Search This Blog

Monday 19 December 2022

QUEEN MONICA (3) - 2

  







Simulizi : Queen Monica (3)
Sehemu Ya Pili (2)


Hakuna ulazima wowote wa kufanya uchunguzi.Sulala hapa ni moja tu ,Ernest amefanya usaliti hivyo lazima auawe.Kitendo cha kumuacha mpaka sasa ni kosa kubwa kwani anaendelea kujiimarisha na kutufyeka taratibu.Ernest is a very smart guy,anajua kuzicheza vizuri karata zake.Kwa kipindi hiki chote amekuwa akitusoma na baada ya kutufahamu vyema ameanza kutufyeka taratibu na tuspokuwa makini sote tutakwenda na maji.” Jeremiah akanyamaza na kuwatazama wenzake ambao wote walikuwa kimya “Mnaonaje juu ya wazo langu? Akauliza Jeremiah “Wazo lako si baya lakini huu ni usaliti mwingine ndani ya jumuiya kwa kwenda kinyume na maazimio ya kikao kikubwa kama kile.Ni vipi endapo Alberto mkuu akafahamu kuhusu hiki tunachotaka kukifanya? Mnadhani akigundua tutakuwa salama? Akauliza Makamu wa rais “ Alberto he’s not here,we are.Albeto is not a Tanzania ,we are.Kwa hiyo basi haya tunayoyafanya ni kwa ajili ya nchi yetu.Alberto anatutegemea sisi katika mabadiliko anayotaka kuyafanya hapa Tanzania kwa hiyo hatuwezi kukaa kimya tukishuhudia mambo yakienda ndivyo sivyo .Ndugu zangu tumejitahid sana kuifikisha jumuiya hapa ilipofika kwa hiyo basi tusikubali juhudi zetu zote zikaenda bure.We must do something and we must do it fast” akasisitiza Jeremiah “Binafsi nakubaliana na Jeremiah” akasema bi Agatha “Ernest ametufanyia kitu kibaya mno ambacho sikuwahi kutegemea kama angekuja kukifanya kwa namna ninavyomfahamu.Ni mume wangu ambaye kuna wakati tulipendana sana lakini kwa hili alilolifanya siwezi kumtetea.Nilikula kiapo cha kuitetea jumuiya hata kwa damu yangu kwa hiyo nakubaliana na Jeremiah kwamba Ernest must die.Ernest si wa kuonewa huruma hata kidogo.Amebadilika mno,si mwenzetu tena na tukitaka mabadiliko haya yafanikiwe basi hatuna budi tumuondoe haraka sana.Me and him we’re over” akasema Agatha kwa hasira “ Ahsante Agatha .Sasa umebaki peke yako makamu wa rais,tafadhali fanya maamuzi” akasema Jeremiah.Makamu wa rais akafikiri kwa muda kisha akasema “Ok I’m in.Let’s do it” “Good. Kama sote tunakubaliana hivyo naomba tuendelee kuwa kitu kimoja.Asitokee mmoja kati yetu akabadili mawazo na kutusaliti.Kuhusu namna ya kuutekeleza mpango huu yote niachieni mimi.Ndani ya siku mbili zijazo nitakuwa tayari na mpango wa namna tutakavyoweza kumuondoa mwenyekiti.Nikiwa tayari nitawaiteni na kuwajulisha lakini wakati mchakato huo ukiendelea Agatha unatakiwa uwe karibu sana na chanzo chako cha taarifa ili tujue nini makao makuu wanafikiria kukifanya” akasema Jeremiah kisha wakaendelea na maongezi mengine ****************** Boaz alikifungua kitabu kile na kuanza kupitia ukurasa mmoja baada ya mwingne.Kila alipoufungua ukurasa sura yake ilionyesha mabadiliko.Katikati ya kitabu kile kulikuwa na karatasi akaifungua haraka haraka na kuanza kuisoma.Ilikuwa ni barua.Iliandikwa hivi Kwako Marcelo Nimeamua kukuandikia ujumbe huu na kuuficha humu kwani sikutaka ujumbe huu uupate angali bado niko mzima.Nimeandika barua hii nikiwa katika siku za mwisho za uhai wangu.Naandika huku macho yangu yakiwa yamejaa machozi.Dhumuni kuu la kukuandikia barua hii kwanza ni kutaka ufahamu mimi baba yako ni nani na maisha ya aina gani ambayo nimeyaishi.Nimekuchagua wewe kati ya watoto wangu kwani ndiye ninayeona unastahili kuyafahamu haya. Kwa muda mrefu umekuwa masomoni kwa hiyo hujapata nafasi ya kukaa nami na kunifahamu vyema.Mimi baba yako ni mmoja wa madaktari maarufu barani Afrika.Nimekuwa bingwa wa upasuaji wa moyo na kichwa ,vile vile nimekuwa bingwa wa saratan ya damu.Nimekuwa bingwa wa kuokoa maisha ya watu jambo lililonipa umaarufu mkubwa lakini katika siku hizi za mwisho za uhai wangu nimegundua kwamba hakuna atakayeweza kuyaokoa maisha yangu.Natamani sana kama angetokea bingwa wa kuyaokoa maisha yangu ili niendelee kuishi lakini hakuna mwenye uwezo huo so I must die.Baada ya kutambua kwamba sintaweza kupona nimeyatafakari maisha yangu niliyoishi na kama nilitimiza vyema wajibu wangu wa kuwapo hapa duniani.Robo tatu ya maisha yangu nimetumia katika kazi yangu ya udaktari na nimeokoa maisha ya watu wengi .

Nilijitoa kwa hali na mali kuhakikisha kila mgonjwa ninayemtibu anapona.Naweza kusema asilimia tisini ya wagonjwa niliowatibu walipona na kuendelea na maisha yao na hii ndiyo iliyonifanya kuwa daktari maarufu.Nilitimiza vyema wajibu wangu kama daktari.Pamoja na mazuri hayo yote bado kuna mambo ambayo wengi hawayafahamu kuhusiana na maisha yangu.Sehemu ya kwanza ya maisha yangu ni hiyo niliyokueleza ambayo niliishi kama daktari,kama baba,mume,mlezi,mtu mwenye nafasi katika kanisa na jamii na zaidi nilijulikana kama tajiri mwenye moyo wa huruma.Hivi ndivyo wengi na hata wewe mnavyonifahamu.Lakini maisha yangu yana upande wa pili pia ambao wengi wenu hamuufahamu na upande huu ndio sababu ya kuandika barua hii Nikisema nikueleze kwa kina kuhusiana na upande huu nitahitaji maelezo marefu lakini kwa kifupi tu ni kwamba mimi ni mfuasi wa kikundi au imani ya Alberto’s.Sina hakika kama unakifahamu au umewahi kukisikia kikundi hiki lakini asili ya kundi hili ni nchini Italia .Ni kundi linaloongozwa na mtu anayeitwa Alberto mkuu .Aliyeanzisha kundi hili ni Alberto mkuu wa kwanza ambaye aliwahi kuwa kiongozi katika kanisa .Alivulia daraja na kufukuzwa katika kanisa baada ya kutaka kuleta uasi ndani ya kanisa akidai mabadiliko ambayo hayaendani na imani ya kanisa hilo.Baada ya kufukuzwa ndipo alipoanzisha kikundi chake cha Alberto’s na lengo kubwa la kuanzisha kikundi hiki ni kuyaendeleza yale ambayo yalisababisha akafukuzwa na kanisa na kwa sasa alitaka mabadiliko haya yawe ni ya kidunia .Alberto mkuu wa kwanza alianza kwa kuwashawishi viongozi wa mataifa makubwa kuwa wafuasi wake.Alifanikiwa katika hilo na akaanza kuyatumia mataifa hayo makubwa yenye nguvu kuusambaza mtandao wake sehemu mbali mbali za dunia na hivyo kupelekea nchi nyingi kuyakubali mabadiliko yake.Mabadiliko aliyokuwa anayataka Alberto’s ni kila nchi duniani kutambua haki za wapenzi wa insia moja,haki ya wanawake kutoa mimba,haki za uvutaji wa mihadarati n.k.Karibu mambo hayo yote yanapingana na imani ya dini zote na ndiyo maana Alberto’s anawatumia wakuu wa nchi ili kutumia nguvu na madaraka yao kushinikiza kutungwa kwa sheria katika nchi zao kuyatambua mambo hayo.Kwa kurahisisha tu kuhusu Alberto ni kwamba hawa ni waabudu shetani.Wengi wa wafuasi wake ni matajiri wakubwa,viongozi wa kisiasa wenye nguvu na ushawishi mkubwa,wengine ni watu wenye nafasi kubwa katika imani zao,lakini ukifika usiku huweka pembeni imani na kumuangukia Mungu wa giza.Mimi pia ni mmoja wao.Nilipewa nguvu yaakuweza kutibu magonjwa mbali mbali na ndiyo maana nimekuwa daktari wa kusifika sana kwa sababu wengi niliowatibu wamepona. Pamoja na nguvu na uwezo huo wa kuponya,nilikuwa na kazi nyingine kubwa na ya muhimu sana kwa Alberto’s.Ili upate picha kamili ngoja nikupe maelezo kidogo.Alberto’s wameifikia sehemu kubwa ya dunia kwa sasa na serikali nyingi zinaongozwa na vongozi ambao ni wafuasi wao.Wanawatumia wakuu wa nchi ambao ni wafuasi wao kufanikisha mambo yao.
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Moja ya mambo ambayo mkuu wa nchi aliye chini ya Alberto’s anapaswa kufanya ni kuhakikisha katika nchi yake wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya hawaguswi wala kubughudhiwa na kwamba ahakikishe wanatengenezewa miundo mbinu mizuri ya kuweza kuifanya kazi yao kwa uhuru.Madawa ya kulevya ni chanzo kikubwa cha mapato kwa Alberto’s kwani wafanyabiashara hawa hutoa kiasi kikubwa cha pesa kwa jumuiya ambazo huisaidia jumuiya iweze kujiendesha.Kwa hapa Tanzania mimi ndiye niliyepewa jukumu la kuhakikisha ninawasimamia wafanya biashara wote wa dawa za kulevyua walio chini ya alberto’s na kuhakikisha biashara zao zinakwenda vizuri na wanalipa michango yao kwa jumuiya kwa wakati.Hiki ndicho chanzo cha utajiri wangu mkubwa Mimi ni mmoja kati ya wale waliochangia vijana wengi kuharibu maisha yao kwa kujiingiza katika matumizi ya dwa za kulevya kwani ndiye niliyeratibu shughuli zote za uingizwaji wa dawa za kulevya nchini. Huo ni upande wangu wa pili ambao wewe na wengine wengi hamuufahamu .Ni kutokana na upande huu nilipata pesa nyingi zilizoniwezesha mimi na familia yangu tuishi maisha ya anasa kubwa lakini kwa siku hizi za mwisho ninayajutia maisha niliyoishi .Nimekuwa nikijiwa na picha zile mbaya za yale mabaya niliyoyafanya na nyakati nyingine ninaota malaika anapambana na jitu la kutisha wananipigania mimi.Nilimuasi Mungu na kuchagua kumuabudu shetani kwa tamaa ya mali utajiri na umaarufu wa dunia.Ninachokiona katika dakika hizi cha mwisho ni kigumu hata kusimulia.Nimeamua kuyafichua haya kwako kwa sababu nataka nikuachie kazi ambayo si nyepesi.Sina hakika kama utaiweza lakini lazima ujaribu au ufe ukijaribu. Nataka uhakikishe kikundi cha Alberto’s kinafutika nchini Tanzania.Hiki ni kikundi hatari mno na madhara yake kwa nchi ni makubwa.Alberto’s wako hapa ,wameotesha mizizi yao na tayari wana nguvu kubwa.Viogozi wengi wa juu wa serikali ni wafuasi wao kwa hiyo yale yote wanayoyataka Alberto’s tayari yamefanyika au yanaendelea kufanyika. Taifa hili linakwenda kubomolewa na ndani ya miaka michache ijayo ile misingi yote imara iliyosimamisha taifa hili itabomolewa na zitaletwa tamaduni mpya kabisa ambazo hazikuwahi kuonekana hapa nchini.Vizazi vijavyo vitarithi taifa ambalo limebomolewa . Nafahamu mapambano na Alberto’s si kitu chepesi lakini fanya kila uwezalo kuhakikisha unapambana na kufanikiwa.Huwezi kupambana peke yako tafuta mtu au watu ambao utashirikiana nao na kwa pamoja mtasaidia kuliondoa kundi hili hapa nchini.Sikutaka kukuingiza katika mapambano haya na watu hawa lakini sina mtu mwingine ninayeweza kumuamini kuifanya kazi hii zaidi yako Marcelo.Nafahamu unasumbuliwa na kansa ya damu lakini hiki si kigezo cha kukufanya ushindwe kupambana. Kitabu hiki nilichokupa ndani yake kuna kumbu kumbu zangu za namna nilivyoweza kutibu magonjwa mbali mbali ,namna nilivyoweza kuponya watu mbali mbali ,dawa nilizotumia n.k.

Ni kitabu ambacho kitakuwa na msaada mkubwa kwako katika kazi yako ya utabibu.Kama nilivyokueleza wakati nakukabidhi kitabu hiki kwamba muda wowote ukipatwa na tatizo lolote katika kazi zako za kitabibu,kifungue na ukisome na utapata maelekezo kwani nimeandika mambo mengi .Silaha kubwa ambayo nakuachia ambayo unaweza kuitumia katika kuidhoofisha na kuifutilia mbali Alberto’s hapa nchini ni kitabu ambacho ndani yake kina orodha nzima ya mtandao wa dawa za kulevya hapa nchini.Utawafahamu ni akina nani ,wako wapi,wanamiliki biashara zipi hapa nchini,mtiririko wao mzima wa fedha,akaunti zao katika mabenki mbalimbali na hadi michango yao inavyowafikia Alberto’s.Kama nilivyokueleza kuwa hiki ni chanzo kikubwa cha mapato kwa Alberto’s kwa hiyo ukifanikiwa kuukata mrija huu wa mapato kutakuwa na upungufu mkubwa wa mapato kwani Tanzania ndiyo hasa njia kuu ya kupitishia madawa hayo kwa hiyo utakapoiziba njia hiyo mapato yatapungua kutoka Afrika.Kitabu chenye mambo haya yote nimekihifadhi kwa katika kasiki lililo nyuma ya picha ya Swala chumbani kwa Vera.

Namba ya simu niliyokupa upige ili uwasiliane na mtu atakayekupa maelekezo ya namna ya kukitumia kitabu hiki ,ukweli ni kwamba hakuna maelekezo yoyote kuhusiana na kitabu hiki kwani kila kitu kinajieleza chenyewe bali lengo langu ni kutaka ufahamiane na mtu huyo ambaye ni mmoja kati ya wafanya biashara wakubwa wa dawa kulevya .Ukifanikiwa kumuangusha huyo basi utakuwa umefanikiwa kuiteteresha biashara nzima ya dawa za kulevya hapa nchini.Wafanya biashara wote wa dawa za kulevya hapa nchini huyo ndiye baba yao.Unatakiwa uwe makini sana naye kwani ni mtu hatari sana.Atakufundisha njia zote za kuhusiana na dawa za kulevya yanakotoka hadi yanafika hapa.Usithubutu kuhusisha chombo chochote cha usalama katika suala hili.Mtandao huu ni mpana na umesambaa katika sehemu kubwa na hadi katika vyombo vya usalama.Narudia tena kukukumbusha kwamba watu hawa wanalindwa na serikali kwa hiyo umakini mkubwa sana unahitajika viginevyo utapoteza maisha kabla hujafanya lolote. Kuna wale rafiki zangu watatu ambao niliwahi kukupa angalizo usiwape nafasi wakakuzoea.Ni wat hatari .Ni wafanya biashara wa dawa za kulevya na wanafanya kazi kwa huyu mtu niliyekupa namba zake.Kaa mbali nao ni wauaji hatari.Mwisho kabisa nataka nikuweke wazi kwamba hata mimi tayari nimewekeza mtaji katika biashara hiyo kwa hiyo mtu niliyekupa namba zake ndiye anayefahamu kila kitu na atakupa maelekezo na hiyo ndiyo njia rahisi ya kujenga mazoea naye kwani ataamini kwamba unaendeleza mradi wa baba yako kumbe una ajenda nyingine. Marcelo narudia tena kukusisitiza kwamba wewe ndiye pekee ambaye ninaamini unaweza kuokoa nchi yetu.Wewe ni kijana mwenye akili na jasiri na ninaamini utafanya kila unaloweza kulifanya ili kufanikisha jambo hili.Ukishindwa au kupuuzia utakuwa umefanya kosa kubwa sana na taifa letu zuri litabomolewa. Mwishi kabisa naomba haya mengi niliyokueleza kuhusu maisha yangu yabaki kuwa siri yako na asifahamu mtu mwingine yeyote na hasa uhusika wagnu katika biashara ya dawa za kulevya. Natumai umenielewa na utayatekeleza yale yote niliyokuagiza .Jambo la mwisho kabisa naomba kila siku kabla ya kulala usiache kuniombea kwa Mungu ili anifutie makosa yangu.Nimekosa sana na katika saa zangu za mwisho ninauona ubaya wa yale yote niliyoyatenda.Niombee bila kuchoka.Wewe ni kijana mwenye hofu ya Mungu usije kutenda yale niliyoyatenda mimi katika maisha yangu Mungu akulinde na akubariki Dr Richard Boaz akashusha pumzi .Uso wake ulionekana kuloa jasho jembamba. Kwa sekunde kadhaa alionekana kama amechanganyikiwa “ Is everything ok Mr Boaz? Akauliza Julieth “Your father was a devil !! akasema Boaz kwa hasira “Laiti kama ningemfahamu kabla Dr Richard ni mtu wa aina gani naapa ningemuua kwa mkono wangu mwenyewe” akasema Boaz huku akihema kwa kasi. “What’s wrong Boaz? Nini kimetokea? Akauliza Julieth “Unamfahamu Vera? Boaz akauliza “Vera?!!..Julieth akaonekana kushangaa “Ndiyo.Unafahamumahala anakoishi? Huku akionekana kuzidi kushangaa Julieth akacheka kidogo..Boazi akamtazama kwa macho makali na kusema “Julieth this is a very very serious matter.Tell me where Vera is please!!! Akasema Boaz “ Boaz I’m not jocking.I real don’t know where Vera is.Whos is Vera ? Boaz akaendelea kumkazia macho Julieth halafu akampa barua ile aisome.

“Oh my gosh !! akasema Julieth baada ya kumaliza kuisoma barua ile “Sasa umefahamu namna baba yako alivyo shetani.Naapa kama ningemfahamu yuko hivi kabla hajafariki ningemuua kwa mikono yangu.How could he do this to me? Nimestuka sana.Sikutegemea kabisa kama Dr Richard anaweza akanifanyia hivi” akasema Boaz “Hata mimi nimestuka sana .Hili ni jambo la kushangaza mno” akasema Julieth.Boaz akakishika kitabu kile na kumtupia Julieth “Kitabu hiki sicho kile nilichokuwa nakitafuta .Hiki kimejaa upuuzi mtupu na hakina msaada wowote kwangu .Kitabu ninachokihitaji ni hicho ambacho amemuelekeza Marcelo kwamba amekihifadhi kwa Vera na ndiyo maana nahitaji sana kumfahamu huyo Vera ni nani? Ninaamini huyo Vera anafahamu alipo Marcelo na kama tukifanikiwa kumpata atatuelekeza mahala alipojificha.Kwa sasa tumerudi katika sifuri.” Akasema Boaz na kuinamisha kichwa “I’m so sorry Boaz.Hata mimi sikujua” akasema Julieth “Si kosa lako Julie.Hata hivyo tunatakiwa kuanza upya tena na tunatakiwa kufanya kila ,liwezekanalo kuhakikisha kwamba kwa gharama zozote zile tunampata Marcelo na hicho kitabu.Bila kumpata Marcelo au hicho kitabu tumekwisha kwani kitabu hicho kina maelezo yote kuhusiana na sisi kama ulivyosoma katika barua .Naamini tayari Marcelo atakuwa amekwisha anza kutekeleza maagizo ya baba yake na tayari anao watu anaoshirikiana nao ambao ni watu wenye uwezo mkubwa .Namna alivyoweza kutolewa hospitali ni kithibitisho tosha kwamba watu anao shirikiana nao si watu wa mchezo.” Akasema Boaz huku sura yake ikionyesha wasi wasi mkubwa. “Rais Ernest amewasaliti wenzake na kwa sasa anaendelea kuwaondoa Alberto’s katika nyadhifa zao ndani ya serikali na hii ni hatari kubwa kwetu kwani tulikuwa tunafanya biashara zetu kwa uhuru kwa kivuli cha Alberto’s kwa hiyo endapo hakuna Alberto’s biashara yetu itakuwa ngumu sana kufanyika.Kama hiyo haitoshi,Marcelo naye ametoweka na kitabu chenye kumbu kumbu zetu wote.Hii ni hatari kubwa sana kwetu .
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sina hakika lakini najaribu kujenga hisia kwamba inawezekana labda Marcelo akawa katika mtandao wa rais Ernest na wanafanya kazi pamoja.Kama ni hivyo basi vita hii itakuwa na ushindi mkubwa kwao kwani hawahitaji kutumia nguvu kubwa kila kitu kinajieleza chenyewe katika hicho kitabu.Hizo ni hisia zangu tu lakini kubwa kuliko yote ni kumtafuta Marcelo apatikane akiwa hai au amekufa.” Akasema Boaz .Julieth akafikiri kidogo na kusema “Boaz nadhani ipo njia ambayo inaweza kutusaidia kujua au kupata mwanga wa kujua aliko Marcelo” “Ni njia gani hiyo ulieth? “Marcelo anao watu wake wa karibu lakini miongoni mwao kuna watu wawili ambao ni wa muhimu sana kwake.Kwanza kuna rafiki yake anaitwa Daniel Swai.Huyu ni rafiki yake wa muda mrefu sana na wamekuwa marafiki wa muda mrefu na ndiye msiri wake mkubwa.Urafiki wao ni mkubwa kiasi Daniel amekuwa ni kama ndugu yetu.Mambo mengi ya Marcelo Daniel anayafahamu na hata akiwa hospitali walikuwa karibu sana na kuna mambo walikuwa wakaiongea kwa siri na hawakutaka mimi niyafahamu.Mtu wa pili anaitwa Monica Benedict.Kwa siku za hivi karibuni Marcelo na Monica wamekuwa na ukaribu mkubwa sana na hata alipolazwa hospitali Monica hakuwahi kukosa kuja kumtazama.Monica na Marcelo nahisi watakuwa na mahusiano ya kimapenzi japo niliwahi kumuuliza Monica na akakana lakini ninamini watakuwa katika mahusiano.Moja ya vitu nilivyovichukua katika kasiki la Marcelo ni faili la matibabu yake ya kansa ya damu na nililipeleka kwa Monica.Lengo la kufanya hivi lilikuwa ni kumfanya Monica aufahamu ugonjwa wa Marcelo na lakini wameendelea kuwa na ukaribu mkubwa.Huyu naye alikuwa akiwasiliana kwa siri na Marcelo kwa njia ya maandishi na hata nilipotaka kujua walichokuwa wakiwasiliana hakuwa tayari.Kwa namna walivyokuwa wakiwasiliana ninaamini kabisa kwamba kuna jambo walilokuwa wanalificha.Naamini kabisa mmoja kati ya watu hawa kama si wote atakuwa anafahamu alipo Marcelo.Nashauri tuanze na hawa wawili na tukiwapata tunaweza kupata mwanga Fulani.” Boaz akafikiri kidogo na kusema “That’s a good idea.Kuna mtu mmoja ambaye ninakwenda kuonana naye jioni ya leo nitampa hiyo kazi ya kuwapata hawa watu wawili .Ni mtu mahiri sana katika shughuli hizo ,atawatafuta kokote waliko,atawapata na atawafanya waseme mahala aliko Marcelo kama wanajua” akasema Boaz huku akiuma meno kwa hasira. *********************** Austin aliwasili katika kiwanda cha viatu cha Ndura kama alivyoelekezwa na Amani.Alishuka garini akaenda katika geti waliko walinzi akasalimiana nao na kumuulizia mtu anayeitwa Amani mjeledi .Huyu alifahamika sana hapo kiwandani kwani alimpata kwa haraka “Habari yako bwana Amani” Austin akamsalimu “Nzuri kabisa.Natumai wewe ndiye bwana Austin” “Ndiye mimi” akajibu Austin “Karibu sana .Nadhani tusipoteze muda twende nikupeleke mara moja ukaonane na rafiki yako.”

 Akasema Amani wakaingia garini na safari ikaanza. “Habari ya wapi Austin? Akauliza Amani aliyeonekana muongeaji sana “Ninaishi Afrika ya kusini .Nimepotezana na Job kwa miaka zaidi ya kumi.Nimekuja mara moja kusalimia ndugu na jamaa nikaona si vibaya nikimtafuta huyu rafiki yangu nimjulie hali a.Nimekwenda mahala alikokuwa anaishi nikapata taarifa za matatizo yaliyompata.Nimesikitika sana” “Ni kweli Job alipatwa na matatizo ya akili.Chanzo ni mke wake ambaye tumeambiwa na mtaalamu kuwa alimtupia jini awe kichaa ili yeye aweze kuolewa na mwanaume mwingine” akasema Amani “Vipi hali yake kwa sasa? Akauliza Austin “Hali yake siwezi kusema ni nzuri kwani bado hajapona japokuwa kuna nyakati huwa anatulia na baada ya muda mfupi uchizi unamjia lakini bado hatujakata tamaa,tunaendelea kumshughulikia.Hivi sasa kuna mtaalamu mmoja anakuja kutoka mkoani Rukwa anakuja kumshughulikia” akasema Amani Hatimaye waliwasili eneo la Tegeta mji mpya anakoishi Amani.Austin akakaribishwa ndani.Kulikuwa kimya kabisa “Austin karibu ndani jisikie nyumbani.Mama ametoka amekwenda mihangaikoni kidogo.Job huwa anabak peke yake hapa nyumbani na mara nyingi huwa anashinda shambani.Nisubiri hapa nikamlete” akasema Amani “Unaweza kwenda sote huko shambani kumuona? “Hakuna tatizo” akasema amani wakaongozana kuelekea shambani kumtafuta Job Walielekea katika shamba lililokuwa na minazi mingi .Baada ya kuzunguka zunguka hatimaye wakamkuta Job akiwa amekaa chini ya mti wa mkorosho akiwa na kitabu.Alipowaona akina Austin akakifunika kitabu alichokuwa nacho na alionyesha mstuko mkubwa alipomuona Austin “Job nimekuletea rafiki yako wa siku nyingi anaitwa Austin.Unamkumbuka? akauliza Amani.Job hakujibu kitu akawatazama halafu akaangua kicheko kikubwa. “Job !! akasema Amani kwa ukali “It’s ok Amani.Wewe nenda niache nibaki naye hapa nitafute namna ya kuweza kumfanya anikumbuke.Pengine anaweza akanikumbuka” akasema Austin “Sawa nitakuwa kule nyumbani nashughulikia mifugo.Naona kichaa chake leo kimepanda ila huwa hana vurugu.

Ukimfokea tu anatulia.Ukishindwa kuzungumza naye labda ujaribu tena kesho pengine atakuwa vizuri.” Akasema Amani na kuondoka akamuacha Austin na Job .Austin akamsogelea Job akaacha kucheka na kumtazama kwa mshangao “Job!!..Job..NimimiAustin.Unanikumb uka? Job hakujibu kitu akapanda juu ya mti wa korosho akakaa huko juu kwa dakika kama tano halafu akashuka akamsogelea Austin na kumpa mkono na kucheka kidogo “ Austn January !!! Austin akastuka sana na uso wake ukajenga tabasamu kubwa “Job umenikumbuka? “Ndiyo.Siwezikukusahau Austin.Karibu sana.Siamini ni wewe kweli au ni mzimu wako? Akasema Job huku akimshika mkono Austin na kuubonyeza. “Kweli ni wewe.Umejuaje kama niko hapa? Akauliza Job “oh my God !!!..akasema Austin na kumkumbatia Job “What happened to you Job? Akauliza Austin hukuakifuta machozi yaliyokuwa yanamtoka “Usilie Austin wala usiongee kwa sauti kubwa.I’m not crazy.Sina tatizo lolote la uchizi.Mimi ni mzima kabisa “ akasema Job na kumfanya Austin amshangae “Tafadhali usishangae Austin.Mimi si kichaa kama wote wanavyodhani.Imenilazimu kuishi katika hali hii kutokana na masahibu yaliyonipata” “Oh Mungu wangu !! Nini kilikupata Job? Akauliza Austin “Ni hadithi ndefu Austin ambayo hatuwezi kuongea hapa.Usiku wa leo naomba tukutane pale Rozana night club.Tutaongea zaidi” “Rozana? Akauliza Austin “Ndiyo” “How will you get there? Hatawagundua hawa ndugu zako kuwa umeondoka? Utatumia usafiri gani? Do you have a phone? Austin akauliza maswali mfululizo na Job akacheka kidogo “Austin nadhani tayari umenisahau mimi ni nani” akasema na kucheka tena “Tukutane kuanzia saa nne usiku wa leo pale Rozana.Ukifika kaa kaunta ya juu nitakukuta hapo.” Austin akataka kusema jambo lakini Job akamzuia baada ya kusikika sauti ya mtu akipiga mluzi akielekea pande zile.


 “Kuna mtu anakuja pande hizi ,atakuwa ni Amani.Tukutane mida hiyo ,fika bila kukosa” akasema Job na kwenda kuketi chini ya mkorosho akiwa na kitabu chake .Ni kweli aliyekuwa akipiga mluzi alikuwa ni Amani kaka yake Job “Vipi kuna maendeleo yoyote? Ameweza kukukumbuka ? akauliza Amani “ Hapana hajaweza kunitambua.Toka ulipoondoka hajainuka pale chini ya mti.Nadhani kama ulivyosema kuwa leo hajaamka vizuri.” “Dah! leo una bahati mbaya sana.Umekuta kimeamka.Kuna baadhi ya siku huwa anakuwa vizuri kabisa anaoga na kujiweka safi lakini siku nyingine unamkuta kama hivi” akasema Amani “Poleni sana kwa tatizo hili.Namuombea sana rafiki yangu huyu aweze kupona na kurejea katika maisha yake ya kawaida kama awali.Kwa kuwa bado naendelea na mapumziko nitakuja tena siku nyingine kumjulia hali” akasema Austin na kugeuka akaanza kupiga hatua kuondoka “Job rafiki yako Austin anaondoka” akasema Amani lakini Job hakujbu kitu.Amani na Austin wakaondoka na kumuacha Job peke yake.Baada ya kufika katika gari lake Austin akafungua droo ya gari na kutoa bunda la noti akahesabu shilingi laki tatu akampatia Amani “Kiasi hiki kidogo kitakusaidia katika kuuguza.Nitakuja tena siku nyingine ili kushauriana namna ya kufanya “ akasema Austin na kuagana na Amani akaondoka “Nahisi kama vile natazama filamu.Job!! nini kimempata na kumsababisha aishi katika hali ile? Akawaza Austin akiwa garini “Lazima kuna jambo kubwa lililomtokea hadi akaamua kuishi maisha yale ya kujifanya kichaa.Huu ndio ubaya wa hizi kazi zetu.Ukiingia katika kazi hizi fahamu hadi kufa kwako you’ll never have a normal life.Hiki ndicho kilichonitokea mimi na ndicho kinachomtokea Job.Nitafahamu kila kitu nitakapoonana naye usiku wa leo.Kama anahitaji msaada lazima nimsaidie.Yule ni mtu muhimu sana kwangu.Namuhitaji sana” akawaza Austin *******************

CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Boaz na Julieth waliwasili katika jengo la ghorofa tano linalomilikiwa na bilionea Peter Chui.Hili ni duka kubwa la magari ya kifahari.Peter Chui akawapokea wageni wake na kuwaongoza hadi ghorofa ya juu kabisa kulikokuwa na ofisi yake kubwa.Ndani ya ofisi yake ile kubwa na nzuri walikuwemo watu wengine wawili ,wote wakasimama kumlaki Boaz. “Karibu tena nyumbani Boaz” akasema mmoja wa wale watu waliokuwamo katika ile ofisi “ Nashukuru sana mzee Chimo.Tayari nimerejea kwa hiyo msiwe na hofu tena” “Hiki kilichotokea ni kitu cha kustusha sana.Sielewi huyu rais amepatwa na nini hadi akafanya haya aliyoyafanya.Hatujui nini hasa lengo lake na hivyo anatuweka katika mashaka makubwa.Kama ameweza kuwasaliti wenzake hawezi kushindwa kuanzisha vita na sisi.Nimefurahi umekuja kwa wakati muafaka ili uweke sawa jambo hili.Peter aliponitaarifu kwamba umerudi nilifurahi sana ikanilazimu nije haraka haraka kukuona ili nijue mipango yako namna ya kulikabili jambo hili kwani baada ya Dr Richard kufariki wewe ndiye uliyebaki mtu tunayekutegemea katika kuweka mambo yote sawa” akasema mzee Chimo “Tuanzie na hapo kwa Dr Richard” akasema Boaz “Kama mnavyofahamu Yule ndiye aliyekuwa kama mlezi wetu na aliwekwa na mkuu Alberto kutusimamia na kuhakikisha mambo yetu yote yanakwenda sawa.Katika siku za mwisho wa uhai wake Dr Richard alinieleza kwamba anataka mwanae arithi nafasi yake pindi atakapofariki.

Ombi lake hili liliwasilishwa kwa Alberto mkuu wa tatu na akakubali kwamba ikitokea Dr Richard atafariki dunia basi mwanae afundishwe kazi kwanza na itakapothibitika kwamba amefahamu kazi vyema basi anaweza akakabidhiwa nafasi ya baba yake.Kwa mujibu wa makubaliano yangu na Dr Richard,ni kwamba mara tu atakapokuwa amefariki basi atamuachia maagizo mwanae Marcelo anitafute ili niweze kumpa maelekezo na kumfundisha kazi.Baada ya Dr Richard kufariki muda ulizidi kusonga bila ya Marcelo kutokea na nilipoulizwa nikamtetea kwamba bado yuko masomoni na atakapomaliza atajiunga nasi hivyo nikaendelea kuyabeba majukumu yote ya Dr Richard.Hata alipohitimu masomo yake na kurejea Tanzania bado Marcelo hakufanya juhudi zozote za kunitafuta.Nilianza kuingiwa na shaka kama Marcelo ana nia ya dhati ya kujiunga nasi hivyo ikanilazmu kuchukua hatua.Kitu cha kwanza tulichokihitaji toka kwake ni kitabu alichopewa na baba yake ambacho kina orodha ya wafanya biashara wote wa dawa za kulevya ambao Dr Richard alikuwa anawasimamia.

Kitabu hicho kinaonyesha mahala walipo,biashara na mali wanazomiliki,akaunti zao za benki na mtiririko wao mzima wa fedha na mwisho ni namna wanavyochangia katika jumuia.Ilinilazmu kumtumia dada yake Marcelo anaitwa Julieth ambaye ndiye huyu niko naye hapa kuingia chumbani kwa Marcelo akafungua kasiki na kuchukua kitabu nilichomuagiza.Kwa bahati mbaya baada ya kukiona kitabu hicho muda mfupi uliopita nimegundua kwamba kitabu hicho si chenyewe.Si kile tunachokitafuta chenye taarifa zetu.Ndani ya kitabu hicho nimekuta barua ambayo Dr Richard alimuandikia Marcelo.Ni barua ndefu kidogo“ akaitoa barua ile akampa mzee Chimo aisome.Ukimya ukatawala mle ofisini wakati mzee Chimo akiendelea kuisoma ile barua.Kadiri alivyoendelea kuisoma ndivyo sura yake ilivyobadilika na uso ukajikunja kwa hasira na mshangao “Bastard !!! akagonga meza kwa hasira baada ya kumaliza kuisoma barua ile “I hope he’s now burnng in hell!! Sikutegemea kabisa kama Rich....” Mzee Chimo akatulia kidogo baada ya simu ya Peter Chui kuita,akasogea pembeni akaipokea.Baada ya maongezi mafupi na mtu aliyempigia ,Peter akamfuata Boaz “Waziri mkuu Jeremiah anataka kuongea nawe” Boaz akaichukua simu na kusogea pembeni. “Hallow mheshimiwa waziri” akasema Boaz “Hallo Boaz.Nimefurahi kusikia uko Tanzania.Nimekutafuta sana leo.Nimepiga afrika ya kusini nikaambiwa uko Comoro nikapiga tena namba niliyopewa ukiwa Comoro nikataarifiwa kwamba haupo tena Comoro.Nikaona nimpigie Peter Chui akaniambia kwamba tayari umerejea Tanzania.Karibu sana nyumbani japokuwa mambo si shwari huku.Upepo mbaya unavuma kwa kasi ya ajabu hivi sasa lakini naamini kabisa kwamba ujio wako unaweza ukaimaliza dhoruba hii” “Ahsante sana mheshimiwa waziri .Kwanza kabisa pole sana kwa masahibu yaliyokupata.Nimelazmika kusimamisha kidogo shughuli zangu nyingine na kuja haraka Tanzania kutokana na hiki kilichotokea” “Imekuwa vizuri sana umekuja Boaz.Ninahitaji mno kuonana nawe jioni ya leo kuna mambo ya msingi nahitaji kuzungumza nawe.Saa ngapi utapata nafasi ? “Leo jioni kuna mtu nitaonana naye na nitakapotoka huko nitakuja kuonana nawe.Tukutane wapi? “Karibu katika makazi yangu” “Sawa waziri mkuu,nitakuja baada ya kumaliza kikao changu na huyo mtu ninayekwenda kuonana naye usiku” akasema Boaz na kukata simu akaenda kuendelea na maongezi na wenzake “Nadhani tayari nyote mmekwisha isoma barua hiyo ambayo Dr Richard alimuandikia Marcelo na tayari mnalo jibu ni kwa nini Marcelo hakuweza kujiunga nasi kama tulivyokubaliana na baba yake.Nina uhakika kama alivyopewa maelekezo na baba yake tayari amekwisha pata watu wa kushirikiana nao na lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanatumaliza kabisa .Ni hao watu anaoshirikiana nao ndio waliomtorosha hospitali .Kwa taarifa nilizopewa namna tukio la kumtorosha Marcelo hospitali lilivyofanywa,lilikuwa ni tukio la kitaalamu sana na hiyo ni picha ya wazi kwamba watu wanaotutafuta bila ya sisi kufahamu ni watu hatari sana.They are very professional na wamejipanga vizuri.Hata hivyo tayari nimeanza kuchukua hatua na usiku wa leo kuna mtu ambaye ninakwenda kuonana naye ,kuna kazi nitampa aifanye na baada ya hapo nitawataarifu hatua itakayofuata .

Nawahakikishia lazima Marcelo apatikane pamoja na kitabu tunachokitafuta.Nawaomba msiwe na wasi wasi kabisa mimi ndiye mtuliza rabsha na dhoruba” akasema Boaz kwa kujigamba kisha wakaendelea na maongezi mengine kuhusu biashara zao ******************** Saa kumi na mbili na dakika kumi,Austin aliwasili katika makazi yake akasalimiana na Marcelo na kuelekea chumbani kwake.Kichwa chake kilijaa mawazo mengi na kubwa zaidi ,likiwa ni suala la Job.Alikaa kitandani akaendelea kutafakari na mara mlango wake ukagongwa akaichukua bastora yake iliyokuwa chini ya mto akaenda kuufungua akakutana na Marcelo ambaye alistuka kumuona Austin akiwa na bastora mkononi. “Karibu ndani Marcelo” akasema Austin .Kwa wasi wasi Marcelo akaingia ndani “Nimestuka baada ya kukuona na bastora.Toka niliponusurika kuuawa kwa risasi nimekuwa ninastuka mno kila nionapo bastora au bunduki.Is everything ok Austin? Akauliza Dr Marcelo “Don’t worry.Everything is ok.This is how I am.I don’t trust people” Ukimya mfupi ukupita Marcelo akauliza “Anyword from David Zumo? “Mpaka sasa bado sijapata taarifa yoyote toka kwa rais.Nitawasiliana naye jioni ya leo kama kuna lolote atanieleza nitakwambia” akasema Austin.Dr Marcelo akainama na kushika kichwa baada ya muda akainua kichwa na kusema “Austin kichwa changu kinataka kupasuka kwa mawazo .Kuna mambo mengi yananitatiza na sijui wapi nitaanzia kupata majibu.Naomba sana msaada wako uweze kunikwamua hapa nilipokwama.Bila wewe kunisaidia maisha yangu yatakuwa kama ya ndege.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog