatua inayofuata?
“ Bila shaka Donald,unaweza kuendelea na
hatua inayofuata.Nini kinachofuata baada ya
hapa?
“ Hatua inayofuata ni kumleta nchini rais
mtarajiwa Dr Lucia Mkozumi na tutakuwa na
maongezi ya pamoja mimi,wewe,Dr Lucia pamoja
na mratibu wa mashambulio mawili toka Alqaeda Dr Lucia yuko nchini Afrika ya kusini akiwa
ameambatana na binti mfalme Salhat
nitawasiliana naye usiku huu na kesho atakuwa
hapa nchini na kesho hiyo hiyo jioni tutakutana
hapa kwa ajili ya kukaa kikao kizito cha kupanga
mikakati ya utekelezaji wa matukio yote.”
Akasema Donald.
“ Sawa Donald.Tutaonana hiyo
kesho.Tutakutana hapa hapa kwani ndiyo sehemu
salama zaidi kwa sisi kuongea na kupanga
mipango yetu” akasema Dr Joshua na kuagana
na Donald akamsindikiza hadi lilipo gari lake
akaondoka zake na Dr Joshua akarejea sebuleni
akaketi sofani
“ Mambo aliyotumwa Donald aje anieleze
ni mambo mazito mno lakini endapo yatafanikiwa
kutekelezwa basi nchi yetu itapata manufaa
makubwa kuliko athari zitakazojitokeza katika
utekelezaji wake .Nchi itayumba kidogo lakini
ndani ya kipindi kifupi itakaa sawa na wananchi
watasahau kabisa matukio yote.Suala hili
ukilitazama kwa upana wake ni kweli Marekani wanastahili kulinda maslahi yake kutokana na
kufanya uwekezaji mkubwa sana hapa nchini
kuliko nchi nyingine yoyote afrika.Uwekezaji huu
unawapa nguvu ya kuweza kuingia hadi katika
siasa zetu na kuchagua rais wanayemtaka
ambaye wanaamini atakuwa na manufaa
kwao.Hili si tatizo as long as wananchi wetu
wananufaika kwa misaada mikubwa itakayotolewa
na Marekani.Kipindi changu cha uongozi,serikali
ya Marekani wamekuwa ni wafadhili namba moja
wa bajeti yetu ya serikali na miradi mingi ya
maendeleo na endapo nikifanikisha Dr Lucia awe
rais kama wanavyotaka misaada itaongezeka
maradufu” akawaza Dr Joshua na kukumbuka kitu
akatabasamu
“ Dr Lucia Mkozumi,huyu mwanamamama
japokuwa sijabahatika kuonana naye lakini
anaonekana anafaa sana kuwa rais.Anaonekana
ni mtu jasiri na asiyesita kufanya maamuzi
makubwa “ akawaza Dr Joshua akajimiminia
whisky katika glasi na kunywa funda kadhaa “ Kwa upande wangu nimeahidiwa mambo
mengi makubwa .Kikubwa zaidi ni fedha nyingi.It’s
a lot of money.Maisha yangu baada ya kustaafu
yatakuwa mazuri mno.I’ll be like an angel in
heaven.Laiti kama jambo hili lingekuja mapema
kabla sijaanza mchakato wa kukiuza kirusi Aby
katu nisingeuza kitu kile kilichojaa mikosi na hadi
sasa mke wangu na mwanangu Flaviana
wangekuwa bado hai..”
Mara wazo likamjia Dr Joshua
“ Kwa kuwa kuna huu mpango mpya
umekuja ambao unaonekana ni bora zaidi na una
maslahi mapana kwangu na kw anchi kwa nini
nisiachane na mpango ule wa kukiuza kirusi
Aby?.Kirusi kile naona kama vile kina mkosi kwani
mpaka sasa tayari nimemkwisha wapoteza watu
wangu wawili wa karibu sana halafu kitu kingine ni
kwamba sifahamu Hussein anataka kukitumiaje
kirusi hicho.”
Dr Joshua akanywa tena funda la mvinyo
“ Hapana siwezi kumpa Hussein kile
kirusi.NItamrejeshea fedha zake zote .Najua itakuwa ngumu lakini hakuna namna nyingine
lazima niachane na mpango ule na nielekeze
nguvu katika mpango huu wa Marekani ambao
una maslahi manono kwangu..”
Akatulia tena akanywa funda lingine la
mvinyo
“ Dah ! Imekuwa ni siku ndefu sana
iliyokusanya mambo mengi na kichwa changu
kimechoka.Nahitaji kupumzika lakini kabla ya yote
lazima nikaonane na Yule shetani wa kike
Peniela.Nashukuru amejileta mwenyewe.”
Akawaza Dr Joshua halafu akakumbuka maneno
aliyoambiwa na jaji Elibariki kuhusu Peniela
akapandwa na hasira na kutoka mle sebuleni kwa
hasira akaelekea katika chumba alimokuwamo
Peniela akaminya kitasa lakini mlango ulikuwa
umefungwa kwa ndani.Akagonga kwa nguvu na
taratibu mlango ukafunguliwa akajikuta
akitazamana na sura yenye tabasamu ya Peniela.
Halow my love” akasema Peniela.Dr
Joshua akavuta pumzi ndefu baada ya
kumshuhudia Peniela akiwa amesimama mlangoni akiwa na nguo ya ndani peke.Mapigo ya
moyo wake yakabadilika na kuanza kwenda kwa
kasi alipoushuhudia mwili ule mwororo .Kwa
sekunde kadhaa wakabaki wanatazamana.
“ Karibu ndani mpenzi wangu” akasema
Peniela kwa sauti laini.Dr Joshua hakujibu kitu
akaingia ndani Peniela akaufunga
mlango.Akamfuata Dr Joshua aliyekuwa
amesimama
“ My love sikujua kama uko hapa..”
akasema Peniela lakini Dr Joshua akamkatisha
“ Stop calling me yur love ,you evil witch!!!
Akasema Dr Joshua kwa ukali huku akimsukuma
Peniela akaangukia kitandani.Peniela akainuka na
kumfuata Dr Joshua
“ Whats wrong my love???
“ Don’t touch me you devil !!! akaendelea
kufoka Dr Joshua huku akimtazama Peniela kwa
macho makali yaliyojaa hasira.
“ Shhh..!!My love I’m not here to
fight.Please calm down and tell me whats wrong
with you and why you are so angry at me today.Sijawahi kukuona ukiwa katika hali hiyo
hata siku moja.Lakini kabla ya yote tafadhali
naomba nikupe kile ambacho umekuwa unakihitaji
sana.” Akasema Peniela na kumkumbatia Dr
Joshua na kuanza kumwagia mabusu mfululizo.Dr
Joshua akakosa cha kusema kwani hasira
zikampotea ghafla na kujikuta akipandwa na
mdadi na kumkumbatia Peniela.Peniela
anamfahamu Dr Joshua na anayafahamu maeneo
ambayo yanampa uchizi mzee huyu hivyo
akayatumia vyema kumpagawisha na kumfanya
atoe miguno.
“ You called me devil,I’m going to show you
I’m a real devil” akawaza Peniela na kumsukumia
Dr Joshua kitandani akaanza kumchojoa nguo
moja moja na kuendela na utundu wake huku Dr
Joshua akilalama kama mtoto na kuongea
maneno ambayo hayakuwa yakisikika vizuri,yote
hii ilisababishwa na raha alizozipata.Peniela
alipohakikisha Dr Joshua amepagawa vya
kutosha akajiweka tayari kwa ajili ya mtanange. Mtanange wa dakika thelathini ulimuacha
Dr Joshua akivuja jasho kama mkimbiaji wa mbio
ndefu.
“ This woman is real amazing.Kila
ninapokutana naye ananifanyia vitu ambavyo
sijawahi fanyiwa na kuzidi kunipagawisha.Sijui ni
uchawi gani anaoutumia kunivuruga akili yangu
namna hii.Mambo aliyonifanyia leo yamenifanya
hata hasira zangu zote nilizokuwa nazo juu yake
zipotee.I think I still love this woman so
much.Pamoja na yote ambayo jaji Elibariki
alinieleza kuhusu Peniela but I still love her and I
don’t know what I’m going to do because I cant let
her go..Mara ya kwanza alinisaliti kwa kuanzisha
mahusiano na Edson na kwa namna alivyoniudhi
nilitamani afungwe kifungo kirefu gerezani ili
apotee kabisa lakini ikashindikana na nilipokuja
kuonana naye tena hasira zangu zote juu yake
zikapotea na nikajikuta nikimpenda zadi na
zaidi.Safari hii tena baada ya kupata taarifa za
anachokifanya dhidi yangu nilimchukia na
nikamuweka katika orodha ya watu ninaotaka kuwashughulikia lakini baada ya kuonana naye
hasira zote zimepotea na kwa mara nyingine
ninajikuta nikizidi kumpenda Peniela.Mapenzi
niliyonayo kwa Peniela ni makubwa mno na sijui
kwa nini ameshindwa kulitambua hilo.Ni kiasi gani
anacholipwa na hao watu wanaomtumia?
Ninaamini hakuna kiasi anachoweza kulipwa
kinachoweza kulingana na upendo wangu kwake”
akawaza Dr Joshua na kugeuka akamtazama
Peniela
“ Muda si mrefu nitamaliza kipindi changu
cha uongozi na kwenda kuishi nje ya nchi.Nitaishi
maisha ya kifahari mno kwa nini basi nisiende
kuanza maisha yangu mapya na mrembo huyu
ambaye ametokea kunipagawisha kuliko
wanawake wote hapa duniani? Siwezi kumfanya
chochote Peniela hata kama ni kweli amekuwa
anatumika na watu kutaka kunihujumu kwa
sababu bado ninampenda sana.Ni mwanamke
pekee ambaye ananifanya nijione nina miaka
ishirini kila ninapokuwa naye.Lazima nifanye kila
ninavyoweza mpaka niondoke naye.Utajiri wote nitakaokuwa nao hautakuwa na maana kama
sintakuwa na Peniela..”
“ Dr Joshua ..!!” akaita Peniela kwa sauti
laini na kumuondoa Dr Joshua mawazoni.
“ Unasemaje Peniela? Akauliza Dr Joshua
“ Earlier you called me evil witch ,what was
the meaning to call me that? Am I a witch to you
now? Akauliza Peniela Dr Joshua hakumjibu kitu
akamkazia macho
“ Sikutegemea kabisa kama siku moja Dr
Joshua ungeweza kunitamkia maneno kama
yale.Kitu gani kibaya nilichokufanyia mpenzi
wangu kiasi cha kuniita majina yale mabaya?
Tafadhali nieleze Dr Joshua kama kuna chochote
nilichokukosea”
Dr Joshua akainuka na kukaa kitandani
“ Peniela you you know how much I love
you,right? Akauliza Dr Joshua
“ Yes I know?” akajibu Peniela
“ Toka tumekuwa na mahusiano nimekuwa
tayari kukufanyia jambo lolote ili kukuonyesha ni
kwa namna gani ulivyo muhimu kwangu.Hukuwahi kuniambia chochote nikasema hapana lakini
pamoja na kukupenda kote kwa nini unanifanyia
hivi? Akauliza Dr Joshua
“ Nimekufanyia nini Dr Joshua? Peniela
naye akauliza
“ Usitake kuniudhi Peniela.How much do
they pay you? Tell me please how much??
Akasema Dr Joshua kwa ukali
“ Nani hao? Mbona sikuelewi Dr Joshua ??
akauliza Peniela
“ Team SC41.How much do they pay you?
Peniela akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Team SC41 ni nini? Akauliza
“ Tuokoe muda Peniela.Ninafahamu kila
kitu kuhusu wewe.Ninafahamu kwa nini uko na
mimi na kitu gani unakihitaji toka
kwangu.Nimeskitika sana Peniela baada ya
kufahamu jambo unalonifanyia na ndiyo maana
ninataka kufahamu unalipwa kiasi gani na hao
waliokutuma kwangu?
“ Dr Joshua nashindwa kukuelewa
unazungumzia kitu gani kwani hiyo team sijui nini
sifahamu ni kitu gani na wanahusika na nini?
Umetoa wapi taarifa hizo?
“ Peniela najua machoni unakataa lakini
moyoni umestuka sana na unajiuliza nimefahamu
vipi.Just tell me how much they pay you and I can
pay you back a hundred times.”
“ Dr Joshua I don’t understand what you are
talking about” akasema Peniela.Dr Joshua
akamtazama Peniela kwa sekunde kadhaa na
kusema
“ Kwa nini unanifanyia hivi Peniela? kwa
nini unataka kunifanyia ukatili huu wakati mambo
ninayoyafanya ni kwa ajili yetu sote? Ninataka
nitakapomaliza kipindi changu cha uongozi mimi
na wewe tuishi maisha kama ya mfalme lakini kwa
nini hutaki kulielewa hilo na kutaka kuvuruga
mipango yangu? Nilikupa nafasi ya kuchagua
sehemu yoyote duniani unayotaka kwenda kuishi
ili tukaishi nitakapomaliza kipindi changu cha
uongozi lakini yote haya umeyaweka pembeni
..Why Peniela?? “ Dr Joshua I real don’t understand
you.Mambo unayonieleza ni mambo mageni
kabisa kwangu na siyaelewi.”
“ Peniela ninakupenda sana ndiyo maana
nnakwambia haya ili ufahamu nina lengo zuri na
wewe.Mimi ni rais wa nchi na ninafahamu kila mtu
aliye karibu yangu.Ninafahamu kila
kinachoendelea.Uko hapa na mimi muda huu kwa
sababu nimetaka iwe hivyo kutokana na upendo
mkubwa nilionao kwako vinginevyo muda huu
usingekuwapo katika ulimwengu huu”
Peniela akamtazama Dr Joshua huku
machozi yakimchuruzika akasema
“ Dr Joshua ninaomba unieleze ni nani
aliyekuambia maneno hayo? Ni nani huyo
asiyetutakia mema katika mapenzi yetu na
anataka kukutenganisha? Do you believe them
than me??
“ Peniela mimi ni raisi na ninazungukwa na
watu ambao wamekula kiapo cha kunilinda hata
kama ikiwabidi kuyatoa maisha yao kwa ajili yangu hivyo ninawaamini kwa kila
watakachioniambia”
Peniela akamtazama na kutikisa kichwa
“ Siamini maneno hayo kama yanatoka
kwako.Lini Dr Joshua utaniamini?
“ How can I trust you Peniela? You are a
professional liar.A cheater !!” akasema Dr Joshua
kwa ukali.Peniela akamnasa kibao
“ Iwe ni mara ya kwanza na ya mwisho
kunitamkia maneno hayo machafu.Kama
ningekuwa nina nia mbaya ningekwisha kufanyia
kitu kibaya muda mrefu .You killed Edson na kesi
ikaniangukia mimi.NiIiifahamu wewe ndiye
uliyemuua Edson lakini sikufumbua mdomo
wangu kusema chochote.Nimeteseka gerezani
mwaka mzima lakini sikuwahi kuufungua mdomo
wangu na kutamka neno lolote la kukuhusisha
wewe na kifo cha Edson.Iweje leo hii unitamkie
maneno hayo machafu? Akauliza Peniela huku
akilia “ Do you have any proof? Una ushahidi
kwamba ninahusika katika kifo cha Edson?
Akauliza Dr Joshua
“ Na wewe una ushahidi wa hayo
unayonituhumu kuyafanya? Akauliza Peniela
“Ndiyo nina ushahidi .Usitake niyaanike
mambo yako Peniela.Ninafahamu kila kitu
unachokifanya.Ninaifuatilia kila hatu unayopiga
kwa hiyo ninakufahamu zaidi ya
unavyojifahamu.Nafahamu umetumwa kwangu na
Team SC41,ninafahamu unashirikiana na mtu
anayeitwa Mathew ambaye aliwahi kufanya kazi
katika idara ya usalama w a taifa .Nafahamu
umetembea na Dr Kigomba na ulimtumia ili
kufanikisha mipango yenu.Ulimpa saa ya mkononi
mliyoiwekea kifaa maalum cha kuweza kutambua
kila mahala alipo .Kama haitoshi mliunganisha
simu yake na mtandao wenu na mkayasikia
mawasiliano yake yote.Peniela ninazifahamu
mbinu zako zote chafu..” akasema Dr Joshua
.Peniela akamtazama na kusema “ Dr Joshua kitu gani unakitafuta toka
kwangu? Kwa nini umeukubali uongo huu bila ya
kufanya kwanza uchunguzi? Watu unaosema eti
ninashirikiana nao ni mara yangu ya kwanza
kuwasikia leo hii.I don’t know them.Halafu
unasema eti nilikuwa na mahusiano na Dr
Kigomba? Mimi Peniela naweza kumuonyesha
utupu wangu mtu kama Yule? Sikutegemea
kabisa mtu kama wewe unaweza kuwa mwepesi
kusikia na kuamini maneno ya watu wasiokutakia
mema” akasema Peniela
“ Peniela mambo haya nimeyapata toka
kwa mtu ninayemuamini na ambaye mlikuwa
mnashirikiana naye katika mipango yenu bila ya
ninyi kufahamu kuwa alikuwa ni m tiifu
kwangu.Hamkuwa mkijua kama jaji Elibariki ni mtu
wangu.Hahahahaaa…” akasema Dr Joshua na
kutoa kicheko cha dharau
“ Jaji Elibariki ???..Peniela akashangaa
“Ndiyo.Mbona umestuka ? Humjui? “ Jaji Elibariki Yule aliyehukumu kesi yangu
na kuniachia huru ndiye aliyekuletea habari hizi?
Akauliza Peniela na kutoa kicheko kidogo
“ Nilijua tu kitu kama hiki lazima
kitatokea.You are so fool Dr Joshua.Jaji
Elibarikiamekuingiza katika mtego na wewe kwa
kutokuwa na umakini umeingia katika mtego
wake..” akasema Peniela na kutoa kicheko
kidogo.Dr Joshua hakusema kitu akabaki
anamtazama
“ Ni hivi naomba unisikilize vizuri Dr
Joshua” akasema Peniela
“ Nilikuwa najiuliza sana ni nani ambaye
anaweza kunitungia uongo mkubwa kama huu?
Nilijua tu lazima mtu ambaye amenitungia uongo
mkubwa kama huu atakuwa na lengo baya na
mimi la kuniharibia maisha yangu kwa kutaka
unichukie na uniache kumbe ni jaji Elibariki
!!!!..akasema Peniela na kutulia kidogo halafu
akaendelea
“ Nilimfahamu Elibariki alipoanza kusikiliza
shauri langu .Mahakama haikunikuta na hatia na nikaachiwa huru.Baada ya kuachiwa huru jaji
Elibariki akanifuata na kuanza kunitongoza akidai
kwamba yeye ndiye aliyeniweka huru.Aliendelea
kunisonga sana na siku moja usiku alikuja kwangu
akiwa ametapakaa damu akaniomba nimuhifadhi
kwa madai kwamba kuna watu wanamtafuta na
wanataka kumuua.Nilimuonea huruma
nikamruhusu alale pale kwangu na kesho yake
asubuhi wakati nikioga alinivamia bafuni.Unajua
alinifanya nini?? Akauliza Peniela kwa hasira.Dr
Joshua hakujibu kitu akabaki anamtazama
“ He raped me !!!!..akasema huku machozi
yakimtoka.Maneno yale yalimfanya Dr Joshua
astuke kidogo na kumtazama Peniela kwa hasira
“ Nilikasirika sana na nikamuweka wazi
kwamba lazima nikueleze kuhusu jambo lile
akanitolea vitisho vingi kwamba nikithubutu
kukueleza chochote ataniua.Alipoona nimeshikilia
msimamo wangu wa kuja kukueleza akaondoka
na baadae akarudi akiwa ameongozana na mke
wa rais mstaadfu Rosemary Mkozumi .Kwanza
aliniomba msamaha halafu akaniambia kwamba amemleta Rosemary mkozumi kwangu kuna
jambo wanataka kuzungumza nami.Rosemary
Mkozumi akaniambia kwamba kuna jambo
wanataka kunishirikisha ambalo endapo
litafanikiwa nitapata fedha nyingi sana.Nilitaka
kufahamu ni jambo gani hilo na wakanieleza
kwamba kuna kifaa Fulani unacho ambacho
natakiwa kufanya jitihada nikipate na nkifanikiwa
basi nitakuwa bilionea.Waliniahidi kunipa shilingi
bilioni kumi endapo ningefanikiwa.Nilitaka
wanifafanulie ni kitu gani hicho lakini hawakuwa
tayari na kwa kuwa tayari jaji Elibariki alikwisha
nifanyia kitendo kibaya cha udhalilishaji mkubwa
sikuwa tayari kushirikiana nao kwa lolote.Baada
ya jitihada zao zote za kunishawishi kushidnikana
wakanitolea vitisho na kunipa muda wa kutafakari
na kufanya maamuzi na wakanionya kwamba
nisithubutu kufungua mdomo wangu na pindi
nikikifanya hivyo wataniua.Pamoja na kitisho cha
kuniua lakini sikukubaliana nao na kama
utakumbuka nilikupigia simu na nikakwambia
kwamba ninataka kuonana nawe lengo lilikuwa ni kukueleza kuhusu jambo hili lakini hatukuweza
kuonana kutokana na msiba wa Flaviana.Juzi
usiku nilivamiwa na watu ambao nina hakika
walitumwa kuja kuniua kwa bahati nzuri
nilifanikiwa kutoroka na nyumba yangu
ikachomwa moto.Nilijihifadhi kwa rafiki yangu na
leo hii nimeamua nije katika hii nyumba uliyonipa
niishi.Kwa hiyo Dr Joshua mambo aliyokwambia
jaji libariki hayana ukweli hata kidogo.Amewahi
kuja kwako na kukupa uongo huu mkubwa kwani
alijua lazima ningekuja kukuona na kukueleza
mambo haya.He lied to you na wewe ukawa
mwepesi kuamini.Dr Joshua mimi sina mpango
wowote mbaya nawe ila nisikilize vizuri ,jaji
Elibariki na Rosemary Mkozumi kuna jambo baya
wanalipanga dhidi yako,kuna kitu wanakitafuta
toka kwako.Sikulazimishi uniamini huo ni uamuzi
wako.Mimi nimekwisha kueleza ukweli wangu na
utapima nani mkweli kati yangu mimi au Elibariki”
akasema Peniela
Mathew na Anitha waliokuwa garini
wakifuatilia mazungumzo yote kati ya Peniela na Dr Joshua kupitia kifaa cha mawasiliano
alichokivaa Peniela sikioni,wakatazamana na
Mathew akatabasamu
“ Peniela is real a professional
liar.Sikutegemea kama angeweza kutunga uongo
ule mkubwa kwa haraka” akasema Mathew Anitha
hakujibu kitu naye akatabasamu
******************
Maneno aliyoambiwa na Peniela yalimfanya
Dr Joshua abaki kima akitafakari.
“ Kwa hiyo Dr Joshua “ akasema Peniela
na kumfanya Dr Joshua ainue kichwa
“ Ni juu yako kuchagua na kuamini yupi
mkweli kati yangu na jaji Elibariki”
Dr Joshua akavuta pumzi ndefu na kusema
“ I don’t know anymore the meaning of
these two words,believe and trust.I don’t know
who to believe or who to trust.” Peniel akamtazama kwa makini na kusema
kwa sauti ndogo ya kimahaba
“You don’t believe even the woman you
love the most as you always say? You don’t
believe me? That’s too bad.”
Akamtazama tena Dr Joshua na kusema
“Kila siku umekuwa unaniambia kwamba
unanipenda na uko t ayari kwa lolote kwa ajili
yangu sasa ni wakati wako wa kulithibitisha hilo
kwa vitendo.Nitaumia mno endapo utashindwa
kuniamini na kuchagua kumuamini mtu ambaye
ana lengo la kukuangamiza.One more thing,if y u
choose not to trust me today then there is no any
meaning for us to contnue with our
relationship.We have to put an end to us
!!!!..akasema Peniela kwa ukali kidogo
“ Peniela my love,si kwamba sitaki
kukuamini lakini ….” Dr Joshua akasita
“ Lakini nini Dr Joshua? Unashindwa kweli
kuniamini mimi? Nasikitika sana kwa hilo.Sasa
nimegundua yale maneno yote uliyokuwa
unaniambia kila siku kamba unanipenda hayakuwa ya kweli.Lengo lako lilikuwa ni kutimiza
tu haja zako za mwili na si kweli kwamba ulikuwa
na nia ya dhati ya kufanya jambo lolote kwa ajili
yang….”
“ Peniela stop !!” akasema Dr Joshua
“ Kwanza naomba samahani sana kwa
maneno yale niliyoyatamka mwanzo.NIsamehe
sana Peniela.Nilitamka maneno yale kutokana na
hasira nilizokuwa nazo juu yako kwa sababu ya
maneno niliyolishwa na jaji Elibariki na mimi
nikayaamini.Maneno uliyonieleza ni mazito na
ninakuahidi nitayafanyia kazi kwa haraka na hawa
wote wanaojifanya ni watu wangu wa karibu
kumbe ni chui wanaoiwinda damu yangu
watakiona cha moto” akasema Dr Joshua halafu
akamtazama Peniela kwa sekunde kadhaa
akamsogeza karibu yake akambusu
“ Peniela nakupenda sana malaika wangu
zaidi ya n inavyoweza kukueleza.Sikumbuki ni
mara ngapi nimekutamkia neno hili kwamba
ninakupenda lakini usiku wa leo nataka
nikukumbushe kwamba ninakupenda kuliko chochote hapa duniani.Japokuwa kuna nyakati h
uwa unaniudhi mfano ulipoanzisha mahusiano na
Yule kijana Edson nilichukia sana lakini kila pale
ninapokuwa na hasira juu yako ninapokuona tu
hasira zote hupotea na hutabasamu
tena.Nakuomba Peniela usiwe na shaka yoyote
juu ya upendo wangu kwako na kwa ajili yako niko
tayari kwa lolote “ akasema Dr Joshua na
kumbusu tena Peniela
“ Peniela muda wangu wa uongozi
unakaribia kumalizika .Utafanyika uchaguzi na
atapatikana rais mpya na mimi nitaenda
kupumzika.Ninao u tajiri mkubwa sana ambao
utanifanya niishi maisha mazuri ya kifahari baada
ya kustaafu hadi siku ninaingia kaburini .Hivi
karibui ninatarajia kupata ukaazi wa kudumu
nchini Marekani kwa hiyo baada tu ya kustaafu
nitakwenda kuishi huko.Sintokwenda huko
mwenyewe bali nitaongozana nawe malaika
wangu unayejenga tabasamu usoni pangu kila
niionapo sura yako.Peniela una nafasi ya pekee
kabisa katika moyo wangu kwa hiyo kokote niendako nitaambatana nawe.Nataka tuishi
maisha yenye furaha ,tuzunguke dunia nzima
tukistarehe na kuyafurahia maisha.” Akasema Dr
Joshua na kumbusu Peniela
“ Peniela sitaki kukupoteza wala kuruhusu
jambo lolote baya likutokee.Kwa Elibariki na
mshirika wake Rosemary Mkozumi ntajua n ini
cha kuwafanya .Kwa hiyo basi kuanzia sasa hadi
hapo nitakaporidhika kwamba hakuna shaka ya
usalama wako utakaa humu ndani na hutatoka
hadi hapo nitakapokuruhusu kutoka.”
“ No !Dr Joshua yu cant do that to me
!!.akasema Peniela
“ Yes you will.Thats an order!!! Akasema Dr
Joshua kwa sauti ya ukali
“ Peniela I’m doing this for you,for us,kwa
hiyo naomba usikasirike wala usinione mimi
mkatili .Maisha yako yana thamani kubwa kwangu
na jambo hili ni la muda tu na nitakapohakikisha
hali ya usalama imeboreka basi utakuwa huru
.Utapata kila unachohitaji na ulinzi nitauimarisha
zaidi hapa.Nitakuelekeza Kareem ahakikishe kunakuwa na ulinzi wa kutosha hapa.Kila jioni
nitakuwa nakuja hapa na tunapata wasaa wa
kuwa pamoja.Peniela this is our moment to be
happy.Give me a chance to show you how much I
love you.Mwanamke kama wewe unapaswa kuishi
zaidi ya malkia” akasema Dr Joshua .Peniela
akaachia tabasamu kubwa akambusu Dr Joshua
na kusema
“ Dr Joshua nafahamu unanipenda na una
nia nzuri na mimi hasa kwa wakati huu ambao
usalama wangu uko shakani lakini siwezi kukubali
kufungiwa humu ndani.Nahitaji kuwa huru mpenzi
wangu”
“ Usijali Peniela.This is just for few
days.Nataka ukitoka hapa japokuwa si rasmi
lakini uishi kama mke wa rais kwa hiyo naomba
unipe siku chache tu niweze kuyafanya mambo
makubwa ambayo nataka kukufanyia.Sawa
malaika wangu? Akasema Dr Johsua.Peniela
akatabasamu na kwa sauti laini akasema
“ Dr Joshua you’re the king
here.Nitatekeleza yote unayoyasema but I have one request na endapo utanitekelezea hilo
nitaamini kwamba kweli unanienda and I’ll go with
you anywhere you wat us to go”
“ Peniela,neno lako ni amri
kwangu.Tafadhali nieleze chochote
nitakutekelezea bila kusita” akasema Dr Joshua
kwa kujiamini
Peniela akainamisha kichwa na alipoinua
kumtazama Dr Joshua macho yake yalijaa
machozi.Dr Joshua akastuka
“ Whats wrong my queen? Akauliza Dr
Joshua
“ Dr Joshua nimedhalilishwa sana na jaji
Elibariki .He raped me.He raped the woman you
real love.I want him for what he did.Can you help
me make him pay?
Dr Joshua akamkumbatia Peniela na
kusema
“ My dear Peniela,siwezi kukueleza ni
namna gani nimeumizwa na taarifa hizo za
kitendo kiovu alichokifanya Elibariki.Edson
nilimuondoa kwa sababu moja tu ya kuwa na mahusiano na mwanamke wangu ninayempenda
kuliko wote.Peniela you are mine and mine alone
kwa hiyo yeyote atakayekuumiza wewe atakuwa
ameniumiza mimi pia.Nakuahidi Peniela, Elibariki
will pay very dearly !!!!... akasema Dr Joshua
huku akiuma meno kwa hasira.
“ Ahsante sana my love.Sasa naamini
maneno yako kwamba unanipenda,Unajua
sikuwahi kufikiri hata siku moja kama ninaweza
kudhalilishwa kiasi kile.Inaniumiza sana na sijui
nitafanya nini ili niweze kuliondoa jambo hili katika
akili yangu”
“ Peniela I’m right here.Nitakufuta machozi
na kukusahaulisha jambo hili.Narudia tena
kukuahidi jaji Elibariki lazima atalipa uovu wake..!”
Peniela akaanza tena utundu wake na Dr
Joshua akazidi kupagawa
“ Dah ! hatimaye nimefanikiwa kumteka akili
huyu mzee.Elibariki alifanya kosa kubwa sana
kutusaliti.Nitahakikisha anakosa kila kitu.Dr
Joshua hana tena kauli yoyote kwangu na lazima
mipango yetu yote iende kama tunavyotaka.Kwa kuwa amenitaka nisitoke nje ya nyumba hii ngoja
nimkubalie matakwa yake lakini natakiwa kutafuta
namna ili niweze kulichukua kasha langu na
kuwapelekea akina Mathew.Kitu kizuri ni kwamba
anasema Kareem ndiye atakayekuwa hapa
nyumbani akihakikisha ninakuwa salama.Kareem
hana kauli kwangu atafanya kila
nitakachomuamuru kufanya.” Akawaza Peniela
huku akiendelea kumfanyia Dr Joshua
utundu,ambaye alikuwa anaguna kimahaba kwa
mambo aliyofanywa na muda si muda wakaingia
katika mzunguko wa pili.Peniela akashika usukani
alimpeleka vilivyo Dr Joshua na kumfanya alalame
kama mtoto mdogo.Hadi mzunguko wa pili
unamalizika Dr Joshua alikuwa hoi amechoka
kupita maelezo.
“ I swear Peniela sintamuacha hata itokee
nini.Huyu binti ananipa raha ambayo siwezi
kupewa na mtu yeote.Nitafanya kila
linalowezekana hadi niw…..” Dr Joshua
akashindwa kuendelea kuwaza akapitiwa na
usingzi.
“ Dr Joshua!!.Dr Joshua .!!” akaita Peniela
lakini tayari D Joshua alikuwa katika usingizi
mzito.
“ Kwisha habari yake” akawaza Peniela na
kuinuka akaelekea chooni akakigonga kile kifaa
cha kuwasiliana alichokiweka sikioni.
“ Hallow Mathew,can you hear me?!!!
Akauliza Peniela.
“ Ndiyo Peniela.Tumesikia kila
kilichoendelea hapo ndani.Good job” akasema
Mathew
“ Ahsante.Kama mlivyosikia huyu mzee
hataki nitoke humu ndani . What are we going to
do? Tunatakiw akuonana na Deus Mkozumi,right?
“ Usijali kuhusu hilo tutatafuta namna
nyingine ya kufanya kuweza kuonana na Deus
Mkozumi ila kwa sasa wewe endelea kukaa humo
humo ndani kama anavyotaka.Endelea kumfanya
akuamini tena na wakati ukiwa hapo ndani jaribu
kutafuta chochote kinachoweza kutusaidia katika
mpango wetu wa kukipata kirusi Aby” “ Sawa Mathew,nitafanya nhivyo ila kesho
nitamtuma Kareem alete ule mzigo hapo
nyumbani. Mathew,tutawasiliana kesho.Good
night”akasema Peniela na kurejea chumbani
ambako Dr Joshua alikuwa amelala fofofo.
“ Nini kinafuata baada ya hapa? Akauliza
Anitha wakiwa ndani ya gari baada ya Peniel
kumaliza kuongea na Mathew
“ Tunarudi nyumbani kwani Peniela hawezi
kutoka mle ndani leo,kwa hiyo hatuna haja ya
kuendelea kukaa hapa”
“ Are you sure she’ll be ok? Ninawasi wasi
kidogo kwani mchezo anaoucheza ni wa hatari
sana.Anacheza na akili ya Dr Joshua,unadhani
nini kitatokea endapo dr Joshua atagundua kuwa
Peniela anamdanganya? Akauliza Anitha
“ Hilo haliwezi kutokea kabla
hatujakamilisha mpango wetu.Peniela ni mjanja
mno.Akili yake inafanya kazi haraka sana na
anaweza kufanya jambo lolote muda
wowote.Amenishangaza sana kwa namna
alivyoweza kubadili upepo kati ya Dr Joshua na jaji Elibariki.Ameweza kuuvaa vyema uhusika na
mtu yeyote angeweza kumuamini alichokisema”
akasema Mathew kisha wakaondoka kurejea
nyumbani.
*****************
Watu hawakuwa wengi nyumbani kwa rais
usiku huu uliko msiba wa Flaviana.Wengi wa
waliobaki ni ndugu na watu wa karibu na familia
ya rais.Anna akamuulizia Jaji Elibariki akaambiwa
kwamba ameondoka ameelekea nyumbani kwake
kupumzika
“ Nitamfuata huko huko nyumbani kwake”
akawaza na bila kupoteza wakati akaelekea katika
gari lake na kuondoka kumfuata jaji Elibariki
nyumbani kwake
“ Leo lazima nifahamu ni kitu gani
kinachoendelea kati ya baba na jaji Elibariki.Kama
alivyonieleza Mathew lazima kuna kitu
kinachoendelea kati yao.I must find out” akawaza
TUKUTANE SEHEMU IJAYO...
“ Dr Joshua!!.Dr Joshua .!!” akaita Peniela
lakini tayari D Joshua alikuwa katika usingizi
mzito.
“ Kwisha habari yake” akawaza Peniela na
kuinuka akaelekea chooni akakigonga kile kifaa
cha kuwasiliana alichokiweka sikioni.
“ Hallow Mathew,can you hear me?!!!
Akauliza Peniela.
“ Ndiyo Peniela.Tumesikia kila
kilichoendelea hapo ndani.Good job” akasema
Mathew
“ Ahsante.Kama mlivyosikia huyu mzee
hataki nitoke humu ndani . What are we going to
do? Tunatakiw akuonana na Deus Mkozumi,right?
“ Usijali kuhusu hilo tutatafuta namna
nyingine ya kufanya kuweza kuonana na Deus
Mkozumi ila kwa sasa wewe endelea kukaa humo
humo ndani kama anavyotaka.Endelea kumfanya
akuamini tena na wakati ukiwa hapo ndani jaribu
kutafuta chochote kinachoweza kutusaidia katika
mpango wetu wa kukipata kirusi Aby” “ Sawa Mathew,nitafanya nhivyo ila kesho
nitamtuma Kareem alete ule mzigo hapo
nyumbani. Mathew,tutawasiliana kesho.Good
night”akasema Peniela na kurejea chumbani
ambako Dr Joshua alikuwa amelala fofofo.
“ Nini kinafuata baada ya hapa? Akauliza
Anitha wakiwa ndani ya gari baada ya Peniel
kumaliza kuongea na Mathew
“ Tunarudi nyumbani kwani Peniela hawezi
kutoka mle ndani leo,kwa hiyo hatuna haja ya
kuendelea kukaa hapa”
“ Are you sure she’ll be ok? Ninawasi wasi
kidogo kwani mchezo anaoucheza ni wa hatari
sana.Anacheza na akili ya Dr Joshua,unadhani
nini kitatokea endapo dr Joshua atagundua kuwa
Peniela anamdanganya? Akauliza Anitha
“ Hilo haliwezi kutokea kabla
hatujakamilisha mpango wetu.Peniela ni mjanja
mno.Akili yake inafanya kazi haraka sana na
anaweza kufanya jambo lolote muda
wowote.Amenishangaza sana kwa namna
alivyoweza kubadili upepo kati ya Dr Joshua na jaji Elibariki.Ameweza kuuvaa vyema uhusika na
mtu yeyote angeweza kumuamini alichokisema”
akasema Mathew kisha wakaondoka kurejea
nyumbani.
*****************
Watu hawakuwa wengi nyumbani kwa rais
usiku huu uliko msiba wa Flaviana.Wengi wa
waliobaki ni ndugu na watu wa karibu na familia
ya rais.Anna akamuulizia Jaji Elibariki akaambiwa
kwamba ameondoka ameelekea nyumbani kwake
kupumzika
“ Nitamfuata huko huko nyumbani kwake”
akawaza na bila kupoteza wakati akaelekea katika
gari lake na kuondoka kumfuata jaji Elibariki
nyumbani kwake
“ Leo lazima nifahamu ni kitu gani
kinachoendelea kati ya baba na jaji Elibariki.Kama
alivyonieleza Mathew lazima kuna kitu
kinachoendelea kati yao.I must find out” akawaza na kuanza kuyakumbuka maneno aliyoambiwa na
Mathew
“ Kila nikiyakumbuka maneno ya Mathew
kuhusu baba,mwili wote unanisisimka.Ni mambo
mazito mno.Hatua aliyofikia baba si hatua ya
ubinadamu.Amefikia hatua ya ukatili
uliopitiliza.Amebariki mke wake na mwanae
wauawe kwa sababu ya pesa???..!! Atapata raha
gani kama atazipata hizo pesa lakini hana mtu wa
kutumia naye? Ni ujinga mtupu” akawaza Anna
akiwa katika mwendo mkali akielekea nyumbani
kwa jaji Elibariki
“ Kwa kila nitakavyoweza lazima nimsaidie
Mathew kuhakikisha baba na genge lake wote
wanafikishwa katika vyombo vya sheria ili na
kupata dhabu stahiki.Siwezi katu kulifumbia
macho suala hili kwa vile muhusika mkuu ni baba
yangu.Nitapambana bega kwa bega na Mathew
mpaka tuhakikishe tunashinda” akawaza Anna na
sura ya Mathew ikamjia kichwani
“ Mathew ni mtu shujaa ambaye anastahili
sifa za kipekee kabsa.Ameweza kufukunyua na kugundua mambo mazito kama haya .Lazima
nimuunge mkono.Nadhani nikiwa karibu naye
nitafahamu mambo mengi zaidi.Anaonekana ni
mtu anayefahamu mambo mengi sana mabaya
yanayofanywa na watu mbali mbali wa hapa
nchini.Natakwa kutafuta namna ya kumfanya
aniamini.Halafu kuna kitu Kareem aliniambia ,eti
Mathew na Anitha ni mtu na mpenzi wake.Kuna
ukweli wowote katika hili? Nitamuuliza Mathew
nikionana naye” akawaza
“ Lakini kwa nini nifuatilie mambo binafsi ya
Mathew na Anitha? Kama ni wapenzi mimi
inanihusu nini? Kazi yangu mimi ni kumsaidia na
kuhakikisha tunawafikisha mbele ya sheria baba
na mtandao wake.Lakini mhhh!!Mathew
amenivutia sana.He’s real a gentleman.Anajiamini
na kwa namna nilivyomsoma kwa haraka ni
mwanaume ambaye hana tamaa na wanawake
kama hawa wanaume wengine ..”
Anna aliwaza mambo mengi sana akiwa
njiani kuelekea nyumbani kwa jaji Elibariki.Alifika
katika makazi ya jaji Elibariki ,akasimamishwa na askari wawili wenye silaha ..kulikuwa na ulinzi
mkali eneo lile.Anna akawasalimu askari wale na
kujitambulisha kwao.Mmoja wa askari wale
akaenda kumfahamisha jaji Elibariki kuhusu ujio
wa Anna.Jaji Elbariki akatoa ruhusa Anna
aruhusiwe kuingia ndani.Anna akashuka garini na
kulakiwa na jaji Elibariki akamkaribisha sebuleni.
“ I’m sorry Anna,sina kinywaji kingine
chochote kikubwa humu ndani zaidi ya hii whysky
ninayokunywa” akasema jaji Elibariki ambaye
macho yake yalikuwa mekundu kwani toka
aliporejea amekuwa akinywa pombe kali
“ Usijali Elibariki hata kama kungekuwa na
vinywaji nisingekunywa.Look,Im here for one
reason only.I want to know whats going on
between you and my father? Akauliza
Anna.Elibariki akamtazama kwa sekunde kadhaa
na kusema
“ Anna imekuwa vizuri umekuja .Kuna
mambo kadhaa ambayo nataka tuongee na
itakuwa vyema kama tutautumia usiku hu wa leo
kuongea kila kile kinachotuhusu lakini kabla sijasema chochote naomba kwanza nitumie nafasi
hii kukupa pole sana kwa kifo cha dada
yako.Nimeumizwa mno kwa kifo cha mke wangu”
akasema Elibariki na kuinamisha kichwa.
“ Elibariki I think you know me,huwa si mtu
wa kutaka hadithi nyingi.Nahitaji uende moja kwa
moja kujibu swali langu nililokuuliza,whats going
on between you and my father? Jeshi la polisi
walitangaza msako mkali dhidi yako kwa
kusababisha kifo cha Flaviana.Nikiwa Afrika ya
kusini nilikupigia simu na ukanihakikishia kwamba
hauhusiki kabisa na hicho kinachodaiwa na jeshi
la polisi halafu nikakuuliza kama baba anahusika
katika matukio ya vifo vya mama na dada
ukakubali kwamba ni kweli baba ndiye muhusika
mkuu wa vifo hivyo na kwamba hata wewe
umejificha kuepuka kuuawa kwa vile tayari
unayafahamu madhambi ya baba.Ghafla bila
kutegemea umeibuka toka mafichoni na
unaonekana ukiwa umeongozana na baba mtu
ambaye ulidai anataka kukuua.Na kama
haitoshi,jeshi la polisi lililokuwa linakusaka kwa udi na uvumba wanadiriki kujitokeza mbele ya
watanzania na kukusafisha kwamba ulikuwa
umetekwa na majambazi na kwa hiyo tuhuma
ulizokuwa ukitafutwa kwazo hauhusiki
nazo.Nataka uniondolee hizi picha picha kichwani
kwangu na unieleze ukweli wa nini kinaendelea
kati yako na baba? Nataka unieleze ukweli
wote.You know I do trust you with all my heart so
tell me nothing but the truth.Nataka ukiri tena ile
kauli yako uliyonieleza kwamba baba anahusika
na vifo vya mama na dada.If you real love my
sister you are going to tell me the truth”
Jaji Elibariki akanywa whysky halafu
akainamisha kichwa na alionekana kuzama katika
mawazo mengi.Baada ya ya kufikiri kwa muda
akasema
“ Ok I’m going to tell you the truth”
Jaji Elibariki akainamisha tena kichwa
alionekana kuwa katika majonzi mazito…
“ Anna kwanza kabisa nataka nikiri tena
kwamba yale maneno niliyokwambia ukiwa afrika
kusini kuhusiana na baba yako ni ya kweli kabisa.Yeye ndiye muhusika mkuu wa vifo vya
mama na dada yako.” Akanyamaza akainamisha
kichwa kidogo halafu akainua kichwa na
kumuelea Anna kila kitu kilichotokea toka mama
yake alipofariki .Maneno aliyoyasema jaji Elibariki
ni sawa na yale yale kama Anna aliyoambiwa na
Mathew.
“Kwa hiyo Anna hivyo ndivyo ilivyokuwa”
Mathew akaendelea
“ Baada ya Dr Joshua na kundi lake
kugundua kwamba tayari nimefahamu
wanahusika katika kifo cha Dr Flora wakasuka
mpangowaniue.Nilinusurika katika shambulio
lililoratibiwa na mtandao wa Dr
Joshua.Nawashukuru sana Mathew na wenzake
kwa jitihada zao hadi leo niko hai” akainama
akawaza kidogo kisha akaendelea kumsimulia
Anna kila kitu bila kumficha.UKimya ukatanda
pale alipomaliza.Anna alimtazama Elibariki kwa
jicho la chuki “Kwa hiyo Anna baada ya matukio haya
yote nikajikuta maisha yangu yakibadilika ghafla”
akaendelea jaji Elibariki
“ Sikuwa na muelekeo na nilipoteza kila kitu
katika maisha yangu.Niliishi bila kuifahamu kesho
yangu.Kwa ufupi nilikuwa nimekwama na sikuwa
na namna nyingine ya kujikwamua ili maisha
yangu yasonge mbele kwani nilikuwa sawa na
mtu asiye na uhai na ndipo nilipoamua kufanya
jambo ambalo kila ninapolifikiria nahisi kama
moyo wangu unakatwa katwa na kisu kikali”
akasema jaji Elibariki na kuinama akashika mahali
ulipo moyo wake
“ Moyo unaniuma sana kwa jambo
nililolifanya” akasema jaji Elibariki
“ Ulifanya nini” akauliza Anna
“ Baada ya kuona nimekwama na maisha
yangu yamekwama nililazimika kutafuta namna ya
kujikwamua na njia pekee ya kurejesha tena
maisha yangu ni kwa kujisalimisha kwa Dr
Joshua.Niliwasaliti wenzangu na kwa kumtumia
Rosemary Mkozumi ambaye nilimfungua toka
mahala pa siri alipokuwa amefichwa na
Mathew,nilifanikiwa kuonana na Dr Joshua
,nikaongea naye na ili anisamehe nikalazimika
kumueleza kila mpango mimi na wenzangu
tuliokuwa tumeupanga dhidhi yake.Dr Joshua
alifurahi kwa niliyomuleleza akanisameheh
tukaufungua ukurasa mpya.I’m free now”
Anna akamtazama kwa hasira na kusema
“ Hukupaswa hata kumuoa dada yangu mtu
kama wewe.Kwa nini ukafanya jambo kama hilo la
kijinga Elibariki? Baada ya kufahamu yote ambayo
baba ameyafanya na hadi kuhusika katika
kusababisha kifo cha mkeo kwa nini badala ya
kumfikisha mbele za sheria ukawageuka wenzako
na kuungana na muuaji? Wewe na yeye nyote
mko sawa..You are both monsters!!! Akasema
Anna
“ Yes I’m a monster!! Akasema kwa ukali
jaji Elibariki.
“ I had no choice.Nilifanya kile ambacho
mtu yeyote kama angekuwa mahala pangu
angekifanya.Hupaswi kunilaumu mimi kwani niFlaviana ndiye aliyeniingiza katika vita dhdi ya
rais na baada ya kufariki sikuona sababu ya
kuendeleza vita ile ambayo hata ningefanya nini
nisingeshinda,nikaamua kujisalimisha”
“Is that all you wanted ?only to be free”
akauliza Anna
‘” Nilichokuwa nakihitaji sana nI kuwa huru
ili niendelee na maish a yangu ya kawaida lakini
baada ya kumueleza Dr Joshua mambo yale
makubwa yaliyopangwa dhidi yake amefanya
maamuzi .Anataka niwe rais ajaYe wa Tanzania
baada ya yeye kumaliza muda wake wa uongozi”
akasema jaji Elibariki huku akitabasamu kidogo
“ What??!! Anna akapatwa na mshangao
mkubwa
“ Tell me it’s a lie!! Akasema
“ Its true Anna.I’m going to be the next
president” Anna aliyekuwa amekunja sura
akalazimika kutoa kicheko kidogo.
“ Ama kweli dunia inaelekea ukingoni.You
?? Next president?? That cant be” akasema Anna “ Anna utake usitake nitakuwa rais wa
jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya
baba yako kumaliza muda wake hiyo ni ahadi
aliyonipa.Kwani siwezi kuongoza nchi? Akauliza
Elibariki
“ Kama umeshindwa kuvumilia na
ukawasaliti wenzako itakuwa nchi? Si utaiuza nchi
na watu wake wewe?? Hebu acheni hayo
masihara “
“ Si masihara Anna.Hili ni jambo la kweli na
ndivyo itakavyokuwa”
“ Hivyo ndivyo baba alivyokudanganya?
“ Hajanidanganya .He’s going to make me
the next president .Right now I’m the only one he
trust the most”
“ Elibariki kitu gani kimekuingia kichwani na
kukubadilisha kiasi hiki? I know me and you we
never seen eye to eye but down deep I know you
are a good guy,what turns you to a monster?
“ I’m serving a monster so I have to be a
monster too!! Akasema jaji Elibariki kwa sauti ya
juu akionekana kukerwa na maneno yale ya Anna “ Sikiliza Anna.Hakuna ubishi kwamba
nitakuwa rais ajaye wa Tanzania kwa hiyo badala
ya kunikashifu na kunivunja moyo unapaswa
kuniunga mkono kwani mimi na wewe tuna
maisha marefu huko mbeleni”
“ What do you mean ?? akauliza Anna
akimtazama Elibariki kwa hasira
“ Sikiliza.Kwa sasa sisi sote tumewapoteza
wapenzi wetu.Umempoteza Edson na mimi
nimempoteza Flaviana hivyo basi kwa kuwa
ninaelekea kushika wadhifa mkubwa na wa juu
katika uongozi nahitaji kuwa na mwenza na kwa
vile kwa sasa uko mwenyewe basi si vibaya kama
tukianzisha mahusiano na baada ya mimi kushika
urais you are going to be the first lady” ak asema
Elibariki .Ana akamtazama kwa hasira na kusema
“ You are sick Elibariki and you need
treatment.Hivi unathubutuje kutamka maneno
kama hayo? Unafahamu kabisa kwamba
ninakuchukua sana sana na kwa hili ulilolifanya
limenifanya nikuchukie hata zaidi kwa hiyo naomba usirudie tena kunitusi kwa kunitamkia
maneno hayo ” akafoka Anna
“ Hata mimi si kwamba ninakupenda Anna
bali huo ni ushauri toka kwa baba yako na ndivyo
anavyotaka iwe.Anataka familia yake iendelee
kushika nafasi za juu za uongozi na mimi siwezi
kuipinga kauli yake”
“ You are both devils !!! I’m out of here but
I’ll come back again .Our conversation is not over
yet!!
Akasema Anna na kutoka kwa hasira hadi
katika gari lake akaondoka
“ Dah ! kweli haya ni maajabu ya
Musa.Haya mambo yanayotokea ni kama vile
filamu lakini ni ya kweli kabisa.Is my father a real
human? Akajiuliza Anna akiwa garini
“ mambo anayoyafanya baba yananipa
wasi wasi na wakati mgumu kumuelewa ni kiumbe
mwenye damu ya namna gani.Kwa kumtazama
anaonekana ni mtu mwema lakini kwa ndani ana
moyo wa kishetani.Yaani kwa tamaa ya pesa
anadiriki bila huruma kuutoa uhai wa mwanamke aliyenileta duniani ambaye nilimpenda kuliko wote
.I’ll never forgive him for that.Kwa kusababisha
vifo vya mama na dada amechukua kila kitu cha
thamani katika maisha yangu na lazima
nihakikishe hafanikiwi katika mipango yake
yoyote” akaendelea kuwaza Anna
“ Halafu kituko kingine bila hata ya aibu eti
anataka kumfanya Elibariki awe rais wa Tanzania
baada ya yeye kumaliza muda wake.Hiki ni
kichekesho kabisa.Kwa kuwa Elibariki naye
ameamua kushirikiana na baba naye pia lazima
nihakikishe anaozea gerezani.Hakuna
atakayesalimika”
Anna alifika nyumbani kwao na kukuta
tayari watu wamekwisha lala .Ni watu wachache
tu waliokuwa wamekaa kivikundi wakiongea hili na
lile huku wakiendele a na vinywaji.Alimtafuta baba
yake lakini aliambiwa kwamba alitoka muda mrefu
.Kwa kuwa alikuwa tayari na uchovu mwingi moja
kwa moja akaelekea chumbani kwake
kupumzika.Kabla ya kulala akamtumia baba yake ujumbe katika simu akamtaka waonane asubuhi
kuna jambo la maana sana anataka waongee.
*****************
Mathew na Anitha waliwasili katika makazi
yao na moja kwa moja Mathew akaenda sebuleni
akajitupa sofani .Alionekana kuwa na mawazo
mengi.Anitha akamtazama kwa sekunde kadhaa
na kusema
“ Unaonekana hutaki kabisa kupumzika
siku ya leo.Its been a long day Mathew let us take
some rest”
“ Sina hakika kama jicho langu litafumba
leo”
“ Kwa nini Mathew” Kitu gani kinakunyima
usingizi? Akauliza Anitha
“ Nitawezaje kupata usngzi wakati sina
hakika na usalama wa Peniela? Ni vipi kama Dr
Joshua atagundua wamba Peniela
anamdanganya? Suala hili linaniumiza mno
kichwa changu.I will never forgive myself if anything bad happens to Peniela” akasema
Mathew.Anitha akatumia sekunde kadhaa
kumtazama Mathew halafu akasema
“ Mathew kuna kitu nataka kukuuliza and
please be honest with me.”
“ Uliza Anitha”
“ Ni kuhusu wewe na Peniela.Nikiwatazama
ninyi wawili kuna vitu Fulani naviona kwenu
vinavyonifanya nijiulize maswali mengi.Is there
anything going on between you two?
Mathew akatabasamu kidogo na kusema
“ Hakuna chochote kinachoendelea kati
yetu.”
“ Kama hakuna kinachoendelea kwa nini
kila linapokuja suala la Peniela kutumia mbinu
yake ya kuutumia mwili waake kufankisha jambo
Fulani umekuwa unapinga sana? Unaonekana
kuumia moyoni.Do you love her?
“ Anitha its like this .Peniela ni mtu ambaye
tunamtegemea mno katika operesheni hii kwa
hiyo lazima niwe makini sana kuhusu usalama
wake.Tukimpoteza yeye tumepoteza kila kitu.Kuhusu kutembea na watu mbali mbali ili
kupata taarifa za muhimu na kufanikisha baadhi
ya mambo ni kweli imetusaidia sana lakini toka
ndani ya moyo wangu sifurahii kabisa hali
hii.Peniela hastahili maisha kama haya ya
kuutumia mwili wake kama chambo.Ni jambo la
hatari sana kwake.Ndoto yangu kubwa toka
nilipoyafahamu maisha yake ni kumsaidia aanze
maisha yake yenye staha na amani.Nataka
nimtoe na kumsahaulisha kabisa maisha yake ya
sasa.Kujibu swali lako kama ninampenda Peniela
au la,ni kwamba ninampenda Peniela kama
ndugu yangu,kama mdogo wangu,kama
binadamu wengine na si vinginevyo.Natumai
umeridhika Anitha”
“ Ndiyo Mathew na samahani sana kwa
mawazo niliyokuwa nayo juu yenu.Pamoja na
hayo narudia tena kukuomba kama una hata
chembe moja ya mawazo kuhusu kuwa na
mahusiano na Peniela naomba ufute kabisa wazo
hilo.Peniela is not good for you” “ Ahsante kwa ushauri wako Anitha”
akasema Mathew halafu ukimya ukapita
“ Mathew !! akaita Anitha
“ Kwa sasa wakati tuko peke yetu kuna
jambo nataka kulifahamu”
“ jambo gani hilo Anitha?
“ Kabla hajaaga dunia ,John Mwaulaya
alitaka kuonana nawe na mpaka leo hii hakuna
anayefahamu wewe na John mliongea kitu
gani.Mathew umekuwa ni mtu wangu wa karibu
kupita wote katika hii dunia na hata siku moja
hujawahi kunificha jambo lolote.I think I deserve to
know what you and John Mwaulaya talked”
Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ Ok nitaueleza uweli” akasema na
kunyamza tena halafu akaendelea
“ Kwanza haikuwa rahisi kukubali wito ule
wa John Mwaulaya kutokana na historia yangu
naye kuwa si nzuri.Nafsini mwangu nilichokuwa
nakiwaza ni kisasi tu.Baada ya kutafakari
nikaamua kwenda kumuona.Nilipofika nilikuwa na
hasira na akalitambua hilo akaniomba nisiwe na
hasira kwani anayotaka kunieleza ni ya muhimu
sana kwangu” Mathew akatulia baada ya sekunde
kadhaa akaendelea
“ Kwanza alianza kwa kuniomba samahani
kwa kile kilichotokea wakati ule na kusababisha
mimi na yeye kuwa maadui.John alikuwa katika
maumivu na alikuwa anapumua kwa
shida.Nilimuonea huruma nikamtaka anieleze
alichoniitia pale.Aliniambia kwamba kuna mambo
mawili ,kwanza ni kuhusu Peniela.Alisema
kwamba yeye atakufa na hataweza kuitimiza
ndoto yake ya kubadili maisha ya Peniela kwa
kumtoa Team SC41 ili aweze kuishi maisha ya
kawaida .Alikiri kwamba alikosea sana
kumuingiza Peniela Team SC41 na kuziharibu
ndoto zake nyingi za maisha.kwa hiyo alinikabidhi
mimi jukumu la kwaza kuhakikisha ninamsaidia
Peniela atoke Team SC41 na pili kuhakikisha
Team SC41 inatoweka katika ardhi ya
Tanzania.Kuhusu Peniela aliniambai kwamba
kuna mamo ya siri yanayomuhusu ambayo
ameyaweka katika kisanduku alichompatia akihifadhi.Alisisitiza kwamba katika kisanduku
hicho kuna mambo muhimu na ya msingi ambayo
hatakiwi mtu mwingine kuyafahamu zaidi ya
Peniela na mimi.Alirudia kunisisitiza kwamba
nimlinde Peniela zaidi ya mboni yangu ya jic ho
kwani ni binadamu mwenye thamani kubwa
.NIlimtaka anifafanulie ana maanisha nini kwa
kauli hiyo akasema kwamba kila kitu alichokisema
kimo ndani ya sanduku alilompa
Peniela.Alinielekeza kwa Askofu Edmund Dawson
kwamba ni mtu muhimu na msaada mkubwa
kwetu.Alinipa maelekezo namna ya kufika kwa
askofu Edmund ambaye ndiye aliyetusaidia hadi
hapa tulipofika” akatulia kidogo kisha akaendelea
“ John Mwaulaya alinieleza jambo lingine
linalonihusu mimi” akasema Mathew
“ Jambo gani hilo? Akauliza Anitha.Mathew
akainamisha kichwa
“ tell me Mathew.Ni jambo gani hilo
alilokwambia John?
“ John…John..” Mathew akababaika “ Niambie Mathew.John alikueleza nini?
akasisitiza Anitha ,akaingiwa na hofu
akamsogelea Mathew karibu zaidi
“ Mathew kuna tatizo gani? John alikueleza
nini?
“ Its about my family”
“ Alikueleza nini kuhusu familia yako?
“ Familia yangu bado iko hai.My wife and
children are all still alive”
“ Whats ?? Anitha akashangaa
“ No ! that’s not true.Ulitueleza kwamba
familia yako yote iliteketea kwa moto”
“ Hata mimi nilijua hivyo lakini kumbe
haikuwa hivyo.”
“ What real happened?haya mbona kama
mazingaombwe? Waliotekete katika nyumba yako
kama si familia yako ni akina nani basi?
“ John alisema kwamba lengo lao lilikuwa si
kuiteketeza familia yangu kwani hawakuwa na
kosa ila walitaka kunichanganya akili kwa
kunifanya niamini familia yangu iliteketea kwa
moto ili wanikamate kirahisi.Alisema kwambawatu waliokutwa wameteketea mle ndani yan
nyumba ni maiti walizozitoa katika chuo kikuu cha
utabibu.Kwa hiyo Anitha familia yangu iko salama
kabisa”
“ Jesus Christ !! Anitha akapatwa na
mshangao mkubwa
“ So where are they now?
“ Wanaishi Marekani .Alinipa anuani ya
mahala wanakoishi endapo nitahitaji
kuwatafuta.Kwa bahati mbaya…” Mathew
akainaisha kichwa
“ bahati mbaya gani tena Mathew?
“ Its complicated” akasema Mathew
“ How ?
“ Mke wangu tayari amekwisha olewa na
ana watoto wengine wawili kwa mume wake wa
sasa.”
“ Oh jamani….! Nimeishiwa maneno ya
kuongea.Dunia hii imejaa watu makatili sana.kwa
nini wakakufanyia hivi Mathew? I hope right now
John Mwaulaya is burning in hell for all that he did
” akasema Anitah kwa hasira “ Naye mkeo kwa nini alikubali kuolewa
tena? Nini hasa kilimshawishi afanye hivyo?
Akauliza tena
“ John alikuwa ni mtu mwenye roho mbaya
lakini katika hili ninamshukuru kwani
hakuiteketeza familia yangu.Alikuwa na uwezo wa
kuwateketeza wote lakini akaingiwa na moyo wa
huruma akawaacha hai na kuwatafutia mahala
kwingine kwa kuishi nje ya nchi ambako wanaishi
maisha yaliyojaa furaha hivi sasa.Mke wangu
naye sipaswi kumlaumu kwa sababu sielewi ni kitu
gani hasa kilichomfanya anisahau na aamue
kuolewa tena” akasema Mathew na kuinama
chini.Anitha akasema
“ So what are you going to do? When this is
over are you going to find them?
“ I cant..They’ve moved on with their life
and they are happy.Sitaki kuyavuruga maisha yao
ya furaha waliyonayo sasa”
“ Mathew una hakika hutaki kuwatafuta na
kufahamu kilichosababisha mkeo aamue kuolewa
tena? Anitha kwa sasa tuna kazi moja tu kubwa
iliyoko mbele yetu,kirusi Aby kiko katika hatari ya
kutua kwenye mikono isiyo salama ya watu
wenye lengo la kufanya maangamizi makubwa
.Me ,you,peniela and Anna we’re the only people
who can save the world.Tunatakiwa kufanya kila
tuliwezalo kuiokoa nchi yetu na dunia toka katika
maangamizi makubwa yanayoweza kutokea
endapo kirusi Aby kitasambaa hewani.Ni jukumu
zito sana kutokana na watu tunaopambana
nao.Baada ya kulikamilisha jukumu hilo ndipo
hayo mambo mengine yatafuata ila kwa sasa
nataka akili yangu niielekeze sehemu moja tu
mambo ya familia yatafuata baadae kwa hiyo
naomba tusiongee chochote kuhusiana na suala
hilo la familia.” Akasema Mathew
“ Sawa Mathew nimekuelewa ila naomba
uniahidi kwamba baada ya mambo haya
kumalizika mimi na wewe tutapata wasaa wa
kuzungumzia suala hili “
“ sawa ninakuahidi hivyo Anitha” “ Thank you.Now let us g to sleep.I’m
sleeping with you tonight”
“ Nini ? Mathew akashangaa
“ Mbona umeshangaa Mathew niliposema
kwamba nitalala nawe usiku wa leo?
“ Lazima nishangae Anitha.Kwa nini tulale
wote wakati k ila mmoja ana chumba chake?
“ Mathe I’m sorry to say this but you and I
we’ve been in a sea of loneliness.Toka
tumefahamiana sijawahi kukuona hata mara moja
na mwanamke halikadhalika hujawahi kuniona au
kusikia nina mpenzi.Sote tulichagua kuishi
maisha haya ya upweke kutokana na mambo
tuliyoyapitia.Baada ya kifo cha Noah nilijifunza
kwamba maisha ni zawadi na ni mafupi
sana.Noah died so yung.What happened to Noah
can happen to us at anytime”
“ Unamaanisha nini Anitha?
“ Ninamaanisha kwamba tumeelekeza
nguvu na akili zetu zote katka kazi na tumejisahau
wenyewe.Kazi zetu zina mafanikio na tunapata
pesa nyingi za kutuwezesha kuishi maisha mazuri but we’re not happy.All we think day and night is
work,work,work,nothing else.Kama si kwa nguvu
ya Mungu pengine hivi sasa ningekwisha kuwa
marehemu.Tayari Rosemary angekwisha
niua.Baada ya kunusurika katika mikono ya Yule
shetani mla watu, nimefanya maamuzi.” Akatulia
kidogo na kuendelea
“ Baada ya mambo haya kukamilika vizuri
na kama tutajaaliwa kubaki salama nitaachana na
hizi kazi.Nataka kuanza aina mpya ya maisha .I’m
dreaming to have a family and be
happy.”akasema Anitha.Ilimkuchukua Mathew
zaidi ya dakika moja kusema chochote kuhusiana
na kauli ile ya Anitha
“ I’m glad to hear that.Its a good
idea.Unachokisema ni cha kweli kabisa.Mawazo
yako ni kama ya kwangu.Hata mimi zaidi ya mara
moja nimekuwa nafikiria kuachana na shughuli
hizi na kuanza maisha mapya”
“ Wow Mathew.Ahsante sana kama nawe
umeliona hilo .We both need to be happy
again.Kwa kuwa sote tuna mawazo yanayofanana,tonight we’re going to sleep
together We weed to comfort each other.Please
Mathew don’t say no to this.I need someone to
comfort me tonight so do you.I need strong arms
to hug me tight tonight and tell everything will be
ok.I need you Mathew” akasema Anitha.Mathew
akajikuta akishindwa kumkatalia Anitha kwani
naye alihisi kuhitaji faraja kwa usiku ule..
Tukutane sehemu ijayo...
“ Wow Mathew.Ahsante sana kama nawe
umeliona hilo .We both need to be happy
again.Kwa kuwa sote tuna mawazo yanayofanana,tonight we’re going to sleep
together We weed to comfort each other.Please
Mathew don’t say no to this.I need someone to
comfort me tonight so do you.I need strong arms
to hug me tight tonight and tell everything will be
ok.I need you Mathew” akasema Anitha.Mathew
akajikuta akishindwa kumkatalia Anitha kwani
naye alihisi kuhitaji faraja kwa usiku ule..
Endelea.....
Tayari usingizi ulikwishaanza kumchukua
Peniela lakini alifumbua macho baada ya kusikia
mlio wa simu ya mkononi mle chumbani.Akainuka
na kumtazama Dr Joshua aliyekuwa amelala
fofofo anakoroma.Akainuka taratibu na kuzifuata
nguo za Dr Joshua ambako mlio ule wa simu
ulitokea.Ndani ya koti akatoa simu na ilionyeshga
mpigaji alikuwa ni Abel Mkokasule
“ Abel Mkokasule,ni nani h uyu? Akajiuliza
Peniela na kwenda kumuamsha Dr Joshua
ambaye alifikicha macho na kutazama katika kioo cha simu na alipoona jina la mpigaji akainuka
haraka haraka na kubonyeza kitufe cha
kupokelea.
“ Hallow Abel” akasema Dr Joshua
“ Mzee samahani kwa usumbufu”
“ Bila samahani Abel”
“ Mzee nimekupigia kukutaarifu kuhusu Dr
Kigomba na Jacob Kateka.” Akasema Abel
Mkokasule .Dr Josha akagundua kwa sauti ya
simu ilikuwa kubwa na Peniela alikuwa akisikia
walichokuwa wanakiongea ,akainuka pale
kitandani na kwenda chooni hakutaka kabisa
Peniela kusikia chochote.
“ Nipe taarifa Abel” akasema Dr Joshua
“ Dr Joshua tumeendelea na zoezi la
kumfuatilia Dr Kigomba na usiku huu amekuwa na
maongezi marefu na Jacob Kateka hapa
Mananzana Royal Club.Mzee hisia zako zinaweza
kuwa sawa kutokana na maongezi yao yalivyo
wanaonekaa kuna kitu kikubwa wanakipanga.”
Dr Joshua akavuta pumzi ndefu na kusema “ Mmeweza kunasa sauti zao kufahamu
wanachokiongea?
“ Hapana mzee hatujafanikiwa kwa hilo
lakini wanaonekana kujadili mambo kwa kina
sana.Kama kuna jambo wanalipanga basi
litakuwa kubwa”
Dr Joshua akafikiri tena kidogo na kusema
“ Sikiliza Abel”
“ nakusikiliza mzee” akasema Abel
“ Edeleeni kuwafuatilia na watakapoondoka
hapo ,take down Jacob Kateka but do it ina
professional way,make it like an accident”
“ What about Kigomba? Akauliza Abel
“ Kigomba muache kwa sasa.Abel nataka
tukio hilo liwe ni habari kuu ya kesho
asubuhi.Umenielewa?
“ Nimekuelewa mzee,tutalitekeleza kama
ulivyoagiza”
“ Good” akasema Dr Joshua na kukata
simu
“ Nikiwachia Kigomba na Jacob wanaweza
kuniharibia kila kitu.Lazima niwawahi kabla hawajaniwahi.Jacob nimekuwa namtafuta siku
nyingi kwani ni mtu ambaye hatuelewani na
amekuwa akinifuatilia sana katika shughuli zangu
sasa Muda wake umefika na lazima nimuondoe”
akawaza Dr Joshua na kutoka mle chooni na
kuelekea moja kwa moja zilipo nguo zake
akaanza kuvaa
“ Peniela I have to go now” akasema
“ Ouh Dr Joshua my love kwa nini
usiendelee kukaa nami hadi asubuhi? I need you
darling”
“ Peniela mimi ni rais na muda wote niko
kazini.Kuna masuala muhimu natakiwa
kuyashughulikia usiku huu.Tutaonana kesho
jioni.Nitakuwa na wageni wangu muhimu kesho
jioni hapa hapa kwa hiyo baada ya kuzungumza
nao nitapata tena wasaa wa kukaa nawe
ikiwezekana hadi asubuhi.Usalama hapa ni
mkubwa na kesho asubuhi Kareem atafika hapa
kuhakikisha unakuwa salama na unapata kia
unachokihitaji ila naomba uzingatie jambo
nililokueleza kwamba usithubutu kutoka humu ndani hadi hapo nitakapokuruhusu.Lengo langu ni
kukutengenezea mazingira mazuri ya maisha na
usalama wako kwani wewe ni mke wa rais ingawa
bado si rasmi.” Akasema Dr Joshua huku akivaa
nguo zake.Peniela akambusu wakaagana
akatoka.Dr Joshua akatoa maelekezo ya kubaki
askari wawili kulinda nyumba ile na kuhakikisha
Penila anakuwa salama.
“ Kama si Peniela kuniamsha baada ya
Abel kupiga simu ningejikuta nimelala hadi kesho
saa mbili asubuhi.Na hii imesababishwa na
mambo aliyonifanyia Peniela.Yule mmwanamke
anajua mno kunipa raha.Anajua kucheza na mwili
wangu.Naapa sintomuacha Peniela hata
iweje.Yeye ndiye mwanamke pekee ambaye
ninataka kuishi naye baada ya kumaliza kipindi
changu cha uongozi lakini…” Akawaza Dr Joshua
na kitu Fulani kikamstua alipokikumbuka
“ Yale maneno aliyonieleza Peniela kuhusu
Elibariki ni ya kweli? Nani nimuamini kati ya
Elibariki na Peniela? Akajiuliza “ lakini namuamini Peniela Hawezi
kunidanganya.Maneno yote aliyonieleza Elibariki
ni ya uongo kutaka kunifarakanisha na
mwanamke ninayempenda kumbe wao ndio
wenye nia ovu na mimi.Elibariki ni chui mwenye
ngozi ya Kondoo.Sikupaswa kabisa
kumuamini.Hata mimi ni likuwa na mashaka naye
sana.Kumbe yeye na Rosemary Mkozumi
wanashirikiana kunihujumu? Hili ninaweza kabisa
kuliamini.Dah ! yaani kila mtu anayenizunguka ni
msaliti nani nitamuamini? Kigomba nae
nilimuamini mno lakini kumbe naye ana mipango
yake ya siri ya kunizunguka na Jacob
Kateka.Haya yote yanatokea kwa sababu ya
kirusi kile.Nahisi kina laana na ndiyo maana toka
nilipoanza mchakato wa kukiuza matukio
yamekuwa yanatokea mfululizo.Nimempoteza
mke wangu,mwanangu na watu wangu wa karibu
niliowaamini kama Captain Amos ambao
waligeuka wasaliti.Ngoja nifanye haraka haraka
nimpatie Hussein mzigo wake ili nipate nafasi
nzuri ya kulishughulikia lile suala la serikali ya Marekani” akawaza Dr Joshua akiwa garini
kurejea nyumbani.
“ Abel Mkokasule ….” Peniela akasema
kwa sauti ndogo akiwa amekaa kitandani baada
ya Dr Joshua kuondoka.
“ Ni nani huyu Abel Mkokasule? Kabla Dr
Joshua hajainuka na kwenda kujificha bafuni
nilisikia huyo mtu anasema kwamba anataka
kumpa taarifa kuhusu Kigomba na Jacob
Kateka.Who is Jacob Kateka? Ana mahusiano
gani na kigomba? Is Dr Joshua spying on
Kigomba? Nahisi hivyo.Kama ni kweli Dr Joshua
anamchunguza Kigomba ambaye ni mshirika
wake wa karibu basi lazima kuna jambo
linaendelea kati yao.Mathew anatakiwa
kulifahamu jambo hili alifanyie uchunguzi “
akawaza Peniela na kulala.
****************
Mlio wa simu ulimuamsha Dr Joshua toka
usingizini.Tayari imekwisha timu saa kumi na dakika nane za alfajiri.Mpigaji alikuwa ni Dr
Kigomba.
“ Hallow Kigomba” akasema Dr Joshua
Mheshimiwa samahani kwa kukupigia
muda huu bu I have a bad news” akasema Dr
Kigomba
“ Kuna taarifa gani mbaya Kigomba?
“ Nimepigiwa simu sasa hivi Jacob Kateka
mkuu wa idara ya usalama wa taifa amepata ajali
mbaya usiku huu wakati akirejea nyumbani kwake
na inasemekana yeye na dereva wake hali zao ni
mbaya sana na tayari wamekimbizwa hospitali
.Mimi niko njiani sasa hivi naelekea huko hospitali
kupata uhakika wa hali zao”
Dr Joshua akavuta pumzi ndefu akakaa
kimya kidogo na kusema
“ Hizi ni taarifa za kustusha sana
.Nashangaa kwa nini mpaka sasa sijataarifiwa
kuhusu suala hilo.Naomba unipe taarifa za hali
zao mara tu utakapowasili hospitali ” akasema Dr
Joshua “ Sawa mzee nitakutaarifu mara moja
nitakapofika hospitali” akasema Dr Kigomba na
kukata simu.Dr Joshua akatabasamu
“ Good job Abel.Napenda sana kuwatumia
vijana wachapakazi kama huyu.Kazi yoyote
ukimpatia unakuwa na uhakika itakamilika kama
unavyotaka.I hope Jacob is dead.Mipango yao
yote waliyoipanga na Kigomba imekwama na
ndiyo maana Kigomba amechanganyikiwa .Na hii
ni taa nyekundu kwake asipobadilika naye lazima
nitamuondoa.He should never try to cross me !!”
Dr Joshua akainuka kitandani na kwenda katika
kabati dogo zilimo chupa kadhaa za mvinyo
,akamimina mvinyo mkali katika glasi na
kugugumia wote huku amefumba macho
“ Sasa baada ya Jacob ,watakaofuata ni
Elibariki na mshirika wake Rosemary
Mkozumi.Hawa wawili wanajifanya wema kwangu
kumbe ni nyoka wa vichwa viwili.Hawa nao
natakiwa kuwaondoa haraka sana” akawaza Dr
Joshua na kuchukua simu akampigia Abel
Mkokasule “ Hallow mzee” akasema Abel baada ya
kupokea simu
“ Abel nimepokea taarifa usiku huu kuhusu
Jacob”
“ Samahani mzee kwa kutokutaarifu
mapema kuhusu kazi uliyonituma hadi ukapata
taarifa toka kwa watu wengine.”
“ Usijali kuhusu hilo.You did a good
job.Nashukuru sana kwa kazi uliyoifanya.Hata
hivyo bado nataka uendelee kuwafuatilia
Kigomba na jaji Elibariki.Kwa jaji Elibariki nataka
uchunguze anakutana na akina nani na halafu
nitakupa maelekezo nini cha kufanya”
Sawa mzee nitafanya hivyo.” Akajibu Abel
“ Once again,thank you Abel.Thank you so
much.” Akasema Dr Joshua na kukata simu na
ndipo akakumbuka kusoma jumbe kadhaa katika
simu yake ambazo hakuwa amezisoma
bado.Moja ya ujumbe ulitoka kwa Anna ,akimtaka
waonane asubuhi kuna jambo la muhimu la
kuzungumza. “ Anna mwanangu amebaki na ukiwa
mkubwa sana baada ya kuondokewa na mama na
dada yake.Natakiwa kufanya kila linalowezekana
kuhakikisha kwamba anakuwa na furaha tena”
akawaza Dr Joshua na kurejea tena
kitandani.Baada ya dakika kumi Dr Kigomba
akampigia simu na kumtaarifu kwamba Jacob
Kateka na dereva wake wamefariki dunia mara tu
baada ya kufikishwa hospitali.Uso wa Dr Joshua
ukachanua kwa tabasamu .
***************
Mlango wa chumba cha Anna ukagongwa
akainuka na kwenda kuufungua akakutana na
baba yake wakasalimiana kisha Anna akawaomba
radhi marafiki zake watatu waliokuwamo mle
chumbani kumfariji watoke kidogo kwani ana
maongezi muhimu na baba yake.
“ Vipi maendeleo yako Anna? Akauliza Dr
Joshua baada ya kubaki wawili mle chumbani “ Ninaendelea vizuri japokuwa siko sawa
kama nilivyokuwa kabla ya matukio haya mfululizo
kutokea.” Akasema Anna
“ Yes I k now.Hii ni mipango ya Mungu na
mafundisho yanatufundisha kwamba tujifunze
kushukuru kwa kila jambo.Tushukuru kwa haya
yaliyotupata katika familia yetu.Anna haya ni
mapito tu katika maisha and I promise you that Im
with you and we’ll get through this together.’
Akasema Dr Joshua
“ Muangalie kwanza anavyoongea kama
malaika lakini kumbe ni shetani mwenye mkia”
akawaza Anna akimtazama baba yake kwa
macho makali
“ Anna leo tunamalizia shughuli za hapa na
tutarejea ikulu kuendelea na maisha yetu ya
kawaida.Asubuhi hii tutakwenda kuwasha
mishumaa katika kaburi la dada yako halafu
tutarejea hapa kumaliza taratibu kisha tutakwenda
ikulu.Nimepata ujumbe wako unasema kuna
jambo la muhimu la kuongea.I’m here now tell me” “ Ndiyo baba kuna jambo nataka
tuzungumze” akasema Anna
“ Ok karibu .I’m here to listen”
“ Ni kuhusu Elibariki” akasema Anna na
kumstua Dr Joshua
“ Nimeonana na jaji Elibariki jana
usiku.Nilitaka kufahamu kuhusu kilichotokea
kwani siku chache zilizopita alikuwa anatafutwa
na jeshi la polisi kwa kusababisha kifo cha dada
lakini ghafla amejitokeza toka mafichoni na
zikafuata taarifa toka jeshi la polisi kwamba
alikuwa ametekwa na majambazi waliokuwa
wanamtumia kwa lengo la kujipatia fedha na
akafanikiwa kutoroka.” Anna akanyamaza kidogo
akameza mate kulainisha koo lakini kabla
hajaendelea Dr Joshua akasema
“ Do you believe him?
“ Yes I do.I believed him because you did
too” akasema Anna
“ Good” akajibu Dr Joshua kwa sauti ndogo “ Kuna kitu Elibariki aliniambia ambacho
kimenifanya nitake kuonana nawe asubuhi hii ya
leo” akasema Anna
“ Amekwambia kitu gani? Akauliza Dr
Joshua kwa sauti yenye kuonyesha wasi wasi
kidogo
“ Ameniambia kwamba umemuahidi
atakuwa rais wa Tanzania baada ya wewe
kumaliza kipindi chako cha uongozi.Is that true?
“ You know uhhmmm…I.. I Told hime that
in order..” Dr Joshua akajikanyaga katika kujibu
swali lile
“ Kama hiyo haitoshi Elibariki aliniambia eti
mmepanga mimi na yeye tuwe na mahusiano na
tuoane.Hilo nalo ni la kweli?
“ Listen my dear Anna,alichokwambia
Elibariki ni kitu cha kweli kabisa.Ni kweli alikuwa
ametekwa na majambazi ambao walimtumia
kutaka kujipatia pesa.Baada ya kufanikiwa
kuwatoroka alinifuata akanieleza nami nikampigia
simu mkuu wa polisi kanda ya Dar es salaam
nikamueleza kuhusiana na watu hao na usiku huo huo polisi wakapambana na watu hao
wakafanikiwa kuwaua baadhi na wengine
wakatoroka na hadi sasa msako unaendelea.Kwa
kitendo cha kishujaa alichokifanya niliona ni mtu
anayefaa kabisa kuwa mrithi wangu baada ya
kumaliza kipindi change cha uongozi kwani katika
chama tumeazimia sasa hivi kuwa na mgombea
kijana kabisa.Niliahidi kulifikisha suala hilo kwa
wadau ila sikumpa uhakika wa moja kwa moja
.Kuhusu yeye na wewe kuwa na mahusiano
nilifikiria hilo ili kuifanya familia yetu iendelee
kuwa katika nafasi za juu za uongozi.”
“ Kwa nini ukafanya hivyo baba? Kwa nini
ukataka kuyaingilia maisha yangu na kupanga
mambo bila kunishirikisha?I’m not a child
anymore..”
“ Anna I’m sorry .I don’t know what I was
thinking at that time.I Think I was drunk.But forget
about that because it wont happen
anymore.Siwezi tena kumfanya Elibariki awe rais
wa nchi hii.Baada ya kutafakari kwa kina nimeona
hana sifa za kuwa rais kwa hiyo sahau kabisa suala la wewe na yeye kuwa na mahusiano.”
Akasema Dr Joshua kwa ukali kidogo.Anna
akamtazama na kuuliza
“ Endapo Elibariki angekuwa chaguo lako
la kurithi kiti cha urais ,bado ungesisitiza mimi na
yeye tuwe na mahusiano”
Dr Joshua akakuna kichwa na kusema
“ Ndiyo.Ingekuwa ni kwa faida yako Anna”
“ Faida yangu? What kind of a father are
you? Yaani kulazimisha niwe katika mahusiano na
mwanaume ninayehisi kutapika nikimuona kwa
sababu ya maslahi yako unasema ni faida
yangu?Akauliza Anna kwa ukali
“ Anna tafadhali usiongee na mimi katika
lugha ya namna hiyo.I’m your father and I’m the
one who decides whats good for you so if I want
you to be with Elibariki or whoever I want you cant
say No!!! akasema D Joshua kwa ukali
“ A father? Have you been a father to us?
Where were you when me and my sister needed a
father? Muda wote unashughulika na mambo
yako yenye faida kwako..”“ Stop that Anna!! Akafoka Dr Joshua na
kusimama akamtazama Anna kwa hasira
“ Don’t you dare talk to me like that
again.Leo unadiriki kusema eti I wasn’t there
when you needed me,are you sure?? Akauliza Dr
Joshua kwa ukali.Anna hakujibu kitu
“ Anna my dear,ndani ya kipindi kifupi
familia yetu imepitia mambo magumu sana.Hii ni
mitihani na ili tuishinde mimi na wewe lazima
tushikamane.Kuna mambo mengi makubwa na
mazuri yanakuja kwa ajili yako.Wewe pekee
ndiye uliyebaki furaha yangu.Nitakulinda zaidi ya
mboni yangu ya jicho.Si muda mrefu topka sasa
nitamaliza kipindi changu cha uongozi na kwa
pamoja tutaizunguka dunia tukifurahia uumbaji wa
mwenyezi Mungu.Kitu kingine ambacho nataka
nikuahidi ni kwamba sintoingilia tena masuala
yako ya kimahusiano .Mwanaume yeyote ambaye
utampenda mimi nitamridhia kwani nahitajhi uwe
na furaha” akasema Dr Joshua .Akamtazama
Anna kwa sekunde kadhaa na kusema “ Now get ready,tunakwenda makaburini
muda si mrefu” akasema Dr Joshua na kutoka
mle chumbani .
“ Nasikitika sana kuwa na baba kama huyu
ambaye hana roho ya ubinadamu hata
chembe.Anyway siku zake zinahesabika,lazima
akumbane na mkono wa sheria.Ngoja nimjulishe
Mathew kwamba nitakwenda kuonana naye
baadae baada ya kutoka makaburini” akawaza
Anna na kumuandikia Mathew ujumbe mfupi
akimfahamisha kwamba wataonana baadae
*******************
Mlio wa ujumbe wa simu ,ulimstua Mathew
akafumbua macho.Pembeni yake alilala Anitha
.Wote walikuwa watupu
“ Dah ! siamini kama kweli nimelala na
Anitha mwanamka ambaye ni rafiki yangu
mkubwa.Sifahamu nilikuwa nawaza wapi hadi
nikakubali kufanya kitu kama hiki.Hata hivyo
baada ya miaka zaidi ya kumi kupita bila kukutana na mwanamka yeyote kimwili,usiku wa jana
niliona kama siko katika ulimwengu huu.Anitha
amenifanya nijione mimi ni mwanaume wa
shoka.Aliniondoa katika dunia ya upweke
mkubwana kunirejesha katika dunia ya
kawaida.Last night was my beautiful night ever
since I lost my wife.Anitha amenikumbusha
umuhimu wa kuwa na familia tena” akawaza
Mathew na kumtazama Anitha ambaye bado
alikuwa amelala
“ She’s beautiful.Ujuzi wake si katika
teknolojia tu bali hata kitandani mambo
anayaweza lakini sitaki turudie tena mchezo
huu.Mambo tuliyoyafanya jana usiku yataishia h
apa kwani tukiendelea tunaweza kujikuta
tumezama mapenzini na mimi sitaki kuingia katika
mapenzi na Anitha.She deserve a better man than
me” akawaza na kukumbuka kilichomstua
usingizini ni ujumbe wa simu.Akaichukua simu
akaufungua ujumbe ule uliotoka kwa Anna
akimjulisha kwamba wataonana baadae “Namuonea huruma sana Anna kwa
mambo yaliyomkuta.Baada ya kuufahamu upande
wa pli wa baba yake ameumia zaidi lakini
hakukuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya
kumueleza ukweli ili aweze kutusaidia” akawaza
Mathew na kuinuka akatoka mle chumban na
kwenda kufanya mazoezi mepesi ya viungo halafu
akaingia jikoni kuandaa kifungua kinywa..
“ Natamani kujua Penila
anaendeleaje.Endapo hadi mchana wa leo
hatakuwa ametujulisha chochote kuhusu
maendeleo yake nitakwenda kumtoa ndani ya lile
jumba mimi mwenyewe.I don’t care what will
happen ila jukumu langu ni kuhakikisha Penila
yuko salama.Lakini alisema wamba atamtuma
kareem leo alete kasha alilopewa na John
mwaulaya.Halafu siku ya leo alitakiwa aongee na
Deus Mkozui ili tuone kama anaweza kutuelekeza
chumba kilimohifadhiwa kirusi aby lakini kwa k
uwa Peniela ndiye aliyepaswa kwenda kuonana
na Deus na kwa kuwa hawezi kutoka ndani ya
jumba lile itabidi kazi hiyo niifanye mimi na Anitha.Tutakwenda kuonana na Deus Mkozumi”
akawaza Mathew wakati akiandaa mlo wa
asubuhi .Kisha maliza kuandaa akamfuata Anitha
chumbani akamuamsha.
“ Wake up pretty angel ….” Akasema
Mathew.Anitha akafumbua macho na kutabasamu
“ C’mon Mathew I was dreaming..”
akasema kwa sauti laini
“Umeiharibu ndoto yangu”
“ I’m sorry Anitha muda wa ndoto
umepita.Huu sasa ni muda wa kazi so wake up”
akasema Mathew.Anitha akainuka huku akiona
aibu kidogo kwani alikuwa mtupu.Akavaa nguo na
kumtazama Mathew
“ Thank you Mathew.Sijawahi kuwa na
usiku mzuri kama wa jana.You are real
amazing.Last night I felt like….ouh gosh I dont
know how to explain it” akasema Anitha.Mathew
akatabasamu na kusema
“ Thank you too but that wont happen again
Anitha.Let us forget what happened and pretend
like nothing happened” “ Its ok Mathew it wont happen again .Lakini
narudia tena kukushukuru kwa namna
ulivyoufanya usiku wangu kuwa mzuri.Leo
nimeamka vyema na akili yangu imetulia na tayari
kwa kazi.Lets get back to work” akasema Anitha
“ Breakfast is ready” akasema Mathew na
baada ya Anitha kujiswafi wakaelekea kupata
kifungua kinywa.
“ Any news from Peniela or Anna?
Akauliza Anitha.
“ Anna kanitumia ujumbe kanitaarifu kuwa
atakuja baadae ila kwa Peniela bado sijapokea
taarifa yoyote toka kwake kwani hakubeba
simu.Nina wasi wasi sana na usalama wake ndani
ya jumba lile”
“ She’ll be fine don’t worry.If anything
happens she can handle it” akasema Anitha
“ Lazimaniwe na wasi wasi kwa sababu
John Mwaulaya kabla ya kifo chake alinisisitiza
kwamba kwa namna yoyote ile hata ikibidi kuweka
rehani maisha yangu nihakikishe Peniela yuko
salama kwa hiyo endapo mpaka mchana wa leo sintapata taarifa yoyote toka kwake itakwenda
kumtoa mle ndani mimi mwenyewe.I don’t know
wh….” Kaba hajamaliza sentesi yake kengele ya
getini ikalia.Mathew akainuka na kwenda katika
chumba chenye luninga zilizounganishwa na
kamera za ulinzi
“ Kareem !! akasema Mathew na kutoka
akaelekea getini akamfungulia Kareem geti
akaingia
“ Karibu Kareem.Naamini Peniela
amekutuma” akasema Mathew
“ Ndiyo nimetumwa na Peniela”
“ Anaendeleaje? Is she safe there?
“ She’s mopre than safe.Amenituma
nikuletee huu mzigo na h ii bahasha” akasema
Kareem na kutoka kuondoka Mathew akamuomba
asubiri akaenda chumbani na kuchukua simu
akampatia
“ Mpe Peniela hii s imu”
Kareem akaondoka ,Mathew na Anitha
wakaelekea katika ofisi yao na kitu cha kwanza ilikuwa ni kuifungua ile bahasha iliyokuwa na
karatasi ndogo ndani yake iliyoandikwa
“ ABEL MKOKASULE..Find out who is he?
Mathew na Anitha wakatazamana.
***************
Taratibu za mwisho za kimila zilikamilika
nyumbani kwa Dr Joshua na hivyo kumpa nafasi
Dr Joshua ya kuondoka kuendelea na majukumu
mengine ya kitaifa.Mtu wa kwanza kuonana naye
baada ya kurejea ikulu ni Dr Kigomba
“ Kigomba nimekuita hapa kuna mambo
kadhaa ambayo nataka tongee” akaanzisha
maongezi Dr Joshua
“ Kwanza kabisa nataka nikupe pole sana
kwa kifo cha Jacob Kateka.Nafahamu wewe na
Jacob mlikuwa marafiki wakubwa .Hata mimi kifo
chake kilimuumiza sana.Nasubiri taarifa za
uchunguzi wa kifo chake ili tufahamu nini
kilisababisha hiyo ajali.Tumempoteza mchapakazi
mzuri sana.Mungu amempumzisha mapema” akasema Dr Joshua halafu ukapita ukimya mfupi
akaendelea
“ Tukiachana na taarifa hizo za kustusha za
kifo cha Jacob ,ninataka nikushukuru binafsi kwa
ushirikiano wako mkubwa katika msiba wa
mwanangu.Kazi uliyoifanya ni kubwa na mimi na
familia yangu tunawiwa deni la shukrani.Kwa
niaba yao nasema ahsante sana Kigomba .Wewe
ni rafiki wa kweli.”
“ Nashukuru sana mheshimiwa rais.Ule
ulikuwa ni msiba wetu sote kwa hiyo juhudi za kila
mmoja wetu zilihitajika” akasema Kigomba
“ Jambo lingine ni kuhusiana na
sintofahamu iliyojitokeza katika ule mpango
wetu.Yalijitokeza mambo kadhaa likiwamo na hili
la msiba na ndiyo maana nikasimamisha zoezi
zima”
“ Tukiachana na hilo la msiba ,nini kingine
kilitokea? Nahitaji sana kufahamu”
“ Kama utakumbuka usiku ule tukiwa
msibani,niliondoka ghafla bila kukutaarifu
naelekea wapi.Nilipigiwa simu na Rosemary Mkozumi akanitaka niende nyumbani kwake
haraka kuna jambo la maana sana anataka
kunieleza.Nilipofika kwake akanikutanisha na jaji
Elibariki.Aliniambia kwamba jaji Elibariki ana
mambo makubwa ya kunieleza.Niliondoka naye
hadi msibani na baadae usiku ndipo nikakaa naye
akaanza kunieleza mambo.Alisema kamba baada
ya kumuacha huru Peniela alitaka kufahamu
kuhusu nani hasa aliyemuua Edson na ndipo
alipoanzisha uchunguzi.Kazi hiyo alimpa rafiki
yake aitwaye Mathew ambaye aliwahi kufanya
kazi katika idara yetu ya usalama wa taifa na
aliacha baada ya familia yake kuteketea kwa
moto.Wakati rafikiye huyo akiendelea na
uchunguzi Dr Flora akafariki na Flaviana
akamuomba Elibariki amsaidie kwa kila nama
awezavyo kufahamu kilichomuua mama
yake.Elibariki naye akamkabidhi kazi hiyo Mathew
ambaye alifanikiwa kugundua kilichomuua Flora
na ndipo akatuletea ile ripoti tuliyoikataa.Mpango
wa kumuua ulishindwa kwani aliokolewa na Jessica Yule aliyewahi kuwa mlinzi wangu kama
unakumbuka”
“ Jessica? Kigomba akashangaa
“ Ndiyo,aliokolewa na Jessica”
“ How? Jessica alifahamuje kuhusu
mpango ule wa kumuua Elibariki?
“ Alielekezwa na Amos.He was a
traitor.Amos alikuwa anafanya kazi na Team
Sc41”
“ Team Sc41? Ni kampuni gani hiyo?
Akauliza Dr Kigomba
“ Hii si kampuni .Hiki ni kikundi
kinachofanya kazi kwa siri hapa nchini kwa ajili ya
kulinda maslahi ya Marekani.Hata mimi bado
sijakifahamu kiundani zaidi naendelea kutafuta
taarifa zake.Kwa mujibu wa Elibariki hawa Team
SC41 wanakitaka kile kirusi na Amos ndiye
aliyekuwa mtu wao waliyempandikiza.Si yeye
peke yake bali na Peniela”.
“ Ndiyo Peniela “ akasema Dr Joshua na
ukimya mfupi ukapita “ kwa mujibu wa Elibariki walikuwa na timu
yao ya kuhakikisha nao wanakipata kirusi
Aby.Timu hiyo iliongozwa na huyo
Mathew,akawepo pia Elibariki mwenyewe,Peniela
na msichana mwingine nimesahau jina.Elibariki
alidai kwamba baada ya kutafakari sana aliona
hataweza kupambana na mimi kwa hiyo akaamua
kuwasaliti wenzake na kumuachia huru Rosemary
mkozumi ambaye alikuwa anashikiliwa katika
jumba la Mathew.Alimtumia Rosemary ili kunifikia
mimi.Alinielezea mipango yote waliyokuwa
wameipanga ili kukipata kirusi hicho na ndiyo
maana nikachukua tahadhari kwa kusitisha kila
kitu hadi hapo tutakapojipanga upya vizuri
ikiwamo kumuondoa Hussein na ujumbe wake
pale walipokuwa wamefikia na kuwapeleka
sehemu nyingine.Kwa hiyo Kigomba hiyo ni
sababu kuu iliyonipelekea nisitishe kila kitu hadi
hapo tutakapojipanga upya”
Ukimya ukatawala mle ofisini,baada ya
dakika mbili Dr Kigomba akasema “ Ahsante sana Dr Joshua kwa kueleza
mambo hayo mazito lakini kwa nini unieleze
sasa? Nilikufuata zaidi ya mara moja kutaka kujua
nini kimetokea na hukuwa tayari kunieleza
chochote.You didn’t even trust me” akasema Dr
Kigomba
“ What do you expect me to do Kigomba?
I’m surrounded by traitors so I chose not to trust
anybody especially you Kigomba!! Dr Joshua
akawa mkali kidogo
“ I sent you to spy n Peniela,what did you
do? Akauliza Dr Joshua.
“ Nothing…I didn’t do anything wrong Mr
President”akajibu Dr Kigomba.Dr Joshua
akamtazama kwa macho makali na kusema
“ Kigomba wewe ni mmoja wa watu wangu
wa karibu sana.Please tell me the truth.Ulitembea
na Peniela na akakupa ile saa ya dhahabu kama
zawadi .Is that that true?
Dr Kigomba akamtazama Dr Joshua kwa
macho makali na kuuliza
“ Elibariki ndiye aliyekueleza hivyo? Do you
believe him? After all that you and I we’ve been
through you choose not to trust me and you trust
that good for nothing judge?Ahsante sana Dr
Joshua.Ahsante sana kwa kuchagua kumuamini
Elibariki.Kesho asubuhi nitawasilisha kwako barua
yangu ya kujiudhuru ili nikupe nafasi ya kufanya
kazi na watu unaowaamini” akasema Dr Kigomba
na kuinuka akataka kuondoka
“ It’s not like that Kigomba.Please sit
donw.Usiwe mwepesi kukasirika kiasi hicho”
akasema Dr Joshua lakini bado Dr Kigomba
alikuwa amesimama
“ Sit down Kigomba” akaamuru Dr Joshua
na Kigomba akaketi
“ Nisamehe Kigomba kama maneno
niliyoyatamka yamekukwaza.Sikuwa na lengo
hilo.Naomba nikuweke wazi Kigomba kwamba
Peniela ni mwanamke wangu.” Dr Kigomba
akastuka sana akamtazama Dr Joshua kwa
sekunde kadhaa kisha akasema
“ I didn’t know that” “ I’m telling you now” akasema Dr Joshua
“ Elibariki aliponieleza kuhusiana na wewe
kutembea na Peniela nilichukia sana sana.I love
Peniela so much and she’s mine alone”
akanyamaza akamtazama Kigomba na kuendelea
“ Jana nimekutana na Peniela akanieleza
ukweli wote”
“ Amekueleza nini? akaulizia Kigomba kwa
wasi wasi.
“ She told me the truth”
“ What truth Dr Joshua? Akauliza Kigomba
huku wasi wasi ukimzidi
“ Kuhusu Elibariki.Yale yote aliyonieleza
Elibariki ni uongo mtupu.Kumbe amekuwa
akishirikiana na Rosemary Mkozumi kupanga
mipango ya kunihujumu.Wanapanga mipango ya
kukipata kirusi na kibaya zaidi alichokifanya
Elibariki amekuwa akimtaka peniela kimapenzi
kwa kisingizio eti yeye ndiye aliyemuachia
huru.Baada ya peniela kumkatalia ,jaji Elibariki
alimbaka!!!!..Sura ya Dr Joshua ikabadilika na
hasira za wazi wazi zikaonekana “ Kibaya zaidi baada ya kumbaka alimtolea
vitisho vya kumuua endapo atanieleza suala
hilo.Juzi usiku Peniela alivamiwa na watu
nyumbani kwake waliokuwa na lengo la kumuua
lakini akafanikiwa kutoroka na watu wale
wakaichoma moto nyumba yake wakateketeza
kila kitu.Elibariki is a snake!!! Akasema Dr Joshua
kwa hasira
“ Peniela anaishi wapi kwa sasa?
“ Anaishi kwenye ile nyumba yangu ya
ufukweni.Elibariki ameniudhi sana na nitamfunza
adabu.Alinifanya niwachukie watu wangu wa
maana kwa maneno yake ya uongo” akasema Dr
Joshua na kumfanya Dr Kigomba ashushe pumzi.
“ Wakati mwingine ukiletewa taarifa kama
hizo unatakiwa kujadiliana kwanza na wenzako”
akasema Dr Kigomba
“ Usemayo ni ya kweli Kigomba.Mambo
yetu mengi yamekwama.Hivi sasa tayari
tungekwisha maliza biashara yetu na Hussein.” “ Baada ya kuufahamu ukweli nini
kitafuata? MIpango yetu inaendelea ? akauliza
Kigomba
“ Tutaendelea Kigomba ila si sasa
hivi.Tutasubiri kidogo mambo yatulie ili tuendelee
na mpango wetu.Macho ya wengi tayari yameona
kwa hiyo ni hatari kwetu.Nahitaji muda wa
kusafisha kwanza njia ndipo tuendelee na
mipango yetu tukiwa na uhakika kuwa hakuna mtu
yeyote atakayekuwa kikwazo
kwetu.Nitazungumza na Hussein ili nimfahamishe
kuhusu maamuzi haya na ninaamini atanielewa
na atasubiri.Endapo hatanielewa basi sintakuwa
na namna nyingine ya kufanya zaidi ya
kumrejeshea fedha zake”
“ Dr KIgomba najua maamuzi haya
yamekunyong’onyeza sana kwani tumetoka mbali
na jambo hili na mengi yametokea hadi hapa
tulipofika lakini hakuna namna nyingine ya
kuendelea na jambo hili kabla kwanza ya
kusafisha njia kwa kuwaondoa njiani wale wote
ambao wanaonekana kuwa kikwazo kwetu.Usiogope Kigomba hata kama jambo hili
halitawezekana mimi na wewe bado tuna fursa
nyingi za kutengeneza fedha nyingi za
kutuwezesha kuishi kama malaika baada ya
kustaafu.Nipe muda kidogo Kigomba na
nitakushirikisha katika jambo Fulani kubwa zaidi
ya hili la kirusi” akasema Dr Joshua
“ Dr Joshua mimi sina kipingamizi chochote
na maamuzi yako.Ni kweli tumetoka mbali na
suala hili na kweli mengi yametokea huko njiani
hadi hapa tulipofika na kwa hali ilivyo nakuunga
mkono kwamba tusimamishe mipango yetu kwa
muda .Ni hasara kubwa lakini hatuna namna
nyingine ya kufanya” akasema Dr Kigomba na
kumfanya Dr Joshua atabasamu
“ Nafurahi sana kusikia kauli hiyo
Kigomba.Pamoja na hayo kuna jambo moja bado
nahitaji msaada wako”
“ Sema chochote unachohitaji Mr President”
“ Leo jioni nitaonana na Donald pale pale
nyumbani kwangu ufukweni kwa hiyo naomba
unifanyie maandalizi kama uliyoyafanya jana.Nataka kiandaliwe chakula cha usiku kwa ajili
ya watu wanne kwani nitakula chakula cha usiku
na wageni wangu usiku wa leo”
“ Sawa mheshimiwa rasi nitalifanya hilo”
akasema Dr Kigomba kisha wakaagana akatoka ili
kwenda kufanya kazi aliyotumwa.Mara tu baada
ya Dr Kigomba kutoka Dr Joshua akachukua simu
na kumpigia Kareem
“ Hallow mzee” akasema Kareem baada ya
kupokea simu
“ Kareem Peniela anaendeleaje?
Amekwisha amka? Amepata kila anachokihitaji?
Akauliza Dr Joshua
“ Ndiyo mzee.Peniela anaendelea vizuri
,tayari amekwisha amka na amepata kila
alichoagiza” akajibu Kareem
“ good to hear that.Kareem nitakuwa na
wageni wangu hapo nyumbani usiku w a leo na
nitakula nao chakula cha usiku hapo hapo
nyumbani.Nimemtuma Dr Kigomba yule katibu
wangu aje afanye maandalizi,please please
hakikisha hamkaribii Peniela.Umenielewa
kareem?
“ Nimekuelewa mzee,Nitalitekeleza hilo”
“ Good” akasema Dr Joshua na kukata
simu.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO...
PENIELA SEASON 5
SEHEMU YA 5
ILIPOISHIA
Kareem Peniela anaendeleaje?
Amekwisha amka? Amepata kila anachokihitaji?
Akauliza Dr Joshua
“ Ndiyo mzee.Peniela anaendelea vizuri
,tayari amekwisha amka na amepata kila
alichoagiza” akajibu Kareem
“ good to hear that.Kareem nitakuwa na
wageni wangu hapo nyumbani usiku w a leo na
nitakula nao chakula cha usiku hapo hapo
nyumbani.Nimemtuma Dr Kigomba yule katibu
wangu aje afanye maandalizi,please hakikisha hamkaribii Peniela.Umenielewa
kareem?
“ Nimekuelewa mzee,Nitalitekeleza hilo”
“ Good” akasema Dr Joshua na kukata
simu
“
Endelea....
“ Ingawa hakutaka kuonyesha wazi wazi
lakini Dr Kigomba amestushwa sana na maamuzi
yangu ya kusitisha ile biashara yetu ya
kirusi.Sitaki kabisa kushirikiana chochote na Yule
msaliti.Nina hakika yeye na Jacob kuna njama
walikuwa wanaipanga dhidi yangu.Hata yeye
Kigomba naamini siku zake zinahesabika kwani
nafahamu namna alivyo na kiu ya pesa atatafuta
kila namna ili aweze kupata pesa nyingi kupitia
kirusi kile.Nilifanya kosa kubwa kumshirikisha
katika mpango ule .” Simu ya mezani iliyoita
ikamtoa Dr Joshua katika mawazo akaipokea
“ Mheshimiwa rais kuna mtu anahitaji
kuzungumza nawe katika laini ya simu namba
moja” akaambiwa Dr Joshua na bila kupoteza
muda akabonyeza laini namba moja
“ Hallow !! akaita “ Hallow Dr Joshua.It’s me Rosemary
Mkozumi.Vipi maendeleo yako? Nimekuwa
nakutafuta niongee nawe jambo la muhimu lakini
sikupata nafasi hii hadi sasa nilipoomba sana
wasaidizi wako wanisaidie niongee nawe.”
Dr Joshua akavuta pumzi ndefu na kuuliza
“ What do you want Rose?
“ Dr Joshua I need your help.Something
happened yesterday here at my place”
“ Kitu gani kilitokea?
“Unakumbuka kuna Yule msichana
niliyekuambia kuwa anashirikiana na Mathew na
Peniela ambaye nilikuwa namtegemea sana
atueleze mahala alipo Mathew?
“ Ndiyo nakumbuka ulinieleza kitu kama
hicho.”
“ Basi Yule msichana ametoroka na sijui
nitampataje.Ninaomba msada wako ili aweze
kupatikana kwani anahatarisha usalama
wetu.Mipango yetu yote haitaweza kufanikiwa
endapo huyu msichana hatapatikana.She knows too much” akasema Rosemary.Dr Joshua
akapatwa na kigugumizi akashindwa aseme nini
“ Dr Joshua are you there? Akauliza Rose
baada ya kuona kumekuwa kimya
“ Uhhmm Rose are you sure about that?
“ About what?
“ About that woman.Is she real?
“ Dr Joshua how come you ask me such a
silly question.You don’t trust me now? You think
I’m lyin g? akauliza Rosemary mkozumi kwa ukali
“ Sikiliza Rose,kwa sasa nina mambo
mengi ya kushughulikia.Tafadhali naomba mambo
yako yashughulikie mwenyewe.If that woman real
do exist find her by yourself” akasema Dr Joshua.
“ Dr Joshua ni wewe kweli unayethubutu
kuniambia maneno hayo leo? Akaulizia Rose kwa
ukali.Dr Joshua hakutaka kuendelea na
maongezi akakata simu
“ Huyu naye ni miongoni mwa watu
waliomo katika orodha ya watu wanaotakiwa
kuondolewa.Yeye na mumewe Deus ni vizingiti
vikubwa katika kufanikisha mipango yangu.Katika mpango wa kumuua Deus Mkozumi huyu naye
lazima awepo” akawaza Dr Joshua na
kutabasamu
“ Ngoja nijiandae nikaonane na
Hussein,nimfahamishe kwa kina ugumu uliopo
kwa sasa katika kuufanikisha mpango wetu na
kama ikiwezekana basi anisubiri na kama hataki
kusubiri basi nimrudishie pesa zake zote
alizotoa.Sintaathirika na chochote kwani tayari
serikali ya Marekani imeleta mpango
utakaoniingizia fedha nyingi mno kwa hiyo
sibabishwi na pesa zake”s akawaza Dr Joshua.
***************
“ Dr Joshua ni shetani.Najuta kushirikiana
na mtu kama Yule. Nina hakika kabisa anataka
kunizunguka na kuchukua pesa zote
mwenyewe.No! I wont let him do that
.Nitapambana naye!! Akawaza Dr Kigomba akiwa
garini kuelekea nyumbani kwa Dr Joshua kufanya
kazi aliyotumwa. “ Tayari nina mipango mingi mikubwa ya
kufanya baada ya kuzipata zile fedha na kwa hiyo
nisipozipata mipango yangu yote itakuwa
imeyeyuka.Hapana siwezi kukubali hilo.Nimefanya
kazi kubwa kuhakikisha jambo hili linafanikiwa
lakini leo baada ya pesa kuwasili Dr Joshua
ananiondoa kimya kimya katika mpango kwa
sababu ambazo hazina kichwa wala
miguu.Anadai eti kuna tishio la usalama na eti jaji
Elibariki na Rosemary Mkozumi tayari
wanafahamu kuhusu mpango huu na kwamba eti
wana njama za kumzunguka na kuuchukua ule
mzigo,that’s a big lie.Najua lazima kuna kitu
kinachoendelea kati yake na jaji Elibariki
.Nitautafuta ukweli” akawaza Dr Kigomba na mara
akakumbuka kitu.
“ Peniela !!..oh my God..Dr Joshua na
Penila kumbe ni wapenzi.Kwa nini hakunieleza
kuhusu jambo hili wakati ananituma
nikamchunguze? Inawezekana kweli Peniela na
Elibariki wakawa wanafahamiana kwa sababu
mambo ambayo Elibariki alimueleza Dr Joshua ni ya kweli k abisa.Ni kweli nilitembea na Peniela na
akanipa zawadi ya saa ya mkononi.Lakini je ni
kweli saa ile aliyonipa Peniela ilikuwa ni mtego? Ni
kweli yeye na wenzake anaowasema Dr Joshua
walikuwa wakifuatilia maongezi yangu ya
simu?.Dr Joshua amesema pia eti Peniela na
Amos walikuwa wanafahamiana na kwamba eti
walikuwa wanashirikana sijui na kikundi gani
nimekisahau jina lake.Haya yote ni ya kweli?
Akaendelea kujiuliza Dr Kigomba.
“ Mmmhhh ! naanza kupata mashaka
kidogo kuhusu huyu Peniela.Lazima kuna kitu
kinachoendelea kati yake na Elibariki.Nani mkweli
k ati yao? Nadhani natakiwa kuonana na Elibariki
.Anaweza akanipa ukweli .Kabla ya kwenda
kuonana naye natakiwa kwanza kutafuta mahala
Dr Joshua alikompeleka Hussein.Natakiwa
kuongea naye kufahamu kinachoendela kati yake
na Dr Joshua na kama ameshakabidhiwa mzigo
wake ama bado.Najua hawezi kunificha chochote
kwani anafahamu mimi na Dr Joshua ni washirika
na mimi n diye niliyefanya naye mchakato mzima hadi hapa tulipofika.Nitamuonyesha Dr Joshua
kuwa mimi nina akili zaidi yake.” Akawaza Dr
Kigomba
****************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment