Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

PENIELA (2) - 1

 




IMEANDIKWA NA : PATRICK CK



*********************************************************************************



Simulizi : Peniela (2)

Sehemu Ya Kwanza (1)




TUKUTANE KATIKA SEASON 2 YA PENIELA



SEASON 2



SEHEMU YA 1



Shughuli ya kuuaga mwili wa Dr Flora Joshua mke wa rais zilihudhuriwa na watu wengi sana.Viwanja vya ukombozi vilifurika watu waliokuja kutoa heshima zao za mwisho kwa mama huyu ambaye katika enzi za uhai wake aliweka mkazo mkubwa katika kuwawezesha kiuchumi akina mama ..Alikuwa na taasisi yake ambayo iliwasaidia sana wanawake kwa kuwapatia mikopo ya biashara.

Wakati shughuli za kuuaga mwili wa Dr Flora zikiendelea Flaviana mtoto mkubwa wa marehemu alikuwa katika mawazo mengi sana kuhusiana na kile kilichomuua mama yake.

“ Usiku uliotangulia siku ya kifo chake,mama alitupigia simu mimi na Anna na akatuomba jioni ya siku ile akutane nasi kuna jambo kubwa analotaka kutueleza.Kwa bahati mbaya sana hatukufanikiwa kulifahamu jambo hilo ambalo alitaka kutueleza kwani alifariki ghafla mchana kabla ya kukutana nasi.Ni kitu gani alichotaka kutuambia? Ninahakika lazima litakuwa ni jambo kubwa kwa sababu aliweka msisitizo mkubwa .Lakini ni nani aliyemchoma dawa ile kwa kiwango kikubwa na kusababisha kifo chake? Ni kwa nini alimchoma? Akaendelea kujiuliza

“ Ninavyofahamu ni kwamba mama alikuwa akihudumiwa na daktari wa familia Dr Amos.Nina hakika yeye atakuwa akifahamu nini kilitokea.Huyu ndiye anayetakiwa abanwe na aeleze ni nani aliyemchoma mama sindano ile.Kitu kingine kuna mfumo wa kamera za ulinzi ,nina hakika lazima zitaonyesha kila mtu aliyeingia chumbani kwa mama siku ile.Lazima tumpate mtu aliyefanya kitendo hiki cha kikatili na tujue ni kwa nini alifanya vi…………….” Flaviana akastuliwa toka katika lindi la mawazo baada ya kusikia kitu Fulani cha baridi kikimgusa shingoni.Akageuka ghafla ghafla na kukutana na sura ya mwanadada aliyekuwa amejitanda sare zilizovaliwa na akina mama pale msibani ambaye sura yake ilikuwa na simanzi na alionekana kama ni mtu aliyeguswa sana na msiba ule

“ Flaviana unahitajika mara moja kule wenye gari la wagonjwa” akasema yule mwanadada.Flaviana akamtazama kwa makini lakini hakuwa akimfahamu.Hakuwa na kumbukumbu kama wamewahi kuonana.Bila kuhoji kuna kitu gani huko katuika gari la wagonjwa Flaviana akainuka na kuongozana na Yule mwanadada kuelekea katika gari la wagonjwa lililokuwa limeegeshwa pembeni kidogo ya viwanja vile kwa ajili ya dharura endapo ingetokea mtu yeyote Yule kuzidiwa.Walipolikaribia lile gari la wagonjwa Flaviana akaanza kuhisi kizungu zungu na kutaka kuanguka.Macho yake hayakuwa yakiona vizuri,akamuomba Yule mwanadada amsaidie kwani hali yake ilibadilika ghafla.Mara wakatokea wanaume watatu waliokuwa na mavazi yaliyowatambulisha kama wafanyakazi wa msalaba mwekundu wakamshika Flaviana na kumuingiza katika lile gari la wagonjwa halafu likawashwa na kuondolewa pale viwanjani huku likipiga king’ora kuashiria kwamba kulikuwamo na mgonjwa ndani yake.Macho ya Flaviana yalipoteza nguvu ya kuona taratibu na mara kukawa giza.Mmoja wa wale jamaa waliokuwamo mle garini akachukua simu na kuwasiliana na mtu Fulani



“ Dr Kigomba kazi imekamilika.Tayari muhusika tunaye na tunataka kulifanya lile zoezi” akasema Yule jamaa

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Good job,fanyeni kama nilivyowaelekeza halafu mumpeleke hospitali ili atakapozinduka ajikute akiwa kule na asigundue lolote lililotokea.Hakikisheni dawa aliyopakwa kumpoteza fahamu si nyingi sana kiasi cha kuweza kumletea madhara.” akasema Yule mtu wa upande wa pili.

“ Sawa mzee tutafanya kama ulivyoelekeza” akasema Yule jamaa na kukata simu,akafungua mkoba mdogo na kutoa kifaa Fulani mithili ya kompyuta akakiunganisha katika simu ya Flaviana waliyoichukua toka katika pochi yake halafu akabonyeza namba kadhaa katika kile kifaa na kusubiri kwa muda wa dakika kama tano hivi kikawaka taa ya kijani halafu akakitoa kile kifaa na kukirudisha katika kile kisanduku kidogo.

“ Kila kitu tayari.Kuanzia sasa yeyote atakayewasiliana naye tutasikia kila watakachokiongea.” Akasema Yule jamaa na kisha safari ikaendelea kuelekea hospitali





******










Saa tano za mchana Mathew na Anitha walirejea nyumbani wakitokea uwanja wa ndege kuwasindikiza Dr Michael na familia yake ambao waliofanikiwa kupata ndege iliyokuwa ikielekea Nairobi na kutokana na mambo yaliyowakuta ,hawakutaka kuendelea kupoteza muda tena hapa nchini hivyo wakaamua kuitumia nafasi hiyo kuondoka.



“Whats next Mathew? Akauliza Anitha wakati wakiingia ndani

“Kwa sasa baada ya kumaliza ile kazi ya Elibariki tunarejea katika shughuli yetu ya msingi ambayo ni kuchunguza kifo cha Edson” akasema Mathew ,Anitha aliyekuwa dereva akasimamisha gari wakashuka na kumkuta Noah amekaa sebuleni na wote wakaelekea katika chumba ambacho hukitumia kwa majadiliano ya kazi.



“Tunaendelea na zoezi letu.” Akasema Mathew

“Tunaendelea na kazi yetu ya kumtafuta muuaji wa Edson.Ile kazi ya kufanya uchunguzi wa kilichosababisha kifo cha Dr Flora iliingilia kati kati na kwa kuwa tumeimaliza basi tuko huru kuendelea na kazi yetu ya awali. Kabla ya kuingia katika kazi ile iliyojitokeza ,tulitakiwa kuchunguza mahusiano yaliyopo kati ya Peniela na Team SC41. Kama Peniela naye ni Team SC41 basi tutakuwa na uhakika kwamba Edson aliuliwa na Team SC 41 na Peniela atakuwa akifahamu sababu ya ya kifo chake .” akasema Mathew



“ Nakubaliana nawe Mathew kwamba kunaweza kuwa na mahusiano kati ya Peniala na Team, Sc 41 au hata Peniela mwenyewe akawa ni mmoja wao lakini ninachojiuliza ni kwamba kama Peniela ni mwenzao kwa nini basi wamuache ahusishwe na kesi ile kubwa ya mauaji ya Edson na kunusurika kufungwa? Kwa nini wamuache mwenzao ateseke gerezani kwa karibu mwaka mzima? Jambo hili ilinanipa shaka kidogo “ akasema Anitha.

“Hata mimi wakati mwingine nimekuwa nikijiuliza swali kama hilo unalojiuliza wewe Anitha.Inakuwa ni vigumu kuingia akilini kwamba Team Sc 41 wanaweza wakafanya mauaji halafu wakamuacha mmoja wa watu wao abebe mzigo ule wa kesi.Ninavyowafahamu Team SC 41 hufanya mambo yao kwa siri kubwa kwa hiyo kumuacha mwenzao akashikiliwa na vyombo vya dola ni kujihatarisha hata wao wenyewe na ndiyo maana hata matibabu ya John Mwaulaya yalikuwa ya siri mno na walipogundua kwamba tunamfuatilia wakamuhamisha haraka mno.Hivi ndivyo Team SC41 wanavyofanya kazi zao.Hiki ni kikosi ambacho kinafanya kazi zake kwa siri kubwa sana.” Akasema Mathew akainma akafikir kidogo na kusema

“ Kuna wazo limenijia,yawezekana kuna watu waliomuua Edson na Peniela ambaye kwa wakati huo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Edson akajikuta amenaswa katika mtego.Kama ni hivyo ni nani basi waliomuua Edson na kumtupia Peniela mzigo wa kesi ile ya mauaji? Kuna ulazima wa kumfahamu zaidi Peniela.Kuna kitu tunaweza tukakipata toka kwake” akasema Mathew

“ Kuna zile kamera kipepeo ulizozitega nyumbani kwa Penny zinaweza zikawa na msaada mkubwa sana kwetu.Zinaweza kutusaidia kufahamu kuhusu nyendo za Penny na ni akina nani anaohusiana nao” akasema Anitha



“ Ni kweli Anitha lakini hatutazitegemea kamera tu,lazima twende ndani zaidi.Lazima tumfahamu Peniela kiundani na katika hilo tutamtumia Jaji Elibariki.Naomba niwaweke wazi kwamba Jaji Elibariki na Peniela wana mahusiano ya siri ya kimapenzi.Hilo alinihakikishia Elibariki mwenyewe.Kwa hiyo basi tukitaka kumfahamu Peniela tunatakiwa tumtumie Elibariki.” Akasema Mathew na kuchukua simu yake akampigia Elibariki



“ Hallow Elibariki,” akasema Mathew baada ya Jaji Elibariki kupokea simu



“ Elibariki samahani kwa kukusumbua.”

“ Bila samahani Mathew.Kuna taarifa gani mpya?

“ Hakuna taarifa mpya ila ninahitaji kukuona.Kuna jambo Fulani nataka tuongee kuhusiana na Peniela.”



“ Ok Mathew nitafika baadae kidogo ,kwa sasa niko hapa viwanja vya Ukombozi kuna shughuli ya kuuaga mwili wa Dr Flora.Mara tu shughuli zitakapomalizika hapa nitakuja hapo mara moja” akasema Elibariki .Baada ya kumaliza kuongea na Elibariki simuni,Mathew akawageukia wenzake



“ Nilimtaka Elvis afike hapa ili tuonge naye kuhusiana na suala hili lakini hataweza kufika kwa sasa kwani wako katika shughuli ya kuuaga mwili wa Dr Flora.Lakini atafika baadae baada ya shughuli ile kumalizika”



“ What about Jason? Hatuwezi kumtumia yeye? Jason na Jaji Elibariki ni marafiki na wote wako pamoja katika jambo hili.” Akashauri Anitha



“ Ninadhani ingefaa zaidi endapo tutamtumia El………………”kabla hajamaliza sentensi yake simu yake ikaita.Alikuwa ni Eva.



“ Hallow Eva” akasema Mathew

“ Mathew samahani kwa usumbufu lakini naomba msaada wako”



“ Kuna tatizo gani Eva?



“ Mathew , I guess I’m in trouble”

“ Eva kuna tatizo gani? akauliza Mathew



“ Kuna watu wananifuatilia .”



“ Wanakufuatilia?!

“Ndiyo.Wamekuwa wakinifuatilia toka nilipotoka nyumbani na sijui lengo lao ni nini kwangu.Nimejaribu kuzunguka mitaa kadhaa ili nihakikishe kama ni kweli wananifuata mimi lakini ni kweli wananifuatilia kwani kila nikisimama nao husimama nikianza safari nao huanza.”

“ Unawafahamu watu hao? Akauliza Mathew

“ Hapana Mathew siwafahamu watu hao ni akina nani na nini lengo lao kwangu.Please Mathew help me I dont know what to do.Nina hakika watu hawa wana lengo baya nami”



“ Ok Eva.Uko wapi mida hii?

“ Nimeishika hii barabara ya Jakaya ninaelekea baharini kuingia katika barabara ya ile ya majimaji Drive.”

“ Ok fanya hivi,ukifika pale kwenye mzunguko karibu na hoteli ya Panda Ocean view,ifuate barabara inayoeeleka chuo cha utalii ,kabla hujafika pale chuo cha utalii ,kuna jengo kubwa la maegesho limefunguliwa hivi karibuni maarufu kama maegesho ya mchina.Ingia ndani ya jengo lile hadi ghorofa ya juu kabisa.Mimi najitahidi kufika pale ndani ya kipindi kifupi.Ukifika kabla sijafika nipigie simu unitaarifu.” Akasema Mathew



“ Ahsante Mathew.Samahani lakini kwa kukusumbua”



“ Usijali Eva.Fanya kama nilivyokuelekeza” akasema Mathew na kukata simu

“ Kuna tatizo lingine limetokea.Kuna watu wanamfuatilia Eva.Unajua Eva ndiye aliyetusaidia mpaka tukampata Kanali Adolf kwa hiyo lazima tumsaidie awapo matatizoni.” Akasema Mathew



“ Eva ni nani? Akauliza Noah



“ Hakuna muda wa maswali Noah.Lazima tuwahi kumsaidia Eva.Anitha jiandae tuondoke,Noah utaendelea kubaki hapa hadi tutakapohakikisha umepona jeraha lako” akasema Mathew na kukimbia kuelekea chumbani kwake akakusanya baadhi ya vifaa vyake vya kazi na kutoka.Anitha naye alikuwa tayari,ili kuwahi ikawalazimu kupanda piki piki .Mara chache sana Mathew hutumia pikipiki ili kuepukana na msongamano mkubwa wa magari jijini Dar.



“ Nakumbuka Eva aliniomba nimsaidie kumsaka msichana aliyetekwa na kufichwa mahala kusikojulikana.Nani waliomteka msichana huyo na kwa nini ? Je ni hawa wanaomfuatilia hivi sasa ndio hao waliomteka huyu msichana? Hapa inaonekana kuna kazi nyingine inaweza kujitokeza.Ngoja kwanza tuwafahamu watu hawa wanaomfuatilia na tujue nini wanakitaka kwake” akawaza Mathew wakiwa katika mwendo mkali kuwahi mahala walikopanga wakutane na Eva







*******





Nyumbani kwa John Mwaulaya kulikuwa kimya sana tofauti na ilivyozoeleka.Ni watu wawili tu walioonekana pale nyumbani kwa John.Kijana mwenye taaluma ya udaktari ambaye amekuwa akimtibu John na Josh mlinzi wa siku nyingi wa John Mwaulaya



“ Leo kuna nini hapa mbona kumekuwa kimya sana? Siku zote kabla hawajaelekea katika kazi zao vijana wote hupita hapa kunijilia hali lakini leo imekuwa tofauti,sijawaona kabisa vijana,wako wapi? Laiti ningekuwa na uwezo wa kuinuka na kwenda kujua nini kinaendelea huko nje,manake hata Osmund leo sijamuona toka nilipoamka” akawaza John halafu akanyoosha mkono na kubonyeza kitufe cheusi chini ya kitanda chake na mlango ukafunguliwa haraka akaingia Desmond kijana mwenye taaluma ya udaktari ambaye ndiye amekuwa akimuuguza John .

“ Desmond,vijana wote wako wapi ? Sijawaona wote toka asubuhi.” Akauliza John

“Mzee,vijana leo hawapo,niko mimi na Josh pekee.Wengine wote wametawanyika”

“ Wamekwenda wapi? Akauliza John kwa sauti dhaifu



“ Kuna matatizo yalitokea jana”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Matatizo gani? Tafadhali naomba unieleze”

“Mzee nadhani si wakati muafaka kwa wewe kufahamishwa kuhusiana na mambo haya kutokana na afya yako.Endelea kulala upumzike.Mambo yote yanashughulikiwa kikamilifu “

“Desmond,nimelala hapa kitandani ninaumwa sina nguvu za kuweza kufanya jambo kubwa lakini kichwa changu bado kina uwezo wake mkubwa wa kufikiri na kufanya kazi sawasawa.Ninafahamu mambo mengi sana kuliko yeyote katika Team Sc41 kwa hiyo tafadhali naomba unieleze ni kitu gani kimetokea?

Desmond akamtazama John Mwaulaya kana kwamba anaogopa kumweleza kile kilichotokea lakini baada ya tafakari ndogo akaamua kumweleza

“ Kuna shambulio lilitokea jana usiku na vijana wetu sita wakauawa”



“ What ?! John akastuka



“Vijana wetu sita waliuawa katika shambulio jana usiku.Leo hii watu wote wametawanyika wanakwenda kuwazika katika sehemu mbali mbali ndiyo maana umeona nyumba iko kimya leo” akasema Desmond



“ Kwa nini Ossy hakunieleza jambo lolote kuhusiana na suala hili? Nadhani ni kwa sababu niko kitandani na siwezi kufanya lolote.Alikosea sana ,mimi nina uwezo mkubwa wa kuwaongoza hata kama niko kitandani” akawaza John.



“ Ni akina nani waliofanya shambulio hilo na kusababisha vijana wetu wote hao kuuawa? Akauliza John

“ Bado haijafahamika ni akina nani lakini watu hao walikwenda kumkomboa mke wa daktari aliyekuwa ametekwa ili kumshinikiza daktari huyo akufanyie upasuaji.”

“ Kwa nini Osmund alifanya hivi? Hakupaswa kufanya hivi hata kidogo.Team SC41 si watekaji wa watu hata simu moja na jukumu letu ni kushughulika na maslahi ya serikali ya marekani tu na si kuingia katika suala la utekaji.Hili ni kosa kubwa alilolifanya na kwa nini hakunieleza mapema ili nimpe ushauri? Akajiuliza John.Pamoja na kuumwa lakini alionekana wazi kuchukizwa na kitendo cha Osmund kuamrisha kutekwa kwa mke wa Dr Michael.

“Desmond naomba uniitie Josh.” Akasema John Mwaulaya.Desmond akatoka na kwenda kumuita Joseph kijana mlinzi wa John wa muda mrefu.



“ Josh kuna jambo nataka nikueleze” akasema John Mwaulaya



“ Nakusikiliza mzee” akajibu Josh kwa adabu



“ Mimi kwa sasa ni mgonjwa lakini nina hakika nitapona na kurejea katika hali yangu ya kawaida.Bado nina matumaini hayo na Mungu ananisaidia hali yangu si mbaya sana japokuwa kuna watu ambao wamekuwa wakinidharau kwa hali yangu hii ,wakitegemea kwamba ninaweza kufariki muda wowote.They are all wrong.Wataanza kufa wao na mimi nitabaki.Anyway tuachane na hayo.Kuna kazi nataka nikupe na nimekuchagua wewe kama kijana wangu mtiifu sana na ninayekuamini.Katika vijana wote ndani ya Team SC41 ni wewe pekee ninayekuamini.Uko tayari kwa kazi nitakayokupatia? Akauliza John

“ Niko tayari mzee” akasema Josh



“ Ok nashukuru kwa hilo.Kuna mtu ambaye anatumwa kutoka makao makuu marekani kwa ajili ya kuja kunichunguza ugonjwa wangu.Ki ukweli ni kwamba mtu huyu haji kwa dhumuni la kunichunguza ugonjwa wangu,bali anakuja kuniua.Dr Burke is a devil.Nimemtahadharisha Osmund kuhusu jambo hili lakini haonekani kunielewa.I want you to stop him.Stop Dr Burke for me” akasema John.Josh akatafakari kidogo na kusema



“ Unataka nimfanye nini Dr Burke? Akauliza Josh.John akamtazama kwa muda kidogo kisha akasema



“Kill him”



“Mzee niko tayari kuifanya kazi hiyo lakini kuna tatizo kidogo hapa.Ni namna ya kupata taarifa za kuhusiana ujio wa Dr Burke.Kila kitu anakifahamu Osmund pekee.”akasema Josh



“ Usijali kuhusu hilo.Nitakupatia kadi ya kuufungulia mlango wa ofisi ya Osmund pamoja na namba za siri ambazo zitakuwezesha kuingia katika kompyuta yake na utafahamu kila kitu kuhusiana na Dr Burke” akasema John na kumuelekeza afungue kasiki lililokuwa ukutani akampatia kadi maalum ya kufungulia mlango wa ofisi ya Osmund pamoja na Josh namba za siri ambazo angezitumia katika kuingia katika kompyuta ya Osmund.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Mzee nashukuru sana kwa kuniamini.Nitafanya kama ulivyoniagiza.” akasema Josh na kutoka

“ Osmund alikosea sana kunidharau na kuamini kwamba sina uwezo wa kufanya chochote kwa sababu tu niko kitandani na sina nguvu za kutembea lakini alisahau kwamba akili yangu bado ina nguvu sana na ninaweza kufanya mambo makubwa tofauti na anavyofikiri.Nilimweleza Ossy kuhusu Dr Burke lakini hajanielewa.Alisahau kwamba pamoja na kwamba ninaumwa ,mimi ndiye niliyeanzisha Team SC 41 na bado kuna vijana wengi wanaoendelea kunitii.” akawaza John na sura ya Dr Burke ikamjia .

“Dr Burke !!..akasema kwa sauti ndogo na kumbukumbu zikamrejesha mbali sana

“ I killed his father.Dr Burke aliapa kulipa kisasi kwa wote waliohusika katika kifo cha baba yake” akawaza John na kumbu kumbu zikamrejesha jijini Washington DC





WASHINGTON DC



1988



Gari la kifahari linafunguliwa geti na kuingia katika jengo moja kubwa na la kupendeza.Baada ya kuegeshwa kijana mmoja aliyekuwa amevalia suti nzuri nyeusi akalisogele gari lile na kuufungua mlango na kijana mmoja mtanashati aliyevalia nadhifu akashuka toka ndani ya ile gari



“ This way Sir” kijana Yule aliyeufungua mlango akamuelekeza kijana Yule aliyeshuka garini ka adabu.Wakaingia ndani ya lile jengo na kulifuata varanda moja refu hadi katika mlango mmoja wa kioo,akaufungua kisha wakaingia ndani,na kuingia tena katika chumba kingine ambamo kulikuwa na watu watano.Wote walionekana kuwa walikuwa wakimsubiri kwa hamu kubwa Yule kijana .



“John Mwaulaya !! akasema mmoja wa wale wazee na kuinuka akamkubatia John kwa furaha kubwa.

“ Karibu sana John.” Wale wazee wengine nao wakamsalimu John kwa furaha kubwa.

“ nashukuruni sana” akasema John na bila kupoteza muda wakaanza kikao



“ John tumekuita hapa kuna kazi ambayo unatakiwa uitekeleze mara moja.Kama unavyofahamu kwamba Team SC41 inafanya kazi kwa siri kubwa kwa ajili ya kuyalinda maslahi ya Marekani katika afrika ya mashariki.Hata ndani ya serikali ya Marekani ni watu wachache sana wanaofahamu kuhusiana na suala hili.Kuna Seneta mmoja anaita Joe Burke kutoka chama cha Republican,huyu amepata taarifa za kuwapo kwa Team SC41 kwa hiyo kwa sababu zake za kisiasa anataka kuja kuliweka wazi suala hili kwa raia wa Marekani.Najua wamarekani wengi hawatafurahishwa kabisa na suala hili na ni suala linaloweza kuleta mgawanyiko mkubwa kwa raia wa marekani.Hatutaki suala hili lifahamike.Hatutaki Team SC41 ijulikane” Akasema Profesa Edward McNill .Akatulia akamuangalia John halafu akaendelea

“ Hivi tunavyoongea Joe Burke amekwenda afrika mashariki kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa vyama vya upinzani ili waweze kulipinga suala hili kwa kuanzisha maandamano makubwa.Kwa taarifa tulizonazo tayari amekwisha zungumza na kiongozi wa chama kikubwa cha upinzani nchini Tanzania ndugu Elisante mkulwe na mazungumzo yao yanaendelea na siku ya jumamosi anatarajiwa kuelekea nchini Kenya kuzungumza na viongozi wa upinzani wa kule na kisha ataelekea Uganda ili kuwasha wishi viongozi hawa waweze kulianika suala hili kwa pamoja.Endapo jambo hili litafanikiwa basi litampandisha sana kisiasa seneta huyu ambaye anatajwa sana katika watu wanaopewa nafasi kubwa ya kuwania urais wa Marekani hapo baadae.Ili kulizima jambo hili,seneta Joe Burke na viongozi wa upinzani ambao tayari amekwisha ongea nao lazima wote wauawe.Hilo ndilo jambo kuu tulilokuitia hapa “ akasema Edward McNill na kuifungua droo yake akatoa picha mbili.Moja ikiwa ya seneta Joe na nyingine ya Elisante Mkulwe akampatia John.

John Mwaulaya akafumba macho baada ya kumbu kumbu ile kumjia



“ Ubongo wangu umejaa kumbu kumbu za mauaji niliyowahi kuyafanya huko nyuma.Kumbu kumbu hizi zinanjia kama jinamisi na kunitesa mno” akawaza John





******





Mathew na Anitha waliwasili katika jengo lililojengwa maalum kwa maegesho ,maarufu kama maegesho ya mchina kutokana na jengo hili kumilikiwa na raia wa china.Mathew akatoa simu na kumpigia Eva

“ Hallow Eva,umefika wapi?

“ Ninakaribia kufika katika maegesho ya mchina,niko hapa katika hospitali ya macho”

“ Ok sisi tayari tumekwisha fika.Imetulazimu kutumia piki piki ili kuwahi kufika kwa sababu ya foleni kubwa.Ukifika pitiliza moja kwa moja ndani hadi juu halafu sisi tutashughulika nagg wale jamaa wanaokufuatilia” akasema Mathew na kukata simu

Mathew na Anitha waliendelea kusubiri pale nje ya jengo lile na baada ya dakika kumi na mbili gari moja likawasha endiketa kuashiria kwamba linakata kona kuingia katika jengo lile la maegesho,na mara simu ya Mathew ikaita.Alikuwa ni Eva



“ Mathew ninaingia sasa katika jengo,gari yangu umeiona? Ninatumia hii BMW nyekundu”

“ Nimekuona Eva.Jamaa wao wanatumia gari gani?



“ Wanatumia Harrier yenye rangi nyeusi”

“ Ok Good ,Endelea kwenda mpaka juu kabisa.UKifika egesha gari na utoke garini ujifiche mahala ili tujue lengo lao ni nini” akasema Mathew na kukata simu.Gari la Eva likaingia ndani ya jengo lile na baada ya dakika mbili Toyota Harrier lenye rangi nyeusi nalo likakata kona kuingia ndani ya jengo lile.



“ Jamaa wenyewe ni hawa hapa.Its show time” akasema Mathew akaiwasha piki piki yake nao wakaingia ndani ya jengo lile wakiifuata ile gari iliyokuwa ikimfuatilia Eva.





Lile gari lililokuwa likimfuatilia Eva ,lilipanda ghorofani na nyuma yake walikuwepo Mathew na Anitha wakiwa na piki piki

“Watu hawa ni akina nani? Kwa nini wanamfuatilia Eva? Akaendelea kujiuliza Mathew.Wakapanda hadi walipofika ghorofa ya pili ,watu wale wakasimamisha gari na mmoja wao akashuka na kuangaza angaza katika magari yaliyokuwa yameegeshwa ,alikuwa akilitafuta gari la Eva.Alipolikosa akarejea garini wakaendelea na kupanda juu zaidi.Mathew akachukua simu na kumpigia Eva

“ Eva jamaa wanapandisha huko juu.Egesha gari kisha shuka ujibanze mahala.Sisi tunaendela kuwafuatilia ili kufahamu nini lengo lao.” Akasema Mathew

“ Tayari nimekwisha shuka nimejibanza katika chumba cha mlinzi “ akasema Eva

Mathew na Eva waliendelea kulifuatilia lile gari hadi maegesho ya juu kabisa.Watu watatu wakashuka toka ile gari.Walianza kuangaza angaza huku na kule kana kwamba kuna gari walikuwa wanalitafuta.Mawazo ya Mathew yalikuwa sawa kwani watu wale walikuwa wakilitafuta gari la Eva.Jamaa mmoja akachungulia ndani ili kuona kama kuna mtu lakini hakukuwa na mtu ndani.Akatoa kidude Fulani kidogo na kukinasisha chini ya gari la Eva kwa haraka.Mathew ambaye macho yake alikuwa ameyaelekeza kwa Yule jamaa alikiona kile kitendo

“ Kuna kidede amekiweka katika gari la Eva.Ninahisi ni kifaa cha kumfuatilia na kuonyesha kila mahala alipo” akasema Mathew kwa sauti ndogo wakiwa wamejificha nyuma ya gari moja

Baada ya kuweka kifaa kile mtu Yule alirejea katika gari lao halafu wakaondoka.

“ Endesha piki piki tuendelee kuwafuata” akasema Mathew wakarukia piki piki yao na kuendelea kuwafuata wale jamaa.Mathew aliyekuwa nyuma akatoa simu na kumpigia Eva.

“ Eva tunaendelea kuwafuatilia wale jamaa ili tuwafahamu ni akina nani .Kuna kitu wamekitega katika gari lako nadhani ni kwa ajili ya kutaka kukufuatilia na kuzijua nyendo zako.Nataka tufahamu nini lengo la kutaka kukufuatilia na kujua kila mahala unakokwenda? “ akasema Mathew

“ Mathew nashukuru sana.Lakini watu hawa ni akina nani na kwa nini wanifuatilie? Akauliza Eva

“ Ni mapema sana kufahamu watu hawa ni akina nani na kwa nini wanakufuatilia .Kwa sasa endelea na kazi zako kama kawaida isipokuwa kitoe kifaa kile na ukibandike katika gari lolote la karibu Nitakupigia simu baadae kukufahamisha tumefikia wapi.Mpaka muda huo nitakapowasiliana nawe tena tafadhali chukua tahadhari” akasema Mathew na kukata simu

Waliwaendelea kuwafuatilia wale jamaa kwa ufundi sana bila ya wao kufahamu kama walikuwa wakifuatiliwa.Wale jamaa walizunguka sehemu kadhaa na hatimaye wakasimama katika mgahawa mmoja mkubwa ulioko kati kati ya jiji maarufu kama City centre.Wakashuka na kuelekea sehemu ya baa.Anitha na Mathew nao wakawafuata ndani ya ile baa,wakatafuta sehemu moja nzuri ambayo iliwawezesha kuwafuatilia wale jamaa vizuri.Waliagiza nyama choma na vinywaji baridi ,wakaendelea kula huku macho yao yakiwa makini kwa kila walichokifanya wale jamaa ambao walikuwa wakipata nyama choma na bia na waliendelea na maongezi yao bila wasi wasi

“ Mathew hawa jamaa hawaonekani kama wana mpango wa kuondoka hapa hivi karibuni.Wameagiza tena raundi nyingine ya vinywaji.Tutakaa sana hapa tukiwafuatilia na kupoteza muda mwingi ambao tungeutumia kwa kazi nyingine.Tunataka kujiingiza katika kazi nyingine wakati tayari tuna jukumu zito mbele yetu na bado hatujafika popote.Tumekwisha gundua lengo lao lilikuwa ni kumfuatilia Eva na anachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuongeza umakini na endapo atahitaji msaada wetu tena katika kuwafahamu zaidi watu hawa basi tutamsaidia baada ya kumaliza shughuli yetu ya msingi” akasema Anitha.Mathew bado aliendelea kuwakazia macho wale jamaa

“ Mathew are you listening to me? Akauliza Anitha

“ Anitha wait for a second” akajibu Mathew na kuendelea kuwakazia macho wale jamaa

Baada ya kama dakika tano hivi mmoja wa wale jamaa aliyekuwa amevaa suruali ya jeans ya bluu na shati jeupe akaitoa simu yake mfukoni ,alikuwa amepigiwa na mtu akabonyeza kituife cha kupokelea akaongea na alipomaliza akaufungua mkoba wake na kutoa simu ile kubwa aina ya Tablet akaelekezana jambo na wenzake wakagonganisha mikono ishara kwamba jambo lao limekwenda vizuri kisha Yule jamaa akatoka akiwa na ile tablet.

“ Nisubiri nakuja sasa hivi” akasema Mathew na kuinuka akatoka nje kumfuata Yule jamaa ambaye alielekea katika maegesho ya magari hadi katika gari moja aina ya Rav 4 rangi nyeusi.Kioo cha mlango wa dereva kikafunguliwa na ndani ya lile gari akaonekana mtu moja aliyevaa miwani myeusi.Jamaa aliyetoka ndani ya mgahawa akasalimiana na Yule jamaa ndani ya gari halafu wakaongea kidogo na akamkabidhi ile tablet.Yule jamaa wa ndani ya gari akaitazama tablet ile halafu wakaonekana kama wanaelekezana jambo Fulani na kisha akaiweka pembeni akafungua mkoba wake na kutoa bahasha ya khaki akamkabidhi Yule mwenzake ,kisha akafunga kioo cha gari lake na kuondoka.Mathew akampigia simu Anitha na kumtaka atoke mara moja.Bila kupoteza muda Anitha akatoka wakapanda piki piki na kuanza kumfuata yule jamaa aliyekuwa amepewa ile tablet

Toka katika mgahawa wa City Centre Yule jamaa alielekea hadi katika jengo Fulani zuri la ghorofa nne .Kabla ya kuingia ndani ya jengo lile kulikuwa na geti lililokuwa likilindwa na walinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi.Yule jamaa mwenye Rav 4 alipita pale getini bila matatizo na walipofika akina Mathew wakasimamishwa na askari ambaye shida yake ilikuwa ni kujua mahala walikokuwa wakielekea.

“ Tunamfuata huyu jamaa aliyeingia na gari sasa hivi”

“ Arnold? Akauliza Yule mlinzi

“ Ndiyo tunamfuata Arnold.Tumeongozana naye” akasema Mathew na Yule mlinzi akawaruhusu wapite na kuwalekeza sehemu ya kuegesha piki piki.

“ Hizi ni ofisi za kampuni gani? akauliza akauliza Anitha wakati wakishuka katika piki piki yao.

“ hata mimi sifahamu .We’ll find out soon” akasema Mathew halafu wakaanza kupiga hatua kuelekea nsdani ya jengo lile

Walifika katika sehemu ya mapokezi na kumkuta mwanadada mmoja mrembo aliyewasalimu kwa heshima huku uso wake ukpambwa na tabasamu mwanana.Naye alitaka kufahamu ni ofisi gani ya lile jengo akina Mathew walikuwa wanaelekea.

“ Tunaelekea katika ofisi ya Arnold” akasema Mathew huku akitabasamu na mara Arnold akaonekana akishuka ngazi..Mathew akatabasamu na kusema

“ Ouh mtu mwenyewe tuliyekuwa tunamfuata ndiye huyo anashuka”

“ Hallow Atnmold” akasema Mathew huku akimpa mkono kana kwamba anamfahamu vizuri.

“ Hallow “ akasema Arnold huku akitoa tabasamu lenye mshangao kidogo kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuonana na Mathew.

“ Arnold nina shida nawe ya kiofisi.Unatoka? akauliza Mathew

“ Yah ! ninatoka kidogo.Una shida gani? Akauliza Arnold

“Kama unatoka tunaweza tukaongelea hata nje” akasema Mathew kisha yeye na Anitha wakatangulia nje na kumuacha Arnold akitoa maelekezo Fulani kwa yule mwanadada wa mapokezi kisha akatoka na kuwafuata akina Mathew

“ Una shuda gani kaka? Halafu bado hatujafahamiana.Umetokea wapi?akauliza Arnold huku akionekana ni mwenye haraka sana ya kutaka kuwahi sehemu

“ Ninaitwa Mathew na yule dada anaitwa Anitha”

“ Ndiyo Mathew nikusaidie nini?akauliza Arnold

“ Arnold kwa kuwa una haraka can we talk in your car? Kuna kitu nataka kukuonyesha ” akasema Mathew huku akiingiza mkono mfukoni kana kwamba kuna kitu anataka kutoa.Arnold alisita kidogo lakini kwa kuwa alikuwa na haraka akaongozana na Mathew katika gari lake.Akafungua mlango na kungia garini

“Mathew nieleze shida yako.Nina haraka sana kuna mahala ninawahi” akasema Arnold huku akiwasha gari

“ Ghafla kwa kasi ya umeme ,Mathew akachomoa bastora toka katika mfuko wa koti na kumuwekea Arnold tumboni.Jicho likamtoka hakuamini alichokiona

“ Usithubutu kupiga kelele ndesha gari twende” akaamuru Mathew.Arnold alikuwa akitetemeka mikono akakanyaga mafuta na gari ikaanza kuondoka.Anitha akawasha pikipiki na kuwafuata.



******



Taarifa za Falviana kukimbizwa hospitali zilimfikia jaji Elibariki na kumstua sana.Bila kuaga mtu yeyote akaingia garini na kuondoka kuwahi hospitali

“ Flaviana alikuwa mzima kabisa na hakuonekana kuwa na tatizo lolote,nini kimemtokea na kusababisha akimbizwe hospitali? Akajiuliza Elibariki akiwa garini kuelekea hospitali

“ Inawezekana akawa alizidiwa baada ya kuona mwili wa mama yake? Lakini kama ni fahamu angepoteza kule hospitali tulipokwenda kuuchukua mwili na yeye na Anna wakapewa nafasi ya kutosha ya kuuaga mwili wa mama yao na aliweza kuhimili iweje aje apoteze fahamu huku uwanjani? Nitakwenda kufahamu huko huko hosspitali ,nini kimemtokea” akawaza Elibariki akiwa katika mwendo mkali akiwahi hospitali.Alipofika alipelekwa moja kwa moja katika chumba alichokuwa amelazwa Flaviana

“ Flaviana ..!! akasema Eli mara tu alipoingia mle chumbani na kumkuta mke wake akiwa amelala kitandani

“ Eli .!!! akasema Flaviana .Elibariki akamsogelea na kumbusu

“ Pole sana.Nini kimetokea?akauliza

“ Hata mimi sifahamu Eli.Sielewi nini kimetokea.Ninachokumbuka…..!!” akanyamaza kidogo na kusema

“Unakumbuka nini? Akauliza Elibariki

“Ninachokumbuka tukiwa pale uwanjani shughuli ikiendelea,alinifuata dada mmoja na kumiambia kwamba kuna mtu anahitaji kuniona katika gari la wagonjwa.Dada yule simfahamu lakini alikuwa amejitanda sare zilizovaliwa na akina mama pale msibani.Nikaongozana naye hadi tulipolikaribia gari la wagonjwa lililokuwa limeegeshwa pembeni ya uwanja mara nikahisi kizunguzungu na miguu ikaishiwa nguvu na macho yakashindwa kuona tena.Ninachokumbuka ni kwamba nilitaka kudondoka chini na watu Fulani wakanidaka na nilipozinduka nimejikuta hapa hospitali.Sielewi ni kitu gani kilinitokea na kunisababishia hali ile lakini nilikuwa mzima kabisa na sikuwa na tatizo lolote ”akasema Flaviana

“Pole sana mke wangu.Kwa sasa unajisikiaje?akauliza Elibariki

“Kwa sasa ninajisikia vizuri na madaktari wamesema hakuna tatizo hali yangu inaendelea vizuri na baadae nitaruhusiwa kurejea nyumbani nikapumzike” akasema Flaviana na mara daktari akaingia.Jaji Elibariki akamuuliza kuhusiana na kilichosababisha mke wake kupoteza fahamu ghafla

“ Tumempima lakini hatujaona tatizo lolote kila kitu kinafanya kazi vizuri.Inawezekana hali hii ikawa ilisababishwa na vitu vingine kama vile uchovu mwingi,msongo wa mawazo,n.k.Anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika .” akasema daktari na kuendelea kumpima Flaviana na alipohakikisha kila kitu kiko vizuri akatoka

“ Flaviana dada huyo aliyekwambia kwamba unahitajika katika gari la wagonjwa unaweza kumkumbuka ukimuona?

“ Ndiyo ! nikimuona lazima nitamkumbuka”

“ Alikueleza ni nani aliyekuwa anakuhitaji katika gari hilo la wagonjwa?

“ Hapana hakunieleza nilikuwa naitwa na nani lakini nilimuamini kutokana na na muonekano wake.”akasema Flaviana .Jaji Elibariki aliyekuwa amekaa kitandani pembeni ya mkewe akamtazama na kusema

“ Kuanzia sasa tafadhali usimuamini mtu yeyote yule ambaye humjui.Hata wale ambao unawafahamu kuwa nao makini sana.Dr Flora amefariki katika mazingira yenye utata mkubwa na mpaka hapo tutakapobaini ni akina nani waliosababisha kifo chake tunatakiwa tuwe makini sana”akasema Jaji Elibariki

“Unayoyasema ni ya kweli kabisa.Inanibidi kuwa makini sana “akasema Flaviana

“Ni nani lakini aliyekuwa anataka kuonana na Flaviana? Akajiuliza jaji Elibariki

“Suala hili linanipa mashaka sana.Nina wasiwasi sana na maisha ya mke wangu.Watu waliomuua Dr Flora wako ndani ya ikulu na hawatasita kufanya kila linalowezekana ili kujilinda wasijulikane.We’re in great danger.I have to talk to Mathew about this ”akawaza Elibariki akachukua simu yake na kumpigia Mathew lakini simu ikaita bila kupokelewa,akapiga tena bado haikupokelewa



********

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

John Mwaulaya alikuwa ameiweka mikono kifuani pake.Alionekana kuwa katika mawazo mengi

“Hali yangu inazidi kuwa dhaifu na ninafahamu kwamba sintopona ugonjwa huu lakini siko tayari kuja kuuliwa na mkono wa Dr Burke.Nina hakika Josh atafanikiwa kumuwahi kabla hajaniwahi. Nilifanya makosa makubwa kumpendekeza Osmund katika nafasi kubwa na kuwaacha vijana watiifu kama Josh.Endapo atafanikiwa kumuondoa Burke ,nitajitahidi kwa kila niwezavyo kabla pumzi zangu hazijakata kuhakikisha Josh anakuwa katika nafasi za juu kabisa ndani ya Team SC41”akawaza John na kumbukumbu zake zikamrejesha mbali

“ Bado naikumbuka siku ile nilipomuua seneta Joe Burke na yule rafiki yake mwanasiasa Elisante.Ni miaka mingi imepita lakini nahisi ni kama jana .” akawaza John Mwaulaya akafumba macho na kuikumbuka siku aliyofanya mauajiya seneta Joe Burke baba yake na Dr Burke

Kiza kimenza kutanda jijini Dar es salaam .Pilika pilika za jioni watu wakishughulika na usafiri wa kuwarejesha makwao ziliendelea kama kawaida.Katika hoteli ya Salama Spring hali ilikuwa ni ya utulivu mkubwa.Watu waliendelea kupata vinywaji chakula na kuburudika na muziki wa bendi

Saa mbili kasoro dakika nane ,gari moja aina ya Nissan Patrol ikapita katika geti la kuingilia hotelini hapo na kuelekea moja kwa moja katika maegesho.Haraka haraka mlango ukafunguliwa akashuka kijana mmoja na kuwahi kuufungua mlango wa mbele.Mtu mmoja mzee wa makamo akashuka na kuongozana na yule kijana kuelekea ndani ya hoteli.Huyu alikuwa ni Mr Elkisante kiongozi wa chama kikubwa cha siasa nchini ambaye amefika katika hoteli hii kukutana na seneta Joe Burke toka chama cha Republican cha nchini Marekani

Wakati Dr Elisante akiingia hotelini hapo hakuwa na habari kwamba kuna watu wanne waliokuwa wakimfuatilia.Akiwa ameongozana na mlinzi wake mmoja walielekea hadi katika chumba cha Seneta Burke

“ He’s in” John Mwaulaya akiwa amekaa katika sehemu ya baa akipata kinywaji akiwa amezungukwa na warembo wawili ,alitaarifiwa na kijana wake aliyekuwa amekaa ghorofa ya kwanza kuhusiana na kuwasili kwa Dr Elisante.Mara tu alipoipokea taarifa iIe John akainuka na kuwaomba wasichana wale waendelee kupata kinywaji na angerejea baada ya muda mfupi,kisha akatoka

Mara tu baada ya kuachana na wale warembo John akatoa simu na kumpigia mmoja wa vijana wake na bila kuchelewa kijana Yule akampa maelekezo

“ John ,nenda ghorofa ya pili ingia chumba namba 108,utakuta kila kitu tayari kimeandaliwa .Chumba cha Seneta Burke ni namba 123 ghorofa ya nne” akasema Scola muhudumu wa hoteli hii ambaye ni mmoja kati ya vijana wa John mwaulaya na ndiye alifanikisha mpango huu kwa kiasi kikubwa

Kwa mwendo wa kujiamini John akatembelea hadi chumba alichoelekezwa,akaangaza kama kuna mtu yeyote ambaye alikuwa anamfuatilia kisha akajitoma ndani ya ile chumba ambacho mlango wake ulikuwa wazi.Juu ya kitanda kuliwekwa suti nyeusi ,shati jeupe na tai nyekundu mavazi ambayo huvaliwa na wahudumu wa kiume wa hoteli hii.Haraka haraka akavua nguo zake na kuvaa zile sare za wahudumu akajitazama katika kioo alionekana kama kweli muhudumu wa hoteli .Ndani ya chumba kile kulikuwa na torori la kubebea vyakula na vinywaji lililokuwa na chupa kadhaa za vinywaji.Akaiweka bastora yake yenye kiwambo cha sauti chini ya kitambaa cheupe kilichofunika lile torori na kuanza kulisukuma akatoka na kupanda hadi ghorofa ya nne.Kila aliyekutana naye hakumtilia shaka hata kidogo kama si muhudumu wa hoteli ile.

John mwaulaya akafika hadi katika mlango wa chumba cha Seneta Burke akagonga na mlango ukafunguliwa na mlinzi wa Dr Elisante

“ Halow’ John akamsalimu yule muhudumu

“ Hallow ,nikuidie nini? Akauliza yule mlinzi

“ Nimeelekezwa nilete vinywaji katika chumba hiki” akasema John

“ Umeelekezwa na nani?

“ Kuna simu imepigwa na kuagiza vinywaji viletwe “ akasemaJohn. Mlinzi yule akamtazama John kwa makini na kumuomba asubiri palepale ili akamuulize bosi wake kama ni kweli vinywaji vimeagizwa.Kitendo cha kumpa mgongo John ni kosa kubwa alilolifanya yule mlinzi.Hazikupita hata sekunde tano kwa kasi ya ajabu John akaichukua bastora yake na kumiminia risasi mfululizo yule mlinzi ,ambaye alianguka chini .Haraka haraka John akaliingiza ndani lile torori la vinywaji na kufunga mlango.Chumba alichopanga seneta Burke kilikuwa na vyumba vitatu yaani sebule chumba cha chakula na chumba cha kulala.Sauti za watu wakijadiliana jambo zilisikika katika chumba cha kulia chakula.Hakutaka kupoteza muda akaufungua mlango ule kwa kasi na kujitoma ndani.Kitendo kile kiliwastua sana wazee wale waliokuwemo mle ndani.Kufumba na kufumbua bila hata kutamka neneo moja John akaanza kuifanya kazi iliyompeleka mle,aliwamiminia risasi wazee wale ,Seneta Joe Burke na DrElisante wakaanguka chini hawakuwa na uhai tena,Risasi nyingi zilizotoka katika bastora mbili za John zilizokuwa na viwambo vya sauti ziliwasambaratisha na kuwaharibu vibaya.Bila kupoteza hata sekunde moja John akakusanya makaratasi yote yaliyokuwapo pale mezani,akayapakia katika sanduku dogo akaenda chumbani na kuchukua kompyuta ndogo ya seneta Burke pamoja na kila kitu ambacho alikiona kinafaa kuchukuliwa halafu akaufunga mlango na kurejea katika chumba kile alichoacha mavazi yake akavua zile nguo za wahudumu wa hoteli akaziweka katika sanduku dogo na kuondoka.

“That’s how I killed seneta Burke.Baada ya miaka mingi kupita mwanae anakuja kulipiza kisasi,he’s coming to kill me”

Akawaza John Mwaulaya



Arnold alimtazama Mathew machoni na kugundua kwamba hakuwa akihitaji masihara.Aliogopa sana.

“Brother unanipeleka wapi? Kama una shida ya pesa tafadhali naomba uniambie” akasema Arnold huku akitetemeka na uso wake tayari ulikwisha loa jasho

“ Drive !..akasema Mathew kwa ukali.Mita kama mia tano toka waliache jengo lile Mathew akafanya kitu kimoja ambacho Arnold hakuwa amekitegemea.Kwa kasi ya ajabu alimpiga pigo moja kichwani kwa kitako cha bastora na Arnold akapoteza fahamu.Mathew akaudaka usikani wa gari na kulizuia gari lisiyumbe na taratibu akaliongoza gari hadi pembeni ya barabara akalisimamisha .Hakuna aliyeweza kuona kilichokuwa kinatendeka ndani ya ile gari kutokana na kuwa na vioo vyeusi.Anitha aliyekuwa analifuatilia gari lile kwa nyuma naye alisimamisha piki piki na kujiweka tayari kwa chochote ambacho kingejitokeza

Kwa haraka Mathew akachukua waya na kumfunga Arnold mikono na miguu halafu akamrushia katika kiti cha nyuma akaukalia usukani na kuliwasha gari akaendelea na safari

“Huyu jamaa ni nani?Mbona haonekanai kama nimtu hatari? Mbona hana silaha yoyote? Akajiuliza Mathew

“ Tutapata majibu muda si mrefu” akawaza Mathew na safari ikaendelea hadi nyumbani kwake.Wakamtoa Arnold na kumuingiza katika chumba kilichokuwa na kitanda cha chuma.Wakamlaza juu ya kile kitanda

“Huyu jamaa haonekani kama ni mtaalamu wa mambo haya.Nimempekua na hana silaha yoyote.Katika mkoba wake kuna vitu vya kawaida tu pamoja na ile tablet aliyopewa na wale jamaa kule City centre”akasema Mathew

“ Hata mimi ninahisi hivyo .Haonekani kama ni mtu anayefahamu chochote.Lakini lazima tumfahamu ni nani na nini lengo la kumfuatilia Eva.”akasema Anitha

“ Inawezekana akawa anatumiwa na watu Fulani.Anatakiwa ahojiwe na aseme kila kitu” akasema Noah.

Mathew akatoka mle chumbani na baada ya muda akarejea kiwa ameshika kitu Fulani mkononi mithili ya dawa,akakifungua na kukiweka katika pua za Arnold na baada ya sekunde kadhaa Arnold akapiga chafya mfululizo.Akafumbua macho na kujikuta ndani ya chumba akiwa amelazwa kitandani na kufungwa mikono.Akaangaza huku nahuku na kumbu kumu za nini kilichotokea zikamjia

“ Mmenileta wapi? Ninyi ni akina nani? Mnataka nini kwangu? Kama mnahitaji fedha niambeni m,mnataka kiasi gani niwapatie? Akasema Arnold huku machozi yakimtoka

“ Relax Arnold.Hatutakufanya kitu chochote kibaya .Kuna mambo tunayohitaji kuyafahamutoka kwako na baada ya hapo tutakuachia uendelee na shughuli zako lakini endapo utashindwa kutupatia kile tunachokihitaji basi itatulazimu kutumia nguvu ”

“ Tafadhali naombeni mnifungue ninasikia maumivu.Nitawapa kila mnachokihitaji lakini mniachie huru.Mimi si mtu mbaya .” Akasema Arnold.Mathew akatazamana na Anitha na kumpa ishara amfungue mikono

“ Arnold kuna kitu kimoja tu tunachokihitaji toka kwako”

“Kitu gani ? Pesa? Gari ? Chukueni chochote lakini mniache mzima” akasema Arnold

“ Hatuna shida na pesa Arnold.Tunahitaji utuambie ukweli.Kuna vijana Fulani wanne ambao mmoja wao ulikutana naye pale City center na akakupa kifaa chenye muundo kama tablet walikuwa wakimfuatilia dada mmoja anaitwa Eva.Vijana wale walitega kifaa Fulani katika gari la Eva ambacho hutuma taarifa katika ile tablet.Tunataka kufahamu ni kwa nini mnamfuatilia Eva? Kwa nini mnataka kujua mizunguko yote ya Eva? Ukitupa majibu ya kuridhisha basi tutakuachia huru uende zako lakini endapo utatudanganya ni wazi itatulazimu tutumie nguvu.Ninakushauri usitufanye tufike huko .Utapata maumivu makali sana ambayo hujawahi kuyapata toka uzaliwe” akasema Mathew

“ Jamani naombeni msitumie nguvu.Nitawaeleza chochote mnachokitaka” akasema Arnold

“ Kusema ukweli mimi simfahamu huyo msichana Eva na wala sijawahi kumuona.” Akasema Arnold

“ Tafadhali Arnold usitulazimishe tutumie nguvu .Sipendi tufike huko .Tueleze ukweli kwa nini mnamfuatilia Eva?

“ Nawaelezeni ukweli ndugu zangu,huyo Eva simfahamu na wala sijawahi kumuona.Ninaomba mniamini ndugu zangu.Mimi ni mtaalamu wa program za kompyuta na nina ofisi yangu katika jengo lile mlikonikuta.Ninachofahamu mimi kuhusu huyu msichana unayemuita Eva ni kwamba wiki iliyopita walikuja watu Fulani wawili ofisini kwangu na kuniomba niwafanyie kazi yao fulani na wakaahidi kunilipa pesa nyingi kama nikiifanya wanavyotaka.Waliniambia kwamba wanahitaji niwatengenezee program ya kompyuta kwa ajili ya kumfuatilia mtu Fulani bila ya yeye kufahamu kama anafuatiliwa.Waliahidi kunipa shilingi million kumi na mbili endapo ningefanikisha kazi hiyo ambayo ilionekana ni ya muhimu sana kwao.Sijawahi kuifanya kazi yenye malipo makubwa kama hii kwa hiyo nilishawishika kukubali kufanya kwa sababu nilikuwa na uwezo wa kuifanya .Nilitengeneza program ambayo ingeweza kuonyesha mizunguko yote ya mtu huyo waliyemtaka.Baada ya kuikamilisha program hiyo kilichofuata ilikuwa ni kukiweka kifaa hicho katika gari la mlengwa.Ili kuifanyakazi hiyo ilinilazimu kuwakodisha wale vijana mliwaona kule City centre kwaniwao ni wazoefu wa mambo kama hayo.Walifanikiwa kukiweka kifaa kile katika gari la Eva na programu yetu ikafanya kazi vizuri jinsi inavyotakiwa.Hicho ndicho ninachokifahamu .Huyo Eva simjui na wala sijawahi kumuona.” akasema Arnold

“ Baada ya kuikamilisha kazi uliyopewa nini kitafuata? Akauliza Anitha

“ Kinachofuata baada ya hapo ni kuwakabidhi kazi yao na wao kunipatia malipo yangu yaliyobaki.”

“Hao jamaa walikupa sababu ya kwanini wanataka kumfuatilia Eva? Akauliza Noah

“ Hapana hawakunieleza chochote kuhusiana na sababu ya kumfuatilia huyo mtu.” Akasema Arnold

“ saa ngapi utaonana nao ili uwakabidhi kazi yao?

“Tumepanga tukutane leo saa moja jioni.Wamesemawatanipgia simu kunipa maelekezo ya mahala kwa kukutana” akasema Arnold

“ Ok vizuri.sasa utaendelea kukaa hapa hadi jioni na tutakwenda sote katika hayo makabidhiano na halafu tutakuacha uende zako.Sisi hatuna shida na wewe hata kidogo.Sisi shida yetu ni hao jamaa waliokupa hiyo kazi” akasema Mathew

“ Tafadhalini jamani nimekwisha waeleza kila kitu mlichokuwa mnataka ,niachieni basi niende zangu” akasema Arnold

“ Usijali Arnold,tutakuachia uende zako ,lakini hadihapo tutakapohakikisha kwamba makabidhiano yamefanyika” akasema Mathew halafu wakaufunga mlangowa kile chumba wakatoka wakaingia katika chumba cha kupangia kazi .

“Wakati tunasubiri kuonana na Elibariki ili kuliweka sawa suala la Peniela,limeibuka suala hili la watu hawa wanomfuatilia Eva na hatuwezi kuliacha.Eva ni rafiki yangu mkubwa na wa miaka mingi na ni mtu ambaye nina hakika anaweza akawa ni wa msaada mkubwa sana kwetu .Ametusaidia katika kulifanikisha suala lile la kuipata ripoti ya kifo cha Dr Flora.Bila yeye tusingeweza kumpata kanali Adolf.Kwa hiyo wakati tunamsubiri Elibariki naombeni mnisaidie kuwabaini watu hawa ni akina nani na nini wanakitafuta kwa Eva? Nina imani kuna kitu tunaweza kukigundua hapa” akasema Mathew

“ Mathew ! akaita Noah

“ Wewe ni rafiki yangu mkubwa na ni kwa msaada wako nimefika hapa nilipo.Umenitoa mbali sana.” Akanyamaza kidogo halafu akaendelea

“ Umetuita hapa ili tukusaidie kazi ya kutafuta nani muuaji wa Edson, Lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda sielewi ni kazi gani iliyotuleta kwani kila siku kazi zinabadilika na hatuelewi kazi ya msingi ni ipi.Jana tumefanya kazi isiyotuhusu na ilibaki kidogo tungepoteza maisha.Leo tena imeibuka kazi nyigine mpya.Mathew tumeyaweka maisha yetu rehani kwa ajili ya kukusaidia ,tuko hapa kwa ajili ya kusaidiana nawe kama ulivyotuomba lakini naomba utuweke wazi ,tunakusaidia kufanya kazi ipi? Akauliza Noah

“Noah !!...akasema Anitha

“ No ! Anitha,Noah ana haki ya kuuliza .Ni kweli niliwaiteni kwa ajili ya kunisaidia kufanya uchunguzi wa suala la Edson lakini kadiri tunavyoendelea na uchunguziwetu mambo mengine zaidi yanaibuka .Ni sawa na unapotafuta madini.Ili uyafikie utakutana na vizingiti vingi kama mawe n.k lakini kwa vile nia yako nikupata madini basi itakulazimu kuyaweka pembeni ili upate njia ya kukufikisha yalipo madini.Hilo ndilo linalotutokea sisi.Tunafanya uchunguzi wa kifo cha Edson tufahamu ni nani alimuua na kwa nini,lakini ndani ya uchunguzi huo yanaibuka mambo mengine mfano Team SC41.Hatuwezi kuacha kuchunguza kila kitu kinachoibuka mbele yetu ambacho tunahisi kinaweza kuwa na mahusiano na kifo cha Edson.Suala lililojitokeza jana na hili la leo ni mambo ambayo nisingeweza kukataa kuyafanya.Elibariki ndiye aliyetupa kazi hii ya kuchunguza kuhusu kifo cha Edson na ndiye anayetulipa kwa hiyo alipokuja na kazi nyingine nakuomba tumsaidie ili kuwa ngumu kukataa.Hata hivyo tumefanikiwa kugundua jambo kubwa sana kuhusiana na kifo cha Dr Flora mke wa rais.Leo hii Eva naye amepatwa na matatizo.Eva ni rafikiyangu wa siku nyingi na amekuwa ni mtu mwenye msaada mkubwa kwangu.Ni yeye aliyetusaidia tukampata kanali Adolf jana na mkumbuke pia kwamba tulikuwa na makubaliano kwamba atanisaida kumpata kanali adolf lakini naye ana kazi yake ambayo anahitaji msaada na niliahidi kumsaidia.Leo hii amenipigia simu na kuniomba tena msaada kuna watu waliokuwa wakimfuatilia toka alipotoka nyumbani kwake.Ilikuwa vigumu sana kwangu kukataa kumsaidia .Kwa kujibu swali lako Noah ni kwamba bado hatujatoka nje ya kazi yetu ya msingi.Bado tunaendelea na uchunguzi kuhusiana na kifo cha Edson lakini hatuwezi kuachana na mambo madogo madogo yanayojitokeza wakati wa uchunguzi huo”akasema Mathew

“ Ninakuelewa Mathew .lakini je ni lini basi tutamaliza kazi hii kama tukiendelea na mpango huu wa kuifanya kila kazi inayojitokeza mbele yetu ? Akauliza Noah

“Noah Please stop that !!..akasema Anitha ambaye alionekana kukerwa na maswali yale ya Noah.

“ I’m sorry Anitha but I need to know .Jana almanusura nipoteze uhai wangu kwa hiyo nahitaji kufahamu kuhusu mpangilio maalum wa kazi tunazozifanya.”akasema Noah

“Usihofu Noah.Kazi itaendelea hata kama hautakuwepo.Inavyoonekana hauko tayari kuendelea na kazi hii.Endapo unahitaji kuondoka uko huru kufanya hivyo.Simzuii mtu yeyote kuondoka.Nina watu wengi ambao wanaweza wakanisaidia katika kazi hii lakini niliona ninyi ni chaguo langu la kwanza ndiyo maana nikawaita.Kwa hiyo kama kuna yeyote kati yenu ambaye hajisikii kuendelea kuifanya kazi hii anaweza akaondoka” akasema Mathew

“ Please Mathew don’t say that.You know I’m always with you.Tumefanya kazi nyingi pamoja na tumepitia hatari nyingi sana kuliko hata hizi za sasa.kwa hiyo siwezi katu kukuacha .Noah kama unajisikia kutaka kuondoka you can just leave!! Akasema Anitha

“Jamani naomba msinielewe vibaya .Sina maana ya kwamba ninataka kuondoka.Siwezi kuondoka na kuwaacha kwani hii ni kazi yetu sote.Samahani kama niliwakera kwa maneno yangu .Tusipoteze muda tuendelee na kazi.”akasema Noah

“Kabla hatujaendelea na kazi nahitaji kufahamu who is with me ? akauliza Mathew

“ I’m with you Mathew” akasema Anitha

“ Me too “ akasema Noah

“ Ok good.Nawashukuruni sana .Saa moja jioniya leo Arnold anakwendda kuonana na watu waliompa kazi na kuwakabidhi kile kifaa ambacho kazi yake ni kuonyesha mienendo yote ya Eva.Katika tablet ile kuna ramaniyote ya jiji la Dar es salaam kwa hiyo kila sehemu aliko Eva ataonekana.Kitu cha kufanya Anitha utaichukua tablet hii na kuiwekea programu nyingine ya siri ya kutuwezesha sisi kuifuatilia.Arnold atakabidhiana nao na baada ya hapo sisi tunatakiwa kuwafuatilia watu hao na kuwafahamu ni akina nani na nini lengo lao kwa Eva.Can you do that Anitha?akauliza Mathew

“Yes I can.Ni kazi ndogo sana hiyo kwangu”akasema Anitha

“Ok thank you.Do it” akasema Mathew na kutoka akaelekea chumbani kwake na kumpigia simu Eva

“ Halow Mathew” akasema Eva baada ya kupokea simu

“ Eva unaendeleaje?

“Ninaendelea vizuri Mathew.Nipe habari.Mmegundua nini kuhusu wale jamaa?

“ wale jamaa hawakuwa na hatari yoyote,walipewa kazi ya kukiweka kifaa kile cha kukufuatilia katika gari lako na kazi yao ikaisha.Tumempata mtu aliyetengeneza program ile na amedai kwamba alipewa kazi hiyo na watu wawili ambao waliahidi kumlipa pesa nyngi.Kwa namna Programu hiyo ilivyotengezwa ni kwamba kifaa kile kilichowekwa katika gari lako hutuma taarifa katika kifaa kingine muundo wa tablet ambacho kina ramani nzima ya jiji la Dar es salaam na hivyo kila sehemu utakayokwenda utaonekana .”

“ watu hao ni akina nani? Na kwa nni watumie gharama kubwa hivyo kunichunguza? Mathew nimeanza kuingiwa na woga .Inaonekana maisha yangu yako hatarini.Inaoenekana hawa jamaa ni watu wanaonifahamu sana”

“Bado hatujawafahamu watu hawa ni akina nani lakini hautapita usiku wa leo kabla ya kuwafahamu ni akina nani.Mpaka wakati huo tutakapolifahamu lengo lao ni nini nakushauri chukua tahadhari kubwa”

“ Ahsante Mathew kwa msaada wako mkubwa.Ninahamu sana ya kuwafahamu watu hawa ni akina nani na kwa nini wanamfuatilia”

“ Usijali Eva.Nitafanya kila linalowezekana ili kuwafahamu watu haoi” akasemaMathew na wakati huo huo ikaingia simu ya jaji Elibariki.Akamuomba Eva akate simu ili aweze kuipokea

“ Hallow Elibariki “akasema Mathew

“ Mathew utanisamehe nilishindwa kufika hapo nyumbani mchana kuna tatizo lilitokea.Mke wangu alipoteza fahamu ghafla na kukimbizwa hospitalini.Lakini mazingira ya kupoteza kwake fahamu yananipa shaka sana”

“ Ilikuaje hadi akapoteza fahamu? Akauliza Mathew

“ Wakati shughuli ya kuuaga mwili wa Dr Flora zikiendelea katika viwanja vya ukombozi,mke wangu alifuatwa na mtu Fulani na kumwambia kwamba anahitajika katika gari la wagonjwa na alipoelekea huko alijikuta akipoteza fahamu na kukimbizwa hospitali.Mathew mazingira ya tukio hilo yanatia shaka sana”

“ Ni kweli Mathew,mazingira hayo yanatia shaka sana .Ninachokuomba kwa sasa chukua tahadhari kubwa.Watu waliomuua Dr Flora ni watu toka ndani ya ikulu na watafanya kila njia kuhakikisha kwamba hawajulikani.Yeyote yule ambaye ataonekana kuwa ni hatari kwao watamshughulikia kwa namna wanavyojua wao kwa hiyo mpe tahadhari mke wako awe makini sana kwa wakati huu.Elibariki tutaliongea vizuri zaidi suala hili jioni naomba ujitahidi usikose kuna jambo la muhimu sana la kuongea kuhusiana na Peniela”

“ Peniela? !..Jaji Elibariki akastuka

“ Kuna nini kuhusu Peniela?

“ Kuna jambo la muhimu sana la kujadili kuhusu Peniela”

“ Ok Mathew nitafika baadae lakini endapo nitashindwa kufika basi tutaonana kesho jioni au kesho kutwa kwa sababu kesho tutakwenda kumzika Dr Flora kijini kwao alikozaliwa na tutarejea jioni na endapo hatutaonana hiyo jioni basi tutaonana kesho kutwa asubuhi”

“ sawa Elibariki.Tutaonana utakapopata nafasi” akasema Mathew na kukata simu

“ Kuna kitu gani kinachoendelea pale ikulu ? Dr Flora ameuawa na nina uhakika mkubwa waliofanya jambo hili wako ndani ya ikulu.Nguvu kubwa imetumika kutaka kuzuia sababu ya kifo cha Dr Flora isijulikane lakini tumefanikiwa kujua nini kilimuua.Kuna kitu gani kinachoendelea ikulu? Lazima liko jambo kubwa hapa linalotakiwa kuchunguzwa.Kwa vile suala hili liko tayari mikononi mwa rais basi nina hakika litashughulikiwa ipasavyo.Kazi yangu mimi ilikuwa ni kuchunguza na kuwapa majibu” akawaza Mathew na kuelekea katika chumba cha kulia chakula .Alihisi njaa.Noah aliyekuwa amebaki nyumbani alikwisha andaa chakula

“ Watu hawa wanaomfuatilia Eva ni akina nani? Nafahamu Eva ana fanya kazi kwa siri katika idara ya usalama wa taifa.lazima kuna wau watakuwa wanataka kumchunguza.Hizi kazi niza hatari sana.Siku zote unaishi kama ndege.” Akawaza Mathew na mara Anitha na Noah wakaingia kujumuika naye pale mezanihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Anitha umefikia wapi kuhusu ile program ?

“ Ninaendelea na hiyo kazi .Lakini huyu jamaa Arnold anaonekana ni mtu anayeifahamu sana kompyuta .Nimeangalia namna alivyoitengeneza ile program dah ! yuko vizuri sana” akasema Anitha

“ Nimezungumza na Elibariki kwamba atajitahidi kufika jioni ya leo ili tuweze kuongea naye kuhusu lile suala la Peniela.Yeye ndiye tutakayemtumia katika kumchunguza Peniela.Peniela lazima kuna kitu anakifahamu kuhusiana na kifo cha Edson na Team SC41.Ili tuufahamu ukweli yatubidi tumfanyie uchunguzi mkubwa sana na nina hakika yeye ndiye atakayetuongoza kwenye ukweli ”akasema Mathew





Jua limeanza kupungua nguvu yake kuashiria kwamba siku inaelekea ukingoni.Shughuli ya kuuaga mwili wa Dr Flora ilimalizika katika viwanja vya ukombozi halafu ukapelekwa katika makazi binafsi ya rais ambako ungelala kule kabla ya kusafirishwa kesho yake asubuhi kuelekea kijijini alikozaliwa kwa mazishi.Zoezi lilichukua muda mrefu zaidi ya ilivyokuwa imetazamiwa kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kumuaga mwanamama huyu ambaye katika kipindi cha uhai wake alijitoa sana katika kuwakomboa kiuchumi wanawake na vijana.

Nyumbani kwa rais mwili wa Dr Flora uliwekwa katika chumba maalum ambako watu mbali mbali ambao hawakupata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho katika viwanja vya ukombozi walikuwa wanaendelea na zoezi hilo.Watu walikuwa wengi sana na ulinzi ulikuwa mkali

Saa kumi na mbili na dakika nane za jioni Dr Joshua akaingia katika chumba alichokuwamo Flaviana akiwa na mdogo wake Anna pamoja na binamu zao watatu

“ Flaviana pole sana.Nilipata taarifa kwamba ulipoteza fahamu ghafla ukakimbizwa hospitali.Nilimuagiza Amos aje akutazaame.Unaendeleaje hivi sasa?akauliza Dr Joshua

“ Ninaendelea vizuri sana baba.Madaktari walinipima wakasema kwamba uchovu wa mwili na mawazo mengi ndivyo vilisababisha hali ile kunitokea.Dr Amos naye ametoka hapa kunipima muda si mrefu na kila kitu kinakwenda vizuri hakuna shida yoyote” akasema Flaviana

“ Pole sana Flaviana hali kama hiyo ni ya kawaida sana kwa nyakati kama hizi.Unachotakiwa ni kujipa mapumziko ya kutosha.Tomorrow we’ll have a big day.I need you all to be strong” akasema Dr Joshua

“ Usihofu baba,tutajitahidi “ akajibu Anna

“ Ok ! Kuna watu ninaohitaji kuonana nao mida hii .Tutaonana baadae “ akasema Dr Joshua na kutaka kutoka Flaviana akamuita

“ baba vipi kuhusu lile suala ? Umekwishaanza kulifanyia kazi?

“ Ndiyo .Tayari limekwisha fanyiwa kazi na tayari nimepokea taarifa ya madaktari walioufanyia uchunguzi mwili wa mama yenu ili kujua chanzo cha kifo chake”

“ really? Akauliza Flaviana

“ Inasemaje? Wamegundua nini?akauliza Anna

“ Bado sijaifungua na kujua kilichomo ndani yake .Nilitaka tuifungue tukiwa wote kesho baada ya kurejea toka katika mazishi.Ile ni taarifa ya familia kwa hiyo inabidi ifunguliwe na sisi sote.Nadhani tulifanye zoezi hilo kesho baada ya kurejea toka katika mazishi”akasema Dr Joshua

“ Dady can we open it today? Akauliza Flaviana

“ It’s ok .Tunaweza kuifungua ripoti hiyo hata leo.Tukutane katika chumba cha maongezi baada ya dakika ishirini .Kuna watu ambao nahitaji kuonana nao sasa hivi”akasema Dr Joshua na kutoka akiwa ameongozana na walinzi wake.Baada tu ya Dr Joshua kutoka,Flaviana akachukua simu na kumpigia mumewe

“ Hallow Flaviana unaendeleaje? Akauliza jaji Elibariki

“Ninaendelea vizuri.Dr Amos ametoka hapa kunipima muda si mrefu na kila kitu kinaendelea vizur.Uko wapi ?

“ Niko na wafanyakazi wenzangu wamekuja kutupa pole kwa msiba” akasema Elibariki

“ Ok vizuri.Eli unaweza ukaja mara moja huku ndani ? Baba anatuhitaji kuna kitu anataka kutuambia” akasema Flaviana

“ Ok ninakuja” akasema jaji Elibariki

Baada ya dakika ishirini Dr Joshua akafika katika chumba cha maongezi kama alivyokuwa amewaahidi wanae.Alionyesha mshangao Fulani baada ya kumkuta Jaji Elibariki ndani ya kile chumba.Ilionekana wazi hakuwa amependezwa kumkuta jaji Elibariki mle ndani.Wakasalimiana halafu akaketi

“ Elibariki nimeshukuru na wewe umefika katika kikao hiki.Nimewaambia wenzako tukutane hapa kuna jambo nataka tulizungumze” akasema Dr Joshua .Flaviana ,Anna,jaji Elibariki walikuwa kimya kabisa wakimsikiliza

“ Kufuatia kifo cha ghafla cha mama yenu ,ilinilazimu kufanya uchunguzi kuhusiana na nini kilisababisha kifo chake” akanyamza kidogo halafu akaendelea

“Niliunda timu ya madaktari bingwa toka katika hospitali kuu ya taifa kwa ajili ya kufanya uchunguzi huo na kubaini sababu ya kifo cha ghafla cha mma yenu.Leo mchana wametoa ripoti yao.Anna hebu fungua mlango na mwambie Captain Amos ailete ile ripoti hapa atusomee ” akasema Dr Joshua.Jaji Elibariki ambaye alionekana kuwa katika mshangao kidogo akauliza

“ Mzee ni uchunguzi gani tena uliofanyika? Ulifanya uchunguzi mwingine kuhusiana na kifo cha Dr Flora ukiacha mbali ule ambao tuliufanya sisi?

“Najua utashangaa Elibariki kwamba kuna uchunguzi mwingine ulifanyika lakini ilinilazimu kufanya uchunguzi kwa kuwatumia madaktari bingwa ili kubaini nini chanzo cha kifo cha Dr Flora” akasema Dr Joshua katika sauti ambayo ilionyesha wazi kwamba hakuwa akihitaji tena maswali yoyote toka Elibariki

“ Lakini mzee uchunguzi si tulishaufanya na nikawaletea ripoti kuhusiana na kilichosababisha kifo cha mama na wewe mwenyewe ukaahidi kulifanyia kazi sasa uchunguzi juu ya uchunguzi inakuwaje hapa? Akauliza Jaji Elibariki

“ Elibariki suala hili ni suala zito linahusu uchunguzi wa kifo cha mtu ,tena mke wa rais,hivyo lazima ufanyike uchunguzi mkubwa na kina.Ninashukuru kwa kujitahidi kufanya uchunguzi wako lakini sisi katika serikali huwa hatufanyi kazi kwa kutegemea taarifa ya kutengenezwa,taarifa isiyokuwa na kichwa wala mkia,taarifa isiyo na uthibitisho wowote wa daktari anayetambuliwa na serikali.Nakupongeza kwa juhudi zako na kwa kujali lakini wataalamu wangu hawakuwa tayari kuifanyia kazi taarifa uliyoitoa.Taarifa itakayofanyiwa kazi ni taarifa ambayo imefanyiwa kazi na madaktari bingwa na kuthibitshwa na daktari mkuu wa serikali na si taarifa ya kuokoteza okoteza.” Akasema Dr Joshua katika hali iliyoonyesha wazi alikuwa akimkebehi Jaji Elibariki kwa ripoti aliyoileta.Jaji Elibariki akasimama na kutaka kusema jambo lakini kabla hajasema chochote Captain Amos daktari wa familia ya rais akaingia akiwa na bahasha mkononihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Karibu sana Captain Amos.Familia yote imekutana tayari kuipokea ripoti ya madaktari.Tafadhali tusipoteze wakati ifungue na utuambie ni kitu gani kimeandikwa na madaktari” akasema Dr Joshua

“ Ripoti hii ni ya uchunguzi wa kubaini sababu ya kifo cha ghafla cha Dr Flora.” Akasema Captain Amos.Akaipitia ripoti ile yenye karatasi tano ,kisha akasema

“ Kwa mujibu wa madaktari bingwa waliofanya uchunguzi huu wamebaini kwamba kifo cha ghafla cha Dr Flora kilisababishwa na shinikizo la damu.Hawajaona kitu kingine chochote kilichosababisha kifo chake” akasema Captain Amos daktari wa familia ya rais

“ Ahsante Amos.Unaweza kwenda”akasema Dr Joshua.Captain Amos akatoka

“ Nyote mmeisikia taarifa ya madaktari bingwa .Mama yenu alikufa kutokana na shinikizo la damu na si sababu nyingine yoyote. Taarifa hii ya madaktari bingwa inapingana na taarifa aliyotuletea mheshimiwa jaji ambayo inasema kwamba kifo cha mama yenu kilisababishwa na sumu.Ukiachana na taarifa hiyo nimepokea pia taarifa toka kwa vijana wangu niliowatuma wafanye uchunguzi kuhusiana na mambo yale mliyoniambia kwamba inawezekana kuna watu walihusika katika kusababisha kifo cha mama yenu.Taarifa ya vijana wangu inasema kwamba hakuna mtu yeyote ambaye alihusika katika kusababisha kifo cha Dr Flora na wala hakuna uzembe wowote uliofanyika.Mlimzungumzia Dr Kigomba kwamba alisikika akipiga simu kuzuia uchunguzi usifanyike lakini ukweli ni kwamba Dr Kigomba alipata taarifa ya kwamba kuna watu waliokuwa wakifanya uchunguzi wa siri na ndiyo maana akatoa amri kwamba watu hao wazuiliwe haraka sana kwa sababu tayari kulikuwa na mpango wa kuufanyia uchunguzi wa kina mwili wa mama yenu kwa kuwatumia madaktari bingwa .Dr Flora ni mtu mkubwa kwa hiyo uchunguzi wa kifo chake unatakiwa uwe maalum pia na si kwa kuwatumia madaktari wa kuokoteza mitaani.Sijaongea chochote kuhusiana na kitendo cha kihuni kilichofanywa na Elibariki na wenzake .Naomba leo niweke wazi kwenu kwamba nimechukizwa sana na kitendo kile na ninaomba kisijirudie tena.Sijataka kuchukua hatua zozote kwa sababu Elibariki wewe ni mwanangu na ninakuheshmu sana lakini wewe na wenzako mlipaswa kupewa adhabu kali sana kwa kitendo cha kihuni mlichokifanya.Mmefanya uhuni na kutuletea taarifa ya uongo ambayo imetusababishia matatizo makubwa ndani ya familia yetu na kwa watu wetu wa karibu tunaowaamini.Dr Kigomba ambaye mmemtuhumu kwamba anahusika katika kusababisha kifo cha Dr Flora ni mtu wangu wa karibu na nimefanya naye kazi kwa muda mrefu ni mtu ninayemuamini sana lakini mmetaka kunifanya niamini kwamba ni mtu mbaya.Sintafanya lolote kuhusiana na jambo lile lakini naomba mfahamu kwamba nimechukizwa sana .Kwa maana hiyo basi mjadala mzima wa kuhusina na sababu ya kifo cha mama yenu nimeufunga rasmi leo na sitaki kabisa kuendelezwa kwa mambo yasiyokuwa na ukweli wowote.Tayari madaktari bingwa wamekwisha thibitisha kwamba mama alikufa kifo cha kawaida kilichosababishwa na shinikizo la damu.” Akasema Dr Joshua halafu akamuomba Flaviana watoke wakaongee nje.Jaji Elibariki alibaki amepigwa na butwaa hakujua aseme nini.Alikuwa na hasira zisizomithilika.Dr Joshua na Flaviana wakatoka nje ya kile chumba

“ Flaviana I’m so disappointed with you” akasema Dr Joshua ambaye uso wake ulionyesha wazi kwamba alikuwa amechukia sana

“ Why father?akauliza Flaviana

‘ kwa nini umemjumuisha Elibariki katika kikao cha familia?

“ Baba,Eli ni mume wangu na ni sehemu ya familia yetu pia.Mbona katika mambo yetu mengine mengi ya kifamilia anashirikishwa? Niliona nimuite kwa sababu hata yeye kikao kile kilimuhusu kama mmoja wa wanafamilia

“ Ulifanya kosa kubwa Flaviana.Elibariki hakutakiwa kuwepo katika kikao kile.Kikao kile kilituhusu sisi pekee na si watu wengine wa hovyo hovyo”

“ dady ! Elibariki ni mume wangu na si mtu baki wala wa hovyo hovyo”

“ Vyovyote unavyomchukulia I don’t care lakini ninachokwambia na kwamba sitaki kumuona katika vikao vyetu vyovyote vya kifamilia.Ni kijana mshenzi sana yule.Ametaka kunisababishia matatizo makubwa na watu wangu wa karibu ninaowaamini na kufanya nao kazi kwa karibu.Ameleta ripoti ya kihuni na kutusababishia matatizo makubwa ndani ya familia yetu.Ninakuweka wazi kwamba ninamchukia sana huyo unayemuita mumeo.Ninasikitika sana kwa kukubali kuolewa na mtu kama yule.Ninashangazwa pia na jinsi unavyosimama na kumtetea leo wakati ni hivi majuzi tu ulikuja hapa ukilia na kusema humtaki tena yule mwanaume.”akasema Dr Joshua kwa ukali

“ dady ,Elibariki hapaswi kulaumiwa katika hili.Mimi ndiye ninayepaswa kubeba lawama kwa sababu ni mimi ndiye niliyemtuma baada ya kuhisi kwamba kuna sintofahamu kuhusiana na sababu ya kifo cha mama na hasa baada ya daktari mmoja pale katika hospitali kuu ya jeshi kuniambia kwamba kuna taarifa iliwafikia kwamba wasifanye uchunguzi wa kuhusiana na kifo cha mama.Yawezekana taarifa aliyopewa Elibariki na madaktari waliomsaidia kufanya uchunguzi ndiyo yenye matatizo na haikuwa na ukweli.Mimi ndiye ninayepaswa kuzibeba lawama hizi kwa sababu Elibariki alifanya kazi ile kwa shinikizo langu” akasema Flaviana

“ Flaviana naomba unisikilze mwanangu,hata wewe ulifanya kosa kubwa sana,ulipaswa kabla ya kushirikiana na mumeo kufanya jambo la hatari kama lile uje kwanza kwangu kunieleza na kwa pamoja tungeona nini cha kufanya.Lakini pamoja na hayo endapo angeleta taarifa yenye ukweli ndani yake basi kusingekuwa na tatizo lakini yeye ameleta taarifa ya uongo mkubwa ambayo imetusababishia sisi matatizo makubwa ndani ya familia,hata mimi taarifa ile imenipa wakati mgumu sana.Sielewi lengo lake ni nini hasa kwa kutuletea taarifa ile ya uongo.Nimejizuia kuchukua hatua zozote kwa sababu yako lakini kama angekuwa si mumeo angepata adhabu kali sana.Siku nyingine kama kuna jamo unataka kulifanya tafadhali usimuamini mumeo,njoo kwangu moja kwa moja.” Akasema Dr Joshua halafu akaondoka na kuelekea katika chumba chake akachukua simu na kumpigia Dr KIgomba

“ Hallow mzee” akasema Dr Kigomba

“ Dr Kigomba naomba tuonane ndani ya dakika tano”

“ Ok mzee ninakuja sasa hivi” akasema Dr Kigomba

Dr Joshua akavuta pumzi ndefu akakaa juu ya kitanda

“ Tayari nimekwisha limaliza lile suala ambalo lilitaka kutuletea matatizo makubwa.Nimewaondoa hofu kuhusiana na kifo cha mama yao kwa kuwasomea ripoti ile.Kwa sasa wote wanaamini kwamba kilichomuua mama yao ni shinikizo la damu.Tatizo linabaki kwa mtu mmoja tu ambaye ni Elibariki.Huyu ndiye anayeufahamu ukweli japokuwa tayari nimemjengea mazingira ya kutokuaminiwa tena lakini bado ni hatari kwetu.Kumuacha hivi hivi ni sawa na kulishikilia bomu mkononi na muda wowote linaweza kutulipukia.Siko tayari Elibariki awe ni mtu wa hatari kwetu eti kwa kuwa tu nimume wa mwanangu.Sintojali hilo na lazima ashughulikiwe haraka sana.Vile vile wanatakiwa wafahamike watu ambao alishirikiana nao kuifanya kazi ile ili nao washughulikiwe haraka sana .Jambo hili si la kufanyia mzaha hata kidogo.Na yotehaya yamesababishwa na Flaviana .Bila yeye tusingefika hapa tulipo hivi sasa.” Akawaza Dr Joshua

Flaviana alihisi kuchanganyikiwa na hakujua afanye nini.Alishindwa amuamini nani kati ya baba yake au mumewe Elibariki

“ Who is telling the truth? Nimuamini nani? Akajiuliza

“Lakini inawezekana baba akawa sahihi kwamba taarifa aliyoileta Elibariki haikuwa imejitosheleza.Haikuwa na usahihi ndani yake .Sina uhakika na uwezo wa madaktari waliomsadia kuufanya uchunguzi huo.Taarifa ile ya baba nadhani ndiyo sahihi kwani imefanyiwa kazi na madakari bingwa.Kinachofuata hapa sasa ni kulifunga rasmi jambo hili ililisiendelee kutuchanganya.” akawaza Flaviana na kurejea katika chumba cha maongezi alikomuacha mumewe.Jaji Elibariki alikuwa ameinama akiwaza.Flaviana akamsogelea karibu

“ Eli naombausiwaze sana mume wangu kuhusu mambo aliyoyasema baba” akasema Flaviana

“ Flaviana please believe me,taarifa hiyo anayoisema baba yako haina ukweli wowote.Rais amedanganywa,amepewa taarifa isiyo ya kweli.Tafadhali naomba usiiamini taarifa hiyo hata kidogo.Kuna kitu kinafichwa hapa ,believe me something is going on” akasema Elibariki

“ Elibariki hata mimi nimechanganyikiwa na sijui niamini lipi lakini nimeamua ni vyema endapo tutaachana na suala hili kwani litatuchanganya sana.” akasema Flaviana

“ Flaviana my love, kama kuna wakati unaopaswa kuniamini basi ni sasa.Please believe me,we did everything to get that report.Uhai wa mtu umepotea katika kuutafuta ukweli lakini matokeo yake taarifa yangu inakataliwa na kuonekana ni ya kuunga unga .Fumbua macho Flaviana something is going on here”

“ Eli I’m confused right now.Sielewi niende upande upi.Ninyi nyote ni watu ninaowaamni lakini …” Flaviana akasita kidogo

“ lakini nini? Akauliza Elibariki

“ Nashindwa nifanye nini.Please Eli I need to be alone for now” akasema Flaviana.Elibariki akamtazama kwa makini na kuuliza.

“ So you don’t trust me?

“Si kwamba sikumaini Eli but ……” akajibu

“ Its ok ..ninajua unachotaka kukisema” akasema Elibariki na kutoka kwa hasira akaubamiza mlango



*******



Dr Kigomba alifika haraka kuitika wito wa mheshimiwa rais

“ Kigomba tayari nimelimaliza lile suala”akasema Dr Joshua

‘ “That’s good news Mr President”akasema Dr Kigomba huku akitabasamu

“ Nimetoka kuongea na familia na wote wameridhika na ripoti ile uliyoileta.Umefanya kazi nzuri sana .Kwa sasa wote wanaamini kwamba mama yao alifariki kwa shinikizo la damu na si kwa kuchomwa dawa yenye sumu kama alivyodai yule muhuni.Pamoja na hayo bado tuna tatizo “

“ Tatizo gani mheshimiwa rais?

“ Ni Jaji Elibariki.Lile ni bomu tumelishika na siku moja linaweza kutulipukia na kutujeruhi.Sitaki nitakapokuwa nimemaliza muda wangu wa uongozi nianze tena kupata usumbufu wa aina yoyote ile.Ninataka baada ya kumaliza uongozi wangu niishi maisha ya raha mustarehe kwa hiyo kitu chochote kinachoonekana kuwa ni kikwazo katika mpango wetu basi nitakiondoa mara moja kama nilivyofanya kwa Flora.Elibariki anaufahamu ukweli wa kifo cha Flora na nina hakika siku moja anaweza akatulipua.Ninahitaji ashughulikiwe haraka iwezekanavyo.” Akasema Dr Joshua

“Unataka tumshughulikie vipi mzee? Ukumbuke huyu ni mkweo”

“ Take him away,but in a proffesional way.No mistake “ akasema Dr Joshua

“ Are you sure about this Mr President? Akauliza Dr Kigomba

“ Yes I’m sure.Hili ni bomu na tunatakiwa kulitegua haraka sana.Lakini kazi hii inatakiwa ifanyike kwa uangalifu mkubwa sana.Wakabidhi kazi hii vijana ambao wana ujuzi wa hali ya juu.Ninarudia tena no Mistake this time.Elibariki ni hatari sana kwetu kuliko hata Flora.Baada ya Elibariki tutaangalia namna ya kumuondoa pia na Captain Amos” Akasema Dr Joshua

“ Ok Mr president nimekwisha kuelewa.Nitalifanyia kazi hilo suala” akasema Dr Kigomba na kuondoka

“ Siko tayari kuona kizingiti chochote katika mpango wangu huu mkubwa ambao uo mbioni kukamilika.Yeyote atakayeonekana kuwa ni kikwazo kwangu nitamuondoa hata kama ni mwanangu “akawaza Dr Joshua



*******



“ Kuna jambo linaendelea hapa ikulu si bure.Ukweli wa kifo cha Dr Flora unazidi kufichwa na sasa hata rais amekubali kudanganywa na taarifa ya uongo na akaiamini.Hata familia yake wote wameonekana kuiamini taarifa ile.Nimeumizwa sana na maneno aliyoyasema Dr Joshua dhidi yangu.Amediriki kuniita mimi muhuni .Mimi na heshima zangu leo hii ninaitwa muhuni .Ninajuta kwa kukubali kuifanya kazi ile ya Flaviana.Juhudi zote za kutaka kuupata ukweli zimekuwa ni kazi bure na badala yake nimeambulia matusi.Kinachoniumiza kichwa ni kwa nini ukweli unafichwa? Kwa nini Dr Flora aliuawa? Akajiuliza jaji Elibariki

“ Ninamuamini sana Mathew na katu hawezi kunipa taarifa isiyo ya kweli.Yeyena timu yake wamehangaika sana na kuhatarisha maisha yao kwa sasabau tu ya kuipata taarifa ile .Hapana siwezi kukubali juhudi zao zipotee bure.Lazima tufahamu ni kwa nini ukweli wa kifo cha Dr Flora unafichwa? Lazima kuna kitu kinaendelea pale ikulu.Lazima nionane na Mathew na nimueleze kuhusu jambo hili ili tuone namna ya kuweza kulifanyia uchunguzi na kuubaini ukweli.NImeanza kuwa na wasi wasi sana hata kuhusiana na kifo cha Edson kwani hata naye alikuwa ni mfanyakazi wa ikulu” akawaza Elibariki halafu akachukua simu na kumpigia Mathew

“ Hallow Mathew” akasema jaji Elibariki

“hallow Elibariki”

“ Mathew kuna tatizo limetokea tena ndugu yangu”

“ Tatiza gani Eli?

“ Siwezi kukuelaza simuni.Uko nyumbani”

“ Ndiyo niko yumbani lakini nitatoka muda si mrefu kuna mahala nitaelekea”

“ Ok nakuja sasa hivi” akasema Elibariki na kukata simu akaelekea katika gari lake na kuondoka”





Shughuli ya kuizika miili ya vijana sita waliopoteza maisha katika shambulio la kumuokoa mke wa Dr Michael ilimalizika saa kumi na moja na dakika ishirini na tatu.Mtu wa mwisho ambaye ni Aron mkibala alizikwa katika makaburi ya mkoroshini.Baada ya shughuli ile kukamilika vijana wote wa Team SC41 walitakiwa wakutane makao makuu

Wakati yote haya yakiendelea ,Josh kijana ambaye kwa muda mrefu amekuwa mlinzi wa John Mwaulaya alikuwa katika ofisi ya Osmund akikitafuta kile alichotumiwa na John.Si rahisi kuingia katika ofisi ya Osmund lakini Josh alifanikiwa kuingia katika ofisi hiyo kwa msaada mkubwa wa John Mwaulaya aliyempatia kadi maalum ya kufungulia mlangowa ofisi hiyo pamoja na namba za siri za kufungulia kompyuta ya Osmund.Baada ya kupata kile alichokuwa anakitafuta ,akatoka na kurejea katika makazi ya John mwaulaya

“ Mzee nimefanikiwa ulichonituma.Nimekwisha pata taarifa zote kuhusiana na Dr Burke kwa hiyo usijali nitaifanya kazi yako kikamilifu” akasema Josh

“ Ahsante sana Josh.Ahsante sana kwa kuendelea kuwa mtiifu.Nitakufanyia jambo kubwa kabla ya pumzi zangu kukatika” akasema John

“ Mzee tafadhali usiwaze kuhusiana na masuala hayo ya kifo.Be strong John.You can fight this”akasema Josh

“ I was as strong as a lion but now I’m very weak and I cant fight anymore.I cant fight this Josh .I’m going to die soon.” Akasema John Mwaulaya na kufumba macho na kwa mbali michirizi ya machozi ikaonekana machoni pake.Josh akamuonea huruma mzee yule aliyekuwa amelala pale kitandani ambaye ndiye aliyemuingiza katika Team SC41

“ John what can I do for you? Akauliza Josh

“ Leave me alone for now” akasema John na Josh akatoka mle chumbani na kumuacha John peke yake

“ Nilizoea kuzitoa roho za watu.Sikujua kama siku moja na mimi nitakufa.I’m so scared of death”akawaza John

“ Nimefanya mambo mengi sana mabaya katika kipindi chote cha masha yangu na zaidi baada ya kujiung a na TeamSC41 .Nimeua watu wengi,nimetesa watu wengi lakini ni kitu kimoja tu ambacho nina uhakika nilikifanya sawa.Sikumuua Peniela.Alikuwa mtoto mdogo na hakuwa na kosa lolote” akaendelea kuwaza John na sura ya Peniela ikamjia akatabasamu

“ Ni msichana mzuri sana lakini kuna kitu kimoja nimekikosea .Nilikosea sana kumuingza katika Team SC41.Japokuwa anapata kila kitu anachokihitaji lakini hana furaha ya maisha .Siku nilipomuingiza Team SC41 niliyaharibu maisha na ndoto zake zote.Peniela amekuwa akitumika katika mambo mengi ya hatari na hivyo kuhatarisha usalama wa maisha yake.Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba mwili wake mzuri umekuwa ukitumika kama silaha ya Team SC41 katika kufanikisha mambo mengi.Inaniuma sana kuyaharibu maisha yake namna hii” John akauma meno kwa uchungu

“ It’s not too late.kabla sijakata pumzi lazima nihakikishe kwamba Peniela amekuwa na maisha ya kawaida kama wasichana wengine.lazima nimuondoe katika Team SC41 .Lazima nihakikshe anaishi maisha ya kawaida.” Akawaza John na kumbukumbu zikamrejesha mbali siku Peniela alipomaliza elimu yake ya msingi

Ni siku ya mahafali ya darasa la saba katika shule ya St Patrick shule ambayo husoma watoto wa matajiri ..Peniela akiwa ni miongoni mwa wahitimu alikuwa na furaha isiyo kifani.Katika miaka yote saba aliyoitumia katika elimu yake ya msingi Peniela amekuwa ni mmoja kati ya wanafunzi hodari sana na mwenye kutiliwa mfano katika bidii ya masomo darasani,michezo,tabia njema na hata usafi.Kwa upande wa maisha ,japokuwa ni mtoto yatima lakini alikuwa akiisha maisha mazuri mno..Aliwezeshwa kupata kila alichokihitaji .sKulikuwa na gari maalum ya kumpeleka shuleni kila siku asubuhi nakumrejesha nyumbani,alipelekwa kila mahala alikotaka kwenda.Watu wengi hawakuamini kama Peniela ni mtoto yatima kutokana na maisha aliyokuwa akiishi.Peniela alitamani sana siku moja akutane na mtu yule ambaye amekuwa akimuwezesha kuishi maisha ya namna ile.Alijiona ni mtoto mwenye bahati kubwa kumpata mfadhili wa aina ile ambaye alimuwezesha kuishi maisha ya hali ya juu kiasi kile.Kila siku alikuwa akimlilia mama Bernadetha amuwezeshe kumkutanisha na huyo mfadhili wake ili aonane naye na amfahamu kwa sura lakini hadi anamaliza darasa la saba hakuwa amefanikiwa kukutana naye

Saa nne za asubuhi John Mwaulaya akiwa katika gari lake la kifahari aliwasili St Patrick school ili kuhudhuria sherehe za mahafali.Alikuwa na furaha usiyo kifani kwa Peniela kumaliza elimu yake ya msingi

“ She’s growing up so fast.Ni juzi tu alianza darasa la kwanza na leo tayari amemamliza darasa la saba ,Dah ! miaka inakimbia sana” akawaza John akishuka katika gari lake la kifahari na kuungana na watu wengine waliokuwa wamekuja katika mahafali haya

Sherehe zilikwenda vizuri na kabla ya sherehe kumalizika Bi Bernadetha akamuomba Peniela waongozane kuelekea sehemu Fulani kuna kitu anataka akamuonyeshe.Peniela aliingia katika gari wakaondoka bila kujua walikuwa wanaelekea wapi.

Safari yao iliwafikisha katika jumba moja kubwa lenye uzuri wa kipekee.Mlinzi alifungua geti wakaingia ndani.Uso wa Peniela ukapambwa na tabasamu la mshangao baada ya kuishuhudia mandhari ya kuvutia sana iliyokuwemo mle ndani.

Watu wanne walikuwa wamesimama katika mlango wa kuingilia sebuleni.Wote walikuwa na nyuso zenye tabasamu.

“ mama Bernadetha hapa ni wapi? Nani anaishi hapaauni hoteli ? Akauliza Peniela

“ Peniela sikuwa nimekwambai toka mwanzo nilitaka nikushangaze kidogo.Hi si hoteli mwanagu.Hii ni nyumba ya kuishi.Kuanzia dakika hii ni nyumba hii ni yako.Mfadhili wako amekuzawadia i kama zawadi yake kwako kwa kuhitimu elimu ya msingi na kuanzia le o utaishi hapa.Leo utayaanza maisha mapya Penny.” Akasema Bi Bernadetha na kumuacha Peniela akiwa na mshangao

“ mama Bernadetha ! akasema Penny kwa mshangao

“ Peniala najua umestuka sana na hata mimi nilistuka sana lakini na nimeumia sana kwamba hatutakuwa pamoja ,kwani wewe ni mtoto ambaye nimekuzoea sana na ninakupenda mno lakini haya ni matakwa ya mfadhili wako kwamba anataka aanze kukujengea maisha ya kujitegemea.Pamojana hayo naomba usijali Penny mimi bado nitaendelea kuwa mama yako na nitaendelea kuwa karibu nawe kwani nafahamu bado unahitaji sana msaada wangu” akasema Bi Bernadetha kisha wakakumbatiana na Peniela.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Walishuka katika gari na kuelekea ndani ,Bi Bernadetha akamtambulisha Peniela kwa watumishi ambao watakuwa wakimsaidia katika maisha yake ndani ya jumba lile.Alikuwepo mtumishi wa kazi za ndani,mpishi,na mtumishi mwingine ni wa kumsaidia peniela katika kazi zake ndongondogo na vile vile alikuwepo pia dereva wake maalum.Wote walifurahi kukutana na Peniela.Wakamzungusha Penny katika jumba lote na alifurahi sana

“ Mama bernadetha huyu mfadhili wangu anayenifanyia mambo haya makubwa ni nani? Kwa nini hutaki kunikutanisha naye ili nimfahamu na kumshukuru? Watu wa namna hii ni nadra sana kupatikana siku hizi.” Akasema Peniela baada ya kumaliza kutembezwa katika jumba lote

“ Peniela usijali siku moja utakunana na mfadhili wako na utamfahamu.Hata naye ana hamu sana ya kukutana nawe lakini ni mwingi wa safari za nje ya nchi” akasema Bi Bernadetha.

Peniela aliyaanza maisha mapya ndaniya jumba lile kubwa .Alijiona ni kama malkia.Saa tatu za usiku akiwa amejilaza katika kitanda kikubwa chumbani kwake simu iliyokuwa mezani ikaita akainuka na kuipokea.

“ Halow” akasema

“ hallow Peniela” ikasema sauti nzito ya kiume upande wa pili wa simu

“ Ninaongea na nani? Akauliza Peniela

“ Unaongea na John.Mimi ndiye mfadhili wako.”

Peniela akapatwa na furaha ya ajabu sana kwa kuisikia sauti ya mtu ambaye amekuwa akitamani kumuona kwa miaka mingi.

“ Baba John nakushukuru sana kwa kila kitu ulichonifanyia.Sina neno zuri la kuweza kukushukru ila ninakuombea kwa Mungu akupe Baraka nyingi na mafanikio katika shughuli zako” akasema Penny huku akilengwa na machozi kwa hisia kali

“ Peniela nashukuru kwa Baraka zako lakini naomba tu ufahamu kwamba kukosa wazazi si kigezo cha kukufanya uishi maisha ya shida.Unastahili kuishi maisha mazuri kama watoto wengine na hicho ndicho ninachojitahidi kukifanya kuhakikisha kwamba maisha yako yanakuwa mazuri.Umeionaje nyumba yako? Inakufaa?

“ baba John,sina cha kusema ,kila kitu ni kizuri .Siamini kama hata mimi yatima leo hii ninaweza kuishi ndaniya jumba kubwa na zuri kama hili.Mungu akubariki sana baba” akasema Penny

“ Penny kuna picha moja kubwa ya bahari ukutani umeiona?

“ Ndiyo baba nimeiona”

“ Ok nenda kaitoe ile picha na nyuma yake utakuta kuna kasiki lina namba kisha lifungue kasiki hilo kwa namba hizi” akasema John na kumtajia Peniela namba za kufungulia kasiki lile.Peniela akafanya kama alivyoelekezwa

“ Tayari baba nimelifungua”

“ Ok Vizuri .Ndani ya kasiki hilo kuna hati ya nyumba na kadi ya gari ,kadi ya benki na nyaraka nyinginezo .Kila kitu kina jina lako.” Akasema John

“ Baba ahsante sana lakini nina kitu kimoja bado kinanisumbua sana akili yangu”

“ Kitugani Peniela?

“ Ninataka kukuona.Moyo wangu utakuwa na furaha kubwa kama nikikuona.Tafadhali baba naomba uniruhusu nikuone, walau niione sura yako” akaomba Peniela.John akacheka kidogo nakusema

“Usijali Peniela siku moja tutaonana.Nitakuwa nikiwasiliana nawe kila siku kujua maendeleo yako.Kwa heri peniela” John akakata simu

Kumbu kumbu ile ikayafanya macho ya John yaloe machozi.

“ She was so beautiful na maisha yake yalikuwa na furaha sana .Lazima nimrudishie furaha yake aliyokuwa nayo wakati ule.Lazima nimuondoe teamSC 41” Akawaza John



******



Mathew,Anitha na Noah walikuwa katika chumba chao cha kazi.Pamoja nao alikuwepo mtaalamu wa program za kompyuta Arnold ambaye walikuwa wakimshikilia .Wote macho yao yalikuwa katika simu iliyokuwepo mezani wakisubiri simu kutoka kwa watu ambao walitakiwa kukutana na Arnold jioni ile.Simu nyingi zilikuwa zikipigwa na kila simu iliyopigwa Arnold alidai haikuwa yenyewe

“ Arnold una hakika hao jamaa watapiga? Akauliza Mathew baada ya kuona muda unazidi kuyoyoma na hakuna simu yoyote iliyopigwa

“ Watapiga tu,makubalinao yetu ni kwamba leo hii lazima niwapatie mzigo wao na wao wanilipe fedha zangu zilizobaki.Kama nilivyowaambia kwamba tulikubaliana kukutana kuanzia saa moja za jioni leo “

Waliendelea kusubiri na ilipotimu saa kumi na mbili na dakika ishirini na tatu simu ikapigwa na Arnold akaitambua kwamba ,ni ya wale jamaa.Wote wakatega masikio .Arnold akabonyeza kitufe cha kupokelea

“ Hallow “ akasema

“ Arnold .Kila kitu kiko tayari? Ikauliza sautiya upande wa pili

“ Ndiyo kila kitu kiko tayari.Ninasubiri maelekezo yenu”akasema Arnold

“ Ok Vizuri .Tukutane Triple S casino ghorofa ya tatu kaunta C.Jitahidi hadi saa moja na robo uwe umewasili ”akasema yule jamaa

“sawa nitafika kabla ya muda huo” akajibu Arnold na simu ikakatwa

“haya kumekucha “ akasema Mathew

“ sasa tunaelekea tena kazini.Noah wewe kwa kuwa bado haujapona vizuri jeraha lako utabaki hapa na nitaongozana na Anitha.”

“ sawa hakuna shida Mathew” akajibu Noah

“ Anitha kila kitu ulikiweka sawa katika ile tablet? Akauliza Mathew

“ Kila kitu kiko tayari.”akasema Anitha kisha Mathew akamgeukia Arnold

“ Arnold tunakwenda sote huko Casino na utawakabidhi hao jamaa kifaa chao lakini nakuonya tutakuwa karibu tukifuatilia kila kinachoendelea kwa hiyo usijaribu kwa namna yoyote ile kuwatamkia kitu chochote kwamba tunawafuatilia.Wakabidhi kifaa chao kisha utatuachia sisi kazi ya kuendelea kuwafuatilia.Ukienda kinyume na tunachokuamuru fahamu kwamba jua la kesho hutaliona.Tumeelewana Arnold? Akauliza Mathew kwa ukali

“Tumeelewana ndugu zangu.Ntafanya kama mlivyoniamuru lakini kuna mambo bado nahitaji kuyafahamu,ninyi ni akina nani? Na hawa jamaa walionipa hii kazi mnawafahamu? Akauliza Arnold

“ Watu hawa waliokupa hii kazi hatuwafahamu lakini tunahitaji k uwafahamu ni akina nani na ndiyo maana tunawafuatilia Ili tuwafahamu na vile vile tufahamu ni kitu gani wnachokitafuta kwa Eva.”akasema Mathew

“Nina wasi wasi kama hawa jamaa ni watu wabaya wanaweza wakanifanyia kitu kibaya au hata kuniua mara tu nitakapowakabidhi kifaa chao “akasema Arnold

“Usijali Arnold sisi tutakuwepo karibu tunakufuatilia na tutakulinda” akasema Mathew

Noah akamchukua Arnold na kumpeleka bafuni akaoga kisha akapewa suti moja ya Mathew akavaa na kujiweka tayari kwa safari ya kuelekea Triple S casino.Baada ya dakika kumi wote walikuwa tayari wakaingia garini na kuondoka wakimuacha Noah peke yake nyumbani

Dakika kumi tu toka akina Mathew waondoke jaji Elibariki akawasili na kumkuta Noah peke yake .

“ Mathew ametoka kuna mahala amekwenda ila amesema hatachelewa sana kurudi na amesema ukifika umsubiri” akasema Noah Jaji Elibariki akajiegemeza katika sofa na kuvuta pumzi ndefu. Alionekana ni mchovu na mwingi wa mawazo

“ Bado sielewi ni kwa nini rais anakubali kudanganywa na wasaidizi wake kiasi hiki ? Kwa nini amekataa kuikubali taarifa yangu ya ukweli? Kitu gani kinaendelea ndani ya Ikulu? Lazima tufanye uchunguzi wa kina tubaini kinachoendelea ndani ya jengo lile.” Jaji Elibariki akastuliwa toka mawazo nina simu yake iliyokuwa ikiita.Akaichomoa toka mfuko wa koti na kutazama mpigaji alikuwa ni mkewe Flaviana

“ Hallow Flaviana”akasema

“Eli uko wapi? Mbona sikuoni hapa? Nimetuma watu wakutafute lakini wamekukosa.Ninakuhitaji kukuona” akasema Flaviana.Elibariki akafikiri kidogo na kusema

“ Flaviana nimetoka kidogo .Mzee amenichefua sana leo”

“ Unaweza ukaja kidogo tukaonana Eli?

“ Niko mbali kdogo.Kunanini?

“ Nataka tuongee kuhusiana na lile suala”

“ Hakuna cha kuongea Flaviana.Hakuna kati yenu anayetaka kuniamini .Hakuna anayetaka kuiamini taarifa niliyowapa.Nyote mnakubaliana na alichokisema baba yenu”

“ Eli si kwamba hatukuamini lakini mambo haya yanachanganya sana .Hapa nilipo nimechanganyikiwa na sijui nielekee upande upi”

“ Flavina ni wewe ndiye uliyeniambia nikusaidie kutafuta kilichomuua mama yako na nilifanya ulivyoniomba.Hujui ni mambo gani yaliyotokea hadi taarifa ile ikapatikana.lakini pamoja na hayo sikulazimishi wewe wala yeyote katika familia yenu akubaliane na mimi lakini siku moja ukweli utadhihiri” akasema jaji Elibariki

“ Eli tafadhali naomba tuachane na hili suala kwani limekuwa gumu sana.Vyovyote vile itakavyokuwa mama yangu amekwisha fariki na hatafufuka.Jambo la msingi nililoamua mimi ni kuachana kabisa na suala hili.Kama mama aliuawa basi waliofanya hivyo siku moja watahukumiwa mbele za haki.” Akasema Flaviana

“ Flaviana mimi ni jaji wa Mahakama kuu na siku zote kazi yangu ni kuhakikisha haki imetendeka.Siwezi kuliacha suala hili hadi nifike nalo mwisho na ukweli lazima ujulikane” akasema jaji Elibariki

“ Eli tafadhali nakuomba usiliendeleze tena suala hili kwani tayari baba amekwisha lifunga. .Liache kama lilivyo”

“ Hapana Flavina siwezi kuliacha hivi hivi.Baba yako amenidharau sana na kuniona kama kitu kisicho na thamani yoyote.Nataka nimdhihirishie kwamba siku zote huwa na simama katika haki na ukweli.Sintalala usingizi hadi nimdhihirishie kwamba nilikuwa sahihi na siku zote huwa niko sahihi”akasema jaji Elibariki

“Eli tafadhali naomba kabla hujafanya chochote naomba kwanza tuonane.Please Eli “ akasema Flaviana

“ Ok ninakuja” akasema Elibariki na kukata simu

Wakati Flavina na jaji Elibariki wakiongea simuni,maongezi yao yalikuwa yanasikika katika gari moja jeusi aina ya Ford lililokuwa na watu watatu ndani, kupitia katika chombo Fulani kilichokuwa kimeunagnishwa na simu ya Flaviana bila ya yeye kujua wakati alipopoteza fahamu mchana na kupakiwa katika gari la wagonjwa na kukimbizwa hospitali.Flaviana hakufahamu chochote kuhusiana na simu yake kuunganishwa na chombo maalum ambacho kingeweza kunasa maongezi yoyote ambayo angeongea kupitia simu yake.Mara tu simu ilipokatwa mmoja wa wale jamaa watatu akachukua simu na kuzitafuta namba za Dr Kigomba akapiga

“ Hallow Austin.Kuna habari gani? Ikauliza sauti ya upande wa pili ya Dr Kigomba

“Dr Kigomba tumefanikiwa kunasa maongezi kati ya Flaviana na mumewe.Nina kutumia sasa hivi uyasikilize halafu utuambie nini cha kufanya” akasema Austin na kisha akamtumia Dr Kigomba maongezi yale ya Flaviana na Jaji Elibariki ambayo tayari yalikwisha rekodiwa katika kompyuta.

Dr Kigomba aliyasikiliza kwa makini maongezi yale kati ya Flaviana na mumewe akayarudia kuyasikiliza tena halafu akampigia simu Dr Joshua na kumuomba waonane.Baada ya dakika kumi wakakutana.

“Kuna nini Kigomba? Akauliza Dr Joshua.Dr Kigomba akatoa simu yake na kumpa Dr Joshua asikilize maongezi yale.Akasikiliza na kuyarudia tena kisha akamgeukia Dr Kigomba

“ Dr Kigomba nilikueleza toka mapema kwamba huyu jamaa ni hatari sana.Kama alivyomwambia mkewe kwamba hatalala hadi ahakikishe ametulipua.” akasema Dr Joshua

“ Unashauri nini Dr Joshua” akauliza Dr Kigomba

“ Muondoeni haraka iwezekanavyo.Ila kumbuka kwamba umakini mkubwa unahitajika katika jambo hili ili kuwafanya watu wasiwe na aina yoyote ya shaka.”akasema Dr Kigomba

“ What about an accident? akauliza Dr Kigomba

“ Yes ! do it.Make it looks like real” akasema Dr Joshua

“ Ok Mr President.Hivi sasa Elibariki yuko njiani anakuja na kazi itafanyika usiku wa leo” akasema Dr Kigomba





Peniela alisimama katikati ya sebule akaitazama namna inavyoonekana akatabasamu

“ Kila kitu kinakwenda kama nilivyotaka .Sebule nzuri sana na inapendeza.Nashukuru Mungu nimehamia sehemu salama na sina shaka yoyote.Ninaamini nitakuwa salama na hata lile kasha alilonipa John litakuwa salama.”akawaza halafu akachukua chupa ya mvinyo na kuelekea sehemu ya juu ya ghorofa kulikokuwa na sehemu nzuri ya kupumzikia.Upepo mwanana wa bahari ulikuwa unavuma na sauti ya mawimbi ya maji ilisikika na kupafanya mahala pale pawe na mandhari ya kuvutia sana

“ Nimepapenda mahala hapa.Ni sehemu nzuri ,tulivu na salama.Kuna kila kitu ninachokihitaji lakini tatizo ni moja tu.This house is too big for me.I feel so lonely.Laiti ningekuwa na mtu wa kuishi naye humu ndani ningefurahi sana.Lakini maisha haya si muda mrefu yatafikia mwisho na nitakuwa huru tena kuishi vile nitakavyo.Baada ya kazi hii sitaki tena kuendelea kuwa sehemu ya Team SC41 .Laiti ningepata nafasi ya kutosha ningemuuliza John ni kwa nini aliniingiza katika kikundi hiki? Kwa nini alitaka niishi maisha haya? Kwa nini hakutaka niishi maisha ya kawaida kama wengine ? Akajiuliza Peniela na kukumbuka mambo mengi sana toka alipokuwa mdogohttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Toka nikiwa mdogo John Mwaulaya amekuwa ni kila kitu kwangu.Amekuwa mfadhili wangu kwa kila kitu.Ameniwezesha kuishi maisha ya hali ya juu sana tofauti na watoto yatima wengine.Hata watoto wengine ambao wana wazazi wao hawajaishi maisha kama niliyoishi mimi.Nilijiona ni mwenye bahati sana kwa kumpata mfadhili mzuri kama yule lakini kwa sasa ninajuta ni kwa nini John alikuwa kunifadhili.Maisha yangu yameharibika kwa sababu yake.Maisha yangu hayatakuwa kawaida tena” Akaendelea kuwaza Peniela na kupiga funda la mvinyo

“ Nilitamani sana kumuona John toka nikiwa mdogo lakini nimefanikiwa kuonana naye katika siku ambazo naweza kuziita ni za mwisho za uhai wake kutokana na kuumwa sana.Nilitamani nimfahamu na kumuuliza maswali mengi hasa ni kwa nini aliniingiza katika Team SC41 ,lakini sikupata nafasi ya kumuuliza kutokana na hali yake..John anaumwa sana na sijui anaumwa nini.Japokuwa ninamlaumu kwa kuniingiza katika Team SC41 lakini namuonea huruma sana kwa namna alivyokuwa amelala pale kitandani hajiwezi .Ugonjwa gani unamsumbua? Mbona hakuwa tayari kunieleza? Itanilazimu nizungumze na Osmund ili niweze kuipata tena nafasi ya kuonana na John Mwaulaya na kufahamu nini kinachomsumbua .Pamoja na kunifutia ndoto zangu za maisha niliyokuwa nikitakakuishi lakini ndiye mtu aliyenilea na kunifikisha hapa nilipofika.Ninamchukulia kama baba yangu ,amenisaidia sana katika maisha yangu .NImeishi maisha ya kifaharikwa sababu yake yeye,nimesoma shule nzuri kwa gharama zake kwa hiyo lazima na mimi nitoe mchango wangu japo harta kama ni kwa siku moja.Nashindwa kuelewa ni kwa nini TeamSC 41 wameshindwa kumtibu John .Nikipata nafasi ya kukaa na John nitafahamu pia kuhusu jambo hili ” Peniala akachukua glasi na kupiga funda kadhaa akamkumbuka Jaji Elibariki na Jason

“ Natamani sana kufahamu maendeleo ya Jaji Elibariki na Jason.Toka ulipotokea ugomvi ule jana na jaji Elibari akapigwa chupa kichwani sifafuatilia maendeleo yake. Inaniuma sana kwa watu wale ambao wote ni watu wangu wa karibu kupigana namna ile..Jason amekuwa na mimi toka kesi ilipoanza na jaji Elibariki ndiye aliyeniachia huru.Bila wao nisingekuwa huru sasa hivi lakini hata hivyo kitu walichotaka kukifanya ni cha hatari sana.Jambo walilotaka kulichunguza lingewasababishia matatzo makubwa na hata kuwagharimu uhaiwao .Hakukuwa na njia nyingine ya kuweza kuwazuia wasiendelee na uchunguzi wao zaidi ya kuwagombanisha ili wasiwe na umoja kati yao.Nilifanikiwa kwa hilo na ninatumai mpango ule wa kuchunguza kifo cha Edson umekufa lakini naamini wataendelea kuwa maadui wakubwa.Sina hakika kama wataelewana tena.Nilimpenda sana Jason, ni kijana mzuri ,mwenye kila sifa ya mwanaume mzuri.Baada ya tukio la jana nina hakika nimekwisha mpoteza..Anyway najua siku moja nitampata mwanaume mwingine ambaye anasifa kama zake.Dunia hii bado imejaa vijana wengi wazuri .Jaji Elibariki naye ni mwanaume mzuri,ana sifa ya kuwa mume bora.Anafahamu mahitaji ya mwanamke ,na anajua kumridhisha.Wote wawili kila mmoja alikuwa nasifa zake nawote walinipenda ” Akaendelea kuwaza .

“Lakini kuna jambo moja ambalo linaniumiza kichwa mpaka leo. Kwa nini Dr Joshua alimuua Edson? Nikweli kwamba alimuua kwa sababu ya wivu wa kimapenzi? Hapana sina hakika kama alimuua Edson eti kwa vile nilikuwa katika mahusiano naye.Lazima kuna sabau nyingine iliyopelekea Edson kuuawa .Anyway anajua mwenyewe kitu kilichopelekea amuue Edson lakini ajue hata yeye siku si nyingi atalia na kusaga meno.Nilibebeshwa mzigo wa kesi ya mauaji na kama si Jason na Elibariki hivi sasa ningekuwa ninasota gerezani.Asifikiri kwamba jambo hili limekwisha,lazima siku moja nitalipiza kisasi.” Akawaza Penny halafu akaichukua simu yake akazitafuta namba za jaji Elibariki akataka kumpigia akasita.Akafikiri kwa sekunde kadhaa na kuirudisha tena simu chini

“ Natamani sana kujua hali ya Elibariki lakini ninaogopa kumpigia.Sina hakika kama atakubali hata kupokea simu yangu kutokana na kitendo cha jana.Ngoja nisubiri kwanza siku zipite na hasira zake zipungue.”akawaza Peniela nakuendelea kupiga mafunda ya mvinyo huku akipulizwa na kiupepo mwanana cha bahari



*******



Watu walikuwa ni wengi Triple S Casino.Gari alilokuwa amepanda Arnold liliingia katika eneo la maegesho .Kabla hajashuka ,gari walilokuwamo akina Mathew nalo likaingia na kuegesha pembeni mwa ile taksi aliyokuwa amepanda Arnold.Hawakutaka kupanda gari moja ili kuondoa aina yoyote ya mashaka kwanbi waliamini lazima Arnold atakuwa akifuatiliwa nyendo zake ili kuhakikisha kwamba hajaongozana na mtu yeyote.

Arnold akashuka toka katika ile taksi na kuelekea ndani.Mathew naye akashuka garini na kumfuata kwa nyuma.Anitha alibaki garini .Moja kwa moja Arnold akaelekea ghorofa ya tatu kaunta C kama alivyokuwa ameelekezwa.Aliagiza kinywaji na kukaa katika kiti kirefu cha pale kaunta na baada ya dakika mbili simu yake ikaita akaipokea.

“ Ondoka hapo kaunta nenda meza namba 21” akapewa maelekezo mengine.Arnold akaondoka pale kaunta na kuelekea katika meza aliyoelekezwa.Alikuwa na wasi wasi mwingi.Alijaribu kutazama huku na huko lakini hakuna mtu yeyote aliyekuwa akimjali.Akaenda kuketi katika meza aliyoelekezwa.Baada ya dakika mbili watu wawili wakatokea.Ni wale wale ambao walimuomba awatengenezee ile program ya kuweza kumfuatilia Eva.

“ Hallow Arnold.habari yako? Akasema mmoja wa wale jamaa

“ Habari nzuri sana .” akajibu Arnold huku sauti yake ikionyesha woga

“ Arnold mbona unaonekana unaogopa sana?

“ Ni mara yangu ya kwanza kuingia sehemu kama hii . Katika maisha yangu yote sijawahi kuingia katika casino.”akasema Arnold na kuwafanya wale jamaa wacheke

“ Ok Arnold tusikupotezee m,uda kwani inaonekana hupendi kukaa sehemu kama hizi.Tuingie moja kwa moja katika biashara yetu .Umekujana kifaa chetu?

“ Ndiyo ninacho hapa.”akajibu Arnold na kuufungua mkoba wake akatoa kile kifaa akakiweka mezani na kukiwasha.Akaanza kuwalekeza namna kinavyofanya kazi.Wale jamaa wakafurahi sana

“ Una hakika kwamba kifaa hicho kimeunganishwa katika gari la mlengwa ambaye tulikuelekeza?

“ Nina uhakika huo.Kifaa kile kimwekwa katika gari la mtu mnayemuhitaji.” Akasema Arnold.Wale jamaa wakatulia kama dakika tano hivi wakikitazama kifaa kile halafu mmoja wao akasema

“ Ok kazi nzuri sana Arnold.”akaingiza mkono mfukoni na kutoa bahasha akampatia Arnold

“ Mzigo wako uliobakia huu hapa.Milioni tano taslimu.Tunashukuru kwa kazi nzuri.Ila tunakupa angalizo kwamba endapo kutakuwa na aina yoyote ya udanganyifu basi tunajua sehemu ya kukupata.Tunafahamu unakosihi,tunakufahamu zaidi ya unavyojifahamu kwa hiyo sekunde yoyote tukikuhitaji tunaweza kukupata” akasema mmoja wa wale jamaa

“Msihofu ndugu zangu,Kila kitu k imefanyika kama mlivyotaka na endapo kutakuwa na tatizo lolote basi nitafuteni nitakuja kurekebisha”akasema Arnold akaagana na wale jamaa akainuka na kuanza kushuka ngazi kuelekea chini.Mathew aliyekuwa amekaa katika meza ya pembeni ambayo haikuwa na watu alishuhudia kila kilichokuwa kinaendelea.Akampigia simu Anitha

“ Anitha tayari biashara imefanyika na Arnold anashuka.Ninaendelea kuwafuatilia hawa jamaa bado wamekaa hapa mezani.Niko meza ya pemb……” Mathew akasita kidogo baada ya kumuona mmoja wao akichukua simu na kupiga.Kwa kuwa hakuwa mbali aliweza kusikia maongezi ya yule jamaa

“Mathew whats going on? Nimemuona Arnold ametoka ameingia katika taksi,tumuache aondoke? Akauliza Anitha lakini Mathew hakujibu kitu alikuwa ametega sikio kusikiliza alichokuwa anaongea yule jamaa.

“ Tayari amekwishatukabidhi kifaa na yuko njiani anashuka.Fanyeni kazi yenu na rudisheni fedha zote ” akasema yule jamaa aliyekuwa akiongea na simu.Mathew akainuka katika ile meza aliyokuwa amekaa na kuanza kushuka chini kwa kasi hadi katika gari lao.

“ Anitha ,they are going to kill him.Nimemsikia mmoja wa wale jamaa aliyewakabidhi kile kifaa akitoa maelekezo kwamba Afuatiliwe.Wanakwenda kumuua na kuchukua fedha zote walizompatia..Nilitegemea kitu kama hiki kutokea.” Akasema Mathew

“ Gari alilopanda Arnold limeondoka hapa kama dakika mbili zilizopita.”

“ Endesha gari tunamfuatilia ,tukamuokoe Arnold.” Akasema Mathew.

“ Mathew hebu subiri kwanza,ninaona kile kifaa kinaondoka .Inaonekana wale jamaa wamehamamezaau wanaondoka ” akasema Anitha

“ Ouh my God what are we going to do? Mathew akajiuliza

“ Tuchague moja Mathew.Tumfuatilie Arnold au tuwafuatilie hawa jamaa wenye kifaa? Akauliza Anitha.Mathew akafikirikwa sekunde chache na kusema

“ Ok ngoja tuachane na Arnold ,tuwafuatilie hawa jamaa.Wait for me here I’m going in” akasema Mathew na kutembea kwa kasi kuelekea ndani.Katika mlango wa kuingilia ndani ya Casino akakutana na wale jamaa wawili wakitoka.Alipishana nao ili wasiweze kumstukia kama anawafuatilia.Akatoa simu na kumpiga Anitha

“ Anitha kuna watu Fulani wawili wametoka sasa hivi ndani ya casino na wanaelekea katika maegesho mmoja amevaa sutiya bluu na mwingine nyeusi hao ndio wenye kile kifaa.Hao ndio tunaotakiwa kuwafuatilia” akasema Mathew.Anitha aliyekuwa ndani ya gari akafungua mlango akashuka na kuangaza angaza macho katika eneo la maegesho ni kweli aliwaona watu wawili alioelekezwa na Mathew

“ Mathew nimewaona hao jamaa ulioniambia.Wanaingia kati agari Fulani la bluu”

“ Ok Anitha hao ndio tunaopaswa kuwafuatilia” akasema Mathew huku naye akipiga hatua ndefu kuelekea maegesho lilipo gari lao akainga tayari kabisa k uanza kuwafuatilia wale jamaa ambao kwa muda huo gari lao lilikuwa katika geti la kutokea..Anitha akawasha gari nao wakaondoka wakiwafuata wale jamaa ambao hawakuwa na habari kama wanafuatilia.

“ leo lazima tuwafahamu watu hawa ni akina nani,inaonekana ni watu wenye mtandao mkubwa “ akasema Mathew.Anitha aliyekuwa makini katika usukani akasema

“ Kwa nini tusimtaarifu Arnold kwamba anafuatiliwa ili atafute namna ya kujiokoa?

“ Wazo lako zuri lakini Arnold akijua kwamba anafuatiliwa sehemu yake ya kwanza kwenda ni polisi na hiyo inaweza ikawa mbaya kwa upandewetu.Hatuhitaji misuguano na vyombo vya usalama”

“So how are we going to help him? Are going to let him die? Akauliza Anitha

“ I’m sorry Anitha kwa sasa hatuna namna tunayoweza kufanya kumsaidia Arnold” akasema Mathew

“ Ouh my God ! he’s so young to die” akasema Anitha kwa masikitiko.

“ Anitha katika kazi hizi kuna nyakati ambazo inakulazimu kufanya maamuzi magumu sana ili kuweza kupata kitu cha muhimu.Kwa sasa hawa jamaa tunaowafuatilia ni muhimu sana kwetu.” Akasema Mathew na mara simu yake ikaita.likuwa ni jaji Elibarii

“ hallow Elibariki”

“ Mathew nimekuja kwako nimekukosa,nimetoka kidogo ninakwenda k uonana na mke wangu ameniita mara moja lakini nitarudi muda si mrefu.Nimeongozana na Noah ametaka kutoka ili apunge upepo kidogo kwani ameboreka sana palenyumbani peke yake.Nitakaporejea kuna jambo kubwa nataka kukwambia .”

“ Ok Elibariki,kuna kitu nakifuatilia sintakawia sana.” akasema Mathew na kukata simu wakaendelea na safari ya kuwafuatilia wale jamaa



*******



Katika jengp linalotumiwa kama ofisi kuu za Team SC41 ,hali ilikuwa ni ya ukimya sana.Kutwa nzima shughuli ilikuwa ni moja tu,kuizika miili ya vijana sita waliouawa katika mapambano na akina Mathew.Ndani ya chumba kikubwa kinachotumiwa kwa mikutano watu wapatao 27 walikuwa wamekaa kuizunguka meza kubwa wakisubiri kuunganishwa na kiongozi mkuu wa Team SC41 kutoka nchini marekani.Mitambo ilipokuwa tayari Luninga kubwa iliyokuwa ndani ya kile chumba ikawashwa na mtu mmoja akaonekana.Osmund aliyekuwa amekaa mbele kabisa ya meza ile kubwa akasema

“ Mr Albert,mbele yako ni Team SC41 afrika mashariki. Ndani ya chumba hiki kuna vijana 27 wenzetu sita waliuawa jana na watatu wanamuhudumia John Mwaulaya.Vijana wote waliouawa jana tumekwisha wazika na kwa sasa tunajiandaa kuanza kuwatafuta wale wote waliofanya shambulio lile la jana.Karibu Mr Albert uongee na vijana”akasema Osmund

“ Nashukuru sana Osmund kwa kunipa nafasi hiiya kuongea nanyi machache.Ni muda mrefu hatujafanya kikao cha pamoja kama hiki.” Akazema Mr Albert akiongea moja kwa moja toka Marekani

“ Awali ya yote nawapeni pole sana kwa kuwapoteza wenzenusita.Ni mara ya kwanza kwa Team SC 41 afrika ya mashariki kupoteza watu wengi kiasi hicho.Tukio hili limetustua sana makao makuu na tunataka tufanye uchunguzi wa kina tufahamu ni kwa nini vijana wote hao wameuawa? Naomba kwa dakika moja niwakumbushe madhumuni ya kuundwa Team SC 41.Kikundi hiki kiliundwa kwa ajili ya kuyalinda maslahi ya Marekani katika eneo la afrika mashariki,kuhakikisha uwekezaji wa Marekani katika eneo hili unakuwa salama na ndiyo maana kazi zake hufanyika kwa siri kubwa bila kujulikana.Hata ndani ya serikali ya Marekani ni watu wachache sana wanaofahamu uwepo wake.Team SC 41 si kikundi cha mapambano japokuwa inapolazimu kutumia nguvu huwa tunatumia lakini ni hadi pale inapobidi.Tukio lililotokea jana inaonekana wazi kabisa kwamba kulikuwa na mapambano yaliyosababisha kuuawa kwa vijana hao sita.Kufuatia tukio hili tunatuma timu ya wataalamu sita kuja kuchunguza nini hasa kilitokea na kutupa taarifa ili tuchukue hatua zipasazo.Kwa hiyo kuanzia dakika hii naomba mfute kabisa mipango yote ya kulipiza kisasi mnayoipanga hadi hapo wachunguzi wetu watakapokamilisha uchunguzi wao.Narudi tena sitaki kusikia tena aina yoyote ya mapigano.Kama kuna tatizo lolote lile kabla ya kulikabili ombeni kwanza ushauri makao makuu au kwa John Mwaulaya.Ingawa anaumwa lakini ni mtu ambaye binafsi ninamuamini sana.Wakati wa uongozi wake hakujawahi kutokea tukio kama hili.John anaifahamu vilivyo Team SC41 na nini malengo yake kwa hiyo endapo mkihitaji ushauri mnaweza mkaupata toka kwake.Nimeelezwa kwamba Dr Burke anawasili k esho ili kuja kuangalia afya yake na kutushauri nini cha kufanya.Kama mnavyojua John hawezi kutibiwa katika hospitali yoyote nchini Tanzania na hata hapa Marekani kwa hiyo tutatafuta namna bora ya kuweza kushughulikia suala la ugonjwa wake..Narudia tena kwamba sitaki kusikia aina yoyote ya mapigano .Kujulikana kwa Team SC 41 ni hatari sana kwa mahusiano ya Marekani na nchi za Afrika ya mashariki.Kujulikana kwake kunaweza kuhatarisha uwekezaji mkubwa wa marekani katika eneo hili na ndiyo maana nimewakumbusha tena misingiya kuanzishwa Team SC 41.Kitu cha mwisho ninachotaka kuwakumbusha ni kuongeza juhudi katika opereshi 26 B. Kumeonekana kuwa na uzembe mkubwa na kusua sua katika operesheni hii ambayo ni muhimu sana kwa usalama wa taifa la Marekani.Endapo mtashindwa katika operesheni hii basi maelfu ya raia wa Marekani watapoteza maisha .Nawaombeni ndaniya mwezi mmoja toka sasa muwe mmekwishapiga hatua ya kuridhisha katika operesheni hiyo.Nawatakia kila la heri ahsanteni”akasema Mr Albert Mackson na Luninga ikazimwa.Osmund akawageukia vijana wake

“ jamani nadhani mmemsikia mkuu alivyosema.Mipango yote tuliyokuwa tuipange kuhusiana na kilichotokea jana tunaivuruga yote.Hakuna tena mpango wowote wa kuwatafuta wale jamaa.Kwa sasa tunaelekeza nguvu katika operesheni 26 B.Peniela ndiye tegemeo letu katika kuifanikisha operesheni hii.Tunatakiwa kumpatia kila aina ya msaada ili aweze kuifanikisha operesheni hii.Tumepewa mwezi mmoja tuwe tumepiga hatua.Kuanzia sasa hakuna kulala,tutafanya kazi usiku na mchana hadi tuhakikishe tumemaliza jambo hili kwani kama mlivyosikia wenyewe ,usalama wa Marekani uko mikononi mwetu hivi sasa kwani tuko hapa kwa maslahiya Marekani na endapo tutashidwa katika operesheni hii basi tutakuwa tumeshndwa kazi yetu kama Team SC41.Kwa kuwa tulikuwa na siku ndefu sana nawaombeni mkapumzike na kesho asubuhi tukutane tena ili kuanza mikakati mipya ya kuifanikisha operesheni 26 B.” akasema Osmund na vijana wote wakatawanyika.Alipohakikisha vijana wote wametoka mle ndani akachukua simu na kumpigia Peniela

“ Hallow Peniela” akasema Osmund baada ya Penny kupokea simu

“ Osmund” akasema Penny

“ Peniela nimetoka kuongea na makao makuu Marekani sasa hivi na wanasisitiza kwamba tufanye haraka iwezekanavyo kukamilisha operesheni 26 B.Nataka tuonane kesho ili tuweke mikakati mipya ya namna tutakavyoimaliza operesheni hii ndani ya kipndi cha mwezi mmoja”

“ Osmund naomba tuelewane.Mlinikabidhi kazi hii kwa hiyo niachieni nilishughulikie jambo hili kwa namna ninavyoona linafaa.Sitaki shinikizo lolote.Nipeni wiki mbili nitakuwa na jibu zuri la kuwapa. Halafu Osmund ninataka kuonana na John Mwaulaya .Kuna mambo ya maana ambayo nahitaji kuongea naye” akasema Paniela

“ Unataka kuongea naye jambo gani?

“ Ni mambo binafsi”

Osmund akafikiri kidogo halafu akasema

“ Ok nitaongea naye na kumtaarifu kwamba unataka kumuona ila naomba tuwasiliane mara kwa mara kuhusiana na operesheni yetu.”

“ Wanatumwa watu kuja kuchunguza kilichosababisha mapigano yale.Ni wazi nilifanya makosa makubwa kumteka mke wa Dr Michael kwani ndiye chanzo cha haya yote kutokea.Lakini nilifanya hivyo kwa ajili ya kumsaidia John Mwaulaya .Lakini nini kitatokea endapo nitabainika kwamba ni mimi ndiye niliyesababisha vijana wale wote kuuawa? Tuhuma zote zinaniangukia mimi .I have to do something very fast.i have to kill john



Noah na jaji Elibariki waliendelea na safari .Noah aliyekuwa akiendesha gari kuupa mazoezi mguu wake aliendesha kwa uangalifu mkubwa hadi walipofika katika makazi binafsi ya rais ambako Elibariki alikwenda kuonana na mke wake Flaviana..Watu walikuwa ni wengi na kwaya mbali mbali ziliendelea kutumbuiza kuwafariji waombolezaji

“Noah kama hutajali naomba unisubiri humu humu garini kwa sababu sintachukua muda mrefu.Nataka nimsikie tu mke wangu anataka kuniambia kitu gani halafu ninakuja tuondoke tukamsubiri Mathew.Lazima nionane naye usiku wa leo.Kuna mambo ya msingi sana ya kuongea naye. “ akasema jaji Elibariki halafu akashuka na kumuacha Noah mle garini.Kutokana na watu kuwa wengi ikamlazimu Elibariki kumpigia simu mke wake atoke nje ili waonane.Bila kupoteza muda Flaviana akatoka wakaelekea bustanini ambako hakukuwa na watu

“ Vipi maendeleo yako? Unajisikiaje sasa hivi? Akauliza Elibariki



“ Kwa sasa ninaendelea vizuri sana.Sina tatizo lolote.Dr Amosa kanipima na kasema hakuna tatizo lolote ” akasema Flaviana

“ Good.Kuna mabadilio yoyote katika ratiba ya kesho kuhusu mazishi? Akauliza Elibariki



“ Mpaka sasa hakuna mabadiliko yoyote ya ratiba.Ninadhani kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa” akasema Flaviana

“ Ok Flaviana nimekuja mara moja kukuona kama ulivyonitaka .Kuna sehemu nahitaji kufika usiku huu.Niambie ni kitu gani ulichotaka kuniambia ? akasema jaji Elibariki



“ Elibariki nimekuita ili tuongee kuhusiana na kile kilichotokea jioni ya leo kuhusu zile ripoti za uchunguzi wa kifo cha mama” akasema Flaviana

“ Flaviana tuongee kuhusu nini? Mjadala kuhusiana na suala lile umekwisha fungwa na baba yako amesema hataki tena jambo hili liendelee na hata wewe mwenyewe umekwisha ridhika na matokeo.Nilihangaika na kuwaletea ripoti ya ukweli mmeikataa tena kwa maneno ya kashfa sana.Sasa tuongee kuhusu nini? Akauliza jaji Elibariki



“ Elibariki naomba uelewe kwamba ripoti yako haijadharauliwa.Ninakushukuru kwa kazi kubwa na ngumu uliyoifanya hadi ukaipata ripoti ile lakini naomba uelewe kwamba suala hili ni gumu sana kwangu kiasi cha kuniweka njia panda .Nashindwa kuamua taarifa ipi ni sahihi.Lakini kwa hali halisi hata kama ungekuwa ni wewe uko mahala pangu ni wazi ungekubalina na taarifa ile ya madaktari bingwa.Sisemi kwamba taarifa yako haikuwa na ukweli lakini inawezekana madaktari uliowatumia katika kuipata taarifa hiyo kuna kitu walikikosea ama waliifanya kwa haraka na ndiyo maana wakaja na majibu yale.Taarifa yako inasema kwamba mama alikufa kwa kuchomwa sindano yenye sumu lakini taarifa ya madaktari bingwa inasema kwamba hakukuwa na aina yoyote ya sumu iliyokutwa iliyopelekea mama kufariki.Taarifa hizi mbili zinakinzana kwa hiyo ninapata wakati mgumu sana wa kuamua ni taarifa ipi iko sahihi lakini kutokana na mazingira yalivyo ninalazimika kuiamini taarifa ya madaktari” akasema Flaviana.Jaji Elibariki akatabasamu kidogo na kusema

“ Flaviana kama nilivyokwambia awali kwamba sikulazimishi uniamini au kuiamini taarifa niliyokupa.Najua unamuamini baba yako kuliko mimi.Hata hivyo ninashukuru kwa dharau za baba yako alizozionyesha kwangu leo ila kinachonisikitisha ni kwamba uhai wa mtu ulipotea katika kuipata taarifa ile lakini juhudi zote hizi zimekuwa kazi bure na badala yake ninaambulia dharau na matusi.Nilikosea sana kukubali kuifanya ile na kusahau kwamba ni familia hii hii ambayo imekuwa iinidharau kila uchao na kuniona kama takataka.” Akasema jaji Elibariki



“ Eli nimekwambia usiyajali maneno ya baba.Nina hakika aliyasema maneno yale kutokana na hasira na pengine hasira zake zikipoa mnaweza mkakaa na kumaliza tofauti zenu.”

“ si mara ya kwanza kwa baba yako kunitamkia maneno ya kejeli kama aliyoyatamka leo.Nimeyapokea yote lakini nakuhakikishia kwamba siku moja nyote mtakubaliana na kile nilichowaambia,lakini mpaka mtakapoubaini ukweli tayari mtakuwa mmekwisha chelewa sana“

“ Eli naomba tafadhali tusifikie hatua ya kuanza kulumbana.Mama yangu bado hajazikwa na sitaki machungu mengine kwa hivi sasa.Nilikuita ili tuongee kama watu wazima lakini naona mwenzangu bado umepandwa na hasira na umenikasirikia mimi kama ndiye niliyekutamkia maneno yale”



“ Hatulumbani Flaviana ila ninakueleza ukweli kwamba kuna jambo linaloendelea hapa ikulu lakini nyote hamtaki kuniamini.Nina hakika kuna siku itakuja mtayaamini maneno yangu” akasema jaji Elibariki



“ Eli naomba usiendee kuniumiza kichwa changu .Nina mambo mengi ya maana yanayopaswa kuumiza kichwa changu na si suala hili ambalo halina umuhimu wowote tena.Ninadhani hatutaweza kuelewana kwa sababu bado una hasira.You can just leave.Nenda unakotaka kwenda” akasema Flaviana akionekana kukasirika

“ Ahsante sana Flaviana.Ni kweli hatuna tena kitu cha kuongea.Mimi ninaondoka nitarejea baadae au asubuhi kwa ajili ya kuwahi ndege ya kuelekea kijijini” akasema jaji Elibariki na kuondoka .Hakutaka kukaa tena pale msibani .Maneno aliyokuwa ametamkiwa na Dr Joshua yalimchefua sana.Moja kwa moja akaelekea katika gari lake ambako alikuwemo Noah.Akakishika kitasa kwa ajili yakuufungua mlango lakini kabla hajaufungua simu yake ikaita.Akaichukua na kutazama mpigaji.Zilikuwa ni namba ngeni kabisa katika simu yake



“ Halow” akasema jaji Elibarki



“ Elibariki don’t get in that car” ikasema sauti ya mwanamke upande wa pili wa simu



“ What ?! jaji Elibariki akastuka na kusogea pembeni



“ Usiingie ndani ya hilo gari.” Ikasema tena sauti ile



“ Wewe ni nani na kwa nini nisiingie ndani ya gari langu? Akauliza jaji Elibariki



“ Ninakuonya usiingie ndani ya gari lako.You are going to die”

“ I’m going to die? Akauliza

“ yes you are going to die.Please listen to me and don’t get in that car” akasema Yule mwanamke



“ Wewe ni nani? Uko wapi.Who are going to kill me?” akauliza Elibariki

“ Elibariki tafadhali sina muda wa kupoteza.Naomba tafadhali unisikilize ninachokwambia na kama huniamini basi ingia ndani ya hilo gari lako” ikaonya sauti ya Yule mwanamke.Jaji Elibariki akabaki amesimama hajui afanye nini.Akageuka akalitazama gari lake halafu akasema

“ Sikufahamu wewe ni nani na siwezi kukuamini.Goodbye” akasema jaji Elibariki



“ Elib…………..” kabla Yule mwanamke hajamaliza , Elibariki akakata simu.Akavuta pumzi ndefu .Alionekana kuchanganyikiwa

“ Ni nani huyu aliyenipigia simu? Kwa nini ananionya nisiingie katika gari langu? Ni akina nani wanaotaka kuniua? Akajiuliza

“ I have to talk to Mathew.Yeye ndiye anayeweza kunishauri kitu cha kufanya” akawaza na kuzitafuta namba za Mathew akapiga lakini hazikuwa zikipatika

“ Ouh my God ! Mathew hapatikani.Nitafanya nini? Akawaza kwa sekunde kadhaa

“Ngoja tu niingie garini niondoke.Hakuna lolote litakalotokea.Vitisho kama hivi nimevizoea.” akawaza jaji Elibariki huku akiufungua mlango wa gari lake na kuingia.



“ Eli kwema huko utokako ? Akauliza Noah baada ya kumuona namna jaji Eibariki alivyobadilika

“ Kwema Noah.Ni mambo ya kawaida ya wanawake” akasema huku akijifuta jasho

“ Can we go? Akauliza Noah



“ Yes .Let us go” akasema jaji Elibariki Noah akawasha gari wakaondoka.Jaji Elibariki alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa.Alikuwa akitazama huku na huku.



“ Noah umekumbuka kutembea na bastora yako? Akauliza jaji Elibariki

“ Hapana Eli,sikuchukua bastora.Kwani kuna tatizo lolote? Akauliza Noah

“ Hapana Noah.Hakuna tatizo nilitaka tu kujua kama ulikumbuka kuchukua bastora yako”

“ Sikuichukua .Katika matembezi ya kawaida kama haya huwa sitembei na silaha “ akasema Noah huku akiendelea kukanyaga mafuta.Bado jaji Elibariki aliendelea kumtafakari mwanamke Yule simuni

“Simfahamu mwanamke Yule na sifahamu amezitoa wapi namba zangu za simu.Kwa nini aniambie maneno kama yale? Akaendelea kujiuliza



“ Yawezekana ikawa ni moja ya njama za Flaviana kunitaka niendelee kukaa pale msibani ,akampa mmoja wa marafiki zake namba zangu anipigie na kunitisha.Lazima atakuwa ni mwenyewe kwani hakuonekana kufurahi nilipomwambia kwamba kuna mahala ninakwenda.Labda anadhani kwamba ninakwenda kwa mwanamke mwingine.Lakini wivu wa nini wakati hanithamini mimi kama mume wake? Angejua kwamba kwa hivi sasa moyo wangu haudundi kwake hata kidogo wala asigethubutu kuwa na wivu.Kwa sasa akili yangu yote inamuwaza mtu mmoja kwa sasa,Peniela.Sijui ni kwa nini msichana yule ameniingia katika damu yangu kiasi hiki.Pamoja na tukio lile lililotokea la kugombana na Jason lakini bado akili yangu haiachi kumuwaza.Bado amejaa tele katika kichwa changu.Natamani sana kumuona na kuongea naye” akawaza jaji Elibariki na kumbu kumbu ya ugomvi uliotokea nyumbani kwa Peniela kati yake na Jason ikamjia akauma meno kwa hasira.



“ Sikujua kama Jason ni kijana mshenzi kiasi kile.Nimetokea kumchukia sana kwa kitendo alichokifanya cha kuingia na kuanzisha ugomvi huku akijinadi kwamba Peniela ni msichana wake.Mbona hakuwahi kuniambia kama ana mahusiano na Peniela? Asicheze na mimi Yule kijana nitamuhamisha huu mji.Sisi ndio wazawa wa jiji hili na akitaka mashindano na mimi nitamfanyia kitu kibaya.Lakini inawezekana akawa kweli na mahusiano na Peniela? Halafu siku ile ya ugomvi kuna wale watu walitokea na kuondoka na Peniela na mimi wakanipeleka hospitali ni akina nani wale? Wana mahusiano gani na Peniela? Mbona walikuwa wamevalia nadhifu sana na hata magari yao yalionekanakuwa ni ya kifahari sana? Peniela alikwenda wapi na wale jamaa usiku ule? Kuna haja ya kumuuliza Peniela na kuufahamu ukweli.Kuna hajaya kumfahamu msichana yule kiundani.Inawezekana akawa na mabwana kibao . ” Akawaza jaji Elibariki







*********







Mara tu gari ya jaji Elibariki ilipotoka katika makazi binafsi ya rais,mtu mmoja aliyekuwa amesimama nje ya gari moja jeusi akiwa amevalia suti nyeusi ,akachukua simu yake ya mkononi na kupiga katika namba Fulani

“ He’s moving out now” akasema Yule jamaa

“ We’ re in position waiting”

“ Kunaonekana watu wawili ndani ya gari.Take them all.Remember no mistake “ akasema Yule jamaa



“ Ok tumekusoma” ikasema sauti ya upande wa pili.

Yule jamaa akaingia katika gari lake na kuondoka maeneo yale.Akiwa ndani ya gari lake akazitafuta namba za simu za Dr Kigomba akampigia



“ Hallow Festo” akasema Dr Kigomba baada ya kupokea simu



“ Mzee kila kitu kinakwenda sawa.Tayari jamaa yuko barabarani na vijana wamekwisha jipanga.Ila kama nilivyokufahamisha awali kwamba kwa mazingira haya ya jiji la Dar es salaam kutengeneza ajali ambayo inaweza ikamuondoa Yule jamaa ni magumu sana kutokana na msongamano lakini tutakwenda na plan B.”

“ Vyovyote itakavyokuwa Festo lakini hakikisheni mmeikamilisha kazi.Wakumbushe vijana kuwa makini sana”

“ Vijana wako makini sana.Nitakupa taarifa baada ya nusu saa.” akasema Yule jamaa na kukata simu







*******





Mathew na Anitha waliendelea kuwafuatilia wale jamaa japokuwa haikuwa kazi rahisi kwa usiku ule . Iliwalazimu kutumia mbinu za hali ya juu sana kuwafuatilia wale jamaa .Mathew alikuwa makini katika usukani na Anitha hakubandua jicho katika kompyuta yake iliyokuwa ikionyesha mwendo wa ile tablet waliyopewa wale jamaa kwani aliiwekea program maalum ya kuweza kuifuatilia .

Safari yao iliwafikisha hadi Kigamboni katka nyumba moja kubwa iliyokuwa na uzio mrefu kiasi kwamba haikuwa rahisi kutazama kilichokuwa kinaendelea mle ndani.Mathew na Anitha waliipita nyumba ile na kwenda kusimamisha gari mbele kidogo kulikokuwa na baa

“ Anitha utabaki ndani ya gari.Mimi ninarudi katika ile nyumba nataka nikawafuatilie wale jamaa.” Akasema Mathew



“ Mathew ni hatari sana kama ukienda peke yako.Hatuwajui watu wale ni akina nani kwa hiyo kuna kila ulazima wa kuchukua tahadhari.Naomba tuongozane wote.Nitakulinda” Akasema Anitha



“ Anitha wewe ndiye mtu ninayekutegemea sana katika kazi zangu nyingi kwa hiyo sitaki kabisa upatwe hata na mkwaruzo.Hakuna ajuaye yawezekana kule ndani kukawa na makabiliano ya risasi na wewe huna uzoefu sana na mambo kama kwa hiyo niachie mimi nikaifanye hii kazi.Nitakuwa nikikupa taarifa ya kila kinachoendelea” akasema Mathew huku akilifungua begi lake na kutoa kisanduku Fulani kidogo na kuchukua kidude kidogo akakiweka sikioni na kubonyeza kitufe chenye rangi ya kijani katika kile kisanduku taa nyekundu ikawaka.

“ Good.Kila kitu kinakwenda vizuri” akasema na kulivaa begi lake mgongoni akashuka na kuanza kupiga hatua kuelekea katika ile nyumba waliyoingia wale jamaa.



“ Anitha nipe ripoti.Kuna mabadiliko yoyote katika kompyuta yako? “ akasema Mathew akiwa hatua chache kuifikia ile nyumba

“ bado kifaa kipo ndani na hakijatoka”



“Ok good .Nimekaribia sana“ akasema .Alitaka kuzunguka kwa nyuma lakini akagundua kwamba mlango mdogo katika geti ulikuwa haukuwa umefungwa,ulikuwa umerudishwa tu, akausukuma taratibu na kuchungulia ndani.Kulikuwa na gari mbili zimeegeshwa na nyingine namoja ilionekana mbovu kwani ilikuwa imefunikwa na turubai.Mbwa mkubwa alionekana kuzunguka zunguka mle ndani.

“ Kitu cha kwanza ni kumnyamazisha yule mbwa,kwa sababu akibweka tu atawastua watu waliomo ndani.” Akawaza Mathew na kisha akaitoa bastora yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti akajiweka vizuri na kumlenga mbwa aliyekuwa amesimama pembeni ya gari.

“ Help me Lord.Nikimkosa huyu mbwa nitakuwa nimeharibu kila kitu”akawaza Mathew na kuachia risasi iliyompata yule mbwa kichwani ,akatoa ukelee mdogo na kuanguka chini akatapa apa.Kabla mbwa yule hajakata roho tayari Mathew aliingia ndani na kukimbia kama paka hadi nyuma ya gari moja akajibanza .Aliangza angaza kama kuna mtu yeyote aliyesikia ukulele uliotolewa na yule mbwa lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyetoka .Ndani ya ile nyumba taa zilikuwa zinawaka na sauti za watu wakicheka kicheko kikubwa zikasikika..Taratibu akanyata na kuzunguka hadi nyuma ya ile nyumba ambako kulikuwa na mlango ambao haukuwa umefungwa.Akaufungua taratibu mlango ule na kuingia ndani.Alijikuta ametokea jikoni.Hakukuwa na mtu pale jikoni na kwa mbali alisikia sauti za watu wakiongea na kucheka.Akiwa bado anatafakari namna ya kufanya mara akasikia hatua za mtu akielekea maeneo yale ya jikoni.Hakukuwa na sehemu ya kujificha kwa haraka hivyo ikamlazimu kujibanza pembeni ya mlango.



“ Yvone..!! mtu yule aliyekuwa akielekea kule jikoni akaita na kuchungulia lakini hakuona mtu akaondoka.Bado sauti za watu wakiongea nakucheka kwa nguvu zilisikika..Mathew akaufungua ule mlangowa jikoni taratibu na kuchungulia .Katika Chumba kilichofuata kulikuwa na meza ya duara na viti sita.Moja kwa moja akajua kile ni chumba cha kulia chakula.Alipohakikisha kwamba hakuna mtu yeyote katika kile chumba akatoka jikoni na kuingia katika kile chumba cha chakula.Bado aliendelea kuzisikia sauti za watu wakiongea na kucheka.Kulikuwa na mlango mkubwa wa kioo akachungulia na kuwaona watu wanne wamekaa katika sebule wakiongea na huku ile tablet iliyotoka kwa Arnold ikiwa mezani.Mathew akawasoma vizuri na kujiweka sawa kwa ajili ya kuwakabili wale jamaa lakini mara akatokea mtu mwingine na kumfanya Mathew asite kidogo.Mtu yule aliyeingia sebuleni alikuwa amekasirika na alikuwa akiongea kwa sauti kubwa hadi Mathew akasikia



“ Yule mtoto mpumbavu sana na leo pia amegoma kula.Tutamfanya nini? Hali yake inazidi kuwa mbaya.Tukifanya mchezo atakufa yule binti” akasema yule jamaa

“ Sijui tutamfanya nini huyu binti lakini hata kama akigoma kula lazima tutaupata mzigo wetu.Kwa sasa tuna uhakika asilimia mia moja kuupata. Ninahakika lazima atakuwa ameuficha kwa huyu msichana .” akasema mwingine huku akiitazama ile tablet



“ Lakini Kwa nini yule kijana aliyetutengenezea hii program tumuue? Ana kosa gani? Akauliza mmoja wao

“ Yule kijana ni hatari sana kwetu.Vijana kama wale mara nyingi huwa wanaingiwa na tama kwa hiyo angeweza hata kuja tena siku za usoni na kututishia kuturipoti kwa vyombo vya dola na kudai pesa nyingi.Kwa kuwa hatuna kazi naye tena,basi kinachofuata ni kumuua tu.Hivyo ndivyo mambo huwa yanakwenda”akasema mmoja wa wale jamaa aliyekuwa ameishika ile tablet.

“Hebu twendeni tukamuone yule binti tujue namna ya kufanya.Haliyake si nzuri hata kidogo” akasema yule jamaa aliyewafuata wenzake pale sebuleni.Wote wakainuka na kumuacha mtu mmoja aliyekuwa ameishika ile tablet.Mathew alikuwa akiona kila kitu kilichokuwa kinaendelea kupitia kioo cha mlango.Wale jamaa walipoondoka pale sebuleni ,akaufungua ule mlango taratibu .Mtu yule aliyekuwa pale sebuleni akiwa hana hili wala lile ameiinama ile tablet mara akahisi kama kuna mtu amesimama mbele yake.Akainua kichwa na kukutana na bastora ikimtazama.Akastuka sana na kuiangusha chini ile tablet



“Shhhhhh!!!!..Usijaribu kufanya chochote.Kaa hivyo hivyo”akasema Mathew kwa sauti ya chini .Yule jamaa alikuwa anatetemeka.Hakuamini kama ni kweli alikuwa akitazamana na bastora



“ tafadhali naomba usiniue.Kuna fedha nyingi ndani nitakupatia”akasema yule jamaa kwa sauti yenye kitetemeshi.Alikuwa ameogopa sana



“ Wenzako wamekwenda wapi? Akauliza Mathew



“ wamekwenda ..wamekwenda….’ akasita,alikuwa anatetemeka



“ Niambie wenzako wako wapi la sivyo nitakifumua kichwa chako kwa risasi” akafoka Mathew



“ Usi.usi..usiniue tafadhali..Wamekwenda kumtazama mgonjwa amegoma kula.”

“ kwa nini mnamfuatilia Eva? Akauliza Mathew.Yule jamaa aliyekuwa amekaa akitetemeka akashindwa kujibu

“Nakuuliza kwa nini mnamfuatilia Eva? Akauliza Mathew.Yule jama alishindwa aseme nini midomo ilikuwa inamcheza.Mathew hakutaka kupoteza muda akamsogelea na kumuwekea bastora kichwani



“ Niambie kwa nini mnamfuatilia Eva? Akauliza Mathew.Kabla yule jamaa hajajibu kitu ukasikika mlio wa glasi kuanguka na kuvunjika .Mathew akageuka haraka haraka na kuangalia kilichotokea.Msichana mmopja alikuwa ameangusha sinia alilokuwwa amelibeba baada ya kuingia pale sebuleni na kumkuta Mathew akiwa amemuelekezea yule jamaa bastora.Yule mwanamke aligeuka haraka na kuanza kukimbia huku akipiga kelele.Kufumba na kufumbua Mathew akampiga yule jamaa pigo moja kichwani na kumpoteza fahamu.Kelele za yule mwanamke zakuomba msaada ziliwastua jamaa wale wengine na kuwafanya watoke mbio kuja kuangalia nini kimetokea.Mathew alikwishawaona na bila kupoteza muda akacheza vizuri ma bastora yake kama vile alizaliwa nayo na kuzimimina risasi .Lilikuwa nishambulio la kustukiza na kutahamaki wote wakajikuta wakiwa chini wamelalia sakafu iliyojaa damu.Hawakuwa na uhai tena.Yule msichana aliyekuwa akipiga kelele alikuwa ameanguka chini akilia akiomba ahurumiwe.Mathew ambaye kwa sasa alikuwa mithili ya Simba akamuamuru ainuke.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Kulikuwa na watu wangapi humu? Akauliza Mathew.Huku akitetemeka yule msichana akajibu

“Kulikuwa na watu..” akasita kidogo kama vile anajaribu kukumbuka idadi ya watu



“ Kulikuw ana watu wangapi ? akauliza Mathe kwa ukali

“Kulikuwa na watu sita .Hawa jamaa wanne uliowapiga risasi na yule mwingine kule sebuleni na mmi.halafu kuna……”akasita



“ Kuna nini?



“Kuna msichana mwingine yuko chumbani”

“ Anafanya nini chumbani? Akauliza Mathew.Yule msichana akabaki kimya
ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog