Simulizi : Mauaji Yaliyojaa Utata
Sehemu Ya Nne (4)
Moyo wa Bwana Seppy haukuridhika kabisa, japokuwa aliendelea kufanya mauaji lakini uwepo wa Benjamin ulimkosesha amani kabisa. Alikosa furaha kabisa, kuna kipindi alikuwa akikaa chumbani kwake na kujifikiria sana.
Mtu huyo alikuwa muhimu sana, kila kilichokuwa kikiendelea, aliona kama Benjamin alikifahamu hivyo kama mtyu huyo asingekufa haraka iwezekanavyo basi ilikuwa ni lazima kujulikana na hivyo kumletea matatizo katika maisha yake.
Hakuwa na mfariji yeyote yule zaidi ya demu wake mwenye asili ya Urusi aliyeitwa Maria Kontekov, msichana mrefu, mrembo mwenye macho ya bluu ambayo yaliwachanganya wanaume wengi kipindi hicho.
Mara kwa mara alikuwa akionana na huyu msichana wake, alioa na kubahatika kupata watoto wawili lakini kipindi kirefu cha maisha yake alipenda kukaa na Maria zaidi ya mke wake ambaye naye umri ulikwenda sana kama alivyokuwa.
Nyumbani hakukulalika, kama alitaka kuonana na vijana wake, alikuwa na jumba jingine la kukutaniana na kupanga vitu vingine. Alipokuwa na mawazo mengi kama kipindi hicho, kimbilio lake pekee lilikuwa Maria ambaye alikuwa akitoka Urusi na kwenda Marekani, wanafanya mambo yao na kisha kurudi huko.
Fedha iliongea, Maria hakuwa akiongea chochote mbele ya Bwana Seppy, alipata chochote alichokitaka lakini kwa sharti kwamba hakutakiwa kuwa na mwanaume yeyote zaidi yake.
Hilo, kwa Maria wala halikuwa tatizo, alikuwa radhi kumridhisha mzee huyo tu kwani kitu pekee alichokihitaji kilikuwa ni fedha tu. Alipewa fedha za kutosha na hata pale ambapo alikuwa na fedha nyingi, nyingine akaongezewa, akaunti yake benki ikajaa fedha nyingi, akanunuliwa jumba la kifahari jiji Moscow nchini Urusi, akanunuliwa magari ya kifahari pamoja na kufunguliwa biashara kubwa.
Mawazo juu ya Benjamin yalipomzingua kichwani mwake, harakaharaka akamwambia Maria afike haraka iwezekanavyo nchini Marekani. Hakukuwa na umbali mkubwa kutoka Marekani mpaka Urusi lakini mzee huyo akaamua kumtumia ndege yake na hatimaye wakutane jijini New York, wazungumze kama kawaida yao na kuingia chumbani kufanya mambo yao.
Ndani ya saa tatu, tayari msichana huyo alikuwa mikononi mwake, walikuwa chumbani, wakafanya kila kitu huku muda mwingi mzee huyo akihitaji kuchuliwa mgongo wake kitu ambacho wala hakikuwa tatizo kwa Maria.
“Kuna nini mpenzi?” aliuliza Maria kwa sauti ndogo iliyojaa mahaba.
“Hakuna kitu kipenzi!”
“Hapana! Huwezi kunidanganya, ninakujua, nimekaa nawe kipindi kirefu, unapokuwa kwenye mawazo, najua, hebu niambie, tatizo nini,” alisema Maria huku akiwa kifuani mwa Bwana Seppy.
“Hakuna kitu!”
“Kweli?”
“Ndiyo mpenzi! Hebu nichue kidogo mgongo,” alisema mzee huyo, haraka sana Maria akaanza kazi hiyo.
Siku hiyo walishinda chumbani tu, Bwana Seppy alijisikia amani moyoni mwake, msichana huyo ndiye alikuwa kila kitu katika maisha yake, ilikuwa ni rahisi kugombana na mkewe ila si Maria, hata kama ungetaka kumchukiza, mtongoze Maria, alikuwa radhi kukuua ila si kama ambavyo ungemtongoza mkewe wa ndoa.
Wiki nzima Bwana Seppy hakurudi nyumbani, alikuwa akijifariji na Maria tu chumbani. Fedha ilikuwa kila kitu, ilibadilisha kila muonekano wa kitu, kile kilichokuwa hakiwezekani, ilikifanya kiwezekane, tena kwa urahisi kabisa.
Maisha yalikuwa ni ya raha na starehe, vijana wake waliendelea na kazi kubwa ya kumtafuta Benjamin huku yeye akiwa hotelini akila raha kabisa. Hakutaka kusikia lolote kuhusu familia yake, hakutaka kusikia kuhusu watoto wake, Jericho na Vanessa, kitu alichotamani kusikia ni kuhusu Maria tu.
“Umekuwa mnyonge kwa kipindi kirefu sana, naomba leo usiku unitoe mtoko,” alisema Maria kwa sauti ndogo huku akiwa kifuani mwa mzee Seppy.
“Unataka twende wapi?”
“Tukaangalie mechi ya kikapu, leo La Lakers anacheza,” alisema msichana Maria.
“Sawa! Tutakwenda kutazama, ninataka uwe na furaha kipindi chote mpenzi,” alisema mwanaume huyo.
Haraka sana Bwana Seppy akampigia simu Dracula na kumwambia kwamba siku hiyo alihitaji kwenda kuangalia mchezo wa kikapu baina ya Timu ya LA Lakers na Memphis ambazo zilitarajiwa kucheza katika mchuano mkali wa timu za Magharibi.
Hilo wala halikuwa tatizo, haraka sana Dracula akaenda kukata tiketi mbili, tena katika upande wa VIP, alipozipata akampelekea mzee huyo hotelini kitu kilichomfanya Maria kuwa na furaha sana.
“Nakupenda mpenzi,” Maria alimwambia Bwana Seppy.
“Nakupenda pia.”
Walilala mchana huo na usiku wakaamka na kuanza safari ya kwenda katika uwanja wa La Lakers, Staple Center. Ndani ya gari ulikuwa ni muda wakupeana mahaba motomoto. Japokuwa Bwana Seppy alikuwa mtu mzima kama baba yake lakini halikuwa tatizo kwa Maria kubadilishana naye mate na kufanya mambo mengine ya aibu, alifanya hivyo kwa sababu nyuma ya pazia kulikuwa na fedha.
Walipofika, wakataremka na kisha kuingia ndani. Ilikuwa vigumu kumgundua Bwana Seppy kwamba alikuwa yeye, kichwani alivalia kofia, akavaa fulana kali, jinzi na raba zilizokuwa na chata ya Nike, kwa muonekano, alionekana kama kijana mwenye miaka thelathini.
Wakaingia mpaka katika sehemu ambayo walitakiwa kukaa. Huko, ni watu wenye fedha ndiyo waliokuwa wakikaa, tiketi zao zilikuwa ni dola elfu themanini ambazo zilikuwa ni sawa na milioni mia moja sitini, na watu walilipia bila malalamiko.
Kule walipokuwa wakikaa, mbele yao kulikuwa na kioo kikubwa, walikaa kibosi na wote waliokuwa huko walikuwa na wasichana wao wadogo, ni mambo ya kifuska ndiyo yaliyokuwa yakiendelea huko.
Katika kipindi hicho, mchezaji aliyekuwa na jina ambaye alikuwa akichipukia alikuwa Paul McKenzie, miongoni mwa wachezaji waliokuwa mwiba kipindi hicho, huyu jamaa alikuwa akitisha. Alikuwa na umri wa miaka kumi na tisa tu lakini uwezo wake ulikuwa mkubwa kana kwamba alikuwa na miaka thelathini.
Mpaka katika kipindi hicho, alivunja rekodi nyingi mno na rekodi moja tu ndiyo alikuwa akiifukuzia, ya kufunga pointi nyingi kama ilivyokuwa kwa mkongwe wa mchezo huo, Michael Jordan, au MJ kama alivyojulikana na watu wengi.
Mafanikio makubwa ndiyo yaliyomfanya kujituma kila siku. Timu ya La Lakers ikapata mtu sahihi wa kuchukua nafasi ya mkali mwingine, Shaq O’Neil ambaye alistaafu kipindi kilichopita huku akiwa ameipa timu hiyo mafanikio makubwa.
Mbali na uwezo mkubwa aliokuwa nao, Paul alikuwa na sura nzuri, aliwavutia wasichana wengi, katika kipindi hicho ndicho alisemekana kuwa mwanaume mwenye sura nzuri zaidi ya wanaume wote chini ya jua. Wanawake walimpenda kwa sababu hakuwa na makuu, hakuwa na kashfa yoyote ile, kitu alichokuwa akikiangalia ni mpira wa kikapu ambao ulimpa magari, majumba ya kifahari na vitu vingine vingi, hata akaunti yake benki ilikuwa ikisomeka na kutuna kila siku.
Wakati tv kubwa iliyopachikwa ukumbini hapo ilipomuonyesha Paul kwa karibu, tena kwa kumvuta, msichana Maria akashtuka, hakuamini kama kweli duniani kulikuwa na mwanaume mwenye sura nzuri kama yule aliyemuona.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mapigo yake ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu, akajikuta akianza kuangukia katika penzi la mwanaume huyo, hakuishia kuangalia kwenye televisheni ile tu, akayatupa macho yake uwanjani, kila aliposhika mpira, wanawake walisikika wakipiga kelele hali iliyoonyesha kwamba hata wanawake waliokuwa humo walimpenda mno.
Moyo wake ukamia mno, kwa jinsi Paul alivyokuwa mzuri, hakutaka kumuona mwanamke yeyote anakuwa naye zaidi yake yeye, hakutaka kubaki kule juu, akajifanya kuvurugwa na tumbo hivyo alitakiwa kwenda chooni, Bwana Seppy hakuwa na wasiwasi wowote ule, akamruhusu msichana huyo aende huko.
Maria akaanza kutembea kwa harakaharaka, akashuka chini mpaka kule katika viti vya chini kabisa, alitaka kumuona Paul kwa ukaribu kabisa kwani alihisi telvisheni ile ilikuwa imemdanganya, alipofika huko, akajipenyeza katikati ya watu mpaka katika kiti ambacho hakikuwa na mtu na kukaa hapo.
Macho yake yakaanza kumwangalia vizuri Paul, aliuona uzuri wa mwanaume huyo, wanawake ambao walikuwa jirani yake, muda wote walikuwa wakimsifia mwanaume huyo, tena huku wakimuita kila alipogusa mpira.
Maria alikasirika, alitamani kuwaambia wasimuite kwani alimuona kama kuwa mpenzi wake. Wakati mpira ukiwa umepigwa na kuelekea nje katika upande aliokuwa Maria na wanawake wengine.
Paul akaufuata, wanawake wote wakasimama, wakazidi kuliita jina lake, Paul akawaangalia, tabasamu pana lilikuwa usoni mwake, alipomuona msichana Maria tu, hakufanya kitu chochote zaidi ya kumkonyeza kitu kilichowafanya wanawake wote waliokuwa hapo kumuonea wivu msichana Maria, kwani kwa muonekano tu, hata naye Paul alionekana kuvutiwa naye, ila hakujua kama angeweza kuonana naye baada ya mechi hiyo kumalizika.
Maria hakutaka kuondoka, akanogewa kukaa mahali hapo, baada ya dakika kumi na tano ndipo akakumbuka kwamba alikuwa ameaga anakwenda chooni hivyo kama angechelewa zaidi kungekuwa na tatizo, harakaharaka akasimama na kuanza kuondoka kuelekea juu alipomuacha mwanaume wake.
Alipandisha ngazi harakaharaka mpaka juu ambapo akaingia katika chumba hicho. Bwana Seppy wala hakuwa na wasiwasi, ndiyo kwanza akawa anazungumza na wazee wenzake wenye fedha, Maria akakaa katika kiti na kuendelea kuufuatilia mchezo huo.
Mawazo yake yalikuwa kwa Paul tu, kila aliposhika mpira, alitetemeka, mapigo yake ya moyo yalimdunda mno, mwanaume huyo alimtetemesha kupita kawaida.
Hata Paul mwenyewe, muda mwingi alikuwa akiangalia katika sehemu aliyokuwa Maria, pale, hakuweza kumuona, hakujua kama mwanamke huyo aliondoka au alitoka na angerudi baada ya muda fulani.
Kipindi cha kwanza kilipofika, wakiwa mapumziko, Maria alikuwa akimfuatilia Paul kwa karibu kabisa, macho ya Paul hayakutulia, alikuwa akiangalia huku na kule, kwa muonekano wake tu ilionyesha kwamba alikuwa akimtafuta mtu fulani, alitamani kujitokeza lakini alishindwa kabisa kufanya hivyo.
“Au nimfuate?” alijiuliza huku akiendelea kumwangalia mwanaume huyo.
Paul alichanganyikiwa, tayari moyo wake ulitekwa na msichana huyo, hakuwa radhi kuendelea kucheza na wakati moyo wake ulichanganyikiwa, kipindi cha pili hakuingia, alifikiria kuingia kipindi cha tatu.
Alikaa kwenye benchi lakini macho yake yaliendelea kutalii huku na kule, alitamani kumuona msichana huyo ambaye aliutetemesha moyo wake kwa kipindi hicho.
Wanawake walikuwa wakimuita lakini hakuwa na habari nao, alikuwa akimtaka msichana mmoja tu, alikuwa Maria ambaye hakujua aliondoka na kuelekea wapi na wala hakujua kama alikuwa akifuatiliwa na msichana huyo.
Mchezo uliendelea, La Lakers hawakuwa wakali kipindi hicho, staa wao alikuwa nje, ila kipindi cha tatu kilivyoingia, akaingia, timu ikapata uhai na kujikuta akifunga pointi nyingi sana.
Mpaka mchezo unamalizika, bado Paul alikuwa na mawazo tele, alishindwa kuvumilia, hakutaka kuingia chumbani kuzungumza na wachezaji wenzake, alibaki akizunguka huku na kule.
Watu wakaanza kutoka, naye akatoka uwanjani, alipofika kwenye korido tayari kwa kwenda chumbani walipokuwa wenzake, akakutana na mchezaji mwenzake wa akiba, akamfuata na kisha kumpa kikaratasi kilichokuwa na namba, alipoiangalia namba hiyo, hakuifahamu ila chini kulikuwa na jina la Maria, akaisevu na kisha kuangalia picha katika Mtandao wa Whatsapp, picha aliyokutana nayo, ilikuwa ni ya msichana huyo aliyekuwa akimtafuta sana kipindi hicho. Msichana Maria.
****
Mpaka mechi inamalizika, Maria alichanganyikiwa, hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kuwasiliana na Paul. Hakutaka kubaki humo, alijua kwamba kama angeendelea kubaki asingeweza kuonana na mwanaume huyo, ilikuwa ni lazima ateremke ili aende akaonane naye huko huko.
Hakutaka kusubiri, alichokifanya ni kumuaga Bwana Seppy kwamba anakwenda tena chooni kwani tumbo lilikuwa likimsumbua. Mzee Seppy hakuwa na tatizo, alikuwa amenogewa na maongezi na mzee mwenzake tena huku wakinywa pombe kali, akamruhusu.
Maria akaondoka kuelekea chini, huko, alimsubiri Paul lakini hakutokea, hakujua nini cha kufanya, kitu kilichomjia kichwani mwake ilikuwa ni lazima amwachie namba mwanaume huyo ili kama kumtafuta, amtafute kwani kuonana naye tayari ilionekana kuwa tatizo kubwa.
Akachukua kikaratasi, akaandika jina lake na namba yake ya simu. Kwa sababu hakumuona mwanaume huyo, alichokifanya ni kumgawia mchezaji mmoja na kumwambia kwamba ampe Paul kwani alitaka kuwasiliana naye, hilo halikuwa tatizo, mchezaji huyo akachukua kikaratasi hicho na kumuahidi kwamba angeweza kumpa.
“Naomba usisahau, nakuomba,” alisema Maria.
“Usijali! Nitaifikisha...”
“Nakuomba usikose...tafadhali nakuomba!”
“Usijali dada!”
“Nitashukuru sana!”
****
Muda wote Maria alikuwa akiiangalia simu yake, alikuwa na presha kubwa ya kuona akipigiwa na Paul na kumwambia kwamba alikuwa akimpenda kama alivyokuwa akimpenda.
Hakuwa na raha, hata ndani ya gari alikuwa kimya kabisa, moyo wake ulikuwa kwenye mawazo tele, hakumfikiria Bwana Seppy tena, mtu aliyekuwa akimfikiria alikuwa Paul tu ambaye aliuburuza vibaya moyo wake.
Bwana Seppy aliyaona mabadiliko, akajaribu kuuliza sababu ya mpenzi wake kuwa vile lakini wala hakupata jibu lolote lile, ilimuuma kwani kati ya watu ambao hakutaka kabisa awaone wakiwa na majonzi mioyoni mwao, alikuwa huyu Maria.
Alijaribu kumuuliza tatizo lilikuwa nini lakini hakupewa jibu la kuridhisha kwani msichana huyo alimwambia wazi kwamba alikuwa poa na hakukuwa na tatizo lolote lile.
Upande wa pili, bado Paul alikuwa akikiangalia kikaratasi kile, japokuwa hakuwa akimfahamu msichana huyo lakini akahisi kwamba ndiye yule aliyemuona uwanjani wakati mechi ikiendelea na ghafla akapotea.
Naye kuanzia kipindi hicho akawa na mawazo tele, alikuwa na namba lakini alihofia kuipiga na kuzungumza na msichana huyo. Alibaki akijiuliza, kujiuliza huko hakukuisha mpaka alipolala usiku.
Kesho, kitu cha kwanza kabisa kukikumbuka kilikuwa ni namba ya Maria, hakutaka kusubiri, alichokifanya ni kuchukua simu yake na kuanza kumpigia simu Maria. Simu ilianza kuita, ikaita, hapohapo ikakatwa.
Mara ya kwanza alihisi kwamba ni network, alichokifanya ni kupiga tena na tena lakini majibu yalikuwa yaleyale kwamba simu ilikatwa kila alipopiga, na baadaye alipojaribu kuipiga tena, haikuwa ikipatikana kitu kilichouumiza moyo wake kupita kawaida.
****
Nahitaji kurudi nyumbani nikapumzike mpenzi,” alisema Maria huku akimwangalia Bwana Seppy usoni.
“Mbona mapema jamani! Si ulisema unakaa mwezi mzima?” aliuliza Bwana Seppy huku akionekana kushtuka.
“Kuna mambo mengi natakiwa kufanya, ila wiki ijayo nitarudi tena, si unajua mama atakuwa amenikumbuka sana,” alisema Maria.
Kwa jinsi alivyokuwa akizungumza, ilikuwa ni vigumu sana kugundua kwamba msichana huyo alikuwa na lake kichwani. Aliiona simu ngeni ikiingia, haikuwa kawaida simu ngeni kuingia katika simu yake, akajua kwamba moja kwa moja mpigaji alikuwa Paul.
Alitamani kupokea lakini ilishindikana kabisa kwani alikuwa jirani na Bwana Seppy hivyo kuikata kila ilipokuwa ikiita. Baadaye alipoona kwamba inasumbua sana na angeweza kushtukiwa, akaizima kabisa.
Moyo wake ulikuwa na furaha tele, hakukuwa na kitu kingine alichokifikiria zaidi ya kumpigia mwanaume huyo ili azungumze naye na ikiwezekana wakutane sehemu, hata kama angemuomba penzi, kwake hakuwa na kinyongo, alikuwa tayari kumpa kwani hakukuwa na mwanaume aliyekuwa akimpenda kama ilivyokuwa kwa Paul.
Alihakikisha anaondoka siku hiyo, hakutaka tena kuendelea kukaa nchini Marekani, iwe isiwe ilikuwa ni lazima kuondoka. Hilo wala halikuwa tatizo, Bwana Seppy akakubaliana naye, hivyo mchana wa siku hiyo akapanda ndege ambayo ilimrudisha mpaka nchini Mexico.
“Nitakukumbuka mpenzi,” alimwambia Bwana Seppy.
“Nitakukumbuka pia, ila usisahau kurudi wiki ijayo!”
“Nitarudi tu,” alisema Maria na kisha kummwagia mabusu mfululizo.
Wakati ndege ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Benito Juarez nchini Mexico, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumpigia simu Paul. Wakati simu inaita, moyo wake ulikuwa na presha kubwa, alitamani kuisikia sauti ya mwanaume huyo. Simu wala haikuita sana, ikapokelewa.
“Nazungumza na nani?”
“Mimi! Maria, yule binti wa uwanjani,” aliitikia Maria huku akiachia tabasamu, fikra zake zilimwambia kwamba mwanaume huyo alikuwa akimwangalia.
“Nimefurahi sana kusikia sauti yako! Kumbe upo Mexico?” aliuliza Paul kwa mshangao, kwani code ya simu ile ilionyesha kwamba mpigaji alikuwa Mexico.
“Ndiyo!”
“Ninatamani nikuone, naweza kuja?”
“Naweza!”
Walizungumza mengi, siku hiyo, Paul hakutaka kabisa kukaa nchini Marekani, kutoka hapo mpaka Mexico haikuwa mbali, siku hiyohiyo akapanda ndege na kuelekea huko ambapo alipokelewa na msichana huyo kisiri.
Hawakutaka kwenda kwenye hoteli kubwa kwani walihisi kwamba huko wangeshtukiwa mapema, kwa kuwa ilikuwa usiku, wakaenda katika hoteli ya chini, tena uswahili kabisa ambapo walikuwa na uhakika kwamba wasingeweza kugundulika kwa urahisi.
“Ninakupenda Paul,” alisema Maria huku tayari wakiwa kitandani.
“Nakupenda pia na ndiyo maana nimesafiri kuja huku, kwa ajili yako tu,” alisema Paul huku akimmwagia mabusu mfululizo msichana huyo.
“Una mchumba?” aliuliza Maria.
“Hapana! Wewe?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ninaye, ni mzee mmoja hivi, sina jinsi, ilinipasa kuwa naye,” alijibu Maria.
“Kwa nini?”
“Basi tu! Maisha yalinipasa kuwa na mzee huyo.”
“Yupi?”
“Bwana Seppy!”
“Yule bilionea?”
“Ndiyo! Ila moyo wangu haupo kwake kabisa, ninakupenda Paul, ninataka uupoze moyo wangu!” alisema Maria kwa sauti ya kulalamika kimahaba.
“Akija kujua je?”
“Sidhani na ndiyo maana ninataka tufanye vitu kisiri sana.”
“Basi hakuna tatizo!”
Usiku huo ulikuwa ni usiku wa raha, hakukuwa na karaha, walianza kubusiana hapa na pale na mwisho wa siku wakajikuta wakiwa watupu kabisa, kilichofuatia ni miguno ya mahaba na kelele za chumbani kitandani humo.
Huo ndiyo ukawa mwanzo wa kila kitu, mara kwa mara walikuwa wakikutana, safari za Paul kwenda nchini Mexico hazikukata, mara kwa mara alikuwa akisafiri kwenda huko.
Kwa Maria, naye alichanganyikiwa mno, kila alipopata nafasi ya kwenda nchini Marekani, alihakikisha anakutana na Paul na kufanya mambo yao kimyakimya pasipo mtu yeyote kufahamu.
Safari za Maria kwenda nchini Marekani kumuona Bwana Seppy zikaanza kupungua, kila alipoambiwa aende, akajifanya kuwa bize. Bwana Seppy akaanza kupatwa na machale, haikuwa kawaida kabisa, Maria alionekana kubadilika, alihisi kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia.
Kuna kipindi aliamua kumtafuta Maria, simu yake haikuwa ikipatikana lakini alipojaribu kumtumia ujumbe katika Mtandao wa Whatsapp, meseji ilikwenda na kusomwa.
“Upo wapi?” aliuliza Bwana Seppy.
“Nyumbani!”
“Una uhakika?”
“Ndiyo mpenzi! Mama anaumwa!”
“Haupo Marekani?”
“Mimi? Marekani! Nije bila taarifa! Inawezekana vipi?” aliuliza Maria.
“Kweli upo Mexico?”
“Ndiyo mpenzi! Halafu nimekumisi sana, nataka wikiendi hii nije kukuona,” aliandika Maria.
“Sawa! Karibu,” alijibu Maria. Hakujua kama Bwana Seppy alikuwa akimfuatilia hatua kwa hatua kupitia simu yake kwa kitu kiitwacho GPS na alijua kwamba kipindi hicho hakuwa nchini Mexico, alikuwa Marekani katika Hoteli ya Greenland iliyokuwa Kaskazini mwa Jiji la New York.
“David, niambie nini kinaendelea,” alisema Benjamin kwenye simu.
“Nimeendelea kufuatilia mawasiliano kwa njia ya simu,” alijibu David.
“Umegundua nini?”
“Kuhusu nini?”
“Juu ya hizo fedha, unajua hizi zitakuwa na maana yake, nini umegundua?” aliuliza Benjamin huku siku ikiwa sikioni mwake, Harry alikuwa pembeni akimsikiliza.
“Bado! Nitaendelea kufuatilia, hata mimi ninahisi kwamba kuna kitu,” alisema David.
Hilo ndilo lililowasumbua kichwa kipindi hicho, hawakujua ni kitu gani walitakiwa kufanya kwani kwa jinsi hali ilivyokuwa, ilionyesha kabisa kwamba huyo muuaji ambaye waliamini ni Bwana Seppy alitumia noti zile za fedha huku akiwa na maana yake.
Benjamin akakata simu na kisha kwenda kutulia kwenye kochi, kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi, moyo wake ulimwambia wazi kwamba kulikuwa na maana kubwa juu ya zile noti lakini hakujua zilikuwa na maana gani.
Alisimama kutoka pale alipokuwa na kuanza kutembea huku na kule, alikuwa na akili nyingi, alitumia muda wake mwingi kufikiria maana ya fedha zile lakini bado hakupata jibu lolote lile.
Alichokifanya ni kuchukua kalamu na karatasi na kisha kuziandika fedha zile kwa majina, alikumbuka, ilikuwa ni noti ya Yen, Dola, Paundi na Euro. Akaziandika zote na kisha kuanza kuziangalia kwa makini.
“Umegundua nini?” alimuuliza Harry.
“Bado sijagundua lolote lile,” alijibu Harry.
“Kweli?”
“Ndiyo!”
Mtu aliyekuwa akihusika na mauaji walikuwa wakimfahamu, alikuwa Bwana Seppy lakini tatizo lilitokea ni kwamba hawakujua sababu iliyompelekea kutumia fedha zile kuficha kilichokuwa kikiendelea.
Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya Benjamin ni kuandika jina la mzee huyo, tena yote mawili, David Seppy na kisha kuanza kuyaangalia kwa umakini kabisa.
“Harry, hebu yaangalie haya majina vizuri,” alisema Benjamin, akayatumbulia macho.
“Umegundua lolote?”
“Hapana!”
“Kweli?”
Alichokifanya Harry ni kuyaangalia tena majina yale, tena kwa wakati huu kwa umakini mkubwa kabisa, aliangalia vya kutosha lakini hakubahatika kitu. Alichokifanya Benjamin ni kulifuta jina la David, likabaki jina la Seppy.
“Na hapo?”
“Bado sijapata kitu.”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
Benjamin akatoa tabasamu pana, hakuamini kama mwisho wa siku angepata jibu kutokana na zile fedha zilizokuwa zikiwekwa kila tukio lilipokuwa likifanyika. Harry alikuwa kimya, kila alipomwangalia rafiki yake, alikuwa akitabasamu tu kitu kilichompa wakati mgumu kama kweli alijua maana ya fedha zile au la.
“Inamaanisha nini?” aliuliza Harry.
“Ni jina lake, alitaka kila mtu ajue kwamba yeye ndiye anafanya mauaji haya,” alijibu Benjamin.
“Unamaanisha Bwana Seppy?”
“Ndiyo!”
“Hebu nifafanulie...”
“Sawa. Hebu niandikie hizi alama za fedha kwenye karatasi...”
“Alama kivipi?”
“Kama dola ina alama gani?”
Alichokifanya Harry ni kuandika kama alivyoambiwa, fedha zote, yaani dola, euro, rubui na paundi, na alama zake zote kisha kumuonyeshea Benjamin. Benjamin akaichukua karatasi hiyo, akachukua kalamu na kuanza kumuonyesha.
“Alama hii ni alama ya dola ($), ukitoka hapa, kuna alama hii pia (£) ambayo ni paundi, ukiachana na hiyo, kuna hii (?), hii ni fedha ya Urusi, ila pia kuna (¥) hii ni fedha kutoka nchini Urusi, hizi zimekuwa fedha ambazo amekuwa akizitumia mara kwa mara. Sasa ziunganishe, yaani $+£+?+¥ ambayo unapata $£?¥, yaani SEPPY. Bado hujapata kitu hapo?” aliuliza Benjamin baada ya kutoa maelezo ya kutosha.
Harry alipigwa na mshangao, hakuamini kile kilichokuwa kimemaanishwa juu ya fedha zile zilizokuwa zikiwekwa kila tukio lilipokuwa likitokea. Moyoni mwake, aliamini kwamba Benjamin alikuwa na akili sana kwani kugundua kitu kama hicho, kwamba mtu alikuwa akifanya mauaji na kuweka fedha kama alama ya jina lake, hakika ilimshangaza sana.
“Mmh! Nimekuelewa, na hii noti ya euro vipi?” aliuliza Harry.
“Aliiweka kwa kuwa kitambo jina lake lilikuwa Seepy, ila baadaye akaamua kutoa E moja na kubaki Seppy, kwa hiyo alitumia euro kama kuongezea alama yake ambayo ni € ili watu wasielewe kile alichokimaanisha,” alijibu Benjamin huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
“Nimekuelewa. Kilichobaki?”
“Ni kuwataarifu polisi tu, akamatwe na afungwe gerezani,” alijibu Benjamin. Wakagongesheana mikono na kuahidiana kwamba asubuhi ya siku inayofuatia, ilikuwa ni lazima kwenda katika kituo cha polisi kutoa taarifa.
****
Moyo wa Bwana Seppy uliwaka kwa hasira, hakuamini kile kilichokuwa kikiendelea kwamba msichana aliyekuwa akimpenda, alikuwa akitembea na mwanaume mwingine.
Hakuamini, alichanganyikiwa, kila wakati alikuwa akitembea peke yake ndani ya nyumba yake huku akizungumza kama kichaa. Hakumjua mwanaume aliyekuwa akitembea na mpenzi wake ila aliambiwa kwamba mara kwa mara wawili hao walikutana katika hoteli moja iitwayo Greenland iliyokuwa huko New York.
Alichokifanya ni kuwaandaa vijana wake, ilikuwa ni lazima mwanaume huyo ajulikane ili kama kumuua amuue kwani asingeweza kumuua msichana Maria kwa kuwa alikuwa akimpenda mno kutoka ndani ya moyo wake.
Siku ziliendelea kusogea mbele, alijua ukweli lakini kila alipomwambia Maria kwamba alikuwa mdanganyifu katika uhusiano wao msichana huyo alimwambia wazi kwamba hakuwa akimdanganya kabisa na alimpenda yeye tu, nyuma yake hakukuwa na mwanaume yeyote yule.
Bwana Seppy akajipanga, ilikuwa ni lazima ajue ukweli wa kile kilichokuwa kikiendelea. Kijana wake wa kompyuta bado alikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha anafahamu mahali anapokuwa msichana huyo ili aweze kutoa taarifa inayotakiwa kutolewa.
“Mkuu! Maria amekuja tena Marekani,” Tim, kijana wa kompyuta alimwambia bosi wake.
“Amekuja lini?”
“Leo hii! Ila hayupo New York.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yupo wapi?”
“Los Angeles kwenye hoteli iitwayo Scandnavia Hill,” alijibu Tim.
Bwana Seppy hakutaka kuchelewa, harakaharaka akawatuma vijana wake waliokuwa Los Angeles kwenda kuhakikisha kile walichokuwa ameambiwa. Huku nyumbani, moyo wake ulizidi kuuma, alimpenda sana Maria, hakutaka kumpoteza, aliuburudisha moyo wake vilivyo hivyo kumuwia vigumu sana kumfanya lolote baya.
Alijua kwamba msichana huyo alihitaji uhuru wake, alitakiwa kuwa na mwanaume mwingine kwani yeye, kwa jinsi alivyokuwa na umri mkubwa, kitandani hakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mapenzi, kama msichana ambaye damu inachemka, ilikuwa ni lazima kutafuta kijana machachari, mwenye nguvu ya kufanya mapenzi hata kwa zaidi ya saa mbili kitandani.
Yote hayo alikubaliana nayo lakini tatizo likawa ni kusalitiwa huku akijua kwamba anasalitiwa. Hakutaka kuona hilo likitokea na hivyo alikuwa tayari kwa kila kitu, alimgharamia sana msichana huyo, hakukuwa na mtu mwingine aliyeingiza mkono katika kumpa fedha na kumjengea nyumba, sasa iweje mwanaume mwingine amchukulie msichana huyo?
Kitu alichokuwa akikisubiria ni kuhusu mwanaume aliyekwenda na mpenzi wake hotelini, hakujua kama alikuwa na fedha kuzidi yeye, hakujua kitu chochote kile, kitu alichokisubiri kilikuwa ni taarifa tu.
Vijana hao walifanya uchunguzi wao katika hoteli hiyo tena kwa kutumia wahudumu ambao walilipwa vizuri na kutoa jibu kwamba msichana Maria alikuwa na mwanaume, supastaa wa mchezo wa kikapu, Paul McKenzie, hivyo kumpa taarifa mzee huyo.
“Nani? Paul?” aliuliza mzee huyo huku akionekana kutokuamini.
“Ndiyo!”
“Hapana!”
“Ndiyo mzee, tumeangalia vizuri! Ni yeye,” alisema kijana wake.
Bwana Seppy alipigwa na butwaa, hakuamini alichokisikia, alikuwa shabiki namba moja wa Paul, alimpenda sana kwa kuwa alionyesha kuwa kijana anayesaka mafanikio kwa nguvu kubwa, kila siku katika maisha yake alipambana, alimpenda lakini mwisho wa siku ndiye huyohuyo aliyekuwa akitembea na mpenzi wake.
Kabla ya kutoa uamuzi wa nini cha kufanya, akatulia kwenye kochi lake, akaanza kufikiria kitu kwamba ni uamuzi gani alitakiwa kuuchukua, machozi yalikuwa yakimbubujika, alijifikiria kwa muda na mwisho wa siku, akaamua kutoa uamuzi wake.
“Muueni kama wengine,” alisema mzee huyo.
“Hakuna tatizo!”
“Kesho, Dracula atasafiri mpaka huko kuja kuwasaidia kukamilisha kazi hiyo,” alisema Bwana Seppy.
“Sawa bosi.”
****
Hawakuwa wakijua kama walikuwa wakifuatiliwa, Paul na Maria walikuwa chumbani huku wakiyafurahia maisha kama kawaida yao. Hawakutaka kwenda katika Hoteli ya Greenland jijini New York bali walichokifanya ni kubadilisha hoteli na kwenda Los Angeles na kuingia katika Hoteli ya Scandnavia Hill.
Huko, walikuwa huru, waliamini kwamba kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angefahamu kama walikuwa humo. Hawakujua kama wahudumu wa humohumo ndiyo waliwapa taarifa vijana wa Bwana Seppy hasa baada ya kupewa kiasi kikubwa cha fedha.
Walijiachia usiku kucha na ilipofika asubuhi, Paul hakutaka kuondoka, bado alitamani kuwa na mpenzi wake huyo kwa kuwa hakukuwa na mechi yoyote na hata mazoezi hayakuwepo pia.
“Naomba ukae huku wiki nzima,” alisema Paul huku akimwangalia Maria usoni.
“Kwa ajili yako tu, hakuna tatizo!”
Kweli, hicho ndicho alichokifanya, hakutaka kurudi nchini Mexico, aliamua kukaa humohumo hotelini huku Bwana Seppy akiwasiliana naye kwa kutumia Whatsapp tu, tena huku akiwa ameifunga simu yake.
Hakujua kama mzee huyo alifahamu kila kitu, tayari Dracula ambaye alikuwa akisubiriwa alikwishafika na hivyo ni mipango ya mauaji ndiyo yaliyotakiwa kufanyika.
“Hakuna taarifa zilizosambaa kwamba tunakuja?” aliuliza Dracula, alikuwa akimuuliza dada wa mapokezi.
“Hakuna!”
“Sawa. Chukua kwanza hii,” alisema Dracula huku akimpa bahasha iliyokuwa na dola elfu ishirini.
Wakapewa kadi iliyokuwa na uwezo wa kufungua kila mlango ndani ya hoteli hiyo, kitu kingine walichokifanya ni kuwasiliana na watu wa IT ambao walikuwa wakisimamia kamera zote zilizokuwa humo hotelini, kuhitaji ulinzi wa hali na mali ili wasiweze kukamatwa, kwani walitaka kuingia ndani wakati msichana Maria alipokwenda bafuni kuoga.
Walichokifanya ni kuondoka na kwenda katika korido iliyokuwa na chumba hicho, walipoifikia, kwa kuwa kwenye mlango kwa chini kulikuwa na nafasi fulani hivyo wakachukua kamera ndogo waliyokuja nayo na kuipitisha kwa chini ambayo iliunganishwa na kichuma kirefu, kamera ile ambayo kama zilizokuwa zikitumiwa na FBI, zikaanza kuonyesha kilichokuwa kikiendelea ndani, tena huku wao wakifuatilia kila kitu kwa nje.
“Wamelala....” alisema jamaa mmoja.
“Usingizi?”
“Hapana! Wamekumbatiana,” alijibu jamaa huyo, baada ya dakika kadhaa, wakamuona msichana Maria akiamka, akachukua taulo lake, akampiga Paul kibao cha kimahaba na kuelekea bafuni kuoga.
“Amekwenda kuoga.”
“Nani?”
“Msichana...”
“Basi tuingieni,” alisema Dracula huku kila kitu alichokuwa ameambiwa awe nacho akiwa nacho. Hakukuwa na muda wa kupoteza, hicho ndicho walichokuwa wakikitaka, kwa haraka sana, wakaingia ndani kwa kutumia kadi ile waliyopewa na mhudumu kama funguo ya kuingia katika chumba chochote kile.
****
Hawakutaka kupoteza muda hapo mlangoni, walishakubaliana kuingia ndani hivyo wakaingia. Paul aliyekuwa kitandani, akakurupuka lakini Dracula akamuwahi palepale kitandani na kumbana vilivyo, akauziba mdomo wake, kijana mwingine akasogea na kumshikilia miguu ili asilete purukushani kitandani pale.
Walipoona wameweza kumzuia, mwingine akaufuata mlango wa bafuni na kuufunga kwa nje ili Maria asiweze kutoka ndani ya bafu lile. Huku kitandani, Dracula akachukua mto na kisha kuufunika uso wa Paul ili amuue kwa kumziba pua na mdomo, akose hewa na kufa, ndivyo ilivyotokea.
Paul alikukuruka na kukuruka lakini ilishindikana kabisa, hakuweza kujinasua kutoka katika mikono ya wanaume hao waliokuwa wamemkandamiza vilivyo kitandani pale, zoezi hilo lilifanyika kwa dakika tano mpaka walipohakikisha amekufa hapo kitandani ndipo Dracula alipotoa mto ule na kumwangalia Paul.
“He is gone,” (Amekufa) alisema Dracula huku uso wake ukianza kutoa tabasamu pana.
Kama kawaida yao, Dracula akachukua bomba la sindano lililokuwa kwenye mfuko aliokuwa nao, akalitoa, akachomeka sindano, akavuta madawa ya kulevya yaliyokuwa katika majimaji na kisha kumchoma Paul huku akimshikiza kwa mkono wake mwingine, alipohakikisha imekuwa poa, akachukua kiplastiki kilichokuwa na alama za vidole vya Benjamin na kisha kumuwekea katika shingo ya mwili wa Paul na katika sehemu zingine za mwili, kabla ya kuondoka, pia wakaweza zile noti ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya utambulisho wa mauaji yale.
Hawakutaka kupoteza muda, waliingia harakaharaka na kufanya kazi yao haraka sana, walipomaliza, wakaondoka zao huku wakiwa wamekamilisha kazi hiyo kwa mafanikio makubwa.
“How was the work?” (Kazi ilikwendaje?) aliuliza Bwana Seppy kwenye simu.
“Simple as usual,” (Nyepesi kama kawaida) alijibu Dracula.
Ndani ya bafu lile, wakati mlango ukifungwa, Maria hakuwa akijua kitu chochote kile, hakujua kama kulikuwa na watu walikuwa wameingia na kumuua mpenzi wake.
Aliendelea kuoga huku akiimba, alipomaliza, akachukua taulo lake akajifuta na kisha kuufuata mlango. Akakishika kitasa ili aufungue, mlango haukuwa ukifunguka, ulionyesha kwamba ulifungwa kwa nje.
Akaanza kuugonga huku akiliita jina la Paul, mara ya kwanza alifikiri ni utani na hata uitaji wake ulikuwa ni wa kiutani sana lakini mlango haukufunguliwa na wala hakusikia sauti yoyote ile kutoka ndani ya chumba hicho.
“Paul, just open the door,” (Paul, fungua mlango) alisema Maria huku akiugonga mlango ule lakini hali iliendelea kuwa kimya.
Aliendelea kusubiri kwa dakika thelathini, alipoona Paul hafungui mlango ndipo alipoanza kuugonga kwa nguvu huku akikitekenya kitasa kile. Ilikuwa kazi kubwa lakini hakuacha kwani pasipo kufanya hivyo, basi angeendelea kuwa ndani ya chumba kile tu.
Alichukua dakika zaidi ya thelathini nyingine, kukipiga kitasa kile mpaka kilipovunjika ndipo akafanikiwa kutoka ndani ya bafu lile. Alichokutana nacho kitandani, hakuamini, mwili wa mpenzi wake, Paul ulikuwa tuli kitandani.
Maria hakuweza kuvumilia, akaanza kupiga kelele, wala hazikupita dakika nyingi, mlango ukafunguliwa, watu wa kwanza kuufungua mlango hawakuwa wahudumu bali walikuwa wageni kutoka katika vyumba vingine ndani ya hoteli hiyo.
Wao wenyewe wakapigwa na butwaa, walichokutana nacho, hawakuamini hata mara moja, mwili wa Paul ulikuwa kitandani, alivyoonekana, ni kama mtu aliyejiovadozi madawa ya kulevya kwani sindano ilikuwa mwilini mwake, katika mkono wake wa kushoto, udenda ulikuwa ukimtoka.
Hakukuwa na mtu aliyeugusa mwili ule, wakapiga simu mapokezini ambapo wahudumu wakafika haraka sana. Wao wenyewe hawakuamini kile walichokiona, wakaona jambo la busara kumuita meneja wa hoteli ile ambaye haraka sana akafika.
“Mungu wangu!” alisema meneja huku akionekana kutokuamini, hivyo kupiga simu polisi.
Japokuwa hoteli hiyo ilikuwa na wahudumu wengi, lakini kulikuwa na mhudumu mmoja ambaye alihusika, yeye ndiye aliyewapa kadi ya kufungulia mlango na hata kuwaelekeza chumba alichochukua Paul na Maria.
Muda wote wakati watu wapo hapo chumbani, Maria alikuwa akilia tu, hakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makubwa.
Hakutoa maelezo yoyote yale kwani aliamini chochote kile ambacho angekisema mahali hapo, kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angemuelewa.
Baada ya dakika kumi, polisi wakafika hotelini hapo, moja kwa moja wakapandisha ngazi na kuanza kuelekea kule kilipokuwa chumba kile, kwa kuwa kilikuwa ghorofa ya tatu, hawakuchukua muda mrefu, wkaafika.
“Nani alikuwa humu chumbani tofauti na marehemu?” aliuliza polisi mmoja.
“Mimi hapa!” alijibu Maria huku akijifuta machozi.
“Hakuwepo mwingine?”
“Hakuwepo.”
“Nini kilitokea?”
“Hata mimi sijui, nilikuwa naoga, nilipotoka, nikakuta hiki kilichotokea,” alisema Maria.
Walichokifanya ni kumfunga pingu kwani yeye ndiye alikuwa mshukiwa namba moja wa mauaji yale. Wakamchukua na kuondoka naye kwenda kituoni huku polisi wengine wakiangalia kitu cha kufanya.
Waandishi wa habarai tayari walikuwa wamefika, hawakuamini kile kilichokuwa kimetokea, mtu aliyekuwa amekufa chumbani humo, walimfahamu, alikuwa staa mkubwa wa kikapu, alipendwa na wasichana wengi kutokana na uzuri wa sura yake.
Hakuwa mtu wa kashfa, aliishi na watu vizuri, alipendwa kutokana na upole wake pia. Siku hiyo, hakukuwa na aliyeamini kama kweli Paul alikuwa amekufa, majonzi yasiyokwisha yakaikumba mioyo yao na hivyo watu haohao waliokuwa ndani ya chumba hicho, wakaanza kusambaza taarifa hizo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Njia nzima Maria alikuwa akilia, polisi hawakutaka kusikia lolote lile, kilichowaambia ni kwamba msichana Maria alikuwa akijua kilichotokea hivyo walitaka kushirikiana naye ili kujua nini kilitokea.
Mauaji yale, yalikuwa yaleyale ambayo yalitokea kwa masupastaa waliopita. Walikufa vilevile, wengi walihisi kwamba walijidunga madawa ya kulevya lakini baada ya miili yao kuchunguzwa, wakagundua kwamba kulikuwa na mtu aliyeitwa Benjamin ambaye ndiye alikuwa amehusika katika mauaji yale.
Hawakujua kuhusu Paul lakini bado mioyo yao iliwaambia kwamba inawezekana muuaji alikuwa huyohuyo ambaye mpaka kipindi hicho hakuwa amepatikana japokuwa alitafutwa sehemu yote nchini Marekani.
Kuna watu wengine walihisi kwamba Benjamin aliondoka na kukimbilia Mexico, nchi iliyokuwa na wauzaji wengi wa madawa ya kulevya. Hakukuwa na dalili za kupatikana kwake, kila watu walipokwenda huku na kule, hawakupata kitu.
Taarifa juu ya kifo cha Paul zikaanza kutangazwa kila sehemu, watu waliambiana kwenye mitandao ya kijamii, kila mtu aliyezipata, hakuamini kama kweli aliyekuwa ameuawa alikuwa Paul, yule mcheza kikapu mwenye jina, sura nzuri aliyekuwa akifagiliwa na wasichana wengi.
“Hebu tuambie nini kilitokea,” alisema ofisa wa FBI ambaye alikuwa katika chumba cha mahojiano na msichana Maria ambaye muda wote alikuwa akilia tu. Pembeni mwa ofisa huyo, alikuwepo mwingine ambaye naye alivalia suti kama aliyokuwa nayo.
“Sikumuua Paul,” alisema msichana Maria huku akiyafuta machozi yake.
“Nini kilitokea?”
Hapo ndipo Maria alipoanza kusimulia kile kilichotokea, hakutaka kuficha kitu, alikamatwa na kitu pekee ambacho kingemuweka huru kwa wakati huo ni kuzungumza ukweli juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
“Kwa hiyo muuaji haumfahamu?” aliuliza ofisa mmoja.
“Hapana! Simfahamu kabisa.”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
Polisi hawakutaka kumuachia Maria, ilikuwa ni lazima kumshikilia kwani mshukiwa namba moja wa mauaji yale alikuwa yeye, akawekwa sero, huko, alikuwa akilia sana, alijuta hatua aliyochukua ya kuwa na Paul na kwenda naye katika hoteli ile.
Hapo ndipo lilipokuja jina la Benjamin. Aliwahi kusikia mastaa wengi wakiwa wameuawa na mtu aliyeitwa Benjamin, hakumfahamu mtu huyo na hakujua sababu iliyomfanya kuwaua mastaa. Alimchukia Benjamin ambaye kwa kipindi hicho, alikuwa adui wa nchi nzima, yaani Enemy of the State.
****
Walipanga kwamba siku inayofuata ilikuwa ni lazima kwenda kituyo cha polisi na kuwaeleza polisi juu ya kile kilichokuwa kikiendelea. Benjamin hakuwa muuaji, hilo ndilo ambalo lingeweza kuzungumzwa kwani pasipo kufanya hivyo, Benjamin alikuwa katika wakati mgumu.
Tayari Benjamin na Harry waliwasiliana na David na kumwambia juu ya kile kilichotakiwa kufanywa, yaani piga ua ilikuwa ni lazima wakutane katika kituo cha polisi kwani yeye ndiye alikuwa na mawasiliano ya Bwana Seppy, Dracula na watu wengine katika upangaji wa mipango yao ya mauaji.
Wakakubaliana lakini ilipofika saa nne usiku wakapata taarifa zilizowashtua kwamba supastaa wa mchezo wa kikapu, Paul McKenzie alikuwa ameuawa ndani ya chumba cha hoteli, mauaji yake yalikuwa yaleyale, yaani kama Todd, Carter.
Walichanganyikiwa, hata kama majibu ya vipimo vya mwili ule havikutolewa, walijua fika kwamba taarifa zingesema kwamba Benjamin ndiye aliyeua, yaani kama ilivyokuwa katika mauaji mengine.
Hilo ndilo lililowafanya hata ule mpango wao wa kwenda kituo cha polisi kuusitisha, ilitakiwa wajipange upya wajue ni kitu gani wangetakiwa kufanya kwani pasipo kufanya hivyo, mambo yangekuwa mabaya zaidi.
“Tufanye nini?” aliuliza Harry.
“Dah! Hapa nimechanganyikiwa. Hebu subiri kwanza, naomba dakika kama tano hivi peke yangu,” alisema Benjamin huku akionekana kuwa na mawazo mengi.
Harry akamuacha, Benjamin akasimama na kwenda chumbani, alihitaji muda wa kuwa peke yake kwani kulikuwa na mengi ya kujifikiria, hakutaka kukurupuka katika kufikiria ni kitu gani alitakiwa kufanya.
“Nini cha kufanya?” alijiuliza huku akitembea huku na kule.
Alikuwa akiishi kwa hofu, hakuwa na amani, alijua kwamba kila kitu kilichokuwa kikitokea, Bwana Seppy alijua kwamba ilikuwa siri, kwa sababu yeye mwenyewe hakuwa na furaha, ilikuwa ni lazima hata Bwana Seppy naye akae akiwa na hofu kama alivyokuwa yeye.
“Umefikiria nini?” aliuliza Harry baada ya kukaa kwa dakika kumi nzima.
“Sioni sababu ya Bwana Seppy kuwa na furaha na wakati mimi nina hofu, kwa nini naye asiishi na hofu moyoni mwake?” aliuliza Benjamin.
“Unamaanisha nini?”
“Nataka niwasiliane naye!”
“Ben! Umechanganyikiwa?”
“Hapana! Hii ni njia ya kwanza, lazima akae kwa presha, ajue kwamba ninajua kila kitu, yaani hapo ndipo tutafanikiwa, kwanza tutakusanya ushahidi wa kutosha kwani atafanya maamuzi ya ghaflaghafla kitu ambacho kinaweza kuwa ushindi mkubwa,” alisema Benjamin.
“Umefikiria nini mpaka kusema hivyo?”
“Wala usijali! Nipe muda, nataka kwenda kumpigia simu, nitatumia simu ya barabarani,” alisema Benjamin.
Jambo alilozungumza halikumuingia akilini kabisa, hakujua alimaanisha nini, hakuona kama kulikuwa na sababu ya kufanya kile alichotaka kukifanya ila kwa sababu yeye mwenye mhusika ndiye aliamua kufanya hivyo, hakuwa na jinsi.
Alichokifanya Benjamin ni kuchukua namba ya simu ya Bwana Seppy na kisha kuondoka nayo kwenda mtaani. Kwa sababu ilikuwa usiku wa saa tano hakukuwa na mtu yeyote aliyemtambua kwani mbali na mwanga hafifu pia alivalia kofia kubwa aina ya pama.
Hakutaka kutumia simu ya mtaani hapo, alijua kwamba mara watakapogundua simu ambayo ilitumika ilikuwa ni lazima kumtafuta kuanzia hapo. Alichokifanya ni kupanda basi na kwenda katika mji mwingine ambao ulikuwa mbali na hapo, kama kilimeta thelathini kutoka hapo.
Huko ndipo alipotafuta kibanda cha simu za mitaani, alikipata katika kituo cha mafuta cha Total, akakifuata na kuanza kupiga namba ya Bwana Seppy. Wala simu haikuita muda mrefu, ikapokelewa.
“Bwana Seppy hapa, nani mwenzangu?”
“Benjamin Saunders...” alijitambulisha Benjamin, Bwana Seppy aliyekuwa upande wa pili, akashtuka.
****
Bwana Seppy akahisi kama mtu akija kumkaba kooni mwake, alichanganyikiwa sana kusikia sauti ya Benjamin, mwanaume aliyekuwa akimsumbua katika kipindi chote hicho, mtu ambaye alitaka afe haraka iwezekanavyo.
Mwanaume huyo alizungumza kwa kujiamini, hakuonekana kuwa na wasiwasi wowote ule mpaka wakati mwingine Bwana Seppy kuhisi kwamba Benjamin alikuwa na ulinzi wa kutosha huko alipokuwa.
“Ni lazima ufungwe maisha yako yote, ni lazima unyongwe kwa mauaji unayoendelea kuyafanya,” alisema Benjamin kwa sauti ya juu iliyosikika vizuri masikioni mwa Bwana Seppy.
“Hahaha!” akabaki akicheka.
“Cheka, ni vizuri kucheka kwa sababu siku ya hukumu yako inakaribia,” alisema Benjamin.
“Nani atajua? Wewe ndiye muuaji, vipimo vya madaktari na polisi vimeonyesha alama za vidole vyako, unahisi nani atakuamini?” aliuliza Bwana Seppy kwa dharau.
“Uwepo wa fedha katika kila tukio!”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hilo linaweza kuwa ushahidi tosha?”
“Ndiyo!”
“Zina maana gani?”
Benjamin hakutaka kuchelewa, hapo ndipo alipomwambia mzee huyo maana ya fedha zile zilizokuwa zikiwekwa katika kila eneo la tukio la mauaji lilipofanyika.
Bwana Seppy akachanganyikiwa, hakuamini kama kungekuwa na mtu ambaye angegundua kile kilichokuwa kimetokea kwamba Benjamin agundue maana ya uwekaji wa fedha zile.
Hilo lilikuwa jambo la kwanza ambalo hakutaka mtu yeyote afahamu, si mke wake, hata Dracula mwenyewe ambaye alikuwa akimtumia katika mauaji hakumwambia maana ya kuweka fedha zile katika kila tukio la mauaji aliyokuwa akiyafanya.
Hakutaka kuzungumza kitu, alichokifanya ni kukata simu na hapohapo kumpigia simu Dracula, kitu cha kwanza kabisa kumuuliza ni mahali gani walipofikia tangu waanze kumtafuta Benjamin ambaye bado aliendelea kutafutwa kila kona.
“Ndiyo tunaendelea, kuna nini kwani?” aliuliza Dracula.
“Amenipigia simu!”
“Amekupigia simu?”
“Ndiyo! Hebu niambie ukweli! Hivi atapatikana kweli?” aliuliza Bwana Seppy, kwa kumsikiliza tu, alinekana kuchanganyikiwa, hakuwa sawa kama siku nyingine.
“Atapatikana tu! Tuvute subira.”
****
Baada ya kuzungumza na Bwana Seppy na simu kukatwa, Benjamin akatulia huku akimwangalia Harry, alikuwa akitabasamu tu, mbele yake aliyaona mafanikio makubwa, alikuwa akifanikiwa kwa kila kitu alichokuwa akikifanya.
Walichokifanya, usiku huohuo ulikuwa ni wa kutoka na kwenda katika kituo cha polisi, huko, wangezungumza ukweli juu ya kile kilichotokea kwani tayari ushahidi walikuwa nao.
Wakatoka na kuanza safari ya kwenda huko. Japokuwa walikubaliana kwenda huko saubuhi lakini wakaiona mbali, ilikuwa ni lazima ifanyike siku hiyohiyo.
Walitembea mitaani, Benjamin hakutaka kuuficha uso wake kwani hata kama angekamatwa, bado alikuwa akienda kituo cha polisi. Walipishana na watu wengi, cha ajabu kabisa watu hawakumgundua kutoka na mwanga hafifu hasa katika kipindi hicho cha usiku.
“Tukifika, ni kutoa maelezo, hata kama nitapelekwa mahakamani, nitaeleza ukweli,” alisema Benjamin huku wakiendelea kwenda huko.
Walitembea kwa mwendo wa haraka, wakati wakikaribia kufika, simu ya Harry ikatoa mlio kwamba kulikuwa na ujumbe ulikuwa umeingia, harakaharaka akaichukua simu yake na kuangalia nini kilikuwa kimeingia, ilikuwa ni habari iliyoingizwa kutoka katika programu ya Shirika la Habari la CNN ambayo ilieleza kwamba kulikuwa na mauaji yalikuwa yametokea katika Hoteli ya Scandnavia Hill.
“Hebu subiri...” alisema Harry.
“Kuna nini?” aliuliza Benjamin.
“Paul McKenzie ameuawa,” alisema Harry, Benjamin akashtuka.
“Unasemaje?”
Hawakutaka kuendelea na safari, walichokifanya ni kwenda pembeni na kuanza kuisoma habari hiyo. Kwa jinsi mauaji yalivyotokea, walijua fika kwamba mzee huyo ndiye aliyehusika kwani mauaji yale yalifanana sana na yale mengine yaliyowahi kutokea.
Walibaki wakiangaliana tu, hawakujua ni kitu gani walitakiwa kufanya kwani kwa jinsi hali ilivyoonyesha, basi polisi wangeanza kumtafuta tena kwa nguvu kubwa.
Hawakuwa na sababu ya kuendelea mbele, safari yao iliishia hapo na hivyo kurudi nyumbani. Vichwani mwao walikuwa na mawazo tele, walijua fika kwamba mara baada ya mwili ule kupimwa, ilikuwa ni lazima alama za vidole vya Benjamin vionekane kwa sababu ndivyo Bwana Seppy alivyokuwa akifanya kwenye kila staa aliyekuwa akiuawa.
“Kwa hiyo tufanye nini?” aliuliza Hans.
“Subiri, nafikiri mpaka asubuhi nitakuwa na majibu, wala usijali,” alijibu Benjamin.
****
Msako mkubwa wa Benjamin ulikuwa ukiendelea, kamera ziliongezeka mitaani kwa ajili yake, ilikuwa ni lazima apatikane kwani kitu alichokuwa amekifanya, hakikuweza kuvumilika, ilikuwa ni lazima akamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuhukumiwa kwa yale yote aliyokuwa ameyafanya.
Maofisa wa FBI walikuwa wakihangaika, walitoa uangalizi kwa watu waliohusika na kamera mpya za barabarani ambazo walikuwa wamezifunga ili kuhakikisha Benjamin anakamatwa na mambo mengine kuendelea. Watu waliowekwa kwa ajili ya kuziendesha kamera zile, kila siku hawakuona kitu, waliendelea kufuatilia kwa wiki nzima lakini hakukuwa na mtu aliyeitwa Benjamini, yaani hata dalili zake kuwepo sehemu fulani, hazikuwepo.
“Na jana uliangalia?” aliuliza Bwana Swan, kiongozi aliyepewa kusimamia kamera hizo mpya ambazo zilifungwa sehemu nyingi nchini Marekani na taarifa kupelekwa moja kwa moja makao makuu.
“Ndiyo!”
“Na hamjamuona?”
“Ndiyo! Ila bado tunaendelea...”
Hivyo ndivyo alivyoambiwa. Wakati mwingine aliona kama hakukuwa na umuhimu wa kuwa na watu hao kwani alijitahidi kuwapa maneno mengi ya kuwafanya waone kwamba kulikuwa na umuhimu wa kumkamata mtu huyo lakini hiyo wala haikusaidia kabisa.
Ilimuumiza, hakupenda kuwasimamia watu ndiyo kazi ifanyike, kwa kumwangalia, alionekana kuwa mwanaume mpole, na hivyo ndivyo alivyokuwa ila alipotaka kitu fulani kifanyike, alikuwa kwenye presha kubwa sana.
“Hebu angalieni kamera vizuri, haiwezekani sehemu nzima asionekane,” alisema Bwana Swan.
“Sawa mkuu!”
Hakukuwa na kitu kilichobadilika, yaliendelea kuwa yaleyale kwamba Benjamin hakuonekana. Hawakujua alikuwa watu, ilikuwa vigumu sana mtu kutafutwa na nchi nzima, FBI halafu asionekane, hilo lilikuwa jambo gumu sana.
Wakati mwingine walihisi kama Benjamin alikimbia nchi, akaenda kujiunga na kundi la Kiislamu la ISIS, wakati mwingine waliisi kwamba Benjamin alikwenda kujiunga na Kundi la Born To Kill la nchini Cuba, yaani kumkosa Benjamin nchi nzima lilikuwa jambo lisilowezekana kabisa.
“Bosi...njoo uone hii,” alisema kijana mmoja, alikuwa mbele ya kompyuta yake, tangu asubuhi hakuwa ameondoka ofisini, yeye ndiye aliyepambana kwa nguvu zote kumtafuta Benjamin kila kona.
Alianzia jijini New York, akaenda Washington, akaenda Los Angeles na sehemu nyingine kwa kutumia kamera zilizowekwa lakini kote huko hakuambulia kitu.
Dakika za mwisho kabisa, alimuona mtu kama Benjamin, alipouona uso wake, akatafuta picha ya Benjamin na kuambatanisha na picha ile aliyoiona kwenye kamera, maneno yaliyotokea ni 100 MATCH, yaani imefanana kwa asilimia mia moja, hapo akajiona kuwa mshindi, ilikuwa ni lazima kumpa taarifa Bwana Swan.
“Yupo wapi?”
“Nawaona vijana wawili wakiwa wamesimama, mmoja yupo ndani ya kibanda cha simu na mwingine yupo nje, Benjamin ni huyu aliyekuwa ndani, aliyekuwa nje simfahamu,” alisema kijana huyo aliyejiita Genius.
Alichokisema Bwana Swan ni kuunganishwa kwa kompyuta ile katika televisheni kubwa iliyokuwa ndani ya chumba hicho huku akimtaka kila ofisa wa FBI aliyekuwa humo ndani aangalie kile kilichokuwa kikiendelea.
Sehemu iliyoandikwa Location ikiwa na maana ya eneo ilionyesha kwamba ilikuwa ni Macberth 25W, sehemu ambayo ilikusanya watu wenye maisha ya kati katika Jiji la Boston, huko ndipo ambapo huyo Benjamin alipokuwa.
Kumuona tu hawakuridhika, waliamini kwamba wangeweza kutorokwa kwani huyo Benjamin hakuwa mtu wa kawaida hata kidogo. Walichokitaka ni kumfahamu mtu ambaye alikuwa naye, alikuwa nani na alikuwa akiishi wapi.
Hiyo wala haikuwa kazi kubwa, alichokifanya Genius ni kuivuta sura ya Harry, akaruhusu sura kadhaa zianze kupita katika kompyuta yake huku ikiitafuta sura ya mwanaume huyo aliyekuwa pamoja na Benjamin.
Ilikuwa kazi kubwa, kila mtu aliyekuwa ndani ya jengo hilo alikuwa kimya, Bwana Swan alibaki akiwa amesimama, mkono wake mmoja ulikuwa mfuko na mwingine aliupeleka katika shavu lake, alikuwa akifuatilia kwa ukaribu sana.
Zaidi ya sura milioni mbili zilipita kwa kasi kubwa mno, ndani ya dakika ishirini, kompyuta ikasimama katika sura moja na kujiandika 100 MATCH kwamba sura ya mtu huyo ilifanana na huyu aliyekuwa ametafutwa.
“Ni nani huyo?” aliuliza Bwana Swan, jamaa mwingine akachukua kalamu na karatasi.
“Anaitwa Harry Hoff, kijana mwenye asili ya Ujerumani, anaishi jijini Boston, nyuma namba 278 katika Mtaa wa Vivien View Barabara ya St. Peters, anasoma katika Chuo cha Kikuu cha Harvard,” alisema Genius, maelezo ya wananchi wote wa Marekani, data zao zilikuwa zimechukuliwa kutokana na vitambulisho wa taifa walivyokuwa wamepewa.
“Safi sana...ninahitaji maofisa kumi waende huko anapoishi Harry. Hakuna kuua, mnachotakiwa ni kuwapata wote wakiwa hai,” alisema Bwana Swan na maofisa wote kuitikia na hivyo kuanza kwenda huko.
****
Vivian hakuwa na raha, moyo wake ulikuwa na majonzi tele, hakuamini kile kilichotokea kwamba mpenzi wake alikuwa akitafutwa kila kona huku sababu kubwa ikiwa ni kufanya mauaji.
Alijua kwamba hakuwa muuaji bali kulikuwa na mtu ambaye alifanya mauaji, hakumfahamu na hivyo ndivyo alivyowaeleza maofisa wa FBI lakini hakukuwa na mtu aliyemuelewa.
Aliruhusiwa kwenda nyumbani, hakukukarika, kila alipokaa, alimkumbuka mpenzi wake tu. Maofisa wa FBI hawakutaka kumuacha, walihakikisha wanamfuatilia kila hatua.
Nje ya nyumba hiyo kulikuwa na gari lao, ndani ya gari hilo kulikuwa na kompyuta nyingi pamoja na kamera zilizokuwa na uwezo wa kupiga picha na kuona kile kilichokuwa kikiendelea ndani.
Mbali na hivyo, waliendelea kufuatilia mpaka mawasiliano ya simu zake, kuanzia ile ya mezani mpaka ya mkononi kwani waliamini kwamba msichana huyo alikuwa na nafasi ya kuwasiliana na mpenzi wake ambaye alikuwa akitafutwa kwa udi na uvumba kipindi hicho.
“Nini kinaendelea?” aliuliza Bwana Swan ambaye aliwagawa vijana wake sehemu mbalimbali.
“Bado tunaendelea kufuatilia, tunamuwekea ulinzi wa kutosha huyu msichana wake,” alijibu ofisa mmoja.
“Simu zake?”
“Tumeziwekea ulinzi pia.”
“Sawa.”
****
Maofisa wa FBI wakaelekea nyumbani kwa Harry, walikwenda na gari lao, ilikuwa asubuhi sana muda ambao waliamini kwamba hata watu hao hawakuwa wameamka, walitaka kuwavamia na kisha kumchukua mtu wao ambaye aliwatesa sana huku usiku uliopita tu akiwa amefanya mauaji katika hoteli moja huko Los Angeles.
Walifika katika nyumba hiyo huku wakiwa na bunduki zao mikononi mwao, waliamini kwamba wangeweza kumpata kwani kwa jinsi walivyoona siku iliyopita, wawili hao wangeendelea kuwa ndani ya hiyo nyumba na ilionyesha kwamba kwa kipindi kirefu Benjamin alikuwa mahali hapo ila tu hawakuwa wakijua hilo.
Walipofika nje ya nyumba hiyo, kitu cha kwanza kabisa walichokifanya ni kuizunguka nyumba hiyo na ndipo mmoja wao akaanza kuugonga mlango na kutaka kufunguliwa.
Nyumba ilikuwa kimya, japokuwa alipiga kelele na kusema “FBI, FBI” lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyefungua mlango. Hawakutaka kuendelea kubaki hapo ndani, walikuwa na hofu kwamba inawezekana Benjamin angekimbia hivyo walichokifanya ni kuingia ndani ya nyumba hiyo kwa kuuvunja mlango.
Bunduki zilikuwa mikononi mwao, walioingia hawakuwa wao peke yao bali kulikuwa na askari wa SWAT ambao kazi yao ilikuwa ni kuvamia sehemu zilizokuwa na hatari, yaani kule ambapo kulikuwa na watu waliokuwa na silaha nzito, walitumika hao kwa ajili ya kuwalegeza kwanza.
Ndani, hakukuwa na mtu, walijaribu kuingia humu na kule, walitembea huku na kule lakini hawakukuta mtu yeyote. Mwisho kabisa wakaamua kukifuata chumba kimoja, kilikuwa chumba cha Harry, walipokifikia, wakaingia ndani, hawakumuona Benjamin, mtu pekee waliyemuona humo alikuwa Harry.
“You are under arrest....” (Upo chini ya ulinzi...) alisema ofisa mmoja huku wote kwa pamoja wakimnyooshea bunduki Harry ambaye aliamka na kuanza kuwaangalia.
“What the hell is going on?” (Nini kinaendelea?) aliuliza huku akiwaangalia.
Hawakutaka kumjibu swali lake, walichokifanya ni kumshika na kumlaza chini kisha kumfunga pingu huku wakimtaka kuwaambia mahali alipokuwa Benjamin.
“Benjamin, I don’t know where he is,” (Benjamin, sijui yupo wapi) alisema Harry huku uso wake ukionyesha tabasamu pana.
“Tell us where he is,” (Tuambie yupo wapi)
“I dont know men, he left last night,” (Sijui jamani, aliondoka usiku uliopita) alijibu Benjamin, kwa kumwangalia tu, alionyesha dhahiri kwamba aliwadanganya.
****
Benjamin alikuwa kama mtu mwenye machale, usiku wa siku hiyo hakulala, alibaki macho huku akiwa na wasiwasi mno, alijua kama kulikuwa na kitu ambacho kingetokea hivyo asingeweza kulala kabisa.
Alikesha, mpaka mwanga unaanza kuchomoza asubuhi, alikuwa macho, akatoka kitandani na kwenda jikoni ambapo akaandaa kahawa na kisha kuelekea sebuleni kuangalia televisheni.
Kipindi hicho televisheni ndiyo ilikuwa faraja yake, hakuwa na cha kufanya, hakuwa na uhuru wa kufanya kitu chochote kile, alipokuwa kwenye televisheni, ndiyo ulikuwa muda wa kujua kitu gani kilikuwa kikiendelea katika ulimwengu aliokuwa akiuogopa.
Mara kwa mara alijiona kwenye televisheni, alikuwa mtu maarufu kwa sababu ya matukio yaliyokuwa yametokea. Watu wengi walihojiwa, kilio chao kilikuwa ni kumuona Benjamin akikamatwa na kufikishwa mahakamani na kisha kushtakiwa kwa makosa ambayo dunia nzima ilijua kwamba aliyafanya.
“Ila kwa nini huyu mzee anafanya hivi?” alijiuliza pasipo kupata jibu.
Akasimama, akaanza kutembea ndani ya sebule ile huku akiwa na mawazo lukuki, aliongea peke yake kama kichaa, akatoka pale alipokuwa mpaka katika dirisha kubwa, akafungua pazia na kuanza kuangalia nje.
Alitamani kuwa huru, aliwaona watu wakitembea barabarani huku wakiwa wamejiachia, alitamani na yeye kuwa vile lakini ilishindikana kabisa, hakuweza kuwa huru kama watu wale walivyokuwa huru kipindi kile.
Wakati akiwa amesimama katika dirisha lile ndipo alipoliona gari moja likija na kusimama karibu na eneo la nyumba ile barabarani. Kwanza akaanza kuwa na wasiwasi, hakutaka kujipa uhakika kwamba watu waliokuwa ndani ya gari hilo walikuwa watu wazuri, akagundua kwamba kulikuwa na kitu.
Hakutaka kuwa na wasiwasi mwingi, akasubiri kuona ni watu gani wangeteremka kutoka ndani ya gari lile. Wakati akiwa amelikodolea macho, likatokea gari jingine ambalo kwa ubavuni liliandikwa S.W.A.T.
Harakaharaka wanajeshi waliokuwa na mavazi yaliyoandikwa S.W.A.T wakatoka ndani ya gari lile, walikuwa na bunduki kubwa hasa AK 47 ambazo ndizo zilikuwa maalumu kwa kazi yao.
Mavazi yao, yalikuwa yale mazito ambapo tumboni mpaka kifuani walikuwa na vazi jingine lililokuwa na uwezo wa kuzuia risasi. Benjamin alipowaona watu hao, hakutaka kusubiri, alijua fika kwamba walikuwa mahali hapo kwa ajili yake.
Hakutaka kujiuliza, wanajeshi wale na FBI tayari walianza kuelekea kule ilipokuwa nyumba ile, aliamini kwamba kama angekwenda jikoni na kutoka nje kupitia mlango wa nyuma, angechelewa na hivyo kukamatwa, wazo pekee lililomjia kichwani ilikuwa ni lazima aingie ndani ya ‘chimney’.
Sebuleni hapo kulikuwa na sehemu maalumu ambayo nyumba nyingi za Marekani na Ulaya au hata sehemu zenye baridi kali huweka kama jiko kwa ajili ya kuchoma kuni na kuleta moto ambapo moshi wake ulipita katika bomba kubwa lililokwenda juu ya bati na kupotelea huko.
Yeye alitaka kuingia katika bomba hilo, halikuwa kubwa sana lakini lilitosha kwa mwili wake kuenea kwani hakuwa mnene ila alikuwa mrefu. Hakutaka kuchelewa, haraka sana akaelekea katika sehemu ile, kulikuwa na kuni, akazisogeza pembeni na kisha kuanza kujiingiza, hakuanza kukiingiza kichwa, alibinuka na kuanza kuiingiza miguu yake kwenda kwenye bomba lile kwa juu.
Ilikuwa kazi kubwa lakini haikumsumbua sana, hakuchukua sekunde nyingi, akafanikiwa kuingia ndani ya bomba lile na kutulia, masikio yake yalikuwa ni hapo sebuleni, tangu maofisa wa FBI walipoanza kuugonga mlango na kuuvunja, yeye alikuwa ndani ya bomba lile sebuleni pale huku akisikiliza kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Maofisa wa FBI walijua fika kwamba Harry alikuwa akijua mahali alipokuwa Benjamin ila hakutaka tu kuwaambia ukweli. Walichokifanya ni kumchukua na kumpeleka kituoni.
Huko wakamuingiza ndani ya chumba cha mahojiano na kuanza kuzungumza naye, walitaka aeleze ukweli mahali alipokuwa Benjamin, vinginevyo wangemfanya kitu kibaya.
“Nina haki ya kusikilizwa pia,” alisema Benjamin kwani tayari aliona maofisa wale walikuwa wamekasirika.
“Sawa. Benjamin yupo wapi?”
“Sijui! Kwani nyie wa nini?”
“Amefanya mauaji!”
“Hapana! Benjamin hakuwahi kuua,” alisema Harry.
“Usibishane na sisi, aliua na hata jana aliua pia,” alisema ofisa huyo.
“Jana kuna mauaji yalitokea huko Los Angeles, wote mnasema kwamba Benjamin ndiye aliyehusika, si ndiyo?” aliuliza Harry.
“Ndiyo!”
“Sawa! Kwenye maelezo yenu mlisema kwamba jana usiku mliniona nikiwa naye, ilikuwa saa tano usiku, si ndiyo?”
“Ndiyo!”
“Mauaji yalitokea saa nne na nusu, si ndiyo?”
“Ndiyo!”
“Sasa jamani! Huyo Benjamin awe ameua saa nne na nusu usiku, atatumia usafiri gani kutoka Los Angeles mpaka hapa Boston kwa mwendo wa nusu saa? Kwa ndege haiwezekani, alitumia usafiri gani sasa?” aliuliza Harry huku akiwaangalia maofisa wawili aliokuwa nao humo ndani.
“Labda niwaulize kitu kimoja. Nyie mnaamini Benjamin ni yupi? Yule aliyefanya mauaji huko Los Angeles au huyu aliyekuwa pamoja nami?” aliuliza Harry. Maofisa wakabaki wakiangaliana tu.
Alichokisema Harry kilikuwa ni ukweli mtupu. Kutoka Los Angeles mpaka hapo Boston ilikuwa ni mwendo wa saa moja na nusu kwa ndege, sasa ilikuwaje huyo Benjamin afanye mauaji Los Angeles halafu ndani ya nusu saa aonekane jijini Boston? Hilo likawapa wakati mgumu maofisa hao, hawakujua washike lipi, kama Benjamin alionekana hapo Boston majira ya saa tano usiku, je aliyefanya mauaji saa nne na nusu usiku huko Los Angeles alikuwa nani? Wakabaki na maswali kibao.
****
Dunia ilikuwa ikijiandaa kwa ajili ya kumuona msichana mrembo ambaye angeibuka kidedea katika Mashindano ya Miss Dunia ambayo kwa kipindi hicho yalitegemewa kufanyika jijini Texas nchini Marekani.
Watu walitaka kushuhudia ni msichana yupi angeibuka mshindi kwani wasichana wote ambao walitegemewa kushiriki walikuwa wale warembo, waliowavutia watu wengi nchini mwao.
Kila mtu anawa na uhakika kwamba msichana Angelica Sanchez kutoka nchini Mexico angechukua taji hilo lililokuwa likishikiria na mrembo kutoka nchini Venezuel, Maria alejandro.
Kwa kumwangalia, Angelica alikuwa msichana mrembo mno, alikwenda juu, hipsi zake zilionekana vilivyo, alikuwa na sura nzuri uliopendezeshwa na vishimo viwili vilivyokuwa mashavuni mwake. Muda wote, alikuwa kwenye tabasamu pana kana kwamba hakujua maana ya kukasirika.
Huyo ndiye alikuwa gumzo kipindi hicho. Tangu alipochukua taji la urembo nchini Mexico, kila mtu alitokea kumpenda, kampuni mbalimbali zinazojihusisha na mambo ya mitindo ikamtafuta, yeye alijiona mrembo, watu wengine wakamuona mrembo lakini makampuni hayo yaliona fedha.
Walijua kwamba kama wangemtumia msichana huyo katika matangazo yao mbalimbali, wangepata fedha nyingi, hivyo wakaingia naye mikataba mingi kwa kutegemea kuwa angeweza kuchukua taji hilo.
Mbali na Angelica, pia kulikuwa na msichana aliyeitwa Jenny Chu, msichana kutoka nchini China, alikuwa mrembo, alisoma na kuwa na PhD ya udaktari, hakuangalia elimu yake, alichokuwa akikiangalia kilikuwa ni masuala ya urembo tu, tangu zamani aliwaahidi wazazi wake kwamba kuna siku angekuwa mrembo wa dunia, na muda huo, aliona ndiyo kipindi chenyewe.
Kulikuwa na wasichana wengi, japokuwa wengi waliwafikiria wasichana hao warembo lakini wakasahau kwamba mbali na wasichana hao kulikuwa na msichana mmoja aliyekuwa mrembo mno, inawezekana kuliko wote hao, msichana huyo aliitwa Stacie Lawrence.
Kwa kumwangalia msichana huyo kutoka nchini Australia, alikuwa mrembo haswa, sura ya kitoto, lipsi pana kidogo, macho ya goroli, shingo ya upanga, aliumbika, alijua kutembea, yaani kwa kumwangalia harakaharaka, ingekufanya kudhani kwamba umekutana na mzimu wa mwanamke mrembo kuliko wote, Cleopatra.
Stacie hakuwa mzungumzaji, alikuwa kimya, alionekana kama kuwa na wasiwasi, hakuonekana kujiamini kabisa. Alikuwa msomi, alikuwa na PhD ya mambo ya uandishi, alitamani kusoma lakini pia alipenda sana mambo ya urembo na huo ukawa ndiyo muda wake wa kukamilisha kile alichokuwa akikiota kila siku.
Alimuogopa msichana Angelica kwa kuwa alitangazwa sana, hakuwa na uhakika kama angeweza kushinda kinyang’anyiro hicho, kila wakati alipokuwa akimuona Angelica, alitamani kumsogelea na kumsalimia kisha kumwambia kwamba alitamani sana kuwa kama yeye.
Hakujua watu walimfikiria vipi. Wasichana wengi waliokuwa katika kinyang’anyiro hicho walimpa ushindi, alionekana kustahili hata zaidi ya Angelica ambaye mara kwa mara alikuwa akipigiwa promo kutoka sehemu mbalimbali.
Wasichana wengine wakashindwa kujizuia, walimsogelea na kumwambiia wazi kwamba alikuwa mrembo, kila msichana alitamani kuwa kama yeye lakini kila alipoambiwa, aliwajibu kitu kimoja kwamba inawezekana hawakumuona Angelica.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unajua wewe mzuri sana,” aliambiwa na msichana Priscilia, mrembo kutoka nchini Italia.
“Nani? Mimi?”
“Ndiyo! U mrembo sana...”
“Hapana! Labda hujamuona Angelica...”
“Nimemuona lakini wewe, hakika unastahili kuwa mshindi katika shindano hili,” alisema msichana Priscilia.
Kwa kumwangalia, alionekana kutokutania, alimaanisha kile alichokuwa akikizungumza. Hiyo haikuwa kwa msichana huyo tu, alipoondoka walimfuata wasichana wengine na kumwambia jinsi alivyokuwa mrembo.
Alipoambiwa, alijisikia aibu, hakujiamini hata kidogo. Kwa Angelica, tayari alianza kuona wivu, jinsi wasichana wengine walivyokuwa wakimzungumzia Stacie, moyo wake uliuma kupita kawaida.
Walikaa kambini huku wakiendelea na mazoezi kama kawaida, saa zilizidi kukatika, siku zikaenda mbele mpaka siku ya tukio kufika. Kila mtu alitaka kuona msichana Angelica akichukua taji hilo na kuwa mrembo wa kwanza kushinda kutoka nchini Mexico.
Wakati Angelica akiendelea kuwa gumzo ndipo watu wakafanikiwa kumona msichana Stacie. Kwanza kila mmoja akashtuka, hawakuamini kile walichokiona, hawakuamini kama kulikuwa na msichana mwingine mrembo hata zaidi ya Angelica ambaye alikuwa gumzo.
Mioyo ya watu ikaanza kubadilika, ikatoka kwa msichana Angelica na kuhamia kwa Stacie, watu wakaanza kumtafuta katika mitandao mbalimbali, picha zake, urembo wake ukawadatisha sana, hakukuwa na aliyeamini kama dunia hiihii ingekuwa na msichana mrembo kama alivyokuwa Stacie.
Watu wakaanza kutumiana picha za msichana huyo katika mitandao ya kijamii, kila mtu aliyemuona Stacie katika picha zile, alitaka kumuona uso kwa uso kwani mioyo yao ilikataa kabisa kwamba katika dunia hiihii, kipindi hikihiki kungekuwa na msichana mrembo kama Stacie.
“Ni lazima nitakwenda kutazama kinyang’anyiro,” alisema jamaa mmoja, alikuwa ameshika simu yake akimwangalia Stacie.
“Si ulisema hauendi!”
“Nitakwenda, nimebadili mawazo,” alisema jamaa huyo.
Watu walitaka kuona ushindani mkubwa kutoka kwa wasichana wawili warembo, mmoja kutoka nchini Australia na mwingine kutoka nchini Mexico. Kila kona, wawili hao walawa gumzo, japokuwa kipindi cha nyuma Angelica alikuwa akizungumziwa sana lakini katika kipindi hicho upepo ukabadilika kabisa, hakuzungumziwa Angelica peke yake bali alizungumziwa Stacie, tena kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda mbele, aliendelea kusikika zaidi.
“Unahisi nani atachukua ushindi?”
“Mmh! Wala sijui manake nishanchanganyikiwa!”
Watu walisubiri mpaka pale kinyang’anyiro kilipoanza. Mwana huo, watu walifuatilia kinyang’anyiro hicho kuliko vipindi vingine vyote, kila kona, watu walikuwa wakifuatilia katika televisheni zao na kitu kilichokuwa kikiwavuta zaidi ni urembo wa wasichana hao wawili.
Vipengele vyote vikapita na mwisho wa siku mshindi kutarajiwa kutangazwa. Katika tatu bora alibaki Stacie, Angelica na mrembo mwingine kutoka Afrika Kusini, ThandiMbokani.
Ukumbi mzima ulibaki kimya, mtu aliyetakiwa kutangaza matokeo, akasimama, akachukua matokeo kutoka kwa majaji na kisha kusimama, hakuanza na mtu wa kwanza, alianza na mtu wa tatu.
Lilipotajwa jina la Thandi, kila mtu alikaa kimya, walilitegemea hilo, walijua kwamba msichana huyo angeshika nafasi hiyo na mbili za juu zingekuwa kwa hao warembo waliowafanya watu wengi kujaa ndani ya ukumbi huo.
Mtangazaji, hakutaka kutangaza kwa pupa, alitaka kila mtu awe na presha mahali hapo, kwanza akarekebisha tai yake, akajikoholesha, akafanya mambo mengi yasiyokuwa na msingi ili kuwafanya watu kuwa na presha ndani ya ukumbi huo.
Kila mmoja alikuwa akimwangalia, mapigo yao ya moyo yalikuwa yakidunda sana, wote walikuwa na mshindi wao mioyoni mwao, walitaka kumsikia mtangazaji huyo alikuwa nani kwani kama ni urembo, wote walikuwa warembo japokuwa msichana Stacie alizidi kidogo.
Moyo wa Bwana Seppy ulikuwa mweupe kabisa, alichokuwa akitaka kukiona ni kuwa peke yake katika penzi la msichana Maria, kuua, kwake hakukuwa na tatizo lolote lile, kitu pekee alichokitaka ni kuwa na furaha kipindi chote.
Alipata taarifa kutoka kwa watu wengine kwamba yule mchezaji wa mpira wa kikapu aliyekuwa akitamba sana kipindi hicho, Paul alikuwa amekufa chumbani katika hoteli moja huko Los Angeles, hakutaka kujali sana kwani yeye ndiye aliyekuwa nyuma ya mpango wake.
Hakutaka kumuuliza Maria kuhusu Paul, alijua kwamba msichana huyo alikuwa na hofu kubwa kwa kuhisi kwamba angejua, akamuacha na uzuri ni kwamba kila taarifa iliyokuwa ikiandikwa, hakutajwa msichana, ilitajwa kwamba kama kawaida Benjamin alikuwa amekwenda chumbani humo na kumuua kijana huyo.
“Hakikisheni huyo msichana anakuwa huru, si mnajua kwamba huyo ni msichana wangu?” alizungumza Bwana Seppy katika simu, alikuwa akizungumza na polisi.
“Ndiyo mkuu!”
“Basi fanyeni hivyo!”
Hela zilikuwa kila kitu, alikuwa miongoni mwa matajiri wakubwa, aliheshimika kila kona, polisi wengi waliokuwa na tamaa ya fedha walikuwa chini yake na ndiyo maana wakati mwingine alikuwa huru kufanya kitu chochote alichotaka kukifanya kwa kuwa alijua hakukuwa na mtu aliyekuwa akimbabaisha hata mara moja.
Polisi walipewa maelekezo juu ya nini cha kufanya na wao walitakiwa kufanya vilevile, harakaharaka wakamuita Maria katika chumba cha mahojiano, wakaanza kuzungumza naye, hawakuchukua muda mrefu wakaamua kumwachia huku wakimwambia kwamba angehitajika kituoni hapo mara kwa mara.
Hilo ndilo alilolitaka Bwana Seppy, akawasiliana na Maria ambaye alimwambia kwamba yupo nyumbani, akamwambia kuwa alitaka kumuona wiki hiyo lakini msichana huyo akasema kwamba hakujisikia vizuri, alihitaji muda wa kupumzika.
“Si utakuja kupumzika huku mpenzi!” alisema Bwana Seppy.
“Hapana mpenzi! Naomba wiki moja ya mapumziko!”
“Sawa. Upo poa lakini?”
“Ndiyo! Najisikia kuchoka tu,” alisema Maria.
Bwana Seppy aliusoma mchezo, alijua fika kwamba msichana huyo alikuwa katika kipindi cha majonzi, alimpenda sana Paul na hakuona kama kungekuwa na mtu ambaye angelivuruga penzi lake, hata mapenzi aliyokuwa nayo juu ya Bwana Seppyy alipungua kwa kiasi kikubwa kwani hata kama fedha, Paul alikuwa nazo japokuwa hazikuwa nyingi kama za Bwana Seppy.
Siku zikaendelea kukatika, wiki ikakatika lakini msichana Maria hakufika nchini Marekani, kila alipopigiwa simu, alisema kwamba alikuwa kwenye kipindi kigumu, matatizo ya kifamilia yalikuwa yakimwandama hivyo asingeweza kabisa kwenda nchini Marekani.
Kwake, hayo yalikuwa majibu makali, yaliyouumiza moyo wake kupita kawaida, hakutaka kuona akishindwa, alichokifanya ni kuondoka Marekani na kuelekea nchini Mexico kwa kuamini kwamba uwepo wake mbele ya msichana huyo ungeweza kubadilisha kila kitu.
“Kisa nini Maria?” aliuliza Bwana Seppy huku akimwangalia msichana huyo usoni.
“Sipo vizuri kiafya,” alisema.
“Najua na ndiyo maana naona umekonda sana. Tafadhali mpenzi, kama kuna tatizo, naomba uniambie.”
“Hakuna tatizo lolote lile.”
“Kweli?”
“Hakika!”
Siku hiyo Bwana Seppy alitumia muda wake wote kuwa chumbani na msichana Maria, hata walipofanya mapenzi, haikuwa kama kipindi cha nyuma, hakupewa ushirikiano kama ilivyokuwa kipindi kingine. Moyoni mwake aliumia lakini hakuwa na jinsi, alimpenda msichana Maria na kama kuzunguka, alizunguka sehemu nyingi, aliwaona wasichana wengi lakini alikiri kwamba hakuwahi kumuona msichana kama Maria kwa jinsi alivyokuwa mzuri.
“Hii yote ni kwa sababu nakupenda Maria?” aliuliza Bwana Seppy ilipofika asubuhi.
“Kivipi?”
“Kwa unavyonifanyia!”
“Kwani nimekufanyaje mpenzi?”
“Sawa. Si umesema una matatizo ya kifamilia, ngoja nikuache uendelee nayo,” alisema Bwana Seppy.
Moyo wake ulikasirika, alimfahamu Maria, hakuwa namna ile, alijua kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikimuuma, kitendo cha mwanaume aliyekuwa akimpenda kuuawa, ndicho kilichomfanya kuwa katika hali ile.
Alikasirika kwa kuwa yeye kama yeye alikuwa na nafasi yake lakini pia hakutakiwa kukasirikiwa au kuonyeshewa hali yoyote ya kutokujali kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa akimuweka mjini msichana huyo.
Uamuzi wa mwisho kabisa kuupanga ulikuwa ni kuondoka mahali hapo, hakutaka kurudi tena, kama kuumia, aliumia vya kutosha na huo ulikuwa muda wa kuulizwa moyo wake huku akijitahidi kutafuta msichana mzuri ambaye angempenda kama alivyokuwa akimpenda Maria.
****
Hakukuwa na aliyeamini kama Stacie alikuwa amembwaga Angelica katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss World ambacho kilifanyika nchini Marekani katika jiji la Texas.
Ukumbi mzima ulipiga makofi, watu wengine walibaki midomo wazi, wapo wengine waliocheza kamari na kubashiri kwamba msichana Angelica angeibuka mshindi kutokana na kunyakua taji hilo.
Stacie alikuwa na furaha kubwa moyoni mwake, alipita huku na kule akiwapungia watu mikono, ndoto yake aliyokuwa nayo tangu kipindi cha nyuma hatimaye Mungu aliifanikisha na kuwa kweli.
Machozi ya furaha yalimbubujika, kuna kipindi hakuwa akiamini, alihisi kwamba alikuwa katika moja ya ndoto yenye msisimko ambapo baada ya kipindi fulani angeamka na kujikuta akiwa kutandani kitu ambacho hakikuwa kweli, kila kitu kilichokuwa kikitokea, kilikuwa katika maisha halisi.
Jina lake siku hiyo likapata umaarufu, waandishi wa habari wakampiga sana picha na wengine kuiweka habari yake katika mitandao ya kijamii, jina lake, yaani kwa kipindi cha dakika kadhaa, lilikuwa maarufu mno.
Uzuri wake uliendelea kuwatetemesha wanaume wengi, hawakuwa wakiamini kama kweli duniani kulikuwa na msichana aliyekuwa na sura nzuri kama alivyokuwa Stacie, wanaume wenye fedha wakajipanga, kila mtu alihitaji kuwa na msichana huyo, hawakujua kama angekubaliana nao au la, kitu walichokihitaji ni kuwa naye kimapenzi, yaani hata kama ni kutumia fedha, watumie lakini mwisho wa siku wampate msichana huyo.
Siku hiyo Stacie akapelekwa katika hoteli kubwa ya nyota saba na kukaa huko. Usiku mzima alikuwa na furaha tele, hakuamini kama kweli angefanikiwa kunyakua taji hilo lililokuwa na heshima kubwa duniani katika masuala ya urembo.
Siku iliyofuata akawasiliana na rafiki yake wa kipindi kirefu, Robert Steph ili awe meneja wake kwani mbele yake aliyaona mafanikio makubwa hasa ya kuingia mikataba minono.
Kama alivyohisi ndivyo ilivyotokea, siku hiyihiyo akapigiwa simu na watu wa Jarida kubwa la Forbes ambao walitaka kuonana naye na kuzungumza naye kuhusu masuala ya kibiashara, hilo wala halikuwa tatizo, alichoangalia kwanza ni kupiga pesa tu.
****
Fedha zikaanza kunukia kwa msichana Stacie, hakukuwa na kitu alichokiona mbele yake zaidi ya mafanikio makubwa, alijiona akiwa mtu mkubwa, mwenye fedha na heshima kubwa.
Kitendo cha kunyakua tuzo na kuwa mrembo wa dunia kilimpa uhakika wa kuishi maisha ya kuwa na fedha mpaka anakufa, kupitia uzuri wake, alishinda tuzo hiyo na hivyo kumshukuru Mungu kila siku kwa kile alichokuwa amempa.
Baada ya kusaini mkataba na Jarida la Forbes na kulipwa kiasi cha dola milioni mbili ambazo zilikuwa zaidi ya bilioni nne za Kitanzania, makampuni mengi yakamfuata, hakuwa na hiyana, alichokifanya ni kuendelea kukusanya fedha kama kawaida.
Jina lake halikushuka, liliendelea kuwa juu na kwa sababu tayari alikuwa na jina, aliona kuwa na umuhimu wa kuwa na mbunifu wake wa mavazi. Kulikuwa na watu wengi walioomba nafasi hiyo, kila siku alipokea barua pepe, watu walikuwa wakimuomba nafasi ya kuwa mbunifu wake wa mavazi kiasi kwamba akachanganyikiwa amchukue yupi kwani kila mmoja alionekana kuwa mtaalamu kwa kazi hiyo.
“Kwa hiyo utamchukua nani?” aliuliza Robert.
“Labda huyu Muitaliano, Alejandro Petrescu,” alijibu Stacie.
Alichokifanya ni kuwasiliana na mbunifu huyo wa mavazi na kumtaka kufika nchini Marekani haraka iwezekanavyo, alimtumia tiketi ya ndege, gharama za kukaa hotelini lakini mwisho wa siku walitaka kuona kila kitu kinakuwa kama kinavyotakiwa.
Tangu achukue taji hilo alikwenda nyumbani kwao Australia mara mbili tu, baada ya hapo, maisha yake yakaendelea kuwa nchini Marekani ambapo aliishi kwa kuheshimika kupita kawaida.
Alejandro ndiye aliyemfanya Stacie kupendeza zaidi, kila siku alikuwa mtu wa kumbunia mavazi mbalimbali, na kila alipovaa, alivutia kiasi kwamba wanaume wengi wakazidi kumpenda.
Jina lake lilikuwa kubwa, ni ndani ya miezi sita tu tayari aliingiza kiasi kikubwa cha fedha kwa sababu tu alikuwa mrembo na hata mastaa wa filamu walitamani kuigiza naye kitu kilichowafanya kuwaomba waongozaji wafanye kitu.
“Hakuna tatizo, nitamuita kwenye hii filamu!”
Muongozaji kutoka katika Kampuni ya Filamu ya Marvel alikuwa akizungumza na muigizaji wake mwenye jina kubwa, Tom Hardy ambaye alikuwa akihitaji kuigiza na msichana Stacie.
Hilo wala halikuwa tatizo, kwa sababu wao wenyewe walikuwa wakitafuta fedha, waliamini kuwa kama wangemruhusu msichana huyo ashiriki katika muvi yao hakika wangepata kiasi kikubwa cha fedha, hivyo bila ubishi, wakawasiliana naye na kumuita.
Stacie hakuamini, hakuwahi kufikiria hata mara moja kwamba ingetokea siku angepokea simu kutoka kwa mmoja wa waongozaji katika kampuni hiyo na kumtaka kuigiza filamu, hakukataa, kwa kuwa naye alizitaka hizo fedha na kuwa maarufu zaidi, akakubaliana nao.
Baada ya siku kadhaa, wakaanza kuigiza filamu mpya ya Black Panther. Japokuwa alikuwa muigizaji mchanga lakini alifanya vizuri sana kitu kilichoonyesha kwamba angekuwa muigizaji mkubwa sana hapo baadaye.
Hayo ndiyo yalikuwa mwanzo wa mafanikio makubwa aliyoanza kuyapata. Kila siku akawa mtu wa kuingiza fedha, uzuri wake uliwachanganya watu wengi na hivyo kuanza kumfutailia bila mafanikio makubwa.
Miongoni mwa watu wengi waliokuwa wakimfuatilia alikuwa Bwana Seppy. Mzee huyu alimpigia simu Stacie na kumwambia kwamba alitaka kuonana naye kwa kuwa kulikuwa na mambo mengi ya kuzungumza.
Jina la Bwana Seppy halikuwa geni, alimfahamu mzee huyo, alikuwa miongoni mwa watu wenye fedha ambao waliitetemesha Marekani kipindi hicho. Kwake ilikuwa furaha tele hivyo kupanga mipango ya kuonana.
Siku mbili zilizofuata, walikuwa katika Mgahawa wa SamSam ambapo hapo Bwana Seppy alikuwa na walinzi wake waliokuwa kimya kila wakati.
Bwana Seppy alibaki akimwangalia msichana huyo, alikuwa mrembo sana, tangu aachane na mpenzi wake, Maria miezi kadhaa iliyopita hakupata mtu ambaye angeziba pengo kubwa lililoachwa na msichana Maria.
Alimtafuta msichana wa kuziba pengo hilo ila kwa kipindi chote hicho, hakufanikiwa kabisa. Kila alipomwangalia Stacie, aliona kabisa kwamba msichana huyo alikuwa akielekea katika kuliziba pengo hilo lililomtesa kwa kipindi kirefu.
Kuhusu kutumia fedha, kwake halikuwa na tatizo lolote lile, kitu pekee alichokihitaji kilikuwa ni mapenzi kutoka kwa msichana huyo tu. Macho yake tu yalionyesha kila kitu, mapenzi aliyokuwa nayo moyoni hayakubaki huko bali yalizunguka mpaka machoni mwake.
Alitaka kumwambia ukweli lakini hakujua mahali pa kuanzia, alivuta pumzi huku akiagiza kahawa, kipindi chote hicho msichana Stacie alikuwa akimwangalia tu machoni mwake.
“Nashukuru sana kwa kuitikia wito wangu,” alisema mzee huyo huku akimwangalia msichana huyo.
“Usijali...”
“Nimekuita kwa jambo moja...”
“Lipi hilo? Biashara?”
“Ndiyo! Lakini sidhani kama la biashara linatakiwa kuzungumzwa leo, nadhani leo tunatakiwa kuzungumzia jambo jingine kabisa,” alisema mzee huyo.
“Lipi hilo?”
Bwana Seppy akashusha pumzi ndefu na kuangalia pembeni kama kulikuwa na watu waliokuwa wakiyafuatilia mazungumzo yao, alipoona hakukuwa na mtu aliyekuwa akifanya hivyo, hapo ndipo alipoamua kutumbua jipu.
Hakutaka kuteseka moyoni mwake, ilikuwa ni vigumu mno kuendelea kuumia, kuwa na mawazo na wakati alikuwa na uwezo mkubwa wa kumwambia msichana huyo kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Hakutaka kuficha, kama ni siri, aliamua kuitoa na hivyo kumwambia jinsi alivyokuwa akimpenda. Muda wote msichana Stacie alikuwa kimya, alibaki akimwangalia mzee huyo usoni, uso wa Stacie ulikuwa kwenye tabasamu pana ambalo lilimpa matumaini mzee huyo kwamba angefanikiwa kile alichokuwa akikitaka.
“Umemaliza?” aliuliza Stacie baada ya kumsikiliza mzee huyo kwa dakika tatu.
“Ndiyo!”
“Haitowezekana!” alijibu kwa kifupi.
“Kwa nini tena jamani?”
“Jua kwamba haitowezekana, hakuna sababu, jua tu kwamba haitowezekana,” alisema Stacie na hapohapo kusimama, hakutaka kusubiri, japokuwa mzee huyo alionyesha muonekano uliomtia huruma, hakutaka kujali, akachukua kila kilicho chake na kuondoka zake huku Bwana Seppy akiishia kula kwa macho tu.
Benjamin hakutaka kutoka kule alipokuwa, alikuwa kimya, japokuwa katika bomba lile kulikuwa na joto kali na uchafu mwingi hasa moshi hakutaka kutoka, alibaki humohumo akiendelea kusubiri mpaka maofisa wale wa FBI waondoke ndiyo atoke ndani ya bomba lile.
Alimsikia rafiki yake, Harry alivyokuwa akiwaambia maofisa hao kwamba yeye hakuwepo, alikuwa amekwishaondoka na hakujua mahali alipokuwa. Maofisa wale walimtafuta, muda wote mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kule alipokuwa lakini hakutaka kutoka.
Walimtafuta bila mafanikio yoyote na kuamua kuondoka ndani ya nyumba hiyo. Hapo ndipo Benjamin alipoona ni muda muafaka kutoka ndani ya bomba lile, alianza kuangalia huku na kule, hakuwa akijiamini hata kidogo.
Hakukuwa a mtu nyumbani hapo, alikuwa peke yake, senhemu hiyo haikuonekana kuwa salama tena, kama maofisa wa FBI walikuja na kuondoka, aliamini kwamba wangerudi tena mahali hapo, alichokifanya ni kuanza kutoka.
Alitembea kwa mwendo wa tahadhali, alihofia kukamatwa, alitembea huku kichwani akiwa na kofia yake, hakuwa na usafiri, ingekuwa rahisi sana kama angefanikiwa kupata usafiri, magari yalikuwepo lakini hilo halikuwezekana.
Akachukua simu yake na kuanza kumpigia mpenzi wake, Vanessa, alitaka kuonana naye na kupanga ni kwa namna gani angeweza kuwa naye na mwisho wa siku kuondoka nchini hapo na kuelekea Urusi ambapo hakukuwa mbali sana.
Simu ikaanza kuita, alikuwa mvumilivu, wakati akipiga simu hiyo, alihakikisha anakuwa katika sehemu ambayo itakuwa vigumu kuonekana, alijibanza sehemu na watu wote waliokuwa wakipita pale alipokuwa, hakukuwa na aliyemgundua.
“Upo wapi?” aliuliza Benjamin mara baada ya simu kupokelewa.
“Nipo nyumbani!”
“Kuna usalama huko?” aliuliza.
“Nadhani. Hakuna mtu, nipo peke yangu!”
“Na FBI je?”
“Hawapo!”
“Hebu chungulia dirishani, angalia kwa umakini, kweli hawapo?” aliuliza Benjamin na Vanessa kufanya hivyo.
“Hakuna mtu!”
“Sawa! Nakuja!”
Japokuwa aliambiwa na msichana wake kwamba hakukuwa na maofisa wa FBI pale nyumbani alipokuwa lakini alishindwa kabisa kujiamini, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda na kuona kwamba kama angekwenda huko ilikuwa ni lazima kukamatwa.
Wakati anafikiria hayo, upande mwingine wa moyo wake ukamwambia kwamba hakukuwa na tatizo lolote lile, kama alitaka kwenda huko, aende na kila kitu kingekuwa vizuri.
Kutoka hapo alipokuwa mpaka alipokuwa akiishi Vanessa, katika nyumba ambayo aliamua kuipanga kwa muda haikuwa mbali sana, hakuchukua muda mrefu akawa amefika katika mtaa huo.
“Ni lazima tuondoke na kuelekea nchini Urusi, hapa Marekani si salama tena,” alijisemea Benjamin.
****
Wakati Benjamin akiwasiliana na Vanessa, vijana wa Bwana Seppy walikuwa wakifahamu kila kitu na walikuwa wakifuatilia neno moja baada ya jingine. Bado Benjamin alionekana kuwa mtu muhimu sana, walijua kwamba kama wasingefanikiwa kumpata mtu huyo na kumuua basi bosi wao angekuwa kwenye wakati mgumu sana.
Mawasiliano yale wakamuonyeshea Bwana Seppy ambaye alionekana kuwa na mawazo mno ya kukataliwa na msichana Stacie, alichoagiza ni kwamba Benjamin na mpenzi wake, Vivian watafutwe na kuuawa haraka iwezekanavyo.
“Hakuta tatizo mkuu! Tunawafuata hukohuko,” alisema Dracula na kisha kuwakusanya watu wake kuelekea kule ambapo Benjamin alitakiwa kuonana na mpenzi wake, Vanessa.
****
Benjamin alianza kupiga hatua za taratibu kuifuata nyumba aliyokuwemo Vanessa, hakujiamini kabisa na alijua fika kwamba inawezekana kuna sehemuu maofisa wa FBI walikuwa wamejificha.
Aliangalia huku na kule, hakuona mtu, hakujua kama maofisa hao walikuwa kwenye gari ambalo mbele hakukuwa na mtu, walikuwa kwa nyuma huku wakimfuatilia katika televisheni walizokuwa nazo na hata mazungumzo yake na Vanessa waliyasikia kwani tayari walikuwa wakimfuatilia msichana huyo tangu siku ile walipomruhusu kutoka katika kituo cha polisi.
“What should we do?” (Tufanye nini?) aliuliza jamaa mmoja.
“There is no time, let’s roll,” (Hakuna muda, twendeni)
Hicho ndicho walichokifanya, hawakutaka kusubiri mahali hapo, wakateremka huku wakiwa na bunduki zao mikononi. Wakati Benjamin akiendelea kupiga hatua kuelekea katika nyumba ile, ghafla akaliona gari likija kule alipokuwa, alionekana kuogopa, hakujua gari hilo lilikuwa la kina nani, alichokifanya ni kuanza kukimbia kuelekea katika nyumba ile.
Hao waliofika hawakuwa maofisa wa FBI, walikuwa ni vijana kutoka kwa Bwana Seppy, walifika hapo na kuhisi kwamba walikuwa peke yao, kitendo cha Benjamin kukimbia kuelekea ndani, wakaanza kumkimbiza huku wakiwa na bunduki.
Benjamin akaingia ndani, nao wakamfuata na kuingia ndani. Msichana Vanessa ambaye alikuwa ndani ya nyumba hiyo, akaanza kupiga kelele, watu wale hawakutaka kujali, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumkamata Benjamin na kisha kumkamata na Vanessa ambaye muda wote alikuwa akiomba msamaha tu kwamba aachwe.
“Mlidhani mtatusumbua miaka yote, kwisha habari yenu,” alisema Dracula huku akiachia tabasamu pana, uso wake ulionyesha jinsi gani alikuwa na furaha.
Wakawachukua na kuanza kutoka nje. Hawakujua kama maofisa wa FBI walikuwa hapo nje, kitendo cha kutoka tu, milio ya risasi ikaanza kusikika, walichokifanya ni kujificha pembezoni mwa nyumba hiyo.
“Who are they?” (Ni wakina nani?) aliuliza jamaa mmoja.
“I don’t know.” (Sifahamu)
“They are cops,” (Ni polisi) alisema Dracula.
“Who call them?” (Nani aliwapigia simu?)
“I don’t know,” (Sijui) alijibu Dracula.
Hakukuwa na muda wa kuulizana maswali mengi zaidi, kama walivyokuwa wakirushiwa risasi nao wakaanza kujibu mapigo. Yalikuwa ni mapigano makubwa, maganda ya risasi yalikuwa yakidondoka chini tu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sehemu hiyo ikabadilika na kuwa uwanja wa vita. Vijana wa Bwana Seppy walikuwa na silaha nzito hivyo kuionekana kuwa na kazi nyepesi kabisa. Kwanza walianza kulishambulia gari la maofisa wale bila tatizo lolote lile.
Kwa maofisa wale ilikuwa ni kazi ngumu kuwarushia risasi kwani watu hao walikuwa na Benjamin mtu ambaye walimtaka kwa udi na uvumba. Wasiwasi wao ndiyo uliosababisha kushambuliwa sana.
Benjamin ambaye alikuwa amekaa nyuma alipoona mashambulizi yanazidi na wote wamemsahau na kuwa bize na maofisa wale, akarudi ndani haraka sana, hakutaka kumshtua Vanessa kwani mahali alipokuwa ilikuwa vigumu sana.
Mmoja wa vijana wale alimuona Benjamin akikimbia lakini hawakuwa na muda wa kumkimbiza kwani bado mashambulizi kutoka kwa maofisa wa FBI yalikuwa yakiendelea kama kawaida.
“He is running....he is running...” (Anakimbia....anakimbia...) alisema jamaa huyo lakini hakuna aliyajali, wote walikuwa bize na mapambano.
****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment