Simulizi : Zawadi Toka Ikulu (2)
Sehemu Ya : Pili (2)
Mzee Manguli anawekwa ukutani na kisha Jesca anapiga hatua kama kumi kurudi nyuma kisha anaielekeza Bastora yake kifuani kwa baba yake kana kwamba alikuwa akilenga shabaha. Walinzi walikuwa wakishika vichwa maana walijua lolote likitokea ni juu yao, walilaumiana kwanini wamemkabidhi rais kwa binti yake. Jasho lilikuwa likimtiririka mzee Manguli, aliangua kilio kama mtoto akihofia kifo taratibu Jesca anashusha bastora huku akimsogerea.
“baba nimekukosea nini katika maisha yangu?”
“hapana mwanangu hujawahi hata siku moja …. Kunikosea”
“sasa kwanini unanifanyia hivi”
“mwanangu nisamehe sikujua kama tutafika huku”
“sawa msamaha wangu kwako ni kumuona Jamae akifika hapa tena akiwa hai tofauti na hapo nitakachokifanya hauto kiamini, nikipoteza mpenzi amini usiamini stakuwa na haja tena yakuwa na baba katika maisha yangu hasa baba kama wewe asiyejua thamani ya furaha kwa binti yake” Baada ya kusema hayo ulisikika mlio wa bastora na kuzua tafarani kwa walinzi.
Hali ilipotulia mzee Manguli alikuwa kajiinamia chini akilia huku Jeska akiwa bado kashika bastora na alikuwa makini zaidi. Upande wa juu kidogo ya kichwa cha mzee manguli kulionekana tundu lililotobolewa na risasi iliyofyatuka kutoka kwenye bastora ya Jesca na sasa ndani kulijaa hekaheka. Mama Jesca anaingia huku akilia kwa hofu maana aliamini huenda lolote limetokea kutokana na kishindo alichokisikia Mungu saidia aliwakuta wote wako salama alishukuru Mungu, binti yake alikuwa bado kashika bastora na ameielekeza kichwani kwa baba yake. Pamoja na kumsihi kwa muda bado haikuzaa matunda alionekana kutokukijali alichoambiwa aliendelea kuwa bize na shabaha yake, hakuonekana kuteteleka bali alizidi kuwa kimya na makini zaidi.
“Jesca unataka nini mwanangu, na kwanini unayafanya haya? ….. hivi huna hofu ya laana kumfanyia hivi baba yako?”
“Mama aliyonifanyia baba yanatosha na sasa nimemwambia neno moja tu ninamhitaji Jamae hapa na si vinginevyo” alijibu bila hata kupepesa macho.
“Baba Jesca tafadhali msikilize mtoto haya mambo yaishe hii ni aibu kwa familia, kumbuka tumetoka kwenye aibu k bwa ya ndoa kuahirishwa msinirudishe kwenye aibu nyingine ya mwaka hapa vymbo vya habari vikijua hatutaishi kwa amani tafadhari ninaomba yaishe”
Mzee Manguli anaomba simu yake ya mkononi anajaribu kuongea na vijana wake, lakini katika mazungumzo hayo anaishiwa nguvu ghafla na kufanya hofu izidi kutanda mioyoni mwa wahusika. Lakini Jesca anagundua huenda ni janja ya kumdhoofisha kisaikolojia lakini alibaki na msimamo wake.
“Hujaanza leo kuigiza mzee Manguli hivyo usicheze patapotea nitakuangamiza bira huruma” Jesca aliongea kwa sauti kubwa huku akiikoki vyema bastora yake na kidole chake kikakaa vyema kwenye trigger. Hakuna aliyetegemea kwani risasi kama tatu zilifyatuliwa mfululizo na zote zikazama ukutani huku kila mtu akiwa chini kwa hofu.
“sijui utaelewa lini kuwa stanii na sijui utaacha lini ujinga wa kunijaribu… kifupi ni kwamba usitegemee huruma kutoka kwa kiumbe hiki ulichokizaa maana nakujua kuliko unavyodhania unatabia yakuuigiza uhalisia na kwa bahati nzuri huwa unashinda ila si kwa leo, mimi na wewe ili tuelewane… na ili nisikupoteze katika ulimwengu huu ninamuomba Jamae Justine ndani ya masaa mawili narudia tena ndani ya masaa mawili” Baada ya kusema hayo aliseti saa yake vyema na huku bastora yake ikiendelea kuelekezwa kwa mzee Manguli.
Ni nusu saa inapita baada ya mzee Manguli kupiga simu na sasa msafara mfupi wa magari yapatayo manne ya kifahari unaingia pale nyumbani na baada ya kufika wanashuka walinzi waliovalia suti nyeusi huku mtu mmoja akiwa na pingu mikononi lakini alikuwa kafunikwa uso. Walipandisha ngazi na kuingia mpaka ndani. Katikati ya sebure kubwa kijana aliyefunikwa uso alifunguliwa ule mguko aliofunikwa na alikuwa ni Jamae Justine alionekana kuwa na makovu kadhaa usoni ambayo yalikuwa yakiendelea kupona. Na sasa alikabidhiwa kwa Jesca walikumbatiana na kubusiana bila kujari hali ile ilizidi kumkera kiasi gani mzee Manguli lakini hakuwa na jinsi.
****
Juhudi za kulipigania penzi zinafanikiwa, sasa Jamae Justine anafanikiwa kuwa mmoja wa wanafamilia wa familia ya mzee Manguli. Bila kuchelewa mama Jesca anamshauri mumewe na hatimaye wanakubaliana kuliharakisha swala la ndoa ya watoto wao na ndoa iliyofanyika nchini marekani na vijana hawa walifanya fungate lao katika miji ya Hongnkong nchini china, Moscow nchini urusi kabla ya kuhitimisha fungate lao katika nchi ya Qatar huko katika falme za kiarabu.
Taarifa za ndoa hii zilikuwa siri kubwa hakuna aliyejua zaidi ya wazazi wa pande mbili nina maanisha wazazi wa Jamae Justine na wazazi wa Jesca Manguli. Hakuna chombo chochote cha habari kiliarifu habari hii kutokana na kukwepa aibu na tuhuma nzito kama walizokutana nazo mwanzo familia ya rais haikuwa tayari kukutana na sakata kama lililopita la fanilia ya Mzee Gao. Lakini Ilikuwa ni furaha kwa wapenzi hawa wawili maana walipendana sana na ilikuwa ndoto yao kuishi pamoja katika maisha yao yote. Tayari walikuwa wamefunga ndoa na maisha yalitakiwa kusonga mbele. Kila wakati walikumbatiana na kucheka huku Jamae akitoa pongezi kwa Jesca kwa juhudi kubwa alizozionesha katika kulipigania penzi lao na hatimae imekuwa kama walivyotarajia.
Hatimaye baada ya fungate walirejea nyumbani na kuendelea na maisha yao kama kawaida, mzee Manguli alimpa mkwe wake kiasi kikubwa cha fedha kama zawadi fedha hizo zikawa chachu ya kuanza tena kwa ustawishaji wa viwanda na makampuni yake na sasa Himaya ChapaKazi ilifufuka baada ya kujengwa kiwanda kikubwa cha mavazi huko mkoani pwani, kiwanda hiki kilitumia malighafi za ndani na kulilenga soko la mataifa ya ulaya, marekani, kusini mwa America na Asia. Mafanikio hayakuwa madogo na sasa Himaya ChapaKazi ilirejea kwa muundo wa kimataifa zaidi. Ni Jamae Justine mkurugenzi mkuu wa Himaya ChapaKazi alikuwa bado akiliongoza Jahazi kwa makini zaidi na sasa amerejea katika mapambano.
Si tu kupendwa bali kulingana na Tabia yake yaunyenyekevu, kujishusha na kupenda kushauriwa, Jamae alijikuta akiheshimiwa sana na Mh. Rais mbali na kuwa mkwe sasa alikuwa ni rafiki mkubwa mno na mshauri mkuu wa rais Manguli Himaya ilizidi kuongeza bidhaa sokoni huku ikiongeza ushindani kwa makampuni makubwa ya nguo duniani na kuifanya kuwa moja ya kampuni kubwa ya uzalishaji wa Mavazi kutoka Afrika yanayouzwa ughaibuni na iliwatumia wabunifu wa kimataifa katika tasinia ya mavazi yanayokwenda na wakati hali hiyo ilitia hamasa na kumfanya Jamae kuwa moja ya matajiri vijana katika nchi hii.
******************
Baada ya mawazo mazito yaliyonikumbusha mengi Jesca ananikaribisha chakula na tukaketi mezani, tulikaa mezani na kuanza kupata chakula, kila siku mke wangu hakuwahi niangusha kwenye swala la mapishi hivyo kila nilapo chakula chake huwa nahisi ndiyo kwanza kanipikia kwa mara ya kwanza. Lakini pamoja na kuwa mtoto wa rais bado alipenda kuishi maisha ya kawaida sana alipenda kupika, pia alipenda kujichanganaya kama watu wengine lakini pia hakuwa anapenda kuwa na wasaidizi wa kazi nyumani kwani si mtu wakujikweza, tangu tumeoana na kuamua kujitegemea hatujawahi kuwa na msaidizi wa kazi za ndani mbali na kuwa na walinzi wetu wa getini wanaolinda usalama wa nyumba yetu.
Wakati familia hii ikiendelea kupata chakula ni simu ya mkurugenzi msaidizi wa kampuni ya Himaya ChapaKazi ilipigwa na alitaka kuongea na Mkurugenzi mkuu, Jesca anaipokea
“ hallo shemeji habari za Marekani?”
“ni nzuri sana hapa Washington mambo ni mazuri sana shemeji, vipi huko mnaendeleaje?”
“Aaaha! Tunaendelea vizuri shemeji yangu, karibu sana nyumbani bwana urudi tumekukumbuka sana”
“Haya nitarudi nadhani baada ya miezi sita ijayo usijali shemeji yangu tutakuwa pamoja….. Vipi Jamae yupo?”
“ndiyo yupo hapa ila nilikukumbuka ndiyo maana nikaidaka simu na kuipokea kabla yake”
“sawa nashukuru sana shemeji …. Okey naomba niongee naye kidogo”
“sawa huyu hapa”
“OOOh! Kimbo habari bwana mkubwa?
“Safi kaka za Dar ES salaam?”
“Ni nzuri kaka”
“usiniambie mzigo unapelea sokoni …. Sijui umejuaje nadhani kuna haja yakuongeza viwanda kaka na pia marighafi hazitutoshi inapaswa kuangalia kwenye mataifa jirani, kwa hali ilivyo Himaya imewavuruga kabisa wazungu”
“upande wa China pia nimeambiwa hali ni nzuri vijana wetu wanatengeneza pesa mpaka wachina wameanza kuikopi nembo yetu, si unajua tena wazee wakutengeza bidhaa feki tunaogopa hata kuwafungulia kesi maana tutajitafutia shida tu, hahaaaa! Ni jambo zuri, Kimbo sasa tunafanyaje?”
“hakuna cha kufanya maana fedha ipo tunahitaji kuongeza viwanda tu na ubora uongezeke katika bidhaa zetu”
“sawa tutatumia kama trioni nne za Tanzania kaka katika kuliboresha hilo ondoa shaka, tafuta wahandisi wazuri tuwape kandarasi nadhani mwezi ujao kazi ianze”
“ la mwisho una habari gani Juu ya Von Gao?”
“Gao… staki hata kujua habari zake”
“Ooh sasa wapaswa kujua, anakuwinda wewe na familia yako kibaya zaidi Domi yupo Kibaha amerejea kutoka Kanada alikokuwa kakimbilia inasemekana wameungana na Mmexico Paolo Mendez kwenye biashara zake za madawa yakulevya na sasa wao ndiyowasambazaji wakuu barani Afrika . Jamaa anafedha chafu namaanisha ni tajiri wakutupya na mbaya zaidi wameungana tena na familia ya Gao sasa Von Gao na Dominic Martine ni pete na kidole na mbaya zaidi wameungana kuku kupambana na wewe. Taarifa ya ndoa yako wameesha ipata nazani wanatafuta tu kujua unaishi wapi ili walikamilishe lengo lao, tafadhali kuwa makini watakuharibia”
“Duh! Sasa Kimbo unanishaurije brother ”
“Ah! Kwa usalama zaidi rudi Ikulu wewe na familia yako itakuwa salama tofauti na hapo peleka familia yako uhamishoni kwako wewe, Dar kwa sasa siyo sehemu salama kwa familia yako”
Jamae wakati akiongea na simu alijitahidi kuficha hisia ili mkewe asijue kama kuna tatizo na alifanikiwa na mwisho wakakamilisha mazungumzo yao.
Jamae anajikaza kwa tabasamu la uongo anamalizia kula kisha anampongeza mkewe kwa chakula kitamu kisha ananyanyuka na kwenda chumbani ambako anaketi na kushusha pumzi kwa nguvu. Alimtizama mwanane ambaye alikuwa na umri mdogo sana ni takribani miezi mitatu tu tangu auone ulimwengu, Eric Jamae ni mtoto wa kiume na kipenzi kwa wazazi wote wawili. Eric alikuwa kajilaza asijue hili wala lile lakini wazazi wake wanapita katika mitihani migumu kila kukicha na sasa kazi inaelekea katika kuyanusuru maisha ya familia ya Jamae Justine. Jamae alikuwa akilia kwa uchungu kwani aliijua vita iliyombele yake, vita ya Von Gao pamoja na Domic Martine si vita ya masihara maana tayari ameesha pigana nao mara kadhaa hivyo ni watu anaowajua vyema na ni watu walio na mpango wa kupambana nae na kuhakikisha wanampoteza katika ulimwengu huu.
Dominic Martine na Von Gao sasa ni marafiki wakutupwa wanaopendana na wanashauliana kwa kila kitu, uswahiba wao ulianza miaka kadhaa iliyopita huko jijini mwanza kipindi hicho martine akifanya kazi Himaya ChapaKazi alishiriki kwa asilimia tisini kumuuza bosi wake ambaye ni Jamae kwa Von Gao. Nasasa wameungana kwa lengo moja tu ni kuhakikisha wanamteketeza Jamae.
Ndani ya jumba moja la kifahari, anaonekana Von Gao na kushoto alikuwepo Dominic wakati upande wa kulia alikuwepo mwanadada mrembo Maria Kimaro ambaye kwa sasa wanaonekana kushibana sana na Dominic. Mazungumzo yao ungeweza kuyatabili kwani yalijikita katika sehemu moja tu nayo ni kuunganisha nguvu ili kuuangamiza uhai wa Jamae kwa gharama yoyote. Nimazungumzo ambayo hayakuwa na kingine chamaana zaidi ya unafiki, wivu na ulimbukeni.
Ungezisikia sababu za kutaka kumpoteza Jamae bila shaka zingekushangaza moja ilikuwa ni Von kutaka kulipa kisasi cha kunyang’anywa mchumba wake ambaye ni Jesca Manguli, Maria pia alitaka kulipiza kisasi kwani aliamini kuwa amemkosa Jamae kwasababu ya Jesca manguli hivyo hayuko tayari kumuona mwanamume aliyempenda akitanua na mwanamke mwingine wakati huo yeye akisota kwa kukosa mume.
Dominic yeye alikuwa na sababu zake yakwanza ni kuimarisha usalama wake na mali zake alizochuma kutoka Himaya ChapaKazi ambayo bila shaka ilikuwa ni kampuni ya Jamae Justine na sasa anatamani kumuangamiza Jamae Justine ili apoteze ushahidi na kuupoteza uwezekano wa kushitakiwa iwapo ataonekana nchini.
Baada ya kila mtu kueleza kwanini anatamani Jamae aangamie na sasa ilianza mikakati ya kumpoteza katika ulimwengu huu. Von Gao kijana wa mzee Pius Gao waziri mkuu wa zamani wa taifa hili, alikuwa bado akitumia nguvu ya madaraka aliyokuwa nayo baba yake bila hofu aliwaendesha watu mbalimbali atakavyo yeye bila kujali hadhi zao wala nguvu ya madaraka waliyonayo serikalini.
Simu ya Von ilikuwa masikioni akijaribu kupeleleza ni wapi angempata Jamae Justine, kupitia washirika wake haikuwa kazi kubwa kwani tayari walimuelekeza mtaa anaoishi mpaka namba ya nyumba. Na sasa maandalizi yalikwenda sawa na sasa kilichobaki ni kukamilisha mikakati ya kuiangamiza familia hiyo.
Simu iliyopigwa Jana usiku kutoka kwa Kimbo ilibaki kuwa kikwazo ndani ya moyo wake na sasa Jamae hakuwa na budi kumueleza mkewe ukweli kuhusiana na kile kinachoweza kutokea ndani ya familia yao iwapo hawatachukua tahadhari. Jamae alitumia busara sana ili mkewe amuelewe, ingawa ilikuwa ngumu lakini mke hakuwa na budi kuelewa. Kama familia waliapa kupambana mpaka mwisho walikumbatiana na kubusiana.
“Jesca ninaapa kuilinda familia yangu hata kwa kutoa uhai wangu”
“familia yako utaweza kuilinda iwapo utakuwa hai na siyo kupoteza uhai wako, iwapo utakuwa tayari kupoteza uhai wako kwaajili ya familia yako je familia yako italindwa na nani baada yawewe kupoteza uhai wako?. Shujaa ni yule anaehakikisha usalama wake yeye na wale awapendao wewe ni shujaa kwangu na mimi ni shujaa kwako usithubutu kujiombea kifo bali omba maisha marefu kila siku… tuko pamoja mume wangu tutapambana kwaajili ya maisha yetu na mwanetu Eric”.
Ni kiapo cha Jamae na Jesca na sasa walikuwa tayari kwaajili ya mapambano, ni vita kubwa waliyoitarajia kutoka upande wa wapinzani wao uliokuwa ukiongozwa na Von Gao.
Jamae alikuwa kaketi sebureni akijaribu kutafakali, aliwaza ni nini kitafuata iwapo yaliyosemwa na Kimbo niyakweli na sasa tafakuli ilienda mbali zaidi kwasababu alikuwa akiyawaza sana maisha ya mwanae Eric ambaye ndo kwanza ameuona ulimwengu hajamaliza hata mwaka mmoja.
Mbali na Eric pia Jamae alikuwa akiutafakali upendo mkuu kutoka kwa mama Eric uliooneshwa kwake kutoka siku yakwanza mpaka sasa Jesca amekuwa akisimamia misimamo yake na hayuko tayari kuteteleka na ilikuwa dhahili kuwa anampenda Jamae kwa mapenzi ya dhati. Jamae alijinamia huku mikono ikiwa kichwani na uso kaulaza juu ya mapaja yake ambayo yalipanda juu baada ya mikuu kuipandisha na kuiweka juu ya sofa alipokuwa kaketi. Alikuwa akiwaza na kuwazua ni namna gani angeweza kuiokoa familia yake maana sasa alijua maisha yake na familia yake yako hatalini kutokana na taarifa alizozipata.
Naweza kusema hakuwa sawa kabisa kutokana na alivyoonekana maana aliketi, akasimama pasipo kupata muafaka na mwisho wa siku simu ya mezani iliita. Haikuwa rahsi kuisikia kwa maramoja kutokana na lundo la mawazo aliyokuwa nayo, lakini baada ya simu kuita marakadhaa hatimaye Jamae ananyanyuka na kuifuata pale mezani.
“hallo!”
“hongera bwana kwa ndoa hatimaye mlifanikiwa”
“ahsante ninazungumza na nani?”
“hupaswi kujua maana nilikupigia kukupa pongezi”
“Oooh ni hilo tu!, si ndoa tu sema hongera kwa familia maana tayari ndoa ilishajibu, tu watatu sasa mimi mke wangu na mwanetu pia”
“sawa endekeza jeuri ila ipo siku zitakutokea puani”
“Sawa Gao nashukuru kwa simu yako na Mungu akubariki pia”
“inaonekana umekuwa na kiburi sana baada ya kumuoa huyo kibwengo mwenziyo siyo?, unatamba umepata mke … kwa mke gani sasa uliyenae? Hicho kituko nacho unasimama mbele za watu na kutamba kuwa unamake?”
“aaah! Unauliza kuhusu mke…? ni yuleyule aliyekuwa anakunyima usingizi mpaka unateka watu na hata kuwauwa wengine… ninachoshukuru ni kwamba nilikuzidi kete nikamchukua …. Alishanizalia na mtoto… nashukuru kwa kuniachia bwana na mungu anazidi kutubariki”
Maswali ya dharau yalizidi kujibiwa kwa dharau kama yalivyoulizwa kama msemo wa Kiswahili usemao “maswali ya kipumbavu hujibiwa kipumbavu kwa wapumbavu”. Ni maswali ya Von Gao kwa Jamae Justine lakini Jamae alikuwa imara sana kuyajibu mara tu baada ya kuigundua sauti ya Jamae sasa aliyajibu kwa kiburi sana na kujiamini.
Ni usiku ambao naweza kusema ulikuwa ni usiku wa hofu kwa Jamae kwanza umeme ulikatika mapema, kibayazaidi kukawa na wingu zito la mvua, jenereta iligoma kuwaka kabisa siku hiyo pamoja na juhudi zote za ,mapema kuchukuliwa na wasaidizi wa Jamae pale nyumbani lakini ilishindikana.
Hakukuwa na jinsi ilibidi kukubaliana na hali. Majira ya saa sita usiku mvua yenye ngurumo kali radi na upepo mkubwa katikati ya giza nene ilizidi kuporomoka. Naweza kusema binadamu huhisi jambo baya liajalo mbele yake usiku huu haukuwa mzuri kwa familia ya Jamae Justine. Akiwa chumbani Jamae anaonekana kuwa na hofu kuu, alimgeukiwa mkewe akitetemeka lakini mke alionekana kuwa imara zaidi alimsihi mmewe kuondoa hofu ili waendelee kulala.
Baada ya kuendelea kulala mlango ulivunjwa na watu wasiojulikana na wanafanikiwa kupenya mpaka ndani, watu hawa wakiwa wamefunika nyuso zao kwa maski nyeusi. Jamae anajaribu kupambana nao kwa kutumia bastora yake lakini walionekana kuwa na siraha nzito zaidi yake wanafanikiwa kumchapa risasi ya bega na anaanguka chini huku akipoteza uelekeo wanamkamata na wanafanikiwa kuingia mpaka chumbani. Bila huruma wanamkamata mke wake pamoja na mtoto wake wanatoka nao ndani na wanakuja nao sembureni wale watu waliofunika nyuso sasa wanafunua nyuso zao mbele ya Jamae na familia yake.
Basi baada ya kufunua nyuso zao lilikuwa ni jopo la wanaume wa shoka wasipopungua saba ambao Jamae hakumtambua hata mmoja, basi walimkamata mtoto Eric na kumning’iniza juu na walidhamilia kumuangamiza kwani mwanaume mmoja alikuwa akimurusha juu na kumdaka pamoja na mtoto Eric kulia kwa uchungu bado majambazi haya hayakuona haja yakuwa na huruma jibaba hili lilizidi kumrusha mtoto bila kujali umri wake na maumivu waliyokuwa wakiyapata wazazi wake.
Matukio haya yote yalikuwa yakifanyika Jamae akiwa kafungwa mikono nyuma huku mitutu miwili aina ya SMG iliwa imeelekezwa kwenye paji lake la uso hiyo haikutosha bali mijibaba yote saba ilikuwa na siraha za kuogofya. Jamae akidhidi kutafakari juu ya ujio wa hawa watu nyumabani kwake akitaka kujua nani kawatuma na wanataka nini lakini kabla hajahoji chochote Ghafla anaingia Von Gao ambaye alifika akiwa na wapambe wake wapatao wawili na kuifanya idadi ya vidume kufikia kumi, alifika na kufungua zipu ya suluali yake na nadhani alikuja kwa lengo moja tu alitaka kumuingilia kimwili Jesca mbele ya uso wa Jamae. Kilikuwa ni kitendo cha aibu na unyama wa hali ya juu kilicholeta maumivu makali ndani ya moyo wa Jamae.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment