Search This Blog

Wednesday, 22 March 2023

MBWA WA GETINI - 4

   

Simulizi : Mbwa Wa Getini 

Sehemu Ya : Nne (4)



“Usiku wakati umelala chief alipiga simu kwako,nikaipokea,kisha akanipa maelekezo flani ambayo yalikuwa yanakulenga wewe!”


“Alisemaje!!?”


Alisema popote tulipo tunahitajika kuungana na na vijana waliokufa kutegua mtego unaotegwa hapa Dodoma,lakini kubwa ni kuwa ofisi inajua wewe na wale vijana ndo mlihitajika hapa na mlitakiwa kufikia hotel hii tuliopo”


Mina akakuna kichwa kuweka sawa fikira zake na hapo akakubaliana na Ziga ya kuwa kuna nyoka anawala visigino ndani ya idara yao na kwa hayo machache tu,waliona ugumu wa kazi maana adui anaeza kuwa amekita mizizi yake kila idara ndani ya nchi.


Mina akachukua mkoba wake na kuanza kutoka ndani ya chumba huku nyuma akifuata ziga.


Waliingia ndani ya gari yao na kabla hawajaondoka Mina akauliza


“Twaenda wapi muda huu”


Ziga akamtazama kisha akamjibu


“Sehemu salama ni nyumbani kwa Zedi”alisema hayo huku akianza kuondoa gari kwenye maegesho na kisha akaimakata barabara


“Yah wazo zuri na pia tunaeza mshawishi akatusaidia mawili matatu ndani ya huu mji” aliongezea Mina huku tayari gari yao ikiyapita magari kadhaa kwa mwendo wa kawaida.


Ila ni kwa kuwa hawakujua na laiti wangejua!!!!!!





Ila ni kwa kuwa hawakujua na laiti wangejua!!!!!!


****


Burizozo alikuwa amekaa kwenye sofa akitizamana na Tausi,huku kushoto kwao kukiwa na mtoto mdogo umri wa miaka kama mitano ama sita hivi


Tausi alikuwa akimtizama Burizozo kwa chuki kubwa sana.


Tausi alitaka kusema kitu lakini alikatishwa na sauti ya mtoto aliekuwa karibu yake ,mtoto alilalama njaa ,alitaka kunyanyuka ili ampe walau chai ahsubuhi ile lakini akapata onyo kutoka kwa Burizozo


“usimpe chai ama kitu cha moto,atakufa maana ametoka kutema mzigo sasa hivi….”


Kilifuata kilio kutoka kwa Tausi,alilia kwa kuona mwanae amegeuka kuwa mbeba madawa ya kulevya.


Na hapo akamatazama tena mwanae yule na Kama ndio anamwona kwa mara ya kwanza,akaona vile mtoto amedhoofu,akamfunua shati alilokuwa amevaa na hapo akaona kovu kubwa lililokuwa tumboni kwa yule mtoto mdogo.


Tausi hakutaka kujiuliza lile kovu ni la nini,tayari alishajua hutumika kutolea tembe zinazosalia tumbobi baada ya kushindwa kutoka kwa njia ya haja .


Tausi alilia na kama mtoto mdogo lakini kilio chake hakikufika mbali wala hakikuwa na thamani zaidi kilimwamsha Kabah aliekuwa kalala juu gorofani na akashuka kwa kasi na kipensi tu na kuwakuta Tausi na mwanae wamekumbatiana,hakujali.


Kwa kasi akamfikia Tausi na kumvuta juu na haraka akamchapa makofi kama sita mfululizo na kumchana usoni kisha akamsukuma kwa nguvu na kumtupa juu ya sofa na bila huruma akanyoosha mkono ili amtandike kofi mtoto aliekuwa amesimama kando akitizama mama yake akisulubiwa,lakini konde lile halikufika likadakwa na Burizozo,


“We need him more than you think” alisema kwa lugha ya kusihi na maneno yakamwingia Kabah akagairi kutoa kipigo kwa mtoto aliefanana na Zedi kwa kila kitu.


Hasira zake bado zilikuwa kwa Tausi na akaendelea kumshushia makonde na kufanya damu zijae kwenye sura ya mwanamama yule sura ambayo ilikuwa imeanza kutota kwa utumizi wa dawa za kulevya.


Kabah alipoona roho yake imesuuzika kwa kipigo alichotoa akaanza kumburuta Tausi kuelekea kwenye chumba ambacho huwa hakifunguliwi mara kwa mara na huko akamtupia humo kama mzoga kisha akakifunga kwa nje.


Tausi alijikunyata kama mtoto mdogo huku kilio kikiwa ni kwikwi,alijuta kwa alioyafanya na alijuta kwa kumsaliti mwanaume aliempenda kuliko kitu chochote.


Mara nyingi Tausi akiwa katika hali kama ile hujituliza kwa dozi ya sindano ama mnuso wa cocaine.


Na tayari mwili ulikuwa unahitaji kupata hicho kitu,lakini hakuwa na wa kumpa ndani ya chumba kile cha giza totoro.


Matanio yalizidi uwezo,akanyanyuka,lakini hakupiga japo hatua mbili akawa yupo chini maumivu ya kipigo yalikuwa yapo kila sehemu,tena ni bora angelikuwa amepigwa na mtu kama mimi au wewe ambao hatujui hata silaha inashikwa vipi,lakini huyu alikuwa amepigwa na komando la waasi wa huko Somalia,tangu utoto hadi ujana wake anacheza na roho za watu tu.


Tausi hamu ya kuvuta unga ilimzidia,akajongea hadi kwenye mlango,akaugonga mara kadhaa na punde ukafunguliwa ila alieufungua hakuwa msemaji akafanya alichoagizwa,akamwaga maji ya baridi ndani ya chumba alichomo Tausi kisha akaufunga ule mlango na kumwacha Tausi akiwa anaelea juu ya maji ya baridi.


Kwa kiasi chake ilimsaidia kumwindolea zile hisia za uhitaji wa kuvuta unga,lakini nafuu ile haikudumu kamwe.


Tausi akawa anayapitia mateso ya kujitakia!!!

****

Ziga alikuwa anaikata kona ya nkuhungu chama na akapunguza kidogo mwendo kulingana na ukali wa kona ile.


Safari yao ilikuwa ya ukimya,haikuwa safari ya mbwembwe kama walivyokuwa wamezoea wawapo wa wili ndani ya gari.


Mbele kidogo ya mtaa wa nkuhungu vibandani Ziga alikata kulia na kupita pembeni kidogo ya ukuta wa nkuhungu sekondari kisha akasogea mwendo wa mita mia mbili na kisha akasimisha gari mbele ya geti kubwa jeusi.


Ziga akapiga honi kadhaa lakini hakuna alietoka kufungua,ikabidi Mina ashuke na kulisogelea geti lile na hapo akaona kitu kilichoamsha hisia mbalimbali ndani ya kichwa chake.


Kimuonekano tu ilionekana eneo lile halijakaliwa na watu kwa muda mrefu kidogo.


Mina akalisogelea zaidi lile geti na kujaribu kusukuma na hapo mshangao mwingine ukamvaa geti la nyumba ya Zedi lilikuwa wazi na kwa tahadhari kabisa akaingia ndani ya uzio wa geti lile nako akazidi kupigwa na butwaa.


Palionekana kutofanyiwa usafi kwa muda mrefu hali iliopelekea kuote majani marefu huku uchafu wa kila aina ukiwa umejaa pote .


Mina akazidi kujongea kuingia ndani ya nyumba ya Zedi na huko akapigwa na mshangao ambao hakuutegemea.


Ni wakati anaingia ndani ya nyumba ya Zedi,mlangoni tu akakutana na matone ya damu yalioganda na Kukauka kabisa na yalionesha ni ya muda mrefu kidogo na pia mlangoni kulionesha kumeparazwa na kitu kama risasi hivi.


Akausukuma mlango na kuingia ndani kabisa kwa mwendo wa tahadhari kabisa.


Hakuwa mgeni wa matukio na moja kwa moja akajua kabisa pale ndani palitokea ugomvi wa aina yake na wapambanaji walionesha wanaujua mchezo,Mina akabaki akishangaa na kujiuliza kulikoni kimemkuta nini Zedi.

***

Ziga akiwa ndani ya gari aliona vile Mina alivyokuwa ananyata kuingia ndani na hapo akajua kabisa huko si salama nae akataka kushuka ili aungane na Mina.


Ni wakati alipokuwa akikaribia kufungua mlango wa gari akili yake ikamtuma atazame kwenye kioo na hapo hakuwia kugundua hawapo peke yao pale,kuna macho ya watu wawili yalikuwa yanawatizama,na sio kuwatizama tu yalikua yanawatizama kwa husda.







Ni wakati alipokuwa akikaribia kufungua mlango wa gari akili yake ikamtuma atazame kwenye kioo na hapo hakuwia kugundua hawapo peke yao pale,kuna macho ya watu wawili yalikuwa yanawatizama,na sio kuwatizama tu yalikua yanawatizama kwa husda.


Ziga akashuka na bila kujali nae akazama ndani na kuyashudia yale alioyashuhudia Mina na kisha wakajikuta wote wapo ndani ya sebule iliojaa vumbi huku kukionekana kuna vurugu zilifanyika hapo ndani na matone ya damu yakiwa yameganda sakafuni.


Walitazamana


Kisha kila mmoja akaanza kukagua upande wake na kila mmoja akijaribu kuwaza alichokiona.


Lakini wote mawazo yao ni kama yalikuwa sawa wakajikuta wakielekea kwenye chumba cha Zedi maana walikijua na huko nako wakakutana na mapya.


Chumba kile kilionekana kina kaliwa na mtu na mtu yule ni mvuta sigara maana vipisi kadhaa vilikuwa chini na kiti kilikuwa kimewekwa pembeni kidogo ya mlango kuonesha mtu yule alipenda kukaa pale.


Kila mmoja alijua nini maana ya kiti kile,ilimaanisha mkaaji huwa anamsubiri mtu,mtu gani hawakumjua.


Ziga alishika hiki akashika kile ili mradi alijua anachokifanya.


“Nyumba hii inaonekana haikukaliwa na mwanamke muda mrefu zaidi kuliko siku alizokaa mwanaume”..yalikuwa maneno ya Ziga na yalisikiwa vizuri na Mina.


Namna ya upangiliaji wa muonekano wa chumba na baadhi ya sehemu za nyumba ile ndizo ziliwapa uhakika ya kuwa mwanamke hakuwa amekaaa pale ndani kwa muda mrefu kuliko mwanaume na ndivyo ilikuwa lakini Mina aliiuliza kitu.


“kwanini umeona mke wa Zedi hajakaa hapa kitambo kuliko Zedi!?”


“Nimeona mpangilio wa hiki chumba vitu vingi vimepangwa kiume na vitu vingi vipo mwonekano wa kiume japo kama huelewi utaona ni sawa tu..” alizungumza Ziga kisha akaendelea huku sasa akishika kitanda


“chumba chochote anachoishi mwanamke, lazima kitanda ukikute kushoto mwa chumba lakini pia kitanda anacholalia mwanamke lazima ukute kaambatanisha mito na mashuka.”alizungumza zedi huku wakati huo akikaribia kabati la nguo na kulifungua


“ona hata namna ya kukunja nguo,mwanamke hakunji hivi”alisema Ziga huku akimwonesha Mina nguo kadhaa zilizokuwa ndani ya kabati.


“Pia naona ni nguo za kiume tu zipo humu za mtoto na za mke hazipo hata moja.”alisema Mina huku sasa wakianza kutoka ndani ya nyumba ile


“kuna tatizo na Zedi yupo matatizoni”alisema Ziga huku sasa wakikaribia gari lao lililokuwa nje na walipolifikia wakapanda huku Ziga akirudia tena kutazama upande ule aliona watu wakitizama,hawakuwepo nae akatia moto wakatokomea eneo lile.


Licha ya mwendo waliokuwa wanatumia kuwa mkali kidogo lakini Ziga hakukawia kujua nyuma kuna gari inawafuata na ilikuwa nyuma yao kwa tofauti ya magari mawili tu.


Wakati wanafika forway,Mina akashauri wagawane lakini kisomi na hapo wakapaki ndani ya bar ya forway bar kisha wakateremka na wakapanga kukutana kwa Rpc Mabeyo .


Walipoingia ndani ya ile bar gari lilikokuwa linawafuata likapita na kuingia kituo cha kujazia mafuta kisha wakateremka vijana wawili shupavu na wakarudi kwa miguu hadi forway bar,lakini walichoenda kukishuhudia hawakukikuta,si mwanamke wala mwanaume zaidi waliona gari ikiwa imepaki pembeni na kijana mmoja akihangaika kuisafisha.


Mmoja wao akanyanyua simu na kupiga anakokujua kisha wakaondoka,lakini Ziga aliwaona na sasa wao ndio walianza kufuatiliwa yaani ile muwinda huwindwa.


*****


Mapambazuko yalimkuta Zedi akiwa nakuru nje kidogo ya jiji la Nairobi na huko alikuwa anaitafuta bank ya KCB ambayo aliakuwa na tetesi na tetesi za kuhusu mambo kadhaa.


Akamlipa dereva taxi aliemleta pale kisha akajongea hadi kwenye mgahawa uliokuwa pembeni ya bank ile na akatafuta pembe moja ya mgahawa na kukaa huku akimtizama kila aliengia na kutoka eneo mgahawani pale lakini pia aliona eneo zima la Kcb lililokuwa bado limefungwa kwa sababu muda wa kazi ulikuwa bado haujatimia.


Akaagiza supu ya mbuzi na chapati nne na kupoza njaa.


Muda ulizidi kusogea na sasa bank ile ya Kcb ilikuwa ipo wazi na watu walianza kuingia na kutoka huku magari kadhaa yakiwa yanapaki na kuondoka mbele ya bank ile.


Akasimama na kulipa pesa kisha akapiga hatua kutoka pale mgahawani huku uso wake akiwa kauweka nyuma ya mawani kubwa na kichwa kimezibwa na kofia ya kibitozi,miguuni alikuwa kavaa raba nyeusi na mwili wake ulisitiriwa na suruali nyeusi ya jeans na fulana mpauko


Akavuka barabara kuingia ndani ya bank ile na moja kwa moja akaelekea pahali pa huduma kwa wateja


“Dada naomba kuoneshwa ofisi ya meneja!!” aliomba Zedi huku akiwa yupo makini na kumtazama yule dada na hapo akauona mstuko wa wazi kabisa na akashindwa kujua kwanini yule dada alistuka na hapo Zedi tena akacheza pata potea


“ooh u mrembo sana wewe waitwa nani vile!” aliamua kuchombeza hata kabla hajajibiwa swali lake la awali na akaona tabasamu la aibu kwenye uso wa yule dada


“Naitwa Wambui”

“ooh Wambui!! Jina zuri sana unaishi wapi!?”


“naishi Kibira,vipi wataka kuonana nami!?”


“Ndio ningelifurahi sana Kama ingelikuwa hivyo”


“ok utanipigia kwa namba hii” Wambui alisema huku akimpa Zedi kadi ya biashara na alipokwisha kuipokea akawapisha wateja wengine huku akipokea maelezo machache kuhusu meneja na ofisi yake,Zedi akajivuta hadi kwenye mlango wa meneja na kugonga kidogo kisha akasubiri na ndani ya muda mfupi mtu alitoka ndani ya ofisi ile na wakati wanapishana na mtu akietoka ndani ya ofisi ya meneja Zedi akapata kugeuka na hapo macho yake yakakutana na macho ya Wambui akimtizama huku mkono wa kushoto ukiwa na simu kuonesha ametoka kuwasiliana ndani ya dakika moja iliopita.


Zedi akatabasamu huku akijua kabisa yule dada amepiga simu sehemu hatari,hakujali akausukuma mlango na kuingia hadi ndani na alipoingia tu akakuta meneja nae anashusha chini simu ya mezani.


Haraka haraka Zedi alikuwa ameona picha kadhaa zilizokuwa zimebandikwa ukutani hakuzijali na hapo macho yake yakadaka jina la meneja yule aliemkuta mle E. KWASI.


Zedi akasimama mbele ya meza iliokuwa mle ofisini na kufanya kuwe na utenganisho baina yao.


‘naomba kujulishwa ilipo ofisi ya bwana Kamau' aliongea zedi huku macho yake yakiwa makini juu ya mwili wa meneja Kwasi.





Zedi akasimama mbele ya meza iliokuwa mle ofisini na kufanya kuwe na utenganisho baina yao.


‘naomba kujulishwa ilipo ofisi ya bwana Kamau' aliongea zedi huku macho yake yakiwa makini juu ya mwili wa meneja Kwasi.


“ooh aliacha kufika hapa ofisini wiki tatu sasa na ndio nikakaimu nafasi yake” alijijibu bwana Kwasi huku akiachia tabasamu la dhihaka na Zedi akajua anadhihakiwa makusudi


“hakuna taarifa zozote kumhusu!! Aliuliza tena Zedi


“Yeye ndie wa kutoa taarifa ofisini na si ofisi ijue taarifa zake” alijibu kijeuri Kwasi.


“ok naomba kujua taarifa za akaunti hii…”.(huku akitaja namba)


Kwasi akimtizama na bila kupepesa alimwambia hiyo ni ngumu kulingana na utaratibu wa kazi ulivyo ukizingatia Zedi sio mmliki wa akaunti ile na hapo tena Zedi akaongeza swali lingine


“Mzee matare na Kamau nasikia walikuwa wote ni wahudumu wa hii ofisi” hapo akaona msituko wa wazi kwa meneja yule japo alijitahidi kuuficha msituko ule na hicho ndicho alichokitaka Zedi.


Zedi hakuwa na pa kuanzia harakati zake za kuzima na kujua yaliojificha nyuma ya utafiti ule uliokuwa unateketeza mamia ya watu nchini Kenya na kuwanyima usingizi viongozi wazalendo na nchi yao,hivyo kwa kufauata maelekezo machache ya marehemu Matare alifanikiwa kupata kadi za bank ndani kwake na kuamua kwenda nazo huko ili japo aone mapokeo ya huko hivyo sasa akajua kuna mengi yamejificha nyuma ya kutekwa kwake na mzee Matare.


“Basi naondoka meneja ahsante kwa ushirikiano”alizungumza Zedi huku akianza kupiga hatua ili aufikie mlango,lakini akaona kundi la watu wakiwa kule mapokezi na kila mmoja alikuwa na bastola mkononi na walikuwa wanapokea maelekezo kutoka kwa Wambui huku akinyoosha kidole kuelekea kule kwenye mlango wa meneja.


Zedi akapagawa na haraka akageuka huku aliko meneja na hapo akapigwa na butwaa jingine.


Meneja alikuwa ameshika bastola double colt akiwa amemwelekezea huku tabasamu feki likiwa usoni pake.


Zedi hakuwa na pa kutokea hata dirisha lililokuwa mle halikutosha kupita mtu maana lilidhibitiwa kwa nondo imara kabisa.


Zedi akatazama juu ya dali la ofisi ile na hapo akatabasamu kimoyomoyo akatabasamu japo hakujua kwanini ofisi ile imejengwa kwa namna ile alioiona.


Watu wale haraka wakawa wanakuja kwa kasi na Zedi akawa bado amenyoosha mikono juu huku kila mara akipokea onyo kutoka kwa meneja Kwasi ya kuwa asijaribu kufanya ujinga wowote la sivyo angeliondoka na uhai wake.



Kitu kimoja meneja Kwasi hakujua ni kuwa bastola alioishika ilikuwa na umuhimu sana kwa Zedi maana hadi muda huo hakuwa na silaha yoyote zaidi ya mikono na akili yake .


Zedi akawa anamtazama meneja machoni tu na hapo akapata kuona alichokusudia kuona ndani ya macho ya meneja yule.


Meneja Kwasi alikuwa anatazama mlangoni huku akirudi kumtazama Zedi ni wakati macho yake yalipokuwa yakitizama mlangoni tena akashangaa kuona kitu cha ajabu.


Kule mapokezi kulikuwa kunafuka moshi kutokea chini kwenda juu huku watu wale waliokuwa wakijongea kwenda kwenye ofisi yake wakianza kurudi tena kule mapokezi kulikokuwa kunafuka moshi mzito huku sasa vingora vya tahadhari vikianza kulia jengo zima huku mashine za kumwaga maji kwa dharura ya moto zikianza kufunguka na kumwaga maji.


Zedi akaitumia vyema nafasi ile na kwa kasi ya ajabu kabisa akaruka na kutua juu ya meza huku mikono yake tayari ikiwa imekamata shingo ya meneja Kwasi na mkono wenye bastola ulikuwa umekamatwa na kuwekwa katikati ya miguu ya Zedi.


Mikono ilielekea kulia pamoja na shingo ya meneja huku miguu ikielekezwa kushoto na mkono wa meneja hivyo ikawa shingo imevunjwa na mkono umevunjwa na kisha bastola ikawa ndani ya himaya ya Zedi na hapo ndipo Zedi akaamua kutazama kule mlangoni japo sasa kioo cha mlango kilianza kufifia kuonesha upande wa pili kwa sababu ya moshi ule.


Zedi hakutaka kuhadaika kivile maana hakujua nani hasa kafanya vile maana kwa uzoefu wake alijua ule ni moshi wa smoke mashine na huwa unatumiwa maalumu na makomando watakapo kutoroka kwa adui na pia moshi ule ulikuwa na tabia ya kuwa kama unalevya kwa mtu awae karibu na kuuvuta.


Aliamini hakuna anaemjua pale Kenya hivyo hakutaka imani imweke matatizoni.


Haraka akasimama juu ya meza na kushika pangaboi lililokuwa linabembea juu kisha akabana pumzi kwa nguvu,hii ilimsaidia kupunguza uzito hivyo pangaboi lile likahimili kumbeba nae akalitumia na kujivuta kwa kasi huku mkono mmoja ukiwa umetangulia na akafanikiwa kugonga kijimlango kidogo kilichokuwa kule juu nacho kikafunguka huku kamba ikishuka chini na kwa haraka akaingia huko na kukifunga tena.


Ni wakati anamalizia kufunga na kugeuka ndipo akaona jambo lingine ambalo mwanzo alilitilia shaka.




Ni wakati anamalizia kufunga na kugeuka ndipo akaona jambo lingine ambalo mwanzo alilitilia shaka.


Huko juu alikuta si dari tena,ilkuwa ni uwazi mkubwa tu uliotosha mtu kutembea na kulikuwa na boksi kadhaa na kulionekana kufanyika shuguli za kuyapaki maboksi yale na hapo akaamua kufungua boksi moja.


Hakuamini macho yake alikutana na mabomu ya c4 yakiwa yamepangwa vizuri na kulikuwa na mabomu mengine ya baruti.


Zedi akazidi kuyafungua maboksi yale na kukutana na silaha nyingi za kila aina,akazitamani baadhi na akachukua bastola mbili na kuzisunda kiunoni hivyo akawa na jumla ya bastola tatu.


Akazidi kuyafungua maboksi yale na kukutana tena na dawa za kulevya zikiwa zimewekwa kwenye mfuko ya chumvi huku juu kukiwa na jina la MZURI.


Hakuwa na muda zaidi wa kukaa kule juu,hivyo haraka akatafuta namna ya kutoka.


Alikutana na sehemu iliokuwa imetengenezwa kama mlango wa dharura na akatumia hiyo sehemu kutoka mle ndani na huko akajikuta anatokea kwenye ngazi zilizoonesha yupo kwenye floor ya juu na kuna ngazi zinashuka chini,hakuzijali.


Akapita kwenye korido pana iliokuwa inatenganisha vyumba kaadhaa vilivyokuwa ni ofisi kimuonekano,huku akishuhudia ukimya wa hali ya juu na nafsin mwake akajua wenyewe wamekimbia baada ya king’ora cha hatari kulia pale ndani.


Hakutaka kushuka ngazi za chini zaidi akaambaa na korido na kutokea upande wa maliwato na huko akatembea kidogo na kukutana na uwazi uliokuwa unampeleka hadi dirishani akalifikia na kulifungua kisha akatazama nje na kuona namna majengo mengine yalivokaa,yalikaa kwa kupeana migongo.


Akatazama kulia na kushoto akaona alichokuwa anakitafuta.


Bomba la kupitisha maji machafu kutoka juu gorofani hadi chini na yeye akafanya jitihada kidogo na kulifikia kisha akalitumia kushuka chini na kutokomea mtaani huku swali likiwa ni nani aliefanya vile ndani ya bank ile,na alifanya kwa malengo gani hakupata majibu na hadi muda huo alikua anavuka barabara na kuita taxi alioomba imrudishe Nairobi West mtaa wa South b dereva akatii bila kujiuliza sana.


Mjini Naivasha wadudu wasioeleweka walikuwa wanashambulia watu na wanyama waliokuwa wakifugwa huko na,serikali ilikuwa imejaribu kwenda kutoa msaada lakini walizidiwa kasi na wadudu wale,watu walikufa na wachache waliofanikiwa kutoroka,huku sumu ya kuuwa wadudu ikimwagwa huko angalau kuzuia shambulizi hilo lakini wadudu wale hawakufa na ndo walizidi kuleta maafa huku wakiwa na kasi ya ajabu.


Mji wa Nairobi ulitangaziwa hali ya hatari na kila mtu hakujua aelekee wapi kwa wakati huo……


Hayo yalisikika kutoka kwenye radio ndani ya taxi huku mtangazaji akiwa ni Leonard mambo mbotela.


Zedi aliekuwa ameegemea kiti na kujilaza yote aliyasikia na hapo ndipo akili yake ikatakiwa kufanya kazi zaid maana aliona hatari ya shambulio lile la wadudu ambao yeye tu ndie alijua wanatoka wapi japo hakujua chanzo ni nini hasa na kwanini watu wale wanataka kuchukua nchi kwa kutumia ukatili wa namna ile.

****


Dereva wa taxi alisimamisha nyuma ya jengo la KRA(KENYA REVENUE AUTHORITY)kisha akaomba ujira wake na Zedi akazama mfukoni na kumpa kisha yeye akashuka na kulitizama jengo lile namna lilivyokuwa refu.


Akapiga mwendo kidogo na kuingia kwenye kiuchochoro kilichikuwa kimetenganisha majengo kadhaa na kisha akanyoosha na kutokea upande wa mbele wa jengo lile na hapo akaingia ndani yake.


Macho yake yakafanya kazi moja tu kusoma vibao vya maelezo ya ofisi na kazi zake na hapo akapata ofisi alioitaka.


Ilikuwa ni ofisi ya usajili wa magari.

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog