Simulizi : Jino Kwa Jino (2)
Sehemu Ya : Tano (5)
Gari ilipotoka tu na kufuatiwa kufungwa kwa geti nyuma yake dreva aliliingiza barabarani hapo Chilamwena aliye katika meza ya peke yake aligeukia meza ya tano toka alipo na macho yake yakakutana na macho manne yakimuangalia kwa pamoja yakiwa mawili ya Agent Hansen Nicholaus Blade na mawili ya Special Agent Simone Joseph Silla, macho yao yaliongea jambo kwa kasi huku mbele ya glocery gari ikipita ikiwa ni gari anayoendesha mtu aliyepewa jukumu la kwenda mitaa ya katikati ya jiji la Salvador kumchukua Brigedia Mcdonald Grannell ambaye naye alitoroka nchini Guatemala kwakuwa alikuwemo katika list ambalo lilitajwa na wafuasi wengine wanaoshikiliwa na serikali kwa kosa lla kushirikiana na genge hatarishi la biashara ya ulanguzi wa madawa genge la The Red Jaguar (chui wekundu).
Detective Chilamwena aliinuka toka katika kiti alichokaa baada ya kukisukuma nyuma kwa eneo la nyuma la mapaja kisha akatoa wallet akatoa pesa ya noti dola tano ya kimarekani akaiacha mezani akiiwekea glasi kwa juu ili isipeperuke huku papo hapo uso wake ukiwa na tabasamu murua mwanaume huyu mweusi wa weusi wa maji ya kunde alionyesha ishara kwa muhudumu ilipo pesa ambapo kama angetaka angerudishiwa iliyobaki lakini haraka aliyonayo hakuona kama kuna umuhimu wa kurudishiwa iliyobaki.
Alipotoka nje ya glocery hii ndogo lakini nzuri sana kwa maua na miti iliyopandwa mbele, hakutoka peke yake nyuma yake alikuwa anakuja Special Agent Silla, wote wakafungua milango ya kimkebe chao (gari yao ndogo) kisha Chilamwena akaiwasha na kuiondoa kuelekea ilipoelekea Cadillac XTS 2016 zikiwa imeshapita dakika moja hivyo ilimbidi asiogope lolote aingie haraka barabarani na kuongeza mwendo wa kasi baada ya kufika kwenye kona na kuiacha kona.
Dreva Chilamwena alipangua magari kama matano akiyapita ndipo kwa umbali wa kama mita hamsini akaiona gari kwa mbele ikipanda kwenye muinuko.
“Ile pale” Akaongea Detective Chilamwena macho yakiwa kayakaza mbele anapokwenda.
“Yes!... Pangua gari mbili za mbele kisha utakwenda kikawaida tutakuwa tushaisogelea!” Silla akaongea hivi ikifuatishwa na kitendo cha dreva kufanya vile alivyoelekezwa.
“Piga kwa TSC kumpa taarifa juu ya kuufukuza mkia tusiojua unaenda wapi..” Chilamwena akaongea akiwa hamuangalii anayemwambia.
“Hallooo!” Haikuchukua hata dakika mbili mbele tayari S.A Silla alikuwa hewani kuongea na Agent Kai.
“Halloo! Nimetumiwa meseji na Hans kuwa kuna mkia umenona”
“Ndiyo.. Tunaangalia wa mnyama gani tutawataarifu kinachoendelea..!”
“Sawa sawa.. Hans macho makali kuangalia zizi naamini hakijaaribika kitu mgawanyo mzuri.. mtaingia whatsapp kuna maelekezo nimeweka kwenye group”
“Sawa.. Baadaye kidogo”
Simu zilikatwa kwa pande zote, toka waingie katika jiji la Salvador mfumo uliozoeleka kwa Kai na hata majasusi wengine kutumia mawasiliano kwa mfumo wa kamtambo kadogo ambacho uwa wanafunga sehemu kisha kufanya mawasiliano yao binafsi hawakufanya kwa sababu ambazo zilikuwa ni kutokuja na kamtambo husika hapa jimboni Bahia hivyo simu za kawaida ndizo zilitumika wakipita zaidi kwenye mitandao hasa whatsapp licha ya huko Guatemala walitumia sana ‘SCNG’ saa za mkononi na vifaa vidogo vya kupachika masikioni kwenye tundu vilivyo katika ‘bluetooth earphones’.
‘Loja Samsung Salvador Shop’ duka la vifaa vya kielektroniki vya kampuni ya Samsung lililopo eneo la Avenida Tancredo Neves mtaa wa Camihno Das Arvores, ni duka ambalo ni kituo kwa bidhaa za kampuni hii katika jimbo la Bahia linalolimiki jiji la Salvador, kampuni inayosambaza bidhaa zake dunia nzima zikiwa ni bidhaa bora sana kiushindani katika masoko ya bidhaa za kielektroniki hasa simu za smartphones, mafriji nakadhalika kampuni ambayo makao yake makuu na uzalishaji mkuu wake ni Korea Kusini katika mji wa Samsung, Seoul mwanzilishi akiwa Bwana Lee Byung-Chul mwaka 1938.
Dreva mwendesha gari aina ya Cadillac XTS 2016 alipaki gari kwenye maegesho ya jengo hili refu na la kisasa la duka hili kubwa sana lililojengwa kwa vioo kwa asilimia nyingi kuliko vitu vingine, mtaa ulikuwa umechangamka sana siku ya jumanne, kulikuwa na maduka mengine makubwa makubwa yanayouza bidhaa mbalimbali za makampuni mengine.
Aliposhuka tu toka ndani ya gari kuna mtu mmoja wa makamo ya umri wa miaka inayokaribia sitini aliinuka kwa kasi katika moja benchi zege yaliyo katika kieneo kidogo cha bustani ambacho kina mabenchi zege kama manne yaliyotengenezwa vizuri na kurembwa kwa rangi za bluu na nyeupe zilizo katika nembo ya alama za kampuni ya Samsung.
“Brigedia Mcdonald Grannell..!” Mtu yule akasema huku akisimamisha hatua ndefu alizokuwa anazitupa kumsogelea aliyeshuka kwenye na mkono wake wa kulia ulikuwa umetangulia mbele ili wapeane mikono.
“Karibu Salvador, Bahia! Mr. Grannell.. Naitwa Marcelo!” Akajibu dreva kisha akampokea begi lililo la wastani na pia akampokea na briefcase pia akamuonyesha kwa ishara mgeni wake kuwa azunguke upande wa pili.
Wakati mgeni! Brigedia Grannell anainuka toka kwenye benchi zege, gari waliyomo Detective Chilamwena na Special Agent Silla ilikuwa upande wa pili wa barabara ambayo ni barabara ya njia mbili ikitenganishwa na kiukuta cha chini kabisa urefu wa nchi nne katikati yake kukiwa kumepandwa mikokono wao wakiwa katika maegesho ya jengo lingine lenye maduka makubwa linaloangaliana na jengo hili la Samsung, walikuwa makini kufuatilia yanayoendelea huku kamera ndogo ya kijasusi aina ya Nikon D4 Stock Photos ilikuwa ikiinuka kwa chati kisha inapiga picha mbili mbili halafu mpigaji ambaye ni S.A Silla anaishusha nay eye kukaa s awa kwa kujiegemea mgongo kwenye kiti chake.
“Zinatosha kaka hizo picha.. Acha watupite kwanza..!” Chilamwena akaongea akimuangalia Silla ambaye siu mbili hizi walizo wote wamekuwa kama marafiki wa karibu bila kuwa wamejuana kwa siku nyingi, utani kwao ulikuwepo na hata kuelekezana kazi kwao ilikuwa kwa haraka tu.
“..Naam.. Kwenye gari alikuwepo dreva peke yake hakukuwa na mtu mwingine.. Huyu mtu sura yake kwangu si ngeni.. Ngoja nikumbuke..!” Aliongea Silla akiiweka kamera kwenye mtoto wa dashboard ya gari.
Cadillac XTS 2016 iliingizwa barabara kuu toka kwenye maegesho ya duka kuu la Samsung na kuvuka upande kwenda upande ambao ingerudi kule ilipotoka wakati inakuja.
“Nafikiri wanarudi Metropolitan..!” Akaongea Chilamwena akitia gia tayari kuondoka kuanza kuwa mkia tena kuifuata kwa nyuma gari wanayoinyapia.
“Yah! Nimemkumbuka huyu mtu.. Yes! Hakika ni muaguatemala huyu.. Tena mwenye cheo kikubwa.. Ngoja niingie kwenye mitandao ni mechi picha yake moja itamleta yeye nani?!” Akaongea S.A Silla yeye akkiwa ametulia kwenye simu yake ya smartphone kufanya vile anavyoviongelea kwa matendo, akiacha dreva Chilamwena aliye makini asipoteze windo lao afanye kazi yake.
Walio ndani ya Cadillac walifuata barabara moja kwa moja mpaka walipofika kwenye kibao cha juu kinachoonyesha kushoto ni Avenida Parabia na kulia ni Avenida ACM Retorno, wakati wanakuja huku walinyoosha tu laini hapa walikunja kushoto na kuingia barabara ya inayoelekea Avenida Parabia.
“Wanaenda kwingine si Metropolitan.. Waambie kwenye group wajue hili.!” Chilamwena akaongea akiongeza spidi ya kimkebe chao hili waifikie kona waliyokata Marcelo na mgeni wao Brigedia Grannell.
Walikwenda vile vile mchana huu kukiwa na magari mengi yanayopita barabara hii walienda wakilipita eneo la Avenida Paulo VI ambapo barabara hii ya eneo hili nayo ikiitwa jina hilihili wakaenda wakikamata barabara ya Candeal walipofika eneo hili wakazunguka mzunguko unaounganisha barabara ya eneo hili la Candeal na eneo la Itaigara, mkia uliendelea kufuata kila kona kila mnyooko wa barabara mpaka wakafika eneo ambalo kibao cha juu wao kina Chilamwena wakagundua wamefika eneo ambalo kitaarifa walipewa taarifa na kina Agent Hansen kuwa ndipo eneo ambalo liliwafanya wao kwenda kule Metropolitan, eneo hili la eneo la Old Quarter Pelourihno ndivyo kibao kilivyosomeka.
“Nafikiri sasa tunaweza jenga taswira tunaenda wapi?” Akaongea Silla akiendelea kuangalia mbele mita zaidi ya mia moja ambako gari wanalolifuatilia lilikuwa limewatangulia.
“…Yah!..Old Quarter Pelourihno ni skani ya washukiwa wetu nakumbuka ulitajwa mtaa kuwa unaitwa mtaa wa Largo, taarifa ziwafikie tena kwenye group wawekee taarifa hii pia” Detective Chilamwena akaongea tena akiweka na agizo kwa mwenzake anayecheza na simu.
Ni kweli dakika mbili mbele walifika mtaa wa Largo, mwenyeji wa mtaa anayeendesha Cadillac XTS 2016 alikwenda akasimama kwenye geti lao akashuka haraka na kulifungua kisha akarudi kwenye gari akafunga mlango na kuingiza gari ndani, wakati wanaingia kwenye geti nyuma yao Detective Chilamwena alipitiliza na kigari chao na kuiingiza pembeni ya barabara katika ukuta unaozunguka jengo hili kisha wote wawili wakashuka wakiwa na maelekezo toka kwenye group lao la whatsapp lenye ‘members’ 7 tu, admin akiwa yupo Marekani jijini Washington DC mwanadada genius Lizy Roby, mikononi mwao walikuwa na bastola kila mmoja wakiakikisha zinakuwa kwa mbele zilipo zipu za suruali zao zisiweze kuonekana na wapiti njia waliokuwa wakipita barabara hii kama kawaida kwakuwa ni njia kuu kwa waendesha vyombo vya moto, baridi (baiskeli) na wapita kwa miguu.
Wakati Marcelo anarudi kufunga geti lao ambalo ni geti la kusukumwa upande kabla hajaligusa watu wawili wanaume wakamtokea kwa kushtukiza, jamaa hakutaraji jambo hili hivyo alisimama macho yamemtoka kama yanataka kujichomoa katika fremu yake.
“Tulia vivyo hivyo.. Usijitingishe wala kuinua mdomo wako mpaka sisi tuseme ongea ndipo utaongea… Ubishi wowote utakupeleka kwenye usingizi usiojulikana kwa wanadamu kuwa ni usingizi wa aina gani?!” Aliongea S.A Silla macho yake yakiwa hayatulii kwa kuangalia kule kwenye gari ambako mgeni aliyeenda kupokelewa alitaka kushuka garini kisha akarudi na kuufunga mlango akicheza pata potea ya hisia pengine wavamizi hawajamuona kama yumo garini akiamini wavamizi awa watakuwa wakisubiri hapa kwenye nyumba muda wote kusubiri yoyote atakayefika.
Kiishara wakamrudisha nyuma Marcelo kisha Chilamwena akalirudisha geti kama vile ambavyo Marcelo angefanya, geti lilipokwisha fungwa Silla akaitumia fursa kumsachi kwa stahili ya kumpapasa mwilini mateka wao akamkuta na bastola aliyokuwa kaiweka ndani ya koti refu alilovaa urefu wake ukiwa umeishia katikati ya mapaja.
“Twende kwenye gari yako.. Tunataka kumchukua na Brigedia Grannell kuingia naye ndani kuna kazi mtatufanyia..!” Akaongea Special Agent Silla kilichofanya Marcelo ageuke kumuangalia usoni Silla asiamini anachosikia toka kwenye mdomo wa mzungu huyu mwenye nywele za blonde.
“…Kina nani nyinyi?” Akauliza Marcelo swali kisha akageuza shingo yake kumuangalia Chilamwena ambapo akakutana na jicho kali lenye karipio kali.
“Tahadhali Silla.. Aliye ndani ya gari ni Brigedia mstaafu wa jeshi.. Muweke ndugu yake ngao vizuri wakati tunalikaribia gari lao..!” Akaongea Chilamwena huku wote wakiwa wamemtanguliza mateka wao mbele.
Ndani ya gari Brigedia Mcdonald Grannell alikuwa amekamatia bastola yake anawaona vizuri wanaokuja akiwa kainuka pale alipo siti ya mbele ya abiria, sura za watu hawa zikimchanganya kuwa wapi aliwai kuziona, maswali kibao yalikuwa yakigongana.
‘Sheeenzy kabisa.. Yaani hata kuingia ndani ya nyumba nikapumzika sijaingia wanaharamu hawa sijui wametokea wapi hata.. Acha niwaonyeshe mimi si Grannell wanayemuhisi kuwa alivyo kwakuwa kazeeka nawaliwa taiming kali ya kikatili nawafyeka wote bila kujali hata huyu wanayemuweka ngao wakiamini namjali nampasua ubongo wake muda si mrefu niwawekee tisho la kwanza la ghafla” Aliwaza Brigedia Grannell.
Kupasua kioo cha gari aliona si vizuri hivyo alitaka aone watekaji watamuelekezea upande gani mateka wao yeye ndipo aanzishe cha kuanzisha kukumbukia enzi za jeshini akilitumikia jeshi la nchi yake ya Guatemala.
Kweli kama alivyopanga katika mpango wa akili yake alijua kuwa watekaji watakuwa si watu wa kawaida kawaida aliwaona wanavyoinama nyuma ya teka lao kiufundi ilimjuza vijana wale si mbumbumbu eneo la uwanja wa vita na mawindo.
Wakiwa wameshalikaribia gari wanajisogeza kwa pembeni hapo jambo ambalo Si Silla, Chilamwena wala Marcelo waliweza kuhisi hili, gari iliwashwa kwa ghafla kisha dreva ndani ya gari akalirudisha nyuma kwa kasi ya kushtukiza ‘hatari’.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na ishirini na moja (121)
Koki ya mapigano imefunguliwa Largo street, Brigedia mstaafu wa jeshi la Guatemala anataka kuwaonyesha nini kina Detective Chilamwena na Special Agent Silla?
Hatari na nusu! Twende sehemu inayofuata katika sehemu za mwisho mwisho za riwaya yetu ndefu na ya kusisimua haswa.
TUKUTANE SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHIRINI NA MBILI (122)
BY K M M M @2019
Riwaya: JINO KWA JINO
(Tooth For Tooth)
Sehemu Ya…………….121
Location: Mixer
Mtunzi:Kaichi M Mussa
Wtssp: +255 652202560
Location: Moro Town
ILIPOISHIA SEHEMU YA 120…!!
“Umesema mtu wako amegundua hoteli walizofikia watu awa.. Je unaonaje kama ungesubiri nguvu kazi uliyoiomba toka Argentina ndiyo wavamiwe? Maana tunatambua hapa Salvador mtu aliyefika akiwa na uzoefu na mikiki ya kazi hizi ukiacha wewe mwenyewe ni mimi na walinzi wetu watano tuliofika nao hapa Salvador wengine wote ni watu wa kawaida ambao si wazoefu katika hili na hata vijana awa wa kibrazili si wazoefu kama tunavyoweza kudhania pia kumbuka hawapambani na watu walio wanafunzi katika kazi za ukachero, ujasusi na uhalifu wa kimataifa.. Wazo langu naomba kazi hii ingesogea mpaka kuanzai jioni ya leo na tena itakuwa vizuri sababu kiuhalisia na uzoefu wangu majasusi na makachero uwa wanaanza kuranda randa kunusa taarifa wanazozitafuta kwa watu wanaofikiri watawasogeza mbele… Langu ni hili mkuu!” Aliongea Puto Sergio Lopez huyu ni rafiki mkubwa wa Feca ambaye alikuwa ameshika mipango ya genge lao nchini Marekani alirudi Mexico baada ya kupata taarifa juu ya hali ya hatari iliyotokea nchini Guatemala na ni kweli alilokuwa akiliongelea juu ya watu walio hapa katika jiji la Bahia kuwa si watu wa kazi sana kama ilivyokuwa awali wakati genge la TRJ linaanza watu kama kina Ivan ‘alto genius’ mtu makini mwenye akili za kutosha kuchanganua mambo ambaye alikufa akiwa kwenye helkopta kwa kombora la lililoidungua wakati wanaenda jimboni San Marcos kutoa msaada baada ya taarifa ya uvamizi wa kina Agent Kai, walikuwepo watu makatili mmexico mwenye asili ya ujerumani Wolfs Klauben Gend (Mnyama), Cisco Murlindo a.k.a Tocon (kisiki) na wengineo kama awa walio na ukatili na ujuzi.
Kingpin Feca kabla hajaanza kuijadili hoja iiyotolewa na rafiki yake simu yake iliingia meseji katika mtandao wa whatsapp akaonyesha ishara kwa mkono wake usiokuwa umeshika bastola kuwa watulie asome meseji kwanza.
“Brigedia Grannell amenitumia meseji amefika hapa Salvador yuko kwenye katika maduka ya katikati ya jiji, naomba Marcelo umfuate uwe makini sana maana mtu huyo alikuwa ni mkurugenzi wa uhamiaji hivyo anaweza kuwa anafuatiliwa nitaomba umpeleke kwenu baada ya kuhakikisha kuko salama salimini itakapofika usiku ndiyo ataletwa hapa kwa usalama zaidi ndiyo maana nimeweka hiyo taratibu isije kusogeza nzi..!”Alitoa maelekezo huku anamuangalia aliyemtaja jina anaitwa Marcelo.
“Nitamjuaje?”Akauliza.
“Nimemuelekeza ulivyovaa pia naye amenielekeza atakapokaa kwenye duka la kuuza bidhaa za Samsung kwakuwa wewe mwenyeji utakuwa unapajua, sawa nenda sasa na utabaki naye huko kwenu mpaka nitakapowajuza mje” Akafafanua Feca.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!!
FUNGA KAZI XIV
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
Detective Omar Chilamwena alikuwa macho yake hayatembei mahali pengine zaidi ya akiinama kichwa kunywa kinywaji chake sekunde tu anainua kuangalia umbali wa mita zaidi ya mia mbili toka walipo, anaangalia lilipo geti lililoshikana na ukuta unaozunguka jengo la ghorofa lenye urefu wa orofa tano kwenda juu huku ya geti juu ya geti lile rangi nyeusi kukiwa na kenop.
Gari aina ya Cadillac XTS 2016 ambazo ni gari zilizo zaidi ya nne ambazo ni aina hii zilizo katika banda la kuwekea magari lililo katika ndani ya kuta zinazozunguka jengo hili viziwa sasa na majasusi awa wa CIA, gari hizi aina moja zilinunuliwa ili kuzuia maadui kujua mtu wanayemlenga yuko kwenye gari gani kwakuwa zote zilifanana hivyo ilitakiwa uzijue namba za hizi gari ndipo ungeweza elezea gari ya mtu yupi unayemuhitaji endapo kutatokea tatizo.
Gari ilipotoka tu na kufuatiwa kufungwa kwa geti nyuma yake dreva aliliingiza barabarani hapo Chilamwena aliye katika meza ya peke yake aligeukia meza ya tano toka alipo na macho yake yakakutana na macho manne yakimuangalia kwa pamoja yakiwa mawili ya Agent Hansen Nicholaus Blade na mawili ya Special Agent Simone Joseph Silla, macho yao yaliongea jambo kwa kasi huku mbele ya glocery gari ikipita ikiwa ni gari anayoendesha mtu aliyepewa jukumu la kwenda mitaa ya katikati ya jiji la Salvador kumchukua Brigedia Mcdonald Grannell ambaye naye alitoroka nchini Guatemala kwakuwa alikuwemo katika list ambalo lilitajwa na wafuasi wengine wanaoshikiliwa na serikali kwa kosa lla kushirikiana na genge hatarishi la biashara ya ulanguzi wa madawa genge la The Red Jaguar (chui wekundu).
Detective Chilamwena aliinuka toka katika kiti alichokaa baada ya kukisukuma nyuma kwa eneo la nyuma la mapaja kisha akatoa wallet akatoa pesa ya noti dola tano ya kimarekani akaiacha mezani akiiwekea glasi kwa juu ili isipeperuke huku papo hapo uso wake ukiwa na tabasamu murua mwanaume huyu mweusi wa weusi wa maji ya kunde alionyesha ishara kwa muhudumu ilipo pesa ambapo kama angetaka angerudishiwa iliyobaki lakini haraka aliyonayo hakuona kama kuna umuhimu wa kurudishiwa iliyobaki.
Alipotoka nje ya glocery hii ndogo lakini nzuri sana kwa maua na miti iliyopandwa mbele, hakutoka peke yake nyuma yake alikuwa anakuja Special Agent Silla, wote wakafungua milango ya kimkebe chao (gari yao ndogo) kisha Chilamwena akaiwasha na kuiondoa kuelekea ilipoelekea Cadillac XTS 2016 zikiwa imeshapita dakika moja hivyo ilimbidi asiogope lolote aingie haraka barabarani na kuongeza mwendo wa kasi baada ya kufika kwenye kona na kuiacha kona.
Dreva Chilamwena alipangua magari kama matano akiyapita ndipo kwa umbali wa kama mita hamsini akaiona gari kwa mbele ikipanda kwenye muinuko.
“Ile pale” Akaongea Detective Chilamwena macho yakiwa kayakaza mbele anapokwenda.
“Yes!... Pangua gari mbili za mbele kisha utakwenda kikawaida tutakuwa tushaisogelea!” Silla akaongea hivi ikifuatishwa na kitendo cha dreva kufanya vile alivyoelekezwa.
“Piga kwa TSC kumpa taarifa juu ya kuufukuza mkia tusiojua unaenda wapi..” Chilamwena akaongea akiwa hamuangalii anayemwambia.
“Hallooo!” Haikuchukua hata dakika mbili mbele tayari S.A Silla alikuwa hewani kuongea na Agent Kai.
“Halloo! Nimetumiwa meseji na Hans kuwa kuna mkia umenona”
“Ndiyo.. Tunaangalia wa mnyama gani tutawataarifu kinachoendelea..!”
“Sawa sawa.. Hans macho makali kuangalia zizi naamini hakijaaribika kitu mgawanyo mzuri.. mtaingia whatsapp kuna maelekezo nimeweka kwenye group”
“Sawa.. Baadaye kidogo”
Simu zilikatwa kwa pande zote, toka waingie katika jiji la Salvador mfumo uliozoeleka kwa Kai na hata majasusi wengine kutumia mawasiliano kwa mfumo wa kamtambo kadogo ambacho uwa wanafunga sehemu kisha kufanya mawasiliano yao binafsi hawakufanya kwa sababu ambazo zilikuwa ni kutokuja na kamtambo husika hapa jimboni Bahia hivyo simu za kawaida ndizo zilitumika wakipita zaidi kwenye mitandao hasa whatsapp licha ya huko Guatemala walitumia sana ‘SCNG’ saa za mkononi na vifaa vidogo vya kupachika masikioni kwenye tundu vilivyo katika ‘bluetooth earphones’.
‘Loja Samsung Salvador Shop’ duka la vifaa vya kielektroniki vya kampuni ya Samsung lililopo eneo la Avenida Tancredo Neves mtaa wa Camihno Das Arvores, ni duka ambalo ni kituo kwa bidhaa za kampuni hii katika jimbo la Bahia linalolimiki jiji la Salvador, kampuni inayosambaza bidhaa zake dunia nzima zikiwa ni bidhaa bora sana kiushindani katika masoko ya bidhaa za kielektroniki hasa simu za smartphones, mafriji nakadhalika kampuni ambayo makao yake makuu na uzalishaji mkuu wake ni Korea Kusini katika mji wa Samsung, Seoul mwanzilishi akiwa Bwana Lee Byung-Chul mwaka 1938.
Dreva mwendesha gari aina ya Cadillac XTS 2016 alipaki gari kwenye maegesho ya jengo hili refu na la kisasa la duka hili kubwa sana lililojengwa kwa vioo kwa asilimia nyingi kuliko vitu vingine, mtaa ulikuwa umechangamka sana siku ya jumanne, kulikuwa na maduka mengine makubwa makubwa yanayouza bidhaa mbalimbali za makampuni mengine.
Aliposhuka tu toka ndani ya gari kuna mtu mmoja wa makamo ya umri wa miaka inayokaribia sitini aliinuka kwa kasi katika moja benchi zege yaliyo katika kieneo kidogo cha bustani ambacho kina mabenchi zege kama manne yaliyotengenezwa vizuri na kurembwa kwa rangi za bluu na nyeupe zilizo katika nembo ya alama za kampuni ya Samsung.
“Brigedia Mcdonald Grannell..!” Mtu yule akasema huku akisimamisha hatua ndefu alizokuwa anazitupa kumsogelea aliyeshuka kwenye na mkono wake wa kulia ulikuwa umetangulia mbele ili wapeane mikono.
“Karibu Salvador, Bahia! Mr. Grannell.. Naitwa Marcelo!” Akajibu dreva kisha akampokea begi lililo la wastani na pia akampokea na briefcase pia akamuonyesha kwa ishara mgeni wake kuwa azunguke upande wa pili.
Wakati mgeni! Brigedia Grannell anainuka toka kwenye benchi zege, gari waliyomo Detective Chilamwena na Special Agent Silla ilikuwa upande wa pili wa barabara ambayo ni barabara ya njia mbili ikitenganishwa na kiukuta cha chini kabisa urefu wa nchi nne katikati yake kukiwa kumepandwa mikokono wao wakiwa katika maegesho ya jengo lingine lenye maduka makubwa linaloangaliana na jengo hili la Samsung, walikuwa makini kufuatilia yanayoendelea huku kamera ndogo ya kijasusi aina ya Nikon D4 Stock Photos ilikuwa ikiinuka kwa chati kisha inapiga picha mbili mbili halafu mpigaji ambaye ni S.A Silla anaishusha nay eye kukaa s awa kwa kujiegemea mgongo kwenye kiti chake.
“Zinatosha kaka hizo picha.. Acha watupite kwanza..!” Chilamwena akaongea akimuangalia Silla ambaye siu mbili hizi walizo wote wamekuwa kama marafiki wa karibu bila kuwa wamejuana kwa siku nyingi, utani kwao ulikuwepo na hata kuelekezana kazi kwao ilikuwa kwa haraka tu.
“..Naam.. Kwenye gari alikuwepo dreva peke yake hakukuwa na mtu mwingine.. Huyu mtu sura yake kwangu si ngeni.. Ngoja nikumbuke..!” Aliongea Silla akiiweka kamera kwenye mtoto wa dashboard ya gari.
Cadillac XTS 2016 iliingizwa barabara kuu toka kwenye maegesho ya duka kuu la Samsung na kuvuka upande kwenda upande ambao ingerudi kule ilipotoka wakati inakuja.
“Nafikiri wanarudi Metropolitan..!” Akaongea Chilamwena akitia gia tayari kuondoka kuanza kuwa mkia tena kuifuata kwa nyuma gari wanayoinyapia.
“Yah! Nimemkumbuka huyu mtu.. Yes! Hakika ni muaguatemala huyu.. Tena mwenye cheo kikubwa.. Ngoja niingie kwenye mitandao ni mechi picha yake moja itamleta yeye nani?!” Akaongea S.A Silla yeye akkiwa ametulia kwenye simu yake ya smartphone kufanya vile anavyoviongelea kwa matendo, akiacha dreva Chilamwena aliye makini asipoteze windo lao afanye kazi yake.
Walio ndani ya Cadillac walifuata barabara moja kwa moja mpaka walipofika kwenye kibao cha juu kinachoonyesha kushoto ni Avenida Parabia na kulia ni Avenida ACM Retorno, wakati wanakuja huku walinyoosha tu laini hapa walikunja kushoto na kuingia barabara ya inayoelekea Avenida Parabia.
“Wanaenda kwingine si Metropolitan.. Waambie kwenye group wajue hili.!” Chilamwena akaongea akiongeza spidi ya kimkebe chao hili waifikie kona waliyokata Marcelo na mgeni wao Brigedia Grannell.
Walikwenda vile vile mchana huu kukiwa na magari mengi yanayopita barabara hii walienda wakilipita eneo la Avenida Paulo VI ambapo barabara hii ya eneo hili nayo ikiitwa jina hilihili wakaenda wakikamata barabara ya Candeal walipofika eneo hili wakazunguka mzunguko unaounganisha barabara ya eneo hili la Candeal na eneo la Itaigara, mkia uliendelea kufuata kila kona kila mnyooko wa barabara mpaka wakafika eneo ambalo kibao cha juu wao kina Chilamwena wakagundua wamefika eneo ambalo kitaarifa walipewa taarifa na kina Agent Hansen kuwa ndipo eneo ambalo liliwafanya wao kwenda kule Metropolitan, eneo hili la eneo la Old Quarter Pelourihno ndivyo kibao kilivyosomeka.
“Nafikiri sasa tunaweza jenga taswira tunaenda wapi?” Akaongea Silla akiendelea kuangalia mbele mita zaidi ya mia moja ambako gari wanalolifuatilia lilikuwa limewatangulia.
“…Yah!..Old Quarter Pelourihno ni skani ya washukiwa wetu nakumbuka ulitajwa mtaa kuwa unaitwa mtaa wa Largo, taarifa ziwafikie tena kwenye group wawekee taarifa hii pia” Detective Chilamwena akaongea tena akiweka na agizo kwa mwenzake anayecheza na simu.
Ni kweli dakika mbili mbele walifika mtaa wa Largo, mwenyeji wa mtaa anayeendesha Cadillac XTS 2016 alikwenda akasimama kwenye geti lao akashuka haraka na kulifungua kisha akarudi kwenye gari akafunga mlango na kuingiza gari ndani, wakati wanaingia kwenye geti nyuma yao Detective Chilamwena alipitiliza na kigari chao na kuiingiza pembeni ya barabara katika ukuta unaozunguka jengo hili kisha wote wawili wakashuka wakiwa na maelekezo toka kwenye group lao la whatsapp lenye ‘members’ 7 tu, admin akiwa yupo Marekani jijini Washington DC mwanadada genius Lizy Roby, mikononi mwao walikuwa na bastola kila mmoja wakiakikisha zinakuwa kwa mbele zilipo zipu za suruali zao zisiweze kuonekana na wapiti njia waliokuwa wakipita barabara hii kama kawaida kwakuwa ni njia kuu kwa waendesha vyombo vya moto, baridi (baiskeli) na wapita kwa miguu.
Wakati Marcelo anarudi kufunga geti lao ambalo ni geti la kusukumwa upande kabla hajaligusa watu wawili wanaume wakamtokea kwa kushtukiza, jamaa hakutaraji jambo hili hivyo alisimama macho yamemtoka kama yanataka kujichomoa katika fremu yake.
“Tulia vivyo hivyo.. Usijitingishe wala kuinua mdomo wako mpaka sisi tuseme ongea ndipo utaongea… Ubishi wowote utakupeleka kwenye usingizi usiojulikana kwa wanadamu kuwa ni usingizi wa aina gani?!” Aliongea S.A Silla macho yake yakiwa hayatulii kwa kuangalia kule kwenye gari ambako mgeni aliyeenda kupokelewa alitaka kushuka garini kisha akarudi na kuufunga mlango akicheza pata potea ya hisia pengine wavamizi hawajamuona kama yumo garini akiamini wavamizi awa watakuwa wakisubiri hapa kwenye nyumba muda wote kusubiri yoyote atakayefika.
Kiishara wakamrudisha nyuma Marcelo kisha Chilamwena akalirudisha geti kama vile ambavyo Marcelo angefanya, geti lilipokwisha fungwa Silla akaitumia fursa kumsachi kwa stahili ya kumpapasa mwilini mateka wao akamkuta na bastola aliyokuwa kaiweka ndani ya koti refu alilovaa urefu wake ukiwa umeishia katikati ya mapaja.
“Twende kwenye gari yako.. Tunataka kumchukua na Brigedia Grannell kuingia naye ndani kuna kazi mtatufanyia..!” Akaongea Special Agent Silla kilichofanya Marcelo ageuke kumuangalia usoni Silla asiamini anachosikia toka kwenye mdomo wa mzungu huyu mwenye nywele za blonde.
“…Kina nani nyinyi?” Akauliza Marcelo swali kisha akageuza shingo yake kumuangalia Chilamwena ambapo akakutana na jicho kali lenye karipio kali.
“Tahadhali Silla.. Aliye ndani ya gari ni Brigedia mstaafu wa jeshi.. Muweke ndugu yake ngao vizuri wakati tunalikaribia gari lao..!” Akaongea Chilamwena huku wote wakiwa wamemtanguliza mateka wao mbele.
Ndani ya gari Brigedia Mcdonald Grannell alikuwa amekamatia bastola yake anawaona vizuri wanaokuja akiwa kainuka pale alipo siti ya mbele ya abiria, sura za watu hawa zikimchanganya kuwa wapi aliwai kuziona, maswali kibao yalikuwa yakigongana.
‘Sheeenzy kabisa.. Yaani hata kuingia ndani ya nyumba nikapumzika sijaingia wanaharamu hawa sijui wametokea wapi hata.. Acha niwaonyeshe mimi si Grannell wanayemuhisi kuwa alivyo kwakuwa kazeeka nawaliwa taiming kali ya kikatili nawafyeka wote bila kujali hata huyu wanayemuweka ngao wakiamini namjali nampasua ubongo wake muda si mrefu niwawekee tisho la kwanza la ghafla” Aliwaza Brigedia Grannell.
Kupasua kioo cha gari aliona si vizuri hivyo alitaka aone watekaji watamuelekezea upande gani mateka wao yeye ndipo aanzishe cha kuanzisha kukumbukia enzi za jeshini akilitumikia jeshi la nchi yake ya Guatemala.
Kweli kama alivyopanga katika mpango wa akili yake alijua kuwa watekaji watakuwa si watu wa kawaida kawaida aliwaona wanavyoinama nyuma ya teka lao kiufundi ilimjuza vijana wale si mbumbumbu eneo la uwanja wa vita na mawindo.
Wakiwa wameshalikaribia gari wanajisogeza kwa pembeni hapo jambo ambalo Si Silla, Chilamwena wala Marcelo waliweza kuhisi hili, gari iliwashwa kwa ghafla kisha dreva ndani ya gari akalirudisha nyuma kwa kasi ya kushtukiza ‘hatari’.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na ishirini na moja (121)
Koki ya mapigano imefunguliwa Largo street, Brigedia mstaafu wa jeshi la Guatemala anataka kuwaonyesha nini kina Detective Chilamwena na Special Agent Silla?
Hatari na nusu! Twende sehemu inayofuata katika sehemu za mwisho mwisho za riwaya yetu ndefu na ya kusisimua haswa.
ILIPOISHIA SEHEMU YA 121…!!
“Tahadhali Silla.. Aliye ndani ya gari ni Brigedia mstaafu wa jeshi.. Muweke ndugu yake ngao vizuri wakati tunalikaribia gari lao..!” Akaongea Chilamwena huku wote wakiwa wamemtanguliza mateka wao mbele.
Ndani ya gari Brigedia Mcdonald Grannell alikuwa amekamatia bastola yake anawaona vizuri wanaokuja akiwa kainuka pale alipo siti ya mbele ya abiria, sura za watu hawa zikimchanganya kuwa wapi aliwai kuziona, maswali kibao yalikuwa yakigongana.
‘Sheeenzy kabisa.. Yaani hata kuingia ndani ya nyumba nikapumzika sijaingia wanaharamu hawa sijui wametokea wapi hata.. Acha niwaonyeshe mimi si Grannell wanayemuhisi kuwa alivyo kwakuwa kazeeka nawaliwa taiming kali ya kikatili nawafyeka wote bila kujali hata huyu wanayemuweka ngao wakiamini namjali nampasua ubongo wake muda si mrefu niwawekee tisho la kwanza la ghafla” Aliwaza Brigedia Grannell.
Kupasua kioo cha gari aliona si vizuri hivyo alitaka aone watekaji watamuelekezea upande gani mateka wao yeye ndipo aanzishe cha kuanzisha kukumbukia enzi za jeshini akilitumikia jeshi la nchi yake ya Guatemala.
Kweli kama alivyopanga katika mpango wa akili yake alijua kuwa watekaji watakuwa si watu wa kawaida kawaida aliwaona wanavyoinama nyuma ya teka lao kiufundi ilimjuza vijana wale si mbumbumbu eneo la uwanja wa vita na mawindo.
Wakiwa wameshalikaribia gari wanajisogeza kwa pembeni hapo jambo ambalo Si Silla, Chilamwena wala Marcelo waliweza kuhisi hili, gari iliwashwa kwa ghafla kisha dreva ndani ya gari akalirudisha nyuma kwa kasi ya kushtukiza ‘hatari’.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!!
FUNGA KAZI XVI
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
Detective Chilamwena hakuwa na ugeni na mchezo haraka alimpiga push nzito ndugu yake S.A Silla wakadondoka chini kwa pamoja ukafuatia kujiviringisha kwa kasi kwa wote wawili, gari likamsukuma chini Marcelo baada kumkumba kwakuwa wakati tukio hili la kushtukiza lilipokuwa linatokea alisukumwa mbele.
Brigedia Grannell alisikia kiumbe kimegongwa kutokea nyuma ya gari akazidisha spidi kisha akafunga breki gari likaserereka kwa sababu ardhi ya hapa ilikuwa imemwagwa kokoto eneo lote la mbele karibu na geti hivyo mserereko ulifanya eneo la nyuma la gari ligonge geti na kutoa mlio, akainuka toka katika muinamo wake ndipo akaona wavamizi wamejiinua goti moja chini lingine juu huku tundu za bastola zao sura zao wote hata kama macho yao yalikuwa yako ndani ya miwani waliyovaa zilionyesha wanamshambulia si kuwa bastola zao zimeinuliwa yeye aweze kujisalimisha la hasha! Mara moja risasi zilianza kufyatuka kama kufuatana kuelekea kwenye kioo cha mbele ikamfanya ainame tena akijiangusha kiubavu kulala siti zote mbili za upande wa dreva. gari kwa kuyumbisha usukani wa gari huku akiwa kainama.
Wakati huohuo Marcelo hali yak echini alipo ilikuwa taabani alipandwa na matairi usoni kiasi cha kubonyezwa eneo lote la usoni akabaki anatapa tapa kutaka msaada, maumivu makali ya kuhisi mtoa roho amemsimamia yalikuwa yamemkalia kooni.
“Tutoke hapa katikati eneo wazi sana tumejianika twende sehemu salama.. Mzee anaonekana anataka kujibu mashambulizi ya silaha sasa..” Akaongea Detective Chilamwena akisimama na pia S.A Silla akasimama wote wakarudi kinyume nyume bastola zao walizoacha kurusha risasi zilibaki zimesogea mbele kwa mikono waliyoinyoosha.
Haraka wakatumia nafasi ya jamaa kuhofia kuinua kichwa chake kwa wao kila mmoja kusogelea nguzo zinazoshika ‘kenopi’ ya juu ya mlango wa orofa ya kwanza.
“Unahisi hatujamgusa kabisa?” Akauliza Silla bila kuangalia upande alipo Chilamwena.
“Sina hakika lakini ndivyo.. Ngoja nifanye kitu..!” Akajibu Detective Chilamwena hapo wakaangaliana na wote wakatabasamu, awa jamaa wao hawakuwa wamevaa sura za bandia walikuwa na sura zao halisi bila kuongeza kitu.
Detective aliinama chini kisha akaokota jiwe kubwa kati ya mawe mengi yaliyo chini, jiwe akalirusha kwa nguvu likaenda kupiga kwenye bodi ya gari mlango wa kulia na kutoa sauti ya jiwe na bati kugongana, brigedia Grannell akahisi kuna mtu anataka kufungua mlango wa gari hapo akashambulia kwa kupiga risasi na bastola yake haikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti hivyo mlio ulianikiza alichotaka Chilamwena kikatimia.
Gari ilikuwa imevunjika vioo cha mbele kilikuwa kimevunjika kwa mashambulizi ya risasi chache zilizopigwa na wazee wa kazi lakini ilipojigonga kwa nyuma katika geti ilisababisha kikaachia kabisa, wataalamu waliona wapi alipo brigedia na ni mzima mpaka ameweza kutumia bastola yake, wakaangaliana na kukonyezana, vichwa vyao vilipogeuka mbele mlango wa gari upande wa kushoto siti za mbele ulifunguliwa kwa kasi kisha bila wao kutarajia akadondoka chini Brigedia Grannell akajiviringisha macho yake yakamuona Silla kwa uzuri kwakuwa alikuwa kaka upande ulio sanjali na upande huu wa mlango wa gari.
Macho ya Silla yangekuwa hayapo ndani ya miwani basi macho kwa macho yangegongana na kila mmoja kuona katika hisia nini anawaza mwingine, S.A Silla alifyatua risasi lakini zilikuta hewa na kupita zikaenda gonga kwenye geti, mzee huyu wa makamo mwanajeshi aliyeachia jeshi akiwa na cheo cha ubrigedia alijizungusha kifundi chini sentimita moja tu kwenda juu ya nguo alizovaa ilipita risasi moja kwa wepesi mwingine tena akiwa chini vile vile akafyatua risasi na yeye kwenda aliposimama Silla katika nguzo ya kenopi ya baraza Mungu saidia kwa S.A Silla aliinama chini risasi moja ikachimba nguzo na kurusha chokaa naye ikimkosa sentimita chache lakini hii ya kumtoa uhai ilimkosa ikampata ingine isiyo na uwezo wa kumtoa roho kwa papo hapo kama atawaiwa kupewa huduma ilikita kwenye bega lake la upande wa kulia unapoanza mkono ikipasua mfupa mkubwa, bastola ilitoka kiganjani kilazima huku mpigwa risasi Special Agent Silla akipaishwa kurudi akaijipiga kwenye nguzo kisha akadondoka chini hapo hakutaka kuzubaa licha ya kuwa anaona kama nyota nyota mwili wake kufika tu chini kwenye kokoto alijitambalisha kwa kasi kujiondoa asionekane uzuri na mshambuliaji.
Brigedia Grannell kuruka kwa damu kutoka kwenye mwili wa aliyemshambulia kulimzubaisha akahisi tayari kamtoa roho hivyo licha ya kuwa anamuona akaona asipoteze risasi zake kwakuwa bado kuna adui yake mwingine lakini alipojipindua kuangalia uzuri alipo jamaa ikiwa matendo yote haya yanafanyika kwa kasi ya nukta kumeta akaoana miguu inamalizia kujivuta upande ambao yeye atamuona vizuri kwakuwa alizibwa na bodi ya gari sehemu za mbele, hapo hakusubiri akaona kumbe mzima akafyatua tena risasi moja ambayo hii ilienda kita kwenye kiatu raba alichovaa S.A Silla hapa ikivunja mfupa wa unyayo maumivu mara mbili yalimfanya Silla apige yowe kisha akajivuta juu ya baraza kwa kasi na kujiziba mdomo.
“Mbwaa huyu ananiua.. Ananiua mbwa.. Chila kuwa makini atatumalizaa.. Oooo phuuuu!!” Kwa sauti kavu yenye donge kooni akaongea S.A Silla, yote haya yalishuhudiwa na Detective Chilamwena.
“Polee pole sana ndugu yangu ndiyo kazi zetu.. Acha nimpoteze nikuwaishe hospitali kabla ya madhara zaidi jibanze papo hapo..!”Akaongea kwa sauti aliyohakikisha anaisikia ndugu yake lakini ghafla komeo la getini lilisikika linafunguliwa lilikuwa ni aina ya mkaomeo ambayo makavu yanaposuguana wakati wa kufunguliwa yanaliwa ‘kwiichi kwiichi kwiichi kwiiichi’. Wote walisikia hili.
“…Omar! Anatoroka kuwa makini hatakiwi kuondoka hapa..!” Akaongea Silla akijitahidi kuzuia damu inayomtoka begani, ikawa kama mtaka mawili kwa Detective Omar Chilamwena anataka amsaidie ndugu yake damu isimtoke pia anataka akimbie kuzuia utorokaji wa Brigedia Grannell lakini tamaa ya kwenda kuzuia iliisha baada ya mtoto wa geti kufunguka na mara kama kivuli kikapita kwenda nje.
“Sheeenzy.. Sheeenzy kabisa.. Kaenda..!” Akaongea kwa hasira uso ulikuwa umekunjwa unaweza sema hautaki uso wake hadi vipovu vya kona za kwenye mdomo wake zilitoka haraka akakimbia alipolala Marcelo akamgusa shingoni akakutana na salamu za kuwa tayari Israel malaika mwenye sifa ya kuwa yeye ndiyo mtoa roho alikuwa kashachukua chake alimvua shati alilovaa baada ya kumuondoa koti la suti alilovaa, shati akakimbia nalo kurudi alipo Special Agent Silla.
“Vumilia kaka nikufunge kuzuia damu kutoka.. Mpuuzi ana bahati sana na tulimdaharau kuwa mzee kumbe mzee kijana.. sheeenzy kabisa..!” Aliongea huku anamfunga jeraha la begani lisiendelee kutoa damu iliyokuwa ikitoka kama maji yanatoka kwenye chemchem.
“Ms..ge! Ms..ge kanivunja mfupa mkubwa… Dah! Sijui nilizubaa vipi mpaka akanishambulia.. Loooh!”Akapayuka kwa hasira na uchungu Silla, wakati Chilamwena anamtoa kiatu mguuni hili napo amfunge damu isitoke zaidi.
“Inatubidi tuondoke haraka sana hapa.. Ving’ora vya gari za polisi navikisia kwa mbali..!” Alimaliza kumfunga mguuni eneo la unyayo ambapo napo mfupa mkubwa ulikuwa umevunjwa na risasi kukwamia ndani kama ilivyo bega hali ilitisha sana kwa Special Agent Silla hapa ndipo wapeleleza na majasusi uilaani kazi yao hii na pia wengine ufikia kujiapiza hawataendelea kufanya hii kazi wanapokutwa na masahibu kama haya.
“Twen’zetu! Akaongea Chilamwena kisha akachukua mkono mmoja ulio mzima wa ndugu yake akaupachika kwa shingoni mwake kisha mkono mwingine akauzungusha kwa mgongoni kwa Silla akaanza kumkokota lakini ving’ora vilizidi kusogea kupitia masikio yao wote ilionyesha si gari moja la polisi ni magari zaidi ya moja yanakuja, hapo Chilamwena akamuangalia ndugu yake kisha akamnyanyua na kumuweka mgongoni.
“Polisi watatukamata na kuharibu mambo mengi acha nikubebe tujaribu kuwai wakitukuta basi tutajisalimisha..!Hakuna njia ingine..! Shiiit!” Akasema tena Chilamwena.
“Hapana tutapunguza nguvu kazi kwa wenzetu weee niache kama tukiona tunafika getini nao wamefika niache kimbia utaruka ukuta kwa nyuma..!” kwa tabu akaongea Silla machoni mwake akianza kuona tofauti kidogo na kawaida.
Na kweli kabla hawajagusa kiambaza cha mtoto wa geti (geti mlango kwenye geti kubwa) magari yalifunga breki kwa nje mbele ya ukuta unaozunguka ghorofa hili.
“Ondoka Chila.. Ondoka Chila..Ondoka haraka sana.. Nitajaribu kujitambulisha pia mtapiga simu ubalozini haraka wanisaidie..!”Akasema S.A Silla kisha akajidondosha toka mgongoni mwa Detective Chilamwena wote wakatoa miwani machoni mwao wakaangaliana kwa sekunde kumi kisha wakakunja ngumi na kugonga tano halafu kwa kasi ya mashindano ya mbio za mita 100 Chilamwena akainuka na kupotea akizunguka upande jengo kuelekea nyuma ya hili la ghorofa.
***** ***** *****
“Halooo! Chila..!”
“Hali si nzuri kiongozi!”
“Vipi tena?”
“Kama tulivyokuwa tunawataarifu katika group kila hatua tunayopiga toka tutoke huko Metropolitan mpaka mlivyotoa ushauri tuvamie kabla hawajaingia ndani, mzee ametuzidi maarifa ametushambulia na kumjeruhi mwenzangu kwa risasi..!”
“Mpo wote hapo? Ana hali gani?”
“Wakati nimemaliza kumpatia huduma ya kumfunga damu isitoke kwa wingi mapolisi walifika na magari yao akanishauri nimuache mimi nikimbie, nikatorokea kwa kupitia nyuma ya jengo kwa kuruka ukuta”
“Mzee kijana amefanya hayo?”
“Ndiyo kiongozi ametushangaza sana haendani alivyo na aliyofanya”
“Dreva wake imekuwaje?”
“Mwenyeji wake! Tulimteka na kumuweka chini ya ulinzi tukasogea naye vizuri tu ikatokea tusilotarajia jamaa akagongwa na gari matairi yakampanda usoni na shingoni akatokwa na uhai kabla sisi hatujatoka na mzee kijana kututoroka kwa kutokea kwenye mtoto wa geti”
“Aiseeh! Poleni sana.. Basi ngoja nipige simu ubalozini wawai kutoa taarifa kwa mapolisi kuhusu mwenzetu.. na pia washughulikie apatiwe huduma bora ikiwemo kurudishwa Marekani haraka sana kwa matibabu bora zaidi”
“Ndicho nilichokupigia kiongozi, uwai kutoa taarifa kwa wenzetu wa ubalozini..!”
“Kwahiyo wewe huko wapi?”
“Niko barabara ya Candeal karibu na njia panda inayozikutanisha hii Candeal na Itaigara nakiona kibao kinachoonyesha migawanyiko hii mita kama mia moja mbele”
“Sawa… Hans bado yupo palepale mgahawani anafukuzia nzi hivyo kajiunge naye, ratiba yetu ilivyo utaikuta kwenye group”
“Nafikiri mzee kijana atakuwa anakuja huko mara tu alivyofanya aliyofanya”
“Namuelekeza Hans azidishe umakini kuweka jicho”
“Sawa sawa.. Nachukua taxi, baadaye!”
Yalikuwa ni maongezi baina ya Agent Kai aliyepigiwa simu na Detective Omar Chilamwena akitoa taarifa ya vumbi lililowakuta.
“Vipi tena?” Alipoweka simu yake kwenye meza tu swali likabandikwa kwake kutoka kwa Special Agent Rebecca, ikabidi Agent Kai awahadithie kile alichohadithiwa na Detective Chilamwena, wote waaipokea taarifa atika hali ya huzuni kama ilivyo timu inapopokea taarifa isiyofurahisha ya matokeo kunakuwa hakuna mchezaji anayefurahia kuona ‘team mate’ anakuwa katika hali isiyo kawaida ndivyo wao wote walivyoipokea taarifa ya kujeruhika mwenzao.
Alipomaliza kuwaeleza akachukua tena simu yake toka mezani na kupiga namba za kiofisi yao huko Washington DC, Marekani zinazotumiwa na fundi muongoza shughuli kisasa Elizabeth Robert ‘Lizy Rob’.
“Hallloo mwanaume!” Upande wa pili alikopiga, mpigiwa simu alipokea haraka kana kwamba alikuwa akiisubiri simu husika kwa hamu kubwa sana.
“Hali si nzuri mwanamke!”
“Nini tena?” Akauliza kwa pupa Lizy Rob.
“S.A S amepatwa tatizo.. Hatujui ana hali gani mpaka dakika hii, ameshambuliwa kwa mkali wetu akiwa kazini na Chila”
“Yuko wapi?”
“Naomba umpigie balozi msaada wake unahitajika haraka sana kwakuwa ilimbidi Chila amuache eneo la tukio kuzuia wao wote kuingia katika mikono ya polisi waliofika baada ya kusikika kwa milio ya bastola toka kwenye bastola ya mzee ambaye kimsingi ni mwanajeshi mstaafu hivyo si mtu wa kudharauliwa lakini wenzetu walizidiwa maarifa kidogo naye!”
“Poleni sana… Nampigia balozi mwenyewe kwa simu yake ya mkononi amerudi huko Brazil leo asubuhi kutoka huku, jamaa yupo wapi?”
“Yupo mikononi mwa polisi, hili apate huduma nzuri isiyo na maswali mengi itakubidi umpe taarifa balozi kuwa haraka apige simu kwa maafisa wake waliopo hapa Salvador wakatoa huo msaada kisha ukaandaliwa usafiri arudishwe nchin kwetutaratibu zingine zitafanyika….inatakiwa haraka aondolewe mikononi mwa polisi”
“Sawa.. Nitaweka mambo mengine yanayoendelea katika group acha kwa sasa nishughulikie dharura iliyotokea”
Maongezi yaliishia hapa simu ikakatwa kupisha Lizy kushughulikia dharura ya kujeruhiwa kwa Special Agent Simone Joseph Silla.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na ishirini na mbili (122)
Brigedia Mcdonald Grannell aliwaonyesha kile ambacho kiliwashangaza Special Agent Silla na Detective Omar Chilamwena pale alipowashambulia ghafla baada ya kutoka ndani ya gari kifundi kazi.
Taarifa za kujeruhiwa kwa S.A Silla zimefika kwa Agent Kai naye akatoa taarifa kwa mwanadada muongoza shughuli kisasa Lizy Roby.
Kwa mwenendo sambamba wa tukio baada ya tukio ungana name katika sehemu inayofuata kwa mapigo ya kisasa zaidi toka kwa mafundi wa pande zote kati ya timu hasimu mbili.
Alipomaliza kuwaeleza akachukua tena simu yake toka mezani na kupiga namba za kiofisi yao huko Washington DC, Marekani zinazotumiwa na fundi muongoza shughuli kisasa Elizabeth Robert ‘Lizy Rob’.
“Hallloo mwanaume!” Upande wa pili alikopiga, mpigiwa simu alipokea haraka kana kwamba alikuwa akiisubiri simu husika kwa hamu kubwa sana.
“Hali si nzuri mwanamke!”
“Nini tena?” Akauliza kwa pupa Lizy Rob.
“S.A S amepatwa tatizo.. Hatujui ana hali gani mpaka dakika hii, ameshambuliwa kwa mkali wetu akiwa kazini na Chila”
“Yuko wapi?”
“Naomba umpigie balozi msaada wake unahitajika haraka sana kwakuwa ilimbidi Chila amuache eneo la tukio kuzuia wao wote kuingia katika mikono ya polisi waliofika baada ya kusikika kwa milio ya bastola toka kwenye bastola ya mzee ambaye kimsingi ni mwanajeshi mstaafu hivyo si mtu wa kudharauliwa lakini wenzetu walizidiwa maarifa kidogo naye!”
“Poleni sana… Nampigia balozi mwenyewe kwa simu yake ya mkononi amerudi huko Brazil leo asubuhi kutoka huku, jamaa yupo wapi?”
“Yupo mikononi mwa polisi, hili apate huduma nzuri isiyo na maswali mengi itakubidi umpe taarifa balozi kuwa haraka apige simu kwa maafisa wake waliopo hapa Salvador wakatoa huo msaada kisha ukaandaliwa usafiri arudishwe nchin kwetutaratibu zingine zitafanyika….inatakiwa haraka aondolewe mikononi mwa polisi”
“Sawa.. Nitaweka mambo mengine yanayoendelea katika group acha kwa sasa nishughulikie dharura iliyotokea”
Maongezi yaliishia hapa simu ikakatwa kupisha Lizy kushughulikia dharura ya kujeruhiwa kwa Special Agent Simone Joseph Silla
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!!
FUNGA KAZI XVII
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
“Saa tano kamili usiku kwa saa za hapa.. Tumepata muda mzuri wa kupumzika amkeni jamani mnalala sana.. Jade amka.. Reby! Reby amka kumekucha” Sauti hii nzito toka kwa Agent Kai ilikuwa ni sauti yake ya kawaida ingawa yeye ni mmoja wa watu waliobarikiwa vipaji lukuki hadi kipaji cha kuongea sauti mbalimbali za tofauti tofauti lakini hii ni yake ya kawaida, alikuwa akiwaamsha Agent Jade Poul Brown mwanamama wa umri unaokaribia kuondoka kwenye miaka thelathini kwenda arobaini lakini kwa mazoezi ayafanyayo na matuzno mazuri aliyonayo kiuhakika yalimfanya aonekane kama bado ndiyo anahama miaka ya ishirini kwenda ya thelathini pia alikuwa akimuamsha Special Agent Rebecca Smith huyu sina la kumuelezea kivyovyote sababu ni mtu ambaye alipo Agent Kai kikazi basi uambatana naye ni mtu anayemuamini na kumkubali kwakuwa siku ya kwanza tu kumuona alihisi amekutana na mtu sahihi kwake kikazi damu zimeendana ikiwa walikutana kwa mara ya kwanza nchini Malaysia katika mkasa wa kutekwa kwa wanasayansi wa kimarekani nchini Malaysia kisha kwa wao kutekwa wakaja kutekwa wapelelezi na majasusi wengine wa kimarekani ndipo kupelekea Agent Kai kusogea Malaysia kikazi wakakutana na Rebecca Smith aliyekuwa ni Agent wa siri wa CIA nchini humo (kwa utamu zaidi soma riwaya ya Mshangao utayapata kwa uzuri humo haya).
“..Aisee nilikuwa naota so amazing, toka nifike hapa jana sikulala kama hivi..!” Rebecca alikuwa wa kwanza kuongea huku anafikicha macho yake.
“Jade! Jade! Amka Jade kumekucha mama yangu… Amka tukale posho iliyobakia na hamu nayo mimi na ndiyo maana sikuwa nimelala vizuri kwa kuwaza huyo mwalimu wa wanajeshi tunamfunzaje adabu hahaha hahahah aiseee ukiwa umetoka kuamka unakuwa mzuri sana” Agent Kai aliamia kumtingisha Jade ambaye amsha ya kwanza haikumshtua ila hii ya kutingishwa ilimfanya afumbue macho kwa maneno ya Agent Kai ikamfanya atabasamu.
“Khaaah! Hujaacha tu matani yako ya toka tuko shule za jeshi.. Haahaah” Akaongea Jade akikumbusha enzi zao za shule ya kijeshi ambazo walikutana na Agent Kai darasa moja.
“.. Jasiri haachi asili.. Ucheshi asili yangu.. Naam!”
“Huo ujasiri wa ucheshi.. Haya bhana, kumekucha”
Waliaanza kujiandaa kwa kila mmoja kwenda kuoga maliwatoni kwa zamu kwakuwa bafu hapa katika hoteli hii ya Wish Hotel Da Bahia, walipomaliza wakajiandaa mpaka ilipofika saa sita kasoro robo wakawa tayari.
“Vipi huko?” Hakuwa anaongea na mmoja wa aliyekuwemno humu ndani ya chumba namba 118 orofa ya nane hotel nzuri ya nyota tano ya Wish Hotel Da Bahia alikuwa akiongea kwa simu aliyopiga kwenye namba za simu za Agent Hansen Nicholaus Blade.
“Nzuri tu.. Tunaanza au?”Akajibu aliye upande wa pili Agent Hansen.
“Ndiyo.. Tangulieni mkifanikiwa kuingia ndani ya uwa mtatujuza kwa meseji, nawaamini sana hamjawai iangusha Marekani, Mungu awatangulie! Inshaallah!”
“Usihofu juu yetu wazee wa hizi kazi kitambo hatuwezi babaishwa na sisimizi wasio na kelele za kunyima mwenye chumba kulala… USA First!”
“USA First!”
Walimaliza hivyo kwa kutakiana kila la kheri kisha Agent Kai akakata simu na kugeuka kuwaangalia wanawake alio nao hapa alipo ambao wao walikuwa bize kufanya mengine katika mabegi madogo yao.
“Mko tayari?” Swali liliulizwa na Agent Kai akiwa anapanga visu vidogo katika moja ya vimifuko vidogo vya ndani ya begi lisilo kubwa la wastani ambalo mara nyingi uwa analining’iniza begani kutegemea na alipo ingawa muda mwingine uwa alipo mwilini mwake lakini haliwi mbali na alipo sababu ubeba vifaa vyake vya kazi.
“Kiakili na mwili, twende tukamalize kazi kwa faida ya vizazi vyetu” Agent Jade Poul Brown akajibu akiwa anaweka kamba kwenye kibegi kilicho kwenye meza huku amesimama kama wenzake wote wakiwa wameizunguka meza ya kioo umbo la duara iliyo katikati ya sebule ya chumba namba118.
“Swahiba mpiga vichwa jiwe huko kimya.. Usiwaze leo hakuna mvua kama kule Putatan.. Hahaha hahahah! Unanifurahisha sana unatisha sana swahiba..” Agent Kai akamgeukia Special Agent Rebecca walipoangaliana wote wakatabasamu akaona amtanie maana alikuwa kwenye mawazo mazito na hilo lilimjuza mzee wa hisia zisizo na mipaka anapoyaangalia macho ya mabinti hata akiwa ni mpelelezi na jasusi kama Rebecca yeye uweza kuhisi anawaza nini.
“Hatari na nusu.. Ujikuta tu kichwa kimechomoka chezea kujihami wewe. Hahahaha hahahaha eeeeeh! Sitaki kaka niache kwanza muda huu uwa ni muda wa kutuliza akili na kutafakari kwa fikra kwa upeo wa juu sana, wewe mwenzetu huko na moyo ulio na ganzi kama umeupaka vumbi la Kongo” Akajibu Rebecca na kusababisha wote kuangua kicheko bila kupenda kwa alichoongea.
“Vumbi la Kongo? Ndiyo nini hilo?” Kicheko cha Jade kilikatizwa ghafla akauliza maana asije kuwa anacheka tu kumbe anafuata mkumbo usiotakikana.
“..Hahahaaaah! mi silijui nimecheka tu.. Reby sema mwenyewe vumbi la Kongo ndiyo vumbi gani?” Agent Kai akaongea huku anatabasamu kwa bashasha tele, hii ikiwa ni mbinu ambayo makomandoo wengi uitumia wanapokaribia kwenda kufanya kazi ambayo kwao uwa ni kufa na kupona na ndicho Kai alichokileta hapa kuanzisha soga ya kumfanya kila mmoja kuwa na furaha bila kujali kilicho mbele yao (furaha muhimu hata nyakati ngumu za vita).
“Jade! Achana naye huyo.. Wala usitake kulijua hilo vumbi la Kongo lenye kutia ganzi maana ukilijua utataka kujua matumizi yake ni nini mi akhuuuu!”
“Akhuuu nini? Si useme tu.. Sikia Jade, vumbi la Kongo tukimaliza kazi yetu huko tunakoenda utamuuliza Detective Chilamwena atakupa jibu maana yeye kihalisia ndiyo nchini kwao.. mimi mtanzania mmarekani na hayo maganzi wapi na wapi” Aliongea huku anatizama saa yake ya mkononi ikawa kaambukiza na kwa wengine wote wakaangalia saa.
“Muda wa onyesho umefika..!”Hatua mbili mbele huku anaongea alikuwa Agent Kai.
“Hans na Chila wako kimya.. Naamini muda makubaliano wako ndani ya jengo muda huu..” Kicheko kilikatwa akaongea kwa sauti kavu sauti ambayo ilikuwa na ujumbe flani wa kuvutia.
“Hatutaongozana… Pia hatutashuka kwa njia aina moja.. Mimi nitashuka chini kupitia dirisha la stoo ya vyombo vya usafi katika vyoo vya jumuiya vilivyo floor hii, nimeshachunguza kulivyo nikishuka pale hatua chache kuna bustani ambayo mbele kuna swimming pool hapo nitaamua kama nikapitie getini kama kawaida au niruke ukuta kutokana na mazingira yalivyo kwa kuruka ukuta itakuwa ni bora zaidi hivyo nitapenda kufanya hivyo ikiwa nitaona hali inaruhusu.. Jade utashuka kwa ngazi na utaenda kushoto ukitoka kwenye langu kuu hapo utasogea hadi kwenye mgahawa wa hoteli wa nje hapo kuna vyoo utajifanya unaenda kupata huduma za choo hapo utakwepa macho ya watu kwa kuzunguka nyuma huko utaruka ukuta upande wa pili utajikuta ufukweni mwa bahari nami nitakuwa nishafika hapo kama nitafanikiwa kuruka ukuta nitakuwai… Reby utatumia lifti kushuka wewe utaenda pita getini, wewe utatuwai kufika chini hivyo utazunguka kwenda ufukweni tutakutana huko kuna minazi upande wa juu mita mia hapo ndipo yatakuwa makutano kutokea hapo hadi kwenye ukuta uliozunguka jengo tunalolinyatia ni mita mia moja na ishirini… Kazi njema.. USA First!” Alipomaliza kuongea hivi akaminya kitasa cha mlango ukakubali akavuta kwa ndani naye kutoka nje tayari kwa safari ya matumaini kazi za kazi.
***** ***** *****
“Hatuna budi sote kupita hapa kwa pamoja… Walinzi wanafanya ulinzi kwa stahili ya kupishana na wanapishaniana eneo lile pale ikitokea hawajakutana basi ukaribia kwa eneo lile.. Umeusoma mchezo eeeh?”Aliongea Agent Hansen akimuonyesha mtaro unaotoa maji machafu ya kutoka ndani ya uwa wa jengo wanalohitaji kuingia kama watangulizi ikiwa kina Agent Kai nao wanakuja.
“Yah ni sahihi.. Acha nitangulie mimi,. Kuna tope hivyo tuwe makini ramani ya hatua zetu kuziacha” Detective Chilamwena wakati akiomba kutangulia alikuwa tayari kashusha miguu yake kwenye mtaro bila kusubiri kama Hansen atamruhusu atangulie ambapo alimtizama tu huku akizungusha macho yake huku na huko nyuma ya ukuta unaozunguka jengo hili la ghorofa lenye urefu wa orofa tano kwenda juu.
Akitanguliza kichwa baada ya kuinama na kuwa anatambalia magoti katika mtaro ambao kulikuwa na giza totoro laiti angekuwa hana miwani ya ‘kazi za kazi’ basi angeweza kuogopa kusogea bila kusita kila hatua ya mtambao wake anayopiga, nyuma yake Hansen alikuwa yupo anafuata akiwa mtambao wa mjusi.
Safari yao ilisita kusogea mbele baada Detective kukutana na sehemu ambayo ni mwisho wa safari yao kulikuwa na matobo makubwa ya mfano wa mdomo wa chupa ya soda ndiyo yaliyomfanya aache kusogea zaidi akili yake kazi za kazi ilikuwa ikichangnua anawezaje kuliondoa funiko zege lililowekwa matobo matobo kushusha maji kwenye mtaro kutoka uwa unaozunguka jumba la ghorofa, kuganda kwake kulifanya Hansen kumsogelea wakawa sambamba sababu mtaro ulimudu kuwaweka watu wawili kwa pamoja.
“Tope hapa kunakopokea maji limekuwa zito zaidi.. Hapakuwa mahala pazuri sisi kupitia.. Pengine tungelazimisha sehemu ingine..” Aliongea Detective Chilamwena akipapasa kwenye kingo za mfuniko kuona kama kuna urahisi wa kulisukuma kwa juu kupitia pembeni.
“Khaah! Tutalipush litafunuka tu kwa juu.. Zile CCTV kamera za kule tusingeziweza zingetuuza kwa bei rahisi sana kwa adui zetu kabla hata hatujavuka hatua yoyote.. Pia mbwa wanaonekana ni wenye mafunzo yaliyotimilika” Akajibu hoja Agent Hansen.
“Agent Kai na wanawake zake soon watakuwa ufukweni wakiamini tutakuwa tayari tuko ndani.. Twende na muda kaka mkuu hatujawai shindwa kitu hivyo tusirudi nyuma nilikuwa natoa maoni tu kuwa hatukuwa na hakika kama hapa kutakuwa na kikwazo chochote.. Tutumie nguvu zetu za wote wawili kuusukuma juu umesilibwa kwa zege zito mtu mmoja hawezi… Yah hapa pana kauwazi unaoonekana tunaweza fanya kitu njoo upande wangu tusukume kwa pamoja Agent!” Akipapasa papasa kuna kitu alikiona ni sahihi kwao kukifanya kilaleta tija, Hansen alisogea naye akapitisha kiganja ambacho kimo ndani ya gloves kama anavyofanya Detective Chilamwena aliyegundua kuwa kuna kitu cha ziada hapa, wote makomandoo hawa waligundua wanaweza fanya kitu.
Kijasho kiliwatoka wakati wanasukuma kwa kwenda juu iliwalia dakika mbili ndipo upande walioukazania kuusukuma upande ulioonyesha unaweza kuleta jibu na taratibu ukasogea sogea na kuinuka upande.
“Kazana kazana hapo hapo yaaah! Yaaah mwangaza.. Kuna meseji imeingia nasikia mtetemesho kutoka kwenye moja ya mifuko ya suruali yako” Akaongea kuhamasisha Agent Hansen ikiwa kuna mafanikio na wakati huo huo meseji iliingia katika simu ya Detective Chilamwena lakini hakuacha kuendelea kusukuma kuondoa zege lilijaziwa kwa pembeni kuzuia mfuniko wa mtaro kwa ndani ya uwa unaozunguka jengo la ghorofa.
Mfuniko ulisalimu amri ukafunukia kwa ndani, Detective Chilamwena akausogea na kuitokeza sura yake akaona mahala wanapoibukia endapo wakitoka ilikuwa kuna kibonde kimetengenezwa kwa sakafu ngumu kwa juu yake kulikuwa na ufito ulionyooshwa kwa ustadi zinaanza nyasi zinazopewa matunzo yake yanayotakiwa maana zilikuwa na afya ya kutosha, kwa upande wa juu kabisa kwenda kulia kulikuwa na dalili kuwa kuna watu moshi wa sigara uliuza taarifa kupitia macho aliyovaa miwani ya kazi za kazi.
Chilamwena akarudi chini na kumuangalia ndugu yake kikazi Agent Hansen ambaye alikuwa na maswali ya kutamamani kujua kunani bila kuuliza.
“Vipi mbwa umewaona?” Hansen akaona amuulize hivi kwa kuanzia.
“Mita nazokadiria zaidi thelathini kutoka hapa kuna mtu au watu inaonyesha ni walinzi.. Funiko hili ni funiko aminiwa kuwa hakuna anayeweza pita kupitia hapa na kuhusu mbwa tope hili na tope linalonuka hivyo si rahisi kwao kusikia harufu ya binadamu wa tofauti na waliyemzoea”
“Nini kinaendelea? Twende tuondoke hapa au umeona kitu cha kutuzuia?”
“Hapana… Agent Kai na timu yake tayari wako nyuma ya hapa.. Meseji yake inauliza kama tayari tupo ndani ndiyo namjibu kwanza”
“Ooooh! Sawa fanya haraka muda unakimbia muelekeze tumekwama hapa na ni kwa sababu gani”
Meseji za majibizano baina ya Chilamwena na Kai ziliwalia dakika mbili tena wakielekezana kisha ya hapo simu ya Chilamwena ikarudi mahala pake.
“Twen’zetu! Natangulia kama kawaida tutatambaa mpaka kwenye muinuko utauona ukitokeza tu..” alipomaliza kueleza hivi akageuka na kujivuta kwenda juu akatokeza akiwa katika mtambao huku nyuma akafuata Hansen ambaye alipotoka aliurudishia mfuniko eneo lake ingawa kwa sasa ulikuwa si uliokazwa ulikuwa ulioegeshwa tu.
Walitambaa kama mijusi mpaka kwenye muinuko walioelekezana hapo sasa wakawa wanaona kwa upande huu walipo kwa uzuri zaidi, macho yao yalifanya usahili wa kutosha kuona wapi salama wapi si salama wakiwa wamejilaza kulalia matumbo yao lakini wakiwa wamelala hivi kuna mbwa mmoja anayeonekana ni mbwa jike alisogea halafu akahisi kitu akawa anaangalia kwa umakini sana walipojilaza watu hawa kukiwa kimya kabisa.
Mbwa aliendelea kusimama akiangalia na kujaribu kunusa harufu halafu akawa anavutiwa kusogeza hatua moja kisha anaganda kidogo anapiga tena hatua moja.
“Shiit! Mbwa jike wanakuwaga wanoko sana” Akanong’ona Agent Hansen huku akizidi kujikandamiza kwa chini kuondoa uonekano wake.
“Hawa mbwajike wakiwa wananyonyesha ndiyo uwa hawasikii harufu za watu walio tofauti na eneo husika lakini wakiwa hawanyonyeshi ni shida sana hili litatufanya tushtukiwe haraka zaidi… Mwache asogee tumtangulize akhera kwa risasi potelea mbali” Akaunga mkono Detective Chilamwena akiweka ufafanuzi wa uelewa wake akipapasa kiwambo cha kuzuia sauti ya mlipuko wa risasi toka kwenye bastola (sailensa).
Mwisho wa sehemu ya mia moja na ishirini na tatu (123)
Je jengo hili lilinyatiwa na wapelelezi majasusi hawa litakuwa ndiyo mwisho wa Brigedia matata Kingpin Feca?
Nini kitatokea walipolala Agent Hansen na Detective Chilamwena?
Tusipige porojo nyingi na kuweka ufafanuzi wa kitu kilichosomwa tayari, twende tukaone itakuwaje katika sehemu zilizobaki za riwaya hii.
Meseji za majibizano baina ya Chilamwena na Kai ziliwalia dakika mbili tena wakielekezana kisha ya hapo simu ya Chilamwena ikarudi mahala pake.
“Twen’zetu! Natangulia kama kawaida tutatambaa mpaka kwenye muinuko utauona ukitokeza tu..” alipomaliza kueleza hivi akageuka na kujivuta kwenda juu akatokeza akiwa katika mtambao huku nyuma akafuata Hansen ambaye alipotoka aliurudishia mfuniko eneo lake ingawa kwa sasa ulikuwa si uliokazwa ulikuwa ulioegeshwa tu.
Walitambaa kama mijusi mpaka kwenye muinuko walioelekezana hapo sasa wakawa wanaona kwa upande huu walipo kwa uzuri zaidi, macho yao yalifanya usahili wa kutosha kuona wapi salama wapi si salama wakiwa wamejilaza kulalia matumbo yao lakini wakiwa wamelala hivi kuna mbwa mmoja anayeonekana ni mbwa jike alisogea halafu akahisi kitu akawa anaangalia kwa umakini sana walipojilaza watu hawa kukiwa kimya kabisa.
Mbwa aliendelea kusimama akiangalia na kujaribu kunusa harufu halafu akawa anavutiwa kusogeza hatua moja kisha anaganda kidogo anapiga tena hatua moja.
“Shiit! Mbwa jike wanakuwaga wanoko sana” Akanong’ona Agent Hansen huku akizidi kujikandamiza kwa chini kuondoa uonekano wake.
“Hawa mbwajike wakiwa wananyonyesha ndiyo uwa hawasikii harufu za watu walio tofauti na eneo husika lakini wakiwa hawanyonyeshi ni shida sana hili litatufanya tushtukiwe haraka zaidi… Mwache asogee tumtangulize akhera kwa risasi potelea mbali” Akaunga mkono Detective Chilamwena akiweka ufafanuzi wa uelewa wake akipapasa kiwambo cha kuzuia sauti ya mlipuko wa risasi toka kwenye bastola (sailensa).
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!
FUNGA KAZI XVIII
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
Mbwa yule angalia yake huku anasogea iliweza kuwavutia mbwa wengine wawili nao wakasogea alipo mwenzao wakaanza lazimisha kuona upande ule huku pua zao zikitanuka kusaidia macho yao kwa kunusa.
“Jiandae Detective.. Hapa watawavutia mabwana zao muda si mrefu kama unavyoona kule unapoibuka moshi usioleweka kama wa bangi au ni nini” Alinong’ona Agent Hansen na kweli sekunde kumi mbele mtu mmoja wa asili ya watu watokao bara la Afrika aliibuka kutokea ukuta uliokuwa umeziba alipo kutokea na walipo lala chini wavamizi wao, alikuwa amevaa pensi ya jeans, miguuni buti la njano aina ya ‘buyu’ na juu ana kikoti cha jeans cha mikono mirefu kichwani ana kofia aina ya pama ya ngozi.
Jamaa alisogelea walipo mbwa huku anaendelea kuvuta sigara hakuwa na silaha yoyote aliyoshika akakaza macho kisha akatoa ishara ya mkono wake mmoja mbwa wasogee mbele baada ya kuhisi kitu na yeye, mbwa aliye mbele akatoka mbio wenzake wakafuata kwa kasi kama wanafukuzana.
Mita tano kabla alipo mbwa wa mbele na wazee wa kazi za kazi wa mbele akabweka kwa sauti kuwa kaona kitu wengine nao wakaunga kubweka papo hapo Detective Omar Chilamwena akainuka kwa kasi toka walipojilaza bastola ikiwa mbele tayari kushambulia, Agent Hansen naye akafanya vivyo hivyo risasi zikachomoka ikiwa Detective Chilamwena kuwalamba risasi za vichwa mbwa wote huku Agent Hansen akimshambulia jamaa aliyeibukia kutokea nyuma ya kuta isiyojulikana kwa kina Hansen kama ni kibanda au ni nini.
Mbwa wote umauti uliwalaza chini miili yao iliyotobolewa kichwani na kuacha matundu ya risasi ilibaki ikijisuka suka katika hali ya viumbe kutenganishwa roho na mwili, huku risasi mbili za kifuani zilimdondosha mbrazil mweusi na papo hapo kuna mwingine akatokeza akiwa na bunduki mkononi alitokeza kuangalia kunani kisha akarudi kwa kasi alikotoka risasi moja ikimkosa na kuchimba katika nguzo chuma.
Wakiwa ndiyo wameinuka wote kwa pamoja wakapiga mbio kutoka pale walipo hadi kwenye ukuta wa jengo na mara taa nyekundu zikaanza kuwaka kila kona ya jengo hili, zinawaka na kuzima kwa stahili ya kama ‘alarm’.
“Kumekucha.. Tumestukiwa hata kabla hatujaingia ndani ya jengo kama ujuavyo mbwa wanavyoharibu shughuli” Taarifa ya kinachoendelea ndani ilitumwa kwa njia simu toka kwa Agent Hansen kwenda kwa Agent Kai aliye nje huko na kampani yake ya watu wawili Specila Agent Rebecca na Agent Jade Poul Brown.
“Naam.. Tumezipata taarifa baada ya milio ya mbwa kubweka tukaju tayari wameharibu hali ya hewa.. Gawaneni majukumu haraka kuzuia utorokaji wa yoyote aliye ndani tunawahitaji wote walio ndani..”Akatoa maelekezo ‘TSC’.
“Msipitie kwenye mtaro.. Hapa sisi hatutamaniki kwa tope ni mwendo wa kujichoresha tu tunakopita tunaacha alama hivyo ni bora mkatafuta namna mimi nataka wajue tuko sisi kwa kuharibu cctv kamera kwanza kazi nje..!” Akaeleza tena Agent Hansen lakini maelezo yake yakiwa bado anaelekeza yalikatizwa na mabomba ya maji yaliyoota ardhini yakipanda toka sakafu ya vitofali vidogo vilivyopangwa, yaani ardhi hii (sakafu hii) kulikuwa na vitofali vinaachi auwazi kisha linaibuka bomba jembamba likiwa na koki zeney midomi mitatu, Agent Hansen pamoja naye Detective Chilamwena kwa haraka walihisi kuna kushambuliwa ila je na nini? Maji au silaha gani itatema baada ya kufika usawa wanaotaka wanayoyaongoza, walishikwa na butwaa!.
“Kuwa makini Hansen tunashambuliwa muda si mrefu hii inamaanisha wanatuona tokea huko ndani.. Tutatakiwa kuruka juu kwa stahili ya mtupu mtupu” Akiwa kakazia macho kila bomba kati ya mabomba kadhaa yanayoibuka toka ardhini (kitendawili kikuu kwao).
“Ruuukaaa..!” Akapaza sauti Agent Hansen kisha akajirusha juu kwa kuuzungusha mwili ‘mtupu mtupu’, hapo alikwepa maji yaliyotoka kwenye koki yakizunguka pia aliyekuwa amepaziwa sauti alifanya alilohitajiwa kufanya, walijikuta wakitua upandea wa pili kwa miguu yao na maji yaliweza kuwapata kwenye suruali wote hapo ndipo walipojua nini haswa kilichozingatiwa na adui zao, yalikuwa ni maji ya kuwasha maji yaliyochanganywa kitaalamu na kemikali za kuwaha mwili pindi zinapogusana na ngozi ya binadamu.
Koki zilikuwa zikizunguka na kumwaga maji chini juu kwa kasi yaani ukikwepa hivi basi yatakukuta hivi kutoka miguuni mwao walipogeuka yakatua mengine maeneo ya kiunoni.
“Tuondoke kwa mbio kaka!” Akaongea akijikaza kujikuna mwilini ingawa ilikuwa ni ngumu sana kujikaza kutojikuna.
Mbio bila kujali koki za maji zilikuwa karibu eneo lote walilo karibu na wao, mbio hatua ndefu ndefu mguu kama unataka kugusa kichogo zilipigwa na wanaume hawa na mara wakaanza kushambuliwa kwa risasi kutokea kwa dirishani ikawa pona pona kwao kwakuwa mshambuliaji alishambulia katika migongo yao na wao ndani walikuwa wamevaa fulana ngumu ya kuzuia risasi (bullet Proof) lakini risasi ni risasi tu hasa za mashine ya udunguaji iliyokuwa ikitumiwa na mshambulizi, ziliwafanya wote wawili kurushwa kama mpira uliopigwa shuti uinuke kwenda juu kama umeondoshwa na kipa timu ikashambulie.
Detective Chilamwena alidondokea kifua bastola ilimtoka mkononi ikiburuzika kwa mbele wakati naye anaburuzika kuifuata nyuma alipoona anaenda kujipiga kwenye ukuta nguzo unaoshika paa ya gereji ya kuhifadhi magari alijipindua akapita kama mshale (uzuri wa ujuzi na kuwa makini) Alhamdulillah sentimeta moja tu alipita na kupishana na hatari ya kupasua kichwa alipoona kasi ya kuburuzika inapungua akajilazimisha kugaragara kwa kuuzungusha hii ilifanya apotee nukta kumeta nyuma ya mojawapo ya magari kama saba ya kifahari yaliyopo eneo hili.
Hali ilikuwa mfanano na kwa Agent Hansen alikitwa na risasi ya mdunguaji katikati ya mgongo akajikuta anapaa juu mikono ikitangulia mbele hapo bastola haikuweza kuhimili kubaki mkononi aliiachia kilazima akiwa juu akaona hatari ya kujipiga kwenye nguzo chuma hivyo akakinga kwa mikono asijipige lakini nguvu ya mtupo ilikuwa kubwa hivyo nguvu hiyo ya kiasili ilimzungusha akabwagika chini akajikaza asiendelee zaidi maana alihisi sasa atalengwa kichwa na mdunguaji akajipindua akakita magoti chini hakujali maumivu ya kuchanika kwa suruali hadi ngozi ya eneo hili la magoti akajidundisha kama chura na kweli kama aliota au alikuwa akiendeshwa kwa rimoti na mtu fulani vile risasi ya mdunguaji ilimkosa padogo kukita kwenye mapaja ikakita ardhi na kuchimba, fundi Hansen akahama kwa kasi ya kimbunga mpaka nyuma ya ukuta lakini huko macho yakakutana ana kwa ana na mtu ambaye wao walimkosakosa na risasi wakati wanawashambulia mbwa na mtu aliyetokeza muda mfupi wakiwa wamelala chini baada ya kutoka kwenye mtaro wa maji.
“Tulia hivyo hivyo lasivyo na kumwaga ubongo” Yule mtu akaongea akimnyoshea mdomo wa mtutu wa bunduki aina ya Norinko QBZ-03 Assault Rifle ikiitwa hivi kwa kiingereza na kwa wazalishaji wenyewe walikuwa wakiita ‘Qing Buqiang Zidong’, bunduki ambazo magaidi na wahalifu wengine wa kimataifa uzipata kwa urahisi kutokana na soko la China kuwa soko huria sana lisilobagua katika mauzo yake ya silaha.
Mtu huyu ni bora angemshindilia risasi Agent Hansen lakini alitaka kumuweka chini ya ulinzi akiwa hajui inamletea athari gani? Bisu kubwa lilizama katikati ya shingo kwa pembeni likikita mpini wake huku makali yote yakipenya kutokea upande wa pili alibaki kasimama anatetemeka mwili mzima ahamini kilichomtokea na kinachokwenda kumtokea, bunduki ikamdondoka akajikuta anapiga magoti kwa nguvu ukafuata mwili wake kujibwaga chini damu zikichuruzika kiwembamba sana kufuata mpini ulipotoka kifo chake kikawa cha kimya kimya kana kwamba hana dhambi zozote mtenda mwema maana hakuwa mwenye kupaparika (lol) pepo inamuita haaah hapana jehanamu ya moto alikuwa anaiona machoni anajijua kwa dhambi alizonazo anaenda huko macho yalipaona wakati yanashindana na roho yake iliyokuwa ikitoka na kuzima kila kitu chake mwilini.
Alikuwa ni Detective Chilamwena kafanya kazi hii murua lakini walipotulia sekunde kumi wakiangaliana baada ya kuitizama kwa pamoja maiti iliyo mbele ya macho yao, miili yao ikaanza fujo waliyokuwa wameikimbia ilikuwa ni muwasho ambao unaweza tamani uivue ngozi yako ubaki na nyama tupu walikuwa wanajikuna hasa miguuni ndipo kulipoathirika.
“Haaah! Bahati kwetu mwilini maji hayajatupata zaidi ya pambeni ya mikono bullet proof imetusaidia..” Aliongea Detective Chilamwena macho yake yakizunguka huku na huko bila kumuangalia ndugu yake aliyebaki kakaa chini anajikuna kwenye vigimbi vya miguu yake kwa kujikwangua na kiubao alichokiokota pale pale chini.
“Wanatuona na hapa, hapo juu yako kuna cctv kamera.. Nyoosha mkono uinyofoe yenyewe au kata waya yake inaonekana vizuri karibu yako..!”Akaelekeza Hansen uso ukiwa umekunjwa kwa hasira na maumivu aliyonayo sehemu mbalimbali za mwili wake.
Chilamwena alitizama juu yake anapoelekezwa akaiona cctv kamera akanyoosha mkono akaivuta kwakuwa sifa ingine ya Chilamwena ni urefu hivyo alifanya kilichotakiwa kufanywa kwa kunyoosha tu mkono akiruka kidogo.
“Weee mbona huwashwi?” Akauliza Agent Hansen akiwa pale pale chini alipo akiwa kazibwa na nguzo zege kumuuliza Detective Chilamwena.
“Ndiyo tofauti ya ngozi zetu inapokuwa hapa.. Wee mweupe kiasili unapokutwa na kitu kama hiki ni tofauti na mimi mwenye ngozi hii ya kiafrika inahimili sana matatizo.. Acha nimpe taarifa Kai na wenzake wewe endelea kujificha papo hapo ukitokeza pua tu utajianika kwa mdunguaji..”Akafafanua Chilamwena akitabasamu akiwa kasimama umbali wa hatua tano toka alipo Hansen yeye akizibwa na gari kutokea kule kwenye madirisha ya ghorofa, alitoa simu akaandika meseji na kuituma kwa namba ya Agent Kai.
Akitumia kiubao alichokuwa akijikwangulia aliivuta bunduki ya marehemu kuja alipo akafanikiwa kuisogeza akaikamatia mkononi akaichunguza na kukoki risasi akajigeuza akihakikisha mwili wake haujianiki kama alivyotahadharishwa na mwenzake.
“Acha tuondoe mwanga kwanza kwa kuvunja hizi taa.. Taa zinamwanga mkali kama nini..” Akaongea huku anachungulia aweze kulenga moja ya balbu kubwa ya taa iliyo katika nguzo zege ikileta mwanga mkali eneo hili walipo, risasi moja tu ilitawanya taa mwanga ukapungua kidogo, wakatizmana na ndugu yake wakatabasamu kisha wakaonyeshana dole gumba kuwa mambo yanaenda sawa.
“Rusha hapa nivunje ya pale naiona uzuri..” Akaomba apewe bunduki kwakuwa wote walikuwa hawana silaha ni kama waliporwa wakati wanakimbia maji kuwashwa huku wanashambuliwa maana hadi mabegi yao yalidondoka.
Bunduki ilidakwa kwa mikono miwili kisha ya hapo mdomo wa mtutu ukainuliwa mara moja tu mvunjiko wa taa ukasikika ukiambatana na mlio mzito wa silaha hii, eneo hili la upande wa jengo ghorofa giza hafifu lenye kuacha vivuli vivuli likachukua hatamu.
Wakati watu hawa wapelelezi na majasusi waandamizi na wabobezi wanapambana kujiokoa baada ya kufanyiwa shambulizi la kushtukizwa, ndani ya jengo kulikuwa na hali ya sintofahamu imekuwaje wamevamiwa katika jengo lao ambalo asilimia mia moja waliamini ni jengo la siri ikizingatiwa katika zile sura ambazo ni ‘most wanted’ hakuna aliyetoka wala kuchungulia dirishani tu kukwepa aina yoyote ya wao kushtukiwa kama wapo kwenye jengo hili ikiwemo hata Madam Millian alipoletwa hapa aliletwa katika hali waliyohakikisha hakuna kiumbe kilichokuwa kinawafuatilia iwe kificho au kisayansi.
“Wamejuaje hapa? Wamejuaje kama tupo hapa? Boza kati yenu kuna msaliti, mmenisaliti mmetusaliti.. Nauliza Chasco niambieeenii? Tumevamiwa hapa pumbavuu zaoo.. Haya zuieni fisi hao hakuna kuingia humu pua yoyote..” Katika chumba kilichopo orofa (floor) ya mwisho ya tano ya jengo hili alikuwa akifoka Brigedia mfukuzwa wa jeshi la Mexico usiku huu baridi haikumsaidia kuupoza mwili wake jasho lilimtoka mwili mzima kama mtu aliyetoka kuoga kisha hajajifuta maji kwa nguo ama taulo.
“Boss! Hapana mi sijui chochote.. Ukweli hakuna anayeweza kukusaliti kivyovyote vile” Akajibu aliyetajwa jina anaitwa Boza.
“Teremkeni chini kuzuia kiumbe chochote kupanda huku juu.. Sitaki kosa lolote lifanyike nachotaka kuona maiti za fisi hao, potea wote!” Akafoka tena akielekeza akifoka kwa sauti.
Walioambiwa wapotee walikuwa ni walinzi wake binafasi na vijana wa kibrazil ambao walikuwa wanatumika katika genge la TRJ kama tawi dogo katika jimbo la Bahia ingawa katika Brazil kijigenge hiki ndicho kilikuwa kigenge kikuu nchi nzima ya Brazil kwa genge la TRJ hivyo majimbo mengine yaliyopo nchini hayakuwa na watu zaidi ya watatu walikuwa ni kama wasambazaji wadogo wa genge lao lakini hapa Bahia ndipo palipokuwa na makao makuu na hata watendaji wengine wa genge walipohitaji kufanya mawasiliano ya kibiashara za ulanguzi wa madawa wa kulevya basi waliwasiliana na Bahia, mbio ziliwatoa katika ukumbi mdogo wa mikutano.
“Amerika.. Amerika wamefika hapa lakini skrini hazinionyeshi sura ya adui kiongozi.. Kati ya wawili hayupo Agent Kai hii inamaanisha hawa sisi hatukuwajua, tumemjua Agent Kai na yule malaya wake anayependa kuongozana kama mkia na sehemu za kunyea za mnyama kila anapoenda yuko naye anaitwa Rebecca Smith.. Hawa wapuuzi kawatanguliza ama nini?” Akiwa amesimama karibu na pazia la dirisha aliongea ‘kingpin Feca’ akili na mawazo yake pamoja na macho akiwa anaangalia skrini kubwa iliyoko ukutani kati skrini tatu zilizofungwa ukutani.
“Jamaa historia yake amekuwa akifanya kazi kwa kivuli cha sura za plastiki za kizungu anazovaa.. Mara nyingi ndicho kitu kinachomlinda na kumpa sifa hasizostahili, nafikiri miongoni mwao wawili wale yupo yeye mule mtu mweusi mchawi..!” Kiunyonge akiwa bado mgonjwa aliongea Mr. Villa Nandez Guti kuweka kitu katika ubongo wa mshirika wake na kiongozi mwenzake wa ngazi za juu katika genge la TRJ.
“Hapana! Hayumo pale niamini mimi.. Aisee kuna mawili ambayo ni muhimu kwetu.. Moja kuwaondoa hawa wamarekani hili tuishi kwa amani au sisi tuuliwe sote humu humu ndani hakuna mtu kukamatwa hivyo hakuna atakayejisalimisha na ninaposema hivi uwa namaanisha.. Atakayejisalimisha tu kabla hajamalizia kurefusha mikono yake kuzidi kichwa atakuwa wa kwanza kutangulia ahera kabla yangu.. Naamini nimeeleweka!” Kwa sauti ya kitemi sauti nzito licha ya umri kuwa umekimbia sana magharibi inayokaribia na insha aliongea akiwa kakunja uso ‘Kingpin Feca’, macho yake yakizunguka katika kila sura yenye macho yanayomtizama, macho yenye uwoga uliokosa ujasiri wa kawaida kwa baadhi ya miongoni mwao.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na ishirini na nne (124)
Ngome ya siri imevamiwa na wazee wa fitina, wazee wa kazi za kazi, wazee wa kujilipua kiakili, kuiingia hatari bila kuiogopa hatari.
Maji ya kuwasha yalifikiriwa na waliyoyatumia kuwa yatawaweka chini kama kondoo wanaosubiria kuchinjwa lakini haikuwa vile walivyotaraji, walinzi wawili wote walioachwa wakililinda jengo hili katika hali ya kuzuia maswali kutokana na kuhisiwa kama wangekuwa wengi basi ingewafanya watu wengine kushuku kwanini? Kwanini jumba hili la ghorofa linalindwa na mambwa pamoja na idadi kubwa ya walinzi, waliweka kificho kupitia hapa.
Agent Kai na wanadada anaoambatana nao ana kwa ana walikuwa bado wa nje wakipanga namna watakavyoweza kupita ikiwa tayari walikuwa wamepewa taarifa juu ya maji muwasho na mambo mengine hivyo umakini mzito ulitakiwa katika wao kuingia.
Nini kitakachowatokea?
Walioambiwa wapotee walikuwa ni walinzi wake binafasi na vijana wa kibrazil ambao walikuwa wanatumika katika genge la TRJ kama tawi dogo katika jimbo la Bahia ingawa katika Brazil kijigenge hiki ndicho kilikuwa kigenge kikuu nchi nzima ya Brazil kwa genge la TRJ hivyo majimbo mengine yaliyopo nchini hayakuwa na watu zaidi ya watatu walikuwa ni kama wasambazaji wadogo wa genge lao lakini hapa Bahia ndipo palipokuwa na makao makuu na hata watendaji wengine wa genge walipohitaji kufanya mawasiliano ya kibiashara za ulanguzi wa madawa wa kulevya basi waliwasiliana na Bahia, mbio ziliwatoa katika ukumbi mdogo wa mikutano.
“Amerika.. Amerika wamefika hapa lakini skrini hazinionyeshi sura ya adui kiongozi.. Kati ya wawili hayupo Agent Kai hii inamaanisha hawa sisi hatukuwajua, tumemjua Agent Kai na yule malaya wake anayependa kuongozana kama mkia na sehemu za kunyea za mnyama kila anapoenda yuko naye anaitwa Rebecca Smith.. Hawa wapuuzi kawatanguliza ama nini?” Akiwa amesimama karibu na pazia la dirisha aliongea ‘kingpin Feca’ akili na mawazo yake pamoja na macho akiwa anaangalia skrini kubwa iliyoko ukutani kati skrini tatu zilizofungwa ukutani.
“Jamaa historia yake amekuwa akifanya kazi kwa kivuli cha sura za plastiki za kizungu anazovaa.. Mara nyingi ndicho kitu kinachomlinda na kumpa sifa hasizostahili, nafikiri miongoni mwao wawili wale yupo yeye mule mtu mweusi mchawi..!” Kiunyonge akiwa bado mgonjwa aliongea Mr. Villa Nandez Guti kuweka kitu katika ubongo wa mshirika wake na kiongozi mwenzake wa ngazi za juu katika genge la TRJ.
“Hapana! Hayumo pale niamini mimi.. Aisee kuna mawili ambayo ni muhimu kwetu.. Moja kuwaondoa hawa wamarekani hili tuishi kwa amani au sisi tuuliwe sote humu humu ndani hakuna mtu kukamatwa hivyo hakuna atakayejisalimisha na ninaposema hivi uwa namaanisha.. Atakayejisalimisha tu kabla hajamalizia kurefusha mikono yake kuzidi kichwa atakuwa wa kwanza kutangulia ahera kabla yangu.. Naamini nimeeleweka!” Kwa sauti ya kitemi sauti nzito licha ya umri kuwa umekimbia sana magharibi inayokaribia na insha aliongea akiwa kakunja uso ‘Kingpin Feca’, macho yake yakizunguka katika kila sura yenye macho yanayomtizama, macho yenye uwoga uliokosa ujasiri wa kawaida kwa baadhi ya miongoni mwao.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!
FUNGA KAZI XVIV
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
“Kama mlivyosikia juu ya wenzetu ambao tayari wapo ndani ya huu ukuta hali ya uwa huu kwa ndani ni cctv kamera zilizopangwa karibu kila kona.. Tayari maaadui washafahamu kuwa ndugu zetu wako ndani ya ngome yao ya siri lakini tunaweza tumia akili zetu tatu kufanya tukaingia kama nyoka anayeingia ndani ya pango kinyemela wakati wa usiku wa giza.. Nipeni mawazo yenu wanawake mashupavu wapigania nchi” Agent Kai aliongea akiwa kachuchumaa chini huku mbele yake yupo Agent Jade Poul Brown akiwa naye kachuchumaa kama alivyochuchumaa yeye huku kulia kwake yuko Special Agent Rebecca wote walikuwa wamevaa miwani ya kisasa yenye kazi kama zifahamikazo kwa watu wa kazi zao kuivaa wakiwa maeneo ya kazi.
“Kwanza tutakata umeme kwa kuharibu nyaya inayoingiza umeme humu ndani hili zoezi letu liwe na mafanikio na pia kuwwasaidia wenzetu walio tayari ndani ya ngome na washashtukiwa kuwa wamevamia..” Akaanza kueleza alichonacho fikirani S.A Rebecca akimuangalia Kai mara moja moja wakati anaeleza kisha anamuangalia Jade halafu kichwa kinazunguka huku na huko, walikuwa karibu na bustani ambayo kwa pembeni ya bustani kuna makaburi ambayo wao hawakuweza kujua kama ni ya familia au ukoo wa watu walio na majirani na hapa karibu na ufukwe wa bahari hivyo sauti ya mawimbi ya maji yanayokuja ufukweni katika stahili ya maji kupwa na maji kujaa yalikuwa yakisikika kwa uzuri katika masikio yao ambapo kwa eneo la mbele ya macho yao ndipo kulikuwa na ukuta unaozunguka jumba ghorofa ambalo wanaamini ndimo alimo Feca na vibaraka wake na ndugu zao kuwa wameshaingia ndani ya ngome kupitia mtaro wa maji ziada na maji machafu kama yatazalishwa na wakazi wa jumba ghorofa hili la kisasa.
“Huko sahihi.. Lakini kwa tulivyochunguza mchana umeme unaoleta umeme ndani ya hili ghorofa huko kwa mbele” Akaunga mkono Agent Jade hapa wakitizamana na Agent Kai bila kuzungusha zungusha macho kila mmoja akiwa katika fikra nzito cha kufanya.
“Naam! Tutagawana upande.. Rebecca utaenda mbele kutafuta waya unaoingiza umeme ndani, wakati mimi nitapita kushoto, umeme ukizimika tu haraka nitakwea ukuta mpaka ndani wakati Jade utapita kulia pia utafanya hivyo nafikiri utadondokea walipo kina Hansen.. Haya Rebecca ungeanza kuondoka kabisa kwenda kufanya kazi ya kukata umeme” Wazo la kukatwa umeme lilipita bila kupingwa katika kichwa cha Agent Kai akaongea kwa kuamua kila mmoja atafuata hamsini yake waingie ndani ya uwa wa ukuta.
Walipena mikono kwa kushikana kutakiana kila la kheri kwa hisia kali walipomaliza kila mmoaja akainuka toka alivyochuchumaa wakainama kwa kupinda migongo yao kifuatacho wakaanza kufuata ukuta wakipita minazi mingi iliyo upande huu baada ya kupapita karibu na eneo la makaburi, walipokaribia wakaanza kugawana kufuata maelekezo ya mwisho toka Agent Kai.
S.A Rebecca alikwenda akipita kwa kufuata vivuli vya miti akiwa anainama upande wake ambao ulikuwa ni upande ambao ungeweza kumpeleka kwa upande wa mbele, ilikuwa si njia pitiwa na watu kulikuwa na waya za senyenge zilizowekwa na jengo la jirani na jengo hili nyatiwa ambalo nalo ni jengo la ghorofa lenye urefu wa floor (losheni) tatu ni zuri sana ukiweza kuliona ila mwenye nalo hakulizungushia ukuta alilizungushia wigo wa asili wa michongoma kisha akazungushia nyaya za senyenge hivyo mwanadada huyu wa kizungu akiwa kavaa kikazi haswa anapopita huku silaha aina ya bastola ikiwa imekamatiwa laiti ungemfumania ungeweza sema kifungu cha giza kilichoinama kinatembea.
Umakini wake uliongezeka katika kiwango kile cha juu kabisa alipokuwa anakaribia eneo ambalo aliona kwa juu kuna nyaya za umeme zinazoleta umeme katika majumba haya mawili yaliyopeana ubavu, jicho moja la upande wa kulia lililo ndani ya miwani aliyovaa lilibinywa huku mkono wa kulia alioshika bastola yake pendwa aina ya 357 S&W Magnum ukiinuka kulenga kikombe kimoja kilichoshika nyaya inayotokea huko inakotokea kuja kwenye nguzo hii inayopeleka umeme majengo haya mawili akaachia risasi moja kikombe kikasambaratika umeme ukakata majengo yote mawili, angeweza sababisha umeme ukate jengo kusudiwa tu lakini hakutaka hivyo kwa kusudi maalumu.
Agent Kai umeme ulipokuwa unazima alikuwa hatua mbili tu toka kwenye mti ambao upo karibu na kona ya ukuta uzio, hivyo kitu alichokuwa akikisubiri kilipotimia kilimfanya atimize hesabu zake alizokuwa akizipiga jinsi atakavyoukwea mti kwa kasi kana kwamba nyani aina ya gendaheka anamkimbia simba mwindaji aliyekuwa akimvizia, aliuparamia mti huu aina ya mng’ongo kwasekunde tano tu akawa juu ya kilele kisha bila kujiuliza usalama wake ulivyo aijifyatua akatua juu ya ukuta gloves zikimsaidia asikatwe na chupa hakujali hili sababu kila kitu kishapangiwa hesabu, taharuki ya butwaa kwa walio ndani ya jengo ilikuwa ni fursa yake aliyoihitaji imsababishe awe ndani ya uwa wa ukuta wa uzio, aliganda juu pale kwa sekunde kumi macho yaliyo ndani ya miwani yakitupwa huku na huko kwa eneo la ndani kisha akajiachia kama furushi akatulia miguu akiwa na bastola mbili kila mkono wake mmoja moja.
Si kwamba alipofika akasubiri tu la hasha! Alipotua miguu tu akaangalia huku na huko kwa kasi ya kuweza kuivunja shingo isiyo na mazoezi akanyooka mpaka usawa wa ukuta alipofika hapa akatizama chini maana alikuwa na maelekezo kuwa uwa kuna vibomba vinavyofyatuka kwa alivyo na uzoefu ilimfanya kuwa na utaalamu katika vamia vamia zake kuwa vitu kama hivyo uwa vinaendeshwa kwa saini maalumu kati ya mahala husika na kiumbe kama binadamu kwa alivyotaka mtu anayeviweka, kweli kama alivyofikiri aliona vitofali vinajisogeza pembeni hapo hakutaka kujiuliza nini kitamkuta maana yeye anajua tofauti na kina Chilamwena na ndiyo waliowajuza wao kuwa kuna kitu icho hivyo Agent Kai fundi mtaalamu mpelelezi na jasusi mbobezi alikuwa kashajua atafanya nini hapa, alirudisha bastola zake sehemu zake salama kisha akaangalia viganja vyake ambavyo si kama alikuwa anaviona sababu vilikuwa ndani ya ‘gloves’ maalumu akavuta zipu iliyo kwa pembeni ya ‘gloves’ kisha alichofungua hapo akakizungusha kuja nyuma ya kiganja akakinasisha katika sehemu ambayo akitaka kutoa basi anakuwa kama anachana akaamia ‘gloves’ la mkono wa kushoto napo akafanya hivi sasa hapa kwa ndani ya kiganja gloves kulikuwa na kile kinachoitwa ‘magnetic blocks gloves’ kwa kasi akaanza kukwea juu akinasisha kiganja ukutani kisha anasisha kiganja kingine, hapa msomaji kunahitajika mazoezi haswa si pa kipoapoa sababu kunakula pumzi na nguvu kubwa hasa kwa wale wa miili mikubwa, miguu ilikuwa ikisapoti kukwea lakini haikuwa na kazi kubwa kama mikono, miguu ilikuwa ikikanyaga kwa nguvu na kusukuma juu katika nguzo ya pembe nne inayopanda toka chini mpaka juu kabisa ikiwa inashikamana na kila ‘floor’ inayoanza.
Futi tano kwenda sita wakati anakwenda juu alisikia zile koki zinarusha maji yakijichapa katika kuta ikawa zali kwake kutumia kasi ya mambo aliyojaliwa na mwenyezi Mungu, hakupatwa hata na tone moja, alipofika floor ya kwanza akajivuta na kuingia ndani ya baraza akasogea kwenye kona ya baraza kujibanza.
Sekunde mbili alipoinama kujibanza mwanga wa taa ukawaka na kufanya pote hapa kuwa peupe hii ilimaanisha kuna jenereta limewashwa na wahusika huko ndani.
‘Nimecheza kama Messi kuwai kufika hapa sidhani kama na wao watakuwa wamejua kama kuna mtu katumia muda mfupi hivi kuwa hapa.. Ngoja niwataarifu wenzangu’ Aliwaza Agent Kai akichomoa bastola yake moja toka mahala salama pa kuhifadhi kitendea kazi ama unaweza iita ‘peni’ kama yeye Agent Kai anayependa kuiita bastola yake kuwa ni peni yake ya kazi.
Alitumia muda huu kuchunguza hili eneo kwa kutokea pale alipo macho yake yaliyo ndani ya miwani aliweza kuona ‘cctv kamera’ iliyo kwa juu ya pale alipo lakini haikuwa inachukua eneo alipo ilikuwa ikichukua kwa ukutani na eneo la chini la ghorofa, aliendelea kutulia akiandika meseji ambazo zilikuwa na maelekezo kwa wenzake katika group lao dogo la mtandao wa whatsapp.
Mnyato ulimsogeza toka alipokuwa hadi kwenye dirisha la kwanza kubwa lililo kwenye baraza hii akachunghulia ndani na kumuonyesha chumba hiki ni chumba cha kulala kwakuwa kulikuwa na kitanda kimoja seti ya televisheni, friji ndogo, meza na sofa moja la kukaliwa na watu watatu, kitandani kulikuwa na kitabu ambacho kimewekewa alama na kalamu karibu na katikati ya kurasa za kitabu hii ilimaanisha mtu aliyekuwa katika chumba alikuwa akijisomea kitabu kabla ya kuondoka katika hiki chumba.
Macho yaliyo ndani ya miwani ya kazi za kazi ambayo inaweza kutumika kwa mengi shukrani zote ziiendee kampuni iliyotengeneza hii miwani kwa oda maalumu ya shirika la ujasusi la CIA, aliweza kuona kila kitu kwa usahihi kisha akajaribu kusukuma kioo dirisha kama anaweza kukuta zali la mentali kukuta liko wazi, alikuwa wazi lilikuwa limefungwa kwa ndani hapo hakusubiri kuelekezwa na mtu mwingine ikiwa yeye si mgeni wa kazi haraka akatoa begi lake toka mgongoni mwake akaliweka mapajani mwake akiwa kachuchumaa akasachi kwenye kisehemu cha mfuko mdogo baada ya kufungua zipu huko akaibuka na peni maalumu akaikamatia na kuchora umbo la duara lenye ukubwa wa chapati au sahani ya duara ya udongo katika kioo cha dirisha la chumba ambalo kama nilivyoeleza awali ni zile nyumba ambazo ujengwa kwa kuwekwa madirisha mapana (makubwa), alipomaliza kuchora mduara akigandamiza peni kwa nguvu alipindua upande wa nyuma wa peni kisha akabonyeza kitufe fulani kilicho katikati ya peni upande wa nyuma ukatoka haina fulani ya wino akagandamiza eneo hili la nyuma ya peni au niseme eneo la juu ya peni panapopachikwa kizibo mtumiaji peni anapoitumia kuandika. Mgandamizo huu ulifanya peni inate katikati ya kioo alichokichora duara sekunde tatu za mgandamizo zilifanya peni igande pale kama imegandishwa na gundi akavuta kwa upande wake yaani kwa nje kioo kikaachia kikifuata mulemule kulikochorwa duara, sasa pakawa na tundu, fundi mtaalamu akapitisha mkono ndani na kutoa ‘lock’ (vibanio) za dirisha kisha kiulaini kama anamsukuma mlevi kwenye dimbwi la maji akalisukuma upande mmoja dirisha usawa wa yeye kupita akakamata begi lake vizuri ikiwa karudisha zana yake peni hii baada ya kuichomoa kwenye kioo alichokibandua kisha kukiacha sakafuni katika baraza.
Mdundo mmoja tu toka barazani ulimfanya miguu itue kitandani hakujali kama anachafua shuka jeupe lililotandikwa kitandani ‘potelea mbali’, akaiweka pazia vizuri ikiwa mtu ataingia ghafla humu chumbani basi asione tundu la kioo.
Bastola aina ya ‘Glock 43 Single Stack 9mm’ ilikuwa tayari kwa matumizi akasogea mlangoni kwa taratibu akihakikisha hasikiki na kiumbe chochote kilicho upande wa pili akaminya kitasa mpaka usawa aliojilizisha akavuta kwa ndani ukagoma kuvutika akasukuma kwa nje nako ukagoma ikamjuza mwenye chumba wakati anatoka alitoka kisha akaufunga kwa nje, si mahala pa kujiuliza mara mbili mbili wakati hamsubiri mvivu hivyo yeye si mvivu akachomoa fungu la funguo toka kimfuko kidogo kilicho katika suruali ya mifuko mingi aliyovaa.
Akasoma aina ya kitasa kinatokea nchi gani na ni kampuni gani? Jibu lilipopatikana akaanza pekua katika fungu la funguo, ilimla dakika moja na sekunde thelathini kuweza kuipata akaiset ajuavyo maana hizi funguo uwa zimetengenezwa maalumu kufungua vitasa vya kampuni mbalimbali lakini haziwi kama funguo za kawaida unazoweza kudhania au wewe msomaji kufikiria ni funguo ambazo zinakuwa kama si funguo kwa haraka ukiitizama lakini ndiyo kiboko ya vitasa vya kampuni husika (lol).
Alipoitumbukiza akaizungusha zungusha ajuavyo kimlio cha kikomeo kinachoshika kitasa unapofungwa kikasikika kwenye masikio yake kikiwa kimesalimu amri hapo akaichomoa na kurudisha fungu la funguo kule alipoitoa mlango ukaminywa kitasa tena kwa mara ya pili kwa taratibu ukavutiwa ndani ukakubali kuja hapo akatulia kwanza kupisha upepo kwanza alipona hasikii hata mnyato fulani toka upande wa pili akavuta tena kwa ndani uwazi wa kumuwezesha kutoa kichwa chake ili macho yake yakapate kufanya ziara kuona nini ni nini? na yaliyomo yamo?.
Kichwa kikatokea na macho yaliyo ndani ya miwani yalishuhudia eneo la korido ndefu sana ikiwa kuna taa juu zenye kumulika kwa mwanga mkali kukawa kweupe kama vile mchana kwa chati akaendelea kuchungulia ndipo kona ya mwisho kabisa akaona vijicho vya ‘cctv kamera’ vinamulika usawa wa katikati ya korido chochote kikitokea basi inachukua kupeleka huko inakopeleka.
Fundi mtaalamu! Akarudi ndani na kuurudisha mlango akatoa simu yake ya mkononi na kutuma ujumbe kwa wanatimu wenzake ambako jumbe zilifika lakini hakuna aliyezisoma kwa wakati huo hii ilijuza kila mmoja yupo katika harakati fulani.
Wakati yeye akiwa hapa katika chumba cha ‘floor’ ya kwanza, Agent Hansen na Detective Chilamwena bado walikuwa wamekwama katika gereji ya kuhifadhi magari wakihofia kutokeza walau hata pua tu kwakuwa wadunguaji walikuwa wameelekeza macho yao eneo lile lile wao wakiwa katika floor ya nne walikuwa wawili katika moja ya dirisha na floor ya tano alikuwepo mmoja, wakiamini adui zao waliowavamia ni hao tu na pia waliamini katika dakika mbili tu ambazo umeme ulikatika na wao kuwashwa jenereta isingewezekana kwa mwingine kama yupo na awa walio hapa kwenye gereji lakini yeye alibaki nje asingeweza kuparamia ukuta wenye vyupa juu kwa dakika hizo kisha aingie ndani kwa kudondokea ndani ukuta uzio, walijidanganya hivi lakini tayari ndani ya uwa huu kulikuwa na mtu wa tatu kaongezeka na pia ndani ya jengo katika ‘floor’ ya kwanza katika chumba fulani alikuwemo Agent Kai.
Mwisho wa sehemu ya mia moja ishirini na tano (125)
Vita ya wavamia na wavamiwa ndiyo imepulizwa filimbi yake ya kuanza kwa watu wawili wa timu vamiwa kuondolewa uhai wao pamoja na mbwa watatu tegemezi na aminika nao kupelekwa kwenye usingizi wa milele mwili kuoza.
Mipango inaenda kama pande zote walivyokuwa wanatamani iende katika moja kudhibiti hakuna anayeingia ndani ya jengo lao kwa vyovyote vile hakuna wa kuwasogelea na huku pande ingine ikisema inatumia kila aina ya ujuzi na ufundi wao wa kikazi hizi za kazi.
Agent Kai yumo ndani ya jengo ‘floor’ ya kwanza huku mtu mwingine ambaye hakutajwa jina kuwa ni nani naye alikuwemno ndani ya ukuta wa uzio unaozunguka jengo husika.
Alipoitumbukiza akaizungusha zungusha ajuavyo kimlio cha kikomeo kinachoshika kitasa unapofungwa kikasikika kwenye masikio yake kikiwa kimesalimu amri hapo akaichomoa na kurudisha fungu la funguo kule alipoitoa mlango ukaminywa kitasa tena kwa mara ya pili kwa taratibu ukavutiwa ndani ukakubali kuja hapo akatulia kwanza kupisha upepo kwanza alipona hasikii hata mnyato fulani toka upande wa pili akavuta tena kwa ndani uwazi wa kumuwezesha kutoa kichwa chake ili macho yake yakapate kufanya ziara kuona nini ni nini? na yaliyomo yamo?.
Kichwa kikatokea na macho yaliyo ndani ya miwani yalishuhudia eneo la korido ndefu sana ikiwa kuna taa juu zenye kumulika kwa mwanga mkali kukawa kweupe kama vile mchana kwa chati akaendelea kuchungulia ndipo kona ya mwisho kabisa akaona vijicho vya ‘cctv kamera’ vinamulika usawa wa katikati ya korido chochote kikitokea basi inachukua kupeleka huko inakopeleka.
Fundi mtaalamu! Akarudi ndani na kuurudisha mlango akatoa simu yake ya mkononi na kutuma ujumbe kwa wanatimu wenzake ambako jumbe zilifika lakini hakuna aliyezisoma kwa wakati huo hii ilijuza kila mmoja yupo katika harakati fulani.
Wakati yeye akiwa hapa katika chumba cha ‘floor’ ya kwanza, Agent Hansen na Detective Chilamwena bado walikuwa wamekwama katika gereji ya kuhifadhi magari wakihofia kutokeza walau hata pua tu kwakuwa wadunguaji walikuwa wameelekeza macho yao eneo lile lile wao wakiwa katika floor ya nne walikuwa wawili katika moja ya dirisha na floor ya tano alikuwepo mmoja, wakiamini adui zao waliowavamia ni hao tu na pia waliamini katika dakika mbili tu ambazo umeme ulikatika na wao kuwashwa jenereta isingewezekana kwa mwingine kama yupo na awa walio hapa kwenye gereji lakini yeye alibaki nje asingeweza kuparamia ukuta wenye vyupa juu kwa dakika hizo kisha aingie ndani kwa kudondokea ndani ukuta uzio, walijidanganya hivi lakini tayari ndani ya uwa huu kulikuwa na mtu wa tatu kaongezeka na pia ndani ya jengo katika ‘floor’ ya kwanza katika chumba fulani alikuwemo Agent Kai.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!
FUNGA KAZI XVV
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
“Vipi miwasho imepungua miguuni?” Swali liliulizwa na Detective Chilamwena kumuuliza Agent Hansen.
“Uvumilivu ndiyo mafunzo yetu.. Sijui wewe? Lakini sijaona ukijikuna.. Hahah..!”
“..Najivunia uwa sina tatizo na mambo haya mpaka yawe mazito zaidi si kwa mpako mdogo kama ule.. Tuko kazini Hans, tumechelewa kuondoka hapa wakati kulivyokuwa giza tumekuwa waoga kudunguliwa”
“Tungetokaje wakati umeme ulivyokatika jamaa walipiga risasi eneo hili kama kutaka kutufahamisha kuwa wako makini tusingeweza kufanya ulichotaka lakini kuweka umakini wao hapa umesababisha Agent Kai kuwa yumo ndani ya jengo lao bila wao kujua, aisee mtu huyu wa ajabu sana. Mungu amemjalia sana ukweli tuuseme najivunia sana kwa nchi yangu kuwa na mtu kama yeye”
“Hakika kaka.. Dakika mbili au tatu zimemtosha kutoka nje kabisa mpaka ndani kabisa ya jengo.. Aliyependekeza aitwe TSC alimpatia sana kwa jinsi alivyo juu kwenye unyemela, hahahah!”
“Kutokea hapa ulipo na hiyo bunduki uliyonayo tunaweza fanya wakawa bize nasi zaidi ya ilivyo kumpa nafasi Agent Kai kufanya kazi yake… Agent Jade naye yumo ndani uzio wa ukuta kama sisi lakini yuko kwa mbele.. Sisi ndiyo wa kuwasaidia wao kufanya kazi kwa wepesi” Agent Hansen alielekeza akibadili maongezi ya kumuongelea mpelelezi na jasusi mwenzao Kai.
“Nimekuelewa!”Akajibu kifupi Detective Chilamwena kisha akajivuta kukaa aweze kuona kupitia kwenye vioo vya madirisha ya gari hapo hakuona vizuri kuelekea yalipo madirisha ya jengo, akainama na kupita eneo hili safari ikampeleka mpaka kwenye kona ya gari hapo akajitokeza kichwa kidogo kuwezesha macho yake yaliyo ndani ya miwani kuona madirisha ambayo alishakadiria kuwa ndipo wadunguaji wapo pale ‘floor’ ya nne, akaseti miwani yake kiufundi zaidi kama ujuavyo miwani si miwani ya kawaida.
Kwa alipojiweka akiwa sambamba na gari, lenzi za darubini zilizokuwa zinatumika kwa kufungwa moja kwa moja kwenye bunduki za udunguaji aina ya UKARMS 300 FPS Airsoft Snipers Rifle, mashine hii tata ya udunguaji toka nchini Uingereza, moja ya bunduki bora sana kati ya bunduki bora za udunguaji hapa duniani, zingeweza kumuona na kumfanya fundi mdunguaji yoyote kuruhusu kidole chake kilicho sambamba na kifyatulio (trigger) kuachia risasi moja tu ambayo ingeweza kumuondoa duniani hivyo hakuthubutu kusogea zaidi lakini vimdomo vya mitutu katika dirisha la chini ambalo ni floor ya tatu na dirisha la juu floor ya nne aliweza kuiona hapo Chilamwena akageuka kwa Hansen akainua kidole kimoja juu ishara yenye kumaanisha awe makini kumuangalia kuna jambo walizungumze kwa vitendo kupitia mikono yao, maelekezo yalifanyika wakaelewana.
Agent Hansen alielewa alichoelekezana na ndugu yake akanyoosha mkono alioshika kibao kuelekea kwenye mwili uliolala chini ukiendelea kumwaga damu, aliutingisha tingisha mkono wa marehemu na mara risasi iligonga kibao chake ikiwa imekuja bila kuacha mlipuko huko ilipotoka ikimaanisha imetoka katika bunduki iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti (sailensa), ilileta athari kibao kilivunjika na kutoka mkononi mwa Hans.
Wakaangaliana na kutabasamu kisha wakaelekezana jambo lingine hapo Agent Hansen akainuka ghafla kisha akakaa kasi hapo tena risasi ilimkosa sentimita chache na kwenda kutua kwenye dumu la oil likapasuka na likiwa hewani kurushwa mpaka kwenye ukuta oil ilirushwa na kutawanywa mpaka alipo yeye na kumuongezea uchafu mpya baada ya matope ya mtaroni.
Wakati jamaa anashambulia risasi toka kwenye bunduki yake kidogo aliutokeza mwili kutoka kwenye pazia ikawa fursa kwa Detective Chilamwena kijana wa kimarekani mwenye asili ya nchi ya Kongo ya Kinshansa kumuona mdunguaji anavyosogeza pazia kwa kutumia mtutu wa bunduki, sifa ya Chilamwena iliyomfanya kuchukuliwa na jeshi la Marekani wakati alipopata nafasi ya usahili ilikuwa ni uwezo wa kulenga shabaha kwa kushtukiza yaani anapotaka kulenga kitu uwa anatokea ghafla na kushambulia kwa usahihi, risasi moja aliyoachia baada ya kutokeza mwili wake aweze kushambulia ilifanikiwa kutua juu kidogo ya mwamba wa pua ya mdunguaji ikiwa ghafla sana kwake bila kutarajia alirushwa kwa ndani na uhai kumchomoka pale pale, haraka Chilamwena akarudi mahala pake akiwa kashaongeza idadi ya kuua mtu kati ya watu aliowaondoa duniani iwe kwa risasi kama leo au kwa aina nyingine yoyote ya uuaji.
Wakaangaliana na Agent Hansen ambaye alihama kwa kasi kwenda upande wa pili toka pale alipo bila mdunguaji kumuona kwa haraka anamaliza kupita kwa mdunguaji aliyebaki ilikuwa kama kaona kivuli ikilinganishwa na uoga aliokuwa nao kusikia mwenzake aliye floor ya chini yake kadunguliwa na wote Chilamwena na Hansen walikuwa wanalijua hili hivyo wote walitumia fursa kugawana eneo ikiwa silaha waliyonayo ni moja tu bunduki aliyonayo Detective Chilamwena ambaye muda huu alijisogeza mbele zaidi kwenye ubavu wa gari ingine ambayo kwa lipo sasa mita kadhaa kwenda juu alikuwa analiona dirisha alilo mdunguaji mwingine.
Alipojisogeza Agent Hansen ilikuwa na karibu na ambapo begi la Detective Chilamwena lilianguka, aliokota moja ya chuma refu akaanza kulivuta bila kujali bomba linatoa mikwaruzo katika sakafu iliyopangwa vitofa vidogo vidogo, sauti iliyomvutia mdunguaji aliye floor ya juu ya ile ambayo aliyekuwepo hapo alishapelekwa kuzimu, kwa chati jamaa akawa anatamani aone kupitia lenzi yake ya darubini ambayo kikawaida uwa haikosi katika bunduki za wadunguaji, hakutaka uso wake au mwili wake uonekane akihofia kukutwa na kile kilichomkuta mwenzake, kwenye macho ya Detective Chilamwena alikuwa akiona tukio lote naye ikamvutia kuvizia zaidi akawa anajivuta aweze kuachia risasi sahihi katika eneo sahihi.
Bega moja la mdunguaji lilikuwa likionekana likizibwa na pazia kisha pazia inarudi linaonekana tena na kila alivyokuwa akijitahidi kuweka darubini vizuri ndipo alipozidi kulifanya bega lake litokee zaidi kwenye upeo wa macho yaliyo ndani ya usaidizi wa miwani aliyovaa Chilamwena akainua mdomo wa bunduki na kulenga kwenye pazia upande anaoliona bega likisukwa, jicho moja likabinywa akabana pumzi alipoachia tu ikawa amevuta nyuma kifyatulio (trigger) kilicho ndani ya kidole cha shahada cha kiganja chake cha mkono wa kulia, risasi moja aliyojitahidi pale itakapotua itue kwa ndani kidogo licha ya kuwa hakuwa anamuona vizuri mtu iliweza kupenya juu kidogo ya moyo wa muhusika na kufanya kukata eneo la juu linaloshika moyo papo hapo mpigwa risasi alirushwa kwa ndani hapana chezea Norinko QBZ-03 Assault Rifle, roho hatimaye ikauchia mwili papo hapo bila kuomba maji giza zito likafunika macho yake huku anayeitwa malkia mtoa roho akiwa amechukua roho kuifikisha inapotakiwa kwenda.
Agent Hansen aliona alichofanya ndugu yake akajua sasa kazi ni kwao kufanya maajabu yanayotakiwa akamuonyesha alama ya dole tokea pale alipo ambaye naye akamjibu dole kisha akaonyesha ishara ingine kuwa imekwisha.
Wakati wao wakifanya haya kwa ushirikiano kama timu, mwanadada Agent Jade Poul Brown baada ya kuruka ukuta kipindi umeme umekatika kwa kazi iliyofanya na mwenzano aliyepewa jukumu hilo, yeye alitokea katika upande wa mbele karibu na geti kuu la kuingilia, taa zilipowaka tena kwa kazi iliyofanywa na jenereta lililowashwa na wahusika waliopo ndani ya mjengo ilimkuta akiwa pembeni ya ngazi za baraza huku kukiwa na mitungi kadhaa mikubwa ya maua kwa ajili ya kuremba eneo hili kuwa la kupendeza zaidi hivyo alijidondosha chini haraka na kujilaza sambamba na kiukuta cha ngazi za baraza, akanyooka kabisa kutulia kwa dakika kadhaa kisha akainua kichwa chake kuona hali iliyopo hapa mbele kama inamruhusu kuwa hapa bila kuingia matatizoni.
Wakati akiendelea kuangalia usalama wake aliona kufuli katika ardhi likionekana limefunga vyuma viwili vilivyobanana hapo kwa ujuzi wake ikamvutia atambae kusogea pale, akatambaa mpaka pale kwa kutumia mikono akasogeza majani ya maua kisha akasukuma michanga sasa akaona kufuli lile limefunga mfuniko wa bati ngumu, macho yakatupwa huku na kule kisha akaliangalia kufuli vizuri likiwa na chata ya kiwanda kilichotengezea kufuli hili kuwa ni kampuni ya utengenezaji wa chuma ya Jalisco Plancha, akili ya Jade ikazidi kujisogeza katika mmiliki wa kiwanda hiki kuwa ni Feca na mke wake, mkono wa mwanadada ukalileta begi lake mbele akafungua zipu akiwa amelala chali akatoa kifaa ambacho ni spesho kwa kuvunja mitego ya kufunga kufuli aina yoyote kifaa hiki kama kufuli ingekuwa ni kiumbe hai basi ingekuwa ikikiona tu inakiogopa.
Akapachika katikati kisha kubonyeza kitufe kilicholifyatua kufuli mara moja tu akazungusha na kulitoa, alipoinua juu likafuata kwa chati akachungulia ndani hapa masikio yake yakasikia muungurumo wa kama injini ya pikipiki, Jade akatulia dakika moja kisha akatizama huku na huko alipoona hakuna shida akainua upenyo wa kuweza kumpitisha akapita akitanguliza miguu kisha akazama ndani kufuatia na kurudisha mfuniko ulivyo, macho yakakutana na ngazi akazifuata zinavyoshuka huku muungurumo ukizidi kila anavyopiga hatua moja kushuka ngazi, alipomaliza akatokea kwenye korido akaifuata ndipo akaona kinachounguruma ni nini? Lilikuwa ni jenereta bila kufikiri hatua zake zilisogea kwa kunyata lakini usoni alilimwaga tabasamu la kutosha akakumbuka kabla hawajaondoka kwenye kikao chao cha dakika nne kilichofanyika nyuma ya jengo hili karibu na makaburi yaliyopo pia karibu na ufukwe.
Alipolifikia akatoa begi lake kisha akatoa bomu dogo la kutega kisha akaliweka karibu na mfuniko wa mafuta wa jenereta hili kubwa lenye uwezo wa kutumika hata kwenye uwanja wa mpira wa basketball na taa kubwa zaidi ya ishirini zikaweza kuwaka kuwamulikia wachezaji wanaocheza na mashabiki waliofika kushuhudia mchezo, safari ya kuelekea mbele zaidi ilianza mwisho wa chumba alikuta ngazi zinapanda juu akapandisha nazo mpaka mwisho wa ngazi akiwa katika hali ya tahadhari kubwa sana mpaka ulipo mlango wa mbao akaminya kitasa hakuogopa kama kitasa kitakuwa ni kati ya vile vitasa vikavu ambavyo ukiminya ili ufungue kinatoa mlio wa kulalamika hiki hakuogopa kwa sababu ya muungurumo wa jenereta hadi hapa ulikuwa muungurumo dume haswa.
Mlango hakukuwa umefungwa akauvuta kwa ndani kidogo kisha kuchungulia upande wa pili macho yaliyo ndani ya miwani yalishuhudia korido ndefu inayoendelea mbele na hakukuwa na mtu lakini juu ya dari ya korido hii kwa mbele kabisa karibu na mwisho wa korido kulikuwa na balbu iliyo na ‘cctv kamera’ ndogo ambapo kama si mjuzi wa vitu hivi huwezi juwa kama katika balbu ile kuna ‘cctv kamera’ ikichukua korido yote kwa kuja huku kwenye mlango wa kuingia chumba cha jenereta.
Agent Jade Poul Brown mwanadada machachari sana kwenye kazi na mzoefu mkubwa wa michezo hii ya gizani alijitokeza kwa kasi kisha akafunga mlango kwa nyuma yake kikafutia na kubonyeza kwa rimoti ndogo ya kulipua vilipuzi vya kutegwa, mzinga mkubwa wa mlipuko wa bomu ukasikika kisha kufuatiwa na giza nene za zito la ghafla likashika hatamu ndani ya eneo lote kuanzia ndani ya mjengo na nje pia, wapenda giza kama nawaona huko walipo wakiwa wamejigawanya kikazi mahala mbalimbali kulizunguka jengo na hata wawili hawa kuwa wamo ndani kila mmoja kati yao alishangilia kilichotokea kwa stahili yake.
Mshindo wa mlipuko ulifanya jengo la ghorofa hili kutingishika na kuwashtua wote waliomo ndani ya jengo hili hasa wale wa upande wa kushoto (waliovamiwa) hawakutegemea kama si kulitarajia hili walilolisikia kwa masikio yao na macho kushuhudia likitokea giza lakini upande wa kulia (uliovamia) kila mmoja ukiacha yeye mwenyewe Agent Jade ulitambua kuwa kazi imefanywa na mmoja wao kazi nzuri yenye manufaa maana kati yao wote imani yao uwa kuwa ‘giza kwanza kwa manufaa ya kazi za giza’ hata wachawi, wanga na vinyamkera wote akiweno baba la maasi duniani (shetani) kwa ujumla wao wanalipenda giza na kutumia msemo wao huo kuwa ‘giza kwanza kwa manufaa ya kazi za giza’.
Hali ilikuwa hali changanyikiwa kwa upande wa mtu wa hatari ambaye uamini katika msemo wake kuwa ‘ng’ombe hazeeki maini’ na shetani kila anavyozeeka uzidisha ujuzi, unyama na ukatili wake basi, mtu kiongozi wa genge ambalo hatujui hatima yake kwa sasa ingawa asilimia sabini ya nguvu zake pamoja na nguvu kazi watu lilikuwa limesambaratika, kingpin Feca ambaye si Kingpin Feca yule wa miaka kumi iliyopita uzee ulikuwa umemla pamoja na jitihada zake za kujiweka kimazoezi lakini kasi ya uzee na anayoyataka vilikuwa haviendani, taharuki naye ilimkumba woga ukamuingia katika viunga vya mifupa yake na maeneo ya hisia ndani ya mwili wake alihofu akajishika kujipapasa sehemu ambazo ameweka silaha zake kusubiri yoyote anayetokea kufika katika eneo walilopo yeye na wenzake wengine watatu basi silaha zitasema nao na ujuzi huu wa kucheza na silaha ni kweli hauzeeki bwana.
“..Jamaa wamelipua jenereta letu..”Akaongea yeye mwenyewe kana kwamba anajiambia peke yake maana sauti haikutoka vizuri hata lile ‘bass’ (sauti lake zito) lenye mikwara halikuwepo tena hii ilisababisha walio karibu yake kuingiwa na ubaridi ndani ya mifupa yao ukizingatia wote hawakuwa mafundi haswa wa michezo hii ukiacha Feca mwenyewe na aliyekuwa kamishina mkurugenzi wa uhamiaji nchini Guatemala Brigedia Mcdonald Grannell
“Nahisi kama tunaweza ingia matatizoni mkuu.. Awa vijana tuliokuwa tumewaweka hapa Bahia si vijana waliopita mafunzo vizuri katika ulinzi na kujihami wameshindwa linda eneo la jenereta mpaka linalipuliwa hii inamaanisha jamaa watatufikia hapa tusipokuwa makini mheshimiwa.. Nimeona jinsi walivyoruhusu watu kuingia ndani ya ngome yetu kirahisi na pia kuona hili lililotokea sasa..!” Alizungumza Rafael Ceni aliyekuwa mheshimiwa waziri wa ulinzi wa nchini Guatemala na swahiba watoka utotoni wa Rais wa nchi ya Guatemala.
“Tafadhali usiwashe tochi.. Zima tochi na pia zima mwanga wa simu itafanya adui watuone tulipo, kumbukeni tunacheza na watu wenye ujuzi na hapa tuliopo wenye ujuzi ni wachache hivyo kila mmoja atafuata maelekezo yangu mimi au ya Brigedia Grannell” Onyo la kuhitajika kuzimwa kwa tochi lilitolewa na ‘Kingpin Feca’ aliyemkemea mdogo wake Alexis Codrado Feca.
“Tusiwategemee tena walinzi waliokuwa wanatulinda ni zamu yetu sasa kujiokoa toka mikononi mwa maadui kwa stahili ya kuamua kufa au kupona au jin o kwa jino kwa kuanza sote tutadhibiti hakuna mtu kufika katika floor hii ya mwisho sababu ngazi za kujia huku tunaziona pia futeni wazo la kusubiri mtu asogee huko huko alipo tuna m shoot bila kusubiri sababu nawaambieni watu hawa hawajaja kucheza hapa Bahia wamekuja kikazi tena kikazi haswa ndiyo maana siku mbili tu zimewatosha wao kupajua mahala hapa tulipoamini ni salama kwetu kwa asilimia 99” Maelezo ya Brigedia Grannell yalishuka kwa kasi huku macho yake yakiangalia zilipo ngazi zinazojia hii floor ya mwisho.
“Sergio Puto aliomba akawe mdunguaji sababu ni mtu anayevutiwa na udunguaji lakini mpaka tunakumbwa na kadhia hii ya giza naamini atakuwa kadunguliwa yeye baada ya kuwa kadungua yeye..” Feca akaeleza tena akitikisa kichwa huku nywele zake zenye mvi lakini akiwa kafungua kimchicha alichokifunga na kuzifanya zimwagike pande zote mapka akiongea inambidi azitingishe aweze kuwaangalia wenzake.
“Ulinzi uimarishwe maradufu na sote tujigawanye wao wamekuja kwenye ngome yetu si kutembea na kufanya nasi maongezi huku tukinywa kahawa wamekuja hapa kutufanyia angamizo na hawatasita kutuangamiza labda tujisalimishe hivyo hawana budi kuja tulipo baada misako yao kufeli kutuona huko orofa za chini… Kwa kuanzia na hili giza lililopo hapa tutakaa kwa kujificha katika kona na kona mimi na mhehimiwa Feca tutakuwa mbele kuongoza ulinzi tukiangamiza kila anayetokeza pua yake, hamna kudangayika na nguo kuwa zinafanana na mmoja wa walinzi wetu kumbukeni hilo jamaa wana ghiliba zote” Maelezo ya Brigedia Mcdonald Grannell yalitoka akisikilizwa kwa umakini mkubwa sana.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na ishirini na sita (126)
Kazi bado ya moto!
Pande zote mbili zinazosigana ziko eneo moja katika ghorofa lenye urefu wa floor tano kwenda juu.
Kama kawaida nisilembe sana mwandiko nikuache utafakari kisha uruhusu twende hatua inayofuata..!
“Tafadhali usiwashe tochi.. Zima tochi na pia zima mwanga wa simu itafanya adui watuone tulipo, kumbukeni tunacheza na watu wenye ujuzi na hapa tuliopo wenye ujuzi ni wachache hivyo kila mmoja atafuata maelekezo yangu mimi au ya Brigedia Grannell” Onyo la kuhitajika kuzimwa kwa tochi lilitolewa na ‘Kingpin Feca’ aliyemkemea mdogo wake Alexis Codrado Feca.
“Tusiwategemee tena walinzi waliokuwa wanatulinda ni zamu yetu sasa kujiokoa toka mikononi mwa maadui kwa stahili ya kuamua kufa au kupona au jin o kwa jino kwa kuanza sote tutadhibiti hakuna mtu kufika katika floor hii ya mwisho sababu ngazi za kujia huku tunaziona pia futeni wazo la kusubiri mtu asogee huko huko alipo tuna m shoot bila kusubiri sababu nawaambieni watu hawa hawajaja kucheza hapa Bahia wamekuja kikazi tena kikazi haswa ndiyo maana siku mbili tu zimewatosha wao kupajua mahala hapa tulipoamini ni salama kwetu kwa asilimia 99” Maelezo ya Brigedia Grannell yalishuka kwa kasi huku macho yake yakiangalia zilipo ngazi zinazojia hii floor ya mwisho.
“Sergio Puto aliomba akawe mdunguaji sababu ni mtu anayevutiwa na udunguaji lakini mpaka tunakumbwa na kadhia hii ya giza naamini atakuwa kadunguliwa yeye baada ya kuwa kadungua yeye..” Feca akaeleza tena akitikisa kichwa huku nywele zake zenye mvi lakini akiwa kafungua kimchicha alichokifunga na kuzifanya zimwagike pande zote mapka akiongea inambidi azitingishe aweze kuwaangalia wenzake.
“Ulinzi uimarishwe maradufu na sote tujigawanye wao wamekuja kwenye ngome yetu si kutembea na kufanya nasi maongezi huku tukinywa kahawa wamekuja hapa kutufanyia angamizo na hawatasita kutuangamiza labda tujisalimishe hivyo hawana budi kuja tulipo baada misako yao kufeli kutuona huko orofa za chini… Kwa kuanzia na hili giza lililopo hapa tutakaa kwa kujificha katika kona na kona mimi na mhehimiwa Feca tutakuwa mbele kuongoza ulinzi tukiangamiza kila anayetokeza pua yake, hamna kudangayika na nguo kuwa zinafanana na mmoja wa walinzi wetu kumbukeni hilo jamaa wana ghiliba zote” Maelezo ya Brigedia Mcdonald Grannell yalitoka akisikilizwa kwa umakini mkubwa sana.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!
FUNGA KAZI XVV
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
“..Feca nina wazo kabla hatujapiga hatua kufuata kile anachosema bwana Grannell hapa”
“Ongea tunakusikiliza!”
“Ahsante nafikiri tumpatie taarifa Kamanda Antonio Luna atupatie msaada kuwa tumevamiwa na majambazi wanataka kutuua.. Navyomjua Luna atawai kufika hapa haraka sana kama alivyotuahidi juzi kuwa atatusaidia katika kutulinda katika hili au unaonaje kiongozi?” Lililetwa wazo hili toka kwa Villa Nandez Guti akiwa kaushika mkono wa kiongozi wake Kingpin Feca, ambapo haraka akachukua simu toka katika meza ambayo ilikuwa meza ya kioo ambayo kikao chao licha ya kuwa wote walisimama walikuwa wameizunguka meza hii.
Alimtafuta Kamanda Antonio Luna kwenye simu na alipopiga haikuchelewa ilianza kuita upande wa pili huko.
“Halloo!” Upande wa pili ukaongea baada ya kupokea simu.
“Unaongea na Ferna hapa.. Watu ambao tulikuwa tukihitaji habari zao na kuwasaka hatimaye wako hapa, wametuvamia tunaomba msaada wa kipolisi katika hili” Hakuacha msikilizaji wake wa upande wa pili hajibu chochote ama kuongea lolote alikuwa. Alimpa ujumbe huu kwa kasi.
“Hapo ulipo ndiyo wamekuja?” Akauliza kimshangao Kamanda Luna.
“Aiseeeh! Niko tayari kwangu ngoja nitume taarifa kwa kiongozi wao askari walio doria usiku huu.. Dakika ishirini mbele watakuwa njiani kuja huko mjitahidi kuwazuia shezni zao mimi pia silali nakuja huko nitakutana nao” Akaongea Kamanda Antonio kisha akakata simu bila kusubiri mpiga simu kama ana lingine la kumwambia.
“Imekuwa poa sana ameonekana kushtushwa sana.. Nashukuru kwa wazo lako ndugu yangu Guti, kwakuwa wewe unaumwa naomba ukakae kule kwenye kona nyuma ya mabox.. Na wewe Alexis naomba muongozane na Guti pale kwenye kona msijitokeze hata iweje kwa usalama wenu maana jamaa nao ni mafundi na wako na mtu ambaye habari zake nyote mnazijua” Feca alimshukuru Guti kwa wazo alilopewa kisha akatoa maelekezo kwake na Alexis kuwa wasiwe eneo la kulinda wavamizi kufika katika ukumbi huu ulioko juu kabisa ya floor ya tano ambayo ni floor ya mwisho katika ghorofa hili lakini juu kukiwa na bati.
“Familia yako itakuwaje Brigedia?” Guti akamuuliza tena Feca wakiwa wanatizamana.
“Ndiyo nataka nichati na mke wangu awachukue watoto waingie katika boksi la dharura..” Akajibu Feca huku anakuna kichwa chake mawazo yakaanza kupandiana hapa baada ya kuwa amekumbushwa juu ya familia yake ambayo wakati wanakuja juuyeye na wenzke aliwaacha katika ‘floor’ (losheni) ya nne ambayo ndiyo hata yeye alikuwa anaishi aliwaacha chini ya uangalizi wa Sergio Puto ambaye sasa ni marehemu baada ya kujipa kazi ya udunguaji lakini akajikuta anadunguliwa yeye na mdunguaji aliye mjanja zaidi yake, tendo la yeye kudunguliwa halikuweza kuonekana kwa mke wa Feca Bi Millian kwakuwa alikuwa chumbani wakati linatokea jambo hili hivyo hakuwa anajua lolote alikuwa akijua bado Puto yupo yeye akawa anaendelea kuwaza na kuwazua jinsi gani watatoroka hapa akiwa na watoto zake wawili wadogo na si kwamba aliona kuna umuhimu wa kuondoka na mfanyakazi wake nah ii ilikuja kichwani mwake kwakuwa kulikuwa na boksi la linaloitwa boksi la dharura ambalo walishaambiwa wakiona mambo yanazidi kuwa shagalabagala basi wanaingia katika boksi hili la plastiki lenye ukubwa wa kama ndege ndogo kisha ya hapo kuna mahala watabonyeza ukutani litajifunga kisha Madam atabonyeza swichi fulani humo humo ndani basi litapanda juu dirisha la chumba litafunguka ndege hii isiyo ndege itatoka na kufuata nyaya ngumu ambazo zimetoka ndani ya jengo hili mpaka nje kabisa kisha baharini ndipo itadondokea kwenye maji hapo inajiseti yenyewe inakuwa kama nyambizi ndogo inazama majini hapo safari ya ndani kwa ndani ya maji ya bahari inaanza wanakuwa washatoroka.
“Nafikiri umejisahau kidogo kiongozi au umejichanganya na mambo haya.. Umeme hamna dirisha haliwezi kufunguka hivyo tumefeli hapa ndugu yangu.. Tuangalie tunazuiaje shemeji na watoto wasidhurike..!” Guti akatahadharisha.
“Hahaa! Shiiiit! Nilisahau kabisa sikujua kama jenereta watajua lilipo mpaka wamelilipua… Naapa kuwaangamiza awa wapumbavu nina hasira nao sana.. Naenda iokoa familia yangu, naenda ilinda familia yangu… Vitalis na Zakheem nifuateni tunashuka floor ya nne.” Alipayuka Feca hasira pomoni zimefura kama kiboko aliyetolewa kwenye maji kiuchokozi na mnyama asiyehusika maji husika.
“Mkuu ni hatari, hatujui wamefika wapi adui zetu kuzifuata ngazi ni hatari kwetu na kwako” Akajibu aliyetajwa jina kuwa anaitwa Vitalis huyu ni mmoja wa mabodigadi zake binafsi bwana Feca.
“Amri yangu uwa haipingwi au kuhojiwa hasa pale linapokuja suala la familia yangu… Wewe ni nani wa kunipa maoni yako” Alipomaliza kuongea hivi Bastola yake bwana mkubwa huyu aina ya Berreta 92FS zao la Italia ikiwa na oda maalumu aliyojiwekea Brigedia huyu wa zamani ikitengenezwa kwa kuweka kitako cha dhahabu kana kwamba akiua mtu basi mtu aliyeuliwa na bastola hii hafi kwa maumivu, ilitema risasi moja ikatua katikati ya paji la uso la Vitalis ambaye wakati wanaongea alikuwa hatua tatu toka alipo boss wake, mwili ukadondoka chini ukimwaga damu kutokea kwenye tundu la risasi.
Waliopo pale wote walishtuka sana hawakutegemea kama Feca atafanya alichofanya kwa mtu ambaye anamuamini sana yeye na Zakheem maana kila alipoenda Feca basi aliongozana na hawa watu wawili kwa miaka kadhaa sasa toka uzee uanze kugonga nanga katika mwili wa Feca.
“Tuko vitani mtu anakatisha tamaa wenzake hafai kabisa acha atangulie kuzimu kwanza mi sipendi kujibizana jibizana ovyo.. Twende Zakheem!” Feca akaongea tena akiwa kashatangulia mbele.
Wakati wakuu hawa wakipanga na kupangua juu ya iweje, Agent Kai alikuwa katika floor ya nne akinyata katika giza kufuata mwisho wa ngazi baada ya kuwa aliouona mwanga wa simu katika moja ya dirisha kubwa la kioo ambalo lilikuwa lina pazia, alifika mwisho wa ngazi akasimama na kunyooka kabisa kisha akachungulia dirishani ikiwa si rahisi kuona kwa ndani kutokana na pazia lakini mwanga wa simu uliendelea kuwa unaonyesha kama huko katika maonyesho na akiwa kasimama anatafafakari ukazimika kisha akasikia kitu kama mlango unafunguliwa.
Masikio yalijitega kunasa kinachofanyika ndani ya dirisha hapo mkanyago wa nyayo ulisikika mlango ukirudishwa, tafakuri kali ilikuwa ikizunguka katika halmashauri ya kichwa cha Agent Kai, maswali yasiyo na majibu yalikuwa yakitawala kichwani asipate jibu mwisho akaamua aingie kujionea mwenyewe nini ni nini?, Akazama kwenye mfuko wa suruali aliyovaa eneo la pembeni lililo chini ya goti, mkono ukaibuka na kifaa chake cha maujanja kinachoogopewa na vioo vya aina yoyote na si kama inavunja vioo hivyo la hasha! Haivunji lakini inavikata eneo atakalo na kuliondoa bila ukelele wowote kama tulivyoona alivyofanya kwenye kioo cha dirisha la floor ya pili, alichora duara sehemu aliyotaka duara la ukubwa wa sahani ya kujazwa msosi na mama nijazie alipomaliza mduara huo akageuza peni yake kama kawaida na kubonyeza katikati palipo kijitufe kidogo ikamwaga wino gundi akagandamiza katikati na kipande kilichokatwa duara kikavutika kwa nje kufuata peni hapo mkubwa akaitoa peni yake hii ambayo ukiiona huwezi tambua kama ina maajabu haya, mkono ukazama ndani akafungua ‘lock’ ya dirisha akasukuma upande halikusogea hapo akatambua kuna komeo ikamfanya azamishe tena mkono ndani akapapasa kona ya mwisho akaigusa ‘lock’ akaipandisha juu hapo alipolisukuma likakubali kusukumika bila kusubiri akakamata juu yake taaap yuko ndani haraka akarudisha kwa kuliegesha mtu mwingine akija iwe kwa nje au kwa ndani inamjuza dirisha liko sawa tu.
Mandhari ya eneo alilotokea baada ya kuingia ndani haikuwa tabu kuonekana kwenye macho yake kwakuwa miwani yake ilikuwa ikimsaidia kuona vizuri palikuwa ni maliwatoni, akasogea mpaka kwenye mlango ambao alifahamu ni mlango ambao hata ukitaka utumie ujuzi mkubwa sana ni mlango wa kusaliti pale unapofunguliwa basi mlio kwake ni kawaida na ndiyo maana mtu wa mwisho kuingia humu maliwatoni kabla yake alijaribu sana kuhakikisha mlango haupigi kelele lakini yeye aliweza kusikia, ulikuwa ni mlango wa fremu ya ‘alluminium’ katikati kukiwa na vioo vigumu ambavyo vilinakshiwa kwa tinted kwa aliye nje ya choo hiki ambapo ni upande wa pili wa alipo sasa Agent Kai hakuwa anaweza kuona aliye ndani ya choo lakini aliye kwa nje alikuwa akionekana na aliye ndani hasa akisogea usawa wa mbele, fundi mtaalamu wetu aliusogeza uso wake na kuchungulia kupitia usawa wa kioo kigumu akaweza kuona kwakuwa miwani iliweza msaidia kuona, macho yalishuhudia nje ya hiki choo ni chumba kikubwa cha kulala kwa maana kulikusanya vitu ambavyo mara nyingi vinakuwa chumbani.
Hakukuwa na vitu bali kulikuwa na watu pia, wote wakiwa macho na wote ni wazungu kwa jinsi rangi yao ilivyoonekana kwa Kai lakini pia walikuwa wawili ni watoto wadogo wa umri unakaribiana lakini si wa kuvuka miaka saba na wote walikuwa ni wa kike kwa nguo walizovaa ilimjuza hivyo fundi mtaalamu ‘The Sole Cat’ (TSC), mwanamke mtu mzima mwenye umri ambao ukikadiriwa na wataalamu wa kukadiria mwili basi watamuweka katika umri wa miaka 55 kwenda mbele lakini pesa iliweza kumfanya aonekane kama binti mdogo wa miaka 23 mpaka 25, mfanano wake ni kama wa mwanamuziki Jenifer Lopez (JLO) wa Marekani akiwa kavaa suruali ya jeans kama walivyovaa wanawe na wote wana viatu muonekano wa kirahisi tu kwa mtu yoyote akiwaona kugundua wako kisafari, wakati akiendelea kuangalia huku anatafakari cha kufanya alitokea mwanamke mwingine mule mule chumbani akiwa kashika nguo ya kike akaongea jambo na mwanamama mzee kijana mambo waliyoongea walihakikisha wanaongea wakiwa wamesogeleana kwa ukaribu hii ilimaanisha walikuwa na hofu ya maeongezi yao kusikika kwa wengine sasa sijui ni kwa watoto walio karibu nao au namna gani.
Akili ya kazi ilikuwa ikizunguka kufanya kazi kwa spidi ya kilometa moja kwa sekunde kumi, akamtizama vizuri yule mama, kisha akavutika kutoa simu yake toka mahala ilipo akageuzia mgongo mlango hili mwanga wa simu usije ukaleta onekano upande wa pili, akafungua upande wa gallery file akaanza kutafuta picha kadhaa mpaka akaipata aliyokuwa akiihitaji akageuza kichwa kwenye kioo cha mlangoni kumtizama mwanamama hapo akaweza kupata mfananano ulio sahihi baina ya picha na mtu halisi anayemuanagalia, alikuwa ni Madam Millian Fernandes Carlos Codrado.
Kabla hajaamua kuwa aendelee na kitu gani ikiwa kashairudisha simu mahala alipoitoa mlango wa kuingilia ndani ya chumba anachokichungulia kupitia mlango wa chooni ulifunguliwa na wakaingia watu wawili mmoja mzungu na mwingine mwenye asili ya Afrika, akitangulia mtu mzima mzungu mwenye nywele nyingi kichwani ambazo zina mvi na uso wake maeneo ya kuzunguka akiwa na ndevu mpaka mdomo wake ukiwa hauonekani vizuri, wote walikuwa na bastola mikononi mwao.
Agent Kai akaongeza umakini katika kutumbua macho yaliyo ndani ya miwani aweze kuupekenyua uso uliozingwa na mandevu, moyo ulipiga kinde! Alipogundua babu huyu wa kizungu ndiye ambaye picha zake zilisambazwa kwenye ubao wa maelekezo katika kikao kilichokuwa kimesimamiwa na mkurugenzi mkuu wa taasisi kuu ya usalama wa taifa wa Marekani (NSA), hapa aligundua zile picha ambazo wao walikuwa nazo ni picha ambazo ni za zamani au huyu mtu ameamua kujiweka hivi akaendelea kumuangalia akagundua mtu huyu aigizi ni kweli umri wake umesogea, huyu ndiye kiongozi mkuu wa genge hatarishi la ulanguzi wa dawa za kulevya ambalo lilitishia amani viunga vya Mexico na nchi za jirani na nchi hii mpaka Marekani yenyewe, genge la THE RED JAGUAR (TRJ).
Macho yalimshuhudia mtu ambaye alikuwa ana hamu ya kumuona mubashara si katika picha maana alikuwa adimu kweli kweli katika miaka ya hivi karibuni alikuwa si mtu wa kuonekana hadharani hata picha ambazo ‘NSA’ na ‘CIA’ walikuwa nazo zilikuwa ni picha ambazo wakati akiwa na miaka hamsini mpaka hamsini na tano alipokuwa jeshi la wananchi la Mexico na zingine alipokuwa amesogea sogea juu kiumri akiwa ameanza kusifika katika uhalifu wake wa kujihusisha na ulanguzi wa dawa za kilevya kutokea hapo akawa adimu kweli kweli akionekana zaidi mke wake na mtoto wake mkubwa ambaye anasoma chuo huku akisaidiana na mama yake kusimamia biashara zao mbalimbali, alikuwa ni komando na mwalimu wa wanajeshi Fernandes Carlos Codrado.
Kwa kukadiria Agent Kai akamkadiria Feca kuwa kwa sasa atakuwa na miaka sabini anajitahidi mazoezi katika ratiba sahihi na kula vyakula vilivyo katika mpangilio bora, aliona wakiingia wakakumbatiana Madam Millian na Feca na watoto wakamrukia kwa furaha, wakiwa wameachiana halafu wanaelekezana jambo ambalo yeye Agent Kai hakuwa anaweza kusikia kutokana na mlango kutengenezwa kwa stahili ambao sauti ya chochote toka upande wa chumba na upande wa maliwatoni ilikuwa hazisikiki, alitamani awasikie wanaongea juu ya nini lakini uvumilivu aliuhitaji sana kwa wakati huu.
Wakiwa wanaendelea kuelekezana kuna jambo inaonyesha lilisimamisha maongezi kati yao kwani mkono wa kulia wa Feca ulitoa simu mfuko wa suruali aliyovaa ikaonyesha inaita akapokea kwa haraka na kuanza kuongea nako haikuwezekana kujua nini anaongea na huyo aliyempigia simu alipomaliza akamuinua mtoto mmoja aliye mdogo zaidi akamuweka kwa kifuani mwake akaongea jambo tena kisha mke wake naye akamkamata mkono mtoto mwingine wakaanza hatua za kutoka nje walipofika mlangoni kuna maelekezo mengine akayatoa akimuelekeza aliyeonekana mlinzi wake binafsi, mlinzi huyu akawapita na kutangulia mbele ambapo akaufungua mlango kisha akatoa kichwa chake kuchungulia huku na huko alipojiridhisha akaonyesha ishara kwa mkono wake usio na silaha kuwa wanaweza kutoka.
Chumba kikaachwa cheupe! Hapo Agent Kai hakutaka kusubiri akatoka ndani ya chumba cha maliwato akili yake ikimtuma kuwa watu hawa wanataka jaribu kutoroka hivyo kwa hatua za haraka haraka akatembea mpaka mlangoni alipominya kitasa uligoma kuvutika kwa ndani ikimaanisha ulifungwa kwa nje.
“Shiit!” Akajisemea kisha akainama kuchungulia kwenye tundu la kuangalia mtu anayegonga mlango kwa nje akiwa amefika kwa ajili ya kuomba ruhusa kwa aliye ndani kuingia au kumuhitaji aliye ndani, hapa akaona korido inayokwenda kwenye ngazi zinazopanda juu na kushuka kuja kwenye floor hii ngazi ambazo yeye alizitumia kupanda kuja hadi floor kabla hajazunguka akaona mwanga wa simu uliomvutia kusogea mpaka kuingia kupitia njia zake tulizozishuhudia kana kwamba nasi tulikuwa naye eneo hili, hapa alitamani wangekuwa wanatumia mfumo wa mawasiliano wa ‘SCNG’ akajiambia ni kosa kubwa la kiufundi wamefanya walipoingia Bahia bila kimtambo chao icho ambacho kikawaida uwarahisishia mambo yao.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na ishirini na saba (127)
Kazi bado inaendelea kazi inaonekana bado haijapikwa ikapikika zaidi ya kuwa kuni za moto wa kuipika kazi ndiyo unakokwa.
Je Kamishina mkuu wa polisi kanda ya jimbo la Bahia Kamanda Antonio Luna aliyeamrisha kikosi chake cha kazi za dharura kufika kutoa msaada kwa kile kilichoitwa kudhibiti uvamizi wa kijambazi atafanikiwa kuwadhibiti walioitwa majambazi kina Agent Kai?
Na je Feca na mkewe pamoja na watoto wanataka kutoroka toka katika jengo hili kama ambavyo anahisi fundi mtaalamu mpelelezi na jasusi Agent Kai?
Majibu ya yote haya ni katika sehemu tatu zilizobaki za riwaya hii ya JINO KWA JINO!
Wakiwa wanaendelea kuelekezana kuna jambo inaonyesha lilisimamisha maongezi kati yao kwani mkono wa kulia wa Feca ulitoa simu mfuko wa suruali aliyovaa ikaonyesha inaita akapokea kwa haraka na kuanza kuongea nako haikuwezekana kujua nini anaongea na huyo aliyempigia simu alipomaliza akamuinua mtoto mmoja aliye mdogo zaidi akamuweka kwa kifuani mwake akaongea jambo tena kisha mke wake naye akamkamata mkono mtoto mwingine wakaanza hatua za kutoka nje walipofika mlangoni kuna maelekezo mengine akayatoa akimuelekeza aliyeonekana mlinzi wake binafsi, mlinzi huyu akawapita na kutangulia mbele ambapo akaufungua mlango kisha akatoa kichwa chake kuchungulia huku na huko alipojiridhisha akaonyesha ishara kwa mkono wake usio na silaha kuwa wanaweza kutoka.
Chumba kikaachwa cheupe! Hapo Agent Kai hakutaka kusubiri akatoka ndani ya chumba cha maliwato akili yake ikimtuma kuwa watu hawa wanataka jaribu kutoroka hivyo kwa hatua za haraka haraka akatembea mpaka mlangoni alipominya kitasa uligoma kuvutika kwa ndani ikimaanisha ulifungwa kwa nje.
“Shiit!” Akajisemea kisha akainama kuchungulia kwenye tundu la kuangalia mtu anayegonga mlango kwa nje akiwa amefika kwa ajili ya kuomba ruhusa kwa aliye ndani kuingia au kumuhitaji aliye ndani, hapa akaona korido inayokwenda kwenye ngazi zinazopanda juu na kushuka kuja kwenye floor hii ngazi ambazo yeye alizitumia kupanda kuja hadi floor kabla hajazunguka akaona mwanga wa simu uliomvutia kusogea mpaka kuingia kupitia njia zake tulizozishuhudia kana kwamba nasi tulikuwa naye eneo hili, hapa alitamani wangekuwa wanatumia mfumo wa mawasiliano wa ‘SCNG’ akajiambia ni kosa kubwa la kiufundi wamefanya walipoingia Bahia bila kimtambo chao icho ambacho kikawaida uwarahisishia mambo yao.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!
FUNGA KAZI XVVI
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
Njia hii haikuwa sawa tena kwake akarudi mbio mbio hadi chumba cha maliwatoni simama yake ikawa dirishani, dirisha ambalo ndilo lililomfanya akawemo humu ndani ya chumba hiki mpaka kumuona kwa sura ‘Kingpin’ Feca mtu ambaye ndiye kisa cha yeye na wenzake kuwepo katika mji wa Salvador jimbo la Bahia, alifunua pazia na ndipo akawaona wanapanda ngazi zinazoelekea juu floor ya mwisho ya jengo la ghorofa lenye urefu wa ‘floor’ tano.
Sekunde ishirini mbele zilimkuta Agent Kai akiwa ametoka kwenye chumba cha maliwato kupitia dirishani kama alivyoingia ikiwa mara hii ametoka kilaini kabisa si kama alivyoingia.
Wakati anaenda kwa kuinama kufuata uelekeo wa ngazi aliona kitu hivyo haraka akasimama huku anainama zaidi taratibu ikiwa yuko eneo la wazi hatua moja kufikia ngazi, ilikuwa pembeni ya ngazi kwa chini yake kuna kiumbe kimejishika kwa miguu aliyogandisha ukutani ukuta wa upande wa pili na mikono nayo imenyooka kukamata upande mwingine hivyo akawa ananing’inina kimaajabu kabisa kama joka kubwa linaloishi kwa kumeza wanyama linaloweza kuweka mkia wake mti mwingine na kichwa chake mti mwingine, nguo alizovaa zilimtambulisha Agent Kai kuwa mtu yule ni Agent Jade Poul Brown ambaye naye alikuwa amemuona Kai hivyo kwakuwa watu aliokuwa amewapsiha wapiti walikwisha pita alitokeza kwa juu na kumuonyesha ishara kwa kupunga mkono, ikabaidi Kai akimbie na kuzikwea ngazi mpaka alipo Jade.
“Ilikuwaje tena?” AkahojI Agent Kai.
“Nilisikia nyayo za watu wakati nikiwa katikati ya juu na chini ya ngazi hizi ikanibidi nifanye ulichonikuta nafanya nikatereza kama joka kama ujuavyo nina mwili mzuri wa kufanya haya mambo.. Hahahah hahahah!”
“Hukuweza kuwaona watu hawa kuwa kina nani?”
“Nisingeweza maana nilipozama na kukamata kuta na kuta ilikuwa ngumu kuinua kichwa kuchungulia bila kuonekana”
“Ila mimi ulioniona?”
“Ndiyo wakati nilipomaliza kuhesabu hatua za waliokutangulia nikataka nione ndipo nikakuona wewe wakati najirudisha kukwepa nikagundua ni Agent Kai Hamisi wa SAD haraka nikaweka ishara yetu usije nilipua maana hamkawii nyinyi kwa ushapu wenye uharaka katika maamuzi eneo la kazi za kazi… Vipi wewe ulifanikiwa kujua ni kina nani wale na wanatokea wapi?”
“Feca yumo pale na mkewe pia pamoja nao watoto naohisi ni wake na mwingine ni mtu ninayefikiria ni mlinzi binafsi wa Feca” Akajibu Agent Kai jibu lililofanya Agent Jade ageuke kumuangalia, muda huu walikuwa wamemaliza ngazi wapo kwenye kona inayowapelekea kwenye korido ndogo hapa kitaalamu na uzoefuna akili zao wasingesogea zaidi hivyo waligawana kila mmoja upande mwingine.
Walisimamisha maongezi baada ya kusikika mlio wa risasi wa bunduki aina ya Norinko QBZ-97, mlio ulikuwa mmoja tu kisha ukfuatia ukimya, Agent Jade akamtizama Agent Kai walipoangaliana akamuonyesha ishara kuwa mlio umetokea orofa za chini ya walipo wao.
Mara wakamuona mtu anakuja akipanda ngazi kwa kunyata akitembea sambamba na ukuta wote wakamtizama baada ya kuonyeshana kwa mikono.
“Reby.. Rebecca ndiyo anakuja.. Asije kutulipua tu..” Akaongea Agent Jade akiinama kwa kuuburuta mgongo wake sambamba na ukuta asionekane kirahisi na mtu anayekuja ambaye ni Specila Agent Rebecca.
“Acha nimjuze asije shambulia maana dunia tamu!... Pyiiiiiiiii pyiiiiiiii!!” Akaongea Agent Kai kwa sauti ya chini ambayo itaweza sikiwa na Jade peke yake aliye umbali wa hatua tatu tu toka alipo kisha akamalizia kwa kupiga mluzi ambao ni mluzi ambao yeye na S.A Rebecca uutumia kustuana.
Kimluzi kiliwasaliti na kuwajuza adui walio kona ya juu tu kuwa kuna mtu anafanya mawasiliano na mwezake kama si wenzake.
Vumbi la simenti iliyochimbwa na risasi na kupita sentimita moja tu katika bega la Agent Kai ilimfanya arudi kwa ndani zaidi katika kona aliyopo, risasi ilikuja kimya kimya bila silaha iliyotumika kurusha hii risasi kutoa mlio ikimaanisha ngoma iliyotumika imefungwa kiwambo cha kuzuia mlio wa mlipuko (sailensa).
“Tumeonekana wanatushambulia.. Haaa!” Agent Jade akaongea baada naye kukoswa koswa, wote wakakaa sawa na kona kiambaza kwa usalama wao hakukuwa hata na nafasi ya wao kutokeza bastola walizoshika.
Wakati wao wakiwa hapa pembeni ya kibambaza kwa kila mmoja na upande huku Rebecca alikuwa amekuja lakini vumbi za risasi zinazovyofyatua nchi za kona ya ukuta na cheche kutoka zilimfanya ainame chini na kuacha kusogea mbele alibaki ameshika bastola yake anasubiri kwa kuangalia juu tu, ikiwa hivi upande wa Agent Hansen na Detective Chilamwena walikuwa wakisukumana kwenda juu kwa kupeana mikono kutoka floor na floor iliwafikisha juu kabisa wakawa wamewaona kupitia nyuma walipo Feca na wenzake lakini hakuweza kuondoka zaidi pale walipo maana walitaka kuona usalama wao kwa umakini bomba la kupeleka moshi wa kuni za kuota juu angani likawa kinga yao.
“Nashuka kuingia katika ukumbi naomba nilinde”Detective Chilamwena akaomba baada ya kuona jamaa wanajipanga zaidi kwa mashambulizi wakiwa katika pande za ukuta.
“Sawa.. Inaelekea wamewaona Agent Kai na wenzake” Akakubali Agent Hansen, panda yao iliyowafikisha hapa juu ilikuwa na manufaa makubwa kwao kwa sababu walitokea mahala sahihi kwa wakati sahihi ingawa si eneo salama kwao.
Chilamwena akajilaza chini kabisa baada ya kujiingiza kwenye ukumbi baraza akatambaa mpaka karibu na kona kisha kama joka akajikunja asionekane na watu aliowaona hatua kama tano tu toka alipo, walikuwa wamejificha nyuma ya meza kubwa ya mbao macho yao yakiwa yanatupwa tupwa huku na huko, aliweza kumtambua mmoja kati yao kuwa ni Mr. Villa Nandez Guti lakini kina Guti hawakuwa na wazo wala hisia kuwa nyuma yao kuna mtu yaani ni watu ambao akili zao walizielekeza mbele kabisa ya ukumbi mpana na mrefu ulio juu kabisa ya jengo hili la ghorofa.
Bastola mkononi akijiamini anaangaliwa na kulindwa kwa umakini mkubwa aliamua kuwashughulikia hawa kwa kukumbuka neno la mkurugenzi wa usalama wa taifa la Marekani aliyewaambia kuwa wanamtaka Feca akiwa hai akahukumiwe kwa makosa yake nchini Marekani au akiwa maiti ikawekwe hadharani watu wakaishuhudia hivyo watu hawa kwake hakuona kama wana umuhimu wowote kwake, taratibu akatoa bastola yake iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti akakikaza vizuri akiw katika tahadhari kuu ya kuhakikisha hausikiki mlio wa aina yoyote ule wakati anakikaza chombo hiki kilicho kama bomba katika mdomo wa bastola.
Adui walikuwa hatua tano tu toka alipo walikuwa watatu ambao ni mdogo wake Feca afahamikaye kama Alexis Carlos Codrado, Mr. Villa Nandez Guti mtu muhimu katika genge la TRJ akiwa ni namba mbili katika safu ya uongozi pia alikuwemo mheshimiwa waziri wa usalama wa zamani wa nchi ya Guatemala mheshimiwa Rafael Ceni ukipita kwa hawa mabwana kwa mbele hatua kama saba ilikuwepo familia ya Kingpin Feca.
Chilamwena aligeuka kumuangalia ndugu yake Agent Hansen ambaye alikuwa kalala chini ya bomba linaloleta moshi wa kuni za kuota kutoka katika sebuke pekee yenye huduma, sebule ya boss mkubwa Feca, walipoangaliana kuna ishara wakapeana wakaelewana vizuri, kurudisha kichwa upande walipo watu adui zao macho yake yaliyo ndani ya miwani yakakutana na macho ya mheshimiwa Rafael Ceni ambaye alishtuka kwa kiwango kikubwa sana akainuka toka alipo.
“Mmoja huyu huku ja..!!” Hakumalizia kauli yake ya kutuma taarifa umbeya, risasi moja ilipasua juu ya sikio lakena kutokea upande wa pili kutokana na bastola iliyotumika kufaytua risasi hii iliyo katika mkono wa kulia wa Detective Chilamwena ilikuwa mita sita toka alipo mpigwa risasi hivyo ilimtawanya vizuri na kuuviringa ubongo ndani kwa ndani kisha ikatokea upande wa pili sauti kelele ilizimwa kwa mwanga wa radi, Israel mtoa roho akachukua chake kabla hajatua hata chini vizuri miguu ikanyooka tuli.
Kelele za Ceni na kushambuliwa kwa risasi kulifanya Guti kugeuka kwa kasi upande alioamini ndipo mshambulizi yupo alikuwa na bastola yake mkononi lakini kabla hajainua bastola hiyo kuelekeza tundu upande huo alijikuta naye anarushwa kutoka alipo kurudi kinyumenyume kwa shambulizi la risasi katika ya pembeni mwa shingo yake naye ukaribu wa mita chache toka bastola iliyomtungua kuwa karibu ilipasua upande mmoja kwenda upande wa pili mpigwaji risasi akipaa kiubavu mpaka karibu na ilipo familia ya Feca.
Alexis Carlos Codrado alishuhudia kwa haraka ya kimbunga wenzake aliokuwa nao hapa wakipewa tiketi ya akhera akainuka akinyoosha mikono juu anaomba kujisalimisha.
Kelele za watoto wa familia ya Feca zilisikika vizuri kwa mkuu wa familia aliyekuwa yuko kwenye kona moja akili yake yote ilikuwa kwenye kushambulia upande wa ngazi zinazokuja juu kwenye ukumbi wao, aligeuka kuona kunani baada ya makelele kufika kwenye kuta za masikio yake ndipo aliposhuhudia kwa macho yake katika giza lakini si giza la kumfanya yeye asione nini kinatua chini kwakuwa macho yake yalikuwa yamezoea giza, alitahamaki akitamani atokea pale alipo kwenda kuwatuliza wanae na kuwaondoa pale hakuwa amejua moja kwa moja wapi alipo mshambuliaji aliyewashambulia kina Guti hivyo akainama chini kwa kuchuchumaa.
“Boss jamaa wengine wako kwa nyuma ndiyo wamewashambulia kina Guti..” Mlinzi binafsi wa Feca akaongea kwa sauti iliyosikika vizuri kwa watu wote walio karibu na ukumbi huu.
“Nimeona ila sikujua wako kwa wapi.. Grannell kuwa makini ulipokaa umejianika.. Tupambane mpaka tone la mwisho la damu” Akajibu Feca pia akamtahadharisha Brigedia mstaafu Mcdonald Grannell.
“Tulieni papo hapo mke wangu.. Mchezo huu nyie hamuhusiki” Feca akaongezea tena.
Chilamwena akasimama kisha akamuweka ngao Alexis Codrado akimtanguliza mbele kisha akamsukuma asogee mbele.
“Sogea mbelee” Akapaza sauti kumuamrisha pia akitaka na wengine wote waliopo pale wasikie watambue kuwa kuna mwenzao mmoja kawekwa chini ya ulinzi.
Kwakuwa wote waliokuwa katika hali ya kuchukua jukumu la kulinda pua yoyote ya adui zao haigusi eneo walilopo walikuwa washaona nini kimetokea baada ya kelele za wanafamilia wa Feca, hivyo kuwekwa mateka ngao kwa Alexis iliwafanya washtushwe zaidi na kukumbwa ba taharuki vichwani mwao wakihisis kama muujiza ama ndoto kile wanachokiona ikiwemo hata wataalamu wakubwa wa michezo ya giza na hata mapigano ya kivita kama Mcdonald Grannell na Feca mwenyewe lakini butwaa iliwakumba kwa asilimia za juu kabisa kwakuwa walikuwa wakizuia kwa kupiga risasi kila inapoonekana dalili ya wanaowazuia kutaka kutokeza, swali kuu kwao lilikuwa jinsi gani aliyewashambulia Guti na Ceni kisha kumdhibiti kama ngao Alexis kafika nyuma yao? Njia ilikuwa ngumu sana kwa mtu wa kawaida kufika juu hapa na ndicho kidogo kilichokuwa kikiwawazisha kwa muda huu.
“Namtawanya ubongo huyu mtu pale mtakapokuwa mnaendelea na zoezi lenu huku mkiwa mmejificha naomba wote mtokeze haraka sana na wote mjisalimishe sababu hakuna njia ingine ya kuweza kutoka kwenu hapa tayari tumezunguka kote mko katikati..!” Akaongea tena Chilamwena huku Agent Hansen akiendelea kuwa pale pale kwenye bomba la kutolea moshi juu macho yake yaliyo ndani ya miwani yakiwa makini kuangalia maeneo ambayo walihisi ndipo wamejificha adui zao wasio waona kwa wakati huu, akiweka ulinzi kwa ndugu yake lisije mkuta lolote la tofauti.
Feca akiwa kazibwa na pipa la ‘simtank’ la lita 2000, macho yakiwa yamezoea giza anaona kikawaida sana alibaki ameinama kuendelea kuzibwa na upande wa alipo Detective Chilamwena lakini akili yake ilikuwa ikifanyia kazi vitu vitatu kwa pamoja ni vipi anafanya jambo kuhusu familia yake ni vipi anamuokoa mwanafamilia yake mwingine ambaye kiuhalisia wamechangia baba na tatu je anafanyaje kuhusu walio kwenye kona ya korido ndogo kuijia huku walipo wao.
“Nahesabu mpaka tano haraka jitokezeni haraka lasivyo nampeleka ahera mtu wenu… Moja. Mbil..!” Hakufika mbili katika kuimalizia itimie maana kamili jambo la ajabu ambalo hata yeye Chilamwena hakulitegemea lilitokea kwa ghafla na ajbu haswa, Alexis Codrado alipigwa risasi ya mguu wa kulia na mtu ambaye alitokeza kwa kudondoka chini kimserereko wa ubavu shukrani kwa ‘tiles’ zilizosakafiwa sakafuni na kufanya kuwa inatereza hata ukijiburuza ama kuburuzwa huwezi patwa na shida kwenye mwili wako, basi mtu huyu muhuni mlinzi binafsi wa Feca aitwaye Andrwez Cannon Ricky, mlinzi mwenye jitihada kubwa sana katika kumlinda Feca aliyeajiriwa na bwana mkubwa huyu miaka minne iliyopita akimtoa nchini Cuba, moja ya makomandoo waliofuzu vizuri sana katika jeshi la nchini Cuba, hakuwa amempiga risasi ya mguu Alexis kama kakosea la hasha! Alikuwa amefanya jambo kusudi akiwa na kusudio kubwa, shabaha ya ajabu sana bastola mkononi huku anatereza kiupande chini kwenye ‘tiles’, mpigwa risasi ya mguu na kumvunja alipiga yowe kubwa sana huku akidondoka licha ya Detective Chilamwena kujitahidi kumzuia asidondoke aendelee kumkinga ilishindikana ikabadi naye atumie akili ya ziada akadondoka naye hili aendelee kukingwa naye.
Nafasi ndogo ya kuonekana kwake wakati anazuia kudondoka kwa Alexis ilimgharimu Detective Chilamwena, risasi toka katika bastola ya Andrwez ilikita na kupasua kwenye kioo cha miwani ikapita hapo na kutua pembeni ya jicho lake la kushoto, akajikuta anamuachia Alexis na si Alexis tu akaachia bastola yake akarushwa hatua mbili nyuma, hali ikawa si hali kwa Detective Omar Mutua Chilamwena mutu ya asili ya Kongo ukawa mwisho wa uhai wake akitupa tupa miguu kisha akatulia tuli, simanzi kuu na pigo kuu kwa shirika la ujasusi la Marekani ‘CIA’ simanzi kwa taasisi kuu ya kijasusi ya Marekani ‘NSA’ na pia simanzi kwa kitengo cha ‘Special Activities Division’ (SAD) kumpoteza mpelelezi na jasusi nguli kama huyu (R.I.P Omar Mutua Chilamwena).
Tukio lilimstua kiasi kikubwa aliyepewa jukumu la kumlinda wakati Chilamwena anaondoka walipokuwa wamejificha Agent Hansen naye hakutegemea kama katika watu wale walio katika ukumbi kuna mtu hatari na fundi kama aliyefanya tukio hili kwa hasira naye akafyatua risasi tokea alipo akimtwanga risasi tatu mfululizo za mgongoni mbili na moja kichwani haraka naye akabadilika jina na kuitwa marehemu Alexis.
Kasi ya kimbunga ndicho unachoweza kuita kwa muuaji huyu fundi wa ki cuba ngozi nyeusi kama mimi mwandishi wa riwaya za Agent Kai, alipita kwa kasi ile ile ikamfkisha upande alipo Feca haraka akajiinua na kuchuchumaa sambamba na alipo boss wake.
“Nitakulinda boss mpaka tone la mwisho la uhai wangu hapa piga ua garagaza tunaondoka usihofu mkuu” Akaongea Andrwez akihema kwa nguvu pumzi kadhaa kujiweka sawa maana alitumia nguvu na akili wakati anajiburuza toka pande alipokuwa na Brigedia Grannell.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na ishirini na nane (128)
Namba za uhai wa watu waliopo ndani ya jengo la ghorofa lenye urefu wa floor tano ulikuwa unazidi kupungua.
Agent Kai, Agent Jade na Special Agent Rebecca wanajikuta wamezuiliwa kusonga mbele kwa kila anayetaka kuitokeza pua yake inatupiwa risasi.
Agent Hansen na Detective Chilamwena wanatumia ufundi walionao kufika juu walipo husika lakini bahati mbaya inawakuta wao kwa kumpoteza Detective Chilamwena mutu ya Kongo aliyejikuta anazaliwa kuwa ni mmarekani.
Fundi mlinzi binafsi wa Feca anafanya jambo linalodhihirisha yeye komando fundi anayeamua na kujiwekea mkakati kazi kisha anautekeleza, anafanya jambo ambalo anaamini ni moja ya njia ya kuzuia baya lolote lisimkumbe boss wake ‘Kingpin’ Feca.
Nini kitafuata?
Nafasi ndogo ya kuonekana kwake wakati anazuia kudondoka kwa Alexis ilimgharimu Detective Chilamwena, risasi toka katika bastola ya Andrwez ilikita na kupasua kwenye kioo cha miwani ikapita hapo na kutua pembeni ya jicho lake la kushoto, akajikuta anamuachia Alexis na si Alexis tu akaachia bastola yake akarushwa hatua mbili nyuma, hali ikawa si hali kwa Detective Omar Mutua Chilamwena mutu ya asili ya Kongo ukawa mwisho wa uhai wake akitupa tupa miguu kisha akatulia tuli, simanzi kuu na pigo kuu kwa shirika la ujasusi la Marekani ‘CIA’ simanzi kwa taasisi kuu ya kijasusi ya Marekani ‘NSA’ na pia simanzi kwa kitengo cha ‘Special Activities Division’ (SAD) kumpoteza mpelelezi na jasusi nguli kama huyu (R.I.P Omar Mutua Chilamwena).
Tukio lilimstua kiasi kikubwa aliyepewa jukumu la kumlinda wakati Chilamwena anaondoka walipokuwa wamejificha Agent Hansen naye hakutegemea kama katika watu wale walio katika ukumbi kuna mtu hatari na fundi kama aliyefanya tukio hili kwa hasira naye akafyatua risasi tokea alipo akimtwanga risasi tatu mfululizo za mgongoni mbili na moja kichwani haraka naye akabadilika jina na kuitwa marehemu Alexis.
Kasi ya kimbunga ndicho unachoweza kuita kwa muuaji huyu fundi wa ki cuba ngozi nyeusi kama mimi mwandishi wa riwaya za Agent Kai, alipita kwa kasi ile ile ikamfkisha upande alipo Feca haraka akajiinua na kuchuchumaa sambamba na alipo boss wake.
“Nitakulinda boss mpaka tone la mwisho la uhai wangu hapa piga ua garagaza tunaondoka usihofu mkuu” Akaongea Andrwez akihema kwa nguvu pumzi kadhaa kujiweka sawa maana alitumia nguvu na akili wakati anajiburuza toka pande alipokuwa na Brigedia Grannell.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!
FUNGA KAZI XVVI
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
“Jeshi la polisi la Brazili, kanda ya jimbo la Bahia limeizunguka nyumba namba BBRS/A4-22… Tukiwa tumepewa taarifa jengo hili limevamiwa na majambazi kwa dhumuni la kufanya uhalifu na uporaji.. Hivyo basi kwa usalama wa watu waliomo ndani ya jengo pamoja na mali zao tunaomba kila aliye ndani ya jengo hili kujisalimisha mara moja” Spika ya matangazo ya polisi ilisikika ikitoa sauti kutangaza amri ya kipolisi inayohitaji watu waliomo katika jengo la ghorofa tano tajwa namba husika kuwa wajisalimishe wenyewe mikononi mwa polisi, tangazo lilirudiwa mara mbili kisha ukavutwa utulivu kidogo na kurudiwa tena mara mbili.
“Tunatoa dakika kumi na tano kabla ya kikosi chetu cha operesheni za dharura hakijaingia kazini kufanya kile kinachotakiwa kufanywa na jeshi la polisi” Mtoa tangazo akasikika tena akieleza muendelezo wa kitisho.
Tangazo lilisikiwa vizuri na watu wote waliomo ndani ya jengo na kila upande ulipokea tangazo katika namna ambayo yenyewe inaona iko vile kimsaada au kiukandamizi, upande wa Feca na watu wake aliobakia nao uliona kwao tangazo hilo limekuja kama Nabii Mussa alivyowaendea wana Israel na kuwaahidi kuwatoa katika makucha ya firauni lakini upande wa timu Agent Kai ulilaani sana polisi kufika na pia kwa haraka waliona ni mbaya sana kwao wakiwa katika hatua ambayo ni kama kumla ng’ombe mzima.
Ukimya ulishika hatamu ndani ya jengo na hata nje ya jengo dakika zikasogea mpaka zikafika dakika kumi na tano ambazo zilifuatiliwa na watu wote kutoka makundi yote hasimu ambao kila mmoja kati yao alikuwa kajificha mahala pake na silaha yake mkononi, lakini haikusikika tangazo kuwa dakika zimeisha ukimya ukaendelea, huu ukimya haukuwa wa bure ni kwamba huko kulikotolewa onyo kitangazo alikuwa amewasili Kamanda mkuu wa jimbo la Bahia kamishina Antonio Luna akawa anafanya maongezi na waliomtangulia kufika alisikiliza na kusikilizaw kisha akachukua kipaza sauti na kusogea mbele akiwa anataka kutoa tangazo lakini kabla hajawasha kipaza sauti hili aanze simu yake ikaita akasimama na kuitoa mfukoni kuona nani anampigia, ilikuwa ni simu ambayo ilimstua sana na kuona ina umuhimu mkubwa aweke kipaza chini asogee pembeni zaidi akafanya hivyo.
“Halloo mheshimiwa waziri!” Akaongea pale alipoiruhusu ikae hewani.
“Huko wapi? Kamishina”
“Kuna tukio la ujambazi hapa Salvador eneo la Metropolitan karibu na beach ya jiji ya Lauro De Freitas hapa kuna jengo la ghorofa tano lina wafanyabiashara walikuwa na kikao chao cha kibiashara wamenipigia simu kuwa wamevamiwa na majambazi ndiyo tumefika hapa kudhibiti hao wavamizi mheshimiwa”
“Ooooh! Saa saba usiku hii Kamishina.. Mmeshafanikiwa?”
“Hapana hatujafanikiwa bado wavamiwa wako ndani na wavamizi nao wako ndani pia ya jengo husika, tushatoa onyo la kuwatahadharisha kuwa jeshi la polisi tayari limefika kuzuia aina yoyote uhalifu toka kwa wahalifu”
“…Vizuri! Je mnawajua hao wafanyabiashara waliokuwa na kikao hapo?”
“Hapana mimi nimepigiwa simu tu kuwa kuna tukio hili”
“Nani alikupigia?”
“Mmoja wa maafisa wangu ambaye naye alipigiwa na mmoja wa hao wafanyabiashara”
“Kamishina hapo Bahia kuna shida katika udhibiti wa wahalifu na ndiyo maana wahalifu wengi wanakimbilia kujificha hapo kila wanapofanya matukio ya uhalifu sehemu nyingine na safari hii mmeacha mtu anayetafutwa kwa kila hali na mataifa mengine ameweka kimbilio hapo Bahia na ni kama mmempa hifadhi na ndiyo huyo aliyewapigia kuwaomba msaada kuwa kavamiwa na majambazi wanataka kumdhuru na kumpora, Kamishina nimesikitishwa sana na msaada huo mnaotaka kuutoa pengine kwa kujua au kwa kutokujua mnatoa msaada wa aina gani kwa mtu wa aina gani? Sasa nataka nikwambie mtu huyo ni mfanyabiashara za ulanguzi wa dawa za kulevya mmexico muasisi wa genge hatari la TRJ lililokuwa na maskani yake Mexico na Guatemala huku sisi nchi nyingine wakiweka vimatawi vyao.. Hao mnaowaita majambazi ni wapelelezi majasusi wa kimarekani wako kazini kwa faida ya urafiki na ushirika baina ya nchi zetu nakuomba muweke ulinzi kudhibiti Fernandes Carlos Codrado maarufu kwa jina la Feca hatoroki kuwakimbia hao majasusi kama waziri wa ulinzi na usalama ninakuja Bahia kwa helkopta kusimamia hilo linatimia, waacheni wamarekani wafanye kazi yao hii ni amri hao si majambazi na si waporaji.. Kazi njema na kwaheri tutaonana muda si mrefu” Maelezo marefu yaliitimishwa kiamri namna hiyo na mpigaji simu Waziri wa Ulinzi na Usalama wa nchi ya Brazil akakata simu, kijasho kilijikuta kikiweka makazi katika makwapa ya Kamanda mkuu Kamishina Antonio Luna.
Uso ulimshuka morali na munkari yote ikamkata na pia mshtuko ulimkumba hakutegemea kupokea amri hii ila pia alishangazwa na yeye kutumika kumlinda mhalifu na mlanguzi mkubwa sana wa dawa za kulevya kwa kudanganywa na rafiki yake mkubwa aitwaye Christopher Josee Lima ambaye ni mmoja wa maafisa wa juu wa taasisi ya kijasusi ya Brazil, alimtumia bila yeye Luna kujua akitumia urafiki wao hivyo akajikuta naye anawatumia maaskari wenzake akitumia ukuu wake kwao papo hapo akageuka kwa askari wenzake ambao walikuwa wakisubiri amri yake wafanye jambo katika kuendeleza kilichowaleta hapa, akawasogelea akiwa kapooza uso umesawijika kabisa.
“Kuna mabadiliko ya kitaarifa za kiintelejensia hivyo msiendelee na kutaka kuingia ndani imarisheni ulinzi kuzunguka jengo lote asitoke mtu yoyote ndani bila kumuweka chini ya ulinzi bila kutumia silaha zenu kama hajafanya shambulizi kwenu” Akatoa maelekezo macho yakiwa kwenye madirisha ya floor ya juu yanayoonekana uzuri kutokea nje.
Tukirudi ndani! Agent Kai akiwa ubavu kwa ubavu na Special Agent Rebecca Smith upande wa kushoto pembezoni mwa ngazi mwisho wake kabla haijaanza korido inayoingia katika ukumbi ambao wasingeweza kujitokeza bila mmoja wao kama si wote kushambuliwa na risasi toka kwa watu ambao waliwai kuwaona wao na kuhakikisha wanadhibiti eneo lao, upande wa pili wa mwisho wa ngazi kulikuwa na mwanadada machachari wa kizungu Agent Jade Poul Brown akiwa naye hajatulia tu kama wenzake alikuwa akichungulia kwa chati chini kabisa ya pembe kama paka anayevizia panya anayekuja mbio upande wake.
“Meseji yangu kwa Lizy nahisi imeleta jibu la ukimya kutoka nje kwa askari waliofika” Akavunja ukimya Agent Kai simu yake ya mkononi ikiwa kwenye kiganja cha mkono wake wa kulia akisubiri kwa hamu kama kuna elekezo lolote kutoka kwa Lizy Roby fundi mtaalamu.
“Huko fasta sana… Kumbe ulikuwa ukituma taarifa, safi sana…” Akajibu Rebecca yeye macho yake yaliyo ndani ya miwani ambayo kila mmoja kati yao alikuwa amevaa, macho yalikuwa yakimuangalia Agent Jade anavyochungulia.
“Shiiiit!!” Akajikuta anaongea kisha uso ukabadilika kwa kukusanya mikunjo (hasira).
“Nini tena?” Kwa haraka akauliza Rebecca akimuangalia usoni boss wake.
“… Aiseee tumempoteza mtu mmoja katika jengo hili.. Ameuliwa, ameuliwa Chilamwena.. Eeeh Mungu wangu najilaumu sana”
“Kwanini unasema unajilaumu? Eeeeh! Ilikuwaje? Kakupa taarifa nani?”
“Nisingependekeza kuja naye huku asingekumbwa na kifo hakika..” Akaongea Agent Kai kwa uchungu akitamani ajitokeze naye atoe roho ya mmoja ya watu wanaowashambulia.
“Hujasema ilikuwaje?”
“Amepigwa risasi akiwa amemdhibiti mmoja wa adui zetu.. Apumzike kwa amani” Akajibu na kumuombea dua njema kwa imani ya dini yake bila aliye pembeni yake kumsikia, wakati akiendelea kuomba dua meseji mpya ikaingia kupitia mtandao wa whatsapp, akamaliza dua lake kwa imani yake ya dini ya kiislamu kisha akaifungua meseji iliyotumwa kila anavyoteremka kuisoma ndivyo alivyoonekana machoni mwa Rebecca uso wake ukikunjua ndita zake taratibu mpaka zikaisha alipomaliza kuisoma akainua macho na kugeuka kumuangalia swahiba wake mdogo wake dada yake mdogo Rebecca.
“Kama nilivyotarajia polisi wameshapewa amri watulize kipago kazi ifanyik.. Nataka nimnyooshe aliyemuua Chila, kwa kweli siwezi kuvumilia najitokeza hili nione nani yuko mahala gani huyo mtu bora liwalo na liwe” Akaongea Agent Kai akataka kusogea lakini mikono miwili ya Special Agent Rebecca ikamzuia kwa nguvu kwa kumkumbatia asisogee ingawa mwili wake wa kike ilikuwa kazi kuzuia mwili wa Agent Kai.
“Hapo kabla uliwai nifundisha kuwa nyie watumia lugha ya kiswahili mna msemo kuwa hasira za mkizi ni furaha ya mvuvi, boss usilete hasira za mkizi tumempoteza Chila na ninaamini kujiamini sana kulimponza naomba tulia tuangalie upepo na tutulize akili kweli kweli kumbuka wanaojihami uwa na nguvu na subira kuliko wanaowahitaji… Tafadhali tulia!” Alionngea kwa utulivu licha ya kuwa alikuwa akitumia nguvu kumzuia lakini hakupaza sauti wala kuongea kwa kasi hapo akili zikamtulia kijana mwenye asili ya Afrika ambaye kuuliwa kwa kijana mwenzie mwenye asili ya bara analotoka tena akiamini bila yeye kumuomba aongozane naye kuja naye huku kwenye ‘operesheni maliza kazi’ basi asingekutwa na umauti uliomkuta.
“Tumalize kazi Rebecca.. Simtaki hata huyo Feca mimi… Jino kwa jino wamemuua Chila na wao hawatakiwi kuishi napitisha hii hukumu ya jino kwa jino mdogo wangu” Akaongea Agent Kai kisha akaleta begi lake lililo mgongoni mbele akaliweka kwenye mapaja yake kisha akalifungua wakati huohuo Jade aliye upande wa pili na Rebecca aliye pembeni yake walikuwa wakimuangalia kwa umakini anafanyaje, mwamba akatoka na bomu la kutupwa (kiazi).
“Boss! Usirushe bomu lako tafadhali ebu relax mkuu.. Si mara ya kwanza sisi kupoteza mwenzetu eneo la pambano kumbuka hilo kuwa hatujui Hansen yuko eneo gani hapo kwenye ukumbi maana yeye ndiyo aliongozana na Chila mpaka huko kwa njia zao sasa ukirusha bomu la kurusha, huoni unaweza ongeza idadi ya mtu wetu wa pili?” Busara za Special Agent Rebecca Smith mwanadada wa kizungu zikaendelea hapo napo akili zikamkaa sawa boss wake.
“Kwani hutaki tumalize kazi?” Akahoji Agent Kai akimtizama Rebecca usoni.
“Napenda.. Napenda! Ila si kama unavyotaka wewe siwezi kukubali kumpoteza mtu mwingine kumbuka ulivyotutahadharisha mimi na Jade tukiwa nje huko… Ulisema Feca umri umeenda lakini ujuzi wake haujazeeka, sote tunafahmu ubora na ujanja wa Komandoo Chilamwena lakini kosa moja limemuondoa” Akaendelea kumtahadharisha mtu ambaye laiti angekuwa yuko peke yake hapa basi ingeweza kuwa hasara kwake ambayo ingewapa furaha ya ushindi adui zake au hasara kwa hao adui zake.
“Sawa niongoze Rebecca! Mi nimechanganyikiwa kwa sasa hasira zimekaa kwenye kona ya mzunguko wa ubongo wangu nikiwa hivi uwa nasikia harufu ya damu ya binadamu kwenye tundu za pua zangu na hapo uwa nashindwa kuzuia hisia zangu hili jambo unisaidia na pia unigharimu mara nyingine” Kama kijana mtoto Agent Kai akajiegemeza kwa mwili wa Special Agent Rebecca kana kwamba analalia bega la mkewe bi Shufania. Akili yake ilikuwa imefungwa na hasira kubwa mdomo wote aliuona mzito wakati anaongea.
Agent Jade alikuwa akiona na kusikia kwa mbali wanayoongea Agent Kai na S.A Rebecca na alikuwa akitambua mtu anayekuwa na hasira za kutaka alipe kisasi kwa haraka eneo la mapambano anavyokuwa, alifurahia kazi iliyofanywa na Rebecca kumtuliza Kai, mahala alipo aliweza kuona upande wa kina Kai na pia aliweza kuona eneo lile ambalo giza ndiyo lilitawala kwa ukubwa lakini kwa macho yake akisaidiwa na miwani aliweza kuona vinavyotikisika ikimaanisha kuna mijongeo ya minyato fulani ya kimawindo hivyo alichokuwa akikisubiri ni kosa lolote lifanywe na watu wale na yeye aruhusu risasi toka kwenye bastola yake aipendayo sana aina ya ‘Mark XIX 429 De Semi-Automatic Pistol’ kitako chake kikijaa kiganjani na kidole chake cha shahada kikiwa tayari kwenye kifyatulio (trigger).
Jade akiwa kama paka anayechungulia kwa wizi windo lake na kwa ‘Kingpin Feca’ pembeni yake akiwepo mlinzi wake binafsi muaminifu sana mwenye ufundi usiomithilika kwenye medani za mawindo na mashambulizi akiwa katoka kutoa roho ya komandoo mwenye ujuzi na uzoefu kutoka kikundi bora zaidi kati ya vikundi kadhaa vilivyoundwa na taasisi ya usalama wa taifa ya Marekani ‘NSA’ pamoja na shirika lake tanzu la kijasusi ‘CIA’, na wao wakiwa sambamba wamejificha nyuma ya mbao zilizokuwa kama ngazi za waliokuwa wakipaka rangi jengo hili kukiwa na gunia kwa mbele pia na kiroba kigumu cha ‘punching bag’, hawakuwa wameona alipo Jade akili zao zilielekezwa kona ambayo waliona mtu katokea kisha akarudi kwenye kona baada ya wao kushambulia kwa risasi eneo hilo.
Ni kama anahesabu hesabu za mtoto wa darasa la kwanza anayejifunza kuhesabu mojaa mbiliii taatuu nnee tanoo bega likaaanza kusogea likitokeza kwenye kona jitihada kubwa zikifanyika asionekane kwa nyuma ambako kuna adui na mbele ambako akili zake kotekote zilitaka umakini uliomakinika huyu alikuwa Brigedia mstaafu wa jeshi Mcdonald Grannell, kitu chenye ncha kali kilitua nyuma ya bega uchungu wake wakati kinapekecha kuingia kama bolt inayopenya kwenye nati kilimfanya atambue amepigwa risasi kutokea kwa nyuma tena kwa bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti, alitamani kupiga yowe lakini akajikaza akagumia kwa kujibinya asitoe sauti papo hapo akarudi chini kuchuchumaa kama ilivyokuwa akiwa kavunjwa mfupa wa bega unaoshika mkono.
Mgumio wake wa sauti inayojaribu kujizuia isitoke kwenda juu zaidi iliwajuza wenzake walio upande wa pili hatua chache kutambua mwenzao Grannell ameshajeruhiwa kwa kupigwa risasi, shambulizi lilikuwa limefanywa na mtu ambaye alikuwa nyuma ya meza karibu na walipo familia ya Feca akiwaona vizuri tu na wao wakimuona vizuri tu wakiwa wamejikunyata kwa kukumbatiana kana kwamba wanajikinga mvua au baridi ya barafu inayoporomoka, mtu huyu ni Agent Hansen.
Maajabu! Wakati Hansen anahesabu na Jade naye alikuwa akihesabu kana kwamba ameingia kwenye kichwa cha Hansen naye akawa anahesabu namba tano ya kisirisiri iliyotajwa humo humo kifuani mwake, Jade naye akawa amefikia namba ileile akashuhudia mtu akitokeza nusu mwili akitangulia bega na mara akaona damu ikiruka mtu yule akarudi chini kwa kasi akigumia kwa maumivu, macho ya Jade yakashuhudia kujirudisha kwake mtu yule akilisukuma gunia lililo na mzigo ndani yake mzigo usiojulikana ni mzigo wa aina gani? Kulisukuma kwake kulifanya aonekane kitu kinachoitwa ni kosa la mwenye shamba la mahindi kuacha kulilinda wakati shamba liko eneo ambalo kuna ngedere wengi juu ya kichwa alichokuwa kakiinamisha hili mkono wake usio na majeraha uweze kushika eneo alilojeruhiwa kosa lililomgharimu kwa risasi moja takatifu toka mkono wa Jade ilipenya zinapoishia nywele zake za singa zilizo nyeusi zilizoanza kupokea mvi, Israel alimfyekelea mbali papo hapo tena wenzake walishuhudia alivyokuwa amerushwa na kudondokea matako ukawa mwisho wa uhai wa Brigedia Mcdonald Grannell.
Sasa wakawa wamebaki watu wawili tu ambao ni Brigedia mfukuzwa katika jeshi la wananchi wa Mexico pamoja naye mlinzi wake binafsi kapteni mtoro wa jeshi la wananchi wa Cuba aliyefikia kiwango cha kuwa Kapteni muongozaji bwana Andrwez Cannon Ricky, waliangaliana kisha wakaongea kwa ishara wanajeshi hawa waliopitia mafunzo na baadaye wao pia kuwa walimu wa kijeshi wakiwafunza wanajeshi wa mataifa yao kabla hawajaingia katika kazi hizi za uroho wa pesa.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na ishirini na tisa (129)
Jeshi la polisi la kanda ya Bahia kitengo cha operesheni za dharura likiongozwa na Kamanda mkuu wa jimbo Kamishina Antonio Luna linafika na kulizunguka jengo la ghorofa tano lakini wakati wakijiandaa kufanya lililo katika kusudio lake anapokea simu toka kwa waziri wa ulinzi na usalama ikimuamrisha asiingilie wanaopambana ndani ya jengo husika bali aimarishe ulinzi asitoroke mtu.|
Agent Kai na wenzake nao wakiwa wamejenga mtindo wa yai bila kupanga ikiwa imetokea tu wanaendelea kusogeza matumaini baada ya Ageng Jade kumalizia vizuri kazi iliyoanzwa na Agent Hansen na kumuondosha duniani Brigedia mstaafu Mcdonald Grannell mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya uhamiaji nchini Guetemala.
Tuache porojo twende tusonge mbele katika sehemu ya mwisho ya riwaya yetu!
Maajabu! Wakati Hansen anahesabu na Jade naye alikuwa akihesabu kana kwamba ameingia kwenye kichwa cha Hansen naye akawa anahesabu namba tano ya kisirisiri iliyotajwa humo humo kifuani mwake, Jade naye akawa amefikia namba ileile akashuhudia mtu akitokeza nusu mwili akitangulia bega na mara akaona damu ikiruka mtu yule akarudi chini kwa kasi akigumia kwa maumivu, macho ya Jade yakashuhudia kujirudisha kwake mtu yule akilisukuma gunia lililo na mzigo ndani yake mzigo usiojulikana ni mzigo wa aina gani? Kulisukuma kwake kulifanya aonekane kitu kinachoitwa ni kosa la mwenye shamba la mahindi kuacha kulilinda wakati shamba liko eneo ambalo kuna ngedere wengi juu ya kichwa alichokuwa kakiinamisha hili mkono wake usio na majeraha uweze kushika eneo alilojeruhiwa kosa lililomgharimu kwa risasi moja takatifu toka mkono wa Jade ilipenya zinapoishia nywele zake za singa zilizo nyeusi zilizoanza kupokea mvi, Israel alimfyekelea mbali papo hapo tena wenzake walishuhudia alivyokuwa amerushwa na kudondokea matako ukawa mwisho wa uhai wa Brigedia Mcdonald Grannell.
Sasa wakawa wamebaki watu wawili tu ambao ni Brigedia mfukuzwa katika jeshi la wananchi wa Mexico pamoja naye mlinzi wake binafsi kapteni mtoro wa jeshi la wananchi wa Cuba aliyefikia kiwango cha kuwa Kapteni muongozaji bwana Andrwez Cannon Ricky, waliangaliana kisha wakaongea kwa ishara wanajeshi hawa waliopitia mafunzo na baadaye wao pia kuwa walimu wa kijeshi wakiwafunza wanajeshi wa mataifa yao kabla hawajaingia katika kazi hizi za uroho wa pesa.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!
FUNGA KAZI XVVI
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
“Kushoto kwangu kuna familia yako bwana Fernandes Carlos Codrado au mwenyewe kama unavyopenda wafuasi wako kukuita Brigedia Feca, nilipo hapa wananiona na wao wananiona pia nimeshawapa onyo la ishara kuwa yoyote kati yao bila kujali umri wake akiinuka tu ncha ya risasi toka kwenye bastola yangu itamnyofoa roho kama wengine niliowatoa roho muda mfupi uliopita… Mmebaki wawili tu na mara zote mwanajeshi mzuri ni yule anayekubali kujisalimisha pale anapoona hali inakwenda halijojo kwake kwa usalama wako na maisha ya familia yako kwa niaba ya wenzangu mimi Agent Hansen Nicholaus Blade nakuomba bwana Feca na kibaraka wako mjisalimishe mara moja kwakuwa njia yako imefika mwisho wa sakafu na hakuna njia ingine..!” Sauti ya kupazwa ya Agent Hansen toka mahala alipojificha nyuma ya meza kubwa ya bati ilipanga maneno kwa kasi kana kwamba anataka hadi walio chini ya jengo wamsikie lakini haikuwa hivyo alikuwa akitaka asikiwe na anayemuarisha ajisalimishe kwa usalama wake.
“Nahesabu mpaka tano kisha ya hapo nitaanza kuangusha mtoto wako mmoja mmoja halafu nitamalizia mkeo Madam Millian.. Feca unanisikia, unanisikia hapo ulipoo?” Agent Hansen akaongea tena kwa sauti ile ile ya kitisho ikiunguruma kwa uzito kama simba wa nyika aungurumaye ikimalizika kwa swali kwenda huko anapotaka.
Ajabu ilikuwa wakati sauti ya kitisho isiyo na masihara inatoka kinywani mwa Agent Hansen kutokea pale alipo, mahala walipokuwa Feca na mlinzi wake binafsi kulikuwa hakuna mtu tena, mahala pale palikuwa na funiko maalumu ambalo ilikuwa ndiyo sababu kubwa ya Feca kusimama na kujificha eneo hili ikiwa kama itatokea kuzidiwa basi aweze kufunua na kutereza ndani yake na ndicho kilichotokea kabla ya onyo la Agent Hansen la kwanza yeye na mlinzi wake Andrewz walikuwa washafunua kimya kimya wakaingia na kutokea kwenye ngazi za chuma zilopangwa kuteremka katika eneo dogo la kama dohani la moshi hii ni njia ya siri iliyotengenezwa na mkandarasi aliyetengeneza jengo hili la ghorofa tano, njia ambayo inafika mpaka chini kabisa kisha inatembea chini ya ardhi mpaka pembezoni mwa ufukwe wa bahari.
Agent Jade alishtuka kuna badiliko alipokuwa akilitizama eneo lile alikuwa akiona uzito fulani lakini sasa macho yake yaliyo ndani ya miwani yalihakikisha alichokuwa akiwazia kama ni fikra tu kwake akajitokeza kwa kuinuka pale alipoinama mwisho wa ngazi kwenye kona kutokea chini, kusimama kwake iliwastaajabisha kina Agent Kai wote wakawa wanamtizama kwa hofu kuu kuwa kwanini anajianika? Haogopi kuwa mhanga wa pili katika timu yao kuondokewa na uhai?.
“Vipi Jade?” Akauliza S.A Rebecca mikono yake ikiwa imefunguka kiishara licha ya kuwa mikono yake yote ilikuwa imekamata bastola.
“Hawapo walipokuwa.. Wametorokaaa..!” Aliongea Jade kisha akafunguka mbio akielekea pale walipokuwa wamejificha Feca na mlinzi wake.
Kundi zima likaunga tela kukimbia kona ya Agent Kai na Rebecca mbio kufuata nyuma na kule alipokuwa Agent Hansen hakusimama naye mbio akielekea pale akiwaacha familia ya Feca pale pale bila kujali itatokea nini kuwaacha.
“Eeeee hiiiii shiiiit! Kuna mfuniko hapa hii inamaanisha walikuwa eneo hili wakijua ikitokea wakazidiwa basi watatutoka kama walivyotutoka.” Akaongea wa kwanza kufika Agent Jade baada ya kusogeza ubao uliokuwa ukiwaziba Feca na Andrewz.
Hansen alikuwa wa pili wa kufika kwa kasi yake hakutaka kuremba wala kuchunguza akainama kufunua mfuniko lakini hakufanikiwa kuuvuta Agent Kai akamsukuma pembeni kuwa aache.
“Tutaisha hapa.. Tutaisha hapa Agent Hansen, achaa huo mfuniko.. kichaa mzee hawezi kutuacha salama.. Tuangalie kingine kuzia wasitutoroke si kufunua huu mfuniko..” Akaongea Agent Kai huku akiangalia walipo familia ya Feca.
“Tunafanyaje sasa?” Akauliza Agent Hansen swali kwenda kwa wote lakini alishakuwa anahisi nani atajibu.
“Ndiyo cha kujiuliza kwa sasa maana hakuna muuza unga wa madawa ya kulevya ambaye ameamaliza wakati wake wa kuishi duniani akiwa salama kiakili na ndivyo Feca sasa alivyo hana akili kama alizokuwa nazo enzi zake yuko jeshini na enzi akiwa mpya katika kuunda genge lao la chui wekundu..Ramani ya jengo hili hatuna lakini akili tunazo kwenye timu yetu hatuwezi shindwa.. Tutafuata linavyoenda eneo hili kwa floor ya pili kutakuwa na majibu huko twendeni haraka ila mmoja abaki na hawa wanafamilia yake watatu twendeni chini” Akajibu Kai kisha akaanza mwendo wa haraka kuondoka pale huku nyuma watu wa kazi wakaangaliana.
“Mimi nabaki nao hawa pia nataka niuweke vizuri mwili wa marehemu Chila..” Agent Hansen akaona abaki juu huku, upendo wake kwa aliyekuwa rafiki yake Detective Omar Mutua Chilamwena ilimfanya akubali yeye ndiyo abaki wenzake wakaendelee na kutafuta namna ya kuzuia Feca na mlinzi wake kuwatoroka iwe imekuwa kazi bure kwao kuja Bahia.
“Hapa.. Ramani ya kufikirika inaonyesha funiko lile njia yake inashuka hadi hapa hatuna namna ya kuweza kuvunja tukaona kunani ila kitaalamu hii njia itakuwa inashuka mpaka chini kwa jinsi navyotizama na uzoefu wangu nafikiri sote tulio hapa ni genius ambao tunaojuana na ndiyo maana tuko hapa.. Naomba nisikie kwenu pia mnafikiriaje?” Alimalizia kwa swali Agent Kai baada ya kueleza kile anachofikiria akiwa katikati ya watu wawili wanadada awapendao na kufurahia kazi anapofanya nao kazi Rebecca na Jade, alikuwa akishika shika ukuta na kuupapasa na mara nyingine anaweka kichwa chake kugandamiza kwa upande akilenga sikio lake la upande wa kulia lisikie na kabla hajasikia jibu la swali alilouliza akawaomba watulie kwa kuweka ishara ya kidole cha shahada katikati ya papi (lips) za mdomo wake.
“Yaah! Kuna ngazi! Jamaa wanateremka na inaonekana wako mbali ingawa hatuwaoni lakini hatua zinavyoshuka si hapa tuliposimama sisi ni hatua zinazoenda chini zaidi” Akafafanua wakati ametega sikio na wenzake wakawa wamefanya kama alivyofanya yeye kutega sikio zao katika ukuta kwa karibu karibu hivyo wakawa sambamba.
“Hii njia na umbali wa mitembeo ya kushuka ngazi nahisi wana handaki humu… Hili jengo limeanzia chini boss!” Akiwa kaondoa sikio lake na kainua kichwa akaleta wazo lake.
“Ndiyo lakini kwa akili yangu ya kazi hii ni njia ya kutoroka tusije tukajidanganya kuwa chini kuna handaki na hata kama litakuwepo hawatakaa hapo.. Changamoto yetu ni kujua wanaelekea wapi.. Twendeni orofa ya kwanza ambako mimi sikuingilia huko.. Nani aliingilia huko kati yenu?” Akaeleza na kuuliza swali akiwatizama wanadada lakini akiwa katika msimamo wa tuondokeni hapa hakuna kusubiri.
“…Mimi hapa..!” Akajibu S.A Rebecca akiwa kaweka mkia wote wakiondoka kwa mtembeo wa mwendo kasi wakishuka ngazi kutoka floor ya nne kuelekea floor ya tano.
“Kuna nini huko?”
“Sebule kubwa yenye fenicha za kisasa tu..!”
“Twendeni ongezeni mwendo lasivyo hii mtu tutaipoteza kumbukeni ana deni na mimi ana deni Marekani yeye hata kama aliyemuua Chila si yeye, sitakubali atukimbie tena kama alivyokimbia Mexico”
Mbio za kushuka ngazi ziliwafikisha ‘floor’ (losheni) ya kwanza, hawakuwa wanatembea kwa kizuizi chochote cha kuogopa walijiamini kama kazi ya kuondoa uadui wa kuwadhuru ilikuwa washauondoa wakawa kama wenyeji wa mjengo husika.
“Mkondo wa ngazi za siri unapita hapa.. Ebu Jade inua meza hiyo iliyo kushoto kwako kisha funua zulia kwa hapo” Akaelekeza Agent Kai kana kwamba ni mwenyeji wa nyumba hii mwenye kujua kila kitu kilichopangwa kwa juu ya zulia hadi vya kufichwa chini ya zulia, Jade hakuwa na hiyana akamuangalia kiongozi wake kisha akafanya kama alivyoelekezwa ilikuwa ni kwenye moja ya kona kati ya kona nne zilizo katika sebule hii kubwa ya kupendeza yenye maurembo urembo juu ya dari hadi chini kwa maua plastiki mbalimbali na hata maua ya asilia ya kupandwa ambayo yalikuwa katika maglasi makubwa maalumu kwa kazi ya kupandwa maua, hakika sebule ilikuwa ni moja ya sebule ya kuvutia kati ya sebule zinazovutia sana machoni mwa mtu pindi aingiapo hapo na raha zaidi uwe umekaribishwa na mwenyeji hivyo itakufanya upate huduma stahili kwa raha mustarehe kuliko sasa ambapo Kai na wenzake walikuwa hapa kikazi tena wakivujwa na majasho maana hakuna aliyekuwa na uhakika kama nini kitatokea, watampata mtu anayetafutwa na wao kwa udi na uvumba au itakuwaje? Hili lilikuwa ni swali linalozunguka kwa kila mmoja kati yao.
“Hakuna kitu?” Akauliza Agent Kai akiwa na shahuku hata kabla Jade hajamaliza vizri kulifunua zulia la manyoya manyoya ya sufi yaliyonakshiwa rangi nyekundu.
Agent Jade hakujibu akawatizama kisha akaonyesha ishara kwa mkono kuwa waje haraka kwa jinsi kiganja kilivyokuwa kinapungwa kwsa hali ya uharaka sana, mbio za watu wawili zikawafikisha kwa pamoja waje jionee icho wanachoitiwa kwa haraka.
“Naaam! Nilimaanisha iki na ndicho nilichohisi” Akaongea Agent Kaiakiangalia anachomaanisha ambacho kama ni mimi nisiyejua mambo mengi katika mambo ya siri yaliyojificha ficha basi nisingeweza tilia maanani kinachoonekana ningeangalia pengine ningezania ni ufa mwembamba tu ullio katika maungio ya sakafu na kuta yake inayoenda juu.
“Kisu kikubwa kinahitajika nani anacho?” Akauliza Agent Kai huku anajilaza chini kifudifudi akiweka sikio kwenye ufa mwembamba.
Akiwa bado kajilaza anasikiliza kisu kikawekwa mbele ya kiganja chake cha mkono wa kulia na mmoja wa wanadada.
“Hakusikiki tena zile hatua” Akaongea tena kaka mkuu kisha akakita kwa ncha ya kisu kwenye ufa kikazama akabinjua kwa nguvu zake zote za mkono wa kushoto, sakafu ile ikavunjika ndipo wote wakagundua ule ulikuwa ubao mfuniko, wakaangaliana kisha akabinjua tena zaidi akivuta kwa nje likatokea tundu kubwa hapo akaweka kisu pembeni akatumia mikono yake yote miwili kuvuta ukawa uwazi mkubwa akachungulia ingawa si chungulia ya kujiamini sana kimoyomoyo alikuwa ana hofu pengine anaweza jikuta amerejesha namba kwa ‘Sir God’ kwa risasi moja tu.
Wote wakashuhudia ngazi zikiendelea kushuka chini huku eneo lenyewe likiwa ni eneo dogo sana ni la kupita mtu mmoja bila kupishana na mtu mwingine.
“Mimi nitaendelea kufuatilia kwa nje ya ghorofa naomba nyie wote wawili muingie hapa kufuata ngazi zinavyokwenda.. Nawaamini sana naomba umakini wenu humo sababu panaweza kuwa ndipo palipo na hatima ya safari yetu ya Bahia.
“Sawa” Akajibu kukubaliana na maelekezo Agent Jade huku Rebecca akikubali kwa kichwa kisha akawa wa kwanza kutumbukiza miguu ndani ya shimo alipozama tu Jase akatizamana na Kai kisha wakagonga tano naye akazama ndani wakimuacha Kai ndani ya hii sebule.
“Lizy Roby! Lizy Roby! Unanisikia vizuri huko?” Agent Kai baada ya kuhakikisha warembo wake wametokomea tayari akatoa simu yake mfukoni kisha akapiga namba za ofisi yao ya Tehama huko Washington DC, Marekani. Alipata wazo hili wakati akiwa anachungulia dirishani kabla hajatoka nje akili yake ikiwa kama yupo kwenye msitu mnene usiku wa manane akiwa haoni njia ya kutokea, moyoni alikuwa na hasira zaidi ya kawaida hii ni mara chache uwa inamfika awapo eneo la kazi, alikuwa na wasiwasi wanampoteza Feca na huyo mtu wake ambaye yeye kwa mujibu wa taarifa aliyopewa Agent Kai na Agent Hansen ndiye aliyempiga risasi Detective Chilamwena na kumuondoa uhai wake.
“Kai nakusikia vizuri.. Sijatoka ofisini kwa ajili ya usiku wenu bado nipo maana usiku wenu huko Bahia ni usiku wote sote napewa taarifa na sekretari wa mkurugenzi mkuu wa taasisi kuu ya usalama wa taifa kuwa mkurugenzi pia anafuatilia kwa ukaribu usiku wenu kutokea katika chumba cha mawasiliano.. Nipe taarifa niitume kwao maana kila robo saa wanauliza maendeleo yenu” Lizy Roby akaongea kama cherehani baada ya kuulizwa na Kai kama anamsikia vizuri.
“Nitatoa taarifa ila hali si hali kwetu tumekula ng’ombe mzima lakini mkia unagoma unataka kutuponyoka Lizy.. Naomba msaada wako tumia mitambo yako kuokoa jahazi hili, fuatilia kwa umakini cctv camera zote za mahoteli yote yaliyo jirani na hapa angalia fukwe za bahari zote zinazozunguka eneo hili hasa fukwe ya nyuma na hapa, naweka simu mlio chochote utakachokiona ambacho ni tofauti utanijuza kwa haraka...!”
“Huko wapi? Kai”
“Muda si mrefu nafungua dirisha kutoka ndani ya jengo na akili yangu inanituma niruke ukuta kwenda nje upande wa ufukweni hivyo pia nitaomba umpigie balozi awaambie hao askari kuwa wakiona mtu anaruka ukuta wasimchalange risasi ni mimi”
“Sawa.. Dakika tatu zitatosha kutimia hayo punguza munkari nitafanya hivyo nawe utahesabu dakika na uzuri ni kuwa balozi naye anaufuatilia huu usiku wenu, usiku wa kumapata mshenzi huyo.. Come on! Ebuu tulia nikuulize usikate simu Kai…Ulifanikiwa kumuona Feca ukiwa humo ndani?” Akiwa anaeleza kuna jambo aliliona akaona amshirikishe Kai kwa haraka akaongea hivi.
“Ndiyo nilimuona, nilimuona amevaa koti jeusi na pia ana fulana ndani ambayo kiuzoefu ni fulana ya bullet proof, vipi Lizy?”
“Koti lina kola ya manyoya kola iliyopanda mpaka pembezoni na masikio, anavaa hereni masikio yote mawili?”
“Kitu kama icho… Yuko wapi?”
“Kuna mtu anatembea kwa mwendo wa kilaghai yuko kama tunayemuongelea na vizuri ulivyomuona.. Yuko na kijana mwingine shababi mweusi kama wewe, wanavuka kuingia eneo ambalo kunaboti inaonekana inawasubiri utatakiwa ufanye kitu Agent Kai… Haraka ufike ufukweni kama si mfike ufukweni kuzuia asitoroke..”
“Sawa..Niliwapanga Jade na Reby wapite njia aliyopita sijui imekuwaje kwao walipopita huko, fanya nao mawasiliano mimi sina muda tena.. Siwezi acha wauaji wa Chila watutoroke.. Wape taarifa ubalozini kama sitamuwai warushe helkopta kufuatilia..!”
“Kuna polisi wamemuona na wakapewa amri na mmoja wao mwenye cheo kuwa waache apite tu hivyo si wa kuwaamini hata kidogo, hofu yangu watakuzuia usifanye kazi hivyo kuna mtihani mkubwa mbele yako kama si mbele yenu.. Kazi njema kwenu”Lizy alimaliza hakusubiri Kai ataongea nini akakata simu.
Kukata simu kwa Lizy kulimkuta Agent Kai akiwa anaangalia nguzo inayopandisha juu kushika paa ya gereji ya kuhifadhia magari, muangalio wake uliitimishwa na kuikwea kwenda juu mpaka kwenye paa akakamata juu na kujipindua mpaka juu ya paa kisha ya hapo akatambaa mpaka mwisho wa paa kwa juu ambako sasa akawa anauona ukuta unaozunguka jengo hili akatambaa vile vile akawa usawa na ukuta akatizama kwa nje upande wa pili inakopatikana fukwe ya bahari ambako dakika moja iliyopita alikuwa akipokea taarifa juu ya Feca kuonakena huko akikaribia boti iliyo tayari kwa matumizi ya kumpakia yeye na aliye naye.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na thelathini (130)
Feca tena katika jaribio la kuwakimbia wamarekani!
Nini tena kitatokea kwao Feca na mtu wake pamoja naye Kai?
Je Agent Jade Poul Brown na Special Agent Rebecca Smith wamekwama wapi?
Majibu ya yote haya kwa sasa ni kitendawili tu twende katika sehemu ya mwisho ya mia moja na thelathini na moja kukamilisha safari yetu ndefu ya jino kwa jino.
“Ndiyo nilimuona, nilimuona amevaa koti jeusi na pia ana fulana ndani ambayo kiuzoefu ni fulana ya bullet proof, vipi Lizy?”
“Koti lina kola ya manyoya kola iliyopanda mpaka pembezoni na masikio, anavaa hereni masikio yote mawili?”
“Kitu kama icho… Yuko wapi?”
“Kuna mtu anatembea kwa mwendo wa kilaghai yuko kama tunayemuongelea na vizuri ulivyomuona.. Yuko na kijana mwingine shababi mweusi kama wewe, wanavuka kuingia eneo ambalo kunaboti inaonekana inawasubiri utatakiwa ufanye kitu Agent Kai… Haraka ufike ufukweni kama si mfike ufukweni kuzuia asitoroke..”
“Sawa..Niliwapanga Jade na Reby wapite njia aliyopita sijui imekuwaje kwao walipopita huko, fanya nao mawasiliano mimi sina muda tena.. Siwezi acha wauaji wa Chila watutoroke.. Wape taarifa ubalozini kama sitamuwai warushe helkopta kufuatilia..!”
“Kuna polisi wamemuona na wakapewa amri na mmoja wao mwenye cheo kuwa waache apite tu hivyo si wa kuwaamini hata kidogo, hofu yangu watakuzuia usifanye kazi hivyo kuna mtihani mkubwa mbele yako kama si mbele yenu.. Kazi njema kwenu”Lizy alimaliza hakusubiri Kai ataongea nini akakata simu.
Kukata simu kwa Lizy kulimkuta Agent Kai akiwa anaangalia nguzo inayopandisha juu kushika paa ya gereji ya kuhifadhia magari, muangalio wake uliitimishwa na kuikwea kwenda juu mpaka kwenye paa akakamata juu na kujipindua mpaka juu ya paa kisha ya hapo akatambaa mpaka mwisho wa paa kwa juu ambako sasa akawa anauona ukuta unaozunguka jengo hili akatambaa vile vile akawa usawa na ukuta akatizama kwa nje upande wa pili inakopatikana fukwe ya bahari ambako dakika moja iliyopita alikuwa akipokea taarifa juu ya Feca kuonakena huko akikaribia boti iliyo tayari kwa matumizi ya kumpakia yeye na aliye naye.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!
FUNGA KAZI XVVI
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
Kutokea juu ya ukuta Agent Kai aliona ufukweni kwa msaada wa miwani aliyovaa lakini miti miti ilimfanya asione vizuri zaidi, ufukwe usiku huu ulikuwa unaonekana umetulia na mawimbi makubwa makubwa yalikuwa yakionekana dhahiri shahiri machoni mwake, alicheza na miwani kwa kubonyeza vibatani viwili vitatu vilivyo pembeni ya miwani hivyo akawa anaivuta kwa ukaribu zaidi bahari kuangalia kama ataona kile kilichosemwa na fundi mipango wake Lizy Roby, kushoto zaidi baada ya kujivuta zaidi juu ya ukuta ndipo akaona boti imesogezwa kwa karibu na fukwe katika eneo la kipando cha boti ambacho si rahisi kujua kinamilikiwa na nani zaidi ya kujipa utambuzi kitakuwa kipando cha manispaa ya jiji au wanaomiliki ufukwe huu wa nyuma ya nyumba hii ya ghorofa ambayo yeye sasa yuko juu ya ukuta aking’aza macho kuona kulikoni.
Kando ya ufukwe kulikuwa na maaskari polisi kama watatu wakiwa wanaranda randa huku ba huko kana kwamba hawaioni boti, Agent Kai alitamani apaze sauti kuwaomba msaada wamsaidie kuizia boti isiondoke lakini taarifa ya Lizy Roby kuwa mmoja wa kiongozi wao aliwaambia wawaache watu hawa ilimshangaza sana na kumpa hofu kubwa sana hivyo akaamua ateremke chini kisha akaone anaweza vipi kuzuia mtoroko huu wa Feca na mlinzi wake, alipo kwa pembeni mita tano mpaka sita kulikuwa na mti hivyo akatambaa juu ya ukuta hadi usawa na mti kisha akachuchumaa juu ya ukuta giza lililokuwa totoro pamoja na nguo nyeusi alizovaa juu mpaka chini ikiwemo hadi buti alizovaa miguuni vilimsaidia kutoonekana na alijiamini kwa hilo, sekunde kumi tu za toka alipochuchumaa pale juu zilimtosha akajirusha na kudaka tawi kubwa la mti ule alipolidaka akatulia sekunde mbili kuweka sawa mtikisiko wa mti usije vutia askari wa polisi waliokuwa umbali wa kukadirika mita thelathini tu kando kando ya ufukwe wa bahari, kulipokuwa kumeacha kutikisika akajiterezesha kurudi kwenye kipago cha mti hapo alipokufikia akakita miguu na kujirusha stahili ya sarakasi mpaka chini kwenye majani mengi ya miti mbalimbali yaliyoanguka anguka chini na kufanya kuwa kama yenyewe ndiyo ardhi ya udongo wa kawaida, akabingirika juu ya majani yale yaliyojichanganya na matawi madogo madogo ya miti yaliyokatika toka mitini.
Kwa hatua ndefu zenye mnyato wa haraka alitembea akifuata miti iliyojipanga mpaka eneo ambalo mwanzo nililielezea kuna makaburi yanayoonekana ni makaburi ya miaka mingi sana akapapita sasa akajiegemeza kwenye moja ya mti ambao alikuwa karibu na eneo ambalo askari polisi hawa walikuwa wakipishana baada ya muda fulani tena walikuwa wakikutana wote watatu baada ya mmoja kwenda kushoto hatua nyingi lakini za usawa wa eneo la nyuma la jengo waliloambiwa waliekee ulinzi na mwingine naye kwenda kulia hatua ambazo ilikuwa ni usawa wa eneo la nyuma ya mjengo na watatu alikuwa akija akipita kwa eneo makaburi anazunguka zunguka kisha wanarudi wanakutana mahala ambapo Agent Kai alishawachora wakati yupo juu ya ukuta na kuona wanachofanya ambako utumia dakika mbili mpaka tatu wakiongea ongea wanachojua wao huku wakiiangalia boti ambayo ndiyo iliyosemwa na Lizy Roby kuwa Feca amesogea kwenye boti hiyo kama vile wameambiwa walinde usalama wa boti na waliomo ndani ya boti.
Ilikuwa kama ajabu kwa Kai kuona boti haiondolewi kama vile waliokuwa ndani ya boti hawataki kutoroka mara moja ikiwa tayari wamo ndani ya boti (kitendawili) hivyo yeye Kai aliweka hesabu zake sawa kuwa awamalize askari polisi maana wazembe wa makusudi kisha aangalie anawezaje kufanya juu ya ile boti ambapo hata nanga haikuwa imeondolewa kulikuwa kimya kana kwamba hamna watu ndani ya boti husika.
Hesabu zilienda alivyotaka askari wale walisogea karibu yake wakakutana ikiwa ni hatua tano toka mti ambao Agent Kai amejificha kwa nyuma anawachungulia kwa chati, bastola moja kwa kila mkono wake hivyo alikuwa kakamata bastola mbili, tundu za pua zake mbili zikapokea ile hisia yake ambayo ni kama kilema sasa kwake, harufu ya damu ambayo inapomjia harufu hii macho yake ubadilika na kuwa mekundu yakiwa ndani ya miwani aliyovaa ndivyo yalivyofanya muda huu, akataka kujitokeza awashambulie lakini akasikia jambo kutoka kwa mmoja wa watu hawa pale walipokutana wote na kuwa karibu karibu kabisa.
“Mkuu anasema tuvumilie dakika kumi na tano mbele.. Wanamdanganya Kamanda Antonio Luna kuwa mama wa watoto amejeruhiwa kwa kitu kizito kichwani hivyo haina budi kupelekwa hosptali ndipo watawaleta huku, hapo kazi yetu itakuwa imeisha” Akaongea mtu huyo akisikika vizuri na Agent Kai kwa lugha yao ya kireno.
“Upuuzi Afande Lito hivi tunajua kwanini tumeahidiwa pesa nyingi kuruhusu watu hawa watoroke? Halafu kwanini wanataka lazima na mkewe awepo? Si wangeondoka tu” Mwingine akaongea.
“.. Khaah! Achana nao si tujali kuwa hatujawaona wakiingia kwenye boti na pia hilo la kuileta hiyo family yake ni kazi ya Koplo Cruz si yetu, muhimu pesa isome kwenye akaunti kwa kazi nyepesi tu ya kukubali watoroke tusiowajua ni kina nani?” Akaongea tena wa kwanza kuongea akisikika vizuri kwa Agent Kai.
“Mmmh! Muda unaenda mwisho Luna atashtukia dili itakuwa noma sana.. Mi zikifika dakika kumi na tano naenda kwenye boti kuwaambia jamaa waondoke sitaki ujinga wao watakutana tu na mke wake” Akarudia kuongea wawili wakiwa kama wao ndiyo waongeaji wakuu kati yao watu watatu mwenzao mmoja akiwa hajasikika akiongea alikuwa akivuta sigara tu huku kakamata bunduki mkono mmoja.
“Loko huongei kitu mbona?” Akauliza wa kwanza akionekana kumuangalia anayeshambulia sigara.
“Watajijua wenyewe mi nachotaka pesa tu… Luna alibadilika baada ya kupigiwa simu na mtu asiyejulikana ni nani? Lakini tulikuwa tumekuja hapa kuzuia hao wavamizi wasiwadhuru hawa wakubwa tunaambiwa ni taita mwenye pesa zake, inasemekana kadhulumiana na mataita wenzake hivyo wamemtumia kikosi kazi cha kukodishwa toka Marekani kumchukua hadi kwa hao aliowadhulumu, tusubiri mwenyewe aliyetupa dili atatujulisha kama wameshindwa mshawishi Kamanda Kamishina Luna basi ataruhusu waondoke lakini sisi haituhusu kabisa bwana afandeMack, pesa nzuri kwa kuruhusu wawatoroke hao wauaji waliotumwa kwetu ni subira tu tupa woga kule ndugu yangu..!” Akaongea mvuta sigara kwa fujo aliyeitwa jina kuwa Loko au waweza muita Afande Loko.
Agent Kai sasa hapa akawa kaelewa nini hasa kinachosababisha boti isiondoke pale ilipo ikiwa tayari ndani yake kuna Feca na mtu wake, akajiuliza nini kimemkuta Agent Hansen huko alipo mpaka mke wa Feca na watoto pamoja na yule dada mwingine anayeonekana ni msaidia kazi wa Madam Millian watoke mikononi mwake? Jibu la haraka alikataa wazo la kuwa kazulika bali aliwaza inaelekea tayari maaskari wameingia ndani na huyo Koplo Cruz kampa somo laghai limemkolea kaiachia familia ya Feca pia akawaza na mengine lakini akaona hana uwezo na hayo mengine ya nyuma huko ambayo kama yametokea hana uwezo ya kurudi na kuzuia labda angeweza kuchukua simu yake na kuitumia kupiga kwa Hansen au kumtumia meseji lakini asingeweza tumia simu kwa mahala alipo sababu kuitoa simu na kuruhusu kioo kitoe mwanga tu basi angeweza kuwajulisha askari polisi hawa kuwa kuna mtu karibu yao, akajitokeza toka nyuma ya mti akaachia risasi toka katika bastola zake alizozifunga viwambo vya kuzuia sauti, bastola moja iliyo mkono wake wa dhahabu wa kushoto wenye sahabaha na nguvu ilitema risasi mbili kila moja ikienda kwenye vichwa vya maaskari polisi wawili huku risasi moja toka katika bastola ya mkono wa kulia ikichimba kidevu cha askari polisi aliyebakia ikizama na kutokea nyuma ya shingo, wote walidondokeana pale pale walipo kwa vishindo vidogo visivyotoa sauti iliyoenda mbali.
Kwakuwa walikuwa eneo la kuonekana na yoyote ambaye angetokea ikiwemo hata aliye ndani ya boti ambaye angechungulia nje basi angewaona hivyo Agent Kai akawasogelea akarudisha bastola zake sehemu ambazo anahifadhi bastola zake, akakamata kwenye nguo zao vifuani akaburuta wawili hadi nyuma ya mti aliokuwa kajificha akamrudia aliyebaki naye akamleta pale walipo wenzake akainua majani akawafunika funika kidogo huku akiongea kwa sauti ndogo anayoisikia mwenyewe tu.
“Poleni sana, mtanisamehe nimewakatizia uhai wenu kwa sababu ya kosa lenu msilolijua kama kosa kutamani pesa haramu ya mwanaharamu Feca, hamkuwa watu wabaya sana tamaa zenu tu zimewaponza kushirikishwa katika hujuma ya kumtorosha mtu ambaye sisi kwetu muhimu sana.. Mungu aweke roho zenu mahala salama” Akamaliza kuwafunika akageuka kuangalia ilipo boti mwili ukamsisimka.
Akatizama saa yake ya mkononi hapa akatamani tena alichokuwa kakitamani mara kadhaa wakati wakiwa ndani ya jiji la Salvador kama wangekuja na kamtambo chao kidogo cha mawasiliano ambacho mara nyingi aendapo sehemu ukumbuka yeye au kukumbushwa na mtaalamu na fundi wake mwanadada Lizy Roby kimtambo kinachowafanya wawe wanawasiliana kwa urahisi zaidi na hata kufanikisha mambo yao kwa urahisi katika mawasiliano ‘Small Call Network Group’ (SCNG), alitamani angeweza kujua wenzake wako wapi? Wanafanya nini? Kimewakuta kitu gani hawaoni?.
Wakati anawaza alikuwa kashaingia ndani ya maji ya bahari akiwa na nguo zake na mabuti yake pamoja na begi dogo alilovaa mgongoni, mawimbi hayakumsumbua na wala hakujali tena kama kwenye begi kuna vitu visivyofaa kulowa maji akazama ndani ya maji akiogelea kufuata ilipo boti ambayo ndani yake yupo Feca na mlinzi wake ajulikanaye kwa jina la Andrwez komandoo wa miaka minne iliyopita wa jeshi la wananchi wa Cuba, aliyeacha kazi za kulitumikia jeshi la wananchi hili afanye kazi binafsi za u ‘bodyguard’ ndipo akaangukia kwenye mikono ya Feca ambaye alisikia sifa zake akaona anastahili kulindwa na mtu bora na fundi kama huyu.
Fundi toka Marekani mwenye asili ya Afrika mzaliwa wa nchi ya Tanzania kabila la kiyao ukoo wa Mkarambati alifika ilipo boti pembezoni akaibuka na kuwa anaonekana kichwa tu hakuishika wala kuisukuma kwakuwa alitambua badiliko lolote ambalo angelifanya kwa kuigusa boti basi ingetikisika na kujisuka suka isivyo kawaida hivyo akaweka subira litokee wimbi kubwa na kuisuka boti ndipo naye afanye jambo na kweli sekunde kumi na tano tu likaonekana wimbi kubwa linakuja ilipo boti na eneo lingine lote kuelekea ufukwe wa bahari, wimbi likapiga wakati linapiga Agent Kai akakamata kamba moja ya katani iliyokuwa imetoka juu akapanda nayo wakati kusukwa sukwa kukiendelea kuwa kukubwa akawa tayari pembezoni anajiachia kimya kimya kwa ndani kuzunguka kinyumba cha boti kinachokuwa katikati.
Akanyata mpaka pembezoni mwa kidirisha cha nyuma aweze kuchungulia ndani, akajiweka kwa pembeni na kuchungulia kwa chati kabla hajaona chochote kinachohusiana na kiumbe kinachovuta hewa ya oxygen kulia kwake alisikia mlango unafunguliwa ikambidi achukue tahadhari kwa kuondoka pale akijiburuta sawa na ukuta wa boti kichumba kuelekea kushoto, mtu aliyetoka ambaye yeye hakuwa anamuona kwa kutokea ‘angle’ alipo alisikika masikioni mwa Kai akiongea kwa simu kwa sauti ambayo ilionyesha hataki iende mbali lakini kwa Kai alisikia upande mmoja.
“Miguel vipi mbona sielewi?” Akaongea.
Ukapita ukimya akisikiliza kwa utulivu kama dakika moja.
“Sawa fanya upesi kutimiza hilo tumechoka kusubiri na siwezi kuiacha familia yangu, wasiliana naye Koplo mwambie naongeza dau akisaidia hili” Akasikika tena na kisha ukimya ukashika hatamu yakasikika mawimbi yanayopiga pembezoni mwa boti na kuifanya boti isukwe sukwe kwa kunesa nesa huku na kule.
Mara mlango ukasikika ukifungwa ikimaanisha muongeaji amemaliza kufanya mawasiliano na huyo aliyemuita kwa jina la Miguel, Agent Kai akarudi dirishani ambako ni dirisha la kioo akachungulia ndani na ndipo sasa akamuona Feca (Fernandes Carlos Codrado) akiwa wamesimama kwa pamoja yuleyule mtu mwenye asili ya ngozi nyeusi aliyemuona akiwa naye katika chumba ambacho alikuwemo Madam Millian ambaye ni mke wa Feca, mtu huyu ndiye yeye Agent Kai alipewa taarifa na Agent Hansen kuwa ndiye alimuua kwa risasi marehemu Detective Omar Mutua Chilamwena.
Akili ya kazi ikazunguka kwa haraka kichwani mwa Agent Kai akatoa begi lake dogo linalobeba silaha hasizoweza kuzibeba katika mavazi anayovaa, akafungua zipu akapapasa kwa mkono wake ndani ya kibegi hiki kilichokuwa kimeloa maji kama mavazi yake yote yalivyokuwa yameloa maji ya baharini ikiwemo na mabuti yake ambayo maji yalikuwa mpaka ndani lakini kwake haikuwa kitu sana, akatoa kichupa kidogo kama pafyumu ndogo kama ungekiona wewe au hata mimi tungezania hivyo kuwa ile ni pafyumu ama spray ya marashi ya kuvutia kwa harufu nzuri lakini kwakuwa imetoka kwenye kibegi cha mtu mtundu na mwenye maarifa ya kuzaliwa pamoja na kuongezewa katika mafunzo aliyopita pita Agent Kai, kibegi hiki chenye kazi ya kubeba silaha za ziada basi tusubiri tuone kina kazi gani katika kile kilichomo ndani yake, akarudi kuchungulia tena dirishani akaona bado wamesimama palepale wakielekezana kwa midomo yao kutamka wanavyotamka ambavyo kwa Kai hakuwa anasikia lakini mkono yao pia ilikuwa ikielekezana kwa kuonyesha kule na kule tena wakiwa katika hali ya kutokuwa na amani kabisa, akarudi kawaida akiacha kuchungulia kisha akanyata mpaka ulipo mlango.
Akazungusha kichwa chake kusapoti macho yake yaliyo ndani ya miwani kutafuta kama kwenye mlango kuna kauwazi cha kumfanya aone ndani akapata mwanya mdogo karibu na bawaba ya mlango wa kuingia ndani ya boti hii ya kisasa, kwa mikono miwili akafungua kifuniko cha juu cha kichupa ya spray akalengesha kwenye upenyo na kubinya hewa iingie ndani kwa uwingi wake ikitoa sauti ya ‘psiiiiiiii psiiiii psiiiiiiii!!! Na kufanya jamaa walio ndani kushtuka kama wameona joka kubwa ndani wote wakatoa bastola zao toka katika mahala wanakohifadhi bastola zao, harufu ya kilichopulizwa ikatua katika viunga vya tundu za pua zao ndipo wakashtuka kuwa hewa isiyo salama imepulizwa na mtu aliye nje kwa mlangoni wote wawili wakakamata bastola zao kwa mkono mmoja na mwingine wakiziba pua zao hewa ile isiingie zaidi kwenye pua zao kwa pamoja wakaanza piga risasi kuelekea mlangoni kwa dabo dabo ikiwa tayari mwamba ameshajiweka pembeni ya mlango hivyo risasi zote zilitoboa mlango na kuugeuza kama tundu za sahani ya jiko la mkaa na risasi zikaisha kwenye bastola zao kwa pamoja wakatulia wakiangaliana kwa kasi kisha kuridi kuangaliaa mlangoni.
Spray iliyopulizwa ilikuwa ni spray yenye sumu yenye nguvu sana inayochukua fahamu za mtu kuwa kawaida kwenda katika hali ya kutojitambua kiasi kidogo tu ukivuta hivyo mara kila mmoja alihisi anaishiwa nguvu pamoja na miguvu yao waliyonayo na hali ya akili zao kutaka kujizuia wasizidiwe ilikuwa kazi bure tayari kila mmoja aliathirika wakajikuta kwa mfuatano wanadondosha bastola walizoshika kila mmoja akatamani aongee kitu lakini midomo yao ikawa mizito wakashikana mikono wakijizuia kuanguka na mara wakaona mlango unafunguliwa mwanaume mmoja akaingia ndani ‘mask’ maalumu ikiwa eneo la puani na mdomoni akiwatizama huku kashika bastola mkono wake wa kushoto akiwa, waathirika kiakili walikuwa wakitamani kutumbua macho kuendelea kumtizama na wafanye kitu lakini wapi wakadondoka kwa kufuatana fahamu zikawatoka pamoja wakiwa ndani lindi kubwa la hasira kali kwa mtu aliyeonekana amewazidi ujanja.
Mwamba ‘TSC’ akatafuta tafuta kitu na kukiona ilikuwa ni kamba za manila ndizo akawafunga vizuri kwa kila kuanzia mikononi mpaka miguuni, akawapekua katika nguo zao sehemu zile ambazo mara nyingi silaha za aina mbalimbali kwa uzoefu wake uwa zinawekwa silaha mbalimbali akawatoa kila kitu na kuwaacha na nguo zao tu kisha akaenda upande wa ‘cabin’ dreva akaikuta funguo ya boti iko mahala pake akaiwasha akiiacha inakolea mambo akaenda kwenye kamba ya nanga akafyatua nanga, wakati anafyatua nanga aliona taa za gari zinakuja hapo hakutaka kujiuliza mara mbili akajua ndiyo waliokuwa wakisubiriwa akarudi mahala kwa nahodha wa boti akatia gia na kuiondoa kwa kasi akiacha mshangao kwa wanaokuja na gari huko ufukweni.
“Lizy Roby! Nimempata” Aliongea baada ya simu yake kuita na kuipokea.
“Nimeshuhudia hilo mpenzi wangu, balozi na kikosi chetu cha wanajeshi wa ubalozini wapo kwenye helkopta wanakuja kutoa msaada Agent Jade na mwenzake S.A Rebecca wamekwama kwenye njia ya chini kwa chini baada ya hao wapuuzi kutega mlipuko”
“Eeeeeh! Wazima?”
“Agent Hansen anasema wazima kabisa ila njia imeziba kwa kutokea na pa kuingia ni shida kwao, askari wa uokozi wa Brazil wameanza kazi ya kufukua kifusi”
“Hatari sana..Naelekea pande za fukwe za upande mwingine tofauti na hizi mi sijui jina zake fukwe hizi za Bahia nitakapoona salama basi nitatia nanga ndipo nitakujulisha niletetewe gari”
“Sawa.. Na hongera kwa kazi nzuri”
Mwisho wa sehemu ya mia moja na thelathini na moja (131)
Hatimaye Kingpin Fernandes Carlos Codrado ‘Feca’ pamoja na Komandoo Andrewz wako chini ya ulinzi wa Agent Kai akiwa kawazinga kamba vizuri.
Nini kitatokea katika sehemu inayokuja ya riwaya yetu?
Je Feca na Andrewz ndiyo mwisho wao umekuwa laini kihivyo?
Spray iliyopulizwa ilikuwa ni spray yenye sumu yenye nguvu sana inayochukua fahamu za mtu kuwa kawaida kwenda katika hali ya kutojitambua kiasi kidogo tu ukivuta hivyo mara kila mmoja alihisi anaishiwa nguvu pamoja na miguvu yao waliyonayo na hali ya akili zao kutaka kujizuia wasizidiwe ilikuwa kazi bure tayari kila mmoja aliathirika wakajikuta kwa mfuatano wanadondosha bastola walizoshika kila mmoja akatamani aongee kitu lakini midomo yao ikawa mizito wakashikana mikono wakijizuia kuanguka na mara wakaona mlango unafunguliwa mwanaume mmoja akaingia ndani ‘mask’ maalumu ikiwa eneo la puani na mdomoni akiwatizama huku kashika bastola mkono wake wa kushoto akiwa, waathirika kiakili walikuwa wakitamani kutumbua macho kuendelea kumtizama na wafanye kitu lakini wapi wakadondoka kwa kufuatana fahamu zikawatoka pamoja wakiwa ndani lindi kubwa la hasira kali kwa mtu aliyeonekana amewazidi ujanja.
Mwamba ‘TSC’ akatafuta tafuta kitu na kukiona ilikuwa ni kamba za manila ndizo akawafunga vizuri kwa kila kuanzia mikononi mpaka miguuni kisha akaenda upande wa dreva akaikuta funguo ya biti iko mahala pake akaiwasha akiiacha inakolea mambo akaenda kwenye kamba ya nanga akafyatua nanga, wakati anafyatua nanga aliona taa za gari zinakuja hapo hakutaka kujiuliza mara mbili akajua ndiyo waliokuwa wakisubiriwa akarudi mahala kwa nahodha wa boti akatia gia na kuiondoa kwa kasi akiacha mshangao kwa wanaokuja na gari huko ufukweni.
“Lizy Roby! Nimempata” Aliongea baada ya simu yake kuita na kuipokea.
“Nimeshuhudia hilo mpenzi wangu, balozi na kikosi chetu cha wanajeshi wa ubalozini wapo kwenye helkopta wanakuja kutoa msaada Agent Jade na mwenzake S.A Rebecca wamekwama kwenye njia ya chini kwa chini baada ya hao wapuuzi kutega mlipuko”
“Eeeeeh! Wazima?”
“Agent Hansen anasema wazima kabisa ila njia imeziba kwa kutokea na pa kuingia ni shida kwao, askari wa uokozi wa Brazil wameanza kazi ya kufukua kifusi”
“Hatari sana..Naelekea pande za fukwe za upande mwingine tofauti na hizi mi sijui jina zake fukwe hizi za Bahia nitakapoona salama basi nitatia nanga ndipo nitakujulisha niletetewe gari”
“Sawa.. Na hongera kwa kazi nzuri”
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!
FUNGA KAZI XVVI
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
Catussaba Resort Hotel ni hotel inayomiliki eneo la fukwe ya Catussaba moja ya fukwe bora sana kati ya fukwe zilizopo jijini Salvador mji mkuu wa jimbo la Bahia moja ya jimbo kati ya majimbo yanayounda nchi ya Brazil, ilikuwa ni saa nane na dakika arobaini usiku unaoitwa usiku wa manane, usiku huu ulishuhudia fukwe hii ikitiwa nanga boti ya kisasa aina ya Aquland 37 rangi nyeupe bodi yake na cabin (kichwa) vikiwa vya alluminium yenye ukubwa wa futi 12 kiurefu wa kutoka nyuma mpaka mbele ikiwa na uwezo wa kubeba watu 15, lakini kwa muda huu ilikuwa na mtu mmoja tu aliyekuwa akionekana kwa walinzi wanaolinda hotel hii upande wa fukwe ambao hawakuwa wamekumbwa na hali ya kibinadamu kusinzia, mtu huyu alikuwa ndiye nahodha anayeendesha chombo hiki cha kisasa lakini hakuwa peke yake ndani ya boti walikuwepo watu wengine wawili katika ‘bodi’ yeye akiwa kwenye ‘cabin’.
Alikuwa ni Agent Kai anafika hapa akiwa na mateka wake wawili wa muhimu sana ndani ya boti hii akiwa anaendesha boti yeye mwenyewe, akili yake ikiwa ina furaha sana kuwa hatimaye imekuwa vile alivyokuwa akitaka wakati akiwa ndani ya ndege kwa mara ya kwanza kabisa wakati anaingia nchini Guatemala, akiwa njiani anakuja hii fukwe ya Catussaba akiwa haijui hata jina kuwa inaitwa fukwe ya Catussaba, Agent Kai alipigiwa simu na katibu wa balozi kuwa ameelekezwa na balozi aongozane na maafisa kadhaa kujua yeye yuko wapi waje wampokee na kuzuia lolote baya toka kwa maaskari polisi wanaoonekana wanataka kumsaidia Feca kutoingia mikononi mwa majasusi wa Marekani.
Walinzi wa fukwe hii usiku huu hawakuwa wanaozidi wanne hivyo wawili walisogea katika eneo ambalo kama Agent Kai angehitaji kushuka basi angeshukia na kufuata njia ambayo wao wapo wamesimama wakiwa na shaukwa wa kujua nani au nani anafika/wanafika hapa Catussaba Resort Hotel lakini kwakuwa Agent Kai alikuwa ana jambo anasubiri kitokee kwanza alibaki akijifanya ana jambo analifanya linalomfanya asitoke kwanza ndani ya boti akiwa kule kule kwenye ‘cabin’.
Dakika tatu toka boti itie nanga hapa simu ya Agent Kai ikaingia meseji aliyoisubiri kwa hamu, meseji toka kwa katibu wa ubalozini kumjibu amekubali kuwa afike afisa mmoja tu toka ubalozini akiwa na gari yenye mwendo kasi lakini wao katibu na maafisa wengine waandae ndege ama helkopta itakayowabeba Feca na mtu wake kuwapeleka moja kwa moja Marekani huku yeye Kai akienda walipoenda balozi na maafisa wengine ambako kina Agent Jade na Specia Agent Rebecca walipatwa na tatizo kidogo la kiufundi kazini, meseji hiyo alipokuwa anamaliza kuisoma ikaingia ingine ya huyo afisa kuwa ameingia tayari getini geti la Catussaba Resort Hotel anazunguka kwa gari eneo la hotel kuja ufukweni.
Hapa sasa ilimfanya Agent Kai anyanyue kibegi chake akakivaa mgongoni akagusa gusa sehemu mbalimbali za mifuko yake kuanzia mifuko ya suruali akiwa anakagua baadhi ya vitu vyake muhimu kisha akachungulia nje kupitia dirishani, halafu akaangalia saa yake ya mkononi iliyomtambulisha kuwa muda huu ni saa tisa na dakika kumi na nane kwa saa za jimbo la Bahia, alipoinua macho kutoka kuangalia saa akachungulia tena nje kupitia dirishani sasa akaiona gari inatokea eneo la majengo ya hoteli hapo akarudisha kuwaangalia walinzi ambao na wao sasa walikuwa wakiangalia kule inapotokea gari nyeusi ambapo kwakuwa ilikuwa ni mita kama mia hivi hawakuwa wakiona aina yake.
Akafungua mlango wa kutoka eneo la nahodha wa boti kwenye ‘cabin’ kisha akatoka lakini kabla hajavuta hatua zaidi tumbo likabana na kutoa muungurumo kama gesi imezidi tumboni na moyo wake ulipiga mshindo wa kushtuka akanyoosha macho kuangalia pale alipokuwa amewalaza kwa kuwafunga kamba mtuhumiwa namba moja Feca na mlinzi wake binafsi Andrwez haraka akahisi kitu katika mlango wake wa fahamu namba sita unaohifadhi vitu ambavyo binadamu wengine wenye milango mitano ya fahamu wanakuwa hawana, mlango huu sita ndiyo wengine uwa tunauita mlango wa bahati au michale ya kuhisi hatari na inakuwa kweli kuna hatari, kama upepo Agent Kai ‘TSC’ akainama na kweli kuinama kwake kulimnusuru na shambulizi la ghafla la chuma kizito kilichokuwa kimerushwa kikiwa mkononi na mtu ambaye alitumia nguvu nyingi kutaka kitue kichwani mwa anayemshambulia mkito ule ukaparaza bega lake lakini mshambuliaji hakukata tamaa alipomkosa akamkita kwa nguvu na mguu wa kulia katika tako la kushoto hapo ilikuwa hakuna ujanja Kai akaenda chini kifudifudi lakini hakulamba sakafu ya boti bali alikinga mikono yake yote miwili akataka kugeuka kwa kasi lakini haikuwa bahati tena kwake kwakuwa anayeshambulia alikuwa makini kutotoa nafasi wala pumzi iliyo kamili kwa anayemshambulia hivyo aliachia teke likamkuta ‘TSC’ mkono wake wa kushoto ikawa kama kachotwa mtama hapo shavu la kushoto lililamba sakafu na mguno ukasikika haraka akauachia mwili chini kisha akagaragara kuhama na hapo sasa ndiyo akamuona ni nani anayemshambulia kwa kasi hivi alikuwa ni mlinzi wa Feca ambaye ndiye huyuhuyu aliyemuaa Detective Omar Mutua Chilamwena rafiki wa damu wa Agent Kai waliyeshibana haswa.
Kama mbogo mjeruhiwa na kana kwamba hakuwa ametoka kwenye hali ya kuzirai komandoo huyu toka nchini Cuba alisogea kasi akataka kuruka akite kwenye mwili wa Kai hapo akitumia miguu yake miwili fundi mjanja mjanja alikita viganja vyake viwili chini kuufanya mwili urushe miguu vizuri akakita kwenye mapaja ya Andrwez na kumfanya apotee step zake akataka adondoke akajizuia hapo Kai akatumia fursa kujiinua kwa stahili ya kujifyatua sasa akasimama huku akili yake ikitaka atoe bastola yake amalize kazi lakini icho nacho kilikuwa kimesomwa kwenye akili ya Andrwez kwakuwa macho ya watu wa kazi za kazi uwa yanpoangaliana usoma macho ya mwingine yanawaza nini katika kifuatacho hivyo mwamba huyu wa ki cuba akalirusha chuma alilolishika kwenda kwa Agent Kai ambaye aliinama likapita juu yake na kwenda kuvunja kioo cha dirisha la boti eneo hili la bodi, akakaa sawa na jamaa akasogea akiwa kakunja ngumi mkao wa kushambulia ‘TSC’ akajiweka tayari kwa mpambano huku akijiuliza wapi alipo Feca hii ilimfanya asiwe makini sana kwakuwa yeye anachotaka kwa huyu aliye mbele yake akiwa kamkingia ngumi wapambane ilikuwa ni kumtoa roho yake aende akashikane kisasi na Chilamwena huko dunia ya kusadikika.
Akang’ata meno kwa nguvu akitulia atoe kitu ambacho kitatoa funzo kwa huyu mtu bila kujali muonekano wake wa ufundi.
“Yuko wapi bwana wako?” Akamuuliza huku kila mmoja akizunguka upande macho kwa macho kuzuia ulaghai wa miili yao (mafundi hawa wanajua hasara ya kupambana huku ukifuata viungo baada ya macho).
“Unanifananisha mjomba, siwezi kuwa na bwana mimi”
“Sasa mbona kila sehemu anapokwenda na wewe unaenda, sasa kama siyo kakuoa ni nini kingine? Wewe ulivyo unaonekana shoga mzoefu umempa Feca mpaka kachizika akakuoa kiboga kimemzidia utamu” Agent Kai alimuongelesha hivi hili ampandishe hasira amvuruge asiwe makini awaze kuwa amezalilishwa tu na ni kweli midomo ya Andrwez ilikosa la kujibu akitaka kuongea anajikuta anatetemeka tu papi (lips) zinagongana tu.
“Ongea sasa shoga wee unaitia aibu ngozi yetu unaliwa hadi unaolewa kama mwanamke kabisa mtu usiyetambua jinsia yako wee mp…!” Hakumaliza kuongea kashfa zake alizokuwa anatoa jamaa aliruka teke ikambidi Kai arudishe kichwa nyuma maana hakutegemea shambulizi la kujifyatua vile ingawa alikuwa tayari anatambua wepesi wa mtu huyu katika mapigano hivyo inahitajika akili sana kupambana naye, jamaa akazungusha teke la kuzungusha nalo likakuta hewa Kai akainama likapita hapo naye akaachia teke kisu kwenda kwenye ugoko wa jamaa lilikuwa teke zito na buti alilovaa lilkuwa ni butu lenye eneo la mbele lililo na ugumu si ‘soft’ likamyumbisha huku likimuachia maumivu ya kumchubua ugoko Andrwez alizidisha kukasirika akarusha ngumi mbili kushoto ikamkosa Kai aliyerudisha kichwa nyuma akaachia ya kulia ikapanguliwa mpanguo wa kwa nguvu yaani ngumi iliputwa akilazimishwa ayumbe aache wazi uso na kweli ikawa hivyo ngumi ya mkono wa kulia toka kwa Agent ikapenya na kukisabahi kidevu cha Andrwez haikuwa nzito sana hivyo ni kama ilimpapasa akayumba kinyume mawashi-teke la mguu wa kulia likatupwa kwa nguvu likatandika nyonga yake hii sasa ilimuingia akayumba kuelekea kushoto lakini hakutaka kwenda bure akaachia teke la mguu wake kushoto kwenda kwa Kai lakini lilionekana linavyokuja sehemu hizi ndizo ambazo ‘TSC’ uchukulia sia na ufundialirudi nyuma hatua mbili mwili ukajikuta umegota kwenye kuta za boti akadunda kidogo aliacha teke liende juu kidogo kisha naye kwa nguvu zote kurukia akapiga kwa chini kwenye dochi-teke kama kipa anabutua mpira usiwaiwe na fowadi katika ‘one by one’, pigo lilikuwa ni pigo takatifu licha ya mazoezi ayafanyayo mguu ulitenguka eneo la kigimbini na kumuachia maumivu ambayo asingeweza kuyavumilia wakati anaweka mguu uliopigwa chini hapo uso wake uliakisi maumivu ikawa fursa ingine kwa Kai akamchota ngwara mguu uliobaki hapo jamaa akaenda chini alipofika akaangalia upande wa kushoto kwake kwa nyuma ya Kai, hisia za mlango wa sita zikagonga kwa mara ingine Kai akajirusha pembeni kama ndoto chuma ambalo ukilitizama unaweza sema ni tufe la duara likapita likimkosa sentimita chache kwa bahati mbaya likaenda alipo Andrwez ambaye aliliona lakini kwakuwa alikuwa amekaa chini kwenye sakafu ya boti akiwa kakalia matako yake alijitahidi kuliepa lakini lilimpata tumboni laiti angekuwa si mtu wa mazoezi likaweza kumpatia maumivu zaidi ya aliyoyapata.
‘TSC’ akageuka nyuma ndipo akamuona Feca amesimama hatua tano toka alipo yeye shukrani iende kwa maamzui yake sahihi ya awali kuamua kuwachukulia silaha zao zote watu hawa wangeweza kumuua bila tabu kabisa kama angewaacha na silaha zao akawatizama wote wawili kwa kuangalia na huku kwa haraka akachomoa bastola yake kutoka nyuma ya kiuno hakutaka tena kuchelewashana nao kwa kupambana nao.
Aliye chini bwana Andrwez alianza kupata matumaini kuwa ainuke mpambano uendelee kwakuwa wakati anadondoka chini na pia kupigwa na chuma lile alitambua kwa watu wa ‘career’ ya ukomandoo kama Agent Kai kupoteza kwake ‘step’ ni kosa ambalo linaenda mgharimu na ajiandae kukabiliana na changamoto zinazokuja hivyo kumuona Feca amezinduka ilimpa matumaini lakini kosa lake likawa amemuangalia kimshangao ili kumpoteza mawazo anayemshambulia aache kuendelea kumshambulia lakini kutoa bastola kwa Agent Kai kulimfanya agwaye tena na akate tamaa ya kujitetea kwao kama si kwake.
“..Vipi tena? Ni mara yangu ya kwanza naona wanaume wamekutana halafu mwanaume mwingine mwenye sifa kedekede katika medani za ujasusi na upelelezi na hata kijeshi anakimbilia kutumia silaha kwa watu ambao hawana silaha…Komandoo Agent Kai mbona umekuwa muoga shusha silaha chini tupambane bwana mkubwa..” Mtu mzima ‘Kingpin Feca’ alijikuta anaongea wakati Kai anajisogeza upande akiwa kawekwa mtu kati hivyo alikuwa akisogea aweze kuwaona wote kwa uzuri huku mikono yake yote miwili alikuwa kakamata bastola huku moja na huku moja.
“Mimi silipwi kama Mayweather au John Cena kupambana na nyie mi naangalia muda na hali zaidi iliyopo kwa wakati huo… Feca umeshajiishia huna lolote hapo ulipo, sikuwai kukuona wakati ule una sifa zako unaitikisa Amerika Kaskazini na Kusini Feca ni Feca kwelikweli, sasa unataka nipambane na wewe kwa kipi haswa ambacho nitasema baadaye nimekipata toka kwako? Nishapambna sana na watu wenye ujuzi mbalimbali katika medani za kijeshi, kipelelezi na kujasusi kwa leo naomba nikwambie ingekuwa amri ni yangu ningekutia shaba nyingi ufie hapa kisha nikutupe baharini kaburi lako liwe matumbo ya samaki uwe kinyesi wakunye huko lakini amri ya mkurugenzi wa usalama wa taifa wa Marekani anakuhitaji ndiyo inafanya nikuache h..!” Risala yake inayosikilizwa na wasikilizaji ambao vichwani mwao walikuwa kila sekunde wanaitumia kuona wanajilipua vipi kumdhibiti ilisitishwa kutiririka toka mdomoni mwa Kai alipokuwa katika angalia kushoto kulia alipogeuka kushoto akamuona Andrwez ananyoosha mkono kutaka kulinyanyua chuma lililotupwa na boss alipomrushia Kai ambaye aliliepa likaenda mtulia yeye hapa Agent Kai kwakuwa alishapanga kumuua kulipiza kisasi cha jino kwa jino kwa Andrwez kumuua Chilamwena aliona wakati ndiyo huu sababu ndiyo hii aliachia risasi mbili kwenda usoni mwa mtu huyu ambaye alijitahidi kutaka ainame moja ilitua puani ingine ikatua juu ya utosi damu zikaruka lakini haikuwa imepita kwa Kai kwani aliye kulia kwake ‘Kingpin Feca’ brigedia na mwalimu wa wanajeshi alijirusha kwa nguvu zake zote kumkumba bila kujali anavyomvamia upande ule kuna bastola alikuwa anajua nini anafanya, wakati wanadondoka kwa pamoja akampiga karete ya juu kidogo ya kiganja kilichoshika bastola ikafanya fundi Agent Kai aachie bastola bila kupenda maana pigo lilikuwa ambalo analijua dhahiri endapo atang’ang’ana kukaza mkono atapasua moja ya misuli yake muhimu inayopitisha damu mkononi.
Mzee huyu hakuwa amesahau mapigano kitu ambacho Kai alijifanya kukidharau huku anakijua kuwa wanasema ujuzi hauzeeki kinachozeeka ni nguvu na wepesi tu, miili yao ilitua chini konde kali la mkono wa kulia likatua kwenye shavu la Agent Kai la kulia kwa mbali akahisi mchaniko wa ndani kwakuwa ngozi na meno vilisigana kwa gumi hili zito shukrani ikawa bwana Feca mkono wake wa kulia hakuwa amevaa mapete yake makubwa ambayo kikawaida uwa anayavaa kwa ngumi hii angemchana vibaya sana, chini Kai alikuwa amedhibitiwa amekaliwa uzito wa mwili wote wa Feca ulikuwa kwake ilikuwa hatari kubwa kwake, Feca akatupa ngumi akilkenga kichwani kwakuwa mkono mmoja wa kushoto wa Kai ulikuwa umebanwa kwa mguu na kumfanya atumie nguvu kwanza kuunasua huku mpinzani akitumia nguvu kukandamiza mkono ule usitoke hii ngumi ya mkono wa kushoto ilikuwa inakwenda kwenye jicho la kulia vidole vya Feca vyote vilikuwa na mapete makubwa ‘vito vya thamani’ hatari kubwa wakati inakuja kama upepo anaiyona hisia za Kai zilikumbwa na hofu kuu akajiinua kwa nguvu zake zote mwili kwenda juu akulazimisha mwili wa Feca ukubali anachotaka kisha akakunja shingo yake ngumi ikapita na kupiga sakafu ya boti kiganja cha Feca cha mkono huu kilitenguka na angekuwa si mtu wa mazoezi angevunjika kabisa, uso wake uliakisi maumivu akakunja sura mate yakigoma kumezeka pumzi ikaziba kwa uchungu alioupata, Kai akatumia mkono wake kulia ulio huru kumsukuma adui yake arudi nyuma kidogo ikawa alivyotaka papo hapo akatumia goti (futi) kumpiga kwa matakoni kwa nguvu hapo Feca akasogea tena kuja karibu na uso wa Kai wakawa karibu macho ana kwa ana mkono wa kushoto wa Kai uliokuwa umedhibitiwa ukatoka hapo akamsukuma kwa nguvu jamaa atoke kurudi juu akafanikiwa kushawishi hapo akakunja tena magoti yake akayapachika katikati ya pachipachi ya Feca akasukuma tena kwenda juu akafanikiwa kumtoa adui haraka akajifyatua kistahili na kusimama kijasho chembamba kilimtoka akamshukuru Mungu kutoka hapa.
Feca hofu ikamtawala mkono wake wa kushoto kiganja chote ulivimba ghafla hata kukunja ngumi akawa hawezi hivyo akarudi nyuma kujihami akijiandaa kupambana zaidi kwa mateke hilo lilionekana kwa Kai akamsogelea akiwa kakunja ngumi uso ameukunja kwa hasira hana tena utani utani ndita zinapokuwa zimekaa usoni anataka atoe adhabu inayomstahili huyu Kingpin.
Akatisha anamsogelea kwa kasi Feca akarudi nyuma kisha akarusha teke la mguu wa kulia hapo Agent Kai ni kama alikuwa analitarajia hilo akazunguka teke la kuzunguka ‘round-kick’ likakutana na lile teke ilikuwa kwa wepesi wa hali ya juu sana mguu wa Feca ukaingia mushkeri maana ulitandikwa haswa eneo la katikati akayumba akatupa ngumi ya mkono wake ulio na uzima ikatua kwenye bega la ksuhoto la Kai ambaye si kama alikuwa hajaiona aliiona lakini alitaka ipite hili atoe anachotaka na yeye haraka akajisogeza hatua moja akawa karibu akaachia konde la nguvu la mkono wa kulia katika mbavu za kushoto eneo muhimu kwenye maungano na tumbo hapo akamfanya Feca aruke nyuma kuepesha mkono wake mbovu usishambuliwe.
Mwisho wa sehemu ya mia moja na thelathini na mbili (132)
Safari ya mpambano huu inaendelea sehemu ya mwisho ya riwaya yetu! Mafundi wamekutana mmoja umri ukiwa umemtupa mkono kidogo na mwingine akiwa ndiyo kwanza kama joka basi ni joka lililojivua gamba lake kwa mara ya kwanza bado lina hamu ya kufanya mambo pale mambo hayo yanapohitajika.
Nani atakaa kwenye huu mpambano?
Twende pamoja katika sehemu ya mwisho ya riwaya yetu ambayo kukweli imekuwa ndefu katika mtindo wa series ikiwa ina series zaidi ya kumi zenye epsd kumi mbili au kumi na tatu kila moja.
Feca hofu ikamtawala mkono wake wa kushoto kiganja chote ulivimba ghafla hata kukunja ngumi akawa hawezi hivyo akarudi nyuma kujihami akijiandaa kupambana zaidi kwa mateke hilo lilionekana kwa Kai akamsogelea akiwa kakunja ngumi uso ameukunja kwa hasira hana tena utani utani ndita zinapokuwa zimekaa usoni anataka atoe adhabu inayomstahili huyu Kingpin.
Akatisha anamsogelea kwa kasi Feca akarudi nyuma kisha akarusha teke la mguu wa kulia hapo Agent Kai ni kama alikuwa analitarajia hilo akazunguka teke la kuzunguka ‘round-kick’ likakutana na lile teke ilikuwa kwa wepesi wa hali ya juu sana mguu wa Feca ukaingia mushkeri maana ulitandikwa haswa eneo la katikati akayumba akatupa ngumi ya mkono wake ulio na uzima ikatua kwenye bega la kushoto la Kai ambaye si kama alikuwa hajaiona aliiona lakini alitaka ipite hili atoe anachotaka na yeye haraka akajisogeza hatua moja akawa karibu akaachia konde la nguvu la mkono wa kulia katika mbavu za kushoto eneo muhimu kwenye maungano na tumbo hapo akamfanya Feca aruke nyuma kuepesha mkono wake mbovu usishambuliwe.
ENDELEA NA MAPIGO MAKALI…!
FUNGA KAZI XVVI
SALVADOR, BAHIA-BRAZIL
Kueepesha mkono wake ilikuwa ni kosa la jinai kwa mtu anayepigana kwa kutegemea ujanja ujanja na kosa la adui yake apale anapokuwa kwenye mapambano ya ana kwa ana, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu hili ni jambo ambalo kwake Agent Kai ndicho ukiweka mbele zaidi ujanja na umakini zaidi ya mamba mtoni anapopigana sababu anajua fika kwenye kupigana hasa wanapokutana mafundi basi ujuzi zaidi wa kimafunzo ndiyo unaotumika kwao hapa ndipo linapohitajika jambo hili linaloitwa ujanja na umakini wa kuligundua kosa la adui kabla hajajua kama kakosea na kulirekebisha kosa lake, mkono ulipoepeshwa usiguswe mwili wake ilibidi urudi nyuma huku mkono mzima ukitanua mbawa kiwiko ‘kosa’, kwapa la mkono ulio mzima lilistuka katikati likipokea ngumi nzito ya mkono wa kushoto mkono wa dhahabu kama mwenyewe anavyopenda kuuita ukiwa una nguvu na shabaha anaposhambulia iwe kwa silaha ama kawaida.
Ngumi hii ni kama ilikata mawasiliano ya nguvu za bwana mkubwa Feca pumzi ilimkata kwakuwa alibana pumzi kuzuia uzito wa ngumi anapoipokea lakini, Kai akarusha ngumi ya kusakiza ya mkono wa kulia Feca akainama kukwepa ikapita naye akarusha ngumi ambayo hata angemrusghia binti yangu basi isingempa wakati mgumu za ya kumuogopesha binti kuwa kashambuliwa na mara mlango wa boti kuja hapa kwenye bodi ukafunguliwa ikawa kosa Feca akageuza shingo kuangalia mgeni huyo ni nani? Wakati yeye Kai hakuangalia sababu alikuwa amemuona aliyekuwa kaingia kwenye daraja la kuja kwenye boti wakati wanaendelea kupigana hivyo yeye hakumuangalia akatumia fursa akaachia shoto lingine la moja kwa moja kwenda usoni bwana mkubwa Feca alipokuwa anarudisha macho kwa uoga ngumi ilitua katikati ya mwamba wa pua ambao ukiguswa vizuri kwa mkong’oto basi lazima utokee mpasuko nje na ndani ya pua, hapa konde hili lilimrudisha nyuma akiyumba bwana mkubwa Feca macho yakiona nyota nyota hakuwa amewai kupigwa ngumi nzito na kali kama hii maisha yake yote iwe alivyokuwa jeshini wala katika nyakati zake hizi alizokuwa akila starehe zaidi bila kashikashi.
Teke la kuzunguka hewani kama muangalia movie haya uwa yanapigwa na watu wazito kwenye medani ya sinema kama kina Scott Adkins au wa zama za miaka ya tisini kina Dolph Lundgren ama Jean-Claude Van Damme ‘round kick’ ilizungushwa na fundi Agent Kai akizunguka kwa kasi hewani kisha akaukita mguu wake wa kulia pembeni usoni shavuni mwa bwana mkubwa, mwili wote ulizidiwa na pigo hili akadondoka kwa kasi chini kama kasukumwa toka katika chombo cha usafiri kilichopata ajali.
‘Jino kwa jino’ Akawaza Agent Kai wakati akitua chini toka kwenye shambulizi, hasira zilikuwa zimepanda kichwani hata yeye mwenyewe hajui zilipotoka akasogea kasi hatua mbili alipo Feca akakita kwa nguvu kwenye goti la mguu wa kulia la Feca na kulivunja papo hapo mguu ukipinda goti likizungushwa nyuma mbele, brigedia komandoo Feca alitamani kupiga kelele kwa maumivu aliyoyasikia kuvunjwa mguu si kitu kidogo lakini alikunja uso na kung’ata meno akipinda pinda mwili na kukata mauno kama anatafuta goli la pili katika mechi ya kikubwa, Kai akasogea na kutisha anataka kupiga teke la kufumua usoni mwa Feca haraka bwana mkubwa akajikunyata akijikusanya hapo likawa kosa mguu wake wa kushoto ukawa umejianika kikatili zaidi ‘TSC’ akaruka mkito mzito wa nguvu zake zote za miguu akakita miguu yote miwili katikati ya ugoko hapa ulisikika mlio uliokuwa unafichwa kwa ujasisri ndani ya Feca kwani bwana mkubwa alipiga yowe kubwa, mguu ukikatika kama mua uliovunjwa katikati, haikuwa mwisho wa Kai kumuacha Feca alimstua teke la kufunika la matako ya bwana mkubwa ‘Kingpin’ Feca kwa nia amsogeze kukaa mkao anaouhitaji alipokaa kifuatacho kilifanya hata yule aliyeingia mlangoni na kuwakuta mafahari hawa wanatiana pembe za kupimana ubavu kufumba macho sababu Agent Kai ‘TSC’ mwamba mwenye asili ya Afrika alipiga dochi-teke katika mbavu changa za Feca kana kwamba anaupiga mpira shuti kali hili kufunga penalty, Feca alirushwa kwa shuti hili akajipiga ukutani kichwani na kupoteza fahamu, pumzi nzito ikatoka mdomoni mwa Kai akashukwa na munkari akabaki anahema kama mwanariadha aliyemaliza mbio za mita mia nne akiwashindwa wanariadha bora kabisa duniani.
“Haya ndiyo malipo ya jino kwa jino Kingpin Feca… Kwa mapigo haya utazinduka ukiwa Marekani shubamiiit ulitesa sana watu natamani nikung’oe koromeo lako na wewe ulipie kifo cha Chilamwena na wote waliouliwa na kuteswa kwa amri zako au vibaraka wako mjusi guruguja mweupe weee..!” Akaongea kwa sauti huku anajitahidi kushusha pumzi zinazomtoka kwa kasi ziwe kawaida Agent Kai.
“Karibu Afisa kutoka ubalozini..!” Akamkaribisha mgeni aliyeingia huku anamtizama alivyosimama mlangoni kana kwamba naye anaogopa mkong’oto jazz band kutoka kwa fundi mtaalamu ‘TSC’.
“Pole sana Agent Kai.. Naitwa Mr. Lawrence Tryphone Call kama ulivyosema ni afisa kutoka ubalozini… Huyu ndiyo Feca?” Akajibu akijitambulisha afisa huyu na kisha kumalizia kwa swali kwenda kwa Kai.
“Ahsante sana Mr. Lawrence Tryphone Call.. Yaah! Ndiyo huyu.. Tusichelewa hapa tumbebe na kuondoka naye”
“Mzima? Maana umemtwanga haswa Mr. Kai”
“Amezirai tu… Ila yule mbwa unayemuona pale nilishajipanga kumtoa roho na nimetimiza hilo… Huyu bwege ndiyo alimuua Detective Chilamwena”
Walimaliza haraka taratibu za pale wakawapa taarifa walinzi wa pale juu ya mtu wanayemchukua na yule maiti waliyemuacha kwenye boti aliyokuja nayo Agent Kai, baada ya yote wakaondoka pale kuelekea ilipo ndege iliyokuja maalumu hapa Salvador, Bahia kwa ajili ya kumchukua Kingpin Fernandes Carlos Codrado.
***** ***** ***** *****
“Karibu sana… Naitwa Balozi Paul William Lambert”
“Agent Kai Hamis wa CIA.. Nimefurahi sana kukutana na wewe balozi wetu nchini hapa.. Vipi hali ya hapa?”
“Kwa kushirikiana na kikosi cha uokozi cha jeshi la polisi la Brazil tumefanikiwa kuwatoa wote wawili katika wakati mmoja, Agent Jade hakukutwa akiwa amezirai kwakuwa yeye hakuguswa na maporomoko ya udongo na zege lakini bado anahema kwa msaada wa hewa ya gesi na..!” Hakuendelea alikatiziwa alichotaka kusema na anayehitaji kujua hali ya mahala hapa.
“Vipi Rebecca? Ana hali gani?” Akauliza kwa sauti ya kasi huku anatizama hatua kumi mbele lilipo gari la misaada kwa wagonjwa na huduma ya kwanza ambako kulikuwa kumezungukwa na jopo la watoa huduma ya kwanza wakiwa wameizunguka stecha moja iliyo na mtu anayepatiwa huduma.
“Madaktari wetu wanajitahidi kuokoa maisha yake kwakuwa alikutwa amebanwa na udongo pamoja na zege lililovunjika amezirai tu na kwa mujibu wa wataalamu wetu wanasema atakaa sawa akifikishwa hospitali kwa matibabu zaidi.. Usiwe na hofu Agent Kai juu ya ndugu zako hawa”
“Ahsante sana mheshimiwa balozi acha nikawaone na mie” Akatoa shukrani.
“Vipi na wewe mmekamilisha kila kitu?”
“Naam.. hivi tunavyoongea chombo iko mawinguni kuelekea Pentagon”
“Vizuri!.. Wametaka apelekwe huko Pentagon?”
“Ndiyo! Ndege iliyofika kumchukua ilitokea Guatemala kikosi cha kijeshi toka huko kikiongozwa na Sajenti Ramazani Asmani walikuwa wamechukua na watu wengine watano waliokuwa ndani ya TRJ katika nafasi za juu na kati ambao nao wanapelekwa Pentagon mambo mengine juu ya hukumu zao tutajua hukohuko Marekani”
“Shukrani kwako umefanya kazi ya kuongoza kikosi kazi kwa mafanikio pia poleni na kumpoteza mshirika mwenzenu ndiyo kazi hizi zilivyo mkiingia kwenye mapambano kunakuwa na mambo mawili kufa au kupona, sawa unaweza kwenda kuwaona ndugu zako mambo mengine tutaongea vizuri utakapokuja ubalozini kwa maongezi zaidi asubuhi”
“Shukrani na wewe pamoja na maafisa wako wengine wote.. USA First!”
“USA First!”
wakapeana mikono kila mmoja kumshukuru mwenzie, Agent Kai alipogeuka hili kuondoka akakutana macho na Agent Hansen anamuangalia huku anatabasamu.
“Baba vipi?”Akasalimu kumsalimia kwa ulizo.
“Poa sana, hongera kwa kazi nzuri na pole kwa mpambano naamini haikuwa kazi rahisi ila mara zote haki ushinda uovu”
“Naam ahsante sana kwa kweli ilikuwa si kazi rahisi lakini uzoefu na ujanja ujanja siku zote utubeba.. Yule mpuuzi aliyetufanya tutoe machozi nimemfanyia jino kwa jino nimemtoa roho kwa risasi kama alivyotufanyia kwa ndugu yetu… Vipi umeongea na Jade?”
“Kidogo sababu madaktari hawakuruhusu iwe hivyo ila kwakuwa tupo wote tunaweza enda kuongea naye”
Walipiga hatua za haraka wakiwapita maaskari polisi pamoja na watu wa vikosi maalumu vya uokozi katika majanga mpaka ilipo gari ya ambulance, Jade alikuwa wa kwanza kuwaona na ndipo wao wakamuona kila mmoja kati yao akaachia tabasamu.
“Karibuni jamani.. Hans karibu tena” Agent Jade akaongea huku anatabasamu tabasamu ambalo kikawaida uwa si kama tabsamu lake zoeleka.
“Tushakaribia bibie fundi langu..Kama kawaida yako kama hakuna lolote kwako lililotokea.. Pole sana na pia poleni sana, una hali gani?” Agent Kai akaongea akimpapasa nywele zake.
“mimi nishapoa naumwa kidogo mbavu na kifuani kuna maumivu kwa mbali” Akajibu Agent Jade.
“Naweza kujua ilikuwaje? mpaka kutokea yaliyo tokea” Ingewezekana angeweza msubiri wakaambiana baadaye yaliyotokea lakini Agent Kai alikuwa na shauku ya kujua kipi kiliwapata wanawake hawa hasa katika moyo wake hamu yake ilikuwa ni kujua kwanini Special Agent Rebecca amekutwa na tatizo kama alilokumbwa nalo.
“Wakati tunashuka ngazi na kuzifuata zinapoelekea kama ulivyotutaka kufanya hivyo tulikwenda tukiwa tunakaribia kufika kwenye mlango ukatokea mtetemeko kisha kusikika mlio wa mlipuko ndipo yakatokea yaliyotokea… Mimi nilijikuta nadondokewa na madongo mara nikadondoka hapo sikumuona tena Rebeccca mpaka nakuja muonea hapa nje nilipoweza fungua macho baada ya huduma ya kusafishwa macho ni hivyo tu”
“Poleni sana.. Mungu awape nguvu mpone upesi… Kazi imeisha hapa Bahia tunasubiri uzima wenu ulio kamili mpaka asubuhi kisha tutaona kama tunaweza ondoka kurudi nyumbani”
“Uliwapata?”
“Ndiyo na sasa hivi wako angani kuelekea Marekani yule aliyemuua Chila nimempa alichostahili jino kwa jino”
“Apumzike kwa amani Omar Mutua Chilamwena swahiba wangu mwenyewe toka jeshini.. Nimeumia sana juu ya kifo chake”
“Kesho mwili wake utaagwa ubalozini naamini nanyi pia mtakuwa mmetoka hospitali tushiriki kuagwa kwake” Agent Hansen aliyekuwa kimya akisikiliza Kai na Jade wakiongea kwa mara ya kwanza aliongea kutoa taarifa.
Kai akaondoka pale kwenda alipo Rebecca ambaye alikuwa ndiyo anamaliziwa kufungwa bandeji ngumu ‘P.O.P’ katika mkono wake wa kulia na hakuwa amerejewa na fahamu, alimtizama akiwa na huzuni kubwa sana ndani ya kifua chake akawa anaomba dua kwa mwenyezi Mungu amfanyie wepesi swahiba wake huyu apone upesi.
“Saa kumi na nusu kunakucha muda si mrefu twende tukapumzike angalau masaa matatu… Ndege ya kwenda Brasilia ulipo ubalozi wetu itaondoka hapa saa nne asubuhi hivyo muhimu tukapumzike..” Agent Hansen alimshika bega Agent Kai kisha akamwambia.
Kwa pamoja wakamuaga Jade ambao kwa pamoja na S.A Rebecca walikuwa wakisubiri kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Hatimaye ukawa mwisho wa genge la TRJ ‘THE RED JAGUAR’ kwa bwana mkubwa wao kuingia katika mkono wa chuma wa Marekani, katika umri wake wa uzee hatimaye anapelekwa Marekani kwa ajili ya hukumu itakayomstahili katika kulipia yote aliyoyafanya kuifanyia Marekani na hata nchi nyingine za mabara mbalimbali hapa duniani, kuna wale walioombwa waelekee nchi ya Argentina ambao si viongozi wa juu bali ni wa chini tu pia walikuwepo waliokuwa chini ya TRJ lakini tawi la Colombia ambao nao hawakuwa na nguvu ni kama waliokuwa hapa Bahia walikuwa ni wasimamizi tu wa biashara za ulanguzi wa dawa za kulevya hawa hawakukumbwa na balaa la kuingia mikononi mwa kina Agent Kai ambapo wapo waliokuwa na vimitaji vya biashara yao hii.
***** ***** ***** *****
Mwisho wa Riwaya ya JINO KWA JINO imeishia hapa katika sehemu ya mia moja na thelathini na tatu, riwaya hii ya kubuniwa ambayo ilikuwa na mikasa ambayo pengine ilikuwa ni kama umewai isoma au kuisoma sehemu kwa hili sikatai sababu ni mambo ambayo yanatokea katika jamii ya uhalifu, ujasusi na upelelezi.
Riwaya yangu inayofuata Inshaallah Mwenyezi Mungu akinipa ruhusa yake itachapwa kitabu hivyo siwezi sema wala kuahidi kama walio mitandaoni wataipata.
Kwa wale watu na wapenzi wa Agent Kai nipeni subira kidogo kisha mje misapoti pale nitakapotangaza kibali nilichopewa na Mungu kwa rukhsa yake kuwa kitabu kinaingia sokoni basi nitaomba sapoti yenu katika mkasa huo mabao nao unavutia sana na kuamsha hisia za kusoma kwako iwe kama unaangalia movie katika ubongo wako wewe mwenyewe.
Ahsante kwa wote mnao nisapoti katika Page yangu ya ‘Riwaya Za Agent Kai ‘The Sole Cat’ na wale pia ambao hawajaniacha kunisapoti kwa kunipigia simu na kunitumia meseji za kunishukuru kwa kazi zangu, sina cha kuwalipa kwa kweli zaidi ya hii burudani ninayotoa katika kichwa changu.
Shukrani za pekee ziende kwa waandishi na watunzi wote ambao uwa wananipa ushauri na kunielekeza mambo kadhaa wa kadha mbarikiwe sana, sina uwezo wa kuwataja mmoja wote mnajijua na kwa wale wasomaji nao nawaomba nirudie tena kuwashukuru sana wapo naoweza kuwataja mmoja lakini ni wengi so patakuwa hapatoshi hapa.
Twende kazi katika ‘WHEN ALIVE’ ikiwa katika kitabu! Twendeni mnisapoti huko wakati ukifikia mtapata taarifa tayari Agent Kai yupo katika kitabu ndani ya mkasa mtamu wenye mapigo ya kisasa nilioupa jina hilo.
MSISITE KUNIKOSOA JAMANI MAANA MIMI SIJUI KILA KITU BADO NA SAFARI NDEFU SABA KWENDA JUU WAPO WALIO JUU NA NYIE PIA MSIWE WACHOYO WA KUNIKOSOA JAMANI.
NAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA KWENU NYOTE, NAWAPENDA SANA! NA HII NDIYO ILIKUWA NDIYO ZAWADI YANGU YA MWAKA 2019 KWENYE PAGE YANGU.
BY K M M M @2019
MWISHO
MWISHO
0 comments:
Post a Comment