“There is this new handsome guy
from south Africa,Austin.Ni kijana mzuri.Japokuwa simfahamu tabia zake laini ni
kijana mzuri mtanashati na ,mstaarabu .Yule jamaa nahisi anaweza akanifaa kwa
sababu kwanza yeye si mkaazi wa hapa,makazi yake ni afrika kusini kwa hiyo hata
kama nikifanya naye mapenzi hataweza kufanya matangazo na nikimtazama
anaonekana ni kijana mwelewa.Isitoshe ana hadhi yangu.Tatizo ni namna ya kuweza
kumpata kwani siwezi kukurupuka tu na kumfuata kumtaka tufanye mapenzi.Lazima
nitafute njia itakayomfanya ashawishike kutaka kufanya nami mapenzi.Lazima
nimsisimue.Tena nimekumbuka aliniomba kama tunaweza kutoka kwa chakula cha
usiku nikamwamia kwamba nitampa jibu.Nadhani hapo ndipo sehemu nzuri ya kuanzia
.Nitakubali kutoka naye kesho nitamchunguza nimfahamu ni mtu wa aina gani ”
akatabasamu “Nadhani sasa nimepata muafaka na suluhisho la tatizo hili.Austin
anaweza kunifaa.Najua sintakuwa namfanyia vizuri David lakini sina namna
nyingine ya kufanya vinginevyo nitaikuta nimezidiwa na kufanya mambo mengine
yasiyofaa.” Akachukua simu yake na kumuandikia Austin ujumbe mfupi wa kukubali
ombi lake la kupata chakula usiku pamoja. Taratibu Monica akajilaza kitandani
na kuanza kuutafuta usingizi alikuwa amechoka sana **************** Austin
alikaribia sana kufika Rozana night club ukaingia ujumbe katika simu yake
akapunguza mwendo wa gari na kuufungua akausoma kisha akatabasamu.Ujumbe ule
ulitoka kwa Monica ambao ulisomeka “Dinner tomorrow. 8 Oclock” “Thank you
Monica.Good night” Austin akaandika uumbe na kuutuma kwa Monica “Mambo yanazidi
kukaa sawa.Monica amekubali ombi langu la kukutana naye kwa chakula cha
usiku.Hii ni hatua kubwa na nzuri katika kuikamilisha kazi ya rais.Wakati mambo
yangu yanakwenda vizuri Boaz na Maria wameibuka na wanataka kuharibu kila
kitu.Hapana siko tayari kuifanya kazi ya Boaz.Eti nimteke Monica na
kumtesa.Sintokubali kumgusa malaika Yule.Lazima nitafute namna ya kumlinda
kwani hivi sasa tayari amekwisha anza kuwindwa na Boaz.Naona kuna mgogoro
mkubwa unanukia kati yangu na Boaz.Nikiingia katika mgogoro na Boaz moja kwa
moja nitakuwa nimeingia katika mgogoro na Maria.Dah ! sikutaka jambo kama hilo
litokee lakini endapo itabidi iwe hivyo sintakuwa na namna nyingine zaidi ya kuingia
katika mgogoro.Vyovyote itakavyokuwa lazima nimlinde Monica” akawaza Austin
huku akipunguza mwendo akakata kushoto na kushika ujia ulioeleka Rozana night
club.Kulikuwa na idadi kubwa ya watu na magari kutokana na klabu hii kutoa
huduma ya burudani kwa saa ishirini na nne.Alielekea sehemu ya maegesho
akaegesha gari na kushuka akaangaza huku na huku kuhakiki usalama akaridhika
kila mtu alikuwa na hamsini zake “Pamechangamka sana mahali hapa.Burudani zipo
za kutosha” akawaza Austin akaingia klabuni na kupanda ngazi kuelekea ghorofani
kama alivyokuwa amekubaliana na Job.Watu walikuwa ni wengi ndani ya klabu na
viti vyote vya kaunta vilijaa.Austin akapiga jicho pande zote na kuwaona watu
wawili wakiinuka katika mojawapo ya meza iliyokuwa karibu na kaunta akaenda
kuketi.Muhudumu aliyevalia nadhifu akafika haraka haraka na kumudumia kinywaji
akaendelea kunywa taratibu huku akivuta muda akimsubiri Job.Mara akashikwa bega
na mtu akageuka haraka haraka na kuiona sura iliyomstua “Jo......!!” akataka
kusema neno lakini Yule mtu akaweka kidole mdomoni ishara ya kumtaka anyamaze
halafu akamfanyia ishara kwa kichwa amfuate.Austin akainuka na kuangaza pande
zote kisha akamfuata Yule mtu “Haya ni kama maajabu.Kweli Job ni jasusi wa hali
ya juu.Mchana ni kichaa lakini usiku ni mtanashati namna hii kiasi kwamba ni
vigumu hata kumtambua.Mchana anavaa matambara na usiku anavaa suti kali .Dah !
amenifurahisha sana kwa hii staili yake .Huyu haswa ndiye mtu ninayemuhitaji
katika operesheni hii” akawaza Austin na kuendelea kumfuata Job aliyeelekea
katika maegesho ya magari ,akaingia katika gari moja jeusi,Austin naye akaingia
katika gari lake na kuondoka akilifuata gari alilopanda Job Walivuka daraja la
Nyerere na kuingia Kigamboni halafu wakaelekea eneo la mto Kazi.Kwa kutumia kifaa
cha kufungulia toka mbali Job akalifungua geti na kuingia ndani,Austin naye
akafuata kisha geti likajifunga “Hapa ni wapi? Nani anaishi katika jumba hili
kubwa? Austin akajiuliza maswali mara baada ya kushuka garini “Karibu Austin”
Job akasema na kumfanyia ishara Austin amfuate wakaelekea hadi katika sebule
kubwa ambayo karibu samani zake zilikuwa zimefunikwa na ilionyesha wazi kwamba
hakukuwa na mtu aliyekuwa akiishi pale.Job akafunua kitambaa kilichofunika sofa
na kupukuta vumbi “Karibu uketi Austin” “Job,first of all ,tell me what is this
place? Nani anaishi hapa? Why are we here? Akauliza Austin “Relax
Austin,utafahamu kila kitu lakini kabla ya yote kuna jambo nataka kufanya”
akasema Job akatoka pale sebuleni na baada ya kama dakika tano akarejea akiwa
na kompyuta ndogo akaiweka mezani akaiwasha na kuanza kubonyeza halafu
akamgeukia Austin “Austin karibu sana .Utanisamehe kwani humu ndani hakuna
kinywaji chochote.No body lives here” “Job you are amazing.How can ....” Kabla
Austin hajamaliza alichotaka kukisema Job akadakia “I know what you want to
say.I’m not crazy Austin.I repeat I’m not crazy” akasema Job huku akitabasamu
“Hii ni nyumba yangu ya siri.Hakuna anayeishi humu ila huwa ninakuja mara kwa
mara hasa nyakati kama hizi au wakati nina kazi za kufanya” “Umewezaje kufanya
hili likawezekana na watu wasikutilie shaka? Akauliza Austin “Hahahaa!!!.Austin
umenisahau kwamba mimi ndiye Job.Kwa kifupi tu ni kwamba imenilazimu kuishi
katika maisha haya kwa miaka mitatu sasa na nmekuw anikija hapa mara kwa mara
nyakati za usiku.Kila ni japo hapa huwa nachukua tahadhari kubwa.Ninazo kamera
saba za siri ambazo nimezitega kwenye miti katika njia ya kujia hapa ambazo si
rahisi kuonekana .Niingiapo hapa ndani huwa ninafuatilia kamera zote za njiani
kuhakiki kama hakuna anayenifuatilia.Kwa hapa nyumbani pekee ninazo kamera kumi
na tatu na hata niwapo kule kwa kaka huwa ninaweza kujua kila kinachoendelea
hapa kupitia kifaa kidogo mithili ya simu ninachotembea nacho kila sehemu.”
Akasema Job na kumuonyesha Austin mfumo mzima wa kamera ulivyo “That’s
good.Kumbe umejizatiti haswa.” Akasema Austin “Nilinunua shamba hili toka kwa
mama mmoja wa kiarabu ambaye kwa sasa anaishi Oman.Sikuwahi kumueleza mke wangu
juu ya shamba hili .Ni eneo kubwa la ekari ishirini na saba.Kuna nyumba saba za
waliokuwa watumishi wa huyo mama na niliponunua sikuwaondoa watu hao bali
niliboresha zaidi makazi yao na kuwapatia kila mmoja sehemu ya kulima na kufuga
kwa hiyo hawa pia ni walinzi wengine wazuri wa nyumba hii.Kwa hiyo Austin hayo
ndiyo maelezo mafupi ya nyumba hii.Vipi unaendeleaje na maisha yako? Unaishi
wapi kwa sasa? Akauliza Job halafu akamtazama Austin na kutikisa kichwa huku
akitabsaamu “Nikikutazama siamini kama kweli ni wewe Austin.Nilipokuona leo
nilipatwa na mstuko mkubwa nikadhani labda ni mzimu wako umenijia kwani
sikutegemea kabisa kukuona tena katika maisha haya kutokana na taarifa ya
mwisho niliyoipata kuwa ulipotea wakati wa operesheni ya kuwakomboa wale
watanzania waliotekwa na Alshabaab nchini Somalia.Welcome back to life brother..”
akasema Job huku akicheka.Austin naye akacheka kidogo na kusema “I’m back to
life.They wanted me dead but now I’m back to haunt them.I’ll haunt each soul
that signed for my death !! akasema Austin kwa hasira “What real happened
brother? Please tell me how you survived” akasema Job akavuta pumzi ndefu
akainama akawaza halafu akasema “Nilipata tetesi nikiwa katika kozi fupi nchini
Korea kusini kuwa mke wangu Monalisa ana mahusiano na mwanaume
mwingine.Sikuzipuuza tetesi hizo na nilipanga kufanya uchunguzi wangu pindi
nitakaporejea nyumbani.Baada ya kumaliza mafunzo na kurudi nyumbani nilimkuta
Monalisa akiwa na gari lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia
mbili.Nilistuka na kuuliza alikopata gari lile akanieleza kuwa amechukua mkopo
benki na ameanza biashara ya madini inayomuingizia fedha nyingi na faida
anayoipata ndiyo iliyomuwezesha kununua gari lile la kifahari.Ni kweli alikuwa
na ofisi yake ya kununua na kuuza madini ya vito.Sikutaka kuonyesha wasi wasi
wowote bali nilianza uchunguzi wangu kimya kimya ili kubaini
ukweli.Nilipochunguza nikagundua kwamba ni kweli Mona alikuwa na mahusiano na
mtu mmoja anaitwa Dogo Bill.Huyu ni mfanya biashara bilionea na jina hilo
alipewa kutokana na kupata utajiri mkubwa akiwa bado kijana mdogo.Jina Dogo Bill
lina maamisha Dogo Bilionea.Jina lake halisi ni Eliah Mkobweka.Niliendelea
kufanya uchunguzi na kugundua kuwa huyu Dogo Bill ndiye aliyemnunulia gari lile
na ndiye aliyempa mtaji wa biashara ya madini.Niliumia sana hasa nikikumbuka
nilikotoka na Monalisa.Nilikwenda mbali zaidi na kugundua kuwa Dogo Bill ni
mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya Afrika mashariki na
kwa kiasi kikubwa utajiri wake unatokana na biashara hiyo.Niligundua kuwa huyu
jamaa anaifanya biashara hiyo kwa siri kubwa kiasi cha kuwa vigumu kumfaham
kuwa anahusika na biashara hiyo.Nilikwenda mbali zaidi nikagundua kuwa kuna
mtandao ambao unafanya kazi ya kuteka watu toka mikoa mbalimbali kuwaua na
kisha hutengeneza nyaraka Bandia za kuonyesha kuwa ni watu kutoka mataifa ya
nje na husafirisha maiti hiyo kwenda nje ya nchi.Maiti hiyo hutolewa kila kitu
ndani na kujazwa dawa za kulevya kisha husafirishwa.Kila mwezi maiti zaidi ya
kumi zimekuwa zikisafirishwa kwenda nje ya nchi zikiwa zimejaa dawa za
kulevya.Mtandao huu ni mpana na umesambaa katika sehemu zote muhimu na ndiyo
maana hadi leo hii hakuna yeyote aliyewahi kuripotiwa kukamatwa kwa jambo
hili.Kilichonistua zaidi ni kwamba kuna watu watatu wakubwa kabisa waliokuwa
karibu na rais ambao nao wanajihusisha na biashara hii.Primusi Buke aliwahi
kuwa waziri alifariki kwa maradhi ya kansa ya ini,Philipo Muro alifariki kwa
ajali ya gari na ambaye yuko hai mpaka sasa ni msaidizi wa rais anaitwa Wilson
Mukasha.Sina hakika kama rais anamfahamu huyu msaidizi wake ni mtu wa namna gani
kwani kama angemfahamu naamini asingekubali kumuweka karibu yake.” Austin
akasimama kwa mstuko alioupata “Vipi Austin mbona umestuka? “Umesema Wilson
mukasha? Akauliza “Ndiyo,unamfahamu? Akauliza Job lakini Austin hakujibu kitu “
Austin !! akaita Job “ Umestuka baada ya kumtaja Wilson Mukasha ,unamfahamu?
“yes I know him” akajibu Austin “Wakati nikiendelea na uchunguzi wangu ili
kubaini mambo mengi yanayohusiana na mtandao huo,kuna kosa moja nililifanya
ambalo lilisababisha niingie katika hali hii” akanyamaza akashusha pumzi na
baada ya muda akasema “Niligundua kwamba ndani ya mtandao ule kulikuwa na watu
wengine wakubwa zaidi ya akina Mukasha.Usiku moja niliondoka kuwahi jambo
Fulani linalohusiana na uchunguzi niliokuwa naendelea kuufanya kumbe nilifanya
kosa moja kubwa.Nilisahau kuuficha ushahidi wote nilioupata kuhusiana na
mahusiano ya Monalisa na Dogo Bill.Huku nyuma Mona aliweza kugundua kuwa
ninamchunguza baada ya kuuona ule ushahidi.Sikurejea nyumbani usiku ule na
niliporejea oh my gosh !!..” Job akanyamaza “What happened Job? Akauliza Austin
“My wife and my daughter were already gone.Aliondoka na kila ushahidi niliokuwa
nimeupata kuhusu yeye na dogo Bill.I was left alone.Kwa kuwa simu yake tayari
nilikuwa nimeiwekea program maalum ya kurekodi mawasiliano yake yote
anayoyafanya niliweza kusikia mazungumzo ya mwisho kati yake na dogo Bill,Mona
akimfahamisha Bill kwamba tayari nimegundua kuhusu mahusiano yao na Bill
akamwambia kwamba wakati umefika kwa yeye kuondoka kwani kama angeendelea kukaa
kwangu mambo yao yote yangeharibika.Mwisho alimuuliza Mona kama yuko tayari
kuachana nami na bila kigugumizi Mona akajibu kuwa yuko tayari.Bill akamwambia
kwamba aanze kujiandaa anatuma watu kwenda kumchukua.Mwisho kabisa
alimhakikishia Mona kwamba asihofu nitashughulikiwa na sintakuwa kikwazo tena
kwao.Hayo ndiyo yalikuwa maongezi ya mwisho ya mke wangu na simu yake
ikazimwa.Haikuwahi kupatikana tena hadi leo hii na sielewi yeye na mwanangu
wako wapi.Kwa mujibu wa mipango yao kilichokuwa kinafuata ilikuwa ni kunimaliza
na kwa mtandao wao namna ulivyo mkubwa lazima wangenimaliza haraka sana hivyo
ikanilazimu kujifanya nimerukwa na akili.Wengi walistushwa mno kwa hali ile ya
ghafla lakini hakuna anayeufahamu ukweli .Wote wanajua kwamba nilipatwa na
uchizi baada ya kuachwa na mke wangu.Ndugu zangu walinichukua wakanipeleka kwa
mganga wa kienyeji kutibiwa wakiamini kuwa nimerogwa.Waliuza nyumba na vitu
vyangu vyote yakiwamo magari mawili kwa kigezo cha kupata hela ya kunitibu
lakini fedha yote waligawana wakijua kuwa mimi ni kichaa.Baada ya kuona kuwa
sipati nafuu wakanihamishia kule kwa kaka ninakoishi na hakuna hata mmoja
anayenijali tena.Wote wanajua kuwa tayari mimi ni kichaa na sintopona
tena.Pamoja na hali yangu hiyo lakini nimekuwa nikiendelea na uchunguzi wangu kimya
kimya” akanyamaza na kumeza mate “Unaendelea na uchunguzi upi? Akauliza Austin
“Ukiacha wewe ,kuna mtu mwingine mmoja ambaye anafahamu kuwa mimi si
kichaa.Anafahamu kuwa nini niko hivi nilivyo na ndiye ambaye ananisaidia katika
uchunguzi.Naendelea kumchunguza Dogo Bill na mtandao wake ili nipate taarifa za
kutosha kabla ya kuamua kufanya kitu.Mtu huyo ambaye ninashirikiana naye
anaitwa Amarachi Inyike.Ni raia wa Nigeria lakini kwa sasa anao uraia wa
Tanzania na anajulikana kama Winifrida Osward ama Winnie kama
alivyozoeleka.Ninaye rafiki yangu mmoja anaishi nchini Nigeria aliniomba
nimsaidie dada yake ambaye aliwahi kutekwa na kundi la Boko Haram akakaa
msituni kwa miaka sita hadi yeye na wenzake sitini walipookolewa na majeshi ya
serikali.Akiwa msituni,Amarachi aliozwa kwa mmoja wa kiongozi wa wanamgambo hao
na akazalishwa mtoto mmoja.Kwa miaka sita wakiwa msituni walikuwa wanapewa
mafunzo mbali mbali ya kijeshi wakiwaandaa kuja kuwa wanamgambo wa kikundi
hicho.Walifundishwa namna ya kutengeneza na kutega mabomu,kutumia silaha nzito
za kivita,mbinu mbali mbali za medani,kwa ujumla waliandaliwa kuwa magaidi na
walikuwa wameiva barabara.Baada ya kukombolewa na kurudishwa uraiani,maisha ya
Amarachi hayakuwa mazuri na yenye furaha.Jamii iliwatenga na hakuna aliyetaka
kuchangamana nao.Mtoto wa Amarachi aliuawa na watu wasiojulikana kwa madai
kwamba ni damu ya magaidi na siku moja naye angekuwa gaidi.Zaidi ya mara tatu
Amarachi alinusurika kuuawa lakini alijinusuru kutokana na kuwa na uwezo mkubwa
wa kujihami” Job akanyamaza kidogo halafu aakendelea “Nilipoombwa na kaka yake
nimsaidie sikusita kufanya hivyo ikanilazimu nimuandalie nyaraka za kuweza
kumuingiza na kumuwezesha kuishi nchini Tanzania.Kaka yake ni mtu mwenye uwezo
mkubwa kifedha hivyo akamjengea hoteli kubwa hapa Dar inaitwa Silver peak hotel
.Amarachi au Winnie ndiye pekee ambaye amekuwa akinipa msaada kila ple
ninapohitaji.Ninapohitaji kuja hapa ni yeye ambaye huja kunichukua katika
sehemu tuliyoipanga kukutana na hunileta huku nikafanya kazi zangu kisha
hunirudisha .Amejitahidi kwa kadiri alivyoweza na amefanikiwa kujenga urafiki
na dogo Bill na hivyo amekuwa akimchunguza lakini mpaka sasa hajawahi kumuona
Bill akiwa na mke wangu Mona au hata kumtaja jina.Bado haijulikani kama Mona
yuko hapa nchini au ameama nchi.Sijui kama yuko hai au amekufa lakini sitaki
kuumiza kichwa kujua hali yake bali akili yangu ni kwa mwanangu Millen.Kwa
kumtumia Amarachi nimeweza kupata taarifa nyingi za kuhusiana na mtandao wa
akina Bill.Kwa ufupi hayo ndiyo yaliyonisibu na kunifanya niishi maisha kama
haya lakini kilichomo moyoni mwangu ni kisasi kibaya sana.Nataka niumalize
mtandao huu nikianzia na dogo Bill lakini nimechelewa kufanya hivyo nikitaka
kwanza kufahamu alipo mwanangu Millen.Nitakapopata taarifa za uhakika za mahala
alipo mwanangu wingu jeusi litatanda Dar es salaam kwani nitalisimamisha jiji
wakati nikiwashugulikia watu hawa waliosababisha nikaishi maisha
haya.Ninachofikiria kukifanya ni Mungu pekee anayefahamu.” “Pole sana Job.Haya
ndiyo madhira tunayokutana nayo katika kazi zetu hizi.Tunajitoa mno kwa ajili
ya kupigania usalama wa nchi yetu lakini kinachotupata ni majuto matupu.Mara
nyingi huwa ninawaza na kujuta kwa nini niliingia katika kazi hii.Sikuwahi
kufikiria eti siku moja nitaukana uraia wangu na kwenda kuishi nchi za
ugenini.Naamini hata wewe haukuwahi kufikiri kuwa iko siku ambayo utaishi kwa
kujifanya kichaa.Lakini haya yote yanasababishwa na watu wachache waliomo
katika madaraka.Ukigusa maslahi yao they make your life a living hell” akasema
Austin .Ukapita ukimya “Tell me why are you here Austin? What are you doing
here? Aren’t you scared of them anymore? Akauliza Job.Austin akainuka na kwenda
kufunua pazia akachungulia nje baada ya muda akageuka na kumtazama Job “Niko
hapa kwa kazi maalum” akanyamaza kidogo halafu akasema “Kwa sasa mimi ni meneja
wa kampuni ya A.A Safaris ltd nayomilikiwa na baba mkwe wangu.Ninaishi maisha
mazuri nchini afrika kusini.Sikuwa nimepanga kurejea Tanzania tena au kufaya
tena kazi hizi lakini nilipigiwa simu na rais Ernest Mkasa akaniomba nirejee
Tanzania kuna kazi anataka kunipa.Sikuwa tayari kwa hilo lakini akanieleza
jambo moja kuwa mdogo wangu Linda amefungwa nchini China kwa kosa la kujaribu
kuingiza dawa za kulevya nchini China.Ernest aliahidi kunisaidia kumtoa mdogo
wangu gerezani endapo ningekubali kumfanyia kazi yake.Kwa ajili ya mdogo wangu
nilikubali kurejea Tanzania kuifanya kazi ya rais.Kama alivyoahidi alifanya
kila aliloweza na mdogo wangu akatolewa gerezani kwa hiyo ni zamu yangu kufanya
kazi yake” akanyamaza kidogo baada ya sekunde kadhaa akaendelea “Ernest Mkasa
rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anataka nimsaidie kupata sampuli toka
kwa mwanamke mmoja ambaye ameelezwa kuwa ni mwanae,kwa ajili ya kufanay kipimo
cha vinasaba kubaini kama kweli ni mwanae.Tayari nimeianza kazi hiyo ambayo si
ngumu na nina uhakika wa kuikamilisha ndani ya kupindi kifupi kijacho lakini
ndani ya kazi hiyo kumejitokea tena kazi nyingine ambayo ni kubwa zaidi na
ambayo imenibadili msimamo wangu na kunirudisha tena kazini” akatulia kidogo
halafu akaendelea “Nilikueleza awali kuwa sababu kubwa ya mimi kutaka kuawa ni
baada ya kugundua mpango wa kumuua rais Ferdinand.Kuna kikundi kijulikanacho
kama Alberto’s ambacho kimesambaa katika sehemu mbalimbali za dunia.Historia ya
kikundi hiki kuna kiongozi mmoja wa kanisa aliyeitwa Alberto aliwahi kufukuzwa
katika kanisa lake baada ya kuchochea uasi ndani ya kanisa kwa kutaka yafanyike
mabadiliko ambayo hayapo katika imani ya kanisa hilo. Mambo ambayo Alberto
alitaka yakubaliwe na kanisa ni kuwaruhusu makasisi na watawa kuoa na
kuolewa,kukubaliana na kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.Utoaji Mimba,matumizi
ya mihadarati n.k.Aliyekuwa kiogozi wa kanisa kwa wakati huo hakufurahishwa na
jambo hilo hivyo akamvua daraja Alberto na kumtimua katika kanisa.Baada ya
kufukuzwa alianzisha kikundi chake ambacho yeye anakiita jumuiya ya Alberto au
the Alberto’s.Aliendeleza yale yaliyomfanya akafukuzwa na kanisa.Alianza kwanza
kwa kuhakikisha wakuu wa mataifa makubwa yenye nguvu wanakuwa wafuasi wake.Alberto
anatumia nguvu za giza kwa hiyo alifanikiwa kuwapata wakuu hao na mataifa mengi
makubwa ya amerika na ulaya yakakubaliana na mambo yake ,wakayapa nafasi
.Wamehalalisha mapenzi na ndoa za jinsia moja,utoaji mimba,matumizi ya
mihadarati n.k.Baada ya kusambaa katika sehemu kubwa ya dunia Alberto’s
walielekeza nguvu zao bara la Afrika ambako walianza ushawishi kwa viongozi wa
mataifa ya Afrika wakiyatumia mataifa makubwa .Rais aliyekuwa madarakani wakati
huo Ferdinand alikataa kata kata kushawishiwa na ndiyo sababu ya kifo chake ili
nafasi ya rais ishikwe na mtu wanayemtaka wao” Austin akanyamaza na kumtazama
Job “Sikufahamu chochote kuhusu suala hili” akasema Job “Si rahisi kufahamu
kwani ni mambo yanayokwenda kwa siri kubwa na kwa kiapo kikali hivyo yeyote
anayethubutu kwenda kinyume adhabu yake ni kifo” “Dah !” akasema Job kwa
mshangao “Kabla ya kuianza kazi ya rais nilitaka kufahamu kama naye ni mmoja wa
Alberto’s.Awali aligoma kunijibu lakini baadae akakiri kuwafahamu Alberto’s ila
yeye si mmoja wao.Alinieleza kwamba Alberto’s walitumia nguvu yao wakamuweka
madarakani ili waweze kumtumia katika kazi zao mbali mbali.Kwa ufupi ni kwamba
rais Ernest yuko pale kama picha tu hana maamuzi yoyote.Anapangiwa kila kitu na
Alberto’s.Makamu wa rais,waziri mkuu,mawaziri na wakuu wa vyombo vya usalama
wote ni watu wa Alberto’s.Karibu sehemu zote za muhimu Alberto’s wamezishika
.Alberto’s pia tayari wamewaweka katika himaya yao asilimia kubwa ya wabunge na
hii inawafanya wawe na nguvu kwani miswaada yote yenye manufaa kwao itapita
kirahisi bila matatizo yoyote.Wanatumia pesa nyingi kila mwezi kuwalipa wabunge
hawa” akasema Austin kisha akanyamaza akavuta pumzi na kusema “Baada ya
kujihakikishia kwamba nchi iko mikononi mwao waliandaa muswaada wa sheria ya
haki za binadamu muswada ambao ndani yake una kipengele cha kutambua haki za
wapenzi wa jinsia moja,haki za utoaji mimba ,haki za watumia mihadarati
n.k.Muswada huo ulitarahjia kuwasilishwa bungeni hivi karibuni na kwa sababu
tayari Alberto’s wana idadi kubwa ya wabnge basi muswada huo ungepita kirahisi
na kuwa sheria.Nilimsoma Ernest hakuwa amependezwa na kitendo cha yeye kuwa
kama rais picha asiye na maamuzi kuhusu masuala ya nchi.Niliona namna
alivyokuwa na hamu ya kuondokana na jambo hilo.Niliamua kutumia fursa hiyo vizuri
kwa kumpa darasa kuhusu athari za Alberto’s na nini kitatokea kwa kizazi
kijacho endapo ataacha Alberto’s waendelee kuiongoza nchi hii.Aliona msingi wa
kile nilichomueleza na akakubali kuungana nami kupambana na Alberto’s.Haikuwa
kazi rahisi kumshawishi lakini nashukuru Mungu alikubali na kitu cha kwanza
nilichomtaka akifanye ni kuufuta muswada ule usipelekwe bungeni na badala yake
uandaliwe muswada mwingine unaotaja kuwa ni kosa la jinai kujihusisha na
mapenzi au ndoa ya jinsia moja,matumizi ya mihadarati na utoaji mimba.Jambo la
pili nililomtaka alifanye ni kumvua wadhifa waziri mkuu na kulivunja baraza
lote la mawaziri ili ateue wapya ambao si wafuasi wa Alberto’s.Tatu nilimtaka
amuondoe mkuu wa majeshi na nikamshauri mtu wa kumpa nafasi hiyo ambaye
ninamuamini ni mzalendo wa kweli.Ernest alikubaliana na mawazo yangu yote na
tayari amekwisha yafanyia kazi.Muswada umefutwa,waziri mkuu ameondolewa,baraza
la mawaziri limevunjwa,mkuu wa majeshi ameondolewa na kwa haya aliyoyafanya
tayari ametoa tamko la vita kati yake na Alberto’s” Austin akamtazama Job
aliyekuwa ametulia akimsikiliza.Job akavua koti “Ninahisi joto.Mambo haya si
mambo madogo.Ni mambo mazito mno” akasema Job “Ni kweli haya si mambo
madogo.Hii ni vita kubwa lakini tumeamua kuipigana kwa ajili ya nchi yetu,kwa
ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.Ni vita ngumu lakini lazima tuipigane huku
Mungu tukimtanguliza mbele.Alberto’s ni mtandao mkubwa na wenye nguvu ,wana
uwezo wa kufanya jambo lolote kwa wakati wowote wanaotaka kwa hiyo mimi na mheshimiwa
rais tayari tumeyatoa maisha yetu kupambana na mashetani hawa na lolote
litakalotokea tuko tayari.Tumeanza mapambano kwa kuukata mzizi mkuu wa
Alberto’s hapa nchini ambao ni ofisi ya rais.Hii ni sehemu waliyokuwa
wakitegemea mno .Tumekata mzizi mwingine ambao ni waziri mkuu na baraza la
mawaziri.Tumekana mzizi mwingine ambao ni mkuu wa majeshi.Haya yote yamefanyika
katika kipindi kifupi na kuwastua sana Alberto’s.Pamoja na mizizi hiyo mikubwa
kukatwa bado kuna kazi kubwa inatakiwa kufanywa.Makamu wa rais ni mfuasi wa
Alberto’s na kibaya zaidi hata mke wa rais naye ni mfuasi wa mtandao huu.”
“Even first lady??!! Job akashangaa “Ndiyo.Tena yeye ndiye aliyetumiwa
kumshawishi Ernest akubali kuwa rais” “Kama ni hivyo basi mheshimiwa rais yuko
katika hatari kubwa!! Akasema Job “Ni kweli rais yuko katika hatari kubwa sana
na muda wowote kitu chochote kinaweza kufanyika.Kabla ya kutoa hotuba yake ile
aliyotangaza kulivunja baraza la mawaziri,watu wawili asiowafahamu waliingia
chumbani kwake wakiwa na bastora na kumtisha asihutubie lakini kwa kuwa tayari
amekwisha jitoa mhanga akaamua kuhutubia.He’s in great danger.Na hilo ndilo
hasa lililonifanya nikakutafuta .Tayari nimeongea na rais nikamfahamisha hatari
inayomkabili na yeye mwenyewe ameiona hatari hiyo kwa hiyo tumeshauriana
kufanya jambo moja.Nitaunda kikosi kidogo cha watu wenye weledi mkubwa katika
masuala ya usalama kwa ajili ya kumlinda rais.Alberto’s wamesambaa kila kona
kwa hiyo hata walinzi wake wa sasa wanaweza wakatumika kumuua kwa hiyo kwa
kutumia mamlaka yake atawaondoa walinzi wake wa sasa na tutaweka walinzi wapya
tutakaowateua .I need you in that team.” Akasema Austin.Job akacheka kidogo na
kusema “Austin you’re my brother.Mimi na wewe tumetoka mbali .Umenifundisha
mambo mengi .I respect you so much but I cant be part of that team” “C’mon
Job.This is serious. I need you” akasisitiza Austin “No Austin” akajibu Job
“Kwa nini Austin? Wewe ni mmoja wa watu wachache ninaotaka kushirikiana nao
katika hii vita.Hii vita si ya kwangu na rais pekee bali tunapigana kwa ajili
ya nchi yetu kwa hiyo ungana nami tafadhali.Nakuhitaji sana uwepo katika kikosi
cha kumlinda rais.Huyu ndiye mwangaza wetu katika mapambano haya hivyo
anatakiwa alindwe.Ikitokea rais akauawa kabla hatujaimaliza vita hii then we’re
done.The war will be over.Ili tusifike hapo tunatakiwa kumlinda rais kwa nguvu
zetu zote.” Akasema Austin “Austin ninaelewa unachokisema na niko tayari
kusaidiana nawe katika mapambano haya lakini naomba nisiwe sehemu ya timu ya
kumlinda rais.Nitakusaidia katika upande mwingine” “Sikia Job.Vita hii si vita
nyepesi.Inahitaji watu wenye ujuzi na uzoefu wa hali ya juu katika mapambano
kama haya na mmoja wa watu hao ni wewe” akasema Austin na kuinamisha kichwa
kisha kwa sekunde kadhaa halafu akamtazama Job “Kuna jambo ambalo sikuwa
nimekueleza bado ambalo labda linaweza kukushawishi ukakubaliana nami” “Jambo
gani hilo? Akauliza Job “Hata mimi sikuwa nalifahamu ni rais ndiye aliyekuja
kunieleza.Ni kwamba katika kila nchi ambayo rais wake ni mfuasi wa Alberto
anapaswa kuhakikisha anawalinda na kuwawezesha wafanya biashara wakubwa wa dawa
za kulevya wafanye biashara yao kwa uhuru bila kubughudhiwa na chombo chochote
cha usalama.Hiki ni chanzo kikubwa cha mapato kwa Alberto’s kwani wafanya
biashara hao walio chini yao hutoa kiasi kikubwa cha fedha kama mchango wao kwa
ajili ya kuendesha jumuiya.Ernest mkasa naye akiwa chini ya Alberto’s alipewa
sharti hilo na amelitekeleza na ndiyo maana utaona katika kipindi cha uongozi
wake biashara ya dawa za kulevya imeshamiri sana hapa nchini.Hii ni kwa sababu
wafanya biashara hawadhibitiwi na wako huru kufanya biashara zao.Nilimtaka
anipe orodha ya wafanya biashara hao ili tuweze kupambana nao na ameahidi
kunipatia orodha hiyo .Baada ya kuisikia historia yako ninahisi kuna uwezekano
mkubwa hata huyo dogo Bill aliyepelekea ukaishi katika maisha haya naye yumo
katika hiyo orodha .It’s tme to fight back.Ni wakati wetu wa kuwa huru.Hatuwezi
kuwa huru endapo hatutawaondoa wale wote waliotufanya tuishi maisha ya namna
hii ,wale ambao wameibinafsisha nchi hii na kuifanya yao,hatutakuwa huru endapo
hatutafanikiwa kuwaondoa Alberto’s hapa nchini.Mpaka lini nitaikimbia nchi
yangu? Makaburi ya wazazi wangu yako hapa Tanzania kwa hiyo hata kama
nitabadili uraia lakini sintaweza kuibadili damu ya Tanzania.Lazima mambo haya
yafike mwisho na yatafika mwisho endapo tutaweza kuwaondoa Alberto’s na mizizi
yake hapa nchini.Nani wa kuwaondoa Alberto’s hapa nchini? Ni mimi ,wewe na
wazalendo wengine wachache walio tayari kuifia nchi yao.Tunaweza tusifanikiwe au
tusifike mbali katika vita hii lakini tukianzisha tutaungwa mkono na watu wenye
nia njema na nchi hii.Naomba usiogope Job,hii ni nafasi ya pekee imejitokeza
ambayo itakusaidia kulipiza kisasi kwa wale wote waliofanya maisha yako kuwa
hivi pia kupata ukweli kuhusu mke na mtoto wako walipo.This is our chance
brother” akasema Austin .Michirizi ya machozi ikaonekana machoni mwa Job
“Austin umenichoma mno moyo wangu na kuyaamsha tena machungu niliyonayo dhidhi
ya Dogo Bill na kundi lake.Wamenifanyia unyama mkubwa kuniachanisha na mke
wangu.I loved Mona so much lakini kwa tamaa ya pesa akachagua kunikimbia.You
are right.Its pay back time.Austin nitaungana nawe katika haya mapambano lakini
si kwa kuingia katika timu ya kumlinda rais.Nataka niwe pembeni yako tupambane
kwa pamoja.Nitakusaidia kutafuta watu watakaounda hicho kikosi cha ulinzi wa
rais.Nataka niwepo katika uwanja wa mapambano na nihakikishe ninamkamata dogo
Bill kwa mikono yangu mwenyewe.Nikubalie kwa hilo Austin” akasema Job .Austin
akamtazama kwa muda halafu akatabasamu na kumpa Job mkono “Karibu katika
operesheni fagio.Tunakwenda kufagia nchi hii na kuuondoa uchafu wote na
kuifanya safi tena kama ilivyokuwa awali enzi za waasisi wetu” akasema Austin
“Mungu atusaidie “ akasema Job “Austin baada ya kuwa tumekuwa kitu kimoja
naomba sasa unipe mikakati yako namna ulivyopanga kuiendesha operesheni
hii.Lakini kabla hujanieleza chochote nina ombi moja kwako” “Omba chochote Job”
akasema Austin “Ahsante sana.Naomba ukubali kumuingiza Amarachi katika operesheni
hii.She’s a great asset to us” Austin akakuna kichwa akafikiri kidogo halafu
akamtazama Job “ Job I have to be honest with you.Hii ni opereseni tofauti sana
na nyingi ambazo tumewahi kuzifanya kwa hiyo napata ugumu kidogo kulikubali
ombi lako.Tunakwenda kupambana na adui mwenye nguvu na mbinu nyingi kwa hiyo
tunahitaji kuwa na watu wenye uwezo mkubwa kama wewe.Zaidi ya yote I cant work
with people I don’t trust” akasema Austin “Nafahamu msimamo wako Austin lakini
naomba uniamini ninachokwambia.This woman is wonderfull.Ana uwezo mkubwa kiasi
cha kunishangaza hata mimi .Nakuhakikishia anaweza kuwa na msaada mkubwa
kwetu.She’s well trained .Please let her in” Austin akafikri tena kidogo na
kusema “Sawa Job ,nimekuelewa lakini kabla sijaamua chochote kama nimjumuishe
ama vipi I’ll have to talk to her in person. I want her to understand how
important this mission is for me,you and for our nation” akasema Austin “Thank
you”akajibu Job “Ningetaka sasa nifahamu mikakati yako kuhusiana na suala hili”
akasema Job “Kitu cha kwanza tunachotakiwa kukifanya ni kutafuta namna ya
kumlinda rais.Nguvu aliyonayo ni msaada mkubwa sana kwetu kwa hiyo lazima
tumlinde kwa nguvu zetu zote.Tunatakiwa haraka sana tupate kikosi kipya cha
kumlinda.Kwa sasa tunaendelea kujipanga ,nitakapomaliza kazi aliyonipa rais
tutakaa pamoja na kujadili nini cha kufanya na wapi kwa kuanzia.” Akasema
Austin “Austin we have to make things faster.Tukizidi kuchukua muda mrefu
tutawapa nafasi ya kujipanga na wakatuzidi maarifa.Naamni hivi sasa watakuwa katika
mstuko mkubwa kwa hili lililotokea so we have to take them by surprise.Tusiwape
nafasi” akasema Job “Uko sahihi Job,lakini watu hawa wamejiimarisha sana na
mizizi yao tayari imesambaa katika sehemu kubwa kwa hiyo basi inabidi tukae
chini tujipange namna ya kuwakabili.Kwa pamoja tutaamua namna bora ya kuwandoa”
Austin akanyamaza kidogo na kusema “Job kuna jambo lingine ambalo nadhani
itakuwa vyema endapo ukilifahamu.Ukiacha kazi aliyonipa rais ya kutafuta
sampuli kutoka kwa Monica,alinipa pia kazi nyingine.Alinitaka nikamtoe
hospitali daktari mmoja aliyekuwa katika hatari ya kuuawa anaitwa Dr
Marcelo.Mtu huyu alipigwa risasi lakini kwa juhudi za madaktari waliyaokoa
maisha yake.Watu waliotaka kumuua bado waliendelea kumfuata hadi hospitali na
kutaka kummaliza ndipo rais aliponitaka nikamtoe kwa siri.Nilifanikiwa kwa hilo
na Dr Marcelo niko naye mahala ninapoishi.Leo hii nikiwa sina hili wala
lile,amekuja ghafla mpenzi wangu Maria akiwa ameongozana na baba yake Mr Boaz
.Huyu Boaz ndiye aliyenikomboa toka mikono ya Alshabaab kwa hiyo ni mtu
ninayemuheshimu na kumthamini mno.Ujio wake kwangu jioni ya leo ulikuwa ni
kuniomba nimfanyie kazi yake.Amenipa kazi ya kumtafuta Dr Marcelo na kukipata
kitabu ambacho anakihitaji toka kwake. Alinipa maelezo marefu kidogo kuhusiana
na kitabu hicho na umuhimu wake.Boaz anafahamu kuwa Marcelo anashirikiana na
watu Fulani na ndio waliomtorosha hospitali lakini hafahamu ni akina nani kwa
hiyo amenipa jukumu la kuwafahamu pia watu hao .Alienda mbali zaidi na kunitaka
niwatafute na kuwapata watu wawili wa karibu na Marcelo ambao ni Danel Swai
rafiki wa karibu wa Marcelo na Monica Benedict ambao anahisi wanafahamu mahala
aliko Marcelo.Anataka nikiwapata niwatese na waeleze wanachofahamu kuhusu
Marcelo na kisha niwaue.Huyu Monica ndiye ambaye rais anataka athibitishe kama
ni mwanae kwa kutumia sampuli aliyonipa kazi ya kuitafuta.” “Oh my God !!!
akasema Job “Nimewekwa kati kati na sasa ni jukumu langu kuamua niende upande
upi.Nikichagua upande wa Boaz ina maana nitakuwa nimemsaliti rais na mapambano
dhidi ya Alberto’s hayataweza kufanikiwa.Nikichagua upande wa rais nitaingia
katika mgogoro na mtu aliyeyaokao maisha yangu na kunifikisha hapa nilipoona
endapo nitaingia katika mgogoro na Boaz moja kwa moja nitakuwa nimeingia katika
mgogoro na Maria ambaye ni mwanamke ninayempenda kuliko wote.Hata hivyo
nimechagua kusimama upande wa rais.Niko tayari kumkosa mpenzi wangu Maria kwa
manufaa ya nchi.Haya ni maamuzi magumu sana nimeyafanya kwani mimi na yeye
tutapita lakini Tanzania itabaki daima kwa hiyo nitapigana kwa ajili ya
Tanzania.Kwa hiyo Job tuna kazi kubwa ya kufanya kumlinda Monica kwani endapo
nitashindwa kutekeleza matakwa ya Boaz lazima atatafuta watu wengine wa
kuifanya kazi yake .Sababu nyingine ya kumlinda Monica ni kwamba Alberto’s
wanaweza wakafahamu kuwa Monica ni mtoto wa Ernest kwa hiyo wanaweza wakamtumia
kama silaha katika kumlazimisha Ernest afanye yale wanayoyataka.” Austin
akanyamaza kidogo kisha akaendelea. “Jambo la pili nikwamba baada ya kulivunja
baraza la mawaziri,rais anahitaji kuunda upya baraza lingine.Kabla ya kuunda
baraza jipya anahitaji kwanza kumpata waziri mkuu.Rais amekuwa na wakati mgumu
wa kumpata mtu wa kumpa nafasi ya waziri mkuu ambaye atakuwa ni mzalendo na
ambaye si mfuasi wa Alberto’s.Jana alikuja kwangu na kunipa taarifa kuwa tayari
amefanya maamuzi nani awe waziri mkuu mpya wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
na mtu anayefikiria kumpa nafasi hiyo ni Wilson Mukasha” Job akapatwa na mstuko
mkubwa akainuka na kumsogelea Austin “No ! That can’t happen!! Akasema kwa
sauti ya juu “Hivyo ndivyo ilivyo Job.Mukasha ndiye ambaye rais amemuona anafaa
kwa ajili ya kuwa waziri mkuu mpya wa Tanzania ndiyo maana uliponitajia jina
hilo kuwa ni mmoja wa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya
nilistuka sana.” Akasema Austin “Austin rais atafanya kosa kubwa sana endapo
atamteua Mukasha kuwa waziri mkuu.Hamfahamu vizuri Mukasha ni mtu wa aina
gani.Austin you have to stop that.Do whatever you can to stop that from
happening” akasema Job na kuinamisha kichwa “Nini kinatokea kwa hili taifa?
Akasema kwa sauti ndogo halafu akamtazama Austin. “Austin we have to stop
that.Tukiruhusu rais akafanya kitu kama hicho vita hii ambayo tumejitolea
kuipigana itakuwa kazi bure.All our sacrifices will be for nothing !! “Nimekuelewa
Job lakini kuna tatizo moja .Rais anamuamini mno Mukasha.Ni mmoja kati ya watu
wachache ambao rais anawaamini mno.Ili tumzuie asifanye hicho alichokusudia
kukifanya yaani kumteua Mukasha kuwa waziri mkuu yatupasa tuwe na ushahidi wa
kutosha kumuhakikishia rais kuwa Mukasha hafai na anashiriki katika biashara ya
madawa ya kulevya.Kumueleza kwa maneno matupu hataweza kutuelewa” akasema
Austin “Austin una uhakika hata wewe ukimueleza hatakuelewa? Akauliza Job “Kwa
muda mfupi niliomfahamu rais Ernest Mkasa nimeshuhudia namna anavyomuamini
Mukasha.Hata akielezwa na nani itakuwa vigumu kumuamini bila kuwa na ushahidi
wa kujitosheleza.Hivyo basi tunatakiwa kufanya juu chini kutafuta kila aina ya
ushahidi utakaoweza kumfanya rais abadili maamuzi yake” “Hiyo nayo ni kazi
nyingine akasema Job “Ni kazi mpya ambayo lazima tuifanye.Lazima tuzuie jambo
hili lisifanikiwe.Tunapaswa kuanzia sasa kuanza kumchuguza Mukasha kwa siri.”
Akasema Austin “Kwa nini tusiutumie ukaribu wako na rais kama sehemu ya
kuanzia? Rais anakuamini kwa hiyo tafuta namna unavyoweza kuitumia nafasi hiyo
kumchunguza Muk...” “Wait .! Austin akamkatisha Job “Kuna kitu nimekikumbuka
.Wakati rais ananitambulisha kwa Mukasha alinieleza kwamba Yule ni rafiki yake
,msiri wake na ndiye aliyempa taarifa zangu.Hii ina maana kwamba Mukasha
ananifahamu vizuri na anafahamu kuwa niko kwa Boaz na ndiye aliyewasiliana na
Boaz.Nakumbuka suala la kunikomboa toka mikononi mwa Alshabaab lilikuwa la siri
kubwa kwa hiyo endapo Mukasha anafahamu basi lazima atakuwa ameelezwa na
Boaz.Lazima yeye na Boaz watakuwa na ukaribu.” Akasema Austin na kutabasamu
“Boaz ni sehemu nzuri ya sisi kuanzia kumchunguza Mukasha.Hawa wawili kuna
mambo wanashirikiana na endapo tutachimba kwa undani zaidi kuna mambo mengi
tutayagundua” akasema Austin “Boaz is your father in law,right? Akauliza Job “
Yes he is” akajibu Austin “ Umekuwa naye karibu kwa kipindi kirefu,unaweza
ukamuelezeaje? “Ninamfahamu Boaz ni mfanya biashara ambaye ni mbunifu na aliye
tayari kufanya lolote linalowezekana ili mradi biashara zake zikue.Ni mtu
mwenye ushawishi na malengo.Ni mtu mpambanaji.Toka nimefahamiana naye sijawahi
kugundua jambo lolote baya na hata biashara zake nyingi ni halali,hana rekodi
mbaya katika biashara zake ila ninafahamu kuna biashara chafu anazifanya ambazo
hajawahi kuniweka wazi ila sikutaka kufuatilia kwa sababu sikutaka kuanzisha
mgogoro na familia ile.kazi aliyoniomba nimfanyie leo imenipa mwanga kuwa Boaz
ni mtu katili na hatari.Huu ni wakati muafaka wa kumfahamu ni nani hasa”
akasema Austin Job akamtazama Austin kwa makini na kuuliza “Your girlfriend
Maria,how much do you love her? “More that I can explain.Why do you ask? “Going
after his father will complicate things between you two so I want you to be
sure of what you want to do” Austin akainamisha kichwa akatafakari kidogo
halafu akasema “Sijawahi kuzama mapenzini kama nilivyozama kwa Maria lakini kwa
maslahi ya nchi ni tayari kwa lolote” “Good” akasema Job “Ninacho chumba cha
mahojiano humu ndani ambacho tutakitumia kumuhoji Boaz.Kina zana maalum kwa
ajili ya kumfanya mtu aseme kwa hiyo nakuhakikishia Boaz akiingizwa humo lazima
atasema” “Nategemea muda wowote kuanzia kesho kuipata sampuli ninayoitaka toka
kwa Monica ambayo itatuwezesha kufanya kipimo cha vinasaba na kuupata
ukweli.Baada ya hapo tutaifungua rasmi operesheni fagio” “So tell me about this
woman Monica Benedict.Is she pretty? “C’mon Job huu si muda wa kuwaza mambo
kama hayo” akasema Austin “Its just a joke Austin” akasema Job huku akicheka
“Job nadhani tumeongea mengi na ninahitaji kuondoka kwani natakiwa kumuhoji Dr
Marcelo usiku huu.Kuna mambo ambayo nahitaji kuyafahamu toka kwake.Kabla
sijaondoka kuna jambo nataka nikuombe” “ Jambo gani Austin? “ Kwa hali ya mambo
inavyokwenda nahitaji kuhamisha makazi yangu na vile vile natakiwa kumlinda pia
Marcelo na Monica.Pale mahala ninapoishi kwa sasa tayari pamekwisha julikana
kwa kuwa katika nyumba hii hakuna mtu yeyote anayeishi unaonaje endapo nitaweka
makazi ya muda humu mimi na Marcelo? Hii ni sehemu salama na inaweza kunifaa sana”
“Hakuna tatizo lolote katika jambo hili Austin.Hata mimi nilikuwa nafikiria
jambo kama hilo Karibu tuishi sote hapa.Ni nyumba kubwa ina vyumba vya kutosha
na usalama ni mkubwa.Hata hivyo kuna jambo nataka ulifahamu” akanyamaza kidogo
na kusema “ Sintarejea tena katika maisha yangu ya uwazimu.Nimechoka kuishi
maisha yale.Nimeteseka sana Austin na ninashukuru kwa ujio wako ambao umenipa
nguvu ya kuweza kuweka nukta katika maisha yale magumu.Sikuwahi kufikiri eti
mtu kama mimi siku moja nitaweza kuokota chakula majalalani,laini imenilazimu
kufikia hali hiyo ili kuwakimbia wanaonitafuta waniue.Mwanzoni hawakuamini na
walikuwa nawaona wakinifuata na kunichunguza ili wapate uhakika kweli nimekuwa
kichaa .Walinifuatilia kwa miaka miwili ndipo walipokata tamaa wakiamini kuwa
kweli nimekuwa kichaa.Uchungu nilio nao siwezi kuuelezea Austin” Job akasema
kwa hisia kali huku machozi yakimtoka “It’s ok brother,they‘ll all pay” akasema
Austin “Sure they must pay.Kikubwa ninachokitaka kwa sana ni kufahamu aliko
mwanangu kwani mateso yote haya ninayavumilia kwa ajili yake.” “Nakuhakikishia
Job kati kati ya sinema hii utafahamu alipo mwanao” akasema Austin na wote
wakacheka “By the way,umewezaje kujenga nyumba kubwa namna hii Job? Umepata
wapi pesa? Akauliza Austin.Job akatabasamu na kusema “Niliwahi kushiriki katika
operesheni moja huko Darfur kumtafuta mtu aliyeitwa Hussein Hafidh Abdullah.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment