Simulizi : Queen Monica (3)
Sehemu Ya Tatu (3)
Nitaendelea kujificha humu hadi lini? Lazima nitafute njia ya kujikwamua hapa nilipokwamba na wewe pekee ndiye unayeweza kunisaidia nikatoka katika giza hili.Please help me Austin” Austin aliyekuwa anamtazama Marcelo kwa makini akavuta pumzi na kusema “Unataka nikusaidiaje Marcelo? “Kuna mambo mengi yamenizunguka ambayo nahitaji kuyapatia ufumbuzi.Ninahisi kuna jambo linaloendelea na mimi ni kama mlengwa mkuu bila kujifahamu.Nataka kujua n.....” Saa ya mkononi ya Austin ikatoa mlio na kumfanya Marcelo anyamaze kwanza.Austin akabonyeza kitufe katika simu yake na ikatokea picha ya mtu aliyekuwa getini vans.!! Akasema Austin kwa sauti ndogo “Who is Evans? Akauliza Marcelo “Ni mlinzi wa rais.Marcelo nenda chumbani kwako tutaongea baadae yawezekana rais amekuja” “Kama ni rais tafadhali nahitaji kuzungumza naye” “Sawa nitamweleza” akasema Austin na kufutika bastora kiunoni akatoka na kuelekea getini.Akachungulia katika tundu dogo la getini na kuliona gari moja.Taratibu na kwa tahadhari kubwa akalifungua geti na gari lililokuwa nje likaingia ndani.Akafunga geti na kulisogelea gari lile kwa tahadhari.Mlango wa dereva ukafunguliwa akashuka Evans mlinzi wa rais “Hello Austin” Evans akamsalimu Austin “Hi Evans.Karibu san.....” Austin akastushwa na mlango mwingine wa gari uliofunguliwa na akashuka mtu aliyemstua “Mr Boaz..?!!!!.. akasema Austin kwa mshangao “Hallo son !! akasema Boaz “Surprised to see me here? Akauliza Boaz huku akitabasamu “Umejuaje kama niko hapa mzee? Akauliza Austin “Iam Boaz remember,hakuna ninachokihitaji katika hii dunia nikakikosa.Nilihitaji kufahamu mahala ulipo na maendeleo yako and here I am .I’m happy to see you” akasema Boaz “Austin nimeelekezwa na mheshimiwa rais niwalete wageni hawa hapa kwako” akasema Evans “Wageni? Kuna mgeni mwingine tena? Akauliza Austin akiendelea kumkazia macho Boaz “Yes ! A very big surprise !! akasema Boaz na kuufungua mlango wa gari akashuka Maria “M..ma..ma...Mar...Maria...!!! Austin akastuka sana.Alihisi kama miguu inamuisha nguvu “Hallo my love” akasema Maria hukuakitabsamau na kwend akumkubatia nma kumwagia mabusu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Oh my God ! I cant believe this “ akawaza Austin “How are you my king? Nimefurahi mno kukuona tena Austin” akasema Maria lakini Austin hakuongea chochote aliendelea kumtazama kwa macho makali.Maria akautambua mstuko alioupata Austine na kuuliza “Are you ok my love? Aren’t you happy to see me? Akauliza Maria .Austin akastuka kama mtu aliyetoka usingizini akajilazimisha kutabasamu na kusema “This is a big surprise na ndiyo maana nimekosa neno la kusema.Karibuni sana ndani” akasema Austin na kumshika mkono Maria akawakaribisha sebuleni,Evans akabaki nje. “Umekuja lini Tanzania? Austin akamuuliza Maria “Nimekuja jana ila utanisamehe nimekuja bila taarifa.I only wanted to surprise you.Siwezi kueleza furaha niliyonayo kukuona tena mfalme wangu” akasema Maria “Karibu sana Tanzania.Karibu Dar es salaam” akasema Austin “What a beautiful house” akasema Maria baada ya kuingia sebuleni.Austin akatabasamu na kuwakirimu wageni wake vinywaji “Austin kwanza kabisa nataka nikuombe radhi kwa kukuvamia bila taarifa.Nimekuja Dar es salaam kwa shughuli zangu lakini nikaona si vyema endapo nitaondoka bila ya kuonana na mwanangu hivyo nikawasiliana na rais akanipa mtu wa kunileta hapa.Nilipofika Dar es salaam nikamkuta Maria tayari amefika naye alikuwa na lengo moja tu la kuja kuonana nawe hivyo nikaona si vibaya endapo nitaongozana naye kuja kukuona .Vipi maisha ya Dar es salaam? Akauliza Boaz “Nashukuru ninaendelea vizuri.Maisha hapa ni mazuri kama mnavyoona.Hata mimi nimefurahi mno kuwaoneni watu wangu wa muhimu.Kwa mara nyingine karibuni sana” akasema Austin
“Ahsnate Austn.” Wakasema Boaz na Maria “Austin naomba unielekeze ulipo msalani tafadhali” akasema Boaz na Austin akamuelekeza.Mara tu Boaz alipotoka pale sebuleni,Austin akamfuata Maria “I told you not to come to Tanzania,what are you doing here ??? ..akauliza Austin kwa sauti ndogo “Austin I real don’t understand you.What’s going on? Kwa nini hutaki nije Tanzania? Kuna nini hutaki nikijue? “Sikiliza Maria,kesho natakiwa uondoke urejee afrika ya kusini.Hutakiwi kuwepo hapa.This place is dangerous”
“Austin umekuwa ukirudia hilo neno la kuhusu usalama mara kwa mara.What’s going on? I’m not going back to South Africa until you tell me whats going on ? Are you back on your old job? Akauliza Maria lakini kabla Austin hajajibu Boaz akarejea.Austin na Maria wakatabasamu na kubadili maongezi “You missed each other huh !!.. Boaz akasema huku akitabasamu “Yes father.I missed Austin so much.Siku moja bila kumtia machoni ni sawa na mwaka mzima.Nimekaa Dubai kwa zaidi ya wiki tatu nadhani unaweza kupata picha how I missed him” akasema Maria na wote wakacheka “By the way Austin,safari ya maria Dubai imekuwa ya mafanikio makubwa.Amesaini mikataba mitano na makampuni makubwa.Mikataba hiyo itatuwezesha kuvuna pesa nyingi sana.Mnastahili pongezi kubwa kwa namna mnavyoendesha biashara zetu kwa mafanikio.” Akasema Boaz na wote wakapongezana .Boaz akaitazama saa yake ya mkononi na kusema “Austin,naweza kupata kama dakika kumi na tano za mazungumzo nawe? Sitaki kuchukua muda mwingi hapa.Kuna mtu ambaye natakiwa kuonana naye usiku huu wa leo.Nadhani wewe na Maria mtapata nafasi nzuri ya kuzungumza kesho” akasema Boaz “Sure.Let’s go to study room” akasema Austin “Maria naomba ubaki hapa kuna mambo nataka kuzungumza na Austin.It’s men’s talk.” Boaz akamwambia Maria. “Feel at home Maria” Austin akamwambia na kumuongoza Boaz hadi katika chumba cha kusomea “Now,let’s have a short and serious talk” akasema Boaz “Nakusikiliza mzee” akasema Austin “Austin you are my son.Ninakupenda na kukuamini zaidi ya ninavyoweza kukueleza.Toka wakati ule nilipokutoa mikononi mwa Alshabaab umekuwa ni mwanangu.Umefanya mambo mengi ya mafanikio kwa familia yetu,ahsante sana kwa hilo” akasema Boaz na kunyamaza kidogo halafu akaendelea “Baada ya utangulizi huo,Austin nimekuja kwako kuna mahali nimekwamba ahitaji msaada wako” aaksema Boaz “Sijapata kukuomba msaada katika jambo lingine lolote zaidi ya biashara lakini kwa sasa nimelazimika kukuomba msaada wako kwani suala hili si langu binafsi bali ni la familia nzima kwa ujumla.” Akanyamaza kidogo na kuendelea “Kuna mtu mmoja aliitwa Dr Richard ambaye aliwahi kuwa mshirika wangu mkubwa katika biashara lakini kwa bahati mbaya alifariki kwa maradhi ya saratani ya damu.Enzi za uhai wake biashara zetu yeye ndiye aliyekuwa akizisimamia na alipofariki mtoto wake ndiye aliyeshika umiliki wa mali zote zikiwamo zile ambazo mimi na baba yake tulikuwa na ubia.Mtoto huyo anaitwa Dr Marcelo” “Dr.Marcelo? Austin akamkatisha Boaz “Ndiyo.Mbonaumestuka.
Do you know him? Boaz akauliza “Hapana simfahamu.Endelea” “Huyo Marcelo anataka kuniondoa katika ubia ili biashara zote zibaki mali yake. Kuna kitabu ambacho baba yake aliweka kumbu kumbu zote kuhusiana na biashara zetu na Marcelo amekificha kitabu hicho ili kupoteza ushahidi.Kwa bahati mbaya ubia wetu hatukuufanya kisheria na ilikuwa ni kati yetu sisi wawili kwa kuwa tulikuwa tukiaminiana sana .Marcelo anaamini kwamba kukificha kitabu hicho ni kupoteza ushahidi wote.Nilijaribu kumtumia ujumbe mara kwa mara ili tuonane tulimalize suala hili kwa njia ya mazungumzo akapuuzia ikanilazimu nitumie nguvu kidogo ili niweze kukipata kitabu hicho chenye kumbu kumbu zote.Niliwatuma vijana wangu kukitafuta kitabu hicho lakini Marcelo akawa jeuri na kuwafyatulia risasi vijana wangu na wao wakajibu shambulizi na katika kurushiana risasi Marcelo akajeruhiwa na kukimbizwa hospitali ambako baada ya siku mbili akatoroka na hadi sasa hajulikani alipo.Austin ubia huo nilioingia na Dr Richard ni mkubwa na niliwekeza fedha nyingi mno ambazo siwezi kukubali zipotee kwa hiyo ninahitaji msaada wako.Nataka unisaidie kumtafuta huyo Marcelo na kukipata kitabu hicho chenye kumbu kumbu zote za biashara kati yangu na baba yake ii niweze kurejesha fedha zangu.Inawezekana ikawa ngumu kidogo kumpata Marcelo kwa sasa kwani tayari amejificha baada ya kufahamu kwamba ninamsaka hata hivyo kuna watu wawili ambao ni watu wake wa karibu sana na ambao wanaweza wakatuongoza mahala aliko Marcelo.Wa kwanza ni mwanamke mmoja anaitwa Monica Benedict ambaye hivi majuzi alitangazwa kuwa ni mrembo kuliko wote Afrika.Huyu ni mtu wa karibu sana na Marcelo na kuna tetesi kwamba wana mahusiano ya kimapenzi.Wa pili anaitwa Daniel Swai.Huyu ni rafiki wa muda mrefu wa Marcelo na ni mtu wake wa karibu .Huyu ni mtoto wa mfanya biashara mmoja tajiri.Watu hawa wawili endapo unaweza kuwapata watakuongoza aliko Marcelo.Nina uhakika mkubwa lazima wanafahamu chochote kuhusu mahala aliko Marcelo.Find them and make them talk!!! Akasema Boaz Austin alihisi kama nyundo kubwa imekipiga kichwa chake baada ya kumsikia Monica akitajwa na Boaz kama mtu anayepaswa kutafutwa aeleze aliko Marcelo.Alistuka vile vile kusikia kwamba Marcelo na Monica wana mahusiano. “Austin !! akaita Boaz baada ya kuona Austin haongei chochote “Najua ninachokuomba ukifanye si kitu chepesi na hukuwa umekitarajia lakini sina namna nyingine zaidi ya kukuomba msaada.Tafadhali nisaidie katika hilo kijana wangu” akasema Boaz na Austin akainamisha kichwa akazama mawazoni “Please help me son” akasema Boaz.Austin akainua kichwa na kusema “Ulilipa kiasi kikubwa cha pesa kunikomboa kutoka mikono ya Alshabaab.Wewe ni sababu ya mimi kuwa hivi nilivyo leo.Umenipokea na kunijumuisha katika familia yako.Wewe ni mtu wa thamani sana kwangu na kwa ajili hiyo basi nitaifanya kazi uliyonipa” “Ahsante sana Austin.Thank you so much my son.Sipati neno zuri la kukushukuru.Ninaamini kwa uwezo ulio nao unaweza kabisa kulikamilisha suala hili ndani ya muda mfupi ili niweze kupata pesa zangu .” Akasema Boaz kwa furaha “ Mr Boaz uchunguzi wangu utaanzia kwa hao watu wawili uliowataja ambao wana ukaribu na Marcelo lakini kabla sijaifanya kazi yangu nataka uwe na uhakika.I want you to be 100% sure that one of them or both knows where Marcelo is.
I dont want 97%,98% or 99% I need 100% .Sitaki kumuumiza mtu asiye na hatia.So mr Boaz I’m going to ask you again are you sure these two people knows where Marcelo is? Boaz akavuta pumzi ndefu na kumtazama Austin kisha kwa sauti yenye kitetemeshi akasema “ I’m not 100% sure but just do it son.These two are the only lead to Marcelo.Take them and use whatever methods you know to make them talk and show us where Marcelo is.Nina uhakika lazima kuna kitu wanakifahamu kuhusiana na Marcelo.Austin you are my family and the money I’m talking here belongs to our family.So do this for our family.What I have is yours too so do whatever you can to find this bastard Marcelo.He’s somewhere hiding here in Dar es salaam.” Akasema Boaz .Austin akamtazama kwa makini na kusema “Ni vipi endapo baada ya kuwahoji nitajiridhisha kwamba wawili hawa hawafahamu chochote kuhusu Marcelo? “Endapo hawafahamu chochote hakuna haja ya kuwacha kill them all...” akasema Boaz .Austin akainama akawaza kidogo halafu akasema “Mr Boaz,nitaifanya hiyo kazi kama ulivyoniomba lakini nataka nikuweke wazi kwamba haitakuwa kazi rahisi kama unavyodhani.Itachukua muda lakini kuna kitu kimoja ambacho nataka nikuombe.Nataka ufanye kila uwezalo kuhakikisha kwamba Maria anaondoka hapa nchini haraka iwezekanavyo.Ikiwezekana hadi kufikia kesho jioni awe amerejea afrika ya kusini.This place is dangerous for her” “Kwani rais amekupa kazi gani Austin? Akauliza Boaz
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kuna kazi yake binafsi ninamfanyia.Si kazi kubwa lakini kama unavyoelewa historia yangu watu waliotaka kuniua bado wako hapa hivyo wakifahamu kwamba niko hai na nimerejea watatafuta kila namna ya kuniangamiza kwa hiyo hapa nilipo nimezungukwa na hatari kubwa.Sitaki Maria adhurike au aingie katika hatari.Naomba umuondoe haraka sana” “Ok sawa niachie suala hilo nitalishughulikia na kesho Maria atarejea afrika ya kusini.Ahsante sana kwa kumjali mwanangu.By the way Austin,tumia kiasi chochote cha fedha unachokihitaji toka katika akauti ya kampuni na endapo kuna msaada wowote unahitaji usisite kunieleza” “Sawa mzee nitakapohitaji chochote nitakujulisha” “Austin ahsante sana .Nitakuwepo hapa Dar hadi jambo hili litakapokamilika kwa hiyo nitakuwa nikija hapa mara kwa mara kukutazama.Vipi kuhusu mawasiliano? Tayari umekwisha pata laini ya simu ili kurahisisha mawasiliano apana bado sijapata laini ya simu kama unavyofahamu laini zote huwa zinasajiliwa na mimi si raia wa Tanzania kwa hiyo kuna ugumu wa mimi kupata laini hata hivyo nitajitahidi ”Marcelo akadanganya “Usijali nitakufanyia mpango wa laini simu kesho.Nadhani tumeelewana.Twende sasa sebuleni ili Maria asipate wasiwasi.Tafadhali naomba usimueleze chochote kuhusiana na kazi hii.Hatakiwi kufahamu kama umerudia tena kufanya kazi hizi” akasema Boaz wakarejea sebuleni. “Austin ahsante sana kwa kutupokea na kutukaribisha japokuwa tumekuja bila taarifa.Maria amefurahi kukuona na kiu yote aliyokuwa nayo imekwisha baada ya kujua uko salama.Hana hofu tena.Si ndiyo Maria?akasema Boaz na Maria akatabasamu “Kwa hiyo Austin sisi tunaondoka,tutapanga tena siku ya kuja kukutembelea ila utakapomaliza shughuli zako urejee mara moja Afrika ya kusini”
“Dady !! .Maria akahamaki kwa kauli ile ya baba yake na kusimama “ Tumekuja kumtazama Austin ,kwa nini tukimbie? Sijaonana na Austin kwa zaidi ya wiki tatu ,nina mambo mengi ya kuongea naye kwa hiyo siondoki sasa hivi.Kama wewe una haraka ya kuondoka nenda kaendelee na shughuli zako mimi ninabaki hapa na Austin atanirejesha hotelini baadae” akasema Maria “Maria we have to leave now.Tumekuja bila taarifa na kwa kuwa tayari tumekwisha onana naye tumuache aendelee na shughuli zake hadi kesho tutakuja kumtembelea tena.” Akasema Boaz “ No day ! you can go I’m staying here !! akasisitiza Maria.Austin akainuka na kumuendea “It’s ok my love you can go now.Mimi na wewe tutapanga tena siku nyingine ya kuonana” Maria akapatwa na mshangao kwa kauli ile ya Austin akashindwa aseme nini.Akawatazama Austin na baba yake kwa zamu “Austin what’s going on?Why aren’t you happy to see me? “Are you hiding something ? Akauliza Maria kwa ukali “I’m not hiding anything from you my love.Kama alivyosema mzee tutawasiliana na tutapata nafasi nzuri ya kuongea yale yanayotuhusu” akasema Austin.Kwa hasira Maria akachukua pochi yake ndogo na kutoka kwa kasi kuelekea garini huku akilia.Boaz na Austin wakatoka hadi katika gari wakaagana na Austin akafungua geti gari likaondoka “Maria tafadhali usilie my princess.Haikuwa vizuri kwa sisi kuendelea kukaa pale kwa muda mrefu wakati Austin ana ratiba zake nyingine hasa ukichukulia kwamba kilichomleta huku ni masuala ya kifamilia.” Akasema Boaz wakiwa garini baada ya kuondoka nyumbani kwa Austin.Maria aliyekuwa ameinama akainua kichwa na kumtazama baba yake kwa hasira na kuuliza “Whats going on dady? Kitu gani ulichoongea na Austin na hamkutaka kunishirikisha? na halafu mlipomaliza ukanitaka tuondoke mara moja wakati unafahamu kabisa kwamba nimesafiri toka Dubai kwa ajili ya jambo moja tu la kuja kuonana na Austin.Why you didn’t let me spend time with the man I love? Why dady? Akauliza Maria.Boaz akakohoa kidogo na kusema “Maria there is one more thing you have to know” “Whats that? Akauliza Maria “Kesho utaondoka kurejea Afrika kusini.Anatakiwa mtu wa kuwepo kule kusimamia biashara zetu.Kwa hiyo nitafanya utaratibu wa ndege kesho na utarejea nyumbani mara moja.Najua nitakuwa nimekuumiza kwa hili and I’m so sorry” akasema Boaz “What?!! Dady that cant happen.
Whats going on? Kuna kitu gani wewe na Austin mnakificha? Je Austin ndiye aliyekushauri hivi? Toka awali nilipomueleza juu ya mimi kuja Dar es salaam alipinga vikali na hata leo aliponiona hakuonyesha kufurahi.I need to know the truth,whats going on? Why Austin is here? Whats he doing here? Akaulza Maria “Haya si mawazo ya Austin bali ni mimi ndiye niliyeamua hivyo.Kuhusu kazi anayofanya Austin hapa Dar es salaam ni mambo yake binafsi ya kifamilia ambayo hatuwezi kuyaingilia .The guy has done a lot for us so we have to respect him whe he needs a privacy” akasema Boaz.Maria hakuongea tena akaendelea kulia kwa kwikwi.Boaz aliumia lakini hakuwa na namna nyingine ya kufanya “Lazima kuna jambo linaloendelea hapa kati ya baba na Austin ambalo hawataki nilifahamu.Toka mwanzo Austin alipinga vikali nisije Dar na hata leo aliponiona alionyesha wazi kutokufurahishwa na ujio wangu.Wakaenda kuongea kwa siri bila kunishirikisha kitu ambacho si cha kawaida na kama hiyo haitoshi naambiwa kwamba kesho natakiwa kuondoka kurejea afrika ya kusini.Kuna nini kinaendelea hapa ambacho ninafichwa? Mimi si mtoto mdogo wa kushindwa kung’amua kwamba kuna kitu kinaendelea hapa na ndiyo maana ninaondolewa haraka haraka.Ninaanza kuhisi kama vile baba ameanza kumtumia Austin katika kazi zake .
I Must find out the truth.Usiku huu nitarejea tena huku nyumbani kwa Austin” akawaza Maria *********************** Baada ya akina Boaz kuondoka Austin alirejea ndani kama mtu aliyerukwa na akili .Moja kwa moja akaelekea katika kabati kulimohifadhiwa chupa za mvinyo akachukua moja na kumimina katika glasi akagugumia yote “ Aaaaggghhhh !!!! akatoa ukelele wa hasira “ Hii si ndoto bali ni kitu cha kweli kabisa.Sikuwahi kufikiri kama siku moja ningeweza kujikuta nikiwa njia panda kama sasa.Kumbe ni Boaz anayetaka kumuua Marcelo? Ni vigumu sana kuamini.Imekuwa bahati sana Marcelo hakujitokea kwani endapo angefahamu yuko hapa hivi sasa tungekuwa tunaongea mambo mengine ” Akawaza Austin na kuvuta pumzi ndefu akamininina tena mvinyo akanywa “Marcelo anatafutwa kwa udi na uvumba na Boaz na ninatakiwa nihakikishe ninawapata Monica na Daniel ili wanieleze mahala aliko Marcelo.Boaz anataka nimtese malkia wa Afrika.Anataka nimuumize mtoto mzuri kama Yule ambaye hana hata chembe ya mkwaruzo.Boaz ananiweka katika mtihani mgumu sana” Kichwa cha Austin kilijaa mawazo mengi na mara akakumbuka kwamba anatakiwa kwenda Rozana night club kuonana na Job Israel “Sikutaka kujihusisha katika suala la Marcelo lakini nimejikuta nimeingia katika suala hilo bila kutaka.Ninahisi kuja Tanzania ulikuwa ni mpango wa Mungu ili niweze kuwaokoa watu wake wasio na hatia kama hawa akina Marcelo.Ngoja kwanza niliweke pembeni suala hili hadi hapo baadae nitakaporejea na kuongea na Marcelo ili niupate ukweli.Naamini kuna sababu kubwa iliyopelekea Boaz anitake nimsake kwa kila namna niwezavyo.Lazima nikiri jambo hili limenitikisa sana ndani ya dakika hizi chache.Nimewekwa kati kati ya watu wawili wa muhimu .Rais Ernest amemtoa mdogo wangu kutoka kifungoni nchini
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
China kama malipo kwa kazi anayotaka nimfanyie ambayo ni kuhakikisha ninapata sampuli toka kwa Monica kwa ajili ya kufanya kipimo cha vinasaba ili kujua kama ni mwanae au vipi kwa hiyo natakiwa kumlinda kwa namna yoyote ile.Kwa upande wake Boaz ameniokoa kutoka katika mikono ya Alshabaab kwa kulipa kiasi kikubwa cha fedha.Amenikaribisha katika familia yake na amenitunza kama mwanae wa kumzaa lakini malipo ya kila alichonifanyia ni kumuua Monica mwanamke ambaye hana kosa lolote.Nimesimama kati kati na itanilazimu nifanye maamuzi magumu.Ngoja kwanza niachane na jambo hili niende Rozana club kuonana na Job.Nitatafakari na nitapata ufumbuzi ila siwezi kuifanya kazi ya Boaz” Austin akaelekea katika chumba cha Marcelo. “Rais ameondoka tayari? Akauliza Marcelo “Hapana hakuwa rais bali ni mlinzi wake kuna maagizo alipewa aniletee” “Still no word from David? Akaulzia Marcelo “Hapana bado” akasema Austin.Marcelo akashika kichwa ishara ya kukata tamaa “Marcelo ninatoka kidogo kuna sehemu ninakwenda.Nitakaporejea tutakuwa na mazungumzo mazito.Usimfungulie geti mtu yeyote Yule.Nitakuachia kifaa ambacho kitakuwezesha kuona picha za kamera zote zilizofungwa hapa .Mimi pia ninacho kifaa cha kuniwezesha kujua kila kinachoendelea hapa kwa hiyo endapo kutakuwa na tatizo lolote hapa nyumbani nitajua na nitakuachia simu ambayo tutawasiliana nitakuelekeza nini cha kufanya.” Austin akaenda chumbani kwake kujiandaa na kisha akamuaga Marcelo akaondoka. “Bado mwili unanitetemeka kwa kuwaona Boaz na Maria.Sikuwa nimetarajia kabisa kuwaona .Nilimkatalia ombi lake la kuja Dar es salaam na kama haitoshi nikakata kabisa mawasiliano naye lakini kwa kumtumia baba yake ameweza kunipata.Imekuwa rahisi kwa Boaz kujua mahala nilipo kwani amewasiliana moja kwa moja na rais akamuelekeza nilipo.Ninachojiuliza Maria ana fahamu kinachoendelea? Anafahamu mipango ya baba yake? Naanza kuhisi kama vile mimi na Maria tunaelekea katika sintofahamu kubwa.
I love her and I don’t want anything happen to us.So what am I going to do? Tell her the truth what I’m doing here? No I cant do that.Ngoja tu niachane naye.Siwezi kumweleza ukweli wa ninachokifanya hapa Tanzania.” Austin akaendelea kuwaza ********************* Ni siku iliyokuwa na pilika pilika nyingi kwa Monica.Alikuwa na mizunguko kadhaa vile vile alikuwa na vikao mbali mbali.Hadi giza linaingia tayari Monica alikuwa amechoka sana.Saa tatu kasoro dakika nane alitoka ofisini akaenda katika gari lake na kuondoka kuelekea nyumbani “Niliwaahidi baba na mama kuwa ningeenda kuonana nao jioni ya leo lakini nimechoka sana nitakwenda siku nyingine.Ninahitaji mapumziko” Monica akastuliwa mawazoni na simu yake iliyoita.Akatazama mpigaji alikuwa ni David Zumo “Oh ! its David.Siwezi kuzungumza naye sasa hivi wakati ninaendesha .Nitampigia nikifika nyumbani.Leo nataka anieleze mahala aliko Marcelo.Nahitaji sana kuonana naye kujua hali yake” akawaza Monica huku simu ikiita na kukata,akatabasamu baada ya sura ya David kumjia kichwani. “Inaonyesha tayari David ameanza kuzama kichwani kwangu.I feel like I’m missing him.The way he was holding me gently,the way he kissed me,oh gosh ! it was so lovely.Should I say I’m luckt to have him? Akajiuliza. “Ndiyo ninaweza kusema ninayo bahati.Mwanaume kama David ukitoa utajiri wake ana mambo mengi ambayo kila mwanamke anayapenda.Kitandani nampa digrii tano.Ni mjuvi wa mambo.Mapenzi anayafahamu.Ana pumzi kama farasi.Alinipeleka hadi nikahisi kutaka kupoteza fahamu.Au inawezekana ni kutokana na ugeni wangu katika mambo haya ya mapenzi?
Lakini pamoja na ugeni wangu katika mapenzi lazima nikiri David is a real man.Alinifikisha mahala ambako sikuwahi kufika.Kila mara ninapokumbuka mambo tuliyoyafanya mwili wote hunisisimka na kwa uchovu huu nilio nao natamani kama ningefika nyumbani na kumkuta David akinisubiri” akatabasamu “It looks like I’m going crazy.Kumbe mapenzi matamu kiasi hiki.Naweza sema bado sijachelewa kwani subira yangu ndiyo iliyonifanya nikutane na David.Endapo ningekuwa tayari nina mpenzi au tayari nimeolewa leo hii nisingekuwa najianda kuolewa na mtu mkubwa kama David zumo tajiri namba moja Afrika” Safari nzima Monica alikuwa akiwaza mambo mengi kuhusu maisha yake yatakavyokuwa.Aliwasili nyumbani kwake akawajulia hali watumishi wake wote halafu akaelekea chumbani kwake akachukua simu na kumpigia David Zumo. “Hallow mpenzi “ akasema David Zumo mara tu alipopokea simu “Hallow mpenzi” akasema Monica na kumfanya David astuke na kuvuta pumzi ndefu “Hatimaye umeniita mpenzi.Mungu mkubwa .Ahsante sana Monica.Niliisubri kwa hamu kubwa siku ambayo ungewez kuniita hivyo na leo imetimia” akasema David.Uso wa Monica ukachanua kwa tabasamu “Kwa nini nisikuite hivyo David wakati tayari nimekwisha ufungua moyo wangu kwako? Tayari nimeukubali ukweli kwamba mimi na wewe tumeumbwa ili tuwe pamoja.Vipi hali yako? Anaendeleaje Pauline? “Sisi huku tunaendelea vizuri,hofu ni kwako wewe.Sijui kwa nini kila wakati ninakuwa na hofu sana juu yako huko uliko.Natamani ungekuwa karibu ili nikuone kila wakati na nihakikishe uko salama.Monica una hakika uko salama? Monica akatabasamu na kusema “Usihofu David niko salama.” “Nafurahi kusikia hivyo.Vipi wazazi hawajambo? Umewaeleza kuhusu sisi? Wamesemaje? Akauliza David “Wazazi hawajambo na tayari nimewaeleza kila kitu na hawana tatizo.Wanajiandaa kuupokea ugeni utakaoutuma kama ulivyoahidi” “Ahsante .Nimefurahi kupita maelezo.Vipi maendeleo yako kwa ujumla?Kazi zako zinakwendaje? “Kwa ujumla kila kitu kinakwenda vizuri.Leo hii nilikuwa na vikao kadhaa kufanya maandalizi ya ujenzi wa ile shule.Bado naendelea kukushukuru sana kwa msaada wako ule mkubwa kwa ile shule” “Usijali Monica.Nitakuunga mkono katika miradi yako yote unayofanya kwa jamii.U mwanamke wa pekee kabisa” akasema David na ukimya mfupi ukapita “David !! Monica akaita “Naam malaika wangu” “Samahani ,sikupokea simu yako uliponipigia nilikuwa barabarani” “Usijali mpenzi.Hata mimi nilihisi hivyo.Hivi bado unaendesha gari mwenyewe? Hauna dereva wa kukuendesha ? Unaendesha gari la namna gani? “Ndiyo ninaendesha mwenyewe.Madereva wapo lakini napenda kuendesha mwenyewe.Gari ninayoendesha ni Marcedece benz.” “ Ouh Monica,unatarajia kuwa malkia wa Congo kwa hiyo unapaswa kuanzia sasa kuendesha gari la hadhi ya kimalkia.Najua hili hulipendi lakini naomba unipe nafasi ya kukuhudumia Monica.
Mtu kama wewe unatakiwa uendeshwe katika gari lenye hadhi kubwa kama Limousine au uwe na helkopta yako.” “Ahsante David kwa kunijali .Si kwamba ninakataa usinihudumie lakini kwa muda huu mfupi kabla ya kufunga ndoa niruhusu niendelee na maisha yangu ya kawaida.Tutakapokuwa tayari katika ndoa utakuwa ni mfalme wangu na kila utakalolisema litakuwa ni amri kwangu.” “Sawa Monica” akasema David.Ukimya mfupi ukapita tena “David” akaita Monica kwa sauti laini “Unasemaje Monica? “Nahitaji kuonana na Marcelo.Umewasiliana na rais wa Tanzania akakuelekeza mahala alikohifadhiwa? “Samahani kwa kutokufahamisha mapema juu ya jambo hili lakini leo sikuweza kuzungumza na rais Ernest.Nimemtafuta sana kutwa nzima ya leo bila mafanikio.Nadhani ni kutokana na mambo yanayoendelea Tanzania kwa sasa ndiyo maana imekuwa vigumu kumpata.Nitamuwahi kesho asubuhi na mapema halafu nitakujulisha.Usihofu mpenzi utaonana na rafiki yako kwani yuko salama .Je utamsaidiaje dhidi ya watu wanaotaka kumuua? “Bado sina mpango wowote hadi hapo nitakapoonana naye ndipo tutapanga kwa pamoja.Kwa sasa nahitaji sana kuonana naye” “Sawa Monica ila kumbuka endapo utahitaji msaada wowote katika suala hili mimi niko tayari kukusaidia” “Ahsante sana David” akasema Monica wakaendelea na maongezi mengine ya kuhusu maisha yao,kila mmoja akamueleza mwenzake historia ya maisha yake lengo kubwa likiwa ni kufahamiana vizuri zaidi.Baadae wakaagana “Oh my gosh ! David is so sweet.Ana sauti nzuri anaongea toka moyoni.Utatamani uendelee kumsikiliza usiku mzima.Anajua kubembeleza .Hapa nilipo mwili wote unanichemka baada ya kuongea naye.Huku sirini nahisi kama vile ..mhh !! Monica akaupeleka mkono sirini “ oh no ! I’m so wet !!. Haraka haraka akainuka na kuingia baduni kuoga “Baada ya kuongea na David nahisi kama ninahitaji kufanya mapenzi.” Akawaza huku akiendelea kuoga “This is very serious. I real need a man.What am I going to do ? Hizi ndizo athari za kuyajua mapenzi ukubwani.” Akawaza “Nitaiondoaje hali hii na mwanaume wangu yuko mbali? Laiti kama David angekuwa karibu ningemfuata usiku huu huu.Natakiwa kutafuta namna ya kuidhibiti hali hii endapo itanitokea kwa wakati huu ambao niko mbali na David vinginevyo nitateseka mno kila mara itakaponitokea kama hivi nitesekavyo sasa.Sikuwahi kutokewa na hali hii kabla sijayaanza mapenzi lakini kwa sasa baada ya kuingia rasmi katika ulingo wa mapenzi ni wazi kwamba hali hii itaendelea kunitokea tena na tena.” Akawaza akiendelea kuoga. “Niliwahi kusikia kwamba kuna vifaa ambavyo unaweza ukatumiwa mwenyewe kujiridhisha pale ambapo unashikwa na hamu ya kufanya mapenzi na mpenzi wako yuko mbali nawe lakini vile vile nasikia athari zake ni kubwa na endapo utazoea mchezo huo ni hatari kubwa.Nitafanya nini basi? Nitafute mwanaume wa kuwa naye kwa siri kwa wakati huu ninaosubiri kuolewa na David?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hili linaweza lisiwe wazo zuri lakini inaweza ikawa ni njia nzuri ya kunisaidia kuondokana na hali hii.I don’t want to fali in love .I want a man only for sex and nothing else.Nitakapoolewa na David nitaachana naye” akawaza na kuondoa sabuni mwilini na kuzama tena mawazoni “Mawazo gani haya yanaanza kunijia kichwani? Jambo kama hili ni ktendo cha usaliti kwa David.Ni vipi endapo atagundua kwamba ninaye mwanaume mwingine? Nitajuaje kama hajaweka watu wa kunifuatilia na kuchunguza maisha yangu? Natakiwa kuwa makini sana ama sivyo nitajikuta ninaharibu kila kitu.Lakini je nisipofanya hivyo nini litakuwa suluhisho la hali hii? Kwa vyovyote vile itakavyokuwa lazima nipate suluhisho la jambo hili kwani bila kufanya hivyo nitateseka mno.Suluhu peke hapa ninayoiona ni kutafuta mwanaume wa siri kwa ajili ya kazi moja tu ya kuniridhisha kila pale ninapokuwa na hamu ya kufanya mapenzi ila kama nikifanya hivyo inatakiwa nilifanye jambo hilo kuwa siri yangu kubwa.” Monica akatoka ndani ya jakuzi na kujifunga taulo akarejea chumbani “Daniel ananipenda lakini siwezi kumpa mwili wangu mtu kama Yule mwenye wanawake karibu kila kona ya jiji.Marcelo ambaye tayari nilianza kuvutiwa naye lakini matatizo yake ni kama haya kwanza ni mgonjwa halafu yuko mafichoni.Who else? Hao wawili ndio ambao kidogo akili yangu iliwahi kuwafikiria” Mara akakumbuka kitu na kutabasamu “There is this new handsome guy from south Africa,Austin.Ni kijana mzuri.Japokuwa simfahamu tabia zake laini ni kijana mzuri mtanashati na ,mstaarabu .
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment