Search This Blog

Wednesday 22 March 2023

MBWA WA GETINI - 5

   

Simulizi : Mbwa Wa Getini 

Sehemu Ya : Tano (5)



Akaelekea moja kwa moja hadi kwenye mlango wa kuingilia ndani ya ofisi ile na kisha akagonga mlango na kama utaratibu usio rasimi ulivyosambaa ndani ya ofisi za waafrika wengi,hakuitikiwa.Na yeye hakungoja kuitikiwa maana aliujua utaratibu huo.


Akakinyonga kitasa na kuzama ndani.


Nyuma ya meza ya ofisi alimkuta kijana wa makamo yapata miaka thelathini na tano hivi,akavua kofia na mawani yake kisha akakaa bila kukaribishwa kwenye kiti kilichokuwa mbele ya meza huku sasa wakiwa wanatazamana na kijana yule ambae hadi muda huo alikuwa ameshaijua sura ya mtu aliekuwa mbele yake.Aliijua kwa sababu ni ahsubuhi hiyo aliposikia matangazo kwenye radio na tv ya kuwa mtu huyo amefanya jaribio la kutaka kulipua jengo la bank ya KCB mjini Nakuru.


Zedi aliona ubabaikaji wa mwenyeji wake,hakutaka kuuliza lolote zaidi ya kile kilichompeleka pale.


“Naomba kufahamu umiliki wa namba hii K369D” alianza kusema Zedi.


“Wewe ni askari?!” aliuliza mwenyeji yule.


Zedi akamtazama na haraka akajua mtu yule anajikaza kuongea ila anamwogopa,hivyo akaamua kutumia udhaifu huo kama silaha Ya kupata kile alichokihitaji


“sihitaji swali lolote naomba kujua umiliki wa gari hii” alizungumza huku akisimama na hapo akaona mtu yule akitetemeka zaidi na kuanza kupekua kwenye komputa yake na punde akawa na majibu


“Anaitwa Jafo kairuki na makazi yake yako Kibera”


Zedi hakutaka kungoja maneno zaidi akatoka ndani ya jengo lile na wakati anatoka tu hata kabla hajavuka barabara ili kufuata kituo cha madereva taxi,akaona gari la polisi likisimama pale kwa kasi na askari wale wakashuka haraka haraka na kuingia ndani na hapo hakutaka kufanya ujinga wowote haraka akakimbia na kupanda taxi ambapo aliomba apelekwe Kibera na dereva akatii haraka wakawa wapo barabarani wakikunja kona ya uwanja wa ndege wa Nairobi west.


Safari yao ilikuwa imewafikisha hadi langata road na kuifuata hiyo barabara hadi walipotokea kwenye makutano ya southern bypass kisha wakakunja kulia na walipofika Uhuru garden Zedi akaomba kusimama hapo ,akalipa na kumruhusu dereva aondoke kisha yeye akaamua kufuata barabara kwa miguu hadi kwenye mahakama ya National housing na macho yake yakavutiwa na harakati za eneo lile.


Akazidi kusogea na kufika karibu na nyumba alioihitaji na kisha akawa kama anaipita hasa baada ya kuona geti lipo wazi na alipopita tu akaona kuna watu wanajadili kitu huku wakitoka nje nae akainama chini na kuyasikia maongezi yao.


“tayari mbinu ya kuwahamisha imefanya kazi na sasa bado nyaraka moja tu,wahi ukaitafute na wambie mbwa weupe wahamishe kule Nakuru west tunapahitaji kufikia hadi kesho ahsubuhi”


Mtoa maelezo akamaliza na kuanza kurudi ndani huku mpewa maelezo akipanda gari iliokuwa pale na kuondoka kwa kasi .


Zedi alihitji kuingia pale ndani na alihitaji kujua chanzo cha mauji yale kila siku na pia alihitaji kujua hao mbwa weupe kazi yao.





Zedi alihitji kuingia pale ndani na alihitaji kujua chanzo cha mauji yale kila siku na pia alihitaji kujua hao mbwa weupe kazi yao.


Akapita kwa kwenda mbele huku nafsini mwake akijionya kutokufaya lolote maana hakujua nguvu iliokuwa pale nyumbani kwa jafo.


Swali moja likabaki kwanini jafo aliingilia harakati za wenzie huku kwa haraka ikionekana lote ni kundi moja?!


Muda ulikuwa unamtupa mkono na hapo akakumbuka namba za siri alizopewa na mtu aliekua mateka kwenye ngome ya kabah.


“za nini zile namba!?” ajajiuliza peke yake huku sasa akiwa yupo nyuma ya mahakama na alikuwa anajaribu kuona uwezekanao wa yeye kuingia kinyemela ndani ya nyumba ya Jafo.


Akaona ugumu wa kuingia pale jioni ile akagairi na hapo akaikumbuka namba ya simu ya Wambui na akaona yule binti kuna kitu anajua akatabasamu huku mawazo yakiwa kusogea hadi zilipo ofisi za kupiga simu kwa kulipia.


*****

Burizozo ndie aliekuwa amesalia kwenye nyumba ya Kabah.


Na alikua anatazama chumba alichofungiwa Tausi,huku mikononi mwake akiwa kamshika mtoto wa Tausi aliekuwa kasizi akitoa udenda,lakini yeye kuna kitu alikuwa anakitaka muda huo.


Ngono !!!

Ngono kutoka kwa Tausi.


Akamweka mtoto pembeni kisha akapiga hatua kwenda hadi chumba alicholafungiwa Tausi akakifungua na kukutana na mwili wa Tausi ukiwa umelelala juu ya dimbwi la maji huku akitetemeka kwa baridi na njaa na kubwa zaidi alitetemeka kwa kuhitaji furaha ya ajabu,furaha ambayo ni ngumu kuipata.


Burizozo akamnyanyua na kwenda nae hadi sebuleni kisha akamkaliza na kumletea chakula,Tausi alikifakamia kama hana akili nzuri na ndani ya muda mfupi akawa amemaliza.


Lakini si njaa tu iliokuwa inamtesa Tausi,hata kule kukosa unga tu kulimtesa tena kuliko hata njaa ya chakula.


Tausi akaomba dawa na hiyo ndio ilikuwa tiba yake.


Kuomba kwake kulingojewa kwa hamu na Burizozo aliekuwa amemgeuza mke wa rafiki yake kuwa wake na sasa alikuwa anataka tena kujiridhisha.


Kwa kuwa alitaka basi hakuwa na budi kukubali masharti ya Burizozo,akavua nguo sebuleni mbele ya mwanae aliekuwa kalala kwenye kochi nae akiwa hajitambui kwa dozi.


Burizozo akanyoosha mkono ili ampe dawa ila akarudisha haraka baada ya kuona mikono ya Tausi kutaka kushika.


Burizozo alikuwa anatoa tabasamu la kifedhuli na kisha akatamka jambo gumu kufanyika kwa binadamu mwenye damu na nyama kisha akajaliwa akili timamu.


Alikuwa anataka tarabu ya Tausi na hapo Tausi akacharuka akajitazama alivyouchi wa mnyama kwa kuwa tu alihitaji kupata kete lakini sasa mtu wa kumpa kete anataka kuzunguka ukuta ndo atoe,hakika ulikuwa ni udhalilishaji wa hali ya juu sana.


Akatamani akatae lakini tamaa ya kupata dozi ikamzidi,lakini kukubali ikawa ndio ngumu akabaki akilia huku nafsi ikiwa inataka japo kupata hata tone tu la unga.


Burizozo matamanio ya kumuona Tausi akiwa uchi yakamzidi na akaona anacheleweshwa,haraka akamfikia na kumlaza kwa nguvu,kisha akaanza kumwingilia kwa nguvu huku Tausi akipiga makelele yaliomstua hadi mtoto aliekuwa anaelea kwenye bahari ya amani.


Mtoto alishuhudia mama yake akiwa analazimishwa kutoa tarabu kwa makofi na bado kumbukumbu zake hazikuwa mbali hasa alipokumbuka yakuwa ni jana tu walipigwa yeye na *****,lakini mtoto yule hakuwa na nguvu za kupambana akabaki kuwa mtazamaji wa filamu ile ya kufedhehesha.





Mtoto alishuhudia mama yake akiwa analazimishwa kutoa tarabu kwa makofi na bado kumbukumbu zake hazikuwa mbali hasa alipokumbuka yakuwa ni jana tu walipigwa yeye na *****,lakini mtoto yule hakuwa na nguvu za kupambana akabaki kuwa mtazamaji wa filamu ile ya kufedhehesha.


***

Tangu utoto wake hakuwa anapenda kuona mtu anamdharau na alikuwa tayari hata kuacha kitu anachokipenda kwa sababu tu ya dharau.


Alijikuta akiwa mgomvi shuleni hadi nyumbani kwa sababu ya kutokupenda dharau na sasa alikuwa amemweka kwene rada zake Burizozo kwa kuwa alikuwa akimdharau na pia aliona kitendo cha Kabah kumuua kijana wake ni sawa na kumdharau kupita kiasi.


Kabah alimwachia maagizo ya kupeleka wadudu flani huko Chamwino Ikulu.


Temba hakuwa anawajua wadudu wale na madhara yake ila alihisi tu ni wa hatari kwa mwonekano wao na tayari alikuwa ameagiza vijana wakatekeleze jukumu hilo yeye akiwa amebaki kuangalia usalama wa jumba lile na mzigo utakaokuwemo.


Wakati akiwa anawaza hili na lile akakumbuka Mina.


Mbali ya kumjua askari yule lakini walikuwa ni marafiki wakubwa waliokutana kwenye mkasa wa SIKU KABLA YA LEO ulioandikwa na mwandishi anaekuja kasi Bahati Mwamba.


Aliona kuingizwa Mina katika kesi ya mauji ya askari polisi aliekuwa anafuatilia nyendo zao ilikuwa ni kumsogeza karibu yeye kuwa adui wa Mina hakutaka hilo litokee,lakini pia hakutaka Mina ajue kama bado anaendelea na ujambazi wa kuua watu.


Akapanga kufanya kitu ili awe mbali na mikono ya Mina lakini kabla hajafanya hilo alitaka kwanza kuwasiliana na Mina amtahadharishe kuhusu wadudu wa ajabu wanaoenda kumwagwa maeneo ya Ikulu Chamwino.


Akatoa simu yake na kuzitafuta namba za Mina kisha akapiga na akasikia zikiita,akakata haraka na kuandika ujumbe mfupi afu akazima simu.


Wakati akijua kawauza wenzie kwa askari mtata Mina akanyanyuka alipokuwa na kujinyoosha kisha akaanza kuzunguka maeneo ya jumba lile na hapo ndipo aliponasa sauti ya hamaniko kutoka ndani.


Alizoea kusikia Tausi akilia kila siku,lakini sauti ya leo ilikuwa inautata,ilikuwa sio ya kilio alichozoea kukisikia wakati Tausi akipigwa,hiki cha leo kilikuwa ni kilio cha maumivu na majuto makubwa lakini pia alisikia killio cha mtoto mdogo


Akashawishika kutazama kupitia dirisha pana la vioo na hapo akaona jambo gumu kuvumilia na akachanganya na chuki yake kwa burizozo akaamua kusaliti mazima.


****


Mikono yake ikiwa imelowa mafuta kwa kukurukakara za kutaka kumruka ukuta Tausi,Burizozo alikuwa bado anafanya jitihada za kumdhibiti Tausi ili atimize haja zake.


Akampiga kofi lenye uzani wa kilo kadhaa na kumwangusha Tausi juu ya zulia na kisha akamfuata huku wololo yake ikiwa imesimama kama kijiti cha mwembe koi huku tabasamu la kifedhuli likiwa limemkaa usoni.


Akainama ili ammiliki Tausi.


Ni wakati mkono wake ukiwa unataka kushika wololo m, hapo ndipo akajikuta akipaa juu na kurudi chini kwa kasi ya umeme huku mbavu zake zikiwa zinauma.


Burizozo akatazama aliemfanyia shambulizi lile hakuamini kuona ni kutoka kwa kibaraka wao Temba.


Akasimama kwa jazba ili amshambulie,lakini ni kwa kuwa hakujua uwezo wa Temba upo vipi,yeye alikuwa anamchukulia kama mjinga flani hivi lakini hakujua ujuzi wa Temba kwenye uwanja wa vita vya mkono au silaha.


Akasimama kwa pupa ingali yu uchi,akaunguruma kwa hasira na kwenda kumvaa Temba,ila alikutana na pigo moja tu lililoondoka na ufahamu wake huku akijibwaga chini kama kiroba cha unga.


Temba hakutaka kukaa pale,akamhimiza Tausi avae nguo na achukue kile kinachomfaa kwa muda huo na watoke pale ndani.


Alimwacha ndani Taus akijiandaa na yeye akaenda kuchukua gari lake lililokuwa limepaki pale uwanjani,walinzi wenzie waliona tu hekaheka za Temba aliejiita Mbwa,lakini hawakujua ni za nini hekeheka zile.




Alimwacha ndani Taus akijiandaa na yeye akaenda kuchukua gari lake lililokuwa limepaki pale uwanjani,walinzi wenzie waliona tu hekaheka za Temba aliejiita Mbwa,lakini hawakujua ni za nini hekeheka zile.


Tausi na mwanae na mkoba wenye nguo kidogo wakapanda ndani ya gari ile na kutokomea mjini huku wakipitia njia ya Area A,na katikati ya safari Temba akatoa kete mbili na kumpa Tausi aliezibugia na kumpa faraja ya ajabu huku mwili wake ukiwa umesahau maumivu.

****


Mina alikuwa anatoka ofisini kwa Rpc ndipo alipoona simu yake ikitetema,mwanzo alidhani ni Ziga,lakini alipoitoa ndipo akapigwa na butwaa,ilikuwa ni namba ya Temba.


Akiwa bado anashangaa Temba kumtafuta baada ya muda mrefu kupita,akaona ujumbe mfupi kutoka tena kwa Temba.


“Wahi Ikulu T620HHH,” mara moja Mina akaelewa ujumbe ule ni taarifa fulani ya hatari na pengine angelipuuzia kama ungelitoka kwa mtu mwingine,lakini ulitoka kwa mtu wake wa karibu na mtu wa matukio na kazi.


Haraka akarudi ofisini kwa Rpc na kuomba usafiri wa gari na difenda ya polisi yenye kasi na askari wenye ujuzi.


Rpc Mabeyo bila kuuliza akatoa magari mawili la kwake na la askari wa kawaida na msafara huo akauacha kwa Mina askari mwenye weledi wa hali ya juu .


Ziga nae alipata taarifa kutoka kwa Mina akiwa anapata taarifa kutoka kwa wenyeji wa nyumba ya Zedi na haraka akaondoka kwenda huko Ikulu ambako wote wawili hawakujua kuna kitu gani kwenye hiyo gari.


Mina ndie alikuwa wa kwanza kuliona gari lile likiwa linatembea taratibu sana haraka akatoa taarifa kwa askari wenzie waliokuwa nyuma kwenye difenda na silaha za mkononi.


“Oya kozo eeh kuna njangu nyuma wapo kishari sana” dereva wa gari lile lililokuwa likifuatwa na polisi alinwambia mwenzie aliekuwa kushoto kwake.


“mmh usitie Shaka watakuwa na ruti zao hao”


Hawakumaliza maongezi yao wakaona taa za kuwaashiria wasimame kutoka kwenye gari iliokuwa nyuma,gari ya polisi.


Dereva akasema na wenzie waliokuwa wako nyuma kama abiria wenye mizigo yao ndani ya kenta ile,nao wakajua kumekucha,haraka wakatoa silaha zao na bila kuuliza wakaanza kushambulia gari ya polisi.


Barabara ikawa haitoshi risasi zikisikia huku gari zikiwa kwenye mwendo mkali sana.


Mina hakutaka kushambulia kwanza maana alihitaji kwanza kufanya kitu haraka akahamia upande wa kulia yanakopita magari yanayotoka Dar.


Akaongeza kasi na kwa aina ya gari alilokuwa nalo haraka akaifikia ile kenta na hakutaka kupita ila akaamua kuwa nayo sambamba na kwa kutumia mkono wa kushoto akachomoa bastola yake na kulenga usawa wa dereva wa kenta ile na alipoachia risasi ikaenda kutua kwenye kichwa na gari lao likakosa mwelekeo na kwenda kujingonga kwenye mti na kubinuka.


Haraka askari wakashuka na kuwafikia watu waliokuwa kwenye kenta ile na kuwakuta baadhi wakipigania uhai wao huku mmoja kati yao akiwa amekufa tayarim.


Askari mmoja akakimbilia kwenda kufanya wokozi,lakini wakati anainama ili kumvuta mtu aliekuwa upande wa nyuma akaona kitu cha ajabu na haraka akaruka na kurudi nyuma.


Kitendo kile kilifanya wengine wajiweke tayari kwa lolote na hapo akawa amefika Mina ambae moja kwa moja bila woga akaongoza kwenda kuangalia.


Hakika hakuamiani kuona kile alichokiona.


Walikuwa ni wadudu wengi sana waliokuwa wanashambulia miili ya watu wale na waliobekana kutoka kwenye maboksi fulani ya vioo na tayari walianza kutafuta njia ya kutoka nje ya gari ile.


Ziga alisimamisha gari na kushuka haraka na bila kuuliza akawaomba askari wote warudi nyuma ni baada ya kuwaona wadudu wale waliokuwa wameanza kupanda juu ya gari ile.




Ziga alisimamisha gari na kushuka haraka na bila kuuliza akawaomba askari wote warudi nyuma ni baada ya kuwaona wadudu wale waliokuwa wameanza kupanda juu ya gari ile.


Ziga akaachia risasi ilioenda kulenga tank la mafuta la kenta ile na kukatokea mlipuko mkubwa uliosababisha kupotea kwa kila kitu ndani ya gari ile.


“huu mradi bado upo!!” alisema Ziga lakini sauti yake ilimfikia Mina na hapo Mina akajua Ziga anajua kuhusu kitu hicho.


Akaagiza uchunguzi zaidi ufanyike kuhusu gari ile huku Mina na Ziga wakipanda gari moja na kuelekea sehemu nyingine kukutana na mtu mwingine.


*****


Saa mbili ya usiku ilimkuta Zedi akiwa anaingia nyumbani kwa Wambui.


Wakati anaingia tu akapokelewa kwa namna ya kipekee,japo alitegemea,lakini hakudhani kama itakuwa gafla kiasi kile.


Wakati anaingia tu mlangoni akapokelewa kwa teke kali la kifua na alipojaribu kurudi nyuma ili atoke nje akashangaa kutandikwa teke la mgongo na kumfanya aingie ndani bila kupenda na huko akakutana na watu watatu wakiwa wamesimama na mitutu ya bunduki ikiwa tayari kutoa roho yake.


Akaamuliwa kunyosha mikono juu nae akatii na punde akatokea Wambui na kamba mkononi akamfunga Zedi na wakamkalisha kwenye kiti,mateso yakaanza.


Wakati watesaji wa Zedi wakidhani wao wapo salama,walikuwa wanakosea.


Kulikuwa na mtu hatua chache nyuma ya sebule ile waliokuwa wameigeuza kama uwanja wa mazoezi kwenye mwili wa Zedi.


Risasi iliotoka kwenye silaha iliofungwa kiwambo cha kuzuia sauti iliondoka na wawili kati ya wanne waliokuwa mle kisha pasipo kutarajia mlango ukasukumwa akaingia mtu kwa kasi ya ajabu huku akiachia mapigo safi yaliomfanya hadi Zedi atabasamu japo alikuwa bado amefungwa kwa kamba.


Zedi aliyaona yote na hata mtu yule alipotaka kutoa pigo la kifo kwa binti mrembo Wambui aliliona na akaachia ukulele wa kumzuia mtu yule asifanye vile.


Mtu yule kwa jinsi alivyokuwa amevaa Zedi hakupata shida kujua ndie mtu aliemwona akiadhibu watu waliokuwa wamebeba mzigo kutoka kwenye nyumba ya mzee Matare na ndie mtu aliepambana nae ndani ya nyumba hiyohiyo ya mzee Matare.


Mtu yule akajifunua sura yake na hapo Zedi akatabasamu baada ya kumjua

“Zedi nilikwambia tupatane Nairobi”


“na tumepatana Mao Waira” alizungumza huku akimalizia kujifungua kamba alizokuwa amefungwa na punde akawa huru huku jicho lake likinasa hila alizokuwa akitaka kuzifanya Wambui nyuma ya mgongo wa Mao Waira.


Haraka Zedi akaachia teke safi lililomkuta Wambui kifuani na kumtoa uhai wake kabla hata hajafika chini.


“Nilitaka kummaliza ukatetea ili umue wewe” Mao Waira alisema huku akicheka na kumpiga Zedi begani kisha wakaanza kutoka ndani ya nyumba ile huku Mao waira akipiga simu kituo cha polisi ili waje kuendelea na taratibu nyingine.


“Idara ya usalama ya Kenya,haikuwa imelala bwana Zedi,tulijua kabisa hizi ni hila za watu wenye pesa kutaka kuchukua hii nchi kihuni na hivyo tumefanya jitihada na kiasi chake tumefanikiwa kudhibiti na kuwakamata baadhi waliokuwa wakituhujumu ila bado kisa cha yote haya bado hakijajulikana japo wanaohusika wanajulikana.” Alizungumza Mao waira aliekuwa amejitambulisha kuwa ni mtu kutoka idara ya usalama ya nchini Kenya.


“Ni wewe ulifyatua smoke mashine pale KCB jana”aliuliza Zedi


“Yah tangu usiku ule tulipopambana kule NHC kwenye nyumba ya mzee yule,sikukimbia kama ulivyodhani,wakati unatoka na unarudi nilikuwa nyuma yako na ulipoamua kulala nikaacha vijana pale kukuwekea ulinzi na ulipotoka ahsubuhi nikaunga tela hadi nilipoona wale mbwa weupe wanakuja mle nikaamua kutumia uhuni wa kukusaidia japo ulivyotoka sikujua hadi nilipokukuta Langata Court kwa Jafo,nikaweka vijana wakulie rada”


Ok ahsante kwa msaada wako Waira,lakini hawa mbwa weupe ni kina nani hasa”




Ok ahsante kwa msaada wako Waira,lakini hawa mbwa weupe ni kina nani hasa”


“haka kakikundi ka wapuuzi flani kazi yao ni kumwaga wale wadudu na kuua watu..anyway twende tukate mzizi wa fitina kwa Jafo anakikao usiku huu” walizungumza hayo huku wakiwa wanapaki gari yao nyuma ya NHC court,kisha wakaanza kutembea kwa miguu hadi walipoingia ndani ya uzio wa nyumba ile inayomilikiwa na Jafo.


Wakagawana


Mmoja alipita upande wa nyuma na mwingine alipita upande wa mbele

*****



Ziga alikuwa amesimama huku akimtizama Tausi aliekuwa amekaa kwenye sofa na mtoto alikuwa mikononi mwa Mina huku Temba akiwa nae kasimama.


Shemeji kilitokea nini hadi ukajikuta mikononi mwa mtu kama yule” aliuliza Ziga huku akionekana dhahiri anahasira na mwananke yule


Mwaka mmoja nyuma


Zedi alitambua ndoa yake imeingiliwa na mdudu pesa na tayari aliona kabisa mkewe Tausi haambiliki.


Uwezo wa kumpiga alikuwa nao,lakini hakutaka kufikia huko maana aliamini uwezo wake wake na kupambana si kumpiga mwanamke.


Pengine alikuwa sahihi,lakini ilikuwa ni tofauti kwa mkewe Tausi ambae alimua kuutumia huo uhuru kuutesa moyo wa Zedi ambae hadi wakati hakuwa na kauli yoyote kwa mkewe huyo aliekuwa ameanza tabia ya kuchelewa kurudi na akirudi huwa amelewa pombe chakari.


Zedi majukumu ya kulea mtoto yalikuwa juu yake huku kila mara akishuhudia mkewe akiondoka na kurudi na mabunda kadhaa ya pesa.


Sio kama hakuwa na pesa la alikuwa nayo ila hakutaka itumike vibaya kama mkewe Tausi alivyotaka.


Tausi raha za dunia zikamdanganya na nyumbani hakukumbuka tena,akaanza safari za kusafiri nchi za nje huku akiwa na bwana ake Kabah.


Siri ya safari zao Tausi aliijua,alijua wanapitisha dawa za kulevya kimagendo.


Haikuwa kusafirisha tu,akaanza na kutumia,hatimae akakolea.


Kabah amwambie nini asitake


Akashauriwa kudai taraka kwa mwanaume suruali Zedi,nae akaomba na Zedi akatoa.


Akashauriwa tena kudai mtoto, hapo ikawa pagumu,ikabidi ustawi waingilie na mwenye haki ya kuishi na mtoto akawa ni Tausi Zedi anahudumia tu.


Zedi hakutaka kukubali akataka kujua jeuri ya Kabah.Akarudi tena kwenye kazi ya upelelezi bila kupenda


Mwanzo tu wa upelezi wake akagundua biashara haramu ya Kabah,Kabah alikuwa anasafirisha watu na madawa ya kulevya.


Kitu ambacho Zedi hakujua ni kuwa Kabah aliingilia familia yake kama kulipiza kisasi maana alijua Zedi ndie aliemuulia baba yake katika mkasa uliopewa jina KIKOSI CHA PILI.


Kabah alitaka amtese Zedi kisaikolojia kabla hajamuua,hilo alifanikiwa,alisambaratisha familia yake na sasa anaimiliki yeye na alikuwa ameanza kuitumia atakavyo.


Kabah aligundua nyendo zake zinafuatiliwa na komando hatari Zedi hivyo haraka akasuka mpango kabambe wa Zedi kutekwa ndani kwake,hilo nalo alifanikiwa japo kwa mbinde sana.


Tausi tofauti na alivyotegemea kupata mapenzi,akajikuta akianza kula joto la usaliti,safari za nje zikaisha huku kila mara akipigwa na kuingiliwa kingono na marafiki wa Kabah.


Kabah akamletea wanawake wengine ndani na kufanya nao ngono mbele yake.


Tausi akashuhudia Mwanae akiachishwa shule na kuanza kutumika kubeba mizigo kadhaa ya dawa za kulevya.


Alipojaribu kuzuia akaambulia kipigo na vitisho.


Akajuta,akajuta!!


Ikaja siku aliosaidiwa na Temba na sasa yupo mbele ya shemeji yake Ziga na mke mwenzie Mina aibu ilioje!!


****


Zedi ndie aliepita upande wa nyuma na kufanikiwa kuona kikao kilichokuwa kinaendelea kupitia dirishani


Zedi alishangaa kumuona kabah,ila alishangaa zaidi kumuona waziri wa uchukuzi na madini wa nchini Tanzania huku wabunge wawili nao wakiwa miongoni mwao.


Akiwa bado anatazama akashudia Mao Waira akiingia kwa kasi pale ndani na kuvamia ule mkutano na kuwaweka chini ya ulinzi watu wote.


Akiwa bado anajaribu kufungua dirisha apitie hapo akashudia Kabah akiruka na kumpiga Waira kwa pigo safi kisha hakutaka kusubiri akakimbilia nje


Zedi hakutaka kuachwa nae akatoka kasi kuwahi upande wa mbele lakini alikuwa amechelewa alikutana na moshi wa gari


Hakuhangaika nae





Zedi hakutaka kuachwa nae akatoka kasi kuwahi upande wa mbele lakini alikuwa amechelewa alikutana na moshi wa gari


Hakuhangaika nae


Akaingia ndani haraka na kuongeza nguvu pale ndani huku nje vikisikika vingora vya polisi vikipiga kelele kusogea pale.


Wahalifu wote wakatiwa pingu kisha Zedi akaomba awasiliane na Ikulu Tanzania,na alipomaliza akaomba kuwasimamia wabunge wale na waziri wao had ndege binafsi itakapo kuja kuwachukua.


Waira akabaki na kazi moja tu kuchoma maabara zote zilizokuwa chini ya mbwa weupe na wanajeshi wa Kenya walielekea Karura forest kulikokuwa na kambi ya Mbwa weupe.


Kasiki ilioibwa kutoka kwenye nyumba ya mzee matare ilimshinda Mao Waira kuifungua,akamuomba Zedi na Zedi akatumia namba 0258 alizopewa wakati akiwa ametekwa na mzee matare.

Kasiki ile ndio ilibeba siri ya mkasa ule.


Mzee matare alikuwa ni dokta na mara nyingi alijikita kufanya tafiti za wadudu na hapo ndipo akapata wazo la kutengeneza aina ya wadudu watakao kuwa kama tiba kwenye mimea yaani wadudu watakao kuwa wanakula wadudu waharibifu wa mazao


Mzee huyu alitengeneza fomula za kisayansi na hatimae akafanikiwa wadudu wale.


Furaha yake ikapata doa baada ya kupata ugeni kutoka nchi za mbali,wao wakaja na wazo la kutengeneza wadudu wala nyama.


Kadri wafadhili wale walivyokuwa wakimfadhili wakaleta na watalamu wao,nasasa Mzee matare akaanza kuona hatari na kibaya zaidi akagundua mpango uliokuwa nyuma ya yote


Mpango ulikuwa ni kuwasambaza wadudu wale maeneo yote ya nchi za Afrika mashariki,kisha wao waje na tiba ya kuwaua wadudu wale,watapata pesa nyingi sana.


Lakini kikubwa walikuwa wanamwaga wale wadudu sehemu zilizokuwa zimegunduliwa madini na mafuta na ugunduzi huo ulikuwa haujafika mikononi mwa serikali yoyote katika nchi hizo.


Maeneo athirika yote wakazi wangehama hivyo,wao wangeingia ubia na serikali kuyamiliki kwa kigezo cha kutoa dawa ya kuwaangamiza wadudu wale.


Mzee yule akafanya hila akaiba ramani ya maeneo hayo yanayolengwa na akaificha ndani kwake na wakati anafanya jitihada za kuzuia akaangukia mikononi nwa wa wasaliti hatimae akaiaga dunia mbele ya macho ya Zedi.

****


Zedi alipokelewa kama shujaa uwanja wa Dodoma na waziri mkuu,IGP na CDF bwana Salim Komba.


Watuhumiwa wakachukuliwa na kupelekwa mahabusu.


Zedi akatoa ramani nzima na mpango mzima ulivyokuwa huko Kenya ila hakuwaambia kuhusu kutoroka kwa Kabah,alimhitaji akiwa mzima au mfu yeye mwenyewe.


****


Wakati Kabah akiwa ndani kwake na kudhani yupo salama,akashangaa kuona Burizozo anaingia kwa kasi na bastola mkononi.


“Tumevamiwa asee,Temba ana…” hakumaliza kauli yake Kabah akachukua bunduki yake na kutoka nje.


Kama alidhani vita ni ya kitoto alikosea


Alipata kushuhudia watu watatu tu wakiua kama mchezo tena kwa kasi na weledi wa hali ya juu.


Akamwacha Burizozo aendelee kupambana yeye akarudi ndani na kutaka kutumia mlango wa nyuma kutoka.


Ziga alimuona wakati akijaribu kukimbia,akamfuata huku sasa burizozo akiwa amebakia kutazamana na Temba na Mina akagwaya.


Temba akamrukia kwa aina ya Tailand kiki na goti lake likakutana na kifua cha Burizozo na kumpeleka chini,haraka akatak kujinyanyua lakini akachelewa kasi ya Temba ilikuwa ni kubwa akamtandika teke la mbavu.


Temba akataka kumuua lakini Mina akawahi na kumzuia kisha akampiga pingu na punde gari za polisi zikaingia kwa fujo na kukutana na maiti kadhaa za vijana wa Mbwa wa geti.


Kitu ambacho askari wale hawakujua ni kuwa Temba ndie alikuwa kiongozi wao ,ikabaki siri ya Mina,Ziga na Temba mwenyewe.


Wakati kabah anataka kutoka nje tu akaukatana na mtu ambae hakutegemea


Zedi alikuwa kasimama wima mlangoni huku silaha ikiwa mkononi na alipomuona tu akaitupa na bila kuulizana ukaanza mkono wa adabu.


Ziga alikuwa kasi kuwahi kummkamata Kabah lakini akakuta rafiki yake akiwa anapambana na jasusi Kabah,yeye akabaki kuwa mtazamaji.


Mpambano ulikuwa ndani ya dakika tano tu lakini tayari Kabah alikuwa amevunjwa mkono na Zedi.


Zedi kwa hasira alizokuwa nazo akapaa hewani ili kummliza Kabah lakini kabla hajashuka Mina akaingia na kumpitia kwa kasi Kabah kisha akamtia pingu huku RPC Mabeyo akiingia pale na kuwapigia makofi huku akiwapongeza vijana kwa kazi waliofanya ndani ya muda mfupi sana.


Kabah alikaguliwa nyumba yake na kukutwa shehena ya dawa za kulevya na watu kadhaa waliokuwa mateka pale ndani.

***


Zedi,Ziga,Mina na Temba waliingia ndani ya nyumba waliokuwa wameweka hifadhi kwa muda na walichokutana nacho hawakukitarajia.


Tausi alikuwa amelala juu ya sofa huku povu likimtoka,mtoto nae alikuwa amekaa tu huku hajui kipi cha kufanya.


Zedi akamkimbilia mwanae,huku kwa mara ya kwanza Ziga na Mina wakilishuhudia chozi la mbabe yule.


Zedi hakuumizwa na kifo cha mkewe Zaidi aliumizwa na mwonekano wa mwanae.


Taratibu zikafanyika na mtoto wa Zedi akapelekwa soba.


****

Baada ya Wiki mbili ndani ya gereza la Isango kulitokea mauaji ya askari magereza zaidi ya hamsini huku wafungwa kadhaa wakitoroka akiwemo na Kabah,huku gereza likiachwa na maandishi makubwa MBWA WA GETI.


Taarifa hizi Zedi alizipata akiwa anamwogesha mwanae ahsubuhi huku Ziga na Mina wakizipokea taarifa hizi wakiwa ndani ya hoteli ya nyota tano huko Zanzibar.


“Karibu tena kiumeni,safari hii nakuua Kabah” alijisemea Zedi huku akilitizama kovu la mwanae tumboni.



MWISHO



Ahsanten sana kwa kuwa nami mwanzo hadi mwisho wa riwaya hii.

Yule mwenye kuhitaji kutoa wazo ama ushauri basi fanya hivyo.


Mwisho wa riwaya hii ni mwanzo wa riwaya nyingine tena ahsanten

0 comments:

Post a Comment

Blog