Huyu ni kiongozi
wa ukoo mmoja na alikuwa anatafutwa kwa kuchochea watu wa ukoo wake kuvamia na
kuwachinja kikatili watu wa ukoo mwingine.Hussen alikuwa ni mtu tajiri sana na
ilituchukua muda kufahamu maficho yake.Tulivamia nyumba yake na yakatokea mapambano
makali baina yetu na walinzi wake,kati kati ya mapambano hayo Hussein
akafanikiwa kutoroka.Tulipoipekua nyumba yake tulikuta kuna chumba kimejazwa
fedha .Hatukuacha hata senti moja.Tulikuwa watu kumi na tano,tukagawana fedha
zote na ndizo ambazo nilizitumia kujenga jumba hili kwa siri bila ya mke wangu
kujua.Amarachi ndiye aliyekuwa akisimamia ujenzi wa jumba hili wakati nikiwa
Darful hadi lilipokamilika kwa hiyo hakuna mtu wangu yeyote wa karibu
anayefahamu kuwa jumba hili ni langu zaidi ya Amarachi.Hii ni siri yako Austin
hatakiwi mtu mwingine kufahamu kwani tulichokifanya haikuwa sahihi” akasema Job
na wote wakacheka.Job akamtembeza Austin sehemu mbali mbali za jumba lile kisha
wakaagana “Usiku wa leo nitakuwa na kazi moja tu ya kufanya usafi humu ndani na
kuweka mazingira safi kabla hamjahamia humu” akasema Job ,Austin akaondoka
alipotoka kuonana na Austin,Boaz alimrejesha Maria hotelini kisha akakodisha
gari la hotelini hapo na kuondoka.Usiku huu alikuwa na miadi ya kuonana na
aliyekuwa waziri mkuu. “Austin amepewa kazi gani na rais? Amekataa kabisa
kuniweka wazi ni kazi ipi anaifanya .Ujio wa Austin Tanzania unaweza kuwa na
uhusiano na hiki alichokifanya rais Ernest? Nimefikiria sana kuhusu jambo hili
kwani baada tu ya Austin kuja Tanzania ndipo rais alipobadilika ghafla.Sina
hakika sana kuhusu jambo hilo lakini linatakiwa lifanyiwe uchunguzi .Natakiwa
kufahamu ni kazi gani ambayo Austin anaifanya hapa Tanzania.Kuna mtu mmoja tu
ambaye ninaamini anaweza kunisaidia kupata jibu.Wilson Mukasha.Huyu ni mtu wa
karibu mno na rais na nina uhakika lazima atakuwa anafahamu kazi ambayo Austin
anaifanya hapa Tanzania.Nitaongea naye baada ya kuonana na waziri mkuu” akawaza
Boaz akiwa njiani kuelekea katika makazi ya waziri mkuu aliyevuliwa madaraka
“Bado suala la Marcelo linaniumiza kichwa changu mno.Amejificha wapi?
Anashirikiana na akina nani? hii ni vita nyingine imeanzishwa ambayo lazima
niipigane ili kukipata kitabu pamoja na Austin.Kitabu kile ni muhimu mno na
endapo hatutakipata mimi na wenzangu tutakuwa katika hatari kubwa.Kwa vyovyote
vile lazima kitabu kipatikane.Kwa nini lakini Dr Richard ametufanyia hivi? Kwa
nini ametusaliti kiasi hiki? Nilimuamini mno na hakuna aliyetegemea kama siku
moja angeweza kutuuza kiasi hiki.Kwa hiki alichokifanya ni fundisho kwangu kuwa
sitakiwi kumuamini mtu yeyote tena.Unayemuamini leo huyo ndiye atakaye
kuangamiza kesho.Tulifanya kosa kubwa kumuamini Dr Richard na kosa hilo
linakwenda kutugharimu. Akaendelea kuwaza Boaz Aliwasili katika makazi ya
aliyekuwa waziri mkuu na kupokewa kwa furaha na mwenyeji wake mheshimiwa
Jeremiah “Karibu sana Boaz.Karibu tena nyumbani” akasema Jeremiah akimuongoza
Boaz katika chumba cha maongezi “Ahsante sana Jeremiah” “Hebu nipe siri yako
Boaz,miaka inazidi kusonga lakini huzeeki.Whats your secret? Akauliza Jeremiah
na wote wakacheka “Nitakueleza siku nyingine Jeremiah mzizi ninaoutumia”
akajibu Boaz “Pole sana Jeremiah kwa hiki kilichokutokea.Sote tumestuka sana
kwa mambo yanayoendelea.Nini kimemfanya Ernest akabadilika ghafla namna hii?
“Ahsante sana Boaz.Kilichotokea kimemstua kila mtu ni kitu ambacho hakuna
aliyekuwa amekitegemea.Ni jambo lililotokea ghafla sana.Hatujui ni kitu gani
kilichomfanya Ernest akabadilika namna hii.Hata hivyo tunaendelea kujipanga
kukabiliana naye” akasema Jeremiah “Mpaka sasa kuna hatua zozote mlizochukua?
Makao makuu ya Alberto’s wanasemaje? “Hicho ndicho kilichonifanya nikuite hapa
Boaz.Toka limetokea jambo hili hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya kukaa
kikao ambacho hakikuwa na suluhu yoyote ya maana ya kulikabili suala
hili.Hatujui Ernest anashirikiana na akina nani ila tunachojua ni kwamba he’s
not alone.Kikao kiliamua kulipa muda suala hili kwa ajili ya kufanya uchunguzi
kufahamu ni akina nani anashirikiana nao.Kanuni za jumuiya zinaeleza wazi
kwamba yeyoye anayekwenda kinyume au kukiuka masharti au kufanya usaliti adhabu
yake ni kuuawa lakini cha kushangaza mwenyekiti wetu kwa makusudi amezuia hilo
lisifanyike eti kwa lengo la kufanya uchunguzi kubaini watu ambao Ernest
anashirikiana nao.Huu ni upuuzi mkubwa kwani hatuna uhakika uchunguzi huo
utachukua muda gani na kipindi hicho uchunguzi unafanyika Ernest atazidi
kujiimarisha na kuitokomeza kabisa Alberto’s hapa nchini.Mimi,makamu wa rais na
mke wa rais tumekutana na kulijadili suala hilo kwa upana wake na tukafanya
maamuzi kwamba ili tuweze kuiokoa jumuiya hapa Tanzania basi mwenyekiti Obi
auawe haraka sana na kisha ifanyike kampeni na mimi nichaguliwe mwenyekiti wa
muda na hapo nitaidhinisha rais auawe mara moja.Baada ya Ernest kuuawa makamu
wa rais atakaimu nafasi ya rais kwa muda na katika kipindi hicho atakachokaimu
atatengua maamuzi yote aliyoyafanya Ernest.Ataurudisha tena ule muswada
ukajadiliwe bungeni pia atanirejeshea wadhifa wangu wa waziri mkuu na
atamrejesha mkuu wa majeshi.Hilo likifanyika sote tutakuwa salama.Biashara zenu
zote zitafanyika kwa uhuru na amani .Endapo hilo halitafanyika nakuhakikishia
Boaz kuwa hatutabaki salama.We’ll all go down.Ernest amekwisha onyesha dhamira
ya wazi ya kuifuta Alberto’s katika uso wa Tanzania.We have to act very
fast.Nimekuita hapa kukupa taarifa hiyo na kukuomba msaada wako.Nafahamu wewe
unafahamiana na watu wengi hivyo naomba unisaidie kumpata mtu atakayefanya kazi
ya kumuua mwenyekiti Obi.I need someone very professional.Can you help me with
that? Akauliza Jeremiah.Boaz aliyekuwa anasikiliza kwa makini akasema
“Nimekuelewa Jeremiah na kwangu mimi hilo si tatizo.Ninafahamu watu wengi wenye
ujuzi wa hali ya juu wa kuifanya kazi yako kwa ufanisi.Lakini nina swali moja
nini kitatokea endapo Alberto mkuu akifahamu juu ya njama hizi? Ukumbuke pia
kwamba Alberto mkuu ni mtu mwenye nguvu kubwa na uwezo wa kung’amua mambo nina
wasi wasi hata mpango huu wa kumuua mwenyekiti wenu anaweza akalifahamu na sote
tukaingia katika matatizo makubwa.Kwa upande Fulani nadhani mwenyekiti wenu
anatumia busara kwani ni wazi Ernest kuna watu anashirikiana nao na hao ndio
wanaompa ujasiri na nguvu ya kufanya hayo anayoyafanya.You have to be sure
about what you want to do Jeremiah” akasema Boaz.Jeremiah hakuonyesha
kufurahishwa na maneno yale ya Boaz akasema “Nielewe vizuri Boaz hali
imechafuka .Kila kitu kimesimama na hatujui nini mipango ya kesho ya
Ernest.Biashara yenu inafanyika na kufanikiwa kwa mwavuli wa Alberto’s na kama
Alberto’s hawapo basi hata ninyi hamtaweza kufanya tena biashara zenu.You are
nothing without us.Suala hili si langu peke yangu ni suala letu sote.Alberto
mkuu yuko Italia na sisi tuko hapa Tanzania.Hii ni nchi yetu na endapo
tutashindwa kufanya mabadiliko basi misaada itakatwa na tutawekewa vikwazo vya
kiuchumi.Taifa hili litazidi kudidimia katika umasikini.We have to fight for
our nation.Hata Alberto mwenyewe endapo atagundua na halafu akaona faida za
tulichokifanya ninaamini atatupongeza kwani lengo lake kubwa ni kuibadili dunia
na katika Afrika Tanzania ni nchi anayoipa umuhimu mkubwa mno.So are you going
to find me what I asked or not? Akauliza Jeremiah.Boaz akamtazama kwa muda
kisha akasema “I’ll find someone to do your job” “Thank you.Unadhani kufikia
lini utakuwa umempata ? “Nipe siku mbili” “Good” akasema Jeremiah na ukimya
mfupi ukapita.Boaz akasema “Jeremiah kuna jambo nimelifikiri kwa haraka haraka
na sina uhakika kama linaweza kuwa na maana yoyote kwako” “Nieleze Boaz.Kwa
hali ya sasa kila ushauri una maana kwangu”: “Baada ya kuyasikia maelezo yako
nimegundua kuwa tatizo hapa ni rais Ernest Mkasa.Kama hivyo kwa nini basi
isitafutwe namna ya kuweza kumuondoa Ernest na kumaliza matatizo yote bila ya
kumgusa mwenyekiti Obi? Hii inaweza kuwa njia muafaka kabisa ya kuepusha mambo
mengine yasitokee ndani ya jumuiya” Jeremiah akavua miwani akatoa kitambaa na
kufuta macho kisha akasema “Boaz wazo lako ni zuri na la msingi ,lakini tatizo
lililopo ni kwamba kwa mujibu wa taratibu zetu mwenyekiti wa jumuiya nchini
ndiye mwenye uwezowa kutoa ruhusa ya kumuua mtu ambaye amekwenda kinyume na
jumuiya na ndiyo maana nataka nishike nafasi ya uenyekiti ili kusitokee mkwamo
wa aina yoyote .Kwa hiyo Boaz nitafutie huyo mtu wa kuifanya hiyo kazi yangu”
akasema Jeremiah halafu wakaendelea na maongezi mengine na baadae Boaz akaondoka
kwenda kupumzika “Mhh !! hili jambo linakoelekea limeanza kunitisha.Hii ni kama
filamu ya usaliti.Dr Richard ametusaliti wenzake na kutuuza kwa mwanae
Marcelo,Ernest Mkasa amewasaliti Alberto’s na sasa Jeremiah na wenzake wanataka
kufanya usaliti mwingine kwa kwenda kinyume na makubaliano ya kikao chao cha
pamoja.Sifahamu nini mwisho wa filamu hii lakini huko tunakoelekea si kuzuri
hata kidogo.Watu wamechanganyikiwa hawafikiri sawasawa.Mimi nadhani suluhu
pekee hapa ni kumuua rais ambaye ndiye anayeonekana kuwa kikwazo.Tukiendelea
kumuacha hai hatujui nini malengo yake.I’m confused!! Akawaza Boaz.Kwa upande
wangu nadhani nisijiingize sana katika mambo haya ya Alberto’s bali nijikite
katika kujihakikishia usalama wetu mimi na wenzangu.Tuhakikishe kitabu kinapatikana
na papo hapo tuanze kubuni mikakati ya kuifanya biashara yetu iendelee endapo
mambo hayatakuwa mazuri.Tunatakiwa tujenge uwezo wa kuendesha mambo yetu bila
ya kuwategemea sana Alberto’s.Hata hivyo nina uhakika mkubwa Alberto’s
hawatakubali kushindwa na Ernest.Nina imani huko makao makuu yao hivi sasa
watakuwa wanapanga mikakati mikubwa namna ya kufanya” akawaza Boaz na kukumbuka
kuwa alihitaji kuongea na Wilson Mukasha.Akachukua simu na kuzitafuta namba za
Mukasha akapiga “Boaz !! akasema Mukasha kwa mshangao “Hallo Wilson” “Hallo
Boaz.Nimestuka kidogo ,sikutegemea kama ungenipigia mida hii” akasema Mukasha.
“Usistuke Mukasha.Unafahamu mimi huja na kuondoka kama mvua.Samahani kwa
kukupigia mida hii .Bado uko kazini? “Hapana nimefika nyumbani muda huu”
“Poleni sana kwa mambo yaliyotokea na yanayoendelea kutokea” “Ahsante Boaz.Ni
kweli kuna upepo mbaya unavuma sasa hivi na hali si nzuri sana” akasema Mukasha
“Hicho ndicho hasa kilichonirudisha nyumbani haraka.Kwa namna mambo
yanavyokwenda unadhani yanaweza yakatulia hivi karibuni? Akauliza Boaz “Hapana
sina uhakika Boaz.Hii ni vita ngumu.Ernest amejipanga sana kwa mapambano.Ni
wakati wa kuwa waangalifu mno” “Nalifahamu hilo Wilson na tayari tumekwisha
anza kuchukua tahadhari.Wilson kilichonifanya nikupigie usiku huu ni kutaka
kufahamu jambo moja” “ Jambo gani Boaz? Ni kuhusu Ernest na Austin.Unaweza
kufahamu Ernest amempa Austin kazi gani? Boaz akauliza “Ernest ni mtu wangu wa
karibu sana na siri zake nyingi amekuwa ananieleza ila kwa hili amekuwa mgumu
kidogo kunieleza.Ni siri yake na Austin pekee kwani hata wanapozungumza
hawataki mtu mwingine awe karibu na asikie wanachokiongea.Ninachoweza kuhisi
lazima kuna jambo kubwa ambalo Austin analishugulikia kwani ilimlazimu Ernest
kulipa ujira mkubwa ili Austin aweze kumfanyia kazi yake.Kwa hiyo naweza kusema
kazi ambayo Austin anamfanyia Ernest ni kazi yenye umuhimu mkubwa sana kwa
Ernest” akasema Mukasha “Umesema kuna ujira Ernest ametoa? Ni kiasi gani
amemlipa Austin? “Ndiyo kuna ujira ametoa lakini si pesa ila kuna kitu kikubwa
amemfanyia Austin na ndicho kilichomfanya Austin akubali kuifanya kazi hiyo ya
Ernest” “Alimfanyia jambo gani? akauliza Boaz.Mukasha akavuta pumzi ndefu na
kusema “ Alimtoa Linda mdogo wake Austin gerezani nchini China.” Boaz akahisi
kama vile amemwagiwa maji ya barafu ghafla gari likayumba kidogo kwa mstuko
alioupata ikamlazimu kuegesha pembeni. “Boaz are you there? Akauliza Mukasha “
Wilson I’m....I’m just shocked.Hii ni taarifa ambayo imenistua sana.Amewezaje
kumtoa Linda? “He’s a president kwa hiyo ametumia madaraka yake kufanya hilo
liwezekane.Amebadilishana wafungwa na seriali ya China.Kwa hiyo hivi sasa Linda
yuko huru” akasema Mukasha.Boaz akavuta pumzi ndefu “Wilson nimestuka
sana.Sikutegemea kabisa kama lingetokea jambo kama hili.Yule binti anafahamu
mambo yangu mengi na anaweza akamueleza kaka yake kila kitu kuhusu mimi kuwa
ndiye niliyemuingiza katika biashara hii ya dawa za kulevya .Kwa hivi sasa yuko
wapi? “Kwa hivi sasa anaishi kwa balozi wa Tanzania nchini China” akasema
Mukasha. “Wilson tafadhali naomba unishauri nifanye nini? Linda hapaswi kuwa
huru.Ni hatari mno kwangu.Austin hapaswi kufahamu chochote kuhusu mimi na mambo
yangu.Endapo atafahamu mambo yangu basi tutakuwa maadui wakubwa na kazi zangu
nilizompa azifanye hazitafanyika.Hiki ni kipindi ambacho ninamuhitaji mno
Austin.Kuna kazi nyingi ambazo nahitaji azifanye” akasema Boaz “Boaz kitu pekee
ambacho unaweza kukifanya hapa ni kumuua Linda” “Wilson hilo si jambo rahisi
hata kidogo kwani kuingia katika ubalozi wetu na kumuua Linda si jambo
dogo.Hata hivyo niachie mimi nitajua nifanye nini.Ninahitaji kujua kitu kimoja
ambacho kinaweza kunipa picha .Wewe ndiye uliyenitambulisha kwa rais.Mimi na
yeye hatukuwa tukifahamiana.Ilikuaje hadi akafahamu kuwa mimi niko na Austin?
“Boaz I don’t think that’s necessary.Kuna mambo mengi ambayo tunapaswa
tuyajadili kwa sasa na si suala hilo” akasema Mukasha “Wilson jambo hili ni
muhimu sana kwangu.I want to know the bottom of this.I want to know how it
started? Wilson akavuta pumzi ndefu na kusema “ Ernest met with this woman...”
“ What woman? Boaz akauliza “ Anaitwa Janet mwamsole.Huyu ni rafiki wa siku
nyingi wa Ernest na huwa wanakutana mara kwa mara .Ni watu wanaofahamiana kwa
miaka mingi toka wakiwa shuleni.Baada ya kutoka kuonana na na Janet ndipo
alipotaka nimtafutie mtu mwenye sifa maalum amfanyie kazi yake na ndipo
nilipomkumbuka Austin.” Akasema Mukasha “Unadhani huyo mwanamke alimueleza nini
Ernest? Unahisi anaweza kuwa na mahusiano na hiki alichokifanya Ernest? Siwezi kuwa
na uhakika sana wa hilo labda tufanye uchunguzi” akasema Mukasha “Hakuna
haja.Tujikite katika masuala ya msingi.Kuna jambo nataka
kukufahamisha.Unamkumbuka marehemu Dr Richard? “Ninamkumbuka uliwahi
kunikutanisha naye ukatutambulisha lakini si kuwahi kuwa na ukaribu naye.”
“Usingeweza kuwa na ukaribu naye kwa kuwa wewe si mwanachama wa Alberto’s.Dr
Richard alikuwa anahusika na wafuasi wa Alberto’s pekee.Leo hii nimeipata barua
ambayo kabla hajafa alimuandikia mwanae Marcelo.Katika barua hiyo alimueleza kila
kitu kuhusu Alberto’s na sisi pia.Mwisho wa maelezo yake akamtaka ahakikishe
anapambana kufa na kupona kuwafyeka Alberto’s na sisi pia tunaojihusisha na
biashara ya dawa za kulevya.Alimuachia kitabu Fulani ambacho kina orodha ya
wafanya biashara wote wa dawa za kulevya hapa nchini ,mahala walipo ,mali zao
na hadi mtiririko wao mzima wa fedha.Dr Marcelo ametoroshwa na watu
wasiojulikana na mpaka sasa hatujui yuko wapi.Tunachofahamu ni kuwa hayuko peke
yake kuna watu anaoshirikiana nao.Kwa hiyo hivi sasa ninajiandaa kwa operesheni
nzito kuhakikisha ninampata Austin na hicho kitabu .Bila kumpata Austin au
hicho kitabu basi hatutakuwa salama.Kuna watu ambao wanajipanga kutuzimisha
kabisa” akasema Boaz “ Hizo ni taarifa za kustusha sana.Una sehemu yoyote ya kuanzia
kufanya uchunguzi huo? Akauliz Mukasha “Ninazo tetesi Fulani ambazo
ninazifanyia kazi .Nina imani ndani ya siku mbili nitakuwa na jibu la uhakika
.Ninachokuomba Mukasha endelea kufanya uchunguzi ufahamu ni kazi gani ambayo
rais amempa Austin.Ni muhimu sana kwangu” “Sawa Boaz mimi nitajaribu kufanya
uchunguzi wangu na chochote nitakachokipata nitakutaarifu” “Ahsante
Mukasha.Kuwa makini sana hasa katika nyakati hizi.Jitahidi kadiri uwezavyo
kuendelea kuwa karibu na rais ili asigundue upande wako wa pili” “Ahsante Boaz
nitajitahdi” akasema Wilson Mukasha na kukata simu.Boaz aliyekuwa ameegesha
gari pembeni ya barabara akawasha gari akaendelea na safari ya kurejea hotelini
“Habari ya Linda kutolewa gerezani ni habari ambayo naweza kusema ni mbaya
zaidi.Yule binti anafahamu mambo yangu mengi kwani nilikuwa namtumia kimapenzi
na kumuingiza katika biashara ya dawa za kulevya.Endapo akipata nafasi ya
kumueleza Austin mambo anayoyajua kuhusu mimi sijui nini
kitatokea.Ninachotakiwa kufanya kwa sasa ni kumuhimiza Austin anifanyie kazi
zangu haraka haraka na baada ya kumaliza I’ll have to kill him.Sitaki apate
nafasi ya kuonana na Linda.Nikiruhusu hilo litokee basi nimekwisha na Austin
ataniua kwani nmaamini lazima Linda amueleze kila kitu wakionana .Austin must die”
akawaza Boaz ustin alirejea katika makazi yake tayari ilikwisha timu saa saba
za usiku.Mara tu alipoingia ndani akaenda moja kwa moja kubisha hodi katika
chumba cha Marcelo.Mlango haukufunguliwa akaingiwa na wasi wasi akaitoa bastora
yake na kukinyonga kitasa mlango ukafunguka akaingia ndani.Marcelo alikuwa
amelala usingizi mzito sana.Austin akashusha pumzi,akamfuata Marcelo na
kumuamsha. “Austin you are back” akasema Marcelo kwa uchovu huku akipiga
mwayo.Austin akamtazama kwa makini na kusema “Marcelo huu si muda wa kulala
namna hiyo.Huu ni muda wa mapambano ni muda wa kukesha macho .Ni muda wa
kujilinda .Si muda wote utakuwa na mimi kwa hiyo unapokuwa peke yako unapaswa
kujilinda .Ni vipi endapo ni adui ndiye aliyegonga mlango na akaufungua bila
hata ya kustuka? Don’t do that next time” akasema Austin “Nimekuelewa
Austin.Hii imetokana na hizi dawa ninazotumia zina nguvu sana.I’m sorry it wont
happen again” akasema Marcelo “Good!!! Akasema Austin na kwenda kuketi katika
kochi dogo lililokuwamo mle chumbani “Nilikuahidi kwamba tutaongea
nitakaporejea kwa hiyo naomba unisikilize kwa makini sana.” Akasema Austin na
kumtazama Marcelo kwa makini sana akasema “Naitwa Austin January.Ni mtanzania
mwenye uraia wa Afrika kusini.Nimerudi Tanzania kwa ajili ya kazi maalum”
akatulia kidogo halafu akaendelea “Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nafanya kazi
katika idara ya usalama wa taifa kitengo cha ujasusi wa kimataifa .Nimefanya
kazi nyingi na za hatari nilizotumwa na nchi yangu.Kazi ya mwisho niliyoifanya
ilikuwa kuongoza kikosi maalum kilichokwenda kuwakomboa watanzania waliotekwa
na wanamgambo wa Alshabaab nchini Somalia.Katika operesheni hiyo nilipigwa
risasi na mmoja wa wenzangu nilioongozana nao nikatelekezwa hapo na kuchukuliwa
na Alshabaab.Kilichosababisha nitake kuuawa ni baada ya kugundua mpango wa
kumuua rais Ferdinand uliosukwa na watu ndani ya serikali” akatulia na kumeza
mate akaendelea “ Nilikombolewa toka kwa Alshabaab na mtu mmoja anaitwa Boaz
ambaye ni baba wa mpenzi wangu Maria.Kwa msaada wake nimefanikiwa kuanza maisha
mapya na yeye ndiye sababu mimi kuwa hapa nilipo leo.Sikuwahi kurejea tena
Tanzania hadi hivi sasa nilipoitwa na rais kwa kazi maalum.Jioni ya leo kama
utakumbuka nilikuomba uende chmbani kwako kwa kujua kuwa rais amekuja.Hakuwa
rais kama nilivyotegemea bali alikuwa mlinzi wake aliyekuwa ametumwa kuwaleta
wageni ambao ni Boaz na mpenzi wangu Maria.Nilistuka sana kwani sikuwa
nimewatarajia kabisa.Boaz aliniomba tuongee pembeni na akanieleza
kilichomleta.Amekuja kuniomba nimfanyie kazi yake moja.Alinieleza kwamba
aliwahi kuwa na rafiki yake anaitwa Dr Richard ambaye kwa sasa ni marehemu” “Dr
Richard ?!! ..Dr Marcelo akastuka sana “Ndiyo Dr Richard .Alisema kwamba
walikuwa na mahusiano ya kibiashara .Walikuwa na miradi ambaye Dr Richard walikuwa
na miradi kadhaa ya pamoja ambayo Dr Richard ndiye aliyekuwa msimamizi
mkuu.Alipofariki Dr Richard alimuachia majukumu yote mwanae anaitwa Dr Marcelo
.” “What??!! Dr Marcelo akazidi kushangaa “Subiri nimalize Marcelo” akasema
Austin “Dr Macelo ndiye aliyekuwa msimamizi mkuu wa miradi yote baada ya baba
yake kufariki.Kwa mujibu wa maelezo ya Boaz ni kwamba Marcelo alibadilika na
kutaka kujimilikisha miradi ile ya ubia jambo ambalo halikumfurahisha.Anadai
kwamba Aliwatuma vijana wake wakamuhoji lakini akawafyatulia risasi na wao
ikawalazimu wajibu na kumjeruhi kwa risasi akaenda kulazwa hospitali lakini
ghafla akatoweka hapo hospitali alikokuwa amelazwa na hajulikani yuko wapi
.Boaz anadai kwamba kuna kitabu ambacho Dr Richard alimkabidhi Marcelo ambacho
ndicho kina maelekezo yote kuhusiana na miradi hiyo ya ubia baina yao.Marcelo
ametoweka na kitabu hicho.Kazi aliyonipa Boaz ni kumsaka Marcelo na kuhakikisha
ninampata yeye na hicho kitabu.Kunirahisishia kazi zaidi amenipa majina ya watu
wawili ambao ana uhakika mkubwa kuwa wanafahamu mahala ulipo.Ametaka niwateke
,niwatese waonyeshe mahali alipo kisha niwaue.Watu hao ni Daniel Swai na
mwingine anaitwa Monica Benedict” “No!!...No!!...noo !! akasema Marcelo. “Let
me finish Marcelo” akasema Austin.Uso wa Marcelo ulikuwa umeloa jasho
“Nilimkubalia kufanya kazi yake kwa hiyo hivi sasa niko katika zoezi la kumsaka
Marcelo.Natumai Marcelo ambaye Boaz anamtafuta si wewe...” “Austin please dont
do it! Mimi ndiye Marcelo ambaye huyo Boaz anamtafuta.Dr Richard ni baba yangu
na kweli amekwisha fariki” akasema Dr Marcelo .Kwa dakika mbili Austin na
Marcelo wakabaki wanatazamana “Please don’t do it” akasema Marcelo huku macho
yake yakichuruzika machozi “Boaz alipomtaja Dr Marcelo nilistuka sana na
nilifahamu moja kwa moja kuwa ni wewe ila sikumueleza chochote kama
ninakufahamu.Ninachotaka unieleze kwa ufasaha kabisa historia yako na mahusiano
yako na Boaz na kama alichokizungumza Boaz ni kitu cha kweli .I need to hear
the truth..” Dr Marcelo akafuta machozi na kusema “ Baba yangu marehemu Dr
Richard alikuwa ni daktari bingwa wa saratani na vile vile alikuwa na uwezo
mkubwa katika mambo ya upasuaji.Ni daktari aliyejizolea sifa kubwa kutokana na
umahiri katika kazi yake.Alinivutia sana kwa kazi zake na mimi nikajikuta
nikivutiwa kuwa daktari .Naweza kusema kwamba sikutumia muda mwingi kuwa na
baba kwani mara nyingi alikuwa ni mtu wa kusafiri katika nchi mbali mbali mimi
muda mwingi nilikuwa masomoni.Nikiwa masomoni China nilipigiwa simu kuwa baba
ni mgonjwa sana na anahitaji kuniona.Nilirudi haraka sana kuonana naye.Hakuwa
na matumaini ya kupona hivyo akanieleza mambo kadhaa ya muhimu ambayo alitaka
niyatekeleze baada ya yeye kufariki.Alinipa vile vile kitabu alichokisema ni
mwongozo katika kazi zangu za kitabibu.Alisema kwamba kila nitakapokuwa na
tatizo lolote katika kazi yangu basi nitampata ufumbuzi wake katika kitabu
hicho.Alinipa vile vile namba za simu akasema kwamba nizipige kabla sijaanza
kukitumia kitabu hicho ili niweze kupewa maelekezo na huyo mtu aliyenipa namba
zake.Alinitaka nisikifungue kitabu kile hadi atakapokuwa amefariki.Hata baada
ya baba kufariki sikuwahi kukifungua kitabu kile wala kumpigia simu huyo mtu
aliyenielekeza nimpigie.Nilikihifadhi kitabu kile katika kasiki na sikuwahi
kukigusa hadi hivi majuzi nilipokuta kasiki langu limefunguliwa na baadhi ya
nyaraka zangu zikachukuliwa likiwemo faili langu la matibabu.Nilipochunguza
vizuri nikagundua kwamba hata kitabu hicho alichonipa baba nacho kilikuwa
kimechukuliwa.Jioni ya siku hiyo nikapigwa risasi na watu nisiowafahamu
nashukuru madaktari walifanikiwa kuokoa maisha yangu.Nikiwa hospitali nilimuona
mtu mmoja aliyewahi kuwa na urafiki na baba na ambaye aliwahi kunionya kwamba
nisiwe na mazoea naye kabisa .Niliogopa sana nikajua tayari maisha yangu yako
hatarini ikanilazimu kuomba msaada kwa mtu ambaye ninamuamini naye ni Monica
Benedict ambaye Boaz anataka umtafute umpate.” “Monica Benedict ? akauliza
Austin “Ndiyo” akajibu Marcelo “Ok endelea” akasema Austin “Nilimuomba Monica
anisaidie niweze kutoka pale hospitali bila mtu mwingine yeyote kueleza
sikutaka hata ndugu zangu wafahamu.Monica aliahidi kunisaidia lakini ghafla
akapotea na sikuonana naye tena hadi leo hii.Sielewi nini kilitokea hadi David
Zumo akapata taarifa zangu akamuomba rais wa Tanzania ambaye alikutuma wewe
ukaja kunitoa pale hospitali.Kwa hiyo Austin simfahamu Boaz ,sijawahi kumuona
na wala baba hakuwahi kunieleza au kunitajia jina kama hilo.Mambo yote
aliyokueleza siyafahamu na ninaweza kusema kwamba si ya kweli.Nakuomba
tafadhali usifanye alichokuomba ufanye.Usiwafanye chochote Daniel na
Monica,hawafahamu chochote kuhusu mahali nilipo na zaidi ya yote ni watu wangu
wa karibu mno.Naomba uniamini Austin” akasema Dr Marcelo.Austin akamkazia macho
Marcelo kwa muda kidogo na kusema “Ofcourse I believe you” “Ahsante sana Austin
kwa kuniamini” akasema Marcelo “Nilifahamu toka awali Boaz alikuwa
ananidanganya.Hapa lazima kuna jambo linaendelea ambalo Marcelo halifahamu.Kuna
jambo limefichwa katika hicho kitabu ambacho Boaz anaonekana kukihitaji kwa gharama
zozote.Boaz asingeweza kufunga safari kuja kuniomba nimfanyie kazi yake hii
kama haina umuhimu mkubwa kwake” akawaza Austin akiendelea kumtazama Dr Marcelo
“Marcelo unadhani ni nani aliingia chumbani kwako akafungua kasiki na kuchukua
kitabu na nyaraka zako nyingine? Unaweza kumuhisi mtu yeyote? Akauliza Austin
“Toka lilipotokea tukio lile nimekuwa najiulza sana nani anaweza akafanya
kitendo kile? Nimetafakari mno lakini mpaka sasa sina yeyote niyaweza kumuhisi.
“Unahisi na nani nyumbani kwako? “Ninahisi peke yangu ila ninaye mfanyakazi wa
ndani ambaye ni mtu mzima anayejiheshimu na hawezi kufanya kitu kama hicho.Huja
asubuhi na kuondoka saa kumi jioni.Hajawahi kuingia chumbani kwangu hata mara
moja.” “Huna mke? “Hapana sina” “Je mpenzi ambaye huja na kuondoka mara kwa
mara? “Hata mpenzi sina” Austin akaonekana kushangaa “ Marcelo nitafurahi
endapo utakuwa mkweli kwangu ili nitafute namna ya kukusaidia.Right now I’m
your only help. So tell me the truth” akasema Austin “Nimekueleza ukweli
Austin,sina mke wala mpenzi.Mbona unaonekana kushangaa? “Inashangaza kidogo kwa
mtu kama wewe kukosa mke au hata mpenzi. “Sikiliza Austin ,sababu ya mimi
kukosa mke au mpenzi ni kwa kwamba mimi ni mgonjwa.Ninasumbuliwa na kansa ya
damu kwa hiyo sitaki kujiingiza katika mahusiano yoyote.Ila niliwahi kuwa
katika mahusiano na msichana mmoja anaitwa Lily wakati fulani” akasema Marcelo
“Nini kilitokea? “It didn’t work” “Where is she now? Akauliza Austin “I don’t
know.Tulipoachana hatukuwahi tena kuwasiliana “ Aliwahi kuingia chumbani
kwako?Anazifahamu namba za siri za kufungulia kasiki? “Tulikuwa wapenzi kwa
hiyo chumbani kwangu kulikuwa ni kama chumbani kwake.Alikuwa akija mara kwa
mara.Kuhusu namba za kufungulia kasiki hazifahamu” Austin akafikiri kidogo na
kusema “Tell me about Monica Benedict.Una mahusiano gani naye? Are you two
dating? “Mimi na Monica ni marafki wa kawaida na hatuna mahusiano ya
kimapenzi.Nimefahamiana na Monica siku si nyingi .Daniel ndiye
aliyenitambulisha kwake na toka tulipoonana tumekuwa watu wa karibu sana.”
Akajibu Marcelo “Inavyoonyesha Boaz anazo taarifa zako zote.Kila unachokifanya
anakifahamu na ana uhakika mkubwa kwamba mmoja kati ya hawa watu wawili Daniel
na Monica anafahamu mahala ulipo.Inaonekana amekuwa anakufuatilia au ameweka
watu wa kukufuatilia kila ukifanyacho bila wewe kufahamu. Inaonekana
anachokitafuta toka kwako ni kitu kikubwa na ninahisi miongoni mwa watu wako wa
karibu kuna mtu kapandikizwa ili kukuchunguza.Unapaswa uchekeche akili na ujue
ni nani ambaye unahisi anaweza akawa ni pandikizi la Boaz? “Austin nakubaliana
nawe kwamba inawezekana katika watu wangu wa karibu kuna mtu anayenichunguza
lakini nakuomba ufanye kila uwezalo kuwalinda Daniel na Monica.Dont let anybody
hurt them especially Monica” akasema Marcelo kwa msisitizo “Nitajitahdi kadiri
niwezavyo kuwalinda hao rafiki zako lakini kuna mambo mawili ninajiuliza
.Kwanza kitabu ulichopewa na baba yako ambacho Boaz anakitafuta ambacho
kimeibwa kwako lakini Boaz hajakipata nani anacho? Ninahisi aliyekichukua
kitabu hicho hana mahusiano na Boaz na ndiyo maana Boaz hafahamu kama kitabu
hicho kimeibwa.Nini kilichomo ndani ya hicho kitabu na kukifanya kiwe na
thamani kubwa namna hii? Jambo la pili najiuliza rais wa Cngo David Zumo
ameingiaje katika suala hili? Marc......” Austin akakatishwa na mlio uliotoka
katika saa yake ya mkononi “Somebody is at the door” akasema na wote
wakashangaa “ Una miadi ya kuonana na mtu usiku huu ? akauliza Marcelo “Hapana
ni usiku mwingi tayari na sitegemei mgeni yeyote.” Akasema Austin na kuchukua
kile kifaa kidogo mithili ya simu ya mkononi alichokuwa amemuachia Marcelo
akakibonyeza na picha kutoka katika kamera zikaanza kuonekana.Kamera ya getini
ilionyesha kulikuwa na mtu amesimama,alikuwa ni mwanamke.Austin akastuka na
kuongea kwa sauti ya mshangao “ Maria?!! “ You know her? Akauliza Marcelo “
Amekuja kutafuta nini usiku huu? Akajiuliza Austin halafu akamgeukia Marcelo “
Marcelo ujio wa Maria usiku huu unanipa mashaka sana.Chukua bastora ile
niliyokupa na utajificha katika maua karibu na mlango mkubwa wa kuingila
sebuleni.You are going to cover me.” Akasema Austin wakatoka mle ndani na
kuelekea nje.Marcelo akajificha katika maua kama alivyoelekezwa na Austin na
kwa tahadhari Austin akaelekea getini.Akachungulia katika kijitundu kidogo
akamuona Maria akiwa amesimama akisubiri kufunguliwa geti.Hakukuwa na mtu
mwingine hapo karibu.Taratibu na kwa tahadhari kubwa Austin akaufungua mlango
mdogo wa geti na kutoka bastora ikiwa mkononi “Austin don’t shoot!! its me
Maria !! akawahi kujitambulisha Maria baada ya kuona namna Austin alivyotoka
pale getini. “Are you lone? “Yes I’m alone.Nililetwa na gari ya hotelini lakini
tayari imeshaondoka” akasema Maria .Austin akamtaka aingie ndani haraka na
kufunga geti “I’m sorry Austin” akasema Maria kwa sauti ya woga “Twende ndani”
akaamuru Austin na Maria akamfuata .Dr Marcelo aliyekuwa amejibanza katika maua
kama alivyokuwa ameelekezwa na Austin alihisi mwili kuingiwa baridi baada ya
kumtazama mwanamke Yule aliyekuwa ameongozana na Austin “Lilian??!! Akajiuliza
“Sidani kama ninaota.Japokuwa ni muda mrefu hatujaonana lakini macho yangu
hayanidanganyi that’s Lily.What is she doing here? Amefahamianaje na Austin?
Ama kweli milima haikutani binadamu hukutana.Baada ya miaka hii yote kupita
hatimaye leo ninakutana tena na Lily! Akawaza Marcelo .Austin na Maria
walipoingia sebuleni,Marcelo akatoka katika maua na kusogea mlangoni akajibanza
kusikia walichokuwa wanakizungumza Austin na Maria “Maria why are you here? Why
are you back? akauliza Austin mara tu walipoingia sebuleni. “Maria !!!...Her
name is Maria? Mbona mimi namfahamu kwa jina la Lilian? Halafu ana jina lingine
anaitwa Shamim” Dr Marcelo akazidi kushangaa. “Nisamehe Austin lakini
imenilazimu kurudi tena.I need answers.What are you doing here and why you
don’t want me to be here with you? What are you hiding? akauliza Maria huku
macho yake yakiingiwa machozi.Kabla Austin hajajibu kitu Marcelo akaingia pale
sebuleni.Austin na Maria wakastuka wote wakageuka na kumtazama. “Lilian !!
akasema Marcelo “Marcelo !! akasema Maria kwa sauti yenye
kitetemeshi.Alionekana kustuka na kuogopa sana. “Do you know him? Austin
akauliza kwa mshangao.Maria akaitika kwa kutikisa kichwa.Wote watatu wakabaki
wanatazama “Habari yako Lily.Habari za miaka mingi?Akasema Dr.Marcelo huku
akitabasamu kwa mbali.Kabla Maria hajafumbua mdomo wake kujibu chochote Austin
akauliza kwa mshangao “ Lilian ? Austin na Marcelo wakatazamana kisha Marcelo
akasema “Austin tunaweza kuzungumza pembeni tafadhali? “Sure” akajibu Austin
kisha wakaingia katika chumba cha pembeni chenye mlango wa kioo “Marcelo
umefahamiana wapi na Maria? Akauliza Austin “Ni hadithi ndefu kidogo lakini
mimi na Maria tuliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.Huyu ndiye mwanamke
ambaye nilikueleza kuwa niliwahi kuwa naye katika mahusiano lakini tukaachana.Ninamfahamu
kwa jina la Lily.Ni muda mrefu hatujaonana hadi nilipomtia machoni usiku
huu.Anafanya nini hapa? Akasema Marcelo.Austin alionekaa kushanagzwa na habari
ile ya Marcelo. “Huyu haitwi Lilian anaitwa Maria.Huyu ni mtoto wa Boaz mtu
anayekutafuta kwa udi na uvumba na ndiye mpenzi wangu kwa sasa.Huyu ndiye
aliyemshawishi baba yake anikomboe toka Alshabaab kwa kiasi kikubwa cha fedha”
akasema Austin na wote wakaendelea kutazamana.Marcelo akasema “Umesema anaitwa
Maria” “Ndiyo anatwa Maria” “Hii imenishangaza kidogo kwani mimi ninamfahamu
kwa jina la Lilian.Ninazihamu nyaraka zake zote zina jina la Lilian Bakile.Pasi
zake za kusafiria ,kadi zake za benki,na vyeti vyake mbalimbali vyote
vinaonyesha kwamba jina lake ni hilo.Kitu ambacho kilisababisha mimi na Lily
kushindwa kuelewana na hatimaye kutengana ni pale nilipogundua kuwa ana pasi
nyingine ya kusafira yenye jina la Shamim.Nilipohoji kuhusu hilo ukaibuka
mkwaruzano na tukatengana.Nimestuka kidogo kusikia anaitwa Maria. ” Akasema
Marcelo Austin akainama akafikiri kidogo na kusema “Nimeshangaa sana kwanza
sikufahamu kama wewe na Maria mnafahamiana na kwamba mpenzi wangu aliwahi pia
kuwa mpenzi wako.Mimi ninamfahamu kwa jina la Maria .Nyaraka zake zote
zinaonyesha anaitwa Maria Boaz Abrahams. Kwa hili uliloniambia kuna taa
nyekundu imewaka kichwani kwangu.Kuna kitu Maria anakificha.Kwa nini awe na
majina zaidi ya moja? Nadhani kuna ulazima wa kumfahamu vizuri.Nadhani bado
sijamjua vizuri mtu ninayedhani ni mpenzi wangu.Ahsante Marcelo kwa kunifumbua
macho” akasema Austin “Tutafanya nini Austin? Huyu ni mtoto wa Boaz na tayari
amekwisha niona na akitoka hapa lazima ataenda kumueleza baba yake kuwa niko
hapa.Naomba unisaidie Austin” “Usijali Marcelo.She wont get out of here” Austin
akafungua mlango na kutoka akamuendea Maria na bila kupoteza hata sekunde
akatoa bastora na kumuelekezea Maria “Nataka unieleze what’s your real name?
Are you Maria,Lilian or Shamim? Akauliza Austin kwa ukali.Maria hakujibu kitu
akabaki anamtazama Austin kwa woga. “Answer me !! what’s your real name?
akauliza tena Austin kwa ukali lakini Maria hakujibu kitu akabaki anatetemeka
.Austin aliyekuwa amefura kwa hasira akamnasa kibao kikali Maria “Answer me !!
akasema Austin.Maria hakujibu kitu akaendelea kulia.Austin akamuinamia pale
sofani “Nafahamu unanidanganya kuhusu mambo yako mengi lakini leo ni siku yako
ya kunieleza ukweli, wewe ni nani? I don’t care how much you love me but I want
to hear the truth.Kwa nini uwe na jina zaidi ya moja? Kwa nini una pasi zaidi
ay moja za kusafiria? Jina lako halisi ni lipi?Usiponieleza ukweli
nakuhakikishia nitakufanyia kitu kibaya sana.Look at me !! Look at me ! akasema
Austin kwa ukali na kumlazimisha Maria amtazame usoni “Right now,I’m not Austin
you know.I’m at work and when I’m doing my job I become a monster so if you
don’t tell me the truth I’ll do smething very painfull to you.Usinilazimishe
nikufanyie hivyo Maria tell me who are you ?Kwa nini ubadilishe majina ?
akauliza Austin lakini Maria hakujibu kitu akaendelea kulia “Maria tafadhali
usinilazimishe nikufanyie jambo ambao sikuwa nimekusudia kulifanya.Niambie
ukweli kuhusu wewe.” “Austin give her a chance to expl....” Marcelo akataka
kusema kitu lakini Austn akamzuia “Marcelo nenda chumbani kwako kajiandae.We’re
leaving this place” akasema Austin halafu akachukua waya akamfunga Maria mikono
na miguu na kumfunga kitambaa usoni. “Austin why are you doing this to me?
Akauliza Maria huku akilia “I warned you don’t come to Dar es salaam because I
didn’t want this to happen to you.Now I don’t have a choice I have to do
this.Wewe utakuwa chanzo cha kupata kile ninachokihitaji” “Nani kakubadilisha
namna hii Austin hadi ukanifanyia haya? Nini unakitafuta toka kwangu? “The ruth
!! akasema Austin kwa ukali “I want to know who you real are? Kwa kuwa umekuwa
mgumu wa kunieleza ukweli unanifanya niamini kwamba kuna mambo mengi ambayo
bado umenificha kuhusu wewe .Inaniuma kukufanyia hivi lakini hata kama angekuwa
ni mama yangu mzazi lazima ningemfanyia hivi.I don’t have a soul whem I’m doing
my job” akasema Austin na kupanda kwa hasira ghorofani akakusanya vitu vake
vyote vya muhimu akavipakia katika gari halafu akambeba Maria na kumpakia
katika gari. Akamuamuru Dr Marcelo aingie garini wakaondoka Austin akaongeza
sauti ya muziki hakutaka kusikia Maria alivyokuwa akilia. “ I hate this
job.Sikufikiria kama siku moja nitamfanyia hivi mwanamke ninayempenda .Maria ni
sababu ya mimi kuwa hapa nilipo leo lakini hayo yote lazima niyaweke pembeni
kwanza kuna vitu ambavyo natakiwa kuvifahamu toka kwake.Kwa nini awe na majina
matatu?Kwa nini hajawahi kunieleza kuhusu majina yake mengine? Kuna kitu gani
anakificha na ambacho hataki kukiweka wazi? Ninahisi kuna jambo haliko sawa
hapa.Ngoja nitaufahamu ukweli kabla hakujapambazuka” akawaza Austin Wilson
Mukasha alishindwa kupata usingizi akainuka na kwenda kusimama
kibarazani.Alionekana kujawa na mawazo “Rais amempa kazi gani Austin? Si
kawaida yake kunificha jambo lolote lakini katika hili ameniweka pembeni.Kwa
nini hataki nifahamu kazi aliyompa Austin? Amehisi nini hadi asinishirikishe
katika jambo hilo wakati mimi ndiye niliyemsaidia akampata Austin? Sina hakika
kama atakuwa amehisi kitu juu yangu kwani endapo angekuwa amehisi au kusikia
kitu chochote basi asingefikiria kunichagua kuwa waziri mkuu wa Tanzania.” Akawaza
Mukasha “ Ujio wa Austin umekuwa kama na mkosi kwani ni baada ya yeye kuja
ndipo rais alipobadilika ghafla.Sifahamu nini kinaendelea kati yao lakini
nahisi lazima Austin atakuwa anahusika katika mabadiliko haya ya ghafla ya
rais.Jambo hili si la kupuuzia kwani bila kuchukua tahadhari mambo mengi
yanaweza yakafichuka hapa.Nimeanza kuwa na wasi wasi sana na
Austin.Nitachunguza nijue kazi anayoifanya hapa Tanzania na nikitaka kujuia ni
kazi gani natakiwa kumuhoji Janet kwani baada tu ya rais kutoka kuongea naye
ndipo alipoanza kumtafuta mtu mwenye sifa kama za Austin.Nina hakika Janet kuna
kitu atakuwa anakifahamu” akawaza Mukasha ********************* Austin
aliwasili katika makazi ya Job. “Job imenilazimu kuja mapema zaidi ya
nilivyotegemea” akasema Austin baada ya kushuka garini “Hakuna tatizo
Austin.Hapa unakaribishwa muda wowote.Nini hasa kimetokea? “Something happened
Job.Tutaongea baadae lakini ndani ya gari kuna watu wawili ambao nitakuwa nao
hapa” akasema Austin na kuufungua mlango wa gari na kumtaka Marcelo ashuke
“Huyu anaitwa Dr Marcelo” Austin akamtambulisha Marcelo kwa Job halafu
akamfungua Maria kitambaa usoni na waya aliomfunga miguuni akamuamuru ashuke
“Huyu anaitwa Maria” akasema kwa ufupi kisha wakaingia ndani “Austin you are a
devil.Sikutegemea kama siku moja ungeweza kunifanyia hivi.Yaani kukupenda
kwangu kumbe nilifanya kosa na leo hii unanifanya mimi kama mhalifu? Nilifanya
kosa kubwa sana kukupenda shetani kama wewe.I swear Austin you’ll pay for
this..!!!! akasema kwa hasira Maria “Shut up !!! Austin akafoka Austin
akawataka Maria na Marcelo waketi pale sebuleni halafu yeye na Job wakapanda
ghorofani. “Austin what’s going on? Who is that woman? Job akauliza.Austin
akavuta pumzi ndefu na kusema Anaitwa Maria.Ni mtoto wa Boaz na ndiye mpenzi
wangu niliyekueleza awali” “Your girlfriend? Nini kimetomkea hadi akawa katika
hali ile? Austin akamsimulia Job kila kitu kilichotokea “ Dah ! Austin una
akili nyepesi sana ya kutambua mambo.Ninakubaliana nawe kuwa hapa kuna kitu
kimejificha.Haiingii akilini awe na majina mawili tofauti,awe na pasi zaidi ya
moja?.Kuna kitu gani anakificha? Ni vipi endapo atakuwa na majina zaidi ya hayo
matatu? Tunapaswa tumchunguze huyu mpenzio.Inawezekana yeye na baba yake kuna
mambo wanayafanya.” Akasema Job “ Boaz ndiye pekee ambaye anaweza akatupa
taarifa tunazozitaka kuhusiana na Mukasha na ili kumfanya Boaz atupe
tunachokitaka tunatakiwa kumtumia Maria .Anampenda mno mtoto wake na hatakubali
jambo lolote limtokee Maria kwa hiyo atatueleza kile tunachokitaka.Kesho nitampata
Boaz na atatueleza kila kitu.” Akasema Austin Job akamtazama Austin kwa makini
na kusema “Austin are you sure about this? What we’re going to do is not easy
so you must be sure that you are going to hurt the woman you real love.” Austin
akavuta pumzi ndefu na kusema “ Yes ! I’m sure” Job akamuongoza katika chumba
maalum cha mahojiano kilicho ndani ya jumba lile.Ni chumba kilichojengwa kisasa
sana kiasi kwamba ukiwa nje unaweza kumuona mtu aliyemo ndani kupitia kioo
maalum bila ya yeye kukuona. Sebuleni Dr Marcelo alikuwa ameketi akitazamana na
Maria.Hakuna aliyekuwa akimsemesha mwenzake.Bastora ambayo Marcelo alipewa na
Austin kwa ajili ya kujilinda ilikuwa mezani. “Marcelo nimefurahi sana
kukuona.Ni muda mrefu hatujaonana.Nimekuwa nakukumbuka sana lakini sikujua
ningekuona vipi.kwa sasa mimi makazi yangu ni afrika ya kusini na huja mara
chache hapa Dar es salaam kibiashara.Umefahamiana vipi na Austin? Maria
akauvunja ukimya uliokuwepo pale sebuleni “ Shut up lily !! akasema Marcelo “
Marcelo tafadhali usinifanyie hivi.Usiwe kama Austin .Tena nakushauri Marcelo
usiwe na urafiki na huyu mtu he’s a monster.Siamini kama anaweza akamfanyia
jambo kama hili mwanamke anayempenda.Kwa taarifa yako mimi ndiye sababu ya yeye
kufika hapa alipofika leo lakini ameyasahau hayo yote na ananifanyia
hivi.Sintomsamehe kamwe katika maisha yangu” akasema Maria huku akilia
machozi.Marcelo akaonekana kuguswa na kumuonea huruma. “Lilian pole sana
.Lakini kwa nini usimueleze ukweli kuhusu wewe na mkayamaliza mambo haya?
Anakupenda sana na haachi kukuzungumzia kila dakika lakini umemchanganya wewe
mwenyewe kutokana na utata wa majina yako.Hata mimi umenishangaza sana.Who you
real are? Akauliza Marcelo akati nikiwa nawe nilikufahamu kama Lilian baadae
nikagundua jina lako la Shamim na sasa unaitwa Maria ,what’s your real name?
Did you change your name? haya ndiyo mambo ambayo Austina anahitajiku yafahamu
.Funguka na mambo haya yatamalizika amani itakuwepo.Hata mimi sifurahi kukuona
katika hali hii” akasema Marcelo.Maria akamtazama kwa huruma na kusema
“Fine.Nitawaeleza kila kitu .Mnataka ukweli basi mtaujua lakini naomba kwanza
unifungue nikajisaidie.Nimebanwa sana” akasema Maria huku akiibana miguu
kuonyesha namna alivyobanwa. “ Siwezi kufanya hivyo.Wasubiri akina Austin
wanakuja sasa hivi” akasema Marcelo “Marcelo nimebanwa sana tafadhali.Usiniache
nikajisaidia hapa .Mimi si mhalifu na sistahili kufanyiwa hivi.Nimesema
nitawaeleza kila kitu kwa hiyo basi naomba unifungua Marcelo nikajisaidie.Una
bastora hapo ,itume endapo nitafanya jambo lolote la kipuuzi.Ninakwenda
kujisaidia na nikimaliza utanifunga kamba zenu.” Akasema Maria.Marcelo
akamtazama kwa wasi wasi mwingi “Amebanwa sana na halitakuwa jambo jema
kumuacha akajisaidia hapa.Ngoja nimfungue akajisaidie” akawaza Marcelo na kwenda
kumfungua Maria waya aliofungwa mikononi. “Thank you Marcelo for this.You are
real a gentleman.Show me the toilet” akasema Maria na Mara tu Marcelo
alipogeuka bila kutarajia akajikuta amepigwa pigo zito kichwani lililompeleka
chini na kumpoteza fahamu. Haraka haraka akaichukua bastora iliyokuwa juu ya
meza. “Its my turn now.He wants to know who I am and now the time has come to
know who I real am” akasema Maria kwa sauti ndogo na kwa tahadhari akaenda
kuchungulia dirishani “Sioni mtu yeyote nje.What is this place? I need to get
out of this place now before these monsters comes down” akasema Maria kwa
kunong’ona na kwa haraka akaenda mlangoni akakinyonga kitasa kwa lengo la
kuufungua mlango “Stop right there !! ikasema sauti kali ya Austin aliyekuwa
amesimama katika ngazi akitokea ghorofani. “Slowly put your gun down and push
it to me !!!.akasema Austin kwa sauti kali Taratibu Maria akaushusha chini
mkono uliokuwa na bastora kwa lengo la kuiweka chini kama alivyoamriwa lakini
kabla bastora ile haijagusa chini kukatokea kitendo ambacho Austin hakuwa
amekitarajia.Kwa wepesi wa aina yake Maria akageuka na kuvurumisha risasi
upande aliokuwa amesimama Austin ambaye alianguka huku akivuja damu.Bastora
yake ikifuka moshi Maria akamuendea Austin aliyekuwa amelala akivuja
damu,machozi yakamtoka “I’m sorry my love.Sikutegemea kama siku moja tungefika
hapa.Ni afadhali nikuue kuliko kukupa nafasi ya kunifahamu mimi ni nani.I love
you Austin and God will forgive me for what I’m going to do” akaema Maria kwa
sauti ndogo na kuelekeza bastora katika kichwa cha Austin na ukasikika mlio wa
risasi. AUSTIN ANAPIGWA RISASI NA MPENZI WAKE MARIA,NINI HATIMA YAKE? MARIA NI
NANI NA KWA NINI HATAKI AUSTIN AMFAHAMU? MCHAKATO WA NDOA YA RAIS DAVID ZUMO NA
MONICA BENEDICT UMEANZA ..JE WATAFANIKIWA LENGO LAO? MPENZI MSOMAJI KUPATA
MAJIBU HAYA NA MENGINE MENGI USIKOSE QUEEN MONICA SEASON 4
MWISHO
0 comments:
Post a Comment