Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

TSSI 01 PRISONER - 5

 







    Simulizi : TSS 01 Prisoner

    Sehemu Ya Tano (5)







    Uvivu ulimponza wa kukifuata choo kilichokuwa ubavuni mwa majengo hayo. Au labda pengine hata huko pia yangemkuta kama hayo yanayoenda kumkuta hivi punde maana pande tatu za majengo hayo zilikuwa zimezungukwa na maadaui. Akiwa tayari kwa kutoa haja yake. Alisikia michakacho kwenye majani yaliokuwa karibu na uzio wa fensi ya kituo hicho. Akaghairisha alichotaka kufanya na kupiga jicho la kiuvivu kule sauti ile ilipotokea. Hakuona kitu!.



    Muda huo Pijo alikuwa ameshahama kitambo eneo lile na hivi sasa alikuwa nyuma ya askari yule. Akamgusa begani kitaratibu na askari yule akageuka kwa pupa huku akiikatisha haja yake. Ngumi ya pua ilitosha kuikatisha pupa aliyokuwa nayo na kuleta taharuki nafsini mwa yule askari. Hofu ikawa nae moyoni mwake. Nini hiki? Mzuka!? Ama shetani? Hakupata jibu!.



    Akaruka nyuma kwa kiroho huku akijiandaa kupiga mayowe ya hofu baada ya kukishuhudia kiumbe kisichoeleweka. Kabla hajafanya alichotarajia. Ngumi mbili za mdomo zilimkata kauli. Akarudi nyuma huku akiinama kwa mbele baada ya kuzidiwa na mashambulizi hayo ya ghafla. Huenda angeweza kupambana na adui yake lakini kutokana na mashambulizi ya kushtukiza. Ilitosha kumpotezea nguvu zote alizokuwa nazo. Hofu!. Uoga!. Wasiwasi wa kifo vilivyochagizwa na kiroho cha mshtuko. Vilimpotezea ujasiri kabisa.



    Ni dakika mbili tu mbele askari yule alikuwa chini akipapatika kama kuku aliechinjwa na kuachiwa kabla ya kukata roho. Akatulia kimya baada ya muda. Kifo kikamchukua kabla haja maizi ni nani msababishi wa kifo chake. Pijo akamvuta hadi karibu na uzio na kumlaza hapo. Ni mapigo yasiyoweza kuandikika kwa urahisi ndio ambayo yaliondoka na roho ya askari kutoka kwa Pijo.



    Askari ambae alikuwa lindo upande ule ambao Deva alikuwa ametega akimtega yeye akae kwenye kumi na nane ili aruke nae. Alisikia michakacho na miguno kadhaa kule ambapo mwenzake alipokuwapo. Wasiwasi ukamuingia na kiroho cha kutaka kuiridhisha nafsi yake kwamba pako salama kikamuingia. Akaweka silaha tayari kwa lolote na kuelekea upande ule kwa umakini ili asije akaleta hofu kwa mwenzake kama akimkuta salama.



    Sehemu ambayo alikuwa akipita ndipo Deva alipokuwa ameweka kambi ya muda kumiwinda yeye. Deva akarudi nyuma kidogo ili amvizie windo lake kwa urahisi. Moja.... Mbili... Tat.... Alipiga hatua moja kubwa na kumchota mtama yule askari. Bila ubishi wowote alienda chini akifuatiwa na kishindo chake huku mguno wa taharuki ukimtoka. Deva aliinua guu lake juu tayari kulishusha kwenye shingo ya askari ili amalize mchezo.



    Askari alihama haraka kwa kujibiringisha pembeni kisha akarusha teke lililo na dhamira ya kumuangusha chini Deva akiwa vile vile amelala chini akigaagaa. Hamadi!. Ile guu la Deva linatua chini sehemu ambayo shingo ya askari ilikuwa mwanzo kabla hajahama. Ndipo teke la yule askari liliupiga ule mguu ambao ulikuwa umesimama wima na kumfanya Deva akose stamini kutokana na kuwa ule mguu mwengine ndio unatua chini sasa. Mara hii alikuwa chini akigaagaa akijitahidi kuinuka kabla ya yule askari hajainuka.



    Wote wakainuka. Wakawa tayari tayari kwa mapambano huku kila mmoja silaha yake ikiwa chini pembeni yake baada ya kuponyoka mikononi pindi walipokuwa chini. Wakaangaliana kwa sekunde kadhaa kila mmoja akimtegea mwenzake auanzishe mchezo.



    Vishindo vya Deva na yule askari. Vilimshtua askari ambae nae alikuwa lindo ubavuni mwa majengo hayo. Akatoka mbio mbio kwenda nyuma ya majengo kuangalia kunani huko. Zinah ambae nae alikuwa upande ule ule majira haya akiwa tayari ndani ya uzio. Alimuona yule askari anavyokuja upande wake akiwa amehamanika vibaya kwa sauti za vishindo vile. Akajiweka tayari iwapo askari yule atafika pale alipo basi amfanyie shambulizi la kushtukiza.



    Askari bila kujua chochote. Bila ya kujua kama analiwa ‘taiming’ akijaa kwenye boksi ashambuliwe kwa ghafla. Alipita eneo lile huku Zinah akimsubiria afike mbali kidogo ili afanye shambulizi. Hatua kama nne mbele. Zinah alichomoka kwa kasi mkononi mwake akiwa ameshika bisu kubwa kama yale ya kukatia nyama buchani akiwa na lengo la kumchinja yule askari. Muda huo Ata aliekuwa upande huo alikuwa akiuangalia mchezo ule vizuri.



    Ghafla!. Tena ghafla sana bila mtu yoyote kutarajia kati ya wale watatu. Zinah bisu lilimdondoka taratibu mkononi mwake. Mikono yote miwili aliihamishia shingoni mwake palipokuwa pakionekana kisu kidogo kikining'inia. Ilastaajabisha!. Mwanzo kisu kile kidogo hakikuwepo shingo pale lakini katika namna isiyotarajiwa kilionekana kikiwa kimekita pale. Macho yalimtoka pima huku akikishika kile kisu akijaribu kukivuta pasi na mafanikio yoyote.



    Akageuka taratibu mahali ambapo alikuwapo Ata huku akiwa bado amekishika kile kisu pale shingoni mwake. Ata alihamanika baada ya kumuona Zinah akiwa katika hali ile ya kustajabisha. Damu zilikuwa zikitoka mahala pale huku mdomoni ndio usiseme kwa uchuruzikaji wake. Kimya kimya bila kusema lolote alianguka na kuacha kishindo kikuu kilichomshtua yule askari ambae alikuwa akienda eneo la nyuma kwenda kujua nini kimetukia huko baada ya kusikia vishindo huko.



    Yowe dogo la Hofu likamtoka askari yule na kujikuta akiiachia bunduki iliyokuwa mikononi mwake na kwenda kujiigamiza ukutani huku akiushangaa mwili ule unavyopapatika pale chini. Nini hii!?. Hakuelewa!.







    Askari baada ya kuona jambo la ajabu usiku ule. Akaiwahi bastola yake pale chini na kuweka ulinzi haraka huku akiwa anaangalia pande zote nne kwa umakini mkubwa. Yote hiyo ni kujilinda kabla hajauendea ule mwili pale chini ili aweze kumaizi ni wa nani? Aliusogelea taratibu huku akisahau ule msemo unaosema kuwa ‘maiti haidhuru’. Pengine labda hakujua kama kuna mtu mwengine mahala hapo. Kimya kimya aliuendea ule mwili pale chini.



    Kule upande wa nyuma. Deva na yule askari kila mmoja alikuwa makini na mwenzake wote wakiwa tayari kwa mapigano ya kimya kimya. Kutokana na giza kuwa kubwa tofauti na mwanga ambao ulikuwa ni hafifu eneo hilo. Halafu pia mavazi meusi aliyovaa Deva. Vilitosha kumbabaisha Askari hata asijue Deva alifika saa ngapi karibu yake. Akapokea ngumi mbili za kifua huku ya tatu akijitahidi kuikwepa na kufanikiwa hilo.



    Teke kali la shingo lilimkuta askari na kumfanya ababaike kidogo na kabla hajakaa sawa. Teke jengine la usawa wa kiuno lilikuwa likimfuata ila hili alifanikiwa kuliona vyema na kulikwepa. Akabenjuka juu huku akitanguliza kigoti maeneo ya kifua cha Deva. Hakika pigo hilo Deva hakulitarajia hata kidogo. Pamoja na kuwa ni mwepesi sana kurusha mateke kutokana na urefu wake. Ila kulikwepa pigo lile alishindwa. Kigoti cha askari kikatua kifuani kwake na wote wakaenda chini huku Deva maumivu yakiwa nae sambamba kifuani.



    Wakati mpambano kati ya Askari na Deva ukiendelea. TSSI 01 alikuwa nyuma ya Pijo muda huu akiwa ameshahama tayari kule ubavuni mwa jengo. Alikuwa kimya nyuma ya Pijo ambae hakuwa na hili wala lile. Yeye macho yake aliyaelekeza mbele yake tu kuhakikisha usalama wake. Hakuweza kujua kama nyuma yake kulikuwa kuna mtu aliekuwa akimuangalia yeye muda wote.



    “Hey” TSSI 01 aliita kwa sauti ya chini lakini iliyopenya kwa ukubwa masikioni mwa Pijo baada ya kushtushwa na sauti hiyo. Hakutarajia kama kutakuwa na mtu yoyote nyuma yake. Akageuka haraka huku bastola yake akiielekeza kule aliposkia sauti ile.



    Moyo ukamuenda mbio ghafla baada ya kukutana na kiumbe ambacho hakuweza kukitafsiri haraka. Aliona kiumbe kile kikimtabasamulia kikiwa ndani ya vazi la soksi usoni ambalo liliacha macho na mdomo tu kwa uwazi. Akiwa kamuelekezea bastola Hemedy. TSSI 01 alimtaka aweke bastola chini ili wapimane uwezo na Pijo nae akaweka bastola chini akiwa tayari kupambana bila silaha.



    “Wewe ni nani?” Pijo aliuliza huku akiwa tayari kwa pambano.



    “Mwokozi” TSSI 01 alijibu huku akiwa tulivu zaidi kama hakuna chochote kibaya kitakachoweza kumkuta.



    Pijo alimuendea TSSI 01 kwa mapigo ya haraka lakini yote yalihepwa kwa ustadi mzuri. Akamuendea tena kwa mapigo mengine lakini sasa ikawa kama mwanzo tu. Alihepwa na kujikuta akipiga hewa. Ikawa sasa kama ni mchezo tu. Wakati Pijo akijitahidi kupiga mapigo yeye aliyohisi ni makali. Lakini yote yalihepwa na TSSI 01 asimdhuru kwa chochote. Ebwana eee!. Pijo alitamani kupiga kelele za kuomba msaada baada ya kuona akitumia nguvu nyingi kumpiga adui yake. Lakini adui yake akitumia nguvu chache sana kumhepa na wala asimdhuru kwa chochote.



    Hofu ikamuingia zaidi baada ya kujua kuwa anaepambana nae hakuwa saizi yake hata kidogo. Alichoona kinafaa kwa wakati huo ni kuiwahi silaha yake iliyokuwa chini ili amalize mchezo kwa kumdhuru kwa namna hiyo. Maana kwa mapigano alishaona ameshindwa dhahiri. Alijaribu kumchebacheba ili awe karibu na silaha yake. Ni kweli alifanikiwa baada ya Hemedy kumhepa tu bila kumaizi mawazo ya Pijo.



    Pijo aliruka sarakasi ndogo kuiendea bastola yake. Alipofika alipiga goti na kuiokota. TSSI 01 kuja kutahamaki na kugundua mchezo wa Pijo ikiwa Pijo tayari ameshaifikia bastola yake. Alichomoka kwa wepesi wa ajabu na kwenda kuukanyaga mkono wa Pijo na buti lake kwa nguvu. Pijo alichia yowe kubwa la maumivu. Haraka kwa mkono wake wa kushoto alichomoa kisu na dhamira yake ilikuwa ni kumkita adui yake kwenye ule mguu uliouminyiza mkono wake pale chini.



    Kisu kile alikishusha kwa kasi kubwa kuukita mguu wa TSSI 01. TSSI 01 aliona na kuhamisha mguu wake kwa haraka na kutokana na kasi na nguvu aliyoitumia Pijo kukishusha kile kisu. Akajikuta akijichoma mwenyewe mkononi mwake na kuachia yowe kubwa la maumivu. Kelele zake zilimshtua kila mtu aliekuwa eneo lile. Si askari waliokuwa lindo usiku huo wala wale wenzake. Ata ambae alikuwa na nia ya kumuua yule askari ambae alikuwa akiusogelea mwili wa Zinah. Alighairisha kumfuata na kuanza kupiga hatua kubwa kubwa kuenda kule nyuma ambapo mayowe yaliskika.



    TSSI 01 aliskia vishindo vya hatua za mtu akija kwa kasi upande huo. Akampiga pigo moja matata Pijo. Pigo ambalo alibenjuka kinyume na mguu wake wa kulia uliovishwa buti kubwa ulipiga kidevuni mwa Pijo na kumfanya arushwe nyuma huku akicheua damu nyingi sana. Alibaki akikoroma tu akiwa hawezi tena kuongea kutokana na taya zake kupindishwa. TSSI 01 alipotelea Gizani baada ya kumnyamazisha mtu wake kwa namna hiyo.



    Ata alikuja mbio mbio hadi pale alipokuwa amelala Pijo akikoroma chini chini huku damu zikimtoka nyingi mdomoni mwake na juu ya kiganja chake cha mkono akiwa bado na kile kisu alichojikita nacho mwenyewe baada ya kukosa lengo. Ata aliangalia huku na huko kama kuna mtu mwengine mahala hapo. Kimya!. Hivi ni kweli askari ndio amefanya mambo haya? Alijiuliza Ata pasi na kupata jibu. Akamuinua haraka Pijo na kupotelea nae gizani.



    Kundi kubwa la askari lilikuwa likienda mbio mbio kule nyuma baada ya kusikia kelele za Pijo kipindi ambacho anapokea kichapo kwa Hemedy. Deva aliona akiendelea kucheka na yule askari ambae walikuwa wakipambana anaweza kuja kukutwa na hatimae kukamatwa. Alitasfiri kukamatwa hapo ni kukamatwa kizembe.



    Aliiwahi bunduki yake iliyokuwa chini kwaajili ya kumaliza mchezo haraka. Ila kabla hajaifikia bunduki yake. Teke zito lilipita karibu na uso wake. Akarudi nyuma kidogo na hiyo ndio ikawa ponya yake dhidi ya lile teke. Deva akarusha teke na yeye usawa wa kifua cha askari na bahati mbaya ikawa kwake askari. Teke lilimkuta na kumrusha nyuma mbali na Deva. Deva akaona hiyo ndio nafasi yake ya kumaliza mchezo. Akaifuata bunduki yake tayari kumfyatulia mbali yule askari mbishi.



    Yule askari baada ya kuona kifo kikimnyemelea. Aliinuka haraka na kumuendea kwa kasi kubwa Deva. Alipofika karibu yake alimrukia kama nyani arukiavyo tawi. Wote wakaenda chini tena. Kazi sasa ikawa kuipata ile bunduki ambayo kwa sasa ilikuwa imeng'ang'aniwa na wote wawili wakitaka kila mmoja iwe mikononi mwake. Askari alipoona anaweza kuzidiwa nguvu kisha kudhuriwa. Akataka kufanya jambo ambalo litawajulisha wenzake kuwa kuna uvamizi umetokea kwenye kituo hicho upande wa nyuma.



    Wakiwa bado wanavutana na ile bastola pale chini. Askari alipapasa hadi alipoipata ‘trigger’. Aliiminya na risasi ikatoka huku mlio mkubwa ukisikika. Ghafla yowe kubwa la maumivu liliskika upenuni mwa ukuta wa jengo la kituo. Yowe ambalo lilimtoka askari ambae alikuwa kwenye kundi yeye wenzake watatu wakiwahi huko. Askari yule ile risasi iliyoachiwa na yule askari aliekuwa akimamaniana na Deva. Risasi ile ilimkuta yeye kwenye mguu. Wenzake watatu walirudi nyuma mbio huku wakitoa mayowe ya hofu baada ya kumuona mwenzao akigaagaa chini kwa maumivu.



    Yule askari aliekuwa akiminyana na Deva pale chini. Alitaharuki baada ya kujua kuwa kumbe ile risasi aliyoiachia kama kiashirio cha kuwaita wenzake waje kutoa msaada ilimpata askari mwenzake aliekuwa akija mbio huko. Aliingiwa na mfadhaiko hata akasahau kwamba alikuwa kwenye kiminyano cha kugombania bunduki na adui yake. Deva akatumia muda huo vizuri kumpokonya haraka askari bunduki na kumpiga na kitako cha bunduki na askari yule akapoteza fahamu pale pale. Deva akatoka mbio na kuuruka uzio wa Seng'enge. Yowe dogo la uchungu lilimtoka baada ya kujichoma na miba iliyokuwa juu ya uzio huo. Akapotelea gizani huku akimshukuru mungu wake kimya kimya kwa kuokoka katika zahma hilo.



    Wale askari watatu waliokuwa wakikimbia baada ya kumuona mwenzao akigaagaa chini kwa maumivu. Walijikuta wakiingia mtegoni mwa Robart na Atu. Walichezea kichapo si mas'hara na kujikuta wakiwa hoi chini hawajiwezi. Punde kuliskika milio ya breki za gari mbele ya kituo hicho huku ikifuatiwa na vishindo vingi vya watu. Polisi!. Wote wawili waliwaza. Wakatoka nje ya uzio na kukimbilia gizani.



    Kundi kubwa la askari liliingia kituoni hapo baada ya askari mmoja aliekuwapo kituoni hapo kutoa taarifa kwa mkuu wa kituo hicho. Na mkuu wa kituo akatoa taarifa kwa askari wake waliokuwa doria usiku huo mitaani na kuwaambia warudi haraka kituoni kuwa kuna uvamivi umetokea huku yeye akijianda haraka nyumbani kwake akiwahi huko kituoni.



    Askari wale waliokuja muda huo wakishirikiana na askari wawili waliokuwa lindo upande wa mbele wa kituo hicho. Walikizunguka kituo kwaajili ya kuweka ulinzi. Walisogea hadi wakajikuta wakikaribiana na hakuna chochote cha kuogopesha walichokiona. Wakawasha tochi zao maana taa za hapo hazikuweza kuwasaidia kuona vizuri baada ya taa baadhi kuvunjwa. Miili ya askari wenzao iliwapokea chini ikiwa kimya na isijulikane kwa haraka haraka kuwa ni wafu au bado wapo hai.



    Wakaikagua haraka haraka na kuona kati ya miili ya wenzao watano na kukuta miwili kati ya hiyo ikiwa sio hai tena. Huku ile mitatu ikiwa mahututi. Mara ghafla walisikia yowe la askari aliekuwa akiwaita haraka upande aliopo na kujikuta wote wakiiacha ile miili na kukimbilia huko. Huko waliukuta mwili mmoja wasio utambua ukiwa kimya chini huku shingoni ukiwa na kisu kilichojaa damu. Haraka haraka askari mmoja alivaa ‘gloves’ mikononi mwake na kuivua ile soksi iliyoziba uso wa mtu yule.



    Wote macho yao yakawa kwenye uso wa Zinah. Hawakumtambua!. Taratibu za kuibeba ile miili ya mahututi na ile ya wafu zilifanyika kwa haraka. Waliingiza kwenye gari na safari ya kuelekea hospitalini ikaanza. Dakika chache baadae mkuu wa kituo kile alifika na kupewa taarifa ya uvamizi ule kwa haraka haraka. Akauliza maswali mawili matatu na akajibiwa yote. Akaingia ofisini kwake akiwaacha askari wake wakijadili tukio hilo huko nje.



    Dakika ishirini nyuma kabla ya askari wengine kuja kutoa msaada kwa wenzao. Ata alimpeleka Pijo kwenye gari waliokuja nalo aliekuwa hoi baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Hemedy TSSI 01. Queen alihoji kwa taharuki ni nini kimetukia huko ila muda wakujibiwa na Ata haukuwepo. Baada ya kumuweka vizuri Pijo. Akajianda kurudi tena kule kituoni kwaajili ya kuendeleza mashambulizi. Mara hii hakuwa na nia tena ya kupora silaha. Nia yake ilibadilika na kuwa ni ya kufanya maafa kwa yoyote atakae kuwa karibu yake.



    Hasira zilimuongoza huku umakini ukimtoka kabisa. Mara ghafla Deva alikuja akihema mahala hapo. UHASAMA uliokuwa baina ya watu hao wawili waliuacha kwanza na kujali kazi iliyowaleta hapo. Ata akahoji ni kwanini Deva amerudi mapema yote ilhali kazi bado ilikuwa ikiendelea? Akajibu kwa kiroho na asieleweke na Ata anayoyaongea. Ghafla walishuhudia gari la polisi likipita kwa kasi barabarani karibu na gari yao walipoiegesha vichakani. Wakajua huko tayari kumenuka.



    Wakiwa bado hawajui wafanye nini kwa wakati huo. Waliwashuhudia wenzao wawili Robart na Atu wakija mbio eneo hilo. Wakahoji kunani huko na kujibu kwa haraka kuwa hapafai tena wao kuendelea kubaki hapo. Wakahoji yuwapi Pijo na Ata aliwaambia kuwa Pijo alikuwa ndani ya gari hajiwezi. Wakahoji tena yuwapi Zinah. Ata akawajibu kuwa hawapo nae tena maana alikutana na kifo huko huko. Walihuzunika kisha wakapakia kwenye gari na safari ya kuondoka hapo ikaanza.



    Kwenye kichaka kilichokuwa karibu na walipopaki gari ya kina Ata. TSSI 01 alikuwa akishuhudia na kusikia kila kilichokuwa kikiongelewa pale. Aliposikia watu wale wamepanga kuondoka muda huo. Aliwahi haraka kule ambako Inspekta Salum alikuwa ametega. Akamuambia ashuke haraka nae akafanya hivyo. Wakaongozana mbio mbio hadi kichakana mahali ambapo gari la Hemedy alikuwa amelificha. Wakazama ndani na safari ya kuwafuatilia wakina Ata ikaanza.









    ENDELEA..



    TSSI 01 aliiondoa gari kwa fujo kiasi ambacho baadhi ya majani yaling'oka huku na huko. Yote hiyo ilikuwa ni kuwawahi maadui zake ili walau ajue kambi yao ilipo na ikiwezekana amalize kazi yake siku hiyo hiyo. Vumbi lilitimuliwa kiasi ambacho nyuma hapakuonekana chochote zaidi ya taa nyekundu za gari ya Hemedy. Tena zilionekana kwa kufifia sana kutokana na uwingi wa vumbi lile.



    Alinyoosha mguu kiasi ambacho Inspekta Salum alijua kama si kupata ajali basi wanaweza kufa kabla ya kupata ajali kutokana na mwendo wa kasi aliokuwa akiuendesha TSSI 01. Njia nzima hawakuona kitu zaidi ya vumbi lililoanza kufifia kuashiria kuna gari lilipita muda si mrefu kwenye barabara hiyo.



    Alitembeza gari hadi alipokuja kuipata barabara kuu ya Muheza. Akakunja kushoto kuifuata barabara hiyo. Majira hayo yalipata saa nane na nusu za usiku. Njia ilikuwa kimya haina magari mengi zaidi ya magari makubwa tu ya mizigo. Ambayo nayo yalikuwa yakiendeshwa kwa mwendo wa kasi.



    Gari waliyopanda wakina Ata. Nayo pia ilikuwa ikiendeshwa kwa kasi si mchezo na mwanadada Queen aliekuwa nyuma ya usukani. Wakiwa maeneo ya Pongwe kabla ya kuipata njia ambayo itawapeleka kwenye kambi yao. Nyuma yao walisikia muungurumo wa gari iliyokuwa ikija kwa kasi ya swala. Wote wakageuka nyuma kuiangalia. Ilikuwa mbali na wao kama mita miatano hivi. Wote wakashangaa. Hii gari inayokuja inatuwahi sisi ama?



    Hofu yao kuu walidhani ni gari ya polisi. Kwahiyo ilikuwa ikiwafukuzia. Ikabidi wamkemee Queen aongeze mwendo zaidi na asiingie na njia ya kuingilia kambini kwao. Walimshauri anyoonshe na njia hiyo hiyo hadi watokezee mjini na huko ndipo watajua ni jinsi gani ya kuwatoka hao waliodhani kuwa ni askari. Queen ni kama vile alichochewa moto na magunzi ya mahindi. Aliongeza gea na kukanyaga mafuta na mwendo ukaongezeka zaidi.



    Gari aliiendesha katika mwendo ambao uliwatisha hata wenzake. Ulikuwa ni mwendo ambao kama kutatokea hatari yoyote mbele yao. Labda kudra za muumba ndio zinaweza kuwaokoa lakini si vinginevyo.



    Waliipita Kange kama upepo na sasa walikuwa maeneo ya Sabasaba. Mwendo ulikuwa ni ule ule usio mithilika hata kidogo. Majira haya walikuwa wameshajua kwamba ile gari iliyokuwa ikiwafuata nyuma haikuwa ya polisi ila ilidhamiria kuwafuata wao. Swali likabaki vichwani mwao. Ni akina nani waliokuwa wakiwafuata kwa mwendo ule? Hawakupata jibu!.



    Kutokana na ugeni wa mji huo. Queen alihofia kukutwa mapema maana hakuwa akizifahamu njia nyingi za mji huo. Lakini akajiapisha kuwa ni lazima awatoke kivyovyote watu hao. Kwenye mzunguko wa Kwaminchi. Njia ambayo inatoka kwa mkuu wa mkoa. Kulikuwa kuna gari kubwa la mizigo lililokuwa likija upande huo kwa mwendo wa wastani maana sehemu hiyo ilikuwa ni lazima kupunguza mwendo ili kuweza kuuzunguka mzunguko huo ndipo uendelee na safari.



    Quee alipoliona gari hilo. Alipanga hapo ndipo pakuwatoka maadui zao. Akaongeza mwendo kuliwahi gari hilo kabla halijazunguka yeye awe tayari ameshapita. Mwendo aliokuwa akiingia nao hapo ulimshangaza mpaka yule dereva wa Lori. Akapita honi nyingi kuipa habari gari ile ndogo kwamba yeye ndie alietakiwa awe wa kwanza kuingia pale kabla ile gari ndogo.



    Ila Queen hakutaka kujali zaidi ya kuingiza gari kwenye mzunguko ule. Kelele za msuguano wa matairi na lami zilisikika kwa sauti kubwa kutokana na kasi aliyokunja nayo huku akinyunyizia breki. Kisha uelekeo ule ule uliokuwa ukija lile gari kubwa Queen alienda nao. Dereva wa Lori alipunguza mwendo ikiwa tayari ameshafika kabisa kwenye mzunguko. Gari ikapungua mwendo ikawa inaenda mwendo mdogo. Huku dereva akiwa haamini macho yake kama kuna watu wanaweza kuwa na akili mbovu za kusababisha ajali za makusudi kama huyo dereva wa gari ndogo.



    TSSI 01 nae alikuwa tayari ameshafika eneo hilo. Bahati mbaya kwake alizidiwa njia na lile gari kubwa lililokuwa likienda kwa mwendo mdogo zaidi. Akalazimika kufunga breki za ghafla ili asije akasababisha ajali. Ebwana wee!!. Sauti za msuguano wa tairi za gari na lami zilisikika kwa sauti kuu kiasi ambacho ziliweza kuleta hofu kwa walevi wachache waliokuwa ndani ya baa ya Tanga Pazuri.



    Kelele za hofu zilisikika ndani ya baa hiyo huku wakijitahidi kuwahi kutoka nje wapate kushuhudia kinachoendelea. Dereva wa Lori aliingiwa na hamaniko asielewe yanayomtokea kwa siku hiyo. Akabaki kupiga mayowe ya hofu yaliyochagizwa na honi aliyokuwa akiipiga mfululizo na asijue kama anafanya hivyo. Gari la Hemedy liliserereka kwa kasi na kujikuta likigeuka kule kule walipotokea huku likizidi kulifuata lile gari kubwa. Mara hii lilikuwa likiifuata kinyume kinyume baada ya mbele kugeuka nyuma.



    Ilikuwa ni kama pua na mdomo jinsi ilivyokuwa kitako cha gari la Hemedy na ubavu wa lile gari kubwa. TSSI 01 Alifanya kitendo cha ajabu kilichowaacha walevi waliotoka nje kushuhudia na kuwafanya washangilie baada ya kuhamanika muda mfupi uliopita. Hemedy aliigeuza gari katika namna ya ajabu ikielekea kule kule walikokuwa wakielekea. Vifijo na makofi viliwatoka walevi huku wakishangilia baada ya dereva wa gari lile dogo kuonyesha mautundu.



    Akalipita lile Lori kwa mbele na kuendelea na safari yake akimuacha dereva wa Lori akistajabu kwa anayoyaona usiku huo. “Shit!” Hemedy aling'aka baada ya kutojua ni uelekeo upi ulishika lile gari walilokuwa wakilifukuzia. Akanyoosha na barabara ya Chumbageni. Mara hii alikuwa katika mwendo wa kawaida. Inspekta Salum Mzanzibar alishusha pumzi nzito za ahueni. Kisha akamuangalia usoni na kumuuliza kwa taratibu.



    “Tunaenda wapi?”



    “Home” Hemedy alijibu huku akitabasamu baada ya kugundua kumbe muda wote Inspekta Salum alikuwa na hofu sana.



    * * * *



    Majira ya saa tisa na na robo usiku. Gari iliyowabeba wakina Ata iliingia kwenye mjengo wao baada ya kufanikiwa kuwatoroka wakina Hemedy. Ikafika hadi sehemu maalum kwaajili ya kuegesha magari. Gari ikawekwa hapo na wote wakashuka. Pijo alikokotwa na Ata wakaaingia ndani. Kutokana na purukushani za hapa na pale. Mr Hanein na Mrutu walitoka vyumbani mwao na kuenda sebuleni na kuwakuta vijana wake wakiwa wamerudi huku Pijo akiwa hoi.



    Mr Hanein aliuliza yaliyotukia huko na Ata alimuambia kila kitu kuhusu kufeli mpango wao. Mr Hanein alichoka ghafla. Maana yeye matarajio yake yalikuwa ni ushindi tu kutokana na kuwaamini sana vijana wake. Ghadhabu zilimshika juu ya Inspekta Kiulason. Mawazo yake yalimnong'oneza na kumuambia kuwa Kiulason ameuchoma utambi wa mchezo na ndio maana picha limeungua.



    Ghafla tu aliwauliza vijana wake kuwa ni adhabu gani itamfaa Inspekta Kiulason kwasababu amewauza kama mawazo yake yalivyomtuma. Wote wakashangaa. Inakuaje Inspekta adhabu imuangukie yeye? Ikabidi wamuulize. Akawajibu kuwa ni lazima ni Kiulason tu ndio ameuharibu mpango wao. Wakatafakari na kuona huenda ikawa kuna ukweli wa maneno hayo.



    Badala ya kujibu lile swali. Wakabaki kimya na isieleweke kwamba wameshindwa kumchagulia Kiulason adhabu ama ndio wanaifikiria. Kimya kilichukua nafasi muda huo hadi pale Pijo alipotoa sauti ya mkoromo wa maumivu. Wote wakashtuka badala ya kugundua kuwa mwenzao alikuwa katika hali mbaya. Mr Hanein aliwaambia kuwa ni lazima Pijo apatiwe huduma ya kwanza kabla mambo mengine hayajaendelea.



    Kwa vile Atu alikuwa na uwezo kidogo wa kitabibu. Wakamkokota Pijo hadi katika chumba chake anachotumia kulala. Wakamlaza huko na kumuachia Atu afanye kazi yake ya kumpa huduma ya kwanza Pijo. Wakarudi tena sebuleni kuja kuendelea na mazungumzo. Kila mmoja alichukua nafasi yake na kumtazama Mr Hanein machoni ishara ya kwamba wapo tayari kwa lolote atakalo waagiza juu ya Inspekta Kiulason.



    “Nataka ifikapo kesho asubuhi niskie taarifa ya kifo cha huyu mbwa askari. Maana hawezi kunifanya mimi ni mtoto mdogo kama alivyo yeye” Mr Hanein alitoa agizo.



    Wakakubalina nae na jambo jengine likaingizwa. Ni juu ya mwili wa Zinah ambao hadi muda huo hawakujua utakuwa mahala gani. Mr Hanein aliwaambia kuwa wauache tu na wasijaribu kufuatilia jambo hilo. Maana kufanya hivyo ni kuwapa mwanga askari wa kuwapata wao. Wakakubalina nae na wakauliza swali jengine. Hili lilikuwa ni juu ya kutekeleza mauaji ya Kiulason. Mr Hanein akawajibu kuwa kazi hiyo wakaifanye muda huo na ifikapo asubuhi apate taarifa ya kifo cha askari huyo. Akanyanyuka na kuanza kupiga hatua kuifuata kordo inayoelekea vyumbani. Hatua nne mbele akageuka na kuwatazama.



    “Mtajichagua wenyewe ni wangapi mtaenda. Ila ni sasa na sio baadae” akamaliza na kupotelea huko.



    Wakaangaliana na Ata ikabidi achukue jukumu ya kuwachagua. Akamtaka Robart na Deva waongozane wote. Deva akatoa sababu kuwa kwa wakati huo hali yake sio nzuri sana kutokana na kuleteana tabu sana na yule askari kule kituoni kabla hajamzimisha. Ata akasema basi wataenda wenyewe wawili. Wakanyanyuka pale na kutoka nje. Wakapanda kwenye gari jengine tofauti na lile walilotoka kufanya nalo tukio muda mfupi uliopita. Safari ya kuenda Makorora nyumbani kwa Inspekta Kiulason ikaanza.



    Dakika ishirini zilitosha kuwafikisha huko. Wakapaki gari karibu na Kanisa la Angrikana lililopo mtaa huo. Wakashuka na kutembea kwa miguu hadi nje ya uzio wa nyumba ya Kiulason. Kimya kilitawala maeneo hayo. Ni sauti za wadudu tu ndio zilikuwa zikisikika masikioni mwao. Wakatafakari jinsi ya kuingia ndani ya nyumba hiyo kimya kimya bila kuleta hofu yoyote kwa ambae atakuwa ndani ya nyumba hiyo ilhali akiwa macho muda huo.



    Bahati ikawa kwao baada ya kujua kuwa ukuta wa nyumba hiyo ulikuwa ukipandika kiurahisi bila tabu yoyote. Wakashauriana kuwa kila mmoja apitie na upande wake ili hata kama kutakuwa na tatizo basi waweze kusaidiana. Robart akazunguka upande wa kulia na Ata akabaki upande wa kushoto. Kila mmoja akauparamia ukuta kwa namna yake anayoijua na sekunde kadhaa mbele wakawa ndani ya nyumba hiyo.



    Kimya kiliwapokea ndani humo. Taa sebuleni ilikuwa ikiwaka. Mlinzi getini alikuwa amelala fofofo na asijitambue kwa lolote lile. Ata akafanya hila ya kumzimisha mlinzi kimya kimya na muda huo mlinzi akalala usingizi tofauti na ule aliokuwa amelala mwanzo. Alikuwa amezima!. Hatua ndogo ndogo ziwafikisha hadi kwenye dirisha la sebuleni. Wakachungulia ila hawakuona chochote kutokana na uzito wa pazia lililowekwa hapo.



    Kimya kimya wakauendea mlango na kujaribu kufungua. Ukafunguka!. Na hata kama usingefunguka walikuwa na namna nyengine ya kuufungua mlango huo bila kuuvunja. Wakazama ndani na bahati ikawa kwao baada ya kumkuta Kiulason akiwa amejilaza kwenye sofa. Hakuwa amelala usingizi. Ila alionekana kama mtu mwenye mawazo mengi yanayomsumbua.



    Inspekta Kiulason alishtuka kwenye lindi la mawazo baada ya kuhisi kuwa mlango wa sebuleni umefunguliwa. Ebwana eee!! Macho yalimtoka pima baada ya kukutana na vijana aliyowajua kuwa ni vijana wa Mr Hanein. Wamefuata nini nyumbani kwangu? Hakujua!. Uoga ulimshika ghafla baada ya kuhisi hali ya hatari iliyokuwa mbele yake.



    Akajiinua pale kwenye sofa na kukaa kitako akiwatizama kwa hofu watu hao walioingia kwake kama mizuka. Akauliza kwa ujasiri huku akijikaza kisabuni asionekane kama ameanza kuingiwa na hofu. Hakupata jibu lolote kwa watu hao. Hofu ikaongezeka zaidi baada ya kuona watu wale wakimuangalia kwa macho ya shari. Kengele ya hatari ikazidi kulia kichwani mwake.



    Ghafla aliinua mto aliokuwa ameulalia na kuchomoka na bastola. Akawanyooshea watu wale kwa zamu huku akiwa amewakazia macho. Kitendo cha kuihamisha bastola kwenye uelekeo wa Robart na kumuelekezea Ata. Sekunde hiyo hiyo Robart aliitumia kufanya jambo lililomuacha mdomo wazi Kiulason. Kwa kasi isiyoyakawaida. Robart alimuwahi kwa teke kali kwenye mkono ambao ulikuwa umeshika bastola. Kabla bastola haijamruka mikononi mwake. Alijaribu kuminya ‘trigger’ na bastola ikatoa mlio wa hafifu wa vyuma. Bastola hakuwa ameitoa usalama kabla!.



    Ghafla aliinua mto aliokuwa ameulalia na kuchomoka na bastola. Akawanyooshea watu wale kwa zamu zamu huku akiwa amewakazia macho. Kitendo cha kuihamisha bastola kwenye uelekeo wa Robart na kumuelekezea Ata. Sekunde hiyo hiyo Robart aliitumia kufanya jambo lililomuacha mdomo wazi Kiulason. Kwa kasi isiyoyakawaida. Robart alimuwahi kwa teke kali kwenye mkono ambao ulikuwa umeshika bastola. Kabla bastola haijamruka mikononi mwake. Alijaribu kuminya ‘trigger’ na bastola ikatoa mlio hafifu wa vyuma. Bastola hakuwa ameitoa usalama kabla!.



    Bastola ikaruka pembeni. Robart aliinua mguu juu na kuushusha kwa kasi pale alipokuwa amekaa Kiulason kwa nia ya kumshindilia. Kiulason aliuona na kuupisha kwa kusogea pembeni. Kule pembeni alipo. Alirusha teke lililokuwa likienda kupiga kwenye goti la Robart. Robart aliliona na kujaribu kurudisha mguu wake nyuma kulihepa ila alichelewa kidogo. Teke la Kiulason lilienda kupiga kwenye ugoko wa Robart na Robart alitoa mguno wa maumivu. Muda wote Ata alikuwa amesimama kimya akiuangalia mchezo huo unavyoendelea.







    ENDELEA..



    Robart alijiweka sawa tena kipindi hicho Kiulason akiwa na yeye amesimama tayari kwa mapambano. Bastola yake ilikuwa usawa wa miguu ya Ata kwahiyo hakuwa na uwezo wa kuiwahi kabla hajawahiwa yeye. Hofu bado ilikuwa nae ya kupambana na watu wawili waliooenakana kuwa na uwezo mzuri wa kimapigano na hadi muda huo bado asielewe watu hao wanataka nini kutoka kwake.



    “Mnataka nini nyie? Mbona hamuongei?” Inspekta Kiulason aliwauliza kwa sauti iliyojaa mashaka muda huu akiona kabisa uwezo wa kuchomoka hapo ni mdogo. Bado waliendelea kuwa kimya vile vile.



    Robart akaona sio tabu kumjibu kwa vitendo. Akamfuata tena kwa mateke makali makali. Kiulason aliyahepa pembeni na kumfanya Robart aifumue vibaya Tv ya ‘Flat Screen’ iliyokuwa imeegeshwa ukutani. Ikasambaratika chini vipande vipande. Kkabla Robart hajakaa sawa. Kiulason akavuta Deki iliyokuwa imepangwa vyema kwenye meza na kufanya nyaya zikatike huko na huko. Kisha akampiga nayo kwa nguvu Robart ya kichwa. Deki ikasambaratika sakafuni huku Robart nae akiyumba yumba kama mlevi kwa kiwewe cha kupigwa kichwani.



    Robart alikuwa na mawenge mengi muda huu baada ya kuachwa na maumivu mengi kichwani kwake. Macho yalimuwia vigumu kuona mbele. Akayapikicha kisha akajaribu kutazama tena akiangalia kama ataweza kuona tena kwa uzuri. Bado ukungu ulikuwa umetanda machoni mwake. Akayapikicha tena na kupepesa kwa sekunde kadhaa. Walau sasa aliweza kumuoana vyema adui yake. Hasira zilimjaa pomoni baada ya kuona aliwekwa katika kilevi cha muda mfupi asichokitarajia.



    Akamuendea Kiulason kwa mapigo ya Tik taka yaliyomkuta kifuani. Kiulason akarushwa hewani na kwenda kujipigiza kwenye kabati la vyombo. Akalisambaratisha vibaya kwa kulivunja vioo huku yeye muda huo akiwa ameliegemea akimuangalia Robart kwa roho ya huruma. Alikuwa hoi kwa pigo hilo. Robart akiwa na hasira vile vile. Alimfuata Kiulason. Kiulason alikiona kifo kikiwa mbele yake.



    Ghafla aliinua kikombe cha dongo ambacho kilidondoka kutoka kabatini na kumrushia Robart kwenye paji la uso. Kikombe kikapiga kwenye paji la uso na kwavile kilikuwa na ufa kabla. Kikavunjika kabla hakijasambaritika vibaya sakafuni. Damu zilichuruzika kwenye viganja vya mikono ya Robart ambaye muda huo alikuwa ameiweka pale alipo jeruhiwa.



    Ghafla bila kutarajia Kiulason wala Robart. Ata alichomoka kwa kasi kule alipokuwa amesimama na kuenda kumkwida Kiulason. Akamning'iniza juu juu kama nyama buchani. Kisha akachia mkono mmoja na kumchezea kwenye shingo sekunde moja na sekunde iliyofuata alimuachia akiwa tayari ni mfu. Kitendo cha kupigana kati ya Kiulason na Robart aliona ni upotevu wa muda tu. Akapangusa mikono na kuanza kupiga hatua kutoka ndani humo akimuacha Robart mdomo wazi asitambue kama Kiulason alikuwa amekufa ama amepoteza fahamu kama sio kulala tu. Kimya kimya akiwa na mshangao wake akafuata nyuma na kupotelea huko.



    * *



    Siku iliyofuata taarifa zilienea haraka karibia mji mzima. Kuwa kuna askari ameuawa nyumbani kwake na watu wasiofahamika. Mr Hanein alipozipata taarifa hizo alifurahi sana na kuwapongeza vijana wake. Siku hiyo aliwapa kiasi kikubwa cha pesa na kuwataka wakafurahike popote wanapotaka ndani ya mji huo.



    Nyumbani kwa Kiulason palifurika vilio kutoka kwa mke wa Kiulason na watoto wake. Walikuwa wakilia sana huku wakisaidiwa na majirani kuomboleza msiba huo. Askari walijaa nyumbani hapo ikiwa pia ni katika kuhudhuria katika kifo cha mfanyakazi mwenzao. Kila mmoja alikuwa na majonzi kwa kumpoteza mpendwa wao. ‘Bwana ametoa na Bwana ametwaa.’ Ndio msemo uliosikika sana mahali hapo.



    TSSI 01 taarifa za msiba wa Inspekta Kiulason zilimchanganya sana. Maana alimuahidi mkuu wake kuwa atajitahidi kuzuia vifo vya askari mpaka pale watakapopatikana wauaji hao. Alijua lawama zitakazotoka kwa mkuu wake sio ndogo na pengine asiweze kuzivumilia. Hammadi!. Simu yake iliita na alipoangalia kwenye kioo nani anapiga akakuta kuwa ni mkuu wake ndie anaempigia. Akajishauri aipokee ama asiipokee.



    Simu ikakata yenyewe akiwa bado anajishauri. Mara simu ikaita tena akaitwaa na kuipokea. Baada ya salamu Mr Kaoneka alimpa pole kwa kufiwa na afisa mwengine wa jeshi la polisi. TSSI 01 hakujua kama hiyo pole ni ya kweli ama amedhihakiwa tu. Akaipokea kwa unyonge. Mkuu wake akamtaka maelezo na yeye akamueleza kila kitu hadi hapo alipofikia kwenye uchunguzi wake. Zaidi alimueleza pia tukio lililotokea siku iliyopita la kujaribu kuzuia uporaji wa silaha.



    Mr Kaoneka akashtuka. Inamaana kumbe wale watu tulio wadhibiti huku ndio na hao wa Hanein walikuwa pamoja? Akajiuliza mwenyewe. Na yeye akamuelezea tukio lililotokea siku chache nyuma la Hilda kuwashuku vijana wawili kuwa wanampango hasi na wakakuta ni kweli walikuwa na mpango wa kununua silaha katika mji huo. Ila ambapo walitaka kununua ndipo ambapo hapakujulikana. Mr Kaoneka ndipo alipopata jibu kuwa watu wale walikuwa na mpango wa kununua silaha hizo kutoka kwa kundi la Mr Hanein.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    TSSI 01 akajifanya kushtuka kwa taarifa hiyo ili asimshtue mkuu wake kuwa alishaelezwa kabla na Hilda taarifa hizo. Mwisho Mr Kaoneka alimuambia Hemedy kuwa anampa siku tano tu za kumaliza kazi hiyo na kama zikipita basi itabidi arudi kitengoni ama atumwe mtu mwengine wakuja kusaidiana nae. Taarifa hiyo Hemedy aliipokea kwa unyonge kwa kuona kuwa anaonekana anachelewa kuimaliza kazi hiyo mapema tofauti na alivyoahidi kipindi anakabidhiwa.



    Akajibu kwa kujiamini kuwa ndani ya siku hizo tano atakuwa ameshaimaliza kazi hiyo na atarudi kitengoni na ushindi. Mr Kaoneka alifurahi baada ya kuona kijana wake amemjibu kwa kujiamini na kumhakikishia ataimaliza kazi hiyo ndani ya siku hizo alizompa. Akamuuliza kama kuna anachokihitaji aongezewe na yeye akajibu kuwa kila kitu kipo sawa. Simu ikakatwa.



    TSSI 01 alibaki na tafakuri nzito akiwaza ni vipi ataimaliza kazi hiyo ndani ya siku hizo alizopewa? Akiwa anaendelea kuwaza. Simu yake ikaita tena. Alikuwa ni Hilda ndie anaempigia. Wakasalimiana wapenzi hao wanaofanya kazi kitengo kimoja na kuzungumza machache. Hemedy alimpasha siku alizopewa na mkuu wao za kumaliza kazi hiyo. Hilda akampa moyo kwa kumuambia kuwa anaamini ataimaliza kazi hiyo ndani ya siku hizo. Kwa kiasi fulani akafarijika na kuingiwa na nguvu mpya na matumaini ya kuifanikisha ‘mission’ hiyo ndani ya hizo siku alizopewa.



    Simu ikakatwa. Sekunde kadhaa mbele simu yake ikaita tena ikiwa bado mkononi mwake. Akaangalia anaempigia na kukuta ni IGP Taure ndie ambae aliekuwa akimpigia. Akaipokea na baada ya salamu. IGP Taure akamtaka afike kituoni muda huo. Akaahidi kuwa ndani ya dakika thelathini atakuwa huko. Simu ikakatwa na Hemedy akaenda chumbani kwake kwenda kujiandaa.



    Alipomaliza. Akatoka nje na kupanda gari lake la kawaida akiliacha lile alilopewa na kitengo. Safari ya kuenda kituo cha Polisi Chumbageni ikaanza. Dakika kadhaa mbele akawa amefika. Akaingia moja kwa moja ofisini kwa IGP. Hapo alimkuta Inspekta Salum akiwa amekaa na IGP Taure wakimsubiri yeye. Akakaa kwenye kiti baada ya kuwasalimu.



    “Nadhani taarifa za kifo cha Inspekta Kiulason umezipata” IGP alianza hivyo. Hemedy alijibu kwa kichwa kukubali.



    “Bilashaka kifo chake ni muendelezo wa vifo vilivyopita vilivyosababishwa na vijana wa Mr Hanein tunaowashuku. Sasa wewe unalipi la kusema mpaka hapa” TSSI 01 alikuna kichwa kwa sekunde kadhaa.



    “Kama ulivyosema kifo cha Inspekta ni muendelezo wa vifo vya askari waliopita. Naweza nikakubaliana na hilo na....”



    “Kivipi?” IGP alimkatisha kwa kumuuliza.



    “Kwasababu jana usiku tulikuwa kwenye tukio mimi na Inspekta hapa....” Akakatishwa tena na swali kutoka kwa IGP iliyomtaka amjulishe ni tukio gani walilokuwa wakilifanya huo usiku. IGP alionekana kutokuwa na subira hata kidogo. TSSI 01 alimtazama Inspekta Salum kisha akamtazama IGP. Akamuhadithia mwanzo mwisho tangu ‘mission’ hiyo fupi ilivyoanza kwasababu ya maelezo yasiyoeleweka ya marehemu Inspekta Kiulason hadi hapo ilipofikia. Na siku hiyo kupatikana kwa taarifa ya kuwa Inspekta ameuawa.



    IGP alishusha pumzi za mshangao na kuwatazama vijana hao waliokuwa mbele yake. Hakuweza kulaumu kwa kutojulishwa mapema swala hilo kwasababu alijua kazi hiyo haikuwa ikihusika kwa jeshi la polisi maana lilishaachishwa mapema kufuatilia vifo vile vilivyokuwa vikitokea siku kadhaa nyuma. Sasa alipata mwanga wa tukio lilitokea siku iliyopita ya uvamizi wa kituo cha polisi huko Muheza.



    Akawauliza ni nini wafanye na TSSI 01 akamuambia kuwa ni lazima jambo hilo libaki siri ya kwamba uvamizi ule ulikuwa ni wakujaribu kupora silaha zilizosemekana kuwa zilikuwa katika ghala lililokuwa ndani ya kituo kile. Inspekta Salum akapata nguvu ya kuuliza swali lake. Yeye alitaka uhakika ya kuwa. Je ni kweli kituo kile kilikuwa na ghala la kuhifadhia silaha? IGP Taure alimtazama kwa muda kisha akamjibu kuwa hakuwa na uhakika kama ni kweli kituo kile kilikuwa na ghala la kuhifadhia silaha.



    Kwasababu mara nyingi silaha husambazwa vituoni na gari maalumu na zinatokea makao makuu ya jeshi la polisi. Sasa kama kuna usemi wa kuwa katika mji huo kuna ghala la lililokuwa likihifadhia silaha. Hapo hawezi kujibu kitu kwasababu hana uhakika wa hilo jambo japokuwa yeye ana cheo cha juu katika jeshi la polisi. Kwa maelezo hayo ilitasfirika kuwa Kiulason aliwadanganya watu hao waliomtaka kuwatafutia ukweli wa hilo jambo.



    Ndio!. Ni kweli marehemu Kiulason alitumia mbinu hiyo ya kumdanganya Mr Hanein ili apate kuokoka yeye na familia yake. Siku ile ambayo aliingia kwenye ofisi ya IGP Taure kwa siri. Alikuwa akitafuta namna ya kufanya ili atakapompa maelezo Mr Hanein yafanane na ukweli. Na kwa vile alijua amemdanganya Mr Hanein. Alijua kivyovyote endapo ikigundulika ni uongo basi mtu huyo anaweza kumdhuru yeye kama si wote yeye na familia yake. Na ndio maana muda mwingi alikuwa ni mtu mwenye mawazo mengi sana.



    TSSI 01 alimuomba IGP isije akatoka askari yoyote kuenda kumuhoji mke wa marehemu Inspekta Kiulason. Maana alijua mama yule atakuwa na mengi ya kumueleza kuhusu kifo cha mume wake. IGP alikubaliana nae kwa kumuambia kuwa hatokwenda askari yoyote hadi yeye atakapoenda. Ukafungwa mjadala na TSSI 01 akaondoka akimuacha Inspekta Salum akielekea ofisini kwake kuendelea na majukumu mengine kabla hajaenda kwenye msiba.



    Hemedy alipotoka kituoni. Moja kwa moja alienda nyumbani kwa marehemu Kiulason. Alipofika alikuta umati wa watu ukiwa umefurika nyumbani hapo. Akawapita na moja kwa moja hadi sebuleni. Huko aliwakuta wakina mama wakiwa wamekaa kihuzuni na katika kona ya sebule hiyo. Alimuona mke wa Kiulason.



    Akasalimia na kumuomba mke wa Kiulason amfuate. Mke wa Kiulason aliinuka katikati ya kundi lile na kina mama na kutoka nje alipokuwa ametoka Hemedy. Wakatafuta sehemu nzuri nyuma ya nyumba hiyo. Hemedy alianza na kumpa pole na pole hiyo ikasababisha kilio kutoka kwa mke wa Kiulason. Alilia sana huku Hemedy akimuangalia tu na wala asifanye jitihada zozote za kum'bembeleza. ‘Kilio hupunguza walau theluthi ya uchungu’. Alizingatia msemo huo na ndio maana alimuacha mama huyo alie pekeake.



    Baada ya dakika kadhaa mbele. Mke wa Kiulason alinyamaza. Akafuta machozi na kumuangalia Hemedy usoni.



    “Mume wangu jana asubuhi alivyokuja na kuondoka ghafla. Alirudi tena usiku majira ya saa nne. Muda wote kabla hajarudi mi nilikuwa nahofu hadi pale aliporejea tena majira hayo. Nikajaribu kukaa nae chini nikimuuliza ni kipi hasa kinachomsibu hadi kuwa katika hali ile aliyokuwa nayo. Mara ya kwanza alinijibu tu kwa upole akiniambia kuwa ataniambia kesho yake ambayo ni leo. Ila nilipomfosi sana huku nikijaribu kumshawishi kwa kumuambia kwamba ni lile tukio la kutekwa wote siku chache zilizopita ndio lilikuwa likimchanganya. Akanijia juu kwa kunikaripia akiniambia hata kama ikiwa ndio hivyo mimi nitafanya lipi? Akanisihi niondoke mahala pale kabla hajanishushia kipigo. Kwa vile wakati huo watoto walikuwa ndani wamelala. Mi sikuona ni vizuri kuendelea kulumbana nae na kuwaletea watoto kero. Mi nikaondoka nikijua siku ya leo nitaambiwa kila kitu kinachomsumbua...” Akatulia na kufuta chozi lililokuwa lilitoka kwenye jicho lake la kulia.



    “Mi kinachonitia wasiwasi na kuhisi kuwa waliofanya mauaji ya mume wangu ni wale waliotuteka wote siku ile ni ile kauli ya mume wangu aliponijibu kuwa kama ikiwa ni wao mi nitafanya lipi.....” Akatulia na kumuangalia mtu aliekuwa akija mahala hapo. Alikuwa ni mwanamke. Akamuambia kuwa kulikuwa kuna mtu anamuhitaji yeye. Akamjibu kuwa anakuja hivi punde. Yule mwanamke akaondoka na mke wa Kiulason akawa huru kuendelea kumueleza Hemedy.







    “Jana usiku majira ya saa ngapi sijui. Ila ulikuwa ni usiku mwingi. Mi nikiwa chumbani nimelala lakini sio usingizi, nikitafakari ni vipi nitamsaidia mume wangu arudi kwenye hali yake ya kawaida. Nilisikia minong'ono ya mume wangu sebuleni. Nikadhani basi atakuwa akiongea na simu. Lakini muda mfupi mbele nikaanza kusikia purukushani sebuleni. Nikaona ninyanyuke nikajue kunani huko. Wakati napiga hatua kuifikia sebule. Nikaona kuna watu wawili, mmoja akiwa amesimama na mwengine alikuwa akipigana na mume wangu. Nikarudi nyuma na kujibanza upenuni mwa ukuta wa kordo nikatulia kimya nione nini kitatokea. Nilikuwa na hofu sana kuona mume wangu akipigana na yule mtu. Waliumizana sana lakini ghafla tu yule mtu ambae mwanzo alikuwa amesimama alienda kumminya mume wangu shingoni na mume wangu akalala chini na wao wakaondoka. Mi nikajua basi atakuwa amezimia tu. Nikakimbia hadi pale alipolala na kuenda kumuamsha. Nilimuamsha sana ila mwisho ndipo nikagundua kuwa amekufa. Nililia sana na nikazimia na sikujua chochote kilichoendelea hadi hii alfajiri nilipozinduka na kujikuta chumbani huku nikipewa taarifa kuwa mume wangu amepelekwa hospital akiwa tayari ni mfu. Ila nakiri kuwa waliofanya mauaji ya mume wangu ni walewale waliotuteka siku ile maana yule aliekuwa akipigana na mume wangu niliwahi kumuona ile sehemu tulipohifadhiwa. Jamani mume wangu hatunae tenaaa aaa!.”



    Baada ya maelezo marefu mke wa Kiulason akalia kwa uchungu. Mara hii Hemedy alim'bembeleza kumpoza machungu. Akamuuliza kuwa wakati yote yakitokea mlinzi wa nyumba hiyo alikuwa wapi? Nae akajibu alikuwepo hapo hapo nyumbani. Hemedy akashukuru na kumtaka waondoke hapo. Wakaondoka na mke wa Kiulason akaelekea kule alipotakiwa na Hemedy alimfuata mlinzi kwenda kumuoji chochote.



    Maskini ya mungu mlinzi hakujua chochote kilochokuwa kikiendelea muda huo. Yeye alikuwa amelala na aliamka akiwa anajua ametoka kulala na taarifa za msiba wa bosi wake alizipata alfajiri ya siku hiyo. Hemedy akaona hana anachokijua mlinzi huyo. Akajua hao watu waliofanya mauaji walifanya kitu kwa mlinzi kabla ya kwenda ndani. Akamuaga na kuondoka zake.



    * * * *



    Siku mbili mbele. Mazishi ya Inspekta Kiulason ndio yalikuwa yakifanyika siku hiyo. Ndugu jamaa zake na marafiki walikusanyika nyumbani hapo kuja kumuaga ndugu yao vya mwisho. Nyimbo za kuomboleza zilisikika kutoka kwa wakina mama waliokuwa wamekaa hapo.



    Muda wa kuuaga mwili wa marehemu ulifika na jeneza likafunuliwa. Watu wakapanga mstari kwenda kumuona vya mwisho kabla hajapelekwa kwenye makazi yake ya milele. Akaanza mke wake ambae alipofika pale alilia sana kiasi ambacho alilikumbatia jeneza. Wakina mama waliokuwa karibu nae muda wote walienda kumtoa mahala pale huku wakimnasihi. Wakafuata watu wengine.



    Zoezi hilo lilipoisha. Sala ya kumuaga ikafuata chini ya Askofu wa kanisa alilokuwa akisalia. Baada ya muda. Watu wakajiandaa kwenda mazikoni katika makaburi ya Makorora Mzingani. Watu wakapanda magari tayari kwenda kulifanikishwa swala hilo.



    Kwasababu hapakuwa mbali sana. Dakika kumi na tano zikatosha kuwafikisha. Taratibu za maziko zikafanyika chini ya Askofu yule yule. Muda wote huo mke wa marehemu Inspekta Kiulason alikuwa akilia akiwa hataki kuamini kirahisi ati ya kuwa ndio anaenda kumfukia mume wake na hatomuona tena maishani kwake. Ilikuwa ni huzuni sana kwa familia hiyo kwa kuondokewa na kichwa cha familia.



    Wakati ibada za mwisho mwisho zikiwa zinaendelea. Deva, Ata na Robart walikuwa hapo kila mmoja sehemu yake. Walikuwa wamekuja kushuhudia mazishi ya Inspekta. Ikiwa pia wapo kuchunguza kama watamuona TSSI 01. Wajue nini wafanye ikiwezekana kuondoka nae wakamfanye vile wanavyotaka maana walishagundua yeye ni mmoja wapo aliekwamisha mpango wao wa kupora silaha kule Muheza kwenye kituo cha polisi.



    Macho yao yalikuwa hayatulii sehemu moja. Mara huku mara kule wakiangalia ni wapi wanaweza kubahatisha kumuona. Walikuwa wakiwasiliana kwa kutumiana ujumbe kwa njia ya simu wakipashana lolote atakalo hisi mmoja wao. Ata alikuwa katikati ya umati wa watu kimya akiendelea na uchunguzi wake. Deva yeye alikuwa upande wa kushoto wa umati ule wa watu huku Robart akiwa nyuma kabisa.



    Kwakuwa sio wote waliokuwa karibu na umati ule ambao ulikuwa karibu kabisa na kaburi. Wengine walikuwa vikundi vikundi mbali kidogo na umati ule na wengine walikuwa wamekaa juu ya makaburi mengine yaliyokuwa eneo hilo. Hiyo ikiwa pia ni kuhudhuria mazishi hayo.



    Katika watu waliokuwa nyuma nyuma ya umati ule. Kulikuwa kuna mzee mmoja alie ndani ya suti za bei ya chini huku kichwani akiwa amevaa kofia ya mkeka. Machoni akiwa amevaa miwani. Alikuwa kimya amesimama. Pamoja na kuonekana ni mtulivu sana. Lakini macho yake yaliyofichwa ndani ya miwani. Yalikuwa hayana utulivu hata kidogo. Alikuwa akiyapepesa huku na huko mahala hapo.



    Mara nyingi alikuwa akimtazama Robart ambae alikuwa hana utulivu. Robart katika pepesa yake ya macho. Akamuona mzee yule akiwa anamtazama yeye. Na alijua kuwa anatazamwa yeye kwasababu yule mzee alikuwa amegeuza shingo na kule alipo yeye. Yule mzee alipoona anatazamwa na aliekuwa akimtazama. Akarudisha shingo yake taratibu na mbele. Akamtazama kwa jicho pembe Robart na akamuona akiwa bado akimtazama yeye.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yule mzee alitabasamu na kuanza kupiga hatua ndogo ndogo kwenda upande ulipokuwa hakuna umati wa watu. Robart akajikuta akivutiwa na mzee yule. Akaangalia huku na huko kuwatazama wenzake na kuwaona kila mmoja akiwa makini kivyake. Akaanza kupiga hatua kuelekea kule anapoelekea yule mzee. Yule mzee alikuwa akienda mbali na kabisa na ulipo umati ule sehemu kulipokuwa na mti mkubwa wa Mkuyu uliozungukwa na vichaka vichache lakini vyenye uwezo wa kutomuwezesha alieko upande mmoja asiweze kuona upande mwengine hadi azunguuke.



    Yule mzee alipofika pale vichakani. Akatulia kimya na kutoa sigara kwenye mfuko wake wa koti. Akatoa na kiberiti cha gesi kutoka kwenye mfuko mwengine na kuiwasha ile sigara. Akavuta hewa ndani na kukirudisha kile kiberiti mfukoni mwake. Mara punde Robart alitokea eneo lile. Mzee akatoa moshi wa sigara na kutabasamu baada ya kumuona Robart. Akakohoa kidogo na isijulikane kuwa amepaliwa na moshi ama ni uzee ndio unamsumbua.



    “Naona kijana wangu umeamua unifuate mpaka huku nilipokuja... Vipi unataka sigara ama nikupatie kiberiti uwashe ya kwako?” Yule mzee alimuuliza Robart kwa sauti ya kukwaruza huku akitabasamu. Robart akajua kuwa mzee huyo alikuja huku kuja kuvuta sigara, aliondoka kule kukwepa kuwaudhi watu. Bila kumjibu chochote akageuka na kuanza kupiga hatua kuondoka hapo.



    “Mpo vyema sana kuua askari. Kwani mmepanga ni idadi ipi mkifikia ndio muache kuua?” Yule mzee alimuuliza huku akiwa anaipigapiga ile sigara kwa juu akiondoa vumbi sehemu iliyokwisha kuvutwa. Robart akageuka nyuma kwa kasi baada ya kushtuliwa na kauli ya mzee yule.



    “Unasemaje wewe mzee?” Alimuuliza kwa taharuki huku akimkazia macho ya mshangao.



    “Umeniskia ila sema jeuri tu” Mzee akajibu. Kisha akaipeleka tena mdomoni ile sigara. Akavuta hewa ndani na kupuuliza moshi juu kwa jeuri.



    “Wewe ni nani?” Robart akauliza kwa hofu.



    “Mwokozi”



    La haula!.



    Kidogo tu Robart azimie kwa presha baada ya kusikia kaulia ya mzee huo. Mwokozi!. Hili neno hata Pijo aliambiwa siku ile walipoenda kuvamia kule kituoni. Inamaana aliemvunja taya Pijo ndio huyu ama? Robart alijiuliza huku kwenye paji la uso pakikunjikana na macho akiyafinya na kuyafanya yawe madogo kama ya wajapani. Hatari!. Nini afenye?



    Akaingiza haraka mkono wake wa kulia kwenye mfuko wa suti aliyoivaa kisha akachomoka na bastola. Kitendo bila kuchelewa. Mzee akairusha ile sigara ambayo bado muda huo ilikuwa na moto. Akairusha kwa ustadi mzuri na moja kwa moja ikaenda hadi kwenye jicho la Robart la kushoto. Ikachoma na kuanguka chini. Robart alipiga kelele za maumivu huku akiisahau kabisa bastola aliyoitoa japokuwa bado ilikuwa mkononi kwake.



    Robart aliinuka kwa hasira baada ya kupiga mayowe ya uchungu na kumnyooshea bastola Mzee, jicho lake la kushoto akilifumba akitumia jicho moja tu kuona. Ila alikuwa amechelewa sana. Bastola ilibetwa na pembeni na kuenda kuruka vichakani. Papo hapo akapigwa ngumi ya taya na kumalizwa na nyengine ya pua. Maumivu aliyokuwa akiyasikia hayakuwa madogo hata kidogo.



    Akiwa bado anababaika kwa maumivu. Alishikwa kichwa na kupigwa vigoti vingi vya kidevu. Kisha akamaliziwa na ngumi kali ya sikio ambayo ilimfanya Robart kujirusha pembeni na kwenda kugaagaa chini akihisi maumivu mengi sana. Mdomoni alikuwa akitoa udenda uliochanganyikana na damu. Yule mzee alikuwa kimya akimtazama vile alivyokuwa akigaagaa pale chini kama nyoka aliemwagiwa mafuta ya taa.



    Robart akajizoa zoa pale chini. Akainuka huku mkononi akiwa amekamata kigongo alichokiokota pale pale chini. Akiwa anayumbayumba kama mlevi. Akamuangalia kwa hasira mzee yule aliekuwa akimtabasamulia kwa dharau. Akafinya finya jicho lake ambalo lilikuwa zima huku lile jengine likiwa halina tena uwezo wa kuona baada ya moto wa sigara kuchomo kwenye mboni ya jicho. Lilikuwa likitoa maji maji yaliyokuwa yakichuruzika hadi mashavuni na kwenda kuungana na damu zilizokuwa zikitoka mdomoni kwa wingi.



    Robart akajizoa zoa pale chini. Akainuka huku mkononi akiwa amekamata kigongo alichokiokota. Akiwa anayumbayumba kama mlevi. Akamuangalia kwa hasira mzee yule aliekuwa akimtabasamulia kwa dharau. Akafinya finya jicho lake ambalo lilikuwa zima huku lile jengine likiwa halina tena uwezo wa kuona baada ya moto wa sigara kuchoma kwenye mboni ya jicho. Lilikuwa likitoa maji maji yaliyokuwa yakichuruzika hadi mashavuni na kwenda kuungana na damu zilizokuwa zikitoka mdomoni kwa wingi.



    “Ningekuacha uende ukawape salamu wenzako uwaambie kuwa mwisho wenu umefika. Ila nasikitika kukuambia kuwa siwezi kurudia tena ujinga wa kumuacha yoyote kati yenu hai pindi nikikutana nae uso kwa uso kama wewe hivi sasa. Maana mkiachiwa mkajifunze, mnaua tena. Bahati hiyo iliwatokea wenzako wale mapacha na hivi punde mtaungana nyote kuzimu mkafanye uhalifu huko” Mzee aliongea kwa jeuri. Akatoa tena sigara nyengine na kuiwasha. Robart akachomoka mbio na kile kigongo kwenda kumvaa Mzee. Mzee akamtupia kiberiti ambacho kilienda kugonga kwenye meno ya Robart yaliyokuwa nje kipindi ambacho Robart amefumbua mdomo na kupiga kelele za ghadhabu.



    Kile kiberiti kikaanguka chini na sigara nayo ikafuata chini baada ya kuachiwa na Mzee mdomoni kwake. Akabonyea chini akilipisha gongo lipite baada ya kurushwa usawa wa kichwa chake. Gongo likapita na ile kofia ya mkeka, na nywele nyingi zikaonekana kwenye kichwa cha yule mzee. Nywele ambazo zilimshangaza Robart maana hazikuwa na hata dalili ya kuota mvi tofauti kabisa na umri wa mzee yule ambae kwa muonekano tu alitakiwa awe tayari na mvi kichwani.



    Hakuachwa kushangaa sana nywele za mzee. Akapigwa ngumi tatu za kifua na kumaliziwa moja ya tumbo kabla hajapigwa ‘kata funua ya kidevu’. Akarushwa hewani huku gongo likimtoka mkononi na kudondokea pembeni na yeye kwenda kujibwaga chini vibaya kwenye kisiki kilichomchoma mgongoni na kumuachia maumivu makali sana. Akapiga mayowe ya uchungu huku akijibenua kwa mbele na mkono wake mmoja akiupeleka mgongoni kwake kupashika pale alipoumia.



    Machozi yalimtoka kwa uchungu huku akimuangalia Mzee kwa hasira na jicho lake moja. Akataka kuinuka ila alishindwa, akarudi tena chini. Alikuwa akilia kwa uchungu si mas'hara. Akatoa simu yake ili awajulishe wenzake kuwa anapata tabu huku na anahitaji msaada. Muda wote yule mzee wa ajabu alikuwa akimuangalia anachofanya. Akamfuata kwa hatua za taratibu hadi pale chini. Akamuinua juu na Robart simu ikamdondoka chini.



    Akamuangalia usoni kwa muda kisha akamrusha hewani na kumpiga teke kali la kiuno lililomrusha hadi kwenye ule mti wa mkuyu. Akajipigiza vibaya maeno ya kichwani na kutua chini kwa kishindo kisha akawa kimya pale. Damu zilizidi kutoka mdomoni na sasa hata puani pia zilikuwa zikitoka. Mzee akaiokota ile simu ya Robart na kuiangalia. Alikuta ujumbe ambao haukumaliziwa kuandikwa kwenye uwanja wa meseji.



    ‘Msaada wa haraka nak’ ilisomeka hivyo. Akacheka kidogo na kuumalizia ule ujumbe. Aliandika hivi. ‘Msaada wa haraka nimeshakufa huku nahitaji maiti yangu muiwahishe monchwari’ Akautuma ule ujumbe na ile simu akaiweka pale pale. Akaanza kukimbia baada ya kusikia sauti za vishindo vya watu wakija kwa kasi hapo.



    Walikuwa ni Deva na Ata waliokuwa wakija hapo baada ya kumtafuta sana mwenzao na wasimuone. Mara kadhaa walisikia mayowe lakini hawakuyapatiliza, walidhani ni makelele ya vijana wa bodaboda waliokuwa karibu na eneo hilo la makaburi. Ila baada ya kusikia kelele zinazidi na mwenzao hawamuoni na majira hayo watu walikuwa wameshatawanyika mahala hapo. Ikabidi wakimbilie huko wakajue kunani.



    Wakati wanafika pale. Walimuona mtu akiruka makaburi na kupotelea kwenye nyumba zilizokuwa eneo lile. Hawakumjali sana badala yake macho yao wakayahamishia kwa mwenzao aliekuwa chini ya mti akiwa kalala kimya. Wakamsogelea kwa tahadhari maana hali waliyomuona nayo haikuwa ya kawaida hata kidogo. Mwili mzima alitapakaa damu. Wakajaribu kumuangalia kama atakuwa ni mzima.



    Wakagundua kuwa alikuwa ni mfu kitambo. Ghadhabu zikawaingia. Ata akamtaka Deva haraka amfuatile yule mtu aliepotelea kule kwenye nyumba maana walishahisi huenda ikawa ndie aliefanya mauaji ya mwenzao. Deva akatoka mbio kuelekea kule alipopotelea yule mzee. Alipofika akashika na kichochoro kilichokuwa mbele yake. Alikimbia na kukimaliza chote. Akatokea katikati ya mtaa. Akasimama akiwa haelewi aende wapi maana vichochoro vilikuwa vingi sana sehemu hiyo.



    Kwenye nyumba moja iliyokuwa na duka la nafaka. Alionekana TSSI 01 akiwa amekaa kwenye kibaraza akinywa juisi ya ukwaju iliyokuwa ndani ya kichupa. Deva hakumjua mtu yule kwasababu hakuwahi kukutana nae ila TSSI 01 alijua kuwa ni mmoja kati ya wale wabaya wake. Deva akawaza amuulize mtu yule juu ya mtu wake anaemtafuta. Lakini alishwanda atamuelekeza vipi ilhali hata sura ya yule mtu hakuiona. Aling'aka kwa ghadhabu na kurudi kule alipotoka. TSSI 01 akatabasamu na kuchukua kofia ya mkeka iliyokuwa pembeni yake. Akaivaa na kuenda kule Deva alipoelekea.





    ENDELEA.



    Deva alipofika alimpa taarifa Ata ya kuwa hakufanikiwa kumuona yule mtu aliekimbia na kule. Ata akashusha pumzi na kutoa simu yake mfukoni. Ghafla alikunja uso na kisha kuachia cheko refu. Deva akashangaa na asijue ni kipi akichekacho mwenzake. Ata alimpatia simu Deva na Deva akausoma ujumbe uliotumwa na Robart. Ulimshangaza sana. Hii ni nini? Akajiuliza. Akamuangalia usoni Ata na kumkuta akiwa amekunja sura kwa ghadhabu. Ina maana Robart kabla ya kufa alituma ujumbe huu? Kivipi? Ajabu sasa hii!.



    Ata alimuambia Deva waondoke. Deva akahoji kuhusu mwili wa Robart na Ata akamjibu kuwa waondoke wauache hapo hapo. Deva alitaharuki kwa maamuzi ya Ata. Inakuaje tuuache mwili wa mwenzetu ilhali uwezo wa kuondoka nao upo? Akajiuliza. Akajua kuwa thamani yao inaonekana wakiwa hai tu ila wakiwa wafu hawathaminiwa tena. Hilo alilithibitisha kwenye mwili wa Zinah kule kituoni walipouacha na alipohoji akaambiwa kuwa utawaletea matatizo. Kwa vile aliesema ni mtoto wa mkuu wake. Akafuata tu.



    TSSI 01 aliwaona watu wale wakipakia kwenye gari lao na kupotelea huko. Akaanza kurudi kule alipotoka. Ila kuna wazo lilimjia. Kwanini nisiwafuatilie nijue mwisho wao? Akajiuliza. Ghafla akanywea baada ya kukumbuka kuwa gari lake ameliacha msibani. Hata hivyo pia anauwezo wa kukodisha bodaboda na ikampeleka mpaka huko wanapoenda watu wale. Akalipitisha wazo hilo na kuamua kulifanya haraka. Akakimbia kuifuata barabara waliyoingia nayo watu wale.



    Japokuwa kuna gari nyingi zilionekana barabarani hapo ila gari anayoitaka hakuiona na pia hakujua imeingia na njia gani. Akajua amewakosa tena kwa siku hiyo. Ila alijipongeza kwa kumpunguza mmoja. Akarudi kule alipotoka na kukifuata kile kichochoro alichotokea nacho. Akarukia dirisha la kwenye boma la nyumba. Na ndani humo akatoka na begi la mgongoni na kuruka tena nje. Akapotelea mitaani.



    TSSI 01 alipofika msibani. Akakuta umati wa watu ulikuwa umeshapungua mahala hapo. Akamtafuta Inspekta Salum na kumpata. Akamueleza yote yaliyotukia kule Mzingani muda mfupi uliopita. Salum alibakia mdomo wazi asiamini. Kumbe ndio maana nilikuwa nikikutafuta sana lakini sikukuona? Akamuuliza.



    “Sasa tunafanyaje?” Hemedy alimuuliza.



    “Inabidi tumpe taarifa IGP ya hili tukio ikiwezekana hiyo maiti ikachukuliwe haraka kabla haijagundulika na watu na kuleta hofu” Hemedy akamuambia basi afanye hivyo. Na taarifa zilipomfikia IGP Taure, akaagiza askari waende huko.



    “Ok. Na sisi tunaenda wapi?” Hemedy alimuuliza.



    “Nipeleke hom ndipo uendelee na shuhuli zako maana mimi nilikuja na gari ya kazi na tayari ishaondoka” Wakapakia gari ya Hemedy na safari ya kuenda nyumbani kwa Inspekta Salum ikaanza.



    * *



    Ata na Deva walifika kambini kwao. Walikuwa wanyonge hasa hasa Deva ambae mwenzao aliuliwa na mwili wameutelekeza huko kwa amri ya Ata. Walipofika ndani ya nyumba. Waliwakuta Pijo na Queen wakiwa wanacheza karata. Mara hii kidogo siha ya Pijo ilianza kutengemaa baada ya kupewa huduma na Atu. Wakapitiliza moja kwa moja hadi ndani na kumkuta Mr Hanein akizungumza na Atu huku wakicheka.



    Wakakaa kwenye viti wakiwaacha watu wakiwatazama kwa mshangao. Pijo na Queen waliingia ndani nao na mara hiyo Mrutu nae akafika hapo. Ikawa kikosi cha Mr Hanein kilichobakia kimekamilika huku Paskali yeye akiwa mjini anasimamia mali za Mr Hanein.



    Wakaulizwa ni vipi waondoke watatu na warudi wawili? Mwenzao yupo wapi? Wakatoa maelezo yote. Hilo lilikuwa ni pigo jengine kwa Mr Hanein. Ni vipi vijana wake wapungue namna hiyo? Huyu mshenzi ni lazima tumfanyie kitu. Aliwaza Mr Hanein baada ya kupewa taarifa hiyo. Akawauliza ni wapi mwili Robart ulipo, na Ata akajibu wameuacha huko huko kwasababu wameshindwa kuuchukua.



    Queen na Pijo walihuzunika sana baada kusikia kuwa Robart amekufa na cha zaidi mwili wake umetelekezwa huko huko. Kama alivyowaza Deva na wao pia wakawaza hivyo hivyo, kuwa thamani yao ilikuwa ikionekana wakiwa wazima tu kama hivyo, ila kama watakuwa wafu basi huweza kutelekezwa popote pale kama ilivyokuwa kwa Zinah na Robart. Je kama angeuliwa Atu ama angekufa Ata. Na wao pia miili yao ingetelekezwa?



    “Tunafanyaje? Maana naona huyu fala anataka kunipanda kichwani sasa” Mr Hanein aliongea huku uchungu ukionekana dhahiri kwenye macho yake.



    “Kwani kwake si panajulikana?” Pijo akauliza. Jibu likatoka ni ndio. “Kama kwenye msiba hakuepo, basi afuatwe kwake watu wakamalize kazi huko huko”



    Wakakuna vichwa kuitafakari rai ya Pijo. Wote wakaona ni kweli kuna ulazima wa kufanya hivyo. Maana mtu huyo amekuwa mwiba kwao na aliwafanya washindwe kufanikisha mambo yao mengi. Mr Hanein akalibariki amuzi hilo na kuwatayari kuwatuma vijana wake waende huko.



    Pamoja na kuwa kwa muda mrefu alikuwa katika kundi hilo. Ila bado ile kauli ya uchungu wa mwana aujuae mzazi ilitembea nafsini kwake. Mrutu hakujua ni kwa namna gani anaweza kumuepusha TSSI 01 Hemedy Bhachu na kifo kilichokuwa kikipangwa angali yeye pia yupo hapo. Kutoka ndani ya nyumba hiyo hakuwahi kutoka hata siku moja na hajui kama anaruhusiwa kutoka ama laa! Sasa nini afanye ilikumuokoa Hemedy na kifo? Hakujua!.



    Mpango wa kumuendea Hemedy nyumbani kwake ukakamilika. Ata na Deva wakaonelewa waende wao huku Queen akibaki kuangalia hali ya Pijo. Na Atu abaki na Mr Hanein waendelee na soga zao. Kwakuwa kauli ilitoka kwa mkuu wao. Hawakuwa na chakupiga tena. Wakaenda kubadilisha nguo na kujipanga zaidi maana mtu wanaeenda kukabiliana nae hakuwa mdogo kwenye mapigano.



    Wakatoka na safari ya kwenda nyumbani kwa adui yao ikaanza. UHASAMA uliopo kati ya Deva na Ata haikujulikana umeishia wapi baada ya kufanya ‘mission’ mbili wakiwa pamoja na wasionekane kutofautiana kwa lolote. Hiyo ilimpa moyo Deva na kuhisi kuwa ule ugomvi wao ulikuwa tayari umeisha na sasa amani imetawala kati yao. Hata Ata alisahau kabisa ugomvi wake na Deva na hii ilichagizwa na uchanganywaji wa akili zao na TSSI 01.



    NJIANI walikuwa wakizungumza ni jinsi gani ya kumuingilia adui yao na wafanikiwe kumdhibiti wamuue ama waondoke nae. Ata hakuonekana kuwa na hofu hata kidogo na Hemedy. Na hii ilitokana na alivyowahi kukutana nae kule hospitali na kuhisi Hemedy hakuwa mjuvi sana kimapigano kumshinda yeye labda uviziaji tu. Akapanga akifika na akifanikiwa kukutana nae. Waonyeshane kwanza ubavu kabla ya kumdhibiti.



    Walifika karibu na nyumba hiyo. Wakapaki gari mbali kidogo na kushuka. Walitembea mwendo wa kujiamini hadi karibu na nyumba hiyo. Nini wafanye ili waingie ndani? Swala la kuruka ukuta likipitishwa. Ila kikwazo kikawa ni jinsi gani ya kuruka ukuta huo. Ukuta ulikuwa mrefu usioweza kupandika kirahisi. Wakaangalia huku na huko na kuona mahala hapo pakiwa pamepoa sana. Hapakuwa na mzunguuko mkubwa wa watu.



    Wakashauriana warukie ndani kwa kutumia miti mirefu iliyokuwa imepandwa nje ya nyumba hiyo. Wakapanda ’chap chap’ hadi juu na mzingira ya ndani wakawa wanayaona vyema. Kwakuwa ukuta huo kwa juu ulikuwa una nyaya za shoti ya umeme. Ikabidi wawe makini na nyaya hizo zisije zikawaletea matatizo. Wakachumpa na ndani. Tiii!! Hadi chini. Wakatazama usalama na kukuta ukiwa mzuri zaidi. Ukimya ulitawala ndani humo na isijulikane kama kuna watu ama hakukuwa na watu au mtu.



    Wakasogea taratibu na kwa umakini kuuendea mlango wa kuingilia ndani huku bastola zao zikiwa mikononi. Mdogo mdogo hadi mlangoni. Ata akajaribu kuufungua na kukuta ukiwa umefungwa. Akatoa funguo mfukoni kwake na kufungua mlango huo. Funguo ya kwanza, ya pili ya tatu ikakubali. Mlango ukawa wazi!. Wakazama ndani huku bastola zikitangulia. Zikaangalizwa kila pahali hapo sebuleni. Patupu!.



    Wakaendelea upekuzi wao. Wakazifuata ngazi za kupanda juu. Wote wakiwa makini. Wakapanda hadi juu na kukagua chumba kimoja baada ya chengine. Viwili havikuweza kufunguka. Ikiwa ni kile anachotumia Hemedy kulala na kile ambacho kilikuwa na mitambo ya ulinzi wa nyumba hiyo. Lakini vyote vilivyofunguka vilikuwa vitupu. Wakaamua warudi chini.



    TSSI 01 majira hayo ndio alikuwa akirudi kutoka nyumbani kwa Inspekta Salum alipompeleka. Kwakuwa hakuwa na mlinzi nyumbani kwake. Ikamlazimu kushuka kwenye gari na kuenda kufungua geti. Akaingiza gari ndani na kufunga tena geti. Taharuki ilimpata baada ya kuona mlango wa kuingilia ndani ukiwa wazi!. Inamaana sikufunga mlango wakati naondoka? Hapana bwana nilifunga. Aliwaza mwenyewe.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipiga hatua kuufuata mlango huku akiwa hafikirii kabisa kama ndani humo kunaweza kuwa na mtu ama watu walioingia kabla yake. Alipoingia ndani. Macho kwa macho na Ata na Deva waliokuwa wakishuka ngazi kuja chini. Wakamnyooshea bastola huku wakimtaka atulie vile vile. TSSI 01 ni kweli alikuwa na uoga lakini hakutaka kuuonyesha mbele za adui zake. Alitabasamu na kuendelea kupiga hatua kuingia ndani.



    “Naona mwenyeji nimekuwa mgeni ghafla na wenyeji wangu mmenikaribsha kwa ukarimu mzuri. Niruhusini basi nikae” TSSI 01 aliongea hayo akiwa bado anatabasamu. Ata na Deva walishuka chini huku Ata akiwa ameshusha bastola chini lakini Deva akiwa bado amemnyooshea.



    “Nadhani leo ndio ile siku itakayo fahamika kuwa mimi na wewe fala, nani mshindi” Ata aliongea huku akikaa kwenye sofa. Hemedy nae akakaa kwenye sofa jengine, wakawa wanaangaliana.



    “Bado hajajulikana fala ni nani kati yangu mimi na wewe. Atakae shindwa mchezo ndio fala” TSSI 01 aliongea.



    “Sawa. Uwanja ni upi? Au hapa hapa ndani patafaa?” Ata aliuliza. TSSI 01 aliiangalia sebule hiyo kwa kuizungushia macho utafikiri ndio kwanza anaiona. Kisha akasema.



    “Dhumuni la mchezo huu ni mapigano bila ya silaha na humu ndani kuna silaha nyingi sana ambazo kwa macho yako ya kawaida hutoweza kuziona hata nikikuachia uishi nyumba hii mwaka mzima. Sasa ili kuepuka mimi kutumia silaha. Tuhamie kule nje ambako kuna usalama zaidi” TSSI 01 aliongea. Na Ata akakubali. Wakatoka nje wote watatu na kuenda katika bustani zilizokuwa ndani ya uzio wa nyumba hiyo. Hapo pakaonekana patafaa zaidi.



    “Muambie huyu marehemu mtarajiwa kijakazi wenu ashushe silaha chini. Sio vizuri kutishiana amani kwenye jambo la furaha kama hili bwana” TSSI 01 alisema hivyo akimaanisha Deva aweke bastola pembeni. Deva alishikwa na hasira kwa kuitwa marehemu mtarajiwa kijakazi. Lakini atafanyaje ilhali mapigano yalikuwa kati ya Ata na adui yao. Akaweka bastola pembeni na kutulia.



    “Sawa. Sasa jengine la mwisho. Ningependa kuwashauri muwape taarifa wenzenu kabisa kuwa watangulie katika ufukwe wa Jeti wakazisubiri maiti zenu kule kabla....”



    TSSI 01 alisema maneno hayo na kabla hajamaliza kuzungumza. Ata alikuwa tayari ameshamvaa zamani baada ya kuona mtu huyo akipoteza muda kizembe kwa maneno yake ya kuudhi. Lilikuwa ni teke kali kutoka kwa Ata lililotua sawia kifuani kwa Hemedy na kumfanya arushwe nyuma kwa msukumo wa teke hilo. Akajibwaga chini. Ata alimfuata pale pale. Akampiga dochi la kiuno na Hemedy alitoa mguno wa maumivu huku akibiringita pembeni.



    Ata alimfuata pale alipo na kuinua guu lake juu kwa nia ya kushindilia la kifua. Hemedy alilizuia kwa mikono japokuwa ilimpa shida kidogo na kurusha teke akiwa vile vile amelala chini. Teke lake likampata Ata maeneo ya nyuma ya kiuono. Ata akapelekwa mbele na kwavile mguu wake bado ulikuwa umeshikwa na Hemedy. Alikosa stamini na kupepesuka. Hemedy aliuvuta ule mguu ambao bado alikuwa ameushikilia na kumfanya Ata aangukie tumbo. Wote sasa wakawa chini!.



    Wakainuka wote kwa pamoja na kukaa tayari kwa mapigano. Wakaangaliana kwa umakini kila mmoja akimuangalia mwenzake ni wapi alipokosea ili mchezo uwe rahisi upande wake. Ata alimuita Hemedy kwa kidole cha kati. Hemedy akatabasamu na kushusha mikono akiwa kama ameghairisha mpambano. Akaanza kupiga hatua kama anaondoka mahala hapo. Ata alivyoona hivyo. Akakimbia kama hatua mbili na kuruka sarakasi ya juu ambayo alikuwa na lengo na kumpanda Hemedy kichwani na kumjeruhi kama si kumuua kabisa.



    Hemedy alimuhepa na Ata akapita hewa. Akiwa juu bado kabla hajatua chini. Hemedy alibenjuka na kumisindikiza Ata na teke kali la shingo. Ata akatua chini bila mpangilio na kujibwaga kwenye bustani ya majani. Akaviringita na mbele baada ya kuona Hemedy akimjia kwa kasi pale alipo yeye. Akajaribu kuinuka lakini akasaidiwa kuinuliwa na dochi kali la mbavu kutoka kwa Hemedy. Akagumia kwa uchungu huku akiyumba yumba akiwa amesimama.



    Hemedy alimfuata kwa mateke ya tik tak ambayo kidogo yalimchanganya Ata na kujaribu kuyapangua lakini si yote aliweza kuyapangua. Akarusha ngumi iliyokuwa na lengo kwenye pua. Hemedy aliipangua na kumshushia ya kwake ambayo ilikuwa na lengo kuharibu mfumo mzima wa taya. Bahati nzuri nae Ata akaiona na kuipisha. Papo hapo akamzunguuka Hemedy kwa nyuma na kumkwida roba huku akimshushia ngumi za mbavu.



    Maumivu yalikuwa mengi kwa Hemedy wakati mbavu zake zikishambuliwa kwa ngumi kali kali. Akampiga vifuti viwili vya tumbo na Ata akamuachia na kurudi nyuma. Hemedy akarusha teke la shukurani ya punda. Ata akaudaka mguu wa Hemedy kwa nia ya kuuvunja kabisa. Hemedy aliusoma mchezo wake na kupiga sarakasi ya mbele na mguu wake ule ambao ulikuwa huru ukapiga kwenye kidevu cha Ata na kumrusha nyuma. Kisha akatua chini kwa kishindo.



    Ata wakati akitua chini kwa kishindo, na Hemedy nae ndio anatua chini baada ya kuruka sarakasi. Akageuka kule ambako alikuwapo Ata. Akamkuta akiwa amesimama tayari kwa mapigano. Ata alifuta damu zilizokuwa zikitoka mdomoni mwake na kuziangalia. Hasira zilimpanda maradufu baada ya kushuhudia damu yake ambayo ilitolewa na adui yake.









    Mapigano yaliendelea. Yalikuwa makali sana ikiwa kila mmoja hakutaka kushindwa kizembe na mwenzake. Bustanini paligeuzwa uwanja wa mapigano. Nyasi walizichangua changua huku na huko na kupafanya pasiwe katika hali nzuri mahala hapo.



    Mpambano ulikuwa mkali sana hasa upande wa Ata ambae alionekana dhahiri anazidiwa. Na hiyo ilisababishwa na kutawaliwa na hasira za kipuuzi. Na kwa vile Hemedy alishajua kwamba adui yake alikuwa na hasira za karibu. Alizidi kumfanyia dharau ambapo kama akimpiga na kumuangusha chini. Humcheka huku akimtolea maneno ya kejeli. Basi Ata huinuka na kuanza kupambana kwa hasira bila kutumia maarifa wala akili na kujikuta akipokea kichapo kikali kila mara.



    Deva alipoona mwenzake alikuwa akizidiwa. Aliingilia na yeye mapigano. Ikawa ni watu wawili kwa mmoja. Lakini pamoja na kuwa wawili. Bado walisanda kwasababu Deva hakuwa na ujuvi mkubwa kumshinda Hemedy. Na kwavile Ata alikuwa amechoka sana. Wakajikuta wote wakichezea kichapo japokuwa mara kadhaa walimbahatisha.



    Kwakuwa walizidiwa sana na hawakuona dalili yoyote ya adui yao kuchoka. Walitumia kanuni ya mwisho kwenye mapigano. Kanuni ya kukimbia!. Kama vile waliambiana. Wote wawili walijikuta wakitoka mbio kuliwahi geti kwaajili ya kutoka. Ashukuriwe Hemedy aliekuwa hakufunga geti dogo huku Hemedy akijuta ni kwanini hakufunga geti hilo. Na ile ilitokana na taharuki lililomkuta mwanzo baada ya kuona mlango wake upo wazi.



    Waliponyoka na getini na kukimbilia nje mahali walipoliacha gari lao. Hemedy alitoka na yeye mbio baada ya kuona adui zake wakikimbia. Akipofika alikuta jamaa wale wakiingia kwenye gari. Akarudi ndani mbio na kufungua geti kubwa. Kisha akaingia ndani ya gari lake la kawaida akiliacha lile alilopewa na Kitengo. Akalitoa ndani mbio na kuelekea kule ambapo adui zake walielekea akiacha geti wazi.



    Walikuwa wakifukuzana barabarani wakishika uelekeo wa Tanga Beach. Njia nzima watu walikuwa wakiwashangaa wao kwa jinsi walivyokuwa wakiendesha magari kwa mwendo wa kasi. Huku Ata huku Hemedy kila mmoja akionyesha umahiri wake katika kuvichezea vyombo vile vya moto.



    Walipofika kwenye kona ya uwanja wa Lowassa. Gari zile zilikunja kona ile zikiwa katika mwendo ule ule wa kasi. Bodaboda na watu wengine waliokuwa maeneo yale walishika vichwa kwa hofu kwa jinsi gari zile zilivyokuwa zimekunjishwa kwenye kona ile. Milio mikali ya msuguano wa matairi na lami ilisikika na kuleta kero na hofu kwa wengine, iliyowafanya wazibe masikio kabisa.



    Kona ilimalizwa na gari zikaendelea kufukuzana. Hemedy alijuta ni kwanini hakuchukua lile gari lake jipya. Kwasababu gari alilokuwa nalo halikuwa na uwezo wa kuenda mbio nyingi kulishinda lile la kina Ata. Akabaki kuwa nyuma akijitahidi hivyo hivyo kuwafukuzia hata japo auone mwisho wake. Maana alijua uwezo wa kuwapata kabla hawajasimama hana.



    Gari zile ziliipita hotel ya Tanga Beach kwa mwendo ule ule. Magari mengi yalilazimika kupisha barabara ili kuepuka ajali zisizokuwa za lazima. Kila alieona mwendo uliokuwa ukiendeshwa gari zile. Mawazoni mwake alitafsiri ajali tu. Zilikunja kona na sasa zilikuwa ukuta wa mbolea. Kila mmoja hakutaka kushindwa na mwenzake.



    TSSI 01 alianza kukosa matumaini ya kuwapata baada ya kuona mafuta kwenye gari yake yakielekea kuisha. Akan'gaka kwa ghadhabu huku akipiga kwa nguvu na mikono yake kwenye usukani. Gari iliyumba kidogo akaiwahi na kuiweka sawa. Ikabidi apunguze mwendo na kusimamisha kabisa. Aliwaona adui zake wakiambaa kwa kasi wakiwa mbali mbele yake. Akasonya kwa nguvu na kuendelea na safari yake. Ila hivi sasa hakuwa tena akiwafuata wakina Ata maana alijua hatofika popote kabla gari haikuzima.



    Sababu ya kuisha mafuta haraka kwa gari lake ni kutokana na kuwa siku hiyo alifanya safari nyingi na gari hilo. Akakunja kona kushoto na mbele kidogo akakunja tena kushoto baada ya kuiona sheli ya GBP. Akajaza mafuta na safari ya kurudi nyumbani kwake ikaanza hapo huku akiwa na hasira nyingi sana kuwakosa adui zake kirahisi rahisi hivyo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kule kwenye jumba la maficho. Baada ya Ata na Deva kuondoka kuenda nyumbani kwa TSSI 01. Queen alitoka tena na Pijo nje kwenda kuendelea mchezo wao wa karata. Mr Hanein, Mrutu na Atu walikuwa sebuleni wakiongea hili na lile. Baada ya muda Mr Hanein aliaga anaenda chumbani kupumzika. Atu nae akatoka nje kwenda kuungana na Queen na Pijo katika mchezo wa karata. Sebuleni akabaki Mrutu pekeake.



    Muda wote Mrutu hakuwa na amani moyoni mwake. Alikuwa na hofu tele kwa kufikiri kwamba mwanae Hemedy ameenda kuuliwa. Muda wote alikuwa akitafuta namna ya kuweza kumuepusha na kifo hicho. Wakati akiwa anaendelea kuwaza. Macho yake yalitua juu ya meza iliyokuwapo hapo sebuleni. Kulikuwa na simu. Simu aliyokuwa akiitumia Queen. Ningezijua namba zake ningempigia. Aliwaza mwenyewe.



    Mara tabasamu la hofu lilijiunda usoni kwake baada ya kukumbuka kuwa siku za nyuma Queen alitumwa kumfuatilia Hemedy na kufanikiwa kumnasa kwenye mitego yake hadi ikatokea kubadilishana namba watu hao wawili. Sijui itakuwepo? Akajiuliza. Haraka haraka akaiendea simu ile. Akaingia upande wa majina akiwa na hofu kuu. Akaangalia jina moja, moja lilivyoseviwa. ‘Adui’ jina la tatu lilikuwa limeseviwa hivyo.



    Kivyovyote akajua huyo aliesevia adui ndio Hemedy. Akajaribu kuangalia na majina mengine. Akaona yote yameseviwa kwa majina ya kawaida tu. Akalitafuta lile ‘Adui’ na kulipiga.



    TSSI 01 Akiwa maeneo ya Dunia Hotel akirudi kwake. Simu yake ndogo iliita. Namba ilikuwa ngeni na hakujua ni nani anaempigia. Namba ya Queen alikuwa nayo siku za nyuma baada ya kubadilishana pale kwenye mgahawa wa Afrikana walipokutaniana mara ya kwanza bila Hemedy kumjua vizuri Queen ni nani.



    Baada ya kushtukia janja ya Queen siku chache mbele kwenye Hotel ya Nyinda walipoenda kukodisha chumba kwaajili ya kula raha. TSSI 01 aliifuta ile namba baada ya kuona haina maana tena kwake baada ya kujua kuwa yule mwanamke alikuwa si mwema kwake. Mara hii namba ile ilimpigia. Lakini asiijue wala asiikumbuke. Akaipokea.



    “Halo Hemedy!” Sauti yenye kitetemeshi ilisikika kwenye spika ya simu ya Hemedy. Sauti ambayo hakuwa na shaka yoyote kumaizi kuwa ni ya baba yake mdogo Mrutu. Akatoa simu haraka sikioni na kuitazama ile namba kwa taharuki. Akairudisha tena sikioni na kusikia tena maneno yale yale ya mwanzo.



    “Ndio. Nani wewe?” Akajibu na kuuliza ikiwa ni kupata uhakika wa kwamba yupo sahihi na mawazo yake ama ni vipi.



    “Mrutu! Baba yako hapa naongea”



    “Babaa!...” aliuliza kwa hamaniko. “Upo wapi wewe?”



    “Nipo Pongwe huku na kama upo nyumbani kwako ondoka haraka kuna watu wanakuja kukuua huko...” Wakati Mrutu akiongea na Hemedy. Aligeuza macho yake huku na huko ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu mwengine aliekuwepo karibu na eneo hilo? La haulaa!!.



    Macho yake yalikutana na macho ya Mr Hanein aliekuwa akimuangalia yeye. Simu ikamponyoka mkononi na kitetemeshi kikachukua nafasi mwilini mwake. Alikuwa akitetemeka zaidi ya mgonjwa wa kifafa. Hofu ilitawala usoni mwake. Mashaka tele nafsini kwa kufumaniwa akiongea na adui wa Mr Hanein.



    Mr Hanein aliifuata ile simu pale chini na kuangalia ni nani aliekuwa akiongea na Mrutu? Adui!. Akamuangalia usoni kwa chuki Mrutu na kuikata ile simu bila kuiangalia na kisha kuizima kabisa. Mrutu alikuwa bado akitetemeka kwa hofu na mara hii alitoa chozi la majuto huku uso wake ukionyesha huruma. Alikuwa akimuomba msamaha Mr Hanein bila kufungua mdomo.



    Hofu ya kuadhibiwa kama sio kuuliwa kabisa ilimkamata mithili ya Jogoo aliekamatwa na bwana wake kwaajili ya kuchinjwa awe kitoweo cha wageni. Mr Hanein bado aliendelea kumuangalia kwa hasira kiasi ambacho mashavu yalimcheza cheza huku sharubu zake zikipepesuka huku na huko mithili ya nyasi ndefu kwenye upepo mkali. Alimtazama na asijue ni nini afanye kwa wakati huo.



    Mara hiyo Ata na Deva waliingia huku nyuma yao wakifuatiwa na Atu, Queen na Pijo. Wote waliishanga ile hali waliyowakuta nayo Mr Hanein na Mrutu. Mrutu alikuwa amepiga goti moja chini huku akitetemeka na Mr Hanein akiwa amekaa kwenye sofa hasira zikionekana waziwazi. Wakahoji kunani tena mbona hali hiyo na Mr Hanein aliwaangalia tu pasi na kusema kitu. Donge zito la hasira lilimkwaa kooni kwake na kumfanya asiweze kuongea chochote.



    “Mpelekeni chini huyu” Alipopata kauli, aliongea maneno hayo kwa ghadhabu. Wakahoji ana nini na Mr Hanein aliwakaripia kwa nguvu huku akiwatolea macho ya hasira na kumfanya afananiane na Dudumizi la mwituni. Wote wakahofu kwa hali hiyo. Hawakujua nini kimetokea hadi kuwa hivyo.



    Bila kusema kitu. Deva na Atu walimchukua Mrutu mzobe mzobe huku Mrutu akiomba msamaha kwa Mr Hanein asamehewe. Walienda nae hadi chini ya nyumba hiyo ambapo kulitisha haswaa. Wakamfungia katika chumba kimoja. Deva akamuuliza Queen ni nini kimetukia hadi Mrutu ambae walizoea kumuita ‘Brother’ kufungiwa huko. Atu akasema hajui na pale wakati wanaingia wao ndio walikuwa wakiingia wote na sababu ya Mrutu kutakiwa kufungiwa huko hawakuijua.



    Wakatoka kule chini kwenda sebuleni. Wakachukua nafasi wote wakimtazama Mr Hanein ambae alikuwa kimya akitetemeka kwa hasira. Walimuangalia pasi na kumuhoji chochote maana waliitambua hasira aliyonayo mkuu wao. Wakaangaliana wenyewe na kila mmoja alimuona mwenzake akiwa na viulizo vingi machoni kwake.



    Mr Hanein akapoa baada ya dakika tano na kuwataka Ata na Deva wamueleze yaliyotukia huko. Ata alimueleza ila alimficha wao kukimbia badala yake alimzushia Hemedy kuwa ndie aliewakimbia. Na kwavile wao hawazijui njia nyingi za mji huo, akawapotea. Mr Hanein alizidi kuwa na hasira mara dufu na shari ikawa inamzunguuka ubongoni mwake dhidi ya Mrutu.



    Akachukua nafasi hiyo kuwaeleza yaliyotukia kipindi ambacho hawakuwepo na wote wakashangaa wasiamini kwamba Mrutu waliekuwa wakiishi nae hapo kwa muda mrefu amewageuka. Swali likaja. Amempigia simu adui yao na kumtahadharisha na kifo ili iweje?. Wote hawakujua kwamba Mrutu na adui yao ni mtu na mwanae. Mr Hanein akashauri waende kule chini wakamhoji vizuri kabla hajaamua ni adhabu gani itamfaa.



    TSSI 01 alitaharuki baada ya kuongea na baba yake mdogo. Alijua kwamba baba yake mdogo anashirikiana na adui zake. Lakini simu yake ya kumtahadharisha na kifo hakuitegemea kabisa. Alijikuta akiingiwa na kiroho cha kutaka kuongea nae tena. Alipaki gari pembeni kisha akajaribu kuipiga ile namba. Lakini haikupatikana. Akajaribu kuipiga mara nyingi na jibu likaja lile lile kuwa haipatikani.



    Kichwani kwake alikuwa na mzigo mzito wa mawazo. Mwili mzima uliingiwa ganzi. Kuna wazo likapita kichwani kwake. Akachukua simu yake na kumpigia TSSI 05 Feysal. Baada ya salamu akamueleza shida yake. Akamuambia kuwa kuna namba atamtumia hivi punde na anaomba amuangalizie ’location’ ilipo hiyo namba. Feysal akamuambia ni jambo dogo sana hilo yeye atume tu hiyo namba. Akakata simu na TSSI 01 akafanya taratibu za kumtumia namba ile. Na alipofanikisha, akawasha gari kuwahi nyumbani kwake.



    Alipofika alikuta geti lake likiwa wazi vile vile alivyoliacha. Akaingiza gari ndani na kufunga geti. Akaingia ndani ya nyumba na kabla hajashika chochote ndani humo. Akakimbilia kwenye chumba cha mitambo ya ulinzi wa nyumba hiyo. Huko aliiendea Kopyuta ambayo ilikuwa ikionyesha na kurekodi matukio yaliyokuwa yakifanyika nje na ndani ya nyumba hiyo kupitia kamera zilizofungwa kila mahali kwenye nyumba hiyo.



    Akaangalia na kuona tangu wakina Ata walivyokuja. Wakaruka ukuta na kuzama ndani. Akaona vyote vilivyoendelea na mwisho akajiridhisha kuwa hakuna chochote kibaya walichokiacha kwenye nyumba hiyo. Akiwa hapo simu yake iliita. Aliangalia na kukuta Feysal ndie aliekuwa akimpigia. Akapokea.



    “Ndio ‘Code One’. Namba hii inayonyesha ipo katika mji mdogo wa Pongwe. Ni pembezoni kidogo mwa mji huo” Feysal aliongea.



    “Sawa. Sasa mimi nafunga safari muda huu kuelekea huko. Naomba uniongoze hadi tuipate ‘location’ inaposoma simu hiyo”



    “Sawa ‘Code One’. ‘Code Five’ nipo nyuma yako” Simu ikakatwa na TSSI 01 akatoka kwenye chumba hicho na kuingia chumbani kwake.



    Huko aliingia chooni na kwenda kuoga kwanza. Na alipotoka, akavaa suruali ya mpira, juu alivaa fulana ya mikono mirefu na juu yake akavaa na kikoti ambacho kilikuwa na mifuko mingi nje na ndani. Juu alivaa kofia aina ya mzula ambayo ndani yake kulikuwa kuna pini kadhaa alizozichomeka. Pini hizi ni kama zile ambazo Ata na Atu walizitumia kule uwanja wa shule ya sekondari Tanga School kuwashambulia nazo askari na Inspekta Salum na kusababisha vifo vya askari watatu huku Inspekta Akiwa taabani.



    Akachomeka na bastola mbili ndogo kwenye ile suruali kwa ndani. Visu sita vikachomekwa ndani ya kile kikoti alichovaa. Kamba ndefu kidogo aliifunga kwa kuiegesha kiunoni kwake. Alichomeka silaha nyingi kwenye zile nguo alizovaa na nyengine akazihifadhi kwenye begi lake la mgongoni. Na mikononi mwake alivaa ‘gloves’ ngumu zisizoweza kupitisha kitu chochote kilicho na ncha kali ambacho hakikuwa na uzito, kama sindano. N. K. Akatoka ndani humo akiwa kamili tayari tayari kwa kazi. Aliingia kwenye gari aliloletwa na kina Fady ambalo hakulijua jina lake. Safari ya kwenda Pongwe ikaanza.



    Kutokana na mwendo wa kasi aliokuwa akiutumia. Alifika katika mji huo mdogo wa Pongwe ndani ya dakika ishirini. Alikunja kushoto na kupaki gari lake kando ya nyumba moja iliyokuwa karibu na barabara hiyo ya vumbi. Akatoa simu yake kwa nia ya kumjulisha TSSI 05 kuwa ameshafika na anataka muongozo wake ili afike huko. Kabla hajampigia, simu yake ikaita na aliekuwa akipiga ni Feysal.



    “‘Code One’ nakusoma vizuri. Sasa fuata uelekeo huo huo uliokuwa nao nitazidi kukupa maelekezo zaidi” Feysal alizungumza. Hemedy akaiingiza tena gari kwenye barabara hiyo ya vumbi. Majira hayo yakiwa ni saa kumi na mbili za jioni. Kigiza kikianza kulitawala anga.



    Akashika uelekeo wa njia hiyo na mbele huko akazidi kupata maelekezo kutoka kwa Feysal mwenye taaluma nzuri ya ‘I.T’. Mjuvi mzuri wa kucheza na kompyuta na alikuwa akimpata Hemedy kwa kupitia simu yake. Muongozo uliendelea hadi mbali kidogo na barabara kuu. TSSI 01 Kwa mbali kidogo aliona jumba kubwa lililo zungukwa na miti mirefu iliyokuwa imepandwa pembezoni mwa jumba hilo.



    Akatabasamu na kufurahi mno baada ya kuhisi kuwa jumba hilo huenda ikawa ndio makazi ya adui zake. Akaingiza gari lake kwenye msitu wa miti mirefu ya mitiki iliyopadwa na kuliegesha hapo. Kisha akashuka. Simu ikaita. Feysal alikuwa akimpigia. Akapokea.



    “‘Code One’ umekaribia kwenye ‘location’. Ni mita hamsini kutoka hapo ulipo”



    “Ok. Comred ‘Code Five’ nashukuru kwa msaada wako”



    “Pamoja Comred na endapo utahitaji msaada usisite kutujulisha haraka iwezekanavyo ili tujue namna gani tunakusaidia. TSSI tupo nyuma yako” Simu ikakatwa.



    Kutokana na giza lililotanda eneo hilo huku miti hiyo ikachagiza kwa asilimia zake. TSSI 01 alitoa miwani ya kijasusi ambayo ilikuwa na uwezo wa kuona vyema kwenye giza. Akaivaa na machoni kwake pakatawala mwanga badala ya giza. Akavuta begi lake na kulivaa mgongoni. Kimya kimya, akaanza kupiga hatua kulisogelea jengo lile.



    Hakujua uwingi wa watu waliokuwepo ndani ya jumba lile. Ila akajiaminisha kuwa atatumia akili kupambana nao hadi akamilishe ‘mission’ yake. Kulikuwa na ukimya mwingi kiasi ambacho alizisikia sauti za pumzi zake. Mivumo ya upepo iliyokuwa ikipepea miti hiyo. Ilisikika kwa sauti ndogo kwasababu hakukuwa na upepo mwingi.



    Mara hii alikuwa yupo karibu kabisa na ukuta wa uzio wa jumba lile. Akazunguuka kwa nyuma akiwa anatafuta namna ya kuingia ndani yake. Ukuta ulikuwa mrefu sana na juu yake kulikuwa na nyaya za shoti ya umeme. Akatoa kamba ngumu kwenye begi lake. Akaifunga kwa mbele mfano wa kitanzi kisha akairusha kwenye chuma moja kati ya mengi yaliyokuwa yamezishikilia vizuri zile nyaya. Kamba ikanasa!.







    Hata kama kukiwa na shoti. Basi haitoweza kumdhuru kwasababu kamba aliyoitumia ilikuwa ni kavu. Akajaribu kuivuta vuta akiangalia uimara wake na kuikuta ikiwa thabiti kabisa. Akapanda juu kwa kutumia ile kamba na alipofika karibu na zile nyanya. Akaachia mkono mmoja na kutoa koleo. Akakata nyaya za shoti na nyaya zile zikaachia.



    Uwazi wa kupita bila shida ukapatikana. Akajivuta juu zaida na mara hii akawajuu kwenye ukuta huo amechuchumaa. Giza lilikuwa limetawala ndani ya nyumba hiyo. Ni taa za kwenye vyumba ndizo ambazo zilikuwa zikionekana kuwaka. Kama alivyoupanda ule ukuta ndivyo ambavyo alivyo shuka kwa ndani. Alipofika chini kabisa, akaangalia usalama. Akaona pako shwari. Akajaribu kuivuta ile kamba lakini ikamgomea baada ya kushika vizuri kwenye lile chuma kule juu. Akaachana nayo!.



    Akakimbia mbio kuuende mti wa muembe uliokuwa bustanini. Akajibanza nyuma yake akiangalia usalama. Wakati akitaka kuhama hapo iliaende mbele zaidi. Akaona mlango wa mbele ukifunguliwa. Akatulia na kuwa makini na mlango huo. Alionekana Pijo akitoka ndani huku mkononi kwake akishika tochi kubwa. Alikuwa akimulika mulika kwenye bustani hiyo alionekana kama kuna kitu anatafuta hapo.



    Hatua nne mbele akazipiga na kuinama chini. Akaokota simu iliyokuwa mahala hapo. Bilashaka aliisahau mchana wa siku hiyo wakati wakicheza karaka. Akapiga hatua kurudi ndani. “Hey!” TSSI 01 Aliita hivyo. Pijo akageuka haraka na kumulika kila pahali akimtafuta alietoa sauti hiyo. Hakumuona!. Kwenye mti wa muembe aliona kivuli kama cha mtu. Akapitisha mwanga wa tochi kulia kwenda kushoto na kuona kivule kile kikihama. “Mmmh!” Akaguna!.



    Akapiga hatua ndogo ndogo kuuendea mti ule. Alipofika karibu, alikutana na jambo lililozua taharuki moyoni mwake. Akataka kupiga kelele za hofu, ila aliwahi kwa kuzibwa mdomo huku akiwa ameekewa kisu shingoni. Alikuwa akitetemeka si mas'hara.



    “Nakukumbuka sana, tuliwahi kukutana siku chache nyuma. Nilikujeruhi ili kukutia adabu lakini leo nakuhakikishia kuitenganisha roho yako na mwili kama ambavyo ulikuwa ukifanya kwa watu wasio na hatia yoyote. Jambo ambalo naenda kulifanya muda huu pindi nimalizapo kukuambia maneno haya” TSSI 01 alikuwa akimnong'oneza sikioni Pijo. Na ghafla kisu kikazama kwenye shingo ya Pijo. Damu zilidhihirisha uchungu aliokuwa akiupata Pijo. Akamuachia na kudondoka chini huku akigaagaa. Na baada ya dakika moja. Akatulia kimya.



    TSSI 01 Alifuta ile damu kwenye kile kisu na kukirudisha alipokitoa. Akakamata bastola na kuanza kuufuata mlango ambao alijua kivyovyote utakuwa wazi baada ya Pijo kuufungua alipotoka. Akanyonga kitasa taratibu kwa kutumia mkono wa kushoto huku wakulia ukiwa umekamata bastola yake madhubuti kabisa.



    “Tulia hivyo hivyo. Tupa bastola mbele na ingia ndani kwa utulivu. Usitake nikuwahishe kuzimu ilhali muda bado” Ata alimtahadharisha baada ya TSSI 01 kuufungua mlango. Akatupa bastola mbele. Mikono juu huku akiingia ndani humo kwa utulivu kama alivyoambiwa. Sebuleni aliwakuta watu wanne wakiwa wamekaa na watano alikuwa ni Ata aliemnyooshea bastola. Nyuso zao zilikuwa na furaha baada ya kuona adui yao amejileta mwenyewe.



    “Mtoto wa Bhachu Muheshimiwa. Msumbufu unaejifanya kuingilia mambo usiyayajua. Nimezipata taarifa zako kwa baba yako mdogo Mrutu ambae kama ungechelewa kidogo ungemkuta ni mfu. Sasa afadhali umewahi kuja kuhudhuria mazishi yenu yatakayofanyika muda mfupi baadae baada ya kuwafumua vichwa vyenu maji” Mr Hanein aliongea kwa majigambo. Akawaamrisha vijana wake wamkamate kisha wamkamfunge chini.



    Deva na Queen waliifanya kazi hiyo. Ila kabla hawajamkamata. Queen alimpiga kofi kali la uso TSSI 01 na kumfanya agugumie kwa maumivu. TSSI 01 alitabasamu huku akiwa bado mtulivu vile vile. Akavuliwa kile kikoti, ‘gloves’ mikononi zikavuliwa na akapapaswa kila sehemu na silaha zote zilizoonekana zikatolea. Ashukuriwe mungu hawakumvua kofia yake ya mzula wala viatu vyake alivyovaa. Kisha hapo Mr Hanein akawataka wakamfunge kwenye kile chumba ambacho alifungiwa Mrutu.



    Alipelekwa huko akiwa chini ya ulinzi mkali ambao kama angethubutu tu kunyanyua mdomo wake angegeuzwa tenga kwa matobo-tobo ya risasi ambazo angemiminiwa. Akafungwa karibu na kiti alichofungwa Mrutu. Majira haya Mrutu alionekana kuchoka mithili ya mgonjwa mahututi baada ya kushushiwa kipigo kikali pindi alipohojiwa. Japokuwa kila alichoulizwa alijibu bila shida lakini bado walimpiga kwa kile walichokiita Usaliti. TSSI 01 akafungwa hapo na kuachwa.



    TSSI 01 alitumia nafasi hiyo kuzungumza na baba yake mdogo ambae hawakuonana miaka saba sasa. Japokuwa Mrutu alizungumza kwa taabu sana. Alimuomba msamaha TSSI 01 kwa yote aliyowahi kuyafanya nyuma. Pia akamuomba msamaha kwa kumuingiza kwenye matatizo. Maana alijua kama si yeye kumpigia simu. Huenda muda huo angekuwa huru bila kufungwa fungwa hivyo na wala mwanae asingeweza kukamatwa.



    Wote walijikuta wakilia machozi ya uchungu pale TSSI 01 alipokumbuka kuwa. Ni huyo ndugu yake wa pekee aliekuwa duniani baada ya kuondokewa na familia yake yote. Sawa alikuwa na ndugu wengine. Lakini hakuwajuwa na pia alijua hata wao hawamjui. Kilio kilipokwisha. TSSI 01 alimueleza mambo yake yote. Hakutaka kumficha chochote. Alimueleza kuwa yeye ni nani na hata hapo alipo yupo kwenye ‘mission’ iliyomleta katika mji huo wa nyumbani.



    Mara ghafla mlango ulifunguliwa na Mr Hanein aliingia na kundi lake lote lililobaki. Hata Paskali mara hii pia alikuwapo. Mr Hanein akavuta kiti na kukaa katikati ya watu hao. Akawaangalia kwa zamu kisha macho yake akayatuliza kwa TSSI 01. Akaachia cheko kali huku akimuangalia kwa dharau.



    “Kumbe ni kitoto kidogo namna hii ndio kinachojifanya kunisumbua. Sasa wewe si umri wa hawa wanangu kabisa. Hivi huoni haya kusumbuna na baba yako? Halafu nimekumbuka kitu. Kumbe wewe baba yako Mzazi alikuwa ni mzee Muheshimiwa? Hahaha kweli Muheshimiwa kaacha jembe. Ila nasikitika jembe lake limechimba kaburi ambalo litajifukia lenyewe”



    Akawaangalia vijana wake. Na kuwaambia kuwa adui yao wanae mikononi mwao. Kwahiyo kama yupo anaejisikia kufanya chochote afanye. Queen akajitokeza mbele. Akamfuata TSSI 01 hadi pale alipo. Akamuangalia kwa jeuri kisha akamtandika kofi kali la shavu lililoacha alama za vidole vyake. Hemedy aligugumia kwa uchungu lakini asiache kutabasamu.



    “Yani leo hii umesahau utamu niliokupa siku ile unanipiga mbele ya mabwana zak....” Kabla hajamalizia. Queen alimshushia ngumi kali ya mdomo. Kisha akampiga kwa hasira kila sehemu aliojisikia kumpiga. Alimpiga sana hadi pale alipokuja kuzuiliwa. TSSI 01 alitema damu kutoka mdomoni huku uso mzima ukimchuruzika damu. Akaipulizia damu ambayo ilichuruzika kutoka puani kuja mdomoni. Ile damu ikaruka mbele vitone vitone. TSSI 01 aliitazama damu kisha akatabasamu tena.



    “Ama kweli shukurani ya punda mateke. Pamoja na kukupa raha siku ile mpaka ukakiri bwana wako hakuwahi kukupa raha kiasi kile leo hii ndio unanifanya hivi?” TSSI 01 aliongea maneno hayo bila kujua anampa ghadhabu Ata. Ghafla Ata alimfuata na kumpiga kipigo kikali na kumfanya Hemedy atoe kelele za maumivu kila pigo litakalo tua mwilini mwake.



    Baada ya kumpiga sana. Alimuacha na kurudi nyuma huku akitweta kwa hasira. Akamkata jicho kali Queen na Queen akakwepesha macho yake haraka na kuangalia pembeni huku hofu ikimjaa nafsini. TSSI 01 alikuwa amechoka ghafla baada ya kushushiwa kipigo hicho. Kichwa alikilaliza chini huku mikono iliyofungwa kwenye kiti ikilegea. Nguvu aliona hivi hivi zikimsaliti na matumaini ya kupona yakiwa finyu kwasababu hakutegemea kupata msaada wa haraka mahali hapo.



    “Hey wewe!?” Mr Hanein alimuita. Kisha akaendelea. “Nataka ushuhudie kifo cha baba yako kwa macho yako usije ukasema sikukuambia utazame” Kisha akaomba bastola na alipopewa. Akaitoa usalama na kumnyooshea Mrutu.



    Ghfla mlio mkubwa wa risasi ulisikika kwenye chumba hicho huku damu iliyo changanyikana na ubongo ikimrukia TSSI 01. Aliinua kichwa chake kwa mshtuko na kuangalia kule ziliporuka damu zile. La haulaa!. Kichwa cha baba yake mdogo kilitawanyishwa vibaya. Ilikuwa ni picha ya kutisha kutazama. Na iliogopesha haswaa.



    TSSI 01 alichia ukelele wa ghadhabu huku akimtazama Mr Hanein kwa hasira. Alijaribu kuinuka kwenye kile kiti na papo hapo akatulizwa na teke kali la uso na Ata. Nguvu alizozipata ghafla zikatoweka ghafla. Alirudi chini na mara hii alikuwa akilia kwa uchungu. Uchungu wa kuondokewa na mtu pekee aliebaki duniani kama ndugu yake. Japokuwa Mrutu pia alishirika kwenye vifo vya wazazi wake. Lakini hakutaka kujali hilo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliinamisha kichwa chini huku akilia kwa uchungu sana. Alitamani hata patokee muujiza kamba zifunguke awaonyeshe kazi. Lakini hapakutokea kitu kama hicho. Mr Hanein alicheka sana na alipokuja kutulia. Aliwataka vijana wake wapande juu wakaongee kidogo kabla hawajaamua wafanye nini juu ya TSSI 01. Wakapanda juu tena.



    Huko walishaurina nini wafanye juu ya TSSI 01. Wapo walioshauri wamuue tu lakini Mr Hanein alipinga. Akatoa rai yake na kusema. Ana wazo la kumtumia Hemedy kwenye kazi zake. Hasa hasa zile hatari zaidi. Wote wakashangaaa. Yani wamtumie adui yao kwenye kazi zao za hatari? Hawakumuelewa hata kidogo.



    Wakasema inakuaje adui yao atumike kwenye kazi zao. Itawezekana vipi wamshawishi hadi akubali? Mr Hanein akawatoa hofu na kuwaambia. Rafiki yake Mr Tanganyika atalifanyia kazi suala hilo na wala haitokuwa tabu. Lakini wanae wakampinga kwa nguvu zote. Waliona sana ni jinsi gani baba yao anaanza kuwadharau. Hasira zikawapanda mara dufu juu ya Hemedy.



    Wakamuabia kwa kiburi kwamba. Endapo atafanya lolote kwa Hemedy na isiwe kumuua. Basi wataondoka Tanzania na kurudi Marekani. Na Mr Hanein asijaribu kuwatafuta hata kidogo na wala asifikirie kwamba ana watoto wa dizaini hiyo. Ata aliongea maneno hayo huku Atu akitia ‘suport’. Mr Hanein akagwaya kwa vitisho vya watoto wake. Akaghairisha maamuzi yake na kuwaruhusu wafanye vile watakavyo.



    Furaha ikarejea kwa mapacha wale. Siku hiyo waliiona ni ya furaha sana baada ya kumtia mikononi adui yao. Wakaona sasa mipango yao itafanyika kikamilifu pindi watakapomuondoa adui yao duniani. Kwavile ilikuwa ni siku ya furaha. Vilevi vikaagizwa vikaletwe haraka. Na shuhuli hiyo waliifanya Queen na Atu. Wakatoka kwenda kutafuta vinywaji.



    Nusu saa mbele walirudi wakiwa na vinywaji vya vilevi vingi. Tafrija fupi ikaanza wakisherekea ushindi wa kumnasa adui yao. Walikunywa sana na Mr Hanein ilibidi aingilie kati suala hilo. Akawaambia wanafurahi ilhali adui yao bado mzima. Walitakiwa wafurahi kipindi ambacho adui yao akiwa ni mfu tayari. Wakamuunga mkono na muda wa kumuondoa TSSI 01 Duniani ukaonelewa uwe huo. Majira hayo yalikuwa ni saa saba za usiku.



    Wakaacha vinywaji vyao na kushuka chini. Pamoja na kunywa sana lakini walikuwa vizuri. Hakuna ambae aliekuwa akipepesuka. Wote walionekana wakiwa ngangari. Walipofika. Ata na Atu wakaomba wafanye mchezo. Mchezo ambao kwenye chemba ya bastola ya kuwekea risasi, kunawekwa risasi moja tu. Kisha inazungushwa ili risasi ijichanganye ndani ya bastola. Kisha waanze mmoja mmoja kufyatua risasi na atakae bahatisha risasi ikiwa kwenye lengo na akafanikiwa kumuua Hemedy, ndie mshindi. Jambo hilo likaungwa mkono na wote na zoezi hilo likafanywa haraka haraka.



    Ikachukuliwa bastola na kutolewa risasi zote. Kisha ikawekwa risasi moja. Chemba ikazungushwa na bastola ikafungwa. Nani aanze kufyatua risasi kati ya hao wawili? Kila mmoja alimtaka mwenzake aanze. Mr Hanein aliamua kukata mzizi wa fitina. Ata akatakiwa aanze kwavile yeye ndie alikuwa mkubwa. TSSI 01 Alijionea huruma kwa kuona maisha yake yanatumiwa kama mchezo fulani hivi wa kutisha. Akainua uso taratibu na kuwaangalia. Akawaona wakiwa na nyuso za furaha kama kile wanachotaka kumfanyia ni kitu cha kawaida sana. Akashusha kichwa chini na kumuachia mungu yote.



    Ata akachukua bastola. Akaiweka usawa wa kichwa cha Hemedy. Taratibu huku akitabasamu. Alibonyeza ‘trigger’ pole pole na ilipofika mwisho, ikatoa mlio wa vyuma kumaanisha kuwa chemba hiyo haikuwa na kitu. Atu alifurahi kwa kurukaruka huku TSSI 01 akishusha pumzi nzito za hofu. Atu akaichukua yeye bastola. Akaiweka usawa wa kichwa cha Hemedy. Akaanza kubonyeza ‘trigger’ taratibu na ilipofika mwisho. Bastola ikatoa mlio wa vyuma. Ata nae akafurahi huku akimpokonya Atu bastola.



    Wote waliokuwa hapo wakajua sasa Ata hawezi kumkosa TSSI 01 kwa mara hiyo ya tatu. Hata TSSI 01 mwenyewe alijua hawezi kuchomoka hapo. Akamuomba mungu wake ampokee kwa amani huko aendapo muda mfupi ujao. Ata aliminya ‘trigger’ taratibu huku mikono ikimtetemeka sana. Muda huo TSSI 01 alikuwa ameshakata tama ya kuishi tena. Chozi la uchungu lilimdondoka na kuangukia chini mahali ambapo damu zake zilitapakaa.



    Mara ghafla tu wote pua zao zilinasa rihi ya manukato mazuri ambayo hapo mwanzo hayakuwa yamenaswa na pua yoyote kati yao. Wote wakageuka nyuma na macho yao yakakutana na mtu ambae amesimama mlangoni. Alikuwa na mavazi meusi mwanzo mwisho. Usoni akiwa amevaa ‘maksi’ nyeusi ambayo ilionyesha macho yake tu. Na bilashaka alikuwa ni mwanamke kutokana na umbo lake lilivyojichora vizuri kwenye mavazi yale. Alionekana na ghadhabu kubwa kupitia macho yake tu. Mkononi akiwa na bunduki kubwa aina ya AK 47 ambayo iligunduliwa na Alexander Kalashnikov. Mrusi, mwaka 1947. TSSI 01 aliinua kichwa chake taratibu na kumuangalia mtu yule. Tabasamu likajiunda ghafla usoni kwake na kudondosha chozi. Huyu mtu ni nani? Hakuna aliejua!.









    Jijini Daresalam. Masaa Sita nyuma kabla kufika saa saba usiku. TSSI 05 Feysal. Alikuwa ndani ya chumba chake cha kazi. Kompyuta ya kisasa ikiwa mbele yake. Kwenye kioo cha kompyuta hiyo, kilikuwa kikionyesha ramani ya jiji la Tanga kwenye mji mdogo wa Pongwe. Katika ramani hiyo kulikuwa na kidonti cha bluu kilichokuwa kikitembea kidogo kidogo kwenye njia za ramani hiyo.



    Alikuwa kimya akikiangalia bila kufanya chochote. Dakika ishirini mbele. Alikiona kidonti kile kimetulia sehemu moja bila kujisogeza popote. Akaanza kuingiwa na mashaka. Inamaana.....huyu ni vipi? Akajiuliza mwenyewe. Akatulia tena kwa dakika tano akisubiri aone kama kitahama ama laa!. Kidonti kikawa pale pale!.



    Hofu ikaongezeka zaidi. Akachukua simu yake na kupiga namba ya TSSI 01 lakini majibu yalikuja kuwa haipatikani. Akajaribu kwa mara ya pili lakini majibu yakawa yale yale. Haraka haraka akahamia kwenye kompyuta nyengine. Akapofya bofya haraka haraka kama dakika moja. “Shit!” akang'aka kwa mfadhaiko. Kisha pale pale akaandika ujumbe kwenye ile Kompyuta. ‘You have to come back in the Unit. There is a problem wich has been are protude. Now!’ akautuma ujumbe ule akimaanisha kuwa wanatakiwa warudi kitengoni kuna tatizo limejitokeza muda huo.



    Pamoja na kuwa kompyuta hiyo imeunganishwa na kompyuta zote za kwenye kitengo hicho. Pia ziliunganishwa kitaalamu na simu maalumu walizokuwa nazo wote sita wakitengo hicho cha siri. Kwahiyo ujumbe ule uliwafikia wote kupitia simu zao majira hayo kila mmoja akiwa nje ya kitengo hicho. Ni Feysal ndie aliebaki baada ya kuombwa na Hemedy mchana wa siku hiyo amsaidie kazi yake.



    Dakika ishirini mbele. Walianza kuingia mmoja mmoja na wa kwanza kufika alikuwa ni mwana dada Tracy Daniel TSSI 04. Akafuata Hilda na Fady akamalizia. Wakawa wanamsubiri mkuu wao na ndani ya dakika hiyo hiyo Mr Kaoneka nae akaingia. Kwakuwa Feysal aliwaambia tokea muda kuwa Hemedy alimuomba msaada. Sasa akatumia nafasi hiyo kuwaeleza mashaka yake. Wote roho ziliwaenda mbio mbio baada ya kuona ni kweli kidonti kilichotumika kama ‘signal’ ya Hemedy kilikuwa kimetulia sehemu moja.



    Mr Kaoneka bila kuchelewa. Akamtaka Hilda TSSI 03 ajiandae haraka kuelekea Tanga usiku huo huku akisindikizwa na Tracy TSSI 04 na Fady TSSI 02 kuenda kumkomboa mwenzao maana walihisi atakuwa kwenye matatizo. Kipindi ambacho Mr Kaoneka akiwa anatoa maelezo. Hilda aliona kama ni upotevu wa muda tu. Akataka kumkatisha lakini akaona ataonekana hana adabu. Akatulia huku akiwa na kiroho baada ya kuhisi mpenzi wake atakuwa kwenye hatari muda huo.



    Haraka haraka baada ya Mr Kaoneka kuwaruhusu wakajiandae. Kila mmoja akaingia kwenye chumba chake. Na dakika kumi wakatoka wakiwa tayari. Tracy yeye alienda kwaajili ya kutoa matibabu kama patahitajika. Akatoka akiwa tayari huku mgongoni kwake akiwa amebaba begi.



    Chopa likaandaliwa na Fady mwenyewe ndie akawa dereva wa chombo hicho. Katika uwanja uliokuwepo nyuma ya Hotel hiyo. Waliingia na Fady akaliondoa chopa lile. Mara hii likawa angani na chini Mr Kaoneka na Feysal walikuwa wakiwatakia wenzao safari njema. Baada ya chopa lile kupotea angani. Feysal alirudi kwenye chumba chake kwaajili ya kuwapa wenzake maelekezo.



    Kutokana na kasi iliyokuwa ikiendeshwa kwenye chopa hilo. Lisaa limoja na nusu lilitosha kuwafikisha ndani ya jiji la Tanga. Majira hayo yakiwa ni saa nne usiku. Chopa likapakiwa umbali mrefu na ilipo ‘location’ wanayoifuata na hapo wakatumia miguu kufika huko. Karibu na ‘location’ ilipo. Waliliona gari la Hemedy likiwa limepakiwa kwenye miti ya mitiki. Wakalichunguza haraka haraka na kukuta likiwa salama.



    “Sasa sikilizeni. Acheni mimi niende na kama kutahitajika msaada zaidi, nitawshtua” TSSI 03 Hilda aliwaambia.



    “Hakikisha huchelewi kutoa ‘signal’ ya kuomba msaada kama kutakuwa na tatizo. Na sijui kwanini ‘Code One’ hakutoa ‘signal’ haraka”



    “Hayo sio ya kujadili sasa. Acha mimi niwahi” Hilda alianza kukimbia kuwahi kwenye jumba lile. Akashtuliwa na Sauti ya Tracy aliemtaka asimame. Akasimama na kugeuka huku akionyesha mfadhaiko usoni kwake. Tracy alimpatia kidonge na kumuambia. Ampatie Hemedy endapo akimkuta katika hali mbaya. Akamuambia kuwa kidonge hicho ni maalumu kwaajili ya kuongeza nguvu kwa muda kama atakuwa katika hali mbaya. Hilda alikipokea na kukihifadhi kwenye nguo. Akashukuru na kuendelea na safari yake.



    * *



    Muda huu sasa ambao upo kipindi ambacho aliingia yule mtu wa ajabu ambae sasa tumemjua kumbe ni TSSI 03 Hilda Ganjo.



    Taa ghafla zikazima ndani humo na moshi mkali ukatanda. Moshi ambao uliwakohoza waliokuwa ndani ya chumba hicho. Mara ghafla milio ya risasi ikasikika humo na kila mmoja akakimbilia mapipa yaliyokuwa yamezagaa ndani humo akijificha nyuma yake. Baada ya dakika moja milio ya risasi ikakoma na ule moshi ukapungua taratibu. Mwisho kabisa taa zikawaka tena.



    Chumba kilikuwa kimyaa!. Wakatoa vichwa vyao kuchungulia kunani. Na kila mmoja akimuwazia mwenzake kuwa huenda ikawa amedhurika kama sio kufa kwa risasi zile. Wakajikuta wakichunguliana wenyewe kwa wenyewe. Ebwana wee!! Kwenye kiti walipomfunga Hemedy. Hakuwepo!!. Wakatazama pale mlangoni na kuiona ile bunduki ikiwa chini na mwenyewe asionekanae.



    Ata ambae aliinuka taratibu huku akitanguliza bastola yake yenye risasi moja. Akachunguza vizuri na kugundua kuwa maadaui zao hawakuwepo. Lakini hata hivyo pia aligundua kuwa ile bunduki pale chini. Ilikuwa ikitoa baruti tu na zile zilizokuwa zikilia sio risasi. Akaawaambia wenzake wasimame. Mr Hanein aliinuka akiwa na ghadhabu nyingi kwa kumkosa adui yake kirahisi kama hivyo. Akatoa amri kwa vijana wake haraka iwezekanavyo watafutwe watu wale na wauawe mara moja. Wakatoka kwaajili ya kuanza masako muda huo.



    SMG. ‘Sub Machine Gun’. Silaha nyingi zilizokuwa zimetawala ndani humo. Kila mmoja akakamata yake kwaajili ya kuanza msako ndani na nje ya jumba hilo. Wakipania kuwa wawatie mikononi wote waliowaingilia kwenye anga zao. Walibaki sita. Watatu wakabaki chini na watatu wakapanda juu. Atu, Queen na Paskali, wao walibaki chini. Huku Mr Hanein mwenyewe, Ata na Deva wakiwa juu. Kwakuwa huko chini kulikuwa ni kukubwa sana. Kila mmoja akashika njia yake kuendeleza msako.



    Taratibu na kwa umakini. Hatua ndogo ndogo huku ameshika vyema bunduki yake. Atu alikuwa akiusogelea mlango wa chumba ambacho kilikuwa mbele yake. Mlango ukiwa wazi. Alipofika mlangoni. Akazama haraka ndani kwa umakini. Lakini hakukuta mtu.



    Akarudi tena kutoka nje iliaendelee na msako wake. Mbele yake akakutana na yule mtu aliewavamia ghafla akiwa amesimama akimuangalia yeye. Atu alimnyooshea bunduki lakini yule mtu alikuwa vile vile na wala hakutetereka. Mara hii hakuwa ameshika silaha yoyote mkononi kwake.



    “Wewe ni mwanamke kama mimi. Na siku zote mwanamke ni kujiamini. Unaonaje ukaweka bunduki lako pembeni halafu tukajaribu kupambana kabla sijakuua?” TSSI 03 alimuambia Atu. Atu akatupa bunduki pembeni huku akicheka kwa dharau.



    Mpambano ukaanza. Walipigana sana huku kila mmoja akiwa makini zaidi ya mwenzake. Hilda alipigwa na yeye akapiga. Atu nae alipigwa na yeye akapiga. Kiuhalisia ilionekana kama uwezo wao ulikuwa sawa kwa kiasi fulani. Walipigana sasa hadi ikawa wanaangaliana na kila mmoja akitweta huku akimtegea mwenzake aanze. Waliangaliana kwa kitambo kirefu. Kisha wakaendeleza mpambano.



    Kule juu pia waligawana hivyo hivyo kama walivyogawana kule chini. Kila mmoja alishika upande wake. Na upande alioushika Deva aliujutia. Alikutana na TSSI 01 aliekuwa amefuraha kwa ghadhabu baada ya kuuliwa baba yake mdogo mbele yake. Deva akajiweka tayari kwa mapambano. Huruma zimuendee Deva maana alikutana na mzimu na wala sio mtu wa kawaida kama yeye alivyodhani. Alichezea kichapo kiasi ambacho aliona afadhali akimbie.



    Unadhani basi hata alifika mbali? TSSI 01 Alichomoa ile kamba ambayo ilikuwa kiuononi kwake. Akairusha kwa ustadi mzuri na kamba ile ikaenda kujifunga kwenye miguu ya Deva. Deva akaangukia pua. TSSI 01 alimfuata pale pale na kwenda kumnyonga na ile kamba kwenye shingo. Deva alitapatapa kujaribu kuokoa uhai wake. Ikashindikana na kifo kikawa hatamu yake.



    TSSI 01 akahama upande kwenda kumtafuta mwengine. Mara hii sasa alikutana na Ata uso kwa uso. Ata alikuwa akimuhofia sana TSSI 01. Baada ya kupokea kichapo mchana wa siku hiyo na kukimbia baada ya kuzidiwa. Lakini muda huu akajipa moyo kuwa walimrostisha mwanzo kabla kutoroshwa kule chumbani. Akajipa moyo kwamba hatakuwa na uwezo wa kupigana. Ni bora angekimbia kama alivyokimbia mchana. Kuliko kujaribu kupambana na TSSI 01 wa muda huu ambae ametawaliwa na ghadhabu nyingi kwa kifo cha baba yake mdogo.



    Nae alichezea kipigo zaidi ya kile alichopekea mchana wa siku hiyo. Alipigwa mpaaka akaomba msamaha lakini wala TSSI 01 asisikie alichozungumza. Na mwisho wa ghadhabu zake. Akamchinja kwa kisu alichokichomoa kwenye kiatu chake. Mbele yake nyuma yetu. Ata kitabu cha historia yake kikafungwa hapo.



    Kule chini baada ya Atu kuona anazidiwa. Alikimbia na kupotelea kusikojulikana. Hilda alishikwa na hasira baada ya hasimu wake kumtoroka. Akaanza kumtafuta. Wakati akiendelea kumtafuta. Alishtukia akipigwa teke la mgongo. Akajibwaga chini na kuinuka haraka. Akakutana na mtu mwengine na huyu alikuwa ni Queen.



    Mpambano ukaanza kati ya Queen na Hilda. Unadhani nae Queen alichukua hata dakika tano? Ndani ya dakika hizo alikuwa mfu tayari. Wakati Hilda anamalizia kumuaa Queen. Paskali alitokea na bunduki. Akaanza kumimina risasi nyingi upande ule. Hilda akachumpa kwenye chumba kilichokuwa karibu na pale alipo huku risasi zikimsindikiza.



    Paskali aliacha kupiga risasi na kuenda kule Hilda alipoingia. Ghafla akiwa hajatarajia. Hilda alichomoka akiwa hewani na kuenda kumvaa Paskali usoni. Wakaenda wote chini huku paskali bunduki ikimtoka mikononi. Kwakuwa Paskali hakuwa na ujuvi wowote wa kimapigano. Ilichukua dakika moja tu kumalizwa. Na sasa Hilda akawa anamtafua Atu.



    Kule juu muda huu Mr Hanein alikutana ‘tit for tat’ na TSSI 01. Alikuwa amemnyooshea bastola huku akimtaka aache makeke yake anaweza kummaliza muda huo huo. Hasira alizokuwa nazo TSSI 01 juu ya Mr Hanein hazikuwa ndogo. Ni kama vile ile bastola alionyooshewa hakuiona ama aliiona lakini alisahua kwamba inamatumizi gani. Akamfuta Mr Hanein mbio kwa hasira. Akamvaa lakini nae akiwa amejeruhiwa begani na risasi.



    Mr Hanein alichezea kichapo kikali huenda kushinda wote. Maana Hemedy hakutaka kumuua mapema. Alimpiga kama dakika ishirini na mwisho akachukua kipande cha taa ya mshumaa uliokuwa umevunjika baada ya purukushani hizo. Akamchoma nacho cha shingo na damu zikaruka huku na huko. Zikatapakaa eneo zima. Kwa hasira alizokuwa nazo akakapembeni na kuanza kulia mwenyewe. Maana bado alikuwa na ghadhabu na hakupatikana wa kummalizia nazo ghadhabu hizo.



    Kule chini mpambano ulikuwa ukiendelea kati ya Hilda na Atu walioonana tena kwa mara ya pili. Bado Atu aliendelea kuchezea kichapo. Mwisho akaona akiendelea kubakia hapo. Anaweza akauliwa. Hakujua wenzake wapo wapi muda huo. Akaanza kukimbia huku Hilda mara hii akiwa nyuma yake hataki kumuacha hata hatua moja.



    Kule ambapo anakimbilia Atu. Ni kwenye kile chumba ambacho Mr Hanein kwa mara ya kwanza aliwaonyesha na kuwaambia kuwa kuna mlango wa kutokea kwenye bomba kubwa ambalo linatokeza kwenye barabara kuu. Atu alipofika kwenye kile chumba. Alibonyeza kile kioo mara tatu kama alivyosema baba yake siku ile. Kioo kile kikajifungua na Atu akapita. Muda huo huo nae Hilda ndio alikuwa anafika. Alikuta kioo kile ndio kinamalizikia kujifunga.



    Akang'aka kwa hasira na kujaribu kuvunja kioo kile. Alivyotegemea sio ilivyotokea. Kioo kilikuwa kigumu mithili ya chuma. Akaangalia huku na huko ndani humo na kukuta nondo kubwa imejilaza chini. Akaiokota na kuanza kukishambulia kioo kile. Lakini hakikuweza kutoa hata ufa. Mara saa yake ya mkononi ikaanza kulia alam. Akaiangalia na kuanza kutoka mbio ndani humo. Mara kadhaa alichanganyikiwa kwa kutoijua njia ya kupandia juu.



    Dakika mbili mbele aliipata na kupandisha kwa kasi. Mara hii akawa ndani ya chumba amabcho kilikuwa na uwazi huo. Akatoka mbio tena huku saa yake ikizidi kupiga alam. Alipotokeza sebuleni alimkuta Hemedy amechuchumaa huku kwenye bega lake kukitoka damu. Akamvuta mkono na kuanza kutoka nae mbio. Kwenye ukuta wa uzio wa jumba hilo. Kulikuwa kuna kamba. TSSI 03 alimuambia TSSI 01 atangulie kupanda yeye haraka huku yeye akiwa nyuma yake.



    TSSI 01 alipanda kwenye kamba ile kwa shida kutokana na mkono wake mmoja kujeruhiwa huku TSSI 03 akiwa chini akimuangalia anavyopanda mara kadhaa akiangalia saa yake kwa hofu. TSSI 01 alirukia kwa nje na TSSI 03 alipanda na yeye haraka kwenye ile kamba. Akaruka kwa nje baada ya kufika juu. Alipotua chini alimshika mkono na wakaanza kukimbia mbio kuenda kule wenzao walipo. Na dakika hiyo hiyo mlipuko mkubwa ukafuata kwenye lile jumba na kulipuka likiwaka moto mkubwa.



    TSSI 01 alisimama na kutazama nyuma. Akawa anaangalia jumba lile. TSSI 03 nae akagauka na kuangalia kule alipokuwa Akiangalia TSSI 01. Wote wakatabasamu na kukumbatiana. Hilda aliona kumbato halitoshi. Akataka kupeleka kinywa chake kwenye kinywa cha Hemedy. Lakini Hemedy alimkatalia. Akamuambia kuwa muda huo bado kinywa chake hakipo sawa. Hilda kwa aibu akamkumbatia tena.



    “Hahaha kumbe ndio maana ulikuwa una wahka sana. Ulitaka ukamuokoe baba chanja kabla hawajakuwahi” Fady alichomekea utani na wenzake wakacheka. Kisha hapo simu ya Fady ikaita. Alikuwa ni Mr Kaoneka ndie anaepiga.



    “‘Code Five’ Nini kinaendelea huko? Mbona hatuoni mabadiliko yoyote” Mr Kaoneka alisikika akiongea.



    “‘Mission Complete’ Ndege mjanja alienasa kwenye tundu bovu ameokolewa na ndege mtundu namba tatu. ‘Soon’ tutakuwa nae huko” Sauti za furaha zilisikia zikitoka kwa Feysal kwenye simu huku Mr Kaoneka akicheka kwa furaha. Akauliza mbona ‘signal’ ya TSSI 01 imepotea ghafla. Swali hilo Fady akamuhamishia Hemedy nae ndio akakumbuka kuwa simu yake ilichukuliwa na Mr Hanein kwahiyo itakuwa imelipuka kwenye nyumba ile. Akamrudishia jibu hilo Mr kaoneka. Nae akamuambia kuwa ametoa likizo fupi kwa wote ya wiki moja kabla hawajarudi kitengoni.



    Furaha ikawajia vijana wale. Wakamuomba mkuu wao likizo yao waimalizie katika mji huo na Mr Kaoneka akasema ni wao tu wenyewe. Lakini inabidi chopa irudishwe kitengoni. Fady hakuwa na budi kurudi Daresalam usiku huo huo kurudisha chopa huku akiwaahidi wenzake kuwa kesho mapema asubuhi atatokea katika mji huo akiwa na Feysal. Wakacheka kwa furuha na Fady akaenda kudanda chopa safari ya kurudi kitengoni ikaanza.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Vipi mrembo? Uko poa wewe?” Hemedy alimuambia Tracy.



    “Acha zako wewe. Embu twendeni ma_hom nikakufanyie tiba kisha upate masaji safi kutoka kwa Hilda” Wote wakacheka na kisha wakaingia ndani ya gari alilokuja nalo Hemedy. Hilda akakaa kwenye usukani huku pembeni yake akikaa Hemedy. Hilda alimtazama Hemedy kwa jicho tatanishi. Hemedy akahamisha macho yake na kuangalia nje huku akitabasamu. Hilda aliondoa gari kwa mbwembwe mahala hapo kurudi mjini.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog