Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

PENIELA (STORY YA KIJASUSI) - 5

 





    Simulizi : Peniela (Story Ya Kijasusi)

    Sehemu Ya Tano (5)


    “nahitaji Jina”

    “ Anaitwa Dr Albert kigomba.”

    “ yeye alipewa maagizo hayo na nani?

    “ Sifahamu aliambiwa na nani.Sisi ni watendaji tu na tukipokea agizo tunalifanyia kazi” akasema Adolf

    “ Ok sasa kilichonifanya nikutafute ni kwamba unatakiwa uufanyie uchunguzi mwili wa Dr Flora na kubaini kilichomuua usiku wa leo”

    “ What ?!!...Adolf akashangaa

    “ Nataka ufanye uchunguzi wa kubaini kilichomuua Dr Flora usiku wa leo”

    “ No ! I cant do that!!..Tumekatazwa kufanya hivyo na siwezi kwenda kinyume na maagizo hayo”

    “ Ninasema kwamba utafanya ninavyokuelekeza.Ninataka ufanye uchunguzi wa mwili wa Dr Flora usiku wa leo”

    “ No ! Nimesema siwezi kufanya hvyo”

    “ Utafanya nimekwambia.Kama ukikataa kufanya hivyo utaozea gerezani kwa maisha yako yote” akasema Mathew.Kanali Adolf akainama akafikiri kwa muda na kusema

    “ Kwa nini unataka kufahamu kilichomuua Dr Flora? Wewe ni nani?

    “Huna haja ya kufahamu mimi ni nani na kwa nini ninataka kufahamu kilichomuua Dr Flora ,nataka kusikia jibu moja tu ,utafanya au hutafanya?

    Adolf akafikri kidogo na kusema

    “ ok I’ll do it.Lakini kwa sharti moja “

    “ Sharti gani hilo?

    “ Hii iwe ni mara ya kwanza na ya mwisho kunitaka nikufanyie kitu cha namna hii.After this we’re done.Sitaki unibughudhi tena.Ukithubutu kunifuata tena I swear I’ll kill you.Do we have a deal?

    “ deal “akasema Mathew.

    “ Ok itanilazimu vile vile kuwataarifu baadhi ya madaktari ambao nitafanya nao uchunguzi huo siwezi kufanya peke yangu”

    “ Huna haja ya kufanya hivyo.Tunaye daktari wetu ambaye utashirikiana naye kufanya huo uchunguzi.”

    “ Yuko wapi huyo daktari?

    “ Usijali utamuona tu.Twende tuondoke” akasema Mathew.Anitha alikwisha rejea garini akimsubiri Mathew,wakaingia garini na kuondoka.





    Tayari jua limezama na kiza kimechukua nafasi yake.Watu walikuwa wengi sana katika makazi ya rais kuliko na msiba wa Dr Flora Joshua mke wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Karibu viongozi wote wa serikali walikuwepo katika eneo hili la msiba na hivyo kulifanya eneo hili kuwa na ulinzi mkali mno.Kila aliyeingia mahala hapa alikaguliwa kwa kutumia mitambo maalum ili kuhakikisha kwamba hakuna anayeingia na silaha wala kitu kingine chochote cha hatari.Jaji Elibariki alikuwa katika pilika pilika nyingi akiwa kama sehemu ya familia ya rais.Kila mara alikuwa akiitazama saa yake ya mkononi na ilipotimu saa moja na nusu akampigia simu mkewe na kumuomba waonane.

    “ Flaviana,nimeona nikufahamishe kwamba ninatoka kidogo ninakwenda kushughulikia lile suala.” Akasema jaji Elibariki

    “ Ahsante sana Eli.Umefikia wapi mpaka hivi sasa kuhusu suala hili kwa sababu kwa mujibu wa ratiba mazishi ni kesho” akasema Flaviana

    “ Siwezi kukupa jibu kwa sasa ila nitakaporejea nitakuwa na jibu la kukupa”

    “ Ok My love,nakutakia kila la heri ila tafadhali kuwa makini sana” akasema Flaviana na kumkumbatia mumewe akambusu. Jaji Elibariki akaingia garini na kuondoka .Licha ya kuwa na mawazo mengi lakini kichwani kulikuwa na picha moja tu iliyokuwa imetawala,picha ya msichana mrembo ,mwenye uzuri usio na mfano,Peniela.

    “ Ama kweli Peniela ameichanganya akili yangu sana kiasi kwamba nashindwa hata kukaa msibani.Kila dakika picha yake inanijia kichwani.Dah ! sikuwahi kuchanganywa na mtoto wa kike kiasi hiki.Sijui Yule msichana anatumia nini kiasi cha kuifanya akili yangu imuwaze yeye tu kila dakika.” akawaza Jaji Elibariki akiendelea na safari yake ya kuelekea kwa Peniela.

    “ Ngoja nimpigie simu nimtaarifu kwamba niko njiani ninakwenda kwake” akapunguza mwendo wa gari na kuzitafuta namba za simu za Penny akampigia

    “ Hallow Elibariki” ikasema sauti tamu ya Penny baada ya kupokea simu

    “ Hallow Peniela,hujambo mtoto mzuri?

    “Sijambo Elibariki,unaendeleaje?

    “ Ninaendelea vizuri sana .Unafanya nini hivi sasa?

    “ Nimejilaza hapa kitandani,akili yangu yote inakuwaza wewe tu.Ninakusubiri kwa hamu sana Elibariki.Mchana ulinionjesha kidogo nataka tuendelee pale tulipoachia .Bado uko msibani? Akasema Penny kwa sauti laini na kuufanya mwili wote wa Elibariki kusisimka.

    “ Niko njiani ninakuja.Ndani ya dakika kumi na tano au ishirini nitakuwa nimefika.Hata mimi nina hamu sana na wewe.Kutwa nzima nimekuwa nikikuwaza wewe tu” akasema Elibariki

    “ Ok Elibariki ninakusubiri.” Akajibu Penny na kukata simu

    “ Dah ! huyu mtoto sijui ana kitu gani jamani ,kwa sababu kuongea naye tu hadi mwili wote umenisisimka.Anajua kumchanganya mwanaume.Vitu alivyonifanyia mchana sijawahi kufanyiwa na mwanamke yeyote Yule.hata mke wangu hajawahi kunifanyia mambo kama aliyonifanyia Penny.Sasa nimegundua kumbe wanawake nao wanaweza kuchangia sana ndoa zao kuporomoka.Kama mwanamke anashindwa kumfanyia mume wake mambo yanayoweza kumchanganya na badala yake anafanya mambo kwa mazoea tu,siku huyo mwanaume akikutana na mwanamke kama Peniela,mwenye kuyajua mambo,mwenye kufahamu nini mwanaume anahitaji,hiyo ndoa haitabaki salama.Lazima isambaratike “ akaendelea kuwaza Elibariki huku akikumbuka mambo aliyoyafanya na Peniela mchana wa siku hiyo.

    Jaji Elibariki aliwasili nyumbani kwa Peniela ,akapiga honi na Penny akaenda kumfungulia geti.Usiku huu Penny alikuwa amevaa gauni fupi la kulalia lililokuwa likionyesha kila kitu cha ndani.jaji Elibariki alipomuona alipandwa na midadi.Tayari ikulu kulikwisha chachamaa.

    “ karibu sana Elibariki” akasema Penny na kumkumbatia halafu akampiga busu zito na mkono mmoja ukashuka chini maeneo ya ikulu na kumfanya jaji Elibariki aanze kuvuta pumzi kwa kasi.Mapigo ya moyo yalibadika.Penny akamuongoza Elibariki hadi katika sofa sebuleni.

    “ I missed you a lot Elibariki.Umenifanya nikuwaze kila dakika kwa mambo uliyonifanyia mchana.Please naomba kwanza unikate kiu yangu .” akasema Peniela kwa sauti laini ya kimahaba iliyozidi kumchanganya Elibariki

    “ I need to take a shower first ” akasema Elibariki.Penny akambusu na kumshika mkono akamuongoza kuelekea bafuni .Wakati Elibariki akioga Penny akachukua simu yake akaenda sebuleni na kumpigia simu Jason na kuongea kwa sauti ya chini.

    “ Hallo Penny.How are you my queen’ akasema Jason baada ya kupokea simu

    “ I’m ok Jason.Uko wapi?

    “Niko nyumbani.Uko wapi Penny mbona unaonekana kama una wasi wasi sana?

    “ Ndiyo Jason.Nina wasiwasi sana.Kuna mtu yuko hapa kwangu ,ambaye amekuwa akinitaka kimapenzi kwa siku nyingi lakini nimekuwa nikimkatalia leo amekuja kwangu na anasema kwamba ameshindwa kuvumilia kuteseka kila siku kwa ajili yangu.Nina wasi wasi ana lengo baya.Please hurry up Jason.Sina amani hapa mtu huyu anaweza kunibaka” akasema Penny

    “Ok Penny,ninakuja hapo sasa hivi.Kuna haja ya kuja na askari?

    “ hapana hakuna haja ya kuja na askari. Nataka uje sasa hivi ili nimuonyeshe kwamba nina mpenzi wangu.Please hurry” akasema penny

    “ Ok penny I’m on the way” akasema Jason .Penny akatabasamu

    “ Kila kitu kimekwenda kama ninavyotaka.Ninachosubiri ni bomu tu kulipuka.Nataka Jason na Elibariki wachukiane wao kwa wao ili mpango wao wa kuchunguza kifo cha Edson usiendelee.Wakigombana hakuna kitakachoendelea.Nasikitika kufanya hivi kwani nitawakosa wote lakini ni kwa faida yao wenyewe.Jambo wanalotaka kulichunguza ni la hatari kubwa na hakuna namna ninayoweza kuwafanya wakaachana nalo zaidi ya kutumia njia hii.” Akawaza Penny.

    “ Inaniuma sana kumkosa Jason,kwani ni mwanaume ambaye sina hakika kama nitampata kama yeye.Najutia kuingia katika maisha kama haya.Ninapata kila kitu ninachohitaji lakini siko kama wanawake wengine.Siwezi kuwa na maisha kama waliyonayo wengine.Lakini nitaendela na maisha haya mpaka lini? “akajiuliza Penny na mara akatokea Elibariki akiwa amejifunga taulo .Penny akaiweka simu mezani na kwenda kumkumbatia akaanza kumporomoshea mabusu mfululizo.Jaji Elibariki naye akajibu mapigo ,akamuinua Penny na kumpeleka sofani na kuanza kumshughulikia.

    Mpambano ulikuwa mkali sana.walihama kabisa katika ulimwengu huu na kuhamia katika sayari nyingine kabisa yenye raha zisizoelezeka.Kilio na miguno kuashiria raha waliyoipata ndivyo vilivyokuwa vikisika.

    Wakati Penny na jaji Elibariki wakijivinjari katika sayari ya mahaba,Jason alikuwa akiendesha gari kwa kasi ya aina yake kuwahi nyumbani kwa Penny.Maneno aliyoambiwa na Penny yalimstua sana.Alitamani apate na kufika mara moja nyumbani kwa Penny ili amfundishe adabu mwanaume huyo ambaye yuko nyumbani kwa penny kwa lengo la kufanya mapenzi.

    “ Leo nataka nimfundishe adabu huyo bazazi ambaye anapenda kuvamia wanawake wa watu.Haelewi ni kiasi gani nimewekeza hadi kumfanya Penny awepo hapa alipo sasa hivi. I’ve sacrificed a lot for her.Siwezi kuruhusu mwanaume mwingine aje na kuanza kufanya mambo ya kipuuzi kwa mwanamke ambaye ninategemea awe mke wangu.” Akawaza Jason akiwa na hasira nyingi.

    Alifika nyumbani kwa Penny akasimamisha gari nje akashuka na kufungua mlango mdogo wa geti ambao haukuwa umefungwa,akaingia ndani.Kitu cha kwanza kukiona ni gari alilolifahamu .

    “ Elibariki!!..akasema kwa mshangao

    “Hili ni gari la Elibariki.Anatafuta nini hapa kwa penny? Yawezekana labda Penny amempigia ili kuomba msaada” akawaza Jason na kupiga hatua ndefu kuelekea ndani.Akaufikia mlango wa sebuleni na kusimama,akajaribu kusikia sauti za watu lakini ni muziki tu ndio uliokuwa ukisikika.Akakinyonga kitasa mlango ukafunguka akaingia ndani .Akapiga hatua tani akakivuka kichumba kidogo na kuingia sebuleni.Alitamani ingekuwa ni ndoto lakini haikuwa ndoto bali ni kitu cha kweli alichokuwa akikiona mbele yake.Alipatwa na mstuko mkubwa na kuhisi miguu yake inaisha nguvu akaegemea ukuta.Mwili wote ulikuwa unamtetemeka.Katika sofa jaji Elibariki na Peniela walikuwa wakifanya mapenzi.Mwili wote ukamtetemeka kwa hasira

    “ Elibariki !!!...akaita kwa hasira Jason.Jaji Elibariki akastuliwa na sauti ya Jason akageuka ghafla na kukutana na sura iliyojaa hasira

    “ Jason !!!..akasema jaji Elibariki kwa mshangao mkubwa.Hakuwa akitegemea kumuona Jason maeneo yale mida ile

    “ What are you doing here Jason? Akauliza Elibariki kwa mshangao huku jasho likimtiririka.

    “ What are you doing here Elibariki? Akauliza Jason kwa hasira.Elibariki akasimama

    “ Nakuuliza Elibariki unafanya nini hapa na mpenzi wangu? Akauliza Jason kwa hasira huku akimsogelea Elibariki

    “ Mpenzi wako? Toka lini Peniela akawa mpenzi wako? Huyu ni mwanamke wangu.Nashangaa ulivyokosa adabu na kuingia katika nyumba za watu bila kubisha hodi.” Akasema kwa ukali jaji Elibariki

    “ Peniela is your woman? Akauliza Jason kwa hasira

    “ Peniela is your woman?akauliza tena Jason

    “ Is she your woman? Jaji Elibariki naye akauliza

    “ Nakuuliza Jason Peniela ni mwanamke wako? Akauliza Elibariki huku naye hasira ikizidi kumpanda.

    “ Yes Peniela ni mwanamke wangu…”

    “ You are idiot!! ..akasema Elibariki .Kauli ile ikamkasirisha sana Jason na kufumba na kufumbua akarusha ngumi nzito iliyompata Elibariki shavuni akaanguka chini.Vurugu kubwa likaibuka mle sebuleni.Penny akaogopa sana kwa namna walivyokuwa wakirushiana makonde. Wakati wakiendelea kupigana,Jason akachukua chupa ya mvinyo na kumpiga nayo Elibariki kichwani, akaanguka na kupoteza fahamu.Peniela alikuwa amejificha katika pembe ya sebule akitetemeka.Baada ya Jaji Elibariki kuanguka chini huku damu zikimtoka Jason akaogopa na kudhani ameua,akatoka mbio.Penny akamkimbilia Elibariki pale chini .Aliogopa sana .Alichanganyikiwa na hakujua afanye nini.Mara mle sebuleni wakaingia watu watatu.

    “ Hello Penny.Nini kimetokea hapa? Akauliza mmoja wa wale jamaa.Penny hakuweza kujieleza,alikuwa amechanganyikiwa .Mmoja wa wale jamaa akaliokota taulo akamfunika kwani alikuwa bado mtupu,halafu akamshika mkono na kumuinua

    “ Its ok Penny.Go to your room and wash yourself.We’re going to take care of this” akasema Yule jamaa aliyekuwa akiongea kwa upole.Akamsindikiza Penny hadi chumbani kwake halafu akarejea sebuleni .Penny akakaa kitandani alikuwa akitetemeka.Picha ya tukio lile ilimuogopesha sana.

    “ Sikutegemea kama jambo hili lingekuwa baya kiasi hiki.Nimeogopa sana.Wale wanaume karibu wangetoana roho mbele yangu.lakini nashukuru kwa kufanikiwa kuwavuruga.Kwa sasa mipango yao yote imevurugika.Nim

    ewakosa wote wawili lakini watakuwa salama.Walikokuwa wakielekea si kuzuri hata kidogo.” Akawaza Penny

    “ Nimefanya ulaghai mkubwa sana.Nimecheza na akili za watu.Niwamedanganya kwa mapenzi na wakadanganyika.They are all going to hate me.I’m a monster.” Akawaza halafu akaingia bafuni kuoga

    “ Watu wale walioingia ghafla pale ndani ni akina nani? Wametoka wapi? Wamenifahamu vipi? Sina hakika kama nimewahi kukutana nao sehemu yoyote.Yawezekana ni wale wale jamaa waliokuja kupekua nyumba yangu wakati sipo.” akajiuliza Penny.

    Watu wale watatu walimpatia Jaji Elibariki huduma ya kwanza na kuizuia damu isiendelee kumwagika.Alipozinduka alihisi maumivu makali mno hasa sehemu za kichwani.Mmoja wa wale jamaa akamfuata Penny chumbani kwake na kumgongea.Penny akafungua mlango

    “ Penny mtu wako amezinduka na tayari tumezuia damu isiendelee kumwagika.Vijana wangu watanmpeleka hospitali ili akapatiwe matibabu na kushonwa jeraha lake.Hatuna haja ya kufahamu klilichotokea kwani hayo ni mambo yako binafsi lakini tuko hapa kukuchukua na kukupeleka mahala unakojitajika usiku huu. “ akasema Yule jamaa

    “ Nyie ni akina nani? Akauliza Penny

    “ 0065 “ akasema Yule jamaa na Penny akawa ameelewa ni akina nani.

    Penny hakusema kitu akatoka mle chumbani na kuelekea sebuleni.Alisikitika sana kwa kumuona jaji Elibariki akiwa katika hali ile.Hakutaka kuongea naye chochote,vijana wawili wakambeba Elibariki na kumpakia katika gari lao .

    “ Penny ,tutahakikisha mtu wako anapatiwa matibabu yenye uhakika na anakuwa salama” akasema Yule jamaa ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake

    “ Nitashukuru sana.hakikisheni tafadhali anapatiwa huduma ya uhakika” akasema Penny akaingia katika gari lingine na Yule jamaa wakaondoka.Jaji Elibarii akapelekwa hospitali

    ********

    Saa na nne na dakika nane,Mathew,Anitha,na Dr Michael ,wakiongozwa na kanali Adolf wakawasili katikahospitali kuu ya jeshi wakitumia gari la Kanal Adolf ambalo halikukaguliwa getini.Baadakushuka walielekea moja kwa moja katika ofisi ya kanali Adolf ambako walivaa makoti meupe ya kidaktarina kisha wakaanza kuelekea katika chumba cha kuhifadhia maiti.Haikuwa kawaida kwa chumba hiki kulindwa ,lakini toka mwili wa Dr Flora ulipoletwa katika chumba hiki kumekuwa na ulinzi mkali.

    Kanali Adolf akajitambulisha kwa wale wanajeshi wawili waliokuwa wakilinda usalama wa chumba kile cha maiti halafu wakaingia ndani .Kwa usiku huu ndani ya chumba kile kulikuwa na wafanyakazi wawili tu.Wote wanamfahamu kanali Adolf na walipomuona wakamsalimu kwa heshima .Akamuita mmoja akamuagiza aupeleke mwili wa Dr Flora katika chumba cha kufanyia uchunguzi wa maiti haraka sana.Ndani ya dakika tano tayari mwili ukaletwa na kulazwa juu ya kitanda.Kwa pamoja Kanali Adolf na Dr Michael wakaaanza kuufanyia uchunguzi huku Mathew na Anitha wakiwa katika tahadhari kubwa sana.

    *********

    Penny hakujua anapelekwa wapi na hakutaka kuhoji ili kufahamu anapelekwa wapi.Akili yake yote ilkuwa ikiwaza kuhusu tukio lililotokea usiku huo .Picha ya Jason na jaji Elibariki wakipigana ikamrudia na kumtoa machozi.

    “ Nimefanya mambo mengi mabaya lakini hili la leo limenisikitisha sana.Nmeumia sana.Nimewaumiza watu walionipenda na kunipigania. Kwa sababu yangu wanaume wale watajenga uadui mkubwa kati yao na sina hakika kama suala hili litaishia pale,lazima litaendelea.Lazima kutakuwa na uhasama mkubwa mno.Lakini Kwa upande mwingine nimewasaidia kutokujiingiza katika matatizo kwa kitu cha hatari walichotaka kukifanya.Mpango wa kuchunguza kifo cha Edson umeisha” Akawaza penny

    Safari ilikuwa ya kimya kimya namuda mwingi penny alikuwa ameinama huku mkononi mwake akiwa na kitambaa cha kufutia machozi yaliyokuwa yakimchuruzika kila alipokumbuka picha ya ugomvi ule.

    Hatimaye walikata kona na kuingia katika jumba moja kubwa la ghorofa zipatazo nne lililozungukwa na miti mingi.Magari zaidi ya ishirini yalikuwa yameegeshwa katika maegesho kubwa iliyokuwamo ndani ya jumba hili.Kijana mmoja aliyevaa suti nyeusi akafika na kumfungulia mkono Penny na bila kujitambulisha akamuomba amfuate.Penny aliendelea kujiuliza mahala pale ni wapi .Akaendelea kumfuata yule kijana wakaanza kupanda juu ghorofani hadi walipofika ghorofa ya nne.Kote walikopita walikutana na watu kadhaa na wote wakiwa wamevalia suti.Kila mmoja alionyesha heshima kubwa kwa Peniela na kuzidi kumshangaza.Hakuwahi kufika mahala pale wala hakuna aliyemfahamu lakini wao walionekana kumfahamu na kumuheshimu sana.

    “ Nimeletwa hapa kufanya nini? Mbona kila mtu ninayekutana naye anatoa heshima kubwa? Akajiuliza na mara Yule kijana aliyeongozana naye akasimama akaongea na mtu mmoja hivi pande la mtu.Mtu Yule akamsalimu penny kwa heshima kubwa halafu akamuomba amfuate.Penny akazidi kushangaa.



    Kikao cha kamati ya kushughukikia mazishi ya Dr Flora kilikuwa kinaendelea katika makazi ya rais .kikao hiki kiliwashirikisha pia viongozi wa juu wa serikali akiwemo Dr Joshua rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Mazishi ya mke wa rais yalipangwa kufanyika kijijini kwao Itogole mahala alikozaliwa.Wakati kikao kikiendelea katibu wa rais Dr Albert Kigomba akapigiwa simu akasimama na kutoka nje ya chumba na kuipokea.Baada ya kumaliza kuongea na simu ile sura yake ilionyesha wasi wasi mwingi.Akasimama na kufikiri kidogo akavuta pumzi ndefu halafu akamuendea rais.

    “ Mheshimiwa rais ninaomba tuongee kidogo” akasema Dk Albert Kigomba .Dr Joshua akaomba samahani kidogo halafu akatoka nje .Wakajificha katika kona Fulani isiyokuwa na watu.

    “ What is it Dr Kigomba ?akauliza Dr Joshua

    ‘ Mheshimiwa nimepokea simu sasa hivi toka kwa Brigedia Abasana anasema kwamba kuna madaktari wameingia katika chumba cha maiti hospitali kuu ya jeshi na mpaka sasa hawajatoka wanaufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora” akasema Dr Albert

    “ What ?!!..Dr Joshua akahamaki.

    “ Who are they? Akauliza Dr Joshua

    “ Haijulikani ni akina nani lakini inasemekana wanaongozwa na kanali Adolf”

    “ kanali Adolf?!!..Dr Joshua akashangaa

    “Ndiyo kwa mujibu wa vijana waliowekwa kulinda katika kile chumba cha kuhifadhia maiti ha hospitali kuu ya jeshi ,Kanali Adolf aliongozana na madaktari wengine wameingia usiku huu ndani ya chumba cha maiti na wanafanya uchunguzi kwa mwili wa Dr Flora.”

    “ Ouh my God !!!..akasema Dr Joshua huku akishika kichwa .Alihisi kuchanganyikiwa.Akainama na kuzama mawazoni

    “ What are we going to do Mr President? Akauliza Dr Albert

    “ Do something to stop them as quick as possible.Hakikisha wote wamekamatwa na hakuna yeyote atakayefanikiwa kutoroka.” Akaamrisha Dr Joshua na mara moja Dr Albert akasogea pembeni na kuanza kupiga simu.

    Wakati Dr Albert akiongea na simu ,hakujua kama katika chumba cha karibu na pale alipokuwa amesimama ,kulikuwa na mtu akisikiliza kila alichokuwa akikiongea.Anna mtoto wa rais alikuwa amejipumzisha ndani ya chumba kile .Alistushwa sana kusikia Dr Albert akimuelekeza mtu kwamba ahakikishe madaktari wote wanaoendelea na uchunguzi kwa mwili wa Dr Flora wanakamatwa haraka sana.

    “ Mwili wa mama unafanyiwa uchunguzi halafu madaktari wote wanaofanya uchunguzi huo wanatakiwa kukamatwa? Anna alistuka sana .

    “ Kwa nini Dr Kigomba atoe amri ya kukamatwa madaktari wanaofanya uchunguzi kubaini kilichomuua mama? Kuna tatizo lolote katika kufanya uchunguzi huo? Je baba anafahamu kinachoendelea ? Something is going on.I have to see Flaviana” akawaza Anna halafu akaufungua mlango wa kile chumba alichokuwamo akatazama huko na huko kuhakikisha kwambahakuna mtu halafu akatoka na kuelekea katika vyumba vyenye watu kumtafuta dada yake, wakaenda sehemu isiyokuwa na watu

    “ Anna kuna tatizo gani? Mbona umeniogopesha? Akauliza Flaviana

    “ Sikuwa nikijisikia vizuri na sikutaka kusikia kelele za aina yoyote ile hivyo nikaenda kupumzika katika chumba cha kule mwisho ambacho alikuwa akikaa bibi na kwa sasa hakikaliwi na mtu.Wakati nimejipumzisha kule nikasikia Dr Kigomba akiongea na simu ,alikuwa akitoa maelekezo kwa mtu kwamba ahakikishe madaktari wote wanaofanya uchunguzi kwa mwili wa mama wakamatwe haraka sana kabla hawajaendelea na uchunguzi wao na asitoroke hata mmoja.Nilistushwa sana na maagizo yalenikajiuliza ni kwa nini wakamatwe wakati wanataka kufahamu kilichomuua mama? Flaviana kuna kitu hakiko sawa hapa.” akasema Anna na kumstua sana Flaviana ambaye alishika kichwa kwa mikono yake

    “ Elibariki !! ..Flaviana akasema kwa mstuko huku akiichukua simu yake na kuzitafuta namba za simu za Elibariki akapiga.

    “ Hallow Flaviana” akasema Elibariki baada ya kupokea simu

    “ Elibariki uko wapi? Akauliza Flaviana.Elibariki hakujibu kitu akabaki kimya

    “ Elibariki nakuuliza uko wapi mida hii? Bado Elibariki hakujibu kitu

    “ C’mon Eli answer me where are you? akauliza Flaviana huku machozi yakimlenga

    “ Niko..niko hapa..hospitali” akasema Elibariki kwa wasiwasi akitegemea maswali kutoka kwa mkewe akitaka kujua ni kwa nini alikuwepo pale hospitalini

    “ Elibariki get out of there now!!!..” akasema Flaviana akifikiri kwamba mumewe alikuwapo katika hospitali kuu ya jeshi kufuatilia uchunguzi wa mwili wa Dr Flora

    “ What ?!... Elibariki akashangaa

    “ Eli,please get out of there now !! Achana na kila kitu unachokifanya,get out.Tayari wamekwisha jua mko hapo hospitali” akasema Flaviana kwa ukali

    “ Whats going on flaviana” akauliza Elibariki huku akigugumia kwa maumivu aliyokuwa akiyasikia kichwani

    “ Kuna amri imetolewa kwamba madaktari wanaoendelea na uchunguzi wa mama wakamatwe wote.Nina hakika uko pamoja nao tafadhali ondokeni mara moja.”akaonya Flaviana

    “ Ahsante sana Flaviana kwa tahadhari,tunatoka sasa hivi” akasema Elibariki na kukata simu.Kijasho kikamtoka kwa mbali.Hakutaka kupoteza muda akampigia simu Mathew

    “ Hallow Elibariki” akasema Mathew baada ya kupokea simu

    “ Mathew uko wapi?

    “ Niko hapa hospitalini tunaendelea na uchunguzi.Wewe uko wapi?

    “ Mathew,get out of there now.Tayari mmekwisha fahamika mnachokifanya humo.Please you are in great danger” akasema Elibariki

    “ Ok Thank you Eli” akajibu Mathew na kukata simu akawageukia wenzake.

    “Guys we haveto stop everything,they know we’re here and the’re after us.Lets get out of here now !!” akasema Mathew.Wote mle ndani wakastuka sana.

    “Please let’s get out of here.!! “akasema Mathew kwa ukali.

    Kwa haraka Dr Michael akakata kipande kidogo cha ini akakiweka katika kimfuko kidogo cha nailoni halafu akachukua tena na sampuli za vitu alivyokuwa akivihitaji akaviweka katika vifuko vidogo vidogo .

    “ Are we going to leave her like this? Akauliza Anitha

    “ Lets go. We don’t have much time here ” akasema Mathew huku akitoa bastora moja na kumrushia Anitha .Yeye alikuwa na bastora mbili mkononi.Kwa tahadhari kubwa akaufungua mlango na kuchungulia nje hakukuwa na mtu yeyote .http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Its clear ,lets go’ akawataarifu wenzake wakatoka .Kwa kupitia kioo kidogo cha dirishani Mathew akachungulia nje na kuwaona wale wanajeshi wawili waliokuwa wakilinda nje ya chumba cha maiti.Akamfanyia ishara kanali Adolf atangulie nje akaongee nao.Kanali Adolf akafungua mlango na kutoka nje.Akawaita wale wanajeshi wawili akaanza kuongea nao.Walionekana kama wanabishana kitu Fulani

    “ It’s our chance now” akasema Mathew na kisha akamfanyia ishara Anitha ailenge kwa risasi taa kubwa iliyokuwa ikimulika eneo lile ili kupafanya mahala pale pawe na giza.Anitha akafungua mlango kidogo na kuilenga ile taa kwa kutumia bastora yenye kiwambo cha kuzuia sauti .Eneo lote likawa giza.Kitendo kile cha taa kuzimika ghafla kikawastua sana wale wanajeshi.Wakati wakishangaa kilichotokea, Ghafla Mathew na Anitha wakatokea na ndani ya sekunde kadhaa wanajeshi wale walikuwa wamelala chini hawakuwa na fahamu.Kanali Adolf alibaki akishangaa kwa namna wanajeshi wale walivyopigwa na kupoteza fahamu ghafla namna ile.

    “ Hakuna muda wa kupoteza ,twendeni tuondoke.” Akaamrisha Mathew wakaanza kutembea kwa kasi .Walifika katika maegesho ya magari wakaingia katika gari la kanali Adolf na kuondoka kwa kasi.

    “ Tunaelekea wapi? Akauliza kanali Adolf

    “ Some where safe” akasema Mathew na kumuelekeza sehemu wanakoelekea.Umbali wa mita kadhaa wakakutana na gari tatu za jeshi zilizojaa wanajeshi.

    “ Tungechelewa kidogo sana wangetukuta.Thanx to Elibariki” Akasema Mathew

    “ Ulijuaje kama wanajeshi wanakuja? Akauliza Kanali Adolf

    “ Tunapofanya kazi tunafanya kama timu” akasema Mathew

    “ Who are you guys” akauliza Adolf .Hakuna aliyemjibu,safari ikaendelea.

    *******

    Bado Flaviana alikuwa ameiweka mikono kifuani kwa woga,alikuwa na mawazo mengi sana kuhusiana na usalama wa mume wake .

    “ Flaviana ni kitu gani kinaendelea hapa? Shemeji Elibariki yuko wapi? Mbona hutaki kunieleza chochote? Akahoji Anna.Bado Flaviana alikuwa ameiweka mikono yake kifuani akimuomba Mungu amsaidie mume wake.

    “ Ngoja kwanza Anna,nitakueleza kila kitu.” Akasema Flaviana huku akitazama simu yake kana kwamba kuna simu anasubiri apigiwe.Dakika zilizdi kwenda ikamlazimu azitafute namba za simu za Elibariki akampigia

    “ Hallow Flaviana ,” akasema Elibariki

    “ Elibariki mmeshaondoka hapo hospitali? Akauliza

    “ Flaviana naomba unisubiri kidogo nitakupigia” akasema Elibariki na kukata simu

    “ Flaviana, Elibariki anafanya nini huko hospitali? Kuna nini kinaendelea? Naomba unieleze tafadhali

    “Ok Anna nitakwambia.” Akasema Flaviana halafu akafikiri kidogo na kusema

    “ mama alifariki ghafla kabla hajatueleza jambo alilotaka kutueleza na mpaka sasa bado hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusiana na nini kilisababisha kifo chake.Niliwasil

    iana na daktari mmoja wa pale hospitali kuu ya jeshi ili kumuuliza nini sababu ya mama yangu kufariki ghafla akaniambia kwamba hawawezi kufanya uchungzui kubaini kitu gani kilimuua mama kwa sababu wamekatazwa kufanya hivyo.Hakuniambia ni nani aliyezuia uchunguzi ule usifanyike.Baada ya kufikiri sana nililazimika kumuomba Elibariki anisaidie kutafuta ukweli wa nini kilichomuua mama.Elibariki yeye ana watu wengi anaowafahamu ambao wanaweza kumsaidia kuutafuta ukweli.Aliondoka hapa jioni akaniambia kwamba anakwenda kushughulikia suala hilo.Nadhani walionekana na ndiyo maana taarifa zikafika hapa haraka na hivyo kutumwa kikosi kwenda kuwakamata.Anna kuna kitu kinaendela hapa ambacho kinafichwa kuhusiana na kifo cha mama”akasema Flaviana na kumstua sana mdogo wake

    “ Ahsante sana Flaviana kwa kunifumbua macho.Unajua mimi sikuwa nikifikria kabisa kitu kama hicho.Ninafahamu mama alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na niliamini ndicho kilichomuua.Taarifa hii uliyonipa imenistua sana.”

    “ Ni kweli Anna,mama alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na nisingekuwa na tatizo lolote kama kusingetolewa amri ya kuzuia mwili wake kufanyiwa uchunguzi kufahamu kilichosababisha afariki ghalfa namna ile.Ukumbuke kwamba kuna jambo ambalo alitaka kutueleza jioni ya siku ile.Ni kwa nini sababu ya kifo chake isijulikane? Kwa nini uchunguzi wa kifo chake unazuiwa? Kuna nini kinafichwa?akauliza Flaviana.Anna akainama akafikiri kwa muda na kusema

    “ Ninakubaliana nawe Flaviana.Kama ni shinikizo la damu ndilo lililomuua basi hakuna sababu ya kuficha.Lakini kuzuai kabisa mwili wake kufanyiwa uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake inatia shaka sana.Inaonekana wazi sababu ya kifo chake haitakiwi kujulikana.kwa nini isifahamike?

    “ Hilo ndilo swali ambalo tunatakiwa tujiulize,ni kwa nini sababu ya kifo cha mama inafichwa?.Sisi ni watoto wake na tuna haki ya kufahamu kilichosababisha kifo cha mama yetu” akasema Flaviana

    “Kwa hiyo Flaviana unafikiri nini?mama aliuawa? akauliza Anna

    “Siwezi kusema moja kwa moja kwamba aliuawa lakini kwa mazingira yaliyopo yanajenga hisia hizo .Hii ni sababu iliyonifanya nimuombe Elibariki anisaidie kuufahamu ukweli wa jambo hili ili niweze kuondokana na duku duku nililonalo.Baad

    a ya kupatikana kwa taarifa ya nini kilisababisha kifo cha mama,tutajua kama aliuawa ama kulikuwa na uzembe wa aina yoyote wa madaktari na wasaidizi wake.Mungu amsaidie Elibariki aweze kutoka salama na tuone kama anaweza kuwa amefanikiwa kupata chochote” akasema Flaviana

    “ Flaviana umemuingiza shemeji Elibariki katika hatari kubwa.Endapo akikutwa huko hospitali lazima atafanyiwa kitu kibaya sana.”

    “ Ni kweli Anna.Najutia uamuzi wangu wa kumtaka anisaidie kuutafuta ukweli.Nimemuweka mume wangu katika hatari kubwa sana.Lolote baya linaweza kumkuta” Akasema Flaviana kwa uchungu mwingi

    “Flaviana unadhani baba atakuwa anafahamu chochote kuhusiana na suala hili? Akauliza Anna

    “ Sina hakika kama analifahamu kwa sababu wakati mama anafariki dunia yeye alikuwa mkutanoni jijini Arusha na alipofika hapa tayari mama alikwisha pelekwa hospitali.” Akasema Flaviana

    “ kwa maana hiyo haya mambo yalifanyika wakati baba akiwa hayupo,namaanisha taarifa hiyo ilitolewa wakati hata baba hajafika.Ninadhani kuna ulazima wa kumueleza baba ukweli wa hili jambo.Inawezekana akawa hafahamu chochote kinachoendelea.Yawezekana akawa amepewa taarifa zisizo za kweli” akashauri Anna.Flaviana akafikiri kwa muda na kusema

    “ Unashauri tumweleze baba?

    “ Ndiyo.Ninadhani litakuwa ni jambo la busara kumueleza baba kuhusiana na kinachoendelea ili afahamu mambo yanayofanywa na watu wake wa karibu na ikiwezekana achukue hatua kulichunguza suala hili.Na hii inaweza kuwa njia nzuri ya kumsaidia Elibariki.Unaonaje kuhusu jambo hili?

    “ Si vibaya ingawa nilipenda sana kulifanya jambo hili kwa siri lakini tufanye kama ulivyoshauri.Twende tukamuone baba tumueleze kuhusiana na suala hili” akasema Flaviana.

    “ Ni mapema sana kufikiria hivyo lakini katika sehemu kama hizi kila kitu kinawezekana.Kwa muda wa miaka sita nimekaa ikulu na nimejifunza kitu kimoja kikubwa , kuutoa uhai wa mtu kwa ajili ya kulinda maslahi Fulani ya wakubwa au ya nchi ni kitu kidogo sana kwa hiyo japokuwa silipi uzito mkubwa suala la mama kuuawa lakini linawezekana kabisa kutokea na kama ikitokea ni hivyo,itakuwa ni kwa sababu nzito” akasema Flaviana.Baada ya kushauriana wakaondoka wakamfuata baba yao.Flaviana akaongea na mmoja wa walinzi wa rais akamuomba awaitie baba yao aliyekuwa ndani ya kikao.Mlinzi Yule akaingia ndani ya kile chumba ambacho kulikuwa na kikao kinachohusiana na mazishi ya Dr Flora akamtaarifu rais kwamba wanae wanahitaji kumuona.Dr Joshua akawaomba radhi wanakamati akatoka na kwenda kuonana na binti zake

    “ Flaviana ,Anna kuna tatizo gani? Akauliza

    “ Baba tunajua una mambo mengi kwa sasa lakini kuna suala la muhimu ambalo tumekuitia na tunaomba tukaliongelee katika chumba cha maongezi” akasema Flaviana .Dr Joshua akaongozana na wanae hadi katika chumba cha maongezi

    “ Kuna tatizo gani Flaviana? Akauliza Dr Joshua

    “ Baba kuna tatizo.Ni kuhusu kifo cha mama” akasema Flaviana na Dr Joshua akatikisa kichwa

    “ Baba ,tumekuwa tukijiuliza maswali mengi sana kuhusiana na kifo cha ghafla cha mama ..Mpaka sasa hatuelewi nini kilisabisha kifo chake,hatujui kama ni shinikizo la damu ambalo lilikuwa likimsumbua kwa muda mrefu au ni kitu kingine. Mpaka sasa hatujapata ripoti yoyote kuhusiana na suala hilo.Kuna daktari mmoja pale katika hospitali kuu ya jeshi ninafahamiana naye ,nilimuuliza kama wanafahamu nini kilisababisha kifo cha mama alisema kwamba hawafahamu chochote kwa sababu walizuiliwa kutokufanya uchunguzi wowote katika mwili wa mama.Binafsi nilistushwa sana na taarifa hizo ingawa hakunieleza ni nani aliyetoa amri hiyo.Baada ya kufikiri sana nikaamua kutumia njia zangu mwenyewe kuutafuta ukweli wa suala hili na ndipo niliposhirikiana na Elibariki kutaka kujua nini sababu ya kifo cha mama.Baba tumegundua kwamba wasaidizi wako wanakuzunguka.Kuna mambo ambayo huyafahamu kuhusia na kifo cha mama.Kuna mambo ambayo hujawekwa wazi.Usiku huu katibu wako Dr Kigomba amesikika akitoa amri kwamba madaktari walioko katika uchunguzi wa kifo cha mama wakamatwe na washughulikiwe haraka sana.Miongoni mwa watu waliomo ndani ya chumba hicho cha uchunguzi ni mume wangu Elibariki ambaye tunashirikiana naye kuutafuta ukweli.Kwa nini wazuiwe kufanya uchunguzi wa kifo cha mama? Tumeona tukuite na tukufahamishe kuhusiana na suala hili ili kwanza uwazuie watu waliotumwa kuwakamata madaktari aho ambao miongoni mwao yumo Elibariki na waachwe waendelee na uchunguzi wao na pili suala hili ulifanyie uchunguzi wa kina ” akasema Flaviana.Dr Joshua akainama akafikiri kwa muda na kusema

    “ Nawashukuruni sana wanangu kwa taarifa hizi ambazo hata mimi zimenistua sana.Sikuwa nikifahamu chochote kilichokuwa kinaendelea .Kama ulivyosema Flaviana ni kweli yawezekana nimefichwa mambo mengi.Niachieni suala hili nilifanyie uchunguzi.Kuhusu sababu ya kifo cha mama yenu nimekwisha zungumza na madaktari wa kutoka hospitali kuu ya taifa na wataufanyia uchunguzi mwili wa mama yenu kesho asubuhi na tutapewa ripoti ya nini kilisababisha kifo chake.Kuhusu uchunguzi huo ulioufanya kwa siri ni jambo zuri lakini ulitakiwa kunifahamisha mapema ili nifahamu na pengine tungeweza kushirikiana kuutafuta ukweli.Kumuacha Elibariki kwenda peke yake kufanya uchunguzi wa jambo hili ni hatari kubwa.Lazima atakuwa hatarini na hata taarifa anayoweza kuipata inaweza isiwe sahihi na ndiyo maana nimeomba timu ya wataalamu kutoka hospitali kuu ya taifa wakafanye uchunguzi na kutupa ripoti sahihi.Msiwe na wasi wasi wanangu kesho tutafahamu kila kitu kuhusiana na nini kilimuua mama yenu.Kuhusu Elibariki nitawasiliana na wakuu wa jeshi ili kufahamu kinachoendelea hapo hospitali na kama atakuwa amekamatwa nitaamuru aachiwe.kwa sasa naombeni mkapumzike na mniachie suala hili nilifanyie kazi.Nina njia nyingi za kuupata ukweli na kama kuna jambo lolote ambalo limefanywa na watendaji wangu nitawaeleza .Ila nawashukuru sana kwa taarifa mlizonipa.Ninafurahi sana kwa kujaaliwa watoto wenye akili nyingi kama nyie.” Akasema Dr Joshua .Flaviana na Anna wakaondoka

    Dr Joshua akavuta pumzi ndefu baada ya wanae kutoka mle chumbani.Alibaki ameegemea kiti chake akiwaza.mambo aliyoambiwa na watoto wake yalimstua sana

    “ Tayari wameanza kuhisi kitu.This is too dangerous.We have to act so quick to stop any suspicious.Dr Kigomba is very stupid.Suala hili amelifanya kizembe sana hadi watu wameanza kustuka..” Akawaza Dr Joshua.

    “ Nimestuka sana ,sikutegemea kabisa kamaFlaviana na Anna wanaweza wakahisi chochte kuhusiana na kifo cha mama yao.Mambo yameanza kuharibika na endapo Elibariki na timu yake watakuwa wamefanikiwa kugundua lolote I’m finished.lazima atamweleza mke wake na wanangu wakigundua kama mama yao aliuawa sijui nitawaeleza kitu gani” akawaza Dr Joshua na kuchukua simu yake akampigia simu Captain Amos daktari mkuu wa familia pamoja na katibu wake Dr Kigomba akawaomba wakutane mara moja ofisini kwake.Aliwataka radhi watu waliokuwa kikaoni kwamba amepatwa na dharura na moja kwa moja akaelekea ofisini kwake..Kichwa chake kilijaa mawazo mengi.Suala aliloambiwa na wanae lilimstua mno

    Baada ya kuachana na baba yao Flaviana akampigia simu mumewe Elibariki lakini simu yake haikuwa ikipatikana.Hofu ikamjaa

    “ Nina wasi wasi sana na usalama wa Elibariki.Sina hakika kama waliwahi kutoka mle ndani kabla wanajeshi hawajawakuta.If anything happens to him I’ll never forgive myself.Mimi ndiye chanzo cha haya yote.Ee Mungu mlinde mume wangu asipatwe na jambo lolote baya na arejee salama” akaomba Flaviana akiwa amejifungia chumbani akilia machozi.

    Dr Joshua aliwasili ofisini kwake na kuwakuta tayari Kaptain Amos na Dr Kigomba wamekwisha fika.Bila kuchelewa kikao kikaanza

    “ Dr Kigomba kuna ripoti yoyote kutoka hospitali? Akauliza Dr Joshua

    “ Nimepokea taarifa wakati nakuja huku ofisini kwamba hawakufanikiwa kumkamata mtu yeyote.Askari waliokuwa wakilinda eneo lile wamekutwa wakiwa hawana fahamu,vile vile mwili wa Dr Flora umekutwa ukiwa katika chumba cha uchunguzi,na inaonekana watu waliokuwa wakifanya uchunguzi ule walipewa taarifa na mtu aliyeko nje na kwa haraka wakaacha kazi ile waliyokuwa wakiifanya wakakimbia.Lakini hakuna uhakika kama wamepata walichokuwa wanakitafuta kwa sababu shughuli ile ilihitaji muda wa kutosha na wao walikimbia wakati kazi bado haijamalizika.Hata hivyo bado msako unaendelea kumsaka Kanali Adolf ambaye inasemekana ndiye aliyeongoza kundi hilo la madaktari waliojaribu kufanya uchunguzi huo.” Akasema Dr Kigomba .Dr Joshua akakuna upara wake

    “ Sasa ndugu zangu sikilizeni,kuna mambo ambayo yanahitajika kufanywa kwa haraka sana.Kaptain Amos you did your job well lakini kazi yako inataka kuharibiwa na uzembe unaofanywa na Dr Kigomba .” Dr Joshua akamgeukia Dr Kigomba

    “ Kigomba how could you do such a stupid things ? Unafahamu kabisa jambo hili ni nyeti na la hatari lakini bado hauko makini.Umesikika usiku huu ukipiga simu na kutoa amri kuwa madaktari wakamatwe,bila kujali mahala ulikokuwa umesimama kuna mtu anakusikilza.Mambo kama haya ni ya siri na unatakiwa ufanye kwa siri kubwa.Sasa hata watoto wangu wameanza kuhoji kuhusu nini kimemuua mama yao.Wanataka kupata ripoti ya daktari .Katika watu waliokuwamo mle wakifanya uchunguzi na mume wa mwanangu alikuwemo pia.Hii ilitokana na kuingiwa na shaka .Sina hakika kama watakuwa wamefanikiwa kufahamu kilichomuua Flora lakini endapo wakifanikiwa kujua,litakuwa ni anguko letu vinginevyo itatulazimu kufanya maamuzi magumu sana ili tuendelee kubaki salama.Kwa kuwa bado hatujui ni kitu gani wamekigundua hao madaktari kuna mambo ambayo lazima tuyafanye.Kwanza kesho asubuhi Kaptain Amos utashughulikia ripoti ya uongo ya kuhusu kifo cha Flora ripoti ambayo nitawaonyesha wanangu ili waridhike kwani nimewadanganya kwamba uchunguzi utafanyika kesho.Pili Mwanangu Flaviana anatakiwa aanze kuchunguzwa sana nyendo zake.Yeye ndiye atakayetupeleka mahala aliko mumewe Elibariki na tukimpata Elibariki tutakuwa tumewapata wengine wote walioshiriki katika jambo hili.Nataka mpaka kufika kesho asubuhi niwe nimepata ripoti kuhusiana na jambo hili.Kwa hiyo kuanzia sasa hakutakuwa na kulala.We’re going to work day and night to make sure we’re safe.You’ve messed it now you’ll have to fix it.!! Akasema kwa ukali Dr Joshua





    Jaji Elibariki alikuwa amepumzishwa kwa muda baada ya kushonwa jeraha lake alilokuwa amepigwa na chupa kichwani.Alikuwa ametundikiwa chupa ya damu kwani ilionekana amepoteza damu nyingi.Akiwa amelala kitandani mawazo yake yote yalikuwa kwa akina Mathew kama walifanikiwa kutoka salama.Kingine kilichomuumiza kichwa ni namna gani angemueleza mkewe kuhusiana na jeraha lile .

    “ Nimekwisha pata jawabu.Nitamueleza kwamba niliumia katika harakati za kutoroka hospitali.Ninadhani kwa uetetezi huo atanielewa.” Akawaza halafu picha ya tukio zima lililotokea nyumbani kwa Peniela ikamjia kichwani

    “ Bastard !!..akasema kwa hasira na kutaka kuinuka lakini akahisi maumivu makali sehemu yenye jeraha akajilaza tena

    “ Kilichotokea nyumbani kwa penny ni kitendo cha aibu sana.Ninashukuru sehemu ile si sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu kumetulia na hakuna watu wengi.Endapo kungekuwa ni sehemu zenye watu wengi sijui ni aibu gani ningeipata.Mtu ninayeheshimika kama mimi,jaji wa mahamakama kuu ninagombana kwa sababu ya mwanamke ni aibu kubwa sana.Ingekuwa sehemu zile zlizojaa wadaku sijui ningeuwekawapi uso wangukwani picha zangu zingesambaa katika kila gazeti la kesho.Ingekuwa ni aibu kubwa kwa sababu Yule mshenzi amenikuta nikiwa mtupu kabisa ” Akawaza Elibariki na kuuma meno kwa hasira

    “ Kuna klitu ambacho ninajiuliza na sipati jibu.Peniela na Jason walikuwa na mahusiano? Ninahisi hivyo kwa sababu Jason alikuwa akijitapa kwamba Peniela ni mwanamke wake.Aliongea kwa kujiamini sana..Kama walikuwa katika mahusiano kwa nini basi peniela akubali kuanzisha mahusiano na mimi? Nakumbuka Peniela ndiye aliyenishawishi hadi tukafanya mapenzi.Yeye ndiye aliyeniita kwake akidai ana shida kubwa lakini nilipofika kwake akaniambia shida yake ilikuwa ni kufanya mapenzi na mimi kwani alinitamanisiku nyingi.Iweje anitamkie manenohayo na wakatyi huo huo akawa na mahusiano na Jason wakati anaelewa kabisa kwamba mimina Jason ni washirika? Hili suala linanichanganya sana.Peniela lazima anipe maelezo kwa nini ametufanyia hivi .Kwa atuchezee kiasi hiki? “ akawaza na picha mbali mbali za Penny zikamjia kichwani.

    “ Lakini pamoja nayote yaliyotokea bado ninampenda penny.Bado yuko moyoni mwangu na siko tayari kumuona akiwa nayule kijana.Jason ni kijana mshenzi sana na asiye na adabu hata kidogo.Ninaapa nitamuonyesha kazi mimi ni nani hapa mjini.Ninataka nimfunze adabu ili siku nyingine asizoee kuingilia mali za watu.Mimi ndiye ninayestahili kuwa na Peniela kwa sababu ndiye niliyemuachia huru.Anajua ni mambo gani nimeyapitia hadi Peniela akawa huru? Nitamuonyesha kwamba nchi hii ina wenyewe .Nataka amuone pen……………” akastuliwa toka mawazoni na simu.Akaichukua na kutazama mpigaji alikuwa ni Mathew

    “Hallow Mathew,nipe habari.Mmefanikiwa kuwahi kutoka?akauliza

    “ Ndiyo Eli,tumefanikiwa kuwahi kutoka .Wewe uko wapi?akauliza Mathew na jaji Elibariki akabaki kimya

    “ Elibariki uko wapi ? akauliza tena Mathew

    “ Niko hapa Brahmaputra hospital”

    “ Unafanya nini hapo hospitali?

    “ Nimekuja kutibiwa jeraha nililoumia.Mmefanikiwa lile zoezi?”

    “ Eli,ninakuja hapo hospitali.I need to talk to you.”akasema Mathew na kukata simu

    “ Ahsante Mungu Mathew na timu yake wamefanikiwa kutoka salama.Lakini Flaviana amepataje taarifa hizi za kutaka kuwakamata madaktari wanaofanya uchunguzi ? Akajiuliza

    “ Mambo haya yanazidi kunichanganya.Inaonekana wazi kwamba sababu ya ya kifo cha Dr Flora haitakiwi kujulikana.Ni kitu gani kinafichwa? Nadhani Flaviana alikuwa sahihi,kuna kitu hakiko sawa kuhusiana na kifo cha Dr Flora.Ninaanza kuhisi yawezekana Dr Flora akawa aliuawa.Kama ni hivyo ni nani aliyefanya hivyo na kwa nini? Akajiuliza na kushindwa kupata jibu.

    Nusu saa toka Elibariki awasiliane na Mathew,mlango wa chumba alimolazwa ukafunguliwa akaingia daktari akiw ameongozanana Mathew na Anitha

    “ hallo Eli.Pole sana.Nini tatizo? akauliza Mathew

    “ Ah ! Mathew nilipata jeraha kidogo.”

    “Ulifanya nini?akauliza Mathew

    “ Nilikuwa naamulia ugomvi sehemu fulani basi ikarushwa chupa na kunipata kichwani.I’m ok now.Vipi kuhusu nyie mmefanikiwa kupata chochote?akauliza Elibariki

    “ Eli hatuwezi kuongea sasa hivi,naomba uinuke tuondoke.” Akasema Mathew na kumgeukia daktari

    “ Daktari naomba uchomoe chupa hiyo ya damu kwa mgonjwa wetu tunaondoka naye sasa hivi” akasema Mathew na kumfanya daktari Yule mwenye asili ya India abaki akishangaa

    “ Usishangae daktari ,chomoa huo mpira wa damu,tunaondoka na mgonjwa wetu” akaamuru Mathew.

    “Mgonjwa bado anahitaji kupatiwa huduma.Jeraha lake limesababisha akapoteza damu nyingi kwa hiyo anatakiwa kuongezewa damu mwilini.Mkimchukua kwa haraka namna hii inaweza kuwa ni hatari kwa mgonjwa”

    “ Dakatri nimesema chomoa huo mpira wa damu sasa hivi.Hatuna muda wa kuendelea kusubiri hapa”akasema Mathew.Daktari Yule akaogopa na kuisimamisha damu ile aliyokuwa ametundikiwa jaji Elibariki.Wakati akifanya hivyo simu ya jaji Elibariki ikaita,alikuwa ni mkewe Flaviana.Mathew akamsaidia kubonyeza kitufe cha kupokelea na kumuwekea sikioni

    “ Hallow Flaviana”akasema Elibariki

    “ Hallo Eli.Uko wapi? Uko salama?

    “ Niko salama mke wangu,ninaendelea vizuri usihofu”

    Flaviana akavuta pumzi nefu baada ya mumewe kumuhakikishia kwamba yuko salama.

    “ Kwa hiyo ukowapi Eli? I need to see you” akasema Flaviana

    “ kwa sasa niko mbali kidogo lakini baadae nitakuelekeza mahala tunakoweza kuonana.Nini kinaendelea hapo? Kuna taarifa gani?

    “ Usihofu Eli,nimeongea na baba na kumfahamisha kila kitu kuhusiana na kinachoendelea na mlichokuwa mnakifanya.Inaonekana kuna watendaji wake waliokuwa wakimzunguka na kufanya mambo bila ya yeye kufahamu.Ameahidi kulishughulikia suala hili kwa hiyo usiogope tafadhali,babat ayari anafahamu mlichokuwa mnakifanya na ameshukuru,ila ameahidi kwamba kesho asubuhi kuna timu ya madaktari kutoka hospitali kuu ya taifa wanakwenda kufanya uchunguzi kufahamu chanzo cha kifo cha mama.”akasemaFlaviana.Mathew akamfanyia ishara akate simu ili waondoke

    “Flaviana I have to go now.I’ll talk to you later”akasema Elibariki na kukata simu.Tayari daktari alikwisha maliza kazi yake akamuomba waongozane hadi katika dirisha la dawa ili akamuandikie dawa ambazo angeendelea kuzitumia.Jaii Elibariki akapatiwa dawa na kisha wakaingia katika gari wakaondoka.Safari ilikuwa ya kimya hadi walipowasili nyumbani kwa Mathew.Mara tu baada ya kuingia ndani Dr Michael akamshika mkono Mathew na kumvuta pembeni

    “ Mathew tayari nimefanya kila ulichotaka kukifanya.Ni zamu yako sasa kumtafuta mke wangu yuko wapi.”akasema Dr Michael

    “ Dr Michael nakushukuru sana kwa msaada wako .Nilikuahidi kwamba mke wako atapatikana.Niamni ninavyokwambia kwamba mkeo atapatikana.kwa sasa tuangalie namna tutakavyoweza kumalizia ile kazi tuliyokwenda kuifanya kule hospitali.”

    “ Nina sampuli kadhaa hapa ambazo zinatakiwa zifanyiwe uchunguzi,lakini sintaendelea na kazi hii mpaka hapo nitakapompata mke wangu.” Akasema Dr Michael

    “ Dr Michael nilikupa ahadi hiyo na lazima nitaitimiza lakini kwanza nahitaji kuimaliza kazi tuliyokwenda kuifanya.Ni muhimu sana.”

    “ Mathew nimekwisha kueleza kwamba sintofanya kazi yoyote ile hadi mke wangu atakapopatikana.” Akasema Dr Michael.Mathew akamtazama na kugundua kwamba hakuwa akitania.

    “ Ok Dr Michael tutamtafuta mkeo.Nipe muda nikae na timu yangu.”akasema Mathew na kuingia ndani.Ile ametia mguu sebuleni akakutana na Kanali adolf

    “ Nini kinaendelea hapa? Ninafanya nini hapa? Kazi yenu nimekwisha imaliza na sina deni tena kwako.I need to go back.I need to clean my mess” akasema Adolf.Mathew akamshika mkono na kumsogeza pembeni

    “ Adolf,kwa sasa huna sehemu nyingine ya kwenda.Hapa ni sehemu pekee ya wewe kuwepo kwa sasa.Utaendelea kukaa hapa hadi tutakapokamilisha uchunguzi tuliokwenda kuufanya na baada ya hapo nitashughulikia suala lako.Niamini Adolf,nitalimaliza suala hili na utarejea tenakazini kwako lakinikwa sasa utaendela kubaki hapa ” akasema mathew

    “ Uchunguzi wetu uliingiliwa kati kati na hakuna namna tutakayoweza kujua nini kilimuua Dr Flora.”

    “ hapanaAdolf,bado uchunguzi wetu unaendelea.Kabla ya kuondoka mle ndani,Dr Michael alichukua sampuli kadhaa za kufanyia uchunguzi.Yeye anafanya kazi katika hospitali kubwa hapa nchini kwa hiyo tutaitumia maabara ya hospitali hiyo anakofanyia kazi kufanya uchunguzi wa sampuli zile alizochukua.Kwa sasa kuna kazi ambayo tunatakiwa kuifanya ili aweze kumalizia uchunguzi .Tunatakiwa kumpata mkewake aliyetekwa”

    “ Mke wake ametekwa? Akashangaa Adolf

    “ndiyo ametekwa”

    “Ametekwa na akina nani?

    “ Hatuna uhakika ni akina nani mpaka sasa hivi.”

    “ Kitu gani kinaendelea hapa nchini? Ninyi ni akina nani? Akauliza Kanali Adolf

    “Adolf kaa upumzike na utuache tufanye kazi,tutaongea zaidi baade”akasema Mathew na kumfuata Anitha

    “ Anitha nenda kaweke sawa mitambo yako tunaanza zoezi la kumtafuta mke wa Dr Michael”

    Anitha akaelekea chumba cha mawasiliano halafu Mathew akamuendea Jaji Elibariki

    “ Elibariki,kuna mambo ambayo yanaendelea ambayo nimeona nikufahamishe.Kwanza usistuke kuona kuna watu tuko nao hapa.Yule mzungu anaitwa Dr Michael na Yule mwingine anaitwa kanali adolf ambaye ni daktari mkuu wa hospitali kuu ya jeshi.Kwa pamoja wote wako hapa kwa sababu maalum.Siwezi kukueleza kila kitu hapa kwa kuwa hatuna muda wa kutosha. Kikubwa ninachotaka kukueleza nikwamba tumefanikiwa kuufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora lakiniwakati tukiwa katikati ya uchunguzi ndipo ulipotupigia simu na kutupa ile taarifa ikatulazimu kuondoka haraka sana.Pamoja na hayo lakini tumefanikiwa kuondoka na sampuli kadhaa ambazo Dr Michael ataendelea kuzifanyia uchunguzi lakini ni baada ya mke wake kupatikana.”

    “ Mke wake yuko wapi? akauliza Elibariki

    “Mke wake ametekwa na watu wasiojulikana na kwa sasa tunaingia katika zoezi la kumtafuta.Tukishampata mke wake Dr Michael ataendelea na uchunguzi.Tukimpata majibu ya uchunguzi huo tutajua nini kilimuua Dr Flora.Ninachotaka kufahamu toka kwako ni nani aliyekupa taarifa za kwamba tumegundulika tunafanya uchunguzi?

    “Ni mke wangu Flaviana ndiye aliyenipigia simu na kunipa taarifa hizo”akasema Elibariki

    “ Alikwambia ni wapi alizipata taarifa hizo?

    “ Hapana sijaongea naye lolote kuhusiana na suala hilo “

    “ Ok itakubidi umpigiie simu umuulize alizipataje taarifa hizo za sisi kuwapo mle ndani.Tukifahamu tutajua nini cha kufanya.Vilevile anatakiwa awe makini sana.Mwambie achukue tahadhari kubwa kwa kila anachokifanya kuanzia sasa hadi hapo tutakapojua ninikilichomuua mama yake”

    “ Kwa niniunasema hivyo mathew?

    “Ni kutokana na hali halisi ilivyo.Kuna kila dalili zinazoonyesha kwamba kuna jambo lilsilo la kawaida linaloendelea hapa.Mpaka tulifahamu ni jambo gani mnatakiwa mchukue tahadhari kubwa.”

    “ Kuna uwezekano Dr Flora akawa aliuawa? Akauliza Elibariki

    “ Kuna uwezekano huo kutokana na hali ya mambo ilivyo.Kuna juhudi kubwa za kujaribu kuficha chanzo cha kifo chake kwahiyo inashawishi kuamini kwamba Dr Flora aliuawa lakini tusubiri kwanza majibu ya vipimo yatatuambia nini” akasema Mathew na kumuacha jaji Elibariki ameduwaa.Akachukua simu na kumpigia mkewe.

    “ Hallo Elibariki” akasema Flaviana baada ya kupokea simu

    “ Flaviana uko wapi?

    “ Niko hapa msibani,kuna nini Elibariki? Akauliza Flaviana

    “ Kuna watu hapo karibu ambaowanasikia unachoongea simuni?

    ‘ Hapana niko chumbani peke yangu nimejifungia”

    “ Ok vizuri,kuna jambo nahitaji kulifahamu.Nahitaji kufahamu namna ulivyozipata zile taarifa “

    Flavina akamueleza mumewe kila kitu kilichotokea

    “ Kwahiyo hapa inaonekana Dr Kigomba ndiye aliyetoa amri ya kuzuia mwili wa Dr Flora usifanyiwe uchunguzi”

    “ Inaonekana hivyo kwa sababu Anna amemsikia kwa masikio yake akielekeza kwamba madaktari wanaoendela na uchunguzi wakamatwe haraka sana.”

    “ Ok ahsante sana nashukuru ,lakini kuna jambo moja nataka kukuonya.Kuanzia sasa kuwa makini sana na kila unachokifanya.Kuha jambo linaloendelea hapo ikulu ambalo tunatakiwa tulifahamu.Kesho tunaweza kupata majibu ya uchunguzi wa kifo cha Dr Flora lakini mpaka wakati huo kuwa makini sana.Nitakupigia tena simu baadae” akasema Elibariki ina kukata simu kisha akamfuata Mathew

    “ Mathew nimeongea na mke wangu anasema kwamba aliyesikika akitoa amri ya kukamatwa kwa madaktari wanaofanya uchunguzi wa kifo cha Dr Flora ni Dr Albert Kigomba katibu wa rais.

    ‘unasema Dr Kigomba? Akauliza Mathew kwa mshangao

    “ Ndiyo .Dr Kigomba ndiye aliyetoa amri hiyo”

    “ Kwa mujibu wa kanali adolf Dr Kigomba ndiye aliyetoa amri kwamba mwili wa Dr Flora usifanyiwe uchunguzi na leo hii ni yeye ambaye anatoa tena amri kuwakamata madaktari wanaofanya uchunguzi wa kifo cha Dr Flora.Kuna jambo hapa si bure” akawaza Mathew halafu akawageukia Anitha na Noah

    “ Guys tumepata tena mtu mwingine tunayetakiwa kumchunguza.Dr Albert Kigomba anaingia rasmi katika mikono yetu.Tunatakiwa kuchunguza uhusika wake katika kifo cha Dr Flora.Tutalifanya hili baadae lakini kwanza tuelekeze nguvu kumpata mke wa Dr Michael ili aweze kumaliza kufanya uchunguzi na baada ya hapo tutajua nini cha kufanya.Anitha umefikia wapi?

    ‘ Kila ktu kiko tayari.Naombeni simu ya Dr Michale ili niiunganishe na kompyuta yangu “

    Dr Michaela kaitwa mle chumbani ,simu yake ikachukuliwa ,Anitha akaichomeka katika kifaa Fulani kilichounganishwa na kompyuta yake halafu akaendelea kubonyeza bonyeza namba kadhaa na baada ya muda akawageukia akina Mathew

    “ mambo tayari.Nitaipiga simu ya mkewa Dr Michael na kama haijazima basi tutaonyeshwa mara moja yuko sehemu gani.Lakini hata kama imezimwa basi tutaitafuta kwa njia nyingine ” akasema Anitha na kisha akabonyeza kitufe cha kupigia simu kilichoonekana katika kompyuta yake.Katika runinga kubwa iliyokuwa ukutani kukaonekana kitu Fulani mfano wa taa ndogo ikiwaka na kuzima.

    “Simu yake inaita.Haijazimwa.Tusubiri sekunde kadhaa tutajua mahala alipo.” Akasema Anitha .Watu wote walikuwa kimya.Baada ya sekunde kadhaa kile kitaa chekundu kilichokuwa kinawaka na kuzima kikabadilika rangina kuwa cha kijani halafu kukatokea picha fulani mithili ya ramani..

    “ Done.Tayari nimejua mahala alipo mke wa Dr Michael.”akasema Anitha halafu akaanza kubonyeza kompyuta yake baada ya dakika mbili akaenda katika runinga ilena kuikuza ile picha picha iliyokuwa inaonekana

    “ .Simu ya mke wa Dr Michael inaita toka katika jengo hili “ akasema Anitha na kuwalekeza akina Mathew

    “Good Job Anitha .Noah jiandae tundoke.” Akasema Mathew

    “Na mimi ninawafuata” akasema Dr Michael

    “ Hapana Dr Michael utabaki hapa.Ni hatari sana kuongozana nasi .”

    “ Mathew huyu ni mke wangu na ninatakiwa nishiriki katika kumuokoa.Hebu pata picha ingekuaje angekuwa ni mke wako ndiye aliyetekwa? Ungeweza kukaa hapa na kusubri wakati mkeo yuko katika hatari? Akauliza Dr Michael.Mathew akainama akafikiri na kusema

    “ Hapana.Nisingeweza kufanya hivyo”

    “ Kama ni hivyo na mimi naungana nanyi.Ninaweza kulenga shabaha vizuri,naninajua kutumia bastora.Ninaweza kupambana” akasema Dr Michael.

    Mathew akaenda chumbani kwake akachukua silaha na vitu vingine ambavvo aliona vitamsaidia katika kazi ile halafu akampatia Dr Michael fulana ya kuzuia risasi pamoja na bastora moja na kisha akaenda sebuleni na kumrushia Kanali Adolf bastora

    “ we’re going out.”

    “ Out where?

    “ To rescue a woman.get ready ” akasema Mathew na kumfuata Anitha

    “ Anitha tunakwenda kumchukua mke wa Dr Michael.Tunakutegema sana wewe katika operesheni hii.I promised to get his wife back and that’s what we’re going to do..” Akasema Mathew na kuchomeka sikioni kifaa cha mawasiliano akajaribisha na kuona kiko sawa

    “ Usihofu Mathew kila kitu kimekaa sawa.Nitaona kila kitu kutokea hapa kwa kutumia satellite.” Akasema Anitha

    Mathew,Noah ,Dr Michael na kanali Adolf wakaingia garini na kuondoka .







    Peniela akiongozwa na yule jamaa wa miraba minne walifika katika mlango mmoja mkubwa wenye nakshi za kupendeza.Nje ya mlango ule kulikuwa na watu wanne wenye kuvalia suti nyeusi kila mmoja.Kama ilivyokuwa kwa watu wengine aliokutana nao katika jengo hili,watu wale pia walionyesha heshima kubwa sana kwake.Penny aliendelea kushangaa kwa kitendo kile cha kupewa heshima kubwa namna ile na watu wale ambao hakuwahi kuonana hata na mmoja wao.

    “ Hello Peniela” akasema mmoja wa wale jamaa waliokuwa wamesimama mlangoni huku akimpa Penny mkono

    “ Hallow” akasema penny .Alikuwa nwasi wasi sana lakini alijitahidi kwa kadiri alivyoweza asionyeshe aina yoyote ya wasi wasi mbele ya watu wale

    “ karibu sana penny.Nadhani ni mara ya kwanza tumeonana ana kwa ana.Mimi ndiye Code is 00P688 na kwa jina naitwa Osmund mgano.Yule pale ni Victor Alfred,anayefuatia ni Bashir Hussein,Amani sufa,na yule pale ni Ezekiel Sadoe.” Akasema Osmund.

    “ Nafurahi kuwafahamu” akasema Penny.Osmund akafungua mlango na kumkaribisha Penny

    “ karibu ndani Penny.Tafadhali usiogope” akasema Osmund na Penny akaingia ndani na kukutana na sebule moja kubwa na nzuri yenye samani za kuvutia.Akatabasamu kwa uzuri wa sebule ile.Osmund akamkaribisha sofani akaketi.

    “ Penny ,nafahamu utakuwa ukijiuliza ni kwa nini leo tumeamua kukuita mahala hapa.Kwa miaka mingi umekuwa ukipata maelekezo yetu kwa kupitia simu na leo imetulazimu kukuita ili tuonane ana kwa ana.” Akasema Osmund akamtazama Penny kwa sekunde kadhaa kisha akaendelea

    “ Hapan ndiyo makao yenu makuu? Akauliza Penny

    “ Hapa si makao yetu makuu ,ila hapa ndipo anapoishi mkuu wetu ambaye ndiye anayetaka kuonana nawe leo hii.Ni mgonjwa sana na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji muda wowote lakini kabla ya kufanyiwa upasuaji huo anahitaji kukuona,kuna jambo anataka kuongea nawe” Akasema Osmund halafu akasimama

    “ Naomba sasa bila kupoteza wakati nikupeleke kwa mkuu wetu ana jambo la kuongea nawe” akasema na kuanza kupiga hatua Penny akamfuata.Walifika hadi katika mlango mmoja wenye rangi nyeupe ,Osmund akasimama na kugonga mara tatu,mlango ukafunguliwa na mtu mwenye mavazi ya kidaktari.Osmund akaongea naye kwa sekunde kadhaa halafu mtu yule akatoka nje na kisha Osmund na Penny wakaingia ndani ya chumba kile kikubwa cha kulala.Macho ya penny yakatua katika kitanda kikubwa alichokuwa amelala mtu mmoja aliyeonekana mgonjwa sana huku akiwa ametundikiwa chupa ya maji .Pembeni ya kitanda chake kulionekana mashine kadhaa na zote zikiwa zimeunganishwa mwilini mwa yule mtu aliyekuwa amelala pale kitandani.Penny alimtazama mtu yule lakini hakuweza kumtambua.Hakuwahi kuonana naye hata mara moja.

    “ Huyu mtu ni nani? Sijawahi kuonna naye hata mara moja.Anataka kunieleza nini? Akajiuliza .Osmund akakisogelea kitanda cha yule mgonjwa akamuinamia na kuongea naye kidofo galafu akabonyeza kitufe Fulani ukutani na sehemu ya juu ya kitanda ikanyanyuka yule mgonjwa akaweza kukaa.Penny akamtazama vizuri ,alikuwa ni mzee ambaye kwa kukadiria umri alipata miaka themanini au zaidi ya hapo.Alionekana dhaifu sana.Akamuomba Osmund ampatie miwani yake akavaa .Osmund akamsogelea Penny na kumwambia

    “ Penny ,huyu ndiye kiongozi wetu.Ni mgonjwa sana ,anaomba kuongea nawe mambo kadhaa.Tafadhali jitahidi kumsikia kwa makini kile atakachokwambia.Ni mtu anayefahamu mambo mengi sana usimuogope” akasema Osmund na kumshika mkonoPenny akamsogeza karibu na kitanda cha yule mgonjwa akamvutia kiti akakaa.Moyo ulikuwa ukimdunda hakujua yule mzee alitaka kumweleza kitu gani.Yule mzee akageuza shingo na kumtazama Penny akamfanyia ishara asogee karibu

    “ Come closer” akasema kwa sauti ya chini.Penny akamsogelea karibu

    “ Nipe mkono wako” akasema.Penny kwa uoga akausogeza mkono wake yule mzee akaushika halafu akaonekana kuzama katika mawazo

    “ Peniela !..akasema kwa sauti ndogo.

    “ I’m glad to meet you before my last breath.”akasema yule mzee halafu akafumba macho yake kana kwamba kuna jambo analifiki kisha akasema

    “ I’m sick and I’m going to die soon my princess lakini nimeona kabla sijafa nikuite kuna mambo ya muhimu ambayo natakiwa nikueleze”.

    Akanyamaza akafumba tena macho akafikiri halafu akasema

    “ Ninaitwa John Mwaulaya.Mimi ndiye kiongozi wa team SC 41 ,kikosi ambacho unafanya nacho kazi.Mimi ndiye niliyekuwa nikiwasiliana nawe kwa miaka hii yote hadi niliposhindwa kuhimili majukumu yangu kutokanana afya yangu kuwa mbovu.” Akanyamza kidogo akafumba macho kwa sekunde kadha halafu akaendeleahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Mimi ndiye ambaye nimekuwa nikikuangalia toka angali ukiwa mchanga hadi hivi sasa japokuwa hukunifahamu.Peniela una historia ndefu sana na ambayo siwezi kukueleza kila kitu kwa sasa.Kuna mambo mengi ambayo huyafahamu kuhusu wewe na hakuna yeyote anayefahamu zaidi yangu.” Akasema John na macho ya Peniela yakalengwa na machozi.Mtu yule ambaye alikuwa na hamu kubwa ya kumuona na ambaye amekuwa akiongea naye simuni kwa miaka mingi leo hii amefanikiwa kuonana naye ana kwa ana.

    “ hatimaye leo nimekuona ana kwa ana John mwaulaya.Sikuwa nikikufahamu hata kwa jina.Nilikufahamu kwa sauti tu.Nina maswali mengi sana ambayo unatakiwa unipatie majibu yake? Akawaza Penny

    “ Penny natamani sana nikueleze wewe ni nani na umefikaje hapa ulipofika lakini sina nguvu tena,sina uwezo wa kuongea kwa muda mrefu..” Akasema John halafu akamuomba penny azunguke upande wa pili wa kitanda,akamtajia namba za kufungulia kasiki lililokuwa ukutani,baada ya kubonyeza namba zile kasiki lile likafunguka na ndani yake kulikuwa na vitu vingi.Akamuelekeza achukue kasha lenye nakshi za dhahabu.Penny akalitoa kasha lile akalitazama halafu akalifunga lile kasiki.

    “ Peniela,ndani ya kasha hilo kuna kila kitu kinachokuhusu wewe.Thats who you are.”akasema John.

    “ John,mbona sielewi? Akauliza Penny

    “ Ndani ya hilo kasha kuna kila kitu kinachohusiana na wewe,kuna kila kitu kinachoelezea wewe ni nani.Historia nzima ya maisha yako iko humo ndani ya hilo kasha,kwa hiyo nakuomba ulitunze kama mboni ya jicho lako.Ukilipoteza na kila kitu chako kimepotea.Nimelitunza kwa miaka mingi kwa hiyo na wewe litunze sehemu salama.Watu wanalitafuta kasha hilo na wakilipata you are finished my princess so.Kwa hiyo lilinde kwa kila namna unavyoweza.” akasema John.Penny akalichunguza kasha lile lilikuwa limefungwa

    “Mbona limefungwa ? Funguo yake iko wapi? Akauliza

    “ Nitakuelekeza namna utakavyoweza kuipata funguo lakini kwanza kuna jambo la muhimu sana nataka kukwambia.” Akanyamaza akafumba tena macho kwa sekunde kadhaa halafu akasema.

    “Nilikuingiza katika kazi hii kwa sababu niliamini ndiyo kazi sahihi kwa wewe kuifanya.Kwa mara ya kwanza katika maisha yngu najutia uamuzi wangu wa kukuingiza katika kazi hii.Ni wakati wako sasa wa kuishi maisha huru na ya kawaida.Baada ya mimi kufariki hautakuwa na ngao wala mtu yeyote anayekulinda na kukuchunga kwa hiyo utakuwa katika hatari kubwa.Ndoto yangu ni wewe kuachana na kazi hii na kuishi maisha ya kawaida yenye furaha na amani.With this job you’ll never have a normal life.Lakini hii itawezekana tu kama utaikamilisha kazi uliyopewa sasa.Operesheni hii ni muhimu sana kwa nchi na dunia nzima kwa hiyo lazima uhakikishe kwa kila namna imefanikiwa.Baada ya kuikamilisha operesheni hii ndipo ulifungue kasha hili.Kasha hili halijakamilika.Lina sehemu tatu.Ukihakikisha kazi imekamilika nenda kanisa la bwana na uonane na mchungani Edmund dawson yeye ndiye mwenye funguo na atakuongoza mahala yalipo makasha yaliyosalia.” Akasema JohnMwaulaya ambaye alianza kupumua kwa shida.

    Wakati Penny na John Mwaulaya wakiwa ndani Osmund aliyekuwa amesimama nje ya mlango wa Joh Mwaulaya akapigiwa simu.Baada ya kuongea na simu ile akamgeukia mwenzake aliyekuwa amesimama naye pale mlangoni

    “ We have a situation.Kuna watu wamevamia mahal tulipomficha mke wa Dr Michael na hivi sasa kuna mapambano yanaendelea .Tuma kikosi haraka sana kwenda kutoa msaada.Hakikisha kwa kila namna hawafanikiwi kumchukua mke wa Dr Michael.Hali ya John inazidi kuwa mbaya na tunamtaka sana Dr Michael amfanyie upasuaji ili kuokoa maisha yake.Bila kuendelea kumshikilia mke wake hataweza kuifanya hiyo operesheni.Tafadhali hakikisheni vijana wanarejea hapa wakiwa na mke wa Dr Michael na wale wote waliojaribu kufanya uvamizi huo” akaamrisha Osmund.



    Peniela alisimama pembeni ya kitanda cha John Mwaulaya akiwa ameshika lile kasha huku akionekana kuchanganyikiwa asijue afanye nini.Alitamani sana John angemfafanulia kuhusiana na kile alichomweleza.

    “ Mr John,…” akaita Penny lakini bado John mwaulaya aliendelea kuyafumba macho yake

    “ Mr John,please listen to me…” akasema Penny na John akafumbua macho yake akatabasamu na kusema

    “ Peniela come closer,hug me” Penny akamsogelea John pale kitandani akainama na kumkumbatia.Katika macho ya John Mwaulaya kulionekana michirizi ya machozi

    “ Sasa ninaweza kwenda kwa amani” akasema John Mwaulaya kwa sauti ndogo

    “ Penny you can go now.Siku zote usisahau kwamba ninakupenda sana” akasema John

    “ Mr John,..Mr John..!! akaita Penny

    “Go Penny…go…!! Akasema John mwaulaya halafu akaupeleka mkono chini ya kitanda chake akabonyeza kitufe Fulani na mlango ukafunguliwa akaingia Osmund kwa haraka na moja kwa moja akamfuata John Mwaulaya pale kitandani.

    “ John ..!! akaita

    “Ossy nataka uniahidi kitu kimoja” akasema John kwa sauti ya chini sana

    “ I need you to take a very good care of Penny after I’m gone.Make sure she’s always safe.” akasema John

    “ Usijali John nitamuangalia penny ,na atakuwa alama.”

    “ One more thing” akasema John

    “ Once this mission is over,please let her go.Give her a chance to start her own life.Can you promise me that? Akauliza John

    “ Yes ! I give you my word John.I’ll let her go.I’ll help her” akasema Osmund

    “ Thank you Osmund.Now escort her out.I need to be alone for a while” akasema John .Osmund akamuangalia halafu akamfuata Peniela na kumuomba amfuate.

    “ Amekwambia nini John?akauliza Osmund wakati wakishuka ngazi.

    “ Nothing important,alinieleza tu kuhusiana na operesheni inayoendelea.Alinisisitiza kwamba nijitahidi sana kuhakikisha inamalizika haraka iwezekanavyo.”

    “ Good.” Akasema Osmund wakati wakishuka ngazi kuelekea chini

    “ Katika hilo kasha kuna nini? Akauliza tena Osmund

    “ Ni zawadi amenipa”akajibu Penny

    “ He loves you so much” akasema Osmund,Penny hakumjibu kitu akatabasamu

    Walielekea moja kwa moja hadi katika maegesho ya magari.

    “ Penny ningekupeleka nyumbani lakini kuna tatizo limetokea hapa muda si mrefu ambalo linahitaji kushughulikiwa haraka sana.Vile vile John anahitajika kufanyiwa upasuaji kwani hali yake inazidi kuwa mbaya.Kijana huyu atakupeleka nyumbani kwako na nitawasiliana nawe tena baadae.” Akasema Osmund

    “ Will he be ok? Akauliza Penny

    “ yes ! He’ll be ok.”

    “ Nashukuru sana Osmund kukufahamu na kumfahamu pia John Mwaulaya.Namuombea apate nafuu ya haraka na apone ugonjwa unaomsumbua.” akasema Penny na kuingia katika gari.

    “ Hata mimi nimefurahi sana kukufahamu Penny.”

    “ Hali yake itakapoboreka ninaweza kupata nafasi ya kuonana naye tena?

    “ Usijali Penny,nijakujulisha pindi hali yake itakapoboreka na utapata wasaa wa kuonana naye” akasema Osmund aliyeonekana kuwa na haraka ,akaagana na Penny kisha akakimbilia ghorofani.Gari aliyopanda Penny ikaondoka

    “ Bado naona kama ndoto ,kuonana na mtu ambaye nimekuwa nikihitaji sana kuonana naye ili anipe majibu ya maswali yangu mengi.Kwa bahati mbaya sana nimekutana naye katika siku zake za mwisho.Kwa hali aliyonayo sina hakika kama bado ana maisha marefu.Laiti ningepata nafasi ya kuonana naye tena”akawaza Penny akiwa garini akirejeshwa kwake

    “ John Mwaulaya amekuwa akiyaongoza maisha yangu toka nikiwa mtoto mdogo.Kila nilichokuwa nikikifanya ni nilikifanya kwa maongozi yake.Nimefurahi sana kumuona lakini pamoja na furaha hiyo bado sijaweza kupata kile nilichokuwa nikikihitaji kukipata toka kwake .Nilihitaji sana anieleze kwa mdomo wakemimi ni nani? Familia yangu iko wapi? Kwa nini nikalelewa katika nyumba ya yatima?Kwa nini aliniingiza katika kazi hii?Akaendelea kujiuliza halafu akalishika lile kasha akalitazama kwa makini

    “ Kasha hili ndilo lenye kila kitu kuhusiana na mimi.Kwa mujibu wa John ni kwamba kasha hili haliko peke yake.Kuna mengine matatu kama hili na nikiyapata yote ndipo nitakapoweza kufahamu kila kitu.Mchungaji Edmund Dawson nitampata wapi? Anahusika vipi na team SC41? Mambo haya yanachanganya sana “akainama akazama katika mawazo.

    “ Nitalihifahdhi wapi kasha hili sehemu yenye usalama? Kwa mujibu wa john ninatakiwa nilihifadhi sehemu salama sana.Siwezi kulificha kwangu kwa sababu tayari watu wale wanaweza wakafika kwangu muda wowote na wakaingia wakalichukua” akawaza



    ********



    Alipohakikisha Peniela ameondoka ,Osmund akarejea haraka chumbani kwa John.

    “ Penny tayari ameondoka” Osmund akamweleza John

    “ Thank you Ossy,” akajibu John kwa sauti ya chini

    “ Kwa sasa unajisikiaje John?

    “Hali yangu si nzuri hata kidogo.I don’t know if I’m going to make it”

    “ John don’t worry.You are going to make it.You are going to be ok.Kila kitu kinaandaliwa hivi sasa ”akasema Osmund.John akamfanyia ishara kwamba atoke mle chumbani anahitaji kuwa peke yake.Akafumba macho na kumbu kumbu Fulani ikamjia

    “ Its been years…!!! Akanong’ona na kumbu kumbu zikamrejesha tarehe 26 April 1986



    26 April 1986

    Saa saba za usiku ,mvua kubwa inayesha jijini Dar ,mitaa mingi imefurika maji.Nje ya nyumba moja yenye uzio wa michongoma,gari moja imesimama ikiwa na watu wanne ndani yake. Mtu mmoja aliyekuwa amekaa pembeni ya dereva alikuwa akiongea na simu

    “ Frederick ,tayari niko nje ya nyumba ya akina Pamela.Are you sure you want to do this? Akauliza mtu yule

    “ John please please you have to do it.Kesho yule msichana na mama yake wanakwenda katika vyombo vya habari na kunitangaza.Tayari nimekwisha taarifiwa na vyanzo vyangu vya habari kwamba kesho Pamela na mama yake wanakutana na waandishi wa habari na wanawaeleza kila kitu.Lengo lao ni kutaka kuniangusha kisiasa.Nina wabaya wangu wengi ambao hawalali wanatafuta namna watakavyoweza kuniangusha.Nimejaribu kutafuta suluhu na Pamela na mama yake lakini hawako tayari kunisikiliza kwani wameahidiwa pesa nyingi sana na wabay wangu kama wakifanikiwa kuniangusha.Sitaki wafike kesho.” Akasema Frederick

    John akanyamaza kidogo akafikiri na kuuliza

    “ What about the baby?

    “ Kill them all” akasema Fred.

    “ Ok Fred nitakupigia baada ya dakika ishirini.”akasema John kisha akawageukia vijana wake

    “ It’s a go.” Akawaambia vijana wale aliokuwa nao garini wakajifunika nyuso zao kwa kofia na kuacha macho tu,wakavaa gloves na kisha wakachukua silaha zao wakashuka na kupenya uzio wa michongoma wakaingia ndani.Mvua kubwa bado iliendelea kupiga ,hivyo hakuna aliyesikia wakati mlango ukifunguliwa .Waliingia ndani na moja kwa moja wakaanza kukagua chumba kimoja baada ya kingine.Nyumba ile ilikuwa na vyumba vitatu vya kulala.Katika chumba kimoja walimkuta msichana mmoja aliyejitambulisha kama msichana wa kazi,chumba cha pili alikutwa msichana Pamela na mtoto wake mchanga,chumba cha tatu kilikuwa ni cha mama yake Pamela ambaye alikuwa amelala na mdogo wake aliyekuja kumtembelea toka kijijini.Wote walikusanywa sebuleni na kufungwa mikono na miguu na kisha kwa amri ya John wakamiminiwa risasi kutoka katika bastora zenye viwambo vya kuzuia sauti.Yalikuwa ni mauaji ya kinyama sana.

    “ Vipi kuhusu mtoto?akauliza mmoja wa wale vijana

    “ Don’t kill that baby.Tunaondoka naye” akasema John ambaye alimbeba yule mtoto Walikagua nyumba yote na kujaribu kuchukua kila walichoona kinaweza kufaa kuchukuliwa wakaondoka.Wakiwa garini John akampigia simu Fred

    “halo Fred…Kazi imemalizika” akasema John

    “Ahsante sana John.Sijui nikulipe kitu gani kwa kuniokoa na janga hili.Ninakuahidi John sintokusahau katika maisha yangu kwa namna ulivyonisaidia.Usihofu kitu makubaliano yetu yako pale pale”akasema Fred

    “ Usijali Fred wewe ni mtu wangu wa karibu .Pamoja na hayo ninaomba tuonane usiku huu,kuna jambo la muhimu nataka tuongee”

    Fred akakaa kimya kwa sekunde kadhaa halafu akasema

    “ Kuna jambo gani John? Kuna jambo halikwenda vizuri?

    “ Hapana Fred ,kila kitu kimekwenda vizuri.Kuna kitu nataka nikukabidhi” akasema John

    “ Tukutane wapi John?

    “ Tukutane daraja la mamba”

    John na vijana wake walielekea hadi katika darajala mto Mamba wakasimamisha kandoni mwa daraja.Eneo lile lilikuwa kimya sana.Mto mamba ulikuwa umefurika maji kutokana na mvua kubwa zlizoendelea kunyesha.Baada ya kama dakika arobaini hivi likatokea gari aina ya Range rover Vogue rangi nyeusi.Gari likazima taa na baada ya dakika tano John akashuka ndani ya gari akaliendea lile range rover vogue.Mlango wa ile range rover Vogue ukafunguliwa akashuka mtu mmoja mnene akiwa na mwavuli.Akamkumbatia kwa furaha John

    “ Ahsante sana John kwa msaada wako.”akasema yule jamaa

    “ Usijali Fred.kazi imemalizika.Kwa sasa uko huru” akasema John

    “ Ahsante sana.Umeniokoa sana John.” Akasema Fred

    “ Fred,hatuna muda mwingi wa kukaa hapa.Kuna kitu nataka nikakukabidhi katika gari langu.” akasema John wakaelekea katika gari la John.Akaufungua mlango na kumulika tochi .Fred akapatwa na mshangao mkubwa

    “ Mtoto !..akashangaa

    “ Yah..”

    “ Umemtoa wapo huyu mtoto? Akauliza Fred

    “ This is your daughter .”

    “ My daughter? Fred akashangaa

    “ Yah ! Huyu ni mwanao.Hii ni damu yako”akasema John.Fred akamtazama kwa macho makali.

    “ You didn’t kill her? Akauliza

    “ Sikumuua”

    “ kwa nini John? Nilikwambia wamalize wote.Sitaki aina yoyote ya ushahidi.John suala hili si la kufanyia mchezo hata kidogo.These people will haunt me and make sure the take me down”akasema Fred

    “ Fred I cant kill an Innocent baby.Huyu ni malaika asiye na kosa lolote.Siwezi kufanya ukatili mkubwa kiasi hiki.I cant kill her” akasema John.Fred akamtazama kwa hasira

    “ So what are you going to do with her? Akauliza

    “ I don’t know.But right now this is what I’m going to do” akasema John na kwa kasi ya umeme akachomoa bastora yake na kumchakaza Fred kwa risasi.Akaanguka chini.

    “ Siko tayari kumuua mtoto mdogo kama huyu asiye na kosa lolote.Sijawahi kufanya ukatili mkubwa kama huo.” Akasema John kisha akaenda katika gari la Gred akalikagua na kuchukua simu ya fred na vitu vingine kadhaa akaingia katika gari lake na kuondoka

    Kumbu kumbu ile ikamfanya John afumbe macho kwa uchungu

    “ I saved her.I saved Peniela.Nilimuua mama yake na baba yake hakutaka Penny abaki hai.” Akawaza John.

    “ Nimefanya mambo mengi mabaya lakini Mungu anaweza akanisamehe kwa jambo hili jema nililolifanya.Nilimuokoa mtoto malaika asiuawe.Mtoto ambaye alitakiwa kuuawa leo hii ndiye aliyejitolea maisha yake kuifanya nchi hii iwe salama” Akawaza John.



    *******http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Peniela alifikishwa nyumbani kwake.Baada ya kuingia ndani alisimama sebuleni kwake akiangalia namna vitu vilivyokuwa vimesambaratika kutokana na ugomvi wa akina Jason.Akaenda kuketi sofani.

    “ Ilibaki kidogo wanaume wale wangeuana hapa ndani.Niliogopa sana kwa namna walivyokuwa wakirushiana makonde.Natamani kufahamu Jaji Elibariki yuko katika hali gani hivi sasa.Aliumizwa sana chupa aliyopigwa na Jason.Niliogopa nikadhani amekufa ”akawaza.

    “ Sijui Jason naye yuko wapi mida hii.Nimefanya jambo baya sana la kuwagombanisha wanaume wale.Wote wawili ni watu wangu muhimu na kwa msaada wao nimeweza kuwa huru tena.Bila wao hivi sasa ningekuwa nikiozea gerezani.Nitawatafuta kila mmoja kwa wakati wake wakati wametulia na hawana tena hasira na nitamalizana nao.Nitawaweka sawa .Nitaendelea na kila mmoja kwa wakati wake kwani bado ninawahitaji lakini sitaki tena wawe marafiki na waendelee na mpango wao wa kuchunguza kifo cha Edson kwani ni hatari kwao.Kitu kikubwa ninachotakiwa kukifikiria kwa sasa hivi ni kuhusiana na jambo lililotokea leo,nimeonana na John Mwaulaya mtu ambaye nimekuwa nikihitaji sana kuonana naye kwa miaka mingi.Sikukipata nilichokuwa nikihitaji toka kwake lakini amenipa hili kasha na kudai kwamba kila kitu ninachohitaji kukifahamu kuhusiana na mimi kipo ndani ya hili kasha na mengine mawili ambayo yako sehemu Fulani.Ninatamani sana kulifungua kasha hili hata leo hii lakini John alisema nilifungue baada tu ya kumaliza operesheni hii. “ akalishika tena lile kasha akalitazama

    “Nahitaji sehemu salama nikalihifadhi hili kasha kama alivyosema John.Hapa kwangu si sehemu salama hata kidogo.Watu kama Team SC41 wanaweza wakaingia na kufanya chochote wanachokitaka muda wowote.I need somewhere safe”

    “ Kama ningekuwa sijawakorofisha akina Jason ningemuomba mmoja wao anihifadhie hili kasha lakini kwa sasa hakuna hata moja anayeweza kulikubali hilo.” Akajaribu tena kufikiri halafu akapata wazo.Akaenda chumbani kwake akachukua simu ile ambayo huitumia kuwasiliana na rais akaishika mkononi.

    “ Dr Joshua Yuko katika wakati mgumu sana hivi sasa,kwa kifo cha mkewe lakini sina namna nyingine nahitaji sana msaada wake kwa sasa.” Akawaza Penny na kumpigia Dr Joshua

    “ Hallo Penny” akasema Dr Joshua

    “ hallow Dr Joshua.How are you?” akasema Penny

    “ Niko katika matatizo Penny lakini nimefarijika sana baada ya kuisikia sauti yako malaika wangu.Unaendeleaje?

    “ Ninaendela vizuri sana.Iwish I could be there with you right now” akasema Penny kwa sauti ndogo

    “ You don’t have an idea of how much I need you by my side Penny.Kwa nyakati kama hizi ni wewe pekee ambaye unaweza ukanifariji na kuniondolea ukiwa.Uko wapi mida hii?

    “ Niko nyumbani nimejipumzisha” akasema Penny

    “ Maandalizi ya mazishi yanakwendaje?

    “ Tunatarajia kuzika kesho kutwa alasiri kijijini kwao.Kesho kutakuwa na zoezi la kuuaga mwili hapa nyumbani “ akasema

    “ Pole sana Dr Joshua”

    “Ahsante sana Peniela.Nimekwisha poa.Ni mapenzi ya Mungu .Ninatamani sana baada ya shughuli za msiba kumalizika nipate wasaa wa kukaa nawe tuongee.Tatizo ni kwamba siwezi kufika hapo unapoishi.kwanini lakini ulikataa kuishi katika ile nyumba niliyokupatia penny? akauliza Dr Joshua

    “Hiyo ndiyo sababu iliyonifanya nikupigie simu Dr Joshua.Niko tayari kuishi katika ilenyumba.”

    “ Unasema kweli Penny?

    “kweli Dr Joshua niko tayari kuishi pale ili mradi unihakikishie ni sehemu salama”

    “ Penny nimefurahi sana kusikia kwamba uko tayari kuishi pale.Kuhusu usalama usihofu,pale ni sehemu salama mno.Nitakuwekea ulinzi wa kutosha kila sehemu utakayokuwa kwa hiyo usiwe na wasiwasi wowote kuhusiana na usalama wako.”

    “ Dr Joshua nitaishi pale lakini kuna jambo moja ninalotaka kukuomba”

    “ Omba chochote penny katika dunia hii nitakupatia isipokuwa roho yangu”

    “ Sihitaji ulinzi wa aina yoyote.Sihitaji mtu wa kunifuatilia kuhusu maisha yangu.Siku nikigundua kwamba umeniwekawalinzi hata wa siri,Dr Joshua kutakuwa na mgogoro mkubwa kati yangu na wewe”

    “ lakini peniela hii ni kwa ajili ya usalama wako.Kama mke wa rais mtarajiwa unahitaji ulinzi .Ok sintakuweka walinzi lakini promise me that we’ll talk about this”

    “ Yes Dr Joshua we’ll talk about this ” akasema Penny.

    “ Nimefurahi sana Penny kwa jambo hili .Lini unahamia? Akauliza Dr Joshua

    “ Kesho” akajibu

    “ Kesho?! Akauliza Dr Joshua

    “ Ndiyo kesho.Kuna tatizo lolote?

    “ Hakuna tatizo Peniela.Nitamkabidhi Kareem jukumu hili atalishughulikia yeye kesho.Wewe usisumbuke na kitu chochote.”

    “nashukuru sana Dr Joshua.” Akasema penny

    Kimya kikapita halafu Dr Joshua akasema

    “ Penny I love you.More than you can imagine”

    Penny akatabasamu na kusema

    “ I love you too Joshua “ akasema Penny na kukata simu ingawa Dr Joshua alihitaji sana kuendelea kuongea naye



    ******

    Osmund alionekana kuwa na hofu kubwa sana.Kila alipojaribu kupiga simu kwa vijana wake waliokuwa katika mapambano na watu waliokuwa wamekwenda kumkomboa mke wa Dr Michael.Alimuhitaji sana Dr Michael kwa ajili ya kumfanyia upasuaji John Mwaulaya.Hali ya John iliendelea kuwa mbaya na alihitajika daktari kwa haraka na daktari pekee ambaye walimtegemea ni Dr Michael.Aliishika tena simu yake na kupiga

    “ hallow bosi” ikasema sauti ya upande wa pili

    “ Victor ni kitu gani kinaendelea huko? Kwa nini hampokei simu?

    “ Bosi,hali huku ni mbaya sana.Wale jamaa ni hatari sana.Wamefanikiwa kumchukua Yule mwanamke na wameondoka.Watu wetu sita wameuawa lakini na sisi tumefanikiwa kumuua mmoja wao”

    Osmund alihisi miguu ikimuisha nguvu akakaa juu ya msingi.





    “ Whats happening to me? Nimeshika tu uongozi ndiyo mambo yote haya yanaanza kutokea.Ugonjwa wa John Mwaulaya,na hawa watu wanaoanza kutufuatilia” Akajiuliza Osmund akiwa amekaa juu ya jiwe.

    “ Lakini watu hawa ni akina nani? Wanatafuta nini kwetu? Wametumwa na nani? Kwanini walikuwa wakimfuatilia John?.Wamefahamuje mahala alipokuwa amefichwa mke wa Dr Michael? Osmund akaendelea kujiuliza maswali mfululizo bila kupata jibu

    “ Nina wasi wasi kuna watu kati yetu wanaotoa taarifa zetu.Si rahisi kwa mtu wa kawaida kufahamu mahala tulipokuwa tumemficha mke wa Dr Michael.Inabidi tufanye uchunguzi haraka sana ili tubaini kama kuna yeyote ambaye atakuwa akitoa habari zetu na kuwapa hawa jamaa .Nina hakika lazima kuna mtu ambaye anatoa habari zetu na ndiyo maana hawa jamaa wamekuwa wakifahamu kila tunachokifanya.Nitafanya uchunguzi na kama nikifanikiwa kumpata ninaapa nitatoa somo kwa wengine.” Akawaza Osmund halafu akakumbuka kwamba hakuwa ameikata simu akaiweka tena sikioni

    “ Hallow Victor ! akaita

    “ Hallow bosi,wale jamaa wameondoka na tunasubiri maelekezo yako”

    “ Ondokeni sehemu hiyo haraka sana muda wowote polisi wanaweza wakafika.Hakikisheni hakuna mtu yeyote anayebaki hapo hapo.Hakikisheni miili ya watu wote inarejea hapa.Mtu wao aliyeuawa muacheni hapo hapo lakini kata kidole gumba chakulia ili tuweze kumfahamu ni nani.Chukueni pia simu yake na chochote mnaachoona kinaweza kutusaidia.Nawahitaji hapa haraka sana” akasema Osmund na kukata simu.

    “ Ninaanza kuwa na wasiwasi sana na Peniela.Nyendo zake zinanitia shaka sana na nina mashaka labda yeye anaweza akawa ndiye anaye toa taarifa zetu kwa wale watu. Nyendo zake sizielewi kabisa.Siku hizi havai tena kile kifaa cha mawasiliano ambacho kinatuwezesha sisi kuwasiliana naye kwa urahisi kila wakati ambacho ni salama zaidi kuliko kutumia simu.Kuna kila sababu ya kuanza kumchunguza Peniela na kuzifahamu nyendo zake.Tunatakiwa kufahamu anafanya nini,anashirikiana na watu gani na tunaweza kugundua kitu.Nina hakika kabisa kwamba tukimchunguza Pennykuna kitu tutakigundua.Nimekuwa na mashaka naye sana” Akawaza Osmund wakati akipanda ngazi kwa kasi kuelekea chumbani kwa John Mwaulaya.Alifungua mlango na kumfuata John kitandani

    “ John……John..”akaita.John mwaulaya akafumbua macho

    “ Unajisikiaje hivi sasa?

    ‘ I’m weak, I’m very weak Ossy.” Akasema John Mwaulaya kwa sauti ndogo.Roho ikamuuma sana Osmund kumuonaJohn Mwaulaya akiwa katika hali ile.Akaenda kuegemea kabati

    “ Nitafanya nini kuhusiana na John? Nitamtibu vipi? Hali yake inazidikuwa mbaya.Hapa hakuna namna zaidi ya kuwasiliana na makao makuu niwape taarifa hii kwamba tumeshindwa kumtibu John ili waweze kuona namna ya kumsaidia.Daktari tuliyekuwa tukimtegemea ni Dr Michael pekee lakini naye kwa hivi sasa hatutaweza kumpata tena” Osmund akatoka nje akaingia katika chumba kimoja kilichokuwa na kompyuta kadhaa akawakuta vijana wawili.

    “ Stanley wataarifu watu wote tukutane hapo chini haraka sana.Kuna jambo zito la kuwafahamisha” akasema Osmund na kutoka akaelekea chini mahala alikoelekeza wakutane

    “ Kwa mara ya kwanza ninahisi mambo kutaka kunishinda.I don’t know what I’m going to do.” Akawaza wakati akishuka ngazi.Mara tu baada ya kupata mwito ule toka kwa Stanley watu wote waliokuwepo pale katika nyumba ya John wakakusanyika chini.

    “ Ndugu zangu,nimewaita hapa kwa dharura kuna mambo makubwa matatu ambayo nataka kuwaeleza.Jambo la kwanza ni kuhusiana na afya ya mkuu wetu.Kama sote tunavyofahamu kiongozi wetu anaumwa sana na hali yake inazidi kuwa mbaya.Jitihada za kumfanyia upasuaji ili kuokoa maisha yake zinaonekana kugonga mwamba kwani daktari tuliyekuwa tukimtegemea kwa ajili ya upasuaji huo hatutaweza kumpata tena.Kwa sasa ninajaribu kuwasiliana na makao makuu ili tuone namna tunavyoweza kuokoa maisha ya John.Nimeona niwaeleze kuhusu hili kwa sababu kwa hatua aliyofikia hivi sasa anything can happen so we have to be prepared.” Akanyamaza akameza mate na kuendelea

    “ Jambo la pili ninalotaka kuwaeleza ni kwamba kuna watu wanatufuatilia.Bado sijafahamu wana tafuta nini kwetu lakini watu hawa wanaonekana ni watu hatari na wanafahamu kila tunachokifanya.Inaonekana kati yetu kuna mtu anayetoa taarifa zetu kwa hawa jamaa.Ninatoa onyo kwamba kwa yeyote atakayebainika kufanya jambo kama hilo adhabu yake ni kali sana.Kila mmoja wakati akijiunga na Team SC41 aliapa kwamba hatatoa siri za aina yoyote lakini inaonekana kuna mtu au watu waliokiuka kiapo chao na kuanza kutoa siri.Uchunguzi mkali unaendelea ili kwanza kuwafahamu wale watu wanaotufuatilia ni akina nani na vile vile kumfahamu mtu anayetoa taarifa zetu kwa wale jamaa.” Akanyamaza tena akawaangalia watu wake na kuendelea

    “ Jambo la tatu ninalotaka kuwaeleza ni kwamba usiku huu yametokea makabiliano kati ya watu wetu na hawa jamaa niliwaeleza kwamba wanatufuatilia na katika mapambano hayo tumewapoteza vijana wetu sita na tumefanikiwa kumuua mmoja wao.Hili ni pigo kubwa kuwahi kutokea katika team SC41 .Ninaahidi kwamba tutawasaka watu hawa na kuwapata wote .Usiku huu tutawazika watu wetu ili kesho tuamkie jambo moja tu.Kuwasaka wavamizi hawa.Miili italetwa hapa na tuatwaaga wenzetu na usiku huu tutawazika” akasema Osmund. Halafu akareja katika chumba walichokuwamo wale vijana wawili na kumuita Stanley nje

    “ Stanley wewe ni kijana ambaye ninakuamini sana na sina shaka nawe hata kidogo.Kuna kazi ambayo ninahitaji unisaidie kuifanya.”

    “kazi gani mkuu? akauliza Stanley

    “ Nadhani umefuatilia niliichokuwa nawaeleza wenzako kule chini.Kuna watu wanatufuatilia na wanapata taarifa zetu.Hili ni jambo hatari sana kwetu na kwa serikali ya Marekani na Tanzania kwa maana hiyo basi ninataka ufanye kazi moja ya muhimu sana.Ninataka umchunguze mtu mmoja mmoja katika Team SC41 ,angalia mawasiliano yao katika siku hii ya leo hii ili tuone kama kuna yeyote anayetoa taarifa zetu kwa watu hawa.Jambo hili sitaki mtu mwingine yeyote alifahamu.This is between us .Can you do that for me? Akauliza Osmund

    “ Ndiyo ninaweza kufanya hivyo ingawa inaweza kuchukua muda kidogo lakini nitafanya hivyo.Lakini ninaweza kufanya hivyo kwa kutumia vifaa vilivyopo kule makao makuu .”

    “ Ok Stanley go, do it”akasema Osmund na kurejea tena katika chumba cha John mwaulaya.Akamfuata palekitandani

    “John…”akaita na John akafumbua macho

    “ John,nasikitika upasuaji wako hautaweza kufanyika.Daktari tuliyemtegemea hatutaweza kumpata tena.kwa hivi sasa ninawasiliana na makao yetu makuu ili kuona uwezekano wa kukuhamisha na kukupeleka nje ya nchi kwa matibabu ”akasema Osmund kwa masikitiko.John akamfanyia ishara kwamba akipandishe kitanda.Osmund akabonyeza kitufe ukutani na kitanda kikainuka upande wa juu,na kumuwezesha John kukaa

    “ Osmund,listen to me my boy.Tafadhali usiwasiliane na makao makuu.Muda wangu umefika and please dont do anything. Its my time to go on rest now”akasema John

    “ No John! Don’t give up.Tunafanya kila linalowezekana ili uweze kupona.Ninakwenda kuongea na makao yetu makuu ili tuone uwezekano wa kupata ndege na ukakimbizwa mara moja Marekani kwa matibabu”

    “ Osmund tafadhali usisumbuke kijana wangu.You have done enough.Stop wasting your time.”

    ‘ John ninakuomba usikate tamaa.Tutakushughulikia na utapona”

    John akamtazama Osmund na kumwambia

    “ Ossy tafadhali naomba uniache mwenyewe.I need to be alone now”akasema John.Osmund akamtazama halafu akatoka kwa kasi .John Mwaulaya akafumba macho na kuendelea kukumbuka

    Mambo yaliyotokea usiku ule .Picha ya mtoto mdogo akiwa amelala katika kiti cha nyuma ya gari ikamjia na kwa mbali akatabasamu

    “ She was so cute.I didn’t even know her name that night.” akasema kwa sauti ndogo



    27 April 1986

    Bado mvua kubwa iliendelea kunyesha.John alikuwa amembeba yule mtoto mdogo ambaye tayari alikuwa amelala.

    “ You’ll be safe little angel.You’ll be fine.I’ll do everything I can to make sure that you are safe” akawaza John

    “ Bosi tunaelekea wapi? Akauliza mmoja wa vijana wake.John hakujibu kitu akachukua simu yake na kuzitafuta namba fulani za simu akapiga.

    “ Hallow Martha.” Akasema John baada ya simu yake kupokelewa

    “Hallow John” ikasema sauti ya mwanadada aliyeonekana kujawa na usingizi.

    “ Samahni nimekuamsha usiku huu”akasema John

    “ Bila samahani John.Una tatizo gani?

    “ I need to see you”

    “ Now? Akauliza Martha

    “ yes.Now” akajibu

    “ Uko wapi mida hii?

    “ Niko barabarani katika hii njia inayoelekea Mkuse Lodge”

    “ Ok,naomba unisubiri pale Eusebio night club, nitafika pale muda si mrefu” akasema Martha na kukata simu.John akamuelekeza dereva aliyekuwa akiendesha gari lile mahala walikokuwa wakielekea.Walifika Eusebio Night club na kuegesha gari,bado mvua kubwa iliendelea kunyesha.Baada ya dakika kama kumi na tano hivi ikatokea gari moja ndogo .John akaitambua gari ile.Akachukua koti la mvua na kumfunika yule mtoto akashuka na kuwaamuru vijana wake waendelee na safari ,yeye akaenda hadi katika lile gari ,akafunguliwa mlango na kuingia

    “ John..whats going on? akauliza Martha .John hakujibu kitu akalitoa lile koti la mvua na kumstua Martha baada ya kukiona kitoto kidogo.

    ‘John !!..akasema Martha kwa mshangao

    “ What are you doing with this baby? Akauliza

    “ Usiulize maswali mengi sana Martha.Mtoto huyu anahitaji sehemu salama na ya siri.Nahitaji msaada wako katika hili” akasema John.Martha akamtazama yule mtoto mdogo akamshika usoni halafu akawasha gari

    “ Mama yangu mdogo rafiki yake anayemiliki kituo cha kulelea watoto yatima.Ngoja niwasiliane naye anipe namba zake za simu nimpigie.” Akasema Martha na kusimamisha gari pembeni ya barabara akachukua simu yake na kumpigia mama yake mdogo wakaongea kwa dakika kama tatu akampatia namba za huyo rafiki yake mwenye kituo cha kulelea yatima.Baada ya kuongea na mama yake mdogo,Martha akampigia simu yule mama mwenye kituo cha kulelea watoto yatima akamtaarifu kwamba anahitaji kuongea naye.Ilikuwa ngumu kidogo kwa mama yule kukubali ombi la Martha hadi alipomtajia jina kwamba ameelekezwa na mama yake mdogo ndipo alipokubali kwani ni rafiki yake mkubwa.Alimuelekeza mahala aliko na bila kupoteza wakati wakachoma mafuta kuelekea huko.

    Bi Bernadetha Usuwo mmiliki wa kituo kile cha kulelea watoto yatima akawapokea na kutaka kufahamu shida iliyowapeleka kwake usiku ule.John akamdanganya kwamba mtoto yule aliyekuwa amemshika amezaa na mwanamke mmoja ambaye amekuwa ni mlevi na anakesha katika kumbi za usiku akifanya biashara za kujiuza.Aliendelea kudanganya kwamba alipigiwa simu na majirani wa mwanamke huyo ambao walimtaka aokoe maisha ya mwanae kwa kwenda kumchukua na ndipo alipoamua kwenda kumchukua mwanae na kumleta pale ili aweze kupatiwa uangalizi makini.

    “ Ouh Jamani kwa nini wasichana wa siku hizi wamekuwa hivi? Unawezaje kumfanyia mambo kama hayo malaika kama huyu? Mtoto huyu bado mdogo tayari anaanza kuruka ruka katika starehe ! Mwanamke mwenye vitendo kama hivyo hafai kabisa kuachiwa mtoto amlee.Umefanya jambo la maana sana kumchukua mwanao.Hapa atalelewa na kupata malezi anayostahili” akasema Bi Bernadetha

    “ Ninashukuru sana mama kwa msaada wako huu mkubwa.Pamoja na hayo kuna jambo lingine ambalo ninataka unisaidie”akasema John

    “ Jambo gani hilo?

    “ Nataka mtoto huyu alelewe kwa siri.Sitaki watu wafahamu kwamba ni mwanangu na wala sitaki mtoto huyu anijue mimi kama baba yake na wala asifahamu kama ana mama.Nitakulipa fedha nyingi kama utanisaidia katika hilo.”

    “ kwa nini unataka iwe hivyo John?

    “ Ni kwa ajili ya usalama wa mtoto.Yeyote atakayekuuliza kuhusiana na mtoto huyu sema kwamba aliletwa kutokea huko Singida au sehemu nyingine yeyote mbali kabisa na Dar es salaam.Tafadhali mama nakuomba sana unisaidie katika hilo” akaomba John

    “ Hii ni ajabu sana.Kwa nini mtoto asifahamu kuhusu wazazi wake ni akina nani?

    “ Mama Bernadetha ni vigumu kukuelewesha kwa sasa lakini naomba unisaidie sana katika hilo.Mimi nitagharamia gharama zote za matunzo na malezi yake na atapata kila kitu kinachotakiwa isipokuwa tu hataniona.Nitakuwa karibu nawe ili kuhakikisha anakua katika malezi mazuri na ninakuahidi ataishi maisha ya raha mustarehe kuliko hata mtoto wa rais lakini kitu kimoja tu atakikosa ambacho ni wazazi.” akasema John..Bi Benrnadetha alijaribu kufikiri kuhusu suala lile lakini kiasi kikubwa cha pesa alichoahidiwa na John kikamfanya akubali kufanya vile anavyotaka John

    “ Jina lake nani huyu malkia? Akauliza Bi Bernadetha.John na Martha wakaangaliana.Hakuna aliyekuwa akilfahamu jina la yule mtoto.Mara John akajikuta akitamka

    “ Peniela.Her name is Peniela”akatamka John.



    ********



    “ Ahsante Mungu kwa kuturejesha nyumbani salama” akasema Dr Michael baada ya kuwasili nyumbani kwa Mathew.Gari lilisimama lakini hakuna aliyetaka kushuka.Wote walionekana kuwa katika hali ya kutoamini kama ni kweli wamerejea salama.Anitha ambaye naye alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa baada ya kupoteza mawasiliano na akina Mathew ilipoanza kusikika milio ya risasi mfululizo alikuwa amesimama katika kibaraza akiwa na Jaji Elibariki.Wote walishangazwa kuona sekunde zinasonga mbele na hakuna mtu yeyote aliyeshuka mle garini.Kwa wasi wasi mwingi wakalisogelea lile gari .Ilikuwa vigumu kujua nani alikuwamo ndani kutokana na vioo vyeusi vya gari lile.Jaji Elibariki akagonga katika kioo cha mbele upande wa dereva.Taratibu mlango ukafunguliwa akashuka Mathew akiwa ameloa damu.

    “ Ouh my God ! Mathew..”akasema Jaji Elibariki.Anitha alistuka sana akamfuata Mathew

    “ Pole sana Mathew. ?akauliza Anitha huku machozi yakimlenga.Mathew alitaka kuongea kitu lakini alihisimaumivu makali. Mlango mwingine ukafunguliwa akashuka Noah naye akiwa katika hali kama aliyokuwa nayo Mathew.Alikuwa amechafuka kwa damu.

    “Ouh Mungu wangu ! Noah..” akasema Anitha na kwenda kumkumbatia na kumsaidia kusimama vizuri kwani alionekana kushindwa kusimama.Jaji Elibariki akafika mara moja na kumtegemeza akampeleka ndani.Katika mlango wa kati kati akashuka Dr Michael akifuatiwa na mke wake.

    “ Dr Michael !! akasema Anitha na kumkumbatia kwa nguvu

    “ Ahsante Anitha.Ahsante sana kwa kila kitu.Umetuokoa ” akasema Dr Michael.Mke wa Dr Michael bado aliendelea kumwaga machozi.Mume wake akamkumbatia na kumtuliza akimuhakikishia kwamba anyamaze kulia kwani tayari alikuwa huru.

    Mathew alikuwa ameegemea gari lililokuwa na matundu mengi ya risasi.Anitha akamsogelea

    “ Pole sana Mathew.Nashindwa kuelezea wasi wasi niliokuwa nao baada ya kuanza kusikia milio ya risasi na ghafla mkapotea.Sijawahi kuogopa kama leo hii.” Akasema halafu akanyamaza kidogo na kuuliza.

    “ Where is A…….” kabla hajamaliza kusema alichotaka kukisema Mathew akamkatisha

    “ We lost him….”

    Anitha akainama.

    Dr Michael akamfuata Anitha na kumuomba ampeleke mke wake ndani halafu akamfuata Mathew

    “Mathew ,nina mambo mengi ambayo ninataka kuyasema kwako na timu yako lakini kwa sasa nataka niseme maneno mawili tu ahsante sana.Uliniahidi kunirejeshea mke wangu na umefanya hivyo.Mmepambana kufa na kupona ,mmetukinga kwa risasi mimi na mke wangu na mkajeruhiwa kwa risasi ambazo zilipaswa kutupata sisi na mmeturejesha salama.Ninyi ni mashujaa ambao nchi ya Tanzania imejaaliwa kuwapata.Nchi hii inapaswa kujivunia watu kama ninyi.Papo hapo nawapa pole sana kwa kumpoteza Dr Adolf.Naomba nikiri nimekuwa nikiyatazama matukio kama yale katika filamu na leo nimeshuhudia kwa macho yangu namna watu wanavyobadilishana risasi.Nimeogopa sana.Picha ile haitaweza kamwe kufutika kichwani kwangu.” Akasema Dr Michael huku michirizi ya machozi ikionekana mashavuni pake.

    “ Dr Michael ahsante nawe pia kwa ushirikiano wako.Sote tumepambana mpaka tukatoka salama.Katika mapigano kama yale mtu mmoja au timu nzima kufa ni kitu cha kawaida sana” akasema Mathew

    “ Mathew jeraha linatoa damu nyingi,tafadhali naomba tuingie ndani ili niweze kuwatibu majeraha haya”akasema Dr Michael halafu Jaji Elibariki akamshika mkono Mathew na kumsaidia kutembea kuelekea ndani.

    Ndani ya jumba hili la Mathew kulikuwa na chumba maalum cha matibabu.Aliifahamu vyema kazi yake kwamba imezungukwa na hatari muda wote hivyo akatenga chumba maalum kwa ajili ya matibabu pale anapokuwa ameumia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Mathew umejiandaa sana.Hapa una kila kitu kinachohitajika.Hii ni kama hospitali ndogo”akasema Dr Michael wakati akiviweka sawa vifaa kwa ajili ya kumtibu Mathew aliyepigwa risasi mkono wa kushoto.Mathew akalala kitandani na Dr Michael akaanza kumuhudumia akianzia na jeraha la risasi katika mkono wa kushoto.

    “ Una bahati sana Mathew.Risasi ile haikupiga mfupa.Imepita pembeni kidogo.Ingepiga mfupa ingekuwa ni hatari zaidi”akasemaDr Michael wakati akiendelea kulitibu jeraha la Mathew.Baada ya kumaliza kulitibu jeraha la Mathew akaendelea pia kumtibu Noah ambaye alikuwa amepigwa risasi ya paja.Wakati Dr Michael akiendelea kumtibu Noah,Mathew alikuwa sebuleni na Anitha na jaji Elibariki ambao walitaka kufahamu kila kitu kilichotokea katika kumkomboa mke wa Dr Michael.

    “ Sikuwa nimetegemea kama mapambano yale yangekuwa makubwa kiasi kile.” Akasema Mathew

    “ Maelekezo uliyokuwa ukitupatia yalitufikisha katika kanisa lililokuwa likiendelea kujengwa.Tuliwakuta watu wanne waliokuwa wakimlinda mke wa Dr Michael ambao tulipambana nao na kuwamaliza wote na tukafanikiwa kumuokoa mateka.Ghafla wakati tukijiandaa kuondoka,ziliwasili gari tatu na tukajikuta tumezingirwa.Hapo mapambano yakaibuka upya.Inavyoonekana kuna wenzao waliwapa taarifa kwamba tumevamia na ndiyo maana wakaja kwa kasi namna ile.Mapambano ya kujiokoa yalikuwa makali sana .Watu wale walikuja wakiwa wamejipanga vizuri sana wakiwa na silaha kali.“ akasema Mathew

    “ Nakumbuka mara ya mwisho ulinitaarifu kwamba tayari mateka mko naye na mnajiandaa kurudi lakini ghafla nikasikia milio ya risasi nadhani ni hapo ndipo wale jamaa walipowazingira.Mawasiliano yalikata ghafla na sikuweza kuwapata tena.”akasema Anitha

    “ Eneo lote lilikuwa giza kwa hiyo yalikuwa ni mapambano makali sana.Wale jamaa walikuwa na kifaa kilichokuwa kikifuatilia masafa tuliyokuwa tukitumia kwa hiyo ilikuwa rahisi kwao kuweza kufahamu mahala tulipokuwa tumejificha na hivyo kutuelekezea mashambulizi hivyo tukalazimika kuvitupa.” Akasema Mathew.

    “ Tulipambana sana na tukafanikiwa kupata upenyo wa kukimbia. Wakati tukiingia katika gari kuna mtu mmoja alivurumisha risasi ambazo zilitakiwa kumpata Dr Michael lakini anali Adolf akalazimika kumkinga na risasi zile zikampata na kumuua pale pale.Tulishindwa namna ya kuondoka naye kwa namna risasi zilivyokuwa zikivurumishwa kwetu.” Akasema Mathew

    “ Watu hawa ni akina nani?akauliza jaji Elibariki kwa uoga

    “ Team SC41 “ akasema Mathew

    “ Team SC41? Elibariki akauliza kwa mshangao

    “ Ni nani haoTeam SC41? akauliza Elibariki

    “ Ni habari ndefu sana nitakueleza baadae kwa sasa bado kuna kazi ya muhimu sana ambayo tunatakiwa kuikamilisha.” Akasema Mathew na kuinuka akamfuata Dr Michael ambaye alikuwa akimalizia kumtibu Noah Jeraha la risasi katika paja lake.

    “ Dr Michael tayari nimeitimiza ahadi yako na sasa ni zamu yako kumalizia ile kazi yetu” akasema Mathew.Dr Michael akamgeukia na kumtazama akatabasamu

    “ Mathew nilidhani utahitaji muda zaidi wa kupumzika baada ya tuko lile la usiku wa leo na isitoshe jeraha lako lilikuwa linavuja damu nyingi .”akasema Dr Michael

    “ Dr Michael,sisi tuko vitani na tunapokuwa vitani tunapambana hadi dakika ya mwisho bila kuchoka,we fight like devils.We never give up.Majeraha ni kitu cha kawaida katika mapambano kama haya kwa hiyo usitishike na jeraha kama hili.Kazi ile lazima imalizike usiku wa leo.”akasema Mathew.Dr Michael akamfunga Noah bandeji halafu akamchoma sindano halafu akamuomba Mathew wasaidiane kumpeleka chumbani kupumzika.Noah aliachwa chumbani akipumzika ,Mathew na Dr Michael wakaelekea sebuleni.

    “ Dr Michael kutokana na hali halisi ilivyo hivi sasa wale jamaa wataendelea kukufuatilia kwa karibu sana.Sikushauri uchunguzi wa zile sampuli ukaufanyie pale hospitalini kwako.Hakuna sehemu ambako tunaweza kwenda usiku huu ukafanya uchunguzi huo? Tunahitaji majibu kabla ya jua kuchomoza “ Akasema Mathew.Dr Michael akafikiri kidogo na kusema

    “Kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Dr Robert yeye anamiliki hospitali yake binafsi.Ana maabara kubwa pale na ninaweza kwenda na kuzifanyia uchunguzi sampuli zile tulizonazo”

    “ Vizuri sana Dr Michael.Anitha msaidie Dr Michael awasiliane na rafiki yake kwani simu yake haitakiwi kutumika.Team SC 41 lazima watakuwa wakifuatilia ili wafahamu mahala alipo.” akasemaMathew na kuelekea chumbani kwake.Akaegemea kabati lake kubwa na kuyafuta machozi.Picha ya Kanali adolf akimiminiwa risasi ilimjia akilini na kumuumiza sana.

    “I’m so sorry Adolf.Umekufa kishujaa “ akasema Mathew halafu akachukua baadhi ya vifaa vyake na kuwafuata akina Anitha

    “ Mathew tayari nimekwisha wasiliana na Dr Robert na ameniambia hakuna tatizo naweza kwenda kuitumia maabara ya hospitali yake.” Akasema Dr Michael.

    “ Ok Good.Elibariki wewe utabaki hapa pamoja na Noah na familia ya Dr Michael.Sisi tunaenda kuzifanyia uchunguzi sampuli tulizochukua ili kubaini chanzo cha kifo cha Dr Flora.Tutakaporejea tutakuwa tayari na jibu lenye uhakika nini kilimuua” akasema Mathew na kumfuata Noah.

    “Noah endelea kupumzika ,tunakwenda kutafuta majibu ya zile sampuli.Elibariki na familia ya Dr Michael watabaki hapa.Protect them.Anitha tunaondoka naye yeye ndiye atakayetuendesha kwani mkono wangu bado una maumivu makali sana.” akasema Mathew kisha akaongozana na Dr Michael,na Anitha wakaingia garini wakaondoka

    “ Nilifahamu toka mapema team SC41 ni watu hatari sana.Kwa mara nyingine tena leo hii nimenusurika toka katika mikono yao.Nitapambana nao.safari hii sintaogopa wala kukata tamaa lazima nihakikishe nimepambana nao na kulipa kisasi cha familia yangu na wenzangu walioteketezwa kikatili.Tukio la leo ni salamu kwao kwamba watu wanaopambana nao kwa sasa si wa kawaida.” Akawaza Mathew wakiwa garini

    “ kwa sasa tunahamia kwa Peniela.Kwa sasa inabidi tuanze kumchunguza Peniela.Katika hili itabidi kuwatumia akina Elibariki.Tunatakiwa kuzifuatilia nyendo zake.Siku ile wale watu wa Team SC41 walitokea kwake ndipo wakaelekea hospitali kwa John Mwaulaya.Ninashawishika kuamini kwamba yawezekana kabisa Peniela akawa na mahusiano naTeam SC41.Endapo tutagundua kwamba Penny ana mahusiano na Team SC41 basi nitawaunganisha katika kifo cha Edson.Baada ya hapo tutaanza kuitafuta sababu ya kumuua.Kama ni kweli TeamSC41 walihusika katika mauaji ya Edson it’ll be for something big.very big”akawaza Mathew





    Waliwasili katika hospitali inayomilikiwa na Dr Robert.Kwa kutumia simu ya Mathew Dr Michael akamfahamisha Dr Robert kwamba tayari wamekwishafika ,akawafuata katika maegesho halafu akawachukua na kuwaongoza hadi ndani ya hospitali.Mathew na Anitha wakaombwa wakae katika viti vilivyokuwa katika sehemu ya kupumzikia wakati Dr Michael na mwenzake wakiendelea kuzifanyia uchunguzi sampuli toka kwa mwili wa Dr Flora .Kabla hawajaanza kazi Dr Robert akamuuliza Dr Michael

    “ Michael,kuna tatizo gani? Kwa nini jambo hili lifanyike usiku na haliwezi kusubiri hadi kesho? Akauliza Dr Robert

    “ Dr Robert kuna sampuli ninazotakiwa kuzichunguza usiku huu na siwezi kusubiri hadi kesho.” Akasema Dr Michael.Robert akamtazama kwa sekunde kadhaa kisha akauliza

    “ Niambie Michael, nini kimetokea? Macho yako yanaonyesha kabisa kwamba kuna tatizo Fulani.Na hawa watu ulioongozana nao ni akina nani?

    “ Robert wewe ni rafiki yangu mkubwa na siwezi kukuficha kitu lakini naomba nitakachokueleza kiwe ni kati yetu wawili.”

    “ Niambie Michael kitu gani kimetokea?

    “ Mke wangu alitekwa nyara na watu wasiojulikana ambao walitaka kunilazimisha nimfanyie upasuaji mgonjwa wao waliyemtorosha toka hospitali.Vijana hao nilioongozana nao ndio waliopambana hadi wakafanikiwa kumuokoa mke wangu toka katika mikono ya watekaji.Mwenzao mmoja alifariki dunia katika mapambano hayo kwa hiyo unapowaona hapo wako katika majonzi makubwa lakini bado hawakati tamaa wanaendelea na mapambano.Kuhusu kilichonileta hapa usiku huu ni kwamba mke wa rais alifariki ghafla na mpaka sasa sababu ya kifo chake haijajulikana na imetolewa amri ya kutochunguza chanzo cha kifo chake.Vijana hawa wanataka kuufahamu ukweli wa kilekilichomuua mke wa rais .Tulifika katika hospitali ulikohifadhiwa mwili wa mke wa rais kwa dhumuni la kuufanyia uchunguzi kwa siri lakini wakati tukiendelea na kazi hiyo wakapokea taarifa kwamba tumegundulika tunaufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora.Ilitulazimu kuacha kila tulichokuwa tunakifanya na kukimbia.Kabla ya kutoka nilichukua sampuli kadhaa kwa ajili ya kuendelea kuzifanyia uchunguzi.Kwa hiyo niko hapa na wale vijana ili kuufahamu ukweli wa nini kilimuua mke wa rais” akasema Dr Michael.

    “ Michael umejiingiza katika matatizo makubwa na vyombo vya dola.Kwa nini ulikubali kufanya kitu cha hatari kama hiki? Unafikiri ikijulikana kwamba ulishiriki katika jambo kama hili utakuwa salama? Akauliza Dr Robert

    “ Robert nililazimika kukubali kufanya hivi kwa sababu waliahidi kunisaidia kumpata mke wangu na wamefanya hivyo kwa hiyo na mimi nalazimika kutimiza ahadi yangu.Lazima niwasaidie kufahamu chanzo cha kifo cha mke wa rais.Kuhusu usalama wangu usijali kuhusu hilo tayari nina mpango mzuri baada ya kumaliza kazi hii” akasema Michael.Robert akamtazama kwa muda kidogo na kusema

    “ Sawa Michael mimi nitakusaidia kufanya uchunguzi huo lakini tafadhali kuwa makini sana,na sitaki ijulikane kwamba hospitali yangu imehusika kwa namna yoyote ile na jambo hili.Je unaweza ukanihakikishia hilo?akauliza Robert

    “Ndiyo Robert.Nakuhakikishia kuhusu hilo”akasema Michael.Robert akavaa koti tayari kwa kuanza kazi

    “ Katika uchunguzi mliokwisha ufanya mligundua chochote?

    “ Tuligundua kwamba mishipa ya damu ilipasuka ishara kwamba kulikuwa na mgandamizo mkubwa wa damu,tunachotaka kufahamu ni kitu gani kilisababisha hali hiyo kutokea?.Hapa nina sampuli kadhaa ambazo tunatakiwa tuzifanyie uchunguzi na tutapata jibu.”akasema Dr Michael na mara moja shughuli ya uchunguzi ikaanza.

    “ Mathew whats next? Akauliza Anitha wakiwa katika sehemu ya kupumzikia.

    “ Baada ya kupata majibu ya nini kilimuua Dr Flora ,tutaendelea na kazi yetu ya msingi yaani kuchunguza kuhusu kifo cha Edson.Kazi hii ya kuchunguza kiini cha kifo cha Dr Flora imeingia tu kwa dharura na haikuwa katika mpangilio wetu wa kazi.Kuanzia kesho tutaelekeza nguvu katika kuchunguza kama Team SC41 walihusika katika kifo cha Edson.Tutaupata ukweli wa jambo hilo kwa kumchuguza Peniela.Tukifahamu mahusano yake na Team SC41 basi itatuwia rahisi sisi kufahamu kama walihusika katika mauaji ya Edson na kwa nini.” Akasema Mathew

    “ Kuna zile kamera mbili ulizozitega nyumbani kwa penny zinaweza kutusaidia sana kufahamu nyendo zake”akasema Anitha

    “Kweli Anitha.Kamera zile zitatusaidia sana kufahamu kila kinachoendelea nyumbani kwa Penny lakini hata hivyo tutawatumia rafiki zake wa karibu,Jason na Elibariki katika kupata taarifa tunazozihitaji”akasema Mathew



    *******



    Miili ya vijana sita waliouawa katika mapambano na akina Mathew ikawasili katika makazi ya John Mwaulaya ambako vijana wote walikuwa wamekusanyika.Gari lile ilimokuwamo ile miili ilikuwa imechafuka kwa damu.Osmund alitaarifiwa kuwasili kwa miili ile akashuka kwa kasi na kwenda kushuhudia.Alipandwa na hasira zilizochangayika na mstuko baada ya kuzishuhudia maiti zile namna zilivyochakazwa kwa risasi.

    “ Whoever did this must be in our hands by sunset tomorrow “akawaza .

    “ Lakini ni nani huyu ambaye anaweza kuwa amefanya kitu kama hiki? Nani huyu ambaye anathubutu kucheza na team SC41 na kuua vijana wetu sita? Hii haijawahi kutokea kuanzia kuanzishwa kwake.Lazima tuwatafute watu hawa na tuwafahamu ni akina nani.” Akaendelea kuwaza Osmund akiwa amesimama kandoni mwa gari lililobeba miili.Mara akastuliwa na sauti ya Victor

    “ Bosi, kile kidole ulichoniambia nikichukue hiki hapa.”akasema Victor na kumkabidhi kidole gumba cha mkono wa kulia ambacho kilikuwa ndani ya kifuko kidogo cha nailoni

    “ Poleni sana Victor” akasema Osmund

    “ Ahsante sana bosi.Yalikuwa ni mapambano makali .Ilikuwa ni kama vita” akasemaVictor

    “ Watu hawa ni akina nani?

    “ Ni vigumu kusema ni akina nani lakini ninaweza kusema kwamba watu wale ni wapiganaji hasa wenye ujuzi na uzoefu wa hali ya juu.Wanatumia vifaa vya hali ya juu vya mawasiliano.They are professionals.Hata yule mwenzao tuliyemuua alikufa wakata kiwakinga wenzake wasishambuliwe na risasi ” akasema Victor

    “ Tukimfahamu huyu mwenzao ni nani basi tutaweza kuwafahamu watu hao ni akina nani”akasema Osmund

    “ Kitu kingine,nimeahirisha mazishi ya vijana wetu niliyokuwa nimepanga tuyafanye usiku wa leo.Vijana wetu wamekufa kishujaa na tutawazika kwa heshima zote.Kuanzia kesho tutaanza kuwazika mmoja mmoja katika makaburi tofauti tofauti.Kesho asubuhi shughulikia suala hilo.Kila kitu kuhusu jambo hilo ninakuachia wewe,hakikisha mpaka kesho saa tatu asubuhi kila kitu kuhusiana na maziko ya vijana wetu kiwe kimekamilika na kuanzia saa tano tuanze kuwazika mmoja mmoja”akasema Osmund

    “ Sawa bosi ninalishughulikia suala hilo.” Akasema Victor na mara simu ya Osmund ikaita akaipokea na kuiweka sikioni

    “ Hallow Joseph” akasema

    “ Bosi ,Edwin Mackson yupo katika laini anakusubiri”akasema Joseph

    “ Ok Joseph ninakuja sasa hivi”akajibu Osmund na kukata simu

    “ Victor tutaendelea na maongezi baadae lakini kwa sasa hakikisha kila aliyeumia anapatiwa matibabu na wanapewa mapumziko katika zahanati yetu kule makao makuu. Hakikisha kila kitu kimekwenda sawa,nina mambo mengi ya kufanya siku ya leo”akasema Osmund na kuondoka kwa kasi kuelekea juu ghorofani hadi katika chumba cha mikutano ya ana kwa ana kilichokuwa na runinga nne kubwa ukutani..Kwa kutumia remote control akawasha runinga namba mbili.

    “ Hallow Edwin”akasema Osmund

    “ Osmund .Habari za Tanzania?

    “habari za huku si njema sana”

    “ Kuna tatizo gani?

    ‘ tatizo la kwanza ni kuhusiana na ugonjwa wa John mwaulaya.Anaumwasana.Tulitegemea kumfanyia upasuaji lakini daktari tuliyemtegemea kufanya upasuaji huo hataweza tena kupatikana.Hali yake inazidi kuzorota kila dakika na kama asipofanyiwa upasuaji wa haraka tunaweza tukampoteza.” Akasema Osmund

    “ Osmund,tulipokukabidhi nafasi kubwa kama hii ya kuongoza kikosi chenye nguvu kama hiki tulitegemea kwamba una uwezo wa kushughulikia masuala madogo madogo kama haya.Suala kama hili si suala la kutaka maelekezo toka makao makuu.Unatakiwa kuomba msaada wa makao makuu kama kuna jambo kubwa na zito lakini katika masuala kama haya ya ugonjwa tumewapa uhuru huko huko wa kufanya kila linalowezekana kutafuta matibabu..Umenielewa Osmund ? akasema Edwin.

    “ Nimekuelewa Edwin lakini John Mwaulaya anahitaji kutibiwa.Huyu ni mtu mkubwa katika Team SC41.Suala la ugonjwa wake si la kulichukulia kirahisi rahisi namna hiyo” akasema Osmund huku akionyesha wazi kukakasirishwa na matamshi ya Edwin

    “ Ni kweli John ni mtu mwenye wadhifa mkubwa katika Team SC41 lakini tunaweza tu kutoa msaada endapo utatuhakikishia kwamba mmeshindwa kabisa kumtibu.”

    “ Edwin mpaka kufikia hatua hii ya kukupigia simu na kukuomba msaada ni wazi tumeshindwa”akasema Osmund

    “ Sawa Osmund ,tutamtuma Dr Marcus burke atafika huko ndani ya siku mbili zijazo kuangalia ukubwa wa tatizo la John halafu atashauri nini cha kufanya”

    “ Ahsante sana Edwin kwa kulipa uzito suala hili.Kuna suala lingine vile vile. “

    “ suala lipi tena?

    “ Kuna tatizo limetokea usiku wa leo”

    “tatizo gani?

    “ Kuna vijana wetu sita wameuawa katika shambulizi .”

    “Mbona sikuelewi Osmund,wameuawa vipi? Nani kawaua? Akauliza Edwin

    “ Bado hatufahamu ni nani lakini tumegundua kuna watu ambao wamekuwa wakitufuatilia.”

    “ Umechukua hatua gani mpaka hivi sasa za kuwafahamu watu hao ni akina nani na wanataka nini? Akauliza Edwin

    “Bado hatujawafahamu watu hao ni akina nani na wanataka nini toka kwetu lakini tutalishughulikia suala hilo kuanzia kesho.kwa hivi sasa ninashughulikia kwanza kuihifadhi miili ya vijana waliopoteza maisha na baada ya kukamilisha shughuli za mazishi yao kesho tutaanza rasmi kuwasaka na kuwafahamu watu hao ni nani na wanataka nini.”

    “ Osmund lipe uzito mkubwa suala hili kwani ni suala zito sana.lazima tuwafahmu watu hawa ni akina nani na wametufahamu vipi na nini wanatafuta toka kwetu.Team SC41 ni kikosi kinachofanya kazi zake kwa siri kubwa kiasi kwamba hata ndani ya serikali ya marekani ni watu wachache wanaofahamu uwepo wake kwa hiyo kwa watu hao kuanza kutufuatilia ina maana kwamba tayari wanatufahamu sisi ni akina nani.Kujulikana kwa Team SC41 na kazi zetu kutahatarisha kwa kiasi kikubwa maslahi ya marekani katika afrika mashariki .Pamoja na kumtuma Dr Marcus Burke kuja kuangalia afya ya John,ataambatana vilevilena timu ya watu watatu ambao watakuja kusaidiana nanyi katika kuwabaini watu hawa ni akina nani.Nataka ndani ya kipindi kifupi tuwe tumewafahamu na kuchukua hatua zipaswazo.Nitaongea nawe tena kesho saa saba mchana kwa saa za Afrika mashariki ili kufahamu namna mnavyoendelea na kama mmekwisha wafahamu watu hao” akasema Edwin na kutoka katika laini..

    “ Afadhali aje daktari toka Marekani kuja kuangalia afya ya John.Lazima apatiwe matibabu anayostahili.Hakuna sababnu ya kuendelea kusumbuka wakati kuna uwezekano mkubwa wa kumpeleka Marekani au nchi nyingine yoyote na akatibiwa ” Akawaza Osmund wakati akipanda ngazi kuelekea chumbani kwa John.Moyo wake ulifarijika sana baada ya kuhakikishiwa ujio wa Dr Burke.Aliufungua mlango wa chumba cha John na kumuomba daktari aliyekuwa akimuhudumia atoke nje .

    “ Kuna nini Ossy?akauliza John kwa sauti ya chini

    “ John nimeongea na makao makuu,wameahidi kumtuma daktari haraka iwezekanavyo.Ndani ya siku mbili hizi Dr Marcus Burke atakuwa amewasili kuja kuangalia afya yako na kutoa ushauri wa nii kifanyike” akasema Osmund.Pamoja na kuwa dhaifu lakini aliposikia jina la Marcus Burke John akastuka sana.Akamfanyia ishara Osmund asogee karibu

    “ Umesema Dr Marcus Burke?

    “ Ndiyo John.Anakuja Dr marcus Burke kuja kuangalia afya yako”

    “ No Ossy.Dont let him.” Akasema John Mwaulaya

    Osmund akamtazama kwa mshangao

    “ Do you know him? Akauliza

    “ yes I know him” akajibu John

    “ John unaumwa na Dr Marcus anakuja kuangalia afya yako na kutoa ushauri nini kifanyike.Unatakiwa ufanyiwe upasuaji wa haraka ili kuokoa maisha yako“ akasema Osmund.John akaushika mkono wa Osmund na kusema

    “ Osmund listen to me my boy.Ninamfahamu Dr Burke.He’s coming for one reason only”

    “ One reason? Osmund akashangaa.

    “ Yes.He’s coming to kill me.Please don’t let him.I need to die a natural death” akasema John na kuzidi kumshangaza Osmund

    “ John nashindwa kukuelewa una maanisha nini.Dr Marcus anakuja kuangalia afya yako na si kukuua” akasema Osmund

    “ Osmund please listen to what I’m telling you.Nilikataa kwenda kutibiwa marekani kwa sababu nilifahamu lazima wataniua.”

    “ kwa nini wakuue John?

    “ Kuna siri nzito ambayo hauifahamu kwa hiyo tafadhali usimruhusu Dr Burke kuja kuniangalia.Ninajua sina maisha marefu sana lakini ninataka nife kifo cha kawaida.”

    “ John ni siri gani hiyo ambayo ingepelekea uuawe endapo ungeenda kutibiwa marekani?

    “ Siwezi kukwambia Ossy.Ni siri ambayo nitakwenda nayo kaburini.” Akasema John.

    “ John unataka nikusaidie na wakati huo huo unanificha siri uliyonayo.Tafadhali niambie na nitakusaidia”

    “ Hapana Osmund siwezi kukwambia.Lifanyie kazi hilo nililokueleza .You can go now I need to be alone.”akasema John.Osmund akamtazama na kuondoka .

    “Nitakufa hivi karibuni.Sifahamu kama ninaweza kusamehewa kwa mambo niliyoyatenda hapa duniani.Nimefanya mambo mengi mabaya lakini kuna jambo moja tu linalonipa faraja hata kama nikifa muda huu nitakufa huku nikitabasamu.I didn’t kill an Innocent child.I didn’t kill Peniela” akawaza John na kumbu kumbu zikamrudisha May 30 1990



    30 May 1990



    Gari la kifahari linafunga breki katika maegesho ya shule ya kimataifa ya watoto wadogo.John Mwaulaya anashuka ndani ya gari lile huku akivuta sigara .Kwa mbali akasikia kelele za watoto wakicheza.Akachukua simu na kumpigia mtu aliyekuwa akimtafuta.Baada ya dakika tano akatokea Bi Bernadetha mlezi wa kituo cha yatima anakoishi Peniela

    “hallo mama Bernadetha.Habari za siku?

    “ habari nzuri sana John.Pole na safari”

    “ahsante sana mama nimekwisha poa.NashukuruMungu nimerejea salama.Peniela anaendeleaje?

    “ Peniela anaendelea vizuri sana na zawadi zote ambazo umekuwa ukimtumia kutoka Marekani amezipata na anafurahi sana.John unamjali sana mwanao .Kwa nini lakini hutaki akuone wala akujue?

    “ Mama Bernadetha,kama nilivyokwambia siku ninamkabidhi kwako ,sihitaji Peniela anifahamu kwa sasa.Hii ni kwa ajili ya usalama wake .Yuko wapi mida hii?nahitaji kumuona”akasema John.Bi Bernadetha akamchukua John na kumpeleka katika ofisi ya mkuu wa shule ile na kumtambulisha kama mfadhili wa Peniela.Waalimu walifurahi sana kumfahamu John na kumpongeza kwa namna alivyojitolea kumsomesha peniela katika shule ile ya gharama kubwa.Wote walimsifu Peniela kwamba ni mtoto mwenye bidii sana ya kujifunza.John akaomba akaonyeshwe mahala alipo Penny,akaongozana na mwali mmoja pamoja na bi Benrnadetha hadi katika uwanja wa michezo,kulikokuwa na michezo mbali mbali.Peniela alikuwa amejumuika na watoto wenzake wakicheza na kuruka kwa furaha.John alihisi furaha ya ajabu baada ya kumuona Peniela.

    “She’so cute.Ni mtoto mzuri na mrembo.Nitahakikisha kwa kila nitakavyoweza anakuwa na maisha yenye kujaa furaha kubwa” akawaza John huku uso wake ukiwa umepambwa na tabasamu .Alitamani akae pale kwa siku nzima ili aendelee kumuangalia peniela .

    “ Natamani kama ningekuwa na mke ningemchukua Peniela niishi naye.Kwa mara ya kwanza natamani na mimi kuitwa baba lakini kazi hii hainiruhusu kuwa na familia.Anyway nitaendelea kumtunza Peniela kwa siri .”akawaza John halafu akaondoka na kurejea garini.Akafungua albamu lililojaa picha za Peniela ambazo alikuwa akitumiwa na Bi Bernadetha wakati akiwa kikazi nchini marekani

    “ You are such a cute baby.I’ll take a good care of you Penny.You’ll never see me but I’ll always take very good care of you.”akasema John.



    ********





    “ Mathew ..mathew..” akaita Anitha na kumstua Mathew toka katika usingizi uliokuwa umempitia. Aliitazama saa yake ilipata saa kumi na dakika kumi na tatu.Mbele yake walikuwa wamesimama Anitha,Dr Michael na Dr Robert.

    “ Pole sana Mathew” akasema Dr Michael huku akitabasamu

    “ Sorry nilipitiwa na usingizi kidogo “

    “ Usijali Mathew,ni kutokana na zile dawa nilizokupa.Zina nguvu sana “akasema Dr Michael

    “Nini kinaendelea Dr Michael? Akauliza Mathew

    “ Tumemaliza kuzifanyia uchunguzi zile sampuli ingawa imetuchukua muda mrefu”

    “Good.tayari mna majibu?

    “Ndiyo Mathew,tayari tuna kila kitu” akajibu Dr Michael na kuketi kitini.

    “ Mathew kilichosababisha kifo cha mke wa rais ni sumu iitwayo Spinolin .Tumekuta chembe chembe za sumu hii katika sampuli ya ini tuliyochukua.Sumu hii inapatikana katika dawa iitwayo Encozynes ambayo hutumiwa na watu wenye shinikizo la damu.Matumizi ya dawa hii mgonjwa hutumia mara moja kila baada ya mwezi mmoja tena kwa kiwango kidogo kwa sababu endapo ikitumiwa kwa kiwango kikubwa ina madhara makubwa na husababisha kifo kwa mgonjwa.Inaonekana mke wa rais alichomwa kiwango kikubwa cha dawa hii na hivyo kusababisha kifo chake.Nina mashaka na mtu aliyemchoma dawa hii kama alikuwa akifahamu madhara yake au alidhamiria kufanya alichokifanya.Inatakiwa kuchunguza ni nani aliyemchoma sindano hiyo kama ni daktari wake au ni mtu mwingine ili kufahamu dhamira yake ilikuwa nini .” akasema Dr Michael na kumkabidhi Mathew bahasha iliyokuwa na majibu ya vipimo walivyovifanya

    “ Ahsante sana Dr Michael.Nashukuru sana kwa msaada wako.”akasema Mathew akasimama.Akapeana mkono na Dr Robert wakaagana wakaingia garini na kuondoka

    “ Dr Flora alichomwa sindano iliyokuwa na kiwango kikubwa cha dawa tofauti na inavyotakiwa.Hapa inaonyesha wazi kwamba aliyemchoma alidhamiria kumuua.Naikataa hoja ya kwamba mchomaji hakuwa na ufahamu kuhusu madhara ya dawa ile.Ni nani basi aliyemchoma sindano ile na kwa nini? Hilo ndilo swali ambalo tunatakiwa kujiuliza kwa sasa.Tukimfahamu ni nani aliyemchoma Dr Flora sindano ile tutakitegua kitendawili hiki.” Akawaza Mathew wakiwa garini wakirejea nyumbani

    “ Mathew ! akaita Dr Michael

    “ Nimeikamilisha kazi yangu.Nadhani hatudaiani tena” akasema .Mathew akatabasamu kidogo na kujibu

    “ Ahsante sana Dr Michael kwa msaada huu mkubwa.Pole sana kwa misukosuko mikubwa iliyokupata katika siku ya leo.Ninatumai ni mara yako ya kwanza kupitia misukosuko mikubwa kama hii.Ninashukuru kwamba baada ya misuko suko kumalizika nyote mu salama.Wewe na familia yako yote mko salama salimini.Hatuna deni tena mimi na wewe lakini ninachoweza kukushauri ni kwamba usifikirie kwenda nyumbani kwako wala kazini katika kipindi cha wiki moja au mbili mpaka hapo tutakapohakikisha kumekuwa salama.Wale jamaa wataendelea kukutafuta bila kuchoka hadi wahakikishe wamekutia mikononi.Kama hutajali naomba wewe na familia yako muendelee kukaa pale kwangu hadi hapo tutakapohakikisha kwamba hali ya usalama imeboreka.” Akasema Mathew.Dr Michael akatabasamu na kusema

    “ Mathew nakiri kwamba kwa mara ya kwanza uliponifuata pale ofisini kwangu na kunielekezea bastora nilikuchukia mno.Nilikuona ni mtu mbaya sana na kwa hasira nilizokuwa nazo nilitamani hata nitafute kitu nikupige nacho nikuue kabisa.Lakini baada ya kukaa nawe kwa saa kadhaa nikagundua kwamba uko tofauti na nilivyokuwa nakufikiria.Wewe ni mmoja wa mashujaa wa taifa hili.Wewe ni kijana mwenye roho nzuri na huruma.Sina shaka yoyote kuhusu kukaa pale kwako ambako ni sehemu salama sana kwangu na kwa familia yangu kwa sasa lakini baada ya matukio ya leo tayari nimekwisha fanya maamuzi.Ninaondoka hapa nchini.”

    “Unakwenda wapi?

    “Mwezihuu nilikuwa namalizia mkataba wangu wa miaka mitano na hospitali ile ninayofanya kazi .Tayari nimekwisha pata kazi nyingine nchini Philipines katika jiji la manila.Ninataka kuelekea huko.Sitaki kuendelea kupoteza muda tena hapa.Kwa maana hiyo basi kuna jambo moja ambalo nitataka unisaidie.”

    “Hizo ni habarinzuri.Umefanya maamuzi mazuri na familia yako itaendela kuwa salama.Ni kitu gani ambacho unataka nikusaidie?akauliza Mathew

    “ Ninahitaji unisaidie kupata ndege .Kwa sasa mimi na familia yangu hatuwezi kutoka na kuanza kuzunguka kutafuta ndege.Naomba unisaidie kuifanya kazi hiyo.Nataka ndege ya kunitoa hapa na kunifikisha afrika ya kusini na kutokea pale nitakuwa salama. “ akasema Dr Michael

    “ usijali kuhusu hilo Dr Michael ,tukifika nyumbani Anitha ataingia mtandaoni na kuangalia kama anaweza akapata ndege ya kukufikisha Afrika ya kusini na pale unaweza ukawa salama kutafuta ndege ya kuelekea kokote unakotaka”akasema Mathew

    “Nitashukuru sana Mathew.”akasema Dr Michael na safari ikaendelea

    Saa kumi na moja na dakika ishirini na saba wakawasili nyumbani kwa Mathew.Ni Noah peke yake ambaye hakuwa amelala licha ya kuwa na maumivu makali ya mguu.

    “ Poleni sana.”akasema Noah

    “Ahsante Noah.Elibariki yuko wapi? Akauliza Mathew,Noah akamfahamisha kwamba yuko chumbani amelala,akamfuata akamuamsha

    “ Mathew !!..akasema jaji Elibariki kwa uchovu uliochanganyika na maumivu ya kidonda alichokuwa nacho kichwani mahala alijkopigwa chupa na Jason.Akaitazama saa yake ilikuwa ni saa kumi na mbili kasoro za asubuhi.

    “Its morning.!! Akasema

    “ yah ! Kumekucha.”

    ‘ Kuna taarifa gani ?akauliza Elibariki

    “ Ile kazi yako imekamilika.”

    “ Thank you Lord ! akasema

    “Ripoti ya uchunguzi hii hapa.kwa ufupi tu ni kwamba Dr Flora alichomwa dawa iitwayo Encozynes yenye kiambata kijulikanacho kama Spinolin.Dawa hii hutumiwa na watu wenye matatizo ya shinikizo la damu lakini ni kwa kiwango kidogo sana.Mgonjwa akipewa dawa hii kupita kiwango chake basi husababisha kifo ndani ya muda mfupi kutegemea na kiwango alichopewa.Kwa hiyo tunatakiwa tuchunguze ni nani aliyemchoma dawa hiyo na kwa nini alimchoma.Tukimpata mtu aliyemchoma tutakitegua kitendawili hiki”akasema mathew

    “ Kwa maana hiyo kuna kila dalili zinazoonyesha kwamba Dr Flora aliuawa kwa kuchomwa kwa makusudi sindano ile .Na hii ni sababu kumekuwa na jitihada kubwa za kutaka kuzuia uchunguzi wa kifo cha Dr Flora usifanyike kwa sababu waliogopa itabainika kwamba aliuawa.” Akasema Jaji Elibariki





    “ Kwa namna jambo hili lilivyotokea na hali halisi ilivyo kuna kila sababu za kunifanya niamini kwamba Dr Flora alichomwa dawa ile kwa makusudi kabisa na aliyemchoma alikuwa na lengo la kumuua.Hebu jiulize ni kwa nini uchunguzi wa kifo cha Dr Flora ulizuiwa na kulikuwa na kila jitihada za kuhakikisha kwamba hakuna uchunguzi unaofanyika? Ni wazi walifahamu kwamba ukifanyika uchunguzi itagundulika kwamba Dr Flora aliuawa.”akasema Mathew

    “ kwa hiyo nini kinafuata baada ya hapa? Nimeanza kuogopa Mathew ” akasema jaji Elibariki

    “ Kwa upande wangu ,kazi yangu nimeikamilisha.Nilihitajika kupata ukweli wa kilichomuua Dr Flora na tayari nimekwisha upata.Kinachotakiwa hapa ni kuifikisha taarifa hii sehemu husika kwa mheshimiwa rais ili aweze kutumia vyombo vyake vya uchunguzi kulifanyia uchunguzi jambo hili.Nguvu yangu mimi inaishia hapa na kwa kuwa jambo hili limefanyika ndani ya ikulu sina nguvu ya kuweza kuingia mle na kufanya uchunguzi.Mheshimiwa rais ana uwezo mkubwa wa kulichunguza suala hili na kujua ni nani aliyefanya kitendo hiki na kuchukua hatua zipasazo” akasema Mathew

    “ Mathew nakushukuru sana kwa msaada wako huu mkubwa.Bila wewe tusingeweza kuupata ukweli huu.Nitafanya utaratibu wa kumkabidhi mheshimiwa rais ripoti hii mapema asubuhi ya leo ili aweze kuchukua hatua zipasazo “ akasema jaji Elibariki

    “ Jitahidi Elibariki ripoti hii ifike katika mikono husika ili iweze kufanyiwa kazi “

    “ Ahsante sana Mathew” akasema jaji Elibariki .

    “ Ok Elibariki ,I need to take some rest now.Utanifahamisha baadae utakapokuwa umemkabidhi taarifa hii mheshimiwa rais”akasema Mathew na kutoka mle chumbani akaelekea katika chumba alichokuwamo Anitha .http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Anitha ninakwenda kupumzika kidogo,jitahidi nawe ukapumzike baada ya kumaliza kazi zako .Usiku ulikuwa mrefu sana.Mambo mengi yametokea usiku wa kuamkia leo.”

    “ Pole sana Mathew.Umechoka sana .Hata mimi ninaenda kupumzika muda si mrefu .Nataka kwanza nishughulikie lile suala la ndege alilo omba Dr Michael” akasema Anitha

    “ Ok Anitha.Nilisahau kusema ahsante sana.Bila wewe tusingeweza kufanikiwa zoezi lile la kumuokoa mke wa Dr Michael”akasema Mathew na kutabasamu kisha akaondoka na kwenda katika mlango wa chumba cha Dr Michael akagonga na mlango ukafunguliwa

    “ Hallow Mathew” akasema Dr Michael

    “ Dr Michael mkeo anaendeleaje?

    “ Anaendelea vizuri sana Mathew”

    “ Sawa Dr Michael ,mimi ninakwenda kupumzika kidogo .Ninachoweza kusema ni ahsante sana kwa msaada wako mkubwa.Bila wewe tusingeweza kufanikiwa kuufahamu ukweli wa kilichomuua Dr Flora.Kwa sasa mnaweza kuendelea kupumzika wewe na familia yako Anitha anaendelea kufanya utaratibu wa kupata ndege na atakapofanikiwa atawafahamisha.”

    “ Ahsante sana pia Mathew.Familia yangu iko salama sasa kwa sababu yako .Bila wewe na timu yako tusingeweza kuwa pamoja tena.Sintokushau katika maisha yangu yote.Lakini kuna jambo moja dogo ninahitaji kukuomba.”

    “ Omba chochote Dr Michael”

    “ Tutahitaji kwenda nyumbani kwetu kuchukua vitu vyetu muhimu kama vile mavazi,nyaraka za kusafiria n.k kwa hiyo tutahitaji ulinzi”

    “Usijali Dr Michael,tutawapeleka nyumbani kuchukua kila kitu mnachokihitaji” akasema Mathew na kuondoka akaelekaa chumbani kwake na kujilaza kitandani

    .Picha ya matukio yote yaliyotokea usiku ule ikajirudia kichwani

    “ Ulikuwa ni usiku mbaya sana.Damu imemwagika na tumempoteza kanali Adolf.Pamoja na hayo tumefanikiwa kupata kile tulichokuwa tukikihitaji.Tumempata mke wa Dr Michael na tumefanikiwa kufahamu kile kilichomuua Dr Flora.Ngoja niipumzishe akili yangu kidogo kabla ya jua kuchomoza “ akawaza Mathew na kufumba macho na hazikupita dakika tano kijiusingizi kikampitia



    *******



    Ulikuwa ni usiku mrefu sana kwa Jason.hakuweza kupata usingizi usiku ule kwa mawazo mengi yaliyokijaa kichwa chake.Kubwa lililoisumbua akili yake ni tukio lililotokea nyumbani kwa peniela.Picha ya Jaji Elibariki na peniela wakifanya mapenzi katika sofa sebuleni kwa Peniela ilimtesa sana.Picha nyingine iliyokuwa ikimfanya atetemeke na uogopa kila akiikumbuka ni ile ambayo Elibariki alikuwa amelala chini huku damu nyingi ikimtoka baada ya kumpiga na chupa.

    “ Mwili wote unanitetemeka sana kila nikilikumbuka tukio lile.Sijui nimeua! ..akawaza Jason

    “ Sijui nini kitatokea endapo nitakuwa nimeua.Sielewi nini kilinitokea hadi nikachukua uamuzi ule wa kumpiga Elibariki na chupa.Nadhani ni hasira zilivuka mipaka ndiyo maana nikaamua kuchukua uamuzi ule” akaendelea kukumbuka .Akaumia sana

    “ Katika maisha yangu sijawahi kupigana na mtu yeyote yule jana ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kupigana tena na mtu ninayeheshimiana naye sana kama Elibariki.”

    Picha ya Elibariki na Peniela ikamrudia tena

    “ Sikujua kama Elibariki ni mtu mshenzi namna ile.Ni mtu niliyemuheshimu sana lakini kwa tukio la jana sintomuheshimu kamwe.Siku zote kumbe alikuwa akimtamani Peniela.Kumbe mipango yake yote ya kutaka kumtafuta muuaji wa Edson ni kwa ajili ya kujiweka karibu na Penny.Baada ya kuona juhudi zake za kumpata Peniela zinashindikana akaamua kutumia nguvu.Angejua namna ninavyompenda Peniela katu asingethubutu kufanya vile alivyofanya.” Akainuka na kwenda nje baada ya dakika tatu akarudi tena ndani

    “ Natamani nimpigie simu Peniela nifahamu anaendeleaje na nini kilitokea baada ya ugomvi ule.” Akaichukua simu yake na kuzitafuta namba za Peniela akampigia.Simu ya Penny haikuwa ikipatikana.

    “ Amezima simu.Inawezekana kukawa na tatizo kubwa lililotokea na ndiyo maana amezima simu yake.Nitamtafuta tena baadae. Sintoweza kukimbia ,kama nitakuwa nimeua basi nitasubiri hapa nije nikamatwe na hatua stahiki zichukuliwe Pamoja na yote bado ninampenda sana Peniela na siku zote ataendelea kuwa ni mwanamkeninayempenda kuliko wote katika hii dunia na kama jaji Elibariki hatakuwa amekufa nitafanya kila linalowezekana mpaka mimi na Penny tuishi pamoja kwani hata yeye mwenyewe amekwisha onyesha kila dalili kamba ananipenda . Ngoja nilale nisubiri kama watakuja askari asubuhi kunikamata kwa mauaji endapo Elibariki atakuwa alifariki baada ya kumpigana ile chupa kichwani.He deserved that” Jason akawaza na kulala kwani macho yalikuwa mazito sana kwa usingizi



    ******



    Kumepambazuka Dar es salaam na kijua tayari kimechomoza.Jaji Elibariki alistuka toka usingizini akatazama saa yake ilipata saa moja na dakika nane.Simu yake ilikuwa imezima haikuwa na chaji.Alihitaji kuwasiliana na mke wake Flaviana akatoka mle chumbani na kuelekea sebuleni ,akamkuta Noah

    “Noah,habari za asubuhi ? Unaendeleaje na jeraha? akauliza

    “ Habari za asubuhi nzuri,ninaendelea vizuri .Vipi wewe unaendeleaje?

    “ Hata mimi ninaendelea vizuri japokuwa nasikia maumivu kwa mbali.Watu wote bado wamelala?

    “Ndiyo bado wamelala.Wamechoka sana kwa kazi ya jana usiku”

    “ yah ! kazi ya jana haikuwa ndogo.Noah unaweza ukaniazima simu yako nahitaji kumpigia mke wangu simu yangu haina chaji hata kidogo ” akasema Elibariki.Noah akampatia simu yake akaziandika namba za Flaviana akampigia

    “ Hallow “ akasema Flaviana

    “ Hallow Flaviana ,samahani nimetumia simu nyingine kukupigia simu yangu imekwisha chaji” akasema Elibariki

    “Eli,uko wapi? Are you ok? Akauliza Flaviana

    “ I’m ok Flaviana.Unaendeleaje?

    “ Ninaendelea vizuri sana.Vipi wewe unaendeleaje? Akauliza Flaviana

    “ Ninaendelea vizuri pia.Kuna habari gani hapo msibani ?

    “ Ratiba imeshatolewa na leo kutakuwa na zoezi la kumuaga mama ambalo litafanyika katika viwanja vya ukombozi ili kuwapa nafasi watu wengi waweze kumuaga.Kesho tutaelekea kijijini kwa mazishi.Vipi kuhusu lile suala umefikia wapi?”

    “ Flaviana ninahitaji kuonana nanyi wewe na Anna asubuhi hii .Naomba tukutane pale kwenye mgahawa wa Maria Stella.Utanikuta ninakusubiri pale.Tafadhali kuweni makini sana”

    “kwani kuna nini Eli mbona unaniogopesha?

    “Ni kuhusiana na lile suala .Kuna mambo ambayo nahitaji kuwafahamisha.” Akasema Elibariki na kukata simu.

    “Noah kuna jambo lingine ambalo naomba unisaidie. Nahitaji kufika sehemu fulani asubuhi hii lakini siko na gari langu.Nahitaji kuongea na Mathew ili kama kuna uwezekano aniazime gari lake moja linifikishe sehemu Fulani nikaonane na mke wangu.”

    “ Mathew bado anapumzika mida hii lakini usihofu nitakupeleka mimi” akasema Noah

    “ Noah utaweza kuendesha gari na maumivu uliyonayo?

    “Usijali Elibariki,nitaweza kuendesha.Maumivu ni vitu tulivyovizoea ”akasema Noah na kuinuka wakaingia katika mojawapo ya gari la Mathew wakaondoka na kuelekea moja kwa moja katika mgahawa unaomilikiwa na dada mmoja aitwaye Maria stella.Noah akamuacha Elibariki pale akarejea.Baada ya dakika kama ishirini hivi toka awasili pale mgahawani Flaviana na Anna wakatokea .Walikuja na gari la kukodi.Flaviana akastuka baada ya kumuona mume wake akiwa na jeraha kichwani

    “Eli umefanya nini hilo jeraha ? Akauliza

    “ Ni katika purukushani za jana.Kulikuwa na kazi nzito”akasema jaji Elibariki.

    “Pole sana mpenzi wangu.Najuta ni kwa nini nilisababisha ukaingia katika jambo la hatari kama lile.Usiku kucha wa leo sijaweza kupata usingizi hata kidogo nikifikiria kama utakuwa salama”akasema Flaviana

    “ Usihofu mke wangu,ilikuwa ni kazi ya hatari sana lakini namshukuru Mungu imemalizika na niko salama”

    “Pole sana shemeji”akasema Anna

    “Nimekwisha poa Anna” akasema Jaji Elibariki halafu akafika muhudumu na kuwahudumia supu halafu Flaviana akauliza

    “kwa hiyo umelala wapi leo?

    “ Ilinilazimu kulala sehemu salama kutokana na hali ilivyokuwa.”akasema

    “ Ile kazi haikuwa rahisi lakini nashukuru Mungu imekwisha salama na tayari tumegundua nini kimemuua Dr Flora”

    “ Ouh thanks God”akasema Flaviana

    “Mmegundua ni nini? akauliza Anna

    “ Tulifanikiwa kuingia katika hospitali ile ya jeshi tukaanza kufanya uchunguzi lakini wakati tukiendelea,ukanipigia simu ikatulazimu kuondoka haraka sana lakini tuliondoka na sampuli kadhaa ambazo tulikwenda kuzifanyia uchunguzi katika maabara nyingine.Katika uchunguzi huo ilibainika kwamba Dr Flora alichomwa dawa iitwayo Encozynes ambayo hutumiwa na wagonjwa wa shinikizo la damu.Natumai hata Dr Flora alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu”akasema Mathew

    “ Ndiyo alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu kwa muda mrefu”akasema Flaviana

    “ Dawa hiyo ina kiambata kiitwacho Spinolin ambacho huweza kusababisha madhara kwa mgonjwa endapo itatumika kwa kiwango kikubwa na ndiyo maana dawa hii hutumika katika kiwango kidogo sana.”akanyamza kidogo halafu akaendelea

    “ Vipimo vinaonyesha kwamba Dr Flora alichomwa kiasi kikubwa cha dawa hii hatari na hivyo kusababisha kifo chake ghafla”

    Anna akainama akashindwa kuyazuia machozi kumtoka.Flaviana naye michirizi ya machozi ikaonekana mashavuni pake.

    “Ladies please not now.Tafadhali msianze kuangua kilio humu mgahawani ”Jaji Elibariki akatoa angalizo

    “ They killed my mother”akasema Anna

    “ Anna please futa machozi.Huu si wakati wa kulia tena.Ni wakati wa kuutafuta ukweli wa jambo hili”akasema Elibariki.Baada ya Flaviana na mdogo wake kufuta machozi akaendelea

    “ Kutokana na majibu haya kuna mambo ambayo lazima tujiulize.Kubwa ni kwa nini uchunguzi wa kifo cha Dr Flora uzuiliwe? Nyote ni mashahidi juhudi kubwa zimefanyika ili kuhakikisha kwamba mwili wa Dr Flora haufanyiwi uchunguzi ili kubaini ni kitu gani kimemuua.Waliokuwa wakifanya juhudi ili jambo hili lifanyike ni wazi walielewa kilichokuwa kinaendelea.Jambo lingine la kujiuliza ni je dawa hii ilichomwa kwa uzembe au mchomaji alidhamiria kufanya alichokifanya? Majibu ya maswali haya ni magumu kwetu sisi kuyafahamu kwa hiyo ripoti hii anatakiwa apewe mheshimiwa rais yeye atatumia vyombo vyake kufanya uchunguzi wa jambo hili na kulipatia jawabu.” Akasema Jaji Elibariki

    “ Dr Kigomba lazima atakuwa anajua kuhusu jambo hili”akanong’ona Anna

    “ Unasemaje ana? akauliza Elibariki

    “Dr Kigomba lazima atakuwa akilifahamu suala hili.Yeye ni katibu wa baba na ndiye niliyemsikia akipiga simu akitoa amri madaktari wanaofanya uchunguzi kwa mwili wa mama wakamatwe haraka sana.Lazima ni yeye atakayekuwa amemuua mama” akasema Anna na macho yake yakaonyesha hasira za wazi.

    “Nakubaliana nawe Anna kwamba huyo Dr Kigomba anaweza akawa anahusika katika suala hili lakini lazima jambo hili lichunguzwe kuanzia mzizi wake.Kama ni kweli Dr Flora alichomwa dawa ile kwa makusudi kwa lengo la kuutoa uhai wake basi lazima kutakuwa na watu wengi wanaohusika na suala hili.Dr Kigomba hawezi kuwa peke yake.Unatakiwa ufanyike uchunguzi wa kina ili kuwabaini wote waliohusika katika suala hili aidha kwa uzembe au kwa makusudi. ” Akasema jaji Elibariki.

    “ Moyo wangu unakataa kabisa kuhusu ushauri wako Elibariki ,kwa nini suala hili tusilifanye wenyewe na kuubaini ukweli? Akasema Flaviana

    “Flaviana ushauri wako ni mzuri na tungeweza kulifanya suala hili sisi wenyewe kama tungeweza lakini hili ni suala kubwa zaidi ya unavyolifikiria.Huu ni uchunguzi wa kifo cha mke wa rais,huyu si mtu mdogo.Kama aliuawa basi ni kwa sababu nzito na kuifahamu sababu hiyo kunahitaji vyombo vya usalama.Kwa hiyo basi naomba ukubali tumuachie mheshimiwa rais suala hili atumie vyombo vyake vya usalama vifanye uchunguzi na kuufahamu ukweli wa jambo hili” akashauri jaji Elibariki.Flaviana akakubaliana na mawazo ya mume wake na bila kupoteza muda wakaingia katika gari na kuelekea moja kwa mojakatika makazi ya rais.

    Asubuhi hii katika makazi ya rais kulikuwa na pilika pilika nyingi.Ni siku ya kumuaga mke wa rais Dr Flora .Flaviana hakupoteza muda akaomba kuonana na baba yao kisha wakiambatana na jaji Elibariki wakaingia katika chumba cha maongezi.

    “ Pole sana mheshimiwa jaji.Ilikuwa ni ajali? ” Dr Joshua akampa pole jaji Elibariki baada ya kumuona na jeraha kichwani

    “ Ahsante sana mheshimiwa rais.Haikuwa ajali bali mkwaruzo mdogo tu,nilijigonga mahala” akasema Jaji Elibariki

    “ Flaviana mbona tumeitana asubuhi asubuhi namna hii kuna nini? Akauliza Dr Joshua

    “Baba kuna taarifa tunataka kukupatia.Ni kuhusiana na kilichosbabisha kifo cha mama”

    “ Ouh Flaviana,nilikwisha kueleza toka jana kwamba nitalifanyia uchunguzi suala hili na hivi tunavyoongea tayari madaktari wako katika uchunguzi.Kabla ya mwili kupelekwa viwanja vya ukombozi kwa kuagwa tayari tutakuwa tumepata majibu nini kilisabisha kifo cha mama yenu.Msihofu wanangu tutafahamu tu muda si mrefu nini kilimuua mama yenu.” Akasema Dr Joshua

    “ Baba tayari tunafahamu nini kilimuua mama “

    “Mmefahamuje” akauliza Dr Joshua kwa mstuko kidogo

    “ Unakumbuka jana nilikufahamisha kwamba nimemuomba mume wangu anisaidie kufanya uchunguzi wa siri?

    “Ndiyo nakumbuka”

    “ Basi Elibariki na jopo lake walifanikiwa kuufanya uchunguzi huo kwa siri licha ya amri ya kuusimamisha iliyotolewa na ripoti yake ni hii hapa” akasema Flaviana na kumkabidhi Dr Johua bahasha yenye ripoti.

    “ Mheshimiwa jaji pole sana kwa misuko suko.Jana alinifuata mwenzako akiwa na mdogo wake na kunieleza mambo mazito ambayo sikuwa nikiyafahamu.Kwa kuwa ndiyo kwanza niliyasikia ninahitaji muda wa kuyachunguza zaidi na kuubaini ukweli.Ripoti yenu inasemaje? Mmegundua ni kitu gani kilimuua Dr Flora? Akauliza Dr Josha akimuelekezea macho jaji Elibariki

    “ Mheshimiwa rais ,uchunguzi tulioufanya unaonyesha kuwapo kwa sumu aina ya Spinolin .Hiki ni kiambata kinachopatikana katika dawa aina ya Encozynes inayotumiwa na watu wenye shinikizo la damu.Dawa hii hutumiwa katika kiwango kidogo sana na endapo ikitumika katika kiwango kikubwa inaweza kusababisha kifo.Uchunguzi unaonyesha kuwapo kwa kiwango kikubwa cha spinolin dalili kwamba Dr Flora alichomwa kiwango kikubwa cha dawa hii na hivyo kusababisha kifo chake.Maelezo ya kitaalamu zaidi namna dawa hiyo inavyofanya kazi yapo ndani ya hiyo bahasha”akasema Jaji Elibariki.Uso wa Dr Joshua ukabadilika .Akamtazama jaji Elibariki kwa muda wa kama sekunde Arobaini hivi halafu akasema

    “ Nashukuru sana mheshimiwa jaji.Good job.Taarifa hii imenistua sana na ninaombeni mnipe muda niwezekulifanyia kazi ili kuwabaini wote waliofanya kitendo hiki” akasema Dr Joshua.

    “ Baba hiki kitu kilicho wazi kabisa.Watu waliofanya hivi wanajulikana kabisa.Dr Kigomba ndiye aliyetoa amri uchunguzi wa kifo cha mama usifanyike.Anatakiwa akamatwe na awataje wenzake”akasema Anna huku akilia.Dr Joshua akamfuata na kumbembeleza

    “ Anna nyamaza usilie.Najua umeumizwa sana kwa jambo hili.Natamani sana ningefanya kama hivyo unavyoshauri nifanye lakini mambo hayaendi namna hiyo.Uchunguzi wa jambo hili ni mkubwa .Naombeni mniachie suala hili nilishughulikie .Nina watu wangu ambao wanaweza wakaifanya kazi hii kwa umakini mkubwa.Yeyote ambaye amehusika katika suala hili lazima apate adhabu stahili.”akasema Dr Joshua

    “ Flaviana na Anna ,tafadhali naombeni mliache suala hili katika mikono ya mzee ili alishughulikie kama alivyoahidi. “ akasema Jaji Elibariki.Flaviana na mdogo wake wakakubali kuliacha suala lile katika mikono ya rais

    “ Muda unakwenda kwa kasi,nendeni mkajiandae mtaongozana na msafara kuelekea hospitali kuufuata mwili .” akasema Dr Joshua na wanae wakatoka kwenda kujiandaa.Dr Joshua akabaki chumbani amesimama akiwaza.Halafu akachukua simu na kuzitafuta namba fulani akapiga

    “ Hallo Mr president” ikasema sauti ya upande wa pili

    “ Dr Kigomba,mambo yamebadilika.Wale jamaa walifanikiwa kufanya uchunguzi na wakagundua kila kitu”

    “ What ?!! Dr Kigomba akashangaa

    “ Hapa nilipo nimeishika bahasha yenye maelezo ya kuhusiana na kilichomuua Flora.Umefanyika uzembe mkubwa sana na tusipofanya juhudi za haraka kila kitu kitaharibika.”

    “ Ok mzee usijali,we’re going to fix this.Hivi tunavyoongea Amos anatengeneza ripoti ya kifo cha Flora.Ikishapatikana ripoti hiyo,ikatae taarifa waliyokuletea,na uwaonyeshe ripoti ya kwetu ambayo itaonekana imetoka hospitali kuu ya taifa na uchunguzi umefanywa na madaktari bingwa.Baada ya hapo tutaangalia namna nyingine ya kufanya”akasema Dr Kigomba

    “ Ok good plan.lakini kuna jambo lingine.”

    “ Jambo gani mzee?

    “ Tunatakiwa tumuondoe Amos katika picha.Yule ni hatari sana kwetu kwani yeye ndiye aliyemchoma Flora sindano ile.”

    “ Una maana tumuue?

    “ yah.Kuendelea kuwa hai ni jambo la hatari kubwa sana kwetu”

    “ Ok nimekuelewa mzee” akasema Dr Kigomba.

    ‘One more thing”

    “Nakusikiliza Mzee’

    “ Keep an eye on my daughters.Wanatakiwa wachunguzwe nyendo zao,wanahusiana na nani ,wanaongea na nani na wanaongea nini.Hawa nao wanaweza kuwa ni hatari kubwa sana kwetu.Endapo itaonekana kwamba wanaweza wakasababisha hatari sintakuwa na njia nyingine zaidi ya kuwaondoa katika picha pia.Mtu mwingine ni jaji Elibariki.Yeye ndiye aliyeshughulikia uchunguzi huu ukafanyika.Huyu ndiye nyoka mwenye sumu kali sana.Huyu naye inatakiwa itafutwe namna ya kumuondoa haraka sana.Tayari anafahamu kilichotokea na hatujui amekwisha mueleza nani .Kabla ya kuanza na Amos,anza kwanza na Jaji Elibariki.“

    “ Ok nimekuelewa mzee,nitalifanyia kazi hilo suala “

    “ Kigomba ,naomba utambue kwamba hii ni nafasi ya mwisho ninakupa.Please don’t mess up.”

    “ I wont mr President” akasema Dr Kigomba na Dr Joshua akakata simu.Alikuwa akiangalia juu ya dari akiwa na mawazo mengi sana.

    “ Suala hili linaanza kufuka moshi.Inatubidi kuwahi mapema kuuzima moto ule kabla haujaanza kuwaka na kusambaa .Ukiwaka moto huu hautazimika na utatuunguza wengi.I wont let that happen.kwa gharama zozote zile lazima nihakikishe ninalizima suala hili” akawaza Dr Kigomba na kutoka mle katika chumba maalum cha maongezi ya faragha cha mheshimiwa rais



    ******



    Jiji la Dare s salaam limeamshwa na habari kubwa ya kifo cha kanali Adolf.Karibu magazeti yote yaliandika kuhusiana na habari ile lakini hakuna hata gazeti moja lilioandika habari ya kweli kuhusiana na nini kilisababisha kifo cha kanali Amos.

    Akiwa bado kitandani ,Peniela alisikia kitu kama mlio wa simu na alipofumbua macho ni kweli ile simu anayotumia kuwasiliana na rais ilikuwa inaita.

    “ Joshua anataka nini asubuhi yote hii?akajiuliza huku akiunyoosha mkono na kuichukua simu ile

    “ Hallo Dr Joshua”

    “ Hallow Penny.Bado umelala?

    “ Bado asubuhi sana Dr Joshua”akasema Penny.Dr Joshua akacheka kidogo na kusema

    “ Ok Peniela.Nimekupigia kukutaarifu kwamba leo inafanyika shughuli ya kumuaga mke wangu katika viwanja vya ukombozi na kesho tutamzika kijijini kwao.Nimemkabidhi Kareem jukumu zima la kukuhamisha siku ya leo.Nitawasiliana nawe tena baada ya kurejea kesho kutoka katika mazishi”

    “Ahsante sana Dr Joshua.Nakutakia safari njema hapo kesho.Nina hamu sana ya kuongea nawe mambo mengi lakini tutaongea ukisharudi” akasema Peniela

    “Usijali malaika wangu ,hata mimi nina mambo mengi sana ya kuongea nawe.Kwa heri kwa sasa”akasema Dr Joshua na kukata simu

    Hazikupita hata dakika tano toka akate simu,kengele ya getini ikalia akaamka na kwenda kufungua akakutana na kareem

    “ Kareem karibu sana “ akasema Penny na kumkaribisha Kareem ndani

    “ Penny ,mheshimiwa rais amenikabidhi mimi kazi ya kuhakikisha leo unahamia katika lile kasri.Nimekuja mapema namna hii nataka tuelekee katika maduka ya fenicha na uchague kila kitu unachokihitaji kiwepo ndani ya ile nyumba .Hutakiwi kuchukua kitu chochote toka huku kwako hata nguo.Kila kitu utanunua kipya..”akasema Kareem.Penny hakujibu kitu akabaki akitabasamu akaelekea chumbani kwake akaoga na kujiandaa kwa ajili ya mizunguko ya siku ile.Alikusanya baadhi ya vitu vyake vidogo vidogo na bila kulisahau kasha alilopewa na John Mwaulaya.

    “Hii yote ni katika kuhakikisha kasha hili linakuwa salama.”akawaza huku akilishika kasha lile akalipakia katika sanduku lle kubwa na kulikokota akatoka mle chumbani.Kareem akamsaidia kulibeba sanduku lile hadi katika gari ,Penny akafunga milango yote ya nyumba yake kisha akaingia garini na kuondoka”

    “Safari ya kuelekea katika maisha mapya imeanza.” Akawaza akiwa garini.

    RAIS WA JAMHURI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JOSHUA AMEIPOKEA RIPOTI YA UCHUNGUZI ULIOFANYWA KWA SIRI NA AKINA MATHEW NINI KITAWATOKEA WATOTO WAKE ANNA NA FLAVIANA PAMOJA NA JAJI ELIBARIKI? PENIELA TAYARI AMEHAMIA KATIKA NYUMBA ALIYOPEWA NA DR JOSHUA .MWISHO WA PENIELA SEASON ONE..


    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog